TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI- Juzuu 22
Kuweka vikundi Qurani tukufu
mwandishi Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
Lugha ya kitabu سواحیلی
mwaka wa kuchapisha 1404

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

IMEANDIKWA NA: SHEIKH MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYA

IMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HASAN MWALUPA

IMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED

IMEPANGWA KATIKA KOMPYUTA NA: UKHT PILI RAJABU

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI

Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London.

Kama lilivyo jina la Tafsiri ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo.

Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyo kujipatia wasomaji wengi sana.

Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana kwenda na wakati.

Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung'ang'ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo, hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea. Hiyo ilimsaidia sana hata kuweza kutoa kitabu kitwacho Al-Fiqh a'laa madhaahabil-khamsah (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka kwa lugha ya kiswahili hivi karibuni Inshaallah).

Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.

Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasayansi kama kina Enstein, wasanii kama Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa.

Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.

Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji.

Mwisho: Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji.

MAKOSA YA CHAPA

Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa, Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa.

Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya msahafu mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswutu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146), Imeandikwa La Ya'alamuun, (hawajui) badala ya Ya'alamuun (wanajua). Mfano wa makosa haya hausameheki.

Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa Fawqahum ila yawmil qiyama badala ya Fawqahum yawamal qiyama. Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile.

Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu Jabal amil 'Makosa ya chapa.'

Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: Hatta idha balagha arbai' na sanah badala ya: Hattaidha balagha ashuddahu arbai ' na sanah"

Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakayoyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefungua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana.

Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: "Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa.” Kama kwamba hakuna kitu chochote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.

Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin(a.s) :"Watu wote ni wapungufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu." Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubalia yale niliyoyapatia na kunisamehe niliyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazi chake, ziwashukie rehema na amani (Amin).

MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH


1

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

Mwendelezo wa Sura Ya Thelathini Na Tisa: Surat Az-Zumar.

فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَبَ عَلَى اللَّـهِ وَكَذَّبَ بِالصِّدْقِ إِذْ جَاءَهُ أَلَيْسَ فِي جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْكَافِرِينَ ﴿٣٢﴾

32. Basi ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na kuikadhibisha kweli imfikiapo? Je! Siyo katika Jahannamu makazi ya makafiri?

وَالَّذِي جَاءَ بِالصِّدْقِ وَصَدَّقَ بِهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ ﴿٣٣﴾

33. Na aliyeleta ukweli na aliyeusadikisha, hao ndio wenye takua.

لَهُم مَّا يَشَاءُونَ عِندَ رَبِّهِمْ ذَٰلِكَ جَزَاءُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٣٤﴾

34. Watapata watakachotaka kwa Mola wao. Hayo ndiyo malipo ya watendao mema.

لِيُكَفِّرَ اللَّـهُ عَنْهُمْ أَسْوَأَ الَّذِي عَمِلُوا وَيَجْزِيَهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٣٥﴾

35. Ili Mwenyezi Mungu awafutie uovu zaidi walioufanya na awalipe ujira wao kwa wema zaidi ya waliokuwa wakiufanya.

أَلَيْسَ اللَّـهُ بِكَافٍ عَبْدَهُ وَيُخَوِّفُونَكَ بِالَّذِينَ مِن دُونِهِ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ ﴿٣٦﴾

36. Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtoshea mja wake? Na wanakutishia kwa wasiokuwa Yeye! Na anayepotezwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumwongoza.

وَمَن يَهْدِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن مُّضِلٍّ أَلَيْسَ اللَّـهُ بِعَزِيزٍ ذِي انتِقَامٍ ﴿٣٧﴾

37. Na anayeongozwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumpoteza. Je! Mwenyezi Mungu si Mwenye nguvu anayeweza kulipiza.

JE, MWENYEZI MUNGU SI WA KUMTOSHEA MJA WAKE?

Aya 32 – 37

MAANA

Basi ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uwongo Mwenyezi Mungu, akamfanyia washirika au mtoto?

Kauli mbaya zaidi ni uwongo na uwongo mbaya zaidi ni kumzulia Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Na kuikadhibisha kweli imfikiapo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia ulimi wa Mtume wake.

Hivi ndivyo walivyo watu wa masilahi na manufaa, mahali popote na wakati wowote, wanaukana ukweli na kuusadikisha uwongo. Kwa sababu masilahi yao yanakuwa kwa uzushi na ubatilifu. Miongoni mwa niliyoyasoma kuhusiana na haya ni kuwa uwongo mkubwa zaidi ni kusema mwongo: “Mwenyezi Mungu anajua kuwa mimi ni mkweli.”

Je! Siyo katika Jahannamu makazi ya makafiri ? Bila shaka ndio makazi yao na makazi ya kila taghuti muovu.

Na aliyeleta ukweli na aliyeusadikisha, hao ndio wenye takua.

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) alikuja na ukweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu na waislamu wakausadikihsa. Hao mbele ya Mwenyezi Mungu ndio watu wema ikiwa watayaogopa aliyoyakataza; vinginevyo kusadikisha bila matendo hakuna maana yoyote.

Watapata watakachotaka kwa Mola wao. Hayo ndiyo malipo ya watendao mema.

Yaani wale wanaogopa aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu. Kwa sababu bado mazungumzo yanawahusu wao. Mwenyezi Mungu hakuanisha malipo, bali amewaachia vile watakavyo.

Ili Mwenyezi Mungu awafutie uovu zaidi walioufanya na awalipe ujira wao kwa wema zaidi ya waliokuwa wakiufanya.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasamehe madhambi yote, makubwa na madogo, kwa yule mwenye kutubia, akaamini na akatenda mema; na atawalipa wale wanaomtii na kushukuru neema zake kwa wema mkubwa kuliko vile walivyokuwa wakitii na kushukuru.

Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtoshea mja wake? Na wanakutishia kwa wasio kuwa Yeye!

Makusudio ya mja wake hapa ni Muhammad(s.a.w. w ) . Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamkinga na shari ya anayemkusudia shari. Makusudio ya wale wasiokuwa yeye ni masanamu. Kundi la wafasiri wamesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) alipoyataja masanamu kwa ubaya, makuraishi walisema: Muhammad asipokoma kuwataja vibaya miungu wetu, basi tutamshtakia kwao apatwe na majanga.”

Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii. Hili haliko mbali na akili za wajinga na wapumbavu. Hakuna mwenye shaka kuwa Mwenyezi Mungu anamtoshea na kumkinga mja wake na mtume wake.

Na anayepotezwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumwongoza. Na anayeongozwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumpoteza.

Wakati tukifasiri Aya ya 23 ya Sura hii tuliyo nayo, kwenye Juz. 23, na kwengineko, tulisema kuwa: Mwenyezi Mungu, anampoteza yule mwenye kufuata njia ya upotevu kwa hiyari yake, na anamwongoza mwenye kuchagua uongofu kwa hiyari yake na akafuata njia yake.

Je! Mwenyezi Mungu si Mwenye nguvu anayeweza kulipiza anayekufuru na akadhulumu kwa hiyari yake tena baada ya kupewa hoja?

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ قُلْ أَفَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّـهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ أَوْ أَرَادَنِي بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ قُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ ﴿٣٨﴾

38. Na ukiwauliza: Ni nani aliyeziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Sema: Je! Mnawaonaje wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondolea dhara yake? Au akitaka kunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake? Sema: Tosha yangu ni Mwenyezi Mungu. Kwake wategemee wanaotegemea.

قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣٩﴾

39. Sema: Enyi watu wangu! Fanyeni muwezavyo, mimi pia nafanya. Basi punde mtajua.

مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُّقِيمٌ ﴿٤٠﴾

40. Ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi, na itakayemshukia adhabu ya kuendelea.

إِنَّا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ لِلنَّاسِ بِالْحَقِّ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَلِنَفْسِهِ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ ﴿٤١﴾

41. Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa Haki. Basi mwenye kuongoka ni kwa nafsi yake, na mwenye kupotoka bila ya shaka amepotoka kwa nafsi yake. Na wewe si mlinzi juu yao.

اللَّـهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَىٰ عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَىٰ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٤٢﴾

42. Mwenyezi Mungu huzipokea roho zinapokufa. Na zile zisizokufa wakati wa kulala kwake. Huzishika zilizohuku- miwa kufa, na huzirudisha nyengine mpaka ufike wakati uliowekwa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri.

أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ شُفَعَاءَ قُلْ أَوَلَوْ كَانُوا لَا يَمْلِكُونَ شَيْئًا وَلَا يَعْقِلُونَ ﴿٤٣﴾

43. Au ndio wamejifanyia waombezi badala ya Mwenyezi Mungu? Sema: Ingawa hawana mamlaka juu ya kitu chochote, wala hawatambui?

قُل لِّلَّـهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا لَّهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٤٤﴾

44. Sema: Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Ni wake Yeye ufalme wa mbingu na ardhi. Kisha mtarejeshwa kwake.

وَإِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَحْدَهُ اشْمَأَزَّتْ قُلُوبُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَإِذَا ذُكِرَ الَّذِينَ مِن دُونِهِ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ ﴿٤٥﴾

45. Na anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake nyoyo za wasioiamini Akhera huchafuka. Na wanapotajwa walio kinyume naye basi wao hufurahi.

SEMA, TOSHA YANGU NI MWENYEZI MUNGU

Aya 38 – 45

MAANA

Na ukiwauliza: Ni nani aliyeziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu.

Jawabu lao hili linatokana na ufahamu wa kimaumbile aliowaumbia watu Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hakuna tafsiri ya kupatikana ulimwengu isipokuwa kuweko Mwenyezi Mungu. Lakini walahidi wanasema: “Sisi hatuamini isipokuwa kwa kujaribu.” Ama maumbile hayo ni maneno ya upuzi. Nasi kwa upande wetu tunawauliza: ikiwa hamuamini isipokuwa majaribio, basi tuonyesheni majaribio yaliyowafahamisha kuwa hakuna Mungu.

Sisi hatuna shaka kuwa mwenye kupinga maumbile haya au kupinga mantiki yake, ndio ameupinga ubinadamu na kupinga yaliyo na thamani zaidi ndani ya binadamu; ukiwemo utashi na uwezo.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 21 (29:66) na (31:25).

Sema: Je! Mnawaonaje wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondolea dhara yake? Au akitaka kunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake?

Washirikina walimtishia Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa masanamu, ndio Mwenyezi Mungu akamwamrisha mtume wake awaambie kuwa masanamu yana uwezo gani kwangu na kwa mwengine? Je, yanaweza kunikinga ikiwa Mwenyezi Mungu anataka kunidhuru? Au yanaweza kuzuia heri anazonitakia Mwenyezi Mungu? Hapana! Masanamu hayawezi kujikinga hata hayo yenyewe ikiwa binadamu anataka kuyavunja kwa shoka au kuyakanyaga kwa kiatu.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:17) na Juz. 11 (10:107).

Sema: Tosha yangu ni Mwenyezi Mungu. Kwake wategemee wanaotegemea.

Ewe Muhammad! Mwambie anayekadhibisha risala yako kuwa mimi nataka msaada kwa Mwenyezi Mungu na kumtaka mwongozo; naye kwangu ni tosha kabisa! Na yeyote mwenye dhiki basi akimbilie kwake. Yeye ana tosha kuwa walii na msaidizi.

Sema: Enyi watu wangu! Fanyeni muwezavyo, mimi pia nafanya. Basi punde mtajua Ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi, na itakayemshukia adhabu ya kuendelea.

Yaani kila mtu abaki kama alivyo, kisha tungoje mwisho utakuwaje. Bila shaka itakuwa ni hasara na moto kwenu nyinyi na baraka na neema kwetu sisi.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:104) na Juz. 11 (10:93).

Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa haki.

Basi fikisha bishara na maonyo, kwa niaba ya Mola wako, kwa kutumia Aya zake; wala usimwachie yoyote udhuru.

Basi mwenye kuongoka ni kwa nafsi yake, na mwenye kupotoka bila ya shaka amepotoka kwa nafsi yake. Na wewe si mlinzi juu yao.

Kila mtu ana majukumu yake na hisabu yake kwa muumba wake, wewe huna majukumu yoyote kwake baada ya kumfikishia na kumpa nasaha.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:104) na Juz. 11 (10:108).

Mwenyezi Mungu huzipokea roho zinapokufa.

Wanaoamini maada wanasema: Mtu ni huu mwili tu, wala hakuna kitu kingine nyuma yake. Tazama kifungu ‘Wanaoamini maada na maisha baada ya mauti’ katika Juz. 13 (13:5-7). Na ‘Pamoja na wanaoamini maada’ katika Juz. 14 (16:78-83).

Waumini wanasema: Mtu ni mwili na roho, na kwamba roho ndiyo inayouendesha mwili na kuupangilia kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mauti ni kukatika mfungamano wa roho na mwili na roho kwenda kwa Mola wake: “Ewe nafsi iliyotua! Rejea kwa Mola wako hali ya kuwa uradhi mwenye kuridhiwa” (89:27-28).

Na hii ndio maana ya kuwa ‘Mwenyezi Mungu huzipokea roho zinapoku- fa,’ ni kuwa anazishika wakati wa kufa miili.

Na zile zisizokufa wakati wa kulala kwake.

Usingizi ni aina ya mauti au ni mauti kimajazi. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ ﴿٦٠﴾

“Naye ndiye anayewafisha usiku.” Juz. 7 (6:60).

Mwenye Majmaul-bayan anasema: “Inayokufa wakati wa kulala ni nafsi ya upambanuzi na akili ambayo inafarikiana na mwenye kulala, kwa hiyo hawi na akili. Ama ile inayokufa wakati wa mauti ni nafsi ya uhai ambayo inaondoka na pumzi na mwenye kulala huwa anapumua. Kwa hiyo tofauti baina ya kushikwa usingizini na kwisha kwenye mauti ni kuwa usingizi ni kutokuwa macho na mauti ni kutokuwa hai. Na kushikwa usingizini roho inakuwa mwilini na kushikwa kwenye mauti ni roho kuondoka mwilini.”

Huzishika zilizohukumiwa kufa, na huzirudisha nyengine mpaka ufike wakati uliowekwa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri.

Mwenyezi Mungu kuzishika roho wakati wa kufa mwili na wakati wa kulala. Zile zilizohukumiwa kufa zinabaki kwake na zile nyingine anaziachia zirudi mpaka muda maalum.

Umar bin Al-Khattab alisema: “Ajabu ni kuwa mtu anaota ndoto inakuwa kama kuchukua kwa mkono na anaota ndoto nyingine, lakini haiwi kitu.” Imam Ali bin Abi Twalib akamwambia: “Hakika Mwenyezi Mungu anazifisha nafsi zote. Ile unayoiona iko mbele yake basi ni ya ukweli na unayoiona baada ya kuiachia basi ni ya uwongo.” Akastaajabu Umar kutokana na kauli ya Imam.

Haya ameyanukuu Sheikh Al-Maraghi katika tafsiri yake kutoka kwa Abi Hatim na Ibn Mardawayh.

Au ndio wamejifanyia waombezi badala ya Mwenyezi Mungu? Sema: Ingawa hawana mamlaka juu ya kitu chochote, wala hawatambui?

Masanamu hayatambui kitu, wala hayawezi kujikinga na madhara, lakini pamoja na hayo washirikina wanawatarajia wawaombee mbele ya Mwenyezi Mungu. Hivi ndivyo wanavyofanya wajinga. Muombezi bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu kwa wale wenye madhambi ni toba na kurejea kwa Mwenyezi Mungu.

Sema: Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu.

Yaani hakuna yoyote anayemiliki uombezi wowote isipokuwa yule aliyemilikishwa na Mwenyezi Mungu:

قُلْ إِنَّ الْأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّـهِ ﴿١٥٤﴾

“Hakika mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu” Juz.4 (3:154).

Ni wake Yeye ufalme wa mbingu na ardhi. Kisha mtarejeshwa kwake.

Mfano wake ni

وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ﴿١٧﴾

“ Na ni wa Mwenyezi Mungu ufalme wa mbingu na vilivyomo baina yake.” Juz. 6 (5:17).

Na anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake nyoyo za wasioiamini Akhera huchafuka. Na wanapotajwa wenginewe asiye kuwa Yeye basi wao hufurahi.

Washirikina walipokuwa wakisikia kauli ya hapana mola ispokuwa Mwenyezi Mungu (Lailaha illa llah) wanakimbia, na wanaposikia kusifiwa masanamu wanafurahi.

Hivi ndivyo walivyo wabatilifu wa zamani na wa sasa. Haiwapumbazi isipokuwa batili wala haiwatishi isipokuwa haki. Kwenye Nahjulbalagha, amesema: “Ambaye inakuwa uzito kwake kuambiwa haki au kuonyeshwa uadilifu, basi kuyatumia mawili hayo inakuwa uzito zaidi.”


2

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

قُلِ اللَّـهُمَّ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ أَنتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِي مَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿٤٦﴾

46. Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Muumba wa mbingu na ardhi! Mjuzi wa yasiyoonekana na yanayoonekana! Wewe utahukumu baina ya waja wako katika waliyokuwa wakikhitalifiana.

وَلَوْ أَنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُ مَعَهُ لَافْتَدَوْا بِهِ مِن سُوءِ الْعَذَابِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَبَدَا لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مَا لَمْ يَكُونُوا يَحْتَسِبُونَ ﴿٤٧﴾

47. Na lau kuwa waliodhulumu wangelikuwa na vyote viliomo duniani na pamoja navyo vingine kama hivyo, bila ya shaka wangelivitoa kujikomboa katika adhabu mbaya Siku ya Kiyama. Na yatawadhihirikia kwa Mwenyezi Mungu wasiyokuwa wakiyatazamia.

وَبَدَا لَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا كَسَبُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٤٨﴾

48. Na utawadhihirikia ubaya wa waliyoyachuma, na yatawazunguka waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.

فَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ ضُرٌّ دَعَانَا ثُمَّ إِذَا خَوَّلْنَاهُ نِعْمَةً مِّنَّا قَالَ إِنَّمَا أُوتِيتُهُ عَلَىٰ عِلْمٍ بَلْ هِيَ فِتْنَةٌ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٤٩﴾

49. Na dhara inapomgusa mtu hutuomba. Kisha tunapompa neema zitokazo kwetu, husema: Nimepewa haya kwa sababu ya ilimu. Sio! Huo ni mtihani! Lakini wengi wao hawajui.

قَدْ قَالَهَا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٥٠﴾

50. Walikwishayasema haya waliokuwa kabla yao, lakini hayakuwafaa waliyokuwa wakiyachuma.

فَأَصَابَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا كَسَبُوا وَالَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ هَـٰؤُلَاءِ سَيُصِيبُهُمْ سَيِّئَاتُ مَا كَسَبُوا وَمَا هُم بِمُعْجِزِينَ ﴿٥١﴾

51. Basi ukawasibu ubaya wa waliyoyachuma. Na wale ambao wamedhulumu miongoni mwa hawa utawasibu ubaya wa waliyoyachuma. Nao si wenye kushinda.

أَوَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٢﴾

52. Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia? Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaoamini.

UTAHUKUMU BAINA YAO

Aya 46 – 52

MAANA

Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Muumba wa mbingu na ardhi! Mjuzi wa yasiyoonekana na yanayoonekana! Wewe utahukumu baina ya waja wako katika waliyokuwa wakikhitalifiana.

Aya hii inafungamana na ile iliyotangulia: ‘Na wewe si mlinzi juu yao.’ Maana yake yako wazi. Kwa ufupi ni, sema ewe Muhammad, baada ya kufikisha ujumbe na kutoa nasaha: ewe Mwenyezi Mungu wewe ni muumba wa ulimwengu, Mfalme wa wafalme, Mjuzi wa yaliyoko kwangu na kwa wakadhibishaji. Hukumu ni yako peke yako katika kila kuhitalifiana na kuzozana baina ya waja wako kwenye maisha haya.

Na lau kuwa waliodhulumu wangelikuwa na vyote viliomo duniani na pamoja navyo vingine kama hivyo, bila ya shaka wangelivitoa kujikomboa katika adhabu mbaya Siku ya Kiyama. Na yatawadhi- hirikia kwa Mwenyezi Mungu wasiyokuwa wakiyatazamia.

Walikuwa wakipupia dunia na wakikusanya mali juu mali, wakiwa wameghafilika na kukutana na Mwenyezi Mungu na hisabu yake. Wakati watakaposimima mbele yake kwa ajili ya hisabu na kuwafunukia waliyokuwa wakiyapuuza, basi watauma mikono wakijuta. Lakini wapi!

Jahannam haiwezi kukombolewa. Umetangulia mfano wake katika Juz. 3 (3:91), Juz. 11 (10: 54) na Juz. 13 (13:18)

Na utawadhihirikia ubaya wa waliyoyachuma, na yatawazunguka waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.

Walikuwa wanapoambiwa iogoponi siku ambayo mtarejeshwa kwa Mwenyezi Mungu, walikuwa wakiifanyia masikhara kauli hii na yule aliyeisema.

Lakini watakapohudhurishwa siku iliyoagwa, hapo ndio haki- ka itawadhihirikia na adhabu itawashukia kulingana na msimamo wao wa madharau na kumdharau yule aliyewaonya.

UDHURU MBAYA KULIKO DHAMBI

Na dhara inapomgusa mtu hutuomba. Kisha tunapompa neema zitokazo kwetu, husema: ‘Nimepewa haya kwa sababu ya ilimu.’

Makusudio ya mtu hapa ni kila mwenye sifa hiyo iliyotajwa ambaye anamtaka msaada Mwenyezi Mungu wakati wa shida na kumsahau wakati wa raha huku akisema kwa kujidai: ‘Neema hii ni kwa mipango na ufundi wangu.’

Wakati nikiandika maneno haya, nimekumbuka siasa ya Marekani aliyoitangaza Rusk, alipokuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, alisema: “Hapana budi kwa Marekani kuonyesha umuhimu wake katika dunia nzima, ikiwemo anga yake, maji yake na pambizo zake zinazoizunguka.”

Anamaanisha kuwa ni lazima Amerika itawale dunia yote na vilivyomo ndani yake.

Tangazo hili lilikuwa mnamo mwaka 1966, kabla ya Marekani kupeleka chombo chake mwezini. Kwa hiyo ingelikuwa leo angeuanganisha mwezi na sayari nyinginezo.

Baada ya magazetu ya kimataifa kutangaza siasa hii ya kikoloni, aliyoitangaza waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, kibaraka mmoja aliandika makala ya kutetea siasa hii, kwa kusema:

“Marekani ndio dola kubwa kielimu na kiutajiri. Imeonyesha ushindi mkubwa katika uwanja wa elimu na viwanda. Kwa hiyo basi inayo haki ya kuingilia ulimwengu kwa sura mbalimbali, kutawala kila inachokitaka, kugeuza kanuni za nchi yoyote, vile inavyotaka, na kuielekeza kiuchumi, kuiwekea bajeti yake na kuipangia nchi hiyo itakachouza nje na itakochonunua.

Vile vile Marekani inayo haki ya kutumia siasa kwenye nchi yoyote kwa mfumo wowote, hata ikibidi kutumia nguvu, kwa mapinduzi ya kijeshi na kuunga mkono harakati za upinzani, ili kuleta utulivu.

Marekani inayo haki hii na zaidi, kwa sababu:

kwanza : Haki hii ni ya kielimu.

Pili : Marekani inamiliki silaha za maangamizi, na kila mwenye kumilki silaha hizi ana haki ya kutawala dunia nzima na vilivyomo ndani yake.”

Yote yaliyoandikwa kwenye makala hii kupitia mwandishi huyu ni ubainifu wa siasa halisi ya Marekani kama ilivyo. Mwenye kutaka kuhakikisha haya naangalie siasa ya Marekani katika Vietnam, Asia, Afrika na Latin Amerika.

Vile vile msimamo wake wa kiadui kwa nchi za kiarabu, jinsi inavyotoa msaada usiokuwa na mpaka kwa adui Israil na inavyopinga jaribio lolote la amani katika tatizo la Palestina na mahali popote penye tatizo mashariki na magaharibi.

Mzandiki huyu aliyejitolea kuitetea Marekani, kubariki siasa zake na kusema kuwa inayo haki ya kushibisha matamanio yake ya kiuadui, kwa kuwa eti inamiliki viwanda vya silaha, tunamuuliza hivi: Ikiwa elimu inaruhusu kuua, kubomoa na kupora, maana yake ni kuwa elimu ni ya shari sio ya heri na ni ya ufisadi wala sio ya utengenezaji?

Na kwamba mwenye elimu anayoruhusa kuitumia elimu yake kuiba, kudanganya na kuzua? Na mwizi atakuwa ni mwenye kushukuriwa na kulipwa; na kila anavyozidi kuwa hodari wa hatia na kuwa na ufisadi mwingi na upotevu basi atakuwa anastahiki heshima?

Ikiwa elimu inaboresha uadui, kwanini basi Marekani inainua nembo za haki za binadamu na kujaribu kila juhudi kuwakinaisha watu kwamba wao wanafanya ibada wana zuhudi na wanupiga vita ukomonisti kwa jina la imani ya Mungu na siku ya mwisho?

Zaidi ya hayo mzushi huyu mwenye dhambi amaesahau kuwa anafichua hiyana yake na upotevu wake, huku akiwa anatetea matamanio ya Marekani kwa mantiki yake ya kufedhehesha akitoa udhuru kwa yaliyo mabaya zaidi ya dhambi yake.

Sio! Huo ni mtihani!

Makusudio ya mtihani hapa ni neema. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamneemesha mja wake ili amjaribu kuwa atashukuru au atakufuru. Akishukuru humzidishia neema duniani na malipo akhera, na akikufuru basi Jahannam imeandaliwa makafiri.

Lakini wengi wao hawajui kuwa Mwenyezi Mungu anawapa mtihani waja wake ili vidhihirike vitendo vinavyostahiki thawabu na adhabu.

Walikwishayasema haya waliokuwa kabla yao, lakini hayakuwafaa waliyokuwa wakiyachuma.

Yaani haya ya kusema kuwa nimepewa kwa elimu yangu. Maana ni kuwa msemaji huyu mjinga ana wanaofanana naye katika historia, lakini mali haikuwazuia na ghadhabu za Mwenyezi Mungu na adhabu yake iliyotolewa kiaga. Tazama Juz. 20 (28:76-82).

Basi ukawasibu ubaya wa waliyoyachuma. Na wale ambao wamedhulumu miongoni mwa hawa - waliomkadhibisha Muhammad – utawasibu ubaya wa waliyoyachuma.

Mwenye kufanya wema atalipwa nao wala hatapata msaidizi asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Hii imethibiti kwa wote bila ya kuvua wala kuhusika na uma zilizotangulia au zijazo. Ni desturi ya Mwenyezi Mungu, wala hutapata mabadiliko katika desturi ya Mwenyezi Mungu.

Nao si wenye kushinda.

Kwani inawezekana muumbwa kumshinda muumba wake?

Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia? Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaoamini.

Umetangulia mfano wake katika Juzuu zifuatazo: Juz.13 (13:27), Juz.15 (17:30), Juz.20 (28:82), Juz.21(29:62), Juz.21 (30:37) na Juz.22 (34:36,39).

Na tumezungumzia kwa ufafanuzi zaidi kuhusu suala hili katika Juzuu zifuatazo: Juz. 6 (5:64-66), kifungu cha ‘Riziki na ufisadi,’ Juz. 7 (5:100) kifungu ‘Je riziki ni bahati au majaliwa?’ Juz. 13 (13:26-29) kifungu ‘Mtu na riziki’ na Juz. 20 (29:56-63) kifungu ‘Riziki na kumtegemea Muumba si kiumbe.’

قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿٥٣﴾

53. Sema: Enyi waja wangu waliozifanyia israfu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ ﴿٥٤﴾

54. Na rejeeni kwa Mola wenu, na silimuni kwake, kabla ya kuwajia adhabu. Kisha hapo hamtanusuriwa.

وَاتَّبِعُوا أَحْسَنَ مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ بَغْتَةً وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ ﴿٥٥﴾

55. Na fuateni yaliyo bora zaidi katika yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu, kabla haijawajia adhabu kwa ghafla, na hali hamtambui.

أَن تَقُولَ نَفْسٌ يَا حَسْرَتَىٰ عَلَىٰ مَا فَرَّطتُ فِي جَنبِ اللَّـهِ وَإِن كُنتُ لَمِنَ السَّاخِرِينَ ﴿٥٦﴾

56. Isije ikasema nafsi: Ee masikitiko yangu kwa yale niliyopoteza upande wa Mwenyezi Mungu; na hakika nilikuwa miongoni mwa wanaofanya maskhara!

أَوْ تَقُولَ لَوْ أَنَّ اللَّـهَ هَدَانِي لَكُنتُ مِنَ الْمُتَّقِينَ ﴿٥٧﴾

57. Au ikasema: Ingelikuwa Mwenyezi Mungu ameniongoa, bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa wenye takua.

أَوْ تَقُولَ حِينَ تَرَى الْعَذَابَ لَوْ أَنَّ لِي كَرَّةً فَأَكُونَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٨﴾

58. Au ikasema inapoona adhabu: Lau kuwa ningelipata kurudi, ningeli kuwa miongoni mwa wafanya mema.

بَلَىٰ قَدْ جَاءَتْكَ آيَاتِي فَكَذَّبْتَ بِهَا وَاسْتَكْبَرْتَ وَكُنتَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٥٩﴾

59. Wapi! zilikwishakujia Ishara zangu, nawe ukazikadhibisha, na ukajivuna, na ukawa miongoni mwa makafiri!

MWENYEZI MUNGU ANASAMEHE MADHAMBI YOTE

Aya 53 – 59

MAANA

Sema: Enyi waja wangu waliozifanyia israfu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

Huu ni mwito wa wazi, kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa wale waliodhulumu nafsi zao kwa kufanya madhambi na maasi. Akaahidi msamaha kwa kila dhambi kadiri itakavyokuwa kubwa. Kwa hiyo amefungua mlango kwa yule mwenye kutaka kufuta maovu yake yeye mwenyewe na kutengeneza yaliyoharibika.

Kuna Hadith inayosema:“Hakika Mwenyezi Mungu hachoki mpaka mchoke. Mkiacha naye anaacha.” yaani mkiacha toba naye anaacha maghufira. Katika Hadith nyingine Mtume(s.a.w. w ) anasema:“Hakuna ninachopenda zaidi katika dunia na vilivyomo kuliko Aya hii.” Imekua mashuhuri kauli ya kuwa hii ni Aya yenye matarajio zaidi katika Qur’ani.

Miongoni mwa madhambi makubwa zaidi ni kukata tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu:

قَالَ وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ ﴿٥٦﴾

“Na ni nani anayekata tamaa na rehema ya Mola wake isipokuwa wale waliopotea.” Juz. 14 (15:56).

Tumelizungumzia hilo kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 5 (4:56). Pia tumeweka kifungu maalum cha toba ’Toba na umbile’ katika Juz. 4 (4:17-18).

Na rejeeni kwa Mola wenu, na silimuni kwake, kabla ya kuwajia adhabu. Kisha hapo hamtanusuriwa.

Chukueni fursa enyi wenye dhambi wala msiipoteze. Tubieni kwake na mumfanyie ikhlasi kwa kauli na vitendo.

Na fuateni yaliyo bora zaidi katika yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu, kabla haijawajia adhabu kwa ghafla, na hali hamtambui.

Hakuna kitu, katika alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kilicho bora zaidi ya kingine kwake. Kila alichokisema ni kizuri zaidi na adhimu. Ama kwa wenye dhambi basi kitu bora zaidi walichoteremshiwa ni mwito wa toba na kukubaliwa hata ikiwa dhambi ni kubwa kiasi gani. Na yasiyokuwa hayo ni kiaga na hadhari.

Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akabainisha matokeo ya atakayepuuza toba; kama ifuatavyo:

Isije ikasema nafsi: Ee masikitiko yangu kwa yale niliyopoteza upande wa Mwenyezi Mungu katika kumtii. Masikitiko ni miongoni mwa adhabu kubwa ya nafsi. Hasa ikiwa hakuna kimbilio wala pa kutokea.

Na hakika nilikuwa miongoni mwa wanaofanya maskhara!

Kesho mwenye madhambi atasema kwa majuto na masikitiko: Sikutosheka na kumwasi Mwenyezi Mungu na kupuuza toba mpaka nikawafanyia masihara wanaomtii Mwenyezi Mungu na wenye kuogopa adhabu yake.

Au ikasema: Ingelikuwa Mwenyezi Mungu ameniongoa, bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa wenye takua.

Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Watasema walioshirikisha: Lau angelitaka Mwenyezi Mungu tusingelishirikisha” Juz. 8 (6:148).

Au ikasema inapoona adhabu: Lau kuwa ningelipata kurudi, ningeli kuwa miongoni mwa wafanya mema.

Mfano wake ni:

قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ ﴿٩٩﴾ لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ ﴿١٠٠﴾

“Husema Mola wangu nirudishe ili nitende mema badala ya yale niliyoacha” Juz. 18 (23:99-100).

Wapi! Mambo hayako kama unavyotaka zilikwishakujia Ishara zangu, nawe ukazikadhibisha, na ukajivuna, na ukawa miongoni mwa makafiri!

Zilimjia ishara za Mwenyezi Mungu akazikanusha na akasema hazitoki kwa Mwenyezi Mungu. Akafanya kiburi na imani na akamkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha akakadhibisha na akasema: hakuna chochote kilichonijia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mtume wake.

Kwa hiyo akachanganya maovu ya kufuru, uwongo na kiburi. Lau angelichukua fursa ya kutubia ingelikuwa hana haja na malalamiko yote haya; na angelikuwa kwenye raha bila ya kuwa na hizaya.


3

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ تَرَى الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَى اللَّـهِ وُجُوهُهُم مُّسْوَدَّةٌ أَلَيْسَ فِي جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْمُتَكَبِّرِينَ ﴿٦٠﴾

60. Na Siku ya Kiyama utawaona wale ambao wamemsingizia uwongo Mwenyezi Mungu nyuso zao zimesawijika. Je! Si katika Jahannamu makazi ya wanaotakabari?

وَيُنَجِّي اللَّـهُ الَّذِينَ اتَّقَوْا بِمَفَازَتِهِمْ لَا يَمَسُّهُمُ السُّوءُ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦١﴾

61. Na Mwenyezi Mungu atawaokoa walio na takua kwa ajili ya kufuzu kwao. Hapana uovu utao wagusa, wala hawatahuzunika.

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿٦٢﴾

62. Mwenyezi Mungu Mungu ndiye Muumba wa kila kitu; na Yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu.

لَّهُ مَقَالِيدُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٦٣﴾

63. Anazo funguo za mbingu na ardhi. Na wale ambao wamezikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye hasara.

قُلْ أَفَغَيْرَ اللَّـهِ تَأْمُرُونِّي أَعْبُدُ أَيُّهَا الْجَاهِلُونَ ﴿٦٤﴾

64. Sema: Je! Mnaniamrisha nimwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, enyi majahili?

وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٦٥﴾

65. Na kwa hakika umepewa wahyi na waliokuwa kabla yako: Bila ya shaka ukishirikisha amali zako zitapomoka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kuhasirika.

بَلِ اللَّـهَ فَاعْبُدْ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ ﴿٦٦﴾

66. Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru.

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٧﴾

67. Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungu haki ya kadiri yake. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume. Ametakasika na Ametukuka na wanayomshirikisha nayo.

WALIOMSINGIZIA UWONGO MWENYEZI MUNGU

Aya 60 – 67

MAANA

Na Siku ya Kiyama utawaona wale ambao wamemsingizia uwongo Mwenyezi Mungu nyuso zao zimesawijika. Je! Si katika Jahannamu makazi ya wanaotakabari?

Kila anayemnasibishia Mwenyezi Mungu yale asiyokuwa na ujuzi nayo basi atakuwa amemsingizia Mwenyezi Mungu; iwe amemnasibishia kuwa na washirika, mke na mtoto, au kazi za Mwenyezi Mungu; kama kuingilia utume ukhalifa, hukumu au kutoa fatwa kwa jina la dini.

Aliulizwa Imam Ja’far As-sadiq(a.s) kuhusiana na maana ya Aya hii, akasema:“Mwenye kudai uimamu usiotokana na Mwenyezi Mungu, atakuwa amemsingizia uongo Mwenyezi Mungu” Muulizaji akasema: Hata kama ni Alawi. Imam akasema: hata kama ni Alawi. Muulizaji akaendelea kuuliza: Hata kama ni Fatimi, Imam akasema:Hata kam ni Fatimi.”

Malipo ya mwenye kumzulia Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ni kufufuliwa akiwa na uso uliosawijika, katika kundi lililoandaliwa Jahannam na Mwenyezi Mungu, makazi mabaya kabisa.

Kauli yake Mwenyezi Mungu ‘wanotakabari’ baada ya kauli yake ‘wale ambao wamemsingizia Mwenyezi Mungu,’ inaashiria kuwa kumsingizia Mwenyezi Mungu ni kiburi.

Na Mwenyezi Mungu atawaokoa waliona takua kwa ajili ya kufuzu kwao. Hapana uovu utaowagusa, wala hawatahuzunika.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwahadharisha wasingiziaji na moto wa Jahannam, sasa anawabashiria wakweli na wenye takua, kuokoka na moto na kila ubaya. Zaidi ya hayo hawatakuwa na huzuni wala majuto kwa yale waliyoyakosa duniani.

Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu.

Kila kilichoko akiwemo mtu, mnyama mimea na mawe, kinafahamisha kuweko kwa Mwenyezi Mungu kwa sura ya ufundi wa mjengaji kutokana na jengo lenyewe na aliyekitengeneza na kila jingo

Na Yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu.

Yaani ni mwenye kusimamia, kwa sababu kila kitu kimepatikana kwa uweza wa Mwenyezi Mungu na kitabaki chini ya uangalizi wake mpaka atakapotaka, vinginevyo itakua hakina maana.

Anazo funguo za mbingu na ardhi.

Funguo ni kinaya cha kuwa Mwenyezi Mungu ni mzingatiaji wa ulimwen- gu na ni mjuzi wa yote yanayopita humo kuanzia chembe ndogo hadi sayari kubwa: “Na ziko kwake funguo za ghaibu” Juz. 7 (6:59).

Na wale ambao wamezikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye hasara.

Makusudio ya ishara za Mwenyezi Mungu ni ulimwengu na nidhamu yake ya ajabu ambayo lau itakoseka kwa kiasi cha unywele tu, basi utaharabika.

Maana ya kuzikataa ishara za Mwenyezi Mungu ni kutozikubali dalili za nidhamu hii kuwa kuna aliyezipanga na uhandisi na mhandisi wake.

Wakadhibishaji wamezitia hasara akili zao na dalili hizi, kwa sababu zimepofuka na hisia. Vile vile wamezitia hasara nafasi zao na akhera, kwa vile wamezichagulia ukafiri na inadi; na Jahannam yatakuwa ndio makazi ya kila kafiri mwenye inadi.

Sema: Je! Mnaniamrisha nimwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, enyi majahili?

Kuna mapokezi yanayosema kuwa washirikina walimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) na kusema: Tutakupa mali itakayokufanya uwe tajiri zaidi ya wote katika Makka na tutakuoza msichana unayemtaka, kwa sharti ya kuwa uache mwito wako. Ndio ikashuka Aya hii.

Iwe riwaya hii ni sahihi au la lakini inafafanua zaidi na Aya hii. Ni vizuri tudokoe maneno yafuatayo kutoka katika makala ya marehemu Mustafa Sadiq Ar-rafii, yenye kichwa cha maneno ‘Dirhamu na dinari’: “Nimewaona baadhi ya mafakihi wakitoa mawaidha na kuwaambia watu halali na haramu, lakini hakika wanawafanyia maskhara vile anavyomfanyia maskhara mwizi anayempa mawaidha mwizi mwingine na kumwambia usiibe.”

Hali hii pia iko kwa waandishi wanasiasa na wengineo wanaobeba nembo za uzalendo na ubinadamu. Ar-rafii anaendelea kusema: “Mwenye kutukuza dirhamu na dinari (pesa) huwa anautukuza unafiki, tamaa na uwongo… Hakika haiba ya Uislamu ni kujitolea maisha sio kupupia maisha, na kuwasaidia waumini sio kuwafanyia uadui. Na utajiri unapimwa kwa inavyofanya kazi mali sio kukusanya mali.”

Na kwa hakika umepewa wahyi na waliokuwa kabla yako: Bila ya shaka ukishirikisha amali zako zitapomoka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kuhasirika.

Makusudio ya kupomoka (kuanguka) amali ni kukosa thawabu. Kushirikisha ni muhali kwa mitume, lakini kukadiria muhali sio muhali. Zaidi ya hayo ni kuwa kutahadharishwa kitu hakufahamishi kuwa aliyehadharishwa anadhaniwa kuwa atafanya alilohadharishwa.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu hakubali ibada ya yeyote ila ikiwa imetakata na kuwa safi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu. Mwenye kumwabudu Mwenyezi Mungu pamoja na mwingine, basi hastahiki thawabu; hata akiwa ni kama mtume. Tumefafanua kuanguka amali katika Juz. 2 (2:216 – 218), kifungu cha ‘Kupomoka.’

Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru.

Kwa dhahiri hii ni amri, lakini kwa hakika ni kuelezea kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) haabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu tu wala hamshukuru yeyote asiyekuwa yeye. Imekuja kwa tamko la amri kutanabahisha waja kuwa ibada na shukrani ni lazima iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mmoja tu.

Zaidi ya hayo Mwenyezi Mungu (s.w.t) mara nyinyi huwaambia wote kwa kumtuma Mtume wake mtukufu: “Na kwamba elekeza uso wako kwenye dini safi, wala usiwe miongoni mwa washirikina.” Juz. 11 (10:105), “Basi simama sawa sawa kama ulivyoamrishwa wewe...” Juz. 12 (11:112) na “Na simamisha Swala katika ncha mbili za mchana...” Juz. 12 (11:114).

Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungu haki ya kadiri yake kwa sababu wao wamemkataa na kuamini masanamu na pesa.

Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume.

Hiki ni kinaya cha ukuu wa Mwenyezi Mungu na uweza wake; na kwamba mbingu na ardhi na vyote viliomo baina yake vinanyenyekea amri yake.

Ametakasika na Ametukuka na wanayomshirikisha nayo.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametakasika na kila shirki na wanayoyasema kuwa ana mkono wa kuume. Na pia ametakasika na ufananisho wanaomsifu nao majahili.

وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَصَعِقَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ ثُمَّ نُفِخَ فِيهِ أُخْرَىٰ فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنظُرُونَ ﴿٦٨﴾

68. Na itapulizwa parapanda, wazimie waliomo mbinguni na waliomo ardhini, ila ambaye Mwenyezi Mungu amemtaka. Kisha itapulizwa mara nyengine. Hapo watainuka wawe wanangojea.

وَأَشْرَقَتِ الْأَرْضُ بِنُورِ رَبِّهَا وَوُضِعَ الْكِتَابُ وَجِيءَ بِالنَّبِيِّينَ وَالشُّهَدَاءِ وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْحَقِّ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٦٩﴾

69. Na ardhi itang’ara kwa Nuru ya Mola wake, na Kitabu kitawekwa, Na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa haki, wala hawatadhulumiwa.

وَوُفِّيَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَا يَفْعَلُونَ ﴿٧٠﴾

70. Na kila nafsi italipwa kwa yale iliyoyafanya, na Yeye anayajua sana wanayoyatenda.

وَسِيقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ زُمَرًا حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا فُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَتْلُونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِ رَبِّكُمْ وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا قَالُوا بَلَىٰ وَلَـٰكِنْ حَقَّتْ كَلِمَةُ الْعَذَابِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٧١﴾

71. Na wale ambao wamekufuru watasukumwa kwenye Jahannamu kwa makundi. Mpaka watakapoifikia itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakuwajia Mitume miongoni mwenu wakiwasomea Aya za Mola wenu na kuwaonya kukutana na siku yenu hii? Watasema: Ndio! Lakini limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya makafiri.

قِيلَ ادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا فَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ ﴿٧٢﴾

72. Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Basi ni ubaya ulioje wa makazi ya wanaotakabari.

WALIOKUFURU WATASUKUMWA

Aya 68 – 72

MAANA

Na itapulizwa parapanda, wazimie waliomo mbinguni na waliomo ardhini, ila ambaye Mwenyezi Mungu amemtaka.

Kupuziwa parapanda ni kinaya cha ukelele. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

يَوْمَ يَسْمَعُونَ الصَّيْحَةَ بِالْحَقِّ ذَٰلِكَ يَوْمُ الْخُرُوجِ ﴿٤٢﴾

“Siku watakaposikia ukelele kwa haki, hiyo ndiyo siku ya kutoka.” (50:42).

Katika baadhi ya tafsiri imeelezwa kuwa ukelele au mpulizo huu utakaririka mara tatu: Wa kwanza ni ule ilioelezwa katika Aya isemayo:

وَيَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَفَزِعَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ وَكُلٌّ أَتَوْهُ دَاخِرِينَ ﴿٨٧﴾

“Na siku itakapopuziwa parapanda, watafazaika waliomo mbinguni na waliomo ardhini, ila amtakaye Mwenyezi Mungu.” Juz. 20 (27:87).

Ambaye Mwenyezi Mungu amemtaka ni yule mwenye takua ambaye umemtangulia wema.

Mpulizo wa pili ni wa mauti ulioashiriwa kwenye Aya hii tuliyo nayo. Na makusudio ya ila ambaye Mwenyezi Mungu amemtaka ni kuwa watu wa ardhini watakufa wote na wa mbinguni hawatabaki isipokuwa ambaye Mwenyezi Mungu atamtaka.

Wafasiri wametofautiana kuhusiana na huyo ambaye Mwenyezi Mungu atamtaka katika wa mbinguni. Ikasemekana kuwa ni Jibril na Israfil. Wengine wakasema ni mashahidi. Mwingine hata akathubutu kusema ni Mwenyezi Mungu – Tunamuomba msamaha Mwenyezi Mungu na tunatubu kwake.

Sio mbali kuwa kusema ila ambaye Mwenyezi Mungu amemtaka, sio hakika bali ni majazi ya kuwa amri siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu peke yake na kwamba:

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ ﴿٢٦﴾ وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٢٧﴾

“Kila kilichoko juu yake kitatoweka na itabaki dhati ya Mola wako mwenye utukufu na heshima” (55:26-27).

Mpulizo wa tatu ni wa ufufuo amabao amaeuashiria Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kusema:Kisha itapulizwa mara nyengine. Hapo watainuka wawe wanangojea hukumu ya Mwenyezi Mungu kwao.

Kwenye Nahajul-balagha imeelezwa: “Na itapulizwa parapanda, kila chenye uhai kitakufa na kila sauti itakuwa bubu, milima na majabali yataporomoka na mawe yageuke mchanga na iwe tamabarare. Hakutakuwa na muombezi wa kuombea wala ndugu wa kutetea wala udhuru utakaonufaisha.[1]

Na ardhi itang’ara kwa Nuru ya Mola wake.

Makusudio ya ardhi hapa ni ardhi ya ufufuo na mkusanyiko. Nayo itang’arishwa na nuru ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa sababu yenyewe ni twahara isyokuwa na aina yoyote ya upotevu na ufisadi; haku- na isipokuwa haki na uadilifu.

Na Kitabu kitawekwa, yaani mandishi ya matendo yote:

وَنُخْرِجُ لَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كِتَابًا يَلْقَاهُ مَنشُورًا ﴿١٣﴾

“Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu atakachokikuta kimekunjuliwa.” Juz. 15 (17:13).

Mulla Sadra anasema katika Al-asfar: “Mwenye kutenda kitendo au kusema kauli, athari yake inajitokeza kwenye nafsi yake na moyo wake.

Athari hii inayopatikana kwenye moyo na roho iko kama nakshi na maandishi katika vitabu na mbao. Nyoyo na roho hizo, ambazo zina athari ya vitendo na kauli, kwa lugha ya sharia zinaitwa kurasa za matendo.”

Na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa haki, wala hawatadhulumiwa. Na kila nafsi italipwa kwa yale iliyoyafanya, na Yeye anayajua sana wanayoyatenda.

Makusudio ya mashahidi hapa ni manaibu wa mitume katika kufikisha ujumbe wao na desturi zao kwa watu. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu kesho atawafufua watu kwa ajili ya hisabu. Atawaleta manabii wawe mashahidi kwa manaibu wao kuwa wao walichukua ujumbe kwa manabii ili waufikishe kwa watu.

Kisha manaibu nao watatoa ushahidi kuwa wao waliwafundisha watu na waliufikisha ujumbe kwa ukamilifu. Baada ya kupatikana ushahidi wa manabii kwa manaibu na wa manibu kwa watu, hapo Mwenyezi Mungu atawahukumu wote kwa uadilifu bila ya kumpunguzia thawabu mtiifu wala kumzidishia adhabu Muasi.

Yeye anawajua zaidi wote, wakiwemo manabii na mashahidi, kuliko nafsi zao. Amewaita hapa kwa ushahidi kukamilisha hoja na kuondoa visababu vyote.

Tazama Juz. 2 (2:143).

Na wale ambao wamekufuru watasukumwa kwenye Jahannamu kwa makundi. Mpaka watakapoifikia itafunguliwa milango yake.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja, katika Kitabu aina kwa aina ya dhabu ya wakosefu; kama vile: udhalili na utwevu, upofu na kusawijika uso, minyororo na nguo za moto, chakula cha Zaqqum na kinywaji cha usaha na kusukumwa na malaika kupelekwa kwenye Jahannam ili wawe kuni zake. Hao malaika wana miadi nao ya kuwangoja, ndio maana watakuta milango tayari iko wazi.

Na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakuwajia Mitume miongoni mwenu wakiwasomea Aya za Mola wenu na kuwaonya kukutana na siku yenu hii?

Makusudio ya swali hili ni kutahayariza na kwamba wao ndio waliojichagulia mwisho huu mbaya.

Watasema: Ndio! Lakini limekwishathibiti neno la adhabu juu ya makafiri.

Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴿١٠﴾ فَاعْتَرَفُوا بِذَنبِهِمْ فَسُحْقًا لِّأَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴿١١﴾

“Na watasema: lau tungelikuwa tunasikia au kutia akilini, tusingelikuwa katika watu wa Motoni! Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa motoni!” (67:10-11).

Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo.

Basi ni ubaya ulioje wa makazi ya wanaotakabari kwenye haki na kutoka kwenye uadilifu.

Lau kusingelikuwa na dalili nyingine ya kuandaliwa Jahannam isipokuwa kwa wenye kiburi, mataghuti, wafisadi na wapotevu tu, ingelitosha. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ ﴿١٤٥﴾

“Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini motoni. Juz. 5 (4:145)

Akasema tena:

إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا ﴿٢١﴾ لِّلطَّاغِينَ مَآبًا ﴿٢٢﴾

“Hakika Jahannam inangojea. Ni marejeo kwa wenye kupetuka mipaka” (78:21-22).

Huko nyuma tumewahi kusema kuwa lau kusingeliku na mahakama, huko akhera, ya kisasi cha aliyedhulimiwa kwa dhalimu, basi ingelikuwa aliyeuliwa kidhulma ana hali mbaya zaidi ya aliyemuua.

Tazama Juz. 11 (10:3-4) kifungu cha: ‘malipo ni lazima.’

وَسِيقَ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ زُمَرًا حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا وَفُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ ﴿٧٣﴾

73. Na waliomcha Mola wao watapelekwa Peponi kwa makundi, mpaka watakapoifikia, nayo milango yake imekwishafunguliwa, walinzi wake watawaambia: Salaamun Alaikum, (Amani iwe juu yenu!) Mmekua wema. Basi ingieni humu mkae milele.

وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي صَدَقَنَا وَعْدَهُ وَأَوْرَثَنَا الْأَرْضَ نَتَبَوَّأُ مِنَ الْجَنَّةِ حَيْثُ نَشَاءُ فَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿٧٤﴾

74. Na watasema: Alhamdulillah, (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) aliyetutimizia ahadi yake, na akaturithisha ardhi, tunakaa katika Bustani popote tupendapo. Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao!

وَتَرَى الْمَلَائِكَةَ حَافِّينَ مِنْ حَوْلِ الْعَرْشِ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْحَقِّ وَقِيلَ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٧٥﴾

75. Na utawaona Malaika wak- izunguka pembeni mwa Arshi ya Mwenyezi Mungu, wakimsabihi na kumsifu Mola wao. Na patahukumiwa baina yao kwa haki na patasemwa: Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote!

WALIOMCHA MOLA WAO WATAPELEKWA PEPONI

Aya 73 – 75

MAANA

Na waliomcha Mola wao watapelekwa Peponi kwa makundi, mpaka watakapoifikia, nayo milango yake imekwishafunguliwa, walinzi wake watawaambia: Salaamun Alaikum, (Amani iwe juu yenu!) Mmekua wema. Basi ingieni humu mkae milele.

Wakosefu watapelekwa kwenye Jahannam huku Malaika wa adhabu wakiwasukuma kwa nguvu na kwa udhalili. Wenye takua wanaingia Peponi wakiwa wamezungukwa na Malaika kwa taadhima na takrima na watasema:

Alhamdulillah, (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) aliyetutimizia ahadi yake, na akaturithisha ardhi, tunakaa katika Bustani popote tupendapo. Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao!

Wanaosema hayo ni waumini. Makusudio ya ardhi hapa ni ardhi ya Peponi. Wataitumia kama vile anavyotumia mrithi, mali aliyoachiwa. Kule duniani waliifanyia kazi Pepo wakitegemea na kuamini aliyoahidi Mwenyezi Mungu kwa wenye takua na subira. Watapoiona watafurahia na kumsifu Mwenyezi Mungu wakijua kuwa ahadi yake ni ya kweli na haki.

Imeelezwa kwenye Nahajul-balagha: “Malaika watawazunguka watu Peponi, watawashukia kwa upole, na watawafungulia milango ya mbingu. Watawaandalia sehemu za heshima alizowafahamisha Mwenyezi Mungu, akaridhia mahangaiko na kusifia makazi yao”[2] .

Na utawaona Malaika wakizunguka pembeni mwa Arshi ya Mwenyezi Mungu, wakimsabihi na kumsifu Mola wao.

Katika Juz. 8 (7:53), tumebainisha, kwa ushahidi wa Qur’ani, kuwa Makusudio ya Arshi ni kuwa amri yote ni ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo maana yake hapa ni kuwa Malaika hawafanyi lolote ila kwa amri ya Mwenyezi Mungu; kama ulivyokuja wasifu wao katika kauli yake Mwenyezi Mungu:

بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ ﴿٢٦﴾ لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ ﴿٢٧﴾

“Bali hao ni waja waliotukuzwa. Hawamtangulii kwa neno nao wanafanya kwa amri yake.”

Juz. 17 (21:26-27)

Na patahukumiwa baina yao kwa haki na patasemwa Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote!

Yaani muasi hatazidishiwa adhabu, wala mtiifu hatapunguziwa thawabu. Kuna tafsiri nyingine zinazasema kuwa Mwenyezi Mungu alipoanza kuumba alisema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote.

Baada ya kufa viumbe na kuwafufua na kutulia watu wa peponi atasema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote, ili awafundishe waja wake adabu yake ya kuanza kila jambo kwa sifa njema na kumalizia kwa sifa njema.

MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA TISA: SURAT AZ-ZUMAR


4

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

Sura Ya Arubaini : Surat Al-Ghaafir.

Ina Aya 85. Imeshuka Makka. Imesemekana Aya mbili hazikushuka Makka. Pia inaitwa Sura Mumin

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

حم ﴿١﴾

1. Hamim.

تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٢﴾

2. Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye kujua.

غَافِرِ الذَّنبِ وَقَابِلِ التَّوْبِ شَدِيدِ الْعِقَابِ ذِي الطَّوْلِ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ إِلَيْهِ الْمَصِيرُ ﴿٣﴾

3. Mwenye kughufiria dhambi na anayekubali toba, Mkali wa kuadhibu, Mwenye fadhila. Hakuna mungu ila Yeye. Marejeo ni Kwake.

مَا يُجَادِلُ فِي آيَاتِ اللَّـهِ إِلَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَا يَغْرُرْكَ تَقَلُّبُهُمْ فِي الْبِلَادِ ﴿٤﴾

4. Hawabishani katika Ishara za Mwenyezi Mungu ila wale ambao wamekufuru. Basi kusikughuri kutangatanga kwao katika nchi.

كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَالْأَحْزَابُ مِن بَعْدِهِمْ وَهَمَّتْ كُلُّ أُمَّةٍ بِرَسُولِهِمْ لِيَأْخُذُوهُ وَجَادَلُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ فَأَخَذْتُهُمْ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ ﴿٥﴾

5. Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuh na makundi baada yao. Na kila uma ulikuwa na hamu juu ya Mtume wao wamkamate. Na walibishana kwa upotovu ili kuipindua haki. Kwa hivyo niliwakamata. Basi ilikuwaje adhabu yangu!

وَكَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّهُمْ أَصْحَابُ النَّارِ ﴿٦﴾

6. Namna hivi limewathibitikia makafiri neno la Mola wako kwamba wao ni watu wa Motoni.

MWENYE KUSAMEHE DHAMBI NA KUKUBALI TOBA

Aya 1 – 6

MAANA

Hamim.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1(2:1).

Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa sababu ni mizani ya haki na ya uadilifu na ni nuru inayoongoza kutokana na giza la upotevu na ujinga.

Mwenye nguvu, Mwenye kujua, Mwenye kughufiria dhambi na anayekubali toba, Mkali wa kuadhibu, Mwenye fadhila.

Kila sifa katika wasifu huu ina mfungamano na athari katika ulimwengu na binadamu na mwenendo wake: Mwenye kuumba ulimwengu ni lazima aujue na awe na uweza. Ndio ikaja sifa ya mwenye nguvu mwenye kujua. Kuwa na nguvu ni kuwa na uwezo.

Dhambi na toba ni vitendo vya mtu, lakini kukubali toba na kusamehewa ni kwa Mwenyezi Mungu. Yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t) husamehe kwa toba au kwa utiifu, kwa sababu mema yanafuta maovu. Vile vile Yeye ni mkali kwa anayeng’ang’ania uasi, wakati huohuo yeye ni mwenye fadhila kwa sababu anampa anayemuomba na asiyemuomba na anamuongezea mengi mtenda mema

Hakuna mungu ila Yeye.

Amepwekeka na sifa ya Tawhid, elimu ya ghaibu na uwezo juu ya kila kitu. Wenye madhambi wote wanahitajia msamaha wake na huruma yake.

Marejeo ni kwake.

Hakuna pa kukimbia kuepuka kukutana naye na hisabu yake na malipo yake. Heri zote ni za yule asiyeona yeyote mwenye kustahiki sifa hizi isipokuwa Mwenyezi Mungu, na wala asiogope yeyote asiyekuwa Yeye.

Hawabishani katika Ishara za Mwenyezi Mungu ila wale ambao wamekufuru, wasiotaka haki na uadilifu wala kuamini chochote isipokuwa hawaa na masilahi yao tu.

Pamoja na hayo wanajitafutia visababu, wakidai kuwa wao ndio walio na haki na kuijadili Qur’ani wakisema kuwa ni ngano za watu wa kale, tawhid ni upotevu na kufufuliwa ni uzushi. Dalili yao ya kwanza na ya mwisho ni kuwa wao wanawaiga mababa zao na kufuata masilahi.

Basi kusikughuri - ewe Muhammad -kutangatanga kwao katika nchi kwa ajili ya biashara na kwenda kwao Sham katika msafara wa kusi na Yemen katika msafara wa kaskazi. Yasikughuri haya, kwa sababu mwisho wake ni maangamizi:

إِنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ لِيَزْدَادُوا إِثْمًا وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٧٨﴾

“Hakika tunawapa muda na wanazidi tu katika dhambi na wana adhabu idhalilishayo.”

Juz. 4 (3:178).

Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuh na makundi baada yao. Na kila uma ulikuwa na hamu juu ya Mtume wao wamkamate. Na walibishana kwa upotovu ili kuipindua haki.

Makusudio ya makundi hapa ni kila watu waliounda kikosi dhidi ya haki na watu wake.

Maana ni kuwa vita vyako ewe Muhammad, pamoja na washirikina, sio vita vyako wewe binafsi; isipokuwa ni vita baina ya haki na batili na kufuru na imani. Ni desturi ya waliopita na wanokuja.

Uma zilizopita ziliwakadhibisha mitume na viongozi wema. Wakawajadili kwa ujinga na inadi. Kila uma ulijaribu kumuua Nabii wao na muonyaji wao; sawa na walivyokupangia njama makuraishi ukiwa umelela kitandani mwako.

Tazama Juz. 9 (30 – 35).

Kwa hivyo niliwakamata. Basi ilikuwaje adhabu yangu!

Ilikuwa kali ya kuvunjavunja.

Namna hivi limewathibitikia makafiri neno la Mola wako kwamba wao ni watu wa Motoni.

Haya ni maonyo na hadhari kwa makuraishi kama waking’ang’ania ukafiri na upotevu, yasije yakawapata, yaliyowapata watu wa Nuh, A’d na Thamud.

Lakini kumhofisha asiyemuogopa Mwenyezi Mungu hakuna manufaa yoyote, isipokuwa kusimamisha hoja na kukata visababu vyote.

الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ ﴿٧﴾

7. Wale wanaobeba Arshi, na wanaoizunguka, wanamsabihi kwa kumuhimidi Mola wao, na wanamuamini na wanawaombea msamaha walio amini. Mola wetu! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe ambao wametubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu.

رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدتَّهُمْ وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٨﴾

8. Mola wetu! Na waingize katika Bustani za Milele ulizowaahidi. Na pia waliofanya mema miongoni mwa wazee wao na wake zao na dhuriya zao. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

وَقِهِمُ السَّيِّئَاتِ وَمَن تَقِ السَّيِّئَاتِ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمْتَهُ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿٩﴾

9. Na waepushe na maovu; kwani umwepushaye maovu siku hiyo, hakika umemrehemu; na huko ndiko kufuzu kukubwa.

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنَادَوْنَ لَمَقْتُ اللَّـهِ أَكْبَرُ مِن مَّقْتِكُمْ أَنفُسَكُمْ إِذْ تُدْعَوْنَ إِلَى الْإِيمَانِ فَتَكْفُرُونَ ﴿١٠﴾

10. Kwa hakika wale waliokufuru watanadiwa: Bila ya shaka kuchukia Mwenyezi Mungu ni kukubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu, mlipokuwa mnaitwa kwenye imani mkakataa.

WANAOBEBA ARSHI

Aya 7 – 10

MAANA

Wale wanaobeba Arshi, na wanaoizunguka, wanamsabihi na kumsifu Mola wao, na wanamuamini.

Katika Juz. 8 (7:54), tulisema kuwa makusudio ya kuwa kwenye Arshi ni kutawala. Na katika Aya ya 75 ya sura iliyopita, tukasema kuwa makusudio ya Malaika kuizunguka Arshi ni kuwa hawamtangulii Mwenyezi Mungu kwa kauli na wanafanya kwa amri yake. Nasi tuna mategemeo kuwa kauli yetu hii, kwa kulinganisha na mfumo wa maneno, inaendana na tafsiri hii.

Ama mfumo wa Aya hii tuliyo nayo na ile inayosema: “Na wanane juu ya wao watachukua Arshi ya Mola wako” (69:17) unatufanya tutafute maana nyingine ya Arshi inayochukuliwa; ingawaje kuchukua Malaika Arshi hakulazimishi kuwa Mungu amekaa juu yake.

Ikiwa hivyo basi itabidi Mwenyezi Mungu awe ana mwili na pia awe yuko mahali fulani na kwengine hayuko.

Ikiwa utauliza : Kama Mwenyezi Mungu hakukaa katika Arshi (kiti cha enzi), kwa nini basi ikanasibishwa kwake, na kusemwa ‘Arshi ya Mola wako.’

Jibu : suala la kunasibisha ni la kawaida na jepesi sana; kwa mfano inaweza kuitwa barabara ya fulani, wakati huyo fulani mwenyewe hata haijui barabara hiyo; sembuse muumba wa ulimwengu wote? Majumba yote ya kuabudu mashariki na magharibi, sikwambii Al-Kaaba tukufu, yanaitwa ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hiyo inamaanisha kuwa Mwenyezi Mungu anaishi humo?

Inawezekana kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametengeneza Arshi na kuamrisha Malaika wake waizunguke; kama alivyomwamrisha Ibrahim kujenga nyumba kongwe na kulazimisha kuizuru na kuizunguka kila mwenye kuweza kuifika.

Vyovyote iwavyo ni kuwa Malaika wanamwamini Mwenyezi Mungu na kumtukuza kwa kumsifuna wanawaombea msamaha walio amini kwa kusema:Mola wetu! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe ambao wametubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu.

Waumini wenye ikhlasi wana aina nyingi ya malipo; zikiwemo Bustani zinazopitiwa na mito chini yake, kuwa marafiki wa manabii na mashahidi na kwamba Malaika wanawatukuza kwa kuwasifu na kuwaombea Mungu wawe na daraja ya juu na kukingwa na ghadhabu yake na adhabu yake.

Mola wetu! Na waingize katika Bustani za Milele ulizowaahidi. Na pia waliofanya mema miongoni mwa wazee wao na wake zao na dhuriya zao. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Malaika watamuomba Mwenyezi Mungu kesho awakusanye familia kwenye Pepo yake; kama walivyokuwa duniani ili wazidi kuwa na furaha. Kauli yake: ‘waliofanya mema,’ inaashiria kukatika udugu baina ya mumin na kafiri, hata kama mmoja ni baba wa mwingine;

فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ فَلَا أَنسَابَ بَيْنَهُمْ يَوْمَئِذٍ ﴿١٠١﴾

“Basi itakapopuziwa parapanda, hapo hakutakuwa na nasaba baina yao.” Juz. 18 (23:101).

الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ ﴿٦٧﴾

“Siku hiyo marafiki watakuwa maadui wao kwa wao isipokuwa wenye takua” (43:67).

Na waepushe na maovu; kwani umwepushaye maovu siku hiyo, hakika umemrehemu; na huko ndiko kufuzu kukubwa.

Wakinge na kila ubaya siku ya kiyama. Hakuna mwenye shaka kwamba mwenye kupata daraja hii mbele ya Mwenyezi Mungu atakuwa amefuzu fadhila zake na rehema zake.

Kwa hakika wale waliokufuru watanadiwa: Bila ya shaka kuchukia Mwenyezi Mungu ni kukubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu, mlipokuwa mnaitwa kwenye imani mkakataa.

Watu wa motoni watachukia wakiwa humo ndani kutokana na yaliyowaleta humo. Huko duniani walikuwa wakiyapenda na kuyaridhia. Mwito utawajia huku wakijilaani wenyewe kuwa, alivyokuwa Mwenyezi Mungu akichukia kufuru yenu duniani ni zaidi sana ya mnavyojichukia nyinyi hivi sasa. Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwalingani kupitia mitume wake, lakini mkakataa isipokuwa ukafiri. Basi onjeni adhabu leo, na madhalimu hawana msaidizi.

قَالُوا رَبَّنَا أَمَتَّنَا اثْنَتَيْنِ وَأَحْيَيْتَنَا اثْنَتَيْنِ فَاعْتَرَفْنَا بِذُنُوبِنَا فَهَلْ إِلَىٰ خُرُوجٍ مِّن سَبِيلٍ ﴿١١﴾

11. Watasema: Mola wetu! Umetufisha mara mbili, na umetuhuisha mara mbili! Basi tunakiri madhambi yetu. Basi je, ipo njia ya kutoka?

ذَٰلِكُم بِأَنَّهُ إِذَا دُعِيَ اللَّـهُ وَحْدَهُ كَفَرْتُمْ وَإِن يُشْرَكْ بِهِ تُؤْمِنُوا فَالْحُكْمُ لِلَّـهِ الْعَلِيِّ الْكَبِيرِ ﴿١٢﴾

12. Hayo ni kwa sababu alipoombwa Mwenyezi Mungu peke yake mlikataa. Na akishirikishwa mnaamini. Basi hukumu ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Mkubwa.

هُوَ الَّذِي يُرِيكُمْ آيَاتِهِ وَيُنَزِّلُ لَكُم مِّنَ السَّمَاءِ رِزْقًا وَمَا يَتَذَكَّرُ إِلَّا مَن يُنِيبُ ﴿١٣﴾

13. Yeye ndiye ambaye anawaonyesha Ishara zake, na anawateremshia riziki kutoka mbinguni. Na hapana anayekumbuka ila anaye rejea.

فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ ﴿١٤﴾

14. Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye, wajapochukia makafiri.

رَفِيعُ الدَّرَجَاتِ ذُو الْعَرْشِ يُلْقِي الرُّوحَ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ لِيُنذِرَ يَوْمَ التَّلَاقِ ﴿١٥﴾

15. Ndiye Mwenye daraja za juu. Mwenye Arshi. Hupeleka Roho, kwa amri yake, juu ya amtakaye katika waja wake, ili kuonya Siku ya kukutana.

يَوْمَ هُم بَارِزُونَ لَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّـهِ مِنْهُمْ شَيْءٌ لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْمَ لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ ﴿١٦﴾

Siku watakayodhihiri wao. Hapana kitachofichikana chochote chao kwa Mwenyezi Mungu. Ufalme ni wa nani leo? Ni wa Mwenyezi Mungu Mmoja Mtenza nguvu.

الْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٧﴾

17. Leo kila nafsi italipwa kwa iliyoyachuma. Hapana dhulma leo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.

UMETUFISHA MARA MBILI NA UMETUHUISHA MARA MBILI

Aya 11 – 17

MAANA

Watasema: Mola wetu! Umetufisha mara mbili, na umetuhuisha mara mbili! Basi tunakiri madhambi yetu. Basi je, ipo njia ya kutoka?

Watakaosema hivyo ni watu wa motoni. Mauti ya kwanza ni kabla ya kuto- ka matumboni mwa mama zao na ya pili ni haya mauti yaliyozoeleka. Uhai wao wa kwanza ni uhai wa duniani na wa pili ni wa ufufuo baada ya mauti.

Maana ni kuwa watu wa Jahannam, wakiwa katikati ya moto wakiadhibi- wa, watamnyenyekea Mwenyezi Mungu huku wakisema: Ewe Mola wetu! Wewe ni muweza wa kila kitu. Ulituleta duniani, ukatutoa kwenye mauti, kisha ukatufufua baada yake.

Hivi sasa tuko mbele yako tukijuta na kukiri makosa na dhambi zetu. Je, kuna njia yoyote, kutokana na karama yako, kutuwezesha kutoka motoni, tukikuahidi utiifu na kufuata amri?

Hayo ni kwa sababu alipoombwa Mwenyezi Mungu peke yake mlikataa. Na akishirikishwa mnaamini.

Hili ni jawabu la kauli yao ‘Je, ipo njia ya kutokea?’ Ufupisho wa jawabu ni kuwa mlinganiaji haki aliwapa mwito wa haki, duniani, mkaukataa. Na mlinganiaji shetani aliwapa mwito mkaukubali. Hivi sasa mnaita hamtajibiwa.

Kauli yake Mwenyezi Mungu:Basi hukumu ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Mkubwa, inaashiria kuwa kesho hukumu ni ya Mwenyezi Mungu tu peke yake, hakuna mkubwa isipokuwa Yeye tu:

وَعَنَتِ الْوُجُوهُ لِلْحَيِّ الْقَيُّومِ وَقَدْ خَابَ مَنْ حَمَلَ ظُلْمًا ﴿١١١﴾

“Zitanyenyekea nyuso kwa aliye Hai, Mwangalizi Mkuu. Na hakika ameharibikiwa mwenye kubeba dhulma.” Juz. 16 (20:111).

Yeye ndiye ambaye anawaonyesha Ishara zake, na anawateremshia riziki kutoka mbinguni. Na hapana anayekumbuka ila anayerejea.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametuonyesha ushahidi mwingi juu ya kuweko kwake, utukufu wake, dalili za upangiliaji wake na hekima yake katika mbingu, ardhi, watu, wanyama na hata katika mvua na mimea na mengingineyo yasiyokuwa na ukomo.

Ilivyo ni kuwa dalili hizi, pamoja na wingi wake, hazijitokezi ila kwa mwenye busara na kufikiria, lakini mpofu wa moyo hayaoni hayo. Anasema Tagore:

“Hakika Mwenyezi Mungu anadhihirisha kuweko kwake katika mfumo hai wa sura mbali mbali za maumbile. Ameudhihirisha kwenye mfumo ulioko baina ya nguvu za maumbile zinazopambana katika umoja wao kwenye kanuni iliyopangiliwa isiyoepukika, wakati huo huo zikielekea kuhakikisha malengo. Kila kitu katika maumbile kina wadhifa wake maalum na malengo maulumu yaliyopangiliwa. Mbegu inafanya kazi kwa bidii ili itoe mti, mti nao unajitihidi ili utoe mau na maua nayo yana kazi ya kutoa tunda. Haya hawezi kuyatambua isipokuwa mwenye moyo ulio salama.”

Makusudio ya mwenye moyo salama ndio yale hasa yaliyokusudiwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na hapana anayekumbuka ila anayerejea.’

Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye, wajapochukia makafiri.

Wanaambiwa waumini. Makusudio ya kuomba hapa ni ibada na dini ni utiifu. Maana ni kuwa mwabuduni Mwenyezi Mungu peke yake na mumtii katika amri zake na makatazo yake, wala msijali lawama. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewasahilishia waja wake njia ya kumtii, pale alipowaongoza akiwahadharisha, akawakalifisha kwa wepesi; na hakumwachia udhuru mwenye kutafuta visababu.

Ndiye Mwenye daraja za juu.

Hiki ni kinaya cha utukufu wake. Imesemekana kuwa Makusudio ya daraja hapa ni tofauti ya wanaomojua Mungu katika maarifa yao.

Kuanzia maarifa ya mtu wa kawaida hadi maarifa ya wanafilosofia na manabii.

Mwenye Arshi.

Ni kinaya cha umiliki na utawala.

Hupeleka Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake, ili kuonya Siku ya kukutana.

Makusdio ya roho hapa ni wahyi. Siku ya kukutana ni Siku ya Kiyama ambapo kila mtu atakutana na malipo ya amali yake. Na makusudio ya kuonya siku hii ni kuonya adhabu. Imekuja ibara ya kuwa Yeye Mwenyezi Mungu ndiye muonyaji, kutokana na ukali na vituko vya siku hiyo.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamteremshia wahyi anayemtaka katika waja wake, ili awaonye watu, kwamba wao watafufuliwa baada ya mauti, katika siku ambayo itakuwa mbaya kwa wenye kuvuka mipaka na waasi na kuulizwa yale waliyokuwa wakiyafanya.

Siku watakayodhihiri wao.

Yaani itadhihiri hakika yao.

Hapana kitachofichikana chochote chao kwa Mwenyezi Mungu.

Huu ni ubainfu wa kauli ya: ‘Siku watakayodhihiri.’

Ufalme ni wa nani leo?

Wataulizwa siku ya kiyama, wakiwa wametokeza kwa ajili ya hukumu: amri na hukumu ni ya nani? Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawajibia, kwa sababu jawabu liko wazi.

Au wao wenyewe watajibu kihali na kimaneno kuwa:Ni wa Mwenyezi Mungu Mmoja Mtenza nguvu waja.

Leo kila nafsi italipwa kwa iliyoyachuma. Hapana dhulma leo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.

Aya hii iko wazi, na imetangulia katika Juz. 13 (14:51).


5

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْآزِفَةِ إِذِ الْقُلُوبُ لَدَى الْحَنَاجِرِ كَاظِمِينَ مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ ﴿١٨﴾

18. Na waonye siku inayokaribia, wakati nyoyo zitakapofika kooni, nao wamejaa huzuni. Madhalimu hawatakuwa na rafiki, wala mwombezi wa kuitikiwa.

يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ ﴿١٩﴾

19. Anajua hiyana ya macho na yanayoficha vifua.

وَاللَّـهُ يَقْضِي بِالْحَقِّ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَقْضُونَ بِشَيْءٍ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿٢٠﴾

20. Na Mwenyezi Mungu huhukumu kwa haki. Na wale ambao wanaomba kinyume chake hawahukumu chochote. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye Kusikia, Mwenye kuona.

أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ كَانُوا مِن قَبْلِهِمْ كَانُوا هُمْ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَآثَارًا فِي الْأَرْضِ فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْ وَمَا كَانَ لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مِن وَاقٍ ﴿٢١﴾

21. Je, hawatembei katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa waliokuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao na athari katika nchi. Na Mwenyezi Mungu aliwakamata kwa sababu ya madhambi yao. Na wala hapakuwa wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu.

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَكَفَرُوا فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ إِنَّهُ قَوِيٌّ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢٢﴾

22. Hayo ni kwa sababu walikuwa wanawajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, lakini wakawakataa, ndipo Mwenyezi Mungu akawakamata. Bila ya shaka Yeye ni Mwenye nguvu, Mkali wa kuadhibu.

WAONYE SIKU INAYOKURUBIA

Aya 18 – 22

MAANA

Na waonye siku inayokaribia, wakati nyoyo zitakapofika kooni, nao wamejaa huzuni. Madhalimu hawatakuwa na rafiki, wala mwombezi wa kuitikiwa.

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume(s.a.w. w ) na wanaotakiwa kuonywa ni washirikina wa kiarabu. Maana ni kuwa kazi yako ewe Muhammad ni kuwaonya washirikina na adhabu ya siku ambayo nyoyo zitayeyuka kwa fazaa; ambapo hakutakuwa na rafiki wala mwombezi. Na siku hii iko karibu tu bila shaka itafika.

Mwenyezi Mungu anajua hiyana ya macho na yanayoficha vifua. Na Mwenyezi Mungu huhukumu kwa haki.

Hakuna jambo alilolidhamiria mtu au kuliangalia kwa jicho la hiyana, ila Mwenyezi Mungu atakuwa analijua na atalitolea hukumu kesho kwa ilimu yake na uadilifu, kwa kila mhaini mwenye hatia. Hukumu yake itakuwa ya mwisho haina rufaa.

Na wale ambao wanaomba kinyume chake Mwenyezi Mungu hawahukumu chochote.

Makusudio ya kinyume chake ni kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu wanchokiabudu watu; iwe ni sanamu, mali, cheo au mengineyo.

Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye Kusikia, Mwenye kuona.

Hii ni ibara nyingine baada ya ile isemayo:

وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا ﴿١٢﴾

“Na kwamba Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kwa elimu.” (65:12).

Je, hawatembei katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa waliokuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao na athari katika nchi. Na Mwenyezi Mungu aliwakamata kwa sababu ya madhambi yao. Na wala hapakuwa wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu.

Huku ni kutahadharishwa kunakotoka kwa Mwenyezi Mungu kwa wakosefu, kwamba mwisho wao utakuwa kama mwisho wa waliokuwa kabla yao. Walikuwa wengi na wenye mali nyingi, lakini ilipokuja adhabu hawakupata wa kuwasaidia wala wa kuwalinda. Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (12:109), Juz. 17 (22:46), Juz. 21 (30:9) na Juz. 22 (35:44).

Hayo ni kwa sababu walikuwa wanawajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, lakini wakawakataa, ndipo Mwenyezi Mungu akawakamata. Bila ya shaka Yeye ni Mwenye nguvu, Mkali wa kuadhibu.

Yametangulia maelezo mara nyingi, kwamba mwisho wa waliokadhibisha mitume ni kuvunjika na kubomoka. Kesho hakutakuwa na tofauti baina ya waliowakataa mitume na wale waliowamini lakini wakahalifu mafunzo yao na wakazima desturi zao; hata kama duniani watachukuliwa kuwa ni waislamu.

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٢٣﴾

23. Na kwa hakika tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na hoja zilizo wazi.

إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَقَارُونَ فَقَالُوا سَاحِرٌ كَذَّابٌ ﴿٢٤﴾

24. Kwa Firauni na Hamana na Qaruni. Wakasema: “Ni mchawi, mwongo mkubwa.

فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْحَقِّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا اقْتُلُوا أَبْنَاءَ الَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ وَاسْتَحْيُوا نِسَاءَهُمْ وَمَا كَيْدُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَالٍ ﴿٢٥﴾

25. Basi alipowaletea Haki inayotoka kwetu, walisema: ‘Waueni watoto wanaume wa wale waliomuamini na wawacheni hai wanawake wao.’ Na haviwi vitimbi vya makafiri ila katika upotovu.

وَقَالَ فِرْعَوْنُ ذَرُونِي أَقْتُلْ مُوسَىٰ وَلْيَدْعُ رَبَّهُ إِنِّي أَخَافُ أَن يُبَدِّلَ دِينَكُمْ أَوْ أَن يُظْهِرَ فِي الْأَرْضِ الْفَسَادَ ﴿٢٦﴾

26. Na Firauni akasema: Niachieni nimuuwe Musa, naye amwite Mola wake! Hakika Mimi nachelea asije kubadilisha dini yenu, au akadhihirisha uharibifu katika nchi.

وَقَالَ مُوسَىٰ إِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُم مِّن كُلِّ مُتَكَبِّرٍ لَّا يُؤْمِنُ بِيَوْمِ الْحِسَابِ ﴿٢٧﴾

27. Na Musa akasema: Hakika Mimi najikinga kwa Mola wangu na Mola wenu anilinde na kila mwenye kiburi asiyeiamini Siku ya Hisabu.

وَقَالَ رَجُلٌ مُّؤْمِنٌ مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَكْتُمُ إِيمَانَهُ أَتَقْتُلُونَ رَجُلًا أَن يَقُولَ رَبِّيَ اللَّـهُ وَقَدْ جَاءَكُم بِالْبَيِّنَاتِ مِن رَّبِّكُمْ وَإِن يَكُ كَاذِبًا فَعَلَيْهِ كَذِبُهُ وَإِن يَكُ صَادِقًا يُصِبْكُم بَعْضُ الَّذِي يَعِدُكُمْ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ كَذَّابٌ ﴿٢٨﴾

28. Na akasema mtu mmoja Muumini, katika watu wa Firauni, anayeficha Imani yake: Mtamuuwa mtu kwa sababu anasema Mola wangu ni Mwenyezi Mungu? Na hali amewajia na hoja zilizo wazi? Na akiwa ni mwongo basi uwongo wake ni juu yake mwenyewe, na akiwa ni mkweli yatawafika baadhi ya hayo anayowaahidi; Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi apindukiaye mipaka, mwongo mkubwa.

يَا قَوْمِ لَكُمُ الْمُلْكُ الْيَوْمَ ظَاهِرِينَ فِي الْأَرْضِ فَمَن يَنصُرُنَا مِن بَأْسِ اللَّـهِ إِن جَاءَنَا قَالَ فِرْعَوْنُ مَا أُرِيكُمْ إِلَّا مَا أَرَىٰ وَمَا أَهْدِيكُمْ إِلَّا سَبِيلَ الرَّشَادِ ﴿٢٩﴾

29. Enyi watu wangu! Leo mna ufalme, mmeshinda katika nchi; basi ni nani atakayetusaidia kutuokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu kama ikitufikia? Firauni akasema: Siwapi rai ila ile niliyoiona, wala siwaongozi ila kwenye njia ya uwongofu.

MUSA

Aya 23 – 29

MAANA

Maelezo kuhusiana na Musa yamepita mara kadhaa, tukiwa tunaashiria jina la sura na Aya iliyopita kila inapokuja Aya nyingine. Hivi sasa kimerudi kisa cha Musa na kitaendelea kurudi kwenye Aya za mbele.

Katika Juz. 16 (20:9 – 16) kifungu cha ‘kukaririka kisa’ tumebainisha sababu za kukaririka huku. Na hivi sasa tunaunganisha tuliyoyabainisha huko na hapa; kwamba sio mbali kuwa kila Aya, hata kama ikikaririka, huwa inatoa mwanga mpya uliofichika kwetu, kwa kuwa sisi hatukufikia utafiti wake au hatukuwa na uwezo wa kuutambua. Vyovyote iwavyo, jipya katika Aya hizi tulizo nazo sasa, ni kuwa zinamzungumzia mumin wa watu wa Firauni.

Na kwa hakika tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na hoja zilizo wazi, kwa Firauni na Hamana na Qaruni,

Hamana ni waziri wa Firauni na Qaruni alikuwa tajiri mkubwa kuliko wote wakati wa Firauni. Inasemekana alikuwa waziri wa fedha wa utawala wa Firauni. Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimtuma Musa kwa watu wote wa zama zake. Wamehusishwa kutajwa hawa watatu, kwa sababu wao ndio msingi wa ufisadi na chimbuko la upotevu. Kama wangeliamini hawa, basi wangeliamini wote.

Wakasema: Ni mchawi, mwongo mkubwa; sawa na walivyosema waliokuwa kabla yao na baada yao, kumwambia kila anyayewajia na ubainifu na hoja.

Basi alipowaletea Haki inayotoka kwetu, walisema: Waueni watoto wanaume wa wale waliomuamini na wawacheni hai wanawake wao.

Aliamrisha kuuliwa watoto wa kiume kwa kuwahofia na kuwabakisha wa kike kwa ajili ya kuwahudumia. Unaweza kuuliza: Firauni alitoa amri hii kabla ya kuzaliwa Musa. Je kuna makusudio gani ya kukaririka tena?

Baadhi ya wafasiri wamejibu kuwa Firauni alizuia kuuliwa watoto baada ya kuzaliwa Musa, lakini Musa alipotumwa na Mwenyezi Mungu, Firauni alirudia kuua. Kauli hii inahitaji kuthibitishwa. Sio mbali kuwa amri ya pili ya kuua ni kuendeleza ile amri ya kwanza; kwamba kuua kuendelee tu wala kusisimamishwe kwa hali yoyote.

Na haviwi vitimbi vya makafiri ila katika upotovu.

Yaani: “Na vitimbi viovu havimpati ila mwenyewe. Basi hawangoji ila desturi ya wa zamani.” Juz. 22 (35:43).

Na Firauni akasema: Niachieni nimuuwe Musa, naye amwite Mola wake!

Hii inaashiria kuwa badhi ya watu wa Firauni walimshauri asimuue Musa kwa kuhofia Mola wake atalipiza kisasi.

Firauni aliendelea kusema:Hakika Mimi nachelea asije kubadilisha dini yenu, au akadhihirisha uharibifu katika nchi.

Firauni ni mzuri kwa vile yeye anasema, mimi ndiye mola wenu mkuu na mimi simjui Mungu mwingine kwenu zaidi yangu. Na Musa ni mharibifu kwa vile yeye ana mwito wa kuwakomboa watu kwenye utumwa wa watu wengine! Haya siyo mageni. Ndio mantiki ya viongozi wa mabavu kila wakati na kila mahali.

Na Musa akasema: Hakika Mimi najikinga kwa Mola wangu na Mola wenu anilinde na kila mwenye kiburi asiyeiamini Siku ya Hisabu.

Musa anajilinda kwa Mwenyezi Mungu asiwe na kiburi na kutomwogopa Mwenyezi Mungu na hisabu yake na adhabu yake. Kwa sababu mtu duni zaidi ni yule aliye na mambo haya mawili.

Na akasema mtu mmoja Muumini, katika watu wa Firauni, anayeficha Imani yake: Mtamuuwa mtu kwa sababu anasema Mola wangu ni Mwenyezi Mungu? Na hali amewajia na hoja zilizo wazi?

Haki huwa haikosi mtetezi, ijapokuwa ni kwaneno la ikhlasi linaloelekezwa kwa watu wa batili na upotevu. Huyu hapa mtu katika watu wa Firauni, aliyemwamini Mwenyezi Mungu kwa ukweli na yakini, lakini alificha imani yake, kwa kuhofia kuuliwa.

Firauni alipotaka kumfanyia shari Musa, imani halisi iliugusa moyo wake, kiasi cha kulipinga hilo na kulihadharisha, lakini kwa mfumo wa kiakili na kihekima, akasema: Amekosa nini mtu huyu mpaka akastahiki kuuliwa? Ni kwa vile tu amesema: Mola wangu ni Mwenyezi Mungu, akiwa na hoja mkataa zilizowaziba mdomo na kuwashinda; kama vile mkono mweupe na fimbo iliyomeza mliyokuwa mkiyazua?

Sheikh Maraghi, katika tafsiri yake, anasema, ninamnukuu: “Mtu mmoja mumin ni binamu yake Firauni, mrithi wake na mkuu wa polisi. Huyu aliokoka pamoja na Musa. Na ndiye aliyekusudiwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَجَاءَ مِنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ رَجُلٌ يَسْعَىٰ قَالَ يَا قَوْمِ اتَّبِعُوا الْمُرْسَلِينَ ﴿٢٠﴾

“Na akaja mtu mbio kutoka upande wa mbali wa mjini” Juz. 22 (36:20).

Ikumbukwe kwamba Sheikh Maraghi alipokuwa akifasiri sura Yasin alisema kuwa mtu huyu aliyekuja mbio kutoka mjini alikuwa katika zama za Isa; kama walivyosema hivyo wafasiri wengineo. Sasa ni nani aliyemfufua wakati wa Musa, ambapo kati yake na Isa kuna zaidi ya miaka 1200; kama walivyosema wanahistoria? Lakini wasiokosea ni wale maasum (waliohifadhiwa na makosa).

Na akiwa ni mwongo basi uwongo wake ni juu yake mwenyewe, mwacheni na uwongo wakena akiwa ni mkweli yatawafika baadhi ya hayo anayowaahidi; iwe mtamuua au mtamuacha. Alisema baadhi ya anayowaahidi na wala hakusema yote anayowaahidi, kwa sababu baadhi yanatosha kuangamiza.

Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi apindukiaye mipaka, mwongo mkubwa.

Mmedai kuwa yeye ni mwongo, basi mwacheni apate malipo ya uwongo. Hapa kuna ishara kuwa wasifu huu ni wa Firauni na kwamba yeye atapambana na malipo ya uwongo wake na kupaetuka kwake mipaka tu.

Enyi watu wangu! Leo mna ufalme, mmeshinda katika nchi; basi ni nani atakaye tusaidia kutuokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu kama ikitufikia?

Bado maneno yanatoka kwa mumin kuwaambia watu wake, watu wa Firauni. Maana yake ni kuwa, nyinyi hivi sasa mko katika amani na mnao ufalme ulioshinda. Basi neema hii aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu, msiiondoe kwa kumuua anayesema Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu. Basi ni nani atakayetuokoa na uovu wake akitujia usiku au mchana?

Kwa ufupi ni kuwa mumin alimkinga Musa kwa njia nzuri na akawajadili maadui wa Mungu kwa hekima na mawaidha mazuri; kwanza alimwepusha Musa na makosa. Pili akawatishia maadui zake kwa hatari na madhara. Tatu akawakumbusha neema ya Mwenyezi Mungu kwao na akawahadhrisha wasiibadilishe na kufuru.

Kwa mfumo huu aliweza kubadilisha azma ya taghuti na kushikilia kwake kumuua Musa, mpaka Firauni akasema:

Siwapi rai ila ile niliyoiona, wala siwaongozi ila kwenye njia ya uwongofu.

Kauli hii ya Firauni inafanana na kuomba msamaha kutokana na yale aliyoyaazimia, kumuua Musa. Na hiyo ni kutokana na nasaha za mumin. Maana ni kuwa mimi sikutoa shauri ya kumuua Musa ila baada ya kufikiria vizuri; na sikutaka haya ila kwa masilahi yenu.


6

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَقَالَ الَّذِي آمَنَ يَا قَوْمِ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُم مِّثْلَ يَوْمِ الْأَحْزَابِ ﴿٣٠﴾

30. Na akasema yule aliyeamini: Enyi watu wangu! Hakika mimi nawahofia mfano wa siku za makundi.

مِثْلَ دَأْبِ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَالَّذِينَ مِن بَعْدِهِمْ وَمَا اللَّـهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعِبَادِ ﴿٣١﴾

31. Mfano wa hali ya watu wa Nuh na A’di na Thamudi na wale wa baada yao. Na Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu waja.

وَيَا قَوْمِ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ يَوْمَ التَّنَادِ ﴿٣٢﴾

32. Na enyi watu wangu! Hakika mimi nawahofia Siku ya kunadi.

يَوْمَ تُوَلُّونَ مُدْبِرِينَ مَا لَكُم مِّنَ اللَّـهِ مِنْ عَاصِمٍ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ ﴿٣٣﴾

33. Siku mtakapogeuka kurudi nyuma, hamtakuwa na wa kuwalinda kwa Mwenyezi Mungu. Na ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, basi huyo hana wa kumwongoa.

وَلَقَدْ جَاءَكُمْ يُوسُفُ مِن قَبْلُ بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا زِلْتُمْ فِي شَكٍّ مِّمَّا جَاءَكُم بِهِ حَتَّىٰ إِذَا هَلَكَ قُلْتُمْ لَن يَبْعَثَ اللَّـهُ مِن بَعْدِهِ رَسُولًا كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ مُّرْتَابٌ ﴿٣٤﴾

34. Na alikwishawajia Yusuf zamani kwa dalili zilizo wazi, lakini nyinyi mliendelea katika shaka kwa yale aliyowaletea; mpaka alipokufa mkasema: Mwenyezi Mungu hataleta tena Mtume baada yake. Kama hivyo Mwenyezi Mungu humpoteza yule aliyepita kiasi mwenye shaka.

الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّـهِ بِغَيْرِ سُلْطَانٍ أَتَاهُمْ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ وَعِندَ الَّذِينَ آمَنُوا كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ قَلْبِ مُتَكَبِّرٍ جَبَّارٍ ﴿٣٥﴾

35. Wale ambao wanajadiliana katika Ishara za Mwenyezi Mungu bila ya dalili yoyote iliyowafikia, ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya walioamini. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu apigavyo chapa juu ya kila moyo wa jeuri anayejivuna.

MWENYEZI MUNGU HADHULUMU WAJA

Aya 30 – 35

MAANA

Na akasema yule aliyeamini: Enyi watu wangu! Hakika mimi nawahofia mfano wa siku za makundi. Mfano wa hali ya watu wa Nuh na A’di na Thamudi na wale wa baada yao.

Makusudio ya makundi hapa ni watu waliounda vikundi dhidi ya mitume wao; kwa dalili ya kauli yake: “Mfano wa hali ya watu wa Nuh na A’di na Thamudi na wale wa baada yao.”

Aliposema Firauni: ‘Wala siwaongozi ila kwenye njia ya uongofu’ yule mumin naye akasema: ‘mimi vile vile si kusema niliyowaambia ila kwa kuhofia yasiwapate maangamizi kama yalivyowapata wa mwanzo, pale walipowakadhibisha manabii wao.

Na Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu waja, lakini wao wenyewe wanajidhulumu kwa kuwakadhibisha mitume na kuifanyia jeuri amri ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya yule mumin kuwahadharisha na adhabu ya dunia, aliwahadharisha na adhabu ya Akhera kwa kusema:

Na enyi watu wangu! Hakika mimi nawahofia Siku ya kunadi.

Siku ya kunadi ni Siku ya Kiyama, ambapo watu watanadiwa kwa ukulele; kama ilivyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

يَوْمَ يُنَادِ الْمُنَادِ مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ ﴿٤١﴾

“Siku atakaponadi mwenye kunadi kutoka mahali karibu” (50:41).

Siku mtakapogeuka kurudi nyuma mkijaribu kukimbia adhabu ya moto, lakini wapi! Hamtakuwa na wa kuwalinda kwa Mwenyezi Mungu.

Vipi mtaweza kumkimbia na hali yeye ndiye mwenye nguvu, kwenye jambo lake, hapingwi wala hazuiwi.

Na ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, basi huyo hana wa kumwongoa.

Yaani atakayefuata njia ya upotevu basi Mwenyezi Mungu atampoteza; kama vile anayekunywa sumu, Mwenyezi Mungu atamuua tu, wala hutap- ata atakayemponesha na kumpa uhai.

Na alikwishawajia Yusuf zamani kwa dalili zilizo wazi, lakini nyinyi mliendelea katika shaka kwa yale aliyowaletea.

Yaani enyi wamisr! Yusuf aliwajia mababa zenu, wakatia shaka utume wake; kama hivyo nanyi mnatia shaka utume wa Musa. Katika Kamusi ya Kitabu kitakatifu, imeelezwa kuwa Yusuf ni jina la kiibrania (Hebrew) lenye maana ya anayezidisha. Mama yake alimwita hivyo, ili apate ziada ya mtoto mwingine. Naye alikufa akiwa na miaka 110.

Mpaka alipokufa mkasema: Mwenyezi Mungu hataleta tena Mtume baada yake.

Hii inaashiria kuwa wao walifurahi kwa kufa Yusuf, kwa vile watakuwa huru na taklifa za Mwenyezi Mungu. Wakasema bila ya kujali, kwa msukumo wa matamanio kwamba Mwenyezi Mungu hatapeleka tena Mtume baada ya Yusuf mpaka Siku ya Mwisho.

Kama hivyo Mwenyezi Mungu humpoteza yule aliyepita kiasi mwenye shaka kuhusu Mwenyezi Mungu na haki. Mwenyezi Mungu anampoteza mwenye kupita kiasi, kwa sababu ametoka katika uongofu na akaingia kwenye upotevu kwa uchaguzi wake mbaya na upofu.

Wale ambao wanajadiliana katika Ishara za Mwenyezi Mungu bila ya dalili yoyote iliyowafikia.

Makusudio ya wale wanaojadiliana ni wale wenye kupita kiasi wenye shaka. Ishara za Mwenyezi Mungu ni dalili za umoja wake, unabii wa mananbii wake na hoja wazi. Maana ni kuwa wakosefu wanajibu hoja za Mwenyezi Mungu kwa matamanio yao na kuiga mababa zao.

Ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya walioamini kujadili wakosefu bila ya ujuzi wala mwongozo au kitabu.

Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu apigavyo chapa juu ya kila moyo wa jeuri anayejivuna.

Kiburi na kujidai ndio sababu hasa ya kupigwa chapa moyoni. Hilo limetegemezwa kwa Mwenyezi Mungu kwa vile Yeye ndiye aliyejaalia kiburi kuwa ndio sababu ya upofu wa moyo; sawa na alivyoujaalia ujinga kuwa ndio sababu ya kudangana na kuwa mbali na haki na akajaalia kusoma na kufanya utafiti ni sababu ya elimu na mwamko.

وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَّعَلِّي أَبْلُغُ الْأَسْبَابَ ﴿٣٦﴾

36. Na Firauni akasema: Ewe Hamana! Nijengee mnara ili nipate kuzifikia njia.

أَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ كَاذِبًا وَكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِفِرْعَوْنَ سُوءُ عَمَلِهِ وَصُدَّ عَنِ السَّبِيلِ وَمَا كَيْدُ فِرْعَوْنَ إِلَّا فِي تَبَابٍ ﴿٣٧﴾

37. Njia za mbinguni ili nikamwone Mungu wa Musa. Na kwa hakika mimi bila ya shaka namjua kuwa ni mwongo tu. Na hivi ndivyo Firauni alivyopambiwa ubaya wa vitendo vyake, na akazuiliwa Njia. Na vitimbi vya Firauni havikuwa ila katika kuangamia tu.

وَقَالَ الَّذِي آمَنَ يَا قَوْمِ اتَّبِعُونِ أَهْدِكُمْ سَبِيلَ الرَّشَادِ ﴿٣٨﴾

38. Na yule ambaye aliamini alisema: Enyi watu wangu! Nifuateni, nitawaongoza njia ya uongofu.

يَا قَوْمِ إِنَّمَا هَـٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا مَتَاعٌ وَإِنَّ الْآخِرَةَ هِيَ دَارُ الْقَرَارِ ﴿٣٩﴾

39. Enyi watu wangu! Hakika maisha haya ya dunia ni starehe yenye kupita tu, na hakika Akhera ndiyo nyumba ya daima.

مَنْ عَمِلَ سَيِّئَةً فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ يُرْزَقُونَ فِيهَا بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٤٠﴾

40. Mwenye kutenda uovu hatalipwa ila sawa na huo, na mwenye kutenda wema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi, waruzukiwe humo bila ya hisabu.

NIZIFIKIE NJIA

Aya 36 – 40

MAANA

Na Firauni akasema: Ewe Hamana! Nijengee mnara ili nipate kuzifikia njia. Njia za mbinguni ili nikamwone Mungu wa Musa. Na kwa hakika mimi bila ya shaka namjua kuwa ni mwongo tu.

Firauni alimtaka waziri wake Hamana amjengee mnara mrefu ili apande mbinguni kwenda kumtafuta Mungu wa Musa. Alifanya hivi akiwa anajua kabisa kwamba yeye hawezi kufanya hivyo, lakini vile vile anajua kuwa katika anaowatawala kuna wenye akili fupi wasiokwa na mwamko, watakaomsadiki atakayosema. Kwani kauli yake hii sio kubwa zaidi ya kusema: Mimi ndie Mola wenu mkuuu; na asingejasiri kusema hivyo lau sikuweko watakaomwambia: ndio, wewe ndiye Mola mkuu.

Hivi sasa tukiwa katika karne ya ishirini, karne ya maendeleo hadi mtu kufika mwezini, lakini bado Dalai Lama anapata wanaomwambia: Wewe ni Mungu, na Agha Khan naye anapata wanaomwambia; Wewe ni nusu mungu. “Kila mahali kuna Al-kaaba na imam”

Na hivi ndivyo Firauni alivyopambiwa ubaya wa vitendo vyake, na akazuiliwa njia.

Mambo mawili yanampambia mtu matendo yake mabaya: Kufuata matamanio na kuendelea na ujinga. Matamanio yalimpambia Firauni kudai ungu na ujinga ukawapambia wanaomtii.

Na vitimbi vya Firauni havikuwa ila katika kuangamia tu; yaani katika hasara.

Kila aliyejaribu na atakayejaribu kuwahadaa watu na kuwafanyia vitimbi, atakuwa katika hasara; hata kama atakuwa na utawala wa Firauni na mali ya Qaruni.

Na yule ambaye aliamini alisema: Enyi watu wangu! Nifuateni, nitawaongoza njia ya uongofu.

Mumin aliwahadharisha watu wake mara ya kwanza na ya pili. Na hii sasa ni mara ya tatu anawahimiza wakubali nasaha zake, kwa sababu anataka kuwaokoa na wapate kheri. Lakini wengineo wanawaongoza kwenye shari na maangamizi.

Enyi watu wangu! Hakika maisha haya ya dunia ni starehe tu, na hakika Akhera ndiyo nyumba ya daima.

Starehe za dunia zitakwisha tu, hilo halina shaka, lakini maisha ya Akhera yatabakia daima. Basi ni maisha gani kati ya haya mawili yanayofaa kuyafanyia kazi? Katika Nahjul-balagha, imesemwa: “Anafanya nini na dunia aliyeumbiwa Akhera? Na anafanya nini na mali ambaye muda mchache atanyang’anywa na kubakia athari yake mbaya na hisabu yake?” Vile vile imesemwa: “Uchungu wa dunia ni tamu ya Akhera na tamu ya Akhera ni uchungu ya dunia/”

Mwenye kutenda uovu hatalipwa ila sawa na huo, na mwenye kutenda wema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi, waruzukiwe humo bila ya hisabu.

Mwenyezi Mungu ni mwadilifu mkarimu. Uadilifu wake unajitokeza kati- ka adhabu ya muovu. Hiyo mbele ya Mwenyezi Mungu inalingana sawa na malipo. Na hupunguza adhabu kwa huruma zake. Ama mwema huzidishiwa ziada nyingi bila ya hisabu, awe mwanamume au mwanamke. Pepo ni malipo tosha kabisa.

Aya inafahamisha wazi kuwa Pepo ni wakf hususi wa mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, kwa imani isiyokuwa na shaka. Ama yule mwenye kufanya kheri kwa ajili ya kheri tu na huku anamkufuru Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, malipo yake yatakuwa sio Peponi, kwa sababu Pepo si ya makafiri. Tazama Juz. Juz. 4 (3:176 – 178), kifungu: ‘Kafiri na amali njema.’

Kuna mapokezi yanayosema kuwa Mtume(s.a.w. w ) amesema: “Hakufanya wema mwislamu au kafiri ila Mwenyezi Mungu humlipa.” Akaulizwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni yapi malipo ya kafiri? Akasema: mali, watoto, afya nk. Akaulizwa: malipo yake akhera yatakuwa nini? Akasema: Ataadhibiwa adhabu ya chini”

وَيَا قَوْمِ مَا لِي أَدْعُوكُمْ إِلَى النَّجَاةِ وَتَدْعُونَنِي إِلَى النَّارِ ﴿٤١﴾

41. Na Enyi watu wangu! Kwa nini mimi ninawaita kwenye wokovu, nanyi mnaniita kwenye Moto?

تَدْعُونَنِي لِأَكْفُرَ بِاللَّـهِ وَأُشْرِكَ بِهِ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ وَأَنَا أَدْعُوكُمْ إِلَى الْعَزِيزِ الْغَفَّارِ ﴿٤٢﴾

42. Mnaniita nimkufuru Mwenyezi Mungu na nimshirikishe na yule ambaye simjui, nami ninawaita kwa Mwenye nguvu, Mwingi wa maghufira?

لَا جَرَمَ أَنَّمَا تَدْعُونَنِي إِلَيْهِ لَيْسَ لَهُ دَعْوَةٌ فِي الدُّنْيَا وَلَا فِي الْآخِرَةِ وَأَنَّ مَرَدَّنَا إِلَى اللَّـهِ وَأَنَّ الْمُسْرِفِينَ هُمْ أَصْحَابُ النَّارِ ﴿٤٣﴾

43. Bila ya shaka mnayeniitia, hastahiki wito duniani wala Akhera. Na hakika marejeo yetu ni kwa Mwenyezi Mungu. Na wanaopita kiasi basi hao ndio watu wa Motoni!

فَسَتَذْكُرُونَ مَا أَقُولُ لَكُمْ وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿٤٤﴾

44. Basi mtayakumbuka ninayowaambia. Nami namkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwaona waja.

فَوَقَاهُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِ مَا مَكَرُوا وَحَاقَ بِآلِ فِرْعَوْنَ سُوءُ الْعَذَابِ ﴿٤٥﴾

45. Basi Mwenyezi Mungu akamlinda na ubaya wa hila walizozifanya. Na adhabu mbaya itawazunguka watu wa Firauni.

النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ ﴿٤٦﴾

46. Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapofika Saa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!.

NINAWAITA KWENYE WOKOVU NYINYI MNANIITA KWENYE MOTO

Aya 41 – 46

MAANA

Na Enyi watu wangu! Kwa nini mimi ninawaita kwenye wokovu, nanyi mnaniita kwenye Moto? Mnaniita nimkufuru Mwenyezi Mungu na nimshirikishe na yule ambaye simjui, nami ninawaita kwa Mwenye nguvu Mwingi wa maghufira?

Maneno haya na yanayofuatia mpaka Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwaona waja, anayasimulia Mwenyezi Mungu kuhusu mumin anayetoa nasaha.

Maana ni, niambieni enyi washirikina kuhusu hali yangu na nyinyi. Mimi nawalingania kwenye kheri itakayowaokoa na adhabu na maangamizi; ambayo ni kumwamini Mwenyezi Mungu mwenye nguvu asiyekuwa na mfano na yoyote; na mwenye kumsamehe anayetubia na kurejea Kwake; na nyinyi mananiita kwenye adhabu ya kuungua na kwenye shirki asiyoisamehe Mwenyezi Mungu wala kuingia akilini. Haifuati isipokuwa mwenye kupotea njia.

Bila ya shaka mnayeniitia, hastahiki wito duniani wala Akhera.

Bila shaka yule mnayenitaka nimwabudu, kama Firauni na mwenginewe, hana faida yoyote duniani na Akhera:

إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ﴿١٤﴾

“Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu. Na wakisikia hawajibu. Na Siku ya Kiyama watakataa shirki yenu.” Juz. 22 (35:14).

Na hakika marejeo yetu ni kwa Mwenyezi Mungu.

Kila kiumbe kitarudi kwa Mwenyezi Mungu kesho, sio kwa Firauni wala kwa mwenginewe. Watasimama wote mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hisabuna malipo na wanaopita kiasi basi hao ndio watu wa Motoni!

Amenukuu Tabari na Razi kutoka kwa Mujahid, kwamba makusudio ya wanaopita kiasi hapa ni waliomwaga damu bila ya haki.

Basi mtayakumbuka ninayowaambia yale ya ukweli na nasaha pale mtakapoona adhabu na kuwashukia balaa Nami namkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwaona waja.

Muhyiddin Bin Arabi anasema katika Futuhatil-makkiyya kuwa neno ufawwidhu (tulilolifasiri kwa maana ya kutegemeza), limechukuliwa kutoka neno fadha lenye maana ya kumimina chombo kikiwa kimejaa na hakiwezi kuchukua ziada.

Kwa hiyo mumin akibebeshwa zaidi ya uwezo wake, huipeleka ile ziada kwa Mwenyezi Mungu, naye Mwenyezi Mungu (s.w.t) hupokea ziada hiyo na kumpunguzia mzigo mumin. Na yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi na mwenye kumuona mwenye kuamini na akamtegemea na yule anayeelekea kwingine.

Basi Mwenyezi Mungu akamlinda na ubaya wa hila walizozifanya. Na adhabu mbaya itawazunguka watu wa Firauni.

Firauni alimdhamiria ubaya Musa na mumin mwenye kutoa nasaha, Mwenyezi Mungu akawaokoa na vitimbi vyake, akaangamia Firauni na watu wake kwenye maji. Namna hii Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawaondolea ubaya wenye ikhlasi, na majanga yanawarudia viongozi wa uhaini. Hii ni kabla ya mauti.

Ama baada ya mauti, basi wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni.

Kuna riwaya iliyopokewa kutoka kwa Imam Ja’far Assadiq(a.s ) akisema:Hiyo itakuwa baada ya mauti na kabla ya Kiyama. Kwa sababu siku hiyo haitakuwa na asubuhi wala jioni. Lau angeliadhibiwa mwenye hatia asubihi na jioni tu, basi ingelikuwa afadhali kwake.

Na itapofika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!

Kila mkosefu ataambiwa Siku ya Kiyama: Ingia Jahannam na ni marejeo mabaya; ni sawa awe ni katika watu wa Firauni au wengineo. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amehusu kutaja Firauni kwa sababu mazungumzo yanamuhusu yeye hivi sasa.


7

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَإِذْ يَتَحَاجُّونَ فِي النَّارِ فَيَقُولُ الضُّعَفَاءُ لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا نَصِيبًا مِّنَ النَّارِ ﴿٤٧﴾

47. Na watapohojiana huko Motoni, wanyonge watawaambia wale waliotakabari: Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu, basi je, mtatuondolea sehemu ya huu Moto?

قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُلٌّ فِيهَا إِنَّ اللَّـهَ قَدْ حَكَمَ بَيْنَ الْعِبَادِ ﴿٤٨﴾

48. Watasema waliotakabari: Hakika sote sisi tumo humo humo! Hakika Mwenyezi Mungu ameshahukumu baina ya waja!

وَقَالَ الَّذِينَ فِي النَّارِ لِخَزَنَةِ جَهَنَّمَ ادْعُوا رَبَّكُمْ يُخَفِّفْ عَنَّا يَوْمًا مِّنَ الْعَذَابِ ﴿٤٩﴾

49. Na walio Motoni watawaambia walinzi wa Jahannamu: Mwombeni Mola wenu atupunguzie siku moja ya adhabu.

قَالُوا أَوَلَمْ تَكُ تَأْتِيكُمْ رُسُلُكُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا بَلَىٰ قَالُوا فَادْعُوا وَمَا دُعَاءُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَالٍ ﴿٥٠﴾

50. Watasema: Je! Hawakuwa wakiwafikia Mitume wenu kwa hoja zilio wazi? Watasema: Kwani? Watasema: Basi ombeni! Na maombi ya makafiri hayawi ila ni kupotea bure.

إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ ﴿٥١﴾

51. Hakika tunawanusuru Mitume wetu na wale ambao wameamini katika uhai wa duniani na siku wataposimama mashahidi.

يَوْمَ لَا يَنفَعُ الظَّالِمِينَ مَعْذِرَتُهُمْ وَلَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ ﴿٥٢﴾

52. Siku ambayo hautawafaa madhalimu udhuru wao, nao watapata laana, na watapata makazi mabaya.

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْهُدَىٰ وَأَوْرَثْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ ﴿٥٣﴾

53. Na kwa hakika tulimpa Musa uwongofu, na tukawarithisha Wana wa Israili Kitabu.

هُدًى وَذِكْرَىٰ لِأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿٥٤﴾

54. Ni Uwongofu na Ukumbusho kwa wenye akili.

فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ ﴿٥٥﴾

55. Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Na, omba maghufira kwa dhambi zako na umsabihi Mola wako kwa kumhimidi jioni na asubuhi.

WANAHOJIANA MOTONI

Aya 47 – 55

MAANA

Aya hizi zimekwishatangulia kimaneno na kimaana. Kwa hiyo tutazifasiri kwa kupitia tu na tutaashiria Aya zilizotangulia zilipo:Na watapohojiana huko Motoni, wanyonge – yaani wafuasi –watawaambia wale waliotakabari: - yaani waliofuatwa -Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu, basi je, mtatuondolea sehemu ya huu Moto?

Mtu huko Akhera atakuwa pamoja na aliyempenda duniani na akamtii. Mwenye kuwapenda waongofu hapa duniani, atakuwa pamoja nao katika neema ya Pepo na atawashukuru kwa kupata uwongofu kwenye njia ya amani na uwokofu.

Lakini yule atakayewafuata mataghuti, basi atawalaani kesho na atawaambia nyinyi ndio sababu ya uovu wangu, sasa je, mtanipunguzia adhabu ninayoipata.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (14:21).

Watasema waliotakabari: Hakika sote sisi tumo humo humo! Hakika Mwenyezi Mungu amekwishahukumu baina ya waja!

Waliofuatwa watawajibu wale waliowasikiza na kuwatii: Leo hapana mjadala wala maneno. Mwenyezi Mungu amekwishaihukumu kila nafsi kwa kila ilichokichuma, na amekwishatuhukumia sisi na wale waliotufuata kwenda motoni

Na walio Motoni watawaambia walinzi wa Jahannamu: Mwombeni Mola wenu atupunguzie siku moja ya adhabu.

Wanafikiria adhabu ya Jahannam ni kama jela ya duniani, wafungwa wanavyopata mapumziko nje ya jela. Hapo wataomba wafanyiwe motoni kama wanavyofanyiwa katika jela ya duniani.

Watasema: Je! Hawakuwa wakiwafikia Mitume wenu kwa hoja zilio wazi? Watasema: Kwani? Watasema: Basi ombeni! Na maombi ya makafiri hayawi ila ni kupotea bure.

Walinzi watawajibu kuwa Mwenyezi Mungu amekwishamaliza udhuru kwenu, kupitia mitume yake; kama mlivyokiri wenyewe. Kwa hiyo hakuna lawama ikiwa hatajibu maombi yenu ila mjilaumu wenyewe tu. Umetangulia mfano wake katika Juzuu hii tuliyo nayo (39:71) na kwa upana zaidi kwenye Juz. 7 (7:50-53).

Hakika tunawanusuru Mitume wetu na wale ambao wameamini katika uhai wa duniani na siku wataposimama mashahidi.

Siku ya mashahidi ni Siku ya Kiyama ambapo wakasofu watatolewa ushahidi na malaika maulama wanaofikisha na hata viungo vya mkosaji:

حَتَّىٰ إِذَا مَا جَاءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ وَجُلُودُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٢٠﴾

“Hata watakapoufikia Moto yatawashuhudia masikio yao, na macho yao na ngozi zao kwa waliyokuwa wakiyatenda.” (41:20).

Aya hii inafahamisha, kwa uwazi, kuwa Mwenyezi Mungu anawanusuru mitume na waumini wenye ikhlasi kuwa washindi duniani na Akhera. Ushindi wa Akhera uko wazi, lakini ushindi wa duniani una sura mbali mbali.

Unaweza ukawa ni nguvu ya kumshinda adui au kuenea itikadi na misingi au hata kuinuka jina na kuwa na shani daima. Kuna baadhi ya mashahidi, makaburi yao yamekuwa kama Al-Ka’aba, yanatembelewa na mamilioni. Historia ni shahidi wa hayo.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 (22: 38-41) kifungu cha ‘Mwenyezi Mungu huwakinga walioamini.’

Siku ambayo hautawafaa madhalimu udhuru wao, nao watapata laana, na watapata makazi mabaya, pasipokuwa na wa kuwakinga wala udhuru utakaowafaa waasi. Kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekata nyudhuru zote. Na mwema ni yule asiyetaka udhuru kwa kufanya matendo mema.

Na kwa hakika tulimpa Musa uwongofu, na tukawarithisha Wana wa Israili Kitabu, ni Uwongofu na Ukumbusho kwa wenye akili.

Makusudio ya uwongofu hapa ni miujiza inayofahamisha utume wa Musa(a.s ) na yale aliyopewa wahyi, ya halali na haramu. Makusudio ya Kitabu ni Tawrat ya kweli.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja kuwa anawanusuru mitume na waumini, hapa anaashiria Musa na wale waliokuwa na ikhlasi katika wana wa Israil. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwanusuru na Firauni na watu wake.

Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli.

Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad(s.a.w. w ) , akiamrishwa kuvumilia, kama walivyovumilia mitume ulul-azm na kuashiria ahadi Yake aliyoieleza katika kauli yake:

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ ﴿٣٣﴾

“Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na dini ya haki ili ipate kushinda dini zote, ijapokwa washirikina wamechukia.” Juz. 10 (9:33).

Ahadi ya Mwenyezi Mungu haiwezi kuachwa.

Na omba maghufira kwa dhambi zako.

Amri ya kuomba msamaha wa dhambi haimaanishi kuwa kuna dhambi. Mtume alimuomba Mola wake ahukumu kwa haki, ingawaje anajua kuwa hahukumu isipokuwa haki:

قَالَ رَبِّ احْكُم بِالْحَقِّ ﴿١١٢﴾

“Akasema: Mola wangu! Hukumu kwa haki.” Juz. 17 (21:112).

Unaweza kuuliza : Kuna faida gani basi ya kufanya istighfari ya dhambi?Jibu : Hakuna isipokuwa ibada; kama amri ya tahalili, takbira na tasbih, kama alivyosema:

Na umsabihi Mola wako kwa kumhimidi jioni na asubuhi.

Neno jioni limefasiriwa kutokana na neno la kiarabu ibkar lenye maana ya kuanzia kupinduka jua hadi usiku. Na asubuhi kutoka Ashiyy lenye maana ya kuanzia Alfajiri hadi mchana.

Zaidi ya hayo ni kuwa kuamrishwa Mtume kuomba msamaha na hali hana dhambi, kunafahamisha kuwa kutubia wenye dhambi ni bora zaidi.

Aina hii ya maneno inaitwa kuuashiria mlengwa. Kwa sababu anayesikiliza atatambua kuwa hukumu inayothibiti kwa anayeatamkiwa inathibiti kwa aliyenyamaziwa vile vile, kwa kiasi cha kusikia tu.

MWENYEZI MUNGU NA WAISRAIL

Katika Juz. 1 (2:40-46) tulisema kuwa maana ya neno Israil ni Abdallah (mtumishi wa Mwenyezi Mungu), kwa kutegemea wafasiri, akiwemo Tabariy, Razi na mwenye Majmaul-bayan.

Lakini tulipoanza Juzuu hii tuliyo nayo, tukaona kuwa kauli hii inahitaji uthibitisho na kwamba haikufaa kutegemea kauli za wafasiri, au angalau tungelitegemeza kauli kwa msemaji (kusema kuwa Fulani ndiye aliyesema hivi); kama inavyotakikana katika mantiki ya elimu. Lakini kuwategemea wajuzi hasa waliotangulia, lilikuwa na linaendelea kuwa ni tatizo la waaandishi na watunzi na hata wapokezi wa Hadith.

Basi nikawa natafuta kitabu Talmud, lakini sikupata, badala yake nikapata kitabu: Treasure provision in the rules of the Talmud na Kamusi ya Kitabu (Bible Dictionary), nikavinunua. Waliochangia kutengeneza kamusi hii ni wasomi wa kikiristo 28, wakiwemo makasisi 17, na wengine ni madokta, mashemasi na waalimu. Humo kuna nukuu hii: "Israil: Maana ya neno hili ni yule anayepigana jihadi na Mwenyezi Mungu au aliyepigana miereka na Mwenyezi Mungu. Hilo ni jina la Yakobo alilopewa na Mungu aliyepigana naye hadi alfajiri" (Biblia Mwanzo 32:28).

Kwa hiyo maana ya Israil ni yule anayepigana miereka na Mwenyezi Mungu, kwa nukuu ya Tawrat. Kuna tofauti kubwa baina ya mja au mtu- mishi na mpiganaji. Kwa sababu mpiganaji anapigana na yule aliyefanana naye, lakini mtumishi anakuwa mnyonge.

Hii inatubainikia kuwa Tawrat ya sasa sio ile aliyoiashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliposema: 'Na tukawarithisha wana wa Israil Kitabu ni uwongofu na ukumbusho' kwa sababu Tawrat ya sasa ni ya matamanio na upofu, kwa vile inasema kuwa Ya'qub alipigana na Mungu mpaka Alfajiri, Lut alilala na mabinti zake mpaka akazaa nao na Daud naye aliwapora wake za watu na kuwaua waume zao.

Watafiti wamekongamana kuwa Tawrat iliyoko sasa, iliandikwa baada ya Musa kwa muda mrefu. Tazama Qamusul-kitabul-muqaddasa (kamusi ya kitabu kitakatifu ya kiarabu), ukurasa 763 na 1120 chapa ya Al-injilya ya Beirut 1964. Vile vile Al-asfarul-muqaddasa,' (Vitabu vitakatifu) cha Abdul-wahid Wafi, ukurasa 16 chapa ya kwanza 1964.

Vile vile imetubainikia kuwa wana wa Israil wa mwanzo waliorithishwa Kitabu, wako mbali sana kinasabu na kushabihiana na dola ya Israil, kambi mpya ya ukoloni mashariki ya kati.

Jarida la A-Majalla la Misr la mwezi January 1970, limechapisha makala yenye kurasa 20, kwa anuani ya 'Tawrat ya Mayahudi' ya mwandishi Hussein Dhul-fiqar Sabri.

Ndani ya makala hiyo kuna mahali anamnukuu Mzayuni Stehr, kwamba Mungu wa Israil, kama inavyoona fikra ya Kiyahudi, ana mfungano na historia ya wana wa israil. Ikiondoka Israil, basi dalili za kufahamisha kuweko Mungu nazo zitakuwa zimeondoka. Kwa hiyo inamlazimu kila myahudi apamabane na dhati hiyo isiyojulikana - yaani Mwenyezi Mungu - mpaka alfajiri, kama alivyofanya Ya'qub, iwe mapambano haya ni ya kushindwa au kushinda.

Vile vile mwandishi amemnukuu mzayuni, Popper, kwamba maana yaliyo katika akili za mayahudi wengi ni kuwa Ya'qub alikuwa na nguvu kuliko Mwenyezi Mungu.

Mwisho, baada ya utafiti wa kina wa mwandishi huyu, akatoka na natija aliyoipata kutoka Tawrat na vitabu vingine vya kiyahudi na pia kutoka katika kauli za wanafikra wa kizayuni, kwamba kiini cha itikadi ya kiza- yuni ni kuweko Israil na kupambana na tishio lolote, hata kama chimbuko la tishio hilo ni Mungu. Na kwamba Tawrat ya sasa ni uchambuzi tu wa uyahudi na kupingana na Mwenyezi Mungu. Yeye yuko pamoja nao na wakati huohuo yuko dhidi yao, katika Tawrat yao Mungu amechanganyika: hatakikani, lakini pia ni mwenye huruma.

Huu ndio Uzayuni. Itikadi yake ni kuwa kuna watu wana nguvu zaidi ya Mwenyezi Mungu, na kwamba kuweko Mungu kunategemea kuweko Israil. Ikiondoka Israil Mungu naye ameondoka.

Ndio maana Uzayuni ukajiunga na ukoloni wa kimataifa, dhidi ya mataifa mengine, dini na ubinadamu kwa ujumla. Matokeo ya muungano huu yakawa ni kupatikana Israil, ndani ya ardhi ya Palestina. Lakini Alhamdulillah, roho ya uadui dhidi ya ukoloni na uzayuni imeenea kwenye miji yote ya kiarabu. Dalili kubwa ya hilo ni mapambano ya Wapalestina na kukubaliana waarabu kuisaidia Palestina. Kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, matunda yatapatikana, kama si leo ni kesho.

إِنَّ الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّـهِ بِغَيْرِ سُلْطَانٍ أَتَاهُمْ إِن فِي صُدُورِهِمْ إِلَّا كِبْرٌ مَّا هُم بِبَالِغِيهِ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿٥٦﴾

56. Hakika wale ambao wanabishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu bila ya dalili yoyote iliyowafika, hawana vifuani mwao ila kutaka ukubwa tu, na wala hawaufikii. Basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu; hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.

لَخَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٧﴾

57. Hakika umbo la mbingu na ardhi ni kubwa zaidi kuliko umbo la watu. Lakini watu wengi hawajui.

وَمَا يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَلَا الْمُسِيءُ قَلِيلًا مَّا تَتَذَكَّرُونَ ﴿٥٨﴾

58. Na kipofu na mwenye kuona hawawi sawa; na walioamini na watendao mema hawawi sawa na muovu. Ni machache mnayoyakumbuka.

إِنَّ السَّاعَةَ لَآتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٥٩﴾

59. Hakika Saa, itafika, haina shaka, lakini watu wengi hawaamini.

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ ﴿٦٠﴾

60. Na Mola wenu amesema: Niombeni nitawaitikia. Kwa hakika wale ambao wanajivuna kufanya ibada yangu wataingia Jahannamu wadhalilike.

اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٦١﴾

61. Mwenyezi Mungu ambaye amewafanyia usiku ili mpate kutulia humo, na mchana wa kuonea. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru.

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٦٢﴾

62. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu, Muumba wa kila kitu. Hapana mungu ila Yeye; basi mnageuzwa wapi?

كَذَٰلِكَ يُؤْفَكُ الَّذِينَ كَانُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ ﴿٦٣﴾

63. Hivyo ndivyo walivyogeuzwa wale ambao walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.

KUUMBA MBINGU NA ARDHI

Aya 56 – 63

MAANA

Katika Hakika wale ambao wanabishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu bila ya dalili yoyote iliyowafika, hawana vifuani mwao ila kutaka ukubwa tu, na wala hawaufikii.

Makusudio ya wanaobishana hapa ni wapenda anasa. Kwani wao wanapinga kitu kikiwa hakikubaliani na ukubwa wao. Ushahidi wa hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘ila kutaka ukubwa tu’ Yaani kwa sababu ya kiburi chao na kujikuza, hawaikubali haki na wanabishana. Ingelikwa bora kama wangelitubia na kukubali makosa.

Basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu na kiburi na mwisho mbaya.

Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona, kiburi chao wana- choking’ang’ania kwa sababu ya jaha na utajiri wao. Katika Nhajul-bal- agha, imesemwa: “Jikingeni kwa Mwenyezi Mungu na majivuno kama mnavyojikinga na majanga.”

Hakika umbo la mbingu na ardhi ni kubwa zaidi kuliko umbo la watu. Lakini watu wengi hawajui.

Kila elimu inavyoendelea, ndio maana ya Qur’ani nayo yanavyozidi kwa nguvu kufunguka kwenye akili. Wataalamu wa zamani walisema: Mtu ndiye kiumbe wa ajabu ardhini na katika anga za juu na kwamba ardhi ndio kituo cha ulimwengu. Kisha ikaja elektroni na ala nyingine za elimu ya kisasa, ili ziseme:

Hapana! Mtu sio kiumbe wa ajabu wala ardhi zio kituo cha ulimwengu. Kwani ulimwengu una mamailio ya vituo na kila kituo kina mamlioni ya nyota, na kwamba hakuna yoyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu anayejua au anayeweza kujua idadi ya vituo hivyo au idadi ya nyota na vinginevyo vilviyomo kwenye kila kituo; na ardhi katika ulimwengu ni kama chembe tu.

Hapa ndio tunapata tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Hakika umbo la mbingu na ardhi ni kubwa zaidi kuliko umbo la watu.’ Ndio! Lakini ndani ya binadamu kuna ulimwengu wa ajabu, jinsi alivyo, hakika yake, mapendeleo yake hisia zake na matamanio yake.

Na kipofu na mwenye kuona hawawi sawa; na walioamini na watendao mema hawawi sawa na muovu. Ni machache mnayoyakumbuka.

Tofuti ni kubwa sana baina mjuzi na mjinga baina ya mwema na mfisadi na baina mwenye kufanya mazuri na mwenye kufanya maovu. Hapana! Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu wala mbele ya watu wenye insafu mwamko. Umetangulia mfano wake katika Juz.7 (6:50), Juz. 13 (13:16) na Juz. 22 (35:19).

Hakika Saa ya Kiyamaitafika, haina shaka, na itatupelekea kusimama mbele za mwenye uwezo aliye mjuzi, batilil zitaondoka, uhakika utathibiti na visababu vyote vitakatika.

Lakini watu wengi hawaamini kwamba wao watafufuliwa siku itakayokuwa kubwa na wataulizwa waliyokuwa wakiyafanya.

Na Mola wenu amesema: Niombeni nitawaitikia.

Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa maana yake ni niabuduni nitawalipa. Wametoa dalili kuwa Qur’an inatumia neno dua kwa maana ya ibada kwa Aya ya isemayo:

إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا ﴿١١٧﴾

“Huwamuombi asiyekuwa yeye isipokuwa (masanamu) ya kike.” Juz. 5 (4:117).

Sisi tuko pamoja na wanaosema kauli hii; hasa katika Aya hii, ambapo mfumo wa maneno unarudia kwenye maana hii, pale aliposema moja kwa moja:

Kwa hakika wale ambao wanajivuna kufanya ibada yangu wataingia Jahannamu wadhalilike.

Kwa hiyo kusema kwake: ‘ambao wanajivuna na ibada yangu,’ ni tafsiri na ubanifu wa kauli yake: ‘niombeni.’ Kwa vyovyote iwavyo, ni kuwa Uislamu ni dini ya matendo sio dini ya maneno. Na Mwenyezi Mungu humruzuku mwenye kufanya juhudi na akawa na subira:

هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا ﴿١٥﴾

“Yeye ndiye aliyeifanya ardhi mororo kwa ajili yenu” (67:15).

Tumezungumzia kuhusu dua (mombi) katika Juz. 2 (2: 186).

Mwenyezi Mungu ambaye amewafanyia usiku ili mpate kutulia humo, na mchana wa kuonea. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:67).

Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu, Muumba wa kila kitu. Hapana mungu ila Yeye; basi mnageuzwa wapi?

Vipi mnageuzwa kumtii Mwenyezi Mungu na kumwabudu na hali Yeye peke yake ndiye Muumba na Mwenye kuruzuku? Makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Amewafanyia, Mwenye fadhila na Muumba wa kila kitu,’ ni kubainisha kuwa Yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekusanya sifa zote za uungu za ukamilifu na kwamba sifa hizo zote ziko wazi kwa mwenye macho na akili nzuri, lakini watu wengi wameghafilika na yale wanayotakiwa kuyafanya na yanayolengwa kwao.

Hivyo ndivyo walivyogeuzwa wale ambao walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.

Kila mwenye kughafilika na kupuuza dalili zinazofahamisha ukuu wa Mwenyezi Mungu, lazima awe anaachana na ibada ya Mwenyezi Mungu na twaa yake. Kwa sababu watu ni maadui wa yale wasiyoyajua.


8

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ قَرَارًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٦٤﴾

64. Ni Mwenyezi Mungu aliyewafanyia ardhi kuwa ni pahala pa kukaa, na mbingu kuwa jengo. Na akawatia sura, na akazifanya nzuri sura zenu, na akawaruzuku vizuri. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu. Basi amekuwa na baraka Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote.

هُوَ الْحَيُّ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦٥﴾

65. Yeye yuko hai - hapana mungu isipokuwa Yeye. Basi muabuduni Yeye mkimsafia Dini Yeye. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.

قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَمَّا جَاءَنِيَ الْبَيِّنَاتُ مِن رَّبِّي وَأُمِرْتُ أَنْ أُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦٦﴾

66. Sema: Hakika nimekatazwa kuwaabudu wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, ziliponijia hoja zilizo wazi kutokana na Mola wangu. Na nimeamrishwa nisilimu kwa Mola wa walimwengu wote.

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ يُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ ثُمَّ لِتَكُونُوا شُيُوخًا وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ مِن قَبْلُ وَلِتَبْلُغُوا أَجَلًا مُّسَمًّى وَلَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٦٧﴾

67. Yeye ndiye ambaye amewaumba kwa udongo, kisha kwa tone, kisha kwa pande la damu, kisha akawatoa katika hali ya mtoto mchanga, kisha mpate kufikia utu uzima, kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanaokufa kabla, na ili mfikie muda uliokwishawekwa, na ili mpate kutia akili.

هُوَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ فَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٦٨﴾

Yeye ndiye ambaye anahuisha na anafisha. Akihukumu jambo liwe, basi huliambia: Kuwa! Likawa.

AMEWATIA SURA NA AKAZIFANYA NZURI

Aya 64 – 68

MAANA

Ni Mwenyezi Mungu aliyewafanyia ardhi kuwa ni pahala pa kukaa, na mbingu kuwa jengo.

Mwenyezi Mungu (s.w.t), hapa, ameisifu ardhi kuwa ni mahali pa kukaa, mahali pengine ameipa sifa ya tandiko na pengine kitanda. Maana yote hayo ni mamoja. Na ameisifu mbingu hapa kuwa ni jengo na mahali pengine kuwa ni sakafu na yenye buruji na yenye mpangilio.

Makusudio ya sakafu ni kufananisha, kwa sababu inaonekana kama hivyo kwenye macho. Kundi la wafasiri limesema kuwa makusudio ya buruji ni nyota na mpangilio. ni njia. Ama makusudio ya jengo ni kuwa aliiumba kwa mpangilio mzuri na akaipamba kwa pambo la nyota; kama ilivyo katika Juz. 23 (37:6).

Na akawatia sura, na akazifanya nzuri sura zenu, na akawaruzuku vizuri. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu. Basi amekuwa na baraka Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemuumba mtu, akalifanya vizuri umbile lake, kimo na viungo, kwa mpangilio wa hali ya juu; kuongezea ubainifu, utambuzi, na mengineyo, kama vile utambuzi n.k. Hali hii ya uwiano wa ajabu baina ya mtu na ulimwengu; kiasi ambacho muundo wake umekuja kwa namna ambayo mtu anaweza kutumia nishati na heri zote zilizo ulimwenguni kulingana na haja na masilahi yake, huenda ndiyo inayomfanya mtu awe kiumbe wa aina yake.

Lau kusingelikuwa na dalili yoyote inayofahamisha kuweko Mwenyezi Mungu, isipokuwa kiumbe huyu wa ajabu (mtu), basi ingelitosha. Hapa ndio tunapokuta tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na katika ardhi zimo Ishara na katika nafsi zenu, je hamuoni?” (51:20-21). Tumeyazungumzia hayo kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 15 (17:70).

Yeye yuko hai - hapana mungu isipo kuwa Yeye. Basi muabuduni Yeye mkimsafia Dini Yeye. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.

Yeye yuko hai kwa sababu Ndiye anayetoa uhai na ni Mmoja wa peke Yake kwa sababu ni Mungu. Kwani uungu unapelekea kuwa wa pekee mmoja tu. Maana ya kumsafia dini ni kumwamini na kumwelekea Yeye tu peke Yake, katika kauli zote na vitendo vyote. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:29) na Aya ya 14 ya sura hii tuliyo nayo.

Baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kusema kuwa Yeye ndiye aliyewatia sura, anaashiria kuwa inatakikana mtu amshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema yake ya kuumba na kuruzuku.

Sema: Hakika nimekatazwa kuwaabudu wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, ziliponijia hoja zilizo wazi kutokana kwa Mola wangu. Na nimeamrishwa nisilimu kwa Mola wa walimwengu wote.

Huu ni mfumo mzuri wa kujadili na kudadisi. Washirikina walipomwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) : abudu masanamu tunayoyaabudu, ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Mtume wake waambie kuwa vipi niabudu masanamu na hali Mwenyezi Mungu amenikataza kuyaabudu na akaniamuru kusalimu amri Kwake Yeye peke yake.

Pia amenifahamisha dalili za kutosha kwamba mnavyoviabudu hav- istahiki kuabudiwa kabisa, kwa sababu ni mawe tu, yasiyodhuru wala kunufaisha. Umetangulia mfano wake katika Aya 41 ya sura hii tuliyo nayo.

Yeye ndiye ambaye amewaumba kwa udongo, kisha kwa tone, kisha kwa pande la damu, kisha akawatoa katika hali ya mtoto mchanga, kisha mpate kufikilia utu uzima, kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanaokufa kabla, na ili mfikie muda uliokwishawekwa, na ili mpate kutia akili

Umetangulia mfano wake katika Juz. 14 (16:70), Juz. 17 (22:70), Juz. 18 (23:14) na Juz. 22 (35:11).

MWANAFALSAFA RUSSEL NA MUDA ULIOWEKWA

Yeye ndiye ambaye anahuisha na anafisha. Akihukumu jambo liwe, basi huliambia: Kuwa! Likawa.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye anayeleta mauti na uhai katika vitu vya asili ya maumbile na Ndiye aliyeleta maumbile yote, zikiwemo sayari zake, kwa neno ‘kuwa’ kutokana na kutokuweko chochote. Sio kutokana na ukungu; wala mengineyo. Kama muulizaji atauliza: Ni nani basi aliyemuumba Mwenyezi Mungu? Tutajibu: maana ya neno Allah (Mwenyezi Mungu) ni kuwa Yeye ni muumba asiyeumbwa na kwamba dhati yake inapelekea kupatikana wala haihitaji mwenye kuipatisha.

Akisema mara ya pili kuwa hayo ni madai tu yanyohitaji uthibitisho, na kwamba huo ukungu huuhitaji mwenye kuupatisha, tutamjibu hivi: Maisha haya na nidhamu hii haiwezi kufasiriwa na ukungu wala na kitu chochote kisichokuwa na uhai wala utambuzi. Kwa sababu asiyenacho haiwezi kuitoa.

Kwa hiyo basi haitabakia kwa mwenye akili kufasiri uhai na nidhamu katika maumbile isipokuwa kukubali kuweko Mwenye uwezo, Mpangiliaji aliyemuumba wa kila kitu na asiyehitajia chochote. Makadirio yoyote yasiyokuwa haya hayakubaliki kiakili.

Na mwenye kupinga basi na alete lililo bora kuliko hili na amwachie mtu kufuata atakalo nasi tutakuwa pamoja naye.

Kwa ufupi ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemumba mtu katika umbile zuri, akamgurisha kutoka hali moja hadi nyingine mpaka kufikia muda wake uliowekwa. Ikiwa hatujamuona muumba basi tumeona athari na dalili zinazofahamisha kuwa Yeye ni Mkuu katika uumbaji Wake.

Kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘na ili mfikie muda uliokwishawekwa, na ili mpate kufahamu.’ Tunakumbuka tukio lililomtokea mwanafalsafa mkubwa Bretrand Russel, alipokuwa na umri wa miaka 76.

Mnamo mwaka 1948, alisafiri kwa ndege kutoka Oslow hadi London. Ndege ilipokuwa inakurubia ufukwe wa Norway, mhudumu mmoja wa ndege alimuuliza kama ni lazima avute sigara? Alikuwa amekaa kwenye viti vya mbele, akamjibu: “Nisipovuta nitakufa.”

Basi akamuonyesha viti vya nyuma aende akakae huko, ataruhusiwa kuvuta sigara. Mara tu baada ya kukaa, ndege ikaanguka baharini, watu waliokuwa viti vya mbele wakafariki na waliokuwa vya nyuma wakapona.

Hatuwezi kupata tafsiri ya hili ispokuwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘na ili mfikie muda uliokwishawekwa, na ili mpate kufahamu.’ Mwenyezi Mungu ametanabisha kufika muda uliowekwa na kufahamu, ili awaeleze walahidi wanaofasiri tukio kama hili na mfano wake kuwa ni sadfa.

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّـهِ أَنَّىٰ يُصْرَفُونَ ﴿٦٩﴾

69. Je, Huwaoni wale ambao wanabishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu wanageuziwa wapi?

الَّذِينَ كَذَّبُوا بِالْكِتَابِ وَبِمَا أَرْسَلْنَا بِهِ رُسُلَنَا فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿٧٠﴾

70. Ambao wamekadhibisha Kitabu na yale tuliyowatuma nayo Mitume wetu. Basi watakuja jua.

إِذِ الْأَغْلَالُ فِي أَعْنَاقِهِمْ وَالسَّلَاسِلُ يُسْحَبُونَ ﴿٧١﴾

71. Zitakapokuwa pingu shingoni mwao na minyororo, huku wanabururwa.

فِي الْحَمِيمِ ثُمَّ فِي النَّارِ يُسْجَرُونَ ﴿٧٢﴾

72. Katika maji ya moto, kisha wataunguzwa Motoni.

ثُمَّ قِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تُشْرِكُونَ ﴿٧٣﴾

73. Tena wataambiwa: Wako wapi mliokuwa mkiwashirikisha.

مِن دُونِ اللَّـهِ قَالُوا ضَلُّوا عَنَّا بَل لَّمْ نَكُن نَّدْعُو مِن قَبْلُ شَيْئًا كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ الْكَافِرِينَ ﴿٧٤﴾

74. Badala ya Mwenyezi Mungu Watasema: Wametupotea, bali tangu zamani hatukuwa tukiomba kitu! Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu huwapoteza makafiri.

ذَٰلِكُم بِمَا كُنتُمْ تَفْرَحُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَبِمَا كُنتُمْ تَمْرَحُونَ ﴿٧٥﴾

75. Haya ni kwa sababu mlikuwa mkifurahi katika ardhi pasipo haki, na kwa sababu mlikuwa mkijishaua.

ادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا فَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ ﴿٧٦﴾

76. Ingieni kwenye milango ya Jahannamu, mdumu humo. Basi ni maovu yaliyoje makazi ya wanaotakabari!

فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ فَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ ﴿٧٧﴾

77. Basi subiri, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Na ama tukikuonyesha baadhi ya yale tuliyowaahidi au tukikufisha, lakini wao watarudishwa kwetu tu.

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِيَ بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ فَإِذَا جَاءَ أَمْرُ اللَّـهِ قُضِيَ بِالْحَقِّ وَخَسِرَ هُنَالِكَ الْمُبْطِلُونَ ﴿٧٨﴾

78. Na kwa hakika tuliwatuma Mitume kabla yako. Wengine katika hao tumekusimulia na wengine hatukukusimulia. Na haiwi Mtume alete Ishara yoyote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi ikija amri ya Mwenyezi Mungu huhukumiwa kwa haki, na hapo wapotofu watapata hasara.

MLIKUWA MKIFURAHI

Aya 69 – 78

MAANA

Je, Huwaoni wale ambao wanabishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu wanageuziwa wapi?

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamwambia Mtume wake mtukufu akipinga ubishi wa kibatili wa washirikina, kuwa umeona ewe Muhammad jinsi washirikina na wapenda anasa wanavyozifumbia macho hoja mkataa na ubainifu ulio wazi juu ya ukuu wa Mwenyezi Mungu na utume wako? Na pia vile wanavyoikimbia haki na kwenda kwenye ujinga na upotevu wa kuabudu mawe?

Ufafanuzi zaidi wa Aya hii na ufupisho wake ni kauli ya Imam Ali(a.s) :“Mwenye kukithirisha mzozo wake kwa ujinga hudumu upofu wake na haki.”

Ambao wamekadhibisha Kitabu yaani Qur’anina yale tuliyowatuma nayo Mitume wetu. Basi watakuja jua.

Siku hiyo uhakika utadhihirika na wakosefu wataiona adhabu yao,zitakapokuwa pingu shingoni mwao na minyororo, huku wanabururwa katika maji ya moto, kisha wataunguzwa Motoni.

Wataburuzwa kupelekwa motoni wakiwa wamefungwa minyororo, kinywaji chao kitakuwa maji ya moto na mikono itafungwa shingoni na utosi utakutanishwa na nyayo:

يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالْأَقْدَامِ ﴿٤١﴾

“Watajulikana wakosefu kwa alama zao, watakamatwa kwa nywele za utosi na kwa miguu” (55-41).

Tena wataambiwa: Wako wapi mliokuwa mkiwashirikisha badala ya Mwenyezi Mungu na mkiwaweka akiba ya wakati wa shida? Basi waiteni wawaitikie ikiwa nyinyi ni wakweli.

Watasema: Wametupotea, wala hatuwaoni hata athari yao.bali tangu zamani hatukuwa tukiomba kitu! Kumbe walikuwa ni mangati tu.

Hivyo ndivyo Mwenyezi huwapoteza makafiri, kwa sababu wameamua kufuata njia mbaya kwa hiyari yao, baada ya kukatazwa na wakafa kwenye uovu na kufuru na hali wameamriwa kutubia na kurejea kwa Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu. Mwenye kuingia mlango wa uovu, ajilaumu mwenyewe tu.

TUNATAFUTA DUNIA KWA DINI

Haya ni kwa sababu mlikuwa mkifurahi katika ardhi pasipo haki, na kwa sababu mlikuwa mkijishaua.

Wakifurahi kwa mambo duni ya dunia yanayoisha wala hawatilii umuhimu neema za daima za akhera zinazowapita. Lakini wasifa huu hauwahusu washirikina tu; bali unatuhusu sisi pia. Tofauti ni kuwa wao wanaikabili dunia wakiwa wanikana Akhera waziwazi na kwa ndani, lakini sisi tunaikabili dunia na kuipupia kwa kutumia imani ya Mwenyezi Mungu na Siku ya mwisho. Sasa ni lipi kati haya mawili linastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu?

Ingieni kwenye milango ya Jahannamu, mdumu humo. Basi ni maovu yaliyoje makazi ya wanaotakabari!

Ataambiwa haya mwenye kutakabari na kila mwenye kuitumia dini na nchi kujinufaisha na akachezea akili za watu wasio na hatia; ni sawa ameyafanya hayo kwa makusudi au kutojua hakika na hali halisi. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا ﴿١٠٣﴾ الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا ﴿١٠٤﴾

“Sema je, tuwaambie wale wenye hasara mno ya vitendo? Ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kuwa wanafanya kazi nzuri? Juz. 16 (18:103 – 104).

Ulama wameafikana kwa kauli moja kwamba mjinga (asiyejua) kwa uzembe hana udhuru mbele ya Mwenyezi Mungu.

Basi subiri, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli.

Imetangulia kwa herufi zake katika Aya 55 katika sura hii tuliyo nayo.

Na ama tukikuonyesha baadhi ya yale tuliyowaahidi au tukikufisha, lakini wao watarudishwa kwetu tu.

Maneno yanelekezwa kwa Muhammad(s.a.w.w) kuhusiana na washirikina. Maana ni kuwa tunaweza tukawaadhibu duniani wale wanaokukadhibisha na kukuudhi wewe ukiwaona na tunaweza tukakuhitari ukaja kwetu kabla ya hayo. Katika hali zote hizo, marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu peke yake.

Aya inashiria kwamba mumin wa kweli anatakikana afurahi kwa yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu, awe na yakini na dini yake na afanye juhudi kadiri atakavyoweza kupiga vita ubatilifu na upotevu, kisha malipo amwachie Mwenyezi Mungu:

وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٢﴾

“Na Mola wako si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda” Juz. 8 (6:132)

Na kwa hakika tuliwatuma Mitume kabla yako. Wengine katika hao tumekusimulia na wengine hatukukusimulia.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 6 (4:164). Tazama kifungu ‘Je, mitume wote ni wa mashariki?

Na haiwi Mtume alete Ishara yoyote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Makusudio ya ishara hapa ni muujiza. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hudhihirisha muujiza mikononi mwa mitume, kulingana na inavyotaka hekima na masilahi; sio kama wanavyotaka wenye kiburi na inadi.

Basi ikija amri ya Mwenyezi Mungu huhukumiwa kwa haki, na hapo wapotofu watapata hasara.

Hapo ni hapo Siku ya Kiyama; nayo ni siku mbaya sana kwa wabatilifu na siku njema sana kwa wenye haki.

اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَنْعَامَ لِتَرْكَبُوا مِنْهَا وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ ﴿٧٩﴾

79. Mwenyezi Mungu ndiye ambaye amewajaalia wanyamahowa ili muwapande baadhi yao na wengine muwale.

وَلَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ وَلِتَبْلُغُوا عَلَيْهَا حَاجَةً فِي صُدُورِكُمْ وَعَلَيْهَا وَعَلَى الْفُلْكِ تُحْمَلُونَ ﴿٨٠﴾

80. Na katika hao mna manufaa Na manapata kwao haja zilizo vifuani mwenu; Na mnachukuliwa juu yao na juu ya majahazi.

وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ فَأَيَّ آيَاتِ اللَّـهِ تُنكِرُونَ ﴿٨١﴾

81. Na anawaonyesha ishara zake, basi ni ipi katika ishara za Mwenyezi Mungu mtaikataa?

أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ كَانُوا أَكْثَرَ مِنْهُمْ وَأَشَدَّ قُوَّةً وَآثَارًا فِي الْأَرْضِ فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٨٢﴾

82. Je, hawatembei katika ardhi wakaona ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao na wakilima ardhi, lakini hayakuwafaa waliyokuwa wakiyachuma.

فَلَمَّا جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَرِحُوا بِمَا عِندَهُم مِّنَ الْعِلْمِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٨٣﴾

83. Basi walipowajia Mitume wao kwa dalili zilizo wazi walifurahia elimu waliyokuwa nayo na yakawazunguka waliyokuwa wakiyafanyia sti- hzai.

فَلَمَّا رَأَوْا بَأْسَنَا قَالُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ وَكَفَرْنَا بِمَا كُنَّا بِهِ مُشْرِكِينَ ﴿٨٤﴾

84. Walipoiona adhabu yetu wakasema: Tumemwamini Mwenyezi Mungu peke yake na tumekataa tuliyokuwa tukimshirikisha naye.

فَلَمْ يَكُ يَنفَعُهُمْ إِيمَانُهُمْ لَمَّا رَأَوْا بَأْسَنَا سُنَّتَ اللَّـهِ الَّتِي قَدْ خَلَتْ فِي عِبَادِهِ وَخَسِرَ هُنَالِكَ الْكَافِرُونَ ﴿٨٥﴾

85. Lakini imani yao haikuwa ni yenye kuwafaa walipoiona adhabu yetu. Ni desturi ya Mwenyezi Mungu iliyopita kwa waja wake. Na hapo waliokufuru watapata hasara.

MWENYEZI MUNGU AMEWAJAALIA WANYAMAHOWA

Aya 79 – 85

MAANA

Mwenyezi Mungu ndiye ambaye amewajaalia wanyamahowa ili muwapande baadhi yao na wengine muwale.

Wanyamahowa ni ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewatumikisha kwa ajili ya manufaa ya binadamu; kama vile kula na kupanda.

Amewahusu kuwataja, pamoja na kuwa neema zake hazina idadi, kwa kuungana kwake na maisha ya waarabu wakati huo, na mpaka sasa bado wana mahitaji mengi sana katika baadhi ya miji.

Na katika hao mna manufaa mengine; kama vile kunufaika na manyoya yake na ngozi zake. Na manapata kwao haja zilizo vifuani mwenu; kama vile kubeba mizigo mizito na bidhaa mbalimbali kutoka mji mmoja hadi mwingine.Na mnachukuliwa juu yao na juu ya majahazi.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (6:142) na Juz. 14 (16:66).

Na anawaonyesha ishara zake, basi ni ipi katika ishara za Mwenyezi Mungu mtaikataa?

Yaani mtaikataa pamoja na hoja na dalili? Ndio walikata kwa vitendo ishara za Mwenyezi Mungu na hukumu zake. Kwa sababu mema kwao ni maovu na maovu kwao ni mema.

Je, hawatembei katika ardhi wakaona ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao na wakilima ardhi.

Historia ya watu wa ardhi imejaa mazingatio na mawaidha kwa mwenye kuzingatia na kupata somo. Ni uma ngapi zilifikia ukomo wa starehe na maendeleo, lakini walipopetuka mipaka, Mwenyezi Mungu aliwakamata kwa dhulma zao kwa mshiko wa Mwenye nguvu na uweza.Basi hayakufaa waliyokuwa wakiyachuma; kama vile utawala, mali na makasri na ngome walizozijenga. Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (12:109), Juz. 17 (22:46) na Juz 21 (30:9).

Basi walipowajia Mitume wao kwa dalili zilizo wazi wakifurahia elimu waliyokuwa nayo.

Makusudio ya furaha hapa ni kughurika. Na makusudio ya elimu ni sababu za utajiri, yaani elimu ya kuzalisha chakula na mavazi. Hilo linaashiriwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao na wakilima ardhi.’ Qarun naye alipoambiwa: “Na utafute kwa aliyokupa Mwenyezi Mungu makazi ya Akhera” Alijibu: “Nimepewa haya kwa sababu ya elimu” Juz 20 (28:77-78)

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu aliwatuma mitume, kwa hoja mkataa, wakati uliopita kwenye umma zilizokuwa na utajiri; kama vile viwanda n.k. Wakaghurika kwa sababu hizi au kwa elimu na wakawafanyia maskhara manabii wa Mwenyezi Mungu na vitabu; sawa na mashirika ya leo yanayohodhi kila kitu ambayo yanaikataa haki na ubinadamu na kudharau thamani yake na amani ya mataifa

Na yakawazunguka waliyokuwa wakiyafanyia stihzai.

Mwenyezi Mungu aliwaadhibu kwa kupituka kwao mipaka na yakawasibu yale waliyokuwa wakiyadharau. Huu ndio mwisho wa kila mwenye kupituka mipaka na kuasi, hata kama muda utarefuka kiasi gani.

Walipoiona adhabu yetu wakasema: Tumemwamini Mwenyezi Mungu peke yake na tumekataa tuliyokuwa tukimshirikisha naye.

Walipokuwa katika amani ya Mwenyezi Mungu walimkufuru, lakini walipoiona adhabu yetu wakasema tumeamini,lakini imani yao haikuwa ni yenye kuwafaa walipoiona adhabu yetu. Kwa sababu hii sio imani yoyote ispokuwa ni kukimbia adhabu, lakini watakimbia wapi?

Ni desturi ya Mwenyezi Mungu iliyopita kwa waja wake, ambayo ni kuwa Mwenyezi Mungu anasikiliza toba na kuzikubali katika nyumba ya taklifa na matendo sio katika nyumba ya hisabu na malipo.

Na hapo waliokufuru watapata hasara.

Kila mkosefu ni mwenye hasara na mtupu.

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI: SURAT AL-GHAAFIR

9

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

Sura Ya Arubaini Na Mmoja: Surat Fussilat. Imeshuka Makka, ina Aya 54.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

حم ﴿١﴾

1. Haa Mim.

تَنزِيلٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٢﴾

2. Ni uteremsho kutoka kwa Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

كِتَابٌ فُصِّلَتْ آيَاتُهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٣﴾

3. Ni Kitabu kilichopambanuliwa Aya zake. Qur’an ya Kiarabu kwa watu wanaojua.

بَشِيرًا وَنَذِيرًا فَأَعْرَضَ أَكْثَرُهُمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ ﴿٤﴾

4. Inayotoa bishara, na inayoonya. Lakini wengi wao wamepuuza; kwa hiyo hawasikii.

وَقَالُوا قُلُوبُنَا فِي أَكِنَّةٍ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ وَفِي آذَانِنَا وَقْرٌ وَمِن بَيْنِنَا وَبَيْنِكَ حِجَابٌ فَاعْمَلْ إِنَّنَا عَامِلُونَ ﴿٥﴾

5. Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayotuitia, na masikio yetu yana uziwi, na baina yetu na wewe kuna pazia. Basi wewe tenda, nasi tunatenda.

قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَاسْتَقِيمُوا إِلَيْهِ وَاسْتَغْفِرُوهُ وَوَيْلٌ لِّلْمُشْرِكِينَ ﴿٦﴾

6. Sema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; ninapewa wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake maghufira. Na ole wao wanaomshirikisha.

الَّذِينَ لَا يُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ ﴿٧﴾

Ambao hawatoi Zaka nao ndio wanaoikataa Akhera

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٨﴾

8. Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema watakuwa na ujira usiosimbuliwa.

KITABU KILICHOPAMBANULIWA

Aya 1 – 8

MAANA

Haa Mim.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1). Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameianza sura hii kwa kuitaja Qur’ani na kuisifu kwa sifa zifuatazo:

1.Ni uteremsho kutoka kwa Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Qur’ani imetoka kwa Mwingi wa kurehemu Mwenye kurehemu, nayo ni rehema kwa walimwengu. Pia aliyeshuka nayo kuileta kwa Muhammad(s.a.w. w ) ni rehema, kwa sababu yeye ni roho mwaminifu. Na Mwenyezi Mungu amemtolea ushahidi Mtume wake mtukufu kuwa yeye “anawahangaikia sana; kwa waumini ni mpole mwenye huruma” Juz. 11 (9:128)

Kwa hiyo basi Qur’ani ni rehema, aliyetumwa kuifikisha kwa Mtume ni rehema, Mtume ni rehema na Yule ambaye ameiteremsha ndiye msingi na chimbuko la rehema. Basi natija ya uhakika ya rehema (huruma) hizi nne ni kuwa mwenye kushikamana na Qur’ani na akaitumia, hushukiwa na mmiminiko wa rehema, na mwenye kuachana nayo, atakuwa ameidhulumu nafsi yake na ameichagulia maangamizi na balaa.

2.Ni Kitabu kilichopambanuliwa Aya zake.

Zinazobainisha halali ya Mwenyezi Mungu, haramu yake, nasaha zake na mawaidha yake, wala hazikumwachia udhuru mwenye kutafuta udhuru na visababu.

3.Qur’ani ya Kiarabu kwa watu wanaojua.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameiteremsha Qur’ani kwa Kiarabu, kwa vile hamtumi Mtume ispokuwa kwa lugha ya watu wake, ili waweze kumfahamu. Ilikuwa hivyo kwa Ibrahim, Tawrat ya Musa na Injil ya Isa(a.s) .

Nabii Muhammad(s.a.w. w ) alimwandikia Kisra, Kaizari, viongozi na wafalme wengineo wasiokuwa wa kiarabu, kwa lugha ya kiarabu, akiwaita kwenye Uislamu. Yametangulia maneno kuhusiana na hilo katika Juz. 12 (12:2) na Juz. 22 (36:1-12) kifungu ‘Mdundo wa ndani katika Qur’ani’.

Vyovyote iwavyo ni kuwa siri ya ukuu wa Qur’ani haiwi kwenye lugha na mfumo peke yake; bali inakuwa katika maana yake na malengo yake ya kudumu yasiyokuwa na mipaka ya kibaguzi, kizazi wala wakati.

4.Inayotoa bishara, na inayoonya.

Qur’ani inampa mtiifu habari njema ya rehema za Mwenyezi Mungu na pepo yake, na inamuonya muasi kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu na hasira yake.

Lakini wengi wao wamepuuza; kwa hiyo hawasikii.

Wamepuuza haki kwa ujinga na kung’ang’ania kuiga mababa au tamaa ya manufaa ya haraka haraka; hata kama ni njozi na mawazo tu.

Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayotuitia, na masikio yetu yana uziwi, na baina yetu na wewe kuna pazia. Basi wewe tenda, nasi tunatenda.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) aliwapa, wapenda anasa wakishirikina mwito wa kumwamini Mwenyezi Mungu peke yake na kutumia Kitabu chake, lakini jawabu lao lilikuwa nyoyo zetu zina kizuizi na wewe, na masikio yetu hayakusikilizi na sisi na wewe tuko mbali mbali. Jitahidi utakavyo na utoe vitisho sisi hatutishiki.

Hivi ndivyo yafanyavyo matamanio – yanaua moyo na kupofusha macho na yanatoa uhuru wa ujinga na upotevu.

Sema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; ninapewa wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake maghufira.

Mataghuti walimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kuwa baina yetu na wewe kuna kizuizi, Mwenyezi Mungu akamwamuru Nabii wake mtukufu awaambia, kizuizi hiki na nyinyi kimetokea wapi?

Kwani mimi si ni mtu tu kama nyinyi, kiroho na kimwili, nikifanya manayoyafanya? Je, wahyi ulionijia kuwa mimi na nyinyi tumwamini Mungu mmoja na tusimshirikishe na yeyote, tutubie kwake na twende sawa kwenye njia ya haki na uadilifu, ndio unaniweka mbali na nyinyi? Au hiyo ndio ingekuwa njia bora ya kutuunganisha kwenye heri na takua? Lakini nyinyi mmekataaa ispokuwa upofu tu na upotevu.

Na ole wao wanaomshirikisha ambao hawatoi Zaka nao ndio wanaoikataa Akhera.

Katika tafsir Albahrul-muhit imeelezwa kuwa sura hii imeshuka Makka na sharia ya zaka ya mali ilishuka Madina, kwa hiyo hapa hapana budi kuifasiri zaka kwa maana ya kutoa tu kwa aina yoyote ya heri au kuifasiri kwa maana ya kuitwaharisha nafsi na ushirikina.

Sisi tunaitilia nguvu tafsiri ya kwanza, kwa sababu kama tukifasiri kwa maana ya kutwaharika nafsi na washirikiana tayari wanajulikana kuwa haawakutwaharika na shirk, itakuwa ni kama kufasiri maji kwa maana ya maji. Kwa hiyo maana yanakuwa washirikina wamekusanya mambo mabaya matatu: Ushirikina, kupinga Akhera na ubakhili.

Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema watakuwa na ujira usiosimbuliwa.

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawalipa na kuwapa thawabu bila ya kuwasimbulia kwa sababu wao wanastahiki kila ukarimu. Neno kusimbulia tumelifasiri kutokana na neno mann ambalo pia hufasiriwa kwa maana ya kukatika. Kuifasiri Aya kwa maana yoyote kati ya hayo mawili inafaa, lakini tunaona ya kwanza iko karibu zaidi.

قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِالَّذِي خَلَقَ الْأَرْضَ فِي يَوْمَيْنِ وَتَجْعَلُونَ لَهُ أَندَادًا ذَٰلِكَ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٩﴾

9. Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliyeumba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyo ndiye Mola wa walimwengu wote.

وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ مِن فَوْقِهَا وَبَارَكَ فِيهَا وَقَدَّرَ فِيهَا أَقْوَاتَهَا فِي أَرْبَعَةِ أَيَّامٍ سَوَاءً لِّلسَّائِلِينَ ﴿١٠﴾

10. Na akaweka humo milima juu yake na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Ni sawa kwa wanaouliza.

ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَا طَائِعِينَ ﴿١١﴾

11. Kisha akaielekea mbingu, na ilikuwa moshi, akaiambia hiyo na ardhi: Njooni, kwa hiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni watiifu.

فَقَضَاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ فِي يَوْمَيْنِ وَأَوْحَىٰ فِي كُلِّ سَمَاءٍ أَمْرَهَا وَزَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَحِفْظًا ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿١٢﴾

12. Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akaipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya dunia kwa mataa na kwa ulinzi. Hayo ndio makadirio ya Mwenyezi nguvu Mwenye Kujua.

MWENYEZI MUNGU AMEUMBA ARDHI

Aya 9 – 12

MAANA

Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliyeumba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyo ndiye Mola wa walimwengu wote.

Kabla ya kuumbwa ulimwengu hakukuwa na wakati wala mahali. Hakukuwa na kitu chochote ispokuwa Mwenyezi Mungu tu mmoja mwenye nguvu.

Kwa hiyo basi makusudio ya siku mbili yatakuwa ni mikupuo miwili au nyakati mbili, kama ilivyosemekana. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:53). Kutokana na haya, tunataja waliyosema baadhi ya wafasiri: “Hakika mfumo wa Qur’ani unatofautiana na mifumo yote.

Inapoashiria suala lolote la kielimu hailionyeshi kama wanavyolionyesha wataalamu wa sayansi kwa ulinganishi na ufafanuzi; huwa mara nyingine hulileta kwa ishara, au alama za siri (code) au kwa kudokeza kwa neno ambalo huenda likampita anayelisikia wakati ule. Lakini inajua kuwa historia na mustakbali utalifafanua neno hilo na kulithibisha kwa uwazi.”

Hakika hii ilikuja mdomoni mwa Ibn Abbas tangu karne 14 zilizopita, pale aliposema: “Msifasiri Qur’ani, zama zitaifasiri” yaani msizame sana katika Aya za kilimwengu (kisayansi), kwa sababu maendeleo ya elimu itafichua siri zake.

Na akaweka humo milima juu yake.

Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ ﴿١٥﴾

“Na akaweka katika ardhi milima ili isiyumbe nanyi.” Juz. 14 (16:15)

Na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Ni sawa kwa wanaouliza.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) alibariki humo mimea, petroli n.k. Makusudio ya kukadiria chakula chake ni kuwa vyote vilivyo katika ardhi viko kwa kiasi cha mahitaji ya waliohai wote, kadiri idadi yao itakavyokuwa.

Kundi la wafasiri wamesema kuwa siku mbili zilizotajwa mwanzo ni kati- ka jumla ya siku nne; yaani kuumbwa ardhi na kukadiriwa chakula chake kulitimia ndani ya siku nne katika siku za Mwenyezi Mungu.

Makusudio ya wenye kuuliza hapa ni kila mwenye kuhitajia chakula. Na usawa ni kuwa Mwenyezi Mungu hakujaalia manufaa ya ardhi kwa jinsia fulani au taifa fulani tu; bali viumbe wote wako sawa katika riziki yake na fadhila yake. Akipatikana mwenye njaa basi ni kwa dhulma ya mwenye nguvu dhidi ya mnyonge. Tazama Juz. 8 (7:54-56) kifungu ‘Mwenyezi Mungu ameitengeneza ardhi na binadamu akaiharibu’

NINI UFUMBUZI WA TATIZO LA NJAA?

Kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘na akakadiria humo chakula chake,’ tutaashiria kauli ya wale waliosema kuwa sababu ya kwanza ya tatizo la njaa ulimwenguni ni wingi wa watu wanaozidi siku baada ya siku kufikia kutotosha chakula cha ardhi na heri zake; na kwamba hakiendani na ongezeko la uzazi. Kisha wakatofautiana kuhusu njia ya kutatua tatizo hili.

Kuna waliosema ufumbuzi ni vita vya maangamizi vitavyowaua watu wengi ili upatikane uwiano wa idadi ya watu na uzalishaji wa chakula. Fikra hii wameiunga mkono wenye viwanda vya silaha na walanguzi wa vyakula wanaotafuta utajiri kwa kukandamiza mailioni ya watu.

Wengine nao wakasema, kama sio vita basi kuwe na maradhi ya kuambukiza. Kisha ikaenea rai ya tatu ya kupanga uzazi. Hakuna neno kwa rai hii, kwa sababu kupanga uzazi ni haki ya kimaumbile na kisharia kwa kila mtu, kwa sharti ya kupanga kabla ya kupatikana uzazi; yaani kabla ya tone la manii halijatua kwenye mfuko wa uzazi kwa ajili ya kutengeneza mtoto.

Ama ile rai ya kwanza, inatosha tu kuwa haifai kutokana na walioitoa – wafanya biashara ya silaha na wenye mashirika ya kilanguzi kwenye mataifa masikini.

Sababu kubwa ya tatizo la njaa, inatokana na nguvu ya shari kwenye kheri za ardhi na kuzihodhi, anasa za wachache zinazotokana na kuwakandamiza wengi, kuangamiza mazao kwa ajli ya kulinda soko la kupandisha bidhaa, kutupa maelfu ya tani ya kemikali kwenye vijiji na mashamba ya Vietnam na kwengineko na kuielekeza elimu kwenye uzalishaji wa silaha.

Lau elimu ingeelekezwa kwenye uzalishaji wa usalama tu, ingelitosha kuzidi heri za ardhi kwa watu na riziki zingelikuwa kama mchanga. Jarida la UNESCO linaandika utafiti uliosema: Gharama za kombora moja tu kubwa inatosha kujenga Hospitali 75, kila hospitali moja ikiwa na vitanda 100, vikiwa na mahitaji yake yote. Au kutosha kununua majembe 50,000 ya kukokotwa, yanayoweza kulima mamilioni ya heka badala ya kulima makombora ya kuangamiza. Serikali ya Marekani imetumia $ 400, Bilioni kwenye vita vya Vietnam kabla ya kumalizika[3] .

Je, mabilioni yote haya si katika heri za ardhi na baraka zake? Lau yangelitumika katika kilimo si yangelitosha kulima mapori yote na hata bahari na kwenye sayari nyingine? Watu wote ardhini wangeliishi maisha ya raha.

Zaidi ya hayo, lau ingelikuwa kweli kauli ya aliyesema kuwa watu wamezidi mahitaji yao ardhini, maana yake ingelikuwa Mwenyezi Mungu hakupangilia vizuri makadirio na makisio, na kwamba Yeye anakosea mahisabu ya wakazi wa ardhini kila wakati unavyozidi kupita au kuwa Yeye anakosea kukadiria mahitaji ya chakula! Mwenyezi Mungu Mtukufu ametukuka na ametakata na wayasemayo wajinga.

Tatizo la njaa duniani haliwezi kutatuka kwa vita, maradhi ya kuambukiza wala kwa kupanga uzazi. Kutakua na faida gani ya yote haya ikiwa katika watu kuna dhalimu na mwenye kudhulumiwa na mlaji na mwenye kuliwa?

Ufumbuzi pekee wa tatizo hili ni kuondoa vikwazo baina ya mtu na nyenzo za maisha, kuitumia vizuri ardhi kuzalisha chakula na mavazi na kukidhi mahitaji ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kisha akaielekea mbingu, na ilikuwa moshi, akaiambia hiyo na ardhi: Njooni, kwa hiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni watiifu.

Kusema ‘tumekuja nasi ni watiifu’ ni kinaya cha uweza wa Mwenyezi Mungu na jinsi ulimwengu unavyofuata amri yake. Aya inaashiria kuwa anga kabla ya kuumbwa nyota ilikuwa na kitu kama moshi.

Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili.

Mbingu saba ni anga za aina saba za ulimwengu na wala sio nyota saba Tazama Juz. 18 (23:12-17). Kifungu ‘maana ya mbingu saba.’ Ama kuhusu siku mbili ni mikupuo miwili au nyakati mbili, kama ilivyosemekana.

Na akaipangia kila mbingu mambo yake.

Yaani ameumba katika kila mbingu nyota na vinginevyo ambavyo anayevijua ni Yeye ti.

Na tukaipamba mbingu ya dunia kwa mataa.

Ambayo ni sayari zinazoangaza kama taa.

Na kwa ulinzi.

Mwenyezi Mungu anazihifadhi sayari katika kuendelea kwake na mfumo mmoja.

Hayo ndio makadirio ya Mwenyezi nguvu, Mwenye Kujua.

‘Hayo’ ni hayo yaliyotangulia ya kuumbwa ardhi na manufaa yake, kuumbwa mbingu na kupambwa kwake na kuhifadhiwa kwake. Hayo hayawi ispokuwa kutoka kwa mwenye uweza anayepangilia vizuri mambo na mwenye ujuzi.

Haya ndio tuliyo nayo katika fahamu na elimu ya kufasiri Aya hizi. Tunayataja kwa kujichunga tukiwa na imani na Mwenyezi Mungu na uweza wake na kwa kila ghaibu aliyoiashiria katika Kitabu chake kwa tamko tusilolijua maana yake kwenye njia yake wala kutambua uhakika wa siri yake.

Kama tukitaka ziada ya maarifa hatupati ispokuwa kunakili kutoka katika vitabu vya wataalamu, ambapo wao hawaleti dalili za kuthibitisha au kukanusha ispokuwa mara chache.

Anayetaka maelezo zaidi ya kauli zao na arejee kwenye kitabu Alkawnul-a’jib (ulimwengu wa ajabu) cha Hafidh Twawqan, Maallah fis samai (Pamoja na Mwenyezi Mungu katika mbingu) cha Ahmad Zakiy na vinginevyo.


10

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

فَإِنْ أَعْرَضُوا فَقُلْ أَنذَرْتُكُمْ صَاعِقَةً مِّثْلَ صَاعِقَةِ عَادٍ وَثَمُودَ ﴿١٣﴾

13. Basi wakipuuza, sema: Nawahadharisha ukelele mfano ukelele wa A’di na Thamudi.

إِذْ جَاءَتْهُمُ الرُّسُلُ مِن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ قَالُوا لَوْ شَاءَ رَبُّنَا لَأَنزَلَ مَلَائِكَةً فَإِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ ﴿١٤﴾

14. Walipowafikia Mitume mbele yao na nyuma yao wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu! Wakasema: Angelitaka Mola wetu bila ya shaka angeliwateremsha Malaika. Basi sisi hakika tunayakataa hayo mliyotumwa.

فَأَمَّا عَادٌ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَقَالُوا مَنْ أَشَدُّ مِنَّا قُوَّةً أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَهُمْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ ﴿١٥﴾

15. Ama kinaA’di walitakabari katika ardhi bila ya haki, na wakasema: Nani aliye na nguvu zaidi kuliko sisi? Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu ambaye amewaumba ni Mwenye nguvu zaidi kuliko wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu!

فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِي أَيَّامٍ نَّحِسَاتٍ لِّنُذِيقَهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَخْزَىٰ وَهُمْ لَا يُنصَرُونَ ﴿١٦﴾

16. Basi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku za nuhusi, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwahizi katika uhai wa duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina hizaya zaidi, na wala wao hawatanusuriwa.

وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ فَأَخَذَتْهُمْ صَاعِقَةُ الْعَذَابِ الْهُونِ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٧﴾

17. Na ama Thamudi tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko uwongofu. Basi uliwachukua ukelele wa adhabu ya kuwafedhehi kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma

وَنَجَّيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ ﴿١٨﴾

18. Na tukawaokoa wale ambao wameamini na wakawa na takua.

NAWAHADHARISHA UKELELE

Aya 13 – 18

MAANA

Basi wakipuuza, sema: Nawahadharisha ukelele mfano ukelele wa A’di na Thamudi. Walipowafikia Mitume mbele yao na nyuma yao wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu!

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) kuhusiana na washirikina wa kiarabu. Mbele yao na nyuma yao ni kinaya cha msisitizo wa mitume na jitihadi zao katika kubashiria na kuonya, na kwamba wao walifuata kila njia kwa ajili ya kuwaongoza wao, lakini shetani akawapambia na akawaingizia dhana yake, pale aliposema:

ثُمَّ لَآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَائِلِهِمْ وَلَا تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ ﴿١٧﴾

“Kisha hakika nitawaendea kwa mbele yao na nyuma yao na kuumeni kwao na kushotoni kwao; wengi katika wao hutawakuta wenye kushukuru.” Juz. 8 (7:17).

Maana ni kuwa, sema ewe Muhammad kumwambia yule anayekukanusha wewe na risala yako kuwa A’d na Thamud waliwakadhibisha waliowalingania kama haya ninayoyalingania – Tawhid, na wakatoa juhudi zao kwa ajili ya uongofu wao.

Lakini walipong’ang’nia kwenye upotevu, Mwenyezi Mungu aliwakamata kwa adhabu ya dunia na Akhera na kwam- ba mimi nawaonya yasije yakawasibu yale yaliyowasibu wao.

Wakasema: Angelitaka Mola wetu bila ya shaka angeliwateremsha Malaika. Basi sisi hakika tunayakataa hayo mliyotumwa.

A’d na Thamud waliwajibu mitume kwa kuwakadhibisha kwa sababu Mwenyezi Mungu, kwa madai yao, hatumi ispokuwa Malaika. Kauli yao hii tumeipinga katika kufasiri Juz. 7 (6:9).

Ama kina A’di walitakabari katika ardhi bila ya haki.

Kauli yake Mwenyezi Mungu: bila ya haki ni katika upande wa kufafanua na kusiitiza tu. Kwa sababu hakuna kiburi cha haki; hasa ikiwa ni kumfanyia kiburi Mwenyezi Mungu.

A’di walifanya kiburi wakawadharau wanyonge na wakasema hakuna yoyote anayetuweza.

Na wakasema: Nani aliye na nguvu zaidi kuliko sisi? Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu ambaye amewaumba ni Mwenye nguvu zaidi kuliko wao?

Hili ni wazi, halihitaji dalili. Imam Aliy(a.s) anasema:“Kila mtukufu asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni dhalili, na kila mwenye nguvu asiyekua yeye Mungu ni dhaifu, na kila mfalme asiyekua Yeye ni mmilikiwa, na kila mjuzi asiyekua yeye ni mwanafunzi na kila muweza asiyekua Yeye ni dhaifu.

Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu!

Walizikana dalili za ulimwengu zinazofahamisha umoja wa Mwenyezi Mungu na ukuu wake. Wakasema kila kilichomo ulimwenguni pamoja na mpangilio wake na nidhamu ni kazi ya maumbile.

Basi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku za nuhusi, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwahizi katika uhai wa duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina hizaya zaidi, na wala wao hawatanusuriwa.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwadhibu duniani kwa upepo uliokuja na baridi katika siku za mkosi na hizaya, kisha watakamilisha adhabu kali zaidi na ya kufedhehesha huko Akhera kuliko adhabu ya duniani.

Na ama Thamudi tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko uwongofu. Basi uliwachukua ukelele wa adhabu ya kuwafedhehi kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.

Aya hii ni dalili wazi kwamba mtu ana hiyari wala halazimishwi, kwa sababu inasema Mwenyezi Mungu aliwaongoza Thamud kwenye njia ya uokovu, akawaamrisha kuifuata na akawakataza maasi, akawabainishia njia ya maangamizi akawakataza na kuwahadharisha na mwisho mbaya kama wataifuata, lakini wakaathirika nayo kuliko ya uokovu; ikawa malipo yao ni balaa na hasara.

Na tukawaokoa wale ambao wameamini na wakawa na takua.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwaokoa kwa sababu walifuata njia ya uokovu. Yametangulia mazungumzo kuhusu A’di katika Juz.12 (11:50) na kuhusu Thamud katika Juzuu hiyo hiyo na sura hiyo Aya 50.

وَيَوْمَ يُحْشَرُ أَعْدَاءُ اللَّـهِ إِلَى النَّارِ فَهُمْ يُوزَعُونَ ﴿١٩﴾

19. Na siku watakapokusanywa maadui wa Mwenyezi Mungu kwenye Moto, nao watazuiliwa.

حَتَّىٰ إِذَا مَا جَاءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ وَجُلُودُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٢٠﴾

20. Hata watakapoufikia Moto yatawashuhudia masikio yao, na macho yao na ngozi zao kwa waliyokuwa wakiyatenda.

وَقَالُوا لِجُلُودِهِمْ لِمَ شَهِدتُّمْ عَلَيْنَا قَالُوا أَنطَقَنَا اللَّـهُ الَّذِي أَنطَقَ كُلَّ شَيْءٍ وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢١﴾

21. Na wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye ametamkisha kila kitu! Na Yeye ndiye aliyewaumba mara ya kwanza, na kwake Yeye mtarejeshwa.

وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّـهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٢٢﴾

22. Na hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, na macho yenu, na ngozi zenu, zisiwashuhudie. Lakini mlidhani kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika mliyokuwa mkiyatenda.

وَذَٰلِكُمْ ظَنُّكُمُ الَّذِي ظَنَنتُم بِرَبِّكُمْ أَرْدَاكُمْ فَأَصْبَحْتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٢٣﴾

23. Na hiyo dhana yenu mliyokuwa mkimdhania Mola wenu, imewaangamiza; na mmekuwa miongoni mwa waliopata hasara.

وَذَٰلِكُمْ ظَنُّكُمُ الَّذِي ظَنَنتُم بِرَبِّكُمْ أَرْدَاكُمْ فَأَصْبَحْتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٢٣﴾

23. Basi wakisubiri Moto ndio makazi yao. Na wakitoa udhuru hawakubaliwi.

MASIKIO YAO NA MACHO YAO YATAWASHUHUDIA

Aya 19 – 24

MAANA

Na siku watakapokusanywa maadui wa Mwenyezi Mungu kwenye Moto, nao watazuiliwa.

Aya hizi tulizo nazo zinaungana na Aya iliyopita inayosema: ‘Basi wakipuuza, sema: nawahadharisha ukelele mfano ukulele wa A’di na Thamudi.’ Yaani pia waambie ewe Muhammad kuwa Malaika wa adhabu watawapeleka wakosefu kwenye Jahannam kwa nidhamu.

Atakayechelewa watamkemea na atakayejaribu kukimbia watamzuia. Makusudio ni kuwa hawana pakukimbia.

Hata watakapoufikia Moto yatawashuhudia masikio yao, na macho yao na ngozi zao kwa waliyokuwa wakiyatenda.

Hakuna kitu Siku ya Mwisho ispokuwa hisabu na malipo. Baadhi ya Aya za Qur’ani, ikiwemo hii tuliyo nayo,zinafahamisha kwamba Mwenyezi Mungu hatamwaadhibu mkosefu siku hiyo mpaka amkinaishe kuwa ana dhambi na anastahili adhabu.

Hii ni miongoni mwa tofauti zilizoko baina ya hakimu wa duniani anayetoa hukumu yake kwa hali yoyote iwayo; awe mwenye kuhukumiwa amekinai kuwa kweli amekosea au la, na hukumu ya Mwenyezi Mungu huko Akhera; ambapo Mwenyezi Mungu kesho hatatoa hukumu mpaka mhukumiwa akinai kuwa anastahili adhabu.

Kwa ajili hii ndio kutakuwa na ushahidi mwingi dhidi ya mkosefu. Wachukuzi wa dini watashuhudia kuwa walimfikishia halali ya Mwenyezi Mungu na haramu yake, Malaika watatoa ushahidi kua aliasi na akafanya jeuri na kitabu cha matendo yake kitasajili kila kauli na kitendo. Ikiwa hatatosheka, ngozi yake itashuhudia kuwa iligusa haramu, kama zina na utangulizi wake, masikio yatatoa ushahidi kuwa yalisikia haki na yakaikataa na macho nayo yatatoa ushahidi kuwa yaliona dalili za umoja wa Mungu yakazikataa na mengineyo.

Aya inaashiria maana ya ndani yakuwa sharti la shahidi ni kutopendelea. Pengine mkosefu anaweza akatuhumu kwamba wafikisha dini na Malaika wanaweza kuwa upande wa Mwenyezi Mungu kwa vile wanafanya mambo kwa amri yake. Ndio maana Mwenyezi Mungu (s.w.t) akaleta ushahidi wa mtu mwenyewe binafsi ili kuondoa tuhuma hii hata kama si ya kweli.

Kuna Hadith isemayo kuwa mja kesho atamwambia Mola wake: Je, hukunikataza dhulma? Atajibiwa: ndio! Basi atasema: Mimi sitakubaliana na ushahidi ispokuwa ushahidi wa nafsi yangu. Basi hapo Mwenyezi Mungu Mtukufu ataviamuru viungo vitoe ushahidi. Mja mwenye dhambi atasema: Potoleeni mbali! Mara ngapi nimewapinga!

Na wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia?

Kauli yao hii inaonyesha kuwa baadhi wa wakosefu hawatakubali ushahidi wa wafikishaji dini na wa Malaika na kwamba wao watafikiria kuwa kukataa kwao huku kutawafaa, lau si Mwenyezi Mungu kuwawekea ushahidi wao wenyewe.

Zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye ametamkisha kila kitu! Na Yeye ndiye aliyewaumba mara ya kwanza, na kwake Yeye mtarejeshwa.

Viungo vyao duniani vinatamka kwa lugha ya kihali na kushuhudi hekima na mpangilio uliomo duniani kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mwanzilishi na mrejeshaji. Na akhera vitatamka hivyo hivyo kwa uwazi kabisa. Wametofautiana wafasiri katika namna ya ushahidi wa viungo kesho.

Kuna wanaosema kuwa kutajitokeza alama za kuonyesha makosa yaliyofanyika. Wengine wakasema kuwa Mwenyezi Mungu atavitamkisha hasa kiuhakika. Hii ndio kauli iliyo wazi, kwa sababu dhahiri ya Aya inaonyesha hivyo, na akili hailikatai hilo.

Na hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, na macho yenu, na ngozi zenu, zisiwashuhudie. Lakini mlidhani kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika mliyokuwa mkiyatenda.

Makusudio ya kudhani hapa ni kuitakidi. Yaani mliamini enyi wakosefu kuwa mnafanya makosa kujificha mkihofia watu na sio kumhofia Mwenyezi Mungu, kwamba hajui mnayoyafanya kwa kujificha, na kwamba viungo vyenu havitawafichua siku ya hisabu.

Na hiyo dhana yenu mliyokuwa mkimdhania Mola wenu, ime- waangamiza; na mmekuwa miongoni mwa waliopata hasara.

Itikadi ya ubatilifu ndiyo iliyowapeleka kwenye Jahannam na ni mrejeo mabaya. Hii vile vile inalingana na wale wanaoiamini Akhera kinadharia na kuikana kimatendo; pale wanapojificha na watu na hawajifichi na Mwenyezi Mungu.

Bali hawa ni wabaya zaidi kuliko wale wanaopinga ufufuo na uweza wa Mwenyezi Mungu, kwa sababu wamemuasi Mwenyezi Mungu wakiwa na uhakika kuwa yuko nao akisikia na kuona; na kwamba hakifichiki kwake chochote katika mbingu na ardhi.

Basi wakisubiri Moto ndio makazi yao. Na wakitoa udhuru hawakubaliwi.

Wakivumilia moto wakosefu basi ndio sawa na ndio makazi yao wala hawataokoka. Na wakiomba radhi kwa Mwenyezi Mungu hawaridhii.” Na wakiomba msaada watapewa maji kama mafuta yaliyotibuka yanayobabua nyuso. Kinywaji kibaya kilioje na mahali pabaya palioje pa kupumzika!” Juz. 15 (18:29).

وَقَيَّضْنَا لَهُمْ قُرَنَاءَ فَزَيَّنُوا لَهُم مَّا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ إِنَّهُمْ كَانُوا خَاسِرِينَ ﴿٢٥﴾

25. Na tukawawekea marafiki, na wakawapambia yaliyo mbele yao na nyuma yao. na ikawathibitikia kauli wawe pamoja na uma zilizopita kabla yao, miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa ni wenye kuhasirika.

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَسْمَعُوا لِهَـٰذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُونَ ﴿٢٦﴾

26. Na wale ambao wamekufuru walisema: Msiisikilize Qur’ani hii, na timueni zogo, huenda mkashinda.

فَلَنُذِيقَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا عَذَابًا شَدِيدًا وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَسْوَأَ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٢٧﴾

27. Basi wale ambao wamekufuru hapana shaka tutawaonjesha adhabu kali, na hapana shaka tutawalipa malipo ya mabaya zaidi waliyokuwa wakiyafanya.

ذَٰلِكَ جَزَاءُ أَعْدَاءِ اللَّـهِ النَّارُ لَهُمْ فِيهَا دَارُ الْخُلْدِ جَزَاءً بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ ﴿٢٨﴾

28. Hayo ndiyo malipo ya maadui wa Mwenyezi Mungu - Moto! Humo watakuwa na nyumba ya kudumu, ndiyo malipo yao kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara zetu.

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا رَبَّنَا أَرِنَا اللَّذَيْنِ أَضَلَّانَا مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ نَجْعَلْهُمَا تَحْتَ أَقْدَامِنَا لِيَكُونَا مِنَ الْأَسْفَلِينَ ﴿٢٩﴾

29. Na wale ambao wamekufuru watasema: Mola wetu! Tuonyeshe waliotupoteza miongoni mwa majini na tuwaweke chini ya miguu yetu, wapate kuwa miongoni mwa walio chini kabisa.

WALIOKUFURU WALISEMA MSISIKILIZE QUR’ANI

Aya 25 – 29

MAANA

Na tukawawekea marafiki, na wakawapambia yaliyo mbele yao na nyuma yao.

Makusudio ya yaliyo mbele yao ni dunia na balaa yake, na ya nyuma yao ni Akhera ambayo kwa wapinzani ni uzushi. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaandalia mataghuti marafiki wabaya wanaowavutia na maovu na kuwaweka mbali na mema.

Unaweza kuuliza : ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyewapangia watakaowahadaa kwenye upotevu na maasi, basi si itakuwa ni dhulma kuwaadhibu na kusema: ‘Basi ikiwathibitikia kauli;’ yaani adhabu.

Jibu : Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewafanyia hivyo baada ya wao wenyewe, kwa uchaguzi wao mbaya, kufuata njia ya upotevu. Hilo amelifafanua Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliposema:

وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ ﴿٣٦﴾

”Anayeyafanyia upofu maneno ya Mwingi wa rehema tunamwekea Shetani kuwa ndiye rafiki yake.” (43:36)

Pia akasema:

فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ ﴿٥﴾

“Walipopotoka Mwenyezi Mungu alizipotosha nyoyo zao” (61:5).

Hayo yamekwishaelezwa huko nyuma mara kadhaa.

Na ikawathibitikia kauli wawe pamoja na uma zilizopita kabla yao, miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa ni wenye kuhasirika.

Waliasi na wakafanya uovu, wakastahili adhabu, sawa na walivyostahili mfano wao katika umma zilizopita. Aya hii inafahamisha kuwa majini wana umma na vizazi, wana mitume na manabii; na miongoni mwao kuna wema na wengine waovu, sawa na watu.

Na wale ambao wamekufuru walisema: Msiisikilize Qur’ani hii, na timueni zogo, huenda mkashinda.

Mataghuti walishangaa walipoona athari ya Qur’ani na inavyoatwala kwenye nafsi za watu; wakawa wamedangana hawajui wafanye nini baada ya kushindwa kukabili hoja kwa hoja. Kisha wakaafikiana waipige vita kwa mambo yasiyosawa – waipe sifa ya uchawi na vigano na waifanyie vurugu. Wakaona kuwa hiyo ndiyo njia iliyobaki ya kuishinda.

Hii ya kufanya vurugu inafahamisha kukubali kwao kushindwa, na kwamba Qur’ani ni ngome ya Mwenyezi Mungu iliyoshinda fikra zote za bianadamu, wakati wote.

Basi wale ambao wamekufuru hapana shaka tutawaonjesha adhabu kali, na hapana shaka tutawalipa malipo ya mabaya zaidi waliyokuwa wakiyafanya.

Makosa yanagawanyika sehemu mbili: Kuna yale mabaya na yale yaliyo mabaya zaidi. Vile vile malipo kwa sababu:

مَنْ عَمِلَ سَيِّئَةً فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا ﴿٤٠﴾

“Mwenye kutenda uovu hatalipwa ila sawa na huo,” (40:40).

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja mabaya zaidi waliyoyafanya ili kubainisha kuwa malipo nayo yatakuwa mabaya zaidi, sawa na matendo yao.

Hayo ndiyo malipo ya maadui wa Mwenyezi Mungu - Moto! Humo watakuwa na nyumba ya kudumu, ndiyo malipo yao kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara zetu.

Hayo ni ishara ya hayo malipo ya mtendo mabaya zaidi ambayo ni kudumu katika moto wa Jahannam. Kudumu huku, Mwenyezi Mungu amekufanya ni malipo ya kila mpinzani mwenye inadi na mshirikina, mambo ambayo hayana udhuru wowote kabisa.

Ujinga unaweza kuwa ni udhuru, lakini sio katika shirki na kupinga. Kwa sababu dalili za umoja wa Mwenyezi Mungu na utukufu wake hazikujificha, ziko waziwazi. Kuzijua kunahitaji kuangalia kusikokuwa kwa kuiga au kufuata mapenzi ya moyo.

Na wale ambao wamekufuru katika wadhaifuwatasema: Mola wetu! Tuonyeshe waliotupoteza miongoni mwa majini na watu katika wale waliofuatwa,tuwaweke chini ya miguu yetu, wapate kuwa miongoni mwa walio chini kabisa.

Walimuomba Mwenyezi Mungu awaletee wale waliowapoteza katika mashetani watu na majini ili wawakanyage na wawe sehemu ya ndani kabisa ya Jahannam, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekwishawafanyia mabaya na mabaya zaidi.pale alipomkamata kila mmoja kwa dhambi yake.


11

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ ﴿٣٠﴾

30. Hakika wale ambao wamesema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakawa na msimamo. Huwateremkia Malaika: Msiwe na hofu, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa.

نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ ﴿٣١﴾

31. Sisi ni mawalii wenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinachotamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyovitaka.

نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ ﴿٣٢﴾

32. Ni takrima itokayo kwa mwingi wa Maghufira, Mwenye kurehemu.

وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّـهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٣٣﴾

33. Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?

وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ ﴿٣٤﴾

34. Mema na maovu hayawi sawa. Zuia uovu kwa lilio jema zaidi. Mara yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki mkubwa.

وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ ﴿٣٥﴾

35. Lakini hawapewi hayo ila wanaosubiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٣٦﴾

36. Na kama Shetani akikuchochea kwa uchochezi basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

WALISEMA MOLA WETU NI MWENYEZI MUNGU KISHA WAKAWA NA MSIMAMO

Aya 30 – 36

MWENYEZI MUNGU NA MTU NA MATENDO

Mwenye kufuatilia Aya za Qur’ani yenye hekima, atakuta kwamba mantiki yake yote na ufahamu wake unajulisha kuwa matendo na imani ndio kila kitu kwa mtu. Hebu angalia dalili zifuatazo:

1. Aya zinazofahamisha kuwa lengo la kwanza na hekima kubwa ya kuweko mtu ni kutenda mambo mema; miongoni mwa Aya hizo ni:

الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ ﴿٢﴾

“Ambaye ameumba mauti na uhai ili kuwajaribu ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi” (67:2).

Tazama Juz. 21 (31:33) kifungu ’Kwa nini Mungu akamuumba mtu?’

2. Aya zinazofahamisha kuwa matendo ndio mizani ya kumpima mtu kwenye msingi wake; mfano kauli hizi za Mwenyezi Mungu mtukufu:

كُلُّ امْرِئٍ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ ﴿٢١﴾

“Kila mtu atalipwa alichokichuma” (52:21)

وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٣٩﴾

“Na hamtalipwa ila mliyokuwa mkiyafanya” Juz. 23 (37:39)

وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِّمَّا عَمِلُوا وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٢﴾

“Na wote wana daraja mbalimbali kutokana na yale waliyoyatenda” (Juz. 8 (6:132) na nyinginezo.

3. Ama kauli yake Mwenyezi mungu Mtukufu:Hakika wale ambao wamesema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakawa na msimamo, ni dalili wazi na mkataa kwamba vitendo ndio dhahiri ya pekee inayoakisi imani ya kweli ya Mwenyezi Mungu iliyo halisi na kwamba yeyote mwenye kusema kuwa mimi ni mumin bila ya kuitafsiri imani yake kwa vitendo katika mfungamano wake na wa muumba wake na nafsi yake na jamii yake, basi huyo atakuwa ni muongo mzushi.

Kuongezea zaidi ni kuwa makusudio ya Qur’ani kuhusu matendo ni matendo ya kujenga yenye kuzaa matunda. Tumezungumzia kwa ufafanuzi zaidi kuhusu msimamo katika Juz. 12 (11: 110 – 115) kifungu cha ’Msimamo.’

4. Zaidi ya yote ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amefahamisha kuweko kwake na utukufu wake kwa matendo. Anasema:

سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ ﴿٥٣﴾

“Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli.” (41:53)

Kisha akataja Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aya kadhaa zinazohusiana na haya, tutatosheka na hizi tu:

خَلَقَ الْإِنسَانَ ﴿٣﴾ عَلَّمَهُ الْبَيَانَ ﴿٤﴾ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ ﴿٥﴾

“Amemuumba mtu, akamfundisha kubaini. Jua na mwezi (huenda) kwa hisabu” (55:3-5).

Huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiwe na hofu, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa.

Kila jambo lina muda maalum. Utakapokuja muda wa wale waliokuwa na msimamo katika njia ya Mwenyezi Mungu, Malaika watawateremkia na rehema kwa utulivu na habari njema kwamba Mwenyezi Mungu ameyaona matendo yao na kuridhia mahangaiko yao. Kwa hiyo amewaandalia makazi ya heshima aliyowaahidi kupitia kwa manabi na mitume wake.

Sisi ni mawalii wenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinachotamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyovitaka.

Ni takrima itokayo kwa Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

Bado yanaendelea mazungumzo baina ya Malaika wa rehema na wale waliokuwa na msimamo. Yaani watiifu na wenye msimamo watakuwa kwa Mola wao Mwenye kurehemu na watapata kila wakitakacho kutokana na riziki ya ukarimu.

Ibn Al-arabi katika Futahitil-Makkiya anasema kuhusu Aya hii, kwamba Malaika watawaambia wenye ikhlasi kabla ya kutoka kwenye makazi ya kuisha kwenda kwenye makazi ya kudumu: Sisi tumekuwa mawalii wenu duniani kwa sababu shetani aliwajaribu kuwahadaa muache njia iliyonyooka na sisi tukiwakataza na mlikuwa mkitusikiliza. Vile vile sisi ni mawalii wenu Akhera kwa sababu tunawatolea ushahidi wa imani na msimamo mbele ya Mwenyezi Mungu.

Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?

Tukiunganisha Aya hii na ile isemayo “Hakika wale ambao wamesema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu kisha wakawa na msimamo,” tutapata maana kuwa imani ya kweli iko sehemu tatu: Kwanza, kutangaza kumwamini Mwenyezi Mungu. Pili, kutenda kwa mujibu wa sharia ya Mwenyezi Mungu. Na matendo yaliyo muhimu na adhimu zaidi ni kuwahudumia watu. Tatu, ni kutoa mwito wa Mwenyezi Mungu.

I. Ya kwanza inafahamishwa na kauli: “Wale ambao wamesema Mola wetu ni Mwenyezi Mungu;” yaani wamelitangaza hilo mbele ya watu.

II. Ya pili inafahamishwa na kauli: “Kisha wakawa na msimamo.”

III. Na ya tatu: “Aitaye kwa Mwenyezi Mungu.” Mwenye kukusanya sifa tatu hizi anayo haki ya kusema “Hakika mimi ni katika Waislamu.” Lakini atakayesema hivyo bila ya kumwamini Mwenyezi Mungu au amemuamini Mwenyezi Mungu bila ya kuwahudumia watu na bila ya kulingania kwa Mwenyezi Mungu, basi huyo si Mwislamu kitu; ingawaje duniani anachukuliwa kama Mwislamu.

Mema na maovu hayawi sawa. Zuia uovu kwa lilio jema zaidi. Mara yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki mkubwa.

Makusudio ya mema hapa ni mema ya mjumbe anayelingania kwa Mwenyezi Mungu ambayo ni jihadi yake na uvumilivu wake wa maudhi kwenye njia hii. Na makusudio ya uovu ni uovu wa safihi aliye mjinga wa dini.

Maana ni kuwa tofauti ni kubwa baina yako wewe Muhammad, ukiwa unalingania kwa Mwenyezi Mungu na unavumilia maudhi kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, na yule ambaye ameitika mwito wako kwa upinzani, maudhi na kukuzulia. Matendo yako ni baraka na wema na matendo yao ni uovu na laana. Lakini pamoja na yote hayo ni juu yako kuwachukulia kwa upole na kuwasamehe, ukivumilia usafihi wao, kwani miongoni mwao wako ambao lau utawakabili kwa namna hii basi wanaweza kurudi kwa Mola wao na uadui ukageuka kuwa mahaba na chuki ikawa mapenzi.

Mtu yeyote anaweza kupata marafiki watakaomsaidia kwa maneno mazuri na anaweza kujitengenezea maadui kwa maneno machafu. Maneno ya watu wema yameweza kuwaongoza waovu wengi na kutatua matatizo mengi. Lau si hayo basi mito ingelijaa damu.

Lakini hawapewi hayo ila wanaosubiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.

Hayo ni hayo ya kuzuia uovu kwa wema. Mwenye bahati kubwa ni yule anayeridhiwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Maana ni kuwa kuzuia uovu kwa wema ni daraja kubwa ambayo haipati isipokuwa mwenye kuwa mvumilivu wa shida na akawa ana mwelekeo wa Mwenyezi Mungu.

Kwenye Nahjul-balagha imesemwa:“Subira katika imani ni kama kichwa katika mwili. Hakuna kheri katika mwili usiokuwa na kichwa wala katika imani isiyokuwa na subira.” Imesemwa tena:“Iondoe shari iliyoko kifuani kwa mwenzako kwa kuing’oa kifuani mwako.”

Na kama Shetani akikuchochea kwa uchochezi basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad(s.a.w. w ) . Tukiibia Aya ufahamu wake ni kuwa inapaswa mtu achukue hadhari wala asijione ni msafi hata akiwa na dini, elimu au akili kiasi gani. Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 9 (7:200).


12

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ ﴿٣٧﴾

37. Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliyeviumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu.

فَإِنِ اسْتَكْبَرُوا فَالَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ يُسَبِّحُونَ لَهُ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَهُمْ لَا يَسْأَمُونَ ﴿٣٨﴾

38. Na ikiwa watafanya kiburi, basi hao walioko kwa Mola wako wanamtakasa Yeye usiku na mchana, na wao hawachoki.

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ إِنَّ الَّذِي أَحْيَاهَا لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٣٩﴾

39. Na katika Ishara zake ni kwamba unaiona ardhi imetulia, lakini tunapoiteremshia maji mara unaiona inashtuka na kututumka. Bila ya shaka aliyeihuisha ardhi ndiye atakayehuisha wafu. Hakika Yeye ni Muweza juu ya kila kitu.

إِنَّ الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي آيَاتِنَا لَا يَخْفَوْنَ عَلَيْنَا أَفَمَن يُلْقَىٰ فِي النَّارِ خَيْرٌ أَم مَّن يَأْتِي آمِنًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ اعْمَلُوا مَا شِئْتُمْ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٤٠﴾

40. Hakika wale ambao wanaupotoa ukweli uliomo katika Ishara zetu hawatufichikii Sisi. Je, Atakayetupwa Motoni ni bora au atakayekuja kwa amani Siku ya Kiyama? Tendeni mpendavyo, kwa hakika Yeye anayaona mnayoyatenda.

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالذِّكْرِ لَمَّا جَاءَهُمْ وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ ﴿٤١﴾

41. Hakika wale ambao wanakataa dhikiri inapowajia. Na hayo bila ya shaka ni Kitabu chenye nguvu.

لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ ﴿٤٢﴾

42. Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa.

مَّا يُقَالُ لَكَ إِلَّا مَا قَدْ قِيلَ لِلرُّسُلِ مِن قَبْلِكَ إِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ وَذُو عِقَابٍ أَلِيمٍ ﴿٤٣﴾

43. Haambiwi ila yale yale waliyoambiwa Mitume wa kabla yako. Hakika Mola wako bila ya shaka ni Mwenye maghufira, na ni Mwenye adhabu chungu.

وَلَوْ جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا أَعْجَمِيًّا لَّقَالُوا لَوْلَا فُصِّلَتْ آيَاتُهُ أَأَعْجَمِيٌّ وَعَرَبِيٌّ قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ فِي آذَانِهِمْ وَقْرٌ وَهُوَ عَلَيْهِمْ عَمًى أُولَـٰئِكَ يُنَادَوْنَ مِن مَّكَانٍ بَعِيدٍ ﴿٤٤﴾

44. Na lau tungeliifanya Qur’ani kwa lugha ya kigeni wangelisema: Kwa nini Aya zake hazikupambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na mwarabu? Sema: Hii Qur’ani ni uwongofu na ponyo kwa wenye kuamini. Na wasioamini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako mahali mbali.

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ ﴿٤٥﴾

45. Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini pakatokea hitilafu kati yake. Na lau kuwa halikwishatangulia neno la Mola wangelihukumiwa. Na hakika wao wamo katika shaka nayo yenye kuwatia wasiwasi.

مَّنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ ﴿٤٦﴾

46. Anayetenda mema basi anajitendea mwenyewe, na anayetenda uovu basi ni juu ya yake; na Mola wako si mwenye kuwadhulumu waja.

HAUTAKIFIKIA UPOTOVU MBELE YAKE WALA NYUMA YAKE

Aya 37 – 46

SAFARI YA MWEZINI

Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja, katika Kitabu chake Kitukufu, Aya kadhaa za kilimwengu na zinavyomfahamisha Muumba na sifa Zake. Miongoni mwa Aya hizo ni zile za kutofautiana usiku na mchana, kuumbwa jua na mwezi n.k. Tazama Juz. 3 (3:27) Juz. 23 (36:37 – 40) na (39:5). Humo mumetajwa usiku, mchana, jua na mwezi.

Kutokana na kutajwa mwezi tutaashiria tukio muhimu lilitokea ulimwenguni la safari ya anga za mbali ya waamerika wawili Neil Amstrong na Edwin kwenda mwezini, katika majira ya kiangazi ya mwaka 1969. Watu walilizungumzia sana tukio hili na wengi wakaniuliza kuhusu maoni ya dini kuhusiana na safari hii. Nikajibu kwa makala iliyosambazwa magazetini, kisha nikaiunganisha na Tafsir Al-kashif kulingana na Aya zinazotaja mwezi. Basi kabla ya kuchapishwa tafsiri, mfanyakazi mmoja wa kiwanda cha uchapishaji akanishauri niiondoe makala hiyo, nami nikakubali bila ya kujua sababu.

Baada ya kupita muda mchache tangu kuchapishwa Tafsir Al-kashif , ikanibainikia kuwa ilikuwa vizuri sikuweka makala hiyo kwenye Tafsiri. Hiyo ilitokana na kuwa nilisoma kwenye gazeti la Al-akhabar la Misr la 6-2-1970, makala, iliyofasiriwa kutoka kwenye gazeti la Pravda la Urusi, ya wanasayansi wawili wa kirusi, Mikhail Vassin na Alexander Cherbakov.

Wataalamu hawa wawili walichunguza matokeo waliyoyatangaza wamarekani katika uchunguzi wao wa mchanga wa mwezini na madini yaliyopatikana kwenye ardhi ya mwezi, wakasema: “Somo hili linakataa nadharia zote zilizoenea kuhusiana na asili ya mwezi, wala halikubali isipokuwa tafsiri moja tu; kwamba mwezi umetengenezwa kwa usanii wa hali ya juu wenye mpangilio. Na iliyoutengeneza ni nguvu ya ajabu yenye uwezo usioweza kufikiwa na chochote.”

Hii inamaanisha kwamba wanavyoamini wamaada kuhusu ulimwengu ni njozi tu. Makala hii inaendelea kusema: “Uchunguzi wa kielimu wa kisasa unakataa nadharia zote na makisio yote kuhusu chanzo cha mwezi na kuan- za fikra mpya ya kutatua kitandawili hiki inayosema: Usanii wa mwezi umetokana na kitu kilichoendelea sana kielimu na kifani, kisha kikaunda harakati ya mwezi kwa vifaa vilivyoendela sana. Ndani ya mwezi kuna mamabo ya ajabu yasiyowezakana kupatikana kwa sadfa.”

Gamba la nje la mwezi liko na tabaka mbili za kimsingi: ya kwanza ni tabaka ya kutenganisha joto lenye unene wa 4 km. La pili lina unene wa 300 km. Juu yake kuna aina mbalimbali ya vifaa vilivyoundwa kuzuia mtingishiko. Kwa hiyo mwezi unaweza kuhimili safari bila ya kuondoka sehemu yake kwa mamilioni ya mamilioni ya miaka.”

Lakini kuna swali linataka majibu: Ikiwa mwezi umetengenezwa na kitu chenye akili iliyoendela, basi kitu hiki kimetoka wapi? Kwa nini kikafanya bidii ya kutengenza sayari hii? Ni kwa ajili ya kuzunguka kwenye sayari tu basi?

Nadharia ya kisasa haiwezi kujibu swali hili. Lakini inaamini kuwa makisio ya karibu zaidi kuliko jambo lolote ni kuwa mwezi umetengenezwa na kwamba mtenegenzaji wake amekuwa na mpangilio wa kiajabu.”

Wakomonisti wawili wanasema: “Akili inakataa makadirio na tafsiri yoyote isipokuwa moja tu, kwamba mwezi umetengenezwa na ilioutengeneza ni nguvu ya ajabu.”

Ndio! Ni kweli umetengenezwa, na mtengenezaji wake hana mshirika wala wa kufanana naye. Uhandisi wake ndio uliotuongoza kujua hilo.

Ama kauli ya wataalamu wawili kuwa umetengenezwa na kitu kilichoendelea sana na mfumo wake ni wa ajabu sana, kauli hii ni kukiri waziwazi kwamba kwenye mwezi kuna mpangilio ambao hauwezi kutokea kwa yeyote isipokuwa kwa aliye Muweza, Mwenye hekima ambaye hana mfano na chochote naye ni Muumba aliye Mjuzi.

Tuna uhakika kwamba hivi karibuni tutasoma kukiri wazi zaidi ya hivi, kutakakovunja kauli za wamaada na nadharia za walahidi. Na itathibitika kwa hisia na majaribio kwamba nyuma ya ulimwengu huu kuna nguvu inayoshinda nguvu zote inayokiamabia kitu kuwa na kikawa.

Hili haliwezi kuepukwa na maendeleo ya elimu na akili huru. Hapa ndio inakuwa siri ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

أَوَلَمْ يَنظُرُوا فِي مَلَكُوتِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ ﴿١٨٥﴾

“Je, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi na alivyoviumba Mwenyezi Mungu?”

Juz. 9 (7:185).

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٤﴾

“Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanotia akilini (mambo).” Juz. 13 (13:4)

هَـٰذَا خَلْقُ اللَّـهِ فَأَرُونِي مَاذَا خَلَقَ الَّذِينَ مِن دُونِهِ بَلِ الظَّالِمُونَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١١﴾

“Huu ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Basi nionyesheni wameumba nini hao wasiokuwa Yeye?” Juz. 21 (31:11)

Msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliye- viumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu.

Aliyeviumba, ni aliyeumba usiku, mchana, jua na mwezi au aliyeumba sayari na nyota zote. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameleta ibara ya jua na mwezi, kwa sababu ndivyo vilivyojitokeza zaidi kwa watu.

Mafakihi wameafikiana kwa kauli moja kwamba ni wajibu kusujudu kwa mwenye kuisoma au kuisikia Aya hii. Wengine wakasema, bali hata aliyesikia bila ya kukusudia pia atasujudu.

Aya inawaambia wasabai, walioabudu nyota, kutokana na manufaa yake, kuwa Mwenyezi Mungu ndiye ambaye ameumba sayari na akazifanya ziwe na manufaa kwa waja, nazo ni viumbe tu kama sisi, zinamwelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumsujuduia na kukubali utumishi.

Na ikiwa watafanya kiburi, basi hao walioko kwa Mola wako wanam- takasa Yeye usiku na mchana, na wao hawachoki.

Yaani ikiwa hao waabudu nyota watang’ang’ania ushirikina, basi Mwenyezi Mungu hana haja nao wala ibada yao, kwa sababu anao waja – Malaika – hawaachi kumsabihi Mwenyezi Mungu usiku na mchana.

Na katika Ishara zake ni kwamba unaiona ardhi imetulia, lakini tunapoiteremshia maji mara unaiona inashtuka na kututumka. Bila ya shaka aliyeihuisha ardhi ndiye atakayehuisha wafu. Hakika Yeye ni Muweza juu ya kila kitu.

Maana haya yamekaririka kwenye Aya kadhaa na kwa mifumo mbali mbali; miongoni mwazo ni: Juz. 17 (22:5)

Hakika wale ambao wanaupotoa ukweli uliomo katika Ishara zetu hawatufichikii sisi.

Washirikina waliitia ila Qur’ani wakasema ni uchawi na wakasema ni ngano, lakini Mwenyezi Mungu anajua kauli zao na atawauliza nazo na kuwaadhibu.

Je, Atakayetupwa Motoni ni bora au atakayekuja kwa amani Siku ya Kiyama?

Swali hili linabeba jawabu lake. Ni nani mwenye akili anayeweza kusema moto ni bora kuliko pepo au hofu ni nzuri kuliko amani? Lakini wakosefu wameghafilika na msingi huu, na wao hasa wameathirika na moto kuliko pepo na hofu kuliko amani.

Tendeni mpendavyo, kwa hakika Yeye anayaona mnayoyatenda.

Hii ni hadhri na onyo kwamba wao watakutana na adhabu baada ya kuifu- ata kwa njia ya kufuru na upotevu.

Hakika wale ambao wanakataa dhikiri inapowajia.

Makusudio ya dhikiri hapa ni Qur’ani. Hapa kuna maneno ya kukadiriwa, kuwa wataadhibiwa.

ISRAIL NA QUR’AN

Na hayo bila ya shaka ni Kitabu chenye nguvu. Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameisifu Qur’ani kuwa ina nguvu na kwamba haifikiwi na upotofu wowote. Maana ya kuwa na nguvu ni nguvu za hoja zake na dalili zake zilizo wazi. Ama kuwa haifikiwi na upotovu, wafasiri wametaja njia tano; iliyokaribu zaidi ni ile isemayo kuwa kila itikadi, sharia habari na mengineyo yaliyomo ndani yake ni haki isiyokuwa na shaka.

Yametangulia maelezo kwa ufafanuzi zaidi katika Juz.14 (15:9). Huko tumeeleza kuwa Israili ilichapisha maelfu ya nakala za Qur’ani na kuziko-roga baadhi ya Aya zake; mfano ile isemayo: “Na mwenye kutaka dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwake.” Juz. 3 (3:85), wakaandika: “Na mwenye kutaka dini isiyokuwa Uislamu itakubaliwa kwake.” Hili lilitokea mwaka 1968. Chuo kiku cha Al-azhar kilikusanya nakala hizi na kuzizuia zisisambae.

Israil ikarudia tena mnamo mwaka 1969 na ikakoroga Aya nyingine: “Walisema Mayahudi: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndiyo iliyofumba, na wamelaaniwa kwa waliyoyasema.” Juz. 6 (5:64), wakabadilisha neno ‘wamelaaniwa’ likawa ‘wameamini.’ Nakala hizi za Qur’ani ya kiisrail zikaenea kwenye maduka ya Lebanon na kwenye miji mingi ya Uarabuni. Pia ilisambazwa huko Malesia, Pakistan, India, Indonasia, Guinea, Ivory coast (Cote de vory) Iran n.k.

Leo hii tarehe 25-2-1970. Gazeti la An-nahar la Beirut limeandika kuwa wakili Faruq Sa’d amepeleka mshtaka kwa niaba ya Ofisi na wachapishaji wa Mash-had Alhusayniy ya Cairo ya kumtia hatiani mwenye kuivuruga Qur’ani Takufu, kuiiga, kuipotoa na kuirekebesha. Pia limeandika kwamba nakala za kupotoshwa zimechapisha Ujerumani Magharibi na wachapishaji wa Cologne – Doits.

Israil haikutosheka hapa na vita vyake dhidi ya Uislamu na waislamu, wakaitangaza Qur’ani ya kukorogwa kwenye idhaa yake. Idhaa ya Cairo ilitumia mwezi mzima kurikodi Qur’ani kutoka idhaa ya Israil.

Vile vile Israil imetengeneza radio ya mkono wanayoiuza kwa bei rahisi kabisa, ambayo haishiki idhaa yoyote isipokuwa idhaa yake inayopotosha Qur’ani tu. Israili inafanya yote haya na mengineyo kwa kuitikia msingi wa kizayui alioutangaza mmoja wa viongozi wake, aliposema: “Ni lazima tuifanye Qur’ani ni silaha ya kuwamaliza waislamu.”

Tumeyaeleza yote haya kama mfano wa vita vya Israil dhidi ya Uislam, ili pengine waweze kuzinduka baadhi ya wafalme na maraisi; bali hata baadhi ya masheikh wanaojiita waislamu, lakini wanafanyakazi kwa siri kwa manufaa ya Israil na wasaidizi wake.

Nilishangazwa na kauli ya sheikh mmoja mpotofu akisema: “Israil ina afadhali kuliko wengine kwa sababu inasoma Qur’ani kwenye idhaa yake.” Ndio ewe sheikh! Wacha kutangaza, bali inachapisha na kusambaza pia, lakini ile iliyopotoshwa na kukorogwa ili kumaliza Uislamu; sawa na baadhi ya wenye vilemba vya usheikh vya upotovu.

Huambiwi ila yale yale waliyoambiwa Mitume wa kabla yako.

Washirikina wa uma zilizotangulia waliwaambia mitume na manabii wao: “Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayotuitia…Hayakuwa haya isipokuwa ni vigano vya wakale…Hakuwa huyu isipokuwa ni mchawi mzushi.” Na hivi ndivyo walivyokuambia mataghuti wa watu wako ewe Muhammad! Kwa sababu Mola aliyekutuma wewe na aliyewatuma waliokuwa kabla yako ni mmoja na risala yake ni moja, na masilahi ya mataghuti ambayo yanasigana na wafuasi wa haki ni hayo hayo wakati wowote na mahali popote.

Hakika Mola wako bila ya shaka ni Mwenye maghufira, na ni Mwenye adhabu chungu.

Aya imekusanya vinyume viwili: msamaha wa mwenye dhambi ikiwa atatubia, na adhabu ikiwa ataendelea. Namna hii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anafanya katika Aya kadhaa, anakutanisha ahadi na kiaga, kupendekeza na kuhadharisha, ili aogope mja adhabu ya Mungu apate kumcha, na wala asikate tamaa na rehema yake atubie na arejee.

Na lau tungeliifanya Qur’ani kwa lugha ya kigeni wangelisema: Kwa nini Aya zake hazikupambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na mwarabu?

Qur’ani iliwateremkia waarabu kwa lugha yao wanayoipenda na kuitukuza, lakini baadhi ya mataghuti wao waliwaambia wengine: Lau ingeliteremka kwa lugha nyingine wangelitaaradhi na kusema itakuwaje Mtume mwarabu na lugha ya kigeni? Hivi ndivyo wanavyouandalia kila mlango ufunguo na kila usiku na taa. Hakuna lengo isipokuwa kuikimbia haki tu.

Sema: Hii Qur’ani ni uwongofu na ponyo kwa wenye kuamini.

Qur’ani ni mwongozo kwa mwenye kutaka uongofu na ni haki kwa njia ya haki na ni ponyo kwa mwenye kutaka kupona maradhi ya ukafiri na unafiki. Imam Ali(a.s) anasema:“Hakika katika Qur’ani kuna ponyo la ugonjwa mkubwa zaidi ambao ni unafiki na dhulma.”

Na wasioamini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni.

Qur’ani ni uongofu na mwangaza kwa wenye ikhlasi, lakini ni upofu machoni mwa wanafiki, ni uziwi masikiano mwao na maradhi nyoyoni mwao.

Hao wanaitwa nao wako mahali mbali.

Qur’ani iliwaita duniani kwa mwito wa Mwenyezi Mungu, lakini hawakuitikia kama kwamba hakuna mwito au kwamba uko mbali hausikiki. Vile vile itawaita Siku ya Kiyama: “Ehe! Kila mpanda mbegu ana wasi-wasi na matokeo ya kazi yake; isipokuwa aliyepanda Qur’ani,” kama ilivyo katika Nahajul-balagha. Wafasiri wanasema kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘nao wako mahali mbali,’ ni ishara kwamba wao hawasikii wala hawafahamu, sawa anayeitwa kwa sauti ya mbali asiyoisikia wala kuifahamu.

Lakini maana haya yanapingana na lengo la kuita, kwa sababu kutakuwa hakusikiwi. Maana yaliyo na nguvu zaidi ni kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Nao wako mahali mbali,’ ni ishara yakuwa mwito unatoka mbinguni, lakini unasikiwa na wote. Hilo linafahamishwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

يَوْمَ يُنَادِ الْمُنَادِ مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ ﴿٤١﴾ يَوْمَ يَسْمَعُونَ الصَّيْحَةَ بِالْحَقِّ ﴿٤٢﴾

“Siku atakaponadi mwenye kunadi kutoka mahali karibu, siku watakaposikia ukele wa haki.” (50:41-42).

Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini pakatokea hitilafu kati yake.

Makusudio ya Kitabu hapa ni Tawrat. Walihitalifiana kwenye hiyo iliposhuka. Kuna walioisadiki na walioikadhibisha. Kadhalika Qur’ani, iliposhuka, kuna walioisadiki na walioikadhibisha.

Na lau kuwa halikwishatangulia neno la Mola wangelihukumiwa.

Imetaka hekima yake Mtukufu kuiahirisha adhabu ya wakosefu hadi siku ya ufufuo. Vinginevyo asingebakia taghuti wala mwenye dhambi yoyote.

Na hakika wao wamo katika shaka nayo yenye kuwatia wasiwasi.

‘Wao’ ni washirikina wa kiarabu, ‘nayo’ ni hiyo Qur’ani. Makusudio ya shaka hapa ni ubishi bila ya ilimu na haki. Maana ni kuwa wao wanabishana kuhusu Qur’ani, lakini kwa ujinga na upotofu. Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 12 (11:110).

Anayetenda mema basi anajitendea mwenyewe, na anayetenda uovu basi ni juu ya yake; na Mola wako si mwenye kuwadhulumu waja.

Maana ya Aya hii yamekaririka kwenye Aya kadhaa; zikiwemo hizi zifuatazo:

فَالْيَوْمَ لَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٥٤﴾

“Basi leo nafsi yeyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyokuwa mkiyatenda Juz. 23 (36:54)

Na ile iliyo katika Juz. Hii tuliyo nayo:

الْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ ﴿١٧﴾

“Leo kila nafsi italipwa kwa iliyochuma. Hapana dhulma leo.” (40:17)

Na nyinginezo zinasema kuwa mtu anakuwa na hiyari halazimishwi.


13

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

إِلَيْهِ يُرَدُّ عِلْمُ السَّاعَةِ وَمَا تَخْرُجُ مِن ثَمَرَاتٍ مِّنْ أَكْمَامِهَا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ أَيْنَ شُرَكَائِي قَالُوا آذَنَّاكَ مَا مِنَّا مِن شَهِيدٍ ﴿٤٧﴾

47. Ilimu ya Saa (ya Kiyama) inarudishwa kwake (Mwenyezi Mungu). Na matunda hayatoki katika mafumba yake, wala mwanamke hachukui mimba, wala hazai, ila kwa kujua kwake. Na siku atakayowaita, akawaambia: Wako wapi washirika wangu? Hapo watasema: Hapana miongoni mwetu anayeshuhudia.

وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَدْعُونَ مِن قَبْلُ وَظَنُّوا مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٍ ﴿٤٨﴾

48. Na wakawapotea wale waliokuwa wakiwaomba hapo mwanzo, na wakaona kuwa hawana pa kukimbilia.

لَّا يَسْأَمُ الْإِنسَانُ مِن دُعَاءِ الْخَيْرِ وَإِن مَّسَّهُ الشَّرُّ فَيَئُوسٌ قَنُوطٌ ﴿٤٩﴾

49. Mwanaadamu hachoki kuomba kheri, na inapomgusa shari, mara huvunjika moyo akakata tamaa.

وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ رَحْمَةً مِّنَّا مِن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ هَـٰذَا لِي وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِن رُّجِعْتُ إِلَىٰ رَبِّي إِنَّ لِي عِندَهُ لَلْحُسْنَىٰ فَلَنُنَبِّئَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِمَا عَمِلُوا وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ ﴿٥٠﴾

50. Na tukimwonjesha rehema itokayo kwetu baada ya kumgusa dhara, bila ya shaka husema: Hii ni yangu, wala sidhani kuwa Kiyama kitakuwa. Na hata nikirudishwa kwa Mola wangu bila ya shaka nina mema yangu kwake! Basi kwa yakini tutawaelezea wale ambao wamekufuru walioyoyatenda, na kwa yakini tutawaonjesha adhabu ngumu.

ELIMU YA SAA INARUDISHWA KWAKE

Aya 47 – 50

MAANA

Ilimu ya Saa (ya Kiyama) inarudishwa kwake (Mwenyezi Mungu.)

Hakuna yoyote anayejua Kiyama kitakuwa lini isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake. Katika Nahjul-balagha imesemwa: ”Nyinyi na Kiyama kimewatia kamba” Yaani mnacho. Mwenye kufa ndio kiyama chake kimeanza.

Na matunda hayatoki katika mafumba yake, wala mwanamke hachukui mimba, wala hazai, ila kwa kujua kwake .[4]

Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:59).

Na siku atakayowaita, akawaambia: Wako wapi washirika wangu? Hapo watasema: Hapana miongoni mwetu anayeshuhudia.

Kesho Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawaambia washirikina kwa kuwatahayariza: Wako wapi wale mliokuwa mkiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu? Je, watawasaidia? Nao watamwambia Mwenyezi Mungu, hakuna yeyote miongoni mwetu mwenye ushahidi leo, kuwa wewe una mshirika.

Na wakawapotea wale waliokuwa wakiwaomba hapo mwanzo.

Siku ya Kiyama mtu hatapata sanamu, wala mali, mtoto, mbinu wala wasila au chochote kile isipokuwa hisabu na malipo ya matendo waliyoyatenda.

Na wakaona kuwa hawana pa kukimbilia.

Kesho vifuniko vitawafanukia wakosefu na watajua kuwa hakuna kwa kuikimbia adhabu.

Mwanaadamu hachoki kuomba kheri, na inapomgusa shari, mara huvunjika moyo akakata tamaa.

Mtu huwa anataka sana kupata mali, cheo, afya na amani; anakuwa na bidii ya kuyafikia hayo bila ya kuchoka. Lakini likimsibu jambo lolote katika dunia yake basi anavunjika nguvu na kukata tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu.

Na tukimwonjesha rehema itokayo kwetu baada ya kumgusa dhara, bila ya shaka husema: hii ni yangu.

Anatafuta dunia kwa bidii na anakata tamaa akikosa kitu chochote kwenye hiyo dunia. Kama Mwenyezi Mungu akimwokoa na misukosuko husema: Nimeokoka kwa nguvu zangu na uwezo wangu wala hakuna yeyote aliyenifadhili.

Hakuna mwenye kusalimika na ghururi hii isipokuwa mtu wa haki na mwenye akili salama.

Wala sidhani kuwa Kiyama kitakuwa. Na hata nikirudishwa kwa Mola wangu bila ya shaka nina mema yangu kwake!

Bado mazungumzo ya mjinga aliyeghurika yanaendelea. Maana yake ni kuwa anasema mpumbavu huyu, kuwa mimi ndiye niliyefanya katika maisha ya dunia. Ama yale wanayonihofisha nayo ya baada ya mauti hayo ni njozi tu; na hata ikiwa ni kweli basi mimi huko Akhera nitakuwa na riziki bora zaidi kwa sababu mimi ni katika watu watukufu.

Mjinga huyu hata kama hana dhambi isipokuwa ufedhuli huu tu, unamtosha kuwa ni dhambi. Umetangulia mfano wake kwa upana zaidi katika Juz. 15 (18:32 – 44).

Basi kwa yakini tutawaelezea wale ambao wamekufuru walioyoyatenda, na kwa yakini tutawaonjesha adhabu ngumu.

Hakuna ovu lolote analolitenda mtu ila atalikuta kesho kwa Mwenyezi Mungu na kuulizwa nalo, kisha aadhibiwe kwalo kwa kiasi anachostahiki. Ikiwa ni katika aina ya madhambi makubwa, kama kufuru ushirikina na dhulma, basi atapata adhabu kubwa.

Na likiwa ni chini ya hapo atapata adhabu hafifu, lakini ieleweke kuwa kila balaa lisilokuwa moto wa Akhera basi si chochote.

وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَىٰ بِجَانِبِهِ وَإِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ فَذُو دُعَاءٍ عَرِيضٍ ﴿٥١﴾

51. Na tukimneemesha mwanadamu hugeuka na kujitenga upande, na inapomgusa shari, huwa na madua marefu marefu.

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ثُمَّ كَفَرْتُم بِهِ مَنْ أَضَلُّ مِمَّنْ هُوَ فِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ ﴿٥٢﴾

52. Sema: Mnaonaje! Ikiwa haya yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, kisha mkayakataa, ni nani aliyepotea zaidi kuliko aliye katika upinzani wa mbali?

سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٥٣﴾

53. Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je! Haikutoshi Mola wako kuwa Yeye ni Shahidi wa kila kitu?

أَلَا إِنَّهُمْ فِي مِرْيَةٍ مِّن لِّقَاءِ رَبِّهِمْ أَلَا إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ مُّحِيطٌ ﴿٥٤﴾

54. Ehe! Hakika wao wamo katika shaka ya kukutana na Mola wao! Ehe! Hakika Yeye amekizunguka kila kitu.

TUTAWAONYESHA ISHARA ZETU

Aya 51 – 54

MAANA

Na tukimneemesha mwanadamu hugeuka na kujitenga upande, na inapomgusa shari, huwa na madua marefu marefu.

Akiwa amejitosha anakuwa makini, lakini akiwa fukara anakata tamaa na kuwa mnyonge; kama alivyosema Imam Ali(a.s ) . Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:12), Juz. 12 (11:9) na Juz. 15 (17:83).

Sema: Mnaonaje! Ikiwa haya yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, kisha mkayakataa, ni nani aliyepotea zaidi kuliko aliye katika upinzani wa mbali?

Wanaambiwa walioikadhibisha Qur’an. Upinzani wa mbali ni inadi. Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwamrisha Mtume wake mtukufu kuwaambia kuwa mnadai Qur’an ni vigano, hebu niambieni itakuwaje hali yenu ikiwa Qur’an ni haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu na hali nyinyi mnaipinga kwa inadi na kiburi? Je, hamjihurumii na mkajitoa shakani na adhabu ya moto?

ULIMWENGU NI QUR’AN KUBWA YA MWENYEZI MUNGU

Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) analeta dalili kwa waja wake ili awakinaishe kuwa yeye yuko na dini yake ni sahihi na mitume na vitabu vyake ni vya kweli. Amewawekea dalili ya hilo kwa hisia na ushahidi kutoka kwao wenyewe na kwenye ulimwengu wa dhahiri ya macho; anazifunua dalili hizo na anazitanabahisha akili kwa muumba wa mbingu na ardhi, kutofautiana mchana na usiku, kuvuma pepo na mawingu, kuhuishwa ardhi baada ya kufa harakati za nyota na manufaa yake, kuumbwa katika uzuri wa sura na mengineyo anayoyatambua mtu ambayo hisia zake zinafahamisha kuweko Mwenyezi Mungu kwa dalili mkataa na kwamba Yeye ndiye muumba wa pekee wa kila kitu.

Ikiwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametegema dalili za hisia kuwakinaisha waja wake na kuwaambia:

فَاعْتَبِرُوا يَا أُولِي الْأَبْصَارِ ﴿٢﴾

“Basi zingatieni enyi wenye busara” (59:2),

“Je, hawapati busara.” (32:15).

Sasa inakuwje kusemwa kuwa dini ni ya ghaibu ndani ya ughaibu, haitegemei hisia wala majaribio?

Hapana! Dini inathibitika kwa hisia na ushahidi; sawa na tunavyothibitisha akili ya mwenye akili kutokana na kauli yake na vitendo vyake. Wataalamu wa kisayansi wanathibitisha mambo mengi yasiyohisiwa wala kuonekana.

Kwa hiyo yanatubainikia makosa ya mwanafasihi mmoja aliyesema: “Mwenyezi Mungu daima anawatakabalia wale ambao wanaamini ghaibu bila ya kuwa na haja ya dalili wala kuona” Jarida la Sabahul-khayr la 26-2-1970.

Zaidi ya hayo maulamaa wa kiislamu wamekongamana kuwa ni wajibu kuchunguza na kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumwamini. Wametegema hukumu ya kiakili na Aya za Qur’an katika hilo. Lakini anayoyasema mwanafasihi huyo ni kinyume na yanagongana na tafsiri ya Qur’an.

Ibn Al-Arabi anasema katika Futuhatil-makkiyya: “Wewe huwezi kuyakana unayoyaona; kama ambavyo huwezi kuacha kuyajua unayoyajua. Wewe unaona na kujua kwa uhakika kuweko herufi, matamshi sura na Aya zinazotamka kuweko mwandishi wake ambaye ni Mwenyezi Mungu, hata kama humuoni.

Kwa hiyo kuweko Mwenyezi Mungu ni Qur’an ambayo haifikiwi na upotofu mbele yake wala nyuma yake. Tazama Juz. 7 (6:4-6), kifungu cha ‘Hakuna udikteta Ardhini wala mbinguni.’

Je! Haikutoshi Mola wako kuwa Yeye ni Shahidi wa kila kitu?

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kusema kuwa yeye anasimamisha dalilili kwa waja wake katika mbingu na ardhi na katika nafsi zao kuwa Mwenyezi Mungu ni kweli, Qur’an ni kweli na utume wa Muhammad ni kweli, sasa anasema kuwa inatosha kuwa dalili zake ni ushahidi wa ukweli na uadilifu wa hilo. Sufi wanasema kuhusu maana ya Aya hii kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayeshuhudia na kufahamisha kupatikana kingine, lakini Yeye haihitajii shahidi mwingine wa kumjulisha kuwa yuko.

Ehe! Hakika wao wamo katika shaka ya kukutana na Mola wao!

Wao wameikadhibisha Qur’an kwa vile tu wao hawaamini ghaibu na malipo. Hii inafahamisha kwamba asiyeamini kukutana na Mwenyezi Mungu, basi hawezi kuongoka kwenye kheri.

Ehe! Hakika Yeye amekizunguka kila kitu.

Anajua dhahiri ya waja na undani wao na atamlipa kila mmoja kwa yaliyochumwa na mikono yake. Ikiwa kheri basi ni kheri na ikiwa shari basi ni shari. Kwa ajili hii ndio atawaadhibu wale ambao wamekana kukutana naye na wakakadhibisha kitabu chake, yakiwa ni malipo kwa yale waliyoyachuma.

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI NA MMOJA: SURAT FUSSILAT


13

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

Sura Ya Arubaini Na Mbili: Surat Ash-Shura. Ina Aya 53.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

حم ﴿١﴾

1. Haa Mim.

عسق ﴿٢﴾

2. A’yn Siin Qaaf.

كَذَٰلِكَ يُوحِي إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ اللَّـهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٣﴾

3. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mwenye hikima anavyokuletea Wahyi wewe na walio kabla yako.

لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٤﴾

4. Ni vyake vilivyomo mbinguni, na vilivyomo ardhini. Na Yeye ndiye Mtukufu, Mkuu.

تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِن فَوْقِهِنَّ وَالْمَلَائِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِمَن فِي الْأَرْضِ أَلَا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿٥﴾

5. Zinakaribia mbingu kutatuka juu yao. Na Malaika wakimsabihi Mola wao kwa kumhimidi na wakiwaombea maghufira waliomo kwenye ardhi. Ehe! Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ اللَّـهُ حَفِيظٌ عَلَيْهِمْ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ ﴿٦﴾

6. Na wale waliowafanya mawalii wengine badala yake Yeye, Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi juu yao; wala wewe si wakili juu yao.

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِّتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا وَتُنذِرَ يَوْمَ الْجَمْعِ لَا رَيْبَ فِيهِ فَرِيقٌ فِي الْجَنَّةِ وَفَرِيقٌ فِي السَّعِيرِ ﴿٧﴾

7. Na namna hivi tumekupa wahyi Qur’an kwa kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa miji na walio pembezoni mwake. Na uhadharishe na Siku ya Mkutano, haina shaka hiyo. Kundi moja litakuwa Peponi, na kundi jengine Motoni.

وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَهُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن يُدْخِلُ مَن يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ وَالظَّالِمُونَ مَا لَهُم مِّن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿٨﴾

8. Na Mwenyezi Mungu angelipenda angewafanya umma mmoja. Lakini anamwingiza katika rehema yake amtakaye. Na madhalimu hawana walii wala msaidizi.

HIVYO NDIVYO MWENYEZI MUNGU ANAVYOKULETEA

Aya 1 – 8

MAANA

Haa Mim. A’yn Siin Qaaf.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1). Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa ni majina ya Sura hii kubainisha ubora wake juu ya Sura za Hamim nyingine.

Razi amesema: kuzungumzia mianzio hii kunatia dhiki na ni kufungua mlango wa porojo. Lilio bora ni kuachia ujuzi wake kwa Mwenyezi Mungu

Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mwenye hikima anavyokuletea Wahyi wewe na walio kabla yako.

Mwenye nguvu na uweza ambaye anapanga mambo kulingana na kipimo chake na hekima, ameleta wahyi kwako wewe Muhammad na kwa mitume wengine waliokuwa kabla yako.

Ni vyake vilivyomo mbinguni, na vilivyomo ardhini. Na Yeye ndiye Mtukufu, Mkuu.

Yeye peke yake ndiye mfalme wa ulimwengu na viliomo ndani yake, bila ya kuweko mwengine yoyote.

Zinakaribia mbingu kutatuka juu yao.

Makusudio ya mbingu ni sayari za juu; na juu yao ni juu ya hizo mbingu. Maana ni kuwa sayari ambazo zimepandana juu ya nyingine zinakurubia kupasuka kutokana na kauli ya anayesema kuwa Mwenyezi Mungu ana washirika. Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا ﴿٩٠﴾ أَن دَعَوْا لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدًا ﴿٩١﴾

“Zinakurubia mbingu kutatuka kwa hilo na ardhi kupasuka na milima kuanguka vipande vipande, kwa kudai kwao kuwa Mwingi wa rehema ana mwana.” Juz. 16 (19:90-91).

Na Malaika wakimsabihi Mola wao kwa kumhimidi.

Lau kama Mwenyezi Mungu angelikuwa na washirika, Malaika wasingelimsabihi kwa kumsifu Mwenyezi Mungu ambaye hakuna Mola mwingine isipokuwa Yeye. Imam Ali(a.s ) anasema:“Lau kama Mola wako angelikuwa na mshirika, wangelikujia mitume wake na ungeliona athari za ufalme wake na usultani wake na ungelivijua vitendo vyake na sifa zake.”

Na Malaikawakiwaombea maghufira waliomo kwenye ardhi, waumini na wenye kutubia; kama ilivyoelezwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ ﴿٧﴾

“Na wanawaombea msamaha walio amini. Mola wetu! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe ambao wametubu na wakaifuata Njia yako.” Juz. 24 (40:7).

Ehe! Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.

Hamnyimi mwenye kuomba rehema na maghufira, vyovyote atakavyokuwa, lakini kwa sharti ya kufuata njia yake ambayo ni toba na ukweli wa nia.

Na wale waliowafanya mawalii wengine badala yake Yeye, Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi juu yao. Wala wewe si wakili juu yao.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamwambia Mtume wake kuwa wewe ni mfikishaji unatoa bishara na kuonya tu, na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuwadhibiti waja na matendo yao, kauli zao na makusudio yao na kuwahisabu nayo. Maana haya yamekaririka kwenye Aya kadhaa.

Hakuna mwenye shaka kuwa hakuna kulazimishwa katika imani, lakini anayevunja heshima ya watu niwajibu kumtia adabu na kumrudi, kwa sababu atakuwa amejivunjia heshima yeye mwenyewe. Na mwenye kuzaliwa Mwislamu kisha akartadi ni wajibu kumuua.

Vile vile Mwislamu akiacha swala au saumu kwa kupuuza atazinduliwaa na kuaziriwa, akiendelea atauawa baada ya kuzinduliwa mara ya nne. Kwa hiyo basi kauli hii ‘wala wewe si wakili juu yao’ itakuwa haihusiki kwenye masula haya au tuseme ilishuka wakati ambapo Mtume hakuwa na nguvu za kutia adabu.

Na namna hivi tumekupa wahyi Qur’an kwa kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa miji na walio pembezoni mwake.

Makusudio ya mama wa miji ni Makka. Yaani mwanzo kabisa utakavyoanza mwito wa Uislamu, ewe Muhammad, uanze na mji wako wa Makka na miji inayoizunguka, kisha ndio uueneze ulimwenguni pote; kama ilivyo miito mingine inaanzia alipozaliwa mtu kisha ndio aieneze kwengine. Tazama Juz.7 (6:92)

Na uhadharishe na Siku ya Mkutano, haina shaka hiyo. Kundi moja litakuwa Peponi, na kundi jengine Motoni.

Siku ya mkutano ni siku ya Kiyama ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameitolea shaka kutokea kwake, na kuwapambanua siku hiyo watu wa Peponi na wa Motoni. Imeitwa siku ya mkutano kwa vile viumbe watakusanyika siku hiyo kwa hisabu na malipo:

ذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّجْمُوعٌ لَّهُ النَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّشْهُودٌ ﴿١٠٣﴾

“Hiyo ndiyo siku itakayokusanyiwa watu na hiyo ndiyo siku itakayoshuhudiwa.”

Juz. 12 (11:103).

Na Mwenyezi Mungu angelipenda angewafanya umma mmoja.

Lau Mwenyezi Mungu angeliwachukuwa watu kwenye dini moja kwa nguvu, sifa ya utu ingeliondoka; ambapo angelikuwa, katika hali hii, ni sawa na unyoya kwenye upepo. Umetangulia mfano wake katika Juz. 6 (5:48), Juz. 14 (16:93) na tumelizungumzia hilo kwa ufafanuzi katika Juz. 12 (12:118)

Lakini anamwingiza katika rehema yake amtakaye ambaye ni mumin, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٣٢﴾

“Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemiwa.” Juz. 4 (3:132).

Na madhalimu hawana walii wala msaidizi kwa sababu wamestahabu upofu kuliko uongofu kwa hiyo ikawanyakua adhabu ya kufedhesha kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.

أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ فَاللَّـهُ هُوَ الْوَلِيُّ وَهُوَ يُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٩﴾

9. Au wamechukua mawalii wengine badala yake! Lakini Mwenyezi Mungu ndiye walii hasa. Na Yeye ndiye anayehuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu.

وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبِّي عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ ﴿١٠﴾

10. Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu ninayemtegemea na kwake Yeye narejea.

فَاطِرُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَمِنَ الْأَنْعَامِ أَزْوَاجًا يَذْرَؤُكُمْ فِيهِ لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١١﴾

11. Muumba mbingu na ardhi. Amewajaalia mke na mume katika nafsi zenu, na katika wanyama howa dume na jike, anawazidisha namna hii. Hakuna chochote kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.

لَهُ مَقَالِيدُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٢﴾

12. Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila kitu.

شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ اللَّـهُ يَجْتَبِي إِلَيْهِ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَن يُنِيبُ ﴿١٣﴾

13. Amewapa sharia ya Dini aliyomuusia Nuh na tuliyokupa wahyi wewe, na tuliyowausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba simamisheni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayowaitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, Na humwongoa kwake aelekeaye.

وَمَا تَفَرَّقُوا إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى لَّقُضِيَ بَيْنَهُمْ وَإِنَّ الَّذِينَ أُورِثُوا الْكِتَابَ مِن بَعْدِهِمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ ﴿١٤﴾

14. Na hawakufarikiana ila baada ya kuwajia ilimu kwa sababu ya uhasidi baina yao. Na lau si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako mpaka muda uliowekwa, basi bila ya shaka palingelihukumiwa baina yao. Na hakika waliorithishwa Kitabu baada yao wanamtilia shaka inayowahangaisha.

SIMAMISHENI DINI WALA MSIFARIKIANE

Aya 9 – 14

MAANA

Au wamechukua mawalii wengine badala yake! Lakini Mwenyezi Mungu ndiye walii hasa. Na Yeye ndiye anayehuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kusema katika Aya ya 6: ‘Na wale waliowafanya mawalii wengine badala yake Yeye, Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi juu yao,’ hapa amerudia tena kauli hii na kuzidisha kuwa Yeye peke yake ndiye Mwenye kunusuru, Mwenye kusaidia, Mwenye kuhuisha, Mwenye kufisha na Muweza wa kila kitu.

Amerudia pamoja na ziada hii ili kumpinga anayemfanyia washirika; kwamba asiyekuwa Yeye hawezi kuleta uhai wala mauti au kusaidia, kwa vile hawezi kila kitu.

Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu.

Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu ninayemtegemea na kwake Yeye narejea.

Haya ni masimulizi ya maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) akiwaambia watu wote kwamba kila kitu watakachikhitalifiana kuwa ni haki au batili, basi rejea ni Qur’an; kauli yake ni ya upambanuzi na hukumu yake ni ya uadilifu.

Mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na kama mkipingana katika jambo, basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake mkiwa mwamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Hilo ni bora zaidi na mwisho mzuri.” Juz. 5 (4:95).

Muumba mbingu na ardhi.

Ameziumba na akazipangilia, wala hakuna tofauti kwa Mwenyezi Mungu baina ya kuumba mbingu na ardhi na kuumba mdudu chungu. Amempangilia vizuri hivi, kama alivyoupangilia ulimwengu.

Amewajaalia mke na mume katika nafsi zenu, ili mpate utulivu:

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١﴾

”Na katika ishara zake ni kuwaumbia wake kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Na akajaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya kuna ishara kwa watu wanaofikiri.” Juz. 21 (30:21).

Na katika wanyama howa dume na jike, anawazidisha namna hii.

Yaani Mwenyezi Mungu amewafanya watu na wanyama waume na wake ili wazidi kuwa wengi. Na kuzidi huku ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Hakuna chochote kama mfano wake, si katika dhati yake wala sifa zake, kwa vile Yeye ni zaidi ya kila kitu. Hakuna Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja Mwenye nguvu.Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona, anasikia kauli zote na kuona matendo yote.

Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila kitu.

Riziki za mbinguni na ardhini ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpanulia amtakaye na humfinyia amtakaye kutokana na hekima yake inavyotaka. Hakuna mwenye shaka kwamba uchache wa mali pamoja na afya, amani, dini na utengenevu ni bora mara elfu kuliko kuwa na mali nyingi pamoja na hofu, ugonjwa, ukafiri na ufisadi. Tumezungumzia rizi kwa anuani ya: ‘Riziki na ufisadi’ Juz. 6 (5:66), ‘Je, riziki ni bahati au majaliwa’ Juz. 7 (5:100) na ‘Mtu na riziki’ Juz. 13 (13:26).

Amewapa sharia ya Dini aliyomuusia Nuh na tuliyokupa wahyi wewe, na tuliyowausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba simamisheni Dini wala msifarikiane kwayo.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwatuma mitume wote kwa tamko la Tawhid, kuamini siku ya mwisho, kusimaisha Swala na kutoa Zaka. Vile vile kuharamisha dhulma, ghushi, uongo na zina. Pia kuharamisha kuoa mama, binti, dada na mengineyo ya misingi ya dini na sharia, lakini sio matawi ya dini ambayo yanatofautiana kulingana na wakati na masilahi; kama alivyoashiria Mwenyezi Mungu kwa kusema:

لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا ﴿٤٨﴾

“Na kila (umma) katika nyinyi tumeujaalia sharia (yake) na njia” Juz. 6 (5:48).

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemuhusisha kumtaja Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad, kwa vile tu wao ni mitume ulul-azm, vinginevyo ni kuwa huyo anayeusiwa ni mmoja kwa mitume wote.

Ikiwa Mungu ni mmoja, dini ni moja na mwito ni mmoja, basi kuna haja gani ya uadui na kuchinjana katika dini? Kuna sababu gani ya vita vilivyosajiliwa na historia kwa herufi za fedheha na aibu?

Tumezungumza kwa ufafanuzi zaidi kuhusu mwito wa mitume na kwam- ba wao wako kwenye dini moja katika Juz. 3 (3:18–20) kifungu cha ‘Dini ya Mwenyezi Mungu ni uislamu’ na tukafuatishia kuzungumzia tofauti baina ya dini na madhehebu kwenye kifungu ‘Vikundi sabini na tatu.’

Vile vile tumezungumzia kwenye Juz.1(2:111) kifungu cha ‘Ualanguzi wa Pepo’ na tukafuatishia na kifungu cha: “Kila mmoja avutia kwake’

Ni magumu kwa washirikina hayo unayowaitia ewe Muhammad, kwa sababu kwanza, wewe si mfalme wala huna mali. Pili, wewe unalingania kwenye haki, wala hakuna kitu kizito zaidi kuliko hicho kwa watu wa matamanio na wabatilifu. Tatu, kuwa wewe umewaita mababa zao wajinga na wapotevu.

Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na amekuchagua wewe ewe Muhammad kuwa ni mtu wa risala yake na akakuishilizia kwa mitume wote, ambapo huna kifani na yeyote kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho.

Na humwongoa kwake aelekeaye.

Kila anayekimbilia kwa Mwenyezi Mungu kwa ukweli na ikhlasi basi Mwenyezi Mungu humwitikia na kumwongoza:

وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ ﴿١١﴾

“Na mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake.” (64:11).

Na hawakufarikiana ila baada ya kuwajia ilimu kwa sababu ya uhasidi baina yao.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 2 (2:213) na Juz. 3 (3:19)

Na lau si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako mpaka muda uliowekwa, basi bila ya shaka palingelihukumiwa baina yao.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:19), Juz. 12 (11:110), Juz. 16 (20:110) na Juz. 24 (41:45)

Na hakika waliorithishwa Kitabu baada yao wanamtilia shaka inayowahangaisha.

Makusudio ya waliorithishwa kitabu ni mayahudi na manaswara. Baada yao ni mtume au uma zilizotangulia na wanayemtilia shaka ni Muhammad kutokana na inavyofahamisha kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye.’ Maana ni kuwa watu wa Kitabu walipinga aliyokuja nayo Muhammad(s.a.w. w ) pamoja na ushahidi wazi wa utume wake na ukweli wa risala yake.


14

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

فَلِذَٰلِكَ فَادْعُ وَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَقُلْ آمَنتُ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِن كِتَابٍ وَأُمِرْتُ لِأَعْدِلَ بَيْنَكُمُ اللَّـهُ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ لَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ لَا حُجَّةَ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ اللَّـهُ يَجْمَعُ بَيْنَنَا وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ ﴿١٥﴾

15. Basi kwa hiyo waite! Nawe simama sawa sawa kama ulivyoamrishwa, wala usifuate matamanio yao. Na sema: Naamini aliyoteremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu. Na nimeamrishwa nifanye uadilifu baina yenu. Mwenyezi Mungu ni Mola wetu, na Mola wenu. Vitendo vyetu ni kwa ajili yenu, na vitendo vyenu ni kwa ajili yenu. Hapana ugomvi baina yetu na yenu. Na Mwenyezi Mungu atatukusanya pamoja, na marejeo ni kwake.

وَالَّذِينَ يُحَاجُّونَ فِي اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا اسْتُجِيبَ لَهُ حُجَّتُهُمْ دَاحِضَةٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ﴿١٦﴾

16. Na wanaohojiana juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kukubaliwa. Hoja zao ni batili mbele ya Mola wao, na juu yao ipo ghadhabu, na itakuwa kwao adhabu kali.

اللَّـهُ الَّذِي أَنزَلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ وَالْمِيزَانَ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ قَرِيبٌ ﴿١٧﴾

17. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeteremsha Kitabu kwa Haki na Mizani. Na nini kitakujulisha pengine Saa ipo karibu.

يَسْتَعْجِلُ بِهَا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِهَا وَالَّذِينَ آمَنُوا مُشْفِقُونَ مِنْهَا وَيَعْلَمُونَ أَنَّهَا الْحَقُّ أَلَا إِنَّ الَّذِينَ يُمَارُونَ فِي السَّاعَةِ لَفِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ ﴿١٨﴾

18. Wasioamini huihimiza hiyo Saa ifike upesi, lakini wanaoamini wanaiogopa, na wanajua kwamba hakika hiyo ni kweli. Ehe! Hakika hao wanaobishana katika hiyo Saa wamo katika upotofu wa mbali kabisa.

KUWA NA MSIMAMO KAMA ULIVYOAMRISHWA

Aya 15 – 18

MAANA

Basi kwa hiyo waite! Nawe simama sawa sawa kama ulivyoamrishwa,

‘Hiyo’ ni hiyo dini. Maana ni kuwa ewe Muhammad! Lingania kwenye dini safi aliyowausia Mwenyezi Mungu (s.w.t) mitume wote; na uwe imara kwenye hiyo dini na kwenye mwito wake. Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 12 (11:113). Huko tumezungumzia kusimama na sawa sawa (msimamo) na mafungu yake.

Wala usifuate matamanio yao.

Nabii ni maasumu anafuata anayopewa wahyi, wala hafuati matamanio ya wengine. Mara nyingi tumesema kuwa kukataza kitu hakufahamishi kuwa kinaweza kutokea kwa anayekatazwa, na kwamba aliye juu anaweza kumkataza yeyote anachotaka. Jumla hii Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 6 (5:48).

Na sema: Naamini aliyoteremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu. Na nimeamrishwa nifanye uadilifu baina yenu. Mwenyezi Mungu ni Mola wetu, na Mola wenu. Vitendo vyetu ni kwa ajili yenu, na vitendo vyenu ni kwa ajili yenu. Hapana ugomvi baina yetu na yenu. Na Mwenyezi Mungu atatukusanya pamoja, na marejeo ni kwake.

Ewe Muhammad! Tangaza imani yako kwa watu katika vitabu vyote alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwa vyovyote iwavyo; na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mola wa wote. Wewe unahukumu kwa uadilifu ukichunga haki ya mdhulumiwa kutoka kwa dhalimu, unachukua kisasi cha mnyonge kutoka kwa dhaifu hata kama ni ndugu. Vile vile utangaze kwamba kila mtu ana majukumu ya matendo yake mbele ya Mwenyezi Mungu yeye peke yake, huna ugomvi na mtu yeyote na kwamba marejeo ni kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu ailipe kila nafsi ilichokichuma.

Kwa njia hii iliyo sawa na mantiki yaliyo salama, utaweza kusimamisha hoja kwa maadui zako na hawatabaki na vijisababu vyovyote.

Na wanaohojiana juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kukubaliwa. Hoja zao ni batili mbele ya Mola wao, na juu yao ipo ghadhabu, na itakuwa kwao adhabu kali.

Watu wa Kitabu walikuwa wakibishana na waislamu na wakijaribu kuwatoa kwenye dini yao baada ya Mwenyezi Mungu kuwaongoza kwenye Uislamu. Kuna mapokezi katika Tafsir At-Tabari kwamba mayahudi na wanaswara walikuwa wakiwaambia waislmu: “Kitabu chetu kimekuja kabla ya chenu na Mtume wetu ni kabla ya wenu, kwa hiyo sisi ni bora kuliko nyinyi.”

Haya si mageni katika ubishi wa maadui wa haki na dini, lakini hoja yao ni batili, kwa sababu ubora unakuwa kwa matendo sio kwa wakati na kutangulia; vinginevyo angelikuwa ibilisi ni bora kuliko Adam (a.s.), kwa vile amemtangulia.

Vyovyote iwavyo, mwisho wa ubishi wa batili ni maangamivu na hasara dunini na Akhera.

Mwenyezi Mungu ndiye aliyeteremsha Kitabu kwa Haki na Mizani.

Makusudio ya Kitabu ni Qur’an na mizani ni uadilifu. Maana ni kuwa kushuka kwake ni haki, kila kilichomo ndani yake ni haki na inakubali kila lilio haki. Maana ya kushuka kwake kwa uadilifu ni kuwa inahukumu baina ya watu kwa uadilifu. Uadilifu unahitaji pande mbele kinyume cha haki; yaani haki ni kwa ujumla. Kwa hiyo kila uadilifu ni haki, lakini sio kila haki ni uadilifu. Jua ni haki liko, lakini sio uadlifu.

Na nini kitakujulisha pengine Saa ya Kiyamaipo karibu.

Hili ni jawabu la kauli ya wanaofanya stihizai wakiuliza: Kiyama kitakuwa lini? Kuhusu ukaribu wake ni kuwa kila kinachokuja kiko karibu na mwenye kufa kiyama chake kimeanza.

Wasioamini huihimiza hiyo Saa ifike upesi kwa stihzai.

Mara ngapi anayehimiza jambo likimfika hutamani angelikuwa mbali nalo kwa umbali wa mashariki na magharibi.

Lakini wanaoamini wanaiogopa, na wanajua kwamba hakika hiyo ni kweli.

Ndio! Kwa sababu wanaijua hakika yake kama vile wamekiona, ndio maana wakakihofia. Miongoni mwa aliyoyasema Imam Ali(a.s ) kuhusiana nacho ni: “Hofu imewachoma kama mshale.

Mtu akiwaangalia anawadhania ni wagonjwa, lakini jamaa hawana ugonjwa wowote. Wanasema: wamechanganyikiwa! Ndio kuna jambo kubwa limewafanya wachanganyikiwe.”

Kuna mshairi mmoja alitunga kuhusiana na maana haya: ref nguzo pg 518. Wanaambiwa ni wagonjwa wala sivyo, Au wamechanganyikiwa kamwe sivyo, Hofu imekuwa sawa na matarajio, Si kikomo cha hofu wala matamanio,

Ehe! Hakika hao wanaobishana katika hiyo Saa wamo katika upotofu wa mbali kabisa.

Upotevu wa mbali ni kuzama kabisa kwenye upotevu, kwa sababu wanakanusha ufufuo wa mwisho na hali wao wameona ufufuo wa kwanza.

اللَّـهُ لَطِيفٌ بِعِبَادِهِ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ ﴿١٩﴾

19. Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. Humruzuku ampendaye. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.

مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ ﴿٢٠﴾

20. Mwenye kutaka mavuno ya Akhera tutamzidishia katika mavuno yake, na mwenye kutaka mavuno ya duniani tutampa katika hayo, lakini katika Akhera hana fungu.

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ وَلَوْلَا كَلِمَةُ الْفَصْلِ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٢١﴾

21. Au wana washirika waliowawekea dini asiyoitolea idhini Mwenyezi Mungu? Na lau lisingekuwako neno la kupambanua basi wangelikatiwa hukumu baina yao. Na hakika wenye kudhulumu watapata adhabu chungu.

تَرَى الظَّالِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا كَسَبُوا وَهُوَ وَاقِعٌ بِهِمْ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فِي رَوْضَاتِ الْجَنَّاتِ لَهُم مَّا يَشَاءُونَ عِندَ رَبِّهِمْ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ ﴿٢٢﴾

22. Utawaona hao madhalimu wanavyokuwa na hofu kwa sababu ya waliyoyachuma, nayo yatawafika tu. Na walioamini na wakatenda mema watakuwamo katika mabustani ya Peponi. Humo watapata wayatakayo kwa Mola wao. Hiyo ndiyo fadhila kubwa.

MWENYEZI MUNGU NI MPOLE KWA WAJA WAKE

Aya 19 – 22

MAANA

Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. Humruzuku ampendaye. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja kuwa Yeye ni mpole Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu na Mwenye kushinda. Makusudio ya upole ni kufanya wema. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾

“Hakika Yeye ndiye mwema Mwenye kurehemu.” (52:28).

Maana ya kuruzuku ni kuwa Mwenyezi Mungu anampa mtu nguvu zote za maandalizi ya kufanya kazi ya kupata riziki na kumuongoza kwenye njia yake, kuongezea kuwa kheri zote zilizo ardhini na mbinguni ameziten- geneza Yeye kwa ufadhili wake. Ama kuwa na nguvu na kushinda ni kuwa Yeye hashindwi na lolote wala hakuna kitu asichokiweza ardhini au mbinguni.

Mwenye kutaka mavuno ya Akhera tutamzidishia katika mavuno yake, na mwenye kutaka mavuno ya duniani tutampa katika hayo, lakini katika Akhera hana fungu.

Mwenye kuitumikia Akhera atapata malipo ya aliyoyafanya na Mwenyezi Mungu atamzidishia ziada nyingi tu, na hatapunguziwa kitu duniani.

Hakuna mwenye shaka kwamba kufanya bidii kwa ajili ya maisha ni katika kuitumikia Akhera vile vile, lakini mwenye kuitumikia dunia peke yake na kuiacha Akhera, atastarehe siku kidogo tu, kisha atahamia kwenye adhabu ya daima. Watakokuwa na hali mbaya zaidi ni wale wanaoifanyia biashara dini na kuitafuta dunia kwa kazi ya Akhera kiunafiki na ria.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (3:145), Juz. 15 (17; 18-19).

Au wana washirika waliowawekea dini asiyoitolea idhini Mwenyezi Mungu?

Ni swali la kukana na kutahayariza. Makusudio ya washirika ni mashetani watu na majini. Kuwawekea ni kuwadanganya na kuwapambia pambia. Maana ni kuwa, kwa nini wakosefu wanaitumikia dunia na kuisahau Akhera? Je, ni kwa kuwa wana mashetani wanaowazuia nayo kwa kuwatia wasiwasi na mambo yasiyokuwa kwenye dini?

Kisha Mwenyezi Mungu amewatishia kwa kusema:Na lau lisingekuwako neno la kupambanua basi wangelikatiwa hukumu baina yao. Na hakika wenye kudhulumu watapata adhabu chungu.

Hekima Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu imetaka kuiahirisha adhabu ya wakosefu hadi siku ya ufufuo; vinginevyo angelimpatiliza kwa adhabu kila mkosefu mwenye dhambi.

Utawaona hao madhalimu wanavyokuwa na hofu kwa sababu ya waliyoyachuma, nayo yatawafika tu. Na walioamini na wakatenda mema watakuwamo katika mabustani ya Peponi. Humo watapata wayatakayo kwa Mola wao. Hiyo ndiyo fadhila kubwa.

Kesho itapita hisabu kwa matendo yote. Mwenye kutenda mema atakuwa katika amani na Pepo, humo atapata kila analolipenda na kulitaka; na mwenye kufanya maovu atakuwa katika hofu ya hasira za Mwenyezi Mungu na adhabu yake. Adhabu hiyo itamfika tu, ikiwa ni malipo kwa iliyochuma mikono yake.

NITII UTAKUWA MFANO WANGU

Hapo mwanzoni nilikuwa nikizitilia shaka Hadith mbili nilizokuwa nikizisikia mara kwa mara masikioni mangu: Ya kwanza ni Hadith Qudsi isemayo:“Ewe mja wangu nitii utakuwa mfano wangu, utakiambia kitu kuwa na kinakuwa.” Na nyingine ni ya Mtume isemayo: “Hakika Mwenyezi Mungu ana waja wakitaka naye hutaka.”

Nilikuwa nikitilia shaka mategemezi ya Hadith mbili hizi, kwa vile sikuzionea athari yoyote katika maisha haya. Kisha nikagundua, wakati nikifasiri Aya za Qur’an yenye hekima, kuwa maudhui ya Hadith hizi ni ya Akhera si ya dunia, basi shaka yangu ikaniondokea na nikawa na yakini kuwa Hadith mbili hizi ni tafsiri na ubainifu wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na walioamini na wakatenda mema watakuwamo katika mabustani ya Peponi. Humo watapata wayatakayo kwa Mola wao.’

Na mfano wa Aya hiyo.

ذَٰلِكَ الَّذِي يُبَشِّرُ اللَّـهُ عِبَادَهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَىٰ وَمَن يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَّزِدْ لَهُ فِيهَا حُسْنًا إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٢٣﴾

23. Hayo ndiyo aliyowabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walioamini na wakatenda mema. Sema: kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu. Na anayefanya wema tutamzidishia wema. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwingi wa shukrani.

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا فَإِن يَشَإِ اللَّـهُ يَخْتِمْ عَلَىٰ قَلْبِكَ وَيَمْحُ اللَّـهُ الْبَاطِلَ وَيُحِقُّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٢٤﴾

24. Au wanasema: Amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Mwenyezi Mungu akipenda atapiga muhuri juu ya moyo wako. Na Mwenyezi Mungu anaifuta batili na anaithibitisha Haki kwa maneno yake. Hakika Yeye anayajua yaliyomo vifuani.

وَهُوَ الَّذِي يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ وَيَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ ﴿٢٥﴾

25. Naye ndiye anayepokea toba kwa waja wake, na anasamehe makosa. Na anayajua mnayoyatenda.

وَيَسْتَجِيبُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضْلِهِ وَالْكَافِرُونَ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ﴿٢٦﴾

26. Na anawaitikia walioamini na wakatenda mema, na anawazidishia fadhila zake. Na makafiri watakuwa na adhabu kali.

NI NANI HAO NDUGU?

Aya 23 – 26

MAANA

Hayo ndiyo aliyowabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walioamini na wakatenda mema.

‘Hayo’ ni hayo ya fadhila kubwa ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia wenye takua huko Akhera. Ameyaeleza kwenye kitabu kuwa ni bishara ili nyoyo zao zitulie.

Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu.

Katika tafsiri ya Al-Bahrul-muhit ya Abu Hayan Al-Andalusi na Ruhul-bayani ya Ismail Haqqi, kuna maelezo haya: “Iliposhuka Aya hii, Mtume(s.a.w. w ) aliulizwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: ni kina nani hao ndugu zako tuliowajibishiwa kuwapenda?Akasema: Ali, Fatima, Hasan na Husein.”

Ibn Al-arabi anasema katika Futuhati, kwa anuani ya ‘La takhunullah war-rasul’ (msimfanyie hiyana Mwenyezi Mungu na Mtume): “Mtume wa Mwenyezi Mungu ametutaka tuwapende akraba wake na watu wa nyumba yake (Ahlbayt) na yeye pia anaingia, kwa vile pendo la Ahlu Bayt haligawanyiki.

Kwa sababu mwenye kuwafanyia hiyana watu wa nyumba ya Mtume ndio amemfanyia hiyana Mtume. Na haishii hapo, kwa sababu mwenye kumfanyia hiyana Mtume wa Mwenyezi Mungu ndio amemfanyia hiyana Mwenyezi Mungu.”

Baadhi ya wafasiri wamenukuu riwaya katika mategemezi yake Muawiya kuwa maana ya Aya hii ni, sema ewe Muhammad kuwaambia makuraishi kuwa msiniudhi na ndugu zangu.

Katika Tafsir Gharaibul-Furqani ya Nidhamuddin Al-Hasan bin Muhammad An-naysaburi, amesema: “Imepokewa kwa Sai’d bin Jubayr, kuwa iliposhuka Aya hii walisema: Ni nani hao ambao Mwenyezi Mungu amewajibisha kuwapenda? Akasema: Ali, Fatima na watoto wao wawili. Hapana shaka kwamba hii ni fahari kubwa na utukufu uliokamilika.

Hiyo inatiliwa nguvu na riwaya kuwa Ali siku moja alimshtakia Mtume husuda ya watu kwake. Mtume akamwambia: “Kwani huridhii kuwa wane wa wane! Wa kwanza atakayeingia Peponi ni mimi na wewe na Hasan na Husein, na wake wetu wakiwa kuumeni kwetu na kushotoni kwetu na dhuria wetu wakiwa nyuma ya wake wetu.”

Imepokewa kutoka kwa Mtume amesema: “Pepo imeharamishiwa mwenye kuwadhulumu watu wa nyumba yangu na akaniudhi kwa kizazi changu.” Na alikuwa akisema: “Fatima ni sehemu yangu linaniudhi lile linalomuudhi.”Imethibiti kwa nukuu mutawatir kwamba yeye alikuwa akimpenda Ali, Hasan na Hussein na akatuwajibishia kuwapenda.

Ni utukufu kwa watu wa Mtume kuishilizwa tashahhud kwa kutajwa wao na kuswalia katika kila swala. Na akasema: mfano wa watu wa nyumba yangu ni kama Safina ya Nuh, mwenye kuipanda aliokoka na aliyeiacha aliangamia.” Mwisho wa kunukuu.

Na anayefanya wema tutamzidishia wema.

Mfano wake ni:

مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ﴿١٦٠﴾

“Mwenye kufanya vizuri atalipwa mfano wake mara kumi.” Juz. 8 (6:160).

Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwingi wa shukrani; yaani anawapa thawabu wenye kushukuru.Au wanasema: Amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Mwenyezi Mungu akipenda atapiga muhuri juu ya moyo wako.

Wazushi wanasema kuwa wewe Muhammad unamzulia Mwenyezi Mungu kwa kudai kwako utume na hawajui kwamba Mwenyezi Mungu amekuhifadhi na makosa na hatia. Na hata kama ungejaribu – kukisia muhali sio muhali – basi Mwenyezi Mungu angelipiga muhuri moyo wako na kukuzuia kwa nguvu.

Na Mwenyezi Mungu anaifuta batili na anaithibitisha Haki kwa maneno yake.

Wewe Muhammad uko kwenye haki na maadui zako wako kwenye ubatilifu; na Mwenyezi Mungu ataiondoa batili na ataithibitisha haki kwa dalili na ubainifu ulio wazi aliokuunga mkono nao Mwenyezi Mungu na kulifanya neno lako liko juu na neno la maadui wako liko chini pamoja na wingi wao na wanavyokuduilia wewe na Uislamu.

Hakika Yeye anayajua yaliyomo vifuani.

Anayajua yanayofichwa na nyoyo zilizo vifuani na atawalipa wenye nyoyo hizo wanayostahiki iwe ni thawabu au adhabu.

Naye ndiye anayepokea toba kwa waja wake, na anasamehe makosa.

Mwenye kufanya dhambi kisha akatubia, Mwenyezi Mungu humkubalia toba yake na humsamehe dhambi yake isipokuwa haki ya watu.

Vile vile akiwa na mema yaliyo sawa na maovu, yasiyohusika na haki za watu, basi Mwenyezi Mungu humsamehe maovu yote na kubakia kama mtu ambaye hakufanya wema wala uovu. Ikiwa mema yatayazidi maovu basi atabakiwa na yale yaliyozidi.

Haya yanasadikishwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ ﴿١١٤﴾

“Hakika mema huondoa maovu. Hiyo ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.” Juz. 12 (11:114)

Pia kauli yake:

وَآخَرُونَ اعْتَرَفُوا بِذُنُوبِهِمْ خَلَطُوا عَمَلًا صَالِحًا وَآخَرَ سَيِّئًا عَسَى اللَّـهُ أَن يَتُوبَ عَلَيْهِمْ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٠٢﴾

“Na wengine wamekiri dhambi zao; wakachanganya vitendo vyema na vingine viovu. Huenda Mwenyezi Mungu akapokea toba zao.” Juz.11(9:102).

Na anayajua mnayoyatenda katika mema na maovu.

Ambaye mizani yake ya maovu itakuwa nzito atakuwa miongoni mwa waliohasirika na ambaye mizani yake ya wema itakuwa nzito basi atakuwa miongoni mwa wenye kufaulu.

Na anawaitikia walioamini na wakatenda mema, na anawazidishia fadhila zake. Na makafiri watakuwa na adhabu kali.

Yaani waumini wanasikia mwito wa Mwenyezi Mungu na kuuitikia, kwa hiyo naye anawalipa kutokana na kuitkia kwao na utiifu na anawazidishia ziada nyingi kutokana na fadhila zake. Na wakosefu hawataki mwito wa Mwenyezi Mungu, kwa hiyo anawadhibu adhabu kubwa kutokana na upinzani wao na uasi.


15

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَلَوْ بَسَطَ اللَّـهُ الرِّزْقَ لِعِبَادِهِ لَبَغَوْا فِي الْأَرْضِ وَلَـٰكِن يُنَزِّلُ بِقَدَرٍ مَّا يَشَاءُ إِنَّهُ بِعِبَادِهِ خَبِيرٌ بَصِيرٌ ﴿٢٧﴾

27. Na lau Mwenyezi Mungu angeliwakunjulia riziki waja wake basi bila ya shaka wangeliasi katika dunia, lakini anaiteremsha kwa kipimo akitakacho. Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye habari, Mwenye kuona.

وَهُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ الْغَيْثَ مِن بَعْدِ مَا قَنَطُوا وَيَنشُرُ رَحْمَتَهُ وَهُوَ الْوَلِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٢٨﴾

28. Naye ndiye anayeiteremsha mvua baada ya wao kukata tamaa, na hueneza rehema yake. Naye ndiye Walii Mwenye kuhimidiwa.

وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَثَّ فِيهِمَا مِن دَابَّةٍ وَهُوَ عَلَىٰ جَمْعِهِمْ إِذَا يَشَاءُ قَدِيرٌ ﴿٢٩﴾

29. Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na wanyama aliowaeneza humo. Naye ni Mwenye uweza wa kuwakusanya apendapo.

وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ﴿٣٠﴾

30. Na misiba inayowasibu ni kwa sababu ya yaliyotendwa na mikono yenu. Naye anasamehe mengi.

وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿٣١﴾

31. Na nyinyi si wenye kushinda ardhini wala mbinguni. Na hamna walii wala msaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu.

وَمِنْ آيَاتِهِ الْجَوَارِ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ ﴿٣٢﴾

32. Na katika Ishara zake ni vyombo baharini kama vilima.

إِن يَشَأْ يُسْكِنِ الرِّيحَ فَيَظْلَلْنَ رَوَاكِدَ عَلَىٰ ظَهْرِهِ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ ﴿٣٣﴾

33. Akitaka, huutuliza upepo navyo husimama tutwe juu ya bahari. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri akashukuru.

أَوْ يُوبِقْهُنَّ بِمَا كَسَبُوا وَيَعْفُ عَن كَثِيرٍ ﴿٣٤﴾

34. Au huviangamiza hivyo vyombo kwa sababu ya waliyoyatenda. Naye husamehe mengi.

وَيَعْلَمَ الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِنَا مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٍ ﴿٣٥﴾

35. Na ili wajue wale wanaojadiliana katika Ishara zetu kwamba hawana pahala pa kukimbilia.

RIZIKI NI KWA KUFANYA KAZI SIO KWA DUA

Aya 27 – 35

MAANA

Na lau Mwenyezi Mungu angeliwakunjulia riziki waja wake basi bila ya shaka wangeliasi katika dunia.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameitegemeza riziki kwa waja wake kwa kuchuma kwao na kufanya kazi si kwa matakwa yao na matamanio; vinginevyo ingelienea vurugu na kufanya ufisadi katika ardhi.

Lakini anaiteremsha kwa kipimo akitakacho.

Yaani anamrukuzu kwa kadiri ya utendaji wake wa kazi. Mara nyingine Mwenyezi Mungu hutoa riziki nyingi kwa kazi chache au riziki chache kwa kazi nyingi kulingana na hekima anayoijua Yeye zaidi. Ama utajiri unaotokana na haramu; kama vile kughushi na kupora, hiyo ni riziki ya shetani sio ya kutokana na kutoa kwa Mwingi wa rehema; vipi isiwe hivyo na hali mwenye riziki hiyo amepewa kiaga cha adhabu chungu?

Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye habari, Mwenye kuona.

Anamjua anayeishi kwa hisabu ya kupora na anayeishi kwa jasho lake. Wa kwanza amemwahidi hizaya na adhabu na wa pili ni heshima na thawabu.

Naye ndiye anayeiteremsha mvua baada ya wao kukata tamaa, na hueneza rehema yake.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja riziki, anasema kuwa sababu za hizo riziki, kama vile mvua, ziko mikononi mwake. Huipeleka anapotaka na huizuia anapotaka. Basi ikichelewa kidogo, wao hukata tamaa, lakini anawawahi kwa rehema yake iliyoenea katika kila kitu.

Naye ndiye Walii anayewasimamia waja wake kwa wemaMwenye kuhimidiwa anyestahiki sifa njema na kushukuriwa.Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na wanyama aliowaeneza humo.

Makusudio ya mbingu ni kilicho juu, iwe sayari au anga; na makusudio ya wanyama hapa ni kila mwenye uhai wakiwemo malaika ndege au yoyote mwenye uhai anayeishi nchi kavu au baharini na kwenye anga au kwenye nyota. Wote hao wanaonyesha kuweko mtengenezaji wake na mtia sura wake.Naye ni Mwenye uweza wa kuwakusanya apendapo; sawa na alivyoweza kuwaumba na kuwaeneza mbinguni na ardhini.

Na misiba inayowasibu ni kwa sababu ya yaliyotendwa na mikono yenu.

Aya hii inafahamisha waziwazi, wala haikubali taawili yoyote, kuwa dhulma na ufukara unatokana na watu sio Mwenyezi Mungu na wala hautokani na hukumu ya Mwenyezi Mungu na sharia yake; hata kahati na kuzuilika mvua, sababu yake ni dhulma na ufisadi; kama ilivyoelezwa katika Hadith na katika kitabu cha Mwenyezi Mungu: “Lau wangelisimamisha Tawrat na Injil na yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Mola wao, kwa hakika wangelikula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. ‘Juz. 6 (5:66), kifungu cha ‘Riziki na ufisadi’

Naye anasamehe mengi katika madhambi isipokuwa shirki na dhulma, kwa sababu Yeye ndiye aliyesema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ﴿٤٨﴾

“Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kufanyiwa mshirika, lakini husamehe yasiyokuwa hayo.” Juz. 5 (4:48).

Na akasema:

يَوْمَ لَا يَنفَعُ الظَّالِمِينَ مَعْذِرَتُهُمْ وَلَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ ﴿٥٢﴾

“Siku ambayo hautawafaa madhaalimu udhuru wao, nao watapata laana, na watapata makazi mabaya kabisa.” Juz. 24 (40:52).

Na nyinyi si wenye kushinda ardhini wala mbinguni. Na hamna walii wala msaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu.

Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 20 (29:22)

Na katika Ishara zake ni vyombo baharini kama vilima.

Ikiwa jahazi limetengenezwa na mtu lakini maji linayoyapitia na upepo unaolisukuma ni katika matengenezo yake Mwenyezi Mungu na hata miti iliyotengenezewa nk. Pia ndege zinazopaa kwenye anga ya Mwenyezi Mungu, magari yanayotembea kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu na vingenevyo hata mtu mwenyewe pia. Vyote hivyo vinadhihirisha uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu na rehema zake.

Akitaka, huutuliza upepo navyo hivyo vyombo husimama tutwe juu ya bahari.

Akizuia upepo au akiyagandisha maji basi majahazi yatasimama tu.

Hakika katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri akashukuru.

Mwenye kuwa na subira ya tafakuri na kuutazama ulimwengu na maajabu ya siri zake, hana budi kuishia kwenye imani ya Mwenyezi Mungu na utukufu wake, na atamshukuru kwa fadhila zake na mwongozo wake.

Au huviangamiza hivyo vyombo kwa sababu ya waliyoyatenda hao watu.Naye husamehe mengi; yaani hawaharakishi pamoja na dhambi zao nyingi.

Na ili wajue wale wanaojadiliana katika Ishara zetu kwamba hawana pahala pa kukimbilia.

Wanaojadiliana katika ishara za Mwenyezi Mungu ni wale wanaosema kuwa hakuna kitu kinachofahamisha kuwa Mwenyezi Mungu yuko. Maana ni kuwa makafiri hawamuamini Mwenyezi Mungu na kupinga kila dalili inayotamka kuweko kwake.

Hata hivyo iko njia moja ya kuamini na kukiri kwao ambayo ni kuona maangamizi kwa macho yao na kujua kuwa hakuna pa kukimbilia; mfano jahazi likisimama baharini au upepo mkali. Kwa maneno mengine hawaamini mpaka waone adhabu.

فَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ لِلَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ ﴿٣٦﴾

36. Basi vyote mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora, na cha kudumu zaidi. Kwa ajili ya walioamini na wakawa wanamtegemea Mola wao.

وَالَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ وَإِذَا مَا غَضِبُوا هُمْ يَغْفِرُونَ ﴿٣٧﴾

37. Na wanayaepuka madhambi makubwa na mambo machafu na wanapokasirika wao husamehe.

وَالَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِرَبِّهِمْ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَمْرُهُمْ شُورَىٰ بَيْنَهُمْ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣٨﴾

38. Na wanaomwitikia Mola wao na wakasimamisha Swala. Na mambo yao ni kwa kushauriana baina yao na wanatoa katika yale tuliyowapa.

وَالَّذِينَ إِذَا أَصَابَهُمُ الْبَغْيُ هُمْ يَنتَصِرُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na ambao wanapofanyiwa jeuri hujitetea.

وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِّثْلُهَا فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ ﴿٤٠﴾

40. Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu.

وَلَمَنِ انتَصَرَ بَعْدَ ظُلْمِهِ فَأُولَـٰئِكَ مَا عَلَيْهِم مِّن سَبِيلٍ ﴿٤١﴾

41. Na wanaojitetea baada ya kudhulumiwa, hao hapana njia ya kuwalaumu.

إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَظْلِمُونَ النَّاسَ وَيَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٤٢﴾

42. Bali njia ya lawama ipo kwa wale wanaowadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika ardhi bila ya haki. Hao watapata adhabu iliyo chungu.

وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ ﴿٤٣﴾

Na anayesubiri, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.

KILICHOKO KWA MWENYEZI NI BORA NA KITABAKIA

Aya 36 – 43

MAANA

Basi vyote mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu,

Starehe za dunia ni kila kinachostarehesha katika maisha haya; kama vile afya cheo, mali, wanawake, watoto, majengo, samani na mengineyo. Anasa za dunia hata zikiwa nyingi, zinaondoka na kuisha. Ama neema za Akhera zinabaki kwa kubakia kwake:

مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ وَمَا عِندَ اللَّـهِ بَاقٍ ﴿٩٦﴾

“Mlivyo navyo vitakwisha na vilivyoko kwa Mwenyezi Mungu ndivyo vitakavyobakia.”

Juz. 14 (16:96).

Anaendelea kusema Mwenyezi Mungu:lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora, na cha kudumu zaidi.

Kila amali itakayotekeleza haja yoyote katika maisha basi hiyo ni akiba mbele ya Mwenyezi Mungu kwa Masharti yafuatayo:-

1.Kwa ajili ya walioamini Mwenyezi Mungu. Ama wale waliomkufuru hawana chochote mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa adhabu, kwa vile wao hawakiri isipokuwa kuweko kwake. Kuna Hadithi inayosema: “Mwenye kumfanyia amali asiyekuwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu (s.w.t) atamwachia aliyemfanyia amali, na kesho ataambiwa: chukua malipo yako kwa uliyemfanyia.”

2.Na wakawa wanamtegemea Mola wao katika mambo yao yote, wala hawajienzi isipokuwa kwa kumcha Mwenyezi Mungu na radhi yake.

3.Na wanayaepuka madhambi makubwa na mambo machafu, ikiwemo dhulma, uongo na ufisadi. Tazama Juz. 5 (4:31) na Juz. 8 (6:151)

4.Na wanapokasirika wao husamehe; yaani si wepesi wa kukasirika na wasiokasirika isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu.

5.Na wanaomwitikia Mola wao, hawamuasi katika amri yake wala makatazo yake.

6.Na wakasimamis ha Swala. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameihusisha kuitaja hapa kwa vile ndio nguzo ya dini, na Mtume(s.a.w. w ) alikuwa akiita ‘kitulizo cha jicho.’ Baadhi ya wataalamu wameiita ‘Uhakika wa Mwislamu’

7.Na mambo yao ni kwa kushauriana baina yao.

Kauli ‘mambo yao’ inaashiria mambo mema ya uma na kwamba wao wanasaidiana kuufanyia kazi uma. Kushauriana huku si katika halali ya Mwenyezi Mungu na haramu yake, kwa sababu zinatokana na Mwenyezi Mungu tu peke yake. Tazama Juz. 4 (3:159). Katika Nahjul-balagha amesema: “Kutaka ushauri ni jicho la mwongozo na amejiingiza kwenye hatari anayetosheka na rai yake.”

8.Na wanatoa katika yale tuliyowapa, katika mali.

9.Na ambao wanapofanyiwa jeuri hujitetea.

Unaweza kuuliza : Tutaichanganya vipi Aya hii na ile isemayo: ‘Na wanapokasirika wao husamehe?’

Jibu : Kusamehe uovu ni vizuri ikiwa kutasababisha muovu kujirekebisha na kutubia au ikiwa ni kukinga ugomvi na fitina, lakini si kuzuri ikiwa kutasababisha ujeuri na usafihi kwa muasi. Imam Ali(a.s ) anasema:“Kuwatekelezea ahadi wavunja ahadi ni kuvunja ahadi mbele ya Mwenyezi Mungu na kuvunja ahadi kwa wavunja ahadi ni kutekeleza ahadi.”

Tumeelezea hayo kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 24 (41:34).

Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo.

Mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ﴿١٩٤﴾

“Anayewachokoza nanyi mchokozeni kwa kadiri alivyowachokoza.” Juz.2 (2:194).

Lakini mwenye kusamehe na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu.

Mfano wake ni

وَأَن تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ﴿٢٣٧﴾

“Na kusamehe ndiko kuliko karibu zaidi na takua” Juz. 2 (2:237).

Vile vile:

فَمَن تَصَدَّقَ بِهِ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُ ﴿٤٥﴾

“Lakini atakayesamehe itakuwa kafara kwake.” Juz. 6 (5:45).

Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu.

Makusudio ya madhalimu hapa ni wale wanaopita mpaka wa kisasi.

Na wanaojitetea baada ya kudhulumiwa, hao hapana njia ya kuwalaumu kabisa wala hakuna kuadhibiwa, kwa sababu mwenye kuanza ndiye dhalimu, na mwenye kudhulimiwa anayo haki ya kujitetea; bali akimnyamazia aliyemdhulumu basi atakuwa ni mshirika katika dhulma, kwa sababu kumnyamazia dhalimu kunamtia mori. Na lau dhalimu atajua kuwa mdhulumiwa ataitetea heshima yake basi atajizuia.

Bali njia ya lawama ipo kwa wale wanaowadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika ardhi bila ya haki. Hao watapata adhabu iliyo chungu.

Huko nyuma tumewahi kueleza kuwa dhalimu anahukumiwa kuwa ni kafiri mbele ya Mwenyezi Mungu, ajapotamka shahada mbili. Ndio! Hapa duniani atachukuliwa kama Mwislamu, lakini Akhera atakuwa pamoja na madhalimu. Hilo ni kwa ushahidi wa Aya kadhaa, zinazomwita kafiri kuwa ni dhalimu na dhalimu kuwa ni kafiri. Tazama Juz. 3 (2:254) na Juz. 9 (25:55-62).

Na anayesubiri, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa; yaani ni mambo mazuri ya kuazimiwa kufanywa. Aina bora ya subira ni kuvumilia udhia katika kuithibitisha haki na kuitangaza. Na aina bora zaidi ya kusamehe ni kule kutakakosababisha kuondoa fitina na ufisadi.


16

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن وَلِيٍّ مِّن بَعْدِهِ وَتَرَى الظَّالِمِينَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ يَقُولُونَ هَلْ إِلَىٰ مَرَدٍّ مِّن سَبِيلٍ ﴿٤٤﴾

44. Na ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, hana walii baada yake. Na utawaona madhalimu watakapoiona adhabu watasema: Je, ipo njia ya kurudi?

وَتَرَاهُمْ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا خَاشِعِينَ مِنَ الذُّلِّ يَنظُرُونَ مِن طَرْفٍ خَفِيٍّ وَقَالَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَلَا إِنَّ الظَّالِمِينَ فِي عَذَابٍ مُّقِيمٍ ﴿٤٥﴾

45. Na utawaona wanapelekwa kwenye Moto, nao wamenyenyekea kwa unyonge, wanatazama kwa mtazamo wa kificho. Na walioamini watasema: Hakika waliopata hasara ni hao waliohasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Ehe! Hakika wenye kudhulumu watakuwa katika adhabu ya kudumu.

وَمَا كَانَ لَهُم مِّنْ أَوْلِيَاءَ يَنصُرُونَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن سَبِيلٍ ﴿٤٦﴾

46. Wala hawatakuwa na walii wa kuwanusuru asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemepoteza, basi hana njia yoyote.

اسْتَجِيبُوا لِرَبِّكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا مَرَدَّ لَهُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَكُم مِّن مَّلْجَإٍ يَوْمَئِذٍ وَمَا لَكُم مِّن نَّكِيرٍ ﴿٤٧﴾

47. Mwitikieni Mola wenu kabla haijafika siku isiyoepukika itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo hamtakuwa na pa kukimbilia wala hamtakuwa na cha kukataa.

فَإِنْ أَعْرَضُوا فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا إِنْ عَلَيْكَ إِلَّا الْبَلَاغُ وَإِنَّا إِذَا أَذَقْنَا الْإِنسَانَ مِنَّا رَحْمَةً فَرِحَ بِهَا وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَإِنَّ الْإِنسَانَ كَفُورٌ ﴿٤٨﴾

48. Na wakipuuza, basi hatukukupeleka uwe mwenye kuwalinda. Si juu yako ila kufikisha tu. Na hakika tukimwonjesha mtu rehema kutoka kwetu, huifurahia. Na akisibiwa na ovu kwa sababu ya iliyotanguliza mikono yao, basi hakika mtu huyu anakufuru.

لِّلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ يَهَبُ لِمَن يَشَاءُ إِنَاثًا وَيَهَبُ لِمَن يَشَاءُ الذُّكُورَ ﴿٤٩﴾

49. Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume.

أَوْ يُزَوِّجُهُمْ ذُكْرَانًا وَإِنَاثًا وَيَجْعَلُ مَن يَشَاءُ عَقِيمًا إِنَّهُ عَلِيمٌ قَدِيرٌ ﴿٥٠﴾

50. Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye uweza.

MWENYE HASARA NI YULE ALIYEJIHASIRI MWENYEWE

Aya 44 – 50

MAANA

Na ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, hana walii baada yake.

Mwenye kufuata njia ya upotevu kwa uchaguzi wake mbaya, basi atakuwa ni katika wapotevu. Wala hakuna wa kumlaumu ila yeye mwenyewe. Ambaye Mwenyezi Mungu amemuhizi hawezi kupata wa kumuokoa na hizaya hii.

Na utawaona madhalimu watakapoiona adhabu watasema: Je, ipo njia ya kurudi?

Walijikuza, wakafanya kiburi na kutakabari katika maisha ya dunia, lakini watakapofufuliwa wakiwa dhalili, watanyenyekea na watatafuta njia ya kuokoka na adhabu au kurudi duniani mara nyingine.

Hivi ndivyo walivyo mataghuti, wanajikuza ikiwa hakuna nguvu ya kuwarudi na wananyewa ikiwadhihirikia dalili yake.

Na utawaona wanapelekwa kwenye Moto, nao wamenyenyekea kwa unyonge, wanatazama kwa mtazamo wa kificho.

Wataukabili moto kwa matendo yao, wataichungulia Jahannam wakiwa wanatetemeka kwa hofu kuu, na hapo mwanzo walikuwa wakiifanyia mzaha.

Na walioamini watasema: Hakika waliopata hasara ni hao waliohasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Ehe! Hakika wenye kudhulumu watakuwa katika adhabu ya kudumu.

Waumini watayasema haya watakapowaona wakosefu wakisukumwa kwenye mwisho wa matendo yao, watamshukuru Mwenyezi Mungu aliyewaokoa na hizaya hii. Umetangulia mfano wake katika Juz. 23 (39:15).

Wala hawatakuwa na walii wa kuwanusuru asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

Sharti la kwanza la walii (mlinzi) atakayeweza kusaidia, ni kuwa yeye mwenyewe awe na nguvu za kujikinga na kujisadia au kumsadia mwingine. Siku hiyo hakutakuwa na yeyote atakayekuwa na uwezo au nguvu.

Na ambaye Mwenyezi Mungu amemepoteza, basi hana njia yoyote ya kuokoka na moto.

Hapa tutaufasiri upotevu kwa maana ya moto, kwa sababu mfumo wa maneno unaishiria hilo; sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Juz. 24 (40:34): “Kama hivyo Mwenyezi Mungu humpoteza yule aliyepita kiasi mwenye shaka.” Yaani anamwadhibu.

Mwitikieni Mola wenu kabla haijafika siku isiyoepukika itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo hamtakuwa na pa kukimbilia wala hamtakuwa na cha kukataa

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewakalifisha waja yale yaliyo na manufaa kwao na heri yao, akawapa uwezo wa kuyatekelza yale aliyowakalifisha, akawapa muda wa kuyatenda na kutubia na akwahadharisha na matokeo ya kupuuza na uzembe – hakumwachia yeyote hoja ya kukimbilia siku ile ambayo mtu hataweza kurudishwa kwenye maisha yake ya kwanza wala hataweza kuyakana yaliyofanywa na mikono yake.

Na wakipuuza, basi hatukukupeleka uwe mwenye kuwalinda. Si juu yako ila kufikisha tu.

Maana yako wazi. Umetangulia mfano wake katika Aya kadhaa; kama vile: Juz. 5 (4:80) na Juz. 7(6:107).

Na hakika tukimwonjesha mtu rehema kutoka kwetu, huifurahia. Na akisibiwa na ovu kwa sababu ya iliyotanguliza mikono yao, basi hakika mtu huyu anakufuru.

Makusudio ya rehema ni neema; kama vile afya na mali, na ovu ni balaa; kama vile ufukara na maradhi. Ama Makusudio ya mtu ni wengi katika wao sio kila mtu; vinginevyo ingelikuwa mtu hana taklifa yoyote, ikiwa ndio hivyo alivyo; kama tulivyobainisha katika Juz.13 (14:32-34).

Maana ni kuwa mjinga mwenye hasara huwa anafurahi kwa starehe za dunia akizipata na anakufuru akikosa kitu, hata kama ni kwa rai yake mbaya na matamanio ya nafsi yake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 12 (11:9-10).

Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; anaumba apen- davyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume. Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye uweza.

Hakuna mwenye shaka kwamba mtu hana hiyari wala uweza wowote wa kupata watoto wa kike tu au wa kiume tu au mchanganyiko. Ni Mwenyezi Mungu tu ndiye mwenye uwezo wa kumpa mtu watoto wa kike, wa kiume, mchanganyiko au kumfanya asizae kabisa. Mpaka sasa bado madaktari hawajaweza kutibu utasa kwa mwanamume au kwa mwanamke. Waliloweza ni kuchukua mbegu za mwanamume mwingine, bila ya kufanyika tendo la kujamiaana, na kuzitia kwa mke wa mume tasa.

Tumeweka mlango maalum wa hilo katika kitabu chetu Al-islamu walhay-at (Uislamu na maisha) na tukatoa fatwa ya kuharamisha hilo na kwamba mtoto atakayezaliwa katika njia hiyo hawezi kuwa wa mume, kwa ijimai, na atakuwa ni wa mama.

وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ ﴿٥١﴾

51. Na haikuwa kwa mwanaadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi, au kwa nyuma ya pazia, au kumtuma Mjumbe. Naye humletea wahyi ayatakayo kwa idhini yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hikima.

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٥٢﴾

52. Na hivyo ndivyo tulivyokupa roho kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumeifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunamwongoza tumtakaye katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoza kwenye njia iliyonyooka.

صِرَاطِ اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ أَلَا إِلَى اللَّـهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ ﴿٥٣﴾

53. Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Ehe! mambo yote yanarudi kwa Mwenyezi Mungu.

SURA YA MAWASILIANO BAINA MWENYEZI MUNGU NA MITUME WAKE

Aya 51 – 53

MAANA

Na haikuwa kwa mwanaadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi, au kwa nyuma ya pazia, au kumtuma Mjumbe. Naye humletea wahyi ayatakayo kwa idhini yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hikima.

Maneno ya Mwenyezi Mungu yana maana nyingi; miongoni mwayo ni haya yafuatayo:

Kadha yake na kadari yake: “Na lau si neno lilikwishatangulia kutoka kwa Mola wako.” Aya 45

Kuuumba:

إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّـهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ ﴿١٧١﴾

“Hakika Masih Isa bin Maryamni Mtume wa Mwenyezi Mungu ni neno lake tu alilompelekea Maryam, Juz. 6 (4:171)

Haki:

وَكَلِمَةُ اللَّـهِ هِيَ الْعُلْيَا ﴿٤٠﴾

“Na neno la Mwenyezi Mungu ndilo la juu.” Juz. 10 (9:40).

Ulimwengu aliouleta kwa neno

كُن ﴿٨٢﴾

“kuwa” Juz. 23 (36:82)

Ilhamu kama inavyoelezewa kwenye Aya hii tuliyo nayo: “kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi.”

Maneno yanayosikiwa:

أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾

“Je mnatumaini ya kwamba wataamini na hali baadhi yao walikuwa wanasikia maneno ya Mwenyezi Mungu kisha wanayabadili baada ya kuwa wameyafahamu na hali wanajua? Juz. 1 (2:75).

Maneno haya ndiyo anayoyasikia Mtume nyuma ya pazia au kupelekewa mjumbe.

Katika Aya hii tuliyo nayo Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja njia tatu za kuzungumza kwake Mwenyezi Mungu na mitume na namna ya kuwasiliana nao:

1. Kuyaingiza maana katika moyo wa Mtume moja kwa moja bila ya kuweko kati chochote. Hii ndiyo iliyokusudiwa katika kauli yake: ‘Ila kwa wahyi’

2. Kuumba Mwenyezi Mungu maneno, kama anavyoumba vitu vingine na kuyasikia mtume nyuma ya pazia; yaani bila ya kumuona mzungumzaji. Ndio makusudio ya kauli yake:

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا ﴿١٦٤﴾

“Na Musa akanena na Mwenyezi Mungu maneno.” Juz. 6 (4:164).

3. Kumpeleka Mwenyezi Mungu (s.w.t) Malaika kwa Mtume wake, atakayemfikishia risala ya Mola wake. Mula Sadra anasema katika Asfar: “Usije ukadhani Mtume(s.a.w. w ) alipokea maneno ya Mwenyezi Mungu kupitia kwa Jibril kama unavyosikia wewe kutoka kwa Mtume, au kusema kuwa Mtume(s.a.w. w ) alikuwa akimwiga Jibril.”

Hakuna mwenye shaka kuwa hakuna anayedhania au kusema hivi isipokuwa mjinga tu. Kwa sababu Jibril aliyomfikishia Muhammad(s.a.w. w ) ni maneno ya Mwenyezi Mungu hasa na Mtume(s.a.w. w ) akayaelewa kiuhakika wake.

Kwa hiyo basi kule kujua Mtume maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ndio maneno ya Mwenyezi Mungu, na maneno ya Mwenyezi Mungu ndio kujua Mtume.

Na hivyo ndivyo tulivyokupa roho kwa amri yetu.

Makusudio ya roho hapa ni Qur’an, kwa sababu hiyo ni uhai wa roho na mwili vile vile. Imam Ali(a.s ) anasema:“Kitabu cha Mwenyezi Mungu mnaona kwacho, mnatamka kwacho na manasikia kwacho”

Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala imani.

Makusudio ya Kitabu ni Qur’an na imani ni sharia ya Mwenyezi Mungu ambayo ameibainisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa Nabii wake mtukufu baada ya kumchagua Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa risala yake. Wametofautiana katika tafsiri ya Aya hii kwenye kauli ambazo Razi ameishilizia tano. Yenye nguvu zaidi – kama tuonavyo – ni kauli ya Sheikh Ismail Haqqi, katika Tafsir Ruhul-bayan, ninamnukuu:

“Makusudio ya imani ni ufafanuzi uliokuja kwenye Qur’an ambao akili hauwezi kuupata, sio ile imani ambayo inakuwa kwenye akili na maarifa. Kwa sababu uzoefu wa Mtume(s.a.w. w ) hauna shaka.

Wamekongamana watu wa Usul – kwenye maarifa ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake – kwamba mitume walikuwa ni waumini kabla ya wahyi, wakiwa wamehifadhika (maasumu) na madhambi makubwa na madogo ambayo yangeliweza kuwafanya watu wawakimbie kabla na baada ya utume, zaidi ya kwamba hawakuwa makafiri.”

Lakini tumeifanya hiyo Qur’ankuwa ni Nuru ambayo kwayo tunamwongoza tumtakaye katika waja wetu ambao wametafuta uongofu kwa nia safi na wakaitafuta haki kwa haki. Ama yule aliyeasi na akafanya jeuri, Mwenyezi Mungu anaachana naye:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ ﴿٣﴾

“Hakika Mwenyezi Mungu hamwongozi aliye mwongo kafiri.” Juz. 23 (39:3).

Na hakika wewe unaongoza kwenye Njia Iliyonyooka, njia ya Mwenyezi Mungu.

Nabii(s.a.w. w ) anatoa mwito wa Uislamu, dini ya Mwenyezi Mungu na njia yake iliyonyooka. Mwenye kufuata njia hii atakuwa amefuata njia ya wazi itakayompeleka kwa Mwenyezi Mungu na atasalimika na mwisho mbaya.

Ambaye ni vyake vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Ehe! mambo yote yanarudi kwa Mwenyezi Mungu.

Mwito wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ndio njia ya kueleka kwa Mfalme wa ulimwengu Ambaye atawakusanya Siku isiyo na shaka. Basi mwenye kuusikiliza mwito wa Mtume na akauitikia, kesho atakuwa pamoja na wakweli na manabii.

Hao ndio marafiki wazuri. Na mwenye kuuacha, akajiweka mbali nao, atakuwa katika Jahannam na rafiki yake shetani.

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI NA MBILI: SURAT ASH-SHURA


17

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

Sura Ya Arubaini Na Tatu: Surat Az-Zukhruf. Ina aya 89 Imeshuka Makka. Imesemekana isipokuwa Aya moja haikushuka Makka

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

حم ﴿١﴾

1. Haa-miim.

وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾

2. Naapa kwa Kitabu kinachobainisha.

إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٣﴾

3. Hakika tumeifanya Qur’an kwa kiarabu ili mfahamu.

وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ ﴿٤﴾

4. Na hakika hiyo imo katika mama wa Kitabu kilichoko kwetu, ni tukufu na yenye hiki- ma.

أَفَنَضْرِبُ عَنكُمُ الذِّكْرَ صَفْحًا أَن كُنتُمْ قَوْمًا مُّسْرِفِينَ ﴿٥﴾

5. Je, tuache kuwakumbusha kwa kuwa ni watu mliopita mipaka?

وَكَمْ أَرْسَلْنَا مِن نَّبِيٍّ فِي الْأَوَّلِينَ ﴿٦﴾

6. Na manabii wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani!

وَمَا يَأْتِيهِم مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٧﴾

7. Na hakuwajia nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli.

فَأَهْلَكْنَا أَشَدَّ مِنْهُم بَطْشًا وَمَضَىٰ مَثَلُ الْأَوَّلِينَ ﴿٨﴾

8. Na tuliwaangamiza waliokuwa na nguvu kushinda wao, na mfano wa watu wa zamani umekwishapita.

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ ﴿٩﴾

9. Na ukiwauliza: Nani aliyeumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi.

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَجَعَلَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٠﴾

10. Ambaye amewafanyia ardhi kuwa tandiko, na akawafanyia ndani yake njia mpate kuongoka.

وَالَّذِي نَزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَنشَرْنَا بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا كَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ ﴿١١﴾

11. Na ambaye ameteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na kwa hayo tukaifufua nchi iliyokufa. Na hivyo ndivyo mtakavyotolewa.

وَالَّذِي خَلَقَ الْأَزْوَاجَ كُلَّهَا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْفُلْكِ وَالْأَنْعَامِ مَا تَرْكَبُونَ ﴿١٢﴾

12. Na ambaye ameumba aina zote, na akawafanyia jahazi na wanyamahowa mnaowapanda.

لِتَسْتَوُوا عَلَىٰ ظُهُورِهِ ثُمَّ تَذْكُرُوا نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا اسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَـٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ ﴿١٣﴾

13. Ili mkae vizuri migongoni mwao. Kisha mkumbuke neema za Mola wenu mnapokaa sawa sawa juu yao hao mnaowapanda na mseme: Ametakasika aliyemfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya haya wenyewe.

وَإِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ ﴿١٤﴾

14. Na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi.

KITABU KINACHOBAINISHA

Aya 1 – 14

MAANA

Haa-miim.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1).

Naapa kwa Kitabu kinachobainisha.

Hiki ni kiapo kutoka kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Qur’an ambayo ndani yake mna ubainifu wa uongofu na upotevu, na halali na haramu.

Hakika tumeifanya Qur’an kwa kiarabu ili mfahamu.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 12 (12:2), Juz. 16 (20:113), Juz. 24 (41:3) na kwenye Juzuu hii tuliyo nayo (42:7). Tumekwishaizungumzia sana Aya hii, na hivi sasa hatuna la ziada.

Na hakika hiyo imo katika mama wa Kitabu kilichoko kwetu, ni tuku- fu na yenye hikima.

‘Hiyo’ ni hiyo Qur’an na mama ni asili. Hakuna mwenye shaka kwamba ilimu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndio asili ya vitabu vyote mbinguni. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameisifu Qur’an kuwa ni tukufu kwa sababu inainua na kuwatukuza wanayoisikiliza na kuitumia. Tumeona jinsi ilivyowatoa waarabu kwenye ujinga wa wajinga kuwapeleka kwenye maendeleo na jinsi ilivyoeneza utawala wao na lugha mashariki ya ardhi na magharibi yake, pale walipohalalisha halali ya Qur’an na wakaharamisha haramu ya yake.

Vile vile Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameisifu kuwa ina hikima kwa sababu imeweka sawa baina ya watu bila ya kubagua, ikatoa mwito wa kusameheana na ikahimiza kufanya kazi yenye manufaa na kusaidiana kwa masilahi ya watu wote.

Je, tuache kuwakumbusha kwa kuwa ni watu mliopita mipaka?

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuitaja Qur’an kwamba ni mtoa nasaha mwaminifu, sasa anawaambia wale walioikadhibisha katika washirikina wa kiarabu: Mnaonaje tuache kuwakumbusha Qur’an kwa vile tu nyinyi mmezipitishia kiasi nafsi zenu na mkazidhulumu kwa ujinga na upotevu? Bali nyinyi ndio mnafaa zaidi kukumbushwa kuliko wengineo.

Na Manabii wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani!

Ni wengi tu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemsimulia Mtume wake habari za manabii kadhaa na akamwambia:

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ ﴿٧٨﴾

“Na kwa hakika tuliwatuma Mitume kabla yako. Wengine katika hao tumekusimulia na wengine hatukukusimulia.” Juz. 24 (40:78).

Na hakuwajia nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli, kama walivyokukejeli wewe ewe Muhammad. Kwa hiyo lisikutie tabu hilo, si mageni hayo. Ni vita baina ya wapotevu na wanaolingania haki na uadilifu, kila mahali na kila wakati.

Na tuliwaangamiza waliokuwa na nguvu kushinda wao.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwaangamiza mataghuti waliokuwa na nguvu katika umma zilizopita kwa kuwanusuru wema walio wanyonge.

Na mfano wa watu wa zamani umekwishapita.

Yaani tumekusimulia katika Qur’an hali ya waongo wa zamani na jinsi walivyoangamia, ili watu wako wapate funzo.

Na ukiwauliza: Nani aliyeumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 21 (29:61), (31:25) na Juz. 24 (39:38)

Ambaye amewafanyia ardhi kuwa tandiko, na akawafanyia ndani yake njia mpate kuongoka. Na ambaye ameteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na kwa hayo tukaifufua nchi iliyokufa. Na hivyo ndivyo mtakavyotolewa.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:99), Juz. 13 (13:3) na Juz. 16 (20:53).

Na ambaye ameumba aina zote.

Yaani aina zote za waanyama, mimea na vitu vigumu.

Na akawafanyia jahazi na wanyamahowa mnaowapanda.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwatajia neema ya maji na ardhi na kwamba wao wanakula, kuvaa na kunywa humo, sasa anawatajia neema ya mawasiliano. Ametaja jahazi na wanyama kwa njia ya mfano tu sio kuwa ndio hayo tu; kwa sababu magari na ndege hayakuwa maarufu wakati huo.

Ili mkae vizuri migongoni mwao.

Yaani migongoni mwa hao mnaowapanda.

Kisha mkumbuke neema za Mola wenu mnapokaa sawa sawa juu yao hao mnaowapanda na mseme: Ametakasika aliyemfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya haya wenyewe. Na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi.

Katika Nahjul-balagha amesema: “Ewe Mola wangu! Ninajilinda kwako na mashaka ya safari, na huzuni ya marejeo na ubaya wa mandhari katika watu wa nyumbani na mali.

Ewe Mola wangu! Hakika wewe ni mwenza safarini na wewe ndiwe wa kuachwa nyuma na familia. Wala hawezi kuyakusanya haya mawili isipokuwa wewe. Kwa sababu mwenye kuachwa nyuma hawezi kuwa mwenza na mwenza hawezi kuachwa nyuma.”

Sheikh Muhammad Abduh anaielezea kauli hiyo ya Imam Ali(a.s) , kwa kusema:“Mwanzo wa maneno haya umepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na akayatimiza Amirul-muminin kwa kusema Wala hawezi kuyakusanya…mpaka mwisho. Dhati ya Mwenyezi Mungu iko sawa mahali pote na wakati wote. Kwa hiyo kuwa safarini na kuwa mjini kwake ni sawa.”

وَجَعَلُوا لَهُ مِنْ عِبَادِهِ جُزْءًا إِنَّ الْإِنسَانَ لَكَفُورٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾

15. Na wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika mwanadamu ni mwenye kukufuru waziwazi.

أَمِ اتَّخَذَ مِمَّا يَخْلُقُ بَنَاتٍ وَأَصْفَاكُم بِالْبَنِينَ ﴿١٦﴾

16. Au amejichukulia watoto wa kike katika vile alivyoviumba, na akawachagulia nyinyi watoto wa kiume?

وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِمَا ضَرَبَ لِلرَّحْمَـٰنِ مَثَلًا ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ ﴿١٧﴾

17. Na mmoja wao akibashiriwa kwa yale aliyompigia mfano Mwingi wa rehema, uso wake husawijika naye amejaa chuki.

أَوَمَن يُنَشَّأُ فِي الْحِلْيَةِ وَهُوَ فِي الْخِصَامِ غَيْرُ مُبِينٍ ﴿١٨﴾

18. Ati aliyelelewa katika mapambo, na katika mabishano hawezi kusema bayana?

وَجَعَلُوا الْمَلَائِكَةَ الَّذِينَ هُمْ عِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ إِنَاثًا أَشَهِدُوا خَلْقَهُمْ سَتُكْتَبُ شَهَادَتُهُمْ وَيُسْأَلُونَ ﴿١٩﴾

19. Na wakawafanya malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa na wataulizwa!

وَقَالُوا لَوْ شَاءَ الرَّحْمَـٰنُ مَا عَبَدْنَاهُم مَّا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ إِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿٢٠﴾

20. Na husema: Angelipenda Mwingi wa Rehema tusingeliwaabudu. Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ila kusema uwongo tu!

أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا مِّن قَبْلِهِ فَهُم بِهِ مُسْتَمْسِكُونَ ﴿٢١﴾

21. Au tuliwapa Kitabu kabla ya hiki, wakawa wameshikamana nacho?

بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّهْتَدُونَ ﴿٢٢﴾

22. Bali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu juu ya desturi na tunaongoza nyayo zao.

وَكَذَٰلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ ﴿٢٣﴾

23. Na kadhalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila wapenda anasa wake walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu juu ya desturi na tunafuata nyayo zao.

قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ ﴿٢٤﴾

24. Akasema: Hata nikiwaletea yenye muongozo bora kuliko mliowakuta nayo baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo.

فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ ﴿٢٥﴾

25. Basi tukawalipizia. Angalia ulikuwaje mwisho wa waliokadhibisha!

AU AMEJICHUKULIA WATOTO WANAWAKE

Aya 15 – 25

MAANA

Na wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika mwanadamu ni mwenye kukufuru waziwazi. Au amejichukulia watoto wakike katika vile alivyoviumba, na akawachagulia nyinyi watoto wa kiume?

Makusudio ya fungu hapa ni mtoto, kwa sababu ni sehemu ya mzazi wake. Ama kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watoto wa kike katika vile alivyoviumba, inaonyesha dalili ya uharibifu wa madai yao kuwa Mwenyezi Mungu ana mtoto, kwa sababu muumbwa hawezi kuwa ni sehemu ya aliyeumba; kama ambavyo nyumba haiwezi kuwa ni sehemu ya mjenzi.

Washirikina hawakutosheka na uzushi huu, mpaka wakamhusisha Mwenyezi Mungu na wale watoto wasiowapenda wao.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:100), Juz. 15 (17:40) na Juz. 23 (37:149-153).

Na mmoja wao akibashiriwa kwa yale aliyompigia mfano Mwingi wa rehema, uso wake husawijika naye amejaa chuki.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwasifu washirikina na ukafiri ulio waziwazi, sasa anawashutumu wale wanaohuzunika na kukasirika wakipata wasichana, wakati huohuo wanamzulia Mwenyezi Mungu na kusema kuwa ana watoto wasichana.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 14 (16:58).

Ati aliyelelewa katika mapambo, na katika mabishano hawezi kusema bayana?

Ewe mshirikina mjinga! Unamnasibishia Mwenyezi Mungu wanawake wanojipamba, na kama ukihojiwa kwenye hilo utashindwa na hoja na dalili? Wafasiri wamesema wamemnasibishia Mwenyezi Mungu wanawake ambao hawawezi hoja na kubishana Dhahiri ya Aya inarudia kwenye tafsiri hii.

Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao?

Vipi wanajasiri washirikina kusema kuwa Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu. Je, walikuwako kwa Mwenyezi Mungu wakati akiwaumba Malaika au aliwapa habari ya hilo? Amesema kweli aliyesema: “Mtu amesema uwongo juu aliye mfano wake, juu ya Mola wake, juu ya Mitume wake na Malaika wake, vile vile amesema uwongo juu ya nafsi yake.”

Mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

أَمْ خَلَقْنَا الْمَلَائِكَةَ إِنَاثًا وَهُمْ شَاهِدُونَ ﴿١٥٠﴾

“Au tumewaumba malaika kuwa ni wanawake na wao wakashuhudia? Juz. 23 (37:150).

Ushahidi wao utaandikwa na wataulizwa!

Kwa Mwenyezi Mungu hakufichiki chochote, Yeye anajua uzushi wao kwake na kwa Malaika wake na kesho atawauliza na kuwahisabu

Na husema: Angelipenda Mwingi wa Rehema tusingeliwaabudu.

Wanadai kuwa Mwenyezi Mungu yuko radhi wao kuabudu Malaika na masanamu; vinginevyo angeliwazuia kwa nguvu. Wamesahau kama Mwenyezi Mungu angelifanya hivyo, mtu angelikuwa sawa na mawe, asingelistahiki thawabu wala adhabu.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (6:148).

Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ila kusema uwongo tu!

Wamenasibisha shirki yao na upotevu wao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu! Hawajui kuwa Yeye, ambaye imetukuka enzi yake, anaamrisha na anakataza kitaklifa na kimongozo, akaacha utekelezaji uwe kwa matakwa ya aliyekalifishwa, ili yadhihiri matendo yake yatakayomfanya astahiki thawabu au adhabu.

Au tuliwapa Kitabu kabla ya hiki, wakawa wameshikamana nacho?

Hapana! Hawana dalili ya akili wala ya nakili kwa madaia yao, isipokuwa dalili hii:

Bali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu juu ya desturi na tunaongoza nyayo zao.

Kwa hiyo kuwaiga mababa ndio kimbilio la kwnza na la mwisho. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameisimulia kauli yao hii katika Aya kadha; miongoni mwazo ni: Juz. 2 (2:170), Juz. 7 (5:104), Juz.17 (21:53), Juz.21 (31:21) na nyinginezo. Tumeweka kifungu kuhusu kuiga na mafungu yake katika Juz. 2 (2:170).

Na kadhalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila wapenda anasa wake walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu juu ya des- turi na tunafuata nyayo zao.

Haya ndio mantiki ya wanaotaka manufaa yao tu, tangu walipoanza kupatikana hadi siku ya mwisho. Tazama kifungu ‘Fikra ya mataghuti’ katika Juz. 13 (13:30-31), Juz. 15 (17:16-21) na kifungu ‘Mantiki ya watu wa pesa ni benki na ardhi.’ katika Juz. 18 (25:7-16).

Akasema: Hata nikiwaletea yenye muongozo bora kuliko mliowaku- ta nayo baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo.

Tunalolifahamu kutokana na kauli yao hii ni kuwa wao wanaikataa haki popote na vyovyote iwavyo; hata kama ingelitoka kwa mababa zao, na kwamba wao hawaamini chochote isipokuwa manufaa na chumo lao tu.

Ama kujiingiza kwenye desturi ya mababa ni visingizio tu, wakihofia kujulikana uhakika wao na watu. Tumewawona wengi wakiwabeza mababa zao, si kwa lolote ila kuwa wanagongana na masilahi na mapendeleo yao. Hakuna malipo kwa mwenye kuipinga haki isipokuwa kumtumilia nguvu:

Basi tukawalipizia. Angalia ulikuwaje mwisho wa waliokadhibisha!

Bila shaka ni fedheha na moto wa Jahannam.


18

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ ﴿٢٦﴾

26. Na pale Ibrahim alipomwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayoyaabudu.

إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ ﴿٢٧﴾

27. Isipokuwa yule aliyeniumba, kwani Yeye ataniongoza.

وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٢٨﴾

28. Na akalifanya liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee.

بَلْ مَتَّعْتُ هَـٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْحَقُّ وَرَسُولٌ مُّبِينٌ ﴿٢٩﴾

29. Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume anayebainisha.

وَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ وَإِنَّا بِهِ كَافِرُونَ ﴿٣٠﴾

30. Na ilipowafikia Haki wakasema: Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa.

وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ هَـٰذَا الْقُرْآنُ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنَ الْقَرْيَتَيْنِ عَظِيمٍ ﴿٣١﴾

31. Na walisema: Kwa nini Qur’an hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?

أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُم مَّعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِّيَتَّخِذَ بَعْضُهُم بَعْضًا سُخْرِيًّا وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ ﴿٣٢﴾

32. Kwani wao ndio wanaogawa rehema za Mola wako? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawainua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wengine wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya.

وَلَوْلَا أَن يَكُونَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً لَّجَعَلْنَا لِمَن يَكْفُرُ بِالرَّحْمَـٰنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفًا مِّن فِضَّةٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا يَظْهَرُونَ ﴿٣٣﴾

33. Na lau isingekuwa watu watakuwa kundi moja tungeliwajaalia wanaomkufuru Mwingi wa rehema nyumba zao zina dari ya fedha, na ngazi zao pia wanazopandia.

وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَابًا وَسُرُرًا عَلَيْهَا يَتَّكِئُونَ ﴿٣٤﴾

34. Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyoegemea juu yake.

وَزُخْرُفًا وَإِن كُلُّ ذَٰلِكَ لَمَّا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةُ عِندَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٣٥﴾

35. Na mapambo. Na hayo yote si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako ni ya wenye takua.

JE, WANAIGAWA REHEMA YA MOLA WAO?

Aya 26 – 35

MAANA

Na pale Ibrahim alipomwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayoyaabudu, isipokuwa yule aliyeniumba, kwani Yeye ataniongoza.

Kaumu ya Ibrahim, akiwemo baba yake, kama inayvofahamisha dhahiri ya Aya, walikuwa wakiabudu masanamu. Basi akawakataza na akatangaza kujitenga nayo, na kwamba yeye anamwabudu aliyemuumba na atamuongoza kwenye lile lililo na heri na masilahi naye.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:73), Juz. 16 (19: 41-44), Juz. 17 (21:51-56), Juz. 19 (26:69-82) na Juz. 23 (37:83-85).

Kusema kwake: ‘Kwani Yeye ataniongoza,’ kunaonyesha yakini yake na kumtegemea kwake Mwenyezi Mungu. Hivi ndivyo anavyokuwa kila mwenye kuitafuta haki na mwongozo kwa nia safi. Anaamini kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja naye, atamtosha na atamwongoza. Hiyo inatokana na kauli zake Mwenyezi Mungu Mtukufu zifuatazo:-

وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ ﴿٣٦﴾

“Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye takua.” Juz. 10 (9:36).

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٣﴾

“Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaosubiri” Juz.2 (2:153).

وَإِنَّ اللَّـهَ لَمَعَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٦٩﴾

“Na hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wema” Juz. 21 (29:69).

Na akalifanya liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake.

Alilolifanya ni hilo neno la Tawhid, likiashiriwa na kauli yake: ‘Hakika mimi najitenga mbali na hayo mnayoyaabudu.’

Makusudio ya kulifanya ni kuliusia; kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na Ibrahim akawausia haya wanawe na Yaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amewachagulia dini; basi msife ila nanyi ni waislamu.” Juz. 1 (2:131).

Ili warejee.

Hii ndio sababu yake Ibrahim kuwazuia wanawe; kwa maana ya kuwa aliwausia neno la Tawhid, ili walijue. Na kama mmoja wao akishirikisha au akijaribu basi akumbuke wasia wa baba yake na aambiwe kuwa wewe umehalifu wasia wa Ibrahim.

Na hilo lilitokea hasa: “Sema: amesem kweli Mwenyezi Mungu. Basi fuateni mila ya Ibrahim aliyeshikamana na haki; wala hakuwa katika washirikina.” Ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye aliwaita waislamu zamani. Juz. 4 (3:95) Juz. 17 (22:78).

KWA NINI ALI KARRAMALLAHU WAJHAH

Mwaka 1389 nilifunga Ramadhan tukufu Dubai kwa mwaliko kutoka huko. Vijana wakawa wananiuliza maswali mengi; miongoni mwayo ni: Kwa nini wanapotajwa maswahaba sunni wanasema: Radhiallah a’nhu (Mwenyezi Mungu awe Radhi naye) na Shia anapotajwa Imam wanasema : Alyhis salaam (Amani ishuke juu yake).

Nikajibu kuwa wote wamechukua kutoka kwenye Qur’an:

رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ﴿١١٩﴾

“Awe radhi nao Mwenyezi Mungu na wao wawe radhi naye” Juz. 7 (5:119).

قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ وَسَلَامٌ عَلَىٰ عِبَادِهِ الَّذِينَ اصْطَفَى ﴿٥٩﴾

“Sema: Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu (Alhamdu lillah) na amani ishuke juu ya waja wake aliowateua” Juz. 19 (27:59).

Kwa hiyo Shia wamechukua hii na Sunni wakachukua ile.

Nilipofikia kufasiri kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Ili warejee,’ nikasoma kwenye Tafsir Ruhul-bayan ya Sheikh Ismail Haqqi, katika ulama wa kisunni, ninamnukuu: “Wamesema baadhi katika kutukuzwa uso wa Ali bin Abu Twalib, kwa kusemwa: Karramallahu wajhah (Mwenyezi Mungu autukuze uso wake), kwamba imenukuliwa kutoka kwa mama yake, Fatima bint Asad, kwamba yeye (Fatma) alipokuwa akitaka kusujudia sanamu, Ali akimzuia akiwa tumboni.”

Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume anayebainisha.

Hawa ni washirikina wa kiquraishi, ambao ni kizazi cha Ibrahim(a.s ) . Makusudio ya haki hapa ni Qur’an na Mtume ni Muhammad(s.a.w.w) . Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemsifu kuwa anabainisha, kwa sababu risala yake iko wazi dalili na muujiza wake umemziba mdomo kila mpingaji.

Maana ni kuwa vigogo wa kiquraishi walimshirikisha Mwenyezi Mungu na wakaupinga wasia wa baba yao Ibrahim(a.s ) wa Tawhid, lakini Mwenyezi Mungu akawapa muda na akawaneemesha fadhila zake, lakini iliwatamalaki ghururi wakapituka mipaka, mpaka alipowajia Mtume kutokana na wao wenyewe na Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinachowapa mwito wa Tawhid ambayo ni mila ya baba yao Ibrahim.

Na ilipowafikia Haki wakasema: Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa.

Waliikataa Qur’an na wakasema ni uchawi uliozushwa na wakamkataa Mtume wakasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِي نُزِّلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ ﴿٦﴾ لَّوْ مَا تَأْتِينَا بِالْمَلَائِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٧﴾

“Ewe uliyeteremshiwa ukumbusho! Wewe ni mwendawazimu. Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli?” Juz. 14 (15:6-7).

Na walisema tena: Kwa nini Qur’an hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?

Muhammad ni fukara ati anasema: Nimeteremshiwa Qur’an si ajabu hii! Mwenyezi Mungu anaweza kumchagulia risala yake mtu mkubwa; kama vile Walid bin Al-Mughira wa Makka na Urwa bin Mas’ud Athaqafi wa Taif. Mmoja wa hawa ndio angefaa kuteremshiwa Qur’an.

Hivi ndivyo walivyoipinga risala ya Muhammad(s.a.w. w ) ; si kwa lolote ila ni kwa vile hamiliki pesa wala ardhi. Hawajui kuwa mali inamilikiwa na mwema au muovu na mumin au kafiri. Lakini risala ni wakfu wa aliye kufu na na aliyesafi kati ya wasafi.

Hakuna tofauti mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) baina ya anayepinga utume wa Muhammad kwa sababu ya ufukara wake na yule anayemtukuza na kumweshimu tajiri kwa sababu ya mali yake na utajiri wake na kumdharau fukara kwa sababu ya ufukara wake. Hakuna tofauti kabisa baina ya hawa wawili; hata mmoja wao akitamka shahada mbili. Isipokuwa tu, atakayetamka duniani atachukuliwa kama mwislamu, lakini huko Akhera atakuwa pamoja na wapinzani na washirikina.

Kwani wao ndio wanaogawa rehema za Mola wako?

Makusudio ya rehema hapa ni utume. Maana ni kuwa, je jambo la utume liko mikononi mwa wapenda anasa, ndio wachague wanayemtaka na wamzuie wasiyemtaka? Kwani utume ni udiwani au ubunge? Hapana! Utume unatoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume anafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ndiye msemaji wake na mbainifu wake.

Sasa wapenda anasa ndio wasemaji rasmi wa Mwenyezi Mungu? Je, wao wanaweza kumruhusu mtu awe msemaji wao rasmi bila ya idhini yao? Vipi wanamfanyia Mwenyezi Mungu ambayo wao hawawezi kujifanyia?

Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawainua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wengine wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya.

Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye, hilo halina shaka, lakini Yeye vile vile ametaka kutoruzuku hivi hivi isipokuwa kwa sababu:

هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِن رِّزْقِهِ ﴿١٥﴾

“Yeye ndiye aliyeidhaliisha ardhi kwa ajili yenu, basi tembeeni katika pande zake na kuleni katika riziki zake.” (67:15).

Sababu hizi za riziki au mahangaiko katika ardhi yako aina nyingi; miongoni mwazo ni; viwanda, kilimo, biashara, utumishi, kama ilivyosema Qur’an: ‘Baadhi yao wanawafanya wengine wawatumikie,’ kama watumishi wa serikali, viwandani, madukani au hospitalini nk. Katika ufahamu wa watu nikuwa bosi yuko juu zaidi ya wengine, lakini mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu na na aliye juu zaidi ni yule mwenye takua zaidi.

إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿١٣﴾

“Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni aliye na takua zaidi katika nyinyi” (49:13)

“Na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, imeandaliwa wenye takua.”

Kwenye Nahjul-balagha Imam Ali(a.s ) anasema:

“Alikuwa na njaa Mtume katika dunia pamoja na umahasusi wake – yaani umahasusi mbele ya Mola wake-na alijiweka mbali na vivutio vya dunia pamoja na kuwa karibu navyo. Basi naatazame mwenye akili, je, Mwenyezi Mungu amemtukuza Muhammad kwa hilo au amemtweza? Akisema amemtweza – basi Wallahil-adhim – atakuwa muongo (anayesema hivyo) na akisema amemtukuza basi naajue kwamba Mwenyezi Mungu amemtweza mwenginewe aliyemkunjulia dunia.”

Unaweza kuuliza : utaifanyaje kauli: ‘Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawainua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi’ inayoonyesha wazi kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayefukarisha na kutajirisha, na anayemfanya huyu ni mfanyikazi na yule ni mfanyiwa kazi?

Jibu : kauli yake hii Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kusimulia hali halisi waliyo nayo watu na ameyategemeza hayo kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa sababu kutofautiana kunatokana na sababu zake za kimaumbile moja kwa moja na zinatoka kwake kwa kupitia kwengine, kwa vile Yeye ndiye muumba wa ulimwengu.

Maana haya yanafahamishwa na kauli yake Mwenyezi Mungu mwisho wa Aya: ‘Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya.’ Ambapo kukusanya mali amekutegemeza kwa watu.

Hapa ndio zinaafikiana Aya zinazoamrisha kuhangaikia riziki na zile zilizoitegemeza rizi kwa Mwenyezi Mungu moja kwa moja. Katika Juzuu hii tuliyo, kwenye (42:27), tumeashiria kwamba Mwenyezi Mungu mara nyingine anawapa baadhi ya waja wake tawfiki na kuwaruzuku kingi kutokana na kichache.

Na lau isingekuwa watu watakuwa kundi moja tungeliwajaalia wanaomkufuru Mwingi wa rehema nyumba zao zina dari ya fedha, na ngazi zao pia wanazopandia na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyoegemea juu yake na mapambo.

Yaani ngazi, milango na vitanda vyote vinatokana na madini ya fedha. Aya inamjibu anayesema kuwa ufukara hauendani na utume, eti kwa sababu ufukara ni hulka pungufu.

Ufupi wa jawabu ni kuwa dunia, mbele ya Mwenyezi Mungu, hailingani hata na bawa la mbu, na Akhera ni bora mbele ya Mola wako na ni yenye kubaki, lakini watu wanaathirika na dunia kuliko Akhera na wanakwenda nayo popote wanapoelekea. Lau si hivyo basi Mwenyezi Mungu angeliwapa makafiri nyumba zenye sakafu za fedha na pia milango, ngazi na samani. Na angeliwazidishia mapambo ya dunia kwa kuidharau. Mtaalamu mmoja alisema: “Watu wamepondokea dunia, lakini Mwenyezi Mungu hakulifanya hilo, je ingelikuwaje lau angelifanya. Aya hii inafahamisha kwamba Mwenyezi Mungu anawachukulia upole waja wake na kuwafanyia yale yatakayowakurubisha kwake na kuwaweka mbali na maasi. Kwa uchache kabisa ni kuwa hawafanyii yatakayowahadaa kwenye maasi.

Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu.

Yaani neema za dunia, kwa vyovyote itakavyokuwa basi itaisha tu. Katika Aya nyingine dunia imeitwa upuzi, mchezo na ghururi. Na Akhera iliyoko kwa Mola wako ni ya wenye takua ambao wamemfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu katika kauli zao na vitendo vyao.


19

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ ﴿٣٦﴾

36. Anayeifanyia upofu dhikri ya Mwingi wa rehema tutamwekea Shetani kuwa ndiye rafiki yake.

وَإِنَّهُمْ لَيَصُدُّونَهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٣٧﴾

37. Na hakika wao wanawazuilia njia na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka.

حَتَّىٰ إِذَا جَاءَنَا قَالَ يَا لَيْتَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ بُعْدَ الْمَشْرِقَيْنِ فَبِئْسَ الْقَرِينُ ﴿٣٨﴾

38. Hata atakapotujia atasema: Laiti ungelikuwako baina yangu na wewe umbali baina ya mashariki na magharibi. Ni urafiki mbaya ulioje?

وَلَن يَنفَعَكُمُ الْيَوْمَ إِذ ظَّلَمْتُمْ أَنَّكُمْ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na kwa kuwa mlidhulumu, haitawafaa leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu.

أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ أَوْ تَهْدِي الْعُمْيَ وَمَن كَانَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٤٠﴾

40. Je, unaweza kumsikilizisha kiziwi, au kumwongoza kipofu na aliyemo katika upotofu ulio wazi?

فَإِمَّا نَذْهَبَنَّ بِكَ فَإِنَّا مِنْهُم مُّنتَقِمُونَ ﴿٤١﴾

41. Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi kwao.

أَوْ نُرِيَنَّكَ الَّذِي وَعَدْنَاهُمْ فَإِنَّا عَلَيْهِم مُّقْتَدِرُونَ ﴿٤٢﴾

42. Au tutakuonyesha tuliowaahidi. Nasi bila ya shaka tuna uweza juu yao.

فَاسْتَمْسِكْ بِالَّذِي أُوحِيَ إِلَيْكَ إِنَّكَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٤٣﴾

43. Basi yashike uliyopewa. Hakika wewe uko kwenye Njia iliyonyooka.

وَإِنَّهُ لَذِكْرٌ لَّكَ وَلِقَوْمِكَ وَسَوْفَ تُسْأَلُونَ ﴿٤٤﴾

44. Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakujaulizwa.

وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ آلِهَةً يُعْبَدُونَ ﴿٤٥﴾

45. Na waulize Mitume wetu tuliowatuma kabla yako: Je, tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Mwingi wa rehma?.

JE, UNAWEZA KUWASIKILIZISHA VIZIWI

Aya 36 – 45

MAANA

Anayeifanyia upofu dhikri ya Mwingi wa rehema tutamwekea Shetani kuwa ndiye rafiki yake.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni mwadililifu na ni hakimu, hawezi kuwasilitia Shetani waja wake ili awadanganye kuwatia kwenye upotevu na uasi; kisha awaadhibu. Itakuwaje hivyo na hali Yeye ndiye aliyesema:

إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ ﴿٤٢﴾

“Hakika waja wangu hutakuwa na mamlaka nao, ispokuwa wale wapotofu waliokufuata.”

Juz. 14 (15:42).

Akasema tena:

وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ ﴿٤٦﴾

“Na Mola wako si mwenye kuwadhulumu waja.” Juz. 24 (41:46).

Kwa hiyo basi maana ya Aya yatakuwa ni mwenye kuitupilia mbali dini ya Mwenyezi Mungu na sharia yake, akafuata matamanio na starehe, Mwenyezi Mungu atamwachia nafsi yake yenye kuamrisha mno uovu na mashetani watu na majini, wamfanye vile watakavyo na kumwongoza kwenye maangamizi. Mwenyezi Mungu hamkatazi mtu mambo maovu kwa nguvu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 24 (41:25).

Na hakika wao wanawazuilia Njia.

Yaani hao mashetani wanawazulia watu njia ya uwongofu.

Na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka.

Mashetani wanawaongoza wafuasi wao kwenye upotevu na wafuasi wanadhani kuwa wako kwenye uwongofu kwa kuwafuata mashetani. Muovu zaidi katika watu ni yule anayefuata njia ya upotevu na mwenyewe anaitakidi kuwa yuko salama:

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا ﴿١٠٣﴾ الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا ﴿١٠٤﴾ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَلِقَائِهِ فَحَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَزْنًا ﴿١٠٥﴾

“Sema je, tuwaambie wale wenye hasara mno ya vitendo? Ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kuwa wanafanya kazi nzuri? Hao ndio ambao wamezikanusha ishara za Mwenyezi Mungu na kukutana naye. Kwa hiyo vitendo vyao vimepomoka; na wala siku ya Kiyama hatutawapa uzito wowote.” Juz. 16 (18:103-105).

Hata atakapotujia atasema: Laiti ungelikuwako baina yangu na wewe umbali baina ya mashariki na magharibi. Ni urafiki mbaya ulioje?

Yaani kesho mfuasi atamwambia mfuaswa: afadhali ningekuwa mbali sana na wewe, kulikoni urafiki huu mbaya:

إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ ﴿١٦٦﴾

“Pindi waliofuatwa watakapowakataa wale waliowafuata, na hali ya kuwa wamekwishaiona adhabu na kuwakatikia mafungamano.” Juz. 1 (2:166).

Na kwa kuwa mlidhulumu, haitawafaa leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu.

Wanaambiwa wafuasi. Maana ni kuwa duniani mtu akipata adhabu na akamuona mwenzake naye anapata adhabu ile basi huwa anapoa kidogo (kifo cha wengi ni arusi), lakini sivyo kwa adhabu ya akhera; inakuwa sawa tu, iwe kwa wafuasi au wafuaswa-kushirikiana kwao hakuwezi kuwapun-guzia chochote wala kuwanufaisha.

Je! Unaweza kumsikilizisha kiziwi, au kumwongoza kipofu na aliyemo katika upotofu ulio wazi?

Starehe zimepiga muhuri kwenye macho yao, nyoyo zao na masikio yao, wataionaje haki na kusikia maneno yao? Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:42), Juz. 20 (27:80) na Juz. 21 (21:52).

Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi kwao au tutakuonyesha tuliowaahidi. Nasi bila ya shaka tuna uweza juu yao.

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume kuhusiana na washirikina. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) hawaachi washirikina walivyo.

Ikiwa mtume atafariki kuelekea kwenye rehema ya Mola wake, kabla ya wao hawajasalimu amri, basi Mwenyezi Mungu atawaadhibu au ikiwa mtume yuko hai basi atampa ushindi juu yao na watanyenyekea amri yake watake wasitake.

Hiyo ilitokea hasa; pale mtume alipoiteka Makka na vigogo wake kusal- imu amri, baada ya kuwa wamemtoa huko kwa hofu na kujificha. Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:46), Juz. 13 (13:40) na Juz. 24 (24:77).

Basi yashike uliyopewa. Hakika wewe uko kwenye Njia iliyonyooka.

Shikamana na Qur’an ewe Muhammad, kwa sababu ni haki, na Mwenyezi Mungu yuko pamoja nawe kwa sababu uko kwenye njia yake iliyo ya sawa. Naye atakutoshea na wanaokufanyia istihzai na inadi.

Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako.

Yaani Qur’an ni heshima kwako na kwa waarabu, kwa sababu imewainua na ikaeneza utawala wao na lugha yao maghiribi mwa ardhi na mashariki yake; kama tulivyotaja katika Aya ya 4 kwenye Sura hii. Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 (21:10).

Na mtakujaulizwa nyinyi waarabu jinsi mlivyoitumia Qur’an; na nyinyi hivi leo mnaipuuza sana; ndio maana mmekua chakula cha kila mwenye tamaa.

Na waulize Mitume wetu tuliowatuma kabla yako: Je! Tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Mwingi wa rehma?

Waulize ewe Muhammad watu wa dini zilizotangulia na mitume kuwa je, wamewahi kumsikia Mtume yoyote aliyeruhusu ushirikina na kuhalisha kuabudiwa masanamu?

Ikiwa mitume wote walilingania Tawhid na kutupilia mbali ushirikina; kama alivyofanya Muhammad, basi kwanini mnanupiga vita mwito wake enyi washirikina?

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَقَالَ إِنِّي رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٦﴾

46. Na hakika tulimtuma Musa kwa Ishara zetu aende kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: Hakika mimi ni Mtume wa Mola wa walimwengu!

فَلَمَّا جَاءَهُم بِآيَاتِنَا إِذَا هُم مِّنْهَا يَضْحَكُونَ ﴿٤٧﴾

47. Lakini alipowajia na Ishara zetu wakaingia kuzicheka.

وَمَا نُرِيهِم مِّنْ آيَةٍ إِلَّا هِيَ أَكْبَرُ مِنْ أُخْتِهَا وَأَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٤٨﴾

48. Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyengineyo. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee.

وَقَالُوا يَا أَيُّهَ السَّاحِرُ ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ إِنَّنَا لَمُهْتَدُونَ ﴿٤٩﴾

49. Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako kwa ile ahadi aliyokuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka.

فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ ﴿٥٠﴾

50. Basi tulipowaondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi.

وَنَادَىٰ فِرْعَوْنُ فِي قَوْمِهِ قَالَ يَا قَوْمِ أَلَيْسَ لِي مُلْكُ مِصْرَ وَهَـٰذِهِ الْأَنْهَارُ تَجْرِي مِن تَحْتِي أَفَلَا تُبْصِرُونَ ﴿٥١﴾

51. Na Firauni alitangaza kwa watu wake, akisema: Enyi watu wangu! Kwani mimi sinao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu? Je, hamwoni?

أَمْ أَنَا خَيْرٌ مِّنْ هَـٰذَا الَّذِي هُوَ مَهِينٌ وَلَا يَكَادُ يُبِينُ ﴿٥٢﴾

52. Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi?

فَلَوْلَا أُلْقِيَ عَلَيْهِ أَسْوِرَةٌ مِّن ذَهَبٍ أَوْ جَاءَ مَعَهُ الْمَلَائِكَةُ مُقْتَرِنِينَ ﴿٥٣﴾

53. Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu, au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama?

فَاسْتَخَفَّ قَوْمَهُ فَأَطَاعُوهُ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ ﴿٥٤﴾

54. Basi aliwachezea watu wake, na wakamtii. Kwa hakika hao walikuwa watu mafasiki.

فَلَمَّا آسَفُونَا انتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٥٥﴾

55. Walipotukasirisha tuliwapatiliza tukawagharikisha wote.

فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِّلْآخِرِينَ ﴿٥٦﴾

56. Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye.

MUSA

Aya 46 – 56

MAANA

Na hakika tulimtuma Musa kwa Ishara zetu aende kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: Hakika mimi ni Mtume wa Mola wa walimwengu wote! Lakini alipowajia na Ishara zetu wakaingia kuzicheka.

Hii ni mara ya kumi na sita kukaririka kisa cha Musa(a.s ) , mbali na zile Aya alizotajwa. Tumekwishazungumzia kisa hiki, mara nyingine kwa ufafanuzi zaidi na mara nyingine kwa ujumla.

Katika Juz. 16 (20:9) tumetaja sababu za kukaririka. Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa Mwenyezi Mungu mtukufu amekirudia kisa cha Musa hapa kwa sababu vigogo wa kikuraishi walimtia ila Muhammad(s.a.w. w ) , ndio akabainisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwamba Yeye alimtuma Musa fukara kwa Firauni tajiri. Aya iliyotangulia inatilia nguvu hili.

Vyovyote iwavyo, maana ya Aya tuliyo nayo yako wazi. Kwa ufupi ni kuwa Mwenyezi Mungu alimtuma Musa kwa Firauni na watu wake na miujiza inayojulisha utume wake; kama vile fimbo na mkono mweupe, lakini wakamdharau yeye, mwito wake na miujiza yake.

Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyengineyo.

Makusudio ya ishara hapa ni adhabu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t):

فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الطُّوفَانَ وَالْجَرَادَ وَالْقُمَّلَ وَالضَّفَادِعَ وَالدَّمَ آيَاتٍ مُّفَصَّلَاتٍ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ ﴿١٣٣﴾

“Basi tukawapelekea tufani na nzige na chawa na vyura na damu kuwa ishara mbalimbali, lakini wakatakabari na wakawa watu wakosefu.” Juz. 9 (7:133).

Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee kutoka kwenye upotevu kwenda kwenye uongofu na kutoka kwenye ufisadi wa nchi hadi kwenye kuitengeneza, lakini ishara na maonyo hayakuwafuaa watu wasioona ispokuwa manufaa na chumo lao tu.

Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako kwa ile ahadi aliyokuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka.

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasimulia kuwa watu wa Firauni walimwita Musa mchawi, na katika Juz.9 (7:134) walimwita kwa jina lake. Sio mbali kuwa kuna wakati walimwambia kwa jina lake na wakati mwingine walimwambia kwa kumwita mchawi. Hili ni jambo la kawaida katika mabishano ya watu.

Basi tulipowaondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi.

Mwenyezi Mungu aliwakamata na adhabu kwa miaka, wakamtaka Musa awaombee kuondolewa adhabu na wakamwahidi kutubia, lakini waliivunja ahadi yao na wakaendelea na kufuru na upotevu baada ya kuondokewa na adhabu.

Na Firauni alitangaza kwa watu wake, akisema: Enyi watu wangu! Kwani mimi sinao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu? Je, hamwoni?

Chini yangu ni kinaya cha kuwa mito iko chini yake akiitumia vile atakavyo. Firauni anautolea dalili ukuu wake na cheo chake kwa mali na ardhi. Hii ndio hali iliyoenea kwa wengi kila wakati na kila mahali. Wenye mali hivi sasa ndio watawala kwenye nchi nyingi.

Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi?

Ni mnyonge eti kwa kuwa ni fukara na kutosema waziwazi ni kwa kuwa alikuwa ana kigugumizi, lakini Mwenyezi Mungu alikiondoa kwa dalili ya kauli yake Musa kumuomba Mola wake:

“Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu.” Na Mwenyezi Mungu naye akamjibu: “Hakika umepewa maombi yako ewe Musa!” Juz.16 (20:27,36). Na Firauni alimwita Musa kwa alivyokuwa si kwa alivyo.

Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu, au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama?

Yaani Malaika wawe wapambe wake; kama wanavyofanya viongozi kuwa na wapambe. Wafasiri wanasema kuwa ilikuwa ni desturi ya watu wa firauni wakimchagua kiongozi wao wanamvisha vikuku na mkufu wa dhahabu, kuwa ndio alama ya uongozi wake. Ndio maana Firauni akasema, atakuwaje Musa ni nabii na hali hana dhahabu mikononi mwake wala shingoni mwake. Lililompa ujasiri wa hilo ni ujinga wa watu wake, upotevu wao na udhaifu wa akili zao; kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t):

Basi aliwachezea watu wake, na wakamtii. Kwa hakika hao walikuwa watu mafasiki.

Mwaka uliopita nilimwita fundi wa umeme anirekebishie kwenye maktaba yangu. Basi alipoona vitabu vimetapakaa huku na huko, aliniambia: “Mke wangu ananichukia sana, nakuomba uniandikie dawa ya mapenzi.” Nikwambia mimi sijui fani hiyo. Akasema: “Kwa nini una vitabu vyote hivi?”

Walipotukasirisha kwa kumkadhibisha Mtume, kuvunja ahadi na kuendelea na ukafiri na upotevu,tuliwapatiliza tukawagharikisha wote, viongozi na wafuasi.

Kisha tukawafanya kuwa watangulizi wa motonina mfano kwa wa baadaye, wapate funzo na mawaidha wale watakaokuja baada yao.

Mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَقَوْمَ نُوحٍ لَّمَّا كَذَّبُوا الرُّسُلَ أَغْرَقْنَاهُمْ وَجَعَلْنَاهُمْ لِلنَّاسِ آيَةً ﴿٣٧﴾

“Na watu wa Nuh walipowakadhibisha Mitume, tuliwagharikisha na tukawafanya ni ishara kwa watu: Juz. 19 (25:37).


20

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ ﴿٥٧﴾

57. Na alipopigiwa mfano Mwana wa Maryam, watu wako waliupigia ukelele.

وَقَالُوا أَآلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ ﴿٥٨﴾

58. Wakasema: Miungu yetu kwani ni bora au Yeye? Hawakukupigia mfano huo ila kwa ubishi tu. Bali hao ni watu wagomvi!

إِنْ هُوَ إِلَّا عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَاهُ مَثَلًا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٥٩﴾

59. Hakuwa yeye Isa ila ni mja tuliyemneemesha na tukamfanya ni mfano kwa Wana wa Israili.

وَلَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَا مِنكُم مَّلَائِكَةً فِي الْأَرْضِ يَخْلُفُونَ ﴿٦٠﴾

60. Na tungelipenda tungeliwafanya badala yenu Malaika katika ardhi kuwa makhalifa.

وَإِنَّهُ لَعِلْمٌ لِّلسَّاعَةِ فَلَا تَمْتَرُنَّ بِهَا وَاتَّبِعُونِ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٦١﴾

61. Na kwa hakika hiyo ni elimu ya Saa. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo njia iliyonyooka.

وَلَا يَصُدَّنَّكُمُ الشَّيْطَانُ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٦٢﴾

62. Wala asiwazuie Shetani. Hakika yeye ni adui yenu wa dhahiri.

وَلَمَّا جَاءَ عِيسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ قَالَ قَدْ جِئْتُكُم بِالْحِكْمَةِ وَلِأُبَيِّنَ لَكُم بَعْضَ الَّذِي تَخْتَلِفُونَ فِيهِ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿٦٣﴾

63. Na alipokuja Isa na dalili zilizo wazi, alisema: Nimewajia na hikima, na ili niwaeleze baadhi ya yale mliyokhitalifiana. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnitii.

إِنَّ اللَّـهَ هُوَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٦٤﴾

64. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu, na Mola wenu. Basi Mwabuduni Yeye tu. Hii ndiyo njia iliyonyooka.

فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِن بَيْنِهِمْ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ عَذَابِ يَوْمٍ أَلِيمٍ ﴿٦٥﴾

65. Lakini makundi yalikhitalifiana wao kwa wao. Ole wao waliodhulumu kwa adhabu ya siku chungu.

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٦٦﴾

66. Hawangoji ila Saa iwajie ghafla na hali wao hawatambui?.

ALIPOPIGIWA MFANO MWANA WA MARYAM

Aya 57 – 66

MAANA

Na alipopigiwa mfano Mwana wa Maryam, watu wako waliupigia ukelele. Wakasema: Miungu yetu kwani ni bora au Yeye?

Anaambiwa Mtume(s.a.w. w ) . Wafasiri wamesema kuwa aliyempigia mfano mwana wa Maryam ni Abdallah bin Ziba’ara. Aya inaashiria tukio lililotokea baina ya Mtume(s.a.w. w ) na makafiri wa kikuraishi; kwa ufupi ni kama ifuatavyo:

Iliposhuka Aya: “Hakika nyinyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannam mtaifikia” Juz. 17 (21:98), makuraishi waliona vibaya sana, wakamwendea Abdallah bin Ziba’ara, kabla ya kusilimu, naye akamwambia Mtume: “Manaswara wanamwabudu Masih, ikiwa Masih atakuwa katika Moto sisi tutakuwa radhi kuwa miungu yetu iko pamoja naye kwa sababu yeye ni bora kuliko hiyo au hiyo siyo bora kuliko yeye” Makuraishi waliposikia walilipuka kwa makelele ili wamnyamazishe Mtume asiweze kujibu na watu wafikirie kuwa ameshindwa kujibu.”

Mapokezi mengine yanasema kuwa Mtume(s.a.w.w) alimwambia Bin Zab’ara: “Ni ujinga ulioje wako kutojua lugha ya watu wako? Hujui kuwa herufi ‘ma’ ni ya wasio na akili?” yaani ‘hayo mnayoyaabudu.’

Hawakukupigia mfano huo ila kwa ubishi tu.

Kukupinga kwako makuraishi kwa kumtolea mfano Masih sio kwa makusudio ya kuihakiksha haki na kuidhihirisha, isipokuwa ni kwa makusudio ya kuikimbia haki na kuvungavunga tu. Wao wanajua wazi kuwa makusudio ya hayo mnayoyaabudu ni masanamu yao hasa.

Bali hao ni watu wagomvi! Wanazidisha ugomvi na uhasama ili kulinda masilahi yao.

Hakuwa yeye Isa ila ni mja tuliyemneemesha na tukamfanya ni mfano kwa Wana wa Israili.

Isa ni mja katika waja wa Mwenyezi Mungu, aliyeneemeshwa kwa utume na kaumbwa bila ya baba, kama Adam, ili awe ni ishara kuwafahamisha Wana wa Israil uweza wa Mwenyezi Mungu na ukuu wake, waweze kuongoka na kuwa na takua. Lakini wao walizidi inadi na ujeuri, wakasema kuhusu Bwana Masih na mama yake mambo ambayo yanaweza kuitingisha Arshi.

Na tungelipenda tungeliwafanya badala yenu Malaika katika ardhi kuwa makhalifa.

Hili ni kemeo na karipio kwa washirikina. Maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu hana haja na nyinyi wala ibada yenu. Kama angelitaka anageliwaangamiza na mahala penu pakachukuliwa na Malaika watakomtakasa na kumsifu kwa sifa njema bila ya kumuasi na jambo lolote.

Mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَإِن تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُم ﴿٣٨﴾

“Na mkigeuka atawaleta watu wengine na hawatakuwa mfano wenu.” (47:38).

Na kwa hakika hiyo ni elimu ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo Njia iliyonyooka.

‘Hiyo’ ni hiyo Qur’an. Maana ni kuwa Qur’an inawaelimisha watu siku ya Kiyama na kuwapa uhakika wake na pia kuwahadharisha na vituko vyake; wala haifai kukitilia shaka. Na hii Qur’an ni njia ya Mwenyezi Mungu iliyonyooka. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ ﴿٩﴾

“Hakika hii Qur’an inaongoza kwenye yaliyonyooka kabisa.” 15 (17:9).

Iliyonyooka kabisa ndio hiyo njia iliyonyooka.

Unaweza kuuliza : kwanini isiwe hakika huyo, yaani Isa, kwa vile Isa ndiye aliyetajwa na Qur’an haikutajwa kwenye Aya?

Jibu : maudhui ya Aya ni mjadala kuhusiana na Isa, na masimulizi yake yamesimuliwa na Qur’an. Kwa hiyo kutajwa Bwana Masih ni kutajwa Qur’an. Hili linatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwenye Aya hiyo hiyo: “Hii ndiyo njia iliyonyooka” ambayo makusudio yake ni Qur’an kama tulivyoeleza. La kushangaza ni mfasiri mmoja aliyeirudisha dhamir kwa Isa na kufasiri njia iliyonyooka kuwa ni mwito wa Muhammad(s.a.w.w) na Qur’an.

Wala asiwazuie Shetani na haki na kuitumia. Hakika yeye ni adui yenu wa dhahiri.

Uadui wa wazi na chuki inamfanya awaghuri kwa mambo machafu. Mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم مِّنَ الْجَنَّةِ ﴿٢٧﴾

“Shetani asiwatie katika fitna, kama alivyowatoa wazazi wenu katika Bustani (Pepo).”

Juz. 8 (7:27).

Na alipokuja Isa na dalili zilizo wazi, alisema: Nimewajia na hikima, na ili niwaeleze baadhi ya yale mliyokhitalifiana. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnitii.

Makusudio ya dalili hapa ni miujiza inayofahamisha utume wa Isa; kama vile kuponesha upofu na ukoma. Na makusudio ya hikima ni elimu ya dini ya Mwenyezi Mungu na sharia yake.

Maana ni kuwa Isa, ambaye utume wake umethibiti kwa dalili wazi, aliwaambia Wana wa Israili: Nimewajia na hukumu zote za dini, kiitikadi na kisharia na kwazo mtamjua mwenye haki na mbatilifu, basi mcheni Mwenyezi Mungu mtaongoka.

Unaweza kuuliza : Kwa nini amesema baadhi ya mnayohitalifiana na asiseme yote?

Wamejibu kundi katika wafasiri kwamba Makusudio yake ni kuwa Isa(a.s) , kwa wasifu wake kama Mtume, huwa anawabainishia mambo ya dini tu, lakini haingilii mambo ya dunia.

Kuna riwaya ya maulama wa kisunni kutoka kwenye sahihi zao kwamba Mtume(s.a.w.w) amesema:“Nyinyi ni wajuzi zaidi wa mambo ya dunia yenu na mimi ni mjuzi zaidi wa mambo ya dini yenu.”

Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu, na Mola wenu. Basi mwabuduni Yeye tu. Hii ndiyo njia iliyonyooka.

‘Hii’ ni ishara ya Tawhid na kukataza shirki. Maana yako wazi, kama alivyosema Razi.

Lakini makundi yalikhitalifiana wao kwa wao. Ole wao waliodhulumu kwa adhabu ya siku chungu.

Makusudio ya makundi ni mayahudi na manaswara kwa upande mmoja, na manaswara wenyewe kwa upande wa pili. Mayahudi walisema kuwa Isa ni mtoto wa zina (mwanaharamu), wakipingana katika hilo na manaswara wote na waislamu wote. Na hao manaswara wenyewe nao walikhitalifiana, baada ya Masihi, makundi mbali mabli. Kuna waliosema Isa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wengine wakasema ni mwana wa Mungu na wengine wakasema kuwa yeye ni mungu hasa. Ametakata Mwenyezi Mungu na wanayomsifia.

Hawangoji ila Saa iwajie ghafla na hali wao hawatambui?

Hili ni karipio na kemeo kwa yule anayemfanya Isa kuwa ni Mungu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (12:107).

الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ ﴿٦٧﴾

67. Siku hiyo marafiki watakuwa maadui, wao kwa wao, isipokuwa wenye takua.

يَا عِبَادِ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ ﴿٦٨﴾

68. Enyi waja wangu! Leo hamtakuwa na khofu, wala hamtahuzunika.

الَّذِينَ آمَنُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا مُسْلِمِينَ ﴿٦٩﴾

69. Ambao waliziamini Ishara zetu na wakawa Waislamu.

ادْخُلُوا الْجَنَّةَ أَنتُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ تُحْبَرُونَ ﴿٧٠﴾

70. Ingieni kwenye Bustani (Pepo), nyinyi na wake zenu katika hali ya kufurahishwa.

يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ وَأَنتُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٧١﴾

71. Watapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; Na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda, na macho yanavifurahia. Na nyinyi mtakaa humo milele.

وَتِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٧٢﴾

72. Na hiyo ni Bustani (Pepo) mliyorithishwa kwa hayo mliyokuwa mkiyafanya.

لَكُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ كَثِيرَةٌ مِّنْهَا تَأْكُلُونَ ﴿٧٣﴾

73. Mnayo humo matunda mengi mtakayoyala.

إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ ﴿٧٤﴾

74. Hakika wakosefu watakaa milele katika adhabu ya Jahannamu.

لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ ﴿٧٥﴾

75. Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa.

وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا هُمُ الظَّالِمِينَ ﴿٧٦﴾

Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio waliokuwa madhalimu.

وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ قَالَ إِنَّكُم مَّاكِثُونَ ﴿٧٧﴾

77. Na watapiga kelele: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako! Atasema: Hakika nyinyi mtakaa humo humo!

لَقَدْ جِئْنَاكُم بِالْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَكُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ ﴿٧٨﴾

78. Kwa yakini tuliwaletea Haki, lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia Haki.

أَمْ أَبْرَمُوا أَمْرًا فَإِنَّا مُبْرِمُونَ ﴿٧٩﴾

79. Au wamekata shauri? Bali ni Sisi ndio tunaopitisha.

أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ ﴿٨٠﴾

80. Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong’ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika.

SIKU HIYO MARAFIKI WATAKUWA NI MAADUI

Aya 67 – 80

MAANA

Siku hiyo marafiki watakuwa maadui, wao kwa wao, isipokuwa wenye takua.

Makusudio ya maadui ni kukatika muungano; iwe ni kwa chuki na kulaaniana au bila chuki. Maana ni kuwa muungano wa mapenzi na urafiki uliokuwa duniani, baina ya watu, siku ya kiyama utaondoka na kukatika; ila ukiwa chimbuko lake ni udugu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kusaidiana kwenye twaa yake.

Kwani huo utadumu bila ya kuwa na kikomo, bali unazidi na kukua kila muda unavyorefuka, kwa sababu yaliyoko kwa ajili ya Mwenyezi Mungu yanazidi.

Zaidi ya hayo ni kwamba watu wa Peponi watakuwa ni familia moja, hata kama walikuwa wanatofautiana duniani: Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ إِخْوَانًا عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ ﴿٤٧﴾

“Na tutaondoa chuki iliyokuwamo vifuani mwao wawe ndugu, juu ya viti wakielekeana.”

Juz.14 (15:47).

Enyi waja wangu! Leo hamtakuwa na khofu, wala hamtahuzunika.

Hii ni amani ya Mwenyezi Mungu kesho kwa wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na wakawa na takua.

Ambao waliziamini Ishara zetu na wakawa Waislamu: Ingieni kwenye Bustani (Pepo), nyinyi na wake zenu katika hali ya kufurahishwa.

Huu ni ubainifu na tafsiri ya waja wa Mwenyezi Mungu na kwamba wao ni wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na wakanyenyekea twaa yake na malipo yao mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kuwaingiza Peponi pamoja na wake zao walio wema.

Maana ya ‘kufurahishwa’ ni kuwa thawabu zao haziishii kwenye amani na kukosa hofu tu; bali zinavuka hadi kwenye shangwe na furaha. Vile vileWatapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; sahani ni za chakula na vikombe ni vya kinywaji.

Na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda katika starehehe za kimaada na za kiroho,na macho yanavifurahia, katika mandhari mazuri.Na nyinyi mtakaa humo milele bila ya kuwa na mwisho.

Na hiyo ni Bustani (Pepo) mliyorithishwa kwa hayo mliyokuwa mkiyafanya. Pepo ni haki yenu enyi waumini mlioifanyia kazi; sawa na mirathi. Kwa sababu nyinyi mliifanyia kazi duniani.

Mnayo humo matunda mengi mtakayoyala. Chakula, kinywaji na matunda pia. Vinavyotamaniwa na nafsi havina idadi, kwa sababu matamanio ya nafsi hayana udhibiti. Vile vile ladha ya jicho.

Hakika wakosefu watakaa milele katika adhabu ya Jahannamu. Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja walioongoka, sasa anataja waliopotea na kwamba wao watakuwa katika adhabu ya daima wakiwa hawana matumaini yoyote ya kwisha wala kupungua.

Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio waliokuwa madhalimu.

Kwa sababu Allah (s.w.t) aliwahadharisha na kawaonya, lakini wakakataa isipokuwa kufuru.Na watapiga kelele waseme:Ewe Malika! Na atufishe Mola wako! Naye atasema: Hakika nyinyi mtakaa humo humo!

Watamuomba Malik, mtunzaji wa Moto, awaombee kwa Mwenyezi Mungu awape mauti, ili waepukane na adhabu. Naye Malik atawajibu kuwa hakuna kuokoka, nyinyi mtakua humo humo tu. Haya ndiyo mliyozifanyia nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkiyafanya.

Unaweza kuuliza : Mwenyezi Mungu (s.w.t), katika Aya iliyotangulia amewaelezea kuwa wao watakata tamaa hata ya kupunguziwa adhabu, sikwambii kukatika. Vipi hapa anawatolea habari kwamba wao watataka mauti ili waondokewe na adhabu? Hii inafahamisha matarajio ambayo yanapingana na kukata tamaa.

Jibu : Watu wa motoni watakuwa na hali ya kukata tamaa na mara nyingine kuwa na matumaini. Zaidi ya hayo inawezekana kuwa mwito wao kwa Malik ni kiasi cha kuelezea shida yao tu.

Kwa yakini tuliwaletea Haki, lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia Haki.

Wanaoipinga haki wako aina mbili: Kwanza, ni wale wanaopinga kwa kutoijua. Pili, ni wale wanaoipinga kwa vile inagongana na masilahi yao na matamanio. Aina hii ndio nyingi zaidi.

Kila atakayeingia motoni kesho atauingia kwa sababu aliipinga haki na kutoitumia, lakini wachache miongoni mwao watastahiki adhabu kwa vile wamezembea kuijua haki. Na wengi watastahiki adhabu kwa vile wameiacha kwa kuwa inagongana na matamanio yao; sio kwa kutoijua.

Au wamekata shauri? Bali ni Sisi ndio tunaopitisha.

Yaani hao makuraishi. Maana ni kuwa washirikina hawakufanya njama zozote kwa Mtume ila Mwenyezi Mungu huvunja njama zao; kama alivyowafanyia makuraishi, pale walipopanga njama ya kumuua mtume akiwa amelala kitandani mwake.

Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong’ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika.

Wao wanapanga njama kwa siri wakidhani kuwa hilo linafichika kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini Yeye anajua siri na yaliyofichika, naye haviongozi vitimbi vya wahaini.

قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ ﴿٨١﴾

81. Sema: Ingelikuwa Mwingi wa rehema ana mwana, basi mimi ningelikuwa wa kwanza kumwabudu.

سُبْحَانَ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿٨٢﴾

82. Ametakasika Mola wa mbingu na ardhi, Mola wa Arshi, na hayo wanayomsifia.

فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ ﴿٨٣﴾

83. Basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao wanayoahidiwa.

وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ ﴿٨٤﴾

84. Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hikima, Mwenye ujuzi.

وَتَبَارَكَ الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَعِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٨٥﴾

85. Na amekuwa na baraka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo kati yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa Na kwake Yeye mtarudishwa.

وَلَا يَمْلِكُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٨٦﴾

86. Wala hao wanoaomba badala yake Yeye hawana uweza wa uombezi, isipokuwa anayeshuhudia kwa haki, na wao wanajua.

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٨٧﴾

87. Na ukiwauliza ni nani aliyewaumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi wanageuzwa wapi?

وَقِيلِهِ يَا رَبِّ إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ قَوْمٌ لَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾

88. Na usemi wake ni: Ewe Mola wangu! Hakika hawa ni watu wasioamini.

فَاصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَامٌ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿٨٩﴾

89. Basi wasamehe, na uwaambie salama. Watakuja jua.

INGELIKUWA MWINGI WA REHEMA ANA MWANA

Aya 81 – 89

MAANA

Sema: Ingelikuwa Mwingi wa rehema ana mwana, basi mimi ningelikuwa wa kwanza kumwabudu.

Mwenye Majamaul-abayan, ameitajia Aya hii ktk njia tano na akarefusha maneno bila ya kuwa na haja ya kufanya hivyo, kwa sababu maana yako wazi nayo ni sema: ewe Muhammad(s.a.w. w ) kumwambia yule anayedai kuwa Mwenyezi Mungu ana mwana kwamba mimi nitakuwa na wewe lakini kwa sharti ya kunithibitishia dalili mkataa ya hilo.

Lakini hakuna dalili ya madai haya; bali kuna dali ya kinyume chake. Kwa hiyo mimi ni katika wanaompwekesha Mwenyezi Mungu kwa kuamini kuwa Mwenyezi Mungu hakuzaa wala hakuzaliwa.

Kwa ufupi ni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) alikufunga kukubali kwake na jambo lilio muhali. Hakuna mwenye shaka kuwa kuli- funga jambo na muhali ni sawa na muhali. Mfumo huu ni maarufu kwa maulama katika kujadiliana, na ni wa kumnyamazisha mbishi.

Ametakasika Mola wa mbingu na ardhi, Mola wa Arshi, na hayo wanayomsifia ya kumnasibishia mtoto na mshirika.Basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao wanayoahidiwa.

Makusudio ya porojo na kucheza ni kusema kuhusu Mwenyezi Mungu bila ya ujuzi. Siku yao ni Siku ya Kiyama.

Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hikima, Mwenye ujuzi.

Mwenyezi Mungu pekee ndiye muumba wa ulimwengu pamoja na ardhi yake na mbingu yake, ndiye mpangiliaji wake kwa ujuzi wake na hekima yake; hakuna yoyote asiyekuwa Yeye anayestahiki ibada.

Na amekuwa na baraka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama.

Kaulia yake ‘na viliomo kati yake’ inaashiria kuwa katika anga kuna vitu tusivyovijua uhakika wake, na hakuna anayejua Kiyama kitakuwa lini isipokuwa Mwenyezi Mungu tu.

Na kwake Yeye mtarudishwa kwa ajili ya hisabu na malipo.

Wala hao wanoaomba badala yake Yeye hawana uweza wa uombezi, isipokuwa anayeshuhudia kwa haki, na wao wanajua.

Wao wanaabudu masanamu kwa kudai kuwa yatawaombea kwa Mwenyezi Mungu. Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawaambia, hapana, hakuna anayeweza kuombea kwake isipokuwa yule anayemtamkia neno la Tawhid, akaliamini kwa ujuzi, na lazima anayeombewa awe anastahiki uombezi na msamaha

Na ukiwauliza ni nani aliyewaumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi wanageuzwa wapi?

Wao wanakubali kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Aliewaumba, lakini bado wanaacha kumwabudu na kuayendea masanamu. Umetangulia mfano wake katika Aya 9 ya sura hii tuliyo nayo.

Na usemi wake Mtume ni: Ewe Mola wangu! Hakika hawa ni watu wasioamini. Basi wasamehe, na uwaambie maneno ya salama. Watakuja jua.

Maana ni kuwa Mtume alimwambia Mola wake kuwa wale ulionituma kwao hawakuniitikia. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akamwambia usijali na upinzani wao, kwani mwisho ni wako sio wao. Makusudio ya salama hapa ni kama makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾

“Na wajinga wakiwasemesha husema: Salama” Juz. 19 (25:63).

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI NA TATU: SURAT AZ-ZUKHRUF


21

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

Sura Ya Arubaini Na Nne: Surat Ad-Dukhan. Imeshuka Makka. Ina Aya 59.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

حم ﴿١﴾

1. Haa Mim.

وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾

2. Naapa kwa Kitabu kinachobainisha.

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ ﴿٣﴾

3. Hakika tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni waonyaji.

فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ ﴿٤﴾

4. Katika huo hubainishwa kila jambo la hikima.

أَمْرًا مِّنْ عِندِنَا إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ ﴿٥﴾

5. Ni amri itokayo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.

رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٦﴾

6. Ni rehema itokayo kwa Mola wako. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ ﴿٧﴾

7. Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake, ikiwa nyinyi mna yakini.

لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿٨﴾

8. Yeye Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha - Mola wenu na Mola wa baba zenu wa mwanzo.

بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ يَلْعَبُونَ ﴿٩﴾

9. Lakini wao wamo katika shaka wakicheza.

TUMEITEREMSHA USIKU ULIOBARIKIWA

Aya 1 – 9

MAANA

Haa Mim.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1)

Naapa kwa Kitabu kinachobainisha. Hakika tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa.

Umebarikiwa kwa kuteremkiwa na Qur’an. Tukiunganisha Aya hii na ile isemayo:

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾

“Hakika tumeiteremsha katika usiku wa heshima (Laylatul-qadr.) (97:1)

Na pia ile isemayo:

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ ﴿١٨٥﴾

“Ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa ndani yake Qur’an.” Juz.2 (2:185),

Tukiunganisha Aya hizi tatu, tunapata maana kuwa usiku uliobarikiwa ni Laylatul-qadr, na kwamba uko ndani ya mwezi wa Ramadhani uliobarikiwa.

Katika Juz. 2 (2: 183-185), Tumesema kwamba mwanzo wa kushuka Qur’an ulikuwa kwenye Layaltul-qadr, sio kuwa ilishuka Qur’an yote usiku huo. Kwa maelezo zaidi rudia huko.

Hakika Sisi ni Waonyaji wa adhabu kali kwa atakayeasi na kufanya ufisadi katika ardhi. Onyo hili limekuja katika Qur’an iliyoteremshwa kwenye moyo wa Muhammad(s.a.w. w ) .

Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima. Ni amri itokayo kwetu.

Wafasiri wametofautiana kuhusu ‘jambo la hikima.’ wengi wameonelea ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anagawanyia waja wake riziki na muda wa kifo katika usiku huu. Pia anasamehe makosa mengi kwa anayemtaka.

Wengine wakasema kuwa Makusudio ya jambo la hikima ni ubainifu wa kila jambo la dini uliokuja katika Qur’an. Lakini ikumbukwe Mwenyezi Mungu amesema katika huu, na hakusema katika hii. Ubainifu zaidi utaku- ja katika Juz. 30 (97).

Hakika Sisi ndio wenye kutuma. Ni rehema itokayo kwa Mola wako.

Yaani Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad kuwa ni rehema kwa viumbe vyote; kama ilivyoelezwa katika Juz. 17 (21:107).

Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.

Anasikia kauli na anajua yaliyo kwenye nia.

Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake, ikiwa nyinyi mna yakini.

Mwenye akili akiuangalia ulimwengu kwa mtazamo safi na kutilia maanani, atashuhudia kwa ikhlasi na yakini kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mmiliki wa ulimwengu na vilivyomo ndani yake na kwambaYeye Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha.

Hakuna yeyote anayeleta uhai isipokuwa Yeye. Na muda ukifika hakuna kinachoweza kuusogeza mbali wala karibu.

Mola wenu na Mola wa baba zenu wa mwanzo . Vipi basi mnaabudu mizimu na kumtii shetani badala ya Mwenyezi Mungu?

Lakini wao wamo katika shaka wakicheza.

Wametia shaka ya kutumwa Muhammad(s.a.w. w ) pamoja na dalili na ubainifu na wanafanya mchezo na mwisho wao na yale wanayotakiwa kuyafanya.

فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ ﴿١٠﴾

10. Basi ingoje siku ambayo mbingu italeta moshi ulio dhahiri.

يَغْشَى النَّاسَ هَـٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١١﴾

11. Utakaowafunika watu. Hii ni adhabu chungu!

رَّبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ ﴿١٢﴾

12. Mola wetu! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.

أَنَّىٰ لَهُمُ الذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مُّبِينٌ ﴿١٣﴾

13. Kutafaa nini kukumbuka kwao? Na alikwishawafikia Mtume mwenye kubainisha.

ثُمَّ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَقَالُوا مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ ﴿١٤﴾

14. Kisha wakamgeuzia uso, na wakasema: Amefunzwa, mwenda wazimu.

إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا إِنَّكُمْ عَائِدُونَ ﴿١٥﴾

15. Hakika tutaiondoa adhabu kidogo, (lakini) nyinyi kwa yakini mtarudia.

يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَىٰ إِنَّا مُنتَقِمُونَ ﴿١٦﴾

16. Siku tutakayowashika kwa mashiko makubwa, hakika sisi ni wenye kutesa.

وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَاءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ ﴿١٧﴾

17. Na hakika kabla yao tuliwajaribu watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.

أَنْ أَدُّوا إِلَيَّ عِبَادَ اللَّـهِ إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٨﴾

18. Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume mwaminifu.

وَأَن لَّا تَعْلُوا عَلَى اللَّـهِ إِنِّي آتِيكُم بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿١٩﴾

19. Na msijitukuze mbele ya Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitawaletea uthibitisho ulio wazi.

وَإِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمْ أَن تَرْجُمُونِ ﴿٢٠﴾

20. Nami najikinga kwa Mola wangu na Mola wenu, ili msinirujumu.

وَإِن لَّمْ تُؤْمِنُوا لِي فَاعْتَزِلُونِ ﴿٢١﴾

21. Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.

SIKU AMBAYO MBINGU ITALETA MOSHI

Aya 10 – 21

MAANA

Basi ingoje siku ambayo mbingu italeta moshi ulio dhahiri, utakaowafunika watu.

Maneno yanatoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Nabii wake mtukufu Muhammad(s.a.w. w ) akimwahidi kumkubalia dua yake. Hiyo ni baada ya Makuraishi kuzidi sana kumuudhi Mtume(s.a.w. w ) . Akawaombea dua mbaya, akasema:“Ewe Mola wangu wafanyie miaka kama ya Yusuf.” Basi mvua ikakatika na ardhi ikawa kame, makuraishi wakapatwa na njaa mpaka wakawa wanakula mifupa na mizoga. Kutokana na njaa mtu alikuwa akiona kama moshi mbinguni.

Wakasema: Hii ni adhabu chungu! Mola wetu! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.

Walimjia Mtume(s.a.w. w ) na kumwambia: Muombe Mwenyezi Mungu (s.w.t) atuondolee adhabu hii na sisi tutaamini risala yako.

Kutafaa nini kukumbuka kwao? Na alikwishawafikia Mtume mwenye kubainisha. Kisha wakamgeuzia uso, na wakasema: Amefunzwa, mwendawazimu.

Walitoa ahadi ya kuwaidhika na kukumbuka kama Mwenyezi Mungu atawaondolea adhabu, lakini wao hawatubii wala hawatekelezi ahadi. Kwani hawakushuhudia dalili za Tawhid, lakini pamoja na hayo wakamshirikisha Mwenyezi Mungu? Je, hakuwajia Mtume na hoja zilizo wazi wakamkadhibisha? Wakasema ni mwendawazimu, anafundishwa baadhi ya matamshi na jinni au mtu, kisha anakuja kutusomea?

Hakika tutaiondoa adhabu kidogo, (lakini)nyinyi kwa yakini mtarudia.

Makusudio ya adhabu hapa ni adhabu ya kahati na njaa. Kurudia, ni kuvunja ahadi kwa kurudia makosa. Maana ni kuwa tutawaondolea shida waliyo nayo, katika baadhi ya wakati, lakini sisi tunajua wazi kuwa watavunja ahadi. Lakini hiyo ni katika upande wa kutimiza na kuondoa visababu.

Siku tutakayowashika kwa mashiko makubwa, hakika sisi ni wenye kutesa.

Hili ni tishio kuwa Mwenyezi Mungu siku ya kiyama atawashika kwa adhabu ya kufedhehesha kutokana na uasi na jeuri yao.

Kwa ufupi ni kuwa makuraishi walimuudhi Nabii(s.a.w. w ) , naye akawombea dua mbaya. Ilipowapata shida walimkimbilia Mtume na kumwahidi kutubia, lakini walivunja ahadi baada ya kupata faraja, ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawatishia kwa Jahannam na makazi mabaya.

Na hakika kabla yao tuliwajaribu watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.

Yaani kabla ya makuraishi. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu aliwapa mtihani watu wa Firauni kwa neema na kumakinishwa katika ardhi; kama walivyopewa mtihani makuraishi kwa kuondolewa adhabu. Mwenyezi Mungu alimtuma Musa kwa watu wa Firauni; kama alivyomtuma Muhammad kwa makuraishi. Wote wakaasi amri ya Mwenyezi Mungu.

Na Musa akamwambia Firauni na watu wake:Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume mwaminifu.

Firauni alikuwa akiwakandamiza wana wa Israil kwa kuwachinja watoto wa kiume na kuwabakisha wa kike kwa ajili ya utumishi. Kwa hiyo Musa akamtaka Firauni amwachie ili aende nao anapotaka. Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

فَأَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَا تُعَذِّبْهُمْ ﴿٤٧﴾

“Basi tuwachie wana wa Israil wala usiwaadhibu.” Juz. 16 (20:47).

Na msijitukuze mbele ya Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitawaletea uthibitisho ulio wazi.

Haya ni maneno ya Musa kwa watu wa Firauni. Maana ni kuwa msijiweke juu ya twaa ya Mwenyezi Mungu, kwani mimi nina hoja za kutosha za kuthibitisha haki.

Nami najikinga kwa Mola wangu na Mola wenu, ili msinirujumu.

Najilinda na ninakimbilia kwake ikiwa mtanikusudia ubaya.

Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami. Achaneni na mimi, kama hamtaki kunisadiki na kuitikia mwito wangu.

فَدَعَا رَبَّهُ أَنَّ هَـٰؤُلَاءِ قَوْمٌ مُّجْرِمُونَ ﴿٢٢﴾

22. Ndipo akamwomba Mola wake kuwa watu hawa ni wakosefu.

فَأَسْرِ بِعِبَادِي لَيْلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ ﴿٢٣﴾

23. Basi nenda na waja wangu usiku. Hakika mtafuatwa.

وَاتْرُكِ الْبَحْرَ رَهْوًا إِنَّهُمْ جُندٌ مُّغْرَقُونَ ﴿٢٤﴾

24. Na iache bahari imetulia, hakika wao ni jeshi litakalozamishwa.

كَمْ تَرَكُوا مِن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿٢٥﴾

25. Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha!

وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ ﴿٢٦﴾

26. Na mimea na mahala pa fahari!

وَنَعْمَةٍ كَانُوا فِيهَا فَاكِهِينَ ﴿٢٧﴾

27. Na neema walizokuwa wakijistareheshea!

كَذَٰلِكَ وَأَوْرَثْنَاهَا قَوْمًا آخَرِينَ ﴿٢٨﴾

28. Ndivyo hivyo! na tukawarithisha haya watu wengine.

فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ ﴿٢٩﴾

29. Mbingu na ardhi hazikuwalilia; wala hawakupewa muda.

وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنَ الْعَذَابِ الْمُهِينِ ﴿٣٠﴾

30. Na hakika tuliwaokoa wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha.

مِن فِرْعَوْنَ إِنَّهُ كَانَ عَالِيًا مِّنَ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾

31. Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupituka mipaka.

وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٣٢﴾

32. Na hakika tuliwachagua kwa ujuzi kuliko walimwengu wengine.

وَآتَيْنَاهُم مِّنَ الْآيَاتِ مَا فِيهِ بَلَاءٌ مُّبِينٌ ﴿٣٣﴾

33. Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi.

WATU HAWA NI WAKOSEFU

Aya 22 – 33

MAANA

Ndipo akamwomba Mola wake kuwa watu hawa ni wakosefu.

Musa alikata tamaa na Firauni na watu wake, ndipo akawaombea mabaya na akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu waharakishie maangamizi duniani kwa sababu ya kufuru yao.” Mwenyezi Mungu akamwitikia dua yake na kumwambia:Basi nenda na waja wangu usiku. Hakika mtafuatwa.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwamrisha atoke Misri yeye na wana wa Israil usiku na akamjulisha kuwa Firauni na watu wake watawafuata.

Na iache bahari imetulia, hakika wao ni jeshi litakalozamishwa.

Fuata njia ya baharini, ukishavuka upande wa pili, wewe iwache kama ilivyo, kwa sababu jeshi la adui litaingia na wataangamia wote.

Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha! Na mimea na mahala pa fahari! Na neema walizokuwa wakijistareheshea! Ndivyo hivyo! na tukawarithisha haya watu wengine.

Watu wa Firauni walikuwa katika starehe za vyakula na vinywaji, wana utawala, makasri, mito na matunda. Mwenyezi Mungu akawatumia Musa kuwalingania kwenye uadilifu na kuacha ufisadi katika nchi, lakini hawakumwitikia mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu. Basi akawaangamiza na akawarithisha watu ambao hawakuwa na uhusiano wowote na wao.

Sheikh Al-Maraghi anasema akifasiri Aya hii: “Wakati fulani wasyria walichukua Misr na wakati mwingine ikachukuliwa na wababilon na pia wahabeshi. Kisha wafursi, wayunani (wagiriki), waroma, na waarabu. Vile vile utawala wa Altoulenion, Alikhchidip, Fatimid, Ayyubids, Mamluk, Uturuki, Ufaransa na Uingereza. Na sisi hivi sasa tunapigana ili kuwatoa katika nchi yetu ili tuweze kumakinika na uhuru wa chi yetu.”

Sheikh huyu alikuwa katika zama za mfalme Faruk Bin Fuad. Nasi tunaunganisha maneno yake kwa kusema: Hivi sasa Uzayuni umepora Sinai na ukanda wa mashariki katika mfereji wa Suez, kwa msaada U.S.A. kambi mpya ya ukoloni.

Na wamisri wanajitahidi na kupigana kuwatoa wavamizi kwenye ardhi yao. Haya ndio maisha ya jihadi na mapigano. Mtu kufa na bunduki mkononi akipigania nchi yake na heshima yake ni bora zaidi kuliko kuishi maisha ya udhalili na utwevu.

Mbingu na ardhi hazikuwalilia.

Hiki ni kinaya cha kutowapa umuhimu watu wa Firauni pale Mwenyezi Mungu alipowagharikisha baharini,wala hawakupewa muda; bali Mwenyezi Mungu aliharakisha maangamizi yao duniani.

Na hakika tuliwaokoa wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha ambayo ni kuuawa watoto wao wa kiume na kutumikishwa wanawake wao na mabinti zao na pia kudhalilishwa wanaume kwa kazi za sulubu

Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupituka mipakaya kila ufisadi, uasi na kiburi. Na hakika tuliwachagua kwa ujuzi kuliko walimwengu wengine.

Mwenyezi Mungu (s.w.t), katika Kitabu chake, amewasifu kwa sifa mbaya wana wa Israil, akasajili

makosa makubwa waliyoyafanya; kama vile usaliti, kuifanyia jeuri haki na kula mali kwa dhulma.

Vile vile amewasifu kwa ukafiri, dhulma na akawalaani katika Aya kadhaa na kuwatishia kwa adhabu kali.

Kwa maana hii ndio wafasiri wakakongamana kuwa makusudio ya walimwengu, katika Aya hii na mfano wake, ni walimwengu wa zama zao si kila zama.

Katika Juz. 1 (2:47-48) tulisema kuwa Mwenyezi Mungu aliwafadhilisha juu ya watu wa zama hizo kwa vile tu Mwenyezi Mungu aliwatuma mitume wengi kutokana na wao. Hivi sasa tumepata wazo kutokana na Aya tuliyo nayo kuwa makusudio ya walimengu ni Firauni na wale walioukubali uungu wake na wala sio watu wote wa wakati ule. Siri ya kufadhilishwa huko ni kuwa waisrail hawakumwabudu Firauni kama wamisri waliotangulia.

Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi.

Makusudio ya ishara hapa ni miujiza; kama kupasuka bahari, kufunikwa na kiwingu, kuteremshiwa Manna na Salwa na kububujika maji kutoka kwenye jiwe. Na Makusudio ya majaribio ni neema. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

وَنَبْلُوكُم بِالشَّرِّ وَالْخَيْرِ فِتْنَةً وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ ﴿٣٥﴾

“Na tutawajaribu kwa mtihani wa shari na heri na kwetu mtarejeshwa.” Juz. 17 (21:35).


22

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَيَقُولُونَ ﴿٣٤﴾

34. Hakika hawa wanasema:

إِنْ هِيَ إِلَّا مَوْتَتُنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ ﴿٣٥﴾

35. Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatu- fufuliwi.

فَأْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣٦﴾

36. Basi warudisheni baba zetu, ikiwa mnasema kweli.

أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ أَهْلَكْنَاهُمْ إِنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ ﴿٣٧﴾

37. Je, wao ni bora au watu wa Tubbaa’ na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.

وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ ﴿٣٨﴾

38. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake kwa mchezo.

مَا خَلَقْنَاهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٩﴾

39. Hatukuviumba ila kwa haki. Lakini wengi wao hawajui.

إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ مِيقَاتُهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٤٠﴾

40. Hakika siku ya Upambanuzi ni wakati uliowekwa kwa wao wote.

يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٤١﴾

41. Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.

إِلَّا مَن رَّحِمَ اللَّـهُ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٤٢﴾

42. Isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu atamrehemu Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.

JE, WAO NI BORA AU WATU WA TUBBAA’

Aya 34 – 42

MAANA

Hakika hawa wanasema: Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.

‘Hawa’ ni ishara ya washirikina wa Makka, walisema hakuna uhai wala ufufuo baada ya mauti na wakatoa hoja kwa kusema:Basi warudisheni baba zetu, ikiwa mnasema kweli. Wao hawaamini kuwa Mwenyezi Mungu anaweza kuwafufua wafu ila wakiona hilo kwa macho; wakasahau umbile la kwanza, kwamba yule aliyeleta mwanadamu, aliyekuwa hayuko, ndiye huyo huyo mwenye uweza wa kufufua mifupa iliyosagika.

Je, wao ni bora au watu wa Tubbaa’ na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.

Watubba’ walikuwa na dola yenye nguvu katika Yemen, na walikuwa na mali na hali nzuri zaidi kuliko makuraishi. Walipoasi amri ya Mola wao, Mwenyezi Mungu aliwakamata na akawaangamiza; kama alivyowaangamiza watu wa Nuh, A’d na Thamud kutokana na kufuru na ufisadi. Lau wangelizingatia wangeliona na wakaamini, lakini wao ni watu wasiofahamu.

Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo kati yake kwa mchezo. Hatukuviumba ila kwa haki.

Mwenyezi Mungu ni mwenye hikima na mwenye hikima hawezi kufanaya mchezo. Kwa hiyo haumbi kitu ila kwa masilahi yanayorudia kuumba. Lengo la kuumbwa mtu ni kuishi maisha mema ya milele yasiyokuwa na mwisho. Kwa hiyo basi hakuna budi kuweko na ufufuo; vinginevyo itakuwa kuumbwa mtu ni kwa mchezo tu. Tazama Juz. 21 (31:33-34) kifungu cha: ‘Kwa nini Mungu akamuumba mtu?’

Lakini wengi wao hawajui kwamba Mwenyezi Mungu ameumba ulimwengu na vilivyomo ndani yake kwa hikima na malengo sahihi.

Hakika siku ya Upambanuzi ni wakati uliowekwa kwa wao wote.

Siku ya upambanuzi ni siku ya Kiyama ambayo Mwenyezi Mungu atawakusanya watu wote kwa ajili ya kuangalia hisabu na malipo. Kuwekewa wakati kwa wote ni ahadi ya huko kukusanywa kwa hisabu na malipo.

Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.

Si cheo, mali, nasabu, urafiki wala chochote kitakachoweza kufaa siku hiyo, isipokuwa matendo mema. Hayo peke yake ndiyo yatakayoweza kusaidia mbele ya Mwenyezi Mungu.

Isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu atamrehemu, lakini Mwenyezi Mungu atamrehemu yule anayestahiki kurehemiwa; kama yule mwenye vitangulizi vya kumkurubisha kwa muumba wake.

Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. Hakuna mwenye kunusuru wala kurehemu kesho isipokuwa Mwenyezi Mungu. Yeye ni mwenye nguvu na rehema, viumbe wananyenyekea nguvu yake na wanahitajia rehema yake.

إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ ﴿٤٣﴾

43. Hakika Mti wa Zaqqum.

طَعَامُ الْأَثِيمِ ﴿٤٤﴾

44. Ni chakula cha mwenye dhambi.

كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ ﴿٤٥﴾

45. Kama mafuta mazito, hutokota matumboni,

كَغَلْيِ الْحَمِيمِ ﴿٤٦﴾

46. Kama kutokota kwa maji ya moto.

خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَاءِ الْجَحِيمِ ﴿٤٧﴾

47. Mkamateni na mburuzeni mpaka katikati ya Jahannamu!

ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ ﴿٤٨﴾

48. Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayochemka.

ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ ﴿٤٩﴾

49. Onja! Hakika wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!

إِنَّ هَـٰذَا مَا كُنتُم بِهِ تَمْتَرُونَ ﴿٥٠﴾

50. Hakika haya ndiyo mliyokuwa mkiyatilia shaka.

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ ﴿٥١﴾

51. Hakika wenye takua watakuwa katika mahali pa amani.

فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿٥٢﴾

52. Katika mabustani na chem-chem.

يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَابِلِينَ ﴿٥٣﴾

Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana.

كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ ﴿٥٤﴾

54. Ndio kama hivyo! na tutawaoza mahurilaini

يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ ﴿٥٥﴾

55. Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani.

لَا يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلَّا الْمَوْتَةَ الْأُولَىٰ وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ ﴿٥٦﴾

56. Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na atawalinda na adhabu ya Jahannamu.

فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿٥٧﴾

57. Ni fadhila zitokazo kwa Mola wako. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٥٨﴾

58. Basi tumeifanya nyepesi hii kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka.

فَارْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ ﴿٥٩﴾

59. Basi ngoja tu, na wao wanangoja.

CHAKULA CHA MWENYE DHAMBI NA CHA MWENYE TAKUA

Aya 43 – 59

MAANA

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwataja wakosefu, katika Aya iliyotangulia, na kwamba ahadi yao ni siku ya Kiyama, sasa anataja hali yao itakavyokuwa, kama ifuatavyo:

Hakika Mti wa Zaqqum, Ni chakula cha mwenye dhambi, ambaye dhambi zake na makosa yake yalikithiri duniani. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameyasifu matunda ya mti huu kuwa ni kama mafuta mazito, hutokota matumboni kama kutokota kwa maji ya moto.

Sio mbali kuwa hiki ni kinaya cha uchungu wa adhabu na ukali wake. Mulla Sadra anasema katika Al-asfar: Mti wa Zaqqum ni itikadi za ubatilifu na tabia mbaya zinazompeleka mtu kwenye moto. Baadhi ya mapokezi yanaeleza kuwa ubakhili ni mti miongoni mwa miti ya Motoni na ukarimu ni mti miongoni mwa miti ya Peponi.

Mkamateni na mburuzeni mpaka katikati ya Jahannamu!

Yaani wataambiwa Malaika wa motoni mburuzeni hadi katikati ya Jahannam,kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayochemka.

Hii inaashiria kuwa kwenye Jahannam kuna matunda, hamamu na mavazi, lakini yote yanatokana na moto.

Onja! Hakika wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu! Hakika haya ndiyo mliyokuwa mkiyatilia shaka.

Malaika wa adhabu watamwambia taghuti mwenye dhambi: wewe ulipinga siku ya ufufuo na ukadai kuwa ni mkubwa na mtukufu, basi hivi sasa onja malipo ya kujitukuza kwako na kiburi chako.

Kadiri ninavyotia shaka, lakini siwezi kutia shaka yoyote kuwa wale wanaopora mali za watu na kuzitengenezea silaha za maangamizi kwa ajili ya kuwaua wasiokuwa na hatia, wakiwemo wanawake na watoto, na wala wasione haki wala uadilifu isipokuwa yale wanayoyataka na kuyatamani, sitii shaka kabisa kwamba hawa wanastahiki aina hii ya adhabu; bali wanastahiki zaidi ya adhabu hii kama ingeliokuwako. Tazama Juz. 13 (14:46-52), kifungu cha ‘Jahannam na silaha za maangamizi.’

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kubainisha hali za wakosefu, sasa anaashiria hali za wenye takua siku ya Kiyama, kwa Aya zinazofuatia:

Hakika wenye takua watakuwa katika mahali pa amani, hawatakuwa na hofu wala kuhuzunika. Katika mabustani na chemchem, wakistarehe kadiri watakavyo.

Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana.

Nguo zao ni hariri laini na nzito na watakaa kwenye viti wakielekeana wao kwa wao, wakibarizi huku wanashukuru kwa kukumbuka neema ya Mwenyezi Mungu na radhi zake.

Ndio kama hivyo! na tutawaoza mahurulaini, ambao hajawagusa mtu kabla yao wala jinni.

Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani.

Watataka matunda bila ya kuhofia kuwa yataisha.

Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na Mwenyezi Munguatawalinda na adhabu ya Jahannamu.

Kila mtu atakufa mauti ya kwanza na baadae ataguria Peponi au Motoni, hakuna kufa huko, lakini kufa ni bora sana kuliko uhai katikati ya Jahannam.

Ni fadhila zitokazo kwa Mola wako. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Kuna kufuzu gani kukubwa zaidi ya kuokoka na adhabu ya moto na ghad- habu ya Mwenyezi Mungu?

Basi tumeifanya nyepesi hii kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka.

Iliyofanywa nyepesi ni Qur’an. Wanaotakiwa kukumbuka ni waarabu na ulimi ni wa Mtume. Maana ni kuwa tumeiteremsha Qur’an kwa kiarabu ili waarabu wanufaike na mafunzo yake na mawaidha.

Basi ngoja tu, na wao wanangoja.

Ngoja kidogo ewe Muhammad, utaona mwisho utakuwa wako. Wao wanakuduia ufikwe na mabaya, lakini: “Ameaangamia mwenye kuduia na amerudi utupu mwenye kuzua na mwenye kuigeukia haki ameangamia,” kama anavyosema Imam Ali.(a.s) .

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI NA NNE: SURAT AD-DUKHAN


23

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

Sura Ya Arubaini Na Tano: Surat Al-Jaathiya, Pia inaitwa Sura ya Sharia. Imeshuka Makka. Ina Aya 37.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

حم ﴿١﴾

1. Haa mim.

تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ﴿٢﴾

2. Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

إِنَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٣﴾

3. Hakika katika mbingu na ardhi kuna Ishara kwa Waumini.

وَفِي خَلْقِكُمْ وَمَا يَبُثُّ مِن دَابَّةٍ آيَاتٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿٤﴾

4. Na katika umbo lenu na katika wanyama aliowatawanya zimo ishara kwa watu wenye yakini.

وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن رِّزْقٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ آيَاتٌ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٥﴾

5. Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayoiteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake. Na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili.

تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَ اللَّـهِ وَآيَاتِهِ يُؤْمِنُونَ ﴿٦﴾

6. Hizo ni Ishara za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki Basi hadithi gani watakayoiamini baada ya Mwenyezi Mungu na Ishara zake?

KATIKA MBINGU NA ARDHI KUNA ISHARA KWA WAUMINI

Aya 1 – 6

MAANA

Haa miim.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1).

Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Makusudio ya kitabu ni Qur’an, na yote kuanzia mwanzo wake hadi mwisho wake ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu si kwa mwenginewe. Mwenye Ruhul-bayan anasema: “Wasifu wa Mwenyezi Mungu kuwa Mwenye nguvu, hapa unafahamisha kuwa Qur’an ni muujiza unaomshinda nguvu kila mwenye kuipinga. Na wasifu wake kuwa ni mwenye hikima unajulisha kuwa Qur’an ina hikima ya hali ya juu yenye kunufaisha. Hakuna mwenye shaka kuwa Qur’an ni muujiza unaomshinda kila mwenye kupingana nayo na kwamba hiyo ni chimbuko la hekima na kianzio chake.”

Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akaishiria kwenye dalili ya hisia zinazotamka kuweko kwake na utukufu wake; miongoni mwazo ni:

Hakika katika mbingu na ardhi kuna Ishara kwa waumini.

Yaani kwa anayetaka kuamini haki kwa kuwa ni haki. Makusudio ya Ishara hapa ni yale yanayovumbuliwa na akili kama vile nidhamu ya ulimwengu na sera yake kwenye desturi isiyokuwa na mabadiliko wala mageuzi. Lau si uthabiti wake isingeliwezekana kuipima na kufaidika nayo; hatimae ilimu ya sayari isingelikuwa na athari yoyote.

Na katika umbo lenu na katika wanyama aliowatawanya zimo ishara kwa watu wenye yakini.

Mwenye kutaka kujua kwa yakini kuweko Mwenyezi Mungu, naafikirie na kujitaamali yeye mwenyewe na katika kila kilicho na uhai, je, atapata kiungo hata kimoja kisicho na kazi au silika yoyote isiyokuwa na hikima?

Hii inafahamisha kwa dalili mkataa ya kuweko utashi na azma, ikiwa hatumuoni huyo mwenye utashi na azma basi tunaona athari yake kwa macho kabisa, kwa hiyo basi imani yetu kwa mambo ya ghaibu inategemea hisia na kuona.

Na kupishana usiku na mchana.

Mara nyingi Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameashiria kuhitalifiana usiku na mchana ili kuizindua akili kwenye siri za ajabu katika mzunguko wa ardhi, kwa vile ndio sababu ya kuja usiku baada ya mchana.

Yote yaliyosemwa kuhusu sababu za mzunguko wa ardhi hiyo yenyewe au kando ya jua na sababu nyinginezo, zote zinaishia kwenye matakwa ya muumbaji wa kwanza na uwezo wake na hekima yake. Ni jambo lisiloingilika akilini kuwa chimbuko la maajabu yote haya liwe ni mada pofu inayohukumiwa na sadfa, bila ya mpangilio, wala makusdio au lengo!

Na riziki anayoiteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake.

Makusudio ya riziki hapa ni kila kitu chenye athari katika uhai; kama vile maji na joto la jua nk. Ambayo ndani yake kuna ufahamisho wa kuweko muumba wa viliomo mbinguni na katika ardhi. Kwa sababu vyote hivyo vimepatikana kwa lengo na hekima iliyo sahihi.

Na mabadiliko ya upepo, kusi na kaskazi, matlai na umande na joto na baridini Ishara kwa watu wenye akili.

Yote hayo na mengineyo ni dalili mkataa ya utashi wa mwenye ujuzi na hikima

Hizo ni Ishara za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki.

Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoweka mbele ya akili ushahidi na dalili za hisia za kumjua muumba na uweza wake.

Basi hadithi gani watakayoiamini baada ya Mwenyezi Mungu na Ishara zake?

Ambaye hakunufaika na ubainifu wa Mwenyezi Mungu na kutokinai na dalili zake basi hakuna hoja yoyote itakayomfaa. Maana ya Aya hii yamekaririka mara nyingi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu; miongoni mwazo ni ile iliyo katika Juz. 2 (2:164).

Katika Nahjul-balagha kuna maelezo haya: “Katika kuumba kwake, kikubwa, kidogo, kizito, chenye nguvu na hafifu, ni sawa tu. Vile vile mbingu hewa, upepo na maji. Hebu angalia jua, mwezi, mimea, miti, maji, na jiwe. Pia kupishana huu usiku na mchana, kububujika hizi bahari, kukithiri milima, urefu wa vilele hivi na kutofautiana lugha na lahaja. Ole wake mwenye kumkataa mkadiriaji na akamkana mpangiliaji. Wanajifikiria ni kama mimea isiyokuwa na mkulima wala kuwa kutofautiana sura zao kusiwe na mtengenezaji. Hawana hoja na wanayodai wala uhakiki kwa waliyoyasikia. Je, jengo linaweza kuwa bila ya fundi? Au hatia bila ya kuweko mkosaji?”

وَيْلٌ لِّكُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ ﴿٧﴾

7. Ole wakekila mtunga uongo mwenye dhambi!

يَسْمَعُ آيَاتِ اللَّـهِ تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ثُمَّ يُصِرُّ مُسْتَكْبِرًا كَأَن لَّمْ يَسْمَعْهَا فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٨﴾

8. Anayesikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anang’ng’ania huku akijivuna, kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu chungu!

وَإِذَا عَلِمَ مِنْ آيَاتِنَا شَيْئًا اتَّخَذَهَا هُزُوًا أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٩﴾

9. Na anapokijua kitu katika Aya zetu hukifanyia mzaha. Hao ndio watakaokuwa na adhabu ya kufedhehesha.

مِّن وَرَائِهِمْ جَهَنَّمُ وَلَا يُغْنِي عَنْهُم مَّا كَسَبُوا شَيْئًا وَلَا مَا اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْلِيَاءَ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٠﴾

10. Nyuma yao ipo Jahannamu. Na waliyoyachuma hayatawafaa kitu, wala mawalii waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu. Na watapata adhabu kubwa.

هَـٰذَا هُدًى وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَهُمْ عَذَابٌ مِّن رِّجْزٍ أَلِيمٌ ﴿١١﴾

11. Hii ni mwongozo. Na wale waliozikataa Ishara za Mola wao watapata adhabu yenye maumivu iliyo chungu.

اللَّـهُ الَّذِي سَخَّرَ لَكُمُ الْبَحْرَ لِتَجْرِيَ الْفُلْكُ فِيهِ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢﴾

12. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeifanya bahari iwatumikie, ili humo yapite majahazi kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru.

وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مِّنْهُ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿١٣﴾

13. Na amefanya viwatumikie vilivyomo mbinguni na vilivyo katika ardhi, vyote kutoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaotafakari.

قُل لِّلَّذِينَ آمَنُوا يَغْفِرُوا لِلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ أَيَّامَ اللَّـهِ لِيَجْزِيَ قَوْمًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٤﴾

14. Waambie walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyokuwa wakiyachuma.

مَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ ﴿١٥﴾

15. Anayetenda mema basi anajitendea mwenyewe, na anyetenda uovu basi ni juu yake; kisha mtarudishwa kwa Mola wenu.

OLE WAKE KILA MTUNGA UONGO MWENYE DHAMBI!

Aya 7- 15

MAANA

Ole wake kila mtunga uongo mwenye dhambi! Anayesikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anang’ng’ania huku akijivuna, kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu chungu! Na anapokijua kitu katika Aya zetu hukifanyia mzaha.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuweka wazi dalili za kihisia zinazofahamisha, kwa mkato na kwa yakini, kuweko Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mwenye akili, na kusema kuwa asiyeziamini hizo basi hawezi kuamini dalili nyingine zozote, sasa anampa onyo na kumwahidi yule asiyezitilia manani dalili hizi na kunufaika nazo kwa kumwita mzushi mwenye dhambi na kumpa kiaga cha adhabu chungu.

Vile vile ammempa sifa ya mpinzani wa haki na kujitia ukubwa, na kwamba hakutosha na hayo bali ameidharau na kuifanyia mzaha haki.

Kafiri huyu mwenye kuidharau haki na watu wake hana tofauti, siku ya hisabu, na yule anayeiamini haki kwa kauli tu, bila ya kufanya, na kwa nadharia tu bila ya matendo. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ قَالُوا سَمِعْنَا وَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ ﴿٢١﴾

“Wala msiwe kama wale wanaosema: tumesikia; na kumbe hawasikii;” yaani hawakubali wala hawatendi. Juz.9 (8:21).

Imam Ali(a.s ) anasema:“Mwenye busara ni yule anayesikia akatafakari, akachunguza akaona na akanufaika na mazingatio.”

Hao ndio watakaokuwa na adhabu ya kufedhehesha. Nyuma yao ipo Jahannamu. Na waliyoyachuma hayatawafaa kitu, wala mawalii waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu. Na watapata adhabu kubwa.

‘Hao’ ni kila mtunga uwongo. Makusudio ya waliyoyachuma ni watoto wao, mali zao na vyeo vyao. Na waliyoyashika ni masanamu na mizimu yao.

Maana ni kuwa wale walioifanyia kiburi haki na wakaidharau, marejeo yao ni kuingia Jahannam; hakuna atakayewaokoa na adhabu hiyo – si masanamu wala watoto wala mali au vyeo.

Hii ni mwongozo.

‘Hii’ ni ishara ya Qur’an. Hakuna mwenye shaka kuwa Qur’an ni mwongozo kwa mwenye kuiamini na ni nguvu kwa mwenye kuitegemea.

Na wale waliozikataa Ishara za Mola wao watapata adhabu yenye maumivu iliyo chungu.

Makusudio ya Ishara hapa ni dalili za kilimwengu za kuwako Mwenyezi Mungu na ukuu wake. Neno adhabu, maumivu na uchungu, yanarudiana au yanakaribiana. Lengo la kukaririka huku ni kusisitiza adhabu atakayokutana nayo mzushi mwenye dhambi ambaye ameikalia juu haki na kuidharau.

Mwenyezi Mungu ndiye aliyeifanya bahari iwatumike, ili humo yapite majahazi kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru.

Fadhila za Mwenyezi Mungu ziko bara, baharini na angani. Miongoni mwa neema zake Mwenyezi Mungu Mtukufu baharini ni chakula, chumvi, mawe ya thamani, mawasiliano, matembezi na hata michezo nk. Umetangulia mfano wake katika Aya kadhaa, ikiwemo Juz.15 (17:66) na Juz.21 (30:46).

Na amefanya viwatumikie viliomo mbinguni na vilivyo katika ardhi, vyote kutoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaotafakari.

Katika ulimwengu huu mpana kuna manufaa na nyenzo zisizokuwa na idadi. Pamoja na kuendelea kwa elimu katika zama zetu hizi, lakini nyenzo zilizofichikana ni nyingi zaidi kuliko zilizobainika, lakini Mwenyezi Mungu amempa mtu maandalizi kamili ya kugundua nguvu na nyenzo zilizomo ulimwenguni na kufaidika nazo, kama atakuwa na mweleko wa elimu ya kibinadamu sio ya kibiashara, na pia kama atafanya juhudi kubwa.

Neno ‘Vyote,’ linaashiria kwamba mtu anayo maandalizi ya kumwezesha kufika mwezini na kwengineko. Tazama Juz. 20 (29:19-27) kifungu cha ‘Qur’an na fikra.’ Pia Umetangulia mfano wake katika Juz. 21 (31:20)

Waambie walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyokuwa wakiyachuma.

Makusudio ya siku za Mwenyezi Mungu hapa ni siku za adhabu yake. Wale wasiozitarajia siku za Mwenyezi Mungu ni washirikina wa kiarabu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwamrisha Mtume wake awaombe waumini wawasamehe washirikina ubaya waliowafanyia na wawalipize wema. Mwenyezi Mungu ndiye mwenye hisabu ya muovu na malipo yake.

Anayetenda mema basi anajitendea mwenyewe, na anyetenda uovu basi ni juu yake; kisha mtarudishwa kwa Mola wenu.

Maana yako wazi. Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:104) na kwa Herufi zake katika Juz. 24 (41:46).


24

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَلَقَدْ آتَيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿١٦﴾

16. Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu.

وَآتَيْنَاهُم بَيِّنَاتٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَمَا اخْتَلَفُوا إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿١٧﴾

17. Na tukawapa maelezo wazi ya amri. Basi hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa ajili ya uhasidi uliokuwa baina yao. Hakika Mola wako atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika waliyokuwa wakikhitalifiana.

ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٨﴾

18. Kisha tukakuweka juu ya sharia katika amri, basi ifuate. wala usifuate matamanio ya wasiojua.

إِنَّهُمْ لَن يُغْنُوا عَنكَ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا وَإِنَّ الظَّالِمِينَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُتَّقِينَ ﴿١٩﴾

19. Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika wenye kudhulumu ni mawalii wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni walii wa wenye takua.

هَـٰذَا بَصَائِرُ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿٢٠﴾

20. Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni mwongozo, na rehema kwa watu wanaoyakinisha.

WANA WA ISRAIL TENA

Aya 16 – 20

MAANA

Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu.

Katika Aya zilizotangulia, Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewataja wazushi wenye dhambi ambao wamezikanusha dalili za Mwenyezi Mungu na wakaidharau haki na watu wake.

Kwa kuwa Wana wa israil ni mfano halisi wa sifa hizi, ndio akafuatishia kuwataja na yale waliyo nayo ya upinzani na madhambi; pamoja na kuwa Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwa Tawrat na Injil alizoziashiria kwa neno Kitab. Akawafahamisha mawaidha na hukumu zilizomo ndani ya vitabu hivyo. Na hayo ndio makusudio ya ‘Hukumu.’

Akawafanyia mitume kutokana na wao na akawateremshia Manna na Salwa, alizoziashiria Mwenyezi Mungu kwa neno ‘Vitu vizuri.’ Pia akawafadhilisha juu ya watu wa Firauni pale alipowagharikisha na waisrail wakapumua kutokana na adhabu yao.

Na tukawapa maelezo wazi ya amri.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwafafanuliwa Wana wa Israil mahitaji yao ya mambo ya dini, hawakubakiwa na udhuru au visababu vya kutofautiana na kufarikiana.

Basi hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa ajili ya uhasidi uliokuwa baina yao.

Waliyajua kwa yakini yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Musa, lakini wao wakajitia kutojua na wakayageuza kulingana na matamanio na masilahi yao:

مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ وَيَقُولُونَ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا ﴿٤٦﴾

“Miongoni mwa mayahudi wako ambao hugeuza maneno kutoka mahali mwake na husema: tumesikia na tumeasi.” Juz. 5 (4:46).

Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Basi hawakukhitalifiana,” inaashiria kuwako wachache kwa nadra waliothibiti katika haki.

Hakika Mola wako atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika waliyokuwa wakikhitalifiana.

Katika maisha ya duniani, mara nyingine asiyekuwa na haki humshinda mwenye haki, lakini akhera itakayokuwa juu ni haki peke yake; vinginevyo mwenye haki angekua ni mbaya kuliko asiyekuwa na haki.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:93).

WAISRAIL WAMEPIGWA NA UDHALILI KWA HUKUMU YA TAWRAT

Qur’an imewazungumzia Wana wa Israil kwa kusema: “Wamepigwa na udhalili popote wanapokutanikana” Juz. 4 (3:112). Huko tumezungumza kwa ufafanuzi zaidi kuhusu Aya hii na tukasema kuwa Israil ni kambi ya kijeshi ya ukoloni na kwamba itaisha tu, sasa au baadaye.

Hivi sasa tutanukuu kitabu kitakatifu kwa Mayahudi yale yanayofahamisha kwa uwazi kuwa Mwenyezi Mungu amewaandikia Waisrail udhalili hadi siku ya mwisho: “Kwa hiyo BWANA akawaghadhibikia Israel sana…. Kwa hiyo BWANA akakitaa kizazi chote cha Israel, akawatesa.”

(2 Wafalme 17:18 – 20)

“Basi BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa nami nitawapa maji ya uchungu wanywe. Nami nitawatawanya kati ya mataifa, ambao hao hawakuwajua; wala baba zao; nami nitatuma upanga nyuma yao, hata nitakapowaangamiza.” (Yeremia 9:15-16)

“Nanyi mtasalia wachache kwa hisabu…..Nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi” Kumbukumbu la (Torati 28: 62-63). Maneno katika nukuu zote hizo yanaelekwezwa kwa Wana wa Israil. Kuna nukuu nyinginezo zaidi ya hizi.

Tunawauliza wazayuni: Ikiwa nyinyi ni taifa teule la Mwenyezi Mungu, kama mnavyodai, basi kwa nini nyinyi na kizazi chenu Mwenyezi Mungu amewahukumia udhalili, kufukuzwa hadi kung’olewa kabisa? Vipi Mola akatoa ahadi kuwa ataifanya Jerusalem ni magofu na makao ya mbweha? Kama ilivyoelezwa katika Yeremia 9:11, “Nami nitafanya Yerusalem kuwa magofu, makao ya mbweha; Nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, isikaliwe na mtu awaye yote.”

Ni kipi hicho Kitabu kitakatifu kwa ajili ya dola yenu ya kidini ya kiubaguzi, kama alivyosema Pompidou, raisi wa ufaransa? Je, ni Tawrat iliyowasifu nyinyi na mji wenu kwa kusema: “Bwana asema hivi; mji – yaani Yerusalem – umwagao damu ndani yake…Tazama, wakuu wa Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya nguvu zake, wamekuwamo ndani yako, ili kumwaga damu.”

(Ezekieli 22: 3,6.)

Vile vile umeshutumiwa mji wa Jerusalemu, kwenye Luka mtakatifu 13:34: “Ewe Yerusalemu, Yerusalemu, wewe uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako!”

Inasema Biblia kuwa kila mahali na kila wakati Mayahudi ni washirika wa hatia ya mababu zao waliomsulubu Bwana Masih, kwa sababu wanaliridhia hilo kwa vitendo vyao kwa kusema kuwa Yeye ni mwanaharamu.

Hayo yanaafikiana na msingi wa kiislamu unaosema kuwa mwenye kufanya dhulma, mwenye kuisaidia na mwenye kuiridhia wote ni washirika.

Ndio maana kanisa la Khufti (Coptic), likaingilia kati kumpinga Baba mtakatifu, wakati yeye na wasaidizi wake walipotoa tamko rasmi la kukisafisha kizazi cha kiyahudi na damu ya Bwana Masih.

Ieleweke kuwa Baba mtakatifu alitoa tamko hili kabla ya muda mchache Israil kuvamia miji ya Kiarabu.

Kisha tukakuweka juu ya sharia katika amri, basi ifuate.

Neno sharia katika Lugha lina maana ya chemchem ya maji. Kisha likaazimwa kutumiwa kwenye hukumu za dini. Kwa sababu zinaipa uhai roho; kama maji yanayvoupa uhai mwili. Makusudio ya amri hapa ni dini. Maana ni kuwa Ewe Muhammad tumekujaalia kwenye itikadi ya Tawhid na kuing’oa shirki na tukakupa sharia nyepesi, basi shikamana nayo. Ama kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:wala usifuate matamanio ya wasiojua, maana yake ni kuwa wakosefu hawafuati isipokuwa matamanio na lengo.

Na wala usizichukulie lawama za mwenye kulaumu, na Mwenyezi Mungu (s.w.t) atakutosha na vitimbi vya wenye vitimbi na shari za wenye njama.

Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu.

Kwa sababu anayeshindwa kujikinga yeye mwenyewe hawezi kumsaidia mwingine.

Na hakika wenye kudhulumu ni mawalii wao kwa wao.

Mwenye hatia duniani hapati wa kumsaidia na kumnusuru isipokuwa aliye kama yeye katika hatia na dhambi, na walio wema ni maadui zake na wagomvi wake. Lakini huko Akhera, wenye hatia watalaniana wao kwa wao.Na Mwenyezi Mungu ni walii wa wenye takua, duniani na Akhera.

Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni mwongozo, na rehema kwa watu wanaoyakinisha.

Ni dalili zinazowaonyesha haki na njia ya uongofu. Hakuna mwenye shaka kwamba mwenye kufuata Qur’an anakuwa na yakini kwamba yeye yuko kwenye uongofu Kutoka kwa Mola na kuingia kwenye rehema yake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 9 (7:203).

أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ اجْتَرَحُوا السَّيِّئَاتِ أَن نَّجْعَلَهُمْ كَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَوَاءً مَّحْيَاهُمْ وَمَمَاتُهُمْ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ﴿٢١﴾

21. Je, wanadhani wanaotenda maovu kuwa tutawafanya kama walioamini, na wakatenda mema, sawa sawa uhai wao na kufa kwao? Ni mabaya wanayohukumu.

وَخَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَلِتُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٢﴾

22. Na Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki. Na ili kila nafsi ilipwe yale iliyoyachuma. Nao hawatadhulumiwa.

أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ وَأَضَلَّهُ اللَّـهُ عَلَىٰ عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِ وَقَلْبِهِ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِ غِشَاوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِن بَعْدِ اللَّـهِ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٢٣﴾

23. Je, umemwona aliyefanya hawaa yake kuwa ndio mungu wake? Basi nani atamwongoza baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?

وَقَالُوا مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا يُهْلِكُنَا إِلَّا الدَّهْرُ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ إِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴿٢٤﴾

24. Na walisema: Hapana ila uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinachotuhilikisha isipokuwa dahari. Lakini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadhani tu.

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ مَّا كَانَ حُجَّتَهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا ائْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٥﴾

25. Na wakisomewa Aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila kusema: Waleteni baba zetu, ikiwa nyinyi ni wakweli.

قُلِ اللَّـهُ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يَجْمَعُكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٦﴾

Sema: Mwenyezi Mungu anawapa uhai, kisha anawafisha, kisha anawakusanya, Siku ya Kiyama isiyo na shaka.

AMEIFANYA HAWA YAKE NDIO MUNGU WAKE

Aya 21 – 26

MAANA

Je, wanadhani wanaotenda maovu kuwa tutawafanya kama walioamini, na wakatenda mema, sawa sawa uhai wao na kufa kwao? Ni mabaya wanayohukumu.

Inawezekana mwema na muovu wawe na daraja sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na katika mtazamo wa kiakili? Basi kutakuwa na haja gani ya kuitwa mwema na mwengine muovu? Nini itakuwa tofauti ya heri na shari?

Wataalamu wa ilimu ya teologia wamechukua madhumuni ya Aya hii na wakasema kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaahidi watiifu thawabu na akawahidi waasi adhabu, na duniani hakutokei kitu katika hayo. Kwa hiyo basi Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawajibisha kurudisha uhai baada ya mauti ili upatikane utekelezaji wa ahadi yake.

Vile vile Mwenyezi Mungu ni mwadilifu, hilo halina shaka, na tunamuona dhalimu akimaliza maisha yake bila ya kulipizwa kisasi na yoyote aliyedhulumiwa. Lau si kurudi kwa hisabu na malipo, basi mdhulumiwa angelikuwa na hali mbaya zaidi ya dhalimu na Mwenyezi Mungu angelikuwa dhalimu. Ametakata sana Mwenyezi Mungu na hayo.

Ama neema za dunia sio alama ya kuridhia Mwenyezi Mungu. Wala shida ya dunia sio dalili ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Imam Ali (a.s.) anasema: “Enyi watu! Hakika dunia ni ya kupita na akhera ni ya kutulia, basi chukueni kutulia kwenu katika mapito yenu…nyoyo zenu zitoeni duniani kabla hazijatoka milini mwenu. Kwenye hiyo dunia mnapewa mtihani na mmeumbwa kwa ajili ya kwengine sio duniani.”

Na Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki.

Hii ni sababu ya kutofanywa sawa mwema na muovu. Ubainifu wake ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameumba ulimwengu kwa haki na uadilifu; vinginevyo ingelikuwa kuumbwa ulimwengu ni kwa mchezo na ubatilifu.

Kwa sababu mwenye kufanya mchezo kwenye jambo moja anaweza kufanya kwenye jambo jingine.

Na ili kila nafsi ilipwe yale iliyoyachuma. Nao hawatadhulumiwa.

Hii ndio njia ya usawa – njia ya haki na uadilifu; mwenye kufanya heri kwa uzani wa chembe ataiona, na mwenye kufanya shari kwa wizani wa chembe ataiona. Tazama Juz. 11 (10:4) kifungu cha: ‘Hisabu na malipo ni lazima.’

Kwa ufupi ni kuwa Mwenyezi Mungu ana hekima na ameepukana na makosa, na hekima yake Mwenyezi Mungu Mtukufu inapelekea kuwafufua watu baada ya mauti, ili kumpambanua mwema na muovu na kumlipa kila mmoja stahiki yake. Kama si hivyo basi kuumbwa ingelikuwa ni kwa mchezo. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Je, mnadhani kuwa tuliwaumba bure na kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa? Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa haki.” yaani ametakasika na mchezo. Juz. 18 (23:115-116)

Je, umemwona aliyefanya hawa yake kuwa ndio mungu wake?

Miongoni mwa watu kuna yule ambaye haamini chochote isipokuwa nafsi yake na masilahi yake tu. Anaweza kuwa anasoma tahlili na takbira; bali anaweza pia kuwa anafunga na kuswali, madamu hilo haliingiliani na anayoyapenda na kuyatamani. Hawa yake ndiyo muabudiwa wa haki peke yake, mengineyo ni nyenzo tu, sio lengo; au ni mazoweya tu sio ibada. Haya ndio makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘aliyefanya hawa yake kuwa ndio mungu wake.’

Neno hawa limetokana na neno la kiarabu linalotamkwa hivyo hivyo ‘Hawaa’ lenye maana pia ya kuanguka chini. Kuna mmoja amesema, hali hiyo imeitwa hawa kwa sababu inamwangushwa kwenye Jahannam aliye nayo. Msemaji amechukua fikra hii kutokana kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٤٠﴾ فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ ﴿٤١﴾

“Na ama yule mwenye kuogopa kusimama mbele ya Mola wake, na akaikataza nafsi na hawa, basi hakika Pepo ndio makazi (yake).” (79:40-41).

Kuna tafsiri inayosema kuwa mshirikina aliye jahili, alikuwa akiangukia jiwe kuliabudu, kisha anaona jingeni analiangukia na kulitupa lile la kwanza. Ndio hivyo anayemtupa Mungu na kuangukia kwenye ‘hawa’ kuwa ndio Mungu wake.

Hakuna mwenye shaka kwamba mshirikina mpumbavu, hatia yake mbele ya Mwenyezi Mungu inazidiwa na kibaraka anyeiuza dini yake na dhamira yake kwenye mnada na kushikana na yule anayezidisha bei.

Na Mwenyezi Mungu akampoteza licha ya ilimu.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) hampotezi. Atampotezaji na hali Yeye ndiye aliyekataza upotevu na akautolea kiaga kikali? Lakini anyefuata njia ya upotevu kwa hiyari anamwachila mbali na upotevu wake, wala hapatwi na upole wake na msaada wake, baada ya kujua kwa mbali upotevu wake na inadi yake.

Ama kauli yake:na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akaweka kizibo machoni mwake, maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anampofusha na kumtia uziwi mwenye inadi baada ya kuitambua haki kwa macho yake na masikio yake, baada ya kubainishiwa na kuhimizwa, lakini akipinga bila ya sababu za maana. Mwenyezi Mungu nasema:

فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿٥﴾

“Lakini walipopotoka, Mwenyezi Mungu akazipotoa nyoyo zao, na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu mafasiki.” (61:5).

Basi nani atamwongoza baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?

Asiyenufaika na mawaidha ya Mwenyezi Mungu basi hayawezi kumfaa mwaidha na nasaha zote.

Na walisema: Hapana ila uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinachotuhilikisha isipokuwa dahari.

Wamaada au wadahari, vyovyote utakavyowaita, wanasema kuwa binadamu ni mchanaganyiko wa vitu vya kimaada vilivyokusanyika kutoka huku na huko na vikafanyika. Kwa hiyo akifa ndio amekwisha, hakuna chochote baada ya mauti, sawa na mimea na wadudu. Na kwamba hizi hisia na utambuzi tunaouna kwa binadamu zimezalishwa na mwili kutokana na mchanganyiko wa hali. Yaani akili ya mwanadamu ni mkondo wa pili usiokuwa na asili na chanzo.

Lakini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadhani tu.

Yaani kauli yao hii ni madai yasiyokuwa na hoja; bali kuna hoja ya kuayavunja. Yule ambaye anaihukumu maada, kuipatia manufaa na kujua mengi zaidi kuihusu, lakini yenyewe isimjue yeye, hapana budi kuwa, mtu huyu wa ajabu, awe ni mkuu na yuko zaidi kuliko maada. Yametangulia maneno kuhisiana na hayo mara nyingi; kama vile kwenye Juz. 14 (16:78).

Na wakisomewa Aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila kusema: Waleteni baba zetu, ikiwa nyinyi ni wakweli.

Hii ni sawa na anayesema, siwezi kuamini kuwa mtofahaa unaweza kuzaa matunda wakati wa kaskazi mpaka niuone una mimba wakati wa kusi. Mtoto huyu akishakuwa mkubwa, atajua kuwa kila kitu kina muda wake na kwamba kila ajali ina maandishi haikawii wala kuwahi. Umetangulia mfano wake katika Juzuu hii tuliyo nayo kwenye (44:36).

Sema: Mwenyezi Mungu anawapa uhai, kisha anawafisha, kisha anawakusanya, Siku ya Kiyama isiyo na shaka.

Ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye anayempa uhai mtu alipokuwa si chochote, atashindwa vipi kumpa uhai mara ya pili? Lakini watu wengi hawajui kuwa kurudishwa mara ya pili ni rahisi kuliko kuumbwa kwa kwanza. Umetangulia mfano wake katika Aya kadhaa, zikiwemo: Juz. 1 (2:28) na Juz.17 (22:66).


25

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI

وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَخْسَرُ الْمُبْطِلُونَ ﴿٢٧﴾

27. Na ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. Na siku itaposimama Saa, siku hiyo watahasirika wenye batili.

وَتَرَىٰ كُلَّ أُمَّةٍ جَاثِيَةً كُلُّ أُمَّةٍ تُدْعَىٰ إِلَىٰ كِتَابِهَا الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٢٨﴾

28. Na utauona kila umma umepiga magoti. Kila umma utaitwa kwenye kitabu chake: Leo mtalipwa mliyokuwa mkiyatenda.

هَـٰذَا كِتَابُنَا يَنطِقُ عَلَيْكُم بِالْحَقِّ إِنَّا كُنَّا نَسْتَنسِخُ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٢٩﴾

29. Hiki kitabu chetu kinasema juu yenu kwa haki. Hakika Sisi tulikuwa tukiyaandika mliyokuwa mkiyatenda.

فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُدْخِلُهُمْ رَبُّهُمْ فِي رَحْمَتِهِ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ ﴿٣٠﴾

30. Ama wale walioamini na wakatenda mema, Mola wao atawaingiza katika rehema yake. Huko ndiko kufuzu kulio wazi.

وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا أَفَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَاسْتَكْبَرْتُمْ وَكُنتُمْ قَوْمًا مُّجْرِمِينَ ﴿٣١﴾

31. Na ama wale waliokufuru: Kwani hamkuwa mkisomewa Aya zangu nanyi mkawa na kiburi, na mkawa watu wakosefu?

KILA UMMA UTAITWA KWENYE KITABU CHAKE

Aya 27 – 31

MAANA

Na ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anaashiria, kwa kauli hii, kwamba aliyeumba mbingu na ardhi na wala asichoke, bila shaka, ni muweza wa kuhuisha wafu.

Na siku itaposimama Saa ya Kiyama,siku hiyo watahasirika wenye batili, kwa sababu makazi yao ni motoni siku hiyo, wala hawatakuwa na wa kuwasaidia.

Na utauona kila umma umepiga magoti.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawafufua watu wakiwa wamepiga magoti wakingoja hisabu na malipo. Sio mbali kuwa hiki ni kinaya cha fazaa na hofu itakayojitokeza.

Kila umma utaitwa kwenye kitabu chake: Leo mtalipwa mliyokuwa mkiyatenda.

Makusudio ya kitabu hapa ni maandishi ya matendo. Maana ni kuwa kila umma na kila mtu atalipwa kwa aliyoyatenda. Kwenye Nahjul-balagha, Imam Ali(a.s ) anasema:“Anapokufa mtu watu husema alichokiacha, na Malaika husema alichokileta”

Hiki kitabu chetu kinasema juu yenu kwa haki. Hakika Sisi tulikuwa tukiyaandika mliyokuwa mkiyatenda.

Kesho wakosefu wataambiwa haya ndiyo tuliyoyaandika kuhusiana na nyinyi. Picha kamili ya matendo haina nyongeza wala upungufu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwaamrisha Malaika kusajili vitendo vyenu na kuvihifadhi kwa pumzi zenu mlizozitumia kwenye maasi.

وَيُنذِرَ الَّذِينَ قَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ﴿٤﴾

Na kiwaonye wanao nena: Mwenyezi Mungu ana mwana. Juz. 15 (18:4).

Ama wale walioamini na wakatenda mema, Mola wao atawaingiza katika rehema yake. Huko ndiko kufuzu kulio wazi.

Walifuata njia ya amani, Mwenyezi Mungu akawaongoza katika rehema yake. Imam Ali(a.s) anasema:“Hatafuzu kwa heri ila mwenye kuifanyia kazi, wala hatafedheheka na shari ila aliyeifanya.”

Na ama wale waliokufuru, wataambiwa: Kwani hamkuwa mkisomewa Aya zangu nanyi mkawa na kiburi, na mkawa watu wakosefu?

Kesho Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawambia waasi waliokuwa na inadi na kiburi, kwa kuwasuta na kuwatahayariza kuwa mliisikia sauti ya haki hamkuitika na mkaona dalili waziwazi mkazipinga kwa inadi na kiburi; mkastarehe kwenye ufisadi na upotevu, basi leo nyinyi ni katika waliohasirika.

وَإِذَا قِيلَ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَالسَّاعَةُ لَا رَيْبَ فِيهَا قُلْتُم مَّا نَدْرِي مَا السَّاعَةُ إِن نَّظُنُّ إِلَّا ظَنًّا وَمَا نَحْنُ بِمُسْتَيْقِنِينَ ﴿٣٢﴾

32. Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, na Saa haina shaka, nyinyi mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini.

وَبَدَا لَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا عَمِلُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٣٣﴾

33. Na ubaya wa waliyoyatenda utawadhihirikia, na yatawazunguka waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.

وَقِيلَ الْيَوْمَ نَنسَاكُمْ كَمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٣٤﴾

34. Na itasemwa: Leo tunawasahau kama mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wa kuwanusuru.

ذَٰلِكُم بِأَنَّكُمُ اتَّخَذْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ هُزُوًا وَغَرَّتْكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا فَالْيَوْمَ لَا يُخْرَجُونَ مِنْهَا وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ ﴿٣٥﴾

35. Hiyo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu; na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru.

فَلِلَّـهِ الْحَمْدُ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَرَبِّ الْأَرْضِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٣٦﴾

36. Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa mbingu, na Mola wa ardhi, na Mola wa walimwengu wote.

وَلَهُ الْكِبْرِيَاءُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٣٧﴾

37. Na ukubwa ni wake, mbinguni na katika ardhi, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

LEO TUNAWASAHAU

Aya 32-37

MAANA

Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, na Saa haina shaka, nyinyi mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini.

Bado mazungumzo ya wakosefu yaaendelea. Kauli yake Mwenyezi Mungu: “Saa haina shaka,’ ni ubaiinifu na tafairi ya ahadi ya Mwenyezi Mungu. Maana ni kuwa wakosfu walipokuwa wakiwaambiwa na waumini kuwa ufufuo ni kweli na hisabu na malipo ni kweli, wao walikuwa wakisema: sisi hatuna uhakika na ufufuo wala hatuji chochote kuhusiana nao isipokuwa dhana. Basi tuleteeni.dalili yake.

Unaweza kuuliza : Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwenye Aya 24 ya sura hii, amewasimulia kuwa wao walikana ufufuo kwa njia ya mkato, kama inavyofahamisha kauli yao: ‘hapana ila maisha yutu ya duniani,’ kisha hapa Mwenyezi Mungu anawasimulia kwamba wao wanadhania na hawana yakini, yaani hawakatai moja kwa moja. Vipi tutazichanganya Aya mbili hizi?

Razi anasema dhana kubwa ni kuwa wao walikuwa vikunndi viwili: kundi liliokanusha ufufuo kwa mkato na kundi jingine walikuwa na shaka.

Lakini sisi dhana yetu kubwa ni kuwa walikuwa kundi moja tu, na kwamba maana ya Aya zote mbili ni kuwa wao hawaamini ufufuo kwa vile wanadai hawana dalili inayoyakinisha isipokuwa ni mambo yaliyo mbali na wao.

Na ubaya wa waliyoyatenda utawadhihirikia, na yatawazunguka waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.

Duniani walipanda makosa na madhambi watayavuna matunda yake Akhera. Waliidharau Jahannam watakuwa ni kuni zake.

Na itasemwa: Leo tunawasahau kama mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wa kuwanusuru.

Waliikana siku ya Kiyama na wakaifanyia dharau na wale wanaoiamini, Mwenyezi Mungu akawapa muda na wala hawatapata rehema ya Mwenyezi Mungu siku hiyo, bali atawaonjesha adhabu ya siku hiyo na atawaonyesha uweza wake na nguvu zake ndani ya siku hiyo waliyoitilia shaka. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:51).

Hiyo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu; na maisha ya dunia yakawadanganya.

‘Hiyo’ ni hiyo adhabu. Maana ni kuwa iliyosababisha adhabu yao ni kukanusha kwao siku ya mwisho, kuipinga Qur’an na kuzidharau Aya zako wanaposomewa na kujituliza kwao na dunia na strehe zake.

Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru.

‘Humo’ ni humo motoni. Maana ni kuwa wao watakaa milele humo, wala hawatatakiwa kumtaka radhi Mwenyezi Mungu kwa kauli au kitendo. Kwa sababu Akhera ni nyumba ya hisabu na malipo sio nyumba ya kuomba radhi.

Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa mbingu, na Mola wa ardhi, na Mola wa walimwengu wote.

Msifuni Mwenyezi Mungu peke yake, kwa sababu Yeye ni muumba wa kila kitu.

Na ukubwa ni wake, mbinguni na katika ardhi.

Makusudio ya ukubwa wake Mtukufu ni kwamba hakuna mkubwa anayehofiwa au kutarajiwa isipokuwa Yeye peke yake. Imam Ali(a.s.) akiwasifu wanaomjua Mwenyezi Mungu kwa kusema:“Amekuwa mkubwa Muumba katika nafsi zao akawa mdogo asiyekuwa Yeye machoni mwao.”

Naye ni Mwenye nguvu, ambaye hakimshindi chochote.Mwenye hikima katika mpangilio wa kuumba kwake.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI


YALIYOMO

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 1

IMEANDIKWA NA: SHEIKH MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYA 1

IMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HASAN MWALUPA 1

IMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED 1

IMEPANGWA KATIKA KOMPYUTA NA: UKHT PILI RAJABU 1

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI 1

MAKOSA YA CHAPA 2

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 3

JE, MWENYEZI MUNGU SI WA KUMTOSHEA MJA WAKE? 3

MAANA 3

SEMA, TOSHA YANGU NI MWENYEZI MUNGU 5

MAANA 5

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 9

UTAHUKUMU BAINA YAO 9

MAANA 9

UDHURU MBAYA KULIKO DHAMBI 10

MWENYEZI MUNGU ANASAMEHE MADHAMBI YOTE 13

MAANA 13

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 15

WALIOMSINGIZIA UWONGO MWENYEZI MUNGU 15

MAANA 15

WALIOKUFURU WATASUKUMWA 18

MAANA 18

WALIOMCHA MOLA WAO WATAPELEKWA PEPONI 21

MAANA 21

MWISHO WA SURA YA THELATHINI NA TISA: SURAT AZ-ZUMAR 22

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 23

MWENYE KUSAMEHE DHAMBI NA KUKUBALI TOBA 23

MAANA 23

WANAOBEBA ARSHI 25

MAANA 25

UMETUFISHA MARA MBILI NA UMETUHUISHA MARA MBILI 27

MAANA 27

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 30

WAONYE SIKU INAYOKURUBIA 30

MAANA 30

MUSA 32

MAANA 32

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 35

MWENYEZI MUNGU HADHULUMU WAJA 35

MAANA 35

NIZIFIKIE NJIA 37

MAANA 37

NINAWAITA KWENYE WOKOVU NYINYI MNANIITA KWENYE MOTO 39

MAANA 39

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 41

WANAHOJIANA MOTONI 41

MAANA 41

MWENYEZI MUNGU NA WAISRAIL 43

KUUMBA MBINGU NA ARDHI 46

MAANA 46

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 48

AMEWATIA SURA NA AKAZIFANYA NZURI 48

MAANA 48

MWANAFALSAFA RUSSEL NA MUDA ULIOWEKWA 50

MLIKUWA MKIFURAHI 51

MAANA 51

TUNATAFUTA DUNIA KWA DINI 52

MWENYEZI MUNGU AMEWAJAALIA WANYAMAHOWA 54

MAANA 54

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI: SURAT AL-GHAAFIR 55

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 56

KITABU KILICHOPAMBANULIWA 56

MAANA 56

MWENYEZI MUNGU AMEUMBA ARDHI 59

MAANA 59

NINI UFUMBUZI WA TATIZO LA NJAA? 59

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 62

NAWAHADHARISHA UKELELE 62

MAANA 62

MASIKIO YAO NA MACHO YAO YATAWASHUHUDIA 64

MAANA 64

WALIOKUFURU WALISEMA MSISIKILIZE QUR’ANI 67

MAANA 67

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 69

WALISEMA MOLA WETU NI MWENYEZI MUNGU KISHA WAKAWA NA MSIMAMO 69

MWENYEZI MUNGU NA MTU NA MATENDO 69

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 73

HAUTAKIFIKIA UPOTOVU MBELE YAKE WALA NYUMA YAKE 74

SAFARI YA MWEZINI 74

ISRAIL NA QUR’AN 76

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 80

ELIMU YA SAA INARUDISHWA KWAKE 80

MAANA 80

TUTAWAONYESHA ISHARA ZETU 82

MAANA 82

ULIMWENGU NI QUR’AN KUBWA YA MWENYEZI MUNGU 82

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI NA MMOJA: SURAT FUSSILAT 83

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 84

HIVYO NDIVYO MWENYEZI MUNGU ANAVYOKULETEA 84

MAANA 85

SIMAMISHENI DINI WALA MSIFARIKIANE 87

MAANA 87

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 91

KUWA NA MSIMAMO KAMA ULIVYOAMRISHWA 91

MAANA 91

MWENYEZI MUNGU NI MPOLE KWA WAJA WAKE 93

MAANA 93

NITII UTAKUWA MFANO WANGU 94

NI NANI HAO NDUGU? 95

MAANA 95

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 98

RIZIKI NI KWA KUFANYA KAZI SIO KWA DUA 98

MAANA 98

KILICHOKO KWA MWENYEZI NI BORA NA KITABAKIA 101

MAANA 101

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 104

MWENYE HASARA NI YULE ALIYEJIHASIRI MWENYEWE 104

MAANA 105

SURA YA MAWASILIANO BAINA MWENYEZI MUNGU NA MITUME WAKE 107

MAANA 107

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI NA MBILI: SURAT ASH-SHURA 109

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 110

KITABU KINACHOBAINISHA 111

MAANA 111

AU AMEJICHUKULIA WATOTO WANAWAKE 113

MAANA 114

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 116

JE, WANAIGAWA REHEMA YA MOLA WAO? 116

MAANA 117

KWA NINI ALI KARRAMALLAHU WAJHAH 117

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 121

JE, UNAWEZA KUWASIKILIZISHA VIZIWI 121

MAANA 121

MUSA 124

MAANA 124

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 127

ALIPOPIGIWA MFANO MWANA WA MARYAM 127

MAANA 127

SIKU HIYO MARAFIKI WATAKUWA NI MAADUI 131

MAANA 131

INGELIKUWA MWINGI WA REHEMA ANA MWANA 133

MAANA 133

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI NA TATU: SURAT AZ-ZUKHRUF 134

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 135

TUMEITEREMSHA USIKU ULIOBARIKIWA 135

MAANA 135

SIKU AMBAYO MBINGU ITALETA MOSHI 137

MAANA 137

WATU HAWA NI WAKOSEFU 139

MAANA 139

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 142

JE, WAO NI BORA AU WATU WA TUBBAA’ 142

MAANA 142

CHAKULA CHA MWENYE DHAMBI NA CHA MWENYE TAKUA 144

MAANA 144

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI NA NNE: SURAT AD-DUKHAN 145

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 146

KATIKA MBINGU NA ARDHI KUNA ISHARA KWA WAUMINI 146

MAANA 146

OLE WAKE KILA MTUNGA UONGO MWENYE DHAMBI! 148

MAANA 149

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 151

WANA WA ISRAIL TENA 151

MAANA 151

WAISRAIL WAMEPIGWA NA UDHALILI KWA HUKUMU YA TAWRAT 152

AMEIFANYA HAWA YAKE NDIO MUNGU WAKE 154

MAANA 154

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 157

KILA UMMA UTAITWA KWENYE KITABU CHAKE 157

MAANA 157

LEO TUNAWASAHAU 158

MAANA 159

SHARTI YA KUCHAPA 160

MWISHO WA JUZUU YA ISHIRINI NA MBILI 160

YALIYOMO 161



[1] . Khutba: 195.

[2] . Khutba 222.

[3] . Haya ni katika miaka ya 70. Je hivi sasa Marekani imetumia Matirilioni mangapi ya dola huko Afghanistan na Iraq? Mtarjum.

[4] . Mwisho wa utafiti wa kitiba (mnamo mwaka 1970) umefikia kuweza kujua aina ya mtoto aliye tumboni kuwa ni wa kiume au kike kuanzia mwezi wa tatu wa mimba. Tazama Juz. 21 (31:34).