TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA- Juzuu 11
Kuweka vikundi Qurani tukufu
mwandishi Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
Lugha ya kitabu سواحیلی
mwaka wa kuchapisha 1404

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

IMEANDIKWA NA: SHEIKH MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYA

IMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HASAN MWALUPA

IMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED

IMEPANGWA KATIKA KOMPYUTA NA: UKHT PILI RAJABU

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI

Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London.

Kama lilivyo jina la Tafsiri yenyewe ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo. Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyo kujipatia wasomaji wengi sana.

Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana kwenda na wakati.

Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung'ang'ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo, hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea, hiyo ilimsaidia sana hata kuweza kutoa kitabu kitwacho 'Al-Fiqh a'laa madhaahabil-khamsah' (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka hivi karibuni Inshaallah).

Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.

Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasyansi kama kina Enstein, Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa.

Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.

Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji.

Mwisho: Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji.

MAKOSA YA CHAPA

Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa, Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa.

Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya msahafu mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswutu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146). Imeandikwa La Ya'alamuun, (hawajui) badala ya Ya'alamuun (wanajua), Mfano wa makosa haya hausameheki.

Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa "Fawqahum ila yawmil qiyama” badala ya “Fawqahum yawamal qiyama", Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile.

Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu jabal amail 'Makosa ya chapa.'

Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: " Hatta idha balagha arbai' na sanah badala ya: Hattaidha balagha ashuddahu arbai ' na sanah"

Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakayoyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefungua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana.

Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: "Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa, kama kwamba hakuna kitu chochote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.

Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin(a.s) :"Watu wote ni wapungufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu."

Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubali- ayale niliyoyapatia na kunisamehe niliyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazi chake, ziwashukie rehema na amani (Amin).

MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH


1

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

Mwendelezo Wa Sura Ya Tisa: Suart At – Tawba.

يَعْتَذِرُونَ إِلَيْكُمْ إِذَا رَجَعْتُمْ إِلَيْهِمْ قُل لَّا تَعْتَذِرُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكُمْ قَدْ نَبَّأَنَا اللَّـهُ مِنْ أَخْبَارِكُمْ وَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٩٤﴾

94. Watawatolea udhuru mtakaporudi kwao, Sema, msitoe udhuru; hatutawaamini, Mwenyezi Mungu amekwishatueleza habari zenu, Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ataviangalia vitendo vyenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi, wa ghaibu na dhahiri awaambie mliyokuwa mkiyatenda.

سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ إِنَّهُمْ رِجْسٌ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٩٥﴾

95. Watawaapia Mwenyezi Mungu mtakaporudi kwao ili muachane nao. Basi achaneni nao, Hakika wao ni uchafu, na makazi yao ni Jahanamu; ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyachuma.

يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِن تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ ﴿٩٦﴾

96. Wanawaapia ili muwe radhi nao. Kama mkiwa radhi nao, basi hakika Mwenyezi Mungu hatakuwa radhi na watu mafasiki.

WATAWATOLEA UDHURU

Aya 94 – 96

MAANA

Watawatolea udhuru mtakaporudi kwao.

Mfumo wa Aya unafahamisha kwamba Aya ilishuka wakati wa kurudi jeshi la Kiislamu kutoka vita ya Tabuk pale Mwenyezi Mungu alipowafahamisha kuwa watakapofika Madina, wanafiki watawakabili na nyudhuru kwa kukaa kwao nyuma, Watatoa nyudhuru za uwongo. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akamwambia Mtume wake:

Sema: msitoe udhuru; hatutawaamini, Mwenyezi Mungu amekwishatueleza habari zenu.

Huu ni ukatazo kutoka kwake Mwenyezi Mungu mtukufu kutokubali udhuru kutoka kwa wanafiki, na ni amri kwa Mtume(s.a.w.w) awaambie kuwa sisadiki chochote katika mnayonitolea udhuru.

Kwa sababu Mwenyezi Mungu amenipa wahyi yale yanayofichwa na nyoyo zenu miongoni mwa shari na unafiki.

Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ataviangalia vitendo vyenu.

Yaani hatukubali nyudhuru zenu mpaka mthibitishe kwa vitendo sio kwa maneno kwamba nyinyi ni wa kweli katika nia zenu na malengo yenu, na wenye ikhlasi katika kumwamini Mwenyezi Mungu kama mnavyodai.

Kisha mtarudishwa Mjuzi, wa ghaibu na dhahiri awaambie mliyokuwa mkiyatenda.

Ghaibu ni yale tusiyoyajua, yanajuliwa na Mwenyezi Mungu.

Maana ni kuwa nyinyi kesho mtasimama mbele ya Mwenyezi Mungu, ambaye halijifichi kwake la kujificha, awape habari ya matendo yenu na awalipe. Ikiwa ni heri basi ni heri na ikiwa ni shari basi ni shari.

Watawaapia Mwenyezi Mungu mtakaporudi kwao ili muachane nao.

Yaani mtakaporudi kutoka katika vita vya Tabuk, Ili muachane nao; yaani mnyamazie unafiki wao ni msiwatahayarize.

Basi achaneni nao.

Yaani wapuuzeni na muwadharau. Baadhi ya wapokezi wanasema kwamba Mtume(s.a.w.w) aliwaamuru waislamu wasiwe na mawasiliano nao. Kisha Mwenyezi Mungu akabainisha sababu ya kuwapuuza na kuwadh rau kwa kauli yake:

Hakika wao ni uchafu, na makazi yao ni Jahanamu; ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyachuma.

Kuna Hadith isemayo: “Tahadharini na kukaa na mauti.” Akaulizwa ni nani hao ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: Kila mwenye kupotewa na imani mjeuri wa hukumu.” Hadith nyingine inasema: “Mwenye hekima zaidi katika watu ni yule anayemkimbia mjinga zaidi katika watu.”

Wanawaapia ili muwe radhi nao. Kama mkiwa radhi nao, basi hakika Mwenyezi Mungu hatakuwa radhi na watu mafasiki.

Aina hii ya kukataza kwa upole ni mfumo fasaha zaidi. Kuwa radhi Waumini kunatokana na radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawi radhi na watu mafasiki.

Sasa vipi Waumini wawe radhi nao? Yeyote anayedai kumwamini Mwenyezi Mungu huku akiwa radhi na yule aliyeghadhabikiwa na Mwenyezi Mungu basi yeye ni mnafiki, hilo halina shaka.

الْأَعْرَابُ أَشَدُّ كُفْرًا وَنِفَاقًا وَأَجْدَرُ أَلَّا يَعْلَمُوا حُدُودَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٩٧﴾

97. Mabedui wamezidi sana katika kufuru na unafiki na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.

وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغْرَمًا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ الدَّوَائِرَ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٩٨﴾

98. Miongoni mwa mabedui wako wanaochukulia kuwa wanayoyatoa ni gharama ya bure, Na wanawangojeleamisiba. Misiba mibaya itakuwa juu yao. Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi, Mjuzi.

وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَاتٍ عِندَ اللَّـهِ وَصَلَوَاتِ الرَّسُولِ أَلَا إِنَّهَا قُرْبَةٌ لَّهُمْ سَيُدْخِلُهُمُ اللَّـهُ فِي رَحْمَتِهِ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٩٩﴾

99. Miongoni mwa mabedui wako wanaomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na wanachukulia wanayoyatoa ndiyo ya kuwasogeza kwa Mwenyezi Mungu na dua za Mtume. Sikilizeni! Hakika hayo ni mambo ya kuwasogeza, Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehema yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu.

MABEDUI WAMEZIDI SANA

Aya 97 – 99

USHAMBA NA KUENDELEA

Mabedui wamezidi sana katika kufuru na unafiki na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.

Hii haina maana ya kuwagawanya watu kwenye ushamba na kuendelea kuwafanya bora watu wa mjini kuliko mabedui. Vipi? Iwe hivyo na hali Mwenyezi Mungu, katika Aya inayofuatia, anaelezea kuwa kuna watu katika mabedui wenye ikhlasi katika imani yao na matendo yao.

Kama ingelikuwa ubedui ni dhambi basi angeliuharamisha, sawa na alivyoharamisha dhulma. Na Qur’ani huwagawanya watu kwa misingi ya takua, yaani kumwamini Mwenyezi Mungu na amali njema, na imebainisha hakika hii na kuisisitiza kwa mifumo mbali mbali, bali hakika hiyo ndiyo lengo la kwanza na la mwisho la kuteremsha Qur’ani, mwito wake, mafunzo yake na sharia yake.

Aya hii tuliyo nayo inaashiria hilo kwani kauli yake hiyo Mwenyezi Mungu:

“Mabedui wamezidi sana katika kufuru na unafiki” inafahamisha kuwa sababu ya kutukanwa ni ukafiri na unafiki na kutojua hukumu za Mwenyezi Mungu alizoteremsha kwa Mtume wake, na wala ubedui sio sababu ya kutusiwa.

Ni kweli kuwa maisha ya ubedui (ushamba) na kuwa kwake mbali na maendeleo na maarifa, yanasababisha tabia ngumu na ya ovyo na kukeuka mipaka, lakini hilo ni kosa la mazingara sio kosa la ubedui, Kuna hadith isemavyo ifahamuni halali na haramu, vinginevyo basi nyinyi ni mabedui.” Yaani mtakuwa kama wao katika ujinga na kuwa mbali na maendeleo.

Baada ya utangulizi huu, sasa turudie kwenye Aya, Maana yaliyo kusudiwa katika Aya ni kuwa katika mabedui kuna makafiri na wanafiki sawa na wakazi wa mjini, isipokuwa makafiri wa kibedui na wanafiki wao ni zaidi kuliko wengine katika wakazi wa mjini.

Hayo ndio maana yanayopatikana katika dhahiri ya Aya, nasi tunaongezea kwamba ikiwa sababu inayowajibisha hilo ni ugumu wa tabia basi vile vile watakuwa ni wenye imani zaidi wakiamini na wenye ikhlasi zaidi watakapokuwa na ikhlasi, kwa vile sababu ni moja.

Kwa mnasaba huu tunadokeza maelezo yaliyokuja katika Kitabu Mizan Sha’rani, mlango wa Shahada, ninamnukuu: “Hambali hawakubali ushahidi wa bedui dhidi ya mtu wa mjini na Malik anaukubali katika kujeruhi na kuua tu, lakini sio katika haki nyingine”.

Tunajua wajihi wa anayesema kuwa haukubaliwi ushahidi wa asiyekuwa Mwislamuu dhidi ya Mwislamuu. Lakini kumlinganisha Bedui mwislamu na asiye kuwa mwislamu katika ushahidi, hatujui kumepitiwa njia gani. Mwenyezi Mungu anasema:

وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ ﴿٢﴾

“Na mshuhudishe mashahidi wawili waadiilifu miongoni mwenu” (65:2)

na wala hakusema katika wakazi wa mjini. Linalozingatiwa katika kukubaliwa ushahidi ni uadilifu sio ushamba wala kuendelea.

Miongoni mwa mabedui wako wanaochukulia kuwa wanayoyatoa ni gharama ya bure.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja kuwa miongoni mwa mabedui wako wanafiki, hapa anataja kuwa wao wanatoa mali zao, lakini wanaona kutoa huku ni gharama za bure sizizokuwa na faida, na kwamba thawabu na malipo yake siku ya Kiyama ni mambo ya kubandikwa tu.

Na wanawangojelea misiba.

Wanangonjea maadui wawashinde waislamu na wanatamani wamalizwe ili wapumzike na gharama hii ya hasara, kama wanavyoitakidi.

Misiba mibaya itakuwa juu yao.

Kuna kundi katika wafasiri wanaosema kuwa hii ni dua kwa wanafiki kuwa yawapate yale wanayowatamania Waumini. Pia inawezekana kuwa ni kutolea habari hali ya adhabu watakayokuwa nayo wanafiki siku ya Kiyama.

Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi Mjuzi,

Anasikia wanayoyasema na anajua wanayoyaficha.

Miongoni mwa mabedui wako wanaomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na wanachukulia wanayoyatoa ndiyo ya kuwasogeza kwa Mwenyezi Mungu na dua za Mtume.

Mabedui ni kama watu wengine wako wanafiki wanaonyesha yasiyokuwa katika nyoyo na kuona wanayoyatoa ni gharama za bure sio wajibu; kama ilivyodokeza Aya iliyotangulia.

Na miongoni mwao wako Waumini wenye ikhlasi wanaotoa kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na thawabu zake na kutaka dua ya Mtume ya kupata baraka na maghufira, kama ilivyoashiria Aya hii.

Sikilizeni! Hakika hayo ni mambo ya kuwasogeza, Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehema yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu.

Dhamiri ya hayo ni yale wanayoyatoa; yaani kutoa huko kunakurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Maana ni kuwa wale walioamini wakatoa kwa kutaka kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atakubali kutoa kwao; atawaingiza katika pepo yake na atawasamehe makosa waliyotekeleza na kuyakosa.

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٠٠﴾

100. Na waliotangulia wa kwanza katika wahajiri na Ansari. Na wale waliowafuata kwa wema. Mwenyezi Mungu yuko radhi nao na wao wako radhi naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele, Huko ndiko kufuzu kukubwa.

وَمِمَّنْ حَوْلَكُم مِّنَ الْأَعْرَابِ مُنَافِقُونَ وَمِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ مَرَدُوا عَلَى النِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ ﴿١٠١﴾

101. Na miongoni mwa mabedui walio pambizoni mwenu wamo wanafiki na katika wenyeji wa Madina wako waliobobea katika unafiki, Huwajui, sisi tunawajua, Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa.

وَآخَرُونَ اعْتَرَفُوا بِذُنُوبِهِمْ خَلَطُوا عَمَلًا صَالِحًا وَآخَرَ سَيِّئًا عَسَى اللَّـهُ أَن يَتُوبَ عَلَيْهِمْ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٠٢﴾

102. Na wengine wamekiri dhambi zao; wakachanganya vitendo vyeman vingine viovu, Huenda Mwenyezi Mungu akapokea toba zao, Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wamsamaha, Mwenye kurehemu.

WALIOTANGULIA WA KWANZA

Aya 100 – 102

MAANA

Katika Aya hizi tatu Mwenyezi ametaja aina nne katika uma, kisha akaongezea aina ya tano katika Aya 106, tutaizungumzia tutakapofika huko. Ama aina nne ni hizi:

Na waliotangulia wa kwanza katika wahajiri na Ansari.

Wote (Wahajiri na Ansari) wamefanywa ni aina mbili zilizotangulia. Hakuna mwenye shaka kuwa makasudio ya kutangulia ni katika Hijra na Nusra (kuhama na kuwasaidia waliohama).

Sifa inatambulisha hivyo, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakuelezea wakati wa huko kutangulia. Ndio maana wakatofautiana wafasiri: Kuna wenye kusema kuwa makusudio ni kuhama na usaidizi kabla ya siku ya Badr. Wengine wanasema kuwa ni kabla ya Baia ya Ridhwani iliyokuwa chini ya mti siku ya Hudaibia. Mwingine anasema ni wale walioswali Qibla mbili.

Tuonavyo sisi ni kwamba waliotangulia kuhama na kusadia (Muhajirin na Ansari) ni kabla ya waislamu kuwa na nguvu ya kuwazuia wanaowa- chokoza na kufitini dini yao; kama walivyofanya washirikiana mwanzo wa dawa.

Kwa hiyo basi kauli ya kwanza ndiyo yenye nguvu, kwa sababu nguvu ya waislamu ilidhihiri siku ya Badr walipohisi washirikina ukakamavu na nguvu ya Uislamu.

Na wale waliowafuata kwa wema.

Nao ni kila mwenye kwenda njia ya waliotangulia wenye ikhlasi. Anasema Tabrasi: Anaingia katika hao kila atakayekuja baada yao hadi Kiyama”.

Yamekuja maelezo ya waliowafuata kwa wema katika Aya isemayo:

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٠﴾

“Na wale waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu! Tughufurie sisi na ndugu zetu waliotutangulia katika imani wala usijaalie katika nyoyo zetu mfundo kwa walioamini. Mola wetu! Hakika wewe ni Mpole sana Mwenye kurehemu” (59:10).

Tunataraji watapata funzo kwa Aya hii wale wanaotoa mwito wa imani na huku wenyewe wamejawa na mifundo ya hasadi.

Aina mbili hizi – waliotangulia na waliowafuatia – ndio ambaoMwenyezi Mungu yuko radhi nao na wao wako radhi naye na amewaandalia Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele.

Mwenyezi Mungu yuko radhi nao kwa twaa yao na ikhlasi yao, na wao wako radhi naye kwa neema alizowamiminia.

Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Yaani hakuna kufuzu kwa maana yake sahihi ila kwa radhi ya Mwenyezi Mungu.

Utauliza : Dhahiri ya Aya inaonyesha kule tu kutangulila kwa kuhama na kusaidia, kunatosheleza kupata radhi za Mwenyezi Mungu, na kwamba huo ni wema usiodhuriwa na uovu. Sasa je, dhahiri hii, ni hoja kiasi ambacho ni wajibu kwetu kumtukuza kila aliyetangulia kwa Hijra na Nusra, hata kama yamethibiti kwake maasi?

Jibu : Makusudio ya waliotangulia wa kwanza ni wale waliomtii Mwenyezi Mungu na wakafa juu ya sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) .

Ama wale waliomwasi na wakafanya uovu baada ya kutangulia hawachanganywi na walio na radhi ya Mwenyezi Mungu; vipi iwe hivyo na hali yeye Mwenyezi Mungu anasema:

مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٢٣﴾

“Mwenye kutenda uovu atalipwa kwa ovu huo, Wala hatajipatia mlinzi wala msaidizi zaidi ya Mwenyezi Mungu.” Juz.5 (4:123)

لِيَجْزِيَ اللَّـهُ كُلَّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٥١﴾

“Ili Mwenyezi Mungu ailipe kila nafsi kwa yale iliyoyachuma, Hakika Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kuhisabu” (14:51).

Na amepokea Bukhari, katika sahih yake Juz.9 Kitabu Alfitan mlango wa kwanza, Hadith isemayo:

“Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) atasema siku ya Kiyama: Hao ni swahaba zangu. Naye ataambiwa: Hujui walifanya nini baada yako. Hapo nitasema: Ole wake! Ole wake, mwenye kuibadilisha (dini yake) baada yangu” [1]

Hakuna mwenye shaka kwamba waliotangulia katika kuhama na kusaidia wahamiaji wana ubora, lakini hili ni jambo jingine na kusamehewa maasi au kuwa wasihisabiwe ni jambo jingine.

3.Na miongoni mwa mabedui walio pambizoni mwenu wamo wanafiki na katika wenyeji wa Madina wako waliobobea katika unafiki, Huwajui, sisi tunawajua.

Amekwisha taja Mwenyezi Mungu (s.w.t) wanafiki katika Aya kadhaa, Hapa anawataja kwa mnasaba wa kuwataja waumini waliotangulia; na ili kumpa habari Mtume wake mtukufu sehemu walikokwamba wao wamemzunguka kila upande.

Wako Madina anapokaa yeye na vitongojini mwake, sehemu za jangwani. Na kwamba wanafiki wa Madina ni mahodari katika fani ya unafiki kiasi cha kuweza kuuficha kwa Mtume pamoja na kuwa nao wakati mwingi. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) anabainisha malipo ya wanafiki kwa kauli yake:

Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa.

Adhabu hii ya mwisho ambayo watarudishwa ni maarufu, Jahanamu. Ama aina na wakati wa adhabu ya mara ya kwanza na ya pili kabla ya adhabu ya Jahanamu, haikuashariwa na Aya.

Sio mbali kuwa adhabu ya mara ya kwanza ni wakati wa kufa kwa sababu ya kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:

وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ يَتَوَفَّى الَّذِينَ كَفَرُوا الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿٥٠﴾

“Na lau ungeliwaona Malaika wanapowafisha wale waliokufuru wakipiga nyuso zao na migongo yao na (kuwaambia) ionjeni adhabu iunguzayo” Juz.10 (8:50).

Ama adhabu ya mara ya pili ni adhabu ya kaburi kutokana na Hadith nyingi kuwa kaburi ya kafiri ni shimo miongoni mwa mashimo ya Jahanamu, na kaburi ya mumin ni bustani katika bustani za peponi.

4.Na wengine wamekiri dhambi zao; wakachanganya vitendo vyema na vingine viovu.

Hawa ni wale waumini ambao mara kwa mara wanafanya mema kwa msukumo wa imani yao na mara nyingine hawaa hushinda imani yao wakafanya uovu, nao ni wengi. “Ni nani ambaye hulka zake zote zinaridhisha” isipokuwa wale waliohifadhiwa na Mola wako. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akabainisha hukumu ya hawa kwa kauli yake:

Huenda Mwenyezi Mungu akapokea toba zao kwa vile wao wametambua makosa na kuyakiri kwa hiyo wamekuwa, kwa hilo, ni mahali pa kutarajia rehema ya Mwenyezi Mungu na maghufira yake.

Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

Katika Majmaul-Bayan imeelezwa: “Wafasiri wanasema: ‘Huenda’ ikitoka kwa Mwenyezi Mungu inakuwa ni hakika; isipokuwa amesema ‘huenda’, ili wawe baina ya tamaa na wasibwete wakupuuza toba.


2

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٠٣﴾

103. Chukua sadaka katika mali zao uwasafishe na uwatakase kwayo. Na uwaombee rehema, Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi, Mjuzi.

أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ هُوَ يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٠٤﴾

104. Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayekubali tob aya waja wake na kuzipokea sadaka. Na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu?

وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾

105. Na sema: Tendeni vitendo Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini wataviona vitendo vyenu na mtarudishwa kwa Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, naye awaambie mliyokuwa mkiyatenda.

وَآخَرُونَ مُرْجَوْنَ لِأَمْرِ اللَّـهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمْ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيْهِمْ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿١٠٦﴾

106. Nawengine wanangojea amri ya Mwenyezi Mungu, ama atawaadhibu au awakubalie toba, Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.

CHUKUA SADAKA KATIKA MALI ZAO

Aya 103 – 106

MAANA

Chukua sadaka katika mali zao uwasafishe na uwatakase kwayo.

Wameafikiana kuwa dhamir katika ‘kwayo’ ni ya sadaka, na wakahitalifiana katika dhamir ya mali zao. Ikasemwa kuwa inawarudia wale waliochanganya amali njema na mbaya Ikasemwa kuwa inawarudia matajiri wote kwa sababu Aya imeshuka katika zaka ya wajibu. Kauli hii iko karibu na maana.

Kwa hiyo maana yatakuwa ni chukua ewe Mtume! Zaka katika mali za matajiri, kwani zinawatakasa na ubakhili kwa haki ya Mwenyezi Mungu. Tumezungumzia zaka katika kufasiri Aya 60 ya Sura hii, na Juz. 3 (2: 274)

Na uwaombee rehema, Hakika maombi yako ni utulivu kwao.

Yaani muombee baraka na maghufira mwenye kutoa zaka, kwani hupata furaha na raha ya nafsi kwa dua yao.

Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi, Mjuzi.

Anasikia na ataitikia maombi yako kwa watoaji zaka, na anajua nia ya anayetoa zaka kwa roho safi, kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu peke yake.

Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayekubali toba ya waja wake na kuzipokea sadaka?

Mfumo unaashiria kwamba toba imetajwa hapa kwa kuashiria kuwa mwenye kuzuia zaka, kisha akatubia na akaitoa, basi Mwenyezi Mungu ataikubali toba yake na kupokea sadaka yake. Maana ya kukubali ni kwamba Mweneyezi Mungu, ambaye limetukuka neno lake atailipa thawabu. Kuna Hadith isemayo: “Hakika sadaka inaingia mkononi mwa Mwingi wa rehema kabla ya kuingia katika mkono wa mwombaji.” Mkono wa Mwingi wa rehema ni fumbo la kukubali.

Na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu?

Yaani anakubali toba na kuwarehemu wenye kutubia.

Na sema: Tendeni vitendo Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wataviona vitendo vyenu.

Katika kitabu Futuhatul-Makkiyaa J4, ameitaja Muhyiddin bin Al-arabi, Aya hii na kuifafanua kuwa maana ya kuona yanatofautiana kulingana na mwonaji. Kwa hiyo maana ya kuona kwa Mwenyezi Mungu ni kukijua kitu kwa pande zake zote. Maana yake kwa Mtume(s.a.w.w) ni kujua kitu kwa njia ya wahyi uliomshukia. Maana yake kwa na mumin mwenye maarifa, ni kujua kwa kadiri ya alivyojua na kufahamu kutokana na wahyi ulioteremshiwa Mtume(s.a.w.w) .

Kwa hiyo basi, mwenye kufanya amali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu anajua hakika ya amali yake na kuiridhia; Mtume naye anajua kuwa amali hii imeridhiwa kwa Mwenyezi Mungu, na mumin pia anajua kuwa ni mwenye kuridhiwa na Mtume. Natija ya mwisho ni kuwa mwenye kufanya amali njema anaridhiwa na Mwenyezi Mungu, Mtume na waumini.

Na wengine wanangojea amri ya Mwenyezi Mungu, ama atawaadhibu au awakubalie toba.

Katika Aya ya 100 na inayofuatia, Mwenyezi Mungu (s.w.t), ametaja aina nne ya watu: Waliotangulia kuhama na waliotangulia kusaidia, waliowa- fuatia hao kwa wema, wanafiki na wenye kukiri dhambi zao.

Katika Aya hii ameashiria watu ambao hakuwapa sifa maalum, kama alivyofanya kwa aina hizo nne, wala hakuweka wazi hukumu yao; isipokuwa amesema kuwa wao wanangojea adhabu ya Mwenyezi Mungu au msamaha wake; yaani jambo lao liko Kwake Yeye Peke Yake, amewaficha. Huenda hekima ya hivi ni kuwa wawe baina ya kuhofia na kutarajia, wasiwe na tamaa wala kukata tamaa.

Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.

Ni Mjuzi, wa yanayowafaa hawa na wengineo, na ni mwenye hekima kati- ka kufanya wangojee hukumu yao na katika kila analolifanya.

Wafasiri wengi wanasema kuwa Aya hii iliwashukia jamaa katika waislam waliobaki nyuma katika vita vya Tabuk, kisha wakajuta.

Lakini Aya 118, imeeleza kuwa masahaba watatu walibaki nyuma katika vita ya Tabuk, kisha wakatubia na kwamba Mwenyezi Mungu aliwatakabalia toba yao na akatangaza kukubali kwake, wala hakuwacha baina ya kuhofia na kukata tamaa.

Haya ndiyo yaliyotudhihirikia katiaka kufasiri Aya hii tuliyo nayo: hatujui tutapata maana gani tutakapofikia Aya hiyo ya 118, Tuonane huko.

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًا بَيْنَ الْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِّمَنْ حَارَبَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ مِن قَبْلُ وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا الْحُسْنَىٰ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١٠٧﴾

107. Na wale waliotengeza msikiti kwa ajili ya kudhuru na ukafiri na kuwafarikisha waumini na mahali pa kuvizia kwa yule aliyempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume hapo kabla. Na bila shaka wataapa kwamba hutakukusudia ila wema; na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao ni waongo.

لَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا لَّمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى التَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُوا وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ ﴿١٠٨﴾

108. Usisimame humo kabisa, Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa takua tangu siku ya mwanzo, unastahiki zaidi wewe usimame humo. Humo mna watu wanopenda kuji takasa; na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaojitakasa.

أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ تَقْوَىٰ مِنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠٩﴾

109. Je, aliyeweka msingi wa jengo lake juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na radhi (zake) ni bora au aliyeweka msingi jingo lake juu ukingo wa shimo linalomomonyoka, na likamomonyoka likaanguka pamoja naye katika moto wa Jahannamu na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.

لَا يَزَالُ بُنْيَانُهُمُ الَّذِي بَنَوْا رِيبَةً فِي قُلُوبِهِمْ إِلَّا أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمْ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿١١٠﴾

110. Jengo lao hilo walilolijenga litaendelea kuwa ni sababu ya kutiwa wasiwasi nyoyoni mwao, isipokuwa nyoyo zao zikikatikakatika. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.

MSIKITI WA MADHARA

Aya 107 –110

MAANA

Aya zilizotangulia zimeonyesha aina mbali mbali za unafiki wa wanafiki. Aya hii inaonyesha aina nyingine ya unafiki wao na hila yao.

Jamaa fulani katika wanafiki wa Madina waliona njia nzuri ya kuufanyia vitimbi Uislam na Mtume wake Muhammad(s.a.w.w) ni kujenga msikiti chini ya sitara ya kujumuika kumwabudu Mwenyezi Mungu na kunadi kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Nyuma ya nembo hii watakuwa wamemkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kuudhuru Uislamu na waislam na kuwagawanya.

Naam walijenga msikiti huu vizuri sana na kuutolea mapesa. Baada ya kuukamilisha walimwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu wakamwambia: Nyumba zetu ziko mbali na msikiti wako inakuwa vigumu kwetu kuhudhuria na tunachukia kuswali swala isiyokuwa ya Jamaa; nasi tumejenga msikiti kwa lengo hili na kwa ajili ya wanyonge na vilema. Kama utaswali humo basi itakuwa ni vizuri na tutabaruku kuswali mahali utakaposwali.

Hivi ndivyo walivyo wanafiki na wahaini kila wakati, wanabeba nembo za kutengeneza kumbe wanataka kubomoa. Lakini mara moja inafichuka aibu yao na kufedheheka mbele ya watu wote; kama walivyofedheheka wenye msikiti wa madhara, pale Mwenyezi Mungu alipomfahamisha Mtume wake hakika yao, kwa kusema:

Na wapo waliotengeza msikiti kwa ajili ya kudhuru na ukafiri na kuwafarikisha waumini na mahali pa kuvizia kwa yule aliyempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume hapo kabla.

Aya tukufu inasema kuwa waliojenga msikit wa madhara wana malengo manne:

1. Kuwadhuru waislamu.

2. Kumkufuru Mwenyezi Mungu na kumtia ila Mtume wake.

3. Kuwagawanya waislamu na kuwaweka mbali na Mtume wa Mwenyezi Mungu.

4. Kuufanya msikiti ni maficho ya yule aliyempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake zamani.

Wameafikiana wafasiri na waandishi wa sera ya Mtume kwamba makusudio ya adui aliyempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni mtu mmoja katika Khazraji anyeitwa Abu Amir Arrahib[2] .

Alikuwa ameingia ukiristo, mwenye cheo katika watu wake, Mtume(s.a.w.w) alipofika Madina alipambana kiuadui na mlanifu huyu ambaye Mtume alikuwa akimwita fasiki.

Alipoona Mtume anazidi kupata nguvu, alikimbilia Makka kuwachochea Maquraish dhidi ya Mtume, Baada ya ushindi wa Makka alikimbilia Taif.

Watu wa Taif waliposilimu alikimbilia Sham. Huko aliwaandikia wafuasi wake wamjengee msikiti kwa sababu yeye atakuja na jeshi la Kaizari kumpiga vita Muhammad(s.a.w.w) .

Iliposhuka Aya hii, Mtume(s.a.w.w) akiwambia baadhi ya masahaba zake: “Nendeni kwenye msikiti huu wa watu madhalimu muuvunje.”

Wakafanya hivyo na Mtume(s.a.w.w) akaamrisha pale mahali pawe ni jaa. Baadhi ya mapokezi yameelezea kufananishwa msikiti wa madhara na ndama aliyeabudiwa na Waisrail na Musa akiwa hai. Kama ambavyo Nabii Musa aliamrishwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) kumvunjavunja ndama, vile vile Mtume aliamrishwa auvunje mskiti wa madhara.

Na, msikiti wowote, taasisi au klabu yoyote inayoundwa kwa sababu ya njama dhidi ya waumini basi hiyo ni ndama wa waisrail na ni msiki wa madhara, ni wajibu kuuvunja na kuufanya jaa.

Tangu yalipopatikana mafuta katika miji ya Kiarabu, mashirika ya nje ya kusimamia mafuta yalikuja na maamia ya misikiti ya madhara kwa sura mbali mbali. Miongoni mwa sura hizo ni kama hizi zifuatazo: Ile iliyobandikwa jina la sehemu ya kuabudia au vyuo, yenye jina la ofisi kuu au taasisi za kidini na yenye majina ya maendeleo ya kijamii au vilabu vya michezo.

Mingine ni ile iliyojitokeza kwa sura ya kitab, gazeti au mhadhara unao tangazwa kwenye idhaa kwa jina la dini au la nchi na mengineyo mengi ambayo dhahiri yake ni rehema na ndani yake ni adhabu. Yote hayo lengo lake ni kuharibu dini na nchi.

Tumezungumzia kuhusu nembo za kidini katika Juz 4 (3:142)

Na bila shaka wataapa kwamba hutakukusudia ila wema; na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao ni waongo.

Yaani hawa wanafiki waliapa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kwamba lengo la kujenga msikiti huu ni ibada tu na manufaa kwa waislamu; na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wao hawakujenga msikiti ila kwa kutaka kuwadhuru waislamu, kumkufuru Mwenyezi Mungu, kuwatenganisha Waumini na maficho ya anayempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Usisimame humo kabisa.

Maneno anaambiwa Mtume, lakini makatazo ni kwa wote; sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu:

أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ ﴿٧٨﴾

“Simamisha Swala jua linapopenduka” (17:78)

Wafasiri wamesema kuwa makusudio ya usisimame, hapa, ni usiswali. Lakini kwa dhahiri hapa, kusimama ni ujumla, kunachanganya swala na mengineyo.

Kwa vyovyote ilivyo, kauli yake Mwenyezi Mungu usisimame humo kabisa ni dalili mkataa ya kutosihi swala katika msikiti uliojengwa kuwadhuru waislamu na kuwatenganisha na kwamba mwenye kuswali humo, basi swala yake ni batil, ni lazima airudie mahali pengine, Kwa sababu ukatazo katika ibada unafahamisha kuharibika.

Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa takua tangu siku ya mwanzo, unastahiki zaidi wewe usimame humo.

Imesemekana kuwa makusudio ni msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kwa sababu ndio uliojengwa siku ya kwanza Madina. Na ikasemekana kuwa ni Msikiti Quba ambao waliujenga Bani Amr bin Auf. Kwa dhahiri ni kwamba makusudio ni kila msikiti uliojengwa kwa ajili ya kumcha mungu, Kwa sababu neno Msikiti limekuja kiujumla (nak`ra).

Na kauli yake:‘Tangu siku ya mwanzo, ’ maana yake ni kuwa umejengwa kwa lengo la uislamu tangu siku ya kuanza kujengwa kwake. Kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Unastahiki zaidi,’ maana yake ni kwa uhakika, na wala sio kuwa huu ni bora zaidi kuliko wa madhara. Kwa sababu msikiti wa Madhara sio bora hata kidogo na haifai kuswali ndani yake kwa vyovyote vile.

Humo mna watu wanopenda kujitakasa; na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaojitakasa.

Yaani, msikiti huu ambao umeasisiwa kwa msingi wa takua, wenye ikhlasi wanaukusudia kwa swala na ibada ya Mwenyezi Mungu tu, si kwa unafiki na njama dhidi ya uislamu na Mtume; kama walivyofanya wenye msikiti wa madhara.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameleta ibara ya swala hapa kwa neno kuji- takasa, kwa sababu swala inamtakasa mtu na madhambi. Kuna Hadith isemayo: “Hakika swala ni kama mto unaopita, mwenye kuoga humo mara tano kila siku hatabakiwa na uchafu; vile vile mwenye kuswali mara tano kila siku hatabakiwa na dhambi.

Haya ndiyo tuliyoyafahamu katika Aya hii, pamoja na kukiri kuwa hakuna mfasiri yeyote aliyefasiri kutakata kwa maana ya swala, kama tunavyojua; na kwamba wengi wao wamefasiri kwa maana ya kutakasa uchafu kwa maji.

Je, aliyeweka msingi wa jengo lake juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na radhi (zake) ni bora au aliyeweka msingi jengo lake juu ya ukingo wa shimo linalomomonyoka, na likamomonyoka likaanguka pamoja naye katika moto wa Jahannamu na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.

Makusudio ya Aya ni kutofautisha baina ya msikiti wa Takua na msikiti wa madhara. Kwani wa madhara hauna uthabiti na unaweza ukaanguka kwenye moto mara moja; sawa na ambaye amejenga ukingoni mwa mto au kwenye mto. Ama jengo la msikiti wa takua ni thabiti lenye msingi imara usiotingishwa na chochote; na watu wake wako katika amani. Aya hii ni mfano wa Aya isemayo:

لَا يَسْتَوِي أَصْحَابُ النَّارِ وَأَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمُ الْفَائِزُونَ ﴿٢٠﴾

“Hawalingani sawa watu wa motoni na watu wa peponi. Watu wa peponi ndio wenye kufuzu” (59:20).

La kushangaza ni kauli ya baadhi ya wafasiri kwamba kauli ya ‘moto wa Jahanamu’ ni ishara ya yaliyotukia duniani kuwa moto ulitoka kwenye mskiti wa madhara na moshi wake ukabakia hadi zama za Abu jafar Al-Mansuru.

Jengo lao hilo walilolijenga litaendelea kuwa ni sababu ya kutiwa wasiwasi nyoyoni mwao, isipokuwa nyoyo zao zikikatikakatika. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.

Makusudio ya wasiwasi hapa, ni kwamba wanafiki hawakuamini utume wa Muhammad(s.a.w.w) . Kukatika nyoyo ni fumbo la kufa. Maana ni kuwa wao walijenga msikiti wakiwa na shaka bila ya kumwamini Muhammad(s.a.w.w) , watabaki na shaka hiyo hadi kufa.

إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّـهِ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١١١﴾

111. Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba wao wapate Pepo, wanapi gana katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hiyo wanaua na kuuawa. Ni ahadi aliyojilazimisha kwa haki katika Tawrat na Injil na Qur’ani. Na ni nani atekelezaye zaidi ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliofanya naye, Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

التَّائِبُونَ الْعَابِدُونَ الْحَامِدُونَ السَّائِحُونَ الرَّاكِعُونَ السَّاجِدُونَ الْآمِرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَالنَّاهُونَ عَنِ الْمُنكَرِ وَالْحَافِظُونَ لِحُدُودِ اللَّـهِ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١٢﴾

112. Wanaotubia, wanaoabudu wanaohangaika, wanaorukuu, wanaosujudu, wanaoamrisha mema na wanaokataza maovu na wanaohifadhi mipaka ya Mwenyezi Mungu, Na wape bishara Waumini.

MUNGU HUUZA NA KUNUNUA

Aya 111 – 112

MAANA

Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba wao wapate Pepo, wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hiyo wanaua na kuuawa.

Mnunuzi ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) muuzaji ni mumin, bidhaa ni nafsi na mali, cha kununuliwa ni pepo, na madalali ni Mitume. Bei yenyewe ni ya mkopo; kwamba muuzaji akabidhi bidhaa kwa mnunuzi atakapoitaka, lakini thamani yake atalipwa baadaye; na Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini; na hakuna mwenye kutekeleza ahadi na tajiri zaidi ya Yeye.

Utauliza : Mungu ni muumbaji wa nafsi na Mwenye kuruzuku mali, sasa vipi mwenye kumiliki kitu akinunue.

Jibu : Huku siko kununua kunakojulikana; isipokuwa ni kuhimiza twaa. Mwenyezi Mungu ameleta ibara ya kununua kwa mambo mawili:

Kwanza : mtiifu ategemee malipo na thawabu ya twaa yake; sawa na anavyotegemea muuzaji thamani badala ya bidhaa yake.

Pili : kuzindua kuwa imani sio tu maneno ya mdomoni, picha za akilini au matamanio yanayohisiwa katika nyoyo; isipokuwa ni kujitolea mhanga kwa nafsi na mali, kutafuta thawabu za Mwenyezi Mungu ambazo ni ghali zisizokwisha; sawa na anavyotoa mnunuzi milki yake katika bidhaa ambayo anaiona ina manufaa na yenye kufaa.

Kitu kikubwa kwa binadamu ni uhai wake na nafsi yake. Ama kupenda kwake mali ni kwa kuwa hiyo ni nyenzo ya kuhifadhi uhai na kutekeleza matakwa yake na hawaa zake.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawatahini wanaodai wana imani kwa vitu wanavyovipenda ili ampabanue mkweli wa imani na mwongo; wala hataweza kutoa hoja kesho kwa saumu yake na swali yake akiwa amefanya ubakhili na kujizuia kujitolea kwa nafsi yake na mali yake.

Ni ahadi aliyojilazimisha kwa haki.

Hii ni sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu:

كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ﴿١٢﴾

Amejilazimisha rehema Juz.7 (6:12)

Yaani yeye mwenyewe ndiye aliyejiwajibshia, Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaahidi wapigania jihadi Pepo ikawa ni haki yao kutokana na ahadi hii;

hasa baada ya kuisajilikatika Tawrat na Injil na Qur’ani. Na ni nani atekelezaye zaidi ahadi kuliko Mwenyezi Mungu?

Lengo la usisitizo huu ni kuwa wapigania jihadi wawe na uhakika wa malipo na thawabu adhimu; mpaka wawe kama walioyaona kwa macho, wafurahi na wapate bishara.

Basi furahini kwa biashara yenu mliyofanya naye, Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

Huu ni usisitizo mwingine wa ahadi ya malipo mema. Watalamu wa elimu ya Tawhidi wanasema kuwa Mwenyezi Mungu akiahidi thawabu, basi atatekeleza aliyoahidi, na akiahidi adhabu basi ana hiyari, akiadhhibu ni kwa uadilifu wake na akasamehe ni kwa fadhila zake; na Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja.

Tumeizungumzia thamani ya Pepo katika kufasiri Juz. 2 (2:155).

Kisha Mwenyezi Mungu akawasifu wale waliouza nafsi zao na mali zao kwa Pepo yake, kwa sifa hizi zifuatazo:

Wanaotubia kwa kila wanalolikosea; hata kama ni la makruh.

Wanaoabudu . Yaani wenye ikhlasi katika matendo yao yote.

Wanaohimidi Mwenyezi Mungu katika raha na dhiki.

Wanaohangaika katika ardhi kutafuta elimu au riziki ya halali.

Wanaorukuu, wanaosujudu, Yaani wanaoswali.

Wanaoamrisha mema na wanaokataza maovu. yaani wanaoneza mwito wa Mwenyezi Mungu na twaa yake na kupamba na kila anayechezea haki yoyote miongoni mwa haki za Mungu na haki za waja wake.

Na wanaohifadhi mipaka ya Mwenyezi Mungu . Mipaka yake ni halali yake na haramu yake

Na wape bishara Waumini walio na sifa hizi, kuwa wao wana fadhila kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.


3

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿١١٣﴾

113. Haimfalii Mtume na wale walioamini kuwatakia msamaha washirikina ijapokuwa ni jamaa. Baada ya kuwabainikia kuwa wao ni watu wa motoni.

وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ ﴿١١٤﴾

114. Na haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake ila ni kwa sababu ya ahadi aliyofanya naye, lakini ilipom pambanukia kuwa yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, alijiepusha naye. Hakika Ibrahim alikuwa Mpole sana wa moyo mvumilivu.

ABU TWALIB NA KUWATAKIA MSAMAHA WASHIRIKINA

Aya 113 – 114

KUSHUKA AYA

Watu wamesema mengi kuhusu Uislamu wa Abu Twalib, ami yake Mtume(s.a.w.w) . Kauli zimetofautiana na viko vitabu vya zamani na karibuni kuhusu suala hilo. Vile vile maudhui haya yaliwahi kutolewa katika kurasa za gazeti la Majallatul-Arabi Na 108 na 110.

Wanaosema kuwa alisilimu, wametoa dalili kwa yale aliyopambana nayo kutoka kwa vigogo vya maquraish na kauli zake katika kumsifu Mtume kishairi n.k. Ama wale waliosema kuwa alikuwa mshirikina, walitoa dalili kwa riwaya inayosema kuwa Aya mbili hizi zilishuka kuhusiana na Abu Twalib.

Nilipofika hapa kufasiri, nilifuatilia riwaya na kauli katika vitabu vya zamani na vya sasa kuhusu sababu za kushuka Aya mbili hizi, nikatoka na natija kuwa wapokezi na wafasiri wametofautiana kwenye kauli tatu kuhusu sababu za kushuka Aya hizi.

KAULI YA KWANZA

Kuwa jamaa katika Waumini walisema, tuwatakie msamaha wafu wetu washirikina; kama alivyomtakia msamaha Ibrahim baba yake, ndipo zikashuka Aya mbili hizi.

Haya yametajwa na Tabari, Razi na Abu Hayan Al-andalusi. Vile vile mwenye Tafsiri Al-manar na wengineo.

Kauli hii ina nguvu kuliko kauli nyingine, kwa sababu katika Aya hizo kuna matamko yanayofahamisha hivyo; kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu “…na wale walioamini kuwatakia msamaha washirikina ijapokuwa jamaa …”

Kwa hiyo kukatazwa waumini kuwatakia msamaha jamaa zao, washirikina, kunatambulisha kuwa wao walikuwa wakiwatakia msamah au walijaribu kufanya hivyo.

Vile vile kauli isemayo:“Na haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake …”

Hilo ni jawabu la kauli ya waumini waliposema: Kama alivyomtakia msamaha Ibrahim baba yake.

KAULI YA PILI

Kwamba Mtume(s.a.w.w) alikwenda kwenye kaburi la mama yake akalia, na kumtaka idhini Mola wake amwombee msamaha, ndipo zikashuka Aya mbili hizo. Kauli hii wameitaja wale tuliowanukuu kwenye kauli ya kwanza.

Kauli hii inaizidi ile isemayo kuwa zilishuka wakati wa kufa Ami yake Abu Twalib. Kwa sababu Abu Twalib alikufa Makka katika mwaka wa huzuni miaka mitatu kabla ya Hijra, na Sura ya Tawba yenye Aya hizo mbili ilishu- ka Madina mwaka wa 9 Hijra – miaka 12 tangu kufa AbuTwalib.

KAULI YA TATU

Kwamba Aya mbili hizi zilishuka kwa Abu Twalib kwa madai ya kwamba Mtume alimwambia Ami yake, AbuTwalib akiwa karibu ya kukata roho: “Ewe Ami sema: “Lailaha illa llah” lakini hakusema, Mtume akasema: “Nitakuombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu maadamu sijakatazwa”

Kauli hii imejibiwa na kundi la maulama kwa kauli mbili:

Kwanza : kuwa Aya mbili, kama tulivyodokeza, zilishuka baada ya kufa Abu Twalib.

Pili : kwamba Abu Twalib alikufa baada ya kusilimu na kuufanyia ikhlasi Uislamu wake, Tazama kitabu Al-Ghadiri cha Aminiy J7 Uk 369 chapa ya mwaka 1967.

HALI HALISI

Kama tukiachana na kauli za wafasiri na wapokezi, tukaiweka itikadi ya Abu Twalib kutegemea alivyokuwa, kulingana na mambo yalivyo, basi natija itakuwa kwamba Abu Twalib alikuwa akiamini utume wa Muhammad(s.a.w.w) katika kauli zake zote na vitendo vyake, Na huo ndio Uislamu hasa.

Mtume aliinukia akiwa ni yatima wa baba na mama – Baba yake alikufa akiwa yuko tumboni na inasemekana kuwa alikuwa mtoto mchanga. Mama yake akafa akiwa na miaka sita, Akabaki katika malezi ya babu yake, Abdul Muttwalib, kiasi cha miaka minane.

Babu yake alipofikiwa na mauti alimkabidhi kwa Abu Twalib. Abu Twalib hakuwa ndiye mtoto mkubwa wa Abdul Mutwalib, wala hakuwa na mali nyingi isipokuwa alikuwa ndiye mwenye heshima, mwenye hulka nzuri na mkarimu sana kuliko ndugu zake wote.

Kwa hiyo Abu Twalib akamlea vizuri; akampenda sana kuliko watoto wake; alitunga kasida ndefu na fupi kumsifu; alikuwa akitabaruku naye na akimtegemea wakati wa balaa kutokana na karama zilizodhihiri kwake.

Imepokewa kutoka kwa Ibn Asakir, kwamba watu wa Makka walipatwa na kahati; akatoka Abu Twalib na Muhammad akiwa ni kijana akaomba mvua kwa uso wake. Ikabubujika mvua na ardhi ikarutubika.

Ismail Haqqi anasema katika Rawhilbayaan katika kufasiri (12:45): “Abu Twalib alimlea na kumhami Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na kumtetea katika uhai wake”.

Ilivyo ni kwamba yeye ni miongoni mwa waliokuwa na imani kama ilivyotangulia kuelezwa.

JE, KUNA SIRI GANI?

Ikiwa Abu Twalib anampenda Muhammad, anajitolea kwa nafsi yake na kuwa tayari kufa ili amsaidie, kutegemea ukweli wake na msimamo wake, naye aliona aliyoyaona katika karama zake, kabla ya utume na baada ya utume, kwa nini basi asiamini utume wake?

Ikiwa ni kweli madai ya kuwa Abu Twalib si Mwislamu basi itabidi kuweko na siri iiyomzuia kuwa Mwislamuu Je, ni siri gani hiyo? Je, Abu Twalib, aliyekuwa akimjua kiuhakika Muhammad, alimwona na mambo yanayopingana na Utume? Hapana! Mwenye kudai hivyo si Mwislamu kabisa!

Kisha itakuwaje Muhammad(s.a.w.w) aweze kuwakinaisha wachunga ngamia na wale waliokuwa hawajui chochote zamani, lakini ashindwe kumkinaisha ami yake, Abu Twalib ambaye alikuwa akimjua chimbuko lake?

Je, Abu Twalib alikuwa na akili ndogo kuliko Bedui wa jangwani, au alikuw ana tamaa iliyomzuia kusilimu, kama walivyozuilika wenye tamaa? Matamanio ambayo yangeweza kumzuia Abu Twalib kuingia Uislamu ni moja kati ya mambo mawili: Ama kuhofia mali yake na utajiri wake, na ilivyo ni kwamba Abu Twalib aliishi maisha ya kifukara na alikufa fukara. Au itakuwa ni kuhofia kuondokewa na uongozi katika nyumba ya Hashim nk, na ni kinyume cha hivyo.

Ikiwa sababu hizo mbili hazipo, na tukiunganisha kukosekana sababu na mambo yanayoelekeza Uislamu wake, ambayo ni kumpenda kwake Muhammad na kujua uhakika wake, basi natija ni kwamba Abu Twalib sio tu kuwa alisilimu bali ni katika waislamu wa mwanzo.

Vile vile ikiwa itabatilika kauli kuwa Aya mbili zilimshukia Abu Twalib na haikuthibitika riwaya sahihi kwamba zilishuka kwa sababu ya mama wa Mtume, basi itabakia kauli ya kwanza, kwamba ziliwashukiwa watu waliokuwa au waliojaribu kuwaombea msamaha watu wao; na dhahiri ya Aya mbili inaliweka wazi hilo.

MAANA

Haimfalii Mtume na wale walioamini kuwatakia msamaha washirikina ijapokuwa ni jamaa.

Imeelezwa katika Tafsir Tabari haya yafuatayo; ninanukuu: “Watu katika maswahaba wa Mtume(s.a.w.w) walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Katika mababa zetu wako waliokuwa na ujirani mwema, wakiunga udugu, wakisadia na kutekeleza madeni; je, tuwatakie msamaha? Akasema: Kwa nini isiwe hivyo, nami nitamtakia msamaha baba yangu, kama Ibrahim alivyomtakia msamaha baba yake, Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hiyo.”

Utauliza : kuwa itakuwaje Mtume(s.a.w.w) atoe idhini kwa masahaba zake kuwatakia maghufira baba zao washirki na ikiwa ni haramu?

Jibu : Kila kitu ni halali mpaka kikatazwe; na wakati Mtume alipotoa idhini kuombea msamaha hakukuwa kumekatazwa; baada ya kukatazwa, aliwakataza.

Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) anabainisha sababu za kukataza kwa kusema:

Baada ya kuwabainikia kuwa wao ni watu wa motoni.

Aya hii inatufahamisha kuwa mtu anahukumia ukafiri wake na imani yake kutokana na dhahiri ya hali yake, na kwamba ambaye dhahiri yake ni ukafiri basi haifai kumtakia msamaha wala kumrehemu.

Utauliza : Ikiwa kuwaombea msamaha washirikina ni haramu, kwanini Mtume aliwaombea msamaha watu wake walipomvunja meno na wakamchana uso wake? Imethibitika kwamba yeye alisema: “Ewe Mola Wangu! Wasamehe watu wangu, kwani wao hawajui.”

Wafasiri wengi wamelijibu swali hii kwamba Aya imekataza kutakiwa msamaha washirikina waliokufa, sio waliohai wanaotarajiwa imani yao.

Jibu : tunaloliona ni kwamba kutaka msamaha kwa Mtume(s.a.w.w) kulikuwa ni kusamehe haki yake ya kibinadamu, sio kusamehe haki ya Mwenyezi Mungu na maghufira kwa ushirikina.

Na, hakuna mwenye shaka kwamba inafaa kwa mtu kusamehe haki yake, inayomhusu yeye tu, kwa mwislamu na kafiri.

Swali la pili : Ibrahim alikuwa akimlingania baba yake kwenye imani na kumhimiza na kumwahidi kumtakia msamaha; kama asemavyo Mwenyezi Mungu:

إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ﴿٤﴾

“… Ila kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele za Mwenyezi Mungu…”(60:4)

Naye alitekeleza ahadi yake hii na akamwombea msamaha kwa kusema:

رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾

“Ewe Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wawili na waumini, siku ya kusimama hisabu.” (14:41)

Sasa vipi Ibrahim(a.s) alimtakia msamaha baba yake, ambapo kumtakia msama mshirikina hakufai? Mwenyezi Mungu (s.w.t) amejibu swali hilo kwa kusema:

Na haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake ila ni kwa sababu ya ahadi aliyofanya naye, lakini ilipompambanukia kuwa yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, alijiepusha naye.

Yaani Ibrahim(a.s) alimtakia msamaha baba yake kwa vile tu, alimwahidi kuwa atamwamini Mungu. Alipovunja ahadi na kumbainikia kuwa yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu alijiepusha naye.

Sio mbali kuwa dua ya Ibrahim(a.s) kwa baba yake, ni sawa na dua ya Muhammad(s.a.w.w) kwa watu wake washirikina; yaani kusamehe haki yake ya kibinadamu, sio haki ya Mwenyezi Mungu na kutakia msamaha ushirikina.

Hilo linatambulika kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu.

Hakika Ibrahim alikuwa Mpole sana wa moyo mvumilivu.

Mpole wa moyo ni yule mnyenyekevu na mvumilivu ni yale anayesamehe akiwa na uwezo. Na, Ibrahim alisamehe kauli ya baba yake:

لَئِن لَّمْ تَنتَهِ لَأَرْجُمَنَّكَ وَاهْجُرْنِي مَلِيًّا ﴿٤٦﴾

“Usipokoma nitakupiga mawe, na niondokelee mbali kwa muda mhache” (19:46)

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِلَّ قَوْمًا بَعْدَ إِذْ هَدَاهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١١٥﴾

115. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwapoteza watu baada ya kuwaongoza; mpaka awabainishie ya kujiepusha nayo Hakika Mwenyezi Mungu anajua kila kitu.

إِنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١١٦﴾

116. Hakika Mwenyezi Mungu ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, huhuisha na hufisha; nanyi hamna mlinzi wala msaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu.

MWENYEZI MUNGU HAWAPOTEZI WATU

Aya 115 –116

MAANA

Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwapoteza watu baada ya kuwaongoza.

Makusudio ya kuwapoteza ni kuwahisabu na kuwachukulia kuwa wamepotea. Na makusudio ya watu ni waumini tu; kwa dalili ya kauli yake, ‘baada ya kuwaongoza.’

Maana ni kuwa waumini wakifanya kitu chochote wasichokijua kuwa ni halali au haramu; kama vile kuwaombea msamaha au kuwarehemu washirikina kwa kutojua uharamu, basi Mwenyezi Mungu (s.w.t) hatawaadhibu, mpaka awabainishie ya kujiepusha nayo kwa ubainifu ulio wazi wa kiasi. Baada ya ubainifu, wakifanya uasi,hapo watastahiki adhabu.

Tafsiri bora ya Aya hii ni kauli ya Mtume mtukufu(s.a.w.w) : “Mtu yoyote aliyefanya jambo kwa kutojua hana neno.” Na kauli ya Imam Ja’far Asswadiq(a.s) : “Kila kitu ni halali mpaka kikatazwe.”

Hakika Mwenyezi Mungu ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, huhuisha na hufisha, nanyi hamna mlinzi wala msaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu.

Aya ikowazi na mfano wake umekwishapita mara nyingi na utaendelea kuja. Lengo ni kuwa binadamu daima awe pamoja na Mungu na kuukumbuka ukuu wake; na kwamba yeye peke yake ndiye bwana wake, ili asiweze kupetuka mpaka wowote katika mipaka yake.

لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١١٧﴾

117. Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Mtume na wahajiri na Answar waliomfuata saa ya dhiki. Baada ya nyoyo za baadhi yao kukurubia kugeuka, Kisha akawakubalia toba. Hakika yeye kwao ni Mpole Mwenye kurehemu.

وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّىٰ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوا أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ اللَّـهِ إِلَّا إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١١٨﴾

118. Na pia wale watatu walioachwa nyuma, mpaka ardhi ikawa finyu juu yao pamoja na wasaa wake; na nafsi zao zikadhikika juu yao, na wakayakinisha kuwa hakuna kwa kumkimbia Mwenyezi Mungu isipokuwa kwake. Kisha akawakubalia toba ili wapate kutubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwingi wa kukubali toba Mwenye kurehemu.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ ﴿١١٩﴾

119. Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wa kweli.

MWENYEZI MUNGU AMEMKUBALIA TOBA MTUME

Aya 117 – 119

MAANA

Bado maelezo ni ya vita vya Tabuk na matukio yake, Vita hivi vina mambo yake mahsusi yasiyokuwa katika vita vingine.

Miongoni mwa mambo hayo au yaliyo muhimu ni kuwa jeshi lilikuwa katika joto, njaa, kiu na uchache wa vipando, Ndio maana jeshi hili likaitwa ‘Jeshi gumu.’

Wapokezi wanasema kuwa kikundi fulani cha jeshi la Waislamu walikuwa wakipokezeana kupanda ngamia mmoja; chakula chao kilikuwa ni shayiri yenye wadudu na tende yenye mabuu, Mmoja wao alikuwa anaweza kufyonza tende akipata ladha yake, humpa mwenzake. Kuhusu maji walikuwa wanapochinja ngamia wanakamua mavi yaliyo katika utumbo wake na kurambisha ndimi zao.

Wanafiki walirudi nyuma kwenye vita hivi, Yamekishatangulia maelezo kuwahusu wao, Ama Waumini, ambao walimfuata Mtume(s.a.w.w) katika vita vya Tabuk, Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewashiria kwa kusema:

Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Mtume na wahajiri na Answar waliomfuata saa ya dhiki.

Ikisemwa kuwa fulani ametubia basi hufahamika kuwa alikuwa na dhambi, kisha akatubia, na ikisemwa kuwa Mwenyezi Mungu amepokea toba hufahamika kuwa amemkubalia toba yake. Lakini vile vile ina maana ya kuelekezwa rehema ya Mwenyezi Mungu na radhi yake kulingana na jumla ilivyo.

Maana ya kukubaliwa toba ndiyo yaliokusudiwa kwa wale watatu. Na maana ya rehema na radhi ndiyo yaliyokusudiwa kwa Mtume na swahaba waliomfuata katika saa ya dhiki. Hii inatokana na hali halisi ilivyo ya isma ya Mtume(s.a.w.w) na utiifu wa waliomfuata katika saa ya dhiki.

Baada ya nyoyo za baadhi yao kukurubia kugeuka.

Waliorudi nyuma walirudi nyuma, na Waumini katika wahajiri na Answari wakamfuata, lakini kikundi katika hawa walipozidiwa na shida na ugumu wa safari walilegea na kukusudia kuachana na Mtume, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwapa uthabiti na kuwalinda. Hivyo wakavumilia na kujitolea.

Kisha akawakubalia toba kutokana na vile walivyoazimia kumwacha Mtume.

Makusudio ya kuwakubalia toba hapa ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwachukulia kuwa hawakudhamiria dhambi, Kwa sababu mwenye kud- hamiria dhambi kisha asilitende, haandikiwi kitu.

Hakika yeye kwao ni Mpole, Mwenye kurehemu.

Kwa vile yeye alijua kwao ukweli katika imani yao na ikhlasi katika nia yao na kwamba dhamira yao ilikuwa ni jambo lililozuka tu na kuondoka bila ya kuacha athari yoyote.

Na pia wale watatu walioachwa nyuma, mpaka ardhi ikawa finyu juu yao pamoja na wasaa wake; na nafsi zao zikadhikika juu yao, na wakayakinisha kuwa hakuna kwa kumkimbia Mwenyezi Mungu isipokuwa kwake.

Wameafikiana wafasiri na wapokezi kwamba watatu hao ni katika waumini wa Kianswari, waliobaki nyuma katika vita vya Tabuk kwa uvivu na kupuuza, sio kwa unafiki na inadi. Hao ni Kaab bin Malik, Mar’wan bin Rabii na Hilal bin Umayya Al-waqif.

Masimulizi ya hao tunamwamchia Twaha Hussein aliyeleta Muhtasari wa yale waliyoyoafikiana wote na yanayofahamika katika Aya, Anasema katika Kitab mir-atul-islam:

“Watatu hawa walikuwa na imani kubwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wenye mapenzi ya ukweli kwake yaliyowafanya wasiongezee kosa la uwongo baada ya lile la kubaki nyuma. Kwa sababu ya ukweli na kuhofia Mwenyezi Mungu kuwafedhehesha waongo, walikiri makosa yao; na Mtume akawasikia na kutangaza kuwa wao ni wakweli, lakini pamoja na hayo hakuwasamehe; akaamrisha waumini wasiwasemeshe. wakawa wametengwa wakiwa mbali kabisa na watu; wakawa katika hali ambayo, jela ilikuwa bora kuliko hali hiyo.

Siku moja Mtume akatuma ujumbe wa kuwaaamuru watengane na wake zao. Hilo sio ajabu, kwa sababu wake zao ni waumini; na amri imetoka kuwa waumini wote watengane nao.

Baada ya kupita siku hamsini wakiwa wamejuta sana, Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya kuwatakabalia toba yao. Waumini wote wakalifurahi hilo wakawa wanawapongeza hawa watatu kwa kutakabaliwa toba. Kaab, alifurahi sana; akadhamiria kutoa sadaka mali yake yote, lakini Mtume akamwamuru atoe sehemu tu, Kaab akaahidi kutosema uwongo mpaka kufa.

Kisha akawakubalia toba ili wapate kutubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwingi wa kukubali toba Mwenye kurehemu.

Utauliza : kuwa dhahiri ya kukubaliwa toba ni kuwa walitubu na wakakubaliwa toba; na dhahiri ya ili wapate kutubu ni kuwa hawajatubia bado; sasa je, kuna wajihi gani?

Swali hilo limejibiwa kwa majibu mengi . Lenye nguvu zaidi ni lile lise- malo kuwa makusudio ya kukukabaliwa toba ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwakubalia toba ili watubu na wasiendelee na dhambi na waseme lau Mwenyezi Mungu atatukubalia toba yetu, basi tutatubu kabisa. Hiyo inafanana na mtu unayempenda akikufanyia uovu nawe unataka kumsamehe, ukamfundisha msamaha ili aombe, nawe umsamehe.

Tumeweka mlango maalum wa toba katika Juz.4 (4: 17).

Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wa kweli.

Wakweli ni Mitume na wale ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na kuwatakasa kabisa kabisa. Kwa maneno mengine, makusudio ya ukweli hapa sio kutosema uwongo tu katika mazungumzo, kwa sababu wako watu wasiosema uwongo lakini haifai kuwafuata katika kila jambo; isipokuwa makusudio ni ukweli katika kauli vitendo na elimu ambavyo vitamwandaa mwenye navyo kuweza kufuatwa.


4

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

مَا كَانَ لِأَهْلِ الْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ الْأَعْرَابِ أَن يَتَخَلَّفُوا عَن رَّسُولِ اللَّـهِ وَلَا يَرْغَبُوا بِأَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ لَا يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلَا نَصَبٌ وَلَا مَخْمَصَةٌ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَطَئُونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٢٠﴾

120. Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio kandoni mwao kubaki nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu; wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake. Hayo ni kwa sababu ya kuwa hakiwapati kiu wala taabu wala njaa katika njia ya Mwenyezi Mungu; wala hawakanyagi ardhi ichukizayo makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na adui, ila huandikiwa kuwa ni amali njema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa watendao mazuri.

وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةً صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً وَلَا يَقْطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمْ لِيَجْزِيَهُمُ اللَّـهُ أَحْسَنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢١﴾

121. Wala hawatoi chochote cha kutumiwa kidogo wala kikubwa wala hawalikati bonde ila wanaandikiwa kuwa Mwenyezi Mungu awalipe mema ya yale waliyokuwa wakiyatenda.

HAIFAI WATU WA MADINA KUBAKI NYUMA

Aya 120 – 121

MAANA

Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio kandoni mwao kubaki nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu; wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake.

Mtume wa Mwenyezi Mungu ni Muhammad(s.a.w.w) . Makusudio yake hapa ni dini ya Mwenyezi Mungu na haki, Kwa sababu dini ya haki inaun- dika katika utu wake mtukufu.

Kuinusuru haki ni wajibu kwa kila Mwislamu, wala hakuhusiki na watu wa Madina na walio kandoni mwao; isipokuwa wametajwa hao kwa kuwa karibu kwao na kuwa jirani, na pia kwa kulingana na mazungumzo ya vita vya Tabuk. Maana ni kuwa ni juu ya kila Mwislamuu kuinusuru haki na kuizuia batili wala asiathirike na manufaa na masilahi kuliko dini ya Muhammad, kwa kutoa visababu vya uwongo, kama walivyofanya wanafiki.

Hayo ni kwa sababu ya kuwa hakiwapati kiu wala taabu wala njaa katika njia ya Mwenyezi Mungu; wala hawakanyagi ardhi ichukizayo makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na adui, ila huandikiwa kuwa ni amali njema.

Hayo ni ishara ya kukataza kubaki nyuma na kuacha kuwapiga jihadi wabatilifu.

Ni jambo la kutia uchungu kwa mtu yeyote, awe Mwislamuu au la, kumwacha akanyage mchanga wa mji wake na nchi yake; pengine awe kibaraka asiye na dini wala dhamiri. Uislamu haumruhusu yeyote, vyovyote alivyo, kukanyaga ardhi ya mwingine ila kwa sababu mbili; Kuzuia madhara ya watu; kama vile kuzima moto kukinga mali na mali ya jirani.

Kuingiza nguvu iliyoadilifu itakayowazuia watu wa hapo na dhuluma na uadui kwa mji mwingine; kama alivyofanya Mtume(s.a.w.w) katika vita vya Tabuk, baada ya Waroma kuazimia kuipiga madina na kuumaliza Uislamu na Mtume wake.

Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa watendao mazuri.

Hakuna kitu rahisi kwa mtu kuliko kufanya wema, maadamu Mwenyezi Mungu anakuandikia wema kukaa kwake, kusimama kwake, na hata unyao mmoja tu anaoukanyaga kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu.

Wala hawatoi chochote cha kutumiwa kidogo wala kikubwa wala hawalikati bonde ila wanaandikiwa kuwa Mwenyezi Mungu awalipe mema ya yale waliyokuwa wakiyatenda.

Haya na yaliyo kabla yake yanafupilizwa na kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾

“Na atakayefanya heri uzani wa sisimizi ataiona” (99:7).

Lengo la ufafanuzi huu ni kuhimiza mali ya heri na kuhimiza kumpiga jihadi anayeeneza ufisadi katika ardhi.

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ ﴿١٢٢﴾

122. Wala haiwafalii waumini kutoka wote, Kwa nini kisitoke kikundi katika kila kundi miongoni mwao kuji funza dini na kuwaonya watu wao watakapowarudia, Ili wapate kujihadhari.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ ﴿١٢٣﴾

123. Enyi mlioamini! Piganeni na wale walio karibu yenu katika makafiri na wakute kwenu ugumu; na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye takua.

KWA NINI KISITOKE KIKUNDI

Aya 122 – 123

MAANA

Wala haiwafalii waumini kutoka wote.

Aya hii inaungana na Aya iliyotangulia kuwa haifai watu wa Madina kubaki nyuma. Njia ya kuungana ni kwamba iliposhuka Aya iliyotangulia Makabila ya Kiislam yalisema: Wallahi kuanzia leo hatutabaki nyuma ya Mtume katika vita. Wakamiminika kutoka madina kwa lengo hili.

Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t) akateremsha Aya hii, tuliyonayo, kuwa hawatakiwi kutoka wote kwa jihadi, bali hali hiyo inatofautiana kwa kutofautiana vita. Mara nyingine jihadi inakuwa ni wajibu kwa kila mtu, mara nyingine inakuwa ni wajibu kifaya, wakitekeleza baadhi basi wajibu umewaondokea wote.

Ama atakayetofautisha kati ya wajib hizo mbili ni Mtume(s.a.w.w) . Watatoka Waislamu wote kama akitaka watoke, na watatoka baadhi akitaka hivyo.

Kwa nini kisitoke kikundi katika kila kundi miongoni mwao kujifunza dini na kuwaonya watu wao watakapowarudia.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kubainisha kuwa si wajibu kwa kundi lote kutoka katika kila vita, sasa ana bainisha kuwa kuna wajibu mwingine usiokuwa jihadi ambao ni wajibu kuutekeleza, sawa na jihadi; kama vile kutoka kikundi katika kila mji au kabila kwenda Madina au mahali penginepo, kujifunza dini ya Mwenyezi Mungu – wajue halali na haramu; kisha warudi kwa watu wao wawongoze na kuwatahadharisha na adhabu ya Mwenyezi Mungu inayotokana na kumwasi na kuhalifu amri zake.

Ili wapate kujihadhari.

Yaani wawasikilize wanowaongoza na wawatii.

Hivi ndivyo tulivyoona katika kufasiri Aya hii, tukiwa tumetofautiana na wafasiri wengi ambao wamefanya ‘kujifundisha’ ni sifa ya watakaobaki, sio watakaotoka; wakasema katika ufanuzi wao kuwa ni wajibu kwa Waislamu kugawanyika makundi mawili: Kundi liende kwenye Jihad na kundi jingine libaki Madina kujifunza sunna na faradhi.

Tafsiri tuliyokwenda nayo sisi ndiyo yenye asili katika riwaya za Ahlu Bait wa Mtume(s.a.w.w) ambao ndio wajuzi zaidi wa Qur’ani na siri zake.

Miongoni mwa riwya hizo ni ile isemayo kuwa Mtu mmoja alimwuliza Imam Ja’far Asswadiq(a.s) kuhusu maana ya kauli ya Mtume(s.a.w.w) : “Kutofautiana umati wangu ni rehema”. Akasema: Makusudio ya kutofautiana sio kuzozana, vinginevyo kuafikiana kwao ingelikuwa ni adhabu; isipokuwa makusudio ni kuhangaika duniani kutafuta elimu. Kisha Imam akaitolea dalili Aya hii kwa makusudio ya maana hayo.

Hakuna mwenye shaka kwamba dalili hiyo haikamliki ila ikiwa kujielimisha ni sifa ya kikundi kinachotoka sio kinachobaki.

Wanachuoni wa usul wameitolea dalili Aya hii kuwa ‘Habari Moja’ inayo nukuliwa kutoka kwa Masumu ni hoja inayopasa kutumiwa katika hukumu za kisharia Njia ya kutoa dalili ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ame- wajibisha kwa ulama kufundisha na kuonya. Na, ukishakuwa wajibu huu kwa ulama, basi imekuwa wajibu kwa asiyejua kukubali kauli ya ulama na kuitumia; vinginevyo itakuwa wajibu wa kujifundisha na kuonya; ni mchezo tu.

Vile vile ikiwa ni wajibu kwa asiyejua kujifundisha, basi imekuwa ni wajibu kwa ulama kufundisha; vinginevyo itakuwa wajibu wa asiyejua kujifundisha ni mchezo tu. Imam Ali(a.s.) anasema:“Mwenyezi Mungu hatawaadhibu wajinga kwa kutojifundisha mpaka awaadhibu wenye elimu kwa kutofundisha”.

Enyi mlioamini! Piganeni na wale walio karibu yenu katika makafiri.

Aya hii inawahimiza Waislamu kulinda mipaka na maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zao. Katika Majmaul-bayan kuna maelezo kuhusu tafsiri ya walio karibu yenu katika makafiri kuwa ni walio karibu zaidi, isipokuwa kama kuna mapatano. Hii ni dalili kuwa ni wajibu kwa watu walio katika hali ya hatari kujilinda wakihofia kuchafuliwa Uislamu au mji wa Waislamu, hata kama hayuko Imam mwadilifu”.

Tumezungumizia kwa ufafanuzi kuhusu kupigana na makafiri katika Juz: (2:193) Kwa anuani ya ‘Uislamu unapiga vita dhulma na ufisadi’.

IMAM ZAINULABIDIN NA MSINGI WA VITA

Na wakute kwenu ugumu.

Ugumu hapa ni fumbo la nguvu na kuilinda vizuri mipaka.

Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye takua.

Ambao wameamini imani ya kweli; wakafanya ikhlasi katika kupigana na adui yao na adui wa Mwenyezi Mungu; wakajiandaa kwa nguvu zao zote, kama alivyo waamrisha Mwenyezi Mungu.

Maelezo ya kupendeza kuhusu maudhui haya ni dua ya Imam Zainul Abidin, Ali Bin Hussein(a.s.) , akimlingania Mola wake na kuwaombea watu walio katika hatari ya kushambuliwa na walinzi wa miji ya Kiislamu. Alisema katika aliyoyasema:

“Ewe Mola Wangu! Mrehemu Muhammad na Ali wa Muhammad. Na uifanye nyingi idadi yao, uzinoe silaha zao, uzilinde nchi zao, uzuie kushambuliwa kwao, ushikamanishe mjumuiko wao, uyaaangalie vizuri mambo yao, uwatoshelezee mahitaji yao, uwasaidie kwa kuwapa subra (uvumilivu), uwahurumie kwa kuwakinga na hadaa, uwafahamishe wasiyoyajua, uwaelimishe wasiyokuwa na ujuzi nayo.

Wanapokutana na adui wasahaulishe kukumbuka dunia yao iliyo na hadaa na ghururi, ufute katika nyoyo zao mawazo ya mali yenye fitna na uijalie pepo machoni mwao.”

Hiyo ndiyo misingi ya ushindi wa kuweza kulizuwiya jeshi lolote kadiri litakavyokuwa na silaha za kisasa; hata tonoradi, mizinga, mapesa ya kuwalipa wapiganaji, elimu ya vita na kutumia silaha pamoja na mbinu zote za kupigana.

Silaha kubwa zaidi ni kuunganisha majeshi na kuzifanya nyoyo ziwe na ikhlasi ya kupigana na kuwa na uvumilivu hadi kufa, kuisahau dunia na kuamini kuwa mtu kufa shahidi, katika kupigania dini yake na nchi yake ndio faida na kufuzu kukubwa.

Je, si Waarabu na Waislamu, wa zamani na wasasa, wamekuwa ni chakula kwa sababu tu ya mali yenye fitina? Dalili ya hayo ni janga la tarehe 5 June,1967.

Maneno haya ya Imam Zainul Abidin yamepitiwa na zaidi ya karne 13, lakini pamoja na hayo lau, hivi sasa, kamanda mkuu angetaka kusoma sababu za ushindi, basi hatahitajia ila kufafanua matamko haya mafupi aliyoyatamka Imam.

وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَـٰذِهِ إِيمَانًا فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ ﴿١٢٤﴾

124. Na inapoteremshwa Sura yoyote, basi miongoni mwao kuna wanaosema: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia imani? Basi wale walioamini inawazidishia imani, nao wanafurahi.

وَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَىٰ رِجْسِهِمْ وَمَاتُوا وَهُمْ كَافِرُونَ ﴿١٢٥﴾

125. Ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi inawazidshia uovu juu ya uovu wao, Na wanakufa hali ni makafiri.

أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَّرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ ﴿١٢٦﴾

126. Je, hawaoni kwamba wao wanajaribiwa kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu wala hawakumbuki.

وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ نَّظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ هَلْ يَرَاكُم مِّنْ أَحَدٍ ثُمَّ انصَرَفُوا صَرَفَ اللَّـهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ ﴿١٢٧﴾

127. Na inapoteremshwa Sura wanatazamana: Je, kuna yeyote anyewaona? Kisha hugeuka, Mwenyezi Mungu amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.

INAPOTEREMSHWA SURA

Aya 124 – 127

MAANA

Na inapoteremshwa Sura yoyote, basi miongoni mwao kuna wanaosema: Ninani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia imani?

Yaani baadhi ya wanafiki walikuwa wakidharau Qur’ani na kuulizana kuwa kuna ajabu gani ya hii?

Kwa hiyo wanazifanya nafsi zao, zilizochafuliwa na tamaa na dhambi, kuwa ni kipimo cha haki na ukweli.

La kushangaza ni kuwa washirikina walikuwa wakiukubali ukuu wa Qur’ani na athari zake zinazoingia nyoyoni, wakuwa wanausiana kuwa wasisikilize, kwa kuhofia kuvutwa kwenye Uislamu bila ya kujitambua. Mwenyezi Mungu anasema:

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَسْمَعُوا لِهَـٰذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُونَ ﴿٢٦﴾

“Na Walisema waliokufuru: Msisikilize Qur’ani hii na fanyeni zogo, huenda mkashinda” (41:26)

Hii inafahamisha, moja kwa moja, kuwa wanafiki wana athari mbaya zaidi kuliko washirikina.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewajibu wanafiki kwa kuwaaambia:

Basi wale walioamini inawazidishia imani.

Yaani, ikiwa katika nafsi zenu enyi wanafiki, haina athari yoyote nzuri, baada ya kupigwa chapa ya matamanio, basi waumini inawazidishia uongofu na yakini. Kwa sababu nafsi zao ni safi hazina taka ya uchafu kama nafsi zenu.

Nao wanafurahi kila inapoteremshwa Sura au Aya katika Qur’ani, kwa sababu inawapa bishara ya Pepo na kuwaongoza kwenye njia iliyo sawa.

Ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi inawazidshia uovu juu ya uovu wao.

Kila mwenye kuwa mbali na haki na hali halisi, na imani yake na rai yake ikavutwa kwenye dhati yake na mawazo yake, basi yeye ni mgonjwa wa moyo na akili. Na anapotakiwa kuwa kwenye hukumu halisi na akakataa huzidi maradhi yake.

Unafiki ni maradhi kwa sababu ni upotevu. Wanafiki wa sasa jinsi wanavyopupia dunia ni kama mfano wa funza; kila anavyozidi kujikunja ndio anakuwa mbali zaidi na kutoka mpaka anakufa.

Na wanakufa hali ni makafiri kwa uchaguzi wao mbaya; kama anavyok- ufa funza kwa sababu yake mwenyewe.

Je, hawaoni kwamba wao wanajaribiwa kila mwaka mara moja au mara mbili?

Makusudio ya kujaribiwa hapa ni kufedheheshwa na kufichuka njama zao kwa wote. Aya hii inaambatana na Aya iliyo tangulia: “Na inapoteremshwa Sura …”

Njia ya kuungana ni kuwa wanafiki walikuwa wakimlia njama Mtume(s.a.w.w) na wakimshutumu; kama vile kusema kuwa ni sikio, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) alikuwa akimfahamisha Mtume wake njama zao, na Mtume akiwafedhei. Mara nyingine hilo hukaririka zaidi ya mara moja katika mwaka.

Katika hilo kuna dalili mkataa juu ya ukweli wa Mtume na kwamba Qur’ani inatoka mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo ilikuwa ni wajibu kwao wapate mawaidha na wamwamini badala ya kudharau na kucheza chere kwa kusema: Ni nani miongoni mwenu amezidishiwa imani hii na hii?

Kisha hawatubu wala hawakumbuki.

Na hawakumbuki ila wenye akili; na hawa wamepofushwa akili zao na nyoyo zao kwa matamanio.

Na inapoteremshwa Sura hutazamana.

Ndivyo walivyo wanafiki kila wakati na kila mahali – wanaposhindwa kuikabili haki kwa hoja basi wanakonyezana, kuonyesha kuzama kwao kwenye ukafiri na upotevu.

Je kuna yeyote anayewaona.

Yaani wanayasema haya kwa mdomo au kwa vitendo:

يَسْتَخْفُونَ مِنَ النَّاسِ وَلَا يَسْتَخْفُونَ مِنَ اللَّـهِ وَهُوَ مَعَهُمْ إِذْ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرْضَىٰ مِنَ الْقَوْلِ ﴿١٠٨﴾

“Wanajificha kwa watu wala hawajifichi kwa Mwenyezi Mungu, na yeye yu pamoja nao walipokula njama usiku kwa maneno asiyoyapenda” Juz.5 (4:108)

Kisha hugeuka.

Yaani wanafanya wanayoyafanya kisha hugeukia kwenye shughuli zao; kama vile hawakufanya kitu.

Mwenyezi Mungu amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.

Mwenyezi Mungu amezigeuza nyoyo zao na haki baada ya kuwasimamishia hoja na ubainifu, na baada ya kuwafanyia inadi na kukataa kusalimu amri. Kwa hiyo wao ndio sababu ya moja kwa moja ya kugeuka na ikategemzwa kwa Mwenyezi Mungu kupita kwao.

Ni desturi ya Qur’ani Tukufu kutegemeza mambo mengi ya waja kwa Mwenyezi Mungu, kwa kuangalia kuwa yeye ni muumbaji wao na mwenye kuutengeneze ulimwengu na vitu vyake.

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢٨﴾

128. Hakika amewajia Mtume kutokanana nyinyi wenyewe, Yanamhuzunisha yanayo-wataabisha, anawahangaikieni sana, kwa waumini nimpole, mwenye huruma.

فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ﴿١٢٩﴾

129. Basi wakikengeuka, sema: Anitoshelezeaye ni Mwenyezi Mungu, hakuna Mola (apasaye kuabudiwa) ila yeye tu; kwake ninategemea; naye ndio bwana wa Arshi.

KWA WAUMINI NI MPOLE

Aya 128 – 129

MAANA

Hakika amewajia Mtume kutokana na nyinyi wenyewe.

Msemo huu anaambiwa kila mwanadamu anayetafuta uhakika na kutaka kuongozwa kwake. Mtume ni Muhammad bin Abudullah(s.a.w.w) , aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwa watu wote kuwaokoa na ujinga na upotevu na kuwaongoza kwenye njia ya haki na heri.

Analotakiwa kufanya mwenye kutaka njia ya heri na haki ni kuangalia kwa ufahamu tu sera ya Muhammad(s.a.w.w) na desturi yake na Kitabu alichokuja nacho kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Walimwamini mamilioni tangu zamani na sasa, wakiwemo maulama na wanafalsafa walioacha dini ya mababa na mababu, wakakubali Uislamu baada ya kutulia akili zao na nyoyo zao na kumuona Mtume wake mtukufu, kama alivyomsifu Mwenyezi Mungu kwa kauli yake:

Yanamhuzunisha yanayowataabisha, anawahangaikieni sana, kwa Waumini ni mpole, mwenye huruma.

Anahuzunika kwa kila baya linalomfika yeyote aliye ardhini; hata kama ni mnyama; mwenye kuhangaikia uwongofu na wema wa watu wote. Ama upole wake na rehema yake imewaenea watu wote:

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٧﴾

“Nasi hatukukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu wote” (21:107)

Na miongoni mwa Hadith zake ni: “Mimi ni rehema niliyetolewa zawadi”

“Wenye huruma huwarehemu Mwenyezi Mungu.” “Wahurumieni walio katika ardhi watawahurumia walio katika mbingu”.

Utauliza : Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema kwa Waumini ni Mpole mwenye huruma. Na katika Aya nyingine anasema: Nasi hatukukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu wote; yaani waumini na wasiokuwa waumini, Sasa zinaungana vipi Aya mbili?

Jibu : Makusudio ya kauli yake “Nasi hatukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu wote,” ni kuwa dini ya Muhammad ni dini ya ubinadamu na sharia yake ni rehema kwa watu wote. Lau kama watu wangelifuata na wakaitumia ardhi ingelijaa heri na uadilifu.

Ama kauli yake Mwenyezi Mungu: “Kwa waumini ni Mpole,” maana yake ni kwamba yeye ni Mpole sana na mwenye huruma kwa anayeamini haki na akajizuia kuwaudhi watu.

Ama anayewafanyia uadui na kuichezea haki yeye anamchukulia ugumu wala hamfanyii upole.

Hii nidyo dini ya utu na rehema. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekataza upole katika kutekeleza hadi (adhabu) kwa wakosaji. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّـهِ ﴿٢﴾

“Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mpigeni, kila mmoja katika wao, mijeledi mia wala isiwashike huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu” (24:2)

Anasema Ibin Al-Arabi katika Kitabu Futahahtuli-Makkiyya J2 “Makusudio ya waumini ni wenye kuamini haki na batili, sio wenye kuamini haki tu.” Lakini haya ni katika mambo ya kisufi.

Basi wakikengeuka, sema: Anitoshelezeaye ni Mwenyezi Mungu, hakuna Mola (apasaye kuabudiwa) ila yeye tu; kwake ninategemea; naye ndio bwana wa Arshi tukufu.

Hio ndiyo kazi ya Mtume – kufikisha tu. Mwenye kuongoka ni faida yake na mwenye kupotea ni hasara yake mwenyewe.

Mtume(s.a.w.w) alikuwa na yakini kabisa kwamba Mwenyezi Mungu anamtosha, na ndiye anayempa nguvu za ushindi wake, kwa sababu anamtegemea yeye peke yake.

Tutamalizia Sura hii kwa alivyomalizia Mwenye Tafsir Al-Manar, aliposema:

“Ama uteuzi wake Mwenyezi Mungu mtukufu kwa Bani Hashim, ni kwa kuwa walikuwa wanatofautiana na Maquraishi wote kwa fadhila na ukarimu. Hashim ndiye aliyekuwa mwenye msafara wa Maquraish ambao aliuchukulia ahadi kuuwahami kutoka kwa Kizair wa Roma katika msafara wa kaskazi; na kutoka serikali ya Yemen katika msafara wa kusi.

Yeye ndiye wa mwanzo kuwalisha mafukara na mahujaji wote mkate na mchuzi, Na alimpa malezi ya ukarimu mtoto wake, Abdul-Muttwalib. Kwa ujumla ni kuwa Bani Hashim walikuwa ni wenye tabia njema kuliko Maquraish wote, walikuwa hawana kiburi wala ubinafsi.

Baadhi ya mapokezi yanasema kuwa Aya ya mwisho kushuka ni hii: “Anitoshelezeaye ni Mwenyezi Mungu, hakuna Mola (apasaye kuabudiwa) ila yeye tu; kwake ninategemea; naye ndio bwana wa Arshi tukufu”

MWISHO WA SURA YA TISA: SUART AT – TAWBA


5

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

Sura Ya Kumi: Suart Yunus

Imeshuka Makka, Inasemekana kuwa Aya tatu au nne zilishuka Madina; maudhui yake ni kama maudhui ya Sura za Makka, ya kuthibitisha misingi ya kiitikadi. Ina Aya 109.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

الر تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْحَكِيمِ ﴿١﴾

1. Alif Lam Ra. Hizo ni Aya za Kitab chenye hekima.

أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ رَجُلٍ مِّنْهُمْ أَنْ أَنذِرِ النَّاسَ وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ قَالَ الْكَافِرُونَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ مُّبِينٌ ﴿٢﴾

2. Je, imekuwa ni ajabu kwa watu, kwamba tumempa wahyi mmoja wao, kuwa uwaonye watu na uwape bishara wale walioamini kwamba wana cheo kikubwa mbele ya Mola wao? Wakasema Makafiri: “Hakika huyu ni mchawi aliye wazi.”

HIZO NI AYA ZA KITAB CHENYE HEKIMA

Aya 1 – 2

MAANA

Alif Lam Ra.

Yametangulia maelezo kuhusu herufi hisi katika mwanzo wa Sura Baqara Juz.1

Hizo ni Aya za Kitab chenye hekima.

Hizo ni ishara kwamba kila Aya katika Aya za Qur’ani inakusanya hekima.

Je, imekuwa ni ajabu kwa watu, kwamba tumempa wahyi mmoja wao

Wapinzani waliona ajabu Mwenyezi Mungu kuwasiliana na mja miongoni mwa waja wake. Mshangao huu ulikuwa na sababu zifuatazo:-

1. Walimpima Muhammad(s.a.w.w) na wao wenyewe, kwamba ikiwa Mwenyezi Mungu hawasiliani na wao, basi inatakikana asiwasiliane na mwingine.

Jibu la hilo tunalipata katika Aya isemayo:

اللَّـهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ﴿١٢٤﴾

“Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi, zaidi wa kujua mahali anapoweka ujumbe wake”Juz.8 (6:124)

Yaani Muhammad(s.a.w.w) ana sifa za kumwezesha kuchukua utume kuliko wengine.

2. Wao hawakujua aina ya mawasiliano na Mwenyezi Mungu, wakadhani kwamba kuwasiliana kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu na Muhammad ni sawa na wanavyowasiliana wao kwa wao. Jibu la mawazo haya tunalipata katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا ﴿٥١﴾

“Na haiwi kwa mtu kusema na Mwenyezi Mungu ila kwa wahyi au nyuma ya pazia au humtuma mjumbe…” (42:51)

3. Kwamba Muhammad aliwaletea lile wasiloliitakidi wala kuzoweya. Na hili ndilo muhimu zaidi.

Jibu lake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

قَالَ لَقَدْ كُنتُمْ أَنتُمْ وَآبَاؤُكُمْ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٥٤﴾

“Akasema: Hakika nyinyi na baba zenu mlikuwa katika upotevu uliowazi” (21:54)

Kuwa uwaonye watu na uwape bishara wale walioamini kwamba wana cheo kikubwa mbele ya Mola wao.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kubainisha kustajabu kwa makafiri wahyi kwa Muhammad(s.a.w.w) , anabainisha hakika ya aliyoyatumia wahyi kuwa ni maonyo na bishara – kumuonya na adhabu kali yule anayehalifu na kuasi amri ya Mwenyezi Mungu na kumpa bishara ya thawabu yule anayefuata amri. Thawabu zimetajwa kwa ibara ya cheo kikubwa.

Ikiwa wahyi wenyewe ndio huu na Muhammad(s.a.w.w) akawa na sifa za kuuchukua na kuufikisha, sasa yako wapi maajabu?

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hawezi kuwaacha watu bila ya kuwatumia mjumbe mwaminifu awafikishie wanayoyataka katika heri na wanayoyachukia katika shari, wajiepushe na hili na wafanye lile. Na pia ili wasiwe na hoja, kama wakihalifu. Na Muhammad(s.a.w.w) ndiye mwaminifu wa ujumbe huu kuliko watu wengine. Kwa hiyo imepasa yeye awe ndiye mjumbe wa Mwenyezi Mungu.

Wakasema Makafiri: Hakika huyu ni mchawi aliye wazi.

Walimsifu Muhammad(s.a.w.w) kwa uchawi, kwa vile wao waliikana Qur’ani kuwa ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Vile vile walishindwa kuleta Sura iliyo mfano wake, Kwa hiyo hawakubakiwa na jingine ila kudai uchawi tu. Walishindwa na wakajitia kushindwa kujua kuwa kila lililo katika Qur’ani ni hakika isiyo na shaka, na kwamba uchawi ni uwongo usio na msingi.

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٣﴾

3. Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kasha akastawi juu ya Arshi, Yeye hutengeneza mambo. Hakuwa mwombezi ila baada ya idhini yake, Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu, basi mwabuduni, Je hamkubuki?.

إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا إِنَّهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ بِالْقِسْطِ وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ ﴿٤﴾

Kwake ndiye marejeo yenu nyote, Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli. Hakika yeye ndiye anayeanzisha kiumbe kasha hukirejesha ili awalipe wale walioamini na wakafanya amali njema kwa uadilifu. Na waliokufuru, watapata kinywaji cha maji yachemkayo na adhabu chungu kwa kuwa walikuwa wakikufuru.

KUUMBA KATIKA SIKU SITA

Aya 3 – 4

MAANA

Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akatawala juu ya Arshi, Yeye hutengeneza mambo yote.

Siku za Mwenyezi Mungu si kama siku zetu hizi, Zingelitokea wapi siku kabla ya kuumbwa ulimwengu? Kwa hiyo makusudio ya siku hapa ni awamu au vipindi. Ama Arshi ni kutawala. Aya hii imetangulia pamoja na tafsir yake katika Juz. 8 (7:54)

Hakuna mwombezi ila baada ya idhini yake.

Vile vile hii imetangulia katika Juz.3 (2:255)

Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu, basi mwabuduni.

Kwa sababu yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa, Ama mali, nasabu na ufalme sio Mungu wa kuabudiwa wala nguvu ya kunyeyekewa.

Je, Hamkumbuki?

Kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja peke yake anayestahiki kuabudiwa.

HISABU NA MALIPO NI LAZIMA

Kwake yeye ndiyo merejeo yenu nyote.

Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli.

Hakika yeye ndiye anayeanzisha uumbaji kisha ataurejesha.

Suala la kuanzishwa na kurudishwa kiumbe ni moja ya mushkeli mkubwa wa kifalsafa, Watu wengine wanasema ulimwengu ulipatikana wenyewe tu bila ya kuweko mpatishaji.

Fikra hii ni sawa na mtu aliyeona mandishi, kisha aseme yamepatikana kibahati; kwa vile tu hakumwona mwandishi kwa macho yake. Yule aliyechora ulimwengu ni mkuu zaidi kuliko aliyechora msitari kwa wino juu ya karatasi.

Jicho ni duni sana kuweza kumwona; na akili zimemwona katikati njia zinazosababishia kumwamini.

Tumetunga vitabu viwili kuhusu njia hizo: Allahu Wal-aq’ na Falsafa Tul- Maad. Baadhi yake tumezielezea kwa ufupi katika Juz. 1 (2:21) na Juz. 4 (3: 190)

Ama kufufuliwa wafu, kurudishwa mara ya pili kwa hisabu na malipo kumeelezwa na wahyi na wala akili haikatai, kwa hiyo ni wajibu kuku- sadiki na kukuamini.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amebainisha hekima ya kurudishwa wafu kwa kusema:

Ili awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda mema. Na waliokufuru, watapata kinywaji kinachochemka na adhabu chungu kwa vile walivyokuwa wakikufuru.

Mwenyezi Mungu amemwezesha mtu kutenda na akampa akili inayopambanua kheri na shari akamwamrisha hili na akamkataza lile. Basi akamtii mwenye kumtii na akamwasi mwenye kumwasi.

Kila mmoja akaingia shimo lake, bila ya kupewa thawabu mtiifu wala kuadhibiwa mwasi, Tena waasi wengi wanapetuka mipaka na kufanya dhulma na kuijaza dunia dhulma na jeuri bila ya kuulizwa na yeyote.

Tukichukulia kuwa hakuna ufufuo wala hisabu basi maana yake ni kuwa dhalimu na mdhulumiwa na mumin na kafir ni sawa, bali kafiri atakuwa ni bora kuliko mumin; na taghut mharibifu atakuwa mtukufu kuliko yule aliyekufa shahidi katika njia ya radhi yake.

Hakuna shaka kuwa haya yanapingana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu, na hekima yake na uwezo wake; bali hata na kuweko kwake Mwenyezi Mungu. Ametakata Mwenyezi Mungu na hayo kutakata kukubwa.

Tumeona wadhulimiwa wengi wakipiga kelele wakisema: Lau Mwenyezi Mungu angelikuwako kusingelibakii dhalimu yeyote katika ardhi.

Kauli hii haifahamishi chochote isipokuwa kuakisi matakwa ya kuweko mwadilifu mwenye uwezo atakayemchukulia kisasi mdhulumiwa, Lakini wamefanya haraka kwa uchungu, wakasahau maumbile aliyowaumbia Mwenyezi Mungu[3] , ndio wakasema waliyoyasema.

Nimeandika vitabu na makala kuhusu ufufuo, hisabu na malipo. Vilevile wakati wa kufasiri Aya inayoambatana na hayo, Na sasa Aya hii tena inanirudisha. Nimepata kufahamu kuwa dalili yenye nguvu ya kuthibitisha ufufuo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

الْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٧﴾

“Leo italipwa kila nafsi kwa iliyoyachuma, hapana dhulma leo, Hakika Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kuhisabu.” (40:17)

Ayah hii ni kama Aya tuliyonayo, lakini hii iko wazi zaidi, inajichukulia dalili yenyewe na kujijibu. Inasema: Leo italipwa kila nafsi kwa iliyoyachuma, kwa nini? Kwa sababu hakuna dhulma kwa Mwenyezi Mungu bali yeye ni mwepesi wa kuhisabu.

Utatuzi wa kiakili wa suala hili ni kwamba lau sio siku hii ambayo kila mtu atalipwa, basi Mwenyezi Mungu angelikuwa dhalimu, kuweko kwake ni mateso na sharia zake ni mchezo: Ametakata Mwenyezi Mungu (s.w.t) na wanayombandika.

Kwa hiyo natija ya mwisho ya mantiki haya ni kwamba kila mwenye kukana ufufuo, hisabu na malipo atakuwa amekana kuweko Mwenyezi Mungu, atake asitake.

هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ مَا خَلَقَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِالْحَقِّ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٥﴾

5. Yeye ndiye aliyefanya jua kuwa mwanga na mwezi kuwa nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo ila kwa haki. Anazipambanua Aya kwa watu wanaojua.

إِنَّ فِي اخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَّقُونَ ﴿٦﴾

6. Hakika katika kuhitalifiana usiku na mchana na alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi kuna ishara kwa watu wamchao.

إِنَّ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا وَرَضُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَاطْمَأَنُّوا بِهَا وَالَّذِينَ هُمْ عَنْ آيَاتِنَا غَافِلُونَ ﴿٧﴾

7. Hakika wale wasiotaraji kuku- tana nasi na wakawa radhi na maisha ya dunia na wakatua nayo, na wale walioghafilika na ishara zetu.

أُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمُ النَّارُ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٨﴾

8. Hao makazi yao ni motoni kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُم بِإِيمَانِهِمْ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٩﴾

9. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Mola wao atawaongoza kwa sababu ya imani yao. Itapita mito chini yao katika Mabustani yenye neema.

دَعْوَاهُمْ فِيهَا سُبْحَانَكَ اللَّـهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ وَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٠﴾

10. Wito wao humo ni: Umetakasika eweMwenyezi Mungu! Na maamkuzi yao ni ‘Salaam’ na mwisho wa wito wao ni: ‘Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote.

IDADI YA MIAKA NA HISABU

Aya 5 – 10

MAANA

Yeye ndiye aliyefanya jua kuwa mwanga na mwezi kuwa nuru.

Imesemekana kuwa mwanga na nuru yana maana moja, Na ikasemekana kuwa maana yanatofautiana. Neno mwanga linafahamisha kuwa nuru yake haitegemei kitu kingine; na neno nuru lina maana ya kuwa nuru yake imetokana na kitu kingine; kama vile nuru ya mwezi iliyotokana na jua.

Lakini ilivyo ni kuwa Aya haikuja kubainisha chochote katika hayo, isipokuwa makusudio ni kutanabahisha umoja wake Mwenyezi Mugu na uwezo wake; sawa na Aya iliyotangulia; na kwamba hekima ya jua na mwezi ni ile aliyoashiria Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kauli yake:

Na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu.

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameufanyia mwezi vitu visivyobadilika wala kugeuka; sawa na desturi nyngine za maumbile. Makusudio ya kutogeuka huko ni kudhibiti nyakati ambazo uhai hauwezi kutimia ila kwazo.

Hayo tumeyazungumzia kwa ufafanuzi katika Juz.7 (6:96) na Juz.10 (9:36).

Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo ila kwa haki. Anazipambanua ishara kwa watu wanaojua.

Mwenyezi Mungu amepambanua ishara za ulimwengu kimaumbile na kupatikana, na kwa kufafanua na kubainisha ili azingatie vizuri kila ambaye Mwenyezi Mungu amempa maandalizi ya kuchunguza na kutia akilini jambo ambalo linapelekea kumwamini Mwenyezi Mungu, uwezo wake na hekima yake.

Yametangulia maelezo, mara kadhaa, kuwa Mwenyezi Mungu mtukufu hutegemeza dhahiri za kiulimwengu na mabadiliko kwenye desturi yake ya kimaumbile ili mtu, daima, abakie kukumbuka muumbaji wa yaliyo katika ulimwengu.

Hakika katika kuhitalifiana usiku na mchana na alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi kuna ishara kwa watu wamchao.

Umetangulia mfano wa Aya hii na tafsiri yake katika Juz.2 (2:164).

Hakika wale wasiotaraji kukutana nasi na wakawa radhi na maisha ya dunia na wakatua nayo, na wale walioghafilika na ishara zetu.

Aya hii ni kemeo na kiaga kwa yule asiyeamini akhera na hisabu yake, kwa kusema kuwa aliyekufa yake yamekwisha. Akiyasema haya kwa kusukumwa na hawa zake na matamanio yake akiwa ameghafilika na ulimwengu na yaliyomo ndani yake yakiwa ni pamoja na mazingatio mawaidha na mito ya Mitume na watu wema.

Hao makazi yao ni motoni kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.

Haya ndiyo malipo ya kila mwenye kukadhibisha siku ya malipo na akayafanya matamanio yake ndiyo Mola wake, bila ya kujali haki wala uadilifu.

Ilivyo ni kuwa makemeo haya hayahusiki na mwenye kukana kukutana na Mwenyezi Mungu kwa kauli na vitendo tu, bali yanamhusu pia yule mwenye kuamini kinadharia tu, lakini akakana kimatendo. Kwa hiyo wanaoswali na kufunga wakiwa wanaamini hisabu na adhabu, kisha wasichunge haramu ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika Jahanam pamoja na wanaopinga hisabu.

WAKO WAPI WACHA MUNGU?

Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Mola wao atawaongoza kwa sababub ya imani yao. Itapita mito chini yao katika Mabustani yenye neema.

Makusudio ya kuongozwa hapa ni thawabu; yaani Mwenyezi Mungu atawalipa thawabu kwa sababu ya imani yao.

Mwenyezi Mungu (s.w.t), katika Aya zilizotangulia, amewataja wapinzani na sifa zao na mwisho wao. Katika Aya hii anawataja waumini, sifa zao na mwisho wao; kama desturi yake Mwenyezi Mungu Mtukufu yakutaja vitu na vinyume vyake.

Kwa hiyo waumini wako kinyume na wapinzani, wanatarajii kukutana na Mwenyezi Mungu, wanachunga miko yake kwa mujibu wa dini yao na imani yao. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawapa thawabu ya Pepo ipitayo mito chini yake.

Yamekuja maelezo katika Hadith kuwa Muumba, Mwenyezi Mungu Mtukufu, atasema siku ya Kiyama: “Leo nitaondoa nasabu yenu na niweke nasabu yangu, Wako wapi wacha mungu? Huo ndio mwito wa Mwenyezi Mungu siku hiyo ya haki ‘wako wapi wacha Mungu, walio wakweli katika kauli zao wenye ikhlasi katika vitendo vyao’. Ama mwito wa shetani hapa duniani, nyumba ya dhulma na ufisadi, ni: Wako wapi mataghuti wanaovunja miko walio wafisadi?

Kila mwenye kumtukuza mumin kwa sababu ya imani yake na takua yake, basi atakuwa ametoa mwito wa Mwenyezi Mungu ‘wako wapi wacha Mungu’ Na kila mwenye kumheshimu taghuti kwa makosa yake, basi atakuwa ametoa mwito wa Sheitan ‘wako wapi wakosaji’

Imam Ja’far As-Swadiq(a.s) anasema: “Ni makruh kumsimamia mtu kwa kumheshimu ila mtu wa dini” Na akasema tena: “Usibusu mkono wa yoyote ila mkono wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) au wa anayekusudiwa kwaye Mtume(s.a.w.w) .

Hukumu ya kumheshimu mtu inatofautiana kulingana na hali ilivyo. Ikiwa ni kwa kutia mori wa dhambi na maasi ya Mwneyezi Mung basi ni haramu. Ikiwa ni kwa mapenzi na mshikamano au kutekeleza haja ya mhitaji basi ni kuzuri.

Ama kumheshimu na kumtukuza mpigania jihadi kwa juhudi yake, mwenye ikhlasi kwa ikhlasi yake, msuluhishaji kwa suluhu yake na ulama kwa elimu yake, basi hiyo ni katika kuadhimisha nembo za Mwenyezi Mungu na miko yake, ambako amekuashiria kwa kusema:

وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾

“Na anayezitukuza alama za Mwenyezi Mungu, basi hilo ni katika uchaji wa Moyo” (22:32).

ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ ﴿٣٠﴾

“Na anayevitukuza vitu vitakatifu vya Mwenyezi Mungu, basi hiyo ni heri kwake mbele ya Mola wake…” (22:30).

Wito wao humo ni ‘Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu! Na maamkuzi yao ni ‘Salaam’ na mwisho wa wito wao ni: ‘Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu Wote.’

Aya hii kwa ujumla inaelezea habari za watu wa Peponi wakiwa katika raha hawashughlishwi na lolote katika yale yaliyokuwa yakiwashughulisha duniani ya kutaka masilahi au kukinga madhara; hawataki uadilifu wala amani, au kuzidishiwa malipo na cheo.

Hawataki chochote kwa sababu kila kinachotamaniwa na nafsi na kuburudisha macho kiko tayari; wakitaka kitu kazi yao ni kukifikiria tu katika nyoyo zao.

Kwa ajili hiyo wanajishughulisha na Tasbih na Tahmid tu:

لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا ﴿٢٥﴾ إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا ﴿٢٦﴾

“Hawatasikia humo porojo wala maneno ya dhambi, isipokuwa maneno: Salaam, Salaam”.(56:25–26).

Salam hii waliisikia kutoka kwa Mwenyezi Mungu walipokutana naye:

تَحِيَّتُهُمْ يَوْمَ يَلْقَوْنَهُ سَلَامٌ وَأَعَدَّ لَهُمْ أَجْرًا كَرِيمًا ﴿٤٤﴾

“Maamkuzi yao siku ya kukutana naye yatakuwa ni Salaam” (33:44)

Salaam hiyo wataisikia kutoka kwa Malaika:

وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ ﴿٧٣﴾

“Na walinzi wake watawaambia: Salaamun Alaykum, furahini, iingieni make milele (39:73).

Na, pia wataamkiana wenyewe kwa wenyewe.

Tumezungumzia kuhusu Maamkuzi ya Kiislam katika Juz.7 (6:54).


6

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

وَلَوْ يُعَجِّلُ اللَّـهُ لِلنَّاسِ الشَّرَّ اسْتِعْجَالَهُم بِالْخَيْرِ لَقُضِيَ إِلَيْهِمْ أَجَلُهُمْ فَنَذَرُ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١١﴾

11. Lau Mwenyezi Mungu angeli waharakishia watu shari, kama wanavyoharakishia kheri, hakika wangelikwisha timiziwa muda wao. Basi tunawaacha wale wasio taraji kukutana nasi wakihangaika katika upotevu wao.

وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ الضُّرُّ دَعَانَا لِجَنبِهِ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَائِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَا إِلَىٰ ضُرٍّ مَّسَّهُ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢﴾

12. Na dhara inapomgusa mtu hutuomba naye ameegesha ubavu wake, au katika hali ya kukaa, au katika hali ya kusi mama; lakini tunapomwon dolea dhara yake huendelea kama kwamba hakupata kutuomba tumwondolee dhara iliyomgusa, Namna hii wamepambiwa wapetukao mipaka yake waliyokuwa wakiyatenda.

وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ مِن قَبْلِكُمْ لَمَّا ظَلَمُوا وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ وَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ ﴿١٣﴾

13. Hakika tumekwishaziangamiza kaumu za kabla yenu walipodhulumu; na waliwajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, lakini hawakuwa wenye kuamini, Namna hii tunawalipa watu wakosefu.

ثُمَّ جَعَلْنَاكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ مِن بَعْدِهِمْ لِنَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ ﴿١٤﴾

14. Kisha tukawafanya nyinyi ndio mnaowafuatia baada yao katika ardhi ili tuone jinsi mtakavyotenda.

LAU MWENEYEZI MUNGU ANGELIWAHARAKISHIA SHARI

Aya 11 – 14

MAANA

Lau Mwenyezi Mungu angeliwaharakishia watu shari, kama wanavyoharakishia heri, hakika wangelikwishatimiziwa muda wao.

Makusudio ya heri hapa ni yale yanayowanufaisha watu katika maisha haya, Kwa ajili hii ndio wanaiharakia wala hawana subira nayo. Makusudio ya shari ni yale wanavyodhurika nayo; huyakataa na kuyaachukia kwa maumbile yao; ila kukiwa na sababu; kama vile kuondoa ambayo ni shari zaidi. Mshairi anasema: Navumilia shari kuhofia shari Shari nyingine ni shari kuliko shari.

Au pengine mtu akiwa katika hali isiyo ya kawaida; kama vile mtu anayetaka kujinyonga. Au kuwa katika hali ya inadi ya kumkabili hasimu aliyemshinda kwa hoja; kama vile walivyoshindwa washirikina kumjibu Muhammad(s.a.w.w) wakati Mwenyezi Mungu alipodhihirisha miujiza mikononi mwake wakasema:

“Ewe Mungu! Ikiwa (anayoyasema Muhammad) ni haki, basi tuteremshie mvua ya mawe au tuletee adhabu iumizayo.” Juz. 8 (8:32)

Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimjibu kila anayeharakisha adhabu na shari kwamba hekima ina inapitisha kutomkubalia matakwa yake mpaka wakati mwingine. Pengine linaweza kutokea jambo jengine la heri baada yake; kama ilivyotokea kwa wengi waliosema: Tuteremshie mvua ya mawe. Kuna kundi katika wao walisilimu na wengine wakazaa waumini wengi, Kama Mwenyezi Mungu angehiharakisha muda wao kusingelitokea kitu.

Kwa ufupi ni kwamba wao waliharakisha shari, sawa na wanavyoharak- isha heri, lakini Mungu (s.w.t) aliwachelewesha mpaka alipowatakia heri.

Basi tunawaacha wale wasiotaraji kukutana nasi wakihangaika katika upotevu wao.

Yaani Mwenyezi Mungu Mtukufu haharikishi adhabu kwa yule asiyeamini kufufuliwa katika wale waliomkufuru Muhammad, bali anaachana nao; hata kama wameasi amri yake na kuendelea katika uasi.

Na dhara inapomgusa mtu hutuomba naye ameegesha ubavu wake au katika hali ya kukaa, au katika hali ya kusimama.

Kuegesha ubavu, kukaa na kusimama ni fumbo la unyenyekevu wake kati- ka hali zake zote harakati zake na kutulia kwake.

Maana ni kuwa lau inamshukia chembe ya shari aliyoiharakisha, atakosa subira na atahangaika na kutukimbilia kwa unyenyekevu kwa kujidhalilisha katika hali zake zote ili tumuondolee.

Lakini tunapomwondolea dhara yake huendelea kama kwamba hakupata kutuomba tumwondolee dhara iliyomgusa.

Hali mbaya inaweza kumlazimisha mtu kusema uwongo, ria na kujipendekeza kwa mtu aliye na haja naye. Lakini ni jambo gani linalomlazimisha mtu kuasi, kukana jambo zuri na kumkana ambaye jana alikuwa akimyenyekea amtekelezee haja yake? Na alipompatia tu haja yake akamsahau kwamba hakumwomba kitu?

Hakuna tafsiri nyingine ya hilo zaidi ya kutojali, kuikana haki na misimamo na kupetuka mipaka katika hayo.

Namna hii wamepambiwa wapetukao mipaka yake waliyokuwa wakiyatenda.

Waliopambiwa vitendo vibaya ni wale wasiojali chochote ila manufaa yao na tamaa zao.

Hakika tumekwishaziangamiza kaumu za kabla yenu walipodhulumu; na waliwajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, lakini hawakuwa wenye kuamini, Namna hii tunawalipa watu wakosefu.

Hili ni onyo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa wale waliomkadhibisha Muhammad(s.a.w.w) kwamba nao itawafika adhabu kama iliyowafikia waliokua kabla yao walipowakadhibisha Mitume yao. Umepita mfano wa Aya hii katika Juz.7 (6:6).

Kisha tukawafanya nyinyi ndio mnaowafuatia baada yao katika ardhi ili tuone jinsi mtakavyotenda.

Umma unaondoka na kufuatiwa na mwingine. Ama lengo la kuweko mtu katika ardhi hii ni elimu na amali ya kunufaisha.

Utauliza kuwa : Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾

“Sikuumba majini na watu ila waniabudu” (51:56).

Na wewe unasema kuwa Mwenyezi Mungu amemuumba mtu kwa elimu ya manufaa.

Jibu : Makusudio ya ibada iliyotajwa ni amali njema kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ ﴿١٠﴾

“Na amali njema huiinua…” (35:10)

Bali Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameumba ulimwengu pamoja na ardhi yake na mbingu yake kwa ajili ya amali njema. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ﴿٧﴾

“ Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita na Arshi yake ilikuwa juu ya maji, ili awajaribu ajulikane ninani miongoni mwenu ni mzuri zaidi wa vitendo” (11:7).

Tumebanisha maana ya kujaribiwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika Juz.7 (5:94)

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا ائْتِ بِقُرْآنٍ غَيْرِ هَـٰذَا أَوْ بَدِّلْهُ قُلْ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أُبَدِّلَهُ مِن تِلْقَاءِ نَفْسِي إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥﴾

15. Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasiotaraji kukutana nasi husema: “Lete Qur’ani isiyokuwa hii, au ibadilishe. Sema: Haifai mimi kubadilisha kwa hiyari ya nafsi yangu; sifuati ila niliyopewa wahyi. Hakika mimi naogopa, nikimwasi Mola wangu, adhabu ya siku iliyo kuu.

قُل لَّوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا تَلَوْتُهُ عَلَيْكُمْ وَلَا أَدْرَاكُم بِهِ فَقَدْ لَبِثْتُ فِيكُمْ عُمُرًا مِّن قَبْلِهِ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٦﴾

16. Sema: lau Mwenyezi Mungu angelitaka nisingeliwasomea hiyo wala nisingeliwajuza, Nimekaa kwenu umri kabla yake, basi hamtii akili.

فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْمُجْرِمُونَ ﴿١٧﴾

17. Basi ninani aliye dhalimu zaidi kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uwongo au akadhibishaye Aya zake? Hakika hawafaulu wakosefu.

LETE QUR’AN ISIYOKUWA HII

Aya 15 – 17

MAANA

Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasiotaraji kukutana nasi husema: “Lete Qur’ani isiyokuwa hii, au ibadilishe.

Makusudio ya wale wasiotaraji kukutana na Mwenyezi Mungu ni washirikina. Mtume(s.a.w.w) alikuwa akiwapa hoja wao, mayahudi na wakristo kwa Qur’ani; na alikuwa akijadaliana nao kwa mjadala mzuri. Mjadala wake na washirikina na mayahudi ulikuwa mkali, kwa sababu wao ndio waliokuwa maadui na wapinzani sana; kama ilivyoelezwa katika Aya kadhaa zilizotangulia.

Ama wakristo kuna waliomtembelea na wakakubali kutoa kodi; kama vile wakristo wa Najran. Na wengine walikusudia kumpiga vita Madina, Mtume akawakatia njia na kupigana nao katika ardhi ya Sham.

Washirikina walikuwa wakimpa Mtume maoni ya kila aina ya ujinga wao na mchezo wao; kama vile ilivyodokezwa katika Juz,1(2:118), walipomtaka Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) awazungumzishe Mwenyezi Mungu kwa mdomo.

Aya hii tuliyonayo inasimulia maoni yao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kuwa awaletee Qur’ani nyingine au aibadilishe kwa vile Qur’ani hii imewaletea dini mpya. Inawalingania kwenye Tawhid na kuamini ufufuo na malipo.

Pia inathibitisha misingi ya uadilifu na usawa, kutupilia mbali utabaka na kuharamisha riba na dhuluma; wakati ambapo wao wana dini ya waungu wengi, wanapinga ufufuo na kuharakisha wanayoyatamani. Ndipo wakamtaka Muhammad(s.a.w.w) awaletee Qur’ani itakayothibitisha dini yao na kuiga kwao au angalau, waondoe ile sehemu wasiyoiridhia.

Kuna tofauti gani kati ya maombi haya ya washirikina wa Kijahiliya na vijana wengi wa karne ya ishirini, wasemao kuwa kuna haja gani ya dini na kwa nini kuwe na halali na haramu? Na, maendeleo ya makompyuta hayahitaji msingi na dini.

Sema: Haifai mimi kubadilisha kwa hiyari ya nafsi yangu; sifuati ila niliyopewa wahyi. Hakika mimi naogopa, nikimwasi Mola wangu, adhabu ya siku iliyo kuu.

Mtume ni mwenye kunakili tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu sio mwenye kuweka sharia; sawa na mpokezi wa Hadith kutoka kwa Mtume. Kuna Hadith iliyopokewa kutoka kwake isemayo “Mwenye kunikadhibisha basi na ajichagulie makazi yake motoni,” sasa itakuwaje yeye amkadhibishe Mwenyezi Mungu. Haiwezekani kwa mwenye isma kukosea au kuteleza.

Aya hii inampinga yule mwenye kutoa fatwa na kuhukumu bila ya dalili ya kisharia. Vile vile ni dalili mkataa kuwa Mtume kamwe hakutoa hukumu kwa ijtihadi yake, na kwamba hukumu zake zote zilikuwa ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mwenye kusema kuwa alifanya ijtihad basi, atakuwa hakumtofautisha na mafakihi wengine, Shia wanapinga kuwa Mtume alifanya ijitihadi ambapo Sunni wanatofautiana. Wengine wanaafikiana na Shia na wengi wamesema kuwa alifanya ijitihadi.

Sema: lau Mwenyezi Mungu angelitaka nisingliwasomea hiyo wala nisingeliwajuza.

Dhamir ya hiyo ni ya Qur’ani. Maana ni kuwa lau Mwenyezi Mungu asingeliileta nisingelifanya hayo, lakini nimefanya niliyoyafanya kwa kutekeleza matakwa ya Mwenyezi Mungu.

Nimekaa kwenu umri kabla yake, basi hamfahamu.

Mtu ambaye ameishi kwa watu miaka arubaini kabla ya kupewa wahyi akiwa hakusoma kitabu chochote au kufundishwa na mwalimu, wala hakuwahi kufanya jambo la kulaumiwa; bali maisha yake yote yalikuwa ni mema, mwenye ukweli na uaminifu mpaka akaitwa Amin (mwaminifu). Pamoja na yote haya hamfahamu kuwa mtu aliye hivi yuko mbali na uwongo na uzushi?

Basi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uwongo au akadhibishaye Aya zake?

Maana ya kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo ni kuweka kwenye dini jambo lililo mbali na dini. Maana ya kukadhibisha Aya zake ni kukanusha yale ambayo kwa asili yanatoka kwake. Hii ndiyo bid’a ambayo Mtume ameielezea kwa kusema: “Kila bid’a ni upotevu na kila upotevu ni katika moto.”

Hakika hawafaulu wakosefu.

Kwa sababu njia ya kufaulu na kuokoka ni ukweli na ikhlasi. Ama uwongo na uzushi ni njia ya maangamivu na utwevu, na haifati njia hiyo isipokuwa mwovu mkosefu.

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّـهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿١٨﴾

18. Na wanaabudu wasiowadhuru wala kuwanufaisha badala ya Mwenyezi Mungu, Na wanasema: “Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu.” Sema: Je, mnamwambia Mwenyezi Mungu asiyoyajua katika mbingu wala katika ardhi? Ametakasika na ametukuka na hao wanaomshirikisha naye.

وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً فَاخْتَلَفُوا وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ فِيمَا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿١٩﴾

19. Na hawakuwa watu ila ni umma mmoja tu kisha wakahitalifiana. Na lau si neno lililotangulia kutokana na Mola wako, bila shaka hukumu ingelikwishakatwa baina yao katika hayo wanayokhitalifiana.

وَيَقُولُونَ لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَقُلْ إِنَّمَا الْغَيْبُ لِلَّـهِ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ ﴿٢٠﴾

20. Na wanasema: “Kwanini hakuteemshiwa ishara kutoka kwa Mola wake?” Sema: hakika ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu, basi ngojeni na mimi niko pamoja nanyi katika kungoja.

WANASEMA HAWA NI WAOMBEZI WETU

Aya 18-20

MAANA

Na wanaabudu wasiowadhuru wala kuwanufaisha badala ya Mwenyezi Mungu.

Hawa ni wale waliomwambia Mtume alete Qur’ani nyingine au aibadilishe. Wao walikuwa wakiabudu masanamu; wakiamini kuwa yanawanu- faisha na kuwadhuru; kama anavyosema Mwenyezi Mungu:

Na wanasema: “Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu.

Lakini imani yao hii haina msingi wowote isipokuwa ni njozi na mawazo tu. Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake Muhammad(s.a.w. w ) akanushe madai yao kwa kuwaambia:

Je, mnamwambia Mwenyezi Mungu asiyoyajua katika mbingu wala katika ardhi? Ametakasika na ametukuka na hao wanaomshirikisha naye.

Washirikina walidai kuwa masanamu yao yatawaombea kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa haya ni kweli, basi Mwenyezi Mungu angeliujua uombezi huu na kwa kuwa haujui basi ina maana kuwa washirikina ni waongo na wazushi.

Na hawakuwa watu ila ni umma mmoja tu kulingana na maumbile aliyowaumbia Mwenyezi Mungu; kisha hawa zao zikawatenganisha kutoka asili yao na ufuasi ukawagawa vikundi katika dini yao baada ya kushindana kupata raha za maisha.

Na lau si neno lililotangulia kutokana na Mola wako, bila shaka hukumu ingelikwishakatwa baina yao katika hayo wanayokhitalifiana.

Makusudio ya neno hapa ni kutoharakisha Mwenyezi Mungu adhabu ya waasi na thawabu za watiifu; bali anangojea mpaka siku ya ufufuo; ili kila mtu, kwa hiyari na radhi ya nafsi yake, afikie heri au shari na ubora au uduni.

Lau Mwenyezi Mungu angeliharakisha adhabu ya muovu katika watu basi wangelikuwa sawa, lakini kwa kuhofia tu si kwa utiifu.

Hakuna mwenye shaka kwamba hili ni kinyume na kuondoa maana ya thawabu na adhabu. Vile vile litapingana na hekima yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kudhihirisha hakika ya mtu kulingana na matendo yake na uchaguzi wake. Umetanglia mfano wake katika Juz. 2 (213) na Juz. 6 (6:48).

Na wanasema: “Kwa nini hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake?”

Mwenyezi Mungu alimteremshia Muhammad ishara nyingi na miujiza kadhaa, lakini washirikina waliosema hivi walitaka ishara kulingana na hawa zao na miujiza wanayoitaka wao; kama walivyosema:

“Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi” Juz; 1 (2:218).

لَوْلَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَلَكٌ فَيَكُونَ مَعَهُ نَذِيرًا ﴿٧﴾

“Mbona hakuteremshiwa Malaika akawa muonyaji pamoja naye” (25:7).

Sema : hakika ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu, basi ngojeni na mimi niko pamoja nanyi katika kungoja.

Yaani, ewe Muhammad waambie hawa wenye inadi kuwa ishara mnazozitaka ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu mimi sina langu jambo wala sijui kuwa Mwenyezi Mungu ataiteremsha kutoka mbinguni au Mimi na nyinyi katika hili ni sawa katika hilo. Basi tuone ni kundi gani litasalimika na hasira za Mwenyezi Mungu.


7

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً مِّن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُمْ إِذَا لَهُم مَّكْرٌ فِي آيَاتِنَا قُلِ اللَّـهُ أَسْرَعُ مَكْرًا إِنَّ رُسُلَنَا يَكْتُبُونَ مَا تَمْكُرُونَ ﴿٢١﴾

21. Na tunapowaonjesha watu rehema baada ya dhara kuwagusa, huanza kuzipangia njama Aya zetu, Sema: Mwenyezi Mungu ni mwepesi zaidi wa kupanga njama, Hakika wajumbe wetu wanayaandika mnayoyapanga.

هُوَ الَّذِي يُسَيِّرُكُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ حَتَّىٰ إِذَا كُنتُمْ فِي الْفُلْكِ وَجَرَيْنَ بِهِم بِرِيحٍ طَيِّبَةٍ وَفَرِحُوا بِهَا جَاءَتْهَا رِيحٌ عَاصِفٌ وَجَاءَهُمُ الْمَوْجُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ أُحِيطَ بِهِمْ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ لَئِنْ أَنجَيْتَنَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿٢٢﴾

22. Yeye ndiye anayewaendesha bara na baharini. Hata mnapokuwa majahazini na yakaenda nao upepo mzuri na wakaufurahia, mara upepo mkali ukawazukia yakawajia mawimbi kutoka kila upande na wakaona wamekwishazongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumfanyia ikhlasi: ukituokoa na haya bila shaka tutatakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.

فَلَمَّا أَنجَاهُمْ إِذَا هُمْ يَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا بَغْيُكُمْ عَلَىٰ أَنفُسِكُم مَّتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُكُمْ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٢٣﴾

23. Lakini alipowaokoa, mara wanafanya jeuri katika ardhi pasipo haki. Enyi watu! Hakika jeuri yenu itawarudia nyinyi wenyewe tu. Ni starehe ya maisha ya dunia kisha marejeo yenu ni kwetu ndipo tuwaambie mliyokuwa mkiyatenda.

SEMA: MWENYEZI MUNGU NI MWEPESI ZAIDI WA KUPANGA NJAMA

Aya 21-23

MAANA

Na tunapowaonjesha watu rehema baada ya dhara kuwagusa, huanza kuzipangia njama Aya zetu.

Imesemekana kuwa makusudio ya watu ni washirikina. Kauli hii haiko mbali na mfumo wa maneno, kwa sababu Aya inawazungumzia washirikina lakini haizuwii kuwa makemeo yanamhusu kila mwenye kukana neema za Mwenyezi Mungu, ni sawa upinzani utokane na mu’min au kafiri, kabla ya madhara au baada.

Madhumuni ya Aya hii yanalingana na Aya ya 12 ya Sura hii: “Na dhara inapomgusa mtu hutuomba naye ameegesha ubavu wake au katika hali ya kukaa au katika hali ya kusimama Lakini tunapomwondolea dhara yake huendelea kama kwamba hakupata kutuomba tumwondolee dhara iliyomgusa.” Hiyo inasema kuwa mtu anamkumbuka Mwenyezi Mungu katika saa ya dhiki na hii tunayoifasiri sasa inasema kuwa anapomjaalia wepesi huzipangia njama Aya zake.

Mkusudio ya njama hizo ni kupinga Aya za Mwenyezi Mungu na kukataa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye msababishaji katika kumwondolea madhara na balaa na kufasiri sababu nyingine zizisizo na msingi wala asili; kama masanamu, nyota, sadfa na tafsiri nyinginezo mbovu zinazotofautiana kulingana na watu, mawazo yao na uigaji wao.

Sema: Mwenyezi Mungu ni mwepesi zaidi wa kupanga njama, Hakika wajumbe wetu wanayaandika mnayoyapanga.

Makusudio ya njama za Mwenyezi Mungu ni kwamba yeye anawalipa wapanga njama kwa njama zao na kuwaandalia adhabu kali bila ya wao kutambua. Pia tumelizungumzia hilo katika Juz.3 (3:54).

Makusudio ya wajumbe waandishi ni Malaika. Maana ni kuwa Yeye Mwenyezi Mungu mtukufu anavidhibiti vitendo vya wenye njama na kuwalipa wanayostahiki.

Yeye ndiye anayewaendesha bara na baharini.

Yaani Yeye Mwenyezi Mungu mtukufu amempa mja wake uwezo wa kutembea humo. Makusudio ya ishara hii ni kukumbusha fadhila zake na nema zake ili awe katika wenye shukrani, “Utukufu ni wako ewe Mola wangu! Ni ubainifu ulioje wa ukarimu wako kwa anayekuridhisha na anayekuchukiza”

La kushangaza ni kauli ya Abu Bakr Al-mughafiri katika Kitabu Ahkamul- Qur’an, kwamba Aya hii inafahamisha kuwa usafiri wa baharini ni halali sio haramu; tena akarefusha maneno katika kutoa dalili ya uhalali wa kusafiri bahrini. Amesahau kuwa kawaida ya sharia, ambayo anaijua asiye- jua na Mjuzi, ni uharamu ndio unaohitajia dalili na sio uhalali.

Hata mnapokuwa majahazini na yakaenda nao upepo mzuri na wakaufurahia, mara upepo mkali ukawazukia yakawajia mawimbi kutoka kila upande na wakona wamekwishazongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumfanyia ikhlasi: ukituokoa na haya bila shaka tutatakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.

Aya hii inafahamisha kuwa binadamu ana maumbile ya kumwamini Mungu kwa sababu ya kurejea kwake katika shida. Angalia kifungu: ‘Mwenyezi Mungu na maumbile’ katika Juz.7 (6:41).

Mwenye Al-manar amesema katika kufasiri Aya hii, ninamnukuu: “Washirikina walikuwa hawamuombi yeyote wakati wa shida, isipokuwa Mwenyezi Mungu muumba Mola wao. Ama waislamu wengi, zama hizi, hawamuombi Mwenyezi Mungu, kama wanavyodai hilo hao wenyewe, isipokuwa wanawaomba wafu; kama vile Badawiy, Rifai, Dasuqi, Jaylani, Almatbuli, Abu sarii na wengineo wasiokuwa na hisabu.

Na utawakuta wenye vilemba wa Azhar na wengineo hasa waangalizi wa makaburi yanayoabudiwa wakitumia wakfu na nadhiri zake kutoka kwa wale wanaowahadaa kwa shirki yao wakieguza jina katika Lugha ya kiarabu kwa kuiita tawassul n.k.” Mfano wa maneo haya yamo katika Tafsir ya Maraghi.

Nimesoma katika gazeti la Misri kuwa wamisri wanaandika karatasi wakizitupa kwenye kaburi la waliy, Humo wanaandika mashtaka ya wahasimu wao wakitaraji maiti awalipizie kisasi kutokana na dhulma na uovu walio- fanyiwa. Nimenukuu mashtaka haya katika kitabu Minhuna wa hunaka (Huku na huko).

Ama kuhusu mkusanyiko wa hafla ya mazazi ya walii, tuuchie gazeti la Aljumhuriya la tarehe 1-11-1968, likisema: “Msongamano ulikuwa kama siku ya kufufulia watu; ni kama mawimbi au shamba lililopandwa miti”

Lakini alipowaokoa, mara wanafanya jeuri katika ardhi pasipo haki.

Walimwahidi Mwenyezi Mungu kumcha na kumshukuru akiwaondolea, lakini alipowafanyia walivunja ahadi.

Hii inakariri aya iliyotangulia kwa ibara nyingine. Ile inasema wanazipangia njama Aya zetu na hii inasema wanafanya uovu katika ardhi. Maana ni moja au yanaoana. Lengo ni kuonyesha inadi yao na jeuriyao kwa picha mbaya.

Enyi watu! Hakika jeuri yenu itawarudia nyinyi wenyewe tu.

Kwani mwenye kuchomoa upanga wa jeuri atauliwa kwa huo.

Ni starehe ya maisha ya dunia kisha marejeo yenu ni kwetu ndipo tuwaambie mliyokuwa mkiyatenda.

Mjeuri anaweza kufurahi na kuburudika na ushindi, lakini ni wa muda; kisha inakuja balaa na hasara. Mtume(s.a.w.w) anasema: “Mambo matatu yanawarudia watu wake: Njama, njama za uovu hazimpati ila mwenyewe[4] .

Kuvunja ahadi, basi mwenye kuvunja ahadi anjivunjia ahadi mwenyewe[5] , Ujeuri, enyi watu! Hakika jeuri yenu itawarudia nyinyi wenyewe tu[6] .

إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢٤﴾

24. Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama mfano wa maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kasha ikachanganyika na mimea ya ardhi wanayokula watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipokamilisha uzuri wake na ikapambika. Na wenyeji wake wakadhani kuwa wana nguvu juu yake, amri yetu iliifkia usiku au mchana na tukaifanya imefyekwa, kama kwamba jana haikuweko. Namna hiyo tunazieleza Aya kwa watu wenye kufikiri.

وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢٥﴾

25. Na Mwenyezi Mungu anaita kwenye nyumba ya amani, Na humwongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka.

MFANO WA MAISHA YA DUNIA

Aya 24-25

MAANA

Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama mfano wa maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha ikachanganyika na mimea ya ardhi.

Yaani dunia hii mnayoshindana nayo na kujifaharisha inafanana na mvua iliyotermka ardhini, ikapata rutuba na kuotesha aina za mimea zikachanganyika kutokana na wingi wake na kukua kwake.

Wanayokula watu na wanyama

Kila kiumbe hai kinalishwa na ardhi, inajaza matumbo yaliyo na njaa. Watu wanakula nafaka na mtunda na wanyama wanakula nyasi na vinginevyo.

Mpaka ardhi ilipokamilisha uzuri wake na ikapambika, kama harusi aliyejitengeza ili amfuruhishe harusi mwenzake,

Na wenyeji wake wakadhani kuwa wana nguvu juu yake na kuweza kutumia utajiri wake wakijaza mifuko yao na hazina zao. Baada ya mategemeo haya na kutuliaamri yetu iliifkia ya maafa na maangamizi,usiku au mchana na tukaifanya imefyekwa, kama kwamba jana haikuweko, kutokana na kuondoka kila kitu, haikubaki hata alama ya vilivyokuwepo, matumaini yote na ndoto zote zimeyayuka.

Namna hiyo tunazieleza Aya kwa watu wenye kufikiri kuwa starehe za dunia zinaisha na kwamba mwenye kuzitegemea basi atakuwa ametege- mea kwenye mawingu na kwamba hakuna haja ya kumwagiana damu, kuanzisha vita na kuzidhalilisha akili za wajuzi.

Na Mwenyezi Mungu anaita kwenye nyumba ya amani.

Wafasiri wamesema kuwa makusudio ya nyumba ya amni ni pepo. Hakuna mwenye shaka kuwa pepo ni nyumba ya wema na amani, lakini mwito wa Mwenyezi Mungu unaenea kwenye kila jambo litaklohakikisha raha kwa watu wake; bali Mwenyezi Mungu ameiharamisha pepo isipokuwa kwa watakaotumikia njia hii.

Na humwongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka.

Mwito wa Mwenyezi Mungu wa kutenda heri, unamwenea kila aliye baleghe na mwenye akili timamu bila ya kumtoa yeyote. Basi atakayeasi na akaipuuza atakuwa amepotea na mwenye kutii akaitenda, atakuwa amaeongoka. Inafaa kutegemezwa uongofu wake kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu njia ya kuufuata ilikuwa ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Ama upotevu wa aliyepotea, haifai kuutegemeza kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu ameukataza na Mwenyezi Mungu hawezi kukataza jambo kisha alielekeze lifuatwe.

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٦﴾

26. Kwa wafanyao wema ni wema na ziyada, Na vumbi halitafunika nyuso zao wala udhalili. Hao ndio watu wa Peponi; hao humo watadumu.

وَالَّذِينَ كَسَبُوا السَّيِّئَاتِ جَزَاءُ سَيِّئَةٍ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ مَّا لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مِنْ عَاصِمٍ كَأَنَّمَا أُغْشِيَتْ وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِّنَ اللَّيْلِ مُظْلِمًا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧﴾

27. Na wale waliochuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake. Na utawafunika udhalili, Hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu. Kama kwamba nyuso zao zimefunikwa na kipande cha usiku wenye giza. Hao ndio watu wa motoni hao humo watadumu.

وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا مَكَانَكُمْ أَنتُمْ وَشُرَكَاؤُكُمْ فَزَيَّلْنَا بَيْنَهُمْ وَقَالَ شُرَكَاؤُهُم مَّا كُنتُمْ إِيَّانَا تَعْبُدُونَ ﴿٢٨﴾

28. Na siku tutakayowakusanya wote, kisha tuwaambie wale walioshirikisha: Simameni mahali penu nyinyi na washirika wenu. Kisha tutawatenga baina yao. Na wao walioshirikisha watasema: Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi.

فَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ إِن كُنَّا عَنْ عِبَادَتِكُمْ لَغَافِلِينَ ﴿٢٩﴾

29. Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yetu na nyinyi. Hakika sisi tulikuwa hatuna habari na ibada yenu.

هُنَالِكَ تَبْلُو كُلُّ نَفْسٍ مَّا أَسْلَفَتْ وَرُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٣٠﴾

30. Huko kila nafsi itajua iliyoyatanguliza na watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa haki, na yote waliyokuwa wakiyazua yatawapotea.

KWA WAFANYAO WEMA

Aya 26 – 30

MAANA

Kwa wafanyao wema ni wema na ziyada.

Razi anasema kuwa mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:

هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ ﴿٦٠﴾

“Je, malipo ya hisani si ni hisani tu” (55:60).

Lakini ilivyo ni kwamba hisani inahusika na kumfanyia mtu mwingine, na wema ni ule unaopendeza kimaumbile, ni sawa uwe ni kumfanyia mwingine au la. Huo ni pamoja na itikadi njema, kauli njema vitendo vyema na nia njema; na hata kuhisi dhambi.

Yote hayo yanapendeza kwa Mwenyezi Mungu na kwa maumbile, naye Mwenyezi Mungu (s.w.t) ataulipa wema. Kwa hiyo basi Aya iko katika mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu.

وَمَن يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَّزِدْ لَهُ فِيهَا حُسْنًا ﴿٢٣﴾

“Na anayefanya wema tutamzidishia wema…” (42:23).

Wametofautiana wafasiri katika maana ya ziada, Kwa sababu ikiwa ni katika aina ya wema basi si ziada na kama siyo basi neno litakuwa halijulikani. Lile tunalolifahamu ni kuwa makusudio ya ziada hapa ni kuwa yeye Mwenyezi Mungu mtukufu atawalipa wale waliofanya wema zaidi ya wanavyostahiki. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضْلِهِ ﴿١٧٣﴾

“Ama wale ambao wameamini na wakatenda mema,atawalipa ujira wao sawa, na atawazidishia kwa fadhila yake” Juz.6 (4:173)

Na vumbi halitafunika nyuso zao wala udhalili, Hao ndio watu wa Peponi; hao humo watadumu.

Kila kilichomo moyoni kiwe ni huzuni au furaha, amani au hofu, athari yake hudhihiri usoni wazi wazi, lakini athari ya hofu na kiherehere inadhi- hiri zaidi kuliko nyingineyo; hasa nyuso za watu wa motoni watakapouona. Zitasawajika kwa hofu; kama kwamba zimegubikwa na moshi au vumbi jeusi.

Ama watu wa Peponi nyuso zao zitacheka na kufurahi:

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ ﴿٣٨﴾ ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ ﴿٣٩﴾ وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ ﴿٤٠﴾ تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ ﴿٤١﴾

“Nyuso siku hiyo zitanawiri. Zitacheka na kufurahika. Na nyuso nyingin siku hiyo zitakuwa na vumbi. Zimefunikwa na weusi” (80:38–41).

Na wale waliochuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake.

Hakika Mwenyezi Mungu ni mwadilifu atamlipa anayefanya uovu anayostahiki; wala hatamdhulumu hata uzani wa sisimizi, bali atasamehe mengi. Kwa sababu yeye ni mkarimu; Na kwa ukarimu humwongezea mwenye kufanya wema ziada nyingi.

Na utawafunika udhalili.

Yaani fedheha itawafunika waovu, Hakuna mwenye kudhalilika na kufedheheka zaidi kuliko yule anayefed- heheka mbele ya watu.

Hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu.

Kuwalinda na machukivu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake.

Kama kwamba nyuso zao zimefunikwa na kipande cha usiku wenye giza. Hao ndio watu wa motoni hao humo watadumu.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kusema kuwa watu wema hazitafu- nikwa nyuso zao na vumbi wala udhalili, anasema kuwa wale waovu nyuso zao zitasawajika, kama kwamba ni kipande cha usiku.

Imam Ali(a.s ) amesema:“Heri siyo heri ikiwa baada yake ni moto; na shari si shari ikiwa baada yake ni Pepo , Na kila neema isiyokuwa Pepo ni kazi bure na kila balaa isiyokuwa moto ni nafuu”.

Na siku tutakayowakusanya wote, wale walioefanya wema na, wale waliofanya uovu;kisha tuwaambie wale walioshirikisha: Simameni mahali penu nyinyi na washirika wenu.

Kesho watasimama kwa hisabu, washirikina na wale waliokuwa wakidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu; watakabiliana uso kwa uso ili kila kikundi kitoe dalili kwa hoja yake. Hapo yatayeyuka matumaini waliyokuwa wakiyatamani washirikina na kutaraji manufaa na itawabainikia kuwa wao walikuwa kwenye upotevu katika kushirikisha kwao na inadi yao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na vitabu vyake.

Kisha tutawatenga baina yao

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t), siku ya Hisabu, atapambanua viumbe vyake vyote kwa sifa zao walizo nazo, na kudhihirisha hakika ya kila mmoja. Hapo itawabainikia washirikina kwamba hakuna yeyote anayeza kujidhuru yeye au mwingine au kujinufaisha na kwamba amri ni ya Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika wala mpinzani.

Na wao walioshirikisha watasema: Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi.

Wakati Mwenyezi Mungu atakapowasimamisha, mahali pamoja, washirik- ina na wale waliokuwa wakiwaabudu, na kukabiliana uso kwa uso, wataambiana: Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi; isipokuwa ni mawazo yenu kuwa Mwenyezi Mungu ana washirika na kwamba sisi ndio hao washirika walio katika mawazo yenu tu. Kwa hakika nyinyi hamwabudu chochote, na sisi ni chochote; kwa hiyo hamtuabudu sisi.

Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yetu na nyinyi

Yeye anajua kuwa hao washirika mliowazua kwenye mawazo yenu hawako, Vile vile anajua kuwa sisi tuko mbali na huo ushirikina wenu.

Hakika sisi tulikuwa hatuna habari na ibada yenu.

Hatujui chochote. Hiyo ni kuashiria kukana kuabudiwa na kwamba wao ni waabudu sio waabudiwa.

Huko kila nafsi itajua iliyoyatanguliza na watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa haki, na yote waliyokuwa wakiyazua yatawapotea.

Yaani Mwenyezi Mungu Mtukufu atawakusanya watu kuwahesabu na kumlipa kila mtu aliyoyachuma, wala hatakuta kile alichokuwa akikiitakidi na kukiwazia kuwa kinafaa na kumkinga; isipokuwa mtendo ya ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake. Maana haya yamekaririka kwa mifumo mbali mbali katika Aya kadhaa.


8

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٣١﴾

31. Sema: Ninani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini? Au ni nani anayemiliki usikizi na uoni na ni nani amtoaye hai kutoka maiti na akamtoa maiti kutoka aliye hai na ni nani anayedabiri mambo yote? Watasema ni Mwenyezi Mungu. Waambie: Basi je hamchi?

فَذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمُ الْحَقُّ فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ﴿٣٢﴾

32. Basi huyo ndiye Mweyezi Mungu Mola wenu, tena ni nini baada ya haki isipokuwa upotevu? Basi mnageuzwa wapi.

كَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ فَسَقُوا أَنَّهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٣﴾

33. Hivyo ndivyo lilivyothibiti neon la Mola wako juu ya wale waliofanya ufuska kwamba hataamini.

قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ قُلِ اللَّـهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٣٤﴾

34. Sema: Je, katika Miungu yenu ya ushirikina yuko anayeanzisha kuumba viumbe kasha akakirejesha? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye anayeanzisha kuumba kiumbe kasha akakirejesha, Basi mnadanganywa vipi?

NI NANI ANAYEWARUZUKU?

Aya 31 – 34

MAANA

Nguzo za imani ya haki kwa Mwenyezi Mungu ni tatu: Umoja, Utume na Ufufuo, Qur’ani imeonyesha aina mbali mbali za dalili ya nguzo hizi. Umetangulia ubainifu wake kwa ufanuzi pamoja na Aya hii tunayoifasiri sasa na iliyo baada yake.

Kwani Aya hizi zimekuja kubatilisha ushirikina na madai ya washirikina kuwa masanamu yao yanawakuribisha kwa Mwenyezi Mungu na kwamba hakuna ufufuo wala hisabu, na Qur’ani ni uzushi wa Muhammad kwa Mwenyezi Mungu. Yafuatayo ni kubadilisha madai hayo:

Sema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini?

Kila sababu miongoni mwa sababu za riziki, iwe yakaribu au mbali, haina budi kuwa ni ya mbinguni au ya kiardhi. Miongoni mwa sababu za mbingu ni mvua mwangaza na mengineyo ambayo wameyangudua wataalamu au watakuja kuyagundua. Na, katika sababu za ardhi ni mimea, wanyama na madini.

Sababu zote hizo zinarudia kwa Mwenyezi Mungu peke yake kupita desturi za kiulimwengu; kwa sababu yeye Mwenyezi Mungu mtukufu ndiye muumbaji; na washirikina wanajua hakika hii na kukiri kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji mwenye kuruzuku.

Kwa hiyo hapa linakuja swali kuwa:

Enyi Washirikina! Maadamu mnaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji mwenye kuruzuku, vipi mnamfanyia washirika? Vipi kitu kinaweza kuwa mshirika, na inajulikana kuwa hakina athari naye kabisa? Je, inafaa wewe msomaji uwe mshirika wangu katika kutunga kitabu hiki, na mimi ndiye niliyefikiri, nikavumilia na kuandika?

Tumefafanua maudhui haya katika Juz. 5 (4: 48)

Au ni nani anayemiliki usikizi na uoni?

Mwenyezi Mungu amezihusisha hizi mbili, kwa sababu ndizo nyenzo za kwanza za kupata elimu; hata nadharia pia inatokana na hizo kwa sababu nadharia inakomea kwenye hisia na kuona, Razi anasema katika kufasiri Aya hii.

“Ali (r.a.) alikuwa akisema: “Utakatifu ni wa yule aliyeufanya uoni kwa shahamu na akaufanya usikizi kwa mifupa na akatamkisha kwa nyama”

Ni nani amtoaye hai kutoka maiti na akamtoa maiti kutoka aliyehai.

Yaani anayemiliki mauti na uhai. Miongoni mwa mifano ya kutoa hai kati- ka maiti ni vinavyoliwa na wanyama na kupitia matumboni kisha vinasagwa hatimae zinapatikana chembe mpya za uhai. Na mfano wa kutoa maiti katika hai ni kufa chembe ambazo zinatokana na mwili ulio hai kwa kupumua. Tumezugumza kwa ufafanuzi katika Juz.7 (4:95) kifungu cha ‘uhai umetoka wapi?’

Na ni nani anayeyadabiri mambo yote yaliyo katika ulimwengu?

Watasema ni Mwenyezi Mungu , Waambie basi je hamchi katika washirika mliowazusha?

Wao hawakatai kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja aliyepeke yake, anayeruzuku, anayemiliki usikizi, uoni, mauti, uhai, na mambo yote. Lakini pamoja na hayo wanamfanyia Mwenyezi Mungu washirika.

Siri ya mgongano huu ni kwamba wao wanamtazama muumba kwa mtazamo wa kimaudhui. Wameamini kuwa yeye ndiye muumba na mwenye kupatisha vitu vyote; kisha wakatazama yale yatakayowakurubisha kwake kwa mtazamo wa kimapenzi yao, wakakosea. Badala ya kujikurubisha kwake kwa vitendo na ikhlasi, wamemzuishia washirika na wakajikurubisha kwa hao wanaowashirikisha

Basi huyo ndiye Mweyezi Mungu Mola wenu, tena ni nini baada ya haki isipokuwa upotevu?

Hakuna usaidizi baina yao; ama haki na uongofu au batili na upotevu. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye aliyeumba mbingu na ardhi ambazo ndani yake mna sababu za riziki. Na akaumba usikizi na uoni kwa haki ambazo ndio njia za elimu.

Na yeye anamiliki mauti na uhai kwa haki. Milki hiyo ni dalili ya uwezo na cheo. Naye ndiye mpangaji wa mambo kwa haki, ambako kunafahamisha elimu na hekima. Basi kuna nini tena baada haya yote isipokuwa upotevu, batili, ujinga na inadi.

Basi mnageuzwa wapi kuiacha haki na Tawhid na kufuata upotevu na kufuata shirk? Hivyo ndivyo lilivyothibiti neno la Mola wako juu ya wale waliofanya ufuska.

Hiyo ni ishara ya yale yaliyotangulia kwamba hakuna baada ya haki isipokuwa upotevu. Makusudio ya neno la Mola wako hapa ni adhabu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

قَالُوا بَلَىٰ وَلَـٰكِنْ حَقَّتْ كَلِمَةُ الْعَذَابِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٧١﴾

“Lakini limekwishathibiti neon la haki kwa makafiri”(39:71).

Makusudio ya waliofanya ufuska ni washirikina. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu atawaadhibu washirikina, adhabu ya mwenye kuifanyia inadi haki na akakataa imani kabisa. Hiyo ndiyo stahiki yao kwani walipewa mwito wa Tawhid, zikawasimamia hoja na ubainifu, lakini pamoja na hayo walig’ang’ania shirki na wakafa nayo.

Sema: Je, katika Miungu yenu ya ushirikina yuko anayeanzisha kuumba viumbe kisha akakirejesha? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye anayeanzisha kuumba kiumbe kisha akakirejesha, Basi mnadanganywa vipi?

Yaani sema ewe Muhammad kuwaambia washirikina kuwa Mungu anaumba kitu bila ya kutumia kitu, anamrudishia uhai aliyekufa, Je hao mnaomshirikisha naye wanaweza hilo? Ikiwa hawawezi, basi inakuwaje mnaiacha Tawhid na kuifuata shirk?

Unaweza kuuliza kuwa : hoja ya kuumba iko wazi kwa washirikina, kwa vile wanakubali hilo, lakini hoja ya kurudisha uhai haiko wazi na hilo ndilo jambo wanalolipinga, kuwa hakuna ufufuo, Sasa kuna wajihi gani hapo?

Jibu : Qur’ani katika Aya kadhaa imeleta hoja za kutosha kuhusu kurudishwa uhai na ufufuo kwa ujumla na washirikina wakashindwa kuzijibu. Kushindwa kwao huko ndiyo hoja iliyowalazimu; kwamba Mwenyezi Mungu atavirudisha viumbe kama alivyovianzisha.Kwa maneno mengine ni kuwa hukumu inasimama kwa dalili sio kusalimu amri yule anayehukumiwa.

قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ قُلِ اللَّـهُ يَهْدِي لِلْحَقِّ أَفَمَن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّي إِلَّا أَن يُهْدَىٰ فَمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ﴿٣٥﴾

35. Sema: Je, katika Miungu yenu ya ushirikina yuko aongozaye kwenye haki? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye aongozaye kwenye haki Basi je anayestahiki kufuatwa ni yule aongozaye kwenye haki au ni Yule asiyeongoka isipokuwa aongozwe? Basi mni nini nyinyi? Mna hukumu vipi?

وَمَا يَتَّبِعُ أَكْثَرُهُمْ إِلَّا ظَنًّا إِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا يَفْعَلُونَ ﴿٣٦﴾

36. Na wengi wao hawafuati isipokuwa dhana tu. Hakika dhana haifai kitu mbele yake haki, Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa wanayoyatenda.

وَمَا كَانَ هَـٰذَا الْقُرْآنُ أَن يُفْتَرَىٰ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٣٧﴾

37. Na haikuwa Qur’ani hii imezushwa, kuwa haitoki kwa Mungu. Lakini inasadikisha yaliyotangulia na ni ufafanuzi wa kitab. Haina shaka imetoka kwa Mola wa viumbe vyote.

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ قُلْ فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّثْلِهِ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣٨﴾

38. Je, wanasema ameizuwa? Sema: Basi leteni Sura moja mfano wake na muwaite muwawezao asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli.

بَلْ كَذَّبُوا بِمَا لَمْ يُحِيطُوا بِعِلْمِهِ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ ﴿٣٩﴾

39. Bali wamekadhibisha wasiyoyajua elimu yake, Kabla haujawajia ufafanuzi wake, Kadhalika walikanusha waliokuwa kabla yao Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa madhalimu.

MWENYE KUONGOZA KWENYE HAKI

Aya 35 – 39

MAANA

Sema: Je, katika Miungu yenu ya ushirikina yuko aongozaye kwenye haki?

Aya hii nikumfunga mdomo yule anayeabudu pamoja na Mwenyezi Mungu waungu wengine. Njia ya kufunga huko ni kwamba sifa ya kwanza anayotakikana kuwa nayo yule mwenye kuabudiwa ni kuwa yeye mwenyewe anaongoza kwenye haki bila ya kutegemea mwongozo wa mwingine, Ama yule asiyeongoza kwenye haki hastahiki uungu kabisa. Hakika hii ni wazi haina ubishi.

Kwa hiyo Mwenyezi Mungu amemwamrisha Mtume wake Muhammad(s.a.w.w.) kuwahoji washirikina na kuwatupia swali hili, kwamba je, katika masanamu yenu haya mnayoyaabudu anapatikana anayeweza kuongoza kwenye haki? Hakuna mwenye shaka kwamba wao hawakuthubutu kujibu hili.

Kwa sababu masanamu yao ni mawe tu, waliyoyatengeneza kwa mikono yao, kwa vile Mtume(s.a.w.w.) anayo hoja mkataa kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayeongoza kwenye haki, ndipo akalielekeza swali hili kwao.

Sema: Mwenyezi Mungu ndiye aongozaye kwenye haki sio mwingine.

Na mwongozo huo ni wake mwenyewe hautokani na mwingine. Dalili ya kuwa Mwenyezi Mungu anaongoza kwenye haki ni Mitume aliowatuma kwa waja wake wakitoa bishara na kuonya.

Vile vile vitabu alivyowateremshia ambavyo ndani yake mna Aya zinazobainisha ambazo zinawaon- goza watu kwenye shari yao na wema wao.

Huyu hapa Muhammad anawakabili washirikina ana kwa ana na aki- washinda kwa Qur’ani ambayo ndani yake mna ubainifu wa kila kitu.

Basi wako wapi wajumbe wa waungu wenu wa kishirikina? Viko wapi vitabu vyao, Lau Mwenyezi Mungu angelikuwa na mshirika, tungelimwona Mtume wake.

Ilivyo ni kwamba lengo sio kumlinganisha Mwenyezi Mungu, Mtume na masanamu, hapana! Ispokuwa lengo ni kuwaamsha washirikina na kuwazindua ujinga wao na upotevu wao, huenda wakazinduka.

Basi je anayestahiki kufuatwa ni yule aongozaye kwenye haki au ni yule asiyeongoka isipokuwa aongozwe?

Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja utangulizi huu, hapa anabainisha natija yake, kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kufuatwa, si mwingine.

Natija hii anaidokeza kwa swali lenye jawabu lake; nalo ni: Ni nani anayestahiki kufuatwa na kuongoza? Je, ni Mwenyezi Mungu anayeongoza yeye mwenyewe au ni waungu wenu wa ushirikina wanaongozwa?

Unaweza kuuliza kuwa : washirikina wa Makka wanaoambiwa maneno walikuwa wakiabudu masanamu na inajulikkana wazi kuwa masanamu hayo ni mawe ambayo hayawezi kuongozwa na walimu wala viongozi. Sasa kuna wajihi gani wa kauli ya Mwenyezi Mungu, ‘isipokuwa aongozwe?’

Wafasiri wamejibu kuwa hii ni haki ya kufaradhia na kukisia tu; yaani tufaradhie kuwa lau hayo masanamu yenu yangekuwa yanaongoza si ya takua hayo yenyewe yamefanywa kuongozwa? Na anayekuwa hivyo basi hafai kuwa Mwenyezi Mungu.

Jibu : zuri ni kuwa Aya haikuwashukia washirikina wa Makka peke yao, bali imewashukia wao, na wale wanaoabudu watu au Malaika n.k.

Kwa hiyo maana yanakuwa, kila asiyeweza kuongoza, basi hastahiki kuwa Mungu ni sawa awe hana uwezo wa kuongoza hata kwa kuongozwa; kama mawe, au anaweza kuongoza baada ya kuongozwa; kama binadamu na Malaika, Wote hao hawastahiki kuwa Mungu.

Basi mna nini nyinyi? Mnahukumu vipi?

Mnaamini upotevu na hali dalili ya ubatilifu na ufisadi wake iko wazi

Na wengi wao hawafuati isipokuwa dhana tu.

Wengi wao ni washirikina. Kwa sababu kulikuwa na baadhi ya washirikina waliokuwa na yakini na kukubali ukweli na utume wa Muhammad na wakijua fika kuwa masanamu yao si chochote, lakini wakafanya inadi na kiburi kwa kuchunga masilahi yao na vyeo vyao. Ama wengine ambao ndio wengi walikuwa wakiabudu masanamu kwa kufuata na kuwaiga wazazi wao.

Mwenyezi Mungu ameitolea ibara ya dhana, ibada yao hii, pamoja na kuwa wenyewe walikuwa na yakini kuwa masanamu yao yanadhuru na kunufaisha.

Kwa sababu yakini yao hii haina msingi wa usahihi, Na kila yakini inayotegemea kuiga inafaa kuitolea ibara ya dhana. Tumefafanua zaidi kuhusu kufuata na kuiga tulipofasiri Juz. Baqara (2:170).

Hakika dhana haifai kitu mbele yake haki.

Makusudioa ya dhana hapa sio kutokuwa na uhakika, kama inavyoonyesha katika ibara iliyopita, isipokuwa makusudio yake hapa ni kuamini msingi wowote katika misingi ya dini au tawi katika matawi yake bila ya dalili ya kiakili au ya wahyi; hata kama imani hiyo itaaminiwa kiuhakika; kama vile kuiga washirikina katika kuabudu masanamu na ulahidi kabla ya kufanya utafiti na kuchunguza sababu za kuweko ulimwengu na kupatikana kwake na nidhamu iliyoko ndani yake. Je ilikuwa kwa sadfa au kwa mpango wa mwenye ujuzi na hekima?

Aya hii ni dalili wazi ya kupinga kiyasi (kukisia) na kuwa haifai katika masuala ya dini. Kwa sababu kiyasi ni kutumia dhana ambayo haifai kitu mbele ya haki katika misingi ya kiitikadi na hukumu za sharia.

Ama maswala ya dunia yako nje ya maudhui ya Aya, Vipi Mungu atakataza dhana katika kilimo, biashara na mafungamano ya kijamii. Lau watu wangelingoja elimu na yakini katika kila kitu basi maisha yangedumaa Hata hivyo haifai kumtuhumu mtu na kosa au kuwa shahidi ila baada ya kujua na kupata yakini. Siri ya hilo ni kuyapeleka maisha kwenye njia iliyo sawa.

Kwa ufupi katika mambo ya kidunia kuna maswala ambayo inafaa kufuata dhana na ambayo haifai kufuata dhana na mengine kuna hiyari. Mwenye kutaka kujua ufafanuzi wa hayo na asome kitabu Faraidil-Usul kinachojulikana kama Arrasul cha Sheikh mkuu, Al-Answari. Yeye amezama sana kwenye utafiti wa suala hili na ameandika karibu kurasa

Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa wanayoyatenda

Hili ni kemeo kwa washirikina ambao wanafuata dhana katika kuabudu masanamu na kumkadhibisha Mtume(s.a.w.w) bila ya kuipima dhana yao hii kwa kipimo cha maumbile na akili. Vile vile ni kemeo kwa kila anayefuata dhana katika mambo ya dini.

Na haikuwa Qur’ani hii imezushwa kuwa haitoki kwa Mungu.

Kwa sababu ya mfumo wake wa ajabu na yale yaliyomo ndani yake; kama elimu, sharia ya watu, adabu za kijamii, kutolea habari mambo ya ghaib na mengineyo ambayo ni muhali kuwa hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Lakini inasadikisha yaliyotangulia katika vitabu vya Mwenyezi Mungu, Na ni ufafanuzi wa kitab.

Makusudio ya kitab hapa ni kila sharia aliyoiweka Mwenyezi Mungu ambayo binadamu anaihitajia kwa ajili ya wema wake wa dunia na akhera.

Haina shaka imetoka kwa Mola wa viumbe vyote.

Yaani haitakikani kwa mwenye akili kutia shaka katika Kitab cha Mwenyezi Mungu, kikiwa kimekusanya miujiza na Aya zinazokubalika na kila mwenye umbile safi na akili iliyo salama.

Je, wanasema ameizuwa? Sema: Basi leteni Sura moja mfano wake na muwaite muwawezao asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wa kweli.

Yametangulia maelezo yake kwa ufafanuzi zaidi katika Juz.1(2:23)

Bali wamekadhibisha wasiyoyajua elimu yake.

Ndivyo ilivyo kwa asiyejua, kufanya haraka kusadikisha na kukadhibisha, kabla ya kufanya uchunguzi.

Kusema kwake Mwenyezi Mungu: ‘Wasiyoyajua elimu yake,’ ni ishara ya kwamba akili haiwezi kuthibitisha kitu au kukanusha ila baada ya kukisoma kwa utulivu kwa darasa kamili inayokusanya pande zake zote.

Kabla haujawajia ufafanuzi wake,

Yaani washirikina waliikanusha Qur’ani kabla ya kujua uhakika wake na siri zake. Lau wao wangeyatilia maanani mafunzo yake na hukumu yake, basi wangeliisadiki, ikiwa wanatafuta uhakika.

Imeelezwa katika Tafsir Majmaul-bayan: “Inasemekana kuwa Amirul- mumini, Ali(a.s ) alichukua kutokana na Aya hii kauli yake:‘Watu ni maadui wa wasiyoyajua.’ Na kauli yake:‘Thamani ya mtu ni yale anayoyajua, ’ aliichukuwa katika Aya isemayo:

فَأَعْرِضْ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿٢٩﴾ ذَٰلِكَ مَبْلَغُهُم مِّنَ الْعِلْمِ ﴿٣٠﴾

“Basi mwachilie mbali yule aupaye kisogo ukumbusho wetu na wala asitake ila maisha ya dunia. Huo ndio mwisho wao wa ujuzi” (53:29–30)

Na kauli yake isemayo: ‘Zungumzeni mtajulikana’ aliitoa katika Aya:

وَلَتَعْرِفَنَّهُمْ فِي لَحْنِ الْقَوْلِ ﴿٣٠﴾

“Na hakika utawafahamu kwa namna ya usemi.” (47:30).

Kadhalika walikanusha waliokuwa kabla yao; kama vile watu wa Nuh, Adi, Thamud nk, waliokanusha Mitume yao kabla ya kujua uhakika wa heri na mwongozo waliokuja nao.

Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa madhalimu katika maangamizi na mabalaa.

فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٥﴾

“Ikakatwa mizizi ya watu waliodhulumu; na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote.” (6:45)

وَمِنْهُم مَّن يُؤْمِنُ بِهِ وَمِنْهُم مَّن لَّا يُؤْمِنُ بِهِ وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِالْمُفْسِدِينَ ﴿٤٠﴾

40. Na miongoni mwao wapo wanaoiamini, na miongoni mwao wapo wasioiamini. Na Mola wako anawajua sana wafisadi.

وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ أَنتُم بَرِيئُونَ مِمَّا أَعْمَلُ وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٤١﴾

41. Na kama wakikudhabisha, basi sema: Mimi nina amali yangu na nyinyi mna amali yenu. Nyinyi hamna jukumu kwa ninayoyatenda, na mimi sina jukumu kwa mnayoyatenda.

وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ وَلَوْ كَانُوا لَا يَعْقِلُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na miongoni mwao wapo wanaokusikiliza, Je, wewe unaweza kuwasikilizisha viziwi ingawa hawafahamu?

وَمِنْهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيْكَ أَفَأَنتَ تَهْدِي الْعُمْيَ وَلَوْ كَانُوا لَا يُبْصِرُونَ ﴿٤٣﴾

43. Na miongoni mwao wapo wanaokutazama, Je, wewe unaweza kuwaogoza vipofu ingawa hawaoni?

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ النَّاسَ شَيْئًا وَلَـٰكِنَّ النَّاسَ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٤٤﴾

44. Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu watu chochote, lakini watu wanajidhulumu wenyewe.

MIONGONI MWAO WAPO WANAOAMINI

Aya 40 – 44

MAANA

Na miongoni mwao wapo wanaoiamini na miongoni mwao wapo wasioamini.

Dhamir katika miongoni mwao inarudi kwa washirikina na inayoaminiwa ni Qur’ani. Maana ni kuwa washirikina kwa mtazamo wa Kiqur’ani wako mafungu mawili: Kuna walioacha ushirikina na kuamini Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi. Kimsingi ni kuwa kuamini Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndio kumwamini Mohammad(s.a.w.w) .

Na wengine wameng’ang’ania ushirikina kwa inadi na kupupia manufaa. Hawa ndio wale aliowakemea Mwenyezi Mungu kwa kusema:

Na Mola wako anawajua sana wafisadi.

Hii inaonyesha kuwa neno mfisadi halimuhusu yule anayewafitini watu au kuwafanyia uovu bali linamuhusu kila aliyejua haki na asiitumie.

Na kama wakikudhabisha, basi sema: Mimi nina amali yangu na nyinyi mna amali yenu. Nyinyi hamna jukumu kwa ninayoyatenda, na mimi sina jukumu kwa mnayoyatenda.

Waumini wengi wameniuliza kuhusu jukumu lao kwa watoto wao waliopotea na wakaipuuza dini na hukumu yake.

Nikawajibu kuwa ni jukumu la mzazi kuwalea wanawe wadogo malezi ya kidini na awakuze kwenye misingi ya dharura ya dini, awaeleze misingi ya kiitikadi na kuwazowesha ibada za wajib; kama vile swala na saumu n.k. Vile vile kuwajulisha mambo ya haramu; kama uwongo, kusengenya, ulevi n.k.

Wakifikia makamo ya kujiongoza, basi awe kama muonyaji na mtoa bishara, Ikiwa hawataitikia mwito wake; basi yeye hana lawama mbele ya Mwenyezi Mungu.

Kisha nikawasome Aya hii na Aya nyingine iliyo na maana hii na Hadith; kama kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na sema: Hii ni haki itokayo kwa Mola wenu, basi atakaye na amini na asiyetaka na akatae” (18:29) Mtume Mtukufu(s.a.w.w) anasema:

“Mtoto ni bwana wa miaka saba na mtumwa wa miaka saba na waziri wa miaka saba. Tosheka na tabia yake kwa miaka 21 vinginevyo achana naye, umeshatekeleza majukumu yako kwa Mwenyezi Mungu”

Yaani mtoto ataachwa katika miaka saba ya mwanzo kwa sbabu ya udogo wake na atatiwa adabu katika miaka saba ya pili; kama mtu asiyekuwa na hiyari na ataelekezwa katika miaka saba ya tatu; kama mtu huru. Kusema achana naye ni kukata tamaa, na kwamba mzazi hana majukumu juu ya uovu wa mwanawe.

Na miongoni mwao wapo wanaokusikiliza.

Yaani katika washirikina au wanaokadhibisha wapo wanaomsikiliza Mtume(s.a.w.w) kwa masikio tu. Ama nyoyo zao na akili zao ziko mbali naye, sawa na asiyesikia.

Je, wewe unaweza kuwasikilizisha viziwi, ingawa hawafahamu maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno yako ewe Mtume? Yule anayesikia na asifahamu au anayefahamu na asisikie, Mwenyezi Mungu amemweka daraja ya asiyesikia.

Kwa sababu lengo la hisia za kusikia ni kufaidika na kunufaika nazo. Ikiwa lengo hilo halikutimia, basi ni sawa na kutokuwepo hizo hisia.

Na miongoni mwao wapo wanaokutazama kwa macho yao lakini hawajui cheo chako na daraja yako ewe Mtume; kama kwamba hawana macho.

Je, wewe unaweza kuwaongoza vipofu ingawa hawaoni?

Yaani kama ambavyo huwezi kumfanya kiziwi asikie na kipofu aone, basi vile vile huwezi kumwongoza na Qur’ani yule anayekusikiliza na kukuangalia kwa sababu ya malengo yake na tamaa yake. Walisema wahenga: “Tamaa inapofusha na kufanya uziwi.”

Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu watu chochote, lakini watu wanajidhulumu wenyewe.

Hilo halina shaka kwani Mwenyezi Mungu amewapa uwezo na utambuzi, akawabainishia njia ya kheri na ya shari, akawakataza hili akawaamrisha lile na akawapa hiyari. Basi atakayemtii Mwenyezi Mungu atakuwa amejichagulia yeye mwenyewe kuokoka na atakaye asi atakuwa amejichagulia kuangamia.

Ni ajabu kuwa hakika hii imefichika kwa Ashaira na ikadhihirika kwa Iblis mlanifu, pale atakapowaambia wafuasi wake siku ambayo haitakuwa na ubishi wala hadaa:

فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنفُسَكُم ﴿٢٢﴾

“Msinilaumu bali jilaumuni wenyewe” (14:22).


9

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ كَأَن لَّمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِّنَ النَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيْنَهُمْ قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na siku atakapowakusanya itakuwa kama kwamba wao hawakukaa isipokuwa saa moja tu ya mchana, Watatambuana. Hakika wamehasirika waliokanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuwa wenye kuongoka.

وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ اللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ ﴿٤٦﴾

46. Na vyovyote vile, tukikuonyesha baadhi ya tunayowaahidi au tukakufisha, basi marejeo yao ni kwetu. Kisha Mwenyezi Mungu ni shahidi wa wanayoyafanya.

وَلِكُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولٌ فَإِذَا جَاءَ رَسُولُهُمْ قُضِيَ بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٤٧﴾

47. Na kila Umma una Mtume Basi anapokuja Mtume wao inahukumiwa baina yao kwa uadilifu; nao hawatadhulumiwa.

SIKU ATAKAYOWAKUSANYA

Aya 45 – 47

MAANA

Na siku atakapowakusanya itakuwa kama kwamba wao hawakukaa isipokuwa saa moja tu ya mchana.

Kusema saa moja tu ya mchana ni fumbo la kuwa maisha ya dunia hata yakiwa marefu kiasi gani bado ni mafupi tu, kwa sababu yanaisha.

Maneno ya watu kuhusu kuikashifu dunia kimashairi na kinathari yamejaza kurasa za vitabu. Lakini jambo la kushangaza ni kuwa wanachanganya kuikashifu na kuisifu. Bali watu lau watarudishwa duniani baada ya kufa, wangelirudia yale yale waliyokatazwa. Hii inafahamisha kwamba watu hawatambuliki kwa maneno.

Watatambuana .

Dhahiri ya tamko inajulisha kuwa wenye makosa watatambuana siku ya mkusanyiko; vile vile watu wema.

Unaweza kuuliza : Hii haipingani na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ ﴿٢﴾

“Siku mtakapoiona kila mwenye kunyonyesha atamsahau amnyonyeshaye” (22:2)

Jibu : Kuna tofauti kati ya ufufuo na kukusanywa na vile vile siku ya Kiyama ambayo ni siku ya kuharibiwa ulimwengu. Na Aya ya (22:2) inazungumzia siku ya Kiyama, Na kauli yake Mwenyezi Mungu: “Watatambuana” inazungumzia siku ya kukusanywa. Zaidi ya hayo ni kwamba vituo vya mkusanyiko vitakuwa vingi. Watu wataweza kutambua na hasa siku ya hisabu na vingine hawatatambuana; kama vile wakipelekwa motoni.

Hakika wamehasirika waliokanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuwa wenye kuongoka.

Kila mwenye kufanya kwa ajili ya jambo ambalo haliko, au akapuuza na asifanye kwa ajili ya jambo liliopo ambalo linaambatana naye na mwelekeo wake, basi atakuwa ni katika wenye kupotea wenye kuhasirika. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa yule anayefanya amali kwa ajili ya dunia bila ya akhera, ni sawa awe mkweli au mwogo.

Na vyovyote vile, tukikuonyesha baadhi ya tunayowaahidi au tukakukufisha, basi marejeo yao ni kwetu.

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume(s.a.w.w ) . Maana nikuwa Mwenyezi Mungu anawashtua na kuwaahidi wale wanaowakadhibisha kuhusu hizaya hiyo kuwa hapana budi itawapata tu, iwe ni katika uhai wa Mtume au baada ya kufa kwake. Kwa vyovyote vile, marejeo yao ni kwa Mwenyezi Mungu na atawaadhibu adhabu kubwa.

Kisha Mwenyezi Mungu ni shahidi wa wanayoyafanya.

Yaani anayajua yote wayafanyao, hakifichiki kitu chochote kwake; na kisha atawalipa yale wanayostahiki.

Na kila Umma una Mtume anayewapa bishara na kuwaonya. Na baada ya maonyo itakuwa hisabu na adhabu, Kwani hakuna adhabu bila ya onyo.

Basi anapokuja Mtume wao na akawaeleza yale yaliyowajibu kuyajua katika dini; na kusibakie udhuru wa mwenye kutafatu udhuru,inahukumiwa baina yao kwa uadilifu. Yule aliyetikia mwito wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, atahukumiwa kufuzu na kupata Pepo. Na yule anayeukataa atahukumiwa adhabu

Nao hawatadhulumiwa.

Hakuna upungufu wa thawabu za mtiifu, bali huenda akazidishiwa. Wala hakuna kuzidishiwa aliyeasi, bali huenda ikamfikia rehema.

Hayo ndiyo maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu ‘kwa Uadilifu’ Ni desturi ya Qur’ani kusisitiza kila linaloambatana na akhera na malipo yake ya thawabu na adhabu.

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٨﴾

48. Na wanasema: Ni lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli?

قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ إِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَلَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ ﴿٤٩﴾

49. Sema: Similikii nafsi yangu dhara wala nafuu, isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu, Kila umma una muda, Unapofikia muda wao hawakawii saa moja wala hawatangulii.

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُهُ بَيَاتًا أَوْ نَهَارًا مَّاذَا يَسْتَعْجِلُ مِنْهُ الْمُجْرِمُونَ ﴿٥٠﴾

50. Sema: Mwaonaje ikiwafikia adhabu yake usiku au mchana, Sehemu gani ya adhabu wanaihimiza wenye makosa?

أَثُمَّ إِذَا مَا وَقَعَ آمَنتُم بِهِ آلْآنَ وَقَدْ كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ ﴿٥١﴾

51. Tena, Je, ikishatokea Mtaiamini? Sasa tena? Na hali mlikuwa mkiihimiza?

ثُمَّ قِيلَ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ هَلْ تُجْزَوْنَ إِلَّا بِمَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ ﴿٥٢﴾

52. Kisha waliodhulumu watambiwa: onjeni adhabu ya kudumu. Kwani hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyachuma?

وَيَسْتَنبِئُونَكَ أَحَقٌّ هُوَ قُلْ إِي وَرَبِّي إِنَّهُ لَحَقٌّ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ ﴿٥٣﴾

53. Na wanakuuliza: Je, ni kweli hayo? Sema: Ehe! Naapa kwa Mola wangu hiyo ni kweli nanyi hamuwezi kushinda.

وَلَوْ أَنَّ لِكُلِّ نَفْسٍ ظَلَمَتْ مَا فِي الْأَرْضِ لَافْتَدَتْ بِهِ وَأَسَرُّوا النَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٥٤﴾

54. Na lau kama kila nafsi iliyod hulumu inamiliki kila kilichomo ardhini, ingelitoa vyote kujikombolea. Na watakapoiona adhabu wataficha majuto Na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu; nao hawatadhulumiwa.

أَلَا إِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَلَا إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٥﴾

55. Jueni kuwa hakika vyote vilivyomo katika mbingu na ardhi ni vya Mwenyezi Mungu. Jueni kuwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni haki Lakini wengi wao hawajui.

هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٥٦﴾

56. Yeye ndiye anayefufua na anayefisha na kwake mtarudishwa.

NI LINI AHAD HII?

Aya 48 – 56

MAANA

Na wanasema: Ni lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli?

Katika Aya 45, Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewatishia wale wanaokad- hibisha kuwa watakutana naye, kwamba yeye atawafufua baada ya kufa na awaadhibu kutokana na kukadhibisha kwao. Katika Aya hii 48, Mwenyezi Mungu Mtukufu anaishiria kwamba wao wanajibu vitisho hivyo kwa dharau wakisema kuwa yatakuwa lini hayo?

Sema: Similikii nafsi yangu dhara wala nafuu, isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu.

Yaani nyinyi mnaniuliza jambo ambalo sina uwezo nalo, bali sina uwezo hata wa nafsi yangu sembuse hayo mengine! Mfano wa Aya hii umetangulia katika Juz.9 (7:188).

Kila umma una muda, Unapofikia muda wao hawakawii saa moja wala hawatangulii.

Tumeeleza kwa ufafanuzi, kuhusu mfano wa Aya hiyo katika Juz.4 (3:145).

Sema: Mwaonaje ikiwafikia adhabu yake usiku au mchana, Sehemu gani ya adhabu wanaihimiza wenye makosa?

Washirikina walikadhibisha adhabu ya Akhera, kisha wakaihimiza kwa dharau; ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kuwaambia kuwa Hebu niambieni mtafanya nini ikiwashukia adhabu mkiwa mko macho au mmelala, tena ni adhabu gani hiyo mnayoihimiza enyi wapumbavu? Je, mnangoja adhabu ya dunia au adhabu ya akhera? Vyovyote iwavyo, je, mnaweza kuikinga? Kuna yeyote miongoni mwenu awezaye kumkimbia Mwenyezi Mungu?

Tena, Je, ikishatokea Mtaiamini?

Tumewashuhudia watu wengi wapumbavu wakijaribu kuikabili hatari au wakiacha mambo ambayo yana manufaa kwao. Wanapopewa nasaha na wenye akili na kuwahadharisha na mwisho mbaya, wao wanaziba masikio yao na kuwa na inadi ya kufanya uovu au kuacha kufanya heri wakidharau matokeo yake na yule anayewahadharisha. Inapofikia huanza kusema: ole wetu tulikuwa tukiambiwa sisi.

Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa wale wanaokadhibisha siku ya mwisho. Waliikadhibisha wakati ambao kuiamini kulifaa na wataiamini siku ambayo kuiamini hakuna manufaa yoyote, wamekwisha chelewa.

Sasa tena? Na hali mlikuwa mkiihimiza?

Je, mnaikubali na kuiamini hivi sasa ambapo hakuna manufaa yoyote ya kuiamini, wakati ambao mlitakiwa kuiamini, hamkufanya hivyo. Hakika kumwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho ni kumwamini ikiwa ghaibu, lakini kuamini kiaga chake na siku ya mwisho baada ya kuiona, sivyo inavyotakiwa.

Kisha waliodhulumu watambiwa: onjeni adhabu ya kudumu.

Kifungo cha maisha, katika dunia, kinaishia kwa mauti. Ama kifungo katika Jahannam hakina mwisho, kwa sababu hakuna kufa wala adhabu yake haipunguwi.

Kwani hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyachuma?

Lau wangeliadhibiwa kwa yale wasiyoyachuma, Mwenyezi Mungu angelikuwa dhalimu, Ametakata ambaye ghadhabu zake hazimfanyi kuacha uadilifu wake.

WALLAHI WEWE MUHAMMAD NI MTUME

Na wanakuuliza, Je, ni kweli hayo? Ya adhabu tuliyoahidiwa?

Sema: Ehe! Naapa kwa Mola wangu hiyo ni kweli nanyi hamuwezi kushinda.

Qur’ani mara nyingi imetaja ishara na ubainifu juu ya utume wa Mohammad na ukweli wake wa kauli na vitendo. Miongoni mwa Aya hizo ni Juz, 1 (2:23), Juz. 3 (3:61), Juz,11(10:16) n.k.

Inajulikana kwamba Mtume alikuwa mkweli na mwaminifu kabla ya kutangazwa kuwa Mtume. Kwa hiyo mtu ambaye watu wamemjua kuwa ni mkweli na mwaminifu kwa muda wa miaka arobaini, basi ni juu yao kumwamini katika kauli zake zote mpaka uthibitike uongo wake.

Mwenye kumjua kwa sifa hizi anapaswa amwamini katika madai yake ya utume kwa kuchukulia kuwa Mohammad ni mwaminifu. Lakini tamaa manufaa na hawa za nafsi zinaingia kati ya mtu na akili yake na moyo wake.

Ama wale ambao wameepukana na matamanio ya nafsi na wakaitafuta haki kwa njia ya haki, basi waliamini kuanzia mwanzo. Miongoni mwao wako waliotosheka, kwa kusema tu: mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, bila ya kutaka ubainifu wala kiapo; kama vile Aliy bin Abu Talib. Wengine wakataka ubainifu na wengine wakatosheka kwa kuapa, kama vile Dhamam bin Tha’laba.

Wamesema wapokezi, akiwemo Imam ibn Hambal, Bukhari na Muslim: “Wakati Mtume alipokuwa msikitini, mara aliingia mtu, akaanza kusaili: Ninani Mohammad katika nyinyi? Akaelekezwa, wakaanza mahojiano. Yule mtu akanza kwa kusema: Mimi nitakuuliza maswali mengi kwa hiyo usinichoke.

Mtume: Uliza upendavyo.

Mtu: Ninakuuliza kwa jina la Mola wako na Mola wa aliyekuwa kabla yako, Je, Mwenyezi Mungu amekutuma kwa watu wote:

Mtume: Ndio, kwa jina la Mola wangu.

Mtu: Nakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu: Je, amekuamrisha kuswali swala tano, katika usiku na mchana?

Mtume: Ndio, kwa jina la Mola wangu.

Mtu: Nakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu: Je amekuamrisha kufunga mwezi mmoja katika mwaka?

Mtume: Ndio, kwa jina la Mola wangu.

Mtu: Nakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu: Je, amekuamrisha kuchukua sadaka kutoka kwa matajiri na kuigawanya kwa mafukara. Mtume: Ndio, kwa jina la Mola wangu.

Mtu: Nimeamini uliyokuja nayo, nami nitakuwa mjumbe kwa watu wangu. Mimi ni Dhamam bin Tha’laba ndugu wa Bani Sa’d bin Bakr.

Yule mtu akatoka Msikitini na alikuwa na nywele zenye misokoti miwili, Mtume akasema yule mtu akisadikisha, ataingia peponi.

Alipofika kwa watu wake maneno yake ya kwanza yalikuwa: Lata na Uza hawana maana. Watu wakasema: We! Dhamam nyamaza, usije ukapatwa na mbalanga na ukoma! Akasema: ole wenu! Hao hawadhuru wala kunufaisha, Hakika Mwenyezi Mungu amewaletea Mtume na amemteremshia Kitabu kitakachowaokoa na haya mliyokuwa nayo.

Na mimi Ninushahadia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee hana mshirika; na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja wake na Mtume wake. Nimewaletea kutoka kwake yale mnayoamrishwa na mnayokatazwa.

Kama alivyosilimu yeye kirahisi, vilevile watu wake, waume kwa wake, walisilimu kirahisi.

Hivyo ndivyo alivyo kila ambaye matakwa yake na matamanio yake ni haki, anaiamini pale tu dalili yake inapomweka, kwa namna yoyote ile; sawa na apendaye kuwa kipofu. Ilikwishasemwa zamani: Hekima imempotea mumin, popote aipatapo huichukua. Makusudio ya mumin ni kila anayeiamini haki mara inapomdhihirikia bila ya taklifu yoyote wala mashaka.

Mwenyezi Mungu anasema:

وَالْبَلَدُ الطَّيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُ بِإِذْنِ رَبِّهِ وَالَّذِي خَبُثَ لَا يَخْرُجُ إِلَّا نَكِدًا ﴿٥٨﴾

Na mji mzuri hutoa mimea yake kwa idhini ya Mola wake. Na ule ulio mbaya hautoi ila kwa taabu tu. Juz.8 (7:58)

Na lau kama kila nafsi iliyodhulumu inamiliki kila kilichomo ardhini ingelitoa vyote kujikombolea kutokana na adhabu na ukali wake, lakini hakuna fidia yoyote itakayofaa isipokuwa imani na amali njema. Mwenyezi Mungu anasema:

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا تَنفَعُهَا شَفَاعَةٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿١٢٣﴾

“Na ogopeni siku ambayo nafsi haitafaa kitu nafsi nyingine, wala hakitakubaliwa kwake kikomboleo; wala maombezi (shufaa) hayatafaa, wala hawatanusuriwa” (2:123)

Na watakapoiona adhabu wataficha majuto lakini majuto, ya siri au dhahiri, hayafai kitu.

Na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu; nao hawatadhulumiwa.

Aya hii, kama ilivyo, imetangulia katika Aya ya 47 ya Sura hii, Kule imetajwa kuwahadharisha wale wanaokadhibisha. Na hapa imerudiwa kuelezea kuwa hakuna faida ya fidia wala kikomboleo; hata kama ingeliwezekana kufanya hivyo.

Jueni kuwa hakika vyote vilivyomo katika mbingu na ardhi ni vya Mwenyezi Mungu. Anahukumu na kufanya atakavyo wala hapana mwenye kuzuia matakwa yake.

Jueni kuwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni haki katika kuweko siku ya mwisho, thawabu zake, adhabu zake na kila kilichoahidiwa.

Lakini wengi wao hawajui kwamba Kiyama kitakuja, hakina shaka na kwamba Mwenyezi Mungu, atawafufua walio katika makaburi, Wengi wenye imani hii ya ufufuo hawaifanyii kazi. Ikiwa, kwa ujumla, wengi hawajui na wale wachache wajuao hawayatumii wanayoyajua, basi itakuwa wajuzi wanaoufanyia kazi ujuzi wao ni nadra kuliko dhahabu nyekundu.

Yeye ndiye anayefufua na anayefisha na kwake mtarudishwa ili aadhibiwe aliyejua, na asiutumie ujuzi wake, adhabu kubwa na kali kuliko ya yule aliyezembea kutafuta ujuzi. Ni kweli kuwa mzembe anajukumu, laki- ni jukumu la anayejua na asiutumie ujuzi ni kubwa zaidi.

Kuhangaika kutafuta mali kwa ajili ya kulipa deni ni wajib na mwenye kuacha atapata dhambi. Lakini dhambi ya mwenye kuacha na hali anayo mali ya kulipa ni kubwa na kali sana.

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٥٧﴾

57. Enyi watu! Hakika yamewafikia mawaidha kutoka kwa Mola wenu, na ponyo la yale yaliyomo vifuani mwenu na mwongozo na rehema kwa waumini.

قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ ﴿٥٨﴾

58. Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake, basi nawafurahi. Hayo ni bora kuliko yale wanayoyakusanya.

قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ حَرَامًا وَحَلَالًا قُلْ آللَّـهُ أَذِنَ لَكُمْ أَمْ عَلَى اللَّـهِ تَفْتَرُونَ ﴿٥٩﴾

59. Sema: Je, mwaonaje zile riziki alizowateremshia Mwenyezi Mungu, kisha mkafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali? Sema: Je, Mwenyezi Mungu amewaruhusu au mnamzulia Mwenyezi Mungu uwongo?

وَمَا ظَنُّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٦٠﴾

60. Nini dhana ya wale wanaomzulia uwongo Mwenyezi Mungu juu ya siku ya Kiyama? Hakika Mwenyezi Mungu ana fadhila juu ya watu Lakini wengi wao hawashukuru.

YAMEWAJIA MAWAIDHA

Aya 57 – 60

MAANA

Enyi watu! Hakika yamewafikia mawaidha kutoka kwa Mola wenu, na ponyo la yale yaliyomo vifuani mwenu na mwongozo na rehema kwa waumini.

Sifa hizi mawaidha, ponyo, mwongozo, na rehema ni sifa za Qur’ani Tukufu, na lengo la kuzitaja ni kuwajibu washirikina na kila mwenye kukitilia shaka Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kukikataa.

Njia ya majibu hayo ni kwamba Qur’ani inaonya watu kwa mawaidha mazuri, inaponya nyoyo kutokana na hawaa na uchafu, inaogoza watu kwenye lile lililo sawa nayo ni rehma inayomuokoa na mangamizi na adhabu, yule atakayeitumia. Kwa hivyo basi atakayeikataa, atakuwa amekataa misingi hii ambayo ndiyo mihimili ya haki na heri na njia ya uwokovu.

Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake, basi nawafurahi. Hayo ni bora kuliko yale wanayoyakusanya.

Yaani mwenye akili hafurahi kwa mali na starehe za maisha haya ya dunia, isipokuwa anastarehe kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake. Wafasiri wamerefusha maneno sana kuhusu maana ya fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake na wakabainisha tofauti kati ya maneno mawili hayo.

Mfumo wa Aya unafahamisha kuwa makusudio yake hapa ni kuongoza kwenye njia ya heri na kuokoa; sawa na ilivyo fadhila na rehema katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako na rehema yake, lingedhamiria kundi katika wao kukupoteza” Juz.5 (4:113).

Kwa hiyo kauli yake ‘kukupoteza’ inafahamisha kuwa makusudio ya fadhila yake na rehema yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni uwongofu au kuthibitisha kwenye huo uwongofu, kwa sababu ndio kinyume cha upotevu. Mfano mwingine ni Aya isemayo: Kisha mligeuka baada ya haya,“Na lau kuwa si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema Zake, mngelikuwa miongoni mwa wenye kuhasirika.” Juz.1 (2:64)

Sema: Je, mwaonaje zile riziki alizowateremshia Mwenyezi Mungu, kisha mkafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali?

Maana ya Aya hii yako karibu na maana ya Aya iliyo Juz.7 (5:103) ambayo Tafsiri yake imekwishaelezwa.

Maana yanayopatikana ni kwamba Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake kuwaambia washirikina wa Makka ambao walifanya katika wanyama Bahira na Saiba (ngamia aliyezaa mimba kumi na ngamia wa nadhiri), kuwa hebu niambieni.

Ni jambo gani liliwafanya kufanya halali na haramu katika zile riziki alizowapa Mwenyezi Mungu; mpaka mkagawa mafungu haya?

Swali hapo ni la kukanusha; yaani Mwenyezi Mungu hakujalia hivyo kabisa, bali hayo yanatokana na nyinyi wenyewe peke yenu ndio mmeharamisha mliyo yaharamisha.

Sema: Je, Mwenyezi Mungu amewaruhusu au mnamzulia Mwenyezi Mungu uwongo?

Haiwezekani kudai kuwa Mwenyezi Mungu amewaruhusu hivyo, kwa hiyo nyinyi mnamzulia tu.

Nini dhana ya wale wanaomzulia uwongo Mwenyezi Mungu juu ya siku ya Kiyama?

Yaani je, wanafikiria wale wanaojihalalishia na kujiharamishia kuwa Mwenyezi Mungu atawaacha kesho bila ya kuwaadhibu kutokana na uwongo na uzushi wao? Kama ni hivyo basi itakuwa hakuna tofauti kati ya mwenye kumcha Mwenyezi Mungu na mwenye kuasi.

Itakuwaje hivyo na hali Mwenyezi Mungu amesema: “Je, tuwafanye walioamini na kutenda mema kuwa sawa na wafisadi ardhini? Au tuwafanye wenye takua kuwa sawa na waovu?” (38:28). Kusuta huku ni katika ufasaha zaidi wa kushtua na kutoa kiaga.

Hakika Mwenyezi Mungu ana fadhila juu ya watu kwa yale aliyowaneemesha katika akili na sharia inayowaamrisha heri na kuwakataza shari.

Lakini wengi wao hawashukuru.

Yaani hawajui kwa kutumia akili wala kwa hukumu ya sharia.


10

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ وَمَا يَعْزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثْقَالِ ذَرَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَلَا أَصْغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرَ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٦١﴾

61. Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur’ani, wala hamtendi kitendo chochote ila sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nacho. Na hakifichikani kwa Mola wako chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa ila kimokatika kitabu kinachobainisha.

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٢﴾

62. Juweni kuwa mawalii wa Mwenyezi Mungu hawana hofu wala wao hawahuzuniki.

الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ ﴿٦٣﴾

(Hao) ni ambao wameamini na wakawa na takua.

لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ لَا تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿٦٤﴾

64. Wao wana bishara katika maisha ya dunia na katika Akhera. Hakuna mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu, Huko ndiko kufuzu kukubwa.

HUWI KATIKA JAMBO LOLOTE

Aya 61 – 64

MAANA

Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur’ani, wala hamtendi kitendo chochote ila sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nacho.

Msemo katika huwi unaelekezwa kwa Mtume Muhammad(s.a.w. w ) na katika hamtendi unaelekezwa kwa Mtume na uma wake. Maana kwa ujumla ni kuwa hakuna hali yoyote anayokuwa nayo Mtume na uma wake isipokuwa Mwenyezi Mungu anajua.

Na hakifichikani kwa Mola wako chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa ila kimo katika Kitabu kinachobainisha.

Kitab kinachobainisha ni Lawhin Mahfudh. Kwa ufupi Aya inaeleza kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa, Mjuzi, wa kila kitu. Na makusudio ya kujua kwake hapa ni malipo kwenye kauli za watu na vitendo vyao vya heri au vya shari, vikubwa au vidogo.

Juweni kuwa mawalii wa Mwenyezi Mungu hawana hofu wala wao hawahuzuniki.

Imam Ali(a.s ) anasema katika wasifu wake kwa vipenzi (mawalii) wa Mwenyezi Mungu:“Hao ni wale ambao wameiangalia dunia kwa undani wakati watu wameiangalia kwa nje. Wamejishughulisha na wakati ujao wakati watu wamejishughulisha na wakati wa sasa. Wakaua yale wanayohofia kuwauwa – yaani hawa-na wakaacha katika dunia yale ambayo wanajua kuwa yatawaacha.”

Amesema tena: “Hakika bora wa watu kwa Mitume ni yale anayejua zaidi yale waliyokuja nayo; na kwamba mpenzi wa Muhammad ni yule anayemtii Mwenyezi Mungu, hata kama mwili wake utakuwa mbali naye na adui wa Muhammad ni yule mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu hata kama atakuwa karibu naye kiudugu.”

Maana ya yote hayo ni kuwa kuamini bila ya kumcha Mwenyezi Mungu na vitendo hakuna manufaa yoyote. Ndio Mwenyezi Mungu akaashiria kwa kusema:

Hao ni ambao wameamini na wakawa na takua.

Tumeyafafanua zaidi hayo katika Juz, 2 (2:212) na Juz.4 (3:200)

Wao wana bishara katika maisha ya dunia na katika Akhera.

Wao ni wacha Mungu, na bishara yao katika dunia inatoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume kwamba wao wako katika haki ya itikadi yao na matendo yao. Hapana mwenye shaka kwamba nafsi inatulia na kuona raha, ikiwa ina imani na dini yake na matendo yake.

Ama bishara ya wanaomcha Mwenyezi Mungu katika Akhera ni furaha yao kwa neema za Mwenyezi Mungu na fadhila zake.

يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٧١﴾

“Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu na kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa waumini” (3:171)

Hakuna mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake, na anapotaka kitu hakuna wa kupinga matakwa yake.

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ ﴿١٠٧﴾

“Na kama Mwenyezi Mungu akikugusisha dhara hakuna wa kuiondoa isipokuwa yeye tu na kama akikutakia heri, basi hakuna mwenye kuirudisha fadhila zake.” (10:107)

Huko ndiko kufuzu kukubwa, ambako hakuna kufuzu kwengine zaidi yake, Kila kufuzu kunakotokana na natija ya kuamini haki na jihadi katika njia yake, basi huko ni kufuzu kukubwa.

وَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ إِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٦٥﴾

65. Wala isikuhuzunishe kauli yao. Hakika enzi yote ni ya Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye

mwenye kusikia, Mjuzi,

أَلَا إِنَّ لِلَّـهِ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ وَمَا يَتَّبِعُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ شُرَكَاءَ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿٦٦﴾

66. Juweni kuwa ni wa Mwenyezi Mungu wote waliomo mbinguni na waliomo ardhini. Na wale wanaoomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu hawawafuati kuwa ni washirika, hawafuati ila dhana tu, na hawasemi ila uwongo tu.

هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ ﴿٦٧﴾

67. Yeye ndiye aliyewafanyia usiku ili mtulie humo na mchana wa kuonea. Hakika katika haya kuna ishara kwa watu wanaosikia.

قَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا سُبْحَانَهُ هُوَ الْغَنِيُّ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ إِنْ عِندَكُم مِّن سُلْطَانٍ بِهَـٰذَا أَتَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٨﴾

68. Wanasema: Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto! Ametakata na hayo! Yeye ni mkwasi. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Nyinyi hamna dalili kwa haya, Je, mnasema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua?

قُلْ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ ﴿٦٩﴾

69. Sema: Hakika wale ambao wanamzulia Mwenyezi Mungu uwongo hawatafaulu.

مَتَاعٌ فِي الدُّنْيَا ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ الْعَذَابَ الشَّدِيدَ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ ﴿٧٠﴾

70. Ni starehe katika dunia. Kisha marejeo yao ni kwetu, tena tutawaonjesha adhabu kali, kwa sababu walikuwa wakikufuru Mungu.

ENZI YOTE NI YA MWENYEZI MUNGU

Aya 65 – 70

MAANA

Wala isikuhuzunishe kauli yao. Hakika enzi yote ni ya Mwenyezi Mungu.

Enzi hapa ina maana ya nguvu na ushindi.

Walipagawa wakubwa kutokana na mwito wa Mtume Muhammad(s.a.w. w ) kwenye uadilifu na usawa na kuharamisha dhulma na ukandamizaji. Walipagawa na mwito huu kwa sababu ulikuwa ukiingilia enzi yao na utajiri wao. Kwa hiyo wakajaribu kumzuia na kupambana naye.

Mwanzo wa mapambano yao ulikuwa ni uzushi na kueneza uvumi. Wakasema ni mwenda wazimu, lakini hakuna aliyewaamini, wakasema ni mchawi, lakini hali halisi ikawafanya waongo, Ndipo wakadhamiria kumuua, wakawa wanashauriana katika njia ya kummaliza.

Mwenyezi Mungu akamwambia Mtume wake usijali na yale wanayoyasema na wanayoyapanga kuhusu wewe, kwani nguvu na utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu, sio wa jaha wala mali. Yeye ndiye ambaye humtukuza amtakaye na humdhalilisha amtakaye. Na atawaadhibu wale waliokukadhibisha na kukuambia waliyokuambia na hawatapata msaidizi wala mlinzi atakayewakinga na adhabu na ghadhabu za Mwenyezi Mungu.

Yeye ndiye mwenye kusikia uzushi wao juu yako Mjuzi, wa njama wanazozipanga juu yako na yeye anawagonja.

Unaweza kuuliza : kuwa Aya hii imefahamisha kuwa ushindi wote ni wa Mwenyezi Mungu peke yake, Kuna Aya isemayo:

وَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾

“Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye enzi na Mtume wake, na Waumini.” (63:8).

Jibu : Enzi ya Mtume na ya Waumini inatokana na Mwenyezi Mungu; wana nguvu za ushindi kutokana na yeye na kwake wanategemea.

Juweni kuwa ni wa Mwenyezi Mungu wote waliomo mbinguni na waliomo ardhini.

Mwenye kuwa na yote hayo ana uwezo wa kumnusuru Mtume wake na kumpa nguvu mbele za maadui zake. Mwenyezi Mungu amesema: waliomo na wala hakusema vilivyomo, kwa sababu mazungumzo yanawahusu washirikina ambao wamemzulia uwongo Mwenyezi Mungu

Na wale wanaomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu hawawafuati kuwa ni washirika, wa Mungu.

Ukiwa unamfuata mtu kwa kuitakidi kuwa yuko sawa na akawa amepotea, basi utakuwa hufuati usawa bali unafuata upotevu. Hivyo ndivyo ilivyo wanaoabudu masanamu kwa kuitakidi kuwa ni washiriki wa Mwenyezi Mungu. Kwa hakika hasa ilivyo, ni wao hawaabudu washirika wa Mwenyezi Mungu, kwa sababu sio washirika wa Mwenyezi Mungu kiuhakika.

Maana haya yanafafanuliwa na kauli yake Mwenyezi Mungu. Hawafuati ila dhana tu, na hawasemi ila uwongo tu, kauli ya hawasemi ila uwongo tu, inatia nguvu kauli ya hawafuati isipokuwa dhana tu. Umetangulia mfano wa Aya hii na maelezo yake katika Aya 28 ya Sura hii.

Yeye ndiye aliyewafanyia usiku ili mtulie humo na mchana wa kuonea. Hakika katika haya kuna ishara kwa watu wanaosikia.

Mchana ni wa kuona ili tujishughulishe kwa kazi na usiku ni giza ili tupumzike kutokana na mihangaiko ya mchana. Ufafanuzi zaidi wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu.

وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ آيَتَيْنِ فَمَحَوْنَا آيَةَ اللَّيْلِ وَجَعَلْنَا آيَةَ النَّهَارِ مُبْصِرَةً لِّتَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ ﴿١٢﴾

“Na tumeufanya usiku na mchana ni ishara mbili, kisha tukaifuta ishara ya usiku na tukaifanya ishara ya mchana ya kuonea ili mtafute fadhla itokayo kwa Mwenyezi Mungu.” (17:12)

Wanasema: Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto! Ametakata na hayo! Yeye ni mkwasi. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Nyinyi hamna dalili kwa hayo, Je, mnasema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua?

Umetangulia mfano wa Aya hii katika Juz.1 (2:117). Huko tumezungumzia utatu (mungu baba, mungu mwana na roho mtakatifu).

Sema: Hakika wale ambao wanamzulia Mwenyezi Mungu uwongo hawatafaulu katika Akhera ambayo ni bora na yenye kubaki kulinganisha na maisha yetu haya.

Adhabu yao na maangamizi yao yatakuwa makubwa, ikiwa uzushi wao ni katika dhati yake Mwenyezi Mungu na sifa Zake na kumnasibishia washirika mke na mtoto

Ni starehe katika dunia.

Yaani neema waliyonayo washirikina ni starehe duni, hata kama mali yao ni nyingi na wakawa na jaha kubwa, kwa sababu yote hayo ni ya muda mfupi tena yanachanganyika na matatizo. Nayo si lolote yakilinganishwa na neema za Akhera.

Kisha marejeo ni kwetu tena tutawaonjesha adhabu kali, kwa sababu walikuwa wakikufuru Mungu na neema zake na kumkadhibisha Mtume wake.

وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ نُوحٍ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكُم مَّقَامِي وَتَذْكِيرِي بِآيَاتِ اللَّـهِ فَعَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْتُ فَأَجْمِعُوا أَمْرَكُمْ وَشُرَكَاءَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُنْ أَمْرُكُمْ عَلَيْكُمْ غُمَّةً ثُمَّ اقْضُوا إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ ﴿٧١﴾

71. Na wasomee habari za Nuh alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Ikiwa cheo changu na kukumbusha kwangu Ishara za Mwenyezi Mungu kunawachukiza, basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu, nanyi tengenezeni mambo yenu na washirika wenu, tena mambo yenu yasi- fichikane kwenu, kisha mlitekeleze kwangu wala msinipe nafasi.

فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَمَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٧٢﴾

72. Lakini mkikengeuka, basi mimi siwaombi ujira. Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu, Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa waislamu.

فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ فِي الْفُلْكِ وَجَعَلْنَاهُمْ خَلَائِفَ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنذَرِينَ ﴿٧٣﴾

73. Wakamkadhibisha, basi tukamwokoa na waliokuwa naye katika jahazi na tukawafanya ndio waliobakia, Tukawazamisha waliozikadhibisha Ishara zetu. Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walioonywa.

HABARI ZA NUH

Aya 71 – 73

MAANA

Na wasomee habari za Nuh.

Anaambiwa Mtume Muhammad(s.a.w. w ) awasomee washirikina wa Makka.

Alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Ikiwa cheo changu na kukumbusha kwangu Ishara za Mwenyezi Mungu kunawachukiza, basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu, nanyi tengenezeni mambo yenu na washirika wenu, tena mambo yenu yasifichikane kwenu, kisha mlitekeleze kwangu wala msinipe nafasi.

Mtume Muhammad(s.a.w. w ) aliwaonya watu wake katika washirikina wa Makka akawatahadharisha na adhabu kali, lakini wakachukia mawaidha yake na maonyo yake. Bado aliendelea kuwalingania, wakachukizwa na cheo chake na wakajaribu kumuua.

Ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha awasomee habari za Nuh ambaye aliwaonya watu wake, wakachukia maonyo yake na cheo chake, sawa na ilivyo kwake yeye Muhammad na washirikina wa Makka.

Muhtasari habari za Nuh alizowasomea washirikina wa Makka ni kwamba Nuh alishaindana na waliomkadhibisha na akawaambia kuwa mimi ninamtegemea Mwenyezi Mungu na nitawashinda; hata kama nyinyi ni wengi na wenye nguvu, Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameniahidi kunipa ushindi naye havunji ahadi yake. Ama vitisho vyenu kwangu haviwezi kunizuwiya kuendelea na mwito wa Mwenyezi Mungu.

Kwa hiyo lililobaki kwenu ni kupanga njama kwa kadiri mtakavyoweza, muwakusanye wale wasiokuwa Mwenyezi Mungu, uonyesheni uadui mnavyotaka, endeleeni kuniudhi na yafanyeni hayo.

Lakini mkikengeuka, basi mimi siwaombi ujira.

Yaani kama mtapinga mwito wangu, basi mimi sijali upinzani wenu, kwa sababu hakuna manufaa yoyote nitakayoyakosa wala madhara nitakayopata.

Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu sio kwenu nyinyi, kwani hakika mimi ninamfanyia yeye sio nyinyi.

Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa waislamu.

Mimi nimetii na kutekeleza ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa njia zake.

Baada ya hapo nishauri yenu mkisilimu au mkikufuru.

Wakamkadhibisha, basi tukamwokoa na waliokuwa naye katika jahazi na tukawafanya ndio waliobakia, Tukawazamisha waliozikadhibisha Ishara zetu. Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walioonywa.

Hivyo ndivyo unavyokuwa mwisho wa wanaopinga. Wanaangamia na Waumini wanaokoka na kuchukua mahali pa wanaokadhibisha walioangamia. Basi anagalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale walioonywa. Anaambiwa Mtume Muhammad(s.a.w. w ) awaonye washirikina wa Makka yasije yakawapata yaliyowapata watu wa Nuh. Umetangulia mfano wa Aya hii katika Juz. 8 (7:72).

ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا بِهِ مِن قَبْلُ كَذَٰلِكَ نَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْمُعْتَدِينَ ﴿٧٤﴾

74. Kisha baada yake tukatuma Mitume kwa watu wao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo wazi. Lakini hawakuwa ni wenye kuamini waliyokuwa wameyakadhibisha kabla, Hivyo ndivyo tunapopiga muhuri juu ya nyoyo za wapetukao mipaka.

ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ وَهَارُونَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ بِآيَاتِنَا فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ ﴿٧٥﴾

75. Kisha tukapeleka baada ya hao Musa na Harun kwa Firauni na waheshimiwa wake kwa ishara zetu, Wakafanya kiburi nao walikuwa watu wenye makosa.

فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا إِنَّ هَـٰذَا لَسِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٧٦﴾

76. Basi ilipowafikia haki kutoka kwetu walisema: Hakika huu ni uchawi ulio wazi.

قَالَ مُوسَىٰ أَتَقُولُونَ لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَكُمْ أَسِحْرٌ هَـٰذَا وَلَا يُفْلِحُ السَّاحِرُونَ ﴿٧٧﴾

77. Musa akasema: Mnasema juu ya haki ilipowafikia, je huu ni uchawi? na wachawi hawafanikiwi!

قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَلْفِتَنَا عَمَّا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا الْكِبْرِيَاءُ فِي الْأَرْضِ وَمَا نَحْنُ لَكُمَا بِمُؤْمِنِينَ ﴿٧٨﴾

78. Wakasema: Je, umetujia ili utuondoe katika yale tuliyowakuta nayo baba zetu. Ili ukubwa uwe wenu nyinyi wawili katika nchi, na sisi hatuwaamini nyinyi.

وَقَالَ فِرْعَوْنُ ائْتُونِي بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ ﴿٧٩﴾

79. Akasema Firauni: Nileteeni kila mchawi mjuzi.

فَلَمَّا جَاءَ السَّحَرَةُ قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ ﴿٨٠﴾

80. Basi walipokuja wachawi, Musa akawaambia: “Tupeni mnavyotupa

فَلَمَّا أَلْقَوْا قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئْتُم بِهِ السِّحْرُ إِنَّ اللَّـهَ سَيُبْطِلُهُ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُصْلِحُ عَمَلَ الْمُفْسِدِينَ ﴿٨١﴾

81. Walipotupa, Musa akasema: Mlioleta ni uchawi, hakika Mwenyezi Mungu ataubatilisha, Hakika Mwenyezi Mungu hafanikishi vitendo vya wafisadi.

وَيُحِقُّ اللَّـهُ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ ﴿٨٢﴾

82. Na Mwenyezi Mungu anaihakikisha haki kwa maneno yake, ingawa watachukia wenye makosa.

KISHA TUKAWAPELEKEA MITUME BAADA YAKE

Aya 74 – 82

MAANA

Kisha baada yake tukatuma Mitume kwa watu wao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizowazi. Lakini hawakuwa ni wenye kuamini waliyokuwa wameyakadhibisha kabla.

Yaani baada ya Nuh tulipeleka Mitume kwa watu wao, kama Ibrahim, Hud, Swaleh na wenginio, wakiwa na dalili na miujiza, lakini miujiza hii haikuwatoa kwenye ushirikina, kuwageuza kwenye imani ya umoja wa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.

Wao waliyakadhibisha hayo kabla kuwajia Mitume na hoja zilizo wazi, kwa hivyo waliendelea na kukadhibisha kwao huku hata baada ya kuwajia Mitume na kuwaonya.Kwa maneno mengine ni kuwa hawakunufaika na elimu ya Mitume na mwongozo wao.

UONGOFU NA UPOTEVU

Hivyo ndivyo tunapopiga muhuri juu ya nyoyo za wapetukao mipaka.

Unaweza kuuliza : ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyepiga muhuri juu ya nyoyo zao, basi vipi atawaadhibu?

Jibu : Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaka uongofu uwe na njia yake maalum ambayo ni kufuata Mitume yake. Na upotevu nao uwe na njia yake ambayo ni kufuata matamanio. Kwa hiyo mwenye kufuata njia ya Mitume atafikia kwenye uongofu kwa vyovyote vile, na mwenye kufuata matamanio atafikia kwenye upotevu, sawa na alivyojaalia Mwenyezi Mungu kwamba mwenye kujitupa kutoka juu atakufa na mwenye kujitupa baharini akiwa hajui kuogelea atakufa maji tu.

Kwa kufangamanisha njia hizo mbili na matakwa ya Mwenyezi Mungu ndio ikawa Mwenyezi Mungu ndiye aliyepiga muhuri hizo njia mbili, Yamekwisha elezwa maelezo hayo mara nyingi, Kwa ibara mbali mbali.

Kisha tunapeleka baada ya hao Musa na Harun kwa Firauni na waheshimiwa wake kwa Ishara zetu.

Yaani baada ya Mitume waliokuja baada ya Nuh, tulimtuma Musa na Harun na miujiza, kama vile fimbo kugueka nyoka na mkono kuwa mweupe.

Kusema kwake Mwenyezi Mungu‘na tukawapelekea’ inafahamisha wazi kuwa Harun ni Mtume sawa na nduguye Musa. Inasemekana kuwa Harun ni mkubwa wa Musa kwa miaka mitatu.

Wakafanya kiburi kukubali hakinao walikuwa watu wenye makosa.

Kila anayepinga kukubali haki basi ni mwenye makosa.

Basi ilipowafikia haki kutoka kwetu ambayo ni miujiza aliyoidhihirisha Mwenyezi Mungu mikononi mwa Musa(a.s ) ,walisema :

Hakika huu ni uchawi ulio wazi.

Kama hivyo walisema washirikina wa Kiquraish kuhusu Mtume Muhammad(s.a.w. w ) alipowajia na Qur’ani na muujiza wake. Ni muhali kabisa kupona muongozaji na uzushi wa wafisadi.

Na uzushi wenyewe unakwenda na wakati. Hapo mwanzo watu walikuwa wakiamini mchawi, kwa hiyo kiongozi mwema alikuwa akiitwa mchawi, ama leo ambapo hakuna imani ya uchawi wanamwita ni mvurugaji.

Musa akasema: Mnasema juu ya haki ilipowafikia, je huu ni uchawi?

Vipi iwe hivyo haki ina lengo la kuwaongoza watu ambapo uchawi unapotosha hali halisi na kuwapoteza watuna wachawi hawafanikiwi ! Je, anaweza kufanikiwa mwenye kiini macho.

Wakasema: Je, umetujia ili utuondoe katika yale tuliyowakuta nayo baba zetu.

Huu ni mchezo anaoucheza kila mwenye ufisadi ambao una maslahi kwake. Suala ni kuhofia maslahi tu, sio suala la mababa na masanamu. Dalili ya hilo ni kauli yao anayoisimulia Mwenyezi Mungu:Ili ukubwa uwe wenu nyinyi wawili katika nchi.

Hiyo ni kauli ya Firauni na wakuu wake wa nchi kumwambia Musa na ndugu yake Harun. Walikuwa na maana ya kuwa lengo ni kunyang’anywa ufalme wa Misr sio ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Ndipo wakasema:Na sisi hatuwamini nyinyi. Bali tutapigana kulinda manufaa yetu na vyeo vyetu.

Akasema Firauni: Nileteeni kila mchawi mjuzi, naye hajui matekeo ya hayo.

Basi walipokuja wachawi, Musa akawaambia: Tupeni mnavyotupa. Alisema hivi kwa kuwapuuza wao, uchawi wao na Firauni wao, Kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemwaahidi ushindi.

Walipotupa, Musa akasema: Mlioleta ni uchawi, hakika Mwenyezi Mungu ataubatilisha.

Huo wenyewe ni batili tangu mwanzo, lakini Mwenyezi Mungu atadhihirisha ubatilifu wake kwa watu. Ama fimbo ya Musa haipatwi na ubatil- ifu kwa sababu ni haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu.

Hakika Mwenyezi Mungu hafanikishi vitendo vya wafisadi, Na Mwenyezi Mungu anaihakikisha haki kwa maneno yake ambayo ni hoja mkataa. Ingawa watachukia wenye makosa, kwa sababu chuki yao haiwezi kusimamisha matakwa ya Mwenyezi Mungu.

11

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

فَمَا آمَنَ لِمُوسَىٰ إِلَّا ذُرِّيَّةٌ مِّن قَوْمِهِ عَلَىٰ خَوْفٍ مِّن فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِمْ أَن يَفْتِنَهُمْ وَإِنَّ فِرْعَوْنَ لَعَالٍ فِي الْأَرْضِ وَإِنَّهُ لَمِنَ الْمُسْرِفِينَ ﴿٨٣﴾

83. Basi hawakumwamini Musa, isipokuwa baadhi ya vijana katika watu wake, kwa sababu ya kumwogopa Firauni na wakubwa wao asiwatie msuko suko. Na hakika Firauni alikuwa jeuri katika nchi, na kwa hakika alikuwa miongoni mwa waliopita kiasi.

وَقَالَ مُوسَىٰ يَا قَوْمِ إِن كُنتُمْ آمَنتُم بِاللَّـهِ فَعَلَيْهِ تَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّسْلِمِينَ ﴿٨٤﴾

84. Na Musa akasema: Enyi watu wangu! Ikiwa nyinyi mmemwamini Mwenyezi Mungu, basi mtegemeeni yeye, ikiwa nyinyi ni waislamu.

فَقَالُوا عَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْنَا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٨٥﴾

85. Wakasema: Tumemtegemea Mwenyezi Mungu. Ewe Mola wetu! Usitufanye wenye kutiwa misukosuko na watu madhalimu.

وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٨٦﴾

86. Na utuokoe kwa rehema yako na watu makafiri.

وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ وَأَخِيهِ أَن تَبَوَّآ لِقَوْمِكُمَا بِمِصْرَ بُيُوتًا وَاجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ قِبْلَةً وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨٧﴾

87. Na tukampa wahyi Musa na Harun: watengezeeni watu wenu majumba Misr, Na mzifanye nyumba zenu zenye kuelekea upande mmoja, Na simamisheni swala Na wape bishara waumini.

وَقَالَ مُوسَىٰ رَبَّنَا إِنَّكَ آتَيْتَ فِرْعَوْنَ وَمَلَأَهُ زِينَةً وَأَمْوَالًا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا رَبَّنَا لِيُضِلُّوا عَن سَبِيلِكَ رَبَّنَا اطْمِسْ عَلَىٰ أَمْوَالِهِمْ وَاشْدُدْ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُوا حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ ﴿٨٨﴾

88. Na Musa akasema: Mola wetu! Hakika wewe umempa Firauni na wakuu wake mapambo na mali nyingi katika maisha ya dunia. Mola wetu! Hivyo wanawapoteza watu na njia yako. Mola wetu! Ziangamize mali zao, Na zitie shida nyoyo zao, Na hawataamini mpaka waione adhabu yenye kuumiza.

قَالَ قَدْ أُجِيبَت دَّعْوَتُكُمَا فَاسْتَقِيمَا وَلَا تَتَّبِعَانِّ سَبِيلَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٨٩﴾

89. Akasema Mwenyezi Mungu, maombi yenu yamekubaliwa. Basi muwe na msimamo wala msifuate njia ya wale wasiojua.

HAWAKUMUAMINI MUSA

Aya 83 – 89

MAANA

Basi hawakumwamini Musa, isipokuwa baadhi ya vijana katika watu wake, kwa sababu ya kumwogopa Firauni na wakubwa wao asiwatie msuko suko.

Baada ya Musa kutupa fimbo na Mwenyezi Mungu kudhihirisha haki mikononi mwake, waliamini wachawi na watu wengi. Lakini kabla ya tukio la fimbo, walioamini ni vijana tu, katika Waisrael. Kwa sababu vijana walikuwa na wanaendelea kuwa ni wenye hamasa kwa kila jipya.

Lakini walimwamini Musa huku wakimhofia Firauni na pia wakubwa wa Waisrael, wasiwatie msuko suko kwa kuwaadhibu ili waikatae dini yao. Baadhi ya wanaotafuta maslahi katika Mayahudi walikuwa wakila njama na Firauni dhidi ya watu wao; kama ilivyo watu wa dini kila wakati na kila mahali.

Na hakika Firauni alikuwa jeuri katika nchi, na kwa hakika alikuwa miongoni mwa walipita kiasi katika na utaghuti wake. Na Musa akasema: Enyi watu wangu! Ikiwa nyinyi mmemwamini Mwenyezi Mungu, basi mtegemeeni yeye, ikiwa nyinyi ni waislamu.

Musa hakuwa na chochote isipokuwa haki, na Firauni alikuwa na kila kitu, isipokuwa haki. Alikuwa akimkandamiza na kumtesa kila anayemwamini Musa. Musa akawa anawaambia watu wake, mimi sina nguvu wala nyinyi hamna nguvu za kumzuwiya Firauni na dhulma yake, isipokuwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, na vilevile kutegemea ahadi yake kwamba mwisho ni wa wenye kumcha Mwenyezi Mungu, kwa hiyo tegemeeni mambo yenu kwake Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamtii yeye.

Aliwatajia sifa tatu: Imani ambayo ni kusadikisha moyoni. Ya pili ni Uislam ambao makusudio yake hapo ni kufuata na kusalim amri kwa Mwenyezi Mungu, ya tatu ni kumtegemea Mwenyezi Mungu, nako ni kufanya Ikhlasi na kutegemeza mambo yote kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Mwenye kukusanya sifa hizi atakuwa pamoja na Mwenyezi Mungu.

Wakasema: Tumemtegemea Mwenyezi Mungu, na mambo yote tumemwachia yeye. Ndiye anayejua hali yetu na maslahi yetu, na yeye ni mweza juu ya kila jambo.

Ewe Mola wetu! Usitufanye wenye kutiwa misukosuko na watu madhalimu.

Makusudio ya madhalimu hapa ni makafiri ambao ni Firauni na watu wake. Na misukosuko ni adhabu, kwa maana ya kuwa, usitujaalie ni mahali pa adhabu yao.

Na utuokoe kwa rehma yako na watu makafiri.

Makafiri hapa ni hao madhalimu ambao ni Firauni na watu wake ambao waliwakandamiza Waisrael. Makusudio ya kuokoka hapa ni kuokoka na dhulma yao na ukandamizaji wao. Kwa hiyo Aya hii ni tafsir ya Aya iliyo kabla yake.

Na tukampa wahyi Musa na Harun: watengezeeni watu wenu majumba Misr.

Yaani msiondoke hapo Misr na mfanye maskani kwa ajili ya Waisrael watakapokimbilia na kujilinda.

Na mzifanye nyumba zenu zenye kuelekea upande mmoja.

Yaani nyote mkae kwenye mtaa mmoja.

Imesemekana kuwa maana yake ni ‘mzifanye nyumba zenu ni mwahala mwa ibada,’ lakini tafsir ya kwanza ina nguvu kuliko kuwa majumba yawe miskiti kwa sababu majumba sio miskiti, miskiti ni ya ibada na majumba ni ya kukaa.

Na simamisheni Swala, kwa sababu ndiyo mambo ya Ikhlas na inaziku- sanya nyoyo kwenye hisiya ya umoja.

Na wape bishara waumini ya kuokoka na Firauni na wakubwa wake wa nchi katika dunia na kupata Pepo akhera.

Maneno yameelekezwa kwa Musa, kwa sababu yeye ndiye asili ya ujumbe, na kwa Harun kwa sababu yeye ni mfuasi wake.

Na Musa akasema: “Mola wetu! Hakika wewe umempa Firauni na wakuu wake mapambo na mali nyingi katika maisha ya dunia.

Aya hii ilishuka wakati ambao watu hawakuwa wakijua chochote kuhusu yaliyomo katika makaburi ya mafir’aun, Kisha wachimbaji wagunduzi wakagundua mali na vipambo vilivyoelezwa na Qur’ani. Huu ni ushahidi usiokuwa na shaka yeyote kwamba Qur’ani ni wahyi utokao kwa anayejua ghaibu.

Hivyo wanawapoteza watu na njia yako.

Yaani natija ya kuneemeshwa kwao na Mwenyezi Mungu kwa vipambo na mali, ni kumwasi badala ya kumtii.

Mola wetu! Ziangamize mali zao.

Mtu anaweza kudhani kuwa katika dua, Nabii Musa alimtaka Mwenyezi Mungu kuzuwiya utajiri wa wapotevu, ili wasizidi upotevu, lakini lililokatazwa ni ufisadi ambao ameukataza Mwenyezi Mungu. Tumelifafanua hilo katika Juz; 6 (5:66) kifungu cha ‘riziki na ufisadi.’

Na zitie shida nyoyo zao.

Imesemekana kuwa makusudio ni kuzifunga nyoyo zao wabaki katika miji yao ili waone kwa macho maangamizi ya mali zao. Pia ikasemekana ni kuzifunika nyoyo. Lakini tuonavyo sisi ni kuwa makusudio ni shida.

Yaani Musa(a.s ) alimwomba Mwenyezi Mungu kuleta shida katika nyoyo zao.

Tafsiri hii inanasibiana na ombi lake Musa(a.s) la kuangamizwa mali zao.

Na hawataamini mpaka waione adhabu yenye kuumiza.

Jumla hii inaungana na ‘wawapoteze waja wako’. Yaani mwisho wa neema ya Mwenyezi Mungu kwa Firauni ni kuwapoteza watu na kutoamini mpaka waione adhabu, wakati ambao haitafaa imani. Hapana mwenye shaka kwamba Musa(a.s ) hakuomba haya yote ila baada ya kukata tamaa na kuongoka kwao.

Akasema Mwenyezi Mungu : maombi yenu yamekubaliwa.

Yaani mambo ya kuangamizwa mali ya Firauni na wakubwa wake wa nchi na shida na masaibu kwenye nyoyo zao.

Basi muwe na msimamo katika njia hiyo ya jihad ya kuilingania haki.wala msifuate njia ya wale wasiojua ukubwa wa Mwenyezi Mungu na hekima yake.

Imefaa hapa kukatazwa ambaye hafanyi dhambi (maasum); Kwa sababu makatazo yanatoka kwa Mwenyezi Mungu si kwa mwingine. Ni kawaida aliye mkubwa kumwamuru aliye chini yake kwa namna yoyote alivyo.

وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ بَغْيًا وَعَدْوًا حَتَّىٰ إِذَا أَدْرَكَهُ الْغَرَقُ قَالَ آمَنتُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا الَّذِي آمَنَتْ بِهِ بَنُو إِسْرَائِيلَ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٩٠﴾

90. Na tukawavusha bahari wana wa Israel na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui mpaka kulipomfikia kufa maji, akasema: Nimeamini kwamba hakuna Mola isipokuwa yule wanayemuamini wana wa Israel nami ni miongoni mwa waislam (walionyenyekea).

آلْآنَ وَقَدْ عَصَيْتَ قَبْلُ وَكُنتَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ ﴿٩١﴾

91. Je, sasa! Na hali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa wafisadi.

فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ آيَةً وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ عَنْ آيَاتِنَا لَغَافِلُونَ ﴿٩٢﴾

92. Basi leo tutakuokoa kwa mwili wako ili uwe ishara kwa ajili wa nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu.

وَلَقَدْ بَوَّأْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مُبَوَّأَ صِدْقٍ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ فَمَا اخْتَلَفُوا حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْعِلْمُ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿٩٣﴾

93. Nao hawakuhitalifiana mpaka ilipowafikia elimu. Hakika Mola wako atahukumu baina yao siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana.

NA TUKAVUSHA BAHARI WAISRAEL

Aya 90 – 93

MAANA

Na tukawavusha bahari wana wa Israel na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui.

Umetangulia mfano wake katika Juz.1 (2:50) na Juz.9 (7: 136).

MWISHO WA UTWAGHUTI

Mpaka kulipomfikia kufa maji, akasema nimeamini kwamba hakuna Mola isipokuwa yule wanayemuamini wana wa Israel nami ni miongoni mwa waislam (walionyenyekea).

Jana alikuwa Firauni akisema: Mimi ndiye Mola wenu mkubwa ,na leo anakana, Hali zote mbili hazimfai, si ile ya kwanza wala hii ya sasa. Mlango wa twaa ulipokuwa wazi yeye aliasi, na sasa hakuna nafasi tena ya utiifu wala uasi.

Hivi ndivyo alivyo mtu duni, hujifanya mkubwa wakati wa neema na kujifanya mdogo wakati wa dhiki. Historia huwa inajirudia; yaani desturi ya Mwenyezi Mungu katika viumbe vyake ambayo ameisharia kwa kusisitiza pale aliposema:

فَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّـهِ تَبْدِيلًا وَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّـهِ تَحْوِيلًا ﴿٤٣﴾

“Basi hutapata mabadiliko katika desturi ya Mwenyezi Mungu, wala huta pata mageuko katika desturi ya Mwenyezi Mungu” (35:43)

Israil ya leo, inayokwenda kwa msaada wa ukoloni, inakwenda sawa na desturi ya Firauni hasa.

Firauni alikuwa akiwachinja watoto wa kiume wa Israel na kuwacha watoto wa kike. Leo Israel inafanya hivyo hivyo kwa wapalestina tena zaidi kuliko Firauni.

Firauni alisema:

قَالَ يَا قَوْمِ أَلَيْسَ لِي مُلْكُ مِصْرَ وَهَـٰذِهِ الْأَنْهَارُ تَجْرِي مِن تَحْتِي ﴿٥١﴾

“Enyi watu wangu, je, ufalme wa Misr si ni wangu na hii mito ipitayo chini yangu?” (43:51).

Israel nayo inasema: Je, Palestina si ni yetu pamoja na mali zake zote, ikiwa ni pamoja na milima ya Golan na ukanda wa Gaza. Firauni alisema:

فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٤﴾

“Mimi ndiye Mola wenu mkuu.” (79:24).

Israel na wanaowasaidia wanasema hatuwezi kushindwa sisi

Hazikupita siku nyingi ila ilianza kudhihiri desturi ya Mwenyezi Mungu. Ambapo Elat iliangamia na kuharibiwa vituo vya mabomu na wanaojitoa mhanga, kumemlazimisha Dayan kusema: “Ni lazima Mayahudi wajiandae kupanua uwanja wa makaburi yao.”

Na atasema tu, kama sio leo ni kesho: Nimemwamini yule anayeaminiwa na Waarabu na Waislam; sawa na alivyosema Firauni. Kwa sababu yeye anafuata nyayo zake, basi mwisho wake utakuwa sawa na Firauni tu. Mtu anaweza kusema kuwa vita vya Israael vimekuwa virefu na vyenye kuumiza

Tunaweza kujibu kuwa ni kweli, lakini ushindi wa mwisho ni wa wenye haki, hata kama muda utarefuka kwa kiasi gani. Historia ya zamani na ya karibuni ni shahidi wa hakika hii, kuanzia kwa Firauni na Hamana hadi kwa Hitler na Mussolini.

Je, sasa!

Baada ya kukupata yaliyokupata ndio unasema nimeamini?

Na hali uliasi kabla yake ulipokuwa na hiyari ya kutubia na kurudi kwenye haki, lakini ukafanya dhulmana ukawa miongoni mwa wafisadi.

Kwa hiyo onja malipo ya amali yako kwa kufa maji, na kuangamia.

Basi leo tutakuokoa kwa mwili wako sio kwa roho yako; na mwili wako na tutautupa nchi kavu ili auone yule aliyekuwa akikutukuza.

Ili uwe ishara kwa ajili wa nyuma yako apate mawaidha yule atakayeiweka nafsi yake kwenye ufisadi. Lakini wapi! Ibra ni nyingi lakini mazingatio ni machache, ndio Mwenyezi Mungu akasema:

Na hakika watu wengi wameghafilika na ishara zetu, Nao hawakuhitalifiana mpaka ilipowafikia elimu.

Yaani baada ya kuangamia Firauni, tuliwapa makazi mazuri na ardhi yenye rutuba.

Wafasiri wametofautiana kuhusu mji waliokuwa, wengine wamesema ni Palestina na wengine wakasema ni Misr. Kauli ya Misr ndiyo yenye nguvu kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu. “Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem, na mahazina na mahali pazuri. Kama hivyo, na tukawarithisha hayo wana wa Israel.” (26: 57-59).

Aya hii inaonyesha wazi kuwa Mwenyezi Mungu aliwakalisha wana wa Israel nyumba ya Firauni na wakubwa wake.

Nao hawakuhitalifiana mpaka ilipowafikia elimu.

Makusudio ya elimu hapa nia Tawrat, kama ilivyo teremshwa kwa Musa(a.s ) . Ndani yake mlikuwa na habari ya Mtume Muhammad(s.a.w. w ) . Wana wa Israel walikuwa wamoja katika ukafiri na upotevu wao, kabla ya kuteremshwa Tawrat.

Baada ya kuwajia Tawrat wakatofautiana wakati wa Musa na baadae, wengine waliasi zaidi, wakaabudu ndama na wakamwambia Musa tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi, na nenda wewe na Mola wako na mengineyo yaliyosajiliwa na Qur’ani.

Hakika Mola wako atahukumu baina yao siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana.

Ambapo siku hiyo hakutakuwa na uwongo wala riya au kitu chochote, isipokuwa haki itakayowadhihrikia wote wazi wazi.

فَإِن كُنتَ فِي شَكٍّ مِّمَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ فَاسْأَلِ الَّذِينَ يَقْرَءُونَ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكَ لَقَدْ جَاءَكَ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿٩٤﴾

94. Ukiwa na shaka juu ya tuliyokuteremshia, basi waulize wale wasomao Kitabu kabla yako. Haki imekwishafikia kutoka kwa Mola wako, kwa hivyo kabisa usiwe miongoni mwa wafanyao shaka.

وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ فَتَكُونَ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٩٥﴾

95. Na kabisa usiwe miongoni mwa wanaokadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, usije ukawa miongoni mwa wenye hasara.

إِنَّ الَّذِينَ حَقَّتْ عَلَيْهِمْ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٩٦﴾

96. Hakika wale ambao neno la Mola wako limekwishawathibitikia hawataamini.

وَلَوْ جَاءَتْهُمْ كُلُّ آيَةٍ حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ ﴿٩٧﴾

97. Ijapokuwa itawajia Ishara, mpaka waione adhabu iumizayo.

IKIWA UNA SHAKA

Aya 94 –97

MAANA

Ukiwa na shaka juu ya tuliyokuteremshia, basi waulize wale wasomao kitabu kabla yako.

Makusudioya wale wasomao Kitabu ni maulama wa Injil na Tawrat na kinachoulizwa ni kisa cha Musa na Mitume wengine kulingana na Qur’ani. Hiyo ni kwa kuangalia mfumo wa maneno.

Kwa sababu Aya zilishuka kuhusu kisa cha Musa na Firauni.

Unaweza kuuliza : kuna wajihi gani katika kauli yake Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake.“Ukiwa na Shaka” pamoja na kujua kuwa Mtume hana shaka katika hilo, vipi iwe hivyo na hali yeye amevumilia adha nyingi katika kufikisha ujumbe wake kiasi ambacho hakuwahi kuna nacho Mtume mwingine au kiongozi yoyote.

Jibu : wajihi ni kumwambia Mtume Muhammad(s.a.w. w ) yule anayetia shaka yale yaliyotajwa na Qur’ani kuhusu kisa cha Musa na Mitume wengine, aulize Ulamaa wa watu wa Kitab wasio na upendeleo. Kwani hilo ni lenye kuthibiti katika Tawrat na Injil kama ilivyoeloezwa katika Qur’ani.

Haki imekwishafikia kutoka kwa Mola wako, kwa hivyo kabisa usiwe miongoni mwa wafanyao shaka, Na kabisa usiwe miongoni mwa wanaokadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, usije ukawa miongoni mwa wenye hasara.

Yaani fikisha ujumbe ewe Muhammad kwa yule mwenye kutia shaka au kuikanusha haki iliyoteremshwa kwako, basi yeye ni miongoni mwa wenye kuadhibiwa siku ya Kiyama, hali ya kupata hasara.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameyatolea ibara makatazo haya kwa kumkataza Mtume kutokana na shaka na uongo, ili Mtume Muhammad(s.a.w. w ) aseme kwa watu: Mimi ni mtu mfano wenu na ni mmoja miongoni mwenu, kama nitatia shaka au kukanusha, basi nitahisabiwa na nitaadhibiwa; kama vile mtu yeyote yule atakayetia shaka au kukadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu.

Mfumo huu ni fasaha na wenye kufaulu zaidi katika kuilingania haki ambayo mbele yake inakuwa sawa kwa watu wote

Hakika wale ambao neno la Mola wako limekwishawathibitikia hawataamini, Ijapokuwa itawajia Ishara, mpaka waione adhabu iumizayo.

Makusudio ya neno la Mola wako hapa ni adhabu; yaani hakika wale ambao Mwenyezi Mungu atawaadhibu ni wale wasioiamini haki kwa hali yoyote hata kama ataletewa hoja elfu; isipokuwa kama ataiona adhabu. Na ilivyo ni kwamba imani ya namna hii haifai kitu kwa sababu ni sawa na imani ya Firauni wakati alipoangamia majini; kama iliyoelezwa hivi punde katika kufasiri Aya 90 ya Sura hii.


12

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

فَلَوْلَا كَانَتْ قَرْيَةٌ آمَنَتْ فَنَفَعَهَا إِيمَانُهَا إِلَّا قَوْمَ يُونُسَ لَمَّا آمَنُوا كَشَفْنَا عَنْهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٩٨﴾

98. Kwanini usiweko mji ulioamini na imani yake ikawafaa, isipokuwa kaumu ya Yunus? Walipoamini tuliwaondolea adhabu ya hizaya katika maisha ya dunia na tukawastarehesha kwa muda.

وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَآمَنَ مَن فِي الْأَرْضِ كُلُّهُمْ جَمِيعًا أَفَأَنتَ تُكْرِهُ النَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٩٩﴾

99. Lau angelitaka Mola wako, wangeliamini wote waliomo ardhini, Basi je wewe utawalazimisha watu wawe Waumini?

وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تُؤْمِنَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ وَيَجْعَلُ الرِّجْسَ عَلَى يَعْقِلُونَ الَّذِينَ لَا ﴿١٠٠﴾

100. Na hakuna nafsi inayoweza kuamini isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na hujaalia uchafu kwa wale ambao hawatumii akili.

KAUMU YA YUNUS

Aya 98-100

KISA

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemtaja Yunus kuwa ni katika Mitume na katika watu wema. Vile vile amemwita kwa jina sahiba wa samaki, Pia akamwita mwenye kughadhibika. Kwa sababu aliwalingania watu wake kwenye imani, lakini hawakumwitikia ndipo akawaombea maangamizo na akawaondokea kwa kukata tamaa na imani yao.

Katika Sura Al-Qalam Mwenyezi Mungu amemwamrisha Mtume wake Muhammad(s.a.w. w ) , avumilie na asifanye haraka ya kuwaombea adhabu watu wake, kama alivyofanya Yunus.

فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ الْحُوتِ إِذْ نَادَىٰ وَهُوَ مَكْظُومٌ ﴿٤٨﴾

“Basi subiri hukumu ya Mola wako, wala usiwe kama sahiba wa samaki, aliponadi na hali amezongwa.” (68:48).

Watu wa Yunus walikuwa kiasi cha laki moja (100,000). Mwenyezi Mungu anasema:

وَأَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ مِائَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ ﴿١٤٧﴾

“Na tulimtua kwa watu elfu mia moja au zaidi.” (37:147).

Wapokezi na wafasiri wanasema kuwa watu wa Yunus walikuwa wakikaa katika ardhi ya Mousel, na kwamba wao walikuwa wakiabudu masanamu. Nabii Yunus(a.s ) akawakataza kufru hiyo na kuwaamrisha Tawhid, lakini wakang’ang’ania ushirikina wao; kama ilivyokuwa kwa watu wa Mitume wengine.

Baada ya kuondoka Yunus zikaanza dalili za adhabu kutoka mbinguni, basi wakaanza kutubia kwa Mwenyezi Mungu na wakamuomba kwa ikhlasi kuwa awaondolee adhabu, Akafanya hivyo Mwenyezi Mungu akawabakisha mpaka muda wao. Hayo ndiyo maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Kwanini usiweko mji ulioamini na imani yake ikawafaa, isipokuwa kaumu ya Yunus? Walipoamini tuliwaondolea adhabu ya hizaya katika maisha ya dunia na tukawastarehesha kwa muda.

Wafasiri wanasema kuwa watu wa Yunus walivaa magwanda wakatoka jangwani wakiwa pamoja na wanawake, watoto na wanyama, wakatenganishasha baina ya kila mama na mwanawe awe mtu au mnyama. Wakatoa sauti wote, zikapanda sauti zao na ikachanganyika sauti ya watu wanyama, Basi Mwenyezi Mungu akawaondolea adhabu wakarudi majumbani mwao salama salmini.

Ama Yunus alisafiri akafika ufuo wa bahari akakuta kundi la watu kwenye jahazi, Akawaomba ajiunge nao wakakubali. Walipofikia katikati ya bahari, Mwenyezi Mungu aliwapelekea samaki mkubwa akazuia jahazi yao, wakajua kuwa anataka mmoja wao. Wakaafikiana kupiga kura ambayo ilimwangukia Yunus.

Kwa hiyo wakamtupa Yunus au alijitupa yeye mwenyewe baharini na akamezwa na samaki; kama ilivyoelezwa katika Qur’ani:

وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٩﴾ إِذْ أَبَقَ إِلَى الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ ﴿١٤٠﴾ فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ الْمُدْحَضِينَ ﴿١٤١﴾ فَالْتَقَمَهُ الْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ ﴿١٤٢﴾

“Na hakika Yunus ni miongoni mwa Mitume, Alipokimbia katika jahazi iliyosheheni, Akaingia katika kupigiwa kura na akawa katika walioshindwa, Samaki akammeza hali ya kuwa mwenye kulaumiwa” Yaani mwenye kujilaumu (37: 139-142).

Mwenyezi Mungu akampa ilham samaki kumuhifadhi tumboni[7] mwake bila ya kumpa udhia wowote, Yunus akakimbilia kwa Mola wake na kumwomba akiwa tumboni mwa samaki, kama inavyoashiria Qur’ani.

فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾

“Basi akaita katika giza kwamba hakuna Mola isipokuwa wewe tu, umetakasika, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu,” yaani mwenye kujidhulumu. (21:87)

Kisha samaki akamtema ufukweni baada ya kukaa tumboni kiasi alichota- ka Mwenyezi Mungu, Wafasiri wanasema Yunus alitoka tumboni kama kifaranga kisicho na manyoya, na Mwenyezi Mungu alimwoteshea mmea wa mung’unya kujifunika nao. Katika hilo Mwenyezi Mungu anasema:

فَلَوْلَا أَنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُسَبِّحِينَ ﴿١٤٣﴾ لَلَبِثَ فِي بَطْنِهِ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤٤﴾ فَنَبَذْنَاهُ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ سَقِيمٌ ﴿١٤٥﴾ وَأَنبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِّن يَقْطِينٍ ﴿١٤٦﴾

“Lau angelikuwa si katika wanaomtakasa Mwenyezi Mungu angelikaa tumboni mpaka siku ya kufufuliwa, Lakini tulimtupa ufukweni patupu hali ya kuwa mgonjwa, na tukamwoteshea mmea wa mung’unya’ (37: 143- 146).

Baada ya hapo Yunus, alirudi kwa watu wake wakafurahi sana kwa kufika kwake naye akafurahi kwa imani yao.

Lau angelitaka Mola wako, wangeliamini wote waliomo ardhini.

Yaani lau angelitaka Mwenyezi Mungu kuwalazimisha watu imani au kuwaumba tangu mwanzo, wakiwa Waumini, basi duniani kusingelipatikana kafiri hata mmoja. Na angelifanya hivyo, basi kusingekuwa na thawabu wala adhabu na vitendo vya watu vingelikuwa kama matunda tu ya mti. Umetangulia mfano wa Aya hii katika Juz,7 (6:35), Na tumefafanua zaidi katika Juz. 3 (2:253)

Basi je wewe utawalazimisha watu wawe Waumini?

Yaani hekima ya Mwenyezi Mungu imetaka kwamba hiyari ya kufuata haki au kuipima, iwe mikono mwa watu, ili aweze kupambanuka mwovu na mwema, Na hakuna yeyote anayeweza kupinga matakwa ya Mwenyezi Mungu. Basi kwanini unahuzunika na kusikitika kutokana na ukafiri wao na kukosa kwao imani? Makusudio ni kuwa tahfifu hii anafanyiwa Mtume Mtukufu(s.a.w. w ) .

Maana haya yamekarika kwenye Aya nyingi, Miongoni mwazo ni:

وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِجَبَّارٍ ﴿٤٥﴾

“Wala wewe si mwenye kuwatawalia” (50:45)

Na hakuna nafsi inayoweza kuamini isipokuwa kwa idhi ya Mwenyezi Mungu.

Yaani kila hali ya mtu ina sababu, ikiwemo imani na njia ya kuangalia ishara za Mwenyezi Mungu kwa mtazamo safi. Mwenye kuzijua kwa uhakika wake na kwa njia zake, kwa vyovyote ataishia kwenye kuamini hukumu za Mwenyezi Mungu na anavyotaka.

Hapa ndio anakuwa Mwenyezi Mungu ametaka kuamini kwake, kwa sababu yeye ndiye aliyejaalia kuzingatiwa Ishara zake ndio sababu ya kuamini yeye.

Vilevile mwenye kuzipinga, kwa vyovyote ataishia kwenye ukafiri kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu, Kwa sababu yeye ndiye aliyejaalia kuzipinga Aya ndio sababu ya ukafiri, Lakini amejaalia hiyari mikononi mwa mtu mwenyewe katika kufuata mojawapo ya njia mbili.

Katika maana ya Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu.

قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا ﴿٩﴾ وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا ﴿١٠﴾

“Hakika amefaulu mwenye kuitakasa na amepata hasara mwenye kuitweza” (91:9-10)

Yaani kwa vyovyote kufaulu kunathibiti kwa mwenye kuisafisha nafsi yake kutokana na hawa na matamanio. Na kufeli kwa vyovyote ni kwa mwenye kuichafua nafsi yake kwa dhambi.

Na hujaalia uchafu kwa wale ambao hawatumii akili.

Makusudio ya uchafu hapa ni ukafiri kwa mkabala wa imani ambayo ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Maana ni kuwa kupinga Aya za Mwenyezi Mungu na kuacha kuzizingatia, lazima, kunapelekea ukafiri; kama ambavyo kuzinzingatia kunapelekea imani.

Hapo inatubainikia kuwa makusudio ya idhini ya Mwenyezi Mungu kwenye imani ni utambuzi wa dalili na hoja alizoziweka, ikiwa utambuzi wenywee ni msafi usiokuwa na misukumo ya malengo ya maslahi na matamanio ya nafsi.

قُلِ انظُرُوا مَاذَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا تُغْنِي الْآيَاتُ وَالنُّذُرُ عَن قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠١﴾

101. Sema, tazameni ni yapi yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini! Na dalili na maonyo hayawafai watu wasioamini.

فَهَلْ يَنتَظِرُونَ إِلَّا مِثْلَ أَيَّامِ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِهِمْ قُلْ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ ﴿١٠٢﴾

102. Basi hawangojei isipokuwa siku za watu waliopita kabla yao. Sema, basi ngojeni, mimi pia ni pamoja nanyi katika wenye kungojea.

ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيْنَا نُنجِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠٣﴾

103. Kisha tunawaokoa Mitume wetu na wale walioamini, ndio kama hivyo inatustahiki kuwaokoa Waumini.

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِن كُنتُمْ فِي شَكٍّ مِّن دِينِي فَلَا أَعْبُدُ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِنْ أَعْبُدُ اللَّـهَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُمْ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠٤﴾

104. Sema, Enyi watu! Ikiwa mnayo shaka katika dini yangu, basi mimi siwaabudu wale mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, lakini ninamwabudu ambaye anawafisha, na nimeamrishwa niwe miongoni mwa wenye kuamini.

وَأَنْ أَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٥﴾

105. Na kwamba elekeza uso wako kwenye dini safi, wala usiwe miongoni mwa washirikina.

وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠٦﴾

106. Wala usiwaombe wasiokuwa Mwenyezi Mungu ambao hawakunufaishi wala kukudhuru; kama ulifanya basi wewe utakuwa miongoni mwa madhalimu.

ISHARA NA MAONYO HAYATOSHI

Aya 101 – 106

MAANA

Sema, Angalieni yaliyomo mbinguni na ardhini.

Kwa mnasaba wa kutaja imani katika Aya iliyotangulia, hapa Mwenyezi Mungu anaamrisha kuangalia ulimwengu na maajabu yake. Kwa sababu hiyo ndiyo njia ya kumjua Mwenyezi Mungu na kumwamini, Zimekwishatangulia Aya nyingi zenye mfano huu.

Na ishara zote na maonyo hayawafai watu wasioamini.

Kila dalili ya haki huwa inamuonya kwa adhabu anayeihalifu, na kila Mtume atokaye kwa Mwenyezi Mungu huwa na dalili ya ujumbe wake. Lakini dalili na Mitume haifai kitu isipokuwa kwa yule ambaye haki kwake ni kitu kilichompotea, anaichukua popote atakapoipata, hata kama ni kwa kupoteza maisha.

Ama yule ambaye haangalii katika dini, haki na utu, isipokuwa maslahi yake na manufaa yake tu, basi huyo ni adui wa dalili, hoja Mitume na hata viongozi wema.

Basi je, hawangojei isipokuwa mfano wa siku za watu waliopita kabla yao?

Siku za watu ni siku za utawala wao au siku za misukosuko yao. Na waliopita kabla yao hapa ni watu wa Nuh, A’d na Thamud na wanaongojea ni wale waliomkadhibisha Muhammad(s.a.w. w ) kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Sema, basi ngojeni, mimi pia ni pamoja nanyi katika wenye kungojea. Kisha tunawaokoa Mitume wetu na wale walioamini.

Jumla hii inaungan na jumla iliyokadiriwa, kuwa imepita desturi ya Mwenyezi Mungu kuwapeleka Mitume kwa watu kuwapa bishara na kuwaonya. Baadhi wanawaamini na wengine wanawakidhibisha. Huangamizwa wanaopinga kisha wanaokoka Mitume na waliowaamini. Mwenye Tafsir Al-Manar anasema hii ni miongoni mwa muujiza wa ufasaha wa Qur’ani. Muujiza wenyewe ni kutajwa jumla moja inayofahamisha jumla kadhaa ambazo hazikutajwa.

Ndio kama hivyo inatustahiki kuwaokoa waumini.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kusema kuwa yeye anaokoa waumini, hapa anasema huko kuokolewa ni haki yao. Na kwamba ni juu ya Mwenyezi Mungu kuwapatia haki yao hiyo. Hili ni jibu wazi la wale waliosema kuwa Mwenyezi Mungu ni haki yake kumwadhibu mtiifu na kumpa thawabu muasi, kama ilivyosemwaa katika kitabu Al-Mawaqif Juz 8.

Sema, Enyi watu! Ikiwa mnayo shaka katika dini yangu, basi mimi siwaabudu wale mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, bali ninamwabudu Mwenyezi Mungu ambaye anawafisha nyinyi na nimeamrishwa niwe miongoni mwa wenye kuamini.

Mtume Muhammad(s.a.w. w ) amekwishaitekeleza amana ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake, akawafikishia ujumbe wa Mola wao.Wakamwitikia waliomwitikia na wakakataa waliokataa.Mwenyezi Mungu amemwamrisha awambie wale waliong’ang’ania ushirikina, kwamba kama mnashaka na dini yangu, basi mimi siabudu masanamu yasiyokuwa na akili, kama mnayoyafanya, isipokuwa ninamwabudu Mola mwenye uweza, mwadilifu, mwenye hekima na Mjuzi, Na yeye ndiye anayezichukua roho zenu. Basi ni nani anayefaa kutiliwa shaka?

Huu ni miongoni mwa mifumo ya kulingania kwa hekima na mawaidha mazuri.

Na kwamba elekeza uso wako kwenye dini ya kweli wala usiwe miongoni mwa washirikina.

Makusudio ya uso hapa nia nafsi. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu ameniamrisha kumwelekea yeye nikiwa mwislam kwa kufuata nyayo za Mitume wengine kwa kauli na vitendo.

Wala usiwaombe wasiokuwa Mwenyezi Mungu ambao hawakunufaishi wala kukudhuru, kama ukifanya basi hapo utakuwa miongoni mwa madhalimu.

Ni muhali kwa Mtume kumwomba mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Isipokuwa makusudio hapa ni kumpa habari anayeomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kuwa yeye ni miongoni mwa waliopata hasara.

Ilivyo ni kuwa Aya hizi tatu za mwisho zina maana moja kwa ibara tofauti. Nayo ni kuamrisha imani na kukataza ushirikina. Aya ya kwanza imeamrisha imani na kuashiria kuwa dini ya Tawhid haifai kuitilia shaka na kwamba dini yenye wasiwasi na shaka ni ile ya ushirikina na kuabudu sanamu.

Aya ya pili imeamrisha imani pamoja na kuashiria kuwa Uislam ndiyo dini isiyokuwa kombo kombo, kinyume na dini nyingine. Na Aya ya tatu ikamrisha imani na kutoa ishara kuwa ambaye atafuata dini nyingine isiyokuwa Uislam, basi ni katika madhalim waliojidhulumu wenyewe.

Ni desturi ya Qur’ani kukariri na kulisisitiza kila linaloambatana na itikadi na misingi yake.

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ يُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿١٠٧﴾

107. Na Mwenyezi Mungu akikugusisha dhara basi hakuna wa kuiondoa isipokuwa yeye. Na kama akikutakia kheri, basi hakuna wa kurudisha fadhila yake. Huifikisha kwa amtakaye katika waja wake, Naye ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ ﴿١٠٨﴾

108. Sema, Enyi watu! Haki imekwishawafikia kutoka kwa Mola wenu. Basi anayeongoka hakika anaongoka kwa faida ya nafsi yake tu, na anayepotea anapotea kwa hasara ya nafsi yake tu. Na mimi si mwakilishi juu yenu.

وَاتَّبِعْ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَاصْبِرْ حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللَّـهُ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ ﴿١٠٩﴾

109. Na ufuate yale unayopewa wahyi, na vumilia mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu, na yeye ndiye Mbora wa mahakimu.

KAMA MWENYEZI MUNGU AKIKUGUSISHA DHARA

Aya 107 – 109

MAANA

Na Mwenyezi Mungu akikugusisha dhara basi hakuna wa kuiondoa isipokuwa yeye.

Mtu anaweza kupata madhara kutokana na yeye mwenyewe; kama vile mtu kujidharau au kuacha kufanya kazi na uwezo anao au kufanya kazi bila ya maandalizi. Madhara ya aina hii hayafai kuyanasibisha kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu yeye Mwenyezi Mungu ameamrisha kufanya maandalizi kwa kazi yoyote na amekataza aina zote za madhara.

Mara nyingine Mtu anapata madhara kwa sababu ya ufisadi wa jamii anayoishi. Madhara haya vilevile hayafai kuyanasibisha kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amekataza ufisadi na ameamrisha utengeneo.

Au anaweza kudhurika sio kutoka na yeye mwenyewe wala jamii; kama kuzaliwa na upungufu wa maumbile au akili pungufu, kiasi cha kushindwa kujua mambo ya elimu. Au kupigwa na radi n.k. Aina hii ya madhara ndiyo iliyokusudiwa katika Aya, ingawaje aina zote za madhara Mwenyezi Mungu anaweza kuziondoa. Kwa sababu yeye ni Mjuzi, wa kila kitu.

Na kama akikutakia kheri, basi hakuna wa kurudisha fadhila yake. Huifikisha kwa amtakaye katika waja wake.

Tumetangulia kueleza kuwa haifai kunasibisha madhara kwa Mwenyezi Mungu na Mtume moja kwa moja. Ama heri inafaa kuinasibisha kwa Mwenyezi Mungu, ni sawa iwe imetokana na athari ya matendo ya binadamu.

Kwa sababu yeye Mwenyezi Mungu anataka heri na anaiamrisha. Na yeye ndiye mwenye uweza zaidi kwa mtu.

Naye ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.

Na rehema zake zimeenea kila kitu, kama ilivyo elimu yake na uwezo wake.

Sema: Enyi watu! Haki imekwishawafikia kutoka kwa Mola wenu. Basi anayeongoka hakika anaongoka kwa faida ya nafsi yake tu, na anayepotea anapotea kwa hasara ya nafsi yake tu. Na mimi si mwakilishi juu yenu.

Muhtasari wa maana ya Aya hii uko katika Aya isemayo: “Kila mtu ni rehani ya alichokikimu.” (52:21) Pia umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:104)

Na ufuate yale unayopewa wahyi, na vumilia mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu, na yeye ndiye Mbora wa mahakimu.

Aya hii inaelezea wadhifa wa Mtume katika kufikisha wahyi, kuufanyia kazi na kuvumilia maudhi atakayoyapata katika kazi hiyo mpaka Mwenyezi Mungu aidhihirishe dini yake na neno lake liwe juu. Na haya ni muhimu kwa kila atakayekuwa naibu wa maasum katika kufikisha hukumu za Mwenyezi Mungu na kuzieneza.

MWISHO WA SURA YA KUMI


13

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA

Sura Ya Kumi na Moja: Surat Hud

Imeshuka Makka, baada ya Sura Yunus ina Aya 123.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu.

الر كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ ﴿١﴾

1. Alif laam raa, Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimepangwa kiuhakika, kisha zikafafan uliwa kutoka kwa mwenye hekima mwenye habari.

أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ إِنَّنِي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ ﴿٢﴾

2. Kwamba msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu, Hakika mimi kwenu ni muonyaji mbashiri ninayetoka kwake.

وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَاعًا حَسَنًا إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَهُ وَإِن تَوَلَّوْا فَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ كَبِيرٍ ﴿٣﴾

3. Na kwamba mumtake maghufira Mola wenu kisha mtubie kwake, Atawastarehesha starehe nzuri mpaka muda uliotajwa na atampa kila mwenye fadhila fadhila yake. Na ikiwa mtakengeuka basi mimi nawahofia adhabu ya siku kubwa.

إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٤﴾

4. Marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu, naye ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.

KITABU NA AYA ZAKE

Aya 1 – 4

MAANA

Alif Laam Raa.

Meelezo yake ni kama ya mwanzo wa Sura Baqara, Juz.1 (2:1) Mwenye kutaka arudie huko.

Hiki ni kitabu ambacho Aya zake zimepangwa kiuhakika, kisha zikafafanuliwa kutoka kwa mwenye hekima mwenye habari.

Makusudio ya Kitab hapa ni Qur’ani. Maana ni kuwa hii Qur’ani maana yake yako wazi na imepangwa vizuri, Haina upungufu wala makosa. Kwa sababu inatokana na mpangaji wa mambo anayoyaweka kwa misingi ya elimu na hekima.

Baadhi ya wajuzi wanasema kuwa Mwenyezi Mungu ana vitabu viwili, Kitabu cha kiulimwengu ambacho ndio huu ulimwengu na kitabu cha kurasa ambacho ni hii Qur’ani. Kila kimoja kwa upande wake, kimepang- wa vizuri na kwa ukamilifu.

Wanazuoni wa dini mbali mbali wamezungumzia utukufu na umuhimu wa Qur’ani. Nimenukuu baadhi ya kauli zao katika kitabu changu Al-Islam Wal-Aql (uislam na akili) sehemu ya Utume.

Wakati nikifasiri Aya hii, imetokea sadfa ya kusoma makala inayohusiana na Kitabu kinachoitwa Muhammad cha mtaalam wa kifaransa anayeitwa Marksem Roudinseim. Iliyotolewa na gazeti la Al-Misriya la tarehe, 22, Desemba 1968.

Katika hiyo makala anasisitiza kuwa Qur’ani imewanukulia vizazi vinavyokuja kuhusu binadamu aliyekandamizwa jinsi alivyo jikakamua kutoka katika dhulma na ukandamizaji. Nayo imevipa silaha yenye nguvu ya kupambana na madhalim na wanafiki, Anaendelea kusema mtaalam huyo. “Hakika uislam ni itikadi na mfumo wa maisha na ni mtazamo kamili wa ulimwengu na binadamu.”

Kwamba msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu, Hakika mimi kwenu ni muonyaji mbashiri ninayetoka kwake.

Makusudio ya mimi ni Muhammad(s.a.w.w) , muonyaji ni kuonya adhabu kwa anayeasi na mbashiri ni anayetoa habari njema ya thawabu kwa mtiifu.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kusema kuwa Qur’ani ni Kitabu kili- chopangwa vizuri na kufafanuliwa, katika Aya hii anazungumzia Tawhid na kumfanyia ikhlas Mwenyezi Mungu peke yake katika ibada. Vilevile kuwa Muhammad(s.a.w.w) ni muonyaji na mtoaji habari njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Na kwamba mumtake maghufira Mola wenu kisha mtubie kwake.

Yaani mumwabudu Mwenyezi Mungu, mumwamini Muhammad(s.a.w.w) na utume wake, mtake maghufira na mtubie. Tofauti ya kuomba maghfira na kutubia ni: kuomba maghufira ni kutaka kusamehewa yaliyopita, bila ya kuangalia chochote kijacho. Ama kutubia ni kuomba msamaha yaliyopita na kuahidi kutotenda tena maasi.

Atawastarehesha starehe nzuri mpaka muda maalum na atampa kila mwenye fadhila fadhila yake.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuamrisha Ikhlas, kuamini utume wa Muhammad(s.a.w.w) , kuomba maghfira na kutubia, anataja kwamba malipo ya watiifu katika dunia sio kung’ongolewa kama walivyoong’olewa makafiri waliokuwa kabla yao; bali atawabakisha mpaka muda wao. Ama malipo yao huko akhera ni thawabu kwa kila mtu kulingana na matendo yake, yawe mengi au machache.

Na ikiwa mtakengeuka basi mimi nawahofia adhabu ya siku kubwa kutokana na vituko vyake na shida yake, nayo ni malipo ya kila mwenye kuikataa haki.

Marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu, naye ni mwenye uwezo juu ya kila kitu.

Na kwa uwezo wake atawafufua wafu, awakusanye kwa ajili ya hisabu na amlipe kila mmoja stahiki yake. Ni muweza kwa waja wake wote.

أَلَا إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ لِيَسْتَخْفُوا مِنْهُ أَلَا حِينَ يَسْتَغْشُونَ ثِيَابَهُمْ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٥﴾

5. Sikilizeni! Hakika wao wanakunja vifua vyao ili wamfiche. Sikilizeni! Wanapojigubika nguo zao anajua wanayoyaficha na wanayoyadhihirisha. Hakika yeye ni Mjuzi, wa yaliyomo vifuani.

WANAKUNJA VIFUA VYAO

Aya 5

MAANA

Dhamir ya ‘hakika wao’ ni ya washirikina na ya ‘anayemficha’ ni Mtume

Muhammad(s.a.w. w ) , Maana ya Aya ni kuwa baadhi ya watu walikuwa wakikunja nyoyo zao kwa kumfanyia chuki na uadui Mtume Muhammad(s.a.w. w ) , na hilo walikuwa wakilificha. Lakini Mwenyezi Mungu akaiifichua hakika yao na kwamba yeye Mwenyezi Mungu mtukufu anajua yaliyo nyoyoni mwao na hali yao yote kwa ujumla, na yeye atawaadhibu kutokana na makusudio yao.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA JUZUU YA KUMI NA MOJA


YALIY0M0

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 1

IMEANDIKWA NA: SHEIKH MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYA 1

IMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HASAN MWALUPA 1

IMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED 1

IMEPANGWA KATIKA KOMPYUTA NA: UKHT PILI RAJABU 1

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI 1

MAKOSA YA CHAPA 2

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 3

WATAWATOLEA UDHURU 3

MAANA 3

MABEDUI WAMEZIDI SANA 5

USHAMBA NA KUENDELEA 5

WALIOTANGULIA WA KWANZA 7

MAANA 7

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 10

CHUKUA SADAKA KATIKA MALI ZAO 10

MAANA 10

MSIKITI WA MADHARA 12

MAANA 12

MUNGU HUUZA NA KUNUNUA 16

MAANA 16

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 18

ABU TWALIB NA KUWATAKIA MSAMAHA WASHIRIKINA 18

KUSHUKA AYA 18

KAULI YA KWANZA 18

KAULI YA PILI 19

KAULI YA TATU 19

HALI HALISI 19

JE, KUNA SIRI GANI? 20

MAANA 20

MWENYEZI MUNGU HAWAPOTEZI WATU 22

MAANA 22

MWENYEZI MUNGU AMEMKUBALIA TOBA MTUME 23

MAANA 23

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 26

HAIFAI WATU WA MADINA KUBAKI NYUMA 26

MAANA 26

KWA NINI KISITOKE KIKUNDI 27

MAANA 27

IMAM ZAINULABIDIN NA MSINGI WA VITA 29

INAPOTEREMSHWA SURA 30

MAANA 30

KWA WAUMINI NI MPOLE 32

MAANA 32

MWISHO WA SURA YA TISA: SUART AT – TAWBA 33

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 34

HIZO NI AYA ZA KITAB CHENYE HEKIMA 34

MAANA 34

KUUMBA KATIKA SIKU SITA 36

MAANA 36

HISABU NA MALIPO NI LAZIMA 36

IDADI YA MIAKA NA HISABU 38

MAANA 38

WAKO WAPI WACHA MUNGU? 39

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 41

LAU MWENEYEZI MUNGU ANGELIWAHARAKISHIA SHARI 41

MAANA 41

LETE QUR’AN ISIYOKUWA HII 43

MAANA 43

WANASEMA HAWA NI WAOMBEZI WETU 45

MAANA 45

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 47

SEMA: MWENYEZI MUNGU NI MWEPESI ZAIDI WA KUPANGA NJAMA 47

MAANA 47

MFANO WA MAISHA YA DUNIA 49

MAANA 49

KWA WAFANYAO WEMA 51

MAANA 51

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 54

NI NANI ANAYEWARUZUKU? 54

MAANA 54

MWENYE KUONGOZA KWENYE HAKI 57

MAANA 57

MIONGONI MWAO WAPO WANAOAMINI 60

MAANA 60

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 63

SIKU ATAKAYOWAKUSANYA 63

MAANA 63

NI LINI AHAD HII? 65

MAANA 65

WALLAHI WEWE MUHAMMAD NI MTUME 66

YAMEWAJIA MAWAIDHA 69

MAANA 69

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 71

HUWI KATIKA JAMBO LOLOTE 71

MAANA 71

ENZI YOTE NI YA MWENYEZI MUNGU 73

MAANA 73

HABARI ZA NUH 75

MAANA 75

KISHA TUKAWAPELEKEA MITUME BAADA YAKE 77

MAANA 77

UONGOFU NA UPOTEVU 77

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 79

HAWAKUMUAMINI MUSA 79

MAANA 79

NA TUKAVUSHA BAHARI WAISRAEL 82

MAANA 82

MWISHO WA UTWAGHUTI 82

IKIWA UNA SHAKA 84

MAANA 84

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 86

KAUMU YA YUNUS 86

KISA 86

ISHARA NA MAONYO HAYATOSHI 89

MAANA 89

KAMA MWENYEZI MUNGU AKIKUGUSISHA DHARA 91

MAANA 91

MWISHO WA SURA YA KUMI 92

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA MOJA 93

KITABU NA AYA ZAKE 93

MAANA 93

WANAKUNJA VIFUA VYAO 95

MAANA 95

SHARTI YA KUCHAPA 95

MWISHO WA JUZUU YA KUMI NA MOJA 95

YALIY0M0 96



[1] . Hadith hii katika sahih Bukhari cha kingereza, ni Hadith no.174 uk.144. Pia ina- patikana katika sahihi Muslim Juz. 4 Uk. 1236, hadith no. 5682. –Mtarjumu.

[2] . Fasiki huyu alikuwa na mtoto aitwaye Hantwala ambaye ni katika maswahaba watukufu, aliyekuwa na ikhlas zaidi kwa Mwenyezi Mungu na Mtume. Aliuawa katika vita vya Uhud akiwa na janaba akaoshwa na malaika. Ndipo akaitwa muoshwa na malaika.

[3] . Angalia Juz.7 (6:41) kifungu 'Mwenyezi Mungu na maumbile'

[4] . (35:43)

[5] . (48:10)

[6] . (10:23)

[7] . Lau wangelitanabahi wale wanaowanasibisha wavumbuzi kwenye Qur’ani wangelisema kuwa samaki anaashiria nyambizi. Angalia Juz.1 (2:2) kifungu cha ‘Qur’ani na sayansi’