MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
UTANGULIZI WA MTUMISHI WA SITE
Kitabu hichi kimeandikwa na wanachuoni wa Madhehebu ya Kisunni, kwa hiyo yaliomo ndani ya kitabu hichi ni masuala ya kielimu yanayoendana na Madhehebu hayo, hivyo basi wafuasi wa madhehebu mengine wanatakiwa kusoma ili kufaidika zaidi, na hapa hakuna lengo la kutoa ushawishi wa aina yeyote ile. Na lengo hasa la kuweka kitabu hichi ni kutaka ndugu zetu wa Kisunni nao waweke makala na vitabu vyetu katika site zao bila ya kuvutia upande wowote, jambo ambalo litawasaidia ndugu zetu wa Madhehebu mengine kuzielewa itikadi zetu bila ya chuki ya aina yeyeote, jambo ambalo litasaidia katika kueneza elimu na tamaduni za Kiislamu.
Asanteni sana.
Ngugu yenu:
SALIM SAID AL-RAJIHIY.
SURA YA KWANZA
MAANA YA ELIMU
Elimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji. Wanataaluma wamejitahidi kutoa maana ya elimu kuwa ni mabadiliko ya tabia yanayotokana na ujuzi. Kwa maana hii Elimu haiishii kwenye kuijua tu bali elimu hukamilika inapomwezesha mwenye kujua kutenda kwa ufanisi zaidi kuliko yule asiyejua.
Nani aliye elimika? Kutokana na maana ya elimu tuliyojifunza hapo juu, mtu aliyeelimika ni yule ambaye ujuzi alioupata humuwezesha kutenda kwa ufanisi zaidi kuliko pale alipokuwa hajapata ujuzi huo. Mtu aliyesoma hatachukuliwa tu kwa kirahisi kuwa kaelimika, bali kuelimika au kutoelimika kwake kutathibitika katika matendo na mwenendo wake wa kila siku. Matarajio ni kwamba mtu aliyesoma anapaswa aelimike kwa kutenda kwa ufanisi zaidi kuliko asiyesoma.
Na katika kuzingatia hili Allah (s.w) anatukumbusha katika Qur-an:
﴿قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ﴾
"...Sema, Je! wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu." (39:9)
Jibu la swali hili ni wazi. Mjuzi na asiyejua hawawezi kuwa sawa kiutendaji na kitabia. Endapo mtu atajiita msomi kwa kusoma vitabu vingi au kupewa shahada nyingi lakini kitabia na kiutendaji akawa hatofautiani na wale wasiosoma atakuwa bado hajaelimika na mfano wake ni ule unaopigwa katika Qur-an:
﴿مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴾
"Mfano wa wale waliopewa Taurati kisha hawakuichukua (kwa kuitia katika matendo) ni kama punda aliyebeba (mzigo) wa vitabu vikubwa (bila ya kufaidika kwavyo) ni mbaya kabisa mfano wa watu waliokadhibisha aya za Mwenyezi Mungu.Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu." (62:5).
NAFASI YA ELIMU NA WENYE ELIMU KATIKA UISLAMU
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo:
Kwanza: Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.
Tunajifunza katika Qur-an kuwa jambo la kwanza alilotunukiwa Adam(a.s) mara tu baada ya kuumbwa kwake ni kupewa elimu.
﴿وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا﴾
"Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya vitu vyote..." (2:31).
katika aya hii inaashiria fani zote za elimu ambazo anahitajia mwanaadamu hapa duniani ili afikie kwa ufanisi lengo la kuumbwa kwake.
Pia tunajifunza katika Quran kuwa mwenye elimu na hekima amepewa kheri nyingi.
﴿يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ﴾
(Mungu) humpa hikma amtakaye, na aliyepewa hikma bila shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili. (2.269).
KUTAFUTA ELIMU
Kutafuta elimu (kusoma) ni amri ya kwanza kwa mwanaadamu. Tunajifunza kutokana na historia ya kushushwa Qur-an kuwa Wahay wa kwanza kumshukia Mtume(s.a.w.w) ambao ndio ulimtawazisha rasmi kuwa mtume ni ule unaopatikana katika aya tano za mwanzo za Suratul-'Alaq:
﴿اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ﴾
"Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba.Ambaye amemuumba mwanaadamu kwa 'Alaq (kitu chenye kuning'inia).Soma na Mola wako ni karimu sana. Ambaye amemfundisha mwanaadamu kwa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya) mambo aliyokuwa hayajui" . (96:1-5)
Kutokana na aya hizi, kwa muhtasari, tunajifunza yafuatayo:
1. Kusoma kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni jambo la kwanza waliloamrishwa wanaadamu na Mola wao.
2. Kusoma kwa jina la Mola wako ni kusoma kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu au ili kuweza kumwabudu Allah(s.w) inavyostahiki na kusimamisha Uislamu katika jamii.
3. Radhi za Mwenyezi Mungu zitapatikana pale mwanaadamu atakapoweza kufikia lengo la maisha yake la kumuabudu Allah (s.w) kwa kuzingatia maamrisho na mipaka ya Mwenyezi Mungu katika kila kipengele cha maisha.
4. Amri hii ya kusoma hailengi fani maalum tu ya elimu; bali kila fani itakayomuwezesha mwanaadamu kufikia lengo la maisha yake kwa ufanisi.
5. Chanzo au chimbuko la fani zote za elimu ni Allah (s.w). Hivyo kwa Muislam mlango wa kwanza wa elimu ni kusoma kwa mazingatio Qur-an na hadithi sahihi za Mtume(s.a.w.w) na kusoma maarifa ya Uislamu kwa ujumla kutokana na vyanzo hivi viwili.
KWANINI UISLAMU UMEIPA ELIMU NAFASI YA KWANZA?
Elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislam kwa sababu zifuatazo:
Kwanza : elimu ndio nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kumtambua Mola wake vilivyo na kumuabudu ipasavyo kwa unyenyekevu kama Qur-an inavyothibitisha:
﴿ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ ﴾
"...Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale wataalam (waliozama katika fani mbali mbali)" (35:28).
Pili : elimu iliyosomwa kwa mrengo wa Qur-an ndio nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kuwa Khalifa wa Allah (s.w) hapa Ulimwenguni. Khalifa ni mja anayetawala ulimwengu kwa niaba ya Allah (s.w) kwa kufuata kanuni na sheria zake. Nabii Adam(a.s) aliwathibitishia Malaika kuwa ana uwezo wa kuutawala ulimwengu kwa niaba ya Allah (s.w) baada ya kuelimishwa fani zote za elimu (majina ya vitu vyote) na kuahidiwa mwongozo kutoka kwa Allah (s.w).
Tatu : kutafuta elimu ni Ibada maalumu ya hali ya juu kuliko Ibada zote. Kwa mujibu wa Qur-an Swala ni Ibada maalumu ya hali ya juu na ni dhikri kubwa au zingatio kubwa juu ya Allah (s.w):
﴿ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَلَذِكْرُ اللَّـهِ أَكْبَرُ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ﴾
"Hakika swala humzuilia (mja) na mambo machafu na maovu na ni dhikri kubwa kwa Allah (s.w)" (29:45).
Pia katika Hadith Mtume(s.a.w.w) amesisitiza:
"Nguzo kubwa ya Dini (Uislamu) ni swala, mwenye kusimamisha swala kasimamisha Dini na mwenye kuacha swala kavunja Dini."
Hivyo kwa mujibu wa Qur-an na Hadith sahihi za Mtume(s.a.w.w) , swala ni Ibada yenye hadhi ya juu kuliko Ibada zote mbele ya Allah (s.w); lakini bado Ibada ya kutafuta elimu inachukuwa nafasi ya juu zaidi kuliko swala kwani swala haiwezi kusimama bila ya kuwa na ujuzi stahiki. Nne, mwenye elimu ananafasi bora ya kumuabudu Mola wake inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake kama inavyosisitizwa katika Qur-an:
﴿ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ ﴾
"... Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale wataalamu" (35:28)
Pia Qur-an inasisitiza juu ya umuhimu wa elimu kwa kuuliza:
﴿قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ﴾
"Je,waweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu." (39:9)
Kimsingi wanaojua wanatarajiwa wafanye mambo kwa ufanisi zaidi kuliko wasiojua. Kwa msingi huu Allah (s.w) anasisitiza tena katika aya ifuatayo:
﴿يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴾
"Mwenyezi Mungu atawainua (daraja) wale walioamini miongoni mwenu, na waliopewa elimu watapata daraja zaidi. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda yote" (58:11)
Hivyo, kutokana na aya hizi (35:28, 39:9 na 58:11) tunajifunza kuwa; waumini wenye elimu wana daraja zaidi kuliko waumini wengine kwa sababu wanao uwezo zaidi wa kuona dalili za kuwepo Allah (s.w) na utukufu wake kwa undani zaidi, jambo ambalo huwapelekea kumuogopa Mola wao na kumuabudu inavyostahiki katika kukiendea kila kipengele cha maisha yao kama inavyobainika katika aya zifuatazo:
﴿إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴾
"Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana, ziko hoja (za kuonesha kuwepo Allah (s.w) kwa wenye akili (3:190)
Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima, wakiwa wamekaa na wakiwa wamelala. Na hufikiri (tena) umbo la mbingu na ardhi (wakasema) Mola wetu! Hukuviumba hivi burebure tu. Utukufu ni wako. Basi tuepushe na adhabu ya moto." (3:191).
Pia kutokana na aya hizo tunajifunza kuwa waumini wenye elimu wanao uwezo mkubwa wa kufanya mambo kwa ufanisi, jambo litakalowapelekea kusimamisha ukhalifa wa Allah (s.w) katika jamii.
CHANZO CHA ELIMU
Chanzo cha Elimu ni Allah (s.w) Kama tunavyojifunza katika surat 'Alaq (96:4-5), chanzo cha elimu au mkufunzi wa binadamu ni Allah (s.w). Allah (s.w) huwasiliana na binadamu na kuwaelimisha kwa kutumia mojawapo ya njia zifuatazo zilizoainishwa katika aya ifuatayo:
﴿ وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ ﴾
"Na haikuwa kwa mtu kwamba Mwenyezi Mungu anasema naye ila kwa il-hamu (anayetiwa moyoni mwake) au kwa nyuma ya pazia au humtuma mjumbe (Malaika) naye humfunulia kiasi anachotaka kwa idhini yake (Allah), bila shaka yeye ndiye aliye juu mwenye hekima." (42:51).
Aya hii inatufahamisha kuwa binaadamu hupata habari kutoka kwa Allah (s.w) kwa njia tatu zifuatazo:
(a) Il-hamu (Intution).
(b) Nyuma ya pazia.
(c) Kutumwa Malaika na kufikisha ujumbe kama alivyotumwa. Pia katika Qur-an tunafahamishwa njia mbili nyingine anazozitumia Allah (s.w) katika kumfikishia binaadamu ujumbe kutoka kwake:
(d) Ndoto za kweli (ndoto za Mitume).
(e) Maandishi (mbao zilizoandikwa tayari).
(a) Il-hamu.
Ni mtiririko wa habari au ujumbe unaomjia mwanaadamu bila ya kufundishwa na mtu yeyote au kuona mfano wake katika mazingira yoyote. Mambo mengi mwanaadamu huyafahamu kwa Il-hamu. Wagunduzi wa fani mbali mbali za elimu kama vile Hisabati, Fizikia, Jiografia, n.k. na Wavumbuzi wa vitu mbali mbali katika taaluma mbali mbali za kisayansi wameweza kufanya hivyo kwa kupata Il-hamu kutoka kwa Allah. Hivyo hakuna fani yoyote ya elimu isiyotoka kwa Allah (s.w).
﴿عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴾
"Amemfundisha mwaanadamu mambo yote aliyokuwa hayajui" (96:5)
(b) Kuongea na Allah (s.w) nyuma ya Pazia Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s.w) kwa sauti ya kawaida pasina kumuona. Kutokana na ushahidi wa Qur-an njia hii imetumika kwa Mitume na wateule wengine wa Allah (s.w).
Nabii Mussa(a.s) ni miongoni mwa Mitume waliosemeshwa na Allah (s.w).kama tunavyofahamishwa kisa chake katika Qur-an:
﴿فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى الْأَجَلَ وَسَارَ بِأَهْلِهِ آنَسَ مِن جَانِبِ الطُّورِ نَارًا قَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ جَذْوَةٍ مِّنَ النَّارِ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ ﴿٢٩﴾ فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ مِن شَاطِئِ الْوَادِ الْأَيْمَنِ فِي الْبُقْعَةِ الْمُبَارَكَةِ مِنَ الشَّجَرَةِ أَن يَا مُوسَىٰ إِنِّي أَنَا اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴾
Basi Musa alipotimiza muda, akasafiri pamoja na ahali zake (watu wake kurejea kwao Misri). Aliona moto upande wa mlimani akawaambia ahali zake; 'Ngojeni, hakika nimeona moto, labda nitakuleteeni habari za huko au kijinga cha moto ili muote! (28:29) Basi alipoufikia aliitwa kutoka upande wa kuliani wa bonde hilo katika kiwanja kilichobarikiwa, kutoka mtini: "Ewe Mussa! Bila shaka mimi ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu." (28:30)
Kwa njia ya nyuma ya pazia, Nabii Mussa(a.s) aliongea na Allah mara nyingi na mara zote hizo hakuweza kumuona. Alipoomba amuone alijibiwa kama inavyooneshwa katika aya zifuatazo:
﴿وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ﴾
Na alipofika Mussa katika miadi yetu na Mola wake akazungumza naye, (Mussa) akasema: "Mola wangu! Nionyeshe (nafsi yako) ili nikuone" Akasema (Mwenyezi Mungu): "Hutaniona, lakini tazama jabali (lililoko mbele yako) kama litakaa mahali pake utaweza kuniona".
Basi Mola wake alipojionyesha katika jabali, alilifanya liwe lenye kuvunjika vunjika na Mussa akaanguka hali ya kuzimia. Alipozindukana akasema "Utukufu ni wako.Natubu kwako, na mimi ni wa kwanza wa wanaoamini (haya)" (7:143).
Pia tunafahamishwa katika Qur-an kuwa Bibi Maryam, mama wa Nabii Issa(a.s) naye aliongeleshwa nyuma ya pazia wakati wa kumzaa Issa Bin Maryamu kama ilivyo katika aya zifuatazo:
﴿فَأَجَاءَهَا الْمَخَاضُ إِلَىٰ جِذْعِ النَّخْلَةِ قَالَتْ يَا لَيْتَنِي مِتُّ قَبْلَ هَـٰذَا وَكُنتُ نَسْيًا مَّنسِيًّا ﴿٢٣﴾ فَنَادَاهَا مِن تَحْتِهَا أَلَّا تَحْزَنِي قَدْ جَعَلَ رَبُّكِ تَحْتَكِ سَرِيًّا ﴿٢٤﴾ وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَاقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا ﴿٢٥﴾فَكُلِي وَاشْرَبِي وَقَرِّي عَيْنًا فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ الْبَشَرِ أَحَدًا فَقُولِي إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَـٰنِ صَوْمًا فَلَنْ أُكَلِّمَ الْيَوْمَ إِنسِيًّا﴾
"Kisha uchungu ukampeleka katika shina la mtende, (akawa anazaa na huku) anasema:"Laiti ningelikufa kabla ya haya, na ningekuwa niliyesahaulika kabisa.Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake ikamwambia usihuzunike.Hakika Mola wako amejaalia kijito cha maji chini yako.na litikise kwako shina la mtende, litakuangushia tende nzuri, zilizo mbivu. Basi ule na unywe na litulie jicho (lako). Na kama ukimuona mtu yeyote (akauliza habari juu ya mtoto huyu), sema:"Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa Rehma ya kufunga, kwa hiyo leo sitasema na mtu" (19:23 - 26).
(c) Kuletewa Ujumbe na Malaika kutoka kwa Allah (s.w) Kutuma ujumbe wa Malaika ni njia nyingine anayoitumia Allah (s.w) katika kuwaelimisha wanaadamu hasa katika mambo ya msingi ya maisha ya mwanaadamu hapa ulimwenguni. Hii ni njia maalum aliyoitumia Allah katika kuwasiliana na Mitume na miongoni mwa watu wengine wema. Kuhusu jinsi Mtume(s.a.w.w) aliyofundishwa na Allah (s.w) tunafahamishwa katika aya zifuatazo:
﴿وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ ﴿١﴾ مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ ﴿٢﴾ وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾ عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ ﴿٥﴾ ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَىٰ ﴿٦﴾ وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَىٰ ﴿٧﴾ ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ ﴿٨﴾ فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ ﴿٩﴾ فَأَوْحَىٰ إِلَىٰ عَبْدِهِ مَا أَوْحَىٰ ﴿١٠﴾ مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ ﴿١١﴾ أَفَتُمَارُونَهُ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ﴾
Naapa kwa nyota zinapoanguka.(Zinapokuchwa). Kwamba mtu wenu (huyu Muhammad) hakupotea kwa ujinga wala hakukosa. (na hali ya kuwa anajua); wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake. Hayakuwa haya (anayosema) ila ni wahyi (ufunuo). Uliofunuliwa (kwake).Amemfundisha (malaika) mwenye nguvu sana mwenye uweza. Na yeye yu katika upeo wa kuona (Horizon) katika mbingu kwa juu kabisa. Kisha (ukaribu wao) ni kama baina ya upinde na upinde au karibu zaidi. Na akamfunulia huyo Mtumwa wake (Mwenyezi Mungu) aliyoyafunua. Moyo haukusema uwongo uliyoyaona.(Moyo wake ulisadikisha haya yaliyotokea). Je! Mnabishana naye juu ya yale anayoyaona (daima)? (53:1-12).
Katika mafunzo ya Qur-an na Hadithi tunafahamishwa kuwa malaika Jibril ndiye malaika mkuu aliyehusika na kupeleka ujumbe kwa Mitume wa Allah (s.w). Lakini pia kutokana na aya za Qur-an sio yeye pekee aliyehusika tu na kupeleka ujumbe wa Allah kwa Mitume bali wajumbe wengine pia walihusika. Katika aya zifuatazo tunafahamishwa juu ya wageni (wajumbe) wa Nabii Ibrahim(a.s) ,waliomletea habari njema ya kumpata mtoto Is-haqa na habari ya kuhuzunisha ya kuangamizwa kwa watu waovu wa Kaumu ya Lut(a.s) aliyekuwa mpwawe:
﴿وَنَبِّئْهُمْ عَن ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ ﴿٥١﴾ذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا قَالَ إِنَّا مِنكُمْ وَجِلُونَ ﴿٥٢﴾ قَالُوا لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ ﴿٥٣﴾ قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِي عَلَىٰ أَن مَّسَّنِيَ الْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ ﴿٥٤﴾ قَالُوا بَشَّرْنَاكَ بِالْحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ الْقَانِطِينَ ﴿٥٥﴾ قَالَ وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ﴿٥٦﴾ قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ ﴿٥٧﴾ قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ ﴿٥٨﴾ إِلَّا آلَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٥٩﴾ إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَا إِنَّهَا لَمِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٦٠﴾ فَلَمَّا جَاءَ آلَ لُوطٍ الْمُرْسَلُونَ ﴿٦١﴾ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ ﴿٦٢﴾ قَالُوا بَلْ جِئْنَاكَ بِمَا كَانُوا فِيهِ يَمْتَرُونَ ﴿٦٣﴾ وَأَتَيْنَاكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿٦٤﴾ فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَاتَّبِعْ أَدْبَارَهُمْ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ وَامْضُوا حَيْثُ تُؤْمَرُونَ ﴿٦٥﴾ وَقَضَيْنَا إِلَيْهِ ذَٰلِكَ الْأَمْرَ أَنَّ دَابِرَ هَـٰؤُلَاءِ مَقْطُوعٌ مُّصْبِحِينَ﴾
"Na uwaambie khabari za wageni wa (Nabii) Ibrahim. Walipoingia kwake na wakasema:"Salaam" (Salaamun Alaykum, akawajibu; kisha) akasema (alipoona wamekataa kula chakula alichowawekea). "Kwa hakika sisi tunakuogopeni".Wakasema: "Usituogope, Sisi tunakupa khabari njema ya (kuwa utazaa) mtoto mwenye ilimu kubwa".Akasema: "Oh! Mnanipa khabari hii, na hali ya kuwa uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanipa khabari njema hiyo? Wakasema: Tumekupa khabari njema iliyo haki: basi usiwe miongoni mwa wanaokata tamaa. Akasema: "Na nani anayekata tamaa ya rehema ya Mola isipokuwa wale waliopotea? Akasema: (Tena) kusudi lenu (jingine) ni nini enyi mliotumwa?" Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa wale watu wakosaji (tukawaangamize).(watu wa Nabii Lut.)Isipokuwa waliomfuata Lut.Bila shaka sisi tutawaokoa wote hao (waliomfuata Lut)Isipokuwa mkewe.Tunapimia ya kuwa atakuwa miongoni mwa watakaokaa nyuma (waangamizwe).Basi wajumbe walipofika kwa watu wa Lut (kwa sura za kibinaadamu). (Lut) alisema:"Hakika nyinyi ni watu msiojulikana (na mimi; sikujueni)". Wakasema:"Basi sisi tumekuletea yale ambayo walikuwa wanayafanyia shaka, (nayo ni maangamizo yao).Na tumefika kwako kwa (hilo jambo la) haki (la kuangamizwa) na hakika sisi ni wenye kusema kweli. Basi ondoka na watu wako katika kipande cha usiku (pingapinga la usiku), na wewe ufuate nyuma yao; wala yeyote katika nyinyi asigeuke nyuma (na mwende upesi upesi) mnakoamrishwa.Na tukamkatia (Nabii Luti) jambo hili; la kwamba mizizi yao itakatwa asubuhi (yaani wataangamiziliwa mbali asubuhi)" (15: 51-66).
Zakaria(a.s) mlezi wa Maryamu mama wa Nabii Issa(a.s) aliletewa habari na malaika ya kumzaa Yahya(a.s) kama tunavyofahamishwa katika aya zifuatazo:
﴿هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٨﴾ فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًا بِكَلِمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٣٩﴾ قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَقَدْ بَلَغَنِيَ الْكِبَرُ وَامْرَأَتِي عَاقِرٌ قَالَ كَذَٰلِكَ اللَّـهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ﴿٤٠﴾ قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمْزًا وَاذْكُر رَّبَّكَ كَثِيرًا وَسَبِّحْ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ﴾
Pale pale Zakaria akamwomba Mola wake, akasema: "Mola wangu! Nipe kutoka kwako mtoto mwema.Wewe ndiye usikiaye maombi (ya wanaokuomba).Mara Malaika wakamlingania hali amesimama akiswali chumbani, kwamba Mwenyezi Mungu anakupa khabari njema za (kuwa utazaa mtoto; umwite) Yahya, atakayekuwa mwenye kumsadikisha (Mtume atakayezaliwa) kwa neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu (Naye ni Nabii Issa) na atakayekuwa bwana kabisa na mtawa na Nabii anayetokana na watu wema (Nao ni nyinyi). Akasema (Zakaria): "Mola wangu! Nitapataje mtoto, na hali uzee umenifikia,na mke wangu ni tasa?" Akasema (Mwenyezi Mungu),Ndiyo vivyo hivyo; Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo)". Akasema:Mola wangu! Niwekee alama (ya kunitambulisha kuwa mke wangu kishashika mimba nipate kufurahi upesi).Akasema: Alama yako ni kuwa hutaweza kusema na watu kwa siku tatu isipokuwa kwa ishara tu. Na mtaje Mola wako kwa wingi na umtukuze (kwa kuswali) wakati wa jioni na asubuhi" (3:38 - 41)
Pia Bibi Maryamu aliletewa ujumbe na malaika kutoka kwa Allah kama inavyodhihirika katika aya zifuatazo:
﴿ وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا ﴿١٦﴾ فَاتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا ﴿١٧﴾ قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَـٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا ﴿١٨﴾ قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا﴾
"Na mtaje Maryamu Kitabuni (humu).Alipojitenga na jamaa zake, (akaenda) mahali upande wa mashariki (wa msikiti).Na akaweka pazia kujikinga nao.Tukampelekea Muhuisha Sharia yetu (Jibrili) - akajimithilisha kwake (kwa sura ya) binaadamu aliye kamili. (Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema (Aniepushe) nawe.Ikiwa unamuogopa Mungu (basi ondoka nenda zako). (Malaika) akasema: Hakika mimi ni Mjumbe wa Mola wako: ili nikupe mwana mtakatifu" (19:16-19).
Pamoja na Malaika kuleta ujumbe kwa Mitume na miongoni mwa watu wema, pia kuna Malaika waliokuja kufundisha elimu ya uchawi kama sehemu ya mtihani kwa wanaadamu. Malaika waliotumwa na Allah kufundisha uchawi kama mtihani kwetu ni Haruta na Maruta kama inavyobainishwa katika Qur-an:
﴿وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴾
Wakafuata yale waliyoyafuata mashetani, (wakadai kuwa yalikuwa) katika ufalme wa (Nabii) Suleiman, na Suleiman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru,wakiwafundisha watu uchawi na (uchawi) ulioteremshwa kwa Malaika wawili, Haruta na Maruta, katika (mji wa) Babil. Wala (Malaika hao) hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: "Hakika sisi ni mtihani (wa kutazamwa kutii kwenu); basi usikufuru". Wakajifunza kwao ambayo kwa mambo hayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe (na mengineyo). Wala hawakuwa wenye kumdhuru yoyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.Na wanajifunza ambayo yatawadhuru wala hayatawafaa. Na kwa yakini wanajua kwamba aliyekhiari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera.Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia (starehe za) nafsi zao (za akhera).Laiti wangalijua,(hakika wasingefanya hivi)". (2:102).
Aya hii inazidi kututhibitishia kuwa hapana chochote ambacho anakijua mwanaadamu ila itakuwa amefundishwa na Allah (s.w).
(d) Ndoto za kweli Njia nyingine ya kupata ujumbe kutoka kwa Allah ni njia ya ndoto za kweli. Historia inatuonyesha kuwa ndoto za Mitume daima zilikuwa zikitokea kweli; kwa hiyo ulikuwa ni ujumbe moja kwa moja kutoka kwa Allah (s.w). Ndio maana Nabii Ibrahim(a.s) alipoota kuwa anamchinja mwanawe, hakusita kutekeleza hilo kwa kuwa yeye na mtoto wake Ismail(a.s) walikuwa na uhakika kuwa ni amri kutoka kwa Allah kama inavyobaini katika Aya ifuatayo:
﴿فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَىٰ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّابِرِينَ﴾
"Ewe mwanangu!Hakika nimeona katika ndoto ya kwamba ninakuchinja.Basi fikiri, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Fanya unayoamrishwa, utanikuta Insha-Allah miongoni mwa wanao subiri" (37:102)
Kutokea kweli kwa ndoto ya Nabii Yusuf(a.s) kama inavyobainishwa katika Qur-an ni miongoni mwa ushahidi kuwa ndoto za Mitume ni ujumbe wa kweli na wa moja kwa moja (kama ndoto yenyewe ilivyo) kutoka kwa Allah (s.w). Hebu turejee kisa cha ndoto ya Nabii Yusuf(a.s) katika aya zifuatazo:
﴿إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ ﴿٤﴾قَالَ يَا بُنَيَّ لَا تَقْصُصْ رُؤْيَاكَ عَلَىٰ إِخْوَتِكَ فَيَكِيدُوا لَكَ كَيْدًا إِنَّ الشَّيْطَانَ لِلْإِنسَانِ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴾
"Kumbuka Yusuf alipomwambia baba yake: Ewe baba yangu! Hakika nimeona katika ndoto nyota kumi na moja na jua na mwezi. Nimeviona vyote hivi vinanisujudia.Akasema (babaake): Ewe mwanangu! Usiwasimulie ndoto yako (hii) nduguzo wasije wakakufanyia vitimbi (kwa ajili ya husda itakayowapanda). Hakika shetani kwa mwanaadamu ni adui aliye dhahiri (atawatia uchungu tu). (12:4 - 5)
Kutokea kweli kwa ndoto hii kunabainishwa katika aya ifuatayo:
﴿فَلَمَّا دَخَلُوا عَلَىٰ يُوسُفَ آوَىٰ إِلَيْهِ أَبَوَيْهِ وَقَالَ ادْخُلُوا مِصْرَ إِن شَاءَ اللَّـهُ آمِنِينَ ﴿٩٩﴾ وَرَفَعَ أَبَوَيْهِ عَلَى الْعَرْشِ وَخَرُّوا لَهُ سُجَّدًا وَقَالَ يَا أَبَتِ هَـٰذَا تَأْوِيلُ رُؤْيَايَ مِن قَبْلُ قَدْ جَعَلَهَا رَبِّي حَقًّا وَقَدْ أَحْسَنَ بِي إِذْ أَخْرَجَنِي مِنَ السِّجْنِ وَجَاءَ بِكُم مِّنَ الْبَدْوِ مِن بَعْدِ أَن نَّزَغَ الشَّيْطَانُ بَيْنِي وَبَيْنَ إِخْوَتِي إِنَّ رَبِّي لَطِيفٌ لِّمَا يَشَاءُ إِنَّهُ هُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ﴾
"Na walipoingia kwa Yusuf, aliwainua wazazi wake na kuwaweka katika kiti (chake) cha ufalme.Na wote wakaporomoka kumsujudia. Na (Yusuf) akasema: "Ewe babaangu!Hii ndiyo (tafsiri) hakika ya ndoto yangu ya zamani.Bila shaka Mola wangu ameihakikisha. Na amenifanyia ihsani akanitoa gerezani na akakuleteni nyinyi kutoka jangwani; baada ya shetani kuchochea baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu ni mwenye kulifikia alitakalo. Bila shaka yeye ni mjuzi na mwenye hikima" (12: - 10).
Kutokea kweli kwa ndoto ya Mtume(s.a.w.w) kuwa Waislamu watangia Makka kuhiji kwa salama bila ya kuzuiliwa na mtu yeyote. Ndoto hii ilitokea kweli kama tunavyofahamishwa katika aya ifuatayo:
﴿ لَّقَدْ صَدَقَ اللَّـهُ رَسُولَهُ الرُّؤْيَا بِالْحَقِّ لَتَدْخُلُنَّ الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ إِن شَاءَ اللَّـهُ آمِنِينَ مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمْ وَمُقَصِّرِينَ لَا تَخَافُونَ فَعَلِمَ مَا لَمْ تَعْلَمُوا فَجَعَلَ مِن دُونِ ذَٰلِكَ فَتْحًا قَرِيبًا﴾
Kwa yakini Mwenyezi Mungu amemhakikishia Mtume wake ndoto yake ya haki.Bila shaka nyinyi mtaingia katika Msikiti Mtukufu Insha-Allah kwa salama; mkinyoa vichwa vyenu na mkipunguza nywele (kama ilivyowajibu kufanya hivyo wakati wa Hija).Hamtakuwa na khofu.Na (Mwenyezi Mungu) anajua msiyoyajua.Basi kabla ya haya atakupeni kushinda kuliko karibu. (48:27).
(e) Njia ya Maandishi: Njia nyingine anayoitumia Allah (s.w) katika kuwasiliana na waja wake ni njia ya maandishi, yaani maandishi yaliyoandikwa tayari. Nabii Mussa(a.s) aliletewa ujumbe kutoka kwa Allah (s.w) kwa maandishi yaliyoandikwa tayari katika mbao kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo: "Na tukamwandikia katika mbao kila kitu mawaidha (ya kila namna) na maelezo ya kila jambo.
﴿ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا بِأَحْسَنِهَا﴾
"Basi yashike kwa imara na uwaamrishe watu wako wayashike vema haya" (7:145)
﴿وَلَمَّا سَكَتَ عَن مُّوسَى الْغَضَبُ أَخَذَ الْأَلْوَاحَ وَفِي نُسْخَتِهَا هُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ هُمْ لِرَبِّهِمْ يَرْهَبُونَ﴾
"Na Musa zilipotulia ghadhabu zake, aliziokota zile mbao.Na katika maandiko yake (hizo mbao) ulikuwamo uwongofu na rehema kwa wale wanaomuogopa Mola wao" (7:154).
Kwa ujumla tumeona kuwa chanzo cha elimu ni "Allah (s.w). Lolote tunalolifahamu tumefunzwa na Allah kwa njia mojawapo katika njia tano tulizoziona.
1
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
KATIKA UISLAMU HAKUNA ELIMU YA DINI NA DUNIA
Makafiri na hata baadhi ya Waislamu kutokana na mtazamo wao finyu juu ya maana ya dini iliyowapelekea kuyagawanya maisha ya binaadamu kwenye matapo mawili; maisha ya dini na maisha ya dunia, wameigawanya elimu kwenye matapo hayo mawili. Kwa mtazamo huu potofu elimu ya dini ni ile inayoshughulikia maswala ya kiroho (spiritual life) ya mtu binafsi inayoishia katika kumuwezesha mtu kuswali, kufunga na kutekeleza Ibada nyingine maalumu kama hizi bila ya kuzihusisha na maisha yake ya kila siku ya kibinafsi, kifamilia na kijamii.Hivyo elimu hii haina nafasi ya kumuwezesha binaadamu kuendea maisha yake ya kila siku ya kijamii.
ELIMU YA DUNIA
Elimu ya Dunia kwa mtazamo huu wa makafiri, ni ile inayojishughulisha na masuala ya kijamii kama vile uchumi, siasa, utamaduni, sheria na maongozi ya jamii kwa ujumla kwa kufuata maelekezo na matashi ya binaadamu bila ya kuzingatia mwongozo wa Allah (s.w). Kwa mtazamo wa mgawanyo huu, elimu ya dini ndiyo iliyofundishwa na Allah (s.w) kupitia kwa Mitume na Vitabu vyake na elimu ya dunia imebuniwa na binaadamu wenyewe kwa msukumo wa matashi na mahitaji yao katika kuendea kila kipengele cha maisha yao ya kimaada (Physical or Material life). Kwa mtazamo wa Uislamu (Qur-an na Sunnah) hapana mgawanyo huu wa elimu kwa sababu za msingi zifuatazo: Kwanza, Nabii Adam(a.s) katika kuandaliwa yeye na kikazi chake kuwa Makhalifa wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni alifundishwa majina ya vitu vyote kama Qur-an inavyoainisha:
﴿وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا﴾
"Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya vitu vyote" (2:31)
Majina ya vitu vyote hapa kama tulivyotangulia kusema inaashiria fani zote za elimu zitakazomuwezesha binaadamu kuendea kila kipengele cha maisha yake na kufikia malengo tarajiwa. Pamoja na kufundishwa majina ya vitu vyote, p ia Adam(a.s) na kizazi chake waliahidiwa na Mola wao kuletewa mwongozo utakaowawezesha kutumia fani mbali mbali za taaluma walizonazo kwa kufuata utaratibu utakaowapelekea kukiendea kila kipengele cha maisha yao kwa furaha na amani:
﴿قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴾
"Tukasema: Shukeni humo nyote; na kama ukikufikieni uwongozi utokao kwangu, basi watakaofuata uwongozi wangu huo, haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika." (2:38).
Lakini wale watakaotumia taaluma mbali mbali walizonazo katika kuendea kila kipengele cha maisha yao ya kila siku ya kibinafsi na kijamii bila ya kufuata mwongozo wa Allah (s.w) kupitia kwa Mitume wake na Vitabu vyake, wataishi maisha ya huzuni na khofu na katika maisha ya akhera watakuwa na adhabu kali:
﴿وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾
"Lakini wenye kukufuru na kuyakadhibisha maneno yetu, hao ndio watakaokuwa watu wa motoni, humo watakaa milele" (2:39)
Kwa mujibu wa maelezo haya tunajifunza kuwa fani zote za elimu (majina ya vitu vyote) ambazo amezifundisha Allah (s.w) pamoja na mwongozo maalumu kutoka kwake, vinahitajika kwa binaadamu ili kumuwezesha kuishi maisha ya furaha na amani hapa duniani na huko akhera. Hivyo hapana mwenye uwezo wa kutenganisha maisha ya dini na dunia au elimu ya dini na dunia.
Pili : Amri ya kusoma (kutafuta elimu) aliyopewa Mtume(s.a.w.w) na umma wake, haibagui elimu ya dini na dunia.
Vinginevyo fani yoyote ya elimu inayomuwezesha binaadamu kusimamisha ukhalifa wa Allah (s.w) katika jamii na kufikia lengo la kuumbwa la kumuabudu Allah (s.w) inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake inapaswa isomwe kwa juhudi zote.
Tatu : chanzo cha fani zote za elimu ni Allah (s.w) kama Qur-an inavyosisitiza:
﴿اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ﴾
"Soma na Mola wako ni karimu sana.Ambaye amemfundisha (Binaadamu fani zote za elimu) kwa msaada wa kalamu.Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya mambo) aliyokuwa hayajui". (96:3-5)
Kwa mujibu wa aya hizi hapana fani yoyote ya taaluma iliyoasisiwa na binaadamu. Hivyo suala la kuwa na elimu ya dunia iliyoasisiwa na binaadamu na elimu ya dini ambayo tu ndiyo iliyotaka kwa Allah (s.w), halipo kwa mtazamo wa Qur-an.
Nne : katika Qur-an tunafahamishwa kuwa wanaomcha Allah (s.w) ipasavyo na kumuogopa ni wale wataalamu (ulamaa) waliozama katika fani mbali mbali za elimu. Kwa mujibu wa Qur'an fani hizi mbali mbali haziishii tu kwenye zile fani zinazotazamwa kwa mrengo wa kidini kama vile fiqh, Tawhiid, n.k. bali fani zote za elimu zinazo muwezesha binaadamu kutafakari kwa undani juu ya kuwepo Allah (s.w) na daraja ya utukufu wake, hasa zile fani za kisayansi zinazohusiana na maumbile. Hebu turejee aya zifuatazo:
﴿أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ ثَمَرَاتٍ مُّخْتَلِفًا أَلْوَانُهَا وَمِنَ الْجِبَالِ جُدَدٌ بِيضٌ وَحُمْرٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهَا وَغَرَابِيبُ سُودٌ ﴿٢٧﴾ وَمِنَ النَّاسِ وَالدَّوَابِّ وَالْأَنْعَامِ مُخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ كَذَٰلِكَ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ ﴾
Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji toka mawinguni!Na kwayo tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana. Na katika watu na wanyama wanaotambaa na wanyama (wengine), pia rangi zao ni mbali mbali. Kwa hakika wanaomwogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja Wake ni wale wataalamu (wanavyuoni). Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Msamehevu. (35:27-28)
Katika aya hizi tunajifunza kuwa wenye kumcha Allah (s.w) ipasavyo na katika kiwango cha juu cha unyenyekevu ni wale waumini waliobobea katika taaluma mbali mbali (maulamaa). Je, maulamaa waliotajwa katika aya hizi ni wale tu waliobobea kwenye taaluma zinazoitwa za kidini kama vile fiq-h, Qur-an na Hadith? Maulamaa waliopigiwa mfano katika aya hizi ni wale waliozama katika fani ya Hali ya Hewa (Meteorologist), Maulama waliozama katika uchunguzi wa wanyama (Zoologist), maulamaa waliozama katika fani ya matunda (Horticulturist), Maulamaa waliozama katika fani ya Madini (Geologists) na Maulamaa waliozama katika fani ya kuchunguza watu walivyo kimaumbile, rangi, n.k. (Anthropolagist). Pia katika aya nyingi za Qur-an binaadamu amesisitizwa kuyafanyia utafiti mazingira ya mbingu na ardhi ili kumtambua Mola wake na kumuabudu ipasavyo.
Tano : katika Qur-an Allah (s.w) anatufahamisha kuwa waumini waliobobea kwenye elimu wana daraja kubwa zaidi kuliko waumini wengine:
﴿يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴾
"Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu; na waliopewa elimu watapata daraja zaidi.Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda yote." (58:11)
Aya hii haijabagua wenye elimu.Hivyo yeyote yule mwenye taaluma inayomuwezesha kumcha Mola wake na kumuabudu inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake na ikamuwezesha kuchangia katika kusimamsiha Uislamu katika jamii atakuwa na daraja zaidi kuliko wale wasio na taaluma hiyo kama Qur-an inavyozidi kusisitiza:
﴿إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ﴾
"Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mwenyezi Mungu zaidi katika nyinyi." (49:13)
Sita : hatuoni mgawanyo wa elimu katika Hadith mbali mbali za Mtume(s.a.w.w) zinazozungumzia elimu. Kwa mfano Mtume(s.a.w.w) aliposema: "Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila Muislamu mwanamume na kila Muislamu mwanamke." (Ibn Majah), hakubagua elimu.Pia rejea Hadith zifuatazo: Anas (r.a) ameeleza kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema: Mwenye kutoka nje kutafuta elimu yuko katika njia ya Allah mpaka atakapo rejea. (Tirmidh)
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema: Yeyote atakayeulizwa juu ya jambo alilojifunza kisha akaficha (akakataa kutoa elimu ile) atavalishwa mshipi (mkanda) wa Moto siku ya Kiyama." (Ahmad, Abu Daud, Tirmidh na Ibn Majah).
Pia tunajifunza katika historia kuwa; Mtume(s.a.w.w) aliwaacha huru mateka wa vita vya Badr kwa yule aliyeweza kujikomboa kwa kuwafunza kusoma na kuandika watoto kumi wa Waislamu.
Hadith hizi zinadhihirisha kuwa Mtume(s.a.w.w) naye hakuigawanya elimu katika elimu ya dini na elimu ya dunia. Bali Mtume(s.a.w.w) amewahimiza Waislamu kutafuta elimu yenye manufaa kwa jamii popote pale inapopatikana. "Tafuteni elimu hata China" (Baihaqi)
Laiti kama pangelikuwepo na mgawanyo wa elimu na kuwa elimu ya lazima kutafutwa na Waislamu ni ile iitwayo "elimu ya dini" kwanini Mtume(s.a.w.w) aliwaamuru waende China wakati wahay ulikuwa unamfuata yeye alipo? Ilikuwa inatosha wao kubaki na Mtume Makkah au Madina na asiwatume tena kwenda China kutafuta elimu. Hivyo, kutokana na hoja hizi sita, Uislamu hautambui mgawanyo wa elimu kwenye tapo la elimu ya dini na elimu ya dunia.
MGAWANYO WA ELIMU KATIKA FARADH
Mgawanyo wa Elimu katika Faradh 'Ain na Faradh Kifaya Faradh ya elimu inaweza kugawanywa kwenye faradhi 'Ain na faradh Kifaya.Faradh 'Ain ni faradh inayomhusu kila mtu binafsi isiyo na uwakilishi. Mfano, kusimamisha swala, kutoa Zakat, kufunga, n.k. ni katika faradh 'ain. Faradh Kifaya ni faradh inayoweza kufanywa kwa uwakilishi.Ni faradhi ya kijamii. Wachache wanaweza kuitekeleza kwa niaba ya jamii. Kwa mfano swala ya maiti na yale yote ya faradh anayostahiki kufanyiwa maiti wa Kiislamu ni katika faradh kifaya.
ELIMU YA MAARIFA YA UISLAMU
Elimu ya Maarifa ya Uislamu, itakayompelekea mja kumtambua, Mola wake, vilivyo na kumuabudu inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha ni faradh 'Ain. Kwa maana nyingine ni faradh kwa kila Muislamu kuujua Uislamu vilivyo na kujitahidi kuutekeleza kwa kadiri ya uwezo wake katika kila kipengele cha maisha. Elimu juu ya fani mbalimbali zinazohitajika katika maisha ya jamii ni faradhi kifaya kwa jamii ya Kiislamu. Kwa mfano ni faradhi kwa jamii ya Kiislamu kuwa na madaktari, wahandisi, wanasheria, wanasiasa, wanauchumi, waalimu na wataalamu wengineo katika kila fani ya maisha ya jamii wa kutosha kukidhi mahitajio ya jamii katika kuendea nyanja zote za maisha.
Ikitokezea Waislamu wamezembea kiasi cha kushindwa kutoa wataalamu wanaohitajika kuendesha kila fani ya maisha ya jamii mpaka inapelekea Waislamu kushindwa kumuabudu Mola wao ipasavyo katika kila kipengele cha maisha, jamii yote ya Waislamu itakuwa katika lawama (itapata dhambi) na itaathirika kutokana na dhambi hii.
Hivyo ili Waislamu waweze kusimamisha Uislamu (Ukhalifa wa Allah) katika jamii, kila Muislamu hanabudi kuufahamu Uislamu vilivyo na pawekwe mazingira ya makusudi yatakayomuwezesha kila Muislamu kujielimisha katika fani maalumu ya maisha inayohitajika katika jamii kwa kadiri ya vipaji alivyoruzukiwa na Mola wake.Kwa maana nyingine kila Muislamu mwenye vipaji vya kuwa Daktari au Mhandisi au Mwanasheria au Mchumi au Mwalimu au. ajizatiti kuiendea taaluma hiyo na jamii ijizatiti kumuwezesha. Endapo, kwa mfano Muislamu mwenye kipaji cha kuwa Dak tari, akazembea asiwe Daktari atakuwa mas-uli mbele ya Allah (s.w).Pia endapo jamii ya Waislamu itazembea isitoe Madaktari wanaohitajika itakuwa mas-uli mbele ya Allah (s.w).
ELIMU YENYE MANUFAA
Elimu yenye manufaa ni ile ambayo:
Kwanza : humuwezesha mja kufikia lengo la kuumbwa kwake. Tumeona kuwa elimu imekuwa faradhi ya kwanza kwa waumini kwa kuwa elimu ndio nyenzo kuu ya kuwawezesha binaadamu kufikia lengo la kuumbwa kwao ambalo ni kumuabudu Allah (s.w), ipasavyo katika kila kipengele cha maisha yao. (Qur-an 51:56).
Pia elimu ndio nyenzo kuu ya kuwawezesha waumini kuwa viongozi wa jamii (makhalifa wa Allah) katika ardhi. (Qur-an 2:30 - 31).
Elimu itakayotafutwa kinyume na kumuwezesha mtu kumuabudu Mola wake ipasavyo na kusimamisha ukhalifa wa Allah (s.w) katika ardhi itakuwa si elimu yenye manufaa bali elimu yenye kuhasirisha kama tunavyojifunza katika hadithi zifuatazo: Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:
"Anayetafuta elimu isiyokuwa kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah (s.w), hasomi kwa lengo lolote lile ila la kupata maslahi ya hapa duniani tu.Huyo siku ya kiyama hatapata hata harufu ya Pepo." (Ahmad, Abu Daud, Ibn Majah).
Pia Mtume(s.a.w.w) ametuasa kuwa mwenye kutafuta elimu ili awazidi wasomi wengine au ili kuitumia katika biashara za kijahili au ili kujionesha kwa watu kuwa naye ni msomi, Mwenyezi Mungu atamuingiza motoni. (Tirmidh)
Pili : elimu yenye manufaa kwa binaadamu hapa ulimwenguni na huko akhera ni ile ambayo pamoja na mtu binafsi kuitumia katika kumuabudu Allah (s.w) ipasavyo katika maisha yake ya kila siku, huifundisha au huifikisha kwa wengine pia kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah (s.w). Ni vibaya mno mbele ya Allah (s.w) mtu kukataa au kuacha kufikisha kwa wengine kila anachokijua kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:
"Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:
"Atakayeulizwa juu ya jambo alilojifunza kisha akaficha (akakataa kutoa elimu ile) atavalishwa mshipi wa moto katika siku ya Kiyama". (Ahmad, Ibn Majah, Tirmidh na Abu Daud).
Katika hadith nyingine iliyosimuliwa na Abu Hurairah Mtume(s.a.w.w) amesema:
"Mfano wa elimu isiyonufaisha ni sawa na mfano wa mali iliyokusanywa bila ya kutumiwa katika njia ya Allah". (Ahmad, Darini).
Kutokana na hadith hizi tunajifunza kuwa elimu yenye kunufaisha ni ile iliyofundishwa kwa wengine kinadharia na kiutendaji. Kwa kufundisha watu unachokijua bila ya wewe mwenyewe kutenda ni mfano mbaya mno kwa wale wanaofundisha na chukizo kubwa mno mbele ya Allah (s.w):
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ ﴿٢﴾ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ﴾
"Enyi mlioamini mbona mnasema msiyoyatenda?Ni chukizo kubwa mbele ya Allah (s.w) kusema msiyoyatenda" (61:2-3)
ZOEZI
1. Elimu ni nini?
2."Sema, Je wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?.. ." (39:9) Ni kwasababu gani wanaojua hawawi sawa na wasiojuwa?
3. Unatoa maoni gani iwapo wanaojua na wasiojua wakawa sawa kiutendaji?
4. Toa maelezo yenye ushahidi wa Qur-an kuonyesha kuwa:
(a) Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa binaadamu na Mola wake.
(b) Kutafuta elimu ni amri ya kwanza kwa binaadamu.
5. Onyesha kwa ushahidi wa Qur-an kuwa katika Uislamu mgawanyiko wa elimu katika "elimu ya dini" na "elimu ya dunia" haukubaliki.
6."Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba." (96:1)
Kusoma kwa jina la Mola wako maana yake nini?
7. "....Soma na Mola wako ni karimu sana.Ambaye amemfundisha mwanaadamu kwa kalamu.Amemfundisha mwanaadamu mambo aliyokuwa hayajui". (96:3-5)
Orodhesha njia tano anazozitumia Allah (SW) katika kuwasiliana na wanaadamu.
8. Elimu yenye manufaa kwa binaadamu ni ile.................................
9. Eleza sababu tatu zinazopelekea elimu kupewa nafasi ya kwanza katika Uislamu.
2
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
SURA YA PILI
MAANA YA DINI KWA MTAZAMO WA MAKAFIRI
Makafiri wanatafsiri dini kuwa ni:
(i) "Imani inayohusiana na mambo ya kiroho baina ya binaadamu na Mwenyezi Mungu au njia ya kuhusiana na Mwenyezi Mungu" (Kamusi ya Kiswahili sanifu)
(ii) "Imani juu ya kuwepo Mungu Muumba aliye muweza na mwenye nguvu juu ya kila kitu, Mmiliki wa ulimwengu, ambaye amempa binaadamu roho ambayo huendelea kuishi baada ya kifo cha mwili" (Oxford Advanced Learner's Dictionary of Current English). Kutokana na tafsiri hii ya dini iliyonukuliwa kutoka kwenye kamusi ya Kiswahili na ya Kiingereza, tunajifunza mambo makubwa mawili:
Kwanza : kwa mtazamo wa makafiri dini inahusiana na imani ya kuwepo Allah (s.w). Hivyo wenye dini ni wale tu wanaoamini kuwepo kwa Allah (s.w), na wale wasioamini kuwepo kwake hawana dini. Ni katika mtazamo huu V. I. Lenin katika kitabu chake "Socialism and Religion (Ujamaa na Dini) amedai: "Everybody must be absolutely free to profess any religion he pleases or no religion whatever; i.e. to be an atheist which every socialist is as a rule..." Tafsiri:
"Kila mtu hanabudi kuwa huru kabisa kufuata dini yoyote anayotaka au asiwe na dini kabisa, yaani awe kafiri, jambo ambalo inambidi kila mjamaa awe kama sheria..."
Pili : kwa mtazamo wa makafiri, dini inahusiana na mambo ya kiroho au ulimwengu wa kiroho tu, na haihusiani kabisa na ulimwengu wa kimaada (wa vitu). Ni kwa mtazamo huu kwa makafiri, matendo ya wafuasi wa dini yamegawanywa katika sehemu mbili, matendo ya dini na matendo ya dunia. Katika mtazamo huu pia Waislamu hulaumiwa na makafiri kuwa wanachanganya dini na siasa, dini na uchumi; dini na utamaduni, na kadhalika.
MAANA YA DINI KWA MTAZAMO WA UISLAMU
Kwa mtazamo wa Uislamu"Dini" ni utaratibu wa maisha wanaoufuata binaadamu katika kuendesha maisha yao ya kila siku ya kibinafsi na kijamii.
Ni katika maana hii ya dini Allah (s.w) huuliza katika aya ifuatayo:
﴿أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ﴾
"Je, (watu) wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu na hali kila kilichomo mbinguni na ardhini kimejisalimisha kwake kipende kisipende. Na kwake watarejeshwa wote" (3:83)
Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa:
Kwanza : kuna dini nyingi zinazofuatwa na watu hapa ulimwenguni, lakini dini iliyostahiki watu wenye "akili timamu" waichague, ni ile dini inayofuatwa na maumbile yote.
Pili : dini ya maumbile yote ya mbinguni na ardhini si nyingine, ila ni ile ya kujisalimisha katika kufuata sheria za maumbile alizoziweka Muumba. Tukirejea kwenye sayansi ya maumbile (natural science) tunajifunza kuwa kila kitu kilicho hai na kisicho hai (living and nonliving thing) ili kiwepo ni lazima kifungamane na sheria za maumbile za kibailojia, kifizikia na za kikemia (Biological, Physical and Chemical laws). Kwa mtazamo huu hata miili yetu pia imejisalisha kwa muumba kwa kufuata sheria za maumbile pasina hiari kama inavyosisitizwa katika aya ifuatayo:
﴿فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴾
"Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawa sawa ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu (yaani dini hii ya Kiislamu inawafikiana bara bara na umbile la binaadamu).Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu.Hiyo ndio dini iliyo ya haki lakini watu wengi hawajui." (30:30)
Kwa ufupi, aya hii inatukumbusha kuwa miili yetu imejisalimisha kwa Allah (s.w) bila ya hiari kwa kufuata bara bara sheria za maumbile zinazofungamana na ufanyaji kazi wa kila kiungo cha mwili.Chakula kinayeyushwa tumboni, moyo unasukuma damu, mapafu, ini, figo, na viungo vingine mwilini hufanyakazi kwa kufuata sheria za Muumba na wala sio kwa kufuata sheria walizozitunga wanaadamu katika mabunge yao.
Tatu : Uislamu ni mfumo wa maisha uliofungamana na kanuni na sheria alizoziweka Muumba ili watu waendeshe maisha yao ya kibinafsi na kijamii sambamba na hali halisi ya maumbile yaliyowazunguka. Wale watakaoamua kwa hiari yao kufuata kanuni na sheria alizoziweka Allah (s.w) katika kukiendea kila kipengele cha maisha yao ya kila siku watakuwa ni Waislamu, waliojisalimisha kwa Muumba wao kama ilivyojisalimisha miili yao na maumbile yote ya mbinguni na ardhini. Hawa wataishi kwa furaha na amani hapa ulimwenguni, kwani wataepukana na maisha yale ya kupingana na maumbile yaliyowazunguka. Ama wale watakaokataa kufuata kanuni na sheria alizoziweka Muumba na badala yake wakaweka mfumo wa maisha unaopingana na kanuni na sheria hizo watakuwa ni makafiri, walioamua kupingana na maumbile yote yaliyowazunguka. Kwa vyovyote vile watakuwa wameamua kuishi maisha ya upinzani na vurugu.
Nne : kimantiki, ni lazima iwepo siku ya Hisabu ambapo watu wote watahudhurishwa mbele ya mahakama ya Muumba na Mmiliki wa maumbile yote, ili walipwe kutokana na uamuzi wao katika kuchagua na kufuata "dini". Wale waliojisalimisha kwa Allah (s.w) na kufuata "dini" yake, pamoja na kuishi maisha ya nuru (ya Amani na Heshima) hapa duniani, watakuwa na maisha ya furaha na amani ya kudumu huko Peponi. Ama wale waliompinga Allah (s.w) kwa kuweka na kufuata mifumo ya maisha kinyume na "dini" yake, pamoja na kuishi maisha ya giza (ya khofu na huzuni) hapa duniani, watakuwa na maisha ya dhiki na adhabu kubwa huko Motoni kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
﴿اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾
"Mwenyezi Mungu ni Mlinzi (kiongozi) wa wale walioamini. Huwatoa katika giza na kuwaingiza katika nuru.Lakini waliokufuru, walinzi (viongozi) wao ni Matwaghuut.Huwatoa katika nuru na kuwaingiza katika giza.Hao ndio watu wa Motoni, humo wakakaa milele". (2:257)
Mwanaadamu hawezi kuishi bila Dini Mwanaadamu hawezi kuishi bila dini kwa sababu zifuatazo:
(a) Maana halisi ya dini Tunaona kuwa maana halisi ya dini kwa mtazamo wa Qur'an ni utaratibu au mfumo wa maisha anaoufuata mwanaadamu katika kuendesha maisha yake ya kila siku. Hivyo kwa vyovyote vile mwanaadamu katika kuendesha maisha yake ya kila siku atakuwa anafuata dini moja au nyingine.Hana namna yoyote ya kuishi bila dini.
(b) Umbile la Mwanaadamu ni la kidini Ukizingatia maana halisi ya dini, kuwa dini ni utaratibu wa maisha, utadhihirikiwa kuwa umbile la mwanaadamu ni la kidini. Umbile la mwanaadamu kama maumbile mengine yaliyomzunguka hufuata mfumo maalum bila ya matashi au hiari ya mwanaadamu. Kwa maana nyingine umbile la mwanaadamu limedhibitiwa na sheria za maumbile (natural Laws - biological, chemical, and physical laws). Kwa mfano, ukichunguza hatua anazozipitia mwanaadamu katika tumbo la uzazi mpaka kuwa kiumbe kamili, ni utaratibu madhubuti ambao uko nje kabisa ya uwezo au matashi yake. Kuhusu kuumbwa kwa mwanaadamu Allah (s.w) anatukumbusha katika Qur-an:
﴿وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن سُلَالَةٍ مِّن طِينٍ ﴿١٢﴾ ثُمَّ جَعَلْنَاهُ نُطْفَةً فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ ﴿١٣﴾ ثُمَّ خَلَقْنَا النُّطْفَةَ عَلَقَةً فَخَلَقْنَا الْعَلَقَةَ مُضْغَةً فَخَلَقْنَا الْمُضْغَةَ عِظَامًا فَكَسَوْنَا الْعِظَامَ لَحْمًا ثُمَّ أَنشَأْنَاهُ خَلْقًا آخَرَ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ﴾
Na kwa yakini tulimuumba mwanaadamu kwa udongo ulio safi, kisha tukamuumba kwa tone la manii lililowekwa katika makao yaliyohifadhika. Kisha tukalifanya tone hilo kuwa kitu chenye kuning'inia na tukakifanya hicho chenye kuning'inia kuwa pande la nyama, kisha tukalifanya pande hilo la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivisha nyama,kisha tukamfanya kiumbe kingine. Basi Ametukuka Allah, Mbora wa waumbaji (23:12-14)
Si tu kuwa mwanaadamu hana mamlaka na kuzaliwa kwake, bali pia hana mamlaka na kukua kwake, na kufa kwake kama tunavyokumbushwa tena katika Qur-an:
﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّنَ الْبَعْثِ فَإِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ مِن مُّضْغَةٍ مُّخَلَّقَةٍ وَغَيْرِ مُخَلَّقَةٍ لِّنُبَيِّنَ لَكُمْ وَنُقِرُّ فِي الْأَرْحَامِ مَا نَشَاءُ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ثُمَّ نُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْلَا يَعْلَمَ مِن بَعْدِ عِلْمٍ شَيْئًا وَتَرَى الْأَرْضَ هَامِدَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ وَأَنبَتَتْ مِن كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ﴾
Enyi watu! Kama mumo katika shaka juu ya ufufuo, basi (tazameni namna tulivyokuumbeni)! Kwa hakika tulikuumbeni kwa udongo, kisha kwa manii, kisha kuwa kitu chenye kuning'inia, kisha kuwa kipande cha nyama kinachoumbika na kisichoumbika, ili tukubainishieni. Nasi tunakikalisha tumboni tunachokitaka mpaka muda uliowekwa, kisha tunakutoeni kwa hali ya utoto, kisha tunakuleeni mpaka mfikie baleghe yenu.Na kuna wanaokufa (kabla ya kufikia umri huu). Na katika nyinyi kuna wanaorudishwa katika umri dhalili, asijue chochote baada ya kule kujua kwake (22:5)
Aya hizi zinatukumbusha na kututhibitishia kuwa kuumbwa kwa mwanaadam, kukua kwake na kufa kwake hufuata utaratibu madhubuti uliowekwa na Muumba wake bila ya hiari yake.
Vile vile ukizingatia ufanyaji kazi wa mwili wa mwanaadamu utagundua kuwa mwili wa mwanadamu ni mashine ya ajabu inayofanya kazi kwa kufuata utaratibu uliofungamana na sheria madhubuti. Kwa mfano ukichunguza mwili wa mwanaadamu utakuta kuwa kuna mifumo mbali mbali kama vile mfumo wa usagaji chakula (digestion system), mfumo wa hewa (respiratory system), mfumo wa fahamu (nervous system), mfumo wa uzazi (reproduction system) na kadhalika. Mifumo hii hufanya kazi yake kwa kufuata utaratibu na sheria madhubuti nje kabisa ya mkono wa mwanaadamu. Utaona kuwa mwili wa mwanaadamu hufanya kazi yake na kumwezesha mwanaadamu kuwa katika hali ya uzima alionao, kwa kufuata sheria madhubuti za maumbile zilizowekwa na Muumba wake kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:
﴿ فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴾
Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawa sawa - ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu (yaani dini hii ya Kiislamu inaafikiana bara bara na umbile la binaadamu).Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu.Hiyo ndiyo dini ya Haki, lakini watu wengi hawajui. (30:30)
Katika aya hii tunajifunza kuwa mwili wa mwanaadamu hufuata dini ya Allah (s.w), yaani hufuata bara bara utaratibu au sharia madhubuti alizoweka Allah (s.w). Lakini mwanaadamu mwenyewe katika kuendesha maisha yake ya kila siku ana uhuru kamili wa kufuata dini ya Allah (s.w) kwa kufuata kwa ukamilifu na kwa unyenyekevu sharia madhubuti alizoziweka Allah (s.w) katika kukiendea kila kipengele cha maisha (rejea juzuu ya 2 EKP uk. 33 au kufuata dini za watu kwa kufuata utaratibu wa maisha walioufuma watu katika kukiendea kila kipengele) kinyume na utaratibu wa Allah (s.w). Na katika kuutumia uhuru huu,Allah (s.w) anamtanabahisha mwanaadamu.
﴿أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ﴾
Je, wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu na hali kila kilichomo mbinguni na ardhini kinamtii yeye, kipende kisipende?Na kwake watarejeshwa wote. (3:83).
Aya hii inamtanabahisha mwanaadamu ili achukue uamuzi wa busara wa kufuata dini ya Allah (s.w), ambayo dini hiyo ndiyo inayofuatwa na mwili wake na maumbile mengine yote yaliyomzunguka. Ni dhahiri kwamba atakapoamua kufuata dini nyingine yoyote isiyokuwa dini ya mwili wake, atakuwa ameamua kufuata utaratibu wa maisha unaopingana na umbile lake, na matokeo yake ni kukosa furaha na amani, katika maisha au kuishi maisha ya migongano, vurugu na huzuni.
(c) Vipawa vya Mwanaadamu Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine. Mwanaadamu anatofautiana sana na viumbe wengine, hasa katika suala la kufuata utaratibu wa maisha, kutokana na vipawa alivyotunukiwa na Muumba wake ambavyo hatuvioni kwa viumbe wengine. Vipawa hivi ni: -Akili na fahamu ya hali ya juu ambayo humwezesha kuwaza, kufikiri na kutafakari juu ya yeye mwenyewe na mazingira yake.
-Utambuzi wa binafsi (self consciousness) ambao humuwezesha mwanaadamu kufahamu mambo mbali mbali, kutambua mambo na kuyahusisha, kuyachambua, kuyalinganisha, n.k.
-Elimu (uwezo wa kujielimisha na kuelimika) ambayo humuwezesha mwanaadamu kufahamu mambo mbali mbali na kumuwezesha kutenda kwa ufanisi na kuwa na hadhi ya juu kuliko viumbe vyote.
-Huria (uhuru wa kuamua na kutenda atakavyo) - humuwezesha mwanaadamu kufuata utaratibu wa maisha anaoutaka. Vipawa hivi vyote kwa pamoja humtofautisha sana mwanaadamu na viumbe vingine. Humpa uwezo mkubwa na kumfanya auangalie ulimwengu na umbile lake pamoja na vyote vilivyomo kwa mtazamo wenye kutofautiana mno na ule wa viumbe wengine. Kwa mfano, kutokana na utambuzi binafsi (self consciousness) mwanaadam anatambua uhusiano wake na watu wa familia yake. Kuna baba, mama, dada, kaka, mke, watoto na ndugu wengine ambao anapaswa kushirikiana nao mpaka kufa. Hapa lazima mwanaadam aamue mwendo atakaoufuata ili kuwa na uhusiano unaostahiki baina yake na watu hawa.
Pia mwanaadamu ana uhusiano na watu wasio hesabika ulimwenguni, wengine ni majirani zake, wengine marafiki wengine ni maadui zake. Kuna wenye haki juu yake na wako wenye haki zake. Pia mwanaadamu ana uhusiano na viumbe vingine vyenye uhai na visivyo na uhai. Kwa ujumla vyote hivi vipo kwa kumsaidia yeye lakini mwanaadamu anapaswa aamue namna ya kuvitumia kwa manufaa yake yeye mwenyewe na wale wanaomzunguka.
Hivyo, ni dhahiri kuwa ni lazima mwanaadamu awe na njia iliyojenga mwenendo wake juu ya namna atakavyoshirikiana na wanaadamu wenziwe na viumbe vyote vinavyomzunguka kwa sababu katika hali halisi ya maumbile jambo hili la uhusiano haliendeshwi na silka (instinct) kama ilivyo kwa viumbe wengine.
Njia hii inayojenga mwenendo baina yake na mazingira yake ndio dini yake - njia yake ya maisha.
Pia mwanadamu ameumbwa katika namna ambayo hawezi kujitosheleza mwenye.Kwa namna moja au nyingine ni mwenye kuwategemea wanaadam wenziwe na viumbe vingine. Hivyo utaona kwamba mwanaadam hawezi kuishi bila ya kuwa na maingiliano na wanaadamu wenzake, viumbe vingine na mazingira yake yote kwa ujumla. Kutokana na sababu hiyo basi utaona kuwa kila mwanaadamu anafuata utaratibu wa maisha (dini) ambao hujenga uhusiano wa maisha baina yake na mazingira yake.
Suala lingine ni mwanaadamu kuwa na akili ya hali ya juu kuliko viumbe vingine vyote katika ardhi hii. Hatusemi kuwa wanyama hawana akili kabisa lakini sio katika daraja ya juu kama ilivyo akili ya wanaadamu. Kwao wao hitajio muhimu ni silka inayowawezesha kuishi na kuzaana na akili kama wanayo si hitajio kubwa kama lile la silka. Kazi yake ni kuwawezesha kutambua mahitajio yao ambayo ni lazima wayafuate ili waweze kuishi na kuzaana.
Swali ni kwamba; kwa nini mwanaadamu ana akili zaidi kuliko viumbe vingine (wanyama)? Kwa kweli hakuna sababu nyingine isipokuwa ni kumuwezesha mwaanadam kutambua njia ya maisha inayomfahamisha na kumuelekeza kwenye lengo la maisha yake hapa duniani. Mwanaadamu atakapoacha kutumia akili yake kwa kazi hii atakuwa hana tofauti na mnyama katika kuendesha maisha yake ya kila siku na wakati mwingine atakuwa na mwenendo mchafu zaidi kuliko ule wa mnyama kama Qur-an inavyotutanabahisha:
﴿وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ﴾
Na bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannam - wengi katika majini na watu (kwa sababu hii). Nyoyo (akili) wanazo lakini hawafahamu kwazo, macho wanayo lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotofu zaidi. (7:179).
Kwa hiyo, mwanaadamu ana akili ya juu kuliko jamii ya viumbe vingine ili aweze kuamua ni njia gani ya maisha inayostahiki kufuatwa.
Hivyo, kutokana na vipawa alivyonavyo, mwanaadamu hujisaili maswali kama: Nini chanzo cha ulimwengu na nini lengo la kuwepo dunia na uhai wa mwanaadamu na ni vipi mwanadamu aishi ili afikie lengo hili? Maswali haya ni lazima yapatiwe majibu ili maisha yaweze kuwa na maana na muelekeo. Majibu yatakayotolewa ndio yatakayokuwa msingi wa dini ya mwenye kutoa majibu hayo. Kwa mfano kama mtu atatoa jawabu kuwa chanzo cha ulimwengu ni bahati nasibu (chance creation) yaani hauna muumbaji na uhai ikiwa ni pamoja na maisha ya mwanaadamu hauna lengo, basi mtu huyo atayajenga maisha yake juu ya msingi kwamba hakuna Mungu.Hivyo njia yake ya maisha au dini yake itakuwa ya kikafiri.
Kwa ujumla vipawa hivi vya hali ya juu alivyotunukiwa mwanaadamu, kuliko viumbe wengine humlazimisha mwanaadamu kufungika katika mfumo wa maisha ya kijamii katika kuendea kila kipengele cha maisha yake ya kila siku katika uchumi, siasa, utamaduni, na kadhalika. Mfumo huo wa maisha utakuwa ndio dini yake. Kwa mtazamo wa Uislamu tumeona kuwa dini ni utaratibu au mfumo wa maisha anaofuata binaadamu, katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na kijamii. Hivyo kwa vyovyote vile binaadamu katika kuendesha maisha yake ya kila siku atakuwa anafuata dini moja au nyingine. Akifuata mfumo wa maisha aliouweka Mwenyezi Mungu, ambao ni sawa na mfumo wa maisha unaofuatwa na maumbile yote (Qur-an 3:83) atakuwa anafuata Dini ya Kiislamu - dini ya kujisalimisha kwa Allah (s.w) kwa kufuata kanuni na sheria alizoziweka Allah (s.w) katika kukiendea kila kipengele cha maisha. Binaadamu akiamua kufuata mifumo ya maisha iliyojengwa kwa kanuni na sheria zilizowekwa na watu, zinazopingana na kanuni na sheria za Allah (s.w) atakuwa anafuata dini za Kikafiri - Mifumo ya maisha inayopingana na mfumo wa maisha aliouweka Allah (s.w).
Hivyo katika kuishi hapa duniani watu wanagawanyika katika makundi makuu mawili - kundi la Waislamu wanaoufuata mfumo wa maisha aliouweka Allah (s.w) na kundi la Makafiri wanaofuata mifumo ya maisha waliyoibuni watu kama inavyobainika katika Qur-an:
﴿هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ فَمِنكُمْ كَافِرٌ وَمِنكُم مُّؤْمِنٌ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴾
"Yeye ndiye aliyekuumbeni (nyote).Wengine wenu ni Makafiri na wengine wenu ni Waislamu. Na Mwenyezi Mungu anayaona (yote) mnayoyafanya" (64:2)
Kwanini Uislamu Ndio Dini Pekee Inayostahiki Kufuatwa na Watu?
﴿الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ﴾
Hakika dini mbele ya Allah ni Uislamu..." (3:19)
﴿ فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴾
"Basi uelekeze uso wako katika Dini iliyo ya haki kabla ya kufika hiyo siku isiyozuilika, inayotoka kwa Mwenyezi Mungu; siku hiyo watatengana (Waumini wende Peponi na Makafiri wende Motoni)." (30:43)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa pamoja na kuwepo dini nyingi (mifumo mingi ya maisha) hapa ulimwenguni dini ya Haki anayoiridhia Allah (s.w) ni Uislamu. Hivyo Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kufuatwa na watu kwa sababu zifuatazo:
Kwanza : ndio dini ya kweli na ya uhakika kwa sababu imefumwa na Allah (s.w) aliye mjuzi wa kila kitu. Allah (s.w) ndiye aliyemuumba binaadamu kwa lengo maalumu, na hivyo ndiye pekee anayestahiki kumuwekea utaratibu wa maisha utakaomuwezesha kufikia lengo la kuumbwa kwake kwa wepesi. Tunakumbushwa katika Qur-an:
﴿سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى ﴿١﴾ الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٢﴾ وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ﴾
"Litukuze jina la Mola wako aliye Mtukufu.Aliyeumba (kila kitu na) kukitengeneza na akakikadiria (kila kimoja lengo lake) na akakiongoza (kufikia lengo hilo)." (87:1-3)
Dini nyingine zote wanazofuata watu ni dini za upotofu kwa sababu zinabuniwa na wanaadamu wasio na ujuzi wala uwezo wa kazi hiyo. Mifumo yao ya maisha imefumwa kwa dhana wakiongozwa na matashi ya nafsi zao. Tujihadhari na wazushi hawa wa dini kama Allah (s.w) anavyotuasa:
﴿وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ﴾
"Na kama ukiwatii wengi katika (hawa) waliomo ulimwenguni watakupoteza na njia ya Mwenyezi Mungu. Hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kuzua (tu basi)." (6:116)
Pili : Uislamu ndio mfumo wa maisha pekee unaolandana na umbile la binaadamu na maumbile yote yaliyomzunguka. Yaani kanuni na sheria zilizowekwa na Uislamu zinakwenda sambamba na kanuni na sheria zinazofuatwa na maumbile yote, kwani mtunzi wake ni yule yule mmoja, Allah (s.w). Ni kwa msingi huu, Allah (s.w) anatanabahisha watu:
﴿أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ﴾
"Je, (watu) wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu na hali kila kilichomo mbinguni na ardhini kimejisalimisha kwake kipende kisipende?..." (3:83)
﴿فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴾
"Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawa sawa ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu.Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu.Hiyo ndio dini iliyo ya Haki lakini watu wengi hawajui." (30:30).
Hivyo kwa kuwa Uislamu ni dini ya maumbile, ndio pekee inayoweza kuiongoza jamii kwa uadilifu na kuleta furaha na amani ya kweli.
Tatu : ndio dini pekee inayofuatwa na walimwengu wote wa sehemu zote na wa nyakati zote. Mitume wote wa Mwenyezi Mungu kuanzia Adam(a.s) mpaka kuishia kwa Muhammad(s.a.w.w) , wamefundisha na kufuata dini moja- Uislamu-kama tunavyokumbushwa katika aya zifuatazo:
﴿شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ﴾
"Amekupeni sheria ya dini ile ile aliyomuusia Nuhu, na Tuliyokufunulia wewe na Tuliyowausia Ibrahim na Mussa na Issa, kwamba simamisheni dini (Uislamu) wala msifarikiane kwayo..." (42:13)
﴿وَجَاهِدُوا فِي اللَّـهِ حَقَّ جِهَادِهِ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَـٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ﴾
"Na ipiganieni dini ya Mwenyezi Mungu kama inavyostahiki (kupiganiwa).Yeye amekuchagueni (muwe umma ulio bora). Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika dini.(Nayo dini hii) ni mila ya baba yenu Ibrahimu; yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu (katika vitabu vya zamani) huko; na katika (Qur-an) hii pia (mumeitwa jina hilo) ili awe Mtume shahidi juu yenu na nyinyi muwe mashahidi juu ya watu (waliotangulia)..." (22:78).
Pia Uislamu ni dini isiyoruhusu ubaguzi wa aina yoyote kama tunavyokumbushwa katika aya ifuatayo:
﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ﴾
"Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja, Adam) na (yule yule) mwanamke (mmoja, Hawwa). Na tumekufanyieni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane (tu basi). Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari (za mambo yote)." (49:13)
Nne : Uislamu ni utaratibu wa maisha uliokamilika.Uislamu unamuelekeza binaadamu namna ya kuendesha kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na ya kijamii. Uislamu umeweka utaratibu unaozingatia watu kama walivyo. Kwa kutambua kuwa mtu anakamilika kwa kuwa na mwili na roho, Uislamu umeweka utaratibu wa kuustawisha mwili na roho. Uislamu umetuwekea kanuni na sheria zinazotuwezesha kujenga afya zetu na kukuza utu (ucha Mungu) wetu.
Pia, kwa kutambua kuwa watu ni viumbe wanaotakiwa waishi kijamii (social beings) na kutegemeana, Uislamu umetoa mwongozo na kuweka kanuni na sheria ambazo humuwezesha kila mtu binafsi na jamii kwa ujumla kuishi maisha ya furaha na amani. Uislamu umeweka mifumo ya kijamii kama vile siasa, uchumi, utamaduni, na kadhalika juu ya misingi ya haki na Uadilifu.
Tano : ni dini pekee inayomuongoza binaadamu namna ya kumiliki hisia zake.Uislamu unatuelekeza, tufanyeje tunapokuwa katika furaha kubwa. Kwa mfano Uislamu unatuelekeza kuwa tunapokuwa na sherehe, tule na kunywa vilivyo vizuri na halali lakini tusifanye israfu na tumtaje na kumsifu Allah (s.w) kwa wingi.
Pia Uislamu unatuelekeza la kufanya pindi tunapofikwa na jambo la kutuhuzunisha sana. Kwa mfano, Uislamu unatuelekeza kuwa tunapofikwa na msiba wa aina yoyote, tusubiri na tuone kuwa,hilo lililotokea ni katika Qadar ya Allah (s.w), kama tunavyokumbushwa katika aya zifuatazo:
﴿وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴾
"Na Tutakutieni katika msuko suko wa hofu na njaa na upungufu wa mali na wa watu na wa matunda. Na wapashe habari njema wanaosubiri.Ambao uwapatapo msiba husema: Hakika Sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea".( 2:155- 156)
﴿مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٢٢﴾ لِّكَيْلَا تَأْسَوْا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا تَفْرَحُوا بِمَا آتَاكُمْ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ﴾
"Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujaumba.Kwa yakini hilo ni sahali kwa Mwenyezi Mungu.Ili msihuzunike sana juu ya kitu kilichokupoteeni, wala msifurahi sana kwa alichokupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye, ajifaharishaye" (57:22-23)
Sita : Uislamu ni dini ya haki kama inavyobainika katika Qur-an:
﴿هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴾
"Yeye (Allah (s.w) ndiye aliyemleta Mtume wake kwa uongofu na dini ya haki ili aijaalie (dini hii) kushinda dini zote ijapokuwa watachukia washirikina" (9:33)
Dini ya haki hapa ina maana kuu mbili;
Maana ya kwanza : ni kuwa Uislamu ni dini ya Allah (s.w), mjuzi na mwenye Hikima. Allah (s.w) ndiye anayestahiki kuwaundia binaadamu dini kwa kuwa ndiye aliyewaumba kwa lengo maalumu na kwa hiyo ndiye mwenye haki pekee ya kuwawekea wanaadamu utaratibu wa maisha na kuuambatanisha na mwongozo utakaowawezesha kufikia kwa ufanisi lengo hilo.
Maana ya pili : ni kuwa Uislamu ni dini ya kusimamia haki za binaadamu katika jamii kwa uadilifu kuliko dini yoyote ile. Mitume na Vitabu vya Allah (s.w) vimeshushwa ili kuwafundisha watu uadilifu na kuwaamuru wasimamishe uadilifu kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
﴿لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ وَأَنزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ﴾
"Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukaviteremsha vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu. Na tumekiteremsha (tumekiumba) chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu ajulishe anayemnusuru na Mitume yake na hali ya kuwa hawamuoni Mwenyezi Mungu.Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu mwenye kushinda" (57:25).
Katika aya hii tunajifunza kuwa silaha zinatokana na chuma na aina nyingine za madini, nani zana zinazotakaiwa zitumiwe na waumini ili kusimamisha haki na uadilifu katika jamii. Katika aya nyingi za Qur-an waumini wa Kiislamu wameamrishwa kupigana na madhalimu ili kuhakikisha haki inapatikana katika jamii kwa kila raia kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
﴿فَلْيُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يَشْرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ وَمَن يُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيُقْتَلْ أَوْ يَغْلِبْ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٧٤﴾وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا﴾
Basi nawapigane katika njia ya Mwenyezi Mungu wale wanaouza maisha (yao) ya dunia kwa (kununua) ya Akhera.Na anayepigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kisha akauawa au akashinda, tutampa ujira mkuu). Na mna nini hampigani katika njia ya Mwenyezi Mungu na (katika kuwaokoa) wale walio dhaifu - katika wanaume na wanawake na watoto - ambao husema: "Mola wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie tuwe tuna mlinzi anaetoka kwako." (4:74-75).
Wale walioamini wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, lakini waliokufuru wanapigana katika njia ya (Twaghuut).
﴿فَقَاتِلُوا أَوْلِيَاءَ الشَّيْطَانِ إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا﴾
Basi piganeni na marafiki wa Shetani. Hakika hila za Shetani ni dhaifu. (4:76).
Saba : Uislamu ni mfumo wa maisha pekee ulioweka utaratibu wa kumbakisha binaadamu katika maadili ya utu. Uislamu umemuwekea binaadamu ibada maalumu zenye lengo la kumtakasa na kumuwezesha kuwa na maadili mema yatakayopelekea kujenga mazingira ya furaha na amani katika jamii. Ibada hizi maalumu ni Swala, Zakat, Saum, Hija, n.k. Namna ibada hizi zinavyofanya kazi katika kumbakisha binaadamu katika maadili ya utu imefafanuliwa vyema katika kitabu cha pili (Nguzo za Uislamu).
Sababu hizi tano za msingi, zatosha kuwa vigezo vya kumfanya mtu achague Uislamu kuwa utaratibu pekee wa maisha wa kufuata katika kuendea kila kipengele cha maisha yake. Dini zote zilizoundwa na watu, zimekosa kabisa sifa hizi na ni zenye kumhasirisha binaadamu katika maisha ya dunia na akhera.Na hata mazingira yetu yanathibisha hili.
﴿وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴾
"Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake.Naye akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa) (3:85)
ZOEZI
2 1. (a) Maana ya dini kwa mtazamo wa Makafiri ni.............................
(b) Maana ya dini kwa mtazamo wa Uislamu ni............................
2. Katika kuishi hapa duniani watu wamegawanyika makundi makubwa mawili:
(i).............................
(ii).................................................
3. Kwa mtazamo wa Uislamu hakuna mtu anayeishi bila ya kufuata dini moja au nyingine kwa sababu: .....................................
4. Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kufuatwa na watu kwa sababu tano zifuatazo: (i)...................................
(ii)....................................
(iii)....................................
(iv)...................................
(v)...................................
(vi)...................................
(vii)..................................
5. Kwanini Mwanadamu hawezi kuunda mfumo wa maisha utakao watendea haki na uadilifu walimwengu wote?
3
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
SURA YA TATU
IMANI YA KIISLAMU
MAANA YA IMANI IMANI
Imani ni neno la Kiarabu lenye maana ya kuwa na yakini au kuwa na uhakika moyoni juu ya kuwepo kitu au jambo fulani lisiloonekana machoni lakini kuna dalili za kuthibisha kuwepo kwake. Hivyo ili mtu awe na imani juu ya jambo lolote lile asiloweza kuliona, hanabudi kuwa na ujuzi wa kina utakaompa hoja au dalili za kutosha zitakazomkinaisha moyoni juu ya kuwepo jambo hilo.
NANI MUUMINI?
Imani ni kitu cha moyoni kisichoonekana lakini dalili za Muumini huonekana kwenye matendo. Katika Uislamu mtu hatakuwa Muumini kwa kudai tu bali uumini wake utaonekana katika matendo yake. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa:
﴿وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ﴾
"Na katika watu wako wasemao, 'tumemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na hali ya kuwa wao si wenye kuamini."( 2:8).
Si wenye kuamini kwa sababu hawajaingiza imani yao katika matendo, bali wamebakia kwenye kudai tu kuwa wao ni waumini pengine kwa kujiita majina au kuchagua kufanya vitendo fulani fulani tu.Muumini wa kweli ni yule atakayethibitisha imani yake katika mwenendo na matendo yake ya kila siku.
﴿إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ ﴿٢﴾ الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا لَّهُمْ دَرَجَاتٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ﴾
"Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa hofu, na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi).Ambao husimamisha swala na wanatoa katika yale tuliyowapa.Hao ndio wanaoamini kweli kweli, wao wana vyeo (vikubwa) kwa Mola wao, na msamaha na riziki bora kabisa". (8:2-4).
﴿إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ﴾
"Wenye kuamini kweli kweli ni wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kisha wakawa si wenye shaka na wanaopigania dini ya Allah kwa mali zao na nafsi zao.Hao ndio wenye kuamini kweli kweli" (49:15).
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa waumini wa kweli ni wale wenye sifa zifuatazo:
(i) Wana yakini kuwa Allah (s.w) yupo Waumini wa kweli huwa na yakini nyoyoni mwao juu ya kuwepo Allah (s.w) na Mtume wake. Yaani wanashuhudia kwa dhati nyoyoni mwao kuwa Allah (s.w) ni Mola wao pekee na Muhammad(s.a.w.w) ni Mtume wake wa mwisho na katika matendo yao yote huishi kwa kufuata mwongozo wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na daima hukumbuka msisitizo wa aya ifuatazo:
﴿وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا﴾
"Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini,Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi (kabisa)." (33:36)
(ii) Humcha Allah (s.w) kwa kutekeleza amri zake Anapotajwa Mwenyezi Mungu au wanapokumbushwa juu ya maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu, nyoyo zao hunyenyekea na kufuata kama walivyokumbushwa. Hufanya hivyo kwa kuhofu ghadhabu za Mwenyezi Mungu na kutarajia radhi zake.
(iii) Huongezeka imani yao kwa kusoma na kufuata Quran Wanaposoma aya za Mwenyezi Mungu huwazidishia imani. Kwa maana nyingine, waumini wa kweli hufuata mwongozo wa Allah (s.w) katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Hawako tayari kufanya jambo lolote kinyume na mwongozo wa Allah (s.w).
(iv) Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu. Wanamsimamo thabiti na hawayumbishwi na yeyote katika kutekeleza wajibu wao kwa Mola wao. Wana yakini kuwa aliyenusuriwa na Allah (s.w) hakuna wa kumdhuru na aliyeandikiwa kupata dhara na Allah (s.w) hakuna wa kumnusuru.
(v) Husimamisha swala Husimamisha swala katika maisha yao yote. Huswali swala tano kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa, na kwa hiyo hufikia lengo la swala kwa kutojihusisha kabisa na mambo machafu na maovu. Na zaidi huamrisha mema na kukataza maovu katika jamii.
(vi) Husaidia wenye matatizo katika jamii Huwa wepesi wa kutoa msaada kwa hali na mali kwa wanaadamu wenziwe wanaohitajia msaada.
(vii) Hufanya biashara na Allah (s.w) Wanafanya jitihada za makusudi kwa kutumia mali zao na kujitoa muhanga nafsi zao ili kuhakikisha kuwa dini ya Allah inasimama katika jamii. Yaani wanajitahidi kwa jitihada zao zote ili kuzifanya sharia za Allah (s.w) ziwe ndizo zinazotawala harakati zote za maisha ya jamii.
Pia sifa za Waumini zinabainishwa katika Suratul- Muuminuun kama aya zifuatavyo:
﴿قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١﴾ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ ﴿٢﴾ وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ ﴿٣﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَاةِ فَاعِلُونَ ﴿٤﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿٥﴾ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿٦﴾ فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿٧﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ ﴿٨﴾ وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٩﴾ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ ﴿١٠﴾ الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾
Hakika wamefuzu Waumini ambao katika swala zao huwa wanyenyekevu.Na ambao hujiepusha na Lagh-wi (mambo ya upuuzi). Na ambao Zaka wanaitekeleza.Na ambao tupu zao wanazihifadhi isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale iliyomiliki mikono yao ya kuume.Basi hao ndio wasiolaumiwa.Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka. Na ambao amana zao na ahadi zao wanaziangalia.Na ambao swala zao wanazihifadhi.Hao ndio warithi.Ambao watarithi Firdaus (Pepo ya daraja ya juu) wakae humo milele. (23:1-11)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa waumini wa kweli waliofuzu na watakaostahiki kupata pepo ya Firdaus, ya daraja ya juu kabisa ni wale wanaojipamba na sifa zifuatazo:
(viii) Wenye khushui katika swala Waumini wa kweli waliofuzu huwa na khushui (unyenyekevu) katika swala. Yaani huswali kwa kutulizana kimwili, kimoyo,kiroho na kifikra, huku wakizingatia yale wayasemayo mbele ya Mola wao wakiwa na yakini kuwa anawaona na anawasikia.
(ix) Wenye kuhifadhi swala Waumini wa kweli waliofuzu huhifadhi swala kwa kutekeleza kwa ukamilifu shuruti zote za swala nguzo zote za swala na huswali kama alivyoswali Mtume(s.a.w.w) na hudumu na swala katika maisha yao yote: Rejea Qur-an (70:23).
Zingatio :
Swala husimama kwa kuhifadhiwa na kuswaliwa kwa khushui na kudumu na swala katika maisha yote.
(x) Wenye kuepuka lagh-wi Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi. Laghwi ni mambo ya upuuzi yanayomsahaulisha mtu kumkumbuka Mola wake, yanayosababisha ugomvi au bughudha baina ya watu na yanayomsahaulisha mtu kusimamisha swala: Rejea Qur-an (5:91).
Mahala ambapo Allah (s.w) hakumbukwi, shetani huchukua nafasi. Michezo yote ni lagh-wi, isipokuwa ile tu inayochezwa kwa kuchunga mipaka yote ya Allah (s.w) kwa lengo la kukuza ukakamavu na siha.
(xi) Hutoa Zakat na Sadakat Waumini wa kweli waliofuzu hutoa Zakat wakiwa na mali na hutoa misaada na huduma waziwezazo kwa wanaadamu wenziwe kwa kadiri ya haja ilivyojitokeza.Asiyejali kuwasaidia binaadamu wenziwe, huku ana uwezo si Muumini. Rejea Qur-an (107:1-7).
(xii) Huepuka zinaa na tabia za kizinifu Waumini wa kweli waliofuzu hujihifadhi na zinaa au hujiepusha kufanya jimai nje ya mipaka aliyoiweka Allah (s.w). Hatua ya kwanza ya kujilinda na zinaa ni kujiepusha na vishawishi vyote vinavyokurubisha watu kwenye zinaa. Muumini wa kweli hutekeleza pasina kusita ile amri ya Allah (s.w) ya katazo kuwa:
﴿وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَىٰ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا﴾
Wala usiikaribie zinaa; kwa hakika huo ni uchafu na ni njia mbaya kabisa (17:32)
(xiii) Huwa muaminifu Waumini wa kweli waliofuzu huchunga amana. Hutunza amana aliyopewa na kuirejesha au kuitumia kwa mujibu wa maelekezo ya mwenyewe. Amana kuu aliyopewa mwanaadamu na Mola wake ni kule kufadhilishwa kwake kuliko viumbe vingine vyote ili asimamishe Ukhalifa (utawala wa Allah) katika ardhi kama tunavyokumbushwa katika Qur-an:
﴿إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَن يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنسَانُ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا﴾
"Kwa yakini Sisi Tulidhihirisha amana kwa mbingu, ardhi na milima,vikakataa kuichukua na vikaiogopa,lakini mwanaadamu aliichukua. Bila shaka yeye ni dhalimu mkubwa, mjinga sana" (33:72)
(xiv) Wenye kutekeleza ahadi Hutekeleza ahadi zao wanapoahidiana na wanaadamu wenziwao maadamu ni katika mipaka ya Allah (s.w). Ahadi kubwa wanayotoa Waislamu mbele ya Allah (s.w) ni shahada; pale wanapo ahidi kuwa hawatamshirikisha Allah (s.w) na chochote na kwamba wataishi maisha yao yote kwa kufuata mwongozo wa Allah (s.w) kupitia kwa Mtume wake, Muhammad(s.a.w.w) . Rejea (6: 162 -163) Katika Suratul-Fur-qaan sifa za Waumini zinabainishwa tena kama ifuatavyo:
﴿وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾ وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا ﴿٦٤﴾ وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿٦٥﴾ إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿٦٦﴾ وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًاوَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا ﴿٦٨﴾ يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا ﴿٦٩﴾ إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا﴿٧٠﴾ وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا ﴿٧١﴾ وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا بِاللَّغْوِ مَرُّوا كِرَامًا ﴿٧٢﴾ وَالَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَمْ يَخِرُّوا عَلَيْهَا صُمًّا وَعُمْيَانًا ﴿٧٣﴾ وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾ أُولَـٰئِكَ يُجْزَوْنَ الْغُرْفَةَ بِمَا صَبَرُوا وَيُلَقَّوْنَ فِيهَا تَحِيَّةً وَسَلَامًا ﴿٧٥﴾ خَالِدِينَ فِيهَا حَسُنَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا﴾
"Na waja wa Rahmaan; Ni wale wanaokwenda ulimwenguni kwa unyenyekevu; na wajinga wakisema nao (maneno mabaya) huwajibu (maneno ya) salama. Na wale wanaopitisha baadhi ya saa za usiku kwa ajili ya Mola wao kwa kusujudu na kusimama. Na wale wanaosema:"Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea, Hakika hiyo (Jahannamu) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa".Na wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo .Na wale wasiomuomba mungu mwingine pamoja na Allah, wala hawaui nafsi aliyoiharamisha Allah ila kwa haki, wala hawazini; na atakayefanya hayo atapata madhara (papa hapa ulimwenguni). Na atazidishiwa adhabu siku ya Kiyama na atakaa humo kwa kufedheheka milele. Ila yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri, basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.Na aliyetubia na kufanya wema, basi kwa hakika yeye anatubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu. Na wale ambao hawashuhudii shahada za uwongo, na wanapopita penye upuuzi, hupita kwa hishima (yao). Na wale ambao wanapokumbushwa aya za Mola wao hawaziangukii kwa uziwi na upofu. Na wale wanaosema: "Mola wetu! Tupe katika wake zetu na wototo wetu yaburudishayo macho (yetu) (nyoyo zetu), na Utujaalie kuwa waongozi kwa wamchao (Mungu). Hao ndio watakaolipwa ghorofa (za Peponi) kwa kuwa walisubiri, na watakuta humo hishima na amani. Wakae humo milele; kituo kizuri na mahali pazuri (kabisa pa kukaa.) (25:63-76).
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa sifa za Waumini ambao hapa wameitwa "Waja wa Rahman" ni pamoja na:
(xv) Kuishi na watu kwa wema Waumini wa kweli huishi na watu wema kwa kuwathamini na kuwaheshimu; kujizuia na kuwafanyia watu kibri, kujizuia na kujikweza na kujitukuza mbele ya wengine, kujizuia na kuwadhalilisha watu na kuwavunjia heshima.
(xvi) Huepuka ugomvi na mabishano Waumini wa kweli huepuka kabisa tabia ya ugomvi na mabishano. Waumini hufahamu fika kuwa kwenye ugomvi na mabishano shetani huwepo na huchochea faraka baina ya ndugu. (xvii) Hudumu katika kuswali Tahajjud Kuamka usiku na kuswali swala ya "Tahajjud"(kisimamo cha usiku) kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah (s.w) na Rehema zake. Swala hii huswaliwa usiku wa manane hususan katika theluthi ya mwisho ya usiku inayokaribiana na Al-fajiri.
(xviii) Huogopa adhabu ya Allah(s.w) Waumini wa kweli huogopa adhabu ya Allah (s.w) aliyowaandalia watu waovu huko akhera kwa kujitahidi kutenda mema na kujiepusha na maovu na kila mara kuomba:
﴿ وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا﴿٦٥﴾ إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا﴾
"Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea.Hakika hiyo (Jahannamu) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa"(25:65-66).
(xix) Hutumia neema kwa insafu Waumini wa kweli hutumia neema walizopewa na Allah kwa insafu. Hawafanyi ubadhirifu au israfu wa neema kama vile kutumia vibaya mali, wakati, vipaji na ujuzi. Waumini daima huzingatia kuwa Allah hawapendi waja wanaofuja neema alizowatunukia. Mubadhirina ni watu wanaofuja neema walizotunukiwa na Allah (s.w). Wasiotumia neema kwa insafu, ni wafuasi wa shetani. Quran inasema:
﴿وَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرْ تَبْذِيرًا ﴿٢٦﴾ إِنَّ الْمُبَذِّرِينَ كَانُوا إِخْوَانَ الشَّيَاطِينِ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِرَبِّهِ كَفُورًا﴾
"Na wape jamaa wa karibu haki zao,na mayatima (vilevile) na masikini, wala usifanye ubadhirifu. Hakika wafanyao ubadhirifu ni marafiki wa shetani, na shetani ni mwenye kumkufuru Mola wake" (17:26-27).
(xx) Hawamshirikishi Allah (s.w) Waumini wa kweli hawamshirikishi Allah(s.w). Hujiepusha na aina zote za shirk- shirk katika dhati, shirk katika sifa, shirk katika hukumu na shirk katika mamlaka ya Allah(sw). Kufanya shirk ni dhambi kubwa ya daraja la kwanza. Quran inaonya na kutahadharisha kuwa:
﴿إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا﴾
"Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi (dhambi ya) kushirikishwa na kitu na husame yasiyokuwa haya kwa amtakaye. Na anayemshirikisha Allah bila shaka amebuni dhambi kubwa" (4:48)
(xxi) Hulinda na kutetea haki uhai wa nafsi Waumini wa kweli hulinda na kutetea haki ya uhai wa kila nafsi yenye haki ya kuishi. Hivyo, kwa namna yeyote ile ya kisheria, hujitahidi kujiepusha na ushiriki wa kusababisha au kufanya mauwaji ya nafsi ambayo kwa mujibu wa mwongozo wa Allah hustahiki kuishi. Ulinzi na utetezi huu wa haki ya uhai wa nafsi unatokana na mwongozo wa Allah katika Quran kuwa:
﴿مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ﴾
Mwenye kuiuwa nafsi pasina nafsi (hiyo iliyouliwa kuuwa) au kufanya fisadi katika ardhi,huyo itakuwa kana kwamba ameuwa watu wote. Na atakayeilinda nafsi hiyo, huyo atakuwa kana kwamba amelinda uhai wa watu wote (5:32).
(xxii) Hawafanyi uzinzi Waumini wa kweli hawaikaribii zinaa wala kufanya uzinifu. Na zaidi hawashawishi wala kushiriki kwa namna yoyote ile katika mambo yanayosababisha zinaa kufanyika.
﴿وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَىٰ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا﴾
"Wala usikaribie zinaa.Hakika hiyo ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa)." (17:32).
(xxiii) Husema kweli daima Waumini wa kweli husema kweli daima. Hawatowi ushahidi wa uongo au kutetea batili. Wanapowajibika kutoa ushahidi juu ya jambo, husema ukweli hata kama ni dhidi ya nafsi zao wenyewe au watu wao wa karibu.(rej 4:135, 5:8).
(xxiv) Hawavutiwi na mambo ya kipuuzi Waumini wa kweli ni wale ambao hawavutiwi na mambo ya kipuuzi ambayo wafuasi wa ibilisi huyatumia katika kuwavuta watu kwa lengo la kuwapumbaza na kuwateka akili zao. Muumini huwa hana muda wa kupoteza au fursa ya kuikabidhi akili yake kwa twaghuti aichezee. Hivyo, kwenye mambo ya kipuuzi waumini hupita haraka kwa heshima zao, na ikibidi kuweka jambo m-badala lenye maana na manufaa kwa jamii.
(xxv) Humwitikia Allah(s.w) anapowaita Waumini wa kweli humwitikia Allah (s.w) anapowaita kwa makatazo na maamrisho yake katika Quran. Hivyo hutii kwa unyenyekevu maagizo ya Allah (s.w) kila wanapokumbushwa kwa kusomewa au kusoma wenyewe aya za Kitabu cha Allah (s.w). na Allah (s.w) ananadi katika Quran kuwa:
﴿وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ﴾
Na waja wangu wanapokuuliza kuhusu mimi, basi (waambie) hakika Mimi nipo karibu najibu maombi ya mwombaji pindi anaponiomba. Basi na waniitike na waniamini Mimi ili wapate kuongoka (2:186).
(xxvi) Hujenga familia za kiislamu Waumini hujitahidi kujenga familia za kiislamu kwa kumuongoza mke na kuwalea watoto na wale wote walio chini ya mamlaka yake katika mipaka ya Ucha-Mungu kwa kuwaamrisha kutenda mema na kuwakataza maovu. Pamoja na jitihada hiyo huomba msaada wa Allah kwa kuleta dua ifuatayo:
﴿وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا﴾
"Mola wetu! Tupe katika wake zetu na wototo wetu yaburudishayo macho (yetu) (nyoyo zetu), na Utujaalie kuwa Viongozi kwa wamchao (Mungu). (25:74)
Kwa ujumla waumini wa kweli ni wale wanaojipamba na tabia njema kama iliyoelekezwa katika Qur-an na Sunnah.
ZOEZI
3: 1. Imani ni.................................................................................
2. Pamoja na kudai kwao kuwa ni waumini Allah (s.w) anawakatalia.
"Na katika watu wako wasemao, "Tumemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na hali ya kuwa wao si wenye kuamini ..." (2:8)
Allah (s.w) anawakatalia kwa sababu.................................................
3. Orodhesha sifa za waumini wa kweli kama zilivyoainishwa katika Qur-an (8:2-4) na (49:15).
4. Orodhesha sifa za waumini kama zilivyo ainishwa katika aya zifuatazo:
(a) Suratul-Muuminuun (23:1-11)
(b) Suratul-Furqaan (25:63-76)
5. Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita. Zitaje zote. Kwa mpangilio.
4
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa; Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:
1 Kumuamini Allah (s.w)
2 Kuamini Malaika wake
3 Kuamini Vitabu vyake
4 Kuamini Mitume wake
5 Kuamini Siku ya mwisho
6 Kuamini Qadar yake
Hawi Muumini wa Kiislam yule ambaye amekanusha angalau moja ya nguzo hizi kama inavyobainika katika Qur-an:
﴿وَمَن يَكْفُرْ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا﴾
"... Na mwenye kumkanusha Allah (s.w) na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho. basi bila shaka amepotea upotofu ulio mbali (kabisa)" (4:136)
Mtu hatakuwa Muumini kwa kutamka tu hizi nguzo sita, bali pale atakapozijua kwa undani na kuendesha maisha yake yote kwa misingi ya nguzo hizi.
Tunazifahamu nguzo hizi sita kutokana na Hadith ya Mtume (s.a.w) iliyosimuliwa na Umar (r.a) kama ifuatavyo: Siku moja tulipokuwa tumeketi pamoja na Mtume(s.a.w.w) alitutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe kama theluji na nywele zake nyeusi sana, hakuwa na dalili zozote za msafiri, ingawa alikuwa mgeni kwetu sote. Halafu alikaa mbele ya Mtume(s.a.w.w) hali magoti yake yakikabiliana na yale ya Mtume na akaweka mikono yake katika mapaja ya Mtume na akasema:"Ewe Muhammad nifahamishe juu ya Uislamu" na Mtume akasema ;
"Ni kushuhudia ya kuwa hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah, Kusimamisha swalaa, kutoa Zakat, Kufunga Mwezi wa Ramadhani, Kuhiji Makkat kwa mwenye kuweza"
Halafu yule mgeni akasema "umesema kweli".
Tukastaajabu kwa nini aliuliza halafu akasadikisha. Halafu akasema; "Nifahamishe juu ya Iman".
Mtume akasema :
"Ni kumuamini Mwenyezimungu na, Malaika wake , Vitabu vyake, Mitume wake, Siku ya Mwisho na Qadar, Kheri na shari yake . Kisha akasema nifahamishe juu ya Ihsaan" Akasema"Ni Kumuabudu Allah kama kwamba unamuona, ikiwa wewe humuoni yeye anakuona" Halafu akasema nifahamishe juu ya Kiyama" Akasema:"Hajui mwenye kuulizwa juu ya hilo zaidi ya mwenye kuuliza. Akasema: Nifahamishe dalili zake. Mtume akasema: "sNi wakati ambapo mjakazi atamzaa bibi yake, na utakapowaona wachungaji masikini wanaposhindana kujenga maghorofa. "Yule mgeni alipoondoka, Mtume alikaa kimya kwa muda kisha akasema: "eweUmar, unamfahamu muulizaji?' Sote tukamjibu kuwa Allah na Mtume wake wanajua zaidi. Mtume akasema"Huyo ni Jibriil amekuja kuwafundisheni dini yenu" (MUSLIM)
KUMUAMINI ALLAH ( S.W )
Nafasi ya akili katika kumtambua Allah (s.w) Imani ya kweli juu ya Allah (s.w) itathibitika moyoni baada ya kumjua vyema Allah (s.w) na sifa zake zote tukufu. Allah (s.w) hatumuoni kwa macho bali tunamfahamu kwa akili zetu katika kuchunguza dalili mbali mbali zilizotuzunguka. Tunavyojifunza katika Qur-an, matumizi ya kwanza ya akili tulizotunukiwa ni kuyakinisha kuwepo kwa Allah (s.w) na sifa zake. Msisitizo wa matumizi ya akili na fikra zetu katika kazi hii ya kumjua Allah (s.w) na sifa zake tukufu unabainishwa katika aya zifuatazo:
﴿إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ﴾
"Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana ziko hoja (za kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu-Allah) kwa wenye akili" (3:190)
﴿وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١﴾ وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْعَالِمِينَ ﴿٢٢﴾ وَمِنْ آيَاتِهِ مَنَامُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَابْتِغَاؤُكُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ﴿٢٣﴾ وَمِنْ آيَاتِهِ يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَيُحْيِي بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴾
"Na katika ishara zake,(za kuthibitisha kuwepo kwake na uweza wake) ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kutoka kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofahamu.Na katika ishara zake (za kuonyesha uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu na (mengine yenu na hali ya kuwa muumbaji ndiye huyo huyo mmoja). Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi. Na katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na (kuamka) mchana, na kutafuta kwenu fadhila yake. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanaosikia.Na katika ishara zake ni kukuonyesheni umeme kwa (kukutieni) hofu na tamaa (ya kuja mvua), na kuyateremsha (hayo) maji kutoka mawinguni. Kwayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake.Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofahamu" (30:21-24)
Aya hizi chache zatosha kuonesha msisitizo wa Qur-an juu ya kutumia akili na fikara zetu katika kumfahamu vyema Allah (s.w). Kila mtu atakavyozama katika utafiti wa mazingira katika fani yoyote ile ndivyo atakavyoweza kumuona Allah (s.w) na utukufu wake kwa upeo mkubwa zaidi. Allah (s.w) mwenyewe anathibitisha hilo katika aya zifuatazo:
﴿أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ ثَمَرَاتٍ مُّخْتَلِفًا أَلْوَانُهَا وَمِنَ الْجِبَالِ جُدَدٌ بِيضٌ وَحُمْرٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهَا وَغَرَابِيبُ سُودٌ ﴿٢٧﴾ وَمِنَ النَّاسِ وَالدَّوَابِّ وَالْأَنْعَامِ مُخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ كَذَٰلِكَ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ﴾
"Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu Ameteremsha maji mawinguni! Na kwayo Tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali.Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana.Na katika watu na wanyama wanaotambaa na wanyama (wengine), pia rangi zao ni mbali mbali, kwa hakika wanaomcha Allah miongoni mwa waja Wake ni wale wataalamu (wanazuoni): Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu, Msamehevu" (35:27-28)
Wataalamu (wanazuoni) kwa mnasaba wa aya hizi si wale waliobobea kwenye fani ya fiq-h tu na nyinginezo zinazoitwa za "dini" bali ni pamoja na wale walio zama kwenye fani mbali mbali za elimu ya mazingira. Kwa mujibu wa aya hizi, wataalamu waliopigiwa mfano ni wale waliobobea katika taaluma ya hali ya hewa (meteorologists), katika taaluma ya madini (Geologists), katika taaluma ya matunda (horticulturist), katika taaluma ya wanyama (Zoologist) na katika taaluma ya watu na tabia zao (anthropologists).
Wale ambao hawatumii vipawa vyao vya akili katika kumfahamu Mola wao kutokana na mazingira wamefananishwa na wanyama, kama tunavyojifunza katika Qur-an:
﴿وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ﴾
"Na bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannam wengi katika majini na watu (kwa sababu hii) Nyoyo (akili) wanazo, lakini hawafahamu kwazo, macho wanayo lakini hawaoni kwayo na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika" (7:179)
﴿إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِندَ اللَّـهِ الصُّمُّ الْبُكْمُ الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ﴾
"Hakika vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni hawa wanaojipa uziwi na ububu ambao hawayatii akilini (wanayoambiwa au wanayoyaona)" (8:22).
Vilevile Alla(s.w) anawashutumu wale wanaobishana kuhusu Yeye pasina kuwa na elimu.
﴿أَلَمْ تَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَسْبَغَ عَلَيْكُمْ نِعَمَهُ ظَاهِرَةً وَبَاطِنَةً وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَابٍ مُّنِيرٍ﴾
Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu amekutiishieni vilivyomo mbinguni na ardhini, na Akakukamilishieni neema zake zilizo dhahiri na za siri? Na wako watu wanaobishana katika (mambo) ya Mwenyezi Mungu pasipo elimu wala uwongofu wala Kitabu chenye nuru (31:20)
﴿وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَابٍ مُّنِيرٍ﴾
Na katika watu wako wanaojadiliana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya ilimu wala uwongozi wala kitabu chenye nuru (22:8)
Kutokana na aya hizi tunabainikiwa kwa uwazi kuwa katika Uislamu suala la kumuamini Allah (s.w) si suala la kibubusa (la kufuata mkumbo tu) bali ni suala la kitaaluma linalohitaji utafiti wa kina wa kisayansi. Kuna maeneo matano makubwa ambayo tukiyazamia vizuri kisayansi, yanatupatia dalili mbali mbali za uwazi zinazotuthibitishia kuwepo kwa Allah (s.w) na utukufu wake usio na mfano wake. Maeneo haya ni:
(i) Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake
(ii) Nafsi ya mwanaadamu
(iii) Historia ya mwanaadamu
(iv) Maisha ya Mitume
(v) Mafundisho ya Mitume
Umbile la mbingu na ardhi
﴿إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ﴾
"Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s.w) kwa wenye akili." (3:190).
Mungu, Muumba wa kila kitu ndiye mmiliki pekee wa viumbe vyote. Ni Yeye anayebadili mielekeo ya upepo, anayekusanya mawingu, anayewasha jua na kuiangazia dunia na kudhibiti sayari zizunguuke katika mihimili yao. Kudai maisha haya ya dunia na ulimwengu mzima yanatokana na bahati nasibu ni kutokitumia kipawa cha busara alichotunukiwa kila mwanaadamu mwenye akili timamu. Mpango bora wa dunia na ulimwengu kwa ujumla unapinga uwezekano wa kutokea kwa bahati nasibu tu, na kinyume chake ni ishara ya wazi ya uwezo wa Allah(s.w)usio na kikomo unaodhihirisha kuwepo kwake.
Wakati ambapo ni muhali hata kwa kitu chepesi kufanya mzunguko wa moja kwa moja katika njia yake bila kwenda kombo, dunia pamoja na ukubwa wake yenye mkusanyiko wa vitu visivyo na idadi hufanya hivyo. Na imekuwa ikifanya hivyo kwa miaka dahari, na dahari, tangu dunia kuumbwa na kuanza mzunguko wake. Allah anasema Yeye ndiye mfanyaji wa mahesabu ya mzunguko huo.
﴿قَدْ جَعَلَ اللَّـهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا﴾
Hakika Mwenyezi Mungu amekwishakiwekea kila kitu kipimo chake (65:3)
Utaratibu huo bora wa ulimwengu unaendeshwa kwa mfumo wa ajabu unaokwenda kwa kutegemea mihimili isiyo na mashiko.Wengine hudhani kuwa baada ya kuumba, Allah(s.w)amekiacha kila kitu kijiendeshe chenyewe tu. La hasha kila tukio litokealo mahala popote pale ulimwenguni hutokea kwa idhini ya Allah(s.w) na chini ya udhibiti wake.
Qur'an inatufahamisha:
﴿أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَابٍ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ﴾
Je! Hujui ya kwamba Mwenyezi Mungu anajua yaliyoko mbinguni na ardhini? Bila shaka yote yamo kitabuni mwake.Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni sahali. (22:70)
Kwa ujumla, umbile la mbingu na ardhi pamoja na vyote vilivyomo - jua, mwezi, nyota, sayari mbali mbali, milima na mabonde, maji ya mvua, bahari, mito na maziwa, mimea ya kila namna, wanyama wa kila namna na kadhalika ni hoja kubwa ya kuthibitisha kuwepo Allah (s.w) na utukufu wake kwa kila mwenye kutumia akili yake vizuri. Kila mtu atakavyobobea katika taaluma zinazohusiana na maumbile ya mbingu na ardhi kama vile Jeografia, Elimu ya anga (Astronomy), Elimu ya mimea (Botany), Elimu ya wanyama (Zoology), n.k. ndivyo Imani yake ya kuwepo Allah (s.w) itakavyopea.
﴿إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ﴾
Kwa hakika wanaomuogopa Allah (s.w) miongoni mwa waja wake ni wale wataalam..." (35:28)
NAFSI YA MWANAADAMU
﴿وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِّلْمُوقِنِينَ ﴿٢٠﴾ وَفِي أَنفُسِكُمْ أَفَلَا تُبْصِرُونَ﴾
"Na katika ardhi zipo (alama namna kwa namna za kuonyesha kuwepo Allah (s.w) kwa wenye akili.Na katika nafsi zenu (pia zimo ishara hizo) Je, hamuoni?" (51:20-21)
Ukimtafakari mwanaadamu utapata dalili nyingi zinazothibitisha kuwepo kwa Allah (s.w). Maeneo ya kutafakari ni pamoja na:
(I) CHANZO NA MWISHO WA UHAI WA MWANAADAMU
﴿كَيْفَ تَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَكُنتُمْ أَمْوَاتًا فَأَحْيَاكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴾
"Vipi mnamkanusha Allah (s.w) na hali mlikuwa wafu, akakuhuisheni, kisha atakufisheni, kisha atakurudisheni (tena) kisha kwake mtarejeshwa" (2:28)
﴿فَلَوْلَا إِذَا بَلَغَتِ الْحُلْقُومَ ﴿٨٣﴾ وَأَنتُمْ حِينَئِذٍ تَنظُرُونَ ﴿٨٤﴾ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُبْصِرُونَ ﴿٨٥﴾ فَلَوْلَا إِن كُنتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ ﴿٨٦﴾ تَرْجِعُونَهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴾
"Basi mbona (roho) ifikapo kooni,na nyinyi wakati ule mnamtazama. Nasi tunakaribiana naye zaidi (huyo anayetoka roho) kuliko nyinyi,wala nyinyi hamuoni.Kama nyinyi hamumo katika mamlaka (yangu), kwanini hamuirudishi (hiyo roho) ikiwa mnasema kweli?" (56:83-87)
(II) ASILI YA MWANAADAMU
﴿وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ إِذَا أَنتُم بَشَرٌ تَنتَشِرُونَ﴾
"Na katika ishara zake (za kuonyesha kuwepo kwake) ni huku kukuumbeni kwa udongo kisha mnakuwa watu mnaoenea (kila mahali)" (30:20)
(III) KUUMBWA WANAUME NA WANAWAKE
﴿أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَن يُتْرَكَ سُدًى ﴿٣٦﴾ أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَىٰ ﴿٣٧﴾ ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٣٨﴾ فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ ﴿٣٩﴾ أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ﴾
"Je! Anafikiri binaadamu kuwa ataachwa bure(asipewa amri za Mwenyezi Mungu wala makatazo yake)? Je, hakuwa tone la manii lililotonwa?.Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamuumba na akamsawazisha,kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.Je!Hakuwa huyo ni muweza wa kuhuisha wafu?" (75:36-40).
﴿وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴾
"Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya ziko alama (za kuwepo Allah) kwa watu wanaofikiri" (30:21)
(IV) TOFAUTI YA LUGHA, RANGI, MAKABILA, MATAIFA
﴿وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْعَالِمِينَ﴾
"Na katika ishara zake (za kuonyesha kuwepo kwake na uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu.Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi" (30:22)
﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴾
"Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja Adam) na (yule) mwanamke (mmoja Hawwa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane (tu basi). Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Allah ni yule amchaye Allah zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Allah ni Mjuzi Mwenye habari (za mambo yote)." (49:13)
(V) UMBO NA SURA
﴿ يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ ﴿٦﴾ الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ ﴿٧﴾ فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاءَ رَكَّبَكَ﴾
"Ewe mwanaadamu! Nini kikudanganyacho na Mola wako Mtukufu (hata ukamkanusha).Aliyekuumba na akakutengeneza, kisha akakulinganisha sawa sawa. Katika sura yoyote aliyoipenda amekutengeneza" (82: 6-8)
﴿وَفِي خَلْقِكُمْ وَمَا يَبُثُّ مِن دَابَّةٍ آيَاتٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴾
Na katika umbo lenu na katika viumbe alivyovitawanya zimo alama kwa watu wenye yakini" (45:4)
(VI) CHAKULA CHA MWANAADAMU
﴿فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ ﴿٢٤﴾ أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا ﴿٢٥﴾ ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا ﴿٢٦﴾ فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا ﴿٢٧﴾ وَعِنَبًا وَقَضْبًا ﴿٢٨﴾ وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا ﴿٢٩﴾ وَحَدَائِقَ غُلْبًا ﴿٣٠﴾ وَفَاكِهَةً وَأَبًّا ﴿٣١﴾ مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ﴾
"Hebu mwanaadam na atazame chakula chake.Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu(kutoka mawinguni). Tena tukaipasuapasua ardhi.Kisha Tukaotesha humo (vyakula vilivyo) chembe chembe.Na mizabibu na mboga.Na mizeituni na mitende. Na mabustani, (mashamba) yenye miti iliyosongamana barabara.Na matunda na malisho.Kwa ajili ya kukustarehesheni nyinyi na wanyama wenu. (80:24-32)
(VII) UFANYAJI KAZI WA VIUNGO VYA NDANI NA NJE YA MWILI WA MWANAADAMU
﴿فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴾
"Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawasawa - ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu; (yaani dini hii ya Kiislamu inawafikiana barabara na umbo la binaadamu).Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu.Hiyo ndiyo dini iliyo haki, lakini watu wengi hawajui." (30:30)
(VIII) USINGIZI
﴿وَمِنْ آيَاتِهِ مَنَامُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَابْتِغَاؤُكُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ﴾
"Na katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na kuamka mchana na kutafuta fadhila Yake.Hakika katika hayo zimo ishara kwa wenye kusikia.(30:23)
Mwanadamu japo analala kila siku, hajui chanzo cha usingizi.Mtu anapokuwa usingizini hajui chochote kinachoendelea, Je! ni nani anayeleta usingizi na kuuondoa?
(IX) MWANADAMU KUMKUMBUKA ALLAH (S.W) WAKATI WA MATATIZO
﴿قُلْ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ تَدْعُونَهُ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً لَّئِنْ أَنجَانَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ﴾
"Sema: Ni nani anayekuokoeni katika viza (taabu) vya bara na baharini? Mnamuomba kwa unyenyekevu na kwa sauti ndogo (mnasema): Kama akituokoa katika (baa) hii bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru (6:63)
Hata Fir'auni, aliyetakabari sana kiasi cha kudai kuwa yeye ni mkubwa kuliko Allah, alimkumbuka Mola wake pale alipokabiliwa barabara na matatizo.
﴿وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ بَغْيًا وَعَدْوًا حَتَّىٰ إِذَا أَدْرَكَهُ الْغَرَقُ قَالَ آمَنتُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا الَّذِي آمَنَتْ بِهِ بَنُو إِسْرَائِيلَ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴾
"Na tukawapitisha wana wa Israel katika bahari, na Firauni na majeshi yake wakawafuata kwa dhulma na jeuri. Hata kulipomfikia Fir'aun kuzama alisema, "Naamini kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila yule wanayemuamini wana wa Israel na mimi ni miongoni mwa wanaotii". (10:90)
Historia ya Mwanadamu Historia ya mwanadamu ukiichunguza tangu mwanzo wake utakuta matukio mengi yanayothibitisha kuwepo Allah (s.w) Mmiliki wa kila kitu na mwenye nguvu na uwezo juu ya kila kitu. Mara kwa mara tunatanabahishwa katika Qur-an:
﴿أَفَلَمْ يَهْدِ لَهُمْ كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّنَ الْقُرُونِ يَمْشُونَ فِي مَسَاكِنِهِمْ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّأُولِي النُّهَىٰ﴾
"Je! Haikuwabainikia tu kama (kaumu) ngapi tuliziangamiza kabla yao? Na hawa (makafiri wa sasa) wanatembeatembea katika maskani yao, (hawaoni alama za kuangamizwa kwao)?Bila shaka katika hayo zimo ishara kwa wenye akili." (20:128)
﴿أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ كَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَأَثَارُوا الْأَرْضَ وَعَمَرُوهَا أَكْثَرَ مِمَّا عَمَرُوهَا وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴾
"Je! Hawatembei katika nchi na kuona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao na wakilima ardhi na kuistawisha zaidi kuliko wao walivyostawisha. Na mitume wao waliwajia kwa dalili waziwazi, basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu,lakini walikuwa wenyewe wakijidhulumu nafsi zao." (30:9)
﴿أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَابِ الْفِيلِ ﴿١﴾ أَلَمْ يَجْعَلْ كَيْدَهُمْ فِي تَضْلِيلٍ ﴿٢﴾ وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ ﴿٣﴾ تَرْمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ ﴿٤﴾ فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍ مَّأْكُولٍ﴾
"Je!Huoni Mola wako alivyo wafanya watu wenye ndovu?Hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?Na akawapeleka ndege makundi kwa makundi, wakawapiga kwa mawe ya udongo wa kuchoma, Akawafanya kama majani yaliyotafunwa." (105:1-5)
Tukio hili la watu wenye ndovu lilitokea mwaka 570.A.D. miezi michache kabla ya kuzaliwa Mtume Muhammad(s.a.w.w). Mnamo mwaka wa 570 A.D. Abraha, gavana wa Yemen, chini ya himaya ya Kikiristo ya Uhabeshi alikusanya jeshi lenye askari 60,000 na ndovu (tembo) kumi na tatu (13) kwa nia ya kuibomoa na kuisambaratisha Al-Ka'abah, nyumba takatifu ya Allah (s.w) iliyopo Makka. Walinzi wa Ka'abah, kabila la Quraish waliongozwa na Abdul-Muttalib, Babu yake Mtume (s.a.w), walimfahamisha Abraha kuwa wao hawana uwezo wa kupambana na jeshi lake hilo bali mwenye Ka'abah ndiye atakayeilinda. Abraha alipokaidi na kusisitiza kutekeleza azma yake ya kuivunja Ka'abah, Abdul- Muttalib aliwaamuru wakazi wa Makka wampishe na akaingia ndani ya Ka'abah na kumuomba Allah (s.w) kwa unyenyekevu kama ifuatavyo:
"O Allah, mtu hulinda nyumba yake, nawe ilinde nyumba yako. Usiuachie msalaba na hila zao kesho kushinda hila zako. Kama utaamua kuwaachia waifanye watakavyo Qibla yetu, Basi wewe ni muweza wa kufanya upendavyo. Wanusuru leo watumishi wako dhidi ya watumishi wa Msalaba na waabudu wake. Ewe Mola wangu, sina matumaini yoyote toka kwa yeyote dhidi yao isipokuwa kwako. Ewe Mola wangu, ilinde nyumba yako dhidi yao. Adui wa nyumba hii ni adui yako. Wazuie wasiiharibu nyumba yako"
Kesho yake, Abraha na jeshi lake kabla hawajapiga hatua kutoka kwenye kambi yao, kilometa tano (5) tokea Makka, walizingirwa na jeshi la ndege wadogo wadogo walioitwa "Ababil" waliokuwa na silaha ya vijiwe. Kila ndege alimlenga askari wake na kijiwe hicho kilichomchakaza na kumfanya kama majani yaliyotafunwa na kutemwa. Tukio hili la "watu wa ndovu" ni kielelezo tosha kutokana na historia ya binaadamu kuwa Allah (s.w) yupo na anauwezo ulio juu ya hila zote za binaadamu na juu ya kila kitu.
Maisha ya Mitume Ukiyachunguza maisha ya mitume mbalimbali kama yalivyoelezwa katika Qur-an utabaini kuwa wao kweli walikuwa ni wajumbe wa Allah (s.w). Tunayoyaona katika maisha ya Mitume ambayo yanatuhakikishia kuwepo kwa Allah (s.w) ni pamoja na:
(i) Kuwepo kwao na kujieleza kwa watu wao kuwa ni Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w)
(ii) Msimamo wao katika kujieleza kwa jamii zao kuwa wao ni Mitume wa Allah (s.w)
(iii) Mwenendo wao mwema kutoathiriwa na (mazingira) jamii
(iv) Miujiza waliyoionesha katika kuthibitisha utume wao (v) Kuhimili kwao mateso na kujitoa kwao muhanga kwa ajili ya Allah (s.w)
(vi) Ujasiri wao katika kuwakabili viongozi wa jamii zao.
(vii) Ushindi wao dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu
(viii) Mitume kutohitaji malipo yoyote kwa ajili ya kazi yao.
(i) Kuwepo kwao na kujieleza kwa watu wao kuwa ni Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w) Mitume walijieleza kwa uwazi kuwa wao ni mitume wa Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika mifano ifuatayo:
﴿لَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥٩﴾ قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٦٠﴾ قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي ضَلَالَةٌ وَلَـٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦١﴾ أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنصَحُ لَكُمْ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٢﴾ أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ لِيُنذِرَكُمْ وَلِتَتَّقُوا وَلَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٦٣﴾ فَكَذَّبُوهُ فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ فِي الْفُلْكِ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا عَمِينَ ﴿٦٤﴾ وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٦٥﴾ قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي سَفَاهَةٍ وَإِنَّا لَنَظُنُّكَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٦٦﴾ قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي سَفَاهَةٌ وَلَـٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ﴾
"Tulimtuma Nuhu kwa watu wake naye akasema: 'Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika mimi ninakuhofieni adhabu ya siku iliyo Kuu. Wakuu wa watu wake wakasema: "Sisi tunakuona uko katika upotofu uliodhahiri.Akasema (Nuhu):"Enyi kaumu yangu mimi simo katika upotofu lakini mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola wa walimwengu wote. Na kwa Adi (tulimpeleka) ndugu yao Hudi akasema: "Ewe kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu nyinyi hamna Mungu ila Yeye Hamuogopi? Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake:"Sisi tunakuona umo katika upumbavu na tunakuona u miongoni mwa waongo.Akasema: "Enyi kaumu yangu! Mimi sina upumbavu.Lakini mimi ni Mtume niliyetoka kwa Mola wa walimwengu.(7:59-67)
Pamoja na Mitume kujieleza kuwa wanatoka kwa Allah (s.w) mwenyewe Allah (s.w) anatufahamisha kuwa ametuma Mitume:
﴿وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ فَمِنْهُم مَّنْ هَدَى اللَّـهُ وَمِنْهُم مَّنْ حَقَّتْ عَلَيْهِ الضَّلَالَةُ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴾
Na bila shaka tulimpeleka Mtume katika kila umma ya kwamba,"muadubuni Mwenyezi Mungu na mwepukeni muovu (twaaghuut) (16:36)
﴿إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَإِن مِّنْ أُمَّةٍ إِلَّا خَلَا فِيهَا نَذِيرٌ﴾
Bila shaka Sisi tumekutuma (tumekuleta) kwa haki ili ubashirie na uonye. Na hakuna taifa lolote ila alipita humo muonyaji (Mtume kuwaonya). (35:24)
﴿وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِيَ بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ فَإِذَا جَاءَ أَمْرُ اللَّـهِ قُضِيَ بِالْحَقِّ وَخَسِرَ هُنَالِكَ الْمُبْطِلُونَ﴾
Na kwa yakini tuliwatuma Mitume kabla yako.Wengine katika hao tumekusimulia (majina yao na habari zao) na wengine hatukusimulia na haikuwa kwa Mtume yoyote kuleta muujiza wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na itakapokuja hukumu ya Mwenyezi Mungu kutahukumiwa kwa haki, na wafanyao mambo ya batili watapata hasara wakati huo. (40:78).
Hivyo, kuwepo kwa Mitume kunatuthibitishia kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.a.w) kwa namna mbili, kwanza, kama Mwenyezi Mungu (s.w) asingelikuwepo asingelileta Mitume kwa wanaadamu. Pili, Mitume wote waliotokea katika nyakati mbali mbali za historia wasingelitoa dai moja linalofanana kwa wote kuwa wao ni Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w) kama Mwenyezi Mungu hayupo.
(ii) Mwenendo wao mwema kutoathiriwa na jamii Mitume wote takriban walizaliwa na kulelewa katika jamii za kijahili zilizozama katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w) na miungu chungu nzima. lakini jambo la ajabu na kushangaza ni kwamba, Mitume wote tangu utotoni waliepukana na tabia za kijahili na walijiepusha mbali na kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w). Walikuwa na mwenendo wa kiutu (wa Kiislamu) uliowavutia watu wote wa jamii zao na walikuwa ni nyota katika jamii. Kwa mfano, Nabii Ibrahim(a.s) alizaliwa na kuhani Mkuu.
Yaani baba yake Nabii Ibrahim alikuwa ni kiongozi au msimamizi wa ibada ya masanamu. Lakini Nabii Ibrahim kamwe hakuvutiwa na ibada hiyo ya masanamu bali akiwa angali kijana mdogo aliona kuwa ni kinyume kabisa na akili ya mwanaadamu kuwaabudu miungu wengine kinyume na kumuabudu Allah (s.w) aliye mpweke. Mfano wa pili ni ule wa Nabii, Musa(a.s) aliyelelewa katika nyumba ya Firaun aliyetakabari na kujiita mungu. Malezi hayo ya kifalme kamwe hayakumuathiri Nabii Musa(a.s) .Aliinukia kuwa na mwenendo mwema wa kumpwekesha Allah (s.w).
Mfano mwingine ni ule wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) ambaye alizaliwa katika jamii ya Maquraysh iliyobobea katika ujahili na iliyozama katika ushirikina kiasi kwamba kila kitu kwao kiliweza kufanywa mungu na kuabudiwa. Katika wakati huo masanamu ya watu, ndege na wanyama yaliuzwa sokoni kama miungu wa kuabudiwa na hata tende zilifinyangwa na kuabudiwa. Lakini tunavyojifunza katika historia, Mtume(s.a.w.w) tangu utotoni mwake hakuathiriwa kamwe na ibada za masanamu na mwendo wa ujahili. Bali tunajifunza kuwa aliinukia katika kumtambua na kumpwekesha Allah (s.w) na aliwazidi watu wote kwa tabia njema kiasi kwamba watu wake walimtegemea sana kwa ushauri na kuwatunzia amana zao na walimwita "mkweli", "mwaminifu" na majina mengine kama haya yaliyodhihirisha tabia yake njema katikati ya jamii ya kijahili. Ni kitu gani kilichowafanya Mitume kuwa tofauti na watu wa jamii zao?
Je, hakuna aliyewatayarisha na kuwalea katika mwenendo huo ili wawe viigizo vyema katika jamii zao? Bila shaka Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye aliwewaleta Mitume ili wafikishe ujumbe wake na wawe viigizo vyema katika kuutekeleza Uislam kama inavyobainishwa katika Qur-an:
﴿لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ﴾
Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na tukaviteremsha Vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu. (57:25)
(iii) Dalili (miujiza) za kuthibitisha Utume wao Mitume wameletwa pamoja na alama mbali mbali za kuwathibitisha Utume wao kwa watu wao.
﴿لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ﴾
"Kwa hakika tumewapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi" (57:25)
Kila Mtume alipewa dalili za kuwathibitishia watu wake kuwa yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Alama za Utume wa Nabii Musa(a.s) ni fimbo yake kugeuka kuwa nyoka wa kweli na mkono wake kutoa mwan ga mkali kama tunavyojifunza katika Qur-an. (Rejea 28:29-32)
Dalili za Utume wa Nabii Issa(a.s) zilikuwa ni kuwafufua wafu, kuwaponyesha vipofu na wenye mbaranga, kulifanya sanamu la ndege kuwa ndege wa kweli kama inavyobainishwa katika Quran (5:110).
Dalili aliyopewa Mtume Muhammad(s.a.w.w) ya kuthibitisha kuwa yeye ni Mtume wa Allah (s.w) ambayo itabakia mpaka mwisho wa ulimwengu ni Qur-an. Qur-an tofauti na vitabu vingine vya Allah (s.w) imehifadhiwa na uharibifu wa aina yoyote. Qur-an yenyewe inatukumbusha:
﴿أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللَّـهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلَافًا كَثِيرًا﴾
Hawaizingatii nini,hii Qur-an? Na kama ingelitoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi. (4:82).
(iv) Kuhimili mateso na kujitoa kwao muhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w)
Jambo jingine linalopatikana katika historia ya Mitume ni uvumilivu waliokuwa nao dhidi ya mateso mbali mbali waliyofanyiwa na watu wao na bado wakaendelea kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu bila ya kukata tama. Tukirejea katika Qur'an tunapata mifano mbali mbali ya mateso waliyofanyiwa na jamaa zao. Kwa mfano tunajifunza katika Qur-an kuwa ilikuwa ni tabia ya Wayahudi (kizazi cha Israil) kuwauwa Mitume yao pasina haki:
﴿إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ الَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِالْقِسْطِ مِنَ النَّاسِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴾
Wale (Mayahudi) wanaozikataa Aya za Mwenyezi Mungu, na wakawaua manabii pasina haki, na wakaua watu wanaoamrisha kusimamisha haki, wapashe habari ya adhabu kali. (3:21)
Nabii Yahya(a.s) (Yohana mbatizaji) ni miongoni mwa Mitume wa Mwenyezi Mungu waliochinjwa na Mayahudi, kwa sababu tu eti walisimama kidete kufikisha neno la Mwenyezi Mungu, kwa watu wao ili wasimamishe haki katika jamii kwa kufanya mema na kuacha maovu.Pia Mayahudi walikula njama za kumuua Nabii Isa(a.s) . Lakini Mwenyezi Mungu (s.w) alimuokoa na kumnyakuwa kwake kama tunavyojifunza katika Qur-an:
﴿وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّـهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا ﴿١٥٧﴾ بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٥٨﴾ وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا﴾
"Na kwa (ajili ya) kusema kwao: Sisi tumemuua Masihi Isa, mwana wa Maryam Mtume wa Mungu", hali hawakumuua wala hawakumsulubu, bali walibadilishiwa (mtu mwingine wakamdhani Nabii Issa). Na kwa hakika wale waliokhitilafiana katika (hakika) hiyo (ya kumuua Nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo la kusema kauawa).Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo) hili (la kuwa kweli wamemua Nabii (Isa). Isipokuwa wanafuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumua.Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima. (4:157-158)
Naye Nabii Ibrahim alitupwa motoni na jamaa zake, Mwenyezi Mungu (s.w) aliuamrisha moto kuwa baridi na salama kwake:
﴿قُلْنَا يَا نَارُ كُونِي بَرْدًا وَسَلَامًا عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ﴾
"Tukasema: 'Ewe moto! Kuwa baridi na salama juu ya Ibrahim". (21:69)
Mitume pia walitiwa vifungoni na vizuizini (kutengwa na jamii) kama ilivyokuwa kwa Nabii Yusufu(a.s) na Nabii Muhammad(s.a.w.w) . Baadhi ya Mitume na wafuasi wao walifukuzwa nchini mwao na kuhamia ugenini kama ilivyokuwa kwa Mtume(s.a.w.w) na Muhajirina:
﴿لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ﴾
"(Basi) wapewe (mali hayo) mafakiri wa Kimuhajiri ambao walifukuzwa katika nyumba zao na mali zao; (wakakhiari kuyaacha hayo) kwa ajili ya (kutafuta) fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi (yake) na kuinusuru (dini ya) Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi hao ndio waislamu wa kweli. (59:8).
Mitume pia walinyanyaswa kwa matusi na kejeli. Kwa mfano Mtume Muhammad(s.a.w.w) aliitwa mwendawazimu, mchawi, mtunga mashairi, abtair (mkiwa) na matusi mengineyo. Pamoja na kufanyiwa madhila yote hayo, bado Mitume walisimama kidete kuufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa watu wao na wala hawakukata tamaa.Ni nguvu gani iliyowapa Mitume ustahimilivu kiasi hicho? Je,kuna malipo yoyote ya hapa duniani waliyoyapata ndiyo yakawafanya kuwa wastahamilivu kiasi hicho? Je, Mitume hawakuwa na tegemeo la kulipwa na mwenye uwezo juu ya kila kitu anayestahiki kutegemewa na kuogopwa kuliko yeyote yule? Bila shaka uvumilivu na subira ya hali ya juu waliyokuwa nayo Mitume ni alama kuwa yuko mwenye nguvu na uwezo juu ya kila kitu waliyekuwa wakimtegemea na kutaraji ujira mkubwa kutoka kwake.
(v) Ujasiri wa Mitume mbele ya Viongozi wa jamii ya kishirikina Mitume hawakumchelea yeyote katika kuwafikishia watu ujumbe waliotumwa kuufikisha.Hawakufikisha ujumbe wao kwa watu wa kawaida tu bali waliwaendea Wafalme na watawala wa jamii waliokuwa wapinzani wakubwa wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w). Mitume waliwaelekea wakuu hao wa jamii pamoja na takaburi zao na vitisho vingi walivyovitoa dhidi yao. Kwa mfano Nabii Ibrahiim hakumchelea baba yake katika kumfikishia ujumbe wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
﴿إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا ﴿٤٢﴾ يَا أَبَتِ إِنِّي قَدْ جَاءَنِي مِنَ الْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَاتَّبِعْنِي أَهْدِكَ صِرَاطًا سَوِيًّا ﴿٤٣﴾ يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ عَصِيًّا ﴿٤٤﴾ يَا أَبَتِ إِنِّي أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيْطَانِ وَلِيًّا ﴿٤٥﴾ قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنْ آلِهَتِي يَا إِبْرَاهِيمُ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ لَأَرْجُمَنَّكَ وَاهْجُرْنِي مَلِيًّا﴾
(Wakumbushe) alipomwambia baba yake: "Ewe baba yangu! Kwanini unaabudu visivyosikia na visivyoona na visivyo kufaa chochote?Ewe baba yangu!Kwa yakini imenijia ilimu isiyokujia. Basi nifuate nitakuongoza njia iliyosawa.Ewe baba yangu! Usimuabudu shetani, hakika shetani ni mwenye kumuasi (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehma.Ewe baba yangu! Hakika naogopa kukupata adhabu inayotoka kwa Mwingi wa Rehma (Mwenyezi Mungu), ukifanya hivyo) utakuwa mwenziwe shetani".Akasema (yule baba yake):"Je, unaichukia miungu yangu, ewe Ibahimu? Kama huachi (haya unayoyasema) lazima nitakupiga mawe.Na niondokelee mbali, kwa muda mchache (huu). (19:42-46)
Nabii Ibrahim hakuishia kuufikisha ujumbe kwa baba yake tu, bali aliufikisha pia kwa vitendo kwa jamii nzima kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
﴿وَتَاللَّـهِ لَأَكِيدَنَّ أَصْنَامَكُم بَعْدَ أَن تُوَلُّوا مُدْبِرِينَ ﴿٥٧﴾فَجَعَلَهُمْ جُذَاذًا إِلَّا كَبِيرًا لَّهُمْ لَعَلَّهُمْ إِلَيْهِ يَرْجِعُونَ ﴿٥٨﴾ قَالُوا مَن فَعَلَ هَـٰذَا بِآلِهَتِنَا إِنَّهُ لَمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٩﴾ قَالُوا سَمِعْنَا فَتًى يَذْكُرُهُمْ يُقَالُ لَهُ إِبْرَاهِيمُ ﴿٦٠﴾ قَالُوا فَأْتُوا بِهِ عَلَىٰ أَعْيُنِ النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَشْهَدُونَ ﴿٦١﴾ قَالُوا أَأَنتَ فَعَلْتَ هَـٰذَا بِآلِهَتِنَا يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿٦٢﴾ قَالَ بَلْ فَعَلَهُ كَبِيرُهُمْ هَـٰذَا فَاسْأَلُوهُمْ إِن كَانُوا يَنطِقُونَ ﴿٦٣﴾ فَرَجَعُوا إِلَىٰ أَنفُسِهِمْ فَقَالُوا إِنَّكُمْ أَنتُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٦٤﴾ ثُمَّ نُكِسُوا عَلَىٰ رُءُوسِهِمْ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا هَـٰؤُلَاءِ يَنطِقُونَ ﴿٦٥﴾ قَالَ أَفَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكُمْ شَيْئًا وَلَا يَضُرُّكُمْ ﴿٦٦﴾ أُفٍّ لَّكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٧﴾ قَالُوا حَرِّقُوهُ وَانصُرُوا آلِهَتَكُمْ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ﴾
"Na wallahi (kwa haki ya Mungu) nitayafanyia mabaya masanamu yenu haya baada ya kunipa mgongo mkenda zenu." Basi akayavunja (masanamu yote yale) vipande vipande isipokuwa lile kubwa lao (aliliacha), ili wao (hao makafiri) walirudie. Wakasema: "Nani aliyeifanya hivi miungu yetu? Hakika huyo yu miongoni mwa madhalimu (wakubwa).Wakasema: "Tulimsikia kijana mmoja akiwataja anayeitwa Ibrahim.Wakasema: Basi mleteni mbele ya macho ya watu, wamshuhudie (kwa ubaya wake huyo)" Wakasema: "Je!Wewe umeifanya hivi miungu yetu, Ee Ibrahim? Akasema: Siyo,bali amefanya (hayo) huyu mkubwa wao, basi (muulizeni na) waulizeni (pia hao waliovunjwa) kama wanaweza kusema! Basi wakajirudi nafsi zao, (wakafikiri udhalilifu wa waungu hao walio nao, wasioweza kujipigania) na wakasema: "Hakika nyinyi mlikuwa madhalimu (wa nafsi zenu kwenda kuwaabudu wasiokuwa na maana)." Kisha wakainamishwa vichwa vyao, (wakarejea ujingani, ukafirini, wakasema): "Hakika umekwishajua ya kwamba hawasemi, (kwa nini unatucheza shere?).Akasema: "Je! Mnaabudu badala ya Mwenyezi Mungu (miungu) isiyokufaeni chochote(mnapowaabudu) wala kukudhuruni (chochote mnapoacha kuwaabudu? Kefule (udhalilifu) yenu na ya hivyo mnavyoviabudu kinyume na Mwenyezi Mungu. Je! hamfikiri? (21:57- 67)
Pia Nabii Ibrahim(a.s) alimkabili mfalme na kuhojiana naye. - Rejea Qur-an (2:258)
(vi) Ushindi wa Mitume dhidi ya maadui Jambo jingine tunalojifunza katika historia ya Mtime ambalo ni miongoni mwa dalili kubwa za kuonyesha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) ni ushindi waliokuwa wakiupata Mitume na wafuasi wao wachache dhidi ya maadui zao. Mara zote walikuwa wapinzani wakubwa wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w) walikuwa watawala wa walioshikilia dola na matajiri waliokuwa na wafuasi wengi na majeshi yenye nguvu kubwa. Kwa upande mwingine, katika jamii zote, walioamini Mitume walikuwa wachache na wengi wao wakiwa wanyonge wa jamii. Pamoja na hivyo Mitume na waumini wachache wanyonge waliwashinda maadui zao walikuwa na nguvu kwa kiasi kikubwa.
Hebu turejee mifano michache ifuatayo: Nabii Nuhu(a.s) aliwalingania watu wa jamii yake kwa miaka 950. Lakini watu wake pamoja na kutishia kumuua, walimtaka awaletee kutoka kwa Mola wake hiyo adhabu aliyokuwa akiwatahadharisha kwayo ikiwa anasema kweli kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.w). Mwishowe adhabu kweli ililetwa na wakawa ni wenye kugharikishwa kama tunavyojifunza katika Qur-an: Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa motoni wala hawakuwapata wa kuwanusuru mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w). (71:25) Nabii Hud(a.s) alitumwa kwa watu wa Ad na kuwafikishia ujumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w). Lakini wengi wao wakiongozwa na watawala na matajiri walitakabari na kukataa na kuwa dhidi yake na wafuasi wachache walioamini pamoja naye. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w) alimnusuru Mtume wake na walioamini pamoja naye kutokana na madhalimu kama tunavyojifunza katika Qur-an:
﴿٧٢فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَقَطَعْنَا دَابِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَمَا كَانُوا مُؤْمِنِينَ﴾
Basi tukamuokoa yeye na waliokuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukakata mizizi ya wale waliozikadhibisha aya zetu, na (ambao) hawakuwa wenye kuamini. (7:72).
Nabii Musa(a.s) na wana wa Israil waliokolewa kutokana na makucha ya dhalimu Firaun na majeshi yake kama tunavyojifunza katika Qur-an:
﴿فَأَتْبَعُوهُم مُّشْرِقِينَ ﴿٦٠﴾فَلَمَّا تَرَاءَى الْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَابُ مُوسَىٰ إِنَّا لَمُدْرَكُونَ ﴿٦١﴾ قَالَ كَلَّا إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهْدِينِ ﴿٦٢﴾ فَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْبَحْرَ فَانفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَالطَّوْدِ الْعَظِيمِ ﴿٦٣﴾ وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ الْآخَرِينَ ﴿٦٤﴾ وَأَنجَيْنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُ أَجْمَعِينَ ﴿٦٥﴾ ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ ﴿٦٦﴾ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٦٧﴾ وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ﴾
Basi (watu wa Firaun na mwenyewe nafsi yake Firaun) wakawafuata (Nabii Mussa na watu wake) lilipotua jua. Na yalipoonana majeshi mawili (haya, watu wa Nabii Musa wanakimbia, na Firauni na watu wake wanawafuatia). Watu wa Musa walisema: "Hakika tutakamatwa. (Musa) akasema: "La, kwa yakini Mola wangu yu pamoja nami, bila shaka ataniongoza (tuokoke sote)". Mara tulimpelekea Wahyi Musa (tukamwambia): "Piga bahari kwa fimbo yako". Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama jabali kubwa. Na tukawaleta hapo wale wengine (nao ni firauni na watu wake). Na tukamuokoa Musa na wale waliokuwa pamoja naye wote.Kisha tukawagharikisha hao wengine. Hakika katika hayo muna mazingatio: lakini wengi katika wao si wenye kuamini. Na kwa yakini Mola wako ndiye Mwenye Nguvu, mwenye Rehema. (26:60-68)
Mfano wa mwisho ni ule unaopatikana katika historia ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) na wafuasi wake. Vita vya kwanza vikubwa alivyopigana Mtume (s.a.w) na wafuasi wake dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu ni vita vya Badr. Katika vita hivyo jeshi la makafiri wa Kiquraish lililojizatiti barabara lilikuwa na watu 1000 ambapo jeshi la Waislamu lisilojiandaa vizuri kivita lilikuwa na wanajeshi 300 tu hivi. Pamoja na udogo na uduni wa jeshi, Waislamu walipata ushindi mkubwa kwa msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyojifunza katika Qur-an:
﴿إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّي مُمِدُّكُم بِأَلْفٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُرْدِفِينَ ﴿٩﴾ وَمَا جَعَلَهُ اللَّـهُ إِلَّا بُشْرَىٰ وَلِتَطْمَئِنَّ بِهِ قُلُوبُكُمْ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴾
(Kumbukeni) mlipokuwa mkiomba msaada kwa Mola wenu, naye akakujibuni kuwa:"Kwa yakini Mimi nitakusaidieni kwa malaika elfu moja watakaofuatana mfululizo (wanaongezeka tu)". Na mwenyezi Mungu hakufanya haya ila iwe bishara (habari ya furaha) na ili nyoyo zenu zituwe kwayo. Na hakuna msaada (wa kufaa) ila utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na) Mwenye hikima. (8:9-10).
Ushindi wa Mitume na wafuasi wao haukupatikana ila kwa msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w). (vii) Mitume kutohitajia malipo kutoka kwa watu wao:
Mitume, tofauti na viongozi wengine waliojitokeza katika jamii mbalimbali, hawakuifanya kazi yao ya kuwaongoza watu katika njia ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kutarajia maslahi yoyote si ya hali wala ya mali, kutoka kwa watu wao. Waliifanya kazi hiyo kama watumishi wa Mwenyezi Mungu (s.w) na ni yeye pekee waliyemtegemea awalipe kwa kazi hiyo. Daima walikuwa wakiwakumbusha watu wao jambo hili kama tunavyorejea katika Qur-an:
﴿وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴾
"Wala sikutakini juu yake ujira, ujira wangu hauko ila kwa (Mwenyezi Mungu) Mola wa walimwengu wote"(26:127)
Mitume wasingelikuwa wajumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w) wenye uhakika wa kupata ujira mkubwa kwake kwa kazi yao, kitu gani kingeliwazuia wasitake malipo kutoka kwa watu wao, kama viongozi wa kawaida wa jamii za wanaadamu wanavyotaka malipo kutoka kwa watu wao?
5
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
MAFUNDISHO YA MITUME
Mafundisho ya mitume ni eneo lingine linalo thibitisha kuwepo Allah (s.w).Dalili zinazodhihirisha kuwepo Allah (s.w) katika eneo hili ni pamoja na:
(a) Umoja wa ujumbe wa mitume
(b) Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira ya jamii zao
(c) Upeo wa elimu waliyokuwa nayo mitume.
(a)Umoja wa Ujumbe wa Mitume
Kitu kinachodhihirisha kuwa Mitume ambao baadhi yao ulimwengu mzima una shuhudia historia yao, kama vile historia ya Nabii Ibrahim (a.s), Musa(a.s) , Isa(a.s) na Muhammad(s.a.w.w) kuwa ni wajumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) wenye ujuzi na hekima, ni kule kufanana kwa ujumbe wao. Kama dhana ya kutokuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) ingelikuwa kweli, ingelikuwa muhali kwa Mitume waliotokea sehemu tofauti nyakati tofauti, kutoa ujumbe unaofanana. Turejee katika Qur-an mifano michache ya mafundisho ya msingi waliyotoa Mitume kwa watu wao:
(I) NUHU(A.S)
﴿لَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ﴾
Tulipompeleka Nuhu kwa watu wake, naye akasema:"Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu.Nyinyi hamna Mungu ila Yeye.Hakika mimi ninakuhofieni adhabu ya siku (hiyo) iliyo kuu"(7:59).
(II) HUD(A.S)
﴿وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ أَفَلَا تَتَّقُونَ﴾
"Na kwa Adi (tulimpeleka) ndugu yao Hudi, akasema: "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna Mungu ila Yeye.Basi hamuogopi? "(7:65).
(III) SALIH(A.S)
﴿وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴾
"Na kwa thamud (tulimpeleka) ndugu yao, Saleh.Akasema "Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna Mola ila Yeye. Hakika umekwisha kukufikieni muujiza ulio dhahiri kutoka kwa Mola wenu. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye na ishara kwenu (ya Utume wangu). Basi muacheni ale katika ardhi ya Mungu, wala msimtie katika dhara yoyote, isije ikakushikeni adhabu iumizayo" (7:73)
(IV) SHU'AYB(A.S)
﴿وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴾
Na kwa watu wa Madyan (tulimpeleka) ndugu yao, Shu'ayb, akasema: 'Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu, hamna Mungu mwingine isipokuwa Yeye. Zimekwisha kufikieni hoja dhahiri kutoka kwa Mola wenu. Basi kamilisheni sawa sawa vipimo (vya vibaba) na mizani (pia) wala msiwapunguzie watu vitu vyao wala msifanye uharibifu katika ardhi badala ya kutengenea kwake.Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi mumeamini. (7:85).
(V) ISA(A.S)
﴿وَإِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴾
Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Mola wenu. Basi muabuduni.Hii ni njia iliyonyooka. (19:36)
(VI) MUHAMMAD(S.A.W.W)
﴿قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴾
Sema (ewe Muhammad): "Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote; (Mungu) ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi, hakuna aabudiwaye (kwa haki) ila yeye, yeye ndiye ahuishaye na ndiye afishaye.Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, aliye Nabii Ummiyyi (asiyejua kusoma wala kuandika) ambaye humuamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka". (7:158)
﴿وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ فَمِنْهُم مَّنْ هَدَى اللَّـهُ وَمِنْهُم مَّنْ حَقَّتْ عَلَيْهِ الضَّلَالَةُ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴾
"Na bila shaka tulimpeleka mtume katika kila umma ya kwamba, Muabuduni Mwenyezi Mungu na mwepukeni twaghuti. Basi wako miongoni mwao ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa na wako miongoni mwao ambao upotofu umethubutu juu yao. Basi tembeeni katika ardhi na mwangalie ulikuwaje mwisho wa wale waliokadhibisha" (16:36)
Ukirejea katika Qur-an utaona kuwa Mitume wote kwa ujumla wamefundisha yafuatayo:-
(i)TAWHIID
Wamewafundisha watu juu ya kuwepo Allah (s.w) na upweke wake kwa kuwaonyesha dalili zilizo waziwazi.
(II)LENGO
Waliwafundisha watu kuwa lengo la kuumbwa kwao ni kumuabudu Allah (s.w) na kusimamisha ukhalifa wake hapa ulimwenguni na kisha waliwafundisha namna ya kumuabudu Mola wao katika kila kipengele cha maisha.
(III) KUBASHIRIA
Waliwabashiria watu malipo mema ya kudumu ya huko Peponi kwa wale watakaoamini vilivyo na kutenda mema katika maisha yao ya hapa duniani.
(IV) KUHOFISHA
Waliwahofisha watu juu adhabu kali watakayopata huko Akhera wale watakao mkufuru Allah (s.w) na kumwabudu twaghuti. Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira ya jamii zao Takriban Mitume wote walitokea katika jamii zilizozama katika ujahili, lakini kamwe ujumbe wao haukuathiriwa na mitazamo ya ujahili kwa ujumla, wala hawakuingiza utamaduni wa kijahili katika dini ya Allah (s.w). Kwa mfano, maquraishi walipomjia Mtume(s.a.w.w) na rai ya kuchanganya haki na batili katika ibada, Mtume(s.a.w.w) aliamuriwa na Mola wake awape msimamo wa Uislamu kama ifuatavyo:
﴿قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ ﴿١﴾ لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ ﴿٢﴾ وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ ﴿٣﴾ وَلَا أَنَا عَابِدٌ مَّا عَبَدتُّمْ ﴿٤﴾ وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ ﴿٥﴾ لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ﴾
"Sema: Enyi makafiri, siabudu mnachoabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.Wala sintaabudu mnachoabudu.Wala nyinyi hamtamuabdudu ninayemuabudu.Nyinyi mna dini yenu nami nina dini yangu" (109:1-6)
Upeo wa Elimu waliyokuwa nayo Mitume Mitume walikuwa na upeo wa fikra na hekima kuliko mtu yeyote katika jamii zao. Hawakusoma kwa mtu bali walifunuliwa elimu kwa njia ya Wahay kutoka kwa Mola wao. Kwa mfano juu ya Nabii Daudi na Suleimani tunasoma katika Qur-an: "Na bila shaka tuliwapa Daudi na Suleimani elimu (kubwa kabisa na wakamshukuru Allah) wakasema, "Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu aliyetufadhilisha kuliko wengine katika waja wake waliomuamini" (27:15) Sifa za Allah (s.w) Kuthibitisha kuwepo kwa Mungu muumba baada ya kutafakari ishara mbali mbali zilizotuzunguka katika kuiendea Imani ya kweli juu ya Allah (s.w) ni hatua ya kwanza. Hatua ya pili ni kuzifahamu sifa (Attributes) za Allah (s.w). Sifa za Allah (s.w) ni nyingi kiasi kwamba hapana yeyote awezaye kuzimaliza kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
﴿قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا﴾
"Sema hata bahari ingelikuwa ndio wino kwa kuyaandika maneno ya Mola wangu, basi bahari ingelikwisha kabla ya kwisha maneno ya Mola wangu hata kama tungelileta (bahari) kama hiyo kuongezea" (18:109)
﴿وَلَوْ أَنَّمَا فِي الْأَرْضِ مِن شَجَرَةٍ أَقْلَامٌ وَالْبَحْرُ يَمُدُّهُ مِن بَعْدِهِ سَبْعَةُ أَبْحُرٍ مَّا نَفِدَتْ كَلِمَاتُ اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴾
"Na lau kama miti yote iliyomo katika ardhi ingelikuwa kalamu, na bahari hii (ikafanywa wino) na ikasaidiwa na bahari nyingine saba, maneno ya Mwenyezi Mungu yasingelikwisha. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu, mwenye hekima" (31:27)
Pamoja na msisitizo huu Mtume (s.a.w) anataja majina na sifa 99 za Mwenyezi Mungu.
MAJINA 99 YA MWENYE EZI MUNGU
1. Allah Mwenyezi Mungu, Mola Mwenye kustahiki kuwepo. Hili ndilo jina la Dhati la Mungu Mmoja tu. 2. Ar-Rahmaanu Mwingi wa Rehema (huruma). 3. Ar-Rahiimu Mwenye kurehemu. 4. Al-Maliku Mfalme wa kweli wa milele. Mfalme wa Wafalme. 5. Al-Qudduusu Mtakatifu, Ametakasika na sifa zote chafu.
6. As-Salaamu Mwenye Kusalimika, Mwenye kuleta amani, Mwenye Salama. 7. Al-Mu'uminu Mtoaji wa amani. 8. Al-Muhayminu Mwangalizi wa mambo ya viumbe vyake (matendo yao, uhai wao, n.k) Mlinzi, Mchungaji. 9. Al-'Aziizu Mwenye Shani, shahidi katika mambo yake, Muhitajiwa na kila kitu na wala hahitaji kwa yeyote katika viumbe vyake. 10. Al-Jabbaaru Mwenye kuunga mambo yaliyovunjika. Mwenye kulazimisha viumbe wafanye analolitaka yeye bila ya wao kuwa na uwezo wala uhuru wa kumlazimisha yeye kufanya wanalotaka viumbe. 11. Al-Mutakabbiru Mwenye Kibri na Haki ya Kibri (Majestic, Suprem Pride). 12. Al-Khaaliqu Muumbaji, Mbora wa waumbaji. 13. Al-Baariu Mtengenezaji (The maker out of nothing). 14. Al-Muswawwiru Mfanyaji wa sura za namna namna (the Fashioner).15.Al-Ghaffaaru Msamehevu.Mwenye kusamehe.16.Al-Qahhaaru Mwenye Nguvu juu ya kila kitu (Irresistible). 17. Al-Wahhaabu Mpaji Mkuu (The Bestower) 18. Ar-Razzaaqu Mtoaji wa Riziki, Mwenye kuruzuku. 19. Al-Fattaahu Afungua kila kitu. 20. Al-Aliimu Ajuae, Mjuzi wa kila kitu. 21. Al-Qaabidhu Mwenye kuzuia, Mwenye kufisha na kusababisha kufa, Mwenye kunyima (kutia umaskini). 22. Al-Baasitwu: Mwenye kutoa,Mwenye kuhuisha, mwenye kuvipa viumbe uhai, mwenye kutajirisha. 23. Al-Khaafidhu Mfedhehesha waovu. 24. Ar-Raafiu Mpaji cheo, Mpandishaji daraja. 25. Al-Mui'zzu Mtoaji heshima kwa amtakaye. 26. Al-Mudhillu Mnyima heshima kwa amtakaye, mwenye kudhili. 27. As-Samiiu' Mwenye kusikia, Msikivu wa hali ya juu kabisa. 28. Al-Baswiiru Mwenye kuona, Muoni wa hali ya juu kabisa. 29. Al-Hakamu Mwenye kuhukumu, Mwenye kukata shauri,Mwamuzi. Muadilifu, mwenye kutoa ha30.Al-'Adluki asiye dhulumu.31.Al-Latwiifu Mpole, laini, mwenye huruma sana.32. Al-Khabiiru Mwenye khabari zote (mjuzi wa mambo yote). 33. Al-Haliimu Mpole sana, kabisa 34. Al-A'dhiimu Mkuu, Aliye Mkuu. 35.Al-Ghafuuru,Msamehevu.36.Ash-Shakuuru Mwenye shukrani.37.Al-'AIliyyu Aliye juu (The High). 38. Al-Kabiiru Mkubwa wa kuishi Mkongwe. 39. Al-Hafiidhu Haafidhi (The Preserver) Mwenye kuhifadhi kila kitu. 40. Al-Muqiitu Mlishaji (the Feeder), Mtoaji Riziki kwa kila kiumbe, Mwenye nguvu. 41. Al-Hasiibu Mwenye kuhesabu (The Reckoner), Mjuzi wa Hesabu. 42. Al-Jaliilu Mzuri wa hali ya juu (The majestic), Tajiri, Mtukufu, Mjuzi, Mtawala, mwenye Nguvu (yote haya yanajumuisha Al-Jaliil).(Mzuri wa hali zote) 43. Al-Kariimu Mtukufu mwenye ukarimu. 44. Ar-Raqiibu Muoni wa kila linalofanyika, Mwenye kuona yote yanayofanywa, anayaangalia yote yanayofanywa (The Watcher, The Watchful) 45. Al-Mujiibu Mpokeaji wa maombi ya waja wake.Mwenye kuona yote yanayofanywa, anayaangalia yote yanayofanywa. 46. Al-Waasiu Mwenye Wasaa, Mwenye kila kitu.47. Al-Hakiimu Mwenye Hikma (The wise). 48. Al-Waduudu Mwenye Upendo (The Loving), Mwenye kupenda kuwatakia mazuri watu. 49. Al-Majiidu Mtukufu (The Glorious), Mwenye kustahiki kutukuzwa. Jina hili lina changanywa kwa pamoja Al-Jaliil, Al-Wahaab na Al-Kariim. 50. Al-Baa'ithu Mwenye kufufua wafu. 51. As-Shahiidu Shahidi mwenye kushuhudia kila kitu (Witness). 52. Al-Haqqu Wa haki, Wa kweli hasa, Mkweli (The Truth), The True. 53. Al-Wakiilu Wakili (The Advocate), Mdhamini (The Trustee), Mlinzi mwenye kustahiki kuachiwa mambo ya watu.Anayeangalia na kulinda yote (The Representative). 54. Al-Qawiyyu Mwenye nguvu (the Strong). 55. Al-Matiinu,Aliye Madhubuti (The Firm), Asiyetingishika kwa lolote. 56. Al-Waliyyu Mwenye kusifika, kila sifa njema ni zake. 57. Al-Hamiidu Mhimidiwa, Mwenye kustahiki sifa zote nzuri. 58. Al-Muhswiy Mwenye kudhibiti (hesabu), Mwenye kuhesabu. 59. Al-Mubdiu Mwenye kuanzisha (The Producer, The Originator). 60. Al-Mu'iidu Mwenye kurejeza (The producer, The R'estorer). Angalia: Yeye Allah Ndiye Mwenye kuanzisha viumbe na kuvifanya vifu, kisha ndiye mwenye kuvirejesha tena kwenye maisha baada ya kufa.61. Al-Muhyi Mwenye kuhuisha. 62. Al-Hayyu Mwenye uhai wa milele (The Alive). 63. Al-Mumiitu Mwenye kufisha (The Causer of death, The Destroyer). 64. Al-Qayyumu Msimamia kila jambo, Mwendeshaji wa mambo yote. 65. Al-Waajidu Mwenye utaambuzi wa kila kitu.Utambuzi (The Perceiver). 66. Al-Maajidu Wa kuheshimiwa, Mtukufu (The Noble, illustrious). 67. Al-Waahidu,Mwenye kupwekeka, Mmoja tu (The One). 68. As-Swamadu Mwenye kukusudiwa kwa kuabudiwa, kuombwa na kutegemewa. 69. Al-Qaadiru Mwenye uwezo wa kufanya au kutofanya kila kitu, Muweza wa kufanya au kutofanya chochote. 70. Al-Muqtadiru Mwenye kudiriki kila kitu, mwenye uwezo wa pekee juu ya kila kitu (The Dominant, The Powerful).71.Al-Muqaddimu Mwenye kutanguliza, mwenye kumleta mja karibu naye. 72. Al-Muakhiru Mwenye kuakhirisha (The Postaponer). Mwenye kubakisha nyuma Mwenye kumpeleka mja mbali naye(The Deferer). 73. Al-Awwalu Wa mwanzo (The first). 74 Al Aakhiru Wa mwisho (The last). 75. Adh-Dhaahiru Wa dhahiri (The Outward). Haonekani kwa macho, wala hagusiki, wala haonjeki, ila anaonekana kwa akili na hoja zilizo wazi hapa ulimwenguni. 76. Al-Baatwinu Wa siri (The Inward). 77. Al-Waliyyu Gavana (The Governor), Mpanga Mipango ya watu na mwangalizi wa mipango yote. 78. Al-Muta'aali Mtukufu aliye juu (The High Exalted). 79. Al-Barru Mwema (The righteous). 80. At-Tawwaabu Mwenye kupokea Toba za waja wake. 81. Al-Muntaqimu Mwenye kuchukua kisasi, Mlipakisasi kwa waovu. 82. Al-'Afuwwu Mwenye kusamehe madhambi, mfuta madhambi ya waja wake (The Pardoner), Msamehevu. 83. Ar-Rauufu Mpole, Mwenye huruma (The compassionate). 84. Maalikal-Mulki Mwenye kumiliki ufalme wote, Mfalme wa 'Wafalme (The Owner of the Sovereignty) Mwenye kutumia mamlaka yake atakavyo. i85. Dhil-jalaali Wal-Ikraam Mwenye Utukufu na Heshima (The Lord of Majesty and Bounty). 86. Al-Muqsitu Mwenye kukamilisha usawa (The Equitable) Mwenye kutoa usawa, Mtoaji Haki sawa kwa kila anayestahiki. 87. Al-Jaamiu' Mkusanyaji (The gather or The Collector), Mkusanyaji viumbe siku ya mwisho (Kiyama). 88. Al-Ghaniyyu' Mwenye kujitosheleza (The self Sufficient), Hahitaji chochote kwa yeyote (The Independent, The absolute), Tajiri (The Rich). 89. Al-Mughnii Mwenye kutajirisha (The Enricher), mwenye kutosheleza viumbe kwa kila wanachohitajia. 90. Al-Maaniu' Mwenye kusalimisha viumbe kutokana na mabaya, mwenye kuzuia viumbe visidhurike, mwenye kunusuru (The Preventer, The Witholder). 91. Adh-Dhaarru Mwenye kuleta shari (Dhara), Mwenye kudhurisha (The Distresser). 92. An-Naafiu' Mwenye kuleta nafuu (Kheri), Mwenye kunufaisha (The Profitor). 93. An-Nuuru Nuru, Mwenye Nuru, Mwangaza (The Light).94.Al-Haadi Mwenye kuongoza waja wake katika kheri mbali mbali (Elimu, Riziki, n.k) Mwongozaji (The Guide). 95. Al-Badiiu' Mwasisi (The Originator). 96. Al-Baaqy Mwenye kubakia Milele, hana mwisho (The Everlasting, Enduring). 97. Al-Waarithu Mrithi, Mwenye Kurithi kila kitu (baada ya wenyewe kufa). 98. Ar-Rashiidu Mwenye kuongoa, mwenye kuongoa waja wake kuiendea njia ya kheri. 99. As-Swabuuru Mwenye kusubiri, mwenye subira (The Patient).
Katika Qur-an sifa za Mwenyezi Mungu zimeelezwa katika aya mbali mbali lakini si kwa mfululizo huu tulioupanga katika Hadith. Ayatul-Qurusiyyu (2:55)
﴿اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ﴾
"Mwenyezi Mungu hakuna Mola ila Yeye. Ndiye mwenye Uhai wa milele. Msimamizi wa kila jambo, kusinzia hakumshiki wala kulala. Ni vyake (peke yake vyote) vilivyomo mbinguni na ardhini.Na nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyomo mbele yao viumbe na yaliyo nyuma yao; Wala (Hao viumbe) hawajui lolote katika ilimu yake, ila kwa alipendalo (mwenyewe). Enzi yake imeenea mbingu na ardhi, wala kuvilinda hivyo hakumshindi, na Yeye pekee ndiye aliye juu (ya kila kitu) na Ndiye Aliye Mkuu." (2:255)
﴿سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١﴾ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢﴾ هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣﴾هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٤﴾ لَّهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٥﴾ يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَهُوَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٦﴾ آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَأَنفِقُوا مِمَّا جَعَلَكُم مُّسْتَخْلَفِينَ فِيهِ فَالَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَأَنفَقُوا لَهُمْ أَجْرٌ كَبِيرٌ﴾
"Kinamtukuza Mwenyezi Mungu kila kilichomo mbinguni na ardhini, na Yeye ndiye mwenye Nguvu, Mwenye Hekima. Ufalme wa mbingu na ardhi ni wake, na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. Yeye ndiye wa mwanzo na ndiye wa Mwisho, na ndiye wa Dhahiri na wa Siri, Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu. Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika nyakati sita, kisha akatawala katika enzi yake. Anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni na yanayopanda humo. Naye Yu pamoja nanyi popote mlipo na Mwenyezi Mungu anaona yote mnayoyatenda. Ufalme wa mbingu na ardhi ni wake na mambo yote yanarudishwa kwa Mwenyezi Mungu. Anaingiza usiku katika mchana na anaingiza mchana katika usiku.Na yeye anajua yaliyomo vifuani.Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na toeni katika yale aliyokupeni. Basi wale walioamini miongoni mwenu na wakatoa, wana malipo makubwa." (57:1-7)
﴿هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿٢٢﴾ هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٢٣﴾ هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴾
"Yeye ndiye Allah.Ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki ila Yeye tu. Ni Mjuzi wa yaliyofichikana na yaliyo Dhahiri. Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Yeye Ndiye Allah, ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki ila yeye tu.Ni Mfalme Mtakatifu, Mwenye Salama, Mtoaji wa Amani, Mwendeshaji wa mambo yake.Mwenye shani, mwenye kufanya alitakalo, Mkubwa (kuliko vyote vikubwa),Allah ametakasika na hao wanaomshirikisha naye.Yeye Ndiye Allah, Muumbaji, Mtengenezaji, Mfanyaji sura, Mwenye majina (sifa) mazuri.Kinamtukuza kila kilichomo mbinguni na ardhini.Naye ni mwenye nguvu mwenye Hikima." (59:22-24).
﴿قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾ اللَّـهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ﴾
Sema: Yeye ni Allah mmoja tu. Allah ndiye anayestahiki kukusudiwa (na viumbe vyote kwa kumuabudu, kumuomba na kumtegemea) Hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hana anayefanana naye hata mmoja. (112:1-4)
UFAFANUZI WA SIFA ZA ALLAH (S.W)
Ukizichunguza kwa makini sifa zote hizi zilizoorodheshwa katika Qur-an na Hadith tunaona kuwa nyingi ya sifa hizi kama vile Ar-Rahmaan na Ar-Rahiim zinafanana au zinakaribia kufanana kwa kiasi ambacho wafasiri wengi wameshindwa kuzipambanua. Hii inadhihirisha ukamilifu wa sifa za Allah (s.w). Sifa hizi zinakienea kila kitu na kukifanya kila kitu katika mbingu na ardhi kiishi na kiwe kama kilivyo. Hapana mwanya wala nafasi iliyoachwa wazi bila ya kufunikwa na sifa za utendaji wa Allah (s.w).
Ni muhimu kwa kila muumini kuzifahamu sifa hizi kwa undani ili ziweze kumuathiri vilivyo katika utendaji wake wa kila siku. Ili kurahisisha kuzifahamu sifa hizi kwa undani, tumezigawanya sifa hizi katika mafungu yafuatayo:
(a) Sifa au majina ya Allah yanayoonesha kuwepo kwake na umoja wa Uungu wake.
(b) Majina ya Allah yanayoonesha ujuzi wake usio na mipaka.
(c) Majina ya Allah yanayoonesha upweke wake wa utawala na Utukufu wake.
(d) Sifa za Allah zinazoonesha Uadilifu wake usio na mipaka.
(e) Sifa za Allah zinazoonesha Urehemevu, Upendo na Usamehevu wake usio na mipaka.
(A) SIFA AU MAJINA YA ALLAH YANAYOONESHA KUWEPO KWAKE NA UMOJA WAKE, UUNGU WAKE NA UUMBAJI WAKE.
1. Allah Hili ni jina Dhati Pekee la Mungu Muumba Mmoja na Mpweke. Jina hili halifasiriki katika lugha yoyote.Mitume wote wamemtaja Mungu Muumba Mmoja Mpweke kwa jina hili la Allah.
2. Al-Waahid - Mmoja Pekee
3. Al-Ahad - Yeye ni Mmoja Sifa hizi zinasisitiza kuwa Allah (s.w) ni mmoja tu na hagawanyiki kama wanavyodai wakristo na Washirikina. Aya zifuatazo zinafafanua sifa hizi:
﴿وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴾
"Hapana Mungu ila Allah.Hakika Allah ni mwenye nguvu na mwenye hekima" (3:62)
﴿ إِنَّ إِلَـٰهَكُمْ لَوَاحِدٌ ﴿٤﴾ رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ الْمَشَارِقِ﴾
"Kwa yakini Mungu wenu ni Mmoja tu. Mola wa mbingu na ardhi na yaliyomo kati yake, na ni Mola wa mashariki (na Magharibi zote)". (37:4-5)
﴿قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ﴾
"Sema (ee Mtume): Yeye ni Mungu mmoja tu. Na hakika mimi ni mbali na hao mnaowashirikisha (naye)". (6:19)
4. As-Swamad- Mkusudiwa, Mstahiki kutegemewa na kila mtu. Kwake Yeye vinategemea vyote na Yeye ni mwenye kujitosheleza.Hategemei chochote.
5. Al-Haqq Mkweli, Yeye ni wa Haki. Msimamisha Haki.'
6. Al-Awwal Wa mwanzo, yeye ni mwanzo.
7. Al-Aa'Khir Wa mwisho, Yeye ni mwisho.
8. An-Nuur Yeye ni Nuru. Yeye ni mwanga.
9. Adh-Dhaahir Mdhihiri, Aliyedhihirika, Mdhihirishaji.
10. Al-Baatwin Msiri; Mjua yote ya siri. I
11. Al-Muhy Mwenye kutoa maisha, Mwenye kuhuisha.
12. Al-Hayy Aliye hai milele. Yeye ni Mhai.
13. Al-Qayyuum Mwenye Uhai wa maisha. Mwenye Kubakia Milele. Aya ifuatayo inaitaja sifa hii:
﴿ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ﴾
"Mwenyezi Mungu hakuna Mola ila Yeye, Ndiye mwenye Uhai wa Maisha (wa kudumu) " (2:255)
14. Al-Waajid Mwenye kuwepo nyakati zote (hana mwanzo wala mwisho).
15. Al-Badiiu' Mwanzilishi (Mzushi) Pekee wa kila kitu. Aya zinazoidhihirisha sifa hii ya Allah:
﴿بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ﴾
"Yeye ndiye mwanzilishi wa mbingu na ardhi pasina ruwaza; na anapotaka jambo basi huliambia tu "kuwa", nalo huwa" (2:117).
﴿ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ﴾
"Huyo ndiye Allah, Mola wenu, hakuna anayeabudiwa kwa haki ila Yeye. Muumba wa kila kitu.Kwa hiyo mwabuduni Yeye (tu). Naye ni Mlinzi wa kila kitu" (6:102)
16. Al-Mubdiu Mwanzilishi wa kila kitu. Sifa hii inafafanuliwa vema na aya ifuatayo:
﴿أَوَلَمْ يَرَوْا كَيْفَ يُبْدِئُ اللَّـهُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ﴾
"Je,hawaoni jinsi (Mwenyezi Mungu) aanzishavyo viumbe,kisha atavirudisha (mara ya pili). Hakika kwa Mwenyezi Mungu hayo ni sahali" (29:19)
17. Al-Baaqii - Mwenye kubakia milele.Aya zifuatazo zinafafanua sifa hii ya Allah (s.w):
﴿كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ ﴿٢٦﴾ وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ﴾
"Kila kilicho juu yake (ardhi na mbingu) kitatoweka.Inabakia dhati ya Mola wako tu, Mwenye utukufu na heshima" (55:26-27)
﴿وَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ لَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴾
"Wala usimuombe - pamoja na Mwenyezi Mungu - mungu mwingine, hakuna aabuduwaye kwa haki ila Yeye, kila kitu kitakufa isipokuwa Yeye tu. Hukumu ya mambo yote iko Kwake na Kwake mtarejeshwa (nyote)". (28:88)
18. Al-Khaaliq Muumbaji, mwanzilishi wa viumbe.
19. Al-Baariu Mtengenezaji, Mwanzilishi.
20. Al-Muswawwiru Mtengenezaji wa sura, muumbaji wa sura.
21. Al-Mu'iid Mwenye kurejeza. Aya ifuatayo inafafanua sifa hii ya Allah (s.w):
Marejeo yenu nyote ni kwake, na ahadi ya Allah ni haki. Hakika Yeye ndiye aliyeanzisha viumbe na ndiye atakayewarejeza, ili awalipe kiuadilifu wale waliamini na kufanya vitendo vizuri"(10:4)
22. Al-Muhyii Muhuishaji.Mwenye kuvifanya viumbe viishi kutoka kwenye ufu.
23. Al-Mumiitu Mfishaji, Mwenye Uwezo pekee wa kufisha vilivyo hai. Aya ifuatayo inafafanua:
﴿وَإِنَّا لَنَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَنَحْنُ الْوَارِثُونَ﴾
"Na sisi ndio tunaohuisha na tunaofisha, na sisi ndio warithi(wa vyote)".(15:23).
24. Al-Waarith Mrithi, Mrithishaji.
﴿وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ بَطِرَتْ مَعِيشَتَهَا فَتِلْكَ مَسَاكِنُهُمْ لَمْ تُسْكَن مِّن بَعْدِهِمْ إِلَّا قَلِيلًا وَكُنَّا نَحْنُ الْوَارِثِينَ﴾
"Na tumeiangamiza miji mingapi iliyojifaharisha juu ya maisha yao! Hayo maskani yao yasiyokaliwa baada yao tena ila kidogo tu hivi, na sisi tumekuwa warithi (wa sehemu hizo)"(28:58)
25. Al-Baa'ith Mfufua wafu kutoka makaburini.
﴿وَأَنَّ السَّاعَةَ آتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَأَنَّ اللَّـهَ يَبْعَثُ مَن فِي الْقُبُورِ﴾
"Na kwamba Kiyama kitakuja hapana shaka ndani yake; na kwa hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini" (22:7)
26. Al-Jaamiu' Mkusanyaji wa watu wote siku ya Malipo.
﴿رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ﴾
"Mola wetu! Wewe ndiye mkusanyaji wa watu siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi" (3:9)
27. Al-Muakh-khir Mwenye kuakhirisha, Mwenye kuchelewesha viumbe mpaka ufike muda wao.
28. Al-Muqaddim Mwenye kutanguliza, Mtangulizaji. Sifa zote hizi zinatupa picha kamili juu ya Allah (s.w) na uwezo wake wa Kiungu usiopatikana kwa kiumbe yeyote yule. Kwa muhtasari sifa hizi zinatufahamisha kuwa Allah (s.w) ni Mungu mmoja tu na Mpweke, ambaye hana mwanzo wala mwisho. Amekuwepo nyakati zote na atakuwepo milele. Hana mwanzilishi wake bali Yeye mwenyewe ni chanzo na vyote vimetokana na Yeye. Ni mwenye kujitegemea kwa kila kitu, na vyote vinategemea kwake kwa kila kitu kinachohusu kuwepo kwao, uhai wao na maisha yao kwa ujumla. Ndiye pekee anayemiliki maisha ya watu na viumbe vyote baada ya maisha ya hapa duniani.Ni dhahiri kwamba hapana kiumbe yeyote mwenye hata chembe ya sifa hizi. Hivyo kumtegemea kiumbe yoyote badala ya Allah ni ujahili wa hali ya juu.
(B) MAJINA YA ALLAH (S.W) YANAYOONESHA UJUZI WAKE USIO KIKOMO
29. Al-Baasitu Mkunjuaji, anakienea kila kiumbe. Sifa hii inafafanuliwa vyema katika aya ifuatayo:
﴿اللَّـهُ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ وَفَرِحُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا مَتَاعٌ﴾
"Allah hukunjua riziki kwa amtakaye na huidhikisha (kwa amtakaye)".(13:26)
30. Al-'Aliim Mjuzi wa kila kitu. Mjuzi wa yote.
31. Al-Hakiim Mwingi wa Hekima.
32. Al-Khabiiru Mwingi wa khabari, mwenye khabari zote.
33. As-Samiiu' Msikivu, Mwenye kusikia pasina mipaka.
34. Al-Baswiiru Mwenye kuona kila kitu; Mwenye kuona pasina mipaka. Usikivu na uoanaji wa Allah (s.w), hauna mipaka na ni wa kudumu milele.
35. Ash-Shahiid Shahidi, Mwenye kushuhudia kila kitu na kila tukio.
﴿إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئِينَ وَالنَّصَارَىٰ وَالْمَجُوسَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا إِنَّ اللَّـهَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ﴾
"Hapana jambo lolote linalotendeka bila Allah (s.w) kuwa shahidi juu ya jambo hilo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi juu ya kila kitu". (22:17).
36. Al-Mujiib Mwenye kujibu maombi.
37. Ar-Rashiid Mwenyezi Mungu Mwongozi wa njia ya sawa, mwenye kuelekeza katika mwenendo mzuri. Yeye ni mfundishaji na muongozaji. Yeye Mwenyewe ni mwongofu. Sifa hizi za Allah (s.w) zinatupa picha kamili juu ya ujuzi wake uso mipaka. Ni Allah (s.w) pekee anayestahiki kutegemewa kwa kila kitu kwani Ndiye pekee anayetujua fika tulivyo na ndiye pekee anayedhibiti kila tendo letu na kila tukio litokealo popote ardhini na mbinguni. Anatukumbusha hili katika aya zifuatazo:
﴿وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ﴾
"Na ziko kwake funguo za siri, hakuna azijuuaye ila Yeye tu, na Anajua yaliyomo barani na baharini. Na Halianguki jani ila analijua. Wala haianguki punje katika giza la ardhi (ila anaijua). Wala (hakianguki) kilichorutubika wala kilichoyasibika (ila anakijua). (Hapana chochote) ila kimo katika kitabu kidhihirishacho (kila jambo)" (6:59)
﴿أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴾
"Je,huoni kwamba Allah anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini? Haupatikani mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa wanne wao, wala wa tano ila yeye huwa ni wasita wao, wala wa wachache kuliko hao wala zaidi ila Yeye huwa pamoja nao popote walipo; kisha siku ya kiyama Atawaambia waliyoyatenda. Hakika Allah ni Mjuzi wa kila kitu" (58:7)
﴿وَرَبُّكَ يَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴾
"Na Mola wako Anayajua yanayoficha vifua vyao na wanayoyadhihirisha" (28:69)
﴿وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ ﴾
"Na bila shaka tumemuumba mtu, nasi tunajua yanayopita katika nafsi yake.Nasi tu karibu naye zaidi kuliko mshipa wa shingo (jugular vein) (50:16)
pamoja na aya hizi chache tulizozinukuu hapa, sifa hizi zimerejewa mahala pengi katika Qur-an ili kuonesha kwa uwazi ujuzi wa Allah (s.w) usio mipaka. Kwa muhtasari sifa hizi za Allah zinatuyakinishia kuwa Allah (s.w) ni Mjuzi wa kila kitu na ni Mwenye hekima isiyo na mipaka. Hakuna chochote kile kinachofichikana kwake, kiwe kimedhihirishwa kwa kusema au kwa kutenda au kiwe kimefichwa moyoni Allah (s.w) anakiona na anakijua. Hivyo muumini wa Allah (s.w) aliyeelewa fika sifa hizi anatarajiwa awe mkweli mno katika kila kipengele cha maisha yake ya kila siku kwani ana hakika kuwa hakuna siri mbele ya Allah (s.w) na ana uhakika kuwa Allah (s.w) atafichua siri zake zote kama si hapa duniani, huko akhera ni lazima.
(C) MAJINA YA ALLAH YANAYOONESHA UPWEKE WA UTAWALA, NGUVU NA UTUKUFU WAKE
38. Al-AziizMtukufu mwenye nguvu.
39. Al-Jabbaar Mwenye nguvu juu ya kila kitu.
40. Al-Mutakabbir Mwenye kumiliki nguvu zote, Mwenye haki ya kiburi.
41. Al-Maalik Mmiliki wa kila kitu na kila jambo.
﴿مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ﴾
"Mwenye kumiliki siku ya malipo" (1:4)
42. Al-Malik Mfalme wa kila kitu.
43. Maalikul-Mulki Mmiliki wa Ufalme. Mmiliki wa Falme zote zilizomo mbinguni na ardhini. Tunapata ufafanuzi wa sifa hii katika aya ifuatayo:
﴿قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ بِيَدِكَ الْخَيْرُ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴾
Sema (katika kumsifu Mwenyezi Mungu): "Ee Mola uliyemiliki Ufalme wote, humpa ufalme umtakaye, na humuondolea ufalme umtakaye, bila shaka Wewe ni Muweza juu ya kila kitu". (3:26)
44. Al-'Adhiim Mkuu, Mkubwa kwa utukufu, Mwenye enzi.
45. Al-'Aliyuu Mwenye daraja ya juu ya utukufu, Mtukufu wa watukufu.
46. Al-Qawiyyu Imara, Mwenye nguvu. Aya ifuatayo inafafanua sifa hizi
﴿اللَّـهُ لَطِيفٌ بِعِبَادِهِ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ ﴾
Mwenyezi Mungu ni mpole kwa waja wake; anampa riziki amtakaye, naye ni mwenye nguvu, Mwenye kushinda". (42:19)
47. Al-Qahharu Mtenza nguvu. Mwenye nguvu juu ya kila kitu. Aya ifuatayo inafafanua vyema sifa hii:
﴿يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴾
Enyi wafungwa wenzangu wawili! Je! Waungu wengi wanaofarikiana ndio bora au Mwenyezi Mungu mmoja Mwenye nguvu (juu ya kila kitu)" (12:39)
48. Al-Matiin Mwenye nguvu madhubuti, mwenye nguvu za kudumu, mwenye nguvu zisizokatika. Aya ifuatayo inadhihirisha sifa hii:
﴿إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ﴾
"Kwa yakini Mwenyezi Mungu ndiyo mtoaji wa riziki,mwenye nguvu madhubuti". (51:58).
49. Dhuljalaali-wal-Ikraam Bwana mtukufu, Mwingi wa Heshima.
﴿تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴾
"Limetutuka jina la Mola wako Mwenye utukufu na heshima" (55:78)
50. Al-Jaliil Mtukufu na mwenye kuheshimika.
51. Al-Majiid Mtukufu, anayestahiki kutukuzwa. Wakasema (wale Malaika):
﴿قَالُوا أَتَعْجَبِينَ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ رَحْمَتُ اللَّـهِ وَبَرَكَاتُهُ عَلَيْكُمْ أَهْلَ الْبَيْتِ إِنَّهُ حَمِيدٌ مَّجِيدٌ﴾
"Je,unastaajabu amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii. Hakika Yeye ndiye anayestahiki kusifiwa na kutukuzwa" (11:73)
52. Al-Maajid Mtukufu anayestahiki kutukuzwa. 53. Al-Muta'al Mtukufu wa daraja. Aliye juu kwa daraja.
﴿عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْكَبِيرُ الْمُتَعَالِ ﴾
"Mjuzi wa siri na dhahiri, mkuu aliye juu" (13:9)
54. Al-Quddus Mtakatifu. Aliyetakasika na kila udhaifu.
55. Al-Kabiir Mkubwa kwa cheo na kwa kila kitu.
56. Al-Muqtadiru Mwenye uwezo juu ya kila kitu. Mwenye uwezo mkubwa na mwenye nguvu za kudiriki kila kitu na kila jambo. Aya ifuatayo inadhihirisha sifa hii:
﴿كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذْنَاهُمْ أَخْذَ عَزِيزٍ مُّقْتَدِرٍ ﴾
"Wakakadhibisha hoja zetu zote, kwa hiyo tukawatesa kama anavyotesa, Mwenye nguvu, mwenye uwezo". (54:42)
57. Al-Qaadiru Mwenye uwezo mkubwa wa kuendesha kila kitu kama inavyostahiki.
58. Al-Qadiiru Mwenye uwezo mkubwa na Mwenye nguvu. Sifa hizi za al- Qaadir na Al-Qadiiru zina maana sawa na ile ya Al-Muqtadir. Yote haya yanaonesha utawala na mamlaka ya Allah (s.w) juu ya kila kitu. Aya ifuatayo inafafanua:
﴿تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴾
"Ametukuka yule ambaye mkononi mwake umo ufalme (wote): Naye ni mwenye uweza juu ya kila kitu". (67:1)
59. Al-Mu'izzu Mpandishaji wa daraja, mtunuki daraja na cheo.Hatukuki asiyemtukuza.
60. Al-Mudhillu Mwenye kudhili, mwenye kunyongesha, mwenye uwezo pekee wa kumdhalilisha asiyemtukuza. Kwa ufafanuzi wa sifa hizi mbili, hebu turejee tena aya ifuatayo:
﴿قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ بِيَدِكَ الْخَيْرُ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴾
Sema: "Ee Mola uliomiliki ufalme wote! Humpa ufalme umtakaye, na humuondolea ufalme umtakaye, na humtukuza umtakaye, na humdhalilisha umtakaye, kheri imo mikononi mwako.Bila shaka wewe ni muweza juu ya kila kitu".(3:26)
61. Al-Khaafidhu Mfedheheshaji.
62. Ar-Raafi'u Mtukuzaji, Mpandishaji daraja. Sifa hizi mbili zinaonekana katika aya ifuatayo:
﴿إِذَا وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ ﴿١﴾ لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَةٌ ﴿٢﴾ خَافِضَةٌ رَّافِعَةٌ ﴾
"Litakapotokea tukio (hilo la kiyama) ambalo kutokea kwake si uwongo.Lifedheheshalo (wabaya) na litukuzalo (wazuri)" (56:1-3)
Pia katika Qur-an Allah (s.w) amejitaja kwa jina la "Raafi'uddarajaat". Mpandishaji cheo na daraja.
﴿رَفِيعُ الدَّرَجَاتِ ذُو الْعَرْشِ يُلْقِي الرُّوحَ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ لِيُنذِرَ يَوْمَ التَّلَاقِ﴾
"Yeye ndiye mwenye vyeo vya juu kabisa,Mwenye enzi. Hupeleka Wahyi wa amri yake kwa amtakaye miongoni mwa waja wake ili kuwaonya (viumbe) siku ya kukutana (naye)." (40:15)
63. Al-Walliyyu Mlezi wa kila kiumbe.
64. Al-Waaliy Muhifadhi wa viumbe vyote vilivyomo mbinguni na ardhini.
65. As-Salaam Chanzo cha amani na ukamilifu. Mtoa amani. 66. Al-Mu'min Mhifadhi na mlezi wa imani.
67. Al-Muhayminu Mwangalizi, mlezi, mchungaji wa usalama wa viumbe.
68. Ar-Raqiib Mwangalizi, Mchungaji. Sifa hii inadhihirishwa na aya ifuatayo:
﴿ مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ﴾
"Sikuwaambia lolote ila yale uliyoniamrisha ya kwamba: Mwabuduni Mwenyezi Mungu Mola wangu na Mola wenu'.Na nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao, na uliponikamilishia muda wangu. Wewe ukawa mchungaji juu yao, na wewe shahidi juu ya kila kitu". (5:117)
69. Al-Wakiil, Mlinzi
﴿الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ ﴾
"Wale ambao watu (waliokodiwa na Makurayshi) waliwaambia (Waislamu): 'Watu wamekukusanyikieni. Kwa hiyo waogopeni'.Lakini maneno hayo yakawazidishia imani wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha.Naye ni mlinzi bora kabisa" (3:173).
70. Al-Haafidh Muhifadhi, Mlinzi.
71. Al-Hafiidh Muhifadhi, Mlezi, Mlinzi.
72. Al-Waasi'u Mwenye wasaa mkubwa.
73. Al-Muqiitu Mwongozi, Mwangalizi, Mtawala juu ya kila kitu.
74. Al-Muhsiy Mdhibiti wa kila kitu. Hapana jambo lolote linalofanywa na linalotendeka lililo nje ya udhibiti wake.
75. Al-Mughnii Mtajirishaji, mnawirishaji.
76. Al-Maani'u Mzuiliaji.
77. Al-Qaabidh Mwenye kuzuia, mwenye kunyima
78. Adh-dhaarru Mnyongeshaji, Mwenye kudhuru. Hapana anayedhuru, kudhuru Kwake na hapana yeyote anayeweza kuokoa chochote kilichodhuriwa na Allah. Aya ifuatayo inafafanua vyema:
﴿وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ قُلْ أَفَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّـهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ أَوْ أَرَادَنِي بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ قُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ﴾
"Na ukiwauliza: 'Na nani aliyeziumba mbingu na ardhi?" Bila shaka watasema: Ni Mwenyezi Mungu, Je mnawaonaje wale mnaowaomba kinyme cha Allah, kama Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondolea dhara yake?Au akitaka kunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake?" Sema:'Mwenyezi Mungu ananitosha, kwake wategemee wategemeao". (39:38)
Sifa zote hizi zinatupa picha kamili juu ya utalawa wa Allah (s.w) na uwezo wake juu ya kila kitu. Kutokana na sifa hizi tunafahamu kuwa Allah (s.w) Ndiye pekee aliyeumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo na ndiye pekee anayevilea, anayevilinda, anayevikuza na kuviendeleza na ndiye pekee anayeviongoza mpaka kufikia lengo la kuumbwa kwao. Allah (s.w) hahitaji msaada au ushauri kutoka kwa yeyote katika kutekeleza ridhaa yake juu ya viumbe vyake.Pia hahitaji zana au juhudi katika kulitekeleza alitakalo. Akitaka chochote kiwe ni kukiamrisha: "Kuwa" na kikawa pale pale na vile vile atakavyo.
Tukizingatia sifa hizi za Allah (s.w) tutaona kuwa, hapana yeyote anayestahiki kunyenyekewa, kuogopwa na kutegemewa kinyume na Allah (s.w). Ni wazi kuwa hapana yeyote mwenye uwezo wa kumdhuru yeyote, aliyepata hifadhi ya Allah (s.w). Kinyume chake hapana yeyote anayeweza kumnusuru aliyehukumiwa kudhurika na Allah (s.w). Kwa kufahamu hivi, muumini wa kweli hatarajiwi kumuogopa na kumchelea yeyote katika kutekeleza amri ya Allah (s.w). Historia inatuonesha kuwa Mitume wa Allah (s.w) na wale walioamini pamoja nao, hawakutetereka kamwe katika kutekeleza amri za Allah (s.w) kwa kuwa walifahamu kwa yakini kuwa hakuna yeyote atakayewasaidia dhidi ya adhabu ya Allah (s.w). Allah (s.w) anatukumbusha hili katika aya ifuatayo:
﴿قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا﴾
Sema: Waiteni wale mnaodai (kuwa wana uwezo) mkamwacha Yeye (Allah). Hawataweza kukuondosheeni shari wala kubadilisha (kuwa kheri). (17:56).
(D) SIFA ZA ALLAH (S.W) ZINAZOONESHA UADILIFU WAKE USIO NA MIPAKA
Pamoja na kwamba Allah (s.w) anatawala kila kitu na ana uwezo wa kufanya lolote apendalo dhidi ya kiumbe chochote, amejilazimishia uadilifu. Kila kiumbe anayestahiki kupata hiki au malipo fulani kutokana na ahadi yake, atamlipa kwa uadilifu. Sifa zifuatazo zinaonesha uadilifu wake katika kuwahukumu na kuwalipa waja wake.
79. Al-Hakamu Yeye ni Hakimu. Hakimu anayejitosheleza, asiyehitaji ushauri, msaada au ushahidi kutoka kwa yeyote. Ni hakimu aliyemjuzi kamili wa kesi anayoihukumu. Aya zifuatazo zinafafanua sifa hii:
﴿وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ ﴾
"Na Nuhu alimuomba Mola wake (alipomuona mwanawe anaangamia) akasema: "Ee Mola wangu! Mwanangu ni katika watu wa nyumbani kwangu (mbona anaangamia)? Na hakika ahadi yako ni haki, nawe ni mwenye kuhukumu kwa haki kuliko mahakimu (wote)" (11:45)
80. Al-'Adilu Mwadilifu
81. Al-Muqsit Mwenye kuhukumu kwa haki, Muadilifu.
82. Al-Fattaah Jaji Mkuu, Mbora wa mahakimu. Sifa hii inarejewa katika Qur-an kama ifuatavyo:
﴿رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ﴾
"Mola wetu! Hukumu baina yetu na baina ya wenzetu kwa haki, Nawe ndiye Mbora wa wanaohukumu" (7:89).
83. Al-Muntaqim Mwenye kulipa kisasi na kuwaadhibu waovu. Aya zifuatazo zinafafanua sifa hii:
﴿وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ﴾
"Na nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayekumbushwa kwa aya za Mola wake kisha akazikataa?Hakika sisi ni wenye kuchukua kisasi kwa wale wabaya". (32:22)
﴿وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴾
"Na iogopeni adhabu ambayo haitowasibu pekee yao wale waliodhulumu nafsi zao katika ninyi.Na mcheni Mwenyezi Mungu.Hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu" (8:25)
84. Al-Hasiib Mpweke katika kuhesabu. Tunapata ufafanuzi wa sifa hii katika aya ifuatayo:
﴿وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَسِيبًا ﴾
"Na mnapoamkiwa na maamkio yoyote yale, basi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo. Hakika Mwenyezi Mungu anafanya hisabu ya kila kitu" (4:86)
85. As-Sabuur Msubirifu, Mwingi wa subira. Tukizingatia sifa hizi za Allah (s.w) tunaona kwa yakini kuwa mja hana njia yoyote ya kuepa hukumu ya Allah (s.w). Hakimu atakuwa ni Allah (s.w) mwenyewe na hapana njia yoyote ya kupata upendeleo wowote mbele ya mahakama ya Allah (s.w). Muumini yeyote aliyeelewa vyema sifa hizi anatarajiwa awe muadilifu katika kila kipengele cha maisha yake yote na ahukumu kila jambo kwa haki. Kwani kila hukumu iliyopitishwa kinyume na haki, Mwenyezi Mungu ataihukumu kwa haki na kumlipa haki aliyestahiki na kumuadhibu vikali aliyeizuia haki.
(E) SIFA ZA ALLAH (S.W) ZINAZOONESHA UREHEMEVU, USAMEMEHEVU NA UPENDO WAKE KWA WAJA WAKE
Allah (s.w) pia ana sifa zifuatazo ambazo hukamilisha Uungu wake na kukidhi mahitajio yote ya viumbe. Pamoja na sifa za upweke wa Uungu wake, upweke wa uwezo wake wa kuumba, kukuza, kulea, kunawirisha, kuendeleza na kuvimiliki kwa udhibitifu mbingu na ardhi na vyote vilivyomo, na pamoja na upweke wa uadilifu wake katika kuwahukumu waja wake na kuwalipa malipo yanayostahiki, Allah (s.w) vile vile ni mwingi wa rehema, mwingi wa kusamehe, mwingi wa huruma na upendo kwa viumbe vyake. Hebu tuzingatie sifa zifuatazo:
86. Ar-Rahmaan Mwingi wa Rehema, Mwingi wa Ukarimu.
87. Ar-Rahiim Mwenye kurehemu, Mwingi wa Huruma. Sifa hizi zimewekwa pamoja, japo hatuoni tofauti kubwa katika tafsiri, ili kukamilisha sifa ya Urehemevu wa Allah (s.w). Hapana yeyote katika waja wake anayekirimu na kuhurumia viumbe vyake, mfano wa kukirimu na kurehemu kwake.
88. Al-Kariim Mkarimu, Mwingi wa Ukarimu.
89. Ar-Razzaaq Mwingi wa kuruzuku, Mruzuku pekee. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ndiye mtowaji wa riziki, Mwenye nguvu madhubuti (51:58) 90. Al-Mu-'utii Mwingi wa kutoa, Mpaji. Aya ifuatao inafafanua sifa hii:
﴿قَالَ رَبُّنَا الَّذِي أَعْطَىٰ كُلَّ شَيْءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدَىٰ ﴾
(Musa) akasema: "Mola wetu ni Yule aliyekipa kila kitu umbo lake kisha akakiongoza. (20:50)
91. Al-Wahhaab Mpaji mkuu.Mpaji pasina hesabu. Katika Qur-an tunafahamishwa:
﴿رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴾
Mola wetu! Usiache nyoyo zetu kupotea baada ya kuwa tayari umeziongoza, na utupe rehma kutoka kwako. Hakika Wewe ndiwe Mpaji mkuu.(3:8)
92. Al-Barru Mwema pekee. Mfadhili. Qur-an inaieleza sifa hii katika aya ifuatayo:
﴿إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴾
"Hakika sisi zamani tulikuwa tukimuabudu yeye (tu).Hakika Yeye Ndiye Mwema Mwenye rehma" (52:28)
93. An-Naafiu' Mwenye kunufaisha.
94. Ash-Shakuur Mwenye shukurani, Mshukuriwa. Sifa hii tunaipata katika aya zifuatazo:
﴿لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴾
"Ili awape ujira wao kamili na kuwazidishia fadhila zake.Hakika Yeye ni mwingi wa msamaha, Mwenye shukurani" (35:30)
﴿وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي أَذْهَبَ عَنَّا الْحَزَنَ إِنَّ رَبَّنَا لَغَفُورٌ شَكُورٌ ﴾
"Na watasema (katika kushukuru kwao) sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, aliyetuondolea huzuni,kwa yakini Mola wetu ni mwingi wa msamaha, mwenye shukurani". (35:34)
95. Al-Ghaffaaru Msamehevu, Mwingi wa usamehevu. Tunaikuta sifa hii katika aya ifuatayo:
﴿وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِّمَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَىٰ﴾
"Na hakika Mimi ni Mwenye kusamehe sana kwa anayetubia na kuamini na kutenda mema, tena akashika uongofu (bara bara)". (20:82)
96. Al-Ghafuuru Mwenye kusamehe, Mwingi wa Kusamehe.
97. At-Tawwaabu Mwenye kupokea toba.
98. Al-'Afuwwu Mwingi wa msamaha, Mtoaji msamaha.
99. Al-Haliimu Mpole.
100.Al-Waduud Mpenda, Aliyejawa na upendo.
101.Ar-Rauufu Mwingi wa upendo na huruma.
102.Al-Latiifu Mpole, Mwema sana, Laini kwa upole, Mwenye huruma sana.
103.Al-Haadii Mwongozaji.
104.Al-Hamiidu Mwenye kusifika, Mstahiki sifa pekee, Msifiwa. Hizi ndizo sifa za Allah (s.w) kama zinavyojitokeza kwenye Qur-an na Hadithi. Kila muumini hana budi kuzifahamu na kuzizingatia sifa hizi ili aweze kuishi maisha anayoyaridhia Allah katika kila hatua na kila kipengele cha maisha yake ya kila siku.
Mja anayemuamini Allah na kumfahamu vyema kwa sifa zake, anatarajiwa awe na msimamo madhubuti katika kutekeleza amri zote za Allah (s.w) na kusimamisha ufalme wake hapa ulimwenguni, kwani ana yakini kuwa mahitaji yake yote ikiwa ni pamoja na ulinzi, hifadhi, huruma, upendo na msamaha juu ya udhaifu wake yako mkononi mwa Allah (s.w) peke yake. Ana yakini kuwa akimtegemea yeyote kwa mahitaji hayo atakuwa amejiyumbisha na kujidhulumu mwenyewe nafsi yake, kujidhulumu kukubwa kusiko na kifani.
Maana ya Kumuamini Allah (s.w) katika Utendaji wa kila siku Hatua ya tatu na ya mwisho katika kuiendea Imani ya kweli juu ya Allah (s.w) ni hatua ya utendaji. Hivyo kiutendaji anayemuamini Allah (s.w) ni yule anayefuata maamrisho yake yote na kuacha makatazo yake yote pamoja na kuyaendea maisha yake ya kibinafsi na ya kijamii kwa kufuata mwongozo wake pekee - Rejea kurasa za mwanzo juu ya "Nani Muumini?" Aidha Muumini wa kweli ni yule atakayejitenga mbali na aina zote za shirk. Shirk ni kujaalia kinadharia au kiutendaji kuwa yupo mungu au miungu wengine pamoja na Allah (s.w) wanaosaidiana kuendesha nidhamu ya ulimwengu.
Kuna aina kuu nne za shirk:-
1.Shirk katika Dhati ya Allah (s.w). 2. Shirk katika sifa za Allah (s.w).
3. Shirk katika Hukumu za Allah (s.w)
4. Shirk katika Mamlaka ya Allah (s.w).
Shirk katika Dhati ya Allah (s.w) Kumshirikisha Allah (s.w) katika dhati yake ni kuchukua vitu au viumbe kama vile masanamu, hirizi, majabali, moto, ngombe, binadamu, n.k. na kuvinasabisha na Uungu na kuvielekea kwa unyenyekevu kwa kuviomba na kuvitegemea kama anavyostahiki kuombwa na kutegemewa Allah (s.w). Shirk katika Sifa za Allah (s.w) Kumshirikisha Allah (s.w) katika sifa zake ni kukinasibisha au kukipachika kiumbe chochote sifa anazostahiki kusifiwa kwazo Allah (s.w) pekee au kumdunisha Allah (s.w) kwa kumfananisha na viumbe vyake. Hata kumsifu Mtume kupita kiasi ni shirk kama tunavyotahadharishwa katika hadith ifuatayo:
"Imepokelewa kutoka kwa Umar (r.a) kuwa, Mtume (s.a.w.w) amesema: Msizidishe katika kunisifu kama walivyozidisha Wakristo (Manasara) katika kumsifu mwana wa Maryam (Isa (a.s). Mimi ni mja wa Allah tu kwa hiyo niiteni: "Mja wa Allah na Mtume wake" (Sahihi Bukhari).
Pia Waislam wanakatazwa kujisifu na kujitukuza au kuwasifu na kuwatukuza wengine kiasi cha kukiuka mipaka ya Allah (s.w) katika aya ifuatayo:
﴿الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ﴾
"... Yeye ndiye anayekujueni sana tangu alipokuumbeni katika ardhi na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase (msizisifu) nafsi zenu, yeye anamjua sana aliyetakasika" (53:32)
Waumini wa kweli pia wanatarajiwa wawe ni wenye kumtegemea Allah (s.w) pekee kwa kila jambo wanalolihitajia na kuomba moja kwa moja msaada wake, Baraka, Rehema zake, Msamaha wake n.k kwa kutumia sifa zake (majina yake) zinazolandana na yale tuyaombayo:
﴿ قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا﴾
"Sema; mwombeni (Allah) kwa jina la Allah au muombeni (kwa jina la) Rahman, kwa jina lolote mnalomwita (katika haya itafaa); kwani ana majina mazuri mazuri.." (17:110)
Shirk katika Hukumu za Allah (s.w) Kumshirikisha Allah (s.w) katika hukumu zake ni kutoa hukumu kinyume na alivyohukumu Allah (s.w) juu ya masuala mbali mbali. Kwa mfano Allah (s.w) anahukumu kuwa adhabu ya mwizi ni kukatwa kiganja chake cha mkono wa kulia; wazinifu wachapwe viboko mia, n.k. Pakitokea sheria inayotoa hukumu kinyume na Allah (s.w), itakuwa imemshirikisha Allah (s.w) katika hukumu zake. Inasisitizwa katika Qur-an kuwa wale wasiohukumu kwa kufuata sheria ya Allah (s.w) ni Makafiri, Madhalimu na Mafaasiq.
﴿وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ﴾
"Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio Makafiri.Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio Madhalimu.Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio Mafaasiq" (5:44- 47)
Shirk katika Mamlaka (Uongozi wa) ya Allah (s.w) Allah (s.w) ndiye aliyemuumba mwanaadamu kwa lengo na ndiye mwenye haki pekee ya kumuwekea mwanaadamu sharia na mwongozo wa maisha.
Akitokea mtu au kikundi cha watu kuchukua jukumu la kumtungia mwanaadamu sheria kinyume na ile ya Allah na kumtaka atii sheria hiyo ni kuchukua nafasi ya Allah (s.w). Hivyo atakayewaamrisha watu wamtii kinyume na sharia ya Allah (s.w) au atakaye waamrisha watu waishi kinyume na mwongozo wa Allah (s.w) atakuwa amechukua nafasi ya Uungu. Mayahudi na Wakristo wameshutumiwa katika Qur-an:
﴿اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَـٰهًا وَاحِدًا لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴾
"Wamewafanya wanazuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu..." (9:31)
Mtume(s.a.w.w) katika kufafanua aya hii ameeleza kuwa kuwafanya wanazuoni au viongozi wengine kuwa mungu badala ya Allah (s.w) ni kuwatii kinyume na sharia ya Allah (s.w). Hivyo kukitii kiumbe chochote kinyume na utii kwa Allah (s.w) ni kukifanya kiumbe hicho mungu. Kina cha Uovu wa Shirk Shirk ni dhambi kubwa kuliko zote kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:
﴿إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴾
"Hakika Allah hasamehi (dhambi ya) kushirikishwa na kitu na husamehe yasiyo haya kwa amtakaye. Na anayemshirikisha Allah bila shaka amebuni dhambi kubwa" (4:48)
﴿إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴾
"Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi (dhambi ya) kushirikishwa na kitu na husamehe yasiyokuwa haya kwa amtakaye.Na anayemshirikisha Allah bila shaka yeye amepotea upotofu ulio mbali." (4:116)
Dhambi ya shirk hufuta mema yote aliyoyatenda mja kabla ya kushirikisha. "Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa wale waliokuwa kabla yako,kuwa "kama ukimshirikisha (Allah) bila shaka amali zako zitaruka patupu, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye khasara" (39:65)
ZOEZI
2:1 1. Allah (s.w) hatumuoni kwa macho lakini tunamuona kwa akili zetu kwa........................
2."Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana, ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (a.w) kwa wenye akili." (3:190). Ainisha alama kumi (10) zilizo katika maumbile ya mbinguni na ardhini zinazothibitisha kuwepo Allah (s.w).
3. "...Na katika nafsi zenu (pia zimo ishara hizo), Je, hamuoni?" (51:20-22) Orodhesha dalili kumi (10) katika nafsi ya mwanaadamu zinazothibitisha kuwepo Allah (s.w)
4. Kwa kurejea kisa cha watu wa tembo (As-habul-fyl) kilichosimuliwa katika Suratul-fyl (105:1-5) thibitisha kuwepo kwa Allah (s.w).
5. Taja mambo saba (7) katika maisha ya Mitume yanayothibitisha kuwepo kwa Allah (s.w).
6. Taja dalili tatu (3) katika mafundisho ya Mitume zinazothibitisha kuwepo Allah (s.w).
7. Katika Qur-an na Hadithi sahihi tumefahamishwa sifa (majina) mbali mbali za Allah (s.w) ili...........................
8. Eleza kwa muhutasari ni vipi Allah (s.w) hushirikishwa katika: (a) Dhati yake. (b) Sifa zake. (c) Hukumu zake. (d) Mamlaka yake.
9. Kina cha uovu wa shirk kinabainishwa katika Qur-an kuwa:
(a) ............................(b) ...........................(c) ............................
10. Allah (s.w) ameikemea vikali shirk kwa sababu.................
6
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
KUAMINI MALAIKA WA ALLAH (S.W.)
Malaika ni nani? Malaika ni katika waja na viumbe wa Allah(SW) walioumbwa kutokana na nuru. Tunafahamishwa katika hadithi ifuatayo kuwa: Aysha (r.a.) amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:
Malaika wameumbwa na nuru na majini wameumbwa kutokana na ndimi za moto na Adamu ameumbwa kwa udongo kama ilivyoelezwa kwenu (katika Qur'an). (Muslim)
Na katika Qur'an tukufu,Allah(SW) anatubainishia kuwa, katika maumbile yao halisi, malaika ni viumbe wenye mbawa.
﴿الْحَمْدُ لِلَّـهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴾
"Sifa zote njema ni za Allah,Muumba wa mbingu na ardhi. Aliyewafanya malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili-mbili,na tatu tatu, na nne nne.Huzidisha katika kuumba apendavyo.Bila shaka ni mwenye uweza juu ya kila kitu" (35:1)
JE MALAIKA WANAISHI WAPI?
Katika Qur,an tunafahamishwa kuwa Malaika wanayo makazi maalumu lakini si hapa duniani. Allah(SW) anawanukuu malaika wakisema:
﴿وَمَا مِنَّا إِلَّا لَهُ مَقَامٌ مَّعْلُومٌ ﴿١٦٤﴾ وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ ﴿١٦٥﴾ وَإِنَّا لَنَحْنُ الْمُسَبِّحُونَ﴾
Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi. Na kwa yakini katika sisi wapo wajipangao safu. Na wako katika sisi wamtukuzao (Mwenyezi Mungu) (37:164-166)
Kutokana na kazi zao, Malaika wengi tunaishi nao humu humu duniani na wako nasi muda wote.Kila mtu ana malaika wawili wenye kuandika amali zake. Hakika juu yenu kuna wenye kuwatunza, malaika watukufu wenye kuandika.Wanayajua yote mnayoyatenda (82:10-12) Aidha, tunafahamishwa katika Qur,an kuwa kila mmoja wetu ana kundi la malaika mbele na nyuma yake. Ana (kila mtu) kundi (la malaika) mbele yake na nyuma yake.Wanamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. (13:11)
KWANINI HATUWAONI MALAIKA?
Pengine mtu aweza akauliza kuwa kama tumezungukwa na malaika mbele na nyuma, kulia na kushoto, kwanini basi hatuwaoni?
Jibu ni kwamba, mwanadamu yupo kwenye mtihani. Mtihani wenyewe ni kufanya mema kwa kutaraji malipo ya Allah(SW) na kuacha maovu kwa kuogopa adhabu zake.
﴿تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١﴾ الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ ﴾
Ametukuka yule ambaye Mkononi mwake umo ufalme(wote); naye ni mwenye uweza juu ya kila kitu. Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni; ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha (67:1-2)
Malaika ndio wasimamizi wa mtihani huu, na wamefanywa wasionekane machoni petu ili kila mtu atumie uhuru wake wa ama kumuogopa Allah(SW) kwa kutenda mema au kumkufuru Allah(SW) kwa kumuasi.
Lau malaika wangelionekana, watu wengi wangelitenda mema kinafiki(ria) badala ya kufanya kwa ikhilaswi. Mfano wake, ingekuwa kama vile watu wenye dhamira za kufanya uhalifu wanavyojidai watu wema pale wanapokuwepo askari waliovalia rasmi. Utendaji kazi wa malaika ni kama mashushushu au askari kanzu. Mtu muovu anapanga na kutenda maovu akidhani yupo peke yake,kumbe malaika wapo wanaandika.Na ndiyo maana muovu atakapoona kila jambo lake limerikodiwa, atashangaa siku ya kiama kuwa alijulikanaje?
﴿وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَا وَيْلَتَنَا مَالِ هَـٰذَا الْكِتَابِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّا أَحْصَاهَا وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا﴾
Na madaftari yatawekwa mbele yao.Utawaona wabaya wanayaogopa kwasababu ya yale yaliyomo; na watasema: "Ole wetu! Namna gani madaftari haya! Haliachi dogo wala kubwa ila yamelidhibiti.Na watakuta yote yale waliyoyafanya yamehudhuria hapo; na Mola wako hamdhulumu yeyote(18:49)
Siku mtu atakapowaona malaika Kuna siku na muda maalumu ambapo kila mtu binafsi ataanza kuwaona malaika katika umbile lao halisi.
(a) Siku ya kukata roho Hii ni siku na saa ambayo dakika chache baada ya hapo mtu hukata roho na kuiaga dunia. Kwa watu wema, watakuja malaika wa kuwaliwaza:
﴿تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ﴿٣٠﴾ نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ﴾
......Hao huwateremkia Malaika "msigope wala msihuzunike, na furahini kwa pepo mliyokuwa mkiahidiwa. Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na (huku) katika Akhera......"(41:30-31)
Watu wanaotenda maovu watapata mshituko mkubwa na kujawa na huzuni kubwa mno pale watakapowaona Malaika. Watasikitika sana kwa jinsi walivyokuwa wakijidanganya nafsi zao, wakatenda maovu kwa kudhania kuwa hakuna Malaika wanaorekodi matendo yao waliyokuwa wakiyafanya hadharani na mafichoni. Watafadhaika na kusema:
﴿حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ ﴿٩٩﴾ لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ كَلَّا إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَائِلُهَا ﴾
....Mola wangu! Nirudishe(duniani). Ili nifanye mema sasa badala ya yale niliyoyaacha. (Malaika watamwambia): "Hapana! Hakika hili ni neno tu analosema yeye(mtu muovu)....(23:99-100)
(b) Siku ya kiyama Kuanzia pale mtu anapowaona malaika hakutakuwa tena na kizuizi cha kutowaona kama ilivyokuwa hapa duniani. Kuonekana Malaika siku ya kiama itakuwa ni ishara mbaya kwa watu waovu kuwa umeshafika wakati wa wao kuhukumiwa na Allah (s.w) na kuanza kutumikia adhabu za kudumu katika Moto wa Jahannam. Qur'an inatufahamisha kuwa: Siku watakayowaona Malaika haitakuwa furaha siku hiyo kwa wenye makosa; na watasema:
﴿يَوْمَ يَرَوْنَ الْمَلَائِكَةَ لَا بُشْرَىٰ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُجْرِمِينَ وَيَقُولُونَ حِجْرًا مَّحْجُورًا ﴾
"(Mungu) atuepushie mbali adhabu hii iliyotukabili (lakini haitawafaa kitu dua hiyo)(25:22)
(c) Motoni na Peponi Malaika watahudhuria katika uwanja wa hukumu siku ya Kiyama. Kila mtu atawaona wamejipanga safu wakisubiri amri ya Mwenyezi Mungu:
﴿يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّا لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا﴾
Siku ambayo zitasimama Roho na Malaika safu safu; hatasema siku hiyo ila yule ambaye (Allah) Mwingi wa rehema amempa idhini, na atasema yaliyo sawa (78:38)
Wakipewa amri na Allah(s.w) malaika watawakamata waovu na kuwachungachunga kuelekea motoni kuadhibiwa.
﴿وَسِيقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ زُمَرًا حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا فُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَتْلُونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِ رَبِّكُمْ وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا﴾
Na waliokufuru watapelekwa katika Jahannam makundi makundi mpaka watakapoifikia; itafunguliwa milango yake; walinzi wake(malaika) watawaambia: Je! hawakukujieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni aya za Mola wenu na kukuonyeni juu ya makutano ya siku yenu hii(39: 71)
﴿وَسِيقَ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ زُمَرًا حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا وَفُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ﴾
Watu wema watasindikizwa na malaika mpaka kwenye pepo tukufu, na malaika wa huko watawakaribisha. Na walinzi wake(malaika) watawaambia: Amani juu yenu, furahini, na ingieni humu mkae milele(39:73)
SIFA ZA MALAIKA
Malaika Ni viumbe watiifu wasiomuasi Allah(SW) Malaika ni viumbe watiifu kwa Allah(SW). Wakipewa amri ya kumuadhibu mtu muovu,hawagomi wala kumuonea huruma mtu huyo.
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ﴾
Enyi mlioamini! Ziokoeni nafsi zenu na nafsi za watu wenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Juu yake kuna Malaika wakali wenye nguvu.Hawamuasi Allah(SW) katika yale anayowaamuru, na wanatekeleza vile walivyoamrishwa.(66:6)
WANA ELIMU YA KUTOSHA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO
Malaika wana elimu inayowawezesha kutekeleza majukumu yao bila ya kubabaisha. Elimu waliyopewa malaika ni sehemu ndogo sana katika ujuzi wa Allah (SW). Na wenyewe walikiri mbele ya Allah (SW):
﴿قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ﴾
Wakasema: Utukufu ni wako! Hatuna elimu ila ile uliyotufundisha, bila shaka wewe ndiye mjuzi na mwenye hekima (2:32)
HAWANA JINSIA
Malaika hawana jinsia ya kike wala ya kiume.Qur'an inawakosoa watu wanaodhani kuwa malaika ni wanawake. Inahoji:
﴿وَجَعَلُوا الْمَلَائِكَةَ الَّذِينَ هُمْ عِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ إِنَاثًا أَشَهِدُوا خَلْقَهُمْ سَتُكْتَبُ شَهَادَتُهُمْ وَيُسْأَلُونَ﴾
Na wamewafanya malaika ambao ni waja wa Mwingi wa Rehma kuwa ni wanawake. Je wameshuhudia kuumbwa kwao (43:19).
NI VIUMBE WENYE MBAWA
﴿الْحَمْدُ لِلَّـهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴾
"Sifa zote njema ni za Allah, Muumba wa mbingu na ardhi.Aliyewafanya malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili-mbili, na tatu tatu, na nne nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo.Bila shaka Allah ni mwenye uweza juu ya kila kitu". (35:1)
HUWEZA KUJIMITHILISHA UMBILE LA MWANADAMU
Malaika huweza kujimithilisha kuwa kama wanadamu. Hufanya hivyo pale wanapotumwa na Allah (SW) kuleta ujumbe kwa watu maalumu. Kwa mfano, Bibi Maryam, mama yake nabii Isa(a.s) , alijiwa na malaika katika umbo mithili ya mwanaume:
﴿وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا ﴿١٦﴾ فَاتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا﴾
Na mtaje katika kitabu, Maryam, alipojitenga na watu wake katika upande wa mashariki. Tukampelekea Muhuisha sharia Yetu (Jibril) akajimithilisha kwake kwa sura ya binaadamu aliye kamilifu. (19:16-17)
LENGO LA KUUMBWA MALAIKA
Lengo la kuumbwa malaika ni kumtumikia Allah(SW). Katika kutekeleza lengo la kuumbwa kwao, malaika hawana hiyari katika kutekeleza amri za Allah(SW), hufanya mambo yote vile anavyotaka Allah(SW).
﴿لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ﴾
..Hawamuasi Allah(SW) katika yale anayowaamuru, na wanatekeleza vile walivyoamrishwa.(66:6)
KAZI ZA MALAIKA
Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:
﴿وَمَا مِنَّا إِلَّا لَهُ مَقَامٌ مَّعْلُومٌ ﴿١٦٤﴾ وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ ﴿١٦٥﴾ وَإِنَّا لَنَحْنُ الْمُسَبِّحُونَ﴾
Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi. Na kwa yakini katika sisi wapo wajipangao safu. Na wako katika sisi wamtukuzao (Mwenyezi Mungu) (37:164-166)
MALAIKA PIA HUSHUGHULIKIA MAMBO YA WANADAMU KATIKA MAISHA YA DUNIANI NA AKHERA
Miongoni mwa mambo hayo ni:
(1) KULETA UJUMBE KWA WANAADAMU KUTOKA KWA ALLAH (SW)
Kazi ya kwanza ya malaika ni kuleta ujumbe wa Allah(SW) kwa wanadamu. Ujumbe huo huweza kuwa ni mwongozo wa maisha(Wahy) au habari juu ya jambo fulani. Malaika hupeleka ujumbe wa Allah(SW) kwa mitume au watu wa kawaida. Huteremka Malaika na wahy kwa amri yake juu ya anaowataka katika waja wake kuwa
﴿ أَنْ أَنذِرُوا أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاتَّقُونِ﴾
"onyeni kuwa hakuna wa kuabudiwa isipokuwa Mimi, basi niogopeni" (16:2)
Jibril, ambaye ndiye mkuu wa Malaika, ndiye mjumbe mkuu aliyekuwa akiwaletea Mitume wote Wahyi. Yeye ni mwalimu mkuu aliyeteuliwa na Allah(SW) kuwafunza mitume namna ya kuwalingania watu Uislamu kwa maneno na matendo.
﴿إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿١٩﴾ ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ﴾
Hakika hii Quran ni neno lililoletwa na mjumbe mtukufu, malaika mwenye nguvu na hadhi kubwa kwa Mwenyezi Mungu.(81:19-20)
(2) KUANDIKA AMALI ZA WANAADAMU NJEMA NA MBAYA
Kila mtu ana malaika waandishi wawili, kulia na kushoto kwake. Unaposema au kutenda jema au baya hadharani au umejificha peke yako, malaika hawa wanakuona na kurekodi jambo hilo.
﴿إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ ﴿١٧﴾ مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴾
Wanapopokea wapokeaji wawili, anayekaa kuliani na anayekaa kushotoni. Hatoi (mtu)kauli yoyote isipokuwa karibu naye yupo mngojeaji(malaika) tayari (kuandika.) (50:17-18).
(3) KUWALINDA WANAADAMU
Qur'an inatufahamisha Kazi ya tatu ya malaika ni kumchunga na kumlinda kila mtu na vitu vya hatari vilivyo nje ya uwezo wake.
﴿لَهُ مُعَقِّبَاتٌ مِّن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ يَحْفَظُونَهُ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ وَإِذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِقَوْمٍ سُوءًا فَلَا مَرَدَّ لَهُ وَمَا لَهُم مِّن دُونِهِ مِن وَالٍ﴾
Ana (kila mtu) kundi (la malaika) mbele yake na nyuma yake. Wanamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu.Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko nafsini mwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anapowatakia watu adhabu, hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake Mwenyezi Mungu (13:11)
Kwa ulinzi huu wa malaika utokao kwa Allah(SW), mtu hata kama atachukiwa na dunia nzima na kwahiyo wakafanya njama za kutaka kumdhuru, hawataweza mpaka Allah(SW) aondoe ulinzi wake.Vivyo hivyo, kama Allah(SW)atauondoa ulinzi wake huu kwa mtu, hakuna wa kumkinga na shari hata kama atalindwa na mitambo madhubuti ya kisasa pamoja na wataalamu wa ulinzi wa ulimwengu mzima.
(4) KUWAOMBEA WAUMINI MSAMAHA KWA ALLAH (S.W.)
Malaika pia wana kazi ya kumwomba Allah(SW) awasamehe wale watu wanaotubia na kufuatisha vitendo vyema.Humwomba Allah (SW) awasamehe, afute makosa yao, awarehemu kwa kuwalipa pepo na kuwaepusha na adhabu ya Moto.
"Wale wanaokichukua kiti cha enzi (cha Mwenyezi Mungu) na wale wanaokizunguka, wanamtukuza Mola wao na kumsifu na wanamuamini na wanawaombea msamaha waliaomini (Wanasema):
﴿رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدتَّهُمْ وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴾
"Mola wetu! Umekienea kila kitu kwa rehema na Elimu. Basi wasamehe waliotubu na kufuata njia yako na waepushe na adhabu ya Jahannam"(40:8)
Na Mwenyezi Mungu anaahidi kuwa wale wanaotubu kwa kujuta juu ya maovu waliyofanya, wakamuamini Yeye ipasavyo, kwa kujizuia kuyaendea maovu na badala yake wakashikamana na mwenendo mwema; Atabadilisha maovu yao kuwa mema! Qur'an inathibitisha hili katika aya ifuatayo, inasema:
﴿إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا﴾
Ila yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri; basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema, na mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu.(25:70)
(5) KUWASAIDIA WAUMINI VITANI KATIKA KUPAMBANA NA MADHALIMU
Miongoni mwa kazi tukufu za malaika ni kuwasaidia waislamu kupambana na maadui wenye nguvu kubwa kijeshi katika vita. Qur'an inatueleza kuwa:
﴿بَلَىٰ إِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا وَيَأْتُوكُم مِّن فَوْرِهِمْ هَـٰذَا يُمْدِدْكُمْ رَبُّكُم بِخَمْسَةِ آلَافٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُسَوِّمِينَ﴾
Naam.Kama mtasubiri na kujilinda na makatazo yake(Allah) na maadui wakakufikieni kwa ghafla, hapo Mola wenu atakusaidieni kwa Malaika elfu tano washambuliao kwa nguvu(3:125)
(6) KUWAANGAMIZA WATU WAOVU WALIOPINDUKIA MIPAKA
Malaika pia wana kazi ya kuwaangamiza watu waovu waliokubuhu na kupindukia mipaka. Watu wa nabii Lut waliangamizwa na Malaika baada ya kubobea katika maovu na kukataa kwao kujirekebisha. Tunafahamishwa hili pale malaika walipomjibu nabii Ibrahiimu(as) Wakasema:
﴿قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ ﴿٥٨﴾ إِلَّا آلَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ﴾
"Hakika sisi tumetumwa kwa wale watu wakosa (tuwaangamize) Isipokuwa waliomfuata Lut.Bila shaka sisi tutawaokoa wote hao (15:58-59)
(7) KUTOA ROHO ZA WATU
Kuna malaika wengi wanaohusika na utoaji wa roho za wanadamu wakati muda wao wa kuishi duniani unapokamilika. Malaika mkuu wa kazi hii ni Malakul-mauti:
﴿قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ﴾
Atakufisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu, kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu (32:11)
(8) KUWALIWAZA NA KUWAKARIBISHA WATU WEMA PEPONI KABLA YA KUTOLEWA ROHO
kila mtu aliyetenda mema na kutofanya maovu atashukiwa na malaika wa kumliwaza. Watamwambia:
﴿يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ ﴿٢٧﴾ ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً ﴿٢٨﴾ فَادْخُلِي فِي عِبَادِي ﴿٢٩﴾ وَادْخُلِي جَنَّتِي﴾
Ewe nafsi yenye kutulia! Rudi kwa Mola wako hali ya kuwa utaridhika Naye amekuridhia. Basi ingia katika kundi la waja (wazuri) uingie katika pepo yangu.(89:27-30).
﴿وَسِيقَ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ زُمَرًا حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا وَفُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ﴾
Na siku ya Kiama watawapokea na kuwakaribisha kwenye pepo ya Allah (SW) yenye neema za kudumu. Watawaambia: Amani juu yenu, furahini, na ingieni humu mkae milele (39:73)
(9) KUWAADHIBU WATU WAOVU MOTONI
Watu wanaotenda maovu watakuwa katika adhabu kali kwenye Moto wa Jahannam. Mwenyezi Mungu amewaweka malaika maalumu kwa ajili ya kuwaadhibu watu waovu wasiotaka kutubia, kujirekebisha wala kutenda mema. Allah (SW) anamtangazia kila mtu mwenya tabia hizi kuwa:
﴿سَأُصْلِيهِ سَقَرَ ﴿٢٦﴾ وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ ﴿٢٧﴾ لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ ﴿٢٨﴾ لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ ﴿٢٩﴾ عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ﴾
Karibuni hivi nitamtia katika Moto.Na ni nini kitakachokujulisha Moto huo? Haubakizi wala hausazi, unababua ngozi mara moja.Juu yake wako malaika (walinzi) kumi na tisa.(74:26-30).
Mkuu wa malaika hawa wa adhabu katika Jahannam ni Malik. Kutokana na machungu ya adhabu watakayopata, watu waovu watalia na kutamani mauti, watamtaka Malik amwombe Allah (SW) awafishe kuliko hiyo adhabu inayowakabili:
﴿ وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ قَالَ إِنَّكُم مَّاكِثُونَ﴾
Nao watapiga kelele: watasema: "Ewe Malik!Na atufishe Mola wako! (Maliki) atasema: "Kwa hakika mtakaa humu humu"(43:77)
Na Mwenyezi Mungu anasifu kuwa adhabu watakayotoa malaika hao kutokana na uwezo aliowapa haitakuwa na mfano wake katika adhabu hizi za duniani.
Siku hiyo mwanadamu atakumbuka, lakini kukumbuka huko kutamfaa nini.Atasema:
﴿وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٢٣﴾يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي ﴿٢٤﴾ فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ ﴿٢٥﴾ وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ﴾
"Laiti ningalitanguliza(wema) kwa ajili ya uhai wangu (huu wa leo). Basi adhabu ya(Allah) siku hiyo, haitolingana na adhabu aitoayo yeyote (katika wanadamu).Wala hatafunga yeyote jinsi ya kifungo chake (Allah) (89:23-26).
Taathira ya Imani ya Malaika katika maisha ya kila siku Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini. Hii ni kwa sababu:
1. Imani ya kweli juu ya Malaika humuepusha Muumini na kumshirikisha Allah (s.w) na viumbe vyake, hasa vile visivyoonekana, miongoni mwa hivyo ni Malaika na Majini.
2. Muislamu anaamini kuwa Malaika ni viumbe watukufu ambao wametakasika na dhambi na kila aina ya uchafu, lakini binaadamu amepewa daraja ya juu zaidi pindi atakapotimiza wajibu wake kama Khalifa wa Allah (s.w) hapa duniani. Imani hii humpelekea mtu kujitahidi upeo wa uwezo wake kuishi maisha yanayolingana na cheo hiki kikubwa, cheo ambacho Malaika walikitamani (Rejea Qur-an, 2:30)..
3. Muislam anaamini kuwa kila wakati na kila alipo yu pamoja na Malaika watukufu.Imani hii peke yake inatosha kumfanya mtu abadili tabia yake. Hii ni kwa sababu binaadamu ameumbwa na haya, kwa hiyo huhuzunika akifanya mambo maovu mbele ya watu na hasa mbele ya watu anaowaheshimu.
4. Muislamu anaamini kuwa Malaika hao sio tu kuwa wapo naye daima bali wanahudhurisha mbele ya Allah (s.w) kila anachokitenda. Imani hii ikithibiti moyoni humfanya Muislam ajitahidi kufanya mambo mema na ajitahidi kuepuka maovu.
5. Muislamu anajua kuwa Malaika sio tu hupendezwa na mema, bali pia humuombea mtu huyo anayefanya mema, maghfira kwa Allah (s.w) jambo ambalo humzidishia Muislamu hima ya kutenda mema daima na kujiepusha na maovu hata akiwa peke yake.
KUAMINI VITABU VYA ALLAH (S.W)
Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya vitabu vya Allah (s.w). Vitabu vya Allah (s.w) vimeshushwa kupitia kwa Mitume mbali mbali.
﴿لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ﴾
"Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na tukaviteremsha Vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu..." (57:25).
Vitabu vya Allah (s.w) ni vingi lakini tunavyovifahamu ni vile vilivyotajwa katika Qur-an kama ifuatavyo:
(1) Suhufi kwa Ibrahimu(a.s)
(2) Taurati kwa Mussa(a.s)
(3) Zabri kwa Daud(a.s)
(4) Injili kwa Issa(a.s)
(5) Qur-an kwa Muhammad(s.a.w.w)
Lengo la kushushwa Vitabu vya Allah (s.w) Iimebainishwa wazi katika Qur-an kuwa vitabu vya Allah (s.w) vimeshushwa kupitia kwa Mitume wake ili kuwaongoza wanaadamu katika njia iliyonyooka. Njia iliyonyooka ni ile inayomuwezesha mwanaadamu kumuabudu Allah (s.w) katika kila kipengele cha maisha yake kwa kipindi chote cha uhai wake hapa ulimwenguni. Allah (s.w) amechukua ahadi ya kuwaletea watu mwongozo tangu awali pale alipowashusha wazazi wetu, Adamu(a.s) na mkewe (Hawwah) hapa ardhini kama tunavyojifunza katika Qur-an:
﴿قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٨﴾ وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾
"Tukasema, shukeni humo nyote, na kama ukikufikieni uwongozi utokao kwangu, basi watakaoufuata uwongozi wangu huo haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika. Lakini wenye kukufuru na kuyakadhibisha maneno yetu, hao ndio watakaokuwa watu wa Motoni, humo watakaa milele". (2:38-39).
Ahadi hii ameitekeleza Allah (s.w) kwa kuwaleta Mitume mbali mbali baada ya Adamu (a.s) na kuwashushia vitabu vyenye Uongozi na nuru. Qur-an inasisitiza:
﴿إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ﴾
"Hakika tuliteremsha Taurat yenye Uongozi na Nuru.." (5:44)
﴿وَقَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ﴾
"Na tukawafuatishia (Mitume hao) Issa bin Maryam kuyahakikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurat, na tukampa Injili iliyomo ndani yake Uongozi na nuru." (5:46)
﴿شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ﴾
"Ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi) huo (hii) Qur-an ili iwe Uongozi kwa watu na hoja zilizo wazi za Uongozi wa upambanuizi..." (2:185)
Haja ya Mwongozo kutoka kwa Allah (s.w) Mwanaadamu pamoja na elimu aliyotunukiwa, hana uwezo pasina msaada wa muumba wake, kupata majibu sahihi ya maswali ya msingi ya maisha yake hapa duniani na huko akhera. Maswali haya ya msingi ni:
1. Nani chanzo cha maumbile yote?
2. Ni lipi lengo la mwanaadamu hapa ulimwenguni?
3. Atalifikiaje lengo hilo?
4. Ni ipi nafasi halisi ya mwanaadamu hapa ulimwenguni?
5. Ni ipi hatma yake baada ya kufa, je kufa ndio mwisho wa maisha yake?
Mwanaadamu bila ya mwongozo kutoka kwa muumba wake hana uwezo wa kutoa majibu sahihi ya maswali haya. Elimu ya mazingira aliyonayo mwanaadamu ni finyu mno kiasi kwamba haimuwezeshi hata kuijua roho yake kama tunavyokumbushwa katika Qur-an:
﴿وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا﴾
"Na wanakuuliza habari ya roho.Sema: "Roho ni jambo lililohusika na Mola wangu. Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo kabisa" (17:85)
Maana ya Kuamini Vitabu vya Allah Imani ya kweli katika Uislamu haishii moyoni tu bali ni lazima idhihirishwe katika matendo ya kila siku. Hivyo, waumini wa kweli wa vitabu vya Allah (s.w) ni wale wanaoendesha maisha yao ya kila siku katika kila kipengele kwa kufuata bara bara maongozi ya vitabu vya Allah (s.w). Kabla ya Qur-an kushushwa, waumini wa kweli wa vitabu vya Allah vilivyotangulia, vikiwemo Taurat, Injili, Zaburi, n.k. ni wale walioishi kwa mujibu wa maongozi ya vitabu hivyo kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
﴿إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُوا لِلَّذِينَ هَادُوا وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُوا مِن كِتَابِ اللَّـهِ وَكَانُوا عَلَيْهِ شُهَدَاءَ فَلَا تَخْشَوُا النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ﴾
"Hakika tuliteremsha Taurati yenye uwongozi na nuru; ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha (kwa Allah) waliwahukumu Mayahudi; Watawa na Maulamaa pia (walihukumu kwa hiyo Taurat); kwa sababu walitakiwa kuhifadhi kitabu hicho cha Allah; Nao walikuwa mashahidi juu yake. Basi, msiwaogope watu, bali niogopeni (Mimi). Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache (ya maslahi ya dunia).Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Allah, basi Hao ndio makafiri." (5:44)
﴿وَلْيَحْكُمْ أَهْلُ الْإِنجِيلِ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فِيهِ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴾
"Watu wa Injili wahukumu kwa yale aliyoteremsha Allah ndani yake.Na wasiohukumu kwa (kufuata) yale aliyoteremsha Allah, basi hao ndio mafasiki (maasi)" (5:47)
Baada ya Qur-an kushushwa kupitia kwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) kwa ajili ya walimwengu wote, Waumini wa kweli wa vitabu vya Allah (s.w) ni wale wanaoishi kwa kufuata maongozi ya Qur-an na Sunnah ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) katika maisha yao yote. Si muumini yule anayeikataa Qur-an na Mtume aliyeshushiwa hatakama anadai kuwa anaiamini Taurat, Zabur, Injili, n.k. na Mitume walioshushiwa vitabu hivyo kwa mujibu wa aya ifuatayo:
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي أَنزَلَ مِن قَبْلُ وَمَن يَكْفُرْ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا﴾
"Enyi mlioamini! Mwaminini Allah na Mtume wake na kitabu alichokiteremsha juu ya Mtume wake,na vitabu alivyoviteremsha zamani. Na mwenye kumkanusha Allah na Malaika wake na vitabu vyake, na Mitume wake na siku ya mwisho, basi bila shaka amepotea upotofu uliombali (na haki)" (4:136)
Hivi sasa, katika vitabu vya Allah (s.w) vilivyoshushwa hapa ulimwenguni, ni Qur-an pekee iliyobakia katika lugha yake ya asili (Kiarabu fasaha) na katika usahihi wake wa asili. Vitabu vilivyoitangulia Qur-an vinakabiliwa na matatizo makubwa mawili yafuatayo:
1. Lugha zilizotumika katika vitabu hivyo zimekufa (zimetoweka). Kwa mujibu wa Qur-an kila Mtume alilepewa wahay kwa lugha ya watu wake
﴿وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ﴾
"Na hatukumpeleka Mtume yeyote isipokuwa kwa lugha ya watu wake ili apate kuwabainishia..." (14:4).
Tunajua kutokana na historia kuwa lugha hukua na kufa. Hivi sasa kwa mfano Allah (s.w) akituletea kitabu alichoshushiwa Nabii Adam(a.s) katika lugha aliyozungumza Adam(a.s) na wanawe wa karibu wa wakati ule, hatuwezi kupata ujumbe wake.
2. Vitabu vilivyoitangulia Qur-an viliingizwa mikono ya watu, vikabadilishwa na kupotoshwa ili kukidhi matashi ya watu waliodai kufuata vitabu hivyo kinyume na Allah (s.w). Taurat, Zabur, Injili, n.k. Vilikumbwa na tatizo hili.
Qur-an imeepukana na matatizo haya kwani hivi leo, Lugha ya Kiarabu, ni miongoni mwa lugha kubwa zinazokua kwa kasi; pia Kiarabu ni lugha fasaha na tajiri kwa maneno kuliko lugha zote duniani. Pia Qur-an tofauti na vitabu vingine vya Allah (s.w), haitaingiliwa na mkono wa mtu, kwani imepewa hifadhi na Allah (s.w) mwenyewe:
﴿نَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ﴾
Hakika sisi ndio tulioteremsha mawaidha haya (hii Qur-an) na hakika Sisi ndio tutakao yalinda" (15:9).
﴿لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴾
"Haitakifikia batili mbele yake wala nyumba yake; kimeteremshwa na Mwenye Hikma Ahimidiwaye." (41:42).
Hivyo hivi sasa, Muumini wa kweli wa vitabu vya Allah (s.w) ni yule:
1. Anayeamini pasi na tone la shaka kuwa Qur-an yote kama msahafu ulivyo kuanzia sura ya kwanza (Al-Faatiha) mpaka sura ya mwisho (An-Naas) ni maneno kutoka kwa Allah (s.w). Muumini anayakinisha kuwa:
﴿ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ فِيهِ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ﴾
"Hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake, ni uwongozi kwa wamchao Allah" (2:2)
2. Anayaongoza maisha yake ya kila siku kwa kufuata Qur'an na mwenendo au sunnah ya mfasiri wa Qur-an, Mtume Muhammad(s.a.w.w). Qur-an yenyewe inasisitiza:
﴿وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا﴾
"Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi (kabisa)." (33:36)
﴿وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ﴾
"...Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri". (5:44)
﴿وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴾
"... Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu" (5:45) lengo-2 166 1/18/10, 12:28 PM 167
﴿وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴾
"... Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio mafasiki (maasi)" (5:47)
KUAMINI MITUME WA ALLAH (S.W)
Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya Mitume wa Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika Qur-an: "Semeni nyinyi (Waislamu kuwaambia Mayahudi na Wakristo kuwa):"Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu, na Ismail na Is-haqa na Yaaqubu na kizazi (chake Yaaqubu); na waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutafautishi baina ya yoyote katika hao.(Wote tunawaamini), na sisi tumenyenyekea kwake." (2:136) Kuamini baadhi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na kuwakanusha wengine kama walivyo fanya mayahudi na Wakristo ni Ukafiri kama tunavyojifunza katika Qur-an:
﴿إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُوا بَيْنَ اللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ وَنَكْفُرُ بِبَعْضٍ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُوا بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١٥٠﴾ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ حَقًّا وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٥١﴾ وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَلَمْ يُفَرِّقُوا بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ أُولَـٰئِكَ سَوْفَ يُؤْتِيهِمْ أُجُورَهُمْ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا﴾
"Hakika wale wanaomkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume yake, na wanataka kutenga baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume yake, kwa kusema: "Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa," na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya (si ya Kiislamu khasa wala ya Kikafiri).Hao ndio Makafiri kweli.Na tumewaandalia makafiri adhabu idhalilishayo.Na waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mitume yake wala wasimfarikishe yoyote katika wao (bali wamewaamini wote), hao atawapa ujira wao.Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu." (4:150-152).
Mitume wa Allah (s.w) ni wengi sana kama inavyobainishwa katika Qur-an:
﴿وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ﴾
"Na kwa yakini tuliwatuma mitume kabla yako (Muhammad).Wengine katika hao tumekusimulia (majina yao na habari zao) na wengine hatukukusimulia..." (40:78)
Mitume waliosimuliwa katika Qur-an ni hawa ishirini na tano (25) wafuatao:
1. Adam(a.s)
2. Idrisa (Enock)(a.s)
3. Nuhu (Noah)(a.s)
4. Hud (Heber)(a.s)
5. Salih (Metheusaleh)(a.s)
6. Ibrahim (Abrahim)(a.s)
7. Lut (Lot) (a.s)
8. Ismail (Ismael)(a.s)
9. Is-haq (Isaac)(a.s)
10. Yaaqub (Jacob)(a.s)
11. Yusuf (Joseph)(a.s)
12. Shu'aib (Jethro)(a.s)
13. Ayyub (Job)(a.s)
14. Mussa (Moses)(a.s)
15. Harun (Aaron)(a.s)
16. Dhul kifl (Ezekiel)(a.s)
17. Daud ( David)(a.s)
18. Sulayman (Solomon)(a.s)
19. Ilyaas (Elias)(a.s)
20. Al - Yassa' (Elisha)(a.s)
21. Yunus (Johah)(a.s)
22. Zakariya (Zechariah)(a.s)
23. Yahya (John the Baptist)(a.s)
24. Isa (Jesus)(a.s)
25. Muhammad(s.a.w.w)
LENGO LA KULETWA MITUME WA ALLAH (S.W)
Mitume wameletwa kuwa Waalimu na viongozi wa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuusimamisha Uislamu katika jamii kinadharia na kimatendo kama tunavyojifunza katika Qur-an:
﴿ لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ﴾
"Kwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukaviteremsha vitabu na Uadilifu (mizani) pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu. (57:25)
﴿ هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴾
"Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na kwa dini ya haki ili kuifanya ishinde dini zote, ijapokuwa washirikina watachukia." (9:33, 61:9)
MWISHO WA UTUME
Maswali ambayo huweza kuulizwa ni: Kwa nini wahyi ukatike?Kwa nini Mitume wasiendelee kuletwa hadi kiyama? Kwa nini Muhammad(s.a.w.w) afunge mlango wa Utume? Ili kulielewa vizuri suala hili la mwisho wa Utume yafaa kwanza tuzingatie kuwa kilicho muhimu na cha msingi kabisa kwa Mtume yeyote si kule kuwepo kimwili bali ni kule kuufikisha kwake ujumbe aliopewa na Mwenyezi Mungu (s.w) ili watu wake wasiwe na hoja tena iwapo watachagua kupotea. Na lau ingekuwa lililo muhimu kwa Mtume ni kule kuwapo kimwili basi Mwenyezi Mungu angelimpeleka Mtume mara tu baada ya kufariki Mtume aliyetangulia.
Kilicho cha msingi ni mafundisho aliyokuja nayo.Maadamu ujumbe aliouleta uko hai basi Mtume huyo yu hai. Hivyo kifo halisi cha Mtume ni kule kupotea kwa mafundisho aliyoyaleta. Mitume wote waliomtangulia Muhammad(s.a.w.w) mafundisho yao yalipotea, kwani yalichanganyika na hekaya mbali mbali. Katika vitabu vilivyoitangulia Qur-an, kwa mfano Taurat, Injil, na Zaburi hakuna hata kimoja ambacho kipo katika hali ya usahihi wake wa asili. Hata wafuasi wa vitabu hivyo wanakiri kuwa nakala walizonazo leo si zile walizopewa Mitume. Si hivyo tu bali hata historia za maisha ya Mitume waliomtangulia Muhammad(s.a.w.w) zimechanganywa na ngano za kushtusha kabisa, hata inakuwa vigumu kupambanua haki na batili.
Kinyume chake mafundisho aliyokuja nayo Muhammad(s.a.w.w) yako hai kabisa na hayajaharibiwa na katu hayawezi kuharibiwa.Qur-an, kitabu alichoteremshiwa kipo tena katika lugha ile ile ya asili bila ya kupunguza wala kuzidisha japo nukta moja. Historia kamili ya maisha yake, maneno yake, maagizo yake, vitendo vyake, vyote vimehifadhiwa kwa usahihi kabisa kiasi ambacho karne 14 zimepita lakini bado historia yake ni ya wazi na kamili kama kwamba tunamuona kwa macho yetu. Katika kila kipengele cha maisha yetu tunaweza kupata muongozo na mafundisho kutoka kwa Muhammad(s.a.w.w) . hii ndio sababu hakuna haja ya kuletwa Mtume mwingine baada yake.
Zaidi ya hayo yapo mambo matatu ambayo husababisha kuhitajika kuja kwa Mtume mwengine baada ya yule aliyetangulia:
(1) Iwapo mafundisho ya Mtume aliyetangulia yamechanganywa na hekaya za nzushi, kuharibiwa na kupotea. Katika hali kama hiyo Mtume anahitajika ili aje aifundishe dini katika usahihi wake wa awali.
(2) Iwapo mafundisho ya Mtume aliyeondoka hayakukamilika na hivyo kukawa na haja ya kuyakamilisha, kuyarekebisha, au kuongeza jambo fulani.
(3) Iwapo Mtume aliyetangulia alipelekwa kwa watu wa taifa fulani maalum au nchi fulani maalum na hivyo kuwepo haja ya kuletwa Mtume kwa watu wa taifa au nchi nyingine. Au pengine Mtume anaweza kuletwa ili amsaidie Mtume mwingine, lakini kwa kuwa hii si kanuni ya kawaida, hatujaita kama sharti la nne. Katika Qur-an ipo mifano miwili ya hali kama hiyo. Nabii Haruni(a.s) alikuwa msaidizi wa Nabii Musa(a.s) . Nabii Lut (a.s) Ismail(a.s) na Is-haq(a.s) walikuwa wasaidizi wa Nabii Ibrahim(a.s).
Haya matatu ndiyo masharti makuu ya kimsingi yanayohitajika ili aletwe Mtume mwingine. Kati ya hayo hakuna hata sharti moja lililopo leo.
Kwanza : mafundisho ya Mtume wa mwisho, Muhammad(s.a.w.w) yako hai, yamehifadhiwa na yatadumu hadi siku ya Kiyama. Mwongozo aliouleta kwa walimwengu wote ni sahihi na kamili na umehifadhiwa katika Qur-an humo kuna ahadi ya ulinzi wa Allah (s.w) kama tunavyofahamishwa:
﴿نَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ﴾
"Hakika sisi ndio tulioteremsha mawaidha (haya hii Qur-an); na Hakika sisi ndio tutakaoyalinda." (15:9).
Pia sunnah zake zimehifadhiwa kikamilifu kiasi ambacho mtu anaweza kujua pasi na shaka yoyote nini mafundisho ya Mtume juu ya jambo fulani.Hivyo sharti la kwanza linaondoka.
Pili : Mwenyezi Mungu amekamilisha mwongozo wake kwa Nabii Muhammad(s.a.w.w) na hivyo Uislamu ni dini kamilifu kwa ulimwengu wote. Allah (s.w) anasema katika Qur-an:
﴿الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ﴾
"Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu juu yangu na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu (5:3)
Na tukiutafiti Uislamu kwa makini kama mfumo kam ili wa maisha tunaona unadhihiri ukweli wa aya hii ya Qur-an. Uislamu unatoa mwongozo wa maisha haya na ya akhera na hakuna jambo lililo muhimu katika kumuongoza mwanaadamu lisilokuwemo katika mwongozo aliokuja nao Muhammad(s.a.w.w) . Hivyo hoja ya kuhitaji Mtume ili aje kukamilisha dini pia inaondoka. Hata hivyo kuna baadhi ya watu wanaosema kwamba kupita tu kwa muda mrefu ni sababu ya kuhitaji Mtume mwingine. Hii ni kwa sababu wanasema mwongozo ulioletwa karne 14 zilizopita ni wa kale mno kiasi kwamba hauwezi kukidhi mahitaji ya watu wa leo. Mawazo haya hayana msingi kabisa, kwa sababu zifuatazo:
(i) Mafunzo ya Uislamu ni ya milele, kwa sababu ni ufunuo utokao kwa Mwenyezi Mungu mjuzi wa yote ya kale, ya sasa na yajayo, tena basi mwenye uhai wa milele. Elimu ya binaadamu ndiyo yenye ukomo, na ni jicho la binaadamu ambalo haliwezi kuona hata kesho achilia mbali miaka milioni mmoja ijayo. Elimu na hikima ya Mwenyezi Mungu imesalimika na upungufu kama huo.
(ii) Uislamu umeegemeza mafundisho yake juu ya umbile la binaadamu. Na umbile la binaadamu limesalia vile vile katika zama zote. Watu wote wamejengwa kwa majengo yale yale yaliyowajenga watu wa kale kabisa na hivyo umbile lao kimsingi ni lilelile.
(iii) Katika maisha ya binaadamu kuna mizani inayoridhisha kabisa baina ya mambo yanayodumu na mambo yanayobadilika. Misingi muhimu na maadili makuu hayabadiliki na sura ya nje ndiyo inayoweza kubadilika kutokana na kupita kwa muda. Qur-an na sunna zinatoa kanuni au misingi ya kudumu na kwa kutumia ijitihadi misingi hiyo inaweza kutekelezwa kadri hali itakavyobadilika. Uislamu ndio dini pekee iliyoweka utaratibu madhubuti unaoweza kuoanisha maendeleo ya binaadamu na misingi ya Kitabu cha Allah (s.w) na Sunnah ya Mtume wake Muhammad(s.a.w.w).
Na tukirudi katika lile sharti letu la tatu kuhitajia kuletwa Mtume mwingine, tunaona kuwa Muhammad(s.a.w.w) hakuletwa kwa taifa au watu maalum bali kwa walimwengu wote. Qur-an inasema:
﴿قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا﴾
"Sema (Ewe Nabii Muhammad): "Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote". (7:158)
﴿وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ﴾
"Nasi hatukukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu wote" (21:107)
Labda itaulizwa: Kwanini Mtume Muhammad(s.a.w.w) awe Mtume wa walimwengu wote? Ama kuhusu suali hili, hapana jibu lolote lililotolewa katika Qur-an wala katika hadithi za Mtume(s.a.w.w) . Hivyo ni Allah (s.w) pekee anayejua ni kwanini alimleta kwa ulimwengu mzima. Lakini tunaweza kutumia akili zetu finyu tukajaribu kuona hikima iliyopo kwa Mtume(s.a.w.w) kuwa Mtume wa ulimwengu mzima jambo ambalo halikuwezekana kwa Mitume waliotangulia. Hapo awali, kabla ya Mtume(s.a.w.w) , Mitume walikuwa wakitokea kwa kila nchi au kila taifa. Sababu ya msingi tunayoweza kuona kirahisi ni kwamba katika wakati huo wa historia njia za usafiri na mawasiliano yalikuwa finyu sana kwa kiasi ambacho mawasiliano kati ya watu na nchi moja na nyingine yalikosekana kabisa. Kila nchi au ukanda wa jiografia ulikuwa ni ulimwengu wa peke yake.
Katika hali hii ilikuwa ni vigumu mno kuwa na Mtume mmoja kwa ulimwengu wote. Ndio tunakuta kila nchi au kila ukanda wa jiografia ukatumiwa Mtume wake. Sote tunashuhudia kuwa katika umma huu wa mwisho wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) pamekuwa na maendeleo makubwa sana ya mawasiliano kiasi kwamba dunia inakuwa kama kijiji. Suala la "Globalization" (utandawazi) kwa Waislamu sijambo geni. Tunafahamishwa katika Qur-an kuwa umma huu wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) ni umma mmoja na unawajibika kuufanya Uislamu utawale ulimwengu mzima.
Kutokana na hoja hizi tatu itaonekana wazi ni kwanini hakuna haja ya Mtume mwingine baada ya Muhammad(s.a.w.w) . Na ndivyo Allah (s.w) anavyotufahamisha katika Qur-an kuwa yeye Muhammad(s.a.w.w) ni "Khataman-Nabiyyina" - yaani mwisho wa Mitume:
﴿مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴾
Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Allah na mwisho wa Mitume na Allah ni mjuzi wa kila kitu. (33:40)
Na Mtume Muhammad(s.a.w.w) mwenyewe pia anasema:
Palikuwa na Mitume waliowaongoza Banii Israil katika njia sahihi. Kila Mtume alipokufa, alifuatiwa na Mtume mwingine. Lakini hapana Mtume atakayekuja baada yangu.Kazi hii (ya kuufundisha Uislamu na kuusimamisha) inaweza kufanywa na makhalifa (viongozi wa Kiislamu). (Bukhari)
Na katika Hadithi nyengine Mtume(s.a.w.w) amesema:
"Uhusiano wangu na (msururu mrefu) wa Mitume unaweza kueleweka vizuri kwa mfano wa nyumba nzuri ya kifalme. Nyumba hii ikawa imejengwa vizuri sana na ikawa inapendeza lakini pakawa na nafasi moja iliyobakia. Watu wakawa wanaizungumza nyumba hii nzuri na wakawa wanauliza kwa mshangao.Kwanini hii sehemu isiwe imejazwa! Nimejaza pengo hili na ni Mtume wa mwisho". (Bukhari)
Mitume wa Uongo Wafuatao ni baadhi ya wale waliodai utume wakati Mtume (s.a.w) akiwepo na baada yake. Aswad Aus: Alijitangazia Utume wakati wa Mtume(s.a.w.w) na aliuawa kwa amri ya Mtume mwenyewe.
Musailama (Al-kadhaab) Alijitangazia Utume wakati wa Abubakari (Khalifa wa kwanza wa Mtume(s.a.w.w) . Waislamu walimpiga vita na kumuua. Bahau'lla Alijitokeza huko Iran katika karne ya 19 na aliuawa na Waisalmu.
Mirza Gulam Ahmed Alizaliwa huko India katika kitongoji cha Kadiani katika karne ya 19. Japo alilindwa na serikali ya Kikoloni ya Kiingereza, alipigwa vita na Waislamu kwa maneno na kalamu mpaka uwongo wake ukawa dhahiri kwa waislamu pamoja na kutumia kwake Qur-an hii wanayoifuata Waislamu. Pia kwa kukosekana mtu aliyekuja na kitabu cha mwongozo kinachofanana na Qur'an angalau kwa mbali, inazidi kutudhibitishia kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) ni Mtume wa mwisho na Qur'an ni ujumbe wa mwisho wa Allah (s.w) utakaobakia mpaka mwisho wa ulimwengu. Maana ya Kuamini Mitume wa Allah (s.w) katika maisha ya kila siku.
Waumini wa kweli wa Mitume wa Allah (s.w) ni wale wenye tabia ifuatayo:
1. Kuwatii Mitume ipasavyo kwa kufanya yale yote waliyoamrisha na kuacha yale yote waliyoyakataza kama Qur'an inavyosisitiza:
﴿وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا﴾
"... Na anachokupeni Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho..." (59:7)
﴿قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾ قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴾
Sema: "Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni; (hapo)Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu.Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira, mwenye rehema. Sema: "Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na kama mkikengeuka,(Mwenyezi Mungu atakutieni adabu),kwani Mwenyezi Mungu hawapendi Makafiri" (3:31-32)
2. Kuwafanya Mitume vigezo vya maisha yao kibinafsi, kifamilia na kijamii kama inavyosisitizwa katika Qur-an:
﴿ لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا﴾
"Bila shaka mnao mfano mwema (wa kuiga) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kumtaja Mwenyezi Mungu sana". (33:21)
3. Kuwapenda Mitume kuliko nafsi zao kama Qur-an inavyosistiza:
﴿قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴾
"Sema "Kama baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali mlizozichuma na biashara mnazoogopa kuharibikiwa,na majumba mnayoyapenda; (ikiwa vitu hivi) ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kupigania dini yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake; na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu maasi" (9:24)
Kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume si jambo lingine zaidi ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa unyenyekevu na upendo.
Muumini wa kweli hatakuwa tayari kuifurahisha nafsi yake au kumfurahisha yeyote awaye kinyume na kumfurahisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ni katika maana hii Mtume(s.a.w.w) anasema:
"Hatakuwa mmoja wenu ni Muumini wa kweli mpaka anipende zaidi kuliko chochote kile ikiwa ni pamoja na familia yake, mali yake na watu wote" .(Sahihi Muslim)
"Yeyote yule anayependa Sunnah yangu ananipenda, na yeyote yule anayenipenda atajikuta yuko ubavuni kwangu huko Peponi" (Tirmidh)
4. Kuwafanya Mitume kuwa Mahakimu wao pale wanapohitilafiana katika jambo lolote lile kama tunavyojifunza katika Qur-an:
﴿فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا﴾
"Naapa kwa (haki ya) Mola wako (Ewe Muhammad); wao hawawi wenye kuamini mpaka wakufanye hakimu katika yale wanayokhitalifiana, kisha wasione uzito nyoyoni mwao juu ya hukumu uliyopitisha, na wanyenyekee kabisa." (4:65)
﴿وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا﴾
"Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiyari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakika amepotea upotofu (upotevu) ulio wazi." (33:36)
5. Kuwa na yakini kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) ndiye Mtume wa mwisho kama Qur-an inavyosisitiza:
﴿مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا﴾
"Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Mitume, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu." (33:40)
6. Kumswalia Mtume(s.a.w.w) mara kwa mara katika swala na kila anapotajwa. Kumswalia Mtume(s.a.w.w) ni amri ya Allah (s.w) kama inavyotuelekeza ifuatavyo:
﴿إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا﴾
Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia Rehema Mtume;na Malaika wake. Basi; Enyi mlioamini, msalieni Mtume na muombeeni amani. (33:56)
ZOEZI 2:2
1. Malaika ni......................................................................
2. Toa tofauti nne (4) zilizopo kati ya Malaika na binaadamu.
3. Orodhesha kazi kumi (10) za malaika zenye mahusiano na binaadamu.
4. Muumini wa kweli wa Malaika ni yule anayefanya yafuatayo:-
(a) ..........................(b) ......................(c) .....................(d) .........................
5. Taja vitabu vinne (4) vya Allah (s.w) vilivyohadithiwa katika Qur-an na Mitume walioshushiwa.
6. Lengo la kushushwa vitabu vya Allah (s.w) ni..................................
7. "Hakika ni juu yetu kutoa mwongozo." (92:12) Pamoja na binaadamu kupewa akili na elimu hana uwezo wa kujiundia njia sahihi ya maisha kwa sababu zifuatazo:
(a)...............................................
(a)..............................................
(b)..............................................
8. Toa tofauti nne (4) zilizopo kati ya Qur-an na vitabu vingine vya Allah (s.w). 9. Muumini wa kweli wa Qur-an ni yule anayefanya yafuatayo:
(a).............................................
(b)..................................................
10. (a) Mitume wa Allah (s.w) ni ..................................................
(b) Mitume wameletwa ili..................................................
(c) Waumini wa kweli wa Mitume wa Allah (s.w) ni wale wenye tabia zifuatayo:
(i)..........................
(ii)..........................
(iii)..........................
(iv)..........................
(v)..........................
7
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
KUAMINI SIKU YA MALIPO
Kuamini siku ya Malipo ni miongoni mwa Nguzo Muhimu katika Nguzo za Iman ya Kiislamu. Kwa hakika ndiyo Msingi wa nguzo nyinginezo za Iman. Mtu hawezi kuwa muumini wa kweli mpaka awe na yakini kuwa pana maisha mengine baada ya kufa. Katika sehemu mbalimbali katika Qur'an Allah (s.w) ameiambatanisha nguzo hii ya "Kuamini Akhera" na "Kumuamini Allah" ambayo ni nguzo ya kwanza.
Allah (s.w) anatuambia:
﴿وَمَن يَكْفُرْ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا﴾
"Na mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho, basi amepotea upotevu ulio mbali (na haki) (4:136)
Pia anasema:
﴿لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا﴾
"Bila shaka mnao mfano mwema (ruwaza nzuri) kwa mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa Mwenye kumwogopa Mwenyezi mungu na Siku ya Mwisho, na kumtaja Mwenyezimungu sana" (33 :21)
Pia anasema:
﴿لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ﴾
"Sio wema (peke yake tu) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi, bali wema hasa ( ni wale) wanaomwamini Allah na Siku ya Mwisho" (2:177)
Muislamu wa kweli anaamini kuwa maisha haya ya duniani ni maisha yana mwisho, yatakoma na kuna siku nyingine ambayo hakuna siku baada ya siku hiyo, kisha yanakuja maisha ya pili ambayo ndiyo maisha halisi ya kweli ya nyumba ya Akhera. Kupatikana kwa siku hiyo ambayo hakuna siku baada ya siku hiyo, kutakuja baada ya Ulimwengu wote kutoweka na kubaki ufalme wa Allah (s.w) tu yeye peke yake, Aliye dhati ya kweli. Malaika, Milima, Majini, Binaadamu, maji na kila kilicho na uhai kitatoweka kipende kisipende. Allah anatutanabahisha hili kwa kusema:
﴿كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ ﴿٢٦﴾ وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ﴾
"Kila aliye juu ya ardhi atakufa na atasalia Mola wako Mwenye Utukufu (wa kweli) usio na mahitaji na fadhila kamili" (55:26 - 27)
Baada ya kila kilicho hai kutoweka na kubaki Ufalme wa Allah (s.w) kama Alivyokuwa kabla ya kuumba chochote, hapo Allah atawafufua viumbe na kuwakusanya kwake wote ili apate kuwalipa kwa lile walilolifanya katika ardhi hii, wapate Pepo kama walikuwa watiifu kamili kwa Mola wao au wastahili Moto kwa kuwa walishika miungu mingine badala ya Allah (s.w) katika kuendesha maisha yao. Maisha hayo ndiyo maisha halisi na yenye kudumu daima! Allah (s.w) anatubainishia kuwa:
﴿أَلَا يَظُنُّ أُولَـٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ ﴿٤﴾ لِيَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥﴾ يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ﴾
"Kwani hawaelewi kuwa wao watafufuliwa ? Ndani ya Siku tukufu, Siku watasimama watu kwa amri ya Bwana wa viumbe vyote? (83: 4-6).
Pia anasema:
﴿زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ﴾
"Makafiri wanadai kuwa hawatafufuliwa!, (sema Kwanini msifufuliwe?!) Naapa kwa Mola wangu Wallah!: Mtafufuliwa na kisha wallah! Mtaelezwa mlichokifanya duniani, hayo kwa Allah ni sahali (64:7)
Muislamu wa kweli anaamini kuwa Qiyama kitasimama na kila mja atalipwa kwa kila tendo alilolifanya, dogo au kubwa kama Allah (s.w) anavyotubainishia katika Qur'an:
﴿فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾ وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ﴾
"Basi atakayefanya (jambo lolote) la kheri lenye uzito mfano wa Dharra (Atom) ataliona jaza yake. Na atakayefanya (jambo lolote) la shari lenye uzito mfano wa Dharra (Atom) ataliona jaza yake". (99: 7 - 8)
Pia Allah (s.w) anamkumbusha Mtume(s.a.w.w) juu ya wasia wa Mzee Luqmaan kwa kijana wake ambao kwa hakika ndio wasia bora wa kila mzazi kumpa kijana wake, anasema:
﴿ يَا بُنَيَّ إِنَّهَا إِن تَكُ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ فَتَكُن فِي صَخْرَةٍ أَوْ فِي السَّمَاوَاتِ أَوْ فِي الْأَرْضِ يَأْتِ بِهَا اللَّـهُ إِنَّ اللَّـهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ ﴾
"Ewe mwanangu, jambo lolote lililo na uzito wa chembe ya Hardal (au ndogo kuliko hiyo) ikiwa katikati ya jabali, au juu mbinguni au chini ardhini Allah Atalileta (amlipe aliyelifanya) Hakika Allah ni mwingi wa habari na mwenye ujuzi (hasa)" (31: 16)
Dalili (Alama) za Qiyama Ingawa hakuna ajuaye Kiyama kitakuwa lini, kupitia Aya mbali mbali za Qur'an na Hadith kadhaa za Mtume (s.a.w) zinabainisha kwa uwazi juu ya dalili mbali mbali za kusimama kwa kiyama. Ziko Dalili kubwa na Dalili ndogo, na zipo ambazo tayari zimekwishadhihiri nyingine zinaendelea na ambazo bado kudhihiri kwake; Kama Allah Aliyetukuka anavyotubainishia:
﴿فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً فَقَدْ جَاءَ أَشْرَاطُهَا فَأَنَّىٰ لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ﴾
"Kwani wanangoja jingine ila kiyama kiwajie kwa ghafla?Basi alama zake (hicho kiyama) zimekwishakuja.Kutawafaa wapi kukumbuka wakati kitakapowajia?" (47:18)
Pia anasema
﴿وَالذَّارِيَاتِ ذَرْوًا﴾
"Saa ya Kiyama imekaribia; na mwezi umepasuka" (54:1)
Dalili Ndogo za Kiyama:
(i) Watu kumiliki mali na hali ya kuwa ni madhalimu wasio na uadilifu
(ii) Kuenea mno kwa riba kiasi cha kila mtu kuathiriwa nayo
(iii) Kuenea kwa kila aina ya Ulevi
(iv) Wanawake kukithiri katika kuvaa nguo zinazochochea zinaa (nguo nyepesi za kuangaza,fupi na za kubana)
(v) Wanawake watawaiga wanaume katika mavazi kadhalika wanaume watawaiga wanawake katika mavazi. Leo wanaume wanavaa hereni, shanga, bangili,na mengineyo yanayojulikana kuwa mapambo ya kike.
(vi) Kuenea kwa Liwati (kujimai baina ya jinsia mojawanaume kuwaendea wanaume wenzao na wanawake kuwaendea wanawake wenzao) Homosexuality and Lesbiansm. Jambo hili leo limehalalishwa na watu wa Magharibi, pia hapa kwetu Afrika na hasa Kenya na Afrika kusini ni halali Mwanaume kuolewa na mwanamume mwenzake! Subhaanallah!
(vii) Kuenea sana kwa zinaa na itafanyika hadharani.
(viii) Watu hawatawajali tena wazazi wao, ndugu zao na jamaa zao badala yake watawathamini na kuwasaidia rafiki zao.
(ix) Watu watachukia sana kulea watoto.
(x) Unafiki utaenea sana.
(xi) Mauaji yataenea sana, kwa kutoka Taifa moja kwenda kulivamia Taifa jingine na watu baadhi kuwaua wengine kwa maslahi yao binafsi
(xii) Watu wataona uzito sana kutoa sadaka
(xiii) Watawala watakuwa wengi sana lakini hakuna atakayekuwa mkweli na mwadilifu
(xiv) Mtu ataheshimiwa kwa shari yake na si kwa uadilifu na wema wake.
(xv) Kujifaharisha kwa misikiti
(xvi) Pamoja na haya yote,bado kutakuwepo na kundi dogo tu la waislamu ambalo litadumu katika njia iliyonyooka na halitatetereka kwa lolote.
Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya Kiyama Mtume(s.a.w.w) pia ametutajia dalili kubwa za kukaribia kwa siku ya Mwisho. Dalili hizo zinapatikana katika Qur'an na Hadith kama inavyobainishwa hapa chini:
Allah (s.w) anasema:
﴿وَإِذَا وَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَابَّةً مِّنَ الْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ النَّاسَ كَانُوا بِآيَاتِنَا لَا يُوقِنُونَ﴾
"Na kitakapokaribia Kiyama, tutawatolea mnyama kutoka ardhini atawaeleza (watu) kwa kuwa watu walikuwa hawaziamini aya zetu" (27:82)
Pia anasema:
﴿حَتَّىٰ إِذَا فُتِحَتْ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَهُم مِّن كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلُونَ ﴿٩٦﴾ وَاقْتَرَبَ الْوَعْدُ الْحَقُّ فَإِذَا هِيَ شَاخِصَةٌ أَبْصَارُ الَّذِينَ كَفَرُوا يَا وَيْلَنَا قَدْ كُنَّا فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا بَلْ كُنَّا ظَالِمِينَ﴾
"Mpaka watakapofunguliwa Ya'juj na Ma'juj nao wataporomoka kwa kasi, na ikakaribia ahadi ya kweli kufunguliwa, hesabu na malipo, basi wakati huo macho ya makafiriyatatokeza mno juu" (21:96 - 97)
Katika hadith aliyoipokea Imam Ahmad, na kusimuliwa na Khudhaifa Ibn Usaid Al - Ghifaar (r.a) amesema; Alitutokea Mtume (s.aw) kutoka chumbani kwake na sisi tukikumbushana jambo la kiyama, Mtume (s.a.w) akasema: Hakitosimama Kiyama mpaka muone alama kumi;
1. Kuchomoza jua Magharibi 2. Kutokea moshi mkubwa utakaochafua mazingira (pollution)
3. Mnyama atatokeza na kuwasemesha watu (27:82)
4. Kufunguliwa Ya'juj na Ma'juj (21:96 97)
5. Kurudi kwa Issa mwana wa Maryam Kuamini siku ya mwisho ni kuamini kuwa kuna maisha ya milele baada ya maisha haya ya hapa duniani. Kwa mujibu wa mafundisho ya Qur-an, maisha hayo yatakuwa na hatua kuu nne zifuatazo:
(i) kutokwa na roho
(ii) Maisha ya kaburini - Barzakh.
(iii) Kufufuka na kuhudhurishwa mbele ya Allah (s.w) na kuhesabiwa.
(iv) Maisha ya kukaa Peponi milele kwa watu wema au kukaa motoni kwa watu waovu. Aidha kwa kuzingatia matukio yatakayotokea katika hatua nne za maisha yajayo, siku ya mwisho katika Quran imepewa majina mengi yafuatayo:
(i) Siku ya Qiyama (21:47, 75:1, 75:6, 79: 42)
(ii) Siku ya mwisho (2:4, 2:8, 58:22)
(iii) Siku ya malipo (1:4, 82:9, 95:7, 107:1, 83:11)
(iv) Msiba ugongao nyoyo (101:1)
(v) Siku ya hukumu (77:13-14)
(vi) Wakati maalumu (56:49-50)
(vii) Siku ya makamio (50:20)
(viii) Siku ya makutano (40:15)
(ix) Siku iliyokaribu sana kufika (40:18)
(x) Siku ya kuitana (40:32)
(xi) Siku ya kutoka makaburini (50:42)
(xii) Tukio lilokaribu, limesogea
(xiii) Siku zitakapotikisika mbingu mtikisiko wake
6. Kuja kwa Masih Dajal (False Messayah)
7. Kutoka Moto (Volcano) katika pango la Aden
ukiwaendesha watu
8. Dunia kugawika mapande matatu (Three Blocks); Pande la Mashariki (Eastern Block)
9. Pande la Magharibi na (western block)
10. Bara Arab (Mashariki ya kati - Middle East)
Kwa hakika Qur'an imetaja dalili nyingi mno, Rejea Suratul qiyaamah (75:6 - 9) na nyinginezo nyingi zilizotajwa katika hadith mbali mbali.
(xiv) Siku ya kukaa daima (50:42)
(xv) Siku zitakapofichuliwa siri (86:9)
(xvi) Tukio la Haki (69:1-3)
(xvii) Siku ya Haki (78:39)
(xviii) Tukio kubwa (56:1-2)
(xix) Siku iliyokadiriwa (85:2)
(xx) Msiba ukumbao (88:1)
(xxi) Siku iliyokuu (83:5)
(xxii) Siku ya mkusanyiko (64:9)
(xxiii) Siku ya Hisabu
HOJA ZA WAPINZANI WA SIKU YA MWISHO
Wengi wa makafiri wapingao kuwepo siku ya mwisho wanatoa hoja kubwa mbili zifuatazo:
1. Hapana uwezekano wa kupatikana uhai baada ya mtu kuoza na mifupa yake kusagika sagika
﴿يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ ﴿١٠﴾ أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَّخِرَةً ﴿١١﴾ قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ﴾
"(Makafiri) wanasema (kwa stihizai) Je! Tutarudishwa katika hali yetu ya kwanza (tutafufuliwa)?Hata tukiwa mifupa mibovu (iliyooza)? (kwa stihizai wanasema):- Basi marejeo haya ni yenye hasara (kwetu)" (79:10-12)
﴿وَكَانُوا يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ﴾
"Na walikuwa wakisema: "Tutakapokufa na kuwa udongo na mifupa ndio tutafufuliwa? (56:47)
UDHAIFU WA HOJA
Allah (s.w) ameonyesha udhaifu wa hoja hii katika aya zifuatazo:
﴿أَوَلَمْ يَرَ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ ﴿٧٧﴾ وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ قَالَ مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ ﴿٧٨﴾ قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ ﴿٧٩﴾ الَّذِي جَعَلَ لَكُم مِّنَ الشَّجَرِ الْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَا أَنتُم مِّنْهُ تُوقِدُونَ ﴿٨٠﴾ أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم بَلَىٰ وَهُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ ﴿٨١﴾ إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾ فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴾
Je, mwanaadamu hatambui ya kwamba tumemuumba kwa tone la manii? Amekuwa hasimu yetu aliye dhahiri (Sasa)! Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake (kwa manii) - akasema: "Nani atakayeihuisha mifupa na hali imesagika?" Sema: "Ataihuisha yule aliyeiumba mara ya kwanza, naye ni Mjuzi wa kila (namna ya) kuumba. Ambaye amekufanyieni moto katika mti mbichi, mkawa nanyi kwa (mti) huo mnauwasha. Je, yule aliyeziumba mbingu na ardhi (mnaona) hana uweza wa kuumba (mara ya pili) mfano wao (wanaadamu)?Kwa nini? Naye ni Mwumbaji mkuu, Mjuzi (wa kila jambo).Hakika amri yake anapotaka chochote (kile kitokee) ni kukiambia:'Kuwa,' basi mara huwa. Ametukuka yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake mtarejezwa nyote. (36:77-83)
﴿أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُ ﴿٣﴾ بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُ﴾
Anadhani mtu ya kuwa sisi hatutaikusanya mifupa yake?Kwa nini! Sisi tunaweza (hata) kuzisawazisha ncha za vidole vyake (tutakapomfufua mara ya pili,ziwe kama zilivyokuwa duniani) (75:3-4)
﴿أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ ﴿١٧﴾ وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ ﴿١٨﴾ وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ ﴿١٩﴾ وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ﴾
Je! Hawawatazami ngamia jinsi walivyoumbwa? Na mbingu jinsi zilivyoinuliwa. Na milima jinsi ilivyothubutishwa? Na ardhi jinsi ilivyotandazwa? (Basi aliyeyafanya hayo kutamshinda kufufua Binaadamu)? (88:17-20)
﴿وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ وَلَهُ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴾
Na yeye ndiye aliyeanzisha viumbe na ndiye Atakayevirudisha (mara nyingine), na (jambo) hili ni rahisi zaidi Kwake; naye ndiye mwenye sifa nzuri mbinguni na katika ardhi, naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. (30:27)
﴿أَفَعَيِينَا بِالْخَلْقِ الْأَوَّلِ بَلْ هُمْ فِي لَبْسٍ مِّنْ خَلْقٍ جَدِيدٍ ﴾
Je! Tulichoka kwa kuumba kwa mara ya kwanza (hata tushindwe kuumba umbo la pili)? Basi wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya! (50:15)
2. Waliokufa hawajarudi wakatoa ushahidi
﴿وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ مَّا كَانَ حُجَّتَهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا ائْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴾
"Wanaposomewa aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila husema waleteni baba zetu (wazee wetu waliokufa) ikiwa nyinyi ni wasemao kweli (kuwa watu watafufuliwa)" (45:25)
Udhaifu wa Hoja Kutofufuka waliotangulia kufa sio hoja ya kutokuwepo ufufuo, kwani katika utaratibu wa Allah (s.w) watu hawatafufuliwa mmoja mmoja, bali watafufuliwa wote kwa pamoja, wa mwanzo na wa mwisho katika siku hiyo maalumu:
﴿قُلْ إِنَّ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ ﴿٤٩﴾ لَمَجْمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَاتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ ﴾
"Sema "Bila shaka wa kwanza na wa mwisho watakusanywa kwa wakati (uliowekwa) katika siku maalum. (56:49-50).
Ulazima wa kuwepo Siku ya Mwisho Kimantiki kuwepo siku ya malipo (siku ya hukumu) ni jambo lisilo budi ili:
1. WALE WALIOFANYA WEMA HAPA DUNIANI BILA YA KUPATA UJIRA UNAOSTAHIKI, WALIPWE FADHILA YA WEMA WAO.
﴿هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ﴾
"Hakuna malipo ya ihsani ila kulipwa ihsani" (55:60)
2. WALE WALIODHULUMU HAKI ZA WATU HAPA DUNIANI, WARUDISHE HAKI ZA WENYEWE MBELE YA HAKIMU WA MAHAKIMU.
﴿أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ ﴾
"Je!Mwenyezi Mungu si Hakimu muadilifu kuliko mahakimu wote? (95:8)
3. WALE WABABE WALIOFANYA UOVU ULIOKITHIRI HAPA DUNIANI
bila ya kupata adhabu inayostahiki, wahukukumiwe na kupewa adhabu inayolingana na makosa yao mbele ya Mfalme wa Wafalme.
﴿مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ﴾
"Mwenye kumiliki siku ya malipo" (1:4)
4. WATU WAULIZWE VIPI WALISHUKURU JUU YA NEEMA NA VIPAJI MBALI MBALI WALIVYOTUNUKIWA NA MUUMBA WAO.
﴿ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ ﴾
"Kisha kwa hakika mtaulizwa siku hiyo juu ya neema (mlizopewa mlizitumiaje)? (102:8)
5. WABAINIKE NI AKINA NANI WALIOFUATA NJIA SAHIHI YA MAISHA, WAISLAMU AU MAKAFIRI?
﴿وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَا يَبْعَثُ اللَّـهُ مَن يَمُوتُ بَلَىٰ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٨﴾ لِيُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي يَخْتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّهُمْ كَانُوا كَاذِبِينَ﴾
"Nao (wakaapa) kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa kiapo chao cha nguvu (kwamba Mwenyezi Mungu hatawafufua wafao.Kwanini (asiwafufue)? Ni ahadi iliyolazimika kwake,(kuwafufua na kuwalipa) lakini watu wengi hawajui.(Atawafufua) ili kuwabainishia yale waliyohitalifiana ili wajue waliokufuru ya kwamba wao walikuwa ni waongo.(16:38 - 39)
Ushahidi wa Ufufuo kutokana na Historia Tukirejea Qur-an tunafahamishwa matukio kadhaa ya kihistoria yanayotudhihirishia kuwa ufufuo ni jambo jepesi kwa Allah (s.w). Matukio haya ni pamoja na:
1. Kufufuka msafiri na punda wake
﴿أَوْ كَالَّذِي مَرَّ عَلَىٰ قَرْيَةٍ وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحْيِي هَـٰذِهِ اللَّـهُ بَعْدَ مَوْتِهَا فَأَمَاتَهُ اللَّـهُ مِائَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ قَالَ كَمْ لَبِثْتَ قَالَ لَبِثْتُ يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ قَالَ بَل لَّبِثْتَ مِائَةَ عَامٍ فَانظُرْ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمْ يَتَسَنَّهْ وَانظُرْ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجْعَلَكَ آيَةً لِّلنَّاسِ وَانظُرْ إِلَى الْعِظَامِ كَيْفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكْسُوهَا لَحْمًا فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ قَالَ أَعْلَمُ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴾
"Au kama yule aliyepita karibu na mji uliokuwa umekufa akasema:"Mwenyezi Mungu atauhuisha vipi (mji) huu (na watu wake) baada ya kufa kwake?" Basi Mwenyezi Mungu alimfisha kwa miaka mia, kisha akamfufua akamwuliza:"Umekaa muda gani?" Akasema: "Nimekaa muda wa siku moja au sehemu ya siku." (Mwenyezi Mungu) akasema: "Bali umekaa miaka mia; nawe tazama chakula chako na vinywaji vyako, havikuharibika. Na mtazame punda wako (amekuwa mifupa mitupu iliyolikalika).Na ili tukufanye uwe hoja kwa watu (ndio tumekufufua hivi). Na itazame mifupa (ya punda wako) jinsi tunavyoinyanyua,kisha tunaivisha nyama."Basi yalipombainikia (haya yule aliyefufuliwa) alinena: 'Najua kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu." (2:259)
2. KUFUFUKA NDEGE WA NABII IBRAHIMU(A.S)
﴿وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ أَرِنِي كَيْفَ تُحْيِي الْمَوْتَىٰ قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِن قَالَ بَلَىٰ وَلَـٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِي قَالَ فَخُذْ أَرْبَعَةً مِّنَ الطَّيْرِ فَصُرْهُنَّ إِلَيْكَ ثُمَّ اجْعَلْ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٍ مِّنْهُنَّ جُزْءًا ثُمَّ ادْعُهُنَّ يَأْتِينَكَ سَعْيًا وَاعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴾
Na (kumbuka) Ibrahimu aliposema:"Mola wangu!Nionyeshe jinsi utakavyofufua wafu"(Mwenyezi Mungu) akasema:"Huamini?"Akasema: "La, (naamini), lakini (nataka kuona hayo) ili moyo wangu utulie (zaidi)" Akasema: "Basi chukua ndege wanne na uwazoeshe kwako (uwadhibiti vizuri sura zao hata wasikupotee popote unapowaona), kisha (wachinje) uweke juu ya kila jabali sehemu katika wao.Kisha waite, watakujia mbio. Na ujue ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye hikima". (2:260)
3. KUAMKA AS-HABUL-KAHF
﴿ وَلَبِثُوا فِي كَهْفِهِمْ ثَلَاثَ مِائَةٍ سِنِينَ وَازْدَادُوا تِسْعًا ﴾
"Na walikaa katika pango lao miaka mia tatu, na wakazidisha (miaka) tisa" (18:25)
4. KUFUFUKA KWA WATU WA NABII MUSSA(A.S)
﴿ وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْكُمُ الصَّاعِقَةُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ﴾
Na (kumbukeni habari hii pia:) Mliposema:"Ewe Mussa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu wazi wazi" Yakakunyakueni mauti ya ghafla), na hali mnaona. Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu, ili mpate kushukuru. (2:55-56)
5. KUFUFUKA KWA YULE MTU ALIYEULIWA KWA DHULUMA WAKATI WA NABII MUSSA(A.S)
﴿ وَإِذْ قَتَلْتُمْ نَفْسًا فَادَّارَأْتُمْ فِيهَا وَاللَّـهُ مُخْرِجٌ مَّا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٧٢﴾ فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا كَذَٰلِكَ يُحْيِي اللَّـهُ الْمَوْتَىٰ وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴾
Na (kumbukeni khabari hii inayotajwa sasa hivi:) Mlipoiua nafsi, kisha mkakhitilafiana kwa hayo; (wengine wanasema kauawa na Fulani na wengine wanasema Fulani mwingine). Na Mwenyezi Mungu ni Mtoaji wa hayo mliyokuwa mkiyaficha.(Basi akayatoa akajulikana huyo aliyemwua). Tukasema: "Mpigeni kwa baadhi (sehemu) yake (huyu ng'ombe)." Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuisha wafu; na anakuonyesheni Dalili zake ili mpate kufahamu.(2:72-73)
6. NABII ISSA(A.S) ALIFUFUA WAFU KWA IDHINI YA ALLAH (S.W)
﴿ وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنِّي قَدْ جِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ أَنِّي أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللَّـهِ وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ اللَّـهِ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴾
"Na (atamfanya) Mtume kwa wana wa Israili, (kuwaambia): 'Nimekujieni na hoja kutoka kwa Mola wenu, ya kwamba nakuumbieni, katika udongo, kama sura ya ndege, kisha nampuliza, mara anakuwa ndege, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.Na ninawaponesha vipofu na wenye mbalanga, na ninawafufua (baadhi ya) waliokufa,kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na nitakwambieni mtakavyovila na mtakavyoweka akiba katika nyumba zenu. Bila shaka katika haya imo hoja kwenu ikiwa nyinyi ni watu wa kuamini'!" (3:49)
Uthibitisho wa Ufufuo kutokana na maisha ya kila siku Allah (s.w) pia anatupigia mifano kutokana na maisha yetu ya kila siku inayotuyakinisha juu ya ufufuo. Miongoni mwa mifano hii ni:-
1. Kufufuka kwa ardhi wakati wa mvua baada ya kufa kwake wakati wa kiangazi
﴿ وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ إِنَّ الَّذِي أَحْيَاهَا لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴾
"Na katika ishara zake ni kwamba unaona ardhi imedhalilika (kwa kukosa mvua) lakini tunapoiteremshia maji mara unaiona inataharaki na kuumuka; bila shaka aliyeihuisha ndiye atakayehuisha waliokufa. Hakika yeye ndiye mwenye uweza juu ya kila kitu" (41:39)
2. Kufufuka kutoka usingizini
﴿وَمِنْ آيَاتِهِ مَنَامُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَابْتِغَاؤُكُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ﴾
"Na katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na kuamka mchana ,na kutafuta fadhila Yake.Hakika katika haya zimo Ishara kwa watu wanaosikia(30:23)
3. Kufufuka kutoka kwenye kuzimia. Mtu aliyezimia ni kama mtu aliyekufa kwani hajitambui wala hajiwezi kwa lolote, na anapozindukana hajui lolote lililoendelea katika kipindi cha kuzimia kwake.
MAZINGIRA YA MAISHA YA AKHERA
Qur-an Karimu imechukua sehemu kubwa kuelezea maisha ya akhera kuanzia pale roho ya mtu inapokaribia kutoka mpaka katika hatua ya mwisho ya kuingia peponi kwa watu wema au kuingia motoni kwa watu waovu. Hakika iliyowazi ya kufahamishwa maisha ya akhera yatakavyokuwa ndani ya Qur'an ni kumtahadharisha binaadamu na maisha hayo ili aishi kwa uangalifu kwa kuzingatia maisha hayo yajayo.
Muumini baada ya kupewa picha kamili ya maisha ya akhera na Mola wake atajitahidi kufuata mwenendo mwema wa maisha utakaompelekea kupata radhi za Allah na kustahiki kupata mwisho mwema na kuingizwa katika neema za peponi na kujitahidi kujiepusha na mwenendo mbaya wa maisha ili kuepukana na ghadhabu za Allah (s.w) na kuepukana na adhabu kali ya motoni watakayostahiki kupata watu waovu waliomkufuru na kumuasi Mola wao. Ili tupate picha kamili juu ya maisha ya akhera katika sehemu hii tumenukuu na kurejea aya chache za Qur-an na Hadith sahihi za Mtume(s.a.w.w) juu ya kila hatua ya maisha ya akhera kama ifuatavyo:
(i)Wakati wa Kukaribia kufa Mtu anapokaribia kufa na hasa baada ya kumuona malaika aliyehudhurishwa kuchukua roho yake huwa na yakini juu ya maisha ya akhera. Watu wema watafurahia kufa kwa yale maliwazo watakayopewa na malaika:
﴿ يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ ﴿٢٧﴾ ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً ﴿٢٨﴾ فَادْخُلِي فِي عِبَادِي ﴿٢٩﴾ وَادْخُلِي جَنَّتِي ﴾
"Ewe nafsi yenye kutua! Rudi kwa Mola wako hali ya kuwa utaridhika (kwa utakayoyapata), na (Mwenyezi Mungu) aridhike na wewe. Basi ingia katika (kundi la) waja wangu (wazuri) uingie katika pepo yangu" (89:27-30)
Watu waovu watajuta kwa kupoteza muda wao nje ya lengo la kuumbwa kwao na wataomba wacheleweshwe kidogo ili wafanye mema. Juu ya hili Allah (s.w) anatutahadharisha:
﴿ وَأَنفِقُوا مِن مَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَا أَخَّرْتَنِي إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٠﴾ وَلَن يُؤَخِّرَ اللَّـهُ نَفْسًا إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴾
"Na toeni katika yale tuliyokupeni kabla ya mmoja wenu hayajamfika mauti; kisha akasema: Mola wangu: Huniakhirishi muda kidogo (tu) nikatoa sadaqa na nikawa miongoni mwa watendao mema! Lakini Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapokuja ajali yake; Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda" (63:10-11)
﴿ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ ﴿٩٩﴾ لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ كَلَّا إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَائِلُهَا وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ﴾
"Hata yanapomfika mmoja wao mauti husema: "Mola wangu! Nirudishe (katika uhai) ili nifanye mema sasa badala ya yale niliyoyaacha" (23:99-100)
Jambo la kuzingatia hapa ni kuwa muda (wakati) ambao ndiyo rasilimali ya uhai wa binaadamu unahitajika utumike wote katika kuendea lengo la maisha ya binaadamu hapa ulimwenguni. Muda wote uliotumika nje ya lengo utakuwa ni wenye kujutiwa. Lagh-wi (mambo ya upuuzi yanayopoteza muda wa kuendea lengo) ni haramu katika Uislamu. Rejea sifa za waumini Qur-an 23:2) na (25:72).
Hebu turejee hadith za Mtume(s.a.w.w) juu ya hali wanayokuwa nayo watu wanao karibia kufa"Ubaidah bin Swamiti amesimulia kuwa Mtume wa Allah(s.a.w.w) amesema: Yeyote anayependa kukutana na Allah (s.w), naye Allah (s.w) anapenda kukutana naye; na yeyote yule asiyetaka kukutana naye, pia Allah (s.w) hana haja ya kukutana naye. Aisha, au baadhi ya wake zake Mtume(s.a.w.w) wakasema: Hakika ni kweli hatupendi kifo. Alifafanua Mtume(s.a.w.w) "Sio hivyo, bali wakati kifo kinapomjia Muumini, anapewa habari njema juu ya ridhaa ya Allah (s.w) na neema zake. Baada ya habari hizi hatakuwa na kitu chochote atakachokipenda zaidi kuliko kifo (kinachomkaribia). Kwa hiyo atataka kukutana na Allah (s.w) na Allah (s.w) atataka kukutana naye.Na asiye muumini, kifo kinapomkaribia anapewa habari mbaya juu ya adhabu kali ya Allah (s.w). Na hapati kuwa na kitu kisichopendeza mbele yake kuliko hicho kinachomngojea mbele yake.Kwa hiyo Allah pia hataki kukutana naye. (Bukhari na Muslim).
Katika Hadith nyingine: "Anas amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alikwenda kumuona kijana ambaye alikuwa katika hali ya ulevi wa mauti (Mtume(s.a.w.w) alimuuliza: Unajisikiaje? Alijibu (kijana): "Ewe Mtume wa Allah!Ninamtumainia Allah (s.w) na ninaogopa madhambi yangu." Ndipo Mtume(s.a.w.w) . Hivi viwili haviungani pamoja katika moyo wa mja kama hivi kwa wakati mmoja, isipokuwa Allah (s.w) anampa (mja wake) kile anachokitumaini na kumkinga na kila anachokiogopa" (Ibn Majah na Tirmidh)
Katika hadithi hizi tunajifunza kuwa watu wema watapata maliwazo na matumaini wakati wa kukaribia kufa na watu waovu watakata tamaa na kuhuzunika wakati huo.
(ii) Kutolewa roho (kufikwa na kifo) Kifo ni katika ishara kubwa ya kuwepo Allah (s.w) na siku ya mwisho. Binaadamu pamoja na mamlaka yake hana uwezo wa kuzuia kifo kisimfike. Wafalme pamoja na kuzungukwa na walinzi wenye silaha na zana za ulinzi madhubuti wanakufa kila uchao. Zingatia kuondoka kwa wafalme mbalimbali unaowafahamu katika historia kuanzia enzi za Fir'aun mpaka kwa hawa wafalme waliofutika katika uso wa dunia hivi karibuni. Allah (s.w) anatutanabahisha:
﴿ فَلَوْلَا إِذَا بَلَغَتِ الْحُلْقُومَ ﴿٨٣﴾ وَأَنتُمْ حِينَئِذٍ تَنظُرُونَ ﴿٨٤﴾ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُبْصِرُونَ ﴿٨٥﴾ فَلَوْلَا إِن كُنتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ ﴿٨٦﴾ تَرْجِعُونَهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴾
"Basi mbona (roho) ifikapo kooni, na nyinyi wakati ule mnamtazama,nasi tunakaribiana naye zaidi (huyo anayetokwa na roho) kuliko nyinyi wala nyinyi hamuoni. Kama nyinyi hamumo katika mamlaka (yangu) ,kwanini hamuirudishi (hiyo roho) ikiwa mnasema kweli?" (56:83-87)
Kama tulivyojifunza katika Hadith, watu wema baada ya kupata bishara za kuridhiwa na Mola wao watafurahia kufa na roho zao zitatolewa kwa upole. Kinyume chake, watu waovu baada ya kuona dalili za ghadhabu za Allah juu yake hatapenda kufa na kuwalazimu Malaika husika wachukue roho zao kwa nguvu. rejea kazi za malaika.
(iii) Maisha ya Barzakh (Kaburini)
﴿ لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ كَلَّا إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَائِلُهَا وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ﴾
"na mbele yao kuna Barzakh (maisha baada ya kufa) mpaka siku ya kufufuliwa". [23:100]
Kwa mujibu wa aya hii Barzakh ni kipindi cha maisha ya kaburini kinachodumu kwa kipindi chote ba ada ya mtu kufa mpaka siku ya kufufuliwa watu wote. Hiki ni kipindi ambacho roho za watu zinakuwa zimetengana na miili husika. Ambapo roho zitakuwa hai ima katika starehe au katika adhabu kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo: Anas amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema: Hakika mja anapolazwa kaburini na jamaa zake wakawa wanarejea nyumbani anasikia sauti ya miguu yao. Malaika wawili humjia na kumkalisha na kumuuliza: Ulikuwa ukisemaje juu ya huyu Muhammad? Kama ni muumini atajibu: "Ninashuhudia kuwa yeye ni mja wa Allah (s.w.). Ataambiwa kuwa angalia sehemu yako ya motoni uliyobadilishiwa na sehemu katika pepo. Kisha ataziona sehemu zote mbili
Kwa Mnafiki au Kafiri ataulizwa: ulikuwa ukisema nini juu ya huyu mtu (Muhammad)? Atajibu:"Sijui, nilikuwa nikisema kama watu walivyokuwa wakisema. Ataambiwa hukuwahi kujua wala kusoma. Kisha atapigwa dharuba na rungu la kipande cha chuma, kwa kiasi kwamba atapiga kelele ambayo itasikiwa na kila kitu isipokuwa viumbe wa aina mbili (watu na majini)". [Bukhari na Muslim]
Pia katika hadithi nyingine tunafahamishwa: Abdullah bin Umar umesimulia kuwa: Mtume wa Allah (s.w.) amesema:"Hakika wakati miongoni mwenu anapokufa. Mahali anapokwenda huwekwa mbele yake asubuhi na usiku. Kama ni miongoni mwa wakaazi wa peponi (roho yake) itakuwa ni miongoni mwa wakaazi wa peponi. Ikiwa yeye ni miongoni mwa wakazi wa motoni, (pia roho yake) itakuwa ni miongoni mwa wakaazi wa motoni. Kisha ataambiwa: "Hii ndio sehemu yako mpaka utakapofufuliwa siku ya kiyama" . [Bukhari na Muslim]
Aysha amesimulia kuwa mwanamke wa Kiyahudi alimuendea na kumsimulia adhabu ya kaburini. Akamwambia: "Allah akukinge na adhabu ya kaburini.Aysha akamuuliza Mtume(s.a.w.w) juu ya adhabu ya kaburini Mtume(s.a.w.w) akajibu: "Ndio. Adhabu ya kaburini ni jambo la kweli". Aysha alisema: Sikumuona Mtume(s.a.w.w) baada ya hapo kuswali swala yoyote bila ya kumuomba Allah amkinge na adhabu ya kaburini. [Bukhari na Muslim]
Ibn Abbas amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) alikuwa akiwafundisha (kwa msisitizo) dua (ifuatayo) kama alivyokuwa akiwafundisha sura ya Qur'an kwa kuwaambia:"Sema, Ee Allah! Nakijinga kwako na adhabu ya Jahannam na najikinga kwako na adhabu ya kaburi,na najilinda kwako na majaribu ya Dajjal mwenye jicho moja, na najikinga kwako na majaribu ya maisha ya kifo" [Muslim]
Hadithi zote hizi zinatuthibitishia kuwa Roho, katika kipindi cha Barzakh, zitakuwa katika raha au taabu, kulingana na yale mja aliyoyatanguliza kutokana na matendo yake hapa duniani. Ndio maana Mtume(s.a.w.w) akatufundisha dua hiyo na akatusisitiza tumuombe Allah (s.w.) atukinge na adhabu katika maisha ya akhera na atuwezeshe kufaulu mitihani ya majaribio ya maisha ili tuweze kupata maisha ya salama na amani katika makazi ya akhera. Hebu tuzidi kuzingatia hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) wa Allah amesema: Baada ya maiti kuzikwa malaika wawili, mmoja mweusi na mwingine mwenye rangi ya kibluu, watamjia. Mmoja wao anaitwa Munkar na mwingine Nakiir. Watauliza: Unasemaje juu ya huyu mtu? Kama (maiti huyo alikuwa Muumini atajibu).Ni mja wa Allah (s.w.) na ni Mtumwa wake. Ninashuhudia kuwa hapana Mola ila Allah (s.w.) na kwamba Muhammad ni Mtume(s.a.w.w) wake na Mjumbe wake.
Watasema: Tulijua kuwa utajibu hivyo baadaye (baada ya swali). Kaburi lake litafanywa pana kiasi cha dhiraa sabiini kwa kila upande na kisha patakuwa na mwanga na ataambiwa: Lala kama usingizi wa Bwana arusi ambaye hakuna anayeweza kumuasha isipokuwa wapenzi wake katika familia. Mpaka Allah (s.w.) atakapomuinua kutoka kwenye kitanda chake. Kama (maiti) alikuwa Mnafiki, atajibu: Nimesikia watu wakisema neno kama hili linalosema: Simjui. (Malaika) watasema: Tulijua kuwa utasema hivyo.Kisha ardhi itaambiwa M'bane. Kisha itam'bana mpaka pande mbili (ubavu wa kulia na kushoto) zibadilishane.
Hatapumzika na adhabu ya hapo mpaka Allah atakapomuinua kutoka kwenye kitanda chake hicho. [Tirmidh] Katika hadithi nyingine: Abu Hurairah amesimulia kutoka kwa Mtume (s.a.w) wa Allah ambaye alisema: Hakika maiti hupelekwa kaburini na hukaa kaburini bila ya khofu wala fadhaa. Baada ya hapo ataambiwa: Ulikuwa katika nini? Atajibu: "Nilikuwa katika Uislamu". Kisha ataulizwa: Huyu ni nani? Atajibu: Muhammad, Mtumwa wa Allah.
Alitujia na hoja zilizowazi kutoka kwa Allah (s.w.) na kwa hivyo tulimuamini. Ataulizwa tena: Umemuona Allah? Atajibu: Si katika uwezo wa yeyote kumuona Allah.Kisha patawekwa uwazi utakaomwezesha kuona moto unaofoka. Ataambiwa: Angalia kile ambacho Allah amekuokoa (amekukinga) nacho. Kisha patawekwa uwazi utakaomuwezesha kuiona pepo na vile vilivyomo ndani yake. Ataambiwa: Hii ni sehemu yako kutokana na uthabiti wa imani uliyoishi nayo na ukafa nayo na ambayo utafufuliwa nayo, InshaAllah.
Mtu muovu, atakuwa katika kaburi lake kwa khofu na fadhaa.Ataulizwa ulikuwa katika nini? Atajibu: Sijui. Kisha ataulizwa tena: Ni nani huyu? Atajibu: Nilisikia watu wakisema kama ninavyosema. Kisha atawekewa uwazi wa kumuwezesha kuiona pepo. Ataangalia na kuona uzuri wake na vilivyomo ndani yake. Ataambiwa angalia kile ambacho Allah amekukosesha (kutokana na imani yake mbovu). Kisha utawekwa uwazi wa kumuwezesha kuona moto. Ataungalia na ataona muwako wake ulio mkali. Kisha ataambiwa.Hii ndio sehemu yako ambayo uliendesha maisha yako kwa kuwa na mashaka nayo, na umekufa ukiwa na mashaka nayo na utafufuliwa katika hali hiyo hiyo, InshaAllah. [Ibn Majah]
Hadithi hizi zimetuweka wazi juu ya hali zitakazokuwa nayo Roho za waja katika kipindi cha kukaa kaburini.Patakuwa na maswali yatakayoulizwa mara tu mtu anapokufa. Maswali haya yatakuwa ni mtihani kwa mja. Waumini tu ndio watakaoweza kujibu maswali haya kwa usahihi na ndio pekee watakaofaulu na kupewa bishara nzuri ya kupata pepo na neema zake. Kwa hawa kaburi huwa ni Bustani miongoni mwa bustani za peponi. Makafiri, Washirikina na Wanafiki hawataweza kujibu maswali watakayoulizwa, na watashindwa mtihani huu na kuahidiwa adhabu kali ya motoni na wataendelea kupata adhabu kali katika kipindi chote hiki cha maisha ya kaburini kama ujira wa imani yao mbovu juu ya Allah (s.w.) iliyosababisha matendo yao kuwa maovu. Kwa hawa kaburini huwa ni mashimo miongoni mwa mashimo ya motoni. Jambo muhimu linalotubidi tulifahamu kwa uwazi ni kwamba uwezo wa kujibu maswali haya haupatikani kwa kusoma na kukariri majibu kama tufanyavyo katika matayarisho ya mitihani yetu ya kila siku au mahojiano, bali uwezo wa kujibu maswali hayo hupatikana kutokana na uthabiti wa imani katika maneno na matendo ya kila siku. Wanafiki, wenye kuamini kinadharia tu, hawatakuwa na uwezo wa kujibu maswali hayo, hata kama walikuwa ni Masheikh wa kuwasomea watu talakini katika maisha yao yote.
Hivyo si talakini anayosomewa mtu wakati wa kuzikwa itakayomuwezesha kujibu maswali ya Munkar na Nakiir, bali kitakachomsadiia mtu ni ule uthabiti wa imani yake iliyofuatiwa na matendo mema katika utendaji wa maisha yake yote ya hapa ulimwenguni. Kwa ukweli huu Mtume(s.a.w.w) kila baada ya kumaliza kumzika mtu alikuwa akiwaambia Maswahaba wamtakie maghfira ndugu yao na wamuombee uthabiti wa imani ili aweze kujibu maswali yale inavyostahili. Hivi ndivyo tunavyofahamishwa katika hadithi ifuatayo: Uthman amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) alipomaliza kumzika mtu aliyekufa alikuwa akisimama pale (kaburini) na kusema: "Mtakie maghfira ndugu yenu na muombeeni awe thabiti kwani ataulizwa sasa hivi". [Abuu Daud]
Kwa ufupi maisha Barzakh huwa kama mt aliyelala na kuota ndoto, mtu mwema, kwa kipindi chote atakacholala kaburini humo. ataota ndoto nzuri na muovu ataota ndoto mbaya zitakazoudhi nafsi yake kwa kipindi chote atakacholala kaburini humo. Kutokana na Hadith hii hakuna mtu yeyote wa kumuwezesha mtu kufaulu mtihani huu wa Allah (s.w.) mbali na uthabiti wa imani yake na matendo yake katika maisha ya dunia.
8
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
(iv) SIKU YA KUFUFULIWA
Baada ya kipindi cha Barzakh watu watafufuliwa na kuelekea kwenye uwanja wa Hisabu - kama tunavyojifunza katika Qur'an:
﴿ وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَإِذَا هُم مِّنَ الْأَجْدَاثِ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يَنسِلُونَ ﴿٥١﴾ قَالُوا يَا وَيْلَنَا مَن بَعَثَنَا مِن مَّرْقَدِنَا هَـٰذَا مَا وَعَدَ الرَّحْمَـٰنُ وَصَدَقَ الْمُرْسَلُونَ ﴿٥٢﴾ إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً فَإِذَا هُمْ جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ ﴿٥٣﴾ فَالْيَوْمَ لَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴾
Na kisha litapigwa baragumu (la kufufuliwa), tahamaki hao wanatoka makaburini kwenda mbio mbio kwa Mola wao. (Na huku) wanasema: Ole wetu, (Eee adhabu yetu)!Nani aliyetufufua malaloni petu?" (Waambiwe): "Haya ndiyo yale aliyoahidi (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema na waliyoyasema kwa haki Mitume". Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, tahamaki wote wamehudhurishwa mbele yetu. (Waambiwe) "Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa chochote kile wala hamtalipwa ila yale mliyokuwa mkiyatenda".[36:51-54]
Aya hizi zinatufahamisha kuwa hali ya siku hiyo itakuwa ni tofauti kabisa na hali ya hapa ulimwenguni na kwa ujumla itakuwa ni hali ya kutisha na ngumu kwa wanadamu (na majini). Muelekeo wa watu wote baada ya kufufuliwa utakuwa kwa Mola wao katika uwanja wa Hisabu. Japo katika aya nyingi za Qur'an siku ya kufufuliwa imeunganishwa moja kwa moja na siku ya hisabu, bado katika Hadith tunawekwa wazi kuwa patapita muda mrefu wa taabu na mashaka kabla ya kufikia katika hisabu. Patakuwa na jua kali na joto kali sana. Ardhi na mbingu vitakuwa vya shaba kama tunavyofahamishwa katika aya hii:
﴿ يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ﴾
"Siku mbingu zitakapokuwa kama shaba iliyoyeyuka". [70:8].
Katika hali hii joto na jua kali watu watabubujikwa na jasho litakalofurika kama tunavyofahamishwa katika hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:Siku ya kufufuliwa (Siku ya Kiyama) watu watatokwa na jasho kwa kiasi ambacho jasho lao litafurika juu (litakuwa na kina) kiasi cha dhiraa sabini na litawazamisha watu mpaka kufikia masikioni. [Bukhari na Muslim]
Mbubujiko na mafuriko haya ya jasho yatategemeana na matendo waliyoyatanguliza waja. Kama tunavyopata ufafanuzi katika Hadith ifuatayo: Miqdad amesimulia: Nimemsikia Mtume(s.a.w.w) akisema: Siku ya Kiyama jua litashushwa karibu na viumbe kiasi cha umbali wa maili moja. Watu watatokwa na jasho kulingana na matendo yao. Kwa watu wengine litafika kwenye fundo za miguu, wengine litafika mpaka magotini na katika watu kuna wale watakaozamishwa mzamisho mkubwa na jasho lao, akiashiria mdomoni mwake kwa mkono wake" [Muslim]
Watu wataangalia mbinguni juu kwa juu kwa muda wa miaka arobaini. Matumbo yataungua kwa njaa na midomo itapasuka kwa kiu. Kila mmoja siku hiyo atahakikisha kuwa siku aliyoahidi Allah (s.w.) na kuikariri mara nyingi katika ujumbe wake, ndio hiyo iliyowadia na hapana popote pa kukimbilia isipokuwa kwa Mola wako.Kila mmoja ataona matendo yake yamehudhurishwa. Na katika hali hii Qur'an inauliza:
﴿ وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٧﴾ ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٨﴾ يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْئًا وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّـهِ﴾
Ni nini kitakachokujulisha siku ya malipo ni siku gani hiyo. Tena nini kitakachojulisha siku ya malipo ni siku gani hiyo?Ni siku ambayo nafsi hitamilikia nafsi (nyingine) chochote. Na amri siku hiyo itakuwa ya Mwenyezi Mungu tu" [82:17-19]
Kwa ujumla kipindi kati ya kufufuliwa na kufikia hisabu, kitakuwa kigumu sana na kila mtu atahisi ugumu wake na kiasi ambacho hata Mitume wa Allah (s.w.) ambao ni vipenzi vyake watahisi. Hapana nafsi itakayojiamini, kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifuatayo:
Aysha amesimulia kuwa alikumbuka moto na akaangusha kilio. Mtume(s.a.w.w) akauliza:Ni kitu gani kinachokuliza? Akajibu: "Nimekumbuka moto na nikaanza kulia. Je utawakumbuka wake zak siku ya Kiyama?" Mtume (s.a.w.) akasema: "Sikiliza: Katika sehemu tatu (zifuatazo) hakuna atakayemkumbuka yeyote yule - karibu na mizani (hisabu) mpaka ajue kuwa mizani yake itakuwa nyepesi au nzito, na karibu na kupewa kitabu kilichorikodiwa matendo mpaka utakapoitwa: Njoo, soma kitabu chako, na mpaka atakapopewa kitabu chake kwa mkono wa kulia au kushoto au nyuma ya mgongo wake, na karibu na njia nyembamba (siratwa) inakayowekwa baina ya ncha mbili za moto wa Jahannam". [Abuu Daud]
Hata hivyo, tunafahamishwa katika Hadith kuwa katika hicho kipindi kigumu cha baina ya kufufuliwa na kuhukumiwa, waumini waliotenda matendo mema watawekewa kivuli cha Allah (s.w.) na kila Mtume atapewa kisima au haudhi ya maji ya kuwanywesha watu wa ummah wake walioamini pamoja naye. Mtume(s.a.w.w) ameahidiwa Kauthar katika Qur'an:
﴿ إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ ﴾
"Hakika Tumekupa kheri nyingi" [108:1]
Kutokana na Hadith, Kauthar ni Birika (haudhi) aliloahidiwa Mtume(s.a.w.w) ambalo maji yake ni matamu kuliko asali na meupe kuliko maziwa na yanakata kiu milele - yaani kila mwenye kunywa maji hayo hasikii kiu tena.
Hadith ifuatayo inatufahamisha Kauthar ni nini: Abdullah bin Amr amesimulia kuwa Mtume wa Allah (s.w.) amesema: "Haudhi yangu ina urefu wa safari ya mwezi mmoja na ni pembe mraba na maji yake ni meupe kuliko maziwa, na harufu yake ni nzuri kuliko misk na vikombe vyake vinang'ara kama nyota angani. Yeyote yule anywaye maji yake hasikii kiu daima . [Bukhari na Muslim]
Watakaonyweshwa maji haya na Mtume(s.a.w.w) katika kipindi hicho kigumu cha joto kali lisilo kifani, njaa inayounguza matumbo na kiu kikali kisicho kifani, ni wale tu katika waumini waliomfuata Mtume(s.a.w.w) bila ya kumzumulia lolote. Waliozusha jambo lolote katika dini, Mtume(s.a.w.w) atawafukuza na kuwanyima maji yake kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifautayo:
Sahl bin Sa'ad amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema: Hakika nitawatangulia katika Haudhi. Yeyote atakayepita kwangu atakunywa, na yeyote atakayekunywa hatasikia kiu daima. Watu wale nitakaowajua na watakaonijua hapana shaka watakuja kwangu kunywa lakini patakuwa na kizuizi kati yangu na wao, kisha nitasema: "Hakika hawa ni wangu". Patasemwa: Hakika hujui ni uzushi gani waliokuzulia baada yako. Kisha nitasema: Ondokeni, ondokeni nyinyi mlionizulia (mliozua mambo na kuyaingiza kwenye dini) baada ya yangu. [Bukhari na Muslim]
(V) SIKU YA HUKUMU
Siku ya Hukumu ndio Siku Kuu ambapo Ufalme wa Allah (s.w.) utaonekana kwa wazi kwa kila mtu. Kila mtu atayakinisha kuwa Ufalme ni wa Allah (s.w.) Peke Yake hata kwa wale waliokanusha hapo awali katika maisha ya dunia. Hata hivyo Allah (s.w.) atauliza: Leo Ufalme ni wa nani? Wote watakuwa kimya, halafu atajibu Mwenyewe swali hili kama ilivyo katika aya ifuatayo:
﴿ يَوْمَ هُم بَارِزُونَ لَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّـهِ مِنْهُمْ شَيْءٌ لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْمَ لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ﴾
Siku watakayodhihiri (mbele ya Mwenyezi Mungu), na haitafichika habari yao yoyote kwa Mwenyezi Mungu. Leo Ufalme ni wa nani? Ni wa Mwenyezi Mungu Mmoja, Mwenye Nguvu (za kufanya Atakalo). [40:16]
Hukumu itatolewa katika ardhi iliyotambarare kabisa ambapo viumbe vyote vitahudhurishwa.Malaika wote watasimama katika safu:
﴿ يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّا لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا﴾
"Siku ambayo zitasimama Roho (za viumbe wote) na Malaika safu safu; hatasema siku hiyo ila yule ambaye (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema amempa idhini ( ya kusema) na atasema yaliyo sawa". [78:38]
Kisha kiti cha Enzi cha Allah (s.w.) cha kutolea Hukumu kitahudhurishwa pale na Nuru Yake itazagaa kila mahali na kila mmoja atakuwa na uhakika kuwa Allah (s.w.) yupo kwa kuchukua Hisabu. Qur'an tukufu inatupa picha ya Siku hiyo kuwa:
﴿ وَأَشْرَقَتِ الْأَرْضُ بِنُورِ رَبِّهَا وَوُضِعَ الْكِتَابُ وَجِيءَ بِالنَّبِيِّينَ وَالشُّهَدَاءِ وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْحَقِّ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴾
Na ardhi (siku hiyo) itang'ara kwa nuru ya Mola wake, na madaftari (ya vitendo) yatawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi na kutahukumiwa baina yao kwa haki wala hawatadhulumiwa". [39:69]
Kila mmoja atapita katika hisabu, japo wengine hisabu zao zitakuwa ngumu sana na wengine nyepesi sana. Hebu tuzingatie Hadith zifuatazo: Aysha amesimulia kuwa Mtume wa Allah (s.w.) amesema: Yeyote atakayehisabiwa (atakayeulizwa) katika siku ya Hukumu, ataangamia. Nikauliza (Aysha) Je, Allah hakusema:
﴿ فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ﴾
"Basi Yeye Atahisabiwa hisabu nyepesi?" [84:8]
Akajibu: Hayo kwa hakika ni maelezo ya ujumla lakini atakayehisabiwa kila kitu kwa undani wake, ataangamia. [Bukhari na Muslim] Hadith inatufundisha kuwa kila mmoja atahisabiwa, lakini yule ambaye hisabu yake haitafanywa nyepesi, hataweza kufaulu kutokana na maelezo yake na bila shaka atakuwa ni mtu wa motoni. Pia Hadith ifuatayo inasisitiza juu ya kila mtu kuulizwa na Allah (s.w.):
Ad bin Haatim amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:Hapana yeyote kati yenu ambaye hataongea na Mola wake. Hapatakuwa na mkalimani yeyote kati ya Allah na yeye na hapatakuwa na pazia ya kumzuia Allah asionekane. Mja ataangalia kuliani kwake,lakini hatoona chochote isipokuwa matendo yake aliyoyatanguliza.Ataangalia mbele yake, lakini hataona chochote isipokuwa moto unaomjia usoni mwake. Kwa hiyo jikinge na moto (na kutoa sadaka) angalau kipande cha tende. [Bukhari na Muslim] Vile vile tunafahamishwa katika Hadith kuwa hapana yeyote atakayetoka kwenye uwanja wa Hisabu bila ya kuulizwa mambo matano yafuatayo:
1. Ujana wako umeutumiaje?
2. Umri wako umeutumiaje?
3. Mwili wako na vipaji vyako umevitumiaje?
4. Mali yako umeipataje na umeitumiaje?
5. Elimu yako umeitumiaje ?
Maswali haya yataulizwa mbele ya viumbe vyote vilivyoumbwa tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka mwisho wake.Kila mchunga (kila kiongozi katika ngazi yoyote ile) ataulizwa juu ya uchungaji (uongozi) wake. Mitume ndio watakaokuwa wa kwanza kuulizwa. Allah (s.w.) atawauliza Mitume: Ni lipi jibu lenu. Watajibu: Hatuna ujuzi.Hakika Wewe Ndiye Mjuzi wa siri (ghaibu)". Mitume watapumbaa kwa woga baada ya kuulizwa swali hili: Kisha Mtume Nuhu(a.s.) ataitwa na kuulizwa kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifuatayo: Abu Sayyid amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema: Nuhu(a.s.) atahudhurishwa katika siku ya hukumu. Ataulizwa: Je, umefikisha (ujumbe wangu)? "Ndiyo" atajibu.Kisha wafuasi wake wataulizwa: Aliwafikishia (ujumbe wangu)? Watajibu: "Hapana mwonyaji aliyetujia". Ataulizwa (Nuhu ni nani mashahidi wako? Atajibu: Muhammad na Umma wake. Mtume(s.a.w.w) amesema: Kisha mtaitwa (mtahudhurishwa) na mtatoa ushahidi kuwa kwa hakika alifikisha ujumbe (wa Allah kwa watu wake).
Kisha Mtume(s.a.w.w) akasoma (aya ifuatayo): Na hivyo ndivyo Tumekufanyeni umati bora (kama Kibla chenu tulivyokifanya bora) ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume(s.a.w.w) awe shahidi juu yenu. Na hatukukifanya Kibla ulichokuwa nacho (mara ya kwanza kuwa ndio Kibla chako sasa na mwisho wa ulimwengu) ili tupate anayegeuka akarejea nyuma. Na kwa yakini ilikuwa jambo gumu isipokuwa kwa wale aliowaongoza Mwenyezi Mungu. Kwani Mwenyezi Mungu. Kwa watu ni mpole sana (na) mwenye rehma. (2:143) [Bukhari]
Habari juu ya kuulizwa kwa Nabii Issa(a.s.) inatolewa katika Qur'an: Na (kumbukeni) Mwenyezi Mungu atakaposema: Ewe Issa bin Maryam Je, wewe uliwaambia watu 'Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu? Aseme (Nabii Issa): "Wewe umetakasika na kuwa na mshirika. Hainijuzii mimi kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uwongo).Kama ningalisema bila shaka ungalijua; unayajua yaliyomo nafsini mwangu, lakini siyajui yaliyo nafsini mwako; hakika Wewe ndiye ujuaye mambo ya ghaibu".
﴿ ن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا ﴿١١٧﴾ لَّعَنَهُ اللَّـهُ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿١١٨﴾ وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا﴾
"Sikuwaambia lolote ila yale uliyoniamrisha: Ya kwamba mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu'. Na nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao, na uliponikamilisha muda wangu, wewe ukawa mchungaji juu yao, na wewe shahidi juu ya kila kitu. "Ikiwa utawaadhibu basi bila shaka hao ni waja wako, na ukiwasamehe basi kwa hakika wewe ndiye mwenye nguvu na mwenye hikima; (hutaambiwa kuwa wamekushinda kuwatia adabu).Mwenyezi Mungu atasema: Hii ndiyo siku ambayo wakweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mbele yake mito. Humo watakaa milele.Mwenyezi Mungu amewawia (amewapa) radhi,nao wawe radhi naye.Huku ndiko kufaulu kukubwa. [4:117-119)
Waovu na madhalimu watapiga kelele na kila mmoja katika waumini (wa kweli) atasema:
"Nafsi yangu Nafsi yangu" Watakapokuwa katika hali hii moto utalisambaza tena joto lake mara ya pili, na watarudi katika hali ya kuogopa na kutetemeka. Katika mara ya tatu, watu wataanguka kifudifudi na hapo baba atamkimbia mtoto, ndugu atamkimbia ndugu yake na mume atamkimbia mkewe.
﴿ وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا﴾
"Wala jamaa hatamuuliza jamaa (yake)" [70:10]
Kisha watu watahudhurishwa mmoja mmoja mbele ya Mola wao kuulizwa. Hapana yeyote atakayeongea bila ya kuulizwa. Hapatakuwa na ndugu wala rafiki wa kumsaidia au kumuonea huruma mtu mwingine. Mahojiano na Allah (s.w.) itakuwa kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifuatayo: Abu Hurairah amehadithia: Ewe Mtume(s.a.w.w) Tutamuona Bwana wetu Siku ya Kiyama? Akauliza (Mtume(s.a.w.w) Je, mnaona ugumu kuona mwanga wa jua katikati ya mchana wakati halikufunikwa na mawingu?" Hapana" walijibu. Akauliza (tena): Mnaona vigumu kuona mwanga wa mwezi katikati ya mbalamwezi kali wakati ambapo hamna mawingu? Wakajibu: Hapana. Akasema: Naapa kwa yule ambaye maisha yangu yamo mikononi mwake, hamtapata shida katika kumuona Bwana wenu bali mtamuona kama msivyoona shida kuona jua katikati ya mchana na mwezi wakati wa mbalamwezi kali. Kisha (Allah) atakutana na mja na kumuuliza: Ewe fulani sikukutukuza na nikakupa nguvu, na nikakuozesha, na nikakutiishia farasi na ngamia, na sikukupa uongozi na bora (ya ngawira)? Ulifikiria kuwa utakutana na Mimi. 'Hapana'. Atajibu. Atasema Allah (s.w.) Sasa nimekusahau kama ulivyonisahau. Qur'an inatueleza:
﴿ وَقِيلَ الْيَوْمَ نَنسَاكُمْ كَمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّاصِرِينَ﴾
Na itasemwa:"Leo tunakusahauni kama nyinyi mlivyotusahau siku yenu hii, na mahali penu ni motoni, wala hamna wa kukunusuruni". [45:34]
Kisha Allah atakutana na mtu wa pili. (Mtume(s.a.w.w) akatekeleza habari zake kama yule wa kwanza. Kisha Allah (s.w.) akakutana na mtu wa tatu atamuuliza maswali yale yale: Mja huyo atajibu: Ee Bwana, nilikuamini na nikaamini kitabu chako, na Mitume wako, na niliswali, nikafunga na kutoa zaka. Atataja matendo mema aliyoyafanya kwa kiasi atakachoweza.
Allah atamwambia: Njoo hapa (kama unavyosema ndivyo).Sasa tunakuletea mashahidi. Atajiuliza ni nani atakayetoa ushahidi dhidi yangu? Kisha mdomo wake utafungwa na makalio yake yatapewa amri: Sema. Makalio yake, nyama yake na mifupa yake itaongea juu ya vitendo vyake na kwa hivyo ataomba msamaha na huyo atakuwa ni mnafiki ambaye amekasirikiwa na Allah (s.w.). [Muslim]
Kwa ujumla kabla ya kuulizwa na kisha kujitetea kote huku, kila mja atapewa uwezo wa kuona matendo yake aliyoyatanguliza ambayo yamehifadhiwa katika kitabu maalum ambacho atapewa aambiwe akisome mwenyewe kama tunavyofahamishwa katika Qur'an:
﴿وَكُلَّ إِنسَانٍ أَلْزَمْنَاهُ طَائِرَهُ فِي عُنُقِهِ وَنُخْرِجُ لَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كِتَابًا يَلْقَاهُ مَنشُورًا ﴿١٣﴾ اقْرَأْ كِتَابَكَ كَفَىٰ بِنَفْسِكَ الْيَوْمَ عَلَيْكَ حَسِيبًا﴾
"Na kila mwanadamu tumemfungia (jaza ya) vitendo vyake shingoni mwake, tutamtolea siku ya kiyama daftari (iliyoandikwa ndani yake kila alilolifanya) atakayoikuta imekunjuliwa (aambiwe): Soma daftari yako.Nafsi yako inatosha leo kukuhisabu" [17:13-14]
Daftari hili ni daftari la ajabu, litakuwa limenukuu kila kitu mja alichokitenda katika maisha yake. Tunaweza kukiangalia kitabu hiki zaidi ya mfano wa televisheni ya matendo ya mtu ya kila siku kutokea kwenye baleghe yake mpaka kufariki kwake dunia. Televisheni hii itaonesha hata fikra zilizofichikana akilini na siri zilizohifadhiwa vifuani. Kila kitu kitaonekana kwa uwazi katika kitabu hicho. Kitabu hiki kinatolewa picha yake na Qur'an katika aya ifuatayo:
﴿ وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَا وَيْلَتَنَا مَالِ هَـٰذَا الْكِتَابِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّا أَحْصَاهَا وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا ﴾
Na madaftari yatawekwa (mbele yao). Utaona wabaya wanavyoogopa kwa sababu ya yale yaliyomo (madaftarini) na watasema: "Ole wetu, (Ee kuangamia kweli leo). Namna gani madaftari haya!Haliachi dogo wala kubwa ila yamelidhibiti (yameliandika)!"Na watakuta yote yale waliyoyafanya yamehudhuria hapo, na Mola wako hamdhulumu yeyote. [18:49]
Pia tumefahamishwa katika Qur'an:
﴿فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾ وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ﴾
Basi anayefanya wema (hata) kwa kiasi cha uzito wa mdudu chungu (atom's weight) ataona jaza yake. Na anayefanya uovu (hata) wa uzito wa mdudu chungu (atom's weight) ataona jaza yake" [99:7-9]
Pia tunafahamishwa katika Qur'an kuwa dalili ya kufaulu au kufeli kwa mtu itaonekana hata kabla mja hajasoma kitabu chake. Atakayekabidhiwa kitabu chake kwa mkono wa kulia atakuwa ni miongoni mwa wenye kufaulu na atakayekabidhiwa kitabu chake kwa mkono wa kushoto atakuwa miongoni mwa waliofeli kama tunavyofahamishwa katika Qur'an:
﴿فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ ﴿١٩﴾ إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَاقٍ حِسَابِيَهْ ﴿٢٠﴾ فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٢١﴾ فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ ﴿٢٢﴾ قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ ﴿٢٣﴾ كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ ﴿٢٤﴾ وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيَهْ ﴿٢٥﴾ وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ ﴿٢٦﴾ يَا لَيْتَهَا كَانَتِ الْقَاضِيَةَ ﴿٢٧﴾ مَا أَغْنَىٰ عَنِّي مَالِيَهْ ﴿٢٨﴾ هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيَهْ ﴿٢٩﴾ خُذُوهُ فَغُلُّوهُ ﴿٣٠﴾ ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ ﴿٣١﴾ ثُمَّ فِي سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَاسْلُكُوهُ ﴿٣٢﴾ إِنَّهُ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ الْعَظِيمِ﴾
Basi ama yule atakayepewa daftari lake kwa mkono wake wa kuume (kulia) atasema (kwa furaha) "haya someni daftari langu (nililopewa sasa hivi). Hakika nilijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu (kwa vizuri)". Basi yeye atakuwa katika maisha ya raha katika pepo tukufu.Vishada vya matunda yake vitakuwa karibu;(vinachumika bila tabu). (Waambiwe) "Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya vitendo mlivyofanya katika siku zilizopita".Walakini atakayepewa daftari lake katika mkono wake wa kushoto basi yeye atasema: "Oh Laiti nisingalipewa daftari langu.Wala nisingelijua nini hisabu yangu.Laiti (mauti) yangemaliza (kila kitu changu). Mali yangu haikunifaa.Usultani (ukubwa) wangu umenipotea.(Kusemwe): "Mkamateni na mtieni makongwa.Kisha mtupeni motoni. Tena katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini muingizeni, (mtatizeni). Hakika yeye alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu" [69:19-33]
Baada ya kupewa daftari, tukio kubwa litakalofuata ni kupimwa amali katika mizani. Jambo ambalo litakuwa pia ni lenye kutisha sana kwa waja kama tulivyofahamishwa katika Hadith. Patakuwa na makundi matatu ya watu. Kuna watakaoingia peponi moja kwa moja bila hesabu. Hili litakuwa kundi la watu wachache waliojizatiti katika kutenda mema kwa ajili ya kupata radhi ya Allah (s.w.). Atawakaribisha moja kwa moja baada ya kuwafanyia wepesi katika hesabu yao kwa kuwaita:
﴿يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ ﴿٢٧﴾ ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً ﴿٢٨﴾ فَادْخُلِي فِي عِبَادِي ﴿٢٩﴾ وَادْخُلِي جَنَّتِي﴾
"Ewe nafsi yenye kutua: Rudi kwa Mola wako, hali ya kuwa umeridhika (kwa utakayoyapata), na (Mwenyezi Mungu) aridhike na wewe. Basi ingia katika (kundi la) waja wangu (wazuri) uingie katika Pepo Yangu" [89:27-30]
Kundi la pili la wale ambao hawakumuamini Allah (s.w.) hata chembe, hawa wataingizwa motoni moja kwa moja bila ya amali zao kupimwa katika mizani kwani chochote atakachokifanya kafiri au mushriki, au kitakachofanywa kwa ria au kwa unafiki hakitakuwa na malipo yoyote kutoka kwa Allah (s.w.). Hivyo kafiri, mushriki na mnafiki hawatakuwa na lao mbele ya Allah (s.w.) kama tunavyofahamishwa katika Qur'an:
﴿أَفَحَسِبَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن يَتَّخِذُوا عِبَادِي مِن دُونِي أَوْلِيَاءَ إِنَّا أَعْتَدْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ نُزُلًا ﴿١٠٢﴾ قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا ﴿١٠٣﴾ الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا ﴿١٠٤﴾ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَلِقَائِهِ فَحَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَزْنًا ﴿١٠٥﴾ ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُمْ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُوا وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَرُسُلِي هُزُوًا﴾
Je,wale waliokufuru wanadhani ya kwamba kule kuwafanya waja wangu kuwa walinzi (wao) badala Yangu (kutawafaa kitu kufanya hivyo)?Hakika Sisi Tumeiandaa Jahannamu iwe ndio mahala pa kuteremkia makafiri. Sema:Je!Tukujulisheni wenye hasara katika vitendo (vyao)? Hao ambao bidii yao hapa duniani imepotea bure katika maisha ya dunia, nao wanafikiri kwamba wanafanya amali njema? Hao ni wale waliozikataa (waliozikanusha) ishara za Mola wao na (wakakataa) naye.Kwa hiyo vitendo vya vimeruka patupu, wala hatutawasimamishia mizani siku ya kiyama. Hivyo Jahannamu ni malipo yao kwa sababu walikufuru na kuzifanyia mzaha aya zangu na Mitume wangu. [18:102-106]
﴿ وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴾
"Na kwa yakini imefunuliwa kwako na kwa wale waliokuwa kabla yako (maneno haya): "Kama ulimshirikisha (Mwenyezi Mungu) bila shaka amali zako zitaruka patupu (hatazipatia thawabu japo ni amali njema), na lazima utakuwa miongoni mwa wenye hasara". [39:65]
Kundi la tatu ni lile la watu walimuamini Allah (s.w.) lakini katika utendaji wakawa wamechanganya mema na maovu. Mema yao na maovu yao itabidi yapimwe katika mizani ya haki ili kila mmoja alipwe kwa haki kutokana na matendo yake aliyoyatanguliza. Qur'an inatufahamisha juu ya hili:
﴿وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ﴾
Nasi tutaweka mizani za uadilifu siku ya Kiyama na nafsi yeyote haitadhulumiwa hata kidogo. Na hata kama ikiwa (jambo hilo lina) uzito mdogo wa chembe ya hardali nalo tutalileta. Nasi tunatosha kuwa wajuzi (wazuri kabisa) wa hisabu. [21:47]
Wale watakaokuwa na mizani nzito upande wa wema au wale ambao uzito wa mema yao utazidi uzito wa uovu wao, hawa watakuwa ni wenye kufaulu watastahiki pepo. Na wale ambao mizani itaonyesha kinyume chake, utakapokuwa umezidi uzito wa mema yao, hao watakuwa ni watu wa motoni kama tunavyofahamishwa katika Qur'an:
﴿ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٢﴾ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ﴾
Ama wale ambao mizani ya amali zao (nzuri) itakuwa nzito,hao ndio wenye kufaulu. Na wale ambao mizani yao itakuwa nyepesi, hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao, na katika Jahannamu watakaa muda mrefu. [23:102-103]
Ukweli wa mambo ni kwamba, mizani anayo mtu katika maisha yake yote ya hapa ulimwenguni. Kila mja ameshajulishwa ni tabia ipi au mwenendo upi wa maisha akiufuata atafaulu hapa duniani na akhera, na ni tabia ipi au mwenendo upi wa maisha atakapoufuata mja utamhilikisha hapa duniani na huko akhera. Hivyo kila mja anao uwezo wa kukisia kuwa mizani yake itakuwaje kwa kuiangalia tabia yake jinsi anavyolandana na inavyopingana na utaratibu wa Sharia aliyoiweka Allah (s.w.). Makisio haya tutayafanya kwa kutumia mizani aliyotuletea Allah (s.w.) kama Qur'an inavyofufahamisha:
﴿لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ﴾
Kwa hakika Tuliwapeleka Mituma wetu kwa dalili wazi wazi na tukaviteremsha vitabu na mizani (ya mema na maovu) ili watu wasimamie uadilifu [57:25]
Hivyo kila mmoja anao uwezo wa kuiweka mizani yake ikaelemea upande unastahili kwa kulipima kila jambo analolifanya katik a maisha yake kwa mizani aliyoiweka Allah (s.w.) ya kuyaweka bayana mabaya na mazuri kisha mtu akajihukumu. Mafundisho tunayoyapata kutokana na Hadith ifuatayo:
Aysha amesimulia kuwa, alikuja mtu mmoja na kukaa mbele ya Mtume(s.a.w.w) na kuuliza: "Ewe Mtume(s.a.w.w) wa Allah nimeweka mkataba wa watumwa ambao wananikadhibisha na wananifanyia hila na kunidanganya na hawanitii, ninawakemea na kuwapiga.Niwafanyeje? Mtume(s.a.w.w) akasema: "Siku ya malipo itakapofika, hisabu itachukuliwa dhidi yao kiasi walichokuhadaa kwa hila, kiasi walichokataa kukutii na kiasi walichokughadhibisha. Kama adhabu uliyowapa (ya kuwakemea na kuwapiga) itakuwa ni sawa na makosa yao, sawa kwako na kwao, na kama adhabu uliyowapa itakuwa ni ndogo kuliko makosa yao, utaongezewa ufidie sehemu iliyobaki, na kama adhabu uliyowapa itazidi makosa yao basi itabidi fidia itoke (kwenye amali yako) kwkao uwape.". Yule mtu aligeuka pembeni na akaanza kusikitika na kulia. Kisha Mtume(s.a.w.w) akasema:" Hujasoma aya za Allah (s.w.):
﴿وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ﴾
"Tutaweka mizani kwa uadilifu siku ya Kiyama na nafsi yoyote haitadhulumiwa hata kidogo na hata kama likiwa na uzito ndogo wa chembe yardali nalo tutalileta, Nasi tutatosha kuwa wajuzi wa kuhisabu". [21:47].
Yule mtu akasema: "Ewe Mtume wa Allah: Ninaona kuwa hapana jambo lililo bora zaidi kwangu mimi na kwa hawa watumwa, isipokuwa kuachana nao.Ninashuhudia mbele yako kuwa wote sasa wako huru". [Tirmidh]
Hadith inatupa fundisho kubwa kuwa, pamoja na mtu kukosewa, si vema kutoa hukumu kwani anaweza kutoa hukumu isiyolingana na kosa. Kwa ujumla Mtume (s.a.w.w) ametuusia kuwa tujihisabu wenyewe kabla hatujahisabiwa. Huku kujihesabu si lingine bali ni kutubu kikweli kweli kwa moyo mkunjufu kwa makosa yote mtu aliyoyafanya na kwa yale yote aliyoacha kuyatekeleza katika yale aliyoamrishwa. Na kurudisha haki ya aliyedhulumiwa hata kama ni punje moja iliyochukuliwa kwa makosa au kinyume na idhini yake, kumtaka msamaha kwa haki iliyochukuliwa, na wale walioumizwa kwa uonevu kwa ulimi au mkono. Kama mtu aliyefanya makosa haya atafariki bila ya kutubia na kuwaomba msamaha wale aliowakosea au kuwarudishia haki zao kama zinarudishika, atawakuta karibu na mizani katika siku ya hisabu wakidai haki zao na kushitaki: "Ulinigombeza (ulinikemea) bila ya sababu yoyote, ulinitukana, uliniteta, ulinifanyia ubaya ukiwa kama jirani, mtumishi, Rais, hukunihudumia ipasavyo nilipokuwa mgonjwa, ulinikuta nina njaa na hukunilisha na ilihali ulikuwa na uwezo, unilikuta nina kiu hukuninyeshwa, ulinikuta ni uchi hukunivisha, hukuondoa dhulma na ili hali ulikuwa na madaraka na kadhalika. Hapa Allah (s.w.) atasema:
﴿الْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ﴾
"Leo kila nafsi italipwa kwa kila ilichokitanguliza.Hapana atakayedhulumiwa leo".[40:17]
Kwa muhtasari kutokana na haya tuliyojifunza juu ya Siku ya Kiyama mambo matano yafuatayo yamejitokeza:
Kwanza : hukumu itakuwa ya haki na kwamba hakuna mtu hata mmoja atakayedhulumiwa chochote kama Qur'an inavyosisitiza:
﴿الْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ﴾
Leo kila mtu atapewa malipo ya yale aliyoyatenda, hakuna dhulma leo, bila shaka Allah ni Mwepesi kuhisabu. [40:17]
﴿إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ النَّاسَ شَيْئًا وَلَـٰكِنَّ النَّاسَ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴾
Hakika Allah hawadhulumu watu chochote, lakini watu wanajidhulumu nafsi zao [10:44]
Pili : mambo yote siku hiyo yatakuwa wazi kiasi cha kuweza mtu kujihesabu mwenyewe
Tatu : kabla ya hukumu kwa kawaida hutakikana ushahidi. Ushahidi wa siku hiyo ni daftari la amali za mtu ambalo limedhibitiwa vyema na malaika waandishi hodari wa amali za waja kama tunavyofahamishwa katika Qur'an:
﴿مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴾
Hatoi kauli yoyote isipokuwa karibu naye yuko mngojeaji tayari (kuandika) [50:18]
﴿وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ ﴿١٠﴾ كِرَامًا كَاتِبِينَ ﴿١١﴾ يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ﴾
Na hakika juu yenu kuna wenye kuwatunza (Malaika) watukufu wenye kuandika.Wanayajua yote mnayoyatenda.[82:10-12].
Nne : mashahidi siku hiyo ni viungo vyake mtu. Macho yatasema yalichokitazama kinyume na sheria ya Allah (s.w.), mikono itachoiba, miguu iliko kwenda na kadhalika. Maadam mtu hatendi jema wala ovu ila atatumia kiungo fulani cha mwili wake basi ajue hao ni mashahidi waadilifu ambao hawapokei rushwa, na ataitoa wapi rushwa siku hiyo? Tunafahamishwa katika Qur'an:
﴿يَوْمَ تَشْهَدُ عَلَيْهِمْ أَلْسِنَتُهُمْ وَأَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴾
Siku ambayo zitawashuhudia ndimi zao na mikono yao na miguu yao kwa yale waliyokuwa wakifanya. [24:24]
﴿لْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَىٰ أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴾
Siku hiyo tutaviziba vinywa vyao, itazungumza mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma. [36:65]
﴿وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّـهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ﴾
Na hamkuwa mkijificha hata masikio yenu na macho yenu na ngozi zenu zisiweze kutoa ushahidi juu yenu, bali mlidhani ya kwamba Allah hayajui mengi katika (hayo) mnayoyafanya. [41:22]
Tano : kutakuwa na mizani ya kupimia amali za waja. Mizani hii haitapima amali zenyewe bali thamani ya amali. Uzito siku hiyo utakuwa ni kweli na haki. Yaani kweli au haki ndivyo vitakavyokuwa na uzito. Allah (s.w.) amesema:
﴿وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٨﴾ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ﴾
Na siku hiyo kipimo (uzito) kitakuwa ni haki. Basi watakaokuwa na uzani mzito, hao ndio watakaofaulu. Na watakaokuwa na uzani hafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzifanyia jeuri Aya zetu. [7:8-9]
"Na siku hiyo uzito utakuwa ni haki Msemo huu wa Allah (s.w.) una maana kuwa, siku ya Hukumu katika mizani ya haki, hakuna chochote isipokuwa Haki na Ukweli ndivyo vitakavyokuwa na uzito. Uzito utazidi au kupungua kulingana na ukweli utakaokuwa nao mja juu ya nafsi yake na atahukumiwa kwa kipimo cha ukweli huo na si kwa kitu kingine chochote. Maisha ya kinafiki na uasi hata kama yatakuwa marefu na hata kama mtu atakuwa amefanya mambo mengi ambayo yeye atadhani kuwa ni makubwa katika mizani ya Allah (s.w.) hayatakuwa na uzito wowote.
9
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
Je, mtu hufuzu kwa amali zake au kwa rehema ya Mwenyezi Mungu? Kutokana na msisitizo mkubwa wa Qur'an wa kuwahimiza watu kufanya amali njema ili wafuzu huko Akhera, baadhi ya Wakristo mara nyingi huuliza: "Je, Wailsamu mnategemea kunusurika na adhabu kwa sababu tu ya vitendo vyenu na siyo kwa sababu tu ya huruma ya Mwenyezi Mungu kwenu? Ikiwa ni hivyo mtawezaji kuokoka?
Hapana shaka yoyote kuwa, katika mafundisho ya Uislamu ipo nafasi kubwa sana ya rehema ya Mwenyezi Mungu. Lakini rehema hiyo wanaipata wale tu wanaostahiki. Na wanaostahiki kuipata ni wale ambao pamoja na udhaifu wao wa kibinadamu wanajitahidi kadri ya uwezo wao kumtii Mola wao na wanaolipigania neno lake kwa hali na mali. Hivyo rehema hiyo haitolewi holela tu. Atakuwa ni mwislamu wa ajabu yule atakayewaambia wanafunzi wake: "Yeyote yule anaweza kufaulu na si muhimu kabisa kama anajitahidi kuhudhuria masomo au la, au kama anafanya mazoezi, ninayotoa au la, atafaulu kwa huruma yangu tu".
Uislamu unafundisha kuwa kumuamini Mwenyezi Mungu siyo kwa kusema tu; bali aisadikishe hiyo imani yake kwa kufanya aliyoamrishwa na Mola wake na kujiepusha na yale aliyomkataza. Lakini hata mja akifanya hivyo bado hatakiwi kujigamba na kujipiga kifua kuwa eti Pepo ni mali yake kwa sababu ya mambo kadhaa anayoyafanya. Bali aombe rehema ya Mola wake ili ayazidishe mema yake, na amghufirie makosa yake.
Watu wanapata wokovu kutokana na rehema ya Mwenyezi Mungu kwa sababu anaulipa uovu kwa uwiano wa moja kwa moja.Lakini anapoilipa amali njema huilipa malipo bora zaidi thamani ya amali hiyo. Mwenyezi Mungu anatufahamisha katika Qur'an:
﴿مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَى الَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴾
Atakayefanya mema atapata jaza bora kuliko huo (wema alioufanya) na atakayefanya ubaya, basi hawatalipwa wale wafanyao ubaya ule ila sawa na yale waliyokuwa wakiyafanya. [28:84]
﴿إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا﴾
Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu (viumbe vyake hata kitu kilicho sawa na) uzito wa mdudu chungu, na kama likiwa ni jambo jema atalizidisha na kutoa ujira mkubwa unaotoka kwake. [4:40]
﴿وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴾
Afanyaye kitendo kizuri,atalipwa mfano wake mara kumi. Na afanyaye kitendo kibaya hatalipwa ila sawa nacho tu (basi), Nao hawatadhulumiwa. [6:160]
Rehema hii ya Allah (s.w.) pia imetajwa katika Qur'an ifuatavyo:
﴿ذَٰلِكَ الَّذِي يُبَشِّرُ اللَّـهُ عِبَادَهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَىٰ وَمَن يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَّزِدْ لَهُ فِيهَا حُسْنًا إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ شَكُورٌ﴾
Hii ndiyo habari nzuri ambayo Mwenyezi Mungu anawaambia waja wake walioamini na kufanya vitendo vizuri. Sema: "Kwa haya (ninayokufundisheni) siombi, (sitaki) malipo yoyote kwenu; lakini (nataka) myapende mambo ya kukusogezeni (kwa Mwenyezi Mungu). Na anayefanya wema tutamzidishia wema; kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mwingi wa msamaha, mwingi wa shukrani. [42:23]
﴿لِيَجْزِيَهُمُ اللَّـهُ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ وَاللَّـهُ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴾
Ili Mwenyezi Mungu Awalipe (malipo) mazuri kwa yale waliyoyafanya na kuwazidishia katika fadhila zake, na Mwenyezi Mungu Humruzuku Amtakaye pasipo hisabu. [24:38]
Ni dhahiri kuwa, ili mtu aipate rehema hii ya Mwenyezi Mungu itabidi kwanza liwemo hilo jambo jema ambalo Allah (s.w.) atalizidisha. Ndiyo maana Mtume(s.a.w.w) amesema, mtu akitakiwa kutoa hisabu yake reja reja yaani kwa kuangalia kila kipengele kimoja kimoja, basi mtu huyo ameangamia. Hii ni kwa sababu watu wema hutoa hisabu ya jumla na mema yao hufuta makosa yao. Mwenyezi Mungu amesema:
﴿وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَحْسَنَ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ﴾
"Na walioamini na wakafanya vitendo vizuri, kwa yakini tutawasamehe maovu yao, na tutawalipa mema ya yale waliyokuwa wakiyafanya". [29:7]
Hivyo hisabu ya watu wema itakuwa nyepesi na ya waovu itakuwa nzito kama anavyozidi kututhibitishia Mwenyezi Mungu kwa kusema:
﴿فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ ﴿٧﴾ فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا﴿٨﴾وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ ﴿١٠﴾ فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا ﴾
"Ama atakayepewa daftari lake katika mkono wake wa kulia, basi Naye atahisabiwa hisabu nyepesi, lakini atakayepewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake, basi yeye atayaita mauti (yamjie ili afe apumzike, wala hayatamjia)". [84:7-8 na 10-11]
Hivyo lililo muhimu kwetu ni kujitahidi upeo wa uwezo wetu ili tustahili kupata rehema ya Mwenyezi Mungu, na tutakuwa tunajidanganya wenyewe iwapo tutaitaraji rehema hiyo kwa kuchapa usingizi tu.
Maisha ya Peponi Kabla hatujaeleza maisha ya Peponi yatakavyokuwa hebu tuangalie maana ya neno Jannat (Pepo) Jannat ilivyoelezwa katika Qur'an na Hadith ni Bustani nzuri zilizo na matunda na miti mizuri ya kila aina, yenye kupitwa na mito ya maji mazuri na matamu kuliko asali na meupe kuliko maziwa na yenye harufu nzuri kuliko miski. Pia ndani ya bustani hii nzuri isiyo na kifani ni yenye fenicha nzuri zisizo hadithika. Maelezo ya Qur'an na Hadith katika kuelezea uzuri wa pepo ni kama mfano tu kwani vipaji hivi vya fahamu tulivyo navyo ni vya hapa hapa duniani tu na havina uwezo kabisa kuyaingiza katika picha sahihi matukio yote ya maisha ya akhera. Katika maisha hayo ya akhera watu watakuwa na maumbile na vipaji vinavyolingana na maisha hayo na kila mja ataona na kuyahisi maisha ya huko kwa uhakika. Hivi ndivyo anavyotufahamisha Mtume(s.a.w.w) katika Hadith ifuatayo:
Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah kasema:Allah (s.w.) kasema: Nimewaandalia waja wangu mema ambayo hapana jicho lililowahi kuona, na hapana sikio lililowahi kusikia, na hapana moyo wa mtu uliopata kufahamu (kufikiri). Na soma kama unapenda: "Nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho (huko Peponi) ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyafanya".
Kwa maana ya ujumla, neno Jannat limetumiwa katika lugha ya Kiislamu kama kielelezo cha mazingira mazuri katika maisha ya Akhera ambapo watu wema, walioishi hapa duniani kwa wema, kwa kufuata barabara kanuni za maisha ya kila siku kama zilivyowekwa na Allah (s.w.) wataishi milele kwa furaha na amani. Hebu tujaribu kupiga picha ya mazingira ya peponi kwa kutumia mifano iliyotolewa katika Qur'an na Hadith inayolingana na mazingira haya:
Abu Mussa amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema:"Hakika kwa waumini patakuwa na hema moja kubwa la lulu katika pepo. Upana wake (urefu wake) utakuwa maili sitini. Katika kila kona patakuwa na wakaaji ambao hawatawaona wengine. Waumini watayazungukia ambapo patakuwa na bustani mbili ambamo vyombo vyake vyote na kila kilichomo ndani yake kitakuwa cha dhahabu, na kati ya watu na uoni wao kwa Allah patakuwa na pazia ya utukufu wa uso wake itakavyoonekana katika Pepo ya daraja ya juu". [Bukhari na Muslim]
Hizi bustani nne zimeelezewa katika Qur'an katika aya zifuatazo:
﴿وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ﴾
Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake atapata mabustani (Pepo) mawili. [55:46]
﴿وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ﴾
Na zaidi ya hizo yako mabustani mawili (mengine) [55:62]
Katika Hadith nyingine, tunafahamishwa kuwa Pepo imegawanywa kwa uzuri katika daraja mia moja na daraja ya juu ndio bora kuliko zote. Ubaidah bin Samit amesimulia kuwa Mtume wa Allah (s.w.) amesema:Pana milango mia moja katika Pepo. Umbali kati ya kila milango miwili ni kama umbali kati ya mbingu na ardhi,na Firdausi ndiyo yenye mlango ulio juu kabisa kuliko yote. Mito minne ya peponi inamiminika kutoka humo na juu yake ipo arshi. Kwa hiyo,unapomuomba Allah (akuruzuku pepo), muombe Firdausi. [Tirmidh]
Katika Qur'an tunapewa sifa za watu watakaofuzu kuingia katika Firdaus:
﴿قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١﴾ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ ﴿٢﴾ وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ ﴿٣﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَاةِ فَاعِلُونَ ﴿٤﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿٥﴾ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿٦﴾ فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿٧﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ ﴿٨﴾ وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٩﴾ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ ﴿١٠﴾ الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾
Hakika wamefuzu Waumini.Ambao katika sala zao huwa ni wanyenyekevu. Na ambao hujiepusha na mambo ya kipuuzi.Na ambao (nguzo ya) Zaka wanaitekeleza.Na ambao tupu zao wanazilinda. Isipokuwa kwa wake zao na kwa (wanawake) wale iliyomiliki mikono yao ya kuume (kulia). Basi hao ndio wasiolaumiwa.(Lakini) anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka (ya Mwenyezi Mungu). Na ambao amana zao na ahadi zao wanaziangalia wanazitekeleza).Na ambao Sala zao wanazihifadhi.Hao ndio warithi. Ambao watarithi Firdaus wake humo milele. [23:1-11]
Hali ya mazingira ya maisha ya wenyeji au wakazi wa peponi inafafanuliwa katika Hadith zifuatazo: Jabir anasimulia kuwa Mtume wa Allah (s.w.) amesema:Hakika wakazi wa peponi watakula na kunywa lakini hawatakuwa wanatema, wala kwenda haja ndogo au kubwa, wala kutokwa na uchafu puani. Waliuliza (Masahaba): Kitakuwaje chakula? Alijibu (Mtume s.a.w.w) kitabu kama utamu wa miski na watakuwa wamejazwa na Tasbihi na Tahmid kama walivyojaaliwa kupumua. [Muslim]
Abu Sayyid na Abu Hurairah wasimulia kuwa, Mtume (s.a.w.) amesema:Mwenye kunadi atanadi: Kwenu pana afya ya kudumu na daima hamtakuwa wagonjwa, na kwenu kuna maisha ya milele na hapana kufa, na kwenu kuna ujana unaoendelea na daima hamtazeeka, na kwenu mna neema ziendeleazo na daima hamtapungukiwa na mahitaji. [Muslim]
Pamoja na Hadith hizi, Qur'an inatuchorea picha ya maisha ya peponi pamoja na wakazi wake na sifa zitakazowawezesha kuingia humo. Hebu tuzingatie aya chache zifuatazo:
﴿إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُلٍ فَاكِهُونَ ﴿٥٥﴾ هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلَالٍ عَلَى الْأَرَائِكِ مُتَّكِئُونَ ﴿٥٦﴾ لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ ﴿٥٧﴾ سَلَامٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ﴾
Kwa yakini watu wa Peponi leo wamo katika shughuli (zao), wamefurahi. Wao na wake zao wamo katika vivuli, wameegemea juu ya viti vya fahari. Watapata humu (kila namna ya) matunda na watapata watakavyovitaka.Salama (tu juu yao), ndio neno litokalo kwa Mola (wao) Mwenye Rehema. [36:55-58]
﴿قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ﴾
Sema: "Nikwambieni yaliyo bora kuliko hivyo?" Kwa ajili ya wamchao Allah ziko bustani kwa Mola wao, zipitazo mito mbele yake. Watakaa humo milele na wake (zao) waliotakaswa (na kila uchafu na kila ubaya). Na wana radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anawaona (wote) waja (wake). [3:15]
﴿أُولَـٰئِكَ لَهُمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَيَلْبَسُونَ ثِيَابًا خُضْرًا مِّن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ نِعْمَ الثَّوَابُ وَحَسُنَتْ مُرْتَفَقًا﴾
Hao watapata mabustani ya milele yanayopita mito (ya maji) mbele yake. Humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu na watavaa nguo za kijani za hariri laini na za hariri nzito; wanaegemea humo juu ya vitanda vilivyopambwa (makochi).Ni malipo mazuri yaliyoje hayo. Na mahali bora palioje hapo (Pa kupumzika) [18:31]
﴿إِنَّ اللَّـهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَلُؤْلُؤًا وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ﴾
Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza wale walioamini na kufanya vitendo vizuri (katika) mabustani yapitayo mito mbele yake.humo watavishwa mapambo ya mikononi ya dhahabu na lulu, na mavazi yao humo yatakuwa hariri. [22:23]
﴿وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٤٢﴾ وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي هَدَانَا لِهَـٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِيَ لَوْلَا أَنْ هَدَانَا اللَّـهُ لَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ وَنُودُوا أَن تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴾
Na wale wanaoamini na kufanya vitendo vizuri - hatumkalifishi mtu yeyote ila kwa kiasi cha uweza wetu - hao ndio watu wa Peponi. Wao watakaa humo daima.Na tutaiondoa bughudha vifuani mwao (wawe wanapendana wote kweli kweli, mbele yao iwe inapoita mito. Na watasema (katika kushukuru kwao): Sifa zote njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu ambaye ametuongoza katika (neema) hizi. Na hatukuwa wenye kuongoka wenyewe kama asingetuongoza Mwenyezi Mungu. Mitume wa Mola wetu wameleta haki. Na watanadiwa (wataambiwa) ya kwamba: Hii ndiyo pepo mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya". [7:42-43]
﴿إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿٤٥﴾ ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ ﴿٤٦﴾ وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ إِخْوَانًا عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ ﴿٤٧﴾ لَا يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَبٌ وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ﴾
"Na hakika wanaomcha Mwenyezi Mungu watakuwa katika Mabustani na chemchem (zinazoita mbele yao huko; waambiwe): "Yaingieni salama salimini (kwa salama na muwe katika amani)". Na tutaondoa mifundo iliyokuwa vifuani mwao, na (watakuwa) ndugu (wenye kupendana) (waliokaa) juu ya viti vya kifalme, wameelekeana (wanazungumza kwa furaha kubwa).Haitawagusa humo taabu wala pia humo hawatatolewa". [15:45-48]
﴿جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَلُؤْلُؤًا وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ ﴿٣٣﴾ وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي أَذْهَبَ عَنَّا الْحَزَنَ إِنَّ رَبَّنَا لَغَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٤﴾ الَّذِي أَحَلَّنَا دَارَ الْمُقَامَةِ مِن فَضْلِهِ لَا يَمَسُّنَا فِيهَا نَصَبٌ وَلَا يَمَسُّنَا فِيهَا لُغُوبٌ﴾
"Bustani ya milele wataingia humo, humo watapambwa vikuku vya dhahabu, na lulu, na nguo zao humo zitakuwa za hariri. Na watasema (katika kushukuru kwao) "Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Aliyetuondolea huzuni, kwa yakini Mola wetu ni Mwingi wa msamaha (na) Mwenye shukurani". Ambaye kwa fadhila zake ametuweka katika nyumba ya kukaa daima, humo haitugusi taabu wala humo hakutugusi kuchoka". [35:33-35]
﴿يَا عِبَادِ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ ﴿٦٨﴾ الَّذِينَ آمَنُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا مُسْلِمِينَ ﴿٦٩﴾ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ أَنتُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ تُحْبَرُونَ ﴿٧٠﴾ يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ وَأَنتُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٧١﴾ وَتِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٧٢﴾ لَكُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ كَثِيرَةٌ مِّنْهَا تَأْكُلُونَ﴾
"Enyi waja wangu (mlio wazuri) Hamtakuwa na hofu siku hiyo wala hamtahuzunika.(Waja wangu) ambao waliziamini aya zetu na walikuwa Waislamu kamili. Ingieni bustanini (peponi) nyinyi na wake zenu, mtafurahishwa (humo). Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe (vya dhahabu) na vitakuwemo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele. Na hii ni bustani (pepo) mliyorithishwa kwa hayo mliyokuwa mkiyafanya.Muna (nyingi) humo matunda mengi mtakayoyala" [43:68-73]
﴿مَّثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ فِيهَا أَنْهَارٌ مِّن مَّاءٍ غَيْرِ آسِنٍ وَأَنْهَارٌ مِّن لَّبَنٍ لَّمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُ وَأَنْهَارٌ مِّنْ خَمْرٍ لَّذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ وَأَنْهَارٌ مِّنْ عَسَلٍ مُّصَفًّى وَلَهُمْ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَمَغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ كَمَنْ هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ﴾
Mfano wa pepo waliyoahidiwa wacha Mungu (itakuwa hivi): Imo mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa, tena humo watapata matunda ya kila namna, na samahani kutoka kwa Mola wao. Basi hao watakuwa sawa na wale watakaokaa motoni, na kunyeshwa maji yachemkayo yatakayokata chango zao? [47:15]
﴿نَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَعِيمٍ ﴿١٧﴾ فَاكِهِينَ بِمَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ وَوَقَاهُمْ رَبُّهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ ﴿١٨﴾ كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٩﴾ مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ سُرُرٍ مَّصْفُوفَةٍ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ ﴿٢٠﴾ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَانٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَا أَلَتْنَاهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَيْءٍ كُلُّ امْرِئٍ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ ﴿٢١﴾ وَأَمْدَدْنَاهُم بِفَاكِهَةٍ وَلَحْمٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ ﴿٢٢﴾ يَتَنَازَعُونَ فِيهَا كَأْسًا لَّا لَغْوٌ فِيهَا وَلَا تَأْثِيمٌ ﴿٢٣﴾ وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ غِلْمَانٌ لَّهُمْ كَأَنَّهُمْ لُؤْلُؤٌ مَّكْنُونٌ ﴿٢٤﴾ وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٥﴾ قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ ﴿٢٦﴾ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ ﴿٢٧﴾ إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ﴾
"Kwa yakini wamchao Mwenyezi Mungu watakuwa katika mabustani na neema. Wakifurahia yale Aliyowapa Mola wao, na Mola wao amewalinda na adhabu ya moto utakao (kwa nguvu kabisa). (Wataambiwa watu wema):"Kuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya hayo mliyokuwa mkiyatenda, watakuwa wameegemea juu ya viti vya fahari vilivyopangwa safu safu, na Tutawaoza wanawake wanaopendeza wenye macho ya vikombe (makubwa). Na wale walioamini na wakafuatwa na wazee wao na watoto wao katika imani. Tutawakutanisha nao hao jamaa zao, wala hatutawapunja kitu katika (thawabu) vitendo vyao, kila mtu atalipwa kwa kila alichokichuma. Na tutawapa (kila namna ya) matunda na (kila namna za) nyama, kama vile watakavyopenda.Watapeana humo gilasi (zilizojaa vinywaji) visivyoleta maneno ya upuuzi wala dhambi. Iwe wanawapitia watumishi wao (wanaopendeza) kama kwamba ni lulu zilizomo ndani ya chaza. Wataelekeana wao kwa wao wanauliza (wanazungumza).Waseme: "Tulikuwa zamani pamoja na watu wetu tukimuogopa (Mwenyezi Mungu). Basi Mwenyezi Mungu ametufanyia ihsani (ametutia peponi) na ametuokoa na adhabu ya pepo za moto". Hakika sisi zamani tulikuwa tukimuabudu yeye (tu Mwenyezi Mungu): Hakika Yeye Ndiye Mwema, Mwenye Rehema". [52:17-28]
﴿إِنَّ الْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا ﴿٥﴾عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللَّـهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا ﴿٦﴾ يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا ﴿٧﴾ وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا ﴿٨﴾ إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّـهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا ﴿٩﴾ إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا ﴿١٠﴾ فَوَقَاهُمُ اللَّـهُ شَرَّ ذَٰلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا ﴿١١﴾ وَجَزَاهُم بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا ﴿١٢﴾ مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا وَلَا زَمْهَرِيرًا ﴿١٣﴾ وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَالُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا ﴿١٤﴾ وَيُطَافُ عَلَيْهِم بِآنِيَةٍ مِّن فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا ﴿١٥﴾ قَوَارِيرَ مِن فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا ﴿١٦﴾ وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا ﴿١٧﴾ عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًا ﴿١٨﴾ وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَّنثُورًا ﴿١٩﴾ وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا ﴿٢٠﴾ عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا ﴿٢١﴾ إِنَّ هَـٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَاءً وَكَانَ سَعْيُكُم مَّشْكُورًا ﴾
"Hakika watu wazuri watakunywa kinywaji kilichochanganyika na kafuri. (Hiyo kafuri) ni mto watakaokunywa waja wa Mwenyezi Mungu, watautiririsha mtiririsho ( mzuri namna watakavyo). (Watu hao ni hawa) wanaotimiza wajibu (wao) na wanaiogopa siku ambayo shari yake itaenea (sana). Na huwalisha chakula masikini na mayatima na wafungwa, na hali ya kuwa wenyewe wanakipenda (chakula hicho). (Husema wenyewe katika nyoyo zao wanapowapa chakula hicho): "Tunakulisheni kwa ajili ya kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu (tu) hatutaki kwenu malipo wala shukurani".Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu hiyo siku yenye shida na taabu". Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo na kuwakutanisha na neema na furaha. Na atawajazia Mabustani (ya peponi) na maguo ya hariri, kwa sababu ya kusubiri (kwao). Humo wataegemea viti vya enzi, hawataona humo jua (kali) wala baridi (kali), Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yake yataning'inia mpaka chini.Na watapitishwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae. Vigae vya fedha, wamevijaza kwa vipimo. Na humo watanyweshwa kinywaji kilichochanganyika na tangawizi. Huo ni mto ulio humo (peponi) unaitwa Salsabili. Na watawazungukia (kuwatumikia) wavulana wasiochakaa, ukiwaona utafikiri ni lulu zilizotawanywa. Na utakapoyaona (yaliyoko) huko utaona neema (zisizo kuwa na mfano) na ufalme mkubwa. Juu yao wana nguo za hariri laini, za kijani kibichi na za hariri nzito. Na watavikwa vikuku vya fedha na Mola wao atawanywesha kinywaji safi kabisa (Awaambie):"Hakika haya ni malipo yenu, na amali zenu zinakubaliwa" [76:5-22]
Hizi ni baadhi tu ya aya zinazotoa sifa za Peponi na sifa za wale wanaostahiki kuingia Peponi. Kwa ujumla kilele cha lengo la maisha ya mwanadamu ni kukutana na Allah (s.w.) akiwa radhi naye. "Ee Allah! Tuongoze katika njia iliyonyooka na tujaalie tuwe miononi mwa waja wako wema watakaostahiki kuingia peponi"
10
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
MAISHA YA MOTONI
Moto umetumiwa katika Qur'an na Hadithi kuonyesha makazi mabaya watakaposhukia waovu, walioamua kumpinga Allah (s.w.) na kuendesha maisha yao ya hapa duniani kinyume na kanuni na taratibu alizoziweka Allah (s.w.). Maisha ya motoni ni kinyume na maisha ya peponi ambayo picha yake tumeshaiona. Hebu tuelekeze kamera yetu motoni na kupiga picha ya maisha ya huko. Kwanza kabisa tunafahamishwa na Qur'an kuwa motoni kuna daraja au milango saba.
﴿ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٤٣﴾ لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَابٍ لِّكُلِّ بَابٍ مِّنْهُمْ جُزْءٌ مَّقْسُومٌ ﴾
"Na bila shaka Jahannam ndipo mahali pao walipoahidiwa Ina milango saba, na kwa kila mlango iko sehemu yao iliyogawanywa" [15:43-44]
Daraja hizi za moto zimepewa majina kama tusomavyo katika Qur'an: Jahannam: Jina hili limetumiwa katika aya nyingi za Qur'an kama jina la ujumla la maisha ya motoni. Hutwamah:
﴿كَلَّا لَيُنبَذَنَّ فِي الْحُطَمَةِ ﴾
"Moto wa kuvunja vunja - moto uliowashwa kwa ukali barabara". [104:4]
Moto mkali wa kuunguza [4:55]
Moto unaobabua. [74:26]
Moto mkali. Qur'an (26:9 na 102:6]
Moto uwakao kwa ukali. Qur'an (101:9]
Mioto hii itawaunguza wakosaji kulingana na makosa yao.
Kwa ujumla aina yoyote ya moto ulioandaliwa makafiri hata ukiwa na daraja ya chini namna gani, utakuwa ni mkali usiokifani na usiovumilika hata kwa muda mfupi sana kama Allah anavyotufahamisha:
﴿إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴾
"Hakika hiyo (Jahannam) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa (hata kwa muda mfupi) " [25:66]
Hebu tuone pia anavyotufahamisha Mtume(s.a.w.w) juu ya kiwango cha ukali wa adhabu ya motoni: Nuuman bin Bashir amesimulia kuwa, Mtume(s.a.w.w) amesema:Hakika atakayekuwa na adhabu nyepesi kabisa katika wakazi wa motoni atakuwa yule atakayekuwa na viatu vya moto. Kwa moto huu (wa nyayoni) utachemsha ubongo wake kama maji yachemkayo kwenye birika. Haitaonekana kuna mwenye adhabu kali kuliko hii, lakini hiki ndio kiwango cha chini kabisa cha adhabu .[Bukhari na Muslim]
Kwa ujumla moto wa adhabu aliouandaa Allah (s.w.) kwa watu waovu ni mkali sana wenye miale yenye kupanda juu kwa hasira. Moto huu umeunguzwa kwa ukali kwa muda wa miaka elfu moja mpaka ukabadilika kuwa mwekundu. Uliunguzwa tena kwa muda wa miaka mingine elfu moja mpaka ukabadilika kuwa mweupe. Kisha uliunguzwa tena kwa miaka mingine elfu moja mpaka ukabadilika kuwa mweusi. Hivi ndivyo tunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:Abu Hurairah amesimulia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ambaye amesema: Moto uliunguzwa kwa muda wa miaka elfu moja mpaka ukawa mwekundu. Kisha uliunguzwa kwa muda mwingine wa miaka elfu moja mpaka ukawa mweupe. Tena uliunguzwa kwa mara nyingine kwa muda wa miaka elfu moja mpaka ukawa mweusi. Sasa ni mweusi tii. [Tirmidh]
Pia tunafahamishwa kuwa Jahannam kutakuwa shimoni kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifuatayo: Uthman bin Ghazwaan amesimulia: Imesimuliwa kwetu na Mtume(s.a.w.w) kuwa jiwe litatupwa kutoka ukingoni mwa moto. Litaendelea kuanguka kwa miaka sabini bila kufika chini. Naapa kwa jina la Allah kuwa itajazwa. Na tulifamishwa kuwa umbali katika kati ya milango miwili ya moto na mwendo wa siku arubaini na patakuja siku ambapo itajaa watu. [Muslim]
Humo ndani ya shimo la moto wa Jahannam patakuwa na mashimo (mabonde) na shimo baya kabisa kuliko yote ni "Jabal- Huzn", ambapo Jahannam yenyewe inaomba kukingwa na moto huo wa "Jabal-Huzn" mara sabiini kwa siku. Ndani ya mazingira ya motoni pia patakuwa na miti michungu, na miti maarufu kwa uchungu wake hujulikana kwa jina la "Zaquum". Tumefahamishwa katika Hadith kuwa: Ibn Abbas amesimulia kuwa Mtume (s.a.w.w) alisoma aya hii:
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴾
"Enyi mlioamini muogopeni Allah kama ipasavyo kumuogopa,wala msife isipokuwa mmeshakuwa Waislamu kamili". (3:102).
Mtume(s.a.w.w) alisema:Kama tone la Zaquum lingeanguka kwenye nyumba ya dunia hii, lingelitosha kuharibu vitu vyote wanavyovitumia wakazi wa dunia. Sasa itakuwaje kwa yule ambaye hicho kitakuwa ndio chakula chake? [Tirmidh]
Tunapata maelezo kamili ya mti wa Zaquum. Ambao umemea katikati ya Jahannam na watakaostahiki kuula katika aya zifuatazo:
﴿ أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ الزَّقُّومِ ﴿٦٢﴾ إِنَّا جَعَلْنَاهَا فِتْنَةً لِّلظَّالِمِينَ ﴿٦٣﴾ إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِي أَصْلِ الْجَحِيمِ ﴿٦٤﴾ طَلْعُهَا كَأَنَّهُ رُءُوسُ الشَّيَاطِينِ ﴿٦٥﴾ فَإِنَّهُمْ لَآكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ ﴿٦٦﴾ ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِّنْ حَمِيمٍ ﴾
"Je, karibisho la namna hii silo bora au kupata mti wa Zuqquum? (Mti mchungu kabisa watakaolishwa watu wa motoni). Kwa yakini sisi tumeufanya ni adhabu ya (hao) madhalimu (wa nafsi zao). Hakika huo ni mti unaotoka (unaoota) katikati ya Jahannam. (Panda za) matunda yake (zinatisha) kama kwamba ni vichwa vya mashetani. Bila shaka wao watakula katika (mti) huo, na kwa huo wajaze matumbo (yao). Kisha bila shaka utawathubutikia, juu ya uchungu wa mti huo, mchanganyiko wa maji ya moto". [37:62-67]
Pia katika mazingira ya motoni patakuwa na nyoka na nge wakubwa wenye sumu kali ambao watakuwa wanauma wakazi wa humo kama sehemu ya adhabu yao kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifuatayo:
Abdullah bin Harith bin Jazin amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:"Kuna nyoka huko motoni wakubwa kama ngamia. Mmoja wao akikuuma mara moja, uchungu wake hubaki kwa miaka arobaini. Kuna nge huko motoni wakubwa kama nyumba. Mmoja wao atamuuma mtu na uchungu wake utabakia kwa muda wa miaka arobaini . [Ahmad]
Kwa vyovyote itakavyokuwa maisha ya motoni yatakuwa magumu sana kwa wakazi wake. Chakula chao kitakuwa cha moto wa kuunguza kila kitu tumboni, mavazi yao yatakuwa ya moto, kinywaji chao cha moto kitakachochemsha matumbo yao. Picha halisi ya mazingira ya motoni, maisha ya wakazi wake na sifa zitakazowafanya wastahiki kuingia humo, aya zifuatazo zinafafanua zaidi:
﴿وَقَالُوا أَإِذَا ضَلَلْنَا فِي الْأَرْضِ أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ بَلْ هُم بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ كَافِرُونَ ﴿١٠﴾ قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ ﴿١١﴾وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الْمُجْرِمُونَ نَاكِسُو رُءُوسِهِمْ عِندَ رَبِّهِمْ رَبَّنَا أَبْصَرْنَا وَسَمِعْنَا فَارْجِعْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا إِنَّا مُوقِنُونَ ﴿١٢﴾ وَلَوْ شِئْنَا لَآتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَاهَا وَلَـٰكِنْ حَقَّ الْقَوْلُ مِنِّي لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿١٣﴾ فَذُوقُوا بِمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا إِنَّا نَسِينَاكُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴾
"Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?" (Ndio) Bali wao hawakiri kwamba watakutana na Mola wao. Sema: "Atakufisheni malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu".Na ungaliwaona waovu wakiinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao, (na kusema): "Mola wetu! Tumekwishakuona na tumekwisha kusikia, basi turudishe tutafanya vitendo vizuri, hakika (sasa) tumeyakinisha.Na tungalitaka tungempa kila mtu uwongofu wake (kwa lazima kama tulivyowapa malaika, lakini binadamu amepewa nguvu ya kufanya alitakalo lililo jema na baya), lakini imehakikika kauli iliyotoka Kwangu: Kwa yakini nitaijaza Jahannam kwa wote hawa; majini na watu (ambao ni wabaya). "Basi ionjeni (adhabu) kwa sababu ya kusahau makutano ya siku yenu hii, na sisi tutakusahauni (humo motoni) na onjeni adhabu idumuyo kwa yale mliyokuwa mkiyatenda". [32:10-14]
﴿ إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا ﴿٢١﴾ لِّلطَّاغِينَ مَآبًا ﴿٢٢﴾ لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا ﴿٢٣﴾ لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا ﴿٢٤﴾ إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا ﴿٢٥﴾ جَزَاءً وِفَاقًا ﴿٢٦﴾ إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا ﴿٢٧﴾ وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا ﴿٢٨﴾ وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا ﴿٢٩﴾ فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا ﴾
"Kwa hakika Jahannam inawangoja wabaya.Ni makazi ya maasi.Wakae humo dahari nyingi (karne baada ya karne) Hawataonja humo baridi (wala usingizi) wala kinywaji.Ila maji yachemkayo sana na usaha (wanalipwa) malipo yaliyo sawa (na amali zao).Hakika wao hawakuwa wakiogopa hisabu (ya Mwenyezi Mungu).Na wakikadhibisha aya zetu kukadhibisha (kukubwa kabisa). Na (hali ya kuwa) kila kitu tumekidhibiti kwa kukiandika. Basi onjeni (leo adhabu yangu). Nasi Hatutakuzidishieni (kitu) ila adhabu (juu ya adhabu) ". [78:21-30]
﴿وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٢٣﴾يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي ﴿٢٤﴾ فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ ﴿٢٥﴾ وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ ﴾
"Basi siku hiyo italetwa Jahannam.Siku hiyo mwanadamu atakumbuka,lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? Atasema:"Laiti ningalitanguliza (wema) kwa ajili ya uhai wangu (huu wa leo)".Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu Kwake (Mwenyezi Mungu). Wala hatafunga yeyote jinsi ya kufunga Kwake (Mwenyezi Mungu) " [89:23-26]
Aya hizi kwa ujumla zimesisitiza kuwa, watakaostahiki adhabu ya motoni ni wanadamu na majini waovu ambao waliendesha maisha yao ya hapa duniani kwa kibri na kinyume na utaratibu aliouweka na kuuridhia Allah (s.w.). Kuhusu adhabu yenyewe itakavyokuwa tunafahamishwa katika aya zifuatazo:
﴿إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا سَوْفَ نُصْلِيهِمْ نَارًا كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا الْعَذَابَ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴾
"Hakika wale waliozikataa Aya zetu, tutawaingiza katika moto. Kila ngozi zao itakapowiva, tutawabadilishia ngozi nyingine badala ya zile, ili wawe wanaonja (uchungu wa) adhabu (maisha). Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na Mwenye Hikima) " [4:56]
Hawa mahasimu wawili waliohasimiana kwa ajili ya Mola wao. Basi wale waliokufuru watakatiwa nguo za moto na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yachemkayo.
﴿هَـٰذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ فَالَّذِينَ كَفَرُوا قُطِّعَتْ لَهُمْ ثِيَابٌ مِّن نَّارٍ يُصَبُّ مِن فَوْقِ رُءُوسِهِمُ الْحَمِيمُ ﴿١٩﴾ يُصْهَرُ بِهِ مَا فِي بُطُونِهِمْ وَالْجُلُودُ ﴿٢٠﴾ وَلَهُم مَّقَامِعُ مِنْ حَدِيدٍ ﴿٢١﴾ كُلَّمَا أَرَادُوا أَن يَخْرُجُوا مِنْهَا مِنْ غَمٍّ أُعِيدُوا فِيهَا وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴾
"Kwa (maji) hayo vitayayushwa vilivyomo matumboni mwao na ngozi zao (pia). Na kwa ajili yao (yatakuwapo) marungu ya chuma. Kila mara watakapotaka kutoka humo (adhabuni) kwa sababu ya uchungu watarudishwa humo na (kuambiwa): "Ionjeni adhabu ya kuungua".[22:19-22]
﴿وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ ﴿١٠٣﴾ تَلْفَحُ وُجُوهَهُمُ النَّارُ وَهُمْ فِيهَا كَالِحُونَ ﴿١٠٤﴾أَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَكُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ ﴿١٠٥﴾ قَالُوا رَبَّنَا غَلَبَتْ عَلَيْنَا شِقْوَتُنَا وَكُنَّا قَوْمًا ضَالِّينَ ﴿١٠٦﴾ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْهَا فَإِنْ عُدْنَا فَإِنَّا ظَالِمُونَ ﴿١٠٧﴾ قَالَ اخْسَئُوا فِيهَا وَلَا تُكَلِّمُونِ ﴾
"Na wale ambao mizani yao itakuwa nyepesi, hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao, na katika Jahannam watakaa muda mrefu. Moto utababua (utaziunguza) nyuzo zao, nao watakuwa humo wenye kukenya (meno yao kwa adhabu).(Waambie): Je! Hazikuwa aya zangu mkisomewa na nyinyi mkizikadhibisha? Watasema:"Mola wetu: Tulizidiwa na ubaya wetu na tukawa watu wenye kutopea. Mola wetu! Tutoe humu (motoni, uturejeshe ulimwenguni, tukafanye amali nzuri), na tufanyapo tena bila shaka tutakuwa madhalimu (wa nafsi zetu kweli kweli). Atasema (Mwenyezi Mungu):"Hizikeni humo wala msinisemeshe (msiseme nami) ". [23:103-108]
﴿إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ ﴿٤٣﴾ طَعَامُ الْأَثِيمِ ﴿٤٤﴾ كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ ﴿٤٥﴾ كَغَلْيِ الْحَمِيمِ ﴿٤٦﴾ خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَاءِ الْجَحِيمِ ﴿٤٧﴾ ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ ﴿٤٨﴾ ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ ﴿٤٩﴾ إِنَّ هَـٰذَا مَا كُنتُم بِهِ تَمْتَرُونَ ﴾
"Bila shaka mti wa Zaqquum, ni chakula cha (kuliwa na) maasi,(kwa umoto wake ni) kama shaba iliyoyayushwa; huchemka matumboni kama chemko la maji ya moto kabisa. (Kuambiwe):"Mkamateni (huyo asi) na mumtupie katikati ya Jahannam.Kisha mwagieni juu ya kichwa chake (aonje) adhabu ya maji ya moto. (Aambiwe): Onja! Ulikuwa (ukijidai kuwa) wewe ni mwenye nguvu, mhishimiwa, (onyesha leo nguvu zako).Hakika hii ndiyo ile (adhabu) mliyokuwa mkibishana (mkiitilia shaka) ". [44:43-50]
﴿ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا الضَّالُّونَ الْمُكَذِّبُونَ ﴿٥١﴾ لَآكِلُونَ مِن شَجَرٍ مِّن زَقُّومٍ ﴿٥٢﴾ فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ ﴿٥٣﴾ فَشَارِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ الْحَمِيمِ ﴿٥٤﴾ فَشَارِبُونَ شُرْبَ الْهِيمِ ﴿٥٥﴾ هَـٰذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ الدِّينِ ﴾
"Kisha nyinyi, mliopotea (na kukadhibisha) kwa yakini mtakula mti wa Mzaqquum, na kwa huo mtajaza matumbo (yenu).Na juu yake mtakunywa maji ya moto yanayochemka. Tena mtakunywa kama wanywavyo ngamia wenye kiu sana.(Na kila wakinywa kiu haiweshi). Hiyo ni karamu yao siku ya malipo". [56:51-56]
﴿هَـٰذَا وَإِنَّ لِلطَّاغِينَ لَشَرَّ مَآبٍ ﴿٥٥﴾ جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿٥٦﴾ هَـٰذَا فَلْيَذُوقُوهُ حَمِيمٌ وَغَسَّاقٌ ﴿٥٧﴾ وَآخَرُ مِن شَكْلِهِ أَزْوَاجٌ ﴾
"Hivyo (ndivyo itakakavyokuwa).Na kwa hakika wale warukao mipaka, pa kurudia pao patakuwa pabaya: Jahannam - wataingia. Nayo ni matengenezeo mabaya kabisa.(Ndivyo hivyo itakavyokuwa). Basi waonje (wanywe) maji ya moto na usaha. Na (adhabu) nyingine za namna hii nyingi.(Kila likitiwa jeshi jingine huko motoni waambiwe wale waliotangulia". [38:55-58]
﴿وَلِلَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٦﴾ إِذَا أُلْقُوا فِيهَا سَمِعُوا لَهَا شَهِيقًا وَهِيَ تَفُورُ ﴿٧﴾ تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظِ كُلَّمَا أُلْقِيَ فِيهَا فَوْجٌ سَأَلَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَذِيرٌ ﴿٨﴾ قَالُوا بَلَىٰ قَدْ جَاءَنَا نَذِيرٌ فَكَذَّبْنَا وَقُلْنَا مَا نَزَّلَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِي ضَلَالٍ كَبِيرٍ ﴿٩﴾ وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴿١٠﴾ فَاعْتَرَفُوا بِذَنبِهِمْ فَسُحْقًا لِّأَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴾
"Na kwa waliomkufuru Mola wao iko adhabu ya Jahannam (inawaongojea). Na ni marejeo mabaya yaliyoje: Watakapotupwa humo watasikia rindimo (mngurumo) lake, na hali ya kuwa inafoka. Unakaribia kupasuka kwa hasira (yake juu ya wabaya).Kila mara litakapotupwa humo kundi (la wabaya) walinzi wake watawauliza: Je! Hakukufikieni mwonyaji? Watasema: Kwanini? Alitujia muonyaji, lakini tulikadhibisha na tulisema: Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote, nyinyi hamumo ila katika upotofu (upotevu) mkubwa. Na watasema: Kama tungalikuwa tunasikia au tungalikuwa na akili tusingalikuwa katika watu wa motoni (leo). Watakiri dhambi zao; (lakini hapana faida).Basi kuangamia kumewastahikia watu wa motoni". [67:6-11]
﴿إِنَّهُ مَن يَأْتِ رَبَّهُ مُجْرِمًا فَإِنَّ لَهُ جَهَنَّمَ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ﴾
Hakika atakayekuja kwa Mola wake, hali ya kuwa mkosa, basi kwa yakini atapata moto wa Jahannam, hatakufa humo wala hataishi (maisha mazuri). [20:74]
﴿فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ﴾
Basi siku hiyo hataadhibu yoyote namna ya kuadhibu Kwake(Mwenyezi Mungu). [89:25]
Aya hizi chache zimetupa picha ya kutisha ya maisha ya Motoni ambapo wakazi wake hawatakuwa na hata chembe ya furaha na hawatakufa japo watatamani wafe. Na hasara kubwa zaidi watakayoipata ni kutomuona Allah (s.w.). Kwani kumuona Allah (s.w.) ni kilele cha furaha na ilihali watu wa motoni wameharamishwa hata chembe ya furaha. Kwa ujumla marejeo ya motoni ni marejeo mabaya kabisa na kila mja mwema hana budi daima aombe:
﴿وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿٦٥﴾ إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا﴾
"Mola wetu: Tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea. Hakika hiyo (Jahannam) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa (muda mfupi au mrefu). [25:65-66]
11
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
MAANANA YA KUAMINI SIKU YA MALIPO KATIKA MAISHA YA KILA SIKU
Muumini wa kweli wa Siku ya Mwisho ni yule atakaye jitahidi kwa jitihada zake zote kufanya yafuatayo:
1. Kufanya wema kwa kadiri ya uwezo wake ili apate radhi za Allah (s.w) ili astahiki kupata makazi mema katika maisha ya akhera.
Huingia katika biashara na Allah (s.w):
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿١٠﴾ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١١﴾ يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾ وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴾
Enyi mlioamini! Je! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo? (Basi biashara yenyewe ni hii):- Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganieni dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu, haya ni bora kwenu; ikiwa mnajua (kuwa ni bora, basi fanyeni).(Mkifanya haya) Atakusameheni dhambi zenu na atakuingizeni katika Mabustani yapitayo mito mbele yake na (atakupeni) maskani mazuri mazuri katika Bustani za milele: huku ndiko kufuzu kukubwa. Na (atakupeni) kingine mnachokipenda: Nayo ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu na ushindi ulio karibu! Na wapashe habari njema waumini (61:10 -13)
﴿إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّـهِ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴾
Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani.Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa, (9: 111)
2. Kujiepusha na maovu kwa kadiri ya uwezo wake na kila mara kuleta Istighfar na dua, kumuomba Mola wake amuepushe na adhabu ya akhera. Katika Qur-an tunafahamishwa waja wa Rahman (Waumini wa kweli) ni wale waombao:
﴿وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿٦٥﴾ إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا﴾
"Mola wetu tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea. Hakika hiyo (Jahannam) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa" (25:65-66)
3. Kuleta toba ya kweli atakapoteleza kwa kufanya jambo lolote lile kinyume na radhi ya Allah (s.w). Mwenyewe Allah (s.w) anatuamrisha:
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ﴾
"Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allah toba ya kweli, huenda Mola wenu Atakufutieni maovu yenu na kukuingizeni katika pepo zipitazo mito mbele yake,.." (66:8)
﴿وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴾
"Na ombeni msamaha kwa Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa Kurehemu." (73:20)
﴿إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾ وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا﴾
Allah (s.w) ameahidi kuwasamehe wale watakao leta toba ya kweli kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo: Ila yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri; basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu. Na aliyetubia na kufanya wema, basi kwa hakika yeye anatubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu.(25:70-71)
﴿ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُوا السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴾
Kisha hakika Mola wako kwa wale waliofanya ubaya kwa ujinga, kisha wakatubia baada ya hayo na wakatenda mema; bila shaka Mola wako baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu (16:119)
﴿وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ أَنَّهُ مَنْ عَمِلَ مِنكُمْ سُوءًا بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابَ مِن بَعْدِهِ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴾
Na (wewe Mtume) wanapofika wale wanaoamini Aya zetu(na hali wamekosa kidogo; wanakuja kutubia) waambie "Amani iwe juu yenu, Mola wenu amejilazimisha rehema, kwamba atakayefanya miongoni mwenu uovu kwa ujinga, Mwenyezi Mungu atamghufiria kwani yeye ni Mwingi wa Rehema. (6:54)
﴿قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴾
Sema,"Enyi waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu; bila shaka Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote; hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu." (39:53)
Kutokana na aya hizi, tunajifunza kuwa toba ya kweli itapatikana kwa kuzingatia masharti yafuatayo:
1. Mwenye kuleta toba awe amefanya kosa kwa ujinga au kwa kutelezeshwa na vishawishi vya mazingira ya kishetani bila ya kudhamiria.
2. Baada ya kutanabahi kuwa amemuasi Mola wake, Muumini wa kweli atajuta na kuilaumu nafsi yake, na kulalama kwa Mola wake, kama walivyolalama wazazi wetu, Adam(a.s) na Hawwa (r.a):
﴿قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴾
"Mola wetu!Tumedhulumu nafsi zetu, na kama hutatusamehe na kuturehemu,bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye khasara." (7:23)
Pia katika Hadithi iliyosimuliwa na Abubakar Swidiq (r.a) na kukubaliwa na Maimamu wote wa hadith, Mtume (s.a.w) ametufundisha kuleta majuto moyoni mwetu kwa kuomba: "Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika nimedhulumu nafsi yangu dhulma kubwa.Hapana yeyote mwenye kusamehe dhambi isipokuwa wewe tu.Basi nakuomba unipatie msamaha utukao kwako na unihurumie.Hakika wewe ni Msamehevu, Mrehemevu."
3. Kuazimia moyoni kuacha maovu.
4. Iwapo makosa yake yamehusiana na kudhulumu haki za watu, itabidi awatake radhi wale aliowakosea na kuwarejeshea haki zao zile zinazorejesheka.
5. Kuzidisha kufanya amali njema kwa kuzidisha kutoa sadaqa, kuzidisha kuleta swala na funga za sunnah, na kuzidisha juhudi ya kupigania dini ya Allah kwa mali na nafsi. Rejea Qur-an (61:10-13) na (9:111).
Shufaa Ni muhimu baada ya mada hii ya "maana ya kuamini siku ya mwisho", tuiangalie shufaa kwa mtazamo wa Kiislamu. Ni muhimu kwa sababu imetokea kwa baadhi ya watu wanaoitakidi kuwa ni waumini, kwa kupenda kwao njia ya mkato, wanaacha kutekeleza wajibu wao wa kuishi kama anavyotakiwa kuishi muumini wa kweli na badala yake wanaendesha maisha yao ya kila siku kama wafanyavyo makafiri na wakati huo huo wanamatumaini makubwa ya kupata neema za peponi kwa njia ya shufaa.
Maana ya Shufaa: Kwa mujibu wa Qur-an na Sunnah shufaa ni uombezi wa watu wema kuwaombea msamaha watu watakaokuwa katika hali ya udhalili katika maisha ya akhera ili Allah (s.w) awatoe katika hali hiyo ya udhalili na kuwapeleka katika hali bora. Patakuwa na shufaa ya:
(i) Kuwaombea watu hisabu nyepesi na wachukue muda mfupi katika hisabu.
(ii) Kuwaombea waja wema waingie peponi moja kwa moja bila ya hisabu ili kuepukana na mazito ya siku ya Hisabu.
(iii) Kuwaombea waingizwe peponi wale ambao mizani ya mema na mabaya yao imekuwa sawa sawa.
(iv) Kuwaombea watu watolewe kutoka motoni na waingizwe peponi.
(v) Kuwaombea watu wema wapandishwe daraja katika Pepo; watolewe katika pepo ya daraja ya chini na kupandishwa katika pepo ya dara ya juu.
Masharti ya Shufaa: Pamoja na shufaa kuwepo katika siku hiyo ya malipo, Uislamu hauichukulii shufaa kwa mtazamo wa kikristo au mtazamo wa dini nyingine, ambapo hao watakaoshufaia wameitakidiwa kuwa watakuwa na uwezo wa kuwaokoa watu na adhabu ya Allah (s.w) na kuwaingiza Peponi. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Shufaa haitafanyika ila kwa idhini ya Allah (s.w). Ni lazima kwanza Allah (s.w) aridhike kuwa mkosaji anastahiki ndio atoe ruhusa ya shufaa kwa yule aliyemridhia na kisha baada ya msamaha huo kuombwa ni khiari yake Allah (s.w) kusamehe au kutosamehe. Msimamo huu juu ya shufaa umewekwa bayana katika Qur-an:
﴿مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ﴾
" Nani huyo awezaye kushufaia mbele yake (Allah) bila ya idhini yake?" (2:255)
"Na wako Malaika wangapi mbingu ni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia." (53:26). Pia rejea Qu r-an (6:51, 10:3, 19:87, 39:44, 43:86 na 74:48).
Kwa ujumla shufaa ni rehema ya Allah (s.w) atakayo ikunjua kwa wale watakaostahiki kuipata kutokana na jitihada zao za kutenda mema hapa duniani kwa ajili ya Allah (s.w) japo wakati mwingine wanaweza kutekeleza na kumuasi. Muumini wa kweli wa siku ya malipo atajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kutenda mema kwa ajili ya Allah (s.w), kujiepusha na maovu kwa kuchelea ghadhabu za Allah (s.w) na kuomba maghfira kwa haraka haraka kila atakapomkosea Allah (s.w) au kumkosea mwanaadamu mwenziwe. Udhaifu utakaompitia muumini huyu, Allah (s.w) atamsamehe kwa njia mbali mbali na hii ya kuombewa shufaa ikiwa ni mojawapo.
Nani watakao shufaia? Watakaoombea waumini shufaa kama tulivyoona katika aya zilizotangulia ni pamoja na Malaika, Mitume, watu wema ikiwa ni pamoja na watoto wachanga na amali njema kama Swala, Swaumu, Qur-an, n.k. Wa kwanza kushufai katika siku ya kutisha, siku ya Kiyama atakuwa ni Mtume(s.a.w.w) kama tunavyofahamishwa katika hadith nyingi. Baada ya Hukumu kupita,Mitume watawaombea shufaa miongoni mwa wafuasi wao ambao watakuwa wamehukumiwa kuingia motoni. Pia waumini watakoingia Peponi watapewa fursa ya kuwaombea shufaa waumini wenzao ambao kwa njia moja au nyingine walifeli mtihani na ikabidi waingie motoni.
Hebu tuzingatie hadith zifuatazo: Uthman bin Affan amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) kasema: "Watatu watashufaia katika siku ya Kiyama: Mitume, kisha wanachuoni, kisha waliokufa mashahidi". (Ibn Majah). Abu Sayyid amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:Kati ya Umma wangu patakuwa na watakaoshufaia makundi mengi ya watu kati yao kuna watakaoomba shufaa kwa kabila (moja) na kati yao kuna wakaoomba shufaa ya mtu mmoja, mpaka wangie Peponi." (Tirmidh)
Anas kasema: Wakazi wa motoni watapangwa katika mistari, kisha mmoja wa wakazi wa Peponi atawapitia. Mmoja katika wao atasema: Ewe Fulani, hunitambui?Nilikuwa yule niliyekupa maji. Na wengine watasema: Tulikuwa ni wale tuliyekupa maji ya kutawadhia. Hivyo atamuombea (kila mmoja) kwa Allah (s.w) na kumwingiza peponi. (Ibn Majah). Abu Sayyed al-Khudry amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:"Kila mwenye imani uzito wa hardali (atom weight) atatolewa motoni". (Tirmidh).
Jambo la kuzingatia na kusisitiza sana hapa ni kwamba shufaa haitaombwa kwa misingi ya udugu, ukoo, utaifa au kwa misingi ya upendeleo wa aina yeyote, bali itajuzu tu kwa wale Allah (s.w) atakaoridhia waombewe na akatoa idhini juu ya kuombewa kwao. Kwa maana nyingine shufaa itategemeana na matendo mema ya mtu aliyoyatanguliza. Mitume watashufaia wafuasi wao waliowafuata kwa uadilifu, watu wema watawashufaia jamaa zao, jirani zao, rafiki zao, wananchi wenzao, waliowatendea wema kwa ajili ya wema wao, watoto wadogo wawashufaia wazazi wao waliokuwa wema kwao, n.k. Shufaa hizi zitapata ruhusa na kukubaliwa tu iwapo wale wanaoombewa walikuwa waumini ambao kwa njia moja au nyingine waliteleza na kumuasi Allah na wakastahiki kuwa katika hali hiyo ya dhiki. Kwa kafiri au mushriki shufaa ya aina yeyote haitakubaliwa hata kama shufaa hiyo itaombwa na Mitume au vipenzi vya Allah (s.w). katika Qu-an tumeona kukataliwa kwa maombi ya Nabii Muhu juu ya mwanawe aliyestahiki kuangamizwa pamoja na walioangamizwa kwa ukafiri wao:
"Ikiwa hiyo (jahazi) inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamwita mwanawe aliyekuwa mbali (kakataa kuingia jahazini): "Ewe mwanangu!Panda pamoja nasi wala usiwe pamoja na makafiri". Akasema (huyo mtoto): "Nitaukimbilia mlima utakaonilinda na maji". Akasema (Nuhu): "Hakuna leo kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu isipokuwa yule atakayemrehemu (Mwenyezi Mungu)". Mara mawimbi yakaingia baina yao na akawa miongoni mwa waliogharikishwa. Na (baada ya kuangamizwa wote na vyote alivyotaka Mwenyezi Mungu viangamie) ikasemwa:P "Ewe ardhi: Meza maji yako. Na ewe Mingu jizuie (na kuteremsha mvua). Basi maji yakadidimia chini na amri ikapitishwa (ya kuangamizwa makafiri), na (jahazi) likasimama juu ya (jabali linaloitwa) Judi.Na ikasemwa likasimama juu ya (jabali linaloitwa) Judi. Na ikasemwa "Wameangamiliziwa mbali madhalimu"
Na Nuhu alimwomba Mola wake (alipomwona mwanawe anaangamia) akasema:
﴿ وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ ﴿٤٥﴾قَالَ يَا نُوحُ إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ إِنَّهُ عَمَلٌ غَيْرُ صَالِحٍ فَلَا تَسْأَلْنِ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ إِنِّي أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ﴾
"Ewe Mola wangu! Mwanangu ni katika watu wa nyumbani kwangu (mbona anaangamia)? Na hakika ahadi yako ni haki; nawe ni Mwenye haki kuliko mahakimu (wote): Akasema (Mwenyezi Mungu): Ewe Nuhu! Huyu si miongoni mwa watu wako. Yeye ni (mwenye) mwendo usiokuwa mzuri. Basi usiniombe ambayo huyajui Mimi nakunasihi usiwe miongoni mwa wajinga" (11:45-46)
Pia tunafahamishwa katika Hadith jinsi Nabii Ibrahim (a.s) atakavyokataliwa maombi yake kwa Allah (s.w) kumuombea baba yake Azar aepushwe na adhabu kali waliyoandaliwa washirikina: Abu Hurairah amesimulia kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) aliyesema: Ibrahim atakutana na baba yake. Azar katika siku ya Kiyama. Uso wa Azar utakuwa umefunikwa na lami na mavumbi.
Ibrahimu atamsemesha: "Sikukuambia kuwa usiache kunitii (usinikadhibishe)?" Baba yake atamjibu: "Leo sitaaacha kukutii". Ibrahim ataomba: Ewe Mola! Hakika umeniahidi kuwa hutanifedhehesha siku watakapofufuliwa watu.Sasa ni fedheha gani zaidi kuliko kuwekwa mbali na baba yangu? Allah (s.w) atasema: Hakika Nimeiharamisha Pepo kwa Washirikina. Kisha itasemwa kwa Ibrahimu: Angalia ni kitu gani kilichoko miguuni mwako. Ataangalia, hamaki: shingo kubwa itatokeza. Ataburuzwa (Azar) kwa miguu yake na kutupiwa motoni. (Bukhari)
Vile vile tukirejea tena Qur-an tunaona jinsi Mtume(s.a.w.w) alivyokataliwa maombi yake alipowaombea wanafiki:
﴿اسْتَغْفِرْ لَهُمْ أَوْ لَا تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ إِن تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ سَبْعِينَ مَرَّةً فَلَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴾
Waombee msamaha au usiwaombee.Hata ukiwaombea msamaha mara sabiini,Mwenyezi Mungu hatawasamehe. Hayo ni kwa sababu ya kuwa wao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotofu.(9:80)
Hivyo kutokana na maelezo haya, tumeona kuwa shufaa itakuwepo, lakini itawanufaisha tu walioamini na sio makafiri, washirikina na wanafiki. Jambo muhimu kwa Muislamu ni kujitakasa kwa kutenda mema na kuacha maovu na kuwa mwepesi na kurejea kwa Allah (s.w) kwa toba baada ya Kumkosea au kuhisi Kumkosea. Si vyema kwa Muislamu kuzembea katika kufanya mema na kuendelea kufanya maovu kwa matarajio ya kupata shufaa ya Mtume(s.a.w.w) au ya yeyote yule amtegemeaye kuwa atamshufaia. Kuna mambo mawili muhimu ya kuzingatia kwa wale wanaoacha kujitahidi kutekeleza wajibu wao kama anavyoridhia Allah (s.w) na badala yake wakaishi watakavyo kwa tegemeo la kupata uokovu kutokana na shufaa:
Kwanza kutegemea shufaa ni jambo la kubahatisha mno, kwani si jambo lililoko kwenye mamlaka ya yeyote isipokuwa Allah (s.w) pekee. Pili, shufaa nyingine itakuja baada ya mja kuadhibiwa kwanza, adhabu ambayo ni kali mno, inayodhalilisha au kuhilikisha hata kama mja atakaa humo muda mfupi sana. Ni vyema tuzingatie sana aya ifuatayo:
﴿فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ﴾
Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu Kwake (Allah) (89:25)
Hivyo, jambo la busara ni Muislamu kujitahidi kuepukana na adhabu kali ya Allah (s.w) aliyowaandalia watu maasi na badala yake ayaendee kwa juhudi kubwa iliyoambatana na subira na yale yatakayompelekea kustahiki kuingizwa peponi moja kwa moja.
12
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
KUAMINI QADAR YA ALLA
Kwa mujibu wa Hadith iliyosimuliwa na Umar (r.a), kuamini Qadar ni nguzo ya sita ya Imani ya Kiislamu. Katika hadithi hii ndefu, Umar (r.a) anasimulia: Siku moja tulipokuwa tumeketi pamoja na Mtume(s.a.w.w) alitutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe kama theluji na nywele zake nyeusi sana, hakuwa na dalili zozote za msafiri, ingawa alikuwa mgeni kwetu sote. Halafu alikaa mbele ya Mtume hali magoti yake yakikabiliana na yale ya Mtume na akaweka mikono yake katika mapaja ya Mtume halafu akasema:
"Ewe Muhammad nifahamishe juu ya Uislamu" na Mtume akasema: "Ni kushuhudia kuwa hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah, kusimamisha Swala, Kutoa Zakat, Kufunga mwezi wa Ramadhani na Kuhiji Makkah kwa mwenye kuweza" Halafu yule mgeni akasema:
"Umesema kweli.Tulistajaabu kwa nini aliuliza halafu akasadikisha. Halafu akasema: "Nifahamishe juu ya Imani". Mtume akasema: "Ni Kumuamini Allah, Malaika Wake, Vitabu vyake, Mitume Wake, Siku ya Mwisho na Qadar, Kheri yake na Shari yake". Kisha akasema: "Nifahamishe juu ya Ihsan". Na Mtume akamjibu:"Ni kumuabudu Allah kama kwamba unamuona, kwani ingawa humuoni, Yeye anakuona". Halafu akasema: "Nifahamishe juu ya Siku ya Kiyama". Mtume akamjibu kwamba hajui mwenye kuulizwa zaidi ya mwenye kuuliza Akasema:
"Nifahamishe dalili zake" Mtume.Akasema: "Ni wakati ambao mjakazi atamzaa bibi yake, na utakapoona wachungaji maskini, wenye nguo zilizoraruka na wasio na viatu wanashindana kujenga maghorofa".Yule mgeni alipoondoka, Mtume alikaa kimya kwa muda halafu akasema: "Ee Umar, unamfahamu muulizaji?" Sote tukajibu kuwa Allah na Mtume wake ndio wajuao. Mtume akasema: "Huyo ni Jibril, amekuja kuwafundisheni dini yenu". (Muslim)
Maana ya Qadar Neno "Al-Qadar" limetumika katika Qur-an kwa maana ya "kiasi", kipimo", kukadiria kipimo maalumu". Hebu turejee aya zifuatazo ambamo neno Qadar limetumiwa:
﴿إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ ﴾
"Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kiasi (chake makhsusi)" (54:49)"...
﴿وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا﴾
Na (Mwenyezi Mungu) Ameumba kila kitu na Akakikadiria kipimo (chake)" (25:2)
﴿وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ﴾
"Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa (mwembamba) kama chaparare la mtende kuu kuu". (36:39).
Tukizingatia aya hizi, tunajifunza kuwa Allah(s.w) ameumba ulimwengu huu na vyote vilivyomo kwa mujibu wa kanuni zinazotawala mzunguko wa jua, mwezi, nyota, dunia na sayari nyingine. Kutokana na mizunguko ya jua, mwezi na dunia tunapata urefu wa mchana na usiku, hesabu ya miezi, majira, n.k. Kuna kanuni zinazotawala ukuaji wa mimea. Kutokana na kanuni hizo, mimea huzaa matunda yenye rangi na ladha mbali mbali.Kwa ujumla Allah (s.w) ameumba kila kitu kwa lengo, maalumu na ameweka kanuni madhubuti zinazokiwezesha kila kiumbe kifikie lengo lake kama anavyotukumbusha katika Qur-an:
﴿سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى ﴿١﴾ الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٢﴾ وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ﴾
"Litukuze jina la Mola wako aliye Mtukufu.Aliyeumba (kila kitu) akakitengeneza.Na akakikadiria (kila kimoja jambo lake) na akakiongoza (kufanya jambo hilo). (87:1-3)
Pia matukio yote yako katika Qadar ya Allah (s.w).Hapana tukio lolote linalotokea liwe la kheri au la shari kwa mwanaadamu, ila limo katika Qadar ya Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika Qur-an:
﴿ وَاللَّـهُ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ جَعَلَكُمْ أَزْوَاجًا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ وَمَا يُعَمَّرُ مِن مُّعَمَّرٍ وَلَا يُنقَصُ مِنْ عُمُرِهِ إِلَّا فِي كِتَابٍ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ﴾
Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha akakufanyeni wanaume na wanawake. Na mwanamke yoyote hachukui mimba wala hazai ila kwa ilimu Yake (Mwenyezi Mungu). Na mwenye kupewa umri hapewi umri (zaidi) wala hapunguziwi umri wake ila yamo hayo katika Kitabu (cha Mwenyezi Mungu). Bila shaka (kuyapitisha) haya ni sahali kwa Mwenyezi Mungu. (35:11)
﴿مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ﴾
Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwishaandikwa katika Kitabu (cha Mwenyezi Mungu) kabla Hatujauumba. Kwa yakini hilo ni sahali kwa Mwenyezi Mungu. (57:22)
Mtazamo wa Uislamu juu ya Qadar Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, ni makosa makubwa kudhani kuwa mtu anaweza kufanya jambo lolote lile kinyume na Qadar ya Allah (s.w). Na ni makosa makubwa pia kudhani kuwa mtu anaweza kumlaumu Allah (s.w) kwa maovu anayotenda. Utatanishi wote wanaoupata watu juu ya suala hili unaondoka kwa sababu Uislamu umegawanya maisha ya binaadamu katika maeneo makuu mawili:
(a) Eneo ambalo binaadamu hana hiari, na
(b) Eneo ambalo binaadamu anao uchaguzi. Binaadamu hana hiari kabisa katika baadhi ya mambo katika maisha yake. Mambo hayo humtokea atake asitake. Hana uwezo wa kuyachagua wala kuyabadilisha.Kwa mfano mtu hana hiari ya kuwachagua wazazi wake.Hawezi kuchagua tarehe ya kuzaliwa wala nchi atakayozaliwa.Hawezi kuchagua rangi ya ngozi yake wala aina ya nywele, rangi ya macho, kimo au vipawa vingine.
Damu itazunguka mwilini bila kuipangia yeye safari hiyo, moyo wake utadunda bila yeye kuuamrisha.Mwili mzima wa binaadamu unafanya kazi bila yeye kuupigia kura. Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu binaadamu hataulizwa au kuhisabiwa juu ya jambo lolote ambalo yeye hakuwa na hiari nalo.Yaani hakuna mtu atakayeulizwa kwanini wewe ulizaliwa siku ya Jumanne badala ya Jumatano? Au kwa nini ulifariki mwezi wa Shaabani badala ya kusubiri hadi mwezi wa Ramadhani? Au kwanini ulikuwa mrefu namna hii badala ya kuwa na kimo cha wastani? Kwa hakika ni rehema kubwa ya Allah (s.w) kwamba mambo hayo hatuyadhibiti sisi wenyewe.
Hebu fikiria kama moyo ungelikuwa unapiga kwa amri yetu, tungeliwazaje kulihakikisha hilo tunapolala usingizini au tunaposahau? Matatizo yangekuwa hayo hayo lau myeyusho wa chakula (digestion) ungelikuwa uko chini ya udhibiti wetu, n.k.
Kuna eneo ambalo binaadamu anao uhuru wa kuchagua hili au lile. Mtu anaweza kwa mfano kuchukua bastola na kumuulia mtu mwingine na kupora mali yake au anaweza kuchukua chakula na kumpa mwenye njaa. Mtu anaweza kutumia pesa zake kwa kuwanunulia nguo wazazi wake, au anaweza kwenda nazo kilabuni kunywea pombe. Mtu anaweza kumuamini Allah (s.w) na kumtii na anaweza kukataa kumuamini na akaamua kumuasi. Mtu anaweza kusema kweli au akiamua anaweza kusema uwongo.Anaweza kumtendea mwenziwe haki au anaweza kumdhulumu.Katika eneo hili binaadamu ni Mas-uli, yaani atahisabiwa na Allah (s.w) kwa yote aliyoyafanya kwani ni mambo ambayo binaadamu amepewa uhuru wa kuchagua kutenda hili au lile.
﴿إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا﴾
"Hakika Sisi Tumemuongoa, (tumembainishia) njia. Basi atakuwa mwenye shukurani au mwenye kukufuru" (76:3)
﴿وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ فَمَن شَاءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَاءَ فَلْيَكْفُرْ﴾
"Na sema: Huu ni ukweli uliotoka kwa Mola wenu, basi anayetaka naamini na anayetaka na akufuru." (18:29)
﴿ أَلَمْ نَجْعَل لَّهُ عَيْنَيْنِ ﴿٨﴾ وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ ﴿٩﴾ وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ﴾
"Je, hatukumpa(binaadamu) macho mawili? Na ulimi na midomo miwili?Na tukambainishia zote njia mbili?" (90:8-10)
Hivyo ni dhahiri kuwa katika eneo hili binaadamu hajapangiwa na Allah (s.w) lipi aje kulifanya atake asitake. Allah (s.w) amempa mwongozo wa kuufuata lakini kampa na hiari ya kuufuata au kuuacha. Na ndio maana ataulizwa.Ukweli kuwa watu wanaweza kumuasi Allah (s.w) ni ushahidi tosha kuwa watu wanao uhuru wa kuchagua kutenda mema au maovu, kwani lau si hivyo watu wote wangekuwa kama Malaika.
Hata hivyo, kwanza, isidhaniwe kuwa maadamu watu wanao uhuru wa kuchagua kutenda lolote basi Allah (s.w) hajui mpaka jambo hilo litokee.Yeye anayajua yote atakayofanya mja hadi hatima yake ya mwisho siku ya kiyama hata kabla mtu huyo hajazaliwa.
﴿وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ﴾
"Na hakuna mnyama yeyote (kiumbe chochote) katika ardhi ila riziki yake iko juu ya Mwenyezi Mungu. Na anajua makao yake ya milele na mahali pake pa kupita tu (hapa duniani). Yote yamo katika kitabu kinachodhihirisha (kila kitu)" (11:6)
Allah (s.w) anayajua atakayoyachagua mtu kuyafanya lakini hakumshurutisha kuyafanya
Pili, isidhaniwe pia kuwa maadamu mtu amechagua kumuasi Allah (s.w), basi mtu huyo anapotenda uovu huo Allah (s.w) huchukia lakini hana uwezo wa kumzuia. Mtu hawezi kufanya lolote ila kwa idhini ya Allah (s.w). Yaani mtu anaweza tu kutenda jema au ovu kwa sababu ya kutumia vizuri au vibaya neema alizopewa na Allah (s.w).
Kwa mfano tusema mtu amekusudia kwenda kuswali Ijumaa lakini kabla hajaondoka Allah (s.w) akamnyang'anya mtu huyo neema ya akili au fahamu, au akakosa nguvu hata za kukaa, ni dhahiri kuwa hataweza kuswali Ijumaa. Na hivyo hivyo kwa mtu aliyekusudia kwenda kuvunja duka na kupora mali kabla ya kufanya hivyo akavunjika mgongo au akatiwa upofu machoni, ni dhahiri kuwa hawezi kutenda lile alilolikusudia. Hivyo mema au maovu hayatendeki kinyume na uwezo wa Allah (s.w).
13
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
SUALA LA UONGOFU
Badhi ya watu hujiuliza: Kama sote tuna fursa sawa sawa ya kuchagua kutenda mema au maovu mbona Qur-an yasema Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye na humuacha kupotea amtakaye? Uongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu uko wa namna mbili: Kwanza uongofu kwa maana ya kumfahamisha mtu njia sahihi ya kufuata. Na pili uongofu kwa maana ya msaada utokao kwa Mwenyezi Mungu.
Uongofu kwa maana ya kwanza, yaani kujulishwa njia ya heri na ya shari, na kujulishwa jambo lipi mtu atende na lipi aliwache, ni uongofu ambao kila mtu anaupata. Na uongofu huo ni wa namna tatu kwanza ni: fitra, yaani kupandikizwa uongofu katika nafsi yake mtu:
﴿وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا ﴿٧﴾ فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا﴾
Na kwa nafsi na aliyeitengeneza.Kisha akaifahamisha uovu wake na wema. (91:7-8)
Na uongofu wa namna ya pili ni kipawa cha akili, ambacho kinaweza kutumika kuisadikisha imani. Na namna ya tatu ni uongofu aliopewa binaadamu kwa kupitia Mitume na Vitabu vya Mwenyezi Mungu. Hivyo kila mtu amepata uongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu angalau kwa njia mbili za mwanzo.
Uongofu kwa maana ya msaada wanaupata wale tu wanaoamua kuufuata kikweli kweli ule uongofu waliopewa. Tuseme mathalan mtu fulani amepotea mjini au hajui njia ya kwenda mahali fulani akaamua kumuuliza askari: Baada ya kumuelekeza mtu yule aliyepotea aseme: Sikuamini, mwongo mkubwa wee!! Askari atamwambia: Sawa fuata njia unayoijua. Lakini iwapo mtu aliyepotea baada ya kuelekezwa atasema: Ahsante sana kwa kunielekeza nafikiri nitafika ninakokusudia, askari anaweza kumwambia: Subiri kidogo mimi nakwenda huko huko nitakupeleka hadi unapokwenda. Huu ni mfano tu, na Mwenyezi Mungu hawezi kufananishwa na askari au kiumbe yeyote.Kusudio hapa ni kuonesha kuwa watu wanaofuata muongozo wa Mwenyezi Mungu huzidishiwa uongofu:
﴿وَالَّذِينَ اهْتَدَوْا زَادَهُمْ هُدًى وَآتَاهُمْ تَقْوَاهُمْ﴾
Na wale wanaokubali kuongoka anawazidishia uongofu na anawapa (jaza) ya ucha Mungu wao. (47:17)
﴿نَّحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ نَبَأَهُم بِالْحَقِّ إِنَّهُمْ فِتْيَةٌ آمَنُوا بِرَبِّهِمْ وَزِدْنَاهُمْ هُدًى﴾
Sisi tunakusimulia habari zao kwa kweli. Hakika wao walikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao Nasi tukawazidisha uongofu.(18:13)
Ili kuweka wazi zaidi uongofu wa aina hii ya pili hebu tuizingatie kwa makini aya aifuatayo:
﴿إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُم بِإِيمَانِهِمْ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ﴾
Hakika wale walioamini na kufanya vitendo vizuri, Mola wao atawaongoza kwa sababu ya imani yao (wende katika Pepo) Itakuwa inapita mito mbele yao katika mabustani yenye neema. (10:9).
"Allah (s.w) humwingiza katika rahma zake amtakaye na kumwacha kupotea amtakaye" Muradi wa aya zenye melekeo huu ni kuwa Allah(s.w) ametoa sifa za waumini kama zilivyoaminishwa katika Qur'an mf.( 23: 1-11), (25: 63-77), (8:2-4), (49: 1-13,15), (70:19-35), n.k.
Hawa ndiyo "anaowataka" basi anayetaka awepo katika kundi hilo hana budi ajipambe kwazo. lakini pia ametoa sifa za wafiki, washirikina, makafiri, .n.k kama zilivyoanishwa katika qur'an (33:12-20), (2:8-20), (3:166-171), (4:135-152), n.k. Watu watakojipamba na sifa hizi basi Allah huwaacha ( akawaelekezea huko) kupotea, Allah (s.w) ni mwadilifu, humrahisishia mja kila akitakacho cha kheri au cha shari, ndiyo maana pia anasema, "Haakhirishi ya watu mpaka watu wabadilishe yayokuwa katika nafsi zao....." Mbona kuna Uovu na Mateso Duniani? Kuna baadhi ya watu ambao huuliza hivi: Iwapo Mwenyezi Mungu anawapenda waja wake mbona anaacha maovu na mateso yaendelee duniani?Kwa nini asiyazuie?
Kwanza : ni makosa kumhukumu Mwenyezi Mungu ambaye ni Mjuzi wa kila kitu kwa vipimo vya kibinaadamu. Hii ni kwa sababu binaadamu mara nyingi anaathiriwa na hisia zake binafsi na maslahi yake katika kufanya maamuzi yake. Kwa mfano tunaamuaje kuwa kitu fulani ni chema au kibaya? Tuchukue mifano rahisi.Mvua ikinyesha mkulima aliyepanda mazao anamshukuru Mwenyezi Mungu lakini mtu anayekwenda pikiniki au anayefanya sherehe ya harusi, mvua hasa ikinyesha kutwa nzima ni nuksi kubwa kwake!Au tuseme mtu amekodi teksi anawahi ndege uwanjani kwenda kumzika mama yake.
Kwa sababu ya msongamano wa magari barabarani amechelewa kufika uwanjani na hivyo ndege imemwacha na safari kaikosa. Atalaani mtu huyo na kudai kuwa huo ni mkosi mkubwa. Baada ya nusu saa akisikia kuwa ndege ile imeanguka na watu wote wamekufa utamsikia anamshukuru Mungu kwa bahati njema aliyoipata! Binaadamu hawana haki ya kumuuliza Mwenyezi Mungu kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:
﴿لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ﴾
Haulizwi (Mwenyezi Mungu) anayoyafanya lakini wao (viumbe wataulizwa).(21:23)
Hii haina maana kuwa binaadamu wanakatazwa kujaribu kutafuta hikima ya Mwenyezi Mungu katika kuamrisha au kukataza kwake mambo, La!Kinyume chake wanahimizwa kufanya hivyo. Wanachokatazwa ni kujaribu kumhukumu Mwenyezi Mungu au kuyakataa na kuyapinga yale ambayo hikima yake hawaijui. Hivyo katika hizo jitihada za kujaribu kubahatisha kuona hikima ya kuyaacha maovu na mateso yawepo baadhi ya watu wanasema kuwa lau si kuwepo kwa uovu watu wasingejua nini wema, bila kuwepo maradhi watu wasingejua thamani ya afya na bila ya mauti watu wasingeyathamini maisha. Wengine wanasema hata wadudu wabaya tunaodhani wanawabughudhi binaadamu, tunadhani hivyo kwa sababu tu hatujajua thamani yao kwetu.
Jambo la kukumbuka ni kuwa kwa mujibu wa Qur-an binaadamu katika kipindi chote cha maisha yake hapa duniani yupo katika majaribio. Na majaribio hayo yatachukua sura mbali mbali za heri na shari. Na jingine ni kwamba ili mtihani huo uwe na maana yoyote watu lazima wawe na hiari ya uchaguzi. Hii ina maana kuwa watu wanaweza kuchagua uovu pia. Hivyo iwapo Mwenyezi Mungu atawapa watu hiari ya uchaguzi lakini atahakikisha hawachagui kufanya ufisadi na uovu nini maana ya kutoa mtihani? Hii haina maana kuwa baada ya kuumbwa ulimwengu Mwenyezi Mungu ameususa na kuuacha uende vyovyote utakavyokwenda, La!Bali kila kitu kipo katika Qadar yake.
Maana ya Kuamini Qadar katika Maisha ya Kila Siku Kwanza, Kwa kujua kuwa fursa, bahati, vipaji na neema zote alizonazo hakuzipata kwa uwezo wake, hanabudi kuvitumia vitu hivi kama amana aliyokabidhiwa na Mola wake. Hanabudi kuitumia amana hii vizuri ili kumuwezesha kufikia lengo la kuumbwa kwake. Muumini wa kweli ana yakini kabisa kuwa atakapo khini amana aliyokabidhiwa na Mola wake, atakuwa ni mwenye kukosa shukrani na atastahiki kuadhibiwa.
﴿ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ﴾
Kisha kwa hakika mtaulizwa siku hiyo juu ya neema (mlizopewa mlizitumiaje)" (102:8)
Pili : Kwa kujua pia kuwa fursa, bahati, vipaji na neema zote zinatoka kwa Allah (s.w), halalami pale atakapokuwa amekadiriwa vitu hivi kwa uchache. Yaani hatalalama na kukata tamaa pale atakapokosa fursa mbali mbali, atakapofikiwa na bahati mbaya, atakapodhikishwa vipaji na neema mbali mbali. Bali ataridhika na alichokadiriwa na Mola wake na pia atamshukuru Mola wake kwa kumpangia amana ndogo anayoiweza kuitunza, kwani huenda kama angelikabidhiwa amana kubwa zaidi ya hiyo aliyonayo, angelishindwa kuitunza na kuwa miongoni mwa waliofeli mtihani.
Tatu : atajitahidi kutumia fursa, bahati, vipaji na neema zote alizotunukiwa na Mola wake kwa kadiri ya uwezo wake, kisha matunda ya jitihada hizo huyategemeza kwa Mola wake. Akipata matunda mazuri yaliyotarajiwa hafurahi kupita kiasi, bali atakuwa na furaha ya kawaida ikiambatana na kumshukuru Mola wake kwa kuzidisha kutenda wema kwa kuswali Sunnat-shukra, kutoa sadaqa, kufunga sunnah, n.k. Akipata matunda dhaifu asiyoyategemea, hatakata tamaa na kusononeka, bali ataridhika na matokeo hayo, na ataona ndio makadirio ya Allah (s.w) na ndiyo yenye manufaa naye. Atashukuru na kusema "Al-hamdulillah 'Alaa kullihaali"
Nne : anapotokewa na misuko suko mbali mbali iliyo nje ya uwezo na jitihada za binaadamu, huwa ni mwenye kutulizana na kusubiri akijua kuwa:
﴿مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٢٢﴾ لِّكَيْلَا تَأْسَوْا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا تَفْرَحُوا بِمَا آتَاكُمْ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ﴾
"Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika kitabu kabla hatujaumba.Kwa yakini hilo ni sahali kwa Allah, Ili msihuzunike sana juu ya kitu kilichokupateni. Na Allah hampendi kila ajivunaye, ajifaharishaye" (57:22-23)
Muumini wa kweli anajua kuwa misiba na misuko suko mbali mbali ni katika qadar ya Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
﴿وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ﴾
"Na tutakutieni katika misuko suko na hofu, njaa, upungufu wa mali na watu na matunda.Na wapashe habari njema wale wanaosubiri. (2:155)
Tano : Mtu anayeamini Qadar ya Allah (s.w), siku zote huyaweka mategemeo yake yote kwa Allah (s.w) ambaye ndiye mdhibiti wa kila jambo. Huendelea kutimiza wajibu wake kwa ujasiri na subira hata anapokuwa katika mazingira magumu kwa kuwa anayakini kuwa:
﴿قُل لَّن يُصِيبَنَا إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَنَا هُوَ مَوْلَانَا وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ﴾
"... Halitatusibu ila alilotuandikia Mwenyezi Mungu, Yeye ni Mola wetu. Basi waislamu na wamtegemee Mwenyezi Mungu tu" (9:51)
SURA YA NNE
LENGO LA MAISHA YA MWANADAMU
Lengo la maisha Ili mwanaadamu aweze kuishi maisha yenye maana hapa ulimwenguni hanabudi kuwa na ujuzi wa yakini juu ya Lengo, Hadhi na Dhima aliyonayo hapa ulimwenguni.Lengo la kuumbwa watu limebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo:
﴿وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴾
Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu. (51:56)
Aya hii inabainisha wazi kuwa watu hawakuletwa hapa ulimwenguni kwa lengo lingine ila kumuabudu Allah (s.w) tu. Kumuabudu Allah (s.w) ni kufanya Ibada kwa ajili ya Allah (s.w). Maana ya Ibada kwa Mnasaba wa Lengo la Kuumbwa Ibada ni neno la Kiarabu linalotokana na neno "Abd" lenye maana ya Mtumwa au mtumishi. Hivyo kumuabudu Allah (s.w) ni kumtumikia Allah (s.w) kitumwa au kumtumikia Allah (s.w) kikweli kweli bila ya kuwa na hiari katika utumishi huo. Kwa maana hii, lengo la kuumbwa mwanaadamu ni kumtumikia Allah (s.w) kwa unyenyekevu bila ya kumtumikia mwingine yeyote kinyume na mwongozo wake.
Kwa hiyo, ili mwanaadamu aishi kulingana na lengo la kuumbwa kwake, hanabudi kumuabudu Allah (s.w) katika kila hatua na kila pumzi ya maisha yake kwa kuzingatia na kufuata maamrisho yake yote na kuacha makatazo yake yote na kuchunga bara bara mipaka yake kwa kila atakalolifanya. Kwa maana nyingine kila kitendo atakachokifanya mtu kwa lengo la kupata radhi ya Allah (s.w) kitakuwa ni Ibada. Kwa mfano kuchuma mali kwa kuzingatia mipaka ya Allah (s.w) ili kupata riziki ya halali na mahitajio muhimu ya maisha ni Ibada. Kula chakula kizuri na halali ili upate afya nzuri itakayokuwezesha kutekeleza majukumu yako ya kifamilia na ya kijamii kwa ujumla ni Ibada Kulala au kujipumzisha ili uweze kupata nguvu mpya ya kiakili na kimwili itakayokuwezesha kutekeleza majukumu yako kwa jamii ni Ibada. Kwa ujumla kila kitendo kizuri cha halali kilichotendwa kwa kuchunga mipaka ya Allah (s.w) kwa nia ya kumuwezesha mtu kuwa katika hali nzuri ya kutekeleza wajibu wake kwa Allah (s.w) na kwa jamii kwa ujumla ni Ibada.
Mtazamo Potofu Juu ya Maana ya Ibada Baadhi ya watu wameifinya ibada ya Allah (s.w) kwa kuinasibisha na matendo maalumu tu kama vile kuswali, kutoa zakat na sadaqa, kufunga, kuhiji, na ibada nyingine za sunnah zilizoambatana na hizi. Kwa mtazamo huu, matendo yaliyo nje ya Swala, Zakat, Swaum,na kadhalika. si ibada. Je, tutakuwa tumefikia lengo la kuumbwa kwetu kwa kutekeleza tu hizi ibada maalumu? Ukichunguza utaona kuwa muda wanaotumia Waislamu katika kutekeleza ibada hizi maalum ni mdogo sana. Kwa mfano muda tunaotumia kuswali swala tano za siku, ibada ambayo Waislamu wanaitekeleza kwa wingi kuliko ibada nyingine yoyote katika nguzo za Uislamu, ni mdogo sana. Jaalia tunachukua dakika 20 kwa kila swala; hivyo tutahitaji dakika 100 tu katika sa 24 za siku. Hii ni na asilimia 7 (7%) tu ya muda wa siku.
Kuhusu Zakat, kiasi kinachotakiwa kutolewa na tajiri aliye na mali iliyofikia nisaabu ni asilimia 2.5 (2.5%) tu. Vile vile tukichukua mfano wa funga ya Ramadhani, tutaona ni muda mfupi tu tunaotumia katika funga. Jalia tunafunga mwezi mzima wenye siku 30 na kila siku tunafunga kwa saa 14 katika nyakati za kiangazi, ambapo mchana ni mrefu kuliko usiku. Kwa mfano huu kiasi tunachofunga ni sawa na asilimia 5 (5%) ya muda wa mwaka.
Kwa mifano hii michache utaona kuwa lengo la kuumbwa kwetu halitatimia kwa kutekeleza tu hizi ibada za Swala, Zakat, Funga, Hija, n.k. bali tunatakiwa tumuabudu Allah (s.w) muda wote wa saa 24 kwa maisha yetu yote. Hivi ndivyo Allah (s.w) anatuamrisha katika aya zifuatazo:
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴾
"Enyi mlioamini! Ingieni katika Uislamu wote, wala msifuate nyayo za shetani, kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri" (2:208)
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ﴾
"Enyi mlioamini! Mcheni-Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha,wala msife isipokuwa mmekwisha kuwa Waislamu kamili." (3:102)
Aidha, Allah (s.w) anatufahamisha kuwa wale wenye akili miongoni mwa wanaadamu ni wale wanaomuamini Allah (s.w) na kumuabudu katika kila kipengele cha maisha yao kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
﴿إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ﴾
Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana ziko hoja (za kuonyesha kuwepo kwa Allah (s.w) kwa wenye akili.Ambao humkumbuka Allah wakiwa wima, wakiwa wamekaa na wakiwa wamelala. Na hufikiri umbile la mbingu na ardhi (tena na tena kisha wanasema), Mola wetu! Hukuviumba hivi bure (pasina lengo).Utukufu ni wako. Basi tuepushe na adhabu ya Moto (3:190-191).
Aya hizi zinatuusia kuwa tumuabudu Allah (s.w) katika shughuli zetu zote tunazozifanya tukiwa tumesimama, tukiwa tumekaa na tukiwa tumelala. Tutahesabika kuwa katika ibada katika kila sekunde ya maisha yetu pale tutakapofanya kila jambo au kila shughuli ya kibinafsi au kijamii kwa kuzingatia mwongozo wa Allah (s.w) na kuchunga bara bara mipaka aliyotuwekea.
Vinginevyo kumuabudu Allah (s.w) kwa baadhi ya wakati, haikubaliki kabisa kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
﴿أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰ أَشَدِّ الْعَذَابِ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ﴾
"...Je! Mnaamini baadhi ya kitabu na kukataa baadhi (yake)? Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya haya katika nyinyi ila fedheha katika maisha ya dunia; na siku ya kiyama watapelekwa katika adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda" (2:85).
14
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
LENGO LA IBADA MAALUMU
Baadhi ya Waislamu, pamoja na kulifinyisha lengo la kuumbwa mwanaadamu kwa kulinasibisha tu na utakelezaji wa Ibada maalumu kama vile Swala, Zakat, Saumu, pia wamelifinyisha lengo la hizi ibada maalumu kuwa ziko pale ili:
(i) Kutupatia thawabu na kutuingiza Peponi tu na hazina mahusiano yoyote na maisha ya kila siku ya kibinafsi na kijamii.
(ii) Kuwa kifutio cha madhambi, hivyo mtu hufanya maovu kwa furaha, pasina hofu yoyote.
(iii) Kumfurahisha na kumfaidisha Mwenyezi Mungu. Huu nao ni mtazamo finyu wa hizi ibada maalumu kwa sababu.
Kwanza : Allah (s.w) mara tu baada ya kutufahamisha lengo la kuwaumba Majini na Watu, ametoa tahadhari kuwa wasije Majini na Watu wakadhania kuwa Allah (s.w) amewaumba kwa lengo hilo ili wamnufaishe, kwani yeye si muhitaji; bali viumbe ndio wanaomuhitajia kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
﴿وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾ مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ ﴿٥٧﴾ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ﴾
"Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu.Sitaki kwao riziki wala sitaki wanilishe.Kwa yakini Mwenyezi Mungu ndiye mtoaji wa riziki, Mwenye nguvu, madhubuti" (51:56-58)
Pili : Allah (s.w), pamoja na kutuamrisha kutekeleza hizi ibada maalumu, ametufahamisha vile vile lengo la kila ibada. Kwa mfano, kuhusu lengo la Swala tunafahamishwa:
﴿اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَلَذِكْرُ اللَّـهِ أَكْبَرُ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ﴾
"Bila shaka Swala (ikiswaliwa vilivyo) humzuilia (mwenye kuswali na) mambo machafu na maovu" (29:45).
Lengo la utoaji wa Zakat na Sadaqat linabainishwa kuwa ni kumtakasa mtoaji na makosa yanayosababishwa na umilikaji wa mali:
﴿خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴾
"... Chukua Sadaqa katika mali zao uwatakase kwazo na kuwataja kwa uzuri (mbele yangu) na uwaombee dua..." (9:103).
Lengo la Swaumu nalo linabainishwa kuwa ni kumfanya mfungaji awe mcha-Mungu:
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ﴾
"Enyi Mlioamini! Mmeamrishwa kufunga kama walivyoamrishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha-Mwenyezi Mungu (2:183).
Mcha Mungu ni yule anayeishi kwa kufuata mwongozo wa Allah (s.w) na kuchunga mipaka yake katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake.
Ibada ya Hija, pamoja na kumuandaa Al-Hajj kuwa Mcha- Mungu, inamtayarisha pia kuwa tayari kuipigania dini ya Allah (s.w) kwa mali yake na nafsi yake. Hadhi ya Waumini Hapa Ulimwenguni Hadhi tarajiwa ya mwanaadamu hapa ulimwenguni inabainika vizuri kwa kurejea kwa makini aya zifuatazo:
﴿وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾ وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣١﴾ قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٣٢﴾ قَالَ يَا آدَمُ أَنبِئْهُم بِأَسْمَائِهِمْ فَلَمَّا أَنبَأَهُم بِأَسْمَائِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٣٣﴾ وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ﴾
"(Wakumbushe) wakati Mola wako alipowaambia Malaika,Mimi nitajaalia khalifa katika ardhi.Wakasema (Malaika) utaweka humo watakaofanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutukuza kwa sifa zako na kukutaja kwa utakatifu wako? Akasema (Mwenyezi Mungu)"Hakika mimi najua msiyo yajua" "Na Mwenyezi Mungu akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema, "Niambieni majina ya vitu hivi ikiwa mnasema kweli."Wakasema (Malaika): "Utakatifu ni wako! Hatuna ilimu isipokuwa ile uliyotufundisha; bila shaka wewe ndiye Mjuzi na ndiye Mwenye Hekima. Akasema (Mwenyezi Mungu),"Ewe Adam waambie majina yake" Alipowaambia majina yake alisema (Mwenyezi Mungu): "Sikukwambieni kwamba mimi ninajua siri za mbinguni na za ardhi; tena najua mnayoyadhihirisha na mliyokuwa mnayaficha?" Na (wakumbushe watu khabari hii): Tulipowaambia Malaika, "Msujudieni Adam" (yaani muadhimisheni kwa ile ilimu yake aliyopewa) Wakamsujudia wote isipokuwa Ibilis; akakataa na akajivuna; na (tokea hapo) alikuwa katika makafiri" (2:30-34).
Tunajifunza kutokana na aya hizi kuwa mwanaadamu amekusudiwa kuwa Khalifa wa Mwenyezi Mungu hapa ulimwenguni. Ukhalifa ni cheo chenye hadhi kubwa mbele ya Allah (s.w). Kuamrishwa kwa malaika kumsujudia Adam ni dalili tosha kuwa mwanaadamu anapochukua nafasi yake ya Ukhalifa anakuwa na hadhi kubwa mbele ya Allah (s.w) kuliko ile ya Malaika. Pamoja na Adamu kufundishwa majina ya vitu vyote aliahidiwa kuletewa mwongozo utakaomuelekeza kufuata njia sahihi ya maisha.
﴿قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٨﴾ وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾
Tukasema shukeni humo nyote, na kama ukikufikieni mwongozo utokao Kwangu basi watakaofuata mwongozo huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. Lakini wenye kukufuru na kuyakadhibisha maneno yetu, hao ndio watokaokuwa watu wa Motoni humo watakaa milele." (2:38-39)
Nyenzo kuu inayomuwezesha mwanaadamu kuwa Khalifa ni elimu ya mazingira aliyotunukiwa na Mola wake na mwongozo alioshushiwa kutoka kwake. Majina ya vitu vyote inaashiria taaluma ya fani zote anazohitajia mwanaadamu katika kuendesha maisha yake yote ya kibinafsi na kijamii. Khalifa ni kiongozi kwa niaba ya Allah (s.w) hapa ulimwenguni.Yaani, yule anayesimamisha Ufalme wa Allah (s.w) au Dola ya Kiislamu katika jamii kwa kuhakikisha kuwa sharia za Allah (s.w) ndizo zinazotawala katika kuendesha kila kipengele cha maisha ya jamii ili kusimamisha uadilifu katika jamii hiyo. Jamii itaweza kuishi kwa furaha na amani ya kweli pale tu patakapokuwa na utawala unaosimamia haki na uadilifu.
Wanaostahiki Ukhalifa Pamoja na mwanaadamu kukusudiwa kuwa Khalifa katika ardhi, si kila mtu atakuwa Khalifa. Ahadi ya ukhalifa imetolewa kwa watu maalum kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
﴿وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴾
"Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na kufanya vitendo vizuri kuwa atawafanya Makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya Makhalifa wale waliokuwako kabla yao, na kwa yakini, Atawasimamishia dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia amani baada ya hofu yao. Wawe wananiabudu, hawanishirikishi na chochote. Na watakao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wavunjao amri zetu (24:55)
Tunajifunza katika aya hii kuwa wanaostahiki kuwa Makhalifa wa Allah (s.w) ni waumini watendaji. Waumini watendaji ni wale waumini wa kweli kama wanavyobainishwa katika aya zifuatazo:
﴿إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ ﴿٢﴾ الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا لَّهُمْ دَرَجَاتٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ﴾
"Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa Aya zake huwazidishia imani, na wakamtegemea Mola wao tu basi.Ambao wanasimamisha swala na wanatoa katika yale tuliyowapa.Hao ndio wanaoamini kweli kweli.Wao wana vyeo (vikubwa) kwa Mola wao, na msamaha na riziki bora (kabisa huko Akhera) (8:2-4)
﴿إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ﴾
Wenye kuamini kweli kweli ni wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; kisha wakawa si wenye shaka, na wakaipigania dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao.Hao ndio wenye kuamini kweli. (49:15)
Pia kutokana na aya hii ya (24:55) tunajifunza kuwa ishara itakayotuonyesha kuwa Ukhalifa umesimama katika ardhi ni pale sharia za Kiislamu zitakapo tawala katika ardhi au pale dola ya Kiislam itakapokuwa imesimamishwa katika jamii kama ilivyosimamishwa wakati wa Mtume(s.a.w.w).
Dhima ya Waumini katika Jamii Dhima ya kwanza kwa waumini ni kujielimisha au kusoma kwa ajili ya Allah (s.w). Hii ndiyo amri ya kwanza ya Allah (s.w) juu ya waumini kama tulivyoona katika sura ya kwanza ya juzuu hii. Pia tumeona kuwa elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Qur-an kwa sababu ndiyo nyezo kuu inayowawezesha waumini kumuabudu Mola wao ipasavyo na kusimamisha Uislamu katika jamii. Pia tumeona kuwa elimu tuliyoamrishwa kuitafuta ili tuwe makhalifa wa Allah (s.w) katika jamii ni fani zote za elimu zinazohitajika katika kuendesha maisha ya jamii (Qur-an, 2:30- 31) pamoja na elimu ya mwongozo (maarifa ya Uislamu) kutoka kwa Allah (s.w) kupitia kwa Mitume wake na vitabu vyake (Rejea Qur-an, 2:38-39).
Dhima ya pili kwa waumini ni kumcha Allah (s.w) ipasavyo kama anavyotuamrisha:
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ﴾
"Enyi Mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha, wala msife isipokuwa mmekwishakuwa Waislamu kamili" (3:102)
Kumcha Allah (s.w) ni kumtii Allah na kuchunga bara bara mipaka aliyotuwekea katika kuendea njia ya maisha yetu ya kila siku. Aya hii inawaamrisha waumini kufanya jitihada za makusudi za kumuabudu Allah (s.w) katika kila kipengele cha maisha na kudumu na ibada hiyo mpaka mwisho wa maisha yao ya hapa duniani.
Dhima ya tatu kwa waumini ni kulingania kheri au kuufikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu ambao haujawafikia au kuwakumbusha wautekeleze wale ambao umeshawafikia.Hapana Mtume yoyote atakayeletwa baada ya mtume Muhammad(s.a.w.w). Hivyo dhima ya kulingania Uislamu iko juu ya waumini wote. Kufundisha na kulingania uislamu katika jamii ni jambo muhimu mno kwa waumini kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
﴿وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّـهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴾
"Na ni nani asemaye kauli bora zaidi kuliko aitaye (watu) kwa (dini ya) Mwenye zi Mungu na mwenyewe akafanya vitendo vizuri (akawa Muislamu) na husema (kwa maneno yake na vitendo vyake); "Hakika mimi ni miongoni mwa waislamu." (41:33).
Tunajifunza kuwa baada ya Muumini kuufahamu Uislamu vilivyo na kujipamba nao katika maisha yake ya kila siku, hana budi kuulingania na kuufundisha katika jamii. Pia tunajifunza kutokana na aya hii kuwa kazi ya kulingania uislamu na kuufundisha ni bora kuliko kazi nyingine. Hii ndio kazi ya Mitume wa Allah (s.w). Dhima ya nne ya waumini ni kushikamana pamoja. Dhima hii imewekwa bayana katika Qur-an:
﴿ وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا﴾
"Na shikamaneni kwa kamba (dini) ya Mwenyezi Mungu nyote, wala msifarikiane" (3:103).
﴿وَاعْتَصِمُوا بِاللَّـهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ ﴾
Na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa.
﴿إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُم بُنْيَانٌ مَّرْصُوصٌ﴾
"Kwa yakini Mwenyezi Mungu anawapenda w ale wanaopigana katika njia yake safu safu kama kwamba wao ni jengo lililokamatana barabara." (61:4)
Mshikamano wa Waumini umeamrishwa juu yetu na Allah (s.w) kwa sababu ndio msingi wa nguvu za waumini zitakazowawezesha kuwashinda maadui zao na kuuwezesha Uislamu kusimama katika jamii. Mshikamano wa waumini chini ya Uongozi wa Mtume(s.a.w.w) ni mfano wa kuigwa uliowazi:
﴿مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا﴾
"Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama kwa kurukuu na kusujudu (pamoja), wakitafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi (yake). Alama zao zi katika nyuso zao,kwa taathira, (athari) ya kusujudu.Huu ndio mfano wao katika Taurati.Na mfano wao katika Injili (umetajwa hivi.Kuwa (wao) ni kama mmea uliotoa matawi yake; kisha (matawi hayo) yakautia nguvu, ukawa mnene ukasimama sawasawa juu ya kigogo chake, ukawafurahisha walioupanda; ili awakasirishe makafiri kwa ajili yao. Mwenyezi Mungu amewaahidi walioamini na kutenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa. (48:29).
Dhima ya tano ya waumini ni kuamrisha mema kama Allah (s.w) anavyotuamrisha:
﴿وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴾
"Na wawepo katika nyinyi watu wanaolingania kheri (Uislamu) na wanaoamrisha mema na wanaokataza maovu.Na hao ndio watakaotengenekewa" (3:104)
Waumini hata kama hawajafikia hatua ya kusimamisha dola ya Kiislamu, hawana budi kufanya mambo mazuri na kutoa huduma mbali mbali kama vile elimu, afya, ujenzi wa barabara, utunzaji wa mazingira, n.k. zitakazopelekea kuboresha maisha ya jamii kwa ujumla. Pia waislamu wanawajibika kwa mshikamano wao kuweka mazingira ya kufanya mambo mazuri ya kuistawisha jamii kiasi cha kuwafanya watu wengine, kwa haja za kibinaadamu, waunge mkono. Vile vile waislamu kwa umoja wao, wanawajibika kujenga mazingira yatakayowalazimisha watu kufanya mema, hata kama dola ya Kiislamu haijasismama.
Dhima ya sita kwa waumini ni kutakataza maovu yasitendeke katika jamii (Qur-an 3:104).
Hata kama dola ya Kiislamu haijasimama katika jamii waumini hawana budi kujiepusha na maovu yote hata yale yaliyozoeleka katika jamii hiyo. Kisha kwa umoja wao waumini wanawajibika kuweka mazingira ambayo wafanya maovu wataona haya. Pia waumini wanawajibika kuweka mikakati ya makusudi ya kuzuia maovu yasifanyike katika jamii, hata kama dola ya Kiislamu haijasimama. Waislamu watakapofikia hatua ya kukaa kimya na kuacha maovu yakafanywa kwa wasaa katika jamii, wajue kuwa hata wao hawatasalimika na adhabu ya Allah (s.w) itokanayo na maovu hayo hata kama hawakushiriki kuyafanya.
﴿وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴾
"Na iogopeni adhabu (ya Mwenyezi Mungu ya hapa duniani) ambayo haitawasibu peke yao wale waliodhulumu nafsi zao miongoni mwenu (bali itawasibu hata walionyamaza wasiwakataze, bali na wengineo pia); na jueni ya kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu".(8:25).
Katika kusisitiza umuhimu wa kuamrisha mema na na kukataza maovu Mtume Muhammad(s.a.w.w) anatuasa katika Hadithi zifuatazo:
Abu Said Al-Khudhri (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:
"Yeyote miongoni mwenu atakayeona jambo ovu na aliondoe kwa mkono wake, kama hawezi na aliondoe kwa ulimi; na kama hawezi kuliondoa kwa ulimi na achukie moyoni mwake; na huku kuchukia kwa moyo tu ni kiwango cha chini cha imani." (Muslim)
Hudhaifah (r.a) ameeleza: Nimemsikia Mtume wa Allah amesema: "Naapa kwa yule ambaye mkononi mwake yako maisha yangu, mtaamrisha mema na mtakataza maovu, vinginevyo, ni hivi karibuni tu adhabu ya Mwenyezi Mungu itakuwa juu yenu.Kisha mtamuomba Mwenyezi Mungu, lakini hamtajibiwa." Jabir bin Abdullah (r.a) ameeleza:
Nimemsikia Mtume wa Allah akisema: "Hapana mtu ambaye anafanya maovu mbele ya watu ambao wana uwezo wa kumzuia, lakini wasijali kufanya hivyo, ila Mwenyezi Mungu atawaadhibu wote hapa duniani kabla hawajafa." (Abu Daud, Ibn Majah).
Dhima ya saba ya waumini ni kufanya juhudi za makusudi au kuingia katika Jihadi kuhakikisha kuwa Dini ya Allah (s.w) inasimama katika jamii. Dini ya Allah (s.w) itasimama pale sheria za Allah zitakapokuwa ndizo zinazotawala kila kipengele cha maisha ya jamii. Kuusimamisha Uislamu katika jamii ni faradhi kwa Waislamu kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
﴿وَجَاهِدُوا فِي اللَّـهِ حَقَّ جِهَادِهِ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَـٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ﴾
"Na ipiganieni dini ya Mwenyezi Mungu kama inavyostahiki (kupiganiwa).Yeye amekuchagueni (muwe uma ulio bora) wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika dini. (Nayo dini hii) ni mila ya baba yenu Ibrahimu; Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu (katika vitabu vya zamani) huko; na katika (Qur-an) hii pia mumeitwa jina hilo); ili awe Mtume shahidi juu yenu na nyinyi muwe mashahidi juu ya watu waliotangulia..." (22:78)
Aya hii inatuweka wazi kuwa dhima hii ya kusimamisha Uislamu, si kwa Waislamu wa Umma huu wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) bali ni dhima kwa waislamu wa zama zote. Pia tunajifunza katika Qur-an kuwa Dhima aliyokuwa nayo Mtume(s.a.w) na kwa hiyo dhima ya wafuasi wa kweli wa Mtume(s.a.w.w) ni kuutawalisha Uislamu katika jamii kama inavyobainishwa katika aya zifuatazo:
﴿هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴾
Yeye ndiye aliyemleta Mtume wake kwa uongofu na dini ya haki ili aijaalie kushinda) dini zote; ijapokuwa watachukia washirikina. (9:33, 61:9)
﴿هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا﴾
"Yeye (Allah) ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na dini ya haki,ili aijaalie kushinda dini zote. Na Mwenyezi Mungu atosha kuwa shahidi" (48:28)
Mwenyezi Mungu ni shahidi kuwa Mtume(s.a.w.w) pamoja na Waislamu waliokuwa pamoja naye, walisimamisha Dola ya Kiislamu yenye nguvu kuliko dola zote za Kitwaaghuti zilizokuwepo siku zile. Pia ni katika utaratibu wa Mwenyezi Mungu kuwa wakati wowote Waislamu watakapo simama kidete kutekeleze amri yake ya kusimamisha dini yake, atawanusuru na kuwapa ushindi.
Dhima ya nane ya waumini ni kuihami dini ya Allah (s.w) isihujumiwe baada ya kusimama katika jamii. Waislamu wanaamrishwa na Mola wao waingie vitani kuuhami Uislamu kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
﴿ أَلَا تُقَاتِلُونَ قَوْمًا نَّكَثُوا أَيْمَانَهُمْ وَهَمُّوا بِإِخْرَاجِ الرَّسُولِ وَهُم بَدَءُوكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ أَتَخْشَوْنَهُمْ فَاللَّـهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَوْهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٣﴾قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّـهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ ﴾
"Je, hamtapigana na watu waliovunja ahadi zao na wakafunga nia ya kumfukuza Mtume, nao ndio (pia) waliokuanzeni mara ya kwanza? Je,mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumuogope, ikiwa nyinyi mumeamini." piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awafedheheshe na akunusuruni juu yao na avipoze vifua vya Waumini (wafurahi). (9:13-14)
﴿أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَا رَسُولِهِ وَلَا الْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴾
Je, mnadhani kuwa mtaachwa, na hali Mwenyezi Mungu hakuwabainisha wale waliopigania dini miongoni mwenu na wasiwafanye rafiki wa ndani isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyafanya" (9:16)
﴿ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ ﴿٣٨﴾ إِلَّا تَنفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئًا وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴾
"Enyi mlioamini! Mnanini mnapoambiwa 'Nendeni (kupigana) kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu' mnajitia uzito katika ardhi? Je, mumekuwa radhi na maisha ya dunia kuliko ya akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kwa (mkabala wa maisha ya) akhera ni kidogo tu.Kama hamtakwenda atakuadhibuni kwa adhabu iumizayo na atawaleta watu wengine badala yenu, wala hamtamdhuru (Mwenyezi Mungu) chochote (mkitopigania dini yake); na Mwenyezi Mungu ni muweza juu ya kila kitu." (9:38-39)
﴿انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴾
Nendeni (vitani) mkiwa wepesi na mkiwa wazito (wazima au wagonjwa); na piganieni dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu.Haya ni bora kwenu, ikiwa mnajua." (9:41)
Kupigania Dini ya Allah (s.w) ili isimame katika jamii na kuihami isiporomoshwe baada ya kusimama kwake ni Dhima kubwa kwa Waislamu na ni amali bora kuliko amali nyingine yoyote ile atakayoifanya Muumini.Katika kuonyesha ubora wa amali hii ya jihad, Allah (s.w) ameifananisha na biashara yenye kuleta faida kubwa isiyo na mfano wake kwa maisha ya hapa duniani na huko akhera kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿١٠﴾ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١١﴾ يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾ وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴾
"Enyi mlioamini! Je! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo? (Biashara yenyewe ni hii): Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na piganieni dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu, haya ni bora kwenu; ikiwa mnajua.(Mkifanya haya) .atakusameheni dhambi zenu na atakuingizeni katika mabustani yapitayo mito mbele yake na (atakupeni) maskani mazuri mazuri katika Bustani za milele, huku ndiko kufuzu kukubwa. Na (atakupeni) kingine mnachokipenda: Nayo ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu na ushindi ulio karibu! Na wapashe habari njema waumini" (61:10-13)
﴿ إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّـهِ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴾
Mwenyezi Mungu amenunua kwa waumini nafsi zao na mali zao, ili na yeye awalipe Pepo. Wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, wanaua na wanauawa. Hii ndiyo ahadi aliyojilazimisha (Mwenyezi Mungu) katika Taurati na Injili na Qur-ani. Na ni nani atekelezaye zaidi ahadi yake kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyofanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.(9:111).
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa kazi ya kupigania Dini ya Mwenyezi Mungu (Jihadi) imefanywa ni biashara mja anayofanya na Mola wake. Mtaji wa biashara hii ni kutoa mali na nafsi (nguvu kazi na ikibidi kuitoa roho muhanga). Faida ya biashara hii ni:
1. Kuokolewa na adhabu iumizayo hapa duniani chini ya Uongozi wa Twaaghut na huko akhera.
2. Kusamehewa dhambi.
3. Kuingizwa peponi na kufaidika na starehe zake.
4. Kupata nusra ya Allah (s.w) hapa ulimwenguni.
5. Kumshinda adui na kuweza kusimamisha dini ya Allah (s.w) katika jamii na kuleta amani ya kweli ya kudumu.
Umuhimu wa Kusimamisha Uislamu Katika Jamii
﴿إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ﴾
"Bila shaka dini (ya haki) mbele ya Allah ni Uislamu" (3:19)
﴿هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴾
"Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa Uongofu na dini ya haki ili aijaalie kushinda dini zote ijapokuwa washirikina watachukia." (61:9)
Imekuwa muhimu kuutawalisha Uislamu katika jamii kwa sababu kubwa mbili zifuatazo:
Kwanza : bila ya Uislamu kushika hatamu katika kuendesha shughuli zote za maisha ya jamii katika siasa, uchumi, utamaduni na katika kila kipengele kingine muhimu cha maisha ya jamii; Waislamu kamwe hawataweza kumuabudu Mola wao katika kila kipengele cha maisha. Waumini wa kweli ni wale wanaoufuata Uislamu wote katika kila jambo la kibinafsi au la kijamii wanalolifanya katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Aidha waumini wa kweli huishi kwa kuzingatia wito wa Allah (s.w) ufuatao:
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴾
"Enyi mlioamini! Ingieni katika hukumu zote za Uislamu, wala msifuate nyayo za shetani kwa hakika yeye kweni ni adui dhahiri" (2:208)
﴿وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا﴾
"Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu (upotevu) ulio wazi (kabisa)." (33:36)
Kwa mazingatio ya aya hizi, waislamu wanalazimika kufanya jitihada za makusudi, kwa kutumia mali na nafsi zao, kuhakikisha kuwa sheria za Kiislamu zinatumika katika kila kipengele cha maisha ya jamii ili kuweka mazingira ya kufuata hukumu zote za Uislamu katika siasa, uchumi, utamaduni; na kadhalika.
Tukumbuke kuwa, iwapo Waislamu tutabweteka na kuridhika kuishi maisha ya "mseto" ya kumuabudu Allah (s.w) kwa kuswali; kutoa Zaka, Kufunga, n.k. na kumuasi Allah (s.w) kwa kuridhia kufuata mfumo haramu wa siasa, uchumi; utamaduni,na kadhalika, tutastahiki adhabu kubwa ya kuwa dhalili katika jamii na kuwa na marejeo mabaya huko akhera kama tunavyokumbushwa:
﴿أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰ أَشَدِّ الْعَذَابِ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ﴾
"...Je! Mnaamini baadhi ya kitabu na kukataa baadhi (yake)? Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya haya katika nyinyi ila fedheha katika maisha ya dunia; na siku ya kiyama watapelekwa katika adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda." (2:85)
Pili : bila ya Uislam kushika hatamu katika jamii,ni muhali kupatikana furaha na amani ya kweli. Waislamu wanawajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu ili kuhakikisha kuwa panakuwa na maendeleo ya kweli katika jamii, kila mtu anapata haki zake na panakuwa na mazingira ya amani kwa ujumla. Allah (s.w) amewaleta Mitume na Vitabu ili kuwaongoza watu wasimamishe uadilifu katika jamii kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
﴿لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ﴾
"Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukaviteremsha vitabu na hukumu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu..." (57:25)
Kwa mujibu wa aya hii tunajifunza kuwa ni muhali kupatikana furaha na amani ya kweli katika jamii inayoongozwa kinyume na muongozo wa Mitume na Vitabu vya Mwenyezi Mungu, ambamo ndimo Uadilifu unamopatikana. Furaha na amani ya kweli katika jamii hupatikana tu pale maongozi ya jamii hiyo yatakapokwenda sambamba na maongozi ya Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
﴿اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾
"Mwenyezi Mungu ni mlinzi (kiongozi) wa wale walioamini.Huwatoa katika giza na kuwaingiza katika nuru.Lakini waliokufuru, walinzi (viongozi) wao ni matwaghut. Huwatoa katika nuru na kuwaingiza katika giza. Hao ndio watu wa motoni, humo watakaa milele" (2:257)
Katika aya hii Giza, huashiria maisha yaliyogubikwa na dhuluma za kila aina, maisha ya vita na mauaji, maisha ya ubabe, maisha ya uonevu, udhalilishaji na ukandamizaji wa kila namna, maisha ya samaki wakubwa kuwameza wadogo, maisha ya ujanja ujanja na utapeli, maisha ya maangamizi ya kila namna. Nuru katika aya hii inaashiria maisha ya uadilifu, upendo na kujaliana maisha ya kila mtu kupata haki yake inayomstahiki, maisha ya kuhurumiana na kusaidiana, maisha ya furaha na amani.
Matwaghut, katika Qur-an ni viongozi wa jamii wanaoongoza watu kinyume na mwongozo wa Mwenyezi Mungu kama ulivyobainishwa na Mitume wake na Vitabu vyake. Wanaoongoza kwa kuchupa mipaka na taratibu za Allah (s.w). Wanawaongoza watu kwa sheria walizotunga binaadamu zinazopingana na sheria za Allah (s.w).
Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa; ambapo sera ya Allah (s.w) ni kuwatoa watu kwenye giza (maisha ya dhiki na mashaka) na kuwapeleka kwenye nuru (maisha ya furaha na amani) sera ya matwaghut ni kuwatoa kwenye nuru na kuwaingiza katika Giza. Hivyo Waislamu hawanabudi kushika hatamu ya maongozi ya jamii,ili kuinusuru jamii isiangamizwe na matwaghuti na kutumbukizwa kwenye giza.
ZOEZI - 4
1. Nukuu aya ya Qur-an au tafsiri yake inayotufahamisha lengo la kuletwa binaadamu hapa ulimwenguni.
2. "(Wakumbushe) wakati Mola wako alipowaambia Malaika, "Mimi nitaleta khalifa katika ardhi..." (2:30)
Kwa mnasaba wa aya hii khalifa ni...............................................
3. "Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na kufanya vitendo vizuri kuwa atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wale waliokuweko kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia dini yao aliyowapendelea na atawabadilishia amani baada ya hofu yao. Wawe wananiabudu, hawanishirikishi na chochote..." (24:55) Kutokana na aya hii tunajifunza yafuatayo:
(i).........................................................................................
(ii)........................................................................................
(iii)......................................................................................
(iv)......................................................................................
4. Waumini wa kweli katika jamii wanadhima ya kufanya yafuatayo:
(i)........................................................................................
(ii)......................................................................................
(iii).....................................................................................
5. Kwanini Waislamu wanalazimika kuusimamisha na kuuhami Uislamu katika jamii?
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini
YALIYOMO
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 1
UTANGULIZI WA MTUMISHI WA SITE 1
SURA YA KWANZA 2
MAANA YA ELIMU 2
NAFASI YA ELIMU NA WENYE ELIMU KATIKA UISLAMU 2
KUTAFUTA ELIMU 3
KWANINI UISLAMU UMEIPA ELIMU NAFASI YA KWANZA? 3
CHANZO CHA ELIMU 5
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 12
KATIKA UISLAMU HAKUNA ELIMU YA DINI NA DUNIA 12
ELIMU YA DUNIA 12
MGAWANYO WA ELIMU KATIKA FARADH 15
ELIMU YA MAARIFA YA UISLAMU 15
ELIMU YENYE MANUFAA 16
ZOEZI 17
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 18
SURA YA PILI 18
MAANA YA DINI KWA MTAZAMO WA MAKAFIRI 18
MAANA YA DINI KWA MTAZAMO WA UISLAMU 18
ZOEZI 29
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 30
SURA YA TATU 30
IMANI YA KIISLAMU 30
MAANA YA IMANI IMANI 30
NANI MUUMINI? 30
ZOEZI 37
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 38
NGUZO ZA IMANI 38
KUMUAMINI ALLAH ( S.W ) 39
NAFSI YA MWANAADAMU 42
(I) CHANZO NA MWISHO WA UHAI WA MWANAADAMU 42
(II) ASILI YA MWANAADAMU 42
(III) KUUMBWA WANAUME NA WANAWAKE 42
(IV) TOFAUTI YA LUGHA, RANGI, MAKABILA, MATAIFA 43
(V) UMBO NA SURA 43
(VI) CHAKULA CHA MWANAADAMU 43
(VII) UFANYAJI KAZI WA VIUNGO VYA NDANI NA NJE YA MWILI WA MWANAADAMU 44
(VIII) USINGIZI 44
(IX) MWANADAMU KUMKUMBUKA ALLAH (S.W) WAKATI WA MATATIZO 44
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 54
MAFUNDISHO YA MITUME 54
(I) NUHU(A.S) 54
(II) HUD(A.S) 54
(III) SALIH(A.S) 54
(IV) SHU'AYB(A.S) 55
(V) ISA(A.S) 55
(VI) MUHAMMAD (S.A.W.W) 55
(i)TAWHIID 55
(II)LENGO 55
(III) KUBASHIRIA 56
(IV) KUHOFISHA 56
MAJINA 99 YA MWENYE EZI MUNGU 57
UFAFANUZI WA SIFA ZA ALLAH (S.W) 60
(A) SIFA AU MAJINA YA ALLAH YANAYOONESHA KUWEPO KWAKE NA UMOJA WAKE, UUNGU WAKE NA UUMBAJI WAKE 61
(B) MAJINA YA ALLAH (S.W) YANAYOONESHA UJUZI WAKE USIO KIKOMO 63
(C) MAJINA YA ALLAH YANAYOONESHA UPWEKE WA UTAWALA, NGUVU NA UTUKUFU WAKE 64
(D) SIFA ZA ALLAH (S.W) ZINAZOONESHA UADILIFU WAKE USIO NA MIPAKA 68
(E) SIFA ZA ALLAH (S.W) ZINAZOONESHA UREHEMEVU, USAMEMEHEVU NA UPENDO WAKE KWA WAJA WAKE 69
ZOEZI 74
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 75
KUAMINI MALAIKA WA ALLAH (S.W.) 75
JE MALAIKA WANAISHI WAPI? 75
KWANINI HATUWAONI MALAIKA? 75
SIFA ZA MALAIKA 77
WANA ELIMU YA KUTOSHA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO 77
HAWANA JINSIA 78
NI VIUMBE WENYE MBAWA 78
HUWEZA KUJIMITHILISHA UMBILE LA MWANADAMU 78
LENGO LA KUUMBWA MALAIKA 78
KAZI ZA MALAIKA 78
MALAIKA PIA HUSHUGHULIKIA MAMBO YA WANADAMU KATIKA MAISHA YA DUNIANI NA AKHERA 78
(1) KULETA UJUMBE KWA WANAADAMU KUTOKA KWA ALLAH (SW) 79
(2) KUANDIKA AMALI ZA WANAADAMU NJEMA NA MBAYA 79
(3) KUWALINDA WANAADAMU 79
(4) KUWAOMBEA WAUMINI MSAMAHA KWA ALLAH (S.W.) 80
(5) KUWASAIDIA WAUMINI VITANI KATIKA KUPAMBANA NA MADHALIMU 80
(6) KUWAANGAMIZA WATU WAOVU WALIOPINDUKIA MIPAKA 80
(7) KUTOA ROHO ZA WATU 81
(8) KUWALIWAZA NA KUWAKARIBISHA WATU WEMA PEPONI KABLA YA KUTOLEWA ROHO 81
(9) KUWAADHIBU WATU WAOVU MOTONI 81
KUAMINI VITABU VYA ALLAH (S.W) 82
KUAMINI MITUME WA ALLAH (S.W) 86
LENGO LA KULETWA MITUME WA ALLAH (S.W) 87
MWISHO WA UTUME 87
ZOEZI 93
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 94
KUAMINI SIKU YA MALIPO 94
HOJA ZA WAPINZANI WA SIKU YA MWISHO 98
UDHAIFU WA HOJA 98
1. WALE WALIOFANYA WEMA HAPA DUNIANI BILA YA KUPATA UJIRA UNAOSTAHIKI, WALIPWE FADHILA YA WEMA WAO 99
2. WALE WALIODHULUMU HAKI ZA WATU HAPA DUNIANI, WARUDISHE HAKI ZA WENYEWE MBELE YA HAKIMU WA MAHAKIMU 99
3. WALE WABABE WALIOFANYA UOVU ULIOKITHIRI HAPA DUNIANI 99
4. WATU WAULIZWE VIPI WALISHUKURU JUU YA NEEMA NA VIPAJI MBALI MBALI WALIVYOTUNUKIWA NA MUUMBA WAO 100
5. WABAINIKE NI AKINA NANI WALIOFUATA NJIA SAHIHI YA MAISHA, WAISLAMU AU MAKAFIRI? 100
2. KUFUFUKA NDEGE WA NABII IBRAHIMU(A.S) 100
3. KUAMKA AS-HABUL-KAHF 101
4. KUFUFUKA KWA WATU WA NABII MUSSA(A.S) 101
5. KUFUFUKA KWA YULE MTU ALIYEULIWA KWA DHULUMA WAKATI WA NABII MUSSA(A.S) 101
6. NABII ISSA(A.S) ALIFUFUA WAFU KWA IDHINI YA ALLAH (S.W) 101
MAZINGIRA YA MAISHA YA AKHERA 102
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 108
(iv) SIKU YA KUFUFULIWA 108
(V) SIKU YA HUKUMU 110
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 119
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 127
MAISHA YA MOTONI 127
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 133
MAANANA YA KUAMINI SIKU YA MALIPO KATIKA MAISHA YA KILA SIKU 133
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 139
KUAMINI QADAR YA ALLA 139
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 143
SUALA LA UONGOFU 143
SURA YA NNE 146
LENGO LA MAISHA YA MWANADAMU 146
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU 149
LENGO LA IBADA MAALUMU 149
ZOEZI - 4 160