AKIDA

Mwandishi: Sayyid Ali Khamenei
Misingi mikuu ya Dini

AKIDA

MSAMIATI

Adilisha: tendea haki, wema na uadilifu.

Daawa: utangazaji wa mafundisho ya dini ya Kiislamu;

Tablighi: Uhubiri.

Mwanadaawa: mtu anayetangaza mafundisho ya dini ya Kiislamu;

Mubalighi; mhubiri.

Dhahania: mawazo.

hasi: -a kukana; -a kinyume kabisa.

Irfani: mafundisho au imani inayohusiana na maarifa ya hakika ya Mwenyezi Mungu yapatikanayo kwa njia ya mtu kujisahau nafsi yake na kumwabudu Mwenyezi Mungu tu; usufii; uwalii.

Maada: asili au dhati ya kila kitu; meta.

Maadili: (elimu inayohusiana na) tabia njema au mwenendo sahihi wa mtu; akhlak.

Hekima, kauli; fani ya utumiaji wa akili.

Maono: fikra, ufahamu au uonaji wa kimoyomoyo (wa dini moja au mfumo mmoja wa kiitikadi) juu ya ulimwengu mzima,viumbe na vitu; nadharia.

Metafizikia: elimu ihusikanayo na asili ya mwanzo wa uhai, Uungu, n.k.

Nara: matamko mafupi au mwito maalum wa kikundi cha watu, chama au dini ambao unatolewa aghlab katika medani za vita, mikutano, misafara, n.k. kwa lengo la kutia shime, kuhamasisha au kutangaza shabaha yake, n.k. Pia shaari.

Radiamali: jambo au kitendo kinachofanywa kurudia kitendo fulani kilichotendewa.

Shaari:taz.nara.

Shirki: hali ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kiumbe au kitu chochote katika ibada, uumbaji na tadbiri Yake ya ulimwengu; ushirikina.

Stadhaafika:kuwa katika hali ya kukandamizwa kiuchumi, kisiasa, kiitikadi au kitamaduni.

Ustadhaafu: hali ya kustadhaafika.

Mustadhaafu:(wastadhaafu/mustadhaafina): mtu mwenye kukandamizwa kiuchumi, kisiasa, kiitikadi au kitamaduni; mnyonge; mwenye kudhoofishwa au kustadhaafishwa.

Takabari (stakabari); fanya jeuri au kiburi na kuona wengine si kitu; kandamiza watu kiuchumi, kisiasa, kiitikadi au kitamaduni. Utakabari (ustakabari): hali ya kutakabari au kustadhaafisha. Mtakabari/mstakabari (watakabari/ was-takabari): mtu mwenye kukandamiza watu kiuchumi, kisiasa, kiitikadi au kitamaduni.

Taghuti:(ma-) kitu au kiumbe ambacho ni sababu ya uasi au uvunjaji wa sheria za Mwenyezi Mungu, k.v. miungu, masanamu, mashetani, viongozi madhalimu, utawala wa haramu, n.k.; mtu yeyote anayefuatwa bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu; mtu anayependelea mambo yenye kukiuka mipaka (sheriaya Mwenyezi Mungu).

Tasnifu: ithibati (thesis).

Tawhidi:Umoja na Upweke wa Mwenyezi Mungu katika dhati, sifa, vitendo na ibada Zake.


UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu

Ndugu Msomaji ! Kitabu ulichonacho mkononi mwako kimetafsiriwa na mfasiri wetu mmoja.

Taasisi hii ya Fikra za Kiislamu imo katika jitahada za kutafsiri na kuchapisha vitabu vya maarifa na utamaduni wa Kiislamu katika lugha mbalimbali za dunia ili viwe mwongozo katika maisha ya mashaka ya ndugu zetu ambao ni viungo vya kiwiliwili kimoja cha Uislamu; na vilevile viwe ni mnara wa baharini wenye kuwamulika wasio Waislamu ambao wametweka tanga zao kukata mawimbi ya bahari ili kutafuta ukweli, au viwe kama motisho kuzidisha raghba ya msomaji. Tunataraji kwamba jitahada zetu za kidhati zitajibu maswali yanayowatatiza wasomaji wetu. Kwa hakika tumeangalia kwamba vitabu tunavyochagua kuchapishwa vimeandikwa na waandishi mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu.

Huenda unaelewa kwamba utamaduni wa Kiislamu na fasihi yake umetajirika kwa maneno mahsusi na ya asili kwa sababu chemchemi yake ambayo ni Qur'ani, Kitabu cha Mwenyezi Mungu - hububujisha maneno hayo na kuufurisha. Kwa hivyo, huwa ni vigumu kuyazuia mafuriko hayo katika maziwa ya lugha nyinginezo. Inatubidi tuchimbe mifereji kadhaa ili kupunguza uzito na kuhifadhi mito. Na hilo ndilo tulilolifanya. Wakati wowote tulipoona kwamba haiwezekani kutumia neno fulani na wakati huohuo likatoa maana hasa iliyokusudiwa katika lugha ya asili ya Kiarabu na katika istilahi ya Qur'ani, hapo tukatumia neno lake laasili na kulifafanua katika ukurasa wa msamiati na istilahi. Kwa njia hii, utaelewa vizuri maudhui na ujumbe uliokusudiwa katika kitabu hicho, na kwa wakati huohuo utatajirisha msamiati wako wa Kiislamu.

Mwishowe, tunakuomba ukisome kwa makini kitabu hiki ambacho maudhui yake ni msingi muhimu na wa kwanza wa dini ya Kiislamu, nao ni Tawhidi - kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Somo la Tawhidi linaweza kujadiliwa kwa mapana na marefu katika kila kipengee, lakini Sayyid Ali Khamenei, mwandishi wa kitabu hiki, ameashiria baadhi tu ya vipengee vya kijamii, kiuchumi na kisiasa ambavyo tunaamini kwamba havikujadiliwa vya kutosha katika mihafala ya Afrika Mashariki.

Kama kuna makosa yoyote humu ni yetu wenyewe na wala si ya mwandishi; hivyo, tunawaomba wasomaji watuonyeshe ili tuweze kusahihisha katika chapa nyingine.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu awaunganishe Waislamu wote duniani. Amin.

TAASISI YA FIKRA ZA KIISLAMU KUHUSU MTUNGAJI

Mtungaji wa kitabu hiki, Hujjatulislam Sayyid Ali Khamenei, amezaliwa tarehe 15 julai 1939 (28 Safar 1358 Hijria) katika mji mtakatifu wa Mashhad, mashariki mwa Iran. Wazazi wake wote wawili wanatokana na koo za wanazuoni. Babake Ayatullah HaJ Sayyid Jawad Khamenei, alikuwa ni miongoni mwa wanavyuoni wachaMungu katika Mashhad.

Mamake alikuwa binti wa mwanachuoni Hujjatulislam Sayyid Hashim Najafabadi.

Akiwa na umri wa miaka minne, aliingia chuoni kusoma Qur'ani na baadaye akasoma na kumaliza shule ya msingi. Alipokuwa akisoma katika shule ya sekondari, alijiunga katika chuo cha kidini cha Nawab. Alipokuwa na umri wa miaka 18 alimaliza masomo ya kati kwa babake na wanavyuoni wengine wa Mashhad, kama vile Marehemu Haj Hashim Qazwini, Haj Sayyid Ahmad Mudarrisi na Marehemu Haj Sayyid Mahmud Damad.

Baada ya hapo, akaanza kuhudhuria darasa za kharij (darasa za juu) za Hawza (Chuo) ya Mashhad. Maustadhi wake walikuwa Marehemu Haj Hashim Qazwini na Ayatu-llah Milani.

Katika mwaka 1957, alikwenda Najaf (lraq) kwa ajili ya kuzuru maziara ya watukufu ambapo alishiriki na kufaidika na darasa za Ayatullah Sayyid Muhsin Hakim, Ayatullah Sayyid Abul Qasim Khui, Ayatullah Sayyid Mahmud Shah-rudi, Ayatullah Aqa Mirza Baqir Zanjani, Ayatullah Mirza Hasan Yazdi na Ayatullah Mirza Yahya Yazdi.

Katika mwaka 1958, aliendelea na masomo yake katika mji wa Qum (Iran) pamoja na Hujjatulislam Hashimi Rafsan-jani, Rais wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

WALIMU WAKE

Walimu wake walikuwa: Marehemu Ayatu-llah Burujerdi na Imam Khomeini ambaye wakati huo alikuwa akifundisha falsafa katika Madrasa ya Fayziyyah.

Hujjatulislam Khamenei alisomafalsafa ya Mandhumah ya Haj Mulla Hadi Sabziwari kwa Marehemu llyasi na Haj Mirza Jawad Aqa Tehrani. Alisoma kwa Marehemu Ayatullah Allamah Tabatabai faslu kadhaa za vitabu vya kifalsafa vya Asfaar na Shifaa; pia alisoma kwa Ayatullah Muntadhari sehemu ya vitabu vya kifalsafa vya Asfaar na Sharh /shaaraat.

Wakati harakati za kisiasa za maulamaa (wanavyuoni) zilipoanza katika mwaka 1962, Hujjatulislam Khamenei alikuwa miongoni mwao pia. Alishiriki katika harakati za mwaka 1963 zilizoongozwa na Imam Khomeini dhidi ya utawala wa Shah wakati askari wa Shah walipoishambulia Madrasa Fayziyyah mjini Qum. Alikamatwa akiwa na risala ya Imam Khomeini aliyomwandikia Ayatullah Milani kuhusu mauaji ya siku ya Ashura. Kwa jumla, Hujjatulislam Khame-nei alikamatwa na kutiwa ndani mara saba kati ya mwaka 1963 na 1978. Alikamatwa katika mji wa Birjand mahali ambapo Asadullah Alam, Waziri Mkuu wa Shah alipokuwa na nguvu kubwa na mahali ambapo Shah alikuwa akistarehe katika mkoa wa Khurasan. Vilevile alikamatwa katika mji wa Zanjan na akabaidishwa katika mji wa Iranshahr kwa muda mrefu.

Wakati mmoja alianzisha chama cha siri cha Kiislamu, na kilipogunduliwa akakamatwa yeye pamoja na Ayatullah Muntadhari na Marehemu Ayatullah Rabbani Shirazi. Lakini Khamenei aliweza kukimbia jela yeye pamoja na wengine, na akarejea Mashhad katika mwaka 1965. Vifungo hivyo

vya ndani na vya kuhamishwa vilimpatia uzoefu mzuri na kuimarisha harakati zake za Mapinduzi ya Kiislamu. Alitumia fursa ya kuwepo. kifungoni kwa kufasiri Qur'ani Tukufu na kufundisha maarifa ya Kiislamu pamoja na kuandika na kufasiri vitabu kadhaa. Darasa zake za tafsiri ya Qur'ani ziliwavutia sana vijana.

Katika mwaka 1978, yeye pamoja na mashekhe wanaharakati wenzake waliunda Jumuiya ya Wanavyuoni Wakakamavu.

Wakati Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini alipokuwa uhamishoni mjini Paris (Ufaransa), alimteua Hujjatul islam Khamenei kuwa ni mwanachama wa Baraza la Mapinduzi; na baada ya kuundwa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliteuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi katika jeshi, na msaidizi wa mambo ya kimapinduzi katika Wizara ya Ulinzi.

Katika mwaka 1980, Imam Khomeini alimteua Sayyid Ali Khamenei kuwa mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi (Pasdar) na Imamu wa Ijumaa waTehran.

Katika uchaguzi wa kwanza wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge), Khamenei alichaguliwa kuwa mwakilishi (mbunge) wa wakazi wa Tehran na katika mwaka huohuo, Imam Khomeini alimteua kuwa mwakilishi wake katika Baraza Kuu la Ulinzi.

Yeye ni miongoni mwa waanzilishi wa Chama cha Jamhuri ya Kiislamu (Hizbe jamhuriye Islami), na kitabu chake kiitwacho Msimamo Wetu alichokiandika pamoja na Hujjatul-islam Hashimi Rafsanjani kimetumika kuratibu sera ya chama hicho. Sasa ni Katibu Mkuu wa tatu wa chama hicho, na mchapishaji wa gazeti la chama liitwalo jamhuriye Islami.

Mnamo tarehe 27 Julai 1981, wakati Hujjatulislam Sayyid Ali Khamenei alipokuwa akitoa mawaidha baada ya kusalisha sala ya jamaa katika Msikiti wa Abu Dhar, alijeruhiwa sana kwenye mkono na kifua wakati bomu lililokuwa limetegwa na wanafiki katika tepurikoda lilipo ripuka juu ya meza aliyokuwa akihutubia.

Katika uchaguzi wa tatu wa Urais wa jamhuri ya Kiislamu ya Iran uliofanyika katika mwezi wa Oktoba 1981, Khamenei alichaguliwa kuwa Rais kwa asilimia 95 ya kura zote. Katika kipindi cha kwanza cha'miaka minne ya Urais wake, mafanikio mengi yalipatikana ingawa nchi ilikabiliwa na vita na matatizo mengi.

Katika uchaguzi wa nne wa Urais uliofanyika katika mwezi wa Agosti 1985, Hujjatulislam Khamenei alichaguliwa kwa mara ya pili kuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Alishinda kwa kura, 12,203,870 kati ya kura 14,244,630.

Mnamo Septemba 4, 1985, Imam Khomeini aliufawidhi (aliuthibitisha) Urais wa Sayyid Ali Khamenei, na mnamo tarehe 10 Oktoba aliapishwa katika Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu.

Rais Khamenei ni khatibu mahiri, mwandishi hodari, mwanafikra na mwanafasihi. Ameandika na kufasiri vitabu kadhaa katika uwanja wa maarifa ya Kiislamu na historia. Ametarjumi kwa lugha ya Kifarsi (Kiajemi) tafsiri ya Qur'ani ya Shahid Qutb iitwayo Fii Dhilaalil Qur'an.

Hujjatulislam Sayyid Ali Khamenei ameoa binti wa mwanachuoni mmoja katika mwaka 1964 na ana watoto wanne wa kiume na wawili wa kike.

Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu

Siku ambayo Mtume wa Uislamu, Muhammad(s.a.w.w) , alipotangaza mwito (nara) wa : ("Hakuna mungu ila Allah") ili kuwaokoa wanadamu, watu wa kwanza waliosimama kumpinga walikuwa viongozi, wakuu na watu watukufu wa makabila. Mwanzoni, maadui hao walitumia silaha ndogo san a, yaani kumfanyia mzaha na kumtukana, lakini baadaye kila harakati ya Kitawhidi ilipozidi kuimarika na kuratibika, silaha zao pia zikawa kali zaidi. Watu wengine pia walishawishiwa na wapinzani hao, na wakasimama kumpinga na kumfanyia uhasama Mtume Mtukufu na wafuasi wake; na kwa mara nyingine tena mandhari ya kifedheha katika historia iliyokuwepo katika miaka ya kumi na mitatu kabla ya Hijria ikakaririwa.

Uhakika huu wa kihistoria unahitaji kuchunguzwa kwa makini sana kwa ajili ya kuufahamu Uislamu kwa jumla, na hasa Tawhidi ambayo ni kiini cha mafundisho ya Kiislamu.

Katika zama zetu, mojawapo kati ya mambo yenye kusikitisha sana ambalo ni msiba mkubwa kwa zama zetu, ni kupotoshwa maana halisi ya ujumbe wa Mitume wa Mwenyezi Mungu ambayo ni Tawhidi. Kupotoshwa maana ya Tawhidi ni kupotosha msingi halisi wa mafundisho ya dini, kwa sababu hakuna itikadi yoyote nyingine katika historia

nzima ambayo inaweza kwa kadiri hii kuwaokoa watu na kuwakomboa waliokandamizwa.

Kwa kadiri tunavyojua, ujumbe wote wa Mitume ulikusudiwa kuleta mabadiliko ya kimapinduzi kwa faida ya watu, kuwakomboa wanyonge na wanaokandamizwa, na kupinga udhalimu, ubaguzi na uonevu. Kiini cha maadili ya dini zote kuu, kama alivyosema Erich Fromm, ni kuthibitika malengo ya elimu, mapenzi ya kindugu, kupungua shida za watu, uhuru na hisia za majukumu. (Hapana shaka kwamba malengo yaliyo bora zaidi hayawezi kutambuliwa kwa macho ya mchunguzi wa kimaada.)

Malengo yote hayo yanategemea msingi wa Tawhidi. Kwa kupiga nara ya Tawhidi, Mitume walikuwa wakitangaza makusudio na malengo yao yote, na kwa wakati huohuo, kwa kupiga nara hiyo walikuwa wakiandalia mapambano kwa ajili ya kutekeleza malengo hayo katika dunia au kuyakaribia.

Kwa hakika ni jambo la kusikitisha sana, si tu kwa wenye kuitakidi Tawhidi, bali hata kwa wale wote wenye kuyapigania malengo hayo, kuona kwamba katika zama hizi wakati ambapo malengo hayo huhitajika kwa haraka na kwa dharura zaidi - kuna ujinga na upotoshi wa msingi.na maana ya Tawhidi, na kwamba watu hutosheka na tafsiri yake ya juujuu na ya kimawazo tu.

Tumesema kwamba mkabala na upinzani uliokuwepo mwanzoni mwa Uislamu unaweza kufafanua uhakika muhimu wa maana halisi ya Tawhidi.

Uhakika wenyewe ni huu, kwamba shaari (nara) ya Laa ilaaha illallaah - ("Hakuna mungu ila Allah"), kwa hatua ya kwanza, ni pigo zito kwa walewale watu ambao wali-simama kuipinga, yaani tabaka la wenye mamlaka na utawala katika jamii.

Vitendo vya uhasama dhidi ya fikra moja na harakati moja, vinabainisha misimamo yake ya kijamii, kiwango na kina cha taathira zake katika misimamo hiyo. Kwa njia hii, tunaweza kujua misrmamo ya kitabaka na ya kijamii ya harakati hizo kwa kusoma nyuso za maadui wa harakati hizo. Vilevile tunaweza kupima kina na taathira za harakati hizo kwa kuangalia ushadidi na ukali wa upinzani wao.

Kwa sababu hii, njia mojawapo inayoaminika kutumiwa kwa ajili ya kutambua barabara daawa za Mitume, ni kuzichunguza safu za waungao mkono na safu za wapingao harakati hizi.

Tunapoona kwamba tabaka la wenye nguvu na mamlaka katika jamii ni watu wa kwanza waliosimama kupinga dini bila ya kusita hata kidogo katika upinzani wao, hapo ndipo tunapotambua waziwazi kwamba kwa kawaida dini na harakati za kidini zinapinga tabaka hilo. Kimsingi, Mitume walikuwa wakipinga ujeuri na ubepari wao, na nafsi ya tabaka lenyewe ambalo lilikuwa likijitenga mbali na wengine.

lli tuweze kuzingatia suala la Tawhidi katika kipengee hiki cha kuupinga utawala wa kitabaka katika jamii, ni lazima kwanza tujue kwamba kinyume na vile inavyodhaniwa na watu wa kawaida, Tawhidi si nadharia ya kifalsafa na kidhahania peke yake, bali ni nadharia ya kimsingi kuhusu binadamu na ulimwengu, na ni itikadi ya kijamii, kiuchumi na kisiasa pia.

Miongoni mwa istilahi za kidini na zisizo za kidini, ni taabu sana kupata istilahi kama hii iliyojaa maana ya kimapinduzi na kiurekibishaji yenye kuzingatia vipengee mbalimbali vya kimaisha, kijamii na kihistoira vya binadamu. Haikuwa sadfa kwamba miito yote ya Mitume wa Mwenyezi Mungu katika historia nzima ilianzia kwa kutangazwa Upweke na Umoja wa Mwenyezi Mungu na umilikaji Wake Peke Yake.

Ifuatayo ni muhtasari wa vipengee mbalimbali vya maudhui ya Tawhidi:

1) Tawhidi katika Kipengee cha Nadharia juu ya Ulimwengu na Maisha

a) Tawhidi maana yake ni umoja na ufungamano wa ulimwengu mzima na vitu vyote vilivyomo humo.

llivyokuwa mfumo wa uumbaji ni mmoja, na kila kitu kimeanza na kutokana na chanzo na asili moja bila ya kuwepo miungu na waumba wengi tofauti; hivyo, vitu vyote hivyo vinaingia katika mkusanyiko na mfumo mmoja,na ulimwengu mzima ni mmoja, na wote una mwelekeo mmoja.

مَّا تَرَىٰ فِي خَلْقِ الرَّحْمَـٰنِ مِن تَفَاوُتٍ

"Huoni hitilafu yoyote kati'ka uumbaji wa Mwingi wa rehema." (alMulk, 67:3)

أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا فِي أَنفُسِهِم مَّا خَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى

"Je, hawatafakari juu ya nafsl zao? Allah hakuumba mbingu na ardhl, na vlllvyomo baina yao ila kwa [mfumo wa] haki na kwa muda maalum. "(ar-Rum, 30:8).

Kufuatana na mtazamo huu, ulimwengu huonekana kama msafara mmoja ambao wasafiri wake wote hufanya kazi kwa pamoja kuelekea kwenye mahali na lengo moja kama mnyororo ulioshikamanishwa pamoja kwa vikuku na kama vipande vidogo na vikubwa vya mashine. Kila kitu katika mfumo huo hufanya kazi kufuatana na hali na nafasi yake, maana na sababu iliyowekewa. Hivyo, katika mwendo huu wa ukamilifu, kila kitu hukisaidia na kukikamilisha kitu kingine, na vyote ni vitu vya lazima katika mjumuiko huo. Kusimama, kuharibika, kupanguka au kwenda kombo kimojawapo katika vitu hivyo kutasababisha kuharibika, kuparaganyika na kwenda kombo mfumo mzima. Kwa hivyo, ufungamano halisi na wa kiroho wa mfumo

mmoja ndio unao unganisha vitu vyote hivyo.

b) Tawhidi maana yake ni kuwepo shabaha katika uumbaji. Ulimwengu umeumbwa kwa mpango, hesabu na utaratibu maalum; na kila kitu chake kina maana na roho (dhati) pia. llivyokuwa ulimwengu umeumbwa na Muumba Mwenye hekima, hivyo, ni lazima kuwepo hekima, lengo na shabaha katika asili ya kuumbwa kwake kama inavyoonekana katika vitu vingi vya hapa ulimwenguni.

وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ ﴿١٦﴾

"Nu hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yao kwa mchezo [na bila shabaha]." (al-Am- biyaa, 21:16)

Kwa mtazamo huu, hakuna kitu chochote katika ulimwengu kilichoumbwa bila ya kuwa na shabaha au maana yoyote, bali mfano wake ni kama mashine iliyotengenezwa kwa ajili ya kufanya kazi maalum. Tunaweza kuuliza kuhusu shabaha yake, lakini hatuwezi kuuliza kuhusu asili ya shabaha hiyo. Mfano wake ni kama shairi moja la maana ambalo unaweza kulifahamu kwa kuzingatia maana yake, lakini huwezi kulifahamu kwa kutegemea sauti au mizani yake tu.

c) Tawhidi maana yake kubwa zaidi ni kunyenyekea vitu na viumbe vyote vya ulimwengu mbele ya Mwenyezi Mungu. Hakuna kitu chochote katika mkusanyiko huo chenye hiari yake yenyewe. Kanuni zote za ulimwengu (maumbile) na kila kitu kinachofuata kanuni hizo ni lazima kitii, kijitolee na kisalimu amri kwa Mwenyezi Mungu tu.

Kwa hivyo, kuwepo kanuni za kimaumbile katika ulimwengu mzima hakumaanishi kwamba hakuna Mwenyezi Mungu na Muumba wa ulimwengu.

إِن كُلُّ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِلَّا آتِي الرَّحْمَـٰنِ عَبْدًا ﴿٩٣﴾

"Hakuna yeyote aliyemo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Mwingi wa rehema hali ni mtumwa." (Maryam, 19:93)

بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾

"Bali ni vyake vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Vyote vinamnyenyekea Yeye." (al-Bagarah, 2:116)

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٧﴾

"Hawakumheshimu Allah heshima anayostahiki, na (katika) Sfku ya Kiyama ataidhibiti ardhi yote, na mbingu zitakunjwa kwa uwezo Wake. Ameepukana na upungufu na Yu mbali na yale wanayomshirlkishiya." (az-Zumar, 39:67)

2) Tawhidi katika Kipengere cha Uchunguzi na Uamuzi kuhusu Binadamu

a) Tawhidi maana yake ni kwamba: wanadamu wote ni wamoja na ni sawa katika kuhusiana na Mwenyezi Mungu. Yeye ni Mola wa wanadamu wote. Hakuna mtu aliyekuwa na uhusiano mahsusi na Mwenyezi Mungu kwa sababu ya umbile lake la kibinadamu tu, wala hakuna mwenye ujamaa Naye. Yeye si Mungu wa taifa, umma au kabila fulani. Hakuumba wala hakufadhilisha jamii moja kuliko nyingine. Wote ni sawa mbele ya Mwenyezi Mungu. Hakuna mtu mwenye utukufu mahsusi mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kutokana na jitahada zake. Kila mtu anaweza kupata utukufu na fadhila zaMwenyezj Mungu akijitahidi zaidi kutoa huduma njema kwa wanadamu na kwa kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu ambayo ni dhamana ya pekee ya kumtukuza binadamu.

وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا سُبْحَانَهُ بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾

"Wanasema 'Allah amejipangia mwana.' Ameepukana na hilo; bali ni Vyake vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Vyote vina mnyenyekea Yeye. " (al-Baqa-rah, 2:116)

فَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا كُفْرَانَ لِسَعْيِهِ وَإِنَّا لَهُ كَاتِبُونَ ﴿٩٤﴾

"Na atakayefanya vitendo vizuri na hali ni muumini, bas/ haitokataliwa juhudi yake; na kwa hakika Sisi tutamwandiki'a." (al-Ambiyaa, 21:94)

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ ﴿١٣﴾

"Enyi watu! Kwa hakika tumekuunbeni nyote kutokana na mwanamume na mwanamke, na tumekufanyeni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika anae heshimiwa sana miongoni mwenu mbele ya Allah ni yule anayemcha Mungu zaidi katika nyinyi." (al-Hujaraat, 49:13).

b) Tawhidi maana yake ni kwamba wanadamu wote ni wamoja na ni sawa katika kuumbwa kwao na katika asili yao ya ubinadamu. Ubinadamu ni asili moja inayopatikana katika wanadamu wote bila ya kutofautiana. Wanadamu waliogawika katika matabaka mbalimbali ya kijamii si waja wala viumbe wa waungu mbalimbali hata asili na maumbile yao yakatofautiana pia, na matokeo yake ukakuwepo mpaka usiovukika baina yao. Wala hakuna mungu wa tabaka aali (tukufu) aliyekuwa na nguvu zaidi kuliko mungu wa tabaka la chini. Wote ni viumbe wa Mwenyezi Mungu Mmoja, na wote wameumbwa sawa katika maumbile yao ya asili.

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ ...﴿١﴾

"Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja..." (an-Nisaa, 4:1)

c) Tawhidi maana yake ni kwamba wanadamu wote ni sawa na wamoja katika kuweza kujiendeleza na kujikamilisha. Wanadamu wote ni sawa katika asili na maumbile yao ya kibinadamu. llivyokuwa Mwenyezi Mungu Mwenye hekima amempa kila mtu umbile la kibinadamu, hivyo, hakuna mtu yeyote asiyekuwa na uwezo katika dhati na umbile lake wa kufuata njia iliyonyooka na njia ya kujikamilisha. Kwa sababu hii ndiyo maana mwito wa Mwenyezi Mungu ukawa ni kwa watu wote bila ya kuwa ni mahsusi kwa watu, taifa au tabaka fulani. Ingawa mazingira tofauti yanaleta athari tofauti kwa binadamu, lakini athari hasi za mazingira haziwezi kabisa kumfanya binadamu daima awe shetani au malaika, au kumfungia njia ya kujiamulia yeye mwenyewe. Qur'ani inamhutubu hivi Mtume Mtukufu:

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾

"Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui." (Sabaa, 34:28)

"Na tumekutuma kwa watu wote kuwa Mtume." (an-Nisaa, 4:79)

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا ﴿١٧٤﴾ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَاعْتَصَمُوا بِهِ فَسَيُدْخِلُهُمْ فِي رَحْمَةٍ مِّنْهُ وَفَضْلٍ وَيَهْدِيهِمْ إِلَيْهِ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿١٧٥﴾

"Enyi watu! Umekufikieni ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na tumekuteremshieni Nuru iliyo wazi. Ama wale walio muamini Mwenyezi Mungu, na wakashikamana naye, basi atawatia katika rehema yake na fadhila, na atawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka." (An-Nisaa, 174 - 175)

d) Tawhidi maana yake ni kuwakomboa wanadamu wote kutoka katika utumwa n.a unyenyekevu wa yeyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kwa maana nyingine ni ulazima (wajibu) wa kumwabudu Mwenyezi Mungu tu. Tawhidi inapinga mwanadamu kuingia katika utumwa na utiifu usiokuwa wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuzingatia maana pana ya ibada, utumwa huo unaweza kuwa ni wa kifikra, kitamaduni, kiuchumi au kisiasa. Tawhidi inakataza kuishi maisha kama haya ya kujichukulia mtu mwingine kuwa ni mshirika na sawa katika ibada ya Mwenyezi Mungu. Tawhidi humchukulia binadamu kuwa ni mja wa Mwenyezi Mungu tu, na humkomboa kutoka katika utumwa na utiifu wa kila mtu, mfumo au nguvu yoyote ambayo humfanya amshirikishe katika ibada ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, Tawhidi maana yake ni kukubali utawala wa Mwenyezi Mungu tu na kukana na kupinga utawala wowote mwingine usiokuwa wa Mwenyezi Mungu, uwe na sura au umbo la aina yoyote.

إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٤٠﴾

"Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui." (Yusuf, 12:40)

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ﴿٢٣﴾

"Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu...." (al-lsraa, 17:23).

e) Tawhidi maana yake ni kumheshimu na kumthamini binadamu. Umbile tukufu na la fahari la binadamu lina thamani zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu na wala halina haja ya kufanywa mnyonge, dhalili au mtumwa mbele ya yeyote ghairi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu tu Mwenye ukamilifu na jamala mutlaki Ndiye Ambaye anastahiki kuabudiwa na binadamu, kusifiwa na kupendwa. Kutukuza huko ni daraja moja ya mja kupata utukufu.Ghairi ya Dhati Takatifu hakuna kitu wala kiumbe chochote chenye utukufu na hadhi ambayo kwayo inamstahikisha amfanye binadamu kuwa mtumwa wake. Masanamu yote yenye uhai na yasiyo

na uhai ambayo yamejipachika katika fikra, moyo na kiwiliwili cha binadamu na yamechukua kwa nguvu utawala wa Mwenyezi Mungu katika maisha ya binadamu, ni najisi na uchafu unaochafua usafi wa umbile la binadamu. Masanamu hayo humletea binadamu madhila na uduni, hivyo, inambidi ayaangamize na ayasafishe katika ibada yake ili apate kurejesha hadhi yake tukufu. Hakuna mawazo yoyote ya kimaada ya binadamu yaliyoweza kujadili kwa undani na ufasaha utukufu na thamani ya binadamu, kamaTawhidi inavyojadili.

فَاجْتَنِبُوا الرِّجْسَ مِنَ الْأَوْثَانِ وَاجْتَنِبُوا قَوْلَ الزُّورِ ﴿٣٠﴾حُنَفَاءَ لِلَّـهِ غَيْرَ مُشْرِكِينَ بِهِ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَانٍ سَحِيقٍ ﴿٣١﴾

"Basi jiepusheni na uchafu wa masanamu na maneno ya uwongo; mhalisike kwa Allah bila kumshirikisha. Na anae mshirikisha Allah basi ni kana kwamba ameanguka kutoka mbinguni k'isha ndege [tai] wakamnyakua au upepo umemtupa mahali pa mbali." (al-Hajj, 22:30, 31)

لَّا تَجْعَلْ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَقْعُدَ مَذْمُومًا مَّخْذُولًا ﴿٢٢﴾

"Usimfanye mungu mwingine pamoja na Allah, usije ukawa mwenye kushutumiwa (na) kutupwa." (al-lsraa, 17:22)

ذَٰلِكَ مِمَّا أَوْحَىٰ إِلَيْكَ رَبُّكَ مِنَ الْحِكْمَةِ وَلَا تَجْعَلْ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتُلْقَىٰ فِي جَهَنَّمَ مَلُومًا مَّدْحُورًا ﴿٣٩﴾

"Wala usimfanye mungu mwingine pamoja na Allah, usije kutupwa katika jahannam hali ya kuwa mwenye kulaumiwa (na) mwenye kufukuzwa." (al-lsraa, 17:39)

f) Tawhidi maana yake ni ulinganifu na umoja baina ya maisha ya binadamu na kuwepo kwake. Maisha ya binadamu yamefanyika kwa dhamiri na uhakika, fikra na amali (matendo). Ikiwa kimojawapo kati ya vitu viwili hivo, au sehemu moja yake itaathiriwa na nguvu zilizo kinyume cha Uungu kama vile dhamiri ya kumwamini Mungu kuambatana na uhakika usiokuwa wa Kiungu, au uhakika wa kumpenda Mungu kuambatana na moyo wa kutomjua Mungu basi matokeo yake yatakuwa ni kupatikana hali mbili zinazopingana katika maisha ya binadamu na kufanyika shirki (ushirikina) katika kumwabudu Mwenyezi Mungu. Katika hali kama hiyo, binadamu huwa kama akrabu ya dira ambayo huelekea sehemu nyingine kwa sababu ya kuvutwa na uvutano usio wa kawaida, hivyo, kama haitoelekea kwenye ncha ya kawaida itaharibika. Kwa hivyo, ikiwa binadamu atapotoka kwenye njia iliyonyooka na mwelekeo ulio sawa ambao ni umbile aliloumbiwa, basi atapotoka kwenye njia ya Mwenyezi Mungu.

أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰ أَشَدِّ الْعَذَابِ ...﴿٨٥﴾

"Je, mnaamini baadhi ya Kitabu [maarifa na maam-risho ya dini] na kuyakataa mengine? Basi' hakuna malipo kwa mwenye kufanya hivyo kati'ka nyinyi ila fedheha katika maisha ya dunia, na Si'ku ya Kiyama watarudishwa kwenye adhabu kali kabisa. " (Al-Baqa-rah, 2:85)

g) Tawhidi maana yake ni kwenda sambamba binadamu na mazingira yake ya ulimwengu. Upana usio na kikomo wa ulimwengu ni uwanja wa amali na radiamali zisizohesabika za kanuni za ulimwengu. Hakuna tukio au jambo lolote, liwe dogo vipi, ambalo linaweza kuepukana na kanuni hizo. Kutokana na ulingano, utaratibu na umoja wa kanuni za ulimwengu ndipo unapopatikana mfumo wenye utaratibu na umoja katika ulimwengu. Binadamu ni sehemu moja ya mfumo huo, hivyo, yeye pia hutawaliwa na kanuni hizo za kawaida pamoja na kanuni maalum ambazo zinakwenda

sambamba na kanuni nyinginezo.

Lakini binadamu, kinyume cha viumbe vinginevyo ambavyo vinalazimika kufuata maumbile bila ya kuwa na hiari yoyote, ana uwezo wa kuchagua na kujiamulia mwenyewe. Inambidi binadamu achague njia ya asili na ya umbile lake ambayo ndiyo njia inayomnyanyua, kumwendeleza na kumkamilisha. Hii pia ina maana kwamba ana uwezo wa kwenda kinyume na njia hiyo ya umbile (fikra).

"Basi anayetaka aamini, na anayetaka akufuru ." (al-Kahf, 18:29)

Tawhidi humtaka binadamu afuate njia ya kiasili na ya kimaumbile ambayo pia inafuatwa na ulimwengu mzima. Binadamu akiwa ni kiungo muhimu katika ulimwengu, hujitahidi kujiunganisha na kujiambatanisha na viungo vingine vya ulimwengu ili upatikane umoja na ufungamano kamili kati ya binadamu na ulimwengu.

أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾

"Je, wanataka dini ghairi ya Allah na hali kila kilichomo mbinguni na ardhini kinamtii Yeye kwa upendo au karaha, na Kwake watarejeshwa?" (Aali 'lmraan, 3:83)

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَسْجُدُ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ وَالنُّجُومُ وَالْجِبَالُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ النَّاسِ ...﴿١٨﴾

"Je, huoni kwamba kinamsujudia Allah kila kilichomo mbinguni na kllicbomo ardhini, na jua na mwezi na nyota na milima na miti na wanyama na miongoni rnwa watu walio wengi?" (al-Hajj, 22:18)

3 ) Tawhidi katika Kipengee cha Sera ya Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa

a) Tawhidi maana yake ni kwamba hakuna mtu yeyote ghairi ya Mwenyezi Mungu anayefaa peke yake kupanga na kuamua mambo ya ulimwengu na binadamu. Hii ni haki ya Mwenyezi Mungu tu Ambaye Ndiye Muumba wa binadamu na ulimwengu na Mratibu wa vitu vyake vyote. Yeye tu anajua uwezo na mahitaji yao yote. Kwa hakika, Yeye tu hujua kwa ukamilifu nguvu, uwezo na nishati zilizomo katika kiwiliwili na roho ya binadamu, na vilevile hazina zisizohesabika katika ulimwengu, kadiri na matumizi yake na vipi kuvisawazisha.

Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Peke Yake tu Ndiye anayeweza kuratibu ratiba ya maisha ya binadamu na sera ya uhusiano wake katika mfumo wa ulimwengu. Yeye tu anaweza kupanga mifumo ya kisheria na kijamii katika maisha ya binadamu.

Haki hii ya pekee ya Mwenyenzi Mungu inatokana na uhakika huu wa kiasili na kimantiki kwamba Yeye ni Muumba. Kwa hivyo, aina yoyote ya uingiliaji katika kuamua sera ya kimatendo ya wanadamu utakaotokana na wengine, utakuwa ni sawa na kuingilia utawala wa Mwenyezi Mungu na kudai Uungu, na huko kutachukuliwa kuwa ni shirki.

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

"La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa." (an-Nisaa, 4:65)

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦﴾

"Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi. " (al-Ahzaab, 33:36)

1

AKIDA

TAWHIDI

MAANA YA TAWHIDI

b) Tawhidi maana yake ni kwamba: hakuna mtu yeyote aliye na haki ya kutawala na kusimamia jamii na maisha ya binadamu isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Utawala na usimamizi wa mtu mmoja juu ya mwingine kama utachukuliwa kuwa ni haki ya pekee isiyokuwa na jukumu lolote, hapana budi huleta udhalimu na uonevu. jamii inawezekana kuepukana na udhalimu na upotofu ikiwa Nguvu Kuu, itaweka utawala na uongozi wa mambo ya jamii katika mikono ya mtu mmoja au kikundi cha watawala ambao watakuwa na majukumu yatakayoambatana na uwezo. Hiyo Nguvu Kuu, katika lugha ya kidini, ni Allah Mwenye ezi (Mwenyezi Mungu) Ambaye uwezo Wake na upana wa elimu Yake hauwezi kushindwa na uwezo au elimu yoyote.

لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٣﴾

"Hapana kinacho fichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi; ila vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha." (Sabaa, 34:3).

Sifa Zake za kuwa Mkali wa kuadhibu na Mlipizaji hazitoi fursa yoyote kwa wale aliowateua kupotoka kwenye njia Yake.

وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ ﴿٤٤﴾ لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ ﴿٤٥﴾ ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ ﴿٤٦﴾

"Na lau [Mtume] angelizua juu Yetu baadhi ya maneno, bila shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia, kisha kwa hakika tungelimkata aorta.." (al-Haaqah, 69:44-46).

Huyo Allah Mwenye enzi si kama umma au taifa ambalo linaweza kudanganywa au kumilikiwa; wala si kama chama kinachoweza kugeuzwa kuwa ni chombo cha kudhulumu na kukandamiza; na wala si kama viongozi na wakuu ambao wanaweza kununuliwa au kushirikishwa katika hiana.

Kwa kuzingatia kwa undani zaidi, ikiwa kupatikana makini na utaratibu katika maisha ya binadamu kutalazimika vyombo vyote vinavyohusika na maisha vikutanike katika kitovu kimoja, na mambo yote yadhibitiwe na nguvu moja, basi nguvu hiyo haiwezi kuwa kitu kingine isipokuwa nguvu ya Muumba wa ulimwengu na binadamu.

Kwa hivyo, utawala na uongozi wa jamii ya binadamu ni haki mahsusi ya Mwenyezi Mungu. Utawala huo humilikiwa kupitia kwa wateule wa Mwenyezi Mungu ambao ni watu waliochaguliwa kufuatana na sifa na kipimo maalum kilichowekwa na dini ya Mwenyezi Mungu. Wale ambao sifa zao huafikiana na kipimo hicho, hushika hatamu ya utawala na hapo ndipo mfumo wa kidini wa kusimamia sheria za Mwenyezi Mungu unapothibitika na kutekelezeka.

قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٤﴾

"Sema: 'je, nifanye mtawala [msimamizi] ghairi ya Allah, Mwumba wa mbingu na ardhi, Naye hulisha wala halishwi?' Sema: 'Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kutii [amri ya Mofaj',' na [nikaambiwa:] 'Usiwe miongoni mwa washirikina. ' " (al-An'aam, 6:14)

إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ ﴿٥٥﴾

"Hakika mwenye amri (utawala) juu yenu Umma wa Kiislamu] ni Allah na mtume Wake na wale walioamini ambao husimamisha sala na hutoa zaka, na hali ya kuwa wanarukuu. " (af-Maai'dah, 5:55)

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾ مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢﴾ إِلَـٰهِ النَّاسِ ﴿٣﴾ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ ﴿٤﴾

"Sema: 'Najikinga kwa Rabi wa watu. Mmiliki (Mtawala) wa watu. Mwabudiwa wa watu.' " (an-Naas, 114:1-3).

c) Tawhidi maana yake ni kwamba umilikaji mutlaki na wa asili wa neema, maliasili na hazina zote za ulimwengu ni wa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Mtu yeyote hana haki ya kumiliki peke yake kitu chochote. Kila kitu kimewekwa amana kwa binadamu ili akitumie kwa ajili ya kumsaidia katika mwendo wake wa kujikamilisha na kujiadilisha. Hairuhusiwi kwa mtu aliyeneemeka kuharibu, kuangamiza au kutotumia neema za dunia ambazo ni matokeo na matunda ya jitahada za maelfu ya viumbe na matukio. Neema hizo zisitumiwe katika njia yoyote isipokuwa kujiadilisha binadamu. Mali anayomiliki binadamu ingawa ni kwa ajili yake - lakini kwa hakika amepewa na Mwenyezi Mungu, hivyo, ni lazima atumie katika njia ambayo ameonyeshwa na Mwenyezi Mungu; nako ni kutumia katika njia yake ya asili na ya kimaumbile, katika njia ambayo imeumbiwa. Kutumia na kunufaika nayo katika njia yoyote nyingine ni kukwepa njia yake ya kimaumbile, nako huleta ufisadi.

Jukumu la binadamu katika utumizi wa neema anuwai za Mwenyezi Mungu ni kutumia katika njia iliyo sahihi kwa lengo la kuzihuisha na kuzikamilisha.

قُل لِّمَنِ الْأَرْضُ وَمَن فِيهَا إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٨٤﴾ سَيَقُولُونَ لِلَّـهِ قُلْ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٨٥﴾

"Sema: 'Ni ya nani ardhi na vilivyomo ndani yake, ikiwa nyinyi mnajua?' Watasema: 'Ni ya Allah!' Sema: 'Basi je, hamkumbuki?' " (al-Mu 'minuun, 23:84, 85).

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ...﴿٢٩﴾

"Yeye Ndiye aliyeumba kwa ajili yenu [binadamu] vyote vilivyomo katika ardhi." (al-Bagarah, 2:29)

اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُّجِيبٌ ﴿٦١﴾

"Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi." (Huud, 11:61).

وَالَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ ﴿٢٥﴾

"Na wale wanaovunja ahadi ya Allah baada ya kuifunga, na wanakataa aliyoyaamuru Allah yaunganishwe, na wanafisidi katika ardhi; hao ndio watakaopata laana na makao mabaya." (Ar-Ra'd, 13:25)

d) Tawhidi maana yake ni kwamba watu wote wana haki sawasawa katika kutumia neema za ulimwengu. Uwezekano na fursa zote ni sawasawa kwa wanadamu wote ili kwamba kila mtu aweze kunufaika na neema hizo kwa kadiri ya haja yake na jitahada zake. Katika ulimwengu huu wa neema, hakuna eneo lolote lililowekwa kuhodhiwa na kikundi fulani tu. Watu wote wanaweza kutumia hima na uwezo wao kunufaika na neema mbalimbali za ulimwengu

huu. Katika kutumia fursa hii, hakuna ubaguzi wowote kwa sababu ya ukabila, rangi, jiografia, historia au hata itikadi (dini).

وَالْأَنْعَامَ خَلَقَهَا لَكُمْ فِيهَا دِفْءٌ وَمَنَافِعُ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ ﴿٥﴾ وَلَكُمْ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسْرَحُونَ ﴿٦﴾وَتَحْمِلُ أَثْقَالَكُمْ ...﴿٧﴾

Na amewaumba wanyama [ngamia, ng'ombe na kondoo], katika hao mnapata joto na manufaa na wengine mnawala. Na katika hao ni uzuri kwenu mnapowarudlsha jioni na mnapowapeleka malishoni asubuhi. Na hubeba mizigo yenu.. ." (an-Nahl, 16:5-7)

"Yeye Ndlye anayekuteremshieni maji' kutoka mbinguni. . (an-Nahl, 16:10)

". . Kwayo hukuotesheeni mimea. . " (an-Nahl,16:11) ....

"... Na alivyokuumbieni katika ardhi. . " (an-Nahl, 16:13)

"Allah Ndiye aliyekuumbieni wanyama ili mwa

pande baadhi yao na wengine wao muwale. " (Gha-afir, 40:79)

Katika aya hizo zinazofuatana mwanzoni mwa Sura an-Nahl, wanaozungumziwa ni wanadamu wote kwa jumla, bila ya kufadhilishwa kabila au taifa fulani, kama aya hizi zinavyoashiria pia:

"Na lau angelitaka bila shaka angelikuongozeni nyinyi [wanadamu] nyote. " (an-Nahl, 16:9)

"Mungu wenu [enyi wanadamu] ni Mungu Mmoja." (an-Nahl, 16:22)

Hayo tuliyoyataja ni sehemu moja tu ya maana kubwa na pana ya kipengee tofauti vya Tawhidi. Muhtasari huu unaweza kufafanua waziwazi kwamba Tawhidi si nadharia tupu ya kifalsafa na kidhihinia (kimawazo) isiyoweza kuwa ya kimatendo; au kusema kwamba haihusu maisha ya kila siku ya binadamu; au kwamba haiingilii kati katika kuamua malengo, jitahada na vitendo vya binadamu. Tawhidi haitoshi kuwa ni imani tupu inayoaminiwa na watu badala ya itikadi nyinginezo.

Kwa upande moja, Tawhidi ni mtazamo mzima juu ya ulimwengu, binadamu, msimamo wa binadamu juu ya matukio ya dunia, historia pamoja na uwezo, vipaji na mahitaji yake. Tawhidi inatazama malengo na mwongozo wa binadamu katika kujikamilisha na kujiadilisha.

Kwa upande mwingine, Tawhidi ni imani ya kijamii ambayo hupanga na huratibu mfumo ufaao wa mazingira ya binadamu, mazingira ambayo yatamwezesha kwa urahisi na haraka kujiendeleza kufikia utukufu na ukamilifu maalum. Ni pendekezo na kielelezo mahsusi kwa ajili ya jamii na huonyesha sera yake ya kiasili na kimsingi.

Kwa hivyo, wakati wowote sauti ya Tawhidi inapopaazwa katika jamii za kijahili au kishirikina (zilizosimama juu ya msingi wa kutojua uhakika wa binadamu), na jamii za kitaghuti (zilizosimama juu ya msingi wa kudhulumu thamani

za haki za binadamu), huleta mabadiliko ya kimapinduzi katika jamii, huhuisha na kuzindua nyoyo dhaifu na roho zilizokufa, hufanya mawimbi katika bahari iliyotulia ya jamii, na huisawazisha jamii iliyochafuka. Huleta mapinduzi na mabadiliko katika vyombo vya kinafsi, kiuchumi, kijamii, kimaadili na kibinadamu. Kwa ufupi, Tawhidi hushambulia hali iliyopo ya kijahili na nguvu zinazoilinda hali hiyo, na huondoa kabisa mazingira yanayostawisha hali hiyo.

Kwa hivyo, Tawhidi si ufumbuzi mpya peke yake katika masuala ya kinadharia na kiitikadi yenye matendo machache tu, bali ni njia mpya kwa binadamu ambayo licha ya kuchungua masuala ya kidhahania na kinadharia, hudhamiria kuratibu sera mpya kwa ajili ya matendo na maisha.

Kwa kufahamu jambo hili ndipo tunapoitakidi kwamba Tawhidi m kiini na msingi wa dini ambao kwao jengo zima la dini husimama juu yake.

Kusema kwamba Tawhidi ni nadharia inayohusu meta-fizikia au ni tasnifu ya hali ya juu ya kirttaadili na kiirfani peke yake, maana hii haiwezi kupewa itikadi kuu kama ya Kiislamu ambayo inatawala maisha nzima ya kijamii.

Hapanashaka kwamba katika kila zama walikuwepo watu ambao ingawa walimwamini Mwenyezi Mungu na waliitakidi Tawhidi, lakini walighafilika au walipuuza umuhimu wa itikadi hiyo katika matendo, na hasa jamii. Katika kilazama watu hao walio wepesi kuamini waliishi maisha yaliyokuwa sawa na maisha ya wasioamini Tawhidi; na kwa sababu hii ndiyo maana kwamba itikadi yao haikuleta mwamko wowote nyoyoni mwao kuhisi kwamba haiwezekani kwa mwenye kuamini Tawhidi kuafikiana na kujilinganisha na maisha yasiyokuwa na Kitawhidi; au kwamba haiwezekani kupata utulivu katika mazingira mazito na ya kubana ya ushirikina. Katika mwanzoni mwa kudhihiri Uislamu wakati mji wa Makka ulipokuwa ni kitovu na mji mkuu wa ushirikina na masanamu maarufu ya Waarabu, walikuwepo wafuasi wa dini halisi ya Ibrahim. Lakini kwa kuwa katika fikra zao

Tawhidi haikuwa zaidi ya itikadi ya kidhahania na kiroho katika maumbile na matendo yao ya kibinafsi, hivyo, kuwepo kwao hakukuleta taathira yoyote ya kifikra na kijamii katika mazingira ya kijahilia (kishirikina). Kuwepo kwao hakukuhisika hata kidogo, na maisha ya kishirikina yaliendelea kwa salama na amani. Hao waumini wa Umoja wa Mwenyezi Mungu walikuwa wakiishi pamoja na washirikina bila ya kusumbuliwa na mila na desturi mbaya za maisha ya kishirikina. Aina hii ya mtazamo wa kidhahania wa Tawhidi ndiyo iliyowafanya wakose uwezo na satua muhimu katika maisha, na hasa maisha ya kijamii.

Katika mazingira kama hayo ndipo Uislamu ulipotangaza maana ya Tawhidi kuwa ni itikadi inayoahidi kutoa muundo mpya na mpana kwa ajili ya maisha ya kijamii. Katika hatua zake za kwanza, Uislamu ulionyesha sura yake kama ni ujumbe wa kimapinduzi kwa watu wote waumini na makafiri. Wote walielewa kwamba ujumbe huo ulikuwa ni mfumo mpya wa kijamii, kiuchumi na kisiasa ambao haukubaliani na mifumo mingine iliyokuwepo duniani. Uislamu uliyapinga mazingira yaliyokuwepo na badala yake ulisimamisha mfumo mpya.

Kwa sababu ya upambanuzi wake, waumini waliukubali ujumbe wake kwa hamu na shauku na wakajitolea kwa ajili yake; na kwa sababu hiyohiyo wapinzani na makafiri wa ujumbe wa Tawhidi waliupinga kwa vikali na kila siku upinzani wao ulizidi.

Uhakika huu wa kihistoria unaweza kuwa ni kipimo kwa ajili ya kupima na kutathmini usahihi au utovu wa usahihi wa madai ya Tawhidi katika awamu zote za historia. Wakati wowote utakapoonekana kwamba madai ya Tawhidi yanayotolewa na watu yanafanana na madai ya wale waumini wa Umoja wa Mungu wa Makka kabla ya kudhihiri Uislamu, hapo tutaweza kushuku ukweli wa madai yao ya kuitakidi Tawhidi. Tawhidi inayokubaliana na ibada ya masanamu na miungu ghairi ya Mwenyezi Mungu si Tawhidi tena, bali ni

dhana moja iliyo kinyume cha Tawhidi iliyofundishwa na Manabii.

Kwa hivyo, kufuatana na maana halisi ya Tawhidi iliyofundishwa na Mitume, tunaweza kuelewa vizuri sababu ya Uislamu kusambaa na'kuwa na nguvu katika siku za mwanzoni, na sababa ya kuzorota kwake katika zama za baadaye.

Mtume Muhammad (s.a.w.w ) aliwaonyesha watu Tawhidi kama ni njia na mwongozo kwa ajili yao; lakini katika zama za baadaye, Tawhidi ikajadiliwa katika mahafali na mabaraza kama mawazo au dhanio. Katika zama za Mtume Mtukufu, Tawhidi ilikuwa ikiangaliwa kama mtazamo au ono jipya kwa ajili ya dunia na harakati kwa ajili ya maisha; lakini baadaye ikageuzwa kuwa ni maudhui ya kiitikadi tupu kwa ajili ya kuchunguzwa na kujadiliwa na wanavyuoni wakati wa masomo na faragha. Katika zama za Mtume Mtukufu, Tawhidi ilikuwa ni msingi wa mfumo mzima na kitovu cha uhusiano wote wa kijamii, kiuchumi na kisiasa;

lakini baadaye ikafanywa kuwa kama taswira nzuri iliyochorwa kwa usanifu kisha ikatundikwa kwenye'ukuta wa maonyesho kama pambo. jambo gani linaweza kupatikana kutoka katika pambo lisilokuwa na uhai ?

Hayo tuliyokwishasema yanathibitisha wazi kwamba kwa mtazamo wa kimatendo, Tawhidi ni kama kalibu (kielelezo) ambayo kwayo jamii hupata umbo au sera ya kuishi. Ni jina la mfumo uliowekwa na dini ya Kiislamu na kufaa kabisa kwa ajili ya ustawi na maendeleo makubwa ya binadamu. Kwa upande wa kinadharia, ni itikadi ambayo ni msingi wa kifalsafa wa mfumo huo.

Baada ya utangulizi huu, tunaweza kurejea yale tuliyo yasema mwanzoni na tukalichunguza suala hili katika kipengee maalum.

Tumesema kwamba wapinzani wa kwanza wa nara ya

Tawhidi walikuwa ni viongozi na watu wenye fedha, nguvu na utukufu katika jamii; na hii inaonyesha kwamba upinzani mkubwa kuliko wote unatoka katika tabaka linalotawala na linalomiliki katika jamii ambalo linaitwa 'tabaka la wastakabari' katika Qur'ani. Tumesema kwamba mara tu miito ya Kitawhidi inapotolewa katika jamii katika zama yoyote na kutangazwa msimamo wake kwa tabaka la wenye utawalana wastakabari, basi hukabiliwa na radiamali mbili zinazotofautiana kutoka matabaka mawili yanayopingana katika jamii hupingwa na hufanyiwa uadui na wastakabari, na hukubaliwa na huungwa mkono wa wastadhaafu (wanyonge).

Kwa hakika hali hii ya kuwepo radiamali mbili tofauti inaonyesha sura ya asili na ya kweli ya Tawhidi, na inamaanisha kwamba katika kila zama za zamani na baadaye, wakati Tawhidi inapotangazwa katika sura yake sahihi na maana yake halisi, basi hapana budi itakabiliwa na hali hiyo.

Sasa tuangalie ni kipengee kipi kati ya vipengee mbalimbali vya Tawhidi, kinapinga moja kwa moja maslahi na hata kuwepo kwa tabaka lawastakabari (madhalimu)? Kwa maana nyingine, kipengee kipi cha Tawhidi au pendekezo lipi la Kitawhidi kwa ajili ya jamii ambalo linapingwa kwa vikali sana na tabaka la wastakabari ?

Kujua sura za wastakabari katika Qur'ani kutasaidiasana kuelewa vizuri zaidi suala hili.

Katika zaidi ya mahali arobaini, Qur'ani inaonyesha sifa za kinafsi za wastakabari, hali zao za kijamii, ubarakala wao, na shabaha zao.

Kwa jumla, Qur'ani hubainisha sifa hizi za wastakabari:

a) Ingawa mstakabari (mustakbir) humwamini Mwenyezi Mungu kama ni uhakika wa kidhahania au wa kimila, au mwenye utawala wa kiasi fulani, lakini, kwa hakika, humkataa Mwenyezi Mungu kwa maana inayofahamika katika nara (shaari) ya Laa ilaaha illa llaah - kwamba utawala na mamlaka yote inahodhiwa na Mwenyezi Mungu tu.

إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٣٥﴾

"Hakika wao walipokuwa wakiambiwa: 'Hakuna mungu ila Allah,' walikuwa wakitakabari' (waki'-kataa). " (as-Saafaa't, 37:35)

b) Mstakabari hapimi utukufu wa binadamu kwa mujibu wa kipimo sahihi cha ubora, bali hujichukulia mwenyewe kuwa ni bora ha mtukufu kuliko watu wote kwa kutegemea kipimo cha kijahili (kishirikina)cha utajiri na nguvu.

فَأَمَّا عَادٌ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَقَالُوا مَنْ أَشَدُّ مِنَّا قُوَّةً ...﴿١٥﴾

"Ama kina A'di walijivuna katika nchi bila ya haki, na wakasema: Nani aliye kuwa na nguvu kushinda sisi?" (Fussllat, 41:15).

c) Kutokana na mawazo hayo batilifu, mstakabari hupinga aya za Mwenyezj Mungu ambazo ni ujumbe (ufunuo) kwa ajili ya kuunda mfumo mpya na vipimo vya thamani za kweli.

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا وَلَّىٰ مُسْتَكْبِرًا كَأَن لَّمْ يَسْمَعْهَا كَأَنَّ فِي أُذُنَيْهِ وَقْرًا فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٧﴾

"Na' anaposomewa aya Zetu, huzipa mgongo kwa kutakabari, kama hakuzisikia, kana kwamba masikioni mwake mna uzito; basi mpe habari ya adhabu Inayoumiza." (Luqmcian, 31:7).

d) Mstakabari hupinga mwito wa Mtume wa kuleta mabadiliko na ukombozi kwa kutoa visingizio na kusema kwamba: "Lau (Mtume) angekuwa mkweli, tungemtambua mapema zaidi kuliko wengine," au kwamba: "Ni lazima Mwenyezi Mungu azungumze nasi moja kwa moja." Na kwa kutoa visingizio hiyvo, husimama kupigana vita dhidi yaMtume.

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا لَوْ كَانَ خَيْرًا مَّا سَبَقُونَا إِلَيْهِ ﴿١١﴾

"Na waliokufuru waliwaambia walioamini: 'Lau [dini yao] ingelikuwa bora (kheri), wasingetutangulia kwayo [kuifuata].'" (al-Ahqaaf, 46:11)

وَإِذَا جَاءَتْهُمْ آيَةٌ قَالُوا لَن نُّؤْمِنَ حَتَّىٰ نُؤْتَىٰ مِثْلَ مَا أُوتِيَ رُسُلُ اللَّـهِ ﴿١٢٤﴾

"Na inapowafikia aya, husema; 'Hatuamini mpaka tuteremshiwe kama yale waliyoteremshewa mitume waAllah."' (al-An'aam, 6:124).

e) Mstakabari humtuhumu mtangazaji (mwanadaawa) wa ujumbe wa Tawhidi kama ni mtu mwenye kutafutacheo na maslahi, na kwa njia hii hutetea desturi zao za zamani zenye kuunga mkono tabaka lao ili apate kudhoofisha nguvu za mwito wa Tawhidi kati ya watu.

قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَلْفِتَنَا عَمَّا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا الْكِبْرِيَاءُ فِي الْأَرْضِ وَمَا نَحْنُ لَكُمَا بِمُؤْمِنِينَ ﴿٧٨﴾

"Wakasema [kumwambia Musa]: 'je, umetujia ili utuondoe katika [nyendo na mila] zetu tulizowakuta nazo mababu zetu, ili ukubwa (na utawala) uwe wenu wawili katika nchi? Na sisi' hatuwezi kukuaminini.' " (Yuunus, 10:78).

f) Mstakabari hutumia nguvu, mabavu na ujanja kujaribu kuwaweka watu katika hali ya kunyonywa, utumwa na kutii bila ya sharti yoyote, na huwachochea wakatae na wapinge jitahada zozote za kuwakomboa ili wapate kuwaweka watu katika hali wanayoitaka wao. [Hivyo, katika Siku ya Kiyama, wanyonge ambao walikubali kudhulumiwa na wastakabari hao watasema haya:

وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا ﴿٦٧﴾

"Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia.' " (al-Ahzaab, 33:67).

فَيَقُولُ الضُّعَفَاءُ لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا نَصِيبًا مِّنَ النَّارِ ﴿٤٧﴾

Na wanyonge watakapowaambia wale waliotakabari: 'Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu [duniani], basi je, mnaweza [leo kutuondolea sehemu ya [adhabu ya] Moto?'" [Ghaafir, 40:47).

قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٠٩﴾ يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُمْ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ ﴿١١٠﴾

"Wakasema k'ikundi cha wakuu katika kaumu ya Firauni [kuwaambia watu wanyonge]: 'Hakika huyu [Musa] ni mchawi stadi. Anataka kukutoenf katika ardhi yenu; bas mnatoa shauri gani?' " [al-A'raaf, 7:109,110)

g) Mwishowe, wakati Mtume ha wafuasi wake wanapo simama dhidi ya mfumo unaotawala? wa wastakabari ili kuupindua, hukabiliwa na mashambulio, udhia na uhasama mkubwa kutoka kwa wastakabari:

قُتِلَ أَصْحَابُ الْأُخْدُودِ ﴿٤﴾ النَّارِ ذَاتِ الْوَقُودِ ﴿٥﴾ إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌ ﴿٦﴾ وَهُمْ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ بِالْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌ ﴿٧﴾

"Wameangamizwa Watu wa Mahandaki (As'haabul Ukhduud), [waliouwasha] moto wenye kuni nyingi, walipokuwa wamekaa hapo, wakishuhudia yale [mateso] waliyokuwa wakiwafanyia waumini." (cil-Buruuj, 85:4-7)

وَقَالَ فِرْعَوْنُ ذَرُونِي أَقْتُلْ مُوسَىٰ وَلْيَدْعُ رَبَّهُ إِنِّي أَخَافُ أَن يُبَدِّلَ دِينَكُمْ أَوْ أَن يُظْهِرَ فِي الْأَرْضِ الْفَسَادَ ﴿٢٦﴾

'Akasema Firauni [kuwaambia washauri wakej: 'Niachieni nimwue Musa, naye amwite Rabi wake [kadiri anavyoweza! ] Hakika mimi nfnaogopa asije kuibadili dini yenu au kuleta ufisadi katika ardhi [hata watu wakatuasi.' " (Ghaafir, 40:26).

Hii ni sehemu ndogo tu ya aya za Qur'ani zenye kuelezea sifa za wastakabari.

Katika aya nyinginezo, licha ya kuchora taswira, Qur'ani inafafanua zaidi kwa kuonyesha kwamba ustakabari kama ni tabaka moja maalum,au kwamba kilammojawao ni kama nembo au alama inayowakilisha tabaka hilo.

ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ وَهَارُونَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ بِآيَاتِنَا فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ ﴿٧٥﴾

"Kisha baada yao tukamtuma Musa na Haruni kwa Firauni na waheshimiwa wake, kwa Ishara zetu. Wakajivuna, na wakawa watu wakosefu. " (Yuunus, 10:75).

وَقَارُونَ وَفِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَلَقَدْ جَاءَهُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ وَمَا كَانُوا سَابِقِينَ ﴿٣٩﴾

"Na Qarun na Firauni na Hainana; na hakika Musa aliwafikia kwa ujumbe bayana, lakini walitakabari katika ardhi [ya Mungu na mbele ya waja na ujumbe wa Mola." (al- 'Ankabuut, 29:39).

Sote tunamjua Firauni. Hamana alikuwa mshauri muhsusi wa Firauni na waziri mkuu katika utawala wa Misri. Malau Fir'awn ni viongozi na wakuu katika utawala wa Firauni ambao walikuwa washauri na wasaidizi katika mfumo huo wa Kifirauni. (Tazama Sura al-A'raaf, 7:126 na aya nyinginezo.) Qarun alikuwa bepari mkubwa ambaye alihodhi hazina kubwa kwa kadiri kwamba "Kulihitajika watu kadhaa wenye nguvu kuweza kubeba funguo za hazina hizo!"

Baada ya kuangalia aya kadhaa za Qur'ani, tunaweza kuwatambua wastakabari kama ni tabaka linalotawala katika jamii ya kishirikina bila ya kustahiki kushika hatamu za kisiasa na kiuchumi. lli kuendeleza unyonyaji na utawala wao wa kidhuluma, 'wastakabari hudhibiti utamaduni na itikadi za watu, na hutumia mbinu mbalimbali, kwa vile, kupiga msasa bongo za watu, kuwafanya wawanyenyekee na wakubali hali hiyo. lli kuhifadhi maslahi yao, wastakabari huwa tayari kupigana kufa kupona dhidi ya mwito wowote wenye kuleta mwamko, seuze harakati za kimapinduzi.

Sasa turejee tena kwenye maudhui ya asili.

Vipi Mitume na Manabii walikuwa wakitangazaTawhidi? Namna shaari hiyo ya Tawhidi ilivyokuwa ikitangazwa na Mitume ambayo ni msingi wa asili wa mafundisho yao inaonyesha kwa urahisi kipengee kipi cha Tawhidi hakiwezi kuvumiliwa na wastakabari, na sababu ya kuikataa kwao. Kwa nini tabaka hilo haliwezi kuikubali Tawhidi inapoelezwa kwa maana hiyo?

Tunajua kwamba shaari (nara) ya Tawhidi ambayo ni msemo wa Laa ilaaha i'lla llaah ni utangulizi wa mwanzo wa miito yote ya Mitume.

Maneno haya ya Mtume Mtukufu kwamba: "Semeni:

'Hakuna mungu ila Allah' mfaulu," ni maneno yaliyo maarufu sana.

Vilevile tangazo hili linalosema: "Enyi watu! Mwabu duni Allah, [kwani] hamna mungu ghairi Yake" (7:59)

limetolewa na Manabii wakubwa kama Nuh, Hud, Salih, Shu'ayb, n.k. ambalo lilikuwa muhimu sana katika kuhubiri kwao;

na limekaririwa mara kadhaa katika Qur'ani.

Kama tunavyoona katika matamko hayo, jambo linalosi sitizwa ni "kukana ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu";

na Tawhidi inaangalia kwa mtazamo huu kwamba asiabudiwe

yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu.Kwa kutumia matamko hayo, Mitume walikuwa wakiwaonya watu wajinga na waghafilifu ambao walizama katika matope ya mifumo ya kijahili (kishirikina) na kitaghuti, na walikuwa wakiwatahadharisha wasimwabudu mtu yeyote isipokuwa Allah Mwenye ezi. Daawa za Mitume zilianza kwa kutangaza vita dhidi ya wanaodai uungu.

Na nani katika jamii wanaodai uungu? Kupambana na wajigambao uungu kunamaanisha nini? Malengo gani ya kijamii (yaliyoahidiwa na Manabii) yanatazamiwa kutimizwa katika uandalizi huu?

Kwa kawaida, ibara 'kudai uungu' inachukuliwa kwa maana kwamba mtu hujidai mwenyewe kuwa ni 'mungu' mwenye uwezo ule mkubwa ambao watu walikuwa wakiitakidi katika historia nzima. Kwa hakika, hii ni maana ya kijuujuu tu.

Hapana shaka kwamba walikuwepo wahalifu wapumbavu ambao kwa kutumia nguvu zao za kisiasa na kijamii, waliwafanya watu walio wapumbavu zaidi kuliko wao waamini kwamba waungu walikuwa na sehemu ya roho ya Mwenyezi Mungu. Lakini tunapochungua maana pana ya maneno 'ibada' na 'uungu' katika Qur'ani, tunapata natija hii kwamba ibara 'wanaodai uungu' ina maana kubwa zaidi.

Qur'ani inatumia neno 'ibada' kwa maana ya kujitolea na kumtii mtu au kiumbe chochote bila ya sharti lolote. Wakati wowote tunapojitolea kabisa kwa mtu mmoja, tunapotenda kufuatana na amri yake, na tunapojitolea na kutii amri yake tu, hapo huwa 'tunamwabudu' yeye. Vivyo hivyo, ikiwa nguvu yoyote kutoka ndani ya nafsi yetu au nje yake itaweza kutufanya tuwe wanyenyekevu na watiifu kwake kwa kuvidhibiti viwiliwili na roho zetu, na kwa kuzielekeza nishati zetu zote kwenye matakwa yake, basi sisi tutakuwa ni 'waabudu' wake, naye atakuwa 'mwabudiwa' wetu.

Aya zifuatazo zinafafanua jambo hili.

Mwanzoni mwa daawa yake, Musa alimlaumu Firauni kwa kumwambia:

وَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَيَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٢٢﴾

Na hiyo ndio neema uliyonifadhilia ya kuwatia katika ibada yako Wana wa Israill?" (ash-Shu'araa, 26:22).

Firauni pamoja na wakuu na washauri wa utawala wake walikuwa wakisema:

فَقَالُوا أَنُؤْمِنُ لِبَشَرَيْنِ مِثْلِنَا وَقَوْمُهُمَا لَنَا عَابِدُونَ ﴿٤٧﴾

"Je, tuwaamini wanadamu wawili walio mfano wetu na kabila lao ni wenye kutuabudu sisi?" (al-Mu'ini-nuun, 23:47) :

Ibrahim alimwambia baba yake (mdogo);

يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ عَصِيًّا ﴿٤٤﴾

"Ewe baba yongu! Usimwabudu Shetani hakika Shetani ni mwasi kwa [Mola] Mwingi wa rehema." (Maryam, 19:44) :

Mwenyezi Mungu anawauliza wanadamu .wote kwa jumla:

أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَا بَنِي آدَمَ أَن لَّا تَعْبُدُوا الشَّيْطَانَ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٦٠﴾

"Je, sikukuagizeni, enyi wanadamu, kwamba msimwabudu Shetani? Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu." (Yaasii'n,36:60)

Mwenyezi Mungu anawaahidi wale wenye kutumia akili:

وَالَّذِينَ اجْتَنَبُوا الطَّاغُوتَ أَن يَعْبُدُوهَا وَأَنَابُوا إِلَى اللَّـهِ لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فَبَشِّرْ عِبَادِ ﴿١٧﴾

Na wale wanao jiepusha na ibada potovu, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu, watapata bishara njema. Basi wabashirie waja wangu." (az-Zumar, 39:17).

Mwenyezi Mungu anawaambia haya wale wanaowakejeli wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na Utume:

مَن لَّعَنَهُ اللَّـهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ الْقِرَدَةَ وَالْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ الطَّاغُوتَ أُولَـٰئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ ﴿٦٠﴾

"Ni yule ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani na amemkasirikia, na amewafanya miongoni mwao manyani na nguruwe, na wakamuabudu Shet'ani. Hao ndio wenye mahali pabaya na wamepotea zaidi njia iliyo sawa. " (al-Maaidah, 5:60).

Katika aya hizi, kumtumikia na kumtii Firauni na wakuu wa utawala wake, na kuwatii na kuwatumikia mataghuti (madhalimu) na mashetani kunafasiriwa kama ni 'ibada' na .'kuabudu'. Kwa J'umla, aya hizi pamoja na aya nyingine kadhaa za Qur'ani, zinaonyesha kwamba maana ya 'ibada' katjka Qur'ani ni kufuata, kusalimu amri na kuitii kabisa kudura (nguvu) moja ya kihakika au ya kimawazo (kidha-hania), kwa njia ya hiari na raghba au nguvu na lazima, kutakoambatana au hakutokuambatana na hisia ya kiroho ya kuheshimu, kunyenyekea na kutukuza.

Kwa vyovyote vile, kudura .hiyo ni mwabudiwa na mungu, na mtiifu huyo ni mwabudu na abdi.

Kwa maelezo hayo, inafahamika kwamba neno 'Uungu', 'Mungu' au 'Allah' lina maana sawa na 'uabudaji' na 'Mwabudiwa'.

Katika mfumo mpotofu wa kishirikina ambapo watu hugawanywa katika matabaka mawili ya wastakabari (mustak-biruun) na wastadhaafu (mustadh'afuun) - yaani tabaka linalotawala la mabepari na wanyonyaji, na tabaka la wanyonge na maskini - tunaona mfano dhahiri kabisa wa uhusiano baina ya 'mwabudiwa' na 'waabudu' ambao ni huu uhusiano usio sawa na usio wa haki baina ya matabaka mawili haya. Tukitaka kuwajua waabudiwa na waungu wa jamii mbalimbali katika historia, tusihangaike kuwatafuta miungu wa aina ya mtu, mnyama au kitu katika jamii hizo, bali inatosha kuona mfano mzuri sana wa waungu na waabudiwa wao ambao ni haohao wastakabari waliowakandamiza wastadhaafu (wanyonge), wakawatia utumwani, wakawatawala na wakawafanya wawaabudu (wawatumikie) ili washibishe unyonyaji wao na tamaazao za kumiliki.

Katika jamii kama hizo, dini hasa ya watu ni shirki (ushirikina), kwa sababu kuna idadi kubwa ya miungu au waungu wenye kuwa na uwezo na amri juu ya watu, ambao hufumba macho yao na kuziba masikio yao na kuwaelekeza kwenye njia ya matakwa yao kwa utiifu kamili.

Shirki maana yake ni kumtii na kumwabudu mwingine badala au pamoja na Mwenyezi Mungu. Shirki maana yake ni kuweka mambo yote ya maisha katika udhibiti wa mwingine ghairi ya Mwenyezi Mungu. Shirki maana yake ni kusalimu amri mbde ya kudura na nguvu zisizokuwa za Mwenyezi Mungu, na kuzitegemea katika kutimiziwa mahitaji na kupata mwongozo.

Tawhidi inapingana kabisakabisa na shirki, kwa kuwa inakana na inakataa miungu na waungu hao, inapinga kuwatii, inapinga utawala na mamlaka yao, inakataza kutaka msaada kutoka kwao, na mwishowe, inataka uwakatae kabisa na badala yake ujitolee kwa moyo wote mbele ya Mwenyezi Mungu.

Nara ya kwanza iliyopigwa na Mitume wote wa Mwenyezi Mungu ilikuwa ni kukana shirki na kukiri Tawhidi:

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ...﴿٣٦﴾

"Na kwa hakika tulimtuma Mtume katika kila umma, ya kwamba: 'Mwabuduni Allah na waepukenl mataghuti [watawala wenye kumwasi Mungu].' " (an-Nahl, 16:36).

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾

"Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimpa wahyi ya kwamba: 'Hakuna mungu (aabudiwaye) ila Miml, basi niabuduni.' " (al-Ambiyaa,21:25).

Kwa hivyo, kwa kutangaza shaari hiyo, Mitume waliishutumu mifumo ya kifasidi na ya kishirikina, na wakawahimiza watu wapambane dhidi ya mataghuti ambao ni watetezi wa mifumo hiyo, waasi wa thamani halisi za kibinadamu, na ambao huwalazimisha watu wafuate mfumo wao usio na thamani ili waweze kuhifadhi maslahi yao ya kidhalimu.

Kwa hakika, kukataa shirki ni kukataa mifumo yote ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ambayo ni misingi wa asili ya jamii ya kishirikina. Itikadi ya kishirikina ni kifuniko au kisingizio cha kuhifadhi na kuendeleza hali isiyofaa katika jamii.

Kuwapinga waungu na masanamu maana yake ni kuwapinga watu wote ambao wanawakandamiza na kuwastadhaafisha watu, kwa kutumia mabavu au ujanja, ili wapate kuyatosheleza matamanio yao.

Musa alipotangaza shaari hiyo na aliposema kuhusu utawala mkuu na wa pekee wa Mwenyezi Mungu Mola wa ulimwengu, alitangaza vita dhidi ya Firauni na akamkataa. Hapana shaka kwamba wanabaraza wa Firauni walimshutumu Musa kwa kuwapinga waungu wao, na wakamtuhumu kwa kosa la kuwapinga masanamu na waungu wao wa kimila.

وَقَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوْمَهُ لِيُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَآلِهَتَكَ ﴿١٢٧﴾

"Na wakasema wakuu wa utawala wa Firauni: 'je, utamwacha Musa na watu wake walete ufisadi katika ardhi na kukuacha wewe na waungu wako?'" (al-A'raaf, 7:127).

Lakini Firauni mwenyewe pamoja na kikundi chake cha wafisadi, walijua vizuri sana kwamba hao 'waungu' - yaani masanamu yasiyokuwa na roho - hawakuwa kitu isipokuwa ni kisingizio tu kwa ajjli ya kudai uungu wao, na njia muhimu ya kudumisha uungu wao. Kwa hivyo, ilikuwa ni mantiki kabisa kwa Firauni kujibu mwito wa Musa wa kujitolea kwa Mwenyezi Mungu Mmoja, Muumba wa mbingu na ardhi na Mola wa mashariki na magharibi, kwa kumtisha kumfunga na kumwua, na kuwatishia wafuasi wake kuwaadhibu kwa mateso makali.

قَالَ لَئِنِ اتَّخَذْتَ إِلَـٰهًا غَيْرِي لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ الْمَسْجُونِينَ ﴿٢٩﴾

"(Firauni) akasema: 'Kama ukifichagulia mungu mwingine ghairi yangu, kwa hakika nitakuweka miongoni mwa wafungwa.' " (ash-Shu 'araa, 26:29)

Firauni akamjibu haya mshauri wake ambaye alimshawishi achukue hatua kali ya kumtia adabu Musa na Wana wa Israili:

قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبْنَاءَهُمْ وَنَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَاهِرُونَ ﴿١٢٧﴾

"[Firauni] akasema: 'Hivi karibuni tutawaua wavulana wao na tutawaacha hai wanawake wao, na bila shaka sisi ni wenye nguvu juu yao.' " (al-A 'raaf, 7:127).

Firauni akawaambia haya wachawi wake ambao wali mwamini Musa bila yeye kutegemea:

لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٢٤﴾

"Kwa hakika nitaikata mikono yenu na miguu yenu kwa kubadillsha, kisha nitawasulubini nyote " (a{-A'raaf, 7:124).

Unyama huo unaofanywa dhidi ya jina la Allah na mwito wa Tawhidi, unamaanisha kwamba ujumbe huu wa uhuru na ukombozi hauna maana nyingine isipokuwa:

Kuamini kwamba Allah tu Ndiye Mwenye utawala na mamlaka ya pekee j'uu ya maisha.

Kuwakataa wengine wote wanaodai uungu, na kukubali kuwa mja wa Allah tu.

Kukata minyororo yote ya utumwa wa wengine ghairi ya Allah.

Hii ndiyo roho, asili, kiini, na maana halisi ya itikadi ya Tawhidi ambayo ni kipengee kinachong'ara kabisa cha UmoJa wa Mwenyezi Mungu.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU


YALIYOMO

AKIDA 1

MSAMIATI 1

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI 3

TAASISI YA FIKRA ZA KIISLAMU KUHUSU MTUNGAJI 3

WALIMU WAKE 4

AKIDA 14

TAWHIDI 14

MAANA YA TAWHIDI 14

SHARTI YA KUCHAPA 26

MWISHO WA KITABU 26

YALIYOMO 27

AKIDA

AKIDA

Mwandishi: Sayyid Ali Khamenei
: AMIR ALY DATOO
Kundi: Misingi mikuu ya Dini
Kurasa: 4