MUANDAMO WA MWEZI
Mwandishi: Juma Muhammad Rashid Al-Mazrui, Al-Zenjibari.Midahalo na majadiliano kielimu
MUANDAMO WA MWEZI
MAZUNGUMZO BAADA YA KHABARI KUHUSU MUANDAMO WA MWEZI-SAYARI
MAZUNGUMZO NA WANAFUNZI WA SHEIKH NASSOR BACHOO JUU YA SUALA LA MWEZI MUANDAMO
MUANDISHI: JUMA MUHAMMAD RASHID AL-MAZRUI, AL-ZENJIBARI
UTANGULI
Baada ya hayo, sina budi kutoa shukurani na pongezi zangu za dhati kwa juhudi kubwa iliofanywa na ndugu zetu wa "Ansaru Sunna" Zanzibar kwa kutunga kitabu chao kujibu kitabu changu kuhusu miandamo ya mwezi. Mnamo mwezi Rajab, nilitumiwa meseji na mmoja wa ndugu zetu wa Zanzibar akiniambia "Je unajua kuwa kitabu chako cha mwezi kimejibiwa?" Nikamwambia sijui kwani sijaletewa kopi. Mara juzi tarehe 2/8/2009, nikajuilishwa na mmoja wa ndugu hapa Oman kuwa kitabu kimetumwa as soft copy katika E-Mail box yake. Kwa hivyo, nikafanya bidii ya kukipata ili nipate faida ya kile nisichokijua. Kwa bahati nilipokisoma sikuona kitu chochote cha kielimu, wala sikuona kwamba wameweza kuthibitisha dai lao kwamba muandamo mmoja ni hoja kwa walimwengu wote. Bali kilichokuwemo ni "Juma kafanya hivi; Juma kasema hivi". Kwa kweli, kwa habari nilioletewa kotoka Zanzibar ni kuwa waliowengi wanasema kuwa hawakuweza kujibu hoja za kitabu chetu UshahdiUuliowekwa Wazi. Lakini nami nasema kwamba wamejitahidi kadiri ya uwezo wao: kila ndege huruka kwa ubawawe.
Kasoro nyengine kubwa zilizomo katika kitabu chao ukiwacha kukosekana kwa mada ya kielimu ni:
1) Tadlis Kughushi. Mara nyingi wamekuwa wakitumia njia mbali mbali kuyaghushi maneno yangu na maneno ya wanavyuoni kama mutavyoona humu. Katika kufanya hivyo, kwa mfano:
a) Huchukua sehemu ndogo ya maneno yangu ambayo haileti maana kamili halafu ndio wakajibu bila ya msomaji kuweza kujua hoja gani hasa nilitoa.
b) Wakati mwengine hunukuu sehemu ya maneno yangu na kuondosha sehemu nyengine; maana ikafisidika. c) Kuhusu maneno ya Maulamaa pia wamefanya hivyo hivyo.
Jambo hili linanipa masikitiko na kuona kwamba labda watu hawa hawakukusudia kutafuta haki bali wamekusudia kuitetea rai fulani wanayoiamini. Hata hivyo, napenda kuwashukuru kwamba 90% ya kitabu chao kimeandikwa kwa lugha nzuri, sehemu moja moja wameteleza. Tunawapa udhuru, kwani ni vigumu mtu kuweza kuwacha hamasa 100%.
2) Kasoro ya pili ya kitabu chao: ni kutokujua wakisemacho. Hili lina picha tatu:
a) Wamenukuu maneno ya wanavyuoni, kisha wakayakoroga katika kuyafasiri kwa Kiswahili: hata maana yake kwa Kiswahili imewashinda. Sasa watu kama hawa vipi wanathubutu kujadili mambo ya elimu.
b) Wananukuu kanuni za Kiusuli kisha hawajui pa-kuziweka. Mara nyengine hunukuu kanuni iliodhidi yao; wao wanaitolea hoja hawajui kwamba maana ya kanuni hio inawapinga wao.
c) Wanaweza kukulaumu kwa kitu kisha kitu kisha na wao wakakifanya kile kile.
3) Tatu: ni kuwa sehemu kubwa ya kitabu changu hawakuweza kuijadili hata kwa hayo majibu yao dhaifu. Kwa hivyo, kimsingi kitabu kimewashinda.
4) Nne: ni kuwa hawajui Qias kinafanywa vipi na wakati gani, kwa hivyo utaona wanahoji kwa hoja ambazo hata wanavyoni hawazitaji kamwe.
5) Tano: ni kukariri kitu hicho kwa hicho mara baada ya ntyengine. Jambo hili likifanya kitabu kikose utunzi wa kitaalamu. Kwa hivyo, na mwenye kujibu hulazimika kukariri jawabu.
6) Sita: ni kuwa unapowapa hoja ya kielimu iliojengeka katika misingi ya fani za elimu na wakawa hawana jawabu ya kuijibu husema: "Lazima yatolewe madondoo ya tafsiri za Wanavyuoni wenye kutegemewa". Na utaponukuu maneno ya wanavyuoni kuunga mkono hoja yako husema: "Kutegemea maneno, matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila y a kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa ni udhaifu".
7) Saba: ni kuwa wanapotaka kukipinga kitu ambacho hawakitaki nao hawana hoja, husema hili hukulinukuu kutoka kwa "Wanavyuoni wenye kutegemewa"; wakitaka kuthibitisha wao jambo lao hunukuu mpaka maneno ya watu ambao hawakufika hata daraja ya uwanafunzi katika istilahi za kielimu.
8) Nane: ni kuwa jambo wasillolijua husema hakuna mwanachuoni aliyesema hivyo, ilhali wanavyuoni wamejaa waliosema hivyo. Yote haya yanaonesha kwamba wamekiingia kitu wasichokijua.
9) Tisa: ni kuwa kitabu chao chote hawakujadili mambo yenye maana, bali huchagua vile vipengele visivyo na umuhimu ndio wakajadili. Hizi ni baadhi ya kasoro kubwa za jawabu yao hio. Mimi nilitarajia kwamba katika kitabu chao watajadili mas-ala yenye maana. Lakini hatimae nakuta mambo kama kwanini nimesema "Vuta-nikuvute" na mfano wa hayo. Ilhali wale wakuu wetu wote hutumia lugha hizo katika vitabu vyao. Husomi kitabu cha fiq-hi au tafsiri au lugha ila utakuta maneno kama M aulamaa wamevutana, au wamesukumana, na mfano wa hayo. Na zote ni ibara zenye kumaanisha kuwepo kwa ikhtilafu kubwa tu: si kwamba waligombana au kupigana.
Hadi sasa ninapoandika jawabu hii, sijapata hard copy. Kwa hivyo, nitapowanukuu ndugu zangu sitoweza kuweka nambari ya ukurasa. Jawabu hii ni mukhtasari wa jawabu pana tutayoitayarisha katika mfumo wa kitabu baada ya kupata hard copy ya kitabu cha ndugu zetu. Kwa hivyo, kwa sasa ikiwa wana jawabu juu ya haya nitayosema humu, basi wasifanye haraka kuichapisha kwa vile nitatoa kitabu ambacho natarajia kwamba kitakuwa na ziada baada ya kupata kitabu chao na mimi kunafasika zaidi na ambacho yako mengi yaliojikariri humu katika kitabu nitayaondoa.
Kwa ajili ya faida ya ziada, jawabu hii nimekigawa sura mbili:
1) Sura ya kwanza nitanukuu makala ya Sheikh wa Mombasa juu ya suala hili la muandamo wa mwezi na jawabu yangu kwake.
2) Sura ya pili ndio tutazama mazungumzo yetu mimi na ndugu zangu wa Ansari wa Zanzibar. Natumia lugha "Mazungumzo" kwa vile sehemu kubwa ya kitabu chao haina hoja za kielimu: ni mazungumzo ya kawaida tu. Na mimi nilikuwa nasita: je nijibu hiki kitabu au nikiwache na kuwaacha watu wasome kitabu changu Ushahidi Uliowekwa Wazi na Kitabu chao pamoja na cha Sheikh Bachoo halafu watu walinganishe hoja tu? Nilitaraddad baina ya rai hii na hile kwa vile hoja za msingi ni zile zile hata tukiandika vitabu mia. Yanayozidi huwa ni mambo ya kushutumiana na kuongezea hoja ndogo ndogo. Hatimae nikaamua kuwajibu si kwa lengo la kufikisha risala kwa wasomi na watu wenye fahamu sahihi; bali kwa ajili kwamba wako watu wenye fahamu kama zao ni lazima twende kwa mujibu wa fahamu zao.
Na kwa sababu hio, naendelea kushindwa kuipa jawabu hii jina jina lenye kuonesha kuwa ni kitabu cha kielimu? Kukipa jina la kielimu kitabu chenye kujadili hoja za mitaani kinawafanya watu wakuone huna maana. Kwa hivyo, jina nililohisi linafaa jawabu hii ni kuiita :
MAZUNGUMZO BAADA YA KHABARI: KUHUSU MUANDAMO WA MWEZI-SAYARI
Kwa kweli kama ndugu zetu walitafakari na kuijua nafasi yao ya elimu, basi wasingelipoteza wakati wao. Hawaoni hawa kwamba hata Saudia ilikuwa zamani na msimamo kama huo wao. Lakini baada ya kukutana kwa wanachuoni wao wakubwa akiwemo Sheikh Bin Baz na Sheikh Ibn Uthaimin na bodi ya wanachuoni wakuu wa huko, waligundua kwamba msimamo huo ni makosa na sahihi ni kuwa kila watu wafate muandamo wao. Jambo hili lilitaka liwape ndugu zetu mazingatio kwani:
1) Wale wa Saudia ni Maulamaa; wakati hawa hakuna hata aiyefikia daraja ya talib 'ilmi (mwanafunzi) kwa mujibu wa istilahi za kielimu.
2) Wanachuoni wa Saudia walitoa uamuzi huo baada ya kukutana wanachuoni hao wakazungumza kwa pamoja: haikuwa fikra ya mwanachuoni mmoja. Na hili linaifanya kauli iwe na nguvu. Nataka kusema kwamba suala zima la kufata muandamo wa mwezi, hoja yake ya msingi ni kuzielewa Hadithi mbili tu; nazo ni Hadithi isemayo: "Fungeni kwa kuuona mwezi" na Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas. Basi hizi ndio dalili mama za kujadiliwa: yaliobaki ni maelezo, sherehe na shubuhati. Kwa hivyo, mwisho wa kitabu hiki, nitajaribu nifanye mukhtasari juu ya vipi tunaweza kuzifahamu hadithi hizi, na natarajia kwamba kwa anayetaka kufahamu atafahamu.
Pia utaona kwamba mimi katika jawabu hii, sikuacha hata kipengele chao kimoja ila nimekijibu, wakati ndugu zetu hawakuweza kukijibu asilimia kubwa ya kitabu changu. Na hili linaonesha kwamba wanajilazimisha tu fikra fulani japokuwa ni fikra dhaifu kielimu. Katika jawabu hii, nitatumia neno "Munasema" kumaanisha nakala ya maneno yao; na neno "Jawabu" kumaanisha jawabu yangu kwao. Ahsantum Ndugu yenu katika dini Juma Muhammad Rashid Al-Mazrui, Al-Zenjibari.
1
MUANDAMO WA MWEZI
SURA YA KWANZA
Nimesoma makala niliyoletewa na mmoja wa ndugu zetu katika Uislamu kuhusu suala la kuonekana kwa mwezi muandamo na kuhusu je mfungo na mfunguo uwe kwa muandamo mmoja au uwe kwa mujibu wa uoni wa kila mji? Muandishi anasema kwamba muandamo mmoja unatosheleza duniani kote. Baadhi ya hoja za muandishi wa makala hio tayari nimezijadili katika kitabu Ushahidi Ulioekwa Wazi ambacho nitakiambatanisha tena na makala hii ili ikiwa kuna upinzani wa kielimu juu ya nilioyasema nipingwe kwawo kwa faida ya Waislamu.
Hata hivyo, yako baadhi ya mambo ambayo - japokuwa niliyajibu kwa uwazi lakini - muandishi ameyaleta katika sura mpya inayonifanya nami nitoe tena mchango wangu katika kuweka wazi zaidi. Aliyesoma kitabu changu au kusoma vitabu vya wanavyuoni amejua kwamba ushahidi mkubwa wa kimaandishi wa wale wanaosema kwamba kila watu na muandamo wao ni Hadithi ya Ibn Abbaas na Kurayb ambayo utaiona katika kitabu nitachokiambatanisha humu. Hadithi hio nimeielezea kwa urefu na kutoa ushahidi unaopatikana ndani yake na kutoa upinzani wa wale wasiokubaliana na kutoa kwetu ushahidi kwa kutumia Hadithi hio. Pia nilionesha kwa urefu kwamba na sisi tuna jawabu gani juu ya upinzani huo.
Sasa muandishi wa makala niliyemuashiria hapo juu anatwambia kwamba Hadithi ya kurayb tunayoitegemea sisi ni dhaifu, naye - katika kuthibitishi hilo - anatoa maelezo yafuatayo. Anasema: "Hoja kubwa ya wenye kuhalalisha kila nchi kuwa na mwezi wake ni moja tu nayo ni kisa cha Kuraybu mtumwa wa Ibn 'Abbaas walipojadiliyana na Ibn 'Abbaas mwenyewe anasema Kuraybu kuwa "Ummul Fadhli bint Harith [mama yake huyu Ibn 'Abbaas] alinituma kwa Muawiyya katika mji wa Shamu nikafika Shamu na kutekeleza haja zake [zote] na ukaonekana mwezisayari wa mwezi wa Ramadhaan, na mimi nipo Shamu, tukauona mwezisayari usiku wa kuamkiya Ijumaa, baada ya hapo nikarudi Madina mwisho wa mwezi [wa Ramadhaan] akaniuliza Ibn 'Abbaas, kisha akautaja mwezi akasema : lini mliuona mwezi? nikamwambiya usiku wa kuamkiya Ijumaa. Akasema kuniuliza wewe umeuona usiku wa kuamkiya Ijumaa? Nikajibu ndiyo na wameuona watu [wote] na wakafunga, na akafunga Muawiyya [piya] akasema Ibn 'Abbaas lakini sisi tumeuona mwezi usiku wa kuamkiya Jumamosi na tutaendeleya kufunga mpaka tukamilishe siku 30, au tuuone[wenyewe], nikamwambiya [Ibn 'Abbaas] je, hukutosheka kwa kuuona Muawiyya na kufunga kwake akajibu kwa kusema, "hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)."
Ndugu Waislamu hii ndiyo dalili kubwa ya wenye kuhalalisha kila nchi kuwa na mwezi mwandamo wake kwa hakika hawana dalili nyingine zaidi ya kisa hiki, hebu tukichambuwe kwa undani sote ili kila mmoja wetu apate faida je kinafaa kuwa ni dalili ya kutegemeya?
KUMJADILI KURAYBU NA UCHAMBUZI WA KISA HIKI
Kwanza watukufu Waislam kabla hatujasogeya kwenda mbali inabidi mpate faida kumjuwa huyu Kuraybu ni nani? Hili jina la Kuraybu ni la baba yake ambaye na wanachuwoni wa hadith wanamkubali huyu baba yake kuwa alikuwa mtu mkweli sana na anategemewa katika upokezi wa hadithi tazama kitabu 'Tahdhibu' cha Imam Ibn Hajar Al 'Asqalani [jalada la 3 uk 468 chapa ya Beirut tazama mahala pa herufi kaaf] Na tazama vile katika Taqribu Tahdhibu cha huyu huyu Ibn Hajar Al Asqalani jalada la 2, uk 28. Lakini huyu aliye katika kadhiya hii na Ibn 'Abbaas jina lake kamili ni Muhamad Ibn Kuraybu Ibn Abi Muslim Al Hashimiy alikuwa ni mtumwa wa Ibn 'Abbaasi na mama yake Ibn 'Abbaasi Umul Fadhli alikuwa akimtuma sana kwenda Shamu kwa Muawiyya.
Na yeye huyu si Sahaba bali ni katika tabiin na si mtu wa kuaminika katika elimu ya hadith hakubaliki. Hebu tuwasikilize wanachuwoni wetu wa hadith wanavyomchambuwa huyu Muhamad Bin Kuraybu. Amesema Athram toka kwa Ahmad bin Hanbal kuwa, "Huyu Muhammad Bin Kuraybu hadith zake ni 'Munkar" Na amesema Ad Duuriyu toka kwa Ibn Maiyn kuwa "Hadith zake huyu si chochote". Na amesema Ibn Numair; "upokezi wake haufai kabisa ni dhaifu". Na amesema Ibn Hatim toka kwa baba yake kuwa "Huyu Muhamad Bin Kuraybu hazitolewi hoja hadith zake". Na amesema Abi Zur'a kuwa "Hadith zake ni laini mno".
Na amesema Imam Al Bukhaariy kuwa "Hadith zake huyu ni za kuchunguzwa sana". Na akaendeleya kusema Imam Al Bukhaariy kuwa "Hadith zake huyu ni Munkar hazikubaliki". Kumbuka ndugu Muislamu pindi imam Al Bukhaariy anaposema kuwa hadith za mtu Fulani ni munkar basi wanachuwoni wote wa hadith wamekubaliyana kuwa zinawekwa upande wa dhaifu. Na amesema Imam An Nasaaiy "Huyu Muhamad Ibn Kuraybu ni dhaifu". Na vivyo amesema Imam Adaara Qutni. Na amesema Abubakar Al Athram: "Nilimuuliza Imam Ahmad Bin Hanbal kuhusiyana na hadith za huyu Muhamad Bin Kuraybu akasema 'Ni Munkar kwa sababu analeta hadith za ajabu kabisa".
Na amesema Imam Ibn Hibbaan kama alivyonukuliwa katika Mizanul i'tidali ya Imam Adh Dhahabi kuwa "Huyu Muhamad bin Kuraybu alikuwa ni mudalisi [mrongo]". Na amesema Abu Na'im Ad Damishqi kuwa, "Huyu Muhammad Bin Kuraybu alikuwa anachanganya hadith sahihi na dhaifu". Kumbuka ndugu Muislamu hakuna hata mwanachuwoni mmoja wa hadith aliyemtaja huyu Muhamad Ibn Kuraybu kuwa ni mkweli." Mwisho wa kunukuu.
NASAHA
Kabla sijaanza kutoa jawabu juu ya maneno haya, ningependa kutoa nasaha zangu kwa muandishi wa makala. Tunamuomba muandishi wa makala amche Mungu; akumbuke siku ya hisabu; asiseme kitu asichokijua juu ya Mwenyezi Mungu au Mtume wake au dini yake akapoteza watu bila ya elimu. Allah anasema:"Wala usifutilie usichokuwa na elimu nacho." Na anasema: "Sema hakika Mola wangu kakataza maovu na (kakukatazeni nyinyi) kusema musichokijua." Na akasema"Na ni nani aliyedhalimu zaidi (wa nafsi yake) kuliko anayemzulia Allah uwongo ili awapoteze watu bila ya elimu." Na halkadhalika Mtume(s.a.w.w) katoa indhari kubwa katika Hadithi kadha wa kadha kuhusu mtu kusema kitu asichokijua akawapoteza watu. Aya zote hizo zinatupa indhari juu ya kusema kitu katika dini ya Allah bila ya kuwa na ujuzi nacho.
JAWABU
Baada ya nasaha hizo sasa natotoe jawabu juu ya baadhi ya nukta (points) za makala hio, tukianzia na Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas na khususan kuhusu sanad ya Hadithi hio. Jawabu ni kuwa muandishi wa makala kachanganya mambo! Amesema kitu ambacho hata hao wanavyuoni wakubwa wa Hadithi hata waliopinga kutoa ushahidi kwa Hadithi ya Kurayb hawakukisema. Sijui Sheikh umepata wapi kwamba Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Kurayb!!!!!!!!! Kama yupo basi naye tutamdai ushahidi kama tunavyokudai wewe ewe Sheikh muandishi wa makala. Sanad ya Hadithi hii katika masimulizi ya Muslim na wengine ni: "Yahya bin Yahya (bin Bukair) katupa habari Ismail bin Ja'afar kutoka kwa Muhammad (naye ni Muhammad bin Abi Harmala) kutoka kwa Kurayb." Hii ndio sanad ya Hadithi hii. Sasa sijui ni nani aliye dhaifu katika wapokezi hawa?!
Ama Muhammad bin Kurayb unayemzungumzia wewe, yeye hayumo katika sanad hii wala katika Hadithi hii kamwe. Na ushahidi wa haya ni kwamba Hadithi hii imepokewa na: Muslim Sahihu Muslim, Al-Tirmidhi Al-Sunan, Abu Daud Al-Sunan Al-Nnasai Al-Kubra Al-Bayhaqi Al-Kubra Ibn Khuzaima Al-Sahih. Wakati Muhammad bin Kurayb aliye dhaifu - ambaye ni mtoto wa Kurayb aliyekuwa mtumwa mkombolewa wa Ibn Abbaas: yaani baba na mwana wote walikuwa ni Mawali (Freed slaves) wa Ibn Abbaas - unayemzungumzia wewe yeye ni mpokezi wa Ibn Maja tu katika wapokezi sita: wapokezi wengine hawakupokea Hadithi kutoka kwake; wakati Hadithi hii imepokewa na Muslim na hao wengine niliowataja. Kwa hivyo, Muhammad aliyetajwa katika sanad ya Muslim na wengine si Muhammad bin Kurayb bali ni Muhammad bin Abi Harmala naye ni mmoja wa wanafunzi wa Kurayb , baba mtu. Tafadhali rejea hayo hayo Maraji'u (Referernces) uliyotupa yaani Tahdhibu Al-Tahdhib cha Ibn Hajar. Tazama vizuri mfumo wa Ibn Hajar katika kitabu hicho: utaona kwamba kabla ya kumtaja mpokezi juu hukuekea nani aliyesimulia Hadithi kutoka kwake katika wasimulizi sita wakuu wa Kisuni. Na ukitazama hapo utaona kwamba Muhammad bin Kurayb ni msimulizi wa Ibn Maja: si Muslim na wengine: wakati Hadithi hii imesimuliwa na Muslim na wengine.
Kwa ufafanuzi zaidi, kwa vile utafiti wa sanad za Hadithi huwa hautazamwi kwa mpokezi mmoja, basi tazama sanad ya Al-Tirmidhi utaona sanad inasema kwa uwazi: .."Katuhadithia Muhammad bin Abi Harmala katupa habari Kurayb ". Na katika masimulizi ya Abu Daud: ".Katupa habari Muhammad bin Abi Harmala katupa Habari Kurayb" Na katika masimulizi ya Ibn Khuzaima: "Kutoka kwa Muhammad (yaani bin Abi Harmala) k utoka kwa Kurayb". Na katika masimulizi ya Al-Nasaai: "Katuhadithia Muhammad - naye ni Ibn Abi Harmala - kasema kanipa habari Kurayb". Na katika masimulizi ya Al-Bayhaqi: "Kutoka kwa Muhammad bin Abi Harmala kutoka kwa Kuraib".
Kwa hivyo, dai hilo kwamba Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Kurayb si dai sahihi bali ni kutaka kulazimisha kuwa Hadithi hii lazima iwe dhaifu na kwa hivyo kama hakuna mpokezi dhaifu katika Sanad yake basi akachukuliwe mwengine ukooo apachikwe ilimradi Sanad iwe dhaifu, lakini ushahidi wa udhaifu haupo hata mukiomba msada kwa binaadamu wote na majini wote. Bali kama tulivyosema kwamba hata wasiokubaliana na kutoa ushahidi kwa Hadithi hii miongoni mwa wanavyuoni wakubwa kama Al-Shaukani, hawasemi kuwa hii ni Hadithi yenye sanad dhaifu wala hawasemi kuwa imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Kurayb, bali wanasalim amri mbele ya usahihi wa Sanad ya Hadithi hii, tafauti ni katika kuifahamu tu: Al-Shaukani - kwa mfano - akadai kuwa hii ni ijtihad ya Ibn Abbaas, nalo ni kosa kama tulivyobainisha katika kitabu Ushahidi Uliowekwa Wazi.
MATN YA RIWAYA YA KURAYB NA IBN ABBAAS
Baada ya muandishi kutupa utafiti wake wa sanad ya riwaya ya Kurayb, alitupa utafiti wake juu ya matn (text) ya riwaya hio, akasema: "Baada ya kumaliza kumkaguwa huyu Kuraybu ebu sasa ndugu Muislamu tuje kukikaguwa kisa chenyewe, tukianza na qauli ya Ibn 'Abbaas kukataa kufunguliya kwa mwezi ulioonekana katika mji wa Shamu kasema Imam Alqarafi katika kitabu cha "Adhakhira" ya kuwa, "Siku ile habari ya mwezi alipopewa Ibn 'Abbaas kutoka kwa Kuraybu kulikuwa hakuna mawingu yaliyotandaa katika mji wa Madina, na wala haukuonekana mwezi siku hiyo, Ibn 'Abbaas akatanguliza kuuona yeye mwezi kuliko ile habari au taarifa alioletewa na Kuraybu, na ndiyo maana akasema: "Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa maana tusichukuwe habari za dhana na tukaacha yakini, japokuwa hakuna tafauti ya kuutazamiya mwezi kukiwa kuna mawingu au hakuna mawingu, lakini yeye alihukumu kwa kuuona mwezi. Anasema Imam Alqarafi kuwa "Hiki kisa kishakuwa na utata mkubwa".
Na qauli ya Ibn 'Abbaas ya kukataa kufunguliya mwezi ulioonekana Shamu na kusema hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akaishiya hapo hakuendeleya na wala hakufafanuwa zaidi na kisa hiki kikaishiya hapo. Na utata ukawa mkubwa katika safu za Waislamu kutokana na kutokupatikana ufafanuzi zaidi juu ya kisa hiki." Mwisho wa kunukuu. Tunasema: Habari ya Kurayb alioitoa ilikuwa inahusu mwezi muandamo wa mfungo: si wa mfunguo, kama riwaya yenyewe inavyosema: "Ukaniindamia mwezi wa Ramadhani (si wa Shawali) nami niko Sham" na mwezi muandamo wa mfungo unathibiti kwa ushahidi wa mtu moja muadilifu kama wewe mwenyewe Sheikh ulivyotwambia katika makala yako kwamba: "Akiona mwezisayari mtu mmoja na akatoa habari kwa wengine katika eneo lina kiongozi wa Kiislam itawalazimu watu wote wafunge." Kwa maana hii hakuna maana ya kuiita habari ya Kurayb kuwa ni habari ya dhana kwani habari ya dhana yaani ya mtu mmoja inakubalika katika mwezi Muandamo kama vile Mtume(s.a.w.a) alivyoikubali habari ya Ibn 'Umar peke yake. Na kauli ya Al-Qarafi aliposema: "Hiki kisa kishakuwa na utata mkubwa" haina uwezo wa kuibatilisha riwaya hii baada ya kuthibiti kwake kwa sanad sahihi.
Anaendelea Sheikh muandishi wa makala kwa kusema: "Sasa basi tujiulize sote kwa pamoja kaamrishwa na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nini? Wamekhitilafiyana wanazuwoni katika makundi manane juu ya hii amri anayosema Ibn 'Abbaas kaamrishwa na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
1) "Kundi la kwanza la wanazuwoni wanasema kaamrishwa na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asifunge wala kufunguwa katika siku itakayokuwa mawingu yametanda angani wakamilishe 30 Shaabaan au 30 Ramadhaan."
Tunasema: Nayo hii ni kauli ilio na udhaifu wa wazi. Kwani maudhui ni kuwa mwezi umeonekana Sham kabla ya Madina, ikiwa Ibn Abbaas aliuzingatia muandamo wa Sham basi asingelisema kuwa "Hatutoacha kufunga hadi tutimize siku thalathini au tuuone mwezi," kwani kutimiza siku thalathini Madina ni kutimiza siku thalathini na moja huko Sham. Na kwa vile hakuna mwezi wa siku thalathini na moja, basi kwa vyovyote vile Ibn Abbaas kama aliukubali muandamo wa Sham alikuwa atimize siku 29 tu kwani wakati huo itakuwa Sham mwezi kwa hakika umeshamalizika. Ama dai kwamba "Kaamrishwa na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asifunge wala kufunguwa katika siku itakayokuwa mawingu yametanda angani wakamilishe 30 Shaabaan au 30 Ramadhaan" halihusiani na tokeo hili kamwe kwani hapa maudhui ni kuwa mwezi umeonekana Sham lakini haukufatwa Madina: hakuna suala la mawingu hapa.
Anasema muandishi:
2) "Kundi la pili wao wanasema: "Kaamrishwa na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asipokee taarifa ya kufunga au kufunguwa kutoka kwa mtumwa kwa sababu wale wote walioleta habari ya mwezi wa kufunga au kufunguwa zama za Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa si watumwa, na Kuraybu alikuwa ni mtumwa wa Ibn 'Abbaas (radhiya Allahu 'anhu)." Tunasema: Na hii pia ni kauli dhaifu, kwani Kurayb hakuwa mtumwa ambaye kamilikiwa, bali ni Maula yaani mtu aliyekombolewa kutoka katika utumwa, na mawla (freed slave) hukumu zake katika Uislamu ni sawa na Muislamu yeyote yule. Anasema muandishi:
3) "Kundi la tatu wao wanasema kaamrishwa na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asipokee taarifa au habari ya mwezi kutoka kwa mtu mmoja tu mpaka apatikane mwingine mwenye kumshuhudiya huyo mtowa habari." Tunasema: Na hii pia ni kauli dhaifu kwani Mtume(s.a.w.w) kapokea habari ya bedui peke yake nayo japokuwa ni hadithi yenye sanad dhaifu lakini maana yake ni sahihi kwani katika Hadithi nyengine tunapata kwamba Mtume(s.a.w.w) pia alipokea habari iliotolewa na Ibn Umar peke yake. Wala lisipingwe hili kwamba hii ilikuwa ni mahususi kwa Mtume(s.a.w.w) kwani tunasema kwamba matendo ya Mtume(s.a.w.w) ndio kigezo kwa Umma wake ila ikiwa kutakuwa na ushahidi kuwa kitendo kadha ni kwa ajili yake tu. Bali Ibn 'Umar - kama ilivyo katika riwaya alioisimulia Ibn Abi Shaiba kama utavyoona katika kitabu - kaujuzisha ushahidi wa mtu mmoja peke yake na watu wa Madina wakafunga kwa ushahidi huo.
Anasema muandishi:
4) "Kundi la nne wanasema kaamrishwa na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa yeyote yule atakayesafiri kutoka katika mji ambao haukuonekana mwezi na kuelekeya katika mji ambao umeonekana, basi hukumu yake atafunga pamoja na watu wa mji huo na atakuwa ni mmoja kati ya watu wa mji huwo. Kwa mujibu ya mafundisho haya ya Kuraybu, atatakiwa afunge siku 31."
Ninasema: Nadhani umebirukiza au msemaji kabirukiza: nadhani sahihi ni kusema: "Atakayesafiri kutoka katika mji ambao umeonekana mwezi na kuelekeya katika mji ambao haukuonekana" nadhani hivi ndio sahihi ili rai hii iweze kuwiyana na matokeo yalivyotokea. Nayo pia ni kauli dhaifu kwani haihusiani na mjadala wa Ibn Abbaas na Kurayb kwani msafiri alikuwa ni Kurayb wakati aliyekataa kuufata muandamo wa mbali ni Ibn Abbaas naye alikuwa Madina: hakuwa msafiri. Anasema muandishi:
5) Kundi la tano wao wamesema kaamrishwa na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asikubali mwezi aliyouona Muawiyya kwa sababu mtazamo wake yeye Ibn 'Abbaas (radhiya Allahu 'anhu) alikuwa hautambui utawala wa Muawiyya na alisimama pamoja na Aliy bin Abi Twalibu dhidi ya Muawiyya. Kwa mafundisho haya asikubali mwezi ulioonekana na kiyongozi asiyetambulika.
: Nayo pia ni kauli dhaifu kwani kama tulivyoeleza katika kitabu:
a) Mwezi wa Sham haukuonekana na Mu'awiya tu, bali Kurayb kasema kwa uwazi: "Na watu wakauona na wakafunga." Na alipoulizwa Kurayb "Wewe umeuona?" Akasema: "Ndio." Kwa hivyo, dai hilo halina muelekeo kwani mwezi umeonekana na Mu'awiya, na Kurayb na watu wa Sham. Wala suala la kuonekana kwa mwezi halina uhusiano na uovu wa utawala ikiwa Waislamu wameuona.
b) Ibn Abbas katoa sababu ya kuukataa muandamo huo, hatuna haja ya kumtilia maneno katika kinywa chake. Sababu yake ni kuwa "Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume s.a.w." Kwa hivyo, kudai kwamba Ibn Abbas kaukataa muandamo huo kwa sababu ya uasi wa Mu'awiya, ni kutoa sababu tafauti na ile ambayo Ibn Abbas mwenyewe kaisema kwa uwazi. Anasema muandishi:
6) "Kundi la sita wamesema kaamrishwa na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asikubali kufunguwa na kulipa siku badala yake ile waliokula mchana na isipokuwa kwa mashahidi wawili kwa hilo kuhofiya kuwalipisha watu funga ya siku moja iliyowapita kutokana na taarifa ya mtu mmoja".
Ninasema: Na hii pia ni kauli dhaifu kwani - kama tulivyosema - Ibn Abbaas kaukataa muandamo wa mfungo wa Ramadhani: si muandamo wa mfunguo wa Shawaal, na muandamo wa mfungo - kama tulivyosema na kama riwaya zinavyonena kwa uwazi - hauhitaji mashahidi wawili, bali shahidi mmoja anatosha kama wewe mwenyewe pia ulivyotuandikia. Anasema muandishi:
7) "Kundi la saba wanasema kaamrishwa na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kila nchi ina machomozo ya mwezisayari wake na masafa yake, na masafa yanayokusudiwa ni KM 133.056.
Ninasema: Kauli hii ina usahihi na udhaifu na upungufu. Usahihi ni kuwa tafauti za machomozo ya mwezi ni lazima zizingatiwe kwa mujibu wa Qiyas (analogy) sahihi kama zinavyozingatiwa tafauti za machomozo ya jua. Upungufu ni kuwa Illa (sababu) katika tokeo hili ni murakkaba (yaani sababu ni mbili kwa pamoja: si moja: si machomozo tu: ni machomozo na umbali). Udhaifu ni kuukadiria umbali huu kwa KM 133.056. Maelezo zaidi juu ya hili ni katika kitabu. Kundi la nane alilotuahidi Sheikh muandishi wa makala hakututajia.
TANBIHI
Sasa cha kuzingatia hapa ni kuwa tafauti hizi alizotunakilia Sheikh muandishi wa makala katika kuifasiri riwaya ya Kurayb na Ibn Abbaas hazijaifanya riwaya hio kuwa ni dhaifu, vyenginvyo riwaya kadha wa kadha ambazo ni sahihi kwa makubaliano ya Umma basi wanavyuoni hutafautina katika kuzifasiri hadi kufikia makumi ya rai na zaidi. Hadithi Innamaa Al-A'amalu binniyyaat (Hakika ya matendo ni kwa nia) ni sahihi kwa makubaliano ya Umma, lakini w anavyuoni wametafautiana juu ya maana yake. Je tafauti zao juu ya tafsiri sahihi zitabatilisha usahihi wa Hadithi hii? Bali Aya zote za Qur-ani taqriban zina kauli tafauti za wafasirina juu ya tafsiri gani ya Aya hizo ilio sahihi. Je tafauti katika tafsiri hizo zibatilishe uhakika na ukweli na kuthibiti kwa Aya hizo?! Kwa hivyo, tunasema suala la muandishi aliposema: "Sasa basi tujiulize sote kwa pamoja kaamrishwa na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nini? Jawabu ni kuwa baada ya kuzikusanya illa (sababu) zote zinazofaa kuwa illa ya hukumu hii, illa pekeye inayofaa kuwa illa ya hukumu hio ni umbali uliopo baina ya nchi mbili hizo - Sham na Madina. Na tafauti ya machomozo zinatokana na umbali na hizi zinathibiti kwa njia ya Qiyas (analogy) sahihi kama tulivyobainisha katika kitabu.
DAI LA PILI
Watu wengi wenye msimamo wa kufunga kwa muandamo mmoja utasikia mitaani wakisema: "Kile cha Kurayb na Ibn Abbaas ni kisa: si Hadithi!" Kwa baahati mbaya watu kama hawa wanapopata watu waliopapasa karatasi mbili tatu za vitabu wakawambia hivyo hivyo basi huzidi kuamini kwamba hile si Hadithi bali ni kisa. Na hapa muandishi wa makala anatwambia hivi: "Hoja yao kubwa siyo Qur-aan wala Sunnah ya Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambavyo ndiyo dira yetu tunapokhitilafiyana kama alivyosema Allah Taa'ala katika Qur-aan " Na kama mkikhitilafiyana juu ya jambo lolote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, hiyo ndiyo kheri nayo ina matokeo b ora kabisa."
Hoja kubwa ya wenye kuhalalisha kila nchi kuwa na mwezi wake ni moja tu nayo ni kisa cha Kuraybu mtumwa wa Ibn 'Abbaas..". Mwisho wa kunukuu.
Jawabu Sasa tukuulizeni enyi muliosoma elimu ya Hadithi kwani Hadithi ni nini? Wataalamu wa Hadithi wana hiki cha kutwambia:
1) "Kauli ya Sahaba (ataposema): tumeamrishwa kadha au tumekatazwa kadha.na iliofanana na hio, basi kilichosahihi ni kuwa zote hizo hupewa hukumu ya (Hadithi) marfu'u (huzingatiwa kuwa ni Hadithi iliotoka kwa Mtume s.a.w.)."
2) "Ikiwa Sahaba ataitaja amri kwa uwazi akasema kwa mfano: 'Mtume (s.a.w.) katuamrisha, basi hakuna khilafu (ya wanavyuoni) ndani yake (hiyo ni Hadithi marfu'u: ni Hadithi ya Mtume(s.a.w.w) ." Al-Suyuti Tadribu Al-Rawi uk. 161.
3) "Ama Sahaba akileta lafdhi yenye uwezekano wa kuwepo mtu mwengine baina yake na Mtume(s.a.w.w) , kwa mfano akisema: 'Mtume kasema kadha au kaamrisha kadha au kakataza kadha au kahukumu kadha basi Jumhur inasema kuwa (kauli hio) ni hoja (katika hoja za Kisharia)". Al-Shaukani Irshadu Al-Fuhul uk. 92 Faslu Fii Alfadhi Al-Riwaya. Na mfano wake ni maelezo ya Al-Imamu Al-Ghazali katika Al-Mustasfaa uk. 104 Al-Muqaddimatu Fii Bayani Alfadhi Al-Sahaba.
4) "Na katika hio ni kauli ya Sahaba anayejulikana kwa usahaba (wake): (ataposema kwamba) 'Tumeamrishwa tufanye kadha" na"Tumekatazwa kutokana na kadha wa kadha" na "Tulikuwa tunaamrishwa kadha" na "Tulikuwa tunakatazwa kadha" .Ikiwa atayasema hayo Sahaba anayejulikana kwa usahaba (yaani anayejulikana kuwa ni Sahaba), basi hio (inazingatiwa kuwa ) ni Hadithi musnad (kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) na zote hizo zimepokewa katika Masanid (Hadithi zilizotoka kwa Mtume(s.a.w.w) . Tazama Al-Hakim Ma'arifatu 'Ulumu Al-Hadith uk. 22 katika Dhikru Al-Naw'i Al-Sadis.
5) "Sahaba akisema: 'Nimemsikia Mtume(s.a.w.w) anaamrisha kadha au anakataza kadha".(basi kauli) inayotegemewa na walio wengi ni kuwa hio ni hoja" . Al-Aamidi Al-Ihkam j. 2, uk. 325.
6) "Na kauli ya Sahaba (ataposema):'Tumeamrishwa kadha' au 'Tumekatazwa kadha' ni (Hadithi) Marfu'u, Musnad (yaani inazingatiwa kuwa ni Hadithi kutoka kwa Mtume mwenyewe(s.a.w.w) kwa Wanavyuoni wa Hadithi, nayo ndio kauli ya wanavyuoni wengi." Ibn Kathir 'Ulumu Al-Hadith j. 1, uk. 150. Anasema Sheikh Ahmad Shakir katika maelezo yake ya chini katika kitabu hicho: "Nayo ndio (kauli) sahihi."
Sasa mukhtasar wa haya ni kuwa wanavyuoni taqriban wote wamekubaliana bali wengine wamenukuu makubaliano kwamba Sahaba akisema "Mtume(s.a.w.w) katuamuru kadha au katukataza kadha," basi hio inazingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume(s.a.w.w) wala si lazima kuwa Sahaba huyo ainukuu lafdhi alioitamka Mtume(s.a.w.w) . Na mifano ya Hadithi za namna hio ziliokubalika iko mingi sana katika vitabu vya Hadithi. Mfano mmoja ni Hadithi alioipokea Al-Bukhari katika Sahihu yake Hadithi na. 578 na Muslim katika Sahihu yake Hadithi na. 378 "Kutoka kwa Anas kasema: 'Bilal aliamrishwa aifanye adhana kuwa ni shafi'i (Even) na Iqama aifanye kuwa ni witr (Odd)". Utaona kwamba Sahaba hapa kasema tu kwamba Bilal kaamrishwa bila ya kuinukuu lafdhi alioitamka Mtume(s.a.w.w) kumwambia au kumuamuru Bilal kwayo. Na hii imezingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume(s.a.w.w)
Sasa ukirudi kuitazama riwaya ya Ibn Abbaas na Kurayb, utamkuta Ibn Abbaas anasema:"Hivi (ninavosema au ninavyofanya mimi) ndivyo alivyotuamrisha Mtume (s.a.w.w)". Kwa hivyo, hii ni Hadithi marfuu yenye kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) , na kuitwa kuwa ni kisa haina maana kuwa si Hadithi. Bali Hadithi nyingi ambazo ndani yake muna matokeo fulani huitwa kuwa ni visa wala haina maana kuwa hizo si Hadithi. Kisa cha Sahaba Tha'alaba kwa mfano - nacho ni dhaifu - kinaitwa kisa na kinaitwa Hadithi. Kimeitwa kisa kwa sababu ya matokeo yaliokuwemo ndani yake na kimeitwa Hadithi kwa kuhusishwa nacho Mtume(s.a.w.w) . Mimi nahofia kuwa hawa watu wenye fahamu kama hizi kesho watakuja kutwambia kwamba baadhi ya Aya za Suratu Al-Qasas (Sura yenye visa vya Musa na Fir'awna na wengine) si Qur-ani bali ni visa tu kwani imeitwa Sura yenye visa!!!!!!!!!!!! Kwa hivyo, kuyaita maneno ya Ibn Abbaas yasemayo "Hivi (ninavosema au ninavyofanya mimi) ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) ", kuwa ni kisa kwa maana kwamba si Sunna (Hadithi) ya Mtume(s.a.w.w) ni kwenda kinyume na kanuni za Elimu ya Hadithi na kanuni za Usulu Al-Fiqhi.
DAI LA TATU
Muandishi anasema: "Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mwenyewe katika maisha yake kafunga Ramadhan 9 kauona mwezi kwa macho yake mara 2 kaletewa habari za mwezi mara 3 toka Madina na mara 4 toka nje".
JAWABU
Sijui ndugu muandishi unakusudia nini kwa kusema "Na mara 4 toka nje". Je ni kutoka Oman, Yemen, Sham au wapi? Mara zote alizopewa habari ilikuwa ni habari kutoka Madina: wakati mwengine ilikuwa ni habari kutoka katika miji ya Madina na mara nyengine ni habari kutoka katika jangwa la Madina. Kwa hivyo, zote ni habari za Madina.
Hizi ndio nukta muhimu zilizokuemo katika makala ya Muandishi. Ama mengine yote alioyasema tumeyajadili katika kitabu ambacho tutakiambatanisha na makala hii ili wale ambao hawakukipata kitabu hicho waweze kuona hoja za pande zote na mdahalo juu ya hoja hizo.
2
MUANDAMO WA MWEZI
SURA YA PILI
JAWABU KWA WANAFUNZI WA BACHOO JAWABU YA UTANGULIZI
Wahusika ndugu zetu wa Masjid Al-Sunna Zanzibar, wameanza kitabu chao hicho kwa utangulizi wenye kumshukuru na kumuhimidi Allah na kumtakia rehema na amani Bwana wetu Muhammad (s.a.w.) kama zilivyo khutuba na vitabu vya kiislamu. Na hayo yote yamefanyika chini ya utangulizi wenye anwani:
UKWELI JUU YA KUANDAMA KWA MWEZI
Na hii ndio sehemu ya kwanza ya kitabu chao. Wakasema katika utangulizi huo: Msisitizo wetu mkubwa katika kitabu hiki ni ile nukta muhimu ya kwamba suala la kufunga na kufungua kwa muandamo mmoja kwa dunia nzima si jambo jipya kama wanavyodhani baadhi ya watu, ni jambo la kale mno ambalo linaweza kutekelezeka na kwamba huo ndio uliokuwa msimamo wa 'Jamhur' ya wanavyuoni.
Jawabu Nakubali kuwa hili ni jambo la zamani, lakini kudai kuwa hii ni kauli ya Jumhuri ni madai hewa: hayana ushahidi. Leo hii duniani hakuna madhehebu yoyote ambayo inaitendea kazi kauli hio kama ni madhehebu nzima, bali kuna baadhi ya watu tu katika kila madhehebu ambao wanafata kauli hio. Hata zile madhehebu ziliotajwa kuwa ni zenye kufata kauli hio kama vile Malik, Hanbal na Hanafi, basi hawaitendei kazi kauli hio ila baadhi yao tu. Libya, Algeria na nchi nyengine za Afrika Kaskazini na Magharibi - kwa mfano - ni nchi za wafuasi wa madhehebu ya Malik, nao wanafata miandamo yao wenyewe. Kwa hivyo, dai kuwa hii ni kauli ya Jumhur ya wanavyuoni, si dai sahihi.
SEHEMU YA PILI
Katika sehemu ya pili, ndugu waandishi wanasema:
2. Si Fikra Za Shaykh Naaswir Bachuu "Ndugu yetu Juma Muhammad Rashid Al-Mazrui amejitahidi kuandika kitabu alichokiita: "Ushahidi Uliowekwa Wazi Katika Suala La Miandamo Ya Mwezi. Makusudio yake yalikuwa ni kutaka kukijibu kitabu kilichoandikwa na Shaykh Naaswir Abdullah Bachuu kinachojulikana kwa jina la "Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi."
Jawabu Kidogo na mimi naomba niweke wazi kwamba kitabu changu hakikuwa kabisa na lengo la kujibu kitabu cha Sheikh Nassor Bachoo. Hili la kunukuu maneno yake na kuyajadili lilikuwa ni jambo la kutokea tu baada ya mtu Fulani kuniletea kitabu chake. Kwa havyo, kama mulivyosema nyinyi katika kitabu chenu kwamba: Kitabu hiki ni kama nasaha kwa Waislamu wote ili kuweza kudumisha umoja wetu hususan pale ambapo pamejitokeza misimamo tofauti katika mambo ya ibada. Wala lengo la kitabu hiki sio kuendeleza malumbano baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe hata kwa wale wenye misimamo tofauti. Kutajwa ndugu yetu Juma Muhammad Rashid lilikuwa ni jambo lisilobudi wala hapakuwa na lengo la kumkashifu au kumuumbua bali ni kutokana na kuwa hapakuweza kupatikana njia mbadala kwa vile ameshaandika kitabu ambacho ameshakichapisha chapa ya kwanza na ya pili.
Basi na mimi nakuombeni munielewe hivyo hivyo, kwamba wakati mimi naikubali fikra Fulani na kuikataa fikra Fulani, hakuna budi ninukuu fikra pinzani na kuonesha kwanini siikubali; na kwa upande wa pili ni lazima nioneshe kwanini naikubali fikra ninayoikubali. Na nitaposema kuwa kuna watu wana fikra hii, basi nadhani haitokuwa jambo la busara kama watu hao sikuwataja na nikiwataja ni lazima nitaje marejeo. Kwa sababu hii ndio maana nimekuwa nikinukuu maelezo ya Sheikh wetu Nassor Bachoo na kumjadili mule nisimokubaliana naye. Naomba musihuzunike kwani kujibizana katika kutafuta ukweli ni suala mashuhuri katika uwanja wa elimu. Wanavyuoni wakubwa wa kale na wa sasa wamekuwa wakijibizana ili kutafuta ukweli na hatimae huwabainikia woa pamoja na wasomaji. Kwa hivyo, hamukuwa na haja ya kutumia lugha: "Wala hapakuwa na lengo la kumkashifu": hii si kashfa hata kidogo: hii ni elimu.
Lakini, hakuna haja ya kufichana; kitabu chenu mumeandika kwa kujibu kitabu changu. Hamuna haja ya kusema: "Wala lengo la kitabu hiki sio kuendeleza malumbano baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe hata kwa wale wenye misimamo tofauti. Kutajwa ndugu yetu Juma Muhammad Rashid lilikuwa ni jambo lisilobudi wala hapakuwa na lengo la kumkashifu au kumuumbua bali ni kutokana na kuwa hapakuweza kupatikana njia mbadala kwa vile ameshaandika kitabu ambacho ameshakichapisha chapa ya kwanza na ya pili", kwani kitabuchenu kimeanza kwa kunitaja mimi mwanzo hadi mwisho na kuniaga kwa kunipa nasaha mimi. Ama mimi naandika jawabu hii kukujibuni nyinyi: sikufichini wala sisemi uwongo.
Munasema Kutokana na jambo hilo , sisi kwa upande mmoja tunashukuru kwa juhudi yake hiyo na kwa upande wa pili tunatuma masikitiko yetu kwake kwa kutokuwa makini na muadilifu katika kulifafanua jambo hilo muhimu. Kwani kitabu chake hicho kimeandikwa katika mfumo wa chuki, kibri, kejeli na malumbano huku akisisitiza kwa mara nyingi kauli chafu ambazo muandishi hapaswi kuzitumia katika kitabu au katika mijadala ya Dini. Jawabu Hizi chuki, kibri na kejeli, mimi nimezisoma kwenu, kwa hivyo na iwe kama msemo wa Waswahili: "Papa akipea mafuta huwapa wanawe". Je nyinyi munayakumbuka haya:
1) Munaukumbuka muhadhara wa Sheikh Bachoo ambao alisema kuwa wasionyanyua mikono katika sala wanasali kama mipopoo? Jamani! Hii si kejeli? Je katika nyinyi yuko aliyetoa muhadhara au kuandika kitabu ili kumjibu Sheikh wetu. Sasa uadilifu uko wapi?
2) Je munaukumbuka muhadhara wa Sheikh Bachoo aliozungumzia mas-ala ya udhu kasha akasema: "Wengine wakitia udhu kiungo hiki huomba dua hii na kiungo hiki huoma dua hii; upumbavu mtupu". Je haya si matusi? Je hii si kejeli?
3) Siku moja palikuwa na maziko. Maiti alisaliwa msikiti wa wajiitao "Watu wa Sunna". Kijana mmoja akasimama akasema: "Leo tunataka kukuonesheni vipi Mtume (s.a.w.) kamsalia maiti: si kama wanavyofanya Ibadhi na Shia.
4) La nne ni kuwa ikiwa nyinyi mumethubutu kunita mjeuri, mwenye kibri na kejeli; maneno ambayo mimi sikukwambieni wala kumwambia Sheikh Nassor; mimi nimemtoa makosa tu Sheikh wetu: na hii ni kawaida katika uwanja wa elimu; sasa je na nyinyi pia ni majeuri, wenye kibri na kejeli? Katika uwandishi wenu, pia mumesema: "Hatujui dhana hii potofu ameitoa wapi." Mwenye dhana potufu naye ni mpotufu, kwa hivyo na nyinyi hamukutoa nasaha bali mumetukana. Nakupeni mifano hii mitatu ya Sheikh wetu na mmoja wenu nyinyi wenyewe enyi wenye kuandika Radan mardudan na mifano iko mingi. Inatosha kuwaita kwenu watu wengine kuwa ni watu wa bidaa na nyinyi ndio watu wa Sunna. Kwa hivyo, hii hali mumeiuda nyinyi wenyewe: Zanzibar bali Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla haikuwa hivi. Chuki mumeziunda nyinyi; mukijirekebisha kwa kutumia lugha nzuri nadhani hakuna atayekwambieni jambo kwa lugha nzito.
Mnasema Mfano wa kauli zake mbaya ni kama zifuatazo:
(vuta-nikuvute) [uk. 6]
(hii ni ajabu katika ajabu za dunia!) [uk. 124]
(Kwa hivyo, uwezekano huo alioutoa Sheikh hauwashi wala hauzimi [uk. 124]
(Ninasema: Enyi walimwengu wenzangu tazameni hoja za kielimu hizo!!!!!!! Kwani nyinyi Wazanzibari kabla ya kuja fikra hio ya Sheikh Nassor Bachoo ya kufunga kwa muandamo mmoja,)
(Utaona kwamba masuala yote haya si yenye kima katika soko la elimu, bali ni masuala ya kuwababaisha watu wasiojua nini cha kujadiliwa katika mas-ala haya ya funga) [uk. 167]
(Hoja nyengine - nayo pia ni hoja ya mitaani - ni kuwa watu wengi wa kawaida wanapouona mwezi mkubwa husema: "E basi ule ndio mwezi wa leo ule?!!!")
(Jawabu hii ya mwisho, inaufanya upinzani mzima wa Sheikh Bachoo kuwa hauna maana yoyote.) [uk. 132]
(Kwa ufupi ni kuwa hicho walichokidai watetezi wa rai pinzan) [uk. 32]
(utaona jinsi gani mwanamume alivyokuwa bingwa wa kubadilika! Na hili si jengine bali ni lile Waswahili wanalolisema: "Mfa maji hukamata maji.") [uk. 128]
(Hakuna hapa kinachoonesha mas-ala ya kufunga kwa muandamo mmoja wala kumi na moja.)) [uk. 125] (haina maana kwamba usiku ukiingia sehemu moja ndio umeingia dunia nzima. Kwa ufupi ni kuwa hii ni hoja ambayo haina faida yoyote ya kielimu, lakini tunaijadili kwa ajili ya watu wa mitaani tu.)
Jawabu Sikubaliani na nyinyi kwamba humu muna maneno mabaya. Lakini hata nikikubali basi nasema kwamba lugha ya namna hii sababu ni nyinyi, na kwa hivyo, utaona kwamba ninapojadiliana na watu wengine basi lugha yangu hubadilika. Kwa hivyo, tujirekebisheni sote na tujadili tafauti zetu kwa lugha ya kiungwana. Ama ukinita mpopoo, basi usinilaumu na wewe nikikwita mnazi: unanilaumu nini na wewe unakifanya kile kile nikifanyacho?! Bali hata katika kitabu hiki munachonijibu, basi nanyi mumetumia lugha hizo hizo. Katika baadhi ya sehemu umesema: "Kwa hakika katika kitabu chake hicho kwenye uk 6, anajionyesha alivyo na kauli mbili tofauti..". Na mwishoni mwa kitabu mumesema: "Dhana ya pili ya ndugu Juma imejengeka katika msingi dhaifu wala haina nafasi katika uwanja wa fani (kitaalamu) nao ni kule kusukuma kwake juu ya elimu ya Jiografia". Na yamo mengi katika kitabu chenu. Sasa nyinyi mwasema nini na mwatenda nini?
Munasema "Kwa hakika katika kitabu chake hicho kwenye uk 6, anajionyesha alivyo na kauli mbili tofauti: Kwanza anakubali kwamba suala la muandamo wa mwezi lina ikhtilafu katika kufunga kwa kumuelezea Shaykh Naaswir Bachuu kwamba: (Tunampongeza kwa juhudi) Kisha pale pale anageuka kwa kusema: (madamu hili ni suala la khilafu - basi i likuwa ni kutolizungumza kabisa,) Sasa hebu tumuulize ndio anapongeza nini? Na ni nani aliyemwambia kwamba jambo lenye khitilafu halizungumzwi? Yeye angezungumza nini katika kitabu chake kama si masuala ya ikhtilafu? Pia anatwambia haya ni katika mambo ya furui (matawi) za Kidini, kwa hivyo zisizungumzwe. Kwani ni nani aliyemwambia kuwa furui za Kidini hazizungumzwi?"
Jawabu Ikiwa lugha hii ndogo hamukuweza kuifahamu, vipi mutaweza kufahamu kitu chenye kuhitaji fani za lugha na usuli na mengineo. Ikiwa mimi niliingia msikitini kwenu Raha Leo nikakuta juu ya ubao wenu munawasomesha vijana na katika darsa hio Mubtadaa mumemwita Fa'il (vipi mutaweza kujadili masuala haya?!!! Mimi nimempongeza Sheikh Bachoo kwa juhudi au moyo wake; na sikumpong eza kwa kulikuza suala ambalo:
1) Ni la furuu'i
2) Lina khilafu. Na hii haina maana kuwa Furu'i zisizungumzwe; suala la Furu'i huwa halishadidiwi; bali unawaacha watu kama walivyo tu. Lakini yeye anapenda kushadidia katika mas-ala kama haya; ndio maana akashadidi hata katika suala la kufunga mikono hata kuwaita watu mipopoo bali na kuwambia kuwa hawana Sala. Kwa hivyo, nieleweni kwamba ninachokipinga ni kushadidia au kuwakoroga watu katika kitu ambacho ni furu'i za dini ilhali yeye kawakuta na msimamo tafauti tangu zamani. Katika mas-ala ya furu'i, wanavyuoni huwa hawashadidi juu ya Mas-ala kama haya. Mimi leo nikisimama nikaanza kufanya kampeni kwamba watu wasiitikie amina wa kisali, nalo ni jambo la furu'i, si nitakuwa natia fitna tu? Jambo kama hili huwachwa wasomi wakalitafiti kaiha kila mmoja akafanya vile ilivyombainikia. Lakini kufanya kampeni maalumu na da'awa kana kwamba waliotangulia wote ni wapotovu, hili ndilo jambo la kulaumiwa.
Ama kauli yenu: "Kwanza anakubali kwamba suala la muandamo wa mwezi lina ikhtilafu katika kufunga kwa kumuelezea Shaykh Naaswir Bachuu kwamba: (Tunampongeza kwa juhudi) Kisha pale pale anageuka kwa kusema: (madamu hili ni suala la khilafu - basi ilikuwa ni kutolizungumza kabisa,) Sasa hebu tumuulize ndio anapongeza nini?" Mwisho wa kunukuu. Na mimi nikuulizeni nyinyi mumenishukuru kwa juhudi yangu kisha mwisho wa kitabu mukaniambia: "Mwisho tunachukua fursa hii kumuonya ndugu Juma kuwa amuogope Mwenyezi Mungu hususan katika mas-ala ya kielimu. Akumbuke kuwa Mwenyezi Mungu Ameonya juu ya mtu kusema jambo au kufanya asilolijua. Aelewe kwamba ataulizwa juu ya hilo. Lingekuwa jambo la busara kama ndugu Juma angalikubali kuuliza na kufanya utafiti zaidi juu ya mas-ala haya kama agizo la Mwenyezi Mungu linavyotutaka". Sasa na nyinyi munanishukuru nini?
Munasema "Sisi tunapenda kumfahamisha kuwa suala hili la kwamba mwezi ukiandama sehemu moja unatosheleza kufuatwa kwa kufunga au kufungua ulimwengu mzima, si suala jipya bali ni jambo la kale. Tunasikitika kwamba hakuangalia vizuri maoni ya Wanavyuoni wakubwa walivyoelezea msimamo huo. Angalia katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 51-58. Hapa tunanukuu baadhi ya kauli hizo:
Imamun-Nawawy aliyekisherehesha Kitabu cha Sahihi Muslim anasema:
"Na jambo lililo sahihi kwa wenzetu (Mashaffi) ni kuwa muandamo mmoja hauwahusu watu wote bali unawahusu wale walio karibu kwa kiasi ambacho hawaruhusiki kupunguza Sala (Sala ya safari). Pia imesemwa kuwa iwapo matlai ni mamoja watalazimika (watu) kufunga pamoja. Pia imesemwa kuwa ikiwa (wanaishi) katika eneo la Iklimu moja (maili 72 au km 89) (watalazimika kufunga pamoja) vyenginevyo kila mmoja atafunga kwa muandamo wake. Na wakasema wenzetu wengine (Mashaffi) kuwa muandamo katika sehemu moja utawahusu wote wa dunia nzima".
Shaykh Jaadul Haq wa chuo kikuu cha Al-Azhar katika kitabu chake "Bayaanullinnas" J. 2 uk 203 - 204 ameandika yafuatayo juu ya kauli hiyo ya Imamun-Nawawy:
"Hapa Imamu An-Nawawy ametaja kwa mukhtasari kauli zilizomo katika madhehebu ya Kishaffi (juu ya kuandama kwa mwezi) na ambazo pia zimo katika madhehebu mengine ya Kiislamu. Kauli hizo tunaweza kuzigawa katika maf ungu matatu makuu: "...Hapo Imamu An-Nawawy ametaja kwa mukhtasar kauli zilizomo katika madhehebu ya Shaffi (juu ya kuandama kwa mwezi) na ambazo pia zimo katika madhehebu nyengine za Kiislam. Kauli hizo tunaweza kuzigawa katika mafungu matatu makuu: Kauli ya kwanza: "Kila nchi iwe na matlai yake, wala muandamo wa nchi moja hautalazimu nchi nyengine ya mbali wala karibu". Kauli ya pili: "Muandamo wa nchi moja unalazimu nchi zote za dunia hata kama ziko mbali".
Kauli ya tatu: "Muandamo wa nchi moja unalazimu nchi iliyo karibu nayo au inayowafikiana kimatlai". Kisha, Shaykh Jaadul-Haq akaendelea kusema kwamba:
"Na (kauli) zote hizo ni maoni yatokanayo na Ijtihaadi ambazo hazikusimama juu ya hoja kat-ii, si sanad wala matni. Kwa hivyo ingefaa ichaguliwe kauli ambayo inakubaliana na maslahi ya (Waislam wote wa) dunia nzima kwa jumla"."
Jawabu Sikubaliani na mtazamo wa Sheikh Shaykh Jaadul Haq wa chuo kikuu cha Al-Azhar, kwamba zote hizi ni rai na itihad kwani kanuni ni kuwa "Hakuna ijtihadi mbele ya andiko" Ijtihad mwahala mwake ni musimo andiko. Wakatika katika suala hili, utaona kwamba asemaye kuwa tufunge kwa muandamo mmoja, hoja yake ni Hadithi "Fungeni kwa kuuona"; na anayesema kuwa kila mahala na muandamo wake, anatoa ushahidi wake ni Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib. Kwa hivyo, ijtihad ni katika kuyafahamu maandiko: si ijtihad kwa maana ya rai tupu pasi na andiko kama alivyosema Sheikh. Kilichobaki ni kuzijadili riwaya mbili hizi zina maana gani?
Munasema Tungependa kumueleza ndugu yetu kwamba hata hapa Afrika ya Mashariki jambo hili hakulianzisha Shaykh Naaswir Bachuu kama alivyodai mwenyewe (Nd. Juma) kwamba: (Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro)) Inasikitisha hakuweza kuangalia katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 161-163 wametajwa walioonyesha kwa vizuri kabisa misimamo hiyo tofauti. Mashaykh wenyewe ni hawa wafuatao: Al-marhuum Shaykh Juma Abdul Waduud (wa Zanzibar), Shaykh Abdillahi Naaswir ( Nairobi Kenya ), na Shaykh Naaswir Khamis Abdul Rahman ( Mombasa Kenya ).
Jawabu Kwani wapi katika kitabu changu nilisema kuwa Sheikh Nassor Bchoo ndiye aliyeanzisha fikra hii hapo Afrika ya Mashariki hata mukaleta dai hili? Mimi nimeeleza kuwa zamani Afrika Mashariki watu wote wakifata muandamo mmoja. Nilisema: Karne zimepita bila ya sikio la Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro juu ya suala la muandamo wa mwezi. Harakati za elimu zilipobadilika na kuelekea zaidi - kwa kujua au bila kujua - katika mrengu wa Kihanbali na Kiwahabi, pakajitokeza mapinduzi ya ghafla ya fikra na matendo. Dr. Ramadhan Al-butti - miongoni mwa wanavyuoni wakubwa wa ulimwengu wa sasa - anaona kwamba harakati hizi hazisifiki kama ni madhehebu: bali ni hatua (phase) katika mapito ya Historia.
Na katika uk. 97, nimesema:
Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya. Kwa hivyo, ni wazi kwamba mimi nazungumzia Afrika Mashariki. Na mfano wa hilo pia kalisema Sheikh Nassor Bachoo, lakini yeye hamukumjibu. Anasema: "Pamoja na kuwa mgogoro wa kuandama kwa mwezi umeanza kuonekana hadharani katika jamii za Waislam wa hapa Afrika ya Mashariki katika miaka ya hivi karibuni". Inasikitisha kwamba hata maneno yangu mumeyakata na kuchukua yale ambayo hayakamilishi maana nilioilenga. Maneno "Karne zimepita" hamukuyataka kwani hayakufikisheni kule mutakako!
Pili narejea tena kusema kwamba hao wanavyuoni aliowataja Sheikh Nassor, hawajathibitisha habari za kuwa watu wafunge au wakifunga kwa muandamo mmoja Africa Masharik, ukimtoa Sheikh Nassir Khamis wa Mombasa ambaye naye pia ni mtu wa sasa. Ama sheikh Juma Abdu-Wadood yeye, kwa mujibu wa nakala hio ya Sheikh Nassor Bachoo, kasema hivi: Kuona huku kwa mwezi kumekusudiwa kuonekana na Waislam, na kuonekana na Waislamu huko, sio lazima kuonekana na Waislamu wote. Bali inatosha shahada ya mtu mmoja muadilifu".
Pia inampasa mtu mmoja pekee kama ameuona mwezi yeye afunge na kila aliyemuamini; hata akiwa haijakubaliwa shahada yake. Haya ndio maneno ya Sheikh Juma Abdu-Wadood kwa mujibu wa alivyomnukuu Sheikh Bachoo. Sasa ikiwa ndugu zetu mumeshindwa kuyafahamu maneno haya ya Sheikh Juma Abdu-Wadood, bado mutaendelea kupoteza watu bila ya elimu?! Sheikh Juma Abdul-Wadood hapa anazungumzia mas-ala ya ushahidi kwamba si lazima - katika suala la kuonekana kwa mwezi - kwamba kila mmoja auone: bali akiona mtu mmoja basi inatosha kwa wengine kufunga. Hii ndio kauli ya Sheikh Juma Abdul-Wadood na hili nimelieleza kwa urefu katika kitabu changu.
Kisha Sheikh Juma Abdul-Wadood akazungumzia suala la kufunga kwa muandamo mmoja akasema: "Rai za Maimamu wengine wameifasiri hadithi isemayo: (Fungeni kwa kuuona Mwezi) kwamba ukionekana popote mashariki au magharibi (watu) wafunge; hapana kutazama masafa fulani au nini. Hii ni rai nayo na wengi wamesema (hivyo) kama Imamu Malik , Ahmad na kundi kubwa la Hanafi. Inakurubia kuwa n dio rai ya Jamhuri - kufata rai hii ni kuhakikisha umoja wa dunia nzima. Wala hatuwezi kusema kwamba rai ya Shaffiy ndio ya Jamhur". Hapa Sheikh Juma anasimulia rai za Maimamu wengine: si rai za Maulamaa wa Afrika Mashariki. Mimi dai langu nililodai ni kuwa jambo hili la kufunga kwa muandamo mmoja, napenda munifahamu: ni jipya kwa Africa Mashariki. Mimi sikusudii jambo la wanazuoni kuzungumzia rai mbali mbali: bali nazungumzia jambo la watu kufata muandamo mmoja kwamba karne zimepita ya sikio la Muafrika Mashariki wa Kawaida halijiapata kusikia. Na nimetumia maneno "Muafrika wa Mashariki wa kawaida" ili kuwatoa wanavyuoni wao hata kama walikuwa hawafati kauli hio, lakini wanaijua. Kwa hali yoyote ile:
1) Sheikh Juma Abdul-Wadoo hajazungumzia kwamba Afrika Mashariki watu walikuwa wakifunga au wafunge kwa muandamo mmoja, bali kazungumzia rai za wanavyuoni wasio wa Afrika Mashariki - Al-Imamu Shafi, Hanbal n.k. Na mimi sijakanusha tafauti hizi.
2) Kauli yake ilikuwa ni kuhusu suala la mashahidi.
Ama Sheikh Abdillahi Nassir, yeye ni mwanachuoni wa sasa. Na mimi sijasema kuwa sasa hakuna rai hizo. Pili ni kuwa nakala alizotupa Sheikh Bachoo za kitabu cha Sheikh Abdillahi utaona kwamba Sheikh Abdillahi hazungumzii kuwa kauli ya kufatwa ni ile ya muandamo mmoja; bali yeye kasema kuwa hili ni suala la khilafu kwa hivyo tusigombane kila mtu afate rai anayoiona kuwa ni sawa. Sheikh Abdillah kayasema haya baada ya kutokea mizozo hii ya sasa. Kwa hivyo tunarudi pale pale kwamba "Karne zimepita bila ya sikio la Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro juu ya suala la muandamo wa mwezi. Harakati za elimu zilipobadilika na kuelekea zaidi - kwa kujua au bila kujua - katika mrengu wa Kihanbali na Kiwahabi, pakajitokeza mapinduzi ya ghafla ya fikra na matendo". Kwa hivyo, nukta hii hamukuuijibu: na wala sioni kuwa kuna haja ya kuijibu kwani haina umuhimu katika maudhui yetu. Bali kitabu chenu chote, munachagua mambo yasio na umuhimu "Juma kantutukana; Juma kanfanya hivi" nyinyi ndio munajibu baada ya kuzungumzia dalili za kielimu.
Ama Sheikh Nassor: yeye pia ni mtu wa sasa na ni mfuasi wa skuli hio hio munayoifuata nyinyi, kwa hivyo kusema kwake alivyosema hakujapindua nilioyasema kuwa - kimatendo - hili ni suala jipya kwa kwetu Afrika ya Mashariki. Wala mimi sikusema kuwa Sheikh Nassor Bachoo ndiye muasisi wa fikra hio huko kwetu. Naomba munifahamu ninachokisema kwanza kisha ndio munijibu. Na sijui munapinga nini kitu ambacho watu wote wanakijua. Bila ya kusahau kwamba mimi sikusudii kusema kuwa kitu sahihi ni kilichofanywa zamani au kilichofanywa leo: laa! Bali kitu sahihi ni chenye ushahidi sahihi uliojengeka juu ya misingi sahihi ya kielimu. Na kielimu, suala la kuzingatia muandamo mmoja - hamutoweza kulithibitisha.
MNASEMA
Pia Shaykh Ahmad Al Khalil, Mufti wa Omani amethibitisha kwamba Ikhtilaf hii ya muandamo wa mwezi katika hukmu ya kufunga au kufungua ipo na kwamba ni jambo la kale. Kama alivyosema maneno yake yaliyotafsiriwa na Shaykh Muniir Sulayman 'Aziz kwamba: "Hakuna madhehebu iliyokuwa imesalimika na kuwa na Khitilafu baina ya Wanavyuoni wake juu ya suala la kutafautiana miandamo ya mwezi." Jee ndugu Juma anataka kusema kwamba Shaykh Naaswir Bachuu ndiye mwalimu aliyeanzisha madhehebu zote? Au ndiye aliyeanzisha mtafaruku huu kama alivyouita mwenyewe ndugu Juma?
JAWABU
Suala hilo jiulizeni wenyewe; mujijibu wenyewe; kwani nyinyi ndio mulioliunda: mimi sikusema hivyo kamwe bali nilichokisema ni hiki: "Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya". Nami sikusudii kusema kwamba upya huo ni katika kuzungunzwa au kusomwa suala hilo katika vitabu; nakusudia kimatendo sula hili lilikuwa halipo Afrika Mashariki. Sasa ili muwe mumenijibu, twambieni nani alikuwa akifata muandamo mmoja hapa Afrika Mashariki. Jamani! Tafuteni hoja mujadili: musijadili kitu kisichokuwa na umuhimu. Kama hamuna hoja nyamzeni musijitie aibu!
MNASEMA
Katika kudhihirisha udhaifu wake wa kumuandama mtu fulani; Ndugu Juma anasema: (Kama tunavyojua kwamba Sheikh Nassor Bachoo, ni mmoja wa wenye kusisitiza ulazima wa kuwa na muandamo mmoja.) Sisi kwa upande wetu tunasema: Katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu hakuna pahala alipolazimisha watu wafuate huo aliouita ndugu Juma (msimamo wa Shaykh Naaswir). Bali yeye ameonesha mitizamo ya Wanavyuoni kwa kutumia Aya za Qur-aan, Hadiythi na vitabu vinavyokubalika. Lugha aliyotumia Shaykh Naaswir katika huo unaonekana ni msimamo wake ni maneno yaliyozimuliwa kilugha (polite language) kama vile: (inawezekana) ((inaonyesha) .
JAWABU
Na mimi hapa sijasema kuwa Sheikh Nassir Bachoo kalazimisha watu wafunge kwa muandamo mmoja. Nimesema "Anasisitiza ulazima" yaani yeye analingania msimamo huo kwani kwake ndio msimamo sahihi na ndio wajibu kuufata. Naomba tena tuelewane musiseme kitu kinyume na nilivyosema. Wala musitafute kitu kisicho na maana mukajadili eti ndio jawabu! Pili maneno yenu: "Katika kudhihirisha udhaifu wake wa kumuandama mtu fulani". Sasa je na nyinyi pia munaonesha udhaifu huo huo kwa kumuandama mtu fulani katika kitabu chenu?
MNASEMA
Aliyelazimisha rai ni ndugu Juma mwenyewe kama anavyosema: (Lakini kilicho lazima na ambacho tunatakiwa tukubaliane ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali) [uk. 112]
JAWABU
Bali hata Sheikh Bachoo pia kalazimisha kwani ukidai kuwa huu ndio msimamo wa haki au ndio msimamo sahihi au ndio wajibu kufatwa, bila kusema kuwa rai zote zinafaa basi na wewe huwa umelazimisha rai yako. Sasa je Sheikh Bachoo anakubali hivyo kuwa rai zote ni sawa? Mimi kweli sisemi kuwa rai zote ni sawa: nasema kuwa nyinyi mumekosea na sahihi ni kinyume na munavyofanya, na kwa hivyo bado nipo katika msimamo wangu huo huo kwamba: "Kilicho lazima na ambacho tunatakiwa tukubaliane ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali".
MUNASEMA
"Kisha katika uk 85 ndugu Juma anataja kwamba msimamo huu wa muandamo mmoja kwa dunia nzima ni ((kitu kipya)) na kwamba jambo hilo halitekelezeki na ni kauli iliyobaki vitabuni tu baada ya kutaja baadhi ya nchi zinazofuata miandamo yao - yaani kila nchi na muandamo wake kama Al-yaman , Oman , Misri na Saudia. Kisha hapo hapo akataja: ((isipokuwa Imarati katika miaka ya mwisho wamekuwa wakifata Saudia.)) Inafaa ndugu Juma aulizwe masuala yafuatayo:
i) Kama ni jambo lisilotekelezeka vipi tena Imarat wanalitekeleza?
ii) Je hawa wa Imarat nao ni wanafunzi wa Shaykh Naaswir Bachuu?
iii) Kwani hiyo sio kauli ya Jamhuur ambayo ndio msimamo wa maimamu wakubwa wakiwemo Ahmad bin Hanbal, Malik na Abu Hanifa? (Angalia pia sehemu ya 11 na 13 za kitabu hiki)
JAWABU
Kwanza mumemefanya ghushi: maneno yangu hamukuyanukuu yote. Mimi nimesema: "Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya". Nyinyi maneno "Kwa kwetu Afrika Mashariki" mumeyatoa ili ionekane kuwa mimi nasema kuwa hili ni suala jipya kila pahala. Watu kama nyinyi vipi tutakuamini katika dini yenu na uadilifu wenu, ikiwa munaghushi maandiko hivi? Hii ndio kamati ya Msikiti Sunna na hii ndio suna yenyewe?! Halafu mukaendelea na tadlis (ghushi) yenu mukasema: "Na kwamba jambo hilo halitekelezeki na ni kauli iliyobaki vitabuni tu". Mimi sikusema hapa kuwa "Halitekelezeki", bali nimesema:
Lakini ukweli ni kuwa hata katika nchi nyengine zote za dunia taqriban kauli kwamba tufunge kwa muandamo mmoja, ni kauli ilioishia katika vitabu tu, kimatendo (practically) kauli hio haitumiwi isipokuwa na mtu mmoja mmoja. Hadi leo hii: watu Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao, Misr wanafata muandamo wao na nchi zote taqriban ni hivyo, isipokuwa Imarati katika miaka ya mwisho wamekuwa wakifata Saudia.
Haya nionesheni hapa maneno "Halitekelezeki". Mimi nimesema kuwa kimatendo kauli hii, hadi leo haitendewi kazi isipokuwa na baadhi ya watu. Nyinyi mumebadilisha na kuweka ghushi yenu mukasema nimesema halitekelezeki. Kwa hivyo, hilo Sula (a na b) jibuni wenyewe kwani mumesema kinyume na nilivyosema. Suala (d), najibu kuwa sio: hio si kauli ya jumhur bali jumhur kauli yao ni kinyume na hivyo na hili nimelithibitisha katika uk. 189-193 wa chapa ya pili ya kitabu changu au uk. 171 wa kitabu hicho chapa ya kwanza. Na Al-Imamu Malik riwaya zake zimegongana na riwaya kwamba kila watu na muandamo wao ndio ilio bora kwani ni riwaya ya Madina aliko kuweko Al-Imamu Malik, wakati riwaya nyengine ni ya watu wa Irak kulikokuwa na viwanda vya kutunga riwaya!
MNASEMA
Na sisi tunamuongezea habari moja ambayo ni vyema kuielewa, kwamba nchi ya Uganda iliyo katika Afrika ya Mashariki pia inafuata rasmi muandamo mmoja wa duniani. Pia aelewe kwamba huo msimamo wa kila nchi na mwezi wake huku Afrika ya Mashariki haukuwepo tokea zamani. Mashaykh wote wa huku wanakubaliana mwezi ukionekana popote katika nchi hizi tatu ( Kenya , Uganda na Tanzania ) wanafunga pamoja. Yeye anaendelea kushika msimamo wake: (Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao). Lile analoliona yeye halitekelezeki, basi ndio linatekelezeka.
JAWABU
1) Kitu rasmi Uganda hakizingatiwi kwani Uganda kimsingi sin chi ya Kiislamu wala ya Waislamu: Waislamu ni wachache ukilinganisha na Wasio Waislamu. Kwa hivyo, hakuna kitu rasmi. Na jambo hilo ni jambo la sasa. Na mimi sijapinga kwamba sasa fikra hio ipo Afrika Mashariki.
2) Ama kauli yenu: "Mashaykh wote wa huku wanakubaliana mwezi ukionekana popote katika nchi hizi tatu ( Kenya , Uganda na Tanzania ) wanafunga pamoja". Ndio maana nikatumia lafdhi "Kwa kwetu Afrika Mashariki" nikijua kuwa wanavyuoni wote wa kwetu Afrika Mashariki wana msimamo huo. Ama kauli yenu: "Yeye anaendelea kushika msimamo wake: ((Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao,)). Lile analoliona yeye halitekelezeki, basi ndio linatekelezeka". Mwisho wa kunukuu. Inaonesha kuwa kitabu changu mumekijibu bila ya kukifahamu. Nilichosema ni kuwa, ijtihadi ifanywe katika kubainisha wapi hadi wapi watu wafunge pamoja. Kwa vile, hakuna andiko lililobainisha hivyo. Ama muandamo mmoja kwa dunia nzima hili ni kinyume na andiko. Kwa hivyo, wakiwa wanavyuoni wa zamani wamefanya ijtihad hio, sisi tunafata ijtihad yao kwa vile hapa ni mahala pa ijtihad na haikugongana na andiko. Ama madai yenu nyinyi ni kinyume na andiko lilivyoonesha.
MNASEMA
"Kuna suala moja la nyongeza tunapenda tumuulize ndugu yetu Juma: Hata kama hizo nchi alizozitaja ( Al-Yaman , Oman , Misri na Saudia) hazijakubaliana kufuata muandamo mmoja, je hakuna uwezekano (japo wa sadfa) unaoweza kutokea kufunga siku moja ijapokuwa kila mmoja ameona mwezi katika nchi yake? Sasa tuseme kila nchi katika hizo imeona mwezi usiku wa Alkhamisi kuamkia Ijumaa - Wote si watafunga siku moja ya Ijumaa? Basi huo ndio utekelezaji aliosema hautekelezeki. Ni wazi kuwa unatekelezeka.
JAWABU
Munaendelea kuuliza masula haya kwa sababu masuala yenu mumeyajenga katika kitu nisichokisema kamwe. Wapi nimesema kuwa "Hilo halitekezeki" hata mukauliza masuala haya?
3
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA TATU
IKHTILAFU SIO UPINZANI
MNASEMA
"3. Ikhtilafu Sio Upinzani Tunapenda kumfahamisha ndugu Juma kwamba mara nyingi inaweza kutokezea katika jambo moja watu kutofautiana lakini hawapingani. Ni vyema kuelewa kwamba upinzani umo katika Siasa za kilimwengu na mambo mengine sio katika masuala ya Dini. Katika Dini hutokea Ikhtilafu. Masahaba (Radhiya Allaahu 'Anhum) pia walikuwa wakikhitilafiana katika baadhi ya mambo, lakini hawakuwa wakipingana. Kila mmoja aliweza kushika mwendo wake bila kugombana na mwenzake. Ama pale ulipotokea upinzani kwa bahati mbaya - jambo hilo liliwapelekea kugombana au kupigana vita, kwani jambo hilo ni katika amali za Kishetani. Lakini mara walipotanabahi juu ya udhaifu huo waliomba toba kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na kutakana misamaha baina yao Na huo bila shaka ndio mwendo wa watu wema.
Kwa bahati nzuri semina na makongano yote yaliyofanyika ndani na nje ya Zanzibar hapajatokea kuitwa 'pinzani' wala neno 'upinzani' halijatumika hata mara moja. Bali semina zote zilizowahi kufanyika zimekuwa zikisisitiza maneno ya 'umoja' na 'kuelimishana' wala sio 'kupingana.'
Neno 'upinzani' haliko katika midomo ya Wanavyuoni. Tanasikitika sana kuwa Ndugu yetu Juma Muhammad Rashid amelitumia neno ambalo si zuri la 'upinzani' na kulikariri katika kitabu chake zaidi ya mara 33. Kwa kweli hizo si kauli za wenye busara na hikma, bali ni kama alivyozoea kuzitumia. Kwa mfano pale alipokuwa akimlalamikia Shaykh Naaswir Bachuu, alisema: (Tazama pia katika uk. 109-110 uone upinzani alioutoa hapo halafu linganisha upinzani huo na upinzani alioutoa kabla ya hapo, utaona jinsi gani mwanamume alivyokuwa bingwa wa kubadilika! Na hili si jengine bali ni lile Waswahili wanalolisema: "Mfa maji hukamata maji.")
Tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwamba kwa upande wa hapa kwetu Tanzania watu wanaruhusiwa kufunga na kufungua kwa mujibu wa misimamo yao (yote miwili) bila ya kugombana. Swala za 'Iyd kwa upande wa watu wanaofuata mwezi unapoonekana popote duniani wamekuwa wakiswali misikitini na viwanjani bila ya bughudha yoyote. Bali hata katika familia moja yenye misimamo hiyo tofauti, watu hawagombani. Huko ndiko kukhitilafiana sio kupingana".
JAWABU
Nakubaliana na nyinyi sana kwamba ikhtilafu si ugomvi. Lakini nyinyi wenyewe mutakumbuka kwamba munasisitiza kufata wanavyuoni. Wanavyuoni wa Kiislamu wanapozungumzia rai tafauti hutumia maneno haya: "Na ikapingwa kauli hii". Au:"Upinzani wa mwanzo ni kadha wa kadha..". Au: Na wakasema wale watupingao au waliotafauti na sisi. Au "Wakavutana". Au "Wamesukumana". Hizi ndio lugha za wanavyuoni na mimi nimechukua kutoka kwao. Nao kwa lugha hizo huwa hawakusudi kwamba kulikuwa na ugonvi, bali wanakusudia kwa kumekuwa ikhtilafu. Kwa hivyo, mimi sijakusudia upinzani kwa maana ya ugonvi, bali naku sudia kutokuafiki rai au kauli Fulani, na hilo ni jambo linalosemwa na wajuzi.
SEHEMU YA NNE
JUMA AMPINGA AL-IMAMU AL-SHAUKANI
MNASEMA 4.
Ndugu Juma Anampinga Al- Imam Shawkani Jambo jengine la kusikitisha ni kuwa ndugu Juma haonyeshi kuwaheshimu Wanavyuoni au kuwapa hadhi zao wanazostahiki. Wanavyuoni wana heshima zao hata pale wanapokosea. Ni vyema kuelewa kwamba Al Imam Shawkani alikuwa ni miongoni mwa Wanavyuoni wakubwa kama ilivyoelezwa kwenye historia yake fupi katika kitabu cha "Kuandama Kwa Mwezi" cha Shaykh Naaswir Bachuu Uk 35. Al Imam Shawkani aliandika vitabu vingi vya kukubalika pamoja na Tafsiri yake ya Qur-aan Tukufu inayojulikana kwa jina la "Fathul Qadir."
JAWABU
Al-Imamu Al-Shawkani - bali hata aliye chini ya yeye sana kwa elimu - ninamuheshimu sana. Na katika kitabu changu nimemnukuu kwa kumpa laqabu anayostahiki. Sehemu nyingi nimemwita Imamu. Huku ni kukikiri kuwa ni mtu wa maarifa mapana kwani Imamu hawi mtu yeyote bali ni yule aliyekusanya zana nyingi za elimu. Labda sehemu moja tu nilimwita Sheikh, nayo pia ni laqabu ya heshima. Sasa vipi munasema kwamba simpi heshima yake. Tukumbuke kwamba kumuheshimu mwanachuoni, si maana yake kwamba tusimpinge au kujadili maneno yake. Kufanya hivyo si kumuheshimu bali ni kumtakasa, nalo ni kosa. Pili: kwani nyinyi wale Maimamu wakubwa munaowapinga katika suala hili la muandamo wa mwezi huwa ndio mumewavunjia heshima yao?
MNASEMA
Ndugu Juma katika kujikweza kama kwamba yeye ana elimu kubwa zaidi na kwamba anakubalika zaidi kuliko Al Imam Shawkani, anathubutu kusema: ((Huo ndio upinzani wa pili wa Al-imamu Al-shaukaniy, lakini kama unavyoona jawabu yetu ya kwanza inajibu baadhi ya nukta zilizomo katika upinzani huu.)) [ uk : 111]". Kisha akamfananisha Al Imam Shawkani na watu wa kawaida (yaani labda ni mtu wa mitaani asiyekuwa na elimu) kwa kusema: ((Maneno haya ya Al-imamu Al-shaukaniy - kama yalivyo maneno ya watu wengi wa kawaida.))
JAWABU
Haya! Ubaya uko wapi hapa? Sasa nyinyi ndio munamuheshimu au munamtakasa. Kwani nani kasema kuwa mwenye elimu hajibiwi katika kutafuta haki? Ikiwa Ibn Abbaas kapingwa na watu ambao hawamuoni hata vumbi lake, itakujakuwa Al-Imamu Al-Shawkani. Kwani Sheikh Bachoo yeye katika hicho kitabu chake si anawapinga wanavyuoni wote waliotangulia Afrika Mashariki, au tuseme na yeye anajikweza na kujifanya ana elimu?! Kwa kweli haya ni maneno ya aliyefilisika: asiye na hoja.
Ama kauli yenu: "Kisha akamfananisha Al Imam Shawkani na watu wa kawaida (yaani labda ni mtu wa mitaani asiyekuwa na elimu)" hayana maana, kwani nimesema: ((Maneno haya ya Al-imamu Al-shaukaniy - kama yalivyo maneno ya watu wengi wa kawaida.)). Sasa sijui ni mtu gani wa mitaani aliye na daraja ya uimamu! Enyi walimwengu! Hebu fahamuni munayoyasoma. Mimi nafananisha kauli na kauli: si mtu na mtu. Al-Shawkani nimempa hadhi yake ya uimamu, lakini alichokisema hakikubaliki kwani hakina dalili za kisharia. Au munataka tuchukue tu kwa sababu msemaji ni fulani bila ya kutazama kilichosemwa?
MNASEMA
Ndugu Juma katika kumuandama Al Imam Shawkani anaendelea kusema: ((Penye andiko huwa hapana ijtihadi;)) kama kwamba Al Imam Shawkani alikuwa hajui Qur-aan wala Hadiyth. Au kama kwamba Al Imam Shawkani anampinga Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Jawabu Inaonekana nyinyi muko mashariki na elimu iko magharibi! Tafadhali fungeni safari muifate. Kauli ya Imamu yeyote awaye inarejeshwa katika dalili za kisharia. Maimamu wanakosea pia na mifano iko mingi. Na kutajia mifano mitatu tu:
1) Al-Imamu Al-Nawawi kunukuu Hadithi ifatayo:
"Tulikuwa tunasafiri pamoja na Mtume(s.a.w.w) , miongoni mwetu wako waliofunga na wako waliokula, na wako waliotimiza (rakaa za Sala) na wako waliopunguza. Basi aliyefunga hakumtia kasoro asiyefunga; wala asiyefunga (hakumtia kasoro) aliyefunga; wala aliyepunguza (rakaa katika Sala) (hakumtia kasoro) aliyetimiza; wala aliyetimiza (hakumtia kasoro) aliyepunguza." Hadithi hii kainukuu Al-imamu Al-nawawi katika Sharhu Sahihi Muslim na akainasibisha na Sahaba Abi Said Al-khudriy katika masimulizi ya Muslim katika Sahih yake. Wakati Hadithi hii haimo katika Sahihu Muslim. Hadithi ya Abi Said Al-khudriy alioiashiria Al-imamu Al-nawawi - katika mlango huo huo - ni Hadithi na. 95/2612, nayo inasema: "Tulikuwa tunasafiri pamoja na Mtume(s.a.w.w) katika mwezi wa Ramadhani. Hakumtia aibu aliyefunga kutokana na aliyekula, wala aliyekula kwa sababu ya kula kwake."
Na mfano wa Hadithi hii ni Hadithi na. 93/2610 na 96 /26134 na Hadithi nyengine tatu zinazofata mpaka mwisho wa mlango huo, wala hakuna maneno yanayosema: "Wala (hakumtia aibu) aliyepunguza (rakaa katika Sala) juu ya aliyetimiza; wala aliyetimiza juu ya aliyepunguza:" maneno haya hayamo katika Hadithi hio ya Muslim, bali kilichomo ni mas-ala ya kufunga na kutokufunga tu kwa msafiri katika mwezi wa Ramadhani. Na kwa sababu hii ndio maana Al-Shaukaniy akampinga Al-imamu Al-nawawi kwa maelezo yake hayo. Je tuseme Al-Imamu Al-Shawkani naye kafanya kosa kumpinga Al-Imamu Al-Nawawi, au kafanya wajibu wake wa kudhihirisha haki. Na je Al-Imamu Al-Nawawi kawa ndio si mwanachuoni tena kwa sababu hapa kakosea?! Fahamu ziko wapi?!!!!!!!!
Ibn Hisham: Ibn Hisham Al-Ansari ni bingwa mkubwa wa lugha. Katika kitabu chake Qatru Al-Nada anasema kwamba miongoni mwa sharti za kufanya kazi masdar ni kuwa baina yake na mtendwa wake pasiwe na kitu kilichokaa katikati. Anasema (Sharti) ya saba ni kuwa (ili masdar ifanye kazi) basi isiwe yenye kupambanuliwa kutokana na mtendwa wake. Na kwa hivyo, (w atu wa Nahau) wakairejesha kauli ya aliyesema kwamba (neno yawma katika Aya: Yawma tubla Al-Sarair ni mtendwa wa neno "Raj'ihi", kwani baina yao pamekuwa na upambanuzi kwa kuwekwa khabar.
Hayo ni maneno ya Ibn Hisham pamoja na kundi la wanavyuoni. Sasa someni Aya hii:
Neno It'am ni masdar; na neno yatiman na miskinan ni watendwa wa Masdar hio. Hata Ibn Hisham mwenyewe alipoingia kueleza migawanyiko ya masdar 'aamil katoa mfano wa Aya hii hii. Haya je tumfate Ibn Hisham au tufate dalili za kielimu? Na je Ibn Hisha tayari kageuka kuwa mtu wa mitaani kwa sababu hapa kakosea? Kwa hivyo, wanavyuoni wanakosea, na wanapokosea na sisi pakitubainikia kwa dalili sahihi kuwa hili ni kosa huwa tunazinduana kuwa hili ni kosa, hata akiwa aliyelifanya ni nani, wala huko hukumpunguzii mwanachuoni kima chake, kwani hakuna asiyekosea. Na nadhani hivyo ndivyo Uislamu unavyotutaka.
Al-Hafidh Ibn Hajar: Kuna Hadithi inasema: "(Kasimulia Abu Said Al-Khudri) kwamba kikundi cha Masahaba wa Mtume (s.a.w.) walipita kwa kabila moja la Kiarabu, mtu mmoja kati yao akadonolewa (na ng'e), wakasema: 'Kuna mzinguaji kati yenu?' Mmoja wao akamzingua kwa Al-Hamdu. Basi akapewa kikundi cha ghanam (kondoo au mbuzi) akakataa kukichukua. Wakaja kwa Mtume(s.a.w.w) wakamtajia hayo, akasema: 'Aliyechukua kwa zinguo la batili (ndiye aliye chukua haramu), (ama wewe) kwa hakika umechukua kwa zinguo la haki. Chukueni na mie munipe sehemu yangu". Hadithi hii pia kaipokea Al-Bukhari kutoka kwa Abu Sa'id bin Al-Mu'allah na kutoka kwa Ibn Ibn Abbas kwa lafdhi tafauti kidogo.
Al-Hafidh Ibn Hajar kawakosoa waliosema kuwa Hadithi hii imesimuliwa kutoka kwa Abu Sa'id Al-Khudri. Anasema Ibn Hajar: "Al-Ghazali na Al-Fakhr Al-Razi wakifatiwa na Al-Baydhawi wamekinasibisha kisa hiki kwa Abu Sa'id Al-Khudri nalo ni kosa, bali yeye (mwenye kisa hiki) ni Abu Sa'id Al-Mu'alla". Tazama Fat-hu Al-Bari j. 9, uk. 5076, katika sherehe ya Hadithi na. 4474. Nami nasema: lakini maelezo hayo ya Ibn Hajar ya kuwakosoa Al-Ghazali, Al-Razi na Al-Baydhawi, bado ni maelezo ya kufirikiwa kwani kisa hiki kimesimuliwa pia na Muslim Hadithi na. 2201, na Abu Dawud Hadithi na. 3415 na wengine kutoka kwa Abu Sa'id Al-Khudri. Kwa hivyo, Al-Ghazali na wenziwe hawakukosea isipokuwa ikiwa Ibn Hajar anadai kuwa sanad hizo ni dhaifu na ya Al-Bukhari yenye kusema kuwa muhusika alikuwa ni Abu Sa'id Al-Mu'allah ndio sanad sahihi.
Utaona kwamba Ibn Hajar kawakosoa wanavyuoni wengine. Wakati pia na yeye kakosea katika kuwakosoa huko kwani walivyosema wao ndivyo ilivyo katika Sahihu Muslim. Sasa tusema wanavyuoni hawa wakubwa tayari wameshakuwa watu wa mitaani kwa kukosowana huku? Jamani! Sisi tumeambiwa tuwaheshimu Maulamaa: sio tuwatakase na kwamba hata mtu akikosea asiambiwe. Sasa kama kanuni inayokubalika kwa Umma mzima inasema: "Penye andiko huwa hapana ijtihadi", je Al-Imamu Al-Shawkani akenda kinyume na kanuni asirejeshwe kwa sababu yeye ni mwanachuoni mkubwa. Nakukumbusheni maneno yenu yaliomo kitabuni mwenu muliposema: "Kutegemea maneno, matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa ni udhaifu". Haya mumeyasema nyinyi kuzipinga kauli za wanavyuo ni musiokubaliana nao. Sasa vipi munanilaumu kwa kitu mukitendacho?!
Ingelikwa dharau lau nilisema kuwa Al-Shawkani hana akijuacho. Na mimi ni nani hata niseme kuwa Al-Shawkani hajui?! Mimi nadai kuwa hapa kakosea. Sasa nyinyi, ili iwe mumenijibu basi mubainishe kuwa: "Aa si kweli hakukokesea, na kanuni hio si kweli haipo". Hapo itakuwa mumenijibu. Lakin munaleta maneno ya mtu aliyefilisika na hoja munasema: "Kama kwamba Al Imam Shawkani alikuwa hajui Qur-aan wala Hadiyth. Au kama kwamba Al Imam Shawkani anampinga Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)". Kwani nyinyi hao munaowapinga munaitakidi kuwa hawajui Qur-ani na Hadithi au wanampinga Allaah na Mtume Wake(s.a.w.w) , au kwa sababu munahisi kuwa wamejitahidi na kukosea? Kwanini nyinyi mujiweke katika dhana safi na wenzenu muwaweke kwenye dhana mbovu?
Munasema Angalia katika kitabu chake Ndugu Juma kwenye uk 108 - 109 ameeleza misimamo ya Wanazuoni wawili mashuhuri; yaani Al Imam Badru Din na Shaykh Al Khalil ambao wamejaribu kuukosoa msimamo wa Al Imam Shawkan lakini kwa njia nzuri. Wote wawili wameonyesha kwamba ile ni Ijtihadi ya Al- Imam Shawkani katika kumfahamu Ibni ''Abbas katika kisa cha Kuraib wala hawakumfanya Al Imam Shawkani kama ni mpinzani. Ni vyema kuelewa pia kwamba wanaweza kutokea Wanavyuoni wengine wanaoweza kusema pia kwamba na hizo ni Ijtihadi za Al Imam Badru Din na Shaykh Al Khalil katika kumfahamu Al Imam Shawkani. Wala huwezi kusema kuwa Al Imam Shawakani alikuwa halifahamu andiko, Shaykh Al Khalil ndio amelifahamu andiko. Hizo zote ni Ijtihadi katika kukifahamu kisa cha Kuraib.
Jawabu Hapa hakuna sula la nani analifahamu andiko, suala ni kuwa mujibu wa Usulul Hadithi (elimu ya Hadithi), maneno ya Ibn Abbbaas yasemayo: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) ," je yanazingatiwa kuwa ni Hadithi au si Hadithi? Hakuna hapa suala la kumfata Al-Imamu Al-Shawkani wala Al-Imamu Al-Khalili wala Imamu atayekuja: wote wanarejeshwa katika kanuni (pr iciples) zile zile na hakuna mwenye uwezo wa kuwa juu ya kanuni: kanuni ziko juu ya wote. Kwa hivyo, sisi tulipompinga Al-Imamu Al-Shawkani na kumuunga mkono Al-Imamu Badru Al-Din, si kwa sababu yule ni Al-Shawkani na huyu ni Al-Khalili au kwa sababu yule ni mtu wa madhehebu iliotafauti na yetu, bali ni kuwa huyu kasema kitu kilicho sawa na kanuni za Hadithi; yule kenda kinyume na kanuni. Pamoja na hayo, hatupingi ijtihadi ya Al-Imamu Al-Shawkani.
SEHEMU YA TANO
NDUGU JUMA ANATOA RAI BINAFSI
Munasema 5. Ndugu Juma Anatoa Rai Binafsi Katika kitabu chake alichokiandika, Ndugu Juma ameonyesha udhaifu wake wa kulazimisha kujaribu kujibu hoja za kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu. Maneno yake mengi yametawaliwa na ubinafsi. Hakupenda kuwa muadilifu katika kueleza hoja zake ingawa yeye mwenyewe anapokwama kihoja hujifanya kumgomba Shaykh Naaswir Bachuu huku akimwambia: (Kwa ufupi ni kuwa hii ni hoja ambayo haina faida yoyote ya kielimu, lakini tunaijadili kwa ajili ya watu wa mitaani tu).
Jawabu Hizo ni tuhuma zenu baada ya kushindwa kujibu hoja zangu. Sijui nani anayejilazimisha kujibu hoja na ambaye anakwama? Na hayo maneno: (Kwa ufupi ni kuwa hii ni hoja ambayo haina faida yoyote ya kielimu, lakini tunaijadili kwa ajili ya watu wa mitaani tu), niliyatoa baada kuwa nimeshajibu hoja au nilisema hivyo tu ikawa basi? Sasa asiyemuadilifu ni mimi au nyinyi ambao munataka kuonesha kitu tafauti na kilivyo. Mimi niliyasema hayo baada ya kuwa nimeshajibu, kisha ndio nikabainisha kwamba kielimu - yaani kwa watu wa mustawa wa elimu - suala hilo alililolileta Sheikh Nassor Bachoo halina maana lakini kulijadili kwangu ni kwa kuzingatia akili za watu wa mitaani. Nyinyi mumeyachukua maneno haya na kufanya kuwa ni ushahidi kuwa sikujibu bali nimekwama. Munadhani mutawadanganya watu na watu vitabu vyote wanavyo?!
MNASEMA
Ni kweli kwamba mlango wa Ijtihadi uko wazi, lakini si vyema katika wakati wetu huu mtu kutoa rai binafsi za kujikweza bila kunukuu hoja za Wanazuoni waliotangulia tena wanaokubalika. Katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu kuna hoja nyingi mno zilizotajwa kutoka kwenye vitabu vya Wanazuoni wakubwa ambao wameonyesha misimamo mbali mbali juu ya maudhui haya ya muandamo wa mwezi, lakini Ndugu Juma hakuijibu hata moja zaidi ya kumponda Al Imam Shawkani. Angalia misimamo ya Wanazuoni waliotajwa katika kitabu cha 'Kuandama Kwa Mwezi' cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 5 - 11, 51 - 56, 59 - 74, 129 - 133. Pia angalia: 'Makubaliano Katika Mikutano Ya Wanavyuoni' yalivyoelezwa ambayo ndugu Juma ameyafumbia macho uk 134 - 155.
JAWABU
Kwanza mimi si mujtahid, kwa hivyo huo mlango uko wazi kwa mujtahidin. Ikiwa nyinyi wenzangu mumefikia daraja hio, basi musiwache kuupita mlango huo ili nasi tufaidike kwa ijtihada zenu. Lakini maandishi yenu yanaonesha kuwa hata daraja talabatul 'Ilmi hamujafikia. Pili ni kuwa aliyefikia daraja ya ijtihad halazimiki kunukuu maneno ya wanavyuoni wengine. Hata akinukuu basi hanukuu kwamba ndio dalili yake bali ni kuonesha kuwa wako waliosema kauli kadha. Kwa hivyo, kauli yenu: "Lakini si vyema katika wakati wetu huu mtu kutoa rai binafsi za kujikweza bila kunukuu hoja za Wanazuoni waliotangulia tena wanaokubalika" si kauli sahihi. Tatu: Hata mujtahid si kwamba ana haki ya kusema kitu kinyume na kanuni za lugha na usuli. Nakusudia kanuni walizokubaliana Umma mzima au zisizopingana na Qur-ani na Suna.
Nne: Katika mjadala huwa hapategemewi fulani kanena, bali panategemea dalili za Kisharia na maneno ya fulani hurudishwa katika dalili za kisharia. Na hicho ndicho nilichokifanya. Nakukumbusheni kauli yenu muliposema: "Kutegemea maneno, matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa ni udhaifu". Na wanavyuoni nimewanukuu wengi. Lakini narudia tena kauli za wanavyuoni ni hoja pale walipokubaliana: si walipotafautiana. Wakitafautiana, basi huwa kauli zao si hoja, bali kila mmoja anaambiwa lete hoja ya Kisharia.
Sasa mimi hata nikinukuu wanavyuoni wa dunia nzima, ikiwa sikutoa ushahidi unaokubalika kielimu ni kazi bure. Ama Al-Imamu Al-Shaukani yeye tumeyajadili maneno yake kiurefu kwa vile Sheikh Bachoo na wengine wameonekana kuyategemea zaidi maneno yake. Na pia Al-Shawkani ndiye aliyeijadili Hadithi husika kwa urefu kulikoni wengine. Ama madai yenu muliposema: "Kumponda Al Imam Shawkani". Mimi nakanusha kwa nguvu dai hilo, mimi sijamponda bali sikukubaliana naye kwa vile nimeona hoja alizotoa ni kinyume na kanuni za Hadithi na Usuliil Fiq-hi. Sasa ili nanyi muwe mumenisomesha basi onesheni kuwa hoja zake ni sawa kwa mujibu wa kanuni za Hadithi na Usulil-Fiq-hi.
MUNASEMA
Angalia Ndugu Juma alivyokuwa akijenga baadhi ya hoja zake binafsi (za umimi) pale aliposema: (Nasi tunasema kwamba Aya ndio, lakini hoja yake katika Aya hio ni hoja dhaifu sana .) [uk. 71] ((Isipokuwa upinzani ambao - mimi kwa upande wangu - nauona kuwa una muelekeo juu ya tafsiri hii tulioitoa hapa,)) [uk. 62] Ziko wapi hapa hoja za Wanavyuoni wanaokubalika zaidi ya kudai: (Mimi kwa upande wangu nauona) au: (Ninasema bila shaka)
JAWABU
Na nyinyi munasema: "Sisi tunamjibu hivi.." wala hakuna mwanachuoni aliyejibu hivyo mulivyojibu nyinyi, ni rai zenu binafsi tu. Kwa hivyo, na nyinyi muna ubinafsi. Aidhan Sheikh Bachoo anasema: "Ni kweli kwamba msimamo wa upande wetu". Mimi sioni tafauti ya maneno "Sisi" au "Nasi" na maneno "Upande wetu" zote ni dhamiri (pronouns) za ubinafsi. Kwa hivyo, kosa hili nimejifunza kutoka kwenu. Ama kauli yangu (Isipokuwa upinzani ambao - mimi kwa upande wangu - nauona kuwa una muelekeo juu ya tafsiri hii tulioitoa hapa)". Ninasema:
1) Kama hilo nimelisema kwa mtazamo wangu, mulitaka niwadanganye watu niwambie hivi ndivyo walivyosema wanavyuoni. Mimi sighushi kama munavyofanya mimi: langu nasema kuwa hili ni langu; na la wanavyuoni nasema kuwa hili kalinena fulani.
2) Pili ni kuwa mulitakiwa munukuu kile nilichokisema kisha mukijibu kama mulikusudia kutafuta ukweli. Lakini hamukufanya hivyo, na badala yake munatafuta kitu ambacho munadhania kuwa hiki kitamtia aibu Juma ndio munataja. Sasa nikisema ninavyoona mimi, kitu gani kilichokuwa haramu hapa ni hii kauli au ni yale nilioyasema. Kama ni hii kauli, basi uharamuu wanaufanya wanavyuoni wote wa Umma, kwani kwenye rai zao binafsi husema: Au yaani ninavyoona mimi. Kama uharamu uko katika yale nilioyasema, tafadhali yanukuuni kisha muyajadili na kubainisha kosa liko wapi.
3) Tatu ni kuwa narudia tena kwamba kitabu cha mjadala huwa hakitegemei kauli za wanavyuoni, bali huwa kinajadili mambo kwa mujibu wa misingi yake ya kilugha na kiusuli na hivi ndivyo nilivyofanya. Sasa kama nyinyi munadai kuwa nimekosea kwa mujibu wa fani hizi, tafadhali nukuuni maneno yangu na muonesha kosa liko wapi.
4
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA SITA
MUANDAMO WA KIFALAKI NA MUANDAMO WA KISHARI'AH
UTANGULIZI MFUPI JUU YA SEHEMU HII
Kabla sijaendelea na kunukuu jawabu niliojibiwa na ndugu zangu kuhusu maudhui ya sehemu hii, ni vyema kwanza ninukuu nilioyasema katika kitabu ambayo wao ndio wanayajadili. Kufanya hivyo, ni kuwawezesha wasomaji kuona udhifu uko wapi. Katika kitabu, chini ya anwani
MUANDAMO WA KIFALAKI NI NINI?
nilisema yafatayo: Ni ukweli usiopingika kwamba ufahamu sahihi wa kitu chochote kile unafungamana mfungano wa nguvu na walazima na ufahamu wa dhana (concept) yake sahihi. Kwa hivyo, ni kawaida kwamba muhubiri anapohubiri juu ya maudhui fulani, kwa mfano jografia, kama hakufafanua tangu mwanzo na kuweka wazi, basi suala la kwanza ataloulizwa ni "Jografia ni nini?"
Maudhui yetu katika sehemu hii ni hii dhana sahihi ya muandamo wa mwezi: je kuandama kwa mwezi ni nini katika dhana yake ya uhakika? Qur-an Tukufu, imeashiria muandamo wa mwezi katika baadhi ya Aya zake. Na hii ni pale Allah Aliposema:"Na Mwezi tumeupimia vituo mpaka ukarejea (kuwa mwembamba) kama karara kongwe (la mtende) . Na anasema Allah :"Yeye (Allah) Ndiye aliyelifanya jua kua muanga na mwezi kua nuru na akaupimia (huo mwezi) vituo, ili mujue idadi ya miaka na hisabu."
MAELEZO JUU YA AYA HIZI
Aya mbili hizi zinathibitisha kwamba mwezi una Manazil (vituo) ambayo hupitia ndani yake. Watu wa elimu ya falaki wanasema kwamba Manazil haya ni ishirini na nane ambayo yamo katika Buruji (constellations) kumi na mbili. Majina ya buruji hizo ni:
1) Al-hamal (Aries, Kondoo dume).
2) Al-thaur (Taurus. Ngo'mbe dume).
3) Al-jawzaa (Gemini. Mapacha).
4) Al-sartan (Cancer. Kaa).
5) Al-asad (Leo. Simba).
6) Al-sunbula (Virgo. Mashuke).
7) Al-mizan (Libra. Mezani).
8) Al-a'qrab (Scorpio. Nge).
9) Al-qaws (Sagittarius. Upinde).
10) Al-jadyu (Capricon. Mtoto wa mbuzi).
11) Al-dalwu (Aquarius. Ndoo).
12) Al-hut (Pisces. Samaki).
Hayo ndio majina ya buruji kumi na mbili, kwa mujibu wa wanaojihusisha na elimu za falaki. Buruji hizo kumi na mbili zina vituo ishirini na nane (28). Kila Buruji moja ina vituo viwili na thuluth. Vituo hivyo ni:
1) Al-shartan. 2) Al-butain. 3) Al-thurayya. 4) Al-dabran. 5) Al-haq'a. 6) Al-han'a. 7) Al-dhiraa. 8) Al-nnathra. 9) Al-ttarf. 10) Al-jabha. 11) Al-kharatan. 12) Al-sarfa. 13) Al-awaa. 14) Al-simak. 15) Al-ghafr. 16) Al-zubanayan. 17) Al-iklil. 18) Al-qalb. 19) Al-shaula. 20) Al-na'aim. 21) Al-baladda. 22) Sa'adu Al-dhabih. 23) Sa'adu Bula'a. 24) Sa'du Su'ud. 25) Sa'ad Al-akhbiya. 26) Al-far'u Al-muqaddam. 27) Al-far'u Al-muakkhar. 28). Batnu Al-hut.
Haya ndio majina ya manazil ishirini na nane kwa mujibu wa wataalamu wa falaki. Kilichomashuhuri katika vitabu vingi vya kale ambavyo vimezungumzia mas-ala haya ni kuwa buruji ya kwanza ambayo ni Al-hamal (Aries), vituo vyake ni: Al-shartan, Al-butain na thuluthi moja ya Al-thuraya. Miongoni mwa hawa ni Al-qurtubiy kama ilivyo katika tafsiri yake. Na hivyo ndivyo walivyosema wengi wengineo ambao nimebahatika kuona maandishi yao juu ya maudhui hii. Lakini hata hivyo mmoja wa wataalamu wetu waliokuweko Zanzibar, naye ni Sheikh Yusuf alikuwa anasema kwamba buruji haziko thabiti (not constant), bali kila miaka sabiini (70), zinaondoka na kujongea mbele, jambo ambalo linazifanya kuingia katika manazil mengine baada ya miaka. Hatimae nikaikuta kauli hii imo katika kitabu "AHKAMU AL-HAKIM" cha mwanachuoni mashuhuri wa falaki wa Misri Al-ustadh Abdul-fattah Al-sayyid Al-tukhi Al-falaki. Anasema: "Jua kwamba manazil (vituo) ni zile nyota tunazoziona usiku. Na waliotangulia walikuwa wakiziita nyota thabiti (fixed stars), kwa sababu ya kudhani kwao kwamba zimesimama kwa ajili ya kwenda kwake kidogo kidogo. Lakini elimu ya sasa imegundua kwamba zinakwenda lakini kidogo kidogo sana ambapo zinakata daraja moja (one degree) katika (kipindi cha) miaka 66 taqriban." Mwisho wa kunukuu.
Kauli ya Sheikh Yusuf inaashiria kwamba labda yeye anaamini kwamba majina ya manazil ni zile sehemu zilizokaa nyota: si ule mkusanyiko wenyewe wa nyota (constellation). Kwa hali yoyote ile - kumbu kumbu yangu - ni kuwa kwa mujibu wake, Manazil (vituo) hayo tulioyataja kuwa ni ya Al-hamal - nayo ni Al-shartan, Al-butain na thuluth Al-thuraya - kwa sasa yamo katika buruji ya Al-thaur (Taurus. Ngo'mbe dume). Kauli yake hii inawafikiana na kauli ya Al-tukhi katika kitabu chake hicho.
Mwezi unakata kila kituo kimoja kwa muda wa siku moja, ikimaanisha kwamba siku ishirini na nane (28), huwa umekamilisha safari yake. Na hapo hufichika kidogo kwa siku moja au mbili kisha hudhihiri na kuonekana tena duniani. Suala ni kuwa je kukamilika huku kwa mzunguko wa mwezi ndio muandamo wa mwezi Kisharia? Umejua - kutokana na hayo yaliotangulia - kwamba mwezi unakamilisha mzunguko wake kwa muda wa siku ishirini na nane (28), na ili uonekane duniani unahitaji kupitiwa na siku moja au mbili. Kuanzia hapa utaanza kujua tafauti baina ya muandamo wa mwezi kisharia na muandamo wake kifalaki. Pia utaanza kuona namna gani Sh. Nassor Bachoo katika kitabu chake alivyochanganya baina ya hali mbili hizi wakati alipokuwa akizungumzia maudhui hii.
MAELEZO YA SH. NASSOR BACHOO
Sh. Nassor Bachoo ni mmoja wa Wazanzibari waliojitokeza kuzungumzia mas-ala haya. Katika kitabu chake, Sheikh kaizungumzia maudhui hii na akanukuu Aya ya 5 ya Sura ya 10 ambayo ni ya pili katika Aya tulizozinukuu kabla. Baada ya maelezo alisema: "Qur-an inalieleza suala la kuandama kwa mwezi kama ni tukio moja wapo kati ya matukio yaliyopangwa na Mwenyezi Mungu kutukia kila mwezi mara moja duniani kote." Mwisho wa kunukuu.
Ukianzia uk. 5. hadi uk. 8, wa kitabu chake, utaona kwamba Sh. Nassor Bachoo anathibitisha mwenendo wa mwezi kupitia katika Manazil (vituo) yake. Ufupisho wake - kama tulivyotangulia kusema - ni kuwa mwezi unasafiri kwa muda wa siku ishirini na nane (28) kupitia katika vituo hivyo, na siku moja au mbili hupotea kisha kudhihiri na kuweza kuonekana duniani. Sheikh aliishia maneno yake kwa kusema: "Baada ya maelezo haya tunatumai tumeweza kuelewa mtazamo wa Qur-an juu ya kuandama kwa mwezi." Mwisho wa kunukuu. Sasa ukitazama sentensi mbili hizi za Sh. Bachoo, utaona kuwa anakusudia kuthibitisha kitu kimoja kwa Aya ambayo haimpatii malengo yake. Anachokusudia kukithibitisha Sh. Bachoo - kwa inavyoonesha kutokana na maandishi yake - ni kuwa muandamo ni mmoja duniani kote na kwa hivyo - bila shaka anakusudia kusema - kwamba sote tufunge kwa muandamo mmoja huo. Ndio maana akasema: "Qur-an inaeleza suala la kuandama kwa mwezi kama ni tukio moja wapo kati ya matukio yaliopangwa na Mwenyezi Mungu kutukia kila mwezi mara moja duniani kote." Lakini dai kwamba Qur-an inasema kuwa muandamo wa mwezi unatokea mara moja tu dunia nzima - ikiwa anakusudia muandamo wa kisharia nao bila shaka ndio anaouzungumzia - si sahihi. Na sijui wapi Qur-an imesema hivi?!
Qur-an imezungumzia muandamo wa mwezi katika hali mbili: Hali ya kwanza: ni ya muandamo wa kifalaki. Na huu sio ule tunaouita muandamo. Hapa tutatumia tu neno "Muandamo" kwa ajili ya kufahamiana. Huu ndio ambao unazungumziwa na Aya hizo tulizotangulia kuzinukuu. Na ndio unaotokea mara moja duniani kote. Hali ya pili: ni ya muandamo wa Kisharia. Huu umetajwa katika Aya ya 189 ya Sura ya 2, ambapo Allah anasema:
"Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo. Sema hivyo ni vipimo kwa ajili ya watu na Hija." Sasa katika Aya zote mbili hizi hakuna ufafanuzi wowote wenye kuonesha kwamba muandamo wa mwezi wa kisharia ni mmoja au vipi? Bali Aya hii ya pili, inaonesha tu kwamba katika Sharia kuna kitu miandamo ya mwezi. Lakini vipi miandamo hio: hakuna ufafanuzi wowote ule uliotolewa katika Aya hii. Kwa hivyo madai hayo ya Sh. Nassor Bachoo kwamba Qur-an inasema kwamba muandamo ni mmoja ni kitu kimoja na maelekezo ya Aya ni kitu chengine.
Kwa kufahamu zaidi ni kuwa Aya alioitolea ushahidi juu ya fikra yake, inasema:"Yeye (Allah) Ndiye aliyelifanya jua kua muanga na mwezi kua nuru na akaupimia (huo mwezi) vituo, ili mujue idadi ya miaka na hisabu."
Sasa utaona kwamba Aya hii imetaja vitu viwili: jua na mwezi. Na vyote hivi vinazunguka katika falaki (orbits) zake na vinapita katika manazil (vituo) yale yale na vinapita katika buruji (constellations) zile zile. Sasa cha kustaajabisha ni kuwa vipi Sh. Nassor Bachoo ajenge hoja kwa Aya hii kuthibitisha muandamo mmoja na asijenge hoja kwa Aya hii kuthibitisha wakati (time) mmoja wa kusali?! Ninachokusudia kukisema ni kuwa Aya imetaja kwamba Allah ndiye aliyeumba jua na mwezi. Kisha akataja Illa (sa babu) ya kuumba vitu viwili hivyo. Akasema"Ili mupate kujua idadi ya miaka na hisabu (nyengine)." Kwa lugha nyengine sababu ya kuumbwa jua na mwezi, ni kutuwezesha kudhibiti hisabu za miaka na hisabu za mambo mengine. Sasa kama sababu hii - kwa mujibu wa Sheikh Nassor Bachoo - ndio iliohalalisha au kuwajibisha kuuzingatia muandamo mmoja wa mwezi duniani kote kwa mujibu wa Aya hii, kipi kimeharamisha kuuzingatia mtenguko mmoja wa jua kuwa ni alama ya kuthibitisha wakati mmoja wa sala duniani kote, wakati Aya hii kama ilivyoutaja mwezi kuwa ni chombo cha kudhibitia wakati ndivyo ilivyolitaja jua kwa lengo hilo hilo?
Ubainifu wa haya ni kuwa kama Mtume(s.a.w.w) alivyosema kwamba:fungeni kwa kuuona mwezi, vivyo hivyo ndivyo alivyosema Allah"Salini kwa kutenguka jua." Na Aya hio aliotunakilia Sh. Nassor Bachoo inazungumzia mambo yote mawili jua na mwezi. Kwa hivyo, ilitakiwa fiq-hi ya Sh. Bachoo iliojengeka juu ya Aya hio, ilihusishe jua kama ilivyouhusisha mwezi, kwani Aya inazungumzia mwenendo wa jua na mwezi. Na kwa hivyo, jua likitenguka Makka watu wa Zanzibar wasali?!
Kuanzia hapa utaanza kuona kwamba Aya hio ni kitu kimoja na fikra ya Sh. Nassor Bachoo ni kitu chengine. Qur-an imeeleza tu kwamba mzunguko wa jua na mwezi ni kwa ajili ya kujua miaka na hisabu, na miandamo ya mwezi ni vipimo vya nyakati na Hija: haikufafanua kwamba mwezi wa kisharia unaandama mara moja au kumi na moja. Ufafanuzi huu unaweza kupatikana baada ya kuzikusanya dalili zote zinazohusu maudhui hii kutoka katika Hadithi. Ama Qur-an Aya zake katika maudhui hii ni Mujmala (hazikufafanuliwa).
Baada ya haya, utaona kwamba tatizo sugu kwa walio wengi ni kutokutafautisha baina ya muandamo wa mwezi kifalaki (astronomically) na muandamo wake Kisharia. Muandamo wa kifalaki ni kutimiza kwa mwezi msafara wake kutoka katika kituo ulichoanzia hadi kufikia kituo cha mwisho. Muandamo huu ndio ambao ni mmoja dunia nzima, nao sio muandamo wa Kisharia: muandamo wa kisharia wa mwezi ni kitu chengine kabisa. Dhana (concept) sahihi ya kuandama kwa mwezi kisharia ni kuuona kwa macho baada ya siku ishirini na tisa au thalathini au kukamilisha idadi ya siku thalathini, kama Hadithi ilivyoeleza kwa uwazi. Sasa muandamo huu wa Kisharia, si lazima kwamba ukithibiti mahala pamoja uwe umethibiti mahala pengine. Kwa hivyo, Sheikh katika maelezo yake kachanganya baina ya muandamo wa kisharia na muandamo wa kifalaki na akaufanya muandamo wa kifalaki unaothibiti mara moja duniani kuwa ni sawa na muandamo wa kisharia ambao unatafautika kwa kutafautiana jografia ya ulimwengu kama tutavyoeleza baadae Inshaa Allah". Mwisho wa kunukuu nilioyasema kitabuni mwangu.
JAWABU NILILIPATA
Wanasema ndugu zetu wakijibu maelezo hayo: "6. Muandamo Wa Kifalaki Na Muandamo Wa KiShari'ah Kama kawaida yake ndugu yetu Juma amezusha dhana mpya katika mas-ala ya mwezi ambayo inakwenda kinyume kabisa na mitazamo ya Wanavyuoni, katika kulihusisha suala hilo na utaratibu wa kufunga na kufungua Ramadhaan. Amejaribu kuugawa muuandamo wa mwezi katika sehemu mbili kama alivyodai mwenyewe katika kitabu chake uk 18 kwa kusema: ((Hali ya kwanza: ni ya muandamo wa kifalaki.)) na (Hali ya pili: ni ya muandamo wa Kisharia.)
Hatujui dhana hii potofu ameitoa wapi kwani hakuweza kuthibitisha hata kauli moja ya Mwanachuoni yeyote aliyegawa muandamo au aliyesema kuna miandamo miwili (ya Kifalaki na ya Kisheria). Hoja sio kusema unavyoona wewe binafsi, kama mara nyingi alivyojaribu kuonya yeye mwenyewe ndugu Juma kwamba pasitumike 'hoja za mitaani' lakini bahati mbaya yeye mwenyewe anakwenda kinyume na kauli zake hizo".
JAWABU
Kwanza : maneno yenu "Kama kawaida yake" hayaoneshi kuwa muna insafu. Tukichukulia kuwa maneno "Muandamo wa kifalaki" ni istilahi mpya, je kitendo hiki cha kutoa istilahi mpya kimejikariri mara ngapi katika kitabu changu hata iwe "Kama kawaida yake". Ni wazi kwamba lengo lenu si kujadili bali ni kuponda na kutia aibu baada ya kushindwa kukijibu kitabu changu kwa hoja za kielimu zinazokubalika.
pili : Maneno "Inakwenda kinyume kabisa na mitazamo ya Wanavyuoni" yanaonesha kuwa hamujui mukisemacho, mwaporoja tu! Kwenda kinyume ni kuwa moja anasema "Kaja" mwengine anasema "Hakuja", huku ndio kwenda kinyume. Ama kusema kitu kipya tu ambacho hakijasemwa huko hakuitwi kwenda kinyume. Ingekuwa ni kinyume lau kuna wanazuoni waliokataa kwamba hakuna muandamo wa kifalaki, mimi nikauthibitisha, hapo ndio kwenda kinyume.
Tatu : Ilikuwa ni wajibu wenu kunukuu maneno yangu yote niliosema kisha mukayajibu: sio kuwambia watu "Amejaribu kuugawa muuandamo wa mwezi katika sehemu mbili kama alivyodai mwenyewe katika kitabu chake uk 18 kwa kusema: (Hali ya kwanza: ni ya muandamo wa kifalaki.) na (Hali ya pili: ni ya muandamo wa Kisharia."
Nnne : Tazameni maneno yangu vizuri nilisema: "Hali ya kwanza: ni ya muandamo wa kifalaki. Na huu sio ule tunaouita muandamo. Hapa tutatumia tu neno "Muandamo" kwa ajili ya kufahamiana. Huu ndio ambao unazungumziwa na Aya hizo tulizotangulia kuzinukuu. Na ndio unaotokea mara moja duniani kote". Maneno haya yote mumeyaruka ili mupate kufikia lengo lenu; lakini watu hamuwadanganyi kwani wanasoma na kujionea. Kwa hivyo, ni wazi - kwa kila mwenye akili licha ya mwenye elimu - kwamba mimi sikuuita huo kuwa ni muandamo, bali nimetumia lugha hio ili kutaka kuikurubisha maudhii katika fahamu za watu kuwa mwezi unakuwa umekamilisha safari yake baada ya kuvikata vituo ishirini na nane, na hapo huwa umemaliza mzunguko wake. Na huu ndio tuoweza kuuthibitisha kwa Aya zenye kutaja kupita kwa mwezi kwenye manazili.
Tano : Eleweni kwamba kinachotazamwa katika uwanja wa elimu si istilahat (technical terms), bali ni uhakika (facts) Yaani hali hio ya mw ezi kukamilika safari yake ndio uhakika (facts) na hilo jila nililoupa ni istilah tu. Sasa kama mulikuwa ni watu wa kufahamu mungelijadili uhakika (facts) na kubainisha kwamba nilivyosema sivyo. Ama istilahat (technical terms) mtu anawez a kukikipa kitu jina lolote lile kwani muhimu ni kuwa afahamike anakusudia nini. Na hili ni jambo ambalo wanavyuoni wanalizungumzia sana katika vitabu vyao vya Usuli na Furu'i, na ndio makusudio yao pale wanaposema: Hakuna kuvutana ka tika maneno ya kitaalamu au ya kifani (technical terms). Lakini kwa vile wenzetu walivyokuwa masikini wa elimu, basi wameona kule kutaja muandamo wa falaki - pamoja na kuwa nimebainisha kuwa huo si muandamo, bali natumia neno hilo ili kufahamiana - kuwa hilo ni kosa la jinai kwani ni jina ambalo halikutumiwa na wanavyuoni! Maskini wenzetu!
Sita : Ni kudai kwenu kwamba sikunukuu kauli za Maulamaa. Sijui munataka Maulamaa gani tena. Rejeeni maandiko yangu nilipozungumzia mas-ala haya muone kauli za Al-Tukhi, Al-Baghawi, Al-Zamakhshari, Al-Qurtubi na wengine wengi. Au hawa si wanavyuoni?! Saba: Ni kuwa nyinyi katika kukipinga Qias cha Sala na funga mumeleta hoja zenu binafsi: hakuna mjuzi yeyote anayetoa hoja hizo. Nazo ni hoja zenye kuonesha uchache au utovu wa maarifa.
MUNASEMA
"Ukiangalia katika kitabu cha "Kuandama Kwa Mwezi" uk 6 - 7 cha Shaykh Naaswir Bachuu, utaona kwamba yeye hakuporoja, bali amenukuu hoja za Wanavyuoni katika vitabu zaidi ya kumi. Baadhi yao ni kama vifuatavyo:- Tafsiri ya Durul-Manthuur: Imam as-Suyuuty katika tafsiri yake iitwayo "Durul-Manthuur" ameandika hivi "Amepokea Al-Khalib katika vitabu vya nyota kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'Anhu) kwamba kauli ya Mungu isemayo: "Na mwezi tumeupanga vituo husafiri (vituoni humo) hadi kurudi ukiwa kama karara la mtende." Amesema: "Ni vituo ishirini na nane ambavyo mwezi hutua humo kwa muda wa mwezi mzima, kumi na nne kati ya hivyo vipo magharibi na kumi na nne vyenginevyo viko mashariki."
Baada ya kuvitaja vituo hivyo akaendelea kusema: "Utakapomaliza (kusafiri katika) vituo ishirini na nane, hurudi ukiwa kama karara la mtende, kama ulivyokua mwanzo wa mwezi." (Durul-Manthuur: J. 5, uk. 495) Tafsiri ya Qurtubiy: Naye Imam Al-Qurtubiy amesema haya yafuatayo: "Na vituo vilivyotajwa katika aya hii ni ishirini na nane...." Akavitaja kwa majina kisha akasema: "Mwezi unapofika katika kituo cha mwiisho hurudi tena katika kituo cha mwanzo, kwa hivyo humaliza mzunguko mmoja katika siku ishirini na nane, kisha hufichika, kisha huchomoza tena katika sura ya uchanga (mwandamo) na kurejea katika safari yake kwenye vituo vilivyotajwa". (Tafsirul-Qurtubiy J. 8, uk. 21)".
Jawabu
Je katika kitabu changu hayamo hayo mulioyanukuu kutoka kwa Sheikh Nassor Bachoo hata langu liwe porojo lake lisiwe? Je mimi pia sikunukuu kauli za wanavyuoni juu ya Haya. Bali mimi nimenukuu kutoka kwa mtu ambaye alimu ya nyota ndio fani yake, naye ni Al-Tukhi, huyu ni bora katika fani hii kuliko hao wafasirina. Hebu rejeeni ukurasa wa 17-22 wa chapa ya pili ya kitabu Ushahidi Uliowekwa Wazi. Bali mimi nimewasiliana na mtaalamu wa falaki anayekubalika na akasema kuwa hakuna makosa katika nilioyaandika, na barua yangu kwake na majibu yake nimeyaweka katika uk. 11-13, wa kitabu changu. Tafadhali rejeeni huko. Pili ni kuwa Sheikhe wenu Bachoo ndiye aliyekosea alipotoa hoja kwa Hadithi ya kutunga. Kama alivyodai kwamba Kuraib hajulikani na wanavyuoni wa Hadithi, na akadai kuwa Al-Imamu Abu Muslim Al-Rawahi (Ibadhi) ni miongoni mwa waliosema kuwa muandamo mmoja unatosheleza duniani kote. Yote haya nyinyi munayafumbia macho na kusema "Sheikh Nassor hakuporoja". Ni wazi kwamba hamutafuti haki, bali ni ushabiki tu.
MNASEMA
Wala haina maana kwamba Shaykh Naaswir Bachuu, kwa kuzinukuu tafsiri hizo anaashiria kuwa watu wafunge kwa kutumia huo alioita ndugu Juma 'Mwezi wa falaki. Jawabu Mimi nilichokisema ni hiki: Sh. Nassor Bachoo ni mmoja wa Wazanzibari waliojitokeza kuzungumzia mas-ala haya. Katika kitabu chake, Sheikh kaizungumzia maudhui hii na akanukuu Aya ya 5 ya Sura ya 10 ambayo ni ya pili katika Aya tulizozinukuu kabla. Baada ya maelezo alisema: Qur-an inalieleza suala la kuandama kwa mwezi kama ni tukio moja wapo kati ya matukio yaliyopangwa na Mwenyezi Mungu kutukia kila mwezi mara moja duniani kote. Mwisho wa kunukuu.
Ukianzia uk. 5. hadi uk. 8, wa kitabu chake, utaona kwamba Sh. Nassor Bachoo anathibitisha mwenendo wa mwezi kupitia katika Manazil (vituo) yake. Ufupisho wake - kama tulivyotangulia kusema - ni kuwa mwezi unasafiri kwa muda wa siku ishirini na nane (28) kupitia katika vituo hivyo, na siku moja au mbili hupotea kisha kudhihiri na kuweza kuonekana duniani. Sheikh aliishia maneno yake kwa kusema: "Baada ya maelezo haya tunatumai tumeweza kuelewa mtazamo wa Qur-an juu ya kuandama kwa mwezi." Mwisho wa kunukuu.
KISHA NAMI NIKANENA
Sasa ukitazama sentensi mbili hizi za Sh. Bachoo, utaona kuwa anakusudia kuthibitisha kitu kimoja kwa Aya ambayo haimpatii malengo yake. Anachokusudia kukithibitisha Sh. Bachoo - kwa inavyoonesha kutokana na maandishi yake - ni kuwa muandamo ni mmoja duniani kote na kwa hivyo - bila shaka anakusudia kusema - kwamba sote tufunge kwa muandamo mmoja huo. Ndio maana akasema: "Qur-an inaeleza suala la kuandama kwa mwezi kama ni tukio moja wapo kati ya matukio yaliopangwa na Mwenyezi Mungu kutukia kila mwezi mara moja duniani kote." Lakini dai kwamba Qur-an inasema kuwa muandamo wa mwezi unatokea mara moja tu dunia nzima - ikiwa anakusudia muandamo wa kisharia nao bila shaka ndio anaouzungumzia - si sahihi. Na sijui wapi Qur-an imesema hivi?!
Kwa hivyo, ni wazi kwamba mimi napinga kutoa kwake (Sheikh Bachoo) ushahidi kwa Aya hio kama ni dalili ya muandamo wa mwezi. Nasema kuwa Aya haina maana ya muandamo wa mwezi bali ina maana ya kukakamilika mzunguko wa mwezi ambako ndiko nimekuita "Muandamo wa kifalaki" yaani the moon has been astronomically born: not judicially. Ama muandamo wa mwezi kisharia ni:
1) Kuuona kwa macho siku ya mwezi 29.
2) Kutimiza idadi ya siku 30.
Huu ndio muandamo wa mwezi kisharia. Ama kukamilika mzunguko, huo si muandamo kisharia kwani mwezi unaweza kukamilika mzunguko na usionekane duniani wala kusiwe na uwezekano wa kuonekana. Kwa hivyo, bado hamujajibu nilivyosema. Nasema kuwa Sheikhe wetu alivyoihusisha Aya hio, basi kakosea. Lakini hamutaki kukiri kwa sababu hamutafuti haki, mwatafuta kumlinda mtu fulani na kumshambulia fulani; na kuisapoti rai fulani na kuipinga nyengine hata kama ushahidi unakusuteni. Kiufupi ni kuwa Sheikh Bachoo aliposema hivyo, alikuwa anathibitisha muandamo mmoja kwa kutumia Aya hio, sasa vipi tena mutadai kuwa: "Wala haina maana kwamba Shaykh Naaswir Bachuu, kwa kuzinukuu tafsiri hizo anaashiria kuwa watu wafunge kwa kutumia huo alioita ndugu Juma 'Mwezi wa falaki."
MNASEMA
"Kwanza ni vyema kuelewa kwamba hakuna hiyo dhana ya muandamo wa kifalaki lakini kitaaluma kuna: "mwezi mpya" usioonekana (the invisible new moon) na "mwezi mchanga" unaonekana (the visible young crescent ). Ndio maana Shaykh Naaswir Bachuu akaandika katika kitabu chake uk 87 - 88 kwa kusema hivi: Tukirejea katika mada yetu ya kuandama kwa mwezi, itakuwa vizuri hapa kama tutamnukuu mtaalamu wa elimu hii ya annga (Astronomy), Dr. S. K. Abdali katika makala yake iliyochapishwa katika gazeti la Al-Ittihad la Mombasa Kenya, litolewalo mwaka mara nne; la kipindi cha Januari - Julai 1979. Amesema: "... Huu 'mwezi mpya' usioonekana (the invisible new moon) ambao majira yake hupatikana katika makalenda na magazeti, usichanganywe na mwezi mchanga unaoonekana (the visible young crescent) ambao (kutokana na mwezi huo mchanga) huanza mwezi mpya katika kalenda ya Kiislam...".
Hapa tunajifunza jambo moja muhimu kuwa 'mwezi mpya' (new moon) ni tofauti na 'mwezi mchanga' (young crescent). Na mwezi mchanga ndio tunaoutumia Waislam kujua kalenda (tarehe) yetu. Kwa hivyo hapa Shaykh Naaswir anasisitiza jambo la kutumika mwezi unaoonekana katika hukumu ya muandamo. Pili: Katika kitabu kizima cha Shaykh Naaswir kimeandikwa kwa msisitizo wa kutosha wa kwamba hukumu ya kufunga na kufungua ni lazima uonekane mwezi muandamo au kukamilisha siku 30 kama patapatikana udhuru wa kutoonekana mwezi siku ya tarehe 29. Ameyasema hayo Shaykh Naaswir akiwa anajua fika kwamba huo mwezi (aliouita ndugu Juma wa Falaki) hauna hukumu ya kufanya mtu afunge au afungue, kwani hauonekani kwa macho ya kawaida (the invisible new moon). Unajulikana kwa mahesabu ya Kitaalamu au kwa kuangaliwa kwa vyombo vya Kitaalamu.
JAWABU 1)
Kwanza nimeshakujibuni kuwa: wanavyuoni wote wanakubali na wamesema kuwa: Hakuna kujadiliana katika maneno ya kitaalamu au ya kifani. Kwa hivyo, je mwezi huo tuuite ni mwezi wa kifalaki kama alivyouita Juma Mazrui au tuuite 'Mwezi mpya' usioonekana (the invisible new moon) kama alivyouita mtaalamu wa falaki, hili si muhimu kielimu. Muhimu je huo aliouita Juma Mazrui kuwa ni muandamo wa kifali upo au haupo? Tena, je makusudio yake kwa kuuita muandamo wa kifalaki ni sawa na makusudio ya yule mtaalamu wa kifalaki alipouita 'Mwezi mpya' usioonekana (the invisible new moon). au Juma Mazrui anakusudia kitu chengine na mtaalamu wa falaki anakusudia kitu chengine? Haya ndio mambo ambayo wenye elimu huyajadili: sio kujadili majina, bali kinachojadiliwa ni uhakika (facts).
2) ni kuwa kama munatoa hoja kama hizo, basi hata hio dhana ya 'Mwezi mpya' usioonekana (the invisible new moon) pia katika Uislamu haipo. Hii Qur-ani na hizo Hadithi za Mtume (s.a.w.) haya nitoleeni palipoandikwa 'Mwezi mpya' usioonekana (the invisible new moon). Ni wazi kwamba jina hilo halipo katika Uislamu, lakini suala ni kuw a je uhakika (facts) wa 'Mwezi mpya' usioonekana (the invisible new moon) upo au haupo.
Wataalamu huwa wanatafiti uhakika (facts ) kisha wakishakugundua kitu wanakipa jina. Jina huwa ni jipya na uhakika hua upo zamani. Na jina la kitaala mu huwa linatafautika katika nchi hadi nchi; zama hadi zama; bali wakati mwengine baina ya mtaalamu au mpekuzi mmoja na mwengine. Lakini ndugu zetu, hamutaki kujiweka katika nafasi yenu aliokupeni Allah ya uchache wa maarifa, kisha munawambia watu wanajikweza, sijui nani anayejikweza. 3) Tatu: Eleweni tena, mimi nilikuwa najibu kitu gani? Mimi nilikuwa napinga kuhusishwa Aya"Yeye (Allah) Ndiye aliyelifanya jua kua muanga na mwezi kua nuru na akaupimia (huo mwezi) vituo, ili mujue idadi ya miaka na hisabu" na suala la muandamo wa mwezi Kisharia: nasema Aya hii haina uhusiano huo kamwe.
5
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA SABA
NDUGU JUMA ANACHANGANYA MAMBOKATIKA AYA YA QUR-AAN IFUATAYO
MNASEMA 7.
Ndugu Juma Anachanganya Mambo Katika Aya Ya Qur-aan Ifuatayo:
"Yeye (Mwenyezi Mungu) ndiye aliyelifanya jua (kutoa) mwangaza na mwezi (kuakisi) nuru na akaupangia (huo mwezi) vituo (vya kusafiria) ili mpate kujua idadi ya miaka na hesabu (ya nyakati"). (10: 5) Ndugu Juma anaona mwezi na jua ni vitu sawa sawa na kama kwamba vinafanya kazi moja kwa kuwa vimetajwa kwenye Aya moja ya Qur-aani. Huku akisisitiza kwamba: (Sasa utaona kwamba Aya hii imetaja vitu viwili: jua na mwezi. Na vyote hivi vinazunguka katika falaki (orbits) zake na vinapita katika manazil (vituo) yale yale na vinapita katika buruji (constellations) zile zile.) Pia anaona hukumu ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kusema kwamba ((Fungeni kwa kuuona mwezi)) ni sawa sawa na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliposema kuwa:"Swalini kwa kutenguka jua" .
SISI TUNAJIBU HIVI:
a) Mwezi na jua ni vitu viwili tofauti vinavyofanya kazi tofauti katika huo wakati (time). Kila kimoja kinafanya kazi yake maalumu kwa kuashiria huo wakati maalumu uliopangiwa. Angalia pia: (36: 40), (2:187)
b) Hukumu ya ((Fungeni kwa kuona mwezi na Swalini kwa kutenguka jua)) ni vitu viwili tofauti kwa sababu zifuatazo: i. Hadiyth ya kufundisha nyakati za Swala aliteremka Sayyidna Jibriyl ('Alayhi swalaatu was-salaam) kuja kumfundisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala haina khitilafu ya mahala kwa Wanavyuoni karibu wote. Angalia pia Qur-aan Tukufu (17: 78).
ii. Hukumu ya mgonjwa au mtu aliye safarini anayo ruhusa ya kutokufunga hata kama ameona mwezi lakini hana ruhusa ya kutokuswali kabisa hata akiwa mgonjwa au aliye msafiri.
iii. iii) mashariki " jua nyakati za Ibada za watu. Yaani kuweza kujua wakati wa kufunga., kutaja "ikma hkani kabisa, Mwanamke aliye katika siku zake ambaye amepewa ruhusa ya kutofunga Swaum ya Ramadhaan na kutokuswali atakuja kulipa Swaum, lakini hatolipa Swala.
iv. Hutokezea (ijapo kwa Sadfa) watu wa eneo kubwa kama nchi zote za Kiarabu hufunga Swaum zao kwa siku moja kutokana na muandamo wa mwezi. Lakini hawaswali Swala zao za faradhi kwa wakati mmoja - kwa kufuata jua wala hilo halina pingamizi wala mjadala kama ilivyokuwa hakuna ikhtilafu katika kufuturu wakati wa kuzama jua. v. Kumbuka kilichozungumzwa ndani ya kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu pamoja na Wanavyuoni wote wakubwa waliokuja na hoja ya kufunga pamoja. Wameelezea uwezekano wa kufunga dunia nzima katika siku moja, sio dakika au saa moja ya siku. Kwa mfano, dunia nzima inaswali Swala ya Ijumaa siku moja ya Ijumaa. Hakuna Ijumaa mbili duniani bali kuna kupitana na kutanguliana na hayo yanakuwa hata katika nchi moja.[1]
vi. Nyakati za Swala zimetengenezewa Jadweli (Time table) zinazolingana na mitenguko ya jua lakini suala la kufunga (Swaum) halikubaliki kufanyiwa jadweli au kalenda za muandamo wa mwezi sharti mwezi uonekane japo kwa macho ya mtu mmoja. vii. Si sharti kuliona jua kwa macho hata kwa mtu mmoja wakati wa kuchomoza au kutua (kuzama) katika hukumu ya kuanza na kumaliza kufunga. Unahakikisha muda wake tu kama umefika.
viii. Mwezi una Manazil (vipimo maalumu kwa ajili ya mwezi peke yake sio jua). Angalia Qur-aan (36: 39). Mwezi: Umejaaliwa kuashiria hesabu ya masiku 1, 2 28, 29 au/na 30. Kuingia kwa siku iliyoashiriwa na muandamo wa mwezi ndio unaufanya Ummah wa Kiislamu ufunge au ufungue Ramadhaan. Jua: Limejaaliwa kuashiria hesabu ya sekunde , dakika, saa, siku, wiki, miezi (months), miaka pamoja na miongo (Seasons) kwa ujumla. Mwenendo wa jua ndio unaofafanua nyakati za Swala, kula daku na kufuturu. Wala huwezi kutumia mienendo ya mwezi au Manazil yake katika kuashiria nyakati za Swala, kula daku au kufutari. Kusema: (jua likitenguka Makka watu wa Zanzibar wasali?!) kama alivyosema ndugu Juma katika kitabu chake uk 20, hizo ndio hoja za mitaani anazozikataa, kisha akawa anazitumia mwenyewe. Sisi tunamjibu hivi: Basi wakiswali Dar es Salaam na Kigoma waswali? Nizwa wakiswali na Ruwi waswali? Maana wanafunga siku moja". Mwisho wa kunukuu.
Jawabu ya ujumla Aya isemayo:
"Yeye (Mwenyezi Mungu) ndiye aliyelifanya jua (kutoa) mwangaza na mwezi (kuakisi) nuru na akaupangia (huo mwezi) vituo (vya kusafiria) ili mpate kujua idadi ya miaka na hesabu (ya nyakati)" , imetaja khabari nayo ni maneno yasemayo: "Huwa Al-Ladhi Ja'ala" (Yeye ndiye aliyejaalia). Kisha ikaletwa Al-Lamu Al-Ta'aliliya Lita'alamu. Kisha ikaletwa Al-Ma'alul Aya ikasema: 'Adada Al-Sinina Wa Al-Hisab. Kwa hivyuo, kama mulikuwa nyinyi ni watu wa fani za elimu kama munav yodai mungelijua kwamba hapa mumesukuma bila ya elimu. Hii inamaanisha kuwa kujua idadi ya miaka na hesabu ndio sababuu ya kuumbwa jua na mwezi katika Aya hio. Na haya yametajwa katika Aya moja - mf anyaji ni mmoja na illa (sababu) iliotajwa ni moja. Kwa hivyo, Aya kama ilivyolihusisha jua ndivyo ilivouhusisha mwezi katika kazi zile zile.
Ama njia ya kufanya Qiyas baina ya jua na mwezi si kama mulivyodhania. Kumbukeni kuwa vitu viwili vinaweza kuwa vinatafautiana katika baadhi ya mitazamo (in some aspects) na vitawafikiana katika mitazamo myengine. Qiasi hufanywa katika zile sehemu zilizo sawa: si zile ziliotafauti. Wala si kwamba kitu kilichotomika kufantiwa qiasi kitu chengine huwa hakizingatiwi kabisa kwa sababu kuna shemu ziko tafauti kama mulivyodhani nyinyi. Tafadhali rejeeni vitabu vya usuli mujifunze kufanya Qiasi musisukume mukapoteza watu bila ya elimu. Waliofanya kiasi baina ya jua na mwezi, wametazama zile sehemu ambazo vitu viwili hivyo vimelingana. Nayo ni kama nilivyoeleza katika kitabu kwamba:
1) Wajibu wa Sala umefungamanishwa na kutenguka na kuzama kwa jua - kitu cha kimaumbile (Natural phenomenon). Kwa hivyo mtenguko wa jua ni sababu ya kuingia wajibu wa Sala.
2) Wajibu wa funga umefungamanishwa na muandamo wa mwezi - kitu cha kimaumbile (Natural phenomenon). Kwa hivyo kuandama kwa mwezi ni sababu ya kuingia wajibu wa wajibu wa funga.
4) Jua - ambalo kutenguka kwake ndio sababu ya kuwajibikiwa na sala - likitenguka katika nchi moja, watu wa nchi nyengine hawawajibikiwi na sala. Kwa hivyo, Qiyas sahihi ni kuwa kuonekana kwa mwezi - ambayo ni sababu ya kuwajibika funga - katika nchi moja isiwe sababu ya kufunga kwa watu wa nchi nyengine. Hiki ni Qiyas sahihi. Au ukipenda kufanya Qiyas chengine sahihi, basi ni kile tulichokinukuu kutoka kwa Sheikh Al-'Uthaimin, aliposema:
"Na wakati wa mwezi ni kama wakati wa siku Kama vile ambavyo miji inatafautiana katika kuanza kujizuia (na kula na kunywa na jimai: yaani kuanza kufunga) na (inavyotafautiana katika) kufuturu kwa siku (daily au basi vivyo hivyo inawapasa watafautiane katika kujizuia na kufuturu kwa mwezi (monthly). Na (kama) inavyojulikana kwamba tafa uti za kisiku zina athari zake kwa makubaliano ya Waislamu. (Watu) waliyo upande wa mashariki, hakika wao wanaanza kufunga kabla ya waliyo upande wa magharibi na wanafuturu kabla yao.
Wala haiwezekani mtu akasema kwamba kauli yake Allah (S.W. inayosema):"Sasa waingiliyeni (wake zenu) na tafuteni kile Allah alichokuandikiyeni, na kuleni na kunyweni mpaka ukubainikieni uzi mweupe kutokana na uzi mweusi wa alfajiri, kisha timizeni saumu hadi usiku." Na kauli yake Mtume (s.a .w.w):"Usiku ukitokeza kutoka hapa na mchana ukaondoka kutokea hapa na jua likatua, basi aliyefunga ameshafungua (au na-afungue)." (Haiw ezekani mtu akasema kwamba Aya hio na Hadithi hii) kwamba ni za ujumla wa Waislamu wote katika miji yote. Basi vivyo hivyo tunasema kuhusu ujumla wa kauli yake Allah (S.W.):"Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" . Mwisho wa kunukuu.
Na kauli hii - kama unavyoona - ina nguvu yake kwa mujibu wa lafdhi (yake) na mtazamo sahihi na Qiyas sahihi vile vile: Qiyas cha wakati wa siku kwa (kuulinganisha) na wakati wa mwezi (month). Ama vifungu mulivyovileta vyote bado havijajibu hoja hizi. Kifungu cha kwanza kinasema: "a) Mwezi na jua ni vitu viwili tofauti vinavyofanya kazi tofauti katika huo wakati (time). Kila kimoja kinafanya kazi yake maalumu kwa kuashiria huo wakati maalumu uliopangiwa". Ninasema: nukta inayozungumzwa na wanavyuoni ni kuwa vyote viwili:
1) Ni vipimo vya nyakati
2) Kuingia kwake ni sababu za kuwajibika ibada.
3) Ni vitu vya kimaumbile (Natural phenomena).
Natija ni kuwa ikiwa tunakubaliana kwamba kutenguka jua nchi moja au katika watu wenye matalai moja ya jua si sababu ya kuingia wajibu was Sala katika nchi au matalai nyengine, basi vipi mwezi kuonekana katika matalai moja au nchi moja iwe ni sababu ya kufunga watu wa matalai au nchi nyengine?!
Kifungu (b) kinasema: b) Hukumu ya ((Fungeni kwa kuona mwezi na Swalini kwa kutenguka jua)) ni vitu viwili tofauti kwa sababu zifuatazo: i. Hadiyth ya kufundisha nyakati za Swala aliteremka Sayyidna Jibriyl ('Alayhi swalaatu was-salaam) kuja kumfundisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala haina khitilafu ya mahala kwa Wanavyuoni karibu wote. Angalia pia Qur-aan Tukufu (17: 78).
JAWABU
Sijui hata munasema nini!!! Kwanza mimi sikuzungumzia Hadithi ((Fungeni kwa kuona mwezi na Swalini kwa kutenguka jua)) na Hadithi ya Jibril ya nyakati za Sala. Bali nimezungumzia Hadithi hio, na Aya "Simamisheni sala kwa kutenguka jua". Na hoja nilioitoa ni kuwa katika Aya na Hadithi mwote kuna (ujumla) ulio sawa. Huku fungeni na kule Salini; huku kwa kuuona mwezi; kule kwa kutenguka jua - ujm la na illa (sababu) ni sawa katika maandiko yote mawili. Sasa ili iwe mumenijibu, basi inakubidini mujibu yale nilioyasema na muoneshe kuwa ujumla ulio huku na kule ni tafauti, sio mulete Hadithi ambayo mimi sikuitaja kamwe wala haihusiani na kile tunachokizungumza! Pili ni kuwa hata hio Hadithi munayoizungumzia nyinyi haijabatilisha niliyosema bali inayapa nguvu yale ninayosema kwamba kila watu na nyakati zao pamoja na kuwa andiko ni moja lile lile.
MNASEMA
"Hukumu ya mgonjwa au mtu aliye safarini anayo ruhusa ya kutokufunga hata kama ameona mwezi lakini hana ruhusa ya kutokuswali kabisa hata akiwa mgonjwa au aliye msafiri". iii. iii) mashariki " jua nyakati za Ibada za watu. Yaani kuweza kujua wakati wa kufunga., kutaja "ikma hkani kabisa,Mwanamke aliye katika siku zake ambaye amepewa ruhusa ya kutofunga Swaum ya Ramadhaan na kutokuswali atakuja kulipa Swaum, lakini hatolipa Swala.
JAWABU
Yametangulia maelezo kwamba vitu viwili huwa vinaoana katika baadhi ya mazingatio na kufarikiana katika mazingatio mengine. Wanavyuoni wanapofanya Qias baina ya vitu viwili hivyo, huwa hawadai kwamba vitu hivyo ni sawa katika kila kitu; bali huwa wanadai kuwa ni sawa katika zile sehemu walizozifanyia qias. Lau Mtume(s.a.w.w) - kwa mfano - alisema: "Musile samaki Fulani kwani ana sumu: anaua". Basi hapa hutafutwa illa (sababu) ya kukatazwa kula samaki huyo. Illa (sababu) ikipatikana na kwa hapa ni kuwa ana sumu, basi kila chenye sumu hupewa hukumu hio hio. Tukimkuta mnyama wa nchi kavu mwenye miguu mine ana sumu basi hupewa hukumu hio hio. Tukikuta tunda lina sumu hupewa hukumu hio hio. Huwezi tena kuda kwamba "Aa yule ni samaki anaishi baharini; huyu ni mnyama wa nchi kavu ana miguu miwili" au "Aa yule ni samaki anaishi baharini; hili ni tunda". Inayotazamwa ni illa (sababu), ikipatikana basi hukumu huthibiti palipotajwa hukumu na pasipotajwa. Huo ni mfano tu. Sasa tazama mambo ambayo wanavyuoni wameyafanyia Qiyas:
1) Imekuja Hadithi yenye kusema:"Kusengenya na kutia maneno mabaya baina ya watu, kunatoa udhu na kunavunja saumu" . Kama kawaida ya wanavyuoni huwa wanatafuta Illa (sababu) ya hukumu ikiwa Illa (sababu) hio haikutajwa kwa uwazi, kwani hukumu za kisharia ni zenye sababu. Hapa wakatafuta Illa (sababu) na wakaishia kwamba sababu ni kuwa matendo hay o ni katika madhambi makubwa. Kwa hivyo, wenye mtazamo huu wakasema kuwa kila dhambi kubwa inatengua udhu.
Wakati ukizitazama dhambi kubwa zenyewe ziko aina tafauti: kuzini ni tafauti na kulewa; kuiba ni tafauti na kuua n.k. Lakini kinachotazamwa ni kuungana kwa Illa (sababu) ndiko kunakovifanya vitu tafauti kuwa na hukumu moja. Ama ukitazama upande zilizotafautiana dhambi hizo, utaona kuiba hukumu yake ni kukatwa mkon; kuzini hukumu yake ni kupigwa mijeledi au kuuliwa; kuua hukumu yake ni kuuliwa. Lakini katika baadhi ya awajuh (aspects) zake, dhambi hizo ni sawa, nazo ni kuwa zote ni dhambi kubwa zenye kumpeleka mtu motoni kama hakutubia. Kwa hivyo, mfanyaji Qias huwa anatazama je ni katika mambo gani ya vitu viwili hivi mimi nayalinganisha. Ikiwa mambo hayo ni sawa, basi hukumu fulani itakuwa sawa. Na wala haina maana kuwa vitu viwe sawa katika hali zote. Bali hakuna hasa duniani vitu viliosawa katika hali zote, na kwa hivyo ingelikuwa kuna ufahamu huo mulio nao nyinyi, basi ingelikuwa hakuna kamwe kitu Qias.
2) Mtume(s.a.w.w) anasema:"Pombe imeharamishwa kwa sababu ya kulewesha kwake". Illa (sababu) ya kuharamishwa pombe ni hio iliotajwa. Kwa hivyo, kila penye Illa (sababu) hio hukumu inakuwa ni hio hio, ikiwa chenye kulewesha ni pombe au bangi au kokeni? Lakini ikiwa hujui Qias kinafanywa vipi, unaweza kutoa hoja kama hizo zenu ukasema:
a) Aa pombe inafanya kwa matunda mabovu (kwa Warabu wa kale inafanywa hasa hasa kutokana na zabibu) wakati bangi ni majani ya mmea unaoota.
b) Pombe inafanywa kutokana na matunda yaliooza, wakati bangi na kokeni ziko safi: haziozi! c) Pombe ni maji maji; wakati bangi na kokeni ni kavu.
Hivi ndivyo mtu asiyejua Qias kinafanywa vipi - kama nyinyi - anavyoweza kudai. Yaa Nas! Qias kinafanywa katika sehemu zilioafikiana baina ya vitu kwa sababu ya kuwepo sababu ilio sawa baina yao, wala haina maana kuwa vitu hivyo ni sawa katika kila kitu, zindukeni!
3) Mtume(s.a.w.w) alikataza kurembea mawe, kisha akataja Illa (sababu) ya kukataza huko, akasema:"Kwani haliwindi kiwindwa wala halimpigi na kumshinda adui, bali linavunja jino na kutofoa jicho" . Kwa hivyo, baada ya Mtume kutaja Illa (sababu) hizo, basi kinafanyiwa kiasi kila chenye kuwa na sifa hizo (chenye kuvunja jino, chenye kukata mguu, chenye kuvunja mkono) yaani vyenye kuweza kujeruhi: vyote vinaingia katika katazo. Wala huwezi kusema "Aa pigi (kwipi) ni tafauti na jiwe: pigi ni tawi la mti; jiwe limeundika katika ardhi". Tafauti hizi sizo zinazofanyiwa Qiasi: Qiasi kinafanyiwa zile sehemu zilio sawa. Kwa hivyo, vitu viwili vinaweza kuwa tafauti katika baadhi ya mitazamo yake (some aspects) na kuwa sawa katika mitazamo mingine, Qiyasi baina ya vitu hivyo hufanywa katika sehemu zenye kuwiyaana si zenye kufarikiana.
Kwa hivyo, kutafautiana kwa hukumu ya mgonjwa katika kusali na kufunga, na kuruhusika kwa mwanamke kutokulipa sala hakuvunji ukweli kwamba jua na mwezi viko sawa katika mas-ala ya nyakati. Katika mas-ala ya nyakati, kuingia kwa wajibu was ala kumefungamanishwa na jua - natural phenomenon (kitu cha kimaumbile); kuingia kwa wajibu wa saumu kumefungamanishwa na mwezi - natural phenomenon (kitu cha kimaumbile). Kutenguka kwa jua katika matlai fulani hakuwafanyi watu wa matlai mengine walazimikiwe na sala; kwa hivyo, kuandama kwa mwezi katika matlai fulani hakuwafanyi watu wa matlai mengine wawajibikiwe na funga.
Pili: ni kuwa hayo masuala mulioyasema, yamekuwa hivyo kwa sababu ya kuwepo ushahidi mwengine wa kimaandiko - yote yana dalili zake katika Hadithi. Na penye andiko huwa hakuna kufanya Qias kama kanuni zinavyoeleza. Yaani makusudio ya kuwa hapana Qias na andiko, ni kuwa huwezi kuleta Qiyas cha kubomoa andiko: si Qias chanye kuunga mkono andiko: Qias cha kuunga mkono andiko kimebarikiwa na kinatumika sana. Sisi suala letu ni kuwa je suala la kuzingatia matalai - tukiwacha kuwepo kwa maandiko (Hadithi ya Quraib) - je linapata nguvu katika Qiyas sahihi? Hili ndio suala. Nasi tunasema ndio, linapata nguvu ya Qias sahihi kama tulivyobainisha mara nyingi.
MNASEMA
Hutokezea (ijapo kwa Sadfa) watu wa eneo kubwa kama nchi zote za Kiarabu hufunga Swaum zao kwa siku moja kutokana na muandamo wa mwezi. Lakini hawaswali Swala zao za faradhi kwa wakati mmoja - kwa kufuata jua wala hilo halina pingamizi wala mjadala kama ilivyokuwa hakuna ikhtilafu katika kufuturu wakati wa kuzama jua.
JAWABU
1) Mimi sina kumbu kumbu ya nchi zote za Kiarabu kuonekana mwezi sawa au kufunga sawa. Kama nyinyi munazo munaweza kutupa.
2) Mimi katika kitabu changu, nilichokipinga ni kudai kuwa muandamo mmoja unatosha kwa dunia nzima na nikabainisha kuwa hili ni kinyume na Hadithi ya Kuraib. Ama eneo gani tufunge, nilikiri kuwa huu ni uwanja wa ijtihad. Kwa hivyo, kipengele hiki nacho pia kina mushkila.
MNASEMA
Kumbuka kilichozungumzwa ndani ya kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu pamoja na Wanavyuoni wote wakubwa waliokuja na hoja ya kufunga pamoja. Wameelezea uwezekano wa kufunga dunia nzima katika siku moja, sio dakika au saa moja ya siku. Kwa mfano, dunia nzima inaswali Swala ya Ijumaa siku moja ya Ijumaa. Hakuna Ijumaa mbili duniani bali kuna kupitana na kutanguliana na hayo yanakuwa hata katika nchi moja.
JAWABU
Nami napinga kwamba kuna uwezekano huo. Binafsi mwezi wa tano na wa sita 2009 nilikuwa Hong Kong. Nikampigia simu mtu aliyeko U.S.A, nikamuuliza kwenu saa ngapi? Akanambia saa kumi za jioni. Wakati huo mimi nilikuwa nishatoka msikitini kiasi cha saa kumi na moja na nusu au kumi na mbili kasoro kidogo au kumi na mbili. Hii ni kusema kuwa J/tatu asubuhi Hong Kong ni J/pili jioni U.S.A. Ikiingia alfajiri U.S.A, Hong Kong jua limeshatua kwa hivyo ni J/ane. Sasa uko wapi huo uwezekano wa dunia kufunga sawa?
Pili: je nyinyi si ndio muliokataa Qiasi cha Sala na funga, vipi tena hapa munalinganisha uwezekano wa kusali siku moja na uwezekano wa kufunga siku moja? Tatu: Kusali Ijumaa siku moja katika siku inayoitwa ijumaa, ni sawa kwani sababu imeshapatikana na wakati umeshafika, lakini suala letu ni je wanasali sawa sawa au kila mtu ni kwa mujibu wa wakati wake?
MNASEMA
Nyakati za Swala zimetengenezewa Jadweli (Time table) zinazolingana na mitenguko ya jua lakini suala la kufunga (Swaum) halikubaliki kufanyiwa jadweli au kalenda za muandamo wa mwezi sharti mwezi uonekane japo kwa macho ya mtu mmoja.
JAWABU
Na kusali pia ni sharti jua litenguke au lizame. Kusali kwetu kwa kufata jaduweli, ni kwa sababu tuna yakini kuwa wakati tayari: si kwa kutegemea jadueli. Lau na mwezi tulikuwa na yakini basi pia tungefanya hivyo hivyo. Ndio maana mwezi 30, tunafunga bila ya kuutazama kwani tuna yakini kwamba upo. Mas-ala hapa ni kuwepo yakini na kutokuwepo. Ama kwa kuzingatia asili ya amri, basi yote mawili - jua na mwezi - ni lazima vitazamwe.
Pili : jaduweli si jambo la kisharia tunaweza kuzikubali na tunaweza kuzikataa. Bali hio ni ijtihada ya watu tu: hakuna Aya wala Hadithi iliosema "Salini kwa kufata jadueli" bali "Salini kwa kutenguka jua". Tatu: ni kuwa yale niliokufahamisheni kwa urefu kwamba Qias baina ya mambo mawili si lazima kwamba yawe yameafikiana katika kila kitu bali yawe yameafikiana katika zile sehemu zinafantiwa Qias, zinafanya tafauti hii pia iwe haina umuhimu.
MNASEMA
Si sharti kuliona jua kwa macho hata kwa mtu mmoja wakati wa kuchomoza au kutua (kuzama) katika hukumu ya kuanza na kumaliza kufunga. Unahakikisha muda wake tu kama umefika.
JAWABU
Suala letu si mas-ala ya kuona au kutokuona, bali ni kuwa jua likitenguka katika nchi moja: si hoja kwa watu wan chi nyengine; basin a mwezi uwe hivyo hivyo kwani vyote ni vyombe vya kupimia wakati kwa ajili ya kuingia wajibu wa ibada.
MNASEMA
Mwezi una Manazil (vipimo maalumu kwa ajili ya mwezi peke yake sio jua). Angalia Qur-aan (36: 39).
Jawabu Aya ya 39 ya Sura ya 36 inasema:"Na Mwezi tumeupimia vituo mpaka ukarejea (kuwa mwembamba) kama karara kongwe (la mtende)" . Aya hii inathibitisha kwamba mwezi una manazil: haikanushi kwamba jua lina manazil. Wala hakuna mtaalamu yeyote aliyesema kuwa "Mwezi una Manazil (vipimo maalumu kwa ajili ya mwezi peke yake sio jua)" kama munavyosukuma nyinyi bila ya elimu. Nimebainisha katika kitabu changu na kunukuu maneno ya Al-Sayyid Al-Tukhi Al-Falaki kwamba: Manazil ni hizi nyota tunazoziona usiku, kama tulivyotangulia kunukuu maneno ya mtaalamu wa falaki Al-Tukhi kutoka katika kitabu chake kinachoitwa Ahkamu Al-Hakim Katika anga hii ya dunia kuna mijumuiko kumi nambili ya nyota ambayo inaitwa buruji. Kila mjumuiko mmoja ni buruji moja. Nazo ziko katika anga. Anasema Allah: (Naapa kwa anga yenye buruji (mikusanyiko ya nyota). Na kila buruji moja ina vituo ambavyo ndivyo vinavyoitwa manazil. Kwa hivyo, kama mwezi unavyopita katika buruji hizi, ndivyo jua, dunia na sayari nyenginezo zinavyopita: zote zinapita katika buruji zile zile na kwa hivyo zinapita katika manazil yale yale. Hii ni kusema kwamba jua na mwezi vyote viwili vina manazil. Fatilia kalenda zilizoandikwa na wataalamu wa falaki, utaona wanasema jua siku kadha liko katika buruji kadha, manzila (kituo) kadha daraja (degree) kadha. Na mwezi siku kadha uko katika buruji kadha, manzila kadha daraja kadha.
Nimekuelezeni katika kitabu kwamb kutoa ushahidi kwa Aya: "Na Mwezi tumeupimia vituo mpaka ukarejea (kuwa mwembamba) kama karara kongwe (la mtende)" kwamba jua halina manazil ni makosa, kwani ni kutoa ushahidi kwa njia ya Mafhumu Al-Llaqab nayo ni batili - taqriban - kwa makubaliano ya Umma mzima. Mafhumu Al-Llaqab ni kama mtu kusema: "Muhammad ni Mjumbe wa Mungu." Mwengine akasema "Basi Mussa si Mjumbe wa Mungu!" Huyu wa pili kajenga hoja yake kwa kutumia Mafhumu Al-Llaqab nalo ni kosa kwani kusemwa kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allah, haimaanishi kwamba hakuna Wajumbe wengine. Kwa hivyo, na hapa iliposemwa "Mwezi una manazil" nyinyi mukajibu: "Basi jua halina!!!!" Iliposemwa "Jua lina matalai" mukajibu "Basi mwezi hauna." Na haya ni makosa ya kifani. Kwani nikisema fulani alikuwa mwanachuoni wa Zanzibar inamaanisha kwamba yeye alikuwa mwanachuoni; wala haimaanishi kuwa mwengine hakuwa?! Au nikisema "Abu Bakr alikuwa muadilifu," maana yake ni kuwa Umar hakuwa?!
MNASEMA
"Mwezi: Umejaaliwa kuashiria hesabu ya masiku 1, 2 28, 29 au/na 30. Kuingia kwa siku iliyoashiriwa na muandamo wa mwezi ndio unaufanya Ummah wa Kiislamu ufunge au ufungue Ramadhaan. Jua: Limejaaliw a kuashiria hesabu ya sekunde, dakika, saa, siku, wiki, miezi (months), miaka pamoja na miongo (Seasons) kwa ujumla. Mwenendo wa jua ndio unaofafanua nyakati za Swala, kula daku na kufuturu. Wala huwezi kutumia mienendo ya mwezi au Manazil yake katika kuashiria nyakati za Swala, kula daku au kufutari".
JAWABU
Sawa! Lakini huo sio upande uliofanyiwa Qias baina ya vitu hivyo. Qias kimefanyiwa kwa mazingatio kwamba vitu vyote viwili hivyo ni vyombo vya kudhibiti wakati na ni kuingia kwake ni sababu ya kuwajibika ibada ya sala kwa upande wa jua; na kuwajibika kwa ibada ya saumu kwa upande wa mwezi. Jua likitenguka katika matalai moja au mji mmoja huwa si hoja kwa watu wa matalai au wa mji mwengine; kwa hivyo Qias ni kuwa na kuandama kwa mwezi katika matalai moja kusiwe hoja kwa watu wa matalai au wa mji mwengine. Tafadhali tazameni ni juu ya nukta gani Qias kimefanywa: sio mutafute tafauti katika sehemu ambazo sizo wanavyuoni wanazozifanyia Qias; angalieni mule walimofanyia Qias kasha ikiwa muna tafauti ndio mupinge.
Tumesema vitu viwili vinakuwa sawa katika mazingatio fulani kama pombe na bangi au kokeni kwa mazingatio kwamba vyote vinalevya; na vinakuwa tafauti katika mazingatio mengine kama tulivyobainisha kabla. Ukitaka kufanya Qias, kwanza unatazama hukumu unayotaka kuithibitisha. Kwa hapa ni uharamu. Pili unatazama sababu ya uharamu huo katika Aslu (Shina), kwa hapa ni kulewesha. Tatu unatazama je sababu hio ipo katika Far'u (tawi)? Jawabu ndio, bangi na kokeni nazo zinalewesha. Kwa hivyo, hukumu y a bangi na kokeni inakuwa sawa na pombe - vyote ni haramu kwa sababu ya kuungana katika Illa (sababu) ya uharamu. Wala hutazami tafauti za kuwa bangi ni majani; pombe ni maji maji; bangi haikuoza; pombe ni matunda yalioza. Hufanyi hivyo, kwani wewe lengo lako ni kutafuta nini kimesababisha pombe kuwa haramu, ukikipata unakitazama je katika bangi na kokeni kimo au hakimo. Hivi ndivyo Qias kinavyofanywa: sio hivyo mulivyodhania nyinyi. Halkadhalika mwezi na jua, kinachotazamwa ni kuwa jua ni kipimo cha ibada ya sala na ni sababu ya kuingia wajibu wake. Na mwezi pia ni kipimo cha ibada ya funga na ni sababu ya kuingia wajibu wake. Jua likitenguka mahala fulani haliwi sababu ya watu wa sehemu nyengine kusali; kwa hivyo, Qias sahihi ni kuwa kuandama kwa mwezi mahala Fulani isiwe sababu ya watu wa sehemu nyengine.
MNASEMA
Kusema: ((jua likitenguka Makka watu wa Zanzibar wasali?!)) kama alivyosema ndugu Juma katika kitabu chake uk. 20, hizo ndio hoja za mitaani anazozikataa, kisha akawa anazitumia mwenyewe. Sisi tunamjibu hivi: Basi wakiswali Dar es Salaam na Kigoma waswali? Nizwa wakiswali na Ruwi waswali? Maana wanafunga siku moja.
JAWABU
Hili ndilo tatizo lenu moja niliolizungumzia katika utangulizi: hamunukuu maneno yenye kuleta maana kamili. Suala je ilikuwaje hata mimi nikasema:"Jua likitenguka Makka watu wa Zanzibar wasali?! Je nilikuwa nadai kuwa watu wafanye hivyo au nilikuwa najibu hoja? Ufupisho wa kwanini nimesema hivyo, ni kuwa Sheikh Nassor aliichukua Aya isemayo:"Yeye (Allah) Ndiye aliyelifanya jua kua muanga na mwezi kua nuru na akaupimia (huo mwezi) vituo, ili mujue idadi ya miaka na hisabu," kuwa ni ushahidi juu ya muandamo mmoja duniani kote. Nami nikajibu - mukhtasari wake - kwamba Aya hii haina uhusiano na muandamo wa Kisharia, vyenginevyo Aya imetaja jua na mwezi kama ni vyombo vya nyakati. Kisha Aya ikataja illa (sababu) ya kuumbwa vitu hivyo nayo ni kujua idadi ya miaka na hesabu. Sasa nikamwambia Sheikh wangu kwamba, ikiwa yeye kaona kuwa Aya hii ni dalili ya muandamo wa Kisharia na kwamba muandamo mmoja - kwa mujibu wa Aya - unatosha dunia kote; basi Aya imetaja pia jua, kwa hivyo, nalo mtenguko wake mmoja na-utoshe duniani kote. Kwani Aya kama ilivyoutaja mwezi kuwa ni chombo cha kujua wakati ndivyo ilivyolitaja jua kwa lengo hilo hilo - illa ni moja na ma'alul ni moja. Hapa ndio nikasema kwamba, kwa mantiki yake hio ya kutoa ushahidi kwa Aya hii, basi na jua likitenguka Makka watu wa Zanzibar wasali kwani yeye katoa Aya hio kuthibitisha muandamo mmoja; na Aya imetaja jua na mwezi.
Hio ndio hoja yangu. Nyinyi kwa ufahamu wenu finyu au kwa ghushi zenu munakata kipande cha maneno yangu kisha munasema Juma kasema jua likitenguka Makka watu wa Zanzibar wasali!!! Fahamu ziko wapi: mimi sijasema hivyo.
Ama tafauti ya kufuturu Kigoma na Dar-es-salam na kuungana kwa kufunga, mumeikariri sana humu nami nimeieleza nukta hii katika sehemu nyengine kama mbili mutazikuta humu. Ama Niz-wa na Rui wanasali sawa na wanaona mwezi sawa.kuhusiana na jua na mwezi, ni kwamba humo mulimoona nyinyi kuwa muna tafauti simo mulimotumika kufanya Qias baina ya vitu viwili hivyo. Na inaposemwa kwamba vitu fulani vimefanyiwa Qias, haimaanishi kuwa vitu hivyo ni sawa katika pande zake zote; bali ina maanisha kwamba hukumu iliopo katika kitu ambacho hukumu yake imetajwa, inaingia katika kitu ambacho hukumu yake haikutajwa kwa sababu ya kuwepo illa jami'a sababu moja yenye kupelekea hukumu hio kuingia katika vitu viwili hivyo. Vyenginevyo, lau wanavyuoni wanatafautisha kama hivyo mulivyofanya nyinyi basi kusingelikuwepo na kitu Qiasi duniani kamwe kwani kuvikuta vitu viwili au zaidi vimeshabihiana katika pande zote ni muhali.
6
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA NANE
KUTOKUTAJWA KWA MATLAI YA MWEZI NDANI YA QUR-AAN
Katika kitabu changu nilisema hivi: Anaendelea Sheikh Nassor Bachoo na maelezo yake kwa kusema: "Jambo jengine la kuzingatiwa ni kwamba wanavyuoni karibu wote wamekubaliana kuwa machomozo (matlai) yamehusiana na jua na kwamba kila eneo (pahala) linafata majira ya kuchomoza, kupinduka na kuzama kwa jua katika hukumu ya kusimamisha sala ndani ya siku hio hio moja kwa ulimwengu mzima. (Angalia: surat Al-israa (Banii Israil) 17: 78). Lakini hakuna aya hata moja katika Qur-an (bali hata hadithi moja, iliyokuja kujuzisha (kukubalisha) kuwepo kwa tafauti za matlai ya mwezi. Kwa hivyo basi hakuna hoja hata moja ya kisharia iliyokuja kukubalisha kuwepo kwa Matlai ya mwezi 'MATLAI-QAMAR' Neno MATLAI mara zote katika Qur-an limekuja likiambatanishwa pamoja na JUA, 'MATLAIL-SHAMS'. Zifuatazo ni baadhi ya Aya zilizotaja habari ya matlai:-
1)"Unaliona jua linapochomoza" AL-KAHF (18:17)
2)"Hata alipofika matokea ya jua AL-KAHF (18:90).
3)"Na umtukuze Mola wako pamoja na kumsifu kabla halijatoka jua" TAHA (20:130). Mwisho wa kunukuu. Kisha nami nikatoa maelezo yangu kama ifatavyo: Kwa hakika mimi kabla sijasoma kitabu cha Sheikh Nassor Bachoo, nilimsikia kijana mmoja akisema maneno hayo, n a yeye akaongezea kwa kusema: "Bali mwezi una manazil." Bila shaka aliikusudia - kwa usemi wake huo - Aya inayosema: "Na mwezi tumeupimia manazil" (vituo) .
Kwa hivyo watu hawa ni kwamba wametazama Aya ya Qur-an inayosema:"Na mwezi tumeupimia manazil" (vituo), na Aya kama:"Hata alipofiki machomozo ya jua" . Wakaona mwezi ndio wenye manazil na jua ndilo lenye matalai: mwezi hauna matalai wala jua halina manazil!!! Watu wangejua kwamba Qur-an haifasiriwi ila kwa fani zake, basi wangejua kwamba tafsiri yao hio wameijenga katika "MAFHUMU AL-LLAQAB," nayo ni batili - taqriban - kwa makubaliano ya Umma mzima, kama tulivyotangulia kueleza. Tumebainisha huko nyuma nini "MAFHUMU AL-LLAQAB," na kwamba hii ni kama mtu kusema: "Muhammad ni Mjumbe wa Mungu." Mwengine akasema "Basi Mussa si Mjumbe wa Mungu!" Huyu wa pili kajenga hoja yake kwa kutumia "MAFHUMU AL-LLAQAB," nalo ni kosa kwani kusemwa kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allah, haimaanishi kwamba hakuna Wajumbe wengine. Kwa hivyo, na hapa iliposemwa "Mwezi una manazil" wao wakajibu: "Basi jua halina!!!!" Walipoambiwa "Jua lina matalai" wakajibu "Basi mwezi hauna." Jamani! Kwani nikisema fulani alikuwa mwanachuoni wa Zanzibar inamaanisha kwamba mwengine hakuwa?! Au nikisema "Abu Bakr alikuwa muadilifu," maana yake ni kuwa Umar hakuwa?!
Kwa ufupi labda watu hawajui manazil ni nini. Manazil ni hizi nyota tunazoziona usiku, kama tulivyotangulia kunukuu maneno ya mtaalamu wa falaki Al-tukhi kutoka katika kitabu chake kinachoitwa "AHKAMU AL-HAKIM" Katika anga hii ya dunia kuna mijumuiko kumi nambili ya nyota ambayo inaitwa buruji. Kila mjumuiko mmoja ni buruji moja. Nazo ziko katika anga. Anasema Allah:"Naapa kwa anga yenye buruji" (mikusanyiko ya nyota). Na kila buruji moja ina vituo ambavyo ndivyo vinavyoitwa manazil.
Kwa hivyo, kama mwezi unavyopita katika buruji hizi, ndivyo jua, dunia na sayari nyenginezo zinavyopita: zote zinapita katika buruji zile zile na kwa hivyo zinapita katika manazil yale yale. Hii ni kusema kwamba jua na mwezi vyote viwili vina manazil. Fatilia kalenda zilizoandikwa na wataalamu wa falaki, utaona wanasema jua siku kadha liko katika buruji kadha, manzila (kituo) kadha daraja (degree) kadha. Na mwezi siku kadha uko katika buruji kadha, manzila kadha daraja kadha. Ama matalai, ni wingi wa neno, na maana yake ni kuchomoza au mahala pa kuchomoza. Kwa maana ya kwanza itakuwa ni (Jina lililoaanzia na mimu), kama linavyotumika neno Mi'iraj kwa maana ya Al-uruj (Kupaa). Na asili ya muundiko huu wa neno Mi'iraj hutumika kwa jina la chombo au zana kama Miftahu yaani chombo au zana ya kufungulia (ufunguo). Na kwa maana ya pili ya neno Matla'i ni (Jina la pahala). Kwa maana hii, jua na mwezi yote yana matalai, kwani yote yanachomoza na yana sehemu za kuchomoza. Na kwa sababu hii, wale wenye kujua Kiara bu sawa sawa hawakuona tabu - katika kumsifu Mtume(s.a.w.w) - kusema:
Mwezi umetalai kwetu (umechomoza). Na Mtume(s.a.w.w) hakuwambia kwamba mwezi hauchomozi. Sikusudii kusema kwamba Mtume(s.a.w.w) ni mwezi, laa: sio hivyo, lakin i kilichopo katika kasida hii ya Masahaba wa Madina ni kitu kilichofananishwa na kitu chengine: kimoja ni hakika cha pili ni majazi (metaphor au mithali). Lakini cha kufahamu ni kuwa katika kufanya tashbihi (kukifananisha k itu kimoja na chengine kwa maana ya mithali) basi kimoja ni lazima kiwe hakika ndivyo kilivyo. Halkadhalika hakuna aliyemkosoa Mshairi aliposema: Viumbe wote wanasubiri t unuko lake kama Mahujaji wanavyosubiri Mwezi muandamo uchomoze. Halkadhalika ukirudi katika kamusi la Kiarabu mashuhuri na lenye kutegemewa nalo ni Lisanu Al-Arab la Ibn Mandhur, utakuta alipokuwa akilielezea neno: Tala'a (kutalai au kuchomoza) ali sema: Chomoza: Limechomoza jua na mwezi na alfajiri na nyota.
Kwa hivyo jua na mwezi - yote mawili - yana matalai na manazil, na kutokutajwa matalai ya mwezi katika Qur-an haina maana kwamba hicho kitu hakipo kwani Qur-an haikutaja kila kitu kwa ufafanuzi, bali imetaja kila kitu kwa ujumla tu, na Allah kasema:"Alipouona mwezi unachomoza. "Anasema Al-sabuni katika tafsiri yake: "Bazighan ni Taalian: husemwa bazagha Al-qamaru (Mwezi umebazighi) unapoanza kuchomoza." Pili ni kuwa: suala la kuchomoza mwezi ni kitu cha maumbile tunachokishuhudia sote: hatuna haja ya kusubiri ushahidi wa Qur-an. Kwani nikisema kwamba binaadamu wanakwenda aridhini, huwa ninahitaji ushahidi wa Qur-an kuthibitisha maneno yangu? Mwisho wa kunukuu nilioyasema kitabuni.
JAWABU NILILOPATA
Kujibu hoja hio, ndugu zangu wakasema ifatavyo:
8. Kutokutajwa Kwa Matlai Ya Mwezi Ndani Ya Qur-aan Katika kuelezea mada hii Shaykh Naaswir Bachuu kwenye kitabu chake ameelezea kama ifuatavyo:- Lakini hakuna Aya hata moja katika Qur-aan (bali hata Hadiyth moja iliyokuja) kujuzisha (kukubalisha) kuwepo kwa tofauti za Matlai ya mwezi. Kwa hivyo basi hakuna hoja hata moja ya kisheria iliyokuja kukubalisha kuwepo kwa Matlai ya mwezi 'Matlial-Qamar'. Neno Matlai mara zote katika Qur-aan limekuja likiambatanishwa pamoja na Jua 'Matlai-shamsi'. Zifuatazo ni baadhi ya Aya zilizotaja habari za Matlai:"Unaliona jua linapochomoza...." (18: 17)"Hata ilipofika matokea ya jua " (18: 90)Na umtukuze Mola wako pamoja na kumsifu kabla halijatoka jua (Taha 20: 130)
" Na Mtukuze Mola wako kwa kumsifu, kabla ya kutoka jua..." (50: 39) Kwa upande wa Ndugu Juma, yeye anayaona maelezo hayo siyo sahihi, lakini kwa bahati mbaya kama kawaida yake hakuweza kutoa hata Aya moja kuthibitisha hoja yake. Tahamaki anajaribu kutoa hoja ya kuwepo "Matlail - Qamar" kwa hoja za mashairi, maneno ya kiarabu pamoja na kutukumbusha kipande cha Qasida maarufu. Sasa ukirejea tena katika maelezo ya Shaykh Naaswir Bachuu utakuta kuwa bado ndugu yetu Juma ana deni kubwa juu ya uthibitishaji wake katika mas-ala haya. Kwa kuwa Shaykh Naaswir ametulia katika misingi miwili imara ya Qur- aan na Sunnah. Ingetarajiwa Ndugu Juma naye angetoa hoja katika misingi hiyo hiyo lakini anaonesha umahiri wake katika kuhifadhi beti za Qasida wala Shaykh Naaswir hakusema hakuna aliyesema "Mat-lail-Badru" katika Qasida. Kwani Qasida au mashairi hata ndugu Juma anaweza kusema atakavyo wala hakatazwi. Alichosema Shaykh Naaswir ni kwamba hapakutajwa lafdhi ya "Matlail-Qamar" ndani ya Qur-aan lakini pametajwa: "Matlai-Shams."[2][2]
Kwa upande mwengine, Ndugu yetu Juma amejaribu kutaka kuonyesha kwamba yapo Matlai ya mwezi kwa kuinukuu Aya ya Qur-an isemayo:"Na alipouona mwezi unachomoza alisema: "Huu ndio Mola wangu." (6: 77) Hapa ingefaa aelezwe Ndugu Juma kama anakusudia kwamba ni dalili katik a Aya hiyo kuwepo kwa "Matlail - Qamar" basi kwa mujibu wa mtiririko wa Aya zilizotangulia kabla ya Aya hiyo, hazina uhusiano wowote katika masuala hayo. Wala hajulikani mfasiri hata mmoja aliyeifasiri hivyo Aya hiyo hata Ndugu Juma akapata kigezo hicho. Ama kama anakusudia kutujuulisha mtindo wa lugha ya Kiarabu kuhusu neno atakuwa amekwenda kinyume na kanuni, kwani tujuavyo sisi kitabu chake alichokiandika ni cha mas-ala ya mwezi wala hakihusiani na lugha". Mwisho wa kunukuu.
Nayo ni jawabu ya kuchekesha. Kwa ufupi nasema je nyinyi munapinga kwamba mwezi hauchomozi? Kama unachomoza je pale unapochomozea panaitwa vipi kwa Kiarabu na kwa Kiswahili? Na je kwani kitu kutokutajwa katika Qur-ani huwa hakipo? Au kitu kikithibiti katika ulimwengu wa hakika huwa kinatosha kuthibitishwa. Nakukumbusheni mulioyasema: "Jambo la asli halihitaji (kuletewa) dalili, (lakini dalili inahitajika katika jambo lisilo la asili)." Nikisema kuwa binaadamu wanakwenda kwa miguu aridhini huwa nahitaji ushahidi wa Qur-an kuthibitisha hilo? Na nani kakwambiyeni kwamba lugha ya Kiarabu sio msingi mama wa kuifasiri Qur-an hata mukakataa kutoa kwangu ushahidi wa kuwepo kwa matala ya mwezi kwa Aya isemayo:"Na alipouona mwezi unachomoza alisema: "Huu ndio Mola wangu." (6: 77) Ikiwa Aya hii inathibitisha kwamba mwezi unachomoza vipi tena utakataa kwamba mwezi una machomozo?! Hivi si vichekesho?! Pia nimekutajieni maelezo ya Shei kh Al-Sabuni akisema kuwa maana ya neno "Bazagha" ni kuchomoza; halafu munadai hakuna mwanachuoni aliyefasiri hivyo.
Halafu kwa kusukuma kwenu mambo ya elimu bila ya kuyarejesha katika fani zake zinazotumika kufasiria maandiko munasema: "Ingetarajiwa Ndugu Juma naye angetoa hoja katika misingi hiyo hiyo lakini anaonesha umahiri wake katika kuhifadhi beti za Qasida wala Shaykh Naaswir hakusema hakuna aliyesema "Mat-lail-Badru" katika Qasida. Kwani Qasida au mashairi hata ndugu Juma anaweza kusema atakavyo wala hakatazwi". Na munamnukuu Sheikh akisema: "Lakini hakuna Aya hata moja katika Qur-aan (bali hata Hadiyth moja iliyokuja) kujuzisha (kukubalisha) kuwepo kwa tofauti za Matlai ya mwezi". Ninasema: Aya nimekupeni:"Na alipouona mwezi unachomoza alisema" . Kilichobaki munambie ni maana ya kuchomoza katika Aya hii. Kumbukeni kwamba kinachozingatiwa si lafdhi bali ni maana, maana moja ya kitu inaweza kuwa na lafdhi nyingi. Thaub (nguo) inapotajwa kwa jina la libas (kivazi), huwezi kukataa ukasema nguo haikutajwa kwani maneno yote hayo yana maana moja. Ama Hadithi munayoidai, inaonesha hata hamujui Hadithi ni nini? Hadithi au Sunna zimegawika sehemu tatu:
1) Qawliyya (ya maneno). Yaani pale Mtume(s.a.w.w) anaposema au kuamuru au kukataza kitu.
2) Fi'iliyya (ya kimatendo). Yaani pale Mtume(s.a.w.w) anapotenda kitu.
3) Taqririyya (ya kukiri au kukubali). Yaani pale Mtume(s.a.w.w) anapokiona kitu kinatendwa au kinanenwa mbele yake naye asikikitaze.
Kwa hivyo, kama umelifahamu hilo basi utakuwa umeelewa kwamba kipande cha Qasida maarufu katika elimu ya Hadithi huwa kinaitwa Sunna taqririyya ni Hadithi ya kuona kitu ukakikubali. Sasa anayeomba Hadithi juu ya suala la matalai ya mwezi, kwanza na-akasome elimu ya Hadit hi. Kwa ufupi, nahisi sina haja ya kurefusha kwa vile munaonekana hamutaki ukweli bali munataka ushabiki, vyenginevyo musingeliukataa ushahidi wa wazi wa Qur-ani bila ya hoja sahihi. Bali suala lu kuwa mwezi una matala halitaki ushahidi wa Qur-ani kamwe kwani tunauona ukichomoza na sehemu unayochomoza.
7
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA TISA
UFAFANUZI WA NENO 'AHILLAH'
Katika kitabu changu nilisema yafuatayo: "Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo. Sema: Hivyo ni (vipimo vya) nyakati kwa ajili ya watu na Hija" Hapa kuna nukta mbili tatu ambazo tutazijadili kama zilivyotolewa na Sheikh Nassor Bachoo, katika kitabu chake
UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI"
Kuanzia uk. 8 hadi uk. 9 wa kitabu chake hicho, Sh. Bachoo, anazungumzia kuhusu mas-ala ya kuwepo na kutokuwepo miandamo mingi kwa mujibu wa Qur-an. Katika maelezo yake anaona kwamba katika Qur-an hakuna sehemu yoyote ile ilioeleza kwamba kuna miandamo mingi. Na kwa hivyo baada ya kuinukuu Aya hio ya 189 ya Sura ya 2, alisema:
"Baadhi ya watu wa Afrika ya Mashariki wanadhani kwamba Aya hio inakiri kuwepo kwa miandamo mingi. Dhana hio wameijenga kwenye lile neno "miezi miandamo." Ni kweli nen o hilo limekuja kwa wingi (plural) yaani limetaja "miezi mingi" au "miezi michanga" kwa hivyo watu hao tuliowataja wameona kuwa; kwa kuwa Mwenyezi Mungu ametaja miezi mingi katika Aya hii basi anakiri kuwepo kwa miandamo mingi.
Kwa kweli dhana ya watu hawa juu ya tafsiri ya neno: Ahilla, yaani 'miezi miandamo' sio sahihi kwani neno hilo lilotajwa katika Aya hii ingawaje lina maana ya wingi lakini halikukusudiwa kumaanisha maana ya 'miezi mingi.' Kilichokusudiwa hapa ni kule kuelezwa 'hali ya miezi' kuwa nyingi yaani kwa kuwa mwezi huonekana kwa sura tafauti ndani ya kipindi kizima cha mwaka, imezingatiwa kuwa kama ni miezi mingi." Mwisho wa kunukuu.
Kisha Sheikh akanukuu mfano wa maneno hayo kutoka katika tafsiri ya Al-qurtubiy, ili kuipa nguvu tafsiri yake. Nami nina maelezo kidogo juu ya tafsiri ya Aya hii kama ifuatavyo: Kwa kuanzia ni kuwa Sheikh hakutoa ushahidi wa kielimu juu ya usahihi wa tafsiri alioitoa, kwani tafsiri inakwenda na ushahidi wake, ama: 1) Tafsiri ya Aya kwa Aya. 2) Au Aya kwa Hadithi. 3) Au kwa mujibu wa fani za lugha na usuli. Kwa ufupi ni kuwa neno Ahilla (miezi miandamo), kama alivyosema Sheikh, lina maana ya miezi mingi miandamo. Na hii ina uwezekano wa tafsiri mbili. Moja ni hio alioiita kuwa ni tafs iri ya watu wa Afrika Mashariki kwamba lafdhi Ahilla (miezi miandamo), ni dalili ya kuwepo kwa miandamo mingi wakati mmoja.
Tafsiri hii inapata nguvu kwa mambo mawili: Moja ni kuwa sehemu ya pili ya Aya imeifasiri sehemu ya kwanza na kubainisha muradi wake. Sehemu ya kwanza inasema: "Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo." Halafu ikaja sehemu ya pili ikatoa tafsiri kwa kusema: "Sema hivyo ni (vipimo vya) nyakati kwa ajili ya watu na hija." Kwa hivyo ni wazi kwamba kinachozungumziwa hapa ni miandamo yenyewe ya mwezi: wala si hali tafauti za mwezi, kwani vipimo vya nyakati na hija ni miandamo yenyewe: si hali tafauti za mwezi: hali tafauti za mwezi za kuwa mkubwa na mdogo haziwezi kuwa vipimo vya nyakati na hija. Kwa hivyo, tafsiri hio ya watu wa Afrika Mashariki - nao wamekulia katika chemchemu za elimu - ni tafsiri yenye muelekeo madhubuti sana.
Cha pili: chenye kuipa nguvu tafsiri yao hio, ni riwaya yenye kusema: "Kutoka kwa Ibn Umar (r.a.) kwamba Mtume(s.a.w.w) kasema:'Hakika ya Allah kaijaalia miezi miandamo kuwa ni vipimo vya nyakati: mukiuona fungeni na mukiuona fungueni." Ni wazi katika Hadithi hii kwamba kilichokusudiwa kwa neno Ahilla (miezi miandamo), ni miandamo yenyewe : si hali za mwezi. Na kwa hivyo, imesema Kaijaalia miezi miandamo kuwa ni vipimo vya nyakati.
Na akasimulia Abu Ghanim Al-khurasani - mpokezi wa Kiibadhi - Hadithi kama hio kutoka kwa Umar bin Al-khattab (r.a.) akisema: "Miezi miandamo ni vipimo vya nyakati, basi fungeni kwa kuuona na fungueni kwa kuuona, ikiwa wingu litauzi ba (au litauzinga kwa lugha nyengine) basi kamilisheni idadi ya siku thalathini." Sasa tukirudi katika tafsiri ya Sh. Bachoo, ambayo kaipa nguvu pia kwa tafsiri ya Al-imamu Al-qurtubiy, ni kuwa Sheikh - labda - hakutanabahi kwamba tafsiri hio alioitegemea kutoka kwa Al-qurtubiy na wengine, imejengeka katika Hadithi maudhui (ya kutunga). Nayo ni Hadithi alioisimulia Al-wahidiy na akainuku Al-suyutiy kutoka katika kitabu "TA-ARIKH DIMASHQ" cha Ibn Asakir na kutoka kwa Abu Nuaim, kwa njia ya Al-suddiy Al-saghir kutoka kwa Al-kalbiy kutoka kwa Abu Salih kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Muadh bin Jabal na Tha'alaba bin Ghanama walisema: 'Ewe Mjumbe wa Allah, kwanini mwezi unadhihiri na kuchomoza hali ya kuwa ni mdogo sana mfano wa uzi kisha unaongezeka mpaka unakuwa mkubwa na unakamilika na kuwa duara kisha unaendelea kupungua na kua mdogo mpaka unarudi kama ulivyokua, haui katika hali moja. Basi ikateremka Aya hio inayosema:"Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo" .
Na riwaya alioinukuu Al-qurtubiy mwenyewe kabla ya maneno hayo alioyaelezea Sheikh Bachoo, inaeleza kwamba hayo ni maneno ya Mayahudi, japokuwa Muadh ndiye muulizaji. Nayo ni Hadithi dhaifu sana kama alivyosema Sh. Abdul-razzaaq Al-hadi, aliyeitia maelezo tafsiri ya Al-qurtubiy. Na pia kama alivyosema Al-alusi na wengineo. Nao ndio ukweli, kwani katika sanad yake kuna Al-sudiy Al-saghir, naye ni Moh'd bin Mar-wan. Anasema Jarir bin Abdi Al-hamid: "Mwongo." Anasema Al-dawri kutoka kwa Ibn Main: "Si mwenye kuaminika." Anasema Salih bin Moh'd: "Alikuwa dhaifu na alikuwa akitunga (Hadithi)." Anasema Abu Hatim: "Hadithi zake zinaporomoka: Hadithi zake zinaachwa: Hadithi zake haziandikwi kamwe." Anasema Ibn Adey: "Udhaifu katika Hadithi zake uko bayana." Anasema Al-jawzjani: "Hadithi zake zinaporomoka." Anasema Ibn Hibban "Si halali kuandika Hadithi zake ila kwa ajili ya kufatilia (Sanad), na wala hafanywi kuwa ni hoja kwa hali yoyote." Anasema Al-tabari: "Hadithi zake hazifanywi kuwa ni hoja." Anasema Abdullahi bin Numair: "Al-suddiy alikuwa mwongo mkubwa."
Pia katika sanad ya Hadithi hio kuna Al-kalbi, naye ni Moh'd bin Saib bin Bishr. Anasema Mu'utamir bin Sulaiman kutoka kwa baba yake: "Al-kufa palikuwa na waongo wawili: mmoja wao ni Al-kalbi." Anasema Laith bin Abi Sulaim: "Al-kufa palikuwa na waongo wawili: mmoja wao ni Al-kalbi na wa pili ni Al-suddiy." Anasema Yahya bin Main: "Si lolote si chochote." Na akasema katika riwaya ya pili: "Dhaifu."
Na Al-kalbiy kaipokea Hadithi hio kutoka kwa Abi Salih kutoka kwa Ibn Abbas. Anasema Al-suyutiy: "Abu Salih ni dhaif." Anasema Abdul-Razzaq Al-mahdiy katika maelezo yake juu ya tafsiri ya Al-baghawiy: "Abu Salih katika (riwaya zake alizozisimulia kutoka) kwa Ibn Abbas, si mwenye kuaminika. Kwa hivyo, tafsiri hio ya Al-qurtubiy inayosema kwamba maana ya Al-ahilla (miezi miandamo) ni hali zake tafauti, si tafsiri ya kushangiriwa sana kwani imejengeka katika Hadithi maudhui (ya kutunga) au dhaifu sana.
JAWABU NILILOPATA
Ndugu zangu wakanijibu hivi: "Ufafanuzi Wa Neno 'Ahillah' Ufafanuzi wa Aya ya Qur-aan:"Wanakuuliza juu ya miezi. Sema: "Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili (ya mambo) ya watu (mengine) na ya Hijja (zao) . (2: 189) Hapa Ndugu yetu Juma katika kosoa kosoa zake anaona kama hivi ifuatavyo kwa mujibu anavyosema katika kitabu chake uk 56 - 57: (Kwa hivyo ni wazi kwamba kinachozungumziwa hapa ni miandamo yenyewe ya mwezi: wala si hali tafauti za mwezi, kwani vipimo vya nyakati na hija ni miandamo yenyewe: si hali tafauti za mwezi: hali tafauti za mwezi za kuwa mkubwa na mdogo haziwezi kuwa vipimo vya nyakati na hija.)
SISI TUNAJIBU KAMA IFUATAVYO
Neno 'yas-aluunaka' ambalo tafsiri yake ni "Wanakuuliza" tunaweza kuligawa sehemu tatu zifuatazo:-
1. Wenye kuuliza (waulizaji).
2. Mwenye kuulizwa (muulizwaji).
3. Chenye kuuliziwa (kinachouliziwa).
1. Wenye kuuliza (Waulizaji): Kwa hapa bila shaka ima itakuwa ni Waislamu waliokuwa katika hadhara ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) - yaani Masahaba au kama sio Waislamu watakuwa ni makafiri. Lakini kwa mujibu wa Tafsiri nyingi za Wanavyuoni wengi wenye kutegemewa katika fani hii ya tafsiri na baadhi ya vitabu vyengine - vimeeleza kwamba Masahaba ndio waliomuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)".
2. Mwenye kuulizwa hapa bila shaka yoyote atakuwa ni mwenyewe Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kwani yeye ndiye aliyeteremshiwa hiyo Qur-aan Tukufu. Na Aya kama hizi zipo nyingi katika Qur-aani Tukufu. Angalia: (2: 215, 217, 219, 220, 222).
3. Chenye kuuliziwa kwa hapa ni zile hali za mwezi kama yalivyobainishwa hayo na Wanavyuoni katika tafsiri zenye kutegemewa katika fani hii ya tafsiri. Ni vyema kuelewa kwamba Qur-aan ina utaratibu wake maalumu wa kuitafsiri, hususan inapokuwa katika mjadala wa kielimu au katika kutoa hoja juu ya hukumu ya jambo fulani, lazima yatolewe madondoo ya tafsiri za Wanavyuoni wenye kutegemewa. Wala sio busara mtu yeyote kutoa fikra zake binafsi hasa kama mtu huyo hajafikia katika daraja ya "Ijtihaad." Kwa mantiki hiyo, ndio maana ukaona katika kitabu cha "Kuandama Kwa Mwezi" cha Shaykh Naaswir Bachuu kila anapotoa hoja ya jambo fulani huwa anatoa madondoo maalumu hata pale anapotaja tafsiri ya baadhi ya Aya za Qur-aan.
JAWABU
Kwanza : mumepata wapi kwamba mtu lazima ategemee tafsiri za wanavyuoni? Maneno ya wanavyuoni si hoja za Kisharia ila wakikubaliana, na hapo hoja huwa ipo katika katika ijma'a (makubaliano) yao. Nakukumbusheni kauli yenu muliposema: "Kutegemea maneno, matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas b ila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa ni udhaifu".
Pili : ni kuwa wanavyuoni wa tafsiri wametumia riwaya nyingi za kutunga na dhaifu sana katika tafsiri zao. Kwa mfano kisa cha Malaika wanaoadhibiwa huko Iraki hadi leo! Kisa hiki ni katika riwaya za kiisraili. Wakati wanavyuoni wa tafsiri wamekitaja na wengine kwa kukikubali. Na kwa hivyo anasema Al-Imamu Ahmad kuwa riwaya za tafsiri hazina msingi kamwe, ingawa dhahir si kwamba Al-Imamu Ahmad anakusudia kuzikanusha riwaya zote za tafsiri; bali - dhahir ni kuwa - anakusudia kutokuwepo usahihi kwa asilimia kubwa ya riwaya hizo kama alivyosema Al-Zarqani. Chukua kwa mfano tafsiri ya Al-Tha'alabi. Utaona kwamba tafsiri yake ni mashuhuri kwa Hadithi za kutunga. Anasema Abdu-Razzaq Al-Mahdi katika utangulizi wake alioutia katika tafsiri ya Al-Baghawi: "Jua ewe ndugu Muislamu kwamba vitabu vyote vya tafsiri vimekusanya Hadithi dhaifu na za kutunga na riwaya za Kiisraili munkar na visa vibovu havina haja hata ya kuvitaja. Na katika hizo ni Hadithi zilizotungwa kuhusu fadhila za Qur-ani sura moja moja alizozisimulia Al-Tha'alabi katika tafsiri yake.na Maimamu wameeleza kwa uwazi kuwa ni za kutunga."
Anasema Ibn Al-Jawzi baada ya kutaja Hadithi ya kutunga: "Na ameitawanya Hadithi hii Al-Tha'alabi katika tafsiri yake..na akafatiwa na Abu Al-Hasan Al-wahidiy katika hayo, nayo si ajabu kwao kwani wao si watu wa (elimu ya) Hadithi." Hio ni mifano michache katika mingi lau twaikusanya basi tunaandika juzuu nyingi za kitabu. Kwa hivyo, marejeo ni kanuni za tafsiri za lugha, usuli-fiq-hi na Usulil-Hadithi: si mwanachuoni kasema nini. Hadithi ikiwa na sanad dhaifu au ya kutunga hakuna mwenye uwezo wa kuikweza akaifanya sahihi hata akiwa na elimu kiasi gani. Kwa hivyo, nakubaliana na nyinyi muliposema: "Ni vyema kuelewa kwamba Qur-aan ina utaratibu wake maalumu wa kuitafsiri, hususan inapokuwa katika mjadala wa kielimu au katika kutoa hoja juu ya hukumu ya jambo Fulani". Kwa bahati mbaya nyinyi na Sheikh Bachoo taratibu hizo hamukuzifata kamwe. Ama kauli yenu: "Lazima yatolewe madondoo ya tafsiri za Wanavyuoni wenye kutegemewa" hili nakupingeni, bali ni lazima ujue kanuni za tafsiri kisha tafsiri yako iwe kwa mujibu wa kanuni hizo. Ama wafasirina wamesema kauli sahihi na dhaifu; wametegemea riwaya sahihi na dhaifu na za kutunga kama nilivyokunakilieni maneno ya wajuzi.
Cha pili ni kuwa kauli yenu: "Kwa mantiki hiyo, ndio maana ukaona katika kitabu cha "Kuandama Kwa Mwezi" cha Shaykh Naaswir Bachuu kila anapotoa hoja ya jambo fulani huwa anatoa madondoo maalumu hata pale anapotaja tafsiri ya baadhi ya Aya za Qur-aan" maneno haya si sahihi. Sheikh Bachoo kasema Kuraib hajulikani, haya wapi kayapata maneno haya?!
Tatu : Ikiwa nyinyi hamuna uwezo wa kuifahamu tafsiri sahihi ya Aya, au hamuwezi kupambanua baada ya kuzitazama hoja tafauti za wanavyuoni juu ya tafsiri kwa kutokuwa na elimu ya nahau, sarfu, balagha na usuli, basi si kwamba kila mtu yuko hivyo. Kwa ivyo, anayeweza kuzitazama kauli za wanavyuoni na kuzipambanua na-afanye: asiyeweza na-aulize. Nyinyi hamuwezi na kuuliza hamutaki, munashikilia msimamo huo huo tu. Hata wale wenye elimu kukushindeni nyinyi kule Saudia akina Sheikh Bin Baz na Sheikh Ibn 'Uthaimin na wanavyuoni wote wa Saudia wamebadilisha msimamo baada ya kuona kuwa hoja sahihi ni zile walizoshikana nazo wale wenye kusema kwamba kila watu na muandamo wao. Nyinyi pamoja na udhaifu wenu mmekaa kupinga tu ilhali hamuna uwezo wa kifani wa kuweza kufikia natija sahihi.
Nne : ni kuwa mas-ala haya hayahusiani na elimu ya tafsiri; bali ni mas-ala ya riwaya marejeo yake ni wanavyuoni wa Hadithi. Na waliotia maelezo tafsiri za Qur-an na kuielezea riwaya hio wamesema kwa uwazi kwamba riwaya hio si hoja. Anasema Abdul-Razzaq Al-Mahdi katika maelezo yake juu ya tafsir ya Al-Zamakhshari baada ya kuinukuu riwaya hio: "Kaitaja Al-Wahidi katika Asbabu Al-Nuzul bila ya sanad. Na hii haina maana kabisa, kwani mbali na kuwa haina sanad, ni riwaya ya Al-Kalbi na jina lake ni Muhammad bin Al-Saib naye ni mwenye kuachwa mwenye kutuhumiwa (kwa uwongo)." Na katika maelezo yake juu ya tafsiri ya Al-Baghawi, baada ya Al-Baghawi kuitaja riwaya hio, Sheikh Abdul-Razzaq anasema kwamba (ni Hadithi): "Dhaifu sana na sanad hii inaporomoka, Al-Suddiy ni mwenye kuachwa na Al-Kalbi ni mwenye kutuhumiwa (kwa uwongo)." Na hata Al-Alusi - naye ni katika watu wa tafsiri - anasema: "Ameipokea Ibn 'Asakir kwa sanad dhaifu..".
MNASEMA
Kitu cha msingi hapa ni kujua kwamba: Je suala liliulizwa au halikuulizwa? Hata kama waliouliza ni Masahaba au Mayahudi. Bila shaka Aliyesema kwamba paliulizwa suala ni Mwenyewe Mwenyezi Mungu Mtukufu Aliposema: {{Wanakuuliza}}
JAWABU
Suala liliulizwa. Lakini mimi upinzani wangu haukuwa hapo. Mimi nilichokipinga ni kudai kwa Sheikh Bachoo kwamba: Kwa kweli dhana ya watu hawa juu ya tafsiri ya neno: Ahilla, yaani 'miezi miandamo' sio sahihi kwani neno hilo lilotajwa katika Aya hii ingawaje lina maana ya wingi lakini halikukusudiwa kumaanisha maana ya 'miezi mingi.' Kilichokusudiwa hapa ni kule kuelezwa 'hali ya miezi' kuw a nyingi yaani kwa kuwa mwezi huonekana kwa sura tafauti ndani ya kipindi kizima cha mwaka, imezingatiwa kuwa kama ni miezi mingi. Na mimi nimejibu kwamba:
1) Aya inasema kuwa:miandamo ya mwezi ni vipimo vya nyakati na Hija. Kwa hivyo ni wazi kwamba kinachozungumziwa hapa ni miandamo yenyewe ya mwezi: wala si hali tafauti za mwezi, kwani vipimo vya nyakati na hija ni miandamo yenyewe: si hali tafauti za mwezi: hali tafauti za mwezi za kuwa mkubwa na mdogo haziwezi kuwa vipimo vya nyakati na hija.
2) Tafsiri alioitegemea Sheikh Bachoo tegemeo lake ni Hadithi ya kutunga. Kwa hivyo, ili niwe nimejibiwa, basi thibitisheni kuwa:
1) Hali tafauti za mwezi za kuwa mkubwa na mdogo ndio vipimo vya nyakati na Hija. Na mukanushe kwa hoja kwamba kuandama kwa mwezi sio vipimo vya nyakati na Hija.
2) Thibitisheni kwa hoja za kielimu zinazokubalika katika elimu ya Hadithi kwamba riwaya hio ya kuwa Mtume (s.a.w.) aliulizwa kuhusu hali tafauti za mwezi ni riwaya sahihi. Na hili hamutoliweza mpaka ngamia atapita kwenye tundu ya sindano hata mukiomba msada kwa binaadamu na majini wote.
MNASEMA
Masahaba walitaka kujua kwa kina juu ya hali za miezi, mbona mara unakuwa mkubwa, mara mdogo, mara unapotea hauonekani kabisa, mara hali hii mara hali ile? Bila shaka jawabu ingetarajiwa iwe yenye kufafanua hali halisi ya matokeo hayo lakini jawabu ilikuja kutaja "hikma" ya kupatikana hali hizo nazo ni kujua nyakati za Ibada za watu. Yaani kuweza kujua wakati wa kufunga (Swaum), Hijja, Zakka na shughuli nyengine za kimaisha. Ikumbukwe kwamba utaratibu kama huu wa kuulizwa suala na jawabu ikataja hekima ya jambo lenyewe badala ya kufafanuliwa hilo jambo lenyewe ni jambo maarufu katika fani ya "Balagha" ijulikanayo kwa jina la "Uslubul-Hakiim" Angalia kwa makini baadhi ya madondoo kutoka katika kitabu Al-Balaghal - Waadhihah kama ifuatayo: Masahaba walimuuliza Mtume (S walla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu (hali za) miezi, vipi mwezi huonekana mdogo kisha unakamilika nuru yake (kwa kuwa mkubwa) kisha unakuwa mdogo katika hali ya kutoonekana. Mas-ala haya ni miongoni mwa mas-ala yanayohusu elimu ya nyota yanayohitajia uchambuzi mrefu na wa kina, ndio maana Qur-aan Tukufu ikawacha uchambuzi huo, na badala yake ikabainisha kuwa (hali hizi) za miezi ni njia za kujua nyakati za kazi na ibada mbali mbali".
JAWABU
Uslubu Al-Hakim si kazi yake kusahihisha riwaya dhaifu, bali kazi yake ni kuonesha hekima ya jawbu. Tunachokitaka ni sanad sahihi ya riwaya ya uwongo wa Al-Kalbi na Al-Sudi mulioitegemea. Ivo ndio munawalingania watu kukamatana na riwaya yenye sana za waongo halafu munasema nyinyi ndio munafata Sunna?! Tafadhalini leteni sanad sahihi ya riwaya hii, musibabaishe huku na kule. Kama hamuna musione haya kutangaza ukweli.
Pili : lazima mujue kwamba sababu iliompelekea mwenye kitabu Al-Balaghal - Waadhihah na wengine kuiita jawabu hio ya Qur-an kuwa imekuja katika mfumo wa "Uslubul-Hakiim" si kuitazama Qur-ani yenyewe; bali waliitazama hio riwaya dio wakatoa natija hio kwamba jawabu "Hiyo ni vipimo vya nyakati na Hija" ni "Uslubul-Hakiim". Sasa kama ni hivyo, basi el eweni kwamba riwaya hio ni dhaifu mno, bali ni ya kutunga haiwezi kujenga hoja.
Munasema Kwa hiyo tukichunguza Aya hiyo"Wanakuuliza" tutaona kuwa, Aya yenyewe inatuthibitishia wazi kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sa llam) aliulizwa, na waliomuuliza walikuwa ni Masahaba na alichoulizwa ni hali za miezi kama tulivyokwishaelezea.
Jawabu Aya inathibitisha kuwa Mtume (kaulizwa) kuhusu miandamo ya mwezi: si hali tafauti za mwezi. Lakini mumepata wapi madai kwamba: "Aya yenyewe inatuthibitishia kwamba.waliomuuliza walikuwa ni Masahaba na alichoulizwa ni hali za miezi kama tulivyokwishaelezea?". Tupeni ushahidi wa waulizaji walikuwa Masahaba katika Aya. Lakini hili si muhimu natusameheane. Leteni ushahadi wa hali tafauti za mwezi katika Aya hio au katika riwaya sahihi, musilazimishe tafsiri japokuwa ni tafsiri dhaifu kwa ushahidi wa kielimu. Wala musiisahau kauli yenu muliposema: "Kutegemea maneno, matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kuku balika kifani, huo utakuwa ni udhaifu".
MNASEMA
Kwa vyovyote vile kushikamana na Qur-aan ni jambo bora zaidi (aula) hususan inapotokezea khitilafu juu ya jambo au hukumu fulani. Shaykh Saalimiy katika kitabu chake anasisitiza zaidi katika jambo la kushikamana na Qur-aan hasa pale zinapopatikana ikhtilafu juu ya jambo fulani katika Umma:
Mwenye kushikamana na dhahir (ya manen o) ya kitabu cha Mwenyezi Mungu wakati ambapo Umma (wa Kiislam) umetafautiana juu ya hukumu ya jambo (fulani) au habari (fulani) bila shaka (mtu huyo) atakuwa ameshika kishiko madhubuti kisichovunjika.
JAWABU
Sasa nyinyi mumeshikana na sehemu gani katika Aya hio kuthibitisha madai yenu?
MNASEMA
Ama kuitolea hoja Aya hiyo (Wanakuuliza) kuwa ni dalili ya kuthibitisha kuwepo kwa muandamo wa kisheria au kuwa ni dalili ya kwamba kila nchi ifunge kwa muandamo wake au kuthibitisha kuwepo kwa 'miandamo mingi' huko ni kushindwa kuifahamu makusudio ya Aya. Vile vile ni kwenda kinyume na maelezo ya Wanazuoni katika vitabu vyao vya tafsiri, kwani Qur-aan ni lazima itafsiriwe kwa kuzingatia misingi yake maalum na kanuni zake zinazokubalika katika hiyo fani ya tafsiri. Shaykh Ahmad Al-Khaliil (Mufti Mkuu wa Oman ) alipokuwa akielezea rai za Wanavyuoni juu ya aina za tafsiri ya Qur-aan- ameeleza haya yafuatayo:
Kauli yenye nguvu ni kuwa inafaa kutafsiri Qur-aan kwa kutumia rai (lakini) kwa yule aliyekusanya sharti ambazo lazima Mfasiri awe nazo. Sharti zenyewe tumeshazieleza katika darsa iliyopita. Wala Mfasiri huyo asitie (katika tafsiri yake hiyo) matamanio ya nafsi yake. Bali rai yake hiyo iwe ni faida itokanayo na madondoo ya tafsiri za Wanavyuoni zenye kutegemewa katika fani hii ya tafsiri. (Sio kubuni tafsiri isiyoeleweka wala isiyokubalika katika misingi ya Dini) vile vile azingatie vizuri tokeo lililosababisha kuteremshwa Aya hiyo anayoifasiri, (lazima) aangalie "Sababun - Nuzuul"
JAWABU
Kwanza : rekebisheni ghushi zenu au kusukuma kwenu. Maneno ya Sheikh Al-Khalili yasemayo: nyinyi mumeyafasiri Bali rai yake hiyo iwe ni faida itokanayo na madondoo ya tafsiri za Wanavyuoni zenye kutege mewa katika fani hii ya tafsiri. (Sio kubuni tafsiri isiyoeleweka wala isiyokubalika katika misingi ya Dini). Masadir Al-Tafsir (vyanzo au sources za tafsiri) anazozikusudia Sheikh si tafsiri za wanavyuoni, bali ni fani za kutafsiria Qur-an. Mwenyewe kalieleza hilo kuanzia ukurasa wa 20 wa juzuu ya kwanza ya tafsiri yake Jawahiru Al-Tafasir. Sasa nyinyi ndugu zangu ikiwa maneno ya wanavyuoni hata kuyafahamu hamuyafahamu; kitu gani kilichokupelekeeni kujitumbukiza katika kulielezea jambo hili?! Na kama Sheikh anaona kuwa lazima mtu arejee katika tafsiri za wanavyuoni, haya ilikuwaje tena aipe nguvu kauli ya kujuzu kufasiri kwa rai kwa yule mwenye zana za elimu?! Hamuji mukisemacho!
Pili : mimi sikutoa ushahidi kwa kipande cha Aya kisemacho:"Wanakuuliza" tu kuwa ni dalili ya kuthibitisha kuwepo kwa muandamo wa kisheria, kama mulivyobutuwa nyinyi hapa. Dalili ya muandamo wa kisharia katika Aya hii iko katika neno "Ahilla". Tafsiri ya Ahilla ni mwezi miandamo. Na muandamo wa kis haria ni kuuona mwezi au kuthibiti kwa idadi ya siku 30. Sasa kama huu si muandamo wa kisharia ni muandamo gani? Bali Aya yenyewe imejieleza hivyo. Aya - kiukamilifu - inasema:"Wanakuuliza juu ya miezi miandamo. Sema: "Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na vya Hijja (zao) " . Sasa ikiwa Aya inasema kwamba Al-Ahilla(miezi miandamo) ni vipimo vya nyakati na hija vipi nyinyi mutasema kwamba kusema kuwa Aya hii hapa ni dalili ya miandamo ya Kisharia ni makosa? Jamani! Lakini muko makini au basi "Kake kanena namiye nanena tu?!"
Ama kauli yenu kwamba Aya hio ni kosa kuifasiri hivyo.Au kuwa ni dalili ya kwamba kila nchi ifunge kwa muandamo wake au kuthibitisha kuwepo kwa 'mian damo mingi.' Inaonesha kuwa hamukunifahamu nilivyosema. Mimi nilisema hivi: Kwa kuanzia ni kuwa Sheikh hakutoa ushahidi wa kielimu juu ya usahihi wa tafsiri alioitoa, kwani tafsiri inakwenda na ushahidi wake, ama: 1) Tafsiri ya Aya kwa Aya. 2) Au Aya kwa Hadithi. 3) Au kwa mujibu wa fani za lugha na usuli. Kwa ufupi ni kuwa neno Ahilla (miezi miandamo), kama alivyosema Sheikh, lina maana ya miezi mingi miandamo. Na hii ina uwezekano wa tafsiri mbili. Moja ni hio alioiita kuwa ni tafsiri ya watu wa Afrika Mashariki kwamba lafdhi Ahilla (miezi miandamo), ni dalili ya kuwepo kwa miandamo mingi wakati mmoja. Haya ndio maelezo yamgu. Zingatia maneno Na hii ina uwezekano wa tafsiri mbili. Yaani ni dalili yenye uwezekano wa namna mbili:
1) Inawezekana ikawa maana ni kuwa miandamo iko tafauti. Msingi wa hili ni kuwa lafdhi iliotajwa ni Ahillah (miezi miandamo). Na vitu vikitajwa kwa wingi plural form basi kimoja huwa si cha pili au kwa lugha nyengine huwa ni vitu tafauti, ila kukiwa na Qarina kwamba ni kitu kimoja. Ikitajwa Ash-hur mwezi (ya siku 29-30), makusudio huwa ni mwezi tafauti sio mmoja hule hule; wakitajwa watu basi moja huwa si mwengine, n.k.
2) Au ikawa maana ni miandamo ya mwezi tafauti japo ya mji mmoja, yaani mfunguo mosi, pili tatu. n.k. Maana zote hizi zimo katika lafdhi ya neno "Ahillah (miezi miandamo)".
Pamoja na hayo, niliona kuwa tafsiri ya kwanza ni bora kwa sababu ya kupata kwake nguvu katika riwaya tulizozinuku. Pamoja na hayo, kutumia kwangu neno uwezekano kulitakiwa kukufahamisheni kwamba tafsiri hii si ya mkato kwa vile haiko wazi 100%. Inawezekana ikawa makusudio ni ya pili. Ama tafsiri ya hali tafauti za mwezi, hii ndio niliodai kuwa ni batili kwani lafdhi ya neno Ahillah (miezi miandamo) haliingizi; wala haikutegemea riwaya sahihi ikawa ni tafsiri ya Mtume(s.a.w.w) , bali ni tafsiri iliosimuliwa na waongo kama walivyosema wanavyuoni wa wapokezi wa Hadithi.
Ama wanavyuoni, nimeshakujibuni kuwa hawana mamlaka ya kusahisha hadithi ya kutunga. Na tunachokitaka katika uwanja wa elimu na mijadala ya dini si fulani kanena, bali nini kimenenwa au fulani ana hoja gani? Ama Maelezo ya Sheikh Al-Khalili, ukizitoa sehemu mulizozikoroga zenye rangi nyekundu - inasema: Kauli yenye nguvu ni kuwa inafaa kutafsiri Qur-aan kwa kutumia rai (lakini) kwa yule aliyekusanya sharti ambazo lazima Mfasiri awe nazo. Sharti zenyewe tumeshazieleza katika darsa iliyopita. Wala Mfasiri huyo asitie (katika tafsiri yake hiyo) matamanio ya nafsi yake. Bali rai yake hiyo iwe ni faida itokanayo na madondoo ya tafsiri za Wanavyuoni zenye kutegemewa katika fani hii ya tafsiri. (Sio kubuni tafsiri isiyoeleweka wala isiyokubalika katika misingi ya Dini) vile vile azingatie vizuri tokeo lililosababisha kuteremshwa Aya hiyo anayoifasiri, (lazima) aangalie "Sababun - Nuzuul"
Eleweni kwamba makusudio ya kufasiri Qur-ani kwa rai anakokupinga ni kufasiri bila ya kuwa na dalili za kilugha, kiusuli au Hadithi na nyenginezo ambazo zinatumika katika kuifasiri Qur-an: sio kufasiri kwa mujibu wa kanuni. Pili: asbabu nnuzuli hakuna azipingae, na waliozipinga wakasema kuwa hazina maana hakuna muhaqqiq aliyewaunga mkono. Lakini cha kufahamu ni kuwa Sheikh Al-Khalili hapa anahimiza ulazima wa kujua asbabu nnuzuli: si kutegemea Hadithi za kutunga kama hio mulioitegemea nyinyi. Yeye mwenyewe Sheikh katika darsa zake za tafsiri hunukuu baadhi ya riwaya za asbabu nnuzuli kisha akazipinga kwa sababu ya udhaifu. Kwa hivyo, si kila iitwayo sababu nnuzuli ndio ichukuliwe tu, bali ichukuliwayo ni ile iliojengeka katika riwaya sahihi.
MNASEMA
Katika maudhui hii, ndugu yetu Juma amechanganyikiwa kwa kuwa tabia yake anaona ni bora kupinga tu vyovyote iwavyo! Yeye anaona katika Aya hiyo neno 'Ahilla' halizungumzii hali tofauti za mwezi bali linazungumzia miandamo yenyewe - yaan i kama kwamba kusema: Omani itazame mwezi wake, Dubai itazame mwezi wake, Yemen itazame mwezi wake, Saudia itazame mwezi wake na kila nchi itazame mwezi wake. Angalia katika kitabu chake uk 56 - 57. Anasema hivi: (Kwa hivyo ni wazi kwamba kinachozungumziwa hapa ni miandamo yenyewe ya mwezi: wala si hali tafauti za mwezi,) Kisha akasema: (lafdhi Ahilla (miezi miandamo), ni dalili ya kuwepo kwa miandamo mingi wakati mmoja) Angalia uk 56 ndani ya kitabu chake.
JAWABU
Mumenukuu kipande kidogo sana. Ilikuwa munukuu yote nilioyasema au sehemu yenye kuleta maana kamili. Nimesema: Kwa ufupi ni kuwa neno Ahilla (miezi miandamo), kama alivyosema Sheikh, lina maana ya miezi mingi miandamo. Na hii ina uwezekano wa tafsiri mbili. Moja ni hio alioiita kuwa ni tafsiri ya watu wa Afrika Mashariki kwamba lafdhi Ahilla (miezi miandamo), ni dalili ya kuwepo kwa miandamo mingi wakati mmoja.
Tafsiri hii inapata nguvu kwa mambo mawili: Moja ni kuwa sehemu yapili : ya Aya imeifasiri sehemu ya kwanza na kubainisha muradi wake. Sehemu ya kwanza inasema: "Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo." Halafu ikaja sehemu ya pili ikatoa tafsiri kwa kusema: "Sema hivyo ni (vipimo vya) nyakati kwa ajili ya watu na hija." Kwa hivyo ni wazi kwamba kinachozungumziwa hapa ni miandamo yenyewe ya mwezi: wala si hali tafauti za mwezi, kwani vipimo vya nyakati na hija ni miandamo yenyewe: si hali tafauti za mwezi: hali tafauti za mwezi za kuwa mkubwa na mdogo haziwezi kuwa vipimo vya nyakati na hija. Kwa hivyo, tafsiri hio ya watu wa Afrika Mashariki - nao wamekulia katika chemchemu za elimu - ni tafsiri yenye muelekeo madhubuti sana.
Hayo ndio maelezo niliotoa. Sasa nikuulizeni enyi Mashekhe wa msikiti wa Sunna. Ikiwa Aya inasema: "Sema hivyo ni (vipimo vya) nyakati kwa ajili ya watu na hija." Munataka mimi niseme vipi: nisema hali tafauti za mwezi?!
Halafu mukabutua tena maneno yangu, mukasema: "Kisha akasema: (lafdhi Ahilla (miezi miandamo), ni dalili ya kuwepo kwa miandamo mingi wakati mmoja.)". Maneno ya nyuma mumeyawacha. Mwanzo wa maneno ni: "Na hii ina uwezekano wa tafsiri mbili. Moja ni hio alioiita kuwa ni tafsiri ya watu wa Afrika Mashariki kwamb a lafdhi Ahilla (miezi miandamo), ni dalili ya kuwepo kwa miandamo mingi wakati mmoja. Tazama tafauti ya mantiki unayoipata katika maneno kamili na maneno butu mulioyanukuu nyinyi. Na hii ni kawaida yenu katika sehemu nyingi za kitabu chenu. Ni meeleza kwanini nimetumia neno "Uwezekano" rejeeni mutazame maelezo yangu. Sasa kilichobaki munithibitishie kuwa neno Ahillah halibebi maana ya miandamo mingi tafauti, na kama linabeba kipi kimeitoa maana hio katika Aya hio kutoka katika maana yake hio?
MNASEMA
Jambo jengine; ndugu Juma anaona kazi za mwezi na jua ni sawa sawa na kwamba kwa kuwa mwezi una 'Manazil' basi hivyo hivyo na jua lina 'Manazil'. Pia anaona kwamba kwa kuwa jua lina 'Matlai' basi na mwezi vile vile una Matlai. Angalia katika kitabu chake hicho (uk. 153 - 157).
JAWABU
Hili tumeshalizungumzia hatuhitaji kulikariri mara nyingi.
Munasema Jambo jengine ni kwamba ndugu Juma anaona katika tafsiri ya Aya hiyo"Wanakuuliza" imetumika Hadiyth 'maudhui' yaani ya uongo katika hilo linalobainishwa kwenye sababu ya kushuka Aya hiyo [3 na kwamba waliouliza hawakuwa ni Maswahaba bali ni Mayahudi.
Sivyo nilivyosema: nilivyosema ni hivi: Na riwaya alioinukuu Al-qurtubiy mwenyewe kabla ya maneno hayo alioyaelezea Sheikh Bachoo, inaeleza kwamba hayo ni maneno ya Mayahudi, japokuwa Muadh ndiye muulizaji. Kwa hivyo, maneno yenu: "Na kwamba waliouliza hawakuwa ni Maswahaba bali ni Mayahudi" tafadhali yarekebisheni katika chapa ya pili au katika kunijibu tena. Hayo si maneno yangu bali ndivyo ilivyo riwaya alioitaja Al-Qurtubi. Ama kusema kuwa hii ni riwaya ya uwongo, kweli nimelisema na nalisema kwani nina ushahidi nanyi mumeshindwa kuupindua wala hamuna njia ya kuupindua.
Munasema Sisi tunamuelimisha hivi ndugu yetu huyu kwa kumwambia kwamba kwa upande wetu tunazithamini sana tafsiri za watu wenye elimu ambao hapana shaka, wao hiyo Hadiyth wameshaiona na wameitumia baada ya kuipima kwa viwango vya kielimu zao. Halafu hapa katika Aya, hapana mjadala wala utatanishi wowote unaohitaji maelezo makubwa ya sababu ya kushuka kwa Aya hiyo, kwani dhahiri ya Aya iko wazi mno kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Mwenyewe Anathibitisha kwamba:"Ewe Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): (watu) wanakuuliza kuhusu (hali za) mwezi
JAWABU
Utatanishi haupo juu ya Mtume(s.a.w.w) kuulizwa bali upo juu ya kilichoulizwa. Mimi sitaki mupige chenga hii na hile; nataka riwaya sahihi. Na nimekuelezeni kwamba wanavyuoni wote wanakubali kuwa katika tafsiri za Qur-ani kuna riwaya nyingi za kutunga hadi Al-Imamu Ahmad bin Hanbal akasema kuwa tafsiri haina hadithi sahihi. Na nimekunakilieni maneno ya Sheikh Abdul-Razzaq na nimekupeni sanad na wanavyosema wanavyuoni wa wapokezi. Kwa hivyo, tufate misingi au tufate riwaya dhaifu?! Sasa kama munazithamini juhudi za wanavyuoni je munaikubali Hadithi isemayo kwamba tufate kitabu cha Allah na Ahlu Al-Bayt, alioipokea mjuzi kuliko mimi nanyiny, naye ni Muslim. Na munaikubali Hadith Al-Tair alioipokea Al-Hakim kwamba Ali (k.w) ndio awe khalifa baada yake. Zote hizi ni juhudi za wanavyuoni. Au mutachagua kile munachokiona kuwa ni sahihi na kukiwacha kile munachokiona kuwa si sahihi? Ikiwa munathamini juhudi za wanachuoni kwa maana hio, basi nijuilisheni nikunakilieni riwaya zao musizozikubali. Ikiwa munathamini juhudi zao pamoja na kuchagua kilichosahihi, na hivi ndivyo inavyotakiwa, naomba munioneshe usahihi wa riwaya hio, Na natoa changa moto.
Ama kauli yenu: "Kwani dhahiri ya Aya iko wazi mno kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Mwenyewe Anathibitisha kwamba:"Ewe Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): (watu) wanakuuliza kuhusu (hali za) mwezi." si kauli sahihi. Wapi Aya imetaja (hali za) mwezi" ?.
MNASEMA
Hebu tumuangalie mwanachuoni Al- Imam Abil-Hawaary Muhammad Binil - Hawaary Al-Omaniy Al-Ibadhy anayetajwa kama ni mwanachuoni wa karne ya tatu Hijriyah aliyeandika kitabu chake alichokiita: Katika kuitafsiri Aya hiyo ya Qur-aani: Aliandika ifuatavyo kwenye uk 99: Imeteremshwa Aya hii kwa Muadh bin Jabal na Tha'alabah bin Anama ambao ni katika Maansar. Walimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu miezi miandamo. Akasema Muadh: "Ewe Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi w a aalihi wa sallam) wa Mwenyezi Mungu una nini huu mwezi mbona unakuwa (mwembamba) kama uzi kisha unazidi (wembamba huo) tena unajaa (unakuwa mnene) mpaka unakuwa sawa sawa baada ya hapo unapungua unakuwa kama ulivyoanza?" (Baada ya suala hilo, Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akamteremshia Mtume wake aya hiyo: {{Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo. Sema hiyo ni vielelezo vya nyakati kwa ajili (ya mambo) ya watu}} kama kutaka (kujua) nyakati za eda zao, swaum zao, Mikataba yao (na mambo mengine ) na Hijja - yaani kujua nyakati za Hija zao. Kwa hivyo miezi ni vielelezo vya nyakati kwa mambo hayo". Mwisho wa kunukuu.
JAWABU
Na mimi nakuongezeeni mwanavyuoni wengine wa Kiibadhi naye ni Qutbu Al-Aimma, Muhammad bin Yusuf Utfayyish, katika tafsiri yake Al-Taysir j. 1, uk. 277. Halafu baada ya hapo nipatieni ushahidi wa tafsiri hio katika riwaya sahihi. Nipo nasubiri riwaya.
MNASEMA
Sasa tuangalie Wanavyuoni wetu ambao ni wazaliwa wa Zanzibar wenye kutegemewa ambao wameandika tafsiri zao za Qur-aan tukufu:
1. Shaykh Abdalla Saleh Al-Farsy aliyeandika tafsiri ya Qur-aan Takatifu alikuwa na haya yafuatayo katika kuifasiri (yas-aluunaka), alitoa maelezo yafuatayo: "Maswahaba waliuliza nini sababu ya kukhitalifu sura ya mwezi - mara mdo go, mara mkubwa. Wakajibiwa kwa wepesi tu kuwa 'Ipate kuwa kipimo ili wapate watu kujua kuwa sasa wako katika mwanzo wa mwezi au kati yake au mwisho wake.'
2. Shaykh Said Muusa Muhammad Al-Kindy katika Tafsiri yake ya Qur-aan aliyoiita: "Asili ya uongofu" Katika kuifasiri Aya hiyo; Alikuwa na maelezo yafuatayo:-"Kaulizwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu namna ya mwezi kwamba ukiandama mwanzo wa mwezi unakuwa mdogo kisha baada ya siku unakuwa nusu, kisha mkubwa, kisha unapunguka urudi kuwa nusu, na mdogo, na kuwa kama uzi; Jee nini hekima yake?"
Waulizaji waliouliza ni Muadh bin Jabal na Thaalabah bin Ghanam. Wakazidi kumuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba: kwa nini unabadilika hivyo mwezi? Na kwa nini jua halibadiliki kama mwezi? Ndio ikateremka Aya hii:"Wanakuuliza juu miezi, sema: "Ewe Nabii Muhammad uwaambie kwamba: 'Hiyo' kuwa mwezi mara mdogo mara mkubwa: "Ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya mambo ya "watu." Yanayohusu mambo yao ya dunia na pia ya Dini. Kwa ajili wajue: madeni yao wanayodaiana, na kodi zao wanazolipana katika mambo mbali mbali, na hesabu zao na za kujua siku na mwezi na mwaka na nyakati."
"Na wajue eda ya hedhi za wake zao, na wajue siku za Swaum yao, na wajue siku za 'Hijja' zao na na Ameulizwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) sababu ya kubadilika mwezi mara kwa mara. Ndio akawajibu kwamba ingekua mwezi utabaki namna moja tu kama jua, haitajulikana hisabu ya mwezi." "Na muradi wa mwezi yaani ni "Takwimu" au kalenda ya kujua hisabu ya wakati za siku na nyakati za wiki na nyakati za miezi na nyakati za miaka, na mambo mengi ya watu ya maisha yao ya duniani kupeana kama : kodi za nyumba, au mashamba au mfanyakazi au au ...Na mengi mengineyo."
"Na kama mambo ya Dini ambayo tumekwisha kuyataja. Yote hayo ya dunia na ya Dini yamehusika na hesabu ya mwezi kubadilika kwake mara kuwa mdogo na mara kuwa mkubwa."
3. Al -Marhuum Shaykh Ali Muhsin Al-Barwani katika Tafsiri yake ya Qur-aan Tukufu ijulikanayo kwa jina la "Tarjama Ya Al-Muntakhab"katika kuifafanua Aya hiyo ameeleza yafuatayo:- "Na watu wanakuuliza habari za mwezi, unaanza mwezi mchanga kama uzi, kisha unakuwa mpaka unatimia kamili. Tena unapungua mpaka unakuwa kama ulivyoanza. Haukai katika hali moja kama jua. Nini maana ya kugeuka huku hata inakuwa kila siku 29 au 30 unakuja mwezi mpya?"
"Waambie huku kutokea hivi kuandama mwezi na kugeuka yapo ndani yake maslaha ya Dini na dunia pia. Hizi ni alama za kuonyesha nyakati za mambo ya maisha yenu. Zinaonyesha nyakati za Hijja, ambayo ni moja katika nguzo za Dini yenu. Na lau kuwa mwezi ungelibaki namna moja tu kama jua msingelitambua nyakati za maisha yenu na Hijja zenu. Wala huko kutojua hekima ya kugeuka mwezi kusikupelekeeni kutilia shaka hekima ya Muumba"
"Uislamu unahisabu mwezi unapoandama na kugeuka Sura kwa watu kupimia nyakati za ibada, na pia kwa mambo yao ya kidunia, kwa sababu hayo ni mambo ya kuonekana, na kwa hivyo tarehe inajulikana kwa sura ya mwezi. Mwezi kwa hakika ni kama kioo kinachoonyesha mwangaza wa jua huku duniani. Mwezi ukiwa kati baina ya jua na dunia hauonekani, na baadae mwezi mchanga unaandama na wakaazi wa dunia wanajua kuwa mwezi mpya umeanza. Ukifika mwezi katika upande unaokabiliana baina ya jua na dunia ndio unapokuwa wakati wa mbaamwezi, mwezi mpevu. Halafu unaendelea kupungua kama ulivyokuwa kwanza ukizidi kukua. Kwa hivyo tarehe inaanza tangu pale ulipokuwa mwezi mchanga. Pale unapoonekana mwezi mchanga kama uzi ndio mwezi umeandama, huonekana upande wa magharibi, hata kwa dakika chache baada ya kuchwa jua nao hupotea. Hivyo hivyo siku baada ya siku huhisabiwa mpaka zipite siku 29 au 30."
4. Shaykh Al-Amin bin 'Ally Al-Mazrui: "Katika tafsiri yake uk 67 ya Qur-aan Tukufu juu ya Aya isemayo: Alikuwa na haya ya kusema:"Wanakuuliza wewe habari ya miezi !"
Kisha akaendelea kufafanua: "Baadhi ya Masahaba walimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) habari ya miezi - kwa nini huanzia mwembamba, ukaongezeka kidogo kidogo hata ukakamilika kengee yake, kisha ukaanza kupungua mpaka ukapotea kabisa kabisa? Kama suala hili lingejibiwa kisayansi ingewafungulia watu mlango wa kuuliza mengi ambayo hayahusiani na kazi ya Mitume. Kwani Mitume kazi yao ni kuwaongoza watu na kuwafunza yale ambayo hawawezi kuyajua ila kwa Wahyi. Ama mambo yawezayo kujulikana kwa ilimu, kama Falaki (astronomy), utabibu na kadhalika, si mambo ya kufaa kuulizwa Mitume, wala hayahusiani na kazi yao kamwe. Kwa sababu hii Allaah, badili ya kujibu suala lao, Ameeleza faida ya mwezi iliyofungamana na baadhi ya mambo ya manufaa, Shari'ah na mambo ya ibada. Hili lilitosha kuwafunza Masahaba lifaalo kumuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuwakomesha wasiulize suala zisizofaa. Wakaambiwa kuwa mwezi huwajulisha watu nyakati za muamala wao na maslaha yao ya kilimwengu na nyakati za ibada zao kama Hijja, Swaum na kadhalika." Mwisho wa kunukuu.
JAWABU
Haya! Sasa nipatieni ushahidi wa usahihi wa tafsiri hio! Nakukumbusheni maneno yenu muliposema: "Kutegemea maneno, matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya k uonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa ni udhaifu". Kwa ufupi mimi nilijibu hivi kuhusu riwaya hio: Nayo ni Hadithi dhaifu sana kama alivyosema Sh. Abdul-razzaaq Al-Mahadi, aliyeitia maelezo tafsiri ya Al-qurtubiy. Na pia kama alivyosema Al-alusi na wengineo. Nao ndio ukweli, kwani katika sanad yake kuna Al-Sudiy Al-Saghir, naye ni Moh'd bin Mar-wan. Anasema Jarir bin Abdi Al-hamid: "Mwongo." Anasema Al-duri kutoka kwa Ibn Main: "Si mwenye kuaminika." Anasema Salih bin Moh'd: "Alikuwa dhaifu na alikuwa akitunga (Hadithi)." Anasema Abu Hatim: "Hadithi zake zinaporomoka: Hadithi zake zinaachwa: Hadithi zake haziandikwi kamwe." Anasema Ibn Adey: "Udhaifu katika Hadithi zake uko bayana." Anasema Al-jawzjani: "Hadithi zake zinaporomoka." Anasema Ibn Hibban "Si halali kuandika Hadithi zake ila kwa ajili ya kufatilia (Sanad), na wala hafanywi kuwa ni hoja kwa hali yoyote." Anasema Al-tabari: "Hadithi zake hazifanywi kuwa ni hoja." Anasema Abdullahi bin Numair: "Al-suddiy alikuwa mwongo mkubwa."
Pia katika sanad ya Hadithi hio kuna Al-kalbi, naye ni Moh'd bin Saib bin Bishr. Anasema Mu'utamir bin Sulaiman kutoka kwa baba yake: "Al-kufa palikuwa na waongo wawili: mmoja wao ni Al-kalbi." Anasema Laith bin Abi Sulaim: "Al-kufa palikuwa na waongo wawili: mmoja wao ni Al-kalbi na wa pili ni Al-suddiy." Anasema Yahya bin Main: "Si lolote si chochote." Na akasema katika riwaya ya pili: "Dhaifu." Na Al-kalbiy kaipokea Hadithi hio kutoka kwa Abi Salih kutoka kwa Ibn Abbas. Anasema Al-suyutiy: "Abu Salih ni dhaif." Anasema Abdul-Razzaq Al-mahdiy katika maelezo yake juu ya tafsiri ya Al-baghawiy: "Abu Salih katika (riwaya zake alizozisimulia kutoka) kwa Ibn Abbas, si mwenye kuaminika.
Kwa hivyo, tafsiri hio ya Al-qurtubiy inayosema kwamba maana ya Al-ahilla (miezi miandamo) ni hali zake tafauti, si tafsiri ya kushangiriwa sana kwani imejengeka katika Hadithi maudhui (ya kutunga) au dhaifu sana. Hio ndio jawabu yangu kwa riwaya yenu. Nanyi hamukunijibu, mumenambia kuwa wanavyuoni wamesema. Nami nakubali kuwa wanavyuoni wamesema, lakiji je:
1) Wa dalili gani.
2) Je Wamekubaliana?
Nimkunakilieni maelezo ya Sheikh Abdul-Razzaq Al-Mahdi akisema kwamba riwaya hio: "Kaitaja Al-Wahidi katika Asbabu Al-Nuzul bila ya sanad. Na hii haina maana kabisa, kwani mbali na kuwa haina sanad, ni riwaya ya Al-Kalbi na jina lake ni Muhammad bin Al-Saib naye ni mwenye kuachwa mwenye kutuhumiwa (kwa uwongo). Na kwamba (ni Hadithi): "Dhaifu sanana sanad hii inaporomoka, Al-Suddiy ni mwenye kuachwa na Al-Kalbi ni mwenye kutuhumi wa (kwa uwongo).
Na Al-Alusi - naye ni katika watu wa tafsiri - anasema: "Ameipokea Ibn 'Asakir kwa sanad dhaifu..". Anasema Al-Sayyid Muhammad Rashid Ridha: "Hakika ya riwaya hii ya Ibn Abaas ni dhaifu, bali wamesema kwamba riwaya za Al-Kalbi kutoka kwa Abi Salih ndio njia dhaifu zao". Anasema Al-Tabatabai - mfasiri wa kishia - "Na ikapokewa kwamba baadhi yao walimuuliza Mtume(s.a.w.w) kuhusu hali tafauti za mwezi, ikataremka Aya hio. Na hili ndilo tulilolitaja kabla kwamba ni kinyume na dhahir ya Aya hio basi halina mazingatio". Kwa hivyo, sitaki kurefusha, wanavyuoni wako pia ambao hawakukubaliana na riwaya hio kwa sababu ni ya uwongo. Kilichobaki ni kuwa mutuletee riwaya sahihi ili tukubaliane nanyi.
8
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA KUMI
MASIMULIZI YA KURAIB
Kuhusu Hadithi hii mimi nilisema yafatayo:
"Kutoka kwa Kurayb (kasema) kwamba Ummu Al-fadhli bint Al-harith alimtuma Sham (Syria) kwa Muawiya. Akasema: 'Basi nikaenda Sham nikamkidhia haja yake.' Na ukaniindamia (mwezi wa) Ramadhani na mimi niko Sham. Basi nikauona mwezi usiku wa (kuamkia) ijumaa. Kisha nikaja Madina mwishoni mwa mwezi. Basi Abdullahi bin Abbas (r.a.) akaniuliza. Kisha akataja (habari za) mwezi muandamo akasema: 'Lini mumeuona mwezi muandamo?' Nikasema: 'Tumeuona usiku wa (kuamkia) Ijumaa.' Akasema: 'Wewe umeuona?' Nikasema: 'Ndio. Na Watu wameuona na wakafunga na Muawiya akafunga.' Akasema: 'Lakini hakika ya sisi tumeuona usiku wa (kuamkia) Juma Mosi, basi hatuachi kuendelea kufunga mpaka tutimize (siku) thalathini au tuuone.' Nikasema: 'Kwani wewe hutosheki na kuonekana na Muawiya na kufunga kwake?' Akasema: 'Laa' (Sio): Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w )."
SANAD YA HADITHI.
Tunatoa Sanad ya Muslim. Muslim kaipokea Hadithi hii kutoka kwa:
1) Yahya bin Yahya bin Bukayr. Naye ni mwalimu wa Al-bukhariy na Muslim na kasifiwa bila kifani. Kaitwa Imamu wa dunia wa zama zake, mkweli, muaminifu, mwenye elimu kubwa sana na mcha Mungu sana, wala hakuna aliyemjeruhi hata mmoja. Naye kaipokea kutoka kwa:
2) Ismail bin Ja'afar. Naye ni mkweli mwenye kuaminika, bila khilafu.
Naye kaipokea kutoka kwa:
3) Muhammad bin Abi Harmala, naye ni mwenye kuaminika wala hakuna aliyemjeruhi.
Naye kaipokea kutoka kwa:
4) Kuraib, naye ni Kuraib bin Abi Muslim, naye ni mwenye kuaminika bila khilafu.
Naye kaipokea kutoka kwa:
5) Ibn Abbas. Yeye hahitaji maelezo.
Kwa hivyo, Hadithi hii ni thabiti bila ya wasiwasi wowote. Na - natarijia - kwamba hakuna khilafu yoyote juu ya usahihi wake: khilafu iko juu ya maana yake.
FIQ-HI YA HADITHI.
Fiq-hi ya Hadithi hii, na ushahidi tunaopata ndani yake, ni kuwa Ibn Abbas (r.a), alipopewa habari kwamba mwezi umeonekana usiku wa (kuamkia) Ijumaa huko Sham (Syria) alikataa kuufata muandamo huo, na akasema "Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) ." Tukafahamu kwa mujibu wa matamshi haya ya Hadithi kwamba Mtume(s.a.w.w) kafundisha kwamba kila mji kufata muandamo wake. Vyenginevyo hakuna maana ya Ibn Abbas kuukataa mwezi uliothibiti Sham, baada ya kuthibiti kwa habari iliotolewa na mtu muaminifu. Na Kuraib alipomuuliza Ibn Abbas "Kwani wewe hutosheki na kuonekana (huo mwezi) na Muawiya." Akajibu "Laa" (Sitosheki): hivi (ninavyofanya mimi) ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) . Kwa hivyo, amri ya Mtume (s.a.w.) ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali.
UPINZANI NA MAELEZO YA AL-IMAMU AL-SHAUKANIY
UPINZANI WA KWANZA
Anasema Al-imamu Al-shaukaniy - akipinga kutoa hoja kwa Hadithi hio ya Kuraib na Ibn Abbas - : "Na jua kwamba hoja iko katika Al-marfu'u katika riwaya ya Ibn Abbas si katika ijtihadi yake ambayo watu wameifahamu kutoka kwake. Na chenye kuashiriwa kwa kauli yake (Ibn Abbas aliposema): 'Hivi ndivyo Mtume alivyotuamrisha,' na kauli yake 'Hatuachi kufunga mpaka tukamilishe (siku) thalathini.' Na amri yenyewe kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) ni ile (Hadithi) walioipokea Mashekhe wawili (Al-bukhariy na Muslim) na wengineo (yenye kusema): 'Musifunge mpaka muuone mwezi muandamo wala musifunguwe mpaka muuone, ikiwa wingu litakuzibeni basi kamilisheni idadi ya (siku) thalathini." Mwisho wa kunukuu.
Natarajia kwamba maneno haya ya Al-shaukaniy hayako wazi kwa kila mtu, labda yanahitaji kushereheshwa na kuwekwa wazi kabla ya kujibiwa. Anachokisema Al-imamu Al-shaukaniy ni kuwa hoja imo katika Hadithi ya Ibn Abbas alioipokea kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) : wala haimo katika ijtihadi yake, na alichokipokea kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) , ni Hadithi inayosema: "Musifunge mpaka muuone mwezi wala musifungue mpaka muuone, ikiwa wingu litakuzibeni basi kamilisheni idadi ya (siku) thalathini." Na kwa hivyo, Ibn Abbas - katika Hadithi hio ya Kuraib tunayoijadili hapa - alipoukataa muandamo uliothibiti Sham na kusema "Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) " amri yenyewe alioikusudia Ibn Abbas ndio Hadithi hio yenye kusema: "Musifunge mpaka muuone mwezi wala musifungue mpaka muuone, ikiwa wingu litakuzibeni basi kamilisheni idadi ya (siku) thalathini." Sasa kama ni hivyo, basi ukiitazama Hadithi hii, utakuta kwamba haiwahusu watu fulani pasi na wengine. Hivi ndivyo anavyosema Al-imamu Al-shaukaniy. Natarajia kwamba - kwa kusherehesha huku - maelezo yake yako wazi.
AL-IMAMU BADRU AL-DIN, AL-KHALILIY AJIBU
Lakini maelezo haya yakajibiwa na Sheikh Al-khaliliy kwamba, dai la Al-shaukaniy kwamba Ibn Abbas kuukataa muandamo wa Sham ilikuwa ni ijtihadi yake (Ibn Abbas) na kwamba aliposema (Ibn Abbas): "Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) " amri yenyewe alioikusudia ni Hadithi inayosema: "Musifunge mpaka muuone mwezi." Anasema Sheikh Al-khaliliy: "Hio pia n i ijtihadi ya Al-shaukaniy mwenyewe katika kujaribu kubainisha alichokitegemea Ibn Abbas. Na ilivyo ni kuwa kauli ya Sahaba (ataposema kwamba) Mtume(s.a.w.w) alikuwa akituamrisha kadha na akitukataza kadha basi inapewa hukumu ya raf'ibali Jumhuri inasema kwamba kauli ya Sahaba: 'Tulikuwa tukiamrishwa kadha na tukikatazwa kadha inapewa hukumu ya raf'i." Mwisho wa kunukuu.
Anachokisema Sheikh Al-khaliliy katika kumjibu Sheikh Al-shaukaniy, ni kuwa Ibn Abbas katika Hadithi yake hio aliukataa muandamo wa Sham na kusema "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) ." Na maneno haya ya Ibn Abbas yalikuja baada ya kuulizwa na Kuraib: "Kwani wewe hutosheki na kuuona Muawiya?" Ndio Ibn Abbas akajibu hivyo. Kwa hivyo, ni wazi kwamba kutokutosheka na mwezi wa mbali ndio mafunzo ya Mtume(s.a.w.w) . Sasa kudai kwa Al-shaukaniy kwamba Ibn Abbas alitumia ijtihadi yake, ni kinyume na kanuni za Usulu Al-hadith (Elimu ya Hadithi). Kwani - kwa mujibu wa elimu hii - ni kuwa Sahaba anaposema kuwa "Mtume katuamrisha kadha au katukataza kadha," basi maneno haya yanapewa hukumu ya Hadithi yenye kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) . Na hivi ndivyo walivyokubaliana wanavyuoni wote wa Hadithi. Tafauti ipo pale Sahaba anaposema: "Tulikuwa tukiamrishwa kadha," bila ya kumtaja Mtume(s.a.w.w) . Hapa Jumhuri inayapa maneno haya hukumu ya Hadithi inayotoka kwa Mtume(s.a.w.w) na wachache miongoni mwa wanavyuoni hawayapi hukumu hio. Sasa hapa Ibn Abbas kasema: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) ." Kwa hivyo, kukataa kwake muandamo wa Sham ni hukumu ya Mtume(s.a.w.w) .
Ama kudai kwamba Ibn Abbas - kwa kusema kwamba Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) - alikusudia kuiashiria Hadithi inayosema: "Musifunge mpaka muuone mwezi," ni dai lisilo na ushahidi katika riwaya nyengine, wala halifahamiki katika Hadithi ya Ibn Abbas na Kuraib. Kwa hivyo, hio ni ijtihadi ya Al-shaukaniy, na kauli ya Ibn Abbas ndio mafunzo ya Mtume(s.a.w.w) . Huu ndio mukhtasari wa jawabu ya Al-imamu Badru Al-din Al-khaliliy kwa Al-imamu Al-shaukaniy.
UPINZANI WA PILI
Anaendelea Al-imamu Al-shaukaniy na upinzani wake kwa kusema: "Hata tukikubali (kwamba) muelekeo wa ishara katika maneno ya Ibn Abbas (inaonesha) katika kutokulazimika (kufata) kuonekana (kwa mwezi) wa watu wa mji (mmoja) kwa watu wa mji mwengine, basi ingekuwa kutokulazimika huko kumefungamanishwa na dalili ya kiakili, nayo ni kuwa pawe baina ya miji miwili hio umbali ambao kwawo (hupatikana) tafauti za matalai. Na Ibn Abbas kuacha kuutendea kazi uonekanaji (wa mwezi) wa watu wa Sham - pamoja na kutokuwepo (baina ya miji hio) umbali ambao kwao inaweza kupatikana tafauti (ya matalai) - kulifanyika kwa ijtihadi (yake tu) nayo si hoja." Mwisho wa kunukuu.
Anachokisema Al-imamu Al-shaukaniy ni kuwa hata tukikubali kwamba Ibn Abbas aliposema "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) " tukikubali kwamba Ibn Abbas kwa maneno haya kakusudia kwamba kila mji na muandamo wake, basi hilo haliwezi kuwa sahihi ila lifungamanishwe na hoja ya kiakili, na hoja ya kiakili yenyewe ni kuwa baina ya miji hiyo iliotokea miandamo tafauti basi pawe na umbali wa kutosha baina yake ambapo kwa sababu ya umbali huo, basi matalai (machomozo ya mwezi) yanaweza yakatafautiana baina ya miji hio. Sasa Sham (Syria) na Madina hakuna masafa hayo ambayo yanasababisha kutafautika kwa matalai baina ya miji hio. Kwa hivyo, ikabainika kwamba hili lilikuwa si jengine bali ni ijtihadi ya Ibn Abbas, na ijtihadi ya Sahaba si hoja katika hoja za kisharia.
Huo ndio upinzani wa pili wa Al-imamu Al-shaukaniy, lakini kama unavyoona jawabu yetu ya kwanza inajibu baadhi ya nukta zilizomo katika upinzani huu. Na hii ni kudai kwamba ile ilikuwa ni ijtihadi ya Ibn Abbas. Kwa kweli ilivyo ni kuwa hii ni ijtihadi ya Al-imamu Al-shaukaniy, na msingi ni kurudi katika elimu ya Hadithi, ndio itayohukumu Hadithi ni ipi na ijtihadi ni ipi. Na tumeona kwamba kauli ya Ibn Abbas inasema: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w." Tumesema sigha (form) hii ya Hadithi inaipa Hadithi hukumu ya kuzingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume Mwenyewe(s.a.w.w) .
Ama kudai kwamba hata ikithibiti kwamba muelekeo wa kauli ya Ibn Abbas ni kuwa muandamo wa mji mmoja hautendewi kazi kwa watu wa mji mwengine, kwamba hata ikithibiti kuwa huo ndio muradi, ni lazima kuufungamanisha muradi huo na miji yenye tafauti ya matalai, si dai sahihi. Maneno haya ya Al-imamu Al-shaukaniy - kama yalivyo maneno ya watu wengi wa kawaida - chimbuko lake ni kuchanganya pale penye kujuzu ijtihadi na pale isipojuzu. Penye andiko huwa hakuna ijtihadi: ijtihadi mahala pake ni pasipo andiko. Sasa ukirudi kuitazama riwaya hio ya Ibn Abbas, utakuta kwamba kinachoelezwa ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali. Hivi ndivyo andiko linavyoonesha.
Sasa je umbali huu uwe kiasi gani, andiko halikubainisha. Kwa hivyo, "Muandamo wa mbali si hoja kwa walio mbali" ndio andiko ambalo lazima tusalim amri kwa hilo; na je "Umbali huu uwe kiasi gani," huu ndio uwanja wa ijtihadi. Sasa mas-ala ya ulazima wa kutokuuzingatia muandamo wa mji mmoja katika mji mwengine kwa kutafautika matalai, ambayo anayazungumzia Al-imamu Al-shaukaniy, ni mas-ala ya ijtihadi. Hakuna ulazima wa kuwa watu wazingatie ijtihadi hio, wanaweza wakashikana na ijtihadi hio na wanaweza kupitisha ijtihadi nyengine. Lakini kilicho lazima na ambacho tunatakiwa tukubaliane ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali.
Pili : ni dai la Al-imamu Al-shaukaniy kwamba Sham na Madina hakuna umbali ambao kwawo inawezekana kupatikana tafauti za matalai. Lakini akajibiwa na Sheikh Al-khaliliy kwamba masafa yaliopo baina ya Sham na Madina ni zaidi ya meli 500 na katika mikutano iliofanyika kwa ajili ya kulitafiti suala hili la muandamo wa mwezi, na ambayo ilihudhuriwa na wataalamu wa falaki, basi ramani zilichorwa na kubainishwa kwamba masafa ambayo inawezekana mwezi kuonekana sehemu moja na kutokuonekana sehemu ya pili, ni masafa ya meli 500 baina ya sehemu mbili hizo. Kwa hivyo, dai la Al-imamu Al-shaukaniy kwamba Madina na Sham hakuna umbali ambao kwawo inawezekana kupatikana tafauti za matalai, si dai sahihi, kwani baina ya miji miwili hio ni zaidi ya meli 500, na meli 500 zinatosha kusababisha tafauti ya matalai kama wataalamu wa falaki walivyosema.
UPINZANI WA TATU
"Lau tutakubali kutokuwepo ulazima wa kuifungamanisha (Hadithi hio ya Ibn Abbas) na akili, basi (mtu) mwenye elimu (yake) hatii shaka kwamba dalili (ushahidi) zinahukumu kwamba watu wa miji (tafauti) huwa wanazitendea kazi habari na ushahidi wake wanaopeana katika hukumu zote za Kisharia. Na kuonekana kwa (mwezi) ni miongoni mwake." Mwisho wa kunukuu.
JAWABU
ni kuwa hakuna upinzani kwamba watu wa nchi moja watendee kazi ushahidi unaotolewa na watu wa nchi nyengine, ikiwa yatakamilika masharti yake. Lakini tunakubaliana kwamba hio ni hukumu ya ujumla, na kwamba ujumla kinapopatikana kitu cha kuuhusisha basi chenye kuhusisha ndio kinachotangulizwa. Kwa hivyo, kanuni inasema kwamba Hadithi ya Ibn Abbas imeuhusisha ujumla wa kuutendea kazi kila ushahidi unaotolewa na watu wa nchi moja kuwapa nchi nyengine. Na natija ni kuwa ushahidi wote unaotolewa na watu wa nchi moja kuwapa watu wa nchi nyengine - ikiwa umekamilisha masharti yake - basi utendewe kazi isipokuwa ushahidi wa kuonekana mwezi. Kwani ushahidi huu umehusishwa na riwaya hio, na kanuni ni kuwa:
"Andiko la ujumla linakwenda katika ujumla wake mpaka lipatikane andiko lenye kuhusisha." Kwa hivyo, ujumla wa kuutendea kazi kila ushahidi au kila habari, umehusishwa katika ushahi di au habari ya kuandama kwa mwezi, kwani hii ni khaas (specific) na ile ni Aam (general).
Pili : - kama alivyojibu Sheikh Al-khaliliy - ni kuwa Ibn Abbas hakumwambia Kuraib kwamba nina wasi wasi na habari yako ulionipa, bali kamwambia: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w." Kwa hivyo, Ibn Abbas hakukataa kuutendea kazi ushahidi unaotolewa na watu wa mji mwengine, lakini kabainisha kwamba ushahidi huo haulihusu suala la kuandama kwa mwezi.
UPINZANI WA NNE
"Na ni sawa sawa, ikiwa baina ya miji miwili kuna umbali ambao kwawo kuna tafauti ya matalai au hakuna, basi kuhusisha (baadhi ya sehemu) haikubaliki ila kwa dalili (ushahidi)." Mwisho wa kunukuu. Jawabu ni kuwa ushahidi wenye kuhusisha sehemu moja pasi na nyengine ni Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbas, ambapo aliukataa muandamo wa Sham. Na akasema kwamba hivi ndivyo Mtume(s.a.w.w) alivyoamuru.
UPINZANI WA TANO
"Hata tukikubali kwamba Hadithi hii ya Kuraib inafaa kuihusisha (sehemu fulani pasi na nyengine), basi inatakiwa iishie katika sehemu ya andiko tu, ikiwa andiko linajulikana au katika kinachofahamika kutokana na hio (Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbas) ikiwa (andiko) halijulikani, kwa sababu ya kuja kwake (Hadithi hio ya Ibn Abbas na Kuraib) kinyume na Qiyas (Analogy)." Mwisho wa kunukuu. Anachokisema Sheikh Al-shaukaniy hapa, ni kuwa Hadithi hio ya Kuraib ni kinyume na Qiyas, na kitu ambacho kiko kinyume na Qiyas basi huwa kitu chengine hakipimwi juu ya kitu hicho, kama kanuni inavyosema: "Kila ambacho hukumu yake imethibiti kinyume na Qiyas basi kitu chengine ha kipimwi (hakilinganishwi na kupewa hukumu moja) na kitu hicho." Kwa ufafanuzi zaidi, ni kuwa maelezo ya Sheikh Al-shaukaniy ni kuwa Hadithi hio ya Kuraib na Ibn Abbas ni kinyume na Qiyas, kwa hivyo hata kama itafaa kuuhusisha ujumla uliomo katika Hadithi inayosema: "Fungeni kwa kuuona," basi uhusisho huo wa Hadithi hio ya Kuraib na Ibn Abbas uishie Madina na Sham, yaani itendewe kazi na watu wa Sham na watu wa Madina tu: si watu wa miji myengine kwani ni kinyume na Qiyas na kanuni - kama tulivyosema - ni kuwa: "Kila kilicho tafauti na Qiyas basi kitu chengine hakipimwi (hakilinganishwi na kupewa hukumu moja) na kitu hicho." Kwa hivyo, watu wa nchi nyengine hukumu hii haiwahusu!!!
Nasi tunajibu kwamba kanuni inayosema: "Kila kilicho tafauti na Qiyas basi kitu chengine hakipimwi (hakilinganishwi na kupewa hukumu moja) na kitu hicho" hapa si mahala pake, kwani Sham na Madina katika hukumu hio hazikutoka nje ya Sunanu Al-qiyas (njia za kufanya Qiyas). Na kwa hivyo, kuzikisia nchi nyengine kwa kuzipa hukumu sawa na hukumu hio ya Madina na Sham, ni Qiyas sahihi kabisa. Ama kusema kwamba kwa hukumu hio, Sham na Madina hazikutoka nje ya Sunanu Al-qiyas (njia za kufanya Qiyas), ni kutazama ukweli kwamba jua - kwa mfano - likitua Sham, watu wa Madina hawasali magharibi wala hawafuturu; jua likitenguka upende mmoja katika nchi mbili hizo, watu wa upande wa pili hawasali; alfajiri ikichomoza upande mmoja watu wa upande wa pili hawalazimiki kusali wala kuanza kufunga mpaka na kwao alfajiri ichomoze. Sasa vipi atasema Sheikh Al-shaukaniy kwamba hukumu ya kutozingatiwa muandamo wa Sham huko Madina ni kinyume na Qiyas (Analogy)? Bali hukumu hio imo katika Sunanu Al-qiyas (njia za kufanya Qiyas), na kwa hivyo kuikisia miji myengine kwa kuipa hukumu sawa na hukumu ya Madina na Sham ni Qiyas sahihi kabisa, kwani Miji Shina, nayo ni Sham na Madina, haikutoka katika Sunanu Al-qiyas (njia za kufanya Qiyas).
Ama njia ya kuiingiza miji myengine katika hukumu hio, ni kutazama kwamba illa (sababu) ziko za namna mbili kuu: Moja: ni "Sababu ilioelezwa kwa uwazi."
Pili : ni "Sababu ya kutolewa katika maandiko (yaani ambayo haikuelezwa kwa uwazi)." Sasa njia moja ya kujua "Sababu ya kutolewa katika maa ndiko (yaani ambayo haikuelezwa kwa uwazi), ni ile wanayoita: (Kupima na kugawa). Njia hio imeitwa hivyo kwa sababu mwenye kufanya Qiyas kwa kutumia njia hio, huwa anazikusanya sifa tafauti, kisha anatazama ipi inafaa kuwa illa (sa babu) ya hukumu. Njia hii pia huitwa (Kusafisha vyenye kufungamanishiwa). Vyenye kufungamanishiwa ndio illa (sababu) zenyewe.
Sasa njia ya illa (sababu) hapa ni njia hii ya (Kupima na kugawa). Nayo ni kutaza ma kwamba Ibn Abbas alipokataa kuufata muandamo wa Sham na kusema "Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume s.a.w.," ni kuwa Mtume (s.a.w.) atakuwa kawaamrisha hivyo kwa illa (sababu) moja katika mbili: hakuna zaidi: Moja ni kuwa: iwe hivyo ndivyo walivyoamrishwa na Mtume (s.a.w.) kutokuuchukua mwezi wa Sham, kwa sababu huko ni Sham. Kwa hivyo, Sham iwe ndio illa (sababu) ya kutokuuzingatia muandamo. Hii inamaanisha kwamba lau Kuraib alikuwa anatoka Misri au Pemba wangeukubali muandamo huo. Illa (sababu) hii ni dhaifu, haifai kuifanya kuwa ndio illa (sababu) ya hukumu hio ya Mtume (s.a.w.) iliomo katika Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbas. Kwani:
a) Ni (It is an intrasitive cause as opposed to a transitive one). Yaani ni sababu ambayo haivuuki mahala pake, nayo inapingwa na sababu nyengine yenye kuvuuka mahala pake.
b) Ni "Kulifanya jina kuwa ndio sababu." Na inavyotakiwa sifa iwe ndio sababu: sio jina. Naam! Jina linaweza wakati mwengine ku fanywa illa (sababu) ikiwa lina maana ya sifa. Katika jina "Sham" maana hii haipo. Pili ni kuwa: iwe Mtume(s.a.w.w) kawaamrisha hivyo kwa sababu Sham ni mbali. Illa (sababu) hii, ni sahihi na imekamilisha masharti ya utoaji wa illa (sababu).
Kwa hivyo, natija ni kuwa Mtume(s.a.w.w) kawaamrisha hivyo kwa sababu Sham ni mbali, sio kwa Sababu kule ni Sham. Baada ya haya tazama maelekezo katika jaduweli inayofata: Al-aslu ( Shina), ni mji wa Madina na mji wa Sham. Al-far'u (T awi) ni miji myengine ya dunia. Al-illah (sababu) ni kuwa mbali mbali. Al-hukmu (hukumu) ni wajibu wa kutokuzingatiwa muandamo wa mji mmoja katika mji wa pili. Kwa hivyo, tunasema kwamba hiki ni Qiyas sahihi, hakina vumbi, na kimetimiz a masharti yake yote. Na hii inabomowa dhana ya Sheikh Bachoo aliposema maneno yafuatayo:
"Kwa hapa: 1) Asili (shina) ni ijtihad ya Ibn Abbas.
2) Hukumu ya Asili: watu wa madina hawakuukubali mwezi ulioonekana Sham.
3) Illa: haipo.
4) Tawi linalozalika halipo." Mwisho wa kunukuu.
Hivyo ndivyo alivyosema, nalo ni jambo la kusikitisha, kwani - kwanza - hivyo alivyopanga Sheikh Nassor Bachoo vyote sivyo (ni wrong). Asili (shina) si ijtihadi ya Ibn Abbas, bali ni ile miji miwili (Madina na Sham) ambako muandamo wa upande mmoja haukuzingatiwa upande wa pili. Tena hii kuita ijtihadi ni kosa la kielimu, kwani Ibn Abbas kasema "Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) "Tumesema zaidi ya mara moja kwamba sigha (form au namna) hii ya maneno inaifanya Hadithi kuwa marfu'u (yaani kuwa ni Hadithi yenye kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) mwenyewe kama fani zinavyoeleza). Al-illa (sababu): Sheikh Nassor Bachoo anasema: "Haipo." Natarajia ujuzi zaidi wa fani ya usuli unahitajika, kwani illa (sababu) ipo kama tulivyobainisha. Lakini labda Sheikh anadhania kuwa illa (sababu) zote ni "Sababu zinazoelezwa kwa uwazi." Bali Al-ilal (Sababu) - kwa mujibu wa usuli - zinakuwa hizo na zinakuwa: "Sababu z a kutolewa katika maandiko (yaani ambazo hazikuelezwa kwa uwazi)." Na njia zake za kuzijua ni nyingi, moja ni hio tulioitumia hapa nayo ni (Kuzikusanya sifa zinazoelekea kuwa illa (sababu) halafu kuzipima na kuchukua iliokuwa sahih i).
Kuhusu Al-far'u (Tawi), Sheikh anasema: "Tawi linalozalika halipo." Inaonesha Sheikh tawi kalitaja tu bila kulifahamu. Tawi ni nchi nyengine au miji myengine ukiitoa Madina na Sham ambayo ndio miji shina, yaani miji ya asili. Kuhusu Al-hukmu (Hukumu), Sheikh anasema: "Hukumu ya Asili: watu wa Madina hawakuukubali mwezi ulioonekana Sham." Nayo pia si maneno madhubuti, bali hukumu ya asili ni wajibu unaopatikana kutoka katika amri ya Mtume (s.a.w.) ya kuamrisha kutokuufata muandamo wa mbali. Tunakariri kwamba Ibn Abbas - baada ya kuukataa muandamo huo - kasema: "Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume." Kwa hivyo, kuyaita maneno haya kuwa ni maneno ya watu wa Madina ni kinyume na Mustalahu Al-hadith (Elimu ya Hadithi).
UPINZANI WA SITA
Anasema Al-imamu Al-shaukaniy - akiendelea kutoa upinzani wake juu ya hoja ya kutokuzingatia muandamo wa mbali kwa kutegemea riwaya ya Ibn Abbas - :
"Hata tukikubali usahihi wa kufanya Qiyas, na kuuhushisha ujumla kwayo (kwa riwaya ya Ibn Abbas) basi kipeo chake ni kuwa iwe katika mwahala ambamo umbali baina yake, ni (sawa na umbali) wa Madina na Sham au zaidi." Mwisho wa kunukuu. Katika kitabu chake, Sheikh Bachoo kaongezea upinzani huo kwa kusema: "Jambo la kushangaza hapa, mbona hapatumiwi masafa kama haya? Tena hapafuatwi hata mwezi ulioonekana katika nchi jirani au iliyo na masafa punguzu ya haya. Je hoja hapa bado itakuwa ni kisa cha Kurayb na Ibn Abbas (r.a.)?
Huo ndio upinzani wa sita na wa mwisho, nao ndio upinzani dhaifu kuliko wote, kwani umejengeka katika "MAFHUMU AL-LLAQAB," nayo ni batili - taqriban - kwa makubaliano ya Umma mzima. "MAFHUMU AL-LLAQAB" - kama tulivyoeleza katika kitabu chetu "MEZANI YA HAKI - ni kama mtu kusema: "Muhammad ni Mjumbe wa Mungu." Mwengine akasema "Basi Mussa si Mjumbe wa Mungu!" Huyu wa pili kajenga hoja yake kwa kutumia "MAFHUMU AL-LLAQAB," nalo ni kosa kwani kusemwa kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allah, haimaanishi kwamba hakuna Wajumbe wengine. Sasa msingi huu ndio ambao hoja ya Al-shaukaniy imesimama juu yake: iliposemwa kwamba umbali wa Sham na Madina ndio illa (sababu) ya kuzingatia tafauti za miandamo, yeye akasema: "Basi kama katika miji hakuna umbali wa Sham na Madina miandamo tafauti isizingatiwe!"
Sasa tahariri ni kuwa, tumefahamu kwamba illa (sababu) ya kutokuuzingatia muandamo wa Sham, ni umbali: umbali ndio illa (sababu). Sasa je umbali huu uwe masafa gani? Hapa hakuna andiko, kwa hivyo hapa ndio mahala pa ijtihad: ama muandamo wa mbali kutozingatiwa mbali, hili limethibiti kwa Hadithi, kwa hivyo si suala la ijtihadi: ijtihadi iwe katika umbali gani. Hapa wanavyuoni watatoa rai zao, na sisi tutatazama iliokuwa munasib zaidi au iliokuwa na nguvu zaidi.
UPINZANI WA SH. NASSOR BACHOO KWA HADITHI YA KURAIB NA IBN ABBAS
UPINZANI WA KWANZA
Katika maelezo yake, Sheikh Nassor Bachoo aliifasiri na kuielezea Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbas kama ifuatavyo: "Kwanini Kurayb alimuuliza Ibnu Abbas (r.a.): "Je hutosheki na kuona (mwezi) kwa Muawiya na kufunga kwake?" Bila Shaka suali hili linaonesha kuwa lilikuwa ni jambo linaloeleweka kuwa: mwezi ukionekana pahala mbali - Waislamu wa sehemu nyengine watosheke na habari watakazopewa ikiwa zitakuja kwa njia ya kuaminika. Inaelekea kuwa hivyo, ndivyo walivyofahamu watu kama Kurayb ndio maana akamuuliza Ibnu Abbas ili apate uhakika." Mwisho wa kunukuu.
Kwa ufupi ni kuwa, huo alioutaja Sheikh Bachoo ni uwezekano (ihtimal), mmoja. Na inawezekana ikawa Kuraib aliuliza hivyo kwa sababu hakupata kuisikia Hadithi alioitolea Hoja Ibn Abbas. Kwa hivyo jambo hilo linawezekana kuwa hivi na linawezekana kuwa hivi, na kwa hivyo - kama kanuni inavyo sema: "Dalili ikiwa na maana nyingi basi ushahidi wake huporomoka." Kwa hivyo, uwezekano huo alioutoa Sheikh hauwashi wal a hauzimi katika suala hili. Na wala hili la kuisikia Hadithi baadhi ya Masahaba - wachilia mbali Kuraib ambaye ni mfuasi wa Sahaba - pasi na kuisikia wengine si jambo geni. Mifano ni mingi sana juu ya suala hili. Tosheka na ukweli kwamba Abu Bakr (r.a.) na Umar (r.a.) walikuwa wakitaka kutoa hukumu ya kitu nao hawakumbuki Hadithi juu ya suala hilo wanalotaka kulihukumu, basi kwanza huuliza kama yuko aliyehifadhi Hadithi juu ya jambo hilo. Akiwepo basi wanaitumia katika hukumu hio.
Pili : ni kama tulivyosema kwamba, huo alioutoa Sheikh Nassor Bachoo ni uwezekano, lakini Ibn Abbas amesema kwa mkato kwamba: "Hivi ndivyo Mtume s.a.w. alivyotuamrisha." Kwa hivyo, hakuna mazingatio kwa uwezekano huo mbele ya andiko.
UPINZANI WA PILI
Anaendelea Sheikh Nassor Bachoo kuichambua riwaya hio kwa kusema: "Naye Ibnu Abbas (r.a.) akamjibu (Kuraib) kuwa ametosheka, kwani namna hivyo - yaani kuamini habari za mbali juu ya suala la mwezi - ndivyo alivyoamrisha Mtume(s.a.w.w) ."!!!! Mwisho wa kunukuu.
JAWABU
ni kuwa: hii ni ajabu katika ajabu za dunia! Na huku ni kubadilisha maana ya Hadithi ambako wanavyuoni wakubwa wenye kujua lugha ya Kiarabu na fani za tafsiri hawakukusema. Ibn Hajar - alipokuwa akizungumzia mas-ala haya - kaiashiria Hadithi hio ya Kuraib kwa kusema: "Na katika Sahihu Muslim kiko chenye kutoa ushahidi huo (wa kwamba kila watu na muandamo wao). Kwa ufupi ni kuwa Hadithi inasema:
Wau ni wau al-atfi na asil i yake - herufi hio - ilikuwa ikae mwanzo, lakini ilipokuja Hamzat Al-istifham, (Hamza ya kuulizia), ilibidi hamza ikae mwanzo kwani herufi za kuulizia kwa kawaida hukaa mwanzo. Kwa hivyo tafsiri sahihi ya maneno haya ni:
"Wala hutosheki na Muawiya kuuona (mwezi) na kufunga kwake?" Ibn Abbas akajibu (sio). Watu wa Nahau wanajua kwamba jawabu namna hii ikitolewa huwa kuna kitu kimeondoshwa; na kilichotajwa kabla huwa ndio kinakifasiri kile kilichoondoshwa na kutotajwa, na kina kibainisha ni kitu gani hicho kilichoondoshwa. Yaani jumla (sentensi) huondoshwa kwa ulazima au kwa kujuzu ikiwa inafahamika katika Qarina (context). Kwa hivyo, makadirio ya jawabu ya Ibn Abbas ni sentensi ile ile alioitumia Kurai b kumuuliza Ibn Abbas kwayo, na kwa hivyo maana ni:
"Je hutosheki?"
JAWABU
(si) yaani "si-tosheki Sentensi (kutosheka) imeondoshwa na inabainishwa na ile ilio kabla yake, na ni lazima pakae kabla ya sentensi hio, herufi (si) ili maana iwe (si-tosheki)."
Neno "Si" hapa ndilo lililotajwa, na neno "Tosheki" ndilo lililoondoshwa katika jawabu ya Ibn Abbas. Baada ya makadirio ya neno hilo, maana inakuwa: "Si-tosheki."
Herufi "laa" hapa imefasirika hivyo kwa maana ya (si), kwa sababu ni herufi iliokuja baada ya jumla (sentensi) iliondoshwa, ambayo ni lazima iunganishwe na sentensi hio ilioondoshwa - na ambayo inafahamika katika qarina (context) - ili maana iwe sawa. Sasa ukitazama Qarina (context) hapa huwezi kuyafasiri maneno ya Ibn Abbas kwa tafsiri hio ya Sh. Bachoo, kwani Qarina (context) katika maneno yaliotangulia inaonesha kwamba Ibn Abbas alikataa kuufata muandamo wa Sham.
Na hii ni kwa sababu yeye Ibn Abbas alisema: "Hatuachi kufunga mpaka tukamilishe idadi ya siku thalathini au tuuone mwezi." Sasa kama aliukubali muandamo wa Sham, basi asingelisema maneno hayo, kwani kwa hali yoyote ile ikifika siku ya mwezi 29 ya muandamo wa Madina ni lazima watu wa Madina wale idi siku ya pili, ((halafu ikiwa itawathibitikia kwamba Sham mwezi uliandama tarehe thalathini wao watu wa Madina wailipe siku moja)) kwani siku hio ya mwezi 29 wa Madina ni lazima Sham itakuwa ni siku ya tarehe 30 au tarehe mosi. Ikiwa ni tarehe 30 itakuwa Sham wamefunga siku 30, wakati Madina wamefunga siku 29, na Ikiwa Sham ni tarehe mosi siku hio, basi watakuwa wamo ndani ya siku kuu - kwa hali zote mbili, kama Ibn Abbas aliukubali muandamo wa Sham, basi ni lazima watu wa Madina waishie kufunga tarehe 29.
Lakini tunamkuta Ibn Abbas anasema "Hatuachi kufunga mpaka tutimize (siku) thalathini au tuuone mwezi." Kusema "Mpaka tutimize (siku) thalathini" kunabomowa dhana hio ya Sheikh Bachoo, kwani maana ya maneno hayo ni kuwa mwezi wa Sham hakuukubali, kwani thalathini ya Madina ni thalathini na moja ya Sham - kwa mujibu wa miandamo miwili hio - na hakuna mwezi wa siku thalathini na moja kama Hadithi zilivyobainisha. Kwa hivyo, tafsiri hio ya Sheikh Nassor Bachoo haina msingi madhubuti.
Na sijui ni nani katika wanavyuoni wakubwa wenye fani za tafsiri na lugha ya Kiarabu aliyefasiri hivyo? Kama yupo basi jawabu yetu kwake ni hio. Hata Al-shaukaniy, ambaye ana rai kama hio ya Sheikh Bachoo, basi kubwa alilolisema ni kuwa hio ni ijtihadi ya Ibn Abbas, wala hakusema kwamba Ibn Abbas hapa kakubali kuufata muandamo wa Sham, bali maelezo yake yote ni jawabu yenye kuonesha kwamba Ibn Abbas hakuukubali mwezi wa Sham. Al-tirmidhiy naye alipoisimulia riwaya hio alisema: "Mlango wa tisa: kilichokuja kwamba kila mji una uoni wao (wa mwezi muandamo)." Kisha akasema: "Hadithi hii ni hasan sahihi gharib, na kinachotendewa kazi na watu wa elimu ni Hadithi hii, kwamba kila watu wa mji wana uoni wao."
Na Anasema Ibn Khuzaima: "Mlango wa dalili (ushahidi) kwamba kilichowajibu juu ya watu wa kila mji ni kufunga Ramadhani kwa uoni wao (wenyewe wa muandamo) si uoni wa wenzao." Na Al-nnawawi katika Sherehe yake kasema: "Mlango (kuhusu) ubainifu kwamba kila mji una muandamo wake na kwamba wao wakiuona mwezi muandamo katika mji, haithibiti hukumu yake kwa walio baada (yao) kutoka kwao.".
Hivi ndivyo wanavyuoni walivyoifahamu riwaya hio, tafauti ni katika kuifasiri tu, Al-shaukaniy akadai kuwa hio ni ijtihadi, nalo ni kosa kama tulivyobainisha.
UPINZANI WA TATU
Anaendelea Sheikh Bachoo na uchambuzi wake wa riwaya hio, anasema: "Pili kama ingalikuwa hakuna dhana ya kuwa mwezi ukionekana popote watu wafunge, Ibnu Abbas (r.a.) asingekuwa na haja ya kumuuuliza Kurayb juu ya habari za mwezi wa Sham kwa kusema: "Kisha (Ibn Abbas) akataja (habari) ya mwezi na akasema: "Ni lini mliuona mwezi?...akasema: "Wewe um euona?"
Hio ndio hoja nyengine ya Sheikh Bachoo, kwamba lau hakuna dhana ya kuwa mwezi ukionekana popote watu wafunge, basi Ibn Abbas asingekuwa na haja ya kumuuliza Kuraib "Lini mumeuona mwezi!!!" Ninasema: Enyi walimwengu wenzangu tazameni hoja za kielimu hizo!!!!!!! Kwani nyinyi Wazanzibari kabla ya kuja fikra hio ya Sheikh Nassor Bachoo ya kufunga kwa muandamo mmoja, mulikuwa hamuwaulizi watu wanaotoka nchi nyengine masuala kama hayo wanapokuja kwenu na nyinyi muko kati kati ya mwezi pamoja na kwamba nyote zamani mukifata muandamo wenu? Sasa kama nyinyi mulikuwa mukiuliza suala hilo hilo kwanini Ibn Abbas na yeye asiulize hata kama dhana hio haipo? Mimi binafsi nina kawaida ya kuwauliza wageni walioko nchi hii ninayoishi suala hilo, na natarajia kwamba pia nimewasikia watu wengi wenye kuwauliza wageni suala hilo. Kwa hakika shubuhati kama hizi hazifai katika kujadili mambo ya kielimu. Kwa ufupi ni kuwa hata kama dhana hio ilikuwepo, dhana hio inabomolewa na kukataa kwake - Ibn Abbas - kuukubali mwezi wa Sham, na kujenga hoja kwa Hadith marfu'u kwamba hayo ndio mafunzo ya Mtume (s.a.w.) kwao.
Bali tunasema kwamba suala la Kuraib aliposema: "Je hutosheki kwa kuuona Muawiya na kufunga kwake" inawezekana ikawa na maana kinyume kabisa na fikra ya Sheikh Nassor, kwani inaweza ikawa ndio hasa inayomaanisha kwamba watu enzi hizo walikuwa hawazingatii muandamo wa mbali, au ikawa jambo hilo lilikuwa halijulikani kamwe, kwa sababu lau ingelikuwa Mtume(s.a.w.w) kafundisha kutendewa kazi muandamo wa mbali au ingelikuwa katika enzi hizo wanazingatia muandamo mmoja tu basi Kuraib asingelikuwa na haja ya kumuuliza Ibn Abbas suali hilo, bali angelimwambia: "Lipeni siku moja iliokupiteni ya muandamo wa Sham." Kwa hivyo, kumuuliza kwake suali hilo ni dalili ya wazi kwamba hakukuwa na dhana ilioenea kuwa mwezi ukionekana popote watu wafunge. Na kwa hivyo, Kuraib alikuwa hajui kamwe nini hukumu ya tokeo hilo.
UPINZANI WA NNE
Upinzani wa nne - ninafupisha - unaeleza kwamba riwaya ya Kuraib inasema kwamba yeye alikuja Madina mwishoni kwa mwezi. "Mwishoni kwa mwezi" inawezekana ikawa ni tarehe 26-27-28-29, au ikawa ni tarehe 30.
Sasa tuchukulie ni moja katika tarehe za mwanzo (26-27-28-29), hii ina maana kwamba mwezi ulikuwa bado unaendelea: bado haujakwisha. Kwa hivyo Ibn Abbas aliposema kwamba "Hatuachi kufunga mpaka tutimize siku thalathini au tuuone mwezi" ni sawa kwa sababu Mtume (s.a.w.) ndivyo alivyofundisha kwamba tusifunge mpaka tuuone mwezi na tusifungue mpaka tuuone mwezi, na mwezi Madina ulikuwa haujaonekana.
Hio ndio hoja yake - kwa kujaalia kwamba Kuraib karejea Madina tarehe 26 au 27 au 28 na 29. Lakini kama unavyoona kwamba upinzani huu unajibiwa na majibu tuliotoa katika sehemu zilizotangulia. Tumesema kwamba kipengele kinachosema: "Mpaka tutimize siku thalathini" kinabomowa hoja hii. Na hii ni kwa sababu kutimiza siku thalathini kwa watu wa Madina, ni kutimiza siku thalathini na moja kwa watu wa Sham. Na kwa vile hakuna mwezi wa siku thalathini na moja, basi Ibn Abbas alikuwa hana haja ya kutimiza siku thalathini huko Madina, kwani ikifika ishirini na tisa Madina, Sham hakika ni mwezi thalathini au ni mwezi mosi, lazima kwa hali yoyote watu wa Madina waishie kufunga siku ya tarehe ishirini na tisa kama Ibn Abbas aliukubali mwezi wa Sham. Lakini kusema kwamba "Mpaka tutimize siku thalathini" ni andiko la wazi juu ya maudhui hii kwamba muandamo wa Sham Ibn Abbas hakuukubali.
UPINZANI WA TANO
Upinzani wa tano na wa mwisho wa Sheikh Nassor Bachoo, ni kuwa tukijaalia kwamba Kuraib kafika Madina tarehe 30, basi Ibn Abbas alikuwa na sababu madhubuti ya kuukataa ushahidi wake kwani utakuwa ni ushahidi uliotolewa na mtu mmoja, na ushahidi wa mtu mmoja haukubaliki katika mwezi muandamo wa Shawaal (mfunguo mosi).
Hapa ukitazama upinzani wa Sheikh Nassor aliotangulia kuutoa huko nyuma, utaona kuna kitu mgongano baina ya maneno yake ya awali na maneno yake katika sehemu hii. Katika sehemu ziliotangulia upinzani wa Sheikh unasema kwamba Ibn Abbas aliukubali ushahidi uliotolewa na Kuraib, wakati hapa Sheikh anajenga hoja yake kwamba Ibn Abbas hakuukubali ushahidi uliotolewa na Kuraib!!!
Kwa ufupi ni kuwa - tukijaalia kuwa upinzani hapa ni huo basi - jawabu ni kuwa Ibn Abbas hakuukataa Muandamo wa mwezi wa Shawwal (mfunguo mosi): bali alioukataa ni mwezi muandamo wa Ramadhani uliothibiti huko Sham. Na mwezi muandamo wa Ramadhani hauhitaji mashahidi wawili, bali shahidi mmoja anatosha kama tulivyotangulia kueleza katika sura ya kwanza. Sasa cha kufanya - kama Ibn Abbas aliukubali mwezi huo - ilikuwa ikifika mwezi ishirini na tisa, basi lazima iwe ni siku yake ya mwisho ya kufunga, kwani Sham itakuwa hakika mwezi wa Ramadhani umekwisha siku hio, na kufunga siku ya Siku Kuu haijuzu. Badae watu wa Madina watatafuta habari, ikiwafikia kwamba Sham walifunga siku 30, basi watu wa Madina wailipe siku moja yao. Lakini tunamuona Ibn Abbas anatumia lugha yenye kuonesha kwamba hakuukubali muandamo wa Ramadhani (si wa M/mosi) uliothibiti Sham na akasema: "Hatuachi kufunga mpaka tutimize siku thalathini au tuuone mwezi."
Na vipi mtu aseme kwamba Kuraib tukijaalia kuwa kafika Madina mwezi 30, basi Ibn Abbas hakuukubali ushahidi wake kwa sababu ni ushahidi wa mtu mmoja na ushahidi wa mtu mmoja haukubaliki katika kuthibitisha muandamo wa mfunguo mosi? Vipi mtu aseme hivyo? Kwani Kuraib kauona wapi na kauona lini mwezi huo muandamo wa mfunguo mosi hata afike Madina mwezi 30 Ramadhani na kutoa habari ya muandamo huo? Je inaingia akilini kwa zama hizo kwamba Kuraib kaondoka Sham baada ya kuushuhudia mwezi muandamo wa mfunguo mosi kisha akafika Madina mwezi 30 Ramadhani wakati mapishano yao ya muandamo ni siku moja tu? Kwa hivyo, habari ya Kuraib ilikuwa ni ya muandamo wa Ramadhani kama Hadithi yenyewe inavyosema: "Ukaniandamia mwezi wa Ramadhani nami niko Sham." Na muandamo wa Ramadhani ni muandamo ambao unathibiti kwa mtu mmoja.
Pili : Ina maana gani kauli ya Ibn Abbas aliposema kwamba hatutaacha kufunga mpaka tuuone mwezi au tutimize siku thalathini, ikiwa Ibn Abbas kaendewa na Kuraib katika siku ya mwezi 30? Jawabu hii ya mwisho, inaufanya upinzani mzima wa Sheikh Bachoo kuwa hauna maana yoyote. Mwisho wa kunukuu nilioyaeleza kuhusu Hadithi hio ya Kuraib na Ibn Abbaas.
9
MUANDAMO WA MWEZI
JAWABU NILILOJIBIWA
Ndugu zangu wakanijibu hivi:
10. Masimulizi Ya Kuraib Kama kawaida yake, Ndugu Juma ametoa dhana yake binafsi kwamba si lazima mwezi ukithibiti kuandama sehemu moja uwe umethibiti sehemu nyengine, na kwamba kwa mawazo yake ni lazima tusalim amri kwa hilo, yaani yeye anataka kila nchi ifunge kwa muandamo wake. Kwani aonavyo yeye katika jambo hilo kuna andiko. Hilo andiko je alinukuu? Alilolichukua yeye ni katika kisa cha Ibnu ''Abbas na Kuraib.[4]
JAWABU
Jamani! Nyinyi hamuoni haya kusema mambo ovyo ovyo?! Hivyo hii pia munaita rai yangu binafsi. Ivo mimi ndiye wa mwanzo kusema kuwa kila pahala na muandamo wao? Mimi ndiye wa mwanzo kuitumia Hadithi hii katika kuthibitisha hayo? Tena bado munaendelea kufanya makosa ya kifani kwa kudai kwenu: "Kwani aonavyo yeye katika jambo hilo kuna andiko. Hilo andiko je alinukuu? Alilolichukua yeye ni katika kisa cha Ibnu ''Abbas na Kuraib". Nakukumbusheni maneno yenu mazuri sahihi muliposema: "Isipokuwa Sahaba akisema: "Tumeamrishwa kadha" au "Tumekatazwa kadha." Jambo hilo hupewa hukumu ya "Rafii", yaani hio inazingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume (s.a.w.). Sasa bado munakana kuwa hilo si andiko, haya hizi ndio fani zenu mulizosoma?!
Munasema Sisi tunamfahamisha mambo yafuatayo kwamba:
1. Hakuna andiko Takatifu zaidi ya Qur-aan Tukufu, lakini bado Wanavyuoni wakubwa wametofautiana katika baadhi ya tafsiri za Aya nyingi pamoja na Hadiyth sahihi.
2. Maswahaba pia walitofautiana katika kufahamu tafsiri za Aya za Qur-aan na Hadiyth. (Angalia tafsiri ya Shaykh Ahmed Al-Khaliil J. 1)
3. Kama Wanavyuoni waliopita wangekuwa na msimamo kama wa ndugu Juma kwamba katika kisa cha Kuraib kuna andiko, basi kungekuwa hakuna mjadala. Kama ilivyo katika nyakati za Swala hazina tofauti kubwa, kila eneo linaswali kwa mitenguko yake ya jua.
4. Kama kisa chenyewe ni andiko, mbona ndugu Juma anatoa mawazo kwamba suala la umbali gani ndio linatakiwa Ijtihadi? Sasa tunakujibu kwamba hapa ndipo penye mjadala wote wa mwezi, maana mpaka leo hii hapakupatikana makubaliano ya kweli ya kisheria, isipokuwa kila eneo linafuata matakwa yake ya kisiasa na kifalme za nchi zao.
JAWABU
Mimi sijasema kuwa kuna andiko takatifu zaidi ya Qur-an. Pia mimi sijakataa kuwepo kwa khilafu katika tafsiri wala katika fiq-hi. Lakini pamoja na hayo, sisemi kuwa hakuna kauli sahihi na dhaifu. Wanavyuoni wote - mukiwemo nyinyi - wanakubali kuwa kauli ziko sahihi na dhaifu. Kwa hivyo, sisi tunadai kuwa kauli yenu ni dhaifu kwani haikujengeka katika fani za kielimu. Ama kauli yenu muliposema: "Kama Wanavyuoni waliopita wangekuwa na msimamo kama wa ndugu Juma kwamba katika kisa cha Kuraib kuna andiko, basi kungekuwa hakuna mjadala. Kama ilivyo katika nyakati za Swala hazina tofauti kubwa, kila eneo linaswali kwa mitenguko yake ya jua" inathibitisha yale tuliosema kwamba humujui munachokisema: watu wannena nasi twanena.
Kwani mumepata wapi nyinyi kwamba pakiwa na andiko watu huwa hawatafautiani. Si ndio nyinyi muliosema katika kifungu (1): "Hakuna andiko Takatifu zaidi ya Qur-aan Tukufu, lakini bado Wanavyuoni wakubwa wametofautiana katika baadhi ya tafsiri za Aya nyingi pamoja na Hadiyth sahihi". Na mukasema katika kifungu (2): "Maswahaba pia walitofautiana katika kufahamu tafsiri za Aya za Qur-aan na Hadiyth. (Angalia tafsiri ya Shaykh Ahmed Al-Khaliil J. 1)". Sasa Qur-ani si andiko kwa sababu wanavyuoni wametafautiana juu ya tafsiri ya baadhi ya Aya zake? Mimi nahisi hoja hio mumeijibu wenyewe. Halafu je Hadithi "Fungeni kwa kuuona" si andiko? Mbona wanavyuoni wamelifahamu tafauti? Ndugu zeu, hoja hamuna: muna vichekesho tu!!!
Pia tazameni kauli yenu: "Kama kisa chenyewe ni andiko, mbona ndugu Juma anatoa mawazo kwamba suala la umbali gani ndio linatakiwa Ijtihadi?". Nami nauliza ili iwe jawabu:
a) Kama Hadithi za Sala ya safari ni andiko, mbona wanatafautiana juu ya umbali gani ndio tusali safari?
b) Kama Hadithi hizo ni andiko mbona wanatafautiana je ni kwa muda wa siku ngapi safari inaendelea?
Enyi walimwengu! Hizi ndio hoja za kielimu tulizoahidiwa?! Hadithi za sala ya safari ni maandiko ya wazi juu ya mashru'iyya ya sala ya safari. Kilichokuwa hakiko wazi sana ni safari inaanza baada ya umbali gani na inadumu siku ngapi. Na kutokuwa wazi katika mas-ala haya, hayavunji asili ya sharia ya sala ya safari na usahihi wa maandiko yake, bali sala ya safari ni andiko la wazi juu ya sharia hio, na vipengele visivyo wazi ndio vinakuwa sehemu za ijtihad. Halkadhalika, ukweli kwamba wapi hadi wapi tufunge pamoja ni suala la ijtihadi, hakuvunji ukweli kwamba muandamo mmoja si hoja kwa dunia nzima.
MNASEMA
Sasa tunakujibu kwamba hapa ndipo penye mjadala wote wa mwezi, maana mpaka leo hii hapakupatikana makubaliano ya kweli ya kisheria, isipokuwa kila eneo linafuata matakwa yake ya kisiasa na kifalme za nchi zao.
JAWABU
Kitabu chenu au cha Sheikh wetu Bachoo, hakikusisitiza nukta hii, bali kinasisitiza usahihi wa kufunga kwa muandamo mmoja duniani. Anasema: Pia jambo la kuzingatia hapa ni kwamba ilivyokuwa mtu huyo alikuwa ni Bedui yaani mtu wa Majangwani, Mtume(s.a.w.w) angeweza kumuuliza anatoka wapi, lakini hakumuuliza kabisa suala hili jambo ambalo linathibitisha kuwa suala la umbali gani wa kuonekana mwezi Mtume(s.a.w.w) hakuwa akilizingatia hata kidogo!!! Mwisho wa kunukuu.
Na anasema: Ni kweli kwamba msimamo wa upande wetu ni kuwa mwezi ukiandama popote pale ulimwenguni watu wafunge. Nami nikamjibu katika kitabu changu hicho, kwamba hilo ni kinyume na Hadithi ya Kuraib, nayo ni Hadithi marfu'u kwa mujibu wa elimu ya Hadithi kama tulivyobainisha. Ama ukweli kwamba "Mpaka leo hii hapakupatikana makubaliano ya kweli ya kisheria, isipokuwa kila eneo linafuata matakwa yake ya kisiasa na kifalme za nchi zao". Narudia - mutanisamehe - kwamba tatizo lenu ni kutokujua mas-ala ya ijtihad na yasio ya ijtihad. Tumesema kwamba umbali gani au wapi hadi wapi watu wafunge pamoja, hili ni suala la ijtihad kwa sababu ya kutokuwepo andiko la wazi, lakini kufunga dunia nzima kwa muandamo mmoja, hili ni kinyume na andiko. Sasa tukirudi katika mas-ala ya ijtihad, ni kuwa mas-ala ya ijtihad si lazima watu waafikiane, bali mwenye kusibu hupata ujira mara mbili atayekosea hupata ujira wa ijtihad yake. Ama andiko, huwezi kulikwepa na kulipiga chenga hii na ile.
MNASEMA
Hapa chini tutaonyesha namna Wanavyuoni wenye kutegemewa ambao hawakukichukua kisa cha Kuraib kama ni hoja ya kwamba kila nchi au kila eneo lifunge au lifungue kwa muandamo wake. Wanavyuoni wamekhitalifiana kwa sababu kisa chenyewe cha Ibnu ''Abbas na Kuraib kina utata, hakikueleweka kwa mtazamo mmoja. Chambilecho alivyosema Shaykh Ahmed Al-Khaliil kwamba: "Hakuna madhehebu iliyosalimika." Habari hizi zimepatikana katika khutba yake iliyorikodiwa katika kanda (audio cassette) alipozungumza Shaykh Ahmed Al-Khaliil kwenye msikiti Istiqama Zanzibar iliyotafsiriwa na Shaykh Munir Sulayman 'Aziiz.
1. Rawdhatun-Nadiyyah: Kilichoandikwa na Shaykh Alqanuji
"Ama hoja ya aliyetegemea Hadiyth ya Kuraib iliyopokelewa na Muslim na wengineo, (hoja hiyo) sio sahihi kwa sababu Ibnu 'Abbas hakuelez a kama Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewakataza kufuata mwandamo wa nchi nyengine." Mwisho wa kunukuu.
JAWABU
Kwanza tungependa mufahamu kwamba katika kitu chenye khilafu, basi hakuna maneno ya mwanachuoni yeyote ambayo yanakuwa ndio hoja. Bali hoja huwa ni Qur-an, Hadithi na kanuni za tafsiri zilizokubalika. Pili: ikiwa kitu kuna mtu hakukifahamu pia haiwi hoja kwa vile wako waliokifahamu. Mara ngapi utakuta katika vitabu kwamba mwanachuoni mkubwa anadai kuwa kitu hiki hakipo au mimi sifahamu kakusudia nini, kisha mwengine akakibainisha kuwa kipo au kina maana gani. Chukua mfano kwamba Al-Mubarrad ni katika vigogo wa lugha ya Kiarabu. Lakini anadai kwamba kusema Lawlaya au lawlaka au laulahu n.k." anasema mf umo huu katika lugha ya Kiarabu haukupokewa kamwe. Wakati Sibawahi na wenziwe wameuthibitisha kuwepo kwa muundo huo kwa beit za Warabu wa kale kama:
Atutmi'u fiina man araq dimaana**Walawlaka lam ya'ar idh liahsabina hasan Na beit kama: Wakam matinin lawlaya tihta kama hawa**Biajramihi min qunnatin niqin munhawi Na beit kama: Awmat bi'aynayha minal h adaji**Lawlaka fid ha l'ami lam ahjuji Al-Mubarrad na ubingwa wake wote wa lugha hakujua kama kuna beit hizi. Mfano mwengine ni wa Al-Imamu Abu Hayyan. Anasema kuhusu beit isemayo: Fala Wallahi la yulfi Unasu n**Fatan hattaka ya Ibn Ziyad
Anasema Abu Hayyan, naye ni Imamu wa lugha na tafsiri,: "Na kumalizikia kwa ghaya katika hattaka sikufahamu; wala sijui kakusudia nini kwa (kusema) 'Hattaka', labda baiti hii ni ya kutunga (fabricated). Lakini aliyetia maelezo Sharhu Ibn 'Aqil kabainisha nini muradi wa kile ambacho Abu Hayyaan hakukifahamu. Kwa hivyo, kutokufahamu kwa Shaykh Alqanuji muradi wa Ibn Abbaas hakujakufanya kuwa Hadithi hio iwe batili, madamu wengine wamefahamu. Cha muhimu ni kuwa waliofahamu wamefahamu nini. Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib inasema:
"Kutoka kwa Kurayb (kasema) kwamba Ummu Al-fadhli bint Al-harith alimtuma Sham (Syria) kwa Muawiya. Akasema: 'Basi nikaenda Sham nikamkidhia haja yake.' Na ukaniindamia (mwezi wa) Ramadhani na mimi niko Sham. Basi nikauona mwezi usiku wa (kuamkia) ijumaa. Kisha nikaja Madina mwishoni mwa mwezi. Basi Abdullahi bin Abbas (r.a.) akaniuliza. Kisha akataja (habari za) mwezi muandamo akasema: 'Lini mumeuona mwezi muandamo?' Nikasema: 'Tumeuona usiku wa (kuamkia) Ijumaa.' Akasema: 'Wewe umeuona?' Nikasema: 'Ndio. Na Watu wameuona na wakafunga na Muawiya akafunga.' Akasema: 'Lakini hakika ya sisi tumeuona usiku wa (kuamkia) Juma Mosi, basi hatuachi kuendelea kufunga mpaka tutimize (siku) thalathini au tuuone.' Nikasema: 'Kwani wewe hutosheki na kuonekana na Muawiya na kufunga kwake?' Akasema: 'Laa' (Sio): Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) ."
Kwa hivyo, Ibn Abbaas kasema "'Lakini hakika ya sisi tumeuona usiku wa (kuamkia) Juma Mosi, basi hatuachi kuendelea kufunga mpaka tutimize (siku) thalathini au tuuone". Ni wazi kwamba mwezi muandamo wa Sham hakuukubali kwani - kama tulivyoeleza katika kitabu - kwamba kutimiza kwa siku 30 kwa watu wa Madina ni kutimiza 31 kwa watu wa Sham, wakati hakuna mwezi wa siku 31. Hakuna ila tuseme kwamba muandamo wa Sham hakuukubali. Akaulizwa na Kuraib: "Kwani wewe hukutosheka na kuonekana kwa mwezi huko Sham" akajibu "Hapana" (Sikutosheka). Kisha akasema kwamba "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) ".
Sasa kama Ibn Abbaas kakataa kuufata muandamo wa Sham kisha akajibu kwamba hivi (ninavyofanya mimi) ndivyo Mtume (s.a.w.) alivyofunza. Vipi mtu atadai kwamba: Ama hoja ya aliyetegemea Hadiyth ya Kuraib iliyopokelewa na Muslim na wengineo, (hoja hiyo) sio sahihi kwa sababu Ibnu 'Abbas hakueleza kama Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewakataza kufuata mwandamo wa nchi nyengine." Sasa Sheikh huyu alitaka Ibn Abbaas aeleze vipi tena zaidi ya hivi, naye kakataa kuufata muandamo huo na akasema kuwa hayo ndio mafunzo ya Mtume(s.a.w.w) kwao? Je hayo yanamaanisha kuwa dunia iwe na muandamo mmoja?! Kwa hivyo, nasi tunasema kuwa maelezo y Shaykh Alqanuji si sahihi, na ibara za Ibn Abbaas ziko wazi kabisa hata kwa mwanafunzi licha ya mwanachuoni.
MNASEMA
2. Aunul-Maabud, Sherhe Sunanu Abu-Daud: Yaani: aliposema: "hivi ndivyo alivyotuamrisha." kama anakusudia: Ametuamrisha kukubali ushahidi wa watu wawili sio mtu mmoja katika kufungua (siku ya 'Iydl-fitri). Aidha inawezekana pia kwamba anakusudia ametuamrisha tufungue kwa kufuata mwandamo wa nchi tuliyopo siyo nchi nyengine. Abu Daudi ameitegemea hii maana ya pili lakini Ibnul-Qayyim anaona kuwa maneno haya: "hivi ndivyo alivyotuamrisha" yana utata - yaani yanaweza kukusudiwa kwa maana ya kwanza au ya pili. Kwa maana hiyo, maneno hayo hayawezi kuwa hoja kwani hoja haitakiwi kuwa na utata (yaani maana zaidi ya moja). Wanavyuoni wa U sulil - Fiqhi wanasema hivi:
"Dalili ikiwa na maana (nyingi) zaidi ya moja, ushahidi wake huporomoka."
JAWABU
Kwanza naomba tuyanukuu maneno ya Aunul-Maabud, Sherhe Sunanu Abu-Daud kama yalivyo na tuyafahamu kama yalivyo, kwani hivyo mulivyoyaeleza nyinyi sivyo, bali hata hiyo tajama (translation) yake hapa ni mushkeli. Kitabu hicho kinasema: Kauli yake (Ibn Abbaas aliposema): "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) , ina uwezekano kwamba makusudio kwayo ni k uwa yeye (Mtume(s.a.w.w) katuamuru tusiikubali shahada ya mtu mmoja katika kufuturu, au katuamuru kwamba tutegemee uoni wa mji wetu: wala tusitegemee uoni wa wengine. Na hii maana ya pili ndipo inapomili tarjama (yaani heading) ya mtunzi (wa kitabu hiki), lakini maana ya mwanzo ina uwezekano (huu na ule) basi ushahidi wake hauendi sawa kwani uwezekano wa namna tafauti unaifisidi dalili.
Hayo ndio maneno ya mwenye kitabu hicho akimnukuu Ibn Al-Qayyim. Utaona kuwa wenzetu hapa:
1) Wamefanya ghushi kama kawaida yao. Maneno tusiikubali shahada ya mtu mmoja katika kufuturu, wameyaondosha kwani hayakubaliani na lengo lao.
2) Maana ya maelezo yenyewe wameivuruga vuruga. Sijua hawajui au wanafanya kwa kukusudia?
Sasa kwa ufupi ni kuwa, anachokisema Ibn Al-Qayyim, ni kuwa Hadithi hii ina uwezekano wa aina mbili:
1) Tusiikubali shahada ya mtu mmoja katika kufuturu. Huu ndio uwezekano wa kwanza.
2) Tutegemee uoni wa mji wetu: wala tusitegemee uoni wa wengine. Huu ndio uwezekano wa pili.
Sasa Ibn Al-Qayyim anasema kwamba "Lakini maana ya mwanzo ina uwezekano (huu na ule) basi ushahidi wake hauendi sawa kwani uwezekano wa namna tafauti unaifisidi dalili". Kwa hivyo, anachokipinga Ibn Qayyim ni kuwa maneno ya Ibn Abbaas "Hivi ndivyo alivyotuamu Mtume s.a.w." yana uwezekano wa maana kwamba ushahidi wa mtu mmoja usikubalike, lakini maana hii si sahihi: maana hii yeye kaipinga. Ama maana ya pili ya kwamba: "Tutegemee uoni wa mji wetu: wala tusitegemee uoni wa wengine". Hii yeye hakuipinga na kakiri kuwa maana hio imo katika Hadithi hio. Sasa ikiwa ndugu zetu mumeshindwa kuyafahamu mabo simple (mepesi) kama haya, vipi mutaweza kujadili suala hili lenye kuhitaji fani hii na hile?! Ama kanuni: "Dalili ikiwa na maana nyingi basi ushahidi wake huporomoka" ni kanuni sahihi lakini ina sharti zake:
1) Iwe Maana nyingi zenyewe ziwe zinatokana na dalili.
2) Kusiwe na qarina (contex au dalili za nje) ambazo kwazo inawezekana kuipa uzito maana moja. Ama hapa katika Hadithi ya Ibn Abbaas, Qarina (context) inabainisha wazi nini muradi wa Ibn Abbaas kuyasema hayo. Qarina (context) yenyewe ni kukataa kwake kufata muandamo wa Sham na akasema: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w.".
MNASEMA
3. Imamu Suyuti: Aliyesherehesha "Sunanun-Nisai" ametumia maneno yale yale ya Ibnul-Qayyim: Kwa hivyo Imamu Suyuti naye amekuja na msimamo ule ul e wa Ibnul-Qayyim wa kwamba maneno ya Ibnu ''Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu): "Hivi ndivyo alivyotuamrisha." Yana utata, kwa hivyo si hoja ya kutegemewa kisheria.
JAWABU
Al-Imamu Al-Suyuti ni kweli kasema kama alivyosema Al-Imamu Ibn Al-Qayyim. Maneno yake ni haya: Kauli yake (Ibn Abbaas aliposema): 'Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) ,' ina uwezekano kwamba makusudio kwayo ni kuwa yeye katuamuru tu siikubali shahada ya mtu mmoja katika kufuturu, au katuamuru kwamba tutegemee uoni wa mji wetu: wala tusitegemee uoni wa wengine. Na hii maana ya pili ndipo inapomili tarjama (yaani heading) ya mtunzi (wa kitabu hiki), lakini maana ya mwanzo ina uwezekano (huu na ule) basi ushahidi wake hauendi sawa kwani uwezekano wa namna tafauti unaifisidi dalili, kana kwamba wameona kwamba chenye kufahamika akilini ni maana ya pili wakajenga dalili juu yake.
Hayo ndio maneno ya Al-Suyuti, nayo ni sawa na maneno ya Ibn Qayyum, nayo ni hoja yetu dhidi yenu. Lakini mulipolijua hilo, mukaona maneno ya Ibn Al-Qayyim muyaghushi: kipande mukikate; na maneno ya Al-Suyuti muyanukuu kipande kidogo tu kisemacho (Na kusema kwakwe (Ibn Abbaas) hivi ndivyo ali vyotuamuru!
Kwa hivyo, maneno ya Al-Imamu Al-Suyuti ni kama ya Ibn Al-Qayyim, kwamba maneno ya Ibn Abbaaas yana uwezekano wa aina mbili
1) Tusiikubali shahada ya mtu mmoja katika kufuturu, au katuamuru kwamba. Huu ndio uwezekano wa kwanza.
2) Tutegemee uoni wa mji wetu: wala tusitegemee uoni wa wengine. Huu ndio uwezekano wa pili.
Na kwamba uwezekano wa kwanza ni dhaifu na wa pili ndio wenye nguvu na ndio tegemeo - kule la Abu Dau; na huku - la Al-Nasai.
Munasema Baada ya kupimwa maneno ya Ibnu-'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) katika mezani ya Usul-Fiqhi na kuonekana kwamba hayaeleweki kwa maana moja, sasa tuyatie kwenye mezani ya Hadiyth ambapo tutaona maneno ya Ibnu-'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) aliyoyasema: "Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)," yanapewa 'Hukmu Arafi' yaani yanapewa nafasi sawa na Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika hukmu. Hapa mezani ya Mustwalahul-Hadiyth inatoa jawabu ifuatayo:
JAWABU
Ni mezani gani ya usulul-fiq-hi mulioitumia na ni kanuni gani ya usuli mulioitumia kuonesha kuwa maneno ya Ibn Abbaas hayaeleweki? Maneno ya Ibn Al-Qayyim mumeyaghushi; maneno ya Al-Suyuti mumeyabutua. Na yote yanakupingeni nyinyi: si yanakusapotini. Kanuni: "Dalili ikiwa na maana nyingi basi ushahidi wake huporomoka" hamukuifahamu, nayo pia hapa inaipa nguvu tafsiri yetu. Sasa nyinyi ni kanuni gani hio ya usuli mulioitumia hapa kuon esha kuwa maneno ya Ibn Abbaas hayaeleweki?! Pili munasema maneno ya Ibn Abbaas: "Yanapewa 'Hukmu Arafi' Haya ndio kama yale nilioyakuta ubaoni kwenu Al-Rajulu Jaa mukasema Al-Rajulu ni faa'il (mtenda)!!! Na hapa munatwambia: sijui huyu Raafi'u katoka wapi. Sijui na hili hamulijui au kalamu imekupokonyokeni pamoja wingi wenu! Mashekhe hii inaitwa bila ya Alif katika Al-Raa (Ree): sio Sasa kama nyinyi hata hizi istilahi (technical terms) hamuzij ui, ni kitu gani kinachokufanyeni mujitie katika mambo kama haya?! Lakini nakupeni udhuru, labda ni kosa la chapa!
MNASEMA
i. Katika kitabu cha kimeandika yafuatayo: "Itakapo gongana 'Marfuu-hukman' na 'Marfuu-Saraaha' hutangulizwa (katika hukmu) 'Marfuu-Saraaha."
ii. Pia katika tafsiri ya Qur-aan ifuatayo: 383) imeandikwa ifuatavyo: " "Marfuu-Saraa ha ni bora zaidi (aula) kutangulizwa (katika hukmu) kuliko Marfuu-hukman."
JAWABU
Munaendelea kunukuu mambo musioyajua mukijitia katika dhima na jukumu. Maana ya kugongana katika elimu ya Usulil-Fiqhi na usulil-Hadithi, ambako kunalifanya andiko moja liachwe, ni kuwa:
1) Andiko moja lisema hivi na la pili liseme kinyume chake. Wakati hapa hakuna mgongano baina Hadithi ya Ibn Abbaas "Fungeni kwa kuuona" na Hadithi yake: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) ". Kwani hadithi ya kwanza - kwa baadhi ya mazingatio yake ni Aam (ya ujumla) - na ya pili - kwa baadhi ya mazingatio yak e ni Khaas (specific). Na ujumla wenyewe uliomo katika Hadithi hio "Fungeni kwa kuuona" ni - kama tulivyoeleza katika kitabu Ushahidi Uliowekwa Wazi ni kuwa Hadithi hii ni ushahidi kwamba watu wote lazima wafunge kwa kuuona, wala haibanishi suala la ku wa je ukionekana mwezi na watu wan chi moja watu wan chi nyengine nao wafunge au wasifunge: hili katika hadithi hio halimo kwa mbali wala kwa karibu.
Ama mazingatio yenye kuifanya Hadithi yake: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w.", ni ukweli kwamba Hadithi hii inaonesha kwa uwazi kwamba kila watu au kila mji na muandamo wao. Kanuni za kiusuli ni kuwa Aam (andiko la ujumla) likigongana na Khaas (andiko lenye kuvua baadhi ya mambo au specific exceptional), basi Khaas ndilo linalotangulizwa, kwani Khaas ni la hakika na Aam ni la dhana. Na kwa mazinagatio mengine, basi Hadithi "Fungeni kwa kuuona" ni mutlaq na Hadithi "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w." ni muqayyad; kanuni ni kutanguliza muqayyad kabla ya mutlaq. Na kwa ba adhi ya mazingatio, Hadithi: "Fungeni kwa kuuona" ni mumal na Hadith "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w." ni mubayyan. Kanuni ni kutanguliza mubayyan pasi na mujmal. Kwa hivyo, kiufupi ni kuwa hizi ni Hadithi mbili zenye kufasiriana: moja imeifasiri ya pili, wala hakuna mgongano.
Katika kitabu Ushahidi Uliowekwa Wazi, nilitoa maelezo yafuatayo:
a) Tumesema kwamba Hadithi hii ni mujmal (isiofafanuliwa) na kwamba mujmal hurejeshwa katika mubayyan. Kanuni hii ni kwa kuzingatia kwamba Hadithi hii haikubainisha je muandamo ni mmoja au kila watu wana muandamo wao? Bali imesema kwa ujumla tu "Fungeni kwa kuuona mwezi" kama Qur-an ilivyosema "Simamisha sala kwa kutenguka jua."
b) Tumesema pia kwamba Hadithi hii ni mutlaq na kwamba kanuni ni kulirejesha andiko mutlaq katika andiko muqayyad. Na tukasema kwamba ni lazima Hadithi hii ifungamanishwe na Hadithi ya Ibn Abbas. Hadithi ya Ibn Abbas ni muqayyad kwa hivyo ni lazima itangulizwe. Tumeiita Hadithi hii mutlaq kwa kuwa lafdhi yake haikufungamanishwa na sehemu yoyote, na tukaiita Hadithi ya Ibn Abbas kuwa ni muqayyad kwani lafdhi yake imefungamanishwa na sehemu moja pasi na nyengine.
b) Tumesema kuwa Hadithi hii ni Aam (ya ujumla). Ujumla huu ni kwa kuzingatiya wanaoambiwa au wanaohubiriwa (addressees). Na hii ni kuwa Hadithi inawataka Waislamu wote wafunge kwa kuuona mwezi. Lakini tumebainisha kwamba hii haina maana kuwa muandamo uwe mmoja, bali maana yake ni kuwa kila watu ni lazima wafunge kwa kuuona mwezi: sio kwa manazil wala kwa hisabu wala kufunga siku ya shaka. Hii ndio maana ya Hadithi hii, na hiyo ndio mielekeo ambayo kwayo nimezileta kanuni hizo za kiusuli.
2) Jambo la pili lenye kuyafanya maandiko yazingatiwe kuwa yanagongana ni kuwa maandiko hayo yote yawe sawa katika daraja zake.
3) Iwe hakuna njia ya kulipa uzito moja au kila moja kuliweka mahala pake. Kwa hapa kila andiko moja inawezekana kuliweka mahala pake na kuliweka kwenye muradi wake. Andiko: "Fungeni kwa kuuona mwezi" mahala pake ni kuwa kila watu wasifunge mpaka wauone; andiko "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w." mahala pake ni kuwa mwezi wa mbali si hoja walio mbali. Ama yakitokea hayo, na isiwezekane kuyajumuisha au kulipa uzito moja au kila moja kuliweka mahala pake, huwa maandiko yanagongana, na yote huachwa. Kwa bahati Hadithi mbili hizo hazina mgongano huo, bali ni katika milango ya: Al-Mujmal na Al-Mubayyan; Al-'Aam na Al-Khas; Al-Mutlaq na Al-Muqayyad. Na huku si kugongana, bali ni kufasiriana kwa maandiko. Ama maneno ya Sahib Khabaril Wahid aliposema: "Itakapogongana 'Marfuu-hukman' na 'Marfuu-Saraaha' hutangulizwa (katika hukmu) 'Marfuu-Saraaha" inaonesha kuwa nyinyi wenyewe hamukuyafahamu. Nimekuelezeni wakatika gani andiko huambiwa kuwa limegongana. Nayo iwe:
1) Yote ni daraja moja kwa nguvu.
2) Isiwezekane kulipa uzito moja.
3) Isiwezekane kulifungamanisha moja na jengine na kuyapa tafsiri ya pamoja au kila moja kuliweka mahala pake. Wala haikusudiwi kwa kanuni hizo kugongana kwa:
1) Al-Mujmal na Al-Mubayyan.
2) Al-'Aam na Al-Khas.
3) Al-Mutlaq na Al-Muqayyad.
Vyenginevyo Aya za Qur-ani za ujumla huwa vile vile zinagongana na maandiko mengine. Aya za mirathi zimegongana na Hadithi "Mwenye kuua harithi". Katika Qur-ani hakuna "Mwenye kuua harithi" bali kuna mgao wa mafungu tu. Hadithi ya Mtume (s.a.w.) ikawatoa wenye kuua. Sasa kugongana huku hakuitwi kugongana; bali kunaitwa kubainisha andiko mujmal (andiko lisilofafanuliwa). Halkadhalika Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib ni kubainisha andiko mujmal (andiko lisilofafanuliwa) nalo ni Hadithi "Fungeni kwa kuuona".
MNASEMA
Ufafanuzi zaidi wa maelezo hayo ni kwamba Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zilizotajwa hukmu ya kufunga na kufungua zimetaja hukmu hiyo kwa (saraaha) uwazi: "Fungeni kwa kuona mwezi." Hilo ni agizo la ujumla - yaani kwa watu wote. Lakini tukiyachunguza maneno ya Ibnu ''Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) tutayagundua ingawaje kayategemeza kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) bado hayako wazi - yana utatanishi.
JAWABU
Suala hili hili tumeshalijibu kwa urefu katika kitabu Ushahidi Uliowekwa Wazi. Na tunanukuu tena baadhi ya jawabu yetu. Nilisema: Jambo la pili: la kutazamwa katika Hadithi hii ni kuwa Khitabu (Agizo: kama alivyofasiri Sheikh Nassor Bachoo) ya Hadithi hii ni Aam (ya ujumla), kama Sheikh alivyonukuu kutoka katika kitabu cha Al-sayyid Saabiq. Na sisi tunajibu kwa jawabu mbili. Ya kwanza ni kuwa:
Ujumla wa agizo hilo, umehusishwa na Hadithi ya Ibn Abbas, na kanuni ya kiusuli inaeleza kwamba Al-khaas (Andiko maalumu au specific) nd io inayotangulizwa kuliko Al-aam (Andiko la ujumla), kwa kuwa kwake (hio Khaas) ni ya uhakika kinyume na Aam hakika yake ni (kitu) cha dhana. Kwa hivyo kanuni hapa inatutaka kuitanguliza Hadithi ya Ibn Abbas. Na natija ni kuwa ujumla jamala ulioba kia katika Hadithi "Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi" na ambacho tunachotakiwa sote tukifanye kwa mujibu wa Hadithi hii, ni kuwa sote tufunge kwa kuuona mwezi. Ama je muandamo ni mmoja au kila watu wana muandamo wao, Hadithi hii haitoi jawabu hio. Jawabu ya pili ni ile tuliotangulia kuinukuu kutoka kwa Sheikh Ibn Uthaimin aliponukuu jawabu ya wale wenye kusema kwamba kila mji una muandamo wake, ambapo walisema kwamba ujumla uliomo katika Hadithi hio, ni sawa na ujumla uliomo katika Aya inayosema: "Sasa waingiliyeni ( wake zenu) na tafuteni kile Allah alichokuandikiyeni, na kuleni na kunyweni mpaka ukubainikieni uzi mweupe kutokana na uzi mweusi wa alfajiri, kisha timizeni saumu hadi usiku."
Je hapa Allah anazungumza na watu wote au na watu maalumu? Je kuzungumza huku na watu wote inamaanisha kwamba alfajiri ya nchi moja ikichomoza watu wa nchi zote wajizuie, au kila watu na alfajiri yao? Jawabu yako hapa ndio jawabu yetu kwa maneno ulioyanukuu kutoka katika kitabu cha Al-sayyid Saabiq kwamba Hadithi hiyo "Fungeni kwa kuuona" ni: " "Agizo la ujumla linalojumuisha umma wote (wa Kiislamu) kwa hivyo; yeyote miongoni mwao atakayeuona (mwezi) popote pale; kuone kana huko kutakuwa ni kuonekana kwa wote." Halkadhalika tunajibu ujumla huo kwa Hadithi inayosema: "Usiku ukitokeza kutoka hapa na mcha na ukaondoka kutokea hapa na jua likatua, basi aliyefunga ameshafungua (au na-afungue)." Na sisi tunauliza je hapa walikuwa wakiambiwa watu wa Makka tu, au wakiambiwa watu wa nchi zote? Kama walikuwa wakiambiwa watu wa nchi zote, je jua likitua Makka au katika mji wowote ule sote tufuturu? Kwa hakika kila aliyejaaliwa kuwa na mtazamo sahihi, anaona kwamba kujenga hoja kwa ujumla wa Hadithi "Fungeni kwa kuuona" kwamba ni ushahidi wa kuwepo muandamo mmoja, ni kujenga hoja juu ya msingi dhaifu sana. Na kwa maana hio, Ibn Uthaimin (Mwanachuoni wa Kiwahabi) akasema kwamba kauli ya kuwa kila watu wana muandamo wao: "Ina nguvu yake kwa mujibu wa lafdhi (yake) na mtazamo sahihi na Qiyas sahihi vile vile: Qiyas cha wakati wa siku kwa (kuulinganisha) na wakati wa mwezi (month). Mwisho wa kunukuu.
Kwa ufupi ni kuwa, ujumla wa Hadithi inayosema "Fungeni kwa kuuona" ni - kama tulivyotangulia kusema - kwamba watu wote ni lazima wafunge kwa kuuona: si kwa kalenda wala kwa jengine lolote. Huu ndio ujumla unaokusudiwa katika Hadithi hio, au ndio ujumla uliobakia baada ya kuhusishwa au kuvuliwa sehemu ya ujumla huo na Hadithi ya Ibn Abbas na Kuraib.
Jambo la tatu: la kutazamwa katika Hadithi hii, ni kuwa Hadithi hii ni Mutlaq (isiofungamanishwa na kitu) wakati Hadithi ya Ibn Abbas ni muqayyad (iliofungamanishwa). Kanuni ni kuitanguliza muqayyad kuliko mutlaq kama usuli unavyoeleza. Kwa hivyo, kila msingi utaoufata utaona kwamba Hadithi ya Ibn Abbas ndio inayotakiwa itangulizwe.
Ama waliosema kwamba tufunge kwa muandamo mmoja, ukweli ni kuwa wao waliitanguliza rai kuliko kanuni za tafsiri. Walitazama wakaona kuwa mwezi ni mmoja na unakamilisha safari yake mara moja na kwa hivyo muandamo utakuwa mmoja. Lakini tumeona kwamba huu si muandamo wa Kisharia bali ni muandamo wa Kifalaki: muandamo wa Kisharia tunaupata katika kuzijumisha Hadithi tafauti. Pili ni kuwa hio ni rai, na ya Ibn Abbas ni Hadithi; na rai haina uwezo wa kuipinga Hadithi. Kama walivyosema: "Rai haina nafasi mbele ya A ndiko."
Ama utata munaotaja nyinyi mara baada ya nyengine basi hata katika Hadithi "Fungeni kwa kuuona" pia upo; bali hapa upo zaidi kuliko katika Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas; kwani Hadithi hii "Fungeni kwa kuuona" haikubainisha je tufunge kwa muandamo mmoja au kila watu na muandamo wao nayo Hadithi hio katika ujumla wake ni kama Aya "Simamisha Sala kwa kutenguka jua" na Hadithi "Usiku ukitokeza kutoka hapa na mchana ukaondoka kutokea hapa na jua likatua, basi aliyefunga ameshafungua (au na-afungue)." Zote zina ujumla sawa. Wakati - kwa upande wa pili - Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas imebainisha kwamba mwezi wa mbali si hoja kwa walio mbali. Kwa hivyo, utata uko zaidi katika Hadithi "Fungeni kwa kuuona" kuliko Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas.
MNASEMA
Baada ya kuyaona maneno ya Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) kwamba hayako wazi na kama mezani ya fani ya Hadiyth inavyojionesha - ni vyema kuwauliza Wanavyuoni ambao ni wapokezi wa Hadiyth: Je Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) hajawahi kupokea Hadiyth inayotaja kadhia hii ya miandamo ya mwezi nyengine isiyokuwa ile ya Kurayb? Wanavyuoni watajibu kuwa ipo riwaya iliyopokelewa na Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) mwenyewe juu ya suala hili la muandamo wa mwezi.
JAWABU
Hili tumeshalieleza kwamba hakuna kanuni laa ya kiusuli wala ya elimu ya Hadithi ilioifanya Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib kuwa isizingatiwe au iwe haifahamiki. Na kama kuna mtu hakuifahamu basi tatizo liko kwake si kwa Ibn Abbaas wala si katika riwaya yenye: riwaya iko wazi. Ibn Abbaas kaukataa muandamo wa Sham na akasema "Kuwa hivi ndivyo Mtume s.a.w. alivyotuamuru". Sasa alivyowaamuru ni vipi? Je kawaamuru kuwa wauzingatie muandamo wa mbali? Kama ni hivyo, vipi tena Ibn Abbaas asiufate naye ni mwanachuoni, sahaba mcha Mungu. Kwa hivyo, suala liko wazi na halitaki maelezo, lakini mtu akiwa kitu hakitaki huwa anatafuta kipengele dhaifu na shubuha hii na hile ili akikatae.
Ama suala: "Je Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) hajawahi kupokea Hadiyth inayotaja kadhia hii ya miandamo ya mwezi nyengine isiyokuwa ile ya Kurayb?" Jawabu ndio kapokea lakini je riwaya hio nyengine inabatilisha riwaya yake na Kuraib? Hili ndilo la kujiuliza?
Munasema Ifuatayo ndiyo riwaya yenyewe:
(Kutoka kwa Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) kwamba bedui mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Nimeuona mwezi." Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Unashuhudia kwamba hakuna anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)?" akasema: "Ndio." Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Ewe Bilal watangazie watu kesho wafunge.")) (Muslim).
Kama tulivyoona kwamba Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) ndiye aliyeipokea Hadiyth hiyo ya bedui na alivyokuja bedui huyo kumpa habari Bwana Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akazikubali habari hizi za kuambiwa. Jambo alilofanya ni kuzithibitisha tu kwamba yule aliyezileta habari zile ni Muislam. Wala hakumuuliza kwamba bedui yule anatokea wapi, wala pahala alipouona mwezi, wala kutokea masafa gani. Inawezekana kuwa alitokea maeneo ya karibu au vile vile inawezekana alitokea maeneo ya mbali na inaelekea kabisa kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa akimjua bedui yule ndio maana akamtamkisha shahada ili kuhakikisha kama alikuwa ni Muislamu.
Ilivyokuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakumuuliza bedui jambo lolote katika hayo tuliyoyataja, Shari'ah ya 'Usulul-Fiqhi' Wanavyuoni wanasema yafuatayo: "Kuacha kuuliza pahala ambapo ilikuwa inayumkini kuuliza basi inamaanisha kuwa hii ni hukmu ya jumla ('aam) isiyokuwa na mipaka."
Habari hizi zimenukuliwa katika Tafsiri ya Qur-aan Tukufu: i. ii.
Na ndio njia inayoelekea kuwa sahihi kuliko kufuata jambo lenye utatanishi (ihtimaalati). Bora kushikamana na mafunzo sahihi ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo yako wazi na yaliyo mepesi. "Jambo la asli halihitaji (kuletewa) dalili, (lakini dalili inahitajika katika jambo lisilo la asili)."
Kwa hivyo ilivyokuwa Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) alipokea (Hadiyth) maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ya kwamba alimkubali bedui bila ya kumuuliza anatokea wapi; halafu Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) huyu huyu hakuukubali mwezi ulionekana na Kuraib huko Sham, hapa inaonyesha wazi kwamba kitendo cha Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) kimetafautiana na yale aliyoyapokea kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
JAWABU
SANAD YA HADITHI
Katika kitabu changu Ushahidi Uliowekwa Wazi, niliikuu Hadithi hio ya Ibn Abbaas na nikatoa maelezo yafatayo: Hadithi hii - kama unavyoona - imepokewa na wapokezi tafauti. Lakini ina kasoro mbili: Moja ni mgongano katika sanad: wakati katika sanad nyengine Ikrima anaisimulia Hadithi hii mausulan (kwa kuifikisha) kutoka kwa Ibn Abbas kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) , katika sanad nyengine anaisimulia mursalan (bila kumtaja Ibn Abbas wala Sahaba yeyote). Na kwa hivyo, Al-nnasai anasema kwamba kauli ya kuwa Hadithi hii ni mursal (iliosimuliwa bila kutajwa Sahaba aliyeisikia Hadithi hio kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) : "Ndio inayoelekea zaidi kuwa sahihi."
Pia wanavyuoni wengine wakubwa wa Hadithi wanasema kwamba kundi (kubwa) la wasimulizi wameisimulia Hadithi hii kutoka kwa Ikrima kutoka kwa Mtume (s.a.w.) mursalan (bila kutajwa Ibn Abbas wala Sahaba yeyote). Miongoni mwa waliosema hivyo, ni Abu Daud kama ilivyo katika kitabu chake "AL-SUNAN" na akayanukuu maneno yake pia Al-bayhaqiy katika "AL-KUBRA". Na mfano wa maneno ya Abu Daud, ni maneno ya Ibn Majah katika "AL-SUNAN". Na akasema Al-tirmidhiy: "Hadithi ya Ibn Abbas ndani yake kuna khilafu: kaisimulia Sufyan Al-thauri na wengineo kutoka kwa Simak bin Harb kutoka kwa Ikrima kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) mursalan (bila kutajwa Ibn Abbas wala Sahaba yeyote), na wengi wa As-habu wa Simak wameisimulia (hivyo) kutoka kwa Ikrima kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) mursalan (bila kutajwa Ibn Abbas wala Sahaba yeyote)."
Ama Ibn Al-arabiy Al-malikiy yeye anasema: "Hilo kwetu halivunji usahihi wa kutoa habari (yaani usahihi wa kusimulia Hadithi) nayo ndio kauli ya Al-nadhaam kwani mpokezi wakati mwengine huiwasilisha (Hadithi kwa kumtaja Sahaba) na wakati mwengine huiachia (kwa kutokumtaja Sahaba), na (pia) wakati mwengine mpokezi mmoja huiwasilisha (Hadithi kwa kumtaja Sahaba) na mpokezi mwengine akaiachia (kwa kutokumtaja Sahaba)."
Kasoro ya pili ambayo kwayo imetiwa ila Hadithi hii, ni kuwa Hadithi hii kapwekeka nayo Simak bin Harb naye ni dhaifu, na kwa hivyo "Si ambaye anafanywa kuwa ni hoja katika Hadithi alizopwekeka nazo," kama alivyosema Al-nasai katika nakala ya Al-shaukaniy. Na bila shaka Simak bin Harb ni dhaifu. Anasema Abu Talib kutoka kwa Al-imamu Ahmad bin Hanbal akisema kwamba Simak bin Harb: "Hadithi zake zinagongana." Na "Alikuwa Shu'uba akimdhoofisha." Anasema Ibn Ammar: "(Wanavyuoni wa Hadithi) wanasema kwamba alikuwa akikosea." Anasema Ya'aqubu bin Abi Shaiba: "Nilimwambia Ibn Al-madiniy: (Vipi kuhusu) riwaya za Simak kutoka kwa Ibn Abbas? Akasema: "Ni zenye kugongana." Anasema Ibn Al-mubarak: "Simak ni dhaifu katika Hadithi." Anasema Ibn Hibban: "Anakosea." Na wako wengine waliomdhoofisha.
Kwa hivyo, kwa kuzingatia kwamba Hadithi hii, kapwekeka nayo Simak bin Harb kutoka kwa Ikrima, na Simak ni dhaifu, basi wanavyoni wa Hadithi wameihukumu Hadithi hii kuwa ni yenye sanad dhaifu, ingawa maana ya Hadithi hii wameikubali kwa kuzingatia kwamba inapata nguvu kwa Hadithi sahihi ya Ibn Umar ambayo tutainukuu katika sehemu inayofata Inshaa Allah. Anasema Al-shaukaniy kuhusu Hadithi hii ya bedui: "Nayo ni miongoni mwa kile ambacho hoja haisimami kwacho, kwa (sababu ya) kile kilichotangulia (kuelezwa) cha udhaifu wa yule aliyepwekeka nayo (naye ni Simak bin Harb)." Mwisho wa kunukuu.
Kisha baada ya hapo nikatoa tanbihi, nikasema: Jua kwamba udhaifu wa sanad ya Hadithi hii, haimaanishi udhaifu wa matn (text au maneno) ya Hadithi yenyewe. Maana ya Hadithi hii ni sahihi kwa vile kuna Hadithi nyengine - nayo ni Hadithi ya Ibn Umar - yenye kuafikiana na Hadithi hii kimaana. Na kwa hivyo wanavyuoni wengi wameitolea hoja Hadithi hii, na Ibn Hibban alipotaka kuisimulia Hadithi ya Ibn Umar tutayoinukuu baadae Inshaa Allah, alitumia lugha hii: "Kutaja habari (riwaya) yenye kubomoa kauli ya mwenye kudai kwamba habari (riwaya) hii (ya bedui) kapwekeka nayo Simak bin Harb na kwamba kuinasibisha kwake na Mtume(s.a.w.w) si sahihi." Kisha baada ya hapo, Ibn Hibban akasimulia riwaya hio ya Ibn Umar yenye maana sawa na riwaya ya bedui.
Kwa hivyo, ili muwe mumenijibu kwanza thibitisheni usahihi wa lafdhi hii ya Hadithi. Ama usahihi wa maana hauifanyi Hadithi kuwa ni hoja ikiwa ina sanad dhaifu. Kwa hivyo, kisanad, Hadithi hii si hoja na hilo wamelinena wanavyuoni wengi.
10
MUANDAMO WA MWEZI
MATN YA HADITHI
Ama kuhusu matn ya Hadithi hii, na kuhusu madai yenu mulioyakariri bila ya kujibu nilioyasema, mimi nilisema hivi: Suala jengine muhimu katika Hadithi hii na ambalo linahusiana zaidi na mizozo na migogoro yetu ya mwezi muandamo katika Afrika ya Mashariki, ni kuwa je Hadithi hii inathibitisha usahihi wa dai la kwamba muandamo wa mji mmoja ni muandamo wa ulimwengu mzima? Katika kitabu chake Sheikh Nassor Abdallah Bachoo, baada ya kuinukuu Hadithi ya bedui, alitoa maelezo haya:
"Pia jambo la kuzingatia hapa ni kwamba ilivyokuwa mtu huyo alikuwa ni Bedui yaani mtu wa Majangwani, Mtume(s.a.w.w) angeweza kumuuliza anatoka wapi, lakini hakumuuliza kabisa suala hili jambo ambalo linathibitisha kuwa suala la umbali gani wa kuonekana mwezi Mtume(s.a.w.w) hakuwa akilizingatia hata kidogo!!!" Mwisho wa kunukuu.
Lakini nadharia hii ya Sheikh Nassor Bachoo, haikutokana na fikra sahihi. Labda tuulize suala ili iwe ndio jawabu ya madai haya ya Sh. Nassor Bachoo. Suala ni kuwa: je Sheikh Bachoo anadhani kwamba bedui huyo alitoka wapi mpaka akaweza kufika kwa Mtume(s.a.w.w) usiku huo huo wa muandamo wa mwezi na akampa habari hio? Je anadhani kuwa bedui huyo alitoka Sham, Misr, Yemen au Oman? Ni wazi kwamba bedui atayeweza kwenda kwa Mtume(s.a.w.w) kumpa habari hio usiku huo huo au hata usiku wa pili na wa tatu, basi atakuwa ni bedui wa jangwa la hapo hapo Madina. Na kwa hivyo Mtume(s.a.w.w) - naye ndiye mkamilifu wetu kwa akili na elimu - hakuwa na haja ya kumuuliza unatoka wapi. Ivo tuseme katika wakati ambao hapakuwa na ndege wala vyombo vyovyote vyenye kwenda kwa kasi akakujia mtu baada ya Isha akakwambia nimeuona mwezi, nawe upo Bumbwini au Mahonda, utahitaji kumuuliza anapotoka? Ni wazi kwamba mtu huyo atakuwa anatoka katika miji hio hio ya Zanzibar. Kwa hivyo, bedui alikuwa ni bedui wa Madina ndio maana akaweza kufika kwa Mtume(s.a.w.w) usiku huo huo. Na kwa hivyo Mtume(s.a.w.w) hakuhitaji kumuuliza anapotoka.
Lakini baada ya maelezo hayo ya kiakili ambayo yako wazi kwa kila mwenye kutafakari, ni bora tuwaachie wapokezi wa Hadithi watueleze bedui huyo alitokea wapi. Ikrima - mwanafunzi wa Ibn Abbas - anaeleza kwamba bedui huyo alikuwa akitokea Al-harrah nayo ni sehemu yenye mawe mawe katika eneo la Madina. Na kwa maelezo haya mafupi, unabainika udhaifu wa dai hilo la Sh. Bachoo la kukufanya kule Mtume(s.a.w.w) kutomuuliza bedui anapotoka, kuwa ni dalili ya kutozingatia masafa, a kitegemea Hadithi hio ya bedui, kwani bedui huyo anajulikana kwamba anatoka Madina: si mahala pengine.
Hayo ndio nilioyasema na yote haya nyinyi hamukuyajibu - si sanad wala si matn, bali mumekariri kitu kile kile ambacho nimeshakijibu, na huu sio mjadala wa kielimu. Mjadala wa kielimu ni kuwa nukta inayojibiwa kwa uwazi huwa haikaririwi tena bali hutazamwa mule ambamo hamukujibiwa. Lakini hayo, ni kwa wale wenye kujua nini maana ya debate. Ama kanuni isemayo: "Kuacha kuuliza pahala ambapo ilikuwa inayumkini kuuliza basi inamaanisha kuwa hii ni hukmu ya jumla ('aam) isiyokuwa na mipaka." Kanuni hii, haihusiani na riwaya hio ya Bedui. Kanuni hii - nayo ni ya Al-Imamu Al-Shafi kwa ninavyokumbuka - inazun gumzia kitu ambacho hakijulikani na hakikuulizwa; si kitu chenye kujulikana. Na asili ya kanuni hii imejengwa katika Hadithi zenye kusimulia Sahaba aliyesilimu naye ana wake wengi zaidi ya wane. Mtume (s.a.w.) akamuamuru awaache abakishe wane. Yule sahaba hakuuliza Mtume(s.a.w.w) je wa kuachwa ni waliolewa mwisho au wowote tu, na Mtume(s.a.w.w) naye hakumbainishia. Kwa hivyo, Maulamaa - nadhani wa mwanzo wao ni Al-Imamu Al-Shafi - ndio wakatoa kanuni hio kutoka katika Hadithi hio. Ama bedui aliyekwenda kwa Mtume(s.a.w.w) usiku wa muandamo au hata siku ya pili na ya tatu, basi ni badui wa jangwa hilo hilo la Madina: si bedui wa Oman, Yemen au Sham. Nadhani hili - ikiwa hamutaki ubishi - basi liko wazi. Juu ya hayo, riwaya yenyewe imesema kwamba huyo bedui alikuwa akitoka wapi. Ikrima - mwanafunzi wa Ibn Abbas - anaeleza kwamba bedui huyo alikuwa akitokea Al-harrah nayo ni sehemu yenye mawe mawe katika eneo la Madina. Sasa uko wapi uhusiano wa kanuni hii na hadithi ya bedui?!!!!!!!!
Ama kanuni isemayo: "Jambo la asli halihitaji (kuletewa) dalili, (lakini dalili inahitajika katika jambo lisilo la asili)" lau muliifahamu kanuni hii, musingeliniambia kuwa nilete ushahidi wa kuwepo kwa matalai ya mwezi, k wani jambo linalojulikana kwamba ndio lilivyo basi halihitaji ushahidi. Lakini nyinyi ndugu zangu hamusemi kitu kwa maarifa sahihi, bali muna msimamo wenu huo hamutaki kuuwacha na anayekupungeni huwa yeye si mtu wa msimamo. Munasema Je nini hukmu ya kadhia hii? Ni vyema tusogeze karibu mezani yetu ya Mustalahul-Hadiyth ili tuone kipimo sahihi na chenye uzito mkubwa kipo upande gani:
"Atakapokwenda kinyume mpokezi (wa Hadiyth) kwa kile alichokipokea; Je hutangulizwa (katika hukmu ya jambo hilo ) njia (madhehebu) ya mpokeaji (namna alivyofanya yeye) au itatangulizwa habari (yaani) kile alichokipokea? Jamhuri ya Wanavyuoni wa Usulul-Fiqhi na Wanavyuoni wa Fiqhi - wakiwemo Imamu Shafi na Abul-Hassan wameonelea kwamba kilicho wajibu kutendewa kazi ni ile habari aliyoipokea mpokeaji sio ile tafsiri (ya tendo) la mpokezi. Kwani chenye kuzingatiwa juu ya kadhia hii ni kile alichokipokea (Swahaba kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) sio kile anachokiona yeye katika rai yake au alichokitenda."
Habari hizi zinapatikana katika vitabu vifuatavyo: 1. Al - Ihkamu Fii Usulil-Ahkam J. 2
2. Irshadul-Fuhul.
3. Khabaril-Waahid Wahujjiyatuh.
4. Al-Fatawa-Swala, Zakka, Swaum wa Hajj - kitabu cha 1 uk 268.
Jawabu
Kanuni hio ni sahihi, lakini wapi Ibn Abbaas kenda kinyume na riwaya yake. Riwaya ya Ibn Abbaas - pamoja na udhaifu wa sanad yake - inasema: ((Kutoka kwa Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) kwamba bedui mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Nimeuona mwezi." Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Unashuhudia kwamba hakuna anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)?" akasema: "Ndio." Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Ewe Bilal watangazie watu kesho wafunge.")). Haya iko wapi humu kwamba watu wafunge kwa muandamo mmoja, hata iwe Ibn Abbaas kenda kinyume na riwaya hii alipouacha muandamo wa Sham? Naona ndugu zangu munasema tu mambo bila hata ya kufikiri! Ama yale ya Mtume(s.a.w.w) kutokumuuliza bedui atokapo tumeshajibu.
MNASEMA
Baada ya kuona uzito uliopo katika mezani ya Mustalahul-Hadiyth. Ni vyema tuangalie tena mfano mwengine ufuatao:- Kuhusu Sahaba Abu Hurayra (Radhiya Allaahu 'Anhu) alivyopokea hukmu ya chombo kilichorambwa na mbwa. Sahaba huyu ndiye aliyepokea Hadiyth kutoka kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba chombo kilichorambwa na mbwa kisafishwe kwa kuoshwa kwa maji mara saba; moja kati ya hizo isafishwe kwa mchanga. Katika mapokezi mengine Abu Hurayra (Radhiya Allaahu 'Anhu) huyu huyu ameshuhudiwa kutoka kwa Sa'iyd bin Musayab kwamba yeye Abu Hurayra alikiosha chombo mara tatu katika sehemu ambayo ilitiwa mdomo na mbwa.
Imeonekana kitendo hicho cha Abu Hurayra (Radhiya Allaahu 'Anhu) kimetofautiana na maneno aliyoyapokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa jambo hilo , Wanavyuoni wote wa Kishafi wamesema chombo kilichorambwa na mbwa kioshwe mara saba na wala sio mara tatu. Kwa mantiki hiyo wameona washike yale maneno yake Abu Hurayra aliyoyapokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na wameacha kushika kile kitendo chake. Kwa hivyo cha kuzingatia ni yale maneno yaliyopokewa na wala sio kitendo cha aliyepokea. Kwani huenda mpokeaji akaghafilika, lakini maneno yakabaki vile vile na ndiyo yanayostahiki kutendewa kazi. Haya ni kwa mujibu wa misingi ya Shari'ah, Qur-aan na Sunnah. Tokeo hili ni sawa katika hukmu na tokeo la Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) katika kisa cha Kuraib, kama vile Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) alipokea kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikubali habari za mwezi zilizoletwa na bedui asiyetambulika na bila ya kumuuliza anatokea wapi au mwezi aliuona wapi. Halafu Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) huyu huyu hakuukubali mwezi ulioonekana na Kuraib pamoja na watu wengine huko Sham.
JAWABU
Hivyo alivyofanya Abu Huraira ndio mpokezi kwenda kinyume na riwaya yake: sio yale yaliomo katika riwaya ya Ibn Abbaas na Kuraib kwa upande mmoja na riwaya ya Ibn Abbaas na bedui kwa upande wapili. Kule hakuna kwamba katika riwaya moja Ibn Abbaas kaambiwa fungeni kwa muandamo mmoja kisha katika riwaya ya pili akafunga kwa muandamo tafauti. Wala hili halifahamiki katika riwaya hio kamwe kama tulivyobainisha vya kutosha.
MNASEMA
Hapo ndipo tunapowajibika kushika yale maneno aliyoyapokea Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) na kukiacha kitendo chake. Lililo bora ni kushika yale maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yaliyo wazi kuwa mwezi ukionekana (popote) watu wafunge au wafungue na hivyo ndivyo alivyofanya mwenyewe Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya kuzingatia wapi umeonekana mwezi. Kauli yake ilikuwa kama ifuatavyo:"Fungeni kwa kuonekana mwezi - muandamo na fungueni kwa kuonekana mwezi - muandamo"
JAWABU
Ama kudai kwamba: "Hapo ndipo tunapowajibika kushika yale maneno aliyoyapokea Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) na kukiacha kitendo chake. Lililo bora ni kushika yale maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yaliyo wazi".
Hio ni dhana dhaifu sana. Kwa bahati tumekubaliana kwamba twende kwa mujibu wa kanuni. Utakumbuka kwamba riwaya ya Ibn Abbaas na Kuraib inasema: Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) .. Kwa hivyo, kwa mujibu wa fani ya Hadithi 'Ulumul Hadith hii pia ni Hadithun Marfu'u sawa na Hadithi isemayo:"Fungeni kwa kuonekana mwezi - muandamo na fungueni kwa kuonekana mwezi - muandamo" . Na hivi ndivyo walivykobaliana wajuzi. Anasema Al-Suyuti alipokuwa akizungumzia Hadithun Marfu'u: "Akiwa (sahaba) atasema: 'Mtume s.a.w. katuamuru, basi hakuna khilafu ndani yake (hio ni Hadithun Marfu'u)'.
Kwa hivyo, kuifanya Hadithi (Fungeni kwa kuonekana mwezi - muandamo na fungueni kwa kuonekana mwezi - muandamo.) kuwa ndio Hadithi ya Mtume(s.a.w.w) na Hadithi "Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) " kuwa ni maneno ya Ibn Abbas ni kosa la kiminhaj (Methodolocal error); hilo halikubaliki katika elimu ya Hadithi. Zote hizo ni Hadithi za Mtume(s.a.w.w) , na kwa hivyo, kilichobaki ni kutafuta hii ina maana gani na hile ina maana gani. Tena nakukumbusheni kauli yenu muliposema: "Isipokuwa Sahaba akisema: "Tumeamrishwa kadha" au "Tumekatazwa kadha." Jambo hilo hupewa hukumu ya "Rafii" yaani hio inazingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume(s.a.w.w).
Tumesema: ama Hadithi"Fungeni kwa kuuona" ni andiko la wazi juu ya uwajibu wa kufunga kwa kuuona mwezi. Kw a hivyo, lazima tufunge kwa kuuona: si kwa kalenda wala si kufunga siku ya shaka. Hili ndilo linalothibitishwa na Hadithi hio:Fungeni kwa kuuona ." Lamu iliomo katika neno (Liru-uyatihi) ni H arfu Jarri li-tta'alil. Yaani ni harufu yenye kulitia neno kasra na kuonesha sababu ya maneno yaliotangulia au sababu ya hukumu iliotajwa. Kwa hivyo, maana ya haya ni kuwa kuuona mwezi iwe ndio sababu ya kufunga au kwa lugha nyengine sababu ya kufunga iwe ni kuuona mwezi. Hii ndio maana ya meneno"Fungeni kwa kuuona:" Hakuna hapa kinachoonesha mas-ala ya kufunga kwa muandamo mmoja au miandamo tafauti.
Ama Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib, ambayo ndani yake tunapata kuwa Ibn Abbaas aliukataa kuufata muandamo wa Sham na kusema: Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w ) Hadithi hii ni ushahidi kwamba muandamo wa mbali si hoja kwa walio mbali. Hivi ndivyo, taratibu za kifan i zinavyotutaka: tuyakusanye maandiko madamu inawezekana: sio moja tulitendee kazi jengine tulitupe. Kwa hivyo, natija ni kuwa:
a) Lazima tufunge kwa kuuona: si kwa kalenda wala si kufunga siku ya shaka. Hili linathibiti kwa Hadithi: Fungeni kwa kuuona."
b) Muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali. Hili linathibiti kwa kitendo cha Ibn Abbas cha kuukataa muandamo wa Sham na kubainisha kwamba hicho ndicho alichokifunza Mtume(s.a.w.w) . Munasema Suala Jengine: Je masimulizi ya Kuraib na Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) ndio yanakuwa makhsusi katika Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zilizotaja habari za kufunga na kufungua? Ni vyema kuweka wazi kwamba Hadiyth zote za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aali hi wa sallam) ambazo ni nyingi mno (Mutawaatir) zilizotaja habari ya kufunga na kufungua mwezi wa Ramadhaan zote zimekuja kwa ujumla - ('aam) Bila kuhusisha watu wa nchi fulani, masafa au matlai ya aina yoyote. Angalia: Agizo hilo limekuja kwa watu wote. Masimulizi ya Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) na Kuraib yalitokea zaidi ya miaka 30 baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kwamba Makhalifa wote wanne walikwishaondoka duniani. Kwa hivyo kuyafanya masimulizi hayo ya Kuraib kuwa ndiyo 'Khaas' katika Hadiyth hizo za kufunga na kufungua Swaum ni kinyume na kanuni za kifani. Ni vyema kuwaangalia Wanavyuoni wa fani ya Usulil-Fiqhi wanasema nini katika vitabu vyao kwenye huu mlango wa ('aam) - yaani maana ya ujumla na upamoja kwa watu wote:
JAWABU
1) Naam! Masimulizi ya Kuraib na Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) ndio yanakuwa makhsusi, kwa kuwa yanawahusisha watu wa sehemu pasi na wengine; wakati katika masimulizi mengine hili hulipati.
2) Ama dai kwamba "Hadiyth zote za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambazo ni nyingi mno (Mutawaatir) zilizotaja habari ya kufunga na kufungua mwezi wa Ramadhaan zote zimekuja kwa ujumla - ('aam)", si dai sahihi. Sasa riwaya zote zikija kwa uj umla - ('aam), ndio Hadithi ya Ibn Abbaas ishakuwa batili?!!! Au tufate kanuni kwamba andiko mahususi ndilo linalotangulizwa kuliko andiko la ujumla.
3) Pili: Je ujumla huo ni ujmla katika mazingato gani? Ujumla uliomo katika riwaya nyengine ni kama tulivyoeleza ni ujumla kwamba watu wote ni lazima wafunge kwa kuuona: wala hakuna katika Hadithi yoyote ujumla kwamba watu wote wafunge sawa. Suala je tufunge pamoja au tafauti halimo katika riwaya "Fungeni kwa kuuona" wala katika riwaya ziliokurubiana na hii kilafdhi. Bali riwaya hizi zinahimiza kwamba mfungo na mfunguo uwe kwa mujibu wa kuuona mwezi. Ama je muandamo wa mbali unakuwa hoja kwa walio mbali au haui, hilo linabainishwa na riwaya ya Ibn Abbas na Kuraib.
4) Ama dai kwamba: "Masimulizi ya Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) na Kuraib yalitokea zaidi ya miaka 30 baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kwamba Makhalifa wote wanne walikwishaondoka duniani". Sijui dai hili linathibitisha nini? Kwani masimulizi yakiwa baada ya miaka 30 huwa yanabatilisha riwaya? Na kwani Makhalifa wakiondoka ndio riwaya huwa hazisimuliwi tena?! Masimulizi ya riwaya yana sharti zake zikitimia basi riwaya inazingatiwa.
5) Ama kudai: "Kwa hivyo kuyafanya masimulizi hayo ya Kuraib kuwa ndiyo 'Khaas' katika Hadiyth hizo za kufunga na kufungua Swaum ni kinyume na kanuni za kifani". Tunauliza: ni kinyume na fani gani hio? Tuleteeni hio fani inayoonesha kuwa kutegemea ri waya ya Ibn Abbaas na Kuraib ni kinyume na fani. Fani inasema kwamba "Kauli ya sahaba akisema Mtume s.a.w. katuamuru kadha au katukataza kadha" hio ni Hadithi ya Mtume. Kwa hivyo, hii ni Hadithi ya Mtume (s.a.w.). Sasa wapi umesikia kwamba au ni fani gani isemayo kwamba ni kosa kuuhusisha ujumla wa Hadithi moja kwa Hadithi nyengine?
MNASEMA
Ifuatayo ni tafsiri kwa njia ya maana bila ya kutafsiri neno kwa neno: "Ili khaas ikubalike katika misingi ya Shari'ah kama ni hoja sahihi lazima khaas hiyo iepukane na utata. Kuwepo kwa utata ndani ya khaas kutaifanya kukosa kuwekwa mbele kwenye safu za hoja. Kwa hivyo (kielimu) haitaweza kutegemewa kwa namna yoyote ile. Na badala yake itabakia kuwa ni ya ujumla ('aam) katika kuwajumuisha watu wot e popote walipo. Kwani kuwepo kwa utata ni tuhuma zisizo na ushahidi imara zinazoifanya khaas hiyo kwa mujibu wa kanuni za Usulil-Fiqh kutoweza kuzingatiwa.
JAWABU
Kwanza tafsiri yenu inataka kurekebishwa, pamoja kuwa mumejilinda kwa kusema: "Ifuatayo ni tafsiri kwa njia ya maana bila ya kutafsiri neno kwa neno". Na nadhani pia kuna kosa la chapa. Neno inavyoelekea munakusudia Wallahu A'alam. Na neno Ihtimal halina maana ya utata, bali maana yake ni uwezekano wa tafsiri hii na hile. Ama tafsiri ya maneno hayo ni hivi:
Ama (andiko la ujumla) kuwa lina uwezekano wa kuhusishwa (na andiko khaas specific) bila ya kuwepo dalili ya uwezekano huu, basi hilo ni katika yale yasiozingatiwa wala halitazamwi wala halitendewi kazi. Basi (hapo) ushahidi uliomo katika Aam (andiko la ujumla) unaendelea kubakia katika (ujumla wake wa) kukusanya sehemu zake za yakini. Wala kule kuwa kuna uwezakano tu (kwamba andiko Aam, andiko la ujumla) limehusishwa bila ya dalili hakuliathiri (kitu andiko hilo la Aam ujumla), kwani uwezekano huo ni katika kufikiri kitu kimakosa (illusion), na hakuna kuzingatia fikra ya kimakosa wala kufikiri kimakosa."
Hii ndio tafsiri ya maneno hayo. Sasa mumefahamu nini? Haitoshi mtu kufungua kitabu akatafuta kipande akanukuu ikiwa ile fani hajaisoma yote. Kinachozungumzwa hapa ni kuwa je ndiko Aam ni (la dhana) au ni (la uhakika na yakini)? Mahanafi wanasema ni (la uhakika na yakini); Jumhur wanasema ni (la dhana). Sasa wanaosema kuwa andiko hilo ni (la dhana) - nao ni Jumhur wanasema - wanajega hoja kwamba ndiko Aam linauwezekano wa kuwa limehusishwa kwani imesemwa kwamba hakuna ndiko Aam la ujumla ila huwa limehusishwa isipokuwa andiko kama "Hakika Allah ni Mjuzi wa k ila kitu" na yalio mfano wa hilo. Kwa hivyo, kwa kuzingatia kwamba maandiko Aam ya ujumla yote - taqriban - yamehusishwa, basi huwa hatuna yakini tunapolikuta andiko Aam la ujumla kwamba je ni kweli kila chenye kuhusiana na andiko hilo kimeingia au yameingia baadhi tu. Nikisema Wazanzibari ni wakarimu, je huwa kweli ni Wazanbari wote? Inawezekana ikawa wote na inawezekana ikawa si wote. Lakini kwa vile lafdhi Wazanzibari ni wakarimu inawaingiza wote, basi hapo ndio ikawekwa kanuni nyengine kwamba: "Andiko la ujumla linakwenda katika ujumla wake mpaka lipatikane andiko lenye kuhusisha." Nikikuta andiko jengine kwamba Mzanzibari si karimu, basi yeye huwa kahusiswa na andiko Khaas (specif ic au exceptional). Ama andiko khaas specific ni (la uhakika na yakini) kwa mujibu wa Jumhur. Na kwa hivyo, niksema Ali ni mkarimu, basi hili ni andiko la uhakika kwamba Ali kaingia katika ukarimu.
Ama wanaosema kwamba ndiko Aam la ujumla ni (la uhakika na yakini), nao ni Mahanafi, na kwamba andiko hilo linawaingiza wote wanaoingia katika lafdhi ya andiko hilo, ndio wanaosema hivyo: Ama (andiko la ujumla) kuwa lina uwezekano wa kuhusishwa (na andiko khaas specific) bila ya kuwepo dalili ya uweze kano huu, basi hilo ni katika yale yasiozingatiwa wala halitazamwi wala halitendewi kazi. Basi (hapo) ushahidi uliomo katika Aam (andiko la ujumla) unaendelea kubakia katika (ujumla wake wa) kukusanya sehemu zake za yakini. Wala kule kuwa kuna uwezakan o tu (kwamba andiko Aam, andiko la ujumla) limehusishwa bila ya dalili hakuliathiri (kitu andiko hilo la Aam ujumla), kwani uwezekano huo ni katika kufikiri kitu kimakosa (illusion), na hakuna kuzingatia fikra ya kimakosa wala kufikiri kimakosa." N a hao ni Mahanafi: si Jumhur. Kwa hivyo ni wazi kwamba ndugu zetu:
1) Hawakuyafahamu maana ya maneno walioyanukuu: wameyafasiri sivyo.
2) Hawakufahamu hii ni kauli ya akina nani.
3) Hawakufahamu muradi wake ni nini.
Kwa hivyo, maana ya maneno hayo si kwamba andiko lenye maana nyingi au lenye utata kama munavyoita nyinyi huwa halitumika kuhusisha ujumla. Hii sio maana ya maneno hayo. Bali hata ingelikuwa maana ya maneno hayo ni hivyo mulivyodhani nyinyi, basi hii ingekuwa dhidi yenu kwani Hadithi iliosemwa kuwa ina ihtimal uwezekano huu na hule ni Hadithi "fungeni kwa kuuona".
MNASEMA
Mukhtasari Wa Nukta Muhimu i). Kwa kuwa masimulizi ya Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) na Kuraib yana utatanishi - hayaeleweki kwa maana moja; hayawezi kuchukuliwa kama ni hoja kama walivyoeleza hayo Wanavyuoni wa Usulil-Fiqhi na Mustalahul-Hadiyth.
JAWABU
Tumejibu tayari kwamba hakuna utatanishi: utatanishi munao nyinyi. Bali Hadithi "Fungeni kwa kuuona" ndio yenye utata. Munasema
ii). Kwa kuwa Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) ameonyesha kinyume na vile alivyopokea Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakiwezi tena kuchukuliwa kitendo chake kama ni hoja.
Jawabu Tumejibu kwa hoja za kielimu kwamba Ibn Abbaas hakwenda kinyume na alichokipokea kutoka kwa Mtume (s.a.w.) bali kilichopo ni Hadithi moja kuifasiri nyengine, kwani zote mbili - kwa mujibu wa fani - ni Hadithi za Mtume(s.a.w.w) .
Munasema iii). Katika Hadiyth iliyopokelewa habari ya kuonekanwa mwezi muandamo na bedui ambapo ingeyumkinika kuulizwa aliuona wapi mwezi muandamo lakini hakuulizwa.
JAWABU
Bedui anajulikana anapotokea. Ikrima - mwanafunzi wa Ibn Abbas - anaeleza kwamba bedui huyo alikuwa akitokea Al-harrah nayo ni sehemu yenye mawe mawe katika eneo la Madina. Na hata pasitajwe anapotokea, inajulikana kuwa anatoka katika jangwa la Madina kwani hakuna uwezekano katika zama hizo mtu kutoka Sham au Misr akafika Madina usiku wa muandamo au hata baada ya wiki nzima.
MNASEMA
Jambo hilo linapewa hukmu ya 'aam ujumla katika fani ya Usulil-Fiqhi. Wanavyuoni wamekuwa wakisema haya yafuatayo: "Hakika chenye kuzingatiwa baina ya njia aliyopita Sahaba (katika kutenda jambo fulani) na kile alichokipokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam); jambo la k ufaa kuzingatiwa katika hukmu ni kile alichokipokea (wala sio kile alichokitenda). Hata kama kitendo chake hicho kimepata umaarufu na kujulikana sana ." Hiyo ndio maana ya maneno ya Wanavyuoni wa Shari'ah yasemayo: "Chenye kuzingatiwa ni kile alichokipokea Sahaba kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala sio kile alichokitenda kutokana na riwaya hiyo."
JAWABU
a) Maneno yenu na dalili mulioitoa ya kiusuli ni vitu viwili tafauti, jambo ambalo linathibitisha kwamba hamujui munasema nini. "Munasema: Jambo hilo linapewa hukmu ya 'aam ujumla katika fani ya Usulil-Fiqhi. Wanavyuoni wamekuwa wakisema haya yafuatayo".: Kisha mukataja kanuni isemayo: "Kikigongana kitendo cha Sahaba na riwaya yake inatangulizwa riwaya yake". Kanuni ina zungumzia mgongano wa rai na riwaya; nyinyi munaitumia kwamba ni dalili ya ujumla!!!
b) Ama ikiwa munakusudia kwamba Ibn Abbaas kenda kinyume na riwaya yake, hili tumelijibu kwamba si kinyume kwani zote ni Hadithi za Mtume(s.a.w.w) .
c) Katika Hadithi ya bedui hakuna kitu ujumla kamwe, ila vile kuwa bedui hakuulizwa atokapo ndiko mulikokudhania nyinyi kuwa hukumu yake ni ya ujumla. Lakini yeye hakuulizwa kwa sababu unajulikana anapotoka. Nimekuulizeni kama mimi niko Bumbwini katika zama za ngamia na punda ukanijia baada ya isha ukaniambia "Mwezi umeonekana", bado nitahitaji kukuuliza ulipoonekana. Si itakuwa umeonekana miji hio hio ya Unguja?
MNASEMA
iv). Ameandika mwanachuoni mmoja anayeitwa Shaykh Aadaud bin Ibrahim bin Umar kitabu cha Kiibadhi cha Usulul-Fiqh kinachosomeshwa mashuleni. Katika J. 2 uk 15 ameandika yafuatayo:
10. Kisha akafupisha kuandika kwenye Khulasa: Tafsiri yake ni kama ifuatavyo:- Atakapoeleza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya hukmu ya jambo (fulani) na hukmu hiyo ikawa ina utata (yaani ina tafsiri zaidi ya moja) kisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa s allam) akanyamaza bila ya kutoa ufafanuzi mwengine wowote juu ya hukmu ya jambo hilo; itakuwa hukmu ya jambo hilo ni 'aam - yaani ni hukmu ya jambo lenye kuwajumuisha Waumini wote kwa pamoja, pamoja na kuwa jambo hilo lina utata.
JAWABU
Nimeshakufahamisheni nini maana ya kanuni hii. Hii inaeleza kitu ambacho kina uwezekano mwingi na hakijulikani: si kitu chenye kujulikana. Bedui alikuwa akijulikana atoka wapi, kwa hivyo, Mtume (s.a.w.) kutokumuuliza anapotoka haina maana kuwa masafa hayazingatiwi, kwani mtu anajulikana anapotoka. Pili: ni kuwa kilichomuhimu kukifahamu ni kwamba hio yenu ni istimbat; na la Ibn Abbaas ni andiko; na istimbat haina uwezo wa kubomoa andiko. Na kwa hivyo, wamesema katika kawaida za fiq-hi Hakuna kuizingatia dalili (isio wazi) mbele ya andiko lililowazi. Ubainifu wa hili ni kuwa Ibn Abbaas kasema kwa uwazi kwamba "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w." wakati katika hadithi ya bedui hakuna uwazi huu kwamba muandamo ni mmoja, bali hayo munayoyadai nyinyi ni kwa njia ya istimbat na istimbat yunu yote ni makosa kama tulivyobainisha.
11
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
MTAZAMO WA MASAHABA (RADHIYA ALLAAHU 'ANHU) JUU YA KADHIA YA KUFUNGA NA KUFUNGUA MTAZAMO WA MASAHABA
MNASEMA
Mtazamo Wa Masahaba (Radhiya Allaahu 'Anhu) Juu Ya Kadhia Ya Kufunga Na Kufungua Ndugu Juma amekuwa na mtazamo wake juu ya yale aliyoyasema Shaykh Naaswir Bachuu kwamba kwa muda wa miaka 30 ya Makhalifa waongofu hapakupatikana utatanishi wowote juu ya suala la muandamo wa mwezi. Haikuthibiti kwamba Masahaba waliwahi kuzingatia suala la masafa au matlai katika suala la kuandama kwa mwezi.
Ndugu Juma anasema: (Kama ilivyokuwa hakuna ushahidi kwamba wao waliwaamrisha watu wasifate miandamo yao, pia hakuna ushahidi kwamba wao waliwakataza wasifate miandamo yao, au kwamba waliwaamrisha kufata muandamo wa Madina.) Kwa upande wetu tunasema hivi: Ni kweli kuna uwezekano kwamba Masahaba hawakuwaamrisha watu wasifuate miandamo yao au waliwakataza watu kufuata miandamo yao.
Bila shaka jambo hilo linawezekana sana, kwani Masahaba hawana mamlaka ya kuwaamrisha au kuwakataza watu kwani wao hawakuwa wakipata Wahyi. Mwenye mamlaka hayo ni mwenyewe Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Isipokuwa Sahaba akisema: "Tumeamrishwa kadha" au "Tumekatazwa kadha." Jambo hilo hupewa hukumu ya "Rafii." Juu yao Masahaba ni kumsikiliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anavyowaamuru na kumuuliza pale panapotokea mushkeli wowote. Kwa mantiki hiyo tunapenda kusema kuwa hakuna Riwaya hata moja iliyo Sahihi inayoeleza kuwa labda Masahaba walimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa tufunge vipi au wenzetu walioko mbali nao wafunge vipi na wafungue namna gani. Hii ina maana kwamba Masahaba walimuelewa vyema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika maagizo yake hasa katika suala hili la kufunga walielewa vyema kuwa agizo hili ni la Waumini wote, mahala popote walipo.
JAWABU
Dai lenu kwamba: "Kwa mantiki hiyo tunapenda kusema kuwa hakuna Riwaya hata moja iliyo Sahihi inayoeleza kuwa labda Masahaba walimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa tufunge vipi au wenzetu walioko mbali nao wafunge vipi na wafungue namna gani. Hii ina maana kwamba Masahaba walimuelewa vyema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika maagizo yake hasa katika suala hili la kufunga walielewa vyema kuwa agizo hili ni la Waumini wote, mahala popote walipo". Hili si dai sahihi. Utaona kwamba tunakariri yayo kwa yao. Tunasema kwamba kutokuwepo kwa riwaya kwamba aliulizwa, hakumaanishi kuwa hakuulizwa, bali kuna maanisha kuwa hakuna riwaya hii wala hile. Kwa hivyo, huenda ikawa aliulizwa huenda ikawa hakuulizwa - hakuna ithbati. Lakini hali hii haina uwezo wa kuibomoa riwaya iliothibiti kwa sanad sahihi kwamba mafunzo yake ni kutokuuzingatia muandamo wa mbali. Nakukumbusheni tena kauli yenu muliposema: "Isipokuwa Sahaba akisema: "Tumeamrishwa kadha" au "Tumekatazwa kadha." Jambo hilo hupewa hukumu ya "Rafii" yaani hio inazingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume(s.a.w.w) . Kwa hivyo, natija ni kuwa:
1) Hakuna riwaya kwamba Mtume(s.a.w.w) kaulizwa hivi wala vile. Kwa hivyo, hapa hakuna hoja.
2) Kuna Hadithi kwamba Mtume kafunza kutokuuchukua muandamo wa mbali.
MNASEMA
Riwaya itegemewayo juu ya suala hili linalo zingatiwa matlai ni masimulizi ya Kuraib tu. Tukio lililotokea zaidi ya miaka 30 baada ya kufa Bwana Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Pia Makhalifa wote wanne walikwisha ondoka Duniani. Masimulizi ambayo yana utata mkubwa na hayana ufafanuzi wa kina, hususan yanapopimwa katika mezani mbili - mizani ya Usulul Fiqhi na mezani ya Mustalahul- Hadiyth. Baada ya kupimwa vizuri uzito wake katika mezani zote mbili, inabainika kwamba hapana uzito unaostahili kuchukuliwa kama ni hoja sahihi za kutegemewa katika mdahalo huu wa muandamo wa mwezi.
JAWABU
Naona tunaendelea kukariri. Ni mezani gani au ni kanuni gani ya Usulul Fiqhi au ya Mustalahul- Hadiyth muliotumia kubatilisha riwaya ya Kuraib na Ibn Abbaas. Nakukumbusheni tena mulioyasema punde: "Isipokuwa Sahaba akisema: "Tumeamrishwa kadha" au "Tumekatazwa kadha." Jambo hilo hupewa hukumu ya "Rafii" yaani hio inazingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume(s.a.w.w) . Riwaya ya Ibn Abbaas iko hivyo. Sasa ni elimu gani ya Hadithi mulioitumia? Na kanuni zote za kiusuli kama nilivyobainisha katika kitabu zinaifanya Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas itangulizwe.
MNASEMA
Ama tukichukua maneno sahihi ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliyoyasema:"Fungeni kwa kuuona mwezi muandamo" katika mezani, tutaona kina cha uzito wa maneno haya ni kikubwa mno. Ndio maana tukasema kushikamana na man eno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni bora na ndiyo hasa Sheri'ah inavyotuagiza kuliko kushika maneno yenye utata na yenye khitilafu.
JAWABU
Nakukumbusheni tena maneno yenu: "Isipokuwa Sahaba akisema: "Tumeamrishwa kadha" au "Tumekatazwa kadha." Jambo hilo hupewa hukumu ya "Rafii" yaani hio inazingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume(s.a.w.w) . Riwaya ya Ibn Abbaas iko hivyo, kwa hivyo nayo ni mafunzo ya Mtume(s.a.w.w) musiyatoe kwenye uzito.
MNASEMA
Kama tukijadili uwezekano wa utekelezaji wa agizo hilo la kufunga na kufungua katika zama ambazo mawasiliano yalikuwa duni na hafifu sana; tungejiuliza, Masahaba wangewezaje kupeana taarifa za kuandama kwa mwezi katika nchi za mbali? Wengewezaje kwa pamoja kuamka wakiwa wamefunga na hasa pakizingatiwa kuwa taarifa zenyewe zinatakiwa ziwafikie wengine kabla ya kupambazukiwa na alfajiri? Bila shaka jambo hilo lilikuwa ni gumu kiutekelazaji hata katika nchi moja pekee. Lakini ni vyema kuelewa kwamba hilo lilikuwa ni jambo la dharura kwa wakati huo.
JAWABU
1) Illa ya kufunga kwa miandamo tafauti ni kutafautina miadamo: si kupatikana kwa teknolojia mpya katika zama zetu na kukosekana kwake hapo zamani. Kama vile ambavyo illa ya kusali katika nyakati tafauti ni kuingia nyakati hizo tafauti kwa mtenguko na mzamo wa jua. Na sharia haibadiliki isipokuwa kitu kiwe kina illa (sababu) fulani iliojulikana katika andiko kwa njia ya tasrih (uwazi) au istimbat, kisha illa (sababu) hiyo iwe haipo tena. Hapo hukumu pia hubadilika. Kama walivyosema wanavyuoni sababu ikiondoka na hukumu huondoka. Sasa nyinyi wenzetu mumepata wapi kwamba kutofika habari ndio sababu ya kufunga kwa miandamo tafauti ili iwe sasa kwa kupatikana teknolojia mpya t ayari illa (sababu) hio imeondoka na sasa hukumu imebadilika?
2) Pili ni kuwa suala hilo nimelijibu kwamba Ibn Abbas alisema: "Hatuachi kufunga mpaka tukamilishe idadi ya siku thalathini au tuuone mwezi." Sasa kama aliukubali muandamo wa Sham, basi asingelisema maneno hayo, kwani kwa hali yoyote ile ikifika siku ya mwezi 29 ya muandamo wa Madina ni lazima watu wa Madina wale idi siku ya pili, ((halafu ikiwa itawathibitikia kwamba Sham mwezi uliandama tarehe thalathini wao watu wa Madina wailipe siku moja)) kwani siku hio ya mwezi 29 wa Madina ni lazima Sham itakuwa ni siku ya tarehe 30 au tarehe mosi. Ikiwa ni tarehe 30 itakuwa Sham wamefunga siku 30, wakati Madina wamefunga siku 29, na Ikiwa Sham ni tarehe mosi siku hio, basi watakuwa wamo ndani ya siku kuu - kwa hali zote mbili, kama Ibn Abbas aliukubali muandamo wa Sham, basi ni lazima watu wa Madina waishie kufunga tarehe 29. Lakini tunamkuta Ibn Abbas anasema "Hatuachi kufunga mpaka tutimize (siku) thalathini au tuuone mwezi." Kusema "Mpaka tutimize (siku) thalathini". Kama ni hivyo, basi utaona hapa kwamba habari ya muandamo wa mwezi ilikwishafika Madana. Suala je ilitendewa kazi? Kwa hivyo, kufika na kutokufika kwa habari si sababu ya kuwepo kwa miandamo tafauti hapo kale, bali sababu ni umbali na kutafautiana kwa matalai. Na lau ilikuwa sababu ni kutofika habari, basi habari ikifika ingetendewa kazi. Lakini hapa habari imefika wala haikutendewa kazi.
MNASEMA
Msisitizo wetu mkubwa ni kuwa katika masimulizi ya Kuraib hapakupatikana maafikiano ya Wanavyuoni kwa hivyo si jambo la kutegemewa. Kama wanavyosema Wanavyuoni wa 'Usulil-fiqhi.' "Dalili ikiwa na maana (nyingi) zaidi ya moja, huporomoka ushahidi wake."
Jawabu Ikiwa kutokuafikiana kwa wanavyuoni ni sababu ya kuachwa kwa andiko, basi itatubidi tuiache Qur-ani yote ila Aya chache kwani Aya zote taqriban wametafautina kuzifasiri. Bismillahi itabidi tuitoe kwenye misahafu kwani wako wanaosema kuwa si Aya kabisa kama vile watu wa Mailk. Bali kwa mantiki hio pia tuiwache Hadithi "Fungeni kwa kuuona musifunge mpaka muuone.." kwani wanavyuoni pia hawakukubaliana juu ya maana yake. Anasema Ibn Hajar (Na wale ambao hawakuchukua kauli hio, wanasema kwa sababu kauli yake Mtume(s.a.w.w) aliposema) "Mpaka muuone" ni agizo kwa watu maalumu." Anasema Al-san'ani: "Na ikasemwa kwamba (Muandamo wa mbali) hauzingatiwi (mbali), kwa sababu kauli yake (Mtume(s.a.w.w) aliposema:"Mukiuona" ni agizo kwa watu maalumu."
Ama kanuni isemayo: "Dalili ikiwa na maana (nyingi) zaidi y a moja, huporomoka ushahidi wake" haihusiani na hapa. Nyinyi hiki kitabu chenu baada ya kukiandika hamukuwapitishia watu wa fani wakakichungulia?! Kanuni hio haina maana kuwa wanachuoni wakitafautiana basi dalili huporomoka. Basi tusisali sala ya safari, maana wametafautina masafa ya safari: wengine kilomita 12; wengine masafa ya siku 3 nk. Na pia muda wa siku ngapi sala ya safari inakwisha: zote hizi ni tafauti, kwa hivyo Waislamu wasisali sala ya safari!!! Maana ya kanuni hio ni kuwa dalili yenyewe (Aya au Hadithi) ikiwa ina uwezekano huu na ule wala hakuna Qarina yenye kuipa uzito maana moja, basi huwa huwezi kutoa ushahidi kwayo ukasema kuwa maana hii ndio ilikusudiwa madamu huna ushahdi.
MNASEMA
Ikumbukwe kuwa Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni (aula) bora kwa hali yoyote iwayo. Kinachotakiwa ni kuifuata sio kuibeza. Shaykh Al-Qanubiy wa Kiibadhi anasema katika kitabu chake kuwa: "Itakapogongana amri ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na amri nyengine yoyote, basi amri ya agizo la Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni (aula) bora zaidi kutangulizwa (mbele) na ku fuatwa." Shaykh Ahmed Al-Khaliil (Mufti Mkuu wa Omani) naye amesema: "Hakuna kuzingatiwa kauli itakayopingana na Hadiyth sahihi, kwani Sunnah ni hoja juu ya jambo la Kid ini, wala jambo jengine lolote haliwezi kuwa ni hoja dhidi ya Sunnah."
103) Anachokieleza Shaykh Ahmed Al-Khaliil ni kuwa: "Lazima marejeo y a asili (katika misingi ya Kidini) ni kila kilichoelezwa kwa (saraha) uwazi katika Qur-aan Tukufu na kilichoelezwa katika Sunnah Sahihi. "Walikuwa wanavyuoni wema wakionyesha kukereka kwao na hasira zao juu ya yule mtu ambaye anaipuuza (anaibeza) Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa (kuifuata) rai (ya mwanachuoni) au Qiyaas au mapende kezo ya Wanavyuoni au kauli ya mtu yeyote kwa kuipuuza Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)" Katika maudhui yetu hayo ya muandamo wa mwezi, katika kadhia ya kufunga na kufungua kwa kuonekana mwezi, ni vyema kuachana na vitu vyenye utata na kusisitiza kushikamana na maneno katika Hadiyth Sahihi ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo:"Fungeni kwa kuonekana mwezi -muandamo"
Jawabu Munahimiza kufata Hadithi ya Mtume (s.a.w.) kama wanavyohimiza wanavyuoni hao. Hilo hatutafautiani. Lakini tunasema kwamba riwaya zote mbili "Fungeni kwa kuuona" na "Hvi ndivyo alivyotuamu Mtume s.a.w." ni Hadithi. Nakukumbusheni maneno yenu: "Isipokuwa Sahaba akisema: "Tumeamrishwa kadha" au "Tumekatazwa kadha." Jambo hilo hupewa hukumu ya "Rafii" yaani hio inazingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume (s.a.w.). Kwa hivyo, kinachotakiwa ni kuzijumuisha Hadithi hizo na kuzitazama zina maana gani: sio kuitendea kazi moja na kuiwacha moja: kuitendea kazi moja na kuiwacha moja ni kinyume na Al-Minhaj Al-Sahih (methodology) sahihi.
12
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
KUANDAMA KWA MWEZI KATIKA SEHEMU MOJA KUNATOSHELEZA KUANDAMA KWAKE DUNIA NZIMA
MNASEMA
12. Kuandama Kwa Mwezi Katika Sehemu Moja Kunatosheleza Kuandama Kwake Dunia Nzima Katika maelezo yaliyopita tumeeleza kwamba Hadiyth zote za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zilizotaja amri hii ya kufunga na kufungua ni Sahihi na ni zenye kukubalika mbele ya Wanavyuoni wala hazina khitilafu yoyote juu ya usahihi wake. Hadiyth zote hizo zimetaja amri hii ya hukumu ya kufunga na kufungua kwa ujumla - yaani ni jambo linalotekelezeka kwa watu wote katika siku moja. Wala agizo hilo halihusishi nchi fulani pasi na nchi nyengine. Ni agizo la ujumla 'aam.
Pia ni wazi kwamba agizo hilo la Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) halikutaja suala la kuwepo kwa matlai wala masafa gani, wala chengine chochote. Wala hakuna katika maelezo sahihi ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo yanakubalika na Wanavyuoni yaliyotaja kwamba 'kila nchi ifunge na ifungue kwa miandamo yao!' Kama ilivyoelezwa kwamba hoja inayotegemewa na baadhi ya Wanavyuoni wachache juu ya mas-ala haya ni kisa cha masimulizi ya Kuraib, masimulizi ambayo hayana ufafanuzi wa kina kama walivyoeleza hayo baadhi ya Wanavyuoni wengine na kuonyesha kuwa yana utatanishi (ihtimaalati). Jambo ambalo linaifanya hoja yake kuwa dhaifu. Kama yalivyoelezwa hayo na Wanazuoni wa fani ya "Usulul-Fiqhi."
JAWABU
Inaonesha tunaendelea kukariri yayo kwa yayo katika kila sura. Kudai kwamba Hadithi zote ni agizo la ujumla 'aam, ni kweli hilo ni agizo la ujumla lakini je ujumla huo uko mahala gani katika Hadithi hizo. Ujumla upo katika wenye kuamrishwa kwamba "Fngeni kwa kuuona". Kwa hivyo, ujumla unaopatikana ni kuwa watu wote wafunge kwa kuuona. Tumesema kwamba Lamu iliomo katika neno (Liru-uyatihi) inaitwa Harfu Jarri li-tta'alil. Yaani ni harufu yenye kulitia neno kasra na kuonesha sababu ya maneno yaliotangulia au sababu ya hukumu iliotajwa. Kwa hivyo, maana ya haya ni kuwa kuuona mwezi iwe ndio sababu ya kufunga au kwa lugha nyengine sababu ya kufunga iwe ni kuuona mwezi. Hii ndio maana ya maneno:"Fungeni kwa kuuona:" hakuna hapa kinachoonesha mas-ala ya kufunga kwa muandamo mmoja wala zaid i ya mmoja. Yaani ujumla hauambatani na sehemu bali unaambatana na walioamrishwa kwamba watu wote wafunge kwa kuuona: sio watu wote wafunge sawa. Ujumla huo ni sawa na ujumla uliomo katika Aya:"Simamisha sala kwa kutenguka jua" , na ujumla uliomo katika Hadithi isemayo:Usiku ukitokeza kutoka hapa na mchana ukaondoka kutokea hapa na jua likatua, basi aliyefunga ameshafungua (au na-afungue). Wala haina maana kuwa watu wa nchi moja wasali kwa kutenguka jua nchi nyengine, na wala haina maana kwamba usiku wa nchi moja ukiingia watu wa nchi nyengi wafuturu. Bali ujumla uliomo katika Aya ni kuwa watu wote wasali kwa kutenguka jua; na ujmla ulio katika Hadithi ni kuwa watu wote wafuturu kwa kuingia usiku: hakuna ndani ya maandiko haya mas-ala ya ujmla wa sehemu: ni ujumla wa wanaomrishwa.
Ama kauli yenu: "Pia ni wazi kwamba agizo hilo la Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) halikutaja suala la kuwepo kwa matlai wala masafa gani, wala chengine chochote" pia haikujengeka katika misingi ya kielimu. Wanavyuoni inapotajwa hukumu huwa wanaitafuta illa (sababu) ya hukumu hio. Ikiwa sababu imetajwa kwa uwazi, basi ni hivyo: hio ndio maslak njia yake; ikiwa haikutajwa basi huwa wanaitafuta kwa njia tafauti Masalik 'illa njia za kutafuta sababu. Kisha wakiipata ndio huifanyia Qiasi baina yake na baina ya kitu ambacho hukumu yake ha ikutajwa. Kwa hivyo, baada ya kuzikusanya sifa zote zenye kufaa kuwa sababu ya kwanini Mtume(s.a.w.w) akaamuru hivyo, tunapata sababu mbili kama nilivyoeleza katika kitabu, kwamba:
Moja ni kuwa: iwe hivyo ndivyo walivyoamrishwa na Mtume(s.a.w.w) kutokuuchukua mwezi wa Sham, kwa sababu huko ni Sham. Kwa hivyo, Sham iwe ndio illa (sababu) ya kutokuuzingatia muandamo. Hii inamaanisha kwamba lau Kuraib alikuwa anatoka Misri au Pemba wangeukubali muandamo huo. Illa (sababu) hii ni dhaifu, haifai kuifanya kuwa ndio illa (sababu) ya hukumu hio ya Mtume(s.a.w.w) iliomo katika Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbas. Kwani:
a) Ni (It is an intrasitive cause as opposed to a transitive one). Yaani ni sababu ambayo hai vuuki mahala pake, nayo inapingwa na sababu nyengine yenye kuvuuka mahala pake.
b) Ni "Kulifanya jina kuwa ndio sababu." Na inavyotakiwa sifa iwe ndio sababu: sio jina. Naam! Jina linaweza wakati mwengine kufanywa illa (sababu) ikiwa lina maana ya sifa. Katika jina "Sham" maana hii haipo. Pili ni kuwa: iwe Mtume(s.a.w.w) kawaamrisha hivyo kwa sababu Sham ni mbali. Illa (sababu) hii, ni sahihi na imekamilisha masharti ya utoaji wa illa (sababu).
Kwa hivyo, natija ni kuwa Mtume(s.a.w.w) kawaamrisha hivyo kwa sababu Sham ni mbali, sio kwa Sababu kule ni Sham. Tafauti za matlai, kwa sababu ya umbali au kwa sababu za kijografia, ni katika mambo yanayothibiti kwa njia ya Qias. Na Qias, nijuavyo, kwa Sunni, Ibadhi na Jumhur kwa ujumla ni dalili katika dalili za Kisharia. Kwa hivyo, kusema: "Pia ni wazi kwamba agizo hilo la Mtume(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) halikutaja suala la kuwepo kwa matlai wala masafa gani, wala chengine chochote" hakukujengeka katika misingi ya elimu, kwani elimu haiangalii nassun (andiko) tu; bali inaangalia andiko na Qias pia. Ama kauli yenu: "Wala hakuna katika maelezo sahihi ya Mtume(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo yanakubalika na Wanavyuoni yaliyotaja kwamba 'kila nchi ifunge na ifungue kwa miandamo yao" si kauli sahihi. Kwani ikiwa munataka Hadithi iseme "Jamani kila nchi na muandamo wao" basi riwaya yenye lafdhi hii haipo. Ama riwaya yenye maana hii ipo nayo ni riwaya ya Kuraib na Ibn Abbaas, nayo ni Hadithun Marf'u'u kwa mujibu wa lafdhi yake.
Pili ni kuwa kama vile ambavyo hakuna Hadithi ambayo lafdhi yake inasema: "Jamani kila nchi na muandamo wao" pia hakuna Hadithi yenye kusema "Jamani fungeni kwa muandamo mmoja". Kwa hivyo, suala hili linarejeshwa katika dalili zake nyengine kwa mujibu wa fani zinavyoeleza. Na tumeona kwamba Ibn Abbaas kaukataa muandamo wa Sham na akasema "Hivi ndivyo alivyotufunza Mtume(s.a.w.w) ". Kwa hivyo, mafunzo ya Mtume(s.a.w.w) , ni kutokuuzingatia mwezi wa mbali.
Ama kauli yenu: "Kama ilivyoelezwa kwamba hoja inayotegemewa na baadhi ya Wanavyuoni wachache juu ya mas-ala haya ni kisa cha masimulizi ya Kuraib, masimulizi ambayo hayana ufafanuzi wa kina kama walivyoeleza hayo baadhi ya Wanavyuoni wengine na kuonyesha kuwa yana utatanishi (ihtimaalati)" pia si kauli sahihi. Kwanza walioizingatia Hadithi ya Kuraib ndio Jumhur kama tunavyoshuhudia leo practically (kimatendo) kwamba asilimia kubwa ya Waislamu wa madhehebu mbali mbali duniani wanafata msimamo huu. Pili ni kuwa usahihi na udhaifu haupimwi kwa wingi na uchache hata kama ilikuwa munavyodai nyinyi ndio kweli kauli ya Jumhur; bali kipimo ni dalili za Kisharia. Ama kudai kuwa masimulizi ya Kuraib hayana ufafanuzi, sijui munataka ufafanuzi gani. Riwaya imeshaeleza kwa uwazi kwamba Ibn Abbaas kaukataa muandamo wa Sham na akasema kuwa hivyo ndivyo Mtume(s.a.w.w) alivyowaamuru, bado munasema kuwa haina ufafanuzi?! Ni wazi kwamba hamutaki wala sidhanii kuwa mumekuwa musiofahamu kiasi hicho hata ikawa hamuifahamu Hadithi hii.
Ama dai kwamba masimulizi hayo yana utatanishi (ihtimaalati), tumeshayajibu sana na sijui ni utatanishi (ihtimaalati) gani munaoukusudia. Ibn Al-Qayyim katika nakala mulizomnukuu kwa kughushi na Al-Suyuti katika nakala mulioibutua kipande wamesema: Kauli yake (Ibn Abbaas aliposema): 'Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) ,' ina uwezekano kwamba makusudio kwayo ni kuwa yeye Mtume(s.a.w.w) katuamuru tusiikubali shahada ya mtu mmoja katika kufuturu, au katuamuru kwamba tutegemee uoni wa mji wetu: wala tusitegemee uoni wa wengine. Na hii maana ya pili ndipo inapomili tarjama (yaani heading) ya mtunzi (wa kitabu hiki), lakini maana ya mwanzo ina uwezekano (huu na ule) basi ushahidi wake hauendi sawa kwani uwezekano wa namna tafauti unaifisidi dalili, kana kwamba wameona kwamba chenye kufahamika akilini ni maana ya pili wakajenga dalili juu yake. Kwa hivyo, ihtimal wanayoikusudia wao ni kuwa inawezekana kuwa maana iliokusudiwa ni kutokuchukua ushahidi wa mtu mmoja katika kufuturu; na inawezekana ikawa maana iliokusudiwa ni kwamba tutegemee uoni wa mji wetu: wala tusitegemee uoni wa wengine. Kisha wakabainisha kwamba maana ya pili ndio sahihi na kwamba maana ya mwanzo ndio yenye ihtimal (utata kama munavyoita), kwa hivyo maana ya mwazo si sahihi.
Lakini tunasema kwamba bila shaka dai hilo kwamba riwaya hio ina uwezekano kwamba makusudio yake ni kuwa Mtume(s.a.w.w) katuamuru tusiikubali shahada ya mtu mmoja katika kufuturu, ndio maana ya maneno "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w." ni dai dhaifu kwani:
1) Ibn Abbaas aliukataa muandamo wa Ramadhani huko Sham; si muandamo wa mfunguo mosi. Kama riwaya yenyewe inavyosema: "Ukaniandamia mwezi wa Sham nami niko Sham", na muandamo wa Ramadhani hauhitaji mashahidi wawili, bali shahidi mmoja anatosha.
2) Pili katika riwaya mulioitolea hoja - nayo ni riwaya dhaifu: riwaya ya bedui - tunapata kwamba Mtume (s.a.w.) mwenyewe kauchukua muandamo wa mtu mmoja (bedui) katika mwezi wa mfungo.
MNASEMA
Kwa hivyo agizo hilo la kufunga na kufungua kwa pamoja litaendelea kuwa hivyo kwani hakuna riwaya sahihi isiyo na utata yenye kuvua ujumla huu. Tamko hili ni: "Tamko lisilo na mipaka maalum."
JAWABU
Riwaya sahihi isio na utata yenye kuuvua ujumla huo iko: ni riwaya ya Kuraib na Ibn Abbas. Na wala hakuna utata wowote ndani yake; utata munao nyinyi wenyewe.
MNASEMA
Ama jambo la kusema kila watu na mtenguko wao wa jua kwa hivyo wana wakati wao wa kuswali na kufunga (Swaum) ndio hivyo hivyo; ni vyema ieleweke hivyo ni vitu viwili tofauti. Swala imeambatana na mitenguko ya jua na Swaum imeambatana na kuandama kwa mwezi. Mas-ala ya nyakati za Swala yameshaelezwa na kufafanuliwa na Mwenyewe Mwenyezi Mungu katika Qur-aan na pia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelibainisha kwa uwazi kabisa katika Hadiyth. Wala hakuna ikhtilafu yoyote mbele ya Wanazuoni juu ya jambo hilo. Ijmai ya Wanazuoni wamekubaliana kuwa kila sehemu, wala si kila nchi nzima inaweza kusali kwa wakati mmoja. Kwani mtenguko wa jua unaweza kutofautiana hata katika nchi moja. Angalia Dar es Salaam na Kigoma wanaswali na kufuturu tofauti, lakini wanafunga kwa mwandamo mmoja. Kila sehemu itaswali kwa wakati wake kwa kutegemea mtenguko wake wa jua. Mwenyezi Mungu Amebainisha hayo katika Surat Bani Israil (17: 78) kama ifuatavyo:"Simamisha Swala jua linapopinduka (likaenda magharibi) mpaka giza la usiku". Kwa upande wa Swaum hapakupatikana ufafanuzi wa kina ambao unakubali ka mbele ya "Jamhur" ya Wanazuoni. Hakuna hoja isiyokuwa na utata katika jambo la kuanza kufunga na kufungua kwa kutegemea kila nchi au kila eneo moja peke yake. Kwa mantiki hiyo ndio maana "Jamhur" ya Wanavyuoni wetu wakaonelea ni bora kutegemea Sunnah, yaani Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zilizo wazi ambazo zinaashiria umoja katika kufunga kwa pamoja. Kukamata andiko sahihi ni bora kuliko kung'ang'ania jambo lisilofahamika ambalo lina utatanishi.
"Kutumia madondoo kama Qur-aan au Sunnah ni bora zaidi kuliko kuiwacha (au kuipuuza na kuzingatia dalili zenye utata)".
JAWABU
Kuwepo kwa andiko na ijmaa ya nyakati tafauti za Sala na kutokuwepo kwa andiko la wazi juu ya wapi hadi wapi tufunge, ndiko kuliko juzisha kufanya Qias hicho cha sala na funga. Qias sharti yake ni kuwepo kwa msingi nacho ni kitu ambaho hukumu yake imetajwa; tawi nacho ni kitu ambacho hukumu yake haikutajwa; hukumu nayo ni moja katika hukumu tano za kifiq-hi; na illa jami'a (sababu yenye kuvijumuisha) vitu viwili hivyo na - kwa hapa - ni ukweli kwamba:
1) Jua ni kipimo cha wakati.
2) Jua ni sababu ya kuwajibikiwa na ibada.
3) Mwezi ni kipimo cha nyakati.
4) Mwezi ni sababu ya kuwajibikiwa na ibada.
5) Jua likitenguka sehemu moja: haiwi sababu ya watu wa sehemu nyengine yenye matalai tafauti kuwajibikiwa na sala.
6) Kwa hivyo, na kuonekana kwa mwezi katika sehemu ya mbali kusiwe ni sababu ya watu wan chi ya mbali kuwajibikiwa na ibada ya funga.
Ama kauli yenu: "Kwani mtenguko wa jua unaweza kutofautiana hata katika nchi moja. Angalia Dar es Salaam na Kigoma wanaswali na kufuturu tofauti, lakini wanafunga kwa mwandamo mmoja". Haya ndio niliokwambieni kuwa ni mas-ala ya ijtihad, au yanayojuzu kufanyiwa ijtihad. Yaani wapi hadi wapi tufunge sawa, hilo halikubainishwa na riwaya yoyote; lakini ukweli kwamba muandamo wa mbali usiwe hoja kwa walio mbali; hili limebainishwa na riwaya ya Ibn Abbaas na Kuraib. Kwa hivyo, ikiwa watu wa Kigoma wamefata ijtihad fulani ya wanavyuoni juu ya mas-ala ya masafa gani, hili kwa ujumla linakubalika. Lisilokubalika ni kufunga dunia nzima kwa muandamo mmoja. Na hili ndilo ninalotafautiana na nyinyi. Ama ukweli kuwa mbona basi tunafuturi tafauti na watu wa Kigoma; hili halijuzu ijtihadi kwa sababu ya kuwepo andiko la wazi kwamba wasifuturu hadi jua lituwe. Kwa ufupi ni kuwa, masafa gani tufunge sawa; hapa ijtihad inajuzu kwa sababu ya kukosekana andiko lenye kuhadidi masafa; masafa gani tufuturu sawa, hili halijuzu ijtihad kwa sababu ya kuwepo andiko lenye kubainisha suala hili.
Ama kusema kwenu: "Kwa upande wa Swaum hapakupatikana ufafanuzi wa kina ambao unakubalika mbele ya "Jamhur" ya Wanazuoni. Hakuna hoja isiyokuwa na utata katika jambo la kuanza kufunga na kufungua kwa kutegemea kila nchi au kila eneo moja peke yake. Kwa mantiki hiyo ndio maana "Jamhur" ya Wanavyuoni wetu wakaonelea ni bora kutegemea Sunnah, yaani Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zilizo wazi ambazo zinaashiria umoja katika kufunga kwa pamoja". Ninasema: kutopatikana ufafanuzi wa kina ndiko kunakohalalisha kufanya Qias, kwani lau palikuwa na andiko, basi Qias kisingelijuzu kama walivyosema: kwenye andiko hakuna Qias. Lakini sijakufahamuni muliposema : Kwa manti ki hiyo ndio maana "Jamhur" ya Wanavyuoni wetu wakaonelea ni bora kutegemea Sunnah, yaani Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zilizo wazi ambazo zinaashiria umoja katika kufunga kwa pamoja". Ni Jumhur ya wanavyuoni wenu gani?
Pili : ni kuwa na Hadithi ya Kuraib pia ni sunna ya Mtume(s.a.w.w) iliowazi.
Tatu : ni kuwa na Hadithi mulioitegemea nyinyi pia haiko wazi kwani inasema"Fungeni kwa kuuona" . Kweli Hadithi hii ko wazi katika kubainisha kwamba kufunga hakutakiwi ila baada ya kuuona mwezi; lakini haiko wazi katika kubainisha je tufunge kwa muandamo mmoja au kila watu wawe na muandamo wao. Ufafanuzi huu, unapatikana katika Hadithi ya Kuraib ambayo hamuitaki: munaipiga chenga!!!
Ama kauli yenu: "Kukamata andiko sahihi ni b ora kuliko kung'ang'ania jambo lisilofahamika ambalo lina utatanishi". Nimeshakufahamisheni kwamba Hadithi ya Kuraib pia infahamika na haina utatanishi, na kwamba Hadithi: "Fungeni kwa kuuona" ndio ambayo inafaa au inaelekea kuambiwa kuwa ina utata, kwani haikufafanua je tufunge kwa muandamo mmoja au miandamo tafauti.
Ama kanuni isemayo: "Kutumia madondoo kama Qur-aan au Sunnah ni bora zaidi kuliko kuiwacha (au kuipuuza na kuzingatia dalili zenye utata)". Kanu ni hii ni ushahidi wetu dhidi yenu, lakini kama munavyojionea wenyewe nyinyi hizi fani hamuzijui: munasukuma tu. Maana ya kanuni hii ni kuwa ikiwa neno - kwa mfano - halifasiriki katika uhakika wake, basi hupewa hukumu ya majazi: lakini sio kuwa liachwe. Na kwa ufupi ni kuwa andiko lolote likiwa linaweza kutendewa kazi basi haliwachwi: huwa linatendewa kazi. Na kwa maana hii, yanaingia maandiko mawili ambayo dhahir yake ni kuwa yana mgongano. Maandiko hayo huwa hayawachwi yote wala haliachwi moja madamu yanaweza kutendewa kati yote, bali kila moja hupewa maana linoyostahiki. Kwa hivyo, sisi ndio tulioitumia kanuni hii: sio nyinyi, kwani sisi tumezitendea kazi Hadithi zote mbili: Hadithi "Fungeni kwa kuuona", na Hadithi "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) " katika masimulizi ya Kuraib. Kusu Hadithi "Fungeni kwa kuuona", tumesema kwamba maana ni kuwa watu wote ni lazima wafunge kwa kuuona mwezi, yaani kuonekana kwa mwezi ndio kuwe sababu ya mfungo; na Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas tumesema inatoa ubainifu wa kwamba muandamo wa mwezi wa mbali si hoja kwa waliombali. Kwa hivyo, kanuni hio hamukuielewa na mungeielewa musingelipata tabu katika kuzifasiri Hadithi mbili hizo.
MNASEMA
Ama suala la kuingia alfajiri na kujizuilia kula na kunywa katika hukmu ya kuanza kufunga au kuanza kufuturu wakati wa kuzama kwa jua, mambo hayo hayana mjadala au khitilafu kama hizo kwani Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameshayafafanua katika Qur-an Tukufu kama ifuatavyo:"Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swaum mpaka usiku" . (2: 187) Jambo hilo la k utokuwepo khitilafu yoyote katika mas-ala haya, inamaanisha kwamba kila sehemu itajizuilia kula na kunywa kutokana na kuingia alfajiri yake na kila sehemu itafuturu baada ya kuzama jua kwa upande wake.
JAWABU
Haya! Iko wapi hio hoja katika Aya hii?!"Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swaum mpaka usiku" . Je hapa wanaombiwa ni watu wan chi moja au wan chi zote? Nadhani jawabu iko wazi kwamba ni watu wan chi zote. Sasa je usiku ukiingia nchi moja na watu wan chi nyengie nao wafuturu? Kama si hivyo, basi vipi Hadithi "Fungeni kwa kuuona" iwe ni dalili ya kufunga sawa duniani kote; lakini Aya"Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swaum mpaka usiku". isiwe hoja kwamba tufuturu sawa ilhali ujumla ulioko huku ndio ulioko kule? Kwa kweli, ndugu zetu humujui mukisemacho, na Aya hii ni hoja dhidi yene: si hoja yenu.
Ama kauli yenu kwamba: "Suala la kuingia alfajiri na kujizuilia kula na kunywa katika hukmu ya kuanza kufunga au kuanza kufuturu wakati wa ku zama kwa jua, mambo hayo hayana mjadala au khitilafu". Mwiso wa kunukuu. Nami nasema: Eleweni kwamba kwa kutokuwepo khilafu hizo, ndio imewezekana kufanya Qias sahihi kisichopingika kwa wenye kujua taratibu za Qias, kwani ikiwa Aya inasema:"Na kuleni na kunyweni" na hii ni amri ya ujumla kwa watu wote, na pamoja na hayo wanaokula si wote bali ni baadhi tu ambao usiku umeingia kwao; basi na Hadithi "Fungeni kwa kuuona" haijawa dalili ya kuwa watu wote wafate muandamo mmoja. Ukiniambia "Kule kuna dalili kwamba waliokusudiwa ni wale ambao usiku umeigia kwao". Nitakujibu kwamba na huku kuna dalili kwamba wanaomrishwa katika Hadithi"Fungeni kwa kuuona" ni wale ambao mwezi kwao umeandama. Kule dalili ni ijma'a; huku dalili ni Hadithi ya Ibn Abbaas ya kuukataa muandamo wa mbali na kusema: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) ".
MNASEMA
Ama ile hoja inayotolewa na baadhi ya ndugu zetu kama Juma isemayo: "Mbona watu wa nchi fulani wakifuturu nyinyi hamfuturu nao?" Au "Wakifuturu watu wa Saudia na nyinyi mufuturu basi." Bahati nzuri kwa upande wetu tumeshajibu mara nyingi katika makala haya kwamba jambo hili haliingizwi katika mjadala kama huu kwani jambo hilo halizungumzwi hata katika nchi moja yenye kufuata muandamano mmoja. Tumetoa maelezo kwamba katika Tanzania, Mji wa Dar-es-salaam hauwezi kufuturu sawa na mji wa Kigoma kwani kuna tofauti ya zaidi ya dakika 40. Jua linazama au kuchomoza dakika 40 kabla ya Kigoma. Kwa hivyo, Dar es Salaam wanaanza kufuturu mwanzo wakati bado jua halijatua Kigoma. Al-Marhuum Shaykh Abdulla Al-Farsy alipokua akiifasiri Aya ya Quran isemayo:"Kisha timizeni Swaum mpaka usiku" . Aliitolea maelezo yafuatayo: "Na ilipoambiwa:"Fungeni Swaum mpaka usiku" . Muradi ni magharibi - jua likishakuc hwa tu, ndio usiku wenyewe uliokusudiwa, kama alivyobainisha hivi Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na akahimiza watu wafungue jua tu likishakuchwa, na wakawie kula daku"
JAWABU
Kwanza ni lazima tufahamiane ni kwa sababu gani pakatolewa hoja hio. Hoja hio imetolewa kujibu dai kwamba Hadithi "Fungeni kwa kuuona" ni Aam (ya ujumla). Na kwa hivyo, inawahusu Waislamu wote wan chi zote. Hapo ndio na sisi tukajibu kwamba na Aya isemayo: (Simamisha sala kwa kutenguka jua), pia ni ya jumla: haiwahusu watu wa nchi fulani pasi na nyengine. Na Hadithi"Usiku ukitokeza kutoka hapa na mchana ukaondoka kutokea hapa na jua likatua, basi aliyefunga ameshafungua (au na-afungue)" pia ni ya jumla. Sasa je ujumla huu unamaanisha kuwa watu wa Maka au nchi nyengine wakifuturu, watu wote wafuturu pamoja nao? Sisi hapa tunajibu hoja ya kuwepo kwa ujmla katika maandiko haya, kwamba ujumla tu haojatoa jawabu madamu kuna maandiko mengine ambayo nayo ni lazima yazingatiwe ili tuwe tumeyatendea kazi maandiko yote na kufikia maana sahihi.
Sasa ukweli kwamba "Jua linazama au kuchomoza dakika 40 kabla ya Kigoma. Kwa hivyo, Dar es Salaam wanaanza kufuturu mwanzo wakati bado jua halijatua Kigoma" hakujahalalisha kufunga kwa muandamo mmoja duniani madamu kuna andiko sahihi la Hadithi lililoonesha hivyo. Bali hali kama hizi zitabaki kama ni uwanja wa i jtihadi. Ama pale kwenye andiko, ni lazima andiko litendewe kazi.
13
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA KUMI NA TATU
MAANA YA JAMHURI KATIKA MATUMIZI YA KISHARI'AH
MNASEMA
13. Maana Ya Jamhuri Katika Matumizi Ya Kishari'ahKwanza : ni vyema kuelewa kwamba mjadala huu wa mwezi katika hukumu ya kufunga na kufungua ni mkongwe wala haukuanza leo. Wala hii si fikra aliyoianzisha Shaykh Naaswir Bachuu kama walivyofahamu hayo baadhi ya watu kama akina ndugu Juma. Ukweli ni kuwa Shaykh Naaswir ni miongoni mwa Mashaykh wanaoendeleza harakati hizi za kufuata muandamo mmoja. Mtazamo huu wa kufunga kwa pamoja uliokuwepo tokea karne nyingi zilizopita umeshaelezwa katika kitabu cha "Kuandama kwa Mwezi" cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 129 - 133. Wanavyuoni wakubwa kama Dr. Wahbah Zuhailiy, Shaykh 'Abdur-Rahmaan Al-Juzairy, Alqanuji, Sayyid Saabiq, Ibnu Taymiyah, Ibnu Quddama Almaqdisiy, Shaykh Muhammad 'Aliy Assaabuniy na wengine wengi ni miongoni mwa waliosema kuwa msimamo wa kufunga kwa muandamo mmoja ndio "Rai ya Jamhur."
JAWABU
Hakuna katika kitabu changu sehemu niliodai kuwa Sheikh Nassor Bachoo ndiye aliyeanzisha mjadala huu. Nilichokisema ni hiki: Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya. Mutakumbuka kwamba na jambo hili pia kalizungumzia Sheikh Nassor katika kitabu chake aliposema: Pamoja na kuwa mgogoro wa kuandama kwa mwezi umeanza kuonekana hadharani katika jamii za Waislam wa hapa Afrika ya Mashariki katika miaka ya hivi karibuni.
Ama dai kwamba msimamo wa kufunga kwa muandamo mmoja ni rai ya jumhuri, hatuwezi kukubaliana kwani ukweli unaonekana tafauti na hivyo. Kwa ufupi mimi nimelijibu suala hilo hivi: Wengi katika wale wenye msimamo wa kufunga kwa muandamo mmoja huwa wanapenda kudai kwamba rai yao hio ni rai ya Jumhuri (majority) ya Umma, nalo ni kosa kwani ikiwa wanakusudia Jumhuri ni idadi ya wanavyuoni wengi, basi rai ya kwamba kila watu na muandamo wao bila shaka itakuwa ndio yenye kufatwa na wanavyuoni wengi kwani ni rai ya Mashafi nao ndio walio wengi duniani katika madhehebu za Kisuni. Pia rai hii ni rai ya Mashia Imamiyya nao ni wa pili au wa tatu kwa wingi katika madhehebu za Kiislamu.
Ikiwa tunakusudia Jumhuri kwa idadi ya madhehebu, basi - katika madhehebu zilizoko leo duniani - rai ya kuwa kila watu wana muandamo wao ni rai ya Mashafi, Maibadhi, Mashia Imamiyya, pia - kutokana na aliyoyanukuu Al-shaukaniy kutoka kwa Al-imamu Yahya na Al-hadawiyya miongoni mwa Zaidiyya, inaonesha kwamba hii ndio kauli ya madhehebu hio ya Shia-Zaidiyya. Na ndio msimamo wa sasa wa Madhehebu ya Kiwahabi huko Saudia, na ndio kauli sahihi kwa Mahanafi kwa mujibu wa alivyosema Al-sayyid Saabiq kama tutavyonukuu baadae Inshaa Allah..
Pili : ni kuwa kauli ya kufunga kwa muandamo mmoja imenasibishwa kwa Al-imamu Malik. Lakini riwaya hio ya Al-imamu Malik imesimuliwa na watu wa Iraq, ama kule Madina alipokuwepo mwenyewe Al-imamu Malik, watu wa Madina wamesimulia kutoka kwake akisema: "Funga haiwalazimu kwa habari isipokuwa watu wa mji (ule ule) ambao (mwezi) umeonekana."
Tatu : ni kuwa: madhehebu zote ambazo zinajulikana kuwa ndizo zenye msimamo wa kufunga kwa muandamo mmoja zina wanavyuoni si kidogo ambao hawakuiafiki rai hii. Kama Al-kaasaniy, naye ni Hanafi. Na akawanukuu Abu Muslim wanachuoni wengine wa Kihanafi wenye kauli hii. Anasema: "Na alichokichaguwa mwenye kitabu cha "AL-TTAJRID" na wengineo katika Mashekhe wa Mahanafi, ni kuzingatia tafauti za Matalai. Amesema Al-zayla'i naye ni miongoni mwao (Mahanafi): 'Nayo (kauli hio) ndio yenye kuelekea zaidi.' Na amesema Ibn Al-hammam miongoni mwao (Mahanafi) na kushikana na dhahiri ya masimulizi (ya Hadithi ya Kuraib) ni (jambo) lenye hadhari zaidi..na hakuna shaka kwamba hii ni bora kwani ni nassu (andiko la wazi) na ile (Hadithi inayosema: 'Fungeni kwa kuuona') ina uwezekano wa kuwa makusudio ni kuwaamuru watu wa kila matalai kuwa na uoni wao wa mwezi muandamo." Mwisho wa nakala kutoka katika kitabu cha Al-imamu Abu Muslim.
Anasema Al-sayyid Saabiq: "Na akasema Ikrima na Salim na Is-haq na ndio (kauli) sahihi kwa Mahanafi..kwamba watu wa kila mji wanazingatia muandamo wao wala hauwalazimu muandamo wa wenzao." Mwisho wa kunukuu. Ninasema: bila shaka watakuepo wengine wengi ambao vitabu v yao hatujavisoma au hatujaviona kamwe.
Pia ukitazama maneno ya Ibn Rushd Al-qurtubiy - naye ni mwanachuoni wa Kimaliki - utaona hakutoa msimamo wake kwa uwazi, lakini maneno yake yanaonesha kwamba anaelemea katika kauli kwamba kila watu wana muandamo wao. Anasema - baada ya kuinukuu Hadithi ya Kuraib na kutoa maelezo -: "Dhahiri ya Riwaya hii inamaanisha kwamba kila mji una uoni wao (wa mwezi muandamo) ukiwa mbali au karibu. Na Qiyas kinatoa tafauti baina ya miji ya mbali na miji ya karibu."
Mwisho wa kunukuu.
Na Ibn Al-arabiy - naye ni miongoni mwa wanavyuoni wakubwa wa Kimaliki - anasema: "Na wakatafautiana katika kuifasiri kauli hii ya Ibn Abbas (yaani Hadithi ya Kuraib). Ikasemwa: '(Ibn Abbas) Kaikataa (habari hio aliopewa na Kuraib) kwa kuwa ni ya mtu mmoja. Na ikasemwa kwa kuwa miji (miwili hio ya Madina na Sham) matalai yake yametafautiana, nayo ndio (kauli) sahihi..na mfano wake ni lau uliandama usiku wa Ijumaa huko Aghmat (Morocco) na ukaandama huko Ishbiliyya (Mji wa Spain) usiku wa J/mosi, ba si inakuwa kila mji una muandamo wake."
Na mfano wa kauli hii ya kuzingatia tafauti za miandamo kwa kutafautika miji kwa umbali au kwa kutafautika matalai, ndio kauli ya Ibn Majishun na Al-mughira miongoni mwa wanavyuoni wa Kimalik. Anasaema Ibn Rushd Al-qurtubiy: "Na wakakubaliana kwamba hilo halizingatiwi katika miji ilio mbali mbali kama Al-andalus (Spain) na Hijaz (Saudia)." Na kauli hii kaisema pia Ibn Abdil-Barri katika wanavyuoni wa Kimalik. Changanya na ukweli kwamba Al-imamu Malik mwenyewe kuna riwaya mbili juu ya kauli gani aliitegemea, na riwaya ya kwamba kila watu na muandamo wao ndiyo yenye kuelekea zaidi kutoka kwake kwani ndio riwaya iliosimuliwa na watu wa Madina ambako Al-imamu Malik mwenyewe alikuwa akiishi.
Nne ni kuwa: kama tulivyotangulia kusema kwamba mas-ala ya kufunga kwa muandamo mmoja yamo katika vitabu tu: si katika matendo: kimatendo ni Waislamu wachache sana duniani wanaofata rai hio. Kwa mfano nchi za India na Pakistan na Bangladesh - ambazo zina Mahanafi wengi - ukiwauliza wakazi wa nchi hizo wenye kuishi Ghuba: "Kwenu mwezi umeandama lini?" Watakwambia siku tafauti na muandamo wa nchi nyengine ambazo labda zimetangulia. Na nchi hizo zote zina Maulamaa.
Tano : ni kuwa: kauli ya kuwa kila mji na muandamo wake imesimuliwa kutoka kwa Maimamu wengine wakubwa - ukitoa Maimamu wanne - kama Ikrima miongoni mwa Wafuasi wa Masahaba, na Moh'd bin Al-qasim na Salim na Is-haq bin Rahawaih na Al-tirmidhiy akainasibisha na watu wa elimu (Maulamaa). Kwa hivyo, tunasema kwamba kusema kwamba kauli ya muandamo mmoja ni kauli ya Jumhuri ya Umma, ni jambo la kufikiriwa. Kwa hali yoyote ile, mimi sisemi kwamba kilichosawa ni kinachosemwa na Jumhuri,( laa): sisemi hivyo, bali ninachosema ni kuwa kilicho sahihi ni chenye ushahidi madhubuti uliojengeka juu ya misingi ya kielimu, lakini naona watu hapa wamekuwa wakipiga kampeni kwa kutumia jina Jumhuri nayo si sahihi. Na mas-ala kama haya yako mengi: utasikia hii ndio kauli ya Jumhuri, mara ukisoma kitabu chengine utakuta kauli kinyume na hio kwamba ndio kauli ya Jumhuri!!! Cha kustaajabisha zaidi ni kuwa wakati mwengine utakuta kitu chenye tafauti mashuhuri, basi atatokea mtu anayetaka kuipamba rai yake, anasema: "Umma umekubaliana juu ya jambo hili!" Mwisho wa kunukuu nilioyasema kitabuni.
Bila kusahau kwamba hata leo hii, Jumhur ya Waislamu duniani hawafati miandamo ya nchi nyengine. Kwa hivyo, hiki ni kitu tunakishuhudia hatuhitaji andiko. Lakini - kama nilivyosema - ikiwa Jumhur inasema tufunge kwa muandamo mmoja au inasema kama tunavyosema sisi, yote mawili si hoja katika uwaja wa Sharia, bali hoja ni je wana dalili gani, na wapinzani wao wana dalili gani. Chukua - kwa mfano - walio wengi katika Sunni, wanasema tufunge mikono chini ya kitovu, tukichukulia kwamba Sunni wengi ni Hanafi. Au wanasema tufunge juu ya kitovu, tukichukulia kwamba Sunni wengi ni Shafi. Wakati Salafia wana hoja ambazo ndio sahihi kwao kwamba mikoni inafungwa juu ya kifua. Sitaki kusema kipi ni sahihi, nataka kusema kwamba wingi si hoja ya Kisharia. Bali leo, ukitazama katika madhehebu za Sunni utakuta kwamba Salafiyya ndio wachache. Sasa tuseme ndio dalili zao zitakuwa hazifai? Bila shaka kitachotazamwa ni dalili: si wingi na uchache.
MNASEMA
Msimamo huu kwa kweli umejengeka katika misingi imara uliopokewa moja kwa moja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pale aliposema: (Fungeni kwa kuona mwezi - muandamo..)
JAWABU
Tumeshabainisha sana kwamba (Fungeni kwa kuona mwezi - muandamo..) ni Hadithi na "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) " pia ni Hadithi. Na huwezi kuyakataa mafunzo ya Mtume(s.a.w.w) , bali unaweza kuyatafutia maana sahihi
MNASEMA
Wanavyuoni wa Shari'ah wameieleza "Jamhur" kwa maana ya kukubaliana jambo "Maimamu wanne wa Kisunni" na hata kama ikitokea kujitoa Imamu mmoja katika hao wanne kwenye jambo fulani bado jambo hilo litachukuliwa ni la msimamo wa "Jamhur" midam watatu kati yao wana msimamo mmoja.
Ama tukichunguza katika kitabu cha ndugu Juma tunakuta ameeleza maana ya Jamhur kinyume na hivyo. Ameieleza "Jamhur" katika mtindo usioelezwa katika vitabu vya Shari'ah. Miongoni mwa udhaifu alioutaja ndugu Juma katika kueleza maana ya "Jamhur" ni vile alivyoeleza kuwa (tunasema kwamba kusema kwamba kauli ya muandamo mmoja ni kauli ya Jumhuri ya Umma, ni jambo la kufikiriwa.). Sisi tunasema kwamba kitu cha kwanza cha kufikiriwa ni hii tafsiri ya ndugu Juma katika maana ya neno "Jamhur." Tunamuomba nd ugu Juma asijifanye kama yule kipofu aliyeingia kwenye nyumba ya mtu na kujigonga kwa vitu vilivyokuwemo ndani, kisha akawalaumu sana wenye nyumba. Sasa inafaa kujiuliza ni nani wa kulaumiwa baina ya kipofu na mwenye nyumba? Bila shaka wa kulaumiwa ni yule bwana kipofu kwani vitu vilikwishapangwa akamtupia lawama mwenye nyumba. Kwa hivyo nasi tunamtanabahisha vizuri na mwenye nyumba lakini kwa sababu ya kutokuona kwake ndio ndugu Juma kuwa Wanavyuoni wenye kuaminika wamekwishakuieleza maana halisi ya "Jamhur" katika matumizi ya Shari'ah ingawa yeye kwa makusudi akajitia upofu na kuanza kusema: (naona watu hapa wamekuwa wakipiga kampeni kwa kutumia jina Jumhuri nayo si sahihi.) Kisha akaendelea kusema: (basi atatokea mtu anayetaka kuipamba rai yake, anase ma: "Umma umekubaliana juu ya jambo hili!")[5]
Kama kweli ndugu Juma ni msomi ingekuwa jambo la busara atoe majina ya vitabu vya Wanavyuoni wenye kukubalika waliosema kuwa rai ya kufuata muandamo mmoja sio rai ya Jamhur. Pili tunamuuliza ndugu Juma ni rai ipi aliyoikuta yeye ambayo imetajwa kuwa ni rai ya Jamhur kisha isiwe ni rai ya Jamhur? Ilikuwa ni wajibu wake kama anataka kuikosoa atoe ushahidi wa maandiko na madondoo ili uwe ushahidi. Kwani tunavyojua sisi ni kuwa kila rai iliyotajwa kuwa ni ya Jamhur panakuwa na maandiko yenye kukubalisha jambo hilo , hata kama ipo khitilafu ya baadhi ya Wanazuoni.
Tunamnasihi ndugu yetu Juma kuwa anapojaribu kuelezea mas-ala yoyote ya kielimu, basi ni vyema apite katika njia zake zenye kukubalika kitaalamu wala asidhani kuwa anaweza kufaulu bila ya kupita katika njia hizo. Ni vyema aelewe kwamba asipopita katika njia hizo atapotea. Mshairi mmoja wa kiarabu anasema hivi: "Unatarajia kuokoka (kufaulu) bil a ya kupita katika njia zake (Elewa kwamba) jahazi haiwezi kwenda kwenye nchi kavu." Mshairi mwengine anasema: "Ukiliendea jambo (ukitaka kulifanya jambo) bila ya kupita katika njia zake utapotea (na kuwapoteza wenzako). Na ukiliingia jambo katika njia zake utaongoka (na utaongoza wenzako)."
JAWABU
Ni wanavyuoni wa Sharia gani hio waliosema kuwa Jumhur ni kukubaliana jambo kwa "Maimamu wanne wa Kisunni"?! Yaani mulivyowafahamu nyinyi hao wanavyuoni ni kuwa hawa Waislamu wote tokea Masahaba kauli zao ni mataka tu: Maimamu wane ndio wanye haki ya kuzungumzia dini?!!!
Jumhur linatumika kwa maana tafauti. Inatumika Jumhur ya Umma, na hii ndio Jumhur yenye nguvu. Yaani kitu kilichokubaliwa na waliowengi katika Umma, kuanzia Masahaba hadi Maimamu wa madhehebu zote na hadi leo. Pia linatumika kumaanisha Jumhur ya Kisunni, hii ndio hio mulioitaja nyinyi. Na kuna jumhur ya Mashafi, ya Kiibadhi, ya Kishia n.k, yaani walio wengi katika wanavyuoni wa madhehebu hizo. Kwa hivyo, Jumhur halitumiki kwa maana moja. Ndio maana ukisoma vitabu tafauti vya kifi-qhi utaona ibara kama "Jumhuru ya wanachuoni wa madhehebu fulani au wa fani fulani". Na utakuta Jumhur ya Ummah. Na unaweza kukuta kwamba hii ni kauli ya Jumhur; hapa itabidi umfahamu muandishi je anakusudia Jumhur gani.
Anasema Dr. Al-Zuhaili: "Wamekubaliana Jumhur ya watu wa adab (literature)." Na anasema: "Na wakapinga Jumhur ya Mashafi na Mahanafi". Na akasema: "Wakasema Jumhur ya watu wa Usuli". Anasema Al-Imamu Al-Jitali: "Na hio ni kwa sababu kwa (mtazamo wa) Jumhuri ya watu wa elimu". Na anasema: "..Kwa Mashekhe wetu na Jumhur ya Ummah". Anasema Bakli 'Abdil-Rahman: "Na wakasema jumhur ya Maulamaa wetu (wa Kiibadhi)". Anasema Sheikh Al-Khalili: "Na Jumhur ya Umma wakatoa ushahidii". Haya yako katika kila kitabu unachokisoma taqriban utayakuta, wala mtu mwenye elimu yake hayaulizi.
Ama kama Jumhur ni makubaliano ya Maimamu wane wa Kisuni, basi jumhur haitokuwa hoja kamwe, kwani Maimamu wane wametanguliwa na vigogo wengi katika Masahaba na wafuasi wao na Maimamu wakubwa waliokuwa mabingwa sana. Na wote hawa walikuwa na fikra tafauti na za Maimamu wane: yaani mwengine hukubaliana na mwengine hutafautiana. Wametangulia kabla yao akina Jabir bin Zaid na wanafunzi wake; Al-Hasan Al-Basari na wanafunzi wake; Al-Awzai na madhebu yake; Mafaqihi wa Madina; wa Iraq; wa Sham kwa maelfu. Kwa hivyo, kama jumhur:
1) Ni kauli ya Maimamu wane wa Kisuni, itakuwa haina nguvu kwani Umma uliowatangulia ni mkubwa na ulikuwa na vigogo ambao walisifika kushinda wote waliokuja baada yao.
2) Kama ni idadi ya madhehebu, basi madhehebu zenye kufunga kwa miandamo yao leo na zamani ni watu wa madhehebu zote taqriban. Miji ya Pakistan, Bagladesh na India yenye Mahanafi wengi wanafata miandamo yao. Misri ambako Mashafi - nadhani - ndio wengi wanafata muandamo wao. Nchi za Afrika Magharibi zenye Malik wengi pamoja na nchi za Afrika Kaskazini za Kiarabu zenye Malik wengi, zinafata miandamo yao. Nchi za Ghuba, Iraki, Sham na Al-Yaman, Mashariki ya mbali wote hawa wanafata miandamo yao, na waliowengi katika nchi hizo ni Masunni wa madhehebu nne. Kwa hivyo, bado naendelea kusema kwamba kudai kuwa kauli ya muandamo mmoja ni kauli ya Jumhuri ya Umma, ni jambo la kufikiriwa.
MNAEMA
Tukiendelea kumfahamisha ndugu Juma juu ya kauli zake alizoziandika kwenye kitabu chake ambazo sio za kielimu ni kule kusema kwake kwamba: (kama tulivyotangulia kusema kwamba mas-ala ya kufunga kwa muandamo mmoja yamo katika vitabu tu: si katika matendo: kimatendo ni Waislamu wachache sana duniani wanaofata rai hio.) Tunamfahamisha ndugu Juma kwamba kitu cha msingi kinachofaa kuzingatia katika mas-ala yoyote yale ya Dini ni ule usahihi wake, sio kuangalia wingi au uchache wa wafuasi. Mfano mzuri ni haya madhehebu ya Ibadhi yenye wafuasi wachache mno duniani ukilinganisha na madhehebu mengine kama Hanafi na mengineyo. Je kwa sababu ya uchache wao ndio unataka kusema Ibadhi hawako katika haki?
Kwa hiyo uchache wa wafuasi sio kipimo cha haki au batil. Ni vyema ndugu Juma awe makini katika uandishi hususan katika jambo la kujenga hoja, asikubali kutawaliwa na taasub za aina hizo.
JAWABU
Hapa nakubaliana na nyinyi 100%. Na hilo nilikwisha kulisema katika kitabu na humu kabla yakufika hapa pia nimelisema. Kitabuni nilisema: Kwa hali yoyote ile, mimi sisemi kwamba kilichosawa ni kinachosemwa na Jumhuri,( laa): sisemi hivyo, bali ninachosema ni kuwa kilicho sahihi ni chenye ushahidi madhubuti uliojengeka juu ya misingi ya kielimu. Na humu katika jawabu hii, nimekwambieni hivyo kwamba je uchache wa Salafia unawafanya kuwa hawako sahihi?! Na nyinyi mukaniambia je uchache wa Maibadhi unawafanya kuwa hawako sahihi. Kwa hivyo, nukta hii tumekubaliana. Lakini tumetafautiana katika tafsiri ya neno Jumhur.
Ama kauli yenu: "Pili tunamuuliza ndugu Juma ni rai ipi aliyoikuta yeye ambayo imetajwa kuwa ni rai ya Jamhur kisha isiwe ni rai ya Jamhur?" inaonesha hamutaki kusoma: munataka kukosoa tu. Mara ngapi utakuta vitabuni kuwa hii ndio rai ya Jumhur kisha ukisoma kitabu cha pili utakuta rai kinyume kwamba ndio rai ya Jumhur. Kwa mfano, mas-ala ya kuziletea ta-awil Aya za Sifat. Al-Asha'ira wanadai kuwa huo ndio mwenendo wa Al-Salaf (Masahaba, wafuasi wao na Maimamu wakubwa wakiwemo wane); wakati Salafiyya wanadai kutokuziletea ta-awil Aya hizo ndio mwenendo wa Al-Salaf na Maimamu. Na wote wana ushahidi wao wakimaandiko. Bali utakuta kwamba Umma umekubaliana juu ya hili wakati ni kitu chenye khilafu. Kwa mfano, utakuta mara nyingi kwamba "Umma umekubaliana kuwa Hadithi za Al-Bukhari na Muslim zote ni sahihi". Halafu tunakuta Maulamaa wengi, kama Ibn Taymiyya, Ibn Al-Qayyim, Al-Albanni, Al-Qannubi, Ibn Al-Jawzi na mamia ya Maimamu wa Kisuni, wanazidhoofisha baadhi ya Hadithi hizo. Sasa hayo makubaliano ya Umma yako wapi? Kwa hivyo, ndugu zanguni, kwa ujumla vitabu vya binaadamu vyote vina makosa. Haitoshi mtu kutoa hoja kuwa kuwa fulani kasema; ni lazima utafute ukweli wenyewe ukoje.
MNASEMA
Mukhtasari Wa Nukta Muhimu (1) Msimamo wa kufunga na kufungua kwa muandamo mmoja duniani ndio rai ya Jamhur. Wala si rai itokayo kwa Shaykh Naaswir Bachuu. Ndugu Juma hakuwa makini katika kukisoma kitabu alichokiandika Shaykh Naaswir Bachuu: "Kuandama Kwa Mwezi" uk 162 - 163. Wafuatao ni baadhi ya Mashaykh wa Afrika Mashariki waliowahi kubainisha jambo hilo :-
JAWABU
Si kweli huu si msimamo wa Jumhur ya wanavyuoni wa Umma, bali hata ya wanavyuoni wa Kisunni bali hata ya Maimamu wane wa Kisuni. Ama wanavyuoni wa Umma, leo Umma una madhehebu nane kuu: nne za Kisuni, Salafiyya, Ibadhi, Shia Imamiyya Ithnashariyya na Zaidiyya. Wenye msimamo huu kimatendo ni baadhi ya Salafiyya walio nje ya Saudia. Ama wale wa Saudia walikuwa na msimamo huo na baada ya kuuchunguza kupitia kwa wanavyuoni wao wakuu kama Sheikh Bin Baz na Ibn 'Uthaimin na Bodi ya wanavyuoni wakuu, wameweza kugundua kuwa msimamo huo ni makosa na kwahivyo wamebadilisha msimamo huo na sasa wanafunga kwa mujibu wa muandamo wao. Ama nchi zenye Madhehebu za Hanafi na Malik, Maulamaa wao pia wanafata miandamo ya nchi zao. Bali Al-Imamu Malik mwenyewe kuna riwaya mbili juu ya Msimamo gani alifata na riwaya kwamba kila mtu na muandamo wake ndio riwaya iliopokewa huko Madina ambako yeye mwenyewe Al-Imamu Malik alikuwa akiishi. Kwa hivyo, narejea tena kwamba dai kwamba msimamo wenu ni msimamo wa Jumhur - hata kama yuko aliyeandika hivyo - basi ni dai la makosa na vitabu vimejaa makosa tele, kitu muhimu ni tahqiq: sio kuchukua tu fulani kasema.
Ama kudai kwenu: "Ndugu Juma hakuwa makini katika kukisoma kitabu alichokiandika Shaykh Naaswir Bachuu" kunaonesha kuwa nyinyi hamukuwa makini katika kukisoma kitabu changu wala cha Sheikh Nassor, kwani nilichokisema mimi ni kuwa huu ni msimamo mpya kwa kwetu Afrika ya Mashariki, na hivi ndivyo alivyosema Sheikh wetu Nassor Bachoo pia. Nimekupeni marejeo katika sehemu mbili redieni mutazame. Kwa hivyo, nyinyi munanibandika kitu ambacho sikukisema.
MNASEMA
i) Al-Marhuum Shaykh Juma 'Abdul-Waduud wa Zanzibar katika kuelezea msimamo wa kufunga pamoja alisema ifuatavyo: "Hii ni rai nayo na wengi wamesema (hivyo) kama Imamu Malik, Ahmad na kundi kubwa la Hanafi."[7]
ii) Shaykh Abdillahi Naaswir wa Kenya ameeleza yafuatayo: "Wako wanaosema kwamba mwezi ukionekana mji mmoja, basi Waislamu wengine popote walipo wafunge. Hayo ni maoni ya Hanbali, Maliki na Hanafi" (Imenukuliwa kutoka kitabu chake Swaum--Nguzo Ya Nne uk. 22 - 23 chapa ya 1985.).
JAWABU
Kuhusu Al-Imamu Malik, nimeshakujibuni kwamba hakuna uthibitisho kwani riwaya kutoka kwake zinagongana. Na wanavyuoni wa madhehebu yake wametafautiana, lakini pia kusema kwamba walio wengi ni wenye kusema kuwa tufate muandamo mmoja ni kitu cha kufikiriwa kwani Ibn Rushd Al-Qurtubi - naye ni katika vigogo wa Kimalik - anasema: "Na wakakubaliana kwamba hilo halizingatiwi katika miji ilio mbali mbali kama Al-andalus (Spain) na Hijaz (Saudia)." Na haya pia yamenenwa na Ibn Abdil-Barri - naye ni katika Malik pia. Na wanavyuoni wa Kihanafi wametafautiana - kama tulivyoeleza katika kitabu - lakini hadi leo hii wanachokitendea kazi Mahanafi na Malik ni kufata miandamo yao kama tunavyoshuhudia katika nchi zao.
MNASEMA
iii) Al-Marhuum Shaykh Hemed bin Juma bin Hemed -aliyekuwa Mufti Mkuu Wa Tanzania Katika hotuba yake iliyonukuliwa neno kwa neno na gazeti la Al-Jihaad toleo No: 4 la tarehe 18/03/1994 sawa na 6/Shawaal/1416 lililotolewa na MSAUD. Katika maelezo mengi aliyoyatoa Shaykh Mkuu huyo kwenye kadhia iliyosababisha kuandama mwezi siku iliyo ikiaminika kuwa ni mwezi (tarehe) 28 ya Ramadhaan alikuwa na haya ya kusema:
"Nyinyi Waislamu wezangu, mwaniambia mimi, kwa ile tukio lenyewe lote, kadhia nilivyoeleza, mwaweza nambia nimewafungisha siku ishirini na nane? Basi tumefungua, Alhamdulillah rabbil aalamin. Linalofuata, mimi nitoe shukrani kubwa kwa watukufu, kutusaidia namna hiyo, na kuondosha tatizo hilo Pia nashukuru sana, kwa bahati kubwa tuliyoipata mwaka huu, ya kihistoria, kufungua siku moja, sisi na wa Saudia, Cairo na Muscat Oman na wapi, kufungua siku moja, nadhani kihistoria, mimi mpaka leo, nina miaka, huu wa sitini na sita, lakini sikumbuki kupata bahati hii. Sikumbuki kupata bakhti hii. Nimemuuliza mzee wangu, Mzee Gumsani, una miaka mingapi, ananiambia themanini na nne, sijui themanini na ngapi! Je iko siku umebahatika hivyo, asema bado sijapata. Je, bahati iliyoje hii? Hadhi kubwa tuliyoipata ya kufungua siku moja, wa Saudia, Cairo, Maskati Oman na miji kadha kadhaa ya Kiarabu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Aiendeleze bahati hii, ili kuimarisha umoja huu. Mungu ajaalie 'Arafah pia iwe moja. Ndio zina matatizo, na 'Iyd ya mfunguo mosi iwe moja. Matatizo haya yaondoke InshaAllaah!" Mwisho wa kunukuu.
JAWABU
Haya! Hoja yenu iko wapi hapa?! Anachokizungumzia Sheikh Hemed ni kuwa watu mara hio waliuona mwezi muandamo sawa; wakafunga sawa: si kwamba mwezi ulionekana sehemu moja watu wa miji yote wakafunga.
MNASEMA
(2) Imeshawahi kutokezea mara nyingi dunia nzima (au sehemu kubwa ya dunia) kufunga na kufungua kwa pamoja, yaani katika siku moja. Mfano mzuri uliowahi kutokea ni huo hapo juu alioueleza Mufti Mkuu Shaykh Hemed bin Juma katika tokeo la mwaka 1994. Pia katika mwaka wa 2007 takriban dunia nzima ilifunga siku moja ya tarehe 13/09/2007.
JAWABU
Haijapata kutokea dunia nzima kufunga siku moja, wala hata sehemu kubwa zaidi ya dunia; na hilo haliwezekani kifaki wala kijografia. Lakini inawezekana nchi nyingi zikafunga pamoja. Na huu sio mjadala wetu: mjadala wetu ni je walifunga kwa kufata muandamo wan chi moja au walifunga kwa miandamo yao.
14
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA KUMI NA NNE
UFAFANUZI WA AYA ISEMAYO : ATAKAYEUHUDHURIA MWEZI AFUNGE!
MUNASEMA
14.Ufafanuzi Wa Aya Isemayo:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ "Atakayeuhudhuria mwezi afunge!" (2: 185)
Uchambuzi wa neno "shahida" na neno "Shahra"; baadhi ya watu wamedhani kwamba maana ya shahida ni 'kuona kwa macho' na neno Shahra wanadhani kuwa ni 'mwezi - muandamo.' Kwa mujibu wa Wafasirina takr iban wote wamelifasiri neno 'shahida' kwa maana ya "kuwepo" au "kuhudhuria" wala sio maana ya 'kuuona mwezi' hata Shaykh Muhammad 'Aliy Assaabuniy ameona ni makosa kitafsiri kulifasiri neno hilo kwa maana ya "Kuuona mwezi muandamo" kama alivyosema:: 27) "Na wala sio maana ya neno 'shahida' (liliyomo katika Aya hiyo) kwa maana ya kwamba: 'ameuona mwezi." Neno 'shahra' lililomo katika Aya hiyo linaleta maana ya 'mwezi - siku' yaani 'month' kwa lugha ya Kiingereza. Ni mwezi unaoashiria tarehe kuanzia 1 mpaka 29 au 30. Wala neno hilo halina maana ya 'mwezi-sayari' yaani 'crescent' au 'moon' kwa lugha ya Kiingereza.
JAWABU
Kama Shahida ina maana ya kuhudhuria tu, basi maana itakuwa "Atayekuwepo katika mji wa mwezi (month). Na kama ni hivyo, hii ni dalili kwamba kuna miji myengine bado hakuna mwezi (month) kwani Aya imekuja kwa njia ya mafhumu Al-Shati na mafhumu hii ni dalili katika dalili za Kisharia. Na kwa maana hio, itakuwa kuna sehemu mwezi bado haujaonekana; wanaoamrishwa kufunga ni wale ambao mwezi (month) umewaingilia kwa kuuona mwezi (Crecent). Tafsiri yenu inaupa nguvu msimamo wetu: si msimamo wenu. Pili wanavyuoni walioifasiri Aya hio kwa maana ya kuona wako wengi kama nilivyotaja baadhi yao katika kitabu na nitanukuu tena baadae.
MNASEMA
Kitu muhimu ni kuelewa kwamba maneno mawili hayo yaani 'shahida' na 'shahra' yaliyomo katika aya hiyo, yana maana tuliyoieleza hapo juu na ndivyo walivyoeleza Wafasirina wakubwa wote. Ni vyema mtu anapoingia katika mjadala kama huu atoe madondoo sahihi yenye kukubalika sio kuingiza fikra zake tu, hususan katika suala hili la tafsiri. Tukianza kutumia utamaduni huo wa kila mmoja kubuni tafsiri yake mwenyewe na tukaziacha tafsiri za Wanazuoni wenye kutegemewa, jambo hilo litatufanya tuwe na idadi kubwa ya wafasiri 'bandia' ambao sio wafasiri wa kweli.
JAWABU
Wafasirina bandia wamejaa sasa huko Zanzibar, ndio maana ikawa munanukuu kanuni za kiusuli na kuziweka si mwahala mwake bali hata kuzifasiri pia zinakushindeni munafasiri sivyo, halafu munataka kuingia katika mijadala ya elimu kama hii. Pili: Kinachotazamwa si tafsiri za wanavyuoni tu, hususan wasio Masahaba, bali kinachotazamwa ni dalili walizozitoa. Isipokuwa pale walipokubaliana ndio huwa kuna ulazima wa kufata: sio walipotafautiana. Tatu: Kama nilivyosema Wafasirina na Maulamaa wakubwa Mujtahidun walioifasiri Aya hio kwa maana ya kuona wako wengi kama tutavyonukuu maneno yao.
MNASEMA
Vile vile ukizingatia neno 'shahra'﴿ الشَّهْرَ﴾ utaliona katika herufi yake ya mwisho ambayo ni 'Re' imetiwa 'fat-ha' hio haina maana kwamba neno hilo lina maana ya 'mtendwa' kama wanavyodhania baadhi ya watu. Ingaw aje neno hilo limemalizikia 'fat-ha', lakini halina maana ya 'mtendwa' bali neno hilo linaashiria maana ya 'wakati'. Ni muda maalumu kama mfano mtu akisema: "Nitakuja mwezi wa Ramadhaan" hapa hakuna kitu chenye kuonekana bali muda au wakati tu Kinyume na akisema: "Nimeuona mwezi" hapa ndio itakuwa neno 'mwezi' ni 'mtendwa.' Kwa hiyo, wanaotumia Aya hiyo kwa maana ya 'kuuona mwezi kwa macho' sio sahihi kama alivyothibitisha hayo Mwanachuoni - Mufasir katika tafsiri ya 'Al-Kashaaf'. Na vile vile katika kitabu: 'Rawaaiul-Bayaan' yameelezwa hayo hayo.
Kinyume na maneno ya ndugu Juma aliposema: ((Aya hii inawezekana kuchukua tafsiri zote: kushuhudia kwa maana ya kuona na kushuhudia kwa maana ya kuwepo katika mji. Na zote zinakubalika kwa mujibu wa fani za tafsiriInasikitisha sana mar a nyingi kumuona ndugu yetu Juma anavyotoa tafsiri ya baadhi ya Aya za Qur-aan bila kuwapa nafasi Mashaykh wenye kutegemewa katika ulimwengu wa Kiislam. Anachokifanya yeye ni kuingiza fikra zake binafsi katika kufasiri Aya za Qur-aan tukufu. Kitendo ambacho hakikubaliki. Kwani ingekuwa inakubalika hali hiyo bila shaka kusingelikuwa na haja ya kutegemewa tafsiri yoyote, kwani kila mmoja wetu angelikuwa bingwa wa kubuni tafsiri aitakayo mwenyewe - jambo ambalo lingetufikisha pahala pabaya na baya zaidi ni kumsingizia uongo Mwenyezi Mungu katika Maneno Yake Matukufu. Wala hatukusudiwi kwamba hao wafasiri pekee walikuwa kama kwamba wakipata 'Wahyi' na kwamba maneno yao yalikuwa hayawezi kuwa na dosari au kupingwa. La hasha! Kinachokusudiwa ni kuwa anapoingia mtu yeyote katika mjadala wa kutetea hoja juu ya jambo fulani lazima aonyeshe madondoo sahihi yenye kuthibitisha dai lake hilo , sio kutoa fikra zake na zikakubalika. Kinachosisitizwa ni ule umuhimu wa kuonyesha madondoo ya tafsiri ya Aya za Qur-aan alizotegemea sio nafasi ya mtu kutumia akili yake katika maeneo hayo.
JAWABU
Wanavyuoni wa tafsiri hawakukubaliana juu ya suala hili kinyume na munavyodhani nyini. Wako waliosema kwamba neno 'shahra'﴿ الشَّهْرَ﴾ limetiwa fataha kwa kuwa ni dharfu-zaman kama mulivy onukuu nyinyi. Na kuna wengine wengi wanavyuoni wakubwa waliosema kuwa ni 'mtendwa'. Sasa nyinyi ilikuwa mutuoneshe ni ipi kauli sahihi tufate. Anasema Abu Hayyan - baada ya kuitaja hio irabu mulioitoa nyinyi - : "Na wakasema kwamba kunasibika ( kuingia fataha) kwa neno Sha-hr ni kwa kuwa ni (mtendwa). Nayo ni kwa msingi wa kuondoshwa mudhaf na maana ni atayeshuhudia - mtendwa wake akaondoshwa - naye ni mji (misr) au mji (balad)." Na haya yote nilikuelezeni lakini nyinyi hamutazami kilich osemwa: munatazama aliyesema. Kisha Abu Hayyaan akatoa muelekeo mwengine wa neno lililoondoshwa akasema: "Na ikasemwa kwamba kunasibika (kuingia fataha) kwa neno Sha-hr ni kwa kuondoa mudhaf nalo ni neno dukhul". Anasema Mahmud Safi: "(Neno) Al-Shar ni mtendwa, kwa (kukadiria) kuondoshwa mudhaf, na makadirio yake ni dukhulu Al-Shar (kuingia kwa mwezi).
Kwa ufupi ni kuwa wako wanavyuoni waliosema hivi na waliosema vile, tafauti na dhana za ndugu zetu kwamba wanavyuoni wote wamesema kitu kimoja. Na kila tafsiri moja inamuelekeo sahihi. Tafsiri ya kuwa mtendwa hasa ni mudhaf (kaondoshwa), mfano wake ni kama Aya:
﴿وَاسْأَلِ الْقَرْيَةَ الَّتِي كُنَّا فِيهَا وَالْعِيرَ الَّتِي أَقْبَلْنَا فِيهَا ۖ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴾
"Kiulize kijiji ambacho tulikuwamo ndani yake" . Sote tunajua kwamba kijiji hakiulizwi wala hakisemi. Hapa mten dwa pia kaondoshwa na asili yake ni : Waulize watu wa kijiji ambacho tulikuwemo ndani yake". Halkadhalika Aya﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ inawezekana ikawa maana yake ni"Ataye shuhudia miongoni mwenu uingiaji wa mwezi" yaani atayekuwepo katika mji wakati mwezi (month) unaingia. Tafsiri hii - kama nilivyosema - inatupa nguvu sisi. Au ikawa maana ni"Ataye shuhudia miongoni mwenu uingiaji wa mwezi" . Na kwa tafsiri hii, neno shahida litakuwa kwa maana ya kuona. Na - kama invyoleweka - kwamba kuweza kujua ni maana gani neno imekusudiwa, ni pale litapokuwa katika sentensi. Na kama neno sh ahida kwa asili halina maana ya kuona; je haliwezi kuwa na maana hio kwa misingi ya kimajazi zikiwepo Qarina?
MNASEMA
Takriban wafasirina wote wa Qur-aan tukufu wameifasiri Aya hiyo kwa maana ya 'atakayekuwa katika mji katika huu mwezi wa Ramadhaan afunge. Hakuna hata mmoja aliye Mwanachuoni wa kweli aliyeifasiri Aya hiyo kwa maana ya 'atakayeuona' au 'atakayeushuhudia' mwezi afunge. Wala hakuna khitilafu katika tafsiri za Wanavyuoni hao juu ya Aya hiyo. Khitilafu iliyopo ni moja tu: Je mwezi ukiandama sehemu moja duniani italazimu kufunga sehemu nyengine zilizobaki au kila sehemu na muandamo wake?
JAWABU
Kwanza: inaonekana hamukuyasoma maandishi yangu kwa makini wala hamujua mimi naeleza nini. Nilichokisema ni hiki: Wanavyuoni wengi wameifasiri Aya hii, kuwa maana yake ni "Atayeuhudhuria mwezi (Month) basi na-aufunge." Kisha wakabainisha kwamba maana ya atayeuhudhuria mwezi, ni atayekuwa katika makazi yake, yaani si msafiri. Nynyi munanijibu "Takriban wafasirina wote wa Qur-aan tukufu wameifasiri Aya hiyo kwa maana ya 'atakayekuwa katika mji katika huu mwezi wa Ramadhaan afunge". Sasa tafauti iko wapi?!
Kisha mukadai yale yale alioyadai Sheikh Nassor kwamba "Hakuna hata mmoja aliye Mwanachuoni wa kweli aliyeifasiri Aya hiyo kwa maana ya 'atakayeuona' au 'atakayeushuhudia' mwezi afunge". Nalo pia ni kosa kwani nakala za wanavyuoni walioifasiri Aya hio kwa maana ya kuona nimekupeni kwa wingi. Nimesema katika kitabu:
1) Abu Al-Suud - katika Maulamaa wa tafsiri - baada ya kuifasiri Aya hio kama alivyosisitiza Sheikh Nassor Bachoo, anasema: "Na ikasemwa kwamba (maana ya Aya hio ni) mwenye kuushuhudia hilala Al-shahri mwezi muandamo wa mwezi (wa Ramadhani) basi naafunge kama kauli yako (unaposema): 'Nimeshuhudia ijumaa yaani Sala yake (Sala ya ijumaa)." Mwisho wa kunukuu. Ni wazi kwamba kwa mujibu wa Abu Al-suud, kuna kauli ya pili juu ya tafsiri ya Aya hii, amba yo wengine wameshikana nayo. Na bila shaka Abu Al-suud hazungumzii watu wa Afrika ya Mashariki.
2) Ibn Al-arabiy. Anasema: "(Aya hii - yaani "Atayeushuhudia mwezi na-aufunge), inafasiriwa kwa kuushuhudia mwezi (month), nako ni kuuona mwezi muandamo, na vivyo hivyo kasema Mtume (s.a.w.): "Fungeni kwa kuuona na fungueni kwa kuuona." Mwisho wa kunukuu.
3) Ibn Baraka Al-bahlawiy, Al-umaniy, baada ya kuinukuu Aya hio inayosema:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ "Ataye ushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge." Akasema: "Na kushuhudia kuko kwa namna mbili: kushuhudia katika kuuona (mwezi muandamo) na kushuhudia kwa kujua kama kipofu na yule ambaye uoni wake amepungua kwa sababu ya kufichikana kwa (mwezi) au asiweze kuuona mwezi."
4) Abu Zahra kataja tafsiri ya Aya hio:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ "Ataye ushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" kwamba maana yake ni:"Atayeushuhudia miongoni mwenu mwezi muandamo wa mwezi (wa Ramadhani)."
5) Ibn Hazm baada ya kuinukuu Aya:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ "Ataye ushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" anasema: "Atayeuona basi kwa hakika kaushuhudia."
6) Al-Jassas Al-Razi, kaweka mlango aliouita : Babu kayfiyyati shuhudi al-shahri. Hapa Al-imamu Al-jassas, anazungumzia kuandama kwa mwezi ni vipi: nini dhana au mafhum (concept) ya kuandama kwa mwezi Kisheria? Akaanza kwa kunukuu Aya mbili:
Moja : ni Aya inayosema:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" .
Pili : ni Aya inayosema:﴿يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ ﴾ "Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo, sema hivyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na hija" . Kisha akanukuu Hadithi ya Ibn Umar (r.a.), kisha akatoa maelezo mpaka akasema: (Likaonesha hilo kwamba kuuona mwezi muandamo ndio kuushuhudia mwezi (wa siku 29 au 30 yaani month ).
Ni wazi kwamba Al-jassas kaifasiri Aya hii kwa maana ya kuona kwa macho.
Na kabla ya hapa alisema: "Na hukumu zinazopatikana kutoka katika kauli yake (Allah S.W. inayosema):﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" ni kumlazimu kuufunga mwezi yule aliyeshuhudia miongoni mwao. Na kushuhudia kunagawika sehemu tatu: kuujua (kwamba mwezi umeandama), kuwepo katika mji, ..na ikamaanisha pia kwamba aliyeuona mwezi muandamo peke yake basi inampasa kuufu nga." Tazama uzuri maneno haya ya Al-imamu Al-jassas, utaona kwamba kakufasiri kushuhudia kulikotajwa katika Aya kwa tafsiri tatu: moja ya hizo ni kuona.
7) Anasema Al-Imamu Abu Muslim: "Na akauita Allah mwanzo wa mwezi kwa jina la mwezi mzima au pakadiriwe mudhafu (kilichotegemezwa ambacho kimeondoshwa nacho ni Hilal)." Bali Abu Muslim kabla ya hapa kanukuu kauli ya Al-zajjaj akisema "Shahru ni jina la Hilal (mwezi muandamo), ingawa kauli hii Al-imam baadae kaipinga.
8) Sheikh Al-Khalili na Prof Moh'd Bakr Ismail, utaona kwamba dhahiri ya maneno yao katika vitabu vyao ni kuwa Aya hio pia inafasirika kwa maana ya kuona kwa macho, ambapo Sheikh Al-khaliliy anasema hivi: "Na hoja gani basi iliothabiti zaidi na kubwa zaidi kuliko mtu kuuona mwezi muandamo kwa macho yake ambao wajibu wa funga au hukumu ya kufungua zimefungamanishwa nao. Mwenyezi Mungu anasema:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" 9) Ama Prof Moh'd Bakr Ismail yeye anasema kuhusu mtu aliyeuona mwezi peke yake: "Na saumu imemuajibikia peke yake katika hali hii, kwa sababu ya kauli yake Allah (S.W.):﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge".
10) Ibn Uthaimin alipokuwa akielezea tafsiri ya wale wenye msimamo kwamba kila mji na muandamo wake, alisema - kuhusu Aya hio inayosema:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" - maneno haya: "Na inajulikana kwamba haikusudiwi kwa (Aya) hio kw amba kila mtu auone peke yake, basi unatendewa kazi (muandamo huo) katika sehemu (mji) ulioonekana." 11) Al-Sayyid Ahmad Al-Hashimiy, alipokuwa akizungumzia darsa inayoitwa Al-istikhdam katika fani ya balagha, alitoa mfano wa Aya hio:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" kisha akasema: (Makusudio ya mwanzo ya neno Al-shahru (mwezi wa siku 29-30: month, katika Aya hii) ni Al-hilalu (Mwezi muandamo)." Mwisho wa kunukuu.
12) Anasema Dr. Wahbat Al-zuhailiy: "Mfano wa sababu ni kauli yake Allah Mtukufu﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" (basi) kuuona mwezi muandamo ndio sababu ya uwajibu wa kufunga." Je hao wote si wanavyuoni wa kweli? Ama kauli yenu: "Wala hakuna khitilafu katika tafsiri za Wanavyuoni hao juu ya Aya hiyo. Khitilafu iliyopo ni moja tu: Je mwezi ukiandama sehemu moja duniani italazimu kufunga sehemu nyengine zilizobaki au kila sehemu na muandamo wake". Jawabu ni kuwa khilafu ipo, lakini nyinyi munapenda kudai "Wamekubaliana" au "Maulamaa wote wamesema" n.k. Hili ndio tatizo lenu, na si nyinyi tu bali hata wale wenzenu walioko Saudia huo ndio mtindo wao. Hebu rejeeni hizo tafsiri mulizozitoa, kama ya Abu Suud, Abu Hayyan na wengine, mutazame je hamutooana waliosema kuwa maana ya Aya hio tunayoizungumzia hapa ni﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ "Ataye ushudia kati yune mwezi muandamo (crecent) wa mwezi (wa ramadhani" . Sasa kuushudia mwezi muandamo n i vipi?
MNASEMA
Mantiki hiyo ndiyo aliyotumia Shaykh Naaswir Bachuu kila anapotaja tafsiri ya Aya za Qur-aan tukufu huwa anaonesha pahala alipoitoa tafsiri hiyo. Kwa hivyo hakwenda kinyume na kanuni za kielimu na misingi sahihi ya Dini yetu. Alichosisitiza Shaykh Naaswir Bachuu katika Hadiyth isemayo:
(Fungeni kwa kuuona mwezi - muandamo) Ni kuwa Hadiyth hii ni 'aam - yaani ya ujumla, kwa hivyo popote mwezi utakapoonekana na habari hizo zikathibitishwa usahihi wake, basi watu wote wafunge. K adhalika wafungue kama ni mwezi wa kufungua. Pia Shaykh Naaswir ameonesha msimamo wa Wanazuoni juu ya masimulizi ya Kuraib kwamba hayawezi kuwa "hoja sahihi" katika mas-ala haya.
JAWABU
Ama Sheikh Nassor kenda kinyume na kanuni za elimu katika sehemu nyingi za kitabu chake. Kwanza katoa tafsiri na kupinga tafsiri bila kuonesha kwa mujibu wa kanuni za lugha, usuli na nyengine, usahihi wa tafsiri alioichagua: hakuonesha kifani kwanini kakipinga alichokipinga na kukisapoti alichokisapoti. Kwa hivyo, hakuwa na dalili za kielimu isipokuwa fulani kasema; wakati fulani kasema ni hoja ambayo kila kundi inalo. Kinachotakiwa ni kuonesha kuwa hoja hizi ndio sahihi kwa sababu kadha. Ama Hadithi(Fungeni kwa kuuona mwezi - muandamo), tumeshaielezea sana hatuna haja ya kuikariri mara kwa mara. Pia Hadithi ya Kuraib tumeshaielezea na kutoa majibu juu ya tafsiri sahihi ya Hadithi hio, hatuna haja ya kuikariri mara kwa mara.
MNASEMA
Ndugu Juma yeye amezitaja baadhi ya tafsiri za Quran na baadhi ya vitabu vilivyotaja Aya inayoelezewa:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ Akidhania kuwa tafsiri hizo zimeitafsiri Aya hiyo kuwa:"Atakayeushuhudia mwezi afunge." Ukichunguza vyema utaona kuwa ndugu Juma hakuelewa kinachokusudiwa katika tafsiri hizo. Kwanza utaona kuwa kila anapojaribu kulito lea tafsiri neno﴿ شَهِدَ﴾ 'shahida' huliwacha kama lilivyo kwa kusema 'atakayeushuhudia'. Ni kama kusema:"Atakayeushuhudia" maana yake"atakayeushuhudia."
JAWABU
Maana ya kuliwacha neno hilo kama lilivyo, ni kwa sababu wako waliofasiri Shahida kwa maana ya kuwepo; na wako waliofasiri Shahida kwa maana ya kuona. Kwa hivyo, baadhi ya mwahala - kutegemea nakusudia nini - ndio huliwacha kama lilivyo. Lakini kila aliyesoma kitabu changu kaelewa vyema nini nilichokieleza.
MNASEMA
Hebu na tuangalie Wanavyuoni walivyolifasiri neno shahida: Mwanachuoni Dr. Zuhaily ameeleza yafuatayo: "Kuuhudhuria mwezi wa Ramadhaan ni sababu ya kuwajibika kufunga (Swaum) kama ilivyoelezwa katika Qur-aan Tukufu:" Atakayekuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhaan) afunge" .
Dr Zuhaily aliendelea kutoa dalili ya kuonesha wajibu wa kufunga kwa kuonekana mwezi - muandamo kwa kuyanukuu maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pale aliposema:(Fungeni kwa kuonekana mwezi - muandamo) Na jambo la kuonekana mwez i japo na mtu mmoja katika Hadiyth hiyo ni la wote ('aam). Wala hakuna Mwanachuoni yeyote aliyesema kuwa Hadiyth hii inaashiria kila pahala pafuate muandamo wake. Kutegemea maneno matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kuk ubalika kifani, huo utakuwa udhaifu.
JAWABU
kwanza : munatabia ya kutotoa marejeo. Ilikuwa ni jambo la busara munapotaja kauli ya mtu muoneshe kutoka wapi.
Pili : ikiwa Dr. Al-Zuhaili, katika sehemu moja kasema hivyo, sehemu nyengine kasema:"Atayeushudia mwezi na aufunge" . Kuuona mwezi muandamo ndio sababu ya wajibu wa kufunga. Kwa hivyo, Dr. Al-Zuhaili pia kaifasiri Aya hio kwa maana ya kuuona kwa macho. Cha kufahamu ni kuwa mwanachuoni anapotoa maelezo kisha akataja Aya au kinyume chake anapotaja Aya kisha akatoa maelezo, basi huwa maelezo hayo ndio anaifasiri Aya hio.
Ama kauli yenu: "Wala hakuna Mwanachuoni yeyote aliyesema kuwa Hadiyth hii inaashiria kila pahala pafuate muandamo wake. Kutegemea maneno matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa udhaifu". Ninasema: munarejea kosa lile lile alililolifanya Sheikh Nassor la kudai hivyo, nami nimekunukulieni ushahidi k uwa wako wanavyuoni waliosema kwamba Hadithi hio "Fungeni kwa kuuona.." ni mahususi kwa watu maalumu nao ni wale waliouona. Anasema Ibn Hajar: (Na w ale ambao hawakuchukua kauli hio, wanasema kwa sababu kauli yake Mtume(s.a.w.w) aliposema:"Mpaka muuone" ni agizo kwa watu maalumu." Anasema Al-san'ani: "Na ikasemwa kwamba (Muandamo wa mbali) hauzingatiwi (mbali), kwa sababu kauli yake Mtume (s.a.w.w) aliposema:"Mukiuona" ni agizo kwa watu maalumu." Maelezo haya nyinyi mumeyafumbia macho kwani hamukuyapenda.
Ama kauli yenu: "Kutegemea maneno matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa udhaifu" inanifanya nisijue mukitakacho. Ninanapokupeni ushahidi wa kifani juu ya tafsiri fulani, munasema Juma Mazrui anafasiri kwa rai yake wala hategemai mael ezo ya wanavyuoni; mukipewa maneno ya wanavyuoni munasema "Kutegemea maneno matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa udhaifu". Sasa munataka vipi, hebu twambieni mutakavyo!
MNASEMA
Shaykh Al-Amin 'Aliy Mazrui: katika kuifasiri Aya isemayo:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ ameeleza yafuatayo: "Basi mwenye kuwemo katika mwezi huu na afunge." Kisha akaendelea kusema: "Muradi wa 'mwenye kuwamo katika mwezi huu' ni ambaye hakuwa sa farini." (uk. 65)[9][9] Mwanachuoni Shaykh Al-Jassas katika kitabu chake Ahkamul-Qur-aan ameweka mlango unaitwa Kayfiyati Shuhudi Shahri "mlango unaolelezea namna ya kuhudhuria mwezi" Shaykh Al-Jassas akaanza kunukuu aya mbili, ya kwanza "Famman Shahida minkum na aya ya pili "Yas-alunaka 'anil-ahilah" Ifuatayo ni tafsiri sahihi ya aya hizo kama ilivyo katika vitabu vya tafsiri, tafsiri ya aya ya mwanzo:"Atakayekuwa katika Mji katika mwezi huu mwezi (wa Ramadhaan afunge" . Tafsiri ya aya ya pili:"wanakuuliza miezi miandamo sema hiyo ni (vielelezo vya) nyakati kwa ajili (ya mambo) ya watu na hija zao" .
JAWABU
Maneno ya Sheikh Al-Amin hayana upinzani. Na - kwa ujumla - maneno hayo na yalio mfano hayo yalikuwa hayana maana kwani mimi katika kitabu changu sijapinga kwamba kuna wanavyuoni walioifasiri Aya hio kwa maana ya kuwa katika mji. Bali nilisema: Wanavyuoni wengi wameifasiri Aya hii, kuwa maana yake ni "Atayeuhudhuria mwezi (Month) basi na-aufunge." Kisha wakabainisha kwamba maana ya atayeuhudhuria mwezi, ni atayekuwa katika makazi yake, yaani si msafiri.
Kwa hivyo, mimi nanachokipinga ni dai lenu kwamba hakuna mwanachuoni aliyefasiri shahida kwa maana ya kuona: wala sijapinga ukweli kwamba kuna wengi waliosema kwamba neno shahida katika Aya ni kwa maana ya kuwepo katika mji. Bali nilisema kwamba tafsi hii ndio yenye nguvu. Nilisema hivi: Tafsiri hii inapata nguvu kwa kutazama kukabiliana kimaana (Muqabala) - kuliopo katika sehemu ya kwanza ya Aya hii na sehemu yake ya pili. Aya hii inasema: "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu, basi na-aufunge." Neno "Kushuhudia" linatumika kwa maana ya kuhudhuria, na hutumika kwa maana hio na ziada nayo ni maana ya "Kuona" kwani kila muonaji huwa kahudhuria. Sasa "Kuushuhudia" mwezi inawezekana ikawa maana yake ni kuuona kwa macho na inaweza ikawa maana yake ni kuhudhuria kwa maana ya kuwepo katika mji. Sasa ilipokuja sehemu ya pili ya Aya, ikasema:
﴿مَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ ﴾
"Na atayekuwa mgonjwa au kuwa safarini, basi (afunge) idadi (ya siku asizozifunga" katika siku nyengine. " Hapa ikawa tumefahamu kwamba makusudio ya Aya inayosema:"Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu, basi na-aufunge" ni "Atayekuwa katika mji: yaani si msafiri." Na kwa tafsiri hii, Muqabala (opposite au kinyume) utakuwa umepatikana, na maana ya Aya itakuwa hivi: "Huyu ni wajibu kufunga kwa kuwa ni mzima na kwa kutokuwa safarini; na (kinyume chake) yule karuhusiwa kula kwa kuwa ni mgonjwa au kwa kuwemo safarini." Msingi huu wa Muqabala, dhahir ndio msingi wa wale walioifasiri Aya hio kuwa maana yake ni: Atayekuwa katika mji: yaani si msafiri" nao ni msingi madhubuti. Hatimae nikakuta katika tafsiri ya Ibn Jariri Al-ttabari akieleza hivyo hivyo Walillahi Al-hamdu.
Sasa munachokipinga ni nini? Inaonesha hamujui mukisemacho. Ama kuhusu Al-Imamu Al-Jassas Al-Razi, nilisema hivi: Al-jassas Al-raziy, kaweka mlango aliouita: Babu kayfiyyati shuhudi al-shahri. Hapa Al-imamu Al-jassas, anazungumzia kuandama kwa mwezi ni vipi: nini dhana au mafhum (concept) ya kuandama kwa mwezi Kisheri a? Akaanza kwa kunukuu Aya mbili:
Moja : ni Aya inayosema:
﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ﴾
Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge).
Pili : ni Aya inayosema:﴿يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ ﴾ "Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo, sema hivyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na hija" .
Kisha akanukuu Hadithi ya Ibn Umar (r.a.), kisha akatoa maelezo mpaka akasema:(Likaonesha hilo kwamba kuuona mwezi muandamo ndio kuushuhudia mwezi (wa siku 29 au 30 yaani month).
Ni wazi kwamba Al-jassas kaifasiri Aya hii kwa maana ya kuona kwa macho.
Nyinyi maneno:(Likaonesha hilo kwamba kuuona mwezi muandamo ndio kuushuhudia mwezi (wa siku 29 au 30 yaani month) , mumeyafumbia macho kama kawaida yenu, na badala yake mukasema: Mwanachuoni Shaykh Al-Jassas katika kitabu chake Ahkamul-Qur-aan ameweka mlango unaitwa Kayfiyati Shuhudi Shahri "mlango unaolelezea namna ya kuhudhuria mwezi" Shaykh Al-Jassas akaanza kunukuu aya mbili, ya kwanza "Famman Shahida minkum na aya ya pili "Yas-alunaka 'anil-ahilah" Ifuatayo ni tafsiri sahihi ya aya hizo kama ilivyo katika vitabu vya taf siri, tafsiri ya aya ya mwanzo:"Atakayekuwa katika Mji katika mwezi huu mwezi (wa Ramadhaan afunge" . Tafsiri ya aya ya pili:"wanakuuliza miezi miandamo sema hiyo ni (vielelezo vya) nyakati kwa ajili (ya mambo) ya watu na hija zao" . Mwisho wa kunukuu.
Bali kabla ya hapo Al-Jassas kasema kuhusu Aya hio kwamba ina maana tatu; moja yao alisema: "Na ikamaanisha kwamba atayeuona mwezi peke yake basi naafunge". Ni wazi kwamba Imamu huyu anakubali kwamba neno hilo au Aya hio pia inabeba maana ya kuona. Na akasema tena: "Na Waislamu wamekubaliana kwamba Aya hii na Hadithi hio kwamba maana yake ni kuuzingatia uoni wa mwezi muandamo". Yote haya nyinyi mumeyafumbia macho, kwani lengo lenu ni kunusuru rai. Kwa ujumla nilichokipinga si kwamba Aya hio ina maana ya kuwepo katika mji: hili sikulipinga bali nililitilia nguvu. Nilichokipinga ni dai kwamba; HAKUNA WANAVYUONI WALIOFASIRI AYA HIO KWA MAANA YA KUONEKANA MWEZI. Hili nililipinga na nikatoa ushahidi wa wanavyuoni wengi kama ilivyotangulia.
MNASEMA
Ufuatao ni ufafanuzi wa aya hizo. Tunaanza na aya ya mwanzo wanazuoni wengi sana wameitafsiri aya hiyo kwa maana iliyo hapo juu. Ingawa ukilichukua neno mojamoja katika aya hiyo na ukaliangalia katika makamusi ya Kiarabu utalikuta lina maana zaidi ya moja, utaratibu huu sio mgeni katika lugha ya Kiarabu, kanuni ya lugha inasema: "Neno halina maana (moja) mpaka liwemo ndani ya sentensi", kwa hivyo neno "Shahida" liliyomo ndani ya aya hiyo lina maana ya "Kuwepo" (sio maana ya kuona). Na neno "Shahri" lina maana ya mwezi siku, sio maana ya mwezi sayari hiyo ndiyo tafsiri sahihi ama kuitafsiri kwa maana ya "atakayeuona mwezi na afunge" hiyo ni tafsiri ya kuilazimisha.
JAWABU
Natukubaliane kuwa hio ndio tafsiri sahihi, japo kuwa hamukuonesha ushahidi wa elimu, tatizo ni kuwa tafsiri hio itawapa nguvu wale wenye kudai kwamba kila watu na muandamo wao. Kwani ikiwa tafsiri ya neno "Shahida" liliyomo ndani ya aya hiyo lina maana ya "Kuwepo" na tafsiri neno "Shahri" lina maana ya mwezi siku" maana itakuwa "Atayekuwepo katika mwezi siku naafunge" hii mufhumu mukhalafa yake - na kwa hapa ina nguvu kwani ni mafhumu Al-Shart - itakuwa yule ambaye hayupo katika mwezi siku basi asifunge - anayeamrishwa ni aliyepo. Na kusema hivi haiwezekani ila iwe kuna sehemu mwezi siku tayari umethibiti; na kuna sehemu bado haujathibiti. Na hili litawapa nguvu wapinzani wenu. Sijui munafahamu au munanukuu tu?!!!
MNASEMA
Ama uchambuzi wa aya ya pili kama ulivyo katika vitabu vingi vya tafsiri, kwanza wameeleza sababu ya kuteremshwa aya hiyo ni kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameulizwa na kama aya yenyewe inavyothibitisha tokeo hilo Na vilevile Wanazuoni hao wakaeleza kuwa kilichoulizwa hapo ni hali halisi ya mabadiliko ya miezi. Kwa maelezo zaidi rudi katika tafsiri, itakutosha tafsiri ya Dr. Zuhaily. Kwa mantiki hiyo hapa hapazungumziwi kuwepo miandamo mingi wala kuwepo muandamo wa kisheria, wala Aya hii maana ya kuwa kila nchi ifunge na ifunguwe kwa mujibu wa matlai yao , vile vile Aya hii haina maana ya kuwa ni "Khaas" katika zile Hadiyth zilizotaja kwa ujumla kuhusu suala la kufunga na kufungua.
JAWABU
Sasa munaanza kuchanganya mambo. Aya ambayo imesemwa kushuka kwa sababu hio ni Aya "Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo": si Aya:"Atayeushudia mwezi" . Na maudhui yetu hapa ni kuhusu Aya"Atayeushudia mwezi" . Mara mumerukia kwengine. Kwa ufupi, ni kuwa tumeshajibu kwamba wanavyuoni hao wametegemea Hadith maudhui (Hadithi ya kutunga) kwa ushahidi tuliotoa wa sanad na kwa ushuhuda wa wanavyuoni wengine. Nakukumbusheni kaul i yenu muliposema: "Kutegemea maneno, matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa ni udhaifu". Sasa nyinyi mulitumia fani gani hata mukaitegemea sababu hio ya kutremka Aya ambayo sanad ya riwaya y ake ina wapokezi waongo.
MNASEMA
Alichokisisitiza Shaykh Al-Jassas katika kitabu chake ni ule wajibu wa kufunga na kufungua kwa kuzingatia "Suala zima la kuonekana mwezi" Na ndio maana Shaykh Al-Jassas akanukuu Hadiyth zenye kutaja wajibu wa kufunga na kufungua kwa kuonekana mwezi. Na Hadiyth zote hizo zimetaja jambo hilo kwa njia ya Ujumla, yaani hukumu yake inawaenea Waumini wote popote walipo. Katika kuielezea kauli hii ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Shaykh Al-Jassas anasema: "ni jambo linaloeleweka kuwa kauli ya Mtume(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo:(Fungeni kwa kuonekana mwezi na Fungueni kwa kuonekana mwezi) ni ya ujumla haiwahusishi watu wa nchi moja peke yao pasi na wengine.
Na vilevile msimamo kama huu wa kufunga pamoja ameuweleza Dr. Zuhaily katika kitabu chake Al-Fiqhul- Islamiy.
JAWABU
Hatupingi kwamba kuna wanavyuoni waliosema hivyo, wala mimi katika kitabu chamgu sikupinga hilo; tunachodai ni kuwa hoja zao ni dhaifu ukilinganisha na hoja za kundi lapili. Na Hadithi hio tumeshaielezea, tusikariri yayo kwa yayo mara elfu.
15
MUANDAMO WA MWEZI
HOJA YA ABU AMMAR NASSIR AL-MAZRUI JUU YA MASIMULIZI YA KURAIB
MNASEMA
Hoja Ya Abu Ammar Nassir Al-Mazrui Juu Ya Masimulizi Ya Kuraib Katika kitabu cha ndugu Juma chapa ya pili uk 143 amenukuu hoja nyengine ambayo haikuwemo katika chapa yake ya kwanza. Katika hoja hiyo ya Abu Ammar imegundulika kwamba imejengeka katika msingi wa ibara isemayo: "inawezekana." Kwa hivyo ni ibara yenye utata (ihtimal) - yaani inawezekana hivi au kinyume na hivi. Ibara kama hizi zimeshaelezewa mara nyingi kuwa sio za kuzijengea hoja sahihi kama walivyothibitisha hayo Wanavyuoni wa Usulul-Fiqhi. Ingawa hoja hiyo imesemwa na Mwanachuoni mkubwa anayeheshimika sana na InshAllaah Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atamlipa kwa jitihada yake hiyo. Lakini kama alivyoandika ndugu Juma katika kitabu chake baada ya kuinukuu hoja moja ya Shaykh Naaswir Bachuu iliyomo ndani ya kitabu chake uk 37, hatimae kuonyesha mshangao katika hoja hiyo na kuandika hivi: (shubuhati kama hizi hazifai kujadili mambo ya kielimu.)
Nasi tunasema shubuhati kama hizi za kina Abu Ammar hazifai kujadili mambo ya kielimu.
JAWABU
Lakini kwa bahati mbaya hamukunukuu yote yaliosemwa. Mumenukuu kipande kidogo kisemacho "Inawezekana", kisha mukamuacha msomaji hajui kilichoanzia wala kilichokwishia. Nami nakunakilieni sehemu hio yote ili ijulikane Abu Ammar katoa hoja gani na kujibu nini na udhafu uko wapi. Maudhui ilianza hapa: UPINZANI WA TATU: Anaendelea Sheikh Bachoo na uchambuzi wake wa riwaya hio, anasema: "Pili kama ingalikuwa hakuna dhana ya kuwa mwezi ukionekana popote watu wafunge, Ibnu Abbas (r.a.) asingekuwa na haja ya kumuuuliza Kurayb juu ya habari za mwezi wa Sham kwa kusema: "Kisha (Ibn Abbas) akataja (habari) ya mwezi na akasema: "Ni lini mliuona mwezi?...akasema: "Wewe umeuona?"
Hio ndio hoja nyengine ya Sheikh Bachoo, kwamba lau hakuna dhana ya kuwa mwezi ukionekana popote watu wafunge, basi Ibn Abbas asingekuwa na haja ya kumuuliza Kuraib "Lini mumeuona mwezi!!!" Ninasema: Enyi walimwengu wenzangu tazameni hoja za kielimu hizo!!!!!!! Kwani nyinyi Wazanzibari kabla ya kuja fikra hio ya Sheikh Nassor Bachoo ya kufunga kwa muandamo mmoja, mulikuwa hamuwaulizi watu wanaotoka nchi nyengine masuala kama hayo wanapokuja kwenu na nyinyi muko kati kati ya mwezi pamoja na kwamba nyote zamani mukifata muandamo wenu? Sasa kama nyinyi mulikuwa mukiuliza suala hilo hilo kwanini Ibn Abbas na yeye asiulize hata kama dhana hio haipo? Mimi binafsi nina kawaida ya kuwauliza wageni walioko nchi hii ninayoishi suala hilo, na natarajia kwamba pia nimewasikia watu wengi wenye kuwauliza wageni suala hilo. Kwa hakika shubuhati kama hizi hazifai katika kujadili mambo ya kielimu. Kwa ufupi ni kuwa hata kama dhana hio ilikuwepo, dhana hio inabomolewa na kukataa kwake - Ibn Abbas - kuukubali mwezi wa Sham, na kujenga hoja kwa Hadith marfu'u kwamba hayo ndio mafunzo ya Mtume(s.a.w.w) kwao.
Bali tunasema kwamba suala la Kuraib aliposema: "Je hutosheki kwa kuuona Muawiya na kufunga kwake" inawezekana ikawa na maana kinyume kabisa na fikra ya Sheikh Nassor, kwani inaweza ikawa ndio hasa inayomaanisha kwamba watu enzi hizo walikuwa hawazingatii muandamo wa mbali, au ikawa jambo hilo lilikuwa halijulikani kamwe, kwa sababu lau ingelikuwa Mtume(s.a.w.w) kafundisha kutendewa kazi muandamo wa mbali au ingelikuwa katika enzi hizo wanazingatia muandamo mmoja tu basi Kuraib asingelikuwa na haja ya kumuuliza Ibn Abbas suali hilo, bali angelimwambia: "Lipeni siku moja iliokupiteni ya muandamo wa Sham." Kwa hivyo, kumuuliza kwake suali hilo ni dalili ya wazi kwamba hakukuwa na dhana ilioenea kuwa mwezi ukionekana popote watu wafunge. Na kwa hivyo, Kuraib alikuwa hajui kamwe nini hukumu ya tokeo hilo.
Sasa sijui udhifu uko wapi katika hoja hio ya Abu Ammar?! Nyinyi baada ya kuchukua na kuijadili ile maana alioisema na ambayo inafahamika anapinga nini na anasapoti ni nini, munachukua ibara "Inawezekana" ndio mukaijadili. Mumewacha Jawhar (kiini) na mukag'an'gania Qushur (magamba).
MNASEMA
Ikumbukwe kuwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika jambo hili la kufunga na kufungua ni ya pamoja ('aam) kwa watu wote. Hakuna kabisa maneno mengine ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yaliyo "sahihi" yenye kutufunza kuwa kila nchi ifunge na ifungue kwa muandamo wake. Kitu kilichoelezwa juu ya mas-ala haya ni upatikanaji wa mawasiliano ya habari za kuaminika katika utaratibu unaokubalika kishari'ah. Maneno ya Abu Ammar yasemayo: "Kwa sababu lau ingelikua Mtume(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kafundisha kutendewa kazi muandamo wa mbali." Hayo ni mane no dhaifu sana Hakuweza kutoa dalili sahihi isiyokua na utata inayoonesha kuwa amri hiyo ya kufunga na kufungua ina mipaka maalum, au ni ya watu maalumu au inahusisha nchi moja na kuacha nchi nyengine.
JAWABU
Dai lenu kwamba: "Hakuna kabisa maneno mengine ya Mtume(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yaliyo "sahihi" yenye kutufunza kuwa kila nchi ifunge na ifungue kwa muandamo wake" si madai sahihi. Ibn Abbaas kaukataa muandamo wa mbali na kunena: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w.". Nakukumbusheni maneno yenu muliposema: "Isipokuwa Sahaba akisema: "Tumeamrishwa kadha" au "Tumekatazwa kadha." Jambo hilo hupewa hukumu ya "Rafii" yaani hio inazingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume(s.a.w.w) .
Ama kusema: "Kitu kilichoelezwa juu ya mas-ala haya ni upatikanaji wa mawasiliano ya habari za kuaminika katika utaratibu unaokubalika kishari'ah", pia yanahitaji muyafafanue. Ama ikiwa munakusudia kwamba mas-ala ya kupokea habari yamo katika riwaya, hilo ni kweli. Lakini riwaya hizo hazikutoa ufafanuzi wowote juu ya je tufunge kwa muandamo mmoja au kumi na moja. Faida inayopatikana katika habari hizo ni kuwa shahidi mmoja anatosha kuthibitisha muandamo. Ama istintaj yenu kwamba Mtume(s.a.w.w) hakuwauliza watowaji habari wapi wanatokea, si isimbat sahihi kwani:
a) Watoaji habari walikuwa wanajulikana watokapo, nalo ni jangwa la Madina.
b) Ni istimbat inayogongana na andiko la wazi, nayo ni Hadithi ya Ibn Abbaas aliposema "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w.".
Ama nakala yenu mulipomnukuu Abu Ammar akisema: "Maneno ya Abu Ammar yasemayo: "Kwa sababu lau ingelikua Mtume(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kafundisha kutendewa kazi muandamo wa mbali." Hayo ni maneno dhaifu sana Hakuweza kutoa dalil i sahihi isiyokua na utata inayoonesha kuwa amri hiyo ya kufunga na kufungua ina mipaka maalum, au ni ya watu maalumu au inahusisha nchi moja na kuacha nchi nyengine". Mwisho wa kunukuu. Kwanza ningekuombeni muikamilishe nakala hadi ilete maana kamili. Alichokisema ni:
Bali tunasema kwamba suala la Kuraib aliposema: "Je hutosheki kwa kuuona Muawiya na kufunga kwake" inawezekana ikawa na maana kinyume kabisa na fikra ya Sheikh Nassor, kwani inaweza ikawa ndio hasa inayomaanisha kwamba watu enzi hizo walikuwa hawazingatii muandamo wa mbali, au ikawa jambo hilo lilikuwa halijulikani kamwe, kwa sababu lau ingelikuwa Mtume(s.a.w.w) kafundisha kutendewa kazi muandamo wa mbali au ingelikuwa katika enzi hizo wanazingatia muandamo mmoja tu basi Kuraib asingelikuwa na haja ya kumuuliza Ibn Abbas suali hilo, bali angelimwambia: "Lipeni siku moja iliokupiteni ya muandamo wa Sham." Kwa hivyo, kumuuliza kwake suali hilo ni dalili ya wazi kwamba hakukuwa na dhana ilioenea kuwa mwezi ukionekana popote watu wafunge. Na kwa hivyo, Kuraib alikuwa hajui kamwe nini hukumu ya tokeo hilo.
Hoja hii kaitoa kujibu maelezo ya Sheikh Bacho aliposema: "Pili kama ingalikuwa hakuna dhana ya kuwa mwezi ukionekana popote watu wafunge, Ibnu Abbas (r.a.) asingekuwa na haja ya kumuuuliza Kurayb juu ya habari za mwezi wa Sham kwa kusema: "Kisha (Ibn Abbas) akataja (habari) ya mwezi na akasema: "Ni lini mliuona mwezi?...akasema: "Wewe ume uona?" Mukhtasar wa haya ni kuwa Sheikh Nassor kakufanya kule Ibn Abbaas kumuuliza Kuraib "Je wewe umeuona" kuwa ni dalili kwamba mwezi ukionekana popote watu wafunge. Na hili ndilo ambalo halina ushahidi, kwa bahati mbaya lisilo na ushahidi la Sheikh Bachoo hamukuliulizia ushahidi; lisilo ushahidi - kama mulivyo dai - la Abu Ammar mumeliulizia ushahidi - huu ni uchambuzi gani?! Kiufupi mimi nimejibu kwamba hata watu wan chi nyengine, huko kwetu Zanzibar na nchi nyengine, watu huulizana suala kama hilo hata kama wanafata miandamo yao. Sote tunajua kwamba hapo Zanzibar watu kabla ya kuanza fikra hio ya kufunga kwa muandamo mmoja, walikuwa wakiulizana hivyo. Kwa hivyo, hio si dalili ya kielimu. Ama jawabu ya Abu Ammar, ni kitu kisichohitaji ushahidi, kwani kama ilikuwa inaeleweka kwamba mwezi wa mbali utendewe kazi mbali, basi Kuraib angelimwambia Ibn Abbaas kwamba "Mwezi umeonekana Sham kabla yenu kwa siku kwa hivyo, muilipe siku moja". Sasa jawabu hii ina udhaifu gani na nyinyi munata watu wa Madina wafanyeje ikiwa siku moja ya Sham hawakuifunga: wasiilipe: iwe basi?!
Jambo ambalo mtu anaweza kulilahidh (kuliobserve) katika kitabu chenu, nikuwa hamunuu kitu kamili au chenye kuleta maana kamili. Wala hamunukuu jawabu zangu zote; munachagua zile muzitakazo mukanuuu kipande kidogo halafu munatoa jawabu zenu zilio mbali na elimu.
MNASEMA
Mwanachuoni Al-Jassas katika kitabu chake Ahkamul-Qur-aan J. 1, uk 305 katika kuieleza kauli hii ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema hivi: "Ni jambo linaloeleweka kuwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo: ((Fungeni kwa kuonekana mwezi -muandamo na fungueni kwa kuonekana mwezi-muandamo)) ni ya ujumla '(aam), inawahusisha watu wa pande zote za dunia na kwamba haihusu watu wa nchi moja peke yao pasi na wengine." Aidha Shaykh Sayyid Saabiq katika kitabu chake Fiqhus-Sunnah J. 1 uk 436 baada ya kuitaja kauli hiyo ya Mtume(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameandika hivi: "Na kauli hii ni agizo la ujumbe linalojumuisha umma wote (wa Kiislam), kwa hivyo yeyote miongoni mwao atakayeuona (mwezi-muandamo) popote pale; kuonekana huko kutakuwa ni kwa wote"
Kwa marejeo mengine zaidi kama haya angalia:-
1. Rawaaiul-Bayan J. 1, uk 211
2. Naylul-Awttar J. 4, uk 195
3. Sharhu Subulu Sawiyah Li Fiqhi Sunanil Marwiyah
4. Fatawa ya BAKWATA uk 110:.11 mada 14/70
JAWABU
Maelezo haya sijui munayanukuu mara ngapi! Maelezo hayo kayatoa Sheikh Bachoo na nimeyajibu nanyinyi munayakariri bila ya kutoa jawabu juu ya maelezo yangu. Nimesema: Jambo la pili: la kutazamwa katika Hadithi hii ni kuwa Khitabu (Agizo: kam a alivyofasiri Sheikh Nassor Bachoo) ya Hadithi hii ni Aam (ya ujumla), kama Sheikh alivyonukuu kutoka katika kitabu cha Al-sayyid Saabiq.
Na sisi tunajibu kwa jawabu mbili: Ya kwanza: ni kuwa: Ujumla wa agizo hilo, umehusishwa na Hadithi ya Ibn Abbas, na k anuni ya kiusuli inaeleza kwamba Al-khaas (Andiko maalumu au specific) ndio inayotangulizwa kuliko Al-aam (Andiko la ujumla), kwa kuwa kwake (hio Khaas) ni ya uhakika kinyume na Aam hakika yake ni (kitu) cha dhana. Kwa hivyo kanuni hapa in atutaka kuitanguliza Hadithi ya Ibn Abbas. Na natija ni kuwa ujumla jamala uliobakia katika Hadithi "Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi" na ambacho tunachotakiwa sote tukifanye kwa mujibu wa Hadithi hii, ni kuwa sote tufunge kwa kuuona mwezi. Ama je muandamo ni mmoja au kila watu wana muandamo wao, Hadithi hii haitoi jawabu hio.
Jawabu ya pili: ni ile tuliotangulia kuinukuu kutoka kwa Sheikh Ibn Uthaimin aliponukuu jawabu ya wale wenye kusema kwamba kila mji una muandamo wake, ambapo walisema kwamba ujumla uliomo katika Hadithi hio, ni sawa na ujumla uliomo katika Aya inayosema:
﴿فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ ﴾
"Sasa waingiliyeni (wake zenu) na tafuteni kile Allah alichokuandikiyeni, na kuleni na kunyweni mpaka ukubainikieni uzi mweupe kutokana na uzi mweusi wa alfajiri, kisha timizeni saumu hadi usiku."
Je hapa Allah anazungumza na watu wote au na watu maalumu? Je kuzungumza huku na watu wote inamaanisha kwamba alfajiri ya nchi moja ikichomoza watu wa nchi zote wajizuie, au kila watu na alfajiri yao? Jawabu yako hapa ndio jawabu yetu kwa maneno ulioyanukuu kutoka katika kitabu cha Al-sayyid Saabiq kwamba Hadithi hiyo"Fungeni kwa kuuona" ni: "Agizo la ujumla linalojumuisha umma wote ( wa Kiislamu) kwa hivyo; yeyote miongoni mwao atakayeuona (mwezi) popote pale; kuonekana huko kutakuwa ni kuonekana kwa wote."
Halkadhalika tunajibu ujumla huo kwa Hadithi inayosema: "Usiku ukitokeza kutoka hapa na mchana ukaondoka kutokea hapa na jua likatua, basi aliyefunga ameshafungua (au na-afungue)."
Na sisi tunauliza je hapa walikuwa wakiambiwa watu wa Makka tu, au wakiambiwa watu wa nchi zote? Kama walikuwa wakiambiwa watu wa nchi zote, je jua likitua Makka au katika mji wowote ule sote tufuturu? Kwa hakika kila aliyejaaliwa kuwa na mtazamo sahihi, anaona kwamba kujenga hoja kwa ujumla wa Hadithi "Fungeni kwa kuuona" kwamba ni ushahidi wa kuwepo muandamo mmoja, ni kujenga hoja juu ya msingi dhaifu sana. Na kwa maana hio, Ibn Uthaimin (Mwanachuoni wa Kiwahabi) akasema kwamba kauli ya kuwa kila watu wana muandamo wao: "Ina nguvu yake kwa mujibu wa lafdhi (yake) na mtazamo sahihi na Qiyas sahihi vile vile: Qiyas cha wakati wa siku kwa (kuulinganisha) na wakati wa mwezi (month). Mwisho wa kunukuu.
Kwa ufupi ni kuwa, ujumla wa Hadithi inayosema "Fungeni kwa kuuona" ni - kama tulivyotangulia kusema - kwamba watu wote ni lazima wafunge kwa kuuona: si kwa kalenda wala kwa jengine lolote. Huu ndio ujumla unaokusudiwa katika Hadithi hio, au ndio ujumla uliobakia baada ya kuhusishwa au kuvuliwa sehemu ya ujumla huo na Hadithi ya Ibn Abbas na Kuraib.
Jambo la tatu: la kutazamwa katika Hadithi hii, ni kuwa Hadithi hii ni Mutlaq (isiofungamanishwa na kitu) wakati Hadithi ya Ibn Abbas ni muqayyad (iliofungamanishwa). Kanuni ni kuitanguliza muqayyad kuliko mutlaq kama usuli unavyoeleza. Kwa hivyo, kila msingi utaoufata utaona kwamba Hadithi ya Ibn Abbas ndio inayotakiwa itangulizwe. Ama waliosema kwamba tufunge kwa muandamo mmoja, ukweli ni kuwa wao waliitanguliza rai kuliko kanuni za tafsiri. Walitazama wakaona kuwa mwezi ni mmoja na unakamilisha safari yake mara moja na kwa hivyo muandamo utakuwa mmoja. Lakini tumeona kwamba huu si muandamo wa Kisharia bali ni muandamo wa Kifalaki: muandamo wa Kisharia tunaupata katika kuzijumisha Hadithi tafauti.
Pili ni kuwa hio ni rai, na ya Ibn Abbas ni Hadithi; na rai haina uwezo wa kuipinga Hadithi. Kama walivyosema: "Rai haina nafasi mbele ya Andiko." Hii ndio jawabu yangu, nanyi mumeiruka kama mulivyoziruka sehemu kubwa za kitabu changu.
AINA ZA IJMA'
MNASEMA
Aina Za Ijma' Kuna baadhi ya watu kama ndugu yetu Juma ambao wamejenga hoja ya kuwepo miandamo mingi ya mwezi kwa vile maneno ya Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) katika kisa cha Kuraib yalinyamaziwa. Hakuna Sahaba yeyote aliyetoa kauli tofauti na ile ya Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu). Jambo hilo limechukuliwa kama ni hoja kwamba Masahaba wote walikubaliana na Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu).
JAWABU
Kwanza : mimi sikusema hivyo. Na ili nieleweke vyema, lazima munukuu maneno yote. Hapa kuna madai ya Sheikh Nassor na jawabu niliomjibu nainukuu ili nieleweke vyema nini nimekisema. Sheikh Nassor alidai kuwa msimamo wao ndio msimamo wa Makhalifa waongofu. Alisema hivi: "Kipindi chao cha ukhalifa kilichukua kiasi cha miaka 30 kabla ya kutokea utatanishi uliopatikana katika masimulizi ya Kurayb; ukijumuisha nyakati zote walizokamata ukhalifa Sayyidna Abu Bakr (r.a.) Sayyidna Omar (r.a.) Sayyidna Uthman (r.a.) Sayyidna Ally (r.a.), utagundua kwamba Uislamu ulikwishaenea sehemu kubwa ulimwenguni kaskazini mwa Afrika kama Misri na Maghrib (Morocco), baadhi ya nchi za Ulaya lakini haikuthibiti kwamba wao waliwahi kuzingatia suala la masafa au matalai katika suala la kuandama mwezi. Jambo la kujiuliza hapa je kwani wao walikuwa hawaelewi kwamba kulikuweko na nchi nyingi zilizokuwa mbali na Makka na Madina ambazo zilikuwa chini ya himaya zao? Mbona hawakueleza kuwa watu wa kila nchi wafunge kwa kuuona mwezi wao." Mwisho wa kunukuu.
Nami nikamjibu hivi: Jawabu ni kuwa: Hizi ni zile ambazo wataalamu huziita Shubuhati, nacho ni kitu ambacho kinaelekea lakini sio muradi. Kwa ufupi ni kuwa jawabu ya madai hayo ni kama inavyofata: Mosi ni kuwa: Kama ilivyokuwa hakuna ushahidi kwamba wao waliwaamrisha watu wasifate miandamo yao, pia hakuna ushahidi kwamba wao waliwakataza wasifate miandamo yao, au kwamba waliwaamrisha kufata muandamo wa Madina. Na kwa hivyo, Al-qutbu anasema: "Masahaba walikuwa hawawaamrishi watu wa miji ya mbali kufunga kwa kufata muandamo wa miji myengine."
Pili : ni kuwa: Marejeo ya Haya ni Hadithi za Mtume (s.a.w.), na tumesema kwamba Hadithi ya Ibn Abbas ndio iliomaanisha kwamba muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali. Na Hadithi ya Ibn Abbas sigha (form) yake ni ya raf'i (Ya kuinasibisha Hadithi hio na Mtume mwenyewe(s.a.w.w) . Kwa hivyo, ikiwa riwaya haikupokewa na Sahaba fulani, haidhurishi kitu madamu mwengine kaipokea na imethibiti. Na wala huu si mlango wa kuwa lazima Hadithi ipokelewe na kundi kubwa yaani iwe mutawatir. Hadithi mutawatir ni sharti katika itikadi: si katika matendo: katika matendo inatosha riwaya kuwa Ahadi, kama Jumhuri ilivyosema: "Hadithi Ahadi inawajibisha matendo wala haiwajibishi yakini (itikadi)." Tatu ni kuwa: Riwaya ya Ibn Abbas, hajulikani Sahaba aliyeipinga, pamoja na kuwa alikuwa Madina - mji wa Masahaba. Kwa hivyo, kunyamaza kwao kwa uchache iambiwe kuwa ni Al-ijmaa Al-su kutiy (Makubaliano ya kunyamaza), nayo ni makubaliano ambayo mmoja husema kitu wengine wakanyamaza wasimpinge. Kauli hii inaelekea zaidi, kuliko madai ya Sheikh Nassor Bachoo, kwani kusema hivi ni kuijenga kauli juu ya msingi unaokubalika Kisharia nao ni msingi wa kuzingatia Al-ijmaa Al-sukutiy (Makubaliano ya kunyamaza), ikiwa hajulikani aliyepinga katika watu wa zama hizo. Kwa hivyo, unapomjibu mtu kwanza uwe umemuelewa. Mimi sikudai kuwa Ijma' Sukutiy ni hoja waliokubaliana wanavyuoni, ba li ni hoja ambayo inafaa ukilinganisha na hoja ya Sh. Bachoo, kwani Ijma' Sukutiy wako wengi katika wanavyuoni, madhehebu na Maimamu ambao wameikubali, wakati madai ya Sheikh Nassor hayakuwa na tegemezi zozote zile.
MNASEMA
Ni vyema kuelewa kuwa Wanavyuoni wameigawa Ijma' kwenye sehemu mbili kuu:
i) Ijma' Sariyh.
ii) Ijma' Sukutii. Ijma' Sariyh Ni Ijma' ambayo Jamhuri ya Wanavyuoni wa Fiqhi wamekubaliana juu ya usahihi wake kwa vile iko wazi, haina utata wowote. Hoja ya Ijma' hii ni madhubuti na yenye kukubalika zaidi mbele ya Umma wa Kiislamu na wala hakuna khitilafu yoyote juu ya Ijma' hii. Katika kuielezea Ijma' hii, Imam Shaffi (Rahimahu Allaahu) anasema hivi: Anachosema Imam Shaffi hapa, juu ya umuhimu wa Ijma' hii kwa ufupi ni kuwa: "Hakuna yeyote atakayeweza kusema (juu ya umuhimu wa Ijma' hii Sariyh) kinyume na vile ambavyo Wanazuoni wote waliv yosema (kuhusu uzito wa Ijma' hii Sariyh). Kwa maneno mengine ni kuwa: "Mwanachuoni yeyote atakayeonana naye na kumuuliza uzito wa Ijma' hii Sariyh bila shaka jawabu ya Mwanachuoni huyo itakuwa ni ile yenye kuthibitisha umuhimu wa Ijma' - Sariyh, kuliko Ijma' - Sukutiy katika hoja."
JAWABU
Maneno yenu: "Wala hakuna khitilafu yoyote juu ya Ijma' hii" si sahihi. Nilikwambieni mara nyingi kwamba muache kusukuma; khilafu juu ya ijma'a hii pia ipo. Lakini mulikuwa museme tu kwamba kilicho sahihi ni kuwa ijma'a ya aina hii ni hoja yenye nguvu kwa mujibu wa dalili zake. Ama khilafu ipo. Pili: munaendelea na tatizo lenu la kunukuu kitu musichokifahamu. Al-Imamu Al-Shafi hasemi hivyo. Kwanza tafsiri mumeikosea: tafsiri ni: Hutosema wala (hatosema) yeyote miongoni mwa watu wa elimu (wanavyoni) kwamba kitu hiki kimekubaliwa na wote isipokuwa kile ambacho ukimkuta mwanachuoni yeyote milele atakwambi (hivyo hiv yo). Hio ndio tafsiri ya maneno hayo, lakini nyinyi - kama kawaida yenu - mumeyavuruga kichwa chini miguu juu halafu munajadili mambo ya elimu. Sasa baada ya hayo, je mumemfahamu nini Al-Imamu Al-Shafi?! Kwanza nataka mujue kwamba maudhui ya ijmaa ni pan asana na ina vipengele vingi sana. Anachokizungumzia Al-Imamu Al-Shafi ni kuwa ni vigumu mtu kudai kuwa jambo hili Umma umekubaliana. Kwani miji ya Kiislamu iko mingi na wanavyuoni ni wengi. Sisi tulio Zanzibar tukiwa na msimamo fulani hatujui kwamba je watu wote wanatusapoti au wako wasiokubaliana nasi. Lakini - anavosema Al-Shafi ni kuwa - unachoweza kudai kwamba haya ni makubaliano ya Umma ni kile kitu ambacho mwanachuoni yeyote ukimuuliza atakujibu hivyo hivyo. Kwa mfano je sala ni wajibu? Huna utayemuuliza ila atakwambia kwamba ni wajibu. Kwa mukhtasar, Al-Imamu Al-Shafi anazungumzia ugumu wa kuthibitisha ijmaa na hili limehusishwa na wengi hata Al-Imamu Ahmad inadaiwa kuwa kasema: "Atayedai ijmaa kasema uwongo".
MNASEMA
Ijma' - Sukutiy Ni makubaliano ambayo mmoja husema kitu na wengine wakanyamaza wasimpinge. Mtazamo Wa Wanavyuoni Juu Ya Ijma' Hii Sukutiy Takriban ukiviangalia vitabu vyote vya Usulul-Fiqh kuhusu Ijma' hii Sukutiy utaona kwamba ni Ijma' yenye khitilafu (mvutano) mkubwa, hakuna maafikiano ya pamoja. Tofauti na Ijma'-Sariyhi ambayo ina makubaliano yenye uzito wa hoja za kutegemewa katika misingi ya Shari'ah. Chanzo cha khitilafu hizi katika Ijma' Sukutiy ni kule kupatikana ndani yake utata; jambo ambalo huifanya hoja yake kuwa dhaifu. Kama kanuni ya Usulul-Fiqhi inavyosema: "Dalili inapokuwa ina maana nyingi huporomoka ushahidi wake." Shaykh Abu Zuhra amesema: Ifuatayo ni tafsiri kwa njia ya maana: "Ijma' Sukutiy (makubaliano ya kunyamaza) ina khitilafu kubwa mbele ya Wanavyuoni wa 'Usulul -Fiqhi.' Kwa kuwa Wanavyuoni wengi hawakuizingatia Ijma' hii ni dalili imara katika mas-ala ya kielimu. Al-Imam Shaffi ni miongoni mwa wale wasioizingatia Ijma' hii kuwa ni hoja, kama alivyoeleza hayo mwanachuoni M. Abu Zuhra katika kitabu chake cha Usulul-Fiqh. Sababu za msingi zilizoifanya Ijma' hii kutokuwa hoja imara - kwa mujibu wa maelezo ya Abu Zuhra ni kule kupatikana (ihtimaalat) tatanishi."
JAWABU
Na hapa naomba murekebishe tafsiri ya maneno ya Abu Zahra, kwani tafsiri muliodai kuwa ni njia ya maana imepoteza baadhi ya maana. Tafsiri ya maneno hayo ni Kwa hakika haifaii kuzingati kuwa kunyamaza ndio kuwafiki, kwani kunyamaza kuna uwezekano kwamba ni kunyamaza kwa kuwafiki; na kuna uwezekano kwamba yeye (mwenye kunyamaza) bado hajafanya ijtihad katika muwafaka, na inawezekana kwamba yeye ka jitahidi lakini ijtihada yake hakumpelekea kutoa (uamuzi wa) mkato kwa kitu chochote. Na kwa uwezekanu mwingi wa namna hii, haiwezekani kukazingatiwa kunyamaza kuwa ni hoja.
Nyinyi mumeongeza maneno Kwa kuwa Wanavyuoni wengi hawakuizingatia Ijma' hii ni dalili imara katika mas-ala ya kielimu. Wakati madhehebu mbili za Kisunni zimeikubali ijma'i hii na mbili zimeikataa. Kwa hivyo, kwa mujibu wa ufahamu wenu wa maana ya neno Jumhur, nusu ya Jumhur imeikubali ijma'i hio. Ukiongezea na madhehebu nyengine kama Ibadhi na wanavyuoni wengine waliotangulia kabla ya madhehebu nne za Kisuni, hutoweza tena kudai kwamba Kwa kuwa Wanavyuoni wengi hawakuizingatia Ijma' hii ni dalili imara katika mas-ala ya kielimu.
MUNASEMA
Shaykh Abu Zuhra baada ya kutaja udhaifu huo aliendelea kusema: "Kuwepo utata mwingi ndani ya Ijma' hii Sukutiy inaifanya Ijma' hii kutozingatiwa kuwa ni hoja." Kwa hivyo, Ijma' inayofaa kutangulizwa katika mjadala wa kielimu ni Ijma' -Sariyhi na wala sio Ijma'-Sukutiy. Ni vyema ieleweke pia, kwenda kinyume (kuikhalifu) Ijma'-Sukutiy sio makosa wala mtu haambiwi kuwa amefanya jambo la ufasiki kama alivyosema Shaykh Saalimiy: "Mwenye kukhalifu (kwenda kinyume na) Ijma' - Sukutiy haiambiwi kuwa ametenda kosa la ufasiki." 24 - 25) Naye Shaykh Abu Zuhra katika kueleza rai zilizopo juu ya Ijma'-Sukuty na kuonesha uzito wa hoja katika ljmai-Sariyhi amesema ifuatavyo: "Rai nyengine inasema (hii Ijmai-Sukuty) nayo ni Ijma' lakini sio sawa (katika uzito wa hoja) kama ilivyo Ijma'-Sariyhi. 205 - 206) Kutokana na miongozo sahihi ya Wanazuoni wa fani ya Usulul-Fiqhi tumeelewa kuwa: Ijma'-Sariyhi ndiyo yenye uzito wa hoja, na hakuna khitilafu juu ya jambo hilo. Pia tumejifunza kuwa kwa upande wa Ijma'-S ukutiy ni Ijma' yenye mzozo mbele ya Wanazuoni kutokana na kupatikana ndani yake tatanishi (Ihtmaalaat).
Kwa maana hiyo hapawezi kutegemewa Ijma'-Sukutiy kama ni hoja katika mjadala wa khitilafu za miandamo ya mwezi. Miongoni mwa Wanavyuoni ambao hawakuzingatia Ijma' hii kuwa ni hoja; mmoja wao ni Imam Shaffi (Radhiya Allaahu 'Anhu) kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Abu Zuhra.
JAWABU
Jawabu ya ujumla ni kuwa mengi mulioyasema hapa tunakubaliana: hatutafautiani. Suala ni kuwa je nyinyi mumenifahamu vipi mimi hata mukanijibu hivi? Mimi nilichokisema ni kuwa dai la Sheikh Nassor kwamba Masahaba walikubaliana kwamba kufunga ni kwa muandamo mmoja ni dai ambalo halina ushahidi wowote juu ya hilo. Kisha ndio nikamwambia kwamba Ibn Abbaas kasema kwa uwazi kwamba "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w." yaani baada ya kuukataa muandamo wa Sham. Na hakuna ushahidi kwamba kuna sahaba alimpinga Ibn Abbaas kwa kusema hivi, bali ni wazi kwamba Masahaba waliokuwa Madina pia iliwafika habari hio ya Kuraib; haielekei kuwa Kuraib alimwambia Ibn Abbaas tu. Na pamoja na hayo hajulikani sahaba aliyepinga jambo hilo. Kwa hivyo, ndio nikasema:
Riwaya ya Ibn Abbas, hajulikani Sahaba aliyeipinga, pamoja na kuwa alikuwa Madina - mji wa Masahaba. Kwa hivyo, kunyamaza kwao kwa uchache iambiwe kuwa ni Al-ijmaa Al-sukutiy (Makubaliano ya kunyamaza), nayo ni ma kubaliano ambayo mmoja husema kitu wengine wakanyamaza wasimpinge. Kauli hii inaelekea zaidi, kuliko madai ya Sheikh Nassor Bachoo, kwani kusema hivi ni kuijenga kauli juu ya msingi unaokubalika Kisharia nao ni msingi wa kuzingatia Al-ijmaa Al-sukutiy (Makubaliano ya kunyamaza), ikiwa hajulikani aliyepinga katika watu wa zama hizo.
Yaani ukilinganisha madai ya Sheikh Bachoo na kauli hii, hii ni bora zaidi kwani Al-ijmaa Al-sukutiy (Makubaliano ya kunyamaza), hata kama hawakukuba liana wanavyuoni juu yake lakini wako wengi walioikubali. Anasema Dr. Wahbat Al-Zuhail"Wanavyuoni wana kauli tano kuhusu hio Al-ijmaa Al-sukutiy". Akataja wale wasioikubali. Kisha akataja wanaoikubali akasema kwamba hio ndio: " Madhehebu ya Hanafi wengi na Al-Imamu Ahmad (bin Hanbal) (wanasema kuwa hio) inazigatiwa kuwa ni hoja na makubaliano ya uhakika". Kwa hivyo, kwa ujumla Mahanafi na Mahanbali wanaona kuwa Al-ijmaa Al-sukutiy ni hoja ya Kisharia. Anasema Al-Imamu Al-Salimi: "Ama hukumu ya Al-ijmaa Al-sukutiy ni kuwa ni hoja ya dhana inayopelekea kutumika katika matendo wala haileti yakini ni kama vile Hadith Ahadi".
Maana ya maneno ya Al-Salimi "Ni hoja ya dhana" musijemukafikiria dhana kwa maana yake ya Kiswahili, bali anakusudia kwamba inafaa kutumika katika matendo: si katika itikadi. Kwa hivyo, kwa ujmla ni kuwa Al-ijmaa Al-sukutiy ni kitu kinachokubalika kwa vile ziko madhehebu waoikubali na wako wanavyuoni tafauti waliokubali. Kwa ufupi, mimi sikuwa hapa nikitoa hoja kwa Al-ijmaa Al-sukutiy kama mulivyodhania nyinyi; balili nilikuwa nalinganisha dai la Sheikh Nassor na kusema hivi; kwamba hli lina muelekeo zaidi kuliko dai la Sheikh Nassor.
16
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA KUMI NA TANO
FUNGA YA 'ARAFAH
Katika sehemu hii, ni vyema kwanza nikanukuu yote nilioyasema kuhusu maudhui hii, kisha ndio nikanukuu jawabu niliojibiwa na kuijadili. Kuhusu suala hili nilisema: Anasema Sheikh Nassor Bachoo: "Jambo la kusikitisha ni kwamba ikiwa Waislamu watakubali kuwepo tafauti ya siku na tarehe baina yao, hapana shaka watakuwa wanafunga saumu ya Arafa siku tafauti na inavyotakiwa.
Kwa hivyo lengo na faida ya funga yenyewe litakuwa halikupatikana. Mbali na kukosekana huko Makka jambo baya zaidi ni kwamba watakuwa wanafunga siku ya pili yake ambapo watakuwa wanafunga siku ya 'Idul-Adh-ha'; siku ambayo ni Haramu kufunga.
Ni vyema tuzingatie kwamba funga hii ya Arafa pamoja na Iddi yake ni vitu ambavyo havina mahusiano na kuandama mwezi kutokana na kila nchi inavyoona mwezi wake. Bali chanzo cha funga ya Arafa ni uhusiano wa ile siku ambayo mahujaji wanaposimama katika uwanja wa Arafa. Na jambo la kusimama Arafa linapatikana sehemu moja tu ulimwenguni ambayo ni siku inayosadifu tarehe 9 Dhul-Hijjah huko mji wa Makka; sio tarehe tisa ya nchi nyengine yoyote ile. Kwa uthibitisho zaidi wa funga ya siku ya Arafa tunajifunza kuwa Mtume (s.a.w.) alipotueleza umuhimu wa siku hii, na kila alipotaja siku hii ya Arafa alitumia neno 'siku' wala hakutumia neno 'tarehe'.
Funga ya 'siku' ya Arafa." Mwisho wa kunukuu. Sasa tatizo moja linalowatatiza watu kuhusu suala zima la kuwa na miandamo tafauti ni tatizo hili la funga ya Arafa. Kwa kweli hili si tatizo lakini tatizo tunalo sisi wenyewe katika udha ifu wetu wa kukiweka kila kitu mahala pake na kutoa hukumu kwa mujibu wa misingi inavyotuelekeza. Siisahau kauli ya Dr. Al-zuhailiy yenye maana kwamba makosa mengi ya kifiq-hi yanatokana na kuwacha misingi yake ya kiusuli, na kwamba lau watu walikuwa wanaifata misingi hio, basi makosa yasingelitokea au ingelikuwa nadra sana kutokea.
Sasa suala tunaloulizwa ni kuwa kama muandamo kila watu wawe na wao, itakuwaje ikitokea siku ya Arafa kuwa kwetu ni mwezi nane, ilhali Arafa inakuwa mwezi tisa? Tukifunga tutakuwa tumefunga mwezi nane; tukifunga siku ya pili itakuwa Arafa imeshakwisha?
Jawabu ya suala hili: ni kuwa kwanza inatakiwa tujue kwanini tunafunga siku hio: nini sababu: je sababu ni Arafa au sababu ni mwezi muandamo? Tumeeleza huko nyuma nini illa ambayo, kwa Kiswahili, huwa tunaifasiri kuwa ni Sababu. Tukasema kwamba wengine wanatafautisha baina ya sababu na illa. Sababu - kwao - ni kitu kisicho na uhusiano na kitu chenye kupewa hukumu. Tukatoa mfano wa kutenguka kwa jua kuwa ni sababu ya kuwajibikiwa na Sala. Na illa ni kitu chenye uhusiano na kitu chenye kupewa hukumu, kama kuumwa ndio illa ya kuruhusika kula mchana wa mwezi wa Ramadhani.
Kwa maana hii, utakuwa umefahamu kwamba sababu ya:
1) Kutuwajibikia Sala ya Adhuri na Laasiri - kwa mfano - ni kutenguka jua. Ushahidi wake ni Aya inayosema: (Simamisha sala kwa kutenguka jua).
2) Sababu ya kufunga au kuwajibikiwa na funga ni kuuona mwezi. Kama ilivyo Hadithi inayosema:(Fungeni kwa kuuona) . Sasa hapa tuna mambo mawili: Moja: ni munasaba wa kufunga siku hio ya Arafa. Pili: ni sababu ya kufunga siku hio ya Arafa. Kisimamo cha Arafa ni Munasaba: wa kufunga siku hio: si sababu: Sababu: ya kufunga siku hio, ni muandamo wa mwezi wa mfunguo tatu. Wala usidhani kwamba tarehe tisa ya mwezi huo ndio sababu: "laa" (sio hivyo), bali tarehe tisa ni wakati wa kufunga: si sababu ya kufunga. Na hili linabainishwa zaidi na riwaya tuliotangulia kuinukuu huko nyuma, nayo ni riwaya ya Amiri wa Makka, yenye kusema: "Alituusia Mjumbe wa Allah - rehema na amani ziwe juu yake - tuabudu kwa kuuona, kama h atukuuona na wakashuhudia mashahidi wawili waadilifu, tuabudu kwa (kufata) ushahidi wao." Tumesema huko nyuma kwamba neno Nansuk (tuabudu) wengine wameifasiri ibada hii kuwa ni ibada ya hija nayo ndio tafsiri yenye muelekeo madhubuti zaidi, kwani neno hili hutumika sana kwa maana ya ibada ya hija, kama Allah (S.W.) anavyosema kuhusu ibada ya hija: Mukimaliza Nusuki (ibada) zenu (za hija). Na kwa hivyo imekuja katika "A'WNU AL-MA'ABUDI: SHARHU SUNANI ABI DAUD" kuhusu maana ya Hadithi hio tulioinukuu hapo juu kuwa maana yake inahusiana na ibada za hija. Anasema mwenye kusherehesha: "Na maana yake ni: 'Tuhiji kwa kuuona (mwezi), yaani mwezi muandamo wa mfunguo tatu." Ni wazi kwa maelezo haya au kwa mujibu wa Hadithi hii kwamba sababu ya ibada za hija - ikiwemo funga ya Arafa - ni kuandama kwa mwezi wa mfunguo tatu.
Sasa - tukirudi katika munasaba - ni kuwa munasaba si lazima kuwa mtu ausherehekee siku ile ile ya munnasaba huo. Kwa mfano, tunaposherehekea tokeo fulani lililotokea tarehe fulani katika historia, si lazima kuwa tuifanye sherehe yetu siku na tarehe ile ile: "Laa" tunaweza kuweka sherehe yetu siku nyengine. Sikusudii kufananisha sherehe yetu na mas-ala haya, ninachokusudia ni kukupa mfano utaoweza kufahamu kwawo tafauti baina ya Munasaba na Sababu.
Kwa hivyo, funga imeambatanishwa na muandamo wa mwezi, kama vile sala ilivyoambatanishwa na mtenguko wa jua. Utapolifahamu hili, utakuwa umefahamu kwamba, siku ya kufunga ni tarehe tisa mfunguo tatu, sawa siku hio imeafikiana na Arafa au imetafautiana, kwani sababu tayari imepatikana, na kilichotafauti ni kuafikana wakati wa tarehe ya baadhi ya sehemu na kuafikiana wakati mmoja wa Munasaba. Na Munasaba haufanywi kuw a ni illa wala haufanywi kuwa ni sababu ya hukumu. Hilo ni mosi.
Pili : ni kuwa: hata ikiwa kweli kilicho sahihi ni kwamba watu wakisimama Arafa na sisi tufunge hata ikiwa tarehe nane kwetu kwa mujibu wa muandamo wetu - tumeona kwamba kielimu hili ni kosa lakini tujaalie ni hivyo - basi elewa kwamba hili halijahalalisha kwamba na muandamo wa Ramadhani uwe mmoja. Ukitafakari kidogo hapa, utaona kwamba dai hili ni kujenga hoja juu ya Qiyas baina ya mambo mawili yaliotafauti. Arafa ni tokeo ambalo linatokea Makka tu, wakati Ramadhani ni tokeo la dunia nzima. Kwa hivyo, hata tukisema kwamba kilicho sahihi ni kufunga kwa ajili ya tokeo hilo au munasaba huo wa Arafa, basi itakuwa ni kwa sababu munasaba huo unatokea sehemu moja tu: kwetu hautokei. Kwa lugha nyengine, lau na sisi tulioko nje ya Makka ingelikuwa tunatakiwa tusimame Arafa yetu huko tuliko siku ya tarehe tisa, basi tungefanya hivyo kwa mujibu wa muandamo wetu, kama vile tunavyofunga kwa kufata muandamo wetu, na kusali kwa sababu ya mtenguko wetu wa jua. Wakati Ramadhani ni tokeo la dunia: watu wa Makka wanafunga na sisi tunafunga. Kwa hivyo, haya ni matokeo mawili tafauti huwezi kuyafanyia Qiyas kwani miongoni mwa masharti ya lazima ya Qiyas ni "Kupatikana usawa baina ya Shina na Tawi" na usawa hapa haupo. Kilicho sahihi, ni kufanya Qiyas cha Sala na funga. Kwani:
1) Wajibu wa Sala umefungamanishwa na kutenguka na kuzama kwa jua - kitu cha kimaumbile (Natural phenomenon). Kwa hivyo mtenguko wa jua ni sababu: si munasaba.
2) Wajibu wa funga umefungamanishwa na muandamo wa mwezi - kitu cha kimaumbile (Natural phenomenon). Kwa hivyo kuandama kwa mwezi ni sababu: si munasaba.
3) Jua - ambalo kutenguka kwake ndio sababu ya kuwajibikiwa na sala - likitenguka katika nchi moja, watu wa nchi nyengine hawawajibikiwi na sala. Kwa hivyo, Qiyas sahihi ni kuwa kuonekana kwa mwezi - ambayo ni sababu ya kuwajibika funga - katika nchi moja isiwe sababu ya kufunga kwa watu wa nchi nyengine. Hiki ni Qiyas sahihi. Ama kisimamo cha Arafa si Qiyas sahihi, kwani kisimamo cha Arafa ni Munasaba si Sababu wakati muandamo wa mwezi na kutenguka jua ndio Sababu. Au ukipenda kufanya Qiyas chengine sahihi, basi ni kile tulichotangulia kukinukuu kutoka kwa Sheikh Al-uthaimin, aliposema: "Na wakati wa mwezi ni kama wakati wa siku. Kama vile ambavyo miji inatafautiana katika kuanza kujizuia (na kula n a kunywa na jimai: yaani kuanza kufunga) na (inavyotafautiana katika) kufuturu kwa siku (daily au, basi vivyo hivyo inawapasa watafautiane katika kujizuia na kufuturu kwa mwezi (monthly au). Na (kama) inavyojulikana kwamba tafauti za kisiku zina athari zake kwa makubaliano ya Waislamu. (Watu) waliyo upande wa mashariki, hakika wao wanaanza kufunga kabla ya waliyo upande wa magharibi na wanafuturu kabla yao.
Wala haiwezekani mtu akasema kwamba kauli yake Allah (S.W. inayosema):"Sasa waingiliyeni (wake zenu) na tafuteni kile Allah alichokuandikiyeni, na kuleni na kunyweni mpaka ukubainikieni uzi mweupe kutokana na uzi mweusi wa alfajiri, kisha timizeni saumu hadi usiku." Na kauli yake (Mtume) s.a.w.:"Usiku ukitokeza kutoka hapa na mchana ukaondoka kutokea hapa na jua likatua, basi aliyefunga ameshafungua (au na-afungue)." (Haiwezekani mtu akasema kwamba Aya hio na Hadithi hii) kwamba ni za ujumla wa Wa islamu wote katika miji yote. Basi vivyo hivyo tunasema kuhusu ujumla wa kauli yake Allah (S.W.):﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ﴾ (Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge).
Na kauli hii - kama unavyoona - ina nguvu yake kwa mujibu wa lafdhi (yake) na mtazamo sahihi na Qiyas sahihi vile vile: Qiyas cha wakati wa siku kwa (kuulinganisha) na wakati wa mwezi (month). Mwisho wa kunukuu.
Tatu : ni kuwa: kutokukiwahi kisimamo cha Arafa kwa baadhi ya Waislamu wa sehemu nyengine za dunia ni kitu cha lazima. Chukulia - kwa mfano - kuna nchi ambazo siku hio ya mwezi tisa, jua linatua Saudia kwao bado ni usiku au alfajiri ya siku hio hio. Ikiwa watafunga kwa munasaba wa Arafa, inakuwa Arafa haipo tena, labda wawe ni wenye kufata kauli ya wenye kujuzisha kusimama Arafa usiku ndio watakuwa nao wamefunga siku ya Arafa, lakini tatizo bado litabakia katika siku ya Idi.
Siku ya pili - tujaalie ni J/tatu - asubuhi watu wa miji ya Saudia wanasali Idi - wao kwao ni magharibi ya J/pili, na Idi haisaliwi magharibi. Hata wakifika asubuhi - J/tatu kwao - Makka tayari jua limetua, na kwa hivyo ni J/nne. Utaona kwamba mitazamo ya kiakili na hoja za kimaandiko zilizojengeka katika misingi imara ya kifani, inaonesha kwamba kufunga na kufungua - sawa ikiwa Ramadhani au Mwezi tisa mfunguo tatu - basi ni jambo linalofatana na miandamo ya mwezi. Na kilicho sahihi - kama tulivyobainisha - ni kuwa muandamo wa mbali usitendewe kazi mbali. Kwa hivyo, kufunga ni tarehe tisa, sawa imeafikiana na munasaba wa Arafa au haikuafikiana, na kwa kufata tarehe tisa watu wote wa dunia itawezekana kufunga na itawezekana kula Siku Kuu tarehe kumi. Ama tukifata munasaba wa kusimama Arafa, watu wa nchi nyengine hawatoweza kufunga kwani hakuna maafikiano ya wakati wa kufunga baina ya Makka na nchi zao, labda kwa wale wenye kufata kauli ya wenye kujuzisha kusimama Arafa usiku, lakini hata hivyo Idi wataikosa.
Ama tukirudi katika nadharia ya Sheikh Bachoo aliposema: " Ni vyema tuzingatie kwamba funga hii ya Arafa pamoja na Iddi yake ni vitu ambavyo havina mahusiano na kuandama mwezi kutokana na kila nchi inavyoona mwezi wake. Bali chanzo cha funga ya Arafa ni uhusiano wa ile siku ambayo mahujaji wanaposimama katika uwanja wa Arafa." Mwisho wa kunukuu. Tukirudi katika maelezo hayo tunakuta kuwa maelezo hayo yanaifanya ibada ya saumu ianzwe kabla ya kufika sababu yake, kwani Arafa inaanza tarehe tisa baada ya kutenguka jua Adhuhuri, wakati wafungaji huwa tayari wameshafunga tangu kabla ya Alfajiri. Jambo hili la kutangulia "Kilichosababishwa kabla ya kilichosababisha" halipo kamwe katika soko la elimu! Ilivyo ni kutangulia "Kilichosababisha kabla ya kilichosababishwa," kama unavyotangulia mtenguko wa jua au kuzama k wake (ambao ni sababu) halafu ndio ikafatia sala (ambacho ndicho kilichosababishwa).
Ama maneno ya Sheikh Nassor Bachoo aliposema: "Kwa uthibitisho zaidi wa funga ya siku ya Arafa tunajifunza kuwa Mtume (s.a.w.) alipotueleza umuhimu wa siku hii, na kila alipotaja siku hii ya Arafa alitumia neno 'siku' wala hakutumia neno 'tarehe'. Funga ya 'siku' ya Arafa." Mwisho wa kunukuu.
Tunasema kwamba: kuitwa siku hio kuwa ni siku ya Arafa na isiitwe siku ya mwezi tisa si hoja ya kuwa lazima tufunge sawa na Saudia, kwani mtegemezo huu ni kulitegemeza (neno hilo Arafa) kwa ajili ya kuitukuza ile ibada inayofanyika katika eneo hilo." Na hii ni kawaida ya Warabu kuyanasibisha majina ya siku kwa kuyapa majina ya sehemu ambazo kuna matokeo fulani adhimu yaliyotokea au yanatokea katika sehemu hizo. Siku ya vita vya Uhudi - kwa mfano - huiita Yawmu Uhud (Siku ya Uhudi), na Uhudi ni jina la sehemu. Halkadhalika vita vya Hunain: vinaitwa Yawmu H unain (Siku ya Hunain). Anasema Allah kuhusu vita hivyo: "Na siku ya Hunain wingi wenu ulipokupendezesheni." Na Hunain ni jina la mji. Halkadhalika vita vya Badr; Badr ni sehemu. Lakini tunaviita vita hiv yo "Yawmu Badri (Siku ya Badr). Anasema Sahaba Hassan bin Thabit, Mshairi wa Mtume(s.a.w.w):
Nyuso siku ya Badri zilimngojea Mwingi wa rehema alete ushindi. Tazama Sahaba Hassan: ameinasibisha siku hio kwa kuipa jina la sehemu ya Badr, kwa ajili ya utukufu wa yale yaliofanyika hapo. Kwa hivyo kunasibishwa siku ya Arafa na sehemu hio ya Arafa, si kwa sababu tufunge sawa sawa, bali ni kwa utukufu wa yale yanayotendeka. Na yanayotendeka hapo ni Munasaba wa kufunga si Sababu ya kufunga kama tulivyotangulia kubainisha. Na inampasa msomi - mwanachuoni na Talibu Al-ilm (mwanafunzi) - kutafautisha baina ya vitu viwili hivyo. Mwisho wa kunukuu nilioyasema katika kitabu.
JAWABU NILIOJIBIWA NI KAMA IFATAVYO
Baada ya kuyaeleza hayo nilioyaeleza, ndugu zangu walinijibu juu ya maudhui hio kama ifatavyo:
Funga Ya 'Arafah Neno 'Arafah au 'Arafah ni jina linalotokana na uwanja au viwanja maalum vilioko nje kidogo ya Mji Mtukufu wa Makkah. Mahujaji wote ambao wamehirimia kutekeleza Ibada ya Hijja hukusanyika katika viwanja hivyo. Jambo hilo la kwenda kusimama kwenye viwanja hivyo kwa kuomba dua na kumtaja Allaah ni katika nguzo kubwa ya ibada hiyo ya Hijja. Inampasa kila Hajji kusimama au kushiriki hata kwa muda mdogo katika mchana huo. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amebainisha hayo kwa kusema:
(Hijja ni 'Arafah) Jambo hilo linathibitisha kwamba mtu yeyote asiyetekeleza ibada ya kusimama 'Arafah anapokuwa Makkah, atakuwa hakuipata ibada hiyo ya Hijja. Watu humiminika na kusimama kwenye uwanja wa 'Arafah siku ya tarehe 9 - Dhul-Hijjah ya kila mwaka. Ikumbukwe kwamba tarehe 9 hiyo ni ya huko Makkah pahala ambapo inafanyika ibada ya Hijja wala siyo ya pahala pengine popote duniani. Ni vyema kuzingatia kwamba funga hii ya 'Arafah pamoja na 'Iyd yake ni vitu ambavyo havina mahusiano na kuandama kwa mwezi kutokana na kila nchi inavyoona mwezi wake. Chanzo cha funga hii ya 'Arafah ni ule uhusiano wa ile siku ambayo Mahujjaji wanaposimama katika uwanja wa 'Arafah. Ambapo jambo la kusimama 'Arafah linapatikana sehemu moja tu ulimwenguni ambayo ni siku inayosadifu tarehe 9 - Dhul-Hijjah huko mji wa Makkah, sio tarehe 9 ya nchi nyengine yoyote ile.
Kwa maneno mengine ni kuwa tutakapotofautiana katika kufunga Siku ya 'Arafah na 'Iydul-Hajj itakuwa kama kwamba kila nchi ina uwanja wake wa 'Arafah na Makkah yake. Kwa uthibitisho zaidi wa funga ya siku ya 'Arafah tunajifunza kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kila alipokuwa akieleza umuhimu wa siku hii alitumia neno "siku" wala hakutamka neno "tarehe." Ama kwa mujibu wa maelezo ya ndugu yetu Juma, kama kawaida yake yeye anaona kuitwa "Siku ya 'Arafah" haina maana kuwa lazima tufunge sawa na Saudia, bali anaona kuwa hiyo ni "Idhaafatu-Tashriif" (yaani kuitengeneza siku hiyo kwa ajili ya utukufu wa pahala hapo au kwa ajili ya utukufu wa tokeo lenyewe). Sisi kwa upande wetu tunamuuliza ndugu Juma, Je yapo maandiko yoyote ya kilugha au ya kisheria yanayotufunza kuwa pahala pakitumika "Idhaafatu-Tashriif" huwa haparuhusiki tena kutoa mafunzo mengine yaliyomo ndani ya "idhaafa" hiyo? Tujuavyo sisi zipo Aya nyingi za Qur-aan ambazo zimetumika ndani yake hiyo "Idhaafatu-Tashriif" lakini utakuta wanavyuoni wa tafsiri wametoa mafunzo mengine yapatikanayo katika "idhaafa" hizo.
Akaendelea ndugu Juma kutoa kikwazo ambacho anaona kuwa haiwezekani kufunga siku ya 'Arafah sawa na tokeo lenyewe huko Makkah kwa kisingizio cha kuwa kuna nchi zinazotofautiana kwa masaa mengi. Kisha akasema: (Na (kama) inavyojulikana kwamba tafauti za kisiku zina athari zake kwa makubaliano ya Waislamu. Waliyo upande wa mashariki, hakika wao wanaanza kufunga kabla ya waliyo upande wa magharibi na wanafuturu kabla yao). Kama ni hivyo tofauti ni nchi zilizo Magharibi kwa nchi zilizo za Mashariki zinatofautiana, sisi tunamuuliza ndugu Juma vipi tena kwa nchi zilizo jirani kama vile Omani na Dubai , au Omani ya Yemeni, Je! Kuna suala la Mashariki na Magharibi hapa? Au kama ni hivyo basi mbona Juma hakubali uwezekano wa kufunga pamoja nchi zote za Mashariki kwa wakati mmoja na zote za Magharibi kwa wakati mwengine?
JAWABU
Kwanza Kimsingi ni kuwa hamukujibu hoja zangu moja moja kama nilivyoeleza mimi. Mukhtasari wa nilioyaeleza ni kuwa:
a) Ibada za Hija zina Sababu yake.
b) Hadithi imeonesha kuwa sababu ya ibada hizo ni muandamo wa mwezi wa mfunguo tatu. Hadithi imesema: "Alituusia Mjumbe wa Allah - rehema na amani ziwe juu yake - tuabudu kwa kuuona, kama hatukuuona na wakashuhudia mashahidi wawili waadilifu, tuabudu kwa (kufata) ushahidi wao."
Tumesema katika kitabu kwamba neno Nansuk (tuabudu) wengine wameifasiri ibada hii kuwa ni ibada ya hija nayo ndio tafsiri yenye muelekeo madhubuti zaidi, kwani neno hili hutumika sana kwa maana ya ibada ya hija, kama Allah (S.W.) anavyosema kuhusu ibada ya hij a: Mukimaliza Nusuki (ibada) zenu (za hija). Na kwa hivyo imekuja katika "Awnu Al-Ma'abudi: Sharhu Sunani Abi Daud kuhusu maana ya Hadithi hio tulioinukuu hapo juu kuwa maana yake inahusiana na ibada za hija. Anasema mwenye kusherehesha: "Na maana yake ni: 'Tuhiji kwa kuuona (mwezi), yaani mwezi muandamo wa mfunguo tatu." Ni wazi kwa maelezo haya au kwa mujibu wa Hadithi hii kwamba sababu ya ibada za hija - ikiwemo funga ya Arafa - ni kuandama kwa mwezi wa mfunguo tatu.
c) Kwa hivyo, kwa mujibu wa Hadithi hii, sababu ya kuingia ibada ya hijja -funga yake ya mwezi 9 na idi yake mwezi 10, ni muandamo wa mwezi wa mfunguo tatu. Ama kisimamo cha Arafa nimejibu kwamba haiwezekani kuwa ndio sababu ya kufunga kwani, kisimamo kinakuwa baada ya kutenguka jua adhuhuri, wakati wafungaji wameshafunga tangu alfajiri, na sababu hutangulia kwanza kisha ndio kikaja kilichosababishwa; yaani kwa lugha nyengine sababu ya ibada huwa haitanguliwi na ibada yenyewe; bali kwanza hutangulia sababu kisha ndio ikaja ibada ambayo ndio iliosababishwa.
Kwa hivyo, ikiwa sababu ya ibada za hija kikiwemo kisimamo cha Arafa na funga yake ni muandamo wa mfunguo tatu, basi sisi tupo pale pale kwamba Hadithi sahihi ya Ibn Abbaas na Kuraib imethibisha kwamba muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali. Kwa hali hii, sisi Afrika Mashariki, na kwangine, hatuwezi kufunga kwa kufata mwezi tisa wa Saudia, kwani muandamo kila mtu ana wake; wala hatuwezi kufanya hivyo kwa kufata kisimamo cha Arafa kwani kisimamo cha Arafa sio sababu ya ibada za Hijja kikiwemo kifungo hicho; bali muandamo wa mwezi ndio sababu kama Hadithi ilivyosema.
MNASEMA
Ndugu Juma ni vyema aelewe kwamba upo uwezekano wa kufunga 'Arafah siku moja dunia nzima kama tulivyoelezea katika kurasa za nyuma za kitabu hichi kwamba dunia nzima inashirikiana katika mchana mmoja na inashirikiana katika usiku mmoja ingawaje kuna nchi zinazotanguliza na nyengine zinazofuatia. Mfano nchi zote za Afrika zinaweza kushirikiana kufunga siku moja kwani baadhi ya nchi za Afrika zinatofuatiana kwa masaa machache tu sio usiku mzima wala mchana mzima. Katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu imeandikwa kwamba tofauti iliyopo kwa nchi za Kiislamu zilizo Mashariki ya mbali kama Phillipines na Indonesia na zile zilizo Magharibi ya mbali kama Al-Maghrib yaani Morocco ni tofauti ya masaa 9 tu. Kwa hivyo upo uwezekano wa kitaalamu (Kijiografia) wa kuweza kufunga kwa pamoja katika siku hiyo hiyo moja. Tofauti iliyopo ni ya masaa tu. Tunafunga siku moja sio wakati mmoja wala sio dakika moja. Msisitizo upo katika kufunga siku moja sio kuanza wakati mmoja.
JAWABU
Ama kudai kwamba uko uwezekano wa kufunga Arafa duniani kote siku moja, hilo si da sahihi. Nimekupeni mfano wa mimi mwenye mwezi wa 5 na wa 6 2009 nilikuwa Hong Kong, nikampigia simu ndugu yangu aliye Marekani nikamuuliza ni saa ngapi huko kwenu akanijibu ni saa kumi jioni; wakati huo Hong Kong tumeshali Alfajiri tushatoka Msikiti baina ya saa 11 na nusu mpaka 12 au 12 kasoro kidogo. Tazama tafauti iliokuwepo hapo. Hii ina maana jua likitua U.S.A jioni baada ya masaa mawili, labda na nusu, Hong Kong watu wanaingia makazini asubuhi kweupe na jua liko juu. Utaona kwamba, Kiislamu, ikiingia Ijumaa Hong Kong, Marekani bado ni Alkhamisi. Waislamu walioko Hong Kong wakifunga Arafa mchana wa tarehe 9, Marekani bado ni usiku hawawezi kufunga; Waislamu wa Hong Kong wakifuturu jioni, Marekani ni wakati wa mwisho mwisho wa alfajiri au ni asubuhi. Kwa ufupi ni kuwa baadhi ya States za Amerika na Hong Kong, tafauti haipungui masaa kumi na mbili.
Kwa hivyo, dai hilo si sahihi. Na hapa inabainika kwamba kauli sahihi ni ya kufata tarehe 9 mfunguo tatu kwa mujibu wa muandamo wan chi zetu, kwani tukifanya hivyo Waislamu wote duniani wataweza kufunga tarehe 9 na kula siku kuu tarehe 10. Ama tukifata muandamo mmoja hilo halitowezekana kwani mchana wa mwezi 10 wa nchi moja, tuseme hio Hong Kong, ni usiku katika nchi nyengine tuseme hio Marekani; jua likitua Hong Kong itakuwa tayari Kisharia ni mwezi 11, wakati Marekani ndio kwanza wajitayarisha kwenda kusali idi bado kwao ni mwezi 10. Utaona Al-Nadhar, Athar na migawanyiko ya kijografia, yanatoa jawabu sawa kwamba kilicho sahihi ni kila watu kufata muandamo wao.
Ama baadhi ya nchi kama mulivyosema - Za Africa kwa mfano - sipingi kwamba kuna uwezekano, ninachopinga ni kuwa dalili ni tafauti na kitendo hicho. Kama Ibn Abbas kakataa kuchukua muandamo wa Sham wala tafauti baina yake na Madina haifiki masaa hayo ya masaa 9 na akatoa hoja kwamba "Hivi ndivyo alivyotufunza Mtume s.a.w.", basi vipi itawezekana Kisharia kwamba watu wa Africa nzima wafunge sawa sawa.
MNASEMA
Ndugu Juma anasema: (Utapolifahamu hili, utakuwa umefahamu kwamba, siku ya kufunga ni tarehe tisa mfunguo tatu, sawa siku hio imeafikiana na Arafa au imetafautiana,....) [uk. 141]
JAWABU
Nyinyi ndugu zangu munanukuu maneno "Utapolifahamu hili..?" Bila ya ku nukuu maelezo yenyewe yalionipelekea kusema "Utapolifahamu hili". Sasa msomaji atafahamu nini? Huu sio mjadala wa kielimu wenye lengo la kutafuta natija sahihi. Ilikuwa munukuu jawhari ya maneno yangu kasha ndio muyajibu.
MNASEM
a) Sisi tunamjibu kwamba: Sasa kama anaruhusu kutafautiana, tena kwanini imeitwa (Funga ya 'Arafah) isiitwe "Funga ya tarehe 9"? Kisha ndugu Juma anaamini kwamba: (Arafa ni tokeo ambalo linatokea Makka tu, wakati Ramadhani ni tokeo la dunia nzima.) Kama kawaida yake ndugu Juma anajikanganya kila mara, kama kweli anaamini kila nchi ifunge kwa muandamo wake na 'Arafah, kila nchi ifunge kivyake, inakuaje tena Ramadhaan iwe ni ya dunia nzima, 'Arafah iwe kila mtu na yake?
JAWABU
Ama kwanini imeitwa (Funga ya 'Arafah) isiitwe "Funga ya tarehe 9", nimeshakuelezeeni kwa urefu katika Kitabu. Nimesema: Tunasema kwamba: kuitwa siku hio kuwa ni siku ya Arafa na isiitwe siku ya mwezi tisa si hoja ya kuwa lazima tufunge sawa na Saudia, kwani mtegemezo huu ni kuli tegemeza (neno hilo Arafa) kwa ajili ya kuitukuza ile ibada inayofanyika katika eneo hilo." Na hii ni kawaida ya Warabu kuyanasibisha majina ya siku kwa kuyapa majina ya sehemu ambazo kuna matokeo fulani adhimu yaliyotokea au yanatokea katika sehemu hizo. Siku ya vita vya Uhudi - kwa mfano - huiita Yawmu Uhud (Siku ya Uhudi), na Uhudi ni jina la sehemu. Halkadhalika vita vya Hunain: vinaitwa Yawmu Hunain (Siku ya Hunain). Anasema Allah kuhusu vita hivyo: Na siku ya Hunain wingi wenu ulipokupendezesheni." Na Hunain ni jina la mji. Halkadhalika vita vya Badr; Badr ni sehemu. Lakini tunaviita vita hivyo "Yawmu Badri (Siku ya Badr). Anasema Sahaba Hassan bin Thabit, Mshairi wa Mtume(s.a.w.w) :
Nyuso siku ya Badri zilimngojea Mwingi wa rehema alete ushindi. Tazama Sahaba Hassan: ameinasibisha siku hio kwa kuipa jina la sehemu ya Badr, kwa ajil i ya utukufu wa yale yaliofanyika hapo. Kwa hivyo kunasibishwa siku ya Arafa na sehemu hio ya Arafa, si kwa sababu tufunge sawa sawa, bali ni kwa utukufu wa yale yanayotendeka. Na yanayotendeka hapo ni Munasaba wa kufunga si Sababu ya kufunga kama tulivyotangulia kubainisha. Na inampasa msomi - mwanachuoni na Talibu Al-ilm (mwanafunzi) - kutafautisha baina ya vitu viwili hivyo.
Ama kauli yenu: "Kama kawaida yake ndugu Juma anajikanganya kila mara, kama kweli anaamini kila nchi ifunge kwa muandamo wake na 'Arafah, kila nchi ifunge kivyake, inakuaje tena Ramadhaan iwe ni ya dunia nzima, 'Arafah iwe kila mtu na yake?" Mwisho wa kunukuu. Ninasema: hata hili pia nalo munalifanya kuwa ni hoja ya kielimu!!! Zote mbili - Ramadhani na Arafa - ni za dunia nzima, tafauti ni katika kuingia nyakati zake. Ramadhani ni refu Waislamu ni lazima watakutana kwani hakuna tafauti ya muandamo wa mwezi mzima; kuna tafauti ya siku moja mbili, Arafa ni tokeo la siku moja, inapotafautiana miandamo hupelekea kutafautiana kwa tarehe za kufunga na kula siku kuu.
MNASEMA
Hebu tuangalie hoja nyengine ya ndugu Juma katika uk 142 wa kitabu chake anapodai kunukuu maneno ya Shaykh Al-'Uthayminiy, anaposema: ("Na wakati wa mwezi ni kama wakati wa siku Kama vile ambavyo miji inatafautiana katika kuanza kujizuia (na kula na kunywa na jimai: yaani kuanza kufunga) na (inavyotafautiana katika) kufuturu kwa siku (daily) basi vivyo hivyo inawapasa watafautiane katika kujiz uia na kufuturu kwa mwezi (monthly)
a) Suala linakuja: Je! Kama anavyosema miji inatafautiana kufuturu kwa mwezi kama inavyotafautiana kwa siku. Sasa vipi katika nchi moja iliyo kubwa kama Tanzania ambayo ina mikoa inayotafautiana kuanza k ula na kunywa kama Dar es Salaam na Kigoma? Je! Mbona haitafautiani kwa mwezi? Inafunga kwa muandamo mmoja lakini Dar es Salaam na Kigoma zinatafautiana katika kuanza kula na kunywa (kufuturu) kwa zaidi ya dakika 45?
JAWABU
Hatuzungumzii watu wanatenda nini; tunazungumzia nini kinatakiwa Kisharia kitendwe. Watu wa Kigoma ikiwa muandamo kwao ni tafauti na Dar-es-Salam, basi ilivyo ni kuwa wafunge kwa mujibu wa Muandamo wao kama wanavyosali kwa mujibu wa mtenguko wao na kufuturu kwa mujibu wa kuzama jua kwao. Kinachotazamwa si tangazo au amri ya serikali, bali ni muandamo wa mwezi. Na hili - kama munavyojua - ni jambo ambalo wanavyuoni wamelizungumzia na wako walioeleza kama hivyo. Nchi kama Urusi, hasa kabla ya kugawanyika, vipi utamwambia mtu wa State moja ya mbali na iliotafauti kabisa na State nyengine kwamba wafunge sawa. Kinachozinagatiwa si suala la nchi moja bali ni umbali na tafati za matalai.
Pamoja na hayo, kama nilivyokuelezeni mara nyingi kwamba, suala la umbali gani watu wafunge sawa, linabakia kuwa ni uwanja wa ijtihad kwa kutokuwepo andiko lenye kuonesha umbali gani; ingawa andiko limeonesha kwamba muandamo wa mbali si hoja kwa walio mbali, kilichojificha ni umbali gani. Kwa hivyo, ukweli kwamba muandamo wa mbali si hoja kwa waliombali hili ni andiko ambalo lazima tusallim amri mbele yake; na je umabali huo uwe kiasi gani; hapa wenye elimu wana uwanja mpana wa kujitahidi na kutoa fat-wa na sisi tutatazama ilio na nguvu. Kwa hivyo, ikiwa watu wa Kigoma wamechukua ijtihad ya wanavyuoni wetu wakubwa waliotangulia wa Africa Mashariki, hilo linatoa nafasi kwani hapa uwanja wa ijtihad upo. Ama kutwambia kuwa dunia nzima tuwe na muandamo mmoja: hili ni kinyume na andiko na ni kinyume na maumbile yenyewe ya dunia.
MNASEMA
b) Kwa nini basi nchi kama Omani na Dubai zinatafautishwa katika kuangalia mwezi wakati ambapo nchi hizo hazina tofauti kubwa katika kuanza kula na kunywa? Wala hazina tofauti ya matlai wala masaa ya kuanza na kuingia kwa siku?
JAWABU
Imarati ni maamuzi ya serekali zao kufata Saudia; nalo ni kosa kwani wao na Oman ndio walio karibu zaidi na wana matalai sawa. Na nimekwambieni kuwa mjadala wetu si watu wanafanya nini: bali nini kinatakiwa kitedwe Kisharia. Vyenginevyo na mwengine anaweza kukuulizeni mbona Suudia wanafata muandamo wao; mbona Misr wanafata muandamo wao, n.k. Kwa hivyo, tuko pale pale kwamba hatuzungumzii nini watu wanafanya; bali tunazungumzia nini kinatakiwa kifanywe Kisharia.
MNASEMA
c) Tujuavyo sisi nchi zote za Uarabuni zinapata usiku wao mmoja na mchana wao mmoja, kwa hivyo hakuna shida yoyote katika kufunga 'Arafah siku moja kwa wote.
JAWABU
Sijakwambieni kuwa haiwezekani; nimesema kwamba ushihidi tulio nao ni kuwa:
1) Ibada za Hijja ikiwemo funga hio ya Arafa inategemea muandamo wa mwezi: si kisimamo cha Arafa. Kisimamo cha Arafa ni munasaba na muandamo wa mwezi ndio sababu ya ibada hizo.
2) Muandamo wa mbali si hoja kwa walio mbali.
MNASEMA
Shaykh Naaswir Khamiis 'Abdur-Rahmaan wa Mombasa Kenya ameandika kitabu chake "Mwezi Ko-Ongo" na amethibitisha tofauti ya masaa baina ya nchi mbali mbali mfano: "tofauti ya mji wa Mombasa na nchi ya magharibi ya mbali mwa Afrika kama Algeria ni masaa mawili na dakika ishirini na nane (2:28)" - uk 22. Katika jambo la kuonesha ufinyu aliokuwanao ndugu yetu Juma, ule wa kutokufanya uchunguzi wa kina katika mas-ala haya, yeye anaamini kwamba jambo hili limeanzishwa na Shaykh Naaswir Bachuu na wala halikuwepo ulimwenguni kama anavyodai mwenyewe kwa kauli yake ifuatayo: (Ninasema: Enyi walimwengu wenzangu tazameni hoja za kielimu hizo!!!!!!! Kwani nyinyi Wazanzibari kabla ya kuja fikra hio ya Sheikh Nassor Bachoo ya kufunga kwa muandamo mmoja)
JAWABU
Jambo gani hilo ambalo nimedai kuzushwa na Sheikh Nassor Bachoo? Hebu ninukulieni hilo jambo. Fikra ninayosema kuwa kaja nayo Sheikh Nassor Bachoo Zanzibar ni fikra ya kututaka tufunge kwa muandamo mmoja. Kwa Zanzibar yeye ndiye aliyeitangaza, kuilingania na kuitungia kitabu. Wala sikusema kuwa katika dunia yeye ndiye muasisi wa fikra hio. Ama yale mulioyanukuu kutoka kwa Sheikh Nassor Khamis, sio yalionifanya mimi nikapigwa na mshangao huo: ((Ninasema: Enyi walimwengu wenzangu tazameni hoja za kielimu hizo!!!!!!! Kwani nyinyi Wazanzibari kabla ya kuja fikra hio ya Sheikh Nassor Bachoo ya kufunga kwa muandamo mmoja). Kwa hivyo, musichanganye mambo. Mimi nilishagaa hivyo kwa sababu ya maneno haya ya Sheikh Nassor. Alisema Sheikh Nassor: "Pili kama ingalikuwa hakuna dhana ya kuwa mwezi ukionekana popote watu wafunge, Ibnu Abbas (r.a.) asingekuwa na haja ya kumuuuliza Kurayb juu ya habari za mwezi wa Sham kwa kusema:
"Kis ha (Ibn Abbas) akataja (habari) ya mwezi na akasema: "Ni lini mliuona mwezi?...akasema: "Wewe umeuona?" Hapo ndio nikashanga na nikasema: Hio ndio hoja nyengine ya Sheikh Bachoo, kwamba lau hakuna dhana ya kuwa mwezi ukionekana popote watu wafunge, basi Ibn Abbas asingekuwa na haja ya kumuuliza Kuraib "Lini mumeuona mwezi!!!" Ninasema: Enyi walimwengu wenzangu tazameni hoja za kielimu hizo!!!!!!! Kwani nyinyi Wazanzibari kabla ya kuja fikra hio ya Sheikh Nassor Bachoo ya kufunga kwa muandamo mmoja, mulikuwa hamuwaulizi watu wanaotoka nchi nyengine masuala kama hayo wanapokuja kwenu na nyinyi muko kati kati ya mwezi pamoja na kwamba nyote zamani mukifata muandamo wenu? Sasa kama nyinyi mulikuwa mukiuliza suala hilo hilo kwanini Ibn Abbas na yeye asiulize hata kama dhana hio haipo? Mimi binafsi nina kawaida ya kuwauliza wageni walioko nchi hii ninayoishi suala hilo, na natarajia kwamba pia nimewasikia watu wengi wenye kuwauliza wageni suala hilo. Kwa hakika shubuhati kama hizi hazifai katika kujadili mambo ya kielimu. Kwa ufupi ni kuwa hata kama dhana hio ilikuwepo, dhana hio inabomolewa na kukataa kwake - Ibn Abbas - kuukubali mwezi wa Sham, na kujenga hoja kwa Hadith marfu'u kwamba hayo ndio mafunzo ya Mtume(s.a.w.w) kwao. Sasa uko wapi uhusiano wa maneno yangu na nakala ya Sheikh Nassor Khamis?
MNASEMA
Sasa sisi tunataka kumtihibitishia ndugu Juma kuwa wapo watu wengi ambao pengine hawakuwafikiana na Shaykh Naaswir Bachuu katika baadhi ya mambo au misimamo lakini kwa bakhti nzuri katika hili suala la kufunga 'Arafah na kusali siku ya 'Iydul-Adh-ha wanafuata Makkah na wanaungana na ulimwengu mzima. Mfano mzuri kabisa ni ndugu zetu wa Tarika ya Kadiria, takriban wote wanafunga 'Arafah kwa kufuata tarehe 9 - Dhul-hijjah ya Saudia (Makkah). Hayo yanathibitishwa na aliyekuwa kiongozi wao Mkuu wa Tarika hiyo mwanachuoni maarufu Al-Marhuum Shaykh Muhammad Naaswir Abdulla Al-Qaadiry ambaye aliandika kitabu alichokiita: "Kitabu 'Arafah" na kuandika kwenye gamba la kitabu hicho kwamba: "Nguzo Kubwa Ya Hijjah Ni 'Arafah Tarehe Tisa Mfunguo Tatu Na Kuswali 'Iydul-Hajj Sawa Na Makkah." Katika uk 22 wa kitabu chake hicho pia ameandika kama ifuatavyo: "Waislamu wote ulimwenguni wafunge Sunnah ya 'Arafah sawa na 'Arafah ya Makkah."
Kisha katika uk 74 ameandika Fatwa zifuatazo: "'Arafah ya Makkah tarehe 9 mwezi wa Mfunguo Tatu (Dhul-Hajj) ndiyo 'Arafah ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta'ala) na ndiyo 'Arafah ya Waislamu wote popote walipo ulimwenguni." "Wananaokwenda Hijja, kwao ni haramu kufunga siku hiyo ya 'Arafah huko 'Arafaati (Makkah) na waliobaki majumbani, kwao ni Sunnah kubwa kufunga siku hiyo hiyo ya 'Arafah ya Makkah kokote waliko ulimwenguni." "Tarehe 10 Mfunguo Tatu (Dhul-Hajj) ndiyo siku ya 'Iyd ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta'ala) na 'Iyd ya dunia nzima kwa Waislamu wote. Kufunga siku hiyo yote kamili ni haramu. Anayeswali 'Iyd tarehe 10 ya Makkah amefanikiwa na ole wake yule anayeswali 'Iyd siku atakayo mwenyewe. Kwa ujumla kufunga tarehe 9 Mfunguo Tatu kwa Mahujaji 'Arafah ni Haramu. Na kufunga kwa Waislamu wote ulimwenguni tarehe 10, 11, 12 na 13 Mfunguo Tatu ni Haramu."
"Hivyo ni jambo baya kabisa na lenye kutia huzuni sana kuwaona baadhi ya ndugu zetu Waislamu wanaacha kufunga siku ya 'Arafah Aliyoiteua Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta'ala) na badala yake wanafunga siku ya kuchinja tarehe 10 (ya Makkah) wakisingizia kuwa ndiyo siku yao ya 'Arafah waitakayo wao waliyoichagua wao wenyewe ambayo kufunga siku hiyo ni haramu."
JAWABU
Haya! Hoja iko wapi humu! Je hii ni hoja kwamba alivyosema Sheikh Muhammad Nassor ni sahihi au ni hoja kwamba kuna watu wanaafikiana na nyinyi katika hilo? Ikiwa ndio munatoa hoja kwamba alivyosema Sheikh Muhammad Nassor ni sahihi; nitakutakeni dalili ya usahihi huo; ikiwa munatoa hoja kwamba kuna watu wanaafikiana na nyinyi katika hilo; hapo sikupingini. Lakini suala letu bado lipo: 1) Nini sababu ya kufunga Arafa.
2) Je sababu ni kisimamo cha Arafa.
3) Je ni muandamo wa mwezi wa mfunguo tatu.
4) Je tufate muandamo mmoja au kila mtu wake.
Mimi ushahidi nilio nao ni kuwa:
1) Sababu ya kufunga Arafa ni muandamo wa mfunguo tatu, kama ilivyonena Hadithi ya Amir wa Makka.
2) Kisimamo cha Arafa si sababu kwani sababu hutangulia kisha ndio kikija kilichosababishwa. Kama linavyotenguka jua ndio ukaingia wajibu wa kusali; au unavyoingia mwezi wa Ramadhani ndio ukaja wajibu wa Ramadhani. Ama kisimamo cha Arafa kinaanza baada ya kutenguka jua wakati wenye kufunga wanaanza kufunga tangu Alfajiri. Kwa hivyo, kisimamo cha Arafa ni munasaba ni sababu.
3) Kila watu wafate muandamo wao kwa mujibu wa Hadithi ya Ibn Abbas na Kuraib.
17
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA KUMI NA SITA
LAYLATUL- QADRI
MUNASEMA
Laylatul- Qadri: Maelezo Juu Ya Kupatikana Kwa Usiku Ni vyema kujikumbusha kwamba maelezo ya kisayansi yaliyopatikana kwenye Qur-aan Tukufu yanazingatia kwamba "Nyakati" hupatikana kutokana na mipinduko ya jua, mwezi na dunia. Hapana shaka yoyote dunia ina mizunguko yake miwili. Kwanza kuna ule mzunguko wa dunia kulizunguka jua, ambapo mzunguko huo husababisha mabadiliko ya miongo (seasons) mbali mbali kama vile mchoo, vuli, kipupwe au kiangazi. Pili ni ule mzunguko wa dunia kujizunguka yenyewe katika mhimili wake, mzunguko huu wa pili ndio unaosababisha kupatikana usiku na mchana. Kwa kawaida dunia hujizunguka yenyewe kamili kwa muda wa masaa 24 ambayo hupatikana siku moja yenye usiku mmoja na mchana mmoja.
Ni vyema ikumbukwe kwamba hakuna nchi yoyote duniani iliyotafautiana na nchi nyengine katika kupata usiku kwa masaa 24. Nchi zote duniani zinashirikiana katika usiku mmoja pia zinashirikiana katika mchana mmoja huo huo. Isipokuwa nchi nyengine hutangulia na nyengine zitafuatia nyuma.
JAWABU
Hebu tufahamisheni vipi: "Nchi zote duniani zinashirikiana katika usiku mmoja pia zinashirikiana katika mchana mmoja huo huo. Isipokuwa nchi nyengine hutangulia na nyengine zitafuatia nyuma". Mwisho wa kunukuu. Jamani mbona tunaambiana mabo yasio na ukweli! Nimekupeni mfano wa Hong Kong na U.S.A, bila shaka baadhi ya States zake, ambao nimeuona mwenyewe kwamba usiku na mchana haukutani katika nchi hizo, na ninavyodhani ni kuwa Canada na Hong Kong ni hivyo hivyo.
MNASEMA
Sasa tukirudi nyuma katika maelezo ya ndugu Juma katika kuelezea Laylatul-Qadri kwa kupitia fani hii ya Jiografia anaeleza kama ifuatavyo: (Sasa nchi ambazo zimepishana na Makka kwa masaa 12 au zaidi hazitopata nazo LAILATUL-QADRI, kwani LAILATUL-QADRI mwisho wake ni kuchomoza Alfajiri kama Qur-an ilivyosema, na wakati huu kuna nchi bado ni jioni. Sasa vipi hawa wao hawamo au na wao watapata zamu yao baadae?)
Hayo tumeshayaeleza sana kwamba hakuna nchi iliyopishana na nyengine kwa masaa zaidi ya 12. Wala hakuna nchi ya Kiislamu iliyopishana na nchi nyengine ya Kiislamu kwa zaidi ya masaa 9. Kama kweli ndugu Juma anaelewa mambo, ingekuwa jambo la busara akaeleza kwa mfano nchi zote za Kiarabu zina tofauti gani ya usiku au mchana? Au Ulaya (Europe) nzima ina tofauti gani katika kupata usiku au mchana wao? Huku akizingatia kwamba kuna nchi moja kama Canada iliyo na ukubwa kuliko bara zima la Ulaya.
Mara nyinyi tumekuwa tukimfahamisha ndugu Juma kuwa anapojadili jambo lililoambatana na fani fulani basi alijadili jambo hilo kwa kupitia njia sahihi zenye kukubalika kwa mujibu wa fani hiyo. Hususan anapojadili mas-ala ambayo yanahitaji madondoo muhimu kuliko maneno matupu. Kwa uchunguzi zaidi juu ya maelezo ya ndugu Juma tutakuta kuwa hakuweza kutoa ushahidi wa kina hasa anapoelezea tofauti iliyopo katika kutofautiana na baadhi ya nchi juu ya suala zima la kuingia usiku na mchana.
JAWABU
Haya! Hakuna nchi iliopishana na mwenziwe kwa zaidi ya masaa kumi na mbili, je iko iliopishana na mwenziwe kwa masaa hayo kumi na mbili? Je ikiingia alfajiri huko Makka watu hao kwao itakuwa ni saa ngapi hasa siku za joto ambapo Makka Alfajiri yake inaingia saa 10 za usiku. Kama huku saa 10 za usiku, Alfajiri imeingia kule kwenye tafauti ya masaa 12 itakuwa saa ngapi: si itakuwa bado ni jioni? Sasa kama ni jioni, na LAILATUL-QADRI mwisho wake ni alfajiri sasa hoja yenu iko wapi? Kwa ufupi ni kuwa suala hili nilikuwa nikijibu nukta alioileta Sheikh Nassor. Ni vyema nikanukuu hoja yake na jawabu kamili.
Maelezo kamili ni kama inavyofata. Nilisema: Suala jengine ni suala la LAILATUL-QADRI, nayo ni hoja ya mitaani safi. Ufupisho wa hoja hii ni kuwa usiku huo wa Lailatu Al-qadri ni mmoja na unakuwa katika tarehe za witri (Odd numbers: 21-23-25-27-29) za kumi la mwisho. Wakati tokeo hilo hutokea usiku mmoja tu. Sasa kama kila mji au kila nchi watafata muandamo wao, hii ina maana usiku wa mwezi 27 Saudia ni mwezi 26, kwetu. Sasa ni usiku wa nchi gani? Hayo ndio maelezo ya Sheikh Nassor Bachoo kwa ufupi. Kisha nami nikjibu: Tunasema kwamba: suala hili lingekuwa sahihi lau ingelikuwa tuna hakika kwamba tarehe fulani ndio usiku huo wa LAILATUL-QADRI. Lakini hakuna anayejua, hata Mtume (s.a.w.) katika hio Hadithi kasema kausahau usiku huo. Labda na sisi tuulize kwamba je tukio hili ni la dunia nzima au ni la Makka tu. Nadhani jawabu ni "La dunia nzima." Sasa nchi ambazo zimepishana na Makka kwa masaa 12 au zaidi hazitopata nazo LAILATUL-QADRI, kwani LAILATUL-QADRI mwisho wake ni kuchomoza Alfajiri kama Qur-an ilivyosema, na wakati huu kuna nchi bado ni jioni. Sasa vipi hawa wao hawamo au na wao watapata zamu yao baadae? Kama wao watapata zamu yao baadae basi na sisi Pemba hatutokosa.
Kuanzia hapa utajua kwamba hakuna ulazima wa kuwa tarehe ziwe sawa katika tokeo hilo la LAILATUL-QADRI. Lakini kwa kufahamu zaidi udhaifu wa hoja hii, tazama ukweli kwamba Mtume(s.a.w.w) anasema kwamba siku ya Ijumaa kuna Saa ambayo mtu akiisadifia naye yumo katika kusali na kuomba basi hupokelewa maombi yake. Ikiwa ni saa moja au mbili au tatu n.k, suala ni saa ya nchi gani? Cha kuzingatia zaidi ni kuwa wakati Makka ni mchana siku hio ya Ijumaa kuna nchi nyengine bado ni mwanzo wa usiku na jua likitua Makka nchi hizo ni asubuhi au alfajiri. Jawabu yako hapa ndio jawabu yetu kule. Hii ndio jawabu na - kimsingi - nadhani iko wazi kwamba tokeo la Lailatul Qadri si hoja ya kuwa na tarehe moja.
Munasema
Kuhusu Laylatul-Qadri: Bila shaka ni usiku mmoja unaotokea mara moja kila mwaka katika mwezi wa Ramadhaan. Hayo yanathibitishwa na Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) pale Anapoeleza asili ya siku yenyewe katika Qur-aan Tukufu pale aliposema:
﴿إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴾
"Hakika tumeiteremsha (Qur-aan) katika Laylatul-Qadri (usiku wenye heshima kubwa), (usiku wa mwezi wa Ramadhaan" . (87: 1) Katika kuifasiri Aya hii, Shaykh Abdallah Al-Farsy ametoa maelezo yafuatayo: "Qur-aan kama ijulikanavyo ilikuwa ikiteremshwa kidogo kidogo, basi siku ile iliyoanza kuteremshwa ilikuwa katika Laylatul-Qadri (usiku wenye heshima kubwa). Ndio ikaambiwa kuwa Qur-aan imeteremshwa katika Laylatul-Qadri, ni usiku mmoja mtukufu umo katika mwezi wa Ramadhaan, ambao umebarikiwa kuliko miezi alfu, yaani mtu akifanya amali njema katika usiku huo hupata thawabu kama za mwenye kufanya amali ile kwa zaidi ya miezi elfu, na mwenye kufanya maovu naye hupata dhambi za mwenye kufanya maovu kama yale kwa zaidi ya miezi elfu.
Na Mwenyezi Mungu Ameuficha usiku huu haujulikani ni upi, ili watu wajitahidi kufanya Ibada katika mwezi mzima wa Ramadhaan; lakini watarajiwa zaidi kuwa katika kumi la mwisho na hasa usiku wa kuamkia mwezi 23, 25, 27 na 29. Basi atakaye kujua yakini kuwa ameupata usiku huu, bila ya shaka, inamlazimu ajipinde na kufanya ibada mwezi mzima. Wala si lazima kwa mwenye kuupata usiku huu kuona alama yoyote." Kisha Shaykh Abdallah Al-Farsy akabainisha maneno kama hayo alipokuwa akiifasiri Suratud-Dukhaan kama ifuatavyo:
﴿إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ * فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ﴾
"Kwa yakini tumeiteremsha (Qur-aan) katika usiku uliobarikiwa, Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hikima" . (44: 3, 4) Shaykh anaendelea kusema: "Hii 'Laylatin Mubaarakatin Fiyhaa yufraqu Kullu amriin Hakym." Dhahir Shahir hapa kuwa siku hii imo katika mwezi wa Ramadhaan kama yalivyobainishwa haya na Mwenyewe Mwenyezi Mungu katika Aya ya 185 ya Suratul-Baqarah." Ndugu yetu Juma yeye bado anahoji: (Sasa nchi ambazo zimepishana na Makka kwa masaa 12 au zaidi hazitopata nazo LAILATUL-QADRI, kwani LAILATUL-QADRI mwisho wake ni kuchomoza Alfajiri kama Qur-an ilivyosema, na wakati huu kuna nchi bado ni jioni. Sasa vipi hawa wao hawamo au na wao watapata zamu yao baadae?)
JAWABU
Sasa nini uhusiano wa nilioyasema na nakala mulizozitoa za Aya na maelezo ya Sheikh Al-Farisi? Jamani! Munasadiki kuwa hawa watu si watu wa kufahamu: basi wanapenda tu kitu!
MNASEMA
Sisi tunapenda kumuelimisha ndugu Juma kama ifuatavyo: Tunajifunza katika Aya za Qur-aan tulizozitaja kwamba Laylatul-Qadri ni usiku mmoja tu kwa ulimwengu mzima.
JAWABU
Ni sehemu gani ya Aya iliosema hivyo kwamba Laylatul-Qadri ni usiku mmoja tu kwa ulimwengu mzima? Hili ni jambo la ghaibu wala halikufafanuliwa, nyinyi munalisema bila ushahidi unaokubalika. Ikiwa dalilu dhanni haikubaliki katika itikadi, vipi mutasema kitu cha ghaib bila ya ushahidi. Mimi nimekujibuni kwamba ziko nchi ambazo zimetafautiana kwa muda wa masaa kumi na mbili wala hazikutani kamwe katika usiku wala mchana. Sasa kama Laylatul-Qadri ni siku moja katika usiku mmoja na kwa hivyo tarehe iwe moja na mfungo mmoja. Tunauliza Laylatul-Qadri mwisho wake ni wakati gani? Qur-ani imesema mwisho wake ni Alfajiri.
Tuchukulie mwezi mwanzo umeonekana Makka, kwa hivyo usiku wa Laylatul-Qadri Makka, alfajiri ya Makka Laylatul-Qadri itakuwa haipo tena. Sasa wale ambao kwao ni jioni je wao hawatopata Laylatul-Qadri? Kwa sababu hii, ndio maana nikaita hii kuwa ni hoja ya mitaani kwani mwenye elimu hasemi maneno haya kama ni hoja ya muandamo mmoja.
MNASEMA
Mwenyezi Mungu Mtukufu (Subhaanahu wa Ta'ala) Anauadhimisha usiku huo kila mwaka mara moja ndani ya usiku huo kwa amani na baraka nyingi. Hakuna aliyesema kuwa usiku huo hutokea Makkah pekee au kwamba watu wote waitafute Laylatul-Qadri kwa usiku wa Makkah. Kinachozungumzwa hapa ni kwamba usiku huu ni mmoja kwa dunia yote ingawaje kuna nchi zenye kutangulia kabla ya nyengine. Labda ndugu Juma amechanganyikiwa baina ya usiku wa Laylatul-Qadri na 'Arafah, ambayo ilizungumzwa kwamba ibada ya funga ya 'Arafah ina uhusiano wa moja kwa moja na Uwanja wa 'Arafah ulioko Makkah. Kila eneo lina kupambazukiwa kwake na alfajiri kama ilivyo katika hukmu ya kula daku na kuanza kufuturu linapozama jua. Na hayo tumeshayaeleza sana kwamba hata katika nchi moja kubwa kuna kutafautiana alfajiri zao. Kama Dar es Salaam linazama na kuchomoza jua kwa zaidi ya dakika 40 kabla ya Kigoma.
JAWABU
Sikusema kuwa mumedai kwamba Laylatul-Qadri inatokea Makka tu, bali mimi nimenukuu mfano ule ule alioutoa Sheikh Nassor aliposema: "Pindipo itatokea kuwa Laylatul-Qadri? usiku wa 27 kule nchini S. Arabia". Na kwa ujmla bado hamujatoa jawabu katika suala hili kwamba ziko nchi ambazo tafauti ni masaa 12. Alfajiri ya nchi moja ni jioni ya nchi nyengine. Sasa kama Laylatul-Qadri inatoka usiku mmoja na mwisho wake ni alfajiri, tafadhali - musibabaishe - tuelezeni vipi wataupata usiku huo wale ambao bado kwao ni jioni wakati huku ushamalizika. Au kama watapata wao mwanzo huku itakuwa bado ni mchana; jua huku likitua kule alfajiri imechomoza na Laylatul-Qadri itakuwa haipo tena. Kwa kweli, kila mwenye akili - si mwenye elimu - anajua kuwa hii si hoja ya kuonesha kuwepo kwa muandamo mmoja.
18
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA KUMI NA SABA
KUTUMIA QIYAAS CHA KUINGIA WAKATI WA SWALA KWA WAKATI WA SWAUM
MNASEMA
17. Kutumia Qiyaas Cha Kuingia Wakati Wa Swala Kwa Wakati Wa Swaum Katika kuutetea msimamo wake wa kufunga kwa kuzingatia "matlai", Ndugu Juma amejaribu kutoa hoja ya kutumia "Qiyaas" cha "Ibada ya Swala" kwa "Ibada ya Swaum." Kulinganisha kwake huko, Ndugu Juma anatoa taswira ya kuwa: " Kama ilivyokuwa hatuwezi kuswali kwa kufuata machweo ya jua ya nchi ya mbali, vile vile hatuwezi kufunga kwa kufuata nchi nyengine yoyote ile." Sisi kwa upande wetu tunapenda kumzindua ndugu Juma kwa haya yafuatayo: i). Kwanza hakuna mwanachuoni anayekubalika aliyewahi kutumia "Qiyaas" cha wakati wa Swala kwa wakati wa Swaumu katika mas-ala haya ya kuandama kwa mwezi.
JAWABU
Inaonesha mukisoma hamufahamu. Hao wanavyuoni wote waliofanya Qias, Qias chao ndio hicho - Qias cha jua na mwezi. Someni yafatayo kutoka kwa wanavyuoni wenye kuaminika: Mosi: Anasema Al-Imamu Abu Muslim: Na wakaukisia (muandamo wa mwezi kwa kuulinganisha) na kuchomoza alfajiri na (kuchomoza) jua na kutua kwake.
Pili : Anasema Sheikh Al-Khalili alipokuwa akielezea suala hili: "Na kutenguka kwa jua (kwa mfano) katika mji fulani, hakupelekei kuingia wakati wa adhuhuri katika kila mji".
Tatu : Anasema Al-imamu Al-nnawawi: "(Kauli ya) Pili: Haiwalazimu (funga watu wa miji ya mbali) kwani vyenye kuchomoza na vyenye kutua huenda vikatafautika kwa kutafautika miji, hakika kila watu wameamrishwa (kufata) mawio yao na machweo yao. Huoni kwamba alfajiri hutangulia kuchomoza kwake katika mji mmoja na kuchelewa mji wa pili, na vivyo hivyo jua: linatangulia kuzama kwake katika mji na linachelewa katika mji mwengine. Kisha kila mji unazingatia kuchomoza alfajiri yake na kuzama jua lake kuhusu watu wake (mji huo), basi vivyo hivyo mwezi muandamo."
Nne : Anasema Sheikh Ibn 'Uthaimin: "Wakasema: 'Na vivyo hivyo tunasema kuhusu kauli ya Mtume(s.a.w.w) :"Mukiuona fungeni na mukiuona fungueni." Hakika atayekuwa katika sehemu ambayo haiwafikiani na sehemu ya aliyeuona (mwezi) katika matalai ya mwezi basi (mtu huyo anahisabiwa kwamba) hakuuona kwa uhakika wala kihukumu. Wakasema: 'Na wakati wa mwezi ni kama wakati wa siku. Kama vile ambavyo miji inavyotafautiana katika kuanza kujizuia (na kula na kunywa na jimai: yaani kuanza kufunga) na (inavyotafautiana katika) kufuturu kwa siku (daily), basi vivyo hivyo inawapasa watafautiane katika (kuanza) kujizuia na (katika kuanza) kufuturu kwa mwezi (monthly).
Na (kama) inavyojulikana kwamba tafauti za kisiku zina athari zake kwa makubaliano ya Waislamu. Waliyo upande wa mashariki, hakika wao wanaanza kufunga kabla ya waliyo upande wa magharibi na wanafuturu kabla yao. Je ndugu zangu mumewafahamu Maulamaa hawa wanasema nini? Je hakuna mwanachuoni aliyefanya Qias hicho? Hili ndio tatizo lenu: hamuoni tabu kusema kitu bila ya kukijua!
MNASEMA
ii). Pili tunapenda kumfahamisha ndugu Juma kwamba ziko nchi nyingi zinazofuata kama huo msimamo wake ambazo zinashirikiana kufunga siku moja, lakini haziswali wakati mmoja wala hazili daku wakati mmoja. Mfano nchi za Tanzania , Kenya na Uganda zinafunga siku moja lakini haziswali wakati mmoja. Wakati wa Swala kama ya "Adhuhuri" ya Dar es Salaam ni tofauti kabisa na wakati wa "Adhuhuri" ya Kampala .
JAWABU
Hili tumeshalielezea kuhusu suala la Dar na Kigoma, hatuna haja ya kukariri - suala ni moja na jawabu ni moja.
MNASEMA
iii). Wanavyuoni wanakubaliana kwamba kila eneo lina wakati wake wa kuanza kufuturu (kufungua Swaum) wakati wa magharibi linapozama jua, wakati wa kujizuilia kula daku inapokaribia alfajiri na pia kila eneo litatekeleza ibada ya swala zake zote tano kwa kuangalia mipinduko ya jua.
JAWABU
Na hili tushalikariri sana. Ufupisho wake ni kuwa kwa makubaliano hayo, ndio imejuzu kufanya Qias sahihi katika nchi zenye miandamo tafauti. Nayo ni kwamba, kama vile ambavyo watu wenye matalai tafauti ya jua wanavyotafautiana kufunga na kufungua, vivyo hivyo wenye matalai tafauti ya mwezi watafautiane katika kuanza kufunga na kufungua. Na ndio maana ya maneno ya Sheikh Ibn 'Uthaimin: "Na wakati wa mwezi ni kama wak ati wa siku. Na akasema: "Hiki ni Qias sahihi ambacho huwezi kukipinga".
MNASEMA
Na hata kama yupo mwanachuoni aliyesema kuwa Hadiyth fulani inawaruhusu watu wa nchi fulani ambapo wengine haiwaruhusu, maneno hayo pia hayawezi kuchukuliwa kama ni hoja sahihi na yenye mashiko madhubuti kwa sababu zifuatazo: Kwanza: Hadiyth zote zilizotaja wajibu wa kufunga na kufungua zimekuja kwa matamko ya kujumuisha Waumini wote popote walipo. Na kanuni ya Usulul-Fiqhi inatufahamisha tuendelee kushikamana na 'aam mpaka ipatikane Khaas. Pili: Kutegemea maneno, matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa ni udhaifu.
JAWABU
Haya yote tumeshayaeleza mara baada ya mara. Tumeeleza ni ujumla gani uliokuwemo katika Hadithi "Fungeni kwa kuuona", na kwamba hakuna dalili ndani yake kuwa watu wafunge kwa muandamo mmoja; bali kuna dalili kwamba watu wote lazima wafunge kwa kuuona, yaani kuuona iwe ndio sababu ya kufungwa. Hadit hi hii inaonesha sababu ya kufunga kwani Lamul Jarri iliokuwemo ndani yake inaitwa Ta'aliliya yaani ya kuonesha sababu ya amri iliotajwa. Hivi ndivyo kufasiri kwa mujibu wa fani. Ama khaas ni Riwaya ya Ibn Abbaas na Kuraib, alipoacha kuufata muandamo wa mbali na akasema "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w.". Kwa hivyo, khaas imepatikana. Kwa hivyo, udhaifu uko kwenu kwa kutokuweza kuzifahamu dalili za Kisharia.
MNASEMA
iv). Tunapenda kusisitiza maneno yetu ya nyuma ya kwamba cha msingi ni kufunga Swaum na kufungua siku moja kwa Waislamu wote sio kufunga au kufungua kwa saa au dakika moja.
JAWABU
Hata hili haliwezekani. Kwani usiku wa baadhi ya nchi ni mchana kwengine na mcha wa baadhi ya nchi ni usiku kwengine wala hazikutani kamwe.
MNASEMA
v). Haiwezekani kutumika "Qiyaas" cha Swala na Swaum katika misingi ya Shari'ah kwani kwa hapa patakosekana nguzo za kufanyia "Qiyaas." Ni vyema tuelewe kwamba "Qiyaas" hutumika pale tu ambapo hakuna Aya wala Hadiyth juu ya jambo hilo Shar'iah ya Usulul-Fiqhi inasema ifuatavyo:
1. Angalia Kitabu: Kanuni zote hizo mbili zina maana ya kuwa: "Qiyaas" hakitumiki kwa kuwepo dalili za uwazi (yaani: Qur-aan na Hadiyth). Na jam bo hili la muandamo wa mwezi limetajwa wazi katika Hadiyth nyingi za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
JAWABU
Hio sio maana ya kanuni hio. Maana ya kanuni hio ni kuwa hakuna kufanya Qias chenye kugongana na andiko; sio Qias chenye kuwafikiana na andiko. Tegemeo la msingi la wenye kusisitiza kuwepo kwa miandamo tafauti ni Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas. Kwa hivyo, Qias hicho kinakwenda sawa na andiko.
MNASEMA
Wala huwezi kusema kila nchi itaswali wakati mmoja kwani kuna baadhi ya nchi moja kama ambayo ni kubwa sana , yenyewe ina tofauti ya masaa mengi kutoka eneo moja kwenda jengine.
JAWABU
Hili nalo tumeshalielezea zaidi ya mara moja. Mukhtasar wake ni kuwa hapaangaliwi nchi moja au mbili; kinachoangali ni umbali na kutafautiana kwa matalai. Pamoja na hivyo, kama tulivyoeleza, suala la umbali gani linatoa nafasi ya ijtihad kwa kutokuwepo andiko la wazi. Lakini suala la kufunga watu wote kwa muandamo mmoja ndio lililo kinyume na andiko na Qias sahihi pia.
19
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA KUMI NA NANE
KUFUNGWA KWA MASHETANI
MUNASEMA
18. Kufungwa Kwa Mashetani Katika kejeli zake ndugu Juma kwenye hoja za Kidini, hata katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anathubutu kuyaumbua kwa kusema kama ifuatavyo: ((Hoja nyengine - ya mitaani - inasema kwamba Ramadhani inapoingia hupatikana rehema fulani. Miongoni mwa hizo ni kuwa mashetani wote hufungwa kama Bwana Mtume(s.a.w.w) alivyosema: "Ramadhani ikiingia, milango ya mbingu (na katika riwaya ya pili) milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya jahannam hufungwa na mashetani hutiwa minyororo." Na Hadithi nyengine inasema: "Inapoingia siku ya kwanza ya Ramadhani upepo hupiga chini ya Arshi kutoka katika majani ya pepo (kuwapiga upepo huo) Mahuru-Al-ain.)
Maneno kama haya ya kuyakejeli na kuyabeza maneno matukufu ya Mtume(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuyafanya kama kwamba ni maneno ya mitaani au kuifanya haki kuwa batil ni katika mambo yanayompelekea mtu kuingia katika kufru. Kitu cha msingi ni vyema kukumbuka kwamba Shaykh Naaswir Bachuu hakuonesha lugha za kashfa na kejeli hata katika yale maeneo ambayo hakukubaliana nayo basi pia alitumia lugha ya kistaarabu.
JAWABU
Kejeli iko wapi hapa? Je mimi niliyaita maneno ya Mtume(s.a.w.w) kuwa ndio hoja ya mitaani au niliita kule Sheikh Nassor Bachoo kutoa hoja kwa Hadithi hio kuwa ndio hoja ya mitaani? Ebu Soma yote niliosema. Nilisema: Hoja nyengine - ya mitaani - inasema kwamba Ramadhani inapoingia hupatikana rehema fulani. Miongoni mwa hizo ni kuwa mashetani wote hufungwa kama Bwana Mtume(s.a.w.w) alivyosema: "Ramadhani ikiingia, milango ya mbingu (na katika riwaya ya pili) milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya jahannam hufungwa na mashetani hutiwa minyororo." Na Hadithi nyengine inasema: "Inapoingia siku ya kwanza ya Ramadhani upepo hupiga chini ya Arshi kutoka katika majani ya pepo (kuwapiga upepo huo) Mahuru-Al-ain."
Tunachojifunza kutokana na Hadithi hizi ni kuwa:
1) Ramadhani ni moja!!!
2) Neema hizo za kufungwa mashetani na nyenginezo hupatikana siku ya mwanzo ya Ramadhani. Sasa je:
a) Rehema hizi watazipata dunia nzima au wale waliouona mwezi tu?!!!
b) "Inapotokea nchi fulani kama Saudia (Makka & Madina) imeingia katika Ramadhani, Tanzania wanangoja mwezi wao.
Je inaaminika kwamba wale mashetani walioko nchini S. Arabia yatakuwa yamefungwa na mashetani yalioko Tanzania watabaki huru bado? Au tudhani mashetani yalioko S. Arabia yatakimbilia huku Tanzania mbio kuja 'kuvunja jungu' kwa kuwa Ramadhani haijaingia huku bado?"
c) Je mtu aliyeanza kufunga S. Arabia siku ya mwanzo, siku ya pili akaja Tanzania wakati bado watu hawajaanza kufunga, vipi ile rehema ya kufungiwa mashetani ataipata, au watafungwa kwa ajili yake tu?!!!
d) Je mtu huyu aliyeanza kufunga Ramadhani S. Arabia kisha alipokuja Tanzania Ramadhani bado je ataambiwa kaja kufunga Ramadhani au kafunga Ramadhani Saudia na kaja kufunga Shaabani huku Tanzania.
e) Nini hukumu ya saumu ya mtu huyu?!
Masuala haya nimeyanukuu kimaana kutoka katika kitabu cha Sheikh Bachoo , nayo ni masuala ya kuchekesha na kustaajabisha!!! Lau tutakwenda mahala kama Al-azhar au chuo chochote kile kikubwa tukatoa hoja hizi, basi hata yule anayeona kwamba kauli sahihi ni kauli ya kufunga kwa muandamo mmoja basi atacheka sana!!!
Ama kuhusu suala la kwanza kwamba Hadithi hizi zinathibitisha kuwepo Ramadhani moja, Jawabu yake ni kuwa Ramadhani kweli ni moja. Na kwani ni nani kasema kwamba kuna Ramadhani mbili katika mwaka? Ramadhani ni moja katika mwaka isipokuwa inatangulia kuingia katika miji fulani na kuchelewa katika miji myengine, kama vile ambavyo - katika Ramadhani moja hio hio, tunatangulia kufunga katika baadhi ya miji kwa kutangulia kuchomoza alfajiri na tunachelewa kufunga katika miji myengine kwa kuchelewa kuingia alfajiri. Na tunatangulia kufuturu katika miji myengine kwa kutangulia kutua kwa jua na tunachelewa katika miji myengine kwa kuchelewa kutua kwa jua. Na hii haina maana kwamba kuna Ramadhani tano au kumi.
Ramadhani zingelikuwa mbili lau ingelikuwa tunafunga mwezi huo wa Ramadhani, na mwezi mwengine, mathalan tunafunga na mfunguo sita, lakini tunafunga mwezi mmoja, tafauti ni katika kutangulia na kuchelewa tu, basi vipi mtu atatoa hoja kama hio!!! Tazama ukweli kwamba, pia kuna watu wanatangulia kusali Adhuhuri na wengine wanachelewa kwa masaa mengi, wala haisemwi kwamba kuna Adhuhuri tatu au nne. Kwa hivyo, dai hili halina muelekeo kabisa wala halifai kuzungumzwa na wanavyuoni wala wanafunzi, dai hili linafaa kuzungumzwa na watu wasiojua Dalili za Kisharia.
Pili : ni kuwa Hadithi mbili hizo alizozinukuu Sheikh Bachoo hazitoi ushahidi huo kamwe wa kuwa na Ramadhani moja, kwani mantiki ya kusemwa "Ikiingia Ramadhani" ni sawa sawa na kusemwa: "Ikiingia J/tatu" au kusemwa "Ukiingia usiku" na hii haina maana kwamba J/tatu ikianza kuingia sehemu moja huwa imeingia dunia nzima: bali ikianza kuingia sehemu moja - yaani baada ya kutua jua magharibi - sehemu nyengine bado ni J/pili asubuhi. Halkadhalika kusemwa "Ukiingia usiku" kama Allah alivyosema: Usiku ulipomuingilia: haina maana kwamba usiku ukiingia sehemu moja ndio umeingia dunia nzima. Kwa ufupi ni kuwa hii ni hoja ambayo haina faida yoyote ya kielimu, lakini tunaijadili kwa ajili ya watu wa mitaani tu.
Ama suala linalosema: "Je mtu huyu aliyeanza kufunga Ramadhani S. Arabia kisha alipokuja Tanzania Ramadhani bado je ataambiwa kaja kufunga Ramadhani au kafunga Ramadhani Saudia na kaja kufunga Shaabani huku Tanzania Nini hukumu ya saumu ya mtu huyu?!" Jawabu yake ni kuwa: je mtu aliyepanda ndege siku ya J/pili - mathalan - ikamkuta magharibi humo katika ndege katika sehemu fulani ya anga ya dunia akafuturu, kisha baada ya saa moja au mbili akaingia katika anga ya nchi nyengine bado ni saa 9 za jioni ya siku hio hio ya J/pili, funga yake itakuwaje: je ataambiwa kafunga huyu siku ya J/pili au kafunga nusu ya siku hio katika sehemu moja ya dunia na kala katika sehemu nyengine ya dunia?
Tena mara ya pili: je mtu aliyepanda ndege akaanza kusali Adhuhuri humo katika sehemu ambayo jua tayari limetenguka au akasali magharibi katika sehemu ambayo jua tayari limezama na kabla ya kumaliza ikawa ndege imeingia katika sehemu ambayo jua bado halijatenguka au halijazama, je yule aliyesali Adhuhuri ataambiwa kasali Adhuhuri au kasali nusu adhuhuri na nusu Dhuha?! Na yule aliyesali magharibi atakuwa kasali magharibi au kasali sala ambayo nusu yake ni magharibi na nusu yake ni laasiri kipande: yenye rakaa tatu? Jawabu yako hapa ndio jawabu yetu kule. Utaona kwamba masuala yote haya si yenye kima katika soko la elimu, bali ni masuala ya kuwababaisha watu wasiojua nini cha kujadiliwa katika mas-ala haya ya funga.
Sasa cha muhimu kujua ni kuwa Dini ya Kiislamu imeyagawa mambo katika sehemu nne kuu. Moja ni kitu ambacho kimeelezwa katika Qur-an kwa uwazi. Pili ni kitu ambacho kimeelezwa katika Sunnah (Hadithi) kwa uwazi. Tatu ni kitu ambacho Umma umekubaliana juu ya kitu hicho. Mambo matatu haya hayafai kupingwa: ni lazima tufanye vile vile ilivyoelezwa kwa uwazi. Sasa mambo mengine (ambayo ndio ya nne) ni yale ambayo hayakuelezwa kabisa au hayakufafanuliwa nayo ni kama hayo:
1) Aliyefunga katika nchi fulani kisha akaja katika nchi nyengine watu wako katika Shaabani.
2) Kama tulivyosema: "Aliyepanda ndege siku ya J/pili - mathalan - ikamkuta magharibi humo katika ndege katika sehemu fulani ya anga ya dunia akafuturu, kisha baada ya saa moja au mbili akaingia katika anga ya nchi nyengine bado ni saa 9 za jioni ya siku hio hio ya J/pili ya tarehe hio hio alioiwacha katika nchi alioondoka, funga yake itakuwaje: je ataambiwa kafunga huyu siku ya J/pili au kafunga nusu ya siku hio katika sehemu moja ya dunia na kala katika sehemu nyengine ya dunia?"
3) Aliyesali Magharibi katika ndege baada ya kutua jua kabla ya kumaliza sala yake ndege imeingia katika anga ambayo jua lake bado halijatua, je itakuwaje sala yake.
Mas-ala haya na yalio mfano wa haya hayana andiko maalumu lililo wazi, kwa hivyo huitwa mas-ala ya ijtihadi. Kila aliyefikia daraja ya kuitwa Mujtahid atatoa fikra yake akijiongozea kwa dalili za Kisharia (Qur-an, Sunna, Ijmaa (makubaliano ya Umma) au Qiyas (analogy). Kwa hivyo, utaona kwamba bado tuna tatizo la kutokufahamu tafauti baina ya mas-ala ya ijtihadi na yale yasio ya ijtihadi. Mas-ala ya kutokufata muandamo wa mbali yamethibiti kwa Hadithi ya Mtume (s.a.w.) katika riwaya hio ya Ibn Abbas na Kuraib, kwa hivyo haya si mas-ala ya ijtihadi, lakini furui (matawi) tunazozipata katika mas-ala haya na ambazo hazikuelezwa kwa uwazi, ndizo za kufanyiwa ijtihadi.
Sasa kwa ufupi ni kuwa jawabu ya suala "Nini hukumu ya saumu ya mtu huyu" aliyefunga Ramadhani S. Arabia na alipokuja Tanzania akakuta watu wanakula bado ni Shaabani, jawabu ya suala hili ni jawabu ya masuala mawili tulioyatoa, nayo ni masuala ya aliyefuturu na aliyesali kwenye ndege. Na hii ni kuwa:
1) Ima aliyesali basi sala yake aliosali mwanzo aitupilie mbali na aanze upya kwani katika sehemu alio bado wakati wa Sala haujaingia. Halkadhalika aliyefuturu. Ukichukua msingi huu, basi na aliyefunga Saudia Ramadhani na alipokuja Tanzania akaikuta Shaabani bado imo, basi saumu yake asiizingatie na aanze upya kwani katika sehemu alio bado wakati wa kufunga haujaingia.
2) Au asirejee tena sala yake kwani kasali kwa mujibu wa wakati sawa huko alikotoka. Halkadhalika aliyefuturu. Basi na huyu aliyetoka Saudia naye aendelee kufunga kwa kuzingatia kwamba kafunga sawa kwa mujibu wa kule anakotoka. Kwa hivyo, chagua jawabu unayotaka katika mas-ala haya mawili ya aliye kwenye ndege, kisha jawabu yako hio utayoichagua ndio jawabu yetu kwako kwa yule aliyefunga S. Arabia na akaja Tanzania hali ya kuwa bado ni Shaabani.
Ama masuala ya kufungwa mashetani hayana uhusiano kabisa na masuala ya kuthibiti muandamo wa mwezi katika miji pasi na kuthibiti katika miji myengine. Na kipi kinatujuilisha sisi kwamba mwezi ukiandama sehemu moja hufungwa mashetani wa dunia nzima au kila mahala hufungwa mashetani kwa mujibu wa muandamo wa mwezi wa mahala hapo? Kipi kitatujuilisha mas-ala haya. Haya ni mas-ala ya ghaibu wala hayatakiwi kabisa kuhusishwa na mas-ala ya dhahiri. Hadithi inatueleza kwamba mashetani hufungwa. Vipi wanafungwa: hakuna ufafanuzi. Na mas-ala haya ni mas-ala ya itikadi haitakiwi kusema kwa ijtihadi na rai wala kwa kusukuma. Bali Hadithi hio inabidi itazamwe, ikiwa ni Hadithi sahihi na ni mutawatir basi tuikubali; ikiwa sahihi lakini ni Ahadi basi tutatazama ikiwa Umma umekubaliana juu ya maana yake, itakuwa imepata nguvu kwa Ijmaa (makubaliano) ya Umma; ikiwa kuna khilafu nayo ni Hadithi Ahadi basi tuiache kama ilivyo, kwani Hadithi Ahadi haijengewi hoja katika mambo ya itikadi, kama Jumhuri ya Umma ilivyosema. Mwisho wa kunuu nilioyasema katika kitabu.
Hayo ndio nilioyasema. Haya nionesheni hapa wapi nimeyakejeli maneno ya Mtume(s.a.w.w) . Mimi ninachokipinga ni kuzichukua Hadithi hizo za kufungwa kwa mashetani kama ni ushahidi wa kuwepo kwa muandamo mmoja: sio kuzikejeli Hadithi hizo. Bali nimesema katika maelezo ya chini: "Ibn Hajar ana maelezo mazuri kuhusu Hadithi ya kufungwa mashetani. Tazama Al-Fat-Hu katika sherehe ya Hadithi na. 1899". Sasa tuseme ndio mumekuwa hamufahamu kiasi hiki au muna lengo lenu?!
Munasema Tukirudi katika mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya kufungwa kwa mashetani tunazingatia juu ya kuingia kwa mwezi wa Ramadhaan, kwani maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yamekuja katika matamko yasemayo: (Inapoingia siku ya mwanzo ya Ramadhaan mashetani hufungwa)
Ndugu Juma akiendelea kudai kwamba: (Ikiingia Ramadhani" ni sawa sawa na kusemwa: "Ikiingia J/tatu" au kusemwa "Ukiingia usiku" na hii haina maana kwamba J/tatu ikianza kuingia sehemu moja huwa imeingia dunia nzima: bali ikianza kuingia sehemu moja - yaani baada ya kutua jua magharibi - sehemu nyengine bado ni J/pili asubuhi.)
Hayo ndio kama yale tunayomueleza ndugu Juma kila mara kwamba Suala la kutangulia mchana au usiku sio hoja katika mas-ala ya muandamo wa mwezi. Hilo ni jambo lisilowezekana kutumia "Qiyaas" cha mwezi na jua. Hapawezekani kutumiwa "Qiyaas" cha Swala, kuanza kufutari wakati wa magharibi au nyakati za kula daku kabla ya alfajiri hata katika nchi moja kuna kutafautiana katika kuingia mchana na usiku pia kuna kutafautiana katika kuingia "siku." Tuchukulie mfano Dar es Salaam inaingia katika siku ya Jumapili pale jua linapotua, wakati huo huo Kigoma bado iko katika siku ya Jumamosi jioni. Lakini kumbuka kwamba wanafunga siku moja ya muandamo wa mwezi mmoja. Tukichukua mfano mwengine wa nchi kubwa kama Canada au Urusi, ndani ya nchi hizo kuna tafauti ya masaa mengi kutoka mashariki hadi magharibi zake.
JAWABU
Haya yote nimeshayaeleza - mas-ala ya Qias, mas-ala ya kuwa na nyakati tafauti za kufuturu katika nchi moja yote mumeyakariri mara elfu na tumeshayaeleza sana. Lakini pamoja na hayo, hayana uhusiano na maudhui iliopo hapa. Maudhui ya hapa ni kufungwa kwa mashetani na hili pia nimeshakufafanulieni kwamba si hoja ya kuwa tuwe na muandamo mmoja wala mas-ala hayo hayapo kamwe katika uwanja wa elimu.
MNASEMA
Akiendelea kutoa hoja zake ndugu Juma juu ya kufungwa kwa Mashetani anahoji: (Na kipi kinatujuilisha sisi kwamba mwezi ukiandama sehemu moja hufungwa mashetani wa dunia nzima au kila mahala hufungwa mashetani kwa mujibu wa muandamo wa mwezi wa mahala hapo?) Hapa Ndugu Juma amekuja na dhana kwamba mashetani hufungwa pale tu ilipoingia Ramadhaan. Na sisi tunamuuliza ni wapi ameona kuwa ikiingia Ramadhaan hufungwa mashetani wa sehemu hiyo tu iliyoandama mwezi?
JAWABU
Hilo suala jijibuni wenyewe kwani mimi sijasema hivyo wala sijaja na dhana hio, ingawa nadai kwamba inawezekana ikawa hivi na inawezekana ikawa hivi: hakuna ushahidi wa mkato juu ya vipi mashetani wanafungwa. Na mimi nilichokisema ni hiki: Ama masuala ya kufungwa mashetani hayana uhusiano kabisa na masuala ya kuthibiti muandamo wa mwezi katika miji pasi na kuthibiti katika miji myengine. Na kipi kinatujuilisha sisi kwamba mwezi ukiandama sehemu moja hufungwa mashetani wa dunia nzima au kila mahala hufungwa mashetani kwa mujibu wa muandamo wa mwezi wa mahala hapo? Kipi kitatujuilisha mas-ala haya.
Haya ni mas-ala ya ghaibu wala hayatakiwi kabisa kuhusishwa na mas-ala ya dhahiri. Hadithi inatueleza kwamba mashetani hufungwa. Vipi wanafungwa: hakuna ufafanuzi. Na mas-ala haya ni mas-ala ya itikadi haitakiwi kusema kwa ijtihadi na rai wala kwa kusukuma. Bali Hadithi hio inabidi itazamwe, ikiwa ni Hadithi sahihi na ni mutawatir basi tuikubali; ikiwa sahihi lakini ni Ahadi basi tutatazama ikiwa Umma umekubaliana juu ya maana yake, itakuwa imepata nguvu kwa Ijmaa (makubaliano) ya Umma; ikiwa kuna khilafu nayo ni Hadithi Ahadi basi tuiache kama ilivyo, kwani Hadithi Ahadi haijengewi hoja katika mambo ya itikadi, kama Jumhuri ya Umma ilivyosema.
MNASEMA
Tujuavyo sisi ni kuwa tamko la "Ashshayaattwiinu" kwa hapa lina maana ya mashetani wote dun ia nzima. Tamko lililokuja katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kufungwa kwa mashetani inapoingia siku ya mwanzo ya Ramadhaan yaani, lina "Alif na Laam" ambayo linaonesha ni tamko la umumi ('aam). Neno ni na kawaida ya neno "Ismul-jinsi" linawakilisha maana ya ('aam) yaani linazungumzia "ujumla" au "wote". Baadhi ya vitabu vilieleza kwamba "Ismul-jinsi" kuwa ni ('aam)
Ni vyema kuelewa kuwa msimamo wa Shaykh Naaswir Bachuu katika kitabu chake ni kuwataka Waumini wote wafunge na kufungua kwa "Siku moja" na msimamo wake huo unatokana na Hadiyth sahihi ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo na watu wote kwamba: ((Fungeni kwa kuonekana mwezi - muandamo.)) Maneno hayo ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yanawajumuisha Waumini wote, popote walipo kama tulivyokwisha elezea hayo katika kurasa zilizopita. Kwa upande wa utekelezaji wa kufunga na kufungua kwa dunia nzima siku moja, uwezekano huo pia upo kama tulivyokwisha elezea kwa urefu.
JAWABU
Madai yenu: "Tujuavyo sisi ni kuwa tamko la "Ashshayaattwiinu" kwa hapa lina maana ya mashetani wote dunia n zima. Tamko lililokuja katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kufungwa kwa mashetani inapoingia siku ya mwanzo ya Ramadhaan yaani, lina "Alif na Laam" ambayo linaonesha ni tamko la umumi ('aam). Madai haya yanaonesha hamujui mukisemacho. Huu sawa ni ujumla lakini kwa mujibu wa qarina (context) ya Hadithi hakuna ulazima wa kuwa iwe ni ujumla wa dunia nzima. Sababu ni kama ilivyo katika Hadithi: "Ikiingia siki ya kwanza ya Ramadhani" na Ramadh ani haiingii dunia nzima kwa wakati mmoja. Bali kuna sehemu imeingia yaani kwa kuingia magharibi na kuna sehemu ni asubuhi - Ramadhani haijaingia. Ni sawa na kusema "Ikiingia J/tatu", J/tatu huwa haiingi dunia nzima wakati mmoja. Kwa hivyo, ujumla uliomo katika mashetani si lazima uwe ujumla wa dunia, bali inawezekana ikawa hivyo, na inawezekana ikawa pale ilipoingia Ramadhani tu, kwani tamko ikiingia siku ya kwanza ya Ramadhani haliuhusu ulimwengu wote. Kwa hivyo, hili ni suala la ghaib na halina ufafanuzi bali lina ihtimalat uwezekano huu na ule. Kwa hivyo, hii si hoja inayokubalika Kisharia.
MNASEMA
Baada ya maelezo kama hayo: Ndugu Juma anatoa hoja za kutokuwepo uwezekano huo kwa kutoa mifano tofauti kama ifuatayo: ((je mtu aliyepanda ndege siku ya J/pili - mathalan - ikamkuta magharibi humo katika ndege katika sehemu fulani ya anga ya dunia akafuturu, kisha baada ya saa moja au mbili akaingia katika anga ya nchi nyengine bado ni saa 9 za jioni ya siku hio hio ya J/pili, funga yake itakuwaje: je ataambiwa kafunga huyu siku ya J/pili au kafunga nusu ya siku hio katika sehemu moja ya dunia na kala katika sehemu nyengine ya dunia? Tena mara ya pili: je mtu aliyepanda ndege akaanza kusali Adhuhuri humo katika sehemu ambayo jua tayari limetenguka au akasali magharibi katika sehemu ambayo jua tayari limezama na kabla ya kumaliza ikawa ndege imeingia katika sehemu ambayo jua bado halijatenguka au halijazama, je yule aliyesali Adhuhuri ataambiwa kasali Adhuhuri au kasali nusu adhuhuri na nusu Dhuha?!))
JAWABU
yetu kwa ndugu Juma ni pale pale kwamba: a). Hayo ni mas-ala ya Ijtihaad kama alivyotaja mwenyewe ndugu Juma kwenye uk 168 wa kitabu chake. Ndio maana hakuna kauli moja ya Wanavyuoni katika mas-ala hayo.
JAWABU
Kwani mimi nilisema hivi kujibu nini. Tafadhali rejeeni mjadala kamili: musikate maneno vipande bila kutimaza maana. Nukta hii ilikusudiwa kujibu kitu maalumu nayo ni kuwa Sheikh Nassor aliuliza masuala haya:
1) Je mtu huyu aliyeanza kufunga Ramadhani S. Arabia kisha alipokuja Tanzania Ramadhani bado je ataambiwa kaja kufunga Ramadhani au kafunga Ramadhani Saudia na kaja kufunga Shaabani huku Tanzania.
2) Nini hukumu ya saumu ya mtu huyu?!
Hayo ndio masuala yake. Nami nikamjadili kwa kusema: Ama suala linalosema: "Je mtu huyu aliyeanza kufunga Ramadhani S. Arabia kisha alipokuja Tanzania Ramadhani bado je ataambiwa kaja kufunga Ramadhani au kafunga Ramadhani Saudia na kaja kufunga Shaabani huku Tanzania Nini hukumu ya saumu ya mtu huyu?!" Jawabu yake ni kuwa: je mtu aliyepanda ndege siku ya J/p ili - mathalan - ikamkuta magharibi humo katika ndege katika sehemu fulani ya anga ya dunia akafuturu, kisha baada ya saa moja au mbili akaingia katika anga ya nchi nyengine bado ni saa 9 za jioni ya siku hio hio ya J/pili, funga yake itakuwaje: je ataambiwa kafunga huyu siku ya J/pili au kafunga nusu ya siku hio katika sehemu moja ya dunia na kala katika sehemu nyengine ya dunia?
Tena mara ya pili: je mtu aliyepanda ndege akaanza kusali Adhuhuri humo katika sehemu ambayo jua tayari limetenguka au akasali magharibi katika sehemu ambayo jua tayari limezama na kabla ya kumaliza ikawa ndege imeingia katika sehemu ambayo jua bado halijatenguka au halijazama, je yule aliyesali Adhuhuri ataambiwa kasali Adhuhuri au kasali nusu adhuhuri na nusu Dhuha?! Na yule aliyesali magharibi atakuwa kasali magharibi au kasali sala ambayo nusu yake ni magharibi na nusu yake ni laasiri kipande: yenye rakaa tatu? Jawabu yako hapa ndio jawabu yetu kule. Utaona kwamba masuala yote haya si yenye kima katika soko la elimu, bali ni masuala ya kuwababaisha watu wasiojua nini cha kujadiliwa katika mas-ala haya ya funga. Kwa hivyo, huu ndio mnasaba wa mimi kusema hayo mulioyanukuu. Ama ikiwa hamukujilazimisha kunukuu kitu kwa ukamilifu, mutamfanya msomaji asijue nini hasa kimezungumzwa.
MNASEMA
b). Ndugu Juma anapenda kutumia "Qiyaas" cha Sala na Funga (Swaum) ambapo tumeshaeleza kwamba ni jambo lisilokubaliana kabisa. Hayo tumeyaeleza sana , tatizo sio muandamo mmoja au mingi, hata katika nchi moja inatokea, unaweza kusafiri kwa ndege ukasali katika anga la Dar-es-salaam Adhuhuri ukafika Kigoma bado haijaingia Adhuhuri. Je utasema Dar-es-salaam na Kigoma kila moja iangalie mwezi wake? Au kama utaondoka Dar es Salaam umeshafuturu ukafika Kigoma jua halijatua bado utafanyaje?
JAWABU
Ni kweli: hayo mumeyaeleza sana nami nimekujibuni sana nanyi munakariri yayo kwa yao. Suala la miandamo nimekwambieni haitazamwi nchi moja; inatazamwa tafauti za matalai na umbali wa masafa. Kwa hivyo, hii hoja yenu munayoikariri "Hata nchi moja; hata nchi moja" hii si hoja ya kuzingatiwa, kwani kinachotazamwa ni tafauti za matala na umbali: si nchi moja au nchi tafauti. Ama huyu aliyetoka Dar baada ya kufuturu akafika Kigoma bado jua halijatua, sijui kenda kwa chombo gani, maana Unguja na Pemba kwa ndege - nadhani - haipungui nusu saa; sasa Kigoma yenye tafauti ya dakika 40 kwa mujibu wa maneno yenu na masafa ni marefu mno, sijui kapanda chombo gani!
MNASEMA
Kabla ya kuendelea na ufafanuzi zaidi ni vyema kumnukuu ndugu Juma katika maelezo yake anaposema: (Sasa cha muhimu kujua ni kuwa Dini ya Kiislamu imeyagawa mambo katika sehemu nne kuu. Moja ni kitu ambacho kimeelezwa katika Qur-an kwa uwazi. Pili ni kitu ambacho kimeelezwa katika Sunnah (Hadithi) kwa uwazi. Tatu ni kitu ambacho Umma umekubaliana juu ya kitu hicho. Mambo matatu haya hayafai kupingwa: ni lazima tufanye vile vile ilivyoelezwa kwa uwazi. Sasa mambo mengine (ambayo ndio ya nne) ni yale ambayo hayakuelezwa kabisa au hayakufafanuliwa) Kwa maelezo hayo mazuri aliyoyaeleza ndugu Juma tungependa kumuuliza:
Je suala la kufunga na kufungua kwa muandamo mmoja ataliweka wapi katika mafungu hayo? Bila shaka suala hili litawekwa katika kifungu cha pili. Yaani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelieleza jambo hili kwa uwazi. Riwaya zote zilizokuja katika agizo hili ni sahihi na zenye kukubalika mbele ya Wanazuoni wote wa Kiislamu. Na riwaya zote hizo zimekuja kwa Waumini wote popote walipo watekeleze agizo hilo Mwanachuoni maarufu Al-Jassas katika kitabu chake Ahkamul-Qur-aan J. I uk 305 katika kuielezea kauli hii ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema hivi:- "Ni jambo linaloeleweka kuwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo: (Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi), ni ya jumla inawahusisha watu wa pande zote za dunia na kwamba haihusu watu wa nchi moja peke yao pasi na wengine."
JAWABU
Tunaendelea kukariri. Suala la kufunga kwa miandamo tafauti limefafanuliwa na Hadithi ya Ibn Abbaas, kilichojificha ni masafa. Ama Hadithi munazosema nyinyi ni Hadithi Aam. Lakini suala ni kuwa je ujmla wenyewe ni ujmla gani. Tumeshakubainishieni kuwa ujmla wenyewe ni kuwa watu wote wanaamrishwa kuwa wasifunge ila kwa kuuona. Ndio maana katika riwaya nyengine ikaja "Musifunge mpaka muuone". Hakuna katika riwaya zote hizo ufafanuzi juu ya suala la kuwa je tufunge kwa muandamo mmoja au kila watu wawe na muandamo wao. Ufafanuzi huu unapatikana katika Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas ambayo munaikimbia: hamuitaki. Kwa hivyo, maneno ya Al-Jassas si sahihi, na kama mulivyosema, maneno ya mwanachuoni hayana kima ikiwa yatakwenda kinyume na dalili. Madai hayo yanaifanya Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas isizingatiwe: iwachwe wakati kanuni ni kutokuliacha andiko lolote litapowezekana kutendewa kazi. Kwa ufupi ni kuwa, hoja hio niliijibu kama ifatavyo: Jambo la pili: la kutazamwa katika Hadithi hii ni kuwa Khitabu (Agizo: kama alivyofasiri Sheikh Nassor Bachoo) ya Hadithi hii ni Aam (ya ujumla), kama Sheikh alivyon ukuu kutoka katika kitabu cha Al-sayyid Saabiq.
Na sisi tunajibu kwa jawabu mbili. Ya kwanza ni kuwa: Ujumla wa agizo hilo, umehusishwa na Hadithi ya Ibn Abbas, na kanuni ya kiusuli inaeleza kwamba Al-khaas (Andiko maalumu au specific) ndio inayotangul izwa kuliko Al-aam (Andiko la ujumla), kwa kuwa kwake (hio Khaas) ni ya uhakika kinyume na Aam hakika yake ni (kitu) cha dhana. Kwa hivyo kanuni hapa inatutaka kuitanguliza Hadithi ya Ibn Abbas. Na natija ni kuwa ujumla jamala uliobakia katika Had ithi "Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi" na ambacho tunachotakiwa sote tukifanye kwa mujibu wa Hadithi hii, ni kuwa sote tufunge kwa kuuona mwezi. Ama je muandamo ni mmoja au kila watu wana muandamo wao, Hadithi hii haitoi jawabu hio.
Jawabu ya pili: ni ile tuliotangulia kuinukuu kutoka kwa Sheikh Ibn Uthaimin aliponukuu jawabu ya wale wenye kusema kwamba kila mji una muandamo wake, ambapo walisema kwamba ujumla uliomo katika Hadithi hio, ni sawa na ujumla uliomo katika Aya inayosema:
﴿ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ ﴾
"Sasa waingiliyeni (wake zenu) na tafuteni kile Allah alichokuandikiyeni, na kuleni na kunyweni mpaka ukubainikieni uzi mweupe kutokana na uzi mweusi wa alfajiri, kisha timizeni saumu hadi usiku."
Je hapa Allah anazungumza na watu wote au na watu maalumu? Je kuzungumza huku na watu wote inamaanisha kwamba alfajiri ya nchi moja ikichomoza watu wa nchi zote wajizuie, au kila watu na alfajiri yao? Jawabu yako hapa ndio jawabu yetu kwa maneno ulioyanukuu kutoka katika kitabu cha Al-sayyid Saabiq kwamba Hadithi hiyo "Fungeni kwa kuuona" ni: "Agizo la ujumla linalojumuisha umma wote (wa Kiislamu) kwa hivyo; yeyote miongoni mwao atakayeuona (mwezi) popote pale; kuonekana huko ku takuwa ni kuonekana kwa wote." Halkadhalika tunajibu ujumla huo kwa Hadithi inayosema:"Usiku ukitokeza kutoka hapa na mchana ukaondoka kutokea hapa na jua likatua, basi aliyefunga ameshafungua (au na-afungue)." Na sisi tunauliza je hapa walikuwa wakiambiwa watu wa Makka tu, au wakiambiwa watu wa nchi zote? Kama walikuwa wakiambiwa watu wa nchi zote, je jua likitua Makka au katika mji wowote ule sote tufuturu? Kwa hakika kila aliyejaaliwa kuwa na mtazamo sahihi, anaona kwamba kujenga hoja kwa ujumla wa Hadithi "Fungeni kwa kuuona" kwamba ni ushahidi wa kuwepo muandamo mmoja, ni kujenga hoja juu ya msingi dhaifu sana. Na kwa maana hio, Ibn Uthaimin (Mwanachuoni wa Kiwahabi) akasema kwamba kauli ya kuwa kila watu wana muandamo wao: "Ina nguvu yake kwa mujibu wa lafdhi (yake) na mtazamo sahihi na Qiyas sahihi vile vile: Qiyas cha wakati wa siku kwa (kuulinganisha) na wakati wa mwezi (month). Mwisho wa kunukuu.
Kwa ufupi ni kuwa, ujumla wa Hadithi inayosema "Fungeni kwa kuuona" ni - kama tulivyotangulia kusema - kwamba watu wote ni lazima wafunge kwa kuuona: si kwa kalenda wala kwa jengine lolote. Huu ndio ujumla unaokusudiwa katika Hadithi hio, au ndio ujumla uliobakia baada ya kuhusishwa au kuvuliwa sehemu ya ujumla huo na Hadithi ya Ibn Abbas na Kuraib.
Jambo la tatu: la kutazamwa katika Hadithi hii, ni kuwa Hadithi hii ni Mutlaq (isiofungamanishwa na kitu) wakati Hadithi ya Ibn Abbas ni muqayyad (iliofungamanishwa). Kanuni ni kuitanguliza muqayyad kuliko mutlaq kama usuli unavyoeleza. Kwa hivyo, kila msingi utaoufata utaona kwamba Hadithi ya Ibn Abbas ndio inayotakiwa itangulizwe.
Ama waliosema kwamba tufunge kwa muandamo mmoja, ukweli ni kuwa wao waliitanguliza rai kuliko kanuni za tafsiri. Walitazama wakaona kuwa mwezi ni mmoja na unakamilisha safari yake mara moja na kwa hivyo muandamo utakuwa mmoja. Lakini tumeona kwamba huu si muandamo wa Kisharia bali ni muandamo wa Kifalaki: muandamo wa Kisharia tunaupata katika kuzijumisha Hadithi tafauti. Pili ni kuwa hio ni rai, na ya Ibn Abbas ni Hadithi; na rai haina uwezo wa kuipinga Hadithi. Kama walivyosema: "Rai haina nafasi mbele ya Andiko."
20
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA KUMI NA TISA
HITIMISHO
19. Hitimisho Kuna milango katika kitabu alichoandika ndugu Juma ambayo hatukupenda kuizungumza, kwani ukichunguza utakuta maneno yake yote yamejengeka katika dhana mbili. Moja ni ile kauli aipendayo kuikariri kwamba (Penye andiko huwa hakuna ijtihadi:) Bila shaka andiko alilokusudia ni ile kauli ya Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) alipokataa mwezi wa Sham kwa kusema: (La! Hivi ndivyo alivyotuamuru Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?.) Kwa upande wetu tumejaribu kuilezea kifani kauli hii na tumeonesha kwa kutumia ushahidi mbali mbali juu ya udhaifu unaopatikana katika kuitegemea kauli hiyo katika mas-ala haya.
JAWABU
Ni fani gani mulioitumia kubainisha Hadithi hio? Pili ni kosa kusema kuwa hio ni kauli ikiwa munakusudia kuwa ni ijtihad tu; hio si kauli kwa maana ya ijtihad bali ni Hadithi. Nakukumbusheni maneno yenu muliposema: "Isipokuwa Sahaba akisema: "Tumeamrishwa kadha" au "Tumekatazwa kadha." Jambo hilo hupewa hukumu ya "Rafii" yaani hio inazingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume(s.a.w.w) . Kwa bahati mbaya, maneno yenu haya - ambayo ni sahihi kwani ndivyo ilivyo katika elimu ya Hadithi - ni kinyume na matendo yenu. Tazama kwamba hamuiti hio kuwa ni Hadithi bali munasema "Kisa" au "Kauli"; wakati muitakayo nyinyi ndio munaita "Hadithi". Hii inaashiria kwamba hamuutaki ukweli bali munataka kulazimisha rai hata kama ni kinyume na fani za elimu.
MNASEMA
Dhana ya pili ya ndugu Juma imejengeka katika msingi dhaifu wala haina nafasi katika uwanja wa fani (kitaalamu) nao ni kule kusukuma kwake juu ya elimu ya Jiografia. Umeonekana udhaifu wake hasa pale alipokuwa akijaribu kuelezea tofauti iliyopo baina ya nchi na nchi katika suala zima la kutofautiana kwa masaa na kuingia kwa usiku na mchana kwa baadhi ya nchi. Kwa upande wa suala hilo pia tumeshalieleza na kulitolea mifano mbali mbali.
JAWABU
Udhaifu munao nyinyi, kwa kudai kwenu kwamba inawezekana kwa ulimwengu mzima kufunga sawa sawa na kwamba wote wanakutana katika usiku na mchana, ilhali kuna sehemu nyingi ambazo zimepishana kwa masaa mengi: huku usiku kule mchana; jua likitua kule huku ni asubuhi. Sasa vipi watafunga sawa sawa na kukutana kwa usiku na mchana. Nyinyi hamuoni haya munavyosukuma kwa kunukuu kanuni za kiusuli halafu hata kuzifasiri hamujui licha ya kuzitumia?! Kanuni nyengine munazinukuu kutolea hoja nazo ni dhidi yenu, yote hayo nyinyi hamuyajui na munasukuma na wenyewe mumeridhia!
MNASEMA
Mwisho tunachukua fursa hii kumuonya ndugu Juma kuwa amuogope Mwenyezi Mungu hususan katika mas-ala ya kielimu. Akumbuke kuwa Mwenyezi Mungu Ameonya juu ya mtu kusema jambo au kufanya asilolijua. Aelewe kwamba ataulizwa juu ya hilo Lingekuwa jambo la busara kama ndugu Juma angalikubali kuuliza na kufanya utafiti zaidi juu ya mas-ala haya kama agizo la Mwenyezi Mungu linavyotutaka.
Wala usifuate (ukipita ukiyasema au kuyafanya) usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa. (17: 36)
Jawabu
Hii ni nasaha nzuri kwa ndugu kumpa nduguye. Nami nakupeni nasaha yangu kwa udhati: si kwa kukejeli. Tafadhali chukueni vitabu vya fani hususan usulu-fiqhi, usulul-hadith, balagha, nahau na sarfu. chukueni vitabu hivyo, nendeni kwa mtu kama Sheikh Aliyani akusaideni. Au kwa wale walio Pemba nawende kwa mtu kama Sheikh Kabi. Hawa wataweza kukusaidieni kwani wana uwezo mzuri. Vyenginevyo mutakuwa siku zote munasukuma mukinukuu kitu ambacho kukifasiri hamujui wala hamujui mahala pa kukiweka.
Muogopeni Mwenyezi Mungu hususan katika mas-ala ya kielimu. Kumbukeni kuwa Mwenyezi Mungu Ameonya juu ya mtu kusema jambo au kufanya asilolijua. Aeleweni kwamba mutaulizwa juu ya hilo Lingekuwa jambo la busara kama ndugu zetu mungelikubali kuuliza kwani Allah anasema:
﴿ وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ
مَسْئُولًا﴾
Wala usifuate (ukipita ukiyasema au kuyafanya) usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa. (17: 36)
21
MUANDAMO WA MWEZI
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
MUKHTASARI WA MJADALA
Ndugu msomaji bila shaka umejionea kwamba, katika sehemu zake nyingi, huu si mjadala wa kielimu, bali ni mjadala wa hoja za mitaani safi. Ingawa ndugu zetu wamejaribu kunukuu huku na kule, lakini mara nyingi huwa hicho walichokinukuu hawajui hata tafsiri yake licha ya kujua wapi pa-kukiweka. Sasa baada ya hayo, ningependa kukupa maelezo kwa ufupi kuhusu ikhtilafu hizi za miandamo ya mwezi.
Waislamu wametafautiana juu ya suala la mwezi muandamo: je muandamo mmoja wa mwezi unatosha kwa dunia nzima au kila watu wa matalai fulani wawe na muandamo wao. Wengine wakasema kuwa muandamo mmoja wa mwezi unatosha kwa dunia nzima; wengine wakasema kila watu wa matalai fulani wawe na muandamo wao. Wanaosema kwamba tufunge kwa muandamo mmoja wanatoa hoja kwa Hadithi isemayo: "Fungeni kwa kuuona". Hoja yao katika Hadithi hii ni kuwa Hadithi hii ni ya ujmla: haamrishwi kwayo Muislamu pasi na Muislamu; wala watu wa nchi moja pasi na wengine.
Sisi tunaosema kuwa kila watu na muandamo wao, tumekuwa na jawabu tafauti juu ya maana ya Hadithi hio kama ifatavyo: 1) Ujumla uliomo ndani ya Hadithi hio haurejei katika nchi za dunia; bali unarejea katika uoni wa mwezi muandamo. Yaani maana ya Hadithi ni kuwa watu wote wasifunge ila kwa kuuona mwezi. Huu ndio ujumla uliomo katika Hadithi hio. Ama suala je watu wote wafunge kwa muandamo mmoja au vipi? Hadithi hio haitoi ufumbuzi juu ya suala hilo. Bali hilo linapatika katika Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas.
2) Pili ni kuwa Hadithi hio - katika baadhi ya mazingatio yake - ni 'Aam ya ujumla. Na Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib Khaas. Kanuni ya kufasiria mandiko inasema kwamba Khaas inatangulizwa kabla ya 'Aam.
3) Hadithi hio - katika baadhi ya mazingatio yake - ni mujmal (isiofafanuliwa). Wakati Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib ni mubayyan (iliofafanuliwa). Kanuni ya kufasiria maandiko inasema kwamba mubayyan ndio yenye kutangulizwa kabla ya mujmal; yaani andiko mujmal hurejeshwa katika andiko mubayyan. Tumeiita Hadithi "Fungeni kwa kuuona" kuwa ni mujmal kwa kuzingatia kwamba Hadithi hii haikubainisha je muandamo ni mmoja au kila watu wana muandamo wao? Bali imesema kwa ujumla tu "Fungeni kwa kuuona mwezi" kama Qur-an ilivyosema "Simamisha sala kwa kutenguka jua." Na tumeiita Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas kuwa ni mubayyan kwani - katika qadri hii - imebainisha kwamba muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali.
4) Hadithi hio - katika baadhi ya mazingatio yake - ni mutlaq (isiofungamanishwa na sehemu) wakati Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas muqayyad (iliofungamanishwa na sehemu pasi na nyengine). Kanuni ni kulirejesha andiko mutlaq katika andiko muqayyad, yaani muqayyad ndio inayotangulizwa. Na kwa hivyo, Hadithi hio ni lazima ifungamanishwe na Hadithi ya Ibn Abbaas ili kufikia maana sahihi. Tumeiita Hadithi hio kuwa ni mutlaq kwa kuwa lafdhi yake haikufungamanishwa na sehemu yoyote, na tukaiita Hadithi ya Ibn Abbaas kuwa ni muqayyad kwani lafdhi yake imefungamanishwa na sehemu moja pasi na nyengine. Kwa hivyo, kwa mujibu wa kanuni zote za tafsiri, natija ni kuwa Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib ni lazima itangulizwe. Jambo jengine ni kuwa ujumla uliomo katika Hadithi hio, ni sawa na ujumla uliomo katika Aya inayosema
﴿أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ ﴾
Simamisha sala kwa kutenguka jua .
Hapa pia haamrishwi mtu maalumu, lakini pamoja na hayo nyakati za sala za watu duniani haziungani. Kwa hivyo, ujumla uliopo hapa ni kuwa watu wote kila watu ni lazima wasali adhuhuri kwa kutenguka jua.
Pia ujumla huo, ni kama Hadithi isemayo:"Usiku ukitokeza kutoka hapa na mchana ukaondoka kutokea hapa na jua likatua, basi aliyefunga ameshafungua (au na-afungue)." Na bila shaka ujumla huu maana yake ni kuwa kila watu wafuturu kwa kuzama jua: wala haina maana ya kuungana nyakati za kufuturu. Halkadhalika, ujumla uliomo katika Hadithi: "Fungeni kwa kuuona", utaona - hususan baada ya kuzikusanya dalili zote mbili: Hadithi hio na ya Kuraib - kwamba ujumla uliomo ndani yake ni kuwa watu wote kila watu ni lazima wafunge kwa kuuona: si ujumla wa kuwa watu wote wafunge sawa sawa. Vyenginevyo, itabidi tulitendee kazi andiko moja; na tuliwache jengine na hili ni kinyume na minhaj (methodology) ya tafsiri.
Wanaosema kuwa kila watu na muandamo wao, wanatoa hoja kwa:
1) Hadithi ya Ibn ya Ibn Abbaas na Kuraib isemayo :"Kutoka kwa Kurayb (kasema) kwamba Ummu Al-fadhli bint Al-harith alimtuma Sham (Syria) kwa Muawiya. Akasema: 'Basi nikaenda Sham nikamkidhia haja yake.' Na ukaniindamia (mwezi wa) Ramadhani na mimi niko Sham. Basi nikauona mwezi usiku wa (kuamkia) ijumaa. Kisha nikaja Madina mwishoni mwa mwezi. Basi Abdullahi bin Abbas (r.a.) akaniuliza. Kisha akataja (habari za) mwezi muandamo akasema: 'Lini mumeuona mwezi muandamo?' Nikasema: 'Tumeuona usiku wa (kuamkia) Ijumaa.' Akasema: 'Wewe umeuona?' Nikasema: 'Ndio. Na Watu wameuona na wakafunga na Muawiya akafunga.' Akasema: 'Lakini hakika ya sisi tumeuona usiku wa (kuamkia) Juma Mosi, basi hatuachi kuendelea kufunga mpaka tutimize (siku) thalathini au tuuone.' Nikasema: 'Kwani wewe hutosheki na kuonekana na Muawiya na kufunga kwake?' Akasema: 'Laa' (Sio): Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) ."
Hoja yao humu ni kuwa Ibn Abbaas alipopewa habari za muandamo wa mwezi uliotokea Sham usiku wa Ijumaa, alikataa kuufata na akasema "Hivi (ninavyofanya mimi) ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w.". Ikafahamika kwa mujibu wa nakala hii kwamba mafunzo ya Mtume(s.a.w.w) ni kutokuuzingatia muandamo wa mbali. Ama wanaosema kuwa tufunge kwa muandamo mmoja wakajibu kwa hoja tafauti, muhimu zao ni hoja sita za Al-Imamu Al-Shawkani ambazo nimezijadili katika kitabu. Na muhimu katika hizo ni kuwa hii ilikuwa ni ijtihad ya Ibn Abbaas. Hoja hii ikajibiwa kwamba Ibn Abbaas katika riwaya hii kasema: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) ". Na lafdhi kama hii inaifanya hadithi ihukumiwe kuwa ni marfu'u yaani hukumu yake ni kuwa hio ni Hadithi ya Mtume (s.a.w.). Hivi ndivo elimu ya Hadithi inavyosema.
2) Hoja ya pili ya wale wenye kusema kuwa kila watu na muandamo wao, ni Qiyas cha nyakati za funga na nyakati za Sala na kufuturu kama tulivyoeleza juu. Ubainifu wa hili ni kuwa: a) Wajibu wa Sala umefungamanishwa na kutenguka na kuzama kwa jua - kitu cha kimaumbile (Natural phenomenon). Kwa hivyo mtenguko wa jua ni sababu ya kuwajibika sala.
b) Wajibu wa funga umefungamanishwa na muandamo wa mwezi - kitu cha kimaumbile (Natural phenomenon). Kwa hivyo kuandama kwa mwezi ni sababu ya kuingia kwa wajibu wa funga.
c) Jua - ambalo kutenguka kwake ndio sababu ya kuwajibikiwa na sala - likitenguka katika nchi moja, watu wa nchi nyengine hawawajibikiwi na sala. Kwa hivyo, Qiyas sahihi ni kuwa kuonekana kwa mwezi - ambayo ni sababu ya kuwajibika funga - katika nchi moja isiwe sababu ya kuwajibikiwa na funga kwa watu wa nchi nyengine. Hiki ni Qiyas sahihi kama alivyosema Sheikh Ibn
'Uthaimin. Huu ndio mukhtasar wa suala hili la kuonekana mwezi na anayetaka kwa urefu na arudi katika kitabu Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi cha Sheikh Nassor Bachoo na kitabu Ushahidi Uliowekwa Wazi cha Juma Mazrui. Ahsanteni
Ndugu yenu katika dini
Juma Muhammad Rashid Al-Mazrui
Tel: 92213669 Al-Qurm, Muscat Oman
E-Mail: jumamazrui@hotmail.com
Jumamazrui@yahoo.com
Tarehe 6/8/2009
MWISHO
MAREJEO
1- Nilipeleka jawabu hii pamoja na kopi ya kitabu changu kwa wahusika.
2- Yaani katika jawabu hii nilipowapelekea.
3- Tamaza Tah-dhibu Tah-dhibu ya Imam Ibn Hajar Al Asqalani jalada la 3 uk 684-685 chapa ya Beirut. Tazama mahala pa herufi mimu] piya Taqribu Tah-dhibu jalada la 2 ukurasa 86.
4- Tazama Al Jarhu Wataadil cha Imam Ibn Abi Hatim jalada la 8 uk.68 chapa ya India.
5- Mudallis si maana yake mwongo; bali ni mwenye kughushi.
6- Sura 17, Aya 36.
7- Sura 7, Aya 33.
8- Sura 6, Aya 144.
9- Isipokuwa mpokezi wa kwanza ndio wasimulizi wametafautiana.
10 Tazama Tarjama ya Muhammad bin Abi Harmala katika Tahidhi Al-Tahdhib j. 10, uk. 96, tarjama na. 149.
11- J. 9, uk. 373, tarjama (biography) na. 690.
12- Al-Sunan Hadithi na.
13- Si Muhammad bin Kurayb.
14- Pia si Muhammad bin Kurayb, bali ni Kurayb, wala hakuna sanad yoyote ya riwaya hii ambayo ndani yake kuna Muhammad bin Kurayb.
15- Al-Sunan Hadithi na. 2329.
16 - Al-Sahih j. 2, uk. 924 Hadithi na. 1916.
17 - Al-Kubra j. 3, uk. 97, Hadithi na. 2432.
18 - Al-Kubra j. 6, uk. 294 Hadithi na. 8297.
19 - Tazama J. 2 uk 490.
20 - Sunna Za Mtume(s.a.w.w) yaani Hadithi zake zilizothibiti.
21- Qur-aan 4:59.
22- Al-Nawawi Taqribu Al-Nawawi kilicho pamoja na Tadribu Al-Rawi uk. 159-160.
23- Kitabu Ushahidi Uliowekwa Wazi nillikiambatanisha na jawabu kuwafikishia wahusika.
24 - Nassor Bachoo Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi uk. 2.
25 - Nassor Bachoo Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi uk. 162.
28 - Juma Mazrui Ushahidi Uliowekwa Wazi chapa ya kwanza 85, chapa ya pili uk. 97.
29 - Juma Mazrui Ushahidi Uliowekwa Wazi chapa ya kwanza 85, chapa ya pili uk. 97.
30 - J. 4, uk. 450, katika maelezo yake juu ya Hadithi na. 77/2599.
31 - Tazama Al-shaukaniy "AL-NAYLU" j. 3, uk. 212, katika maelezo juu ya Hadithi na. 1/1155 na 2/1156, katika "Babu Ikhtiyar Al-qasri Wa Jawazi Al-itmam."
32- Ibn Hisham Qatru Al-Nada uk. 357.
33 - Ibn Hisham Qatru Al-Nada uk. 361.
34 - Lakini Al-Hafidh Ibn Hajar kawakosoa waliosema kwa Hadithi hii imesimuliwa kutoka kwa Abu Sa'id Al-Khudri. Anasema Ibn Hajar: "Al-Ghazali na Al-Fakhr Al-Razi wakifatiwa na Al-Baydhawi wamekinasibisha kisa hiki kwa Abu Sa'id Al-Khudri nalo ni kosa, bali yeye (mwenye kisa hiki) ni Abu Sa'id Al-Mu'alla". Tazama Fat-hu Al-Bari j. 9, uk. 5076, katika sherehe ya Hadithi na. 4474. Ninasema: lakini maelezo hayo ya Ibn Hajar ya kuwakosoa Al-Ghazali, Al-Razi na Al-Baydhawi, bado ni maelezo ya kufirikiwa kwani kisa hiki kimesimuliwa pia na Muslim Hadithi na. 2201, na Abu Dawud Hadithi na. 3415 na wengine kutoka kwa Abu Sa'id Al-Khudri. Kwa hivyo, Al-Ghazali na wenziwe hawakukosea isipokuwa ikiwa Ibn Hajar anadai kuwa sanad hizo ni dhaifu na ya Al-Bukhari yenye kusema kuwa muhusika alikuwa ni Abu Sa'id Al-Mu'allah ndio sanad sahihi.
35 - Kati ya watu wa hilo kabila.
36 - Abu 'Ubaid Fadhailu Al-Qur-an uk. 224.
37 - Al-Bukhari Al-Sahih Haadithi na. 5006 na Hadithi na. 5736
38 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 5737.
39 - Nassor Bachoo Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi uk. 152.
40 - Sura ya 36 Aya 39.
41 - Sura ya 10 Aya ya 5.
42- Al-Tukhi Ahkamu Al-Hakim j. 1, uk. 55. Al-qurtubiy "AL-JAMI'U LIAHKAMI AL-QUR-AN" j. 15, uk. 30, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura ya 36. Al-zamakhshariy "AL-KASHAF" j. 4, uk. 19. Al-baghawiy "MA'ALIMU AL-TANZIL" j. 2, uk. 410, katika tafsiri ya Aya ya 5, ya Sura ya 10.
43 - Al-tukhiy "AHKAMU AL-HAKIM" j.1, uk. 55. Al-baghawiy "MA'ALIMU AL-TANZIL" j. 2, uk. 410, katika tafsiri ya Aya ya 5, ya Sura ya 10. Hizi ndizo buruji mashuhuri kwa wataalamu wa falaki hususan wa Kiarabu. Ama buruji inayoitwa Ophiuchus au kwa Kiarabu ?????? Al-hawiyya si mashuhuri kwao, na kwa hivyo utaona si aghlabu kuitaja: mara nyingi hutaja hizi kumi na mbili tu. Anasema Al-tukhiy Al-falakiy: "Jua kwamba katika anga kuna buruji - yaani nyota nyingi (ambazo) zinajengeka kutokana na hizo buruji kumi na mbili." Tazama "AHKAMU AL-HAKIM" j. 1, uk. 17.
44- Tazama majina hayo ya buruji katika Al-tukhiy "AHKAMU AL-HAKIM" j.1, uk. 158. Al-baghawiy "MA'ALIMU AL-TANZIL" j. 2, uk. 410, katika tafsiri ya Aya ya 5, ya Sura ya 10.
45 - Al-tukhiy "AHKAMU AL-HAKIM" j. 1, uk. 55. Al-qurtubiy "AL-JAMI'U LIAHKAMI AL-QUR-AN" j. 15, uk. 30, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura ya 36. Al-baghawiy "MA'ALIMU AL-TANZIL" j. 2, uk. 410, katika tafsiri ya Aya ya 5, ya Sura ya 10.
46 - Al-tukhiy "AHKAMU AL-HAKIM" j. 1, uk. 55. Al-qurtubiy "AL-JAMI'U LIAHKAMI AL-QUR-AN" j. 15, uk. 30, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura ya 36. Al-baghawiy "MA'ALIMU AL-TANZIL" j. 2, uk. 410, katika tafsiri ya Aya ya 5, ya Sura ya 10.
47 - Tazama majina ya vituo hivyo katika: Al-baghawiy "MA'ALIMU AL-TANZIL" j. 2, uk. 410, katika tafsiri ya Aya ya 5, ya Sura ya 10. Al-qurtubiy "AL-JAMI'U LIAHKAMI AL-QUR-AN" j. 15, uk. 30, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura ya 36. Al-zamakhshariy "AL-KASHAF" j. 4, uk. 19, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura ya 36. Al-tukhiy "AHKAMU AL-HAKIM" j. 1, uk. 55. Hata hivyo, majina ya manazili - kama tulivyotangulia kodokeza - si jambo ambalo wataalamu wameafikiana. Na kwa hivyo, utakuta huyu anayaita manazili fulani jina kadha, na mwengine anayaita manazili hayo hayo jina jengine. Kwa mfano, manazili ya Shartan wengine wanayaita Nat-hu. Tazama Al-tukhiy "AHKAMU AL-HAKIM" j. 1, uk. 56. Wengine hutaja Manazil Zabra kama ilivyo katika Al-zamakhshariy "AL-KASHAF" j. 4, uk. 19; wengine hawataji jina hilo kamwe, na badala yake hutaja jina la Al-kharatan kama ilivyo katika tafsiri ya Al-qurtubiy "AL-JAMI'U LIAHKAMI AL-QUR-AN" j. 15, uk. 30, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura ya 36. Lakini yote haya si muhimu: kilicho muhimu ni uhakika wa kitu: si jina. Lau mtu atayaita maji ulevi basi hayaharamiki; na lau atauita ulevi maji, basi hauhalalilki; kwani mazingatio yako katika uhakika wa kitu si katika jina lake.
48 - Wako wanaojiuliza: je kuna uhusiano gani baina ya mambo haya na Uislam? Sasa cha kufahamu ni kuwa sisi tunazungumzia uhakika (facts): hatuzungumzii dhana zisizokuwepo (illusion au (Nyota zipo tunaziona, na Allah katwambia kama zipo. Anasema Allah:"Na nyota zimetiishwa kwa amri yake." Sura 16 Aya 14. Na manazil yapo. Anasema Allah: "Na Mwezi tumeupimia manazil (vituo). Na buruji (constellations yaani mikusanyiko ya nyota) zipo. Anasema Allah: (Naapa kwa anga yenye buruji (mikusanyiko ya nyota). Al-allama Sheikh Al-farisy na Sheikh Ali bin Muhsin Al-barwaniy wameifasiri Aya hio hivi: "Naapa kwa mbingu yenye buruji." Lakini - ninavyoona mimi - ni bora kufasiri "Naapa kwa anga yenye buruji" kwani nyota ziko katika anga: si katika mbingu. Na neno al-samaa linafasirika kwa namna nyingi, moja ya hizo ni anga. Na kwa hivyo utaona kwamba Sheikh Al-farisy mwenyewe katika maelezo yake juu ya Aya ya 22 ya Sura ya 2, anasema: "Na samaa ni kila kilicho juu yako." Lakini labda neno "Mbingu" katika Kiswahili pia lina maana ya anga. Ikiwa ni hivyo, basi tafsiri ya Mashekhe wawili itakuwa haina mushkeli. Sasa tukirudi katika mas-ala ya falaki, nyota, manazil na buruji, ni kuwa kilichoharamishwa katika mambo haya ni kuamini kuwa mambo haya yanadhuru au yanafaa. Kuamini hivi ni shirki: ama kusoma myenendo ya sayari na nyota kwa ajili ya kujua hisabu na mengineo, haya sio yaliokatazwa kama Maulamaa wanavyosema. Ama yale majina walioyapa manazil na buruji hizo, sisi hayatudhuru kitu: cha muhimu kwetu ni kuwa uhakika wa kile kitu chenyewe kipo, na jina unaweza kuita unavyoona wewe.
49-. Al-qurtubiy "AL-JAMI'U LIAHKAMI AL-QUR-AN" j. 15, uk. 30, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura ya 36.
50 - J. 1, uk 55.
51- Uk. 57. Kumbuka kwamba maneno haya hapa mimi ninanukuu kwa ajili ya kutoa fikra mbali mbali za wataalamu tu: sisemi kuwa ni sahihi au ni makosa: nayanukuu kwa sababu yakiwa sahihi au si sahihi, basi hayaathiri kitu katika utafiti wetu huu. Lakini wasemaji hawa ni wenye kuaminika sana katika uwanja huu wafalaki kwa kadiri ninavyofahamu.
52 - Anasema Al-zamakhshariy katika "AL-KASHAF" j. 4, uk. 19, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura ya 36: "Unakaa mwezi katika kila moja ya hayo (manazili 28) kwa (muda wa) siku moja." Anasema Al-baghawiy katika "MA'ALIMU AL-TANZIL" j. 2, uk. 410, katika tafsiri ya Aya ya 5, ya Sura ya 10: "Basi unakaa mwezi katika kila moja ya hayo (manazili 28) kwa (muda wa) siku moja." Anasema Al-qurtubiy katika "AL-JAMI'U LIAHKAMI AL-QUR-AN" j. 15, uk. 30, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura ya 36: "Unakaa mwezi kila siku moja katika moja ya hayo (manazili 28)." Anasema Al-sabuni katika "SAFWAT AL-TAFASIR" j. 3, uk. 12: "Nayo ni manazili ishirini na nane, unakaa (mwezi) kila siku moja katika moja ya hayo (Manazili ishirini na nane)."
53 - Anasema Al-qurtubiy katika "AL-JAMI'U LIAHKAMI AL-QUR-AN" j. 15, uk. 30, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura 36: "Basi (Mwezi) unaikata falaki (Orbit) kwa muda wa siku ishirini na nane." Tazama pia maneno hayo katika: Al-zamakhshariy "AL-KASHAF" j. 4, uk. 19, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura ya 36. Anasema Al-tabtabai katika "AL-MIZAN" j. 17, uk. 90: "Manazil ni wingi wa (neno) manzil?..na dhahir ni kuwa makusudio ni manazil ishirini na nane ambayo mwezi unayakata katika (muda wa) siku ishirini na nane taqriban."
54 - Anasema Al-qurtubiy katika "AL-JAMI'U LIAHKAMI AL-QUR-AN" j. 15, uk. 30, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura 36: "Kisha (mwezi) hujificha; kisha huchomoza hali ya kuwa ni mwezi muandamo." Anasema Al-zamakhshariy katika "AL-KASHAF" j. 4, uk. 19, katika tafsiri ya Aya ya 40, ya Sura ya 36: "Kisha (mwezi) hujificha (kwa muda wa) siku mbili; au (kwa muda wa siku) moja ikiwa mwezi (month) ni mpungufu (Yaani ukiwa umeandama 29)." Anasema Al-baghawiy katika "MA'ALIMU AL-TANZIL" j. 2, uk. 410, katika tafsiri ya Aya ya 5, ya Sura ya 10: "Na hujificha (mwezi kwa muda wa) siku mbili ikiwa mwezi (month) ni siku thalathini; na ukiwa (mwezi: month) ni wa siku ishirini na tisa, basi (mwezi: moon) hufichika (kwa muda wa) siku moja."
54 - Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 5.
56 - Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 8.
57- Sura ya 10 Aya ya 5.
58 - Hii haina maana kwamba hakuna sababu nyengine za kuumbwa jua na mwezi, lakini iliotajwa hapa ni hio. Na Aya hii - kwa uoni wangu - inahitaji maelezo marefu sana. Mengine ni ya Kisharia; mengine ni ya kifalaki. Na yote yanahitaji wenyewe waliobobea katika fani hizo.
59 - Juma Mazrui Hoja zilizowekwa Wazi uk. 24, chapa ya pili na 24; chapa ya kwanza uk. 18.
60 - Tazama ukurasa wa 68-70, wa chapa ya pili ya kitabu Ushahidi uliowekwa wazi au uk. 58-59 wa kitabu hicho chapa ya kwanza.
61 - Aya yenyewe ni hii: "Yeye (Allah) Ndiye aliyelifanya jua kua muanga na mwezi kua nuru na akaupimia (huo mwezi) vituo, ili mujue idadi ya miaka na hisabu."
62- Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 5.
63- Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 8.
64- Tazama Ibn Uthaimin "FATAWA ULAMAI AL-BALADI AL-HARAM" uk. 194-195.
65 - Ibn Maja Al-Sunan Hadithi na. 17. 65
66- Sura ya 36 Aya 39.
67 - J. 1, uk 55.
68 - Wa kumi na tatu ni wa buruji inayoitwa Ophiuchus au kwa Kiarabu ?????? Al-hawiyya. Lakini hii si buruji mashuhuri kwa wanavyuoni wa Kiarabu, na kwa hivyo si aghlabu kuitaja: hutaja buruji 12 tu.
69 - Sura ya 85 Aya ya 1.
70 - Tazama Nassor Bachoo: "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI." Uk. 66.
71 - J. 1, uk 55.
72 - Wa kumi na tatu ni wa buruji inayoitwa Ophiuchus au kwa Kiarabu ?????? Al-hawiyya. Lakini hii si buruji mashuhuri kwa wanavyuoni wa Kiarabu, na kwa hivyo si aghlabu kuitaja: hutaja buruji 12 tu.
73 - Sura ya 85 Aya ya 1.
74 - Sheikh Al-mufassirin Badru Al-din Al-khaliliy "AL-HAQQU AL-DAMIGH" uk. 46.
75 - Ibn Mandhur "LISANU AL-ARAB" j. 8, uk. 183.
76 - Al-sabuniy "SAF-WATU AL-TAFASIR" j. 1, uk. 275, katika maelezo ya Aya ya 77 ya Sura ya 6.
77 - Sahihi ni "Mat-lail-Badri" si "Mat-lail-Badru".
78 - Ameipokea Al-hakim - katika "AL-MUSTADRAK" j. 1, uk. 584-585, Hadithi na. 1539, na Al-bayhaqiy katika "AL-KUBRA" j. 6, uk. 196, Hadithi na. 8022, na Abdul-Razzaq katika "AL-MUSANNAF" j. 4, uk. 122, Hadithi na. 7336, na Al-daraqutniy katika "AL-SUNAN" j. 2, uk. 163, Hadithi na. 29 .
79 - Abu Ghanim Al-khurasani "AL-MUDAWANA AL-SUGHRA" j. 1, uk. 168.
80 - Al-wahidiy "ASBABU AL-NNUZUL" uk. 98.
81 - Al-suyutiy "ASBABU AL-NUZUL" uk. 28.
82 - Bali Aya yenyewe inaonesha kwamba Hadithi hii ni ya kutunga. Tazama ukweli kwamba Aya inasema kwamba alichoulizwa Mtume (s.a.w.) ni miezi miandamo, wakati Hadithi inaonesha kwamba alichoulizwa ni hali tafauti za mwezi. Tena kama Hadithi hio ilikuwa sahihi, basi Qur-ani isingelitumia neno "Ahilla" (Miezi miandamo), bali ingetumia neno "Qamar" kwani neno "Hilal" - ambalo wingi wake ndio "Ahilla" - ni mahususi kwa maana ya (Mwezi muandamo), wakati Hadithi inaonesha kwamba alichoulizwa Mtume(s.a.w.w) ni hali ya mwezi kwa maana ya "Qamar," ndio maana akaulizwa kuhusu hatua (stages) unazopita za ukubwa na udogo. Kwa ufupi, ni kuwa kuna mgongano baina ya Hadithi na Aya; ukiongeza na udhaifu mkubwa uliopo wa sanad ya Hadithi hio, basi utakuwa umeongeza chumvi juu ya jaraha!
83- Tazama "TAHDHIBU AL-TAHDHIB" j. 9, uk. 387, tarjama na. 721.
84 - Al-suyutiy "ASBABU AL-NUZUL" uk. 6, katika maelezo juu ya Aya 14, ya Sura ya 2.
85- Tazama tafsiri ya Al-baghawiy "MAALIMU AL-TANZIL" j.1, uk. 144, katika maelezo ya chini yaliotiwa na Abdul-Razzaq Al-mahdiy.
86 - Hatimae ikanibainikia kwamba Hadithi hii ni ya kutunga tu, kwani Al-kalbiy kaisimulia kutoka kwa Abi Salih. Na Al-kalbiy kakiri kwamba riwaya zote alizozisimulia kutoka kwa Abi Salih ni za uwongo. Anasema Al-bukhari: "Katusimulia Yahya kutoka kwa Sufyan kasema: 'Kaniambia Al-kalbiy: 'Kila nilichokusimulia kutoka kwa Abi Salih ni uwongo." Tazama Al-dhahabiy "AL-MIZAN" j. 5, uk. 3, tarjama na. 7574.
87- Al-zarqaniy "MANAHILU AL-U'RFAAN" j. 2, uk. 17.
88 - Al-zarqaniy "MANAHILU AL-U'RFAAN" j. 2, uk. 17.
89 - Abdul-Razzaq katika maelezo yake juu ya Tafsiri ya Al-baghawiy "MA'ALIMU AL-TANZIL" j. 1, uk. 11.
90 - Tazama maelezo haya katika "AL-MAUDHUAT" (HADITHI ZA KUTUNGA) cha Ibn Al-jawziy, j. 1, uk. 240, milango yenye kuhusiana na Qur-an: mlango wa fadhila za Sura.
91 - Tazama maelezo ya Abdul-Razzaq Al-Mahdi katika Al-Kashaf j. 1, uk. 261.
92- Tazama maelezo ya Abdul-Razzaq Al-Mahdi katika Ma'alimu Al-Tanzil cha Al-Baghawi j. 1, uk. 234. Tazama pia maelezo ya Abdul-Razzaq Al-Mahdi huyo huyo katika Al-Jami'u cha Al-Qurtubi j. 2, uk. 339.
93 - Al-Alusi Ruhu Al-Ma'an j. 2, uk. 71.
94 - Tazama Al-Zarkashi Al-Burhan fii 'Ulumi Al-Qur-an j. 1, uk. 22.
95- Tazama Muslim "SAHIHU MUSLIM" katika Sharhu al-nawawiy ni j. 8, uk. 32, Hadithi na. 36- 2408, mlango kuhusu fadhila za Ali bin Abi Talib.
96 - Tazama "TAHDHIBU AL-TAHDHIB" j. 9, uk. 387, tarjama na. 721.
97- Al-suyutiy "ASBABU AL-NUZUL" uk. 6, katika maelezo juu ya Aya 14, ya Sura ya 2.
98 - Tazama tafsiri ya Al-baghawiy "MAALIMU AL-TANZIL" j.1, uk. 144, katika maelezo ya chini yaliotiwa na Abdul-Razzaq Al-mahdiy.
99 - Hatimae ikanibainikia kwamba Hadithi hii ni ya kutunga tu, kwani Al-kalbiy kaisimulia kutoka kwa Abi Salih. Na Al-kalbiy kakiri kwamba riwaya zote alizozisimulia kutoka kwa Abi Salih ni za uwongo. Anasema Al-bukhari: "Katusimulia Yahya kutoka kwa Sufyan kasema: 'Kaniambia Al-kalbiy: 'Kila nilichokusimulia kutoka kwa Abi Salih ni uwongo." Tazama Al-dhahabiy "AL-MIZAN" j. 5, uk. 3, tarjama na. 7574.
100 - Tazama maelezo ya Abdul-Razzaq Al-Mahdi katika Al-Kashaf j. 1, uk. 261.
101 - Tazama maelezo ya Abdul-Razzaq Al-Mahdi katika Ma'alimu Al-Tanzil cha Al-Baghawi j. 1, uk. 234. Tazama pia maelezo ya Abdul-Razzaq Al-Mahdi huyo huyo katika Al-Jami'u cha Al-Qurtubi j. 2, uk. 339.
102- Al-Alusi Ruhu Al-Ma'an j. 2, uk. 71.
103- Al-Sayyid Muhammad Rashid Ridhaa Al-Manar j. 2, uk. 143.
104 - Al-Tabatabai Al-Mizan j. 2, uk. 59.
105 - Hadithi hio kaipokea Muslim "SAHIHU MUSLIM" Hadithi na. 2523, j. 4, uk. 421 katika "Sharhu Al-nnawawi." Al-tirmidhiy "AL-SUNAN" uk. 207, Hadithi na. 693. Abu Daud "AL-SUNAN" uk. 400, Hadithi na. 2329. Al-nnasai "AL-KUBRA" j. 3, uk. 97-98, Hadithi na. 2432. Al-bayhaqiy "AL-KUBRA" j. 6, uk. 294-295. Ibn Khuzaima "AL-SAHIH" j. 2, uk. 924, Hadithi na. 1916. 106 - Tazama "TAHDHIBU AL-TAHDHIB" j 11, uk. 259, tarjama na. 479.
107- Tazama "TAHDHIBU AL-TAHDHIB" j.1, uk. 251, tarjama na. 533.
108 - Tazama "TAHDHIBU AL-TAHDHIB" j 9, uk. 96, tarjama na. 149.
109 - Tazama "TAHDHIBU AL-TAHDHIB" j. 8, uk. 388, tarjama na. 785. Jambo la kusikitisha ni kusema kitu bila ya ushahidi kutoka katika vitabu vyenye kutegemewa, ambapo Sheikh Bachoo alisema katika uk. 58 wa kitabu chake maneno haya: "Kisa cha Kuraib ni "MAJHUUL" yaani Kuraib ni mtu asiyeeleweka vyema katika wapokezi wa Hadithi." Sasa sijui Sheikh Bachoo maneno haya kayapata wapi?! Kuraib huyu ambaye ni Mawla wa Ibn Abbas katajwa katika: "TAHDHIBU AL-TAHDHIB" cha Ibn Hajar tarjama (biography) na 785, na akasema Ibn Sa'ad ni "Mwenye kuaminika." Anasema Uthman Al-darimiy: "Nilimwambia Ibn Main: '(Riwaya za) Kuraib kutoka kwa Ibn Abbas ni bora zaidi kwako au (riwaya za) Ikrima (kutoka kwa Ibn Abbas?)" Akasema (Ibn Main): 'Wote wawili ni wenye kuaminika." Na Kuraib huyu katajwa pia na Ibn Hibban katika "AL-THIQAT" (Kitabu juu ya wapokezi wenye kuaminika), uk. 367, tarjama na. 5124. Tazama maelezo hayo pia katika "TAHDHIBU AL-TAHDHIB" j. 8, uk. 388 Kuraib katajwa pia na Al-bukhariy katika "AL-TAARIKHU AL-AWSAT" j. 1, uk. 371, tarjama na. 824, na akamtaja pia katika "AL-TAARIKHU AL-KABIR" j. 7, uk. 114, tarjama na. 10332. Na akatajwa na Ibn Sa'ad katika "AL-TABAQATU AL- KUBRA" j. 5, uk. 224, tarjama na. 905, na akasema kwamba ni "Mwenye kuaminika." Na akatajwa na Abu Hatim Al-raziy katika "AL-JARHU WA AL-TA'ADIL" j. 7, uk. 168, tarjama na. 955, na akanukuu kauli ya Ibn Main yenye kusema "Wao (Kuraib na Ikrima) ni waaminifu." Na wako wengine wengi waliomtaja Kuraib katika vitabu vya "TAARIKH" na vitabu vya wapokezi wa Hadithi. Tazama maelezo ya chini katika "AL-TAARIKHU AL-KABIR" cha Al-bukhari, j. 7, uk. 114 kilichohakikiwa na Mustafa Abdul-Qadir, utaona marejeo mengine 15 ya ziada ambayo sikuyataja hapa ambamo Kuraib katajwa. Kwa hivyo, kauli ya Sheikh Bachoo kwamba Kuraib hajulikani ni Mujazafa (Kusukuma): kauli hio haina thamani katika gulio la elimu.
110 - Al-shaukaniy "NAYLU AL-AWTAR." j. 4, uk. 200 katika sherehe ya Hadithi na. 1636.
111- Jawabu hii inapatikana katika darsa ya tafsiri ya Aya ya 189 ya Sura ya 2. Sehemu hii ya tafsiri ya Sheikh bado haijachapishwa lakini inapatikana katika kaseti za redio.
112 - Tazama Al-suyutiy: "TADRIBU AL-RAWI" uk. 161.
113- Al-shaukaniy "NAYLU AL-AWTAR." j. 4, uk. 200 katika sherehe ya Hadithi na. 1636.
114 - Wengine wanasema ni zaidi ya meli 700, kama ilivyo pia katika kitabu cha Sheikh Nassor Bachoo.
115 - Al-shaukaniy "NAYLU AL-AWTAR." j. 4, uk. 200 katika sherehe ya Hadithi na. 1636.
116 - Al-shaukaniy "NAYLU AL-AWTAR." j. 4, uk. 200 katika sherehe ya Hadithi na. 1636.
117 - Elewa kwamba ibara hii ya Al-shaukaniy aliposema: "Ikiwa andiko linajulikana" na aliposema: "Ikiwa andiko halijulikani" si ibara sahihi. Ibara hii msingi wake ni kuwa maneno ya Ibn Abbas aliposema: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w." ni ijtihadi yake Ibn Abbas. Nayo si kauli sahihi kama tulivyobainisha. Kwa hivyo, jawabu ni kuwa andiko linajulikana, nayo ni riwaya ya Ibn Abbas na Kuraib.
118 - Al-shaukaniy "NAYLU AL-AWTAR." j. 4, uk. 200 katika sherehe ya Hadithi na. 1636.
119 - Tazama kanuni hii katika Dr. Wahbat Al-zuhailiy "USULU AL-FIQ-HI" j. 1, uk. 637.
120 - Qiyas - kilugha - maana yake ni kipimo. Ama katika fani ya usulu Al-fiq-hi, Qiyas ni "Kukirejesha kitu ambacho hukumu yake haikutajwa, kwa kukilinganisha na kitu ambacho hukumu yake imetajwa, kisha ukakipa kitu ambacho hukumu yake haikutajwa hukumu sawa na ile ya kitu ambacho hukumu yake imetajwa, kwa ajili ya kuwepo illa (sababu) moja katika vitu viwili hivyo." Kwa hivyo, katika Qiyas, tuwe na mambo mane:
1) Aslu. Yaani asili au shina. Shina ni kile kitu ambacho hukumu yake imetajwa.
2) far'u. Yaani tawi. Tawi ni kile kitu ambacho hukumu yake haikutajwa.
3) Illah. Illa ni sababu ambayo ipo katika Aslu. (Shina) na ipo katika far'u (Tawi). Wengine wanatafautisha baina ya sababu na illa. Sababu - kwao - ni kitu kisicho na uhusiano na kitu chenye kupewa hukumu. Kama kutenguka jua kuwa ni sababu ya kuwajibikiwa na Sala. Na illa ni kitu chenye uhusiano na kitu chenye kupewa hukumu. Kama mgonjwa kuruhusiwa kula mwezi wa Ramadhani. Ugonjwa ni illa ya ruhusa hio, na uhusiano baina ya ugonjwa na kuruhusiwa kula uko wazi.
4) hukmu (hukumu) ni moja katika hukumu tano, nazo ni: wajibu, mandub (jambo litakiwalo kufanywa lakini si lazima), haramu, mubaha (ruhusa) na makruhu. Kwa hapa hukumu inaweza ikawa ima ni uharamu wa kuzingatia muandamo wa mbali; au wajibu wa watu wa kila mji kufata muandamo wao.
121 - Tazama darsa hii katika: Al-imamu Al-salimi "SHARHU TAL-ATI AL-SHAMS" j. 2, uk. 135. Dr. Wahbat Al-zuhaily "USULU AL-FIQ-HI AL-ISLAMI" j. 1, uk. 671. Sheikh Muhammad Al-khadhari " USULU AL-FIQ-HI" uk. 381.
122 - Kumbuka kwamba hapa tunafanya (Kuzikusanya sifa zinazoelekea kuwa illa (sababu) halafu kuzipima na kuchukua iliokuwa sahihi).
123 - Makusudio ya sababu isiovuuka mahala pake, ni sababu ambayo ndio iliosababisha kitu fulani kikapewa hukumu fulani, lakini sababu hio ikawa ipo katika kitu hicho tu: haipo katika kitu chengine. Sababu kama hii ni dhaifu, na kwa hivyo ikiwa kuna sababu nyengine ambayo ipo katika kitu hicho na pia ipo katika kitu au vitu vyengine - ambayo ndio huitwa kuwa ni sababu iliovuuka mahala pake - basi wanavyuoni huifanya sababu hio iliovuuka mahala pake kuwa ndio sababu ya hukumu. Si kwamba sababu isiovuuka mahala pake haifanywi kuwa ni sababu ya hukumu, "Laa" inafanywa kwa mujibu wa wanavyuoni wengi, lakini ikigongana na sababu inayovuuka mahala pake basi sababu hio inayovuuka mahala pake ndio ya kuzingatiwa. Na yote haya lau ingelikuwa neno "Sham" linafaa kuwa ni sababu, lakini hata kulifanya neno hilo kuwa ni sababu ya hukumu haiwezekani, kama ulivyoona humu katika maelezo yetu.
124 - Tazama: Sh. Nassor Bachoo: "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 32.
125 - "NAYLU AL-AWTAR." j. 4, uk. 200 katika sherehe ya Hadithi na. 1636.
126 - Neno "Punguzu" ndilo lililomo katika kitabu cha Sheikh Nassor, sijui kama kakusudia neno "Pungufu" au hili ndio neno sahihi kwa mujibu wa Sheikh Bachoo.
127 -Tazama "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 33.
128- Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 37.
129- Ibn Hajar "AL-FAT-HU" j. 5, uk. 2480, katika maelezo ya Hadithi na. 1911.
130 - Wau al-atfi ni wau yenye kuunganisha baina ya maneno mawili au zaidi au sentensi mbili au zaidi. Yaani ni Cojujuctional letter (Herufi ya kuuanganishia). Hii ni kama kusema katika Kishwahili: Ali na Saleh. Herufi "Na" ndio sawa na "Wau au wa" nayo imetumika kuunganisha baina ya maneno Ali na sale. Halkadhalika Wau al-atfi huunganisha maneno au sentensi.
131- Al-tirmidhiy "AL-SUNAN" katika tarjama ya mlango wa 9, maelezo ya Hadithi na. 693.
132- Ibn Khuzaima "SAHIHU" yake katika tarjama ya mlango na. 33, j. 2, uk. 924, Hadithi na. 1916.
133 - Tazama "SHARHU SAHIHI MUSLIM" ya Al-imamu Al-nnawawi, Hadithi na. 2523. Bali Sheikh Bachoo mwenyewe katika uk. 29 kayafasiri maneno hayo ya Ibn Abbas yasemayo: kuwa maana yake ni: "La (Hapana): hivi ndivyo alivyotuamrisha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu." Halafu hapa kageuka na kuyafasiri maneno hayo hayo kuwa Ibn Abbas kasema "Anatosheka:" kule: "Laa" (Sio), huku: "Naam" (Ndio), na Hadithi ni ile ile na msemaji ni yule yule! Tazama pia katika uk. 109-110 uone upinzani alioutoa hapo halafu linganisha upinzani huo na upinzani alioutoa kabla ya hapo, utaona jinsi gani mwanamume alivyokuwa bingwa wa kubadilika! Na hili si jengine bali ni lile Waswahili wanalolisema: "Mfa maji hukamata maji." 134 - Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 37.
135- Hii ni hoja ya Abu Ammar, Nassir bin Mohd bin Rashid Al-mazrui, ambayo aliiongezea hapa. Nilisahau kuweka maelezo haya katika chapa ya kwanza. Na hapa nakamilisha wajibu wangu, kwa vile hoja hii si juhudi yangu, bali ni juhudi yake, nayo ni hoja sahihi, nzuri.
136- Tazama Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 17.
137- Tazama Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 152.
138 - Ibn 'Aqil Shar-hu Ibn 'Aqil j. 1, uk. 11.
139 - Ibn 'Aqil Shar-hu Ibn 'Aqil j. 1, uk. 11.
140 - Ibn 'Aqil Shar-hu Ibn 'Aqil j. 1, uk. 12.
141 - Ibn Hisham Qatru Al-Nada uk. 340.
142- Ibn 'Aqil Shar-hu Ibn 'Aqil j. 1, uk. 14.
143 - Ibn 'Aqil Shar-hu Ibn 'Aqil j. 1, uk. 14.
144 - Hadithi hio kaipokea Muslim "SAHIHU MUSLIM" Hadithi na. 2523, j. 4, uk. 421 katika "Sharhu Al-nnawawi." Al-tirmidhiy "AL-SUNAN" uk. 207, Hadithi na. 693. Abu Daud "AL-SUNAN" uk. 400, Hadithi na. 2329. Al-nnasai "AL-KUBRA" j. 3, uk. 97-98, Hadithi na. 2432. Al-bayhaqiy "AL-KUBRA" j. 6, uk. 294-295. Ibn Khuzaima "AL-SAHIH" j. 2, uk. 924, Hadithi na. 1916.
146 - Yaani Abu Daud, mpokezi wa Hadithi. Kwa hivyo, Abu Daud unasema kama tunavyosema sisi.
147 - Al-Adhim Abad A'wnu Al-Ma'abudi: Sharhu Sunani Abi Daud j. 6, uk. 454-455, katika sherehe ya Hadithi na. 2315.
148 - Yaani Al-Imamu Al-Nasai. Kwa hivyo, Al-Nasai na wengine pia wanawafikiana na sisi.
149- Maana ya kuwa andiko la ujumla ni la dhana na andiko maalum (specific au khaas) ni la uhakika, ni kuwa andiko la ujumla linakusanya vitu vyote vyenye kuhusiana na lafdhi ya andiko hilo, lakini hakuna uhakika kwamba kweli vyote vimeingia au vilivyoingia ni vingi tu, wakati katika andiko maalum (specific au khaas), tuna hakika kwamba kilichotajwa ndivyo kilivyo. Kufahamu hili vizuri, tazama mfano mtu anaposema Wazanzibari ni wakarimu. Andiko hili ni la ujumla linamuingiza kila anayeitwa Mzanzibari, lakini je kweli kila Mzanzibari ana sifa hiyo ya ukarimu? Ukitazama utaona si kweli kwamba Wazanzibari wote wako hivyo, labda hio ni sifa ya waliowengi tu. Lakini nikitumia lafdhi khaas (specific) nikasema Ali ni mkarimu, basi huwa ni kitu cha hakika kwa vile kinamuhusu mtu mmoja maalum. Kwa hivyo, andiko hili si la hakika. Lakini katika andiko maalum (specific au khaas) maneno huwa ni ya uhakika.
150 - Tazama Ibn Uthaimin "FATAWA ULAMAI AL-BALADI AL-HARAM" uk. 194-195.
151 - Al-salimiy "AL-JAWABAAT" j. 1, uk. 45.
152- Kama ilivyo katika "AL-NAYLU" cha Al-shaukaniy j. 4, uk. 192, katika maelezo ya Hadithi na. 1626.
153 - Abu Daud "AL-SUNAN" uk. 401 katika maelezo ya Hadithi na. 2338.
154 - Al-bayhaqiy "AL-KUBRA" j. 6, uk. 211, katika maelezo yake juu ya Hadithi na. 8069.
155- Ibn Majah "AL-SUNAN" uk. 278, katika maelezo yake juu ya Hadithi na. 1652.
156 - Al-tirmidhiy "AL-SUNAN" uk. 206, katika maelezo yake juu ya Hadithi na. 691.
157 - Al-nadhaam ni Ibrahim bin Sayyar, Sheikh wa madhehebu ya Mu'utazila.
158 - Ibn Al-arabiy "AHKAMU AL-QUR-AN" j. 1, uk. 120, katika tafsiri ya Aya inayosema: "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu, basi na-aufunge."
159 - Kapwekeka maana yake kawa peke yake; na kupwekeka na Hadithi ni kuwa kaisimulia yeye tu: hakuna msimulizi mwengine aliyeisimulia. Lihifadhi neno hili kwa sababu limetumika katika sehemu nyengine nyingi za kitabu hiki. 160 - Al-shaukaniy "AL-NAYLU" j. 4, uk. 192.
161- Tazama "TAHDHIBU AL-TAHDHIB" j. 4, uk. 204, tarjama na. 405.
162 - Al-imamu Al-shaukaniy: "NAYLU AL-AWTAR" j. 4, uk. 193 katika maelezo ya Hadithi na. 1625-1626.
163 - Tazama Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 17.
164 - Katika uk. 17-18, Sheikh Bachoo anatoa hoja kwa Hadithi ya mabedui wawili na Hadithi ya Masahaba waliouona mwezi jana (yaani kwa mujibu wa siku waliokwenda kwa Mtume s.a.w.). Na jawabu yetu hapa ni hio hio kwamba watu hao wote walikuwa katika eneo la Madina. Ivo ni mtu gani katika zama za Mtume(s.a.w.w) atayetoka Sham au Oman au mji wowote ule wa mbali akafika kwa Mtume(s.a.w.w) kwa muda wa siku moja - usiku wa jana mpaka magharibi ya leo?! Kwa wakaazi wa Afrika ya Mashariki hili ni rahisi kuweza kulijua: waulizeni Wazanzibari waliokuja Oman zamani: walikuwa wakitoka Ruwi mpaka Niz-wa kwa muda gani? Amenisimulia mmoja wao kwamba walikuwa wakienda Niz-wa kwa punda na ngamia kwa muda wa wiki moja. Na hii kuna sehemu ambazo walikuwa wakipanda gari. Niz-wa kwa leo tunakwenda kwa gari kwa muda wa kama saa na nusu kutokea Ruwi. Ruwi na Niz-wa hapafiki k.m. 200. Ni masafa ya kama 180. Sasa wewe pima mwenyewe bedui huyo alikuwa wapi hata akaweza kufika kwa Mtume(s.a.w.w) - kwa ngamia au kwa punda - kwa muda wa siku moja au mbili au wiki, ikiwa watu hawa wamesafiri masafa ya k.m. mia na thamanini (180) kwa muda wa wiki?
165 - Kama ilivyo katika riwaya na. 8069 ya Al-bayhaqiy katika "AL-KUBRA" j. 6 uk. 211 na Al-hakim katika "AL-MUSTADRAK" j. 1, uk. 587 Hadithi na. 1546 na Abu Daud katika "AL-SUNAN" Hadithi na. 2338 na Al-daraqutniy katika "AL-SUNAN" j. 2, uk. 159 Hadithi na. 14.
166 - Kama ilivyo katika riwaya na. 8069 ya Al-bayhaqiy katika "AL-KUBRA" j. 6 uk. 211 na Al-hakim katika "AL-MUSTADRAK" j. 1, uk. 587 Hadithi na. 1546 na Abu Daud katika "AL-SUNAN" Hadithi na. 2338 na Al-daraqutniy katika "AL-SUNAN" j. 2, uk. 159 Hadithi na. 14.
167 - Al-Suyuti Tadribu Al-Rawi uk. 161.
168 - i. Ahkamul-Qur-aan Cha Al-Jaswas J. 1 uk 305. ii. Fiqhi-Sunnah Cha Sa'iyd Saabiq J. 1 uk 436.iii. Rawaaiul-Bayaan J. 1 uk 211. iv. Naylul-Awtaar J. 4 uk 195 v. Sharhu Subulu Sawiyyah Lifiqhi Sunanil - Marwiyyah vi. Fatawa Za BAKWATA uk 10 - 11 Mada 14/70
169 - Kanuni gani Yaa Nas!
170 - Tazama maudhui hii katika Dr. Al-Zuhaili Usulul Fiq-hi j. 1, uk 244-245. Al-Salimi Sharhu Tal'ati Al-Shams j. 1, uk. 105.
171- Kama ilivyo katika riwaya na. 8069 ya Al-bayhaqiy katika "AL-KUBRA" j. 6 uk. 211 na Al-hakim katika "AL-MUSTADRAK" j. 1, uk. 587 Hadithi na. 1546 na Abu Daud katika "AL-SUNAN" Hadithi na. 2338 na Al-daraqutniy katika "AL-SUNAN" j. 2, uk. 159 Hadithi na. 14.
172 - Ali Muhammad Al-Nadwi Al-Qawa'id Al-Fiqhiyya uk. 417. Muhammad Bakr Isma'il Al-Qawa'id Al-Fiqhiyya uk. 50.
173 - Lakini nyinyi Hadithi ya Ibn Abbaas na kuraib hamutaki kuiba hukumu hio, bali munaona ni kisa tu!!!
174 - Yaani Bismillahi zilio mwanzoni mwa sura: si Bismillahi ilio katikati ya Suratu Al-Naml.
175 - Ibn Hajar Al-Fat-Hu j. 5, uk. 2480, katika sherehe ya Hadithi na. 1907.
176- Al-San'ani Subulu Al-salam j. 1, uk. 415, katika maelezo ya Hadithi na. 610.
177 - Makusudio ya sababu isiovuuka mahala pake, ni sababu ambayo ndio iliosababisha kitu fulani kikapewa hukumu fulani, lakini sababu hio ikawa ipo katika kitu hicho tu: haipo katika kitu chengine. Sababu kama hii ni dhaifu, na kwa hivyo ikiwa kuna sababu nyengine ambayo ipo katika kitu hicho na pia ipo katika kitu au vitu vyengine - ambayo ndio huitwa kuwa ni sababu iliovuuka mahala pake - basi wanavyuoni huifanya sababu hio iliovuuka mahala pake kuwa ndio sababu ya hukumu. Si kwamba sababu isiovuuka mahala pake haifanywi kuwa ni sababu ya hukumu, "Laa" inafanywa kwa mujibu wa wanavyuoni wengi, lakini ikigongana na sababu inayovuuka mahala pake basi sababu hio inayovuuka mahala pake ndio ya kuzingatiwa. Na yote haya lau ingelikuwa neno "Sham" linafaa kuwa ni sababu, lakini hata kulifanya neno hilo kuwa ni sababu ya hukumu haiwezekani, kama ulivyoona humu katika maelezo yetu.
178 - Yaani Al-Imamu Al-Nasai. Kwa hivyo, Al-Nasai na wengine pia wanawafikiana na sisi.
179 - Au saba kwa mujibu wa Mahanafi.
180 - Rejea Ali Muhammad Al-Nadwi Al-Qawa'id Al-Fiqhiyya uk. 393. Muhammad Bakr Isma'il Al-Qawa'id Al-Fiqhiyya uk. 142.
181- Sehemu ya Aya isemayo: ilikuwa haimo kwa Kiarabu chake katika makala ya ndugu zetu. Hapa nimeiongeza kwani tafsiri yake kwa Kiswahili ilikuwemo.
182 - Tazama Juma Mazrui Ushahidi Uliowekwa Wazi Katika Suala La Miandamo Ya Mwezi uk 97 chapa ya pili, au uk. 85 chapa ya kwanza.
183 - Nassor Bachoo Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi uk. 2.
184 - Tazama Al-qurtubiy: "BIDAYATU AL-MUJTAHID" j. 1, uk. 516.
185- Al-kaasaniy "BADAAIU AL-SANAI'I". J. 2, uk. 224-225
186- Al-imamu Abu Muslim "NITHARU AL-JAWHAR" J. 5, uk. 158.
187- Al-sayyid Saabiq "FIQ-HU AL-SUNNA" uk. 293
188 - Al-qurtubiy "BIDAYATU AL-MUJTAHID" j. 1, uk. 516
889 - Ibn Al-arabiy "AHKAMU AL-QUR-AN" j. 1, uk. 121.
190 - Al-qurtubiy "BIDAYATU AL-MUJTAHID" j. 1, uk. 516.
191 - Ramadhani ya mwakaa huu nilikusudia hasa kuwauliza wakazi wa nchi tafauti. Na jawabu ni kuwa: Watu wa jimbo la Kerla India wamefunga sawa na Oman, na Waislamu wa nchi hio wanafata madhehebu ya Shafi. Watu wa Pakistan, Bangladesh na India wamefunga siku ya pili baada ya Oman (ambayo ni siku ya tatu baada ya Saudia). Pakistan na Bangladesh asilimia kubwa ya wakazi wake ni Mahanafi.
192 - Tazama kanuni hii katika Dr. Wahbat Al-zuhailiy Usulu Al-Fiq-Hi j. 1, uk. 677, babu Qiyasi Al-Lugha.
193 - Tazama kanuni hii katika Dr. Wahbat Al-zuhailiy Usulu Al-Fiq-Hi j. 1, uk. 677, babu Qiyasi Al-Lugha.
194 - Tazama kanuni hii katika Dr. Wahbat Al-zuhailiy Usulu Al-Fiq-Hi j. 1, uk. 260..
195- Al-Jitali Al-Qawa'id j. 2, uk. 165.
196 - Al-Jitali Al-Qawa'id j. 2, uk. 56.
197 - Maelezo yake katika kitabu Al-Qawa'id cha Al-Jitali j. 2, uk. 70.
198 - Al-Khalili Al-Fatawa Al-Kitabu Al-Khamis uk. 357.
199- Kwa sasa siwezi kukunakilieni mifano mingi kwani ninapoisoma katika vitabu sidhanii kwamba kuna mtu ataihitaji, lakini hii mifano miwili itatosha kukupeni picha halisi, na nitapoitoa jawabu hii kama ni kitabu nitakunakilieni mifano ya ziada in shaa Allah.
200- Al-qurtubiy "BIDAYATU AL-MUJTAHID" j. 1, uk. 516.
201- Wafasina bandia na maulamaa bandia wamejaa tele leo Zanzibar; ndio maana tukawa na zogo hili. Wallahu Al-Musta'an!
202- Abu Hayyan Al-Bahr j. 2, uk. 47.
203 - Abu Hayyan Al-Bahr j. 2, uk. 47.
204 - Mahmud Safi I'irabu Al-Qur-an j. 2, uk. 371.
205- Tutaeleza kwa urefu katika kitabu inshaa Allah.
206 - Je kanuni hii nyinyi memeifata? Hao muliotolea ushidi katika kitabu chenu wote ni wanavyuoni wa kweli? Mwanachuoni wa kweli si Duktur, bali ni yule aliyefikia daraja ya ijtihad, na nyie munanukuu mpaka kutoka kwa watu wa kawaida! 207 - Abu Al-suud katika tafsiri yake j. 1, uk. 236.
208- Ibn Al-arabiy "AHKAMU AL-QUR-AN" j. 1, uk. 118.
209- Ibn Baraka "KITABU AL-JAMI'I" j. 2, uk. 5.
210- Abu Zahra "USULU AL-FIQ-HI". Kwa sasa ukurasa haunihudhurii kwa vile kitabu hiki sinacho mikononi
211 - Ibn Hazm "AL-MUHALLAH" j. 6, uk. 166.
212 - Al-jassas Al-raziy "AHKAMU AL-QUR-AN" j. 1, uk. 278.
213- Al-jassas Al-raziy "AHKAMU AL-QUR-AN" j. 1, uk. 279.
214 - Al-jassas Al-raziy "AHKAMU AL-QUR-AN" j. 1, uk. 278.
215 - Maana ya maneno haya ya Abu Muslim aliposema: "Na akauita Allah mwanzo wa mwezi kwa jina la mwezi mzima" ni kuwa neno lililotumika katika Aya ni neno Shahr nalo lina maana ya mwezi kwa maana ya kipindi cha siku 29-30 (month), wakati makusudio ya Aya ni atayeushuhudia kwa maana ya kuuona, na unaoonekana ni mwezi ule wa sayari ulioko angani ambao kwa Kiarabu huitwa Qamar au huitwa Hilal unapokuwa muandamo, kwa maana hii itakuwa neno Shahr lililomo katika Aya hio, limetumika kwa maana ya Hilal. Au limetumika kwa maana yake hio hio ya Shahr lakini "Pakadiriwe mudhafu (kilichotegemezwa ambacho kimeondoshwa nacho ni Hilal). Na maana itakuwa "Hilalu Al-shahri" Mwezi muandamo wa mwezi (wa Ramadhani). Hii ndio maana iliomo katika maneno ya Sh. Abu Muslim.
216 - Abu Muslim "NITHARU AL-JAWHAR" j. 5, uk. 13.
217- Abu Muslim "NITHARU AL-JAWHAR" j. 5uk. 25.
218 - Sh. Al-khaliliy "AL-FATAWA" kitabu 1, uk. 309.
219- Prof Moh'd Bakr Ismail "AL-QAWAIDU AL-FIQ-HIYYA" uk 401.
220- Ibn Uthaimin "FATAWA ULAMAI AL-BALADI AL-HARAM" uk. 194.
221 - Al-sayyid Ahmad Al-hashimiy katika "JAWAHIRU AL-BALAGHA" uk. 389
222- Dr. Wahbat Al-zuhailiy "USULU AL-FIQ-HI" j. 1, uk. 43, au uk. 51 kwa chapa nyengine.
223 - Dr. Wahbat Al-zuhailiy "USULU AL-FIQ-HI" j. 1, uk. 43, au uk. 51 kwa chapa nyengine.
224 - Ibn Hajar Al-Fat-Hu j. 5, uk. 2480, katika sherehe ya Hadithi na. 1907.
225 - Al-San'ani Subulu Al-salam j. 1, uk. 415, katika maelezo ya Hadithi na. 610.
226 - Muqabala maana yake ni kusemwa kitu fulani katika sentensi moja kisha katika sentensi ya pili kukasemwa maneno yaliokinyume na yale yalio katika sentensi ya kwanza. Sasa ikiwa maana iliomo katika maneno ya kwanza imefichika, basi tunajiongozea kwa maneno ya pili kuufahamu muradi wa maneno ya kwanza. Tumetoa baadhi ya mifano miwili mitatu katika kitabu chetu: "HOJA ZENYE NGUVU" na si vibaya hapa tukainukuu tena mifano miwili, kwani huenda ikawa mtu kasoma kitabu hiki bila ya kusoma kile. Mfano wa muqabala ni kama Aya inayosema: "Anawahalalishia mambo mazuri na anawaharamishia mambo mabaya." Sura ya 7 aya 157. Na Aya inayosema: "Na wanatarajia rehema yake na wanaogopa adhabu yake." Sura ya 17 aya ya 57. Ukitazama hapa utaona kwamba kila sentensi ya pili ni kinyume na sentensi ya kwanza. Na huu ndio watu wa lugha ya Kiarabu wanaouita Muqabala, yaani opposite au sentensi ilio kinyume ya sentensi nyengine. Sasa kuna wakati inakuwa ni vigumu kuweza kujua maana iliokusudiwa katika sentensi ya kwanza lakini utapoitazama sentensi ya pili katika Muqabala wake, ndio inayokujuilisha muradi wa sentensi ya kwanza.
227- Al-jassas Al-raziy "AHKAMU AL-QUR-AN" j. 1, uk. 278.
228 - Al-jassas Al-raziy "AHKAMU AL-QUR-AN" j. 1, uk. 279.
229 - Al-jassas Al-raziy "AHKAMU AL-QUR-AN" j. 1, uk. 278.
230- Al-jassas Al-raziy "AHKAMU AL-QUR-AN" j. 1, uk. 279.
231- Hii si kanuni muttarid. Neno linaweza kuwa tika sentensi na pia likawa na maana zaidi ya moja ikiwa maana hizo hazigongani. Neno "Sala" katika Aya: Hakika ya Allah na Malaika zake wanamsali Mtume?, lina maana mbili. Sala ya Allah ni maghfira nay a Malaika ni dua.
232 - Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 37.
133 - Hii ni hoja ya Abu Ammar, Nassir bin Mohd bin Rashid Al-mazrui, ambayo aliiongezea hapa. Nilisahau kuweka maelezo haya katika chapa ya kwanza. Na hapa nakamilisha wajibu wangu, kwa vile hoja hii si juhudi yangu, bali ni juhudi yake, nayo ni hoja sahihi, nzuri.
234 - Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 37.
235 - Maana ya kuwa andiko la ujumla ni la dhana na andiko maalum (specific au khaas) ni la uhakika, ni kuwa andiko la ujumla linakusanya vitu vyote vyenye kuhusiana na lafdhi ya andiko hilo, lakini hakuna uhakika kwamba kweli vyote vimeingia au vilivyoingia ni vingi tu, wakati katika andiko maalum (specific au khaas), tuna hakika kwamba kilichotajwa ndivyo kilivyo. Kufahamu hili vizuri, tazama mfano mtu anaposema Wazanzibari ni wakarimu. Andiko hili ni la ujumla linamuingiza kila anayeitwa Mzanzibari, lakini je kweli kila Mzanzibari ana sifa hiyo ya ukarimu? Ukitazama utaona si kweli kwamba Wazanzibari wote wako hivyo, labda hio ni sifa ya waliowengi tu. Lakini nikitumia lafdhi khaas (specific) nikasema Ali ni mkarimu, basi huwa ni kitu cha hakika kwa vile kinamuhusu mtu mmoja maalum. Kwa hivyo, andiko hili si la hakika. Lakini katika andiko maalum (specific au khaas) maneno huwa ni ya uhakika.
236- Tazama Ibn Uthaimin "FATAWA ULAMAI AL-BALADI AL-HARAM" uk. 194-195.
237- Al-salimiy "AL-JAWABAAT" j. 1, uk. 45.
238- Nassor Bachoo: "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 23.
239 - Kainukuu kauli hii Abu Muslim katika "NITHARU AL-JAWHAR" j. 5, uk. 159. Pia kauli hii utaipata katika Fatawa za Al-imamu Al-salimiy j. 2, uk. 114.
240 - Dr. Al-Zuhaili Usulu Al-Fiq-hi j. 1, uk. 521. Al-Qannubi Al-Tufan j. 3, sehemu ya kwanza uk. 23.
241 - Al-Qannubi Al-Tufan j. 3, sehemu ya kwanza uk. 23.
242 - Haya ndio maneno sahihi: sio mudai kwamba wamekubaliana juu ya ijma'i hii.
243 - Ikhtilafu katika Umma ipo, lakini hii ndio kauli yenye nguvu.
244 - Dr. Al-Zuhaili Usulul Fiq-hi j. 1, uk. 526.
245 - Dr. Al-Zuhaili Usulul Fiq-hi j. 1, uk. 527.
246- Al-imamu Al-salimi Sharhu Tal-Ati Al-Shams j. 2, uk. 135.
247- Suala: Je mwezi ukiandama Tanzania au nchi nyengine yoyote ile mwanzo kabla ya Saudia hoja yako kwamba: "Tarehe 9 Dhul-Hijjah huko mji wa Makka; sio tarehe tisa ya nchi nyengine yoyote ile" itakuwa na maana gani? Kumbuka kwamba Saudia haifati muandamo wa nchi nyengine. Kwa kufahamu zaidi, tazama maelezo ya chini (foot note) na. 223. 248- Tazama Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 113-114. 249 - Katika chapa ya kwanza nilisema hivi: "Tukatoa mfano wa kutenguka jua kuwa ni sababu ya kuingia wakati wa kusali." Kilichosahihi ni kusema: "Tukatoa mfano wa kutenguka jua kuwa ni sababu ya kuwajibikiwa na Sala."
250- Tumetaja walioipokea Hadithi hii katika uk. 54-56.
251 - Sura ya 2 Aya ya 200. Na mfano wake ni Hadithi inayosema: "Muhajir (akitaka kukaa Maka basi) akae siku tatu (tu) baada ya (kumaliza) nusuki (ibada) zake (za hija)." 252 - Katika chapa ya kwanza nimeandika "A'YNU" badala ya "A'WNU" basi sahihisha hapa; sahihi ni "A'WNU" si "A'YNU."
253 - Tazama "A'WNU AL-MA'ABUDI: SHARHU SUNANI ABI DAUD" j. 6, uk. 463.
254- Tazama Ibn Uthaimin "FATAWA ULAMAI AL-BALADI AL-HARAM" uk. 194-195.
255- Tatizo pia litabakia kwa wale ambao wakati kwao umetangulia kabla ya Saudia. Kwa mfano Arafa ni J/ane: ambapo alfajiri ya J/ane ikichomoza Saudia wao kwao jua linazama na kwa hivyo ni J/atano. Ikiwa watafunga mchana wa J/ane, basi watafunga kabla ya Arafa. Ikiingia Arafa Makka kwao ni usiku wa J/atano, na hakuna funga ya usiku. Kwa hali hii, ni wazi kwamba funga - yoyote iwayo - ni lazima ifungamanishwe na muandamo wa mwezi. Na kwa kufanya hivyo, Waislamu wote wa dunia wataweza kufunga Arafa mwezi tisa na kula Siku Kuu mwezi kumi.
256- Baada ya kuwa nimeimaliza kazi hii, alinisimulia mmoja wa Sahibu zangu kuhusu nukta alioitoa Sheikh mmoja wa Dar-es-salam katika kuwajibu wale wenye msimamo kwamba tufunge kwa muandamo mmoja. Sheikh aliwaambia watu hao kwamba tunajua kwamba Saudia haifuati muandamo wa nchi nyengine. Sasa suala: je ikiwa mwezi utaandama hapa kwetu kwanza je nyinyi mutafata wapi? Jawabu: Tutafata hapa hapa. Suala. Je ikiwa muko Makka na mwezi umeonekana huku kwanza mutasimama Arafa? Jawabu: Ndio, kwani hakuna Arafa ya mtu peke yake. Suala: Kwani kuna Arafa ya mwezi kumi? Arafa si mwezi tisa? Huoni kwamba ikiwa mwezi umeandama hapa kwanza na wao hawakufata muandamo wa hapa, itakuwa mwezi tisa hapa kule ni nane na tisa kule hapa ni kumi, kwa mujibu wa hisabu yao, wakati nyinyi mwezi munaouzingatia ni ule unaoandama kwanza? Jawabu: Kimya? Kwa hakika nukta hii fupi alioitoa Sheikh huyu inatosha kubainisha ukweli uko wapi.
257 - Kwa hivyo, ni wazi kwamba kisimamo cha Arafa si sababu ya kufunga siku hio bali sababu ni kuandama kwa mwezi wa mfunguo tatu ambao unatangulia kisha ndio zikaja ibada za hija kikiwemo kisimamo cha Arafa. Ama kisimamo hicho ni munasaba tu kama tulivyotangulia kubainisha.
258- Sura 9 Aya 25.
259- Mji uko karibu na Makka. Tazama Yaqut Al-rumi "MU'UJAMU AL-BULDAN" j. 1, uk. 190.
260- Tumetaja walioipokea Hadithi hii katika uk. 54-56.
261- Sura ya 2 Aya ya 200. Na mfano wake ni Hadithi inayosema: "Muhajir (akitaka kukaa Maka basi) akae siku tatu (tu) baada ya (kumaliza) nusuki (ibada) zake (za hija)."
262 - Katika chapa ya kwanza nimeandika "A'YNU" badala ya "A'WNU" basi sahihisha hapa; sahihi ni "A'WNU" si "A'YNU."
263- Tazama "A'WNU AL-MA'ABUDI: SHARHU SUNANI ABI DAUD" j. 6, uk. 463.
264 - Sura 9 Aya 25.
265 - Mji uko karibu na Makka. Tazama Yaqut Al-rumi "MU'UJAMU AL-BULDAN" j. 1, uk. 190.
266 - Anapodai au anaponukuu?!
267 - Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 37.
268 - Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 120-124.
269 - Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 123.
270- Al-imamu Abu Muslim: "NITHARU AL-JAWHAR" j. 5, uk. 157. Rudia pia uk. 194-195 wa kitabu "FATAWA ULAMMAI AL-BALADI AL-HARAM" cha wanachuoni wa Saudia uone walivyoeleza uhusiano wa matalai ya mwezi na matalai ya jua.
271 - Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Fawa: Al-Sala, Al-Zaka, Al-Saum, Al-Haj uk. 314.
272- Al-nnawawi "SHARHU AL-MUHADHAB" j. 6, uk. 183.
273 - Nassor Bachoo "UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" uk. 117-118.
274 - Ibn Hajar ana maelezo mazuri kuhusu Hadithi ya kufungwa mashetani. Tazama "AL-FAT-HU" katika sherehe ya Hadithi na. 1899.
275 - Na pia kwa kufata msingi wa kukamatana na hali ya mwanzo.
276 - Lakini pamoja na hayo tunasema kwamba ilikuwa ni juu ya Sheikh Bachoo kutotoa kabisa hoja hii, kwani Ramadhani inaingia pale tu jua linapotua siku ya mwezi 29 au 30 Shaabani. Sasa kama ni hivyo, vipi anahisi au nini rai yake pale jua linapotua Makka na Madina na ikawa Ramadhani imeingia na mashetani kufungwa, atawapa hukumu gani mashetani wa Marekani ambako ndio kwanza asubuhi au mchana - jua halijatua na Ramadhani haijaingia - je wao wataendelea kuvunja jungu? Au watakimbilia Saudia wakafungwe pamoja na wenzao?
277- Lakini pamoja na hayo tunasema kwamba ilikuwa ni juu ya Sheikh Bachoo kutotoa kabisa hoja hii, kwani Ramadhani inaingia pale tu jua linapotua siku ya mwezi 29 au 30 Shaabani. Sasa kama ni hivyo, vipi anahisi au nini rai yake pale jua linapotua Makka na Madina na ikawa Ramadhani imeingia na mashetani kufungwa, atawapa hukumu gani mashetani wa Marekani ambako ndio kwanza asubuhi au mchana - jua halijatua na Ramadhani haijaingia - je wao wataendelea kuvunja jungu? Au watakimbilia Saudia wakafungwe pamoja na wenzao?
278- Maana ya kuwa andiko la ujumla ni la dhana na andiko maalum (specific au khaas) ni la uhakika, ni kuwa andiko la ujumla linakusanya vitu vyote vyenye kuhusiana na lafdhi ya andiko hilo, lakini hakuna uhakika kwamba kweli vyote vimeingia au vilivyoingia ni vingi tu, wakati katika andiko maalum (specific au khaas), tuna hakika kwamba kilichotajwa ndivyo kilivyo. Kufahamu hili vizuri, tazama mfano mtu anaposema Wazanzibari ni wakarimu. Andiko hili ni la ujumla linamuingiza kila anayeitwa Mzanzibari, lakini je kweli kila Mzanzibari ana sifa hiyo ya ukarimu? Ukitazama utaona si kweli kwamba Wazanzibari wote wako hivyo, labda hio ni sifa ya waliowengi tu. Lakini nikitumia lafdhi khaas (specific) nikasema Ali ni mkarimu, basi huwa ni kitu cha hakika kwa vile kinamuhusu mtu mmoja maalum. Kwa hivyo, andiko hili si la hakika. Lakini katika andiko maalum (specific au khaas) maneno huwa ni ya uhakika.
279- Tazama Ibn Uthaimin "FATAWA ULAMAI AL-BALADI AL-HARAM" uk. 194-195.
280 - Al-salimiy "AL-JAWABAAT" j. 1, uk. 45.
281- Hadithi hio kaipokea Muslim "SAHIHU MUSLIM" Hadithi na. 2523, j. 4, uk. 421 katika "Sharhu Al-nnawawi." Al-tirmidhiy "AL-SUNAN" uk. 207, Hadithi na. 693. Abu Daud "AL-SUNAN" uk. 400, Hadithi na. 2329. Al-nnasai "AL-KUBRA" j. 3, uk. 97-98, Hadithi na. 2432. Al-bayhaqiy "AL-KUBRA" j. 6, uk. 294-295. Ibn Khuzaima "AL-SAHIH" j. 2, uk. 924, Hadithi na. 1916.
YALIYOMO
MUANDAMO WA MWEZI1
MAZUNGUMZO BAADA YA KHABARI KUHUSU MUANDAMO WA MWEZI-SAYARI 1
MAZUNGUMZO NA WANAFUNZI WA SHEIKH NASSOR BACHOO JUU YA SUALA LA MWEZI MUANDAMO 1
MUANDISHI: JUMA MUHAMMAD RASHID AL-MAZRUI, AL-ZENJIBARI 1
UTANGULI 1
MAZUNGUMZO BAADA YA KHABARI: KUHUSU MUANDAMO WA MWEZI-SAYARI 3
MUANDAMO WA MWEZI 5
SURA YA KWANZA 5
KUMJADILI KURAYBU NA UCHAMBUZI WA KISA HIKI 6
NASAHA 6
JAWABU 7
MATN YA RIWAYA YA KURAYB NA IBN ABBAAS 8
TANBIHI 11
DAI LA PILI 11
DAI LA TATU 13
JAWABU 13
MUANDAMO WA MWEZI 14
SURA YA PILI 14
JAWABU KWA WANAFUNZI WA BACHOO JAWABU YA UTANGULIZI 14
UKWELI JUU YA KUANDAMA KWA MWEZI 14
SEHEMU YA PILI 14
MNASEMA 21
JAWABU 21
MNASEMA 21
JAWABU 21
MNASEMA 22
JAWABU 22
MUNASEMA 22
JAWABU 22
MNASEMA 23
JAWABU 23
MNASEMA 23
JAWABU 24
MUANDAMO WA MWEZI 25
SEHEMU YA TATU 25
IKHTILAFU SIO UPINZANI 25
MNASEMA 25
JAWABU 25
SEHEMU YA NNE 26
JUMA AMPINGA AL-IMAMU AL-SHAUKANI 26
MNASEMA 4 26
JAWABU 26
MNASEMA 26
JAWABU 26
MNASEMA 27
SEHEMU YA TANO 30
NDUGU JUMA ANATOA RAI BINAFSI 30
MNASEMA 30
JAWABU 30
MUNASEMA 31
JAWABU 31
MUANDAMO WA MWEZI 33
SEHEMU YA SITA 33
MUANDAMO WA KIFALAKI NA MUANDAMO WA KISHARI'AH 33
UTANGULIZI MFUPI JUU YA SEHEMU HII 33
MUANDAMO WA KIFALAKI NI NINI? 33
MAELEZO JUU YA AYA HIZI 33
MAELEZO YA SH. NASSOR BACHOO 34
JAWABU NILILIPATA 36
JAWABU 37
MUNASEMA 38
Jawabu 38
MNASEMA 39
KISHA NAMI NIKANENA 39
MNASEMA 40
JAWABU 1) 40
MUANDAMO WA MWEZI 42
SEHEMU YA SABA 42
NDUGU JUMA ANACHANGANYA MAMBOKATIKA AYA YA QUR-AAN IFUATAYO 42
MNASEMA 7 42
SISI TUNAJIBU HIVI: 42
JAWABU 45
MNASEMA 45
JAWABU 45
MNASEMA 47
JAWABU 47
MNASEMA 47
JAWABU 47
MNASEMA 48
JAWABU 48
MNASEMA 48
JAWABU 48
MNASEMA 48
MNASEMA 49
JAWABU 49
MNASEMA 50
JAWABU 50
MUANDAMO WA MWEZI 52
SEHEMU YA NANE 52
KUTOKUTAJWA KWA MATLAI YA MWEZI NDANI YA QUR-AAN 52
JAWABU NILILOPATA 54
MUANDAMO WA MWEZI 56
SEHEMU YA TISA 56
UFAFANUZI WA NENO 'AHILLAH' 56
UFAFANUZI WA MGOGORO WA KUANDAMA KWA MWEZI" 56
JAWABU NILILOPATA 58
SISI TUNAJIBU KAMA IFUATAVYO 58
JAWABU 59
MNASEMA 60
JAWABU 60
MNASEMA 61
JAWABU 61
MNASEMA 62
JAWABU 62
MNASEMA 62
JAWABU 63
MNASEMA 64
JAWABU 65
MNASEMA 65
JAWABU 65
JAWABU 66
MNASEMA 66
JAWABU 67
MNASEMA 67
JAWABU 69
MUANDAMO WA MWEZI 71
SEHEMU YA KUMI 71
MASIMULIZI YA KURAIB 71
SANAD YA HADITHI 71
FIQ-HI YA HADITHI 71
UPINZANI NA MAELEZO YA AL-IMAMU AL-SHAUKANIY 72
UPINZANI WA KWANZA 72
AL-IMAMU BADRU AL-DIN, AL-KHALILIY AJIBU 72
UPINZANI WA PILI 73
UPINZANI WA TATU 74
JAWABU 75
UPINZANI WA NNE 75
UPINZANI WA TANO 75
UPINZANI WA SITA 78
UPINZANI WA SH. NASSOR BACHOO KWA HADITHI YA KURAIB NA IBN ABBAS 78
UPINZANI WA KWANZA 78
UPINZANI WA PILI 79
JAWABU 79
JAWABU 79
UPINZANI WA TATU 81
UPINZANI WA NNE 81
UPINZANI WA TANO 82
MUANDAMO WA MWEZI 84
JAWABU NILILOJIBIWA 84
JAWABU 84
JAWABU 84
MNASEMA 85
JAWABU 85
MNASEMA 86
JAWABU 86
MNASEMA 87
JAWABU 88
MNASEMA 89
JAWABU 89
JAWABU 90
MNASEMA 90
JAWABU 90
MNASEMA 92
JAWABU 92
MNASEMA 94
JAWABU 94
JAWABU 95
SANAD YA HADITHI 95
MUANDAMO WA MWEZI 97
MATN YA HADITHI 97
MNASEMA 99
JAWABU 99
MNASEMA 99
JAWABU 100
JAWABU 101
MNASEMA 102
JAWABU 102
MNASEMA 103
JAWABU 103
JAWABU 104
MNASEMA 104
JAWABU 104
MNASEMA 104
JAWABU 105
MUANDAMO WA MWEZI 106
SEHEMU YA KUMI NA MOJA 106
MTAZAMO WA MASAHABA (RADHIYA ALLAAHU 'ANHU) JUU YA KADHIA YA KUFUNGA NA KUFUNGUA MTAZAMO WA MASAHABA 106
MNASEMA 106
JAWABU 106
MNASEMA 107
JAWABU 107
MNASEMA 107
JAWABU 107
MNASEMA 108
JAWABU 108
MNASEMA 108
MNASEMA 109
MUANDAMO WA MWEZI 111
SEHEMU YA KUMI NA MBILI 111
KUANDAMA KWA MWEZI KATIKA SEHEMU MOJA KUNATOSHELEZA KUANDAMA KWAKE DUNIA NZIMA 111
MNASEMA 111
JAWABU 111
MNASEMA 114
JAWABU 114
MNASEMA 114
JAWABU 114
MNASEMA 116
JAWABU 116
MNASEMA 117
JAWABU 117
MUANDAMO WA MWEZI 119
SEHEMU YA KUMI NA TATU 119
MAANA YA JAMHURI KATIKA MATUMIZI YA KISHARI'AH 119
MNASEMA 119
JAWABU 119
MNASEMA 122
JAWABU 122
MNASEMA 122
JAWABU 123
MNAEMA 124
JAWABU 124
MNASEMA 125
JAWABU 125
MNASEMA 125
JAWABU 126
MNASEMA 126
JAWABU 126
MNASEMA 127
JAWABU 127
MUANDAMO WA MWEZI 128
SEHEMU YA KUMI NA NNE 128
UFAFANUZI WA AYA ISEMAYO : ATAKAYEUHUDHURIA MWEZI AFUNGE! 128
MUNASEMA 128
JAWABU 128
MNASEMA 128
JAWABU 128
MNASEMA 129
JAWABU 129
MNASEMA 130
JAWABU 130
MNASEMA 133
JAWABU 133
MNASEMA 133
JAWABU 133
MNASEMA 134
JAWABU 134
MNASEMA 135
JAWABU 135
MNASEMA 137
JAWABU 137
MNASEMA 137
JAWABU 137
MNASEMA 138
JAWABU 138
MUANDAMO WA MWEZI 139
HOJA YA ABU AMMAR NASSIR AL-MAZRUI JUU YA MASIMULIZI YA KURAIB 139
MNASEMA 139
JAWABU 139
MNASEMA 140
JAWABU 140
MNASEMA 142
JAWABU 142
AINA ZA IJMA' 144
MNASEMA 144
JAWABU 144
MNASEMA 145
JAWABU 145
MNASEMA 146
JAWABU 146
MUNASEMA 147
JAWABU 147
MUANDAMO WA MWEZI 149
SEHEMU YA KUMI NA TANO 149
FUNGA YA 'ARAFAH 149
JAWABU NILIOJIBIWA NI KAMA IFATAVYO 153
JAWABU 154
MNASEMA 155
JAWABU 155
MNASEMA 156
JAWABU 156
MNASEM 156
JAWABU 156
MNASEMA 157
JAWABU 157
MNASEMA 158
JAWABU 158
MNASEMA 158
JAWABU 158
MNASEMA 158
JAWABU 159
MNASEMA 159
JAWABU 160
MUANDAMO WA MWEZI 162
SEHEMU YA KUMI NA SITA 162
LAYLATUL- QADRI 162
MUNASEMA 162
JAWABU 162
MNASEMA 162
JAWABU 163
JAWABU 164
MNASEMA 165
JAWABU 165
MNASEMA 165
JAWABU 165
MUANDAMO WA MWEZI 166
SEHEMU YA KUMI NA SABA 166
KUTUMIA QIYAAS CHA KUINGIA WAKATI WA SWALA KWA WAKATI WA SWAUM 166
MNASEMA 166
JAWABU 166
MNASEMA 167
JAWABU 167
MNASEMA 167
JAWABU 167
MNASEMA 167
JAWABU 167
MNASEMA 168
JAWABU 168
MNASEMA 168
JAWABU 168
MNASEMA 168
JAWABU 168
MUANDAMO WA MWEZI 169
SEHEMU YA KUMI NA NANE 169
KUFUNGWA KWA MASHETANI 169
MUNASEMA 169
JAWABU 169
JAWABU 173
MNASEMA 173
JAWABU 173
MNASEMA 174
JAWABU 174
MNASEMA 175
JAWABU 175
JAWABU 175
MNASEMA 176
JAWABU 176
MNASEMA 176
JAWABU 177
MUANDAMO WA MWEZI 179
SEHEMU YA KUMI NA TISA 179
HITIMISHO 179
JAWABU 179
MNASEMA 179
JAWABU 179
MNASEMA 180
MUANDAMO WA MWEZI 181
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA 181
MUKHTASARI WA MJADALA 181
MWISHO 183
MAREJEO 184