TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA Juzuu 21
Mwandishi: Sheikh Muhammad Jawad MughniyyaQurani tukufu
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
IMEANDIKWA NA: SHEIKH MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYA
IMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HASAN MWALUPA
IMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED
IMEPANGWA KATIKA KOMPYUTA NA: UKHT PILI RAJABU
UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI
Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London.
Kama lilivyo jina la Tafsiri ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo.
Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyo kujipatia wasomaji wengi sana.
Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana kwenda na wakati.
Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung'ang'ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo, hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea. Hiyo ilimsaidia sana hata kuweza kutoa kitabu kitwacho Al-Fiqh a'laa madhaahabil-khamsah (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka kwa lugha ya kiswahili hivi karibuni Inshaallah).
Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.
Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasayansi kama kina Enstein, wasanii kama Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa.
Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.
Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji.
Mwisho: Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji.
MAKOSA YA CHAPA
Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa, Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa.
Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya msahafu mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswutu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146), Imeandikwa La Ya'alamuun, (hawajui) badala ya Ya'alamuun (wanajua). Mfano wa makosa haya hausameheki.
Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa Fawqahum ila yawmil qiyama badala ya Fawqahum yawamal qiyama. Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile.
Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu Jabal amil 'Makosa ya chapa.'
Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: Hatta idha balagha arbai' na sanah badala ya: Hattaidha balagha ashuddahu arbai ' na sanah"
Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakayoyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefungua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana.
Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: "Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa.” Kama kwamba hakuna kitu chochote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.
Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin(a.s) :"Watu wote ni wapungufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu." Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubalia yale niliyoyapatia na kunisamehe niliyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazi chake, ziwashukie rehema na amani (Amin).
MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH
1
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
Mwendelezo wa Sura Ya Thelathini Na Tatu: Surat Al-Ahzab.
وَمَن يَقْنُتْ مِنكُنَّ لِلَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتَعْمَلْ صَالِحًا نُّؤْتِهَا أَجْرَهَا مَرَّتَيْنِ وَأَعْتَدْنَا لَهَا رِزْقًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾
31. Na yeyote katika nyinyi atakayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akatenda wema, tutampa malipo yake mara mbili, na tutamwandalia riziki yenye heshima.
يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٣٢﴾
32. Enyi wake wa Mtume! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine kama mtamcha Mwenyezi Mungu. Basi msilegeze sauti, asije akaingia tamaa mwenye maradhi moyoni mwake. Na semeni maneno mema.
وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴿٣٣﴾
33. Na kaeni majumbani mwenu wala msidhihirishe mapambo kwa madhihirisho ya kijahiliya ya zamani.Na simamisheni Swala, na toeni Zaka, na mtiini Mwenyezi Mungu. Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.
وَاذْكُرْنَ مَا يُتْلَىٰ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ وَالْحِكْمَةِ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ لَطِيفًا خَبِيرًا ﴿٣٤﴾
34. Na kumbukeni yanayosomwa majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hikima. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole, Mwingi wa habari.
UTWAHARA WA AHLUL BAYT
Aya 31-34
MAANA
Na yeyote katika nyinyi atakayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akatenda wema, tutampa malipo yake mara mbili, na tutamwandalia riziki yenye heshima.
Kama ambavyo adhabu itakuwa mara mbili kwa atakayejasiri kufanya maasi katika wake wa Mtume, vile vile thawabu zitakuwa mara mbili zaidi kwa atakayemuogopa Mwenyezi Mungu na akamcha.
Enyi wake wa Mtume! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine kama mtamcha Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawaambia wake wa Mtume kuwa nyinyi mko zaidi ya wanawake wengine kiheshima na utukufu, ikiwa mtamcha Mwenyezi Mungu kwa kauli na vitendo. Vinginevyo basi mtakuwa hamna muungano wowote na Mtume.
Al-Hafidh, Muhammad bin Ahmad Al-Kalabiy anasema katika kitabu Attas-hil: “Walipata fadhila juu ya wanawake wote isipokuwa Fatima bint Muhammad, Maryam bint Imran na Asiya bint Muzahim.”
Basi msilegeze sauti asije akaingia tamaa mwenye maradhi moyoni mwake. Na semeni maneno mema na kaeni majumbani mwenu wala msidhihirishe mapambo kwa madhihirisho ya kijahiliya ya zamani.
Zama za Mtume zilikuwa ni bora kuliko zama nyingine, lakini bado Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwahadharisha wake wa Mtume wasilainishe mazungumzo na wanaume na wasitoke majumbani wakiwa wanajionyesha vipambo vyao.
Ikumbukwe kuwa wake wa Mtume walikuwa wakijistahi na kustahiwa kwa hali ya juu isiyokuwa na shaka yoyote. Sasa je, vipi kwenye zama zetu hizi ambapo mwanamke amechomoka nyumbani kwake hadi kwenye mabwawa ya kuogelea na kwenye majumba ya sinema na akaweza kuwa uchi kwa kutumia mfumo wa kustarehe?
Na simamisheni Swala kwa sababu inakataza kujionyesha mapambo na mengineyo ya haramu.
Na toeni Zaka inayosafisha mali, kama Swala inavyosafisha nafsi.
Na mtiini Mwenyezi Mungu katika kila kitu, sio kwenye Swala tu na Zaka wala kwenye kuacha kudhihirisha mapambo au kulegeza sauti.
AHLUBAYT (WATU WA NYUMBA YA MTUME)
Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea ucha- fu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.
Makusudio ya uchafu hapa ni dhambi. Shia wametoa dalili ya isma ya watu wa nyumba ya Mtume kwa Aya hii na wakasema herufi Innama ambayo ki nahw ni chombo cha kudhibiti (adaatul haswr) inafahamisha kudhibiti utwahara wa dhambi kwa watu wa nyumba ya Mtume tu, sio wengineo; wala hakuna maana nyingine ya isma isipokuwa kutwaharika na dhambi.
Katika Sahih Muslim, sehemu ya pili ya Juzuu ya pili, Uk. 116 chapa ya 1348 AH, kuna Hadith hii, ninanukuu: “Aisha amesema: Mtume(s.a.w. w ) alitoka asubuhi na mapema akiwa amejifunika guo – Aina ya kitambaa cha Yemen – kilichofumwa kutokana na sufu nyeusi.
Basi akaja Hasan bin Ali akamwingiza, akaja Husein akamwingiza pamoja naye, tena akaja Fatima akamwingiza, kisha akaja Ali akamwingiza na akasema:“Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume na kuwatakasa kabisa kabisa.”
Kuna Hadith kama hiyo kisanadi, aliyoipokea Tirmidhiy katika Sahih yake, Imam Ahmad katika Musnad yake na wengineo katika maimau wa Hadith wa kisunni.
Katika Tafsir At-Twabariy imeandikwa: “Imepokewa kutoka kwa Abu said Al-Khudriy, Swahaba mtukufu na Ummu salama, mke wa Mtume(s.a.w. w ) , Amesema huyo mke wa Mtume: Iliposhuka Aya hii ‘Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, Mtume(s.a.w. w ) alimwita Ali, Fatima, Hassan na Hussein na akawafunika guo na akasema:“Ewe Mola wangu! Hawa ndio watu wa nyumba. Ewe Mola wangu! Waondolee uchafu na uwatakase kabisa kabisa.’
Ummu Salama akasema: “Mimi si katika wao?” Mtume akasema:“Wewe uko kwenye kheri.”
Kuna mfano wa Hadith hiyo katika Tafsir Al-bahrul- muhit ya Al-andalusi,Tas-hili ya Hafidh, Durrul manthur ya As-Suyuti na Tafsir nyinginezo.
Katika Juz. (2: 35 – 33) Kifungu cha ‘Ahlubayt’ Tumenukuu aliyoyasema Muhyi-ddni Ibnul-Arabiy katika Juzuu ya kwanza na ya pili ya Kitabu Futuhatil-Makkiyya kuhusiana na Aya hii. Sasa tunayanukuu aliyosema kuhusiana na Ahlul-bayt katika Juzuu ya nne ya Kitabu hicho Uk. 139 chapa Darul-kutubil-arabiyya al-kubra ya Misr, anasema: “Hakika mapenzi yetu kwa Mtume(s.a.w. w ) na watu wa nyumba yake ni sawa sawa.
Mwenye kuwachukia watu wa nyumba yake basi amemchukia Mtume(s.a.w. w ) , kwa sababu yeye ni mmoja wao, na mwenye kuwafanyia hiyana atakuwa amemfanyia hiyana Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) .”
Na kumbukeni yanayosomwa majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hikima. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole, Mwingi wa habari.
Makusudio ya hekima hapa ni sunna za Mtume kwa kulinganisha na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Aya zake. Maana ni kuwa enyi wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Shukuruni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, pale alipowajaalia katika majumba ambayo ndani yake mnasikia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume wake ambazo ni nuru ya akili na kiburudisho cha nyoyo.
Unaweza kuuliza : Mfumo wa Aya unafahamisha kuwa makusudio ni kutwaharishwa wake wa Mtume(s.a.w. w ) , vipi wafasiri na wasimulizi wa Hadith wamewatoa?
Jibu :Kwanza : mwenye Tafsir Al-manar akimnukuu ustadh wake Sheikh Muhammad Abduh, katika Juz.2 Uk. 451 chapa ya pili, anasema: “Hakika ni katika ada ya Qur’an kumgurisha mtu kutoka jambo moja hadi jingine, kisha inarudia utafiti wa kusudio moja mara kwa mara.”
Imam Ja’far As-Sadiq(a.s ) naye anasema:“Hakika Aya moja katika Qur’an inakuwa mwanzo wake kuna jambo na mwisho wake ni jambo jingine.”
Kwa hiyo basi haifai kutegemea mfumo wa Aya ya Qur’an yenye hekima kuwa ndio kawaida yake yote.
Pili : Lau tukichukulia kutegemea mfumo wa Aya, kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, ‘kuwaondolea na kuwatakasa,’ imekuja kwa dhamir (kum) ambayo huwa haitumiki kwa wanawake peke yao, kulingana na sarufi ya kiarabu (Nahw).
Tatu : Hakika wafasiri na wasimulizi wa Hadith tuliowataja wametegemea Hadith sahih katika kuwatoa wake wa Mtume. Na waislamu wote wameafikiana kuwa Hadith za Mtume ni Tafsiri na ubainifu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu.
إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿٣٥﴾
35. Hakika waislamu wanaume na waislamu wanawake, na waumini wanaume na waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wakweli wanaume na wakweli wanawake, na wanaume wanaosubiri na wanawake wanaosubiri, na wanyenyekevu wanaume na wanyenyekevu wanawake, na wanaotoa sadaka wanaume na wanaotoa sadaka wanawake, na wanaume wanaofunga na wanawake wanaofunga, na wanaume wanohifadhi tupu zao na wanawake wanohifadhi tupu, na wanaume wanomkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi na wanawake wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi. Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na malipo makubwa.
WANAUME NA WANAWAKE WANAOHIFADHI MIPAKA YA MWENYEZI MUNGU
Aya 35
MAANA
Uislamu ni kukiri umoja wa Mwenyezi Mungu na risala ya Muhammad. Imani ni kukiri kwa ulimi na kufanya kwa vitendo. Kuna Aya inayofahamisha tofauti ya Uislamu na imani:
قَالَتِ الْأَعْرَابُ آمَنَّا قُل لَّمْ تُؤْمِنُوا وَلَـٰكِن قُولُوا أَسْلَمْنَا وَلَمَّا يَدْخُلِ الْإِيمَانُ فِي ﴿١٤﴾
“Mabedui wamesema: Tumeamini, sema: Hamjaamini, lakini semeni tumesilimu. Kwani imani haijaiingia katika nyoyo zenu.” (49:14).
Makusudio ya utiifu hapa ni kutekeleza na kudumu kwenye utiifu. Ukweli ni ikhlasi. Kusubiri ni kuvumilia tabu na mashaka kwa ajili ya haki na kuinusuru. Kunyenyekea ni kujirudisha chini. Kutoa sadaka ni kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Saumu ni ile ile ya kawaida. Pia kuhifadhi tupu ni kule kwa kawaida. Ama kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi ni kinaya cha kudumu kwenye Swala tano.
Mwenye kuwa na sifa zote hizi basi yeye mbele ya Mwenyezi Mungu atakuwa na cheo na malipo makubwa awe mwananmume au mwanamke.
Tazama Juz. 2 (2:228) na Juz. 5 (4:123 – 124) kifungu cha ‘Mwanamume na mwanamke.’
وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦﴾
36. Haiwi kwa muumini mwanamume wala muumini mwanamke, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapoamua jambo, kuwa na hiyari katika jambo lao. Na yeyote mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi amepotea upotevu ulio wazi.
وَإِذْ تَقُولُ لِلَّذِي أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَأَنْعَمْتَ عَلَيْهِ أَمْسِكْ عَلَيْكَ زَوْجَكَ وَاتَّقِ اللَّـهَ وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّـهُ مُبْدِيهِ وَتَخْشَى النَّاسَ وَاللَّـهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَاهُ فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِّنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا لِكَيْ لَا يَكُونَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ حَرَجٌ فِي أَزْوَاجِ أَدْعِيَائِهِمْ إِذَا قَضَوْا مِنْهُنَّ وَطَرًا وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ مَفْعُولًا ﴿٣٧﴾
37. Na pale ulipomwambia yule ambaye Mwenyezi Mungu amemneemsha nawe ukamneemesha: Shikamana na mkeo na mche Mwenyezi Mungu. Ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha, na ukachelea watu na hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea. Basi Zayd alipokwisha haja naye, tulikuoza ili isiwe tabu kwa waumini kuoa wake wa watoto wao wa kupanga watakapokuwa wamekwisha haja nao. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.
2
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
مَّا كَانَ عَلَى النَّبِيِّ مِنْ حَرَجٍ فِيمَا فَرَضَ اللَّـهُ لَهُ سُنَّةَ اللَّـهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلُ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ قَدَرًا مَّقْدُورًا ﴿٣٨﴾
38. Hakuna ubaya kwa Nabii kufanya ambalo amefaradhiwa na Mwenyezi Mungu. Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa waliopita zamani na amri ya Mwenyezi Mungu ni kadara iliyokwisha kadiriwa.
الَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّـهِ وَيَخْشَوْنَهُ وَلَا يَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّـهَ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٣٩﴾
39. Ambao walifikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kumwogopa yeye, wala hawamwogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye anayetosha kuhisabu.
مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٤٠﴾
40. Hakuwa Muhammad ni baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
KISA CHA ZAINAB BINT JAHSH
Aya 36 – 40
JE, MTUME ALIMTAMANI ZAINAB BINT JAHSH?
Maneno yamekuwa mengi kuhusiana na Aya hizi, kutoka kwa wanaoutetea Uislamu na pia maadui zake. Hawa waliutuhumu utakatifu wa Mtume, wakasema kuwa Mtume alimtamani Zainab bint Jahsh As-Saadiyya binti wa shangazi yake Umayma, mke wa huria[1] wake Zayd bin Haritha, na kwamba hilo alilificha kwa kuhofia watu, sio kumuhofia Mwenyezi Mungu. Wakitumia kauli yake Mwenyezi Mungu:“Ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha, na ukachelea watu na hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea.”
Watetezi wa Uislamu wakawajibu kwa kiuhakika na kimantiki, ingawaje wengine wamefuata njia inayoleta tuhuma. Lakini pamoja na hivyo sisi tutakuwa na msimamo usiopendelea, tukilazimiana na dhahiri ya tamko, hatutafanya taawili wala kutoka kwenye dalili za Aya, kisha tumwachie msomaji mwenye kuchunga haki ahukumu mwenyewe. Kabla ya kuanza kufasiri tutatanguliza yafuatayo: Zayd bin Haritha alikuwa mtumishi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) .
Siku moja akaja baba yake kwa Mtume na akamtaka ama amwache huru mwanawe au amuuzie kwa bei yoyote anayotaka. Mtume wa huruma akamwacha huru kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na akampa hiyari ya kwenda na baba yake au abakie.
Zayd akaathirika na Mtume kuliko kwenda na baba yake. Hapo baba yake, Haritha, akasema: “Enyi jamaa wa kikuraishi! Shuhudie kuwa huyu si mwanangu tena.” Mtume(s.a.w. w ) naye akasema:“Shuhudieni kuwa ni mwanangu.” Watu wakadhani kuwa Mtume amemfanya Zayd kuwa ni mwanawe wa kupanga, wakawa wanamwita Zayd bin Muhammad.
Waarabu kabla ya Uislamu walikuwa na desturi ya kumfanya mtoto wa kupanga ni sawa na mtoto wa kiuhakika hata kwenye mirathi na uharamu wa nasaba. Wenye akili wote wema na waovu wanaafikiana kuwa ada inayorithiwa kutoka jadi ni kama sharia na dini, haifai kwa yoyote kuihalifu kwa hali yoyote atakayokuwa.
Hekima yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ikataka kuiondoa ada hii, kwa vitendo sio kwa kauli tu, kwa kumuoza Zayd bin Haritha, ambaye jana alikuwa ni mtumwa asiyekuwa na uwezo wowote, mke mwenye hadhi ya kinasabu na uzuri. Hakuna anayemfikiria kumuoa isipokuwa mwinyi tu. Naye ni Zaynab bint Jahsh. Na mama yake ni Umayma bint Abdul Muttwalib, babu wa Mtume(s.a.w. w ) . Na kwamba Zayd amalize haja yake, ampe talaka kisha aolewe na Mtume(s.a.w. w ) .
Kwa sababu hilo litakuwa na nguvu na ufasaha zaidi wa kukataza desturi hiyo kwa upande mmoja. Na kwa upande mwingine mamwinyi wasione kigegezi kuwaoa waliotalikiwa na mahuria wao na walala hoi. Na zaidi ya hayo asiwe na madharau yule mwenye nasaba tukufu au walii wake kumuoza aliye chini yake kihadhi au kinasaba.
Mwenyezi Mungu akalipitisha hilo na akalikadiria, kama alivyoesema Mwenyezi Mungu (s.w.t):“Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kadara iliyokwisha kadiriwa .” Mwenyezi Mungu (s.w.t) akampa wahyi Mtume wake mtukufu kwa kadhaa na kadari hiyo, akamwamrisha kumuoza Zaynaba kwa Zayd.
Basi Mtume akaja kumchumbia Zaynab kwa ajili ya huria wake Zayd na akaficha moyoni mwake yale aliyompa wahyi Mwenyezi Mungu kuwa amepitisha amuoe yeye baada ya Zayd. Aliuficha Mtume wahyi huu kwa sababu ulikuwa mzito kwa watu kutokana na kuwa mbali na desturi na mila zao. Kuficha huku ndiko alikokuashiria Mwenyezi Mungu kwa kauli yake: ‘Ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha, na ukachelea watu na hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea.’
Hata hivyo Abdallah, kaka yake Zaynab, alikataa kumuoza dada yake kwa mtu ambaye si kufu yake naye mwenyewe pia akakataa kuolewa. Ndipo ikashuka kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ‘Haiwi kwa mumin mwananamume wala mumin mwanamke, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapoamua jambo, kuwa na hiyari katika jambo lao.’ Basi hapo Zaynab na kaka yake wakainyenyekea hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na ikafungwa ndoa.
Baada ya kupita muda uhusiano wa ndoa ukawa una matatizo. Zayd akaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akitaka kumpa talaka Zaynab; hata hivyo akamkataza na akamwamrisha awe na subira, lakini amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima ipite; ikawa talaka. Baada ya kwisha eda Mtume akamuoa na nidhamu ya mtoto wa kupanga ikavunjikilia mbali.
Kwa hiyo basi suala la Mtume kumuoa Zaynab si suala la matamanio na mapenzi; bali ni suala la amri ya Mwenyezi Mungu, kadha na kadari yake kwa nukuu ya Aya zilizo wazi ambazo wazushi wamejaribu kuzipotoa na kuziletea tafsiri ile wanayoitaka wao kulingana na hawa zao.
Hizi hapa nukuu zinazosema waziwazi: ‘Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.’ ‘Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kadara iliyokwisha kadiriwa.’ ‘Ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha, na ukachelea watu na hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea.’
Makusdio ya amri ya Mwenyezi Mungu na yenye kukadiriwa na lile analolidhihirisha Mwenyezi Mungu ni jambo moja – Mtume kumuoa Zaynab ambako Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekutangaza waziwazi kwa kusema: ‘tulikuoza.’
Kama Mtume angelikuwa ameficha matamanio, waliyoyazusha wakuza mambo, basi Mwenyezi Mungu angeliyadhihirisha kutokana na kauli yake:‘Aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha.’
Zaidi ya hayo ni kuwa Zaynab alikuwa mikononi mwa Mtume (alikwa akimjua) na alikuwa akimtii zaidi kuliko viungo vyake. Kama angelikuwa anamtamani basi asingelingoja kwanza amuoze huria wake kisha amalize haja naye ndipo amuoe. Hasha! Bwana wa watu na majini hawezi kuwa na matamanio na hawa hizo. Yuko mbali kabisa na hayo.
Baada ya hayo ni kuwa Aya zote hizi zimekuja kwa maudhui moja, kwa hiyo zinaungana na kushikana; wala haiwezekani kwa hali yoyote kuzitenganisha na kuzigawa mafungu. Ama kuzichukua zote au kuziacha zote.
Mwenye kuchukua kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Ukachelea watu na hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea,’ kuwa ni jumla iliyo peke yake na akaipuuza kauli yake: ‘aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha’ na ‘amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa,’ basi atakuwa ni katika wale wanaoipotosha haki kwa kuifanyia inadi na watu wake.
Kutokana na utangulizi huu, maana ya Aya yatakuwa yako wazi na pia makusudio yatakuwa yamejulikana. Kwa hiyo tutazipitia juu juu, tukiashiria mfuatano wa Aya kulingana na kisa cha ndoa ya kwanza hadi ya pili.
MAANA
Haiwi kwa mumin mwanamume wala mumin mwanamke, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapoamua jambo, kuwa na hiyari katika jambo lao. Na yeyote mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi amepotea upotevu ulio wazi.
Aya hii ilishuka pale Mtume(s.a.w. w ) alipomchumbia Zayanb bint Jahsh kwa ajili ya huria wake, Zayd bin Haritha. Zaynab akakataa yeye na kaka yake kwa vile Zayd sio kufu yake.
Maana ni kuwa ndoa hii ni amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na yeyote katika waumini hana hiyari mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atakayekataa basi atakuwa katika wapotevu wa kuangamia. Basi hapo Zaynab na kaka yake wakaridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na ndoa ikakamilika.
Na pale ulipomwambia yule ambaye Mwenyezi Mungu amemneemsha nawe ukamneemesha.
Huyo ni Zayd bin Haritha. Mwenyezi Mungu alimneemesha kwa uislmu na usuhuba pamoja na Mtume naye Mtume akamneemessha kwa kumwacha huru.
Shikamana na mkeo na mche Mwenyezi Mungu.
Baada ya kupita muda, uhusiano wa ndoa baina ya Zaynab na Zayd ukawa sio mzuri. Akamwambia Mtume(s.a.w. w ) : “Nataka nimtaliki.” Mtume akamuusia kushikamana naye na amche Mwenyezi Mungu katika hali zote. Lakini Mtume alikuwa na hakika kuwa Zayd atakuja mwacha Zaynab kisha amuoe; isipokuwa hakulidhihirisha hilo kwa kuhofia lawama, ndio Mwenyezi Mungu akamwambia kwa kumwelekeza:
Ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha, na ukachelea watu na hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea.
Makusudio ya aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha, ni ndoa ya Mtume kwa Zaynab baada ya kuachwa na Zayd. Mwenyezi Mungu aliidhihirisha kwa kauli yake:
Basi Zayd alipokwisha haja naye, tulikuoza.
Haya ndiyo aliyoyaficha Muhammad(s.a.w. w ) na akayadhihirisha Mwenyezi Mungu. sasa yako wapi hayo matamnio aliyoyaficha Muhammad katika nafsi yake. Kwanini Mwenyezi Mungu alinyamaza baada ya kusema: ‘Aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha.’ Mtume alificha kujua kwake kuwa Zayd atamwacha Zaynab na amuoe yeye. Ni kuficha huku ndiko alikoambiwa na Mwenyezi Mungu kuwa mtu aliye kwenye nafasi yako hatilii umuhimu lawama za anayelaumu na kauli za wanaobobokwa.
Ili isiwe tabu kwa waumini kuoa wake wa watoto wao wa kupanga watakapokuwa wamekwisha haja nao. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.
Ndoa ya Mtume ilikuwa ni ubainifu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waumini na kwa watu wote kuwa hakuna ubaya kuoa wake wa watoto wao wa kupanga ambao wamemaliza haja nao.
Hakuna ubaya kwa Nabii kufanya ambalo amefaradhiwa na Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwamrisha Mtume wake kumuoa mtalaka wa mwanawe wa kupanga, ili kubatilisha desturi hiyo ya kijahilia. Mtume akaitikia amri ya Mwenyezi Mungu.
Kwa hiyo Mtume au mwingine hana lawama kumuoa mtalaka wa mtoto wake wa kupanga, hata kama watu watamlaumu na kumtia kasoro, madamu Mwenyezi Mungu amemuhalalishia.
Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa waliopita zamani na amri ya Mwenyezi Mungu ni kadara iliyokwisha kadiriwa. Ambao walifikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kumwogopa yeye, wala hawamwogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ndiye anayetosha kuhisabu.
Makusudio ya wale waliopita na wale waliofikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu, ni mitume waliotangulia. Maana ni kuwa hakuna Nabii yeyote ila Mwenyezi Mungu alimtuma kulingania haki na kukataza batili, kama vile desturi na maigizo ambayo Mwenyezi Mungu hakuyateremshia dalili yoyote.
Mtume alifikisha ujumbe wa Mola wake kwa uaminifu na kwa ikhlasi, hakulegeza wala hakubabaisha na hakumwogopa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, alipata tabu nyingi sana katika hilo.
Wako waliofanana nawe ewe Muhammad katika mitume waliopita. Hisabu ya wakadhibishaji na wenye inadi ni kwa Mwenyezi Mungu tu peke yake.Hakuwa Muhammad (s.a.w. w ) ni baba wa yeyote katika wanaume wenu kwa nasaba wala kwa kuzaa, kuweza kumzuia kumuoa mtalaka wa Zayd bin Haritha.
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) alizaa watoto wane wa kiume, wa tatu kutokana na Khadija; nao ni: Qasim, Twayyib, na Twahir. Imesemekana kuwa ni wawili, kwamba Twahir ndiye huyo huyo Twayyib. Na mmoja aliyetokana na Maria Qibtiya ambaye ni Ibrahim. Wote walikufa utotoni.
Ama Hasan na Husein ni watoto wa binti yake Fatima aliyewazaa na Ali(a.s ) , lakini Mtume aliwazingatia kama wanawe, pale aliposema:“Wanangu hawa wawili ni maimamu wakisimama au wakikaa.” Pia alisema:“Watoto wa binti wote wananasibiana na baba yao; isipokuwa watoto wa Fatima, mimi ni baba yao.” Tazama Juz. 7 (6:84 – 90).
Bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu
Na Mtume si baba, ingawaje anawashughulikia sana waumini na kuwahu- rumia kuliko baba zao.
Na mwisho wa mitume, hakuna Nabii mwingine baada ya Muhammad(s.a.w. w ) wala sharia nyingine baada ya sharia ya kiislamu.
Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu, ukiwemo ujuzi wa kujua pale atakapouweka ujumbe wake na kuuishiliza kwa Muhammad(s.a.w. w ) .
KWA NINI UTUME ULIISHIA KWA MUHAMMAD?
Waislamu wote wameafikiana kwa kauli moja kwamba hakuna wahyi kwa yeyote baada ya Muhammad(s.a.w. w ) Mwenye kulipinga hilo basi si mwislamu, mwenye kudai utume baada ya Muhammad ni wajibu kuawa na mwenye kutaka dalili ya atakayedai utume huu, kwa kutaraji kumsadiki, basi ni kafiri.
Katika Tafsiri ya Isamil Haqiy, Ruhul-bayan, imeelezwa:“Lau angekuja Nabii baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w. w ) angelikuwa Ali bin Abi Twalib, kwa sababu yeye yuko kwenye daraja ya Haruna kwa Musa.”
Unaweza kuuliza : Kwa nini utume umeishilia kwa Muhammad(s.a.w. w ) ?
Jibu : lengo la kwanza na la mwisho la kutumwa Nabii ni kufikisha kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake. Hakuna kitu chochote alichotaka Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwafikishia waja wake ila kimo kwenye Qur’an Tukufu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:“Na tumekuteremshia Kitabu hiki kubainisha kila kitu.” Juz. 14 (16:89).Na akasema: “Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote.” Juz. 7 (6: 38).
Yaani kitu chochote kinachoamabatana na wadhifa wa mitume na kuhusika kwao katika kuwaongoza viumbe na kuwaelekeza kwenye masilahi yao yanayodhamini ufanisi katika nyumba mbili (duniani na akhera).
Wala hakuna nyenzo ya kuthibitisha hakika hii ila kwa majaribio yasiyokubali shaka wala mjadala; yaani wataalamu wanatakikana waisome Qur’an kwa ukamilifu kuanzia alifu yake mpaka yee yake, kisha wailinganishe na vitabu vingine vya dini. Tuna hakika kabisa kuwa wataishia kwenye mambo mawili:
Kwanza : kwamba Qur’an kwa ufasaha wake, itikadi yake na sharia yake ni zaidi ya vitabu vyote vya kidini.
Pili : ndani ya Qur’an watakuta misingi na misimamo yote ambayo inaona na haja za watu, masilahi yao na maendeleo yao hadi siku ya Kiyama.
Hakuna maendelo yoyote ya kielemu au mapinduzi yoyote ya uhuru, ila Qur’an inayatolea mwito na kuyabariki. Na hakuna sharia yoyote anayoihitajia binadamu katika historia ila wataalam wanaweza kuitoa kutoka katika moja ya misingi ya Qur’an na misingi yake.
Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamemruhusu kila mwenye uwezo na maandalizi kutoa tanzu katika mizizi ya Qur’an na kutoa hukumu iliyo na heri na masilahi kwa watu kwa namna fulani. Maana yake ni kuwa hukumu ya mujtahidi mwadilifu ni hukumu ya Qur’an na ya Mtume. Ndio maana kuna Hadith isemayo kuwa kuipinga hukumu yake ni kama kuipinga hukumu ya Mwenyezi Mungu.
Vile vile hii inamanisha kuwa Mtume yuko kwa kuweko Qur’an ambayo haingiliwi na batili mbele yake wala nyuma yake. Amepatia Ibn Al-arabiy aliposema: “Mwenye kuhifadhi Qur’an ameuunganisha utume mbavuni mwake” lakini kwa sharti ya kuizingatia na kuiamini kwa imani safi.
Zaidi ya hayo, Muhammad ni mtu aliyepewa wahyi; kama Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na mitume wengineo, lakini Mwenyezi Mungu amemuhusu kwa ambayo hakumuhusu nayo yeyote katika mitume. Pamoja na kuwa Mwenyezi Mungu alimpa kila Mtume ubora wote, kwa sababu utume ni mama wa ubora wote, lakini ubora una daraja. Kuna mbora na mbora zaidi, mkamilifu na mkamilifu zaidi, mjuzi na mjuzi zaidi na mkarimu na mkarimu zaidi. Mwenyezi Mungu anasema: “Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya manabii kuliko wengine.” Juz. 15 (17:55).
Mwenyezi Mungu amemuhusu Muhammad(s.a.w. w ) kwa sifa na daraja ya hali ya juu; kiasi ambacho hakuna zaidi yake isipokuwa Mwenyezi Mungu na sifa za Mwenyezi Mungu. Miongoni mwa sifa hizo ni kukamilishwa wahyi ulioteremshwa kwake kukamilika katika pande zote. Dalili ya hilo ni hii Qur’an ambayo ni ubainifu wa kila kitu ambacho kinaingia katika wadhifa wa mitume. Basi wapi na wapi hiyo na vitabu vingine? Haya nawalete wapinzani kimoja tu kilicho na ubainifu wa kila kitu.
Bwana wa mitume na wa mwisho wao aliashiria haya kwa kusema:“Hakika mfano wangu na mfano wa manabii walikokuwa kabla yangu, ni kama mfano wa mtu aliyejenga jengo akalijenga vizuri na akalipamba; ispokuwa sehemu ya tofali moja. Ikawa watu wanapoliona wanastaajabu huku wakisema: “Mbona huweki hili tofali? Basi mimi ndio tofali hilo na mimi ni mwisho wa mitume.”
Tutaishiliza jawabu, kwa yale tuliyoyasema kwenye kitabu Imamatu Ali wal-aql (Uimamu wa Ali na akili): Mtu akisema: “Kwa nini Muhammad(s.a.w. w ) akawa ndiye mwisho wa mitume?
Tutamjibu kuwa Muhammad na dini ya Muhammad ina sifa zote za ukamilifu na imefikia kikomo; sawa na jua lilivyofikia kikomo cha nuru.
Hakuna nyota yoyote wala umeme wowote unaoweza kujaza nuru ulimwenguni kote zaidi ya jua. Kadhalika hakuna Nabii atakayeleta kheri kwa watu baada ya Muhammad(s.a.w. w ) . Maudhui haya yanaungana na tuliyoyaandika kwa anuani ya ‘Dini na maisha’ katika Juz. 9 (8:24), Juz. 15 (17: 9) na Juz. 21 (30:30).
3
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا ﴿٤١﴾
41. Enyi ambao mmeamini! Mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi.
وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿٤٢﴾
42. Na mumtakase asubuhi na jioni.
هُوَ الَّذِي يُصَلِّي عَلَيْكُمْ وَمَلَائِكَتُهُ لِيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا ﴿٤٣﴾
43. Yeye ndiye anayewaswalia na malaika wake, ili awatoe vizani na kuwatia kwenye nuru. Naye ni mwenye kuwarehemu waumini.
تَحِيَّتُهُمْ يَوْمَ يَلْقَوْنَهُ سَلَامٌ وَأَعَدَّ لَهُمْ أَجْرًا كَرِيمًا ﴿٤٤﴾
44. Maamkuzi yao siku ya kukutana naye yatakuwa ni Salaam na amewaandalia malipo yenye heshima.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٤٥﴾
45. Ewe Nabii! Hakika sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na muonyaji.
وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا ﴿٤٦﴾
46. Na mlinganiaji kwa Mwenyezi Mungu kwa idhini yake, na taa iangazayo.
وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ بِأَنَّ لَهُم مِّنَ اللَّـهِ فَضْلًا كَبِيرًا ﴿٤٧﴾
47. Wape bishara waumini ya kwamba wanafadhila kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ وَدَعْ أَذَاهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٤٨﴾
48. Wala usiwatii makafiri na wanafiki na acha udhia wao na mtegemee Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mlinzi.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَكَحْتُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ فَمَا لَكُمْ عَلَيْهِنَّ مِنْ عِدَّةٍ تَعْتَدُّونَهَا فَمَتِّعُوهُنَّ وَسَرِّحُوهُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا ﴿٤٩﴾
49. Enyi ambao mmeamini! Mkiwaoa wanawake waumini kisha mkawaacha kabla ya kuwagusa, basi hamna eda juu yao mtakayoihisabu. Hivyo wapeni cha kuwaliwaza na waacheni muachano mzuri.
NDIYE ANAYEWAREHEMU
Aya 41 – 49
MAANA
Enyi ambao mmeamini! Mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi na mumtakase asubuhi na jioni.
Hii ni amri ya kudumu kwenye Swala tano na kumkumbuka, Mwenyezi Mungu wakati wote, kwa kumbukumbu nzuri.
Yeye ndiye anayewaswalia na malaika wake.
Kuswalia kukitoka kwa Mwenyezi Mungu, maana yake ni maghufira na rehema na kukitoka kwa mwenginewe ni kuombea maghufira na rehema. Kwa hiyo inampasa kila mtu kumswalia na kumwombea amani kila mwenye kuamini na katenda mema.
Ni vizuri kudokeza kwamba Sunni, aghlabu wakimtaja sahaba mtukufu au imam mkuu husema: Radhiallah anh (Mwenyezi Mungu awe radhi naye). Shia wao husema: Alayhissalam (amani ishuke juu yake). Chimbuko la kauli zote mbili ni moja – Qur’an. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Awe radhi nao Mwenyezi Mungu na wao wawe radhi naye.” Juz. 7 (5:119) na akasema:“Amani kwa Ilyasin” (37:130) na amesema kwenye Aya hii tuliyo nayo: “Yeye ndiye anayewaswalia na malaika wake.”
Katika Tafsir Ruhul-bayan imeelezwa: “Bani Israil walimuuliza Musa: “Mola wetu naye anaswali? Basi hili likawa zito kwa Musa.” Hilo si ajabu kwa Waisrail.
Ili awatoe vizani na kuwatia kwenye nuru.
Makusudio ya viza hapa ni viza vya moto; na nuru ni nuru ya neema; yaani Mwenyezi Mungu na malaika wake wanawaswalia waumini ili wawe mbali na adhabu ya moto na waingie kwenye raha. Imesekana kuwa makusudio ya viza ni ukafiri na nuru ni nuru ya imani, lakini hii haiafikiani na kauli yake Mwenyezi Mungu inayofuatia:
Naye ni mwenye kuwarehemu waumini.
Vile vile haiafikiani na kuwa Mwenyezi Mungu na malaika wake hawarehemu makafiri ili awatoe kwenye imani.
Maamkuzi yao siku ya kukutana naye yatakuwa ni Salaam na amewaandalia malipo yenye heshima.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:10) Juz. 13 (14:23).
Ewe Nabii! Hakika sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na muonyaji na mlinganiaji kwa Mwenyezi Mungu kwa idhini yake.
Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad(s.a.w. w ) kulingania haki na akamsheheneza hoja za kutosha, kumpa habari njema ya pepo yule mtiifu na kumwonya na adhabu chungu yule mwenye kuasi. Kesho atakuwa shahidi wa huyu kwamba alipinga na akatupilia mbali na atakuwa shahidi wa yule kwamba alisikia na akatii.
Kwenye Nahjul-balagha kuna maelezo haya: “Alimtuma kuwa ni mlingania kwenye haki na shahidi kwa viumbe. Akafikisha ujumbe wa Mola wake bila ya kubweteka wala kuzembea, na akapigana jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na maadui zake bila ya kudhoofika wala kutafuta visababu. Ni imamu wa mwenye takua na busara ya mwenye kutaka kuongoka.
Na taa iangazayo inayowaongoza wanaohangaika kwenye ufukwe wa salama.
Wape bishara waumini ya kwamba wanafadhila kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Umepita mfano wake katika Juz.11 (9-112)
Wala usiwatii makafiri na wanafiki.
Imetangulia neno kwa neno katika Juzuu iliyopita mwanzo wa sura hii tuliyo nayo.
Na acha udhia wao.
Mtume hakuwaudhi, ispokuwa washirikina ndio waliomuudhi, kiasi cha kufikia kusema: “Hakuudhiwa Nabii mfano wa nilivyoudhiwa mimi.” Kwa hiyo maana ni, achana nao, usikushughulishe ujinga na upumbavu wao.
Na mtegemee Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mlinzi.
Kwenye Nahjul-balagha imesemwa: “ Mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu anamtoshea na mwenye kumwomba atampa na mwenye kumkopesha atamlipa, na mwenye kumshukuru atampa jaza yake.
Enyi ambao mmeamini! Mkiwaoa wanawake waumini kisha mkawaacha kabla ya kuwagusa, basi hamna eda juu yao mtakyoihisabu. Hivyo wapeni cha kuwaliwaza na waacheni muachano mzuri.
Kabla ya kuwagusa ni kabla ya kuwaingilia. Cha kuwaliwaza kisharia ni kitu anachokitoa mtaliki akiwa hajamwingilia na hakutaja mahari yake. Ikiwa ametaja itakuwa ni wajibu kutoa nusu ya mahari. Tazama Juz. 2 (2:236 – 237).
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَحْلَلْنَا لَكَ أَزْوَاجَكَ اللَّاتِي آتَيْتَ أُجُورَهُنَّ وَمَا مَلَكَتْ يَمِينُكَ مِمَّا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَيْكَ وَبَنَاتِ عَمِّكَ وَبَنَاتِ عَمَّاتِكَ وَبَنَاتِ خَالِكَ وَبَنَاتِ خَالَاتِكَ اللَّاتِي هَاجَرْنَ مَعَكَ وَامْرَأَةً مُّؤْمِنَةً إِن وَهَبَتْ نَفْسَهَا لِلنَّبِيِّ إِنْ أَرَادَ النَّبِيُّ أَن يَسْتَنكِحَهَا خَالِصَةً لَّكَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ قَدْ عَلِمْنَا مَا فَرَضْنَا عَلَيْهِمْ فِي أَزْوَاجِهِمْ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ لِكَيْلَا يَكُونَ عَلَيْكَ حَرَجٌ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥٠﴾
50. Ewe Nabii! Hakika sisi tumekuhalalishia wake zako ambao umewapa ujira wao, na uliowamiliki kwa mkono wako wa kuume katika aliokupa Mwenyezi Mungu, na mabinti wa ami zako, na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajomba zako na mabinti wa khalat zako waliohama pamoja nawe, na mwanamke mumin akijitoa mwenyewe kwa Nabii ikiwa Nabii anataka kumuoa. Ni halali kwako wewe tu, si kwa waumini wengine. Tunajua tuliyowafaradhishia wao kuhusu wake zao na wale waliomilikiwa na mikono yao ya kuume. Ili isiwe dhiki juu yako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
تُرْجِي مَن تَشَاءُ مِنْهُنَّ وَتُؤْوِي إِلَيْكَ مَن تَشَاءُ وَمَنِ ابْتَغَيْتَ مِمَّنْ عَزَلْتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكَ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن تَقَرَّ أَعْيُنُهُنَّ وَلَا يَحْزَنَّ وَيَرْضَيْنَ بِمَا آتَيْتَهُنَّ كُلُّهُنَّ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا فِي قُلُوبِكُمْ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَلِيمًا ﴿٥١﴾
51. Unamwakhirisha umtakaye katika wao na na unamsogeza kwako umtakaye. Na unayemtaka katika uliyemtenga si vibaya kwako. Hivyo itakuwa ni karibu zaidi kuburudika macho yao wala wasihuzunike na wawe radhi juu ya kile unachowapa wao wote. Na Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo nyoyoni mwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mpole.
لَّا يَحِلُّ لَكَ النِّسَاءُ مِن بَعْدُ وَلَا أَن تَبَدَّلَ بِهِنَّ مِنْ أَزْوَاجٍ وَلَوْ أَعْجَبَكَ حُسْنُهُنَّ إِلَّا مَا مَلَكَتْ يَمِينُكَ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ رَّقِيبًا ﴿٥٢﴾
52. Hawakuhalalikii wanawake baadaye wala kuwabadilisha kwa wake wengine, ijapo uzuri wao utakupendeza; isipokuwa uliyemmiliki kwa mkono wako wa kuume. Na Mwenyezi Mungu ni Mchungaji wa kila kitu.
TUMEKUHALALISHIA WAKE ZAKO
Aya 50 – 52
MAANA
Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Aya hii ametaja aina ya wanawake walio halali kwa Mtume(s.a.w. w ) na kumwachia hiyari ya kumlalia na kutomlalia anayemtaka. Kisha akamharamishia kuzidisha wale aliokuwa nao au kubadilisha mwingine. Wakati huo alikuwa na wake tisa. Ufuatao ni ufafanuzi:
Ewe Nabii! Hakika sisi tumekuhalalishia wake zako ambao umewapa ujira wao.
Makusudio ya ujira hapa ni mahari. Na kuwapa hayo mahari kunakuwa ni lazima. Aya inaashiria kuwa Mtume anaweza kuoa idadi yoyote anayoitaka. Haya ni katika mambo yanayomuhusu yeye tu.
Unaweza kuuliza : kufunga ndoa kunaswihi hata kama mahari hayakuta- jwa, kwa nini basi Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameufunga uhalali kwa mahari?
Jibu : Ulazima hapa ni wa kuyatoa hayo mahari sio kuyataja kwenye ndoa. Ikiwa mahari hayakutajwa kwenye ndoa, basi ni lazima kutoa mahari kifani; yaani yanayofana na mwingine wa aina yake. Mahari ya mtume, wakati huo, yalikuwa ni Dirhamu 500. wamekadiria Dirhamu moja kuwa ni sawa na Lira 25 za dhahabu.
Na uliowamiliki kwa mkono wako wa kuume katika aliokupa Mwenyezi Mungu katika mateka waliowatekwa nyara na waislamu kati- ka vita na washirikina, ambao wanaitwa masuria. Mwenyezi Mungu amemuhalishia Mtume wake na umma wake, wanawake hawa.
Na mabinti wa ami zako, na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajomba zako na mabinti wa khalat zako waliohama pamoja nawe.
Unaweza kuuliza : Mabinti wa ami, wa shangazi, wajomba na wa khalat (dada wa mama) si wanaingia katika aina ya kwanza ya wanawake, sasa kuna haja gani ya kuhusishwa kutajwa?
Jibu : Inawezekana kuwa makusudio ya kutajwa ni kuwa inavyopendeza ni kuwa hadhi ya Mtume ni kuoa makuraishi aliohama nao kutoka mji wa ukafiri hadi mji wa Uislamu. Ama waumimi wengine ni bora kutowaoa.
Swali la pili : Watu wa sira wamesema kuwa Mtume alikuwa na ami tisa: Abbas, Hamza, Abu Twalib, Zabeir, Harith, Hijla, Muqawwam, Dhirar na Abu Lahab. Na shangazi sita: Swafiya, Ummu Hakim al-baydhau, Atika, Umayma, Arwa na Barra (Assiratu nnabaawiya cha Ibn Hisham).
Na wakasema: “Mtume hakuwa na wajomba wala khalat (mama wadogo au wakubwa), kwa sababu mama yake Amina bint Wahb(a.s) hakuwa na kaka wala dada.” (Tafsir Ruuhul-bayan).
Sasa kuna wajihi gani wa Mwenyezi Mungu kusema: ‘Na mabinti wa ami zako, na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajomba zako na mabinti wa khalat zako?’
Jibu : Makusudio ya wajomba na khalat wa Mtume ni ukoo wa mama yake unaoitwa Bani Zuhra, ambao walikuwa wakisema: “Sisi ni wajomba zake Mtume.”
Na mwanamke mumin akijitoa mwenyewe kwa Nabii ikiwa Nabii anataka kumuoa. Ni halali kwako wewe tu, si kwa waumini wengine.
Katika mambo yanayomuhusu Mtume tu ni kumuoa mwanamke, akitaka, ikiwa atajitoa mwenye kwa Mtume bila ya mahari, kwa masharti ya kuwa mumini. Ndio! Inajuzu kwa mwinginewe kuoa kwa mahari, kisha mke asamehe mahari, kama anavyosamehe mtu yoyote mali yake kwa mwingine.
Tunajua tuliyowafaradhishia wao kuhusu wake zao na wale waliomi- likiwa na mikono yao ya kuume. Ili isiwe dhiki juu yako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
Mwenyezi Mungu, ameweka idadi ya wake waungwana na akaharamisha mwanamke kujitoa mwenyewe bila mahari. Lakini akaliruhusu hilo kwa Mtume ili isiwe dhiki juu yake.
Vile vile kufahamisha utukufu wa cheo chake na juhudi zake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye anayejua zaidi li lilo na masilahi zaidi kwa watu, akiwa anawahurumia na kuwaghufuria.
Unamwakhirisha umtakaye katika wao na na unamsogeza kwako umtakaye.
Katika Aya iliyotangulia Mwenyezi Mungu (s.w.t) amempa uhuru Mtume wake mtukufu katika idadi ya wanawake na katika Aya hii amempa hiyari ya kuongeza au kupunguza zamu ya yeyote anayemtaka.
Na unayemtaka katika uliyemtenga si vibaya kwako.
Yaani anaweza kumrudia aliyemaliza zamu naye na kumwacha aliyekuwa kwenye zamu yake. Kwa ibara ya wanaoimudu lugha ni, anaweza kumtanguliza wa mwisho na kumweka mwisho wa kwanza.
Hivyo itakuwa ni karibu zaidi kuburudika macho yao wala wasihuzunike na wawe radhi juu ya kile unachowapa wao wote.
‘Hivyo’ ni huko kuachiwa hiyari Mtume(s.a.w.w) . Maana ni kuwa wao wakijua kuwa hiyari ni yako sio yao ya zamu sawa, basi kila mmoja ataridhia na vile utakavyokuwa kwake kwa siku kidogo au nyingi kwa kujua kuwa ziada hiyo imetokana na wewe wala si wajibu kwako. Pamoja na hayo, lakini Mtume alikuwa akikaa siku sawa baina ya wake zake.
Na Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo nyoyoni mwenu ya kupondokea zaidi kwa baadhi ya wake zenu kuliko wengine. Mwenyezi Mungu hayachukulii mapenzi yaliyo moyoni au chuki; isipokuwa anachukulia matendo. Hii ndio maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu:
Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mpole.
Hawakuhalalikii wanawake baadaye wala kuwabadilisha kwa wake wengine, ijapo uzuri wao utakupendeza.
Wafasiri wametaja maana tatu za Aya hii; iliyo karibu zaidi na maana ya dhahiri ni ile isemayo kuwa Mwenyezi Mungu baada ya kumhalalishia Mtume wanawake aliowaishiria katika Aya iliyotangulia, amewajibisha katika Aya hii kutosheka na alio nao ambao walikuwa tisa na akaharamishiwa kumwacha yeyote katika wao na kuweka mwingine mahali pake, hata kama atakuwa amempendeza.
Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Ijapo uzuri wao utakupendeza’ inafahamisha kuwa mwanamume anaruhusiwa kumwangalia mwanamke anayetaka kumuoa.
Na ndio mafakihi wakalitolea fatwa hilio kwa kutegemea Aya hii na Hadith za Mtume mtukufu(s.a.w. w ) .
Isipokuwa uliyemmiliki kwa mkono wako wa kuume, aliokupa Mwenyezi Mungu katika mateka.
Na Mwenyezi Mungu ni Mchungaji wa kila kitu, hata kilicho siri na kwenye dhamiri:
وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ﴿٤﴾
“Naye yu pamoja nanyi popote mlipo.” (57:4).
4
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتَ النَّبِيِّ إِلَّا أَن يُؤْذَنَ لَكُمْ إِلَىٰ طَعَامٍ غَيْرَ نَاظِرِينَ إِنَاهُ وَلَـٰكِنْ إِذَا دُعِيتُمْ فَادْخُلُوا فَإِذَا طَعِمْتُمْ فَانتَشِرُوا وَلَا مُسْتَأْنِسِينَ لِحَدِيثٍ إِنَّ ذَٰلِكُمْ كَانَ يُؤْذِي النَّبِيَّ فَيَسْتَحْيِي مِنكُمْ وَاللَّـهُ لَا يَسْتَحْيِي مِنَ الْحَقِّ وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ وَمَا كَانَ لَكُمْ أَن تُؤْذُوا رَسُولَ اللَّـهِ وَلَا أَن تَنكِحُوا أَزْوَاجَهُ مِن بَعْدِهِ أَبَدًا إِنَّ ذَٰلِكُمْ كَانَ عِندَ اللَّـهِ عَظِيمًا ﴿٥٣﴾
53. Enyi ambao mmeamini! Msiingie majumba ya Mtume ila mkipewa ruhusa ya kwenda kula, sio kungojea kiive. Lakini mtakapoitwa, basi ingieni. Na mkisha kula, tawanyikeni wala msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii, naye anawastahi nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa haki. Na mnapowaomba chombo cha nyumbani, basi waulize nyuma ya mapazia. Hilo linasafisha zaidi nyoyo zenu na nyoyo zao. Haiwafalii nyinyi kumuudhi Nabii wala kuwaoa wake zake kabisa. Hakika hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.
إِن تُبْدُوا شَيْئًا أَوْ تُخْفُوهُ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٥٤﴾
54. Mkidhihirisha chochote au mkikificha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
لَّا جُنَاحَ عَلَيْهِنَّ فِي آبَائِهِنَّ وَلَا أَبْنَائِهِنَّ وَلَا إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ أَخَوَاتِهِنَّ وَلَا نِسَائِهِنَّ وَلَا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ وَاتَّقِينَ اللَّـهَ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدًا ﴿٥٥﴾
55. Hapana ubaya kwao kwa baba zao, wala watoto wao, wala kaka zao, wala watoto wa kaka zao, wala watoto wa dada zao, wala wanawake wao, wala wale waliomilikiwa na mikono yao ya kuume. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kushuhudia kila kitu.
MKISHAKULA TAWANYIKENI
Aya 53 – 55
MAANA
Enyi ambao mmeamini! Msiingie majumba ya Mtume ila mkipewa ruhusa ya kwenda kula, sio kungojea kiive. Lakini mtakapoitwa, basi ingieni. Na mkisha kula, tawanyikeni wala msiweke mazungumzo.
Yaani msikae kabisa si kwa mazungumzo wala kwa jambo jingine. Yametajwa mazungumzo kwa vile mara nyingi mtu anakaa kwa kupiga gumzo.
Dhahiri ya Aya inaonyesha kuwa baadhi ya maswahaba walikuwa wakiingia nyumba ya Mtume(s.a.w. w ) bila ya idhini kama ilivyo ada ya kijahiliya; na kwamba wakiona chakula kinapikwa basi wanakingoja na baada ya kula walikuwa wakipiga gumzo.
Hakuna mwenye shaka kwamba aina hii ya upuzi na kukosa adabu inamuudhi binadamu yeyote, awe Mtume au si Mtume. Ni kwa ajili hii Mtume(s.a.w. w ) aliwafundisha adabu mswahaba na wengineo kuwa wasiingie nyumba yoyote bila ya idhini ya wenyewe - hayo yamedokezwa kwenye Juz. 18 (24:28) – na kwamba wasiende kula ila wakiitwa, tena chakula kiwe kimeandaliwa na wakishamaliza kula wasingoje tena.
Haya hayahusiki na nyumba ya Mtume peke yake; isipokuwa Mwenyezi Mungu amemtaja yeye kwa vile ndio sababu ya kushuka Aya. Mara nyingi tumesema kuwa sababu ya kushuka Aya haiifungi na hilo lililoishukia.
Hakika hayo yanamuudhi Nabii, naye anawastahi nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa haki.
Makusudio ya haki aliyokuwa akiistahi Mtume ni haki yake ya kiutu – kuwatoa wapuuzi nyumbani kwake. Mtume aliwanyamazia kwa kuwaonea haya; ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t) akatanabahisha kwamba kubaki kwao baada ya chakula kunamuudhi Mtume, vile vile kuingia kwao nyumbani kwake bila ya idhini yake.
Kuna Hadith isemayo: “Haya ni tawi la imani na asiyekuwa na haya hana dini.” Kuna Hadith nyingine isemayo:“Hakukubakia katika mifano ya mitume isipokuwa kauli ya watu: Kama huna haya basi fanya utakavyo.”
Katika maelezo ya wasifu wa Mtume(s.a.w. w ) ni kuwa yeye alikuwa na haya kuliko mwanamwali kwenye ushungi wake. Katika Nahjul-balagha imesemwa:“Hakuna imani kama haya na subira.” Farazdaq katika kumsifu Imam Zaynul-abdin anasema:
Hufumba macho kwa haya kwa haiba yake. Hazungumzi ila kuonekana tabasamu yake Maajabu ni yale yaliyoandikwa kwenye kitabu Muhadharatul-udabai cha Asfahaniy:
“Doezi mmoja alilaumiwa kwa kudoea kwake, akasema akijitetea: “Ala! Ikiwa bani Israil walimdoea Mungu, je sisi tusidoee watu?”
Na mnapowaomba chombo cha nyumbani, basi waulize ni nyuma ya mapazia. Hilo linasafisha zaidi nyoyo zenu na nyoyo zao.
Yaani mnapowaomba haja wakeze Mtume. Kutaja chombo cha chumbani ni kutolea mfano tu, sio kuhusisha na kuondoa hukumu kwa vingine. Hilo linafahamishwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Hilo linasafisha zaidi nyoyo zenu na nyoyo zao.” Inayotambulisha kuwa kuchanganyika na kuondoa pazia baina ya wanawake na wanaume kunaleta ufisadi na fitna.
Maana yake ni kuwa kuchanganyika ni haramu, au angalau ni bora kuacha. Hapa inatubainikia kuwa kuchanganyika ni sababu ya kuleta matamanio ya kijinsiya, na wala sio kumtia adabu mwanamke na kumkandamiza; kama wanavyodai wale wasemao: “Mungu amesema hivyo na mimi nasema hivi” Ni nani aliye mkweli zaidi kwa mazungumzo kuliko Mwenyezi Mungu?
Haiwafalii nyinyi kumuudhi Nabii wala kuwaoa wake zake kabisa. Hakika hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Hukumu hii inamuhusu Mtume tu peke yake. Kwa sababu wakeze wako katika daraja ya mama wa waumini. Imeelezwa katika Tafsir Arrazi na Ruhul-bayan ya Ismail Haqiy: “Hakika Aya hii ilishuka pale aliposema Twalha bin Abdallah Attaymiy:“Akifa Muhammad(s.a.w. w ) nitamuoa Aisha.”
Hilo linataliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu:
Mkidhihirisha chochote au mkikificha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Hilo ni karipio kwa yule aliyedhamiria kuoa wake za Mtume baada yake.
Hapana ubaya kwao kwa baba zao, wala watoto wao, wala kaka zao, wala watoto wa kaka zao, wala watoto wa dada zao, wala wanawake wao, wala wale waliomilikiwa na mikono yao ya kuume. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kushuhudia kila kitu.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuamrisha kuzungumza na wanawake nyuma ya pazia (hijabu) hapa anavua wale ambao hawawezi kuoana nao, ambao ni: baba, mtoto, kaka, mtoto wa kaka na mtoto wa dada, mtumwa na wanawake. Lakini Mwenyezi Mungu amesema wanawake wao, yaani wanawake wenzao walio waumini, kwa sababu wasiokuwa waumini watawasifia wanaume zao.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 18 (24:31).
إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٥٦﴾
56. Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeami- ni! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.
إِنَّ الَّذِينَ يُؤْذُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَأَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿٥٧﴾
57. Hakika wale ambao wanamuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha.
وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾
58. Na wale ambao wanawaudhi waumini wanaume na waumini wanawake pasi na wao kufanya, hakika wamebeba dhulma kubwa na dhambi kubwa.
MSWALIENI MTUME
Aya 56 – 58
MAANA
Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.
Makusudio ya Mwenyezi Mungu kumsalia Mtume ni kumridhia kumrehe- mu na kumsifu kwa kila kheri, swala ya malaika ni kumsifu, na kutoka kwa waumini ni kumwombea dua ya kuwa na daraja ya juu. Imam Ar-Ridha(a.s) aliulizwa kuhusu maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu: malaika na waumini humswalia Mtume, akasema:“Swala kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni rehema, kutoka kwa malaika ni kumsifu na kutoka kwa waumni ni kumwombea.”
Kuswaliwa huku hakuhusiki na risala ya Muhammad(s.a.w. w ) peke yake. Kila mtu anayetumia desturi ya risala ya Muhammad(s.a.w. w ) , kuifundisha au kuijulisha au kutaja fadhila yoyote katika fadhila zake basi atakuwa amemswalia, awe mumin au sio mumin, akitaka hilo au asitake.
Imam Ja’far As-Sadiq(a.s) anasema: “Mtu kumswalia Muhammad(s.a.w. w ) ni kama kusema:“Subhanallah walhamdulillah walailaha illaha wallahu akbar” (Kutakasika ni kwa Mwenyezi Mungu na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu na hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni mkubwa).
Imam hapa anakusudia kuwa thawabu za kumswalia Mtume ni sawa na thawabu za tasbih, tahmid, tahlil na takbir. Imepokewa Hadith kutoka kwa Mtume mtukufu(s.a.w. w ) , amesema:“Bakhili wa kweli ni yule ambaye nikitajwa mbele yake haniswalii” .
VIPI TUTAMSWALIA MTUME?
Katika Sahih Al-Bukhariy Juz. 8, mlango wa kumswalia mtume, Tafsir At- Tabariy, Tafsir Ar-Raziy, Tafsir Al-Maraghi na wafasiri wengineo, pia katika vitabu vya Hadith, kuna maelezo haya: “Mtume aliulizwa: Vipi tutakuswalia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?Akasema: semeni:
Allahumma swalli a’la muhammdi wa a’la aali Muhammad, kama swal-layta a’la Ibrahima wa a’laa aali Ibrahim, Innaka hamidum majiid Allahumma barik ala muhammdi wa a’la ali Muhammad, kama barakta a’la Ibrahima wa a’la ali Ibrahim, Innaka hamidum majid.
(Ewe Mwenyezi Mungu mswalie Muhammad na kizazi cha Muhammad, kama ulivyomswalia Ibrahim na kizazi cha Ibrahim, hakika wewe ni mwenye kusifiwa mwenye kutukuzwa. Ewe Mwenyezi Mungu mbariki Muhammad na kizazi cha Muhammad, kama ulivyombariki Ibrahim na kizazi cha Ibrahim. Hakika wewe ni Mwenye kusifiwa Mwenye kutukuzwa. )
Katika tafsir Ruhul-bayan ya Ismail Haqiy, amesema: “Inatakikana mwenye kuswali aseme: Allhumma swali a’la Muhammad wa a’la AliMuhammad” kwa kulirudia neno ‘a’la’; kwani Sunni wanaweka neno hilo kabla ya aali, kuwapinga Shia ambao hawaliweki neno hilo.
Sisi hatuoni tofauti yoyote baina ya anayesema: neno hilo na asiyelisema. Ama kuhusu ile Hadith isemayo:“Mwenye kutenganisha baina yangu na kizazi changu, hatapata shafaa yangu,” Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi usahihi wake.
Imam Shafii naye amesema katika shairi lenye maana hii: Enyi watu wa nyumba ya Mtume pendo lenu ni faradhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu amelieleza katika Qur’an. Inawatosha kuwa ni cheo kikuu kwamba nyinyi asiyewaswalia hana Swala
Hakika wale ambao wanamuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha.
Makusudio ya kumuudhi Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kumghadhabisha, na sababu yenye kuwajibisha hilo ni kumpinga, kumnasibishia mshirika au mtoto, au kuasi hukumu miongoni mwa hukumu zake. Na kuumuudhi Mtume(s.a.w. w ) ni kupinga utume wake au kupuuza mwenendo wake.
Laana kutoka kwa Mungu ni kwa kuwekwa mbali na rehema yake na kutoka kwa watu ni shutuma na kuombewa mabaya. Katika Nahjul-balagha imeelezwa:“Mwenyezi Mungu amewalaani wanaoamrisha mema na kuacha kuyatenda na wanaokataza maovu na wanayoyatenda.”
Na wale ambao wanawaudhi waumini wanaume na waumini wanawake pasi na wao kufanya, hakika wamebeba dhulma kubwa na dhambi kubwa.
Pasi na wao kufanya, yaani kufanya kosa linalostahili udhia. Kuudhi kunakuwa ni kwa kusengenya, vitimbi, uzushi n.k. Kuna Hadith zisemazo:
“Mwislamu ni yule ambaye watu wamesalimika na mkono wake na ulimi wake.”
“Utukufu wa mumin ni kwa kujizuia na kuwaudhi watu.”
“Aliye dhalili zaidi katika watu ni yule anayewadharau watu.”
Imam Ali(a.s) anasema:“ Mwenye hali mbaya zaidi katika watu ni yule asiyemwaamini yeyote kwa dhana zake mbaya, na asiyeaminiwa na yeyote kwa vitendo vyake vibaya.”
5
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥٩﴾
59. Ewe Nabii! Waambie wake zako na wake za waumini, wajiteremshie jalbab zao. Hilo ni karibu zaidi kuweza kujulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
لَّئِن لَّمْ يَنتَهِ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْمُرْجِفُونَ فِي الْمَدِينَةِ لَنُغْرِيَنَّكَ بِهِمْ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَا إِلَّا قَلِيلًا ﴿٦٠﴾
60. Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na wale wanaoeneza fitna Madina, hawataacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu.
مَّلْعُونِينَ أَيْنَمَا ثُقِفُوا أُخِذُوا وَقُتِّلُوا تَقْتِيلًا ﴿٦١﴾
61. Wamelaaniwa! Popote waonekanapo, na wakamatwe na wauliwe kabisa.
سُنَّةَ اللَّـهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلُ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّةِ اللَّـهِ تَبْدِيلًا ﴿٦٢﴾
62. Ni desturi ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa kwa wale waliopita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika desturi ya Mwenyezi Mungu.
WAJIBU WA HIJABU
Aya 59 – 62
LUGHA
Kuna kauli nyingi kuhusu neno Jalbab: kuna wanaosema kuwa ni nguo inayomfunika mwanamke kutoka kichwani hadi nyayoni. Wengine wakasema ni ushungi unaofunika kichwa cha mwanamke na uso wake. Kauli hii ndio aliyo nayo mwenye Majmaul-Bayan.
MAANA
Zimekwishatangulia Aya mbili zinazofahamisha wajibu wa hijabu kwa wanawake:
Ya kwanza ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Wala wasidhihirishe uzuri wao ila kwa waume zao.” Juz. 18 (24: 31). Ya pili ni ile Aya ya 53, katika Sura hii tuliyo nayo: “Na mnapowaomba chombo cha nyum- bani, basi waulizeni nyuma ya mapazia.”
Aya iliyo wazi zaidi ya hizi mbili ni hii tuliyo nayo, isemayo:
Ewe Nabii! Waambie wake zako na wake za waumini, wajiteremshie nguo zao.
Kusema kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘wajiteremshie nguo zao’ inaenea kusitiri na kufunika sehemu zote za mwili, kikiwemo kichwa na uso. Hilo linatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu:
Hilo ni karibu zaidi kuweza kujulikana wasiudhiwe.
Waislamu, mwanzoni walikuwa wakitoka bila ya kujitanda, kama ilivyokuwa desturi ya kijahiliya, ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamtaka Mtume wake mtukufu, katika Aya hii, awaamrishe wake zake kujisitiri na kuvaa hijabu. Na amri inafahamisha wajibu. Kwa hiyo hijabu ni wajibu.
Hata hivyo uso na viganja viwili havimo kwenye wajibu huu, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ﴿٣١﴾
“Wala wasionyeshe uzuri wao, isipokuwa unaodhihirika.” Juz. 18 (24:31).
Hilo ni karibu zaidi kuweza kujulikana kutokana na kujistahi na kujichunga. Kwani hijabu ni kinga baina ya mwanamke na tamaa ya watu wenye shakashaka na mafasiki,wasiudhiwe kwa kuangaliwa na mafasiki.
Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
Anasamehe yaliyopita na anamuhurumia mwenye kutubia na kurejea nyuma.
Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na wale wanaoeneza fitna Madina, hawataacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu.
Wanafiki walificha ukafiri na wakadhihirisha imani. Wanaoeneza fitna ni watu katika wananfiki waliokuwa wakieneza propaganda dhidi ya Mtume(s.a.w. w ) na maswahaba na wakawatia shaka wale wadhaifu wa imani ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaletea ibara ya wenye mardhi nyoyoni mwao. Aya inatoa onyo la kuuawa na kufukuzwa wanafiki, waeneza fitna na wale watakaowasikiliza, ikiwa hawatajizuia na upotevu na ufisadi wao.
VITA VYA NAFSI
Siku hizi kueneza fitna kunaitwa ‘vita vya nafsi.’ Nguvu ya shari imetafuta njia nyingi sana za kueneza uongo na mambo ya ubatilifu kwa kila nyenzo. Kuanzia magazeti, radio, runinga, sinema, hotuba, vipeperushi, shule, vyuo, vitabu n.k.
Vyombo hivi vimekaririka masikioni mwa watu kila siku, kiasi ambacho uhakika haupati nafasi kwa watu na wenye ikhlasi, isipokuwa kwa mwamko mkamilifu na elimu itakayotangulia propaganda za wakoloni na wazayuni.
Nimesoma kwenye gazeti linaloitwa Akhabar Al-yawm la Misr, la 13/12/69, kwamba Israil ina magazeti ya propaganda yanayofikia 890 ulimwenguni kwa ajili ya kueneza habari za uongo. Zaidi ya hayo wametawala vyombo vingi vya habari ulimwenguni, kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja; kama vile runinga, radio n.k.
Kwenye mahisabu haya hayaingii magazeti ya Beiruti yenye uhusiano mkubwa na wakoloni na wazayuni.
Kwa vyovyote iwavyo, Alhamdu lillah, Israil imehisi mapigo kutoka kwa waarabu na kwamba propaganda zao zilizotengenezwa na Marekani, na kutangazwa na vibaraka, zimeanza kujulikana.
Wamelaaniwa! Popote waonekanapo na wakamatwe na wauliwe kabisa.
Wamelaaaniwa na kila ulimi, kwa sababu dini yao ni pesa na matendo yao ni udanganyifu, uwongo na hadaa. Hawana dawa isipokuwa kuuawa popote walipo; kama kiungo kilichoharibika, kisipokatwa kitaharibu mwili wote.
Ni desturi ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa kwa wale waliopita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika desturi ya Mwenyezi Mungu.
Makusudio ya desturi ya Mwenyezi Mungu hapa ni hukumu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa mpotevu anayepoteza, ambayo ni kuuliwa ambako amekuwekea sharia, ambaye imetukuka hekima yake, tangu zamani. Hukumu hii itabakia milele bila ya mabadiliko wala mageuzi.
يَسْأَلُكَ النَّاسُ عَنِ السَّاعَةِ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ اللَّـهِ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا ﴿٦٣﴾
63. Watu wanakuuliza kuhusu Saa. Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu tu. Na nini kitakachokujulisha? Pengine hiyo saa iko karibu.
إِنَّ اللَّـهَ لَعَنَ الْكَافِرِينَ وَأَعَدَّ لَهُمْ سَعِيرًا ﴿٦٤﴾
64. Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri moto unaowaka.
خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا لَّا يَجِدُونَ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿٦٥﴾
65. Watadumu humo milele. Hawatapata mlinzi wala wa kuwanusuru.
يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّـهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا ﴿٦٦﴾
66. Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungelimtii Mwenyezi Mungu na tungelimtii Mtume!
وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا ﴿٦٧﴾
67. Na watasema: Mola wetu! Hakika sisi tuliwatii mabwana zetu na wakubwa wetu, wakatupoteza njia.
رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا ﴿٦٨﴾
68. Mola wetu wape adhabu mara mbili, na walaani laana kubwa.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ آذَوْا مُوسَىٰ فَبَرَّأَهُ اللَّـهُ مِمَّا قَالُوا وَكَانَ عِندَ اللَّـهِ وَجِيهًا ﴿٦٩﴾
69. Enyi ambao mmeamini! Msiwe kama wale ambao walimuudhi Musa, lakini Mwenyezi Mungu akamtaksa na waliyoyasema; naye alikuwa ni mwenye heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.
WANAKUULIZA KUHUSU SAA
Aya 63 – 69
MAANA
Watu wanakuuliza kuhusu Saa. Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu tu. Na nini kitakachokujulisha? Pengine hiyo saa iko karibu.
Makusudio ya saa ni Kiyama Umetangulia mfano wake katika Juz. 9 (7:187).
Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri moto unaowaka. Watadumu humo milele. Hawatapata mlinzi wala wa kuwanusuru. Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungelimtii Mwenyezi Mungu na tungelimtii Mtume!
Makafiri na waasi kesho watasukumwa kwenye adhabu ya moto, hawatakuwa na msaidizi wala udhuru. Watauma vidole vyao kwa kujutia walivyomuasi Mwenyezi Mungu na Mtume, lakini ‘majuto ni mjukuu.’
Umetangulia mfano wake katika Juz. 19 (25:27).
Na watasema: Mola wetu! Hakika sisi tuliwatii mabwana zetu na wakubwa wetu, wakatupoteza njia. Mola wetu wape adhabu mara mbili, na walaani laana kubwa.
Makusudio ya mabwana na wakubwa ni viongozi wa dini na dunia. Laana ni kufedheheka. Wadhaifu watawageuzia adhabu na watamtaka Mwenyezi Mungu awaongezee adhabu.
Mwenye kuichunguza historia ataona kwamba aghlabu umma wa kijinga unaongozwa na mataghuti na waovu. Lakini watu wenye mwamko na maarifa hawaamini kuweka masilahi yao isipokuwa kwa waaminifu wenye ikhlasi.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:38).
Enyi ambao mmeamini! Msiwe kama wale ambao walimuudhi Musa, lakini Mwenyezi Mungu akamtaksa na waliyoyasema; naye alikuwa ni mwenye heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.
Waliomuudhi Musa(a.s) ni Wana wa Israil, hilo halina shaka; ambapo walimsifu sifa zisizokuwa za mitume.
Aya hii inaashiria kwamba badhi ya swahaba walimuudhi Mtume mtukufu(s.a.w.w) na wakambandika mambo asiyokuwa nayo, ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawakataza waislamu hilo.
Kuna riwaya inayosema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) siku moja aliapa, basi mtu mmoja katika Answar akasema: “Kiapo hiki hakikusudiwa radhi ya Mwenyezi Mungu.” Hapo uso wa Mtume ukaiva wekundu na akasema:“Amrehemu Musa, hakika aliudhiwa zaidi ya hivi na akasubiri.”
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٧٠﴾
70. Enyi ambao mmeamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni kauli ya sawa.
يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا ﴿٧١﴾
71. Atawatengenezea matendo yenu na atawaghufiria dhambi zenu. Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amefuzu kufuzu kukubwa.
إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَن يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنسَانُ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا ﴿٧٢﴾
72. Kwa hakika tulizitolea amana mbingu na ardhi na milima na vikakataa kuichukua na vikaiogopa, lakini mwanadamu akaichukua. Hakika yeye ni dhalimu mkubwa, mjinga sana,
لِّيُعَذِّبَ اللَّـهُ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْمُشْرِكِينَ وَالْمُشْرِكَاتِ وَيَتُوبَ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٣﴾
73. Ili Mwenyezi Mungu awaadhibu wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na washirikina wanaume na washirikina wanawake; na awapokelee toba waumini wanaume na waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
TULIZITOLEA AMANA
Aya 70 – 73
MAANA
Enyi ambao mmeamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni kauli ya sawa. Atawatengenezea matendo yenu na atawaghufiria dhambi zenu.
Kauli ya sawa ni kusema haki na ukweli, bila ya kuficha kitu; hata kama inamuhusu mwenyewe. Makusudio yake hapa ni ile inayowanufaisha watu kwa kulinganisha na kauli yake Mwenyezi Mungu ‘Atawatengenezea amali zenu;’ ambapo Mwenyezi Mungu (s.w.t) amejaalia kauli ya haki ni sababu ya matendo mema; kwa mfano kumwongoza aliyepotea kwenye njia ya heri na amani, kumsaidia aliyedhulumiwa kwa neno la usawa au kauli ambayo italeta suluhu baina ya watu wawili na mengineyo yanay- owanufaisha watu kwa namna moja au nyingine.
Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amefuzu kufuzu kukubwa.
Atafuzu duniani kwa kufaulu na kuwa na sera nzuri na katika Akhera atafuzu kwa kupata radhi za Mwenyezi Mungu na thawabu zake.
Kwa hakika tulizitolea amana mbingu na ardhi na milima na vikakataa kuichukua na vikaiogopa, lakini mwanaadamu akaichukua.
Wafasiri wametofautiana kuhusu maana ya amana. Kuna waliosema kuwa ni taklifa na twaa. Wengine wakasema ni tamko la Lailaha illahha (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu). Kuna waliosema ni viungo vya mwanadamu; kama masikio yake, macho yake, mikono yake na miguu yake. Kwamba ni juu yake kuvitumia kwa ajili ya lengo lilioumbiwa. Pia kuna wale waliosema kuwa ni amana katika mali.
Tuonavyo sisi maana yake ni kujitolea muhanga kwa ajili ya manufaa ya jamii, si kwa lololote isipokuwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na ya ubinadamu.
Kwa sababu kujitolea huku ni kuzito na kukubwa kiasi ambacho maumbile yenye nguvu zaidi, kama mbingu, ardhi na majabali yangelikataa kubeba, kama yangelikuwa na hisia.
Kwa hiyo lengo la kutaja mbingu na ardhi ni kuashiria ukubwa wa kuji- tolea huku, na kwamba binadamu ni kiumbe pekee anayeweza kupingana na nafsi yake na matamanio yake.
Ama kauli yake Mwenyezi Mungu:Hakika yeye ni dhalimu mkubwa, mjinga sana, maana yake ni kuwa binadamu atajidhulumu yeye mwenyewe na mwingine ikiwa ataifanyia hiyana amana hii na kutojua mwisho muovu utakotokana na hiyana yake hiyo.
Ili Mwenyezi Mungu awaadhibu wanafiki wanaume na wanafiki wanawake ambao wanajionyesha kuwa wanatekeleza amana, lakini kumbe ni wahaini.
Na washirikina wanaume na washirikina wanawake. Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa vile kosa la ushirikina haliwezi kufutwa hata na kujitolea muhanga.
Na awapokelee toba waumini wanaume na waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
Yaani anawaghufiria wenye kutubia na kuwahurumia wanyonge. Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad na kizazi chake, rehema ambayo atatuombea nayo siku tutakapohitajia.
MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA TATU: SURAT AL-AHZAB
5
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
Sura Ya Thelathini na Nne: Surat Saba. Imeshuka Makka. Ina Aya 54.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَلَهُ الْحَمْدُ فِي الْآخِرَةِ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿١﴾
1. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na sifa ni zake katika Akhera. Naye ni Mwenye hekima, Mwenye habari.
يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا وَهُوَ الرَّحِيمُ الْغَفُورُ ﴿٢﴾
2. Anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni na yanayopanda huko na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwingi wa maghufira.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَأْتِينَا السَّاعَةُ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأْتِيَنَّكُمْ عَالِمِ الْغَيْبِ لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٣﴾
3. Na walisema wale ambao wamekufuru: Haitatufikia Saa. Sema: Ndio! Naapa kwa Mola wangu, itawafikia. Mjuzi wa ghaibu. Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo katika hivyo wala kikubwa zaidi; ila vimo katika Kitabu chenye kubainisha.
لِّيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ ﴿٤﴾
4. Ili awalipe wale ambao wameamini na wakatenda mema. Hao watapata maghufira na riziki yenye heshima.
وَالَّذِينَ سَعَوْا فِي آيَاتِنَا مُعَاجِزِينَ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مِّن رِّجْزٍ أَلِيمٌ ﴿٥﴾
5. Na wale ambao wamehangaika kuzipinga ishara zetu wakiona watashinda, hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu.
وَيَرَى الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ الَّذِي أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ هُوَ الْحَقَّ وَيَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿٦﴾
6. Na wale ambao wamepewa ilimu wanaona kuwa uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako ni haki na huongoza kwenye njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.
SIFA NJEMA ZOTE NI ZA MWENYEZI MUNGU
Aya 1 – 6
MAANA
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na sifa ni zake katika Akhera. Naye ni Mwenye hekima, Mwenye habari.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye kustahiki kusifiwa kwa sifa njema katika nyumba mbili. Ni mmliki wa ulimwengu na mpangiliaji wake kwa vyote vilivyomo ndani yake, kulingana na elimu yake na hekima yake.
Kwenye Nahjul-Balagha, imesemwa: “Tunamsifu kwa ukubwa wa hisani yake na wema wa dalili yake na ziada ya fahila zake na neema zake. Sifa ambazo ni haki yake (sisi) kuzitekeleza na kulipa shukrani zake na kujikurubisha kwenye thawabu zake na kutaka ziada ya wema wake.”
Anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo na yanayoteremka kutoka mbinguni na yanayopanda huko na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwingi wa maghufira.
Maana ya Aya hii yamekaririka katika Aya kadhaa; ikiwemo Juz. 7 (6:59) na Juz. Juz. 11 (10:61). Ufupisho wake ni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Na walisema wale ambao wamekufuru: Haitatufikia saa ya Kiyama. Sema: Ndio! Naapa kwa Mola wangu, itawafikia.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 11(10:53).
Mjuzi wa ghaibu. Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo katika hivyo wala kikubwa zaidi; ila vimo katika Kitabu chenye kubainisha.
Kitabu chenye kubainisha ni kinaya cha kuhifadhi. Maana ni kuwa hakuna anayejua wakati wa Kiyama isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake. Tazama Juz. 9 (7:187).
Ili awalipe wale ambao wameamini na wakatenda mema. Hao watapata maghufira na riziki yenye heshima. Na wale ambao wamehangaika kuzipinga ishara zetu wakiona watashinda, hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu.
Huu ni ubainifu wa hekima ya ufufuo, ambayo ni kulipwa mema waliofanya wema na wale waliofanya uovu walipwe kwa uovu wao. Tazama Juz. 11 (10:3-4). Kifungu cha “Hisabu na malipo ni lazima.”
Na wale ambao wamepewa ilimu wanaona kuwa uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako ni haki na huongoza kwenye njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.
Makusudio ya wale waliopewa ilimu ni kila mwenye ilimu aliye na insafu, wakati wowote na mahali potepote. Na makusudio ya uliyoteremshiwa ni Qur’an. Maana ni kuwa yeyote mwenye ilimu atakayeisoma Qur’an kiusahihi, lazima ataishia kuwa ni haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu; kwa sababu iko sawasawa kwenye itikadi yake, sharia yake na mafunzo yake yote.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا هَلْ نَدُلُّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ يُنَبِّئُكُمْ إِذَا مُزِّقْتُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّكُمْ لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ ﴿٧﴾
7. Na wale ambao wamekufuru walisema: Je, tuwajulishe mtu anayewaambia mtakapocham- buliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya?
أَفْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَم بِهِ جِنَّةٌ بَلِ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ فِي الْعَذَابِ وَالضَّلَالِ الْبَعِيدِ ﴿٨﴾
8. Amemzulia Mwenyezi Mungu au ana wazimu? Bali wale ambao hawaamini akhera wamo adhabuni na upotofu wa mbali.
أَفَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِن نَّشَأْ نَخْسِفْ بِهِمُ الْأَرْضَ أَوْ نُسْقِطْ عَلَيْهِمْ كِسَفًا مِّنَ السَّمَاءِ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ ﴿٩﴾
9. Je, hawaoni yaliyo mbele yao na nyuma yao ya mbingu na ardhi. Tungelipenda tungeliwadidimiza ardhini, au tungeliwateremshia vipande vya mbingu. Hakika katika hayo kuna ishara kwa kila mja aliyetubia.
WANAOPINGA SIKU YA MWISHO
Aya 7 – 9
MAANA
Na wale ambao wamekufuru walisema: Je, tuwajulishe mtu anayewaambia mtakapochambuliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya? Amemzulia Mwenyezi Mungu au ana wazimu?
Hivi ndivyo washirikina walivyomwambia Muhammad, ni muongo au mwendawazimu – Mungu apishie mbali. Kwa nini walisema neno la ukafiri kama hilo? Ni Kwa sababu Mtume aliwaambia kuwa mtu atafu- fuliwa baada ya mauti. Hawana dalili yoyote ya kupinga kwao huku isipokuwa kushangaa tu; kama walivyosema:
أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ ﴿٥﴾
“Amewafanya miungu wote kuwa ni mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu.” (38: 5).
Hali yao hii, kama inavyonekana, inategemea vile wanavyofikiria. Maana yake ni kupinga hali halisi kwa fikra na mawazo; pamoja na kuwa fikra haiwi ya kweli ila ikiwa inaakisi hali halisi na kwamba yeyote anayeikum- batia nadharia yoyote hana budi kutafuta dalili ya ukweli wake kwa kuweko uhalisi unaoitafsiri, na haifai kukana uhalisi kwa fikra isiyokuwa na msingi wowote.
Katika hili Imam Ali(a.s) anaashiria kwa kusema:“Watu wanajulikana kwa haki, wala haki haijulikani kwa watu.”
Bali wale ambao hawaamini akhera wamo adhabuni na upotofu wa mbali.
Hao ni wajinga na wapotevu, kwa sababu wameipima haki na uhalisi kwa fikra zao na mawazo yao; na walitakiwa wapime fikra zao kwa haki na uhalisi.
Je, hawaoni yaliyo mbele yao na nyuma yao ya mbingu na ardhi.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawaambia wakadhibishaji: Kuna ajabu gani ya kufufuliwa kwenu baada ya mauti:
أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم ﴿٨١﴾
“Kwani aliyeziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao?” (36:81).
Je, umbile hili halifahamishi umoja wake na ukamilifu wa uweza wake; ukiwemo kuwarudisha watu baada ya mauti?
Tumelizungumzia hilo mara nyingi. Tazama Juz. 1 (2:28 -29), Juz. 5 (4:85 – 87) na Juz. 11 (10:3–4).
Tungelipenda tungeliwadidimiza ardhini, au tungeliwateremshia vipande vya mbingu. Hakika katika hayo kuna ishara kwa kila mja aliyetubia.
Hayo ni ishara ya kuumba mbingu na ardhi. Kwa sabubu hilo, kwa mwenye akili, linafahamisha ukuu wa Mwenyezi Mungu na uweza wake wa kuipa uhai mifupa iliyochakafuka. Ama kauli yake Mwenyezi Mungu:
‘Tungelipenda tungeliwadidimiza ardhini,’ ni karipio na makemeo kwa yule anayepinga siku ya mwisho, kwamba anaweza kumezwa na ardhi au kupigwa na kimondo kutoka mbinguni, kimuunguze.
وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ مِنَّا فَضْلًا يَا جِبَالُ أَوِّبِي مَعَهُ وَالطَّيْرَ وَأَلَنَّا لَهُ الْحَدِيدَ ﴿١٠﴾
10. Na kwa hakika tulimpa Daud fadhila kutoka kwetu. Enyi milima sabihini pamoja naye na ndege. Na tukamlainishia chuma.
أَنِ اعْمَلْ سَابِغَاتٍ وَقَدِّرْ فِي السَّرْدِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١١﴾
11. Kwamba utengeneze nguo za chuma pana na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika ninayaona mnayotenda.
وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ غُدُوُّهَا شَهْرٌ وَرَوَاحُهَا شَهْرٌ وَأَسَلْنَا لَهُ عَيْنَ الْقِطْرِ وَمِنَ الْجِنِّ مَن يَعْمَلُ بَيْنَ يَدَيْهِ بِإِذْنِ رَبِّهِ وَمَن يَزِغْ مِنْهُمْ عَنْ أَمْرِنَا نُذِقْهُ مِنْ عَذَابِ السَّعِيرِ ﴿١٢﴾
12. Na kwa Suleiman upepo. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamtiririshia chemchem ya shaba. Na katika majini kuna waliofanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake. Na anayejitenga na amri katika wao tunamwonjesha adhabu ya moto unaowaka.
يَعْمَلُونَ لَهُ مَا يَشَاءُ مِن مَّحَارِيبَ وَتَمَاثِيلَ وَجِفَانٍ كَالْجَوَابِ وَقُدُورٍ رَّاسِيَاتٍ اعْمَلُوا آلَ دَاوُودَ شُكْرًا وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ ﴿١٣﴾
13. Wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu na masanamu na sinia kubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yasiyoondoka mahali pake. Fanyeni amali enyi watu wa Daud kwa kushukuru. Ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru.
فَلَمَّا قَضَيْنَا عَلَيْهِ الْمَوْتَ مَا دَلَّهُمْ عَلَىٰ مَوْتِهِ إِلَّا دَابَّةُ الْأَرْضِ تَأْكُلُ مِنسَأَتَهُ فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ الْجِنُّ أَن لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ الْغَيْبَ مَا لَبِثُوا فِي الْعَذَابِ الْمُهِينِ ﴿١٤﴾
14. Tulipomkidhia mauti, hapana aliyewajulisha mauti yake ila mnyama wa ardhi aliyekula fimbo yake. Alipoanguka majini walitambua lau kuwa wangelijua ya ghaibu wasingelikaa katika adhabu ya kufedhehesha.
DAUD NA SULEIMAN
Aya 10 – 14
MAANA
Na kwa hakika tulimpa Daud fadhila kutoka kwetu. Enyi milima sabihini pamoja naye na ndege. Na tukamlainishia chuma.
Katika Juz. 6 (4:163) Mwenyezi Mungu anasema: “Na Daud tukamapa Zaburi,” kwenye Juz. 19 (27:15) anasema: “Na hakika tulimpa Daud na Suleiman elimu” na kwenye Aya hii tuliyo nayo anaseama kuwa amempa neema ya sauti nzuri ambayo ilikuwa inakurubia kwenda sambamba na sauti ya milima na ndege.
Katika Juz. 17 (21:79) tulisema kuwa inawezekana kuwa tasbihi ya milima na ndege ni tasbihi halisi hasa pamoja na Daud, Kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. Kuna msemaji aliyesema kuwa makusudio ya kusabihi milima na ndege pamoja na Suleimani ni kuwa ilikuwa ikimfanya asabihi; alipokuwa akiiona husema: “Subhana man khalaqa wa swawwara...” (Kutakasika ni kwa aliyeumba na akatia sura...).
Pia Mwenyezi Mungu alimneeemesha Daud kwa kukifanya chuma vile anavyotaka yeye bila ya kukitia motoni au kukigonga na nyundo. Inawezekana kuwa Mwenyezi Mungu alimfahamisha sababu na nyenzo za kukilainisha chuma.
Kwamba utengeneze nguo za chuma pana na kadiria sawa katika kuunganisha.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Daud atengeneze deraya kutokana na chuma na atengeneze vizuri kuzuia panga mishale na mikuki na ziwe pana kwa namna ambayo mvaaji haitamzuia na harakati zozote.
Na tendeni mema. Hakika ninayaona mnayotenda.
Maneno yanaelekezwa kwa Daud na kizazi chake. Mwenyezi Mungu anawaamrisha wafanye mema na kuwa ameayaandalia malipo na thawabu. Umetangulia mfano wa Aya mbili hizi katika Juz. 17 (21:79 – 80).
Na kwa Suleiman upepo. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja.
Dhahiri ya Aya inaonyesha kuwa upepo ulikuwa ukimchukua Suleiman, anakotaka, kwa amri ya Mungu na kwamba masafa ya mwezi mzima kwa ngamia au kutembea kwa miguu alikuwa akienda kwa asubuhi moja na vile vile jioni.
Na tukamtiririshia chemchemi ya shaba.
Makusudio ya kumtiririshia hapa ni kumyeyushia. Yaani Mwenyezi Mungu Mtukufu alimyeyushia chuma Suleimani kama alivyomyeyushia baba yake Daud. Inawezekana kuwa Mwenyezi Mungu alimuongoza kwenye sababu za kuyeyusha.
Na katika majini kuna waliofanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake. Na anayejitenga na amri katika wao tunamwonjesha adhabu ya moto unaowaka. Wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu na masanamu na sinia kubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yasiyoondoka mahali pake.
Imetangulia pamoja na tafsiri yake katika Juz. 17 (21:82).
Fanyeni amali enyi watu wa Daud kwa kushukuru. Ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru.
Ibn Al-arabi ameitaja Aya hii katika Futuhat Juz. 4, akasema: Shukrani ni kuiona neema kuwa imetoka kwa Mungu si kwa mwingine. Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimpa wahyi Musa akamwambia: Nishukuru kwa haki ya kushukuru. Akasema Musa: “Ni nani anayeweza hilo ewe Mola?” Akamwambia: “Ikiwa unaona neema imetokana na mimi basi umenishukuru.”
Tulipomkidhia mauti, hapana aliyewajulisha mauti yake ila mnyama wa ardhi aliyekula fimbo yake. Alipoanguka majini walitambua lau kuwa wangelijua ya ghaibu wasingelikaa katika adhabu ya kufedhehesha.
Aliyekidhiwa na mauti ni Suleiman. Mnyama wa ardhi ni mchwa anayekula miti. Maana ni kuwa Suleimani alifikiwa na mauti akiwa ameegemea fimbo yake; akabakia hivyo mpaka muda aliotaka Mwenyezi Mungu, majini na watu wakimwangalia na kumdhania kuwa yuko hai, mpaka pale mchwa walipokula fimbo yake kwa ndani, ikavunjika na Suleiman akaanguka; hapo wote wakajua kuwa amekufa; ikadhihirika kwa watu kuwa majini hawajui ghaibu. Kwa sababu lau wangelijua basi wasingelikuwa katika utumishi wa Suleiman akiwa ni maiti.
Ikiwa baadhi ya yaliyo katika Aya hii yanaonekana, kwa kawaida, ni vigumu kutokea, lakini kiakili inakubalika kutokea. Ndio maana tunayasadiki na kuyakubali; tukiwa tunaamini msingi wa wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Mtume(s.a.w. w ) wake mtukufu.
Tazama Juz. 3 (3:45 – 51) kifungu cha “Lisilowezekana kiakili na kidesturi.”
KUPINGA FIKRA YA KIDINI
Kutoka na kutajwa majini na mambo yasiyo ya kawaida katika Aya hii, ni vizuri tutaje yaliyoelezwa kwenye kitabu kilichotoka hivi karibuni, kina- choitwa Naqdu lfikri ddiniy. (Kupinga fikra ya kidini).
Hivi sasa tuko katika mwezi wa Novemba 1969. Yamezungumzwa mengi kuhusu kitabu hicho na mtungaji wake. Mwenye kusoma kitabu hicho mara moja atamhukumu mtungaji wake kuwa ana shaka na wasiwasi na dini zote. Hilo amelisema waziwazi kwenye Uk. 29, 77 na nyinginezo.
Lakini mwenye kukifuatilia kitabu na kuchukua dhahiri yake, ataona kuwa yaliyopelekea shaka na wasiwasi huu ni mambo yafutayo:
Kwanza : Kujaribu baadhi ya waumini kulazimisha kuoanisha nukuu za Qur’an na ugunduzi wa kisayansi, na kuzama sana kuleta taawili iliyo mbali na matamshi. Mtunzi wa kitabu hicho amelitolea ushahidi mwingi hilo, yakiwemo yale aliyoyanukuu katika Uk. 37, kwamba ugunduzi wa chembe za mwanga unafahamisha kuweko malaika na majini.
Mtungaji akielezea kauli hii alisema: “Sijui kuna uhusiano gani baina ya nadharia ya mwanga na kuweko majini.”
Pili : Mazoweya na nembo za kidini zilizoganda haziendani na maendeleo ya karne ya ishirini; kama anavyodai mwandishi.
Tatu: Baadhi ya wakuu wa dini kuunga mkono ukabaila na ukoloni kwa kutumia jina na Uislamu au Ukristo. Kitabu kimejaa ushahidi wa hilo; kama vile kwenye uk. 23: “Dini huko ulaya ilikuwa rafiki mkubwa wa serikali za kikabaila, hali ambayo inaendelea hadi sasa katika miji mbalimbali, hasa ndani ya miji ya kiarabu na nje, na vile dini inavyoungana moja kwa moja na ukoloni mambo leo unaongozwa na Marekani.”
Mtungaji aliongeza katika kupinga kitabu “Almasihiyya wal Islamu fi Lubnan” (Ukiristo na Uislmu Lebanon) ambacho ni mkusanyiko wa mihadhara ya Lebanon ya mwaka 1965, iliyotolewa na wakuu wa kidini wane: mmoja wa kisunni, mwengine wa kishia na wawili wa kikiristo.
Na wengine wane wa wasiokuwa na dini yoyote, lakini walizungungumza kwa niaba ya dini. Wote wakamwahidi Mwenyezi Mungu kuwa watafanya bidii ya kudumu kuondoa pingamizi zinazowekwa baina ya Uislamu na ukiristo.
Miongoni mwa aliyoyasema mtungaji huyu, katika kuwarudi wale waliotoa ahadi, ni yale yaliyo katika ukurasa wa 64, wa Kitabu chake hicho: “Lengo la kwanza la mihadhara na ahadi hizo ni wakristo kuunga mkono serkali ya Lebanon, kwa vile inawanufaisha wao zaidi kuliko waislamu walio na ufukara sana.
Baadhi ya waislamu nao wanaikubali serikali na kuungana na wakiristo, na kuaiachia serikali usimamizi wote wa kisiasa, kijamii na kiuchumi, si kwa lolote ila ni kwa kuwa wanapata manufaa fulani na faida kutoka serikalini. Kiasi ambacho maovu ya serikali yamesahaulika na kuelekea kwenye nembo ya mshikamano wa wakiristo na waislamu.”
Dalili mkataa kuwa malengo ni masilahi sio mshikamano wa kidini, mwandishi anaiweka wazi kwenye Uk. 60, katika kitabu chake, akisema: “Hakika Uislamu hauikubali Biblia, utatu, mhanga, kusulubiwa Bwana Masih, kuzikwa kwake na kutoka kwake kaburini n.k. Kama ambavyo wakiristo nao hawaikubali Qur’an wala utume wa Muhammad(s.a.w. w ) n.k. Sasa hawa wahadhiri na ahadi zao wataondoa vipi pingamizi hizi? Usawa hasa ni kufahamiana na kuelewena Walebanoni kwa uzalendo wao tu na misingi ya ushirikiano kwa masilahi yao, lakini dini aachiwe hiyari kila mtu kulingana na alivyokinai na mazoweya yake.”
Kutokana na kauli ya mwandishi huyu na wengineo wengi, katika kupinga fikra ya dini, inatubainikia kuwa siri ya upinzani wao, kama tulivyodokeza mwanzoni, imetokana na wakuu wa dini kuukumbatia ukoloni, udhalimu na ukandamizaji na kuupamba kwa jina la dini.
Lau wakuu wote wa dini wangeifanyia ikhlasi, wakaifahamisha kwa ufahamu sahihi na wakaibanisha kama alivyoiteremsha Isa na Muhammad na wasiiuze kwa thamani ndogo, basi wapinzani au washambulizi wa kulipwa wasingelipata mwanya wa kuituhumu au kuwa na shaka na dini ya kiislamu wala ya kikiristo.
Lakini jambo la kuvunja moyo ni kuwa watu wamelitumia jina la dini kwa uzushi na wengine wakasimama kuiharibu na kuingiza shaka baada ya kulipwa na maadui wa Mwenyezi Mungu; ndio ikawa radiamali hii kuto- ka kwa mwandishi huyu wa kitabu ‘Kupinga fikra ya dini’ na wengineo. Inasemekana pia mwandishi huyu ni katika wanaolipwa.
Hata hivyo, kwani dini itakuwa imekosea nini ikituhumiwa na wazushi na wenye upendeleo? Ilitakikana mwandishi aangalie ushahidi mwingi ulio katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na suna za Mtume wake na pia katika historia ya Uislamu kuwa dini ni nguvu inayomwelekeza mtu kwenye maisha bora na kwamaba iko mbali na kila jambo lisiloingilika akilini na kugongana na hakika ya maisha.
Hakika hii wanakubaliana nayo wataalamu wengi wa mashariki na wa magharibi wasiokuwa waislamu. Tazama Juz. 1 (2:1-5) kifungu cha ‘Qur’an na Sayansi,’ Juz. 9 (8:24) kifungu cha ‘Dini na maisha,’ na Juz. 15 (17:9-12) kifungu cha ‘Uislamu ni dini ya maumbile.
6
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
لَقَدْ كَانَ لِسَبَإٍ فِي مَسْكَنِهِمْ آيَةٌ جَنَّتَانِ عَن يَمِينٍ وَشِمَالٍ كُلُوا مِن رِّزْقِ رَبِّكُمْ وَاشْكُرُوا لَهُ بَلْدَةٌ طَيِّبَةٌ وَرَبٌّ غَفُورٌ ﴿١٥﴾
15. Hakika ilikuwa ishara kwa wasabaa katika maskani yaobustani mbili, kulia na kushoto. Kuleni katika riziki ya Mola wenu na mumshukuru. Mji mzuri na Mola mwenye maghufira.
فَأَعْرَضُوا فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ سَيْلَ الْعَرِمِ وَبَدَّلْنَاهُم بِجَنَّتَيْهِمْ جَنَّتَيْنِ ذَوَاتَيْ أُكُلٍ خَمْطٍ وَأَثْلٍ وَشَيْءٍ مِّن سِدْرٍ قَلِيلٍ ﴿١٦﴾
16. Lakini wakaacha, basi tukawapelekea mafuriko makubwa na tukawabadilishia bustani zao kwa bustani nyingine mbili zenye matunda makali na mivinje na miti michache ya kunazi.
ذَٰلِكَ جَزَيْنَاهُم بِمَا كَفَرُوا وَهَلْ نُجَازِي إِلَّا الْكَفُورَ ﴿١٧﴾
17. Hayo tuliwalipa kwa vile walikufuru, nasi kwani tunamwadhibu isipokuwa anayekufuru?
وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ الْقُرَى الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا قُرًى ظَاهِرَةً وَقَدَّرْنَا فِيهَا السَّيْرَ سِيرُوا فِيهَا لَيَالِيَ وَأَيَّامًا آمِنِينَ ﴿١٨﴾
18. Na baina yao na miji mingine tuliyoibariki, tuliweka miji iliyo dhahiri na tukaweka humo vituo vya safari: Nendeni humo usiku na mchana kwa amani.
فَقَالُوا رَبَّنَا بَاعِدْ بَيْنَ أَسْفَارِنَا وَظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ فَجَعَلْنَاهُمْ أَحَادِيثَ وَمَزَّقْنَاهُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ ﴿١٩﴾
19. Wakasema: Mola wetu, weka mwendo mrefu baina ya safari zetu. Na wakazidhulumu nafsi zao. Basi tukawafanya ni masimulizi na tukawatawanyatawanya. Hakika katika hayo, bila shaka kuna ishara kwa kila aliye na subira sana mwenye kushukuru.
وَلَقَدْ صَدَّقَ عَلَيْهِمْ إِبْلِيسُ ظَنَّهُ فَاتَّبَعُوهُ إِلَّا فَرِيقًا مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٠﴾
20. Na hakika Ibilisi alisadikisha dhana yake juu yao. Na walimfuata isipokuwa kundi la waumini.
وَمَا كَانَ لَهُ عَلَيْهِم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يُؤْمِنُ بِالْآخِرَةِ مِمَّنْ هُوَ مِنْهَا فِي شَكٍّ وَرَبُّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ ﴿٢١﴾
21. Naye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao, ila ni kwa sababu tujue ni nani mwenye kuamini Akhera na nani anayetilia shaka. Na Mola wako ni mwenye kuhifadhi kila kitu.
SABAA
Aya 15 – 21
LUGHA
Sabaa ni jina la kabila la waarabu, lililotokana na jina la baba ambaye kizazi chao kinatokana naye.
KISA KWA UFUPI
Katika Tarikh almas’ud imeelezwa kuwa mfalme wa kwanza wa Yemen alikuwa ni Sabaa bin Yashjab bin Ya’arab bin Qahtan. Jina lake hasa lilikuwa ni Abdu Shams. Aliitwa Sabaa kutokana na kuchukua kwake mateka[2] . Ardhi ya Sabaa ilikuwa ndio ardhi yenye rutuba na utajiri zaidi katika Yemen.
Kabla yake, ardhi hiyo, ilikuwa ikikumbwa na mafuriko yaliyoangamiza mimea na majengo. Basi akawakusanya wataalamu wa zama hizo kutafuta suluhisho la tatizo hilo. Wakaafikiana kujengwe ukuta baina ya milima miwili na kuweka mlango wa kuyafungulia maji kwa kiasi wanachokitaka.
Ukuta huu ulijulikana kwa jina la mji wa Maaribu uliokuwa karibu na ukuta. Kadiri siku zilivyoendelea kupita ndivyo maji nayo yalivyoongezeka, ukuta ukaharibika na maji yakavunja majumba na mashamba. Watu wakagura na wakatawanyika sehemu kadhaa za nchi. Hapa ndipo ilipochukuliwa mithali: ‘Mikono ya sabaa imetawanyika.’
Katika Tafsir At-Tabari na Majmaul-Bayan imeelezwa kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) kuhusu Sabaa, akasema: ‘Kulikuwa na mtu mmoja mwarabu aliyekuwa na watoto kumi, sita katika wao walikwenda upande wa Yemen na wane wakaenda upande wa Sham.
Waliokwenda upande wa Yemen ni: Kinda, Himyar, Azd, Ash’ar, Madh-hij na Anmar, miongoni mwao ni Khath’am na Bujayla. Ama wale waliokwenda upande wa Sham ni: Amila, Judham, Lakhmu na Ghassan.
Katika Tafsir Al-Ma raghi imeelezwa kuwa watafiti walikuwa wakitilia shaka jambo hili la ukuta, mpaka mgunduzi wa kifaransa Arno alipoweza kufika Maarib mnamo mwaka 1843 na akaona athari yake na kuweza kuchora picha iliyosambazwa kwenye magazeti ya ufaransa mwaka 1874. Baadaye Halevi na Glazr, wakatembelea sehemu hiyo, wakaafikiana na aliyoyasema.
MAANA
Hakika ilikuwa ishara kwa wasabaa katika maskani yaobustani mbili, kulia na kushoto. Kuleni katika riziki ya Mola wenu na mumshukuru. Mji mzuri na Mola mwenye maghufira.
Ishara ni dalili na alama ya neema za Mwenyezi Mungu zilizo nyingi katika mji huo. Bustani mbili kulia na kushoto, ni kinaya cha rutuba na mazao mengi yaliyopatikana kila pembe ya mji huo. Kila aliyepita ardhi ya Sabaa aliweza kuona mazao mengi kulia na kushoto.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwaamrisha watu wa Sabaa, kupitia kwa manabii na Mitume wake, kuwa waneemeke na kheri zake na wamshukuru na wampwekeshe.
Lakini wakaacha, basi tukawapelekea mafuriko makubwa na tukawabadilishia bustani zao kwa bustani nyingine mbili zenye matunda makali na mivinje na miti michache ya mikunazi.
Neema ya Mwenyezi Mungu waliitumia kwa kumuuasi. Akawahadharisha kupitia Mitume wake, lakini halikuwafaa onyo wala kuzingatia mawaidha. Basi Mwenyezi Mungu akawapelekea mafuriko yaliyobomoa ukuta na kuharibu mimea. Mwenyezi Mungu akabadilisha bustani za matunda na konde za mazao kwa miti isiyoshibisha; kama vile: mikwaju, mikunazi na mingineyo inayomea jangwani ambayo wanakula wanyama wenye njaa au mtu aliyeishiwa kabisa.
Hayo tuliwalipa kwa vile walikufuru, nasi kwani tunamwadhibu isipokuwa anayekufuru?
Aliwalipa ufukara, ambao ni malipo ya kufedhehesha zaidi. Kuna Hadith isemayo: “Ufukara unakurubia kuwa ni ukafiri.” Nyingine inasema: “Ufukara unasawijisha uso duniani na akhera.” Imam Ali(a.s) alimwambia mwanawe Muhammad Al-Hanafiya: “Hakika ufukara unapunguza dini –yaani unampeleka mtu kumwasi Mwenyezi Mungu – unazubaisha akili na unaita mateso.”
Na baina yao na miji mingine tuliyoibariki, tuliweka miji iliyo dhahiri na tukaweka humo vituo vya safari: Nendeni humo usiku na mchana kwa amani.
Baina yao ni watu wa Sabaa. Makusudio ya miji ni Sham – kama walivyosema wafasiri-ambao Mwenyezi Mungu aliubariki kwa maji, miti, rutuba na matunda. Iliyodhahiri maana yake ni kuwa karibu ikijitokeza na kuonana.
Kuweka vituo vya safari baina ya mji mmoja na mwengine; kiasi ambacho msafiri anakuwa kwenye mji mmoja asubuhi na jioni anakuwa kwenye mji mwingine. Aya inausifia mji wa Sabaa kabla ya kuharibika. Maana yake ni kuwa miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu na fadhila zake ni kuwa anayetaka kusafiri anakuwa kwenye amani ya nafsi yake na mali yake na hakuwa na haja ya kuchukua masurufu ya safari au kuhofia kiu wala njaa.
Lakini wakachoka na neema wakasema: Mola wetu weka mwendo mrefu baina ya safari zetu.
Yaani weka mbuga na nyika ili tutafute usafiri na tuchukue masurufu ya safari; sawa na walivyofanya wana wa israil walipochoka na Manna na Salwa na kumwambia Musa: “Basi tuombee
Mola wako atutolee vile vinavyooteshwa na ardhi miongoni mwa mboga zake, na matango yake na ngano yake na adesi zake na vitunguu vyake. Akasema: ‘Mnabadili vitu duni kwa vile vilivyo bora?” Juz.1(2:61).
Na wakazidhulumu nafsi zao kwa kupituka mipaka na kukufuru neema. Basi tukawafanya ni masimulizi na tukawatawanyatawanya. Hakika katika hayo, bila shaka kuna ishara kwa kila aliye na subira sana mwenye kushukuru.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwatawanya ardhini mpaka wakawa ni historia kwa vizazi na mazingatio kwa mwenye kuvumilia shida na akushukuru wakati wa raha.
Na hakika Ibilisi alisadikisha dhana yake juu yao. Na walimfuata isipokuwa kundi la waumini. Naye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao.
Shetani aliwahadaa wamuasi Mwenyezi Mungu; wakamsikiliza na kumtii wale waliopetuka mipaka na kukufuru na wakamwasi wale walioamini na kuwa na takua. Aya hii inaashiria kauli ya Ibilisi aliposema:
وَلَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٣٩﴾ إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ ﴿٤٠﴾ قَالَ هَـٰذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ ﴿٤١﴾ إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ ﴿٤٢﴾
“Na nitawapoteza wote; isipokuwa waja wako waliosafishwa. Akasema (Mwenyezi Mungu): Hii ni njia juu yangu mimi iliyonyooka. Hakika waja wangu hutakuwa na mamlaka nao, isipokuwa wale wapotofu waliokufua- ta.” Juz. 14 (15:39 – 42).
Ila ni kwa sababu tujue ni nani mwenye kuamini Akhera na nani anayetilia shaka.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawajua zaidi waja wake kuliko wao wenyewe, lakini anawajaribu kwa raha na dhiki na kwa matamanio na hawaa, ili awadhihirishe ulimwenguni na yaonekane makusudio yao na vitendo vyao ambavyo vinastahiki thawabu na adhabu.
Maana ya Aya hii yamekaririka mara nyingi, ikiwemo Juz. 4 (3: 140).
Na Mola wako ni mwenye kuhifadhi kila kitu.
Hakimpotei chochote kilichomo mbinguni wala ardhini. Kuna Hadith isemayo: “Mche Mwenyezi Mungu kama kwamba wewe unamuona; ukiwa humuoni basi Yeye anakuona.”
قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ ﴿٢٢﴾
22. Sema: Waombeni hao mnaodai kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu. Hawamiliki hata chembe katika mbingu wala ardhini. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala hawana msaidizi miongoni mwao.
وَلَا تَنفَعُ الشَّفَاعَةُ عِندَهُ إِلَّا لِمَنْ أَذِنَ لَهُ حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ ﴿٢٣﴾
23. Wala hautafaa uombezi mbele yake ila kwa yule aliyempa idhini. Hata itakapoondolewa fazaa kwenye nyoyo zao, watasema: Kasema nini Mola wenu? Watasema: Haki, naye ndiye aliye juu, Mkubwa.
قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّـهُ وَإِنَّا أَوْ إِيَّاكُمْ لَعَلَىٰ هُدًى أَوْ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢٤﴾
24. Sema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini? Sema, ni Mwenyezi Mungu! Na hakika sisi au nyinyi bila shaka tuko kwenye uongofu au upotofu ulio wazi.
قُل لَّا تُسْأَلُونَ عَمَّا أَجْرَمْنَا وَلَا نُسْأَلُ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٢٥﴾
25. Sema: Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyoyafanya wala sisi hatutaulizwa kwa mnayoyatenda.
قُلْ يَجْمَعُ بَيْنَنَا رَبُّنَا ثُمَّ يَفْتَحُ بَيْنَنَا بِالْحَقِّ وَهُوَ الْفَتَّاحُ الْعَلِيمُ ﴿٢٦﴾
26. Sema: Mola wetu atatukusanya kisha atatuhukumu kwa haki, naye ndiye Hakimu, Mjuzi.
قُلْ أَرُونِيَ الَّذِينَ أَلْحَقْتُم بِهِ شُرَكَاءَ كَلَّا بَلْ هُوَ اللَّـهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٧﴾
27. Sema: Nionyesheni wale mliowaunganisha naye kuwa washirika. Hapana! Bali Yeye ni Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾
28. Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mtoaji bishara na muonyaji, lakini watu wengi hawajui.
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٩﴾
29. Na wanasema: Ni lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli?
قُل لَّكُم مِّيعَادُ يَوْمٍ لَّا تَسْتَأْخِرُونَ عَنْهُ سَاعَةً وَلَا تَسْتَقْدِمُونَ ﴿٣٠﴾
30. Sema: Mna miadi ya siku ambayo hamtaakhirisha saa wala hamtaitangulia.
SEMA WAITENI MNAODAI KUWA NI WAUNGU
Aya 22 – 30
MAANA
Sema: Waombeni hao mnaodai kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu.
Washirikina waliabudu Malaika na masanamu, Mtume(s.a.w. w ) akawakataza lakini hawakusikia, akawaambia kwa amri ya Mwenyezi Mungu: iko wapi dalili ya mnaowafanya kuwa ni miungu? Waombeni manufaa au kukinga madhara, muone kuwa wanasikia na kuwajibu?
Lengo la matakwa haya ni kusimamisha hoja isiyoshindwa. Ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا ﴿٥٦﴾
“Sema:“Waombeni hao mnaodai badala Yake hawawezi kuwaondolea madhara wala kuyabadilisha.” Juz. 25 (17:56).
Hawamiliki hata chembe katika mbingu wala ardhini. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala hawana msaidizi miongoni mwao.
Maneno yanaelekezwa kwa washirikina. Hata chembe ni kinaya cha kuwa hawamiliki hata kitu kilicho kidogo na duni. Maana ni kuwa hana mshirika wala msaidizi.
Wala hautafaa uombezi mbele yake ila kwa yule aliyempa idhini.
Hii ni kuwarudi washirikina na kauli yao:
مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ ...﴿٣﴾
“Hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu.” (39:3).
Kwa maelezo zaidi Tazama Juz. 1 (47 – 48) kifungu cha ‘Shufaa.’
Hata itakapoondolewa fazaa kwenye nyoyo zao, watasema: Kasema nini Mola wenu? Watasema: Haki, naye ndiye aliye juu, Mkubwa.
Wafasiri wametofautiana kuhusu watakaoondolewa fazaa, watakaouliza na wataoulizwa.
Kauli yenye nguvu zaidi ni watakaoondolewa fazaa ni wote walioko mbinguni na ardhini; kwamba fazaa itawaenea wote isipokuwa atakaowataka Mwenyezi Mungu; kama ilivyoelezwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu:
وَيَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَفَزِعَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ وَكُلٌّ أَتَوْهُ دَاخِرِينَ ﴿٨٧﴾
“Na siku itakapopuziwa parapanda, watafazaika waliomo mbinguni na waliomo ardhini, ila amtakaye Mwenyezi Mungu. Na wote watamfikia hali ya kuwa ni wanyonge.” Juz. 20 (27:87).
Mara kwa mara tumesema kuwa Qur’an inajifasiri yenyewe. Kwa hiyo maana yanakuwa kwamba wakati wa Kiyama, wa mbinguni na wa ardhini watagawanyika mafungu mawili: Kuna kundi litakalokuwa na fazaa kubwa na kundi jingine litakuwa na amani. Hawa ndio walioashiriwa na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Ila amtakaye Mwenyezi Mungu.” Kundi la kwanza ikitulia fazaa yake, watauliza kundil la pili: Mola wenu amesema nini na mwisho wetu ni upi? Watakoulizwa watajibu kuwa Mwenyezi Mungu amesema haki naye ndiye aliye juu, Mkubwa.
Jibu hili kwa ujumla linaashiria kuwa Mwenyezi Mungu hana mshirika wala msaidizi. Pia hakuna atakayeombea kwake isipokuwa aliyempa idhini.
Sema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini?
Maneno yanaelekezwa kwa Mtume(s.a.w. w ) awaambie washirikina. Riziki ya kutoka mbinguni ni mvua na mwangaza na riziki ya ardhini ni mazao ya porini na yanayopandwa.
Sema : ni Mwenyezi Mungu, siyo masanamu au Malaika, wala sio Isa au Uzayr. Kwa vile hili ndio jibu pekee, ndio maana Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake mtukufu awajibie walioulizwa.
Na hakika sisi au nyinyi bila shaka tuko kwenye uongofu au upotofu ulio wazi.
Nabii ana uhakika kwamba yeye yuko kwenye uongofu na kwamba washirikina wako kwenye upotevu, lakini walipoukataa uwongofu na haki ndio akatumia mfumo huu wa hekima na kuwaambia kuwa mja wetu atakuwa kwenye haki na mwingine kwenye upotevu, basi zirudieni akili zenu muone ni nani aliye kwenye usawa?
Huu ndio mfumo wa Mtume wa uwongofu na rehema, kuongezea kuwa mwenye haki anajiamini hata wakimhalifu watu wote wa ardhini.
Sema: Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyoyafanya wala sisi hatutaulizwa kwa mnayoyatenda.
Huu ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t):
وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ أَنتُم بَرِيئُونَ مِمَّا أَعْمَلُ وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٤١﴾
“Na kama wakikukadhibisha, basi sema: Mimi nina amali yangu na nyinyi mna amali yenu. Nyinyi hamna jukumu kwa ninayoyatenda, na mimi sina jukumu kwa mnayoyatenda.” Juz. 11 (10:41).
Sema: Mola wetu atatukusanya kisha atatuhukumu kwa haki, naye ndiye Hakimu, Mjuzi.
Siku ya mwisho ina majina mengi; miongoni mwayo ni siku ya mkusanyiko. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
يَوْمَ يَجْمَعُكُمْ لِيَوْمِ الْجَمْعِ ﴿٩﴾
“Siku atakayowakusanya kwa ajili ya Siku ya mkusanyiko” (64:9).
Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) atatukusanya sisi na na nyinyi ili tuangalie hisabu, malipo na matendo. Hapo pazia litafunuka na mtajua kundi gani ndio lililoelekea njia ya kunyooka.
Sema: Nionyesheni wale mliowaunganisha naye kuwa washirika.
Hapa kuna manaeno ya kukadiria kuwa nionyesheni dalili ya kuwa masanamu ni washirika wa Mwenyezi Mungu au watawajongeza kwa Mwenyezi Mungu.Hapana! Yeye hana mshirika wala msaidizi wala wa kuombea mbele yake isipokuwa aliyempa idhini.
Bali Yeye ni Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Hakuna enzi wala nguvu isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Ama dalili za hekima yake na utukufu wake zinajitokeza katika kuumba ulimwengu na maajabu yake.
Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mtoaji bishara na muonyaji, lakini watu wengi hawajui.
Tazama Juz. 7 (6:92) na Juzuu hii tuliyo nayo (33:40) Kifungu cha ‘Kwanini utume umeishilia kwa Muhammad(s.a.w. w ) ?’
Na wanasema: Ni lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli?”
Imetangulia neno kwa neno katika Juz. 11 (10:48).
Sema: Mna miadi ya siku ambayo hamtaakhirisha saa wala hamtaitangulia.
Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ameahidi ufufuo, hisabu na malipo, naye bila shaka, ni mwenye kutekelza miadi yake, lakini kwa wakati alioupanga yeye ambaye hekima yake imetukuka, hatanguliwi wala hacheleweshwi. Basi yasiwahade mliyo nayo enyi washirikina, kwa sababu yatakwisha tu, muda mfupi au mrefu, kisha marejeo yenu nyote ni kwa Mwenyezi Mungu awajulishe yale mliyokuwa mkiyafanya.
7
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن نُّؤْمِنَ بِهَـٰذَا الْقُرْآنِ وَلَا بِالَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ مَوْقُوفُونَ عِندَ رَبِّهِمْ يَرْجِعُ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ الْقَوْلَ يَقُولُ الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا لَوْلَا أَنتُمْ لَكُنَّا مُؤْمِنِينَ ﴿٣١﴾
31. Na walisema waliokufuru: Hatutaiamini Qur’an hii, wala yaliyokuwa kabla yake. Na ungeliwaona madhalimu watakaposimamishwa mbele ya Mola wao wakirudishiana maneno! wale wanyonge wakiwaambia wale waliojifanya wakubwa: Lau si nyinyi bila shaka tungelikuwa waumini.
قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا لِلَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا أَنَحْنُ صَدَدْنَاكُمْ عَنِ الْهُدَىٰ بَعْدَ إِذْ جَاءَكُم بَلْ كُنتُم مُّجْرِمِينَ ﴿٣٢﴾
32. Wale waliojiona wakubwa watawaambia wale wanyonge: Kwani sisi ndio tuliowazuia na uongofu baada ya kuwafikia? Bali nyinyi wenyewe mlikuwa waovu. Kwani wanalipwa ila kwa waliokuwa wakiyatenda?
وَقَالَ الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا بَلْ مَكْرُ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ إِذْ تَأْمُرُونَنَا أَن نَّكْفُرَ بِاللَّـهِ وَنَجْعَلَ لَهُ أَندَادًا وَأَسَرُّوا النَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ وَجَعَلْنَا الْأَغْلَالَ فِي أَعْنَاقِ الَّذِينَ كَفَرُوا هَلْ يُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٣٣﴾
33. Na wale wanyonge watawaambia wale waliojifanya wakubwa: Bali ni vitimbi vyenu vya usiku na mchana, mlipokuwa mkituamrisha tumkufuru Mwenyezi Mungu na tumfanyie washirika, nao wataficha majuto watakapoiona adhabu. Na tutaweka minyororo shingoni mwa wale waliokufuru kwani wanalipwa ila kwa waliokuwa wakiyatenda?.
HAWATAAMINI QUR’AN
Aya 31-33
MAANA
Na walisema waliokufuru: Hatutaiamini Qur’an hii, wala yaliyokuwa kabla yake, kama vile Tawrat na Injil. Walioyasema haya ni washirikina, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu:
وَقَالَ الرَّسُولُ يَا رَبِّ إِنَّ قَوْمِي اتَّخَذُوا هَٰذَا الْقُرْآنَ مَهْجُورًا {30 }
Na Mtume alisema: Ewe Mola wangu! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur’an ni mahame.” Juz. 19 (25:30).
Wameihama na kuikana kwa sababu inamfanya sawa mweusi na mweupe na ikawaambia:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿١١﴾
“Enyi ambao mmeamini! Wanaume wasiwadharau wanaume wengine, huenda wakawa bora kuliko wao; wala wanawake kwa wanawake wengine, huenda wakawa bora kuliko wao. Wala msitiane kasoro, wala msiitane majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya imani.” (49:11).
Vile vile waliukana utume wa Muhammad(s.a.w. w ) kwa sababu alitaka kuwatoa kwenye ujinga na kurudi nyuma, waende kwenye elimu na maendeleo.
Mtaalamu mmoja wa Ulaya, Jack Rezler, aliyeandika kitabu kuhusu mwamko wa kiislamu na kingine kinachozungumzia maendeleo ya waarabu ambavyo vilichapishwa ufaransa mnamo 1962, alisema: “Hatua ya kwanza ya maendeleo ya waarabu ilianza kwa kujitokeza dini ya kiislamu.
Kuna sababu kadhaa zilizofanya maendeleo haya na kuenea kwake; sababu kubwa zaidi ni kuweko na roho ya kimaana kwa Waislamu kupitia dini hii mpya; jambo ambalo limeleta ushujaa, kiasi cha kufikia kuyadharau mauti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”
Na ungeliwaona madhalimu watakaposimamishwa mbele ya Mola wao wakirudishiana maneno!
Baada ya Mtume(s.a.w. w ) kukata tamaa kuwa washirikina wataamini, Mola Mtukufu alimtuliza na kumwambia kuwa kesho utaona hawa waongo watakavyokuwa dhalili na kuhizika pale watakaposimama mbele ya Mwenyezi Mungu kwa hisabu, jinsi mfuasi atakavyomlaumu aliyemfuata kila mmoja atamtia makosani mwinginewale wanyonge wakiwaambia wale waliojifanya wakubwa: Lau si nyinyi bila shaka tungelikuwa waumini.
Wanyonge ni wale wafuasi; na waliojifanya wakubwa ni viongozi.
Wale waliojiona wakubwa watawaambia wale wanyonge: Kwani sisi ndio tuliowazuia na uongofu baada ya kuwafikia? Bali nyinyi wenyewe mlikuwa waovu, sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu:
كَمَثَلِ الشَّيْطَانِ إِذْ قَالَ لِلْإِنسَانِ اكْفُرْ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِّنكَ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦﴾
“Kama mfano wa shetani anapomwambia mtu: Kufuru. Na akikufuru humwambia: Mimi si pamoja nawe. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu. (59:16).
Sio mbali kuwa shetani katika Aya hii ni kinaya cha viongozi wapotevu wanaopoteza.
Na wale wanyonge watawaambia wale waliojifanya wakubwa: Bali ni vitimbi vyenu vya usiku na mchana, mlipokuwa mkituamrisha tumkufuru Mwenyezi Mungu na tumfanyie washirika.
Wafuasi na viongozi watakapokata tamaa ya kuokoka watatupiana lawama na kutuhumiana, kila kundi likijaribu kuwatupia makosa wengine; sawa na wezi wanapoafikiana kufanya uhalifu, lakini wanaposhikwa wanalaniana wao kwa wao.
Mwisho ushindi utakuwa ni wa wafuasi, kwa kuwakabili waliojifanya wakubwa kwa njama walizozifanya usiku na mchana na kuwadanga na ukafiri na ushirikina kwa njia mbalimbali.
Hata hivyo hilo halitawaondolea adhabu wala kuwapunguzia, maadamu walikuwa na akili na kulifanya hilo kwa hiyari yao: “Wa mwisho wao watawasema wa mwanzo wao: Mola wetu! Hawa ndio waliotupoteza basi uwape adhabu ya moto maradufu. Atasema: Itakuwa maradufu kwenu nyote, lakini hamjui.” Juz. 8 (7:38).
Nao wataficha majuto watakapoiona adhabu. Yaani wafuasi na waliofuatwa. Kila mwenye kuzembea na kupituka mipaka mwisho wake ni adhabu na majuto.
Na tutaweka minyororo shingoni mwa wale waliokufuru, viongozi na wafuasi wao.Kwani wanalipwa ila kwa waliyokuwa wakiyatenda? Kabisa! Mtu atalipwa kwa aliyoyafanya tu na Mola wako si mwenye kuwadhulumua waja.
وَمَا أَرْسَلْنَا فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ ﴿٣٤﴾
34. Na hatukumtuma mwonyaji yeyote kwenye mji ila walisema wapenda anasa wake: Hakika sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo.
وَقَالُوا نَحْنُ أَكْثَرُ أَمْوَالًا وَأَوْلَادًا وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ ﴿٣٥﴾
35. Na wakasema: Sisi tuna mali nyingi zaidi na watoto, wala sisi hatutaadhibiwa.
قُلْ إِنَّ رَبِّي يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٦﴾
36. Sema: Hakika Mola wangu humkunjulia riziki amtakaye na huikunja, lakini watu wengi hawajui.
وَمَا أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُم بِالَّتِي تُقَرِّبُكُمْ عِندَنَا زُلْفَىٰ إِلَّا مَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ جَزَاءُ الضِّعْفِ بِمَا عَمِلُوا وَهُمْ فِي الْغُرُفَاتِ آمِنُونَ ﴿٣٧﴾
37. Na si mali yenu wala watoto wenu watakaowajongeza kwetu muwe karibu, isipokuwa aliyeamini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo maradufu, kwa waliyoyafanya nao watakuwa salama katika maghorofa.
وَالَّذِينَ يَسْعَوْنَ فِي آيَاتِنَا مُعَاجِزِينَ أُولَـٰئِكَ فِي الْعَذَابِ مُحْضَرُونَ ﴿٣٨﴾
38. Na wale ambao wanajitahidi kuzipinga ishara zetu, wakaona watashinda, hao watahudhurishwa kwenye adhabu.
قُلْ إِنَّ رَبِّي يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ لَهُ وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿٣٩﴾
39. Sema: Hakika Mola wangu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake na humkunjia. Na chochote mtakachotoa Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanaoruzuku.
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ يَقُولُ لِلْمَلَائِكَةِ أَهَـٰؤُلَاءِ إِيَّاكُمْ كَانُوا يَعْبُدُونَ ﴿٤٠﴾
40. Na siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia Malaika: Je, hawa walikuwa wakiwaabudu?
قَالُوا سُبْحَانَكَ أَنتَ وَلِيُّنَا مِن دُونِهِم بَلْ كَانُوا يَعْبُدُونَ الْجِنَّ أَكْثَرُهُم بِهِم مُّؤْمِنُونَ ﴿٤١﴾
41. Watasema: Umetakasika! Wewe ndiye walii wetu sio hao. Bali walikuwa wakiwaabudu majini; wengi wao wakiwaamini hao.
فَالْيَوْمَ لَا يَمْلِكُ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ نَّفْعًا وَلَا ضَرًّا وَنَقُولُ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذُوقُوا عَذَابَ النَّارِ الَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ ﴿٤٢﴾
42. Na leo hii hawataweza baadhi yenu kuwaletea nafuu wengine wala kuwadhuru. Na tutawaambia wale ambao wamedhulumu: Onjeni adhabu ya Moto mliokuwa mkiukadhibisha.
WAPENDA ANASA
Aya 34 – 42
MAANA
Na hatukumtuma mwonyaji yeyote kwenye mji ila walisema wapenda anasa wake: Hakika sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo. Na wakasema: Sisi tuna mali nyingi zaidi na watoto, wala sisi hatutaadhibiwa.
Hii ndio fikra ya wapenda anasa na hii ndio lugha yao. Mali ndio ya kwanza na ya mwisho; ndiyo bwana na wao ni watumwa.
Wanabeba bendera ya shari na uchokozi kwa watu kwa ajili ya mali, wanatawala masoko na vyakula, wanaanzisha vita moto na vita baridi, wanatafuta kila namna ya kutawala maisha na kila kitu wanakifungamanisha na chumo lao na faidia yao.
Kwao elimu sio chochote ila ikiwa inazidisha utajiri wao, dini ni ugaidi ila ikiwa inalinda masilahi yao, na amani ni wao wapore na wanayang’anye bila ya ya kuulizwa au kukemewa. Tazama Juz. 15: (17:16,90).
Sema: Hakika Mola wangu humkunjulia riziki amtakaye na huikunja, lakini watu wengi hawajui.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:26) kifungu cha ‘riziki na mtu.
Na si mali yenu wala watoto wenu watakaowajongeza kwetu muwe karibu, isipokuwa aliyeamini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo maradufu, kwa waliyoyafanya nao watakuwa salama katika maghorofa.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) hapimi kheri na fadhila kwa mali na watoto, wala kwa vyeo na nasaba; bali ni kwa imani na matendo mema. Ni kwa mawili haya ndio mja anakuwa ni mwenye kuridhiwa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa thawabu zake na fadhila zake.
Imam Ali(a.s) anasema:“Heri sio kuwa nyingi mali yako na watoto, lakini heri ni kuwa nyingi elimu yako na kuwa na ustahamilivu mkubwa, na ushindane na watu kwa kumwabudu Mola wako. Ukifanya vizuri msifu Mwenyezi Mungu na ukifanya uovu muombe msamaha Mwenyezi Mungu; wala hakuna heri isipokuwa kwa watu wawili: Mtu aliyefanya dhambi akaiunganisha na toba, na mtu anayeharakisha kheri.”
Na wale ambao wanajitahidi kuzipinga ishara zetu, wakaona watashinda, hao watahudhurishwa kwenye adhabu.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 (22:51).
Sema: Hakika Mola wangu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake na humkunjia.
Unaweza kuuliza : Kwa nini Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekariri Aya hii, pamoja na kujua kuwa kuna mtengano wa Aya mbili tu?
Wafasiri wamejibu kwamba Aya ya kwanza inahusika na makafiri na ya pili ni ya waumini. Razi anasema: “Dalili ya hilo ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya ya pili amesema katika ‘waja wake’ na ya kwanza amesema ‘waja’ tu, na mja anayetegemezwa kwake Mwenyezi Mungu anakusudiwa muumini.”
Sio mbali kuwa makusudio ya kukaririka ni mawaidha na kuhimiza kutoa ambako Mwenyezi Mungu amekuashiria kwa kusema:
Na chochote mtakachotoa Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanaoruzuku.
Kuna Hadith ya Mtume mtukufu(s.a.w. w ) , amesema:“Kila usiku kuna mnadi anayenadi kwa kusema: “Ewe Mola wangu! Mlipe kila mtoaji. Na mnadi mwingine ananadi: Ewe Mola angu! Mlipe kila mzuiaji kuangamia.” kwenye Nahjul-Balagha imeelezwa:“Iteremsheni riziki kwa sadaka.”
Na siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia Malaika: Je, hawa walikuwa wakiwaabudu?
Makusudio ya kuelekeza swali hili kwa Malaika ni kuwatahayariza washirikina. Aya inafahamisha kuwa baadhi ya waarabu walikuwa wakiwaabudu malaika. Hayo yanaashiriwa na kauli yake Mwenyezi Mungu: “Je, Mola wenu amewachagulia watoto wa kiume na yeye akajichukulia watoto wa kike katika Malaika?” Juz. 15 (17:40).
Mwenye kumnasibishia Mwenyezi Mungu mwana basi amemfanya Mungu kuwa na mfano na mshirika katika uungu wake.
Watasema: Umetakasika! Wewe ndiye walii wetu sio hao.
Wewe ndiye bwana wetu na wao ni maadui zetu nasi tunajitenga nao.
Bali walikuwa wakiwaabudu majini; wengi wao wakiwaamini hao.
Kundi la wafasiri wamesema kuwa makusudio ya jini hapa ni mashetani na kwamba wao wanawapambia washirikina wawaabudu malaika na wengineo badala ya Mwenyezi Mungu.
Wengine wakasema kuwa ibada ya majini ilikuwa maarufu kwa waarabu; kwa hiyo maana ya Aya yatabaki kwenye dhahiri yake, wala hakuna haja ya kufanya taawili.
Iwe ni majini ndio waliokuwa wakiabudiwa au wengineo kwa kudanganywa na shetani, bado makusudio ya kwanza ya Aya ni kukanusha kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kwamba hakuna uombezi kwake ila kwa idhini yake. Vile vile hakuna kimbilio isipokuwa kwake yeye tu.
Ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akafuatishia na kauli yake:
Na leo hii hawataweza baadhi yenu kuwaletea nafuu wengine wala kuwadhuru.
Si malaika, watu wala majini wanaoweza wao wenyewe kujikinga, sikwambii tena kuwasaidia wengine. Yeye peke yake ndiye mwenye ufalme na sifa njema, naye ni muweza wa kila kitu.
Na tutawaambia wale ambao wamedhulumu: Onjeni adhabu ya Moto mliokuwa mkiukadhibisha.
Walisema kuwa hakuna Pepo wala Moto, wala hatutauamini mpaka tutakapouona waziwazi. Basi ndio Mwenyezi Mungu akawachoma kuitikia matakwa yao.
Aya hii imenikumbusha wanaosema kuwa hakuna elimu wala maarifa ila kwa njia ya kushuhudia au majaribio; hata katika visivyoonekana na kuhisiwa.
8
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالُوا مَا هَـٰذَا إِلَّا رَجُلٌ يُرِيدُ أَن يَصُدَّكُمْ عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُكُمْ وَقَالُوا مَا هَـٰذَا إِلَّا إِفْكٌ مُّفْتَرًى وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٤٣﴾
43. Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi wanasema: Huyu si chochote ila ni mtu anayetaka kuwazuia na waliyokuwa wakiyaabudu baba zenu. Na wakasema: Haya si chochote ila ni uongo uliozuliwa.” Na wale waliokufuru waliiambia haki pale ilipowajia: “Haya si chochote ila ni uchawi ulio dhahiri.
وَمَا آتَيْنَاهُم مِّن كُتُبٍ يَدْرُسُونَهَا وَمَا أَرْسَلْنَا إِلَيْهِمْ قَبْلَكَ مِن نَّذِيرٍ ﴿٤٤﴾
44. Wala hatukuwapa vitabu wavisome, wala hatukuwatumia muonyaji kabla yako.
وَكَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَمَا بَلَغُوا مِعْشَارَ مَا آتَيْنَاهُمْ فَكَذَّبُوا رُسُلِي فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ ﴿٤٥﴾
45. Na walikadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Na hawakufikilia hata sehemu ya kumi ya tulivyowapa hao. Wakawakadhibisha mitume wangu. basi je, kulikuwaje kukanya kwangu?
قُلْ إِنَّمَا أَعِظُكُم بِوَاحِدَةٍ أَن تَقُومُوا لِلَّـهِ مَثْنَىٰ وَفُرَادَىٰ ثُمَّ تَتَفَكَّرُوا مَا بِصَاحِبِكُم مِّن جِنَّةٍ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ لَّكُم بَيْنَ يَدَيْ عَذَابٍ شَدِيدٍ ﴿٤٦﴾
46. Sema: Hakika ninawapa mawaidha kwa jambo moja tu, kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawili na mmoja mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu hana wazimu. Hakuwa yeye ila ni muonyaji kwenu kabla ya kuwafikia adhabu kali.
قُلْ مَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ فَهُوَ لَكُمْ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٤٧﴾
47. Sema: Ujira niliowaomba ni wenu nyinyi. Sina ujira ila kwa Mwenyezi Mungu. Naye ni shahidi juu ya kila kitu.
قُلْ إِنَّ رَبِّي يَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿٤٨﴾
48. Sema: Hakika Mola wangu hutoa haki, Mjuzi mno wa ghaibu.
قُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَمَا يُبْدِئُ الْبَاطِلُ وَمَا يُعِيدُ ﴿٤٩﴾
49. Sema: Haki imefika na batili haijitokezi wala hairudi.
قُلْ إِن ضَلَلْتُ فَإِنَّمَا أَضِلُّ عَلَىٰ نَفْسِي وَإِنِ اهْتَدَيْتُ فَبِمَا يُوحِي إِلَيَّ رَبِّي إِنَّهُ سَمِيعٌ قَرِيبٌ ﴿٥٠﴾
50. Sema: Ikiwa nimepotea basi nimepotea kwa kuidhuru nafsi yangu tu. Na ikiwa nimeongoka basi ni kwa sababu ya kuniletea wahyi Mola wangu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia aliye karibu.
NINAWAPA MAWAIDHA KWA JAMBO MOJA TU
Aya 43 – 50
MAANA
Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi wanasema: Huyu si chochote ila ni mtu anayetaka kuwazuia na waliyokuwa wakiyaabudu baba zenu. Na wakasema: Haya si chochote ila ni uwongo uliozuliwa. Na wale waliokufuru waliiambia haki pale ilipowajia: Haya si chochote ila ni uchawi ulio dhahiri.
Waliosema ni washirikina wa kiarabu, mtu wanayemkusudia ni Muhammad(s.a.w. w ) . Wamempa wasifa wa uzushi na uchawi kwa sababu aliwataka waachane na mizimu na maagizo ya kijahilia. Pia aliwaambia wajizuie na mambo ya haramu, uovu, kumwaga damu na kuwakandamiza wanyonge. Vile vile aliwataka wafanye mambo kielimu na kiuadilifu.
Hilo ndilo kosa la Mtume mtukufu kwao. Kama unavyoona, ni kosa la mjuzi mwenye ikhlasi mbele ya mjinga mhaini, na la tabibu mwenye kutoa nasaha mbele ya mgonjwa anayejiona ni mzima. Amesema kweli yule aliyesema: “Mjinga anajifanyia mwenyewe ambayo hata adui hawezi kumfanyia adui yake.”
Wala hatukuwapa vitabu wavisome, wala hatukuwatumia muonyaji kabla yako.
Walishirikisha ambapo kila kitu kinafahamisha kuwa Yeye ni mmoja, wakawaiga mababa na mababu bila ya kuwa na hoja ya wahyi ulioteremshwa au Nabii aliyetumwa wala athaari yoyote ya ilimu. Tazama Juz. 17 (22: 1-7) kifungu cha: ‘Mjadala wakijinga na upotevu‘.
Na walikadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Na hawakufikilia hata sehemu ya kumi ya tulivyowapa hao. Wakawakadhibisha mitume wangu. basi je, kulikuwaje kukanya kwangu?
Kabla yenu walishirikisha watu wa uma nyingi, waliwakadhibisha mitume; kama manvyokadhibisha nyinyi, nao walikuwa na maendeleo na nguvu zaidi kuliko nyinyi, lakini pamoja na hivyo Mwenyezi Mungu aliwaadhibu kwa dhulma yao na ujeuri wao. Je, hampati funzo na kuhofia kuwafika yaliyowafika wao?
Umetangulia mfano wake katika Juz. 10 (9:70).
Sema: Hakika ninawapa mawaidha kwa jambo moja tu, kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawli na mmoja mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu hana wazimu. Hakuwa yeye ila ni muonyaji kwenu kabla ya kuwafikia adhabu kali.
Kusimama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kushikamana na haki na kuwa mbali na kuiga na kufuata matamanio. Wawili wawili ni mmoja kumrudia mwingine na kuuchunguza mwito na ujumbe. Mmoja mmoja ni kila mmoja kurudia akili yake na dhamiri na kufikiria yale aliyokuja nayo.
Maana ni kuwa ewe Muhammad! Waambie wale wanaokukadhibisha kwamba mimi ninawataka jambo moja tu, uadilifu wa kuchunga haki, mfikirie mkiwa pamoja na mkiwa mbalimbali kuhusu mwito wangu; kisha muangalie, je kweli mimi ni mzushi, mchawi au mwenda wazimu; kama mnavyodai? Au ni mbashiri, muonyaji na mshauri nasaha mwenye busara? Nabii mtukufu aliwapa Watu wa Kitabu mwito kama huu, pale alipowaambia:
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا ﴿٦٤﴾
“Sema: Enyi watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno la usawa baina yetu na baina yenu. Kwamba tusimwabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote.” Juz. 3 (3:64).
Hakuna jambo linalosadikisha zaidi dalili ya ukweli wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) , katika aliyokuja nayo, kuliko kuwapa mwito wa haki na uadilifu mahasimu.
Imepokewa Hadith kutoka kwa Ibn Abbas, kwamba Mtume(s.a.w. w ) siku moja alipanda Swafa na akasema: “Enyi wenzangu! Neno analolitumia anayetaka kuokoka ikiwa kuna jambo kubwa, basi makuraishi wakakusanyika. Akawaambia: “Mnaonaje kama nikiwaambia adui atawajia asubuhi au jioni, mtanisadiki?” Wakasema: “Ndio!” Akasema: “Hakika ninawaonya na adhabu kali. Abu Lahab akamjibu kwa neno la kukana... lakini hazikupita siku ila walisalimu amri wakiwa wanyonge.
Sema: Ujira niliowaomba ni wenu nyinyi. Sina ujira ila kwa Mwenyezi Mungu. Naye ni shahidi juu ya kila kitu.
Makusudio ya ‘ni wenu nyinyi’ ni kukana swali la ujira. Ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu:
فَمَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ ﴿٧٢﴾
“...basi mimi siwaombi ujira. Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu.” Juz. 11 (10:72).
Sema: Hakika Mola wangu hutoa haki, Mjuzi mno wa ghaibu.
Yaani anatoa wahyi kwa haki kuupeleka kwa mitume yake naye anajua vizuri nani wa kumpelekea ujumbe wake mkuu.
Sema: Haki imefika na batili hajitokezi wala hairudi.
Makusudio ya haki hapa ni risala ya Muhammad(s.a.w. w ) na batili ni shir- ki. Kujitokeza na kurudi ni kinaya cha kwisha kabisa batili na kutodhihiri athari yake katika Bara Arabu kabisa baada ya risala ya Muhammad(s.a.w. w ) .
Sema: Ikiwa nimepotea basi nimepotea kwa kuidhuru nafsi yangu tu, wala nyinyi madhara yangu hayawahusu.
Na ikiwa nimeongoka basi ni kwa sababu ya kuniletea wahyi Mola wangu.
Ni kwake Yeye peke yake fadhila za kuongoka kwangu; wala sijimilikii wala kummilikia mwingine isipokuwa yale aliyonimilikisha Mwenyezi Mungu.
Hakika Yeye ni Mwenye kusikia aliye karibu.
Mkisema anasikia, mkidhamiria au mkitenda atajua, kwa sababu yeye yuko karibu zaidi na nyinyi kuliko mshipa wa shingo.
وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ فَزِعُوا فَلَا فَوْتَ وَأُخِذُوا مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ ﴿٥١﴾
51. Na lau ungeliwaona watakapofazaika, basi hapana pa kukimbilia, na watakamatwa mahala pa karibu.
وَقَالُوا آمَنَّا بِهِ وَأَنَّىٰ لَهُمُ التَّنَاوُشُ مِن مَّكَانٍ بَعِيدٍ ﴿٥٢﴾
52. Na watasema: Tumemwamini! Lakini watapata wapi kutoka huko mahali mbali?
وَقَدْ كَفَرُوا بِهِ مِن قَبْلُ وَيَقْذِفُونَ بِالْغَيْبِ مِن مَّكَانٍ بَعِيدٍ ﴿٥٣﴾
53. Na walikwishamkataa hapo zamani, wakiyatupilia mbali ya ghaibu kutoka mahali mbali.
وَحِيلَ بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ مَا يَشْتَهُونَ كَمَا فُعِلَ بِأَشْيَاعِهِم مِّن قَبْلُ إِنَّهُمْ كَانُوا فِي شَكٍّ مُّرِيبٍ ﴿٥٤﴾
54. Na watawekewa kizuizi baina yao na hayo wanayoyatamani, kama walivyofanyiwa wenzao zamani. Hakika wao walikuwa katika shaka ya kutia wasiwasi.
WATAIPATA WAPI?
Aya 51 – 54
MAANA
Na lau ungeliwaona watakapofazaika, basi hapana pa kukimbilia, na watakamatwa mahala pa karibu.
Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad(s.a.w. w ) , kukamatwa mahala pa karibu ni kinaya cha kuwa kwenye uweza wa Mwenyezi Mungu. Maana ni kuwa, ewe Muhammad(s.a.w. w ) lau utaona kesho hofu na adhabu, isiyokuwa na kimbilio, itakayowapata wale wanaokadhibisha utume wako, basi utastaajabu.
Hii ni kemeo kwa washirikina na tulizo kwa Bwana wa Mitume.
Na watasema tumemwamini! Lakini watapata wapi kutoka huko mahali mbali?
Wanayesema ‘tumemwamini’ ni Muhammad(s.a.w. w ) , kwa sababu amekwishatajwa kwenye Aya 46 ‘Mwenzenu hana wazimu.’
Maana ni kuwa, wale waliomkadhibisha Muhammad, watakapoiona adhabu watasema tumemwamini, lakini wataipata wapi imani hii au itawafaa nini huko mbali. Kwa sababu siku ya Kiyama ni siku ya hisabu na malipo sio siku ya imani na matendo.
Imam Ali(a.s) anasema:“Leo ni matendo si hisabu na kesho ni hisabu sio matendo... Enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Jipimeni kabla ya kupimwa na mjihisabu kabla ya kuhisabiwa.”
Na walikwishamkataa hapo zamani. Muda wa kufaa imani umekwisha.
Wakiyatupilia mbali ya ghaibu kutoka mahali mbali.
Kutupilia mbali ni kusema bila ya ilimu, kutoka mahali mbali ni kinaya cha umbali wa kuliza na kutoamini kwao haki. Maana ni kuwa, wao walikuwa wakisema Muhammad ni mzushi, mchawi na mwendawazimu; wala hakuna Pepo au Moto. Waliyasema hayo kwa ujinga na bila ya dalili.
Na watawekewa kizuizi baina yao na hayo wanayoyatamani.
Wanatamani kuokoka na adhbau ya Jahannam, ndio wakakimbilia imani na toba, lakini baada ya kupita muda, basi watazidi majuto na machungu.
Kama walivyofanyiwa wenzao zamani.
Walikuwa na wanaofanana nao katika uma zilizopita; walimpinga Mola wao katika maisha ya dunia na kufazaika akhera. Wataambiwa:
قَالَ اخْسَئُوا فِيهَا وَلَا تُكَلِّمُونِ ﴿١٠٨﴾
“Tokomeeni humo, wala msinisemeshe.” Juz. 18: (23:108).
Hakika wao walikuwa katika shaka ya kutia wasiwasi ya ufufuo.
MWISHI WA SURA YA THELATHINI NA NNE: SURAT SABA
9
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
Sura Ya Thelathini na Tano: Surat Fatir. Imeshuka Makka. Ina Aya 45.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
الْحَمْدُ لِلَّـهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١﴾
1. Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu Muumba wa mbingu na ardhi aliyewafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili mbili, tatu tatu na nne nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye uweza juu ya kila kitu.
مَّا يَفْتَحِ اللَّـهُ لِلنَّاسِ مِن رَّحْمَةٍ فَلَا مُمْسِكَ لَهَا وَمَا يُمْسِكْ فَلَا مُرْسِلَ لَهُ مِن بَعْدِهِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢﴾
2. Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu hakuna wa kuizuia na anayoizuia hakuna wa kuiachia isipokuwa Yeye, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ هَلْ مِنْ خَالِقٍ غَيْرُ اللَّـهِ يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٣﴾
3. Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu. Je, yuko muumba mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu anayewapa riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana Mola ila Yeye basi mnageuzwa wapi?.
SIFA NJEMA NI ZA MWENYEZI MUNGU
Aya 1 – 3
MAANA
Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu Muumba wa mbingu na ardhi aliyewafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili mbili, tatu tatu na nne nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye uweza juu ya kila kitu.
Mwenyezi Mungu amejisifu Yeye mwenyewe ili atufundishe jinsi ya kumsifu na kumshukuru. Aya inafahamisha kuwa katika Malaika kuna walio na mbawa mbili, wenye tatu na wenye nne na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu huzidisha mbawa vile atakavyo. Haya na yanayofanana nayo yanaafikiana na uwezo wa Mwenyezi Mungu na akili haiyakatai. Yasiyokuwa hayo tunamwachia Mwenyezi Mungu (s.w.t), kwa vile sisi hatutaulizwa wala hayana uhusiano wowote na maisha yetu, wala hayana dalili na Aya au Hadith mutawatir.
Ninahofia wale wanaolazimisha kuzifanyia taawili nukuu za dini ziende sambamba na elimu ya kisasa waseme kuwa mbili mbili ni ishara ya ndege yenye injini mbili, tatu tatu ni yenye tatu, nne nne ni yenye nne na kuzidisha katika kuumba ni kuwa ndege zitakazokuja baadaye zenye injini nyingi.
Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu hakuna wa kuizuia na anayoizuia hakuna wa kuiachia isipokuwa Yeye, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Makusudio ya rehema hapa sio mali tu; kama walivyosema baadhi ya wafasiri. Wala sio mali, afya na cheo; kama walivyosema wengine. Kwani mali inapelekea uasi na ukandamizaji. Tumewaona wengi wenye mali wamewageuza wengine wanyonge kuwa ni mashirika wanayoyamiliki na kuwageuza kuwa ni watumwa wao wanaowatumikia au wawe wakimbizi.
Afya nayo inampelekea mtu kwenye hatari. Ama cheo, ndio kabisa, aghlabu kinakuwa ni chombo cha dhulma na uadui. Elimu nayo mara nyingine inakuwa ni afadhali ujinga; kama vile elimu iliyotengeneza bomu la nyukilia na silaha za maangamizi.
Hapana! Makusudio ya rehema yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika Aya hii, sio mali peke yake, wala afya pekee yake wala sio cheo na elimu tu. Isipokuwa makusudio ni huruma ya Mwenyezi Mungu, mwongozo wake wa heri na kinga yake ya shari.
Imam Ali(a.s) anasema:“Shida inapofika kikomo huja faraja na inapokaza sana minyororo ya dhiki hupatikana raha.”
Mara nyingi tumeshuhudia matatizo madogo yanazidi kuwa makubwa kila mwenyewe anavyojitahidi kuyatatua, na tunaona yale makubwa yanatatu- ka kwa wepesi au kwa haraka. Hakuna siri ya hilo ila matakwa ya Mwenyezi Mungu na rehema yake. Amesema kweli aliyesema: “Mtu anaweza kulala kwenye miba, pamoja na rehema ya Mwenyezi Mungu, akaamka kwenye tandiko. Na anaweza kulala kwenye hariri bila ya rehe- ma ya Mwenyezi Mungu akaamka kwenye miba.”[3] .
Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu. Je, yuko muumba mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu anayewapa riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana Mola ila Yeye basi mnageuzwa wapi?
Ukumbusho huu wa neema ya Mwenyezi Mungu na kwamba Yeye peke yake ndiye muumba na mwenye kuruzuku ni kuisisitiza Aya iliyotangulia: ‘Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu...’
Katika Nahjul-Balagha imeelezwa:“Mara ngapi Mwenyezi Mungu amewahusisha na neema yake na akwaunganisha na rehema yake. Mmekuwa uchi akawasitiri, mkafanya ya kuwaadhibu akawapa muda. Basi zikamilisheni neema za Mwenyezi Mungu kwa kuwa na subira ya kumtii na kujiweka mbali na maasi, kwani hakika kesho kuanzia leo ni karibu.”
وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٤﴾
4. Na kama wakikukadhibisha, basi wamekwisha kadhibishwa Mitume kabla yako na mambo yote yatarudishwa kwa Mwenyezi Mungu.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿٥﴾
5. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Basi yasiwadanganye maisha ya dunia, wala mdanganyifu asiwadanganye juu ya Mwenyezi Mungu.
إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمْ عَدُوٌّ فَاتَّخِذُوهُ عَدُوًّا إِنَّمَا يَدْعُو حِزْبَهُ لِيَكُونُوا مِنْ أَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴿٦﴾
6. Hakika Shetani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa motoni.
الَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ ﴿٧﴾
7. Wale ambao wamekufuru watakuwa katika adhabu kali na wale ambao wameamini watapata maghufira na malipo makubwa.
أَفَمَن زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ فَرَآهُ حَسَنًا فَإِنَّ اللَّـهَ يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ فَلَا تَذْهَبْ نَفْسُكَ عَلَيْهِمْ حَسَرَاتٍ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا يَصْنَعُونَ ﴿٨﴾
8. Je, yule aliyepambiwa ubaya wa tendo lake akaliona ni jema - basi hakika Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye na humwongoa amtakaye. Basi roho yako isitoke kwa kuwasikitikia. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyafanya.
WALIKADHIBISHWA MITUME KABLA YAKO
Aya 4 – 8
MAANA
Na kama wakikukadhibisha, basi wamekwisha kadhibishwa Mitume kabla yako na mambo yote yatarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, amlipe thawabu muumini mwenye kusubiri katika jihadi yake na amuadhibu mwenye kuikadhibisha haki kwa sababu ya kukadhibisha kwake.
Lengo la Aya hii ni kumpoza Mtume(s.a.w. w ) na kuwakaripia mahasimu na maadui wake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 ( 3:183) na Juz. 17 (22:42).
Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Basi yasiwadanganye maisha ya dunia, wala mdanganyifu asiwadanganye juu ya Mwenyezi Mungu.
Makusudio ya ahadi hapa ni hisabu na malipo baada ya mauti. Udanganyifu wa dunia ni mali, jaha, wanawake, watoto na udanganyifu wa shetani. Umetangulia mfano wake katika Juz. 21 (31:33).
Hakika Shetani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa motoni.
Shetani ametangaza waziwazi uadui wake na binadamu kwa kusema: “Kwa ulivyonipoteza, basi nitahakikisha ninawazaini hapa ardhini na nitawapoteza wote.” Juz. 14 (15:39).
Kundi lake ni wale wafuasi wake wanaosikiliza wasiwasi wake na udanganyifu wake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametuhadharisha kumtii, kwa sababu mwito wake ni wa ufisadi na wa maangamizi, na Mwenyezi Mungu anatoa mwito wa kheri na rehema.
Wale ambao wamekufuru watakuwa katika adhabu kali na wale ambao wameamini watapata maghufira na malipo makubwa.
Kila mtu atakuwa na mwisho, mtamu au mchungu. Mwisho wa mwenye kukufuru na akafanya ufisadi ni Jahannam, makazi maovu; na mwisho wa mwenye kuamini na akatenda mema ni Pepo ambayo ni raha ya daima.
Je, yule aliyepambiwa ubaya wa tendo lake akaliona ni jema.
Kinahaw, hapa kuna maneno ya kukadiriwa kuwa: ‘ni kama ambaye hakupambiwa’ Hakuna mtu yoyote anayeishi bila ya falsafa na kuchukulia mfano wa juu; hata wale wanaokataa falsafa na mfano, huko kukataa kwao ndio falasafa yao na mfano wa juu. Ndio maana ikasemwa: Mwenye kukataa falsafa ndio amekuwa na falsafa.
Tofauti ni kuwa kuna yale anayeijengea falsafa yake kwenye majaribio na uchambuzi, mwengine anaijengea kwenye akili au dini na kuna yale anayeijengea kwenye dhati yake, mapendeleo yake na kupinga mengine yote.
Hafanyi utafiti wala kufikiri au kufanya uchambuzi, kwa sababu haamini akili wala dini; hakuna kitu isipokuwa kilicho kwenye rai yake na mapendeleo yake.
Mtu wa aina hii anaangalia nafsi zake kuwa ndio kipimo pekee cha haki heri na usawa, na kwamba yeye siku zote yuko sawa, hana upungufu wala hakosei.
Huyu tunaweza kumwita shahidi wa upumbavu na mwenye ghururi ya kuua. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemwashiria mtu huyu, katika Aya kadhaa; miongoni mwazo ni: “Sema je, tuwaambie wale wenye hasara mno ya vitendo?” Juz. 16 (18:103) Nyingine ni:
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ ﴿١١﴾ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ ﴿١٢﴾
“Na wanapoambiwa msifanye ufisadi katika ardhi husema, Hakika sisi ni watengezaji tu. Ehe! Hakika wao ndio wafisadi, lakini hawatambui.” Juz. 1 (2:11-12).
Basi Hakika Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye na humwongoa amtakaye.
Hii ni sababu ya kauli yake Mwenyezi Mungu iliyotangulia ‘Je, yule aliyepambiwa ubaya wa tendo lake akaliona ni jema.’ Yaani kwamba Mwenyezi Mungu amemuweka kwenye upotevu na mwisho mbaya kwa sababu amefuata njia inayopelekea hilo; sawa na alivyomuweka kwenye kifo mwenye kunywa sumu na kufa maji aliyejitia baharini akiwa hajui kuogelea.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:27) na Juz. 14 (16:93).
Basi roho yako isitoke kwa kuwasikitikia. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyafanya.
Usisikitike wala usihuzunike, ewe Muhammad, kwa wale ambao hawakuitikia mwito wako madamu wamefuata wenyewe njia ya uovu na ya maangamizi. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti mambo yao, madogo na makubwa. Umetangulia mfano wake katika Juz. 15 (18:2).
وَاللَّـهُ الَّذِي أَرْسَلَ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَسُقْنَاهُ إِلَىٰ بَلَدٍ مَّيِّتٍ فَأَحْيَيْنَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا كَذَٰلِكَ النُّشُورُ ﴿٩﴾
9. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayezituma pepo ziyatimue mawingu, nasi tukayafikisha kwenye nchi iliyokufa, tukaifufua ardhi baada ya kufa kwake. Ndio kama hivyo kufufuliwa.
مَن كَانَ يُرِيدُ الْعِزَّةَ فَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ جَمِيعًا إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ وَالَّذِينَ يَمْكُرُونَ السَّيِّئَاتِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَكْرُ أُولَـٰئِكَ هُوَ يَبُورُ ﴿١٠﴾
10. Mwenye kutaka enzi basi enzi yote ni ya Mwenyezi Mungu. Kwake hupanda neno zuri na amali njema huuinua. Na wanaopanga njama za maovu watapata adhabu kali, na njama za hao zitaangamia.
وَاللَّـهُ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ جَعَلَكُمْ أَزْوَاجًا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ وَمَا يُعَمَّرُ مِن مُّعَمَّرٍ وَلَا يُنقَصُ مِنْ عُمُرِهِ إِلَّا فِي كِتَابٍ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿١١﴾
11. Na Mwenyezi Mungu amewaumba kutokana na udongo. Kisha tone, kisha akawafanya aina kwa aina. Na mwanamke yeyote hachukui mimba wala hazai ila kwa elimu yake. Wala hapewi umri mwenye umri mrefu wala hapunguziwi umri wake, ila yamo katika Kitabu. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
AMALI NJEMA HUIPANDISHA
Aya 9 – 11
MAANA
Na Mwenyezi Mungu ndiye anayezituma pepo ziyatimue mawingu, nasi tukayafikisha kwenye nchi iliyokufa, tukaifufua ardhi baada ya kufa kwake. Ndio kama hivyo kufufuliwa.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:57).
Mwenye kutaka enzi basi enzi yote ni ya Mwenyezi Mungu.
Enzi ni ya Mwenyezi Mungu na ya dini ya Mwenyezi Mungu hasa; na kwa mawili hayo ndio binadamu anakuwa na enzi. Mwenye kujienzi kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu atadhalilika. Ibn Arabi katika kitabu Futuhatul-Makkiyya, anasema:
“Enzi ya haki hasa ni kuwa hakuna Mola ila Yeye, na enzi ya Mtume wake ni kwa Mwenyezi Mungu, na enzi ya waumini ni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi yanathibiti kwenye tanzu yale yaliyonayothibiti kwenye asili.”
Kudhalilika kwa waislamu leo kumetokana na kuwa wao wanajienzi kwa usiokuwa Uislamu. Hapo mwanzo walikuwa ni wachache kuliko sasa, lakini walikuwa ni wengi kwa kujienzi na jamii na umoja wao dhidi ya adui wa Mwenyezi Mungu na adui wao.
Kwake hupanda neno zuri na amali njema huiinua.
Kupanda maneno na kuinuka matendo kwenda kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kinaya cha kuyakubali na kuyalipa thawabu. Maneno mazuri ni yale yanayonufaisha, na vile vile amali njema.
Aya inaashiria kwamba sababu ya kuenziwa na kutukuzwa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kauli na vitendo vinavyowanufaisha watu.
Na wanaopanga njama za maovu watapata adhabu kali, na njama za hao zitaangamia.
Kupanga njama za maovu ni kupanga kuwaudhi waumini na viongozi wema. Lakini njama zao zitaambulia patupu. Maana ya Aya hii ni kama kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na vitimbi viovu havimpati ila mwenyewe.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 (22:5).
Kisha akawafanya aina kwa aina, mweusi na mweupe na mume na mke.Na mwanamke yeyote hachukui mimba wala hazai, ila kwa elimu yake, kwa sababu yeye amekizunguka kila kitu.
Wala hapewi umri mwenye umri mrefu wala hapunguziwi umri wake, ila yamo katika Kitabu. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
Kupunguziwa umri ni kuwa na umri mfupi; na kuwa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kuwa katika ujuzi wa Mwenyezi Mungu. Maana kwa ujumla ni kuwa umri wote uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Katika Nahjul-Balagha imeelezwa:
“Hampati neema katika dunia ila ni kwa kuimaliza nyingine; wala hapati umri mwenye umri miongoni mwenu ila ni kwa kuumaliza mwingine.” Tazama Juz. 4 (3:144 – 148) kifungu cha ‘Ajali haina kinga’.
10
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
وَمَا يَسْتَوِي الْبَحْرَانِ هَـٰذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ سَائِغٌ شَرَابُهُ وَهَـٰذَا مِلْحٌ أُجَاجٌ وَمِن كُلٍّ تَأْكُلُونَ لَحْمًا طَرِيًّا وَتَسْتَخْرِجُونَ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا وَتَرَى الْفُلْكَ فِيهِ مَوَاخِرَ لِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢﴾
12. Na bahari mbili haziwi sawa; hii ni tamu mno, kinywaji chake kinateremka uzuri, na hii ni chumvi sana. Na kutokana na zote, mnakula nyama freshi. Na mnatoa humo mapambo mnayoyavaa. Na unaona vyombo vikikata maji humo, ili mtafute fadhila yake na mpate kushukuru.
يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ ﴿١٣﴾
13. Anauingiza usiku katika mchana na anauingiza mchana katika usiku. Na amelitiisha Jua na Mwezi, kila kimoja kinaendelea mpaka muda uliotajwa. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu, ufalme ni wake. Na wale mnaowaomba badala yake hawamiliki hata utando wa kokwa ya tende.
إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ ﴿١٤﴾
14. Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu. Na wakisikia hawajibu. Na siku ya Kiyama watakataa shirki yenu. Na hapana atakayekuambia kama Yeye mwenye habari.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَنتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿١٥﴾
15. Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa.
إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ ﴿١٦﴾
16. Akitaka atawaondoa na alete viumbe wapya.
وَمَا ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ بِعَزِيزٍ ﴿١٧﴾
17. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu si gumu.
وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ وَإِن تَدْعُ مُثْقَلَةٌ إِلَىٰ حِمْلِهَا لَا يُحْمَلْ مِنْهُ شَيْءٌ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ إِنَّمَا تُنذِرُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَمَن تَزَكَّىٰ فَإِنَّمَا يَتَزَكَّىٰ لِنَفْسِهِ وَإِلَى اللَّـهِ الْمَصِيرُ ﴿١٨﴾
18. Wala mbebaji hatabeba mzigo wa mwingine. Na kama aliyelemewa akiomba achukuliwe mzigo wake, hautachukuliwa hata kidogo, ingawa ana ujamaa. Hakika unawaonya wale tu wanaomcha Mola wao kwa ghaibu na wakasimamisha Swala. Na anayejitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.
BAHARI MBILI HAZIWI SAWA
Aya 12 – 18:
MAANA
Na bahari mbili haziwi sawa; hii ni tamu mno, kinywaji chake kinateremka uzuri, na hii ni chumvi sana.
Aya hii ni miongoni mwa Aya za kilimwengu, inayoashiria aina za maji tamu na chumvi. Kutofautiana huku, hata kukitegemezwa moja kwa moja kwenye sababu zake za kimaumbile, lakini bado sababu hizo zinakomea kwa muumba wa ulimwengu na mbunifu wake.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 19 (25:53).
Na kutokana na zote, hizo bahari mbili,mnakula nyama freshi [4] ; kama samaki.
Na mnatoa humo mapambo mnayoyavaa. Na unaona vyombo vikikata maji humo, ili mtafute fadhila yake na mpate kushukuru.
Imetangulia neno kwa neno katika Juz. 14 (16:13).
Anauingiza usiku katika mchana na anauingiza mchana katika usiku.
Sayari zinazunguka na nyingine zinazunguka kando kando ya nyingine, na kupatikana vipindi. Wakati mwingine mchana unachukuliwa kutoka kwenye usiku na kipindi kingine usiku unachukuliwa kutoka mchana. Nidhamu hii ya hali ya juu inayoendela katika mamilioni ya miaka ni dalili mkataa wa kuweko mpangiliaji mwenye hekima wa ulimwengu huu; sawa na kinavyofahamaisha chombo kinachotekeleza kazi iliyotakiwa, kuwa kuna aliyekitengeneza na kukipangilia vizuri.
Sadfa inakuwa ni batili katika hukumu ya kukaririka; yaani sadfa haiwezi kukaririka.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 3 (3:27).
Na amelitiisha Jua na Mwezi, kila kimoja kinaendelea mpaka muda uliotajwa.
Imetangulia neno kwa neno katika Juz. 13: (13:2).
Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu, ufalme ni wake. Na wale mnaowaomba badala yake hawamiliki hata utando wa kokwa ya tende.
Utando wa kokwa ya tende ni kinaya cha vitu vilivyo duni zaidi. Maana ni kuwa mambo haya ya kustaajabisha yaliyo dhahiri mnayoyaona katika ulimwengu huu, ni katika matengenezo ya Mwenyezi Mungu, na wale manowabudu na kuwatarajia badala ya Mwenyezi Mungu, hawana wala hawezi chochote.
Mkiwaomba, wakiwa hawana hisia wala utambuzi, kama vile mawe na miti,hawasikii maombi yenu. Na wakisikia , wakiwa ni watu, majini au malaika,hawajibu, kwa vile wao wenyewe hawawezi kujinufaisha wala kujizuilia na madhara, itakuwaje waweze kuwasaidia wengine.
Na siku ya Kiyama watakataa shirki yenu.
Watajitenga na ushirikina na upotevu.
Na hapana atakayekuambia kama Yeye mwenye habari ya mwisho wa hawa wanaokadhibisha utume wako, na wengineo katika waasi, ewe Muhammad.
Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa.
Mahitaji ya muumbwa kwa muumba wake hayakatiki milele; kama mahitaji ya sababu kwa msababishi wake.
Ibn Al-arabi anasema katika Kitabu Futahitul- Makkiya: “Mtu ana pande mbili: upande mmoja anamuhitajia Mwenyezi Mungu na upande mwingine anajitosheleza na ulimwengu. Kwa hiyo yeye ni dhalili muhitaji kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mwenye kujitosheleza kwa yule anayetosheka naye.”
Akitaka atawaondoa na alete viumbe wapya. Na hilo, la kuwamaliza waasi na kuwaleta watiifu,kwa Mwenyezi Mungu si gumu.
Lau Mwenyezi Mungu (s.w.t) akitaka lolote linakuwa tu, kwa sababu Yeye ni Muweza wa kila kitu.
Imetangulia neno kwa neno katika Juz. 13 (14: 19 – 20). Vile vile Umetangulia mfano wake katika Juz. 5 (4:133) na Juz. 8 (6:133).
Wala mbebaji hatabeba mzigo wa mwingine.
Imetangulia neno kwa neno katika Juz. 8 (6:164).
Kila mwenye dhambi atahisabiwa na kuadhibiwa kwa madhambi yake tu, lakini Taurat imeeleza kinyume: “Bwana ni mpole... mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao...” (Hesabu 14:18).
Na kama aliyelemewa akiomba achukuliwe mzigo wake, hautachukuliwa hata kidogo, ingawa ana ujamaa.
Aliyelemewa ni yule mwenye mzigo wa madhambi. Maana ni kuwa siku hiyo hakutafaa kunyenyekea wala kuomba msaada kwa ndugu au mpenzi, kwa sababu kila mtu atajishughulikia mwenyewe:
يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴿٣٤﴾ وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ ﴿٣٥﴾ وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ ﴿٣٦﴾ لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ ﴿٣٧﴾
“Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye na mama yake na baba yake na mkewe na wanawe. Kila mtu siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.” (80:34 – 37).
Hakika unawaonya wale tu wanaomcha Mola wao kwa ghaibu na wakasimamisha Swala.
Wanaoitikia mwito wako, ewe Muhammad ni wale tu wanaomwogopa Mwenyezi Mungu na kutarajia thawabu zake. Ama wale wasiomwamini wala kuamini siku ya mwisho, maonyo na nasaha haziwafai chochote.
Na anayejitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake.
Hii ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu:
مَّنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ ﴿٤٦﴾
“Mwenye kutenda mema ni kwa ajili ya nafsi yake na mwenye kutenda uovu ni juu yake. Na Mola wako si Mwenye kuwadhululumu waja” (41:46)
Katika Nahju-Balagha imeelezwa: “Ihisabu nafsi yako, kwani nafsi nyingine ina wa kuihisabu asiyekuwa wewe.”
Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu, Ampe thawabu mwenye kuamini na akatenda mema na amwadhibu mwenye kufanya ufisadi na uovu.
وَمَا يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ ﴿١٩﴾
19. Hawi sawa kipofu na mwenye kuona.
وَلَا الظُّلُمَاتُ وَلَا النُّورُ ﴿٢٠﴾
20. Wala giza na nuru.
وَلَا الظِّلُّ وَلَا الْحَرُورُ ﴿٢١﴾
21. Wala kivuli na joto.
وَمَا يَسْتَوِي الْأَحْيَاءُ وَلَا الْأَمْوَاتُ إِنَّ اللَّـهَ يُسْمِعُ مَن يَشَاءُ وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ ﴿٢٢﴾
22. Na hawawi sawa walio hai na walio maiti. Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye. Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini.
إِنْ أَنتَ إِلَّا نَذِيرٌ ﴿٢٣﴾
23. Hukuwa wewe ila ni mwonyaji
إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَإِن مِّنْ أُمَّةٍ إِلَّا خَلَا فِيهَا نَذِيرٌ ﴿٢٤﴾
24. Hakika sisi tumekutuma kwa haki, uwe mbashiri na mwonyaji. Na hakuna umma wowote ila alipita humo muonyaji.
وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ وَبِالزُّبُرِ وَبِالْكِتَابِ الْمُنِيرِ ﴿٢٥﴾
25. Na kama wakikukadhibisha, basi hakika wamekadhibisha wale waliokuwa kabla yako. Waliwajia Mitume wao kwa dalili wazi wazi na kwa maandiko na kwa kitabu chenye nuru.
ثُمَّ أَخَذْتُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ ﴿٢٦﴾
26. Kisha nikawakamata wale waliokufuru; basi je, kulikuwaje kukanya kwangu?
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ ثَمَرَاتٍ مُّخْتَلِفًا أَلْوَانُهَا وَمِنَ الْجِبَالِ جُدَدٌ بِيضٌ وَحُمْرٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهَا وَغَرَابِيبُ سُودٌ ﴿٢٧﴾
27. Je, huoni kuwa tumeteremsha kutoka mawinguni maji kutoka mbinguni na kwayo tumetoa matunda yenye kuhitalifiana rangi. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbalimbali na myeusi.
وَمِنَ النَّاسِ وَالدَّوَابِّ وَالْأَنْعَامِ مُخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ كَذَٰلِكَ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ ﴿٢٨﴾
28. Na katika watu na wanyama na wanyama howa pia rangi zao zinahitalifiana. Hakika si mengineyo wanaomcha Mwenyezi Mungu, katika waja wake ni wale wajuzi Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye maghufira.
HAWI SAWA KIPOFU NA MWENYE KUONA
Aya 19 – 28
MAANA
Hawi sawa kipofu na mwenye kuona, wala giza na nuru, wala kivuli na joto. Na hawawi sawa walio hai na walio maiti.
Makusudio ya kipofu ni yule mwenye kuacha njia ya haki na ya uongofu; kinyume chake ni mwenye kuona. Giza ni ujinga na upotevu, na nuru ni elimu na uongofu. Kivuli ni neema na joto ni moto wa Jahannam. Ama walio hai ni wale walio na nyoyo zinazosikia mazuri na zikayafuata; kinyume chao ni wafu.
Maana ni kuwa hawi sawa, mbele ya Mwenyezi Mungu na kihali halisi ilivyo, mwenye kuamini akafanya matendo mema na yule mwenye kukufuru akafanya ufisadi. Bali tofauti baina yao ni sawa na tofauti baina ya kipofu na mwenye macho, mwanga na giza, kivuli na joto na mauti na uhai.
Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye. Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini. Hukuwa wewe ila ni mwonyaji.
Maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu yanaathiri na kufanya kazi katika nafsi za wale wanaotafuta haki kwa ajili ya haki na kuisikiliza kwa ajili ya kutaka kuifanyia kazi.
Ama wale ambao hakuna linalowashtua isipokuwa masilahi yao wala hawafanyi lolote isipokuwa masilahi, wao hawasikilizi maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, wala Yeye, ambaye imetukuka hekima yake, hawasukumi kwenye uongofu. Vinginevyo zitabatilika thawabu na adhabu.
Hakika sisi tumekutuma kwa haki, uwe mbashiri na mwonyaji.
Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad (s.a.w.), kwa hoja za kutosheleza, kulingania kwenye haki na kuwa shahidi kwa viumbe. Basi akafikisha ujumbe kwa ukamilifu na akawa ni rehema kwa viumbe wote, hasa waarabu; pale alipowatoa kwenye ujinga wa wajinga na kuwapeleka kwenye nuru ya Uislamu na karama yake.
Imetangulia neno kwa neno katika Juz. 11 (10:42) na Juz.20 (27:80).
KILA UMMA UNA MTUME
Na hakuna uma wowote ila alipita humo muonyaji.
Katika Qur’an kuna Aya zinazofahamisha waziwazi kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametuma Mtume kwa kila umma; miongoni mwa Aya hizo ni hizi zifuatazo:
Aya hii tuliyo nayo.
فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ ﴿٤١﴾
“Basi itakuwaje tutakapowaletea kila umma shahidi.” Juz. 5 (4:41).
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا ﴿٣٦﴾
“Na kwa hakika tulimtuma Mtume kwa kila umma.” Juz. 14 (16:36).
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولٌ ﴿٤٧﴾
“Na kila Umma una Mtume.” Juz. 11 (10:47).
Kuongezea kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٩٢﴾
“Naapa kwa Mola wako tutawauliza wote Juz. 14 (15:92)
Na pia kauli yake:
أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَن يُتْرَكَ سُدًى ﴿٣٦﴾
“Hivi anadhani mtu kuwa ataachwa bure?” (75:36)
Sio mbali kuwa makusudio ya mjumbe, muonyaji na shahidi ni kila linalosimamia hoja na kukata nyudhuru, liwe limetoka kwa Nabii, Mtume, Kitabu cha dini, kiongozi mwema au hukumu ya akili ya kimsingi, isiyopingika na wenye akili salama na umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu; kama ubaya wa dhulma na hiyana, na uzuri wa uadilifu na uaminifu n.k. Wala hatujui umma ulioishi kwa vurugu bila nidhamu na kumwachia kila mtu afanye atakavyo bila ya kumhisabu kwa kauli na vitendo.
Unaweza kuuliza : Je, hii haipingani na kauli yake Mwenyezi Mungu, iliyo katika Juzuu hii: “Wala hatukuwatumia muonyaji kabla yako.” (34:44). Ambapo Aya tuliyo nayo inathibitisha kuwa kila kaumu ina muonyaji na ya pili inakataa kuwa kaumu ya Muhammad(s.a.w. w ) ilikuwa na muonyaji kabla yake?
Jibu : Muonyaji katika Aya tuliyo nayo inachanganya kila muonyaji awe mtume au la. Ama katika Aya ya pili inahusuiana na Mtume. Kwa hiyo hakuna kupingana baina ya Aya mbili na maana ni kuwa kaumu ya Muhammad(s.a.w. w ) hawakujiwa na Mtume kabla ya kutumwa yeye, lakini walijiwa na muonyaji wa akili na maumbile; nayo ni muonyaji tosha wa kuwapa hoja; hasa katika kuabudu kwao mawe.
Ndio maana Mtume(s.a.w. w ) alikuwa akiwajadili kwa mantiki ya akili na kuwaambia:
قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا وَاللَّـهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٧٦﴾
“Sema: Je, mnamwabudu badala ya Mwenyezi Mungu, ambaye hawezi kuwadhuru wala kuwanufaisha? Juz. 6 (5:76).
Na kama wakikukadhibisha, basi hakika wamekadhibisha wale waliokuwa kabla yako. Waliwajia Mitume wao kwa dalili wazi wazi na kwa maandiko na kwa kitabu chenye nuru.
Makusudio ya maandiko hapa ni hikima na mawaidha. Kitabu chenye nuru ni Tawrat iliyoteremshwa kwa Musa, Injil iliyoteremshwa kwa Isa na vitabu vinginevyo vilivyotermshwa kabla ya Mtume wa mwisho. Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (3:184).
Kisha nikawakamata wale waliokufuru; basi je, kulikuwaje kukanya kwangu?
Makusudio ya kukanya hapa ni adhabu. Yaani Mwenyezi Mungu aliwakanya kwa kauli na vitendo. Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 (22:44) na Juzuu hii tuliyo nayo (34:45).
Je, huoni kuwa tumeteremsha kutoka mawinguni maji kutoka mbinguni na kwayo tumetoa matunda yenye kuhitalifiana rangi na ladha yake na harufu yake.
Hakuna mwenye shaka kwamba kutoafautiana huku kunatokana na sababu za kimaumbile, lakini zote hizi zinaishia kwa muumba wa hayo maumbile. Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:4) katika kifungu cha ‘Sayyid Afghani na wanaomkana Mungu.’
Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbalimbali na myeusi.
Anasema, mkuu wa wasemaji, kwamba Yeye amefanya kwenye majabali njia; kuna nyeupe, nyekundu na nyingine ni nyeusi. Kila moja katika njia hizo tatu inatofautiana rangi.
Mazingatio katika kutofautiana huku ni kufahamisha juu ya uweza wa Mwenyezi Mungu na matakwa yake; sawa na tofauti ya matunda.
Na katika watu na wanyama na wanyama howa pia rangi zao zinahitalifiana.
Kuunganisha wanyama na wanyama hoa, ni katika kuunganisha maalum kwenye ujumla, kwa sababu neno lililotumika kwa wanyama, Dawab, lina maana ya wanaotemebea ardhini, wakiwemo wanyama howa (mifugo) ambao ni ngamia, ng’ombe, kondoo na mbuzi.
Maana ni kuwa kutofautiana rangi za watu na kutofautiana wanyama, kunafahamisha uweza wa Mwenyezi Mungu; sawa na kutofautiana matunda na njia.
Hakika si mwengineyo wanaomcha Mwenyezi Mungu, katika waja wake ni wale wajuzi.
Makusudio ya wenye ujuzi hapa ni wale walioamini kwa kujua, sio kwa kuiga, na wakaujua utukufu wake kwa dalili na hoja.
Hakuna mwenye shaka kwamba mwenye kujua uweza wa asiyeshindwa na kitu wala kupitwa na kitu, hawezi kuacha kumuogopa; ndio maana wanaomjua Mwenyezi Mungu ndio wanaohofia zaidi hasira za Mwenyezi Mungu na ndio walio na matarajio zaidi ya fadhila na msamaha wake.
Sisi ni katika wale wanaoamini kuwa hakuna imani ya kweli bila ya takua wala hakuna takua bila ya mwamko. Ndio maana Mtume mtukufu(s.a.w. w ) akasema: “Ubora wa mjuzi juu ya mwenye kuabudu ni ubora wa mwezi usiku kwenye nyota.” Pia kuna Hadith mashuhuri ya Mtume(s.a.w. w ) :“Usingizi wa mwenye ujuzi ni bora kuliko ibada ya mjinga.”
Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye maghufira.
Mwenye nguvu katika kuwawaadhibu wenye kupituka mipaka na kufanya dhulma, na ni mwenye maghufira kwa mwenye kutubia na kurejea.
11
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّـهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ ﴿٢٩﴾
29. Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakasimamisha Swala, na wakatoa kwa siri na kwa uwazi katika tuliyowapa, wanataraji biashara isiyoangamia.
لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٠﴾
30. Ili awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na awazidishie kutokana na fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye shukrani.
وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ هُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ إِنَّ اللَّـهَ بِعِبَادِهِ لَخَبِيرٌ بَصِيرٌ ﴿٣١﴾
31. Na yale tuliyokupa wahyi kutoka Kitabuni ni haki yenye kusadikisha yaliyokuwa kabla yake. Hakika Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni Mwenye habari, Mwenye kuona.
ثُمَّ أَوْرَثْنَا الْكِتَابَ الَّذِينَ اصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ وَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ ﴿٣٢﴾
32. Kisha tumewarithisha Kitabu wale ambao tumewachagua katika waja wetu. Kati yao yupo aliyejidhulumu nafsi yake, na yupo wa katikati, na yupo aliyetangulia katika mambo ya kheri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo fadhila kuu.
جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَلُؤْلُؤًا وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ ﴿٣٣﴾
33. Mabustani ya milele watayaingia. Humo watavikwa vikuku vya dhahabu, na lulu, na mavazi yao humo ni hariri.
وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي أَذْهَبَ عَنَّا الْحَزَنَ إِنَّ رَبَّنَا لَغَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٤﴾
34. Na watasema: Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu (Alhamdu lillah) ambaye ametuondoloea huzuni. Hakika Mola wetu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye shukrani.
الَّذِي أَحَلَّنَا دَارَ الْمُقَامَةِ مِن فَضْلِهِ لَا يَمَسُّنَا فِيهَا نَصَبٌ وَلَا يَمَسُّنَا فِيهَا لُغُوبٌ ﴿٣٥﴾
35. Ambaye ametuweka katika nyumba ya kukaa, humo haitugusi tabu wala humo hakutugusi kuchoka.
ALIYEJIDHULUMU, ALIYE KATIKATI, NA ALIYETANGULIA KWENYE KHERI
Aya 29 – 35
MAANA
Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakasi- mamisha Swala, na wakatoa kwa siri na kwa uwazi katika tuliyowapa, wanataraji biashara isiyoangamia.
Makusudio ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni Qur’an Tukufu. Kusoma ni kuzingatia maana yake na kuyatumia. Kwa sababu kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu.... ‘iliyokuja baada ya kauli yake: ‘Hakika si mengineyo wanaomcha Mwenyezi Mungu, katika waja wake ni wale wajuzi.’ Inaashiria hivyo.
Katika Nahjul-Balagha kuna maelezo:“... Katika zama hizo hakutakuwa na kitu kisichokuwa na thamani zaidi kuliko kusomwa Qur’an inavyopaswa kusomwa kwake. Wala hakutakuwa na kitu kilicho na thamni zaidi kuliko Qur’an kutowekwa mahali pake.”
Maana ya Aya ni kuwa wale ambao wanazingatia Qur’an na wakatumia hukumu zake, wakikusudia radhi ya Mwenyezi Mungu, basi watakuwa wamepata faida kwenye biashara yao na watakuwa ni wenye kufuzu.
Amesema tena kwenye Nahjul-Balagha:“ Na wameuza machache kati- ka dunia hii isiyodumu kwa mengi ya akhera isiyoisha.”
Ili awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na awazidishie kutokana na fad- hila zake. Hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye shukrani.
Waliamini na wakamfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu, kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, thawabu zake, msamaha wake na rehema zake, na wakapata waliyoyataka.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 3 (2:274) na Juz. 13 (13:22).
Na yale tuliyokupa wahyi kutoka Kitabuni ni haki.
Makusudio ya Kitabu ni Qur’an ikiwa inachukua dalili na hoja za ukweli wake na uhakika wake; ambazo ni hukumu zake na mafundisho yake yanayoipa kipaumbele imani ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu na umoja wake na heshima ya mtu na uhuru wake.
Yenye kusadikisha yaliyokuwa kabla yake katika vitabu na sharia zinazosimama kwenye misingi hii – misingi ya kumwamini Mwenyezi Mungu na utu.
Hakika Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni Mwenye habari, Mwenye kuona yale yaliyo na masilahi kwao na yaliyo na ufisadi. Anawaamrisha lile na kuwakataza hili. Lakini Waislamu wameacha yaliyoamrishwa na Qur’an na wakafanya waliyokatazwa nayo. Wamesadikisha aliyoyasema Mtume mtukufu(s.a.w. w ) aliposema:“Utakuja wakati kwa umma wangu watakataza mema na kuamrisha maovu.” Kwa hiyo si ajabu kusalitika na viumbe waovu.
Kisha tumewarithisha Kitabu wale ambao tumewachagua katika waja wetu.
Makusudio ya Kitab ni Qur’an, hilo halina shaka yoyote; isipokuwa wafasiri wametofautiana katika makusudio ya waliochaguliwa. Wengi wakasema ni umma wa Muhammad(s.a.w. w ) .
Tuonavyo sisi ni Muhammad(s.a.w. w ) , Ahlu bayti wake, maswahaba wake na maulama wa umma wake wanaokwenda na sera yake na wakatumia sunna yake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu hawezi kuwachagua isipokuwa wenye takua walio wema.
Qur’an Tukufu imelitumia neno hili kwa maana haya katika Aya kadhaa; miongoni mwazo ni:
إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٣٣﴾
“Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na watoto wa Ibrahim na watoto wa Imran juu ya walimwengu wote.” Juz. 3 (3:33).
Ama dhamiri katikakati yao yupo aliyejidhulumu nafsi yake, na yupo wa katikati, na yupo aliyetangulia katika mambo ya kheri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inarudia neno waja wetu, kwa vile ndilo lililo karibu.
Mwenye kujidhulumu ni yule ambaye maovu yake yamekuwa makubwa kuliko mema yake. Aliyetangulia katika heri ni ambaye mema yake yamekuwa makubwa kuliko maovu yake; hasa yule ambaye hana maovu. Aliye katikati ni ambaye mema yake na maovu yake yamekuwa sawa.
Hiyo ndiyo fadhila kuu. Mabustani ya milele watayaingia. Humo watavikwa vikuku vya dhahabu, na lulu, na mavazi yao humo ni hariri.
‘Hiyo’ ni hiyo hali ya kurithi na kuchaguliwa. Mabustani ya milele na kuendelea, ni ubainifu wa hiyo fadhila kuu ambayo ameifanya ni malipo ya wale aliowachagua.
Dhahabu, lulu na hariri ni ibara nyingine ya kauli yake Mwenyezi Mungu:
وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ ﴿٧١﴾
“Humo vitakuwemo ambavyo nafsi inavipenda na macho yanavifurahia.” (43:71).
Kuna Hadith kuwa bedui mmoja alimuuliza Mtume: “Je, Peponi kuna samai, yaani nyimbo? Mtume(s.a.w. w ) akasema: “Ndio.”
Na watasema:, sifa njema ni za Mwenyezi Mungu (Alhamdu lillah) ambaye ametuondoloea huzuni. Hakika Mola wetu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye shukrani. Ambaye ametuweka katika nyumba ya kukaa, humo haitugusi tabu wala humo hakutugusi kuchoka.
Watamshukuru Mwenyezi Mungu na kumsifu kwa kuwandolea hofu na kuokoka na moto na adhabu. Pia kuondokana na tabu na mashaka na kudumu kwenye neema na shangwe.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ نَارُ جَهَنَّمَ لَا يُقْضَىٰ عَلَيْهِمْ فَيَمُوتُوا وَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُم مِّنْ عَذَابِهَا كَذَٰلِكَ نَجْزِي كُلَّ كَفُورٍ ﴿٣٦﴾
36. Na wale ambao wamekufuru watakuwa na moto wa Jahannam, hawahukumiwi wakafa wala hawatapunguziwa adhabu yake. Hivyo ndivyo tunavyomlipa kila mwenye kuzidi ukafiri.
وَهُمْ يَصْطَرِخُونَ فِيهَا رَبَّنَا أَخْرِجْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ أَوَلَمْ نُعَمِّرْكُم مَّا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَاءَكُمُ النَّذِيرُ فَذُوقُوا فَمَا لِلظَّالِمِينَ مِن نَّصِيرٍ ﴿٣٧﴾
37. Na humo watapiga makelele: Mola wetu! Tutoe tufanye mema, sio yale tuliyokuwa tukiyafanya. Je, hatukuwapa umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka, na akawajia mwonyaji? Basi onjeni! Na madhalimu hawana wa kuwanusuru.
إِنَّ اللَّـهَ عَالِمُ غَيْبِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٣٨﴾
38. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa siri za mbingu na ardhi. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
هُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ فَمَن كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُ وَلَا يَزِيدُ الْكَافِرِينَ كُفْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ إِلَّا مَقْتًا وَلَا يَزِيدُ الْكَافِرِينَ كُفْرُهُمْ إِلَّا خَسَارًا ﴿٣٩﴾
39. Yeye ndiye aliyewafanya nyinyi makhalifa katika ardhi. Na anayekufuru, basi kufuru yake ni juu yake; na kufuru za makafiri haziwazidishii kwa Mola wao ila kuchukiwa. Wala kufuru za makafiri haziwazidishii ila hasara.
HAWAHUKUMIWI WAKAFA
Aya 36 – 39
MAANA
Na wale ambao wamekufuru watakuwa na moto wa Jahannam, hawahukumiwi wakafa wala hawatapunguziwa adhabu yake.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja aina nyingi ya adhabu kwa waasi; miongoni mwazo ni aina hii: Uchungu wa adhabu, kudumu kwake na kuendelea kwake. Hakuna mauti ya kumaliza adhabu wala sababu ya kupelekea kupunguziwa adhabu.
Hivyo ndivyo tunavyomlipa kila mwenye kuzidi ukafiri.
Ni malipo yanayolingana na kosa lake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 5 (4:56 – 57).
Na humo watapiga makelele: Mola wetu! Tutoe tufanye mema, sio yale tuliyokuwa tukiyafanya.
Watapiga kelele na kutaka usaidizi, lakini hakuna wa kuwaokoa. Watatubia, lakini baada ya kupita muda. Umetangulia mfano wake katika Juz. 18 (23:99 – 100,107).
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:
وَلَوْ رُدُّوا لَعَادُوا لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿٢٨﴾
“Na kama wangelirudishwa, bila shaka wangeyarudia yale waliyokatazwa na hakika wao ni waongo.” Juz. 7 (6:28).
Watapiga kelele na kutaka usaidizi, lakini hakuna wa kuwaokoa. Na watataka kutubia, lakini baada ya kupita muda. Umetangulia mfano wake katika Juz. 18 (23: 99-100, 107).
Je, hatukuwapa umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka, na akawajia mwonyaji?
Wanamtaka Mwenyezi Mungu awaruidishe duniani ili wawahi yale yaliyowapita katika imani na matendo mema.
Mwenyezi Mungu naye anawajibu kuwa mlikuwako duniani hapo mwanzo, mkakaa muda mwingi, akawajia mbashiri na muonyaji, mkafahamishwa njia ya uwongofu, lakini mkakataa.
Basi onjeni adhabu, hivi sasa, kutokana na vile mlivyokuwa mkikufuru.Na madhalimu hawana wa kuwanusuru, kwa sababu wao ndio waliojidhulumu wenyewe kwa uchaguzi wao mbaya. Kwani Mwenyezi Mungu aliwapa hoja na ubainifu.
Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa siri za mbingu na ardhi. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
Anajua siri na dhahiri, na yanayofichikana machoni ardhini na mbinguni, wala hakuna chochote kilichokuwa na kitakachokuwa kinachofichikana kwake.
Yeye ndiye aliyewafanya nyinyi makhalifa katika ardhi. Na anayekufuru, basi kufuru yake ni juu yake; na kufuru za makafiri haziwazidishii kwa Mola wao ila kuchukiwa. Wala kufuru za makafiri haziwazidishii ila hasara.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameumba ardhi katika muundo wa kuweza kuishi watu, wakirithishana vizazi na vizazi. Akawapa akili na uwezo wa kuweza kuitumia kadiri wanavyotaka. Akawaamrisha wamwabudu Yeye peke yake bila ya kumshirikisha na jambo; akawawekea mipaka na kuwakataza wasiikiuke.
Mwenye kusikiliza na akawa na utii basi atapata malipo mema na mwenye kupinga basi atapata adhabu ya moto itakayozidi, na kuzidi kila wanavyozidisha uasi na kupituka mipaka. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:
إِنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ لِيَزْدَادُوا إِثْمًا ﴿١٧٨﴾
“Hakika tunawapa muda ili wazidi katika dhambi.” Juz. 4 (3:178).
قُلْ أَرَأَيْتُمْ شُرَكَاءَكُمُ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا فَهُمْ عَلَىٰ بَيِّنَتٍ مِّنْهُ بَلْ إِن يَعِدُ الظَّالِمُونَ بَعْضُهُم بَعْضًا إِلَّا غُرُورًا ﴿٤٠﴾
40. Sema mnaona hawa washirika wenu mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, nionyesheni wameumba nini katika ardhi? Au wana ushirika wowote katika mbingu? Au tumewapa Kitabu, nao kwa hicho, wakawa na hoja, lakini madhalimu hawaahidiani wao kwa wao ila udanganyifu.
إِنَّ اللَّـهَ يُمْسِكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ أَن تَزُولَا وَلَئِن زَالَتَا إِنْ أَمْسَكَهُمَا مِنْ أَحَدٍ مِّن بَعْدِهِ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ﴿٤١﴾
41. Kwa hakika Mwenyezi Mungu huzuia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka hapana yeyote wa kuzizuia isipokuwa Yeye. Hakika Yeye ni Mpole, Mwingi wa maghufira.
وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِن جَاءَهُمْ نَذِيرٌ لَّيَكُونُنَّ أَهْدَىٰ مِنْ إِحْدَى الْأُمَمِ فَلَمَّا جَاءَهُمْ نَذِيرٌ مَّا زَادَهُمْ إِلَّا نُفُورًا ﴿٤٢﴾
42. Na waliapa kwa ukomo wa kuapa kwao, kwamba akiwafikia mwonyaji bila ya shaka watakuwa waongofu zaidi kuliko taifa jingine lolote. Lakini alipowajia muonyaji hakuwazidishia ila kukimbia.
اسْتِكْبَارًا فِي الْأَرْضِ وَمَكْرَ السَّيِّئِ وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا سُنَّتَ الْأَوَّلِينَ فَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّـهِ تَبْدِيلًا وَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّـهِ تَحْوِيلًا ﴿٤٣﴾
43. Kwa kutakabari kwao katika ardhi na kufanya vitimbi viovu. Na vitimbi viovu havimpati ila mwenyewe. Basi hawangoji ila desturi ya wa zamani. Hutapata mabadiliko katika desturi ya Mwenyezi Mungu wala hutapata mageuzi katika desturi ya Mwenyezi Mungu.
ANAZIZUIA MBINGU NA ARDHI
Aya 40 – 43
MAANA
Katika Aya hii ya kwanza hapa, Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewapa hoja tatu washirikina:
Sema mnaona hawa washirika wenu mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, nionyesheni wameumba nini katika ardhi?
Niambieni enyi washirikina! Ni jambo gani lililowafanya mumfanye Mwenyezi Mungu ana washirika? Je, ardhini kuna kitu chochote kinachofahamisha kuwa kimetengenezwa na wengi? Hapana! Vitu vyote vina- julisha kuweko Mungu mmoja tu, na mpangilio wake ni ushahidi wa utukufu wake na hekima yake.
Au wana ushirika wowote katika mbingu?
Yaani hao mnaowaabudu wana athari yoyote mbinguni kujulisha kuwa wao ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika kuumba?
Au tumewapa Kitabu, nao kwa hicho, wakawa na hoja.
Tuliowapa ni hao washirikina sio washirika wanaoabudiwa. Maana ni kuwa au mumewafanya washirika wa Mungu hao mnaowabudu kwa kutegemea Kitabu kilichoteremshwa au Nabii aliyetumwa? Kwa ujumla ni kuwa hakuna hoja yoyote ya kiakili na kinakili kwa wanavyovishirikisha; bali wao wanamangamanga tu.
Lakini madhalimu hawaahidiani wao kwa wao ila udanganyifu.
Makusudio ya udanganyifu hapa ni ubatilifu. Viongozi wa washirikina walikuwa wakiwaambi wafuasi wao kuwa masanamu yatawaombea kesho. Hakuna mwenye shaka kuwa ahadi hii ni uwongo, uzushi na ubatilifu.
Kwa hakika Mwenyezi Mungu huzuia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka hapana yeyote wa kuzizuia isipokuwa Yeye. Hakika Yeye ni Mpole, Mwingi wa maghufira.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amezizuwia sayari kwa nguvu ya mvutano; sawa na anavyowazuia ndege angani kwa mbawa zao. Mwenyezi Mungu ametegemeza kwake, kwa sababu yeye ni muumba wa ulimwengu na msababishi wa sababu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 (22:65).
Na waliapa kwa ukomo wa kuapa kwao, kwamba akiwafikia mwonyaji bila ya shaka watakuwa waongofu zaidi kuliko taifa jingine lolote.
Walioapa ni washirikina. Katika Bahrul-Muhit imesemwa kuwa watakuwa waongofu ambao hawana mfano. Makuraishi walikuwa wakiwapinga Mayahudi kwa kupotoka kwao na dini yao na kuwaua mitume wao. Wakaapa viapo vya nguvu kwamba akiwajia Mtume kutoka kwa kwa Mwenyezi Mungu watakuwa watiifu zaidi.
Lakini alipowajia muonyaji hakuwazidishia ila kukimbia kwa kutak- abari kwao katika ardhi na kufanya vitimbi viovu.
Hatimaye mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliwajia na hoja na ubainifu, lakini wao walimkadhibisha na wakamkimbia na wakamfanyia kiburi yeye na mwito wake. Vile vile walimfanyia vitimbi yeye na wafuasi wake na wakawazuia watu kuamini utume wake. Hata hivyo mwisho walishindwa na wakasalimu amri wakiwa dhalili na wanyonge.
Na vitimbi viovu havimpati ila mwenyewe.
Vitimbi viovu ni kumdhamiria ubaya ndugu yako na kumpangia njama, bila ya yeye kujua, ili atumbukie. Hata hivyo, akiwa hajui yaliyodhamiri- wa na kupangwa, basi Mwenyezi Mungu anajua na atamlipa mpanga njama malipo ya muongo mwenye hadaa na balaa litamrudia yeye.
Basi hawangoji ila desturi ya wa zamani. Hutapata mabadiliko katika desturi ya Mwenyezi Mungu, wala hutapata mageuzi katika desturi ya Mwenyezi Mungu.
Desturi ya wa zamani ni desturi ya Mwenyezi Mungu kwa watu wa zamani ambayo ni kuangamia waliowakadhibisha mitume wa Mwenyezi Mungu. Maana ni je, hawajui wanaomkadhibisha Mtume wetu Muhammad, kwamba Mwenyezi Mungu aliangamiza kaumu ya Nuh, A’ad, Thamud na mfano wao waliowakadhibisha mitume? Na kwamba hii ni desturi yake Mwenyezi Mungu isiyobadilika wala kugeuka? Je, hawapati funzo kwa wengine?
أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَكَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعْجِزَهُ مِن شَيْءٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ إِنَّهُ كَانَ عَلِيمًا قَدِيرًا ﴿٤٤﴾
44. Je, hawakusafiri katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa waliokuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao. Na hakuna kitu kiwezacho kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala ardhini. Hakika Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye kuweza.
وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّـهُ النَّاسَ بِمَا كَسَبُوا مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهْرِهَا مِن دَابَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِعِبَادِهِ بَصِيرًا ﴿٤٥﴾
45. Na lau Mwenyezi Mungu angeliwachukulia watu kwa waliyoyachuma, basi asingeliwacha katika ardhi hata mnyama mmoja, lakini yeye anawaakhirisha mpaka muda maalum. Ukifika muda wao basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake.
ASINGELIMUACHA HATA MNYAMA MMOJA
Aya 44 – 45
MAANA
Je, hawakusafiri katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa waliokuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao.
Aya hii inaungana na ile ya kabla yake. Ile inasema kuwa desturi ya Mwenyezi Mungu kwa waliowakadhibisha hapo mwanzo ni kuangamizwa na kung’olewa kabisa, na hii inawambia wale wanaomkadhibisha Muhammad(s.a.w. w ) kuwa athari ile ya waliokadhibisha kabla yenu iko wazi na wala sio mbali na nyinyi. Hebu safirini kidogo katika ardhi muone. Pengine mnaweza kuzingatia na mkapata funzo. Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 ( 22:46).
Na hakuna kitu kiwezacho kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala ardhini. Hakika Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye kuweza.
Hampiti aliyepo wala hamshindi mwenye kukimbia. Kila kitu kinanyenyekea uweza wake na kinanyenyekea ukuu wake. Katika baadhi ya tafsiri imeelezwa kuwa viumbe wote wanahusika na dhambi; hata wanyama, ndege na chembe chembe. Kwa sababu Mwenyezi Mungu anawateremshia adhabu, na akiiteremsha inawaenea wote; kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً ﴿٢٥﴾
“Na jikingeni na fitna ambayo haitawasibu wale waliodhulumu miongoni mwenu peke yao”
Juz. 9 (8:25).
Na lau Mwenyezi Mungu angeliwachukulia watu kwa waliyoyachuma, basi asingeliwacha katika ardhi hata mnyma mmoja, lakini yeye anawaakhirisha mpaka muda maalum. Ukifika muda wao basi haki- ka Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake.
Jambo linalofahamisha zaidi maudhi ya mtu kwa muumba wake, ni kuwa yeye anakula riziki yake na anamwabudi mwingine. Hii peke yake inatosha kuadhibiwa. Lakini kila kitu, mbele ya Mwenyezi Mungu, kina muda maalum.
MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA TANO: SURAT FATIR
12
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
Sura Ya Thelathini na Sita: Surat Yasin. Imeshuka Makka isipokuwa Aya moja. Ina Aya 83.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
يس ﴿١﴾
1. Yasin.
وَالْقُرْآنِ الْحَكِيمِ ﴿٢﴾
2. Naapa kwa Qur’an yenye hekima.
إِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣﴾
3. Hakika wewe bila shaka ni miongoni mwa waliotumwa.
عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٤﴾
4. Juu ya njia iliyonyooka.
تَنزِيلَ الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ ﴿٥﴾
26. Ni uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أُنذِرَ آبَاؤُهُمْ فَهُمْ غَافِلُونَ ﴿٦﴾
6. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi ni wenye kughafilika.
لَقَدْ حَقَّ الْقَوْلُ عَلَىٰ أَكْثَرِهِمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٧﴾
7. Imekwishathibiti kauli juu ya wengi wao, kwa hiyo hawaamini.
إِنَّا جَعَلْنَا فِي أَعْنَاقِهِمْ أَغْلَالًا فَهِيَ إِلَى الْأَذْقَانِ فَهُم مُّقْمَحُونَ ﴿٨﴾
8. Hakika tumeweka minyororo shingoni mwao, nayo inafika videvuni, kwa hiyo vichwa vyao viko juu.
وَجَعَلْنَا مِن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا فَأَغْشَيْنَاهُمْ فَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ ﴿٩﴾
9. Na tumeweka kizuizi mbele yao na kizuizi nyuma yao na tumewafunika, kwa hiyo hawaoni.
وَسَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠﴾
10. Ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini.
إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ اتَّبَعَ الذِّكْرَ وَخَشِيَ الرَّحْمَـٰنَ بِالْغَيْبِ فَبَشِّرْهُ بِمَغْفِرَةٍ وَأَجْرٍ كَرِيمٍ ﴿١١﴾
11. Hakika unamuonya yule tu anayefuata ukumbusho na akamcha Mwingi wa rehema kwa ghaibu. Basi mbashirie maghufira na ujira wa heshima.
إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ فِي إِمَامٍ مُّبِينٍ ﴿١٢﴾
12. Hakika sisi tunawahuisha wafu na tunayaandika wanayoyatanguliza na athari zao. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari linalobainisha.
WEWE NI KATIKA MITUME
Aya 1 – 12
MAANA
Yasin
Wafasiri wengi wamesema kuwa tamko hili lina maana kama mianzo mingine ya Sura yenye herufi za mkato; kama ilivyo katika Juz.1 (2:1). Ama kauli yake Mwenyezi Mungu: “Amani kwa Ilyasin” (37:130), makusudio yake ni Ilyas.
Naapa kwa Qur’an yenye hekima. Hakika wewe bila shaka ni miongoni mwa waliotumwa juu ya njia iliyonyooka.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameapa, kwa Qur’an yenye hekima, kwamba Muhammad(s.a.w.w) yuko kwenye dini ya ya sawasawa. Kuapa kwa Mwenyezi Mungu kwa Qur’an pamoja na kuisifu kuwa ina hekima, kunaashiria kwenye utukufu wa Qur’an na ukuu wake na kwamba ni dalili yenye nguvu zaidi juu ya ukweli wa Muhammad(s.a.w.w) katika mwito wake.
Ama kujisifu Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa nguvu na rehema, katika kauli yake:
Ni uteremsho wa Mwenye nguvu Mwenye kurehemu, ni ishara kuwa anawachukulia waasi kwa namna ya Mwenye uwezo na anawahurumia waumini na wenye kutubia.
Imam Ali(a.s) anasema:“Ghadhabu haimshughulishi (asiwe) na rehema, wala rehema haimshughulishi (asiwe) na mateso.”
MDUNDO WA NDANI KATIKA QUR’AN
Mnamo mwaka 1959 Mustafa Mahmud, Mmisri, alitunga kitabu Allahu wal-insan (Mungu na mtu). Katika kitabu hicho alikana Mungu na ufufuo, nami nikamjibu kwa kutunga kitabu Allahu wal-Aqli (Mungu na Akili).
Kisha nikafuatilia makala zake na tungo zake. Nikasoma makala yake katika jarida linaloitwa Ruzil-yusf la tarehe 10-4-1967 akikiri kuweko ufufuo. Hayo nimeyaashiria katika Juz. 1 (2:28 – 29) kifungu cha ‘Ufufuo.’
Mustafa Mahmud ni mwana fasihi, mwenye akili inayogundua undani na siri za lugha. Ushahidi wa hayo ni aliyoyaandika kuhusu Qur’an katika jarida la Sabahul-khayr la tarehe 1-1-1970 kwa anuani ya “Usanifu wa Qur’an” Tunadokoa machache katika makala hiyo, kama yafuatavyo:
“Sijui niseme nini kuelezea hisia niliyoipata katika ibara ya kwanza ya Qur’an... Basi matamshi yake yalikuwa yakiingia kwenye nafsi yangu, kama kwamba ni kiumbe hai chenye maisha ya aina ya peke yake... Nikagundua simulizi za mdundo wa kindani katika ibara za Qur’an Hii ni siri ya ndani sana katika mpangilio wa Qur’an...
Yenyewe sio mashairi wala nathari au lugha ya mjazo; isipokuwa ni ubainifu maalum wa maneno yaliyoundwa kwa njia inayogundua mdundo wa kindani. Mdundo uliozoeleka unakuja kutoka nje na kufika masikioni, na sio ndani bali unatokana na mahadhi, wizani na kina.
Mdundo wa Qur’an hauna wizani wala kina au mahadhi, lakini pamoja na hayo, unashuka kwa kila herufi yake... kutoka wapi na vipi, hiyo ndiyo siri katika siri za Qur’an zisizofanana na mfumo wowote wa kifasihi. Inashangaza na wala hatuwezi kuujua mfumo wake. Ni mfumo wa kipekee haujapatakina katika kila kilichoandikwa kwa lugha ya kiarabu ya zamani na ya sasa. Haiwezekani kuuiga mfumo huu.”
Ndio haiwezekani kuuiga. Na hapa ndio inapatikana siri ya muujiza wa Qur’an. Baada ya mwandishi huyu kuleta ushahidi mwingi wa hakika hii katika maneno ya Mwenyezi Mungu na Aya zake, aliendelea kusema:
“Na sio mdundo wa kindani tu ndio kitu cha aina yake katika Qur’an, bali kuna sifa nyingine inayokutambulisha kuwa hii ni sanaa ya muumba sio ya muumbwa... Hebu isikilize Qur’an ikisifia mfungamano wa maingiliano ya kijinsia baina ya mume na mke, kwa tamako laini na la heshima, jambo ambalo huwezi kulipata kwenye lugha yoyote: “Alipomkurubia [5] 1 alishika mimba nyepesi.” Juz. 9 (7:189).
Tamko hili taghashaha alimfunika (kwa maana ya kumkurubia) linamchanganya mume na mke kama vinavyochanganyika vivuli viwili au kama rangi inavyofunika rangi nyingine. Tamko hili la ajabu linalofahamisha muingiliano mkamilifu wa mume na mke, ni ukomo wa ibara.
Hakika Qur’an ina hali ya kipekee na ya ajabu, inayoleta unyenyekevu katika nafsi na kuathiri moyo, pale tu matamshi yake yanapogusa masikio, kabla ya akili kuanza kuyafanyia kazi. Na ikianza kufanya uchambuzi na kutaamali, inagundua vitu vipya vinavyomzidisha unyenyekevu. Lakini hii ni hatua ya pili; inaweza kutokea na isitokee, inaweza kugundua siri za Aya na inaweza isigundue, na inaweza kuleta busara au isilete, lakini unyenyekevu upo.”
Hii nayo ni aina mojawapo ya muujiza wa Qur’an. Mwandishi huyu wa kitabu Allahu wal insan alimaliza makala yake ndefu kwa kusema: “Hakika Qur’an ni matamshi na maana kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye amekizunguuka kila kitu kwa ujuzi.”
Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi ni wenye kughafilika.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja kuwa Muhammad(s.a.w.w) ni Mtume wa haki na kwamba Qur’an imetoka kwake, sasa anabainisha umuhimu wa Qur’an kuwa inakataza aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu, kwenye masikio ya waarabu, walioghafilika na Mwenyezi Mungu na haki, bila ya kufikiwa na muonyaji kabla ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) .
Huko nyuma kwenye Juzuu hii, kwenye kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na hakuna uma wowote ila alipita humo muonyaji (35:24),” tumesema kuwa makusudio ya muonyaji hapo ni kila linalosimamia hoja, iwe ni akili au nakili na kwamba makusudio ya muonyaji kwenye Aya hii tuliyo nayo ni Mtume hasa.
Imekwishathibiti kauli juu ya wengi wao, kwa hiyo hawaamini.
Makusudio ya kauli hapa ni kiaga cha adhabu, na wengi wao ni hao maba- ba zao; yaani mababa za waarabu waliokuwa wakati wa Muhammad(s.a.w.w) , waliokufa kwenye ushirikina. Ni wachache sana waliokuwa kwenye dini ya Tawhid. Tazama Juz. 15 (17:105–111) kifungu ‘Wanyoofu.’
Hakika tumeweka minyororo shingoni mwao, nayo inafika videvuni, kwa hiyo vichwa vyao viko juu.
Mikono ikifungwa kwa minyororo mpaka shingoni kichwa huinuka juu, na aliyefungwa anakuwa hawezi kugeuka kuume wala kushoto au kuangalia mbele; atakuwa anaangalia juu tu.
Na tumeweka kizuizi mbele yao na kizuizi nyuma yao na tumewafunika, kwa hiyo hawaoni.
Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atawaweka kwenye vizuizi viwili vya moto. Kimoja mbele yao na kingine nyuma yao, hawawezi kwenda mbele wala kurudi nyuma; wala hawezi kuona mbingu, kwa sababu vizuizi viwili vimefunika macho yao.
Sio mbali kuwa hiki ni kinaya cha ukali na uchungu wa adhabu. Kwa vyovyote iwavyo, adhabu haihusiki na washirikina tu, bali itaenea kwa kila mwenye hatia na dhalimu.
Imam Ali(a.s) anasema:“Ama watu wa maasia atawaweka mahali pa baya, atawafunga mikono kwa minyororo hadi videvuni, utosi utafungwa na nyayo, na atawavisha kanzu za lami na nguo za moto. Watu wake watafungiwa mlango katika Moto mkali wenye kuvuma.”
Umetangulia mfano wake katika Juzuu hii (34:33).
Ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye hawataamini.
Ni sawa kwao ewe Muhammad, uwape mawawidha au usiwape, basi hakika wao, hawatafanya lolote isipokuwa kwa hawaa zao na masilahi yao. Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:6).
Hakika unamuonya yule tu anayefuata ukumbusho na akamcha Mwingi wa rehema kwa ghaibu. Basi mbashirie maghufira na ujira wa heshima.
Anayekusikiliza ni yule anayeitafuta haki kwa ajili ya haki na kwenda nayo kwa matokeo yoyote yatakayokuwa. Umetangulia mfano wake katika Juzuu hii (35: 18).
Hakika sisi tunawahuisha wafu na tunayaandika wanayoyatanguliza na athari zao. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari linalobainisha.
Daftari linalobainisha ni kinaya cha elimu ya Mwenyezi Mungu. Maana ni kuwa, Mwenyezi Mungu atawafufua, na ameyahifadhi wanayoyafanya ya kheri na ya shari na athari walizoziacha za manufaa au madhara, na kwamba Yeye atamlipa kila mmoja alilolifanya, nao hawatadhulumiwa.
وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا أَصْحَابَ الْقَرْيَةِ إِذْ جَاءَهَا الْمُرْسَلُونَ ﴿١٣﴾
13. Na wapigie mfano wenyeji wa mji Mitume walipowafikia.
إِذْ أَرْسَلْنَا إِلَيْهِمُ اثْنَيْنِ فَكَذَّبُوهُمَا فَعَزَّزْنَا بِثَالِثٍ فَقَالُوا إِنَّا إِلَيْكُم مُّرْسَلُونَ ﴿١٤﴾
14. Tulipowatuma wawili wakawakadhibisha. Basi tukawaongezea nguvu kwa (mwingine) wa tatu Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu.
قَالُوا مَا أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا وَمَا أَنزَلَ الرَّحْمَـٰنُ مِن شَيْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَكْذِبُونَ ﴿١٥﴾
15. Wakasema nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na mwingi wa rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uwongo tu.
قَالُوا رَبُّنَا يَعْلَمُ إِنَّا إِلَيْكُمْ لَمُرْسَلُونَ ﴿١٦﴾
16. Wakasema: Mola wetu anajua kwamba sisi tumetumwa kwenu.
وَمَا عَلَيْنَا إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿١٧﴾
17. Wala si juu yetu ila kufikisha waziwazi.
قَالُوا إِنَّا تَطَيَّرْنَا بِكُمْ لَئِن لَّمْ تَنتَهُوا لَنَرْجُمَنَّكُمْ وَلَيَمَسَّنَّكُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٨﴾
18. Wakasema: Hakika sisi tunapata mkosi kwa ajili yenu. Kama hamtakoma basi hakika tutawapiga mawe na itawafika adhabu chungu kutoka kwetu.
قَالُوا طَائِرُكُم مَّعَكُمْ أَئِن ذُكِّرْتُم بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ ﴿١٩﴾
19. Wakasema: Mkosi wenu mnao wenyewe. Je, ni kwa kuwa mnakumbushwa? Bali nyinyi ni watu mnaopituka mipaka.
وَجَاءَ مِنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ رَجُلٌ يَسْعَىٰ قَالَ يَا قَوْمِ اتَّبِعُوا الْمُرْسَلِينَ ﴿٢٠﴾
20. Na akaja mtu mbio kutoka upande wa mbali wa mjini akasema: Enyi watu wangu! Wafuateni Mitume.
اتَّبِعُوا مَن لَّا يَسْأَلُكُمْ أَجْرًا وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٢١﴾
21. Wafuateni wasiowaomba ujira nao wameongoka.
وَمَا لِيَ لَا أَعْبُدُ الَّذِي فَطَرَنِي وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٢﴾
22. Na kwa nini nisimwabudu yule aliyeniumba na kwake mtarejeshwa?
أَأَتَّخِذُ مِن دُونِهِ آلِهَةً إِن يُرِدْنِ الرَّحْمَـٰنُ بِضُرٍّ لَّا تُغْنِ عَنِّي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا وَلَا يُنقِذُونِ ﴿٢٣﴾
23. Je, nishike miungu mingine badala yake? Mwingi wa rehema akinitakia madhara, uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa.
إِنِّي إِذًا لَّفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢٤﴾
24. Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotofu ulio dhahiri.
إِنِّي آمَنتُ بِرَبِّكُمْ فَاسْمَعُونِ ﴿٢٥﴾
25. Hakika mimi nimemwamini Mola wenu, basi nisikilizeni.
قِيلَ ادْخُلِ الْجَنَّةَ قَالَ يَا لَيْتَ قَوْمِي يَعْلَمُونَ ﴿٢٦﴾
26. Ikasemwa: Ingia Peponi! Akasema: Laiti watu wangu wangejua.
بِمَا غَفَرَ لِي رَبِّي وَجَعَلَنِي مِنَ الْمُكْرَمِينَ ﴿٢٧﴾
27. Jinsi Mola wangu alivyonighufiria na akanifanya katika waheshimwa.
WAJUMBE WAWILIA WALIOWAONGEZEWA NGUVU KWA WA TATU
Aya 13 – 27
MAANA
Na wapigie mfano wenyeji wa mji Mitume walipowafikia.
Maneno yanaelekezwa kwa Mtume awaambie washirikina wa Kiarabu. Ama mji, wafasiri wengi wamesema ni Antiokia, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakuelezea. Kwa sababu makusudio ya kupiga mfano ni kupata mawaidha na mazingatio, sio jina la mji na sehemu yake.
Dhana kubwa ni kuwa wafasiri wametegemea vitabu vya kinaswara; ambapo imeelezwa kwenye Matendo ya mitume 11:19 – 26, kwamba Barnaba na Sauli walikwenda Antiokia na kuwafundisha watu wengi. Na kwamba mitume ni wanafunzi 12 aliowachagua Bwana Masih(a.s) ili wamsaidie na wamwone atakapotoka kaburini, waelezee walimwengu; kama ilivyoelezwa kwenye Mathayo na Matendo ya mitume.
Barnaba alikuwa ni Mkupro (Cyprus) akaingia kwenye ukiristo katika zama za mitume na akawa ni mhubiri; kama ilivyoelezwa katika ‘Kamusi ya Kitabu kitakatifu’
Tulipowatuma wawili wakawakadhibisha. Basi tukawaongezea nguvu kwa (mwingine) wa tatu.
Katika tafsiri nyingi imeelezwa kuwa mitume walikuwa ni wanafunzi wa Isa(a.s ) na kwamba yeye ndiye aliyewatuma wawili mjini kisha akawaongezea nguvu kwa mwingine wa tatu.
Lakini neno mitume likitegemezwa kwa Mwenyezi Mungu, kama ilivyo katika neno ‘tulipowatuma’ na ‘tukawaongezea nguvu,’ huwa linafahamisha kuwa wao walitumwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu moja kwa moja sio kwa kwa amri ya Isa(a. s ) .
Vyovyote iwavyo, la kuzingatia ni utendaji si majina. Zaidi ya hayo sisi hatutaulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu, wala hilo halina uhusiano wowote na maisha yetu kwa karibu au mbali. Maana yaliyo wazi, ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwatuma mitume watatu kwenye mji huo, watoe mwito wa haki.
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu. Wakasema; nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na mwingi wa rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uwongo tu.
Hii ndio nembo ya wapinzani siku zote. Tazama Juz. 13 ( 14:10), Juz. 15 (17:94), Juz. 17 (21:3), Juz. 18 (23:24) na Juz. 19 (26:154).
Wakasema: Mola wetu anajua kwamba sisi tumetumwa kwenu. Wala si juu yetu ila kufikisha waziwazi.
Baada ya mitume kusimamisha hoja za kusadikisha ukweli wao, waliwaambia wakadhibishaji kuwa sisi tumetumwa kwenu na Mwenyezi Mungu, akatupa ubainifu, kama mnavyouona, na tumetekeleza ujumbe wake, kama inavyotakikana. Basi si juu yetu tena hisabu yenu wala si juu yenu nyinyi hisabu yetu. Yeye ni mjuzi mwenye kuhisabu.
Wakasema: Hakika sisi tunapata mkosi kwa ajili yenu. Kama hamtakoma basi hakika tutawapiga mawe na itawafika adhabu chungu kutoka kwetu. Wakasema: Mkosi wenu mnao wenyewe. Je, ni kwa kuwa mnakumbushwa? Bali nyinyi ni watu mnaopituka mipaka.
Mkosi wenu mnao wenyewe; yaani hakuna mkosi, bali hizo ni dhana zenu tu. Kuna Hadith mashuhuri isemayo:“Hakuna kuambukiza, wala mkosi wala nyuni” Imam As-Sadiq(a.s ) anasema:“Mkosi unaufanya wewe, ukiupuuza utakupuuza, ukiutilia mkazo utakutilia mkazo na ukiufanya si chochote nao hautakuwa ni chochote”
Yaani hakuna kitu kama kisirani, ndege au mkosi; wala hauna athari yoyote kwa mtu; isipokuwa unaathiri nafsi ya mtu na mishipa yake, kwa vile anavyouwazia tu; kama mtoto anavyotishika na zimwi.
Maana ni kuwa wakadhibishaji waliwaambia mitume kuwa mmetuletea mkosi, kwa hiyo tunahofia tutagawanyika; sasa bora mnyamaze, la sivyo tutawanyamazisha kwa kuwapiga mawe na adhabu kali. Ndio Mitume wakawaambia, chimbuko la hofu ya mkosi linatokana na wasiwasi wenu nyinyi wenyewe, kwamba mwito wetu ni mkosi na shari; na hali yakuwa shari inatoka kwenu kwa kufanya shirki, ujahili na ufisadi.
Na akaja mtu mbio kutoka upande wa mbali wa mjini.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakuashiria jina la mtu huyu, lakini wafasiri wengi wakasema jina lake ni Habib An-Najar, na kwamba nyumba yake ilikuwa kandoni mwa mji. Alikuwa mumin. Aliposikia kuwa watu wake wanaazimia kuwaua mitume, alifanya haraka kuja kuwaokoa na kuwasaidia.
Sijui wafasiri wamelitoa wapi jina hili. Mimi nimetafuta mpaka katika Biblia ukurasa wa yaliyomo na kamusi ya Kitabu kitakatifu pia sikulipata.
Vyovyote iwavyo, jina la huyo mtu halina mfungamano wowote na sisi. Wala hakuna linalotushughulisha isipokuwa lile lililofahamishwa na Aya. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemsifu kuwa na imani na wema, kwa sababu alisema:
Enyi watu wangu! Wafuateni Mitume. Wafuateni wasiowaomba ujira nao wameongoka.
Aliwapa nasaha watu wake wakubali mwito wa Mitume wala wasiwapinge, kwa sababu ni kwa masilahi yao. Wanatoa mwito na hawataki malipo wala shukrani; wala uluwa au ufisadi katika ardhi.
Na kwa nini nisimwabudu yule aliyeniumba na kwake mtarejeshwa?
Kauli hii ni ya yule mumin anayetoa nasaha. Maana yake ni kuwa, ni kizuizi gani kitakachonizuia na ibada ya ambaye amenifanya niweko baada ya kutokuweko, kisha atatufufua sote baada ya mauti kwa ajili ya hisabu na malipo?
Hapa anawapinga watu wake walioacha ibada ya Mungu mmoja wa pekee. Anaendelea kuwagonga na kusema:
Je, nishike miungu mingine badala yake? Mwingi wa rehema akinitakia madhara, uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa. Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotofu ulio dhahiri.
Vipi niabaudu masanamu yasiyodhuru wala kunufaisha? Hayaokoi wala hayaombei? Nikifanya hivyo nitakuwa nimepotea, wala sitakuwa katika walioongoka. Hapana!
Hakika mimi nimemwamini Mola wenu, basi nisikilizeni.
Hawi jasiri wa maneno haya isipokuwa yule asiyeogopa mauti katika njia ya haki na kuinusuru. Kuna mapokezi yanayoeleza kuwa alipowajia watu wake na hakika hii, walimuua kwa kumpiga mawe na hakupata wa kumhami. Hili haliko mbali kulingana na sera ya mataghuti na wafisadi. Linalotia nguvu ukweli wa risala hii ni ile kauli ya washirikina kwa mitume: “Kama hamtakoma basi hakika tutawapiga mawe na itawafika adhabu chungu kutoka kwetu.”
Katika Tafsiri ya Zamakhshari na Tha’labi imesemwa: Watangulizi wa umma ni watatu, hawakukufuru hata kwa kupepesa jicho: Ali bin Abu Twalib, Mtu wa Yasin na Mumin wa watu wa Firauni.
Ikasemwa: Ingia Peponi!
Aliiuza nafsi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na thamani ya bei yake ikawa ni Pepo. Hiyo ni tosha kuwa ni thawabu na malipo.
Akasema: Laiti watu wangu wangejua jinsi Mola wangu alivyonighufiria na akanifanya katika waheshimiwa.
Hakusema hivi kwa kuwacheka watu, ingawaje walimkadhibisha, hapana! Watu wema hawawi hivi; bali alisema hivi kuwasikitikia na yaliyowapita, akitamani lau wangelijua kwamba yeye alikuwa akiwapa nasaha na kwamba zilikuwa ni njozi na ujinga kuwa yeye na mitume wana mikosi.
13
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
وَمَا أَنزَلْنَا عَلَىٰ قَوْمِهِ مِن بَعْدِهِ مِن جُندٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَمَا كُنَّا مُنزِلِينَ ﴿٢٨﴾
28. Na hatakuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala sisi si wenye kuteremsha.
إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً فَإِذَا هُمْ خَامِدُونَ ﴿٢٩﴾
29. Hakuwi ila ukelele mmoja tu na mara wamezimia.
يَا حَسْرَةً عَلَى الْعِبَادِ مَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٣٠﴾
30. Ni sikitiko kwa waja. Hawakufika mitume ila wanamfanyia stihizai.
أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّنَ الْقُرُونِ أَنَّهُمْ إِلَيْهِمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿٣١﴾
31. Je, hawaoni umma ngapi tulizoziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei kwao.
وَإِن كُلٌّ لَّمَّا جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ ﴿٣٢﴾
32. Na hapana ila wote watahudhurishwa mbele yetu.
وَآيَةٌ لَّهُمُ الْأَرْضُ الْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَاهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ ﴿٣٣﴾
33. Na ishara kwao ni ardhi iliyokufa, tunaifufua na tukatoa ndani yake nafaka wakaila.
وَجَعَلْنَا فِيهَا جَنَّاتٍ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ وَفَجَّرْنَا فِيهَا مِنَ الْعُيُونِ ﴿٣٤﴾
34. Na tukafanya ndani yake mabustani na mitende na mizabibu, na tukachimbua chemchem ndani yake.
لِيَأْكُلُوا مِن ثَمَرِهِ وَمَا عَمِلَتْهُ أَيْدِيهِمْ أَفَلَا يَشْكُرُونَ ﴿٣٥﴾
35. Ili wale katika matunda yake na hayakufanywa kwa kwa mikono yao, je hawashukuru?
سُبْحَانَ الَّذِي خَلَقَ الْأَزْوَاجَ كُلَّهَا مِمَّا تُنبِتُ الْأَرْضُ وَمِنْ أَنفُسِهِمْ وَمِمَّا لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٦﴾
36. Kutakata na mawi ni kwa ambaye ameumba jozi katika kila vinavyooteshwa na ardhi na katika nafsi zao na katika wasivyovijua.
NAWASIKITIKIA WAJA WANGU
Aya 28 – 36
MAANA
Na hatakuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala sisi si wenye kuteremsha. Hakuwi ila ukelele mmoja tu na mara wamezimia.
Kaumu yake, ni kaumu yake yule mumin aliyesema: ‘Wafuateni mitume.’ Makusudio ya jeshi la mbinguni ni malaika, na ukelele ni adhabu.
Maana ni kuwa kuangamia kwa wakadhibishaji ni jambo rahisi kwetu, lisilohitajia majeshi kutoka mbinguni. Bali ukelele mmoja tu, watakousikia, unawatosha kuyafanya majumba yao ni makaburi ya mili yao.
Ni sikitiko kwa waja. Hawakufika mitume ila wanamfanyia stihizai.
Kunga’ng’ania washirikina kukadhibisha mitume na kuwafanyia madharau ndiko kunakoleta masikitiko.
Unaweza kuuliza : Ni nani anayesikitika na hali tunajua kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) hamsikitikii yoyote?
Jibu : Masikitiko hapa ni kinaya cha mwendo wao mbaya na mwisho wao muovu ambao utawaletea masikitiko watakapoiona adhabu ya Jahannam na kujuta kwao walivyopoteza fursa katika maisha ya dunia.
Je, hawaoni umma ngapi tulizoziangamiza kabla yao?
Wanasikitika na kujuta kwa sababu hawakuchukua somo duniani kwa umma zilizowatangulia zilizoangamizwa na Mwenyezi Mungu walipowakadhibisha mitume.
Hakika hao hawarejei kwao.
Wafasiri wengi wa zamani na wapya, akiwemo Al-Maraghi na mwenye Dhilal, wamesema kuhusu maana ya jumla hii ni: Hawaoni wakadhibishaji kwamba tuliowaangamiza hawarudi tena duniani?
Lakini tafsiri hii inatakikana iangaliwe vizuri. Kwa sababu kukosa kurudi wafu daniani itakuwa ni hoja ya wakadhibishaji kuwa hakuna ufufuo; na wala si hoja juu yao.
Maana ya sawa – kwa tunavyodhania - ni kuwa je, hawakuona wakadhibishaji kwamba Mwenyezi Mungu amewangamiza waliopita wote na hakubaki yeyote wa kuweza kuwarudia wakadhibishaji kuwafahamisha habari ya wakadhibishaji wa mwanzo? Kinachofahamisha kuangamia kwao ni athari tu:
فَتِلْكَ بُيُوتُهُمْ خَاوِيَةً بِمَا ظَلَمُوا إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٥٢﴾
“Basi hizo nyumba zao ni tupu kwa sababu ya walivyodhulumu. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaojua.” Juz. 19 (27:52).
Jumla hii inafanana na kauli yake Mwenyezi Mungu iliyo katika Aya ya 50 ya sura hii tuliyo nayo:“Basi hawataweza kuusia, wala hawatarejea kwa watu wao”
Na hapana ila wote watahudhurishwa mbele yetu.
Watu wote kesho watasimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuchukuliwa hisabau ya matendo yao, hilo ni lazima.
Na ishara kwao ni ardhi iliyokufa, tunaifufua na tukatoa ndani yake nafaka wakaila. Na tukafanya ndani yake mabustani na mitende na mizabibu, na tukachimbua chemchem ndani yake.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 7(6:99), Juz. 13 (13:4) na Juz. 17 (22:5).
Ili wale katika matunda yake na hayakufanywa kwa mikono yao, je hawashukuru?
Neema za Mwenyezi Mungu hazihisabiki wala hazidhibitiki. Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na waliyofanya kwa mikono yao,’ inaashiria kuwa neema ya kweli ni mali ya halali iliyochumwa kwa jasho, lakini mali ya haramu ni moto:
أُولَـٰئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ إِلَّا النَّارَ ﴿١٧٤﴾
“Hao hawali matumboni mwao isipokuwa Moto” Juz. 2 (2:174),
إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ﴿١٠﴾
“Hakika wanakula moto matumboni mwao” Juz. 4 (4:10).
Kutakata na mawi ni kwa ambaye ameumba jozi katika kila vinavyooteshwa na ardhi na katika nafsi zao na katika wasivyovijua.
Ametakasika kutokana na shirk, na ametakata na kutukuka kukubwa ambaye ameumba aina za wanyama, ndege, mimea na binadamu. Pia vile ambavyo hatuvijui katika mbingu na ardhini. Kila aina katika aina hizo inahitalifiana kirangi na kiumbo. Nyingine zinatofauti na kiladha; kama vile mimea na wanadamu kutofautiana kiakhlaki.
Wataalamu wanasema hata vitu vikavu vigumu vinafungamana kutokana na vitu viwili: chanya na hasi, na lau si hivyo basi kusingepatikana vitu. Wala hakuna chimbuko la hayo isipokuwa Mjuzi mwenye hekima. Ama sadfa haina nafasi na hawezi kuuikimbilia ila mzembe mwenye kujikwaza.
وَآيَةٌ لَّهُمُ اللَّيْلُ نَسْلَخُ مِنْهُ النَّهَارَ فَإِذَا هُم مُّظْلِمُونَ ﴿٣٧﴾
37. Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani.
وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٣٨﴾
38. Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua.
وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ ﴿٣٩﴾
39. Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka ukarudi kuwa kama karara la zamani.
لَا الشَّمْسُ يَنبَغِي لَهَا أَن تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ وَكُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ ﴿٤٠﴾
40. Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia.
وَآيَةٌ لَّهُمْ أَنَّا حَمَلْنَا ذُرِّيَّتَهُمْ فِي الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ ﴿٤١﴾
41. Na ni Ishara kwao kwamba tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi ilio sheheni.
وَخَلَقْنَا لَهُم مِّن مِّثْلِهِ مَا يَرْكَبُونَ ﴿٤٢﴾
42. Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda.
وَإِن نَّشَأْ نُغْرِقْهُمْ فَلَا صَرِيخَ لَهُمْ وَلَا هُمْ يُنقَذُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na tukitaka tunawagharikisha; wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi.
إِلَّا رَحْمَةً مِّنَّا وَمَتَاعًا إِلَىٰ حِينٍ ﴿٤٤﴾
44. Isipokuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda.
KILA KITU KINA ISHARA
Aya 37 – 44
MAANA
Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja ishara za ulimwengu zinazofahamisha uweza wake na ukuu wake; kama ifutavyo:
Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani.
Usiku unafuatana na mchana kutokana na kuwa ardhi ni tufe na kuwa inazunguka kama jiwe la kusagia. Wakati ardhi inapozunguka, upande ule unaolielekea jua unakuwa ni mchana na ule usiolieleka jua unakuwa ni usiku. Nao ukifikia kwenye jua unakuwa mchana na ule mwingine unakuwa usiku, na kuendelea namna hiyo.
Hali hiyo ndiyo aliyoitolea ibara Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwa ni kuvua. Na amekutegemeza kwake Yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa sababu ndiye mumba wa ulimwengu na msababishaji wa sababu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 3 (3:27) na Juz. 15 (17:12).
Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua.
Wafasiri wametofautiana katika makusudio ya neno Mustaqarrin lahaa, tulilolifasiri kwa maana ya kiwango chake. Razi ameishilia kwenye kauli nne, lakini zote ziko mbali na ufahamu. Ilivyo hasa ni kinaya cha kwenda kwa nidhamu na mpangilio.
Hilo linatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua’ Mwandishi wa kitabu Al-qur’an wal-ilmulhadith (Qur’an na sayansi) amenukuu wataalamu wa falaki wa kisasa wakisema: Jua linakwenda kwa kasi ya maili 12 kwa sekunde mbali ya kuwa hilo lenyewe linazunguka, na kwamba linatofautiana na mzunguuko wa ardhi.
Yametangulia maelezo yanayoambatana na haya katika Juz. 13 (13:2).
Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka ukarudi kuwa kama karara la zamani.
Vituo hivi havibadiliki au kuondoka mahali pake, wala mwezi haupotei navyo. Wana falaki wanasema kuwa ni 28. Mwezi unashuka usiku kwenye kila kimoja na unajificha nyusiku mbili ikiwa mwezi utakuwa wa siku 30 na usiku mmoja ukiwa na siku 29.
Wakati huo unakuwa kama tawi la mtende kwa wembamba. Haya ndio makusudioya kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘karara.’ Yametangulia yanayofungamana na haya katika Juz.10 (9: 36 – 37) kifungu cha ‘miezi miandamo ndiyo miezi ya kimaumbile’
Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia.
Kila sayari ina njia yake maalum, ikizunguka humo kwa nidhamu na kwenda kwenye kituo chake kilichopangiwa mpaka atakapozikunja Mwenyezi Mungu kama karatasi. Kwenye Nahjul-balagh kuna maelezo haya: “Na akalifanya Jua lake – yaani jua na hizo sayari - kuwa ni ishara yenye kuonwa na mchana wake, na Mwezi wake kuwa unaufuta usiku wake; yaani mwangaza wa mwezi unazidi miangaza ya sayari nyinginezo. Basi akazipitisha katika njia yake ili upambanuke usiku na mchana kwazo na ili ijulikane idadi ya miaka na hisabu kwa makisio ya hizo mbili.
Miongoni mwa niliyoyasoma katika maudhui haya ni Hadith Qudsi aliyoitaja mwenye kitabu cha Al-asfar Jalada la tatu, maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amesema: Lau jua lingewekwa upande maalum, basi matajiri wangelijenga jengo refu kuzuia mwanga wa Jua usiwafikie mafukara, lakini ameliweka kwenye anga likizunguka na kwenda, ili fukara apate sehemu yake, sawa na anavyopata tajiri.
Na ni ishara kwao kwamba tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi ilio sheheni.
Kwao, ni kwao hao Binadamu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawakumbusha neema zake kuu kwao; miongoni mwazo ni kuwabeba kwenye majahazi wao na mizigo yao, wakitolewa huku na kupelekwa kule. Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (14:32) na Juz. 15 (17:66).
Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda.
Yaani mfano wa majahazi. Wafasiri wa kale walisema kuwa makusudio ya mfano wake ni ngamia, farasi, nyumbu na punda. Walisema haya wakati ambapo hakukuwa na ndege wala gari au chombo chote cha angani.
Na tukitaka tunawagharikisha hata kama wako katika manowari na meli.
Lengo ni kuwakumbusha neema ya kuokoka na kuangamia lau kama si rehema yake na usaidizi wake.Wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi, na kuangamia kadiri watakavyotaka usaidizi.
Isipokuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda.
Yaani isipokuwa Mwenyezi Mungu akiwawahi kwa rehema yake na kuwaakhirisha hadi muda malum kulingana na ujuzi wake na hekima yake.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّقُوا مَا بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَمَا خَلْفَكُمْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٤٥﴾
45. Na wanapoambiwa: Ogopeni yalioko mbele yenu na yaliyoko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa.
وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ آيَةٍ مِّنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ ﴿٤٦﴾
46. Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao ila wao huwa ni wenye kuipuuza.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ أَنفِقُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنُطْعِمُ مَن لَّوْ يَشَاءُ اللَّـهُ أَطْعَمَهُ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٤٧﴾
47. Na wanapoambiwa: Toeni katika aliyowapa Mwenyezi Mungu, waliokufuru huwaambia walioamini: Je! Tumlishe ambaye Mwenyezi Mungu angependa angelimlisha? Nyinyi hammo ila katika upotofu ulio dhahiri.
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٨﴾
48. Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?
مَا يَنظُرُونَ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً تَأْخُذُهُمْ وَهُمْ يَخِصِّمُونَ ﴿٤٩﴾
49. Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakaowachukua nao wanazozana.
فَلَا يَسْتَطِيعُونَ تَوْصِيَةً وَلَا إِلَىٰ أَهْلِهِمْ يَرْجِعُونَ ﴿٥٠﴾
50. Basi hawataweza kuusia, wala hawatarejea kwa watu wao.
وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَإِذَا هُم مِّنَ الْأَجْدَاثِ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يَنسِلُونَ ﴿٥١﴾
51. Na itapulizwa Parapanda, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao.
قَالُوا يَا وَيْلَنَا مَن بَعَثَنَا مِن مَّرْقَدِنَا هَـٰذَا مَا وَعَدَ الرَّحْمَـٰنُ وَصَدَقَ الْمُرْسَلُونَ ﴿٥٢﴾
52. Watasema: Ole wetu! Nani aliyetufufua malaloni petu? Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume.
إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً فَإِذَا هُمْ جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ ﴿٥٣﴾
53. Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watahudhuruishwa mbele yetu.
فَالْيَوْمَ لَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٥٤﴾
54. Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyokuwa mkiyatenda.
OGOPENI YALIYO MBELE YENU
Aya 45 – 54
MAANA
Na wanapoambiwa: Ogopeni yalioko mbele yenu na yalioko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa.
Wanaoambiwa ni washirikina wa kiarabu. Makusudio ya yaliyo mbele yao ni kumuasi Mwenyezi Mungu na aliyoyaharamisha, na yaliyo nyuma yao ni adhabu ya hayo. Kwenye Nahjul-balagh imeelezwa: “Hakika Kiyama kimewazingira kwa nyuma yenu.” Maana ni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewakataza kumuasi Mwenyezi Mungu na akwahadharisha na adhabu yake wakimuasi. Akawapa bishara ya rehema yake na thawabu zake wakimtii, lakini waligeuka nyuma.
Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao ila wao huwa ni wenye kuipuuza.
Kila alipowajia Mtume na muujiza wa dhahiri au hoja iliyo wazi, walimkadhibisha kwa jeuri na inadi. Umetangulia mfano wake katika Juz. 19 (26:5).
Na wanapoambiwa: Toeni katika aliyowapa Mwenyezi Mungu, waliokufuru huwaambia walioamini: Je! Tumlishe ambaye Mwenyezi Mungu angependa angelimlisha? Nyinyi hammo ila katika upotofu ulio dhahiri.
Wapenda anasa wana msingi na dini moja tu; kupupia utajiri wao na maslahi yao. Ndio mazungumzo yao na vitendo vyao. Wakiambiwa msifanye ufisadi, wanasema sisi ni watengenezaji. Wakiambiwa aminini kama walivyoamini watu, wanasema: Tuamini kama walivyoamini wapumbavu? Wakiambiwa msujudieni Mwingi wa rehema, wanasema: Ni nani huyo Mwingi wa rehema? Sisi tunasujudia pesa.
Na wakiamriwa kuwapatia wenye haja wanasema Mwenyezi Mungu amewahukumia kuwa mafukara na sisi tuwe matajiri. Hawajui au wamejitia kutojua kuwa ufukara unatokana na yanayofanywa ardhini sio yanayofanywa mbinguni; kama vile ufisadi, serikali za kidhalimu, za unayanyasaji na uporaji.
Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?
Mwenyezi Mungu na Mtume anapowahadharisha na mwisho mbaya, wanasema kwa dharau yatakuwa lini haya? Umetangulia mfano wake kati- ka Aya kadhaa.
Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakaowachukua nao wanazozana.
Yaani wakizozania mambo ya dunia yao. Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
فَأَخَذْنَاهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩٥﴾
“Basi tuliwaachukua kwa ghafla hali hawatambui.” Juz. 9 (7:95).
Basi hawataweza kuusia, wala hawatarejea kwa watu wao.
Ukija ukelele wa adhabu hakuna yeyote atakayepata muda wa kuusia watu wake mambo muhimu, na akiwa mbali nao hataweza kurudi kwao.
Na itapulizwa Parapanda, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (18:99).
Watasema: Ole wetu! Nani aliyetufufua malaloni petu?
Watastaajabu kwa kufufuliwa kwao baada ya mauti, na hapo mwanzo walikuwa wakimfanyia mzaha yule anayewaandalia na kuwamarisha kujianda nao. Baada ya kushuhudia watasema: Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume kwamba Kiyama kitafika tu, bila ya shaka yoyote na kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini.
Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watahudhurishwa mbele yetu.
Kuumba, mauti na ufufuo kwa Mwenyezi Mungu ni sawa, kunakuwa kwa neno moja tu:
مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ ﴿٢٨﴾
“Hakukuwa kuumbwa kwenu wala kufufuliwa kwenu ila ni kama nafsi moja tu.” Juz. 21 (31:28).
Umetangulia mfano wake katika Aya 32 ya sura hii tuliyo nayo.
Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyokuwa mkiyatenda.
Kauli nyingine yenye maana haya ni:
الْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٧﴾
“Leo kila nafsi italipwa kwa iliyoyachuma. Hapana dhulma leo. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kuhisabu” (40:17).
14
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُلٍ فَاكِهُونَ ﴿٥٥﴾
55. Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi.
هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلَالٍ عَلَى الْأَرَائِكِ مُتَّكِئُونَ ﴿٥٦﴾
56. Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya fahari.
لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ ﴿٥٧﴾
57. Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakachokitaka.
سَلَامٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ ﴿٥٨﴾
58. Salaam! Ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mwenye kurehemu.
وَامْتَازُوا الْيَوْمَ أَيُّهَا الْمُجْرِمُونَ ﴿٥٩﴾
59. Na jitengeni leo enyi wakosefu.
أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَا بَنِي آدَمَ أَن لَّا تَعْبُدُوا الشَّيْطَانَ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٦٠﴾
60. Je, sikuagana nanyi, enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shet’ani? Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu.
وَأَنِ اعْبُدُونِي هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٦١﴾
61. Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia iliyonyooka.
وَلَقَدْ أَضَلَّ مِنكُمْ جِبِلًّا كَثِيرًا أَفَلَمْ تَكُونُوا تَعْقِلُونَ ﴿٦٢﴾
62. Na hakika yeye amewapoteza viumbe wengi miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkim- tia akili?
هَـٰذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ ﴿٦٣﴾
63. Hii ndiyo Jahannamu mliyokuwa mkiahidiwa.
اصْلَوْهَا الْيَوْمَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿٦٤﴾
64. Ingieni leo kwa vile mlivyokuwa mkikufuru.
الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَىٰ أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٦٥﴾
65. Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyokuwa wakiyachuma.
وَلَوْ نَشَاءُ لَطَمَسْنَا عَلَىٰ أَعْيُنِهِمْ فَاسْتَبَقُوا الصِّرَاطَ فَأَنَّىٰ يُبْصِرُونَ ﴿٦٦﴾
66. Na lau tungelipenda tungeliyafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wangeionaje?
وَلَوْ نَشَاءُ لَمَسَخْنَاهُمْ عَلَىٰ مَكَانَتِهِمْ فَمَا اسْتَطَاعُوا مُضِيًّا وَلَا يَرْجِعُونَ ﴿٦٧﴾
67. Na lau tungelitaka tungewageuza hapo hapo walipo, basi wasingeweza kwenda wala kurudi.
وَمَن نُّعَمِّرْهُ نُنَكِّسْهُ فِي الْخَلْقِ أَفَلَا يَعْقِلُونَ ﴿٦٨﴾
68. Na tunayempa umri tunampindua katika umbo. Basi je! hawatii akilini?
WATU WA PEPONI NA WATU WA MOTONI
Aya 55 – 68
MAANA
Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi. Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya fahari. Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakachokitaka.
Anachotamani mtu zaidi ni siha, amani, utulivu wa moyo kutokana na tabu na mihangaiko na kupata kuburudika na chakula na kinywaji, maskani, mavazi, kustarehe na wanawake na kuwa na bustani yenye miti na mito. Haya yote yanapatikana Peponi.
Zaidi ya hayo ni Salaam! Ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mwenye kurehemu.
Salaam ya Mwenyezi Mungu ni amani na rehema. Na radhi yake ndio ukomo wa wema na neema. Ndio maana Imam Ali(a.s ) akasema:“Kila neema isiyokuwa Pepo ni upuzi na kila balaa isiyokuwa moto ni faraja.”
Na jitengeni leo enyi wakosefu.
Wakosefu walikuwa duniani wakijionyesha ni watu wema, wakivaa nguo za utawa na kuchanganyika na watu wa takua na wa heri. Hali halisi haikuwa ikijulikana na watu wengi. Ama leo – siku ya hukumu na malipo, Mwenyezi Mungu atawaweka mbali na watu wema na kuwaambia, ingieni motoni pamoja na watakaoingia:
يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالْأَقْدَامِ ﴿٤١﴾
“Watajulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele za utosi na kwa miguu” (55:41).
Je, sikuagana nanyi, enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shet’ani? Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwahadharisha waja kutokana na shetani na wasiwasi wake na akwakataza wasimtii; akawaongoza kwenye njia ya heri na uongofu. Lakini wengi wamemtii Shetani na kumuasi Mwingi wa rehe- ma. Hili ameliashiria kwa kusema:
Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia iliyonyooka.
Na hakika yeye amewapoteza viumbe wengi miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkitia akili?
Kila mwenye kufuata njia ya walioangamia baada ya kuhadharishwa na kuonywa, basi huyo ni katika vipofu wa nuru ya akili na muongozo wake. Wala hakuna malipo ya mfano huu isipokuwa adhabu ambayo amaeiashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa kusema:
Hii ndiyo Jahannamu mliyokuwa mkiahidiwa, kupitia midomoni mwa mitume; mkaidharau na mkawadharau. BasiIngieni leo kwa vile mlivyokuwa mkikufuru, na huu ndio mwisho wa kila mpotevu na aliyepituka mipaka.
Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyokuwa wakiyachuma.
Kila kiungo cha muasi kesho kitatamka kumtolea ushahidi mtu wake yale maovu aliyoyafanya. Mkono utatoa ushahidi kwa ulivyopiga, kuiba, kuandika na kuashiria. Mguu kwa ulivyohangaika. Jicho kwa lililoona n.k.Unaweza kuuliza : Utachanganya vipi kauli hii ‘Tutaziba vinywa vyao’ na ile isemayo:
يَوْمَ تَشْهَدُ عَلَيْهِمْ أَلْسِنَتُهُمْ ﴿٢٤﴾
“Siku ambayo zitawashuhudia ndimi zao” Juz. 18 (24:24).
Ambapo ya kwanza imekanusha kutamka na hii ikathibitisha.
Jibu : Kesho waja watakuwa wana hali tofauti, wengine wataruhisiwa kuzungumza na wengine hawataruhusiwa:
يَوْمَ يَأْتِ لَا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ ﴿١٠٥﴾
“Siku itakapofika, nafsi yoyote haitasema ila kwa idhini yake.” Juz. 13 (11:105).
Na lau tungelipenda tungeliyafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wangeionaje? Na lau tungelitaka tungewageuza hapo hapo walipo, basi wasingeweza kwenda wala kurudi.
Makusudio ya kufutilia mbali macho yao ni kuwa kipofu. Maana ni lau Mwenyezi Mungu angelitaka kuwaadhibu wakosefu dunianai angeliwapofusha macho yao na wasingeweza kuongoka na angeliwageuza wakawa wameganda bila ya kuwa na harakati wala uhai.
Na tunayempa umri tunampindua katika umbo. Basi je! hawatii akilini?
Kupindua kitu ni kukifanya juu chini. Binadamu kila anavyoendelea kuwa na umri mrefu anarudi nyuma: anakuwa mdhaifu baada ya kuwa na nguvu.
Lengo la ubainifu huu ni kuashiria kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amempa maisha ya kutosha ili aongoke na afanye mambo mema. Na lau angelipewa umri zaidi ya kawaida, basi maradhi yangelimweka chini, na umri mrefu ungelikuwa ni balaa na shari:
أَوَلَمْ نُعَمِّرْكُم مَّا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَاءَكُمُ النَّذِيرُ فَذُوقُوا فَمَا لِلظَّالِمِينَ مِن نَّصِيرٍ ﴿٣٧﴾
“Je, hatukuwapa umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka, na akawajia mwonyaji? Basi onjeni Na madhalimu hawana wa kuwanusuru” Juz. 22 (35:37).
وَمَا عَلَّمْنَاهُ الشِّعْرَ وَمَا يَنبَغِي لَهُ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ وَقُرْآنٌ مُّبِينٌ ﴿٦٩﴾
69. Wala hatukumfundisha mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur’an inayobainisha.
لِّيُنذِرَ مَن كَانَ حَيًّا وَيَحِقَّ الْقَوْلُ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٧٠﴾
Ili imwonye aliye hai, na ihakikike kauli juu ya makafiri.
HATUKUMFUNDISHA MASHAIRI
Aya 69 – 70
MAANA
Maadui wa Mwenyezi Mungu walijaribu kwa nyenzo zote kumkadhibisha Muhammad(s.a.w. w ) . Miongoni mwazo ni kauli yao kuwa ni mwenda wazimu, lakini mmoja wao, Walid bin Al-Mughira, aliyekufa akiwa kafiri, akasema: “Hapana, hakika kauli yake – yaani Qur’an – ina utamu na ina mvuto na kwamba juu yake kuna matunda na chini yake kumejaa. Hakika iko juu na haishindwi” Basi wakabadilisha kumtusi na wazimu na kusema: “Huyu ni mchawi muongo” (38:4.) Ilipowabainikia kuwa wao ndio waongo wakasema ni kuhani anakosea na anapatia au ni malenga mwenye kutunga mashairi kwa mawazo.
Ilivyo hasa ni kuwa kutuhumu kwao kuwa Mtume(s.a.w. w ) ni mshairi kunafahamisha kwamba mashairi kwa waarabu si lazima yawe na vina na uzani, bali yana upana zaidi. Ni fani iliyo na uzuri wake; iwe na uzani au la. Hali ni hiyo hiyo hata kwa wanafalsafa wa kale.
Mwenye Tafsir Ruhul-bayani amesema: “Mashairi ya watu wa kale hayakuwa na uzani wala vina wala hivyo sio nguzo ya ushairi.” Fikra hii imeenea leo kwenye somo la fasihi na uchambuzi.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewarudi wanaomtuhumu Mtume Mtukufu kuwa ni mshairi au kuhani kwenye Aya nyingi; miongoni mwazo ni:
إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿٤٠﴾ وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ قَلِيلًا مَّا تُؤْمِنُونَ ﴿٤١﴾ وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٤٢﴾
“Kwa hakika hiyo ni kauli ya Mtume mwenye heshima. Wala si kauli ya mshairi. Ni machache mnayoamini, wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayokumbuka. (69:40 – 42).
فَذَكِّرْ فَمَا أَنتَ بِنِعْمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٍ وَلَا مَجْنُونٍ ﴿٢٩﴾ أَمْ يَقُولُونَ شَاعِرٌ ﴿٣٠﴾
Na wewe kwa neema ya Mola wako si kuhani wala mwendawazimu. Au wanasema ni mshairi (52:29 – 30).
Na wakisema:
وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ ﴿٣٦﴾
“Hivi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mshairi mwendawazimu?” (37:36).
“Bali huyo ni mshairi.” Juz. 17 (21:5). Aya hizi tulizo nazo:
Wala hatukumfundisha mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur’an inayobainisha. Ili imwonye aliye hai, na ihakikike kauli juu ya makafiri.
Makusudio ya aliye hai hapa, ni yule ambaye akili yake iko hai kiuzingatiaji, kutaamali na kufungua moyo wake kwa haki na kheri. Na makusudio ya kauli hapa ni adhabu; sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
وَلَـٰكِنْ حَقَّتْ كَلِمَةُ الْعَذَابِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٧١﴾
“Lakini limekwishahakika neno la adhabu juu ya makafiri.” (39:71).
Washirikina walisema kuwa Qur’an aliyokuja nayo Muhammad si chochote ila ni mashairi yanayoelezea fikra yake na mawazo yake; na wala sio wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawarudi, kwa kuwaambia, kuwa shairi linajikita zaidi kwenye fikra hawa na mapendeleo ya mshairi; anamtetea anayempenda hata kama hana haki na anapamabana na anayemchukia hata kama ana haki. Na Qur’an ni kauli yenye hadhi na ya upambanuzi, na wala si kauli ya hawa na mzaha.
Ni Kitabu cha itikadi na sharia, maadili na mawaidha, ndani yake mna ilimu na fikra. Sasa wapi na wapi ushairi na hayo.
Kama ingelikuwa Qur’an imetengenezwa na Muhammad(s.a.w.w) , angeliweka humo machungu yake na huzuni yake, maisha yake na maazimio; sawa na walivyo malenga.
Kilichobakia ni kudokeza kuwa; hata hivyo Mtume(s.a.w.w) alikuwa akithamini na akiheshimu ushairi, kama fani iliyo na athari nzuri katika kuelezea mapendeleo na matakwa ya watu na amani yao.
Kuna kauli mshuhuri aliyoisema: “Katika baadhi ya ubainifu kuna uchwi na katika baadhi ya mshairi kuna hekima.” Alikuwa akiwaombea tawfiki malenga wanaoipigania haki na watu wa haki.
Aliwahi kumvulia kashida yake Ka’ab bin Zuheir kwa kumtuza, pale alipomsifu kwa kaswida yake iliyo maarufu kwa jina la Burda (kashida); miongoni mwa beti zake ni:
Haki ni nuru rasuli, kwaye twaangaziwa, Upanga wenye makali, wa Mola umechomozwa.
Tazama Juz. 22 (36:4) kifungu cha ‘Mdundo wa ndani katika Qur’an’ na Juz. 19 (26:224).
15
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا خَلَقْنَا لَهُم مِّمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَا أَنْعَامًا فَهُمْ لَهَا مَالِكُونَ ﴿٧١﴾
71. Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyofanya mikono yetu wanyamahowa, na wao ni wenye kuwamiliki.
وَذَلَّلْنَاهَا لَهُمْ فَمِنْهَا رَكُوبُهُمْ وَمِنْهَا يَأْكُلُونَ ﴿٧٢﴾
72. Na tumewatiisha kwao. Basi baadhi yao wako wanaowapanda, na baadhi yao wanawala.
وَلَهُمْ فِيهَا مَنَافِعُ وَمَشَارِبُ أَفَلَا يَشْكُرُونَ ﴿٧٣﴾
73. Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru?
وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ ﴿٧٤﴾
74. Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu wapate kusaidiwa!
لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُندٌ مُّحْضَرُونَ ﴿٧٥﴾
75. Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio jeshi lao watakaohudhurishwa.
فَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ إِنَّا نَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٦﴾
76. Basi isikuhuzunishe kauli yao, hakika Sisi tunayajua wanayoyaweka siri na wanayoyatangaza.
MIKONO YA MWENYEZI MUNGU NDIO DESTURI YA ULIMWENGU NA MAUMBILE
Aya 71 – 76
MAANA
Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyofanya mikono yetu wanyamahowa, na wao ni wenye kuwamiliki. Na tumewatiisha kwao. Basi baadhi yao wako wanaowapanda, na baadhi yao wanawala. Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru?
Wanyamahowa ni wanyama wa mifugo ambao ni ngamia, ngo’mbe, mbuzi na kondoo. Ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake; wanawala, wanakunywa maziwa yao, kutengenza majumba, samani, mavazi kutokana na ngozi, sufu na manyoya. Vile vile kuwabeba wao na mizigo yao kutoka sehemu moja hadi nyingine ambayo wangelifika kwa tabu.
Hilo amelikariri Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Aya kadhaa; kama vile Juz. 8 (6:142) na Juz. 14 (16:5- 8). Lengo ni kuhimiza Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kushukuriwa na kutiiwa. Hilo ameliashiria kwa kauli yake: “Basi je, hawashukuru?” Katika Nahjul-Balagha imeelezwa: “Hata kama Mwenyezi Mungu asingelitoa kiaga kwa kuasiwa kwake, bado ingelikuwa ni wajibu kutoasiwa kwa kushukuru neema zake.”
Makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Kutokana na iliy- ofanya mikono yetu,” ni sababu za kimaumbile. Kwa vile Mwenyezi Mungu sio mwili, mpaka isemwe kuwa ana mikono hasa.
Ibn Al- Arabi anasema katika Futuhat: “Watu wa Mwenyezi Mungu wanawagawanya viumbe kwenye namna mbili: Kuna namna inayopatikana kwa ulimwengu wa amri kwa sababu neno “kun” (kuwa) ni amri. Na aina nyingine inapatikana kwa mikono ya sababu, wanaita ulimwengu wa maumbile. Haya yamefafanuliwa katika Juz. 3 (2:255) kifungu cha ‘Mwenyezi Mungu na desturi ya maumbile.’
Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu wapate kusaidiwa! Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio jeshi lao watakaohudhurishwa.
Yaani hao washirikina ndio jeshi la hayo masanamu. Maana ni kuwa masanamu hayawezi kuwanufaisha washirikina, lakini pamoja na hayo wao wanayalinda. Ni jambo la kushangaza sana kuwa mwenye akili anaabudu mawe yasiyodhuru wala kunufaisha.
La kushangaza sana ni kuwa wao wanayalinda yasiibwe au kuharibiwa na wakati huo huo wanayatarajia yawasaidie katika shida na kuwakurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Hayo yenyewe hayawezi kujisaidia yatawasaidiaje wengine.
Zaidi ya hayo yote, waabudu masanamu walimwambia Mtume(s.a.w. w ) kuwa yeye ni mwendawazimu. Kwa nini? Kwa sababu yeye haabudu mawe. Wao ndio wenye akili kwa sababu wanaaabudu yale wanayoya- chonga. Jambo la kushangaza kabisa.
Basi isikuhuzunishe kauli yao kuwa wewe Muhammad ni mwendawazimu, au mshairi au ni kuhani.
Hakika Sisi tunayajua wanayoyaweka siri na wanayoyatangaza.
Walidhamiria chuki na kinyongo kwa Mtume(s.a.w. w ) na wakatangaza shutuma kwake na kwa mwito wake. Hakuna shaka kwamba Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa hilo na muweza wa kuwahisabu na kuwaadhibu. Basi hakuna haja ya huzuni na uchungu.
أَوَلَمْ يَرَ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ ﴿٧٧﴾
77. Je, haoni mtu kuwa tumemuumba kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndiye mgomvi wa dhahiri!
وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ قَالَ مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ ﴿٧٨﴾
78. Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: ‘Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imemung’unyika?’
قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ ﴿٧٩﴾
79. Sema: Ataihuisha aliyeiumba mara ya kwanza. Na Yeye ni Mjuzi wa kila uumbaji.
الَّذِي جَعَلَ لَكُم مِّنَ الشَّجَرِ الْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَا أَنتُم مِّنْهُ تُوقِدُونَ ﴿٨٠﴾
80. Yeye ambaye aliwajaalia moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa mnauwasha.
أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم بَلَىٰ وَهُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ ﴿٨١﴾
81. Kwani aliyeziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwa nini! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi.
إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾
82. Hakika amri yake anapotaka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kinakuwa.
فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾
83. Basi Ametakata na mawi yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake mtarejeshwa.
AKASEMA NI NANI ATAKAYEIHUISHA MIFUPA?
Aya 77 – 83
MAANA
Je, haoni mtu kuwa tumemuumba kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndiye mgomvi wa dhahiri!
Jana alikuwa ni tone la manii, lakini alipokuwa, kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, ni kiumbe aliye sawasawa mwenye ufahamu, alisahau asili yake na kuanza kumchokoza Mola wake kwa uasi na maneno mabaya.
Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: ‘Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imemung’unyika?’
Anayepiga mfano ni yule anayekana ufufuo. Anapiga mfano wa kutowezekana ufufuo kwa kusema, vipi vitaweza kuungana viungo vya mifupa na kuwa na uhai tena baada ya kuchakafuka na kuwa mchanga unaotawanyika huku na huko? Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamrudi mwenye mfano huu kwa kusema kuwa unastaajabu nini na kukana ufufuo kwa kupiga mfano na unasahahu nafsi yako? Hujui kwamba Mwenyezi Mungu amekuumba kwa mchanga kisha kwa tone la manii? Mwenyezi Mungu amekuleta baada ya kuwa hauko; vile vile basi ana uwezo wa kukurudisha baada ya kuwa mifupa iliyomung’unyika.
Sema: Ataihuisha aliyeiumba mara ya kwanza. Na Yeye ni Mjuzi wa kila uumbaji.
Yaani sema ewe Muhammad kumwambia mpinzani: Kuna ajabu gani kwa mifupa iliyochakaa kupata uhai? Yule ambaye amelifanya tone la manii liweze kusikia, kuona, kuwa na fahamu na ubainifu, ndiye atakayeweza kuirudisha mifupa ilivyokuwa. Umetangulia mfano wake katika Aya kadhaa; miongoni mwazo ni: Juz. 15 (17:49).
Yeye ambaye aliwajaalia moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa mnauwasha.
Mfano huu unaweka wazi fikra ya ufufuo. Ubainifu wa hilo ni kwamba wenye kupinga wameweka mbali fikra ya ufufuo si kwa lolote isipokuwa kwa kudhani kuwa vitu haviwezi kugeuka kuwa kinyume chake.
Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawajibu kuwa fikra hii ni dhana na njozi tu. Kwa sababu mageuko haya yanatokea waziwazi mkiyaona asubuhi na jioni, lakini hamatanabahi.
Mti mbichi unageuka kuwa kuni na ardhi kame inapata uhai na kumea miti mbalimbali ikipata maji. Sasa vipi mnakana kupata uhai mifupa na mnakubali kupata uhai ardhi iliyokufa na miti kugeuka kuwa moto. Yote haya ni mamaoja tu – kugeuka kitu kutoka kilivyo na kuwa kinyume chake.
Kwani aliyeziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwa nini! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi.
Mwenye kuuleta ulimwengu bila ya kutokana na chochote ni rahisi kuleta mfano wake kufanya mfano wake saa yoyote anayotaka. Umetangulia mfano wake katika Juz. 15 (17:99).
Hakika amri yake anapotaka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kinakuwa.
Alianza kuumba kwa neno ’Kuwa’ na atarudisha kwa neno hilo hilo.
Basi Ametakata na mawi yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake mtarejeshwa.
Ametakasika Mola wetu na shirk na Yeye peke yake ndiye mwanzishi na mrudishaji.
MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA SITA: SURAT YASIN
16
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
Sura Ya Thelathini Na Saba: Surat As-Saffat. Imeshuka Makka ina Aya 182.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
وَالصَّافَّاتِ صَفًّا ﴿١﴾
1. Naapa kwa wanaojipanga safu-safu.
فَالزَّاجِرَاتِ زَجْرًا ﴿٢﴾
2. Na kwa wenye kuzuia sana.
فَالتَّالِيَاتِ ذِكْرًا ﴿٣﴾
3. Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.
إِنَّ إِلَـٰهَكُمْ لَوَاحِدٌ ﴿٤﴾
4. Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.
رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ الْمَشَارِقِ ﴿٥﴾
5. Mola wa mbingu na ardhi, na vilivyomo kati yake, na ni Mola wa mashariki zote.
إِنَّا زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِزِينَةٍ الْكَوَاكِبِ ﴿٦﴾
6. Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya dunia (karibu) kwa pambo la nyota.
وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَانٍ مَّارِدٍ ﴿٧﴾
7. Na kuilinda na kila shetani muasi.
لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى الْمَلَإِ الْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ ﴿٨﴾
8. Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande.
دُحُورًا وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ ﴿٩﴾
9. Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.
إِلَّا مَنْ خَطِفَ الْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ ثَاقِبٌ ﴿١٠﴾
10. Isipokuwa anayenyakua kitu kidogo, na mara humfuatia kimondo kinachong’ara.
WANAOJIPANGA SAFU
Aya 1 – 10
MAANA
Naapa kwa wanaojipanga safu-safu. Na kwa wenye kuzuia sana. Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.
Wametofautiana wafasiri katika maana ya wanaojipanga safu, wenye kuzuia na wenye kusoma ukumbusho. Kuna waliosema kuwa ni Malaika.
Wengine wakasema ni waumini wanaokaa safu katika Swala ya jamaa na katika jihadi. Na wenye kuzuia ni makatazo ya Qur’an na Aya zake. Na wenye kusoma ni wasomaji wa Qur’an kwenye Swala na kwengineko.
Sio mbali kuwa makusudio ni aina tatu alizozitaja Imam Ali(a.s ) katika khutba ya kwanza kwenye Nahjul-Balagha, katika wasifu wa Malaika: “Miongoni mwao kuna ambao wamesujudu na wala hawarukui, na kuna waliorukuu na wala hawasimami, kuna waliosimama katika safu na wala hawatawanyiki.” Aliposema: ‘Kuna waliosimama katika safu na wala hawatawanyiki’ inawezekana kuwa ni ishara ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Naapa kwa wanao jipanga safu-safu.”
Kisha Imam Ali(a.s ) akaendelea kusema: “ Miongoni mwao kuna waaminifu wa wahyi wa Mungu, na ni ndimi zitamkazo kwa mitume Wake;” yaani wanaoshuka na wahyi kwa mitume wake; kama vile Jibril(a.s ) . Kauli hii nayo ina uwezekano wa kuwa ni ishara ya kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.” Kwa sababu wao wanasoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu wakati wanapofikisha kwa Mitume.
Akaendelea kusema: “Na miongoni mwao kuna wahifadhi wa waja wake.” Sheikh Muhammad Abduh, katika kuwaelezea hawa, anasema: “Kama kwamba wao ni nguvu inayotiwa katika miili ya binadamu na katika nafsi zao; akiwahifadhi Mwenyezi Mungu binadamu wasiangamie kwa Malaika. Na lau si hivyo, maangamizi yangelikuwa yanamwandama mtu zaidi kuliko amani.”
Sheikh, katika kuleta picha hii, anakusudia kurahisisha kufahamu jinsi Malaika wanavyohifadhi waja; akisema: “Kama kwamba wao.”
Kwa hiyo basi inawezekana hilo linaashiria kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na kwa wenye kuzuia sana,” ikiwa tutasema kuwa kuzia hapa maana yake ni kuzuia udhia kwa waja.
Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja. Mola wa mbingu na ardhi, na vilivyomo kati yake, na ni Mola wa mashariki zote.
Makusudio ya mashariki[6] zote ni mashariki ya Jua kwa kuangalia kwamba kila siku linatokeza mashariki na kutua magharibi. Mwenyezi Mungu amekata kuwa Yeye ni mmoja hana mshirika katika kuumba na kupangilia.
MWENYEZI MUNGU NA KUAPA NA VIUMBE VYAKE
Unaweza kuuliza : Kwa nini Mwenyezi Mungu ameapa kwa Malaika?
Wafasiri wamejibu kuwa Mwenyezi Mungu ameapa kwa Malaika kujulisha ukuu wa daraja na umuhimu wao. Hili ndio jawabu lao kwa kila alichoapia Mwenyezi Mungu; iwe ni wakati, mahali au chochote kilichoko juu au chini. Hata hivyo mwenye Dhilal ameunganisha kuapa huku na kauli ya watu wa jahiliya waliosema kuwa Malaika ni mabinti wa Mungu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:
أَفَأَصْفَاكُمْ رَبُّكُم بِالْبَنِينَ وَاتَّخَذَ مِنَ الْمَلَائِكَةِ إِنَاثًا إِنَّكُمْ لَتَقُولُونَ قَوْلًا عَظِيمًا ﴿٤٠﴾
“Je, Mola wenu amewachagulia waototo wa kiume na yeye akajichukulia watoto wa kike katika Malaika? Hakika nyinyi mnasema kauli kubwa.” Juz. 15 (17:40).
Akasema mwenye Dhilal: Lengo la kuapa kwa Malaika ni kuwarudi wenye kuamini upotofu huu alioita Mwenyezi Mungu ‘kauli kubwa.’
Tuanavyo sisi ni kuwa Mwenyezi Mungu anaapa na kitu chochote kile kwa lengo moja tu – kuwa kila kilichopo kwa asili yake kinafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja hana mshirika.
Hakuna mwenye shaka kuwa Malaika wanaopanga safu na wasiopanga safu wanamwabudu Mwenyezi Mungu na kumtii kwa ujuzi na yakini na kwa utumishi wao. Kwa hiyo kujua kwao hivi ni dalili mkataa kuwa Yeye ni mmoja hana mshirika katika kuuumba umiliki na upangiliaji; sawa na kujua wataalamu hakika ya maudhui waliyoyagundua na kuyafanyia majaribio.
Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya dunia (karibu) kwa pambo la nyota.
Makusudio ya mbingu ni anga ya juu na dunia ni dunia yetu sisi binadamu[7] , sio ulimwengu wote. Makusudio ya nyota ni zile zilizo kwenye anga iliyo karibu zaidi na sisi. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amejaalia nyota, jinsi ziliyvo na mwanga wake katika anga yetu, kuwa ni pambo na urembo; mbali ya manufaa na faida zake:
وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ﴿٩٧﴾
“Na yeye ndiye aliyewafanyia nyota ili muongoke kwazo katika viza vya bara na baharini. Juz. 7 (6:97).
Na kuilinda na kila shetani muasi wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande, wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu. Isipokuwa anayenyakua kitu kidogo, na mara humfuatia kimondo kinacho ng’ara.
Misamiati ya Aya hii iko wazi, isipokuwa miwili-Shetani asi na viumbe watukufu. Mwenyezi Mungu na Mtume wake wameinyamazia, hawaku- tubainishia. Nasi hatuwezi kufasiri bila ya ujuzi. Kwa hiyo tunasema kuwa Aya hizi ni katika zinazotatiza kwetu, lakini inawezekana kuwa ziko wazi kwa wenzetu.
Sio mbali kuwa sababu ya kunyamazia ni kuwa kumjua shetani huyu na kiumbe mtukufu hakuna uhusiano na maisha yetu au kuwa fahamu zetu zinashindwa kufahamu uhakika wake. Na mwenye elimu kadiri atakavyojitahidi, lakini hawezi kujua kila kitu; bali hawezi hata kujua kitu chochote katika vinavyomzunguka uhakika wake hasa kilivyo.
Kujua kwetu misamiati ya Aya; kama kimondo kinachong’ara, adhabu ya kudumu, kunyakua na kufuatiwa, hakuwezi kutosha kufasiri makusudio ya Aya kwa ujumla wake, maadamu hatujui uhakika wa shetani asi na viumbe watukufu.
Baadhi ya wafasiri wamesema makusudio ya shetani asi ni shetani jini. Wengine wakasema ni binaadamu ambaye hafikiri ukuu na utukufu wa nyota na kufahamisha kwake kuweko Mwenyezi Mungu. Masufi wanase- ma: Makusudio ya shetani ni picha na nguvu ya kuwazia. Yote hiyo ni kutupia kwa mbali. Ni afadhali kunyamaza kuliko kusema bila ya kujua. Mwenyezi Mungu anasema:
وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٥﴾
“Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo tu.” Juz. 15 (17:85).
فَاسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَا إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّن طِينٍ لَّازِبٍ ﴿١١﴾
11. Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tuliowaumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unaonata.
بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ ﴿١٢﴾
12. Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara.
وَإِذَا ذُكِّرُوا لَا يَذْكُرُونَ ﴿١٣﴾
13. Na wanapokumbushwa hawakumbuki.
وَإِذَا رَأَوْا آيَةً يَسْتَسْخِرُونَ ﴿١٤﴾
14. Na wanapoona Ishara, wanafanya maskhara.
وَقَالُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾
15. Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio dhahiri.
أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ﴿١٦﴾
16. Ati tukishakufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?
أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ ﴿١٧﴾
17. Hata baba zetu wa zamani?
قُلْ نَعَمْ وَأَنتُمْ دَاخِرُونَ ﴿١٨﴾
18. Sema: Naam! Na hali nyinyi ni madhalili.
فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ ﴿١٩﴾
19. Na hakika ni ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!
وَقَالُوا يَا وَيْلَنَا هَـٰذَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿٢٠﴾
20. Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.
هَـٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿٢١﴾
21. Hii ndiyo Siku ya upambanuzi mliyokuwa mkiikadhibisha.
احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ ﴿٢٢﴾
22. Wakusanyeni waliodhulumu, na wenzao, na hao waliokuwa wakiwaabudu,
مِن دُونِ اللَّـهِ فَاهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْجَحِيمِ ﴿٢٣﴾
23. Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!
وَقِفُوهُمْ إِنَّهُم مَّسْئُولُونَ ﴿٢٤﴾
24. Na wasimamisheni. Hakika hao wataulizwa.
مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ ﴿٢٥﴾
25. Mna nini? Mbona hamsaidiani?
بَلْ هُمُ الْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ ﴿٢٦﴾
26. Bali leo, watasalimu amri.
BALI UNASTAAJABU, NA WAO WANAFANYA MASKHARA
Aya 11 – 26
MAANA
Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tuliowaumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unaonata.
Waulize ewe Muhammad, wale wanaokana ufufuo kuwa kuumba mbingu na ardhi bila ya nyenzo yoyote ni kugumu au kumrudisha mtu kwenye uhai baada ya kufa kwake, na hali Mwenyezi Mungu amemuumba kwa udongo tu uanonata?
Hakika yule ambaye ameuumba ulimwengu bila ya nyenzo yoyote, inakuwa wepesi zaidi kurudisha viungo vya mtu kwenye uhai.
لَخَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٧﴾
“Hakika kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu, lakini watu wengi hawajui.” (40:57)
Unaweza kuuliza : Kwenye Juz.15 (18: 22) Mwenyezi Mungu anasema: “Wala usiulize habari zao kwa yeyote yule.” Kuna njia gani ya kuafikiana Aya mbili hizi?
Jibu : maudhui ya Aya ile yanahusiana na watu wa pango; ambapo Mwenyezi Mungu alimkataza Nabii wake mtukufu kutomuuliza yeyote kuhusiana na wao, baada ya kumweleza habari zao. Na hii tuliyo nayo inahusiana na washirikina tu. Na makusudio ni kuwatahayariza na kuwapa hoja.
Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara.
Wewe Muhammad unawastaajabu washirikina kwa jinsi walivyomfanya Mwenyezi Mungu kuwa na washirika, pamoja na dalili za umoja zilizo wazwazi. Nao vile vile wanakushangaa wewe; bali wanakufanyia maskhara. Kwa sababu dalili za ushirikina ziko wazi kulingana na ufahamu wao na wala sio dalili za tawhid.
Hii inafahamisha kuwa ndio makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili kweli ni jambo la ajabu. (38:5).
Ikiwa mtu atasema pamoja na yule mshairi: “Kila mtu dini yake anaitukuza, laitani usahihi ningejuzwa,” nasi tutajibu:
Kuna misingi na uhakika ulio wazi ambao hawawezi kutofautiana hata watu wawili; ambapo anaweza kuijua mjuzi na asiyekuwa mjuzi; mfano: Elimu ni bora kuliko ujinga, na utajiri ni bora kuliko ufukara.
Ikiwa wawili watatofautiana katika nadharia fulani, yule ambaye kauli yake itaishia kwenye misingi iliyo wazi basi huyo ndiye atakayekuwa na haki.
Na wanapokumbushwa hawakumbuki. Na wanapoona Ishara, wanafanya maskhara.
Kwa sababu mwenye kutii hawaa yake na kuiga mababa zake, huifumbia macho haki: Imam Ali(a.s ) anasema:“Yeyote anayeiacha haki, mazuri huwa mabaya kwake na mabaya huwa mazuri kwake, na hulewa ulevi wa upotevu.”
Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio dhahiri.
Haya wameyakari mara nyingi. Miongoni mwayo ni yale yaliyo katika Juz. 7 (6:7).
Ati tukishakufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa? Hata baba zetu wa zamani?
Maana yako wazi. umetangulia mfano wake katika Aya kadhaa; miongoni mwazo ni: Juz. 13 (13:5), Juz. 15 (17: 98), Juz. 18 (23: 82) na Juz. 20 (27:68)
Sema: Naam! Na hali nyinyi ni madhalili. Na hakika ni ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!
Yaani sema ewe Muhammad, kuwaambia wale wanaopinga ufufuo: ndio, nyinyi mtafufuliwa kutoka kwenye makaburi yenu kwa neno moja tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na mtakusanywa kwake mkiwa madhalili na mtaiona adhabu mliyokuwa mkiikadhibisha kwa macho yenu.
Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo. Hii ndiyo Siku ya upambanuzi -baina ya haki na batili -mliyokuwa mkiikadhibisha.
Haki inapowajia wanapokuwa na fursa ya kuifanyia kazi, wanasema huu ni uwongo na uchawi, hauamini ila mjinga mwenye kuhadaliwa. Na wakati ukipita ukaja wakati wa malipo na kuonja ubaya wa matendo yao, watasema: Ole wetu, sisi tulikuwa kwenye mghafala wa haya, tumejidhulumu wenyewe.
Hali hii mara nyingi inatokea. Mjinga anahangaikia litakalomdhuru, lakini anapopewa nasaha na mwenye akili na kumhadharisha na mwisho mbaya, yeye humdharau na anafura kichwa.
Yakimfika na kutokuwa na pa kukimbilia na kutambua kuwa amehasirika anahangaika na majuto na kusema: laitani nisingelikuwako.
Wakusanyeni waliodhulumu, na wenzao, na hao waliokuwa wakiwaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu.
Aya inaashiria kugawanyika wakosefu; kwamba mshirikina atafufuliwa na washirikina wenzake mahali pamoja kwenye Jahannam wakiwa pamoja na masanamu waliyokuwa wakiyaabudu. Vile vile mwizi pamoja na wezi. Kila aina kwa aina yake; sawa na walivyokuwa duniani.
Waongozeni njia ya Jahannamu!
Ikishamalizika hisabu Malaika wataambiwa: Haya wapelekeni haraka kwenye moto mbaya.
Na wasimamisheni. Hakika hao wataulizwa:
Kabla ya Malaika kuwapeleka kwenye Jahannam watawazuia ili waulizwe yale waliyokuwa wakiyafanya. Katika badhi ya mapokezi imeelezwa kuwa siku hiyo mtu ataulizwa kuhusu alivyomaliza umri wake, mali yake alivyoipata na kuitumia na elimu yake alivyoifanyia kazi.
Ama kulinganisha baina ya Aya hii na ile isemayo:
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُسْأَلُ عَن ذَنبِهِ إِنسٌ وَلَا جَانٌّ ﴿٣٩﴾
“Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.” (55:39)
Tumekuelezea mara nyingi. Kwa ufupi ni kuwa siku ya mwisho itakuwa na hali ya kuulizwa na ya kutoulizwa. Tazama juzuu hii tuliyo nayo (36:65).
Mna nini? Mbona hamsaidiani?
Yaani kesho wataambiwa wakosefu; kwa nini leo hamsaidiani na kule duniani mlikuwa na mshikamano dhidi ya haki na watu wake. Lengo la swali hili ni kutahayariza.
Bali leo, watasalimu amri.
Watafuata amri ya Mwenyezi Mungu na hawatakuwa na hila yoyote.
17
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٧﴾
27. Watakabiliana wao kwa wao kuulizana.
قَالُوا إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ الْيَمِينِ ﴿٢٨﴾
28. Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kuume.
قَالُوا بَل لَّمْ تَكُونُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٢٩﴾
29. Watasema: Bali nyinyi wenyewe hamkuwa waumini.
وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ بَلْ كُنتُمْ قَوْمًا طَاغِينَ ﴿٣٠﴾
30. Na hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi mlikuwa waasi.
فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَا إِنَّا لَذَائِقُونَ ﴿٣١﴾
31. Basi kauli ya Mola wetu imekwishatuthibitika. Hakika bila ya shaka tutaonja.
فَأَغْوَيْنَاكُمْ إِنَّا كُنَّا غَاوِينَ ﴿٣٢﴾
32. Tuliwapoteza kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.
فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ ﴿٣٣﴾
33. Basi hakika wao siku hiyo watashirikiana katika adhabu.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ ﴿٣٤﴾
34. Hivyo ndivyo tutakavyowafanyia wakosefu.
إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٣٥﴾
35. Wao walipokuwa wakiambiwa: Hapana Mola ila Mwenyezi Mungu (La ilaha illa Llahu) tu, wakijivuna.
وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ ﴿٣٦﴾
36. Na wakisema: Hivi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mshairi mwendawazimu?
بَلْ جَاءَ بِالْحَقِّ وَصَدَّقَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣٧﴾
37. Bali ameleta haki, na amewasadikisha Mitume.
WATAKABILANA WAO KWA WAO
Aya 27 – 37
MAANA
Watakabiliana wao kwa wao kuulizana. Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kuume.
Neno yamin, tulilolifasiri kwa maana ya kuume, huwa lina maana nyingi; miongoni mwazo ni: mkono, upande usiokuwa wa kushoto na baraka na nguvu. Makusudo hapa ni kupoteza.
Wahalifu wataulizana na kulaumiana wakati watakapoiona adhabu. Wanyonge watawatupia lawama viongozi kuwa kama si nyinyi tunge- likuwa waumini. Hadaa hii wameiletea ibara ya kuume. Kwa sababu waarabu wanakiona kitu kinachokuja kwa upande wa kuume kuwa ni kizuri. Kwa hiyo kusema kwao mkitujia kwa upande wa kuume ni sawa na anayesema umenilenga hasa au umeniwahi kweli. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:38).
Watasema: Bali nyinyi wenyewe hamkuwa waumini. Na hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi mlikuwa waasi. Basi kauli ya Mola wetu imekwishatuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja. Tuliwapoteza kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.
Hii ni kauli ya viongozi wakiwajibu wale wanyonge, kwamba sisi kazi yetu ilikuwa ni kutoa mwito na kuupamba, nanyi mkauitikia. Nasi tuliwaita kwenye kufuru mkaitikia na mtume akawaita kwenye imani mkamkimbia, kwa sababu ya uhabithi na upotevu wenu. Vinginevyo sisi tuna uwezo gani juu yenu lau mngeliamua kumwamini Mwenyezi Mungu; kama walivyoamini wengine?
Kwa hiyo basi natija ya ukafiri wetu na upotevu wenu na kutuitikia ni kustahiki kauli ya adhabu kwetu na kwenu; kama muonavyo.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 20 (29:25) na Juz. 22 (33:67).
Basi hakika wao siku hiyo watashirikiana katika adhabu.
Haya ni maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Maana yake ni kuwa adhabu itawaangukia wote siku hiyo watakayolaumiana.
Hivyo ndivyo tutakavyowafanyia wakosefu.
Adhabu ya daima bila ya kutofautisha mfuasi na mwenye kufuatwa.
Wao walipokuwa wakiambiwa:Hapana Mola ila Mwenyezi Mungu (La ilaha illa Llahu) tu, wakijivuna.
Walijivuna na wajifanya wakubwa kuliko haki, ndio yakawapata yaliyowapata wajivuni waliokuwa kabla yao.
Na wakisema: Hivi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mshairi mwendawazimu?
Wafasiri wamesema kuwa washirikina walijichanganya kwenye maneno yao; pale walipomsifu Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) kuwa ni mshairi na mwenda wazimu, ambapo mshairi huwa anatumia akili kupangilia maneno yake kwa usanifu wa hali ya juu. Sasa mwendawazimu anaweza kweli kazi hii.
Bali ameleta haki, na amewasadikisha Mitume.
Hapana! Huyo si mshairi wala mwendawazimu isipokuwa ni Mtume mtukufu, ameleta haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na amewasadikisha Mitume waliomtangulia na vitabu vyao.
Baada ya hayo. Kwa hakika mwendawazimu ni bora kuliko yule aliyemsifu Muhammad,(s.a.w. w ) aliyeteulia na Mwenyezi Mungu na kumchagua kwa ujumbe wake na kumjaalia ni bwana na mwisho wa Mitume, kuwa ni mwendawazimu. Tazama tafsri ya (36:69) katika Juzuu hii tuliyo nayo.
إِنَّكُمْ لَذَائِقُو الْعَذَابِ الْأَلِيمِ ﴿٣٨﴾
38. Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.
وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٣٩﴾
39. Wala hamtalipwa ila mliyokuwa mkiyafanya.
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿٤٠﴾
40. Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliotakaswa.
أُولَـٰئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ ﴿٤١﴾
41. Hao ndio watakaopata riziki maalum.
فَوَاكِهُ وَهُم مُّكْرَمُونَ ﴿٤٢﴾
42. Matunda, nao watahishimiwa.
فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٤٣﴾
43. Katika Bustani za neema.
عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ ﴿٤٤﴾
44. Wako juu ya viti wameelekeana.
يُطَافُ عَلَيْهِم بِكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ ﴿٤٥﴾
45. Wakizungushiwa kikombe cha chemchem.
بَيْضَاءَ لَذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ ﴿٤٦﴾
46. Cheupe kitamu kwa wanywao.
لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ ﴿٤٧﴾
47. Hakina madhara, wala hakimaliziki.
وَعِندَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ عِينٌ ﴿٤٨﴾
48. Na watakuwa nao wanawake wenye macho makunjufu.
كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَّكْنُونٌ ﴿٤٩﴾
49. Kama kwamba wao ni mayai yaliyohifadhika.
JUU YA VITANDA WAMEELEKEANA
Aya 38 – 49
MAANA
Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.Wala hamtalipwa ila mliyo kuwa mkiyafanya.
Baada ya Mwenyezi Mungu kusema kuwa wakosefu watashirikiana katika adhabu, sasa anawaambia kuwa adhabu yao ni malipo ya yaliyochumwa na mikonoi yao, wala hawatadhulumia hata chembe.
Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliotakaswa. Hao ndio watakaopata riziki maalumu.
Hii ni desturi ya Qur’an, kuwataja wakosefu na adhabu yao kisha kufuatia kuwataja wema na malipo yao. Malipo yenyewe kwa ujumla ni riziki maalum ya Mwenyezi Mungu kwa ajili yao.
Ama ufafanuzi wa riziki hiyo ni kama ifuatavyo:
Matunda, wanayoyatamani,nao watahishimiwa. Kwa sababu matunda na kudharauliwa ni sumu na huzuni. Kuna mithali isemayo: “Niheshimu wala usinilishe”
Katika Bustani za neema, zinazopitiwa na mito.Wako juu ya viti wamekabiliana, wakiangaliana kwa raha na furaha
Wakizungushiwa kikombe cha chemchem. Vijana watawapatia kinywajicheupe kitamu kwa wanywao, chenye rangi na ladha nzuri.Hakina madhara, Hakiumizi kichwawala kuleta maumivu wala hakimaliziki.
Neno nazaf likitumika kwenye kinywaji lina maaana ya kumalizika na likitumika kwa mtu lina maana ya kuisha akili yake; ndio maana baadhi ya wafasiri wakasema “Hakiwaleweshi;” yaani kinywaji hakimalizi akili yao.
Na watakuwa nao wanawake wenye macho makunjufu
Matunda, heshima, furaha, watumishi na zaidi ya hayo ni wanawake safi warembo wenye macho makunjufu na mazuri,kama kwamba wao ni mayai yaliyohifadhika. Kuwa kama mayai ni kinaya cha usafi wao na kuwa hawajaguswa na mikono wala kutazamwa na mcho.
WANAWAKE NA WATUMISHI
Hivi karibuni nilipata barua kutoka kwa mwananfunzi mmoja wa kike wa Kuwait, ikisema kuwa alikuwa na mazungumzo na rika lake. Yeye akasema kuwa Uislamu haumtofautishi mwanamume na mwanamke.
Wenzake wakampinga na kumwambia kuwa Qur’an imeelezea wazi kuwa Mwenyezi Mungu kesho atawalipa wanaume wema mahurulaini na hakusema vile atakavyowalipa wanawake wema. Kama haki ingelikuwa sawa, basi malipo yangelikuwa ya aina moja. Msichana anasema alishindwa kujibu na akataka nimwandikie ili awakinaishe wenzake.
Majibishano haya mazuri yanatufahamisha kuwa mwanamke ni sawa na mwanamume katika mataminio yake ya kimwili na mapendeleo yake. Na kwamba kupata mume ndio malipo bora zaidi, kama ilivyo kwa mwana- mume kupata mke. Vile vile inatufahamisha kuwa wivu wa mwanamke kwa mwanamume ni kama wa mwanamume.
Basi nikamjibu hivi: “Qur’an imeelezea waziwazi usawa baina ya mwanamume na mwanamke kama msingi wa ujumla. Kwenye hilo inasema:
أَنِّي لَا أُضِيعُ عَمَلَ عَامِلٍ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ ﴿١٩٥﴾
“ …kwamba mimi sitapoteza amali ya mfanya amali miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke” Juz. 4 (3:195).
“Mwenye kufanya mema - mwanamume au mwanamke - hali ya kuwa ni mwenye kuamini, basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kitobwe cha kokwa ya tende.” Juz. 5 (4:124).
Hakuna mwenye shaka kwamba atakayeingia Peponi atapata kila kinachotamaniwa na nafsi na kuburudisha macho awe mwanamume au mwanamke, kama ilivyoelezwa kwenye (43:71).
Vile vile Qur’an imewataja watumishi kama ilivyowataja Hurulaini. Ilipowasifu Hurulaini kuwa ni kama mayai yaliyohifadhika, pia imewataja watumishi kuwa ni lulu iliyotawanywa, kama iliyosemwa kwenye. (76:19)
Sio mbali kuwa kunyamazia kutaja kuwa mwanamke atalipwa kwa kijana mzuri kumefuata ada na desturi iliyozoeleka kwa watu ya kumzungumzia kijana kuoa na kumuuliza, kwa nini huoi? Lakini hawamuulizi msichana, kwa nini huolewi; kwa vile wanakuwa na haya sana. Wakale walisema: “Ana haya kama msichana.”
Vile vile imesemekana kuwa ladha za Peponi zote ni za kiroho si za kimaada au jinsia, na kwamba kutaja hurilaini, matunda na vikombe ni kama ishara na alama ya ladha ya kimwili kwenye ladha ya kiroho na kwamba viti na vitanda ni kinaya cha cheo na daraja.
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٥٠﴾
50. Tena watakabiliana wao kwa wao wakiulizana.
قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينٌ ﴿٥١﴾
51. Aseme msemaji miongoni mwao: Hakika mimi nilikuwa na rafiki.
يَقُولُ أَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُصَدِّقِينَ ﴿٥٢﴾
52. Aliyekuwa akiniambia: Hivyo wewe ni katika wanaosadiki.
أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَدِينُونَ ﴿٥٣﴾
53. Ati tukishakufa tukawa udongo na mifupa, ndio tutahisabiwa?
قَالَ هَلْ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ ﴿٥٤﴾
54. Atasema: Je! Nyie mtachungulia?
فَاطَّلَعَ فَرَآهُ فِي سَوَاءِ الْجَحِيمِ ﴿٥٥﴾
55. Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu.
قَالَ تَاللَّـهِ إِن كِدتَّ لَتُرْدِينِ ﴿٥٦﴾
56. Aseme Wallahi! Ulikaribia kuniangamiza.
وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّي لَكُنتُ مِنَ الْمُحْضَرِينَ ﴿٥٧﴾
57. Na lau si neema ya Mola wangu bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa waliohudhurishwa.
أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ ﴿٥٨﴾
58. Je! Sisi hatutakufa?
إِلَّا مَوْتَتَنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ ﴿٥٩﴾
59. Isipokuwa kifo chetu cha kwanza; wala sisi hatutaadhibiwa.
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿٦٠﴾
60. Hakika huku, bila ya shaka, ndiko kufuzu kukubwa.
لِمِثْلِ هَـٰذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ ﴿٦١﴾
61. Kwa mfano wa haya nawafanye wafanyao.
أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ الزَّقُّومِ ﴿٦٢﴾
62. Je! Kukaribishwa hivi ni bora, au mti wa Zaqum?
إِنَّا جَعَلْنَاهَا فِتْنَةً لِّلظَّالِمِينَ ﴿٦٣﴾
63. Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni fitna kwa waliodhulumu.
إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِي أَصْلِ الْجَحِيمِ ﴿٦٤﴾
64. Hakika huo ni mti unaotoka katikati ya Moto.
طَلْعُهَا كَأَنَّهُ رُءُوسُ الشَّيَاطِينِ ﴿٦٥﴾
65. Mashada yake ni kama vichwa vya mashetani.
فَإِنَّهُمْ لَآكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ ﴿٦٦﴾
66. Basi hakika hao bila ya shaka watakula katika huo, na wajaze matumbo kwa huo.
ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِّنْ حَمِيمٍ ﴿٦٧﴾
67. Kisha juu yake wapewe mchanganyiko wa maji ya moto.
ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى الْجَحِيمِ ﴿٦٨﴾
68. Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu.
KWA MFANO WA HAYA NAWAFANYE WAFANYAO
Aya 50 – 68
MAANA
Tena watakabilaiana wao kwa wao wakiulizana.
Bado maneno yanaendelea kuhusu watu wa Peponi. Katika Aya iliyotangulia, Mwenyezi Mungu (s.w.t) amesema kuwa watu wa Peponi watakuwa na aina mbali mbali za starehe.
Katika Aya hii anasema kuwa watazungumziana wao kwa wao, huku wakiwa na furaha, kuhusiana na maisha yao ya duniani. Miongoni mwayo ni:
Aseme msemaji miongoni mwao: Hakika mimi nilikuwa na rafiki aliyekuwa akiniambia: Hivyo wewe ni katika wanaosadiki ati tukishakufa tukawa udongo na mifupa, ndio tutahisabiwa?
Mumin huyu atawazungumzia wenzake na jirani zake kuhusiana na vile waumini wa malipo ya kiyama walivyokuwa wakifanyiwa masikhara wakisema wasioamini, ati mamake fulani, kweli tukishakufa na kuisha kabisa tutafufuliwa tuwe hai?
Hivi ndivyo alivyo kila mlahidi. Na hiyo hasa inatokana na kuwa kuamini ufufuo ni sehemu ya kuamini wahyi wa Mwenyezi Mungu kwa yule aliyemteua katika waja wake. Ikiwa mlahidi haamini wahyi huu, ataweza kweli kuamini ufufuo baada ya mauti? Kwa maneno mengine ni kuwa ufufuo ni katika mambo ya ghaibu ambayo kwa mlahidi ni vigano tu.
Atasema: Je! Nyie mtachungulia?
Mumin ataendelea kuwaambia wenzake akiwaomba waangalie Jahnnam ili waone mwisho wa aliyekuwa na dharau.
Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu.
Akishawaambia wenzake atachungulia kwenye Jahannam amwone jamaa yuko katikati ya Jahannam.Aseme - kwa kumtahayariza-Wallahi! Ulikaribia kuniangamiza. Yaani kunitia kwenye shaka kwa wasiwasi wako na shaka zako.Na lau si neema ya Mola wangu bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa waliohudhurishwa pamoja nawe katika moto.
Kisha mumin atawageukia wenzake awaambie:
Je! Sisi hatutakufa, isipokuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa. Hakika huku, bila ya shaka, ndiko kufuzu kukubwa.
Atazungumza haya kwa furaha kutokana na aliyoyapata huku akisema alhamudulillah, tumepita mtihani vizuri, hakuna mauti tena wala tabu. Hakuna isipokuwa radhi za Mwenyezi Mungu na neema zake. Katika maana haya ni kauli yake Mwenyezi Mungu: “Hawataonja humo isipokuwa mauti ya kwanza na atawakinga na adhabu ya moto” (44:57).
Kwa mfano wa haya nawafanye wafanyao na washindane wanaoshindana.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaachia waja matendo na amali, akawajibishia kufanya yale yaliyo na kheri nao na masilahi kwao; na akawakataza yale yaliyo na shari yao na ufisadi. Kisha akwaachia hiyari ya kufanya na kuacha. Mwenye kutii akamwahidi Pepo na mwenye kuasi akamwahidi adhabu ya kuunguza.
Hakuna mwenye shaka kuwa mwenye akili atajihurumia na kuchagua lililo na masilahi zaidi. Imeelezwa kwenye Nahjul-balagha: “Hakuna thamani ya nafsi zenu ispokuwa Pepo. Basi msiziuze ila kwayo.”
Je! Kukaribishwa hivi ni bora, au mti wa Zaqum? Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni fitna kwa waliodhulumu.
Kukaribishwa hivi ni kukaribishwa kwenye neema. Makusudio ya fitna hapa ni adhabu. Ama mti wa Zaqum ameubanisha Mwenyezi Mungu kwa kusema:
Hakika huo ni mti unaotoka katikati ya Moto. Mashada yake ni kama vichwa vya mashetani. Basi hakika hao bila ya shaka wataku- la katika huo, na wajaze matumbo kwa huo.
Zaqqum ni kauli ya waarabu kwa chakula kinachochukiza kukila. Kwenye Tafsir Tabari kuna maelezo Haya: “Iliposhuka Aya hii Abu Jahl alisema kwa madharau: “Mimi nitawaletea Zaqqum.” Akaleta siagi na tende kisha akasema: Haya! Nyinyi kuleni Zaqqum. Basi hii ndio Zaqqum anayowatisha nayo Muhammad.
Vichwa vya mashetani, ni kinaya cha ubaya na mandhari ya kutisha ya huo mti. Yule anayesema kuwa Zaqqum ni nembo ya ubaya wa adhabu, hatuwezi kumpinga.
Kisha juu yake wapewe mchanganyiko wa maji ya moto.
Yaani watakula zaqqum na wanywe maji ya usaha; kama anavyosema Mwenyezi Mungu: “Nyuma yake iko Jahannam na atanyeshwa maji ya usaha uliochanganyika na damu” Juz.13 (14: 16).
Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu.
Makusudio ya marejeo ni makazi ya mwisho na makao yao ya kudumu. Maana ni kuwa chakula chao ni Zaqqum na kinywaji chao ni maji moto. Ama kivazi chao, Mwenyezi Mungu amekiashiria kwa kusema:
سَرَابِيلُهُم مِّن قَطِرَانٍ ﴿٥٠﴾
“Nguo zao zitakuwa za lami” Juz. 13 (14:50).
18
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
إِنَّهُمْ أَلْفَوْا آبَاءَهُمْ ضَالِّينَ ﴿٦٩﴾
69. Hakika waliwakuta baba zao wamepotea.
فَهُمْ عَلَىٰ آثَارِهِمْ يُهْرَعُونَ ﴿٧٠﴾
70. Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.
وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٧١﴾
71. Na hakika walikwishapotea kabla yao wengi wa watu wa zamani.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ ﴿٧٢﴾
72. Na hakika tuliwapelekea waonyaji.
فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنذَرِينَ ﴿٧٣﴾
73. Basi tazama jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale walioonywa.
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿٧٤﴾
74. Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa.
وَلَقَدْ نَادَانَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ الْمُجِيبُونَ ﴿٧٥﴾
75. Na hakika Nuh alituita, na Sisi ni bora wa waitikiaji.
وَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ ﴿٧٦﴾
76. Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa.
وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُ هُمُ الْبَاقِينَ ﴿٧٧﴾
77. Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia.
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿٧٨﴾
78. Na tukamwachia kwa walio baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِي الْعَالَمِينَ ﴿٧٩﴾
79. Amani kwa Nuh ulimwenguni kote!
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٠﴾
80. Kwa hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.
إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨١﴾
81. Hakika yeye ni katika waja wetu walio waumini.
ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ ﴿٨٢﴾
82. Kisha tukawagharikisha wale wengine.
WALIPOTEA KABLA YAO WATU WENGI WA ZAMANI
Aya 69 – 82
MAANA
Hakika waliwakuta baba zao wamepotea. Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.
Wanazungumziwa washirikina wa kiarabu waliofuata nyayo za mababu zao bila ya kufanya utafiti wowote au mazingatio. Aya inaashiria kwamba mpotevu na mpotezaji wako sawa katika maasi na kustahili adhabu. Ama yule anayefuata uongofu na utengenevu anakuwa katika amani na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Hilo linafahamishwa na kauli yake Mwenyezi Mungu: “Husema: Bali tuta- fuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala hawakuongoka?” Juz. 2 (2:170). Maana yake ni kuwa, lau baba zao wangelikuwa kwenye uongofu, ingelifaa kuwafuata. Kwa maelezo zaidi tazama Juz.2 (2:168 – 170) kifungu cha ‘Kufuata na misingi ya itikadi.’
Na hakika walikwishapotea kabla yao wengi wa watu wa zamani. Na hakika tuliwapelekea waonyaji.
Ikiwa watakukadhibisha ewe Muhammad na kupotea na haki, basi walikwishapotea kabla yao wengi katika umma, ingawaje Mwenyezi Mungu aliwapeleka mitume na wabashiri; wakawatimizia hoja na kuwabainishia mapenzi yake na machukivu yake, wakaacha hayo wakafuata yale. Basi likastahili kwao neno la adhabu.Basi tazama jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale walioonywa walivyohizika na kubomolewa;isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa, amewaokoa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na adhabu yake na akawalipa ujira wake na thawabu zake.
Na hakika Nuh alituita, na Sisi ni bora wa waitikiaji.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anaashiria yale yaliyoelezwa kwenye Aya nyingine: “Na akasema Nuh: Mola wangu! Usiache Katika ardhi mkazi yeyote katika makafiri” (71:26).
Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa.
Mwenyezi Mungu alimnusuru Nuh na watu wake kutokana na mataghuti. Akawangamiza wote bila ya kubakia, kwa kuitikia maombi ya Nabii wake Nuh. Kwa hiyo akamuokoa yeye na walikouwa pamoja naye na udhia wa ukafiri muovu na kumuhifadhi na msiba na majanga.
SAM, YAFITH NA HAM
Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia, peke yao baada ya tufani.
Katika Tafsir Tabariy imesemwa: “Dhuria wa Nuh ndio waliobakia katika ardhi baada ya kuangamia kaumu yake. Na watu wote baada yake, mpaka leo, ni wa kizazi cha Nuh.
Waajemi na waarabu wanatokana na watoto wa Sam bin Nuh,Waturuki na Waslovenia ni watoto wa Yafith na weusi ni watoto wa Ham. Ulama na mapokezi yameeleza hivyo.”
Tabari alifariki mwaka 310 (A.H.), yaani zaidi ya miaka elfu moja iliyopita. Waliomtangulia na waliokuja baada yake walimbandika jina la sheikh wa wafasiri.
Katika Kamusi ya Kitabu kitakatifu imeandikwa: “Sam ni jina la kiebrania likiwa na maana ya isimu (jina). Yeye ndiye mtoto mkubwa wa Nuh. Kizazi chake ni waarabu, Waarmenia, waashwar na wayahudi. Ndio maana lugha zao wote hao zinatiwa Saamiya, kwa kunasibishwa naye; mfano: lugha ya kiarabu na kiebrania…Yafith huenda maana yake ni uzuri… kizazi chake ni wakazi wa kuanzia magharibi mwa Najad, kusini mwa Bahari ya Kazwin (Caspian sea) na Bahari nyeusi (Black sea) hadi fukwe na visiwa vya Bahri ya kati (Mediterranean Sea) katika asili ya wahindi wa Ulaya–katika hawa wanaingia waturuki na waslovania aliowaashiria Tabariy-Na ham ni jina la kiebrania yaani mwenye kuchemka naye ni mdogo wa watoto wa Nuh”
Na tukamwachia kwa walio baadaye.
Yaani tukamwachia utajo wa sifa katika uhai wake
Amani kwa Nuh ulimwenguni kote!
Yeye yuko kwenye amani ya Mungu kwa kutotajwa na mabaya. Mitume walikuwa wakimwomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwa na utajo mzuri kwa watu wakiondoka. Ibrahim(a.s ) alisema:
وَاجْعَل لِّي لِسَانَ صِدْقٍ فِي الْآخِرِينَ ﴿٨٤﴾
“Na unijaalie kutajwa kwa wema na wengine” Juz. 19 (26:84).
Kwa hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.
Yaani atawafanyia wema Mwenyezi Mungu kwa vile hapotezi amali ya yeyote mwenye kutenda, awe mume au mke.
Hakika yeye ni katika waja wetu walio waumini.
Kwa sababu alifanya wema katika matendo yake, akapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa jihadi yake ya haki. Hii ndio nembo na dalili ya mumin.
Kisha tukawagharikisha wale wengine duniani na akhera watakuwa na adhabu chungu kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.
وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِ لَإِبْرَاهِيمَ ﴿٨٣﴾
83. Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake.
إِذْ جَاءَ رَبَّهُ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ﴿٨٤﴾
84. Alipomjia Mola wake kwa moyo ulio salama.
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَاذَا تَعْبُدُونَ ﴿٨٥﴾
85. Alipomwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?
أَئِفْكًا آلِهَةً دُونَ اللَّـهِ تُرِيدُونَ ﴿٨٦﴾
86. Je, kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?
فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٨٧﴾
87. Mnamdhania nini Mola wa walimwengu wote?
فَنَظَرَ نَظْرَةً فِي النُّجُومِ ﴿٨٨﴾
88. Kisha akapiga jicho kutazama nyota.
فَقَالَ إِنِّي سَقِيمٌ ﴿٨٩﴾
89. Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa!
فَتَوَلَّوْا عَنْهُ مُدْبِرِينَ ﴿٩٠﴾
90. Nao wakamuacha, wakampa kisogo.
فَرَاغَ إِلَىٰ آلِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ ﴿٩١﴾
91. Basi akaiendea miungu yao kwa siri.
مَا لَكُمْ لَا تَنطِقُونَ ﴿٩٢﴾
92. Akaiambia: Mbona hamli? Mna nini hata hamsemi?
فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًا بِالْيَمِينِ ﴿٩٣﴾
93. Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kuume.
فَأَقْبَلُوا إِلَيْهِ يَزِفُّونَ ﴿٩٤﴾
94. Basi wakamjia upesi upesi.
قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ ﴿٩٥﴾
95. Akasema: Je, mnaviabudu vitu mnavyovichonga?
وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ ﴿٩٦﴾
96. Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba nyinyi na mnavyovifanya!
قَالُوا ابْنُوا لَهُ بُنْيَانًا فَأَلْقُوهُ فِي الْجَحِيمِ ﴿٩٧﴾
97. Wakasema: Mjengeeni jengo, kisha mtupeni motoni.
فَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَسْفَلِينَ ﴿٩٨﴾
98. Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini.
وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهْدِينِ ﴿٩٩﴾
99. Na akasema: Hakika mimi nakwenda kwa Mola wangu atakayeniongoza.
IBRAHIM ALIKUWA KATIKA KUNDI LAKE
Aya 83 – 99
LUGHA
Neno kundi limefasiriwa kutokana na neno la kiarabu shia’ lenye maana ya mfuasi anayefuta dini na njia ya yule anayemfuata. Kisha neno hili shia likazoeleka kuwa na maana ya mfuasi wa Imam Ali (a.s.) na yule aliyechukua nafasi yake katika watoto wake.
MAANA
Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake.
Kundi lake, yaani kundi la Nuh. Maana ni kuwa Ibrahim alifuata njia ya Nuh kiitikadi na kimatendo. Mfasiri mmoja wa kale anasema kuwa baina ya Nuh na Ibrahim kulikuwa na miaka 2640. mwenye kauli hii hakutege- meza kwenye rejea za kutegemewa.
Alipomjia Mola wake kwa moyo ulio salama.
Mwenye moyo huu ni yule aliyemfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu peke yake katika kauli zake na vitendo vyake vyote. Kuna Hadith isemyo: “Imani ya mja haisimami sawa mpaka usimame sawa moyo wake.” Kwenye Nahjul-balgha kuna maneno haya: “Heri zote ni za moyo ulio salama uliomtii anayeuongoza na kujiepusha na anayeudekeza.”
Alipomwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini? Je, kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?
Ibrahim alipinga ibada ya masanamu kwa watu wake akawakabili na kauli ya haki kwa kusema kuwa mnataka uzushi na batili kwa kumrejea asiyekuwa Mwenyezi Mungu na kujikurubisha kwa ibada kwa asiyekuwa Yeye? Umetangulia mfano wake katika Juz.7 (6:74).
Mnamdhania nini Mola wa walimwengu wote?
Je, mnamdhania kuwa ni jiwe au nyota naye ameumba ulimwengu? Je, akili yenu haiamki hata kidogo au kuzinduka kutokana na ujinga huu?
Katika Juz. 13 (13:16), kifungu cha ‘akili za watu haziwatoshelezi,’ tumebinisha kwa nini washirikina waliabudu mawe yanayokojolewa na mambwa na vicheche?
Kisha akapiga jicho kutazama nyota, akiwapa dhana watu wake kuwa anatafuta muumba wa ulimwengu, kwa vile wao walikuwa wakiabudu miungu mingi; hasa Nanar, mungu wa mwezi na mkewe Nanjal; kama ilivyoelezwa katika Kamusi ya Kitabu kitakatifu.
Maana ya Aya hii yamekuja katika Juz. 7 (6:74-79).
Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa!
Wafasiri wana kauli nyingi kuhusu makusudio ya ugonjwa. Yenye nguvu zaidi ni ile inayosema kuwa makusudio ya ugonjwa hapa ni shaka. Na maana yanakuwa kwamba Ibrahim aliwaambia watu wake, mimi hivi sasa nimedangana natafuta ukweli na uhakika ili niweze kuongoka kuweza kumjua muumbaji.
Nimeangalia masanamu nikapata uhakika kuwa hayawezi kuwa miungu; kisha nikaangalia nyota na sikupata mwongozo wowote; nimebaki kwenye shaka na kudangana.
Mfumo wa Aya unasaidia maana haya au angalau unayapa nguvu, kwa sababu yanaunganisha baina ya kuangalia kwenye nyota na kuwa mgonjwa.
Wala kauli yake hii ya kusema ana shaka hatuwezi kusema kuwa ni uwongo, kwa sababu ni katika hali ya kwenda na mbishani ili kumchukua kwenye hoja na kumkatia nyudhuru zote.
Nao wakamwacha, wakampa kisogo.
Walimwacha na wakajiendea zao.
Basi akaiendea miungu yao kwa siri.
Alichukua fursa ya kuondoka kwao na kwenda haraka kwenye masanamu. Walikuwa wameyawekea chakula ili yakibariki, akaiambia:
Mbona hamli? Mna nini hata hamsemi?
Alisema hivi kwa kuibeza na kutoa hoja kwa anayeiabudu na kutabaruku nayo.
Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kuume.
Aliavunja masanamu vipande vipande kwa mkono wake wa kuume na kabakisha kubwa lao, angalau waweze kurejea.
Basi wakamjia upesi upesi.
Watu walikuja haraka kwa Ibrahim na kuanza kumuuliza: wewe ndiwe uliyeifanyia hivi miungu yetu?
Akasema: Je, mnaviabudu vitu mnavyo vichonga?
Yaani ole wenu! Msimzulie Mwenyezi Mungu uwongo. Hakika Mola ni Muumba sio muumbwa na Mwenye kuruzuku sio mwenye kuruzukiwa. Nyinyi mmeyatengeneza masanamu haya kwa mikono yenu na mnayalinda, vipi yatakuwa miungu?
Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba nyinyi na mnavyovifanya!
Yeye ndiye Muumba wa kila kitu na marejeo ni kwake.
Wakasema: Mjengeeni jengo, kisha mtupeni motoni.
Walishindwa kuikabili hoja kwa hoja, wakakimbila maguvu; kama ilivyo hali ya mataghuti, huwasha moto na kuwatupa humo wapigania haki na kheri; kama ilivyokuwa zamani. Na elimu ya uvunjaji ilipoondelea sasa wanautupa moto kwa wananchi wanyonge pamoja na wanawake na watoto wao.
Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini, pale alipoufanya moto ni baridi na salama kwa Ibrahim.
Na akasema: Hakika mimi nakwenda kwa Mola wangu ndiye atakayeniongoza.
Baada ya Mwenyezi Mungu kumwokoa Ibrahim na vitimbi vya watu wake, alihama kutoka mji wake wa Urulkaldaniyya (Chaldeans) – Babilon – kwenda Sham.
Katika Kamusi ya Kitabu kitakatifu imeandikwa: “Yaligunduliwa mabaki na michoro ya mika elfu mbili kabla ya miladi (B.C.).
Lilikutwa jina la Ibrahim kwa mfumo wa Abramu au Abrama. Ugunduzi wa historia wa sasa umedhihirisha hali ya mji wa Uru, aliouhama Ibrahim, kama ulivyokuwa wakati huo.”
Umetangulia mfano wake kwa ufafunizi kidogo kwenye Juz. 17 (21:51-60).
19
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
رَبِّ هَبْ لِي مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٠٠﴾
100. Ewe Mola wangu! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.
فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ ﴿١٠١﴾
101. Basi tukambashiria mwana aliye mpole.
فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَىٰ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّابِرِينَ ﴿١٠٢﴾
102. Basi alipofika makamo ya kuhangaika pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa. Utanikuta mimi, Inshallah, katika wanaosubiri.
فَلَمَّا أَسْلَمَا وَتَلَّهُ لِلْجَبِينِ ﴿١٠٣﴾
103. Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji.
وَنَادَيْنَاهُ أَن يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿١٠٤﴾
104. Tulimwita: Ewe Ibrahim!
قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٠٥﴾
105. Umekwishaisadikisha ndoto. Kwa hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْبَلَاءُ الْمُبِينُ ﴿١٠٦﴾
106. Hakika haya ni majaribio yaliyo dhahiri.
وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ ﴿١٠٧﴾
107. Na tukamfidia kwa dhabihu adhimu.
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Na tukamwachia kwa walio baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ ﴿١٠٩﴾
109. Amani kwa Ibrahim.
كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١١٠﴾
110. Hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.
إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١١﴾
111. Hakika yeye ni katika waja wetu waumini.
وَبَشَّرْنَاهُ بِإِسْحَاقَ نَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٢﴾
112. Na tukambashiria Is-haq, Nabii miongoni mwa watu wema.
وَبَارَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَىٰ إِسْحَاقَ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌ وَظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ مُبِينٌ ﴿١١٣﴾
113. Na tukambarikia yeye na Is-haq na miongoni mwa dhuriya zao yuko mwema na mwenye kudhulumu nafsi yake waziwazi.
NIMEONA USINGIZINI KUWA NINAKUCHINJA
Aya 100 – 113
MAANA
Ewe Mola wangu! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.
Ibrahim alifikia uzee sana, wala hakuruzukiwa mtoto. Akamuomba Mola wake ampe kizazi cha waumini na warithi wema.
Basi tukambashiria mwana aliye mpole ambaye ni Ismail, hilo halina shaka, kwa ushahidi wa Qur’an. Ufafanuzi utakuja baada ya tafsiri ya Aya hizi tulizo nazo.
Basi alipofika makamo ya kuhangaika pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchin- ja. Basi angalia, waonaje?
Yaani alipofikia Ismail umri wa kuhangaika pamoja na baba yake. Ibrahim aliota kuwa anamchinja mwanawe. Kafahamu kutokana na ndoto hii kuwa amchinje au amlete machinjioni mwanawe. Na fahamu ya manabii ni yakini. Ndio maana akaamua kuitekeleza ndoto yake. Akampa habari mwanawe na kumtaka maoni yake.
Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa.
Alimjibu bila ya kusita kuwa mimi sina maoni wala amri yoyote kwenye amri ya Mwenyezi Mungu na amri yako. Nichinje tu maisha yangu hayana thamani yoyote mbele ya radhi za Mwenyezi Mungu na rdhi zako. Nikate kichwa na bado wewe utakuwa unanihurumia, maadamu unatekeleza radhi za Mwenyezi Mungu na kuitikia mwito wake.
Kisha Ismail akawa anampoza baba yake na kumwambia:Utanikuta mimi, Inshallah, katika wanaosubiri na kuwa mvumilivu kuweza kukabili kuchinjwa.
Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji, tulimwita: Ewe Ibrahim! Umekwishaisadikisha ndoto. Kwa hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.
Ismail aliponyoosha shingo yake na Ibrahim akapeleka kisu chake, kila mmoja wao akimwachia Mungu, ulikuja mlingano kutoka amri ya juu kwamba hii ndio tafsiri ya ndoto yako - azimio la kujitolea kwako kuchinja kwa ajili ya ikhalasi ya Mwenyezi Mungu na Ismail kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu kwa moyo safi. Kwa hiyo kuchinja halikuwa ndio lengo.
Unaweza kuuliza : Ikiwa lengo halikuwa kuchinja, basi kulikuwa na haja gani ya kuamrishwa?
Jibu : baadhi wanasema kuwa lengo la hilo ni kudhihirisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa watu na vizazi vitakvyokuja, utukufu wa Ibrahim na mwanawe Ismail walivyojitolea muhanga na ikhlasi yao.
Wawe ni sehemu ya kutukuzwa na tukufu hadi ufufuo. Wengine wakasema ni kwa ajili ya kuugeuza wivu wa Sara kwa Hajar, mama wa Ismail na kuzuia ugumu wake kwa Ibrahim.
Nasi tunaongeza kwenye kauli mbili hizo, kuwa vile vile Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alitaka kutoa mfano wa mumin wa haki, kwamba ni yule anayemtii Mwenyezi Mungu katika kila jambo, hata ikibidi kumchinja mwanawe aliye nyongo mkalia ini. Hili linaashiriwa na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t):
Hakika haya ni majaribio yaliyo dhahiri.
Yaani azimio hili la kujitolea muhanga kwa hali na mali kwa kufuata amri ya Mwenyezi Mungu peke yake ndio uthibitisho wa kweli wa mumin na ndio msitari unaogawanya baina ya mumin wa kweli na yule mwenye kuleta njozi za kuwa ni mumin, kumbe si chochote.
Na tukamfidia kwa dhabihu adhimu.
Makusudio ya dhabihu hapa ni mnyama wa kuchinjwa. Inasemkana alikuwa kondoo, wengine wakasema ni mbuzi. Sisi hatuna majukumu ya kujua aina ya fidia ilivyokuwa, wala jambo hilo halina uhusiano wa mbali au karibu na maisha yetu.
La kushangaza zaidi ni kauli ya aliyesema kuwa alikuwa ni kondoo aliyelisha Peponi miaka arubaini na kwamba Ibrahim(a.s ) alimpa Ibilisi wengu na kordani zake. Ikiwa alichunga Peponi miaka arubaini, basi uzito wake utakuwaje?
Na tukamwachia kwa walio baadaye. Amani kwa Ibrahim. Hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema. Hakika yeye ni katika waja wetu walio waumini.
Zimetangulia Aya hizi kwa herufi zake kwenye sura hii Aya (78 – 81).
Na tukambashiria Is-haq, Nabii miongoni mwa watu wema. Na tukambarikia yeye na Is-haq.
Bishara hii kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Ibrahim kupata mtoto wa pili, ni malipo ya subira yake na kumtoa mtoto wake kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu.
Katika Kamusi ya Kitabu kitakatifu imeandikwa kuwa Sara alimzaa Is-haq akiwa na mika 90 na Ibrahim akiwa na miaka mia, na kwamba maana ya neno Is-haq katika Lugha ya Kiebrania ni kucheka. Ama Hajar alimzaa Ismail na umri wa Ibrahim ni miaka 86.
Na miongoni mwa dhuriya zao yuko mwema na mwenye kudhulumu nafsi yake waziwazi.
Mwema katika kizazi hiki ni yule anayefuata mila ya Ibrahim na mwenye kujidhulumu ni yule aliyeiwacha mila hiyo.
JE, DHABIHU ALIKUWA ISMAIL AU IS-HAQ?
Baadhi wamesema kuwa mtoto wa Ibrahim aliyetakiwa kuchinjwa ni Is-haq na wala siye Ismail. Kauli hii haina rejea isipokuwa Hadith za kiisrail za Ka’bul-ahbar na hasadi ya mayahudi kwa watoto wa Ismail. Hili si la kushangaza kwa waisrail. Ama dalili za kuwa aliyetaka kuchinjwa ni Ismail ni kama zifuatazo:-
Kwanza : Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Basi tukambashiria mwana aliye mpole. Basi alipofika makamo ya kuhangaika pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja,’ inafahamisha waziwazi kuwa aliyebashiriwa, aliyehangaika naye na aliyetaka kuchinjwa ni mtu mmoja tu ambaye ni mtoto wa kwanza wa Ibrahim. Na mtoto wa kwanza ni Ismail, kwa maafikano ya waislamu, wanaswara na wayahudi.
Biblia inasema: “Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka themanini na sita, hapo Hajir alipomzalia Abramu Ishmael”
Mwanzo 16:16. Pia inasema: “Ndipo Ibrahim akaanguka kifudifidi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa? Tukiunganisha vifungu viwili hivi, maana yanayopatikana ni kuwa Ismail ni mkubwa wa Is-haq kwa mika 14.
Pili : Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na tukambashiria Is-haq, Nabii miongoni mwa watu wema,’ ambapo bishara hii ilikuwa ni malipo ya utiifu wake Ibrahim kwa Mungu kumchinja mwanawe. Bila shaka malipo yanakuja baada ya kazi. Kwa hiyo Is-haq alipatikana baada ya Ismail.
Tatu : Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Tukampa bishara ya Is-haq na baada ya Is-haq, Ya’qub.” Juz. 12 (11: 71). Vipi Mwenyezi Mungu (s.w.t) atoe bishara ya Is-haq kumzaa Ya’qub kisha wakati huohuo aamr- ishwe achinjwe, kabla ya kupatikana Ya’qub?
Nne : Kama aliyetaka kuchinjwa alikuwa ni Is-haq basi ingelazimika kuchinja, kufanya sa’yi na kupiga vikuta vya shetani kuwe kwenye ardhi ya Sham alipokuwa Sara na mwanawe Is-haq na wala kusingekuwa Makka alipokuwepo Hajar na mwanawe Ismail.
وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١١٤﴾
114. Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Harun.
وَنَجَّيْنَاهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ ﴿١١٥﴾
115. Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na tabu kubwa.
وَنَصَرْنَاهُمْ فَكَانُوا هُمُ الْغَالِبِينَ ﴿١١٦﴾
116. Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio washindi.
وَآتَيْنَاهُمَا الْكِتَابَ الْمُسْتَبِينَ ﴿١١٧﴾
117. Na tukawapa wawili hao Kitabu kinachobainisha.
وَهَدَيْنَاهُمَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿١١٨﴾
118. Na tukawaongoza kwenye njia Iliyonyooka.
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِي الْآخِرِينَ ﴿١١٩﴾
119. Na tukawachia kwa walio baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١٢٠﴾
120. Amani kwa Musa na Harun.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٢١﴾
121. Kwa hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.
إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٢٢﴾
122. Hakika hao ni katika waja wetu walio waumini.
وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٢٣﴾
123. Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume.
إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٢٤﴾
124. Alipowaambia watu wake: Hamna takua?
أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ الْخَالِقِينَ ﴿١٢٥﴾
125. Mnamwomba Baa’li na mnamwacha Mbora wa waumbaji.
اللَّـهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٢٦﴾
126. Mwenyezi Mungu, Mola wenu na Mola wa baba zenu wa zamani?
فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ ﴿١٢٧﴾
127. Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa.
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٢٨﴾
128. Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa.
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿١٢٩﴾
129. Na tukamwachia kwa walio baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ إِلْ يَاسِينَ ﴿١٣٠﴾
130. Amani kwa Ilyasin.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣١﴾
131. Kwa hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.
إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٣٢﴾
132. Hakika yeye ni katika waja wetu walio waumini.
MUSA NA ILYAS
Aya 114 – 132
MAANA
Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Harun.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimfanyia hisani Musa na Harun kwa utume, utajo wa kudumu na kuwashinda maadui. Utume hauwi kwa bidii ya mtu au kazi yake; isipokuwa unatokana na uteuzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi wa kujua mahali anapoweka ujumbe wake.” Juz. 8 (6:124).
Ndio maana utume haufungamani na taklifa yoyote. Kwa hiyo mtu haambiwi kuwa Mtume; kama anavyoambiwa kuwa na takua.
Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na tabu kubwa.
Tabia ya mayahudi ni kukubali kila kitu kwa ajili ya mali; ikibidi hata udhalili na aibu. Hivi ndivyo ilivyowazungumzia historia yao.
Firauni aliwafanya watumwa na hawakufanya lolote mpaka Mwenyezi Mungu alipowapa msaada wa Musa kuwatoa kwenye tabu na shida na kupata faraja.
Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio washindi.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwangamiza Firauni na askari wake, waisrail wakakomboka na utumwa na udhalili.
Na tukawapa wawili hao Kitabu kinachobainisha.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimteremshia Musa na Harun Tawrat ndani yake mkiwa na hukumu zilizo waziwazi.
Na tukawaongoza kwenye njia Iliyonyooka, njia ya haki na uadilifu.Na tukawachia kwa walio baadaye, utajo mzuri na sifa njema.Amani kwa Musa na Harun kutoka kwa Mwenyezi Mungu hapa duniani na akhera.
Kwa hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema. Hakika hao ni katika waja wetu walio waumini.
Yaani malipo ya wema ni wema tu. Yamepita maelezo kuhusu Musa na Harun katika Aya nyingi.
Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume.
Wafasiri wanasema kwamba Ilyas ni mmoja wa manabii wa Bani Israil na kwamba nasabu yake inakomea kwa Harun. Kwenye Tafsiri nyingi imeelezwa kuwa Ilyas huyu ndiye Idris aliyetajwa kwenye Juz. 16 (19:56) na Juz. 17 (21:85).
Katika Kamusi ya Kitabu kitakatifu imeelezwa kuwa neno Iliy ni la kiebrania lenye maana ya Mungu wangu na neno la Kigiriki lenye maana hii ni Ilyas. Pia mara nyingine hutumika katika lugha ya Kiarabu.
Alipowaambia watu wake: Hamna takua?
Aliwaongoza watu wake kwenye tawhidi na kuwahadharisha na shirki, kama walivyofanya mitume wengine.
Mnamwomba Baa’li na mnamwacha Mbora wa waumbaji, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?
Baa’ali ni jina la sanamu, kama unavyofahamisha mfumo wa Aya. Kwenye Kamusi ya Kitabu kitakatifu imeandikwa: “Baa’ali ni jina la Kikanaa’ni na maana yake ni Mola wa ahadi.”
Watu wa Ilyas waliabudu Baa’al, kama walivyoabudu masanamu waliokuwa kabla yao; ndio akawalingania kwenye tawhid; kama alivyofanya Nuh, Ibrahim, Musa na mitume wengineo.
Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa. Yaani walokadhibisha mwito wake, watahudhurishwa Siku ya Kiyama kwa ajili ya hisabu na adhabu.
Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa ambao waliitika mwito wa Ilyas. Hakika wao wataokoka na adhabu na wana wao malipo mema.
Na tukamwachia kwa walio baadaye utajo mwema.
Amani kwa Ilyasin. Kwa hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema. Hakika yeye ni katika waja wetu walio waumini.
Kundi la wafasiri wamesema kuwa jina la baba yake Ilyas ni Yasin na kwamba makusudio ya Ilyasin ni Ilyas hasa, kwa sababu mtoto ni katika watu wa baba.
Vyoyvote iwavyo, makusudio ya Ilyasin hapa ni Ilyas kutokana na mfumo wa mtiririko wa Aya. Kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwenye Aya za nyuma amamtaja Nuh kisha akasema: ‘Amani kwa Nuh,’ akamtaja Ibrahim, akasema: ‘Amani kwa Ibrahim.
Vile vile alipomtaja Musa na Harun. Kisha alipomtaja Ilyas kuwa ni katika Mitume alifuatishia kwa kusema: ‘Amani kwa Ilyasin’ ikajulikna kwamba makusudio ni Ilyas tu.
20
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
وَإِنَّ لُوطًا لَّمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٣﴾
133. Na hakika Lut bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.
إِذْ نَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ أَجْمَعِينَ ﴿١٣٤﴾
134. Tulipomwokoa yeye na ahali zake wote.
إِلَّا عَجُوزًا فِي الْغَابِرِينَ ﴿١٣٥﴾
135. Isipokuwa mwanamke mkongwe katika wale waliobakia nyuma.
ثُمَّ دَمَّرْنَا الْآخَرِينَ ﴿١٣٦﴾
136. Kisha tukawaangamiza wale wengine.
وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِم مُّصْبِحِينَ ﴿١٣٧﴾
137. Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi.
وَبِاللَّيْلِ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٣٨﴾
138. Na usiku. Basi je! Hamtii akilini?
وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٩﴾
139. Na hakika Yunus bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.
إِذْ أَبَقَ إِلَى الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ ﴿١٤٠﴾
140. Alipokimbia katika jahazi lililosheheni.
فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ الْمُدْحَضِينَ ﴿١٤١﴾
141. Wakapiga kura, akawa katika walioshindwa.
فَالْتَقَمَهُ الْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ ﴿١٤٢﴾
142. Basi samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulau- miwa.
فَلَوْلَا أَنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُسَبِّحِينَ ﴿١٤٣﴾
143. Na lau asingelikuwa ni katika wanaomtakasa (Mwenyezi Mungu),
لَلَبِثَ فِي بَطْنِهِ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤٤﴾
144. Bila ya shaka angelikaa tumboni mwake mpaka siku ya kufufuliwa.
فَنَبَذْنَاهُ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ سَقِيمٌ ﴿١٤٥﴾
145. Kisha tulimtupa ufukweni patupu, hali ya kuwa mgonjwa.
وَأَنبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِّن يَقْطِينٍ ﴿١٤٦﴾
136. Na tukamuoteshea mmea wa mung’unye.
وَأَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ مِائَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ ﴿١٤٧﴾
147. Na tulimtuma kwa watu elfu mia moja (laki moja) au zaidi.
فَآمَنُوا فَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ ﴿١٤٨﴾
148. Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.
LUT NA YUNUS
Aya 133 – 148
MAANA
Na hakika Lut bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume. Tulipomwokoa yeye na ahali zake wote; isipokuwa mwanamke mkongwe katika wale waliobakia nyuma. Kisha tukawaangamiza wale wengine.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:80-84), Juz. 12 (11:77 – 83) na Juz. 20 (29:28 – 35).
Maajabu ni yale yaliyoandikwa katika Biblia Mwanzo, (19:30 – 37), kwamba Lut alikuwa na mabinti wawili, wakamlewesha pombe baba yao, kisha akawaingilia, kila mmoja akazaa mtoto wa kiume.
Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi na usiku. Basi je! Hamtii akilini?
Waarabu walikuwa wakisafiri kutoka Hijaz kwenda Sham kwa ajili ya biashara na mengineyo. Njia yao ilikuwa ikipitia ardhi ya kaumu ya Lut. Kwa hiyo walikuwa wakipitia huko asubuhi na jioni wanapokwenda na kurudi safari yao.
Walikuwa wakiona athari ya maangamizi, Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawahadharisha washirikina wa kiarabu waliomkadhibisha Muhammad(s.a.w. w ) , kwa kuwaambia kuwa hampati mazingatio kwa majumba ya kaumu ya Lut yalivyokuwa matupu? Hamhofii kuwafika yaliyowafika wao?
Na hakika Yunus bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.
Yunus huyu ndiye aliyetajwa katika Juz. 17 (21: 87): “Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhabika” na ndiye aliyetajwa katika (68:48): “Wala usiwe kama mmezwa na samaki.”
Mfasiri mmoja amesema: “Yunus ni katika watu wa mji wa Neinawa ambao ulikuwa ni mji mkuu wa Waashwar (Assyrian) na kwamba ulikuwa mashuhuri sana kwenye karne kadhaa. Ulikuwa kwenye ukanda wa mashariki wa mto Dijla (Tigris) na wakazi wake walikuwa wakiabudu Ashtar au Ashtarut (Ashrot au Asterot) ambaye alikuwa akiabudiwa na watu wengi sana wa zamani[8] .”
Alipokimbia katika jahazi liliosheheni. Wakapiga kura, akawa katika walioshindwa.
Yunus aliwalingania watu wake kwenye ibada ya Mwenyezi Mungu, lakini hawakumwitikia. Basi akaona dhiki sana moyoni mwake, akaamua kuhama kwa hasira. Alifika ufukweni akaona jahazi limesheheni watu na mizigo akawaomba ajiunge nao kwenye msafara.
Walipofika katikati ya bahari jahazi likataka kuzama; wakona lazima wamtupe mmoja wao baharini ili wapate kuokoka. Ndipo wakamua kupiga kura, iliyomuangukia Yunus, naye akaamua kujitupa baharini.Basi samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa, kwa vile hakuvumilia adha ya watu wake kama walivyovumilia manabii wengine.
Na lau asingelikuwa ni katika wanaomtakasa (Mwenyezi Mungu), Bila ya shaka angelikaa tumboni mwake mpaka siku ya kufufuliwa.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amebainisha aina ya kutakasa huko (tasbihi) pale aliposema:
فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾
“Basi aliita katika giza (yaani katika tumbo la samaki) kwamba hapana Mola isipokuwa wewe. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu” Juz. 17 (21:87).
Basi Mwenyezi Mungu akamkubalia mwito wake na akamtoa kwenye jela yake inayotembea baharini. Lau sikukimbilia kwa Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi, angelibakia ndani ya jela maisha mpaka Kiyama.
Kisha tulimtupa ufukweni patupu, hali yakuwa mgonjwa. Na tukamuoteshea mmea wa mung’unye.
Wanasema alitoka tumboni mwa samaki akiwa kama kifaranga kisicho na manyoya kikiwa mbungani peke yake. Ndipo Mwenyezi Mungu akamuoteshea mmung’unye ili ajisitiri na majani yake.
Na tulimtuma kwa watu elfu mia moja (laki moja) au zaidi. Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.
Mwenyezi Mungu alimtuma kwa watu hao, mwanzoni, wakampinga. Alipowaacha kwa kukasirika, walihofia wasifikwe na balaa na adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Basi wakamwamini Mwenyezi Mungu na wakamtaka msamaha na rehema. Akawasamehe na maangamizi. Yunus akawarudia na wakafurahi kwa kufika kwake naye akafurahi kwa imani yao.
Tazama Juz. 11 (10:98 – 100) kifungu cha ‘Kisa’ na Juz. 17 (21:87).
فَاسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ الْبَنَاتُ وَلَهُمُ الْبَنُونَ ﴿١٤٩﴾
149. Basi waulize: Ati Mola wako ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wana watoto wa kiume?
أَمْ خَلَقْنَا الْمَلَائِكَةَ إِنَاثًا وَهُمْ شَاهِدُونَ ﴿١٥٠﴾
150. Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?
أَلَا إِنَّهُم مِّنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ ﴿١٥١﴾
151. Ehe! Hakika wao kwa kujitenga kwao wanasema.
وَلَدَ اللَّـهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١٥٢﴾
152. Mwenyezi Mungu amezaa! Na hakika bila ya shaka hao ni waongo!
أَصْطَفَى الْبَنَاتِ عَلَى الْبَنِينَ ﴿١٥٣﴾
153. Je, amechagua watoto wa kike kuliko wa kiume?
مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ﴿١٥٤﴾
154. Mna nini? Vipi mnahukumu?
أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿١٥٥﴾
155. Hamkumbuki?
أَمْ لَكُمْ سُلْطَانٌ مُّبِينٌ ﴿١٥٦﴾
156. Au mnayo hoja iliyo wazi? Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli.
فَأْتُوا بِكِتَابِكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٥٧﴾
157. Na wameweka nasaba baina yake na majini.
وَجَعَلُوا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجِنَّةِ نَسَبًا وَلَقَدْ عَلِمَتِ الْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ ﴿١٥٨﴾
158. Na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa.
سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٥٩﴾
159. Ametakasika Mwenyezi Mungu na yale wanayomsifu.
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٦٠﴾
160. Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliotakaswa.
ATI MOLA WAKO ANA WATOTO WA KIKE NA WAO WANA WATOTO WA KIUME?
Aya 149 – 160
MAANA
Basi waulize: Ati Mola wako ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wana watoto wa kiume? Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?
Qur’an ni hoja ya kihistoria isiyokubali shaka wala mjadala. Nayo imeeleza kuwa baadhi ya makabila yalikuwa yakisema kuwa Mwenyezi Mungu amewafanya Malaika kuwa ni wanawake; kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawarudi kuwa huko ni kuvurumisha na kupofuka na haki, kwa sababu wao hawajui chochote kuhusiana na Malaika.
Katika maana ya hayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na wamewafanya Malaika ambao ni waja wa Mwingi wa rehema kuwa wanawake. Je, wameshuhudia kuumbwa kwao?” (43:19) Vile vile katika Juz. 15 (17:40).
Ehe! Hakika wao kwa kujitenga kwao wanasema: Mwenyezi Mungu amezaa! Na hakika bila ya shaka hao ni waongo!
Neno kujitenga tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu ifk, ambalo mara nyingi hutumika kwa maana ya uzushi, lakini hapa limekuja kwa maana ya kujitenga ambayo pia ni miongoni mwa maana yake; kama lilivyotumika katika Aya isemayo:
قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَأْفِكَنَا عَنْ آلِهَتِنَا ﴿٢٢﴾
“Je, umetujia ili ututenge na miungu yetu?” (46:22).
Kwa hiyo maana yake hapa ni kuwa wao kwa sababu ya kujitenga na Tawhid na kuifuata shirki walisema kuwa Mwenyezi Mungu ana mtoto. Hakuna mwenye shaka kuwa wao ni waongo katika kauli hii.
Je, amechagua watoto wa kike kuliko wa kiume?
Yaani Mungu achague wa kike tu na wa kiume awachie nyinyi; kama mnavyodai. “Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu mabinti. Ametakata na hayo! Na hali wao hupata wanavyovitamani.
Na mmoja wao akibashiriwa msichana uso wake unasawijika naye amejaa chuki.” Juz. 14 (16: 56 -57).
Mna nini? Vipi mnahukumu yaliyo mbali na macho na akili zenu?Hamkumbuki mkakoma na shirki na kauli za uzushi,na hali Mwenyezi Mungu amewakumbusha na akawahadharisha kupitia kwa Mtume wake mwenye amana ya wahyi wake?
Au mnayo hoja iliyo wazi? Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli.
Onyesheni hoja ya kiakili au ya kinukuu kuwa Mwenyezi Mungu ame- wafanya Malaika ni wanawake.
Na wameweka nasaba baina yake na majini.
Wametofautiana wafasiri kuhusu maana ya Aya hii. Tunavyofahamu sisi, kutokana na dhahiri yake ni kuwa washrikina walimnasibishia Mwenyezi Mungu mtukufu mahusiano ya uzazi na majini, kama walivyomnasibishia Malaika.
Kuna tafsiri iliyonukuliwa kutoka kwa Mujahid na Muqatil kwamba Kinana na Khuzaa walisema kuwa Mwenyezi Mungu alitaka uchumba kwa mabwana wa kijini nao wakamuoza binti wao wa ukoo wa kilodi, na ndio akazaa naye Malaika!
Na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa.
Vipi atakuwa na nasaba na majini na hali wao wanajua kuwa Mungu ndiye aliyewaumba na kwamba wao watafufuliwa na kuulizwa yale waliyokuwa wakiyafanya.
Ametakasika Mwenyezi Mungu na yale wanayomsifu, na ametukuka sana na wanayoyasema wenye kufananiza na wapinzani
Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliotakaswa, kwani hakika wao wanamtakasa na shirki na kuwa na mtoto na wanamtakasa kwa kauli na vitendo na yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawalipa kwa imani yao na ikhlasi yao kwa yale mema waliyoyafanya.
21
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ ﴿١٦١﴾
161. Basi hakika nyinyi na mnaowaabudu.
مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ بِفَاتِنِينَ ﴿١٦٢﴾
162. Hamuwezi kuwapoteza.
إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ الْجَحِيمِ ﴿١٦٣﴾
163. Isipokuwa yule atakayeingia Motoni.
وَمَا مِنَّا إِلَّا لَهُ مَقَامٌ مَّعْلُومٌ ﴿١٦٤﴾
164. Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalum.
وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ ﴿١٦٥﴾
165. Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.
وَإِنَّا لَنَحْنُ الْمُسَبِّحُونَ ﴿١٦٦﴾
166. Na hakika sisi ndio wenye kusabihi.
وَإِن كَانُوا لَيَقُولُونَ ﴿١٦٧﴾
Na hakika wao walikuwa wakisema.
لَوْ أَنَّ عِندَنَا ذِكْرًا مِّنَ الْأَوَّلِينَ ﴿١٦٨﴾
168. Tungelikuwa na kumbukumbu ya wa zamani.
لَكُنَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٦٩﴾
169. Bila shaka tungelikuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu waliotakaswa.
فَكَفَرُوا بِهِ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿١٧٠﴾
180. Lakini waliikataa. Basi watakuja jua.
NYINYI NA MNAOWAABUDU
Aya 161 – 170
MAANA
Basi hakika nyinyi na mnaowaabudu hamuwezi kuwapoteza; isipokuwa yule atakayeingia Motoni.
Wanaambiwa washirikina. Maana ni kuwa, enyi washirikina! Hakuna atakayeitikia upotevu wenu na ibada yenu ya masanamu isipokuwa wale walioacha njia ya uongofu inayopelekea radhi za Mwenyezi Mungu na thawabu zake na akafuata njia ya upotevu, inayokomea kwenye hasira za Mwenyezi Mungu na adhabu yake.
Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalum.
Haya ni maneno ya Malaika wakiwarudi washirikina waliosema kuwa Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu na washirikina wakachaguliwa watoto wa kiume.
Maana ni kuwa sisi sote ni waja wa Mwenyezi Mungu tunamtakasa kwa sifa njema zake. Na kila mmoja katika sisi ana wadhifa wake wa kiiibada haupetuki.
Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu. Na hakika sisi ndio wenye kusabihi.
Miongoni mwetu wako waliosimama safu kwa ibada na wengine hawachoki na dhikri na tasbihi. Kuna Hadith inayosema: “Katika wao kuna waliorukui hawasimami na miongoni mwao wapo waliosujudi hawainui vichwa vyao.”
Na hakika wao walikuwa wakisema: Tungelikuwa na kumbukumbu ya wa zamani, bila shaka tungelikuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu waliotakaswa.
Waliokuwa wakisema ni washirikina wa kiarabu ambao walimfanya Mwenyezi kuwa ana mabinti Malaika na wakamfanyia nasaba baina yake na majini. Maana ni kuwa washirikina walikuwa wakisema kabla ya kuja Muhammad(s.a.w. w ) na Qur’an, kwamba lau kitawajia kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa haki, watakiamini na watamwabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Yeye dini.
Lakini yalipowajia yale waliyokuwa wakiyatamani walizidi jeuri na kuikimbia haki. Ndio akaishiria Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kusema:
Lakini waliikataa. Basi watakuja jua, itakavyokuwa adhabu.
وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا الْمُرْسَلِينَ ﴿١٧١﴾
171. Na bila ya shaka neno letu lilikwishatangulia kwa waja wetu waliotumwa.
إِنَّهُمْ لَهُمُ الْمَنصُورُونَ ﴿١٧٢﴾
172. Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakaonusuriwa.
وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ ﴿١٧٣﴾
173. Na kwamba jeshi letu ndilo litakaloshinda.
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿١٧٤﴾
174. Basi waache kwa muda.
وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ ﴿١٧٥﴾
175. Na uwaone, nao wataona.
أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ ﴿١٧٦﴾
176. Je, wanaihimiza adhabu yetu?
فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَاءَ صَبَاحُ الْمُنذَرِينَ ﴿١٧٧﴾
177. Basi itakaposhuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walioonywa.
وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿١٧٨﴾
178. Na waache kwa muda.
وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ ﴿١٧٩﴾
179. Na uone, nao wataona.
سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٨٠﴾
180. Ametakasika Mola Wako, Mola Mwenye enzi, na yale wanayomsifu.
وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ ﴿١٨١﴾
181. Na Salamu juu ya Mitume.
وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٨٢﴾
182. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.
JESHI LETU NDILO LITAKALOSHINDA
Aya 171 – 182
MAANA
Na bila ya shaka neno letu lilikwishatangulia kwa waja wetu waliotumwa. Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakaonusuriwa.
Na kwamba jeshi letu ndilo litakaloshinda duniani kwa hoja na dalili. Imam Ali(a.s ) anasema:“Si mshindi mwenye kushinda kwa dhambi na mwenye kushinda kwa shari ndiye aliyeshindwa. Ama huko Akhera hakuna hila wala nguvu kwa wabatilifu.”
Ar-razi anasema: “Ushindi unaweza kuwa kwa hoja na unaweza kuwa kwa dola na utawala na pia unaweza kuwa kwa kudumu na kuwa imara kwenye haki.
Kwa hiyo mumin hata kama wakati mwingine anashindwa, kwa sababu ya udhaifu na hali ya dunia, lakini bado yeye ndiye anayekuwa mshindi. Si lazima kusemwa kuwa Mitume waliuawa na waumini wengi wakashindwa.”
Kauli ya Razi, kuwa ushindi unaweza kuwa kwa uimara kwenye haki, inaweza kuthibitishwa na ukakamavu wa waarabu leo, kukataa kwao kujisalimisha na azma yao ya kumzuia adui, kwa namna yoyote itakavyokuwa dunia na pamoja na kuonekana kuwa ukoloni na uzayuni unawashinda.
Yametangulia maelezo ya jinsi Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyowalinda wale walioamini katika Juz. 17 (22:38).
Basi waache kwa muda na uwaone, nao wataona.
Anaambiwa Muhammad(s.a.w. w ) aachane na washirikina kisha angoje kidogo atawaona watakavyosalimu amri wakiwa wanyonge. Na kweli haya yalitokea pamoja na majeshi yao makubwa na vikosi vingi dhidi ya Mtume.
Je, wanaihimiza adhabu yetu?
Hili ni jawabu la kauli ya washirikina waliposema: Tuletee uliyotuahidi. Maana ya jawabu ni kuwa vipi mnahimiza adhabu ya Mwenyezi Mungu na hali mnajua kuwa ikiwashukia hamtaiweza wala hamtaweza kuikimbia.
Basi itakaposhuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walioonywa.
Makusudio ya uwanajani kwao ni majumbani mwao na asubuhi ni siku ya adhabu. Maana ni kuwa siku atakayowaadhibu Mwenyezi Mungu baada ya kuwaonya itakuwa mbaya sana kwao.
Na waache kwa muda na uone, nao wataona.
Mwenyezi Mungu amelikariri kwa kutia msisitizo wa kutekeleza ahadi yake na kwamba itakuwa tu.
Ametakasika Mola Wako, Mola Mwenye enzi, na yale wanayomsifu. Na Salamu juu ya Mitume. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.
Mwenyezi Mungu ameishiliza Sura hii kwa kujitakasa na yale yasiokuwa laiki ya ukuu wake, kwa vile kwenye Sura hii amewazungumzia washirikina.
Akajisifu kwa enzi kwa vile Yeye ni muweza wa kila kitu na akajisifu kwa sifa njema kwa sababu yeye ndiye mwenye kunemesha mwenye fadhila. Na salamu kwa mitume, kwa sababu wao walitekeleza amana kwa ikhlasi na wakaibeba. Kwa hiyo basi hakuna enzi wala sifa ila kwa yule aliyemuenzi Mwenyezi Mungu na akamtii.
MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA SABA: SURAT AS-SAFFAT
22
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
Sura Ya Thelathini Na Nane: Surat Saad. Imeshuka Makka, Ina aya 88
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
ص وَالْقُرْآنِ ذِي الذِّكْرِ ﴿١﴾
1. Swaad. Naapa kwa Qur’an yenye ukumbusho.
بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي عِزَّةٍ وَشِقَاقٍ ﴿٢﴾
2. Lakini waliokufuru wamo katika majivuno na upinzani.
كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ فَنَادَوا وَّلَاتَ حِينَ مَنَاصٍ ﴿٣﴾
3. Vizazi vingapi tumeviangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwishapita.
وَعَجِبُوا أَن جَاءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ وَقَالَ الْكَافِرُونَ هَـٰذَا سَاحِرٌ كَذَّابٌ ﴿٤﴾
4. Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anayetokana na wao. Na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo.
أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ ﴿٥﴾
5. Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili kweli ni jambo la ajabu.
وَانطَلَقَ الْمَلَأُ مِنْهُمْ أَنِ امْشُوا وَاصْبِرُوا عَلَىٰ آلِهَتِكُمْ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ يُرَادُ ﴿٦﴾
6. Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililopangwa.
مَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي الْمِلَّةِ الْآخِرَةِ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا اخْتِلَاقٌ ﴿٧﴾
7. Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu.
أَأُنزِلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ مِن بَيْنِنَا بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ مِّن ذِكْرِي بَل لَّمَّا يَذُوقُوا عَذَابِ ﴿٨﴾
8. Ati yeye ndiye aliyeteremshiwa mawaidha kati yetu?” Bali wao wana shaka na mawaidha yangu; bali hawajaionja adhabu yangu.
أَمْ عِندَهُمْ خَزَائِنُ رَحْمَةِ رَبِّكَ الْعَزِيزِ الْوَهَّابِ ﴿٩﴾
9. Au wanazo wao hazina za rehema za Mola wako, Mwenye nguvu, Mpaji?
أَمْ لَهُم مُّلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَلْيَرْتَقُوا فِي الْأَسْبَابِ ﴿١٠﴾
10. Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake? Basi na wazipande sababu zote.
جُندٌ مَّا هُنَالِكَ مَهْزُومٌ مِّنَ الْأَحْزَابِ ﴿١١﴾
11. Ni jeshi litakaloshindwa miongoni mwa makundi yatayoshindwa.
NAAPA KWA QUR’AN YENYE MAWAIDHA
Aya 1 – 11
MAANA
Swaad.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1).
Naapa kwa Qur’an yenye ukumbusho, Lakini waliokufuru wamo katika majivuno na upinzani.
Jawabu la kiapo linakadiriwa kuwa ni ‘Hakika hiyo ni haki.’ Makuraishi walikadhibisha Qur’an ambayo ina kheri yao na enzi yao. Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akaapa kwa Qur’an yenyewe kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwamba hakuna sababu ya kukadhibisha huku isipokuwa kiburi cha wakadhibishaji, kuikimbia kwao haki na uadui wao kwa Muhammad(s.a.w. w ) .
Kuapa kwake Mwenyezi Mungu kwa Qur’an kunaashiria kwamba hiyo Qur’an kushinda kwake kunafahamishwa na ufasaha wake na ukweli wake unafahamishwa na mafunzo yake. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawahadharisha makuraishi na kuwakumbusha maangamizi ya waliotangulia pale walipowakadhibisha mitume, kwa kusema:
Vizazi vingapi tumeviangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwishapita.
Wa mwanzo walijizuia na haki na kuwafanya watu wa haki ni mahasimu wao; sawa na mlivyofanya nyinyi. Walipojiwa na adhabu wakaanza kurudi nyuma na kunyenyekea, lakini muda ulikwishapita tena. Kwa hiyo bora muamini sasa kabla ya kupita muda mkajuta ambapo majuto hayatafaa kitu tena.
KUMWIGA MWENYE KUMPWEKESHA MUNGU NA KUMWIGA MSHIRIKINA
Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anayetokana na wao.
Muhammad(s.a.w. w ) ni Mkuraishi, hilo halina shaka, lakini si katika vigogo wala mataghuti wao, vipi awe ni miongoni mwao? Lau angelikuwa mion- goni mwao angewafanya watu watumwa wake na akawa na hazina au nyumba ya dhahabu. Tazama Juz. 15 (17: 90) kifungu cha ‘Kupenda mali’ na Juz. 18 (25:7) kifungu cha ‘Mantiki ya watu wa pesa ni benki na ardhi.’
Na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo.
Kwa nini ni muongo?
Jibu ni:
Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili kweli ni jambo la ajabu.
Ajabu kwa hawa sio kuwa Muhammad(s.a.w. w ) anapinga shirki na kuweko waungu wengi, ingawaje hilo wanaliwaza, lakini ajabu hasa ni Muhammad(s.a.w. w ) kutoka kwenye maigizo yao na mazowea yao waliyoyarithi tangu jadi na jadi. Wao hasa wanatetea kuiga kwa mababa na mababu zao kuwa ndio dini na msingi; sio kuwa wanatetea masanamu kwa kuwa ni masanamu. Wanatetea masanamu kwa vile ni turathi na urithi kutoka kwa wakale wao:
إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ ﴿٢٣﴾
“Kwa hakika tuliwakuta baba zetu juu ya mila na hakika sisi tunafuata nyayo zao.” (43:23).
Imani ya wajinga hawa ni sawa na imani ya washirikina, kwa sababu chimbuko la imani mbili ni moja nalo ni kuiga. Tofuati ni kuwa kumuiga mwenye kumpwekesha Mungu ni sahihi na kwenye kukubalika kwa sababu kuna msingi wa hali halisi; kama, kwa mfano, nikikuambia:
“Mwenye nadharia ya mvutano ni Newton na mwenye nadhariya ya uwiyano ni Einstein” Lakini kuiga kwa washirikina ni upotevu.
Na mwenye kuiga hivyo atabeba majukumu na atawajibishwa ila akiwa hana ajualo; kama mnyama. Kwa sababu kumshirikisha Mwenyezi Mungu hakuna msingi wowote kwake.
Kwa maneno mengine ni kuwa fikra itakuwa ni ya kweli ikiwa inatokana na uhalisi wa hali; iwe imetokana na elimu au kuiga. Tazama Juz.2 (2:168-170). Kifungu: ‘Kufuata na msingi wa itikadi.’
Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililopangwa. Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu.
Makusudio ya wakubwa wao ni vigogo wa kikuraishi. Kudumu kwenye miungu ni kudumu kuiabudu. Jambo lililopangwa ni kudumu kwenye ibada ya masanamu. Mila ya mwisho ni itikadi ya utatu ya kimasihi (kikiristo). Washirikina waliita ya mwisho kwa vile ndiyo dini ya mwisho kujitokeza wakati wao.
Kwenye Tafsir Tabariy na nyinginezo imeelezwa kuwa wazee wa kikuraishi walimwendea Abu Twalib na kumwambia: “Mwana wa nduguyo na aachane na miungu yetu nasi tutamwacha na Mungu wake anayemwabudu. Abu Twalib alipomwambia hilo Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) alisema:
“Ninawataka neno moja tu waliseme, basi waarabu na waajemi watawafuata.” Wakasema tutakukubalia hilo na mengine kumi, ni lipi hilo? Akasema: “Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu. (Lailaha illa llah)” wakaondoka zao huku wakisema: “Hivi miungu yote ameifanya kuwa mmoja!”
Riwaya hii inaafikiana na dhahiri ya Aya na inasaidiwa na hali halisi ya washirikina na nafasi ya mzee aliyelemewa.
Ati yeye ndiye aliyeteremshiwa mawaidha kati yetu?
Mwenyezi Mungu atamchagua vipi Muhammad na hali hana jaha wala mali?
Bali wao wana shaka na mawaidha yangu,
Wao ni washirikina. Kwa sababu miongoni mwao kuna waliompinga Muhammad(s.a.w. w ) kwa hasadi na wengine wakampinga kwa kulinda masilahi yao.
Bali hawajaionja adhabu yangu.
Wakishaionja shaka itawaondokea na “wataficha majuto” Juz. 11 (10:54).
Au wanazo wao hazina za rehema za Mola wako, Mwenye nguvu, Mpaji?
Makusudio ya hazina za rehema hapa ni utume tu, au utume na neema nyinginezo za Mwenyezi Mungu na hisani yake. Maana ni kuwa kwa nini washirikina wanalalamikia na kupinga rehema ya Mwenyezi Mungu ya kumchagua kwake kuwa mjumbe kwa walimwengu? Je ni kwa kuwa wao wanamiliki hiyari hii badala ya Mwenyezi Mungu?
Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake?
Mmliki wa ulimwengu ni yule anayemiliki utume, kuutoa na kumuenzi nao amtakye. Na washirikina hawamiliki chochote kwa Mwenyezi Mungu kuweza kumpa utume mtu mkubwa kati ya miji miwili.
Kuna jambo moja ambalo wanaweza kwalo kumiliki mbingu na ardhi nalo ni Basi nawazipande sababu zote.
Makusudio ya sababu ni njia na nyenzo. Maana ni kuwa utume anauhukumu ambaye anamiliki ulimwengu na viliomo ndani yake. Basi vigogo wa kikuraishi wakitaka kumchagua kwa utume yule wanayemtaka, kabla ya chochote nawamiliki nyenzo za kufikia kwenye umiliki huu ikiwa wanaweza. Changamoto hii ni ubainifu wa kutosha kabisa.
Ni jeshi litakaloshindwa miongoni mwa makundi yatayoshindwa.
Wale waliokupiga vita, ewe Muhammad, si chochote, watashindwa mbele ya mwito pamoja na wingi wa majeshi na vikosi vyao.
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ ذُو الْأَوْتَادِ ﴿١٢﴾
12. Walikadhibisha kabla yao kaumu ya Nuh, na kina A’adi na Firauni mwenye vigingi.
وَثَمُودُ وَقَوْمُ لُوطٍ وَأَصْحَابُ الْأَيْكَةِ أُولَـٰئِكَ الْأَحْزَابُ ﴿١٣﴾
13. Na Thamud na kaumu ya Lut na watu wa mwituni. Hayo ndiyo makundi.
إِن كُلٌّ إِلَّا كَذَّبَ الرُّسُلَ فَحَقَّ عِقَابِ ﴿١٤﴾
14. Wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahili adhabu yangu.
وَمَا يَنظُرُ هَـٰؤُلَاءِ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً مَّا لَهَا مِن فَوَاقٍ ﴿١٥﴾
15. Na hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio na muda.
وَقَالُوا رَبَّنَا عَجِّل لَّنَا قِطَّنَا قَبْلَ يَوْمِ الْحِسَابِ ﴿١٦﴾
16. Na wao husema: Mola wetu Tuletee upesi sehemu yetu kabla ya Siku ya Hisabu.
اصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَاذْكُرْ عَبْدَنَا دَاوُودَ ذَا الْأَيْدِ إِنَّهُ أَوَّابٌ ﴿١٧﴾
17. Subiri kwa wayasemayo, Na umkumbuke mja wetu Daud. Mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia.
إِنَّا سَخَّرْنَا الْجِبَالَ مَعَهُ يُسَبِّحْنَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِشْرَاقِ ﴿١٨﴾
18. Hakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi
وَالطَّيْرَ مَحْشُورَةً كُلٌّ لَّهُ أَوَّابٌ ﴿١٩﴾
19. Na pia ndege waliokusanywa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake.
وَشَدَدْنَا مُلْكَهُ وَآتَيْنَاهُ الْحِكْمَةَ وَفَصْلَ الْخِطَابِ ﴿٢٠﴾
20. Na tukautia nguvu ufalme wake. Na tukampa hikima na kukata hukumu.
SUBIRI JUU YA HAYO WANAYOSEMA
Aya 12 – 20
MAANA
Walikadhibisha kabla yao kaumu ya Nuh, na kina A’adi na Firauni mwenye vigingi Na Thamud na kaumu ya Lut na watu wa mwituni.
Wote hawa waliwakanusha mitume; baadhi yao wakaangamizwa kwa tufani; kama vile watu wa Nuh, wengine kwa kuzama baharini, kama Firauni.
Kuwa na vigingi ni kinaya cha kujikita ufalme wake kama linavyokitwa hema na vigingi kwenye ardhi.
“Basi Thamud waliangamizwa kwa balaa kubwa (la ukelele wa adhabu). Ama A’d waliangamizwa kwa upepo mkali usiozuilika” (69:5-6).
Kaumu ya Lut majumba yao yalipinduliwa juu chini. Tazama Juz. 12 (11:82). Watu wa mwituni Mwenyezi Mungu aliwaadhibu adhabu chungu. Tazama Juz.14 (15:78) na Juz. 19 (26:176).
Hayo ndiyo makundi. Wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahili adhabu yangu.
Mwenyezi Mungu aliviadhibu vikosi vya shetani kwa sababu ya madhambi yao; ikiwa ni malipo ya yale waliyoyafanya. Je, wanaomkadhibisha Muhammad(s.a.w.w) hawahofii kuwafika yaliyowafika hao.
Na hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio na muda.
Hawa ni waliomkadhibisha Muhammad(s.a.w.w) . Maana ni; wanangoja nini kwa Mungu baada ya kukukadhibisha ewe Muhammad na hali Mwenyezi Mungu, kwa neno moja tu anaweza kuwapelekea adhabu itayowafyeka katika muda ambao hawataweza kuusia wala kurudi kwa watu wao.
Na wao husema: Mola wetu! Tuletee upesi sehemu yetu kabla ya Siku ya Hisabu.
Yaani sehemu yetu ya adhabu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwatishia na adhabu ya Jahannam kupitia kwa Mtume wake mtukufu, lakini wao wakasema kwa madharau kuwa ikiwa ni kweli basi anangoja nini mpaka siku ya Kiyama? Basi na iwe duniani sio akhera.
Subiri kwa wayasemayo, kuwa wewe ni mwongo na mengineyo ya uzushi. Kwani mwisho wa mambo yao ni hasara na kusalimu amri.
Mtume(s.a.w.w) alisubiri na kuvumilia adha ya washirikina kwa muda wa mika 13 na vitimbi vya wanafiki kwa miaka kadhaa huko Madina. Alivumilia muda huu mrefu akiwa na mategemeo ya mustkabali hata kama utachelewa. Hazikupita siku Muhammad(s.a.w.w) akashinda kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, na akaudhihirisha uislamu kuliko dini zote, wajapochukia washirikina.
Na umkumbuke mja wetu Daud.
Hili ni jina la kiebrania lenye maana ya mpendwa (mahboob). Yeye alikuwa mfalme wa pili wa Kiyahudi, wa kwanza alikuwa Talut:
إِنَّ اللَّـهَ قَدْ بَعَثَ لَكُمْ طَالُوتَ مَلِكًا ﴿٢٤٧﴾
“Hakika Mwenyezi Mungu amewachagulia Talut kuwa mfalme.” Juz. 2 (2:247).
Tawrat imemwita Talut huyu kwa jina la Shaul (Saulo). Imeelezwa kwenye Kamusi ya Kitabu kitakatifu’ kwamba Shaul ndiye mfalme wa kwanza wa waisrail na kwamba Daud alipigana katika jeshi lake. Razi anasema kuwa Mwenyezi Mungu amemsifu Daud kwa sifa nyingi. Kisha akazifafanua kwenye kurasa nne. Tutazifupiliza kwenye mistari ifuatayo: Mwenyezi Mungu alimwambia Muhammad(s.a.w.w) :
Subiri kwa wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daud.
Hii ni karama kwa Daud.
Mwenye nguvu; yaani mwenye nguvu ya kumtii Mwenyezi Mungu.
Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia; yaani akiyarudisha mambo yote kwa Mwenyezi Mungu.
Hakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi pamoja naye. Na pia ndege waliokusanywa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake.
Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
يَا جِبَالُ أَوِّبِي مَعَهُ وَالطَّيْرَ ﴿١٠﴾
“Enyi milima sabihini pamoja naye na ndege” Juz. 22 (34:10).
وَسَخَّرْنَا مَعَ دَاوُودَ الْجِبَالَ يُسَبِّحْنَ وَالطَّيْرَ ﴿٧٩﴾
“Na tuliidhalilisha milima na ndege pamoja na Daud ikisabihi.” Juz. 17: (21:79).
Kwa maelezo zaid kuhusu Daud rejea huko.
Na tukautia nguvu ufalme wake.
Na tukampa hikima.
Ambayo ni kukiweka kitu mahali pake. Kwa ibara ya Razi ni elimu na kuitumia. Imeitwa hivyo kwa sababu hekima ni kupanga mambo na kuyaweka sawa.
Na kukata hukumu.
Razi anasema ni uwezo wa kudhibiti maana na kuyatolea tafsiri ya upeo wa juu. Hivi ni zaidi ya tunavyofahamu kuwa kukata hukumu ni elimu ya kuhukumu, kwa uadilifu, mambo ya wanaoteta.
Hivi ndivyo Qur’an ilivyomsifu Daud kwa sifa bora za ukamilifu, lakini Tawrat imemsifu kwa sifa mbaya mbaya; kama dhulma, ufuska, hadaa na kunyanyag’anya wanawake; kiasi amabacho waliochangia kuweka kamusi ya Kitabu Kitakatifu wakasema katika ukurasa 365, chapa ya mwezi Machi 1967, ninanukuu: “Mara nyingine Daud aliweza kufanya mambo ya kufedhehesha na ya aibu.”
23
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
وَهَلْ أَتَاكَ نَبَأُ الْخَصْمِ إِذْ تَسَوَّرُوا الْمِحْرَابَ ﴿٢١﴾
21. Na je, imekufikia habari ya wagombanao walipopindukia ukuta kuingia mihrabu.
إِذْ دَخَلُوا عَلَىٰ دَاوُودَ فَفَزِعَ مِنْهُمْ قَالُوا لَا تَخَفْ خَصْمَانِ بَغَىٰ بَعْضُنَا عَلَىٰ بَعْضٍ فَاحْكُم بَيْنَنَا بِالْحَقِّ وَلَا تُشْطِطْ وَاهْدِنَا إِلَىٰ سَوَاءِ الصِّرَاطِ ﴿٢٢﴾
22. Walipomuingilia Daudi, naye akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Ni mahasimu wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala usipendelee. Na utuongoze kwenye njia iliyo sawa.
إِنَّ هَـٰذَا أَخِي لَهُ تِسْعٌ وَتِسْعُونَ نَعْجَةً وَلِيَ نَعْجَةٌ وَاحِدَةٌ فَقَالَ أَكْفِلْنِيهَا وَعَزَّنِي فِي الْخِطَابِ ﴿٢٣﴾
23. Hakika huyu ndugu yangu ana kondoo wa kike tisini na tisa; na mimi nina kondoo mke mmoja. Akasema: Nipe huyo! Na amenishinda kwa maneno.
قَالَ لَقَدْ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعْجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْخُلَطَاءِ لَيَبْغِي بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَقَلِيلٌ مَّا هُمْ وَظَنَّ دَاوُودُ أَنَّمَا فَتَنَّاهُ فَاسْتَغْفَرَ رَبَّهُ وَخَرَّ رَاكِعًا وَأَنَابَ ﴿٢٤﴾
24. Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao. Isipokuwa walioamini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daud akaona kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba maghufira Mola wake na akaanguka kunyenyekea na kutubia.
فَغَفَرْنَا لَهُ ذَٰلِكَ وَإِنَّ لَهُ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَآبٍ ﴿٢٥﴾
25. Basi tukamghufiria kwa hayo. Naye kwa hakika anao ukuruba na marejeo mazuri kwetu.
KONDOO 99 KWA KONDOO 1
Aya 21 – 25
TAFSIRI NA HADITH ZA KIISRAIL
Baadhi ya wafasiri, wakifafanua Aya hii, wamemnasibishia Nabii Daud mambo ambayo si laiki hata ya mtu wa kawaida mwenye murua na haya; sikwambii tena mtume aliye maasumu. Wakataja kisa kirefu kutoka katika Biblia kitabu cha 2 Samweli: 11 na 12, kutoka agano la kale ambalo mahala pake pamechukuliwa na hukumu ya Qur’an. Nukuu za agano lenyewe kuhusiana na hilo haziingiliki akili.
Muhtasari wa kisa chenyewe ni kuwa Daud alimtamani mke wa mmoja wa watumishi wake aliye pia mwanajeshi wake. Basi akamfanyia hila ya kumuua ili amchukue mkewe. Biblia inasema kuwa Mwenyezi Mungu alikasirika sana na kumkemea kwa kitendo kibaya alichokifanya; miongoni mwa aliyoyasema ni “…Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe ukamtwaa mkewe awe wako… Basi sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau…Nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili. Maana wewe ulifanya jambo hili kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israil wote na mbele ya jua” (2 Samweli 12:9-12.).
Katika 1 Wafalme 1 imeelezwa kuwa jina la mke wa Uria ni Bath-sheba naye ndiye mama yake Suleiman bin Daud.
Daud azini kwa siri na Mwenyezi Mungu, badala ya kumpa adhabu ya hadd ya zina au kumlaumu na kumtaka atubie, badala ya kumfanyia hivyo, anamtia adabu kwa kuwavunjia heshima wakeze wawe uchi na wafanye machafu hadharani kweupe mchana kadmanasi!
Haya ndio maandiko matakatifu yanavyomsifu muumba kwa sifa za unyama. Mwenyezi Mungu Mtukufu ametakata kabisa na hayo wanayomsifu nayo. Huu ni mfano mmoja kati ya mifano kadhaa. Soma kuhusu kupigana miereka Mwenyezi Mungu na Ya’qub na kushindikana kupatikana mshindi, mpaka Ya’qub akalazimika kupiga mfupa wa paja wa Mwenyezi Mungu.
Vile vile soma yaliyoandikwa kwenye biblia, Kumbukumbu la Torat, 7, kwamba Mungu amewahalalishia Mayahudi kula mataifa yote, bila ya huruma. Baadhi ya wafasiri wametegemea Hadith hizi za kiisrail, katika kufasiri Aya za Qur’an yenye mawaidha, biashara na maonyo; ikiwemo hii tuliyo nayo. Kwa hiyo ni juu ya msomaji kuzikabili kauli zao na tafsiri zao kwa jicho la hadhari sana.
MAANA
Na je, imekufikia habari ya wagombanao walipopindukia ukuta kuingia mihrabu. Walipomuingilia Daudi, naye akawaogopa.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamsilmulia Nabii wake mtukufu kisa cha Daud, kwamba siku moja Daud alipokuwa amemwelekea Mola wake kwenye mswala wake, ghafla watu wawili wakajitokeza mbele yake ana kwa ana. Basi kushtukiza huku kulimshtua; tena kuingia kwao kwa njia isiyokuwa ya kawaida.
Hata hivyo kuingia kwao huko, kusikokuwa kwa kawaida, hakufahamishi lolote kuwa ni malaika; kama walivyolitolea dalili baadhi ya wafasiri. Kwa sababu hata binadamu pia anaweza kuingia nyumbani kwa njia isiyokuwa ya kawaida kutokana na sababu fulani. Pia Aya haikuashiria kuwa ni malai- ka. Kwa hiyo hakuna sababu ya kuleta taawili ya kuwa ni malaika.
Wakasema: Usiogope! Ni mahasimu wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala usipendelee. Na utuon- goze kwenye njia iliyo sawa.
Walipoona hofu iliyomjaa, haraka sana wakamtuliza na kusema, sisi tumekuja kwako kuhukumiwa, basi utuhukumu kwa uadilifu na utuongoze kwenye haki wala usikengeuke nayo. Kisha mmoja wao akasema:
Hakika huyu ndugu yangu ana kondoo wa kike tisini na tisa; na mimi nina kondoo mke mmoja. Akasema: Nipe huyo! Na amenishinda kwa maneno.
Hapa hakuna haja yoyote ya kuleta taawili. Dhahiri ya Aya inaonyesha kuwa tukio hili lilitokea wakati wa zama za Nabii Daud; nalo lina mfano wake katika kila zama na kila wakati; hasa wakati wetu huu wa sasa. Kwa hiyo ni wajibu kuichukulia dhahiri yake na kuitumia.
Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake.
Daud aliyasema haya kabla ya kusikiliza ushahidi kutoka kwa mdai na kujibu mdaiwa.
Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao.
Hapa itabidi kuchukulia majazi neno washirikia, kuwa na maana ya wenye mabavu. Kwa sababu hakukua na ushirika wowote kati ya wale mahasimu wawili.
Isipokuwa walioamini na wakatenda mema. Na hao ni wachache.
Nguvu inakuwa ni ya haki ikiwa kwa watu wema, lakini ikiwa kwa waovu basi, bila shaka yoyote, itakuwa dhidi ya haki. Na watu wema ni wachache kwa idadi, lakini wana nguvu katika maadili yao na sifa zao.
Na Daud akaona kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba maghufira Mola wake na akaanguka kunyenyekea na kutubia
Baada ya Daud kutoa hukumu, alitanabahi kuwa amehukumu kabla ya kutaka dalili upande wa pili. Kwa hiyo akajuta na akamuomba msamaha Mwenyezi Mungu.
Basi tukamghufiria kwa hayo. Naye kwa hakika anao ukuruba na marejeo mazuri kwetu.
Mwenyezi Mungu alimsamehe Daud kwa vile alikuwa ni miongoni mwa waliotangulia kumtii Mwenyezi Mungu na kutaka radhi yake.
Katika kitabu Uyunil-akhbar, imeelezwa kuwa mtu mmoja alimuuliza Imam Ar-Ridha(a.s ) kuhusu kisa cha Daud na Uria na mkewe, Imam akapinga yanayonasibishiwa Daud. Muulizaji akauliza: Kosa lake lilikuwa nini ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu? Basi akajibu kwa jawabu refu, miongoni mwake ni: “Daud alifanya haraka kusema: “Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake,” bila ya kumuuliza yule mwingine unasemaje? Basi hilo likuwa ni kosa la rasimu ya mahakama, sio kosa la wanavyosema watu.
Kwani hukusikia Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyomwambia Daud: “Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya uwe Khalifa ardhini.”
Unaweza kuuliza : Vipi Daud alihukumu bila ya ushahidi, na tunajua kuwa mitume wamehifadhiwa na makosa (ni maasumu).
Jibu : kuwa maasumu hakumaanishi kuwa na maumbile mengine yasiyokuwa ya kibinadamu, hapana! Maasumu ni mtu kama watu wengine. Maana ya isma ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamlinda wakati wowote; hata wakijaribu watu kumhadaa kwa mandhari ya uzuri, basi Mwenyezi Mungu mara moja humwongoza kwenye haki na uhakika, kabla ya kuiingia mtegoni. Na hivyo ndivyo ilivyomtokea Daud. Mwenye kondoo mmoja alijaribu kumhadaa kwa namna yake ya kutaka kuhurumiwa, lakini Mwenyezi Mungu alimpa ilhamu ya uhakika kabla ya kutoa hukumu, akafahamu na akatubia.
Mtume alitokewa na yaliyo karibu na haya na akakurubia kuhadaiwa lau si Mwenyezi Mungu kumwimarisha kwa kumwambia: “Hakika tumekuteremshia Kitabu kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kwa alivyokufahamisha Mwenyezi Mungu; wala usiwe mtetezi wa wenye kufanya hiyana. Na muombe maghufira Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu. Wala usiwatetee wale ambao wamezihini nafsi zao...” Juz. 5 (4:105 – 107).
Na akasema Mwenyezi Mungu kumwambia Mtume wake Mtukukufu:
وَلَوْلَا أَن ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًا ﴿٧٤﴾
“Lau sikukuweka imara ungelikurubia kuwaelekea kidogo.” Juz. 15 (17:74).
Kuna Hadith isemayo: “Mimi ni mtu kama nyinyi, isipokuwa ninapewa wahyi tu. Na nyinyi mnakuja kuamuliwa kwangu. Pengine mmoja wenu anaweza kuwa hodari wa kusema kuliko mwingine na nikahukumu kulingana na nilivyosikia.
Ikiwa mtu nitamuhukumia kumpatia kitu katika haki ya ndugu yake, basi ajue ninampatia kipande cha Moto.”
Ingawaje Hadith hii haingii moja kwa moja kwenye maudhui haya tuliyo nayo, lakini tunaweza kuiunganisha nayo. Ama toba ya manabii na kutaka kwao maghufira ya dhambi, hiyo ni aina ya ibada na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Hilo tumeliashiria mara kadhaa.
يَا دَاوُودُ إِنَّا جَعَلْنَاكَ خَلِيفَةً فِي الْأَرْضِ فَاحْكُم بَيْنَ النَّاسِ بِالْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعِ الْهَوَىٰ فَيُضِلَّكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ إِنَّ الَّذِينَ يَضِلُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا نَسُوا يَوْمَ الْحِسَابِ ﴿٢٦﴾
26. Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya uwe Khalifa ardhini. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio, yakakupoteza Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanaopotea Njia ya Mwenyezi Mungu, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا بَاطِلًا ذَٰلِكَ ظَنُّ الَّذِينَ كَفَرُوا فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِنَ النَّارِ ﴿٢٧﴾
27. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake bure. Hiyo ni dhana ya waliokufuru. Ole wao walio kufuru kwa Moto.
أَمْ نَجْعَلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَالْمُفْسِدِينَ فِي الْأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ الْمُتَّقِينَ كَالْفُجَّارِ ﴿٢٨﴾
28. Je! Tuwafanye walioamini na wakatenda mema kama wafisadi katika ardhi? Au tuwafanye wenye takua kama waovu?
كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٩﴾
29. Hiki ni Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.
TUMEKUFANYA UWE KHALIFA ARDHINI
Aya 26 – 29
MAANA
Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya uwe Khalifa ardhini.
Kila mtu aliyeko, au atakayekuweko, ardhini basi huyo ni khalifa wa Mwenyezi Mungu ardhini; kwa maana yakuwa ana majukumu mbele ya Mwenyezi Mungu ya kufanya mambo ya heri duniani na Akhera katika maisha haya.
Hayo ndio maana ya ukhalifa ardhini kwa hali yoyote ile; isipokuwa watu wanatofautiana kulingana na majukumu yenyewe; ambapo kila mmoja anatakiwa atekeleze kulingana na uwezo na wadhifa wake.
Kwa kuwa wadhifa wa manabii ni kutoa bishara na hadhari, ili watu wasiwe na hoja mbele ya Mwenyezi Mungu, basi imekuwa ni wajibu kwao kuwahukumu watu kwa haki na wengine wawasikilize wao.
Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio, kwa sababu unabii uko hivyo kimaumbile.
Kwa maneno mengine ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamchagulia wahyi wake yule anayeiamini haki na kuitumia na inakuwa ni muhali kwake kukosea.
Yakakupoteza Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanaopotea Njia ya Mwenyezi Mungu, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.
Muovu zaidi katika watu ni yule mwenye kumhalifu Mola wake na akafuata matamanio yake. Kuna Hadith isemayo: “Hakika ninalolihofia zaidi kwenu ni hawaa na tamaa nyingi. Hawaa inaipinga haki na tamaa nyingi inasahauliza akhera.”
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo kati yake bure.
Lau katika kuumbwa mbingu na ardhi kungelikua na chembe ya mchezo au hivi hivi tu, basi ulimwengu usingeendelea na nidhamu kwa mamilioni ya miaka.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (3:191).
Hiyo ni dhana ya waliokufuru. Ole wao waliokufuru kwa Moto.
Hiyo inaashiria kuwa hakuna tofauti kati ya aneyepinga kuweko Mwenyezi Mungu kabisa na yule anayekubali, lakini akapinga kuweko hekima katika kuumba kwake. Kwa sababu dalili zake ni wazi na alama zake ziko kweupe.
Imam Ali(a.s ) anasema:“Amekadiria aliyoumba akapangilia makadirio yake; akapangilia akafanya kwa uangalifu mipangilio yake; akaelekeza kwa maelekezo yake, lakini hakupetuka mpaka wa cheo chake wala hakupunguza ukomo wa lengo lake.”
Je! Tuwafanye walioamini na wakatenda mema kama wafisadi katika ardhi? Au tuwafanye wenye takua kama waovu?
Tofauti baina ya mwema na mfisadi na baina ya mwenye takua na muovu ni sawa na tofauti baina ya kipofu na mwenye kuona. Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (5:100) na Juz. 7 (6:50).
Katika kitabu Ahkamul-qur’an cha Kadhi Abi Bakri, ambaye ni maarufu kwa jina la Ibnul-arabiy, amesema: “Aya hii iliwashukia bani Hashim; na kwamba walioamini na kuwa na takua ni Ali bin Abi Twalib, ndugu yake Ja’far, Ubayda bin Tufayl, Al-harth bin Tufayl, Ummu ayman na wengineo, na kwamba wafisadi na waovu ni Bani Abd Shams.
Hiki ni Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.
Hapa anaambiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) . Kitabu ni Qur’an, nayo ina baraka kwa kila mwenye kuiamini, ni dawa ya ukafiri na hulka mbaya na ni uokovu wa shirki na maangamizi. Kwenye Nahjul-Balagha imeelezwa:“Itakeni nasaha kwa nafsi zenu na mzituhumu rai zenu kwayo na mtake uokofu wa hawa zenu ndani yake.”
24
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
وَوَهَبْنَا لِدَاوُودَ سُلَيْمَانَ نِعْمَ الْعَبْدُ إِنَّهُ أَوَّابٌ ﴿٣٠﴾
30. Na Daudi tukamtunukia Suleiman, mbora wa waja. Kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu.
إِذْ عُرِضَ عَلَيْهِ بِالْعَشِيِّ الصَّافِنَاتُ الْجِيَادُ ﴿٣١﴾
31. Alipopelekewa jioni farasi wasimamao kidete, wepesi wakimbiapo.
فَقَالَ إِنِّي أَحْبَبْتُ حُبَّ الْخَيْرِ عَن ذِكْرِ رَبِّي حَتَّىٰ تَوَارَتْ بِالْحِجَابِ ﴿٣٢﴾
32. Basi akasema: Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu. Kisha wakafichikana nyuma ya boma.
رُدُّوهَا عَلَيَّ فَطَفِقَ مَسْحًا بِالسُّوقِ وَالْأَعْنَاقِ ﴿٣٣﴾
33. Nirudishieni! Akaanza kuwapapasa miguu na shingo.
وَلَقَدْ فَتَنَّا سُلَيْمَانَ وَأَلْقَيْنَا عَلَىٰ كُرْسِيِّهِ جَسَدًا ثُمَّ أَنَابَ ﴿٣٤﴾
34. Na tulimtia kwenye mtihani Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake. Kisha akarejea kwa kutubu.
قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَهَبْ لِي مُلْكًا لَّا يَنبَغِي لِأَحَدٍ مِّن بَعْدِي إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٣٥﴾
35. Akasema: Mola wangu! Nighufuirie. Na unipe ufalme usiomwelekea yeyote baada yangu. Hakika wewe ndiye mwingi wa kupa.
فَسَخَّرْنَا لَهُ الرِّيحَ تَجْرِي بِأَمْرِهِ رُخَاءً حَيْثُ أَصَابَ ﴿٣٦﴾
36. Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukienda kwa amri yake, popote alipotaka kufika.
وَالشَّيَاطِينَ كُلَّ بَنَّاءٍ وَغَوَّاصٍ ﴿٣٧﴾
37. Na mashetani, wote wajenzi na wapiga mbizi.
وَآخَرِينَ مُقَرَّنِينَ فِي الْأَصْفَادِ ﴿٣٨﴾
38. Na wengine wafungwao kwa minyororo.
هَـٰذَا عَطَاؤُنَا فَامْنُنْ أَوْ أَمْسِكْ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٩﴾
39. Huku ndiko kutoa kwetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu.
وَإِنَّ لَهُ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَآبٍ ﴿٤٠﴾
40. Naye kwa hakika anao ukuruba na marejeo mazuri kwetu.
SULEIMAN
Aya 30 – 40
MAANA
Na Daudi tukamtunukia Suleiman, mbora wa waja. Kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu.
Katika Kamusi ya Kitabu kitakatifu kumeandikwa kuhusu Suleiman: “Suleiman ni jina la Ibrania na maana yake ni mtu wa amani. Ni mtoto wa mfalme Daud aliyerithi kiti chake cha ufalme, ingawaje alikuwa na ndugu zake wengine sita wa mama mbalimbali. Suleiman ni mtoto wa Bath-sheba aliyekuwa mke wa Uria. Daud alimpenda sana Suleiman kwa vile alikuwa ni mtoto wa mkewe anayempenda zaidi. Na Daud alimwahidi Bath-sheba kuwa atakuwa mfalme baada yake.”
Wameeleza kwa muhtasari hao waliochangia kuweka Kamusi hiyo kutoka kwenye Biblia kitabu cha Wafalme 1 na Samweli 2. Maana yake ni kuwa Tawrat inamuelezea Daud kuwa hafuati amri ya Mwenyezi Mungu wala kutumia wahyi wake, isipokuwa anafuata wahyi wa mwanamke aliyempora kwa mumewe aliyemuua kwa upanga mkali.
Na kwamba yeye mwanamke ndiye muamrishaji na mkatazaji kwake yeye Suleiman na kwa wananchi wake. Ikiwa leo mwanamke anatafuta usawa na mwanamume, basi Tawrat inawafanya wafalme na watawala ni watiifu wa hawaa za wanawake na matamanio yao. Hayo si ajabu, kwani hadi leo jinsia hiyo ndio nyenzo bora ya mayahudi ya kupata faida na kufikia matakwa yao.
Alipopelekewa jioni farasi wasimamao kidete, wepesi wakimbiapo Basi akasema: Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu. Kisha wakafichikana nyuma ya boma: Nirudishieni! Akaanza kuwapapasa miguu na shingo.
Wafasiri hapa wana kauli nyingi. Yenye nguvu zaidi ni ile isemayo kwamba siku moja wakati wa jioni alitaka aonyeshwe farasi wa maandalizi ya vita. Siku hizo ilikuwa ndio silaha ya kumtisha adui.
Kwa maneno mengine ni kuwa alitaka aone gwaride la askari, na akaamrisha kuletwa farasi mbele ya macho yake na akasema haya ninayafanya kwa amri ya Mola wangu sio kwa mapendeleo ya nafsi yangu. Mpaka walipopita akawafurahia. Walipopotea machoni mwake aliaamrisha warudishwe; akawa anawapapasa miguuni na shingoni akiwafurahia na kuwaridhia.
Kwa hiyo makusudio ya kupenda vitu vizuri ni kule kuonyeshwa farasi na kupita machoni kwake. Ama kusema kwake “Kwa kumkubuka Mola wangu,” maana yake ni kuwa ninayafanya haya kwa amri ya Mola wangu sio kwa amri yangu.
Na tulimtia kwenye mtihani Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimpa mtihani Suleiman wa maradhi sugu na akamweka kitandani kama mwili bila roho; sawa na walivyojaribiwa manabii wengineo kwa aina ya majaribu.
Aya inaashiria kwamba mtihani huo ulikuwa ni malipo ya jambo fulani lililomtokea Suleiman, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakulibainisha jambo hilo. Waliyoyataja wafasiri kubainisha jambo hilo hayana msingi wowote. Vyovyote iwavyo ni kuwa Suleiman alitubia kutokana na yaliyotokea; kama walivyotubia manabii wengine na akamtakabalia toba yake kama alivyowatakabalia manabii wengine.
Kisha akarejea kwa kutubu, akasema: Mola wangu! Nighufuirie.
Ilivyo hasa ni kuwa manabii wanatubia kwa kuacha yaliyo bora si kwa kuwa wamefanya maasi. Hayo tumeyabainisha katika Juz. 1 (2:35-39) kifungu cha Isma.
Na unipe ufalme usiomwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye mwingi wa kupa.
Alitaka ufalme wa aina yake kiaina si kiwingi; na kwa aina yake ya muujiza; kama vile kuutumikisha upepo, ndege na majini. Basi Mwenyezi Mungu akamwitikia dua yake kwa ushahidi wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukienda kwa amri yake, popote alipotaka kufika.
na mashetani, wote wajenzi wakijenga anavyotaka Suleiman; kama vile mihirabu n.k.Na wapiga mbizi baharini wakitafuta lulu na johariNa wengine katika mashetaniwafungwao kwa minyororo kwa vile walitoka kwenye amri yake na utii wake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 22 (34: 12-13).
Huku ndiko kutoa kwetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu. Naye kwa hakika anao ukuruba na marejeo mazuri kwetu.
Na kutoa kwa Mwenyezi Mungu hakupunguzi kinachotolewa. Ndio maana Mwenyezi Mungu alimwamrisha Suleiman kutoa kwa ujumla bila ya kipimo akitaka.
Katika Nahjul-Balagha kumeandikwa: “Mwenye uhakika wa kurudishiwa vizuri huwa mkarimu wa kutoa.” Pamoja na hayo lakini Suleiman ni kiumbe dhaifu, kama binadamu wengine: “Anaumizwa na chawa, hufa kwa kusongwa koo na jasho humfanya anuke.”
وَاذْكُرْ عَبْدَنَا أَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ أَنِّي مَسَّنِيَ الشَّيْطَانُ بِنُصْبٍ وَعَذَابٍ ﴿٤١﴾
41. Na mkumbuke mja wetu Ayyub. Alipomwita Mola wake akasema: Kwa hakika Shetani amenifikishia tabu na adhabu.
ارْكُضْ بِرِجْلِكَ هَـٰذَا مُغْتَسَلٌ بَارِدٌ وَشَرَابٌ ﴿٤٢﴾
42. Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Hapa mahali baridi pa kuogea na kinywaji.
وَوَهَبْنَا لَهُ أَهْلَهُ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنَّا وَذِكْرَىٰ لِأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿٤٣﴾
43. Na tukampa ahali zake na wengine kama wao pamoja nao, kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho kwa watu wenye akili.
وَخُذْ بِيَدِكَ ضِغْثًا فَاضْرِب بِّهِ وَلَا تَحْنَثْ إِنَّا وَجَدْنَاهُ صَابِرًا نِّعْمَ الْعَبْدُ إِنَّهُ أَوَّابٌ ﴿٤٤﴾
44. Na shika kitita cha vijiti mkononi mwako, kisha ndio upige kwacho, wala usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu.
وَاذْكُرْ عِبَادَنَا إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ أُولِي الْأَيْدِي وَالْأَبْصَارِ ﴿٤٥﴾
45. Na wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Ya’qub waliokuwa na nguvu na busara.
إِنَّا أَخْلَصْنَاهُم بِخَالِصَةٍ ذِكْرَى الدَّارِ ﴿٤٦﴾
46. Sisi tumewahusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa makao;
وَإِنَّهُمْ عِندَنَا لَمِنَ الْمُصْطَفَيْنَ الْأَخْيَارِ ﴿٤٧﴾
47. Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora.
وَاذْكُرْ إِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَذَا الْكِفْلِ وَكُلٌّ مِّنَ الْأَخْيَارِ ﴿٤٨﴾
48. Na mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhulkifl, na wote hao ni katika walio bora.
AYYUB
Aya 41 – 48
MAANA
Na mkumbuke mja wetu Ayyub.
Ayyub ana kitabu maalum katika Biblia kwenye agano la kale. Zimetumika karibu kurasa arubaini. Kwenye kamusi ya Kitabu kitakatifu imeandikwa kuwa kitabu hicho cha Ayyub mwanzo kiliandikwa kwa mashairi na kwamba baadhi wanaona kuwa kiliandikwa karne ya nne kabla ya Milad (Bc). Na kuna uwezekano kuwa aliishi milenia ya pili kabla ya Milad (Bc). Kisha wakasema waliochangia kuweka Kamusi ya Kitabu kitakatifu kuwa Ayyub aliishi katika nchi ya Usi. Inaaminika kuwa nchi hii iko katika jang- wa la Syria na wengine wanaamini ni Huran.
Alipomwita Mola wake akasema: Kwa hakika Shetani amenifikishia tabu na adhabu.
Watu wamekua wakipiga mfano wa masaibu ya Ayyub katika karne nyingi zilizopita, huku wakiongeza vigano vingi. Aya hii na ile iliyo katika Juz. 17 (21: 83), zinafahamisha kuwa Ayyub alipata masaibu ya hali na mali na kwamba yeye aliyanasabishia yaliyomfika kwa shetani. Hii ndio iliyowafanya jamaa katika wafasiri kutunga riwaya ya ‘Ayyub na shetani.’
Ukiunganisha riwaya zao na yale yaliyoelezwa kwenye Biblia utaona kuwa wao wanaifasiri Qur’an kwa Hadith za kiisrail.
Kwa ufupi ni kuwa Biblia na baadhi ya wafasiri wanasema kuwa Mwenyezi Mungu alimsalitia Ayyub shetani ili amjaribu imani yake. Akaangamiza mali yake na familia yake. Aliposhindwa akauingilia mwili, lakini pia akashindwa.
Ni kweli Aya inaelezea kuwa shetani alimpa Ayyub tabu na mashaka, laki- ni haikusema ni tabu na adhabu ya aina gani? Nasi tunayanyamazia yale aliyoyanyamazia Mwenyezi Mungu, wala hatujikalifishi kuyafanyia utafiti. Lau Mwenyezi Mungu angelitukalifisha angelibainisha. Na kwa kuwa hakuna ubainifu basi hakuna taklifa. Tumeashiria kisa cha Ayyub katika Juz. 17 (21:83 – 91).
Akaambiwa: Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Hapa mahali baridi pa kuogea na kinywaji.
Makusudio ya mahali pa kuogea hapa ni maji. Ayyub alikimbila kwa Mwenyezi Mungu kumshtakia yaliyomfika. Mwenyezi Mungu akamwitikia na akamwamrisha apige ardhi kwa mguu wake, yatatoka maji baridi ya kuoga na kunywa, atapona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Na tukampa ahali zake na wengine kama wao pamoja nao, kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho kwa watu wenye akili.
Mwenyezi Mungu alimponyesha na kumruzuku watoto na wajukuu zaidi ya aliowakosa. Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 (21:83 – 91).
Na shika kitita cha vijiti mkononi mwako, kisha ndio upige kwacho, wala usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu.
Wafasiri wamesema kuwa Ayyub alipokuwa kitandani aliwahi kumkasirikia mkewe kwa jambo lililozuka baina yake na yeye. Akaapa kumpiga, mara kadha, akipona. Mwenyezi Mungu alipompa shafaa, alimwamrisha achukue vijiti kadhaa ampige navyo mara moja tu. Hapo kiapo chake kitakuwa kimefunguka.
Aya haiashiri hilo kwa mbali wala karibu, lakini pamoja na hayo hatupingi kauli ya wafasiri. Kwa sababu kwenye Aya kumetajwa kiapo na kupiga. Kukiweko kupiga, lazima kuwe na kilichopigwa. Mtu akiwa hoi kitandani huwa anaona dhiki hata kwa mambo madogo; hasa yakitokea kwa watu wake mwenyewe. Kwa hiyo basi kauli ya wafasiri haiko mbali.
Unaweza kuuliza : kauli yake Mwenyezi Mungu: Na shika kitita cha vijiti…inafahamisha kuwa inafaa kufanya hila na ujanja katika sharia ya Qur’an na inajulikana kuwa Bani israil walikatazwa kufanya hila ya kuvua Jumamosi, kama ilivyobainisha Aya isemayo: “Na waulize habari za mji uliokuwa kando ya bahari walipokuwa wakivunja Sabato, samaki wao walipowajia juu juu siku ya Sabato na siku wasiyofanya Sabato hawakuwajia. Kama hivyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya ufuska. Juz. 9 (7:163).
Jibu : kwanza aina hii inahusiana na Ayyub tu peke yake wala haienei kwa wengine wanaoapa; vinginevyo suna za Mtume zingeliweka wazi hilo na ulama wote wangelilitolea fatwa. Pili: Hila hii ni kwa ajili ya huruma ya kibinadamu sio kuifanyia hila haki na ubinadamu.
Na wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Ya’qub waliokuwa na nguvu na busara.
Wenye nguvu ni nguvu za matendo mema, na busara ni kinaya cha kumjua Mwenyezi Mungu na dini yake. Maana ni kuwa wakumbuke ewe Muhammad manabii walioijua dini ya Mwenyezi Mungu,wakaitumia kwa ikhlasi na wakafanya jihadi katika njia yake wakiwa na subira. Wakumbuke na uwe na subira kwa wanaokukadhibisha katika watu wako; kama walivyokuwa na subira mitume wengine.
Sisi tumewahusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa makao; yaani makao ya Akhera.
Neno sifa limefasiriwa kutokana na neno Khaliswa lenye maana ya sifa safi kabisa isiyo na doa; nayo ni kuwa wao wanafanya kwa ajili ya akhera na wameathirika na kila kitu.
Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora.
Walimfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu akawahusisha na risala yake, na akawafanya ni katika bora ya viumbe wake.
Na mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhulkifl, na wote hao ni katika walio bora.
Sikupata katika faharasa ya Kamusi ya Kitabu kitakatifu kutajwa Alyasaa na Dhulkifil. Nililolikuta ni jina la la Yashuu bin Nun, khalifa wa Musa. Inasemekana kuwa ndiye Alyasaa. Vyovyote iwavyo, yeye na Dhulkifl ni kama Ismail, Is-haq na Ya’qub katika manabii wateuliwa.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:85) na Juz. 17 (21:83 – 91).
25
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
هَـٰذَا ذِكْرٌ وَإِنَّ لِلْمُتَّقِينَ لَحُسْنَ مَآبٍ ﴿٤٩﴾
49. Huu ni ukumbusho. Na hakika wenye takua wana marudio mazuri.
جَنَّاتِ عَدْنٍ مُّفَتَّحَةً لَّهُمُ الْأَبْوَابُ ﴿٥٠﴾
50. Bustani za milele zitazofunguliwa milango kwa ajili yao.
مُتَّكِئِينَ فِيهَا يَدْعُونَ فِيهَا بِفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ وَشَرَابٍ ﴿٥١﴾
51. Humo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji.
وَعِندَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ أَتْرَابٌ ﴿٥٢﴾
52. Na pamoja nao wapo wenye kutuliza macho, walio marika.
هَـٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِيَوْمِ الْحِسَابِ ﴿٥٣﴾
53. Haya ndiyo mliyoahidiwa kwa Siku ya Hisabu.
إِنَّ هَـٰذَا لَرِزْقُنَا مَا لَهُ مِن نَّفَادٍ ﴿٥٤﴾
54. Hakika hii ndiyo riziki yetu isiyomalizika.
هَـٰذَا وَإِنَّ لِلطَّاغِينَ لَشَرَّ مَآبٍ ﴿٥٥﴾
55. Ndio hivi! Na hakika wenye kupituka mipaka bila ya shaka watapata marejeo maovu.
جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿٥٦﴾
56. Nayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nayo ni malalo movu mno.
هَـٰذَا فَلْيَذُوقُوهُ حَمِيمٌ وَغَسَّاقٌ ﴿٥٧﴾
57. Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha!
وَآخَرُ مِن شَكْلِهِ أَزْوَاجٌ ﴿٥٨﴾
58. Na mengineyo ya namna hii.
هَـٰذَا فَوْجٌ مُّقْتَحِمٌ مَّعَكُمْ لَا مَرْحَبًا بِهِمْ إِنَّهُمْ صَالُو النَّارِ ﴿٥٩﴾
59. Hili ndilo kundi litakaloingia pamoja nanyi. Hapana makaribisho kwao. Hakika hao wanaingia Motoni.
قَالُوا بَلْ أَنتُمْ لَا مَرْحَبًا بِكُمْ أَنتُمْ قَدَّمْتُمُوهُ لَنَا فَبِئْسَ الْقَرَارُ ﴿٦٠﴾
60. Waseme: Lakini nyinyi! Hamna makaribisho! Nyinyi ndio mliotutangulizia haya, napo ni pahala paovu kabisa!
قَالُوا رَبَّنَا مَن قَدَّمَ لَنَا هَـٰذَا فَزِدْهُ عَذَابًا ضِعْفًا فِي النَّارِ ﴿٦١﴾
61. Waseme: Mola wetu! Aliyetutangulizia haya mzidishie adhabu mara mbili Motoni.
وَقَالُوا مَا لَنَا لَا نَرَىٰ رِجَالًا كُنَّا نَعُدُّهُم مِّنَ الْأَشْرَارِ ﴿٦٢﴾
62. Watasema: Mbona hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ni katika waovu?
أَتَّخَذْنَاهُمْ سِخْرِيًّا أَمْ زَاغَتْ عَنْهُمُ الْأَبْصَارُ ﴿٦٣﴾
63. Je, tuliwafanyia maskhara, au macho yamewakosa?
إِنَّ ذَٰلِكَ لَحَقٌّ تَخَاصُمُ أَهْلِ النَّارِ ﴿٦٤﴾
64. Hakika hayo ya kuhasimiana watu wa Motoni ni kweli.
WENYE TAKUA NA WALIOPETUKA MIPAKA
Aya 49 – 64
MAANA
Huu ni ukumbusho.
Yaani huko kutaja Mwenyezi Mungu (s.w.t), katika Aya zilizotangulia, sifa za manabii, kama Ibrahi, Ismail, Daud, Suleiman na wengineo.
Na hakika wenye takua wana marudio mazuri.
Mwenye takua ana mwanzo mzuri duniani na thawabu za Mwenyezi Mungu na radhi zake akhera, nazo niBustani za milele zitazofunguliwa milango kwa ajili yao, wataingia kwa amani bila ya kuulizwa au kuzuiwa.
Humo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji. Na pamoja nao wapo wenye kutuliza macho, walio mari- ka.
Starehe za vyakula na vinywaji na zaidi ya hayo kuna mahurulaini, hawamnyooshei jicho mtu yoyote isipokuwa waume zao. Umetangulia mfano wake katika Juzuu hii tuliyo nayo (37:41).
Haya ndiyo mliyoahidiwa kwa Siku ya Hisabu.
Alioyaahidi Mwenyezi Mungu hayawezi kuachwa.
Hakika hii ndiyo riziki yetu isiyomalizika.
Ndio hivi! Na hakika wenye kupituka mipaka bila ya shaka watapata marejeo maovu kabisa; kinyume kabisa na wenye takua. Wale wana makazi ya amani na hawa wana makazi maovu.
Nayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nayo ni malalo movu mno.
Watakua ni kuni zake nayo itakuwa ni shuka zao.
Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha!
Katika tafsiri Ar-Razi imeelezwa kuwa hapa kuna maneno yaliyotangulizwa na mengine kuja nyuma. Asili yake ni: Haya ni maji ya moto na usaha basi nawauonje.
Na mengineyo ya namna hii.
Adhabu ya watu wa motoni haimalizikii na maji ya moto na usaha tu; bali kuna aina nyinginezo za adhabu zinazofanana kwa ukali na ugumu na zinatofautiana kwa aina; kama vile Zaqqum na nyinginezo ambazo hakuna jicho lililoziona wala sikio lililozisikia.
Hili ndilo kundi litakaloingia pamoja nanyi. Hapana makaribisho kwao. Hakika hao wanaingia Motoni.
Wakosefu wataingia motoni makundi makundi. Likiingia kundi moja likikutana na waliotangulia watawaambia hakuna makaribisho kwenu! Mmekuja kwetu basi mmepata makazi mabaya.
Waseme: Lakini nyinyi! Hamna makaribisho! Nyinyi ndio mliotutan- gulizia haya, napo ni pahala paovu kabisa! Waseme: Mola wetu! Aliyetutangulizia haya mzidishie adhabu mara mbili Motoni.
Maneno haya yote ni ya wale waliofika wakiwajibu waliotangulia. Wamewapokea kwa shari nao wakawarudishia zaidi. Kusema kwao: ‘nyinyi ndio mliotutangulizia haya,’ ni ishara ya kuwa viongozi wa upotevu ndio watakaotangulia motoni kisha wafuatiliwe na wafuasi wao. Kusema kwao ‘haya’ ni hayo ya adhabu. Kisha wafuasi watamtaka Mwenyezi Mungu awaongezee adhabu wale waliowahadaa.
Haya yamekaririka kimaana kwenye Aya kadha, zikiwemo. Juz. 2 (2:166), Juz. 8 (7:37) na Juz. 22 (34:31).
Watasema: Mbona hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ni katika waovu?
Watakaosema ni wale waliopituka mipaka. Makusudioya watu waliohisabiwa kuwa ni katika waovu ni wale wanyonge. Wenye mabavu katika maisha ya dunia walikuwa wakipora mali za wanyonge kisha wakiwaona kama wanyama na vyombo vya kutumia.
Walalahoi ni wanyama na washari. Kwa nini? Kwa vile wao wanakula kutokana jasho lao; wala hawakeshi kwenye makasino, mabaa na madanguro. Ama wale mataghuti, wanaopituka mipaka, basi wao ndio walio bora kwa vile wanastarehe na kufuja mali za wanyonge. Wanyonge ni wapumbavu kwa vile hawaendi mwendo wa kujificha, lakini wapenda anasa hao ndio mabwana kwa vile wanajigeuza kila rangi.
Siku ya hukumu vifuniko vyote vitafunuka na wahaini wataona makazi yao katika moto wa Jahannam, wala hawatumuona yeyote katika wale waliokuwa wakiwaita ni waovu. Watashangaa na kuulizana wako wapi? Hawatachukua muda ila watajua kuwa wako mbele za mfalme muweza. Basi roho zitawatoka kwa majuto na hilo litawazidishia maumivu.
Je, tuliwafanyia maskhara, au macho yamewakosa?
Haya ni maneno ya waliopetuka mipaka watajifanyia masikhara wenyewe Siku ya Kiyama, kwa sababu walikuwa wakiwafanyia masikhara wale walioamini.
Hakika hayo ya kuhasimiana watu wa Motoni ni kweli.
Kuhasimiana kwenyewe ni huko kukaribishana motoni. Na hilo bila shaka litakua tu.
قُلْ إِنَّمَا أَنَا مُنذِرٌ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٦٥﴾
65. Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana Mola ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenza nguvu.
رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ ﴿٦٦﴾
66. Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake, Mwenye nguvu, Mwingi wa maghufira.
قُلْ هُوَ نَبَأٌ عَظِيمٌ ﴿٦٧﴾
67. Sema: Hii ni habari kubwa kabisa.
أَنتُمْ عَنْهُ مُعْرِضُونَ ﴿٦٨﴾
68. Nyinyi mnaipuuza.
مَا كَانَ لِيَ مِنْ عِلْمٍ بِالْمَلَإِ الْأَعْلَىٰ إِذْ يَخْتَصِمُونَ ﴿٦٩﴾
69. Sikuwa na ilimu ya wakuu watukufu walipokuwa wakishindana.
إِن يُوحَىٰ إِلَيَّ إِلَّا أَنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٧٠﴾
70. Sikupewa wahyi isipokuwa kwamba mimi ni mwonyaji tu aliye dhahiri.
إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن طِينٍ ﴿٧١﴾
71. Mola wako alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo.
فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ ﴿٧٢﴾
72. Na nitakapomkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi muangukieni kwa kusujudu.
فَسَجَدَ الْمَلَائِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ ﴿٧٣﴾
73. Wakasujudu Malaika wote pamoja.
إِلَّا إِبْلِيسَ اسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٧٤﴾
74. Isipokuwa Ibilisi alijivuna na akawa katika makafiri.
قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ أَسْتَكْبَرْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ الْعَالِينَ ﴿٧٥﴾
75. Akasema: Ewe Iblisi! Kipi kilichokuzuia kumsujudia yule niliyemuumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu?
قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِّنْهُ خَلَقْتَنِي مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُ مِن طِينٍ ﴿٧٦﴾
76. Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo.
قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ ﴿٧٧﴾
77. Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni mwenye kufukuzwa.
وَإِنَّ عَلَيْكَ لَعْنَتِي إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٧٨﴾
78. Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo.
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿٧٩﴾
79. Akasema: Mola wangu! Nipe muda mpaka siku watakapofufuliwa.
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ ﴿٨٠﴾
80. Akasema: Basi hakika wewe ni katika waliopewa muda,
إِلَىٰ يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ ﴿٨١﴾
81. mpaka siku ya wakati maalumu.
قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٨٢﴾
82. Akasema: Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote.
إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ ﴿٨٣﴾
83. Isipokuwa wale waja wako miongoni mwao waliosafishwa.
قَالَ فَالْحَقُّ وَالْحَقَّ أَقُولُ ﴿٨٤﴾
84. Akasema: Ni haki! Na ndio haki niisemayo.
لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكَ وَمِمَّن تَبِعَكَ مِنْهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٨٥﴾
85. Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao.
قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُتَكَلِّفِينَ ﴿٨٦﴾
86. Sema: Siwaombi ujira juu ya haya, wala mimi si katika wanaojifanya.
إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿٨٧﴾
87. Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote.
وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُ بَعْدَ حِينٍ ﴿٨٨﴾
88. Na bila ya shaka mtajua habari zake baada ya muda.
MIMI NI MUONYAJI TU
Aya 65 – 88
MAANA
Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana Mola ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenza nguvu. Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake, Mwenye nguvu, Mwingi wa maghufira.
Ewe Muhammad! Waambie washirikina kuwa mimi ninawabashiria mumpwekeshe Mwenyezi Mungu na ninawaonya kuwa msimshirikishe na yeyote kwenye ibada.
Yeye peke yake ndiye mwenye ufalme, mwenye nguvu na msamehevu kwa yule mwenye kutubia mwenye kurejea kwa Mola wake.
Sema: Hii ni habari kubwa kabisa. Nyinyi mnaipuuza.
Neno ‘hii’ linarudia kwenye Qur’an na walioipuuza ni washirikina, kwa ujinga au kwa inadi na kupupia masilahi yao. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameisifu Qur’an kuwa ni habari, kubwa kwa sababu imejikita kwenye itikadi, sharia na misingi yote ya asasi za manufaa ya wote na kusaidiana.
UISLAMU NA MSICHANA WA KINGEREZA
Mnamo mwezi January 1970, nilisoma mihadhara miwili ya Roger Garaudy aliyoitoa mjini Cairo, Darul-aharam, mnamo mwezi wa November 1969. Garaudy ni miongoni mwa wataalamu wakubwa wa fikra wa kifaransa. Ni profesa wa falasafa na ni Daktari wa fasihi. Mihadhara yake hiyo iliandikwa kwenye jarida la Attalia namba 1-1970. la Misri.
Miongoni mwa aliyoyasema katika muhadhara wake wa kwanza ni: “Ukombozi wa waarabu haukuwa ni wa kivita wala wa kikoloni; isipokuwa ulikuwa ni wa kuleta fursa katika kila mji kuleta maendeleo kutokana na sanaa ya kiislamu na maendeleo yake. Ukombozi wa waarabu umeleta mwamko wa kiichumi wa ulimwengu, pamoja na kuweko ukabaila katika miaka ya mwanzo ya ukombozi.”
Katika muhadhara wake wa pili alisema: “Sisi tuko kwenye turathi adhimu ya misimamo ya kiislamu ambayo inaweza kutoa mchango mkubwa kati- ka maendeleo ya kiislamu.”
Akaendelea kusema: “Tunamuona mwanafikra mkubwa wa kifaransa, Bacon anasema: “Falsafa yote imechimbuka kutokana na Uislamu.”
Vile vile nilisoma kwenye gazeti la Al-jumhuriya la Misr, la 21/1/ 1970, kwamba msichana mmoja msomi wa kingereza, aitwaye Bridget Honey aliingia kwenye dini ya kiislamu hivi karibuni. Kwa ufupi gazeti linaelezea kuwa msichana huyu alikuwa, kama watu wengine wa kimagharibi, ana chuki na shaka nyingi juu ya Uislamu. Lakini baada ya kusoma, kwa umakini na bila chuki, tarjuma ya Qur’an na vitabu vingine, na akajua mafunzo yake, alijikuta ni mwislamu bila ya kutambua.
Kisha msichana huyu akamwambia mwandishi wa gazeti: “Ni vigumu sana kuubainihsa uhakika wa Uisalmu kwa maneno ya harakaharaka. Kwa sababu huo ni kama aina ya fulani ya kiuhandisi ya ajabu uliokamilika, kila sehemu ikiikamilisha sehemu nyingine. Na siri ya uzuri wake inatokana na kuoana mafungu yake. Sifa hii ya uislmu ndiyo inayoathiri kwa undani ubinadamu.
Hakika mfumo mzuri katika Uislmu wa kutosheleza matakwa ya kimwili naya kiroho una mvuto wa nguvu katika magharibi ya kileo na unaweza kuleta athari kwenye maendeleo ya kisasa. Unawawekea wazi njia ya magharibi kuelekea kwenye usafi na kufaulu kiuhakika.”
Ingelikuwa bora lau vijana wetu, akiwemo yule mwenye kitabu cha fikra ya kupinga dini, wangelifuata njia ya msichana huyu; wakasoma Qur’an na kuyachunguza kwa undani maana yake, wakasoma waliyoandika wataalmu kuhusu Uislamu; kama alivyofanya msichana huyu. Kisha wauhukumu Uisalmu wao wenyewe kulingana na walivyosoma na wakafahamu.
Kwa uchache athari atayoipata mwenye kuisoma Qur’an na kuyazingatia vizuri maana yake ni kujua uadilifu wa mwenye uweza na kwamba Yeye atawalipa wema wanaofanya mema na mabaya wanaofanya mabaya. Atabakia na nini mtu kama atakosa imani hii?
Sikuwa na ilimu ya wakuu watukufu walipokuwa wakishindana. Sikupewa wahyi isipokuwa kwamba mimi ni mwonyaji tu aliye dhahiri.
Makusudio ya wakuu watukufu hapa ni Malaika. Maana ni kuwa sema ewe Muhammad kuwaambia washirikina. Mimi nimewapa habari za Malaika wakati Mwenyezi Mungu alipowambia:
إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ ﴿٣٠﴾
“Mimi nitaweka khalifa katika ardhi” (na wao) wakasema: Utaweka humo watakaofanya uharibifu?” Juz. 1 (2:30).
Nisingeyajua haya lau sikunifahamisha na kunipa wahyi Mwenyezi Mungu; au mnaona mimi ninamzulia Mwenyezi Mungu? Nami sidai lolote kwa ajili yangu, isipokuwa kuwaonya mumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake kwa kutaka thawabu zake na kuhofia adhabu yake.
Mola wako alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo. Na nitakapomkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi muangukieni kwa kusujudu.
Makusudio ya roho ya Mwenyezi Mungu hapa ni uhai. Mwanafasihi mmoja wa kisasa anasema: Bali makusudio ni dhamiri ya mtu hasa, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaamrisha Malaika kumsujudia Adam kwa vile yeye ni elimu. Mara ngapi dhamiri itamwadhibu kiumbe huyo mwenye mwili wa udongo na roho ya Mwenyezi Mungu? “Hakika tumemuumba mtu katika tabu” (90:4). yaani dhiki na mashaka yenye kuendelea.
Wakasujudu Malaika wote pamoja; isipokuwa Ibilisi alijivuna na akawa katika makafiri.
Mwenye kitabu “Kupinga fikra ya dini” anasema katika uk. 90: “Kukataa Iblisi kumsujudia Adam kunaenda sambamba na matakwa ya Mwenyezi Mungu.”
Kauli hii nayo inaenda sambamba na madhehebu ya kisunni, yanayosema kuwa hakuna kulazimiana baina ya anayoyaamuru Mwenyezi Mungu na anayoyataka, wala baina ya anayoyakataza na anayoyachukia. Anaweza kuamuru anayoyachukia na anaweza kukataza anayoyapenda. Tazama Al- mawaqif (8:176).
Miongoni mwa waliyoyatolea dalili ya hilo nikuwa Mwenyezi Mungu alimwamrisha Ibilisi kumsujudia akiwa Yeye Mwenyezi Mungu hataki hivyo, lau angelitaka Mwenyezi, Mungu basi Ibilis angelisujudi tu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu hufanya anayoyataka.
Lakini kauli ya mwenye kitabu cha kupinga dini haiendi sambamba na madhehebu ya Shia wanaosema kuwa Mwenyezi Mungu ana matakwa aina mbili: kutaka kwa kuumba ambako kunaelezwa na ibara ya “Kuwa na ikawa” (kun fayakun).
Na kutaka kwingine ni kwa kisharia ambako kunaelezewa na kuamrisha na kukataza. Tazama Juz. 1 (2:26-27). Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) alitaka kusujudiwa Adam kwa matakwa ya kisharia sio matakwa ya kuumba.
Akasema: Ewe Iblisi! Kipi kilichokuzuia kumsududia yule niliye- muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu?
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anazielezea sababu za kimaumbile kwa ibara ya mikono yake, kwa sababu zinakomea kwake. Mwenyezi Mungu Mtukufu: anasema kwenye Juzuu hii tuliyo nayo:
أَنَّا خَلَقْنَا لَهُم مِّمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَا أَنْعَامًا ﴿٧١﴾
“…kwamba tumewaumbia kutokana na iliyofanya mikono yetu wanyamahowa.” (36:71).
Maana ni, kwa nini umejizuia kumsujudia Adam ewe Ibilisi? Je, umejifanya kuwa na kiburi na ukajiweka kwenye cheo usichokuwa nacho? Au kweli wewe unajiona kuwa ni mkubwa na mtukufu kuliko Adam?
Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo.
Alijibu kuwa ana uhakika yeye ni mkubwa na mtukufu zaidi kuliko Adam, kwa vile ametokana na moto unaokuwa viwandani na kutengenezewa sila- ha za maangamizi, lakini Adamu ametokana na udongo kwa hiyo yeye ni mkulima, kwa vile ni maji na mchanga.
Amesahau au amejitia kusahahu, habithi huyu, kuwa maji ndio asili ya uhai na kwamba maendeleo yote ni tanzu.
Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni mwenye kufukuzwa. Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo. Akasema: Mola wangu! Nipe muda mpaka siku watakapofufuliwa. Akasema: Basi hakika wewe ni katika waliopewa muda, mpaka siku ya wakati maalumu. Akasema: Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote, isipokuwa wale waja wako miongoni mwao waliosafishwa. Akasema: Ni haki! Na ndio haki niisemayo. Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao.
Yametangulia maelezo ya kisa cha kuumbwa Adam, kusujudu Malaika na kukataa Ibilisi kusujudu katika Juzuu zifuatazo:-
• Juz. 1 (2:30 – 34).
• Juz. 8 (7:11 – 18).
• Juz. 14 (15:26 – 44).
• Juz. 15 (17:61-65).
• Juz. 15 (18:50).
Sema: Siwaombi ujira juu ya haya, wala mimi si katika wanaojifanya.
‘Haya’ ni haya ya tabligh na kukumbusha. Makusudio ya kujifanya hapa ni uwongo. Maana ni ewe Muhammad! Waambie wale wanaokukadhibisha kuwa mimi ninawapa nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, sitaki malipo kutoka kwenu wala shukrani, na wala mimi simzulii Mwenyezi Mungu. Vipi nimzulie na hali ninacho kitabu kinachosema kweli, na kilichoshinda ndimi na akili zote kuweza kuleta mfano wake.
Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote walio na moyo au wanaotega sikio na wenyewe ni mashahidi.
Na bila ya shaka mtajua habari zake baada ya muda.
Itawabainikia baada ya muda kidogo katika maisha ya dunia ambapo watu wataingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi makundi. Vile vile itawabainikia haki huko akhera ambapo uhakika utathibiti na batili itapotea.
MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA NANE: SURAT SAAD
26
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
Sura Ya Thelathini Na Tisa: Surat Az-Zumar. Imeshuka Makka ina Aya 75 isipokuwa Aya tatu.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ﴿١﴾
1. Mteremsho wa Kitabu hiki umetokana na Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ فَاعْبُدِ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ ﴿٢﴾
2. Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa Haki. Basi muabudu Mwenyezi Mungu ukimsafia Dini Yeye.
أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِي مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ ﴿٣﴾
3. Ehe! Dini halisi ni ya Mwenyezi Mungu. Na wale wanaowafanya wenginewe kuwa ni walinzi badala yake, (husema): Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika wanayohitalifiana. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongozi aliye mwongo, kafiri.
لَّوْ أَرَادَ اللَّـهُ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا لَّاصْطَفَىٰ مِمَّا يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ سُبْحَانَهُ هُوَ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٤﴾
4. Lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka kujifanyia mwana, basi bila ya shaka angeli teua amtakaye katika aliowaumba. Ametakasika na hayo! Yeye ni Mmoja, Mtenza nguvu.
DINI SAFI NI YA MWENYEZI MUNGU TU!
Aya 1-4
MAANA
Mteremsho wa Kitabu hiki umetokana na Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Qur’an inatoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye ameumba viumbe kwa uweza wake na akaupangilia kwa hekima yake.
Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa Haki. Basi muabudu Mwenyezi Mungu ukimsafia Dini Yeye.
Inaweza kusemwa kuwa : Nabii(s.a.w. w ) ana yakini kuwa Qur’an imetoka kwa Mwenye nguvu Mwenye hekima na kwamba yeye anamwabudu Mwenyezi Mungu kwa kumsafia dini; sasa kuna haja gani ya amri na habari hii?
Jibu : Nabii(s.a.w. w ) aliudhiwa sana na akavumilia mengi, ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamwambia kwamba wewe unalingania kwenye haki; na mwenye kulingania kwenye mazingira kama yako hana budi kujitolea nafsi yake na mali yake. Vile vile wewe unamfanyia ikhlasi Mwenyezi.
Mungu katika kauli na vitendo vyako vyote; na mwenye kumfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu hukumbana na mengi kutoka kwa maadui zake.
Kwa maneno mengine ni kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu: “Tumekuteremshia Kitabu,” sio kutoa habari; wala kauli yake: “ Basi muabudu Mwenyezi Mungu,” sio amri; bali ni ushahidi wa utukufu wa mtume na kumpoza kutokana na anayokumbana nayo kutoka kwa maadui zake.
Ehe! Dini halisi ni ya Mwenyezi Mungu, isiyokuwa na doa, lakini dini iliyo na madoadoa ya ria na hawa, basi ni ya shetani, siyo ya Mwenyezi Mungu. Dini safi ya namna hii haiwi ila kwa yule aliyeifanya ndio mfano wake wa juu, akajitolea nafsi yake na manufaa yake yote, na wala sio kujitolea kwa manufaa yake na masilahi yake.
Na wale wanaowafanya wenginewe kuwa ni walinzi badala yake, (husema): Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewarudia washirikina na kuwaelezea kuwa wao wanawafanya wengine kuwa waungu ili wawaombee kwake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:18).
Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika wanayohitalifiana.
Washirikiana hawatofutiani; isipokuwa wanatofutiana na wanaompwekesha Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atahukumu baina ya makun- di haya mawili – ampe neema mwenye kumpwekesha na ampe adhabu mwenye kumshirikisha.
Hakika Mwenyezi Mungu hamwongozi aliye mwongo kafiri.
Hakika yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwongoza mwenye kufuata njia ya uongofu, anampoteza mwenye kuchagua njia ya upotevu, anamwangamiza mwenye kujitia kwenye maangamivu na anamwokoa mwenye kuchukua hadhari na akajiepusha na maangamizi
Lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka kujifanyia mwana, basi bila ya shaka angeliteua amtakaye katika aliowaumba.
Hii ni katika kukadiria muhali. Na kukadiria muhali sio muhali. Muhali wenyewe ni kuwa kutaka kuwa na mtoto ni kuwa na haja na kuhitajia, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujitosheleza na kila kitu, si muhitaji. Zaidi ya hayo ni kuwa kila mzazi anarithiwa na kila anayerithiwa huwa ametoweka. Kwa hiyo kila mzazi anatoweka; sasa Mwenyezi Mungu atakuwa- je mzazi?
Ametakasika na hayo! Yeye ni Mmoja, Mtenza nguvu, hana mshirika wala wakufanana naye wala hana mwenzahakuna chochote isipokuwa Yeye tu.
خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ يُكَوِّرُ اللَّيْلَ عَلَى النَّهَارِ وَيُكَوِّرُ النَّهَارَ عَلَى اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى أَلَا هُوَ الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ ﴿٥﴾
5. Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Huuzongazonga usiku kwenye mchana, na Huuzongazonga mchana kwenye usiku. Na amelitiisha Jua na Mwezi, kila kimoja kinapita mpaka muda uliotajwa. Ehe! Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kughufiria.
خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ الْأَنْعَامِ ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِّن بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ﴿٦﴾
6. Amewaumba kutokana na nafsi moja, na katika hiyo akamjaalia mkewe. Na amewateremshia wanymahoa namna nane za madume na majike. Anawaumba katika matumbo ya mama zenu, umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu. Ufalme ni wake. Hapana Mola isipokuwa Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi?
إِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنكُمْ وَلَا يَرْضَىٰ لِعِبَادِهِ الْكُفْرَ وَإِن تَشْكُرُوا يَرْضَهُ لَكُمْ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٧﴾
7. Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi. Wala haridhii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru atawaridhia. Wala hatabeba mbebaji mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu. Basi atawaambia mliyokuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ ضُرٌّ دَعَا رَبَّهُ مُنِيبًا إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا خَوَّلَهُ نِعْمَةً مِّنْهُ نَسِيَ مَا كَانَ يَدْعُو إِلَيْهِ مِن قَبْلُ وَجَعَلَ لِلَّـهِ أَندَادًا لِّيُضِلَّ عَن سَبِيلِهِ قُلْ تَمَتَّعْ بِكُفْرِكَ قَلِيلًا إِنَّكَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ ﴿٨﴾
8. Na dhara inapomfikia mtu humwomba Mola wake akielekea kwake. Kisha akimpa neema kutoka kwake, husahau yale aliyokuwa akimwitia zamani, na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze njia yake. Sema: Starehe na kufuru yako kidogo, kwani hakika wewe mi miongoni mwa watu wa Motoni.
HUUFUNIKA MCHANA JUU YA USIKU
Aya 5 – 8
LUGHA
Neno Huuzongazonga limefasiriwa kutokana na neno la kiarabu yukawwir, lenye maana ya kufunika kitu kilicho mviringo; kama mtu anavyozongazonga kitambaa kichwani kufanya kilemba.
MAANA
Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Huuzongazonga usiku kwenye mchana, na Huuzongazonga mchana kwenye usiku.
Huko nyuma tumesema kuwa Mwenyezi Mungu ana vitabu viwili: Kitabu kinachotamka kwa mistari amabacho ni Qur’an na kitabu kilichonyamaza cha kuangaliwa, ambacho ni ulimwengu. Na kwamba yaliyomo katika kitabu hiki; kama vile umoja wenye kuthibiti na hekima iliyopangika, ni dalili mkataa ya umoja wa mwenye kuthibiti na hekima ya mwenye kupangalia. Ama sadfa, kama itatokea, basi hutokea kwenye kitu kimoja wala haikaririki mara nyingi kwenye kitu kimoja.
Mwenye Tafsir Adhilal akizungumzia Aya hii anasema: “Hakika ibara ya kuzongazonga inanilazimisha niangalie vizuri suala la ardhi kuwa ni mviringo, kwamba hiyo yenyewe inazunguka katika kulielekea jua. Kwa hiyo sehemu inayoeleka jua inafunikwa na mwanga na kuwa mchana, lakini sehemu hiyo haitulii kwa vile ardhi inazunguka.
Kila inavyozidi kuendelea ndio usiku nao unaanza kufunika sehemu iliyokuwa mchana. Kufunika huko kunakuwa kwa namna ya kuzongazonga. Kwa hiyo mchana unazongwazongwa na usiku na usiku nao unazongwazongwa”
Kwa hiyo neno kuzongazonga, haliko mbali kuwa linafahamisha mviringo. Ndio maana tunaungana na mwenye Dihilal aliposema ibara ya kuzongzonga inapelekea kuangalia kuwa ardhi ni mviringo. Mustafa Mahmud, katika gazeti la sabahulkhayr amesema kama alivyosema mwenye Dhilal, lakini hakumtaja. Sijui hii ni sadfa ya kuoana mawazo?
Umetangulia mfano wake katika Juzuu hii (36:37), lakini huko halikuja nen o kuzongazonga; bali tulipofafanua tuliashiria kuhusu mzunguko wa ardhi na kwamba upande uanaolelekea jua wakati wa kuzunguka unakuwa mchana na upande wa pili unakuwa usiku.
Na amelitiisha Jua na Mwezi, kila kimoja kinapita mpaka muda uliotajwa. Ehe! Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kughufiria.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:2), 21 (31:29) na 22 (35:13).
Amewaumba kutokana na nafsi moja, na katika hiyo akamjaalia mkewe.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (4:1) na Juz. 9 (7:143)
Na amewateremshia wanymahoa namna nane za madume na majike.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (6:143).
Anawaumba katika matumbo ya mama zenu, umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu. Ufalme ni wake. Hapana Mola isipokuwa Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi?
فَإِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ مِن مُّضْغَةٍ ﴿٥﴾
‘Umbo baada ya umbo’ ni ishara ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Hakika tuliwaumba kutokana na udongo kisha kutokana na pande la damu, kisha kutokana na pande la nyama” Juz. 17 (22:5).
Viza vitatu ni tumbo, tumbo la uzazi na fuko la mtoto. Kuendelea huku kutoka hali moja hadi nyingine ndani ya viza vitatu ni dalili mkataa ya kuweko mpangiliaji mwenye kutengeneza.
Ikiwa kukua huku kunatokana na maumbile moja kwa moja, basi maumbile ni katika usanii wa anayesema ‘kuwa ikawa’ Hili hawezi kupofuka nalo isipokuwa kipofu.
Imam Ali(a.s ) anasema:“Ewe kiumbe uliyembwa sawa sawa na mwenye kutunzwa kwenye viza vya tumbo la uzazi na tabaka za sitara! Umeanzishwa “Kutokana na asili ya udongo [9] .”
Na ukawekwa “mahali palipo madhubuti makini mpaka muda maalum,”[10] na muda maalum. Unataharaki tumboni ukiwa mchanga, huwezi kuita wala kusikia mwito.
Kisha ukatolewa kwenye makazi yako kwenda mahali ambapo hujapashuhudia wala hujui manufaa yake. Basi ni nani aliyekuongoza kutafuta chakula kutoka kwenye matiti ya mama yako na kukujulisha matakwa ya haja yako?”[11] .
Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi
Hayamdhuru maasi ya mwenye kuasi, wala haumnufaishi utiifu wa mwenye kutii “lakini inamfikia takua kutoka kwenu” Juz. 17 (22:37); yaani anawaridhia mkiwa ninyi ni wenye takua;
Ashaira wanasema kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kutaka yote yanayokuwa; hata kufuru ya kafiri, zina ya mzinifu na uuaji wa mwenye kuua kwa dhulma; kwa vile Yeye ni muumba wa kila kitu. Lakini wakati huohuo anakataza kufuru, zina na kuua.
Almawafiq Juz. 8 Uk. 173. Kwa hiyo kukalifishwa lisilowezekana inajuzu kwa Ashaira. Kwa sababu Mwenyezi Mungu hawajibikiwi na kitu chochote wala hakuna kibaya kwake. Almawaqif Juz. 8 Uk. 200.
Hakuna kitu kilicho wazi zaidi kufahamisha ubatilifu wa fikra hii kuliko kauli yake Mwenyezi Mungu:
Wala haridhii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru atawaridhia.
Analoturidhia ni amani kwetu na rehema.
Wala hatabeba mbebaji mzigo wa mwingine.
Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 8 (6:164), 15 (17:15), 22 (35:18).
Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu. Basi atawambia mliyokuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
Kwake Yeye Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya viumbe na mikononi mwake ndio kuna malipo ya matendo na Yeye anajua siri zote na yale wanayoyakusudia.
Na dhara inapomfikia mtu humwomba Mola wake akielekea kwake. Kisha akimpa neema kutoka kwake, husahau yale aliyo kuwa akimwitia zamani, na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze njia yake.
Kumgusa ni kumpata, dhara ni tabu na maudhi na kuelekea kwake ni kurejea kwake. Maana ni kuwa mtu anapopatwa na shida ya nafsi yake au mali yake humkimbila Mwenyezi Mungu kwa kumnyenyekea, lakini shida ikimwondokea basi anasahau unyenyekevu aliokuwa nao.
Sema: Starehe na kufuru yako kidogo, kwani hakika wewe mi miongoni mwa watu wa Motoni.
Hili ni kemeo na kiaga kwa yule anayeamini wakati wa shida na kukufuru wakati wa raha. Hakuna mwenye shaka kwamba starehe ya dunia pamoja kufuru ina mwisho mbaya.
26
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاءَ اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا يَحْذَرُ الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٩﴾
9. Je, Afanyaye ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake. Sema: Je, wanalingana sawa wale ambao wanajua na wale ambao hawajui? Hakika wanaokumbuka ni wenye akili tu.
قُلْ يَا عِبَادِ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا رَبَّكُمْ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ وَأَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةٌ إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿١٠﴾
10. Sema: Enyi waja wangu ambao mmeamini! Mcheni Mola wenu. Wale ambao wamefanya wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni pana. Hakika si mengineyo, wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.
قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ ﴿١١﴾
11. Sema: Hakika mimi nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumsafia Yeye Dini.
وَأُمِرْتُ لِأَنْ أَكُونَ أَوَّلَ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٢﴾
12. Na nimeamrishwa niwe wa mwanzo wa Waislamu.
قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٣﴾
13. Sema: Hakika mimi ninahofia adhabu ya Siku Kubwa nikimuasi Mola wangu.
قُلِ اللَّـهَ أَعْبُدُ مُخْلِصًا لَّهُ دِينِي ﴿١٤﴾
14. Sema: Mwenyezi Mungu ninamuabudu kwa kumsafia Yeye Dini yangu.
فَاعْبُدُوا مَا شِئْتُم مِّن دُونِهِ قُلْ إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَلَا ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ ﴿١٥﴾
15. Basi abuduni mpendacho badala yake. Sema: Hakika waliohasirika ni wale waliojihasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Ehe! hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri
لَهُم مِّن فَوْقِهِمْ ظُلَلٌ مِّنَ النَّارِ وَمِن تَحْتِهِمْ ظُلَلٌ ذَٰلِكَ يُخَوِّفُ اللَّـهُ بِهِ عِبَادَهُ يَا عِبَادِ فَاتَّقُونِ ﴿١٦﴾
16. Watakuwa na vivuli vya moto juu yao, na chini yao vivuli. Kwa hayo Mwenyezi Mungu anawahofisha waja wake. Enyi waja wangu! Nicheni.
HADHARI YA AKHERA NA MATARAJIO YA REHEMA YA MOLA
Aya 9 – 16
MAANA
Hata Manabi Wana Shauku Na Hofu
Je, Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja yule anayeamini wakati wa shida na kukufuru wakati wa raha, anafuatishia kumtaja yule anayeamini wakati wa shida na raha. Neema haimzidishii kitu isipokuwa imani, shukrani, kusujudu na kurukui wakati wa giza la usiku, watu wakiwa wamelala. Hafanyi kitu isipokuwa shauku ya thawabu za Mwenyezi Mungu na kuhofia adhabu yake.
Katika Aya hii kuna ishara kuwa mtu hafanyi ila kwa msukumo shauku na hofu, awe ni mwenye takua au muovu. Tofauti ni kuwa muovu anafanya na kuacha kwa shauku ya starehe za dunia na kuhofia tabu na machungu, lakini mwenye takua anafanya na kuacha kwa sahuku ya shamba la Akhera na neema zake na kuhofia adhabu yake na moto wake.
Hali hii iko hata kwa manabii walio maasumu ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu kwa kusema: “Wakituomba kwa shauku na hofu.” Juz. 17 (21:90).
Sema: Je, wanalingana sawa wale ambao wanajua na wale ambao hawajui? Hakika wanaokumbuka ni wenye akili tu.
Makusudio ya wanaojua hapa sio wale waliohifadhi sherehe na matini, wala sio wale waliogundua elektroni, mabomu ya masafa marefu na kupanda mwezini au kwenye Mars.
Hapana! Sio hao kabisa; isipokuwa makusudio ni wale wanaofanya kheri kwa binadamu wote na kuwakomboa wanaoadhibiwa ardhini na kuwaondoa watu kwenye tabu na mashaka.
Ama ulama wasiojali au wale ambao wameuza dini yao kwa mshetani na maibilisi kwa ajili ya kuwachapa watu na wakagundua silaha za maangamizi, hawa ni kama wanyama; bali wao wamepotea zaidi ya wanyama.
Hawawezi kuitambua hakika hii isipokuwa wale wenye akili na busara.
Sema: Enyi waja wangu ambao mmeamini! Mcheni Mola wenu, kwa sababu imani bila takua wala amali njema haina manufaa yoyote. Ndio maana baadhi ya maulama wamesema kuwa matendo mema ni sehemu ya kuamini haki.
Wale ambao wamefanya wema katika dunia hii watapata wema.
Haya ni maneno mapya hayaungani na yaliyotangulia. Maana yake ni kuwa mwenye kufanya hata chembe ya amali ya kheri ataiona.
Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni pana.
Kwa hiyo atayepata dhiki mjini kwake na akashindwa kutekeleza wajibu wake wa kidini au wa kidunia basi ahamie kwengine. Umetangulia mfano wake katika Juz. 5 (4:97).
Hakika si mengineyo, wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.
Yaani wenye kuvumilia shida kwa subira ya kiungwana na kukataa kusalimu amri kwenye ufukara na udhalili. Ama wale ambao wanawanyeyekea wenye nguvu na kuwa waoga mbele ya mataghuti, hao ndio waliohasirika duniani na akhera na huko ndiko kuhasrika waziwazi.
Sema: Hakika mimi nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumsafia Yeye Dini.
Hakuna tofauti baina ya Nabii na mwenginewe. Yeye anaamrishwa kum- fanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu katika kauli na matendo yake yote; kama binadamu mwingine.
Na nimeamrishwa niwe wa mwanzo wa Waislamu.
Mtume(s.a.w. w ) aliwapa watu mwito wa uislamu baada ya kutangulia yeye mwenyewe kwenye Uislamu, kwa sababu anafanya anayoyasema wala hasemi asiyoyafanya.
Sema: Hakika mimi ninahofia adhabu ya Siku Kubwa nikimuasi Mola wangu.
Muhammad(s.a.w. w ) anamhofia Mwenyezi Mungu kwa sababu Yeye hawezi kumwepuka Mwenyezi Mungu wala hana hoja naye, bali yeye ni hoja ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake wote.
Utukufu zaidi kwa Muhammad(s.a.w. w ) ni kwamba yeye ni mtiifu kwa Mola wake, mwenye kumfanayia ikhlasi na mtangulizi wa mambo ya heri, akipata wahyi kutoka kwa Mola wake na akiutekeleza unavyotakikana:
قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٩﴾
“Sema: mimi si kioja katika mitume; wala sijui nitakavyofanywa wala nyinyi; sifuati ila niliyopewa wahyi na mimi si lolote ila ni muonyaji, mwenye kubainisha.” (46:9).
Sema: Mwenyezi Mungu ninamuabudu kwa kumsafiia Yeye Dini yangu.
Mara nyingine Muhammad(s.a.w. w ) anasisitiza, kwa amri ya Mwenyezi Mungu, kwamba Yeye ni mja mwenye kuamriwa. Mustshriq mmoja wa kingereza, Jeb Hamilton, mwalimu katika chuo kikuu cha Oxford, katika kitabu “Modern trends in Islam” anasema: “Qur’an inakataa fikra ya kuingiliwa kati, baina ya Mwenyezi Mungu na mtu. Unamweka mtu moja kwa moja mbele ya Mola wake bila ya kuweko wa katikati kiroho au kiutu.” Na hii ni tofuati kubwa inayoshindia Uislamu dini nyingine.
Basi abuduni mpendacho badala yake.
Huu ni ufasaha wa hali ya juu kuelezea hasira za Mwenyezi Mungu na makemeo kwa yule anayemfanya muabudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
Sema: Hakika waliohasirika ni wale waliojihasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Ehe! hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri.
Wamezihasiri nafsi zao kwa sababu wamejiingiza kwenye Jahannam, marejeo mabaya kabisa, na wamewahasiri watu wao kwa sababu atakayekuwa mshirikina katika wao ataangamia. Na mumin ni adui wa mwenye kushirikisha duniani na akhera.
Watakuwa na vivuli vya moto juu yao, na chini yao vivuli.
Yaani adhabu ya kuungua itawazunguka kila mahali.
Kwa hayo Mwenyezi Mungu anawahofisha waja wake. Enyi waja wangu! Nicheni.
Mwenyezi Mungu amewabainishia adhabu ya akhera ili waweze kujiepusha nayo wakiwa duniani kwa kufanya utiifu na ikhlasi. Vinginevyo wataionja tu.
Msemaji mmoja alisema kuwa Pepo ni ladha za kiroho na moto ni machungu ya kinafsi na kwamba yote yaliyoelezwa kwenye Qur’an katika sifa za kihisia ni aina ya kupiga mfano na kuleta karibu kwenye akili. Kwa vile mabedui wanapenda sana asali, maziwa, pombe na wanawake mahurilaini. Msemaji wa maneno haya ametolea dalili kauli yake, kwa Aya hii tuliyo nayo: “Kwa hayo Mwenyezi Mungu anawahofisha waja wake.”
Kwamba inavyofahamika ni kuwa Mwenyezi Mungu ametaja matamshi ya adhabu kwa ajili ya kuhofisha tu, wala hakuna hakika[12]
Tunajibu : kila tamko lililokuja katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume wake ni wajibu kuchukulia dhahiri yake, ila ikiwa halingiliki akilini; na hapo tutalitumia kimajazi yanayokwenda na tamko lenyewe.
Hakuna tamshi katika matamshi ya sifa za Pepo na Moto yaliyotajwa na Qur’an, linalokataliwa na akili. Kwa hiyo ni wajibu kubakia tamko kwenye dhahiri yake, bila ya kuweko haja ya kuleta taawili.
Maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Kwa hayo Mwenyezi Mungu anawahofisha waja wake,” ni kuwa anawabainishia uhakika wa mambo, ili wachukue hadhari na wajiepushe na sababu zitakazopelekea hilo. Aya iliyotaja sifa za Moto ndio inayofahamisha maana haya:
إِنَّ ذَٰلِكَ لَحَقٌّ تَخَاصُمُ أَهْلِ النَّارِ ﴿٦٤﴾
“Hakika hayo ya kuhasimiana watu wa Motoni ni kweli.” (38:64).
Ama kauli ya kuwa huruma ya Mwenyezi Mungu haiafikiani na adhabu ya ya Moto kwa kiumbe huyu masikini aliye dhaifu, tunaijibu hivi:
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewandalia adhabu kali na chungu wale wanofanya ufisadi katika ardhi wakamwaga damu, kuwafanya waja wa Mungu kuwa watumwa wao, wakaangamiza watu kwa silaha za maangamizi na kuwaua kwa maelfu ndani ya dakika. Jahannam, pamoja na sifa zake zote, haitoshi kuwa ni malipo kwa hawa; bali wamehurumiwa pia. Amani imshukie yule aliyesema: “Ghadhabu haimshughulishi (asiwe) na huruma, wala huruma haimshughulishi (asiwe) na mateso.”
Tazama kifungu cha ‘Jahannam na silaha za maangamizi’ katika Juz.13 (14:46-52).
وَالَّذِينَ اجْتَنَبُوا الطَّاغُوتَ أَن يَعْبُدُوهَا وَأَنَابُوا إِلَى اللَّـهِ لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فَبَشِّرْ عِبَادِ ﴿١٧﴾
17. Na wale wanaojiepusha na kuabudu taghut, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu, watapata bishara njema. Basi wabashirie waja wangu.
الَّذِينَ يَسْتَمِعُونَ الْقَوْلَ فَيَتَّبِعُونَ أَحْسَنَهُ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَاهُمُ اللَّـهُ وَأُولَـٰئِكَ هُمْ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿١٨﴾
18. Ambao husikiliza maneno, wakafuata mazuri yake zaidi. Hao ndio aliowaongoza Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili.
أَفَمَنْ حَقَّ عَلَيْهِ كَلِمَةُ الْعَذَابِ أَفَأَنتَ تُنقِذُ مَن فِي النَّارِ ﴿١٩﴾
19. Je, Yule mwenye kustahili hukumu ya adhabu, Je, wewe unaweza kumwokoa aliyomo Motoni?.
لَـٰكِنِ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ لَهُمْ غُرَفٌ مِّن فَوْقِهَا غُرَفٌ مَّبْنِيَّةٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَعْدَ اللَّـهِ لَا يُخْلِفُ اللَّـهُ الْمِيعَادَ ﴿٢٠﴾
20. Lakini waliomcha Mola wao watapata ghorofa zilizojengwa juu ya ghorofa; chini yake hupita mito. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَسَلَكَهُ يَنَابِيعَ فِي الْأَرْضِ ثُمَّ يُخْرِجُ بِهِ زَرْعًا مُّخْتَلِفًا أَلْوَانُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَجْعَلُهُ حُطَامًا إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿٢١﴾
21. Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni. Kisha akayapitisha yakawa chem-chem katika ardhi? Kisha kwa maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbali mbali. Kisha hunyauka ukaiona imekuwa kimanjano kisha huifanya imevunjikavunjika. Bila ya shaka katika hayo kuna ukumbusho kwa wenye akili.
WANAOSIKILIZA MANENO WAKAFUATA MAZURI YAKE
Aya 17 – 21
MAANA
Na wale wanaojiepusha na kuabudu taghut, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu, watapata bishara njema. Basi wabashirie waja wangu.
Makusudio ya Tghut hapa ni masanamu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawabashiria wale walioacha shirki wakatubia na wakamtii Mwenyezi Mungu
Ambao husikiliza maneno, wakafuata mazuri yake zaidi. Hao ndio aliowaongoza Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili.
Makusudio ya maneno mazuri sio uzuri wa matamshi na ufasaha wake; isipokuwa ni yale yanayonufaisha duniani na akhera – yakiwa yana madhara basi ni mabaya. Ama maneno yasiyodhuru wala kunufaisha, basi hayo hayawezi kusifiwa kwa ubaya wala kwa uzuri.
Kauli ya Mwenyezi Mungu ni nzuri zaidi kuliko kauli yoyote, wala hakuna kitu bora kuliko kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, iwe kauli au vitendo. Kwa sababu vitu kutoka kwake ni sawa.
Wale wanaosikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu na wakayafanyia kazi ndio walioongoka, mbele ya Mwenyezi Mungu, kwenye maarifa mazuri zaidi na ndio wanaochukua kiini cha maneno sio maganda.
Imam Ali(a.s ) anasema:“Kithirisheni kumtaja Mungu kwa kuwa ni utajo mzuri zaidi, na yafanyieni shauku ambayo (s.w.t) amewaahidi wachamungu, kwa kuwa ahadi yake ni ahadi ya kweli mno, na fuateni mwongozo wa Nabii wenu kwa kuwa huo ni mwongozo bora zaidi, na fanyeni kwa mwenendo wake kwa kuwa ni mwenendo mwongofu bora mno, na jifundisheni Qur’an kwa kuwa hiyo ni maongezi mazuri zaidi, na jitahidini kuifahamu kwa kuwa ni chanuo la nyoyo.”
Je, Yule mwenye kustahili hukumu ya adhabu ni sawa na yule aliyeokolewa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Je, wewe Muhammad unaweza kumwokoa aliyomo Motoni?
Hapana! Hakuna wasila wowote wa kuokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu ila matendo mema na msamaha wa Mwenyezi Mungu, iliyotukuka hekima yake. Hapana mwenye shaka kwamba mwenye kuzama katika upotevu, Mwenyezi Mungu hatamwangalia: “Hao hawatakuwa na sehemu yoyote akhera, wala Mwenyezi Mungu hatasema nao wala hatawatazama siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao watapata adhabu iumizayo. Juz. 3 (3:77).
Lakini waliomcha Mola wao watapata ghorofa zilizojengwa juu ya ghorofa; chini yake hupita mito. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake.
Hii ndio ahadi ya Qur’an – kukutanisha bishara na onyo, ahadi na kiaga, kuwataja wenye takua na thawabu zao na kuwataja mataghuti na adhabu yao. Hawa wana vivuli vya moto na wale wana ghorofa za pepo. Hii ni ahadi yake Mwenyezi Mungu Mtukufu; na ninani mkweli wa maneno zaidi ya Mwenyezi Mungu?
Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni. Kisha akayapitisha yakawa chemchem katika ardhi?
Mvua inashuka kutoka mbinguni na kutirizika juu aya ardhi, kisha maji yananyonywa ndani ya ardhi, yanakuwa chemchem na kuwanufaisha watu. Je, hii yote ni sadfa au ni mipangilio ya Mjuzi Mwenye hekima?
Kisha kwa maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbali mbali.
Je, mimea hii yenye rangi na ladha tofauti imetengenezwa na maumbile asili au ni kwa msaada wa Aliyetengeneza hayo maumbile asili na yaliyo ndani yake?
Kisha hunyauka ukaiona imekuwa kimanjano.
Baadae mimea hunyauka na kuwa manjano inapokomaa; kisha huifanya imevunjikavunjika.
Baada ya kukauka.
Bila ya shaka katika hayo kuna ukumbusho kwa wenye akili.
Katika kuteremshwa mvua, kuoteshwa mimea, kuwa kijani kisha kuwa njano, kisha kuvunjikavunjika kulingana na hekima na masilahi. Yote hayo ni ukumbusho wa muumbaji na mwanzilishaji.
Ikiwa haya yote yametokana na maji na mchanga, basi ni nani aliyeyaleta hayo maji, mchanga na ulimwengu kwa ujumla?
Tazama: Kifungu ‘Uhai umetoka wapi?’ katika Juz. 7 (6:95 – 99) na kifungu ‘Roho inatokana na amri ya Mola wangu’ katika Juz. 15 (17:62 – 85).
27
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
أَفَمَن شَرَحَ اللَّـهُ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ فَهُوَ عَلَىٰ نُورٍ مِّن رَّبِّهِ فَوَيْلٌ لِّلْقَاسِيَةِ قُلُوبُهُم مِّن ذِكْرِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢٢﴾
22. Je! Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfungulia kifua chake kwa Uislamu, na akawa kwenye nuru itokayo kwa Mola wake, Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisizomkumbuka Mwenyezi Mungu! Hao wamo katika upotofu wa dhahiri.
اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ ﴿٢٣﴾
23. Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana. Chenye kuelezewa mara mbili mbili. Husisimka kwacho ngozi za wenye kumhofu Mola wao. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoza amtakaye. Na ambaye amepotezwa na Mwenyezi Mungu, basi hana wa kumwongoza.
أَفَمَن يَتَّقِي بِوَجْهِهِ سُوءَ الْعَذَابِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَقِيلَ لِلظَّالِمِينَ ذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ ﴿٢٤﴾
24. Je! Ajilindae uso wake na adhabu mbaya Siku ya Kiyama. Na wataambiwa wenye kudhulumu: Onjeni hayo mliyokuwa mkiyachuma!.
AMBAYE MWENYEZI MUNGU AMEMFUNGULIA KIFUA CHAKE KWA UISLAMU
Aya 22 – 24
MAANA
Je! Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfungulia kifua chake kwa Uislamu, na akawa kwenye nuru itokayo kwa Mola wake, ni sawa na mwenye moyo mgumu?
Mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu humtosha na mwenye kutafuta uongofu humwongoza. Mwenyezi Mungu akiona kheri kutoka kwa mja na kwamba yeye anataka kuijua haki na kuitumia, basi Mwenyezi Mungu humshika mkono na kumwongoza na humjaalia ubainifu kwenye jambo lake:
وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الْآخِرَةِ نُؤْتِهِ مِنْهَا ﴿١٤٥﴾
“Na anayetaka malipo ya dunia tutampa humo na anayetaka malipo ya akhera tutampa huko” Juz. 4 (3:145).
Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisizomkumbuka Mwenyezi Mungu!
Pamoja na mawaidha, hadhari na bishara, lakini nyoyo zao zimesusuwaa na wala hazikuelekea kwenye uongofu.
Hao wamo katika upotofu wa dhahiri na adhabu ya kufedhehesha.
Amesema Al-Hafidh Muhammad Bin Ahmad Al-Kalabiy, katika kitabu Attas-hil liulumittanzil: “Imepokewa kwamba ambaye amefunguliwa kifua chake kwa Uislamu ni Ali bin Abu Talib na Hamza; na mwenye moyo mgumu ni Abu Lahab na watoto wake”
Kisha Mwenyezi Mungu ameisifu Qur’an kwa sifa zifuatazo:-
1.Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, katika itiakadi yake, sharia yake, mawaidha yake, hekima zake, misingi yake na mafunzo yake yote.
2.Kitabu chenye kufanana kimfumo wala hakuna mgongano katika maana yake, kwa sababu kinatoka kwa Mwenye hekima aliye Mjuzi.
3.Chenye kuelezewa mara mbili mbili; yaani hukumu zake na mawaid- ha yake huja mara mbili mbili – kinachanganya kuamrisha na kukataza, ahadi na kiaga nk. Katika Kitabu ‘Annuwatu fi haqlil hayat’ cha Sheikh Al-Abidy anasema: “Katika Qur’an kuna Sura za kufanana na kinyume chake; kisha inavuma kwako, katika yanayohusiana na ubora, kwa sauti ya kuam- risha ya upole. Na katika yanayohusiana na ubaya kwa sauti ya mwenye kukemea mwenye nguvu. Na ndani ya Qur’an kuna tulizo la mwenye kuabudu na karipio la kiongozi. Imesemekana kuwa makusudio ni kukaririwa. Kwa vyote iwavyo, makusudio ya neno mathani hapa, sio kama ile iliyoko Juz. 14 (15:87).
4.Husisimka kwacho ngozi za wenye kumkhofu Mola wao . Hiki ni kinaya cha hofu ya waumini wanaposikia kiaga cha Mwenyezi Mungu na tishio la Moto. Mfano wake ni kama kauli ya Imam Ali(a.s ) :“Wao na mtoto ni kama waliouona wakiwa ndani wanaadhibiwa.”
5.Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Kinaya cha kutulia kwao wanaposikia ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara yake ya neema: Imam Ali(a.s ) anasema:“Wao na Pepo ni kama waliyoiona wakiwa ndani wakineemeshwa.”
Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoza amtakaye. Na ambaye amepotezwa na Mwenyezi Mungu, basi hana wa kumwongoza.
Je! Ajilindae uso wake na adhabu mbaya Siku ya Kiyama ni sawa na asiyejilinda? Sio sawa yule iliyemvaa adhabu mpaka unyayoni na yule aliye katika amani. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja uso kwa vile ndio kiungo kitukufu kwa mtu na kinachompambanua na wengine.
Na wataambiwa wenye kudhulumu: Onjeni hayo mliyokuwa mkiyachuma!
Sawa na “Kama utakavyofanya nawe utafanyiwa, utavuna utakachopanda na ulichokifanya leo kitakufanya kesho,” kama alivyosema Imam Ali(a.s ) .
كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٢٥﴾
25. Waliokuwa kabla yao walikadhibisha, na ikawajia adhabu kutoka pahali wasipo patambua.
فَأَذَاقَهُمُ اللَّـهُ الْخِزْيَ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٢٦﴾
26. Basi Mwenyezi Mungu akawaonjesha hizaya katika uhai wa duniani. Na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi; laiti wangelijua!
وَلَقَدْ ضَرَبْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ لَّعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٧﴾
27. Na hakika tumewapigia watu kila mifano katika hii Qur’an ili wapate kukumbuka.
قُرْآنًا عَرَبِيًّا غَيْرَ ذِي عِوَجٍ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٢٨﴾
28. Qur’an ya Kiarabu isiyo na upogo, ili wawe na takua.
ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلًا فِيهِ شُرَكَاءُ مُتَشَاكِسُونَ وَرَجُلًا سَلَمًا لِّرَجُلٍ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا الْحَمْدُ لِلَّـهِ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٩﴾
29. Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye washirika wanaohitalifiana, na wa mtu mwengine aliyehusika na mtu mmoja tu. Je! Wako sawa kiufananishi? Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu! (Alhamdu lillahi) Lakini wengi wao hawajui.
إِنَّكَ مَيِّتٌ وَإِنَّهُم مَّيِّتُونَ ﴿٣٠﴾
30. Kwa hakika wewe utakufa, na wao watakufa.
ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ ﴿٣١﴾
31. Kisha hakika mtahasimiana Siku ya Kiyama mbele ya Mola wenu.
QUR’ANI YA KIARABU ISIYOKUWA NA UPOGO
Aya 25 – 31
MAANA
Waliokuwa kabla yao walikadhibisha, na ikawajia adhabu kutoka pahali wasipopatambua. Basi Mwenyezi Mungu akawaonjesha hizaya katika uhai wa duniani. Na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi; laiti wangelijua!
‘Kabla’ yao ni kabla ya hao washirikina wa Makka waliomkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) . Aya inawambia kuwa mnamkadhibisha Muhammad na wala hampati mazingatio kwa kuanangamia umma zilizopita kutokana na kukadhibisha kwao Mitume wao? Maana haya yamekaririka kwenye Aya nyingi; ikiwemo ile ya Juz. 8 (6:148).
Na hakika tumewapigia watu kila mifano katika hii Qur’an ili wapate kukumbuka.
Qur’an imekusanya mafunzo ya kuwalea watu kwa maisha mema na ya amani, katika kila zama na kila mahali. Imewabainishia yaliyo na heri na masilahi na ikawaamuru kuyafanya hayo. Na ikawabainishia yaliyo na shari na ufisadi na ikawakataza kuyafnya. Imefanya hivyo kwa mifumo mbali mbali na mifano iliyowazi ili waweza kupata mawaidha na wanyooke sawasawa.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 15 (18:54) na Juz. 21 (30:58)
TARJUMA YA QUR’AN
Qur’an ya Kiarabu isiyo na upogo, ili wawe na takua.
Qur’an ni ya kiarabu kilugha na ni ya watu wote kidini na kimsingi, haina mpaka wa wakati au mahali wala haibagui rangi au taifa:
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾
“Na hatukutuma ila kwa watu wote, uwe mtoaji bishara na muonyaji, lakini watu wengi hawajui.” Juz. 22 (34:28).
Imenyooka haiko kombokombo, kwa sababu inatoka kwa Mjuzi Mwenye hekima, ikilenga kuwaongoza watu kwenye njia ya haki iliyo sawasawa. Umetangulia mfano wake katika Juz. 12 (12:2), Juz.13 (13:37) na Juz. 16 (20:113).
Unaweza kuuliza : Je, inajuzu kutarjumu Qur’an kwenye lugha nyinginezo? Kama inajuzu, je, tarjuma itakuwa na hukumu ya Qur’an, kwamba isi- guswe bila twahara?
Jibu : Hakuna shaka wala wasiwasi wowote kuhusu kutarjumu Qur’an kwenye lugha zote; bali hilo linatakikana litilwe mkazo, kwa sababu Qur’an ni risala ya Mwenyezi Mungu kwa watu wote, na tarjuma ni kazi ya msingi ya kueneza risala ya Mungu na kuieneza.
Kuna jamaa wengi wamesilimu au wamefahamu hakika ya Uislam kupitia tarjuma ya Qur’an. Ni hivi karibuni tu alisilimu msichana wa kingereza, msomi, baada ya kusoma tarjuma ya Qur’an kwenye lugha yake. Tazama kifungu cha ‘msichana wa kingereza na Uislamu,’ kwenye Juzuu hii.
Kwenye jarida la Arribat la mwezi January 1979, imeelezwa kuwa mpaka sasa Qur’an imetarjumiwa kwenye lugha 27 na tarjuma.
Hakuna shaka kwamba tarjuma ya Qur’an haina hukumu ya Qur’an kwa sababu zifuatazo:-
Kwanza : Kiarabu ndio mhimili wa Qur’an:
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا ﴿٢﴾
“Hakika sisi Tumeiteremsha Qur’an kwa kiarabu” Juz. 12(12:2).
Pili : tarjuma sio Qur’an hasa, bali ni maana ya Qur’an. Kwa maneno mengine ni kuwa Qur’an ni fasihi ya kiarabu na maana yake ya kiuhakika. Kwa hiyo hakuna Qur’an bila ya kiarabu; bali inabaki ni kitu kingine tu. Kwa hiyo hukumu ya tarjuma ya Qur’an, ni sawa na hukumu ya tafsiri yake.
Hata hivyo hukumu ya jina la Mwenyezi Mungu na sifa zake ni hukumu ya Qur’an hasa, inakuwa haramu kugusa kwa lugha yoyote itakayokuwa.
Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye washirika wanaohitalifiana, na wa mtu mwengine aliyehusika na mtu mmoja tu. Je! Wako sawa kiufananishi?
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amepiga mfano huu kwa washirikina wa waliokadhibisha risala ya Muhammad(s.a.w. w ) . Ufafanuzi wake ni kuwa mshirikina anayeabudu waungu wengi ni sawa na mtumishi aliyemilikiwa na watu mbali mbali waliotofauti katika rai na hulka, hawaafikiani kwenye jambo lolote.
Kila mmoja anataka mtumishi atekeleze analolitaka yeye linalotofautiana na wenzake. Mtumishi naye hawezi kutekeleza matakwa ya kila mmoja na kumridhisha; wakati huo huo hataki kuwaudhi wote. Kwa hiyo siku zote anakuwa hajui afanye nini.
Ama mumin mwenye kumpwekesha Mungu mmoja anafanana na mtumishi aliyemilikiwa na mtu mmoja, wala hataki kumridhisha mwingine asiyekua bwana wake anayempangilia katika anayomwamuru na anayomkataza. Kila mmoja ana raha na mwenzake.
Bwana hamkalifishi mtumishi wake asiloliweza na mtumishi anamsikiliza na kumtii huku moyo wake ukiwa umetulia, kwa vile ana uhakika wa kumridhisha bwana wake.
Je, mtu huyu anayehusika na bwana mmoja tu Mwenye hekima na wala hamnyenyekei yeyote isipokuwa yeye tu na mtu yule mwenye mabwana wengi anayetaka kuwaridhisha wote, wako sawa? Hapana!
أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٣٩﴾
“Je, waungu wengi wanaofarikiana ni bora au Mwenyezi Mungu mmoja mwenye nguvu? Juz. 12 (12:39).
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu! (Alhamdu lillahi) ambaye ametia nguvu dini na Mtume wake kwa nguvu za hoja na ubainifu unaofafanua na akawadhalilisha maadui zake wabatilifu, wakarudi nyuma wakiwa vichwa chini.
Lakini wengi wao hawajui.
Kwamba mshirikina ni kama mtumishi mwenye kumilikiwa na wachungaji wengi.
Kwa hakika wewe –Muhammad -utakufa, na wao watakufa.
Kwa sababu mauti ndio mwisho wa uhai wa kila mtu, awe Nabii au sio Nabii, wala hakuna atakayebakia isipokuwa dhati yake tukufu. Lakini maadui wa Muhammad(s.a.w. w ) watakufa kifo cha kikafiri na cha kijahili; haitabaki athari yao isipokuwa laana na matusi. Ama risala ya Muhammad(s.a.w. w ) itadumu wakati wote na jina lake linakutanishwa na rehema na amani mpaka Siku ya Mwisho.
Kisha hakika mtahasimiana Siku ya Kiyama mbele ya Mola wenu.
Makusudio ya kuhasimiana hapa ni kuwa Nabii(s.a.w. w ) atatoa ushahidi mbele ya Mwenyezi Mungu, Siku ya Kiyama, kuwa yeye amewafikishia risala ya Mola wao: “Na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hawa. Juz. 14 (6:89).
SHARTI YA KUCHAPA
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
MWISHO WA JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
YALIYOMO
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 1
IMEANDIKWA NA: SHEIKH MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYA 1
IMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HASAN MWALUPA 1
IMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED 1
IMEPANGWA KATIKA KOMPYUTA NA: UKHT PILI RAJABU 1
UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI 1
MAKOSA YA CHAPA 2
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 3
UTWAHARA WA AHLUL BAYT 3
MAANA 3
AHLUBAYT (WATU WA NYUMBA YA MTUME) 4
WANAUME NA WANAWAKE WANAOHIFADHI MIPAKA YA MWENYEZI MUNGU 6
MAANA 6
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 8
KISA CHA ZAINAB BINT JAHSH 8
JE, MTUME ALIMTAMANI ZAINAB BINT JAHSH? 8
MAANA 10
KWA NINI UTUME ULIISHIA KWA MUHAMMAD? 12
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 15
NDIYE ANAYEWAREHEMU 15
MAANA 15
TUMEKUHALALISHIA WAKE ZAKO 18
MAANA 18
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 21
MKISHAKULA TAWANYIKENI 21
MAANA 21
MSWALIENI MTUME 23
MAANA 23
VIPI TUTAMSWALIA MTUME? 24
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 26
WAJIBU WA HIJABU 26
LUGHA 26
MAANA 26
VITA VYA NAFSI 27
WANAKUULIZA KUHUSU SAA 28
MAANA 28
TULIZITOLEA AMANA 30
MAANA 30
MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA TATU: SURAT AL-AHZAB 31
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 32
SIFA NJEMA ZOTE NI ZA MWENYEZI MUNGU 32
MAANA 32
WANAOPINGA SIKU YA MWISHO 34
MAANA 34
DAUD NA SULEIMAN 35
MAANA 35
KUPINGA FIKRA YA KIDINI 37
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 39
SABAA 39
LUGHA 40
KISA KWA UFUPI 40
MAANA 40
SEMA WAITENI MNAODAI KUWA NI WAUNGU 43
MAANA 43
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 46
HAWATAAMINI QUR’AN 46
MAANA 46
WAPENDA ANASA 49
MAANA 49
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 51
NINAWAPA MAWAIDHA KWA JAMBO MOJA TU 51
MAANA 51
WATAIPATA WAPI? 54
MAANA 54
MWISHI WA SURA YA THELATHINI NA NNE: SURAT SABA 54
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 55
SIFA NJEMA NI ZA MWENYEZI MUNGU 55
MAANA 55
WALIKADHIBISHWA MITUME KABLA YAKO 57
MAANA 57
AMALI NJEMA HUIPANDISHA 59
MAANA 59
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 61
BAHARI MBILI HAZIWI SAWA 61
MAANA 62
HAWI SAWA KIPOFU NA MWENYE KUONA 64
MAANA 64
KILA UMMA UNA MTUME 65
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 68
ALIYEJIDHULUMU, ALIYE KATIKATI, NA ALIYETANGULIA KWENYE KHERI 68
MAANA 68
HAWAHUKUMIWI WAKAFA 71
MAANA 71
ANAZIZUIA MBINGU NA ARDHI 73
MAANA 73
ASINGELIMUACHA HATA MNYAMA MMOJA 74
MAANA 74
MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA TANO: SURAT FATIR 75
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 76
WEWE NI KATIKA MITUME 76
MAANA 77
MDUNDO WA NDANI KATIKA QUR’AN 77
WAJUMBE WAWILIA WALIOWAONGEZEWA NGUVU KWA WA TATU 80
MAANA 80
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 84
NAWASIKITIKIA WAJA WANGU 84
MAANA 84
KILA KITU KINA ISHARA 86
MAANA 86
OGOPENI YALIYO MBELE YENU 89
MAANA 89
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 91
WATU WA PEPONI NA WATU WA MOTONI 92
MAANA 92
HATUKUMFUNDISHA MASHAIRI 93
MAANA 93
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 96
MIKONO YA MWENYEZI MUNGU NDIO DESTURI YA ULIMWENGU NA MAUMBILE 96
MAANA 96
AKASEMA NI NANI ATAKAYEIHUISHA MIFUPA? 98
MAANA 98
MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA SITA: SURAT YASIN 99
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 100
WANAOJIPANGA SAFU 100
MAANA 100
MWENYEZI MUNGU NA KUAPA NA VIUMBE VYAKE 101
BALI UNASTAAJABU, NA WAO WANAFANYA MASKHARA 104
MAANA 104
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 107
WATAKABILANA WAO KWA WAO 107
MAANA 107
JUU YA VITANDA WAMEELEKEANA 109
MAANA 109
WANAWAKE NA WATUMISHI 110
KWA MFANO WA HAYA NAWAFANYE WAFANYAO 112
MAANA 112
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 114
WALIPOTEA KABLA YAO WATU WENGI WA ZAMANI 114
MAANA 114
SAM, YAFITH NA HAM 115
IBRAHIM ALIKUWA KATIKA KUNDI LAKE 117
LUGHA 117
MAANA 117
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 120
NIMEONA USINGIZINI KUWA NINAKUCHINJA 121
MAANA 121
JE, DHABIHU ALIKUWA ISMAIL AU IS-HAQ? 122
MAANA 124
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 126
LUT NA YUNUS 126
MAANA 127
ATI MOLA WAKO ANA WATOTO WA KIKE NA WAO WANA WATOTO WA KIUME? 129
MAANA 129
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 131
NYINYI NA MNAOWAABUDU 131
MAANA 131
JESHI LETU NDILO LITAKALOSHINDA 133
MAANA 133
MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA SABA: SURAT AS-SAFFAT 134
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 135
NAAPA KWA QUR’AN YENYE MAWAIDHA 135
MAANA 136
KUMWIGA MWENYE KUMPWEKESHA MUNGU NA KUMWIGA MSHIRIKINA 136
SUBIRI JUU YA HAYO WANAYOSEMA 138
MAANA 139
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 141
KONDOO 99 KWA KONDOO 1 141
TAFSIRI NA HADITH ZA KIISRAIL 141
MAANA 142
TUMEKUFANYA UWE KHALIFA ARDHINI 144
MAANA 144
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 147
SULEIMAN 147
MAANA 147
AYYUB 150
MAANA 150
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 152
WENYE TAKUA NA WALIOPETUKA MIPAKA 153
MAANA 153
MIMI NI MUONYAJI TU 156
MAANA 156
UISLAMU NA MSICHANA WA KINGEREZA 156
MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA NANE: SURAT SAAD 159
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 160
DINI SAFI NI YA MWENYEZI MUNGU TU! 160
MAANA 160
HUUFUNIKA MCHANA JUU YA USIKU 162
LUGHA 162
MAANA 162
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 165
HADHARI YA AKHERA NA MATARAJIO YA REHEMA YA MOLA 165
MAANA 166
Hata Manabi Wana Shauku Na Hofu 166
WANAOSIKILIZA MANENO WAKAFUATA MAZURI YAKE 169
MAANA 169
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 171
AMBAYE MWENYEZI MUNGU AMEMFUNGULIA KIFUA CHAKE KWA UISLAMU 171
MAANA 171
QUR’ANI YA KIARABU ISIYOKUWA NA UPOGO 173
MAANA 173
TARJUMA YA QUR’AN 173
SHARTI YA KUCHAPA 175
MWISHO WA JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA 175
YALIYOMO 176
[1] . Aliyewahi kuwa mtumwa kisha akawa huru.
[2] . Mateka kwa kiarabu ni sabaya.
[3] . ‘Unaweza kulala maskini ukaamka tajiri’ – Msemo wa kiswahili.
[4] . Katika kufasiri kufasiri neno Twariyya, nimetohoa neno hilo la kiingereza Fresh ambalo linatumika sana kwenya kiswahili cha mitaani; kama walivyotohoa kwenye kiswahili sanifu wakapata neno fremu n.k. –Mtarjumu.
[5] . Neno alipomkurubia limefasiriwa kimaana kutoka neno la kiarabu ‘taghashaha’ tarjuma yake ni alipomfunika. Kwa hiyo mwandishi hapa anasifia jinsi Qur’an ilivyotumia neno kufunika katika tendo la kuonana mume na mke – Mtarjumu.
[6] . Neno mashariki ni la kiarabu lenye maana ya matokeo ya jua (mawiyo) na magharibi ni machweo – Mtarjumu.
[7] . Ndio maana wafasiri wengi wa Kiswahili wamelifasiri neno hilo kwa ‘karibu’ wakimaanisha karibu yetu sisi. – Mtarjumu.
[8] . Mungu wa mahaba na vita. Wagiriki wanamwita Aphrodite–Mtarjumu.
[9] . Qur’an (23:12).
[10] . Qur’an (77:21 – 22).
[11] . Nahjulbalagha hotuba 163.
[12] . Kauli hii ni ya zamani na watu wameachana nayo, lakini Mustafa Mahmud ametaka kuijibu kwa makala aliyoisambaza kwenye gazeti la Sabhul-khayr la 22-1-1970.