MASOMO YA KI-ISLAMU
MUONGOZO KWA WASOMAJI
KIMEANDIKWA NA: OMAR JUMAA MAYUNGA
KIMETOLEWA WAVUNI NA TIMU YA: AHLUL BAYT DIGITAL ISLAMIC LIBRARY PROJECT
Alhamdulillah, Rehma na Amani zimshukie Mtume wetu na Muombezi wetu Muhammad(s.a.w.w) na Aali zake watukufu waliotakaswa. Ninamshukuru zaidi Mwenyeezi Mungu kwa kuniwafiqisha kuchapisha kitabu: Muongozo wa Wasomao, kama alivyoniwafiqisha kabla ya hiki kuchapisha vitabu: Mut'a ndoa sahihi na Meza ya uchunguzi na vingine vingi, Alhamdulillah, Muongozo wa Wasomao, ni kitabu kilichokusanya maudhui nyingi tofauti kwa muhtasari. Ndani yake tumejaribu kufafanua baadhi ya mambo yaliyoeleweka kimakosa, kwa kuonyesha ushahidi na rejea zake. Nataraji hili litakuwa ni kichocheo cha wasomi (masheikh) kutufunulia yaliyofichikana au kufahamika kimakosa katika tarikh ili waislamu wapate ufahamu vyema Uislamu wao. Ee Mola weta! Tuonyeshe Haki tuifahamu kuwa ni haki uturuzuku kuifuata. Na tuonyeshe batil tuifahamu uwa ni batil uturuzuku kuiepuka.
Omar Jumaa Mayunga 9 Shaaban 1413 1 Februari 1993 Dar Es Salaam
MASOMO YA KI-ISLAMU
MUONGOZO KWA WASOMAJI
MWANZO WA WAHY
Amesema Bukhari na Muslim na wengineo kuwa: Imepokewa kutoka kwa Azzuhry naye amepokea kwa U'rwa bin Zubeir naye amepokea kwa Mwana Aisha (mkewe Mtume) kwamba: Malaika Jibril(a.s) alikuja kwa Mtume(s.a.w.w) naye akiwa katika pango la Hiraa akamwambia: Soma, Mtume akajibu: Mimi sijui kusoma. Mtume anasema: Malaika akanikaba kwa nguvu mpaka nikazidiwa kisha akaniambia: Soma, Mtume akajibu: Mimi sijui kusoma. Kisha ndipo Malaika alipomsisitiza kwa nguvu akisema: "Soma kwa jina la Mola wako, ambaye ameumba. Amemuumba mwanadamu kutokana na damu iliyoganda. Soma na Mola wako ni Mtukufu kuliko wote " Qur'an; 96:1-3.
Baada ya hapo, Mtume(s.a.w.w) alirudi kwa mkewe mwana Khadija(a.s) akiwa amejawa khofu kubwa. Alipoingia ndani alijitupa chini na huku akilalamika: "Nifunikeni, nifunikeni!!" Alipotulia akasema: "Ninaogopa sijui kitanipata nini?!" Khadija akamtuliza: "Sivyo! Wallahi Mwenyeezi Mungu hatakuangamiza abadani, wewe unaunga udugu, unavumilia matatizo, unasaidia wanyonge, unasaidia kuleta haki." Hapo Khadija akamchukua Mtume akampeleka kwa Ibnu ammi yake Waraqa bin Nawfal (alikuwa mnasara, mwandishi wa Injili kwa lugha ya kiibrania). Walipofika kwa Waraqa, Khadija akamwambia: "Ewe Ibnu ammi! Msikilize Muhammad aliyo nayo." Waraqa akamuuliza, "una nini?" Muhammad akamwelezea yote kama aliyoyaona, Waraqa akamwambia: "Huyu ni Malaika ambaye amepata kumteremkia vilevile Nabii Musa(a.s) Ee!" Natamani kama nitakuwa hai wakati watakapokufukuza watu wako! Muhammad(s.a.w.w) akashituka: "Watanifukuza?" Waraqa akajibu: "Ndiyo, hakuna mtu yeyote anayeleta jambo kama hili uliloleta wewe isipokuwa atapigwa vita na watu wake".[1]
Madda hii (mwanzo wa Wahy) waandishi wameieleza kwa njia nyingi tofauti zenye kugongana. Hapa tutajaribu kuzitaja chache tu:
A . Khadija na Abubakr walimpeleka Muhammad(s.a.w.w) kwa Waraqa bin Nawfal baada ya kuelezwa Waraqa kuwa Muhammad amepata matatizo, Waraqa akamuuliza Muhammad ana nini? Muhammad(s.a.w.w) akamwambia: "Ninasikia ninaitwa nyuma yangu, ewe Muhammad ewe Muhammad, nikisikia hivyo mimi hukimbia ovyo." Waraqa akamkataza asiwe anakimbia bali akaze roho ili ayasikie anayoambiwa..." Muhammad alishika maelekezo hayo, mara aliposikia akiitwa: Ewe Muhammad! Sema, Bismillahir Rahmanir Rahim, Alhamdulillahi rabbil a'lamina.... mpaka mwisho wa suratul Fatiha. Akaambiwa: Sema: "Laa ilaha illallahu" Muhammad(s.a.w.w) baada ya hapo alikwenda kwa Waraqa bin Nawfal, akamjulisha hali hiyo. Waraqa akambashiria habari njema yakuwa: "Hali kama hiyo alipewa pia Nabii Isa bin Maryam".[2]
B . Khadija alipompeleka Muhammad(s.a.w.w) kwa Waraqa na akamweleza yaliyomtokea. Waraqa alisema: "Huyu ni Nabii wa Umma huu, mwambie atulize moyo."[3]
C . Khadija alimwambia Muhammad(s.a.w.w) atakapokufikia huyo anayekusomesha, unambie, Mtume(s.a.w.w) alipofikiwa na hali hiyo akamjulisha mkewe. Khadija akampakata katika mapaja yake, kisha akavua shungi yake, mara Mtume(s.a.w.w) akaona yule aliyemjia anaondoka haraka. Mtume akamjulisha mkewe hilo, Khadija akasema, "Huyo ni Malaika, na wala siyo shetani, basi kaza roho na furahi".[4]
D . Waraqa bin Nawfal alimwambia Khadija: "Muulize Muhammad(s.a.w.w) nani anaemjia! Ikiwa ni Malaika Mikaeli basi amemletea amani. Na ikiwa ni Malaika Jibril basi amemletea vita na mateka. Khadija Alipomuuliza Mtume(s.a.w.w) akajibu: "Ni Jibril". Khadija akapiga uso wake.[5]
E . Khadija alipewa kipande cha karatasi na mganga mmoja ili ampe Muhammad(s.a.w.w) kama hali hii (iliyomfikia Muhammad) inasababishwa na ugonjwa wa kichaa, basi atapona... Khadija aliporudi kwa mumewe akamkuta anasoma Qur'an, Khadija akamchukua akaenda naye kwa yule mganga, walipofika kwa mganga, akafunua mgongo wa Mtume akaona muhuri wa Utume uko kati ya mabega mawili![6]
F . Muhammad(s.a.w.w) alipofikiwa na hali hiyo (ya kujiwa na Malaika) alikuwa akipanda katika kilele cha mlima mrefu na akitaka kujitupa chini (ili afe).[7]
G . Muhammad(s.a.w.w) alirudi kwa mkewe (kutoka katika pango) akiwa nafuraha kubwa akamwambia mkewe: "Nataka kukueleza habari njema, mimi nimeona katika ndoto kuwa Jibril amenijulisha kwamba ametumwa na Mola wangu aje kwangu... Khadija akamwambia: "Furahi, wallahi Mwenyeezi Mungu hatakufanyia lolote ila lililokuwa la kheri... kisha Khadija akaenda kwa mganga wa kinasara, kuuliza uwezekano wa kumuona Jibril. Mganga alishangaa sana kusikia jina la Jibril katika nchi hiyo, kisha akasema kuwa: "Huyo ni Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu..."[8]
Kwa kweli tukitaka kuijadili mada hii kwa undani zaidi, itatulazimu tutumie muda mrefu katika kuchambua kifungu kimoja baada ya kingine. Na hilo litahitaji kuchukua nafasi ya kitabu kizima ili kujaribu kutatua utata huo. Lakini, kama wasemavyo wataalamu: "Maa Laa yudraku kulluhu laa yutraku kulluhu" yaani, "Yasiyowe za kupatikana yote, hayaachwi yote". Kwa hiyo nasi hatutaacha kutaja japo kidogo:
1. Kutokana na sanad ya Hadithi, ambapo mategemeo yake yamepokelewa katika sahihi mbili (Bukhari na Muslim) na zingine, ambazo zinaonyesha kama: Imepokewa kutoka kwa Az Zuhry kutoka kwa U'rwa bin Zubeir kutoka kwa Mwana Aisha. Sasa: hapa tutaangalia mambo ya fuatayo:
A . Az Zuhry na U'rwa hawa walikuwa wapinzani wa Imam Ali(a.s) na wakimtukana.[9]
Na Mtume(s.a.w.w) amesema juu ya Imam Ali(a.s) kuwa: "Yeyote mwenye kumtukana Ali basi amenitukana mimi na mwenye kunitukana mimi amemtukana Mwenyezi Mungu".[10]
Kwa hiyo, mtu mwenye kumtukana Mtume(s.a.w.w) hawezi kuwa mwema hata kidogo, licha ya kupokea mafunzo ya dini kutoka kwake.
A . Amma kuhusu Mwana Aisha (mkewe Mtume) ambae katika mwaka wa thelathini na sita Hijra, alitoka nyumbani mwake Madina kwenda Basra ili kumpiga Ali bin Abi Talib(a.s) na akafanya hivyo. Kitendo cha mke wa Mtume cha kutoka nyumbani mwake kwenda nje, ni jambo lililokatazwa na Mwenyeezi Mungu: "Na kaeni majumbani mwenu " Quran,33:33.
Mwana Aisha ameipuuza hukumu hii! Aidha, kitendo cha kumpiga Imam Ali(a.s) ni jambo linalomuweka mtu mahala pabaya. Imepokewa kutoka kwa A'diyyi bin Thabiti kutoka kwa Zuhry amesema: "Amesema Imam Ali kuwa: "Ninaapa kwa ambaye ameumba mbegu na akaumba upepo, hiyo ni ahadi ya Mtume kwangu mimi kuwa: Hanipendi mimi isipokuwa mu'umin na hanibughudhi (hanichukii) mimi isipokuwa mnafiki".[11]
Mwana Aisha ameipuuza hukumu hii! Nanikweli Mwana Aisha hampendi kabisa Imam Ali(a.s) . Hilo linathibitishwa na hali halisi, kwanza, amepigana na Imam Ali(a.s) na kupiga hakuanzi kabla ya kuchukia. Na alipopata habari Mwana Aisha kuwa Imam Ali ameuliwa, alisujudu kumshukuru Mwenyeezi Mungu![12]
Mwenyeezi Mungu anasema: "Haiwi kwa mwanamume aliyeamini, Mwenyeezi Mungu na Mtume wake wanapohukumu jambo wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotovu ulio wazi " Quran, 33:36.
1. Riwaya za tukio hilo zinagongana kama unavyoziona - kama utarejea kuzisoma utaliona hilo. Lakini, kwanini Jibril amkamate Mtume kisha amkamuekamue mpaka akaribie kuzimia!? Kwanini Mtume akubali kusoma baada ya kukamuliwa kwa nguvu mara ya tatu? Kwanini asikubali tu kusoma mara ya kwanza kabla ya mateso haya? Na, vipi Mtume arudi kwa mkewe akiwa na khofu kubwa kiasi hiki! Je! Muhammad(s.a.w.w) hakuwa na uwezo wa kumpiga kofi malaika huyo?! Kama alivyofanya hivyo Nabii Musa(a.s) alipoijiwa na Malaika I'zrail ili achukue roho yake, Musa alimpiga kofi moja tu mpaka jicho likang'oka![13]
Haiwezekani kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) alikuwa mwoga hivyo, na Nabii Musa tu peke yake awe shujaa wa kuwang'oa macho malaika!.
2. Kwamba, Mtume(s.a.w.w) aliingiwa khofu kubwa, Khadija na Waraqa walimtuliza mpaka akatulia. Sasa, tuangalie hali hii kama ifuatavyo:
A . Inawezekana kwa Mwenyeezi Mungu, kumpeleka Mtume ambaye hajui Utume wake yeye mwenyewe! Ila kwa Kuthibitishiwa na mwanamke na mnasara? Vipi jambo nyeti hili agundue mwanamke kuwa huo ni Utume na wala si kichaa (kama alivyodhani Muhammad) pia mnasara ajue yaqini kuwa huo ni Utume?! Hili linatupa kufikiri kuwa hawa (mwanamke na mnasara) ni wajuzi na watukufu zaidi kuliko Muhammad(s.a.w.w) .
B . Mwenyeezi Mungu anasema: "Na wakasema waliokufuru: mbona haikuteremshwa kwake Qur'an yote mara moja? Ndivyo ilivyo, ili tukuimarishe kwayo moyo wako na tumeipanga kwa mpango ." 25:32. "Waambie (Muhammad) roho takatifu ameiteremsha kutoka kwa Mola wako kwa haki, ili kuwaimarisha wale walio amini, na kuwa muongozo na habari njema kwa waliosilimu ." 16:102.
katika aya hizi timachunguza ibara isemayo: "Ilu Tukuimarishe Kwayo Moyo Wako ". Kwa hiyo, moyo wa Muhammad uliimarishwa na Mwenyeezi Mungu sikiliza Mwenyeezi Mungu analifafanua hili: "Waambie (Muhammad) hakika mimi ninayo dalili ya wazi itokayo kwa Mola wangu " 6: 57.
"Waambie (Muhammad) Hii ndiyo njia yangu, ninaita kwa ujuzi hasa, mimi na wanaonifuata ." 12:108.
Katika Aya hizi tunaangalia maneno: "Mimi Ninayo Dalili Ya Wazi Itokayo Kwa Mola Wangu" "Ninaita Kwa Ujuzi Hasa" kwahiyo, Mtume Muhammad(s.a.w.w) anajua kuwa anayo dalili (ushahidi) ulio wazi, na kwa ajili hiyo, anawaita watu kwa ujuzi kamili. Hii si sawa na kusema: Muhammad(s.a.w.w) uliimarishwa moyo wake na mnasara (Waraqa bin Nawfal).
Baada ya kujua mwaka wa Kiislaam unaanza tarehe gani ya mwezi gani, kisha umeingia utata juu ya jambo hili kuwa:
Muharram ndiyo mwanzo wa mwaka wa Kiislaamu kwa maana ya Hijra! Ndiyo maana unaona kila uingiapo Muharram baadhi ya Waislam hufanya hafla kubwa kuadhimisha, wakidhani kuwa umeingia mwaka mpya! Ukisoma tarikh utaona kuwa:
A . Imam Ali(a.s) alisema mwaka mpya uanze ile siku aliyofukuzwa Mtume(s.a.w.w) Makka akaenda Madina.
B . Imam Ali aliwaandikia watu wa Najran akasema.... "Na aliandika Ubeidullah bin Abi Rafii tarehe kumi mfungo tisa mwaka wa thalathini na saba kutoka Mtume (s.a.w.w) aingie Madina ".[14]
C . Imam Malik bin Anas anasema: Mwanzo wa mwaka wa Kiislaamu ni mfungo sita, kwa sababu ni mwezi ambao Mtume(s.a.w.w) amehama (kutoka Makka kwenda Madina).[15]
D . Assakhawy amepokea kwa Al'Asmai kuwa wao walikuwa wakiandika mfungo sita, ni mwezi aliohamia Madina Mtume(s.a.w.w) .[16]
E . Amesema Assahib bin U'bbad kuwa: Mtume(s.a.w.w) aliingia Madina tarehe kumi na mbili mfungo sita, na tarehe ikaanzia hapo. Kisha baadae jambo hili liligeuzwa likarudishwa mwezi wa Muharram".[17]
Suala la kuonekana Mwenyeezi Mungu, Waislaamu wamegawanyika makundi mawili, kuna wanaosema kuwa: Mwenyeezi Mungu anonekana hapa duniani na huko akhera. Na kuna wanaosema kuwa: Mwenyeezi Mungu haonekani hapa duniani wala huko akhera. Kila kundi lina hoja zake. Wasemao ataonekana wanategemea hoja mbili: Dalilul a'qly, Dalilun naqly.A. Dalilul a'qly - Kwa kupitia mantiq akili inaona kuwa: kwa kuwa chochote chenye kuwapo lazima uwiano wa kuonekana uwepo.
B . Dalilun naqly: Mwenyeezi Mungu anasema:
i.Na alipofika Musa kwenye miadi yetu, na akazungumza na Mola wake akasema: "Mola wangu! Nionyeshe ili nikuone." Akasema "Huwezi kuniona, lakini tazama jabali, kama litakaa mahala pake ndipo utaweza kuniona " Quran: 7:143.
ii. "Nyuso siku hiyo zitang'aa zikitazama kwa Mola wao " 75: 22-23
Kwanza, ni muhimu kuangalia maana ya tamko la "ARRU-UYA" yaani "KUONA". Taqriban tamko hili linatumika katika nyanja zifuatazo,
(a) Kuona kwa mboni za macho.
(b) Kuona kwa dhana.
(c) Kuona kwa yaqin.
Sasa: Inaposemwa: Mwenyeezi Mungu anaonekana, ni kwa kupitia kigezo gani kati ya vigezo vilivyotajwa hapo juu au chochote kingine. Ikiwa kuwepo kwa kitu ni sharti ya kuonekana, ni nani basi aliyethibitisha mpaka sasa kuwa ameiona Roho, Akili, Nguvu, Sauti, na kadhalika?! Kuhusu aya zilizosomwa kuthibitisha kuwa Mwenyeezi Mungu anaonekana, majibu yake ni kama ifuatavyo:
A . Nabii Musa(a.s) alikuwa akijua vyema kuwa Mwenyeezi Mungu haonekani duniani wala huko akhera. Wala hilo ombi lake hakukusudia kuomba jambo lisilo wezekana, isipokuwa Nabii Musa hapa ametumia uslub (njia) ya kukomesha madai ya watu wake ambao waling'ang'ania kumtaka awaonyeshe Mwenyeezi Mungu waziwazi kama tunavyo soma katika Qur'an: "Ewe Musa, hatutakuamini mpaka tumuone Mwenyeezi Mungu waziwazi ". 2:55
Kwahiyo, Nabii Musa(a.s) alitaka kumaliza ubishi wao, akatumia ibara kati yake na Mola wake ili afute kabisa matumaini ya ombi la watu wake. Qarina ya nukta hii ni pale aliposema Mwenyeezi Mungu kuwa: "Hakika walimuomba Musa makubwa kuliko hayo, na wakasema: Utuonyeshe Mungu wazi wazi ." 4:153
B . Iliposemwa: "Fasawfa Taraani " yaani "Utaniona" ibara hii imetanguliwa na tamko la: " LAN TARAANI " yaani, " HUTANIONA ABADANI " silabi ya " LAN " imekuja katika " NAFYU TAABID " " HUTANIONA ABADAN " matumaini ya kumuona Mwenyeezi Mungu hayako aslan, kwa mujibu wa maweko ya silabi na matumizi yake yaliyokuja katika Aya hii. c. Iliposemwa: " ILA RABBIHA NADHIRA ". yaani,Zikingoja Malipo Kwa Mola Wao " na wala siZikitazama Kwa Mola Wao , hiyo ni tasfiri ya kimakosa kama tutakavyoonyesha. Ku'unganishwa silabi ya "ILA" na silabi ya "Nadhar " hapa kunafidisha maana yaa "Kungojea " Tutaonyesha mfano hapa kuthibitisha hilo kama ifuatavyo: katika kitabu: Lisanul A'rab juzu ya saba ukurasa 72 imeandikwa hivi:- "Innamaa Nandhuru Ila Llahi Thumma Ilayka " akafafanua hapo hapo: "Innamaa Atawaqqau Fadhlallahi Thumma Fadhlak " Maana ya msitari wa kwanza "Kwa hakika tunangojea fadhila za Mwenyeezi Mungu, kisha fadhila zako" katika msitari wa pili, alikusudia kufafanua ibara isemayo: "Nandhuru Ila Llahi " akasema; "Atawaqqau Fadhla Llahi " yaani, "Ninangojea Fadhila za Mwenyeezi Mungu". Hivi ndivyo yalivyo matumizi ya silabi ya "ILA" inapokutana na silabi ya "NADHAR" mara nyingi.
Anasimulia Abu Huraira katika Hadithi aliyoipokea kuwa: (siku ya kiyama) "Mwenyeezi Mungu atawaijia (watu) akiwa na sura tofauti na ile wanayomjua, awaambie: Mimi ndiyo Mola wenu. (Watu) watajibu: Mwenyeezi Mungu atuepushe nawe, sisi tutabaki hapa hapa mpaka Mola wetu (tunayemjua) atufikie, na akija sisi tutamjua. Mara Mwenyeezi Mungu atawafikia kwa sura yake ile wanayomjua atasema: Mimi ni Mola wenu. Nao watajibu: (kweli) wewe ndiye Mola wetu, na watamfuata".[18]
Abu Huraira anaendelea kusimulia: "Watu walimuuliza Mtume(s.a.w.w) 'Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu! Hivi tutamuona Mola wetu siku ya kiyama?' Mtume(s.a.w.w) akajibu: 'Hivi mnapata pingamizi gani kwa kutazama mwezi wa siku kumi na tatu?' Wakajibu: 'Hatupati pingamizi yoyote.' Mtume(s.a.w.w) akauliza tena: 'Mnapata kizuizi gani kutazama jua ambalo halina mawingu?' Wakajibu: 'Hakuna kuzuizi chochote.' Mtume(s.a.w.w) akawaambia: 'Basi ndivyo matakavyomuona". Suhaybu anasimulia kuwa: Amesema Mtume kuwa: "Watu wa peponi watakapoingia Peponi, Mwenyeezi Mungu atawauliza: 'Mnataka niwaongeze kitu gani?' Watasema: 'Oh, umekwisha ng'arisha nyuso zetu, umetuingiza peponi na umetuepusha mbali na moto.' (Hapo) Pazia litaondolewa, eeh, hawajapewa kitu kilicho bora zaidi kuliko kumuona Mola wao. Kisha Mtume(s.a.w.w) akasoma aya: "Wale waliofanya wema watapata wema na zaid ". 10:26
Iliposemwa: (katika Aya iliyotangulia), "Waziyadah " maana yake: Kumuona Mwenyeezi Mungu"[19]
Tamko la "Azziyadah " katika sura ya kumi aya ya ishirini na sita ni: MUB'HAM halionyeshi chochote kuhusu kuona. Kwa hiyo, huwezi kwa tamko hilo kuthibitisha kuwa Mwenyeezi Mungu anaonekana. Bali lililothibiti waziwazi ni hivi asemavyo Mwenyeezi Mungu kuwa, "Maono hayamfikii bali yeye anayafikia "Maono", 6:103. Kwahiyo, zile hadithi zisemazo kuwa Mwenyeezi Mungu anaonekana ni batili kwa sababu zinapinga Aya. Mwenyeezi Mungu anakataa kuwa: "Maono hayamfikii" na maono ni zaidi kuliko macho!!
Ndugu zetu masunni wanaamini kuwa: Qur'an ni ya tangu na tangu (Qadim) Mashia Ithan Ashar wanaamini kuwa: Qur'an imeumbwa. Kwahiyo, hapa tutachunguza kama ifuatavyo:
Katika matumizi ya lugha ya kiarabu, tamko la "JAA'L". Linapotegemezwa kwa Mwenyeezi Mungu huwa kwa maana ya "KHALQ" yaani, "Kuumba ". Na hapa tutataja baadhi ya mifano hiyo:
A . "Wajaa'la min'ha zawjaha " yaani, "Na ameumba mkewe ".
B . "Huwalladhi jaa'la lakumul layla " yaani, "Yeye ndiye aliyewaumbia usiku ".10:6
C . "Inna jaa'lna maa'l ardhi ziinatan laha " yaani, "Kwa hakika tumeviumba vyote vilivyoko juu ya ardhi viwe mapambo yake ". 18:7
D . "Jaa'la laum min anfusikum az'wajan " yaani, "Amewaambieni wake katika jinsi yenu ". 42:11.
E . "Inna jaa'lnahu Qur'anan a'rabiyyan " yaani,hakika tumeifanya (tumeiumba) Qur'an (kwa lugha ya) Kiarabu ". 43:3
f. "Khaaliqu kulli shay'in " yaani, "Muumba wa kila kitu ". 6:102
Sasa, Qur'an ama iwe ni kitu au isiwe ni kitu. Kama itakuwa sikitu, basi yanini kujadili jambo ambalo halipo! Na endapo itasemwa kuwa Qur'an ni kitu, jee! Ni kwa hoja gani Qur'an itatolewa katika umuun ya ibara hii: "Muumba wa kila kitu"? Na hapana shaka yoyote, Qur'an ni kitu, kwa hiyo: kwakuwa vitu vyote vimeumbwa (kama isemavyo Qur'an) Qur'an nayo pia imeumbwa.
Maana ya Taqiyya, kama alivyo tafsiri Sahaba Abdullah ibn Abbas ni "Kusema kwa ulimi na hali moyo unatulia kwa imani". Kwa hiyo, Taqiyya ni kuficha imani ndani ya moyo, na kutamka kwa ulimi yaliyo kinyume na ya moyoni.[20]
Kwakupata ufafanuzi katika somo hili, tumsikilize Imam Bukhari anasema: "Imepokewa kutoka kwa Abu Dardai anasema: 'Hakika sisi wallahi tunawakenulia jamaa ili hali nyoyo zetu zinawalaani."[21]
Abu Dardai anatufahamisha hapa yakuwa: Wao wanapojumuika na baadhi ya watu wasioafikiana nao katika jambo fulani, huchanganyika nao kwa bashashi kubwa kwa kicheko na kukenua mena kama kwamba wanakubaliana na yao. Kumbe ndani ya mioyo yao wanawalaani! Hii ndiyo Taqiyya tunayo izungumza hapa, na ndiyo Taqiyya aliyoisema Mwenyeezi Mungu: "Waumini wasiwafanye makafiri kuwa viongozi badala ya waumini. Na atakaefanya hivyo, basi hatakuwa na chochote kwa Mwenyeezi Mungu, isipokuwa kwa kujilinda nao sana " 3:28.
Iliposemwa: "Na atakaefanya hivyo" maana yake: "Atakaewafanya makafiri kuwa viongozi wake" Mwenyeezi Mungu anamwambia: "Hatakuwa na chochote kwa Mwenyeezi Mungu". Kwa mantiq hii, Mwislamu yeyote anayeongozwa na kafiri, hana chochote kwa Mwenyeezi Mungu. Mpaka hapa hukumu hii itawagusa Waislamu wengi sana! Lakini Alhamdulillah hali haiko hivyo, kwa sababu ibara katika Aya inaendelea kusema: "Isipokuwa kwa kujilinda nao sanasana".
Taqiyya imemuopoa Mwislamu katika hukumu aliyohukumiwa laiti isinge kuwapo Taqiyya. Kwa ajili hii, sahaba Ammar bin Yasir alipoadhibiwa na makafiri, akauliwa mama yake, Sumayya, mbele ya macho yake baada ya kuteswa sana. Hilo halikutosha, akachukuliwa baba yake Yasir akawekwa mbele ya macho yake, akateswa sana hatimae akauliwa, kisha ndipo walipomgeukia naye Ammar, akapigwa na kuteswa, Ammari ndipo alipotamka neno la kufru.
Alipofika kwa Mtume(s.a.w.w) Ammar aliliya sana na kusema: "Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, nitauweka wapi uso wangu ili hali mimi nimesema neno chafu (la kufru) baada ya kuteswa sana, na kuniulia mbele ya macho yangu wazazi wangu wawili baba na mama! Kabla Mtume(s.a.w.w) hajasema lolote Mwenyeezi Mungu akateremsha Aya: "Anayemkataa Mwenyeezi Mungu baada ya imani yake (ataadhibiwa adhabu kali) isipokuwa yule aliyelazimishwa hali moyo wake unatulia kwa imani " 16:106.
Mtume(s.a.w.w) akamsomea Aya hii Ammar bin Yasir, kisha akamwambia: "Basi, kama watarudia (kukutesa) rudia (nawewekuwapa maneno ya kufru).[22]
Hii ndiyo Taqiyya wanayoelekezwa waumini, kama ambavyo Taqiyya inamfikisha Mwislamu katika ngazi ya Uumini. Mwenyeezi Mungu anasema: "Na akasema mtu muumini aliyekuwa mmoja wa watu wa Firauni anayeficha imani yake, jee! Mtamuua mtu kwa sababu anasema Mola wangu ni Mwenyeezi Mungu ? 40:28.
Huyu bwana alionyesha ukafiri, akasihi pamoja najamaa yake Firauni, lakini kwa ndani alikuwa muumini kweli kweli, akatumia Taqiyya ili Firauni asimjue. Mpenzi msomaji! Bila shaka umeona nafazi ya Taqiyya iliyo nayo katika Uislamu, umefahamu kuwa Taqiyya ni kiungo muhimu sana kati ya Islam na Mwislamu. Umesoma Aya zilizozungumza kuhusu Taqiyya umemuona Sahaba Ammar bin Yasir alivyowakejeli makafir kwa kutamka neno Ia kufru, kisha Mtume(s.a.w.w) akaongeza kusema: "Kama Watarudia Nawe Rudia ".
Takriban, kuna aina tano za Tahrif, nazo ni kama ifuatavyo:
1. Kupungua, au kuzidi, harfu au haraka, wakatihuo huo Qur'an isipotee kitu chochote. Tahrif aina hii, inapatikana katika Qur'an, hili linashuhudiwa kama ifuatavyo:
A . Katika Surat Hud Aya 78 inasomwa: "HUNNA AT'HAARU LAKUM" katika silabi ya RAA kumetiwa dhamma, na katika qiraa kingine, inasomwa: "HUNNA AT'HARA" kwa nasbu.[23]
B . Katika Surat Sabai Aya 19 inasomwa: "RABBANAA BAAI'D BAYNA ASFARINA" na katika qiraa kingine, inasomwa:- "RABBANAA BAA'DA" kwa madhi.[24]
C . Katika Suratul Baqara Aya 259 inasomwa: "KAYFA NUNSHIZUHA" na katika qiraa kingine, inasomwa: "KAYFA NUNSHIRUHA" kwa silabi ya RAA badala ya ZAA.
D . Katika Suratul Waqia'h Aya 29 inasomwa:"WATWAL'H'IN MANDHUD" na katika qiraa kingine inasomwa: "WATWAL'I'N MANDHUD" kwa A'YN badala ya H'AA.
E . Katika Surat Saad Aya 23 inasomwa: "LAHU TIS'U'N WATIS'U'NA NAA'JAH" na katika qiraa kingine inasomwa: "LAHU TAS'U'N WATAS'U'NA".
2. Kupungua, au kuzidi neno moja au zaidi. Pamoja na kuwa nafsi ya Qur'an itabaki salama bila ya kupungua au kuzidi kitu. Katika zama za masahaba hali hii imetokea, ambapo Uthman bin Affan aliiunguza moto misahafu mingi. Na akatoa agizo kwa wawakilishi wake wote popote walipokuwa, waichome moto misahafu yote isipokuwa ile aliyoikusanya yeye.[25]
Kuzidi au kupungua katika Aya au sura. Pamoja na kuwepo ukamilifu wa Qur'an, na wakaafikiiana Waislamu wote kuwa: Mtume(s.a.w.w) aliisoma. Hali hii ipo, na mfano halisi ni kama ifuatavyo: "BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIM" Waislamu wote wanakubaliana kuwa, Mtume(s.a.w.w) alikuwa akiisoma kabla ya kila sura isipokuwa Suratut Tawba. Kwa ndugu zetu Masunni imetokea hitilafu kati yao kuwa: "Bismillahi" si katika Qur'an, wengine wakasema: Ni katika Qur'an.[26]
Ama Shia Ithna Ashar, wao wanakubaliana kuwa "Bismillahi" ni sehemu ya kila sura isipokuwa Suratut Tawba.
3. Kuzidi baadhi ya Aya au sura yasiyokuwa Maneno ya Mwenyeezi Mungu. Tahrif aina hii haikubaliwi na Waislamu wote.
4. Kupungua, yaani, Msahafu huu uliopo mikononi mwa Waislamu haukukusanya Qur'an yote iliyoteremshwa na Mwenyeezi Mungu, na kwamba Qur'an nyingine imepotea, Tahrif ama hii ipo, wako wanaothibitisha hilo, na wengine wanakataa kuwa haiko.
1
MASOMO YA KI-ISLAMU
MUONGOZO KWA WASOMAJI
WANAOTHIBITISHA KUWA IPO
A . Amepokea Ibnu Abbas kwamba: "Umar bnul Khattab, siku moja alipokuwa juu ya Mimbar alisema: "Sisi tulikuwa tukisoma katika Qur'an: AN LAA TARGHABU A'N ABAAIKUM FAINNAHU KFRUN BIKUM AN TARGHABU A'N ABAAIKUM"...[27]
B . Umar bnul Khattab alileta Ayatur rajmi ili itiwe katika msahafu, lakini haikuandikwa, kwa sababu Umar alikuwa peke yake hakuwa na shahidi.[28]
Aya yenyewe aliyoileta Umar inasomeka hivi: ASH'SHAYKHU WASH'SHAYKHATU IDHA ZANAYAA FARTUMUHUMAA ALBATTATA NAKAALAN MINALLAHI WALLAHU A'ZIZUN HAKIMUN".[29]
C . Inasimuliwa kuwa: katika mbao za Mwana Aisha ilikuwako Qur'an ikisomeka hivi: "INNA LLAHA WAMALAIKA TAHU YUSWALLUNA A'LAN NABIYY YA AYYUHA LLADHINA AMANU SWALLU A'LAYHI WASALLIMU TASLIIMA WA A'LALLADHI NA YUSWALLUNA ASSUFUFAL AWWALA" Mwana Aisha (mkewe Mtume) alikuwa nayo Qur'an hiyo kabla Uthman bin Affan hajabadilisha misahafu![30]
D . Anasema Mwana Aisha (mkewe Mtume) katika zama za Mtume(s.a.w.w) Suratul Ahzabi ilikuwa inafikia Aya mia mbili, lakini, ulipoandikwa msahafu Aya zikawa hivi kama zilivyo sasa ambazo ni sabini na tatu tu!! Aya mia moja ishirini na saba zimepotea![31]
Mizani ya kupima riwaya zilizo tajwa hapo juu kuonyesha kuwa kuna baadhi ya amma sura au aya zilizopotea, riwaya hizo na za mfano wa kama hizo ni batili, Mwenyeezi Mungu anasema: (Qur'an) "Haitaifikia batili mbele yake wala nyuma yake " 41:42
"Hakika sisi tumeiteremsha Qur'an, na hakika sisi ndio wenye kuilinda " 15:9. Hii ndio itikadi ya Shia Ithna Ashar.[32]
Wako baadhi ya Waislamu wanapinga kumsomea Qur'an maiti, wakisema kwamba kufanya hivyo ni bid'a na bid'a mahala pake ni motoni. Katika kupinga jambo hili wanatoa hoja zao kama ifuatavyo:
A . Imethibiti kuwa: Mtume(s.a.w.w) hakumsomea Qur'an maiti yeyote katika uhai wake, kama jambo hilo ni jema Mtume asingeliacha kufanya kheri hiyo. Kwa hiyo, yeyote leo anae soma Qur'an kwa ajili ya mait, akaamini kuwa itamnufaisha, bila shaka mtu huyo anadai kuwa Mtume amefanya khiyana katika umma huu. Na hilo ni kosa kubwa kuamini kuwa Mtume hakufikisha baadhi ya mambo katika umma wake.
B . Mwenyeezi Mungu anasema: "Na ya kwamba mtu hatapata isipokuwa aliyoyafanyia juhudi " 53:39.
Na kwa Aya hii Imam Shafi amesema kuwa: Kisomo (anachosomewa maiti) thawabu za kisomo hicho hazifiki kwa maiti. Kwa sababu hilo haliko katika matendo yake, na kwa sababu hii, Mtume hakuwawekea umma wake, wala hakuhimiza (wafanye) kwa mtu yeyote. Wala hakupendekeza, wala sahaba yeyote hakuna aliyepokea (jambo hili) [33]
C . Amesema Mtume(s.a.w.w) : "Anapokufa mwanadamu, matendo yake humalizika yote isipokuwa mambo matatu: sadaka ya kudumu, au elimu yenye kunufaisha, au mtoto mwema atakaemuombea baada yake ".
Kwa hiyo, wasomaji wa khitima hupoteza bure muda wao, kwa kufanya jambo haliko katika Uislamu.
Kabla ya kuingia katika majadiliano hayo ni vyema kuzingatia jambo mmoja, nalo ni "NINI QUR'AN"? Taarif ya Qur'an ni: "Maneno ya Mwenyeezi Mungu aliyoyateremsha kwa Mtume wake Muhammad(s.a.w.w) hali yakuwa ni muujiza wake" sasa, Ikisemwa kuwa: Mtume(s.a.w.w) hakuwasomea Qur'an maiti wake, huwa inakusudiwa Qur'an gani?? Kwa sababu, katika salatiil maiti mna Suratul Fatiha, na Mtume(s.a.w.w) aliwasalia mauti wake. Isipokuwa, ikithibitishwa kwa dalili kuwa: Suratul Fatiha si Qur'an[34] . Kuhusu Aya iambiwayo kuwa inazuia thawabu za Qur'an kumfikia maiti 53:39.
Tuangalie matni yake: "WA AN LAYSA LIL'INSANI ILLA MASAA", yaani, "Na yakwamba mtu hatapata isipokuwa aliyo yafanyia juhudi." Hivi ndivyo ananyosema Mwenyeezi Mungu na wala hasemi: "LA YANTAFIU'UL INSANU ILLA MASAA", yaani, "Hanufaiki mwanadamu isipokuwa kwa yale aliyoyafanyia juhudi". Hapa pana tofauti kubwa kati ya ibara ya kwanza na hii ya pili. Ibara ya kwanza inafidisha kuwa: "Mwanadamu atalipwa thawabu kwa mujibu wa matendo yake". Na ibara ya pili inafidisha kuwa: "Mwanadamu hanufaiki kwa chochote isipokuwa kwa matendo aliyoyatenda mwenyewe." Kwa ibara hizi ni sawa na kusema kuwa: "Athumani ana kibanda kidogo cha makuti, na humo ndimo anamoishi. Kwa hiyo, Athumani hana nyumba nyingine yoyote atakayoishi isipokuwa katika kipanda hicho. Lakini hali hii haizuii yeyote mkarimu kumjengea Athumani nyumba kubwa na bora. Mkarimu kama atajenga nyumba iliyo bora na kubwa, kisha akampa Athumani, haiwezi kusemwa: Athumani hawezi kukaa katika nyumba hiyo eti kwa sababu hakuijenga yeye. Amma Hadithi iamiwayo kuwa iazuia thawabu ya Qur'an kumfikia maiti isemayo: "IDHA MATA IBNU ADAMA IN'QATAA A'MALUHU ILLA MIN THALATHA..." yaani, "Anapokufa Mwanadamu matendo yake yote hukatika isipokuwa mambo matatu...." wala Hadithi haisemi: "IDHA MATA IBNU ADAMA IN'QATAA INTIFAU'HU" yaani, "Anapo kufa Mwanadamu humalizika kunufaika kwake". Ibara ya kwanza inafidisha kuwa: "Kinachomalizika ni matendo yake". Na ibara ya pili inafidisha kuwa: "Kinachomalizika ni kunufaika". Kwa mizani ya somo hili, natija inaonyesha kuwa Qur'an ikisomwa kwa ajili ya maiti, lazima thawabu ya kisomo hicho zitamfikia maiti, na hapa tutaonyesha hali tatu zilizo hai:
a . Mtume(s.a.w.w) amesema: "Man Mata Wa A'layhi Siyam Sama A'nhu Waliyyuhu ". yaani,atakae kufa na juu yake kuna saumu atafunga kwa niaba yake walii wake ". Hadithi hii imekubaliwa na Waislamu wote na hata Imam Shafi naye ameikubali. Je! Kama mlango wa kunufaika umefungwa, thawabu ya funga anayofanyiwa maiti na walio hai ingemfikiaje?
b . Mtume(s.a.w.w) alimwambia mwanamke mmoja: "Mhijie mama yako". Na akamwambia mwanamume: "Mhijie baba yako". Hadithi hii pia imekubaliwa na Waislamu wote, Je! Thawabu za hija anayohijiwa na walio hai zinamfikiaje maiti, kumbe mlango wa kunufaika umefungwa?
c . Mwenyeezi Mungu anasema: "Zinamtukuza mbingu saba na ardhi (saba) na vilivyomo ndani yake, na hakuna chochote isipokuwa kinamsabihi kwa sifa zake njema lakini nyinyi hamfahamu kutukuza kwao" 17:44.
Iliposemwa: "Na hakuna chochote isipokuwa kinamsabihi kwa sifa zake njema". Hii inafidisha kuwa: Vitu vyote vinamsabihi Mwenyeezi Mungu, na kwa kuelewa zaidi hili tumsikilize Mtume(s.a.w.w) . Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtume(s.a.w.w) alipita kwenye makaburi mawili akasema: Hawa waliomo katika makaburi haya wanaadhibiwa... Mara akaagiza kuti la mtende, akalipasua vipande viwili kisha akachimbiaa kimoja katika kaburi hili na kingine akachimbia katika kaburi lile, halafu akasema: Bila shaka vitawapunguzia (adhabu) madam havijakauka". Hiposemwa: "Madam havijakauka" inafidisha kuwa: Wakati wote vitakapokuwa vibichi (vipande vya kuti Ia mtende) vitakuwa vinamsabihi Mwenyezi Mungu. Hapa Mtume(s.a.w.w) ana thibitisha kuwa: Tasbihi za kuti zina mpunguzia adhabu maiti, kupunguziwa adhabu ni hatua ya kuingia mtu katika neema (pepo). Mpenzi msomaji! Tasbihi za kuti la mtende zitampa nafuu maiti, lakini Mwislamu akisoma Qur'an kwa ajili ya kumuombea maiti itakosa kumfikia?[35]
Kisha Sheikh Mkuu wa Tanzania alitoa fat'wa kwa kupitia Redio Tanzania kuwa: "Qur'an haikuchanwa" ingawa kwa maelezo yao - kama yalivyo kwenye kitabu: "Taarifa ya ujumbe wa Sheikh Mkuu" ukurasa 14 inasema: "Irshadul Muslimina kilichanwa kwa dharau" mwisho wa kunukuu. Kwa hiyo, Irshadul Muslimina iliyochanwa kwa dharau, ukikifunua kitabu hicho ukurasa wapili katika mlango wa kwanza utaiona Aya ya kumi na nane na ya kumi na tisa nusu yake, za Suratul Jathia. Bakwata inasema: Qur'an haikuchanwa lakini aya mbili katika Suratul Jathia zimechanwa kwa dharau! Sijui kwa Bakwata Qur'an inathubutu kwa vipi! Kwa kukamilika Sura ngapi au Aya ngapi hata isemwe ni QUR'AN? Kwa nini washutumiwe na kulaniwa watu wanaopendekeza kuwa: Sharia ya Mirathi na ya ndoa zifanyiwe marekebisho? Katika Mirathi wanachoomba iondolewe ni Aya isemayo "Lidh'dhakari Mithlu H'adh'dhil Unthayayni " 4:11
katika Ndoa wanaomba iondolewe Aya: "Mathna Wathulatha Warubaa " 4:4, sasa, unaweza kuhesabu silabi za Aya hizi, kisha uhesabu silabi za Aya zilizomo katika vitabu vilivyochanwa. Ndipo utamjua nani mwenye kosa wakufaa kushutumiwa na kulaaniwa! Kwakuwa sheria ni msumeno, hapa napenda kukumbusha baadhi ya matukio kama haya yalioyofanywa na wakubwa. Baada ya kufariki Mtume(s.a.w.w) sheria isemayo kuwa "Katika mafungu manane ya sadaka, fungu moja kati ya haya ni la wale wanaoingia Uislamu. Fungu hili lilifutwa! Na Aya inasomeka hivi: "Wal'muallafati Qulubuhum "[36]
Hukumu ya Aya hii imefutwa, kwa hiyo, maasi ya kunyanyasa sheria ya Mwenyeezi Mungu hayakuanza juzi katika Tarafa ya Nyakato, bali yameanza mbali huko baada ya kufariki tu Mtume(s.a.w.w) .
Israa ni: Mwendo wa usiku, kama ilivyokuja katika Qur'an: "Utukufu ni wa yeye ambaye alimpeleka Mja wake usiku, kutoka Msikiti mtukufu (wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (Falastin) ambao tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake, ili tumuonyeshe baadhi ya ishaara zetu " 17:1.
Miiraji ni: Msafara ulioanzia katika Msikiti wa Falastin kwenda juu. Tukio la Israa limepokewa na waandishi wa Tarikh kwa njia tofauti, kuna wanaosema kuwa Israa ilitokea mwaka wa kumi na mbili baada ya kupewa Utume, Wengine wanasema ilikuwa mwaka wa kumi na moja, wengine mwaka wa kumi, wengine mwaka wa tano, wengine mwaka wa tatu na wengine mwaka wa pili.[37]
Kauli ya sawa katika mjadala huu ni: Israa imetokea katika mwaka wa tatu kwa sababu zifuatazo"
a . Mtume(s.a.w.w) alikuwa akipendelea sana kumbusu binti yake Mwana Fatima(a.s) mpaka Mwana Aisha (mkewe Mtume) likamuudhi sana hilo, akasema: "Ewe Mtume wa Mwenyeezi Mungu! Una nini? Kila mara ninakuona sana unambusu Mwana Fatima kama unayekula asali! Mtume(s.a.w.w) akamjibu: "Ni kweli, ewe Aisha! Mimi nilipopelekwa juu (Miiraji) Malaika Jibril(a.s) aliniingiza Peponi humo nilikula Tunda fulani, likabaki mgongoni, niliposhuka nilimwingillia Khadija (mkewe) mara akapata ujauzito wa Mwana Fatima kutokana na hilo tunda. Na yeye ndiye Tunda bora, kila ninapokumbuka Peponi, humbusu Fatima".[38]
Katika hadithi hii tunajifunza kuwa: Mwana Fatima(a.s) amezaliwa mwaka wa tano baada ya Biitha (kupewa Utume) kwa hiyo, Israa na Miiraji ilikuwa kabla ya kuzaliwa Mwana Fatima, kwa sababu Mwana Fatima ni Tunda la peponi alilokula Mtume siku aliyopelekwa Miiraji. Tunda lililobaki mgongoni kwake hata baada ya miaka miwili akazaliwa Fatima, Bibi bora kabisa katika mabibi wa Peponi - Hadithi. b. Mtume(s.a.w.w) alipopelekwa juu (Miiraji) Malaika walikuwa wakiuliza kila mahala Je! Muhammad amekwisha pewa Utume? Hili linaonyesha kuwa Tukio la Israa na Miiraji lilitokea katika miaka ya awali ya Utume, wala siyo baada ya miaka kumi na mbili. Kwa sababu ingekuwa hivyo bila shaka suala la Utume lingekwisha eleweka zamani pasingekuwepo haja ya kuliuliza. Israa na Miiraji ilitokea kabla ya kusilimu Abubakr bin Abi Quhafa, kwa sababu, Abubakr amesilimu baada ya miaka mitano ya biitha.[39]
Ikiwa Israa na Miiraji imetokea kabla ya kusilimu Abubakr, basi madai ya Laqabu isemwayo kuwa alipata Abubakri ya "SIDDIQ" yanatupwa: Kwa sababu ikiwa laqabu hiyo (kama inavyodaiwa) alupata baada ya kusadikisha msafara wa Mtume(s.a.w.w) aliopelekwa katika Israa na Miiraji. Litawezekanaje hilo, ilihali wakati wa tukio la Israa na Miiraji Abubakri alikuwa kafiri! Hapo tasdiq itapatikana?!
Tukio la Israa, wako baadhi ya Waislamu wanao ona kuwa Mtume(s.a.w.w) alioteshwa na wala hakwenda mwenyewe akiwa macho. Na mategemeo yao ni ile habari aliyoisimulia Mwana Aisha kuwa: "Siku hiyo hakukikosa kiwiliwili cha Mtume".[40]
a . Mwana Aisha wakati wa tukio hilo alikuwa hajaolewa na Mtume, bali yaelekea hata kuzaliwa alikuwa bado!!
b . Mwenyeezi Mungu anasema: "Utukufu ni wa yeye ambaye alimpeleka Mja wake usiku, kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa mbali " 17:1. lliposemwa: "Asraa Bia'bdihi " tamko la "A'BD" hutumiwa kwa roho na kiwiliwili pamoja. Kwa hiyo, Mtume(s.a.w.w) alikkwenda mwenyewe akiwa macho. c. Kama Israa ingelikuwa kwa njozi, basi kusingekuwako na upinzani mkubwa hivyo, na watu wasingeritarddi.[41]
d . Kama Israa ingelikuwa kwa njozi, basi Abu Talib na Bani Hashim wasingetoka kumtafuta, kwa sababu Bani Hashim walitoka kumtafuta siku hiyo.[42]
Imepokewa katika riwaya kuwa: Sala tano zimefaradhiwa wakati Mtume(s.a.w.w) alipopelekwa katika msafara wa Miiraji huko juu Inasemwa kuwa, zilifaradhiwa sala hamsini kwa kila siku, na Mtume(s.a.w.w) alipokuwa akirudi na agizo hilo, alipofika mbingu ya sita akakutana na Nabii Musa(a.s) akamshauri Mtume Muhammad(s.a.w.w) arudi kwa Mola wake amuombe ampunguzie Sala hizo. Mtume alirudi kwa Mola wake na akapunguziwa Sala kumi, aliposhuka katika mbingu ya sita akakutana na Nabii Musa akiwa na sala arobaini. Nabii Musa akamrudisha kwa Mola wake apunguziwe Sala hizo, Mtume akafanya hivyo, Mwenyeezi Muungu akapunguza Sala kumi. Mtume alipofika kwa Nabii Musa, akamrudisha kwa Mola wake akaombe takhfif; Mtume alifanya hivyo, Mwenyeezi Mungu akapunguza sala kumi Mtume akashuka alipofika kwa Nabii Musa akiwa na sala ishirini, Nabii Musa akamtaka arudi kwa Mola wake akampunguzie, kwa sababu umma wake hawawezi hilo. Mtume(s.a.w.w) alifanya hivyo, Mwenyeezi Mungu akapunguza Sala kumi, Mtume akashuka akiwa na sala kumi, alipokutana na Nabii Musa akamrudisha kwa Mola wake ili apunguziwe, Mtume alifanya hivyo, Mwenyeezi Mungu akapunguza Sala tano, Mtume(s.a.w.w) aliposhuka kwa Nabii Musa(a.s) akiwa na sala tano, alipotaka kumrudisha kwa Mola wake, Mtume(s.a.w.w) alisema:- "Kwa hakika, nimerudi kwa Mola wangu mara tano, kuomba takhfif mpaka sasa naona aibu kubwa". Ndipo aliposhuka Mtume(s.a.w.w) akiwa sala tano, ambazo wanapaswa Waislamu kuzisali kwa kila siku.
Tunaamini kuwa: "Mwenyeezi Mungu haweki sheria yoyote isipokuwa ina maslahi ndani yake. Kwa mantiq hii, Mtume(s.a.w.w) asingehitaji kurudi mara zote hizo kwa ajili ya kupunguziwa. Kwa sababu kufanya hivyo ni kutaka sheria isiyo na maslahi, kama ambavyo sababu zilizompelekea Nabii Musa kutaka zipunguzwe Sala hamsini ni kushindwa kuzitekeleza sala hizo. Kama kwamba Nabii Musa anaamini kuwa Sheria hii (ya Sala hamsim) inakwenda kunyume na maslahi, na hilo ni muhali (haliwezekani) kwa Mwenyeezi Mungu. Aidha, vipi Mwenyeezi Mungu hakujua kuwa: Umma wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) hauwezi hilo, bali Musa yeye alijue hilo?? Au tuseme, ni takhfif kwa jambo lisilowezekana, vipi, Mwenyeezi Mungu anatwambia wakati wote: "Mwenyeezi Mungu huwatakieni yaliyo mepesi wala hawatakieni yaliyo mazito ". 2: 185. "Wala hakuweka juu yenu dhiki katika dini " 22:78.
Na vipi Nabii Ibrahim hakushitushwa na misafara ya nenda rudi ya Mtume Muhammad, asimuulize kuna nini! Maana kwa mujibu wa riwaya zinzosimulia tukio hili zinasema kuwa, Nabii Ibrahim(a.s) alikuwa katika mbingu ya saba na Nabii Musa(a.s) mbingu ya sita. Aidha, kwanini Mwenyeezi Mungu asimpe moja kwa moja Mtume wake Sala tano, kuliko usumbufu huu alioupata Mtume wa nenda rudi mpaka akaingiwa na aibu kubwa akashuka kwa shingo upande na sala zake tano!?
Tukitaka kujuwa shabaha na hekima na muujiza wa Israa na Miiraji, lazima kusoma nassi zake na vipengele vyake kwa undani na makini. Na hapa tutaonyesha mambo yafuatayo:
a . Israa na Miiraji ni muujiza mkubwa wa kudumu, na leo katika karne hii ya ishirini tukio hili linakubaliwa na elimu ya sayansi na Teknolojia. Mwanadamu hashangai tena leo kusikia kuwa mtu amekwenda umbali wa maili nyingi zaidi katika upeo wa juu.
b . Mwenyezi Mungu ametaja wazi lengo la msafara huo aliposema: "Linuriyahu Min Ayaatina ", yaani, "Ili tumuonyeshe baadhi ya Aya (ishara) zetu" 17:1. Kwahiyo, lengo ni kumuonyesha Mtume(s.a.w.w) baadhi ya ishara za utukufu wa Mwenyeezi Mungu. Na kwakupelekwa Mtume Israa na Miiraji, kumefunguwa moyo wake na akili yake zaidi kwa kupata taaluma kubwa katika ulimengu huu anaouongoza.
c . Mwanadamu (hasa Mwarabu) wakati huo aijishi katika ulimwengu finyu sana, na akili duni iliyofungwa katika tundu dogo. Kwa sabaha hii ikawa dharura kufunguliwa macho yake na moyo wake ili aujue ulimwengu anaoishi, ambao Mwenyeezi Mungu amemfanya awe khalifa wake.
Inasemekana kuwa: Mtume(s.a.w.w) hakuoa mke yeyote aliye bikira isipokuwa Mwana Aisha tu. Wanasema kuwa: "Mwana Khadija kabla ya kuolewa na Mtume(s.a.w.w) alikwisha olewa na waume wawili kabla ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) na amepata watoto wawili. Tutataja kidogo hapa baadhi ya hoja zinazosemwa juu ya Mwana Khadija kuhusu watoto aliopata kwa waume wengine kabla ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) ni kama ifuatavyo:
i. Wanasema: Shahidi wa kwanza katika Uislamu ni mtoto wa Mwana Khadija aitwae Harithi bin Abi Hala, alipata shahada pale Mtume(s.a.w.w) alipotangaza Uislamu hadharani.[43]
ii. Lakini, hoja hii inaangushwa na riwaya ya Qatada inayosema kuwa: Shahidi wa kwanza katika Uislamu ni Sumayya, mama yake Ammar bin Yasir.[44]
Imepokewa kuwa: Mwana Khadija(a.s) alikuwa na nduguye akiitwa Hala, aliolewa na mtu mmoja katika Koo ya Al'Makhzumi, akazaa mtoto wa kike jina lake Hala, Kisha aliachika akaolewa na mtu mmoja katika Koo ya At'Tamim aitwaye Abu Hindi, akamzalia mtoto jina lake Hind. Huyu Abu Hindi, alikuwa na mke mwingine ambaye alimzalia watoto wawili: Zaynab na Ruqayya. Hatimae Abu Hindi na mkewe wa pili walikufa,akabakia Bi Hala ndugu ya Mwana Khadija, pamoja na watoto wawili: Zaynab na Ruqayya. Yule mtoto wake wa kuzaa: Hind, alikwenda kwa jamaa za mumewe. Ndipo Mwana Khadija alipowakusanya wote akawa nao, Bi Hala na watoto wawili walioachwa na mama yao: Zaynab na Ruqayya. Mwana Khadija alipoolewa na Mtume(s.a.w.w) Bi Hala alifishwa, wakabaki Zaynab na Ruqayya wakilelewa na Mtume(s.a.w.w) . Katika mila za Kiarabu, walikuwa wakiamini kuwa mtoto wa kufikia ni mtoto wako halisi, kwa hiyo, watoto hawa wakapewa ubinti wa Mtume(s.a.w.w) (Zaynab binti Muhammad na Ruqayya binti Muhammad).[45]
a. Katika kitabu "Asha'shaafy" na "At Talkhis" inasema Mtume(s.a.w.w) amemuoa Mwana Khadija akiwa bikira.
b. b. Amesema Abulqasim Alkufy: Mtume(s.a.w.w) alipomuoa Mwana Khadija(a.s) wanawake wa kikuraishi walimkasirikia sana Mwana Khadija wakisema: Wamekuposa mabwana wa kikuraishi wenye heshima, umekataa kuolewa na yeyote kati yao, umekubali kuolewa na Muhammad, yatima wa Abu Talib Lofa hana mali![46]
Amesema Mtukufu Mtume(s.a.w.w) "Watafarakana umma wangu makundi sabini na tatu, kundi moja tu kati ya hayo litaokoka, na yaliyobaki yatatiwa motoni . Ali akauliza: "Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu! Kundi gani litakalookoka? Mtume(s.a.w.w) akajibu: "Wewe na watu wako".[47]
Mfarakano kwa mara ya kwanza ulitokea kwa Waislamu pale tu alipofariki Mtume Muhammad(s.a.w.w) . Mtume(s.a.w.w) kabla ya kufariki dunia, aliweka sera kamili ya uongozi katika Uislamu. Iliposhuka Aya: "Hakika wale walioamini na wakatenda mema, basi hao ndio wema kushinda viumbe vyote " 98:7.
Mtume(s.a.w.w) akamwambia Ali: "Wewe Ali na kundi (pote) lako ".[48]
Mtume(s.a.w.w) amesema: "Ali yu pamoja na Qur'an, na Qur'an ipamoja na Mi, hawataachana mpaka wanifikie katika Haudh ".[49]
Mtume(s.a.w.w) amesema: "Mimi ninakuachieni vizito viwili ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu, Qur'an na Ahlul Bayt wangu, viwili hivi havitaachana mpaka vitakaponifikia katika Haudh".[50]
Imam Ali(a.s) mmoja katika Ahlul Bayt wa Mtume(s.a.w.w) tazama pale iliposhuka Ayatut Tat'hir: "Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni sana sana " 33:33.
Na mke wa Mtume(s.a.w.w) (Ummu Salama) alipotaka kuingia katika nguo hiyo Mtume akamzuia![51]
1. Imam Ali bin Abi Talib(a.s) amezaliwa ndani ya Al' Kaaba siku ya Ijumaa, tarehe kumi na tatu Rajab mwaka wa thalathini (mwaka wa ndovu). Wamekhitilafiana waandishi wa tarikh kujuwa tarehe aliyopigwa dharba Imam Ali, baadhi ya kauli hizo zasema:
a. Alipigwa dharba tarehe 17 usiku wa kuamkia Ijumaa mwezi wa Ramadhan, akafishwa usiku wa kuamkia Jumapili tarehe 19 Ramadhan.
b. Alipigiwa dharba tarehe 19 usiku, akafishwa tarehe 21 Ramadhan mwaka 40.
c. Alipigwa dharba kuamkia tarehe 21, akafishwa tarehe 23 Ramadhani.
d. Alipigwa dharba kuamkia tarehe 23, akafishwa tarehe 25 Ramadhan.[52]
Riwaya nyingine zinasema kuwa:
a. Alipigwa dharba asubuhi ya tarehe 17 Ramadhan.
b. Alipigwa dharba asubuhi ya tarehe 19 Ramadhan, mwaka 40 Hijra.[53]
Abdur Rahman bin Muljam alikutana na msichana mmoja katika khawariji aitwaye Qatwam, ambaye baba yake na kaka yake waliuliwa na Imam Ali katika vita vya Nahrwan. Msichana huyo alikuwa mzuri kupita kiasi, Abdur Rahman alipomtaka Qatwam, alimjibu: "Kama utaweza kunipoza moyo wangu utanipata" Akamuuliza: "Ni lipi litakalo kupoza moyo wako?" Akajibu: "Unipe dirham alfu tatu, mtumishi mmoja, mjakazi, mwimbaji, na umuue Ali bin Abi Talib. Abdur Rahman bin Muljam akasema: "Hayo mengine yote ni mepesi sana, lakini hili la kumuua Ali, ni dalili ya kuwa umenikataa. Kwa sababu haiwezekani kumuua Ali nami nikasalimika, tukaweza kuoana". Ilipofika siku hiyo, kwa kauli zilivyo khitilafiana, kama ulivyoona hapo juu, Abdur Rahman bin Muljam akatimiza lengo lake. Imam Ali amezikwa Kufa katika nchi ya Iraq.[54]
2. Imam Hasan bin Ali(a.s) amezaliwa katika mji wa Madina, tarehe kumi na tano Ramadhan mwaka wa tatu Hijra'. Mu'awiya alipotaka kumtawalisha mwanawe Yazid, alitumia mbinu, akamjenga Juuda bint Al'ash'a'th bin Qays. Huyu alikuwa mke wa Imam Hasan(a.s) . Muawiya akampa sumu ili amtilie Imam Hasan. Na endapo atamuua, basi atamfanyia mambo mawili, la kwanza atampa dirham laki moja na la pili atamuoza mwanawe, Yazidi. Imam Hasan akapewa sumu hiyo na baada ya hapo alibaki siku arobainni akafariki dunia! Amekufa mfungo tano mwaka 50 Hijra.[55]
Wengine wanasema: Amekufa mfungo sita mwaka 49 Hijra.[56]
Baada ya kufa Imam Hasan Juu'da alipeleka ujumbe kwa Yazidi wa kutaka kuolewa naye kama walivyoahidiana na baba yake Mu'awiya, Yazidi aliruka na kusema: "Hukuweza kumhurumia Hasan utanihurumia mimi!? Kama umeweza kumuua yeye mimi utanimaliza mara moja, Yazid akakataa kumuoa.
3. Imam Husein bin Ali(a.s) amezaliwa katika mji wa Madina tarehe tatu Shaaban mwaka wa nne Hijra. Imam Husein(a.s) ameuliwa mwezi kumi Muharram siku ya Ijumaa (wengine wanasema Jumamosi) mwaka wa sitini na moja Hijra. Imepokewa kutoka kwa Anas kwamba Mtume(s.a.w.w) amesema: "Mwanangu Husein atauliwa katika nchi ya Iraq, yeyote miongoni mwenu atakaekuwapo, basi asimame kumnusuru.[57]
Imepokewa kwa mama Ummu Salama (mkewe Mtume) anasema: "Nilimuona Mtume(s.a.w.w) akikipangusa kichwa cha Imam Husein na huku akilia. Nikamuuliza: "Unalilia nini!" Akasema: "Hivi sasa amenijulisha Malaika Jibril kuwa: Mtoto wangu huyu atauliwa katika ardhi litwayo "KARBALA" kisha akanipa gao la udongo na akaniambia: 'Huu udongo ndipo mahala atakapouliwa, utunze, siku yoyote utakapogeuka kuwa mwekundu basi jua yakwamba amekwisha uliwa".[58]
Kama ambavyo, siku aliyouliwa Imam Husein mbingu zilimlilia, na alama ya kuonyesha kuwa zinamlilia ni wekundu unao onekana kwenye mawingu. Kwa hiyo, Imam Husein(a.s) analiliwa na mbingu mpaka leo hii.[59]
4. Imam Ali bin Husein(a.s) amezaliwa katika mji wa Madina tarehe tano Shaaban mwaka thalathini na nane Hijra, kabla ya kufishwa babu yake (Imam Ali) kwa miaka miwili. Imam Ali bin Husein amefariki mwaka wa tisini na nne Hijra, akazikwa katikamji wa Madina katika kiwanja kitakatifu cha Baqii.
5. Imam Muhammad bin Ali(a.s) amezaliwa katika mji wa Madina tarehe tatu mfungo tano (wengine wanasema tarehe moja Rajab) mwaka hamsini na saba Hijra, kabla ya kuuliwa babu yake Imam Husein kwa miaka mitatu. Wamekhitilafiana mwaka aliofia kama hivi:
a. Amefishwa mwaka 114 Hijra.
b. Amefishwa mwaka 117 Hijra.
c. Amefishwa mwaka 118 Hijra.
6. Imam Ja'far bin Muhammad(a.s) amezaliwa katika mji wa Madina tarehe 16 mfungo sita (wengine wanasema tarehe moja Rajab) mwaka 80 Hijra. Imam amefishwa katika mji wa Madina mwaka 149 Hijra, amezikwa pamoja na baba yake na babu yake katika viwanja vitakatifu vya Baqii.[60]
7. Imam Musa bin Ja'far(a.s) amezaliwa katika kijiji cha "AB'WAA" kilicho kati ya Makka na Madina, mahala ambapo kaburi la Mwana Amina bint Wahab mama yake Mtume(s.a.w.w) lilipo. Amezaliwa mwaka 128 Hijra (wengine wanasema mwaka 129). Imam Musa amefariki mwaka 188 Hijra baada ya kutiwa jela na Haruna Rashid kwa miaka kumi moja.[61]
8. Imam Ali bin Musa(a.s) amezaliwa katika mji wa Madina. Wamekhitilafiana kujuwa tarehe aliyozaliwa kama hivi:
a. Amezaliwa mfungo pili mwaka 148.
b. Amezaliwa mfungo tatu mwaka 148.
c. Amezaliwa mfungo sita mwaka 148.
d. Amezaliwa mwaka 153. Kifo cha Imam Ali bin Musa kimetokana na maji ya matunda yenye sumu aliyopewa na Maamun. Baada ya kunywa Imam alibaki siku mbili kisha akafariki dunia, mwaka 203 wengine wanasema mwaka 202 na wengine wanasema mwaka 206.[62]
9. Imam Muhammad bin Ali(a.s) amezaliwa katika mji wa Madina, tarehe kumi na tisa Ramadhan mwaka 195 Hijra. Amefariki Imam Muhammad mwaka 220 wengine wanasema mwaka 225[63]
10. Imam Ali bin Muhammad(a.s) amezaliwa Rajab mwaka 214 Hijra umbali wa maili tatu hivi kutoka katika mji wa Madina. Imam Ali bin Muhammad ameuliwa kwa sumu mwaka 254 Hijra.
11. Imam Hasan bin Ali(a.s) amezaliwa katika mji wa Madina mwaka 231 Hijra. Imam Hasan bin Ali amefariki siku ya Ijumaa tarehe nane mfungo sita mwaka 260 na akazikwa mahala alipozikwa Baba yake.
12. Imam Muhammad bin Hasan(a.s) amezaliwa tarehe kumi na tano Shaaban mwaka 255 Hijra, wengine wanasema tarehe ishirini na tatu Ramadhan mwaka 258 Hijra. Imam Muhammad bin Hasan yuko hai mpaka sasa, alipofiwa Baba yake alikuwa na umri wa miaka mitano. Hawa ni Maimam kumi na wawili katika AhIul Bayt(a.s) walio pamoja na Qur'an. Amesema Mtume(s.a.w.w) "Dini itaendelea kuwa imara mpaka isimame kiama, na mtasimamiwa na viongozi kumi na wawili, wote katika Maquraishi ".[64]
Na ameonya Mtume(s.a.w.w) kwa yeyote ambaye hatawatambua Maimam hawa: "Yeyote atakaekufa na asimjue Imam wa zama zake, atakufa kifo cha kipagani ".[65]
Ukisoma Terikh, na kisha ukafuatilia sera za utawala wa makhalifa watatu, utajua wazi kwamba mabwana hao walizuia kuandikwa Hadithi za Mtume Muhammad(s.a.w.w) bali walikataza hata kuzizungumza mbele za watu. Kwa sababu walijua wazi kuwa sera za utawala wao haziendi sambamba na uongozi wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) . Abubakr amekataza kuzungumza chochote juu ya Mtume(s.a.w.w) na amesema:Yeyote atakaewauliza mseme: "Kati yetu sisi na nyinyi ni Qur'an, basi, halalisheni halali yake na haramisheni haramu yake ". [66]
Kauli hii ya Abubakr imekuja baada ya muda mfupi wa tukio la karatasi, Umar bnul Khattab alipomjibu Mtume kuwa: "Mtume anaweweseka, ipo Qur'an inatutosha", Abubakr anasema: "Kati yetu sisi na nyinyi ni Qur'an"..... Qur'an iliyo kati yetu na Abubakr inasema kuhusu wanaozuia zaka: "Na miongoni mwao wako walio mwahidi Mwenyeezi Mungu, akitupa katika fadhili zake bila shaka tutatoa sadaka na lazima tutakuwa miongoni mwa watendao mema. Lakini alipowapa katika fadhili zake, wa kayafanyia ubakhili na wakageuka, nao ndio wakengeukao. Kwa hiyo akawalipa unafiki mioyoni mwao mpaka siku ya kukutana naye, kwa sababu ya kumkhalifu Mwenyezi Mungu ahadi waliyo mwahidi, na kwa sababu walikuwa wanasema uongo". 9:75-77.
Aya hizi zimeshuka kwa ajili ya Thaalaba aliyezuia zaka wakati wa Mtume(s.a.w.w) . Lakini pamoja na yote hayo Mtume(s.a.w.w) hakumpiga wala hakumnyang'anya mali yake, ingawa Mtume yote haya alikuwa na uwezo nayo. Ambapo suala la Malik bin Nawyira na wenzake waliodaiwa kuwa walizuia Zaka katika utawala wa Abubakr. Huo ni msimamo waliouonyesha dhidi ya utawala wa Abubakr aliyepora madaraka yasiyo kuwa yake. Kwa hiyo, kitendo cha kuzuia zaka kutoupa utawala wa Abubakr ni tafsiri halisi ya kupinga utawala huo na wala si kupinga hukumu ya faradhi ya zaka. Sasa, Abubakr yuko wapi na aya hizi aliyedai kuwa ndiyo sera yake?? Mbona amewaua watu waliozuia zaka kwa kigezo gani? Sera ya Abubakr inasema: "Kati yetu sisi na nyinyi ni Qur'an".
Qur'an inasema: "Wanaume wana sehemu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa walio wakaribia, Na wanawake wanayo sehemu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa walio wakaribia " 4:7.
Mwana Fatima bint Muhammad(s.a.w.w) alipokwenda kwa Abubakr kutaka mirathi iliyoachwa na baba yake, Abubakr akakataa kumpa akidai kuwa amemsikia Mtume akisema: "Sisi Mitume haturithiwi". Hapa Qur'an hana haja nayo, ameshika lile asilokuwa na haja nalo tokea awali, hata hivyo, Abubakr kweli maneno ya Mtume anayakubali? MwanaAisha (Mwanawe) anasimulia tukio hili: Baba yangu alizikusanya Hadithi za Mtume(s.a.w.w) ambazo zilikuwa mia tano, akakesha kucha akizigeuzageuza......kulipokucha akasema: Mwanangu! Niletee Hadithi ulizonazo, ni kampa, akazichoma moto![67]
Je! Ni kweli Abubakr anaitegemea Qur'an tu peke yake? Mwenyeezi Mungu anasema: "Sadaka ni kwa mafakiri tu na masikini na wanaozitumikia na waungiwao.......mioyo yao.....9:60. Iliposemwa: "Na waungiwao mioyo yao" ni wale waislamu wapya ambao ndio kwanza wanasilimu. Abubakr alipotawala, hukumu ya kifungu cha Aya hii akaifuta![68]
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
YALIYOMO
MASOMO YA KI-ISLAMU 1
MUONGOZO KWA WASOMAJI 1
KIMEANDIKWA NA: OMAR JUMAA MAYUNGA 1
UTANGULIZI 1
MASOMO YA KI-ISLAMU 2
MUONGOZO KWA WASOMAJI 2
MWANZO WA WAHY 2
MJADALA WA RIWAYA ZA WAHY 4
MUHARRAM SI MWANZO WA MWAKA 5
KUONEKANA KWA MWENYEEZI MUNGU 6
MAJIBU YETU 6
HADITHI ZISEMAZO KUWA ATAONEKANA 7
MAJIBU YETU 8
QUR'AN IMEUMBWA 8
TAQIYYA 8
TAHRIFUL QUR'AN 10
MASOMO YA KI-ISLAMU 12
MUONGOZO KWA WASOMAJI 12
WANAOTHIBITISHA KUWA IPO 12
WALIOSEMA KUWA HAIPO 12
KUSOMA QUR'AN KWA AJILI YA MAITI 13
MAJIBU YETU 13
ISRAA NA MIIRAJI 15
MTUME ALIKWENDA MWENYEWE AU NI NJOZI? 16
MAJIBU YETU 16
MUSA NA SALA TANO 17
UCHUNGUZI 17
LENGO LA ISRAA NA MIRAJI 18
KHADIJA ALIOLEWA NA YEYOTE KABLA YA MTUME? 18
MAJIBU YETU 19
POTE LENYE KUOKOKA 19
AHLUL BAYT WALIO PAMOJA NA QUR'AN 20
SERA ZA UTAWALA BAADA YA MTUME 23
SHARTI YA KUCHAPA 24
MWISHO WA KITABU 24
YALIYOMO 25
[1] . Taz: Sahihi Bukhari Juz.I uk: 5-6. Sahihi Muslim Juz. I, uk: 97 Almuswannaf Juz. 5, uk: 322. Tarikhut Tabari Juz. 2, uk: 47.
[2] . Taz; Albidayatu Wannihaya Juz. 3, Uk: 9 Assiratun Nabawiyya Juz. 1 uk: 83. Assiratul Halabiyya Juz. 1, uk: 250. Siiratu Mughlataya uk, 15.
[3] . Taz: Albidayatu Wannihaya Juz.3 uk, 12. Siiratu Ibn Hisham Juz. 1 uk, 238 Assiratul Halabiyya Juz. 1, Uk. 239.
[4] . Taz: Assiratul Halabiyya Juz. 1, Uk. 252.
[5] . Taz: Tarikhul Yaa'quby Juz. 2, Uk. 23.
[6] . Taz: Tarikhul Khamisi Juz. 1, Uk. 284. Assiratul Halabiyya Juz. 1, Uk. 243. Assiratun Nabawiyya Juz. 1. Uk. 83.
[7] . Taz: Almuswannaf Juz. 5, Uk. 323.
[8] . Taz: Albidayatu Wannihaya J. 3 Uk. 13.
[9] . Taz: Qamusir Rijal Juz. 6, Uk. 300 Algharat Juz. 2, Uk. 558-560.
[10] . Taz: Mustadrakul Hakim Juz. 3, Uk. 121. Musnad Ahmad Juz. 5, Uk. 30. Alfusulul Muhimma Uk. 111. Tarikh Ibn Asakir Juz. 2, Uk. 184. Manaqibu Ali Uk. 394.
[11] . Taz: Sahihi Muslim, katika kitabul Iman. Sahihat Tirmidhi Juz. 2, Uk. 301. Musnad Ahmad Juz. 1, Uk. 84. Tarikh Bughdad Juz. 2, Uk. 255. Hilyatul Awliyaa Juz. 4, Uk. 185. Kanzul Ummal Juz. 6, Uk. 394. Mustadrakul Hakim Juz. 3, uk 129. Al Istiab Juz. 2, Uk. 214. Addurrul Manthur Aya ya 25 sura 47.
[12] . Taz: Magatilut Talibina Uk. 27. Aljamal, Uk. 83-84.
[13] . Taz: Sahihi Bukhari Juz. 1, Uk. 152. Sahihi Muslim Jz. 7, Uk. 100. Musnad Ahmad Juz. 2, Uk. 315. Almuswannaf Juz. 11, Uk. 274. Sunannun Nasai Juz. 4, Uk. 118. Albidayatu Wannihaya Juz. 1, Uk. 317. Tarikhut Tabari Juz. 1, Uk. 305.
[14] . Taz: Alkharaj Uk. 81. Jamharatu Rasailil ar'b Juz. 1, Uk. 82.
[15] . Taz: Albidayatu Wannihaya Juz. 3, Uk. 207.
[16] . Taz: AI'i'lanu Uk. 78.
[17] . Taz: U'nwanul Maa'rif Uk. 11.
[18] . Taz: Sahihi Bukhari J. 4 Uk. 92 Sahihi Muslim J. 1 Uk. 86 Tafsirul Khazin J. 7 Uk. 137.
[19] . Taz: At'targhib Wat'tarhib J. 4 Uk. 551.
[20] . Taz: Tafsirul Qurtubi, J. 4, Uk. 57.
[21] . Taz: Tafsir ibn Kathir J.1, Uk. 365 Safwatut Tafasir J.1, Uk.196.
[22] . Taz: Tafsir Ibn Kathir J. 2 Uk. 609 Tafsirul Qurtubi J. 10 Uk. 180 Tafsirul Khaazin J. 4 Uk. 117 Tafsirul Maraghi J. 14 Uk. 146.
[23] . Taz: Tafsirul Qurtubi J. 9 Uk. 76.
[24] . Taz: Tafsir Qurtubi J. 14 Uk. 290.
[25] . Taz: Manahilul I'r fani Juz. 1 Uk. 253 3.
[26] . Taz: Tafsirul Alus Juz. 1 Uk: 39 Tafsir lbn Kathir Juz. 1 Uk: 17 Tafsirul Khazin Juz. 1 Uk: 18 Tafsirush Shawkan Juz. 1 Uk; 7.
[27] . Taz: Sahihi Bukhari J. 8 Uk. 26 Sahihi Muslim Juz. 5 Uk. 116.
[28] . Taz: Al' It'qan Juz. 1 Uk. 101.
[29] . Taz: Tafsirul Qurtubi J. 14 Uk. 113 Al' It'qan Juz.2 Uk.32.
[30] . Taz: Al' It'qan Juz. 2 Uk. 33.
[31] . Taz: Tafsirul Qurtubi Juz. 14 Uk. 113.
[32] . Taz: Al'I'tigad Juz. 1 Uk. 16. Tafsir Aalair Rahman Juz. 1 Uk. 25. Albayan fit'tafsiril Qur'an Uk. 213. Tafsirul Qur'an, assayid shubbar Uk. 17.
[33] . Taz: Tafsir ibn Kathir Juz. 4 Uk. 276.
[34] . Tarehe 18-8-1984 katika mkoa wa Mwanza Tarafa ya Nyakato Kijiji cha Buzuruga, kulitokea tatizo kubwa lililosababishwa najeshi la jadi Ia sungusungu. Jeshi la jadi la sungusungu kwa makusudi kabisa, ililiivamia nyumba ya MwisIamu, likaingia ndani na kuchanachana vitabu vitano vitakatifu vya Kiislamu. Yasin Ndogo (B) Majmuul Mubarak (C) Irshadul Muslimina (D) Hadithi Za Mtume (E) Ahlul Badr.
[35] . Taz: Tafsirul Qurtubi J. 10 Uk. 267.
[36] . Taz: Tafasirut Tabari Juz. 10, Uk. 113.
[37] . Taz: Albidayatu Wannihaya Juz. 3, Uk. 108 Tarikhul Khamisi Juz. 1, Uk. 307 Assahihu Minsiiratin Nabi Juz. 1, Uk. 269.
[38] . Taz: Tarikh Bughdad Juz. 5 Uk. 87. Mizanul'itidal Juz. 2 Uk. 297. Mustadrakul Hakim Juz. 3 Uk. 156. Majmauz Zawaid Juz. 9 Uk. 202. Kanzul Ummal Juz. 14 Uk. 97. Dhakhaairul U'qbaa Uk. 36.
[39] . Taz: Assahihu Minsiiratin Nabii Juz. 1, Uk. 274 Usudul Ghaba Juz. 4, Uk. 18.
[40] . Taz: Tarikhul Khamisi Juz. 1 Uk. 308. Al' mawahibul laduniyya Juz. 2 Uk.2.
[41] . Taz: Tafsir ibn Kathir Juz. 3 Uk. 24. Tarikhul Khamisi Juz. 3 Uk. 308. Almuswannaf Juz. 5, Uk. 327.
[42] . Taz: Assahihu Minsiiratin Nabii Juz. 1 Uk. 276.
[43] . Taz: Al' Isaba Juz. 1, Uk. 293 Al'Awaail Juz. 1, Uk. 311-312.
[44] . Taz: Al' Isaba J. 4 Uk. 335.
[45] . Taz: As' Sahihu Minsiiratin Nabi Juz. I, Uk. 123.
[46] . Taz: Al' Istighatha Juz. 1, Uk. 70.
[47] . Taz: Ithbatul Hudat Juz. 2, Uk. 260.
[48] . Taz: Tafsirut Tabari Juz. 30 Uk. 171.
[49] . Taz: Faidhul Qadir Juz. 4 Uk. 358. Musnad Ahmad Juz. 5 Uk. 31. Alfat'hul Kabir Juz. 2, Uk.21. Tarikhul Khulafai Uk. 174. Majmauz Zawaid Juz. 9, Uk. 134. Kifayatut Talibi Uk. 399. Asnal matalibi Uk 136.
[50] . Taz: Tafsir ibn Kathir J. 4 Uk. 122 Tafsir ul Kazin J. 1 Uk. 4 Tarikhu Bughdad J. 8 Uk. 442 Sahihi Muslim Juz. 4 Uk. 1873. Jamiul Usul Juz. 1, Uk. 187. Albidayatu Wannihaya Juz. 7 Uk. 362. Majmauz Zawaid Juz. 9 Uk. 163. Musnad Ahmad Juz. 2 Uk. 17-26. Al Mustadrak Juz. 4 Uk. 109.
[51] . Taz: Sahihi Muslim Juz. 4 Uk. 127. Sahihi Tirmidhi Juz. 4 Uk. 304. Alkhasais Uk. 4. Tarikh Bughdad J. 9 Uk. 126 Al' Isaba J. 1 Uk. 27 Usudul Ghaba J. 5 Uk. 521 Al Mustadrak Juz. 2 Uk. 416. Tafsirut Tabari Juz. 22 Uk. 5-7. Tafsirul Khazin Juz. 5 Uk. 259. Addurrul Manthur Juz. 5 Uk. 198.
[52] . Taz: Kashful Ghumma Juz. 2, Uk. 63.
[53] . Taz: Suratul Aimmatil Ithna Ashar Juz. 1, Uk 452.
[54] . Taz: Kashful Ghumma Juz. 2, Uk. 62. Tabaqatul Kubra, Juz. 6, Uk. 12. Tadhkiratul Khawas Uk. 179 2.
[55] . Taz: Kashful Ghumma Juz. 2 Uk. 207. Tadhkiratul Khawas Uk. 211.
[56] . Taz: Tadhkiratul Khawas Uk. 211.
[57] . Taz: Dhakhairul Uq'baa Uk. 146.
[58] . Taz: Dhakhairul' U'qbaa Uk. 147 Albidayatu Juz. 3 Uk. 174. Albidayatu Wannihaya Juz. 6 Uk. 230. Tarikhul Islam Juz. 3 Uk. 10. Almustadrak Juz. 3 Uk. 176.
[59] . Taz: Tafsirul Qurtubi Juz. 16 Uk. 14.
[60] . Taz: Siiratul' Aimmatil Ithna Ashar Juz. 2, Uk. 225.
[61] . Taz: Tadhkiratul Khawas Uk. 350.
[62] . Taz: Siiratul' Aimmatil' Ithna Ashar Juz. 2, Uk. 341.
[63] . Taz: Siiratul' Aimmatil' Ithna Ashar Juz. 2, Uk. 448.
[64] . Taz: Sahihi Muslim Juz. 6 Uk. 3-4 Sahihi Bukhari Juz. 4, Uk. 165. Sunan Abi Daud Juz. 3, Uk. 106 Musnad Ahmad Juz. 5, Uk. 86-90. Kanzul Ummal Juz. 13 Uk. 26-27. Hilyatul Awliyaa Juz. 4, Uk. 333.
[65] . Taz: Sharhul Maqasid Juz. 2, Uk. 275. Al'mirqat Juz. 2 Uk. 509. Al'ghaadir Juz. 10, Uk. 260.
[66] . Taz: Tadh'kiratul hufaadh Juz. 1, Uk. 3.
[67] . Taz: Kanzul Ummal. Juz. 5, Uk. 237 Tadh'kiratul hufaadh Juz. 1, uk, 5.
[68] . Taz: Tafsirut Tabari Juz. 10, Uk. 113.