TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
IMEANDIKWA NA: SHEIKH MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYA
IMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED
Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London.
Kama lilivyo jina la Tafsiri ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo.
Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyo kujipatia wasomaji wengi sana.
Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana kwenda na wakati.
Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung'ang'ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo, hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea. Hiyo ilimsaidia sana hata kuweza kutoa kitabu kitwacho Al-Fiqh a'laa madhaahabil-khamsah (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka kwa lugha ya kiswahili hivi karibuni Inshaallah).
Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.
Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasayansi kama kina Enstein, wasanii kama Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa.
Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.
Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji.
Mwisho: Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji.
Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa, Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa.
Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya msahafu mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswutu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146), Imeandikwa La Ya'alamuun, (hawajui) badala ya Ya'alamuun (wanajua). Mfano wa makosa haya hausameheki.
Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa Fawqahum ila yawmil qiyama badala ya Fawqahum yawamal qiyama. Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile.
Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu Jabal amil 'Makosa ya chapa.'
Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: Hatta idha balagha arbai' na sanah badala ya: Hattaidha balagha ashuddahu arbai ' na sanah"
Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakayoyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefungua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana.
Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: "Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa.” Kama kwamba hakuna kitu chochote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.
Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin(a.s) :"Watu wote ni wapungufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu." Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubalia yale niliyoyapatia na kunisamehe niliyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazi chake, ziwashukie rehema na amani (Amin).
MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH
1
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
Mwendelezo Wa Sura ya Ishirini Na Saba.
أَمَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَنبَتْنَا بِهِ حَدَائِقَ ذَاتَ بَهْجَةٍ مَّا كَانَ لَكُمْ أَن تُنبِتُوا شَجَرَهَا أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ بَلْ هُمْ قَوْمٌ يَعْدِلُونَ ﴿٦٠﴾
60. Au ni nani yule aliyeziumba mbingu na ardhi na akawateremshia maji kutoka mbinguni na kwayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuotesha miti yake. Je, yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu waliopotoka.
أَمَّن جَعَلَ الْأَرْضَ قَرَارًا وَجَعَلَ خِلَالَهَا أَنْهَارًا وَجَعَلَ لَهَا رَوَاسِيَ وَجَعَلَ بَيْنَ الْبَحْرَيْنِ حَاجِزًا أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٦١﴾
61. Au ni nani yule aliyefanya ardhi mahali pa kutua? Na akaweka ndani yake mito na akaiwekea milima. Na akaweka kizuizi baina ya bahari mbili. Je, yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui.
أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾
62. Au ni nani yule anayemjibu aliyedhikika pale anapomwomba na akaiondoa dhiki? Na akawafanya ni warithi wa ardhi? Je, yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayoyazingatia.
أَمَّن يَهْدِيكُمْ فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَن يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ تَعَالَى اللَّـهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٣﴾
63. Au ni nani yule anayewaongoza katika giza la bara na bahari? Na ni nani yule azipelekaye Pepo kuleta bishara kabla ya rehema yake? Je, yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya yale wanayoyashirikisha.
أَمَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَمَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٦٤﴾
64. Au ni nani yule anayeuanzisha uumbaji kisha akaurejesha? Na ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini? Je, yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni dalili zenu kama nyinyi ni wakweli.
Aya 60–64
Makusudio ya Aya hizi na ile iliyoishia mwisho wa juzuu iliyopita ni kuwatahayariza washirikina na kuwarudi kwa njia ya maswali yasiyohitajia jawabu isipokuwa kusalimu amri; kama yafutavyo:
1.Je, Mwenyezi Mungu ni bora au wale wanaowashirikisha naye?
Aya hii imeishia mwisho wa juzuu ya kumi na tisa tumeileta tena kwa sababu inaungana na hapa Maana ni kuwa ni nani aliye bora na adhimu; ni Mwenyezi Mungu ambaye imetukuka hekima yake au ni mizimu na mengineyo mnayoyaabudu?
Jibu : ni Mwenyezi Mungu hilo halina shaka hata kwa washirikina, kwa sababu hawakanushi kuweko muumba, isipokuwa wanamuomba pamoja na wengine.
2.Au ni nani yule aliyeziumba mbingu na ardhi kwa nidhamu yake na mpangilio wake wa ajabu na wa hali ya juu ambao unafahamisha kuweko mjuzi mwenye hekima? Na akawateremshia maji kutoka mbinguni na kwayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza?
Mwenyezi Mungu huteremsha mvua kutoka mbinguni kwa sababu zake za kimaumbile. Vile vile huotesha kwenye ardhi kila aina ya mimea ya kupendeza kwa sababu za kimaumbile.
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba hayo maumbile na viliyvomo ndani yake, ndio ikasemewa kuwa Yeye ndiye aliyeteremsha mvua na kuotesha bustani.
Nyinyi hamna uwezo wa kuotesha miti yake , bali hata kujua chimbuko la uhai wa mimea na mengineyo, isipokuwa mkifasiri kuweko Mola muweza anayekiambia kitu: ‘Kuwa,’ kikawa.
Mfano wa Aya hi ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
أَفَرَأَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ ﴿٦٣﴾ أَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ ﴿٦٤﴾
“Je, mnaona mnayolima? Ni nyinyi mnayoyaotesha au ni sisi tunayoyaotesha? (56:63 – 64).
Je, yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu waliopotoka kwenye haki, kwa sababu wanamlinganisha Mwenyezi Mungu na wengineo.
3.Au ni nani yule aliyefanya ardhi mahali pa kutua?
Yaani ni mahali pa kutulia kulingana na ilivyo kwa umbo lake, kimo chake, vitenda kazi vyake, vituo vyake na mengineyo ambayo hayawezi kuwa isipokuwa kwa mpangilio wa mjuzi mwenye elimu.
Na akaweka ndani yake mito wanayonufaika nayo viiumbena akaiwekea milima ili isiwayumbishe[1] .
Na akaweka kizuizi baina ya bahari mbili ya maji chumvi na maji tamu. Kizuizi ni kuinama sehemu moja zaidi ya nyingine. Vinginevyo maji tamu yangeliharibika. Tazama Juz. 19 (25:53)[2] .
Je, yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu anayeshirikiana naye katika hayo?Bali wengi wao hawajui, lakini wako wanaojua isipokuwa wanafanya kiburi na inadi kuhofia chumo lao.
4.Au ni nani yule anayemjibu aliyedhikika pale anapomwomba na akaiondoa dhiki?
Mwenyezi Mungu (s.w.t) humpa msaada na tawfiki yule anayemkimbilia Yeye kwa kumtegemea. Humwandalia sababu ambazo zitatekeleza haja zake na humwondolea dhiki na uovu ikiwa ataihangaikia kwa mahangaiko yake yaliyozoeleka. Na yule mwenye kujifungia mahali pake bila ya kuhangaika atakuwa ameidhulumu nafsi yake.
Na akawafanya ni warithi wa ardhi, mkipokezana kizazi baada ya kizazi katika kuimiliki ardhi na kuiendesha.
Hivi karibuni wanasayansi wamegundua kwamba ingawa aina mbili hizi za maumbo ya maji huweza kukutana wakati mto ukiishia baharini, lakini hayawezi kamwe kuchanganyikana kwa vile kuna kizuizi kisichoonekana ambacho huweka aina mbili hizi za maji mbali mbali na tabia zao za wazi.
Je, yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayoyazingatia.
Makusudio ya kuzingatia hapa ni kuzitumia dalili, kunufaika na maonyo na kuwaidhika na mazingatio.
5.Au ni nani yule anayewaongoza katika giza la bara na bahari?
Kupitia milima, nyota na mengineyo yanayoingia kwenye kauli yake Mwenyezi Mungu:
وَعَلَامَاتٍ وَبِالنَّجْمِ هُمْ يَهْتَدُونَ ﴿١٦﴾
“Na alama nyingine. Na kwa nyota wao wanajiongoza.” Juz.14 (16:16).
Na ni nani yule azipelekaye pepo kuleta bishara kabla ya rehema yake?
Umetangulia mfano wake katika Juz.8 (7;57) na Juz. 19 (25:48).
Je, yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya yale wanayoyashirikisha na kuyazua kwa kumnasibishia ushirika na mtoto.
6.Au ni nani yule anayeuanzisha uumbaji kisha akaurejesha?
Mpangilio mzuri katika kuumba unafahamisha kuwa unatokana na mwenye hekima na mpangiliaji. Ikithibitika kuwa uumbaji umeanzia kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi ndio imethibiti kuwa Yeye ndiye mwenye kuurudisha.
Kwa sababu kurudisha ni kwepesi zaidi kuliko kuanzisha, kama isemavyo Aya hii:
وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ ﴿٢٧﴾
“Na yeye ndiye ambaye anaanzisha uumbaji kisha ataurudisha mara nyingine. Na hili ni jepesi zaidi kwake.” (30:27).
Na ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini kwa kuteremsha mvua na kuotesha mimea?Je, yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni dalili zenu kama nyinyi ni wakweli kuwa Mwenyezi Mungu ana mshirika au mtoto.
Kwa ufupi ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameleta dalili na hoja nyingi kwamba yeye yupo na yuko peke yake. Amezifafanua kwa kila mfumo. Basi anayepinga au kumfanya ana mshirika, alete dalili moja tu ya upinzani wake au ya ushirika wake.
Aina hii ya mjadala na mwito wa hukumu ya akili ni dalili mkataa kuwa Uislamu umejikita kwenye umbile ambalo Mwenyeezi Mungu amewaumbia watu. Ni kwa ajili hii ndo Mwenyezi Mungu akausifu kuwa ni dini iliyonyooka.
قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ﴿٦٥﴾
65. Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipokuwa Mwenyezi Mungu; wala wao hawajui lini watafufuliwa.
بَلِ ادَّارَكَ عِلْمُهُمْ فِي الْآخِرَةِ بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ مِّنْهَا بَلْ هُم مِّنْهَا عَمُونَ ﴿٦٦﴾
66. Bali ujuzi wao umefikia kuijua Akhera. Bali wao wamo katika shaka nayo. Bali wao ni vipofu nayo.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَإِذَا كُنَّا تُرَابًا وَآبَاؤُنَا أَئِنَّا لَمُخْرَجُونَ ﴿٦٧﴾
67. Na wakasema wale ambao wamekufuru: Tutakapokuwa mchanga, sisi na baba zetu, hivyo kweli tutakujatolewa?
لَقَدْ وُعِدْنَا هَـٰذَا نَحْنُ وَآبَاؤُنَا مِن قَبْلُ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٦٨﴾
68. Haya tuliahidiwa sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni ngano za watu wa kale.
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٦٩﴾
69. Sema: Nendeni katika ardhi na tazameni ulikuwaje mwisho wa wakosefu.
وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُن فِي ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ ﴿٧٠﴾
70. Wala usiwahuzunikie wala usiwe katika dhiki kwa hila wanazozifanya.
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٧١﴾
71. Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini ikiwa mnasema kweli.
قُلْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ رَدِفَ لَكُم بَعْضُ الَّذِي تَسْتَعْجِلُونَ ﴿٧٢﴾
72. Sema: Asaa ikawafikia sehemu ya yale mnayoyahimiza.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٧٣﴾
73. Na hakika Mola wako ni mwenye fadhila kwa watu, lakini wengi wao hawashukuru.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٤﴾
74. Na hakika Mola wako anayajua yanayoficha vifua vyao na wanayoyatangaza.
وَمَا مِنْ غَائِبَةٍ فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٧٥﴾
75. Na hakuna siri katika mbingu na ardhi ila imo katika kitabu kinachobainisha.
Aya 65 – 75
Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipokuwa Mwenyezi Mungu; wala wao hawajui lini watafufuliwa.
Wapinzani walimtaka Mtume(s.a.w.w) awawekee muda maalum wa ufufuo, ndio Aliye Mtukufu na kutukuka akamwambia: Waambie kuwa hakuna yeyote katika watu majini na hata malaika anayejua ghaibu na muda wa ufufuo isipokuwa Mwenyezi Mungu tu, na kwamba wao watafufuliwa bila ya kujua.
Bali ujuzi wao umefikia kuijua Akhera.
Yaani Mitume waliwapa habari washirikina, lakini hawakumwaamini; watakapofufuliwa na kuiona Akhera kwa macho watajua kuwa yale waliyoelezwa na mitume kuwa ni kweli.
Bali wao wamo katika shaka nayo.
Vipi wanaulizia wakati wa Akhera na hali wao hawaiamini?
Bali wao ni vipofu nayo.
Nyoyo zao zimekuwa na upofu wa Akhera kwa sababu ya upotevu wao na inadi yao.
Na wakasema wale ambao wamekufuru: Tutakapokuwa mchanga, sisi na baba zetu, hivyo kweli tutakujatolewa? Haya tuliahidiwa sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni ngano za watu wa kale.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:5) na Juz. 18 (23: 35 – 36 na 82 – 83).
Sema: Nendeni katika ardhi na tazameni ulikuwaje mwisho wa wakosefu.
Haya ni makemeo kwa yule anayekadhibisha utume wa Muhammad(s.a.w.w) , kuwa atapatwa na maangamizi kama yaliyowapata wengine katika umma zilizotangulia ambao waliwakadhibisha mitume wao.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (3:137).
Wala usiwahuzunikie wala usiwe katika dhiki kwa hila wanazozi- fanya.
Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 14 (16:127).
Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini ikiwa mnasema kweli.
Mtume(s.a.w.w) aliwahadharisha makuraishi na mwisho mbaya wa kukadhibisha kwao na uasi wao, wao wakamwambia kwa kumfanyia maskhara: Hilo litakuwa lini? Kila Mtume alisikia jawabu kama hili la dharau kutoka kwa watu wake pale alipowahadharisha.
Sema: Asaa ikawafikia sehemu ya yale mnayoyahimiza.
Huenda adhabu iko nyuma yenu na nyinyi hamjui. Maana ya Aya hii yako kwenye Aya: “Na watasema: lini hayo? Sema: asaa yakawa karibu.” Juz. 15 (17:51).
Na hakika Mola wako ni mwenye fadhila kwa watu, lakini wengi wao hawashukuru.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anawafadhili kwa kuwapa muda na kuwacheleweshea adhabu ili watubie na warudi kutoka kwenye upotevu wao. Ilikuwa ni wajibu wao washukuru hilo, lakini badala yake wanahimiza adhabu kwa dharau.
Na hakika Mola wako anayajua yanayoficha vifua vyao na wanayoy- atangaza.
Walitangaza kumshirikisha Mwenyezi Mungu na wakaficha njama na shari dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyaficha na wanayoyadhihirisha.
Naye atawalipa tu kwa haya na yale kulingana na wanavyostahili.
Na hakuna siri katika mbingu na ardhi ila imo katika kitabu kinachobainisha.
Hakuna siri katika ujuzi wa Mwenyezi Mungu hilo halina shaka, lakini makusudio ya kulieleza hilo ni onyo na hadhari kwa wahaini na vibaraka ambao wanajificha nyuma ya pazia la unafiki na ria.
2
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَقُصُّ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَكْثَرَ الَّذِي هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿٧٦﴾
76. Hakika hii Qur’an inawasimulia wana wa Israil mengi wanayohitilafiana.
وَإِنَّهُ لَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٧٧﴾
77. Nayo hakika ni uongofu na rehema kwa waumini.
إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُم بِحُكْمِهِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ ﴿٧٨﴾
78. Hakika Mola wako atakata baina yao hukumu yake naye ni mwenye nguvu, Mjuzi.
فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ إِنَّكَ عَلَى الْحَقِّ الْمُبِينِ ﴿٧٩﴾
79. Basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika wewe uko kwenye haki iliyo wazi.
إِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا وَلَّوْا مُدْبِرِينَ ﴿٨٠﴾
80. Kwa hakika wewe huwezi kuwasikilizisha wafu wala kuwasikilizisha viziwi wanapogeuka kurudi nyuma.
وَمَا أَنتَ بِهَادِي الْعُمْيِ عَن ضَلَالَتِهِمْ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨١﴾
81. Wala huwezi kuwaongoza vipofu na upotevu wao. Huwezi kuwasikilizisha ila wale wanaoziamini ishara zetu, basi hao ndio watiifu.
وَإِذَا وَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَابَّةً مِّنَ الْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ النَّاسَ كَانُوا بِآيَاتِنَا لَا يُوقِنُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na itakapowaangukia, tutawatolea mnyama katika ardhi atakayewasemeza, kwamba watu walikuwa hawana yakini na ishara zetu.
وَيَوْمَ نَحْشُرُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ فَوْجًا مِّمَّن يُكَذِّبُ بِآيَاتِنَا فَهُمْ يُوزَعُونَ ﴿٨٣﴾
83. Na siku tutakapowakusanya watu kutoka kila umma, kundi katika wanaokadhibisha ishara zetu. Nao watagawanywa mafungu mafungu.
حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوا قَالَ أَكَذَّبْتُم بِآيَاتِي وَلَمْ تُحِيطُوا بِهَا عِلْمًا أَمَّاذَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨٤﴾
84. Hata watakapofika, atasema: Je, nyinyi si mlizikanusha ishara zangu pasipo kuzijua vyema, au mlikuwa mkifanya nini?
وَوَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِم بِمَا ظَلَمُوا فَهُمْ لَا يَنطِقُونَ ﴿٨٥﴾
85. Na kauli itawaangukia kwa vile walivyodhulumu. Basi wao hawatasema lolote.
Aya 76 – 85
Hakika hii Qur’an inawasimulia wana wa Israil mengi wanayohitalifiana.
Qur’an imezungumzia na kuyakariri mambo ya kushangaza ya wana wa Israil. Imezungumzia mambo yanayohusiana nao, nembo yao na yale waliyohitalifiana wakati wa Nabii Musa na baadaye.
Nembo yao wanayoifuata bila ya kuicha ni: ‘Tumesikia na tumekataa,’ kama ilivyoelezwa katika Juz. 1(2:93) na Juz. 5 (4:46). Yaani tumemsikia Mwenyezi Mungu na mtume wake na tumemuasi Mwenyezi Mungu na mitume wote. Waliendelea na nembo hii wakati wa Nabii Musa(a.s) mpaka akawashtakia kwa Mola wake na akawapa sifa ya ufuska, akisema kwa masikitiko:
رَبِّ إِنِّي لَا أَمْلِكُ إِلَّا نَفْسِي وَأَخِي فَافْرُقْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ ﴿٢٥﴾
“Ewe Mola wangu! Hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu; basi tutenge na watu hawa mafasiki.” Juz. 6 (5:25).
Katika Aya nyingine amewapa sifa ya upumbavu:
قَالَ رَبِّ لَوْ شِئْتَ أَهْلَكْتَهُم مِّن قَبْلُ وَإِيَّايَ أَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ السُّفَهَاءُ مِنَّا ﴿١٥٥﴾
“Alisema: Mola wangu! Lau ungetaka ungeliwaangamiza wao na mimi zamani. Unatuangamiza kwa sababu ya yale waliyoyafanya wapumbavu katika sisi?” Juz. 9 (7:155).
Bado wanaendelea na nembo yao hii hadi leo. Mnamo mwaka 1967, Umoja wa Mataifa, unaowakilisha mataifa yote duniani, kuanzia mashariki hadi magharibi, ulipitisha azimio la kuitaka Israil ijiondoe katika ardhi ya Quds.
Jibu la mjumbe wake lilikuwa ni: “Umoja wa Mataifa ni debe la takataka,” kama ilivyonukuliwa katika magazeti.
Ama yale ambayo walihitilafiana ni walivyoifanyia Tawrat wakati wa Musa mpaka Mwenyezi Mungu akawainulia jabali na kuwatishia kuwaangamiza:
وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاسْمَعُوا قَالُوا سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا ﴿٩٣﴾
“Na tulipochukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu: Kamateni kwa nguvu haya tuliyowapa na sikilizeni. Wakasema: “Tumesikia na tumekataa” Juz 1(2:93)[3] .
Walihitalifiana katika mitume waliokuja baada ya Musa(a.s) . Miongoni mwao ni Bwana Masih(a.s) , kundi moja lilimkadhibisha na kundi moja likataka kumuua; kama ilivyoelezwa katika Juz. 1 (2:87).
Vilevile walihitalifiana kuhusu utume wa Muhammad. Hawakumwamini isipokuwa wachache. Kama wangelikuwa ni watafutaji kweli wa haki wangeliafikiana kuichukua Qur’an ambayo imesimama kwa dalili na hoja juu ya ukweli wake.
Nayo hakika ni uongofu na rehema kwa waumini.
Ni uongofu kwa mwenye kutaka kuongoka na rehema kwa kutumia hukumu zake na mafunzo yake.
Hakika Mola wako atakata baina yao hukumu yake naye ni mwenye nguvu, Mjuzi.
Siku ya Kiyama batili zitaondoka na Mwenyezi Mungu atawahukumu waisrail na wengineo katika yale waliyohitalifiana katika mambo ya dini na dunia.
Basi mtegemee Mwenyezi Mungu.
Mwenye kukimbilia kwake basi yuko katika ngome imara na kizuizi cha nguvu.
Hakika wewe uko kwenye haki iliyo wazi.
Na mwenye haki hajali yanayosemwa juu yake.
Kwa hakika wewe huwezi kuwasikilizisha wafu wala kuwasikilizisha viziwi wanapogeuka kurudi nyuma. Wala huwezi kuwaongoza vipofu na upotevu wao.
Jumla hizi zina lengo moja, kwamba kuna sifa zinazoua moyo na kumfanya mtu anga’ang’anie ukafiri, unafiki na upotevu. Zinamfanya yeye na maiti ni sawasawa; hafaidiki na mawaidha wala maonyo. Miongoni mwa sifa kuu hizo ni tamaa na pupa ya chumo na cheo.
Maana haya yamekaririka kwa mifumo mbalimbali; miongoni mwayo ni Aya hizi zifuatazo:-
Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo, na wana macho, lakini hawaoni kwayo, na wanayo masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotevu zaidi. Hao ndio walioghafilika. Juz. 9 (7:179).
Je, wewe unaweza kuwasikilizisha viziwi ingawa hawafahamu? Je, wewe unaweza kuwaogoza vipofu ingawa hawaoni? Juz.11 (10 42–43).
Huwezi kuwasikilizisha ila wale wanaoziamini ishara zetu, basi hao ndio watiifu.
Anayekusikiliza na kukutii wewe Muhammad ni yule anayeitafuta haki kwa ajili ya haki, kiasi ambacho akipata dalili na hoja anaiamini na kuifuata. Ama watu wa masilahi na tamaa wanakupa mgongo.
Na itakapowaangukia kauli juu yao, tutawatolea mnyama katika ardhi atakayewasemeza, kwamba watu walikuwa hawana yakini na ishara zetu.
Kuwaangukia, ni kuwathibitikia. Makusudio ya kauli hapa ni yale aliyoyaahidi Mwenyezi Mungu ya kutokea Kiyama. Makusudio ya watu ni makafiri.
Ama kuhusu mnyama, maneno yamekuwa mengi kumuhusu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakutubainishia ni yupi. Pia Hadith kutoka kwa maasum hazikuthibiti; hata kama mapokezi yake yatasihi hatuwezi kuitumia, kwa sababu itakuwa imekuja kwa njia moja (Khabarul-waahid) ambayo inakuwa hoja katika hukumu tanzu, si katika maudhui na misingi ya kiitikadi. Na kusema bila ya elimu ni haramu.
Kwa hiyo hakuna kilichobakia isipokuwa kuchukulia dhahiri ya Aya ambayo inafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) atakapowafufua watu kwa ajili ya hisabu atamtoa kiumbe kutoka ardhini atakayetangaza kuwa makafiri walizikana dalili wazi wazi na hoja mkataa za kuweko Mwenyezi Mungu, umoja wake na mitume wake.
Unaweza kuuliza : kwa nini Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakubainisha hakika ya mnyama huyu akawaacha watu wameduwaa, mpaka wengine wakasema bila ya elimu na kuwazia tu?
Jibu : Lengo la kutajwa ni kuwatangaza makafiri na kwamba wao watafufuliwa kesho wakiwa madhalili wamefedheheka mbele ya ushahidi. Lengo hili linapatikana kiasi cha kudokeza tu kuwa kutakuwa na mnyama hata kama jina lake halijulikani wala hakika yake. Aya hii inafanana na kauli yake Mwenyezi Mungu: “Siku ambayo nyuso zitang’aa na nyuso (nyingine) zitasawijika.” Juz. 4 (3:106).
Na siku tutakapowakusanya watu kutoka kila umma, kundi katika wanaokadhibisha ishara zetu.
Neno ‘katika’ ni la kubainisha sio la baadhi; ni kama mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Jiepusheni na uchafu katika mizimu.” akimaanisha mizimu yote sio baadhi.
Maana ni kuwa katika kila umma kuna wanaosadikisha ishara za Mwenyezi Mungu na wenye kuzikadhibisha. Mwenyezi Mungu (s.w.t) kesho atawakusanya wakadhibishaji wote kwa ajili ya hisabu na malipo. Inajulikana wazi kuwa Mwenyezi Mungu atawakusanya wasadikishaji na wakadhibishaji, lakini lengo la kutajwa wakadhibishaji ni ukemeo na kiaga.
Nao watagawanywa mafungu mafungu.
Malaika watawazuia kuumeni na kushotoni na watawachunga kwenda kwenye kisimamo, kama wanyama wakipelekwa machinjioni.
Hata watakapofika, atasema: Je, nyinyi si mlizikanusha ishara zangu pasipokuzijua vyema, au mlikuwa mkifanya nini?
Watakaposimama wakanushaji mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hisabu atawaambia kwa kuwatahayariza, kwa nini mmewakadhibisha mitume wangu na kuacha kuitikia mwito wao? Ikiwa hamkujua ukweli wao kwanini mlipinga dalili za kuwajulisha na msiziangalie kwa mtazamo wa mwenye kutafuta haki kwa njia ya haki? Ni lipi lilo muhimu zaidi ya hilo?
Maulamaa wameafikiana, kwa kauli moja, kuwa akili inahukumiwa kwa wajibu wa kuangalia muujiza wa mwenye kudai utume. Wakasema: Akili haisamehewi kwa lile ambalo ni wajibu ikiwa inaweza kufanya utafiti na kupata maarifa. Kuna Hadith isemayo: “Mja ataambiwa siku ya Kiyama, je ulijua? Akisema, ndio, Ataulizwa tena, je ulifanya? Akisema sikujua (namna ya kufanya), ataulizwa, je ulijifundisha?
Na kauli itawaangukia juu yao kwa vile walivyodhulumu.
Ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu itawapata kwa sababu ya kufuru yao na uzembe wao wa kufanya utafiti na kuuliza.
Basi hao hawatasema lolote, kwa sababu ya kukatikiwa na hoja na mshangao wao kutokana na vituko vya siku ya Kiyama.
أَلَمْ يَرَوْا أَنَّا جَعَلْنَا اللَّيْلَ لِيَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٨٦﴾
86. Je, hawaoni kwamba tumeufanya usiku ili watulie na mchana wa kuangaza. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wenye kuamini.
وَيَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَفَزِعَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ وَكُلٌّ أَتَوْهُ دَاخِرِينَ ﴿٨٧﴾
87. Na siku itakapopuziwa parapanda, watafazaika waliomo mbinguni na waliomo ardhini, ila amtakaye Mwenyezi Mungu. Na wote watamfikia nao ni wanyonge.
وَتَرَى الْجِبَالَ تَحْسَبُهَا جَامِدَةً وَهِيَ تَمُرُّ مَرَّ السَّحَابِ صُنْعَ اللَّـهِ الَّذِي أَتْقَنَ كُلَّ شَيْءٍ إِنَّهُ خَبِيرٌ بِمَا تَفْعَلُونَ ﴿٨٨﴾
88. Na unaiona milima unaidhania imetulia nayo inakwenda mwendo wa mawingu. Ni sanaa ya Mwenyezi Mungu aliyekitengeneza vizuri kila kitu. Hakika yeye ana habari za mnayoyatenda
مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا وَهُم مِّن فَزَعٍ يَوْمَئِذٍ آمِنُونَ ﴿٨٩﴾
89. Watakaokuja na wema watapata bora kuliko hayo. Nao watasalimika na mfazaiko wa siku hiyo.
وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَكُبَّتْ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ هَلْ تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٩٠﴾
90. Na wenye kuja na uovu, basi nyuso zao zitatupwa motoni. Kwani mnalipwa isipokuwa yale mliyoyatenda?
إِنَّمَا أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ رَبَّ هَـٰذِهِ الْبَلْدَةِ الَّذِي حَرَّمَهَا وَلَهُ كُلُّ شَيْءٍ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٩١﴾
91. Hakika nimeamrishwa kumwabudu tu Mola wa mji huu ambaye ameufanya ni mtakatifu; na ni vyake Yeye vitu vyote. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa wenye kunyenyekea.
وَأَنْ أَتْلُوَ الْقُرْآنَ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ وَمَن ضَلَّ فَقُلْ إِنَّمَا أَنَا مِنَ الْمُنذِرِينَ ﴿٩٢﴾
92. Na kwamba nisome Qur’an. Na mwenye kuongoka, basi ameongoka kwa faida ya nafsi yake tu na aliyepotea basi sema: Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji tu.
وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ سَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ فَتَعْرِفُونَهَا وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٩٣﴾
93. Na Sema: Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu (Alhamdu lillah) Atawaonyesha ishara zake mtazijua. Na Mola wako si mwenye kughafilika na mnayoyafanya.
Aya 86 – 93
Je, hawaoni kwamba tumeufanya usiku ili watulie na mchana wa kuangaza. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wenye kuamini.
Imetangulia pamoja na tafsiri yake katika Juz. 11 (10:67).
Na siku itakapopuziwa parapanda, watafazaika waliomo mbinguni na waliomo ardhini, ila amtakaye Mwenyezi Mungu.
Parapanda itapuziwa kutangaza Kiyama, nyoyo za viumbe zitashtuka, kutokana na mpuzio huo, kwa hofu kuu; isipokuwa nyoyo za Mitume wasadikishaji, mashahidi na watu wema ambao Mwenyezi Mungu amewavua kwa kusema: ‘Ila amtakaye Mwenyezi Mungu.’ Hao aliowavua amewashiria katika kauli yake:
وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾
“Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, basi hao (watakuwa) pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii na wasadikishaji na mashahidi na watu wema. Na hao ndio marafiki wema.” Juz. 5 (4:69).
Katika baadhi ya tafsiri imeelezwa kuwa Parapanda itapulizwa mara tatu; Mpulizo wa fazaa, wa kufa watu wote na ule wa ufufuo. Ufufuo wa kwanza unafahamishwa na Aya tuliyo nayo, wa pili na wa tatu unafahamishwa na Aya isemayo: “Na itapulizwa parapanda, wazimie waliomo mbinguni na waliomo katika ardhini, ila aliyemtaka Mwenyezi Mungu. Kisha itapulizwa mara nyingine. Hapo watainuka wawe wanangojea.”
Na wote watamfikia nao ni wanyonge.
Yaani hao wanaohofia watafufuliwa kwa Mola wao wakiwa dhalili.
Na unaiona milima unaidhania imetulia nayo inakwenda mwendo wa mawingu.
Maudhui ya Aya hii na iliyo kabla yake ni mamoja, kuzungumzia Kiyama na vishindo vyake. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ataing’oa milima kutoka sehemu zake na kuiendesha angani, sawa na yanavyopita mawingu, lakini mtu atafikiria kuwa imetulia.
Hiyo inatokana na kuwa umbo kubwa likitembea kwenye mwelekeo mmoja ulionyooka, basi macho hayaoni harakati zake kutoka na ukubwa wake na umbali wa pembe zake; hasa ikiwa mtazamaji yuko mbalia nalo.
Hapa yanatubainikia makosa ya mwenye kuitumia aya hii katika kuthibitisha harakati ya ardhi. Kuna Aya nyingi zinazofahamisha kuwa makusudio ya kutembea milima, katika Aya hii, kutakuwa siku ya Kiyama; miongoni mwazo ni hizi zifuatazo:-
وَيَوْمَ نُسَيِّرُ الْجِبَالَ وَتَرَى الْأَرْضَ بَارِزَةً وَحَشَرْنَاهُمْ فَلَمْ نُغَادِرْ مِنْهُمْ أَحَدًا ﴿٤٧﴾
“Na siku tutakayoipitisha milima na utaiona ardhi iwazi. Na tutawafufua..” Juz. 15 (18:47).
وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا ﴿٢٠﴾
“Na ikaendeshwa milima ikawa sarabi.” (78:20).
يَوْمَ تَمُورُ السَّمَاءُ مَوْرًا ﴿٩﴾ وَتَسِيرُ الْجِبَالُ سَيْرًا ﴿١٠﴾
“Siku itakapotikisika mbingu mtikisiko. Na milima iwe inakwenda mwendo.” (52: 9 – 10).
Maneno ya Qur’an ni mamoja, sehemu moja inaifafanulia nyingine.
Ndio! Watu wa nyumba ya Mtume(s.a.w.w) , ambao wana elimu ya Kitabu na Sunna, waliweka wazi kuwa ardhi ina harakati kabla ya Companicus, kwa miaka elfu moja. Imam Ali(a.s) anasema katika Nahjul-balagha:Na akaiumba ardhi hewani na akiweka bila ya muhimili na akaiinua bila ya nguzo (khutba 186). Na mjukuu wake Imam Jafar Sadiq akasema:“Kufahamisha vitu kuzunguka na vilivyomo ndani yake zikiwamo sayari saba, ni kuwa ardhi ina harakati…”
Ni sanaa ya Mwenyezi Mungu aliyekitengeneza vizuri kila kitu , kuanzia kikubwa sana hadi kidogo sana. Ufundi, mpangilio na nidhamu ni ushahidi mkubwa wa kuweko Mwenyezi Mungu, umoja wake na uwezo.
Hakika yeye ana habari za mnayoyatenda.
Ambaye amemuumba mtu kwa ufundi wa hali ya juu, anajua kila akitendacho kiumbe, kiwe cha heri au cha shari na yale yanayompitikia katika nafsi yake:
وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ ﴿١٦﴾
“Na hakika tumemuumba mtu nasi tunayajua yanayoitia wasiwasi nafsi yake na sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wake wa shingo.” (50:16).
Watakaokuja na wema watapata bora kuliko hayo. Nao watasalimika na mfazaiko wa siku hiyo. Na wenye kuja na uovu, basi nyuzo zao zitatupwa motoni. Kwani mnalipwa isipokuwa yale mliyoyatenda?
Inayofafanua zaidi Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu: “Mwenye kufanya vizuri atalipwa mfano wake mara kumi. Na mwenye kufanya vibaya hatalipwa ila sawa na hivyo tu. Nao hawatadhulumiwa.” Juz. 7 (6:179).
Hakika nimeamrishwa kumwabudu tu Mola wa mji huu ambaye ameufanya ni mtakatifu; na ni vyake Yeye vitu vyote. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa wenye kunyenyekea.
Makusudio ya mji hapa ni Makka Tukufu. amaeuhusisha kuutaja, pamoja na kuwa yeye ni Mola wa ulimwengu wote, ili kuwabainishia makuraishi neema yake kwao kwa sababu ya mji huo. Walikuwa wakitegemeza ubora wao kuliko waarabu wengine kwa taadhima ya mji huo na utakatifu wake na kuwa na amani, kwa kuharamishwa kuua, kupigana, kuwinda, kukata miti na mengine yanayofahamisha utukufu na cheo chake.
Pamoja na yote haya makuraishi waliabudu masanamu wakaichafua Al-ka’ba kwayo, wakimshirikisha nayo Mola wa mji huu mtukufu ambaye amewalisha kutokana na njaa na akawasalimisha na hofu.
Kauli ya Mtume(s.a.w.w) : ‘Nimeamrishwa kumwabudu …’ ni kuwapinga makuraishi na kwamba wajibu wao ni kuacha ibada ya ya masanamu ambayo hayamiliki chochote, na wamwabudu Mola wa mji huu ambaye ndiye muumba, mfalme na mwenye amri. Na yeye ni muweza wa kila kitu na akawafadhili makuraishi kwa vitu vingi.
Na kwamba nisome Qur’an.
Makusudio ya kusoma Qur’an hapa ni kutoa mwito wa kuiamini na kwenda na sera yake.
Na mwenye kuongoka, basi ameongoka kwa faida ya nafsi yake tu na aliyepotea basi sema: Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji tu.
Mtume(s.a.w. w ) ametoa mwito wa uongofu. Mwenye kusikia na akatii, basi amejifanyia uzuri mwenyewe na atakuwa amefuata njia ya kheri na uokovu. Na mwenye kupinga basi atakuwa amejifanyia ubaya yeye mwenyewe na kujiingiza kwenye shari na maangamizi. Mtume(s.a.w.w) hana majukumu ya watu wa upotevu baada ya kuwanasihi na kuwafikishia risala ya Mola wake.
Na Sema: Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu (Alhamdu lillah) kwa kuniwafikisha kufikisha risala yake kwa waja wake kama alivyopenda na kutaka.
Atawaonyesha ishara zake mtazijua.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwaonyesha dalili za ishara zake kwenye nafsi zao na kwenye pambizo, lakini wakazikana. Ndio akawaambia, leo mnazikana na kesho mtazikubali, ambapo kukubali kwenu hakutawafaa kitu.
Na Mola wako si mwenye kughafilika na mnayoyafanya.
Haya ni makemeo na kiaga cha kupinga kwao na kukana ishara za Mwenyezi Mungu na ubainifu wake.
3
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
Sura Ya Ishirini Na Nane: Surat Al-Qasas. Tabrasi amesema imeshuka Makka. Ina Aya 88.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu
طسم ﴿١﴾
1. Twaa Siin Miim.
تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾
2. Hiyo ni Aya za Kitabu kinachobainisha.
نَتْلُو عَلَيْكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرْعَوْنَ بِالْحَقِّ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٣﴾
3. Tunakuosomea habari za Musa na Firauni kwa haki kwa ajili ya watu wanaoamini.
إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَائِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَاءَهُمْ وَيَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ إِنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ ﴿٤﴾
4. Hakika Firauni alitakabari katika nchi akagawa watu wake makundi. Akidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wa kiume na akiwaacha watoto wao wa kike. Hakika yeye alikuwa katika wafisadi.
وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ ﴿٥﴾
5. Na tunataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi na kuwafanya wawe ni viongozi na kuwafanya ni warithi.
وَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَنُرِيَ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا مِنْهُم مَّا كَانُوا يَحْذَرُونَ ﴿٦﴾
6. Na kuwamakinisha katika ardhi. Na kumuonyesha Firauni na Hamana na majeshi yao yale waliyokuwa wakiyahadhari kwao.
Aya 1 – 6
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1)
Hiyo ni Aya za Kitabu kinachobainisha.
Hiyo ni ishara ya Sura hii, Kitabu ni Qur’an na kubainisha ni kupambanua baina ya upotevu na uongofu.
Tunakuosomea habari za Musa na Firauni kwa ajili ya watu wanaoamini.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemsomea Mtume wake mtukufu habari mara kwa mara. Katika Juz. 16 kifungu cha ‘Kukaririka Kisa’ (20:9) tumeeleza lengo la kukaririka kisa cha Musa.
Hakika Firauni alitakabari katika nchi akagawa watu wake makundi.
Alipetuka mipaka na akajifanya jabari, akawagawa wananchi wake kwenye makundi wakigombana, ili udumu utawala wake.
Akidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wa kiume na akiwaacha watoto wao wa kike. Hakika yeye alikuwa katika wafisadi.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:49) na Juz. 9 (7:127).
Mmoja katika wafasiri wa kisasa anasema: “Firauni aliwakandamiza wana wa Israil kwa sababu walikuwa na itikadi isiyoafikiana na itikadi yake. Wao walikuwa wakifuata dini ya babu yao Ibrahim na Ya’qub. Ingawa itikadi yao ilikuwa na upotofu, lakini walibakia na itikadi ya Mungu mmoja.”
Sisi tunamuuliza mfasiri huyu mpya: Umejua vipi kuwa mayahudi waliokuwa wakati wa Firauni walikuwa kwenye dini ya Ibrahim(a.s) na kwamba walibaki na itikadi ya Mungu mmoja? Je, umepata kujua kutokana na kuli yao: “Ewe Musa! Hebu nasi tufanyie waungu kama hawa walivyo na waungu.” Au kauli yao: “Hatutakuamini mpakae tumwone Mungu wazi wazi.”
Au ni kutokana na kuabudu kwao ndama au kwa kuwaua kwao mitume? Ikiwa Firauni aliwakandamiza kwa sababu ya itikadi yao, kwa nini Mtume wao na mwenye ikhlasi zaidi, Musa aliwapa wasifa huu ufuatao? Ufuska, Juz. 6 (5:25), wapumbavu, Juz. 9 (7:155), wabatilifu Juz. 9 (7:153) na ujinga Juz. 9 (7:138). Kama amabavyo Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Aya kadhaa amewasifu kwa ufisadi, uovu na kwa kila aina ya hatia?
Qur’an imetaja kwamba Firauni aliwakandamiza wana wa isaril na kwam- ba yeye alipituka mpaka katika dhulma yake, lakini haikuashiria sababu.
Kwa hiyo maulama wametofautiana katika kuielezea. Kuna waliosema kuwa kuhani alimwambia Firauni kuwa atazaliwa mtoto katika wana waisrail, atakayekuja mvua ufalme wake, wengine wakasema kuwa mitume waliokuwa kabla yake walitoa bishara ya kuja kwake.Firauni alipojua hivyo akahofia na kuanza kuwachinja watoto wa kiume wa wana wa israil. Na sikuona yoyote aliyesema kuwa Firauni aliwakandamiza kwa sababu ya kuwa kwenye dini ya Ibrahim.
Tukiangalia sera ya wana wa israil kwa Mtume wao Musa(a.s) na mitume wengine waliokuja baada ya Musa; ambapo walikuwa wakikadhibisha wengine na wengine wakiwaua. Pia tukiangalia sera yao katika miji wanayoiteka jinsi wanavyoleta fitna, kupanga njama, kujaribu kutawala nyenzo na propaganda zote.
Tukiangalia yote haya basi tunakubaliana na Sheikh Maraghi aliyesema: “Firauni aliwakandamiza wana wa israil kwa vile aliwahofia wanaume ambao walikuwa na ufundi na mikononi mwao mlikuwa na hatamu za uchumi; kuwa muda ukiendelea watakuwa juu kiuchumi waje wawashinde wamisri. Na uchumi ndio wenye nguvu kiutawala.”
Ni kweli kuwa Firauni alipetuka mpaka katika dhulma kwa kuwachinja watoto wa kiume na kuwafanya watumwa watoto wa kike wa wana wa israil, lakini sababu ya yote haya ni wayahudi.
Kwa hiyo lawama ni la wote wawili. Mayahudi kwa sababu ya chuki yao, tabia yao na malengo yao mabaya na pia kwa Firauni kwa sababu aliwatesa wasiokuwa na hatia kwa sababu ya wenye hatia.
LINI MWENYEZI MUNGU ATAWAFADHILI WALIODHOOFISHWA?
Na tunataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi.
Waliodhoofishwa katika ardhi ni wale waliokandamizwa na wenye nguvu, waliotawala nyenzo zao na nguvu zao kimabavu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawafadhili uhuru na kujikomboa kwenye ukandamizaji ikiwa watafanya juhudi na kujitolea kwa ajili ya maisha yao na heshima yao; sawa na mgonjwa atapona ikiwa atafanya matibabu mazuri na mkulima atapata mavuno akilima vizuri.
Mwenyezi Mungu ana desturi katika maumbile yake, na wala hutapata mabadiliko katika desturi ya Mwenyezi Mungu kabisa. Kila mwenye kufuata njia atafika, awe mumin au kafiri. Ama malipo ya kafiri na mumin ni siku ya Kiyama, si katika maisha haya.
Basi atakayemnyenyekea dhalimu, Mwenyezi Mungu humdhalilisha na humwachia atakayemdhulumu, hata kama ataswali, kufunga na kuhiji. Kwa sababu ameidhalilisha haki na akisaidia batili na akhera hana kitu.
Na mwenye kujikomboa kutoka kwa dhalimu na watu wake, na akajitolea mhanga kwa ajili ya heshima yake, Mungu humpa nusra kuwashinda mad- halimu na wababe; kwa sababu atakuwa amekutana na utashi wa Mwenyezi Mungu na amri yake, kwa jihadi na uimara.
Hatuna haja ya kurudia historia ya mbali kutafuta ushahidi wa hakika hii. Kwani ukakamavu wa wananchi wa Vietnam mbele ya taifa hilo na nguvu kubwa ya shari na ufisadi, ni dalili kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na mwenye kudhulumiwa anayepigana jihadi aliye mvumilivu, kwa namna yoyote ile atakayokuwa.
Kwa ufupi ni kuwa Mwenyezi Mungu hapigani kwa ajili ya waliodhoofishwa, lakini anakuwa nao na kuwapa msaada wake, ikiwa watapigana na kupinga kwa lengo la haki, uadilifu na kujikomboa kutoka kwenye makucha ya ukoloni na dhulma. Mwenyezi Mungu yuko pamoja na hawa, kwa sababu, yuko pamoja na kila mwenye kufanya juhudi na akatenda kwa ajili ya maisha.
Haya tumeyafafanua zaidi katika Juz. 13 (13:11).
Unaweza kuuliza : Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwangamiza Firauni na watu wake, akawaokoa wana wa israil na adhabu yao na ukandamizwaji wao. Hii inamaanisha kuwa Mwenyezi Mungu anapigana kwa ajili ya wanyonge; bali kuna Aya isemayo:
إِنَّ اللَّـهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا ﴿٣٨﴾
“Hakika Mwenyezi Mungu huwakinga walioamini.” Juz. 17 (22:38)?
Jibu : Mwenyezi Mungu Mtukufu alimwangamiza Firauni na watu wake kwa sababu ya shirki yao na kuwakadhibisha kwao mitume na sio kuwasaidia wana wa israili; sawa na alivyoangamiza kaumu ya Nuh na washirikina wengineo.
Kwa hiyo wana wa israil na wengineo wakapona na dhulma na ukandamizwaji. Ama makusudio ya walioamini, wanaokingwa na Mwenyezi Mungu ni wale wanopigana jihadi. Na wavivu wako kwenye dini ya wale waliomwambia Musa:
فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلَا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ ﴿٢٤﴾
“Nenda wewe na Mola wako mkapigane, hakika sisi ni wenye kukaa hapa.” Juz. 6 (5:24)
Na kuwafanya wawe ni viongozi.
Yaani tuwafanye mitume miongoni mwao.
Na kuwafanya ni warithi na kuwamakinisha katika ardhi.
Mwenyezi Mungu anawafanya huru kwa muda mrefu baada ya kuwa utumwani.
Na kumuonyesha Firauni na Hamana na majeshi yao yale waliyokuwa wakiyahadhari kwao.
Kwao ni kwa hao wana wa israil. Maana ni kuwa Firauni na watu wake walihofia utawala wao usiingie mikononi mwa wana wa israil, ndio wakachukua hadhari, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawaingiza kwenye yale waliyoyahofia.
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِي الْيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحْزَنِي إِنَّا رَادُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧﴾
7. Na tulimpa wahyi mama wa Musa kuwa mnyonyeshe. Na utakapomhofia basi mtie mtoni. Na usihofu wala usihuzunike. Hakika sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa mitume.
فَالْتَقَطَهُ آلُ فِرْعَوْنَ لِيَكُونَ لَهُمْ عَدُوًّا وَحَزَنًا إِنَّ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا كَانُوا خَاطِئِينَ ﴿٨﴾
8. Basi wakamwokota watu wa Firauni aje kuwa adui kwao na huzuni. Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa.
وَقَالَتِ امْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِّي وَلَكَ لَا تَقْتُلُوهُ عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾
9. Akasema mke wa Firaun: Ni kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuuwe! Huenda akatufaa au tumfanye kuwa mtoto wetu. Wala wao hawakutambua
وَأَصْبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَارِغًا إِن كَادَتْ لَتُبْدِي بِهِ لَوْلَا أَن رَّبَطْنَا عَلَىٰ قَلْبِهَا لِتَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠﴾
10. Moyo wa mamake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kudhihirisha, lau tusingeliuimarisha moyo wake ili awe miongoni mwa waumini.
وَقَالَتْ لِأُخْتِهِ قُصِّيهِ فَبَصُرَتْ بِهِ عَن جُنُبٍ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١١﴾
11. Akamwambia dadake (Musa) mfuatie. Basi akawa anamwangalia kiupande upande na wao hawatambui.
وَحَرَّمْنَا عَلَيْهِ الْمَرَاضِعَ مِن قَبْلُ فَقَالَتْ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ أَهْلِ بَيْتٍ يَكْفُلُونَهُ لَكُمْ وَهُمْ لَهُ نَاصِحُونَ ﴿١٢﴾
12. Na tukamharamishia wanyonyeshaji tangu mwanzo. Akasema (dadake): Je, niwaonyeshe watu wa nyumba watakaowalelea na watakuwa wema kwake?
فَرَدَدْنَاهُ إِلَىٰ أُمِّهِ كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ وَلِتَعْلَمَ أَنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾
13. Basi tukamrudisha kwa mama yake ili yaburudike macho yake na ajue kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Lakini watu wengi hawajui.
Aya 7 – 13
Na tulimpa wahyi mama wa Musa kuwa mnyonyeshe.
Makusudio ya wahyi hapa ni ilhamu; ni mfano kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na Mola wako akampa wahyi nyuki.” Juz. 14 (16:68). Katika Juz. 9 (7: 103 -112).
Tumenukuu kutoka kitabu Qisasul-qur’an, kwamba jina la mama yake Musa ni Yukabid (Jochebed). Kisha tukasoma katika Tawrat kuwa hilo ndilo jina lake na kwamba aliolewa na Amram, mtoto wa kaka yake. Musa ndiye mdogo katika watoto wa baba yake, akiwa ni watatu, baada ya Maryam na Harun.
Na utakapomhofia basi mtie mtoni.
Makusudio ya mto hapa ni mto Nile. Maana ni akimhofia kuchinjwa amtie mtoni kwa mkono wake! Itakuwaje, mwenye akili aweze kujitupa motoni?
Lakini akaambiwa: Na usihofu wala usihuzunike. Hakika sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa mitume.
Usimhofie, hakika Mwenyezi Mungu ndiye mhifadhi na mlinzi. Yule ambaye ameujaalia moto kuwa baridi na salama kwa Ibrahim, ataijalia bahari kuwa amani kwa Musa. Alimpa habari ya usalama wa mtoto wake na kwamba yeye atamlea na pia akampa habari njema kuwa amemchagua kwa risala yake na kumhusu kwa rehema yake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:38).
Basi wakamwokota watu wa Firauni aje kuwa adui kwao na huzuni.
Walimwokota na kumlea kwa kumfanya mtoto wao, lakini akaja akawa ni adui wa itikadi yao na desturi yao. Akaingiza huzuni nyoyoni mwao na mwisho wa ufalme wao ukawa mikononi mwake.
Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa, wapotevu katika vitendo vyao vyote; hasa kuua maelefu ya vijana ili kujiepusha na Musa, lakini ikawa wao wanamwepusha Musa na mauti ili aje awamalize. Katika kamusi ya Kitabu kitakatifu[4] , imeelezwa kuwa maisha ya Musa katika nyumba ya Firauni hayakujulikana kwa ufafanuzi na kwamba wanahistoria wametofautiana kuhusu wakati wake alioishi. Wengine wakasema ni wakati wa Firauni Amenophis (Amenhotep II) (1411 – 1436 Bc), wengine wakasema ni Ramesses II (1223 – 1290 Bc). Pia kuna waliosema ni wakati wa Mernptsh ( 1211 – 1223 Bc).
Akasema mke wa Firaun: Ni kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuue! Huenda akatufaa au tumfanye kuwa mtoto wetu. Wala wao hawakutambua.
Kuburudika macho ni furaha. Mke wa Firauni ni Asiya bint Muzahim. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemsifu pale aliposema:
وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ آمَنُوا امْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِي عِندَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿١١﴾
“Na Mwenyezi Mungu amewapiga mfano walioamini – mke wa Firauni, aliposema: “Mola wangu! Nijengee kwako nyumba Peponi na uniokoe na Firauni na vitendo vyake na uniokoe na watu madhalimu.” (66:11).
Na katika Hadith imesemwa kuwa wanawake bora ni wane: Maryam binti Imran, Asiya binti Muzahim, Khadija bint Khuwaylid na Fatima bint Muhammad. Firauni alipomwangalia mtoto alishtuka na kusema, imekuaje huyu mtoto wa ki Hebrew amepona kuchinjwa? Majasusi hawakumuona au wamenificha?
Mkewe akamtuliza na akamfanya ampende mtoto ili awe kiburudisho cha macho yao, lakini akawa ni kero ya macho yao na huzuni ya nyoyo zao.
Moyo wa mamake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kudhihirisha, lau tusingeliuimarisha moyo wake ili awe miongoni mwa waumini.
Alimtupa mtoto wake baharini akiwa na matumaini ya kuukotwa na ambaye atamwepusha na Firauni. Mara kadari ikamtoa baharini hadi nyumbani kwa Firauni!
Alipopata habari kuwa ameanguka mikononi mwa mchinjaji, alijua mtoto wake amekwisha.
Akafazaika sana na akajisahau na ahadi aliyoahidiwa na Mungu kuwa atamrudisha kwake; akawa karibu adhihirishe fazaa yake kwa kutamka jina la kipenzi chake, lakini Mwenyezi Mungu akampa utuvu, akaufanya thabiti moyo wake ili awe miongoni mwa wanaoamini ahadi yake. Kwa hiyo akawa na subira na akatulia.
Akamwambia dadake (Musa), mfuatie na uchunguze habari yake.
Akaenda na akamkuta kwa Firauni.
Basi akawa anamwangalia kiupande upande na wao hawatambui.
Wengine wamefasiri alimwangalia kwa mbali.
Maana ni kuwa alimwangalia kama vile hataki wala hamkusudii yeye, huku watu wa Firauni hawajui lengo lake au kuwa yeye ni dada wa mtoto waliyemuokota ufukweni.
Na tukamharamishia wanyonyeshaji tangu mwanzo.
Firauni alimsikiliza mkewe, akamwacha mtoto baada ya Mwenyezi Mungu kutia mahaba moyoni mwake na akaamrisha atafutwe mnyonyeshaji atakayemlea na kumtunza.
Wakaletwa wanyonyeshaji kutoka huku na huko, kila mmoja anapendelea akubali matiti yake ili apate hadhi mbele ya Firauni. Lakini mtoto aliwakataa wote.
Akasema (dadake): Je, niwaonyeshe watu wa nyumba watakaowalelea na watakuwa wema kwake.
Dadake Musa alipoona kuduwaa kwa watu wa Firauni kuhusu mtoto alijitokeza kuwaelekeza atakayekubali matiti yake na kumshughulikia bila ya kuzembea. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:40).
Basi tukamrudisha kwa mama yake ili yaburudike macho yake.
Vile vile umetangulia mfano wake katika Juzuu hiyo hiyo.
Na ajue kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli.
Yaani mamake Musa ajue kuwa ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kurudishiwa mwanawe na kuwa miongoni mwa mitume, ni kweli.
Lakini watu wengi hawajui, mipangilio yake Mwenyezi Mungu Mtukufu na undani wa hekima yake.
4
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَاسْتَوَىٰ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٤﴾
14. Na alipofikilia kukomaa kwake na akastawi, tulimpa hukmu na elimu. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.
وَدَخَلَ الْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَـٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَـٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ فَوَكَزَهُ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ قَالَ هَـٰذَا مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ عَدُوٌّ مُّضِلٌّ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾
15. Na akaingia mjini wakati wenyeji wake wako kwenye mghafala. Akakuta humo watu wawili wanapigana – huyu ni katika kundi lake na huyu ni katika adui zake. Yule aliye katika kundi lake alimtaka msaada dhidi ya yule aliye katika adui zake. Musa akampiga, akammaliza. Akasema: Hiki ni kitendo cha shetani; hakika yeye ni adui mpotezaji dhahiri.
قَالَ رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي فَغَفَرَ لَهُ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿١٦﴾
16. Akasema: Mola wangu! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu, basi nisamehe. Akamsamehe; hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
قَالَ رَبِّ بِمَا أَنْعَمْتَ عَلَيَّ فَلَنْ أَكُونَ ظَهِيرًا لِّلْمُجْرِمِينَ ﴿١٧﴾
17. Akasema: Mola wangu! Kwa ulivyonineemesha, sitakuwa msaidizi wa wakosefu.
فَأَصْبَحَ فِي الْمَدِينَةِ خَائِفًا يَتَرَقَّبُ فَإِذَا الَّذِي اسْتَنصَرَهُ بِالْأَمْسِ يَسْتَصْرِخُهُ قَالَ لَهُ مُوسَىٰ إِنَّكَ لَغَوِيٌّ مُّبِينٌ ﴿١٨﴾
18. Akapambaukia mjini akiwa na hofu na hadhari, mara yule aliyemtaka msaada jana anampigia kelele. Musa akamwambia: Hakika wewe ni mpotevu dhahiri.
فَلَمَّا أَنْ أَرَادَ أَن يَبْطِشَ بِالَّذِي هُوَ عَدُوٌّ لَّهُمَا قَالَ يَا مُوسَىٰ أَتُرِيدُ أَن تَقْتُلَنِي كَمَا قَتَلْتَ نَفْسًا بِالْأَمْسِ إِن تُرِيدُ إِلَّا أَن تَكُونَ جَبَّارًا فِي الْأَرْضِ وَمَا تُرِيدُ أَن تَكُونَ مِنَ الْمُصْلِحِينَ ﴿١٩﴾
19. Basi Musa alipotaka kumkamata kwa nguvu, yule aliye adui yao akasema: Ewe Musa! Unataka kuniua, kama ulivyomuua mtu jana? Hutaki ila kuwa jabari katika ardhi, wala hutaki kuwa miongoni mwa wema.
Aya 14 – 19
Na alipofikilia kukomaa kwake na akastawi, tulimpa hukmu na elimu. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.
Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 12 (12:22). Kule imekuja kwa wasifu wa Yusuf na hapa ni wa Musa.
Na akaingia mjini wakati wenyeji wake wako kwenye mghafala. Akakuta humo watu wawili wanapigana – huyu ni katika kundi lake na huyu ni katika adui zake. Yule aliye katika kundi lake alimtaka msaada dhidi ya yule aliye katika adui zake. Musa akampiga, akam- maliza.
Makusudio ya mji hapa ni mji wa Misri.
Siku moja Musa aliingia mitaani bila ya kujulikana na yeyote. Akawaona watu wawili wanagombana na kupigana – mmoja ni Mkibti katika wafuasi wa Firauni na mwingine ni Mwisrail katika jamaa za Musa. Kwa ujumla Wakibti walikuwa wakiwakandamiza waisrail na wakiwahisabu ni watumishi na watumwa wao.
Basi yule Mwisrail akamtaka msaada Musa. Musa naye akampiga ngumi au fimbo kwa kukusudia kumtia adabu na kukinga dhulma, si kwa kukusudia kuua na yule akaanguka ni maiti. Huku kunaitwa kuua kimakosa.
Akasema: Hiki ni kitendo cha shetani; hakika yeye ni adui mpotezaji dhahiri.
Anakusudia kile kitendo cha kugombana wale wawili sio pigo alilopiga Musa. Maana ni kuwa mapigano baina ya wawili, chanzo chake ni wasi-wasi wa shetani na hadaa yake ya kuingiza kwenye uasi na madhambi.
Akasema: Mola wangu! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu, basi nisamehe. Akamsamehe; hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
Mitume na mawili wanajiona mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wapungufu. Hiyo ni katika aina ya kunyenyekea na dua. Hilo halifahamishi kuweko dhambi wala upungufu.
Kwa sababu anayemjua Mwenyezi Mungu kisawasawa huwa anaituhumu nafsi yake kuwa na upungufu wa kumtii Mwenyezi Mungu na kumwabudu.
Ndio maana humwomba msamaha wa dhambi. Wa kale walisema: “Uovu wa watu wema ni wema wa waovu.” Tazama tuliyoyaeleza kwa anuani ya ‘Toba na maumbile’ katika Juz. 4 (4:17-18).
Akasema: Mola wangu! Kwa ulivyonineemesha, sitakuwa msaidizi wa wakosefu.
Musa alimuomba msamaha Mola wake na akamwahidi kuwa atawapiga vita mataghuti na wakosefu; kama vile Firauni na jeshi lake na kumsaidia kila mumin.
Akapambaukia mjini akiwa na hofu na hadhari.
Musa alihofia kuuawa kwa sababu ya Mkibti na kutarajia shari kutoka kwa Firauni na watu wake.
Wakati akiwa katika hali hiyo, mara yule aliyemtaka msaada jana anampigia kelele. Anampigia kelele za kumtaka msaaada. Musa akamwambia: Hakika wewe ni mpotevu dhahiri.
Wewe kazi yako ni kugombana na Wakibti na kutusababishia matatizo. Hebu chunga upotevu wako!
Basi Musa alipotaka kumkamata kwa nguvu yule aliye adui yao,
Musa alitaka kumkamata Mkibti, kwa sababu wakibti ndio waliokuwa wakiwachokoza waisrail na kuwachukulia kuwa ni watumwa wao, kama tulivyoashiria mwanzo. Mkibti alidhani kuwa Musa anataka kumuua, kwa hiyo akasema:
Ewe Musa! Unataka kuniua, kama ulivyomuua mtu jana? Hutaki ila kuwa jabari katika ardhi, wala hutaki kuwa miongoni mwa wema.
Jana ulimuua mtu na leo unataka kuniua mimi, je wewe ni mbabe au mtu mwema? Hii inaashiria kwamba Musa alikuwa ni katika watu wema mwenye tabia nzuri na kwamba kuua hakuendani na tabia yake.
وَجَاءَ رَجُلٌ مِّنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ يَسْعَىٰ قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنَّ الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ النَّاصِحِينَ ﴿٢٠﴾
20. Na akaja mtu kutoka mwisho wa mji akaipiga mbio, akasema: Ewe Musa! Wakubwa wanapanga kukuua. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanaokupa nasaha.
فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ قَالَ رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢١﴾
21. Basi akatoka mjini akiwa na hofu na hadhari. Akasema: Mola wangu! Niokoe na watu madhalimu.
وَلَمَّا تَوَجَّهَ تِلْقَاءَ مَدْيَنَ قَالَ عَسَىٰ رَبِّي أَن يَهْدِيَنِي سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿٢٢﴾
22. Alipoelekea upande wa Madyana alisema: Asaa Mola wangu akaniongoza njia iliyo sawa.
وَلَمَّا وَرَدَ مَاءَ مَدْيَنَ وَجَدَ عَلَيْهِ أُمَّةً مِّنَ النَّاسِ يَسْقُونَ وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا قَالَتَا لَا نَسْقِي حَتَّىٰ يُصْدِرَ الرِّعَاءُ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ ﴿٢٣﴾
23. Alipoyafikia maji ya Madyana alikuta umati wa watu wakinywesha (wanyama wao), na akakuta nyuma yao wanawake wawili wanazuia (wanyama wao). Akasema: Mna nini? Wakasema: Hatunyweshi mpaka wamalize hao wachunga na baba yetu ni mzee sana.
فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ ﴿٢٤﴾
24. Basi akawanyweshea kisha akarudi kivulini na akasema: Mola wangu! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayoniteremshia.
فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا فَلَمَّا جَاءَهُ وَقَصَّ عَلَيْهِ الْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ نَجَوْتَ مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥﴾
25. Basi mmoja wa wale wanawake wawili akamjia naye anatembea akiona haya. Akasema: Baba yangu anakuita akulipe ujira wa kutunyweshea.Basi alipomjia na kumsimulia visa vyake, alisema: Usiogope; umekwishaokoka na watu madhalimu.
قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ ﴿٢٦﴾
26. Akasema mmoja katika wale wanawake: Ewe baba! Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumwajiri ni mwenye nguvu na mwaminifu.
قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَىٰ أَن تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِندِكَ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٢٧﴾
27. Akasema: Mimi ninataka kukuoza mmoja wa mabinti zangu hawa wawili kwa kunifanyia ajira ya miaka minane na kama ukitimiza kumi hiyari yako. Mimi sitaki kukutaabisha. Inshaallah utanikuta miongoni mwa watu wema.
قَالَ ذَٰلِكَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ أَيَّمَا الْأَجَلَيْنِ قَضَيْتُ فَلَا عُدْوَانَ عَلَيَّ وَاللَّـهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ ﴿٢٨﴾
28. Akasema: Hayo yamekwishakuwa baina yangu na yako. Muda wowote kati ya miwili nitakoumaliza nisifanyiwe ubaya na Mwenyezi Mungu ni wakili juu ya haya tunayoyasema.
Aya 20 – 28
Na akaja mtu kutoka mwisho wa mji akaipiga mbio, akasema: Ewe Musa! Wakubwa wanapanga kukuua. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanaokupa nasaha.
Firauni na wapambe wake walijua yaliyotokea baina ya Musa na Mkibti wa kwanza aliyemuua kimakosa na wa pili aliyemwambia unataka kuniua. Kwa hiyo wakashauriana kuhusu mambo ya Musa na kuazimia kumuua. Mmoja wa waumini alipojua hilo alikimbia kwa Musa kumpa habari na akamshauri awakimbie madhalimu.
Wafasiri wengi wamesema kuwa mumin huyu ni yule aliyeashiriwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu:
“Na akasema mumin aliyekuwa mmoja katika watu wa Firauni aliyeficha imani yake: Mtamuua mtu kwa kusema Mola wangu ni Mwenyezi Mungu naye amewajia na hoja zilizo wazi?” (40:28).
Basi akatoka mjini akiwa na hofu na hadhari. Akasema: Mola wangu! Niokoe na watu madhalimu.
Musa alitoka mjini bila ya maandalizi yoyote; hana chakula wala maji, au yeyote wa kuongozana naye. Alitoka kwa hadhari akihofia asionekane na chinjachinja wa Firauni. Zaidi ya hayo alikuwa hajui anakwenda wapi? Basi akamkimbilia Mola wake, akamwachia Yeye mambo yake na akamwomba kuongoka na kuokoka na Firauni na watu wake.
Alipoelekea upande wa Madyana alisema: Asaa Mola wangu akaniongoza njia iliyo sawa.
Musa alitembea bila ya kujua anakwenda wapi, lakini ana yakini kuwa Mola wake atamwongoza njia iliyo sawa ambayo itampelekea kuokoka na kufaulu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamshika mkono na kumwelekeza Madyana, mji wa Shua’yb, ambao baina yake na Misri pana masafa ya mwendo wa siku nane katika jangwa pana sana.
Basi Musa akakata mbuga kwa tawfiki ya Mwenyezi Mungu. Alikuwa akila mimea ya ardhini. Jana alikuwa ikulu ya Firauni akistarehe. Mimea ya ardhi na hofu ni bora mara elfu kwa wenye ikhlasi kuliko starehe pamoja na dhulma; kama alivyosema Imam Husein(a.s) : “Wallahi! Sioni mauti ila ni wema; na sioni kuishi pamoja na madhalimu ila ni uovu.”
Alipoyafikia maji ya Madayana alikuta umati wa watu wakinywesha (wanyama wao) na akakuta nyuma yao wanawake wawili wanazuia (wanyama wao). Akasema: Mna nini? Wakasema: Hatunyweshi mpaka wamalize hao wachunga na baba yetu ni mzee sana.
Mwendo wa Musa uliishia kwenye kisima. Akakuta kundi la watu waki-wanywesha maji wanyama wao na akawaona wanawake wawili pembeni wakiwa na kondoo wao wanataka kunywa maji, lakini wao wanawazuia.
Musa akashtuliwa na hali hii, akawauliza, kwa nini mnawazuia nao wana kiu? Wakasema sisi ni wanawake dhaifu, hatuwezi kusukumana na wanaume. Tunangoja mpaka wamalize ndio nasi tupate nafasi, na baba yetu ni mzee sana, hawezi kuja kuchota maji. Nafsi ya Musa ikataharaki kidini na kiubinadamu, akawasaidia.
Hakuna ajabu kwa Musa kuwasaidia wanawake dhaifu; wala si ajabu kwa Shua’yb na mabinti zake kuishi kwa jasho lao.
Hii ndiyo sera ya mitume na makhalifa wao wenye takua, tangu zamani na baadaye. Bali ajabu ni kuwa roho hii ya Qur’an haina athari yoyote katika nafsi zetu sisi tunaodai kumjua Mwenyezi Mungu, Kitabu chake, na sera ya mitume wake. Ajabu ya maajabu ni kwamba tunashindana katika kuitafuta dunia na mapambo yake.
Basi akawanyweshea, kisha akarudi kivulini na akasema: Mola wangu! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayoniteremshia.
Musa aliwapatia maji wanyama wa wasichana wawili, kisha akaenda chini ya mti kupata kivuli, akiwa na uchovu na njaa. Akamwomba Mwenyezi Mungu fadhila na ukarimu wake. Wala hakung’angania sana au kuomba zaidi, kwa sababu alichokitaka ni kuziba tumbo tu.
Kama angelikuwa anaomba akhera angeling’ang’ania. Katika Nahjul balagha imeelezwa: “Wallahi hakumuomba isipokuwa mkate wa kula tu. Rangi ya kijani ya majani ilikuwa ikionekana kwenye ngozi ya tumbo lake kwa wembamba wake na kutengana na nyama yake.”
Basi mmoja wa wale wanawake wawili akamjia naye anatembea akiona haya. Akasema: Baba yangu anakuita akulipe ujira wa kutunyweshea.
Wale wasichana wawili walirudi kwa baba yao na wakamwelezea yaliyotokea. Basi akamwambia mmoja wao: Nenda kamwite tuje tumlipe hisani yake. Basi akaenda msichana akiwa amegubikwa na haya, ustahi na heshima na kumweleza alivyosema baba yake.
Basi alipomjia na kumsimulia visa vyake, alisema: Usiogope; umekwishaokoka na watu madhalimu.
Musa alikubali mwito, na mzee akamkaribisha na kumshukuru kwa kitendo chake. Musa alipotulia na kumwamini yule mzee, alimsimulia yaliyompitia kwa Firauni na watu wake. Yule mzee akamwambia usihofu, umefika. Hapa kwetu ni ngome ya amani, haifikiwi na Firauni wala mfano wake katika madhalimu.
Wafasiri wametofautiana kuhusu mzee huyu ni nani? Wengi wao wamesema ni Shuaib na wengine wakasema siye. Hakuna ya kutegemewa kwa hawa wala wale. Nasi hatuna haja na tofauti hizi madam hazina uhusiano wowote na imani wala maisha.
Sisi tumechagua jina la Shua’yb kiasi cha kumwelezea huyo mzee tu, sio kuwa tumekubaliana na jina hilo na pia kwa kuwa ni jina liloenea kwa wengi; kama lilivoenea baina ya wanafunzi na ulamaa wa Najaf.
Akasema mmoja katika wale wanawake ambaye alimwita kwa baba yake: Ewe baba! Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumwajiri ni mwenye nguvu na mwaminifu.
Tunasema aliyesema ni yule aliyemwita kutokana na kauli yake ‘mwenye nguvu’ pale alipowasaidia kuchota maji na ‘mwaminifu’ pale alipokuwa na staha wakati wakielekea kwa baba yake.
Akasema: Mimi ninataka kukuoza mmoja wa mabinti zangu hawa wawili kwa kunifanyia ajira ya miaka minane na kama ukitimiza kumi hiyari yako. Mimi sitaki kukutaabisha. Inshaallah utanikuta miongoni mwa watu wema.
Musa mkimbizi, fukara asiyekuwa na chochote, ambaye kwa siku kadhaa, ameishi kwa kula mimea ya ardhi; mpaka akamuomba Mola wake tonge ya kumwezesha kuishi, leo anahiyarishwa kuchagua mke amtakaye. Bila shaka hapa kuna siri ya utu wa Musa na utukufu wake uliomgusa mzee na mabinti zake. Vile vile katika masimulizi yake na sera yake kwa Firauni na watu wake.
Mzee alitambua, kutokana na akili yake safi, kwamba mtu huyu atakuwa na athari ya mbali. Kwa sababu matendo ya mtu aghlabu yanatoka kwenye chimbuko moja. Kwa hiyo mzee, hapa alifuzu kutokana na ukwe huu. Kuna faida gani kubwa zaidi ya kuwa mkwe wa Mtume na mwenye takua.
Mafaqihi wamezungumza mengi kuhusiana na Aya hii, wakaitolea dalili kuwa walii wa mwanamke ndiye atakayetamka tamko la ndoa. Lakini ilivyo ni kuwa inafaa kwa mwanamume au mwanamke mwenyewe kutam- ka. Hilo linafahamika kimsingi bila ya kuhitaji nukuu. Shafii na Imamiya wamesema kuwa ndoa haifungiki isipokuwa kwa tamko la ziwaj na nikah. Hii ni baada ya kuiunganisha Aya hii, yenye tamko la nikah, na ile yenye tamko la ziwaj.
فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِّنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا ﴿٣٧﴾
“Basi Zaid alipokwisha haja naye tulikuoza wewe” (33:37).
Malik na Hambal wakasema pia ndoa inafungika kwa neno hiba, kutokana na Aya yenye neno hiba:
وَامْرَأَةً مُّؤْمِنَةً إِن وَهَبَتْ نَفْسَهَا لِلنَّبِيِّ ﴿٥٠﴾
“Na mwanamke mumin akijitoa mwenyewe kwa Nabii.” (33:50).
Hanafi naye akasema kuwa ndoa inafungika kwa neno lolote linalofahamisha kutaka kuoana.
Mafaqihi wengi wamesema kuwa muda wa kuchunga wanyama miaka minane au kumi haukuwa mahari au sehemu yake. Bali mahari yalikuwa mbali; na kwamba kauli ya mzee: “kunifanyia ajira” maana yake ni kuwa ukichunga wanyama kwangu kwa ajira, nitakuoza mmoja wa mabinti zangu kwa mahari; sawa na kusema: ‘Ukifanya hivi nami nitafanya hivyo.’
Haya ndio maana sahihi ya Aya. Kwa vyovyote iwavyo, hakuna hoja yoyote, katika Aya hii kwa, waliyoyasema mafaqihi. Kwa sababu hizo ni simulizi za sharia zilizotangulia. Nasi tuna uhakika kwamba sharia ya Kiisalmu imefuta sharia zote zilizotangulia, wala haifai kutumia hukumu yoyote miongoni mwa hukumu hizo zilizotangulia, isipokuwa kwa dalili maalum au ya kiujmla kutoka katika Kitab au Sunna. Na hapo itakuwa ni kukitumia Kitab au Sunna, sio kuitumia sharia hiyo.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ﴿٣٨﴾
“Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote.” Juz. 7 (6:38).
Na kauli yake:
وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ ﴿٨٩﴾
Na tumekuteremshia Kitabu hiki kubainisha kila kitu.” Juz.14: (16:89),
Yaani kila kitu katika misingi ya kiislamu na sharia yake.
Mtume(s.a.w.w) naye anasema: “Hakuna kitu kitakachowakurubisha nyinyi Peponi isipokuwa nimewaamrisha, na hakuna kitu kitakachowaweka mbali na moto isipokuwa nimewakataza.”
Akasema: Hayo yamekwishakuwa baina yangu na yako. Muda wowote kati ya miwili nitakoumaliza nisifanyiwe ubaya na Mwenyezi Mungu ni wakili juu ya haya tunayoyasema.
Haya ni maneno ya Musa. Muda wa kwanza ni Hijja nane na wa pili ni Hijja kumi. Maana ni kuwa Musa alimwambia mzee, nimekubali na kuridhia kuoa na kuchunga wanyama.
Mimi nitakuwa na hiyari ya kumaliza nane au kumi. Muda wowote nitakaoumaliza basi usiwe na hoja kwangu na Mwenyezi Mungu ndiye shahidi juu ya haya uliyojiwajibishia na niliyojiwajibishia.
Kuna Hadith isemayo kuwa Musa alichagua muda wa kumi. Wafasiri wengi wanasema kuwa yeye alimchagua mdogo naye ndiye aliyesema, baba yangu anakuita. Na pia kumwambia baba yake, hakika yeye ana nguvu na ni mwaminifu.
5
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى الْأَجَلَ وَسَارَ بِأَهْلِهِ آنَسَ مِن جَانِبِ الطُّورِ نَارًا قَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ جَذْوَةٍ مِّنَ النَّارِ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ ﴿٢٩﴾
29. Basi Musa alipomaliza muda wake na akasafiri na ahli zake, aliona moto upande wa mlima; akawaambia ahli zake: Ngojeni, mimi nimeona moto, pengine nitawaletea kutoka huko habari au kijinga cha moto mpate kuota.
فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ مِن شَاطِئِ الْوَادِ الْأَيْمَنِ فِي الْبُقْعَةِ الْمُبَارَكَةِ مِنَ الشَّجَرَةِ أَن يَا مُوسَىٰ إِنِّي أَنَا اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٣٠﴾
30. Basi alipoufikia aliitwa kutoka upande wa kulia wa bonde, katika eneo lilobarikiwa, kutoka mtini, kwamba ewe Musa! Hakika mimi ndiye Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe.
وَأَنْ أَلْقِ عَصَاكَ فَلَمَّا رَآهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَانٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ يَا مُوسَىٰ أَقْبِلْ وَلَا تَخَفْ إِنَّكَ مِنَ الْآمِنِينَ ﴿٣١﴾
31. Na kwamba, itupe fimbo yako! Alipoiona inatingishika, kama kwamba ni nyoka aligeuka kurudi nyuma wala hakungoja. Ewe Musa! Njoo mbele wala usihofu! Hakika wewe ni miongoni mwa waliosalimika.
اسْلُكْ يَدَكَ فِي جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ وَاضْمُمْ إِلَيْكَ جَنَاحَكَ مِنَ الرَّهْبِ فَذَانِكَ بُرْهَانَانِ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ ﴿٣٢﴾
32. Na ingiza mkono wako katika mfuko wako utatoka mweupe pasipo ubaya na vutia mkono wako kwako kutuliza hofu. Basi hizo ni dalili mbili kutoka kwa Mola wako kwa ajili ya Firauni na wakuu wake. Hakika wao ni watu mafasiki.
Aya 29 – 32
Baada ya kutimia muda walioafikana Musa na baba mkwe, alifungasha virago vyake na akelekea Misri pamoja na ahli zake. Katika Kamusi ya Kitabu kitakatifu, imeandikwa: “Musa alikwenda Misri pamoja na mkewe na wanawe wawili.”
Basi alipofika jangwani alipotea njia kwenye giza la usiku wenye baridi; kama inavyofahamisha kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Mpate kuota.” Wakati akiwa hajui la kufanya, mara akaona moto unawaka, ndipo akawaaambia watu wake, ningojeni niende kwenye ule moto niwaletee habari za njia au angalau niwaletee moto wa kuota. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:10) na Juz. 19 (27:7).
Basi alipoufikia aliitwa kutoka upande wa kulia wa bonde. Yaani upande wa kulia wa Musa.Katika eneo lilobarikiwa, kutokana na Mitume wengi kutokea huko na heri zake nyingi,kutoka mtini, kwamba ewe Musa! Hakika mimi ndiye Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe.
Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “kutoka mtini,” inafahamisha kwamba Mwenyezi Mungu aliumba maneno kwenye mti.
Wale wanaosema kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu ni ya kuzuka na wala siyo ya tangu zamani, wametoa dalili kwa Aya hii. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (19: 52) na (20: 12).
Na kwamba, itupe fimbo yako! Alipoiona inatingishika, kama kwamba ni nyoka aligeuka kurudi nyuma wala hakungoja. Ewe Musa! Njoo mbele wala usihofu! Hakika wewe ni miongoni mwa waliosalimika.
Umetangulia mfano wake katika Juz. Juz. 19 (27:10).
Na ingiza mkono wako katika mfuko wako utatoka mweupe pasipo ubaya na vutia mkono wako kwako kutuliza hofu. Basi hizo ni dalili mbili kutoka kwa Mola wako kwa ajili ya Firauni na wakuu wake. Hakika wao ni watu mafasiki.
Kuvutia mkono ni kuuweka kifuani;yaani hilo linatuliza hofu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 9 (7:108), Juz. 16 (20:22) na Juz. 19 (26:33) na (16:12).
قَالَ رَبِّ إِنِّي قَتَلْتُ مِنْهُمْ نَفْسًا فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ ﴿٣٣﴾
33. Akasema: Mola wangu! Hakika mimi nilimuua mtu katika wao, kwa hiyo nahofia wataniua.
وَأَخِي هَارُونُ هُوَ أَفْصَحُ مِنِّي لِسَانًا فَأَرْسِلْهُ مَعِيَ رِدْءًا يُصَدِّقُنِي إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ ﴿٣٤﴾
34. Na ndugu yangu Harun ni fasaha zaidi kwa ulimi kuliko mimi, basi mtume pamoja nami awe msaidizi. Hakika mimi nahofia watanikadhibisha.
قَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجْعَلُ لَكُمَا سُلْطَانًا فَلَا يَصِلُونَ إِلَيْكُمَا بِآيَاتِنَا أَنتُمَا وَمَنِ اتَّبَعَكُمَا الْغَالِبُونَ ﴿٣٥﴾
35. Akasema: Tutautia nguvu mkono wako kwa ndugu yako. Na tutawapa madaraka hawatawafikia. Kwa sababu ya ishara zetu, nyinyi na watakaowafuata mtashinda.
فَلَمَّا جَاءَهُم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا بَيِّنَاتٍ قَالُوا مَا هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّفْتَرًى وَمَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي آبَائِنَا الْأَوَّلِينَ ﴿٣٦﴾
36. Basi alipowafikia Musa na ishara zetu zilizo wazi wazi, walisema: Haya si chochote ila ni uchawi uliotungwa. Na hatukuyasikia haya kwa baba zetu wa zamani.
وَقَالَ مُوسَىٰ رَبِّي أَعْلَمُ بِمَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ مِنْ عِندِهِ وَمَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٣٧﴾
37. Na akasema Musa: Mola wangu ndiye anayemjua kabisa nani anayekuja na uwongofu kutoka kwake na ni nani atakayekuwa na mwisho mwema wa makazi. Hakika wenye kudhulumu hawatafanikiwa.
Aya 33 – 37
Akasema: “Mola wangu! Hakika mimi nilimuua mtu katika wao, kwa hiyo nahofia wataniua.”
Umetangulia mfano wake katika Juz. 19 (26:14).
Na ndugu yangu Harun ni fasaha zaidi kwa ulimi kuliko mimi, basi mtume pamoja nami awe msaidizi. Hakika mimi nahofia watanikadhibisha.
Hii inaashiria kuwa mwito wowote hauna budi uwe na wasaidizi. Na kwamba ilimu peke yake haitoshi kuitetea haki ikiwa haikwenda pamoja na ufasaha wa ulimi na ubainifu.
Vile vile Aya inafahamisha kuwa Qur’an inaunga mkono nyenzo za uenezaji habari; kama vile idhaa, magazeti n.k., lakini kwa sharti ya kuwa na mwelekeo wa kuithibitisha haki na kuwatetea watu wake na kuibatilisha batili na kuwatangaza wasaidizi wake; sawa na alivyoitumia Harun elimu yake na ufasaha wake dhidi ya utaghuti wa Firaun.
Imesemekana kuwa Harun ni mkubwa wa Musa kwa miaka mitatu. Sijui aliokoka vipi na kuchinjwa. Sio mbali kuwa Harun alizaliwa kabla ya Firauni kuamuru achinjwe kila mwana wa Israili atakayezaliwa. Katika Tawrat, kitabu cha Kutoka 32 imeelezwa kuwa Harun ndiye aliyewatengenezea wana wa israil ndama na kuwajengea dhabihu na wala sio Msamaria, kama ilivyoelezwa katika Qur’an Juz. 16 (20:95).
Akasema: Tutautia nguvu mkono wako kwa ndugu yako.
Mwenyezi Mungu alimwitikia Musa maombi yake, kama alivyotaka. Kauli ya Musa ya kuhofia kuuawa ameijibu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kusema:
Na tutawapa madaraka hawatawafikia. Kwa sababu ya ishara zetu, nyinyi na watakaowafuata mtashinda.
Katika Juz. 16, amesema: “Msiogope! Hakika mimi niko pamoja nanyi. Nasikia na ninaona,” na hapa akasema kuwa nitawapa silaha itakayomtisha Firauni na jeshi lake na mtaneemeka kwayo nyinyi na wale watakaowaamini. Silaha hii au madaraka hayo ni ishara na miujiza; kama vile fimbo kugeuka nyoka, mkono kuwa mweupe, nzige, chawa, vyura n.k.
Basi alipowafikia Musa na ishara zetu zilizo wazi wazi, walisema: Haya si chochote ila ni uchawi uliotungwa. Na hatukuyasikia haya kwa baba zetu wa zamani.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 9 (7:109) na Juz. 16 (20:63).
Na akasema Musa: Mola wangu ndiye anayemjua kabisa nani anayekuja na uwongofu kutoka kwake na ni nani atakayekuwa na mwisho mwema wa makazi. Hakika wenye kudhulumu hawatafanikiwa.
Walimkadhibisha Musa wakamwambia ni mchawi, akawajibu kwa jawabu la asiyejali kukadhibisha kwao na inadi yao, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na ahadi yake.
Kwa ufupi, jawabu ni kuwa Mwenyezi Mungu anajua kuwa mimi niko katika haki na uongofu na kwamba nyinyi mko kwenye batili na upotevu. Vile vile anajua kwamba mwisho mwema ni wangu na wanonifuata, nanyi mtapata mwisho wa maangamizi duniani na adhabu ya moto huko akhera.
وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ مَا عَلِمْتُ لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرِي فَأَوْقِدْ لِي يَا هَامَانُ عَلَى الطِّينِ فَاجْعَل لِّي صَرْحًا لَّعَلِّي أَطَّلِعُ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٣٨﴾
38. Na akasema Firauni: Enyi waheshimiwa! Sijui kama mnaye Mungu asiyekuwa mimi. Ewe Haman! Niwashie moto unichomee udongo, unijengee mnara nipate kumchungulia Mungu wa Musa na hakika mimi namuona yeye ni katika waongo.
وَاسْتَكْبَرَ هُوَ وَجُنُودُهُ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ إِلَيْنَا لَا يُرْجَعُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na akawa na kiburi yeye na majeshi yake katika nchi bila ya haki. Na wakadhani kuwa hawatarudishwa kwetu.
فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ ﴿٤٠﴾
40. Basi tukamshika yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini. Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa wenye kudhulumu.
وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ ﴿٤١﴾
41. Na tukawafanya ni maimamu waitao kwenye moto. Na siku ya Kiyama hawatanusuriwa.
وَأَتْبَعْنَاهُمْ فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ هُم مِّنَ الْمَقْبُوحِينَ ﴿٤٢﴾
42. Na tukawafuatishia laana katika dunia hii. Na siku ya Kiyama watakuwa miongoni mwa wanaokebehiwa.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ مِن بَعْدِ مَا أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ الْأُولَىٰ بَصَائِرَ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na hakika tulimpa Musa Kitabu, baada ya kuziangamiza karne za kwanza, ili kiwafumbue macho watu na kiwe uongofu na rehema ili wapate kukumbuka.
Aya 38 – 43
Na akasema Firauni: Enyi waheshimiwa! Sijui kama mnaye Mungu asiyekuwa mimi.
Alisema hivi kwa vile alipata wa kumsadiki. Nilihifadhi mithali tangu utotoni bado naikumbuka: “Firauni aliulizwa, ni nani Firauni wako? Akasema: Sijapata wa kunipinga”
Watu wengi wangelikuwa mafirauni lau kusingelikuweko upinzani. yatakuja maelezo katika Juz.30 (79:24).
Katika Kamusi ya Kitabu kitakatifu, imeelezwa kuwa neno Firauni ni la kimisri lenye maana ya nyumba kubwa nalo ni msimbo wa wafalme wa Misri.
Ewe Haman! Niwashie moto unichomee udongo, unijengee mnara nipate kumchungulia Mungu wa Musa na hakika mimi namuona yeye ni katika waongo.
Firauni alishindwa kuikabili hoja kwa hoja, akamuhofia Musa na fimbo yake. Akajaribu kuificha hofu yake hii na kushindwa kwake kwa kuwavun- ga watu wake kuhusu Musa, ndipo akadhihirisha shaka ya kuweko Mungu asiyekuwa yeye na kwamba yeye atamchunguza na kumtafuta. Akimpata atapambana naye; vinginevyo basi Musa atakuwa ni muongo.
Ili kusisitiza uvungaji huu machoni mwa wale walio bendera kufuata upepo, alimwambia Haman amwashie moto na atengeneze mnara mrefu utakaomwezesha kupanda mbinguni ili amtafute Mungu wa Musa.
Haman hakujenga mnara, kama tunavyodhani, kwa sababu ana yakini na vitimbi vya Firauni. Ni nani mwenye akili anayeweza kujaribu kujenga jengo lisilo na mwisho na kuwa na njozi za kuwa udongo na miti inaweza kufika kwenye mbingu za juu na kumjua aliyeko huko?
Na akawa na kiburi yeye na majeshi yake katika nchi bila ya haki. Na wakadhani kuwa hawatarudishwa kwetu.
Walijikweza juu ya watu, wakajivuna na wakaeneza ufisadi na shari. Sababu ya kwanza na ya mwisho ni kwamba wao hawamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, wala misingi na dhamiri. Hawaamini kitu chochote isipokuwa nafsi zao na manufaa yao. Kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu akawanyakua mnyakuo wa mwenye nguvu na uweza.
Basi tukamshika yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini. Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa wenye kudhulumu?
Mama yake Musa alimtupa mwanawe kwa kumhofia Firauni, lakini adui huyu wa Mungu na wa Musa akamuokota ili anufaike naye. Musa alipokuwa mkubwa alijaribu kwa juhudi zake kumnufaisha Firauni kwa kumuokoa na maangamizi na adhabu, lakini akakataa na kuwa na kiburi, ukawa mwisho wake ni kuangamia kwenye bahari ile ile aliyomuokota Musa. Katika hayo kuna mazingatio kwa wenye busara, lakini wako wapi?
Na tukawafanya ni maimamu waitao kwenye moto. Na siku ya Kiyama hawatanusuriwa.
Hao ni Firauni na majeshi yake. Maana ni kuwa wao, duniani wamepotea na kuwapoteza wengine na akhera ni wenye hasara.
Maana ya tumewajaalia ni kuwa Mwenyezi Mungu amepitisha kadari kuwa mwenye kufuata njia ya maangamizi basi ataangamia. Hilo tumelibainisha mara nyingi huko nyuma.
Imepokewa riwaya kutoka kwa Imam Jafar Assadiq(a.s) kwamba maimamu katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni aina mbili: Maimamu wa uongofu ambao amewaashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa kauli yake:
وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا ﴿٧٣﴾
“Na tukawafanya maimamu wakiongoza kwa amri yetu. ” Juz. 17 (21:73).
Hao wanatanguliza amri ya Mwenyezi Mungu kabla ya amri yao na hukumu yake kabla ya hukumu yao. Aina ya pili ni maimamu waitao kwenye moto, wakitanguliza amri yao kabla ya amri ya Mwenyezi Mungu na hukumu yao kabla ya hukumu ya Mwenyezi Mungu.
Vile vile wanachukua hawa zao kinyume na ilivyo katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu.
Na tukawafuatishia laana katika dunia hii. Na siku ya Kiyama watakuwa miongoni mwa wanaokebehiwa.
Duniani wana laana ya dunia, ya Mwenyezi Mungu na ya wenye kulaani na Akhera watapata adhabu ya moto.
Na hakika tulimpa Musa Kitabu, baada ya kuziangamiza karne za kwanza, ili kiwafumbue macho watu na kiwe uongofu na rehema ili wapate kukumbuka.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimtermshia Musa Tawrat baada ya kuangamizwa kaumu ya Nuh, A’d na Thamud.
Lengo la kuteremshwa kwake ni kuwapa mawaidha watu na kutumia hukumu yake. Kwa sababu Tawrat, kabla ya kupotoshwa ilikuwa ni nuru, mwongozo na rehema.
Lakini Tawrat ya leo inawambia Waisraili: “ Uweni wanaume, watoto na wanawake, isipokuwa bikra, wabakisheni kwa ajili ya kustarehe nao Na mpore wanyama na milki zote... Mchome miji makazi na makambi.” kama ilivyoelezwa Kitabu cha Hisabu 32.
Je, baada ya haya kuna haja ya kuuliza kwa nini Israil imeuchoma Msikiti wa Aqsa? Itikadi ya kiyahudi ni ya shari na uadui kwa dini zote, sharia na misimamo ya kiubinadamu.
6
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الْغَرْبِيِّ إِذْ قَضَيْنَا إِلَىٰ مُوسَى الْأَمْرَ وَمَا كُنتَ مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٤٤﴾
44. Wala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipompa Musa amri wala hukuwa miongoni mwa walioshuhudia.
وَلَـٰكِنَّا أَنشَأْنَا قُرُونًا فَتَطَاوَلَ عَلَيْهِمُ الْعُمُرُ وَمَا كُنتَ ثَاوِيًا فِي أَهْلِ مَدْيَنَ تَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا وَلَـٰكِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ ﴿٤٥﴾
45. Lakini tuliziumba karne na umri ukawa mrefu juu yao. Wala hukuwa mkaazi wa watu wa Madyana ukiwasomea Aya zetu, lakini ni sisi tuliokuwa tukiwatuma Mitume.
وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الطُّورِ إِذْ نَادَيْنَا وَلَـٰكِن رَّحْمَةً مِّن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أَتَاهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٤٦﴾
46. Wala hukuwa kando ya mlima tulipomuita. Lakini ni rehema itokayo kwa Mola wako ili uwaonye watu wasiofikiwa na muonyaji kabla yako, huenda wakakumbuka.
وَلَوْلَا أَن تُصِيبَهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَيَقُولُوا رَبَّنَا لَوْلَا أَرْسَلْتَ إِلَيْنَا رَسُولًا فَنَتَّبِعَ آيَاتِكَ وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na usije ukawasibu msiba kwa iliyoyatanguliza mikono yao, kisha waseme: Ewe Mola wetu! Mbona hukutuletea Mtume nasi tukafuata ishara zako na tukawa miongoni mwa waumini?
فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا لَوْلَا أُوتِيَ مِثْلَ مَا أُوتِيَ مُوسَىٰ أَوَلَمْ يَكْفُرُوا بِمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ قَالُوا سِحْرَانِ تَظَاهَرَا وَقَالُوا إِنَّا بِكُلٍّ كَافِرُونَ ﴿٤٨﴾
48. Ilipowajia haki kutoka kwetu walisema: Mbona hakupewa kama aliyopewa Musa? Je, hawakuyakataa aliyopewa Musa zamani? Walisema: ni wachawi wawili wanaosaidiana. Hakika tunawakataa wote.
قُلْ فَأْتُوا بِكِتَابٍ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ هُوَ أَهْدَىٰ مِنْهُمَا أَتَّبِعْهُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٩﴾
49. Sema: Basi leteni kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu chenye mwongozo zaidi kuliko viwili nikifuate, ikiwa nyinyi mnasema kweli.
فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكَ فَاعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَاءَهُمْ وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٠﴾
50. Na ikiwa hawakuitikii basi jua kuwa wamejifuatia tu hawaa zao. Na ni nani aliyepotea zaidi kuliko yule anayefuata hawaa yake bila ya mwongozo utokao kwa Mwenyezi Mungu? Hakika Mwenyezi Mungu hawongozi watu madhalimu.
وَلَقَدْ وَصَّلْنَا لَهُمُ الْقَوْلَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٥١﴾
51. Na kwa hakika tuliwafululizia maneno ili wapate kukumbuka.
Aya 44 -51
Wala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipompa Musa amri wala hukuwa miongoni mwa walioshuhudia.
Anaambiwa Muhammad(s.a.w. w ) . Makusudio ya upande wa magharibi ni upande wa magharibi mwa mlima, kama ilivyolezwa katika Tafsir Attabari, mahali alipozungumza Mwenyezi Mungu na Musa. Ama upande wa kuume ulioashiriwa kwenye Juz. 16 (19:52), ni upande wa kuumeni wa Musa. Makusudio ya amri aliyopewa Musa ni ni kuchaguliwa kwake kwa utume na unabii.
Maana ni kuwa kutoa habari Muhammad(s.a.w.w) matukio ya Musa upande wa magharibi mwa mlima ni dalili mkataa kuwa habari hizo ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu atakuwa amepata wapi elimu ya kujua hakika hiyo ya undani na wala hajaisoma katika Kitabu, kuisikia kwa yoyote wala kushuhudia yeye mwenyewe?.
Lakini tuliziumba karne na umri ukawa mrefu juu yao.
Makusudio ya karne ni umma zilizotangulia na kuisha kati ya zama za Musa na Muhammad ambapo kuna karibu mika elfu mbili. Tazama tuliyoyafafanua katika Aya ya 7 ya Juzuu na sura hii tuliyo nayo.
Maana ni kuwa hakukubakia yeyote wa kutoa habari za umma alizoziumba Mwenyezi Mungu baina ya zama za Musa na Muhammad. Na hii ni dalili wazi kuwa elimu ya Muhammad inatokana na wahyi utokao kwa Mwenyezi Mungu.
Kwa hiyo basi muda mwingi ulipita na watu wakawa kwenye ujinga wa wajinga, wakawa wanahitajia Nabii atakayewaongoza na kuwaelekeza kwenye njia ya sawa. Ndipo Mwenyezi Mungu akamtuma Muhammad kuwa mbashiri na muonyaji, akawapa habari za watu wa umma zilizotangulia na mitume yao kwa wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuwa ni dalili kwamba yeye ni Mtume kwa upande mmoja na ni mawaidha kwa upande wa pili.
Wala hukuwa mkaazi wa watu wa Madyana ukiwasomea Aya zetu, lakini ni sisi tuliokuwa tukiwatuma Mitume.
Madyana ni mji wa Shua’yb. Muhammad alimtolea habari Shua’yb, watu wake na watu wa mji wa Madyan; kama kwamba yeye ni Shua’yb akiwasomea watu wake Aya za Mwenyezi Mungu. Muhammad(s.a.w.w) hakuwa Mtume wa watu wa Madyana, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyempa habari hizo kwa kuwa yeye ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake na mwenye amana ya wahyi wake.
Wala hukuwa kando ya mlima tulipomuita.
Yaani hukuwako ewe Muhammad wakati Mwenyezi Mungu alipomuita Musa kando ya mlima.
Unaweza kuuliza kuwa : hakuna tofauti baina ya kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘kando ya mlima’ na ile iliyotangulia ‘upande wa magharibi.’ Sasa je, kuna makusudio gani ya kukaririka huku?
Jibu : Mwenyezi Mungu (s.w.t) alizungmza na Musa na kumwita zaidi ya mara moja. Kwa hiyo inawezekana kuwa Aya ya kwanza ni kuashiria mwito wa kwanza na Aya ya pili kuwa ni ya mwito wa pili. Zaidi ya hayo, kukaririka ni mfumo wa Qur’an. Tazama tuliyoyeleza kwa anuani ya
‘kukaririka katika Qur’an’ kwenye Juz. 1 (2:47 – 48) na Juz.5 (4:116 -122).
Lakini ni rehema itokayo kwa Mola wako ili uwaonye watu wasiofikiwa na muonyaji kabla yako, huenda wakakumbuka.
Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad kuwa ni rehema kwa walimwengu akionya na kutoa bishara kwa watu, ili wafuate njia itakayowapelekea kwenye wema wa nyumba mbili (Dunia na Akhera).
Unaweza kuuliza : Utaiunganisha vipi Aya hii na ile isemayo:
وَإِن مِّنْ أُمَّةٍ إِلَّا خَلَا فِيهَا نَذِيرٌ ﴿٢٤﴾
“Hakuna umma wowote ila alipata humo muonyaji.” (35:24).
Jibu : Tumesema mara nyingi kwamba Aya za Qur’an zinafasiriana, kwa sababu chimbuko lake ni moja. Kuna Aya isemayo:“Enyi watu wa Kitabu! Hakika amewafikia Mtume wetu anayebainishia, katika wakati usio na Mitume.” Juz. 6 (5:19), Yaani ulipokatika utumwaji mitume.
Kwa hiyo basi makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Wasiofikiwa na muonyaji kabla yako,” sio kuwa Mwenyezi Mungu hakupeleka mitume kabla ya Muhammad kabisa; bali makusudio ni kuwa hakufika mtume kwa kipindi fulani.
Na usije ukawasibu msiba kwa iliyoyatanguliza mikono yao, kisha waseme: Ewe Mola wetu! Mbona hukutuletea Mtume nasi tukafuata Ishara zako na tukawa miongoni mwa waumini?
Makusudio ya msiba ni adhabu ya Mwenyezi Mungu duniani. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) alipeleka mitume ili iwe ni hoja kwa watu pale itakapowafikia adhabu kwa sababu ya kufuru yao na utaghuti wao. Umepita mfano wake katika Juz. 6 (4:165) na (5:19).
Ilipowajia haki kutoka kwetu walisema: Mbona hakupewa kama aliyopewa Musa?
Mtume alipokuwa hajawajia walisema, akija tutuamwamini. Alipowajia wanatafuta visababu vya ubatilifu. Usumbufu na uhepaji huu hauhusiki na wale waliomkadhibisha Muhammad tu, waliomwambia Muhammad(s.a.w.w) : Lau ungekuja na fimbo na mkono mweupe wa Musa, tungelikuamini. Hapana! Haya ni mazowea ya mataghuti na wapenda anasa, kila wakati na kila mahali. Ni mazoweya ya wale ambao hawamini chochote isipokuwa masilahi yao na manufaa yao. Ndio wakawa vigeugeu na kuungana na shetani dhidi ya kila wema.
Je, kwani hao hawakuyakataa aliyopewa Musa zamani?
Walimtaka Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kuwaletea mfano wa miujiza ya Musa; ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawajibu kwamba mwenye kuitafuta haki kwa ajili ya haki anaifuata popote pale itakapom- bainikia. Lakini wale ambao hawaamini isipokuwa hawaa na matamanio yao na kuyafanya kuwa ndio mwongozo wao katika mambo yao yote, basi hawa haiwafai dalili na muujiza, uwe wa Musa au wa Muhammad au wa mitume wote.
Dalili ya hakika hii ni kuwa mataghuti waliyakataa aliyokuja nayo Musa; kama ambavyo mataghuti wa kikuraishi walikataa aliyokuja nayo Muhammad. Lau Musa na miujiza yake angelikuwa nafasi ya Muhammad, wangelisema: Lau Musa angelipewa mfano wa aliyopewa Muhammad. Hivi ndivyo walivyo wabatilifu, kila mhali na kila wakati.
Walisema: ni wachawi wawili wamesaidiana. Hakika sisi tunawakataa wote.
Makusudio ya wachawi wawili hapa ni Qur’an na Tawrat na kusaidiana ni kuwa kila moja inaisadikisha nyingine.
Maana ya kiujumla ni kuwa makuraishi walisema Tawrat ni uchawi na Musa ni mchawi. Vile vile wakasema Qur’an ni uchawi na Muhammad ni mchawi na kwamba wanazipinga zote mbili.
Sema: Basi leteni kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu chenye mwongozo zaidi kuliko viwili nikifuate, ikiwa nyinyi mnasema kweli.
Tawrat ni uchawi na mfano wake Qur’an pia ni uchawi, basi ikiwa mnacho kitabu kilicho na kheri kwa watu kuliko Tawrat na Qur’an basi kileteni na mimi nitakifuata na kukitumia. Huu ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ ﴿٨١﴾
“Sema: Ingelikuwa mwingi wa rehema ana mtoto basi ningelikuwa wa kwanza kumwabudu.” (43:81).
Na ikiwa hawakuitikii basi jua kuwa wamejifuatia tu hawaa zao.
Qur’an, kwa ufasaha na balagha yake, imeshinda fasihi na balagha zote. Na imeshinda misingi na mafunzo yote ya binadamu. Hakika Qur’an kwa itikadi yake na sharia yake, inaongoza kwenye usawa zaidi. Na hii ndiyo iliyo mikononi mwa wahakiki na wasomi. Basi na walete kilicho na mwongozo zaidi kwa watu kuliko hiyo au kilicho mfano wake na waite wanayemtaka na wanachokitaka.
Ikiwa watashindwa na wasiamini, basi watakuwa hawana dalili isipokuwa upofu na upotevu unaowaongoza kwenye uovu. Haya ndiyo makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
Na ni nani aliyepotea zaidi kuliko yule anayefuata hawaa yake bila ya mwongozo utokao kwa Mwenyezi Mungu? Hakika Mwenyezi Mungu hawongozi watu madhalimu baada ya kujiingiza wenyewe na kufuata njia ya maangamizi na upotevu.
Na kwa hakika tuliwafululizia maneno ili wapate kukumbuka.
Makusudio ya maneno hapa ni Qur’an ambayo imekwishatoa onyo, haina lawama. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaongoza waja kwenye yale wanayostahiki wao na yale yanayostahiki kwa wengine, ili wawe na utiifu na watende. Atakayetenda na akafanya uzuri, basi huyo yuko katika amani. Na adhabu ni ya mwenye kukadhibisha na akakataa.
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ مِن قَبْلِهِ هُم بِهِ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٢﴾
52. Wale ambao tuliwapa Kitabu kabla yake wanaiamini.
وَإِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ قَالُوا آمَنَّا بِهِ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّنَا إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلِهِ مُسْلِمِينَ ﴿٥٣﴾
53. Na wanaposomewa, husema: Tunaiamini. Hakika hiyo ni haki inayotoka kwa Mola wetu. Hakika sisi kabla yake tulikuwa waislamu (wanyenyekevu).
أُولَـٰئِكَ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُم مَّرَّتَيْنِ بِمَا صَبَرُوا وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٥٤﴾
53. Basi hao watapewa ujira wao mara mbili. Na wanaondoa ubaya kwa wema na wakatoa katika tuliyowaruzuku.
وَإِذَا سَمِعُوا اللَّغْوَ أَعْرَضُوا عَنْهُ وَقَالُوا لَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ لَا نَبْتَغِي الْجَاهِلِينَ ﴿٥٥﴾
55. Na wanaposikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu: Salamun alaykum! Hatuwataki wajinga.
Aya 52 – 55
Wale ambao tuliwapa Kitabu kabla yake wanaiamini.
Yaani waliopewa Kitabu kabla ya Qur’an wanaiamini hii Qur’an. Zimethibiti Hadith Mutawatir kwamba wanaswara (wakiristo) wengi na baadhi ya mayahudi walimwamini Muhammad(s.a.w.w) , kwa sababu Tawrat na Injili zimenukuu wasifu wake, kabla hazijapotolewa:
الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ ﴿١٥٧﴾
“Ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawrat na Injili” Juz. 9 (7:157)
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:121) na Juz. 4 (3:199).
Na wanaposomewa, husema: Tunaiamini. Hakika hiyo ni haki inayotoka kwa Mola wetu. Hakika sisi kabla yake tulikuwa waislamu (wanyenyekevu).
Maulama wa watu wa Kitabu walisoma sifa za Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na Qur’an Tukufu katika Tawrat na injil. Walizisoma hizo kabla ya kutumilizwa Muhammad(s.a.w.w) . Alipotumilizwa aliwasomea Qur’an wakaitambua na wakamtambua Muhammad kwa sifa zake, kama zilivyo katika vitabu viwili; sawa na walivyowajua watoto wao:
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ ﴿١٤٦﴾
“Wale tuliowapa Kitabu wanamjua kama wanavyowajua watoto wao.” Juz.1 (2:146).
Basi baadhi wakaamini na wengine wakaficha haki na hali wanajua, kwa kupupia vyeo na chumo.
Basi hao watapewa ujira wao mara mbili.
Wa kwanza ni kwa sababu ya ikhlasi yao katika dini yao ambayo imewaamrisha kumfuata Muhammad na Qur’an, na wa pili ni kwa walivyovumilia adha ya makafiri wapumbavu, kwa sababu kusilimu kwao kulikuwa ni hoja kubwa kwa yule anayeng’ang’ania ukafiri kwa inadi.
Na wanaondoa ubaya kwa wema.
Waislamu wa mwanzo walipambana na maudhi na mateso, kiasi ambacho Muhammad(s.a.w.w) alikuwa akizomewa na wapumbavu barabarani: “Huyoo mwenda wazimu... Huyoo mwongo... Huyoo mchawi!”
Wakawa na subira wakavumilia bila ya kulalamika. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameiita subira yao wema na maudhi ya washirikina akayaita ubaya.
Katika ibara hii kuna ishara kuwa silaha pekee ya mnyonge ni subira na kwamba hasira na kusimamisha mishipa ni wenda wazimu na kupigana bila ya silaha ni kujitia kitanzi.
Kwa hiyo subira ya mnyonge ni akili na hekima na ni ushujaa na werevu; kwa sharti ya kuhangaika na kufanya juhudi ya kuondoa huo unyonge na visababishi vyake. Lakini atakayebweteka na kufanya uvivu atakuwa amejitweza mwenyewe na kuridhia udhalili na unyonge.
Kwa maneno mengine ni kuwa unyonge ni kama ugonjwa, ni lazima utafutiwe dawa ya kuuondoa, sio kuvumilia kubaki na ugonjwa isipokuwa baada ya kushindwa kabisa na kukata tamaa.
Na wakatoa katika tuliyowaruzuku.
Wanaondoa shari ya uovu kwa kuvumilia. Pia wanafanya wema kwa kutoa kile wanachoruzukiwa na Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake. Imam Ali(a.s) anasema:Muadhibu ndugu yako kwa kumfanyia wema na urudishe uovu wake kwa kumneemesha.
Na wanaposikia upuuzi hujitenga nao.
Makafiri walianzisha matusi na shutuma kwa wale waliosilimu na kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wakavumilia na kujitia hamnazo,na husema: Sisi tuna vitendo vyete na nyinyi mna vitendo vyenu. Nyinyi mmeridhia batili mliyo nayo na sisi tumeridhia haki tuliyo nayo.
Salamun alaykum!
Wafasiri wamesema: Salamu hii ni ya kuwavumilia majahili sio ya maamkuzi; sawa na kumwambia unayetaka uepukane naye: “Niondokee kwa amani.
Hatuwataki wajinga.
Hatuchanganyiki nao wala hatuwi na hulka zao.
7
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾
56. Kwa hakika wewe humuongoi umtakaye, lakini Mwenyezi Mungu humuongoa amtakaye naye ndiye anayewajua zaidi waongokao.
وَقَالُوا إِن نَّتَّبِعِ الْهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفْ مِنْ أَرْضِنَا أَوَلَمْ نُمَكِّن لَّهُمْ حَرَمًا آمِنًا يُجْبَىٰ إِلَيْهِ ثَمَرَاتُ كُلِّ شَيْءٍ رِّزْقًا مِّن لَّدُنَّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٧﴾
57. Na wakasema: Tukifuata muongozo huu pamoja nawe, tutanyakuliwa kutoka nchi yetu. Je, kwani hatukuwaweka imara mahali patakatifu pa amani, panapoletwa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu? Lakini wengi wao hawajui.
وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ بَطِرَتْ مَعِيشَتَهَا فَتِلْكَ مَسَاكِنُهُمْ لَمْ تُسْكَن مِّن بَعْدِهِمْ إِلَّا قَلِيلًا وَكُنَّا نَحْنُ الْوَارِثِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na ni miji mingapi iliyojifaharisha maisha yake tumeiangamiza! Na hayo maskani yao hayakukaliwa tena baada yao ila kwa uchache tu. Na sisi ndio tumekuwa warithi.
وَمَا كَانَ رَبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ حَتَّىٰ يَبْعَثَ فِي أُمِّهَا رَسُولًا يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا وَمَا كُنَّا مُهْلِكِي الْقُرَىٰ إِلَّا وَأَهْلُهَا ظَالِمُونَ ﴿٥٩﴾
59. Na Mola wako haangamizi miji mpaka ampeleke Mtume katika mji wao mkuu awasomee Aya zetu. Wala hatuiangamizi miji mpaka watu wake wawe madhalimu.
وَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَزِينَتُهَا وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٠﴾
60. Na chochote mlichopewa ni matumizi ya maisha ya dunia na pambo lake. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndio bora na yatakayobaki zaidi. Basi je, hamfahamu?
أَفَمَن وَعَدْنَاهُ وَعْدًا حَسَنًا فَهُوَ لَاقِيهِ كَمَن مَّتَّعْنَاهُ مَتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ثُمَّ هُوَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنَ الْمُحْضَرِينَ ﴿٦١﴾
61. Je yule tuliyemuahidi ahadi nzuri tena naye akaipata, ni kama tuliyemstarehesha kwa starehe za maisha ya duniani na kisha siku ya Kiyama akawa miongoni mwa wanaohudhurishwa?
Aya 56 - 61
Kwa hakika wewe humuongoi umtakaye, lakini Mwenyezi Mungu humuongoa amtakaye, naye ndiye anayewajua zaidi waongokao.
Wametofautiana katika sababu ya kushuka Aya hii. Wakasema wafisri wengi katika Sunni kuwa ilishuka kwa ajili ya ami wa Mtume, Abu Twalib. Shia wakasema Aya haikumuhusu yeye wala mwinginewe. Mtume(s.a.w.w) anapenda kila mmoja aongoke, awe ni wa karibu naye au wa mbali naye. Herufi man, katika Aya ni ya kuenea.
Kuitumia Aya kwa kumhusu Abu Twalib peke yake, hiyo itakuwa ni kuyatumia maneno ya Mwenyezi Mungu bila ya dalili. Ama riyawa inayosema kuwa Aya imeshuka kwa Abu Twalib peke yake, hiyo haikuthibiti kwetu.
Kwa hiyo basi Aya hii itakuwa inarudufu Aya nyingine isemayo: “Je, wewe unaweza kuwaongoza vipofu ingawa hawaoni? Juz. 13 (10:43).
Mwenye Tafsiri Fii dhilal amerefusha maneno, kisha akaishia kwenye madhehebu ya mababa na mababu, akategemea dalili za wakale ingawaje zinapingana na maumbile ya kiakili.
Naye amekariri mara kadhaa kuwa Qur’an inazungumza na umbile la akili kwa undani. Nasi tutayahukumu maneno yake kwa mahakama ya maumbile ya kiakili na ya kimaudhui, sio ya kimadhehebu wala ya kiupendeleo. Tunamtarajia msomaji aangalie kauli yetu kwa mtazamo wa kielimu usiokuwa na upendeleo.
Anasema mwenye Fii dhilal, ninamnukuu: “Huyu ami wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , mlezi wake muhami wake na mgombezi wake, Mwenyezi Mungu hamwandikii imani, ingawaje anampenda sana Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mtume wa Mwenyezi Mungu naye anampenda sana, Mwenyezi Mungu hamwandikii kuamini.
Maana ya kauli hii ni kuwa Mwenyezi Mungu alichukia Abu Twalib kusema: Lailaha illa llah, Muhammadu rrasulullah (Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu), lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu alipenda na kung’ang’ani aseme kauli hii.
Tunauliza: Inaingilika akilini kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu apende jambo ambalo Mwenyezi Mungu analichukia? Basi kwa nini Mwenyezi Mungu ameilinganisha sawa twaa yake na ya Mtume, kwenye Aya kadhaa? Ikiwa Mwenyezi Mungu amechukia Abu Twalib asilimu na wala hakumwandikia kusilimu, basi kwanini amwadhibu na amuweke kwenye moto wa ‘juu juu’ kama walivyopokea wazushi? Je, inafaa mwenye nguvu kumwadhibu mnyonge kwa jambo ambalo hakulifanya? Itakuwaje na hali yeye ndiye alisema: “Na mimi si mwenye kuwadhulumu waja?”
Kwa nini Mwenyezi Mungu apende Abu Sufyani asilimu, lakini achukie kwa Abu Twalib? Ni kwa sababu Abu Sufyan alikuwa akimchukia sana Mtume, na kumkusanyia majeshi ya kumpiga vita, akapenda awe mwislamu, lakini Abu Twalib aliyempenda sana Mtume na kumuhami ndio akachukia kuwa mwislamu? Au ni kwa sababu Abu Sufyan ni mzazi wa Muawiya na Abu Twalib ni mzazi wa Ali?
Majibu ya maswali yote haya ni ndio kwa wale wanaodai kuwa Abu Twalib ni kafiri. Kwa sababu wao wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu hawajibikiwi na lolote na wala kwake hakuna jambo baya, na kwamba inafaa kwake kuwaadhibu wema; na wale wanaomwaga damu za watu kuwafanya ni wema.
Je, mwenye Fii dhilal alikusudia kuwa maana haya ndiyo yametokana na umbile la akili la ndani?
Zaidi ya hayo, kuandika tafsiri na isiyokuwa tafsiri kunaathirika na itikadi, mazingira, utamuduni na hali ya mwandishi. Na hili halimwachi mdogo wala mkubwa. Lakini hii haina maana kwamba itikadi na mapondokeo yote hayaafikiani na haki na hali halisi. Vinginevyo ingelikuwa muhali kauli ya haki na uadilifu. Ni wajibu kwa mtu kujitahidi kuitafuta haki kutokana na chimbuko lake, si kutokana na itikadi au mazingira. Na haya ndiyo tunayojaribu na kuyakusudia.
Misitari hii tunaiunganisha na tuliyoyaandika kuhusiana na maudhui haya katika Juz. 11 (9:113).
Na wakasema: Tukifuata muongozo huu pamoja nawe, tutanyakuliwa kutoka nchi yetu.
Kuna riwaya isemayo kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake! Jambo hili nitalitolea mwito kwa mweusi na mweupe, kwa aliye juu ya kilele cha mlima na aliye kwenye kilindi cha maji na nitawatolea mwito watu wa Fursi na Roma.”
Basi vigogo wa kikuraishi waliposikia maneno haya wakayakuza na kumwambia Mtume(s.a.w.w) ; “Vipi tukufuate na wewe nia yako ni hii. Kama tutakuitikia, basi kutakuwa na watu wengi wakiwemo wafursi na waroma na watachukua mali zetu na miji yetu na wataivunja Al-Kaa’ba vipande vipande.”
Iwe ni sahihi riwaya au la, lakini madhumuni yake yanendana na Aya hii. Kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alimlingani mweusi na mweupe, akaendelea na mwito wake. Vigogo wa kikuraishi wakampiga vita.
Zaidi ya hayo pia riwaya inaafikiana na kauli yake Mwenyezi Mungu inayofuatia:
Je, kwani hatukuwaweka imara mahali patakatifu pa amani, panapoletwa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu?
Vipi nyinyi watu wa Makka mnawahofia watu na hali Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameulinda mji wenu huu na mauaji na uporaji tangu siku ya kwanza? Na akajaalia nyoyo za watu zinauelekea mji huu wakileta kila aina ya matunda na mambo mazuri?
Lakini wengi wao hawajui kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameuhusisha mji huu na sifa hizi kuliko miji mingine.
Na ni miji mingapi iliyojifaharisha maisha yake tumeiangamiza! Na hayo maskani yao hayakukaliwa tena baada yao ila kwa uchache tu. Na sisi ndio tumekuwa warithi.
Walimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa tunawahofia watu kama tutakufuata wewe, akawajibu Mwenyezi Mungu, katika Aya iliyotangulia, kuwa mnahofia watu na hali Mwenyezi Mungu ameujalia mji wenu huu ni mtakatifu na wa amani?
Kisha katika Aya hii anawauliza, mnawahofia watu badala ya kumhofia Mwenyezi Mungu? Je, hampati mazingatio kwa umma zilizopita ambazo zilifanya jeuri na kuzikufuru neema za Mwenyezi Mungu, ndipo Mwenyezi Mungu akaziangamiza kwa sababu ya kuzikufuru neema zake, wakaacha miji yao ni magofu isipokuwa michache tu, lakini mingi ikawa haina warithi ila yule atakayeirithi ardhi na waliomo juu yake na kwake ndio marejeo.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:128).
Na Mola wako haangamizi miji mpaka ampeleke Mtume katika mji wao mkuu awasomee Aya zetu. Wala hatuiangamizi miji mpaka watu wake wawe madhalimu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni mwadilifu na ni hakimu hamwadhibu yoyote ila baada ya mawaidha na kuhadharishwa.
Unaweza kuuliza : Dhahiri ya Aya inaonyesha kuwa Mwenyezi Mungu hatumi Mtume katika miji midogo au kama akituma mtume basi watu wake hatawaadhibu kama hawatamsikiliza. Na hii haielekiani na misingi ya usawa katika taklifa na wajibu. Sasa itakuwaje?
Jibu : Aya imekuja kwenye mfumo wa aghlab. Kwani mitume wengi walitumwa kwenye miji mikubwa na kila Mtume alikuwa akituma muongoza- ji kwenye miji midogo. Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:6) na Juz. 12 (11:118).
Na chochote mlichopewa ni matumizi ya maisha ya dunia na pambo lake. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndio bora na yatakayobaki zaidi. Basi je, hamfahamu?
Matumizi mabaya ya maisha ya dunia ni yale yanayomfanya mtu kuwa jeuri na kueneza ufisadi. Vingenevyo hakuna uharamu wa mapambo ya Mwenyezi Mungu na riziki njema isipokuwa kwa asiyejua dini ya Mwenyezi Mungu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2: 103) na Juz.5 (4:77).
Je yule tuliyemuahidi ahadi nzuri tena naye akaipata, ni kama tuliyemstarehesha kwa starehe za maisha ya duniani na kisha siku ya Kiyama akawa miongoni mwa wanaohudhurishwa?
Mwenyezi Mungu aliwaahidi wale ambao wameamini na wakatenda mema Pepo ambazo hupita mito chini yake. Mwenyezi Mungu atatekeleza ahadi yake tu. Hakuna shaka kwamba mwenye kuneemeka na pepo ya milele hawezi kufananishwa na mwenye kustarehe hapa duniani kisha apelekwe Jahannam.
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٦٢﴾
62. Na siku atakapowaita na akasema: Wako wapi mliokuwa mkidai kuwa ni washirika wangu.
قَالَ الَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَغْوَيْنَا أَغْوَيْنَاهُمْ كَمَا غَوَيْنَا تَبَرَّأْنَا إِلَيْكَ مَا كَانُوا إِيَّانَا يَعْبُدُونَ ﴿٦٣﴾
63. Watasema wale iliyothibiti juu yao kauli: Mola wetu! Hawa ndio tuliowapoteza. Tuliwapoteza kama tulivyopotea sisi. Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi.
وَقِيلَ ادْعُوا شُرَكَاءَكُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ وَرَأَوُا الْعَذَابَ لَوْ أَنَّهُمْ كَانُوا يَهْتَدُونَ ﴿٦٤﴾
64. Na itasemwa: Waiteni waungu wenu wa kishirikina. Basi watawaita, lakini hawatawaitikia. Na wataiona adhabu; laiti wangelikuwa wameongoka.
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ ﴿٦٥﴾
65. Na siku atakapowaita na akasema: Mliwajibu nini Mitume.
فَعَمِيَتْ عَلَيْهِمُ الْأَنبَاءُ يَوْمَئِذٍ فَهُمْ لَا يَتَسَاءَلُونَ ﴿٦٦﴾
66. Basi zitawapotea habari siku hiyo. Nao hawataulizana.
فَأَمَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَعَسَىٰ أَن يَكُونَ مِنَ الْمُفْلِحِينَ ﴿٦٧﴾
67. Ama mwenye kutubu na akaamini na akatenda mema, asaa akawa miongoni mwa wenye kufanikiwa.
وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ سُبْحَانَ اللَّـهِ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٨﴾
68. Na Mola wako huumba na huteua atakavyo; hawana hiyari. Mwenyezi Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanaowashirikisha naye.
وَرَبُّكَ يَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٦٩﴾
69. Na Mola wako anayajua yaliyoficha vifua vyao na wanayoyatangaza.
وَهُوَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ لَهُ الْحَمْدُ فِي الْأُولَىٰ وَالْآخِرَةِ وَلَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٧٠﴾
70. Naye ni Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipokuwa yeye. Ni zake sifa njema, mwanzo na mwisho na hukumu ni yake na kwake yeye mtarejeshwa.
Aya 62 – 70
Na siku atakapowaita na akasema: Wako wapi mliokuwa mkidai kuwa ni washirika wangu.
Kesho Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawafufua waabudu mizimu, vyeo na mali awaulize kwa kuwatahayariza, wako wapi mliokuwa mkiwatumikia na kuwasafia matendo yenu badala ya Mwenyezi Mungu?
Watasema wale iliyothibiti juu yao kauli: Mola wetu! Hawa ndio tuliowapoteza. Tuliwapoteza kama tulivyopotea sisi. Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi.
Makusudio ya waliothibitikiwa na kauli ni viongozi wa ushirikina na upotevu. Makusudio ya kauli ni tamko la adhabu lilikuja katika Aya isemayo:
قَالُوا بَلَىٰ وَلَـٰكِنْ حَقَّتْ كَلِمَةُ الْعَذَابِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٧١﴾
“Lakini limekwishathibiti neno la adhabu juu yao” (39:71).
Neno ‘Hawa’ ni ishara ya wafuasi wadhaifu.
Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) wakati atakapowauliza washirikina, wako wapi washirika wangu, wanyonge watajibu: Ewe Mola wetu! Sisi tuliwatii wakubwa zetu wakatupoteza njia.
Wakubwa nao watasema: Hapana, hatukuwalazimisha kufuata ushirikina na upotevu, lakini tuliwaita nao wakaitikia kwa hiyari yao; sawa na sisi tuliyoyaitikia matamanio yetu na kuyatii.
Nasi tunajitenga nao na matendo yao. Hawakuwa wakituabudu sisi, isipokuwa walikuwa wakiabudu masanamu na mashetani.
Hivi ndivyo wanavyofanya watu wa masilahi, wanawadanganya wapumbavu na wajinga na kuwafanya ni njia ya kupatia mlengo yao; mpaka yakiwafika wanawaruka.
Hawa watawaambia kama atakavyosema shetani kesho:
وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا أَن دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنفُسَكُم ﴿٢٢﴾
“Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipokuwa niliwaita mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe” Juz. 13 (14:22)
إِنِّي بَرِيءٌ مِّنكُمْ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ وَاللَّـهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٤٨﴾
“Mimi si pamoja nanyi... Mimi namwogopa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu” Juz. 10 (8:48)
Na itasemwa: Waiteni waungu wenu wa kishirikina.
Itasemwa kesho kwa wasaidizi wa dhulma na wafuasi wao, wako wapi wale mliokuwa mkiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, waiteni waje wawaokoe na adhabu.
Basi watawaita, lakini hawatawaitikia.
Amedhoofika muombaji na anayeombwa.
Na wataiona adhabu; laiti wangelikuwa wameongoka.
Watajua kuwa adhabu inakuja tu. Hapo watatamani lau wangelikuwa waumini.
Na siku atakapowaita na akasema: Mliwajibu nini Mitume.
Mara ya pili Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawauliza kwa kukusudia kuwatahayariza kuwa niliwaletea mitume wangu wakawasomea Aya zangu na wakawaonya na kukutana kwenu na siku hii, basi mtafanya nini? Je, mliwaitikia na mkawatii au mliwapinga na kuwaasi?
Basi zitawapotea habari siku hiyo.
Watakuwa hawana la kujibu kwa jinsi watakavyopigwa na butwaa.
Nao hawataulizana.
Hawataulizana kuhusu litakalowaokoa na adhabu. Vipi wataulizana na hali wao wamekata tamaa na kila kitu.
Ama mwenye kutubu na akaamini na akatenda mema, asaa akawa miongoni mwa wenye kufanikiwa.
Hii ni desturi ya Qur’an – kuuunganisha kutaja utiifu na thawabu zake uasi na adhabu yake na kinyume chake.
Neno‘asaa’ katika maneno ya viumbe linafahamisha kutarajia kitu kinachopendwa na kuhurumia jambo linalochukiza. Ama katika maneno ya muumba linafahamisha ulazima na uhakika. Kwa hiyo basi ni uhakika kuwa mwenye kutubia aliye mwema ni katika wenye kufaulu na wenye kuridhiwa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Na Mola wako huumba na huteua atakavyo; hawana hiyari. Mwenyezi Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanaowashirikisha naye.
Mwenyezi Mungu ndiye muumba na ni mmliki, hakuna anayemiliki kitu kwake. Vitendo vyake vyote ni hekima, heri na usawa. Hakuna yeyote anayeweza kupinga na kutaaradhi, basi vipi wanamnasibishia washirikina?
Na Mola wako anayajua yaliyoficha vifua vyao na wanayoyatangaza.
Vile vile yeye ni mjuzi wa ghaibu na dhahiri na washirika wanaodaiwa hawajui kitu.
Naye ni Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipokuwa yeye peke yake, mwenye kustahiki ibada. Ni zake sifa njema, mwanzo na mwisho.
Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu duniani kutokana na fadhila zake na katika akhera kwa thawabu zake.
Na hukumu ni yake yenye kutokeza katika kila kitu. Na kwake yeye mtarejeshwa.
Wala haiwezekani kulikimbia hili. Mwema ni yule ambaye zitathibiti hoja zake na kukubaliwa udhuru wake.
8
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللَّـهُ عَلَيْكُمُ اللَّيْلَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِضِيَاءٍ أَفَلَا تَسْمَعُونَ ﴿٧١﴾
71. Sema: Mwaonaje, kama Mwenyezi Mungu angeliufanya usiku uwakalie moja kwa moja mpaka siku ya Kiyama, mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaletea mwangaza basi je, hamsikii.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللَّـهُ عَلَيْكُمُ النَّهَارَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِلَيْلٍ تَسْكُنُونَ فِيهِ أَفَلَا تُبْصِرُونَ ﴿٧٢﴾
72. Sema: Mwaonaje, kama Mwenyezi Mungu angeliufanya mchana uwakalie moja kwa moja mpaka siku ya Kiyama, mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaletea usiku mkapumzika humo? Basi je, hamwoni?
وَمِن رَّحْمَتِهِ جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٧٣﴾
73. Na katika rehema zake amewafanyia usiku na mchana mpate kupumzika humo na mtafute fadhila zake na ili mpate kushukuru.
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٧٤﴾
74. Na siku atakapowaita na akasema: Wako wapi mliokuwa mkidai kuwa ni washirika wangu.
وَنَزَعْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا فَقُلْنَا هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ فَعَلِمُوا أَنَّ الْحَقَّ لِلَّـهِ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٧٥﴾
75. Na tutatoa shahidi katika kila umma na tuseme: Leteni hoja zenu! Hapo watajua kwamba hakika haki ni ya Mwenyezi Mungu na yatawapotea yale waliyokuwa wakiyazua.
Aya 71 – 75
Sema: Mwaonaje, kama Mwenyezi Mungu angeliufanya usiku uwakalie moja kwa moja mpaka siku ya Kiyama, mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaletea mwangaza basi je, hamsikii.
Binadamu hufanya kazi na kupumzika kwa usingizi. Kazi inahitajia mwangaza na usingizi kwenye giza unakuwa mzito na unaleta siha ya mwili.
Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akaumba mchana kwa ajili ya kufanya kazi na usiku kwa ajili ya kupumzika. Lau usiku ungeliendelea bila ya asubuhi au mchana ukaendelea bila ya usiku basi maisha yangelikuwa balaa.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) alipotaja usiku amesema: ‘Hamsikii?’ na mchana akasema: ‘Hamuoni?’ kwa sababu usiku unanasibiana na kusikia na mchana kwa kuona.
Huko nyuma tumesema kuwa kufuatana usiku na mchana kunategemezwa moja kwa moja kwenye sababu zake za kimaumbile na kunategemezwa kwa Mwenyezi Mungu kwa kupitia hizo sababu, kwa vile yeye ndiye muumba wa ulimwengu na vilivyomo, na ndiye aliyeupangilia vizuri kwa hekima yake.
Na katika rehema zake amewafanyia usiku na mchana mpate kupumzika humo na mtafute fadhila zake na ili mpate kushukuru.
Yaani amewafanyia usiku mpumzike na amewafanyia mchana mtafute. Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:67), Juz. 15 (17:12) na Juz. 19 (25:47).
Na siku atakapowaita na akasema: Wako wapi mliokuwa mkidai kuwa ni washirika wangu.
Imetangulia punde tu katika Sura hii tuliyo nayo Aya 62. hatujui wajihi wa kukaririka huku isipokuwa kuthibitisha na kusisitiza.
Na tutatoa shahidi katika kila umma na tuseme: Leteni hoja zenu!
Kesho Mwenyezi Mungu (s.w.t) kila umma atauletea nabii wao atoe ushahidi juu yao kuwa alifikisha ujumbe na aeleze upinzani alioupata na kukadhibishwa baada ya kuwawasilishia hoja na kukata nyudhuru zote. Hapo Mwenyezi Mungu (s.w.t) atasema Mtume amenieleza yake, haya nanyi elezeni yenu na kile kilichowafanya muwakadhibishe; sawa na hakimu anavyofanya–kwanza anamsikiliza mwenye madai kisha mshatikiwa anajibu.
Hapo wataziba mdomo wabatilifu na adhabu itawastahili. Umetangulia mfano wake katika Juz. 2 (2:143), Juz. 14 (16:89).
Hapo watajua kwamba hakika haki ni ya Mwenyezi Mungu.
Yaani watajua kuwa hoja ya Mungu itawasimamia juu yao na wao hawatakuwa na hoja kwa Mwenyezi Mungu.
Na yatawapotea yale waliyokuwa wakiyazua, kuwa Mwenyezi Mungu ana mshirika na uwongo walioueneza juu ya watu wema.
إِنَّ قَارُونَ كَانَ مِن قَوْمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيْهِمْ وَآتَيْنَاهُ مِنَ الْكُنُوزِ مَا إِنَّ مَفَاتِحَهُ لَتَنُوءُ بِالْعُصْبَةِ أُولِي الْقُوَّةِ إِذْ قَالَ لَهُ قَوْمُهُ لَا تَفْرَحْ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْفَرِحِينَ ﴿٧٦﴾
76. Hakika Qaruni alikuwa katika kaumu ya Musa, lakini aliwafanyia dhulma. Na tulimpa hazina ambazo funguo zake ziliwaelemea kundi la watu wenye nguvu. walipomwambia watu wake: Usijigambe, hakika Mwenyezi Mungu hapendi wanaojigamba.
وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّـهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللَّـهُ إِلَيْكَ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ ﴿٧٧﴾
77. Na utafute kwa aliyokupa Mwenyezi Mungu makazi ya akhera; wala usisahau fungu lako la dunia. Na fanya wema kama alivyokufanyia wema Mwenyezi Mungu, wala usitafute ufisadi katika ardhi; hakika Mwenyezi Mungu hapendi wafisadi.
قَالَ إِنَّمَا أُوتِيتُهُ عَلَىٰ عِلْمٍ عِندِي أَوَلَمْ يَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَهْلَكَ مِن قَبْلِهِ مِنَ الْقُرُونِ مَنْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُ قُوَّةً وَأَكْثَرُ جَمْعًا وَلَا يُسْأَلُ عَن ذُنُوبِهِمُ الْمُجْرِمُونَ ﴿٧٨﴾
78. Akasema: Kwa hakika nimepewa haya kwa sababu ya elimu niliyo nayo. Je, hakujua kwamba Mwenyezi Mungu amekwishaangamiza karne zilizokuwa kabla yake waliokuwa na nguvu zaidi kuliko yeye na wenye makundi makubwa zaidi. Na wakosefu hawataulizwa dhambi zao.
فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ فِي زِينَتِهِ قَالَ الَّذِينَ يُرِيدُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إِنَّهُ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ ﴿٧٩﴾
79. Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale waliokuwa wanataka maisha ya duniani: Laiti tungelikuwa nayo kama aliyopewa Qaruni! Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa.
وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّمَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا وَلَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الصَّابِرُونَ ﴿٨٠﴾
80. Na wakasema wale ambao wamepewa elimu: Ole wenu! Thawabu za Mwenyezi Mungu ni bora kwa mwenye kuamini na akatenda. Na wala hawatapewa isipokuwa wenye subira.
فَخَسَفْنَا بِهِ وَبِدَارِهِ الْأَرْضَ فَمَا كَانَ لَهُ مِن فِئَةٍ يَنصُرُونَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُنتَصِرِينَ ﴿٨١﴾
81. Basi tukamdidimiza yeye na nyumba yake ardhini; wala hapakuwa na kundi lolote la kumsaidia kinyume na Mwenyezi Mungu wala hakuwa miongoni mwa wanaojisaidia.
وَأَصْبَحَ الَّذِينَ تَمَنَّوْا مَكَانَهُ بِالْأَمْسِ يَقُولُونَ وَيْكَأَنَّ اللَّـهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ لَوْلَا أَن مَّنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا لَخَسَفَ بِنَا وَيْكَأَنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na wakawa wanasema wale waliotamani mahala pake jana: Kumbe Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, katika waja wake, na humdhikisha amtakaye. Asingetufanyia hisani Mwenyezi Mungu angelitudidimiza. Kumbe makafiri hawafanikiwi.
Aya 76 – 82
Hakika Qaruni alikuwa katika kaumu ya Musa, lakini aliwafanyia dhulma. Na tulimpa hazina ambazo funguo zake ziliwaelemea kundi la watu wenye nguvu.
Qaruni alikuwa katika wana wa Israil, kwa sababu yeye alikuwa katika kaumu ya Musa. Inasemekana alikuwa ni binamu yake. Yeye ndiye aliyeweka jiwe la msingi la ubepari wa ukandamizaji au alikuwa ni mwakilishi wake. Kwa sababu yeye alihodhi na akawatawala watu wake, akilitetea hilo kwa kauli yake: “Nimepewa haya kwa sababu ya elimu niliyo nayo,” kama zinazosema Aya zinazofuatia.
Haya ndio madhehebu ya kiuchumi yasemayo: Mtu binafsi kwanza, kisha ndio jamii. Vile vile yanaashiriwa na Aya hii tuliyo nayo, pale ilipokutanisha dhulma na hazina ya mali. Kuna dhulma gani zaidi kuliko kuwa chakula cha viumbe kimezuiwa na mtu au baadhi ya watu mpaka watake wao?
Watu wa Qaruni walijaribu kumkemea kwa njia nzuri, walipomwambia watu wake: Usijigambe, hakika Mwenyezi Mungu hapendi wanaojigamba.
Vipi unafurahi na mali na kuhadaika nayo na kuifanya ni nyenzo ya dhulma, uadui, anasa na israfu, na karibu yako watu wanakufa njaa? Je unajigamba kwa uweza wako wa kufanya dhambi na uovu?
Na utafute kwa aliyokupa Mwenyezi Mungu makazi ya akhera.
Jitahidi na ufanye kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa kila alichokupa Mwenyezi Mungu katika mali siha na akili. Kwani mtu atakuwa na majukumu na kuulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuhusiana na mwili jinsi alivyoutumia, umri wake jinsi alivyoumaliza na mali yake jinsi alivyoichuma na kuitumia.
Wala usisahau fungu lako la dunia.
Usiache mahitaji ya maisha yako na starehe zako. Kula unavyotaka katika vizuri na vya halali na uvae unavyopenda katika nguo nzuri, lakini kutokana na jasho lako sio la wengine. Kwa kufanya hivi utakuwa umepata mafungu mawili: Fungu la dunia na la akhera.
Na fanya wema kama alivyokufanyia wema Mwenyezi Mungu.
Mche Mwenyezi Mungu kwa aliyokuneemesha na umshukuru kwa wema huo kwa waja wake na watu wake; usaidiane nao kwenye yale yaliyo na kheri nawe na wao.
Wala usitafute ufisadi katika ardhi, kwa kufanya jeuri, hiyana, kiburi, ubabe na kufanya israfu na hali kando yako kuna wanaokufa njaa. Huu ndio ufisadi hasa na hakika Mwenyezi Mungu hapendi wafisadi na amewandalia adhabu chungu.
Akasema kwa hakika nimepewa haya kwa sababu ya elimu niliyo nayo.
Yaani mali aliyo nayo imetokana na elimu yake, kipawa chake na ujanja wake. Kwamba mtu anaweza kuitumia elimu yake na kipawa chake kupora, kuiba, kuua na kuwatoa watu katika miji yao.
Hii sio bid’a ya Qaruni peke yake. Serikali ya U.S.A. imeweka mpango wa kununua akili na vipawa kutoka pembe zote za ulimwengu na kuwafanya wataalamu na wajuzi wahamie huko.
Mpango huu wameuita ‘Brain drain;’ yaani kunyonya akili. Lengo la hilo ni kutumia vipawa vya binadamu kupora mali za nchi na vyakula vya waja mashiriki ya ardhi na magharibi yake.
Je, hakujua kwamba Mwenyezi Mungu amekwishaangamiza karne zilizokuwa kabla yake waliokuwa na nguvu zaidi kuliko yeye na wenye makundi makubwa zaidi.
Vipi atajua naye mali na jaha zimemfurisha kichwa, ikampofusha na mwisho wa dhulma na ikamsahaulisha na aliyoyasikia kuhusu karne zilizopita–kwamba zilikuwa na mali na watu wengi zaidi kuliko yeye, lakini walipokiuka mipaka na kufanya dhulma, Mwenyezi Mungu aliwaonjesha adhabu ya kufedheheka duniani na adhabu ya akhera ni kali na ya kufedhehesha zaidi.
Wafasiri wametolea mfano wa kaumu ya Nuh, A’d na Thamud. Kama ningelikuwa wakati wao nigekubaliana nao, nao kama wangelikuwa wakati wangu wangelitosheka na yaliyotokea Libya mwezi huu ninapoandika maneno haya, Septemba1969, ambapo kuna kundi la vijana limempindua mfalme aliyekuwa na nguvu na utajiri kuliko Qaruni, akiwa anasaidiwa na uzayuni na ukoloni. Wamemng’oa na wakachukua madaraka. Vijana hawa waliteswa na mfalme, wakafungwa na kufukuzwa.
Na wakosefu hawataulizwa dhambi zao.
Yaani Mwenyezi Mungu atawaadhibu bila ya hisabu.
Unaweza kuuliza : Aya hii tutaiunganisha vipi na Aya isemayo:
فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٩٢﴾ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٩٣﴾
“Naapa kwa Mola wako, tutawauliza wote yale waliyokuwa wakiyatenda.” Juz. 14 (15:92-93).
Pamoja na Aya nyingine kadhaa zenye maana hiyo?
Jibu : Makusudio ya wakosefu hapa, kulingana na mfumo wa maneno ulivyo, ni wale waliozikosea haki za watu na uhuru, wakazusha fitna na vita kwa ajili ya masilahi yao na manufaa yao. Hawa ndio ambao wataingia motoni bila ya hisabu.
Kwa hiyo kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Hawataulizwa dhambi zao’ inawavua kutoka wale watakoulizwa wote. Yaani kama tutaziunganisha kauli mbili, maana yatakuwa: Tutawauliza wote isipokuwa waliozikosea haki za watu; wao wataingia motoni bila yamaswali.
Basi akawatokea watu wake katika pambo lake.
Watu wake walimpa hadhari ya mwisho mbaya, lakini shetani akampuzia kwenye pua yake, kiburi kikampanda, akawakusanya watumishi wake na wapambe wake. Akapanda kipando cha fahari, kuwaonyesha watu utajiri wake na kiburi chake, kuwaonyesha wale waliomuhadharisha na kumpa mawaidha kutokana na ulevi wa starehe na dhulma.
Wakasema wale waliokuwa wanataka maisha ya duniani: Laiti tungelikuwa nayo kama aliyopewa Qaruni! Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa.
Wadhaifu wa akili walitazama mali na vipambo, wakasahau mwisho wa uovu na kiburi, na wakatamani kuwa na starehe kama za Qaruni ili waangamie kwenye starehe na anasa. Lau wangeliangalia kwa mtazamo wa busara wangelisema kama walivyosema wenye elimu:
Na wakasema wale ambao wamepewa elimu: Ole wenu! Thawabu za Mwenyezi Mungu ni bora kwa mwenye kuamini na akatenda. Wala hawatapewa isipokuwa wenye subira.
Yaani watu wa elimu waliwaambia wale madhaifu wa akili, hayo mnayoyatamka ni ushetani na kwamba vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ni bora na vyenye kubaki.
Yeyote anayemtukuza asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi hudhalilika na kuhizika. Amesema Imam Aliy(a.s) : “Ni mara ngapi aliyepungukiwa akapata faida na aliyezidishiwa akapata hasara” Nahjul Balagha Khutba na 114.
Basi tukamdidimiza yeye na nyumba yake ardhini; wala hapakuwa na kundi lolote la kumsaidia kinyume na Mwenyezi Mungu wala hakuwa miongoni mwa wanaojisaidia.
Dhalimu hawezi kuokoka na kudidimia duniani kabla ya Akhera. Si lazima kudidimia kuwe ni kuzama ardhini, inaweza kuwa ni kwa kufedheheka na kulaaniwa na viumbe wenye kudhulumiwa na kunyimwa haki zao.
Uzoefu unatufahamisha kuwa dhalimu akipatikana na wenye kulipiza kisasi na kutaka haki zao, basi watu wote hujitenga naye; hata wale wasaidizi wake na ndugu zake na kujiona kuwa amedimimia.
Na wakawa wanasema wale waliotamani mahala pake jana: Kumbe Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, katika waja wake, na humdhikisha amtakaye. Asingetufanyia hisani Mwenyezi Mungu angelitudidimiza. Kumbe makafiri hawafanikiwi.
Jana wale wadhaifu wa akili walikuwa wakisema tunatamani kuwa na aliyo nayo Qaruni, kwa vile walikuwa na mtazamo wa dunia na starehe zake; wakasahau hatima ya dhulma na kiburi. Leo wameshuhudia matokeo ya uovu yakimtokea Qaruni.
Wametambua uhakika na wakamsifu Mwenyezi Mungu ambaye hakuwapa kama walivyopewa mataghuti.
Katika Nahjul Balagha, imesemwa: “Ni upungufu mngapi umekuwa faida na ziada ngapi zimekuwa ni hasara?” Kuanzia hapa ndio ikasemwa: ‘Mambo ni mwisho wake.’
تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٨٣﴾
83. Hayo ndiyo makazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasiotaka kujitukuza duniani wala ufisadi. Na mwisho ni wa wenye takua.
مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَى الَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٤﴾
84. Atakayetenda mema atapata malipo bora kuliko hayo. Na atakayetenda uovu, hawalipwi watendao uovu ila waliyokuwa wakiyatenda.
إِنَّ الَّذِي فَرَضَ عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لَرَادُّكَ إِلَىٰ مَعَادٍ قُل رَّبِّي أَعْلَمُ مَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ وَمَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٨٥﴾
85. Hakika aliyekulazimisha Qur’an, bila shaka atakurudisha mahali pa marejeo. Sema: Mola wangu ndiye anayemjua zaidi mwenye kuja na uongofu na aliyemo katika upotofu ulio dhahiri.
وَمَا كُنتَ تَرْجُو أَن يُلْقَىٰ إِلَيْكَ الْكِتَابُ إِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ ظَهِيرًا لِّلْكَافِرِينَ ﴿٨٦﴾
86. Nawe hukuwa unatarajia kuletewa Kitabu lakini ni rehema ya Mola wako. Basi usiwe kabisa msaidizi wa makafiri
وَلَا يَصُدُّنَّكَ عَنْ آيَاتِ اللَّـهِ بَعْدَ إِذْ أُنزِلَتْ إِلَيْكَ وَادْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٨٧﴾
87. Wala wasikuzuie na Aya za Mwenyezi Mungu baada ya kuteremshiwa, na lingania kwa Mola wako, wala usiwe kabisa miongoni mwa washirikina.
وَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ لَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٨٨﴾
88. Wala usimwombe pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwingine. Hapana Mungu ila Yeye. Kila kitu kitaangamia isipokuwa dhati yake, hukumu ni yake na kwake Yeye mtarejeshwa.
Aya 83 – 88
Hayo ndiyo makazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasiotaka kuji- tukuza duniani wala ufisadi. Na mwisho ni wa wenye takua.
Kujitukuza katika ardhi ni kujiweka juu na kuwatawala watu bila ya haki. Ufisadi ni dhulma, uadui, ufuska na uovu.
Maana ni kuwa mwenye kujikweza na kujitukuza kwa watu au kutumia vibaya haki zao, basi Mwenyezi Mungu amemharamishia Pepo na makazi yake ni Jahannam ni makazi mabaya.
Atakayetenda mema atapata malipo bora kuliko huo. Na atakayeten- da uovu, hawalipwi watendao uovu ila waliyokuwa wakiyatenda.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (6160).
Hakika aliyekulazimisha Qur’an, bila shaka atakurudisha mahali pa marejeo.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamwambia Mtume wake kuwa aliyekuwajibishia kuitumia Qur’an ndiye atakayekurudisha Makka walikokutoa watu wako.
Inasemekana kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alipohama Makka kuelekea Madina, akiwa njiani aliutamani, mji wake. Ndipo ikashuka Aya hii kumbashiria kurudi.
Sema: Mola wangu ndiye anayemjua zaidi mwenye kuja na uongofu na aliyemo katika upotofu ulio dhahiri.
Yaani sema ewe Muhammad kumwambia yule usiyemtarajia kuongoka na kung’ang’ania kuwa yeye ni muongofu na wewe ni mpotevu kuwa ni Mwenyezi Mungu peke yake anayeweza kumpambanua muongofu na mpotevu na mwema na muovu. Na atamlipa kila mmoja stahiki yake.
Nawe hukuwa unatarajia kuletewa Kitabu lakini ni rehema ya Mola wako.
Hii ni kumrudi yule aliyemwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu: Wewe si Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, bali unamzulia.
Ubainfu ni kuwa, vipi wanakwambia kuwa wewe ni mzushi na hali hukuwahi hata kuwazia hilo hata siku moja; isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye aliyekuneemesha na akakuteua wewe badala ya wengine?
Basi usiwe msaidizi wa makafiri. Wala wasikuzuie na Aya za Mwenyezi Mungu baada ya kuteremshiwa, na lingania kwa Mola wako, wala usiwe miongoni mwa washirikina. Wala usimwombe pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwingine. Hapana Mungu ila Yeye.
Mwenyezi Mungu amekuteua wewe ewe Muhammad ili uwapige vita wala usiwasaidie. Vile vile amekuchagua kufikisha ujumbe wake kwa waja wake, wala usilaumiwe kwa kuufikisha ujumbe; na umfanyie ikhlasi Mwenyezi Mungu peke yake kwenye kauli zako na vitendo vyako.
Huko nyuma wakati tukifasiri aina ya Aya kama hii inayomwambia maasum kuwa asifanye dhambi tulisema kuwa aliye juu anaweza kumkataza aliye chini kwa aina yoyote ya makatazo anayotaka; kuongezea kuwa jambo linalokatazwa sio lazima anayekatazwa awe anaweza kulifanya.
Hivi sasa tukifasiri Aya hizi, tumepata maana nyingine zaidi. Nayo ni kuwa aina hii ya Aya ni kufichua habari za wenye vilemba na kofia wanaojionyesha kuwa ni watu wa dini kumbe ni askari na wasaidizi wa makafiri waovu na kuelezea hali yao leo na kabla ya leo.
Tumehusisha kutaja baadhi yao hasa, pamoja na kuwa vibaraka wanatokana na kila aina ya watu, kwa vile Aya zinazungumza na anayemlinga- nia Mwenyezi Mungu na sharia yake.
Kila kitu kitaangamia isipokuwa dhati yake, hukumu ni yake na kwake Yeye mtarejeshwa.
Haya ni makemeo na kiaga kwa kila mhaini na kibaraka anayeipangia njama dini yake na nchi yake pamoja na maadui wa Mwenyezi Mungu na wa utu. Na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu atamhukumu mshirikina ambaye amesimamiwa na hoja, lakini akafanya inadi. Kwani hakuna tofauti kabisa baina ya anayemuomba Mungu mwingine na yule anayewasaidia madhalimu mataghuti, akiwatetea na kutoa mwito waungwe mkono.
Unaweza kuuliza : Je, hii inamaanisha kuwa ni wajibu kuwachukulia wahaini na vibaraka kama washirikina katika unajisi, kuacha kurithi, kutooana nao na kutozikwa kwenye makaburi ya waislamu?
Jibu : Ni wajibu wetu kumchukulia kila aliyesema: Ash-hadu alla ilaha illallah wa anna Muhammadarasulullah: (‘Nashudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu,’ kama tunavyomchukulia mwislamu; kwa namna yoyote vitakavyokuwa vitendo vyake au kwa vyovyote moyo wake utakavyokunjika.
Hiyo ni kwa sababu shahada ina athari yake ya kimaudhui haiepukani nayo kwa hali yoyote, ambayo ni utwahara, kurithiana, kuozana na kuzikwa kwenye makaburi ya waislamu. Ama akhera hiyo ni ya Mwenyezi Mungu peke yake wala hahusiki nayo yeyote asiyekuwa Yeye.
Dhahiri za Aya nyingi zimefahamisha kuwa mshirikina na dhalimu, siku ya Kiyama, watakuwa sawa. Tazama tuliyoyasema katika Juz. 19 (55–62).
9
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
Sura Ya Ishirini Na Tisa: Surat A’nkabut. Imesemekana kuwa imeshuka Makka, ina Aya 69.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miim.
أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ ﴿٢﴾
2. Je, wanadhani watu wataachwa waseme tumeamini nao wasijaribiwe?
وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ ﴿٣﴾
3. Hakika tuliwajaribu waliokuwa kabla yao. Kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wakweli na kwa yakini atawatambulisha waongo.
أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ أَن يَسْبِقُونَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ﴿٤﴾
4. Au wanadhani wanaotenda maovu kwamba watatushinda? Ni mabaya wanayohukumu.
مَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ اللَّـهِ فَإِنَّ أَجَلَ اللَّـهِ لَآتٍ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٥﴾
5. Mwenye kutaraji kukutana na Mwenyezi Mungu, basi hakika miadi ya Mwenyezi Mungu itafika. Naye ni mwenye kusikia mwenye kujua.
وَمَن جَاهَدَ فَإِنَّمَا يُجَاهِدُ لِنَفْسِهِ إِنَّ اللَّـهَ لَغَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٦﴾
6. Na anayefanya juhudi basi hakika anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَحْسَنَ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٧﴾
7. Na wale ambao wameamini na wakatenda mema, kwa hakika tutawaondolea maovu yao, na tutawalipa mazuri ya waliyokuwa wakiyatenda.
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حُسْنًا وَإِن جَاهَدَاكَ لِتُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾
8. Na tumemuusia mtu kuwatendea wema wazazi wake wawili. Na wakikushikilia unishirikishe mimi na yale usiyokuwa na ujuzi nayo, basi usiwatii. Kwangu mimi ndio marejeo yenu, na nitawaambia mnayoyatenda.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُدْخِلَنَّهُمْ فِي الصَّالِحِينَ ﴿٩﴾
9. Na wale ambao wameamini na wakatenda mema kwa hakika tutawaingiza katika wema.
Aya 1 – 9
Alif Laam Miim.
Umepita mfano wake katika Juz. 1 (2:1).
Wasidhani watu wataachwa waseme tumeamini nao wasijaribiwe?
Imani sio tamko la kusemwa, bali hapana budi liamambatane na mitihani na majaribu ya aina ya raha na tabu. Mwenye kuvumilia tabu na asitoke kwenye dini yake na akashukuru raha na kunyenyekea, wala cheo na mali isimfanye jeuri na kupetuka mipaka, huyo ndiye mumin wa kweli. Vinginevyo atakuwa sio mumin chochote.
Hivi ndivyo inavyofahamisha dhahiri ya Aya. Tukiiunganisha na Aya nyingine zinazohusiana na maudhui haya, tunapata muhtasari wa kuwa kuna jambo ambalo haliepukani na imani kwa hali yoyote. Nalo ni kuitikia muumini mwito wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kimatendo sio kimatamshi; yaani afanye bidii yake yote kutii amri ya Mungu na makatazo yake na kuambatana hayo na tabia yake na matendo yake. Anapopata mtihani na msukosuko wowote, basi umzidishe imani na unyenyekevu, kwa sababu anamfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu.
Tazama Juz. 2 (2: 153 – 157), kifungu cha ‘Thamani ya Pepo,’ Juz. 2 (2:211 – 212), kifungu cha ‘Hakuna imani bila ya takua’ na Juz. 5 (4: 135 – 136) kifungu cha ‘Baina ya dini na watu wa dini.’
Hakika tuliwajaribu waliokuwa kabla yao.
Wafuasi wa Mitume waliotangulia tuliwajaribu kwa shida, wakavumilia na wakawa na subira ya uungwana na wakazidi kushikamana na dini yao na ikhlasi kwa Mola wao na mitume yao.
Tafsiri inayofafanua zaidi Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Ni manabii wangapi waliopigana pamoja nao waumin wengi, nao hawakulegea kwa yale yaliyowasibu katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakudhoofika, wala hawakudhalilika. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaosubiri.” Juz. 4 (3:146).
Kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na kwa yakini atawatambulisha waongo.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamtahini mja wake kwa kumpa mbele ya dunia na nyuma yake, ili vidhihiri vitendo vyake vitakavyomfanya astahiki thawabu na adhabu. Kwa sababu yeye ambaye, imetukuka hekima yake, hamhisabu mtu kutokana na maandalizi yake ya kheri au ya shari; isipokuwa anamhisabu kwa matendo yake ambayo yanadhihirika.
Au wanadhani wanaotenda maovu kwamba watatushinda?
Waovu wanafikiria kuwa Mwenyezi Mungu hawezi kuwapata? Itakuwaje naye ni muweza wa kila kitu? Ni nani atakayeweza kuwazuia naye na hali yeye hana mpinzani wala mshirika aliye sawa naye?
Ni mabaya wanayohukumu kwamba wao wataponyoka na utawala wa Mwenyezi Mungu na hukumu yake.
Mwenye kutaraji kukutana na Mwenyezi Mungu, basi hakika miadi ya Mwenyezi Mungu itafika.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja wenye kukufuru siku ya mwisho sasa anataja mwenye kumwamini. Akamwambia mumin huyu:
Thibiti kwenye imani yako, kwani saa itafika tu hakuna shaka, basi ifanyie kazi.
Naye ni mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Anasikia unayoyasema na anajua unayoyadhamiria na kuyafanya na atakulipa yaliyopita.
Na anayefanya juhudi basi hakika anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake.
Tafsiri ya Aya hii ni ile Aya isemayo:
فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِ وَمَنْ عَمِيَ فَعَلَيْهَا ﴿١٠٤﴾
“Basi atakayefungua macho ni faida yake mwenyewe; na atakayeyapofua ni hasara yake mwenyewe.” Juz. 7 (6:104).
Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu , haumnufaishi utiifu wa mwenye kutii, wala haumdhuru uasi wa mwenye kuasi.
Na wale ambao wameamini na wakatenda mema, kwa hakika tutawaondolea maovu yao, na tutawalipa mazuri ya waliyokuwa wakiyatenda.
Mwenye kuamini baada ya kukufuru, akawa mwema baada ya kuwa mfisadi, basi Mwenyezi Mungu atamsamehe na kumghufiria yaliyopita. Zaidi ya hayo atapata thawabu kutokana na imani yake na wema wake; sawa na ambaye hana dhambi.
Katika msingi huu wa heri kuna heri zote za utu. Kwa sababu unafungua mlango wa matumaini ya wenye dhambi na makosa na kupata msukumo wa kutubia na kujing’oa kwenye uovu. Hakuna njia nzuri kuliko hii ya kuisafisha jamii na dhulma na ufisadi.
Na tumemuusia mtu kuwatendea wema wazazi wake wawili. Na wakikushikilia unishirikishe mimi na yale usiyokuwa na ujuzi nayo, basi usiwatii. Kwangu mimi ndio marejeo yenu, na nitawaambia mnayoyatenda.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameamrisha kuwatendea wema wazazi wawili na kuwatii katika kila kitu isipokuwa katika lile ambalo haliridhii Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwani hakuna kumtii kiumbe kwa kumuasia muumba.
Tumelizungumzia kwa ufafanuzi hilo katika Juz. 15 (17:23). Na katika vitabu vya Hadith, kuna kisa kinachofahamisha kuwa kuwatendea wema wazazi wawili kunanufaisha wakati wa shida na pia kwamba dua bora ya kumwelekea Mwenyezi Mungu wakati wa shida ni matendo mema.
Imepokewa kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kwamba watu watatu walingia kwenye pango lililokuwa njiani, wakalala humo. Likaanguka jiwe kubwa kutoka mlimani likawazibia mlango. Baada ya kufikiria sana hawakupata njia isipokuwa kuelekea kwenye dua kumuomba Mwenyezi Mungu peke yake awaokoe na maangamizi haya.
Kisha akakumbuka kila mmoja tendo jema alilolitenda: Wa kwanza, akakumbuka jinsi alivyowatendea wema wazazi wake wawili na kuwapatia raha. Basi jiwe likasogea kidogo. Wa pili akakumbuka kumtekelezea haja mwanamke aliyekuwa na dharura bila ya kufanya naye tendo chafu. Jiwe likasogea tena. Wa tatu akasema kuwa alikuwa na mfanyakazi aliyeondoka bila ya kuchukua mshahara wake. Ule mshahara akauhifadhi na ukazaa, ukawa na wanyama wengi sana, basi akampa mshahara wake na ile ziyada. Hapo jiwe likamalizika kufunguka na wakatoka kwenye pango.
Riwaya hii iwe ni sahihi au la, lakini kisa kinauelezea Uislamu na uhakika wake, kwa sababu unadhibiti njia ya uokovu duniani na akhera kwa matendo mema, sio kwa kauli na kujionyesha.
Na wale ambao wameamini na wakatenda mema, kwa hakika tutawaingiza katika wema.
Unaweza kuuliza : Kuna tofauti gani kati ya Aya hii na ile iliyotangulia, isemayo: Na wale ambao wameamini na wakatenda mema, kwa hakika tutawaondolea maovu yao, na tutawalipa mazuri ya waliyokuwa wakiyatenda?
Jibu : Kuingizwa katika kundi la watu wema; kama vile mashahidi na mawalii, ni daraja ya juu zaidi sana kuliko kusamehewa na kulipwa. Ni sawa na kumwambia aliyefanya uovu kisha akatengenea na kuwa mwenye ikhlasi: Nimekusamehe na nitakufanyia wema fulani. Zaidi ya hayo nitakuweka kwenye idadi ya wateuliwa walio bora.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ فَإِذَا أُوذِيَ فِي اللَّـهِ جَعَلَ فِتْنَةَ النَّاسِ كَعَذَابِ اللَّـهِ وَلَئِن جَاءَ نَصْرٌ مِّن رَّبِّكَ لَيَقُولُنَّ إِنَّا كُنَّا مَعَكُمْ أَوَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِمَا فِي صُدُورِ الْعَالَمِينَ ﴿١٠﴾
10. Na katika watu kuna wanaosema: Tumemwamini Mwenyezi Mungu, lakini wanapoudhiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wanayafanya maudhi ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na itakapokuja nusra kutoka kwa Mola wako lazima watasema: Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi. Kwani Mwenyezi Mungu hayajui yaliyomo vifuani mwa walimwengu?
وَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْمُنَافِقِينَ ﴿١١﴾
11. Kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha wale ambao wameamini na kwa yakini atawatambulisha wanafiki.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا اتَّبِعُوا سَبِيلَنَا وَلْنَحْمِلْ خَطَايَاكُمْ وَمَا هُم بِحَامِلِينَ مِنْ خَطَايَاهُم مِّن شَيْءٍ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١٢﴾
12. Na wale ambao wamekufuru waliwaambia walioamini: Fuateni njia yetu nasi tutayabeba makosa yenu. Wala wao hawatabeba katika makosa yao chochote kile. Hakika hao ni waongo.
وَلَيَحْمِلُنَّ أَثْقَالَهُمْ وَأَثْقَالًا مَّعَ أَثْقَالِهِمْ وَلَيُسْأَلُنَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَمَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿١٣﴾
13. Na kwa hakika wataibeba mizigo yao na mizigo mingine pamoja na mizigo yao, na kwa hakika wataulizwa siku ya Kiyama juu ya waliyoyazua.
Aya 10 – 13
Na katika watu kuna wanaosema: Tumemwamini Mwenyezi Mungu. Lakini wanapoudhiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wanayafanya maudhi ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Aya hii inaleta picha ya uhakika ya baadhi ya watu tunaowajua na kuishi nao. Shetani amewapambia watu hawa kwa hila na wasiwasi wake, mpaka wakamsadiki, wakajiona ni katika watu wa takua na imani; kumbe hawaitakidi wala kuona kitu chochote isipokuwa manufaa na masilahi yao.
Hakuna kitu kinachofahamisha zaidi kuwa imani zao ni njozi na sarabi, kuliko kule kuhofia kwao watu japo kwa kitu kidogo tu. Wanawahofia itakapodhihiri haki na usawa kwa kauli au kwa vitendo; sawa na mawalii na wenye takua wanavyomhofia Mwenyezi Mungu.
Imetangulia ishara ya kundi hili katika Aya isemayo:
فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَخْشَوْنَ النَّاسَ كَخَشْيَةِ اللَّـهِ أَوْ أَشَدَّ خَشْيَةً ﴿٧٧﴾
“Walipolazimishwa kupigana, mara kundi moja katika wao wakawaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu au kwa hofu zaidi.” Juz. 5 (4:77).
Huko nyuma tulisema kuwa hakuna yoyote anayeifuata haki ila ataitolea thamani kwa nafsi yake na vitu vyake. Vinginevyo watu wa haki na wanaoinusuru, wasingekuwa na ubora wowote. Tazama Juz. 2 (2: 153 – 157), kifungu cha ‘Thamani ya Pepo.’
Kuna Hadith isemayo: “Mwenye kumwogopa Mwenyezi Mungu huogopewa na kila kitu, na asiyemwogopa Mwenyezi Mungu haogopewi na chochote.”
Na itakapokuja nusra kutoka kwa Mola wako lazima watasema: Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi.
Wao wako pamoja na dini ikiwa ni biashara yenye masilahi, na wao ni maadui wa dini ikiwa itawataka wajitolee muhanga japo kidogo. Kauli fasaha zaidi katika maana haya ni ile ya Bwana wa mashahidi, Husein bin Ali(a.s) pale aliposema:“Watu ni watumwa wa dunia na dini wameilamba kwa ndimi zao tu, inachukulika yanapokuwa mazuri maisha yao. Wapatwapo na misukosuko, wenye dini wanakuwa wachache.”
Umetangulia mfano wake katika Juz. 5 (4:141).
Kwani Mwenyezi Mungu hayajui yaliyomo vifuani mwa walimwengu?
Mnataka kumhadaa Mwenyezi Mungu na kumfanyia hila na yeye ni mjuzi wa mnayoficha na mnayoyadhihirisha?
Kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha wale ambao wameamini na kwa yakini atawatambulisha wanafiki.
Umetangulia mfano wake katika Aya 3 ya sura hii na Juz. 4 (4:154).
Na wale ambao wamekufuru waliwaambia walioamini: Fuateni njia yetu nasi tutayabeba makosa yenu.
Washirikina wa Makka waliwaambia wale walioitikia mwito wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) : Vipi mnamfuata Muhammad na kuvumilia mengi kwa ajili yake? Mwacheni na mrudi kwenye dini yetu. Ikiwa mnahofia adhabu ya Mwenyezi Mungu baada ya mauti, kama anavyowahofisha Muhammad, basi sisi tutawabebea. Walisema hivi wakikusudia kuwa ufufuo baada ya mauti ni porojo.
Wala wao hawatabeba katika makosa yao chochote kile. Hakika hao ni waongo.
Kwa sababu kila mtu atalipwa kwa matendo yake, hatabeba mzigo wa wengine au kuulizwa kwa niaba yake:
قُل لَّا تُسْأَلُونَ عَمَّا أَجْرَمْنَا وَلَا نُسْأَلُ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٢٥﴾
“Sema: hamtaulizwa kwa makosa tuliyoyafanya, wala sisi hatutaulizwa kwa mnayoyatenda nyinyi.” (34:25).
Na kwa hakika wataibeba mizigo yao na mizigo mingine pamoja na mizigo yao.
Kila anayempoteza mwingine atabeba dhambi zake na dhambi za kupoteza; kwa sababu amesababisha kupatikana upotevu na kuenea. Ama yule anayemfuata mpotevu atabeba dhambi zake bila ya kupungua, kwa sababu aliitikia upotevu kwa hiyari yake.
Kwa maneno mengine ni kuwa mpotezaji ana dhambi mbili: Moja kwa upotevu wake na nyingine ni kwa kupoteza. Na mfuasi ana dhambi moja ya kupotea kwa hiyari yake.
Na kwa hakika wataulizwa siku ya Kiyama juu ya waliyoyazua ya kudai kwao kuwa Mwenyezi Mungu ana mshirika, kusema kwao kuwa Mtume(s.a.w.w) ni mchawi, kuwaambia waumini kuwa watawabebea dhambi zao n.k.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٤﴾
14. Na hakika tulimtuma Nuhu kwa kaumu yake, akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini. Basi tufani iliwachukua hali ya kuwa wao ni madhalimu.
فَأَنجَيْنَاهُ وَأَصْحَابَ السَّفِينَةِ وَجَعَلْنَاهَا آيَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٥﴾
15. Tukamwokoa yeye na watu wa safina na tukaifanya kuwa ni ishara kwa walimwengu wote.
Aya 14 – 15
Na hakika tulimtuma Nuhu kwa kaumu yake, akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini. Basi tufani iliwachukua hali ya kuwa wao ni madhalimu. Tukamwokoa yeye na watu wa safina na tukaifanya kuwa ni ishara kwa walimwengu wote.
Dhahiri ya Aya inafahamisha kwa uwazi kuwa Nuhu aliishi miaka 950 na akili hailikitai hilo. Kwa hiyo ni wajibu kulisadiki. Ama kutafuta visababu kwamba siku hizo watu walikuwa wachache ndio maana umri ukarefushwa, kama walivyosema baadhi ya wafasiri, hilo haifai kulitegemea katika kufasiri wahyi.
Katika Kamusi ya Kitabu Kitakatifu imeelezwa kuwa jina la Nuhu ni Samiy na maana yake ni raha na baba yake ndiye aliyemuita hivyo.
Lakini ni lazima ieleweke kuwa jina Samiy linatokana na Sam bin Nuhu, sasa vipi mzazi anasibishwe kwa mwana? Na katika Uk. 448 wa kamusi hiyo hiyo imeelezwa kuwa Sam ni mtoto wa Nuhu na kwamba alizaliwa akiwa Nuhu ana miaka 500. Kamusi haikuasharia tarehe ya wakati wa Nuhu; pengine ni kwa kukosekana rejea. Yametangulia maneno kuhusu Nuhu(a.s) katika Aya kadha; zikiwemo: Juz. 8 (7:59 – 64) na Juz.12 (11:25 – 26).
10
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
وَإِبْرَاهِيمَ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٦﴾
16. Na Ibrahim pale alipowaambia watu wake: Muabuduni Mwenyezi Mungu na mcheni Yeye. Hayo ni kheri kwenu ikiwa mnajua.
إِنَّمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْثَانًا وَتَخْلُقُونَ إِفْكًا إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ وَاعْبُدُوهُ وَاشْكُرُوا لَهُ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿١٧﴾
17. Hakika nyinyi mnaabudu masanamu kinyume na Mwenyezi Mungu na mnazua uzushi. Hakika mnao waabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu hawamilikii riziki yoyote. Takeni riziki kwa Mwenyezi Mungu na mumwabudu na mumshukuru; kwake mtarudishwa.
وَإِن تُكَذِّبُوا فَقَدْ كَذَّبَ أُمَمٌ مِّن قَبْلِكُمْ وَمَا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿١٨﴾
18. Na kama mkikadhibisha basi zimekwisha kadhibisha umma kabla yenu. Na si juu ya Mtume ila kufikisha.
Aya 16 – 18
Na Ibrahim pale alipowaambia watu wake: Muabuduni Mwenyezi Mungu na mcheni Yeye. Hayo ni kheri kwenu ikiwa mnajua. Hakika nyinyi mnaabudu masanamu kinyume na Mwenyezi Mungu na mnazua uzushi. Hakika mnaowaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu hawamilikii riziki yoyote. Takeni riziki kwa Mwenyezi Mungu na mumwabudu na mumshukuru; kwake mtarudishwa. Na kama mkikadhibisha basi zimekwisha kadhibisha umma kabla yenu. Na si juu ya Mtume ila kufikisha.
Hakika mwito wa Ibrahim(a.s) ni mwito wa kila Nabii – Ikhlasi katika kila jambo na kuiondoa shirki kwa sura zake zote, kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mwanzilishi na ndiye mrejeshaji; mkononi mwake ndio kuna madhara na manufaa. Mwenye kukadhibisha na akaukataa mwito huu atakuwa amejidhulumu nafsi yake.
Katika kamusi ya Kitabu Kitakatifu, imeelezwa kuwa Ibrahim ni mwana wa Tarih kutokana na kizazi cha Sam bin Nuhu, yeye anatoka katika mji ulio baina ya mito miwili: mto Dijla na mto Furat na kwamba yeye alikaa hapo miaka 75, kisha akahama pamoja na mkewe na Lut hadi ardhi ya Kanani. Mtungaji wa Kamusi hiyo anasema: “Haiwezekani kuainisha kwa mpangilio tarehe aliyoishi Ibrahim, lakini yeye alizaliwa, kulingana na tarehe aliyoielezea Ashir, kuwa ni kwenye mwaka 1996 kabla ya Kuzaliwa Nabii Isa.”
Yametangulia maelezo kuhusu Ibrahim katika Juz. 7 (6:74 – 84 , Juz. 16 (19:41 – 50) na Juz. 17 (21:52 – 72).
أَوَلَمْ يَرَوْا كَيْفَ يُبْدِئُ اللَّـهُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿١٩﴾
19. Je, hawaoni jinsi Mwenyezi Mungu anavyoanzisha uumbaji na kisha akaurudisha. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni rahisi.
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ بَدَأَ الْخَلْقَ ثُمَّ اللَّـهُ يُنشِئُ النَّشْأَةَ الْآخِرَةَ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٠﴾
20. Sema: Tembeeni katika ardhi na tazameni jinsi alivyoanzisha kuumba, kisha Mwenyezi Mungu ndiye atakayeumba umbo la baadaye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.
يُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ وَيَرْحَمُ مَن يَشَاءُ وَإِلَيْهِ تُقْلَبُونَ ﴿٢١﴾
21. Humwadhibu amtakaye, Na humrehemu amtakaye; na kwake mtapelekwa.
وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿٢٢﴾
22. Wala nyinyi si wenye kushinda ardhini wala mbinguni. Wala hamna mlinzi wala msaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ وَلِقَائِهِ أُولَـٰئِكَ يَئِسُوا مِن رَّحْمَتِي وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٢٣﴾
23. Na wale ambao wamezikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu na kukutana naye. Hao wamekata tamaa na hao watakaopata adhabu chungu.
فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا اقْتُلُوهُ أَوْ حَرِّقُوهُ فَأَنجَاهُ اللَّـهُ مِنَ النَّارِ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٢٤﴾
24. Basi halikuwa jawabu la watu wake ila ni kusema: Muuweni au mchomeni moto! Mwenyezi Mungu akamwokoa na moto. Hakika katika halo kuna ishara kwa watu wanaoamini.
وَقَالَ إِنَّمَا اتَّخَذْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ أَوْثَانًا مَّوَدَّةَ بَيْنِكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ثُمَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُ بَعْضُكُم بِبَعْضٍ وَيَلْعَنُ بَعْضُكُم بَعْضًا وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٢٥﴾
25. Na alisema: Hakika nyinyi mmeyashika masanamu badala ya Mwenyezi Mungu kwa mapenzi baina yenu katika maisha ya dunia. Kisha siku ya Kiyama mtakataana nyinyi kwa nyinyi na mtalaniana nyinyi kwa nyinyi. Na makazi yenu ni motoni wala hamtapata wa kuwanusuru.
فَآمَنَ لَهُ لُوطٌ وَقَالَ إِنِّي مُهَاجِرٌ إِلَىٰ رَبِّي إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ {26 }
26. Akamwamini Lut na akasema: Hakika mimi ninahamia kwa Mola wangu. Hakika Yeye ni mwenye nguvu mwenye hekima.
وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَجَعَلْنَا فِي ذُرِّيَّتِهِ النُّبُوَّةَ وَالْكِتَابَ وَآتَيْنَاهُ أَجْرَهُ فِي الدُّنْيَا وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٢٧﴾
27. Na tulimtunukia yeye Is-haq na Ya’qub na tukajaalia katika kizazi chake Unabii na Kitabu na tukampa ujira wake katika dunia. Naye hakika katika Akhera, bila shaka atakuwa katika wema.
MWENYEZI MUNGU NDIYE MWANZILISHI NA MRUDISHAJI
Aya 19 – 27
Je, hawaoni jinsi Mwenyezi Mungu anavyoanzisha uumbaji na kisha akaurudisha. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni rahisi.
Maana ya hawaoni ni hawajui. Maana yanafupika kwa kauli ya Imam Ali(a.s) :“Namstaajabu anayepinga uumbaji wa mwisho naye anaona uuum- baji wa kwanza.”
Wajihi wa kuungana maumbo haya mawili ni kwa kisababishi ambacho ni uweza wa aliyeyafanya. Kwani aliyeweza kukifanya kitu bila ya kuweko kitu, vile vile anaweza kukifanaya baada ya kutawanyika; bali huko kukufanya ni kwepesi zaidi. Tunasema hivi tukijua kuwa kwa Mwenyezi Mungu hakuna jepesi wala zito, na kwamba yeye anafanya kikubwa na kidogo kwa neno ‘Kuwa.’ Maelezo haya tumeyakariri kwa kukaririka Aya. Angalia Juz.1 (2:28 – 29), Juz. 5 (4:85 – 87) na Juz. 13 (13:5 – 7).
Sema: Tembeeni katika ardhi na tazameni jinsi alivyoanzisha kuumba, kisha Mwenyezi Mungu ndiye atakayeumba umbo la baadaye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.
Qur’an imekataza kuiga na ikaamrisha kufanya utafiti na uchunguzi. Imewasifu wataalamu na wenye kufanya jitihada. Hakuna mwenye shaka kwamba utafiti na uchunguzi ni katika alama za uhai na njia ya kuuen- deleza na kutatua matatizo yake, ikiwa utafiti na uchunguzi utaambatana na subira na kuamua kufikia kwenye malengo hata kama kutakuwa na vikwazo vya namna gani.
Subira na imani inashinda nguvu zote. Binadamu wa zama hizi ameamua kufika mwezini; akajitahidi na akafanya bidii mpaka akakanyaga kwenye uso wa mwezi kwa unyayo wake. Kesho au kesho kutwa atakanyaga mirikh na sayari nyinginezo.
Kwa hiyo, hakuna nguvu isiyoshindwa na binadamu isipokuwa nguvu ya muumba tu. Ndio maana ikasemwa: hakuna zaidi ya binadamu isipokuwa muumba wake.
Kama mtu ataniuliza: Ni kiwango gani cha binadamu? Nitamjibu: Kiwango chake ni kuwa hakuna kiwango cha nguvu zake na maandalizi yake. Ujinga na kuiga ndiko kunakoingilia kati baina ya mtu na mkabala wake na kumtenganisha na nafsi yake na uhalisi wake.
Ndio maana Qur’an ikaharamisha kuiga na kuamrisha kuchunguza na kufuata akili katika hukumu zake zote na kukupa jina la nuru uongofu na dalili.
Unaweza kuuliza : Ni kweli Qur’an imekataza kuiga na kuamrisha kufanya utafiti na uchunguzi, pia ikawasifu wataalamu.
Lakini mfumo au sababu iliyowajibisha kushuka Aya inayohusiana na maudhui haya inafahamisha wataalamu wa dini ndio waliosifiwa kuwa watu wa elimu ya Mwenyezi Mungu na kujua halali yake na haramu yake na kwamba Yeye ameamrisha kuchunguza na kufikiri katika kuumbwa vilivyoko ili mtu aishilie kwa hilo kwenye imani ya Mungu na Siku ya Mwisho, aweze kufuzu kwa kupata pepo na neema zake na kuokoka na moto na ukali wake.
Mfano mzuri wa hayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
أَفَرَأَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ ﴿٦٣﴾ أَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ ﴿٦٤﴾ لَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَاهُ حُطَامًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ ﴿٦٥﴾
“Je, mmeona mnayolima. Je, nyinyi mmeiotesha au tumeiotesha sisi? Lau tungelitaka tungeifanya makapi mkabaki mnastaajabu.” (56:63 – 65).
Ni mwenye akili gani atakayeweza kusema kuwa Aya hii inahimiza elimu ya kilimo?
Jibu :Kwanza : kuna Aya zilizobariki na kusifu kila linalowanufaisha watu; kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
وَأَمَّا مَا يَنفَعُ النَّاسَ فَيَمْكُثُ فِي الْأَرْضِ ﴿١٧﴾
“Ama povu linakwenda bure; ama kinachowafaa watu hukaa kwenye ardhi.” Juz. 13 (13:17).
Hakuna kitu kinachowafaa zaidi watu kama elimu; bali hakuna maisha bila elimu katika zama hizi. Zaidi ya hayo kuna Aya kadhaa zinazohimiza kufanya amali njema na kuwazingatia watendaji wake kuwa ni viumbe bora. Mwenyezi Mungu anasema:
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ هُمْ خَيْرُ الْبَرِيَّةِ ﴿٧﴾
“Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema, hao ndio bora ya viumbe” (98:7)
Na elimu inajitokeza kuwa ni katika matendo mema.
Pili : Ni kweli kuwa sababu za kushuka Aya zilizoamrisha utafiti na uchunguzai au nyingi katika hizo ni kumrudi yule anayemkufuru Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, lakini sababu ya kushuka hailifungi neno na sababu hiyo hiyo peke yake.
Tatu : Elimu yenye manufaa ni nzuri katika mtazamo wa akili. Ndio, elimu ina daraja mbali mbali, zinazopimwa kutokana na faida na manufaa yake.
Elimu ya sharia ya kiislamu na sharia yake ndiyo iliyo na manufaa zaidi kidunia na akhera. Kidunia ni kwa kuwa inaelekeza kila kitu kwenye heri ya watu na masilahi yao. Ama kiakhera, hiyo ndio njia ya kuokoka na hasira za Mwenyezi Mungu na adhabu yake.
Ndio maana waislamu wakamwita mwanachuoni wa kidini: ‘Mwanachuoni huru’ na ‘Mwanachuoni aliyefungwa’ kuwa ni yule wa kidunia.
Nne : wameafikiana mafakihi wa kiislamu kwa kauli moja kwamba kila elimu inayohitajika katika maisha basi ni wajib kifaya.
Kuna hadith isemayo: “ Hakuna Mwislamu yoyote aliyepanda mti au kupanda mbegu, akala humo ndege au mnyama au mtu, ila huwa ni kama sadaka, “Tafuteni elimu katika machimbuko yake ya kidini na kidunia” na “Tafuteni elimu hata kama ni China.”
Kimsingi ni kuwa elimu ya dini inatafutwa katika Kitabu na Sunna sio China!
Humwadhibu amtakaye, katika wanaostahiki adhabu,Na humrehemu amatakaye, katika wanaostahiki rehema.
Kwa sababu Mwenyezi Mungu ni mwadilifu na hakimu, atailipa kila nafsi iliyoyachuma.
Na kwake mtapelekwa . Mtarudishwa siku ya Kiyama kwa hisabu na malipo.
Wala nyinyi si wenye kushinda ardhini wala mbinguni.
Yaani wala aliyeko mbinguni. Katika Nahjul-balagha imeelezwa: “Hamshindi anayemtafuta wala hamponyoki anayemkimbia.”
Wala hamna mlinzi wala msaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Hakuna wa kuzuia hukumu yake wala kumkimbia.
Na wale ambao wamezikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu na kukutana naye. Hao wamekata tamaa na hao watakaopata adhabu chungu.
Kukata tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu ni natija ya kumkana Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na malipo ya mwenye kukata tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu, kwa ukafiri na inadi, ni kuonja adhabu ya kuungua.
Basi halikuwa jawabu la watu wake ila ni kusema: Muuweni au mchomeni moto! Mwenyezi Mungu akamwokoa na moto.
Zinarudi simulizi za Ibrahim(a.s) na sera yake pamoja na watu wake ambao walijaribu kuepukana naye na mwito wake kwa kumuua au kumchoma.
Haya ndio mantiki ya mataghuti kila wakati na mahali. Wanashindwa na hoja wazi basi wanahofia vyeo vyao. Kwa hiyo wanakuwa hawana jingine isipokuwa dhulma waliyo nayo. Hapo wanaanza kutoa amri ya: Wafungeni, waadhibuni, wanyang’anyeni mali, vunjeni majumba, nyongeni, chomeni n.k.
Hapa ndio unaingia uokovu wa Mwenyezi Mungu. Unaweza kuwa ni kwa kuokoka mdhulumiwa kutoka mikononi mwa dhalimu, kuadhibiwa dhalimu na Mwenyezi Mungu au kupitia kwa wanamapinduzi, wakombozi. Umepita mfano wake katika Juz. 17 (21:68).
Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaoamini.
Yaani wanaonufaika na maonyo, kuwaidhika na mazingatio, kuitafuta haki kwa ajili ya haki ili waiamini na kutenda kwa ikhlasi.
Na alisema: Hakika nyinyi mmeyashika masanamu badala ya Mwenyezi Mungu kwa mapenzi baina yenu katika maisha ya dunia.
Ibrahim aliwaambia watu kuwa nyinyi mnayaabudu haya masanamu mkiwa na yakini kuwa hayadhuru wala hayanufaishi, lakini mmeyatukuza kwa kuwaiga mnaowapenda katika maisha haya na kesho haya mapenzi yatabadilika kuwa uadui na chuki.
Kisha siku ya Kiyama mtakataana nyinyi kwa nyinyi na mtalaaniana nyinyi kwa nyinyi.
Imam Ali(a.s) anasema:“Mfuatwa atajitenga na mfuasi, na kiongozi na muongozwa; watafarikiana kwa chuki na watalaaniana wakati wa kukutana.”
Na makazi yenu ni motoni wala hamtapata wa kuwanusuru.
Huu ndio mwisho wa kila mwenye kuipinga haki awe mfuasi au mwenye kufuatwa.
Akamwamini Lut na akasema: “Hakika mimi ninahamia kwa Mola wangu. Hakika Yeye ni mwenye nguvu mwenye hekima.”
Lut ni mtoto wa nduguye Ibrahim. Kundi katika wafasiri wamesema: “Hakuongoka yoyote katika kaumu ya Ibrahim au kumwamini isipokuwa Lut peke yake.” Yakushangaza ni yale yaliyoandikwa katika Biblia Mwanzo: (19:30 – 38)
Imeelezwa kuwa mabinti wawili wa Lut walimlewesha baba yao pombe, wakalala naye na wakashika mimba. Mkubwa akazaa mtoto wa kiume aliyemwita Moabu na mdogo pia akazaa mtoto wa kiume aliyemwita Binamu.
Na tulimtunukia Is-ahq na Ya’qub na tukajaalia katika kizazi chake Unabii na Kitabu na tukampa ujira wake katika dunia. Naye hakika katika Akhera, bila shaka atakuwa katika wema.
Aliyetunukiwa ni Ibrahim(a.s) . Aya hii ni dalili ya wazi kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakutuma mtume baada yake ila anatokana na uti wake wa mgongo.
Tukiiunganisha Aya hii na Hadith isemayo: “Jambo hili liko kwa makuraish... Watu wanawafuata makuraishi Maimamu ni katika makraishi...” tunapata natija ya kuwa mitume wote na maimamu wanatokana na kizazi cha Ibrahim. Kwa sababu nasaba ya Kuraishi inakomea kwake.
Umepita mfano wake katika Juz. 16 (19: 49) na Juz. 17 (21: 72 - 73).
11
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿٢٨﴾
28. Na Lut alipowaambia watu wake: Hakika nyinyi mnafanya uchafu ambao hajawatangulia yeyote kwa hilo katika walimwengu.
أَئِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ وَتَقْطَعُونَ السَّبِيلَ وَتَأْتُونَ فِي نَادِيكُمُ الْمُنكَرَ فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا ائْتِنَا بِعَذَابِ اللَّـهِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٢٩﴾
29. Je, mnawaendea wanaume na mnakata njia na katika mikusanyiko yenu mnafanya uovu? Basi halikuwa jibu la watu wake isipokuwa kusema: Tuletee adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa wewe ni katika wakweli.
قَالَ رَبِّ انصُرْنِي عَلَى الْقَوْمِ الْمُفْسِدِينَ ﴿٣٠﴾
30. Akasema: Mola wangu! Ninusuru juu ya watu hawa mafasiki.
وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا إِنَّا مُهْلِكُو أَهْلِ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ إِنَّ أَهْلَهَا كَانُوا ظَالِمِينَ ﴿٣١﴾
31. Na wajumbe wetu walipomjia Ibrahim na bishara, walisema: Hakika sisi tutawaangamiza watu wa mji huu, kwani hakika watu wake wamekuwa madhalimu.
قَالَ إِنَّ فِيهَا لُوطًا قَالُوا نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَن فِيهَا لَنُنَجِّيَنَّهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٣٢﴾
32. Akasema: Hakika humo yumo Lut. Wakasema: Sisi tunajua zaidi nani aliyemo humo. Bila shaka tutamwokoa yeye na ahli zake, isipokuwa mkewe, aliye miongoni mwa waliobaki.
وَلَمَّا أَن جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالُوا لَا تَخَفْ وَلَا تَحْزَنْ إِنَّا مُنَجُّوكَ وَأَهْلَكَ إِلَّا امْرَأَتَكَ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٣٣﴾
33. Na wajumbe wetu walipomfikia Lut, aliwahuzunikia na akapata dhiki kwa ajili yao. Wakasema: Usihofu wala usihuzunike. Hakika sisi tutakuokoa na ahli zako isipokuwa mkeo aliye miongoni mwa wenye kubaki katika adhabu.
إِنَّا مُنزِلُونَ عَلَىٰ أَهْلِ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٣٤﴾
34. Hakika sisi ni wenye kuteremsha kwa watu wa mji huu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya ufuska wanaoufanya.
وَلَقَد تَّرَكْنَا مِنْهَا آيَةً بَيِّنَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٣٥﴾
35. Hakika tumeacha katika mji huo ishara iliyo wazi kwa watu wanaotumia akili.
Aya 28 – 35
Mwenyezi Mungu alimtuma Nuh kwa jamii ambayo haina mfano wake katika historia mbaya. Wakiwaendea wanaume kwa matamanio badala ya wanawake na ujambazi wa kupora watu njiani. Vikao vyao havikujua kitu isipokuwa uchafu na uovu.
Ndipo Lut akawahadharisha na kuwaonya na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Hayo ndiyo aliyokuwa akiyaweza na kuyamiliki. Lakini wakamkejeli na kumwambia tuonyeshe adhabu ndio tutakuamini. Akamkimbilia Mwenyezi Mungu kumwomba msaada kutokana na watu hao mafasiki.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamwitikia maombi yake, akamsadia kwa Malaika wakali na wenye nguvu, waliopitia kwa Ibrahim na kumpa habari njema ya kupata mtoto kutokana na mkewe kikongwe na wakamwelezea hukmu ya Mwenyezi Mungu kwa kaumu ya Lut.
Akasema; itakuwaje na humo yumo mja mwema Lut. Wakamwambia yeye na wafuasi wake watakuwa katika amani, isipokuwa mkewe ambaye alijitokeza na kupanga njama na makafiri.
Malaika wakaingia kwa Lut kwa nyuso angavu. Akawa na wasiwasi wasivunjiwe heshima na watu wake waovu. Basi wakamfichulia makusudio yao na likatimia neno la adhabu kwa wafisadi, wakabaki ni athari na mazingatio kwa wenye busara.
Baada ya maelfu ya miaka, historia ya ulawiti na ufisadi inajirudia tena katika bunge la Uingereza, lilipothibitisha na kuhalalisha uchafu huu ambao haufanywi hata na wanyama na wadudu. Sisi tuna uhakika kwam- ba aina ya adhabu itaifikia jamii hii na mfano wake, hivi sasa au baadaye; sawa na ilivyowafikia waliokuwa kabla yao.
Katika kamusi ya Kitabu Kitakatifu imeesemwa: “Tunajua kutokana na ugunduzi wa Jiolojia kwamba sehemu za kusini mwa bahari ya chumvi kulichipuka chumvi, huenda sababu ya kuchipuka huku chini ya ardhi kulitokana na tendo la kimungu.”
Aya hizi zimekwishatangulia katika Juz. 8 (7:80 – 87) na Juz. 12 (11:69–83).
وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَارْجُوا الْيَوْمَ الْآخِرَ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٣٦﴾
36. Na kwa wamadyana (tulimpeleka) ndugu yao Shua’yb, akasema: Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu! Na itarajieni siku ya Akhera wala msiende katika ardhi mkifanya ufisadi.
فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٣٧﴾
37. Wakamkadhibisha, ukawanyakuwa mtetemeko wakawa wameanguka majumbani mwao hawajimudu.
وَعَادًا وَثَمُودَ وَقَد تَّبَيَّنَ لَكُم مِّن مَّسَاكِنِهِمْ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَكَانُوا مُسْتَبْصِرِينَ ﴿٣٨﴾
38. Na kina A’d na Thamud na hakika maskani zao zimewabainikia na shetani aliwapambia vitendo vyao na akawazuilia njia na hali walikuwa wenye kuona.
وَقَارُونَ وَفِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَلَقَدْ جَاءَهُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ وَمَا كَانُوا سَابِقِينَ ﴿٣٩﴾
39. Na Qaruni na Firauni na Haman. Na hakika aliwajia Musa na ishara wazi wazi, lakini wakafanya kiburi katika nchi wala hawakuwa ni wenye kushinda.
فَكُلًّا أَخَذْنَا بِذَنبِهِ فَمِنْهُم مَّنْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِ حَاصِبًا وَمِنْهُم مَّنْ أَخَذَتْهُ الصَّيْحَةُ وَمِنْهُم مَّنْ خَسَفْنَا بِهِ الْأَرْضَ وَمِنْهُم مَّنْ أَغْرَقْنَا وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٤٠﴾
40. Kila mmoja tulimtesa kwa dhambi yake; miongoni mwao wapo tuliowapelekea kimbunga cha changarawe;. Na miongoni mwao wapo walionyakuliwa na ukelele na miongoni mwao wapo tuliowadidimiza katika ardhi na miongoni mwao wapo tuliowagharikisha; Wala Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu wenyewe.
Aya 36 – 40
Na kwa wamadyana (tulimpeleka) ndugu yao Shua’yb, akasema: Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu! Na itarajieni siku ya Akhera wala msiende katika ardhi mkifanya ufisadi.
Shua’yb ni mwarabu, kama Hud na Swaleh na watu wa Madyana pia ni waarabu; nayo iko pembeni mwa Sham. Jina hili halipatikani katika Biblia wala kwenye kamusi ya Kitabu kitatatifu; isipokuwa kwamba Yethro ni jina la mmadyani naye ni kuhani wa Madyan, baba mkwe wa Musa[5] ambaye pia anaitwa Rawail. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:85).
Wakamkadhibisha, ukawanyakuwa mtetemeko wakawa wameanguka majumbani mwao hawajimudu.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:78).
Na kina A’d na Thamud na hakika maskani zao zimewabainikia na shetani aliwapambia vitendo vyao na akawazuilia njia na hali walikuwa wenye kuona.
Yaani wanayo macho na akili ambayo inawaongoza kwenye haki, lakini wakamfuata shetani wakawa ni wenye kuangamia. Na nyinyi enyi washirikina mna akili, kama A’d na Thamud na mmeona dalili za kuangamia kwao, jambo ambalo linaweza kuwapa mawaidha na mazingatio. Hivi hamuwaidhiki mkaacha kumfuata shetani?
Na Qaruni na Firauni na Haman. Na hakika aliwajia Musa na ishara wazi wazi, lakini wakafanya kiburi katika nchi wala hawakuwa ni wenye kushinda.
Yaani wenye kuokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu kama walivyookoka waliotangulia.
Qaruni ni yule aliyekuwa na hazina ambazo funguo zake ziliwaelemea kundi la watu wenye nguvu. Firauni ni yule aliyesema: “Mimi ndiye Mola wenu mkubwa,” na Haman ni waziri wake. Hawa wote walijiwa na Musa na miujiza , lakini kujitukuza kwa dhambi, kuliwaangamiza wote.
Kila mmoja tulimtesa kwa dhambi yake; miongoni mwao wapo tuliowapelekea kimbunga cha changarawe; kama vile kaumu ya Lut.Na miongoni mwao wapo walionyakuliwa na ukelele; kama Thamud.Na miongoni mwao wapo tuliowadidimiza katika ardhi; kama Qarun.
Na miongoni mwao wapo tuliowagharikisha; kama kaumu ya Nuhu, Firauni na Haman.
Wala Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu wenyewe.
Kwa nini Mwenyezi Mungu awadhulumu watu? Je, ni kwa kuwa Yeye ana haja ya kudhulumu na hali yeye ni mwenye kujitosheleza na walimwengu? Vipi atawadhulumu waja wake na hali Yeye ndiye aliyesema:
أَن لَّعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿٤٤﴾
“Kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya madhalimu.” Juz. 8 (7:44).
مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٤١﴾
41. Mfano wa wale ambao wamewafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni kama mfano wa buibui aliyejitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu zaidi ni nyumba ya buibui, lau wangelikuwa wanajua.
إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٤٢﴾
42. Hakika Mwenyezi Mungu anajua kila kitu wanachokiomba badala yake. Na Yeye ndiye mwenye nguvu, mwenye hekima.
وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ وَمَا يَعْقِلُهَا إِلَّا الْعَالِمُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na hiyo ni mifano tunawapigia watu na hawaitii akilini ila wenye elimu.
خَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٤﴾
44. Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Hakika katika hayo kuna ishara kwa waumini.
Aya 41 – 44
Mfano wa wale ambao wamewafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni kama mfano wa buibui aliyejitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu zaidi ni nyumba ya buibui, lau wangelikuwa wanajua.
Kwanza ni lazima tuwajue ni akina nani hao waliowafanya wengine kuwa walinzi badala ya Mwenyezi Mungu? Je ni waabudu mawe na mizimu tu, au ni zaidi ya hao?
Kabla ya kulijibu swali hili, kwanza tukumbuke kauli mbili za Mwenyezi Mungu Mtukufu:
مَن كَانَ يُرِيدُ الْعِزَّةَ فَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ جَمِيعًا ﴿١٠﴾
“Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu.” (35:10).
أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا ﴿١٣٩﴾
“Je wanataka kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” Juz. 5 (4:139).
Maana ni kuwa hakuna utukufu wa nguvu ya mali, elimu, utawala wala kwa kitu chochote ila ikiwa utasimama kwa misingi ya kumcha Mungu (takua) na radhi yake na yakawa matokeo yake ni kumtii Yeye na matakwa yake.
Elimu ni nguvu, heri na imani ya Mwenyezi Mungu na ubinadamu, ikiwa inaunga mkono haki na uadilifu na nyenzo za kuendeleza maisha. Elimu ni udhaifu, shari na kumkufuru Mungu na ubinadamu, ikiwa ni nyenzo ya dhulma, uchokozi, uvunjaji na uharibifu. Pia mali, utawala n.k. Ni hivyo hivyo.
Baada ya utangulizi huu, tutakuwa tumejua kuwa wale waliowafanya walinzi wengine badala ya Mwenyezi Mungu, ni waabudu masanamu, wanaompinga Mwenyezi Mungu kwa kughurika na mali, elimu au utawala na wenye kufanya ufisadi katika ardhi.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amezifananisha nguvu za hawa na nyumba ya buibui ambayo ni dhaifu, isiyoweza kuhimili chochote; hata upepo pia unaweza ukaibomoa.
Kwa maneno mengine ni kuwa kila mwenye kumpinga Mwenyezi Mungu kwa kutegemea mizimu, elimu, mali au utawala, huyo ni katika waliowafanya wengine ni walinzi badala ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kufanya hivyo huyo ni miongoni mwa waliopata hasara.
Anasema Jahidh, katika Kitabu lhayawan (kitabu cha wanyama): “Mtoto wa buibui anaweza kutanda utandabui pale tu anapozaliwa kwa kutumia vitu vya nje sio vinavyotoka ndani mwake na kwamba yeye hutumia utando wake kulitanda windo lake.”
Kila mwenye akili anapaswa kujiuliza nafsi yake na akili yake: Ni nani aliyemjulisha buibui malighafi ya kuweza kutengeneza utando mara tu anapozaliwa? Ni mhandisi gani aliyemchorea nyumba hii yenye umbo la mtego wa wadudu? Je, yote haya yamekuja kwa sadfa? Ikiwa sadfa inaweza kuja mara mbili au tatu, je inaweza kukaririka kwa kila buibui wasio na idadi wanaozaliwa?
Hapana! Hakika Yeye ameumba kila kitu akakilinganisha sawa na akakikadiria na akakiongoza. Ametakata Mwenyezi Mungu Mtukufu na hayo wayasemayo wazushi.
Hakika Mwenyezi Mungu anajua kila kitu wanachokiomba badala yake.
Yaani katika mizimu na mengineyo wanayoyategemea badala ya Mwenyezi Mungu; kama vile mali na utawala. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua hakika ya vitu hivi wanavyojikuza navyo na kwamba hivyo haviwatoshi na chochote.
Na Yeye ndiye mwenye nguvu, mwenye hekima.
Mwenye nguvu kwa uweza wake na mwenye hekima katika mipangilio yake.
Na hiyo ni mifano tunawapigia watu na hawaitii akilini ila wenye elimu.
Mifano hiyo ni ile ya buibui na mfano wake na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu anawatanabahisha watu kwenye utukufu wake na umoja wake, lakini mifano hii na mingineyo, katika ishara za Mwenyezi Mungu hawaifahamu isipokuwa wenye akili na busara.
Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa haki.
Yaani kwa njia ya hekima na masilahi; na wala hakuziumba burebure na kwa mchezo. Hekima ya kuumbwa kwake ni kukaliwa na viumbe, wanufaike nayo na wapate dalili, kutokana na usanii wake na maajabu yake juu ya umoja wa Mwenyezi Mungu na utukufu wake.
Hakika katika hayo kuna ishara kwa waumini.
Hayo ya mpangilio na nidhamu ya kuumbwa mbingu na ardhi. Mpangilio huu ni dalili mkataa juu ya umoja wa Mwenyezi Mungu na utukufu wake kwa wale wanaoitafuta haki na kuiamini haki kwa ajili ya haki.
12
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَلَذِكْرُ اللَّـهِ أَكْبَرُ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ ﴿٤٥﴾
45. Soma uliyopewa wahyi katika Kitabu. Na usimamishe Swala, hakika Swala inakataza machafu na maovu. Na hakika dhikri (utajo) ya Mwenyezi Mungu ni kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyafanya.
Aya 45
Soma uliyopewa wahyi katika Kitabu.
Soma ewe Muhammad, mifano hii tuliyowapigia watu katika Qur’an, huenda wakafahamu na wakawa na takua.
Na usimamishe Swala, hakika swala inakataza machafu na maovu.
Unaweza kuuliza : Dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa Swala inamzuia mwenye kuswali kufanya uchafu na mambo mabaya na wala hayafanyi; na lakini inajulikana kuwa wengi wao ni mafasiki; bali baadhi ya wanaoswali wana sera za tabia mbaya kuliko baadhi ya walahidi (wapagani) na washirikina?
Jibu : Hapana! Hakika dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa Swala inamkataza mwenye kuswali asifanye machafu na maovu, inamkataza na kumzuia kwa kauli na mwongozo.
Tofauti ni kubwa baina ya kukataza na kuzuia. Wala hakuna dalili yoyote kuwa mwenye kuswali anakatiza na uchafu na uovu kwa sababu ya Swala.
Hakuna mwenye shaka kuwa kila tamko katika matamko ya Swala na kila harakati katika harakati zake inakataza kumuasi Mwenyezi Mungu na kuamrisha twaa yake.
Kwa maneno mengine ni kuwa swala ni kama Qur’an – inaamrisha na kukataza kisharia sio kimaumbile. Tazama kifungu: ‘Kuumba na kuweka sharia’ katika Juz. 1 (2:26-27).
Ibni Al-arabiy, katika kitabu Futuhatil-makiyya ana maelezo ya ndani na yaliyozama kuhusiana na Aya hii. Ufafanuzi wake ni kuwa mwenye kuswali anakatazwa kusema neno au tendo ambalo linapingana na uhalisi wa Swala na kuivunja, lakini hakatazwi neno au tendo linalooana na Swala; kama kuzidisha tasbih au tahmid katika rukui na sujudi au kutoa sadaqa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu katikati ya Swala; kama alivyofanya Amiru al-mu’minin, Ali(a.s) alipotoa sadaka pete yake akiwa amerukui.
Kwa hiyo basi makusudio ya uchafu na uovu ni kila kauli au tendo linalovunja Swala; yaani kila Swala inamwambia mwenye kuswali: ‘chunga!’ Usifanye kitu kitakachonibatilisha na kunitoa kwenye muundo wangu na hakika yangu.
Na hakika dhikri (utajo) ya Mwenyezi Mungu ni kubwa kabisa.
Maana ya dhikri ni kukumbuka. Makusudio sio kuwa dhikri ni kubwa kuliko Swala, kwa sababu hiyo Swala yenyewe ni dhikri; isipokuwa makusudio ni Mwenyezi Mungu anawadhukuru (anawakumbuka) waja wake zaidi kwa upole wake na huruma zake; wakati huo huo naye ni mwenye kukumbukwa sana.
Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa Mwenyezi Mungu ni mkumbukaji kwa kuwa anawakumbuka waja wake kwa rehma zake na upole wake; naye ni Mwenye kukumbukwa, kwa sababu waja wake wanamkumbuka kwa nyoyo zao kiimani na kiikhlasi, kwa ndimi zao kitasbihi na tahlili na kwa vitendo vyao kwa rukui na sujudi. Kwa hiyo Yeye ni mkumbukaji zaidi ya wengine na ni mwenye kumbukwa zaidi ya wengine.
Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyafanya, ya kheri na shari na kuilipa kila nafsi iliyoyachuma nao hawatadhulumiwa.
وَلَا تُجَادِلُوا أَهْلَ الْكِتَابِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ وَقُولُوا آمَنَّا بِالَّذِي أُنزِلَ إِلَيْنَا وَأُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَإِلَـٰهُنَا وَإِلَـٰهُكُمْ وَاحِدٌ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿٤٦﴾
46. Wala usjadiliane na watu wa Kitabu isipokuwa kwa njia iliyo nzuri kabisa. Isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja na sisi ni wenye kusilimu kwake.
وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ فَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يُؤْمِنُونَ بِهِ وَمِنْ هَـٰؤُلَاءِ مَن يُؤْمِنُ بِهِ وَمَا يَجْحَدُ بِآيَاتِنَا إِلَّا الْكَافِرُونَ ﴿٤٧﴾
47. Na hivyo ndio tumekuteremshia Kitabu. Basi wale ambao tumewapa Kitabu wanakiamini. Na miongoni mwa hao wako wanaokiamini. Na hawazikatai ishara zetu isipokuwa makafiri.
وَمَا كُنتَ تَتْلُو مِن قَبْلِهِ مِن كِتَابٍ وَلَا تَخُطُّهُ بِيَمِينِكَ إِذًا لَّارْتَابَ الْمُبْطِلُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na hukuwa kabla yake unasoma kitabu chochote, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume. Ingelikuwa hivyo wangelifanya shaka wabatilifu.
بَلْ هُوَ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ فِي صُدُورِ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَمَا يَجْحَدُ بِآيَاتِنَا إِلَّا الظَّالِمُونَ ﴿٤٩﴾
49. Bali hicho ni ishara zilizo wazi katika vifua vya waliopewa ilimu; na hawazikatai ishara zetu isipokuwa madhalimu.
Aya 46 – 49
Wala usjadiliane na watu wa Kitabu isipokuwa kwa njia iliyo nzuri kabisa.
Makusudio ya watu wa Kitabu ni mayahudi na manaswara (wakristo). Kujadiliana kwa njia nzuri ni kuwa hoja na dalili ziwe kwa mfumo wa kuvutia sio wa kufukuza, ziwe wazi na sio kufungwa fungwa na kuweko na insafu ya kuusikiliza upande wa pili na kukubaliana nao kwenye lile la haki; ni sawa awe ni katika watu wa Kitabu au wengineo.
Mfano ulio wazi zaidi juu ya hilo ni kauli ya Mwenyezi Mungu kwa washirikina waliosema: “Hakika sisi tuliwakuta baba zetu juu ya desturi; na hakika sisi tunafuata nyayo zao.” Akasema:
أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ ﴿٢٤﴾
“Hata nikiwaletea yenye muongozo bora kuliko mliyowakuta nayo baba zenu?” (43:24).
Upole huu wa kusema: ‘Hata nikiwaletea yenye muongozo bora’ unavunja hoja na unaingia katika moyo wa mwenye kusikiliza vizuri.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amehusisha kuwataja watu wa Kitabu, kwa sabubu wao ndio wanaotakiwa kukubali haki haraka kuliko washirikina, kwa vile wao wanamwamini Mungu, malaika wake, vitabu vyake na mitume wake.
Isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao , ambao ni wale walioifanyia inadi haki na wakang’ang’ania upotevu wala hawajitolei kwa hali yoyote. Basi aina hii ya watu wa kitabu muachane nao wala msijadiliane nao katika dini kabisa.
Mwenye kufuatilia Aya za Qur’an, yenye hekima, ambazo zinawajadili wapinzani na wabatilifu ataona kuwa njia ya mjadala wa kiqur’ani inakuwa kwenye uhuru wa kiakili katika nyanja zote. Uhuru huu unajitokeza pale Qur’an inapoleta dalili mkataa ya usahihi wa madai yake na wajibu wa kuyaamini:
سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ ﴿٥٣﴾
“Tutawaonyesha ishara Zetu zilizo katika upeo wa mbali, na katika nafsi zao, mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli.” (41:53).
Vile vile uhuru huu unadhihiri pale Qur’an inapomtaka mpinzani atoe dalili za kuutetea msimamo wake:
قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١١١﴾
“Sema: Leteni dalili zenu, kama nyinyi ni wasema kweli” Juz. 1 (2:111).
ائْتُونِي بِكِتَابٍ مِّن قَبْلِ هَـٰذَا أَوْ أَثَارَةٍ مِّنْ عِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤﴾
“Nileteeni Kitabu kilicho kabla ya hiki au alama yoyote ya ilimu ikiwa mnasema kweli.” (46:4).
وَلَا يَأْتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئْنَاكَ بِالْحَقِّ وَأَحْسَنَ تَفْسِيرًا ﴿٣٣﴾
“Wala hawatakuletea mfano wowote ila nasi tutakuletea haki na tafsiri iliyo nzuri.”
Juz.21 (25:33).
Huu ndio mjadala wa kiqur’ani ulivyo hasa; kusimamisha hoja kwenye madai yanayohitajia akili, kumtaka hoja anayepinga na kumjibu kwa nguvu ya hoja na fasaha zaidi akiwa ana athari yoyote ya shaka au dalili.
Mtindo huu wa Qur’an umejitokeza kwa mifumo mbali mbali; miongoni mwayo ni hii ifuatayo:
Kutosheka na ubainifu wa jambo na kuchambua maana yake. Qur’an imetumia mfumo huu kuwarudi waabudu masanamu na kuupinga uungu wake; pale ilipoweka wazi kuwa yanashindwa na kitu kidogo:
إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَن يَخْلُقُوا ذُبَابًا وَلَوِ اجْتَمَعُوا لَهُ وَإِن يَسْلُبْهُمُ الذُّبَابُ شَيْئًا لَّا يَسْتَنقِذُوهُ مِنْهُ ضَعُفَ الطَّالِبُ وَالْمَطْلُوبُ ﴿٧٣﴾
“Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu hawatoumba nzi wajapojumuika kwa hilo. Na nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata kwake. Amedhoofika atakaye na anayetakiwa.” Juz. 17 (22:73).
Yaani vipi mtu anaabudu ambacho hakiwezi kuumba hata nzi?
Vile vile Qur’an imetumia mfumo huu katika kuwarudi wale waliodai kuwa Bwana Masih ni mungu:
مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ كَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ انظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الْآيَاتِ ثُمَّ انظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٧٥﴾
“Masih mwana wa Maryam hakuwa ila ni Mtume. Wamepita kabla yake Mitume. Na mama yake ni mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi tunavyowabainishia ishara, kisha angalia jinsi wanavyogeuzwa.” Juz. 6 (5:75).
Yaani anayekula chakula ni muhitaji na Mungu huwa hahitaji kitu isipokuwa yeye ndiye anayehitajiwa. Tazama Juz. 6 (5:76 – 81).
Kutoa dalili ya kuweko kitu kwa kuweko msabibashaji: Qur’an imeutumia mfumo huu kufahamisha kuweko Mwenyezi Mungu, katika Aya kadhaa zikiwemo hizi:
أَفَلَمْ يَنظُرُوا إِلَى السَّمَاءِ فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَاهَا وَزَيَّنَّاهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٍ ﴿٦﴾
“Je, hawaangalii mbingu zilizo juu yao, vipi tulivyozijenga na tuakazipamba wala hazina nyufa.” (50:6).
Haiwezekani jengo hili lilopangiliwa vizuri na kupambwa na nyota liwe limekuja kwa sadfa. Kwa hiyo imewajibisha kuweko mpangiliaji mwenye hekima. Pia Qur’an imetumia mfumo huu kujulisha umoja wa Mungu pale iliposema:
لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّـهُ لَفَسَدَتَا ﴿٢٢﴾
“Lau wangelikuwemo humo miungu wengine isipokuwa Mwenyezi Mungu basi zingefisidika.” Juz. 17 (21:22).
Kwamba kuweko wengi kungeleta ufisadi; na kwa kuwa hakuna ufisadi basi sio wengi. Kwa ibara ya watu wa mantiki ni kuwa kutokuweko linalolazimiana, ambalo ni ufisadi, kunafahamisha kutokuweko linalolazimiwa, ambalo ni kuweko na waungu wengi.
Kutoa dalili kwa umwanzo: Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametumia mfumo huu kutoa dalili ya kuweko marejeo ya ufufo katika Aya 27 ya Sura Ar-Rum kwenye Juzuu hii tuliyo nayo: “Naye ndiye ambaye anaanzisha uumbaji kisha ataurudisha na jambo hili ni jepesi zaidi kwake.” Kwamba mwenye kuweza kukifanya kitu bila ya kuweko kitu kingine, basi ana uwezo zaidi kukikusanya tena baada ya kutawanyika.
Mifumo hii yote ni dalili mkataa kwamba mjadala wa kiqur’ani uko kwenye msingi wa kiakili na uhuru wake; na kwamba lengo ni kuidhi- hirisha haki kwa ajili ya kuiamini na kuitumia au kumjibu mwenye kupinga kwa mfumo wa kumkinaisha mwenye kuitafuta haki kwa ajili ya haki.
Na semeni: Tumeamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja na sisi ni wenye kusilimu kwake.
Maneno yanaelekezwa kwa waislamu. Maana ni kuwa enyi waislamu! Kama ilivyokuwa wajibu kwenu kujadiliana vizuri na yule mnayemtarajia katika watu wa Kitabu, vile vile msiwaonyeshe uadui; bali mchanganyike nao na muwaambie tunayemwabudu sisi ndiye mnayemwabudu nyinyi. Sisi tunamwamini yeye na tunaamini Tawrat iliyoteremshwa kwa Musa na Injil iliyotermshwa kwa Isa; sawa na tunavyoiamini Qur’an iliyoteremshwa kwa Muhammad. Kwa maneno mengine ni: kuweni kwa uislmu ni pambo wala msiwe ni fedheha.
Na hivyo ndio tumekuteremshia Kitabu.
Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad(s.a.w.w) . Makusudio ya Kitabu ni Qur’an. Maana ni kuwa, kama tulivyomteremshia Musa Tawrat na Isa tukamtermshia Injil, kabla yako, vile vile nawe tumekuteremshia Qur’an.
Basi wale ambao tumewapa Kitabu wanakiamini.
Hii ni kuwaishiria wale waliosilimu katika mayahudi na manaswara.
Na miongoni mwa hao wako wanaokiamini.
Ni ishara ya wale waliosilimu katika washirikina wa kiarabu.
Na hawazikatai ishara zetu isipokuwa makafiri.
Unaweza kuuliza kuwa : kukataa ndio kukufuru; hapo basi maana yatakuwa hawazikatai ila wakataaji; sawa na kusema: Hakai ila mkaaji. Na Qur’an haiko hivi?
Jibu : Makusudio ni kuwa dalili za ukweli wa Qur’an ziko wazi kiasi ambacho hawezi kuzipinga, isipokuwa aliyeifanya batili ndio dini. Na ukafiri ni itikadi, mwenye nayo haiachi hata kama ubatilifu wake utadhihiri kama jua; sawa na mayahudi walioambiana: “Wala msimwamini ila yule anayefuata dini yenu.” Juz. 3 (3:73).
Na hukuwa kabla yake unasoma kitabu chochote, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume. Ingelikuwa hivyo wangelifanya shaka wabatilifu.
Wameafikiana wana historia kuwa Muhammad(s.a.w.w) hakusoma kwa mwalimu yoyote, mkubwa wala mdogo. Lakini pamoja na hivyo ameleta Qur’an iliyo muujiza wa miujiza katika itiakadi yake, sharia yake, mafunzo yake, misingi yake yote, kuwatolea habari mitume waliotangulia na mengineyo.
Hii ni dalili tosha kuwa hiyo ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, haikutengenezwa na mtu.
Lau Mtume(s.a.w.w) angeliandika na kusoma au akawa amesoma kwa mwalimu, wazushi wangesema kuwa Qur’an imetungwa na Muhammad, si wahyi wa Mwenyezi Mungu.
Kuna mmoja alisema Muhammad(s.a.w.w) amechukua Qur’an kutoka kwa mtawa wa kinaswara huko Sham. Hatujui ameyatoa wapi haya? Sijui atasemaje kuhusu Aya hizi:
لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ﴿٧٣﴾
“Kwa hakika wamekufuru wale waliosema, Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa utatu.” Juz.6 (5:73).
اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَـٰهًا وَاحِدًا لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٣١﴾
“Wamefanya makuhani wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu na Masih mwana wa Maryam. Wala hawakuamrishwa isipokuwa wamwambudu Mungu mmoja hakuna Mungu ila yeye. Ametakata na wanayomshirikisha nayo.” Juz. 10 (9:31).
Tazama kifungu cha ‘Qur’an na wanaohubiri utatu’ katika Juz. 6 (4:171 – 173).
Bali hicho ni ishara zilizo wazi katika vifua vya waliopewa ilimu; na hawazikatai ishara zetu isipokuwa madhalimu.
Hapana! Qur’an haikutengenezwa na Muhammad(s.a.w.w) , bali ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu wanaiamini na kuitegemea wale wanaotafuta ilimu kwa imani ya haki na kuitumia.
Ama wale ambao wameifanya ilimu ni duka la biashara, basi wataipinga, kwa sababu inapiga vita unafiki na ukandamizaji.
وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَاتٌ مِّن رَّبِّهِ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّـهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٥٠﴾
50. Na walisema: Mbona hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake? Sema: Hakika ishara ziko kwake Mwenyezi Mungu; na mimi kwa hakika ni muonyaji mwenye kubain- isha tu.
أَوَلَمْ يَكْفِهِمْ أَنَّا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَرَحْمَةً وَذِكْرَىٰ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٥١﴾
51. Je, kwani hayakuwatosha kwamba tumekuteremshia Kitabu wanachosomewa? Hakika katika hiyo kuna rehema na mawaidha kwa watu wanaoamini.
قُلْ كَفَىٰ بِاللَّـهِ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ شَهِيدًا يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالَّذِينَ آمَنُوا بِالْبَاطِلِ وَكَفَرُوا بِاللَّـهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٥٢﴾
52. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi baina yangu na nyinyi, anajua yaliyomo mbinguni na ardhini. Na wale ambao wameamini batili na wakamkufuru, hao ndio waliopata hasara.
وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِالْعَذَابِ وَلَوْلَا أَجَلٌ مُّسَمًّى لَّجَاءَهُمُ الْعَذَابُ وَلَيَأْتِيَنَّهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٥٣﴾
53. Na wanakuhimiza adhabu. Na lau si wakati maalum uliowekwa, basi adhabu ingeliwajia na hakika ingeliwatokea ghafla na hali wao hawatambui.
يَسْتَعْجِلُونَكَ بِالْعَذَابِ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿٥٤﴾
54. Wanakuhimiza adhabu na hali Jahannam kwa hakika imewazunguka makafiri.
يَوْمَ يَغْشَاهُمُ الْعَذَابُ مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِمْ وَيَقُولُ ذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٥٥﴾
55. Siku itakayowafunika adhabu hiyo kutoka juu yao na chini ya miguu yao na atasema: Onjeni mliyokuwa mkiyatenda.
Aya 50 – 55
Na walisema: “Mbona hakutermshiwa ishara kutoka kwa Mola wake?” Sema: Hakika ishara ziko kwake Mwenyezi Mungu; na mimi kwa hakika ni muonyaji mwenye kubainisha tu.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2: 118-119), Juz. 7 (6:37), Juz. 11 (10:20) na nyinginezo.
Je, kwani hayakuwatosha kwamba tumekuteremshia Kitabu wanachosomewa?
Kila kilichomo ndani ya Kitabu hicho kinashuhudia kuwa kinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Wao wameshindwa kuleta hata sura mmoja mfano wake. Kimefichua mambo mengi waliyoyadhamiria na kuyaficha; kime- wasimulia visa vya waliopita na wakashuhudia ukweli wake wale wenye insafu katika watu wa Kitabu.
Hayo ni hoja tosha kwa anayeitafuta haki kutoka chimbuko lake. Na washirikina walijikweza na kuifanyia inadi risala ya Muhammad(s.a.w.w) na hali wana uhakika na hilo. Lililowazuia kufuata haki ni tamaa na manufaa tu.
Hakika katika hiyo kuna rehema na mawaidha kwa watu wanaoamini.
Hiyo ni ishara ya Qur’an nayo ni rehema na neema kwa anayeitumia. Pia ni ukumbusho na mawaidha kwa anayeisadiki na kuamini sharia zake na ishara zake.
Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi baina yangu na nyinyi, anashuhudia na kujua kuwa nimefikisha risala yake na kwamba nyinyi mmeikadhibisha na kuipinga. Vile vileanajua yaliyomo mbinguni na ardhini, wala hakifichiki kwake chochote.
Na wale ambao wameamini batili na wakamkufuru, hao ndio waliopata hasara.
Kila yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu ni batili na kila mwenye kumwasi Mwenyezi Mungu huyo ni kafiri aliye fasiki. Yote hayo ni balaa inayostahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na mwisho wake ni Jahannam.
Na wanakuhimiza adhabu. Na lau si wakati maalum uliowekwa, basi adhabu ingeliwajia.
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) aliwalingania makuraishi kwenye Tawhid na uadilifu, akawahadharisha na mwisho wa shirki na dhulma. Wakasema kwa kung’ang’ania ubatilifu wao: “Haya tuletee adhabu chungu.” Kulikuwako na makuraishi walioona ni bora kuangamia kuliko kumnyenyekea Muhammad kwa kuwa na chuki naye.
Tumewaona watu wengi wakipinga mwito wa haki kwa sababu ya anayetoa mwito huo sio kwa kupinga haki yenyewe.
Basi Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawajibu wale wanaoihimiza adhabu kwamba Mwenyezi Mungu amekadiria muda maalum wa adhabu yao, lau si hivyo ingeliwajia saa hiyo hiyona hakika ingeliwatokea ghafla na hali wao hawatambui.
Adhabu itawajia tu, lakini ni kwa ghafla bila ya kutambua, ili wazidi machungu juu ya machungu. Uchungu wa kushtukiziwa na uchungu wa adhabu yenyewe.
Wanakuhimiza adhabu na hali Jahannam kwa hakika imewazunguka makafiri.
Wanaharikisha adhabu ya dunia, lakini hawajui kwamba wao wamezungukwa na dhabu kali na kubwa na kwamba itawafikia ghaflasiku itakayowafunika adhabu hiyo kutoka juu yao na chini ya miguu yao na atasema: Onjeni mliyokuwa mkiyatenda.
Hiyo ni siku ya haki isiyo na shaka; haki itakuwa tu iwe ni sasa au baadaye. Ama moto wa siku hiyo, tunamwomba Mwenyezi Mungu atuepushe nao, utawazunguka pande zote wale walioghadhibikiwa na utaunguza nyama na mifupa na kuwa vumbi; wanarudiwa tena na uhai na moto nao unarudia kazi yake. Hali itaendela kuwa hivyo mpaka pale atakapotaka Mwenyezi Mungu.
Ewe Mola wangu! Najilinda kwako, kwa rehema zako uniepushe na ghadhabu zako na ninkuomba shufaa kwa moyo wangu ulivyojikunja na nasaha na kupenda heri kwa waja wako! Na Wewe ndiwe mjuzi zaidi wa siri zote”.
13
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ أَرْضِي وَاسِعَةٌ فَإِيَّايَ فَاعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾
56. Enyi waja wangu mlioamini! Kwa hakika ardhi yangu ina wasaa, basi niabuduni mimi tu.
كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ثُمَّ إِلَيْنَا تُرْجَعُونَ ﴿٥٧﴾
57. Kila nafsi itaonja mauti, kisha mtarudishwa kwetu.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُبَوِّئَنَّهُم مِّنَ الْجَنَّةِ غُرَفًا تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا نِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na wale ambao wameamini na wakatenda mema, bila shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi yapitiwayo na mito chini yake, wadumu humo. Ni neema iliyoje kwa malipo ya watendaji.
الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ ﴿٥٩﴾
59. Ambao walisubiri na kwa Mola wao wanategemea.
وَكَأَيِّن مِّن دَابَّةٍ لَّا تَحْمِلُ رِزْقَهَا اللَّـهُ يَرْزُقُهَا وَإِيَّاكُمْ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٦٠﴾
60. Wanyama wangapi hawabebi riziki zao. Mwenyezi Mungu anawaruzuku wao na nyinyi. Na Yeye ni Msikizi, Mjuzi.
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٦١﴾
61. Na ukiwauliza ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi, bila shaka watasema ni Mwenyezi Mungu. Basi wanageuzwa wapi?
اللَّـهُ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ لَهُ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٦٢﴾
62. Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake na humdhikisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّن نَّزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ مَوْتِهَا لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿٦٣﴾
63. Na ukiwauliza ni nani aliyeteremsha maji kutoka mbinguni na akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake, bila shaka watasema ni Mwenyezi Mungu. Sema: Alhamdulillah (sifa njema ni za Mwenyezi Mungu), Bali wengi wao hawafahamu.
Aya 56 – 63
Enyi waja wangu mlioamini! Kwa hakika ardhi yangu ina wasaa, basi niabuduni mimi tu.
Wameafikiana mafaqihi kuwa haijuzu kwa Mwislamu kukaa katika mji ambao itakuwa uzito kwake kutekeleza wajibu wa kidini; kama vile Swala na mfano wake; hata kama mji huo ndio nyumbani kwake; na kwamba ni lazima ahame kwenda mahali pengine atakapoweza kutekeleza hayo. Tumezungumzia kwa ufafanuzi zaidi maudhui haya katika Juz. 5 (4:97) kifungu ‘Mafaqihi na wajibu wa hijra’.
Kila nafsi itaonja mauti, kisha mtarudishwa kwetu.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwajibisha kuhama mji uliotajwa, alisema kuwa anayehofia kufa uhamishoni, basi hawezi kuokoka na mauti popote pale alipo, nyumbani au ugenini. Na baada ya kufa ataulizwa wajibu aliouacha na mambo ya haramu aliyoyafanya; yakiwemo kukaa kwenye mji anaolazimika kuacha ibada na kunywa pombe.
Na wale ambao wameamini na wakatenda mema, bila shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi yapitiwayo na mito chini yake wadumu humo.
Atakayetoka nyumbani kwake kwa kufanya Hijra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi Mungu atampa badali bora zaidi yake – ghorofa, miti, na mito katika nyumba na makazi ya amani.
Ni neema iliyoje kwa malipo ya watendaji. Ambao walisubiri na kwa Mola wao wanategemea.
Kuna malipo gani zaidi ya Pepo? Kwa vile ni adhimu basi nayo thamani yake iko ghali na adhimu. Thamani yenyewe ni: kukataa kujisalimisha kwa maadui wa Mwenyezi Mungu, kutomhofia yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, kumfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu peke yake na kuwa na subira kwa ajili yake katika matukio yote, vyovyote yatakavyokuwa.
Wanyama wangapi hawabebi riziki zao. Mwenyezi Mungu anawaruzuku wao na nyinyi. Na Yeye ni Msikizi, Mjuzi.
Watu wengi wanamwamini Mwenyezi Mungu kinadharia; kwamba riziki za viumbe ziko mikononi mwake Yeye peke yake, kwamba hazina yake haishi wala haina ukomo na kwamba Yeye ni mkarimu, hakosi kitu anayemwamini na kumtegemea Yeye.
Wanaamini haya yote kinadharia, lakini wanamkana Mungu kimatendo; wanamtegea kumbe badala ya Muumba na wanajikurubisha kwa kimbe kwa mambo yanayoiondoa dini yao na dhamiri yao kwa kuwa na tamaa ya vilivyo mikononi mwake na wanajiweka mbali na Mwenyezi Mungu wakikata tamaa naye na hazina yake.
Aya hii inamkemea mumin huyu aliye kafiri.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni Muumba wa ulimwengu na vilivyomo ndani yake, aina zote za sababu za riziki zinakomea kwake; nazo ziko tayari kwa kila mwenye kuzitaka na kuzihangaikia. Ikiwa zitakuwa nzito basi zinajiandaa kwa mhitaji kwa ubora zaidi bila ya kutambua; bali viumbe hai vingi haviifanyii kazi riziki wala kuibeba, lakini inawajia pale wanapoihitajia.
Hapa kuna mazingatio kwa vibaraka wahaini na kila mwenye kuiuza dini yake kwa shetani na akayafanya maasi ndio nyenzo ya kupata tonge.
Hasha! Haiwezekeni kwa Mwenyezi Mungu kukataza kitu na azuie sababu za riziki. Vipi iwe hivyo na hali dini yake ni dini ya maisha? Imam Ali(a.s) anasema:“Hakika lile mliloamrishwa lina wasaa zaidi kuliko lile mlilokatazwa na mliyohalalishiwa ni mengi zaidi ya mliyoharamishiwa. Basi acheni yaliyo machache kwa ajili ya yaliyo mengi. Na yaliyo dhiki kwa ajili ya yaliyo na wasaa.”
Akasema tena: “Kuamrisha mema na kukataza mabaya ni maumbile mawili katika viumbe vya Mwenyezi Mungu na kwamba hayo hayakarubishi ajali wala hayapunguzi riziki.”
Huko nyuma tumeweka wazi tofauti baina ya imani ya kweli na imani ya mawazo. Kwamba imani ya kweli ni ile iliyothibiti kwenye moyo na ikaleta kumhofia Mwenyezi Mungu na kujihimu na twaa yake na radhi yake kwa kauli na vitendo.
Lakini imani ya kuwazia haithibiti moyoni; isipokuwa imerambwa na ulimi, na inakuwa ni ya kuwazia tu, sawa na njozi. Ushahidi mkubwa wa imani hii ya kombokombo ni kuwa mtu anamwamini Mwenyezi Mungu kwa kauli na huku anamtarajia kiumbe na kumhofia badala ya Mwenyezi Mungu.
Na ukiwauliza ni nani aliyemba mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi, bila shaka watasema ni Mwenyezi Mungu.
Wanaoulizwa ni wapenda anasa waliokaidi risala ya Muhammad(s.a.w.w) .
Unaweza kuuliza : ikiwa wanakubali waziwazi kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye muumba wa ulimwengu, basi iko wapi sababu ya kupin- gana kwao na mitume?
Jibu : Kimsingi wao wanamkubali Mwenyezi Mungu na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliyewahusu wao kwa mali na utawala na akawachagulia wengine ufukara na utumwa.
Hakuna mwenye shaka kwamba mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu na akaamini kuwa watu wana anayostahiki juu yake na yeye ana anayostahiki juu ya watu, basi huyu ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko huyo anayeamini bila ya matendo
Dalili ya kuwa wao wanamkubali Mwenyezi Mungu kwenye msingi huu ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na wanapoambiwa: Toeni katika yale aliyowapa Mwenyezi Mungu, wale waliokufuru huwambia walioamini: Je, tumlishe ambaye Mwenyezi Mungu akipenda atamlisha? Nyinyi hammo ila katika upotevu dhahiri” (36:47).
Basi wanageuzwa wapi?
Wanaigeuka haki kwa kuzua kuwa Mwenyezi Mungu amewahusu wao tu kuwa na mali kuliko wengine wote.
Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake na humdhikisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:26).
Na ukiwauliza ni nani aliyeteremsha maji kutoka mbinguni na akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake, bila shaka watasema ni Mwenyezi Mungu.
Wakiulizwa kuhusu mumbaji wa ulimwengu wanajibu kwa kukabali kuwa ni Mwenyezi Mungu lakini kwa masharti yao. Na wakiulizwa aliyeteremsha maji na akahuisha ardhi, ambayo ndiyo sababu ya moja kwa moja ya riziki na utajiri ulio mikononi mwao, pia wanasema na kukubali kuwa ni Mwenyezi Mungu peke yake.
Hapo wanajipinga wao wenyewe. Ikiwa sababu za riziki ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na si mikononi mwao, itakuwaje iwe yao tu peke yao na wengine wasipate? Ikiwa Mwenyezi Mungu ni wa wote, vipi heri zake na baraka zake?
Sema: Alhamdulillah (sifa njema ni za Mwenyezi Mungu), ambaye ameidhihirisha haki hata kupitia mdomoni mwa maadui zake wazushi.
Bali wengi wao hawafahamu kwamba wao ni waongo na wazushi wakijipinga wao wenyewe kwa wenyewe.
وَمَا هَـٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٦٤﴾
64. Na maisha haya ya dunia si chochote ila ni upuuzi na mchezo. Na nyumba ya akhera ndiyo maisha hasa, lau wangelikuwa wanajua.
فَإِذَا رَكِبُوا فِي الْفُلْكِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ ﴿٦٥﴾
65. Na wanapopanda katika jahazi, humwomba kwa kumsafia utiifu, lakini anapowavua wakafika nchi kavu mara wanamshirikisha.
لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ وَلِيَتَمَتَّعُوا فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿٦٦﴾
66. Ili wapate kuyakana tuliyowapa na wapate kustarehe, punde watajua.
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا جَعَلْنَا حَرَمًا آمِنًا وَيُتَخَطَّفُ النَّاسُ مِنْ حَوْلِهِمْ أَفَبِالْبَاطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَةِ اللَّـهِ يَكْفُرُونَ ﴿٦٧﴾
67. Je, hawaoni kwamba tumeifanya nchi takatifu ina amani na hali watu wa pambizoni mwake wananyakuliwa. Je, wataamini batili na kuzikataa neema za Mwenyezi Mungu?
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُ أَلَيْسَ فِي جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْكَافِرِينَ ﴿٦٨﴾
68. Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uwongo. Au akadhibishaye haki inapomjia? Je, si katika Jahannam ndio yatakuwa makazi ya makafiri?
وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا وَإِنَّ اللَّـهَ لَمَعَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٦٩﴾
69. Na wale wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, hakika tutawaongoza kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wema.
Aya 64 – 69
Na maisha haya ya dunia si chochote ila ni upuuzi na mchezo.
Makusudio ya dunia hapa ni dunia ya uzembe, uovu, kujifaharisha na israfu kwa hisabu ya wanyonge. Vile vile dunia ya wakoloni na wazayuni waundaji wa mauti, njama za kiuadui na mapinduzi ya kijinga. Dunia ya mashirika ya ulanguzi, unyonyaji, na kuifanyia biashara dini.
Dunia ya vyombo vya habari vya kulipwa ili kutia sumu kwenye fikra na kuvungavunga kuuficha ukweli na propaganda za uwongo.
Hii ndio dunia ya mchezo, ufisadi shari na upotevu, inayomchukiza Mwenyezi Mungu na kuwaandalia wakazi wake adhabu ya kuunguza. Ama dunia ya watu wema, walio huru, waungwana ambao wanaleta masilahi katika nchi na sio ufisadi. Hii ndio dunia ya haki, heri, uongofu na kufaulu ambayo wakazi wake watapata radhi za Mwenyezi Mungu na kufuzu kwa neema yake na Pepo yake.
Na nyumba ya akhera ndiyo maisha hasa, lau wangelikuwa wanajua.
Tunaifasiri kwa kauli yake Imam Ali(a.s) :“Kila neema isiyokuwa Pepo ni upuzi na kila balaa isiyokuwa moto ni faraja.” Na kauli yake katika wasifa wa Pepo “Haikatiki neema yake, haondoki mkazi wake, hazeeki anayedumu humo, wala kukata tamaa anayekaa humo.”
Na wanapopanda katika jahazi, humwomba kwa kumsafia utiifu, lakini anapowavua wakafika nchi kavu mara wanamshirikisha.
Inasemekana kuwa watu wa wakati wa jahiliya walikuwa wanaposafiri baharini huchukua masanamu yao. Dhoruba ikawakumba wanayatupa masanamu na kusema: Yarabi yarabi! (Ewe Mola ewe Mola!). Hili si ajabu. Wengine walikuwa wakitengeneza sanamu ya tende, wakishikwa na njaa wanaila.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:22). Ni vizuri kurudia tuliyoyaandika huko kwenye kifungu ‘Mwenyezi Mungu na maumbile.’
Ili wapate kuyakana tuliyowapa na wapate kustarehe, punde watajua.
Yaani wapate kuacha kushukuru kwa neema ya kuokoka aliyoaneemesha Mwenyezi Mungu kwa ukarimu wake na upole. Basi wataona hizaya ya adhabu itakayowapata kesho.
Je, hawaoni kwamba tumeifanya nchi takatifu ina amani na hali watu wa pambizoni mwake wananyakuliwa.
Wanaambiwa washirikina wa Makka ambao wamempiga vita Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Hiyo ni kutokana na neno ‘Nchi takatifu ina amani.’ Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawakumbusha yale aliyowahusu nayo kuliko watu wengine; kwa kukaa katika mji wenye amani ya nafsi na mali; na jirani zao wanaishi na hofu na wasiwasi wa maisha yao na vitu vyao.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:125), Juz. 4 (3:97) na Juz. 20 (28:57).
Je, wataamini batili na kuzikataa neema za Mwenyezi Mungu?
Kila anayenyenyekea batili na akaridhia yasiyokuwa haki kwa tamaa ya dunia, basi yeye ni katika anayeamini batili na kuzikana fadhila za Mwenyezi Mungu na hisani yake.
Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uwongo. Au akadhibishaye haki inapomjia? Je, si katika Jahannam ndio yatakuwa makazi ya makafiri?
Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:21).
Na wale wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, hakika tutawongoza kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wema.
Juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni mambo mengi; miongoni mwayo ni: kutafuta ilimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kutafuta maisha kwa jasho, kuamrisha mema na kukataza maovu. Ilivyeo bora kabisa kuliko yote ni kuisafisha ardhi na madhalimu na wafisadi.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamwongoza kwenye haki kila Mwenye kum- fanyia ikhlasi katika nia yake na akafanya uzuri katika matendo yake, wala hamuongozi Mwenye kufanya israfu aliye muongo.
14
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
Sura Ya Thelathini: Surat Ar-Rum. Imeshuka Makka ina Aya 60
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu.
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miim.
غُلِبَتِ الرُّومُ ﴿٢﴾
2. Warumi wameshindwa.
فِي أَدْنَى الْأَرْضِ وَهُم مِّن بَعْدِ غَلَبِهِمْ سَيَغْلِبُونَ ﴿٣﴾
3. Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda.
فِي بِضْعِ سِنِينَ لِلَّـهِ الْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ ﴿٤﴾
4. Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo waumini watafurahi.
بِنَصْرِ اللَّـهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٥﴾
5. Kwa nusra ya Mwenyezi Mungu. Humnusuru amatakaye; na Yeye ndiye Mwenye uwezo, Mwenye kurehemu.
وَعْدَ اللَّـهِ لَا يُخْلِفُ اللَّـهُ وَعْدَهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٦﴾
6. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake, lakini watu wengi hawajui.
يَعْلَمُونَ ظَاهِرًا مِّنَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ الْآخِرَةِ هُمْ غَافِلُونَ ﴿٧﴾
7. Wanajua dhahiri ya maisha ya dunia na wameghafilika na Akhera.
Aya 1 – 7
Alif Laam Miim.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1).
Warumi wameshindwa katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda katika miaka michache.
Huko nyuma tumetaja aina za miujiza ya Qur’an; miongoni mwazo ni:
• Kushindwa washirikina kuleta mfano wake japo Sura moja tu.
• Itikadi yake ya kumwamini Mungu na mongozo wake unaoleta maendeleo ya mtu na sharia yake inayotekeleza mahitaji yote ya watu, mahali popote na wakati wowote. Pia kukubaliana na sharia za kutungwa zenye masilahi ya watu kwa namna fulani. Na inajulikana kuwa aliyezifikisha sharia hizo hakukaa kwa mwalimu.
• Maneno ya Mwenyezi Mungu yanachukua njia nyingi, kinyume na maneno ya binadamu. Tumegundua wakati tukitafsiri Aya zake, kuwa siri ya hilo ni ukuu wa mwenye kusema na elimu yake isiyolinganishwa na chochote. Tazama Juz. 18 (24:55), kifungu cha: ‘Njia nyingine ya muujiza wa Qur’an.’
Muujiza mwingine wa Qur’an unaojitokeza ni kutoa habari za mambo yaliyofichikana ambayo hayajui isipokuwa mjuzi wa ghaibu; kama kufichua wanayoyadhamiria wanafiki katika nyoyo zao, ushindi wa Mtume kwa maadui zake, kujitokeza Uislamu juu ya dini zote, kurudi Mtume Makka akiwa ni mshindi baada ya kufukuzwa.
Pia kutolea habari yatakayowatokea maswahaba zake baada yake, kuhusu mayahudi na tabia yao na ushindi wa manaswara wa Roma juu wafursi baada ya miaka kadhaa ya ushindi wa Fursi juu ya Roma. Aya tuliyo nayo inazungumzia tukio hili; kama walivyokubaliana wapokezi na wafasiri wote.
Muhtasari wa tukio hilo ni: Wafursi walikuwa kwenye dini ya kimajusi, hawana Kitabu kama washirikina. Warumi walikuwa kwenye dini ya kinaswara (wakiristo) na walikuwa na Kitabu kama waislamu.
Katika zama za Mtume Muhammad(s.a.w.w) kulitokea vita baina ya Fursi na Rumi katika nchi ya Sham. Washirikina walikuwa wanapendelea upande wa Fursi kwa vile walikuwa washirikina kama wao; na waislamu walipendelea upande wa Rumi kwa sababu wana Kitabu.
Basi zikaja habari za ushindi wa Fursi, waislamu wakaona tabu na washirikina wakaona raha, wakiwaambia waislamu: Wafursi wasio na kitabu wamewashinda warumi watu wa Kitabu. Nyinyi mnadai kuwa mtashinda kwa Kitabu alichoteremshiwa Mtume wenu! Basi sisi tusio na kitabu ndio tutakaowashinda; kama ilivyotokea kwa wafursi na warumi.
Ndio ikashuka Aya hii. Haukupita muda wa miaka tisa ndipo Mwenyezi Mungu akadhihirisha ushindi wa warumi juu ya wafursi. Basi wakafurahi waislamu na wakahuzunika washirikina.
Hapa ndio inakuwa siri ya muujiza wa Qur’an, ambapo ilitolea habari za uhakika sio kubahatisha, kuwa vita vitaanza tena baina ya Fursi na Roma na vitamalizika kwa ushindi wa Roma. Na ikaelezea hata wakati. Neno ‘miaka michache’ limefasiriwa kutokana na neno la kiarabu ‘Bidh’i’ lenye maana ya idadi baina ya tatu na kumi.
Basi ikawa kama ilivyosema Qur’an. Ghaibu hii iliyofichika, haijui ila Mwenyezi Mungu peke yake.
Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake.
Yaani kabla ya ushindi na baada ya ushindi na ni kwake pekee yanarejeshwa mambo yote.
Na siku hiyo waumini watafurahi kwa nusra ya Mwenyezi Mungu.
Watafurahi waislamu siku warumi watakapowashinda wafursi.
Humnusuru amatakaye.
Wawili wakipigana, yule mwenye sababu za kushinda ndiye mshindi, awe na haki au ubatilifu. Mwenyezi Mungu ametegemeza kwake ushindi kwa kuangalia kuwa sababu zote za kilimwengu zinakomea kwake, kwa vile Yeye ndiye Muumba wa ulimwengu na yaliyomo ndani yake.
Na Yeye ndiye Mwenye uwezo, Mwenye kurehemu.
Anamwadhibu dhalimu na kumhurumia mdhulumiwa.
Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake, lakini watu wengi hawajui.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutoa habari za ghaibu, za ushindi wa warumi kwa wafursi, alisisitiza kuwa hilo litatokea tu. Lakini asiyemwamini Mwenyezi Mungu ataamini vipi ahadi yake?
Msisitizo wa uhakika ni ushahidi mkubwa kuwa Qur’an ni wahyi kutoka kwa ambaye kwake ulimwengu wa ghaibu na wa dhahiri ni sawa tu. Lau ingelitokea kinyume, basi maadui wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) wangeliifanya hiyo ni nyenzo ya kuutuhumu ukweli na ujumbe wake.
Wanajua dhahiri ya maisha ya dunia na wameghafilika na Akhera.
Dunia na hali zake ni ulimwengu wa dhahiri unajulikana kwa hisia tano; na Akhera na vituko vyake ni ulimwengu wa ghaibu, haujulikani ila kwa njia ya wahyi na wao hawauamini, basi watajuaje mambo ya Akhera.
أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا فِي أَنفُسِهِم مَّا خَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ لَكَافِرُونَ ﴿٨﴾
8. Je, hawafikiri katika nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake ila kwa haki. Na kwa hakika watu wengi ni wenye kukataa kuwa watakutana na Mola wao.
أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ كَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَأَثَارُوا الْأَرْضَ وَعَمَرُوهَا أَكْثَرَ مِمَّا عَمَرُوهَا وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٩﴾
9. Je hawatembei katika ardhi wakaona ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao na wakiilima ardhi na kuistawisha zaidi kuliko walivyoistawisha wao. Na mitume wao wakawajia na dalili zilizo wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu wenyewe.
ثُمَّ كَانَ عَاقِبَةَ الَّذِينَ أَسَاءُوا السُّوأَىٰ أَن كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ وَكَانُوا بِهَا يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١٠﴾
10. Kisha ukawa mwisho wa waliofanya ubaya ni kuzikanusha ishara za Mwenyezi Mungu na wakawa wanazifanyia stihzai.
اللَّـهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿١١﴾
11. Mwenyezi Mungu huanzisha uumbaji na kisha akaurudisha. Na kisha mtarejeshwa kwake.
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُبْلِسُ الْمُجْرِمُونَ ﴿١٢﴾
12. Na siku itakaposimama Saa wakosefu watakata tamaa.
وَلَمْ يَكُن لَّهُم مِّن شُرَكَائِهِمْ شُفَعَاءُ وَكَانُوا بِشُرَكَائِهِمْ كَافِرِينَ ﴿١٣﴾
13. Wala hawatakuwa na waombezi miongoni mwa waliokuwa wakiwashirikisha nao watawakana washirika wao.
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَتَفَرَّقُونَ ﴿١٤﴾
14. Na siku itakaposimama Saa, siku hiyo watagawanyika.
فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَهُمْ فِي رَوْضَةٍ يُحْبَرُونَ ﴿١٥﴾
15. Ama wale ambao wameamini na wakatenda mema watakuwa katika Bustani wakifurahishwa.
وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ فَأُولَـٰئِكَ فِي الْعَذَابِ مُحْضَرُونَ ﴿١٦﴾
16. Na ama wale ambao wamekufuru na wakazikadhibisha ishara zetu na mkutano wa Akhera, basi hao watahudhurishwa katika adhabu.
Aya 8 – 16
Je, hawafikiri katika nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake ila kwa haki.
Mwenyezi Mungu ni mwenye hekima haumbi kitu chochote isipokuwa kwa haki, na upuuzi kwake ni muhali. Yeye ni Muweza wa kuwarudishia watu uhai baada ya kwisha muda wake uliopangwa.
Mwenye kuangalia vizuri ukuu wa ulimwengu atatambua hekima ya Mwenyezi Mungu katika uumbaji wake na atatambua uweza wake wa kufufua wafu. Kwa sababu kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa kuliko kumrudishia uhai mtu baada ya mauti.
“Je! hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi na hakuchoka kwa kuziumba, ana uwezo wa kuwafufua wafu? Ndio! Hakika yeye ni muweza wa kil kitu” (46:33).
Na kwa hakika watu wengi ni wenye kukataa kuwa watakutana na Mola wao.
Wanakataa kuwa ana uweza wa kurudisha uhai na hawajui kwamba anayeweza kuuanzisha anaweza pia kuurudisha? Kwa vile sababu ni moja tu.
Je hawatembei katika ardhi wakaona ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (3:137).
Na wakiilima ardhi na kuistawisha zaidi kuliko walivyoistawisha wao. Na mitume wao wakawajia na dalili zilizo wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu wenyewe.
Watu wa umma zilizopita walikuwa na maendeleo zaidi ya kilimo na majumba kuliko waarabu, lakini walipodhulumu nafsi zao kwa kufuru yao na kuwakadhibisha kwao mitume, Mwenyezi Mungu aliwapatiliza kwa adhabu na maangamizi. Je, hawaogopi wanaomkadhibisha Muhammad kuwapata yaliyowapata waliokuwa na nguvu zaidi.
Kisha ukawa mwisho wa waliofanya ubaya ni kuzikanusha ishara za Mwenyezi Mungu na wakawa wanazifanyia stihzai.
Mitume wao waliwajia kwa ubainifu ili wawaokoe na upotevu na kuangamia. Wakawafanyia uovu kwa kuwakadhibisha na kuwafanyia stihizai. Ikawa malipo yao ni adhabu na marejeo mabaya.
Mwenyezi Mungu huaanzisha uumbaji na kisha akaurudisha. Na kisha mtarejeshwa kwake.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 20 (29:19).
Na siku itakaposimama Saa wakosefu watakata tamaa.
Siku hiyo ya Kiyama watajua wenye makosa kwamba hakuna mategemeo wala ujanja kwa aliyetanguliza maasi na kuipa muda toba. Wataonja uchungu wa kukata tamaa kwa sababu walizama kwenye upotevu na wakaung’ang’ania.
Wala hawatakuwa na waombezi miongoni mwa waliokuwa wakiwashirikisha nao watawakana washirika wao.
Walikuwa na wale wanaowashirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu duni- ani, wakiwafuata kwenye upotevu na ufisadi kwa ujinga na uigizaji. Walikuwa wakiwatarajia kuwanufaisha na kuwaombea siku ya Kiyama. Lakini watakapokusanyika kwa Mwenyezi Mungu wote na kuiona adhabu na kuhakikisha kuwa hakuna utetezi, basi hapo mfuaswa atajitenga na mfuasi na kiongozi na anayeongozwa.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 2 (2:166 – 167).
Na siku itakaposimama Saa, siku hiyo watagawanyika.
Yaani watagawanyika, wengine ni wa Peponi na wengine ni wa motoni. Yaani wao duniani walikuwa wakikutana sokoni kwenye vyama, masomoni, sehemu za ibada n.k. Lakini siku ya Kiyama hakuna tena makutano.
Ama wale ambao wameamini na wakatenda mema watakuwa katika Bustani wakifurahishwa. Na ama wale ambao wamekufuru na wakazikadhibisha ishara zetu na mkutano wa Akhera, basi hao watahudhurishwa katika adhabu.
Mwenyezi Mungu kesho atawafufua viumbe, awakusanye kwa maswali anayotaka kuwauliza, kisha atawafanya makundi mawili: Kundi la watu wa shirki na la watu wa heri. Hawa atawaneemesha kwa makazi mazuri na Pepo zenye neema; na wale atawaadhibu kwa kuwatia katika moto wa Jahannam.
فَسُبْحَانَ اللَّـهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ ﴿١٧﴾
17. Basi mtakaseni Mwenyezi Mungu mnapofikia jioni na mnapofikia asubuhi.
وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَعَشِيًّا وَحِينَ تُظْهِرُونَ ﴿١٨﴾
18. Na sifa njema zote ni zake katika mbingu na ardhi na jioni na mnapofikia mchana.
يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَيُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَكَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ ﴿١٩﴾
19. Hukitoa kilicho hai kutokana na kilichokufa, na hukitoa kilichokufa kutokana na kilicho hai. Na huhuisha ardhi baada ya kufa kwake. Na kama hivyo ndivyo mtakavyotolewa.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ إِذَا أَنتُم بَشَرٌ تَنتَشِرُونَ ﴿٢٠﴾
20. Na katika ishara zake ni kuwa amewaumba kwa udongo; kisha mmekuwa watu mnaoenea.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١﴾
21. Na katika ishara zake ni kuwaumbia wake zenu kutokana na nafsi zenu. Ili mpate utulivu kwao. Na akajaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya kuna ishara kwa watu wanaofikiri.
وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْعَالِمِينَ ﴿٢٢﴾
22. Na katika ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi. Na kutofautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo kuna ishara kwa wenye elimu.
وَمِنْ آيَاتِهِ مَنَامُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَابْتِغَاؤُكُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ ﴿٢٣﴾
23. Na katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na mchana, na kutafuta kwenu fadhila zake. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaosikia.
وَمِنْ آيَاتِهِ يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَيُحْيِي بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٢٤﴾
24. Na katika Ishara zake ni kuwaonyesha umeme kwa hofu na tamaa, na kuwateremshia maji kutoka mbinguni na kwayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wenye akili.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَن تَقُومَ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ بِأَمْرِهِ ثُمَّ إِذَا دَعَاكُمْ دَعْوَةً مِّنَ الْأَرْضِ إِذَا أَنتُمْ تَخْرُجُونَ ﴿٢٥﴾
25. Na katika Ishara zake ni kusimama mbingu kwa amri yake. Kisha atakapowaita mwito mmoja tu, hapo mtatoka kwenye ardhi.
Aya 17 – 25
Basi mtakaseni Mwenyezi Mungu mnapofikia jioni na mnapofikia asubuhi. Na sifa njema zote ni zake katika mbingu na ardhi na jioni na na mnapofikia mchana.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja watu wa Peponi na watu wa Motoni, anatoa amri ya kutukuzwa kwake asubuhi, jioni, mchana na usiku pia. Kwani Hakika Yeye Mwenyezi Mungu ni msifiwa mbinguni na ardhini.
Kuna riwaya moja inayosema kuwa Suleiman Bin Daud, siku moja alimpi- tia mkulima akasema: “Hakika Bin Daud amepewa ufalme mkubwa.”
Suleiman akamwambia: “Tasbih moja tu anayoikubali Mwenyezi Mungu ni bora kuliko waliyopewa ukoo wa Daud.”
Kwenye Nahjul-balagha, imeelezwa: “Mwenyezi Mungu Amejaalia Alhamdu (kusifiwa na sifa njema) ni ufunguo wa utajo wake na ni sababu ya kuzidi fadhila zake na ni dalili ya uungu wake na utukufu wake.
Hukitoa kilicho hai kutokana na kilichokufa, na hukitoa kilichokufa kutokana na kilicho hai. Na huhuisha ardhi baada ya kufa kwake.
Wanaoamini mada wanasema kuwa mada ndiyo iliyoleta uhai, usikikizi, nyoyo n.k. Kama yangekuwa sahihi haya, basi ingelikuwa kila mada inaona, kusikia na kuwa na akili. Kwa sababu vinavyohusiana na kitu ni lazima viwe navyo wakati wowote. Na kwa kuwa tunaona mada nyingine zina uhai na nyingine hazina, basi tumejua kwamba kuna nguvu nyuma ya mada inayompa uhai amtakaye na kutompa amtakaye.
Na kama hivyo ndivyo mtakavyotolewa.
Yaani kufufuliwa. Kama ambavyo Mwenyezi Mungu ameitoa mimea hai kutokana na ardhi iliyokufa, atamtoa mtu hai kutoka kaburini kwake. Kwa maneno mengine ni kuwa; kama ambavyo alimpa uhai baada ya kuwa si chochote, vilevile atampa uhai mara nyingine baada ya kuwa ni mchanga na mifupa. Basi je, kuna ajabu gani?
Tazama Juz. 7 (6:95 – 99) na Juz. 13 (13:5 – 7) kifungu cha ‘Waanaoamini mada na maisha baada ya mauti.’
Na katika ishara zake ni kuwa amewaumba kwa udongo; kisha mmekuwa watu mnaoenea.
Mwenyezi Mungu amemuumba mtu wa kwanza kutokana na udongo na watu wote wametokana na yeye. Vile vile chakula chao kinachowafanya waishi kinatokana na udongo.
Kwa hiyo, udongo ndio sababu ya kupatikana mtu na kubakia kwake na kuendelea kwake. Vipi mchanga umekuwa mtu mwenye usikizi, uoni, akili, ubainifu, utashi na nguvu zinazofanya maajabu mengi na kuleta maendeleo?
Je, haya ni matengenezo ya sadfa au mada? Na waseme wapinzani watakavyo, lakini akili haiamini isipokuwa kuweko ambaye hana mfano na kitu chochote na ni Mjuzi, Mwenye hekima.
Na katika ishara zake ni kuwaumbia wake zenu kutokana na nafsi zenu. Ili mpate utulivu kwao. Na akajaalia mapenzi na huruma baina yenu.
Maana ya ‘Kutokana na nafsi zenu’ ni jinsi yenu na maumbo yenu; mkibadilishana upendo kwa upendo na utulivu kwa utulivu. Wakale walisema: “Kila shepu inazoena na shepu inayofanana nayo.” Lau mke angelikuwa wa jinsi nyingine inayotofautiana na jinsi ya mume, ingelikuwa vigumu kufahamiana na kushirikiana. Kila mmoja angejiona ni mgeni kwa mwenzake na yuko mbali na tabia yake na hulka yake. Tazama Juz. 4 (4:19 – 21) kifungu cha ‘Ndoa ni kubadilishana roho kwa roho.’
Ya kushangaza ni kauli ya baadhi ya wafasiri waliosema kuwa makusudio ya mapenzi ni kujamiiana; na huruma ni mtoto. Hii inafahamisha tu kuwa wafasiri hao wameelemea zaidi upande wa mambo ya kijinsiya na kumuona mwanamke kuwa ni chombo cha kuzaa watoto tu.
Qur’an Tukufu imeabainisha lengo la ndoa kuwa ni kuzoeana, kuhurumiana, uadilifu na usawa; sio baina ya mume na mke tu, bali familia nzima kwa ujumla. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Enyi watu! Mcheni Mwenyezi Mungu ambaye amewaumba kutokana na nafsi moja.
Na akamuumba mkewe katika nafsi hiyo na akaeneza, kutokana na hao wawili, wanaume wengi na wanawake. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana na ndugu wa damu; hakika Mwenyezi Mungu anawachunga.” Juz. 4 (4:1).
Lengo la kumcha Mwenyezi Mungu katika Aya hii ni kila mmoja katika familia atekeleze haki ya mwenzake, ili familia iwe na maisha mazuri yasiyokuwa na misukosuko wala vikwazo. Inajulikana wazi kuwa familia njema ndio msingi wa jamii njema.
Si vibaya kudokeza kuwa ni Sunna kusoma khutuba ya ndoa wakati wa kutaka kuoa, na wakati wa kusomwa tamko la ndoa kwa kumwiga Mtume(s.a.w.w) na kizazi chake. Khutba yenyewe inakuwa ni kumhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu, shahada mbili, kumswalia Mtume na kizazi chake, kuwausia watu takua na kuwaombea Mungu wana ndoa. Imepokewa Hadith kutoka kwa Imam Zainul-abidin: “Mwenye kumhimidi Mwenyezi Mungu amehutubia.”
Vile vile ni Sunna kutabaruku kwa kusoma Aya za Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Hadith za Mtume wake Mtukufu. Hii imekuwa ni desturi ya wahenga na wa sasa.
Huwa kabla ya kufungisha ndoa wanasoma Aya hii tuliyo nayo. Na katika Hadith wanasoma “Owaneni mtapata kizazi na kuwa wengi. Kwani mimi nitajifaharisha kwa umma nyingine siku ya Kiyama hata kwa mimba iliyoharibika.”
Tumesema kuwa Aya na Hadith hizi zinasomwa kwa kutabaruku tu. Ni makosa kudhaniwa kuwa tabia njema na adabu za Qur’an zitapatikana kwa kusoma Hadith na Aya. Hapana! Tabia njema na adabu zitakuwa kwa malezi tu ya kumlea mtoto ki-qur’ani tangu udogoni; jambo ambalo litampelekea kufahamu lengo alilolikusudia Mwenyezi Mungu katika ndoa.
Ama kuwalea watoto juu ya kupenda mali na kujifharisha na mambo ya kujionyesha ya upuuzi; kama mama kumwambia binti yake: Mungu akujalie upate mume tajiri au baba kumpa nasaha mwanawe kuoa binti wa waziri au wa mfanya biashara mkubwa, malezi haya hayafaidiwi chochote na kusoma Qur’an wala Hadithi.
Hadithi ya owaneni mtapata kizazi, haina shaka yoyote katika usahihi wake, lakini Bwana wa Mitume(s.a.w.w) atajifaharisha kwa waumini wenye takua na wapigania jihadi waungwana na vile vile kwa mimba iliyoharibika. Na atajitenga na waovu wenye ufuska katika vijana wa kike na wa kiume, ambao dini haiwakanyi na lolote.
Vile vile atajitenga na wahaini na vibaraka walio maadui wa Mwenyezi Mungu na wa ubinadamu. Kuna Hadith isemayo: “Kwa hakika watu watafikiwa na wakati ambao mtu hatasalimika na dini ila kwa kukimbia kutoka kilele kimoja hadi kingine.” Wakasema: “Yatakuwa lini hayo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ”Itakapokuwa mtu hapati maisha ila kwa kumuasi Mwenyezi Mungu, basi wakati huo itakuwa halali useja.”
Hakika katika haya kuna ishara kwa watu wanaofikiri.
Lengo la ndoa ni utulivu, mapenzi na kuhurumiana; na kwamba ndoa za kibiashara na kisiasa mara nyingi zinaishia kwenye maisha mabaya ya kifamilia na hatimaye kuvunjika na watoto kutangatanga.
Na katika ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi.
Mwenyezi Mungu anakariri ishara ya kuumbwa ulimwengu, kwa sababu huo pamoja na maajabu na siri zilizomo ndani yake ni katika dalili zilizo dhahiri zaidi za kuweko Mwenyezi Mungu. Vile vile kukumbusha fadhila zake Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na kutofautiana ndimi zenu na rangi zenu.
Yaani kutofautiana lugha na rangi za watu. Pia kuna watu wanatofautiana kwa sura, sauti, alama za vidole n.k. Hekima ya hilo ni kujuana watu na kuwatofautisha. Mzazi amjue mwanawe, mume amjue mkewe, mdai amjue anayemdai n.k. Haiwezekani kabisa kuwa hekima hii ya hali ya juu iwe imepatikana kwa sadfa.
Hakika katika hayo kuna ishara kwa wenye elimu.
Yaani kuna dalili wazi za kuweko mkadiriaji na mpangiliaji mambo.
Na katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na mchana, na kutafuta kwenu fadhila zake.
Mtu anaweza kulala mchana wakati wa adhuhuri (qaylula) na pia anaweza kutafuta riziki usiku. Ama kauli yake Mwenyezi Mungu
وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا ﴿١٠﴾ وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا ﴿١١﴾
“Na tukaufanya usiku ni vazi na tuakaufanya mchana ni maisha,” (78:10 – 11) inachukuliwa kiaghlabu.
Vyovyote iwavyo, lengo ni kukumbusha hekima yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kuyagawanya maisha ya mtu kwenye mateso na raha, ambapo maisha hayawezi kupangika bila ya mawili hayo.
Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaosikia mwito wa Mwenyezi Mungu wakauitikia na mawaidha wakawaidhika nayo.
Na katika Ishara zake ni kuwaonyesha umeme kwa hofu na tamaa na kuwateremshia maji kutoka mbinguni na kwayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wenye akili.
Umepita mfano wake katika Juz. 13 (13:12).
Na katika Ishara zake ni kusimama mbingu kwa amri yake.
Kila kitu kinamhitajia Mwenyezi Mungu katika kubaki kwake na kuendelea kwake; sawa na kilivyomuhitajia katika kuumbwa kwake. Kikikosa ulinzi wake, basi kitakuwa ni bure tu kisicho na maana yoyote.
Kisha atakapowaita mwito mmoja tu, hapo mtatoka kwenye ardhi.
Wito wa Mwenyezi Mungu duniani ni wito wa nasaha na mwongozo, wanauitikia wenye takua na kuupinga wakosefu. Ama mwito wake huko akhera ni wakiutekelezaji, asioweza kuukimbia yoyote. Umetukuka uweza wake.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 15 (17:52).
15
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿٢٦﴾
26. Ni vyake vilivyo katika mbingu na ardhi. Vyote vinamtii.
وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ وَلَهُ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٧﴾
27. Naye ndiye ambaye anaanzisha uumbaji kisha ataurudisha, na jambo hili ni jepesi zaidi kwake. Naye ndiye mwenye mfano bora katika mbingu na ardhi. Na yeye ndiye Mwenye uwezo, Mwenye hekima.
ضَرَبَ لَكُم مَّثَلًا مِّنْ أَنفُسِكُمْ هَل لَّكُم مِّن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُم مِّن شُرَكَاءَ فِي مَا رَزَقْنَاكُمْ فَأَنتُمْ فِيهِ سَوَاءٌ تَخَافُونَهُمْ كَخِيفَتِكُمْ أَنفُسَكُمْ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٢٨﴾
28. Amewapigia mfano kutokana na nafsi zenu. Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kuume mnao washirika katika hivyo tulivyowaruzuku, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mkawahofia kama mnavyohofiana? Namna hiyo tunazipambanua Aya zetu kwa watu wenye akili.
بَلِ اتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَهْوَاءَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ فَمَن يَهْدِي مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٢٩﴾
29. Bali waliodhulumu wamefuata hawa zao pasi na kujua. Basi ni nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza?
Aya 26 – 29
Ni vyake vilivyo katika mbingu na ardhi. Vyote vinamtii.
Ulimwengu na vilivyomo ndani yake ni miliki ya Mwenyezi Mungu na vinakwenda kulingana na utashi wake; hata wale wanaomuasi pia anawafanya atakavyo, bila ya mpinzani.
Naye ndiye ambaye anaanzisha uumbaji kisha ataurudisha, na jambo hili ni jepesi zaidi kwake.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameumba ulimwengu, kisha atauondoa, tena ataurudisha mara nyingine.
Makusudio ya wepesi zaidi hapa ni wepesi tu; sio kuwa kuna mengine ni mepesi kidogo na mengine zaidi; kama vile kusema Mwenyezi Mungu ni Mkubwa zaidi, haimaanishi kuwa kuna mwingine aliye mkubwa na yeye ni mkubwa zaidi. Kwa sababu ambaye hana mfano wa kitu chochote, mambo yote kwake ni sawa. Haifai kusema ni mkubwa zaidi ya mwingine wala hili ni jepesi zaidi ya mengine.
Naye ndiye mwenye mfano bora katika mbingu na ardhi. Na yeye ndiye Mwenye uwezo, Mwenye hekima.
Makusudio ya mfano bora hapa ni sifa bora ambazo hashirikianai na yeyote katika sifa hizo. Nazo ni kuwa: Hakuna Mola isipokuwa yeye na Yeye ndiye Mwenye nguvu ambaye hashindwi na mwenye hekima asiyefanya mchezo.
Amewapigia mfano kutokana na nafsi zenu. Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kuume mnao washirika katika hivyo tulivyowaruzuku, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mkawahofia kama mnavyohofiana?
Mfano huu, Mwenyezi Mungu (s.w.t), anaupiga kwa mataghuti wapenda anasa ambao wanamiliki watumwa na mali na wanadai kuwa Mwenyezi Mungu ana washirika katika kuumba kwake. Ufafanuzi wake ni kuwa: Angalieni enyi washirikina wapenda anasa.
Nyinyi mna watumwa na mali, lakini hamuwashirikishi kwenye mali zenu, wala hamkubali wazitumie ila kwa idhini yenu; wala hamuwahofii, wakati mnapowatumia, kama mnavyowahofia washirika wenu wasiokuwa watumwa na hali ya kuwa wale ambao mmewafanya watumwa sio milki yenu hasa.
Sasa vipi wale ambao ni milki ya Mwenyezi Mungu hasa mmewafanya ni washirika wake katika miliki yake na kuumba kwake. Vipi mnamnasibishia Mwenyezi Mungu yale ambayo nyinyi hamyaridhii. Nyinyi mnachukia kuwa na ushirika na wale mnaodai ni watumwa wenu, lakini Mwenyezi Mungu asichukie kuwa na ushirika na viumbe wake. Ole wenu! Mnahukumu vipi?
Hii ni sawa na kusema kwao kuwa Mwenyezi Mungu ana watoto wasichana na sisi tuna wavulana:
“Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu mabinti. Ametakata na hayo! Na hali wao hupata wanavyovitamani. Na mmoja wao akibashiriwa msichana uso wake unasawijika naye amejaa chuki.” Juz. 14 (16: 57 – 58).
Namna hiyo tunazipambanua Aya zetu kwa watu wenye akili.
Mfano huu ni wazi kabisa kuwa Mwenyezi Mungu hana mshirika, wala hawapofuki na mfano huu ispokuwa watu wa masilahi na matamanio.
Bali waliodhulumu wamefuata hawa zao pasi na kujua.
Ambapo haki iko katika hawa zao na uadilifu uko katika wanayoyatamani. Huu ndio ujinga wa mwisho na upotevu ulio wazi.
Basi ni nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza?
Mwenyezi Mungu amewapoteza kwa vile wameamua kufuata njia ya upotevu. Kila mwenye kufuata njia atafika; iwe njia ya kheri au ya shari; ya kuokoka au ya kuangamia.
Nao hawatakuwa na wasaidizi.
Vipi wawe na usaidizi na hali wao wameamua kufuata njia ya maangamizi kutokana na uchaguzi wao mbaya, wala hawakuonyeka au kukoma na makemeo yoyote.
فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾
30. Basi uelekeze uso wako sawa-sawa kwenye dini–ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini ya sawasawa, lakini watu wengi hawajui.
مُنِيبِينَ إِلَيْهِ وَاتَّقُوهُ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٣١﴾
31. Muwe wenye kurejea kwake na mcheni. Na simamisheni Swala wala msiwe katika washirikina.
مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ ﴿٣٢﴾
32. Katika wale walioigawa dini yao na wakawa makundi makundi. Kila kundi hufurahia waliyo nayo.
Aya 30 – 32
Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye dini–ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini ya sawasawa, lakini watu wengi hawajui.
Aya hii, mara nyingi, inakuwa vinywani mwa mahatibu na kwenye kalamu za waandishi. Kuna wale wanaotosheka na kuitolea dalili tu. Wengine wanaipamba wakisema: Hii ndio dini iliyo sahihi iliyo kubwa n.k.
Bila shaka Aya hii inathibisha msingi unaotiliwa mkazo na itikadi ya Kiislamu na sharia yake. Na inafahamisha wazi kwamba mafunzo ya dini kuanzia alifu mpaka ye (a mpaka z) yanaongoza kwenye uongofu na utekelezaji wa matakwa ya maisha, ukuaji na maendeleo yake.
Kwanza tutanza kufasiri misamiati iliyo katika Aya hii, kisha tutaja maana kijumla.
Neno umbile kwa ujumla linamanisha tabia iliyo ndani ya mtu, inayoikubali kheri inapoijua kuwa ni kheri na kulazimiana nayo kwa vile tu kheri inakubalika. Na tabia hiyo inaikataa shari inapoijua kuwa ni shari, si kwa jingine ila ni kwamba shari inakataliwa na kuepukwa.
Hii ni itakapokuwa umbile la mtu ni safi, halina takataka za desturi na uuigizaji wala halikuchafuliwa na hawaa. Mwanchuoni mkuu Hilli (Allama Hilli) ameipigia mfano tabia hii kwa kusema: “Lau mwenye akili atahiyarishwa kusema ukweli na apewe pesa au aseme uwongo pia apewe pesa, basi atachagua ukweli.”
Tabia hii inayochagua ukweli kuliko uongo ndio ile aliyoizungumzia Mwenyezi Mungu pale aliposema: “Je, mimi si Mola wenu? Wakasema: Kwa nini!” Juz. 9 (7:152). Pia ndiyo iliyokusudiwa na Hadith mashuhuri iliyopokewa kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) : “Kila anayezaliwa anazaliwa na umbile mpaka wazazi wake wamfanye Yahudi au Mnaswara.”
Ama neno ‘kwenye dini’ hapa linamanisha msimamo wa umbile ambalo Mwenyezi Mungu amewaumbia watu la kuwa mbali na hawaa za nafsi.
Makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu,” ni kuwa dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuthibiti kwa msingi wa kimaumbile, hauepukani nayo.
Neno ‘Hiyo’ ni ishara ya yale aliyoyawajibisha Mwenyezi Mungu kwa waja kulazimiana nayo kwa kauli na vitendo. Kwa sababu ndiyo dini ya kisawasawa isiyokuwa na kombokombo.
Ama kwa ujumla wake inafahamisha kuwa dini inafungamana na maumbile ya mtu, lakini hii haimaanishi kuwa umbile ndilo muamrishaji na mkatazaji na dini ielezee hukumu zake, hapana! Mwenyezi Mungu ambaye ameumba dini na maumbile ndiye muweka sharia wa kwanza. Ni Yeye pekee mwenye kuamrisha na kukataza.
Hakika makusudio ya Aya ni kuelezea kipimo tunachopimia dini ya Mwenyezi Mungu na kwamba itikidi, sharia na maadili yake yanenda sambamba na umbile la watu na masilahi yao; na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakuweka hukumu kwa waja wake kupingana na manufaa ya mtu binafsi au jamii.
Huu ndio udhibiti na tofauti iliyoko baina ya hukumu ya Mwenyezi Mungu na hukumu nyinginezo, tofauti baina ya sharia ya haki na sharia ya batili. Ama kauli za maulama wa fiqih, tafsir na falsafa sio msingi wa Uislamu, wala haifai kuwategemea kama dalili ya sharia. Kwa sabau kauli zao hizo zinaakisi tu juhudi na fahamu zao katika dini ya Mwenyezi Mungu na hukumu zake, wala haziakisi uhakika na uhalisi wa dini.
Kwa ufupi ni kuwa Uislamu haukatai yote yaliyo katika dini na madhehbu mengineyo; bali unaangalia kwa mtazamo wa undani na usanifu. Unakubaliana yale yanayoafikiana na umbile la Mwenyezi Mungu na kukataa yasiyokuwa hayo.
Muwe wenye kurejea kwake na mcheni . Rudini kwenye dini hii na mtii hukumu zake zote.
Na simamisheni Swala kwani inawakumbusha Mwenyezi Mungu; wala msiwe katika washirikina.
Mfanyieni ikhlasi Mwenyezi Mungu peke yake kwenye kauli zenu na vitendo vyenu.
Katika wale walioigawa dini yao na wakawa makundi makundi. Kila kundi hufurahia waliyo nayo.
Umepita mfano wake katika Juz. 8 (6:158) na Juz. 18 (23:53).
وَإِذَا مَسَّ النَّاسَ ضُرٌّ دَعَوْا رَبَّهُم مُّنِيبِينَ إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا أَذَاقَهُم مِّنْهُ رَحْمَةً إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ ﴿٣٣﴾
33. Watu yakiwagusa madhara humwomba Mola wao wakiwa wanarejea kwake. Kisha akiwaonjesha rehema kutoka kwake, mara kikundi miongoni mwao humshirikisha Mola wao.
لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ فَتَمَتَّعُوا فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣٤﴾
34. Ili wapate kuyakana tuliyowapa. Basi stareheni. Mtakuja jua.
أَمْ أَنزَلْنَا عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا فَهُوَ يَتَكَلَّمُ بِمَا كَانُوا بِهِ يُشْرِكُونَ ﴿٣٥﴾
35. Au tumewateremshia hoja inayowaambia juu ya yale wamshirikishayo nayo?
وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً فَرِحُوا بِهَا وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ إِذَا هُمْ يَقْنَطُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na watu tunapowaonjesha rehema huifurahia. Na ukiwasibu uovu kwa iliyoyatanguliza mikono yao wenyewe, mara wanakata tamaa.
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٣٧﴾
37. Je, hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaoamini.
فَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ ذَٰلِكَ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يُرِيدُونَ وَجْهَ اللَّـهِ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٣٨﴾
37. Basi mpe jamaa haki yake na masikini na mwananjia. Hayo ni kheri kwa wale watakao radhi ya Mwenyezi Mungu na hao ndio wenye kufanikiwa.
وَمَا آتَيْتُم مِّن رِّبًا لِّيَرْبُوَ فِي أَمْوَالِ النَّاسِ فَلَا يَرْبُو عِندَ اللَّـهِ وَمَا آتَيْتُم مِّن زَكَاةٍ تُرِيدُونَ وَجْهَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُضْعِفُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na mnachokitoa katika riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mlichokitoa Zaka kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watakaozidishiwa.
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَكُمْ ثُمَّ رَزَقَكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَفْعَلُ مِن ذَٰلِكُم مِّن شَيْءٍ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٤٠﴾
40. Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba, kisha akawaruzuku, kisha atawafisha na kisha atawafufua. Je katika mnaowashirikisha yuko awezaye kufanya lolote katika hayo? Ametakasika na ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo.
Aya 33 – 40
Watu yakiwagusa madhara humwomba Mola wao wakiwa wanarejea kwake. Kisha akiwaonjesha rehema kutoka kwake, mara kikundi miongoni mwao humshirikisha Mola wao.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:12) na Juz. 15 (17:67).
Ili wapate kuyakana tuliyowapa. Basi stareheni. Mtakuja jua.
Umetangulia mfano wake katika Juzuu hii (29:66).
Au tumewateremshia hoja inayowaambia juu ya yale wamshirikishayo nayo?
Au hapa ni kwa maana ya mbali. Maana ni kuwa Je, kuna wahyi au akili yoyote inayoshuhudia kuwa ushirikina mlio nao ni sawa na haki? Makusudio ya swali hili ni kupinga na kukemea.
Na watu tunapowaonjesha rehema huifurahia. Na ukiwasibu uovu kwa iliyoyatanguliza mikono yao wenyewe, mara wanakata tamaa.
Huyu ndiye binadamu. Akipata heri anafurahi na kujifaharisha na akipat- wa na shari anakata tamaa. Umetangulia mfano wake katika Juz. 12 (11:9).
Je, hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaoamini.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:26) na Juz. 15 (17:30).
Basi mpe jamaa haki yake na masikini na mwananjia.
Jamaa aliye fukara ana haki kwa jamaa yake aliye tajiri ya kumpa cha kusitiri haja. Shafii na Shia Imamiya wamesema kuwa ni wajibu kumtunza jamaa akiwa ni baba na kuendelea juu na mtoto na kuendelea chini.
Malik akasema: “Hakuna wajibu isipokuwa kwa wazazi na watoto wa karibu tu, sio baba wa baba au mtoto wa mtoto.”
Hambali anasema: “Ni wajibu kumtunza ndugu kwa sharti ya kuwa mtunzaji awe ni mrithi wa anayemtunza.” Ama Hanafi wanaona kuwa sharti la msingi ni kuwa ndugu aliye maharimu kuoana naye. Ufafanuzi uko katika Kitabu chetu Alfiqh ala madhahibil-khamsa (Fiqh ya madhehebu matano).
Ama masikini na mwananjia yametangulia maelezo yao katika Juz. 10 (9:60).
Hayo ni kheri kwa wale watakao radhi ya Mwenyezi Mungu na hao ndio wenye kufanikiwa.
‘Hayo’ ni ishara ya kutoa - kwamba ni wajibu kuwe ni kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyo kwa watu wema na wa kufaulu.
Na mnachokitoa katika riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu.
Kuna kundi la wafasiri waliosema kuwa makusudio ya riba hapa ni ile riba ya haramu. Wengine wakasema makusudioa yake ni riba ya halali; kama vile mtu kumpa zawadi tajiri ili arudishe zawadi kubwa zaidi.
Vizuri ni kuichukulia Aya kwa yote mawili – kwamba zote mbili hazina thawabu mbele ya Mwenyezi Mungu; isipokuwa ya kwanza ina adhabu na ya pili haina thawabu wala adhabu.
Lakini mlichokitoa Zaka kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watakaozidishiwa.
Yaani watazidishiwa thawabu na malipo. Maana ya kiujumla ni kuwa mwenye kutoa kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mwenyezi Mungu humzidishia mali yake duniani na thawabu zake akhera. Imam Ali(a.s) anasema:“Mkifilisika basi fanyeni biashara na Mwenyezi Mungu.” Kauli hii imechukuliwa kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu:“Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, ili amzidishie ziada nyingi?” Juz. 2 (2:245).
Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba, kisha akawaruzuku, kisha atawafisha na kisha atawafufua. Je katika mnaowashirikisha yuko awezaye kufanya lolote katika hayo?
Mnavifanyia ubakhili alivyowapa Mwenyezi Mungu na mnataka riziki kwa wengine; na hali Yeye Mwenyezi Mungu ndiye aliyewafanya muweko baada ya kuwa hamko, akawamiminia baraka zake nyingi. Yeye ndiye anayewafisha na kuwapa uhai kisha awakusanye kwa ajili ya hisabu na malipo? Je, katika hao mnaowatarajia fadhila zao na kutarajia kuwanufaisha kuna anayeweza kutoa uhai na kufisha? Tukikadiria kuwa wanaweza kufanya baadhi ya mambo katika maisha haya, je kesho wataweza kunufaisha na kudhuru?
Ametakasika na ametukuka na hayo wanayomshirikisha naye.
Kuna hadith isemayo: “Shirki imejificha zaidi kuliko kutambaa kwa chungu.” Hapa kuna ishara kwamba shirki ziko aina nyingi, ikiwemo ile ya kumtegemea muumbwa badala ya Muumba.
16
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٤١﴾
41. Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa sababu ya iliyoyafanya mikono ya watu. Ili Mwenyezi Mungu awaonjeshe baadhi ya waliyoyatenda. Huenda wakarejea.
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلُ كَانَ أَكْثَرُهُم مُّشْرِكِينَ ﴿٤٢﴾
42. Sema: Nendeni katika ardhi na tazameni ulikuwaje mwisho wa wale waliotangulia, wengi wao walikuwa washirikina.
فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ الْقَيِّمِ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا مَرَدَّ لَهُ مِنَ اللَّـهِ يَوْمَئِذٍ يَصَّدَّعُونَ ﴿٤٣﴾
43. Basi uelekeze uso wako kwenye dini ya sawasawa, kabla ya kufika siku isiyozuilika, inayotoka kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo watatengana.
مَن كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُ وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِأَنفُسِهِمْ يَمْهَدُونَ ﴿٤٤﴾
44. Anayekufuru basi ukafiri wake utakuwa juu yake, na anayetenda mema basi wanazitengenezea nafsi zao.
لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِن فَضْلِهِ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴿٤٥﴾
45. Ili awalipe walioamini na wakatenda mema kutokana na fadhila yake. Hakika Yeye hapendi makafiri.
Aya 41 – 45
Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa kwa sababu ya iliyoyafanya mikono ya watu.
Kundi la wafasiri limesema makusudio ya baharini hapa ni miji ya pwani na bara ni miji iliyo mbali na pwani. Wengine wamesema makusudio ya bahari ni mji kutokana na wingi wa wakazi wake na bara ni kijiji kutokana na uchache wa wakazi wake.
Tunavyofahamu sisi ni kuwa bara na baharini ni kinaya cha wingi wa ufisadi na kuenea kwake.
Kila aliloliharamisha Mwenyezi Mungu na kulikataza kulifanya ni kosa na ufisadi katika ardhi; kama vile vita dhulma, israfu, uasherati, pombe, kamari, kuzipuuza faradhi za Mwenyezi Mungu na waja wake n.k.
Ikiwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amesifia zama za ujahili kwa kudhihiri ufisadi bara na baharini; ambapo hakukuwa na silaha za kemikali wala mabomu ya atomiki au mashirika ya ulanguzi na unyonyaji wala makasino na mabaa. Je, itakuwaje kwa hivi sasa ambapo nusu ya ulimwengu inahofiwa kuangamizwa wakati wowote, sio kwa kitendo cha Mwenyezi Mungu wala majanga ya asili, bali ni kwa kitendo cha binadamu wenyewe wanaomiliki silaha za maangamizi?
Hakuna njia ya kusalimika watu na shari hii isipokuwa kuangamizwa sila- ha zote. Ama umoja wa mataifa na shirika linalosimamia nguvu za nyuklia halijamhakikishia binadamu usalama wake wala si ya kutegemewa.
Ili Mwenyezi Mungu awaonjeshe baadhi ya waliyoyatenda. Huenda wakarejea.
Ufisadi katika ardhi ni natija ya kuachana na Mwenyezi Mungu na kutojilazimisha na maamrisho yake na makatazo yake. Neno ‘baadhi’ hapa linaashiria adhabu ya dunia na adhabu ya akhera ni mbaya zaidi na ya kufedhehesha. Katika dua zilizopokewa, kuna dua hii: “Ewe Mola wangu! Hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na dhambi inayobadilisha neema na kuteremsha balaa.” Bwana wa Mitume anasema:“Ogopeni dhambi kwani zinafuta kheri.” Inatosha kuwa ni ushahidi wa hilo kauli yake Mwenyezi Mungu:
وَتِلْكَ الْقُرَىٰ أَهْلَكْنَاهُمْ لَمَّا ظَلَمُوا وَجَعَلْنَا لِمَهْلِكِهِم مَّوْعِدًا ﴿٥٩﴾
“Na miji hiyo tuliwaangamiza walipodhulumu na tukawawekea miadi ya maangamizo yao.”
Juz. 15 (18:59).
Sema: Nendeni katika ardhi na tazameni ulikuwaje mwisho wa wale waliotangulia, wengi wao walikuwa washirikina.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (3:137), Juz.7 (6:11) na Juz. 20 (27:69).
Basi uelekeze uso wako kwenye dini ya sawasawa, kabla ya kufika siku isiyozuilika, inayotoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo ni siku ya hisabu na malipo isiyokimbilika. Mwema ni yule ambaye amemfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu katika matendo yake na makusudio yake na akaihisabu nafsi yake kabla ya kuhisabiwa.
Siku hiyo watatengana. Watatawayika makundi mawili: kundi moja Peponi na jingine Motoni. Umetangulia mfano wake katika Juzuu na Sura hii Aya 14.
Anayekufuru basi ukafiri wake utakuwa juu yake, na anayetenda mema basi wanazitengenezea nafsi zao.
Neno kutengeneza, limefasiriwa kutokana na neno Yamhadun lenye maana ya kutandika kitanda. Watu wenye matendo mema wanajitandikia makaburi yao na kufanya maandalizi ya mahitaji ya amani na raha kabla ya kuingia huko; sawa na inavyoandaliwa nyumba ya kuishi duniani. Imepokewa Hadith kutoka kwa Imam Ja’far Sadiq(a.s) :“Hakika matendo mema yanamtangulia mtendaji ili kumwandalia, sawa na mtumishi amwandaliavyo bwana wake.”
Umetangulia mfano wake katika Juz. Juz. 3(2:286).
Ili awalipe walioamini na wakatenda mema kutokana na fadhila yake. Hakika Yeye hapendi makafiri.
Maneno hapa yanafungamana na ‘siku hiyo watatengana.’ Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama atawafanya watu makundi mawili ili awalipe Pepo waumini kutokana na matendo yao, kwa sababu anawapenda na anapenda matendo yao mema. Mwenyezi Mungu anawachukia makafiri na atalipa wanavyostahili.
Katika Nahjul-balagha imesemwa:“Hakika Mwenyezi Mungu anampemda mja na kuchukia matendo yake na anapenda matendo na kumchukia mtendaji wake.” yaani anampenda mumin kwa imani yake na anachukia matendo yake mabaya na anamchukia kafiri kwa kufuru yake na anapenda matendo yake mazuri.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَن يُرْسِلَ الرِّيَاحَ مُبَشِّرَاتٍ وَلِيُذِيقَكُم مِّن رَّحْمَتِهِ وَلِتَجْرِيَ الْفُلْكُ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na katika ishara zake ni kuzituma pepo ziletazo bishara na ili kuwaonjesha rehema yake na ili majahazi yatembee kwa amri yake; na mtafute kutokana na fadhila yake, na ili mumshukuru.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَانتَقَمْنَا مِنَ الَّذِينَ أَجْرَمُوا وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na hakika tulikwishawatuma mitume kwa kaumu zao na wakawajia na hoja zilizo waziwazi. Tukawaadhibu wale waliofanya makosa na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru waumini.
اللَّـهُ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَيَبْسُطُهُ فِي السَّمَاءِ كَيْفَ يَشَاءُ وَيَجْعَلُهُ كِسَفًا فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَالِهِ فَإِذَا أَصَابَ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ ﴿٤٨﴾
48. Mwenyezi Mungu ndiye anayezituma pepo zikayatimua mawingu, kisha akayatandaza mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande mapande, basi ukaiona mvua inatoka ndani yake. Anapowafikishia awatakao katika waja wake, mara wanakuwa na furaha.
وَإِن كَانُوا مِن قَبْلِ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْهِم مِّن قَبْلِهِ لَمُبْلِسِينَ ﴿٤٩﴾
49. Ingawaje kabla ya kuteremshiwa walikuwa wenye kukata tamaa.
فَانظُرْ إِلَىٰ آثَارِ رَحْمَتِ اللَّـهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا إِنَّ ذَٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٥٠﴾
50. Angalia athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Basi hakika huyo, bila shaka, ndiye mwenye kuhuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu
وَلَئِنْ أَرْسَلْنَا رِيحًا فَرَأَوْهُ مُصْفَرًّا لَّظَلُّوا مِن بَعْدِهِ يَكْفُرُونَ ﴿٥١﴾
51. Na kama tungeutuma upepo wakauona umekuwa rangi ya njano, juu ya hayo wangeku- furu.
Aya 46 – 51
Na katika ishara zake ni kuzituma pepo ziletazo bishara na ili kuwaonjesha rehema yake na ili majahazi yatembee kwa amri yake; na mtafute kutokana na fadhila yake na ili mumshukuru.
Kila kitu kinachofungamana na hekima katika kupatikana kwake, ni dalili mkataa ya kukanusha sadfa na kwamba kuna makusudio na utashi katika kupatikana kwake. Dalili hii ndio makusudio ya ishara za Mwenyezi Mungu zinazofahamisha kuweko kwake.
Upepo- ukiwa ni dalili ya umoja wa Mwenyezi Mungu na uweza wakeuna faida nyingi; miongoni mwa faida hizo ni: Kuleta mawingu ya mvua yanayowashiria watu kheri, kutembea majahazi kwenye maji yakiwa yanachukua chakula kutoka mji mmoja hadi mwingine na mengineyo; kama yale aliyoyaashiria Imam Ja’far Sadiq(a.s) kwa kusema:
“Lau upepo utasimama siku tatu, basi kila kitu kitaharibika juu ya uso wa ardhi na kitavunda. Kwa sababu upepo uko kwenye daraja ya kiyoyozi kinachoondosha na kukinga uchafu kwenye kila kitu. Uko kwenye daraja ya roho ikitaka mwilini unaoza na kubadilika... Ametukuka Mwenyezi Mungu mzuri wa waumbaji.”
Na ili mshukuru.
Yaani mpate kuogopa maasi kwa siri na dhahiri. Tumeashiria huko nyuma, zaidi ya mara moja, kwamba Mwenyezi Mungu anapitisha vitu kwa sababu zake na inategemezwa kwake kwa vile yeye ndiye msababishi wa kwanza ambaye sababu zote zinakomea kwake.
Na hakika tulikwishawatuma mitume kwa kaumu zao na wakawajia na hoja zilizo waziwazi. Tukawaadhibu wale waliofanya makosa na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru waumini.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimtuma Muhammad(s.a.w.w) na hoja za kutosheleza; kama alivyowatuma kabla yake Ibrahim, Musa, Isa na wengineo, na hoja zilizowazi. Basi wengi wakawakadhibisha na wachache wakawaamini. Mwenyezi Mungu atawaadhibu wakadhibishaji siku hiyo kubwa na atawanusuru Mitume na walio pamoja nao.
Nusra hii ni wajibu kwa Mwenyezi Mungu aliyojiwajibishia yeye mwenyewe kama alivyojiwabishia rehema. Tazama Juz. 11 (10:3-4) kifungu cha ‘Hisabu na malipo ni lazima’
Lengo la Aya hii ni onyo kwa wale waliomkadhibisha Muhammad(s.a.w.w) kuwa yatawasibu mfano wa yaliyowasibu wale waliokadhibisha mitume yake hapo kabla.
Mwenyezi Mungu ndiye anayezituma pepo zikayatimua mawingu, kisha akayatandaza mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande mapande, basi ukaiona mvua inatoka ndani yake. Anapowafikishia awatakao katika waja wake, mara wanakuwa na furaha. Ingawaje kabla ya kuteremshiwa walikuwa wenye kukata tamaa.
Huu ni ufafanuzi wa Aya ilyotangulia: ‘Na katika ishara zake ni kuzituma pepo ziletazo bishara.’
Kwa ufupi maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anazipeleka pepo kutimua mawingu na kuyatawanya mbinguni, kisha zinayagawa mapande mapande na kulileta kila pande kwenye mji aliooukusudia Mwenyezi Mungu.
Likifika hutoka maji mawinguni na kuanguka kwenye mji uliokusudiwa. Hapo watu wake hufurahi na kupeana habari njema. Na hapo mwanzo walikuwa wamekata tamaa.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:57).
Angalia athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Basi hakika huyo, bila shaka, ndiye mwenye kuhuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu.
Makusudio ya rehema ya Mwenyezi Mungu hapa ni mvua na athari yake ni kuwa hai ardhi baada ya kufa. Uhai huu unaonekana kwa macho ni dalili mkataa kuwa fikra ya uhai baada ya mauti na ufufuo ni sahihi isiyokubali shaka yoyote.
Kwa sababu mwenye akili akitilia maanani na kufikiria vizuri uhai wa ardhi baada ya kufa kwake hana budi kusalimu amri na kuamini fikra ya ufufuo; vinginevyo atakuwa miongoni mwa wanaoamini kuweko kitu na kutokuweko kwa wakati mmoja, jambo ambalo haliwezekani.
Hapa ndio kuna siri ya kukaririka Aya zinazotanabahisha akili juu ya ufufuo wa ardhi baada ya kufa kwake, kama dalili ya uwezekano wa ufufuo wa watu; miongoni mwa Aya hizo ni:
وَاللَّـهُ الَّذِي أَرْسَلَ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَسُقْنَاهُ إِلَىٰ بَلَدٍ مَّيِّتٍ فَأَحْيَيْنَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا كَذَٰلِكَ النُّشُورُ ﴿٩﴾
“Mwenyezi Mungu ndiye anayezituma pepo zikayatimua mawingu, nasi tukayafikisha kwenye nchi iliyokufa tukaihuisha ardhi kwayo baada ya kufa kwake. Ndio kama hivyo kutakuwa kufufuliwa” (35:9)
Nyingine ni:
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ إِنَّ الَّذِي أَحْيَاهَا لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ﴿٣٩﴾
“Na miongoni mwa ishara zake ni kwamba unaiona ardhi ni nyonge, lakini tunapoiteremshia maji mara unaiona inataharaki na kuumuka. Hakika bila shaka aliyeihuisha ardhi ndiye atakayehuisha wafu.” (41:39)
Na nyinginezo nyingi.
Na kama tungeutuma upepo wakauona umekuwa rangi ya njano, juu ya hayo wangekufuru.
Yaani Mwenyezi Mungu akipeleka upepo utakaogeuza mimea yao rangi ya njano baada ya kuwa kijani, watakata tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu na wataipinga hekima yake na kumkufuru Yeye na neema yake.
Hii haifahamishi chochote isipokuwa imani yao kwa Mwenyezi Mungu ni njozi tu. Lau ingelikuwa imejikita moyoni wangelikuwa imara nayo katika shida na raha.
Imam Ali(a.s) amesema:“Katika imani kuna ile iliyothibiti na kutulia moyoni na kuna ile inayokaa nyoyoni na vifuani kwa muda tu.”
Mumin, kama binadamu, anaumia na kuhuzunika, anapopatwa na masaibu yeye mwenyewe, mtoto wake au mali yake, lakini hilo halimtoi kwenye dini yake. Mtume(s.a.w.w) alipofiwa na mtoto wake Ibrahim alisema: “Jicho linalia na moyo unahuzunika wala hatusemi yanayomchukiza Mola.”
فَإِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا وَلَّوْا مُدْبِرِينَ ﴿٥٢﴾
52. Kwa hakika wewe huwezi kuwasikilizisha wafu wala kuwasikilizisha viziwi wanapogeuka kurudi nyuma.
وَمَا أَنتَ بِهَادِ الْعُمْيِ عَن ضَلَالَتِهِمْ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ ﴿٥٣﴾
53. Wala huwezi kuwaongoza vipofu na upotevu wao. Huwezi kuwasikilizisha ila wale wanaoziamini ishara zetu, basi hao ndio watiifu.
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن ضَعْفٍ ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ ضَعْفٍ قُوَّةً ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ قُوَّةٍ ضَعْفًا وَشَيْبَةً يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْقَدِيرُ ﴿٥٤﴾
54. Mwenyezi Mungu ndiye ambaye amewaumba katika udhaifu, kisha akajaalia nguvu baada ya udhaifu, kisha akajaalia udhaifu baada ya nguvu na uzee. Anaumba atakavyo. Naye ndiye Mjuzi, Mwenye uweza.
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُقْسِمُ الْمُجْرِمُونَ مَا لَبِثُوا غَيْرَ سَاعَةٍ كَذَٰلِكَ كَانُوا يُؤْفَكُونَ ﴿٥٥﴾
55. Na siku itakaposimama Saa, wakosefu wataapa kuwa hawakukaa duniani ila saa moja. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakigeuzwa.
وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَالْإِيمَانَ لَقَدْ لَبِثْتُمْ فِي كِتَابِ اللَّـهِ إِلَىٰ يَوْمِ الْبَعْثِ فَهَـٰذَا يَوْمُ الْبَعْثِ وَلَـٰكِنَّكُمْ كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٥٦﴾
56. Na waliopewa ilimu watasema: Hakika nyinyi mlikwisha kaa katika hukumu ya Mwenyezi Mungu mpaka siku ya kufufuliwa. Basi hii ndio siku ya kufufuliwa. Lakini nyinyi mlikuwa hamjui.
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يَنفَعُ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَعْذِرَتُهُمْ وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ ﴿٥٧﴾
57. Basi siku hiyo hautawafaa waliodhulumu udhuru wao wala hawatapokelewa toba yao.
وَلَقَدْ ضَرَبْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ وَلَئِن جِئْتَهُم بِآيَةٍ لَّيَقُولَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ أَنتُمْ إِلَّا مُبْطِلُونَ ﴿٥٨﴾
58. Na hakika tulikwishawapigia watu kila mfano katika hii Qur’an. Na ukiwaletea ishara yoyote bila shaka watasema wale ambao wamekufuru: Nyinyi si chochote ila ni wabatilifu.
كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٩﴾
59. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga muhuri kwenye nyoyo za wasiojua.
فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَا يَسْتَخِفَّنَّكَ الَّذِينَ لَا يُوقِنُونَ ﴿٦٠﴾
60. Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki; wala wasikuhafifishe wale wasiokuwa na yakini.
Aya 52 – 60
Kwa hakika wewe huwezi kuwasikilizisha wafu wala kuwasikilizisha viziwi wanapogeuka kurudi nyuma. Wala huwezi kuwaongoza vipofu na upotevu wao. Huwezi kuwasikilizisha ila wale wanaoziamini ishara zetu, basi hao ndio watiifu.
Zimetangulia kwa herufi zake katika Juz. 20 (27: 80 – 81).
Mwenyezi Mungu ndiye ambaye amewaumba katika udhaifu, kisha akajaalia nguvu baada ya udhaifu, kisha akajaalia udhaifu baada ya nguvu na uzee. Anaumba atakavyo. Naye ndiye Mjuzi, Mwenye uweza.
Mtu hakuwako, kisha akawa na akagura daraja mbali mbali; kuanzia mchanga hadi tone la manii, kijusi hadi kuwa mtoto wa kunyonya, kuachishwa ziwa (kunyonya) hadi kuwa mtoto mdogo na kuanzia ujana hadi uzee na ukongwe.
Udhaifu wa kwanza ulioashiriwa na Aya ni ule wa mwili na utambuzi wa akili kwenye utoto. Imesemekana kuwa ni udhaifu wa kuwa tone la manii. Ama nguvu ni ujana, na udhaifu wa pili ni wa ukongwe; kama walivyoafikiana wafasiri. Ndio maana tukasema udhaifu wa kwanza ni utoto kulinganisha na uzee ambao ndio udhaifu wa pili, kwa maafikiano ya wafasiri.
Kwa vyovyote iwavyo ni kuwa makusudio ya Aya kuashiria mabadiliko ya mtu kutoka hali moja hadi nyingine ni kuwa mtu atambue kuwa yeye yuko mikononi mwa Mwenyezi Mungu akimgeuza vile atakavyo; kumpa uhai, kumfisha, kumpa udhaifu na nguvu. Kisha marejo ni kwake.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 14 (16:70).
Na siku itakaposimama Saa, wakosefu wataapa kuwa hawakukaa duniani ila saa moja.
Makusudio ya Saa ni Siku ya Kiyama. Kusema isipokuwa saa moja ni kukusudia sehemu ya wakati katika maisha ya dunia. Maana ni kuwa wakosefu wakati watakapotolewa makaburini, wataapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa hawakukaa makaburini isipokuwa muda mchache.
Umetangulia mfano wake kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 16 (20:102). Huko tumechanganya Aya tatu: ya kwanza ni ile inayosema:“Watanong’onezana wao kwa wao: Hamkukaa ila siku kumi tu.” Juz. 16 (20: 103) ya pili inasema:“Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku.” Juz. 15 (18:19). Ya tatu ni hii tuliyo nayo. Na tumejibu huko swali la je, zinaoana vipi Aya tatu hizo?
Hivyo ndivyo walivyokuwa wakigeuzwa.
Duniani walikuwa wakigeuza ukweli kuwa uongo huku wakiapa kuwa hakuna ufufuo wala hisabu. Na Akhera vilevile wataapa kuwa hawakukaa isipokuwa saa moja.
Na waliopewa ilimu watasema: hakika nyinyi mlikwisha kaa katika hukumu ya Mwenyezi Mungu mpaka siku ya kufufuliwa. Basi hii ndio siku ya kufufuliwa.
Wakosefu watasema watakayoyasema kuhusu muda wa kukaa kwao makaburini na watu wanaomwamini Mungu na hisabu yake na thawabu zake watawaambia: Mmekaa kiasi alichotaka Mwenyezi Mungu mkae na muda mliokaa makaburi ni wenye kuthibiti katika ujuzi wake Mwenyezi Mungu Mtukufu; wala hakuna aujuae isipokuwa Yeye.
Kuna faida gani ya kuzungumza kwenu kuapa kuhusu muda wa kukaa makaburini na hali nyinyi mlikuwa mkiikana siku hii ambayo leo mnaona vituko vyake kwa macho yenu?
Lakini nyinyi mlikuwa hamjui.
Yaani nyinyi mko kwenye upofu na upotevu ulio wazi.
Basi siku hiyo hautawafaa waliodhulumu udhuru wao wala hawat- apokelewa toba yao.
Kauli nyingine inayofanana na hii ni:
وَإِن يَسْتَعْتِبُوا فَمَا هُم مِّنَ الْمُعْتَبِينَ ﴿٢٤﴾
“Na wakiomba toba hawakubaliwi.” (41:24).
Yaani siku hiyo hakutakuwa na udhuru wala kukubaliwa toba ya mkosefu, baada ya kuhadharishwa na kuonywa akakataa isipokuwa ukafiri.
Na hakika tulikwishawapigia watu kila mfano katika hii Qur’an.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 15 (18:54).
Na ukiwaletea ishara yoyote bila shaka watasema wale ambao wamekufuru: Nyinyi si chochote ila ni wabatilifu.
Wanawaambia mitume, viongozi wema na wakombozi kuwa ni wabatilifu na waongo. Na wale wahaini na vibaraka wanaolipwa, kuwa ndio wenye haki. Hili si jambo geni; kwani mataghuti walio wakosefu wanaipima haki na batili kwa manufaa yao na hawaa zao.
Ikiwa inaafikiana nao basi hiyo ni haki hata kama ni shari na ufisadi; na inayohalifiana nao basi hiyo ni batili hata kama ni heri na wema.
Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga muhuri kwenye nyoyo za wasiojua.
Mwenyezi Mungu amepiga muhuri kwenye nyoyo zao kwa sababu wao walifuata kwa hiyari yao njia inayopelekea hilo. Kuwa kipofu na haki ni natija ya ujinga; na dhulma na utaghuti ni natija ya kuwa kombo na njia ya uongofu. Ama kunasibishwa hilo kwa Mwenyezi Mungu maana yae ni kuwa sababu za natija yake zinalazimiana naye.
Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki; wala wasikuhafifishe wale wasiokuwa na yakini.
Vumilia ewe Muhammad, uendelee na mwito wako na uvumilie adha katika njia yake. Hazitapita siku nyingi ila ujumbe wako utaenea mashariki ya ardhi na magharibi yake jina lako litatajwa pamoja na jina la Mwenyezi Mungu na litaombewa rehema na taadhima.
Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ametuneemesha kwa Muhammad(s.a.w.w) , Mtume wa rehema na kiongozi wa watu kwenye heri. Basi turuzuku shafaa yake, ewe mwenye kubadili mabaya, pamoja na wingi wake, kwa mazuri.
17
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
Sura Ya Thelathini na Mmoja: Surat Luqman. Imeshuka Makka isipokuwa baadhi ya Aya. Ina Aya 34.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miim.
تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْحَكِيمِ ﴿٢﴾
2. Hizo ni Aya za Kitabu chenye hekima.
هُدًى وَرَحْمَةً لِّلْمُحْسِنِينَ ﴿٣﴾
3. Ni uongofu na rehema kwa wafanyao wema.
الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿٤﴾
4. Ambao wanasimamisha Swala; na wanatoa Zaka na wana yakini na akhera.
أُولَـٰئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥﴾
5. Hao ndio walio na uongofu utokao kwa Mola wao na hao ndio wenye kufanikiwa.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٦﴾
6. Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipokujua na wanaichukulia ni mzaha. Hao watapata adhabu ya kufedhehesha.
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا وَلَّىٰ مُسْتَكْبِرًا كَأَن لَّمْ يَسْمَعْهَا كَأَنَّ فِي أُذُنَيْهِ وَقْرًا فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٧﴾
7. Na anaposomewa Aya zetu huzipa mgongo kwa kujivuna, kama kwamba hakuzisikia, kama kwamba masikioni kwake mna uziwi. Basi mbashirie adhabu chungu.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتُ النَّعِيمِ ﴿٨﴾
8. Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema watakuwa na bustani zenye neema.
خَالِدِينَ فِيهَا وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٩﴾
9. Watadumu humo. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kweli. Na Yeye ndiye Mwenye uwezo, Mwenye hekima.
خَلَقَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ ﴿١٠﴾
10. Ameumba mbingu bila ya nguzo mnazoziona na ameweka katika ardhi mlima ili ardhi isiwayumbishe na amewatawanya humo kila namna ya wanyama; na tumeteremsha maji kutoka mbinguni na tukaotesha katika ardhi mimea mizuri ya kila namna.
هَـٰذَا خَلْقُ اللَّـهِ فَأَرُونِي مَاذَا خَلَقَ الَّذِينَ مِن دُونِهِ بَلِ الظَّالِمُونَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١١﴾
11. Huu ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Basi nionyesheniwameumba nini hao wasiokuwa Yeye! Lakini madhalimu wamo katika upotevu ulio dhahiri.
Aya 1 – 11
Alif Laam Miam.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1).
‘Hizo’ ni Aya za Kitabu chenye hekima.
Hizo ni ishara ya Aya za Sura hii, na kwamba hizo zinatokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu amekisifu kuwa kina hekima kwa sababu ndani yake mna hekima ya hali ya juu.
Ni uongofu na rehema kwa wafanyao wema ambao wanaitafuta haki na kuitumia kwa sababu ni haki; wala hawana shaka kwamba Qur’an ni uongofu na rehema kwa kila mwenye kumfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu na haki. Ama wale ambao tamaa zimepofusha nyoyo zao, basi hao ni ugonjwa usiokuwa na dawa isipokuwa kun’golewa.
Ambao wanasimamisha Swala; yaani wanadumu nayona wanatoa Zaka kwa anayestahikina wana yakini na akhera, wala hawana shaka kwamba wao wataulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuhusu kauli zao na vitendo vyao.
Hao ndio walio na uwongofu utokao kwa Mola wao na hao ndio wenye kufanikiwa.
Kipimo cha uongofu na kufanikiwa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kuifanyia ikhlasi haki kwa kauli na vitendo na kutomwabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu wala usifanyie ubakhili fadhila alizokupa Mwenyezi Mungu.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 mwanzo wa sura ya pili.
Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipokujua na wanaichukulia ni mzaha.
Mwenye Majmaul-bayan anasema: “Wafasiri wengi wamesema kuwa makusdio ya maneno ya upuuzi ni nyimbo. Na kutoka kwa Imam Ja’far Sadiq(a.s) imepokewa kuwa ni kuitusi haki na kuifanyia mzaha.”
Tafsiri hii ya Imam ndiyo iliyo karibu zaidi na hali halisi ya mamabo na inaenda na mfumo wa maneno. Kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t) baada ya kutaja waumini waliofaulu, sasa anawataja wakosefu ambao wananunua shutuma kutoka kwa wale wanoifanyia biashara dini na dhamiri, ili wawapoteze watu na haki na kuwavungavunga na mambo ya batili.
Mfano ulio wazi wa hayo ni vile, siku hizi, nguvu ya shari inavyokimbilia kueneza propaganda zake kwa kutoa mamilioni ya pesa kwenye vyombo vya habari ili yaeneze uwongo na uzushi na kuwapa mapesa wahaini na vibaraka ili wawatie shaka wenye wema wenye ikhlasi.
Zaidi ya hayo vyombo hivyo vya kishari vimewavisha vibaraka wake nguo ya dini ili wapandikize bid’a na waifasiri vile watakavyo; kuweza kueneza fitna na mipasuko baina ya mataifa na watu wa dini.
Baada ya vita vya mashariki ya kati vya mwaka 1967, tumeshuhudia aina kwa aina ya propaganda za uwongo na vita vya maneno katika magazeti ya kulipwa. Ama harakati za vibaraka zimefikia kiwango cha kumfanyia ujeuri Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Lakini kila siku zinavyopita zinafichuka njama zao na kufedheheka vibaraka. Wakati wa kuwang’oa utafika tu.
Hao watapata adhabu ya kufedhehesha kwa asababu wameiuza dini yao kwa shetani na wakala njama naye dhidi ya haki na watu wake.
Na anaposomewa Aya zetu huzipa mgongo wa kujivuna, kama kwamba hakuzisikia, kama kwamba masikioni kwake mna uziwi. Basi mbashirie adhabu chungu.
Mumin mwenye ikhlasi anaisikliliza haki na anaizibia masikio batili, lakini habithi mkosefu mwenye malengo ya tamaa anaisikiliza batili na kuiiz- ibia masiko haki. Hana malipo huyu isipokuwa adhabu chungu.
Razi amesema: “Mwenye akili anaitafuta hekima kwa thamani yoyote, lakini wao hawakuitafuta na ilipowajia bure hawakuisikiza.”
Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema watakuwa na bustani zenye neema.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) alipobainisha malipo ya mwenye kuzipinga Aya zake kuwa ni adhabu chungu, sasa anabainisha malipo ya mwenye kuamini kuwa ni Pepo yenye neema.
Watadumu humo na watapata kila wanachokitamani.Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli kwa sababu itatokea tu.
Na Yeye ndiye mwenye uwezo mwenye hekima.
Ni mwenye nguvu kwa uweza wake, usioshindwa, ni mwenye hekima kwa mipangilio yake ambayo haipingi ila jahili au mwenye kiburi.
Ameumba mbingu bila ya nguzo mnazoziona na ameweka katika ardhi milima ili ardhi isiwayumbishe na amewatawanya humo kila namna ya wanyama; na tumeteremsha maji kutoka mbinguni na tukaotesha katika ardhi mimea mizuri ya kila namna.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:2).
Huu ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Basi nionyesheni wameumba nini hao wasiokuwa Yeye!
Kila kilichomo mbinguni ni ushahidi wa kuweko Mwenyezi Mungu na uweza na umoja wake. Basi mna dalili gani nyinyi washirikiana kuwa mnaowaabudu ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenye sifa moja tu katika sifa zake.
Lakini madhalimu wamo katika upotevu ulio dhahiri.
Kila anayeipinga haki yoyote, baada ya kumdhihirikia dalili yake, basi huyo ni dhalimu mwenye dhambi.
Unaweza kuuliza : Mwenye kufuatilia Aya za Qur’an tukufu ataona kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) mara nyingi anapobatilisha ushirikina huwa anasisitiza kwa kueleza vitu vilivyo dhahiri na vinavyoonekana; mfano kauli yake hii: ‘Basi nionyesheni wameumba nini hao wasiokuwa Yeye!’ au ‘Hawawezi kuumba hata nzi,’ Je, kuna siri gani katika hilo?
Siri ya hilo ni kufichua kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwa kikundi kiovu hakiamini hakika yoyote hata kama iko wazi kama mwangaza wa jua, isipokuwa masilahi yake tu. Sifa hii ni mbaya zaidi ya nyingine na ni hatari zaidi; haina dawa isipokuwa nguvu kuu ya upinzani.
وَلَقَدْ آتَيْنَا لُقْمَانَ الْحِكْمَةَ أَنِ اشْكُرْ لِلَّـهِ وَمَن يَشْكُرْ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿١٢﴾
12. Na hakika tulimpa Luqman hekima tukamwambia: Mshukuru Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumshukuru Mwenyezi Mungu basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na aliyekufuru, basi Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifiwa.
وَإِذْ قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ وَهُوَ يَعِظُهُ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ﴿١٣﴾
13. Na Luqman alipomwambia mwanawe akiwa anampa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu na chochote. Hakika shirki ndio dhulma kubwa.
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ ﴿١٤﴾
14. Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake, mama yake amebeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhifu na kumwachisha ziwa (kunyonya) kwa miaka miwili, kwamba unishukuru mimi na wazazi wako. Marudio ni kwangu.
وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٥﴾
15. Na kama wakikushikilia kunishirikisha mimi na yale ambayo huna ilimu nayo basi usiwatii, na kaa nao kwa wema duniani Na fuata njia ya yule anayerejea kwangu. Kisha hakika marejeo yenu ni kwangu mimi, nami nitawaambia mliyokuwa mkiyatenda.
يَا بُنَيَّ إِنَّهَا إِن تَكُ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ فَتَكُن فِي صَخْرَةٍ أَوْ فِي السَّمَاوَاتِ أَوْ فِي الْأَرْضِ يَأْتِ بِهَا اللَّـهُ إِنَّ اللَّـهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ ﴿١٦﴾
16. Ewe mwanangu! Ikiwa kuna jambo la uzito wa hardali likawa ndani ya mwamba au mbinguni au ardhini, basi Mwenyezi Mungu atalileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi, Mwenye habari.
يَا بُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ وَانْهَ عَنِ الْمُنكَرِ وَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا أَصَابَكَ إِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ ﴿١٧﴾
17. Ewe mwangu! Simamisha Swala na uamrishe mema na ukataze mabaya na subiri kwa yanayokusibu, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.
وَلَا تُصَعِّرْ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ ﴿١٨﴾
18. Wala usiwapindie watu uso wako kuwabeua. Wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna anayejifaharisha.
وَاقْصِدْ فِي مَشْيِكَ وَاغْضُضْ مِن صَوْتِكَ إِنَّ أَنكَرَ الْأَصْوَاتِ لَصَوْتُ الْحَمِيرِ ﴿١٩﴾
19. Na ushike mwendo wa katikati. na uinamishe sauti yako. Hakika sauti mbaya zaidi ni sauti ya punda.
Aya 12 – 19
Na hakika tulimpa hekima tukamwambia: Mshukuru Mwenyezi Mungu.
Neno ‘hekima’ hutumiwa kwa maana nyingi; miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kumjua Mwenyezi Mungu na sifa zake, kukiweka kitu mahali pake, maneno yenye mawaidha na kumtii Mwenyezi Mungu. Kuna Hadith isemayo: “Msingi wa hekima ni kumhofia Mwenyezi Mungu”
Luqman alikuwa ni katika wanomjua Mwenyezi Mungu na kumtii, mwenye kulingania kwa Mwenyezi Mungu kwa mfumo mzuri wa utulivu na alikuwa muwazi mwenye kukinaisha.
Na mwenye kumshukuru Mwenyezi Mungu basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na aliyekufuru, basi Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifiwa.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 19 (27:40).
Wametofautiana kuhusu Luqman kuwa je, alikuwa Mtume au mja mwema tu. Tofauti hizi hazihusiani chochote na itikadi au maisha. Lililo wajibu kuliamini ni lile lililonukuliwa na Qur’an - kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimneemesha Luqman kwa hekima ambayo ni elimu ya kumjua Mwenyezi Mungu, kumtii na kutoa mwito kwenye njia yake Mwenyezi Mungu kwa mawaidha mazuri.
Wafasiri na wanahistoria wametaja akili na hekima nyingi za Luqman; miongoni mwazo ni kuwa yeye alikuwa ni mtumwa. Siku moja alitumwa kwenye bustani pamoja na watumwa wengine ili wakalete matunda. Walipofika kwenye bustani wote wakala matunda isipokuwa Luqman. Wakala njama dhidi yake kwa vile hakushiriki kwenye kosa lao.
Wakamfikisha kwa bwana wao na kusema kuwa Luqman amekula matunda yote. Alipoulizwa Luqman akasema: Tunyweshe dawa sote, hapo utadhihiri uhakika. Basi ikawa hivyo. Wote wakatapika matunda isipokuwa Luqman. Vitimbi vikawarudia wao wenyewe.
Tukio jingine ni kuwa siku moja bwana wake alilewa na akaweka rehani ya mali nyingi kuwa anywe maji kwenye ziwa moja huko.
Alipotokwa na ulevi akajuta na akaona amewezwa bila ya kujitambua. Akakimbilia kwa Luqman na kumwambia hii ni siku yako. Luqman akawaambia watu. Hili ziwa lina mito inayomimina maji ndani yake, basi izuwiyeni ili huyu bwana anywe maji ya ziwa. Wakasema hatuwezi kufanya hivyo.
Akawaambia: “Yeye ameweka rehani kunywa maji ya ziwa sio yanyoingia au kutoka ziwani.”
Iwe ni sawa riwaya hii au la, lakini ni mfano wazi kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimpa Luqman hekima na maarifa. Kutokana na kauli za wafasri na wana historia, inaonyesha kuwa Luqman alikuwa zama za Nabii Daud(a.s) Tazama Juz. 17 (21:80).
Na Luqman alimwambia mwanawe akiwa anampa mawaidha:
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja kuwa alimneemesha Luqman kwa hekima, sasa anataja baadhi ya mawaidha yake kwa mwanawe yenye upole na huruma.
Imam Ali(a.s) alimuusia mwanawe Imam Hasan(a.s) wasia mrefu, mwanzo ulikuwa hivi:“Nakuona wewe ni sehemu yangu bali ni mwili wangu wote, kiasi ambacho likikusibu jambo ni kama limenisibu mimi. Na kama kwamba lau mauti yanakujia basi ni kama yamenijia mimi. Jambo lako linanihusu kama linavyonihusu jambo langu.”
Luqman alimuusia mwanawe mambo haya yafuatayo:
Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu na chochote. Hakika shirki ndio dhulma kubwa.
Badhi ya wafasiri wanaona kuwa kauli hii inaonyesha kuwa mwanawe Luqman alikuwa mshirikina. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa kukataza jambo hakufahamishi kuwa anayekatazwa analo. Mwenyezi Mungu alimwambia kipenzi chake: Ibrahim(a.s) :
أَن لَّا تُشْرِكْ بِي شَيْئًا ﴿٢٦﴾
“…kwamba usinishirikishe na chochote” Juz. 17 (22:26).
Pia alimwambia kipenzi chake Muhammad(s.a.w.w) : “Basi usiwatii makafiri” Juz. 19 (25:52). Imam Ali(a.s ) alimwambia Hasan(a.s ) :“Shikamana na Mwenyezi Mungu… awe ndiye unayemwabudu… Lau angelikuwa na mshirika wangelikujia mitume wake.”
Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake. Amebeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu.
Aya hii na iliyo baada yake ni muendelezo wa wasia wa Luqman kwa mwanawe. Neno udhaifu limefasirwa kutokana na neno wahan lenye maana ya udhaifu na mashaka. Kila mtoto anavyokuwa tumboni mwa mama yake humzidisha udhaifu na tabu.
Na kumwachisha ziwa (kunyonya) kwa miaka miwili.
Mama humnyonyesha mwanawe miaka miwili kisha anamwachisha kunyonya Katika muda huo anapata shida kuongezea shida alizozipata wakati wa mimba na uchungu wa kuzaa. Yametangulia maelezo kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 2(2:233).
Kwamba unishukuru mimi na wazazi wako. Marudio ni kwangu.
Yaani siku hiyo nitakuuliza; je ulikuwa ni katika wenye shukrani na twaa au ulikuwa mwenye kuwaudhi wazazi na kuniasi mimi na wazazi wako?Na kama wakikushikila kunishirikisha mimi na yale ambayo huna ilimu nayo basi usiwatii, kwa vile hakuna kumtii kimbe kwa kumuuasi muumba.
Na kaa nao kwa wema duniani kwa kutowakemea na uzungumze nao vizuri na kuwafanyia yale wanayoyapendelea. Yametangulia maelezo ya kuwatendea wema wazazi kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 15 (17:23) na Juz. 20 (29:8).
Na fuata njia ya yule anayerejea kwangu.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuamrisha kushukuriwa Yeye na wazazi, sasa anaamrisha kutiiwa Yeye katika kila jambo, sio kuwatendea wema wazazi tu. Hilo ameliletea ibara kuwafuata watu wema ambao wamemtii Mwenyezi Mungu katika maarisho na makatazo yake.
Imam Zaynul’abidin(a.s) anasema:“Ewe Mola wangu! Niunganishe na watu wema waliopita na unijaalie katika wema waliobakia na unielekeze njia ya watu wema.”
Kisha hakika marejeo yenu ni kwangu mimi, nami nitawaambia mliyokuwa mkiyatenda.
Huu ni ukemeo na kiaga kwa yule anayemuasi Mwenyezi Mungu na wazazi wawili.
Ewe mwanangu! Ikiwa kuna jambo la uzito wa hardali likawa ndani ya mwamba au mbinguni au ardhini, basi Mwenyezi Mungu atalileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi, Mwenye habari.
Neno jambo halikutajwa katika Aya, lakini linafahamika kutokana na mfumo wa maneno. Neno ‘uzito wa hardali’ ni kinaya cha udogo na neno ‘ndani ya mwamba au mbinguni au ardhini,’ ni kinaya cha siri na uficho.
Maana ya kiujumla ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anajua makusudio ya mtu, kauli yake na vitendo vyake vilivyofichika na vilivyo dhahiri, haachi dogo wala kubwa, isipokuwa analidhibiti na kulihisabu.
Makusudio ya maneno haya ni kuwaonya wapotevu wanaopoteza ambao wanaishi na watu kwa ndimi zao na wanaishi na maadui wa Mwenyezi Mungu na wa ubinadamu kwa nyoyo zao, kwamba wajue mwisho ni kufedheheka na balaa.
Baadhi ya wafasiri wamejiuliza na wakasema: Vipi Mwenyezi Mungu ametaja mbingu na ardhi baada ya kutaja mwamba na inajulikana kuwa mwamba lazima uwe ardhini na sio mbinguni?
Mmoja akajibu kuwa mwamba huu hauko mbinguni wala ardhini isipokuwa uko chini ya ardhi saba na ndio mwamba ambao ng’ombe anayeibeba ardhi kwa pembe yake ndio amesimamia hapo. Mwingine akasema mwamba huu uko hewani. Wa tatu naye akasema una rangi ya kijani. Tazama tafsiri ya Razi na Tabariy.
Qur’an, ambayo Mwenyezi Mungu ameisifu kuwa ni nuru na upambanuzi, imeepekuna na tafsiri zote hizi ambazo adui amezifanya ni nyenzo ya kushutumu na kuifanyia stihzai dini. Tafsiri hii na mfano wake inafa- hamisha kuwa walioifasiri hawajui hekima ya Mwenyezi Mungu ya kupeleka mitume yake na kuteremsha Kitabu chake.
Pia hawajui kwamba dini ya kiislamu ni dini ya maumbile na ya maisha na kwamba msingi wa mwito wake ni imani na ikhlasi. Mwangaza wake ni elimu na uadilifu, njia yake ni bidii na utendaji na lengo lake ni wema na raha.
Ewe mwangu! Simamisha Swala, kwa sababu inakukumbusha Mwenyezi Mungu na kukataza kiburi.Na uamrishe mema na ukataze mabaya . Miongoni mwa mema ni kushikamana na waumini na kuwakaba koo wanafiki.
Na subiri kwa yanayokusibu, hakika hayo ni katika mambo ya kuaz- imiwa.
Makusudio ya mambo ya kuazimiwa ni nguvu ya utashi na uthabiti wa haki. Amri ya kuwa na subira baada ya kuamrisha mema inaonyesha kuwa mwenye kutoa mwito wa haki atapata yale anayopambana nayo kila mwenye kufanya jihadi aliye na ikhlasi kutoka kwa wabatilifu.
Wala usiwapindie watu uso wako kuwabeua.
Yaani usiwageuzie uso wako kwa kiburi, bali wakabili na uwanyenyekee. Katika Nahjulbalagha imeelezwa: “Hakuna upweke kama kujiona na hakuna ufahari kama kunyenyekea.”
Wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna anayejifaharisha.
Baada ya kukataza kutembea kwa maringo anabainisha maana yake kuwa ni kujivuna na kujifaharisha; wala hakuna kitu kinachofahamisha ujinga na upunguani kuliko sifa hizi.
Na ushike mwendo wa katikati. Usiende polepole wala haraka na uinamishe sauti yako. Hakika sauti mbaya zaidi ni sauti ya punda.
Hapa kuna ishara ya kuwa kuinua sauti zaidi ya haja kunafahamisha ujinga na pia kunyamaza kabisa. Mwenye kufanya wastani ndio amejua njia.
Pia ieleweke kuwa mazungumzo yatakuwa mazuri, kwa sauti ya wastani, ikiwa kuna haja ya kuzungumza; vinginevyo itakuwa kunyamaza ni bora na ukamilifu zaidi.
Katika maelezo ya wasifu wa Luqman ni kwamba alikuwa akisikiliza sana na kuzungumza kidogo. Anapozungumza basi neno lake linakuwa kama punje ya mtama kwenye changarawe.
Kuna baadhi ya Hadith zisemazo kuwa kunyamaza ni katika milango ya hekima; yaani ni hekima kunyamaza na kusikiliza kwa makini ni hekima.
Ama kauli ya anayesema: “Ikiwa maneno ni fedha basi kunyamaza ni dhahabu,” maana yake ni kunyamaza kwa kuacha batili na ufedhuli; vinginevyo tamko la haki ni nuru na jihadi, hasa likiwa ni dhidi ya dhulma na jeuri. Kuna Hadith isemayo:“Mwenye kuinyamazia haki ni shetani bubu.”
18
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
أَلَمْ تَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَسْبَغَ عَلَيْكُمْ نِعَمَهُ ظَاهِرَةً وَبَاطِنَةً وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَابٍ مُّنِيرٍ ﴿٢٠﴾
20. Je, hamuoni kwamba Mwenyezi Mungu amevifanya viwatumikie vilivyomo mbinguni na kwenye ardhi na akawakamilishia neema zake zilizo dhahiri na siri? Na katika watu wapo wanaojadiliana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya ilimu wala uongofu wala Kitabu chenye nuru.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا أَوَلَوْ كَانَ الشَّيْطَانُ يَدْعُوهُمْ إِلَىٰ عَذَابِ السَّعِيرِ ﴿٢١﴾
21. Na wanapoambiwa: Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu; husema: ‘Bali tutafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu.’ Je, hata kama shetani anawaita kwenye adhabu ya moto?
وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ وَإِلَى اللَّـهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ ﴿٢٢﴾
22. Na ausalimishaye uso wake kwa Mwenyezi Mungu naye akawa anafanya wema, basi huyo hakika amekwishakama- ta kishikilio madhubuti. Na mwisho wa mambo yote ni wa Mwenyezi Mungu.
وَمَن كَفَرَ فَلَا يَحْزُنكَ كُفْرُهُ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ فَنُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٢٣﴾
23. Na mwenye kukufuru, isikuhuzunishe kufuru yake. Marejeo yao ni kwetu, ndipo tutawaambia yale waliyoyafanya. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
نُمَتِّعُهُمْ قَلِيلًا ثُمَّ نَضْطَرُّهُمْ إِلَىٰ عَذَابٍ غَلِيظٍ ﴿٢٤﴾
24. Tunawastarehesha kwa uchache kisha tutawasukuma kwenye adhabu ngumu.
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٥﴾
25. Na ukiwauliza ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi, bila shaka watasema ni Mwenyezi Mungu. Sema: Alhamdulillah (sifa njema ni za Mwenyezi Mungu) Bali wengi wao hawafahamu.
لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٢٦﴾
26. Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na ardhini. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mkwasi, Msifiwa.
وَلَوْ أَنَّمَا فِي الْأَرْضِ مِن شَجَرَةٍ أَقْلَامٌ وَالْبَحْرُ يَمُدُّهُ مِن بَعْدِهِ سَبْعَةُ أَبْحُرٍ مَّا نَفِدَتْ كَلِمَاتُ اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٧﴾
27. Na lau miti yote iliyomo ardhini ikawa ni kalamu na bahari na ikaongezewa bahari nyingine saba, (kuwa wino) maneno ya Mwenyezi Mungu yasingemalizika. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo, Mwenye hekima.
مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ ﴿٢٨﴾
28. Hakukuwa kuumbwa kwenu wala kufufuliwa kwenu ila ni kama nafsi moja tu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.
Aya 20 – 28
Je, hamuoni kwamba Mwenyezi Mungu amevifanya viwatumikie vilivyomo mbinguni na kwenye ardhi na akawakamilishia neema zake zilizo dhahiri na siri?
Neema za Mwenyezi Mungu ni nyingi sana; kama alivyozisifu Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa kauli yake: “Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamuwezi kuzidhibiti.” Juz. 13 (14:34).
Ni nani atakayeweza kudhibiti na kuyajua yaliyo katika mbingu na ardhi zaidi ya aliyeumba hiyo mbingu na ardhi? Wafasiri wametoa mfano wa neema ya dhahiri kuwa ni zile zinazohisiwa na hisia tano na neema za siri kuwa ni nguvu za nafsi na utashi wake. Mulla Sadra anasema katika Juz. 3 ya kitabu chake Al-asfar:
“Watu walio bora wanashindwa kujua mambo ya mbingu na ya ardhi na hawajui hekima yake; bali wengi hawajui hakika ya nafsi ambayo ndiyo mtu mwenyewe. Mambo wanayohusiana nayo yaliyofichika ni mengi zaidi ya yaliyo dhahiri. Ikiwa mtu hajui nafsi yake na mwili wake, vipi ataweza kujua mwili na roho. Nasi, kwa kushindwa huku, hatuna ila kutaamali na kufikiria maajabu ya uumbaji na maumbile ya kushangaza.”
Na katika watu wapo wanaojadiliana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya ilimu wala uongofu wala Kitabu chenye nuru.
Aya hii, pamoja na ufupi wake, imekusanya sababu tatu za maarifa: Kwanza ni hisia na majaribio yaliyoashiriwa na neno ‘ilimu.’ Pili, ni akili ilyokusudiwa kwenye neno uwongofu. Tatu ni wahyi ulioletewa ibara ya Kitabu chenye nuru.
Aya hii Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 17 (22:8).
Na wanapoambiwa: Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu; husema: Bali tutafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu.’ Je, hata kama shetani anawaita kwenye adhabu ya moto?
Umetangulia mfano wake katika Juz. 2 (2:170).
NI NANI MWENYE KUSHIKILIA KISHIKILIO MADHUBUTI?
Na ausalimishaye uso wake kwa Mwenyezi Mungu naye akawa anafanya wema, basi huyo hakika amekwishakamata kishikilio madhubuti. Na mwisho wa mambo yote ni wa Mwenyezi Mungu.
Kishikilio madhubuti ni kinaya cha Qur’an, kamba ya Mungu ni radhi zake na mengineyo anayosalimika nayo mtu na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake. Kila mwenye kusifika na sifa mbili basi atakuwa ameshikilia mpini ulio imara:
Kwanza : ni kumwamini Mwenyezi Mungu kwa kufanya aliyoyaamrisha katika ibada; kama vile Swaumu na Swala. na kuacha aliyoyakataza; kama vile zina, uwongo na pombe.
Pili : ni kuwa mwema. Mwema ni yule ambaye wema wake unaenea kwa wengine wala hajifanyii yeye pekee na watu wake tu. Anashirikiana na watu katika machungu yao anatenda kwa ajili ya kuwakomboa wanaodhulumiwa na kukandamizwa na kwa ajili ya haki na uadilifu popote ulipo na utakapokuwa. Kwa ufupi ni kuwa wema ni sawa na maji twahara; hayo yenyewe ni twahara na yanatwaharisha kingine.
Kwa hiyo basi inatubainikia kuwa watakaosalimika na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake ni wale waumini wanaofanya wema. Ama mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na akamwabudu wala asi- wafanyie wema wengine kwa kusaidiana nao kwenye manufaa ya wote au akafanya wema na asimwamini Mwenyezi Mungu, wote hawa wawili hawana amani ya adhabu ya Mwenyezi Mungu na ghadhabu yake. Kwa sababu watakuwa hawakukamata kishikilio madhubuti.
Kuna Hadith nyingi zinazohusiana na maudhui hii; miongoni mwazo ni hizi zifuatazo:
“Asiyetilia umuhimu mambo ya waislamu basi yeye si mwislamu.”
“Imani ya mja haiwi kweli mpaka ampendelee ndugu yake lile analojipendelea yeye mwenyewe.”
“Mtu anayependeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni yule anayewafaa zaidi watu.”
Kauli yake Mtume mtukufu(s.a.w.w) :“Hakika nimetumwa kukamilisha maadili mema,” ni ushahidi tosha kuwa risala ya uislamu ni risala ya kiutu. Ndio maana baadhi ya wajuzi wakamwelezea mwislamu kuwa ni ‘Mtu ambaye manufaa yake yanaenea kwa jamii ya uma wake wote na sio mtu finyu wa manufaa ya nafsi yake.”
Na mwenye kukufuru, isikuhuzunishe kufuru yake. Marejeo yao ni kwetu, ndipo tutawaambia yale waliyoyafanya. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
Unahuzunikia nini na kupata uchungu kwa sababu ya kufuru ya anayekufuru ewe Muhammad! Wewe umekwishafikisha na ukatekeleza risala kwa ukamilifu. Achana nao hao wakosefu na dunia yao. Sisi tunawajua zaidi na marejeo yao na hisabu yao ni kwetu.
Tunawastarehesha kwa uchache kisha tutawasukuma kwenye adhabu ngumu.
Hizo ni siku chache tu wanacheza nazo na zinacheza nao, kisha iwazingire adhabu kali bila ya kujitambua.
Umetangulia mfano wake katika Aya nyingi; miongoni mwazo ni Juz. 4 (3:176).
Na ukiwauliza ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi, bila shaka watasema ni Mwenyezi Mungu. Sema: Alhamdulillah (sifa njema ni za Mwenyezi Mungu). Bali wengi wao hawafahamu.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 18 (23:84) na katika Juzuu hii tuliyo nayo (29: 61).
Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na ardhini. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mkwasi, Msifiwa.
Sifa njema na ufalme ni wake peke yake, wala hakuna Mkwasi ila yule anayetosheka naye
Na lau miti yote iliyomo ardhini ikawa ni kalamu na bahari na ikaongezewa bahari nyingine saba, (kuwa wino) maneno ya Mwenyezi Mungu yasingemalizika. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo Mwenye hekima.
Bahari saba ni kinaya cha wingi. Makusudio ya maneno ya Mwenyezi Mungu ni uweza wake wa kuvileta vyote vilivyoko wakati wowote anaotaka.
Maana ni kuwa lau tungelikadiria bahari kuwa ni wino na miti ikawa ni kalamu za kuandikia uweza wa Mwenyezi Mungu basi wino na kalamu zingelikwisha na uweza wa Mwenyezi Mungu ungelibakia bila ya kuwa na kikomo.
Kwa manenno mengine ni kuwa uweza wa Mwenyezi Mungu hauna mpaka. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (18:109).
Ibn Al-arabi anasema katika Futahatil – Makkiyya: “Bahari na Miti ni katika jumla ya maneno ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo kama bahari ni wino isingeweza kujiandika isipokuwa hiyo yenyewe tu. Kalamu na mengineyo yangelibakia bila ya kitu cha kuandikia. Hii ni kwa vile amabavyo tayari viko. Je, kwa vile ambavyo haviko lakini vinawezekana kuwako?”
Anakusudia kuwa lau bahari ingelikuwa wino na tukataka kuandika maajabu na siri za bahari tu basi wino ungelikwisha. Ikiwa wino umekwisha kalamu hazitaweza kuandika tena siri na maajbu ya vitu vilivyobaki, zikiwemo hizo kalamu zenyewe.
Na hii ni kwa vile vitu ambavyo tayari vipo. Je, vile amabavyo havipo vinavyopatikana kwa neno ‘kuwa’ wakati wowote anaotaka?
Hakukuwa kuumbwa kwenu wala kufufuliwa kwenu ila ni kama nafsi moja tu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.
Asiyekuwa Mwenyezi Mungu anaweza baadhi ya vitu na vingine vinamshinda. Na vile anavyoviweza kuna vile visivyohitajia juhudi yoyote, kuna vinavyohitajia juhudi kidogo na vile vinavyohitajia juhudi kubwa.
Lakini Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu na kila kitu kwake ni sawa, kiwe kidogo au kikubwa. Kwa hiyo kwake yeye kumuumba mtu mmoja ni sawa na kuumba watu wote. Vile vile kuwafufua na hisabu yao.
Imam Ali(a.s) anasema:“Hakuna kitu kilichoanza kuumbwa kwake ila ni kwa uweza wake aliye mmoja mwenye kushinda nguvu zote ambaye kwake ni marejeo ya mambo yote. Bila ya kukizuia kingelikwisha. Hachoki kukitengenza kitu chochote anapokitengeneza. Wala haoni uzito wa kuumba anachokiumba baada ya kutokuweko.”
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَأَنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٩﴾
29. Je, huoni kwamba huuingiza usiku katika mchana na huuingiza mchana katika usiku. Na amelitiisha jua na mwezi, vyote hupita mpaka wakati uliowekwa. Na Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyafanya.
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الْبَاطِلُ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ ﴿٣٠﴾
30. Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na kwamba wale wanaowaomba badala yake ni batili, na hakika Mwenyzi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ الْفُلْكَ تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِنِعْمَتِ اللَّـهِ لِيُرِيَكُم مِّنْ آيَاتِهِ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ ﴿٣١﴾
31. Je, huoni kwamba majahazi hupita baharini kwa neema za Mwenyezi Mungu, ili awaonyeshe ishara zake. Hakika katika hayo kuna ishara kwa kila mwenye subira nyingi, mwenye shukrani.
وَإِذَا غَشِيَهُم مَّوْجٌ كَالظُّلَلِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ فَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ وَمَا يَجْحَدُ بِآيَاتِنَا إِلَّا كُلُّ خَتَّارٍ كَفُورٍ ﴿٣٢﴾
32. Na wimbi linapowafunika kama vivuli, humuomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafia dini. Lakini anapowaokoa wakafika nchi kavu, wapo baadhi yao huenda mwendo wa wastani. Wala hazikanushi ishara zetu ila kila mhaini mkuu, kafiri mkubwa.
Aya 29 - 32
Je, huoni kwamba huuingiza usiku katika mchana na huuingiza mchana katika usiku.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 3 (3:26) na Juz. 17 (22:61).
Na amelitiisha jua na mwezi, vyote hupita mpaka wakati uliowekwa. Na Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyafanya.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:2).
Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na kwamba wale wanaowaomba badala yake ni batili, na hakika Mwenyzi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa.
Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 17 (22:62).
Je, huoni kwamba majahazi hupita baharini kwa neema za Mwenyezi Mungu, ili awaonyeshe ishara zake.
Miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu ni kusahilisha mawasiliano. Miongoni mwa mawasiliano hayo ni majahazi ambayo yanahitajia maji, upepo na mbingu. Sababu hizi zote zunaishia kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Hakika katika hayo kuna ishara kwa kila mwenye subira nyingi mwenye shukrani, anayevumilia machungu na kuchunguza ishara za Mwenyezi Mungu katika maumbile yake na kushukuru Mungu wake.
Na wimbi linapowafunika kama vivuli, humuomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafia dini. Lakini anapowaokoa wakafika nchi kavu, wapo baadhi yao huenda mwendo wa wastani. Wala hazikanushi ishara zetu ila kila mhaini mkuu, kafiri mkubwa.
Baadhi ya wafasiri wamesema makusudio ya mwenye kwenda mwendo wa wastani hapa ni mwenye kuficha ukafiri wake. Razi akasema ni kafiri wa wastani. Lakini usawa hasa ni yule ambaye hakuidhulumu nafsi yake kwa kuipeleka kwenye hasira za Mwenyezi Mungu na adhabu wala hakuwa ni katika waliotangulia kwenye heri:
فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ وَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ﴿٣٢﴾
“Kati yao yupo aliyejidhulumu nafsi yake na yupo wa wastani na yupo aliyetangulia katika mambo ya kheri” (35:32).
Makusudio ya mhaini mkuu hapa ni yule anayevunja ahadi ya umbile aliloumbiwa nalo kila mwenye kuzaliwa.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 11(10:22-23) na Juzuu hii tuliyo nayo (29:65-66)
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ وَاخْشَوْا يَوْمًا لَّا يَجْزِي وَالِدٌ عَن وَلَدِهِ وَلَا مَوْلُودٌ هُوَ جَازٍ عَن وَالِدِهِ شَيْئًا إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿٣٣﴾
33. Enyi watu! Mcheni Mola wenu na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwanawe wala mwana hatamfaa mzaziwe kwa lolote. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Basi yasiwadanganye maisha ya dunia wala asiwadanganye na Mwenyezi Mungu mdanganyifu.
إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾
34. Hakika ujuzi wa Saa uko kwa Mwenyezi Mungu na huiteremsha mvua na anavijua vilivyo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho, wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, mwenye habari.
Aya 33 – 34
Enyi watu! Mcheni Mola wenu na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwanawe wala mwana hatamfaa mzaziwe kwa lolote. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Basi yasiwadanganye maisha ya dunia wala asiwadanganye na Mwenyezi Mungu mdanganyifu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameamrisha takua kwa sababu ni njia ya kuokoka na siku ambayo mtu atawakimbia wanawe na mama yake na baba yake. Siku hii itakuja bila ya shaka yoyote. Mwenye kuhadaika ni yule anayeghurika na mambo ya batili na uwongo.
Nilisoma mwandishi mmoja akisema: “Miongoni mwa maswali ambayo hayana majibu ni swali hili: Kwa nini Mungu amemuumba mtu?”
Bila shaka kila mmoja anatamani lau angelijua jawabu la swali hili, kwa sababu linafungamana na kuweko mtu na hakika yake moja kwa moja. Sio siri kwamba mimi nimesoma majibu mengi sana ya swali hili kutoka kwa wataalamu, wanafalsafa na wengineo katika waliopita na wa sasa, lakini sikukinai kabisa; igawaje mimi nilipoulizwa swali hili mara nyingi nilijibu kama walivyojibu, kwa vile sina jibu jingine zaidi ya hayo waliyoyasema.
Nilipoingilia kufasiri Aya za Qur’an yenye hekima, nilisahau swali hili na sikuyahifadhi majibu ya wataalamu. Kwa sababu Tafsir Al-Kashif imeninyang’anya kila kitu; hata kumbukumbu yangu pia. Hakuna kitu isipokuwa busara inayoniongoza kwenye maana ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na malengo yake na mfungamano wake na maisha.
Nilipoendela kidogo tu na tafsiri nilipata jawabu lilio wazi wazi, katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, lisilokubali shaka wala taawili. Si uzushi kwamba Muumba wa kitu ndiye anayejua zaidi analolitaka kwa alichokiumba.
Basi nikapata katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu Aya zinazofahamisha kwa uwazi kuwa mtu ameumbiwa akhera sio dunia ili akaishi maisha yasiyokuwa na tabu wala matatizo yoyote.
Lakini hekima ya Muumba imetaka kuwe na mfungamano baina ya maisha mema ya akhera aliyoumbiwa mtu na kuisadiki imani kwa haki na ikhlasi na kuihami; kama ambavyo hekima yake Mtukufu imetaka kuwa asiyeamini mfungamano huu au akauamini kinadhariya bila ya kuufanyia kazi, kuwa atahisabiwa hisabu nyepesi na ataadhibiwa adhabu chungu.
Kwa sababu yeye hakujua au alijitia kutojua lengo aliloumbiwa na akaiacha njia ya sawa kwa uchaguzi wake mbaya baada ya kuongozwa na Mwenyezi Mungu na kuamrishwa kuifuata.
Kwa maneno mengine ni kuwa, ilivyo hasa maisha ya mtu yanabaki kwa kubakia muumba wake na kwamba Yeye amemuweka kwenye nyumba ya dunia kwa muda tu, mpaka wakati maalum kisha agure kwenye nyumba ya kudumu. Naye amemwamrisha kuzishughulikia nyumba zote mbili pamoja, na afanye ihtiyat ya lile linalowezekana kumtokea katika nyumba ya kwanza na lile litakalotokea katika nyumba ya pili ambalo halina shaka.
Ikiwa atafuata amri na akatii basi atakuwa amejichagulia amani na kufaulu; sawa na msafiri mwenye maandalizi kamili ya safari yake. Na atakyepinga na kuasi basi atakuwa amejichagulia mwisho mbaya; sawa na anayesafiri mji wa mbali ugenini bila ya maandalizi yoyote. Tazama Juz. 20 (28:77).
Hebu sasa tutaje baadhi ya Aya zinazofahamisha kuwa lengo la kumbwa mtu ni maisha ya pili; kama ifuatavyo:
1. Kuna zile zinazoisifia dunia kuwa ni upuuzi, mchezo, starehe zinazodanganya na mahali pa kujifaharisha na kujigamba na kwamba dunia itaondoka na kuisha; na kuisifia akhera kuwa ni nyumba ya Mwenyezi Mungu, ya kheri, ya maisha na kuridhiwa.
Vipi Mwenyezi Mungu (s.w.t) amuumbe mtu na ampe siri, ugunduzi na uwezo wa kuleta maendeleo kuweza kuigeuza historia ya mtu, mbingu na ardhi kwa ajili ya mchezo na starehe zenye ghururi na maisha yanayofanana na ndoto; na hali Yeye amesema: “Hakika tumewatukuza wanaadamu.”?
Juz. 15 (17:70). Hakuna kitu kinachooafikiana na kutukuzwa watu na hekima ya Mungu isipokuwa maisha yatakayobakia kwa kubakia muumbaji wake.
2. Aya zinazofahamisha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamjaribu na kumtahini mtu – pamoja na kuwa anamjua zaidi – ili ifichuke siri yake na hakika yake na vijitokeze vitendo vyake vitakavyomfanya astahiki thawabu au adhabu huko mwisho, akhera. Miongoni mwa Aya hizo ni: “Hakika tumevifanya vilivyo katika ardhi kuwa ni pambo lake ili tumjaribu ni nani kati yao mwenye vitendo vizuri zaidi” Juz. 15 (18:7)
وَمَا كَانَ لَهُ عَلَيْهِم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يُؤْمِنُ بِالْآخِرَةِ مِمَّنْ هُوَ مِنْهَا فِي شَكٍّ ﴿٢١﴾
“Naye – Iblisi – hakuwa na mamlaka juu yao ila ni kwa sababu ya (kuwajaribu) tumjue ni nani mwenye kuamini akhera na ni nani anayetilia shaka” (34:21).
3. Lengo sio kutangaza na kuweka wazi tu bali ni “ili awalipe waliotenda ubaya kwa waliyoyatenda na waliotenda mema awalipe kwa memea” (53:31).
Kwa vile malipo haya hayathibiti duniani, basi lazima kuweko na siku nyingine; vinginevyo itakuwa ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kukuza mambo tu. Mwenyezi Mungu ametakata na wayasemayo wajinga.
4. Aya zinazofahamisha kubakia Peponi kwa mwenye kuamini na kufanya wema na kubaki motoni mwenye kukufuru na kufanya uovu.
Unaweza kuuliza : Utaichukulia vipi kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu inayosema: “Sikuumba majini na watu ila waniabudu” (51:56); ambapo inafahamisha waziwazi kuwa lengo la kuumbwa mtu ni kumwabudu Mwenyezi Mungu katika maisha haya ya dunia na wala sio kupewa maisha bora akhera?
Jibu : Makusudio ya ibada hapa ni kila tendo linalomridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujikurubisha kwake. Hakuna mwenye shaka kwamba kumridhisha Mwenyezi Mungu ni njia pekee ya maisha mema ya kudumu. Kwa hiyo maana yanakuwa, sikuumba majini na watu ila wafanye matendo mema yatakayowasababishia kuishi maisha mema ya milele huko akhera. Kwa maneno mengine ni kuwa Aya hii inarudufu kauli yake Mwenyezi Mungu:
وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ﴿٢٣﴾
“Na Mola wako amepitisha kuwa msimwabudu yoyote ila Yeye tu” Juz. 15 (17:23)
na pia kaulu Yake:
وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ﴿٥﴾
“Na hawakuamrishwa ila wamwabudu Mwenyezi Mungu kwa kumsafia dini” (98:5).
Na natija ya usafi wa dini ni maisha ya kudumu na pepo.
Zaidi ya hayo kuna Aya kadhaa amabazo zimeifunga pepo kwa kutenda matendo mema na ya kheri duniani na kuufunga moto na kufanya shari na ufisadi duniani.
Miongoni mwa Aya hizo ni: “Na aliyekuwa kipofu katika dunia hii, basi Akhera atakuwa kipofu na aliyepotea zaidi njia.” Juz. 15 (17:72).
“Je, mwadhani mtaingia Peponi na hali Mwenyezi Mungu hajawajua wale waliofanya jihadi miongoni mwenu na kuwajua wale waliofanya subira?” Juz. 4 (3:142). Makusudio ya jihadi hapa ni jihadi ya kuihami haki na watu wake na kufa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu na makusudio ya subira ni uthabiti dhidi ya wabatilifu na wapetuka mipaka; na wala sio subira ya kujisalimisha kwenye nguvu ya shari na uovu na kuwa dhalili na ufukara.
Baada ya kutubainikia kuwa lengo la kuumbwa mtu ni maisha yatakayobaki na kwamba kupata neema zake ni mpaka mtu afanye heri na wema hapa duniani; na kupata moto ni mpaka mtu afanye shari na ufisadi, tutakuwa tumejua kwamba tafsiri yoyote ya kuelezea lengo la kuumbwa mtu itakayokwenda kinyume na hakika hii basi hiyo itakuwa mbali na usawa na uhalisi wa mambo.
Inatosha kuwa ni dalili ya yote hayo kauli yake Mwenyezi Mungu: “Je, mnadhani kuwa tuliwaumba bure na kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?” Juz. 18 (23:115).
Yaani lau Mwenyezi Mungu asingelimuumba mtu kwa ajili ya akhera basi ingelikuwa Mwenyezi Mungu, ambaye imetukuka hekima yake, anafanya mambo bure tu.
Hakika ujuzi wa saa uko kwa Mwenyezi Mungu na huiteremsha mvua na anavijua vilivyo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho, wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, mwenye habari.
Unaweza kuuliza : Ujuzi wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) hauna kikomo; kama alivyosema: “Hakifichikani kwake kilicho na uzito wa chembe katika mbingu wala aradhini” (34:3) Na akasema tena “Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye; anajua kilichomo nchi kavu na kilichomo baharini; na halianguki jani ila analijua wala punje katika giza la ardhi; wala kibichi au kikavu, ila kimo katika Kitabu kinachobainisha.” Juz. 7 (6:59).
Imam Ali(a.s) naye anasema:“Hakika Mwenyezi Mungu anajua kudondoka kwa tone na kutulia kwake, kusogea kwa chembe na kupita kwake na chakula kinachomtosha mbu.” Sasa kwanini Mwenyezi Mungu (s.w.t) akahusisha kutaja vitu hivi hapa?
Imesemekana kuwa muulizaji alimuuliza Mtume(s.a.w.w) : kuhusu vitu hivi ndipo ikashuka Aya. Razi anasema: Mwenyezi Mungu (s.w.t) alipotaja saa ya Kiyama alinasibisha kutaja vitu hivi.
Sisi tumesema mara nyingi kuwa Qur’an ni Kitabu cha uongofu kinampeleka mtu kwenye jambo moja hadi jingine. Imam Ja’far Sadiq(a.s) amesema:“Hakika Aya inakuwa mwanzo ni jambo jingine na mwisho wake ni jengine; ni maneno yanayoungana yakinyumbuka kwenye njia mabalimbali…” Kwa vyovyote iwavyo nikuwa Aya imekusanya mambo matano:
1.Hakika ujuzi wa Saa uko kwa Mwenyezi Mungu
“Hakuna wa kuidhihirisha kwa wakati wake ila yeye tu.” Juz. 9 (7:187). Hekima katika hilo ni kuwa watu wawe kwenye hadhari, wakitazamia kutokea wakati wowote.
2.Na huiteremsha mvua.
Wafasiri wengi wamesema kuwa makusudio ya kuteremsha mvua ni kuwa ujuzi wa kushuka kwake unahusika na Mwenyezi Mungu tu peke yake.
Usawa ni kulichukulia neno kuteremsha kama lilivyo; kuwa ujuzi wa kuiteremsha unahusika na Mwenyezi Mungu, kwa vile sababu za kushuka kwake zinakomea kwake.
Hii haimzui mtu kujua wakati wa kushuka mvua kutokana na dalili zake. Hata kama tukichukulia kuwa makusudio ya kujua ni kujua wakati wa kushuka kwake.
Kwa sababu mtu anajua wakati wa kushuka kwake baada ya kujitoikeza dalili na alama zake. Lakini hakuna ajuae kuwa dalili na alama hizo zitatokea lini isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake.
Unaweza kuuliza : Wataalamu wanaweza kushusha mvua ya kutengenezwa, sasa itakuwaje kuwa anahusika nayo Mungu tu?
Jibu : Wataalamu wanageuza mawingu kuwa mvua na Mwenyezi Mungu ndiye aliyetengeneza mawingu kisha anayasukuma kutoka mji mmoja hadi mwingine anavyotaka. Tofauti ni kubwa baina ya kukifanya kitu na kukigeuza.
3.Na anavijua vilivyo ndani ya matumbo ya uzazi.
Unaweza kuuliza : Elimu ya kisasa inajua vilevile inajua aliyemo tumboni, kupitia vipimo kuwa ni mume au ni mke?
Jibu : Kipimo kinajua ambacho kimekwishakuwa, lakini hakijui sifa zake na utashi wa aliyemo tumboni; kama vile uzuri na ubaya, werevu na ujinga n.k. Lakini haya yote kwa Mwenyezi Mungu yanajulikana.
Imam Ali(a.s) anasema:“Mwenyezi Mungu (s.w.t) anajua kilicho katika matumbo ya uzazi kuwa kitakuwa mume au mke, mbaya au mzuri, mkarimu au bakhili, mwema au muovu na ambaye atakuwa kuni kwenye moto wa Jahannam au atakayekuwa Peponi pamoja na mitume.”
4.Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho kwa sababu kila siku ina mambo mengine.
Baada ya kupita siku nyingi imethibitika nadharia ya mwanafalsafa wa kigiriki, Heraclitus aliyesema: “Wewe huwezi kuingia mto mmoja mara mbili.” akiashiria kuwa mambo ya dhahiri ya kilimwengu na ya kijamii hubadilika mara kwa mara kutoka hali moja hadi nyingine. Kwa hiyo elimu haiwezi kujua litakalomtokea mtu baadaye.
5.Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani wala wakati gani pia.
Kwa sababu mauti hayazuiliki, yanamchuka mtoto mchanga na kijana mwenye afya na kumwacha mgonjwa na kikongwe.
19
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
Sura Ya Thelathini Na Mbili: Surat As-Sajda. Ina Aya 30. Mwenye Majmaul-bayan anasema: Imeshuka Makka isipokuwa Aya tatu zimeshuka Madina; kuanzia 18 – 20.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miim.
تَنزِيلُ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾
2. Ni uteremsho wa Kitabu kisicho na shaka ndani yake, kinachotoka kwa Mola wa walimwengu wote.
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ بَلْ هُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أَتَاهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ ﴿٣﴾
3. Au wanasema amekizua? Bali hicho ni haki itokayo kwa Mola wako, ili uwaonye watu wasiofikiwa na mwonyaji kabla yako, huenda wakaongoka.
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ مَا لَكُم مِّن دُونِهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا شَفِيعٍ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ ﴿٤﴾
4. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake katika siku sita. Kisha akatawala kwenye Arshi. Hamna walii wala mwombezi isipokuwa Yeye. Basi je hamkumbuki?
يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ ﴿٥﴾
5. Hulipanga jambo kutoka mbinguni hadi ardhini, kisha linapanda kwake katika siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyohisabu.
ذَٰلِكَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٦﴾
6. Huyo ndiye Mjuzi wa mambo ya ghaibu na ya dhahiri, Mwenye uwezo, Mwenye kurehemu.
الَّذِي أَحْسَنَ كُلَّ شَيْءٍ خَلَقَهُ وَبَدَأَ خَلْقَ الْإِنسَانِ مِن طِينٍ ﴿٧﴾
7. Ambaye ametengenza vizuri umbo la kila kitu. Na akaanzisha umbo la mtu kwa udongo.
ثُمَّ جَعَلَ نَسْلَهُ مِن سُلَالَةٍ مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ ﴿٨﴾
8. Kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji hafifu.
ثُمَّ سَوَّاهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِن رُّوحِهِ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ ﴿٩﴾
9. Kisha akamlinganisha sawa na akampulizia roho yake. Na amewajaalia kusikia na kuona na nyoyo. Ni uchache mnavyoshukuru.
Aya 1 – 9
Alif Laam Miim.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1).
Ni uteremsho wa Kitabu kisicho na shaka ndani yake, kinachotoka kwa Mola wa walimwengu wote.
Ushahidi wa hilo tumeuleza kwenye Aya kadhaa; kama vile Juz. 1 ( 2:23 – 25), Juz. 5 (4:80 – 82) na Juz. 18 (24:55 – 57).
Au wanasema amekizua? Bali hicho ni haki itokayo kwa Mola wako, ili uwaonye watu wasiofikiwa na mwonyaji kabla yako, huenda wakaongoka.
Wapenda anasa wanaojitia kwenye upotevu, katika vigogo wa kikuraishi, walisema: “Qur’an ni utungo wa Muhammad.” Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akasema, kuwarudi, kuwa hapana bali ni wahyi wa Mwenyezi Mungu na Muhammad amewajia na yale ambayo hajawaletea yeyote kabla yake wala hatawaletea yeyote baada yake.
Amewajia na kheri ya dunia na akhera akawakataza dhulma na ufisadi mlio nao, ili mpate mawaidha na muache kabla hayajawafikia majanga. Ilitakiwa mumshukuru Muhammad kwa fadhila hii badala ya kumpangia njama za kiuadui na kumfanya ni mwongo mzushi.
Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake katika siku sita. Kisha akatawala kwenye arshi. Hamna walii wala mwombezi isipokuwa Yeye. Basi je hamkumbuki?
Siku sita ni kinaya cha mikupuo au mara. Makusdio ya Arshi ni utawala. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:54), Juz. 11 (10:3) na Juz. 19 (25:59). Katika Juz. 8 (54:56) tumeeleza kauli zilizosemwa kuhusu siku sita na rai yetu.
Hulipanga jambo kutoka mbinguni hadi ardhini, kisha linapanda kwake katika siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyohisabu.
Makusudio ya kupanga jambo ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameumba ulimwengu, kila kiumbe akakipa sifa kwa namna inavyotaka hekima yake. Akamwajibishia kiumbe ambaye amempa uweza na utambuzi kulazimiana na njia aliyomwongoza.
Makusudio ya ‘kupanda kwake katika siku’ ni kuwa matendo ya viumbe yatakwenda kwake Siku ya Kiyama. Miaka elfu ni kinaya cha kurefuka zama.
Maana ni kuwa viumbe wote wamezungukwa na mipangilio ya Mungu na ulinzi wake. Yeye ndiye aliyewaleta na akawapangilia vizuri: “ambaye amekipa kila kitu umbo lake kisha akakiongoza” Juz. 16 (20:50). Ni Yeye atakayekimaliza na kukirudisha, na matendo yatapelekwa kwake siku ambayo itakuwa ndefu na nzito kwa waasi na wakosefu.
Huyo ndiye Mjuzi wa mambo ya ghaibu na ya dhahiri, Mwenye uwezo Mwenye kurehemu.
Muumba wa kila kitu na msimamizi wa kila kitu. Ni Mjuzi wa ya lililokuwa na litakalokuwa, liwe dogo au kubwa, la dhahiri au la kujificha. Ni Mwenye nguvu kwa uweza wake na ufalme wake na Mwenye huruma kwa viumbe wake na waja wake.
Ambaye ametengenza vizuri umbo la kila kitu.
Kila kiumbe kilichopatikana kwa nidhamu kamili basi ni kizuri na kimepangika, kikifahamisha uwezo wa mtengenezaji na utukufu wake. Hakuna kitu chochote kilichopo ila utaona nidhamu na uwiano unaofahamisha kuweko mjuzi mwenye hekima:
مَّا تَرَىٰ فِي خَلْقِ الرَّحْمَـٰنِ مِن تَفَاوُتٍ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ ﴿٣﴾
“Hutaona tofauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa rehema. Hebu rudisha jicho, je unaona kosa lolote” (67:3).
Na akaanzisha umbo la mtu kwa udongo.
Makusudio ya mtu hapa ni baba wa watu, Adam.
Kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji hafifu ambayo ni manii. Kisha akamlimganisha sawa katika umbile zuri na akampulizia roho yake.
Hiki ni kinaya cha uhai. Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:2) na Juz. 18 (23:12 – 14).
Amewajaalia kusikia na kuona na nyoyo. Ni uchache mnavyoshukuru.
Neema ya ubainifu inatokana na neema ya usikizi uoni na utambuzi. Ama matamanio ya chakula ni kwa ajili ya kuishi na matamanio ya jinsia ni kwa ajli ya kubakia. Hakuna matamanio yoyote kwa mtu isipokuwa yana faida na hekima.
وَقَالُوا أَإِذَا ضَلَلْنَا فِي الْأَرْضِ أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ بَلْ هُم بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ كَافِرُونَ ﴿١٠﴾
10. Na husema: Ati tutakapopotea ardhini, kweli tutakuwa kwenye umbo jipya? Bali wao wanakanusha kukutana na Mola wao.
قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ ﴿١١﴾
11. Sema, atawafisha malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu.
وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الْمُجْرِمُونَ نَاكِسُو رُءُوسِهِمْ عِندَ رَبِّهِمْ رَبَّنَا أَبْصَرْنَا وَسَمِعْنَا فَارْجِعْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا إِنَّا مُوقِنُونَ ﴿١٢﴾
12. Na ungeliwaona wakosefu wanavyoinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao. Mola wetu! Tumeona na tumesikia, turejeshe tutatenda mema, kwani hakika sisi tuna yakini.
وَلَوْ شِئْنَا لَآتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَاهَا وَلَـٰكِنْ حَقَّ الْقَوْلُ مِنِّي لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿١٣﴾
13. Na lau tungelitaka tungeipa kila nafsi muongozo wake. Lakini imehakikika kauli kutoka kwangu: Kwa hakika nitaijaza Jahannam kwa wote majini na watu.
فَذُوقُوا بِمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا إِنَّا نَسِينَاكُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٤﴾
14. Basi onjeni kwa sababu ya kusahau mkutano wa siku yenu hii, hakika sisi tumewasahau. Na onjeni adhabu yenye kudumu kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
Aya 10-14
Na husema: Ati tutakapopotea ardhini, kweli tutakuwa kwenye umbo jipya?”
Hii ni sawa na kauli yao:
أَإِذَا كُنَّا تُرَابًا أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ ﴿٥﴾
“Ati tutakapokuwa mchanga, kweli tutakuwa katika umbo jipya?” Juz.13(13:5)
Bali wao wanakanusha kukutana na Mola wao.
Unaweza kuuliza : Washirikina walitangaza waziwazi kufuru yao ya kukutana na Mwenyezi Mungu waziwazi. Sasa kuna haja gani ya kusema wanakanusha kukutana na Mola wao? Si ni sawa na kumwambia aliyetangaza ukafiri kuwa wewe ni kafiri?
Jibu : makusudio ni kuwa wao hawakuipinga akhera kwa ujuzi, bali ni kwa ujinga na kuiga; sawa na kumwambia aliyetangaza ukafiri: wewe ni mjinga.
Sema, atawafisha malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu.
Yaani, ewe Muhammad! Waambie waliokufuru kuwa nyinyi mtakufa tu, hilo halina shaka. Baada ya mauti hakika itawafunukia na mtajua kuwa bila shaka saa ya Kiyama itakuja na kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua walio katika makaburi.
Na ungeliwaona wakosefu wanavyoinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao.
Walipinga ufufuo na wakawafanyia maskhara waliouamini, waliowapa mwito wake na kuwahadhari na mwisho mbaya. Watapofufuliwa na kusimama mbele ya Mola wao kwa ajili ya hisabu watainamisha vichwa vyao kwa kuona haya na majuto na kusema:
Mola wetu! Tumeona na tumesikia, turejeshe tutatenda mema, kwani hakika sisi tuna yakini.
Umetangulia mfano wake katika Juz.7 (6:27) na Juz. 18 (23:99 – 100).
Na lau tungelitaka tungeipa kila nafsi muongozo wake.
Razi anasema: “ Hii ni wazi kuwa madhehebu yetu yako sahihi pale tunaposema: Mwenyezi Mungu hakutaka imani kutoka kwa kafiri na hakutaka kwake isipokuwa kufuru.”
Nasi tunamwambia Razi: Ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyetaka kufuru kwa kafiri, na hakuna anayerudisha matakwa yake, basi kwa nini atamwadhibu. Vipi na Yeye ndiye aliyesema: “Wala hatukuwadhulumu, bali wao ndio waliokuwa madhalimu” (43:76).
Usahihi ni kuwa makusudio ya matakwa ya Mwenyezi Mungu hapa ni matakwa ya kiuumbaji ambayo ni kusema ‘kuwa.’
Yaani lau Mwenyezi Mungu angelitaka kuwalazimisha uongofu wangeliongoka. Na kama angelifanya hivyo, basi kusingekuwa na thawabu wala adhabu. Hayo tumeyaeleza mara kadhaa. Tazama Juz. 6 (5:49 – 50).
Lakini imehakikika kauli kutoka kwangu: Kwa hakika nitaijaza Jahannam kwa wote majini na watu.
Imehakikika kauli kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba ataijaza Jahannam kwa wafisadi na wale walioasi kwa hiyari na matakwa yao wenyewe. Ama wale ambao walimwitikia Mola wao wana maghufira na malipo makubwa. Kuna Hadith Qudsi inayosema: “Nimeiumba Pepo kwa anayenitii hata kama ni mtumwa Muhabeshi; na moto kwa anayeniasi hata kama ni bwana wa kikuraishi.”
Basi onjeni kwa sababu ya kusahau mkutano wa siku yenu hii, hakika sisi tumewasahau. Na onjeni adhabu yenye kudumu kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
Hakuna yoyote aliyefuata matamanio yake na hawa yake ila atamsahau Mwenyezi Mungu na hisabu na ataikufuru haki na dhamiri. Na kesho malaika wa adhabu watamwambia mkosaji huyu: umelewa utamu wa dunia basi leo onja uchungu wa akhera. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:51) na Juz. 10 (9:67).
إِنَّمَا يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا الَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِهَا خَرُّوا سُجَّدًا وَسَبَّحُوا بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ﴿١٥﴾
15. Hakika wanaoziamni Aya zetu ni wale tu ambao wanapokumbushwa hizo huanguka kusujudu na humsabihi kwa kumsifu Mola wao, nao hawatakabari.
تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿١٦﴾
16. Mbavu zao zinaachana na vitanda kumwomba Mola wao kwa hofu na tumaini, na hutoa katika yale tuliyowaruzuku.
فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٧﴾
17. Nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika yanayofurahisha maisha. Ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda.
أَفَمَن كَانَ مُؤْمِنًا كَمَن كَانَ فَاسِقًا لَّا يَسْتَوُونَ ﴿١٨﴾
18. Je, aliye mumin ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa.
أَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ جَنَّاتُ الْمَأْوَىٰ نُزُلًا بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٩﴾
19. Ama wale ambao wameamini na wakatenda mema watakuwa na bustani za makao. Ndipo pa kufikia kwa waliyokuwa wakiyatenda.
وَأَمَّا الَّذِينَ فَسَقُوا فَمَأْوَاهُمُ النَّارُ كُلَّمَا أَرَادُوا أَن يَخْرُجُوا مِنْهَا أُعِيدُوا فِيهَا وَقِيلَ لَهُمْ ذُوقُوا عَذَابَ النَّارِ الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿٢٠﴾
20. Na ama wale ambao wamefanya ufuska, basi makazi yao ni motoni; kila wakitaka kutoka humo watarudishwa humo humo. Na wataambiwa: Onjeni adhabu ya moto ambayo mlikuwa mkiikadhibisha.
وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنَ الْعَذَابِ الْأَدْنَىٰ دُونَ الْعَذَابِ الْأَكْبَرِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٢١﴾
21. Na kwa hakika tutawaonjesha adhabu hafifu kabla ya adhabu kubwa, labda watarejea.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ ﴿٢٢﴾
22. Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayekumbushwa kwa ishara za Mola wake kisha akazikataa. Hakika sisi ni wenye kuwachukulia kisasi wakosefu.
Aya 15 – 22
Hakika wanaoziamni Aya zetu ni wale tu ambao wanapokumbushwa hizo huanguka kusujudu na humsabihi kwa kumsifu Mola wao.
Makusudio ya waumini hapa ni wale wanaoijua haki na kuitumia na kujitolea muhanga kwa ajaili yake; wanamwabudu Mwenyezi Mungu usiku na mchana kwa kumtegemea Yeye na kumfanyia ikhlasi peke yake, asiyekuwa na mshirika. Ama tasbihi, rukui na sujudi kwa msukumo wa chumo na kibiashara kwa dini, yote hayo ni unafiki sio ibada na ni uzandiki sio imani.
Nao hawatakabari; yaani waumini wanaikaribisha haki na kuacha masilahi yao binafsi kwa ajili ya haki; kwa sabu hiyo ndiyo dini yao na masilahi yao.
Ni wajibu kusujudi kwa mwenye kuisoma Aya hii au kuisikiliza na imesemekana hata mwenye kuisikia pia bila ya kukusudia.
Mbavu zao zinaachana na vitanda kumwomba Mola wao kwa hofu na tumaini.
Vitanda ni kinaya cha usingizi. Tukiunganisha Aya hii na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu.” Juz. 18 (24:37), maana yatakuwa: Hakika waumini haiwashughulishi biashara wala usingizi kuacha ibada ya Mwenyezi Mungu, jambo ambalo linaelezea kuhofia kwao adhabu yake na kutumai kwao thawabu zake.
Ibada hiyo ndiyo aliyoikusudia Mwenyezi Mungu aliposema: “Na usi- mamishe Swala, hakika Swala inakataza machafu na maovu.” Kuna Hadith isemayo: Kisimamo cha mja kinamkurubisha kwa Mwenyezi Mungu, kinamkataza dhambi, kinafuta maovu na kufukuza ugonjwa mwilini.” Ama Swala ya kibiashara huwa inaamrisha uovu na ubaya. Kwa sababu ubaya unaelekeza kwenye mfano wake na vile vile wema.
Na hutoa katika yale tuliyowaruzuku.
Wamemwabudu Mwenyezi Mungu kwa nyoyo, miili na mali.
Nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika yanayofurahisha maisha. Ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda.
Makusudio ya nafsi ni nafsi yoyote, iliyokuwa na itakayokuwa katika ardhi au mbingu. Maana ni kuwa hakuna yeyote anayejua uhakika wa thawabu za kufurahisha ambazo Mwenyezi Mungu amewaandalia waumini, wenye kufanya matendo. Mtume anasema katika Hadith: “Mwenyezi Mungu anasema: “Nimewaandalia waja wangu wema ambayo hakuna jicho liliyaona wala sikio lililoyoyasikia, wala moyo uliyoyawazia.”
Je, aliye mumin ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa.
Tafsri nyingi; ikiwemo Jamiu ya Tabariy, Bahrul-muhit ya Andalusi, Ruhul-bayan ya Haqi, zimesema kuwa Aya hii ilishuka Madina kuhusiana na Ali bin Abi Twalib na Walid bin U’qba bin Abi Mu’it. Tutanukuu yale ya Tabariy: “Kulipita maneno baina ya Walid na Ali. Walid akasema: “Mimi nina ulimi mpana kuliko wewe, nina meno makali kuliko wewe na ninafaa zaidi kwenye jeshi kuliko wewe.” Ali akamwambia, nyamaza wewe ni fasiki, ndipo ikashuka: ‘Je, aliye mumin ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa.
Hapana wallah hawawi sawa duniani wala kwenye mauti na akhera pia.
Ama wale ambao wameamini na wakatenda mema watakuwa na bustani za makao. Ndipo pa kufikia kwa waliyokuwa wakiyatenda.
Hii ni kutofautisha baina ya mumin mwenye takua na kafiri muovu; ni sawa na kutofautisha wema na uovu, heri na shari na Pepo iliyoandaliwa wenye takua na moto ulioandaliwa wakosefu.
Na ama wale ambao wamefanya ufuska, basi makazi yao ni motoni; kila wakitaka kutoka humo watarudishwa humo humo. Na wataambiwa: Onjeni adhabu ya moto ambayo mlikuwa mkiikadhibisha.
Waumini watapata Pepo zenye neema na mafasiki watapata moto unaowaka. Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 (22:22).
Na kwa hakika tutawaonjesha adhabu hafifu kabla ya adhabu kubwa, labda watarejea.
Makusudio ya adhabu hafifu ni adhabu ya duniani; kama vile kahati, balaa n.k. Anawaonya kwayo na kwa nguvu za hoja, wale walioghafilika na wanaojishughulisha na mambo ya batili na kuiacha haki, ili waonyeke na wapate mawaidha.
Vinginevyo watafikiwa na adhabu kubwa: “Moto wa Jahanam hali ya kudumu humo. Ni tosha yao. Na Mwenyezi Mungu amewalaani. Na wana wao adhabu ya kudumu.” Juz. 10 (9:68).
Kwa hakika ilivyo ni kuwa viongozi na watawala ndio chimbuko la kwanza la ufisadi na uovu. Kuna Hadith zinayosema: “Watawala wakiwa waongo huzuiliwa mvua, na mtawala akiwa jeuri dola inakuwa dhalili.”
Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayekumbushwa kwa ishara za Mola wake kisha akazikataa. Hakika sisi ni wenye kuwachukulia kisasi wakosefu.
Mwenye kupata mawaidha kisha asiwaidhike nayo basi huyo ni katika wakosefu wakubwa. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaonya kwa ulimi wa mitume wake na kwa madhara na shida, lakini nyoyo zao zikasusuwaa na wakaendelea na dhulma na ufisadi. Ndio Mwenyezi Mungu akawalipiza kisasi na Yeye ni mwenye nguvu Mwenye kulipiza kisasi.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَلَا تَكُن فِي مِرْيَةٍ مِّن لِّقَائِهِ وَجَعَلْنَاهُ هُدًى لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٢٣﴾
23. Hakika tulimpa Musa Kitabu basi usiwe na shaka ya kukipokea kwake, na tukakifanya ni mwongozo kwa wana wa Israil.
وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ ﴿٢٤﴾
24. Na tukawafanya miongoni mwao maimamu wanaoongoza kwa amri yetu waliposubiri, na wakawa na yakini na ishara zetu.
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿٢٥﴾
25. Hakika Mola wako ndiye atakayefafanua baina yao Siku ya Kiyama katika lile walilohitalifiana.
أَوَلَمْ يَهْدِ لَهُمْ كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّنَ الْقُرُونِ يَمْشُونَ فِي مَسَاكِنِهِمْ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ أَفَلَا يَسْمَعُونَ ﴿٢٦﴾
26. Je, haikuwabainikia, ni vizazi vingapi tuliviangamiza kabla yao nao wanatembea katika maskani zao. Hakika katika hayo kuna ishara, basi je, hawasikii.
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا نَسُوقُ الْمَاءَ إِلَى الْأَرْضِ الْجُرُزِ فَنُخْرِجُ بِهِ زَرْعًا تَأْكُلُ مِنْهُ أَنْعَامُهُمْ وَأَنفُسُهُمْ أَفَلَا يُبْصِرُونَ ﴿٢٧﴾
27. Je, hawaoni kwamba tunayapeleka maji kwenye ardhi kame, kisha kwayo tunaitoa mimea wanayokula wanyama wao. Je, hawapati busara.
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْفَتْحُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٨﴾
28. Na wanasema: Ushindi huu utatokea lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
قُلْ يَوْمَ الْفَتْحِ لَا يَنفَعُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِيمَانُهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٢٩﴾
29. Sema: Siku ya ushindi wale ambao wamekufuru haitafaa imani yao, wala hawatapewa muda.
فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَانتَظِرْ إِنَّهُم مُّنتَظِرُونَ ﴿٣٠﴾
30. Basi achana nao na ungoje; hakika wao wanangoja.
Aya 23 – 30
Hakika tulimpa Musa Kitabu basi usiwe na shaka ya kukipokea kwake, na tukakifanya ni mwongozo kwa wana wa Israil.
Wafasiri wengi wamesema kuwa ‘Kwake’ inarudi kwa Musa; kwa maana ya kuwa Muhammad atakutana na Musa usiku wa Miraji. Ilivyo hasa ni kuwa dhamiri hiyo inarudia kwenye Qur’an; kwa maana ya kuwa, ewe Muhammad! Tumekutermshia Qur’an kama tulivyomteremshia Musa Tawrat. Wala haitakikani kutia shaka katika hilo wewe wala mwingine.
Kuhusu kukatazwa Mtume kutia shaka tumekuelezea mara nyingi. Tazama Juz. 3 (3:59-63).
Na tukawafanya miongoni mwao maimamu wanaoongoza kwa amri yetu waliposubiri, na wakawa na yakini na ishara zetu.
Makusudio ya maimamu hapa ni mitume wa Kiisrail; kama vile Musa, na Isa ambaye nasaba ya upande wa mama yake inafikia kwa Daud. Kila Mtume wa kiisraili alipata aina kwa aina ya adhabu na mateso; bali waisrail waliwaua manabii wao kadhaa:
وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ الْحَقِّ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٦١﴾
“Na wakiwaua Manabii pasipo haki. Basi haya ni kwa sababu ya kuasi kwao na kupituka mipaka.” Juz. 1 (2:61).
Pamoja na yote hayo, waliweza kuvumilia wakawa na subira na wakaendelea kutekeleza risala yao. Kwa hiyo nawe Muhammad vumilia maudhui ya watu wako na uendelee na risala yako.
Hakika Mola wako ndiye atakayefafanua baina yao Siku ya Kiyama katika lile walilohitalifiana.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:113), Juz. 11(10:93) na Juz. 14 (16:124).
Je, haikuwabainikia, ni vizazi vingapi tuliviangamiza kabla yao nao wanatembea katika maskani zao. Hakika katika hayo kuna Ishara, basi je, hawasikii.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20).
Je, hawaoni kwamba tunayapeleka maji kwenye ardhi kame, kisha kwayo tunaitoa mimea wanayokula wanyama wao.
Je, hawapati busara kwa jinsi Mwenyezi Mungu alivyoipa uhai ardhi baada ya kufa kwake na akaotesha humo kila aina za mimea wanayokula watu na wanyama? Kama hivyo atawafufua wafu baada ya kuwa ni mchanga na mifupa
Umetangulia mfano wake katika Aya kadhaa; kama Juz. 17: (22:5).
Na wanasema: ushindi huu utatokea lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
Aya hii ni mfano wa ile isemayo: “Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?” Juz. 17 (21:38). Kwa sababu makusudio ya ushindi hapa ni siku itakayohukumiwa kwa haki. Hilo linatiliwa nguvu na kauli inayofuatia:
Sema: Siku ya ushindi wale ambao wamekufuru, na wakaifanyia inadi haki katika maisha ya dunia,haitafaa imani yao huko akhera wakati watakapoiona adhabu. Kwa sababu imani hiyo itakuwa ni kuukimbia moto sio imani ya kweli na yakini.
Wala hawatapewa muda.
Mwenyezi Mungu hawezi kuwapa muda siku ya Kiyama, kwa sababu ali- wapa muda mrefu duniani, lakini hawakuitumia fursa hiyo.
Basi achana nao na ungoje; hakika wao wanangoja.
Wao wanangoja ufikwe na majanga, basi achana nao na ungoje kidogo tu, utaona hukumu ya Mwenyezi Mungu kwako na kwao. Yeye atakunusuru na atawafedhehsha wao:
هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ ﴿٣٣﴾
“Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na dini ya haki ili ipate kushinda dini zote, ijapokwa washirikina wamechukia.” Juz. 10 (9:33).
20
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
Sura Ya Thelathini Na Tatu: Surat Ahzab. Imeshuka Madina, Ina Aya 73.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ اتَّقِ اللَّـهَ وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١﴾
1. Ewe Nabii! Mche Mwenyezi Mungu wala usiwatii makafiri na wanafiki. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.
وَاتَّبِعْ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٢﴾
2. Na fuata uliyoletewa wahyi kutoka kwa Mola wako. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.
وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٣﴾
3. Na mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutegemewa.
Aya 1-3
Ewe Nabii! Mche Mwenyezi Mungu wala usiwatii makafiri na wanafiki. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima. Na fuata uliyoletewa wahyi kutoka kwa Mola wako. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda. Na mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutegemewa.
Katika Aya hizi Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemwamrisha Nabii wake mtukufu, kuwa na takua, kumtegemea Yeye, kuutumia wahyi wake na kutowatii makafiri na wanafiki.
Wafasiri wamejiuliza kuwa Nabii ni maasumu, sasa kuna haja gani ya amri zote hizi na kukatazwa uasi?
Kuna waliojibu kuwa hii ni kusisitiza utiifu na unyenyekevu alio nao Nabii(s.a.w.w) . Wengine wakasema kuwa Abu Sufyan alimtaka Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kutoyatukana masanamu wanayoyaubudu makauraishi. Abu Sufyani wakati huo alikuwa pamoja na kundi la makafiri na wanafiki.
Sisi huko nyuma tumesema mara kwa mara kuwa aliye juu ana uwezo wa kumwamrisha aliye chini na kumkataza maasi hata kama ni maasumu. Hivi sasa tunayaunganisha hayo na haya yafutayo:
Hakuna kitu kizito kwa yule asiyemuogopa Mwenyezi Mungu kuliko tamko la ‘mche Mungu;’ wala hakuna adui mkubwa kuliko atakayelisema tamko hilo kwake. Imenukuliwa kutoka kutoka kwa Abdul-Malik bin Marwani kwamba yeye alipotawala alisema katika hotuba: “Kuanzia leo, atakayeniambia: mche Mungu, nitamkata shingo yake.”
Ama yule mwenye kuhofia kukutana na Mola wake na akaikanya nafsi na matamanio, basi kwake yeye hilo ni tamko la mapenzi na huruma na hutamani lau angelisikia mara kwa mara; hata kama ni maasumu wa makosa na madhambi; bali huko kulipenda na kulisikilza kumetokana na umaasumu na utiifu wake. Mtu adhimu huwa anajituhumu kwa upunguvu kadiri atakavyoweza kujitahidi.
Kwa hiyo basi hakuna haja ya kuleta taawili na tafsiri nyingine. Kuongezea kuwa amri ya takuwa kwa bwana wa watu na majini ni hekima na somo kubwa kwa wenye vyeo na watawala, kwamba kwa vyovyote watakavyokuwa wakubwa, lakini hawako zaidi ya kuamrishwa uadilifu na takua.
Kwenye Nahjul balagha imeelezwa: “Ambaye itakuwa uzito kwake kuambiwa neno la haki au kuelezwa uadilifu basi itakuwa kuyafanya mawili hayo ni uzito zaidi.”
مَّا جَعَلَ اللَّـهُ لِرَجُلٍ مِّن قَلْبَيْنِ فِي جَوْفِهِ وَمَا جَعَلَ أَزْوَاجَكُمُ اللَّائِي تُظَاهِرُونَ مِنْهُنَّ أُمَّهَاتِكُمْ وَمَا جَعَلَ أَدْعِيَاءَكُمْ أَبْنَاءَكُمْ ذَٰلِكُمْ قَوْلُكُم بِأَفْوَاهِكُمْ وَاللَّـهُ يَقُولُ الْحَقَّ وَهُوَ يَهْدِي السَّبِيلَ ﴿٤﴾
4. Mwenyezi Mungu hakumwekea mwanamume nyoyo mbili ndani yake. Wala hakuwafanya wake zenu – mnaowalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu – kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu. Hiyo ni kauli yenu kwa vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu anasema haki, naye huongoza njia.
ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ فَإِن لَّمْ تَعْلَمُوا آبَاءَهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ وَمَوَالِيكُمْ وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُم بِهِ وَلَـٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥﴾
5. Waiteni kwa baba zao. Hilo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Kama hamuwajui mababa zao basi ni ndugu zenu katika dini na rafiki zenu. Si vibaya kwenu kwa mlivyokosea, lakini kwa yale ziliyoyakusudia nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
MWENYEZI MUNGU HAKUMWEKA MTU MMOJA NYOYO MBILI
Aya 4 – 5
Mwenyezi Mungu hakumwekea mwanamume nyoyo mbili ndani yake.
Hata mwanamke pia ni kama mwanamume. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemuhusu mwanmume hapa kwa sababu amemwamrisha Mtume(s.a.w.w) wake mtukufu kuwa na takua, kwa hiyo ikanasibiana kufuatishia amri hii kuwa mwanamume hawezi kuwa na moyo mmoja wa kumcha Mwenyezi Mungu na mwingine wa kucha watu.
Lengo ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) anabainisha kuwa mtu hawezi kuamini mambo mawili yanayopingana kwa wakati mmoja; kwa mfano aamini dini inayokataza dhulma na uchokozi, Uislamu na Ukiristo, na wakati huo huo ahalalishe dhulma na uchokozi.
Ila ikiwa ana nyoyo mbili na nyuso mbili; kama waamerika ambao wameleta kununi mpya, kwamba mmarekani anaweza kuwa ni mwisrail na kupigana na mwarabu kwa jina la Israil na wakati huo bado ni raia wa Marekani.
Au itabidi tuseme kuwa Israil ni kambi ya jeshi la uchokozi la marekani na kwamba urai wa Israil ni jina tu; hata watawala pia; kwa vile ni kikosi tu cha kulinda masilahi ya ukoloni na unyonyaji.
Mtu mmoja alimwambia Imam Ali(a.s ) : “Mimi nakupenda wewe na ninampenda Muawiya.” Imam akamwambia:“Wewe ni chongo, sasa chagua ama uwe kipofu au upone chongo.”
Unaweza kuuliza : Utasemaje kuhusiana na anayesema; mimi ni mwislamu au mkristo kiitikadi, lakini kisiasa ninafuata siasa za mashariki au magharibi. Je inawezekana kuchanganya mawili haya?
Jibu : Mtu yoyote anayeamini haki kwa ukweli na usafi wa nia, inafaa, bali ni wajibu kumuunga mkono kila kwenye msimamo wa kuinusuru haki na uadilifu; awe ni wa mashariki au magharibi. Wala haijuzu kumuunga mkono tu, hivi hivi, bila ya msingi wowote. Kwa maana hiyo basi haiwezekeni kuchanganya baina ya itikadi ya kiislamu na kuunga mkono tu hivi hivi kwa hali yoyote.
Hii ni katika yanayohusiana na Uislamu. Ama yanayohusiana na itikadi ya kikiristo tunawaachia makasisi walio huru waliotangaza hasira zao kwa baba mtakatifu aliyekataa kukutana nao, lakini wakati huo huo akakutana na viongozi wa kimarekani.
Wakasema katika mateta yao: “Mkutano huu wa Baba mtakatifu na viongozi hawa unaonyesha wazi uhusiano wa nguvu ulioko baina ya kanisa kama tasisi ya dini na siasa za kiuchumi zinazosimamia ukandamizaji na dhulma dhidi ya watu wengi.” Makasisi hawa walitangaza kuwa wangejaribu kuuangamiza uhusiano huu[6] .
Wala hakuwafanya wake zenu – mnaowalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu – kuwa ni mama zenu.
Wakati wa ujahiliya mtu alikuwa akimwacha mkewe kwa kumwambia: Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu (Dhihar). Uislamu ukalikataza hilo, kwa sabau mke hawezi kuwa mama kwa kauli hii, na ukawajibisha kafara kwa atakayesema kauli hiyo, yakipatikana masharti yake, ambayo yatabainishwa mwanzoni mwa Juzuu ya 28. (inshaallah).
Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu.
Wakati wa ujahiliya mtu alikuwa akimchukua mtoto wa mwingine kumfanya mwanawe hasa na kumwingiza kwenye ukoo wake, anakuwa na hukumu ya mtoto wake halisi katika kila kitu na watu wakimwita kwa jina la baba aliyemchukua badala ya baba yake. Ndipo Uislamu ukakataza mtindo huu[7] .
Hiyo ni kauli yenu kwa vinwywa vyenu tu.
Na kauli haibadilishi uhalisi wa mambo.
Na Mwenyezi Mungu anasema haki naye huongoza njia.
Kauli ya haki na njia ya sawa ni kuwa mtoto wa kupanga sio mtoto wa kiuhakika; wala mke hawi ni mama kwa dhihari.
Waiteni kwa baba zao waliowazaa sio waliowapanga.Hilo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. yaani hilo la kuwaita kwa ubini wa baba zao.
Kama hamuwajui mababa zao basi ni ndugu zenu katika dini na rafiki zenu.
Neno rafiki limefasiriwa kutokana na neno mawla, pia lina maana ya huria; mtumwa aliyeachwa huru. Mtu alikuwa anaweza kuitwa huria wa fulani.
Wafsiri na watu wa sera wanasema kuwa Zayd Bin Haritha alitekwa nyara akiwa mdogo. Hakim bin Huzam akamnunua kwa ajili ya kumpatia shangazi yake Khadija Bint Khuwalid. Mtume(s.a.w.w) alipomuoa akapewa zawadi na mkewe. Baada ya kushuka wahyi kwa Nabii, akamlingania kwenye Uisalamu na akasilimu. Akamfanya ndugu na ami yake Hamza bin Abu Twalib.
Haritha, Baba yake Zayd, akaja siku moja kwa Mtume(s.a.w.w) na kumwambia, ama uniuzie mwanangu, au mwache huru. Mtume akamwacha huru na kumwambia nenda upendako. Basi akakataa kuachana na Mtume. Ndipo watu wakawa wanamwita Zayd bin Muhammad mpaka iliposhuka Qur’an kubatilisha hilo.
Si vibaya kwenu kwa mlivyokosea, lakini kwa yale ziliyoyakusudia nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
Anayemwita mtu asiyekuwa baba yake kwa kufikiria kuwa ni baba yake, hana lawama; isipokuwa mwenye dhambi ni yule aliyejua na akakusudia: Mtume(s.a.w.w) anasema: “Umma wangu umeondolewa kukosea na kusahau na yale waliyolazimishwa na wasiyoyajua na wasiyoyaweza na wanayokuwa na dharura nayo,” kwa sharti la kutotokea hayo kwa uzembe na kupuuza.
النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ وَأَزْوَاجُهُ أُمَّهَاتُهُمْ وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّـهِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُهَاجِرِينَ إِلَّا أَن تَفْعَلُوا إِلَىٰ أَوْلِيَائِكُم مَّعْرُوفًا كَانَ ذَٰلِكَ فِي الْكِتَابِ مَسْطُورًا ﴿٦﴾
6. Nabii ni aula kwa waumini kuliko nafsi zao. Na wake zao ni mama zao. Na ndugu wa tumbo ni aula wenyewe kwa wenyewe, katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kuliko waumini wengine na wahajiri. Ila muwe mnafanya wema kwa marafiki zenu. Hayo yamekwishaandikwa kitabuni.
وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿٧﴾
7. Na tulipochukua kwa manabii agano lao na kwako wewe na Nuh na Ibrahim na Isa mwana wa Maryam, na tulichukua kwao agano madhubuti.
لِّيَسْأَلَ الصَّادِقِينَ عَن صِدْقِهِمْ وَأَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿٨﴾
8. Ili awaulize wakweli juu ya ukweli wao. Na amewandaalia makafiri adhabu chungu.
NABII NI AULA KWA WAUMINI KULIKO NAFSI ZAO
Aya 6 – 8
Je, Nabii Ni Hakimu Kwa Amri Yake? Nabii Ni Aula Kwa Waumini Kuliko Nafsi Zao.
Neno aula tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu linalotamkwa hivyo hivyo awla lililonyumbuliwa kutokana na neno wilaya na walii, ambalo maana yake yanatofautiana kulingana na yule anayezungumziwa. Akizungumziwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) basi maana yake ni utawala na nguvu zisizoshindwa na yeyote. Akizungumziwa Nabii(s.a.w.w) inakuwa maana ni utiifu usiopingwa. Haya ndiyo maana yaliyokusudiwa hapa.
Sasa unaweza kuuliza: Si itakuwa maana yake ni kuwa Nabii ni hakimu na mtoa amri tu, mwengine hana uhuru. Tutalinganisha vipi hili na lile la msingi wa uhuru ambao ni haki ya kiasili ya kila mtu?
Jibu : Tutalinganisha uhuru wa mtu na utiifu wa Mwenyezi Mungu. Nabii(s.a.w. w ) anamsemea na kumbainishia Mwenyezi Mungu:
وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾
“Hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni wahyi uliofunuliwa” 53 (3 – 4).
Kuna Hadith sahihi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema:“Haamini mmoja wenu mpaka matamanio yake yafuate yale niliyokuja nayo.” Kwa hiyo kufuata na kutii ni aliyokuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu sio kutoka kwake.
Zaidi ya hayo uhuru ni kushikamana na njia ya usawa, kutumia haki na kubeba majukumu kwa utashi wake, huku akiipigania haki kwa nguvu zake zote. Lakini mwenye kuwa na msukumo wa mapendeleo bila ya kujali hisabu wala mchungaji, huyo ni mtumwa wa matamanio. Mwana falsafa mmoja mashuhuri alisema: “Uhuru sio kujifadhilisha kiundani kunakoruhusu tujifadhilishe sisi kuliko majukumu; isipokuwa ni uwezo wa kujenga mustakabali.”
Na wake zao ni mama zao.
Wake za mitume wana heshima na uharamu wa kuolewa baada yake sawa na mama, lakini kwenye mambo mengine ni watu kando kama wengine.
Na ndugu wa tumbo ni aula wenyewe kwa wenyewe, katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kuliko waumini wengine na wahajiri.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 10 (9:75).
Ila muwe mnafanya wema kwa marafiki zenu
Makusudio ya wema hapa ni wasia, na marafiki wanakuwa ni pamoja na walioachwa huru au ndugu wasiorithi. Maana ni kuwa mirathi ni ya ndugu wa karibu wa maiti, lakini wasia ni wa aliyeusiwa awe wa mbali au wa karibu.
Hayo yamekwishaandikwa kitabuni.
Yaani hukumu imekwishathibiti Kitabuni mbele ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuiasi atakuwa miongoni mwa walioangamia.
Na tulipochukua kwa manabii agano lao na kwako wewe na Nuh na Ibrahim na Isa mwana wa Maryam, na tulichukua kwao ahadi ngumu.
‘Kwako wewe,’ anaambiwa Muhammad(s.a.w. w ) . Makusudio ya agano ni kufikisha (Tabligh) risala ya Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu wake na kuwa na subira na yatakayowapata katika njia yake. Amehusisha kutaja Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad, baada ya kuwataja manabii kwa ujumla kwa vile wao ni bora ya manabii wote, na ametangulizwa Muhammad kwa vile yeye ni mbora wao hao watano.
Katika Juz. 26 (46:35) wameashiriwa mitume Ulul-azmi (wenye ustahamilivu). Sababu ya kuitwa hivyo, kama zilivyopokewa baadhi ya riwaya, ni kuwa kila Nabii baada ya Nuh alikwa akifuata sharia ya Nuh, kisha sharia yake ikafutwa na sharia ya Ibrahim nayo ikafutwa na sharia ya Musa, nayo ikafutwa na Isa, kisha ikafutwa na ya Muhammad (s.a.w.) ambayo haitafutwa hadi Kiyama, kwa vile hakuna Nabii mwingine baada yake.
Na tulichukua kwao agano madhubuti.
Hili ndilo agano la kwanza, na amerudia kulitaja ili alisifu kuwa ni imara na lenye nguvu. Mwenyezi Mungu ameyapa sifa ya maagano madhibuti katika sehemu tatu katika Kitabu chake kitukufu:
Kwanza, ni agano la ndoa aliposema: “Na hali wao wamechukua kwenu agano madhubuti?” Juz. 4 (4:21). Pili ni agano alilochukua na wana wa Israil aliposema: “Na tukachukua kwao agano madhubuti.” Juz. 6 (4:154). Agano la tatu ni hili la Manbii tunalolizungumzia.
Sheikh Mahmud Shaltut, alighafilika kidogo pale aliposema: “Wasifu wa agano madhubuti haukuja katika sehemu yoyote ile katika sehemu zake – yaani Qur’an - isipokuwa katika kufunga ndoa.” Kutokosea ni kwa Mungu.
Ili awaulize wakweli juu ya ukweli wao.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewatuma Manabii na akachukua kwao agano la kufikisha ujumbe ili wakawaulize wakweli, walikusudia nini kwenye ukweli wao. Je, walikusudia radhi ya Mwenyezi Mungu au ni kwa ajili ya kuwaambia watu kuwa wao ni wakweli na mengineyo ya kibinafsi.
Imam Ja’far Sadiq(a.s) anasema: “Mwenyezi Mungu akimuuliza mtu kuhusu ukweli wake ni kwa njia gani aliusema, basi atamlipa kulingana nao, je vipi hali ya muongo?”
Na amewandalia makafiri adhabu chungu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) alipowataja mitume sasa anawataja makafiri kwa mkabala wa kuwataja wema.
21
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَاءَتْكُمْ جُنُودٌ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا وَجُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا ﴿٩﴾
9. Enyi ambao mmeamini! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu; pale yalipowafikia majeshi, tukayapelekea upepo na majeshi msiyoyaona na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda.
إِذْ جَاءُوكُم مِّن فَوْقِكُمْ وَمِنْ أَسْفَلَ مِنكُمْ وَإِذْ زَاغَتِ الْأَبْصَارُ وَبَلَغَتِ الْقُلُوبُ الْحَنَاجِرَ وَتَظُنُّونَ بِاللَّـهِ الظُّنُونَا ﴿١٠﴾
10. Walipowajia kutoka juu yenu na kutoka chini yenu; na macho yakakodoka na nyoyo zikapanda kooni. na mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali.
هُنَالِكَ ابْتُلِيَ الْمُؤْمِنُونَ وَزُلْزِلُوا زِلْزَالًا شَدِيدًا ﴿١١﴾
11. Hapo waumini walijaribiwa na wakatikiswa mtikiso mkali.
وَإِذْ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ مَّا وَعَدَنَا اللَّـهُ وَرَسُولُهُ إِلَّا غُرُورًا ﴿١٢﴾
12. Na waliposema wanafiki na wale ambao wana maradhi katika nyoyo zao, Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakutuahidi ila udanganyifu.
وَإِذْ قَالَت طَّائِفَةٌ مِّنْهُمْ يَا أَهْلَ يَثْرِبَ لَا مُقَامَ لَكُمْ فَارْجِعُوا وَيَسْتَأْذِنُ فَرِيقٌ مِّنْهُمُ النَّبِيَّ يَقُولُونَ إِنَّ بُيُوتَنَا عَوْرَةٌ وَمَا هِيَ بِعَوْرَةٍ إِن يُرِيدُونَ إِلَّا فِرَارًا ﴿١٣﴾
13. Na kundi moja miongoni mwao liliposema: Hapana pa kukaa nyinyi leo, basi rudini. Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Mtume wakisema: Hakika nyumba zetu ni tupu. Wala hazikuwa ni tupu; hawakutaka ila kukimbia tu.
وَلَوْ دُخِلَتْ عَلَيْهِم مِّنْ أَقْطَارِهَا ثُمَّ سُئِلُوا الْفِتْنَةَ لَآتَوْهَا وَمَا تَلَبَّثُوا بِهَا إِلَّا يَسِيرًا ﴿١٤﴾
14. Na lau wangeingiliwa kwa pande zake, kisha wakatakiwa fitna, wangelifanya, na wasingelisita isipokuwa kidogo tu.
وَلَقَدْ كَانُوا عَاهَدُوا اللَّـهَ مِن قَبْلُ لَا يُوَلُّونَ الْأَدْبَارَ وَكَانَ عَهْدُ اللَّـهِ مَسْئُولًا ﴿١٥﴾
15. Na kwa hakika walikuwa wamemwahidi Mwenyezi Mungu kabla kwamba hawatageuza migongo. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa.
Aya 9 – 15
Aya hizi tulizo nazo na zinazofuatia hadi 27, zilishuka kuhusu vita vya Ahzab (makundi), ambavyo pia vinaitwa vita vya Khandaq (handaki).
Kwa ufupi ni kuwa kikundi katika viongozi wa kiyahudi waliwahimiza makuraishi na makabila mengine ya waarabu kupigana na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Walitoa mali nyingi sana na wakaweza kuunda jeshi ambalo halikuwahi kutokea katika bara Arabu. Basi jeshi, likiongozwa na Abu Sufyan, likaelekea Madina.
Mtume(s.a.w.w) , alipojua makusudio yao, aliaamrisha lichimbwe shimo kwa ushauri kutoka kwa Salman Al-Farisi. Mtume(s.a.w.w) akafanya kazi kwa mkono wake, na waislamu wengine wenye ikhlasi pia wakafanya kazi. Salmani alikuwa akiwatia hamasa kwa kuwasimulia ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa wanaofanya matendo na wapiganaji jihadi. Wanafiki walikuwa wakijaribu kuivunja azma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na wakiponyoka bila ya Mtume kujua.
Lakini handaki lilikamilika, na vikosi vya majeshi vikaanza kuja kwa maelfu. Waislamu walipowaona, wengi wakajawa na hofu na wakaona wamefikwa na balaa, wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana nyingi. Fazaa yao ilizidi pale Bani Quraydh, kabila la kiyahudi waliokuwa wakikaa na Mtume(s.a.w.w) Madina wakiwa na ahadi ya kutosaidia adui, na kuendelea na ahadi yao hiyo, lakini lilipokuja jeshi la Ahzab wakavunja ahadi na kutangaza vita katika wakati mgumu sana kwa waislamu.
Hivi ndivyo walivyo Mayahudi kila wakati na kila mahali. Wanajidhalilisha kama mbwa, wakiwa hawana nafasi, lakini mara tu wanapoipata wanaanza kuuma. Mtume(s.a.w.w) alimtuma Sa’d Bin Muadh na maswahaba wengine kujaribu kuwaambia Bani Quraydha wasivunje ahadi, lakini wakang’angania kuivunja. Basi Waislamu wakawa wamezungukwa na adui wa nje na wa ndani. Juu kuna adui na chini kuna adui.
Katika kitabu Fiqhu ssira cha Sheikh Ghazali, anasema: “Amru bin Wud, Ikrima bin Abu Jahl na Dhirar bin Al-Khattwab walipitapita wakaona sehemu finyu kwenye handaki, Wakawarusha farasi wao na wakajitoma. Waislamu wakahisi hatari sana. Wapanda farasi wakiongozwa na Ali bin Abu Twalib, wakenda haraka kuziba mwanya.
Ali akamwambia Amru bin Wud, Shujaa mkubwa, mwenye uzoefu: ‘Ewe Amru! Ulimwahidi Mwenyezi Mungu kuwa mwanamume yote wa kikuraishi hatakupa mwito wa mojawapo ya mambo mawili ila utauchukua.” Akasema: “Ndio.” Ali akamwambia: “Ninakupa mwito uje kwa Mwenyezi Mungu kwenye Uislamu.” Akasema: “Sina haja.” Ali akasema. “Ninakuita kwenye mapambano.” Akasema: “Kwa nini ewe mwana wa ndugu yangu. Wallah mimi sipendi kukuua-alisema hivi kwa kumdharau - Ali akamwambia wallahi mimi ninapenda kukuua.
Basi Amru akakasirika, akaruka kutoka kwenye farasi wake, na akapiga uso wake; kisha akamkabili Ali wakaanza kupambana; Ali akamuua. Wakatoka wapanda farasi wa washirikina wakiwa wameshindwa hawana lolote.”
Jeshi la washirikina lilipoona halina mahali pa kuvuka handaki wakaanza kurusha mishale yao kwa waislamu. Mshale mmoja ukampata Sa’ad Bin Mua’dh na ukamjeruhi sana kwenye mboni ya jicho. Mtume(s.a.w.w) akaamuru apelekwe kwa mwanamke anayeitwa Rafida, aliyekuwa akiwatibu majeruhi wa kiislamu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Sa’ad alipoona jeraha lake linaweza kumuua, aliomba dua kwa kusema: “Ewe Mola wangu, Ikiwa bado umebakisha vita na Makuraishi basi nibakishe, kwani hakuna watu ninaopenda kuwapiga jihadi kuliko hawa waliomuudhi Mtume, wakamkadhibisha na kumfukuza. Na ikiwa vita umevimaliza baina yetu na wao basi nibakishe wala usiniue mpaka jicho langu litulie kwa Bani Quraydha.”
Basi Mwenyezi Mungu akamwitikia dua yake akamfanya ni hakimu kwa Bani Quraydha, akawauwa wanume wao na akateka wake zao. Ufafanuzi utakuja kwenye Aya 26 inshallah.
Waislamu wakaendelea kuzingirwa kwa kiasi cha siku ishirini; hakuna kitu isipokuwa kutupiana mishale na mawe. Mara ukaja upepo mkali uliopondaponda kambi ya Ahzab, ukaizua mahema yao, na kila kitu kikaharibika, wakarudi wamedhalilika wakiongozwa na Abu Sufyan.
Mwenyezi Mungu akampa nguvu Mtume wake kwa ushindi; akawa anasema: Lailaha ill- lallha, wahdahu, swadaqa wa’dahu wanaswara abdahu, wa a’zza jundahu wahazama l-a’hzaba wahadau, fala shay-unba’dah” (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, amesma kweli kiaga chake na akamusuru mja wake na akawatia nguvu askari wake na akavishinda makundi akiwa peke yake, basi hakuna kitu baada yake).
Wapokezi wameafikiana kuwa vita hivi vilikuwa mwaka wa tano wa Hijra na wakatofautiana katika mwezi. Kuna waliosema ni Dhul qaada (mfunguo pili) na waliosema ni Shawwal (mfunguo mosi). Kwa ujumla hivyo ndivyo vilivyokuwa vita vya Ahzab (makundi). Ufafanuzi wake ni kama ufuatavyo katika ufafanuzi wa Aya:
Enyi ambao mmeamini! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu; pale yalipowafikia majeshi, tukayapelekea upepo.
Kumbukeni enyi waumini mliokuwa pamoja na Mtume(s.a.w.w) katika vita vya Khandaq, mkizungukwa na maadui kila upande. Kumbukeni hilo na mshukuru neema ya Mwenyezi Mungu kwa kuwa na ikhlasi na subira, pale alipowapelekea madui zenu upepo mkalina majeshi msiyoyaona na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda.
Wafasiri wanasema walikuwa ni malaika. Inawezekana kuwa ni kinaya cha khofu na utishio alioutia Mwenyezi Mungu kwenye nyoyo za majeshi ya Ahzab.
Katika Bahrul-muhit ya Abu Hayan Al-Andalusi imeelezwa kuwa jeshi la wa Ahzab lilikuwa na watu 15,000 na waislamu walikuwa 3000.
Wafasiri na watu wa sera wameafikiana kwamba ulitokea mwamba ndani ya handaki wakati wa kuchimba, ukavunja vyuma na kukawa na uzito. Mtume(s.a.w.w) akachukua sururu kutoka kwa Salman akaupiga mwamba ukatoa cheche, akapiga mara ya pili ukatoa cheche na mara ya tatu pia ukatoa cheche. Mtume(s.a.w.w) akasema:“Kwenye cheche za kwanza nimeona Madain mji wa mfalme Kisra, mara ya pili nikaona kasri ya Kaizari na mara ya tatu nikaona kasri ya Sanaa. Na Jibril amenipa habari kuwa umma wangu utaingia kote huko, basi furahini.”
Yote aliyoyasema, Bwana wa majini na watu, yalitokea.
Walipowajia kutoka juu yenu na kutoka chini yenu.
Yaani jeshi la Ahzab liliwazingira waislamu bila kuwapa mwanya wowote. Kundi la wafasiri wamesema kuwa walikuja Ghatafan, Banu Quraydha na Banun Nadhir katika Mayahudi kutoka upande wa mashariki, wakaja Makuraishi, Banu Kinana na watu Tihama kutoka upande wa magharibi.
Na macho yakakodoka na nyoyo zikapanda kooni.
Hiki ni kinaya cha hofu kubwa na fazaa.
Na mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali.
Baadhi ya walioamini walidhani kuwa Mwenyezi Mungu hatainusuru dini yake na Mtume wake. Baadhi ya wanafiki wakasema Muhammad anatuahidi hazina za Kaizari na leo mtu hawezi hata kwenda chooni.
Hapana mwenye shaka kuwa daima kuna udhuru kwa wanafiki. Lakini mwenye kuamini kisha akajiuliza huku akikereka: Kwa nini Mwenyezi Mungu asiwadidimize madhalimu ardhini au awateremshie kimondo kutoka mbinguni, huyu hatumshangai kuwa yeye ni mwenye kusamehewa kwa Mungu, maadamu anamwamini kwenye moyo wake.
Hapo waumini walijaribiwa na wakatikiswa mtikiso mkali.
Uhakika wa nafsi ulivyo haujitokezi ila wakati wa shida na mtihani wa mambo ya kuhofisha na ya kuchukiza. Vita vya Khandaq vilikuwa ni mtihani mkubwa sana kwa waumini na wanafiki; ambapo hakika ya kila mmoja ilijitokezawaliposema wanafiki walioficha unafiki na kudhihirisha imanina wale ambao wana maradhi katika nyoyo zao . Hawa ni wale wenye imani dhaifu waliowaamini wanafiki bila ya kufikiria. Hawa na wale wakasema:
Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakutuahidi ila udanganyifu.
Hao hawamwamini Mwenyezi Mungu wala Mtume wake. Kwa sababu mumin hawezi kusema maneno haya ya kufuru. Waliyasema haya ili kuwatia shaka wapumbavu na wenye akili dhaifu.
Na kundi moja miongoni mwao liliposema: Hapana pa kukaa nyinyi leo, basi rudini.
Mtume(s.a.w.w) na maswahaba walipoanza kuchimba handaki, kundi moja la wanafiki likasema: “Handaki litafaa nini na vita hivi, halifai lolote hilo.” Walisema hivi kabla ya kufika majeshi. Yalipokuja majeshi wakasema: “Hamuliwezi jeshi hili kubwa wala hamponi isipokuwa kukimbia na kujisalimisha.”
Wakati nikifafanua Aya hizi nimekumbuka vibaraka wa wazayuni na wa wakoloni wanavyoeneza hofu na fazaa kutoka kwa waisrail. Nimekumbuka hivyo kwa kujua kuna wanaofanana nao katika zama zilizopita na kwamba vita vya maneno vilianza zamani; wala havikuanza na uzayuni na ukoloni; lakini la umuhimu ni kuwa hahadaiki nayo isipokuwa mwenye akili finyu na asiyekuwa na mtazamo wa mbali [8] .1
Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Mtume wakisema: Hakika nyumba zetu ni tupu.
Wanafiki walikuwa wakitafuta vijisababu vya kukimbia kambi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kwa kusema kuwa wataibiwa kwa vile nyumba zao hazina watu, lakini Mwenyezi Mungu akafichua uwongo na unafiki wao kwa kusema:wala hazikuwa ni tupu. Hawakutaka ila kukimbia tu kutoka kwenye jihadi na kuinusuru haki.
Na lau wangeingiliwa kwa pande zake, kisha wakatakiwa fitna, wan- gelifanya, na wasingelisita isipokuwa kidogo tu.
Makusudio ya fitna hapa ni kurtadi. Yaani lau jeshi la washirikina lingeingia Madina na likauzingira mji kila upande, na washirikina wawambie wanafiki wartadi na kutangaza shirk, basi wangeliitika haraka sana bila ya kusita au wangelisita kidogo tu.
Ilivyo ni kuwa mumin wa kweli hawezi kurtadi itikadi yake, bali anaipigania akiwa anajua kuwa mwema ni yule anayeigombania dini, vyovyote itakavyokuwa; kama walivyo mashahidi, hawaogopi silaha za wauaji.
Na kwa hakika walikuwa wamemwahidi Mwenyezi Mungu kabla kwamba hawatageuza migongo.
Walitumia uongo kukwepa jeshi la Mtume baada ya kutoa ahadi kwamba watashiriki hadi mauti. Katika Tafisir Tabariy imesemwa: “Bani Haritha na Bani Salama, walidhamiria waislamu washindwe siku ya Uhud; kisha wakamwahidi Mwenyezi Mungu kuwa hawatarudia milele; ndipo Mwenyezi Mungu akawakumbusha ahadi hii waliyoitoa wenyewe.” Tazama Juz. 4 (3:122).
Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa siku ya Kiyama kuhusu utekelezwaji wake,
فَمَن نَّكَثَ فَإِنَّمَا يَنكُثُ عَلَىٰ نَفْسِهِ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّـهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٠﴾
“Basi mwenye kuvunja ahadi kwa hakika anaivunjia nafsi yake tu, na anayetekeleza aliyomwahidi Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa.” (48:10).
قُل لَّن يَنفَعَكُمُ الْفِرَارُ إِن فَرَرْتُم مِّنَ الْمَوْتِ أَوِ الْقَتْلِ وَإِذًا لَّا تُمَتَّعُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٦﴾
16. Sema: Hakutawafaa kukimbia; ikiwa mnakimbia kifo au kuuawa. Na hata hivyo hamtastareheshwa isipokuwa kidogo tu.
قُلْ مَن ذَا الَّذِي يَعْصِمُكُم مِّنَ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَ بِكُمْ سُوءًا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ رَحْمَةً وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٧﴾
17. Sema, ni nani atakayewalinda na Mwenyezi Mungu akiwatakia uovu au akiwatakia rehema? Wala hawatapata mlinzi wala msaidizi asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
قَدْ يَعْلَمُ اللَّـهُ الْمُعَوِّقِينَ مِنكُمْ وَالْقَائِلِينَ لِإِخْوَانِهِمْ هَلُمَّ إِلَيْنَا وَلَا يَأْتُونَ الْبَأْسَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٨﴾
18. Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawajua miongoni mwenu wanaozuilia na wanaowaambia ndugu zao: Njooni kwetu! Wala hawaingii vitani ila kidogo tu.
أَشِحَّةً عَلَيْكُمْ فَإِذَا جَاءَ الْخَوْفُ رَأَيْتَهُمْ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ تَدُورُ أَعْيُنُهُمْ كَالَّذِي يُغْشَىٰ عَلَيْهِ مِنَ الْمَوْتِ فَإِذَا ذَهَبَ الْخَوْفُ سَلَقُوكُم بِأَلْسِنَةٍ حِدَادٍ أَشِحَّةً عَلَى الْخَيْرِ أُولَـٰئِكَ لَمْ يُؤْمِنُوا فَأَحْبَطَ اللَّـهُ أَعْمَالَهُمْ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿١٩﴾
19. Wana choyo juu yenu. Ikija hofu utawaona wanakutazama na macho yao yanazunguka kama ambaye amezimia kwa mauti, lakini hofu inapoondoka wanawaudhi kwa ndimi kali, na wanaifanyia choyo kheri. Hao hawakuamini, basi Mwenyezi Mungu amezipomosha amali zao. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.
يَحْسَبُونَ الْأَحْزَابَ لَمْ يَذْهَبُوا وَإِن يَأْتِ الْأَحْزَابُ يَوَدُّوا لَوْ أَنَّهُم بَادُونَ فِي الْأَعْرَابِ يَسْأَلُونَ عَنْ أَنبَائِكُمْ وَلَوْ كَانُوا فِيكُم مَّا قَاتَلُوا إِلَّا قَلِيلًا ﴿٢٠﴾
20. Wanadhani yale makundi hayajaondoka. Wanatamani wangelikuwa jangwani pamoja na mabedui wakiuliza habari zenu. Na lau wangelikuwa pamoja nanyi wasingelipigana isipokuwa kidogo tu.
Aya 16 – 20
Sema: Hakutawafaa kukimbia; ikiwa mnakimbia kifo au kuuawa.
Walikimbia jihadi kwa kuhofia mauti, na mtu hawezi kuepuka kifo kwa kukimbia, wala mwenye kukipenda pia hawezi kubakia.
Na hata hivyo hamtastareheshwa isipokuwa kidogo tu.
Ikiwa mtasalimika kifo kwenye uwanja wa vita, basi mtakutana nacho baada ya muda mchache tu, kisha muingie motoni. Lakini mashahidi watakwenda kwenye Pepo yenye neema. Imam Ali(a.s) anasema:“Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, mapigo elfu moja ya panga kwangu ni mepesi zaidi kuliko kufa kitandani.”
Sema, ni nani atakayewalinda na Mwenyezi Mungu akiwatakia uovu au akiwatakia rehema? Wala hawatapata mlinzi wala msaidizi asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
Tutaifasiri na kauli yake nyingine Mwenyezi Mungu: “Sema ni nani awezaye kuwasaidia chochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka kuwadhuru au akitaka kuwanufaisha?” (48:11). Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:11).
Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawajua miongoni mwenu wanaozuilia na wanaowaambia ndugu zao: Njooni kwetu! Wala hawaingii vitani ila kidogo tu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawajua wanafiki na kwamba wao wanawazuia watu wasiende vitani na kuwaambia: Kuna haja gani ya vita njooni tule raha. Wanapofichuka basi wanakwenda vitani kwa kujisukuma, kama vile wanapelekwa machinjioni, wanapigana kidogo kidogo na kuwa wazito. Watu wa aina hii wanapatikana kila wakati.
Wana choyo juu yenu kwa mali na ushindi, ubakhili wote Mwenyezi Mungu anausamehe; isipokuwa ubakhili wa jihadi na mali.
Ikija hofu utawaona wanakutizama na macho yao yanazunguka kama ambaye amezimia kwa mauti, lakini hofu inapoondoka wanawaudhi kwa ndimi kali.
Aya hii inaelezea woga wa wanafiki na udhaifu wao kwenye kifo. Wana jeuri ya ya dhambi wakiwa salama, lakini ukianguka mshindo macho yao yanazunguka kwa fazaa na woga, wakishasalimika ndimi zao zinaanza kuwauma waumini wanaopigana jihadi.
Katika Nahjul-balagha kuna maelezo haya:“Hakika mnafiki anazungumza yanayomjia kwenye ulimi wake: hajui anayostahiki na yaliyo wajibu kwake.” Mtume naye anasema:“Haiwi sawa imani ya mja mpaka uwe sawa moyo wake, wala hauwi sawa moyo wake mpaka uwe sawa ulimi wake.”
Na wanaifanyia choyo kheri.
Makusudio ya kheri hapa ni ngawira. Yaani wao wakati wa vita ni waoga, lakini wakati wa kugawanya ngawira wanapandisha sauti kwa kuhoji na kwamba wao wana haki zaidi kuliko wote. Hao hawakuamini; bali walidhihirisha imani wakaficha kufuru, wakapi- gana pamoja nanyi kwa unafiki na riya.
Basi Mwenyezi Mungu amezipomosha amali zao.
Yaani amebatilisha kupigana kwao kwa sababu kulikuwa ni kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
Kuna Hadith inayosema: “Yeyote ambaye kuhama (kuhajiri) kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi kuhama kwake ni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na ambaye kuhama kwake ni ili aipate dunia au mwanamke wa kumuoa, basi kuhama kwake ni kwa lile alilolihamia.”
Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.
Hilo la kupomosha kupigana kwao. Ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa sababu Yeye si dhalimu.
Wanadhani yale makundi hayajaondoka.
Makundi yaliondoka bila ya kurejea, lakini wanafiki hawamini macho yao; si kwa lolote ila ni kwa kuwa wanatamani lau makundi yale yangelimfyeka Mtume na sahaba zake. Matamanio yao haya yakawapa picha kuwa makundi yale bado yako yameuzingira mji wa Madina na kwamba watawamaliza Waislamu kesho au keshokutwa.
Wanatamani wangelikuwa jangwani pamoja na mabedui wakiuliza habari zenu.
Wanafiki wakihakikisha kuwa makundi yameshindwa; kisha yarudi tena mara ya pili Madina, basi watatamani wanafiki lau wangelikuwa mbali na Madina wakikaa jangwani wawe wakiuliza tu yaliyowapata waislamu.
Na lau wangelikuwa pamoja nanyi wasingelipigana isipokuwa kidogo tu.
Huu ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyotangulia ‘Wala hawaingii vitani ila kidogo tu.’
22
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا ﴿٢١﴾
21. Hakika nyinyi mna ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu – kwa mwenye kumtarajia Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi.
وَلَمَّا رَأَى الْمُؤْمِنُونَ الْأَحْزَابَ قَالُوا هَـٰذَا مَا وَعَدَنَا اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَصَدَقَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا ﴿٢٢﴾
22. Na waumini walipoyaona makundi walisema: Haya ndiyo aliyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hayo hayakuwazidishia ila imani na utii.
مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّـهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا ﴿٢٣﴾
23. Miongoni mwa waumini wapo wanaume waliotimiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea; wala hawakubadilisha ahadi yao hata kidogo.
لِّيَجْزِيَ اللَّـهُ الصَّادِقِينَ بِصِدْقِهِمْ وَيُعَذِّبَ الْمُنَافِقِينَ إِن شَاءَ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٢٤﴾
24. Ili Mwenyezi Mungu awalipe wakweli kwa ukweli wao na awaadhibu wanafiki, akipenda, au apokee toba yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
وَرَدَّ اللَّـهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا وَكَفَى اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ وَكَانَ اللَّـهُ قَوِيًّا عَزِيزًا ﴿٢٥﴾
25. Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha wale ambao wamekufuru na ghadhabu yao; hawakupata kheri yoyote. Na Mwenyezi Mungu amewakifia waumini, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye uwezo.
وَأَنزَلَ الَّذِينَ ظَاهَرُوهُم مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِن صَيَاصِيهِمْ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ فَرِيقًا تَقْتُلُونَ وَتَأْسِرُونَ فَرِيقًا ﴿٢٦﴾
26. Na akawateremsha wale waliowasaidia katika watu wa Kitabu kutoka katika ngome zao; na akatia hofu katika nyoyo zao. Badhi yao mkawa mnawaua na wengine mnawateka.
وَأَوْرَثَكُمْ أَرْضَهُمْ وَدِيَارَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ وَأَرْضًا لَّمْ تَطَئُوهَا وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرًا ﴿٢٧﴾
27. Na akawarithisha ardhi yao na majumba yao na mali zao na ardhi ambayo hamjaikanyaga. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.
Aya 21 – 27
Hakika nyinyi mna ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu – kwa mwenye kumtarajia Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi.
Makusudio ya ruwaza hapa ni mfano wa kuigwa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , na kumtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho ni kutaraji thawabu za Mwenyezi Mungu na neema za akhera; na kumkumbuka kwa wingi ni kinaya cha kuswali Swala tano.
Maneno ‘Hakika nyinyi’ yanaelekezwa kwa wale waliomwacha Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) katika vita vya Ahzab. Makusudio ni kuwatahayariza na kuwalalumu, kwa vile walimwacha Mtume wakati mgumu; wakiwa wao wanadai ni waislamu na kuswali na pia kudai wanamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.
Maana ya Aya hii ni kama ile isemayo: “Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio kandoni mwao kubaki nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu; wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake.” Juz. 11 (9:120).
Aya hii iaashiria kuwa mwislamu wa kweli hasa ni yule anayemfuata na kumwiga Mtume wake bila ya kumwasi na jambo lolote.
Unaweza kuuliza : mafakihi wameafikiana kuwa mwenye kusema: Lailaha illallah, Muhadur-rasulullah (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu) atatendewa wanayotendewa waislamu, awe mtiifu au mwasi, sasa itakuwaje?
Jibu : Ndio atatendewa muamala wa kiislamu katika maisha haya ya dunia; kama vile kuozwa, urithi n.k. Lakini muamala katika maisha haya ni jambo jingine na kuzingatiwa kuwa yeye ni mwislamu mbele ya Mwenyezi Mungu ni jambo jingine.
Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa waislamu wanagawanyika mafungu mawili: Kuna mwislamu mbele za watu, lakini sio mbele ya Mwenyezi Mungu; naye ni yule aliyesema: Lailaha illallah, Muhadur-rasulullah (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu) na huku anamwasi Mwenyezi Mungu na Mtume. Huyu atafanyiwa muamala wa Mwislamu duniani tu.
Mwingine ni yule aliyesema Lailaha illallah, Muhadur-rasulullah (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu) na akamtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Huyu atafanyiwa muamala wa Mwislamu duniani na akhera. Imam Ali (a.s.) anasema: “Ufukara na utajiri ni baada ya kuonekana kwa Mungu (Siku ya Kiyama).”
Na waumini walipoyaona makundi walisema: Haya ndiyo aliyotuahi- di Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hayo hayakuwazidishia ila imani na utii.
Wafsiri wa zamani wametaja kauli mbili kuhusiana na Aya hii. Ilio na nguvu zaidi ni ile isemayo kuwa Mtume alikuwa amewaahidi waislamu kupatwa na misukosuko aina kwa aina na kwamba makafiri na washirikina watajitokeza kuwapiga vita na kutaka kuwafyeka kabisa.
Ahadi hii imeelezwa katika Aya ismayo: “Au mnadhani kuwa mtaingia Peponi na hali hamjajiwa na mfano wa wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara” Juz. 2 (2:214).
Waislamu walipoona makundi ya majeshi yakiwazingira kila upande, walisema haya ndiyo aliyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hali hiyo ikawazidishia imani na utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake wakazidi imani juu ya imani. Ama wanafiki na wale walio na maradhi nyoyoni mwao walisema: ‘Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakutuahidi ila udanganyifu.’
Miongoni mwa waumini wapo wanaume waliotimiza waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu katika jihadi na uthabiti wakati wa kukutana na adui, mpaka wakati wa kufa.
Baadhi yao wamekwisha kufa kabla ya vita vya Ahzab; kama mashahidi wa vita vya Badrina baadhi wanangojea kufa shahid au ushindi;wala hawakubadilisha ahadi yao hata kidogo. Vile vile wanafiki na wenye maradhi nyoyoni, hawakubadilika; bali walikufa na unafiki.
Wafasiri wanasema kuwa Anas bin Annadhr hakuwepo kwenye vita vya Badr; akasikitika na akasema: sikuwepo kwa mashuhudio ya kwanza alioshuhudia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , lakini kama Mwenyezi Mungu Mtukufu bado ataniononyesha mashuhudio mengine pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , basi ataona nitakavyofanya.
Basi akawako kwenye vita vya Uhud. Akakutana na Sa’d bin Mua’dh, aka- muliza: “Mpaka wapi ewe Abu Amru?” Akajibu: “Nakimbila harufu ya Pepo. Wallah mimi ninaisikia Uhud.” Basi akapigana mpaka akauwawa. Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe kwake. Kwenye kiwiliwili chake kitukufu kulipatikana majeraha ya panga, mikuki na mishale karibu thamanini.
Ili Mwenyezi Mungu awalipe wakweli kwa ukweli wao na awaadhibu wanafiki, akipenda, au apokee toba yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
Pia ni Mwadilifu na Mwenye hekima; hafanyi upuzi wala mchezo katika matakwa yake na vitendo vyake. Humpa thawabu anayestahiki; kama vile wakweli na wenye imani, ikiwa wataendelea na ukweli wao na imani yao. Na atawaadhibu makafiri na wanafiki, ikiwa watang’ang’ania ukafiri na upotevu. Ikiwa watatubia basi atawapa rehema yake na atawasamehe yaliyopita.
Kusema kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na anawaadhibu wanafiki, akipenda,’ maana yake ni kuwa atawaadhibu ikiwa hawatatubia.
Dalili ya hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Au apokee toba yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.’ Yaani wakitubia atawakubalia toba yao atawasamehe na atawapa rehema yake.
Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha wale ambao wamekufuru na ghadhabu yao.
Ni yale makundi yaliyokusanyika kumuua Mtume(s.a.w.w) kwa kuongozwa na Abu Sufyan. Hawakupata kheri yoyote; yaani lile walilodai kuwa ni kheri; kumuua Mtume na wale walioamini pamoja naye.
Na Mwenyezi Mungu amewakifia waumini na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye uwezo.
Yaani amewatoshea kwenye vita. Abu Hayani Al-Andalusi katika Tafsir yake Al-Bahrul- muhit anasema: “Mwenyezi Mungu aliwatoshea kwenye vita kwa kupeleka upepo na majeshi ambayo ni Malaika. Na imesekana ni Ali bin Abi Twalib na wale waliokuwa pamoja naye. Walipambana, na Ali akamuua Amr.”
Kuna Hadith isemayo: “Pigo la Ali la siku ya Khandaq ni bora kuliko amali za watu na majini.” Riwaya nyingine inasema: “Kupambana Ali na Amr ni amali bora zaidi katika umma wangu hadi siku ya Kiyama.”
Wamenukuu riwaya hizi Al-Hakim katika Mustadrak. Juz. 3 uk. 32, Sayyid Muhsin Al-Amin katika A’yanushia Juz. 2 na Sheikh Al-Mudhaffar katika Dalailussidq Juz. 2.
Na akawateremsha wale waliowasaidia katika watu wa Kitabu kutoka katika ngome zao; na akatia hofu katika nyoyo zao. Badhi yao mkawa mnawaua na wengine mnawateka. Na akawarithisha ardhi yao na majumba yao na mali zao na ardhi ambayo hamjaikanyaga. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.
Yaani waliwasaidia maadui. Makusudio ya watu wa Kitabu hapa ni Bani Quraydha. Ama makusudio ya ardhi ambayo hamjaikanyaga ni bishara ya ushindi wa kiislamu.
Hapo nyuma kidogo tumeeleza kuwa Bani Quraydha walikuwa wakiishi na Mtume(s.a.w.w) huko Madina au kwenye vitongoji vyake na kwamba walikuwa wameahidiana na Mtume kutomsaidia adui. Lakini makundi yalipouzingira mji wa Madina walivunja ahadi na wakatangaza vita; kama ilivyo desturi ya mayahudi wa zamani na wa sasa.
Aya mbili hizi tulizo nazo zinadokeza yaliyowatokea Bani Quraydha baada ya kuvunja ahadi yao na kushindwa jeshi la washirikina; kwa ufupi ni kama ifuatavyo:
Mwenyezi Mungu alipowatoshea waislamu na vita vya Ahzab, msemaji wa Mtume alipiga mbiu ya kuwa watu wawatokee Bani Quraydha. Jeshi la waislamu lilipowafikia lilizingira ngome zao. Mtume akawakaribisha kwenye Uislamu; kwamba watastahiki kama wanavyostahiki waislamu wengine; vinginevyo atawazingira mpaka wasilimu au wapigane.
Kiongozi wao Ka’b bin Asad akawashauri kusilimu na kumwamini Muhammad(s.a.w.w) , akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu! imekwishawabainikia kuwa yeye ni Nabii aliyetumwa na kwamba yeye mnamkuta kwenye Tawrat.” Lakini walikataa na wakasema: “Hatutaiacha dini yetu.”
Vikwazo viliendelea hadi siku ya ishiri na tano, wakawa karibu waangamie kwa kuchoka na hofu. Ndipo wakamtaka Mtume - kwa hiyari yao wenyewe- wahukumiwe na Sa’d bin Mua’dh, aliyekuwa kiongozi wa Aus waliokuwa na urafiki na Bani Quraydha. Mtume akawakubalia ombi lao na akamwita Sa’d akamwambia: “Hawa wametaka kuhukumia na wewe kwa hiyari yao, basi hukumu kwa unalopenda.” Sa’d akasema: “Na hukumu yangu itatekelezwa?” Mtume(s.a.w.w) akasema: “Ndio.”
Basi Sa’d akahukumu kwamba wanaume walioshiriki vitani wauawe. Mali yao ichukuliwe, watoto wao na wanawake wao wachukuliwe mateka na majumba yao yachukuliwe na Wahajiri sio Ansari, kwa sababu Ansar tayari wanayo majumba na Wahajiri hawana.
Basi Nabii(s.a.w.w) akaamuru wauliwe wanaume wale walioshika silaha na wale waliowachochea Bani Quraydha kuvunja ahadi; kama Hayy bin Akhtab, kiongozi wa Bani Nadhir. Kisha mali ikagawanywa, watoto na wanawake wakawa mateka; kama alivyohukumu Sa’d, aliyechaguliwa na Bani Quraydha wenyewe. Hapa ndipo panapoashiriwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Badhi yao mkawa mnawaua na wengine mkawa mnawateka.’
Tumetangulia kuuleza kuwa mboni ya jicho la Saa’d ilidungwa na mshale wa majeshi ya Ahzab naye akaomba asife hadi aridhike kwa watakavyotiwa adabu Bani Quraydha. Basi baada ya kutekeleza hukumu yake kwao jeraha lilitutumka naye akafariki, radhi za Mungu ziwe kwake, moyo wake ukiwa umetulia kwa kufa shahidi na kukubaliwa dua yake.
Unaweza kuuliza : Ilikuwaje Mtume(s.a.w.w) aithibitishe hukumu ya Sa’d iliyokuwa ya nguvu na ukatili; kiasi ambacho maadui wa uislamu wamelifanya tukio hili ni nyenzo ya kuutuhumu na kuutusi Uislamu?
Jibu : Muhammad hakuwadhulumu Bani Quraydha; isipokuwa walijidhulumu wenyewe, kwa kujichagulia wao wenyewe mwishilio huu, kwa ushahidi ufuatao:
Kwanza : wao waliahidiana na Mtume na wakavunja ahadi katika wakati mgumu, kama ilvyo desturi ya mayahudi kuanzia zamani hadi sasa. Mwenyezi Mungu anasema: “Je, kila mara wanapofunga ahadi, kikundi katika wao huitupa? Juz. 1 (2:100).
Pili : Mtume(s.a.w.w) aliwaambia kuwa atawaacha bila ya kuwafanya lolote, kwa sharti waseme: Lailaha illallah, Muhadur-rasulullah (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu). Kiongozi wao, Ka’b bin Asad aliwanasihi wamkubalie Muhammad na watamke shahada mbili, wakakataa.
Tatu : Bani Quraydha walikataa kuhukumiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na wakakubali hukumu ya Saa’d.
Nne, Saa’d aliwahukumu kwa sharia yao wanayohukumia watu na wanayoifuata hadi leo, inayosema: “Utakaposongea karibu ya mji kwenda kupigana juu yake, ndipo utakapowapigia ukelele wa amani.
Itakuwa watakapokujibu kwa amani, na kukufungulia, ndipo watu wote watakaoonekana humo, watafanya kazi ya shoka, na kukutumikia. Na kama hautaki kufanya amani nawe, lakini utafanya vita juu yako, ndipo uhusuru; na Bwana, Mungu wako, autiapo mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga; lakini wanawake na watoto na wanyama wa mji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa Bwana, Mungu wako” (Kumbukumbu 20: 10 – 14)[9] .
Hii inafahamisha kuwa hukumu yao ni kali zaidi ya alivyohukumu Saa’d, kwa sababu hii inasema wazi kuwa mji ukikubli suluhu basi watu wake wote ni watumwa na ukikataa basi wanaume wote wauliwe kwa makali ya upanga, waliopigana na wale wasiopigana na kuchukua mali na kuwateka watoto na wanawake.
Kuna ibara nyingine iliyo kali zaidi ya hii, kwa sababu inaamuru wauliwe wakazi wote, mpaka wanawake na watoto, kisha mji uchomwe na vyote vilivyomo, kwa namna ambayo haitawezekana kujengwa tena; inasema:
“…Hakika yako uwapige wenyeji wa mji ule kwa makali ya upanga, kwa kuwaangamiza kabisa, pamoja na vitu vyote vilivyomo na wanyama na walio humo, kwa makali ya upanga na nyara zake zote uzikusanye katikati ya njia yake; na uuteketeze kwa moto na nyara zake zote, kuwe sadaka kamili ya kuteketezwa kwa Bwana Mungu wako, nao utakuwa magofu milele usijengwe tena” (Kumbukumbu 13:15 – 16).
Je, baada ya yote inafaa kusemwa kuwa Muhammad amewadhulumu Bani Quraydha na kwamba Saa’d aliwaonea kwa alivyowahukumu? Ni katika hukumu ya uadilifu kumpa mtu lile alilolitaka mwenyewe na kuhukumiwa kwa mujibu wa dini na itikadi yake.
Mayahudi wanaitakidi dini yao na kuifuata kwa matendo kwa kuwachinja wanaume kupora mali kuwateka wanawake, kuvunja majumba na kuchoma vijiji na miji kwa watu wote bila ya hata kuwa na vita nao au kuwa wamevunja ahadi au kufanyiwa hata chembe ya ubaya; kama wanavyowafanyia wapalestina hivi sasa.
Je, atahisabiwa ni dhalimu aliyewahukumu kwa wanavyowafanyia watu wengine? Tena Mtume(s.a.w. w ) aliwaua wale waliovunja ahadi tu na wakatangaza vita. Lakini wao wanaua na wanachoma si kwa lolote ila ni kwa kuwa kuua, kuchoma na ufisadi ndio dini yao.
Hata kama wasingevunja ahadi na kutangaza vita, wakahukumiwa kuuawa, kuporwa mali na kuchukuliwa mateka, bado isingelikuwa ni dhulma, kwa sabu wamehukumiwa kwa mujibu wa dini na wanavyofanya wao.
Sharia zote za dini za Mungu na kanuni za kutungwa zimeafikiana kuwa mwenye kufuata dini atalazimiwa na hukumu zake. Hapa ndio kuna siri ya kauli ya Mtume mtukufu(s.a.w.w) aliyomwambia Saa’d: “Umewahukumu kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu kutoka juu ya mbingu saba.”
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ إِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَأُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا ﴿٢٨﴾
28. Ewe Mtume! Waambie wake zako: Ikiwa nyinyi mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni niwape kitokanyumba na niwaache mwachano mzuri.
وَإِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ فَإِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِنَاتِ مِنكُنَّ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٢٩﴾
29. Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia watenda mema, miongoni mwenu, malipo makubwa.
يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ مَن يَأْتِ مِنكُنَّ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ يُضَاعَفْ لَهَا الْعَذَابُ ضِعْفَيْنِ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾
30. Enyi wake wa Mtume! Yeyote kati yenu atakayefanya uchafu dhahiri, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.
Aya 28 – 30
Wake za Mtume(s.a.w.w) walimtaradhia Mtume matumizi zaidi na mapambo, kutokana na ngawira alizompa Mwenyezi Mungu, ndipo ikashuka Aya hii:
Ewe Mtume! Waambie wake zako: Ikiwa nyinyi mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni niwape kitoka-nyumba na niwaache mwachano mzuri. Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia watenda mema, miongoni mwenu, malipo makubwa.
Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake mtukufu awahiyarishe wakeze mambo mawili: Ama awaache pamoja na kitoka-nyumba, ikiwa wanataka, wanayoyataka wanawake wengine, ya dunia.
Kitoka-nyumba ni kitu anachotoa mtaliki kumpa mtalaka wake, kwa kuangalia uwezo wa mwanamume. Tazama Juz. 2 (2:236 – 237).
Au waishi na Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kuvumilia shida [10] 1 na malipo yao mbele ya Mwenyezi Mungu huko akhera yatakuwa makubwa.
Basi wake za Mtume(s.a.w.w) wakachagua akhera na wakaiacha dunia na mapambo yake. Aya hii inaitwa Ayatut-takhyir (Aya ya kuhiyarisha).
Aya ya takhyir ni dalili mkataa ya kukadhibisha madai ya wanaokuza mambo, kuwa Mtume alikuwa na wake kwa sababu ya matamnio ya nafsi. Kwa sababu mwenye pupa ya kustarehe na wanawake – kama alivyosema Mustafa Sadiq Rafi – hawezi kuwahiyarisha baina ya kuachana nao au kuishi maisha ya tabu mpaka siku ya mwisho; bali angeliwabembeleza na kuwaambia kuwa atafanya bidii awatimizie. Kuna mithali isemayo: “Tandiko la harusi liko ghali.”
Anasema Al- aqad katika kitabu chake: Abaqriyatul-Islamiyya: “Lau ladha ya hisia kama ingelikuwa ndio kichocheo cha kuoa baada ya kufa Khadija, basi angeliridhisha hisia zake kwa kuoa wasichana tisa wanaosifika kwa urembo huko Makka na Madina na Bara Arabu kwa ujumla. Na bila shaka angewataka wangelimkubali haraka na kwa kujionea fahari, pia mawalii wao wangeliuridhia na kuuonea fahari ukwe huu ambao haushindwi na ukwe wowote.”
Kisha Al-aqad akataja wake za Mtume mmoja baada ya mmoja na akabainisha sababu zilizopelekea kuwaoa na akasema: “Hakika wanaokuza mambo wamesahahu kila hakika miongoni mwa hakika za maisha haya ya ndoa na wakasahau kuwa Muhammad aliitwa mtakatifu na mtawa wakati wa ujana wake, na kwamba yeye alikaa miaka ishirini na tano na hakuchoka katika kuitafuta halali.
Pia wamesahau kwamba alipotaka kuoa katika miaka hiyo alimuoa mwanamke wa miaka 40 aliyemchagua kwa haja ya kuzoena, wala hakuchagua uzuri uliotakiwa kwa starehe. Wamesahau kwamba mtu waliyempa sifa za hisia za starehe, siku nyingine hakuwa akishiba na mkate wa shairi. Yote haya wameyasahau, na yamethibiti katika historia. Wameyasahau kwa vile wanataka kutia kasoro na kuupotosha uhakika.”
Enyi wake wa Mtume! Yeyote kati yenu atakayefanya uchafu dhahiri, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.
Makusudio ya uchafu hapa ni maasi ya aina yoyote na dhahiri ni waziwazi. Wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu wana daraja tukufu mbele ya Mwenyezi Mungu na ya watu kwa kuungana kwao na Mtume mtukufu(s.a.w.w) . Yeyote atakayefanya maasi atakuwa amehatarisha nafasi yake na kustahiki mara mbili zaidi ya anavyostahiki mwingine. Kwa sababu Mwenyezi Mungu huwahesabu watu kulingana na vyeo vyao; kama wanavyohisabiwa kadiri ya akili zao. Amewalaumu manabii kwa namna ambayo hamlaumu mwingine.
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
YALIYOMO
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 1
IMEANDIKWA NA: SHEIKH MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYA 1
IMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HASAN MWALUPA 1
IMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED 1
IMEPANGWA KATIKA KOMPYUTA NA: UKHT PILI RAJABU 1
UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI 1
MAKOSA YA CHAPA 2
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 3
JE, KUNA MUNGU MWINGINE? 3
MAANA 3
MJUZI WA GHAIBU NA UFUFUO 6
MAANA 7
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 9
QUR’AN INASIMULIA 9
MAANA 9
NEMBO YA ISRAIL NI: ‘TUMESIKIA NA TUMEASI’ 9
MILIMA INAKWENDA MWENDO WA MAWINGU 13
MAANA 13
MILIMA NA HARAKATI ZA ARDHI 14
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 17
AYA ZA KITABU 17
TWAA SIIN MIIM 17
KWA NINI FIRAUNI ALIWAKANDAMIZA WANA WA ISRAIL? 18
LINI MWENYEZI MUNGU ATAWAFADHILI WALIODHOOFISHWA? 19
MAMA WA MUSA 21
MAANA 21
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 24
ALIPOFIKIA KUKOMAA 24
MAANA 24
NJAMA 27
MAANA 27
SHARIA YA KIISLAMU IMEFUTA SHARIA ZOTE 29
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 31
MUSA ANAMALIZA MUDA 31
MAANA 31
NAHOFIA WASIJE WAKANIUA 32
MAANA 33
SIJUI KAMA MNA MUNGU MWINGINE 34
MAANA 34
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 37
MUHAMMAD NA HABARI ZA WALIOPITA 37
MAANA 38
WATAPEWA UJIRA MARA MBILI 41
MAANA 41
SUBIRA NI HEKIMA NA USHUJAA 41
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 43
HUWEZI KUMUONGOA UMTAKAYE 43
MAANA 43
ABU TWALIB NA UISLAMU 43
WAKO WAPI WASHIRIKA WANGU 47
MAANA 47
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 50
HEKIMA YA USIKU NA MCHANA 50
MAANA 50
QARUNI NA UKANDAMIZAJI WA KIBEPARI 52
MAANA 52
ATAKURUDISHA MAHALI PA KUREJEA 56
MAANA 56
KUFICHUA HABARI ZA VIBARAKA NA WAHAINI 56
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 58
IMANI, JIHADI NA SUBIRA 58
MAANA 59
TENA KUWATENDEA WEMA WAZAZI WAWILI 60
KATIKA WATU KUNA WANAOSEMA, TUMEAMINI 61
IMANI AU SARABI? 61
MAANA 61
NUH 63
MAANA 63
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 64
IBRAHIM 64
MAANA 64
MWENYEZI MUNGU NDIYE MWANZILISHI NA MRUDISHAJI 65
MAANA 66
QUR’AN NA FIKRA 66
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 70
LUT 70
MAANA 71
SHUA’YB 72
MAANA 72
NYUMBA DHAIFU ZAIDI NI YA BUIBUI 73
MAANA 73
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 76
MAANA 76
MJADALA KWA NJIA NZURI 77
MAANA 77
Njia Ya Mjadala Katika Qur’an 77
ISHARA ZIKO KWA MWENYEZI MUNGU 81
MAANA 81
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 84
WANYAMA WANGAPI HAWABEBI RIZIKI ZAO 84
MAANA 84
RIZIKI NA KUMTEGEMEA MUUMBA NA SI KIUMBE 85
DUNIA NI UPUUZI NA MCHEZO 87
MAANA 87
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 89
WAROMA WAMESHINDWA 89
MAANA 89
HAWAFIKIRII NAFSI ZAO 92
MAANA 92
USHAHIDI WA ULIMWENGU NA KUUMBWA MTU 94
MAANA 94
NDOA YA KI-QUR’AN 95
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 98
VYOTE VINAMTII YEYE 98
MAANA 98
DINI YA SAWASAWA 100
MAANA 100
Dini Ya Mwenyezi Mungu Na Maumbile 100
DHARA INAPOGUSA WATU 102
MAANA 102
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 104
UFISADI UMEDHIHIRI BARA NA BAHARINI 104
MAANA 104
KATIKA ISHARA YA KILIMWENGU 106
MAANA 106
AKILI NA FIKRA YA UFUFUO 107
AMEWAUMBA KATIKA UDHAIFU 109
MAANA 109
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 112
HUU NI UUMBAJI WA MWENYEZI MUNGU 113
MAANA 113
KUIFANYIA BIASHARA DINI NA DHAMIRI 113
LUQMAN 116
MAANA 116
MWAMBA NA KARNE YA ISHIRINI 118
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 120
KISHIKILIO MADHUBUTI 121
MAANA 121
NI NANI MWENYE KUSHIKILIA KISHIKILIO MADHUBUTI? 121
HUUINGIZA USIKU KATIKA MCHANA 124
MAANA 124
UJUZI WA SAA UKO KWA MWENYEZI MUNGU 125
MAANA 125
KWA NINI MUNGU AKAMUUMBA MTU? 125
UJUZI WA SAA, MVUA NA VILIVYO MATUMBONI 128
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 130
AMETENGENEZA VIZURI UMBO LA KILA KITU 131
MAANA 131
WAKOSEFU WANAINAMISHA VICHWA VYAO 132
MAANA 133
MUUMIN ANAWEZA KUWA SAWA NA FASIKI? 134
MAANA 135
USIWE NA SHAKA YA KUIPOKEA KWAKE 137
MAANA 137
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 139
EWE NABII, MCHE MWENYEZI MUNGU 139
MAANA 139
MWENYEZI MUNGU HAKUMWEKA MTU MMOJA NYOYO MBILI 140
MAANA 140
NABII NI AULA KWA WAUMINI KULIKO NAFSI ZAO 142
MAANA 143
Je, Nabii Ni Hakimu Kwa Amri Yake? Nabii Ni Aula Kwa Waumini Kuliko Nafsi Zao 143
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 145
AHZAB 145
MUHTASARI WA KISA CHA AHZAB 145
KUKIMBIA HAKUTAWAFAA 150
MAANA 150
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI 152
RUWAZA NJEMA KWA MTUME 152
MAANA 153
KISA CHA BANI QURAYDHA KWA UFUPI 155
JE MUHAMMAD ALIWADHULUMU BANI QURAYDHA? 156
EWE NABII, WAAMBIE WAKE ZAKO 158
MAANA 158
MTUME NA WAKE WENGI 158
SHARTI YA KUCHAPA 159
MWISHO WA JUZUU YA ISHIRINI 159
YALIYOMO 160
[1] . Milima: Hivi karibuni wanasayansi wameelezea umuhimu wa milima; kama anavyofafanua Profesa wa Jeolojia mjapani Sievada, yeye anasema: “Milima sio tu kama tunavyoona juu ya ardhi, bali ni mizizi maalumu ambayo inakwenda ndani sana kwenye gamba la ardhi, hivyo huipa milima umbo la kabari”. Frank Press, mwandishi wa kitabu the Earth, anasema: “Kazi ya milima ni kudhibiti na kutuliza gamba la ardhi...” sawa kabisa kama ilivyotajwa katika Juz. 14 (16:15): “Na akaweka katika ardhi milima ili isiyumbe nanyi.”
[2] . Kizuizi baina ya bahari mbili: Mwenyezi Mungu anasema: “Amezikutanisha bahari mbili. Baina yao kuna kizuizi haziingiliani.” (55:19-20) Maumbo makubwa mawili ya maji yanapatikana katika ulimwengu: Moja ni maji matamu yanayotoka kwenye maziwa, mito na chemchemi; umbo lingine ni maji ya chumvi kutoka baharini.
Imegundulika hivi punde na wataalamu wa elimu ya bahari kwamba hata bahari ya jirani haichanganyiki na nyingine, kwa sababu ya utofauti katika kiwango chao cha msongamano, hivyo kutengeneza ukuta mwembamba kati kati ya maumbo hayo mawili ya maji. Upande wa kuvutia ni kwamba, katika kipindi wakati watu hawana elimu ya fizikia, msongamano au utaalamu wa elimu ya bahari, hili tayari limefunuliwa katika Qur'an Tukufu kama muujiza.
[3] . Yakushangaza ni yale niliyoyasoma yaliyonukuliwa kutoka katika Kitabu Talmud, ambacho kwa Mayahudi wengi wanakiona ni kitabu kilichoteremshwa kama Tawrat: “Hakika Mwenyezi Mungu akiteremsha suala gumu huwashauri marabi wakuu kulitatua. Siku moja Mwenyezi Mungu alitoa rai kimakosa, mmoja wa marabi wakuu akagundua kosa hilo na Mungu akakubali.”
[4] . Wakiristo wanaita Tawrat na Injili nne, Kitabu kitakatifu. Kamusi iliyotajwa inafafanua maana ya maneno yaliyo katika Kitabu Kitakatifu, na inadokeza historia, matukio, watu na mengineyo yanayoambatana na Tawrat na Injil.
[5] . Kutoka 3: 1
[6] . Jarida la Al-Jumhuriya la Misr la 17- 10- 1969.
[7] . Hata katika zama hizi pia kuna mtindo unaoitwa adoption. Ambapo mtu anamchukua mtoto asiyekuwa wake na kumfanya ni wake na kukubalika kisharia za kutungwa. – Mtarjumu.
[8] . Nami nakumbuka mwaka huu wa 2007, kabla ya kuanza vita vya Israil, yenye nguvu zote za kijeshi, kupigana na Hizbullah, lilitolewa onyo kali kwa Hizbullah, kuwa wajisalimshe. Onyo hili lilitolewa na hata wale wanaodai ni maadui wa Israil, na kuwaambia. hamtachukua hata siku mbili mtafyekwa nyote. Matokeo yake tuliyaona. Waliweza kupambana kwa zaidi ya mwezi hadi Israili iliposalimu amri – Mtarjumu.
[9] . Kitabu Abaqriyatul-Islamiyya Uk. 219 chapa ya Darul-futuh ya Cairo.
[10] . Baada ya vita vya Ahzab na kuwafurusha Bani Quraydha kutoka Madina, waislamu walipata ngawira na mateka wengi, jambo lililopelekea hali yao ya uchumi kuwa nzuri. Hii iliwathiri wake za Mtume kutaka matumizi zaidi, kwa sababu Mtume aliendelea kuishi vile vile alivyokuwa kimaskini. Inasemekana kuwa jambo hili, la kutaka masurufu zaidi, lilimsikitisha sana Mtume, kiasi ambacho ali- jitenga nao. – Mtarjumu.