TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE- Juzuu 24
Kuweka vikundi Qurani tukufu
mwandishi Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
Lugha ya kitabu سواحیلی
mwaka wa kuchapisha 1404

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

IMEANDIKWA NA: SHEIKH MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYA

IMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HASAN MWALUPA

IMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED

IMEPANGWA KATIKA KOMPYUTA NA: UKHT PILI RAJABU

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI

Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London.

Kama lilivyo jina la Tafsiri ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo.

Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyo kujipatia wasomaji wengi sana.

Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana kwenda na wakati.

Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung'ang'ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo, hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea. Hiyo ilimsaidia sana hata kuweza kutoa kitabu kitwacho Al-Fiqh a'laa madhaahabil-khamsah (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka kwa lugha ya kiswahili hivi karibuni Inshaallah).

Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.

Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasayansi kama kina Enstein, wasanii kama Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa.

Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.

Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji.

Mwisho: Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji.

MAKOSA YA CHAPA

Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa, Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa.

Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya msahafu mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswutu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146), Imeandikwa La Ya'alamuun, (hawajui) badala ya Ya'alamuun (wanajua). Mfano wa makosa haya hausameheki.

Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa Fawqahum ila yawmil qiyama badala ya Fawqahum yawamal qiyama. Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile.

Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu Jabal amil 'Makosa ya chapa.'

Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: Hatta idha balagha arbai' na sanah badala ya: Hattaidha balagha ashuddahu arbai ' na sanah"

Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakayoyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefungua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana.

Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: "Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa.” Kama kwamba hakuna kitu chochote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.

Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin(a.s) :"Watu wote ni wapungufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu." Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubalia yale niliyoyapatia na kunisamehe niliyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazi chake, ziwashukie rehema na amani (Amin).

MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH


1

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Hamsini Na Nane: Al–Mujadala. Imeshuka Madina. Imesemekana kinyume na hivyo, Ina Aya 22.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ ﴿١﴾

1. Mwenyezi Mungu amekwisha­sikia usemi wa mwanamke anayejadiliana nawe juu ya mumewe, na anamshitakia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.

الَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَائِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَاتِهِمْ إِنْ أُمَّهَاتُهُمْ إِلَّا اللَّائِي وَلَدْنَهُمْ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنكَرًا مِّنَ الْقَوْلِ وَزُورًا وَإِنَّ اللَّـهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ ﴿٢﴾

2. Wale miongoni mwenu wanaowafanyia dh h. wake zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale waliowazaa. Na hakika hao wanasema neno linalochusha na la uwongo. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kughufi­ria.

وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٣﴾

3. Na wale wanaowafanyia dhiha­ wake zao kisha wakarudi kuachana na yale walioyase­ma, basi ni kumwacha huru mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa mawaidha kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.

فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا فَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِينًا ذَٰلِكَ لِتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٤﴾

4. Na asiyepata, basi afunge miezi miwili ya kufuatana kabla hawajagusana. Na asiyeweza basi awalishe masikini sitini. Hayo ni hivyo ili mumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu Na kwa makafiri iko adhabu chungu.

DHIHAR

Aya 1 – 4

LUGHA

Dhihar ni mume kumwambia mkewe: ‘Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu;’ akimaanisha kuwa ni haramu kwake kama alivyo mama yake. Akishasema hivyo basi mke anakuwa haramu kwake mpaka atoe kafara; kama yatakavyokuja maelezo.

KISA KWA UFUPI

Wameafikiana wafasiri kuwa Aya hizi zilishuka kwa tukio maalum. Kwa ufupi, tukio lenyewe ni kama ifutavyo:-

Mtu mmoja alimkasirikia mkewe akamwambia: wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu, na hiyo ilikuwa ni talaka wakati wa Jahilia. Basi mwanamke akahuzunika, na mwanamume akajuta kwa haraka yake alioifanya, akamwambia mkewe nenda kwa Mtume umpe habari ya yaliyotokea, mimi ninaona haya kumuuliza.

Mke akaenda na kumsimulia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) na akamsisitiza, huku akisema: Ninamshtakia Mwenyezi Mungu haja yangu. Mwenyezi Mungu akaitikia dua yake na akateremsha Aya hizi. Kisa hiki kinaafikiana na dhahiri ya Aya.

Vyovyote iwavyo ni kuwa: Dhihar ni mlango katika milango ya fiqhi ya waislamu.

MAANA

Mwenyezi Mungu amekwishasikia usemi wa mwanamke anayejadiliana nawe juu ya mumewe, na anamshitakia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamwambia Mtume wake mtukufu kuwa Mwenyezi Mungu amekwishajua hali ya mwanamke na anavyokuelezea kuhusu mumewe. Vile vile amekwishajua mashtaka yake na maombi yake; na amekwishaitikia maombi yake.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona; hakifichiki kwake chochote cha kujificha.

Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akabainisha hukumu ya tukio hili na mfano wake kwa kusema:

Wale miongoni mwenu wanaowafanyia dh h. wake zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale waliowazaa. Na hakika hao wanasema neno linalochusha na la uwongo.

Dhihari imeharamishwa katika dini ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu ni uwongo unaohalifu uhalisia. Vipi mke awe ni mama!

Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kughufiria, yule mwenye kutubia na akarejea nyuma. Baadhi ya mafakihi wame­sema kuwa dhihari ni haramu hilo halina shaka yoyote, kwa sababu Mwenyezi Mungu ameisifu kuwa ni ya kuchukiza na ni uwongo, lakini haina dhambi kwa anayeifanya, kwa sababu ameikutanisha na msamaha.

Lakini kauli ya kutokuwa na dhambi ameirudi Shahidi wa pili kwa kuse­ma kuwa msamaha katika Aya ni wakiujumla na hauhusiki na dhihari.

Na wale wanaowafanyia Dhihar wake zao kisha wakarudi kuachana na yale waliyoyasema, basi ni kumwacha huru mtumwa kabla hawajagusana.

Kurudi na kuyaacha yale waliyoyasema ni wale wanaofanya dhihari kisha wakajuta na kuiacha kauli yao.

Ibn Hisham, katika Mughni anasema: herufi lam inakuja kwa maana ya herufi a’yn (kuachana na) kama ilivyo katika Juz. 12 (11:31). Pia huwa inakuja kwa maana ya herufi fi (katika); kama ilivyo katika Juz. 17 (21:47). Wametofautiana kuhusu kugusana.

Kuna waliosema kuwa ni kugusana kwa maana yake ya kilugha yalivyo. Wengine wakasema ni kuingiliana. Kauli hii haiko mbali na lugha ya Qur’an; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: “Na kama mkiwapa talaka kabla ya kuwagusa…” Juz. 2 (2:237), kwa maana ya kabla ya kuwaingilia; kama walivyoafikina mafakihi

Mnapewa mawaidha kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.

‘Hayo,’ ni hayo ya wajibu wa kafara la dhihari. Makusudio ya mawaidha hapa ni maonyo. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewajibisha kafara la dhihari ili liwe ni onyo na kukemea isifanyike, kwa sababu ni jambo la kuchukiza na ni uwongo. Na Mwenyezi Mungu anamjua muasi na mtiifu na kumfanyia kila mmoja stahiki yake.

Na asiyepata mtumwa wa kumkomboa,basi afunge miezi miwili ya kufuatana kabla hawajagusana. Na asiyeweza basi awalishe maskini sitini.

Wameafikiana kwamba mwenye kumwambia mkewe: Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu,’ haiwi halali kwake kumwingilia mke huyo, mpaka atoe kafara, kwa kumwacha huru mtumwa, akishindwa kupa­ta mtumwa, afunge miezi miwili ya kufuatana na akishindwa kufunga basi awalishe masikini sitini. Vile vile wameafikiana kuwa akimwingilia kabla ya kutoa kafara atakuwa ameasi, lakini Shia Imamiya wamewajibisha kafara mbili kwa hilo.

Shia Imamiya pia wameweka sharti la kuweko waadilifu wawili watakaosikia kauli ya mume na kuwa mke awe katika twahara (asiwe hedhini) ambayo hakuingiliwa na mumewe; sawa na yalivyo masharti ya talaka; kama ambavyo wahakiki miongoni mwao wameweka pia sharti la kuwa awe amekwishawahi kuingiliwa na mumewe; vinginevyo itakuwa hakuna dhihari. Ufafanuzi uko kwenye vitabu vya Fiqh.

Hayo ni hivyo ili mumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameisahilisha sharia kwa waja wake ili waiami­ni na ili iwe ni hoja wazi kwa yule anayeipinga sharia.

Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikeuke.

Na kwa makafiri iko adhabu chungu kwa kupinga kwao sharia ya Mwenyezi Mungu na hukumu yake. Ndani yake kuna ishara kuwa mwenye kuhalifu sharia ya Mwenyezi Mungu basi anahukumiwa kuwa ni kafiri.

إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ كُبِتُوا كَمَا كُبِتَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَقَدْ أَنزَلْنَا آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٥﴾

5. Hakika wanaopingana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, watadhalilishwa kama walivyodhalilishwa wale waliokuwa kabla yao. Na tulik­wishateremsha Ishara zilizo wazi. Na makafiri watapata adhabu ifedheheshayo.

يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا أَحْصَاهُ اللَّـهُ وَنَسُوهُ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٦﴾

6. Siku atapowafufua Mwenyezi Mungu, na awaambie yale waliyoyatenda. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti, na wao wameyasahau! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhu­dia kila kitu.

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٧﴾

7. Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi? Hauwi mnong’ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wanne wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yuko pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyoyatenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نُهُوا عَنِ النَّجْوَىٰ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَيَتَنَاجَوْنَ بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّـهُ وَيَقُولُونَ فِي أَنفُسِهِمْ لَوْلَا يُعَذِّبُنَا اللَّـهُ بِمَا نَقُولُ حَسْبُهُمْ جَهَنَّمُ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٨﴾

8. Kwani huwaoni wale waliokatazwa kunong’ona, kisha wakayarudia yale uadui, na ya kumwasi Mtume? Na wakikujia hukuamkia sivyo anavyokuamkia Mwenyezi Mungu. Na husema katika nafsi zao: Mbona Mwenyezi Mungu hatuadhibu kwa haya tuyasemayo? Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Ni marejeo mabaya sana.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَنَاجَيْتُمْ فَلَا تَتَنَاجَوْا بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَتَنَاجَوْا بِالْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٩﴾

9. Enyi mlioamini! Mnapo nong’onezana. Msinong’onezane kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na kumuasi Mtume. Bali nong’onezaneni kwa kutenda mema na takua. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwake mtakusanywa.

إِنَّمَا النَّجْوَىٰ مِنَ الشَّيْطَانِ لِيَحْزُنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَلَيْسَ بِضَارِّهِمْ شَيْئًا إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٠﴾

10. Kwa hakika minong’ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe walioamini, na wala hatawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi waumini wamtegemea Mwenyezi Mungu. Basi waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu.

KUNONG’ONEZANA

Aya 5 – 10

MAANA

Hakika wanaopingana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, watad­halilishwa kama walivyodhalilishwa wale waliokuwa kabla yao.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja mipaka yake, sasa anampa onyo yule atakayeipetuka mipaka na akampa sifa ya adui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kwamba adhabu yao ni kushindwa na hizaya; kama ilivyokuwa adhabu ya umma zilizotangulia.

Na tulikwishateremsha Ishara zilizo wazi. Na makafiri watapata adhabu ifedheheshayo.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amesimamisha hoja waziwazi za kuweko Yeye na unabii wa mjumbe wake(s.a.w. w ) na akabainisha halali na haramu. Dalili hizi zinafahamisha kuwa kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume ni wajibu na

kwamba mwenye kuhalifu anastahili adhabu itakayomfedhehesha,siku atapowafufua Mwenyezi Mungu, na awaambie yale waliyoyatenda. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti, na wao wameyasahau! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu.

Kesho Mwenyezi Mungu atawakusanya kwa ajili ya hisabu na malipo kwa yale walioyafanya. Mkosefu akisahau madhambi Alioyafanya yote au baadhi yake, Mwenyezi Mungu anakuwa ameyajua yote na atamfedhehe­sha nayo na kumwonjesha adhabu kwa haki na uadilifu wala hatadhulumiwa.

Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyo katika mbin­gu na vilivyo katika ardhi?

Hujui ewe Muhammad kwamba kwa Mwenyezi Mungu hakifichiki chochote mbinguni na ardhini. Vile vile anajua kuwaHauwi mnong’ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wa nne wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yuko pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyoyatenda.

Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘wala wachache kuliko hao,’ ni ishara ya chini ya watatu, na ‘wala walio wengi zaidi,’ ni zaidi ya watano. Kundi la wafasiri wamesema kuwa watu katika mayahudi na wanafiki walikuwa wakikutana kupanga njama dhidi ya Mtume na maswahaba wake, ndio ikawashukia Aya hii.

Hili haliko mbali, kwa sababu dhahiri ya Aya inalitilia nguvu, pia mazowea ya hali. Kwani kusengenya na siri ni mazowea ya wanafiki kila wakati na kila mahali.

Vyovyote iwavyo, maana ni kuwa, usihofu ewe Muhammad njama zao kwako na kwa maswahaba wako! Utahofia nini nawe una yakini kwamba Mwenyezi Mungu anajua siri na dhahiri na minong’ono ya wenye kujificha wawe wachache au wengi? Vile vile unajua kuwa atawakusanya siku ya Kiyama na kuwaadhibu kwa yale waliyokuwa wakiyafanya?

Makusudio ya kutaja tatu na tano ni kiasi cha kutoa mfano tu.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu, hata kutingishika mdomo na kurudia maneno.

Kwani huwaoni wale waliokatazwa kunong’ona, kisha wakayarudia yale waliyokatazwa, na wakanong’onezana juu ya mambo ya dhambi, na ya uadui, na ya kumwasi Mtume?

Hii inaashiria kwamba Mtume(s.a.w. w ) alikuwa amewanasihi wale wenye kujifichaficha na minong’ono kuwa wakome wala wasirudie, lakini hawakukubali, bali walirudia kwa jeuri na inadi. Basi Mwenyezi Mungu akawakaripia kwa tamko la kushangaa alilomwelekezea Mtume wake mtukufu; kama unavyomwambia mwenzako: Unamuona huyu asivyokuwa na adabu?

Na wakikujia hukuamkia sivyo anavyokuamkia Mwenyezi Mungu.

Kuna riwaya kuwa watu katika mayahudi waliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) wakamwamkia: “Assaamu alayka ya Abalqasim” wakimaanisha mauti yakufikie ewe babake Kasim. Mtume naye akawajibu: “Waalykum!” na juu yenu pia. Ndio ikashuka Aya hii.

Sisi hatuna shaka na usahihi wa riwaya hii, kwa sababu inasadikisha zaidi ukosefu wa adabu wa mayahudi na chuki yao kwa haki na watu wake.

Na husema katika nafsi zao: Mbona Mwenyezi hatuadhibu kwa haya tuyasemayo?

Walifanya hivi kisha wakasema: Lau Muhammad angelikwa Nabii basi Mwenyezi Mungu angelituteremshia adhabu kwa jeuri tuliyomfanyia Nabii wake.

Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Ni marejeo mabaya sana.

Msiwe na haraka na hali itakayokuwa, kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaandalia Jahannam ambayo ni marejeo mabaya kabisa na kwamba kesho kuanzia leo ni karibu.

Enyi mlioamini! Mnaponong’onezana msinong’onezane kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na kumuasi Mtume. Bali nong’onezaneni kwa kutenda mema na takua. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwake mtakusanywa.

Watu wengi huwa wanamwamini Mwenyezi Mungu, wakafunga kwa ajili yake na wakaswali kiukweli na haki si kwa uongo wala ria, lakini mara nyingi wanasahau imani hii na wakanong’ona kwa mambo ya dhambi, sawa na wanavyofanya wanafiki na makafiri.

Maneno katika Aya hii yanaelekezwa kwa hawa walioghafilika na imani yao; na Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawaamuru wanong’one kwa mambo ya heri, kwani hilo ndio laiki ya waumini; hawanong’onezani kwa shari kama makafiri na wanafiki.

Kama kwamba Aya hii imezishukia baadhi ya dola zinazojionyesha kuwa ni za kiislamu huku zikiwasaidia waisrail na kuwasheheneza aina kwa aina za silaha ili wawaue wanawake na watoto wadogo; wavunje majumba na kuwafukuza wakazi wake kutoka kwenye miji yao. Ni unafiki gani mkub­wa zaidi ya mtu kudai kuwa yeye ni mwislamu anayemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na huku anasaidiana na maadui wa Mwenyezi Mungu na wa utu; tena anapongeza dhulma na unyanyasaji?

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewakataza waumini kusaidiana na madhalimu hata kama ni kwa neno la siri, na akawaamuru kupambana nao kwa kauli na vitendo kwa siri na kwa jahara.

Kwa hakika minong’ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe walioamini, na wala hatawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Makusudio ya minong’ono hapa ni minong’ono ya shari na ya dhambi. Maana ni kuwa shetani anawahadaa wafuasi wake kwa minon’ono miovu kwa kukusudia kuwaudhi waumini na kuwahuzunisha, lakini waumini wako katika ngao madhubuti hayawapati madhara yoyote isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Basi waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu katika mambo yao yote wala wasiogope madhara kutoka kwa yoyote au kungojea manufaa isipokuwa kutoka kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu tu. Na mwenye kumtegemea shetani atamwongoza kwenye maangamizi.


2

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قِيلَ لَكُمْ تَفَسَّحُوا فِي الْمَجَالِسِ فَافْسَحُوا يَفْسَحِ اللَّـهُ لَكُمْ وَإِذَا قِيلَ انشُزُوا فَانشُزُوا يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١١﴾

11. Enyi mlioamini! Mkiambiwa: fanyeni nafasi katika vikao, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atawafanyia nafasi. Na mki­ambiwa: ondokeni, basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua daraja walioamini miongoni mwenu, na waliope­wa ilimu. Na Mwenyezi Mungu kwa mnayoyatenda anazo habari.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَاجَيْتُمُ الرَّسُولَ فَقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَةً ذَٰلِكَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَأَطْهَرُ فَإِن لَّمْ تَجِدُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢﴾

12. Enyi mlioamini! Mnapo­nong’onezana na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kunong’ona kwenu. Hiyo ni kheri kwenu na usafi zaidi. Na ikiwa hamkupata cha kutoa, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

أَأَشْفَقْتُمْ أَن تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَاتٍ فَإِذْ لَمْ تَفْعَلُوا وَتَابَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٣﴾

13. Mnachelea kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kunong’ona kwenu? Ikiwa hamkufanya hayo, na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu, basi simamisheni Swala, na toeni Zaka, na mtiiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu ana habari kwa mnayoyatenda.

FANYENI NAFASI MWENYEZI MUNGU ATAWAFANYIA NAFASI

Aya 11 – 13

MAANA

Enyi mlioamini! Mkiambiwa: fanyeni nafasi katika vikao, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atawafanyia nafasi.

Maswahaba walikuwa wakiwahi kwenye vikao vya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) na wakipupia kuwa karibu naye. Mara nyingi vikao vilikuwa na msongamano wa watu. Aliyewahi hakuwa akimpa nafasi anayekuja, basi analazimika kurudi au kukalia nyayo zake. Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawafundisha adabu ya kiislamu; Akawaamuru kuwapa nafasi wengine kwenye vikao na akawaahidi kuwapa nafasi Peponi.

Na mkiambiwa: ondokeni, basi ondokeni.

Kwanza Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwaamuru waliokaa wawatengenezee nafasi wengine; kisha akawaamuru kumsikiliza Mtume(s.a.w. w ) akiwataka kuachia nafasi wengine ikiwa nafasi haitoshi.

Kuna riwaya inayosema kuwa Mtume(s.a.w. w ) alikuwa akiwasimamisha baadhi ili wakae wale waliotangulia kwenye mambo mema, na ikawa wengine wanaonyesha kuchukia kwenye nyuso zao. Lakini baada ya kushuka Aya hii walifanya heshima na kuwapisha ndugu zao kwa moyo safi kabla ya kuamuriwa na Mtume(s.a.w. w ) .

Kuna tafsiri nyingine zinazosema kuwa maana ni: mkiambiwa ondokeni kwenda kwenye mambo ya heri basi itikieni. Hili haliko mbali, kwa sababu amri inaenea kwenye maana yote; iwe ni kutoa nafasi, kufanya jihadi au mengineyo.

Ndio! Katika adabu za Qur’an ni mtu kumfanyia nafasi ndugu yake au kumpisha pale alipokaa yeye, lakini sio adabu wala maadili mema kwa yule aliyekuja kumwondoa mahali pake yule aliyekaa.

Mtume(s.a.w. w ) alikuwa akikaa mwisho walipokaa watu, ila ikiwa mwenye kikao atamtaka mtu ampishe ndio anamwitikia, lakini vile vile haitakikani kwa mwenye kikao kumwondoa mtu isipokuwa kwa sababu ya maana; kama vile aliyekaa kukikosea adabu kikao au ikiwa aliyekuja ana shani na daraja mbele ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

Mwenyezi Mungu atawainua daraja walioamini miongoni mwenu, na waliopewa ilimu. Na Mwenyezi Mungu kwa mnayoyatenda ana habari.

Mwenyezi Mungu anawajua watu bora na anajua daraja za ubora naye anampa kila mwenye fadhila haki yake. Bora zaidi katika watu ni yule aliye zaidi kujichunga na aliyoyaharimisha Mwenyezi Mungu. Ikiwa pamoja na kujichunga hivi ana mwamko na ilimu basi atakuwa juu ya walio juu.

Hakuna mwenye shaka kwamba kumwadhimisha aliyeadhimishwa na Mwenyezi Mungu ni faradhi ya lazima. Kuna Hadith inayosema kuwa Mtume alikuwa akiwatukuza watu wa Badr na kuwatanguliza juu ya wengine. Siku moja waliingia baadhi yao kwenye majilisi yake wakakuta watu wamesongamana kwake wala hakuna yeyote aliyewapisha.

Mtume(s.a.w. w ) akawaambia wale waliokaribu yake: ni nani ambaye si katika watu wa Badr. Simama ewe fulani na wewe ewe fulani, na akawakalisha watu wa Badr.

Riwaya hii inaafikiana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Mwenyezi Mungu atawainua daraja walioamini miongoni mwenu…”

KUKAA MBELE KWENYE KIKAO

Mimi ninaposoma makala ya gazeti inayofungamana na maudhui ya Aya yoyote katika Qur’an Tukufu huwa ninaiweka kwenye faili maalum, mpaka nikifikia kuifasiri basi ninairudia ile makala na kuitolea ushahidi.

Pia huwa ninaashiria jina la gazeti na tarehe yake, kwa sababu kizazi kipya wanakinaika na magazeti zaidi kuliko rejea nyingine; kwa mfano kama kwenye Juz. 13 (13:5-7) kifungu cha ‘wanaoamini maada na maisha baada ya mauti.’ Juz. 15 (17: 82-85), kfungu cha: ‘Mwenyezi Mungu na ilimu ya chembe hai,’ Juz. 23 (38: 65-88), kifungu cha: Uislamu na msichana wa kiingereza,’ na Juz. 24 (41:37-46) kifungu cha ‘safari ya mwezini.’

Basi siku moja nilisoma mojawapo ya majarida ya wanasiasa wakubwa kuhusu meza ya maelewano kuwa ni nani atakayekaa mbele, ni nani atakayekuwa nyuma na ni ujumbe upi utatangulia kwenye chumba cha mkutano kabla ya mwingine.

Katika mfano alioutoa mwandishi ni ule wa mwaka 1945 baada ya vita ya pili ya dunia: Waliafikiana Churchill, Stalin na Roosevelt kukutana kwa majadiliano ya mapatano mjini Budabest, lakini wakatofautiana kuwa ni nani atakayeingia kwanza kwenye ukumbi wa mkutano. Ubishi huu uliendelea kwa muda kisha suluhisho likawa wakutane kwenye ukumbi wenye milango mitatu ili wote waingie kwa wakati mmoja.

Nimeikumbuka makala hiyo na kuileta hapa ili aone msomaji kuwa Uislamu unaipa kipaumbele ilimu na ikhlasi. Haya ndio maendeleo ya haki na uadilifu kwa maana yake sahihi, lakini kuwatukuza wanaotengeneza mauti, wanaomiliki makombora ya Menotman na CC, na silaha nyingine­zo za maangamizi, hakuna uzito wowote isipokuwa katika sharia ya shetani na maendeleo ya vita na uchokozi.

Enyi mlioamini! Mnaponong’onezana na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kunong’ona kwenu. Hiyo ni kheri kwenu na usafi zaidi. Na ikiwa hamkupata cha kutoa, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

Sioni tafsiri nzuri zaidi ya Aya hii kuliko ile ya Muqatil bin Hayan, ali­posema: “Matajiri waliwazidi mafukara kwenye vikao vya Mtume(s.a.w. w ) - hii ndio hali yao kila mahali na kila wakati - wakazidisha kum­nong’oneza Mtume mpaka akachukia kukaa kwao sana, ndio Mwenyezi Mungu akaamuru sadaka.

Basi matajiri wakajizuia kutoa na mafukara wakakosa cha kutoa, wakamlilia hali Mtume na kutamani kutoa lau wan­gelikua nacho na kukifikisha kwenye vikao vya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) . Hapo daraja ya mafukara ikazidi, mbele ya Mwenyezi

Mungu na daraja ya matajiri ikaanguka.” Katika tafsiri kadhaa ikiwemo Tafsiru ttabari na Tafsiru rrazi imeelezwa kuwa hakuifanyia kazi Aya hii isipokuwa Ali bin Abu Twalib(a.s ) . Alikuwa na dinar moja akaivunja zikawa dirham 10, akawa kila anapotaka kusemezana na Mtume hutoa sadaka dirhamu moja. Kisha hukumu hiyo ikaondolewa kabla ya kuitekeleze mwingine asiyekuwa Ali.

Mwenye Tafsir Ruhulbayan anasema: “Imepokewa kutoka kwa Imran kuwa Yeye amesema: Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Imran kuwa amesema: Ali alikuwa na mambo matatu, lau ningelikuwa na mojawapo kati ya hayo ingelikuwa bora kwangu kuliko wanyama wekundu: Kumuoa Fatima, kupewa bendera siku ya Khaybar na Aya ya mnong’ono.”

Mnachelea ufukara kuwa hamtaweza kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kunong’ona kwenu? Ikiwa hamkufanya hayo, na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu, basi simamisheni Swala, na toeni Zaka, na mtiii­ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Ilipokuwa uzito kwa matajiri kutoa sadaka kwa kuhofia kuisha mali yao, na Mwenyezi Mungu akalijua hilo, na wakajua kuwa wakati wa Mtume sio wao peke yao tu, ni wakufikisha ujumbe na kupanga mambo ya Waislamu, ndio Mwenyezi Mungu akaruhusu kunong’ona na Mtume bila ya kutoa sadaka na akawasamehe wale wasiotoa, lakini wasizembee swala, Zaka na mengineyo.

Na Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.

Haufichiki kwake wema wa mwenye kufanya wema na uovu wa mwenye kufanya uovu na atamlipa kila mmoja stahiki yake.

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ تَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مَّا هُم مِّنكُمْ وَلَا مِنْهُمْ وَيَحْلِفُونَ عَلَى الْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٤﴾

14. Huwaoni wale waliofanya urafiki na watu ambao Mwenyezi Mungu amewa­kasirikia? Hao si katika nyinyi, wala si katika wao. Na huapa kwa uwongo, na hali ya kuwa wanajua.

أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٥﴾

15. Mwenyezi Mungu amewaan­dalia adhabu kali. Kwa haki­ka waliyokuwa wakiyatenda ni maovu kabisa.

اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ فَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٦﴾

16. Wamefanya viapo vyao ni ngao, na wakaipinga Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi wata­pata adhabu ifedheheshayo.

لَّن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١٧﴾

17. Haitawafaa kitu mali yao wala watoto wao kwa Mwenyezi Mungu, na wao ndio watu wa motoni, wao watadumu humo.

يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا فَيَحْلِفُونَ لَهُ كَمَا يَحْلِفُونَ لَكُمْ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْكَاذِبُونَ ﴿١٨﴾

18. Siku atakayowafufua Mwenyezi Mungu wote, wamuapie kama wanavyo­waapia nyinyi. Na watadhani kuwa wamepata kitu! Ehe! Kwa hakika hao ndio waon­go.

اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمُ الشَّيْطَانُ فَأَنسَاهُمْ ذِكْرَ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ الشَّيْطَانِ أَلَا إِنَّ حِزْبَ الشَّيْطَانِ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٩﴾

19. Shetani amewatawala na akawasahaulisha dhikr ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio kundi la Shetani. Ehe! hakika kundi la Shetani ndilo lenye kuhasirika.

WAMEFANYA VIAPO VYAO NI NGAO

Aya 14 – 19

MAANA

Huwaoni wale waliofanya urafiki na watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia? Hao si katika nyinyi, wala si katika wao. Na huapa kwa uwongo, na hali ya kuwa wanajua.

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume(s.a.w.w) . Waliofanya urafikki ni wanafiki, waliokasirikiwa na Mwenyezi Mungu ni mayahudi na nyinyi, ni nyinyi waislamu. Maana ni kuwa hebu niambie ewe Muhammad kuhusu wanafiki! Wamefanya urafiki na mayahudi na wakapanga njama nao dhidi ya waislamu na uislamu; wakiwa na uhakika kuwa wao si waisalamu wala si katika mayahudi, ni vizabizabina, huku hawako wala kule hawako.

Wameapa kwa kukusudia uwongo kuwa ni waislmu na kwamba hawakuse­ma kitu wala kupanga njama na mayahudi. Kwa ajili ya unafiki wao na viapo vyao vya uwongo,Mwenyezi Mungu amewaandalia adhabu kali. Kwa hakika waliyokuwa wakiyatenda ni maovu kabisa . Kila mwenye kudhihirisha kinyume na yaliyo kwenye dhamiri yake basi ni muovu kwa kauli yake na vitndo vyake, kwa sababu amejitoa kwenye dhati yake na hakika yake.

Wamefanya viapo vyao ni ngao, na wakaipinga Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watapata adhabu ifedheheshayo.

Yaani wanafiki wanajaribu kufanya njama zao kwa viapo vya uwongo na kujikinga navyo; huku wakiwahadaa wale wanaotaka uongofu na kuwazuia na malengo yao, lakini Mwenyezi Mungu hafichwi na kinga yoyote wala dhamiri zozote. Basi ameipasua sitara yao duniani, na Akhera watapata adhabu ya kufedhehesha.

Haitawafaa kitu mali yao wala watoto wao kwa Mwenyezi Mungu, na wao ndio watu wa motoni, wao humo watadumu.

Walipata fursa katika maisha ya duniani, lakini wakaichezea, wala hakuna kitu kwa yule mwenye kuvuta muda na kupuuza isipokuwa adhabu. Na si mali wala watoto inayoweza kurudisha yaliyopita.

Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 4 (3:116).

Siku atakayowafufua Mwenyezi Mungu wote, wamuapie kama wanavyowaapia nyinyi. Na watadhani kuwa wamepata kitu! Ehe! Kwa hakika hao ndio waongo.

Siku ya Kiyama, waja watakuwa na hali mbalimbali; kuna wengine watahurusiwa kuzungumza. Basi Mwenyezi Mungu atakapowapa fursa ya kuzungumza, wakosefu, watamuapia kwa uwongo, kama walivyokuwa wakimwapia Nabii na waislamu duniani; wakiamini kuwa viapo vyao vitawakinga na adhabu. Vipi iwe hivyo na hali Mwenyezi Mungu anajua kuwa wao ni waongo katika imani zao na itikadi zao?

Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:22).

Shetani amewatawala na akawasahaulisha dhikr ya Mwenyezi Mungu.

Shetani wa matamanio aliwaita kwenye upotevu na ufisadi nao wakamwitikia, basi wakapofuka na uwongofu.

Hao ndio kundi la Shetani. Ehe! hakika kundi la Shetani ndilo lenye kuhasirika.

Kwa sababu, vyovyote vile iwavyo, mwenye kumfanya shetani ni kiongozi wake, atamwongoza kwenye kila uovu na maangamizi, iwe kesho au kesho kutwa; hata kama atajisheheni mabomu na makombora.

إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ أُولَـٰئِكَ فِي الْأَذَلِّينَ ﴿٢٠﴾

20. Hakika wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio miongoni mwa madhalili wa mwisho.

كَتَبَ اللَّـهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٢١﴾

21. Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mitume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٢٢﴾

22. Hupati watu wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanapendana na wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au wato­to wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika mabustani yapiti­wayo na mito chini yake. Humo watadumu. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio kundi la Mwenyezi Mungu. Ehe! Hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa.

BILA SHAKA NITASHINDA MIMI NA MITUME WANGU

Aya 20 – 22

MAANA

Hakika wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio miongoni mwa madhalili wa mwisho.

Aya hii ina mshabaha wa jibu la swali la kukisiwa, kwamba maadui wa Mwenyezi Mungu wanaishi wakiwa na nguvu ya maandalizi na idadi, wakiendelea kuwatesa watu wa Mwenyezi Mungu kwa mauaji na kuwa­torosha, vipi Mwenyezi Mungu anawapa muda na kuwapa nguvu?

Aya inajibu kuwa washari ndio viumbe dhalili zaidi kuanzia mwanzo hadi mwisho, kwa sababu mwisho wao ni hizaya na udhalili duniani na Akhera. Hapa duniani ni kuwa Mwenyezi Mungu anawaadhibu kwa mikono ya waliowema:

قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّـهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ ﴿١٤﴾

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awa­fedheheshe, na awanusuru muwashinde na avipoze vifua vya kaumu ya waumin.” Juz. 10 (9:14).

Ama adhabu ya Akhera hiyo ni kali na ni kubwa zaidi.

Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mitume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.

Ushindi utakuwa Akhera, na vile vile utakuwa duniani kwa upanga, adhabu ya kutoka mbinguni, hoja na dalili au kwa kudumu utajo.

Tazama Juz. 17 (38-41) kifungu cha: “Mwenyezi Mungu huwakinga walioamini.” Vile vile Juz. 26 (47:7).

Hupati watu wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanapendana na wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao.

Haiwezekani kabisa imani ichanganyike na mahaba ya makafiri. Itakuwaje hivyo na hali Mwenyezi Mungu ndiye Aliyesema:

مَّا جَعَلَ اللَّـهُ لِرَجُلٍ مِّن قَلْبَيْنِ فِي جَوْفِهِ ﴿٤﴾

“Mwenyezi Mungu hakumwekea mwanamume nyoyo mbili ndani yake.” Juz. 21 (33:4).

Kuna kauli mashuhuri kutoka kwa Imam Ali(a.s ) kuwa rafiki wa adui ni adui. Pia akasema: “Tulikuwa pamoja na Mtume(s.a.w.w) mapigano yakiendela kwa mababa, watoto, ndugu na jamaa. Kila msiba na shida haukutuzidisha isipokuwa imani na kuendelea kwenye haki na kusalimu amri.” Hayo tumeyazungumzia kwa ufafanuzi zaidi kwenye Juz.4 (3:28).

Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake.

‘Hao’ ni ni wale ambao imani yao haiathiriki hata kwa mababa na mama zao. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu amethibitishia imani katika nyoyo za wenye ikhlasi na akawapa nguvu kwa hoja: “Mwenyezi Mungu huwaimarisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika Akhera.” Juz. 13 (14:27).

Na atawaingiza katika Mabustani yapitiwayo na mito chini yake. Humo watadumu. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye.

Maana ya Mwenyezi Mungu kumridhia mja wake ni kumpa fadhila zake, na maana ya mja kumridhia Mola wake ni kuridhia aliyompa. Ibn Al-ara­biy, anasema katika Futuhat: “Mwenyezi Mungu huridhia amali chache ya mja wake na wao wanaridhia thawabu chache walizopata kutoka kwa Mola wao, kwani kadiri Mwenyezi Mungu anavyotoa ni vichache kulingana na vilivyoko kwake.”

Lakini hivi alivyoviita vichache Ibn al-arabiy, ni vichache kwa Mwenyezi Mungu Mtufu na ni vingi kwa waja. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Ili amzidishie ziada nyingi.” Juz. 2 (2:245).

Hao ndio kundi la Mwenyezi Mungu. Ehe! Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa.

Aya hii ni mkabala wa Aya 19 ya Sura hii tuliyo nayo inayosema: “Hao ndio kundi la Shetani. Ehe! hakika kundi la Shetani ndilo lenye kukhasirika.”

Kwa ufupi ni kuwa mtu kadiri atakavyokuwa na uwezo, lakini hawezi kuchanganya kumridhisha Mwenyezi Mungu na kuwaridhisha maadui wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Akiwaridhisha atakuwa amemghadhabisha Mwenyezi Mungu na akimridhisha Mungu atakuwa amewaghadhibisha maadui. Wao hawaridhii isipokuwa yule aliye katika hali yao, kwa ushahi­di wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtufu:

وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ﴿١٢٠﴾

“Hawatakuwa radhi nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila yao.” Juz. 1 (2:120).

Katika Hadith Mtume(s.a.w.w) anasema:“Ewe Mwenyezi Mungu usini­jaalie muovu wala fasiki kwangu, kwani nimekuta katika yale uliyatolea wahyi kuwa: “Hupati watu wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanapendana na wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake.”

MWISHO WA SURA YA HAMSINI NA NANE: AL–MUJADALA


3

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Hamsini Na Tisa: Surat Al-Hashr. Imeshuka Madina. Ina Aya 24.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١﴾

1. Vinamsabihi Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

هُوَ الَّذِي أَخْرَجَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِن دِيَارِهِمْ لِأَوَّلِ الْحَشْرِ مَا ظَنَنتُمْ أَن يَخْرُجُوا وَظَنُّوا أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمْ حُصُونُهُم مِّنَ اللَّـهِ فَأَتَاهُمُ اللَّـهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُوا وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ يُخْرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيْدِيهِمْ وَأَيْدِي الْمُؤْمِنِينَ فَاعْتَبِرُوا يَا أُولِي الْأَبْصَارِ ﴿٢﴾

2. Yeye ndiye Aliewatoa walioku­furu miongoni mwa Watu wa Kitabu katika nyumba zao wakati wa mkusanyiko wa kwanza. Hamkudhani kuwa watatoka, nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda na Mwenyezi Mungu. Lakini Mwenyezi Mungu aliwafikia kwa mahali wasipopatazamia, na akatia woga katika nyoyo zao. Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini. Basi zingatieni enyi wenye busara!

وَلَوْلَا أَن كَتَبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمُ الْجَلَاءَ لَعَذَّبَهُمْ فِي الدُّنْيَا وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابُ النَّارِ ﴿٣﴾

3. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu asingeliwaandikia uhamisho, angeliwaadhibu katika dunia. Na katika Akhera watapata adhabu ya Moto.

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَمَن يُشَاقِّ اللَّـهَ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٤﴾

4. Hayo ni kwa sababu walimpin­ga Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mwenye kumpinga Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

مَا قَطَعْتُم مِّن لِّينَةٍ أَوْ تَرَكْتُمُوهَا قَائِمَةً عَلَىٰ أُصُولِهَا فَبِإِذْنِ اللَّـهِ وَلِيُخْزِيَ الْفَاسِقِينَ ﴿٥﴾

5. Mtende wowote mlioukata au mliouacha umesimama vile vile juu ya mashina yake, basi ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kwa kuwahizi mafasiki.

VINAMSABIHI MWENEYEZI MUNGU

Aya 1 – 5

KISA CHA BANI NADHIR KWA UFUPI

Aya hizi zinahusiana na ushindi wa Mtume(s.a.w.w) dhidi ya mayahudi wa Bani Nadhir. Hawa walikuwa wakiishi viungani mwa Madina. Mtume(s.a.w.w) alipohamia huko, aliwekeana nao mkataba wa amani. Waislamu walipowashinda Makuraishi vita vya Badr, Bani Nadhir walifurahi sana, lakini waliposhindwa kwenye vita vya Uhud walivunja makataba na waka­panga njama za kummaliza Mtume na kiongozi wao, Kaa’b bin Ashraf akaungana na Abu Sufyan dhidi ya Nabii(s.a.w.w) .

Inasemekana kuwa Kaa’b alimshambulia Mtume kwa mashairi, Mtume akamwamuru mmoja wa maswahaba zake kumuua. Kisha Mtume(s.a.w.w) akawaendea Bani Nadhir na akawaamuru kutoka Madina, lakini wanafiki wakiongozwa na Abdallah bin Ubayya, waliwatumia ujumbe kuwa msikubali, sisi tuko pamoja nanyi. Basi wakawa na matumaini na wakashikilia kupigana. Hapo Mtume akawahusuru kwa muda wa siku 21, kama yanavyosema baadhi ya mapokezi.

Mtume(s.a.w.w) aliamuru kukatwa baadhi ya mitende yao. Hakuna yeyote katika wanafiki aliyejaribu kuwasaidia. Basi wakalazimika kusalimu amri, na Mtume akasuluhishana nao kuwa watoke Madina; kila watu watatu wachukue ngamia mmoja atakayewabebea wanachotaka. Basi wakakubali na wakatoka Madina kabisa.

Sura hii imewashukia wao. Ibn Abas alikuwa akiita Sura hii Sura ya Bani Nadhir.

MAANA

Vinamsabihi Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na vilivyo kati­ka ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Vitu vyote vilivyoko vinamsabihi (vinamtakasa) na kutukuza uweza wake Mwenyezi Mungu na hekima yake, kwa lugha ya maneno na lugha ya hali. Umetangulia mfano wake katika Juz. 27 (57:1).

Yeye ndiye Aliyewatoa waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu katika nyumba zao wakati wa mkusanyiko wa kwanza.

Makusudio ya waliokufuru hapa ni Bani Nadhir. Wametofautiana wafasiri kuhusu mkusanyiko wa kwanza. Razi anasema: “Ibn Abbas na wafasiri wengi wamesema kuwa maana ya mkusanyiko wa kwanza ni kuwa hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa watu wa Kitab kutolewa Bara Arabu. Kabla yake walikuwa na nguvu… Hili haliko mbali kwa sababu kutolewa kwa pili kulitokea kwa khalifa wa pili.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwatoa Bani Nadhir kupitia mikononi mwa waislamu. Na hii ilikuwa ni mara ya kwanza kutolewa watu wa Kitabu huko. Na sababu ya kutolewa kwao ni hiyana yao na kuvunja kwao mapatano ya amani waliyowekeana na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) wao wenyewe.

Unaweza kuuliza : Kwanini Mwenyezi Mungu aliwaadhibu kwa kuwatoa na kuchukua mali yao na kuna aina nyingine za kuwaadhibu?

Jibu : Aliwachukulia kwa sharia ya dini yao. Tawrat yao inasema: “Utakaposongea karibu ya mji kwenda kupigana juu yake, ndipo utakapowapigia ukelele wa amani.

Itakuwa utakapokujibu kwa amani, na kukufungulia, ndipo watu wote watakaoonekana humo, watafanya kazi ya shoka, na kukutumikia. Na kama hautaki kufanya amani nawe, lakini utafanya vita juu yako, ndipo uhusuru; na Bwana, Mungu wako, autiapo mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga; lakini wanawake na watoto na wanyama wa mji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa Bwana, Mungu wako” (Kumbukumbu 20:10 -14).

Hakuna mwenye shaka kwamba mwenye kufuata dini au misingi hana budi kufuata hukumu zake zote na kuzitekeleza yeye mwenyewe kabla ya kutekelezea mwenginewe. Tena Nabii(s.a.w.w) aliwahurumia Bani Nadhir, kwa sababu hakuwaua wanaume wao wala kuwateka wanawake na watoto; kama ilivyo nukuu ya Tawrat yao.

Hayo tumeyazungumzia kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 21 (33: 16-20), kifungu cha ‘Je, Muhammad aliwadhulumu Bani Quraydha?’

Hamkudhani kuwa watatoka, nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda na Mwenyezi Mungu.

Yaani waislamu hawakutegemea kabisa kuwa Bani Nadhir watatoka majumbani mwao na kuwaachia maadui zao waislamu, kutokana na inadi yao na nguvu walizokuwa nazo kwa uwezo na idadi yao.

Vile vile Bani Nadhir walikuwa wakijiamini kuwa wana nguvu na uwezo kuwa ni ngome isiyoingiliwa na mkono wowote. Lakini ulikuwa ni uwezo na ngome ya khiyana, haiwezi kumlinda mwenye kuikimbilia.

PROPAGANDA ZA UPOTOFU NA WAKATI MNASABA

Lakini Mwenyezi Mungu aliwafikia kwa mahali wasipopatazamia, na akatia woga katika nyoyo zao.

Walidhani kuwa ngome zao zitawalinda, lakini Mwenyezi Mungu akatia hofu kwenye nyoyo zao baada ya kumjaza haiba Mtume(s.a.w.w) na jeshi lake. Basi ngome zao zikayayuka, kwa sababu nyoyo ndio msingi wa nguvu zote.

Ndio maana waovu na wafanyibiashara wa silaha wanafanya bidii sana kwenye vita vya nafsi na kutafuta nyenzo na pesa, lakini wame­sahau au wamejitia kusahau kuwa hakuna njia ya kuufikia moyo isipokuwa haki, kheri na hisani. Ikiwa propaganda za upotevu zitapata waungaji mkono basi ni kwa muda, kisha zinafichuka; hata kama muda utakuwa mrefu.

Aliulizwa Charles Mwigizaji maarufu wa tamthilia kuhusu mambo ya maisha: Mtu anahitaji nini ili aweze kutengeneza njia yake ya maisha? Akasema: “Jambo muhimu ni kujua wakati mnasaba.” Nasi tunamwambia Charles: “Ndio hakuna budi ya wakati, lakini ni lazima uwe unanasibiana na masilahi ya kheri sio ya shari, na ya haki sio ya batili. Kwa sababu shari inaondoka pamoja na watu wake, hata kama ni kuchelewa kwa kiasi gani.

Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini.

Badhi ya wafasiri wamesema kuwa makusudio ya kubomoa nyumba ni kuziacha na kwa mikono yao ni kuwa wao ndio sababu ya kuondoka kwao; pale walipovunja maelewano na Mtume. Mikono ya waumini ni ishara ya kuwa waislamu ndio waliowatoa Bani Nadhir majumbani mwao.

Wafasiri wengine wakasema kuwa Bani Nadhir waliziharibu hasa nyumba zao ili zisibakie salama mikononi mwa waislamu, na kwamba waislamu walizipondaponda ngome za mayahudi ili wapate kuwafikia. Tafsiri hii iko karibu na maana na inatiwa nguvu na dhahiri ya Aya; wala haipingani na ile ya kwanza, bali ni natija ya kuondoka mji.

Basi zingatieni enyi wenye busara!

Kuzingatia kitu ni kukirudisha kwenye mtazamo na kukihukumu kwa mfano wake. Mwenyezi Mungu aliwatoa Bani Nadhir majumbani mwao yakiwa ni malipo ya hiyana yao. Basi mwenye akili anatakikana kupata somo na ajiepushe na hiyana na njama, ili yasimfike yaliyowafika.

Na lau kuwa Mwenyezi Mungu asingeliwaandikia uhamisho, angeli­waadhibu katika dunia. Na katika Akhera watapata adhabu ya Moto.

Mwenyezi Mungu amewaadhibu duniani kwa kuwahamisha kutoka majumbani mwao na lau si hivyo angeliwaadhibu kwa kuwaua; kama walivyofanywa Bani Quraydha. Na hawataepuka adhabu ya Moto.

Hayo ni kwa sababu walimpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Walistahili adhabu ya dunia na Akhera, kwa sababu wao walimhalifu Mwenyezi Mungu, wakipituka mipaka yake, na kumwekea uadui Mtume wake.

Na mwenye kumpinga Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

Hili ni onyo na kiaga kwa kila jabari mwenye kiburi.

Mtende wowote mlioukata au mliouacha umesimama vile vile juu ya mashina yake, basi ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kwa kuwahizi mafasiki.

Mtume(s.a.w.w) alikuwa ameamrisha kukatwa baadhi ya mitende ya Bani Nadhir ili kuwakasirisha kwa hilo. Baadhi wakadhani kuwa hiyo ni aina ya uharibifu. Ndio Mwenyezi Mungu akabainisha kwamba kila liliotukia kati­ka kukatwa mitende au kuachwa ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu na wala haitoki kwa Mtume(s.a.w.w) , na lengo ni kuwakasirisha makafiri kwa kuikata na pia kuwakasirisha kwa ile ilioachwa kwa vile watanufaika nayo wale wanaowaona ni maadui zao.

Ieleweke kuwa kukata miti na mengineyo wakati wa vita haifai kuchukuli­wa ni msingi maalum; inaweza kuwa ni wajibu na inaweza kuwa ni hara-mu, kulingana na masilahi ya kumpiga adui; sawa na yanavyovunjwa majumba kwa ajili ya kupitisha barabara, siku ambazo si za vita.

وَمَا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْهُمْ فَمَا أَوْجَفْتُمْ عَلَيْهِ مِنْ خَيْلٍ وَلَا رِكَابٍ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٦﴾

6. Na Aliyoleta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwao hamkuyaendea kwa farasi wala ngamia. Lakini Mwenyezi Mungu huwapa mamlaka Mitume wake juu ya wowote awatakao. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.

مَّا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْ أَهْلِ الْقُرَىٰ فَلِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنكُمْ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٧﴾

7. Aliyoleta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu vijijini ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na maya­tima, na masikini, na mwananjia, Ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri miongoni mwenu. Na anachowapa Mtume kichukueni, na ana­chowakataza jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ ﴿٨﴾

8. Wapewe mafukara wahajiri waliotolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake, na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio wa kweli.

MALI ISIZUNGUKE KWA MATAJIRI

Aya 6–8

MAANA

Na Aliyoleta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwao hamkuyaendea kwa farasi wala ngamia.

Neno ‘Aliyoleta’ tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu Fay’i ambalo ki lugha ya kiarabu lina maana ya kurejesha. Fay’i katika sharia ya kiislamu ni mali waliyoipata waislamu kutoka kwa makafiri bila ya vita. Na ghani­ma (ngawira) ni mali iliyopatikana kwa vita.

Vyovyote iwavyo ni kuwa Aya tuliyo nayo inahusika na mali ya Bani Nadhir. Kwa hiyo maana yanakuwa, mali ya Bani Nadhir ameijaalia ni nyara kwa Mtume wake kuifanyia anavyotaka, waislamu hawana chao hapo kwa vile hawakuitolea jasho lolote.

Lakini Mwenyezi Mungu huwapa mamlaka Mitume wake juu ya wowote awatakao.

Miongoni mwa mamlaka hayo ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alitia hofu kwenye nyoyo za Bani Nadhir kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) ili wasalimu amri yake wakiwa dhalili, bila ya vita.

Na Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.

Miongoni mwa hayo ni kudhalilika watu wenye nguvu, ngome na idadi, mbele ya mtumwa miongoni mwa watumwa wa Mwenyezi Mungu.

Aliyoleta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu vijijini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na mwananjia.

Makusudio ya watu wa vijiji hapa ni makafiri wengine wasiokuwa Bani Nadhir. Maana ni kuwa mali ya fay’i isiyokuwa ya Bani Nadhir ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Mwananjia ni msafiri aliyekatikiwa njiani na kushindwa kurudi kwa watu wake.

Kimsingi ni kuwa mali ya Mwenyezi Mungu ni ya Mtume(s.a.w.w) . Wameafikiana kwa kauli moja, isipokuwa kidogo, kwamba makusudio ya jamaa ni jamaa wa Mtume(s.a.w.w) katika Bani Hashim. Ama kuhusu may­atima, masikini na mwananjia, Shia Imamiya wamesema kuwa wanahusi­ka wa Bani Hashim tu. Wengine wamesema ni yeyote awe Hashim au mwinginewe [1] .

Tumeyazungumzia hayo kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 10 (8:41).

Ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri miongoni mwenu.

Uislamu ni dini ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya watu, inachunga masi­lahi ya wote bila ya kuwabagua. Hautatui tatizo la mtu kwa gharama ya mwingine, wala haumkandamizi mtu ili kumnufaisha mwingine. Wote mbele ya uislamu ni sawasawa.

Haya yanajitokeza kwenye hukumu zake na misingi yake. Miongoni mwa misingi hiyo ni kuwa mali isizunguke kwa matajiri tu. Hiyo ni pamoja na kukataza riba, ghushi na unyonyaji.

Ieleweke kwamba hii haifahamishi kwa karibu wala umbali kuwa uislamu unakubaliana na siasa ya ujamaa au haukubali nayo. Ieleweke tu kuwa uis­lamu katika hukumu zake zote kunajengeka fikra ya uadilifu na usawa na unakubaliana na kila lenye heri ya watu na manufaa yao. Hili ni jambo jingine na kutaifisha mali za watu kuwa mali za uma ni jambo jingine.

Tazama Juz. 4 (3:180-182), kifungu cha: ‘Matajairi ni mawakala sio wenyewe.’

Na anachowapa Mtume kichukueni, na anachowakataza jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

Aya hii imeunganisha baina ya kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na ikawajibisha kuzisikiliza kauli zote mbili, kwa sababu kauli ya Mtume inatokana na wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

“Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni wahyi uliotolewa.” Juz. 27 (53:3-4).

Mwenyezi Mungu amesema katika Aya kadhaa: “Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume.”

Akasema tena:

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦﴾

“Na yeyote mwenye kumwasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi amepotea upotevu ulio wazi.” Juz. 22 (33:36).

Zimekuja Hadith mutawatir kwamba Mtume hakuona ndoto yoyote ila ina­jitokeza kama asubuhi. Waislamu wameafikiana kwa kauli moja kuwa hakuna wahyi wala sharia au Ijtihadi baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ila ikiwa kauli ya mujtahidi inatokana na sharia ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Tazama Juz. 22 (33: 36-40) kifungu cha: ‘kwani utume uliishia kwa Muhammad?’ na Juz. 27 (56: 75-96), kifungu cha ‘Uislamu na wanafikra wakuu wa Ulaya.’

Wapewe mafukara wahajiri waliotolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake, na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Makusudio ya wahajiri hapa ni wale waliohama na Mtume kutoka Makka kwenda Madina kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na thawabu zake na katika kuusaidia Uislamu na kupigana jihadi katika njia yake. Hawa ndio waliofaa zaidi kupewa zaka kwa kutangulia kwao na juhudi yao na pia kuwa na haja nayo.

Anasema Tabari akinukuu kutoka kwa Qatada: “Wahajiri hawa waliacha majumba yao, mali na familia kwa kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Wakachagua Uislamu pamoja na shida zake. Hali ilifikia mtu anafunga jiwe tumboni ili kuuzuia mgongo wake na njaa na kuchim­ba shimo wakati wa kipupwe kuwa ndio blanketi ya kujifunika.

Sijaona wasifu wa maswahaba uliokuwa fasaha zaidi kuliko aliousema Imam Zaynul-abidin(a.s) akiwa anawaombea Mwenyezi Mungu (s.w.t) awatakabalie matendo yao; kwa kusema:

“Ewe Mola! Hasa maswahaba wa Muhammad ambao walikuwa na usuhuba mzuri, wakawa na majaribu mema katika kumsaidia kwake. Wakamwitikia alipowaeleza hoja ya ujumbe wake. Wakapigana na mababa zao na watoto wao ili kuuthibisha unabii wake na wakashinda kupitia kwake. Waliozingirwa na mapenzi wakitarajia biashara isiyo na hasara kwa ajili ya kumpenda kwake.

Wakatengwa na jamaa zao waliposhikamana na kamba yake. Udugu ulikwisha walipotulia chini ya kivuli cha udugu wake. Basi ewe Mola usiwasahu kwa yale waliyoyaacha kwa ajili yako. Na uwa­ ridhie kwa radhi zako.”

Hao ndio wa kweli katika imani na jihadi yao, kwa kauli na vitendo.


4

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٩﴾

9. Na waliofanya maskani na imani yao kabla yao, wanawapenda waliohamia kwao wala hawapati dhiki kati­ka vifua vyao kwa walivyope­wa, na wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kue­pushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٠﴾

10. Na waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu! Hakika Wewe ni Mpole Mwingi wa rehema.

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نَافَقُوا يَقُولُونَ لِإِخْوَانِهِمُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَئِنْ أُخْرِجْتُمْ لَنَخْرُجَنَّ مَعَكُمْ وَلَا نُطِيعُ فِيكُمْ أَحَدًا أَبَدًا وَإِن قُوتِلْتُمْ لَنَنصُرَنَّكُمْ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١١﴾

11. Je, Huwaoni wanaofanya unafiki wanawaambia ndugu zao waliokufuru katika Watu wa Kitabu: Mkitolewa na sisi lazima tutatoka pamoja nanyi, wala hatutamtii yeyote kabisa dhidi yenu.

Na mkipig­wa vita lazima tutawasaidia. Na Mwenyezi Mungu ana­shuhudia kuwa hao hakika bila ya shaka ni waongo.

لَئِنْ أُخْرِجُوا لَا يَخْرُجُونَ مَعَهُمْ وَلَئِن قُوتِلُوا لَا يَنصُرُونَهُمْ وَلَئِن نَّصَرُوهُمْ لَيُوَلُّنَّ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ ﴿١٢﴾

12. Wakitolewa hawatatoka pamoja nao na wakipigwa vita hawatawasaidia. Na kama wakiwasaidia basi watageuza migongo; Kisha hawatanusuriwa.

لَأَنتُمْ أَشَدُّ رَهْبَةً فِي صُدُورِهِم مِّنَ اللَّـهِ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ ﴿١٣﴾

13. Hakika nyinyi ni tishio zaidi katika vifua vyao kuliko Mwenyezi Mungu. Hayo ni kwa kuwa hao ni watu wasio­fahamu.

لَا يُقَاتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرًى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَاءِ جُدُرٍ بَأْسُهُم بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّىٰ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ ﴿١٤﴾

14. Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipokuwa katika vijiji vilivyozatitiwa kwa ngome au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili.

كَمَثَلِ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَرِيبًا ذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٥﴾

15. Ni kama mfano wa waliokuwa kabla yao hivi karibuni. Walionja ubaya wa mambo yao. Nao watapata adhabu iliyo chungu.

WANAWAPENDELEA KULIKO NAFSI ZAO

Aya 9 – 15

MAANA

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kubainisha daraja ya wahajiri katika Aya iliyotangulia, sasa anabainisha daraja ya Answar, kwa kusema, kama ifuatavyo:-

Na waliofanya maskani na Imani yao kabla yao, wanawapenda waliohamia kwao.

Makusudio ya maskani hapa ni Madina. Maana ni kuwa Answar, wenyeji wa Madina, walimsaidia Mtume pamoja na wale waliohama naye. Wakajitolea kwa nafsi zao na mali zao; bali waliwapendela wao kuliko nafsi zao; kama itakavyoashiria Aya.

Miongoni mwa Aya zilizoshuka kwa ajili ya Answar ni:

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَالَّذِينَ آوَوا وَّنَصَرُوا أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ ﴿٧٤﴾

“Na wale waliokaribisha na kusaidia, hao ndio waumini kweli, wana wao maghufira na riziki njema.” Juz. 10 (8:74).

Wala hawapati dhiki katika vifua vyao kwa walivyopewa Wahajiri.

Mwanzoni Wahajiri walikuwa ni mafukara zaidi katika Madina wakipata tabu. Lau si Answar wangelikufa na njaa. Mtume(s.a.w.w) alikuwa akiwapa sadaka mafukara na hawapi matajiri na walio na uwezo wa kuchuma.

Kwa hiyo alikuwa akiwapa kipaumbele Wahajiri; mara nyingine akiwapa ngawira wao tu. Answar walikuwa wakiliridhia hilo bila ya kuona choyo wala dhiki nyoyoni, na wakiona ni haki kabisa. Ndio akasajili Mwenyezi Mungu (s.w.t) sifa zao hizi kwenye Kitabu chake.

Na wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.

Kumpendela mwingine kuliko nafsi yake mtu, akiwa na mahitaji, hakuwezi kulinganihswa na jambo lolote isipokuwa kujitolea mhanga. Imeelezwa katika vitabu vya Tafsir na Historia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) aliwaambia Answar: “Mkipenda ngawira hii iwe baina yenu na Wahajiri, lakini mshirikiane nao katika mali yenu, au muwaachie ngawira na nyinyi mbaki na mali yenu. Answar wakasema: bali tutawaachia ngawira na tutashirikiana nao katika mali yetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Hapo Mtume akawaombea dua na kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Warehemu Answar na watoto wa Answar.”

Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.

Uchoyo ni mama wa maovu. Mwenye kuuitikia utamzuia na kila heri, na mwenye kuushinda kwenye nafsi yake basi atakuwa ameikinga na kila uovu na hatari.

Na waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani.

Yaani waliokuja baada ya Answar na Wahajiri. Makusudio ya waliokuja baada yao ni kila mwenye kufuata sera mpaka siku ya Kiyama, wala haku­na njia ya kuwahusisha Tabiina (waliowafuatia maswahaba). Kwa sababu linalozingatiwa ni matendo sio mahali fulani wala wakati. Maswahaba hawakufikia walipokuwa ila ni kwakuwa walisikilza kauli wakafuata mazuri yake.

Wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini.

Ni muhali kabisa kuwa pamoja imani na undani. Inawezekana mtu kujiwekea undani?

Mola wetu! Hakika Wewe ni Mpole Mwingi wa rehema kwa waja wako walioitakasa dini yao na nyoyo zao kutokana undani na unafiki.

Je, Huwaoni wanaofanya unafiki wanawaambia ndugu zao walioku­furu katika Watu wa Kitabu: Mkitolewa na sisi lazima tutatoka pamo­ja nanyi, wala hatutamtii yeyote kabisa dhidi yenu. Na mkipigwa vita lazima tutawasaidia.

Makusudio ya watu wa Kitab hapa ni Bani Nadhir, ndugu wa wanafiki katika ukafiri na uadui kwa Mtume. Aya inaashiria tukio maalum. Pale Mtume(s.a.w.w) alipotangaza vita dhidi ya Bani Nadhir, wanafiki wakion­gozwa na Abadallah bin Ubayya waliwaambia: piganeni na Muhammad na sisi tuko na nyinyi, akiwapiga nasi tutampiga na wakiwatoa Madina tuta­toka nanyi; hatutamsikiliza Muhammad wala mwenginewe.

Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hao hakika bila ya shaka ni waongo kwenye kauli yao na ahadi yao.

Wakitolewa Bani Nadhirhawatatoka pamoja nao wanafiki,na wakipigwa vita hawatawasaidia. Na kama wakiwasaidia basi watageuza migongo;

Hii ndio hali ya mnafiki, ulimi wake unahalifiwa na moyo wake na dhahiri yake inahalifiwa na siri yake.

Kisha hawatanusuriwa wala kunufaika na kwa vitimbi na unafiki wao.

Hakika nyinyi ni tishio zaidi katika vifua vyao kuliko Mwenyezi Mungu. Hayo ni kwa kuwa hao ni watu wasiofahamu.

Wanafiki wanawaogopa waumini kwa ukali wao wa vita, kwa sababu wao wanatazamia shari ya haraka wala hawatazimii adhabu inayokuja Akhera.

Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipokuwa katika vijiji vilivyo zatitiwa kwa ngome, au nyuma ya kuta.

Mayahudi hawakabiliani na waumini uso kwa uso katika uwanja wa vita, bali wanajificha kwenye mitaa yao nyuma ya ngome na kuta na kuwarushia waumini mishale na mawe; kama ilivyo hali ya mwoga.

Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali.

Wao wana nguvu kwa maandalizi yao na idadi yao, lakini masilahi na hawa za nafsi zimewatawanyisha. Wao wamechangukana, hata kama wanajionyesha kuwa na umoja na mapenzi.

Lau wangelikuwa na umoja na kupendana wangeliwatokea kupambana nanyi, lakini hawakupigana nanyi. Hili liko kwa wayahudi na wasiokuwa wayahudi, kwani umoja ni nguvu hata kama idadi na nyenzo ni ndogo, na utengano ni udhaifu hata kama kuna nyenzo na wingi wa watu.

Tumeshuhudia ushindi wa watu wasio na haki wachache juu ya walio na haki wengi na wenye nyenzo. Siri ni utengano wa hawa kwenye haki yao na umoja wa wale kwenye batili yao.

Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili ya kufahamu kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Ni kama mfano wa waliokuwa kabla yao hivi karibuni. Walionja ubaya wa mambo yao. Nao watapata adhabu iliyo chungu.

Mayahudi walijenga uadui na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w ) ; ni sawa na hali ya makafiri wa kikuraishi na wengineo waliompiga vita Mtume; pale walipoishia kwenye fedheha ya duniani na Akhera ni adhabu ya kuungua.

كَمَثَلِ الشَّيْطَانِ إِذْ قَالَ لِلْإِنسَانِ اكْفُرْ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِّنكَ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦﴾

16. Ni kama mfano wa Shetani anapomwambia mtu: kufuru. Na akikufuru humwambia: Mimi si pamoja nawe. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.

فَكَانَ عَاقِبَتَهُمَا أَنَّهُمَا فِي النَّارِ خَالِدَيْنِ فِيهَا وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ ﴿١٧﴾

17. Basi ikawa mwisho wa wote wawili hao ni kuingia Motoni, wadumu humo daima; na hayo ndiyo malipo ya madhal­imu.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٨﴾

18. Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayoyatan­guliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّـهَ فَأَنسَاهُمْ أَنفُسَهُمْ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١٩﴾

19. Wala msiwe kama wale waliomsahau Mwenyezi Mungu, na Yeye akawasa­haulisha nafsi zao. Hao ndio mafasiki.

لَا يَسْتَوِي أَصْحَابُ النَّارِ وَأَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمُ الْفَائِزُونَ ﴿٢٠﴾

20. Hawawi sawa watu wa Motoni na watu wa Peponi. Watu wa Peponi ndio wenye kufuzu.

AKIKUFURU HUMWAMBIA MIMI NIKO MBALI NAWE

Aya 16 – 20

MAANA

Ni kama mfano wa Shetani anapomwambia mtu: kufuru. Na akikufu­ru humwambia: Mimi si pamoja nawe. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.

Wanafiki waliwaambia Bani Nadhir: “Piganeni na Muhammad na sisi tuko pamoja nanyi katika vita,” lakini yalipowafika yaliowafika, walijificha kwenye viota vyao na hawakuonekana hata athari yao.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameifananisha hali ya wanafiki na Bani Nadhir na hali ya shetani na mtu mwenye kutenda dhambi. Huwa anamhadaa kwa ufisadi na upotevu na kumpa tamaa ya amani. Mambo yakichacha humwacha na adhabu na maangamizi na kujitenga naye na kudhihirisha hofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 10 (8:48) na Juz. 13 (14:22).

Basi ikawa mwisho wa wote wawili hao ni kuingia Motoni, wadumu humo daima; na hayo ndiyo malipo ya madhalimu.

Wawili ni shetani na mtu aliyeingia kwenye mtego wake. Maana yako wazi. Kwa ufupi ni kuwa kila mmoja, mwenye kuhadaa na mwenye kuhadaiwa, atakuwa katika Jahannam ambayo ni marejeo mabaya.

Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, ambaye nyinyi mko mikononi mwake, na mwenye kumcha Mwenyezi Mungu humfanyia wepesi mambo yake; kama anavyosema Mwenyezi Mungu katika Qur’an (65:4).

Na kila nafsi iangalie inayoyatanguliza kwa ajili ya Kesho.

Kila analolifanya mtu katika maisha haya huwa amelifanya kwa ajili ya Akhera. Mwenye busara anaangalia kwenye dunia yake kwa mtazamo wa mwenye kuicha kwa wema sio mwenye kuchukua anasa zake.

Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.

Mwenyezi Mungu anamjua mwenye kuamini kwa kauli na vitendo na mwenye kumwamini kwa fikra tu anayoisema na kuisahau kwenye viten­do. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amelikariri jambo la takua kwa ukomo wa kuhimiza na kupendekeza.

Wala msiwe kama wale waliomsahau Mwenyezi Mungu, na Yeye akawasahaulisha nafsi zao.

Walisahau kufanya kwa amri ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu akawasahaulisha kufanya kwa masilahi ya nafsi zao. na aliyedanganyika zaidi katika watu ni yule aliyejisahau na asifanye kwa ajili ya usalama wake kujiepusha na maangamizi.

Hao ndio mafasiki. Kwa sababu hawakunufaika na ubainifu wa Mwenyezi Mungu na kupata funzo kwa mawaidha yake.

Hawawi sawa watu wa Motoni na watu wa Peponi. Watu wa Peponi ndio wenye kufuzu.

Vipi atakuwa sawa mwema na mwovu? Umetangulia mfano wake katika Aya kadhaa miongoni mwazo ni Juz. 21 (32:18).

لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا الْقُرْآنَ عَلَىٰ جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١﴾

21. Lau tungelieiteremsha hii Qur’an juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeliuona ukinyenyekea, ukipasuka kwa hofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo ni mifano tunawapigia watu ili wafikiri.

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿٢٢﴾

22. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu, Mwenye kuya­jua yaliyofichikana na yanay­oonekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٢٣﴾

23. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwangaliaji, Mwenye nguvu, Jabari, Mkubwa; Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanay­omshirikisha nayo.

هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٤﴾

24. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kinamsabihi kilicho katika mbingu na ardhi, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

LAU TUNGELIITERMSHA HII QUR’ANI JUU MLIMA

Aya 21 – 24

MAANA

Lau tungelieiteremsha hii Qur’an juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeliuona ukinyenyekea, ukipasuka kwa hofu ya Mwenyezi Mungu.

Hii ni kiasi cha kukadiria tu, kunakofahamika kutokana na neno ‘Lau.’ Lengo ni kubainisha ukuu wa Qur’an, kwamba ina nguvu na athari; kiasi ambacho lau itateremshwa kwenye jabali basi lingenyenyeka na kulainika pamoja na ugumu wake. Pia lingelipasuka na kuanguka kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu. Basi vipi mtu ambaye anaumizwa na chawa na kufa kwa kusongwa koo na jasho humfanya anuke; kama alivyosema Amirul Muminin, Ali(a.s) ?

Ana nini mtu huyu mnyonge, “anayesikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anang’ng’ania huku akijivuna, kama kwamba hakuzisikia. ” Juz. 25 (45:8).

Je, ni kwa kuwa moyo wake ni mgumu kama jabali ambalo limekazana sana, au ni ujinga, inadi na kung’ang’ania upotevu?

Na hiyo ni mifano tunawapigia watu ili wafikiri, katika hikima ya Qur’an, mawaidha yake, dalili yake, na ubainifu wake, na waongoke, kwa nuru yake, kwenye njia ya usawa, lakini:

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِمَن كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ ﴿٣٧﴾

“Hakika katika hayo kuna ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye ni shahidi.”

Juz. 26 (50:37).

Baada ya hayo yote, hakika ukuu wa Qur’an ni ukuu wa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Walisema wakale: maneno ni sifa ya mwenye kusema; hasa yale yanayorudia ilimu yake.

Ndio maana Mwenyezi Mungu akaisifia Qur’an kwa sifa zake; kama vile nguvu, hekima, utukufu, ukuu, nuru, haki, rehe­ma, ukweli n.k.

Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akajisifu kwa sifa zake tukufu akasema:Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu, apasaye kuabudiwa kwa haki, anayesifika kwa sifa zote nzuri za ukamilifu; zikiwemo hizi zifuatazo:-

Mwenye kuyajua yaliofichikana na yanayoonekana . Anayajua yaliyoghaibu kwa watu na yaliyo dhahiri.

Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu . Sifa mbili hizi zimetokana na rehema kwa maana ya hisani. Inawezekana kuwa kuchanganywa matamko mawili ni kuashiria kuwa rehema yake imeenea kila kitu, hata katika hali ya kughadhibika kwake; na kwamba kuikatia tamaa ni kufuru na upotevu.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Huu ni msisitizo wa tawhid. Yeye niMfalme; ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, Ndiye anayetoa uhai na kufisha.

Mtakatifu; yaani ametakasika na yasiyolaikiana na utukufu wake.Mwenye salama ; kwa sababu inatokana na Yeye mtukufu utulivu na amaniMtoaji wa amani ; Anawapa thawabu waumini na anawapa amani ya adhabu ya moto.Mwangaliaji ; Mwenye kuchunga na kuhifadhi.

Mwenye nguvu ; asiyeshindwa wala kuzidiwa nguvu.Jabari ; Aliye juu bila ya kufikiwa.Mkubwa; Ana ukubwa na utukufu.Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayomshirikisha nayo , ya kuwa na mshirika, mke na mtoto.Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji .

Hizi ni sifa mbili tofauti. Neno mtengenezaji tumelifasiri kutokana na neno Bariu ambalo imesemekana kuwa hapa lina maana ya kuwa mbali na upun­gufu.Mtia sura ; Mwenye kuumba sura na umbo.Mwenye majina mazuri kabisa.

Kila jina lake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni zuri na ni kuu. Tazama Juz. 9 (7:180) Kifungu cha: ‘Je, majina ya Mwenyezi Mungu ni hayo hayo?’

Kinamsabihi kilicho katika mbingu na ardhi, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Tasbihi inakuwa kwa lugha ya maneno na lugha ya hali. Tazama Juz. 15 (15:44) kifungu cha ‘Kila kitu kinamsabihi.

MWISHO WA SURA YA HAMSINI NA TISA: SURAT AL-HASHR


5

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sitini: Surat Al – Mumtahina. Imeshuka Madina. Ina Aya 13.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ يُخْرِجُونَ الرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ أَن تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ رَبِّكُمْ إِن كُنتُمْ خَرَجْتُمْ جِهَادًا فِي سَبِيلِي وَابْتِغَاءَ مَرْضَاتِي تُسِرُّونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَأَنَا أَعْلَمُ بِمَا أَخْفَيْتُمْ وَمَا أَعْلَنتُمْ وَمَن يَفْعَلْهُ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿١﴾

1. Enyi mlioamini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki, mkiwapa mapenzi, na wao wamekwishaikataa haki iliyowajia, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamwamini Mwenyezi Mungu, Mola wenu. Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi yangu, mnafanya upenzi nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayoyaficha na mnayodhi­hirisha. Na mwenye kufanya hayo kati yenu basi amepotea njia ya sawa.

إِن يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا لَكُمْ أَعْدَاءً وَيَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُم بِالسُّوءِ وَوَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ ﴿٢﴾

2. Wakiwakuta wanakuwa maadui zenu, na wanawakun­julia mikono yao na ndimi zao kwa uovu. Na wanapenda muwe makafiri.

لَن تَنفَعَكُمْ أَرْحَامُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَفْصِلُ بَيْنَكُمْ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٣﴾

3. Hawatawafaa jamaa zenu, wala watoto wenu Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu, na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda.

MSIMFANYE RAFIKI ADUI WANGU NA WENU

Aya 1 – 3

KISA KWA UFUPI

Imetangaa kuwa Aya hizi zilishuka kwa Hatab bin Abi Balta’a ambaye ali­pata mtihani mkali siku ya Badr. Kwa ufupi wamesema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) aliaanda jeshi kuipiga Makka. Hatab alipojua hivyo akawaandikia barua Makuraishi kuwahadharisha, akampa mwanamke kuipeleka. Mwenyezi Mungu akampa wahyi Mtume wake habari ya Hatab.

Basi Mtume akawatuma swahaba zake, akiwemo Imam Ali(a.s ) , wakampata njiani. Walipomuuliza kuhusu barua akakataa, baadhi wakamuamini, lakini Ali akamkatalia na akamtishia kumuua, ndipo akaitoa barua kwenye kucha zake.

Wakaja naye kwa Mtume(s.a.w. w ) . Akamuuliza Hatab: ni nani aliyeandika hii? Hatab akasema: “Ni mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Wallah, sijakufuru tangu niliposilimu, wala sijadanganya tangu nilipoamini, lakini nimefanya hivi kwa makuraishi kuwahami watu wangu na shari yao, na nimejua kuwa Mwenyezi Mungu amewafedhehesha.”

Basi Mtume alimwamini na akamkubalia udhuru wake.

MAANA

Enyi mlioamini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki, mkiwapa mapenzi.

Kuna baadhi ya wafasiri wamefasiri: ‘mkiwapeleka (habari) kwa ajili ya mapenzi.’ Lakini tafsiri ya kwanza ndiyo waliyoisema wengi.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwaamrisha waumini wasiwe na muungano wowote wa mapenzi na maadui wa haki, wala wasiwe na mwasiliano nao yoyote kwa sababu zozote ziwazo. Kwa sababu wao ni maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui wa waliomwamini.

Na wao wamekwishaikataa haki iliyowajia, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamwamini Mwenyezi Mungu, Mola wenu.

Aya hii inaashiria sababu za kukataza mapenzi na maadui wa haki, kuwa ni: kwanza, waliikataa Qur’an na Muhammad(s.a.w. w ) kwa inadi. Pili, wao walimtoa Mtume nyumbani kwake na wale walioamini pamoja naye. kwa kuwa walimwabudu Mwenyezi Mungu peke yake na kuyatupilia mbali masanamu.

Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi yangu.

Maadamu mmeacha watu wenu na mji wenu kwa ajili ya kuliinua neno la Mwenyezi Mungu vipi muwafanye marafiki maadui wa Mwenyezi Mungu? Je, yanaweza kuwa pamoja mapenzi ya Mwenyezi Mungu na mapenzi ya maadui zake katika moyo mmoja? Mnapelekwa wapi?

Mnafanya upenzi nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayoyaficha na mnayodhihirisha.

Mnafanya siri mkidhani kuwa Mwenyezi Mungu hawezi kujua siri yenu. Vipi iwe hivyo na hali kila siri kwake ni wazi na kila ghaibu kwake ni dhahiri?

Na mwenye kufanya hayo kati yenu basi amepotea njia ya sawa.

Hiili ni onyo na hadhari kwa kila mwenye kuiacha njia ya uongofu na haki; hasa wahaini na wenye njama.

Wakiwakuta wanakuwa maadui zenu, na wanawakunjulia mikono yao na ndimi zao kwa uovu. Na wanapenda muwe makafiri.

Lau maadui wa haki wangepata fursa wangeliwatukana na kuwaua wau­mini.

Hawatawafaa jamaa zenu, wala watoto wenu Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu, na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda.

Sio mali wala watoto, elimu au nasaba itakayoweza kufaa siku ya hisabu isipokuwa amali njema. Maana haya yamekaririka kwenye Aya kadhaa; ikiwemo Juz. 4 (3:116).

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٤﴾

4. Hakika nyinyi mna kigezo kizuri kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye, walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunawakataa; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapomwamini Mwenyezi Mungu peke yake. Isipokuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea maghufira, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu! Juu yako tumetege­mea, na kwako tumerudi, na kwako ndio marejeo.

رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا وَاغْفِرْ لَنَا رَبَّنَا إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٥﴾

5. Mola wetu! Usitufanyie mti­hani kwa waliokufuru; Na tughufirie, Mola wetu! Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِيهِمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٦﴾

6. Kwa yakini kimekuwa kigezo kizuri kwenu katika mwendo wao, kwa anayemtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na mwenye kugeuka basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa.

عَسَى اللَّـهُ أَن يَجْعَلَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ الَّذِينَ عَادَيْتُم مِّنْهُم مَّوَدَّةً وَاللَّـهُ قَدِيرٌ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٧﴾

7. Asaa Mwenyezi Mungu akatia mapenzi baina yenu na wale mliofanya nao uadui. Na Mwenyezi Mungu ni muweza, na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.

KIGEZO CHEMA

Aya 4 – 7

MAANA

Hakika nyinyi mna kigezo kizuri kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye.

Maneno yanaelekezwa kwa maswahab; hasa Hatab Bin abi Balta’a, ambaye aliwapa mapenzi washirikina. Makusudio ya yaliokuwa pamoja na Ibrahim ni kila mwenye kufuata sera; ni sawa awe wakati wake au baada yake. Inavyojulikana ni kuwa hakuamini katika watu wa Ibrahim isipokuwa Lut.

Maana ni kuwa kipenzi cha mwingi wa rehema (Khalilurrahman), Ibrahim(a.s ) na aliyeamini pamoja naye walipata tabu sana kutoka kwa washirik­ina, mpaka wakaihama miji yao wakaacha wake na watoto; sawa na yaliy­ompata Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na maswahaba.

Ibrahim na waliokuwa pamoja naye walifanya subira na wakavumilia wala mali na watoto waliowaacha hawakuwafadhaisha. Basi ni juu yenu enyi maswahaba wa Mtume muwaige wale walioamini pamoja na Ibrahim, wala msisumbuke kwa mali na watoto, na mkaungana na washirikina kwa ajili ya hilo.

Walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunawakataa; na umek­wisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapomwamini Mwenyezi Mungu peke yake.

Walioamini pamoja na Ibrahim waliwaambia makafiri: Sisi hatuna uhu­siano wowote na nyinyi, ni maadui zetu mpaka siku ya mwisho, maadamu ni maadui wa Mwenyezi Mungu mkiabudu masanamu na nyota.

Isipokuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea maghufira, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu.

Kama kwamba muulizaji aliuliza: Vipi Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema kuwa Ibrahim na walioamini pamoja naye walijitenga na washirikina pamoja na kuwa Ibrahim mwenyewe alisema:

قَالَ سَلَامٌ عَلَيْكَ سَأَسْتَغْفِرُ لَكَ رَبِّي إِنَّهُ كَانَ بِي حَفِيًّا ﴿٤٧﴾

“Amani iwe juu yako (salamun alayka)! Nitakuombea msamaha kwa Mola wangu. Hakika yeye ananihurumia sana.” Juz. 16 (19:47).

Ndio akajibu Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwamba Ibrahim alitaka kum­wombea msamaha baba yake kwa vile alikuwa amemwahidi kuwa ataami­ni. Ilipombainikia kuwa yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, alijitenga naye; kama ilvyokuja katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ ﴿١١٤﴾

“Na haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake ila ni kwa sababu ya ahadi aliyofanya naye, lakini ilipompambanukia kuwa yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, alijiepusha naye. Hakika Ibrahim alikuwa Mpole sana wa moyo, mvumilivu.” Juz. 11 (9:114).

Zaidi ya hayo ni kuwa Ibrahim alimwambia baba yake: “Wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu.” Mambo yote yako mikononi mwa Mwenyezi Mungu.”

Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akabainisha jinsi Ibrahim na wale walioa­mini pamoja naye jinsi walivyoachana na watu wao na miji yao na kukim­bilia kwa Mwenyezi Mungu, wakasema:

Mola wetu! Juu yako tumetegemea . Na mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu anamtosha.Na kwako tumerudi . Tumerudi kwako katika yale yaliyotushughulisha duniani.Na kwako ndio marejeo kwa ajili ya hisabu na malipo.

Mola wetu! Usitufanyie mtihani kwa waliokufuru ; yaani usitusalitie viumbe wako washari wakatutia kwenye mtihani tusiouweza.Na tughufirie, madhambi yetu yaliyopita.

Mola wetu. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, hukosewi wala hakosewi anayekimbilia kwako.Mwenye hikima katika kuupeleka ulimwengu na kuupangilia.

Kwa yakini kimekuwa kigezo kizuri kwenu katika mwendo wao, kwa anayemtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anazidisha kusisitiza kufuata mfano wa Ibrahim na alioamini pamoja naye. Amerudia Mwenyezi Mungu na kuukariri mfano huu, ili akumbuke au awe na matarajio mwenye kutaraji thawabu na akahofia adhabu yake.

Na mwenye kugeuka basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuji­tosha, Msifiwa.

Mwenye kuacha kufuata vigezo vya watu wema, basi Mwenyezi Mungu ni mwenye kujitosha na viumbe wake, mstahiki wa sifa njema katika dhati yake, sifa zake na vitendo vyake vyote. Namna hii Mwenyezi Mungu anawaamuru waovu wapate funzo na mawaidha kwa mwisho mbaya wa waliopita na kuwaamuru waumini kuiga uongofu wa waliopita.

Asaa Mwenyezi Mungu akatia mapenzi baina yenu na wale mliofanya nao uadui.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa hili anaashiria ushindi wa Makka na kwam­ba wengi wa washirikina ambao Mwenyezi Mungu amekataza kufanya urafiki nao, wataingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi makundi. Hapo mtachanganyika na kuwa na mapenzi na waislamu wapya.

Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuondoa uadui na sababu zake na mahali pake kuweka mapenzi na yanayopelekea hayo.Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa Maghufira Mwenye kurehemu, anawaghufiria madhambi waja wake wenye kutubia na kuwafunika kwa rehema yake.

Ndio! Mwenyezi Mungu alitekelza ahadi yake, akamnusuru mja wake, Bara Arabu yote ikawa chini yake, Makka ikasalimu amri, wakaingia watu katika dini ya Mwenyezi Mungu makundimakundi na yakapatikana mapenzi baina ya wale waliokuwa maadui jana.

لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ ﴿٨﴾

8. Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakuwapiga vita, wala hawakuwatoa mak­wenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.

إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَىٰ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٩﴾

9. Hakika Mwenyezi Mungu anawakataza kufanya urafiki na wale tu waliowapiga vita, na wakawatoa makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanaowafanya hao marafiki basi hao ndio madhalimu.

MUNGU HAWAKATAZI WASIOWAPIGA VITA

Aya 8 – 9

MAANA

Dola Rafiki Na Dola Adui

Uislamu umetoa mwito wa usalama na ukakataza vita isipokuwa kwa kujikinga au kumsaidia mwenye kudhulumiwa.

Kwenye hili la kwanza Qur’an imeashiria kwa kusema:

وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿١٩٠﴾

“Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaowapiga, wala msichokoze. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaochokoza.” Juz. 2 (2:190).

Sababu ya pili imeashiriwa na kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ ﴿٩﴾

“Na ikiwa makundi mawili katika waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hayo linadhulumu jingine, basi lipigeni linalodhulu­mu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu.” Juz. 26 (49:9).

Qur’an imepinga na kukana vita vya kuharibu na kutaka kutawala vyaku­la na vyanzo vya mali za watu, ikasema: “Wala msiwatilie kasoro watu vitu vyao. Wala msifanye ufisadi katika nchi mkafanya vurugu.”Juz. 12 (11:85)

Ikasema tena Qur’an:

تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٨٣﴾

“Hayo ndiyo makazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasiotaka kujitukuza duniani wala ufisadi. Na mwisho ni wa wenye takua.” Juz. 20 (28:83).

Aya hizi ni miongoni mwa Aya zinazounganisha dunia na Akhera na ufufuo wa kwanza na wa pili. Tazama Juz. 4 (3:182-183) kifungu cha ‘Thamani ya Pepo.’

Ama kwenye usalama, kuna Aya kadhaa zilizouhimiza; miongoni mwazo ni:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً ﴿٢٠٨﴾

“Enyi mlioamini! Ingieni katika usalama nyote.” Juz. 2 (2:208).

Nyngine ni:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ﴿١٢٥﴾

“Waite kwenye njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora.” Juz. 14 (16:125).

Aya hizi zinathibitisha misingi ya maelewano na na jinsi ya kutatua mata­tizo ya serikali na mengineyo kwa njia ya amani. Bali Qur’an imetoa mwito wa udugu wa kimataifa, unasimama kwenye misingi ya kujuana, mapenzi, wema na uadilifu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Na tumewafanya mataifa na makabila ili mjuane.” Juz. 26 (49:13).

Kwa hiyo kujuana na kuzoeana ndio sababu ya kuweko makabila na mataifa. Ama wema na uadilifu ndio maudhui ya Aya mbili hizi tulizo nazo. Tumwachie Ustadh Khalid bin Khali, aliyesema:

“Hakika msingi unaotuchorea mwongozo wa mfungamno wetu na vita leo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:“Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakuwapiga vita, wala hawakuwatoa makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anawakataza kufanya urafiki na wale tu waliowapiga vita, na wakawatoa makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanaowafanya hao marafiki basi hao ndio madhalimu.”

Hebu tujiulize na tuwaulize wakazi wote wa duniani: Ni dola ipi inayopi­ga vita dini yetu, ikatutoa makwetu? Ni nani aliyewafukuza waarabu kuto­ka Palestina, wakapora mali zao, ardhi zao na majumba yao? Ni akina nani waliowapa silaha Israil, wakawapa mali na kuwaambia kuweni mwiba kwa waarabu? Ni nani aliyetuzuilia silaha zetu na akaiba vyakula vyetu? Ni nani wanaosimama kwenye mikutano ya kimataifa dhidi ya haki yetu na kuwasaidia maadui zetu?”

“Hawa wote, enyi mabwana, ndio wale aliotukataza Mwenyezi Mungu kufanya urafiki nao. Kuna Aya nyingine inatufichulia njia nyingine ya kuishi na hawa, inayosema:

وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ ﴿١٩٠﴾

“Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaowapiga.” Juz. 2 (2:190)”

“Hawa ndio walioungana dhidi yetu. Mwenyezi Mungu anatuhimiza kupi­gana nao kwa vile ndio walioanza na ni madhalimu.

“Hivi ni dini gani waliyoitegemea? Au ni hulka gani waliyoitegemea wakosefu hawa ambao wanataka tuungane na magharibi na kuelewana nao? Mimi sijui sura yoyote ya ulahidi wa dini na kuivunjia heshima haki na wajibu, inayofedhesha kuliko mwito huu. Je, tupigane na walio na amani na sisi na tuwape amani wale wanatupiga na kutuchinja kama kon­doo?

“Itakuwaje na wao walisherehekea kwenye usiku mweusi harusi ya mashariki ya kati na wakazidisha kukalia miji yetu, wakaua nafsi zetu na uhuru wetu na wakaondoa umoja wetu? Basi mwenye akili na anufaike na majaribio na mwenye dini asome kauli ya Mwenyezi Mungu: Piganeni na wale wanaopigana nanyi.”

Naam! Nimedokoa maneno haya kutoka kitabu Addin fi khidmatisha’ab (Dini katika kuwatumikia wananchi) kilichochapishwa 1963.

Lau Ustadh Khalid angekiandika leo asingelizidisha hata herufi moja ya alioyaandika miaka hiyo. Kwa sababu ana uhakika kuwa yaliyotokea mwezi wa Juni 1967 na yanayotokea hivi sasa ni sehemu ya yaliopangwa na wakoloni wazayuni waliopita na wakawasaidia wale wanaopigana kati­ka njia ya wachinjaji wa watu wao, na wachinjaji nao wakiwategemea waarabu wanaopupia maslahi yao.

Wameafikiana mafakihi wa madhehebu kuwa inafaa, dhimmiy (asiyekuwa na vita na waislamu) katika watu Kitabu, kupewa sadaka, isiyokuwa ya wajibu, kutoka kwa Mwislamu. Abu Hanifa akasema, pia inafaa kupewa Zaka ya fitr na kafara.

Vile vile wameafikiana kufaa kumuusia wasiya wa mali na waqf. Hayo wameyatolea dalili kwa Aya hizi tulizo nazo: “Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakuwapiga vita…”.


6

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ وَآتُوهُم مَّا أَنفَقُوا وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ وَاسْأَلُوا مَا أَنفَقْتُمْ وَلْيَسْأَلُوا مَا أَنفَقُوا ذَٰلِكُمْ حُكْمُ اللَّـهِ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿١٠﴾

10. Enyi mlioamini! Wakiwajia wanawake Waumini walio­hama, basi wafanyieni mti­hani. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi Imani yao; Mkijua kuwa ni waumi­ni, basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali yao, wala wanaume hao Si halali yao wanawake hao. Na wapeni hao walichotoa. Si vibaya kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa. Na takeni mlichokitoa, na wao watake walichokitoa. Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu anayowahukumu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.

وَإِن فَاتَكُمْ شَيْءٌ مِّنْ أَزْوَاجِكُمْ إِلَى الْكُفَّارِ فَعَاقَبْتُمْ فَآتُوا الَّذِينَ ذَهَبَتْ أَزْوَاجُهُم مِّثْلَ مَا أَنفَقُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿١١﴾

11. Na akitoroka yeyote katika wake zenu kwenda kwa makafiri, tena ikatokea mkapata ngawira, basi wapeni waliokimbiwa na wake zao kiasi cha mahari waliyoyatoa. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamwamini.

WAKIWAJIA WANAWAKE WAHAJIRI

Aya 10 – 11

MAANA

Mnamo mwaka wa sita wa Hijra Mtume(s.a.w.w) aliwekeana mkataba wa amani wa Hudaybiya pamoja na makuraishi. Tazama Juz. 26 (48: 10) kifungu cha ‘Kisa kwa ufupi.” Miongoni mwa yaliyokuwa kwenye mkata­ba ni atakayekuja kwa Muhammad(s.a.w.w) kutoka kwa makuraishi, basi amrudishe, lakini atakayewaendea makuraishi kutoka kwa Muhammad(s.a.w.w) asirudishwe.

Wafasiri wanasema, baada ya mkataba aliwahi kuja mwanamke mmoja kutoka kwa makuraishi kwa kuhajiri kwa Mtume(s.a.w.w) . Mumewe alim­fuatia na kumwambia Mtume: Ewe Muhammad! Nirudishie mke wangu; kwani ulikubaiana kuwa atakayekujia kutoka kwetu utamrudisha.” Ndio zikashuka Aya mbili hizi, ili kubainisha hali ya kusilimu au kurtadi mmoja kati ya wanandoa. Ufuatao ndio ufafanuzi wake:-

Enyi mlioamini! Wakiwajia wanawake Waumini waliohama, basi wafanyieni mtihani.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawambia waislamu; akiwajia mwanmke aliyemwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi mjaribuni. Wafasiri wametofautiana kuhusu aina ya mtihani. Kauli yenye nguvu zaidi ni ile ise­mayo kuwa ni kupiga shahada. Kwa sababu Mtume alikuwa akitosheka na hilo kuthibitisha uislamu wa mtu. Na hilo ndilo walilokubaliana waislamu.

Sababu nyingine ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu moja kwa moja iliyoungana nayo:Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi Imani yao; yaani nyinyi chukueni dhahiri tu, undani mwachieni Mungu.

Pia Aya nyingine isemayo:

وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا ﴿٩٤﴾

“Wala msimwambie mwenye kuwapa Salaam: Wewe si mwislam.”

Juz. 5 (4:94).

Ikiwa mwenye kutoa salam tu haifai kumwambia kuwa si mwislamu je, mwenye kutamka shahada mbili si ndio kabisa.

Mkijua kuwa ni waumini, kwa kutamka shahada mbili,basi msiwarudishe kwa makafiri Wanawake hao wauminisi halali yao, wala wanaume hao makafirisi halali yao wanawake hao.

Enyi waislamu! Msimrudishe mwanamke mwislamu kwa mume kafiri ambaye amehama akiwa ni mumin, kwa sababu ndoa imekatika.

Kama muulizaji akiuliza : kusema kwake Mwenyezi Mungu: ‘Wanawake hao si halali yao, wala wanaume hao si halali yao wanawake hao.’ Si ni manenno hayo kwa hayo tu, kuna wajibu gani wa kukaririka huku?

Tutajibu : inawezekana ni kuashiria kuwa itikadi ya mshirikina imeondoa athari ya kuwa yeye bado ni mkewe. Pia inawezekana ni kiasi cha kusisi­tiza tu.Na wapeni hao wanaumewalichotoa.

Yaani wapeni waume zao makafiri mahari yale waliyoyatoa. Lakini huku­mu hii ya kurudisha mahari inahusika na kuwapoza washirikina tu, haiendelei baada ya hapo.

Kwa sababu mahari yanathibiti kwa mke kwa kiasi cha mume kumwingilia tu mkewe. Hayaondoki mahari kwa kuvunjika ndoa kwa namna yoyote ile; iwe ni kwa kusilimu mke au kusilimu mume nk.

Si vibaya kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao.

Mwislamu anaweza kumuoa mwanamke mwislamu muhajiri baada ya kuharamishiwa mumewe kafiri, lakini kwa sharti ya kumpa mahari na kutimia ndoa baada ya kwisha eda, ikiwa aliyekuwa mumewe, kafiri alimwingilia.

Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu. Wanandoa wakiwa washirikina na mume pekee akasilimu, basi ndoa yao itavunjika kama ilivyokuwa kwa mwanamke. Vile vile wakiwa waislamu na mmoja wao akartadi.

Na takeni mlichokitoa, na wao watake walichokitoa.

Akisilimu mume anayo haki ya kutaka mahari yake; kama ambavyo mume mshirikina anayo haki ya kutaka mahari aliyompa mkewe aliyesilimu.

Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu anayowahukumu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.

Hukumu hii ni wajibu, haifai kuasi. Mwenyezi Mungu ameiweka kwa hiki­ma anayoijua Yeye zaidi.

Na akitoroka yeyote katika wake zenu kwenda kwa makafiri, tena ikatokea mkapata ngawira, basi wapeni walio kimbiwa na wake zao kiasi cha mahari walioyatoa.

Ikiwa mke wa mwislamu atakimbilia kwa makafri, na wasirudishe mahari, basi nyinyi waislamu mrudishieni huyu mwenzenu kiasi kile alichotoa kutoka kwenye ngawira mtakayoipata kutoka kwa makafiri.

Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamwamini.

Ogopeni aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu na mfuate amri yake, ikiwa nyinyi ni wakweli katika imani yenu.

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا جَاءَكَ الْمُؤْمِنَاتُ يُبَايِعْنَكَ عَلَىٰ أَن لَّا يُشْرِكْنَ بِاللَّـهِ شَيْئًا وَلَا يَسْرِقْنَ وَلَا يَزْنِينَ وَلَا يَقْتُلْنَ أَوْلَادَهُنَّ وَلَا يَأْتِينَ بِبُهْتَانٍ يَفْتَرِينَهُ بَيْنَ أَيْدِيهِنَّ وَأَرْجُلِهِنَّ وَلَا يَعْصِينَكَ فِي مَعْرُوفٍ فَبَايِعْهُنَّ وَاسْتَغْفِرْ لَهُنَّ اللَّـهَ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢﴾

12. Ewe Nabii! Watakapokujia wanawake waumini wakakubai Kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawauwa watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaouzua baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema. Basi peana nao baia na uwatakie maghufira kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kure­hemu.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ قَدْ يَئِسُوا مِنَ الْآخِرَةِ كَمَا يَئِسَ الْكُفَّارُ مِنْ أَصْحَابِ الْقُبُورِ ﴿١٣﴾

13. Enyi mlioamini! Msiwafanye rafiki zenu watu ambao Mwenyezi Mungu ame­wakasirikia. Hao wamek­wishakata tamaa ya Akhera, kama makafiri walivyowaka­tia tamaa watu wa makaburi­ni.

WANAWAKE WAUMINI WAKIKUBAI

Aya 12 – 13

MAANA

Ewe Nabii! Watakapokujia wanawake waumini wakakubai.

Makusudio ya kubai ni kutoa ahadi ya utiifu. Mtume(s.a.w.w) alipopata ushindi wa kuiteka Makka, wanaume walimbai kuwa watamtii na kupigana jihadi; kisha wanawake nao wakambai:

1.Kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote.

Tazama Juz. 5 (4:48-50) kifungu cha: ‘Dalili ya umoja na utatu.

2.Wala hawataiba kutoka kwa waume zao na watu wengine.

Katika vitabu vya Tafsiri na Hadith imeelezwa kuwa Hind, mama wa Muawiya, alimuuliza Mtume kuhusiana na sharti hili: Abu sufyan ni mtu bakhili sana, na nimechukua mali yake? Mtume(s.a.w.w) akamkubalia kutozidisha haja yake na ya watoto wake.

3.Wala hawatazini .

Tazama Juz. 15 (17:26-36) na Juz. 18 (24:1-5)

4.Wala hawatawauwa watoto wao.

Watu wakati wa Jahilia (wakati wa ujinga kabla ya Uislamu) walikuwa wakiwaua watoto wao kwa kuhofia ufukara; kama alivyoashiria Mwenyezi Mungu katika Juz. 15 (17:31).

5.Wala hawataleta uzushi wanaouzua baina ya mikono yao na miguu yao.

Hiki ni kinaya cha tumbo, kwa sababu liko baina ya mikono na miguu. Maana ni kuwa mwanamke asiseme uwongo katika lile analolisema kuhu­siana na mimba, hedhi na utwahara. Asiseme yuko twahara kumbe yuko kwenye hedhi au kinyume wala asidai ana mimba kumbe hana. Mwanamke alikuwa anaweza kumdanganya mumewe kuwa ana mimba kisha anadai imeharibika; au anaweza kuokota mtoto na kumnasibisha na mumewe kwa uzushi.

6.Wala hawatakuasi katika jambo jema.

Mtume(s.a.w.w) haamuru isipokuwa mema, wala hakatazi isipokuwa maovu.

Basi peana nao baia ya kutekeleza yaliyotajwa,na uwatakie maghufira kwa Mwenyezi Mungu kwa yale madhambi yao ya nyuma.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu, anawasamehe wenye kutubia wanaume na wanawake na anawaingiza wote kwenye rehema yake.

Enyi mlioamini! Msiwafanye rafiki zenu watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia. Hao wamekwishakata tamaa ya Akhera, kama makafiri walivyowakatia tamaa watu wa makaburini.

Mwanzoni mwa sura hii Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaambia kuwa wasiwafanye marafiki maadui wa Mwenyezi Mungu, na hapa anaishiliza sura na mfano huohuo. Lengo ni kuwahadharisha waumini na maadui wa Mwenyezi Mungu na wa haki na kutowaamini na habari yoyote ya Mtume(s.a.w.w) na waislmu. Pia wasitegemee uwongo wao na kudanganya kwao. Kwa sababu wao hawatarajii kukutana na Mwenyezi Mungu. Ufufuo kwao ni sawa na kurudi wafu duniani.

Kwa ajili hii ndio Mwenyezi Mungu akawakasirikia na akawaandalia adhabu chungu.

MWISHI WA SURA YA SITINI: SURAT AL – MUMTAHINA


7

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sitini Na Mmoja: Surat As – Saff. Imeshuka Madina. Ina ya 14.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kure­hemu.

سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١﴾

1. Vinamsabihi Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ ﴿٢﴾

2. Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda?

كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ ﴿٣﴾

3. Ni chukizo kubwa kwa Mwenyezi Mungu kusema msiyoyatenda.

إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُم بُنْيَانٌ مَّرْصُوصٌ ﴿٤﴾

4. Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaopigana katika Njia yake kwa safu kama kwamba wao ni jengo lililojengwa kwa risasi.

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ لِمَ تُؤْذُونَنِي وَقَد تَّعْلَمُونَ أَنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿٥﴾

5. Na Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Kwa nini mnaniudhi, nanyi mnajua kuwa hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu niliyetumwa kwenu? Walipopotoka, Mwenyezi Mungu alizipotoa nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu hawaon­goi watu mafasiki

وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٦﴾

6. Na Isa bin Maryam aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Tawrat, na mwenye kubashiria Mtume atakayekuja baada yangu; jina lake ni Ahmad. Lakini alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhahiri!

KAMA KWAMBA WAO NI JENGO

Aya 1 – 6

MAANA

Vinamsabihi Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na vilivyo kati­ka ardhi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Kila kilichoko kinashuhudia uwezo wake Mwenyezi Mungu (s.w.t) na hikima yake, kwa lugha ya maneno au ya hali. Imetangulia kwa herufi zake. Katika Juz. 27 (57:1) na katika Juzuu hii tuliyo nayo mwanzo wa sura 59. na tumelizungumzia hilo kwa ufafanuzi katika Juz. 15 (17:44).

Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda?

Watu wengi wanakusudia uwongo; wanafanya kwa kujificha yale ambayo hawezi kuyadhihirisha. Hakuna mwenye shaka kwamba hawa ni wanafiki kwa kila maana ya neno unafiki.

Basi haifai kuitwa enyi waumini! Hata kama watadhihirisha imani.

Kuna watu wengine wanasema na wanajiandaa kwa nia ya ukweli na kutekeleza, lakini wanapata matatizo yasiyoweza kuzuilika na kushindwa kutekeleza pamoja na juhudi walizofanya. Hawa wanasamehewa, hilo halina shaka.

Na kuna wengine wanasema na wanakuwa na nia ya kutekeleza, lakini uki­fika wakati wananaza kuwa wavivu, waoga au mabakhili. Hawa ni wau­mini lakini ni wapuuzaji, wadhaifu kwenye utashi wao na mbele ya nafsi zao zinazoamrisha sana uovu. Aina hii ya watu ndio wanaokusudiwa kwenye Aya hii.

Ni chukizo kubwa kwa Mwenyezi Mungu kusema msiyoyatenda.

Na mwenye kuchukiwa na Mwenyezi Mungu ameanguka kwenye adhabu ya moto. Wafasiri wengi wamesema kuwa jamaa katika maswahaba walikuwa waki­tamani kupigana kabla ya vita havijaanza, lakini vikija vita na kuwajibishiwa kupigana, basi wanakuwa wazito. Ndio ikashuka aya hii.

Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaopigana katika Njia yake kwa safu kama kwamba wao ni jengo lililojengwa kwa risasi.

Yaani lililojengwa kwa mpangilio na lililothabiti. Imenukuliwa kutoka kwa wanaaikolgia, kuwa wao wamegundua majengo ya zamani yaliyojengwa kwa madini ya risasi. Mwenyezi Mungu amesema akimsimulia Dhulqarnain:

آتُونِي أُفْرِغْ عَلَيْهِ قِطْرًا ﴿٩٦﴾

“Nileteeni shaba iliyoyeyuka nimwagie juu yake.” Juz. 16 (18:96).

Ziyada ya maneno ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anapenda mshika­mano wa watu katika kila lililo na heri na masilahi.

Na Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Kwa nini mna­niudhi, nanyi mnajua kuwa hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu niliye tumwa kwenu?

Swali hili liko pamoja na jawabu lake. Kwa sababu Waisrail ndio wauaji wa manabii kwa nukuu ya kitabu chao kitakatifu; kama ilivyo katika Nehemia (9:26), inasema: “Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako walioshuhudu juu yao wapate kuwarejeza kwako; wakatenda machukizo makuu.”

Qur’an imesajili Aya kadhaa kuhusiana na kuuwa kwao manabii.

Kama muulizajai atauliza: hakuna chochote kinachojulisha kuwa Waisrail walimuudhi Nabii Musa, hasa kwakuwa alikuwa mwokozi na mhisani wao, nasi tutamjibu hivi: Maudhi ya Waisrail kwa Nabii Musa ni mengi; miongoni mwayo ni kumwambia: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu waziwazi, tufanyie Mungu kama wao walivyo na Mungu, hatuwezi kuvumilia chakula kimoja na mengineyo.

Walipopotoka, Mwenyezi Mungu alizipotoa nyoyo zao.

Aya hii inaeleza waziwazi kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) hampotoi mtu mpaka apotoke yeye mwenyewe kwa uchaguzi wake mbaya, wala hamtwezi mtu na kumwangamiza ila akijiangamiza yeye mwenyewe na kujidharau. Aya hii haina tofauti na kauli ya anayesema: “ mwenye kuwa na tamaa ya haramu Mwenyezi Mungu humdhalilisha na kumfedhehsha, na mwenye kukinai na halali, Mwenyezi Mungu humtukuza na kumta­jirisha.

Vile vile Aya hii ni tafsiri ya Aya zinazoonyesha kwa dhahiri kuwa Mwenyezi Mungu ndiye ampotezaye mtu; kama ile isemayo: “Humpoteza Mwenyezi Mungu amtakaye na humwongoza amtakaye.” Yaani Mwenyezi Mungu Mtukufu ametaka kumpoteza anayefuata njia ya upotevu na humwangamiza mwenye kujitia kwenye maangamizi yeye mwenyewe.

Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu mafasiki maadamu wanang’ang’ania ufuska.

Na Isa bin Maryam aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Tawrat, na mwenye kubashiria Mtume atakayeku­ja baada yangu; jina lake ni Ahmad.

Aya ya pili katika maudhui haya inasema:

الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ ﴿١٥٧﴾

“Ambao wanamfuata Nabii asiyesoma wala kuandika ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawrat na Injili.” Juz. 9 (7:157)

Ya tatu inasema:

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنْهُمْ لَيَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٤٦﴾

“Wale tuliowapa Kitabu wanamjua yeye kama wanavyowajua watoto wao. Na hakika kundi katika wao wanaificha haki na hali wanaijua. Juz. 2 (2:146)

Qur’an imeeleza waziwazi kuwa Tawrat ilyoteremshiwa Musa na Injili ili­yoteremshiwa Isa, zimetoa bishara ya unabii wa Muhammad(s.a.w.w) . Na imewakabili kwa hakika hii, ulama wa kiyahudi na kinaswara, na ikashindana nao, kupinga hilo. Lakini Historia haijataja yeyote katika hawa, aliyekana; bali wamethibitisha wale wachunga haki katika wao, wakakiri na wakasilimu; kama vile Abadallh bin Salaam na wengineo; ingawaje walikuwa ni maadui wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

KUPOTOLEWA TAWRAT

Unaweza kuuliza : Mwislamu atamjibu nini Yahudi au Mkristo akisema: Qur’an yenu imesema kuwa Tawrat na Injil imetoa bishara ya Muhammad na hakuna athari yoyote ya bishara hii kwenye nakala ya Tawrat na Injil tuliyo nayo?

Jibu : Atakayeuliza hivi, basi Mwislamu anatakiwa amjibu: Swali hili wamelijibu ulama wa kiyahudi na kinaswara wao wenyewe, pale walipo­kiri waziwazi kuwa Tawrat ya asili iliyoteremshwa kwa Musa imepotea na baada ya kupita miaka akaja mmoja akadai kuwa ameihifadhi moyoni na akaandika madai yake haya; kisha akasema: na iwe ni Tawrat ya Musa, basi ikawa. Hivyo hivyo ikatokea kwa Injil.

Jambo la kushangaza ni kuwa Injil ya Bwana Masih(a.s) , baada ya kupo­tea, yamezaliwa makumi ya Injil zaidi ya hamsini. Mnamo mwaka 325 walikongamana viongozi wa kikiristo na wakakubali injil nne, na hali Isa alikuwa na Injil moja tu, kama wanavyokubaliana manaswara wote. Ni nani basi aliyefanya moja kuwa nne? Lau wangelikubali tatu tungelisema kila mmoja katika watatu (baba mwana na roho mtakatifu) ana yake.

Kinachofahamisha zaidi kuwa Injil hii inatokana na watu wa kanisa, na sio na Masih, ni kuwa ilizuka baada ya kusulubiwa kwake, kuzikwa kwake na kupaa kwake mbinguni. Je alishukiwa na wahyi baada ya kusulubiwa na kuzikwa?

Ikiwa hilo linawezekana, je inawezekana katika hukumu ya kiakili na uhalisia kushukiwa na wahyi ulioandikwa kwenye Injil baada ya yeye kupaa mbinguni?

Swali la pili : Je, kukiri huku kunapatikana wapi kwa ulama wa kiyahudi na kinaswara?

Jibu : Kwenye vitabu vyao kadhaa vya kiarabu na vya lugha nyinginezo. Katika vya kiarabu ni Qamusul kitabulmuqaddas (Kamusi ya Kitabu kitakatifu), ambayo walishiriki wataalamu 27 kuitengeneza. Katika mada ya Yoshua, inasema: “Ni jambo lisilo na shaka kwamba sehemu kubwa ya kitabu kitakatifu iliharibiwa au ilikosekana wakati wa kumritadi Mwenyezi Mungu na vikwazo.” Katika mada ya Vitabu inasema: “Kuna rai inayosema kuwa walioongeza sifa ya kanuni ya agano la kale ni waandishi wenyewe wa kitabu, na rai nyingine inasema ni waandishi wanaosaidiwa na roho mtakatifu, wakiwe­mo viongozi wa kidini wa kiyahudi na wa kimasihi ambao walikubali kita­bu hiki kwa kuongozwa na roho mtakatifu vile vile.”

Huku ni kukiri kusiko na shaka kwamba vitabu vya asili vimepotea na kwamba jamaa waliandika vitabu na kuongeza sifa ya utakatifu wao wenyewe. Na kauli nyingine ni kwa kuongozwa na roho mtakatifu. Tukichukua kauli ya kwanza au ya pili yote ni sawa, natija ni moja tu, kwamba wanakubali kuwa vitabu vilivyoko hivi sasa sio vitabu vya asili vya Musa na Isa; isipokuwa ni vitabu vipya vilivyoandikwa na wale wanaodai ni watakatifu au wanaodaiwa ni watakatifu kwa kupewa nguvu na roho mtakatifu.

Roho mtakatifu, kwao, ni roho wa Mungu katika wale watatu. Mwenyezi Mungu amemwita roho, kwa vile analeta uhai, na mtakatifu kwa vile anaz­itakasa roho za waumini.

Maulama wa Kiislamu wametunga makumi ya vitabu vinavyofahamisha kupotolewa Tawrat na Injil; miongoni mwavyo ni Idh-harulhaqq cha Sheikh Rahmatullah Al-Hindiy.

Ndani yake mna ushahidi 100 wa kuthibitisha upotofu wa Tawrat na Injil, kimatamshi na kimaana. Mwenye Tafsir Al-manar amemwashiria mwandishi huyu alipofasiri sura Annisa aya 46.

Vitabu vingine ni: Arrihlatulmadrasiya cha Sheikh Jawad Albalaghi, Muhammad rasulullah fi bisharatil-anbiya cha Muhammad Abdulghaffar, Muhammad hakadha basharat al-anajil cha Bushra Zachary Michael Kitabu cha mwisho kukisoma katika maudhui haya ni Bisharat wal­muqaranat cha Sheikh Muhammad Assadiq Tehraniy, kilichotoka hivi karibuni. Kimejaa ushahidi mkataa kutoka kwenye vitabu vya kiyahudi na kinaswara, kuhusu kupotolewa Tawrat na Injil zilizoko hivi sasa.

Lakini alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhahiri!

Mayahudi hawakutosheka kumwambia Bwana Masih(a.s) kuwa ni mchawi, bali walithubutu kusema kuwa ni mtoto wa seremala; kama ilivyosemwa kwenya Injil ya Mathayo (13:55) na Injil Marko (6:3). ikinukuu kuwa Mayahudi walimtusi Bibi bikira kuwa alizini.

Lakini pamoja na yote hayo tunawaona wakirsto wengi wanaungana na uzayuni, ulio adui wa dini na utu, hasa kwa Bwana Masihi. Wanaungana dhidi ya Uislamu uliosema:

مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ﴿٧٥﴾

“Masih mwana wa Maryam hakuwa ila ni Mtume. Wamepita kabla yake Mitume, na mama yake ni mkweli.” Juz. 6 (5:75).

Hii inafahamisha tu kuwa umasihi, kwa wale wanaowasaidia waisrail, ni kiasi cha nembo tu ya makusudio mengine na kwamba dini yao na dhamiri zao ni kutawala na kuchokoza; sawa na uzayuni ulivyo.

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُوَ يُدْعَىٰ إِلَى الْإِسْلَامِ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٧﴾

7. Na ni nani mwenye kudhulu­mu zaidi kuliko yule anayem­zulia Mwenyezi Mungu uwon­go, naye anaitwa kwenye Uislamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu mad­haalimu.

يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّـهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ ﴿٨﴾

8. Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo­kuwa makafiri watachukia.

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ ﴿٩﴾

9. Yeye ndiye Aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na dini ya haki ili ipate kushinda dini zote, ijapokwa washiriki­na watachukia.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿١٠﴾

10. Enyi mlioamini! Je, niwajulis­he biashara itakayowaokoa na adhabu iliyo chungu?

تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١١﴾

11. Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua.

يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾

12. Atawasamehe dhambi zenu, na atawatia katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa.

وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٣﴾

13. Na kinginecho mkipendacho ­nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu na ushindi uliokaribu. Na wabashirieni Waumini!

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا أَنصَارَ اللَّـهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّينَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ فَآمَنَت طَّائِفَةٌ مِّن بَنِي إِسْرَائِيلَ وَكَفَرَت طَّائِفَةٌ فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ ﴿١٤﴾

14. Enyi mlioamini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu, kama alivyosema Isa bin Maryam kuwaambia wanafunzi wake: Nani wasai­dizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wakasema wanafun­zi: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu! Basi taifa moja la Wana wa Israili lilia­mini, na taifa jingine lilikufuru. Ndipo tukawaunga mkono walioamini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda.

MWENYEZI MUNGU ANAKAMILISHA NURU YAKE

Aya 7 – 14

MAANA

Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uwongo, naye anaitwa kwenye Uislamu?

Mtume(s.a.w.w) aliwalingania watu wake watupilie mbali ushirikina na kumwamini Mwenyezi Mungu peke yake. Wakaona dhiki, wakampangia njama, wakatengenezea shaka juu yake na wakamzushia. Hivi ndivyo alivyo mbatilifu mwenye inadi, huwa anatengeneza uwongo na kuzua ubatil­fiu kila anapolinganiwa kwenye haki; ni sawa mlinganiaji awe Nabii au la.Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu, wale wanaomzus­hia Mwenyezi Mungu uwongo. Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

لَا تَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا فَيُسْحِتَكُم بِعَذَابٍ وَقَدْ خَابَ مَنِ افْتَرَىٰ ﴿٦١﴾

“Msimzulie Mwenyezi Mungu uwongo, asije akawafutilia mbali kwa adhabu, hakika ameshindwa mwenye kuzua.” Juz. 16 (20:61).

Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia

Walijaribu kuumaliza Uislamu kwa uwongo na kusingizia, wakawa ni sawa na anayepingana na Mwenyezi Mungu katika ufalme wake. Mwenyezi Mungu hashindwi na jambo lake, lakini watu wengi hawajui.

Yeye ndiye Aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na dini ya haki ili ipate kushinda dini zote, ijapokwa washirikina wamechukia.

Makusudio ya Mtume hapa ni Muhammad(s.a.w.w) . Uwongofu ni Qur’an na dini ya haki ni Uislamu. Aya hii na ile iliyo kabla yake zimepita kwa herufi zake katika Juz. 10 (32-33).

Enyi mlioamini! Je, niwajulishe biashara itakayowaokoa na adhabu iliyo chungu?

Dunia ni biashara ya kila mtu. Hakuna yeyote katika maisha haya ila anakusudia masilahi na faida katika matendo yake na matumizi yake. Lakini kuna masilahi mabaya; kama yule anayefanya kwa ajili ya umashuhuri na kurundika mali kwa njia yoyote ile. Masilahi mengine ni mazuri na ya heri; kama yule anayefanya kwa ajili ya haja yake na haja ya wengine.

Kwa kuwa faida ndio msukumo wa kwanza wa kufanya amali, ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawaonyesha waja wake biashara itakayowaokoa na ghadhabu na adhabu yake na kufuzu kwa kupata radhi na thawabu zake. Hakuna faida kama amani na kupata Pepo. Mwenyezi Mungu ameweka masharti ya kupata faida hii, kwa kauli yake:

Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yenu na nafsi zenu.

Hii ndio thamani ‧ imani isiyokuwa na shaka, kujitolea mhanga na kujitolea mali. Likishahakika hilo itatimia kandarasi na Mwenyezi Mungu. Na ninani mwenye kutekeleza ahadi zaidi kuliko Mwenyezi Mungu? Imesemwa katika Nahjulbalagha:“Hakuna thamani ya nafsi zenu isipokuwa Pepo, basi msiiuze ila kwenye hiyo.”

Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua.

Kuokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kufuzu kupata thawabu zake ni bora kuliko nafsi, mali na watoto.

Atawasamehe dhambi zenu, na atawatia katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri katika Bustani za milele.

Huu ni ubainifu na ufafanuzi wa faida inayopatikana kutokana na biashara hii. Faida ya kwanza ni kughufiriwa dhambi. Hakuna uhuru zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kuwa huru na dhambi zake. Faida ya pili, ni makazi ya kudumu na neema ya milele.

Huko ndio kufuzu kukubwa ambako hakuna kufuzu kwingine zaidi yake.Na kinginecho mkipendacho nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu na ushindi uliokaribu. Na wabashirieni Waumini!

Makusudio ya nusura hapa ni ushindi wa kuiteka Makka; kama inavyoku­ja haraka akilini. Maswahaba walikuwa wakitamani sana ushindi huu kutokana na adha waliyokuwa wakiipata kutoka kwa washirikina wa Makka. Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamwambia Mtume wake awabashirie ushindi huu na kuwa uko karibu, baada ya kuwabashiria maghufira na Pepo.

Enyi mlioamini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu, kama alivyosema Isa bin Mariamu kuwaambia wanafunzi wake: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wakasema wanafunzi: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu!

Maneno yanaelekezwa kwa mswahaba, Mwenyezi Mungu akiwaamuru, wawe na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , kama vile walivyokuwa wanafunzi wa Isa kwa kauli na vitendo. Umetangulia mfano wake katika Juz. 3 (3:52). Katika kamusi ya Kitabu kitakatifu imeandikwa: “Yesu anaitwa Mnazareti (mnaswara)… jina hilo linarudia mji wa Nazareti (Naswiriy).

Ama masia (masih) ni msimbo wake. Ameitwa hivyo kwa kujitolea kwake. Waumini wake wameitwa wamasia mwaka 42 au 43. Mwanzoni jina hili lilikuwa ni tusi. Baina ya Isa na Musa kuna miaka si chini ya 1200 na si zaidi ya 1491. kwa sababu wanahistoria wana kauli nyingi juu ya hilo.

Basi taifa moja la Wana wa Israili liliamini, na taifa jingine lilikufuru. Ndipo tukawaunga mkono walioamini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda.

Makusudio ya kushinda hapa ni kushinda kwa hoja na dalili. Maana ni kuwa wana wa Israil walitofautiana kuhusiana na Isa akiwa anatokana na wao. Kuna waliosema ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wengine wakasema ni Mungu na mayahudi wakasema ni mchawi na mtoto wa zina. Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawapa nguvu waliosema ni Mtume wa Mwenyezi Mungu dhidi ya wale waliosema ni Mungu.

Katika Waraka wa Yohana imeelezwa kuwa, aliye dhidi ya Masih ni yule anayekana kuwa na mwili na kuungana umungu wa masih na ubinadamu wake. Ama Qur’an inasema kuwa maadui wa Masih ni wale waliozama sana kuhusu yeye na waliosema dhidi yake.

MWISHO WA SURA YA SITINI NA MOJA: SURAT AS – SAFF


8

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sitini Na Mbili: Surat Al-Jum’a. Imeshuka Madina Ina Aya 11.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ﴿١﴾

1. Vinamsabihi vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hiki­ma

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢﴾

2. Yeye ndiye Aliyempeleka Mtume kwenye watu wasiojua kusoma, aliyetokana na wao, awasomee Aya zake, na awatakase, Na awafunze Kitabu na hikima, Japokuwa hapo kabla walikuwa katika upotofu uliodhahiri.

وَآخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا بِهِمْ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٣﴾

3. Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٤﴾

4. Hayo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu anayompa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.

NDIYE ALIEWAPELEKEA MTUME

Aya 1-4

MAANA

Vinamsabihi vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Kila kilicho katika ulimwengu kinafahamisha umoja wa Mwenyezi Mungu na uweza wake. Hii ni tasbihi na kutukuza, ni ufalme unaotawala, utakati­fu wa kuepuka na vile visivyolaikina naye, ni nguvu isiyoshindwa na hiki­ma katika matumizi yake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 27 (57:1), na katika Juzuu hii tuliyo nayo mwanzo wa sura 59 na 61.

Yeye ndiye Aliyempeleka Mtume kwenye watu wasiojua kusoma, aliyetokana na wao.

Makusudio ya wasiojua kusoma hapa ni waarabu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewasifu kuwa hawajui kusoma kwa vile siku hizo wengi wao walikuwa hawasomi wala hawaandiki.

Neno wasiojua ‘kusoma,’ tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu ummiy, ambalo baadhi wamesema kuwa makusudio ya Ummiy hapa ni watu wa Makka, kwa sababu Makka pia inaitwa Ummulqura, hivyo ummiy liwe limetokana na ummu.

Lakini kauli hii tunaipinga kwa sababu zifuatazo:­

1. Neno la kutojua kusoma ndilo linalokuja kwanza kwenye ufa­hamu.

2. Kauli yake Mwenyezi Mungu kwa kutumia neno hilo hilo ummiy:

وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴿٧٨﴾

“Na wako miongoni mwao wasiojua kusoma; hawajui kitabu isipokuwa matamanio tu.”

Juz. 1 (2:78).

Na Qur’an inajifasiri yenyewe.

3. Kauli yake Mtume(s.a.w. w ) : Sisi ni umma usiosoma, hatuandiki wala hatuhisabu.”

Baaadhi ya watu wa Kitab wamesema kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu: “Yeye ndiye Aliempeleka Mtume kwenye watu wasiojua kusoma, aliyeto­kana na wao, “ inajulisha kuwa Muhammad ni Mtume wa waarabu tu.

Hilo tumelijibu kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 7 (6:91-92) na katika Juz. 22 (33:36 - 40) kifungu cha: “Kwanini utume uliishia kwa Muhammad?

Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akabainisha ufahamu wa risala ya Nabii wake Mtukufu, kama ifuatavyo:- Awasomee Aya zake. Awafikishie risala ya Mola wake ambayo watak­wenda nayo kwenye njia ya maisha na uokovu.

Na awatakase . Azisafishe nafsi zao na shirki, akili zao na ujinga na amali zao na uovu na madhambi.

Na awafunze Kitabu . Awagurishe kutoka kwenye giza la upofu na ujinga kwenda kwenye nuru ya ilimu na uongofu, kwa mafundisho yake ambayo yanaitukuza ilimu na kutupilia mbali upotofu; na yanayojikita kwenye akili na maumbile ya kibinadamu.

Na hikima . kila linaloongoza kwenye heri katika itikadi na maadili basi hilo ni hikima. Ibn Al-arabi anasema: Hikima ni sifa ya kuhukumia wala haihukumiwi; yaani inakua juu wala haikaliwi juu.

Kwa ufupi ni kuwa risala ya Muhammad(s.a.w. w ) ni risala ya ubinadamu kwa ujumla, ikizungumza na watu kwa mazungumzo ya kiakili.

Sifa muhimu ya uislamu inayoutofautisha na dini nyingine, ni kuwa inakaribisha somo lolote la kimaudhui lenye insafu.

Ijapokuwa hapo kabla walikuwa katika upotofu uliodhahiri, wa ushirikina, ujinga, dhulma, chuki na mengineyo mabaya na machafu.

Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao.

Makusudio ya wengine ni kila mwenye kuingia uislamu baada ya Muhammad(s.a.w. w ) mpaka siku ya Kiyama, awe mwarabu au sio mwarabu. Maana ni kuwa Muhammad(s.a.w. w ) ni Nabii wa rehema kwa vizazi vyote na mwito wake ni wa watu wote. Wameuamini waarabu na wasiokuwa waarabu katika wakati wake na wanaendelea kuaamini wanofuatia mpaka siku ya ufufuo.

Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima . Na kwa nguvu yake ameupa nguvu uislamu, akaueneza mashariki mwa ardhi na magharibi yake na kwa hikima yake amemchagua Muhammad(s.a.w. w ) kwa risala yake yenye kuenea.

Hayo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu anayompa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.

Hayo ni hayo ya kumtuma Muhammad(s.a.w. w ) . Ni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na rehema kwa binadamu wote. Mfano ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٧﴾

“Na hatukukutuma ila uwe ni rehema kwa walimwengu.” Juz. 17 (21:107)

مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥﴾

5. Mfano wa waliobebeshwa Tawrati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anayebeba vitabu vikubwa. Mfano muovu mno wa watu waliokadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu.

قُلْ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ هَادُوا إِن زَعَمْتُمْ أَنَّكُمْ أَوْلِيَاءُ لِلَّـهِ مِن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٦﴾

6. Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu pasipo kuwa watu wengine, basi yatamanini mauti, ikiwa mnasema kweli.

وَلَا يَتَمَنَّوْنَهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٧﴾

7. Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyokwisha yatanguliza mikono yao. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhalimu.

قُلْ إِنَّ الْمَوْتَ الَّذِي تَفِرُّونَ مِنْهُ فَإِنَّهُ مُلَاقِيكُمْ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾

8. Sema: Hakika mauti mnayoy­akimbia, bila ya shaka yatawakuta. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kuyajua ya ghaibu yanayoonekana. Hapo atawaambia mliyokuwa mkiyatenda.

KAMA MFANO WA PUNDA WAALIOBEBA VITABU

Aya 5 – 8

MAANA

Mfano wa waliobebeshwa Tawrati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anayebeba vitabu vikubwa.

Mayahudi wanasema sisi ni watu wa Tawrat na ndio kitabu chetu kitakati­fu, lakini pamoja na hayo wanamkana Muhammad aliyenukuliwa kwenye Tawrat. Kwa hiyo hali yao ni kama punda aliyebebeshwa mzigo wa vitabu vya ilimu kwenye mgongo wake, lakini hana akili ya kilichomo ndani yake wala kunufaika nacho.

Mayahudi wameipotoa Tawrat ya Musa na vitabu vingine vitakatifu kwao, hilo halina shaka. Tazama Aya 6 ya sura iliyopita. Kisha baada ya kuipotoa wakayafanyia kazi yale waliyoyapotoa. Tunataja mfano wa hayo katika kitabu walichokinasibisha kwa Ezekieli, ninanukuu:

“Na hao wengine aliwambia, nami nalisikia, Piteni kati ya miji nyuma yake; mkapige jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake…” Ezekili 9: (5-6).

Hii ndio Israil inayofuata misingi hii kila inapopata fursa, kuwaua wazee, vijana, watoto na wanawake, si kwa chochote ila kwa maangamizi na kumaliza.

Unaweza kuuliza : waislamu wengi hawaitumii Qur’an, je mfano wao ni kama mfano wa punda anayechukua mizigo?

Jibu : Waislamu hawakuipotoa Qur’an na kuondoa Aya zinazomkubali Musa, Isa, Tawrat na Injil za asili zilizo sahihi, kama walivyopotoa maya­hudi Tawrat na wanaswara Injil: “Semeni: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is’hak na Yaqub na wajukuu na aliyopewa Musa na Isa na pia yale waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao na sisi tumesilimu (tumenyenyekea) kwake.”Juz. 1 (2:136)

Kwa hiyo basi hakuna njia yoyote ya kufananisha wala kulaumu.

Mfano muovu mno wa watu waliokadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu.

Kila mwenye kukadhibisha haki anakuwa ametoa mfano kutoka kwenye nafsi yake juu ya ukafiri na ufisadi wake. Inafaa kila mtu kumwambia: Ni aibu kwako na huzuni.

Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu.

Wataongoka vipi na hali upotevu umemea kwenye nyoyo zao.

Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu pasipo kuwa watu wengine, basi yatamanini mauti, ikiwa mnasema kweli. Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyokwisha yatanguliza mikono yao. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhalimu.

Mayahudi walidai kuwa wao ni taifa teule la Mwenyezi Mungu na kwam­ba ni vipenzi wa Mwenyezi Mungu na Pepo ni yao tu. Ndio akawarudi Mwenyezi Mungu kwamba wao ni waongo katika madai yao. Kama wangelikuwa wakweli katika madai yao wangelitamani kukutana na Mwenyezi Mungu. Kwa sababu yaliyoko kwake ni yenye kubaki na bora zaidi kuliko fedheha waliyo nayo.

Wapi! Wao wanachukia mauti na wanayahofia, kwa wingi wa madhambi yao. La kushangaza ni kuwa wao bado wanaendelea na kung’ang’ania yale wanayohofia mauti kwayo. Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:94).

Sema: Hakika mauti mnayoyakimbia, bila ya shaka yatawakuta. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kuyajua ya ghaibu yanayoonekana.

Hapo atawaambia mliyokuwa mkiyatenda duniani, yakupotoa Kitabu na mengineyo ya ufisadi na makosa na atawalipa adhabu kali ya Jahannam.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٩﴾

9. Enyi mlioamini! Ikinadiwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, kama mnajua.

فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٠﴾

10. Na itakapokwisha Swala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufaulu.

وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا قُلْ مَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ مِّنَ اللَّـهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ وَاللَّـهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١﴾

11. Na wanapoiona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesi­mama. Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki.

SWALA YA IJUMA

Aya 9 – 11

MAANA

Enyi mlioamini! Ikinadiwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu.

Kunadi swala ni kuadhini.

Swala ya Ijumaa ni wajibu kwa Kitabu, Sunna na Ijmai. Ina rakaa mbili kwa kutanguliwa na khutba mbili. Inaitosheleza swala ya Adhuhuri. Inahusika na wanaume. Hakuna tofauti baina ya waislamu katika hayo. Isipokuwa tofauti inakuwa ni: Je, ni wajibu bila ya masharti au ni lazima aweko kiongozi au naibu wake?

Hanafi na Shia Imamia wamesema, kuweko kiongozi (wa dini) au naibu wake ni sharti, lakini Imamia wameongeza sharti la uadilifu wa huyo kion­gozi; vinginevyo itakuwa kupatikana kwake na kukosekana kwake itakuwa ni sawa. Hanafi wametosheka na kuweko tu huyo kiongozi hata kama si mwadilifu.

Shafii, Malik na Hambali wamesema ni wajibu kwa hali yoyote ile. Imamia wamesema kama hakupatikana kiongozi na akawako fakihi mwadilifu kutakuwa na hiyari baina ya Ijumaa na Adhuhuri. Ufafanuzi uko kwenye Kitabu chetu Fiqh Imam Ja’afar As-swadiq Juz. 1.

Na wacheni biashara.

Makusudio ya biashara hapa ni matumizi yoyote yatakayozuia swala ya Ijumaa, iwe biashara au la. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja biashara, kwa vile mara nyingi huwa inategemea wakati au kwa vile watu wanapen­dela sana biashara kuliko viwanda na kilimo. Mafakihi wametofautiana kuhusiana na biashara inayofanywa wakati wa kunadiwa Ijumaa, je itaswihi au itaharibika na kutokuwa na athari yoyote, lakini ina dhambi kwa muuzaji na mnunuzi?

Biashra hii - kwetu - ni sahihi. Kwa sababu kukatazwa muamala hakufahamishi kuharibika, lakini hilo amelipinga mwenye Majamaul-bayan.

Hayo ni bora kwenu, kama mnajua mambo ya kheri na shari na yanayowadhuru na kuwanufaisha.

Na itakapokwisha Swala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufaulu.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuamuru swala ameamrisha kuhangaika kutafuta riziki na maisha kwa biashara na mengineyo, pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu, katika hali zote. Kwa kipimo hiki ndio kutahakikika kufaulu duniani na Akhera; mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّـهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا ﴿٧٧﴾

“Na utafute kwa aliyokupa Mwenyezi Mungu makazi ya akhera; wala usisahau fungu lako la dunia.” Juz. 20 (28:77).

Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna tofauti mbele ya Mwenyezi Mungu baina ya anayeacha kuifanyia kazi Akhera yake na anayeacha kuifanyia kazi dunia yake.

Na wanapoiona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama.

Katika vitabu vya tafsir na Hadith kuna maelezo kuwa siku moja Mtume(s.a.w. w ) alipokuwa amesima akihutubia swala ya Ijumaa, uliingia msafara wa ngamia uliobeba chakula, basi maswahaba wakautokea, na hawakubakia na Mtume isipokuwa watu 12, ndio ikashuka Aya hii.

Riwaya hii imepokewa kwa njia mbalimbali na kuandikwa kwenye vitaba vya sahih, kwa sababu mmojawapo wa wapokezi wake ni Jabir bin Abdillah Al-answari, ambaye ni katika watu wakweli na mwadilifu. Kwa hiyo riwaya inakuwa ni tafsiri na ubainifu wa Aya.

Kwa mnasaba huu tunaashiria kwamba masilahi ya kimada yana athari kubwa katika maisha ya watu. Kwa sababu uchumi ni mhimili wa maisha. Hilo halina shaka. Ndio maana Mwenyezi Mungu (s.w.t) akasema mkimaliza swala tawanyikeni katika ardhi mtafute.

Hata hivyo si sahihi kuse­ma kuwa uchumi ndio msukumo pekee wa kila harakati na msimamo wa mtu. Hapana! Kuna upande mwingine unamsukuma mtu kwenye harakati na kufanya kazi. Maswahaba wengi walimwacha Mtume akiwa amesima­ma na kwenda kwenye biashara, kama ilivyonukuu Aya, lakini wako waliobakia na Mtume, kama ilivyonukuu riwaya.

Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki.

Kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuna riziki ya dunia na ya Akhera, na baina yake hakuna kizuizi. Si amali ya Akhera inayopunguza riziki ya dunia wala sio amali ya dunia inayopunguza riziki ya Akhera; bali kila amali inay­otekeleza haja ya maisha basi hiyo ni amali ya Akhera vile vile.

Sitakua nimekwenda mbali kama nikisema kuwa kila amali aliyoyahalal­isha Mwenyezi Mungu, katika maisha haya, basi ni ngazi ya Akhera. Na aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni mengi mno. Imam Ali(a.s ) anasema:“aliyowahalalishia Mwenyezi Mungu ni mengi zaidi ya aliyowaharamishia. Basi acheni yaliyo machache mchukue mengi, na muwache yaliyofinyu mchukue yaliyo na nafasi.”

MWISHO WA SURA YA SITINI NA MBILI: SURAT AL-JUM’A


9

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sitini Na Tatu: Surat Al- Munafiqun. Imeshuka Madina. Ina Aya 11.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

ذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَكَاذِبُونَ ﴿١﴾

1. Wanapokujia wanafiki huse­ma: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa hakika wewe ni Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanafiki ni waongo.

اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٢﴾

2. Wamevifanya viapo vyao ni kinga, na wao wakajizuia kuifuata Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika ni mabaya waliyokuwa wakiyafanya.

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ ﴿٣﴾

3. Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo umepigwa muhuri juu ya nyoyo zao nao hawafahamu.

وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ وَإِن يَقُولُوا تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُّسَنَّدَةٌ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٤﴾

4. Na unapowaona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao. Kama kwamba wao ni magogo yaliy­oegemezwa. Wao hudhania kila ukelele ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; jihadhari nao.

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا يَسْتَغْفِرْ لَكُمْ رَسُولُ اللَّـهِ لَوَّوْا رُءُوسَهُمْ وَرَأَيْتَهُمْ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ ﴿٥﴾

5. Na wanapoambiwa: Njooni ili Mtume wa Mwenyezi Mungu awaombee maghufira, huvigeuza vichwa vyao, na unawaona wanageuka nao wamejaa kiburi.

سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَسْتَغْفَرْتَ لَهُمْ أَمْ لَمْ تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ لَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿٦﴾

6. Ni sawa kwao, ukiwatakia maghufira au usiwatakie maghufura, Mwenyezi Mungu hatawaghufiria. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu mafasiki.

HAO NI MAADUI JIHADHARI NAO

Aya 1-6

MAANA

Qur’an imewasifia maswahaba na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na ikawasifia kwa nguvu daraja zao na vyeo vyao. Vile vile imezungumzia aina za wanafiki katika sura kadhaa na jinsi walivyong’ang’ania kuufanyia vitimbi Uislamu na manabii wake. Masimulizi kuhusiana na wanafiki hayana ukomo, kwa sababu uwongo wao na mbinu zao chafu hazina mpaka.

Kwa hiyo si ajabu kukaririka masimulizi yao, na Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwahusisha na sura kamili katika Kitabu chake na kuwasi­fia kwa sifa mbaya; miongoni mwazo ni hizi zifuatazo:-

Wanapokujia wanafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa hakika wewe ni Mtume wake.

Walidhamiria kumkufuru Mwenyezi Mungu na kumfanyia uadui Nabii wake mtukufu, wakadhihirisha mapenzi na imani kwake na kwa risala yake.

Na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanafiki ni waongo.

Makusudio ya kushuhudia kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni kujua. Maana ni kuwa wanafiki wanasema kwa ndimi zao yale yasiyo nyoyoni mwao; na Mwenyezi Mungu anajua wanayoyaficha na wanayoyadhi­hirisha naye anawangojea tu.

Vile vile Nabii anajua hakika yao, lakini ameamrishwa kuwachukulia kwa dhahiri na sio kwa uhalisia; akasema: “Nimeamriwa kupigana na watu mpaka waseme: Lailahaillallah Muhammadur-rasurullah. (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu) wakishasema basi imehifadhika nami damu zao na mali zao, isipokuwa kwa haki yake, na hisabu yao iko kwa Mwenyezi Mungu.”

Ufasaha zaidi niliousoma kuhusiana na maudhui haya ni kauli ya Imam Ali(a.s ) :“Ulimi wa mumin uko nyuma ya moyo wake na moyo wa mnafiki uko nyuma ya ulimi wake.” Yaani ulimi wa mumin unafuata moyo wake, hasemi isipokuwa analoliamini. Lakini mnafiki moyo wake unafuata ulimi wake na ulimi wake unazunguka na hawaa yake na malengo yake. Natija ya hayo ni kuwa mnafiki hana moyo isipokuwa hawa na matamanio.

Wamevifanya viapo vyao ni kinga, na wao wakajizuia kuifuata Njia ya Mwenyezi Mungu.

Mara nyingi njama za wanafiki zilikuwa zikifichuka, nao kila walipokuwa wakizungumza wanafanya kiapo ndio kinga yao kuzuia kughadhibikiwa na Mtume(s.a.w. w ) na kuficha njama zao dhidi ya Mtume na upinzani wao kwa risala yake.

Hakika ni mabaya waliyokuwa wakiyafanya ya vitimbi, hadaa na kuwa vigeugeu.

Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo umepigwa muhuri juu ya nyoyo zao nao hawafahamu lolote.

Makusudio ya waliamini ni kuwa walijulikana na watu kwamba wameami­ni. Vinginevyo ni kuwa wao hawakuwahi kuamini hata chembe. Na makusudio ya wakakufuru ni kujulikana kuwa kumbe walidhihirisha imani na wakaficha ukafiri. Ama makusudio ya kupigwa muhuri juu ya nyoyo zao ni kuwa hawaongoki kwenye heri baada ya kupofushwa na hawaa na upotevu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 5 (4:137).

Na unapowaona, miili yao inakupendeza , Wana mandhari mazuri na hisia mbaya. Kwa ibara ya Imam Ali(a.s ) :“Nyoyo zao zina maradhi na nyuso zao ni safi.”

Na wakisema, unasikiliza usemi wao , kwa sababu wanazungumza maneno ya wenye ikhlasi na wanaizungumzia dunia kwa maneno ya wenye zuhudi.

Kama kwamba wao ni magogo yaliyoegemezwa . Ni mfano wa magogo, lakini wanakula na kunywa. Kila mwenye kupofu­ka na uongofu, basi ni maiti hai.

Wao hudhania kila ukelele ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; jihadhari nao.

Wana roho za woga wa kufichuka siri zao, hawasikii sauti ila wanadhani ni sauti ya adhabu itakayowanyakuwa bila ya kujua. Woga huu ume­wazidishia lawama na uadui kwenu enyi wenye ikhlasi, basi jihadharini na njama zao na msiwape fursa kadiri mtakavyoweza.

Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanageuzwa?

Hii ni shutuma kwa tamko la kuduia na kushangaa. Maana ni kuwa wao wamelaaniwa kwa vile wameiacha haki kwa inadi na jeuri.

Kila sifa walizosifiwa wanafiki wakati wa Mtume(s.a.w. w ) ni sura iliyoko kwa vibaraka wa leo wanaokula njama na maadui wa Mwenyezi Mungu na wa nchi kwa kuufanyia vitimbi uma wao.

Hakuna hatia kubwa kama kuufanyia hiyana uma, na hakuna fedheha kama mtu kumuuza mtu mwenzake.

Na wanapoambiwa: Njooni ili Mtume wa Mwenyezi Mungu awaombee maghufira, huvigeuza vichwa vyao, na unawaona wanageuka nao wamejaa kiburi.

Mtu akiwanasihi na kuwaambia tubieni mliyo nayo na Mwenyezi Mungu atawaghufiria, basi wao wanag’ang’ania batili na kuipinga haki, waki­inamisha vichwa vyao kwa dharau na kiburi. Kwa vile wao ni wakubwa kuliko wanayoyahitajia kwa Mtume; kama wanavyodai.

Ni sawa kwao, ukiwatakia maghufira au usiwatakie maghufira, Mwenyezi Mungu hatawaghufiria.

Hakuna faida ya kuwataka watengenee; kwa hiyo hakuna haja ya kuwatakia maghufira.

Ni kweli Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira mwenye kurehemu, hilo halina shaka, na rehema ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuenea katika kila kitu, isipokuwa kwa mwenye kuikataa na akaifanyia kiburi. Kwa hiyo itakuwa si huruma kumfanyia yule anayeona kuwa haihitajii huruma yako.

Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu mafasiki , maadamu wanang’ang’ania ufuska.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 10 (9: 80).

هُمُ الَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُوا عَلَىٰ مَنْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّوا وَلِلَّـهِ خَزَائِنُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَفْقَهُونَ ﴿٧﴾

7. Hao ndio wanaosema: Msitoe kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, ili wawaondokee. Na hazina za mbingu na ardhi ni za Mwenyezi Mungu, lakini wanafiki hawafahamu.

يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعْنَا إِلَى الْمَدِينَةِ لَيُخْرِجَنَّ الْأَعَزُّ مِنْهَا الْأَذَلَّ وَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٨﴾

8. Wanasema: Tukirejea Madina mwenye utukufu zaidi bila ya shaka atamfukuza aliye mnyonge. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanafiki hawajui.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٩﴾

9. Enyi mlioamini! Zisiwa­shughulishe mali zenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio wenye hasara.

وَأَنفِقُوا مِن مَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَا أَخَّرْتَنِي إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٠﴾

10. Na toeni katika tulichowapa kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, kisha aseme: Mola wangu! Mbona hukuni­akhirishia muda kidogo nika­toa sadaka, na kuwa katika watu wema?

وَلَن يُؤَخِّرَ اللَّـهُ نَفْسًا إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١١﴾

11. Wala Mwenyezi Mungu hata­iakhirisha nafsi yoyote inapofika ajali yake; na Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.

MWENYE NGUVU ATAMFUKUZA MNYONGE

Aya 7 – 11

MAANA

Hao ndio wanaosema: Msitoe kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, ili wawaondokee.

Wanaosema ni wanafiki na walioko kwa Mtume ni wahajiri walio mafukara. Matajiri wa Kianswar walikuwa wakiwasaidia hawa, ndio wanafiki wakawaambia matajiri msitoe mali zenu kwa muhajiri yoyote ili wapate kuona vibaya waweze kuondoka. Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawarudi kwa kuwaambia:

Na hazina za mbingu na ardhi ni za Mwenyezi Mungu, lakini wanafiki hawafahamu.

Mnawaamuru ubahili wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na wakafanya juhudi katika njia yake, na hali Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa viumbe na ndiye anayevimiliki pamoja na mali zao na ndiye mwenye kuviruzuku! Yeye anaweza kuwatajirisha waumini kwa fadhila yake, lakini nyinyi hamjui.

Wanasema: Tukirejea Madina mwenye utukufu zaidi bila ya shaka atamfukuza aliye mnyonge.

Wafasiri wamesimulia kisa cha Aya hii kinachohusiana na kiongozi wa wanafiki Abdallah bin Ubayya na vita vya Bani Mustaliq.

Hawa walikuwa ni sehemu ya Khuza’a na walikuwa wakiishi karibu na Makka. Waliona kuwa Uislamu utakuwa na nguvu katika Bara Arabu, hivyo wakajiandaa kupigana vita na Mtume(s.a.w.w) wakiongozwa na kiongozi wao Harith bin Abu Dhirar. Mtume(s.a.w.w) alipojua hilo akaharakisha kuwatokea na jeshi lake kabla ya wao kufika Madina.

Ibn Ubayya naye akatoka pamoja na jeshi la waislamu kwa tamaa ya ngawira. Basi Mwenyezi Mungu akampa ushindi Mtume wake dhidi ya maadui zake, wakapata mali nyingi ya ngawira. Mtume(s.a.w.w)

akawaongezea mafukara wahajiri katika ngawira ili kupunguza pengo baina ya mafukara na matajiri. Ibn Ubayya akaona vibaya, akawa anawa­chochea Answar; miongoni mwa aliyoyasema ni: “Tukirejea Madina mwenye utukufu zaidi bila ya shaka atamfukuza aliye mnyonge.”

Mtukufu anajikusudia yeye mwenyewe na mnyonge anamkusudia Mtume(s.a.w.w) . Ndio ikashuka Aya hii na Ibn Ubayya akafedheka. Wafasiri wengi wamesema kuwa Ibn Ubayya alisema neno hili la kufuru kutokana na mzozo uliotokea baina ya mmoja wa wafuasi wake na mfanyakazi wa Umar bin Al-Khattab.

Abdallah bin Ubayya alikuwa na mtoto mwema aliyekuwa akiitwa Abdallah pia. Alipojua kuhusu baba yake, alimwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na kumwambia: “Umekwishajua alivyofanya baba yangu. Ukiwa unataka kumuua basi niamuru mimi nimuue, ili nisije nikashindwa kujizuia kumuona aliyemuua baba yangu, nikamuua mumin kwa sababu ya kafiri, nikaingia motoni.”

Mtume(s.a.w.w) akamjibu:“Tutamuhurumia baba yako na tutaishi naye kwa wema muda ule atakaobakia nasi.”

Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu -Yeye, na Mtume wake, na Waumini.

Hii ni kumrudi Ibn Ubayya aliyejisifu kuwa mtukufu zaidi. Utukufu wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni kuwa yeye ndiye mtukufu zaidi kwa waja wake, utukufu wa Mtume ni dini yake kushinda dini nyingine zote na kuwashinda maadui zake, na utukufu wa waumini ni kushinda haki na watu wake.

Lakini wanafiki hawajui kwamba utukufu ni kwa imani na takua. Enyi mlioamini! Zisiwashghulishe mali zenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio wenye hasara.

Mwenye kuitaamali Aya hii na ile iliyo kabla yake ataona kuwa makusudio ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu hapa ni jihadi.

Kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwanza ametaja utukufu wake, wa Mtume na wa waumini; kisha akawakataza na kuwahadharisha waumini, dunia isiwasahaulishe kumkumbuka Mwenyezi Mungu na akajaalia natija ya hayo ni hizaya na udhalili duniani na Akhera.

Hakuna mwenye shaka kwamba hizaya na udhalili ni natija ya kuipenda dunia na kuhofia jihadi na mauti. Hakuna linalosadikisha hakika hii kuliko maisha ya waislamu na waarabu hivi sasa jinsi yalivyo.

Na toeni katika tulichowapa kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, kisha aseme: Mola wangu! Mbona hukuniakhirishia muda kidogo nikatoa sadaka, na kuwa katika watu wema?

Makusudio ya kufikiwa na mauti ni kudhihiri alama zake na utangulizi wake. Maana ni kuwa chukueni fursa ya kutoa kile alichowapa Mwenyezi Mungu. Na mwenye kupuuza akangoja mpaka siku zake za mwisho mwisho atauma vidole kwa kujuta na kumnyenyekea Mwenyezi Mungu ampe muda kidogo, lakini wapi! Yaliyopita hayarudi.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (14:44).

Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapofika ajali yake; na Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.

Ajali imekwishaamriwa haiwahi wala haichelewi. Mwenye kupoteza fursa hana jingine isipokuwa hasara na majuto. Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (3:145) kifungu cha ‘Ajali haina kinga.’ Na Juz. 8 (7:34).

MWISHO WA SURA YA SITINI NA TATU: SURAT AL- MUNAFIQUN


10

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sitini Na Nne: Surat At – Taghabun. Imeshuka Madina Ina Aya 18.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١﴾

1. Vinamsabihi vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi, Ufalme ni wake, na sifa njema ni zake. Na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ فَمِنكُمْ كَافِرٌ وَمِنكُم مُّؤْمِنٌ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢﴾

2. Yeye ndiye Aliyewaumba. Miongoni mwenu yupo aliye kafiri, na yupo aliye Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda.

خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ ﴿٣﴾

3. Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na akawapa sura, na akazifanya nzuri sura zenu Na marejeo ni kwake.

يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٤﴾

4. Anajua vilivyomo mbinguni na ardhini, na anajua mnayoy­afanya siri na mnayoy­atangaza. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.

أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ فَذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٥﴾

5. Kwani haikuwajia habari ya waliokufuru kabla, wakaonja ubaya wa mambo yao? Na wao wana adhabu iliyo chungu.

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالُوا أَبَشَرٌ يَهْدُونَنَا فَكَفَرُوا وَتَوَلَّوا وَّاسْتَغْنَى اللَّـهُ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٦﴾

6. Hayo ni kwa kuwa walikuwa wakiwajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, nao wakase­ma: Hivi binadamu ndio atuongoze? Basi wakakufuru, na wakageuka upande. Mwenyezi Mungu si muhitaji. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, naye ni Msifiwa.

MIONGONI MWENU KUNA KAFIRI NA MUUMIN

Aya 1 – 6

MAANA

Vinamsabihi vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi.

Baadhi ya viumbe vinamsabihi kwa lugha ya maneno na vingine kwa lugha ya hali. Umetangulia mfano wake katika Juzuu hii tuliyonayo, mwanzo wa sura 62.Ufalme ni wake, humpa amtakaye na humvua amtakaye.

Na sifa njema ni zake. Kwa utukufu wa ihsani yake na uangavu wa dalili zake.Na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu bila ya nyenzo wala kufikiria, bali ni kwa neno ‘kuwa.’

Yeye ndiye Aliyewaumba. Miongoni mwenu yupo aliye kafiri, na yupo aliye Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda.

Mtu katika mtazamo wa kiislamu ni kwa uhuru wake na utashi wake. Hakuna utu bila ya uhuru. Anayo hiyari ya kuchagua imani hata kama wazazi wake ni makafiri, na ana hiyari ya kuchgua ukafiri hata kama wazazi wake ni waumini; wala haifai kabisa yeyote kumlazimisha mwingine - hakuna kulazimishana katika dini; vinginevyo taklifa, hisabu na thawabu zitakuwa ni batili.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kumpa mja wake uhuru, unaomfanya kuwa mtu, akamwamuru kufuata imani na kufanya heri na akamkataza ukafiri na kufanya shari, akamwekea dalili za uzuri wa aliyomwamrisha na ubaya wa aliyomkataza; kutokana na akili yake na maumbile yake. Wakaamini baadhi ya watu na wakakufuru waliokufuru; na kila mmoja atapata thawabu au adhabu kulingana na imani na matendo yake.

Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki,

Yaani kwa hikima ya hali ya juu; wala hakuna chochote katika ulimwengu huu kilichoko kwa mchezo, wala hakuna tofauti baina ya kusema kuwa vitu vimepatikana kwa sadfa na kusema kuwa kila kitu, hata nidhamu, kimejileta chenyewe.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 14 (16:3).

Na akawapa sura, na akazifanya nzuri sura zenu.

Msanii anaweza kutengeneza sura ya chochote na kwa ufundi na ustadi wa hali ya juu, lakini kazi yake kubwa inakuwa ni kupamba na kuweka shepu tu; sawa na mjengaji anayeweka jiwe juu ya jiwe jingine, lakini nyenzo za ujenzi na kutengeneza sura inatoka kwa anayekiambia kitu kuwa na kikawa.

Mwenyezi Mungu aliiumba mada ya mtu kwa neno ‘kuwa’ akaitia sura zaidi kuliko viumbe vingine. Umetangulia mfano wake katika Juz. 18 (23:14)

Na marejeo ni kwake awambie mliyokuwa mkiyafanya, na mwenye kuepushwa na moto atakuwa amefuzu.

Anajua viliomo mbinguni na ardhini, na anajua mnayoyafanya siri na mnayoyatangaza. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliomo vifuani. Maana yako wazi. Kwa ufupi ni kuwa Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.

Kwani haikuwajia habari ya walio kufuru kabla, wakaonja ubaya wa mambo yao? Na wao wana adhabu iliyo chungu.

Swali ni la kutahayariza, na maneno yanaelekezwa kwa washirikina waliomkufuru Muhammad(s.a.w. w ) na wakatangaza vita naye na mwito wake. Amewakumbusha Mwenyezi Mungu yaliyowapata waliokuwa kabla yao; kama vile kaumu ya Nuh, A’d na Thamud - waliwakadhibisha mitume yakawasibu maangamizi duniani na adhabu ya Akhera ni kali zaidi na ya kufedhesha.

Hayo ni kwa kuwa walikuwa wakiwajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, nao wakasema: Hivi binadamu ndio atuongoze? Basi wakakufu­ru, na wakageuka upande.

‘Hayo’ ni ishara ya adhabu iliyowafika uma zilizopita kwa vile wali­wakadhibisha mitume. Waliwajia na dalili mkataa juu ya utume wao, lakini bado wao waling’ang’ania kufuru, si kwa lolote ila ni kuwa mitume ni watu kama wao watawaongozaje!

Hawajui kuwa uongozi unatokana na ilimu? Ajabu ni kuwa walipopewa mwito wa tawhid walisema ‘mtu kama sisi atuongoze?’ lakini hawakumwambia hivi aliyewaita kwenye ibada ya mawe, bali walimsikiliza na kumtii bila ya ubishi. Hili si la kushangaza, ndio tabia ya ujinga.

Kadiri nitakavyotia shaka, lakini siwezi kutia shaka kuwa wenye busara lau watahiyarishwa baina ya upofu pamoja na ilimu, na ujinga pamoja na uoni, basi wangelichagua upofu, kwa sababu hauwezi kulikaribisha la mbali wala kulibaidisha la karibu, wala hausawirishi weusi kuwa weupe au weupe kuwa weusi. Lakini ujinga unasawirisha uongofu kuwa ni upotevu, upotevu kuwa uongofu, haki kuwa batili na batili kuwa haki.

Mwenyezi Mungu si muhitaji. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, naye ni Msifiwa.

Kila kilichoko kinashuhudia kwa lugha ya maneno na lugha ya hali kuwa Mwenyezi Mungu hawahitajii viumbe na utiifu wao, mwenye kusifiwa katika sifa zake zote na vitendo vyake.

زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٧﴾

7. Waliokufuru wanadai kuwa hawatafufuliwa. Sema: Kwani? Naapa kwa Mola wangu! Hapana shaka mtafu­fuliwa, na kisha hapana shaka mtaambiwa mliyoyatenda. Na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.

فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالنُّورِ الَّذِي أَنزَلْنَا وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٨﴾

8. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Nuru tuliyoiteremsha. Na Mwenyezi Mungu kwa mnay­oyatenda anazo habari.

يَوْمَ يَجْمَعُكُمْ لِيَوْمِ الْجَمْعِ ذَٰلِكَ يَوْمُ التَّغَابُنِ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿٩﴾

9. Siku atakayowakusanya kwa ajili ya Siku ya Mkusanyiko; hiyo ni siku ya hasara. Na anayemwamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema, atamfutia maovu yake, na atamuingiza katika Bustani zipitiwazo na mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ خَالِدِينَ فِيهَا وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٠﴾

10. Na waliokufuru na waka­ kadhibisha Ishara zetu, hao ni watu wa Motoni, watadumu humo milele. Na hayo ndiyo marudio mabaya.

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١١﴾

11. Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoza moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿١٢﴾

12. Na mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume. Mkigeuka, basi hakika juu ya Mtume wetu ni kufikisha kwa uwazi tu.

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٣﴾

13. Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipo kuwa Yeye. Na juu ya Mwenyezi Mungu nawategemee Waumini.

HII NI SIKU YA HASARA

Aya 7-13

MAANA

Waliokufuru wanadai kuwa hawatafufuliwa. Sema: Kwani? Naapa kwa Mola wangu! Hapana shaka mtafufuliwa, na kisha hapana shaka mtaambiwa mliyo yatenda. Na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.

Tumebainisha njia ya Qur’an katika ufufuo na kuzirudi shaka shaka za wakanushaji na kwamba mwenye kufanya kitu bila ya mali ghafi basi ni rahisi zaidi kwake kuvikusanya viungo baada ya kutawanyika kwake. Tumefafanua kwa mifumo mbali mbali katika kufasiri Aya za ufufuo; kama vile Juz. 11 (10:4) ‘Hisabu na malipo ni lazima.’

Unaweza kuuliza : Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) alitoa mwito wa ufufuo kwa kiapo wakampinga waabudu masanamu; na kimsingi ni kuwa ushahidi ni wa mwenye kudai na kiapo ni cha mwenye kupinga. Msingi huu ni wa kibinadamu uliokubaliwa na sharia zote. Kwa hiyo basi Mtume(s.a.w. w ) anatakiwa alete ushahidi, sio aape. Sasa je, kuna wajihi gani wa Mtume kuleta kiapo na alitakiwa alete hoja za kuwanyamazisha. Je ufufuo utathibitika kwa kuapa tu?

Jibu : Kwanza, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasimulia kuwa wakanushaji hapa walimwuliza Mtume kuhusu ufufuo kama wenye kuchunguza sio wenye kujadiliana; hawakusema:

مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ ﴿٧٨﴾

“Ni nani atakayeiuisha mifupa nayo imemung’unyika?” Juz. 23 (36:78).

Au kusema:

أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ﴿١٦﴾

“Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?” Juz. 23 (37:16).

Kwa kuwa, katika Aya tuliyo nayo, wakanushaji walitosheka na kuuliza tu, sio kushangaa na kujadiliana, basi Mwenyezi Mungu na Mtume wake wametosheka na kujibu tu pamoja na msisitizo wa kiapo.

Ndio maana pale waliposema: ‘Ni nani atakayeihuisha mifupa nayo imemung’unyika,” aliwaambia: “Ataihuisha yule Alieiumba mara ya kwanza. Na Yeye ni mjuzi wa kila jambo.” Jibu linakuja kulingana na swali.

Pili , wale waliokufuru pamoja na wanafiki walikuwa wakiamini kuwa Mtume(s.a.w. w ) hawatakii heri wala masilahi; isipokuwa anataka kujituku­za na kuwa juu yao; kama walivyoamini makafiri, hapo kabla, kwa Nabii Nuh:

فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ مَا هَـٰذَا إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُرِيدُ أَن يَتَفَضَّلَ عَلَيْكُمْ ﴿٢٤﴾

“Wakasema wale wakuu waliokufuru: Huyu si chochote ila ni mtu tu kama nyinyi, anataka kujipatia ubora juu yenu.” Juz. 18 (23:24).

Ndio akaapa Mtume kwamba mwito wake ni wa haki; akimaanisha kuwa hataki isipokuwa haki tu. Mfano wake ni kauli ya Shu’ayb kwa watu wake walipomdhania mabaya:

إِنْ أُرِيدُ إِلَّا الْإِصْلَاحَ مَا اسْتَطَعْتُ وَمَا تَوْفِيقِي إِلَّا بِاللَّـهِ ﴿٨٨﴾

“Sitaki ila kutengeneza kiasi ninavyoweza. Na tawfiki yangu haiko ila kwa Mwenyezi Mungu.” Juz. 12 (11:88).

Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Nuru tuliyoiteremsha.

Maadamu ufufuo ni haki na hisabu na malipo ni haki, basi ni juu ya kila mtu kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nuru; yaani Qur’an. Ameisifu kuwa ni nuru kwa vile inamtoa mtu kwenye giza la ujinga na kufuru kumpeleka kwenye nuru ya ilimu na imani na kumwongoza kwenye njia ya salama:

قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾ سُبُلَ السَّلَامِ وَيُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٦﴾

“Hakika imekwishawafikia nuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Kitabu kinachobainisha. Mwenyezi Mungu huwaongoza kwacho wenye kufuata radhi yake katika njia za amani na huwatoa katika giza kuwapeleka kwen­ya nuru kwa amri yake, na huwaongoza katika njia iliyonyooka.” Juz.6 (5:15-16).

Na Mwenyezi Mungu kwa mnayoyatenda anazo habari. Siku atakayowakusanya kwa ajili ya Siku ya Mkusanyiko; hiyo ni siku ya hasara.

Neno ‘hasara,’ tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu taghabun ambalo wafasiri wengi wamesema kuwa makusudio yake hapa ni kupunjana, ambapo siku ya Kiyama watu wa haki watawapunja watu wa batili, lakini tunavyofahamu sisi ni kuwa makusudio yake ni faida na hasara; ambapo wenye haki watapata faida na wabatilifu watapata hasara. Hata hivyo nati­ja ya maana zote mbili ni moja.

Mwenyezi Mungu anadhibiti kauli za waja wake, vitendo vyao, malengo yao na makusudio yao katika maisha ya dunia na kuyatumia siku ya Kiyama kwa hisabu.

Yakiwa ni heri basi ni heri na yakiwa ni shari basi ni shari. Siku ya mwisho imeitwa ya mkusanyiko kwa vile Mwenyezi Mungu atawakusanya viumbe kwa ajili ya hisabu na malipo.

Na anayemwamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema, atamfutia maovu yake, na atamuingiza katika Bustani zipitiwazo na mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa. Na waliokufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ni watu wa Motoni, watadumu humo milele. Na hayo ndiyo marudio mabaya.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kusema kuwa Yeye atawakusanya watu siku isiyo na shaka, sasa anasema kuwa watu siku hiyo watakuwa aina mbili:

Ya kwanza : ni wale waliomwamini Mwenyezi Mungu, mitume wake na vitabu vyake na wakajitayarisha kwa matendo mema duniani kwa ajili ya Akhera yao. Aina hii ya watu ndio watakaofuzu kesho kwa kupata maghufira ya Mwenyezi Mungu na radhi yake na kwa kupata neema isiyo na ukomo wala kupungua kiwango chake.

Aina ya pili , ni waliopotezwa na dunia wanaoitafuta kwa njia yoyote itakayokuwa; hawajali dini wala dhamiri au halali wala haramu. Aina hi ya watu ndio watakaopata hasara, makazi yao ni Jahannam ambayo ni marejeo mabaya kabisa.

Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa shari yoyote ya duniani ni kwa kadha na kadari yake Mwenyezi Mungu. Na hii inapingana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ﴿٣٠﴾

“Na misiba inayowasibu ni kwa sababu ya yaliyotendwa na mikono yenu. Naye anasamehe mengi.” Juz. 25 (42:30).

Hili tumelijibu kwa ufafanuzi katika Juz. 5 (4:78-79). Ufupi wa jawabu ni kuwa majanga ya kimaumbile; kama vile tetemeko la ardhi kahati nk, yananasibika na maumbile moja kwa moja na yanasabishwa Kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wasita; kwa vile Yeye ndiye Alieyaleta maumbe.

Hii ndio maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.” Na msiba wowote ambao chimbuko lake ni kupuuza na ufisadi, linanasibika kwenye uchaguzi mbaya wa kupuuza na ufisadi. Hii ndio iliyokusudia na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na misiba inayowasibu ni kwa sababu ya yaliyotendwa na mikono yenu.”

Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoza moyo wake.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamchukulia mtu kwa vile inavyochagua nafsi yake. akijichagulia uongofu na heri na kufauata njia iliyonyoka, basi humshika mkono, kumsaidia na kumpatia thawabu za wenye kuongoka. Na akijichagulia upotevu na kuifuata njia yake, humwachilia mbali na kumtweza kisha anamtia kwenye adhabu ya moto.

Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

Anamjua mwenye kujihurumia na anamuhurumia, na mwenye kujiangamiza kwa makusudi basi humwangamiza.

Na mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume. Mkigeuka, basi hakika juu ya Mtume wetu ni kufikisha kwa uwazi tu.

Wajibu wa Mtume ni kufikisha na wajibu wetu ni kusikiliza na kutii. Umetangulia mfano wake katika Aya kadha, ikiwemo ile iliyoko Juz. 7 (5:92).

Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipokuwa Yeye. Na juu ya Mwenyezi Mungu nawategemee Waumini.

Anawatoshea wenye kumtegemea Yeye na ni walii wa wenye ikhlasi.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ وَإِن تَعْفُوا وَتَصْفَحُوا وَتَغْفِرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤﴾

14. Enyi mlioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui zenu. Basi tahadharini nao. Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ وَاللَّـهُ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٥﴾

15. Hakika mali zenu na watoto wenu ni mtihani. Na kwa Mwenyezi Mungu kuna ujira mkubwa.

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنفِقُوا خَيْرًا لِّأَنفُسِكُمْ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٦﴾

16. Basi mcheni Mwenyezi Mungu vile muwezavyo, na sikieni, na tiini, na toeni, itakuwa heri kwa nafsi zenu. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.

إِن تُقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعِفْهُ لَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ وَاللَّـهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٧﴾

17. Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atawazidishia maradufu, na atawaghufiria. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukrani, Mpole.

عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

18. Mwenye kujua ghaibu na dhahiri. Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

UADUI WA WAKE NA WATOTO

Aya 14 – 18

MAANA

Enyi mlioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui zenu. Basi tahadharini nao.

Katika vitabu vya tafsiri na Hadith kuna maelezo kuwa kuna watu waliosilimu Makka na wakataka kuhamia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) , wake zao na watoto wao wakawazuia. Ndipo ikashuka Aya hii kuwahadharisha waumini wasiwatii baadhai ya wake zao na watoto.

Mara nyingi tumesema kuwa sababu ya kushuka haiihusishi Aya na tukio hilo, bali inaenea. Hiyo inakuwa ni sehemu tu miongoni mwa sehemu zake. Kwa hiyo basi kila mke asiyesaidiana na mumewe kwenye lile lilo na masilahi kwa pande zote mbili kidini na kidunia, basi huyo ni adui yake.

Pia mume atakuwa ni adui wa mke akiwa naye ni kikwazo kwa hilo. Vile vile kwa upande wa mtoto na mzazi bali mama na ndugu. Lolote linalofanywa na adui, akilifanya naye pi atakuwa ni adui, kwa hali yoyote itakavyokuwa.

Kwa mnasaba huu tunasema kuwa, kutoka mtu kwenye maisha ya useja kwenda kwenye maisha ya ndoa kunafanana na kwenda Akhera; itakuwa ni Peponi au motoni. Mara nyingi sana ni motoni sio kwenye neema. Kwani maisha ya familia wakati huu ni adhabu na Jahannam - mtoto hawezi kumridhia baba yake ila kwa kutiiwa yeye na kunyenyekewa, wala mke hamridhii mume ila awe yeye ndio mume na mume awe mke!

Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

Hakuna tofauti baina ya msamaha, kupuuza na maghufira isipokuwa kwenye matamshi tu. Makusudio ya kuyachanganya matamko haya ni kiasi cha kusisitiza na kuhimiza tu.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuhadharisha baadhi ya wake na wato­to kwa vile wanafanya wayafanyayo maadui akasema: Mkiwasamehe kwa kuwahurumia na kutumaini kurekebika kwao, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atawafanyia hivyo hivyo nanyi, kwa sababu Yeye humhurumia mwenye huruma na humsamehe mwenye kusamehe, lakini ni pale ikiwa kufanya hivyo ni vizuri; vinginevyo baadhi ya makosa haifai kuyasamehe kwa hali yoyote.

Aya inaashiria kwamba maisha ya famailia hayawezekani isipokuwa kwa subira na kusamehe. Na kwamba lau mtu atahisabu kila linalotoka kwa watoto wake basi mzozo usingemalizika na wangeliishi kwenye Jahannam.

Hakika mali zenu na watoto wenu ni mtihani. Na kwa Mwenyezi Mungu kuna ujira mkubwa.

Kila litakalokuvutia na kukuzuia na majukumu ya kidunia na akhera, hilo ni mtihani; iwe ni mali, mtoto, mke, cheo, usanii n.k. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amehusisha kutaja mali na watoto, kwa sababu ndiyo mambo yanayoongoza kwenye majaribu. Kadiri ladha ya dunia itakavyokuwa kubwa, lakini yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na yenye kubaki. Umetangulia mfano wake katika Juz. 9 (8:28). Katika Tafsir Tabari na nyinginezo kuna maelezo haya: “Mtume(s.a.w. w )

alikuwa akihutubia, akaja Hasan na Husein wakiwa wamevaa kanzu nyekundu, wakijikunguwaa na kusimama. Basi Mtume akashuka akawachukua na kuwabeba mapajani mwake; kisha akasema: Amesema kweli Mwenyezi Mungu: Hakika mali zenu na watoto wenu ni mtihani. Nimewaona hawa na kukatisha mazungumzo yangu ili niwachukue. Kisha akaendelea na hutuba yake.

Basi mcheni Mwenyezi Mungu vile mwezavyo,

Fanyeni bidii kadiri mnavyoweza kuzichunga nafsi zenu na majaribio na mjiweke mbali na aliyoyaharimisha Mwenyezi Mungu wala msifanye chochote cha haramu kwa sababu ya mali au watoto.

Kuna mfasiri aliyesema kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu ipasavyo kumcha.” Juz. 4 (3:102) ni ya mkazo zaidi na kauli yake hii hapa ‘Basi mcheni Mwenyezi Mungu vile mwezavyo,’ ni ya tahafifu; kisha akaongezea hapo kuwa kauli hii imeondoa hukumu ya kauli ile.

Sisi hatuoni tofauti yoyote baina ya Aya mbili hizi, kwa sababu wajibu wa mtu ni kujikinga na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, kadiri atakavyoweza, wala yeye halazimiki na asichokiweza. Tazama Juz. 3 (2:286).

Na sikieni, na tiini, na toeni,

Sikieni mwito wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na muuchunge kwa utiifu na takua, na toeni ziada ya mali yenu katika njia ya Mwenyezi Mungu. Hiyo itakuwa heri kwa nafsi zenu; yaani:

إِنْ أَحْسَنتُمْ أَحْسَنتُمْ لِأَنفُسِكُمْ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا ﴿٧﴾

“Mkifanya uzuri mnajifanyia wenyewe na mkifanya ubaya mnajifanyia wenyewe.” Juz. 15 (17:7)

Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.

Kutoa mali na nafsi ni njia ya kufaulu na kuokoka na kuifanyia ubahili mali na nafsi ni njia ya hasara. Kwa sababu ubahili na uchoyo ni katika nguvu kubwa inayopelekea kujiingiza kwenye maovu.

Imetangulia kwa herufi zake katika Juzuu hii tuliyo nayo (59:9).

Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atawazidishia maradufu, na atawaghufiria. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukrani, Mpole.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anataka mkopo kwa waja wake na hali anazo hazina za mbingu na ardhi, anawazidishia malipo watiifu kwa hisani kutoka kwake, anawaghufiria wenye kutubia kwa kuwahurumia, anawashukuru wenye kufanya ihsani kwa kuwapa kingi kutokana na kichache walichotoa na anawapa muda waasi; kama kwamba amewasamehe. Umetangulia mfano wake katika Juz. 2 (2:245), Juz. 9 (5:12) na Juz. 27 (57:11).

Mwenye kujua ghaibu na dhaahiri hakifichiki kitu chochote kwake.Mwenye nguvu, isiyoshindwaMwenye hikima katika alivyoumba na kupangilia.

MWISHO WA SURA YA SITINI NA NNE: SURAT AT – TAGHABUN


11

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sitini Na Tano: Suarat At-Talaq. Imeshuka Madina. Ina Aya 12.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu.

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ وَاتَّقُوا اللَّـهَ رَبَّكُمْ لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِن بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ لَا تَدْرِي لَعَلَّ اللَّـهَ يُحْدِثُ بَعْدَ ذَٰلِكَ أَمْرًا ﴿١﴾

1. Ewe Nabii! Mtakapowapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao, na fanyeni hisabu ya eda, na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu msiikiuke; na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake Hujui; pengine Mwenyezi Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya.

فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّـهِ ذَٰلِكُمْ يُوعَظُ بِهِ مَن كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا ﴿٢﴾

2. Basi wanapofikia muda wao, muwashike kwa wema, au farakianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi waw­ili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo anavyoagizwa anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anayemcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea.

وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ إِنَّ اللَّـهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّـهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا ﴿٣﴾

3. Na humruzuku kwa upande asiotazamia. Na anayemtege­mea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu amejaalia kila kitu na kipimo chake.

وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِن نِّسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا ﴿٤﴾

4. Na wale waliokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayoshaka, basi eda yao ni miezi mitatu, pamo­ja na ambao hawakupata hedhi. Na wenye mimba eda yao ni mpaka watakapozaa. Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake

kuwa mepesi.

ذَٰلِكَ أَمْرُ اللَّـهِ أَنزَلَهُ إِلَيْكُمْ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُعْظِمْ لَهُ أَجْرًا ﴿٥﴾

5. Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu amewateremshia. Na anayemcha Mwenyezi Mungu atamfutia maovu yake, na atampa ujira mkubwa.

TALAKA KWA WAKATI WA EDA

Aya 1 – 5

MAANA

Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu amewateremshia. Na anayemcha Mwenyezi Mungu atamfutia maovu yake, na atampa ujira mkubwa.

Katika Aya hizi Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja hukumu za talaka, kama ifuatavyo:

1.Ewe Nabii! Mtakapowapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao.

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume(s.a.w. w ) , lakini wanakusdiwa wenye kukalifiwa na sharia wote. Kwa sababu sharia inawahusu wote.

Maana ni kuwa mwislamu akitaka kumpa talaka mkewe, anatakikana angoje wakati mnasaba wa kuingia kwenye eda; kiasi amabacho wakati wa talaka utakuwa ni sehemu ya eda. Madhehebu yote ya kiislamu yamekongamana kwenye hilo.

Lakini Sunni wanasema uharamu huu hauharibu talaka kwa kukosekana sharti hilo; bali talaka itakuwa sahihi na mtaliki atapata dhambi.

Shia Imamiya wamesema talaka itakuwa ni upuzi tu, kwa sababu lil­iokatazwa ni tendo; sawa na kukatazwa kuuza pombe, lengo lake ni kukataza tendo lenyewe sio kukataza tamko lake.

Miongoni mwa waliyoyatolea dalili Shia ni yaliyoelezwa kwenye Sahih Bukhar na Sahii Muslim kwamba Ibn Umar alimpa talaka mkewe akiwa katika hedhi, basi Umar akamuuliza Mtume(s.a.w. w ) kuhusu hilo, akasema Mtume: Mwamrishe amrejee, kisha amwache mpaka atwaharike kisha aingie hedhini tena atwaharike. Hapo sasa akipenda ataamzuia na akipen­da atampa talaka kabla ya kumgusa. Hiyo ndio eda alioyoiamuru Mwenyezi Mungu Mtukufu apewe talaka kwayo.

Kauli yake Mtume(s.a.w. w ) “Akitaka amzuie na akitaka amwache kabla ya kumgusa,” ni ubainifu na tafsiri ya kauli yake: “Amrejee.” Kwamba yaani bado ni mkewe, kwa hiyo amzuie kwa hali yoyote ile wala hakuna hiyari isipokuwa akimpa talaka kwa masharti yake.

Haya ndio maana ya amrejee. Si sahihi kuwa hiyo ni amri ya kumrejea kitalaka; kama walivyosema wanafiqh wa madhehebu mengine. Kwa sababu kumrejea kwa talaka ni kumzuia mke ambako ni natija ya kauli yake ‘Na amrejee!’ na kimsigi jambo haliwezi kuwa hilo lenyewe ndio natija.

Zaidi ya hayo kurejea kwa talaka hakuondoi dhambi iliyotangulia ili kuam­ruwe na Mtume(s.a.w. w ) . Madhehbu yote yameafikiana kwa kauli moja kuwa mke ambaye hajaingiliwa na mumewe anaweza kuachika hata akiwa kwenye hedhi, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Kwa eda yao, na asiyeingili­wa hana eda kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Enyi ambao mmeamini! Mkiwaoa wanawake waumini kisha mkawaacha kabla ya kuwagusa, basi hamna eda juu yao mtakayoihisabu.” Juz. 22 (33:49).

2.Na fanyeni hisabu ya eda.

Mjue mwanzo wa eda na mwisho wake, kwa sababu ina hukumu zinazo­husiana nayo; kama posho ya aliye kwenye eda, haki ya kurejelewa ikiwa ni talaka rejea, haki yake ya kurudia alichokitoa, ikiwa ni talaka ya kujivua (Khul’u), uharamu wa kuolewa mpaka amalize eda na mengineyo waliyoyataja wana fiqh katika vitabu vyao…

Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu katika yale aliyowawajibishia katika hukumu za eda.

3.Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe.

Makusudio ya nyumba zao ni nyumba wanazokaa, sio nyumba za kumiliki; sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na kaeni majumbani mwenu…Na kumbukeni yanayosomwa majumbani mwenu” Juz. 22 (33:33-34).

Wameafikiana mafaqihi kuwa mwenye kuachwa talaka rejea anastahki posho, pamoja na makazi muda ule atakaokaa eda. Wametofautiana katika posho ya aliyeachwa talaka baini.[2]

Hanafi wamesema anastahiki posho, awe ana mimba au la. Malik akasema akiwa hana mimba anastahiki makazi tu na akiwa na mimba basi anastahiki posho kamili. Shafii, Shia Imamiya na Hambali wamesema hana posho akiwa hana mimba, lakini akiwa nayo basi anastahiki posho.

Ikiwa wajibu posho basi ni wajibu kwa mtalikiwa kubakia kwenye nyumba aliyotalikiwa mpaka uishe muda wa eda na ni haramu kutoka au kum­toa; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: ‘Wasitoke …. Wala msiwatoe.’Ila wakifanya uchafu ulio wazi ; yaani utakaothibitika kisharia.

Wameafikiana kwamba zina ni uchafu unapelekea kutolewa nyumbani. Lakini wametofautina katika isiyokuwa zina. Tuonavyo sisi ni kuwa makusudio ya uchafu hapa, (Fahisha), ni zina tu, kwa sababu neno hili likinasibishwa kwa wanawake basi fahamu inayokuja haraka akilini ni zina.

Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu msiikiuke.

Yaani masharti ya talaka na hukumu za eda. Nazo ni hukumu za Mwenyezi Mungu na mipaka yake aliyoibainisha katika Kitabu chake na kupitia kwa Mtume wake.

Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake , kwa sababu ameipeleka kwenye ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake. Aya nyingine inasema:

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٤﴾

“Na mwenye kumwasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akapetuka mipaka yake, atamtia katika moto; ni mwenye kudumu humo, na atapata adhabu idhalilishayo.” Juz. 4 (4:14).

Hujui; pengine Mwenyezi Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya.

Hujui wewe mtaliki labda Mwenyezi Mungu anaweza kuunganisha nyoyo mbili zilizotengana na mambo yakarudi kama zamani. Hapa kuna ishara kwamba nyoyo zina wakati, na inatikakana mtu asiseme jambo kuwa nital­ifanya kesho ila kwa kusema inshallah. Ndio maana Imam Ali(a.s ) akasema:“Nimemjua Mwenyezi Mungu kwa kuvurugika maazimio.’ Yaani kuharibika maazimio ni dalili wazi kuwa kwenye mipango ya mtu kuna mipango ya juu na yenye nguvu zaidi.

4.Basi wanapofikia muda wao, muwashike kwa wema, au farakianeni nao kwa wema.

Ikiwa muda wa eda unakurubia kwisha basi, mtaliki ana hiyari, akitaka atabadilisha azma yake na kumrudisha mtalikiwa kwenye hifadhi yake na akipenda atabakia kwenye hukumu ya kufarikiana na kukatika mfunga­mano baina yao. katika hali zote mbili anatakikana asimdhuru mke, bali amtekelezee haki yake kwa ukamilifu. Haya ndio makusudio ya kumweka kwa wema au kufarikiana naye kwa wema. Umetangulia mfano wake katika Juz. 2 (2:231).

Mtalikiwa anaweza kuwa amekoma kutoka hedhi, ana mimba au hana mimba. Kuhusu wawili wa mwanzo maelezo yao yatakuja.

Ama muda wa eda ya asiyekuwa na mimba ni twahara tatu zikiwa ni pamoja na ile aliyepewa talaka. Hii ni kwa Shia Imamiya, Malik na Shafii. Ama kwa Hanafi na Hambali eda yake ni hedhi tatu. Tazama Juz. 2 (2:228).

5.Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu.

Mafaqihi wa madhehebu wameafikana kuweko ushahidi wa waadilifu wawili kwa mujibu wa Aya hii, lakini wakatofautiana ushahidi uwe kwenye nini? Kwenye kurejea au kwenye talaka? Mafakihi wa kisunni wamesema, unazingatiwa kwenye kurejea, lakini wengine wakasema ni wajib; kama Shafii na wengine wakasema ni sunna; kama Hanafi.

Shia imamiya wanasema kuwa si wajibu ushahidi kwenye kurejea, isipokuwa kwenye talaka. Dkt. Muhammad Yusuf Musa, mhadhiri na raisi wa kitengo cha shariya ya Kiislamu, kitivo cha haki katika chuo Kikuu cha Azhar, anasema katika kitabu chake: Al-ahawalu shakhsiyya Uk. 271, chapa ya 1958:

Shia Imammiya wanaona kuwa miongoni mwa masharti muhimu ya talaka ni kuhudhuria mashahidi wawili waadilifu, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu.”

Na katika hilo anasema mmoja wa ulama wao: Hii ni nyenzo nzuri zaidi ya muungano wa wanandoa, kwa sababu watu wema wana athari katika nafsi kuweza kutuliza mawimbi yawe sawa. Ikiwa nasa­ha zao hazitafaulu, lakini angalau talaka zitapungua kwa kuweko sharti la waadilifu wawili.” Dkt. anaongeza kusema: “Hili halitakikani kufumbiwa macho. Kwa kweli kuichukua rai hii kutaandaa njia ya kutengenea mambo mengi.”

Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Maneno yanaelekezwa kwa mashahidi. Maana ni kuwa msigeuze kitu kati­ka ushahidi, bali utekelezeni kwa njia yake kwa kukusudia kuithibitisha haki, sio kuwaridhisha au kukomoa wanaoshudiliwa.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 3 (2:283).

Hivyo ndivyo anavyoagizwa anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.

Ukweli ni kuwa wanaonufaika na ubainifu wa Mwenyezi Mungu na kutumia hukumu zake ni wale wanaomcha Mungu. Lakini wale wasioamini isipokuwa nafsi zao na masilahi yao, hao ni kama wanyama, hamu yao ni matumbo yao na moto ndio makazi yao.

Na anayemcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea.

kwenye haramu yake kwenda kwenye halali yake na kwenye maasi yake kwenda kwenye twaa yake na humtoshea na kuhitajia wengine,na hum ruzuku kwa upande asiotazamia.

Tunavyofahamu kutokana na Aya hii ni kuwa riziki haina udhibiti maalumu wala kiasi. Inaweza ikaja bila ya kutazamia na inaweza kuondoka bila ya kutazamia. Kuna matukio mangapi mazuri yanamtokea mtu bila ya kutarajia na kuyapanga na ni matukio mangapi mabaya ya kuumiza, yasiyotazamiwa kutokea, yanatokea? Hakuna shaka kuwa baadhi yanatokea kwa kupuuza na mengine ni kwa mipangilio ya mpangiliaji wa viumbe.

Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha.

Kumtegemea Mwenyezi Mungu ni kuchukua desturi yake ya kufanyakazi na kuhangaika kwa kufuata nyenzo: “Basi tembeeni katika pande zake na kuleni katika riziki zake.” (67:15).

Na Hadith inasema:“Tia akili na utawakali.”

Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake . Analolitaka linakuwa na asilolitaka haliwi.

Mwenyezi Mungu amejaalia kila kitu na kipimo chake , hakuna mchezo, wala vurugu au sadfa. Katika Aya nyingine anasema: “Na ameum­ba kila kitu na akikadiria kipimo.” Juz. 18 (25:2). Pia amesema: “Na kila kitu kwake ni kwa kipimo.” Juz. 13 (13:8).

6.Na wale waliokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayoshaka, basi eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawakupata hedhi.

Mafaqihi wa kisunni wametofautiana sana kuhusiana na umri wa kukoma hedhi; kiasi cha kufikia mgongano na kutatizika. Kuna aliyesema ni miaka 50, mwingine akasema ni 55, watatu akasema ni 60, wanne akasema ni 62,watano akatofautisha baina ya wanawake waarabu na wasiokuwa waarabu akasema kuwa waarabu wana nguvu kimaumbile na wa sita akasema, kila mwanamke ataangalia desturi ya ukoo wake. Na wengi katika wao wamenyamaza hawakuweka kiwango cha mwaka wa kukoma hedhi.

Vile vile wametofautiana katika neno ‘ikiwa mnayo shaka.’ Mmoja akasema ni kutia shaka katika hukumu ya eda si katika hali ya mwanamke na kufikia kwake mwaka wa kukoma hedhi. Wengine wakaseam makusudio ni kutia shaka katika hali ya mwanamke na kukoma kwake.

Ama Shia wamesema: Mwaka wa kukoma hedhi kwa mkuraishi ni miaka 60 na kwa asiyekuwa mkuraishi ni miaka 50, wakitegemea riwaya za Ahlulbayt.

Vile vile wamesema kiwango cha chini kuweza kutoka hedhi ni miaka 9. Hii inaafikiana na yaliyoelezwa kwenye kitabu Almughni cha Ibn Quddama, katika sunni: “Uchache wa umri wa kupata hedhi ni miaka 9, kwa sababu marejeo katika hilo ni kupatikana, na amepatikana aliyetoka hedhi katika umri wa miaka 9. Na imepokewa kutoka kwa Shafii kwamba yeye alimuona mwanamke mwenye wajukuu akiwa na miaka 21.”

Nimesoma katika gazeti kuwa kuna msichana aliyepata hedhi kabla ya miaka9.

Wametofautiana Sunni na Shia katika kufasiri Aya hii. Mafaqihi wa kisunni wakasema kuwa makusudio ya waliokoma kupata hedhi ni waliokatikiwa na hedhi kwa sababu ya umri wao mkubwa, na ambao hawakupata hedhi ni wale ambao hawajapata hedhi kwa sababu ya umri wao mdogo. Wote hawa eda yao ni miezi mitatu, wakiwa wameingiliwa na waume zao.

Hii inaafikiana na baadhi ya mafaqihi wakubwa katika Shia imamiya; kama vile Sayyid Almurtadha, Ibn Zuhra, Ibn Samaa na Ibn Shahr Shub. Hata hivyo wengi katika Shia imamiya, wamesema kuwa makusudio ya waliokoma kupata hedhi ni wanaotiliwa shaka kuwa hedhi yao imekatika kwa umri au kwa jambo jingine.

Na wakafasiri kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Ikiwa mnayo shaka,” kuwa ni kutia shaka katika hali yao. Ama makusudio ya ambao hawakupata hedhi ni wale walio katika umri wa hedhi, lakini hawapati hedhi kwa sababu nyingine isiyokuwa ya umri mdogo au mkubwa. Wote hawa eda yao ni miezi mitatu. Wametegemea riwaya za Ahlu bayt katika hilo. Kwa hiyo basi Aya haikuelezea eda ya aliyekoma kutoka hedhi kwa umri mkubwa; si kwa kichanya wala kihasi

Na wenye mimba eda yao ni mpaka watakapozaa.

Mafaqihi wa kisuni na kishia wameafikiana kuwa eda ya mtalikiwa mwenye mimba ni mpaka azae, wakatofautiana katika eda ya aliyefiwa na mumewe akiwa na mimba. Sunni wamesema ni sawa na eda ya mtalikiwa inamalizika kwa kuzaa.

Shia wanasema ataangalia muda utakaorefuka zaidi baina ya kuzaa na miezi mine na siku kumi (yaani akizaa kabla ya miezi mine na siku kumi basi atangoja hadi muda huo uishe). Kwa kuchukulia Aya hii na ile isemayo: “Na wale wanaokufa miongoni mwenu na kuacha wake (hao wake) wangoje miezi minne na siku kumi.” Juz. 2 (2:234). Huko tumefafanua zaidi.

Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi.

Huu ni mfano wa Aya ya 2 na 3 ya Sura hii tuliyo nayo. Hatujui lengo la kukaririka huku isipokuwa kuzidi kuhimiza takua. Kwamba kule kumeku­ja kuhimiza baada ya amri ya kusimamisha ushahidi kwa njia yake. Hapa kumekuja baada ya kubainisha eda ya aliyekoma na mwenye mimba.

Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu amewateremshia. Na anayemcha Mwenyezi Mungu atamfutia maovu yake, na atampa ujira mkubwa.

Manufaa ya takua hayana idadi; mingoni mwayo ni aliyoyataja Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Aya hizi; kama ifuatavyo:-kutoka katika dhiki ya dunia na Akhera, riziki bila ya kutazamia, nusra na kinga kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kuwa mepesi mambo na kufutiwa maovu. Fauka ya yote ni ziada ya malipo. Lakini

أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ أَوْ تَهْدِي الْعُمْيَ وَمَن كَانَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٤٠﴾

“Je, unaweza kumsikilizisha kiziwi, au kumwongoza kipofu na aliyemo katika upotofu ulio wazi?” Juz. 25 (43:40).


12

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

أَسْكِنُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنتُم مِّن وُجْدِكُمْ وَلَا تُضَارُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُوا عَلَيْهِنَّ وَإِن كُنَّ أُولَاتِ حَمْلٍ فَأَنفِقُوا عَلَيْهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ فَإِنْ أَرْضَعْنَ لَكُمْ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ وَأْتَمِرُوا بَيْنَكُم بِمَعْرُوفٍ وَإِن تَعَاسَرْتُمْ فَسَتُرْضِعُ لَهُ أُخْرَىٰ ﴿٦﴾

6. Wawekeni mnavyokaa nyinyi kwa kadiri ya pato lenu, wala msiwaletee madhara kwa kuwadhiki. Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue. Na wakiwany­onyeshea, basi wapeni ujira wao, na shaurianeni kwa wema. Na mkihitilafiana, basi amnyonyeshee mwanamke mwengine.

لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا سَيَجْعَلُ اللَّـهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا ﴿٧﴾

7. Mwenye wasaa agharimie kwa wasaa wake, na mwenye dhiki agharimie katika alichompa Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya alivyoipa. Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya uzito wepesi.

MWENYE WASAA AGHARIMIE

Aya 6 – 7

MAANA

Wawekeni mnavyokaa nyinyi kwa kadiri ya pato lenu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu mwanzoni mwa Sura hii alisema: “Msiwatoe majumbani mwao.” Huko tumesema kuwa ni wajibu kwa mtaliki kumpa makazi aliye katika eda. Aya hii tuliyo nayo inaungana na huko. Kwa sababu inaweka kiwango cha nyumba anayopaswa kukaa mtalikiwa akiwa kwenye eda.

Imeweka kiwango cha uweza wa mtaliki; amuweke kama anavyokaa yeye, akiwa ana nafasi basi amuweke kwa nafasi, akiwa na dhiki basi amuweke kidhiki.

Wala msiwaletee madhara kwa kuwadhiki.

Msikusudie kuwadhuru kwa kuwadhiki katika posho na makazi ili waende zao. Kuwadhuru wengine ni katika madhambi makubwa, hasa mke na jirani.

Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue.

Akimpa talaka na huku ana mimba, itakuwa ni wajibu kumpa posho ikiwa ni pamoja na makazi, mpaka iishe eda kwa kujifungua; ni sawa iwe ni talaka rejea au baini.

Lakini akiwa hana mimba, ikiwa ni talaka rejea itakuwa ni wajibu posho kamili na ikiwa ni talaka baini basi hakuna wajibu wa posho wala makazi.

Kuna kundi la mafiqihi waliosema: Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliposema: ‘wawekeni.’ Aliliachia tamko bila ya kulifunga na mimba, lakini aliposema: ‘wagharamieni,’ amelifunga na mimba. Kwa hiyo natija ni kuwa makazi ni wajibu kwa mtalikiwa yoyote, awe na mimba au la, rejea au baini. Lakini posho inakuwa ni wajibu kwa mwenye mimba hata kama itakuwa ni talaka baini.

Nasi tunajibu: Lau tutachukulia natija hii, basi itakuwa wajibu wa posho ya aliye kwenye eda ni kwa mwenye mimba tu, lakini mwingine haitakuwa ni wajibu hata kama ni talaka rejea, na hakuna anayesema hivyo kabisa; bali yamekongamana madhehebu kuwa ni wajibu posho kwa aliye katika eda ya talaka rejea, kwa nukuu ya Hadith za Mtume, ambazo ndizo zina­zobainisha na kufasiri kitabu cha Mwenyezi Mungu; hasa katika mambo yanayohusiana na halali ya Mwenyezi Mungu na haramu yake. Na hakuna katika Hadith za Mtume zinazobainisha kuwa ni wajib kumpa posho mwenye kupewa talaka baini akiwa hana mimba.

Na wakiwanyonyeshea, basi wapeni ujira wao.

Shia Imamiya wanasema kuwa mama halazimishwi kunyonyesha mtoto wake ila ikiwa kuna ulazima wa hilo; na kama atamnyonyesha katika hali hii au nyingine, basi anayo haki ya kudai ujira wa kunyonyesha; awe kwenye ndoa au ameachika. Ikiwa mtoto ana mali basi ujira wake utatokana na mali hiyo; vinginevyo atatoa baba mwenye uwezo. Akiwa hana basi hapo itakuwa ni wajibu kwa mama kumnyonyesha bure.

Haya yako karibu sana na aliyoyanukuu Ibn Quddama katika kitabu Al-Mughni, kutoka madhehebu mane ya sunni; isipokuwa Malik aliyesema kuwa mke atalazimika kunyonyesha ikiwa walio mfano wake wanawany­onyesha watoto wao. Lakini ikiwa hali yake ni juu zaidi yao basi hatalazimika.

Na shaurianeni kwa wema.

Maneno yanaelekezwa kwa wazazi. Maana ni kuwa shaurianeni na muangalie masilahi ya mtoto kwa ikhlasi katika malipo ya kunyonyesha; msameheane na msahau, ikiwa kwenye nafsi ya mmoja wenu kuna kitu, kwa masilahi ya mtoto ambaye ni amana ya Mwenyezi Mungu juu yenu.

Na mkihitilafiana, basi amnyonyeshee mwanamke mwengine.

Ikiwa baba na mama watatofautiana katika ujira wa kunyonyesha na mama akataka zaidi ya mwingine, basi hapo baba ana haki ya kum­nyang’anya mama na kumpa mwingine amnyonyeshe. Vile vile ikiwa ata­patikana atakayemnyonysha bure na mama akataka malipo. Lakini ikiwa malipo ya mama yako sawa na ya mwingine, basi mama ndiye anayestahi­ki kumnyonyesha. Kwani yeye ndiye aliye na huruma naye zaidi ya mwingine.

Mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na mwenye dhiki atoe katika alichompa Mwenyezi Mungu.

Aya hii inajulisha wazi kuwa hali ya kiuchumi ya mume ni sharti la msingi katika posho ya mke. Atatoa kwa kiasi cha uwezo wake. Ikiwa ana nafasi atatoa kinafasi na akiwa ana dhiki atatoa kidhiki. Hukumu hii ni ya kimsingi wa akili na maumbile ambayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya alivyoipa.

Hukumu ya sharia ikienda sambamba na maumbile ya kiakili, kunaifanya iwe ni ya mkataa isiyokubali taawili au kuihusisha wala kuifuta hukumu yake. Yametangulia maelezo ya kunyonyeshwa mtoto na mama yake na makadirio ya posho yake katika Juz. 2 (2:133).

Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya uzito wepesi.

Hakuna kitu kinachodumu katika hali moja isipokuwa dhati Yake Mtukufu. Mara ngapi dhiki inafuatiwa na faraja! Na shida inapoisha inakuwa ni raha. Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Basi hakika baada ya uzito pana wepesi.” (94:5), hata kama uzito utachukuliwa kwa kukabwa shingo.

وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ عَتَتْ عَنْ أَمْرِ رَبِّهَا وَرُسُلِهِ فَحَاسَبْنَاهَا حِسَابًا شَدِيدًا وَعَذَّبْنَاهَا عَذَابًا نُّكْرًا ﴿٨﴾

8. Na miji mingapi iliyovunja amri ya Mola wake na Mitume wake, basi tuliihisabia hisabu ngumu na tukaiadhibu kwa adhabu kali.

فَذَاقَتْ وَبَالَ أَمْرِهَا وَكَانَ عَاقِبَةُ أَمْرِهَا خُسْرًا ﴿٩﴾

9. Basi ikauonja ubaya wa mambo yake; na mwisho wa mambo yao ulikuwa hasara.

أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ الَّذِينَ آمَنُوا قَدْ أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكُمْ ذِكْرًا ﴿١٠﴾

10. Mwenyezi Mungu amewaandalia adhabu kali. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, mlioamini! Hakika Mwenyezi Mungu amewateremshia Ukumbusho.

رَّسُولًا يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِ اللَّـهِ مُبَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا قَدْ أَحْسَنَ اللَّـهُ لَهُ رِزْقًا ﴿١١﴾

11. Mtume anayewasomea Aya za Mwenyezi Mungu zinazo­bainisha, ili kuwatoa walioamini na wakatenda mema kutoka gizani kuwapeleka kwenye nuru. Na mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu, na akatenda mema, atamwingiza katika Bustani zipitiwazo na mito chini yake, wadumu humo milele. Mwenyezi Mungu amekwishampa riziki nzuri.

اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ وَمِنَ الْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ الْأَمْرُ بَيْنَهُنَّ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا ﴿١٢﴾

12. Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba mbingu saba, na katika ardhi kwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka baina yao, ili mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kukijua.

MIJI MINGAPI

Aya 8 – 12

MAANA

Madhumuni ya Aya hizi yametangulia mara nyingi, kwa hiyo tutazifasiri kwa ufupilizo:

Na miji mingapi iliyovunja amri ya Mola wake na Mitume wake.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwapeleka mitume kwa umma nyingi zilizopita, kuwaamrisha mema na kuwakataza mabaya, lakini wakapinga kwa inadi na kiburi.

Basi tuliihisabia hisabu ngumu na tukaiadhibu kwa adhabu kali.

Mwenyezi Mungu aliwaadhibu kwa adhabu kali baada ya kuwaondolea udhuru kwa hoja na ubainifu ulio wazi.

Basi ikauonja ubaya wa mambo yake; na mwisho wa mambo yao ulikuwa hasara.

Ubaya na mwisho mbaya una maana moja; ndio maana ikafikiriwa kuwa jumla ya pili ina maanaya ya kwanza. Tukichunguza tutaona kuwa ni kama mfano wa kumwambia aliyepata malipo ya uovu: wewe umelipwa malipo ya uovu, kwa sababu mwenye kufanya uovu halipwi ila uovu.

Mwenyezi Mungu amewaandalia adhabu kali.

Adhabu hii inakuwa Akhera, hilo limefahamishwa na neno ‘amewaandalia,’ na hisabu hiyo na adhabu ilikuwa duniani. Hilo limefahamishwa na neno ‘tuliwaadhibu.’ Maana ya Aya mbili hizi yanafupilizwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١١٤﴾

“Wana fedheha katika dunia na katika akhera wana adhabu kubwa.” Juz. 1 (2:114).

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, mlioamini!

Ikiwa mnaamini kweli na kudai kuwa nyinyi ni katika watu wake basi kutanisheni kauli na vitendo na ilimu na kazi; vinginevyo nyinyi mtakuwa si waumini kitu.

Hakika Mwenyezi Mungu amewateremshia Ukumbusho. Mtume anayewasomea Aya za Mwenyezi Mungu zinazobainisha, ili kuwatoa walio amini na wakatenda mema kutoka gizani kuwapeleka kwenye nuru.

Makusudio ya ukumbusho hapa ni Qur’an; na Mtume ni Muhammad(s.a.w.w) . Alimtuma Mtume wake Muhammad kwa Qur’an ili awasomee watu Qur’an na awaongoze kwayo wenye akili awatoe kwenye giza la ukafiri kuwapeleka kwenye mwanga wa haki na imani.

Na mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu, na akatenda mema, atamwingiza katika Bustani zipitiwazo na mito chini yake, wadumu humo milele. Mwenyezi Mungu amekwishampa riziki nzuri.

Waumini walio wema wana ujira mkubwa kwa Mola wao na riziki njema. Maana haya yamekaririka kwenye Aya kadhaa, kwa makusudio ya kuhimiza wema na kufanya heri.

MBINGU SABA NA ARDHI

Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba mbingu saba, na katika ardhi kwa mfano wa hizo.

Kauli zimekuwa nyingi kuhusu mbingu saba na ardhi saba. zinazoingilika akilini ni kama ifuatavyo:-

Kauli ya kwanza : Ni wajibu tuamini kiujumla kuwa kuna mbingu saba na ardhi saba tu basi, na ufafanuzi tuuachie ilimu ya Mwenyezi Mungu.

Kauli ya pili : Ulimwengu mkuu unachanganya tabaka saba za ulimengu. Na kila tabaka ina sayari zisizo na idadi; mingoni mwa hizo sayari ni ardhi. Baina ya kila tabaka moja na nyingine kuna umbali wa mamilioni ya miaka kwa kasi ya mwanga. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amezielezea hizi tabaka saba kwa kusema : mbingu saba. Ama kauli yake: ‘Na katika ardhi mfano wake,” inaashiria kwamba kila tabaka ina ardhi yake. Hayo tumeyadokeza katika Juz. 17 (23: 17).

Kauli ya tatu: Kutajwa mbingu saba hakumaanishi kuwa kuna mbingu saba; isipokuwa wahyi umehusisha kuzitaja kwa vile walioambiwa na Qur’an, wakati huo, walikuwa wakisikia tu sayari saba na nyota zake.

Wana historia wanasema kuwa wakaledonia (Chaldeans) walikuwa maarufu kwa ilimu ya unajimu, na wakafikia kujua kuwa kuna sayari saba.

Vizazi vilivyokuja baadae vikarithi fikra hiyo hadi zama za waarabu ambao Qur’an iliteremshwa kwa lugha yao. Ndio ikawazungumzia mbingu kutokana na walivyozowea kuambiana.

Kauli hii tumeidokeza katika Juz. 1 (2:29).

Inatudhihirikia kuwa kauli hii ndiyo iliyo na nguvu zaidi. Katika kuchaku­rachakura rejea za kufasiri Aya hii tumegundua Hadith na kauli ya Ibn Abbas, zinazotilia nguvu kwamba kutajwa mbingu saba hakukusudiwi kuwa ni hizo saba tu. Hadith yenyewe ameinukuu Sheikh Al-Maraghi kutoka kwa sahaba Ibn Mas’ud: “Mbingu saba na yaliyomo ndani yake na baina yake, na ardhi saba na yaliyomo ndani yake na baina yake, si chochote ila ni kama pete iliyopotea katika ardhi iliyo tamabarare.”

Na Sayansi imethibitisha hakika hii. Tazama Juz. 27 (51:47). Sasa Muhammad(s.a.w.w) ameichukua wapi ilimu hii naye ameinukia kwenye umma usiojua kusoma wala kuandika au kuhisabu.

Je ameichukua kwa mtawa au kwa kuhani? Au Muhammad(s.a.w.w) anamzulia Mwenyezi Mungu, naye analingania Kitabu kinachosema kwa ufasaha na uwazi: Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule amzuliaye uwongo Mwenyezi Mungu. Au mwenye kusema: Nimeletewa Wahyi; na hali hakuletewa wahyi wowote.” Juz. 7 (6:93). “Hakika ameshindwa mwenye kuzua.” Juz. 20 (20:61).

Katika Tafsir Attabariy kuna maelezo kwamba Ibn Abbas, mwanafunzi wa Imam Ali(a.s) , alimuuliza kuhusu kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Mbingu saba, na katika ardhi kwa mfano wa hizo,” Akasema:Lau mtazungumzia tafsiri yake mtakufuru kwa kuikadhibisha.” Yaani akili zao hazitavumilia, kwa hiyo watatia shaka ukweli wake.

Amri zake zinashuka baina yao.

Yaani baina ya hizo mbingu na ardhi. Amezipangilia mbingu na ardhini na vilivyomo ndani yake kwa hikima yake, akazizuia kwa uweza wake na anazijua vizuri kwa ilimu yake.

Ili mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kukijua.

Miongoni mwa hikima kubwa katika kuumba mbingu na ardhi ni mjue kuwa Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu hata ufufuo baada ya mauti, na kwamba yeye ni mjuzi wa kila kitu; mpaka makusudio yenu na vitendo vyenu, basi mtiini na mhofie ghadhabu zake na adhabu yake.

MWISHO WA SURA YA SITINI NA TANO: SUARAT AT-TALAQ


13

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sitini Na Sita: Surat At –Tahrim. Imeshuka Madina. Ina Aya 12.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١﴾

1. Ewe Nabii! Kwa nini unaharimisha alichokuhalilishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta radhi za wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ وَاللَّـهُ مَوْلَاكُمْ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٢﴾

2. Hakika Mwenyezi Mungu amewapa Sharia ya kufungua viapo vyenu. na Mwenyezi Mungu ni Mola wenu. Na Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.

وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِ وَأَظْهَرَهُ اللَّـهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُ وَأَعْرَضَ عَن بَعْضٍ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِ قَالَتْ مَنْ أَنبَأَكَ هَـٰذَا قَالَ نَبَّأَنِيَ الْعَلِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٣﴾

3. Na Nabii alipomwambia mmoja wa wake zake jambo la siri. Basi alipolitangaza yule mke, na Mwenyezi Mungu akamdhihirishia Mtume, alimjulisha sehemu na akaacha sehemu nyengine. Alipomwambia hayo, huyo mke akasema: Nani aliyek­wambia haya? Mtume akase­ma: Kaniambia Mjuzi Mwenye habari!

إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ ﴿٤﴾

4. Kama nyinyi wawili mtatubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwishaelekea kwenye haki. Na mkisaidiana dhidi yake Mtume, basi hakika Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi wake, na Jibrili, na waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia.

عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا ﴿٥﴾

5. Akiwapa talaka, asaa Mola wake akampa wake wengine badala yenu nyinyi, walio bora kuliko nyinyi, wanyenyekevu, waumini, watiifu, walio tubu, wenye kushika ibada, wafanyao kheri, wajane na wanawali.

KWA NINI UNAHARIMISHA ALICHOKUHALILISHIA MWENYEZI MUNGU?

Aya 1 - 5

KISA KWA UFUPI

Wametofautiana wafasiri na wapokezi wa Hadith kuhusu sababu ya kushu­ka Aya hizi. Kwenye Sahih Bukhar na Sahihu Muslim, kuna Hadith iliy­opokewa kutoka kwa Aisha, amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alikuwa akipenda haluwa na asali. Siku moja akanywa asali kwa mkewe Zaynab bint Jahsh. Tukakubaliana mimi na Hafsa, kuwa akiingia kwa mmoja wetu amwambie: Nasikia harufu ya mughafiri[3] .”

Na ikawa hivyo. basi Mtume akasema:“hapana nimekunywa asali kwa Zaynab na sitarudia tena kunywa, lakini usimwambie mtu.”

Katika tafsiri ya Sheikh Al-Maraghi ni kuwa Mtume(s.a.w.w) aliingia kwa Hafsa, kisha akamjulisha Aisha pamoja na kuwa Mtume alimwambia iwe siri. Sheikh anaendelea kusema: Aisha na Hafsa walikuwa wakielewana kuwa dhidi ya wake wengine wa Mtume(s.a.w.w) .

Vyovyote inavyosemwa kuhusu sababu za kushuka Aya hizi, ni kuwa dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa Mtume(s.a.w.w) alijizuia kutumia kitu alichohalalishiwa na Mwenyezi Mungu kutokana na sababu fulani. Na kwamba hilo alilifanya siri na mmoja wa wakeze na kumwamuru asilidhihirishe, lakini mke akakhalifu na kulitoa. Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamnasihi Nabii wake kutojinyima alivyohalalishiwa na Mwenyezi Mungu na akawakemea wakeze wasiosikiliza amri yake.

MAANA

Ewe Nabii! Kwa nini unaharamisha alichokuhalalishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta radhi za wake zako.

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume(s.a.w.w) . Makusudio ya uharamu hapa ni kiasi cha kujizuila tu kuacha halali kwa kumridhisha mwingine; kama vile kuacha kuvuta sigara kwa sababu ya kumridhisha mke ambaye anachukia hilo.

Kwa hiyo makusudio hapa sio kuharamisha kisharia. Ni muhali hilo. Vipi iwe hivyo na Kitabu cha Mwenyezi Mungu alichokiteremsha katika moyo wa Muhammad(s.a.w.w) kinasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٨٧﴾

“Enyi mlioamini! Msiharamishe vizuri alivyowahalalishia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” Juz. 7 (5:87).

Anasema tena;

قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ حَرَامًا وَحَلَالًا قُلْ آللَّـهُ أَذِنَ لَكُمْ أَمْ عَلَى اللَّـهِ تَفْتَرُونَ ﴿٥٩﴾

“Sema: Je, mwaonaje zile riziki alizowateremshia Mwenyezi Mungu, kisha mkafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali? Sema: Je, Mwenyezi Mungu amewaruhusu au mnamzulia Mwenyezi Mungu uwongo?” Juz.11 (10:59).

Inasemekana kitu alichojiharamishia ni asali na kwamba alikusudia kum­ridhisha mkewe Hafsa kwa sababu aliona vibaya kunywa asali kwa mkewe Zaynab bint Jahsh. Basi moyo wa Hafsa ukafurahi kwa hilo

Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

Msamaha na maghufira haumaanishi kuwa kuna dhambi. Mara nyingi inakuwa ni ibara ya thawabu zake na rehema zake. Manabii walikuwa wakiomba msamaha na maghufira kwa Mwenyezi Mungu; mfano: “Juz. 10: (9:43).

Hakika Mwenyezi Mungu amewapa Sharia ya kufungua viapo vyenu.

Inasemekana kuwa Mtume(s.a.w.w) aliapa kuacha kitu alichohalalishiwa na Mwenyezi Mungu, ndio akamwamuru aache kiapo chake na atoe kafara.

Tuonavyo sisi - Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi - ni kuwa Mtume(s.a.w.w) hakuapa, lakini aliahidi kuacha; na ahadi ya maasumu ni wajibu kuitekeleza kwa hali yoyote itakavyokua, ni sawa aliloliahidi liwe ni sunna au halali. Kwa sababu ahadi yake ina nguvu na ni kubwa zaidi kuliko kiapo cha mwingine. Kwa hiyo inafaa kuitwa kiapo.

Na Mwenyezi Mungu ni Mola wenu. Na Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.

Mwenyezi Mungu ndiye mtawala wa mambo ya Nabii na waumini, ndiye anayewanusuru dhidi ya wanaotaka kuwafanyia njama na anajua hikima aliyoifanyia shariya ya hukumu ya viapo na mengineyo.

Na Nabii alipomwambia mmoja wa wake zake jambo la siri.

Hii inafahamisha kuwa Nabii ni mtu kama watu wengine; anafanya siri na wake zake kama wafanyavyo siri watu wengine. Hatofautiani nao isipokuwa kwa kushukiwa na wahyi, na umaasumu unakuwa katika aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu na kila mambo ya aibu. Tazama Juz. 16 (20-17) kifungu cha ‘Hakika ya utume.’

Basi alipolitangaza yule mke, na Mwenyezi Mungu akamdhihirishia Mtume, alimjulisha sehemu na akaacha sehemu nyengine.

Yaani baada ya yule kulitangaza lile aliloambiwa aliweke ni siri, Mwenyezi Mungu alimjulisha Mtume wake mtukufu, naye Mtume akamwambia yule mke baadhi ya mambo aliyoyafichua. Hakumwambia yote kwa kumhurumia. Hapa kuna ishara kuwa huyo alipituka mipaka ya kufichua mambo ya siri.

Alipomwambia hayo, huyo mke akasema: Nani aliyekwambia haya? Mke alimuuuliza Mtume amepata wapi habari hizo,Mtume akasema: Kaniambia Mjuzi Mwenye habari! Ambaye anajua hiyana ya macho na yanayofichwa na vifua.

Kama nyinyi wawili mtatubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwishaelekea kwenye haki.Na mkisaidiana dhidi yake Mtume,basi hakika Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi wake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia.

Dhamiri ya nyinyi wawili inamrudia Aisha na Hafsa; kama ilivyoandikwa katika vitabu vya Tafsiri na Hadith. Tutaonyesha vine; viwili vikiwa vya tafsir na viwili vya Hadith:

Kwenye Tafsir Attabari kuna maelezo haya, ninanukuu: “Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:Na mkisaidiaana dhidi yake , ni yule aliyepewa siri na Mtume(s.a.w.w ) na yule aliyemfichulia siri hiyo, ambao ni Hafsa na Aisha. Watu wa taawili wamesema kama tulivyosema sisi.”

Razi naye akasema: ninamnukuu: “Kama nyinyi wawili mkitubia,” maneno yanaelekezwa kwa Aisha na Hafsa. Bukhari anasema katika Sahih yake Juz. 6 kwa anuani ya ‘Sura Attahrim.” Ibn Abbas alimuuliza Umar Bin Al-khattab: Ni nani hao wawili waliosaidiana dhidi ya Mtume(s.a.w.w) katika wake zake? Akasema: hao ni Hafsa na Aisha. Na mfano wake katika sehemu ya pili ya Juzuu ya pili ya Sahih Muslim kwa anuani ‘Mlango wa kuapa na kujitenga na wanawake.’

Kuna swali pia kuhusu neno ‘Kama nyinyi wawili mkitubia,’ amesema Muslim: Ibn Abbas alimuuliza Umar: Ni nani hao wake wawili katika wakeze Mtume(s.a.w.w) ambao wameambiwa; kama mkitubia? Akasema Umar: ‘’Ni Hafsa na Aisha.’’

Maana ya Aya ni kuwa Aisha na Hafsa walisaidiana dhidi ya Mtume(s.a.w.w) na wakafichua siri yake pamoja na kutaka isitolewe, na Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawamuru kutubia kosa hili. Kwamba wakitubuia na kutengemaa, basi nyoyo zao zitakuwa zimeelekea kwa Mwenyezi Mungu na kumfanyia ikhlas, lakini kama waking’ang’ania kusaidiana dhidi ya Mtume, basi Mwenyezi Mungu atamlinda. Vile vile Jibril, malaika wote, waumini na watu wema.

Unaweza kuuliza : Kwa nini vitisho vyote. kwani Aisha na Hafsa wana nini mpaka wachanganyiwe nguvu ya Mwenyezi Mungu, nguvu ya Jibril pamoja na malaika wengine na walio wema katika waumini?

Jibu : Aisha na Hafsa sio wanaokusudiwa kuhusishwa wao tu na makemeo haya; isipokuwa makusudio kwanza ni kueleza cheo na heshima ya Mtume; kisha kuwafahamisha wote akiwemo Hafsa na Aisha na kila mwenye kumdhamiria kumfanyia ubaya Nabii(s.a.w.w) , kuwa Nabii(s.a.w.w) yuko kwenye ngome imara ya nguvu ya Mwenyezi Mungu, malaika na mawalii wake.

Akiwapa talaka, asaa Mola wake akampa wake wengine badala yenu nyinyi, walio bora kuliko nyinyi, wanyenyekevu, waumini, watiifu, walio tubu, wenye kushika ibada, wafanyao kheri, wajane na wanawali.

Ni jambo gani mnalojidai nalo enyi wake wa Mtume mpaka mkawa dhidi yake? Je, umewahadaa uzuri wenu, dini yenu, utiifu wenu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake au ni kwa nini?

Basi na ajue kila mmoja wenu kwamba lau Mtume(s.a.w.w) atawapa talaka nyote, basi Mwenyezi Mungu atambadilishia walio bora kuliko nyinyi kwa uzuri, ukamilifu, dini na ikhlasi; tena akipenda wajane akitaka au bikra au wote.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ﴿٦﴾

6. Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu. Hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَعْتَذِرُوا الْيَوْمَ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٧﴾

7. Enyi mliokufuru! Msilete udhuru leo. Hakika tu mnalipwa mliyokuwa mkiyatenda.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّـهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٨﴾

8. Enyi mlioamini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba ya kweli! Asaa Mola wenu akawafutia maovu yenu na akawaingiza katika Pepo zipitiwazo na mito chini yake. Siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii. Na walioamini pamoja naye, nuru yao inakwenda mbele yao na kuumeni, na huku wanasema: Mola wetu! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٩﴾

9. Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki, na uwawekee ngumu! Na makazi yao ni Jahannamu. Na hayo ni marejeo mabaya.

KUNI ZAKE NI WATU NA MAWE

Aya 6 – 9

MAANA

Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe.

Makusudio ya mawe ni masanamu kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Nyinyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannam, mtafika.” Juz. 17 (21:98).

Maana ni ikiwa mumin anahisi majukumu mbele ya Mwenyezi Mungu kwa anayoyasema na anayoyafanya na kuhofia ghadhabu yake na adhabu yake, basi ni juu yake kuona kuwa ana jukumu kwa watu wake na watoto wake na kwamba ni wajibu wake kunyoosha mkono wake kwa kazi kwa ajili ya masilahi yao na kunyooka kwao.

Ikiwa baba anafanya kila awezalo kwa ajili ya watoto wake kwa ajili ya mustakbali wao katika maisha haya yanayoisha, basi ingekuwa bora kwake kufanya bidii kwa ajili ya wema wao katika maisha yanayobakia na kuwakinga na jambo kubwa zaidi kuliko misukosuko yote. Lakini baba atafanya nini katika kizazi hiki ambacho kinawataka wazazi wawanyenye­kee watoto?

Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu ya ukakamavu kwa wasiokuwa na maana waliopituka mipaka na kufanya uovu duniani kwa waja wa Mwenyezi Mungu.

Hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa.

Yaani hao malaika wakali, wanaharakisha kumtii Mwenyezi Mungu bila ya kusita, naye anawaambia kwa kila muovu mwenye dhambi:

خُذُوهُ فَغُلُّوهُ ﴿٣٠﴾

“Mshikeni na mumtie pingu.” (69:30).

Enyi mliokufuru! Msilete udhuru leo. Hakika tu mnalipwa mliyokuwa mkiyatenda.

Siku hii ya leo ni siku ya hisabu na malipo ya matendo, sio siku ya toba na kutoa udhuru. Watatubia kitu gani wale ambao viwanda vyao vinafanyakazi usiku na mchana kutengeneza mauti na kuboa?

Enyi mlioamini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba ya kweli! Asaa Mola wenu akawafutia maovu yenu na akawaingiza katika Pepo zipi­tiwazo na mito chini yake.

Asaa ikitoka kwa Mwenyezi Mungu basi maana yake ni kuwa tu. Toba ya kweli ni ile ya kujing’oa kabisa kwenye uovu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke Yake. Nayo iko wazi kwa kila mwenye kufanya madhambi na akaasi. Vile vile ni wema mkubwa unaofuta yaliyo maovu yaliyo kabla yake na inaleta thawabu za Mwenyezi Mungu na Pepo yake.

Siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii.

Hii ni kuwapinga maadui wa Nabii, kwamba wao ndio watakaodhalilika duniani na Akhera; vinginevyo ni nani anayefikiria kuwa Mwenyezi Mungu atamdahalilisha Muhammad(s.a.w.w) siku ya Kiyama, na yeye maisha yake duniani yalikuwa ni rehema kwa viumbe wote?

Na walioamini pamoja naye, nuru yao inakwenda mbele yao na kuumeni, na huku wanasema: Mola wetu! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

Umetangulia mfano wake katika Juz.27 (57:12).

Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki, na uwawekee ngumu! Na makazi yao ni Jahannamu. Na hayo ni marejeo mabaya.

Kabisa! Hakuna upole wala huruma kwa mataghuti, wala hakuna cha kuwafanyia mbele ya haki na uadilifu isipokuwa upanga. Ni sharia gani au kanuni gani inayohurumia na kuwapuuza wanaodharau maisha ya watu na kueneza hofu nyoyoni mwao, huku wakisema: asiyekuwa pamoja na sisi na kuwa mtumwa wetu basi huyo ni adui yetu naye hatapata kutoka kwetu isipokuwa silaha za maangamizi?

Hapo huruma na upole itakuwa ni kuuumaliza uadui na watu wake. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma katika moto wake kama alivyo na huruma katika Pepo yake.

ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ كَفَرُوا امْرَأَتَ نُوحٍ وَامْرَأَتَ لُوطٍ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَالِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا وَقِيلَ ادْخُلَا النَّارَ مَعَ الدَّاخِلِينَ ﴿١٠﴾

10. Mwenyezi Mungu amewapi­gia mfano waliokufuru-mke wa Nuhu na mke wa Luti. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja wetu. Lakini wakawafanyia hiyana, nao wasiwafae kitu. Na ikasemwa: Ingieni Motoni pamoja na wanaoingia!

وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ آمَنُوا امْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِي عِندَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿١١﴾

11. Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walioamini mke wa Firauni, aliposema: Mola wangu! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhalimu.

وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَانَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَاتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِ وَكَانَتْ مِنَ الْقَانِتِينَ ﴿١٢﴾

12. Na Maryam binti Imrani, aliyeilinda tupu yake, na tukampulizia humo kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa watiifu.

MKE WA NUH NA MKE WA LUT

Aya 10 – 12

MAANA

Mwenyezi Mungu amewapigia mfano waliokufuru-mke wa Nuhu na mke wa Luti. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja wetu. Lakini wakawafanyia hiyana, nao wasiwafae kitu. Na ikasemwa: Ingieni Motoni pamoja na wanaoingia!

Hakuna tofauti baina ya mwanamume na mwanamke kiasili na kimajukumu. Kila mmoja ni sehemu ya mwingine. Kila mmoja hawezi kujitosha peke yake. Kuna wanaume wema na waovu na kuna wanawake wema na waovu.

Aya iko mbali kabisa na kutofautisha baina ya mwanamke na mwanamume. Imepigia mfano mwanamke kwa sababu tu ya kuwaonyesha baadhi ya mama wa waumin waliokuwa dhidi ya Mtume(s.a.w.w) ; kama ilivyokuja katika Aya ya nne ya Sura hii tuliyo nayo.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja kuwa baadhi ya wakeze walikuwa dhidi yake, na kuwakemea, sasa anasema kuwa aliye karibu na Mwenyezi Mungu ni yule anayejikurubisha kwake kwa maadili na matendo mema, hata kama yuko karibu na muovu wa waovu.

Na aliye mbali na Mwenyezi Mungu ni yule anayejibaadisha kwa maovu na madhambi, hata kama yuko karibu na mwenye takuwa zaidi ya wenye takua. Hakuna udugu katika hilo. Hakuna kitu kabisa kitakachofaa siku ya Kiyama isipokuwa takua na ikhlasi.

Amepiga mfano Mwenyezi Mungu kwa mke wa Nuh, kwa vile alikuwa akimuudhi mumewe na kumwambia ni mwenda wazimu na alikuwa akifichua siri zake kwa washirikina. Na mke wa Lut alikuwa akiwasaidia mahabithi kwa kuwajulisha juu ya wageni wake. Ndio maana akawapa wasifu wa hiyana ambayo ni kinyume na amana; na wala sio kwa maana ya zina. Kwa sababu waislamu wanaitakidi kuwa mke yeyote wa Nabii hakuwahi kuzini.

Kwa ufupi ni kuwa: Mwenyezi Mungu atamwingiza motoni mke wa Nuh na wa Lut kwa sababu ya ukafiri na unafiki wao, ingawaje walikuwa ni wake wa manabii wakubwa. Basi hivyo hivyo atawaingiza motoni wakeze Mtume mtukufu(s.a.w.w) waliokuwa dhidi yake, iwapo hawatatubia kwa Mwenyezi Mungu na kwake.

Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walioamini mke wa Firauni, aliposema: Mola wangu! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhalimu.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kupiga mfano kuwa ukaribu wa muovu kwa mwema haumfai kitu, sasa analeta mfano wa kuwa pia ukaribu wa mwema kwa kwa muovu haumdhuru kitu. Akapiga mfano wa mke wa Firauni; uhusiano wake na Firauni haukumdhuru. Asiya bint Muzahim alimwamini Mwenyezi Mungu na vitabu na mitume yake na akamkufuru mumewe Firauni.

Basi akamtishia kumuua. Akaathirika na radhi za Mwenyezi Mungu na neema zake kuliko ufalme wa Firauni na usultani wake, akajitenga naye na amali yake; akamwomba Mola wake ampe rehema yake na amneemeshe kwa fadhila yake.

Katika Tafsir Attabariy kuna maelezo kuwa: Firauni alipompelekea watu wake aliwaambia: Muonyesheni jiwe kubwa zaidi mtakalolipata. Akibakia na imani yake ya Mwenyezi Mungu basi mtupieni jiwe na akirejea na kuachana nayo basi atakuwa ni mke wangu.

Basi walipomletea alinyanyua macho yake mbinguni akaona nyumba yake Peponi akasema yale maneno yake na roho yake ikatoka. Wale wakaangusha jiwe kwenye mwili usiokuwa na roho.

Tafsiri nyingine zinasema kuwa: maombi yake ya kujengewa nyumba Peponi, ni kama kusema: Jirani kwanza kabla ya nyumba.

Na Maryam binti Imrani, aliyeilinda tupu yake, na tukampulizia humo kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa watiifu.

Kuhifadhi tupu yake ni kinaya cha usafi wake kutokana na waliyomzulia mayahudi kuwa ni mzinfu muovu. Makusudio ya kupulizia ni kutiwa uhai wa mtoto wake, Bwana Masih; sawa na alivyotia uhai kwa Adam:

فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ ﴿٢٩﴾

“Basi nitakapomkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi muangukieni kumsujudia.”

Juz. 14 (15:29).

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amepiga mfano wa waumini wanawake kwa Bibi Maryam mtakatifu aliyemwamini Mwenyezi Mungu, mitume wake na vitabu vyake na akabeba mimba ya mwanawe kwa neno lake Mwenyezi Mungu.

Umetangulia mfano wake mara nyingi. Tazama Juz. 6 (4:171).

MWISHO WA SURA YA SITINI NA SITA: SURAT AT –TAHRIM


14

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sitini Na Saba: Surat Al-Mulk. Imeshuka Makka. Ina Aya 30.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١﴾

1. Ametukuka ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Muweza juu ya kila kitu.

الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ ﴿٢﴾

2. Ambaye ameumba mauti na uhai ili awajaribu ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwingi wa maghufira.

الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا مَّا تَرَىٰ فِي خَلْقِ الرَّحْمَـٰنِ مِن تَفَاوُتٍ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ ﴿٣﴾

3. Aliyeumba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoy­ote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudisha jicho! Unaona kosa lolote?

ثُمَّ ارْجِعِ الْبَصَرَ كَرَّتَيْنِ يَنقَلِبْ إِلَيْكَ الْبَصَرُ خَاسِئًا وَهُوَ حَسِيرٌ ﴿٤﴾

4. Tena rudisha jicho mara mbili, jicho lako litakurudia likiwa dhalili lililochoka.

وَلَقَدْ زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَجَعَلْنَاهَا رُجُومًا لِّلشَّيَاطِينِ وَأَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابَ السَّعِيرِ ﴿٥﴾

5. Na kwa hakika tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa, na tumeyafanya ili kuwapigia mashetani, na tumewaandalia adhabu ya Moto uwakao.

وَلِلَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٦﴾

6. Na kwa waliomkufuru Mola wao ipo adhabu ya Jahannamu. Na ni marejeo maovu yalioje hayo!

إِذَا أُلْقُوا فِيهَا سَمِعُوا لَهَا شَهِيقًا وَهِيَ تَفُورُ ﴿٧﴾

7. Watakapotupwa humo watausikia muungurumo wake na huku inafoka.

تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظِ كُلَّمَا أُلْقِيَ فِيهَا فَوْجٌ سَأَلَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَذِيرٌ ﴿٨﴾

8. Inakaribia kupasuka kwa hasira. Kila likitupwa kundi humo walinzi wake huwauliza: Kwani hakuwajia mwonyaji?

قَالُوا بَلَىٰ قَدْ جَاءَنَا نَذِيرٌ فَكَذَّبْنَا وَقُلْنَا مَا نَزَّلَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِي ضَلَالٍ كَبِيرٍ ﴿٩﴾

9. Watasema: Kwa nini! Alitujia mwonyaji, lakini tukakadhibisha, na tukasema: Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote. Nyinyi hamumo ila katika upotovu mkubwa!

وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴿١٠﴾

10. Na watasema: Lau tungelikuwa tunasikia, au kuwa na akili, tusingelikuwa katika watu wa Motoni!

فَاعْتَرَفُوا بِذَنبِهِمْ فَسُحْقًا لِّأَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴿١١﴾

11. Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Motoni!

AMETUKUKA MWENYE UFALME WOTE

Aya 1 – 11

MAANA

Ametukuka ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Muweza juu ya kila kitu.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekitukukia kila kitu kwa uwezo wake na nguvu zake, wala hashindwi na lolote; miongoni mwa athari za utukufu huu ni kuwa Yeye ndiyeAmbaye ameumba mauti na uhai ili awajaribu ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na watasema: Lau tungelikuwa tunasikia, au kuwa na akili, tusingelikuwa katika watu wa Motoni!

Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Motoni! Na Yeye ni Mwenye nguvu Mwingi wa maghufira.

Uhai huu umetoka wapi na vipi unatoweka? Hakuna jibu la maswali hayo isipokuwa kuweko aliye hai asiyekufa. Tazama Juz. 7 (6:95) kifungu cha ‘Uhai umetoka wapi?’

Ama hekima ya uhai duniani na umauti kisha ufuufo, ni kudhihirika viten­do vya mtu katika dunia yake, kisha alipwe thawabu au adhabu katika Akhera yake. Imeelezwa katika Hadith kwamba Mtume(s.a.w. w ) , aliposo­ma Aya hii, alifasiri kwa kusema: Ni nani miongoni mwenu mwenye akili nzuri zaidi na mwenye kujichunga zaidi na aliyoyaharimisha Mwenyezi Mungu na aliye mwepesi zaidi wa kumtii?.

Vile vile miongoni wa athari za utukufu Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kwamba Yeye ndiyealiyeumba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudisha jicho! Unaona kosa lolote? Tena rudisha jicho mara mbili, jicho lako litakurudia likiwa dhalili lililochoka.

Kutajwa mbingu saba hakumaanishi kuwa ni hizo tu; Tazama Juz. 28 (65:12). Tabaka Maana yake ni kufuatana katika mpangilio wa kutengenezwa kwake.

Maana ni kuwa hakikisha, uchunguze na utaamali vizuri, tena urudie mara kwa mara, uangalie viumbe, kwa hakika huoni wala hutaona isipokuwa hekima, mpangilio, nidhamu na mfumo wa hali ya juu katika kila kitu; hakuna tofauti kabisa katika mpangilio wa kutengenezwa kwake wala hakuna upungufu au kasoro yoyote, kuanzia kidogo kabisa hadi kikubwa sana.

Ziulize akili zote: Ni nani aliyekipa kila kitu umbo lake na kukikadiria kip­imo chake? Je ni sadfa? Ni lini basi sadfa iliweza kushangaza akili? Hakuna jawabu kwa mwenye akili timamu isipokuwa kurejea kwenye nguvu iliyo nyuma ya maumbile ambayo ni vigumu kuijua hakika yake ni ulivyo ukuu wake.

Kuanzia hapa ndio inakuwa siri ya historia ya kumwamini Mwenyezi Mungu aliyekuwako kwa kuwako mtu, bali kwa kila kiumbe. Tuna uhakika kabisa kwamba mpinzani, lau atafikiria vizuri na kuzingatia umbile la mbingu na ardhi, basi angelimwamini Mwenyezi Mungu atake asitake. Anasema Lord Kelvin, mmoja wa wanasayansi wanaojitokeza: “Ukifikiri kwa undani sana basi ilimu itakufanya ulazimike kuamini kuweko Mwenyezi Mungu.”

Hilo limewekwa wazi na Qur’an pale iliposema:

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ﴿٢٨﴾

“Hakika si mengineyo, wanaomcha Mwenyezi Mungu katika waja wake ni wale wajuzi.”

Juz. 22 (35:28).

Na kwa hakika tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa, na tumeyafanya ili kuwapigia mashetani, na tumewaandalia adhabu ya Moto uwakao.

Makusudio ya mataa ni nyota. Kupiga kunaweza kuwa kwa miali inayounguza - aghlabu - katika anga kabla ya kufika ardhini; au inaweza kuwa ni kwa mawe yanayoanguka kutoka kwenye nyota (vimondo). Kila aliye mfidhuli muasi basi huyo ni shetani; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

وَإِذَا خَلَوْا إِلَىٰ شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ ﴿١٤﴾

“Na wanapokuwa peke yao kwa mashetani wao, husema: Hakika sisi tu pamoja nanyi.”

Juz. 1 (2:14).

Mmoja wa wafasiri amesema: “Walaghai wanafikiri kwamba wao wanajua ghaibu kwa kuangalia nyota; na Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawavurumis­hia miali ya Jahannam kwa vile wao walivyokuwa wakivurumishia ghaibu.” Na sisi tunasema: Tafsiri hii vile vile ni kuivurumishia ghaibu.

Umetangulia mfano wa Aya hii katika Juz. 23 (37:6-10) na Juz. 24 (41:12).

Na kwa waliomkufuru Mola wao ipo adhabu ya Jahannamu. Na ni marejeo maovu yalioje hayo! Watakapotupwa humo watausikia muungurumo wake na huku inafoka. Inakaribia kupasuka kwa hasira.

Mwenye Dhila anasema: “Mtu anaweza kudhania kuwa hii ni ibara ya majazi, lakini Jahannam ni kiumbe hai kina hasira na kuchukia. Hata hivyo wafasiri wengi wamesema makusudio ni kuwa Jahannam ina mvumo mkubwa na kalabi. Mwenye kuiona anaidhania kuwa imewakasirikia makafiri.”

Tafsiri hii iko karibu na ufahamu na usadikisho kuliko tafsiri ya idhla inayofanana na tafsiri ya watu wa dhahiri.

Kila likitupwa kundi humo walinzi wake huwauliza: Kwani hakuwa­jia mwonyaji?

Makusudio ya swali la walinzi ni kuwatahayariza wakosefu na kuwalaumu; sawa na kumwambia anayeadhibiwa kwa kosa lake: “Umejitakia mwenyewe haya.”

Watasema: Kwa nini! Alitujia mwonyaji, lakini tukakadhibisha, na tukasema: Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote. Nyinyi hamu­mo ila katika upotovu mkubwa!

Yaani manabii wamo katika upotevu mkubwa! Kwanini? Kwa vile wao wanatoa mwito wa tawhid na uadilifu. Lakini mataghuti na waasi wanaoabudu mawe na masanamu ndio wenye busara. Haya ndiyo mantiki ya wapotevu na wafisadi kila wakati na kila mahali.

Na watasema: Lau tungelikuwa tunasikia, au kuwa na akili, tusinge­likuwa katika watu wa Motoni! Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Motoni!

Walipowajia mitume kwa hoja wazi wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, wakiwakadhibisha kwa inadi na kiburi na wakawaambia: Nyinyi ni wapotevu mliopotea. Mnamzulia Mwenyezi Mungu uwongo. Lakini adhabu ilipowazunguka walikuwa dhalili na wakajuta; wakakubali kuwa wao ndio wapotevu. Lakini wapi! Wamekwishachelewa! Malipo yao yamekuwa ni kuungua.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (6:130) na Juz. 24 (39:71).

إِنَّ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ ﴿١٢﴾

12. Hakika wanaomwogopa Mola wao kwa ghaibu, watapata maghufira na ujira mkubwa.

وَأَسِرُّوا قَوْلَكُمْ أَوِ اجْهَرُوا بِهِ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٣﴾

13. Na ficheni kauli zenu, au zitangazeni; hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.

أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٤﴾

14. Hivi asijue aliyeumba, naye ni Mpole, Mwenye habari?

هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِن رِّزْقِهِ وَإِلَيْهِ النُّشُورُ ﴿١٥﴾

15. Yeye ndiye aliyeifanya ardhi dhalili kwa ajili yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuli­wa.

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ ﴿١٦﴾

16. Je, mnadhani mko salama kwa alioko mbinguni kuwa hatawadidimiza kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika?

أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ ﴿١٧﴾

17. Au mnadhani mko salama kwa alioko mbinguni kuwa Yeye hatawapelekea kimbun­ga chenye changarawe? Basi mtajua vipi maonyo yangu.

وَلَقَدْ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ ﴿١٨﴾

18. Na walikwishakadhibisha waliokuwa kabla yao; basi kulikuwaje kukasirika kwangu?

أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ فَوْقَهُمْ صَافَّاتٍ وَيَقْبِضْنَ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا الرَّحْمَـٰنُ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ بَصِيرٌ ﴿١٩﴾

19. Je, hawawaoni ndege walioko juu yao wakizikunjua mbawa zao, na kuzikunja? Hawawashikilii ila Mwingi wa rehema. Hakika Yeye ni Mwenye kuona kila kitu.

TEMEBEENI KATIKA PANDE ZAKE

Aya 12- 19

MAANA

Hakika wanaomwogopa Mola wao kwa ghaibu, watapata maghufira na ujira mkubwa.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja aliyowaandaia wakosefu, sasa anataja aliyowaandalia wenye takua, katika misingi ya kuvutia na kuo­gopesha. Wenye takua ni wale wanaojichunga na aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu katika hali zote. Hakuna tofauto kwao wajulikane na watu au wasijulikne, kwa sababu wao wanafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu anayejua yaliyosiri na kujificha.

Na ficheni kauli zenu, au zitangazeni; hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.

Yaani yaliyodhamiriwa. Mwenye kujua yaliyodhamiriwa nyoyoni basi atakuwa anajua yanayosemwa.

Aya hii imetangulia katika Juz. 11 (11:5).

Hivi asijue aliyeumba, naye ni Mpole, Mwenye habari?

Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu, kwa sababu Yeye ni muumba wa kila kitu. Sifa ya upole inaashiria kuwa Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamfanyii haraka muovu kumwadhibu kwa kumhurumia, pengine anaweza kutubia na kujing’oa kwenye dhambi zake.

Yeye ndiye aliyeifanya ardhi dhalili kwa ajili yenu, basi tembeeni kati­ka pande zake, na kuleni katika riziki zake.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni mwenye huruma kwa waja wake, anajua mahitaji yao katika maisha haya. Ndio maana amewaumbia ardhi na akawawekea humo chakula na riziki na akaifanya iitikie matakwa, mahita­ji na masilahi yao. Sheikh Abdul qadir Al-maghribi anasema: “Ardhi ni neema kwetu, ni kipando kilichozoeleka, na ni mtumishi mwenye uzoefu.”

Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu hilo ameliwekea desturi ya kulifanyia kazi na kulihangaikia. Hekima yake imetaka kuzifungamanisha sababu na visababishi pamoja na natija kwa utangulizi wake. Atakayetoka kwenye desturi hii basi atakuwa ameifanyia ujeuri desturi ya Mwenyezi Mungu na matakwa yake.

Na kwake Yeye ndio kufufuliwa.

Hii ni hadhari na kiaga kwa anayetafuta riziki bila ya kusumbuka na kuhangaika kisharia:

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي كَبَدٍ ﴿٤﴾

“Hakika tumemuumba mtu katika tabu.” (90:4).

Yaani asumbuke na kufanya juhudi; kama walivyosema wafasiri wengi.

Je, mnadhani mko salama kwa alioko mbinguni kuwa hatawadidimiza kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko sala­ma kwa alioko mbinguni kuwa Yeye hatawapelekea kimbunga chenye changarawe?

Makusudio ya alioko mbinguni ni muumba wa mbingu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameihusisha mbingu ‧ pamoja na kuwa Yeye ni muumba wa kila kitu‧ kwa sababu watu wanazingatia kupangilia kwake kuwa ni kupangilia mbingu.

Baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kutaja neema ya ardhi na kheri zake, sasa anatoa tahadhari ya mwisho wa dhulma na ufisadi. Kwani neema hii itageuka kuwa shari na balaa kwa wakosefu na wafisadi kwa vile aliyei­jaalia kuwa laini kwa waja ana uwezo wa kuwadidimiza kwa matetemeko na kuwameza wao na wanavyovimiliki. Au awaletee kimbunga kitaka­chowafyeka kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho wao.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 15 (17:68).

Basi mtajua vipi maonyo yangu.

Mwenyezi Mungu aliwaonya na kuwahadharisha na mwisho mbaya, laki­ni mkayakadhibisha maonyo na mkamdharau muonyaji. Basi karibuni itawafikia adhabu mliyokuwa mkiikadhibisha na kuidharau.

Na walikwishakadhibisha waliokuwa kabla yao; basi kulikuwaje kukasirika kwangu?

Kukasirika kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni adhabu yake. Maana ni kuwa mmekwishasikia habari za aliowapatiliza Mwenyezi Mungu kutokana na dhambi zao na mnajua vipi iliwashukia adhabu. Je ham­wogopi kuwasibu yaliyowasibu? Umetangulia mfano wake katika Aya kadhaa; miongoni mwazo ni Juz. 10 (9:69) na Juz. 22 (34:45).

Je, hawawaoni ndege walioko juu yao wakizikunjua mbawa zao, na kuzikunja? Hawawashikilii ila Mwingi wa rehema. Hakika Yeye ni Mwenye kuona kila kitu.

Aya hizi zinawalingania wapinzani wanaomkana Mungu, wafikirie katika kuumba kwa Mwenyezi Mungu na uweza wake Mtukufu. Miongoni mwa athari za uweza huu ni kuumba ndege na kuweko angani. Basi ni nani aliyewaumba kwa umbo linalowawezesha kuruka kiasi cha kukunjua mbawa zake mara nyingi na kuzikunja mara nyingine; kama afanyavyo muogeleji. Je iliyofanya hivyo ni sadfa na maumbile yaliyo mapofu?

“Na hakuna mnyama katika ardhi wala ndege arukaye kwa mbawa zake, ila ni umma kama nyinyi.” Juz. 7 (6:38). Ana utambuzi kama mlivyo nyinyi na anakwenda kulingana na maumbile kama mnavyokwenda nyinyi. Ndege anaruka kwa mbawa zake, na mtu anatembea kwa miguu yake na kusafiri kwa gari, ndege au vyombo vya majini.

Sababu zote hizi ni katika utengenzaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ali­zozileta kama nyenzo za kufikia malengo. Umetangulia mfano wake kati­ka Juz. 14 (14:79).

أَمَّنْ هَـٰذَا الَّذِي هُوَ جُندٌ لَّكُمْ يَنصُرُكُم مِّن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ إِنِ الْكَافِرُونَ إِلَّا فِي غُرُورٍ ﴿٢٠﴾

20. Au ni lipi hilo jeshi lenu la kuwanusuru badala ya Mwingi wa Rehema? Hawako makafiri ila katika udanganyifu.

أَمَّنْ هَـٰذَا الَّذِي يَرْزُقُكُمْ إِنْ أَمْسَكَ رِزْقَهُ بَل لَّجُّوا فِي عُتُوٍّ وَنُفُورٍ ﴿٢١﴾

21. Au ni nani huyo ambaye atawapa riziki kama Yeye akizuia riziki yake? Bali wao wanakakamia tu katika jeuri na chuki.

أَفَمَن يَمْشِي مُكِبًّا عَلَىٰ وَجْهِهِ أَهْدَىٰ أَمَّن يَمْشِي سَوِيًّا عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢٢﴾

22. Je, anayekwenda akisinukia juu ya uso wake ni mwongofu zaidi, au yule anayekwenda sawasawa katika Njia Iliyonyooka?

قُلْ هُوَ الَّذِي أَنشَأَكُمْ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ ﴿٢٣﴾

23. Sema: Yeye ndiye aliyewaum­ba, na akawapa masikio na macho, na nyoyo. Ni kidogo tu mnavyoshukuru.

قُلْ هُوَ الَّذِي ذَرَأَكُمْ فِي الْأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٢٤﴾

24. Sema: Yeye ndiye aliye­watawanya katika ardhi, na kwake mtakusanywa.

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٥﴾

25. Na wanasema: ahadi hii ita­tokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?

قُلْ إِنَّمَا الْعِلْمُ عِندَ اللَّـهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٢٦﴾

26. Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu tu; na hakika mimi ni mwonyaji tu mwenye kubainisha.

فَلَمَّا رَأَوْهُ زُلْفَةً سِيئَتْ وُجُوهُ الَّذِينَ كَفَرُوا وَقِيلَ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تَدَّعُونَ ﴿٢٧﴾

27. Lakini watakapoiona kwa karibu, nyuso za waliokufuru zitahuzunishwa, na itasemwa: Hayo ndiyo mliyokuwa mkiyaomba.

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَهْلَكَنِيَ اللَّـهُ وَمَن مَّعِيَ أَوْ رَحِمَنَا فَمَن يُجِيرُ الْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢٨﴾

28. Sema: Mwaonaje, ikiwa Mwenyezi Mungu ataniangamiza mimi na walio pamoja nami, au akiturehe­mu, ni nani atakayewalinda makafiri na adhabu chungu?

قُلْ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ آمَنَّا بِهِ وَعَلَيْهِ تَوَكَّلْنَا فَسَتَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢٩﴾

29. Sema: Yeye ndiye Mwingi wa Rehema; tunamuamini Yeye, na juu yake tunategemea. Mtakuja jua ni nani aliye kati­ka upotovu ulio dhahiri.

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَصْبَحَ مَاؤُكُمْ غَوْرًا فَمَن يَأْتِيكُم بِمَاءٍ مَّعِينٍ ﴿٣٠﴾

30. Sema: Mwaonaje, yakiwa maji yenu yamedidimia chini, nani atawaletea maji yanayotiririka?

ANAYEKWENDA AKISUNUKIA

Aya 20 – 30

MAANA

Au ni lipi hilo jeshi lenu la kuwanusuru badala ya Mwingi wa Rehema?

Aya hii inaungana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya iliyotangulia: “Je, mnadhani mko salama…”

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwahofisha na kudidimizwa ardhini na kimbunga. Anawauliza, ambaye imetukuka hekima yake, kwa njia ya kutahayariza na kukaripia mtafanya nini ikiwashukia adhabu? Mtakimbia? Na hakuna atakayeokoka na kukimbia au mtakimbilia masanamu yenu nayo hayawezi hata kujisaidia hayo yenyewe?

Jawabu ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:Hawako makafiri ila katika udanganyifu , na dhana za uwongo kwamba wao wako kwenye amani na kusalimika na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake.

Au ni nani huyo ambaye atawapa riziki kama Yeye akizuia riziki yake?

Hili ni swali jingine kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Maana yake ni: Ikiwa Mwenyezi Mungu atawazuilia sababu za riziki, kama vile mvua, ni nani basi atakayewaletea mvua? Je, ni hayo masanamu yenu mnayoyaabudu au ni ujinga na ghururi yenu?

Jibu ni: Bali wao wanakakamia tu katika jeuri na chuki.

Wao wanajua kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuruzuku, lakini pamoja na hayo wanaifanyia inadi haki na wanag’ang’ania kwenye batili, kwa sababu maisha yao yanasimamia batili na kuipiga vita haki na watu wake.

Je, anayekwenda akisinukia juu ya uso wake ni mwongofu zaidi, au yule anayekwenda sawasawa katika Njia Iliyonyooka?

Huu ni mfano wa tamko la swali; mfano wa kuwatofautisha wapotevu waliozama katika ujeuri na kukataa na wale walioongoka wanaosikiliza maneno na wakafuata mazuri yake. Mfano wa wapotevu ni kama anayek­wenda njiani na uso wake umeinamia ardhini huku anajikwaa. Ama walioongoka mfano wao ni kama mfano wa anayekwenda kwenye njia iliyo wazi na mtazamo ulio salama.

Maana ya Aya hii yamekaririka kwenye Aya kadhaa; ikwemo ile isemayo:

مَثَلُ الْفَرِيقَيْنِ كَالْأَعْمَىٰ وَالْأَصَمِّ وَالْبَصِيرِ وَالسَّمِيعِ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٢٤﴾

“Mfano wa makundi mawili ni kama kipofu na kiziwi na anayeona na anayesikia. Je, hawa wawili wanaweza kuwa sawa? Je, hamfikiri?” Juz. 11 (11:24).

Sema: Yeye ndiye aliyewaumba, na akawapa masikio na macho, na nyoyo.

Mwenyezi Mungu amewaumbia masikio, basi waidhikeni kwa mnayoyasikia. Amewajaalia macho, basi zingatieni kwa mnayoyaona, miongoni mwa ishara na miujiza. Amewapa akili, kwanini hamfahamu?

Mmoja wa wafasiri wa zamani alisema: “Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametanguliza usikizi kwa sababu faida zake zina nguvu zaidi kuliko za kuona. Kwa vile usikizi ni wa kuzungumziwa na uoni ni wa kuangalia, na daraja ya kuzungumza ndiyo inayotangulia.”

Mwanafisihi mmoja wa hivi karibuni naye anasema: “Halitangulii neno lolote, katika Qur’an, kulitangulia jingine ila ni kwa sababu fulani, wala halifuati nyuma ila ni kwa sababu; mfano rahisi ni tunavyoona Qur’an ikitanguliza usikizi kuliko uoni katika Aya kadhaa. Jambo hili wanalijua wataalamu wa upasuaji. Wanaona kuwa viungo vya usikizi ni vya hali ya juu, vilivyofungana na laini zaidi kuliko viungo vya uoni.

Mama hawezi kupotewa na sauti ya mtoto wake na anaweza kuitambua hata kukiwa na maelfu ya sauti, lakini anaweza asimuone kukiwa na msongamano.”

Ni kidogo tu mnavyoshukuru , kwa sababu Mungu ameumba masikio na macho kwa ajili ya heri na wema na nyinyi mnavitumia kwa shari na ufisadi.

Sema: Yeye ndiye aliyewatawanya katika ardhi.

Yaani amewafanya wengi kwenye uzazi ili mshindane katika uwanja wa maisha na uimarishaji wake na kugawana kheri zake kwa mujibu wa uwezo wa mtu. Haya ndiyo waliyoyasema wafasiri, lakini kama wange­likuweko hivi sasa ingeliwabidi kuongeza kauli hii: Lakini madola makub­wa yanashindana katika uwanja wa silaha, kuwanyima wenye njaa neema na baraka ya ardhi, ili waweze kulingana na viwanda vya mauti wanavyovimiliki mataghuti walanguzi.

Mahisabu yanaonyesha kuwa matumizi ya silaha ni zaidi ya matumizi ya elimu na afya kwa pamoja.

Na kwake mtakusanywa , awaadhibu wafisadi kwa hatia na makosa yao.Na wanasema: ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?

Swali hili limekaririka mara nyingi sana kutoka kwa wapinzani. Ni ajabu na mshangao, kwa sababu hakuna mwenye akili isipokuwa anataka dalili kwa lile lililo na uwezekano wa kuwa kwa linalofanana na kushabihiana nalo.

Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu tu; na hakika mimi ni mwonyaji tu mwenye kubainisha.

Hii inafanana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلَّا هُوَ ﴿١٨٧﴾

“Wanauliza hiyo saa (Kiyama) kutokea kwake kutakuwa lini? Sema: Ujuzi wake uko kwa Mola wangu. Hakuna wa kuidhihirisha kwa wakati wake ila yeye tu.” Juz. 9 (7:187).

Lakini watakapoiona kwa karibu, nyuso za waliokufuru zitahuzu­nishwa, na itasemwa: Hayo ndiyo mliyokuwa mkiyaomba.

Nabii aliwahadharisha na Siku ya Kiyama, lakini wakamwambia kwa dharau: “Basi tuletee unayotuahidi ukiwa ni miongoni mwa wasemao kweli.”[4] Lakini watakapofufuliwa siku ya Kiyama na kuambiwa: “Haya ndiyo mliyokuwa mkiyahimiza,”[5] watasema: “Ole wetu! Hakika tulikuwa tumeghafilika na haya, bali tulikuwa wenye kudhulumu.”[6]

Hivi ndivyo alivyo kila mjinga anayepanda kichwa na asiyejali yanayose­ma na yanayofanywa kwa ajili yake.

Sema: Mwaonaje, ikiwa Mwenyezi Mungu ataniangamiza mimi na walio pamoja nami, au akiturehemu, ni nani atakayewalinda makafiri na adhabu chungu?

Mwenye kufuatilia Aya za Qur’an yenye hikima ataona kuwa, aghlabu, tofauti iliyokuwako baina ya manabii na washirikina, ilikuwa kwenye ushi­rikina na ufufuo, na kwamba Aya nyingi zilikuwa zikizunguka kwenye misingi miwili hii, kwa mfumo wa moja kwa moja au isiyokuwa moja kwa moja. Washrikina walikuwa wakitoa hoja ya kuabudu masanamu kuwa ni ibada ya mababa na mababu, na wakiukana ufufuo kwa hoja ya kuwa ata­kayegeuka kuwa mchanga vipi anaweza kurudi hai tena?

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemfundisha Nabii wake mtukufu hoja za kuwarudi na kuwaonya na adhabu ya sasa na ya baadae. Yamekwishatangulia makumi ya Aya juu ya hilo. Basi washirikina walis­hindwa kuzijibu hoja, wakabaki kukimbilia kwenye inadi, jeuri na dharau. Mara nyingine wakawa wanamduilia Mtume(s.a.w. w ) aangamie; kama ili­vyoashiria kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “ Au wanasema: mshairi, tunamtazamia kupitilizwa na dahari. Juz. 27 (52:30).

Aya zilizotangulia zimeelezea jinsi Mtume alivyowaambia washirikina kuhusu ufufuo na hadhari ya adhabu ya gharika na vimbunga duniani na adhabu ya Jahannam na marejeo mabaya Akhera.

Kisha ikawa wao wana­muombea dua mbaya Mtume na mwito wake; kiasi cha Mwenyezi Mungu (s.w.t) kumwamrisha kuwaambia: Je, mnanitazamia mimi na aliye pamoja nami kuangamia? Hebu niambieni mtapata faida gani ikiwa yatakuwa hayo mnayoyatamani, je, kutawaokoa na adhabu na hali nyinyi mnaendelea kwenye upotevu? Hapana! Hakuna litakalowafaa isipokuwa toba na kurejea, iwe mtakufa kabla yangu au nife kabla yenu.

Sema: Yeye ndiye Mwingi wa Rehema; tunamuamini Yeye, na juu yake tunategemea.

Hii ndio njia ya kuokoka ‧ kumwamini Mwenyezi Mungu na kwamba Yeye ndiye anayerehemu na kumghufiria mwenye kutubia dhambi zake na akamtegemea katika mambo yake.

Mtakuja jua ni nani aliye katika upotovu ulio dhahiri.

Baada ya Mtume mtukufu(s.a.w. w ) kuwaambia washirikina, kama Mwenyezi Mungu atatuangamiza au kuturehemu, sasa anawaambia: hapana! Nyinyi ndio mtaangamia, kwa sababu ni wapotevu na wapotezaji. Ama sisi tuko katika rehema ya Mwenyezi Mungu na himaya yake na tuna nusura duniani na Akhera, na kesho mtalijua hilo kiuhakika.

Sema: Mwaonaje, yakiwa maji yenu yamedidimia chini, nani atawaletea maji yanayotiririka?

Usawa kwenu enyi washirikina ni kutubia kwa Mwenyezi Mungu na kumshukuru kwa neema zake zisizohisabika; yakiwemo haya maji yenu ambayo ndio chimbuko la maisha yenu. Mwenyezi Mungu angelitaka angeliyadidimiza ndani ya ardhi, na mkafa na njaa na kiu; na wala haku­na mwenye kuzuia matakwa yake.

Kuna mfasiri mmoja aliyesema kuwa Mwenyezi Mungu alikusudia, kwa hili, kulainika nyoyo zao, ili waweze kurudi kwenye uongofu. Hili haliko mbali, kwani mfumo wa kutoa mwito uko namna mbali mbali.

MWISHO WA SURA YA SITINI NA SABA: SURAT AL-MULK


15

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sitini Na Nane: Surat Al- Qalam. Imeshuka Makka. Imesemekana kuwa baadhi imeshuka Madina. Ina Aya 52.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

ن وَالْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ ﴿١﴾

1. Nun. Naapa kwa kalamu na yale wanayoandika.

مَا أَنتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ ﴿٢﴾

2. Kwa neema ya Mola wako wewe si mwendawazimu.

وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ ﴿٣﴾

3. Na kwa hakika wewe una ujira usiokatika.

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ ﴿٤﴾

4. Na hakika wewe una tabia tukufu.

فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ ﴿٥﴾

5. Karibu utaona, na wao wataona.

بِأَييِّكُمُ الْمَفْتُونُ ﴿٦﴾

6. Ni nani kati yenu aliyepandwa na wazimu.

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٧﴾

7. Hakika Mola wako ndiye anayemjua zaidi aliyepotea njia yake na Yeye ndiye anaye­wajua zaidi walioongoka.

فَلَا تُطِعِ الْمُكَذِّبِينَ ﴿٨﴾

8. Basi usiwatii wanaokadhibisha.

وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ ﴿٩﴾

9. Wanatamani lau ungelainisha ili nao wakulainishie.

وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ ﴿١٠﴾

10. Wala usimtii kila mwingi wa kuapa aliye dhalili.

هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ ﴿١١﴾

11. Msingiziaji, apitae akifitini.

مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ ﴿١٢﴾

12. Mwenye kuzuia heri, mwenye kudhulumu, mwingi wa mad­hambi.

عُتُلٍّ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ ﴿١٣﴾

13. Mwenye roho ngumu, juu ya hayo, ni mwanaharamu.

أَن كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ ﴿١٤﴾

14. Ati kwa kuwa ana mali na watoto!

إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٥﴾

15. Anaposomewa Aya zetu, husema: Hizi ni ngano za watu wa kale!

سَنَسِمُهُ عَلَى الْخُرْطُومِ ﴿١٦﴾

16. Tutamtia doa juu ya pua.

WEWE SI MWENDAWAZIMU

Aya 1- 16

MAANA

Nun . kwa kukadiria maneno ya kuwa hii ni sura ya Nun. Hii sio kama mianzo mingineyo ya herufi zinazoanziwa sura, tulizozizungumzia katika Juz. 1 (2:1).

Kuna aliyesema kuwa ni samaki, mwingine akasema ni chombo cha wino, watatu akasema ni wino, wa nne akasema ni nun ya neno rahman, na jamaa wa kisufi wakasema kuwa ni nafsi. Kauli zote hizi zinahitajia dalili.

Naapa kwa kalamu na yale wanayoandika.

Wametofautiana kuhusu kalamu: Kuna waliosema ni kalamu iliyotumika kwenye lawh mahfud[ (ubao maalum uliohifadhiwa). Mwingne akasema ni kila kalamu, na kwamba herufi aliY na la` kwenye neno hili ni ya jinsi, ambayo inamaanisha kuenea.

Hii ndio kauli iliyo dhahiri; kwamba makusudio sio kalamu hasa, bali ni nyenzo yoyote ya kuandikia; kama inavyoashiria kauli inayofuatia inayosema: “Na yale wanayoyaandika.”

Kwa hiyo basi kalamu itakuwa ni kinaya cha chombo cha kuandikia, vyovyote kitakavyokuwa, kilichopo au kitakachogunduliwa karibuni au baadaye. Tumedokeza faida za ubainifu katika Juz. 27 (55:4), kwamba manufaa ya ubainifu ni sawa na manufaa ya maji na hewa.

Kwa neema ya Mola wako wewe si mwendawazimu.

Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad(s.a.w.w) . Hakuna yeyote anayed­hania kuwa Muhammad(s.a.w.w) ni mwenda wazimu. Wale waliompa sifa hiyo walikusudia kuwa ana jinni linalompa wahyi; kama wanavyodai kwamba kila mshairi ana jinni linalomfundisha ushairi.

Hilo linaashiriwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwasimulia:

وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ ﴿٣٦﴾

“Na wakisema: Hivi tuiache miungu miungu yetu kwa ajili ya huyu mshairi mwendawazimu?” Juz. 23 (37:36).

Na kwa hakika wewe una ujira usiokatika.

Neno ‘usiokatika’ tumelifasiri kutokana na neno mamnun, ambalo pia lina maana ya kusimbuliwa au maana zote mbili pamoja (kukatika na kusimbuliwa).

Kimsingi ni kuwa malipo yanapimwa kwa natija ya kazi na athari yake. Bado athari za Muhammad(s.a.w.w) , mwito wake na ukuu wake unaendela hadi leo, kuanzia mashariki mwa ardhi hadi magharibi yake na utaendelea hadi siku ya mwisho. Kwa hiyo si kioja kupata karama ya milele kutoka kwa Mola wake.

Na hakika wewe una tabia tukufu.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakumsifu yeyote katika mitume wake na wasi­fa huu isipokuwa Muhammad.

Maana yake yanafupilizwa na kauli yake Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) : “Mola wangu amenifunza maadili akayafanya mazuri mafunzo yangu,” yaani Mwenyezi Mungu ameelekeza kwa Muhammad(s.a.w.w) maadili yale yale aliyoumba kwa ajli ya nafsi.

Vile vile Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakuwahi kuapa kwa maisha ya mtu isipokuwa kwa maisha ya Muhammad(s.a.w.w) ; pale aliposema:

لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿٧٢﴾

“Naapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao wakiman­gamanga.”

Juz. 14 (15:72).

Ama wasifu wa Muhammad(s.a.w.w) kuwa ni mwisho wa manabii, Maana yake ni kuwa Muhammad alifikia ukomo wa sifa za mtu zisizofikiwa na yeyote kwa ukamilifu. Ni muhali kuja baada yake atakayekuwa bora zaidi kuliko yeye au kuja na sharia bora zaidi ya sharia zake; bali hakuna kium­be yeyote kuanzia wa mwanzo hadi wa mwisho anayefanana naye. Hilo linaashiriwa na kauli yake Mtume(s.a.w.w) : “Mimi ni bwana wa watu wote, wala sisemi kwa kujifaharisha.”

Hii ni kwa kuwa sharia na utume umeishilizwa kwake. Ibn Al-arabiy anasema, katika Futuhat: kuwa Mwenyezi Mungu ameumba viumbe aina kwa aina, akafanya walio bora. Walio bora katika viumbe ni mitume, na katika mitume kuna wateule ambao ni ulul-az` na katika wao kuna mteule zaidi naye ni Muhammad(s.a.w.w) .

Karibu utaona, na wao wataona, ni nani kati yenu aliyepandwa na wazimu.

Hili ni onyo na kiaga, kwamba hivi karibuni itakubainikia wewe na maadui zako kwamba wao ndio wajinga, wapotevu na wendawazimu zaidi katika watu, na kwamba wewe ndiwe ulie juu, mwenye akili na mtukufu wa maadili zaidi ya watu wengine na kwamba ndiwe mtukufu wao zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu.

Hakika Mola wako ndiye anayemjua zaidi aliyepotea njia yake na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.

Mwenyezi Mungu anajua cheo chako ewe Muhammad(s.a.w.w) na uongo­fu na anajua nafasi ya wahasimu wake ya upotevu na mbele yao kuna hisabu na malipo. Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 14 (16:125).

Basi usiwatii wanaokadhibisha.

Washirikina walijaribu kila njia kumzuia Mtume(s.a.w.w) na mwito wake, wakajaribu kumbembeleza kwa cheo na mali, akakataa. Wakatamani lau watakubaliana naye kufanya vile watakavyo, Mwenyezi Mungu akamkataza hilo. Lengo la kumkataza ni kuwakatisha tamaa na wajue kuwa hakuna mjadala wala makubaliano katika twaa ya Mwenyezi Mungu na amri yake. Katazo hili linafanana na anayekutaka mkubaliane naye kwenye dini yako, ukiwa unataka kumkatisha tamaa kabisa, na kumwambia: Mwenyezi Mungu amenikataza hilo.

Wanatamani lau ungelainisha ili nao wakulainishie.

Washirikina walitamani Mtume(s.a.w.w) apunguze baadhi ya yale anayowalingania na wao waache baadhi ya yale aliyowakataza, ijapokuwa ni kwa njia ya kupakaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili kusiwe na mvu­tano baina ya pande mbili.

Mfumo wa maneno unafahamisha kuwa aliyetoa maoni hayo anasifika na sifa aliyoiashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa kusema:Wala usimtii kila mwingi wa kuapa aliye dhalili . Anakithirisha viapo bila ya sababu jambo linalomsababisha kuwa dhalili anayedharauliwa.Msingiziaji anawatia ila sana watu.Apitaye akifitini . Anajaribu kuwavuruga watu kwa kunukuuu ya huku akiyapeleka kule.

Mwenye kuzuia heri , yeye haifanyi na anazuia wengine wasiifanye.Mwenye kudhulumu , haki za watu.Mwingi wa madhambi na makosa.Mwenye roho ngumu, juu ya hayo, ni mwanaharamu, asiyejua nasaba yake. Hii ni sifa mbaya zaidi ya zote zinazofikiriwa na akili.

Wafasiri wengi wamesema kuwa aliyekusudiwa na ushenzi huu ni Walid bin Al-mughira, aliyekuwa ni miongoni mwa vigogo wa kikuraishi, mwenye mali nyingi na watoto; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:Ati kwa kuwa ana mali na watoto! Anaposomewa Aya zetu, husema: Hizi ni ngano za uwongoza watu wa kale!

Wafasiri wamesema kuwa Aya hii ni ya kukataza kumtii mshenzi huyu. Lakini lililo karibu zaidi na usawa ni kuwa huko kuwa na mali na watoto kumemfanya athubutu kusema Qur’an ni simulizi za watu wa zamani; kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾ أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾

“Hakika mtu hupituka mipaka kwa kujiona ametajirika.” (96:6-7).

Sikwambii tena akiwa na nguvu na watu.Tutamtia doa juu ya pua yake. Waarabu wanatumia kutaja pua kwa ajili ya utukufu na udhalii. Wanasema kwa utukufu: ana pua ya kunusa. Kwenye udhalili wanasema: pua yake ikio mchangani.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) atamfedhehesha mjeuri huyu ambaye amejitukuza kwa mali na watoto, atamdhalilisha muda wote, atam laani kwa lugha iliyosajiliwa kwenye Kitabu chake na atamfedhehesha Akhera mbele ya ushuhuda, kwa kusawijika uso na alama nyinginezo za kuakisi madhambi yake.

إِنَّا بَلَوْنَاهُمْ كَمَا بَلَوْنَا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ ﴿١٧﴾

17. Hakika tumewajaribu kama tulivyowajaribu wenye sham­ba, walipoapa kwamba watal­ivuna itakapokuwa asubuhi.

وَلَا يَسْتَثْنُونَ ﴿١٨﴾

18. Wala hawakusema: Inshaallah!

فَطَافَ عَلَيْهَا طَائِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمْ نَائِمُونَ ﴿١٩﴾

19. Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako, nao wamelala!

فَأَصْبَحَتْ كَالصَّرِيمِ ﴿٢٠﴾

20. Likawa kama limefyekwa.

فَتَنَادَوْا مُصْبِحِينَ ﴿٢١﴾

21. Wakaitana asubuhi.

أَنِ اغْدُوا عَلَىٰ حَرْثِكُمْ إِن كُنتُمْ صَارِمِينَ ﴿٢٢﴾

22. Ya kwamba raukeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna.

فَانطَلَقُوا وَهُمْ يَتَخَافَتُونَ ﴿٢٣﴾

23. Basi walikwenda na huku wakinong’onezana.

أَن لَّا يَدْخُلَنَّهَا الْيَوْمَ عَلَيْكُم مِّسْكِينٌ ﴿٢٤﴾

24. Ya kuwa leo asiliingie hata maskini mmoja.

وَغَدَوْا عَلَىٰ حَرْدٍ قَادِرِينَ ﴿٢٥﴾

25. Na walirauka, nao wana nguvu za kunyima.

فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوا إِنَّا لَضَالُّونَ ﴿٢٦﴾

26. Basi walipoliona, wakasema: Hakika tumepotea!

بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ ﴿٢٧﴾

27. Bali tumenyimwa!

قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ ﴿٢٨﴾

28. Akasema Mbora wao: Je, Sikuwambia, kwa nini hamumsabihi Mwenyezi Mungu?

قَالُوا سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٢٩﴾

29. Wakasema: Ametakasika Mola wetu! Hakika tulikuwa madhalimu.

فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَلَاوَمُونَ ﴿٣٠﴾

30. Basi wakakabiliana kulau­miana wao kwa wao.

قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ ﴿٣١﴾

31. Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka!

عَسَىٰ رَبُّنَا أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا رَاغِبُونَ ﴿٣٢﴾

32. Asaa Mola wetu akatubadil­ishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu.

كَذَٰلِكَ الْعَذَابُ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٣٣﴾

Kama hivyo inakuwa adhabu, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi, laiti wangelijua!

LIKAWA KAMA LIMEFYEKWA

Aya 17 – 33

MAANA

Hakika tumewajaribu kama tulivyowajaribu wenye shamba.

Waliojaribiwa ‧ katika neno tumewajaribu - ni washirikina wa kikuraishi waliomkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ambao Mwenyezi Mungu amewaashiria katika Aya ya nane ya surua hii. ‘Basi usiwatii wanaokadhibisha.’ Akiwemo yule mwenye kupituka mipaka mwenye dhambi ambaye, kama walivyosema wafasri, ni Walid bin Almughira, kigogo wa makuraishi msemaji wa wakadhibishaji akielezea ufidhuli na jeuri yao juu ya haki.

Aya hizi tulizo nazo zinampigia mfano yeye na wao, kwamba kulikuwa na watu waliokuwa na shamba lililojaa mazao, lakini wao walikuwa mabahili kwa mafukara na masikini.

Mazao yalipokomaa na kukurubia kuvunwa walipanga njama na kuapa kuwa wavune shamba asubuhi na mapema, mafukara wakiwa hawana habari. Waliazimia hivyo bila ya kuyaunganisha maazimio yao na matakwa ya Mwenyezi Mungu. Waliambiana kuwa wawanyime wahitaji kile walichopewa na Mwenyezi Mungu, wakiwa wamesahau mipangilio ya Mwenyezi Mungu na uweza wake.

Usiku huo huo walioazimia kuvuna, Mwenyezi Mungu alilitermshia shamba janga la mbinguni lilioharibu mazao yote kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Walipoamka asubuhi na kwenda shambani walipigwa na butwaa, wakaan­za kulaumiana wenyewe kwa wenyewe, kila mmoja akimwambia mwen­zake: “Wewe ndiye sababu ya haya.” Miongoni mwao alikuwako mtu mwema aliyewapa nasaha kabla, lakini hawakumsikiliza, ndio akawaambia: Kwani sikuwaaambia, lakini mkakataa. Basi tubieni kwa Mola ili mpate kufaulu. Wakatubia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wakam­womba msamaha na kutaka wahurumiwe na kuneemeshwa kutoka shambani mwao.

Lengo la kupiga mfano huu, ni kupata funzo kila aliyeneemeshwa na Mwenyezi Mungu; hasa watu wa Makka akiwemo yule mshenzi. Wapokezi wa Hadith wanasema watu wa Makka walipatwa na kahati na njaa kwa vile walimkadhibisha Muhammad(s.a.w.w) , ndipo akawaombea majanga na Mwenyezi Mungu akaitikia maombi yake. Kahati iliendelea kiasi cha miaka saba mpaka wakawa wanakula mizoga na mifupa. Pia wapokezi wanasema Mwenyezi Mungu aliingamiza mali ya Walid.

Haya ndio makusudio ya Aya kwa ujumla wake. Ufuatao ni ufufanuzi wa Aya moja moja:-

Walipoapa kwamba watalivuna itakapokuwa asubuhi.

Wenye shamba waliapa kuwa watalivuna mafukara wakiwa hawana habari.

Wala hawakusema: Inshaallah!

Yaani hawakusema tutavuna asubuhi Mungu akipenda.

Tumefasiri wala hawakusema inshaallah! Kutokana na maneno ya kiarabu yastathnuua ambayo tafsiri yake ya moja kwa moja ni ‘hawakutenga au hawakutoa.’ Kwa hiyo baadhi ya wafasiri wakasema maana ni hawakutenga kitu kwa ajili ya masikini. Kila moja kati ya tafsiri mbili hizi inafaa. Vile vile zinaweza kwenda kwa pamoja.

Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako, nao wamelala! Likawa kama limefyekwa.

Wenye shamba walilala raha mustarehe wakiwa na imani ya kulivuna shamba lao asubuhi na mapema, lakini usiku huo likafikwa na janga.

Neno kufyekwa, tumelifasiri kutokana na neno Asswarim, ambalo maana yake nyingine ni weusi, kwa maana ya kuungua na kuwa jeusi kama usiku wa giza

Wakaitana asubuhi, ya kwamba raukeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna.

Ilipofika asubuhi waliitana ili wawahi kwenda shamba bila ya masikini kujua.

Basi walikwenda na huku wakinong’onezana. Ya kuwa leo asiliingie hata masikini mmoja.

Walifanya haraka wakidhamiria kwa siri kuwa masikini asionje hata chembe ya mazao.

Hakuna mwenye shaka kuwa huu ni uchoyo. Ikiwa hawa shamba lilikuwa lao na mazao ni yao hawakuiba, lakini pamoja na hayo Mwenyezi Mungu aliwaghadhabikia na kuwaandalia adhabu; je, itakuwaje kwa yule aliyepituka mipaka kwenye maisha ya watu akawanyang’anya vyakula vyao, akawaua na kuwafukuza kwenye miji, kama wanavyofanya wakoloni hivi sasa katika mashariki ya dunia na magharibi yake?

Na walirauka, nao wana nguvu za kunyima.

Waliingia shambani mwao wakiwa na dhamira kabisa ya kuwanyima mafukara, wakiwa na mawazo kwamba shamba na mazao yake yako mikononi mwao. Hawakujua kuwa mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao.

Basi walipoliona, wakasema: Hakika tumepotea! Bali tumenyimwa!

Walipofika shamba yaliwashangaza waliyoyaona na wakakubali kuwa wamepotea na kusema: sisi ndio tuliokosa fadhila za Mwenyezi Mungu na thawabu zake, na tunastahili ghadhabu za Mwenyezi Mungu na adhabu yake na sio mafukara na masikini.

Miongoni mwao alikuwa mtu mwema aliyekuwa akiaamrisha mema na kuwakataza maovu, lakini hawakusikiliza nasaha zake. alipoona yaliyowafika:

Akasema Mbora wao: Je, Sikuwambia, kwa nini hamumsabi­hi Mwenyezi Mungu?

Yaani hamumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kauli wala kwa vitendo kwa kutoa. alisema hivi kwa kuwahurumia. Kisha akawaamuru kutubia:Wakasema: Ametakasika Mola wetu! Hakika tulikuwa madhalimu wa nafsi zetu kwa kumuasi Mwenyezi Mungu.

Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao.

Kila mmoja anamtupia lawama mwinziwe; kama ilivyo hali ya washiriki­na, wanapofikwa na yale yaliyofanywa na mikono yao.

Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka!

Walirudia akili zao na wakacha kulaumiana, wakakiri dhambi zao kwam­ba wao walikuwa katika upotevu, wakijiombea kufa kwa kusema ‘Ole wetu’ na kumwomba msamaha Mwenyezi Mungu, wakasema:Asaa Mola wetu akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu.

Hii ni dua na matarajio yao kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) awasamehe yaliyopita na awabadilishie yaliyo bora kuliko yaliyopita. Na Mwenyezi Mungu anakubali toba kutoka kwa waja wake, anawasamehe mengi na anaitikia maombi ya anayemuomba kwa ukweli na ikhlasi.

Kama hivyo inakuwa adhabu, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi, laiti wangelijua!

Razi anasema hii iko wazi haihitaji tafsir, lakini sheikh Maraghi amekataa isipokuwa kuifasiri kwa kusema: “Yaani adhabu ya Akhera ni kali na inau­miza zaidi kuliko adhabu ya duniani.”


16

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٣٤﴾

34. Hakika wenye takua watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao.

أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ ﴿٣٥﴾

35. Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu?

مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ﴿٣٦﴾

36. Mna nini? Mnahukumu vipi?

أَمْ لَكُمْ كِتَابٌ فِيهِ تَدْرُسُونَ ﴿٣٧﴾

37. Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma?

إِنَّ لَكُمْ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ ﴿٣٨﴾

38. Kuwa mtapata humo mnayo yachagua?

أَمْ لَكُمْ أَيْمَانٌ عَلَيْنَا بَالِغَةٌ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ إِنَّ لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ ﴿٣٩﴾

39. Au mna viapo juu yetu vinavyofika Siku ya Kiyama ya kuwa mtapata mnayo­jihukumia?

سَلْهُمْ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ ﴿٤٠﴾

40. Waulize: Ni nani miongoni mwao mdhamini wa hayo?

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ فَلْيَأْتُوا بِشُرَكَائِهِمْ إِن كَانُوا صَادِقِينَ ﴿٤١﴾

41. Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao waki­wa wanasema kweli.

يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ ﴿٤٢﴾

42. Siku utakapowekwa wazi muundi, na wataitwa kusu­judu, lakini hawataweza.

خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ وَقَدْ كَانُوا يُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ وَهُمْ سَالِمُونَ ﴿٤٣﴾

43. Macho yao yatanyenyekea fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipokuwa salama.

KWANI TUTAWAFANYA WAISLAMU KAMA WAKOSEFU?

Aya 34 – 43

MAANA

Hakika wenye takua watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao.

Katika Aya zilizotangulia Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwaahidi wakosefu adhabu kubwa, na katika Aya hii anawaahidi wanaomcha Mwenyezi Mungu kuwa na milki ya daima na neema ya kudumu. Namna hii Mwenyezi Mungu analinganisha mwisho wa wakosefu na wa wenye takua; kwa kuvutia na kuhadharisha.

Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? Mna nini? Mnahukumu vipi?

Makusudio ya waislamu hapa sio kila mwenye kusema: Lailaha ilallah muhammadur-rasulullah[ (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu); bali makusudio ni wanaom­cha Mwenyezi Mungu. Kwa sababu mazungumzo hapa yanahusiana na wao na yale waliyo nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya Pepo yenye neema.

Unaweza kuuliza : hatudhani kama kuna yeyote anayehukumu kuwa wenye takua wako sawa na wakosefu; sasa kuna haja gani ya Mwenyezi Mungu kusema: mnahukumu vipi?

Jibu : Ni kweli kuwa hakuna anayehukumu kuwa wakosefu na wenye takua wako sawa, lakini mara nyingi wakosefu wanajiona kuwa ni wacha Mungu na kwamba wao wanastahiki malipo na tahawabu wanazostahiki wenye takua.

Basi ndio Mwenyezi Mungu akalipinga hilo na kuwaambia, vipi mnajifanya mko sawa na wenye takua na kati yenu na wao kuna umbali wa mashriki na magharibi? Linalofahamisha maana haya kuwa ndio makusudio ni maswali haya yafuatayo:

Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma? Kuwa mtapata humo mnayoyachagua?

Je, mna Kitabu kutoka mbinguni au ardhini mnachokisoma kwamba nyi­nyi duniani mtapata mnachokipenda na Akhera mpate mnachokitamani? Wasifu uko sawa na ule wa mayahudi na wanaswara: “Na Mayahudi na Manaswara wanasema: Sisi ni wana wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake.” Juz. 6 (5:18).

Makusudio ya Aya tunayoifasiri ni ya vigogo wa kikuraishi. Ingawaje wao hawakudai kuwa na Kitabu, lakini lengo ni kuwanyamazisha, kwamba hakuna dalili wa mfano wa dalili kuwa wako sawa na wenye takua na kwamba wao watapata wanayoyataka.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 22 (35:30) na Juz. 25 (43:21)

Au mna viapo juu yetu vinavyofika Siku ya Kiyama ya kuwa mtapata mnayojihukumia?

Je, Mwenyezi Mungu amewaapia kiapo kizito na kuwapa ahadi msisitizo kuwa atawaingiza Peponi pamoja na wanaomcha Mungu? Kwamba hatabadilisha ahadi mpaka siku ya Kiyama?

Waulize: Ni nani miongoni mwao mdhamini wa hayo?

Yaani waulize wewe Muhammad! Ni nani aliyeahidiana nao kutekelezewa madai yao?

Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanase­ma kweli.

Makusudio ya washirika hapa ni masanamu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: “Sema: nionyesheni wale mliowaunganisha naye kuwa washirika.” Juz. 22 (34:27).

Maana ni kuwa haya nawalete hao washrikina waungu wanaowaabudu ili washuhudie kwamba wao watapata Pepo pamoja na wenye takua.

Msawali yote aliyoyaelekeza Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa washirikina ni kuwa hakuna kitu kinachofahamisha kwa karibu wala mbali kwamba washirikina wana chochote. Aina hii ya hoja ni katika nyenzo nzuri sana ya kumnyamazisha hasimu, wakati huo ikielimisha na kuleta uhakika.

Siku utakapowekwa wazi muundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza.

Waarabu wanaiita siku ngumu na yenye shida kuwa siku ya kufunuka muundi. Ndio maana siku ya Kiyama imeitwa hivyo. hakuna atakayetaki­wa kusujudi siku hiyo wala kufanya ibada nyingineyo, kwa sababu hiyo ni siku ya hisabu na malipo sio siku ya taklifa na matendo. Kwa hiyo basi kutakiwa kusujudi ni kwa njia ya kutahayariza, sio kwa sharia na taklifa.

Kwa hiyo makusudio ya kutoweza kusujudi siku hiyo ni kwamba hakutawafaa kitu kwa sababu siku hiyo ni ya malipo sio ya kufanya amali. Maana ni kuwa wale ambao wamepituka mipaka au wakafanya uzembe duniani walipokuwa na uwezo wa kufanya, watatahayarizwa na kuadhibi­wa siku ya Kiyama ambayo hakuna hila wala njia ya kuwakurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Macho yao yatanyenyekea.

Kunyenyekea ni sifa ya moyo, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ameileta kwa kinaya cha udhalili wao na utwevu wao uliodhahiri machoni mwao. Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:fedheha itawafunika , ni tafsiri na ubainifu wa hilo.

Na hakika walikuwa dunianiwakiitwa wasujudu, lakini walikataa kwa kiburi.walipokuwa salama, bila ya kizuizi chochote. Baada ya kuiona adhabu sasa ndio wanataka kusujudi, lakini wakati umekwishapita.

فَذَرْنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَـٰذَا الْحَدِيثِ سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٤٤﴾

44. Basi niache na wanaokad­hibisha maneno haya! Tutawavuta kidogo kidogo kwa mahali wasipopajua.

وَأُمْلِي لَهُمْ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ ﴿٤٥﴾

45. Na ninawapa muda; hakika hila zangu ni imara.

أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ ﴿٤٦﴾

46. Au wewe unawaomba ujira, kwa hiyo wanalemewa na gharama?

أَمْ عِندَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ ﴿٤٧﴾

47. Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wanaandika?

فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ الْحُوتِ إِذْ نَادَىٰ وَهُوَ مَكْظُومٌ ﴿٤٨﴾

48. Basi ingojee hukumu ya Mola wako, wala usiwe kama sahibu wa samaki, aliponadi naye amezongwa.

لَّوْلَا أَن تَدَارَكَهُ نِعْمَةٌ مِّن رَّبِّهِ لَنُبِذَ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ مَذْمُومٌ ﴿٤٩﴾

49. Kama isingelimfikia neema kutoka kwa Mola wake, bila ya shaka angeli tupwa ufuk­weni naye ni mwenye kulau­miwa.

فَاجْتَبَاهُ رَبُّهُ فَجَعَلَهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٥٠﴾

50. Lakini Mola wake alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.

وَإِن يَكَادُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَارِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا الذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُ لَمَجْنُونٌ ﴿٥١﴾

51. Na waliokufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanaposikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu.

وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿٥٢﴾

52. Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.

NIACHENI NA WANAOKADHIBISHA

Aya 44 - 52

MAANA

Basi niache na wanaokadhibisha maneno haya!

Wanaokadhibisha ni washirikina wa kiarabu. Maneno ni Qur’an. Neno ‘niache na’ ni lakutangaza vita nao kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwam­ba Mwenyezi Mungu Yeye mwenyewe atatekeleza kuwaadhibu; apumue Nabii na wale walio pamoja naye kutokana nao na shari yao, kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akabainisha, vipi na kwa njia gani atawatesa pale aliposema:

Tutawavuta kidogo kidogo kwa mahali wasipopajua. Na ninawapa muda; hakika hila zangu ni imara.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapa muda wala hawafanyii haraka. Vile vile anawapa mali na watoto na kuwatoa kwenye hali nzuri hadi kwenye hali nzuri zaidi katika dhahiri ya maisha ya dunia, lakini wao kwa undani, wanagurishwa kutoka kwenye hali mbaya hadi kwenye hali mbaya zaidi; mpaka wakifikia kujiona kuwa wako katika ngome madhubuti, ndipo Mwenyezi Mungu huwapatiliza kwa mpatilizo wa mwenye nguvu mwenye uweza. Ili hilo liwe ni la kuumiza zaidi na kutia uchungu moyoni.

Mwenyezi Mungu amekuita huku kuvuta kidogo kidogo kuwa ni hila kwa sababu kunafanana na hila kwa dhahiri; vinginevyo ni kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kutakata na hila na vitimbi. Vipi isiwe hivyo na hali hakimbilii kwake ila mwenye kushindwa, na Mwenyezi Mungu husema kukiambia kitu ‘kuwa kikawa.’ Zaidi ya haya lengo la kutajwa vitimbi ni asihadaike mtu na dunia ikimkabili na kumpa tabasamu. Anatakikana awe na hadhari na yanayojificha.

Au wewe unawaomba ujira, kwa hiyo wanalemewa na gharama? Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wanaandika?

Je, unawataka mali inayokuwa na uzito kwao kuitoa, au wamejua ilimu ya siri kwa hiyo wakafuta yale wanayotakiwa kuamini. Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 27 (40-41).

Basi ingojee hukumu ya Mola wako, wala usiwe kama sahibu wa samaki, aliponadi naye amezongwa.

Sahibu wa samaki ni Nabii Yunus ambaye alipata dhiki na watu wake na akawaacha kwa hasira. Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:97), Juz. 17 (21:87) na.Juz. 23 (37:140). Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemuusia Nabii wake mtukufu(s.a.w.w) kuwa na subira na adha ya watu wake, wala asifanye haraka, kama alivyofanya Yunus, aliyemezwa na samaki, akanadi akiwa tumboni mwa samaki:

أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾

“Hapana Mola isipokuwa wewe, umetakasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.” Juz. 17 (21:87).

Kama isingelimfikia neema kutoka kwa Mola wake, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa.

Yunus alimwomba Mola wake akiwa tumboni mwa samaki, akamwitikia dua yake kwa kumuhurumia, akatemwa na samaki akiwa si mwenye kulau­miwa. Lau si dua yake na kuhurumiwa na Mola wake angelikuwa katika wenye kulaumiwa; bali angelibakia tumboni mwa samaki hadi siku ya ufu­fuo. Ilivyo hasa nikuwa kulaumiwa hapa ni kwa sababu ya kuacha lilo bora sio kwa sababu ya dhambi na uasi.

Lakini Mola wake alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.

Miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kwa Yunus ni kwamba Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu alimtoa tumboni mwa samaki, akiwa radhi naye, na akamrudisha kwa watu wake akiwa Nabii; kama alivyokuwa hapo mwanzo; wakanufaika naye na kwa mawaidha yake.

Lau angelibakia kati­ka tumbo la samaki hadi siku ya ufufuo, unabii wake usingelikuwa na athari yoyote. Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “akamfanya mion­goni mwa watu wema,” ni kuwa atamfufua kesho pamoja na manabii.

Na waliokufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wana­posikia mawaidha

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Maana ni kuwa washirikina wanaposikia Qur’an kutoka kwa Muhammad(s.a.w.w) wanamtazama kwa mtazamo wa kiuadui na chuki, na miguu ya Mtume(s.a.w.w) inakurubia kuteleza kutokana na mtazamo wao mkali kama mshale. Razi anasema: “Waarabu wanasema: Amenitazama kwa kwa mtazamo unaokaribia kuniangusha na kunila. Mshairi anasema: wakikutana macho huyazungusha, mtazamo wa nyoyo kuziangusha

Na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu.

Walimtazama Mtume kwa mtazamo mkali, vile vile wakamtupia maneno makali, kama kusema kwao: Yeye ni mwendawazimu mwenyezi Mungu (s.w.t) amewarudi, mwanzo mwanzo mwa sura hii tuliyo nayo, kwa kuse­ma: “Kwa neema ya Mola wako wewe si mwendawazimu.”

Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.

Makusudio ya ukumbusho ni ukumbusho wa heri na mwongozo wa njia yake. Maana ni kuwa Qur’an ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu aliouteremsha kwa Muhammad(s.a.w.w) ili awaongoze watu wote, kila mahali na kila wakati.

MWISHO WA SURA YA SITINI NA NANE: SURAT AL- QALAM


17

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sitini Na Tisa: Surat Al-Haqqa. Imeshuka Makka. Ina Aya 52.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

الْحَاقَّةُ ﴿١﴾

1. Tukio la haki.

مَا الْحَاقَّةُ ﴿٢﴾

2. Nini hilo Tukio la haki?

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحَاقَّةُ ﴿٣﴾

3. Na nini kitachokujulisha tukio la haki ni nini?

كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَادٌ بِالْقَارِعَةِ ﴿٤﴾

4. Thamudi na A’di walikad­hibisha tukio linalogonga.

فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهْلِكُوا بِالطَّاغِيَةِ ﴿٥﴾

5. Basi Thamudi waliangamizwa kwa tukio kubwa mno.

وَأَمَّا عَادٌ فَأُهْلِكُوا بِرِيحٍ صَرْصَرٍ عَاتِيَةٍ ﴿٦﴾

6. Na ama A’di waliangamizwa kwa upepo mkali wenye nguvu.

سَخَّرَهَا عَلَيْهِمْ سَبْعَ لَيَالٍ وَثَمَانِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومًا فَتَرَى الْقَوْمَ فِيهَا صَرْعَىٰ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ خَاوِيَةٍ ﴿٧﴾

7. Aliowapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magogo ya mitende yalio wazi ndani.

فَهَلْ تَرَىٰ لَهُم مِّن بَاقِيَةٍ ﴿٨﴾

8. Basi je, unamwona mmoja wao aliyebaki?

وَجَاءَ فِرْعَوْنُ وَمَن قَبْلَهُ وَالْمُؤْتَفِكَاتُ بِالْخَاطِئَةِ ﴿٩﴾

9. Na Firaun na waliomtangulia, na miji iliyopinduliwa chini juu, walileta hatia.

فَعَصَوْا رَسُولَ رَبِّهِمْ فَأَخَذَهُمْ أَخْذَةً رَّابِيَةً ﴿١٠﴾

10. Wakamuasi Mtume wa Mola wao, ndipo akawakamata kwa mkamato uliozidi nguvu.

إِنَّا لَمَّا طَغَى الْمَاءُ حَمَلْنَاكُمْ فِي الْجَارِيَةِ ﴿١١﴾

11. Maji yalipofurika tuliwapan­disha katika Jahazi.

لِنَجْعَلَهَا لَكُمْ تَذْكِرَةً وَتَعِيَهَا أُذُنٌ وَاعِيَةٌ ﴿١٢﴾

12. Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalosikia liyahifadhi.

فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ نَفْخَةٌ وَاحِدَةٌ ﴿١٣﴾

13. Na itapulizwa parapanda mpulizo mmoja.

وَحُمِلَتِ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةً وَاحِدَةً ﴿١٤﴾

14. Na ardhi na milima ikaondole­wa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja.

فَيَوْمَئِذٍ وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ ﴿١٥﴾

15. Siku hiyo Tukio litatukia.

وَانشَقَّتِ السَّمَاءُ فَهِيَ يَوْمَئِذٍ وَاهِيَةٌ ﴿١٦﴾

16. Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.

وَالْمَلَكُ عَلَىٰ أَرْجَائِهَا وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَانِيَةٌ ﴿١٧﴾

17. Na Malaika watakuwa kandoni mwake; Na wanane juu ya hawa siku hiyo watabeba Arshi ya Mola wako.

يَوْمَئِذٍ تُعْرَضُونَ لَا تَخْفَىٰ مِنكُمْ خَافِيَةٌ ﴿١٨﴾

18. Siku hiyo mtahudhurishwa ­haitafichika siri yoyote yenu.

TUKIO LA HAKI

Aya 1 – 18

MAANA

Tukio la haki. Nini hilo Tukio la haki?

Makusudio ya tukio la haki ni Kiyama. Kimeitwa hivyo kwa sababu ni wajibu kutokea kwake. Ama kuuliza na kukaririka, ni kwa ajili ya kuhofisha ukali wake na vituko vyake; kwamba ni tukio ambalo masikio hayajawahi kusikia, macho haya­japata kuona wala akili haijawahi kuwazia. Ndio maana Mwenyezi Mungu (s.w.t) akalirudia swali kwa kusema: Na nini kitakujulisha nini hilo Tukio la haki?

Thamudi na A’di walikadhibisha tukio linalogonga.

Thamud ni watu wa Swaleh na A’d ni watu wa Hud. Tukio linalogonga ni katika majina ya Kiyama, kama tukio la haki.

Basi Thamudi waliangamizwa kwa tukio kubwa mno, ambalo ni ukelele wa adhabu. Umeitwa hivyo kwa sababu ya ukali wake.

Na ama A’di waliangamizwa kwa upepo mkali wenye nguvu, wenye kuangamiza.

Aliowapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo.

Upepo uliendelea kwa muda huo bila ya kusita.

Utaona watu wamepinduka ardhinikama kwamba ni magogo ya mitende yalio wazi ndani.

Kila aliye maiti ni gogo lilio wazi; hata kama amevaa hariri.

Basi je, unamwona mmoja wao aliyebaki?

Hapana! Hakuna atakayebaki. Yametangulia maelezo kuhusu A’d na Tahamud kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 8 (7:65-79), Juz. 12 (11:50-68) na Juz. 19 (26:123-1590).

Na Firaun na waliomtangulia, na miji iliyopinduliwa chini juu, walile­ta hatia. Wakamuasi Mtume wa Mola wao, ndipo akawakamata kwa mkamato uliozidi nguvu.

Miji iliyopinduliwa ni miji ya watu wa Lut. Maana yake kwa ufupi ni kuwa Firaun na watu wake na mfano wao katika wale waliotangulia, wakiwemo watu wa Lut, waliwakadhibisha manabii wa Mwenyezi Mungu na mitume wake, na wakafanya vitendo vya hatia; ndio Mwenyezi Mungu akawapatiliza kwa adhabu iliyopita kiasi cha kufikiriwa. Aya na Sura za kumzungumzia Firaun na watu wake ni nyingi; zikiwemo zile zilizo katika Juz. 9 (7:103-137). Vile vile yametangulia maelezo kuhusu Lut na watu wake mara kadhaa; yakiwemo yale yaliyo katika Juz. 8 (7:80-84).

Maji yalipofurika tuliwapandisha katika Jahazi.

Makusudio ya jahazi hapa ni Safina ya Nuh. Hapa kuna maneno ya kukadiriwa; yaani tuliwachukua mababu zenu waumini katika Safina ya Nuh. Vile vile masimulizi kuhusu Nuh na Safina yake, yametangulia mara kadhaa; kama, katika Juz. 8 (7:59-64).

Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu.

‘Hayo’ ni hayo ya kisa cha Nuh na Safina yake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameyakariri kwenye Kitabu chake ili ajue kila mtu kwamba lau si Safina ya Nuh, Adam na Hawa wasingebakiwa na watoto baada ya Tufani. Abul­A’lai ameenda mbali pale alipodai angelikuwa tasa mama yetu Hawa. Kwa sababu kuweko sisi ni neema; kama alivyosema Aristotle na wanafunzi wake.

Na kila sikio linalosikia liyahifadhi.

Kwenye tafsri nyingi za kale na za sasa; ikiwemo ya Razi na ya Sheikh Maraghi, imeelezwa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alimwambia Ali bin Abu Twalib: “Mimi nimemuomba Mwenyezi Mungu ajalie masikio yako ewe Ali.” Imam Akasema: “Sikusikia chochote nikakisahau, na wala sikuwa ni mwenye kusahau.”

Na itapulizwa parapanda mpulizo mmoja.

Kupulizwa parapanda ni kinaya cha ukelele wa kutoka makaburini. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

يَوْمَ يَسْمَعُونَ الصَّيْحَةَ بِالْحَقِّ ذَٰلِكَ يَوْمُ الْخُرُوجِ ﴿٤٢﴾

“Siku watakaposikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kutoka.” Juz. 26 (50:42).

Katika Juz. 24 (39:68), tumetaja maoni ya wafasiri kuhusiana na Parapanda, na kwamba mipulizo itakuwa mitatu: Mpulizo wa fazaa, wa mauti na wa kufufuliwa.

Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja.

Hiki ni kinaya cha kuharibika ardhi na vilivyomo ardhini siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga.” (73:14). Yaani itakuwa kama michanga inayokwenda na upepo.

Siku hiyo Tukio litatukia.

Parapanda ikipulizwa na ardhi na majabali yakivunjwavunjwa, hapo ndio kitasimama Kiyama na wakadhibishaji watajua kuwa ni haki isiyokuwa na shaka.

Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.

Kitachoipata ardhi na mbingu vile vile kitaipata mbingu:

يَوْمَ تُبَدَّلُ الْأَرْضُ غَيْرَ الْأَرْضِ وَالسَّمَاوَاتُ ﴿٤٨﴾

“Siku itakapobadilishwa ardhi kuwa ardhi nyingine na mbingu (pia).” Juz. 14 (14:48).

Yaani mbingu pia itabadilishwa.

Na Malaika watakuwa kandoni mwake ; yaani kandoni mwa mbingu. Maana ni kuwa baada ya kuharibika ardhi na mbingu Malaika watatawan­yika huku na huko katika pambizo za anga.

WABEBAJI ARSHI

Na wanane juu ya hawa siku hiyo watabeba Arshi ya Mola wako.

Je, Mwenyezi Mungu ana kiti cha enzi anachokikalia, kama wafanyavyo masultani na watawala? Watu wadhahiri ya herufi wanasema: Ndio, Yeye ana masikio, macho, mguu na viungo vinginevyo.

Abu Amir Alqurashi amenasibishiwa kauli ya kuwa: Mwenyezi Mungu ni mfano wangu na wako katika umbo lake na sura yake.

Hili haliwezekani kabisa; lau angelikuwa na mwili angelihitajia kuwa na mahali, na muumba hahitajii chochote; isipokuwa chochote ndio kinamhi­tajia Yeye. Vile vile hili litahitajia awe na mahali pawe na zama, na hakuna uzamani ila Mwenyezi Mungu; na mengineyo waliyooyataja wana filosofia na wanateolojia.

Wengine wakasema: “Sisi hatujui Arshi ilivyo wala itakavyobebwa, na wala Mwenyezi Mungu hakutukalifisha kulijua hilo.” Kauli hii ni ya kujitoa shakani (Ihtiyat), kama wasemavyo mafaqihi wenye takua.

Tulipotaamali maana ya Aya hii tulifunukiwa kuwa makusudio ya Arshi (kiti cha enzi) ni utawala; kama tulivyotangulia kuashiria katika Juz. 8 (7:54) na makusudio ya wabebaji arshi ni viumbe vinavomilikiwa na Mwenyezi Mungu. Hilo linatambulika kutokana na yaliyosemwa kwenye

ahjul-balagha: “Na lau si mbingu kumkubali Mwenyezi Mungu kwa uungu na kumtii, asingelizijaalia ni mahali pa Arshi Yake.” Yaani lau sikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anazitumia mbingu vile atakavyo, zisingelikuwa ni milki Yake. Kwa hiyo kutumia atakavyo ni dalili ya umiliki; kama amabavyo umiliki unapelekea utumizi huu.

Kwa hiyo basi kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na watabeba Arshi ya Mola wako,” inashabihiana na jawabu la swali la anayeuliza: Kama mbingu na ardhi ikiondoka itamaanisha ufalme wa Mwenyezi Mungu umeondoka na hakuna kitu anachokitawala?

Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akajibu: Hapana! Kuna viumbe vingine visivyokuwa mbingu na ardhi ambavyo ni vinane, vikiwa kwenye amani na salama, anavitumia Mwenyezi Mungu (s.w.t) vile apendavyo baada ya kupomoka ardhi na mbingu.

Tunasema hivi, kama fikra tuliyoitoa kutoka kwenye neno: ‘Watabeba.’ Fikra hii ‧ kama uinavyo ‧ inawezekana, lakini hii na mfano wake haithibiti isipokuwa kwa nukuu wazi inayofahamisha kwa mkato. Lau ingelikuwa ni katika mlango wa halali na haramu, ingelikuwa dhana ya mwanafiqhi ina njia, kama itategemezwa kwenye dhahiri ya kitabu au sunna.

Siku hiyo mtahudhurishwa -haitafichika siri yoyote yenu.

Viumbe watahudhurishwa kwa Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, kwa ajili ya hisabu na kutekelezewa kila mtu malipo yake. Na Yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamjua zaidi aliyeongoka na aliyepotea njia yake.

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ ﴿١٩﴾

19. Basi ama atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu!

إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَاقٍ حِسَابِيَهْ ﴿٢٠﴾

20. Hakika nilijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu.

فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٢١﴾

21. Basi yeye atakuwa katika maisha ya kuridhia.

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ ﴿٢٢﴾

22. Katika Bustani ya juu.

قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ ﴿٢٣﴾

23. Matunda yake yako karibu.

كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ ﴿٢٤﴾

24. Kuleni na kunyweni kwa fura­ha kwa sababu ya mlivyotan­guliza katika siku zilizopita.

وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيَهْ ﴿٢٥﴾

25. Na ama atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto, Basi atasema: Laiti nisingelipewa kitabu changu!

وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ ﴿٢٦﴾

26. Wala nisingelijua nini hisabu yangu.

يَا لَيْتَهَا كَانَتِ الْقَاضِيَةَ ﴿٢٧﴾

27. Laiti (mauti) yangelimaliza.

مَا أَغْنَىٰ عَنِّي مَالِيَهْ ﴿٢٨﴾

28. Mali yangu hayakunifaa kitu.

هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيَهْ ﴿٢٩﴾

29. Madaraka yangu yamenipotea.

خُذُوهُ فَغُلُّوهُ ﴿٣٠﴾

30. Mshikeni na mumtie pingu!

ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ ﴿٣١﴾

31. Kisha mtupeni Motoni!

ثُمَّ فِي سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَاسْلُكُوهُ ﴿٣٢﴾

32. Tena mtieni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini!

إِنَّهُ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ الْعَظِيمِ ﴿٣٣﴾

33. Hakika yeye alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu.

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿٣٤﴾

34. Wala hahimizi kulisha masiki­ni.

فَلَيْسَ لَهُ الْيَوْمَ هَاهُنَا حَمِيمٌ ﴿٣٥﴾

35. Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu.

وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍ ﴿٣٦﴾

36. Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni.

لَّا يَأْكُلُهُ إِلَّا الْخَاطِئُونَ ﴿٣٧﴾

37. Chakula hicho hawakili ila wenye hatia.

LAITI YANGELIKUWA NI YAKUMALIZA

Aya 19 – 37

MAANA

Basi ama atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu! Hakika nilijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu.

Katika Aya iliyotangulia Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameeleza kuwa siku hiyo watu watahudhurisha. Hapa anabainisha tofauti baina ya watu wa kulia na wa kushoto. Makusudio ya kulia ni heri na kushoto ni shari, kwa kuangalia desturi ya waarabu na istilahi yao. wao wanaita kulia ni heri na kushoto ni shari. Walikuwa wakitabiri kwa kumrusha ndege, akiruka upande wa kuliawanona ni heri na akiruka upande wa kushoto wanaona ni shari[7] .

Kwa hiyo basi maana ni kuwa wema siku ya Kiyama watajitangaza wenyewe kwa fakhri na utukufu, na watamwambia watakayemuona au atakayewauliza hali zao: Ona tulivyo! Hebu soma daftari la matendo yetu! Sisi tulikuwa tukimwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na tulikuwa tukiwekeza kwa ajili ya siku hiyo.

Basi yeye atakuwa katika maisha ya kuridhia, yaani yenye kuridhiwa, yasiyokuwa na bughdha yoyote.Katika Bustani ya juu, matunda yake yako karibu. Waambiwe:

Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa sababu ya mlivyotanguliza katika siku zilizopita . Huu ni ufafanuzi baada ya ujumla; kama kwamba mtu ameuliza: Ni maisha gani hayo ya kuridhiwa? Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) anajibu kuwa ni Pepo ya daraja ya juu, matunda yake yako chinichini kuweza kuchumwa na kuliwa na Malaika watawaambia watu wa Peponi: Kuleni matunda ya Peponi na kunyweni katika kinywaji chake kwa raha, yakiwa ni malipo ya mema mliyoyatenda.

Mwenyezi Mungu ameanzia na tamko la mmoja, kwa kusema atakuwa katika maisha ya kuridhia, na kumalizia na tamko la wengi kwa kusema: Kuleni; kwa kuangalia maana yake ambayo ni wengi.

Na ama atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto.

Huyu ni yule aliyoekadhibisha hisabu na malipo, akapituka mipaka na kuwafanyia dhulma waja. Mwenyezi Mungu amemueleza kwa ibara ya kushoto kwa kuashiria kuwa matendo yake yatamrudia kwa shari; kama tulivyotangulia kueleza.

Basi atasema: Laiti nisingelipewa kitabu changu! Wala nisingelijua nini hisabu yangu. Laiti (mauti) yangelimaliza. Mali yangu hayakuni­faa kitu, madaraka yangu yamenipotea.

Atatamani lau asingelikuwa ameumbwa au asingelifufuliwa kutoka kaburi­ni kwake. Atatamani hivyo baada ya kuwa na uhakika wa adhabu isiy­oweza kukingwa kwa mali wala jaha. Wala si hoja kuwa anamiliki vyote hivyo; isipokuwa ni matamanio ya kukata tamaa.

Hakuna kitu chochote baada hayo isipokuwa kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:Mshikeni na mumtie pingu! Mfungeni mikono yake kwenye shingo yake.Kisha mtupeni Motoni! Kwenye Jahannam.

Tena mtieni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini!

Dhiraa sabini ni kinaya cha uchungu wa adhabu yake. Na ukali wake unapimwa kwa matendo yake na athari aliyoiacha katika jamii. La kushangaza ni kauli ya mfasiri mmoja aliyesema: “Wametofautiana kuhusu dhiraa hii. Ikasemekana ni dhiraa hasa inayojulikana.

Ikasemekana ni dhi­raa ya malaika wa adhabu. Pia imesemekana dhiraa moja ni kipimo cha kuanzia Makka hadi Kufa.” Sijui aliyeyasema hayo ni mtu wa Makka au Kufa?

Hakika yeye alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, Wala hahimizi kulisha masikini.

Huu ni ubainifu wa sababu inayowajibisha adhabu kali; kwamba ni kufuru, uasi na kutohimiza kutoa. Hapa kuna ishara ya kuwa matajiri wanatakikana watoe na wahimize kutoa.

Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu.

Hakuna wa karibu wa kunufaisha wala yeyote wa kuombea.

Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni, unaotoka kwenye mili yao.

Chakula hicho hawakili ila wenye hatia , waliokuwa duniani wakila vyakula vya wanyonge.

فَلَا أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ ﴿٣٨﴾

38. Basi naapa kwa mnavoviona.

وَمَا لَا تُبْصِرُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na msivyoviona.

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿٤٠﴾

40. Kwa hakika hii ni kauli ya Mjumbe mwenye hishima.

وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ قَلِيلًا مَّا تُؤْمِنُونَ ﴿٤١﴾

41. Wala si kauli ya mshairi. Ni machache mnayoyaamini.

وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٤٢﴾

42. Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayoyakumbu­ka.

تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٣﴾

43. Ni uteremsho utokao kwa Mola wa walimwengu wote.

وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ ﴿٤٤﴾

44. Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno,

لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ ﴿٤٥﴾

45. Bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia.

لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ ﴿٤٦﴾

46. Kisha kwa hakika tunge­limkata mshipa mkubwa wa moyo!

فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ ﴿٤٧﴾

47. Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeliweza kutuzuia naye.

وَإِنَّهُ لَتَذْكِرَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٨﴾

48. Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wenye takua.

وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ ﴿٤٩﴾

49. Na hakika bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanaokad­hibisha.

وَإِنَّهُ لَحَسْرَةٌ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٥٠﴾

50. Na hakika hii bila ya shaka itakuwa ni masikitiko kwa wanaokataa.

وَإِنَّهُ لَحَقُّ الْيَقِينِ ﴿٥١﴾

51. Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.

فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ ﴿٥٢﴾

52. Basi lisabihi jina la Mola wako aliye Mkuu.

MNAVYOVIONA NA MSIVYOVIONA

Aya 38 – 52

MAANA

Basi naapa

Wafasiri wengi wamesema kuwa herufi lU hapa ni ziyada kiirabu ya nahau. Bali wengine wamesema kuwa herufi lU hapa ni ya asili, na kwamba maana yake ni ‘Siapi,’ kwa vile jambo liko wazi lisilohotajia kiapo. Maelezo zaidi yametangulia kwenye Juz. 27 (56:75)

Kwa mnavyoviona, na msivyoviona.

Hii inachaanganya ulimwengu wa ghaibu na unaoonekana; yaliyokuwa na yatakayokuwa duniani na Akhera. Hiyo hasa ni kuapa kwa ilimu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), ambayo imekizunguka kila kitu; miongoni mwayo ni:

Kwa hakika hii Qur’anni kauli ya Mjumbe mwenye hishima. Wala si kauli ya mshairi. Ni machache mnayoyaamini. Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayoyakumbuka. Ni uteremsho utokao kwa Mola wa walimwengu wote.

Muhammad(s.a.w.w) ametamka Qur’an hilo hali shaka, lakini hakutamka kama mshairi au kuhani wala kwa sifa zozote za kibinadamu, isipokuwa aliitamka kama msemaji wa Mwenyezi Mungu. Tumezungumzia kwa ufufanuzi zaidi kuhusu ushairi na Mtume katika Juz. 19 (26:224).

Kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Ni machache manyoyaamini, ni machache mnaoyakumbuka.” Maana ni kuwa hawaamini wala wahawaidhiki isipokuwa wachache. Imesemkana makusudio yake ni kuwa hawakuamini wala kukumbuka, wachache wala wengi.

Hiyo ni kufuata desturi ya waarabu wanaosema: “Ni mara chache kufanya; kwa maana hafanyi kabisa. Tafsiri ya kwanza ndio iliyo karibu zaidi na uhalisia, kwa sababu ilivyo ni kuwa baadhi ya washirikina walimwamini Mtume(s.a.w.w) kabla ya kuhamia Madina. Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (1:88).

Unaweza kuuliza : Je, kuapa tu kunathibisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa Muhammad(s.a.w.w) , na kukana ushairi na ukuhani?

Jibu : Kiapo hiki kimekuja baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwataka wakadhibishaji walete mfano wa Qur’an, baada ya kushindwa na hoja. Kwa hiyo makusudio ya kuapa ni kusisitiza haki yenye kuthibiti na dalili, sio kuthibitisha haki kwa kiapo.

Zaidi ya hayo ni kuwa kujadiliana na mpinzani kuna mifumo mbalimbali na kunatofautiana kulingana na fikra na hali. Miongoni mwa mifumo hiyo ni kuleta dalili kwa hoja, kuleta maswali yanaolingana na itikadi na ufasaha wa mfumo. Vile vile kuapa huwa kunaleta hisia na athari.

Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno, bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia, kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo! Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeliwe­za kutuzuia naye.

Yaani lau Muhammad angelituzulia tungelimfanya hivyo. Maana ni kuwa Muhammad(s.a.w.w) ni mwenye kutakaswa na wanayomanasibisha nayo washirikina kuwa anamzulia Mwenyezi Mungu uwongo. Lau angelifanya hivyo, basi Mwenyezi Mungu angelimwadhibu kwa adhabu kali kabisa wala kusingelikuwa na mshirikina au mwinginewe kuweza kumwokoa na adhabu.

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu hakufanya hivyo, basi inamaanisha kuwa Muhammad(s.a.w.w) ni mkweli mwaminifu, na wazushi ndio waliom­nasibishia Muhammad(s.a.w.w) uzushi.

Unaweza kuuliza : Kwa nini Mwenyezi Mungu (s.w.t) hawaharakishii adhabu wanomkadhibisha Muhammad, kama atakavyomharakishia Muhammad(s.a.w.w) lau angekuwa muongo?

Jibu : Hakika utishio huu kutoka kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kwa yule anayedai utume kwa uwongo na uzushi, sio kwa anayekadhibisha utume wa mitume. Tofauti ni kubwa sana baina ya wawili hawa. Zaidi ya hayo utishio wa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake ni kumsafisha Mtume mtukufu na yale wanayomnasibishia ya uzushi, kama tulivyoashi­ria.

Kwa hakika hii Qur’anni mawaidha kwa wenye takua.

Bila shaka ni mwongozo kwa anayetaka kuongoka na akataka kwa ukweli na ikhlasi kujiepusha na ghadhabu za Mwenyezi Mungu na adhabu yake.

Na hakika bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanaokadhibisha.

Haya ni makemeo kwa anayemkadhibisha Mtume na Qur’an.

Na hakika hii Qur’anbila ya shaka itakuwa ni masikitiko kwa wanaokataa, kwa sababu inawalani na kuwafedhehsha na kwa sababu neno lake Mwenyezi Mungu liko juu na la makafiri liko chini. Na pia kwa vile ni hoja juu yao siku ya hisabu na malipo.

Na hakika hii Qur’an bila ya shaka ni haki ya yakini, isiyokuwa na shaka yoyote. Umetangulia mfano wake katika Juz. 27 (56:95).

Basi lisabihi jina la Mola wako aliye Mkuu.

Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad(s.a.w.w) , na makusudio ni kwa wote. Maana ni mtakaseni Mwenyezi Mungu na yale yasiyokuwa laiki yake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 27 (56:75).

MWISHO WA SURA YA SITINI NA TISA: SURAT AL-HAQQA


18

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sabini: Surat Al- Maa’rij. Ina Aya 44. Imeshuka Makka.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ ﴿١﴾

1. Mwenye kutaka alitaka adhabu itakayotokea.

لِّلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ ﴿٢﴾

Kwa makafiri, hapana awezaye kuizuia.

مِّنَ اللَّـهِ ذِي الْمَعَارِجِ ﴿٣﴾

3. Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye daraja.

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ ﴿٤﴾

4. Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka hamsini elfu!

فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا ﴿٥﴾

5. Basi subiri kwa subira njema.

إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا ﴿٦﴾

6. Hakika wao wanaiona iko mbali.

وَنَرَاهُ قَرِيبًا ﴿٧﴾

7. Na Sisi tunaiona iko karibu.

يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ ﴿٨﴾

8. Siku ambayo mbingu zitakuwa kama shaba iliyoyayuka.

وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ ﴿٩﴾

9. Na milima itakuwa kama sufi.

وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا ﴿١٠﴾

10. Wala jamaa hatamuuliza jamaa.

يُبَصَّرُونَهُمْ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ ﴿١١﴾

11. (Ingawa) watafanywa wao­nane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe.

وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ ﴿١٢﴾

12. Na mkewe, na nduguye.

وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْوِيهِ ﴿١٣﴾

13. Na ukoo wake uliokuwa ukimzunguka.

وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ ﴿١٤﴾

14. Na wote waliomo ardhini, kisha aokoke.

كَلَّا إِنَّهَا لَظَىٰ ﴿١٥﴾

15. Sivyo! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa.

نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ ﴿١٦﴾

16. Unaobabua ngozi ya kichwa!

تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٧﴾

17. Utamwita kila aliyoegeuza mgongo na akageuka.

وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰ ﴿١٨﴾

18. Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi.

KADIRI YAKE NI MIAKA HAMSINI ELFU

Aya 1- 18

MAANA

Mwenye kutaka alitaka adhabu itakayotokea.

Neno kutaka tumelitarjumu kutokana na neno la kiarabu sa-ala ambalo mara nyingi hutumiwa kwa maana ya kuuliza, lakini pia huwa na maana ya kutaka au kuomba. Huko nyuma tumewahi kueleza kuwa washirikina waliupinga mwito wa Mtume(s.a.w.w) kwa sababu zifuatazo:

1. Ulikua unapingana na chumo na faida zao.

2. Kwamba Mwenyezi Mungu hawezi kumtuma mtu kuwa Mtume, na kama hakuna budi basi atamtuma tajiri sio fukara, kama Muhammad bin Abdillah. Tatu, Muhammad anaamimi Mungu mmoja na wao wanaamini miungu mingi. Nne, kuwa Muhammad anawahofisha na adhabu na ufufuo.

Hili ndilo walilokuwa wakilipinga sana:

أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ﴿٤٧﴾

“Tutakapokufa na tukawa udongo na mifupa, ati ndio tutafufuliwa?” Juz. 27 (56:47).

Na kama Nabii akisisitiza kuuelezea ufufuo, wao husema:

مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٨﴾

“ Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?” Juz. 23 (36:48).

Mara nyingine wanaifanyia haraka adhabu kwa masikhara na kusema:

وَإِذْ قَالُوا اللَّـهُمَّ إِن كَانَ هَـٰذَا هُوَ الْحَقَّ مِنْ عِندِكَ فَأَمْطِرْ عَلَيْنَا حِجَارَةً مِّنَ السَّمَاءِ أَوِ ائْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٣٢﴾

“Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ni haki itokayo kwako, basi tupige mvua ya mawe kutoka mbinguni au tuletee adhabu iumizayo.” Juz. 10 (8:32).

Ndio maana wafasiri wengi wamesema kuhusu Aya hii tuliyo nayo kuwa ni ishara ya kutaka kuharakishiwa adhabu, na Mwenyezi Mungu (s.w.t) naye akawajibu kwa kusema:Kwa makafiri, hapana awezaye kuizuia . Yaani adhabu itashuka tu kwa wapinzani, hapana awezaye kuizuia, wawe wameitaka kwa haraka au kwa muda ujao.

SHETANI NA UTAFITI WA GHAIBU

Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye daraja.

Ni sifa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Makusudio yake ni utukufu. Mfano wake ni: “Ndiye Mwenye daraja za juu, Mwenye Arshi” Juz. 24 (40:15). Imesemekana kuwa maana ya neno maarij, tulilolitarjumu kwa daraja, lina maana ya mbingu.

Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka hamsini elfu!

Makusudio ya Roho hapa ni Jibril. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemhusisha kumtaja, japo yeye ni miongoni mwa malaika, kwa sababu ya cheo chake kikuu. Kwake ni kwenye yale yaliyo maalum mbele yake na kwa malaika. Miaka hamsini elfu ni kinaya cha urefu wa muda.

Ustadh Ahmad Amin Al-Iraqi, ameitaja Aya hii katika kitabu chake Attakamulu fil islam. Akaeleza kuwa malaika wanakwenda kwa kasi kuliko sauti.

Hivyo ni kwa kuwa upeo wa ulimwengu hauna kikomo. Inatosha kuwa ni dalili ya hakika hii, kwamba baadhi ya nyota mwanga wake umeanza kuja ardhini tangu mamilioni ya miaka iliyopita na bado haujafika; ambapo kasi ya mwanga ni kilomita 300000 kwa sekunde. Kwa hiyo basi malaika wasingeweza kukata masafa yaliyo mapana zaidi, kama wasingekua na kasi zaidi sana.

Katika kufasiri Aya 18 ya Sura iliyo kabla ya hii tuliyo nayo: “Na wanane juu ya hawa siku hiyo watabeba Arshi ya Mola wako,” tulisema kuwa maudhui haya na yanayofanana na haya hayathibiti ila kwa nukuu wazi inayofahamisha kwa mkato, bila ya taawili kwa hali yoyote ile.

Lakini ingelikuwa ni katika masuala ya halali na haramu, basi dhana ya faqih ingelikuwa na mwelekeo kama ingelitegemezwa kwenye dhahiri ya Kitabu au Sunna.

Baadhi ya masufi wanasema makusudio ya miaka hamsini elfu sio ile miaka tunayoijua, bali makusudio ni mizunguko. Sufi mwingine naye akasema kuwa siku za Mwenyezi Mungu ziko kama vile anavyotaka, akitaka anazifanya elfu na akitaka anazifanya maelfu na mamilioni.

Hiyo ni ghaibu ndani ya ughaibu. Sisi hatuna majukumu na ilimu ya Mwenyezi Mungu wala hatukalifishwi kuifanyia utafiti isipokuwa shetani.

Imam Ali(a.s) anasema:“Na ilimu ambayo shetani amekutwisha na wajibu wake kwako hauna athari katika Kitabu wala Sunna ya Nabii (s.a.w.w) na maimamu, basi iwakilishe kwa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa huo ni mwisho wa haki ya Mwenyezi Mungu kwako. Jua kuwa wale waliozama katika elimu ni wale ambao Mwenyezi Mungu amewatosheleza kwa kutoivamia milango iliyofungiwa ghaibu .

Kukiri jumla ya wasiyoyajua ni tafsiri ya ghaibu iliyofichikana. Mungu akawasifu kwa kukiri kushindwa kutambua yale wasiyoyajua. Amekuita kuacha kuzama katika wasiyokalifishwa, kwa kutafuta kumjua alivyo, kuwa ni kuimarika. Basi tosheka na hayo, wala usiupime utukufu wa Mwenyezi Mungu kwa kipi­mo cha akili yako usije ukawa katika walioangamia.”

Basi subiri kwa subira njema. Hakika wao wanaiona siku ya adhabu kuwaiko mbali, na Sisi tunaiona iko karibu.

Nabii(s.a.w.w) aliwahadharisha washirikina na siku ya adhabu, lakini wakaiharakisha kwa dharau, basi kuwa na subira ewe Muhammad na dha­rau yao hii subira isiyokuwa na malalamiko, wala usione kuwa nusra inachelewa. Siku ya adhabu itakuja tu haina shaka, hata kama wanaibadil­isha kuwa ngano, na kila linalokuja liko karibu.

Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akasifu siku hiyo waliyooahidiwa na kuidharau kuwa niSiku ambayo mbingu zitakuwa kama shaba iliyoyayuka .

Gimba la mbingu litayeyuka na kuwa kama matope ya mafuta. Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ ﴿٢﴾

“Na nyota zitakapopukutika.” (81:2).

Na milima itakuwa kama sufi.

Mwenye kuiangalia ataiona kama ni sufi iliyochanguliwa; mfano wake ni kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَبُسَّتِ الْجِبَالُ بَسًّا ﴿٥﴾

“Na milima itaposagwasagwa.” Juz 27 (56:5).

Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake, kwa sababu kila mtu ana shughuli yake itakayomshughulisha. Mwema siku hiyo ni yule atakayejiwekea akiba ya mambo mema.

Ingawa watafanywa waonane.

Yaani hakuna atakayemuuliza mwenzake siku ya Kiyama, hata kama ni marafiki na ndugu, ingawaje wanajuana, lakini watakimbiana kutokana na balaa na majanga ya siku hiyo.

Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwa­toa fidia wanawe, na mkewe, na nduguye, na ukoo wake uliokuwa ukimzunguka, na wote waliomo ardhini, kisha aokoke.

Neno ‘kisha’ linaashiria umbali wa kuokoka. Maana ni kuwa mateka wa Jahannam atatamani lau atafidiwa na watu wote, hata mke na watoto ambao jana alikuwa akiwafidia kwa nafsi yake na kujingiza kwenye hatari kwa ajili yao.

Huu ni ufasaha zaidi wa kuleta picha ya masikitiko ya mkosefu kutokana na yaliyoompita.

Sivyo Enyi wakosefu!Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, Unaobabua ngozi ya kichwa!

Unaondoa viungo kutoka sehemu yake, kisha unavirudisha tena na unaviondoa, bila ya kikomo:

لَا يُقْضَىٰ عَلَيْهِمْ فَيَمُوتُوا وَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُم مِّنْ عَذَابِهَا كَذَٰلِكَ نَجْزِي كُلَّ كَفُورٍ ﴿٣٦﴾

“Hawahukumiwi wakafa wala hawatapunguziwa adhabu yake. Hivyo ndivyo tunavyomlipa kila mwenye kuzidi ukafiri” Juz. 22 (35:36).

Utamwita kila aliyegeuza mgongo na akageuka duniani na kuacha mwito wa haki. Makusudio ya kuita Moto ni kuwa hakuna pa kuukimbia.

Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi.

Aya inatoa hadhari na kiaga kwa mwenye kukusanya mali na akawa na pupa nayo na wala asitoe kwa utiifu wa Mwenyezi Mungu.

Kuwachanganya mwenye kulimbikiza mali na mwenye kukadhibisha mwito wa haki, kunajulisha kuwa wote wako sawa mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya hisabu na malipo.

إِنَّ الْإِنسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا ﴿١٩﴾

19. Hakika mtu ameumbwa na papara.

إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا ﴿٢٠﴾

20. Inapomgusa shari hupapatika.

وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا ﴿٢١﴾

21. Na inapo mgusa kheri huizuil­ia.

إِلَّا الْمُصَلِّينَ ﴿٢٢﴾

22. Isipokuwa wanaoswali,

الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ ﴿٢٣﴾

23. Ambao wanadumisha Swala zao.

وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ ﴿٢٤﴾

24. Na ambao katika mali yao iko haki maalumu.

لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ ﴿٢٥﴾

25. Kwa mwenye kuomba na anayejizuia.

وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿٢٦﴾

26. Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo.

وَالَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ ﴿٢٧﴾

27. Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao.

إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ ﴿٢٨﴾

28. Hakika adhabu ya Mola waosi ya kusalimika nayo.

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿٢٩﴾

29. Na ambao wanazilinda tupu zao.

إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿٣٠﴾

30. Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume, kwani si wenye kulaumiwa.

فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿٣١﴾

31. Lakini anayetaka kinyume cha hayo basi hao ndio wapetukao mipaka.

وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ ﴿٣٢﴾

32. Na wale ambao wanachunga amana zao na ahadi zao.

وَالَّذِينَ هُم بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ ﴿٣٣﴾

33. Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao.

وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٣٤﴾

34. Na ambao wanazihifadhi Swala zao.

أُولَـٰئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُّكْرَمُونَ ﴿٣٥﴾

35. Hao ndio watakuwa Peponi wakiheshimiwa.

NI NANI HAO WANAOSWALI?

Aya 19 - 35

MAANA

Hakika mtu ameumbwa na papara. Inapomgusa shari hupapatika. Na inapo mgusa kheri huizuilia.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) hapa anaashiria kuwa mtu ni dhaifu kwa maumbile yake; kama alivyosema:

وَخُلِقَ الْإِنسَانُ ضَعِيفًا ﴿٢٨﴾

“Na mtu ameumbwa hali ya kuwa dhaifu.” Juz. 5 (4:28)

Na akasema tena:

اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن ضَعْفٍ ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ ضَعْفٍ ﴿٥٤﴾

“Mwenyezi Mungu ndiye ambaye amewaumba katika udhaifu.” Juz. 21 (30:54).

Udhifu huu huwa unajitokeza kwenye sababu zake, kama utajiri na ufukara. Akiwa anajitosheleza basi anakuwa na ubahili na mali yake akihofia ufukara, na akiwa fukara hukata tamaa.

Lakini mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu kikwelikweli na akamategemea Yeye kwa rehema zake, huwa anaushinda udhaifu huu, anakuwa na subira wakati wa shida, kwa subira ya kiungwana akingoja wepesi na faraja na akipata anakuwa mkarimu wa kutoa, akiamini kuwa yalioko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na yenye kubaki.

Kisha Mwenyezi Mungu anataja sifa za waumini kama ifuatavyo:­

1.Isipokuwa wanaoswali, ambao wanadumisha Swala zao.

Hii inafahamisha kuwa hawa hawamo katika kundi la wenye papara na kufazaika. Inafahamaisha wazi kuwa wenye kumswalia Mwenyezi Mungu kiukweli ni wale wanaomtegemea Yeye tu peke yake wala hawamnyenyekei yeyote asiyekuwa Yeye:

“Wewe tu tunakuabudu na wewe tu tunakuomba msaada.”

Ama wale wanasoma takbira na tahalili, kisha wakarukuu na kusujudi kwa ajili ya watu wa jaha na mali kwa tamaa ya yaliyomo mikononi mwao, hawa hawaswali, hata kama watadumu kila siku kwenye faradhi na suna.

2.Na ambao katika mali yao iko haki maalumu kwa mwenye kuomba na anayejizuia.

Maana ni kuwa wanatoa kwa njia ya utiifu na kheri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hawataki kulipwa wala shukrani. Umetangulia mfano wake katika Juz. 26 (51:19).

3.Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo.

Wanamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na wanafanya kwa mujibu wa imani hii; vinginevyo itakuwa imani ya nadharia tu haifai kitu.

4.Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao. Hakika adhabu ya Mola wao si ya kusalimika nayo.

Mumin anakuwa na matarajio na hofu, anaitazama Pepo kwa makini na Moto pia anautizama kwa makini. Anauhofia huu na wala hakati tamaa na ile. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Hawaaminishi hila ya Mwenyezi Mungu ila watu wenye hasara.” Juz. 9 (7:99). Akaendelea kusema:

إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٧﴾

“Hakika hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri.”

Juz. 13 (12:87).

Aliye na dhana nzuri zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni yule anayemhofia zaidi; kama alivyosema Imam Ali(a.s) ; yaani kumhofia Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kiasi cha kujua utukufu wake.

5.Na ambao wanazilinda tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume. Kwani si wenye kulaumiwa. Lakini anayetaka kinyume cha hayo basi hao ndio wapetukao mipaka.

Mumin anatakikana awe na subira na kuridhia mabinti wa Hawa aliopewa na Mwenyezi Mungu, na mumin mwanamke naye anatakiakana awe na subira na aridhie aliyoopewa na Mwenyezi Mungu katika watoto wa Adam. Mwenye kuvumilia na akashukuru basi malipo yake yako kwa Mwenyezi Mungu; vinginevyo mwisho wake ni kukosa Hurula’ini na Pepo. Aya hizi zimetangulia neno kwa neno katika Juz. 18 (23:5-7).

6.Na wale ambao wanachunga amana zao na ahadi zao.

Mumin akiahidi hutekeleza na akiaminiwa hafanyi hiyana, na asiyetekeleza ahadi hana dini wala dhamiri. Vile vile Aya hii imetangulia neno kwa neno katika Juz. 18 (23:8).

7.Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao.

Ushahidi ni amana ya Mwenyezi Mungu kwa shahidi, mwenye kuuficha au kuupindua, atakuwa amemfanyia hiyana Mwenyezi Mungu:

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَتَمَ شَهَادَةً عِندَهُ مِنَ اللَّـهِ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٤٠﴾

“Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule afichaye ushahidi alio nao uto­kao kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo mnayoyafanya.” Juz. 1 (2:140).

8.Na ambao wanazihifadhi Swala zao.

Unaweza kuuliza : Je, hii si ni kurudia Aya iliyotangulia - Ambao wanadumisha Swala zao?

Baahi ya afasiri wamejibu kuwa kudumumisha sio kuhifadhi. Kudumisha ni kuendelea kuswali kila siku na kila wakati wake, lakini kuzihifadhi ni kuzichunga kwa kuzileta kwa masharti yake.

Sisi hatuoni tofauti baina ya kudumisha na kuhifadhi, kwa sababu swala haiwezi kuwa bila ya kuchunga mafungu yake yote na masharti yake, likikosekana mojawapo basi swala imevunjika.

Lililokaribu na ufahamu ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amerudia Aya kwa kiasi cha kutilia mkazo swala na kuzindua kuwa hiyo ni nguzo ya Uislamu.

Hao ndio watakua Peponi wakiheshimiwa.

Hao ni watakaokuwa na sifa zilizotajwa, na kwamba wao watakuwa na daraja na heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.

فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ ﴿٣٦﴾

36. Wana nini wale waliokufuru wanakujia haraka?

عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ ﴿٣٧﴾

37. Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto!

أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ ﴿٣٨﴾

38. Hivi anatumai kila mmoja wao kuingizwa katika Pepo ya neema?

كَلَّا إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ ﴿٣٩﴾

39. Sivyo! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanachokijua.

فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ ﴿٤٠﴾

40. Basi naapa kwa Mola wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza

عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ ﴿٤١﴾

41. Kuwabadilisha kwa waliobora kuliko wao; na Sisi hatushindwi.

فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ ﴿٤٢﴾

42. Basi waache wapige porojo wakicheza, Mpaka wakutwe na hiyo siku yao wanayoahidiwa.

يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ ﴿٤٣﴾

43. Siku watakapotoka mak­aburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia kwenye mzimu.

خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ ﴿٤٤﴾

44. Macho yao yatainama. uny­onge utawafunika. Hiyo ndiyo siku waliyokuwa wakiahidi­wa

WAACHE WAPIGE POROJO

Aya 36 – 44

MAANA

Wana nini wale waliokufuru wanakujia haraka? Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto!

Wana nini hawa ambao wamekadhibisha risala yako ewe Muhammad(s.a.w.w) na kukadhibisha ufufuo, mbona wanakuja haraka kwenye vikao vyako makundi kwa makundi na kuchukua nafasi zao upande wa kulia na kushoto, wakisikiliza Aya za Mwenyezi Mungu kisha wanaambiana huku wakidharau ufufuo na hisabu na kusema, ikiwa haya ni kweli basi sisi ndio bora wa watu na ndio tunaofaa kuingia Peponi, kwa sababu tuna mali nyin­gi na ndio watukufu zaidi kuliko Muhammad.

Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawajibu kwa kusema:

Hivi anatumai kila mmoja wao kuingizwa katika Pepo ya neema?

Hapana! Hamna chenu, enyi wakadhibishaji, katika Pepo ya Mwenyezi Mungu wala thawabu zake. Nyinyi hamna chochote kutoka kwake isipokuwa mwisho mbaya. Vipi mnatumai Pepo na hali nyinyi mnaikadhibisha na mnam­fanyia dharau Mtume aliyoewapa mwito wa kuitumikia. Hivi mnadhani kwamba mali na masanamu yatawakurubisha kwa Mwenyezi Mungu?

Sivyo! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanachokijua.

Wanajua hakika kuwa Mwenyezi Mungu amewaumba kutokana na maji hafifu: “Basi naatazame mtu ni kwa kitu gani ameumbwa. Ameumbwa kwa maji yanayotoka kwa kuruka.” (86:5-6).

Ikiwa asili ya mtu ni moja, basi iweje wengine wawe watukufu kuliko wengine mbele ya Mwenyezi Mungu? Au awe bora kuliko mwenzake? Hapana! Hakuna kuzuidiana kati ya mweupe na mweusi, wala tajiri na masikini, isipokuwa kwa takua na matendo mema.

Kauli yake Mwenyezi Mungu ‘kutokana na wanachokijua’ ina madhumu­ni ya kuwaonyesha wakadhibishaji wa ufufuo, na kuwarudi kwa kuali yao, kwamba hakuna nguvu yoyote inayoweza kurudisha uhai kwa anayegeuka mifupa na udongo. Njia ya majibu ni ikiwa ameweza kuwaumba watu kutokana na maji hafifu basi hawezi kushindwa kuipa uhai mifupa iliyochakafuka.

Basi naapa kwa Mola wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza kuwabadilisha kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi.

Makusudio ya mashariki zote na magharibi ni mashariki na magharibi za sayari, au masahriki za jua na magharibi zake, ambalo linajitokeza machoni na kujificha kutokana na mzunguko wa ardhi mbele yake. Makusudio ya anayeweza kuwabadilisha ni wale waliokufuru.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) imetukuka hikima yake anaapa kuwa Yeye anaweza kuwaangamiza wakadhibishaji na kuwaleta wengine mahala pao wasiomuasi Mwenyezi Mungu kwa wanayoamriwa na kutenda wanayoamriwa, na kama akitaka Mwenyezi Mungu hilo hapana wa kurudisha matakwa yake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 26 (47:38).

Basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao wanayoahidiwa.

Hii ni tahadhari na kiaga. Maana yake ni, achana nao ewe Muhammad, wadharau wafanye sthizai kadiri wawezavyo, lakini mwisho wao ni moto na ni makazi mabaya.

Aya hii imetangulia neno kwa neno katika Juz. 25 (43:83).

Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia kwenye mzimu.

Watatoka haraka makaburini mwao kwenda kwenye mahojiano ya hisabu, kama walivyokuwa wakifanya jana kutoka haraka majumbani mwao kwenda kwenye masanamu na mizimu, lakini mambo ni tofauti baina ya siku mbili hizo. Duniani walikuwa wakiharakisha kwenda kwenye miungu yao wakiwa na amani na utulivu, lakini siku ya Kiyama wataenda haraka kwenda kwa Mwenyezi Mungu huku ardhi ikitetema chini ya nyayo zaoMacho yao yatainama, unyonge utawafunika.

Unyonge na utwevu utawagubika; kama zinavyogubikwa nyuso zao na kipande cha usiku wenye giza.Hiyo ndiyo Siku waliyokuwa wakiahidiwa ambayo walikuwa wakiifanyia dharau na kuiharakishia.

MWISHO WA SURA YA SABINI: SURAT AL- MAA’RIJ


19

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sabini Na Mmoja: Surat Nuh. Imeshuka Makka Ina Aya 28.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

إِنَّا أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ أَنْ أَنذِرْ قَوْمَكَ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١﴾

1. Hakika Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.

قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٢﴾

2. Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhahiri kwenu,

أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ ﴿٣﴾

3. Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche, na munitii.

يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى إِنَّ أَجَلَ اللَّـهِ إِذَا جَاءَ لَا يُؤَخَّرُ لَوْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤﴾

4. Atawaghufiria miongoni mwa madhambi yenu, na atawaakhirisha mpaka muda uliowekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapofika haucheleweshwi. Laiti mnge­jua!

قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوْتُ قَوْمِي لَيْلًا وَنَهَارًا ﴿٥﴾

5. Akasema: Ee Mola wangu! Hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana.

فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَائِي إِلَّا فِرَارًا ﴿٦﴾

6. Lakini mlingano wangu haukuwazidisha ila kukimbia.

وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوا أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِمْ وَاسْتَغْشَوْا ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا وَاسْتَكْبَرُوا اسْتِكْبَارًا ﴿٧﴾

7. Na hakika mimi kila nilipowai­ta ili upate kuwaghufiria, wali­jiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakafanya kiburi kingi!

ثُمَّ إِنِّي دَعَوْتُهُمْ جِهَارًا ﴿٨﴾

8. Tena niliwalingania kwa uwazi,

ثُمَّ إِنِّي أَعْلَنتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًا ﴿٩﴾

9. Kisha nikawatangazia, tena nikasema nao kwa siri.

فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا ﴿١٠﴾

10. Nikasema: Ombeni maghufira kwa Mola wenu; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe.

يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا ﴿١١﴾

11. Atawaletea mvua nyingi.

وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا ﴿١٢﴾

Na atawapa mali na wana, na atawapa mabustani na atawafanyia mito.

NILIWALINGANIA WATU WANGU

Aya 1 - 12

MAANA

Hakika Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.

Sheikh Abdul-qadir Al-Maghrib, akifasiri Aya hizi alinukuu vitabu vya mwanzo mwanzo kwamba Historia ya kuabudu masanamu inaanzia zama za Anush bin Shith bin Adam, na kwamba wakati wa Nuh shirki ilifikia ukomo, ndio akachaguliwa na Mwenyezi Mungu kupambana na shiriki hii na kuwaonya washirikina na maangamizi kama watanga’ang’ania upotevu.

Jina halisi la Nuh ni Raha, na baina ya Nuh na babu yake mkubwa Adam, kuna miaka 1056. Ilipotokea tufani umri wake ulikuwa ni miaka 600, na aliishi miaka 350 baada ya hapo. alimuwahi mjukuu wake Ibrahim na akaishi naye zaidi ya nusu karne. Baada ya Nuh kuokoka na tufani alilima na kupanda kwenye ardhi.

Huu ni muhtasari wa aliyoyanukuu Al-Maghribi kutoka kwenye vitabu hivyo, Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi.

Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhahiri kwenu. Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mum­che, na munitii.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimtuma Nuhu kwa watu kwa mambo matatu: Kwanza, Waache kuabudu masanamu na kumwabudu Mungu mmoja. Pili, wafanye kheri na wajiepushe na shari. Tatu, wamtii katika yale aliy­owaamrisha na kuwakataza. Akawadhaminia mambo mawili kwa Mwenyezi Mungu, kama wataitikia:

La kwanza:Atawaghufiria miongoni mwa madhambi yenu, mliyoy­afanya kabla ya imani, kwa sababu imani inafuta yaliyo kabla yake, lakini yale madhambi mtakayoyafanya baada ya imani mtakua na majukumu nayo. Haya yanashiriwa na neno ‘miongoni mwa dhambi yenu.’

La pili:Na atawaakhirisha mpaka muda uliowekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapofika haucheleweshwi.

Mkimwamini Mwenyezi Mungu peke yake atawaondolea adhabu ya kuangamizwa na tufani nk, atawapa muda wa kumaliza umri wa kawaida na mwenye dhambi atampa muda hadi siku ya Kiyama; vinginevyo atawa­harakishia adhabu ya kuangamia duniani.

Laiti mngejua , kuwa Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na wanay­oyafanya madhalimu.Akasema: Ee Mola wangu! Hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana, Lakini mlingano wangu haukuwazidisha ila kukimbia.

Maana ya usiku na mchana ni daima. Nuhu aliwaita kwenye haki na akawasisitiza, mpaka: “Wakasema: Ewe Nuh! Umejadiliana nasi na ume­zidishi kutujadili.” Juz. 12 (11:32), lakini yeye aliendelea na mwito wake na wao wakaendelea na inadi yao.

Na hakika mimi kila nilipowaita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakaka­mia, na wakafanya kiburi kingi!

Walijiziba masikio kwa vidole ili wasisikie mwito wa haki, na walijifuni­ka nguo ili wasiuone uso wa mwenye kulingania. Hii inaweza kuwa ni hakika hasa, na pia inaweza kuwa ni kwa majazi ya inadi yao. Vyovyote iwavyo, maana ni moja tu, nayo ni kuikataa haki kwa kiburi. Nuh wal­imuona ana daraja ya chini kuliko wao, kwa hiyo wakaona vipi wanaweza kuwa wafuasi wake? Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwasimulia wao:

وَمَا نَرَاكَ اتَّبَعَكَ إِلَّا الَّذِينَ هُمْ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ الرَّأْيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ ﴿٢٧﴾

“Wala hatukuoni wamekufuata ila wale wanaonekana dhahiri kwetu kuwa ni watu duni, wala hatuwaoni kuwa mnayo ziada juu yetu.” Juz. 12 (11:27).

Tena niliwalingania kwa uwazi, Kisha nikawatangazia, tena nikasema nao kwa siri.

Kundi la wafasiri wamesema kauli ya Nuh ya kwanza: Nimewalingia watu wangu usiku na mchana, na kauli ya pili: Tena niliwalingania kwa uwazi na kauli ya tatu: kisha nikawatangazia na nikasema nao kwa siri, zinajul­isha kuwa mwito wake ulikuwa na daraja tatu: aliuanza kwa siri, kisha aka­ufanya wazi, tena mara ya tatu akautangaza na kuufanya siri pamoja.

Kauli hii haiko mbali na dhahiri ya Aya, lakini inawezekana pia kuwa makusudio ya maunganishi haya na kukaririka huku ni kuwa yeye aliwalingania kwa kila mfumo bila ya kuchoka, lakini pia haikufaa kitu.

Nikasema: Ombeni maghufira kwa Mola wenu; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe. Atawaletea mvua nyingi. Na atawapa mali na wana, na atawapa mabustani na atawafanyia mito.

Ikiwa watamwamini Mwenyezi Mungu peke yake na wakamfanyia ikhlasi kwa kauli na vitendo, basi Nuhu atawadhaminia kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) awasamehe maovu yao yaliyoopita na awatoshelezee katika fadhi­la zake kwa mali na watoto; mbingu zimimine heri zake na ardhi nayo itoe mazao yake na wawe na siha, amani, raha pamoja na kuzidi kizazi.

IMANI NA RAHA

Aya hizi zimeifunga raha na amani kuwa lazima ziwe pamoja na imani na takua, lakini inavyoonekana ni kinyume na hivyo. hai ni Marekani (U.S.A.). Inajulikana kuwa hiyo ndio dola iliyo na ubabe kuliko yoyote duniani, ndiyo yenye ufisadi na uadui zaidi; mpaka ikajiwekea msingi kuwa asiyekuwa mtumwa wake basi huyo ni adui yake. Sote tunajua siasa yao hiyo jinsi ilivyoleta majanga - hakuna damu inayomwagika au ufisadi unajitokeza mashariki mwa dunia na magharibi ila Marekani ina mkono wake, kwa namna moja au nyingine. Hakuna mhaini yeyote wa nchi yake ila wanamtukuza.

Pamoja na haya yote hiyo ndio dola tajiri na yenye nguvu zaidi ulimwen­guni. Ushahidi wa hilo ni kuwa pato lake ni asilimia 43 ya pato lote la ulimwengu na hali wakazi wake ni asilimia 6 tu ya wakazi wote waulimwengu[8] .

Sasa kuna wajihi wa kuunganisha haya na dhahiri ya Aya inayoifunga raha na imani?

Jibu :kwanza , Aya hizi zilihusiana na watu wa Nuh, na hakuna dalili ya kuwa zinaenea, ili zihusaiane na wengine. Kuongezea kuwa Mwenyezi Mungu ana muamala maalum na umma unaoonywa na mitume wake moja kwa moja.

Pili , utajiri wa U.S.A. unatokana na shetani sio na Mwenyezi Mungu, kwa sababu zaidi sana umetokana na uporaji na unyang’anyi.

Tatu , Aya hizi zimeunganisha baina ya imani na raha ya dunia na Akhera kwa pamoja. Sio imani na raha ya dunia peke yake: “Wala wasidhanie kabisa wale waliokufuru kwamba muda tunaowapa, ni heri kwa nafsi zao. Hakika tunawapa muda na wanazidi tu katika (kufanya) dhambi na wana wao adhabu idhalilishayo.” Juz. 4 (3:178).

Nne , umejuaje kuwa Amerika na dola nyingine dhalimu ziko kwenye amani? Ni nani mwenye akili anayejiaminisha na majanga? Je, himaya ya Roma ilidumu? Au ya uingereza na himaya nyinginezo zilidumu mpaka udumu ufidhuli wa USA?

Hizi hapa dalili za kuanguka zinaanza kujitokeza, kuanzia mawimbi ya ukombozi ulimwenguni kote hadi kwenye mapinduzi ya watu weusi wap­atao milioni thalathini ndani ya USA. Na kuanzia utawala wa ujasusi wakuua na kuanzisha vita hadi kwenye bangi na madawa ya kulevya, na kuanzia ugomvi na uadui pamoja na watu wa mabara yote matano hadi kwa raisi anayewalinda wezi na wamwagaji damu na mengine yasiyokuwa na kikomo.

Ni muhali kudumu amani na raha kwa mfumo huu wa kushangaza.

Ajabu ni sadfa iliyotokea wakati nikandika maneno haya nikasoma gazeti la Aljumhuriya la Misr la tarehe 10 ‧ 7- 1970, likinukuu magazeti ya New York, kwamba mashoga wapatao elfu tano wazee kwa vijana wamean­damana kwenye barabara za New York, wakibeba mabango wakitaka serikali ihalalishe ulawiti, kwa kuiga wanawake waaliohalalishiwa kujiuza miili yao (umalaya).

Kwenye gazeti la News wee^ la tarehe 12 -7-1970, kuna maelezo kuwa kasisi Barry ambaye ni mashuhuri kwa ulawiti alitoa mwito wa kueneza ulawiti na usagaji, kwa sababu mambo hayo mawili ni katika upendo wa Mungu. Mwito wake huu umeenea na kuwa na wafuasi wengi katika pembe zote za USA.

Hakuna mwenye shaka kwamba katika mashoga na mabasha hawa wata­tokea viongozi watakaotawala siasa za usalama na vita, mambo ya elimu na kazi katika jamii ya Marekani. Hapo ndio itakuwa USA ni duni kuliko nyumba ya buibui.

مَّا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّـهِ وَقَارًا ﴿١٣﴾

13. Mna nini hamumwekei heshi­ma Mwenyezi Mungu?

وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا ﴿١٤﴾

14. Na hali Yeye amewaumba katika hali mbalimbali?

أَلَمْ تَرَوْا كَيْفَ خَلَقَ اللَّـهُ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا ﴿١٥﴾

15. Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyoziumba mbingu saba kwa matabaka?

وَجَعَلَ الْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَجَعَلَ الشَّمْسَ سِرَاجًا ﴿١٦﴾

16. Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?

وَاللَّـهُ أَنبَتَكُم مِّنَ الْأَرْضِ نَبَاتًا ﴿١٧﴾

17. Na Mwenyezi Mungu ame­waotesha katika ardhi kama mimea.

ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا ﴿١٨﴾

18. Kisha atawarudisha humo na atawatoa tena.

وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ بِسَاطًا ﴿١٩﴾

19. Na Mwenyezi Mungu ame­wafanyia ardhi kuwa busati.

لِّتَسْلُكُوا مِنْهَا سُبُلًا فِجَاجًا ﴿٢٠﴾

Ili mtembee humo katika njia zilizo pana.

AMEWAUMBA KATIKA HALI MBALIMBALI

Aya 13 - 20

MAANA

Mna nini hamumwekei heshima Mwenyezi Mungu? Na hali Yeye ame waumba katika hali mbalimbali?

Nuhu anawakana watu wake huku akiwashangaa, vipi hawamwogopi Mwenyezi Mungu pamoja na utukufu wake, na hali wanajua kwamba Yeye amewaumba kwa mchanga, kisha kwa tone la manii, kisha kwa pande la damu. Anaendela hivi hadi kuwa mkongwe.

Vile vile anawaelekeza kuuangalia uwezo wa Mwenyezi Mungu katika kuumba mbingu na ardhi na sayari, akasema:

Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyoziumba mbingu saba kwa matabaka?

Chunguzeni na mzingatie umbile la mbingu na nidhamu yake inayojulisha kupatikana mtengenezaji mwenye hikima. Umetangulia mfano wake kati­ka Juzuu hii tuliyo nayo kwenye sura (67:3). Pia tumeifafanua kidogo kati­ka Juz. 28 (66:12).

Kauli ya Nuh inafahamisha kuwa watu wake walikuwa pia wakiamini kuwa mbingu ni saba na kwamba itikadi hii ilianzia zamani za kale.

Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?

Ndani yake ni ndani ya mkusanyiko wake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amelipa Jua sifa ya taa na mwezi kuwa ni nuru, kwa sababu taa ndio chim­buko la nuru na Jua nalo ni chimbuko la mwezi na mwanga wake unaenea na una manufaa zaidi kuliko wa mwezi. Umetangulia mfano wake katika Juz. 11(10:5).

Na Mwenyezi Mungu amewaotesha katika ardhi kama mimea. Kisha atawarudisha humo na atawatoa tena.

Huyu ndiye mwanadamu. Ameumbwa kutokana na ardhi, kisha arudishwe humo, tena atolewe humo. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:55).

Na Mwenyezi Mungu amewafanyia ardhi kuwa busati ili mtembee humo katika njia zilizo pana.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amefanya njia pana katika ardhi ili watu wayaendee makusudio yao. Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 (21:32).

قَالَ نُوحٌ رَّبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِي وَاتَّبَعُوا مَن لَّمْ يَزِدْهُ مَالُهُ وَوَلَدُهُ إِلَّا خَسَارًا ﴿٢١﴾

21. Nuh akasema: Mola wangu! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila hasara.

وَمَكَرُوا مَكْرًا كُبَّارًا ﴿٢٢﴾

22. Na wakapanga vitimbi vikub­wa.

وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا ﴿٢٣﴾

23. Na wakasema: Msiwaache miungu yenu; msimwache Wadda wala Suwaa wala Yaghutha, wala Yau’qa, wala Nasra.

وَقَدْ أَضَلُّوا كَثِيرًا وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا ضَلَالًا ﴿٢٤﴾

24. Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie waliodhulumu ila kupotea.

مِّمَّا خَطِيئَاتِهِمْ أُغْرِقُوا فَأُدْخِلُوا نَارًا فَلَمْ يَجِدُوا لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ أَنصَارًا ﴿٢٥﴾

25. Basi kwa ajili ya makosa yao kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.

وَقَالَ نُوحٌ رَّبِّ لَا تَذَرْ عَلَى الْأَرْضِ مِنَ الْكَافِرِينَ دَيَّارًا ﴿٢٦﴾

26. Na Nuh akasema: Mola wangu! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri!

إِنَّكَ إِن تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوا إِلَّا فَاجِرًا كَفَّارًا ﴿٢٧﴾

27. Hakika ukiwaacha wata­wapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.

رَّبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًا ﴿٢٨﴾

28. Mola wangu! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliyeingia nyumbani mwangu kuwa ni mumin, na waumini wanaume, na waumini wanawake; na wala usi­wazidishie waliodhulumu

ila kuangamia.

WALA MSIMWACHE WADDA WALA SUWAA

Aya 21 - 28

MAANA

Nuhu akasema: Mola wangu! Hakika hao wameniasi, na wamemfua­ta yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila hasara.

Hii ni ripoti au mashtaka kutoka kwa Nuh kwenda kwa Mola wake, akimwambia Mola wangu na Bwana wangu! Umenituma kuwaongoza waja wako washirikina, nimetekeleza ujumbe kwa njia yake, lakini wao wamenipinga, wakawaitikia viongozi walioingiwa na kiburi kutokana na mali na watoto. Kila wanavyozidi mali na watoto, basi wanazidi kufuru, inadi na kuwa na nguvu ya kupiga vita haki na watu wake, kwa kupupia jaha na chumo lao.

Na wakapanga vitimbi vikubwa.

Yaani hao viongozi waliopituka mipaka. Makusudio ya vitimbi vyao, ni mifumo waliyookuwa wakiitumia kuwazuia wanyonge kuwa na imani; miongoni mwayo ni kusema kwao:Na wakasema: Msiwaache miungu yenu; yaani msiache kuabudu masanamu kwa ibada ya Mungu mmoja.

Walikuwa na masanamu mengi; yaliyokuwa muhimu na shani kwao ni matano, ndio maana wakayahusisha kuyataja na wakasema:msimwache Wadda wala Suwaa wala Yaghutha, wala Yau’qa, wala Nasra.

Nuh alikuwa akitilia mkazo sana kukataza ibada ya haya masanamu matano, kwa sababu ndiyo yaliyokuwa makubwa.

Jamaa katika wafasiri wamesema kuwa haya matano yaliabudiwa wakati wa jahilia hadi wakati wa Mtume Mtukufu(s.a.w.w) , na Wadda alikuwa wa kabila la Kalb, Suwaa ni wa Hudhayl, Yaghutha ni wa Ghatwif, Yau’qa ni wa Hamadan na Nasra ni wa Himyar. Pia kuna masanamu mengine ya watu wengine; kama vile Lata, Uzza, Hubal na Manat.

Na hao walikwishawapoteza wengi, wala usiwazidishie waliodhulumu ila kupotea.

Viongozi waliopituka mipaka wamewapoteza. Makusudio ya kupotea ni kuangamia; mfano kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ ﴿٤٧﴾

“Hakika wakosefu wamo katika upotofu na mioto.” Juz. 27 (54:47).

Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.

Aya hii ni maneno yaliyooingilia kati maneno ya Nuh na dua yake, lakini yameyakamilisha. Maana yake ni kuwa watu wa Nuh waling’ang’ania ukafiri na upotevu, ndio Mwenyezi Mungu akawapatiliza kwa tufani, na adhabu ya Akhera ni kali na yenye kubaki, wala hakuna yoyote atakayeokoka nayo.

Na Nuh akasema: Mola wangu! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri!

Yaani usimbakishe yeyote. Nuh hakuomba dua hii ila baada ya kupata wahyi usemao:

وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُ لَن يُؤْمِنَ مِن قَوْمِكَ إِلَّا مَن قَدْ آمَنَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٣٦﴾

“Akaletewa wahyi Nuh kuwa hataamini katika watu wako isipokuwa yule aliyoekwishaamini.

Basi usisikitike kwa waliyokuwa wakiyatenda.” Juz. 12 (11:36).

Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.

Hii inafahamisha kwamba ukafiri na uovu umepituka mipaka kwenye jamii ya watu wa Nuh, kiasi ambacho kila anayeinukia anakuwa ni kafiri muovu. Inajulikana kwamba nafsi ya mtoto ni kama kioo, inaakisi kila linalomzunguka.

Kuna riwaya inayosema kuwa mtu alikuwa anamchukua mtoto wake hadi kwa Nuh na kumwambia jihadhari na huyu - yaani Nuh - kwa sababu ni muongo, na baba yangu aliniusia kama ninavyokuusia wewe. Basi mkubwa anakufa akiwa na hilo na mtoto naye anainukia nalo.

Mola wangu! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliyoeingia nyumbani mwangu kuwa ni mumin, na waumini wanaume, na wau­mini wanawake.

Baada ya kuwaduilia makafiri, alimuomba Mwenyezi Mungu maghufira yeye na wazazi wake wawili, na kila aliyeamani katika watu wake na wato­to wake aliowakusudia katika kauli yake: ‘aliyeingia nyumbani mwangu.’ Vile vile alimuombea kila mumin mwanamume na mwanamke kuanzia Adam hadi siku ya ufufuo Na wala usiwazidishie waliodhulumu ila kuangamia, kwa yule aliyekataa maangamizi na Moto.

Katika Kamusi ya Kitabu kitakatifu imeelezwa: “Athari zilizofukuliwa zimedhihirisha kuwa tukio la gharika lilikuwa tukio halisi, na kwamba kisa hiki kilianza kuandikwa baina ya miaka 1590 ‧ 1595 BC (kabla ya kuzalia Nabii Isa). Tazama Juz. 12 (11:45-49) kifungu cha “Tufani imethibiti kwa umma nyinginezo.”

Hapa kuna swali linajitokeza: Je, tufani iliyofahamishwa na athari zilizofukuliwa na ikaelezwa kwenye vitabu vya kale ni ya Nuh au ni nyingine?

Jibu : vyovyote iwavyo, ni kuwa Tufani ya Nuh haiwezi kuzuia tufani nyingine kutokea. Kila wakati kunatokea tufani moja au zaidi katika sehemu yoyote katika ardhi. Inawezekena kuwa Tufani ya Nuh ilienea, au ilihusu sehemu fulani katika ardhi. Hakuna nukuu wazi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu inayofahamisha kuwa ilikuwa hiyo tu.

MWISHO WA SURA YA SABINI NA MMOJA: SURAT NUH


20

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sabini Na Mbili: Surat Al-Jinn. Imeshuka Makka Ina Aya 28.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا ﴿١﴾

1. Sema: Nimepewa wahyi ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur’an ya ajabu!

يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا ﴿٢﴾

2. Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu.

وَأَنَّهُ تَعَالَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا ﴿٣﴾

3. Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu umetukuka; hakuji­fanyia mke wala mwana.

وَأَنَّهُ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى اللَّـهِ شَطَطًا ﴿٤﴾

4. Na kwa hakika mpumbavu miongoni mwetu alikuwa akise­ma juu ya Mwenyezi Mungu ya kupituka mipaka.

وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن تَقُولَ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا ﴿٥﴾

5. Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawatasema uwongo juu ya Mwenyezi Mungu.

وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا ﴿٦﴾

6. Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume katika majini; kwa hivyo wakawazidisha mzigo.

وَأَنَّهُمْ ظَنُّوا كَمَا ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَبْعَثَ اللَّـهُ أَحَدًا ﴿٧﴾

7. Na hakika wao walidhani, kama mlivyodhani nyinyi, kuwa Mwenyezi Mungu hatam­tuma Mtume.

KUNDI MOJA LA MAJINI

Aya 1 – 7

MAANA

Sema: Nimepewa wahyi ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur’an ya ajabu!

Jinni ni uhakika na uhalisia, hatii shaka juu hilo mumin, kwa sababu Aya za Qur’an yenye hikima, zimethibitisha hilo, kwa njia isiyokubali shaka wala taawili (tafsiri nyingine). Tutazifanyia vipi taawili kauli zake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu na masanamu na sinia kubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yasiy­oondoka mahali pake.” Juz. 22 (34:13). “Akasema Afriti katika majini: mimi nitakuletea” Juz. 19 (27:39). “Sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa.” Juz. 26 (46:30). Pia Aya zilizo katika sura hii tuliyo nayo.

Je, tuziletee taawili ya virusi vya magonjwa, au redio na vinginevyo katika vifaa vya elektroni?

Ukisema: Sayansi haikuthibitisha kuweko majini, nasi tutasema: Je, katika sayansi kuna linalopinga kuweko majini? Je, sayansi imemaliza kugundua vilivyomo ulimwenguni vyote, vya dhahiri na batini? Ni mtaalamu gani wa zamani au wa sasa anayejijua uhakika wake na akili yake? Au hata kuujua mwili wake wa hisia na wa dhahiri, ikiwemo mishipa na nywele?

Asiyejijua yeye mwenyewe hawezi kumjua mwenginewe; hasa yaliyo katika ulimwengu wa ghaibu.

Wahyi umethibitisha kuweko majini na Malaika, kwa hiyo ni wajibu kuamini kuweko; atakayekanusha, basi ni lazima athibitishe ukanusho wake kwa akili au wahyi; sawa na ilivyothibitishwa.

Baada ya hayo, ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimjulisha Nabii wake mtukufu kuwa kundi la majini walimsikiliza akisoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, wakakifahamu na kuzingatia maana yake; wakapigwa na mshangao kutokana na mpangilio na maana yake makuu; wakaambiana: jamani mnaionaje hii Qur’an? Je, mmeshawahi kusikia kitu mfano wake? Hakika ni muujiza na kwambaInaongoza kwenye uwongofu , inaelekeza, kutoa mwongozo, kuaamrisha na kupendekeza kwenye kila heri. Pia inafahamisha, kukataza na kuonya kila shari.

Kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu.

kwa sababu Yeye ni Muweza wa kila kitu. Na mwenye uweza wa kila kitu basi hahitajii washirika, na kama atataka msaada maana yake ni kuwa anashindwa, na mwenye kushindwa hawezi kuwa Mungu.

Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu umetukuka; hakujifanyia mke wala mwana.

Ametakata Mola wetu na kujifanyia watoto na ametakata kuwagusa wanawake. Vipi awe hivyo na hali Yeye ni mwenye kujitosha mwenye kusifika.

Na kwa hakika mpumbavu miongoni mwetu alikuwa akisema juu ya Mwenyezi Mungu ya kupituka mipaka.

Makusudio ya mpumbavu hapa ni mjinga asiyejua. Hapa kuna ishara kwamba katika majini kuna kikundi kikiamini utatu: Mungu, mwana na mkewe. Hakuna mwenye shaka kwamba hii ni kupituka mipaka na ni upumbavu.

Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawatasema uwongo juu ya Mwenyezi Mungu.

Viongozi wa dini katika majini walikuwa wakiwaambia wafuasi wao ubatilifu na upotevu; miongoni mwayo ni kuwa Mwenyezi Mungu ana mke na watoto. Basi wafuasi wao wenye akili za juu wakawa wanawaamini kwa kuona kuwa hakuna yeyote anayeweza kujasiri kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo na kumsifia kwa sifa zisizokuwa zake. Lakini waliposikia Qur’an wakaamini kwamba viongozi wao wanamzulia Mwenyezi Mungu na kumsifu kwa sifa zisizoafikiana naye.

Jambo la kuangalia hapa ni kuwa majini walisikia hikima ya Qur’an kwa mara ya kwanza, wakaielewa na kuwaidhikia nayo. Na sisi tunasikia Qur’an na kuisoma mara kwa mara na hakuna nyumba yoyote ya mwisla­mu isiyokuwa na msahafu, lakini hatunufaiki na mawaidha yake wala kuongoka kwa mwongozo wake. Je, majini wana nafsi safi au wana akili timamu zaidi au ni kuwa katika maisha yao hawana matamanio na vishaw­ishi? [9] 1

Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume katika majini; kwa hivyo wakawazidisha mzigo.

Wametofutiana katika kufasiri Aya hii. Lillo karibu zaidi na ufahamu‧ tofauti na walivyosema wafasiri wengi. ni kuwa makusudio ya wanaume katika watu ni wale wenye akili za juu juu, na wanaume katika majini ni wale watu wanaowavunga wenzao kuwa wana mawaasiliano na majini na wanaweza kuwaita wakati wowote wanapotaka na kuwatumia watakavyo.

Kwa hiyo maana ni kuwa watu wasiokuwa na akili walikuwa wakitaka hifadhi kwa watu waliokuwa wakidai kuwa na mawasiliano na majini ili wajikinge na hatari ya majini, au wawafahamishe yatakayotokea au wawakurubishie yaliyo mbali au kulipeleka mbali lililo karibu. Ama kuwazidishia mzigo ni kuwa wavungaji walikuwa wakiwataka malipo wasiyoyaweza.

Na hakika wao walidhani, kama mlivyodhani nyinyi, kuwa Mwenyezi Mungu hatamtuma Mtume.

Wao ni makafiri katika watu na nyinyi ni nyinyi majini. Maana ni kuwa waumini wa kijini waliwaambia makafiri katika kaumu yao kuwa nyinyi mna wanaofanana nanyi katika watu wasioamini ufufuo na hisabu.

وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا ﴿٨﴾

8. Nasi tuliigusa mbingu, tukaiona imejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.

وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ فَمَن يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَّصَدًا ﴿٩﴾

9. Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza, lakini sasa anayetaka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!

وَأَنَّا لَا نَدْرِي أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِي الْأَرْضِ أَمْ أَرَادَ بِهِمْ رَبُّهُمْ رَشَدًا ﴿١٠﴾

10. Nasi hatujui kama wanataki­wa shari wale wanaokaa kwenye ardhi au Mola wao anawatakia uwongofu.

وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا ﴿١١﴾

11. Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine kati­ka sisi ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.

وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن نُّعْجِزَ اللَّـهَ فِي الْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُ هَرَبًا ﴿١٢﴾

12. Nasi tulijua kuwa hatu­tomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumshinda kwa kukimbia.

وَأَنَّا لَمَّا سَمِعْنَا الْهُدَىٰ آمَنَّا بِهِ فَمَن يُؤْمِن بِرَبِّهِ فَلَا يَخَافُ بَخْسًا وَلَا رَهَقًا ﴿١٣﴾

13. Nasi tulipousikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake hao­gopi kupunjwa wala kudhulu­miwa.

وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُولَـٰئِكَ تَحَرَّوْا رَشَدًا ﴿١٤﴾

14. Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo katika

وَأَمَّا الْقَاسِطُونَ فَكَانُوا لِجَهَنَّمَ حَطَبًا ﴿١٥﴾

15. Na ama walioacha haki, hao wamekuwa kuni za Jahannamu.

وَأَن لَّوِ اسْتَقَامُوا عَلَى الطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَاهُم مَّاءً غَدَقًا ﴿١٦﴾

16. Na lau kama wangelisimama sawasawa juu ya njia tungeli­wanywesha maji kwa wingi.

لِّنَفْتِنَهُمْ فِيهِ وَمَن يُعْرِضْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِ يَسْلُكْهُ عَذَابًا صَعَدًا ﴿١٧﴾

17. Ili tuwajaribu kwa hayo, na anayepuuza kumkumbuka Mola wake atamsukuma kwenye

adhabu ngumu

TULIZIGUSA MBINGU

Aya 8 – 17

MAANA

Nasi tuliigusa mbingu, tukaiona imejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.

Neno kugusa tumelitarjumu kutokana na neno la kiarabu lamd ambalo asili yake ni kugusa kwa mkono, lakini mara nyingi linatumika kwa kutaka; hasa likinyumbuliwa na kuwa iltimas.

Aya hii inarudi madai ya makuhani na wanaodai kuwa na mawasiliano na majini yaliyooelezwa kwenye Aya zilizotangulia hii. Inavunja madai yao kwa kukiri majini wenyewe kuwa hawana uwezo wa kufika mbinguni kusikiliza, kwa sababu ina ulinzi mkali na vimondo.

Ni sawa liwe hili ni uhakika au ni kinaya cha kutojua majini ghaibu, lakini lengo la kwanza ni kutanabaisha kuwa makuhani na wanaodai kuwasiliana na majini wanamzulia Mwenyezi Mungu na majini, kwa sababu ilimu ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu peke yake:

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ ﴿١٧٩﴾

“Na hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwafunulia mambo ya ghaibu,” Juz. 4 (3:179)

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ﴿٥٩﴾

“Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye.” Juz. 7 (6:59).

Umetangulia mfano wake katika Juz. 14 (15:17-18), Juz. 12 (37: 6-7) na Juzuu hii tuliyo nayo (67:5).

Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusik­iliza, lakini sasa anayetaka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!

Dhahiri ya Aya hii inafahamisha kuwa majini, kabla ya kuja Mtume(s.a.w.w) , waliwahi kupanda sehemu fulani mbinguni, na kwamba walikuwa wakisikia sauti au maneno, kisha wakazuliwa zama za Mtume Muhammad(s.a.w.w) .

Hii haimaanishi kwamba wao walikuwa wakifichua habari za ghaibu mbinguni, hapana! Isipokuwa walisikia kitu tu mbinguni, na si lazima kitu hicho kiwe ni ghaibu; bali haiwezekani kabisa kuwa ni katika aina za ghaibu, kwa sababu ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu peke yake kwa nukuu ya Qur’an.

Mbinguni ni makazi ya Malaika lakini pamoja na hivyo:

قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٣٢﴾

“Wakasema: Utakatifu ni wako hatuna elimu isipokuwa ile uliyotufundis­ha.” Juz. 1 (2:32).

Je, yuko aliye mtukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi kuliko Muhammad(s.a.w.w) , lakini pamoja na hayo alisema:

وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ﴿١٨٨﴾

“Na lau kama ningelijua ghaibu ningejizidishia kheri nyingi, wala isinge­nigusa dhara.”

Juz. 9 (7:188).

Ikiwa mtukufu wa viumbe wa Mwenyezi Mungu hajui ghaibu hata katika mambo yanayomuhusu yeye mwenyewe, vipi majini watajua heri au shari itakayowatokea watu baadae?

Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa kwenye ardhi au Mola wao anawatakia uwongofu.

Hii ni kauli ya majini; maana yake ni kuwa vipi anadhania mpumbavu kwamba sisi tuna ilimu ya ghaibu na kujua heri au shari itakayotokea mbele; na kwamba sisi tunawapa hayo makuhani, na hali sisi hatujui aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu kwa yeyote katika watu wa ardhi wala kwa watu wetu?

Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine katika sisi ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.

Majini wanajisimulia wao wenyewe kuwa miongoni mwao wamo wema na waovu, na kwamba wao wamegawanyika mataifa na madhehebu mbali mbali, sawa na walivyo watu.

Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumshinda kwa kukimbia.

Baada ya majini kuisikia Qur’an waliamini kuwa Mwenyezi Mungu ambaye imetukuka hikima yake, hashindwi na atakayemtaka wala ham­ponyoki atakayemkimbia.

Nasi tulipousikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa.

Makusudio ya mwongozo ni Qur’an. Maana ni kuwa majini waliisikia Qur’an wakaiamini kwa ujumla na kwa ufafanuzi, wakiwa na yakini na uadilifu wa Mwenyezi Mungu, kwamba mwenye kufanya mema akiwa na imani basi hahofii kudhulumiwa wala kupunjwa.

Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo katika sisi wanaoacha haki.

Hili ni fungu la pili la majini baada ya uislamu. Ama fungu la kwanza lil­ioelezwa kwenye Aya 11 ya sura hii tuliyo nayo, wema na walio kinyume, hilo ni kwa mtazamo wa kabla ya kusilimu. Hakuna tofauti katika hilo isipokuwa namna ya kuita tu, wema waliitwa hivyo kabla ya uislamu na wakaitwa waislmu baada ya uislamu.

Basi waliosilimu, hao ndio waliotafuta uwongofu.

Waliosilimu waliutafuta uwongofu wakaupata na wakajichagulia heri wakawa wazuri kwayo.

Na ama walioacha haki, hao wamekuwa kuni za Jahannamu.

Sheikh Ismail Haqi, katika tafsiri yake: uhulbayaa anasema: “Alqasie ni yule aliyoiacha haki na uqsie ni yule anayeiendea haki. Jina qasie limetu­mika sana kuitwa kundi la Muawiya, kutokana Hadith ya Mtume alipokuwa akimwambia Ali bin Abi Twalib: Utapigana na nakithin, na qasitia na mariqiia (wavunja ahadi, walioiacha haki na waliochomoka). Kwa hiyo waliovunja ahadi ni watu wa Aisha waliovunja baia, walioiacha haki ni watu wa Muawiya, kwa vile waliiacha haki pale walipopigana na Imam wa haki na waliochomoka ni makhawariji, kwa sababu walitoka kwenye dini ya Mwenyezi Mungu, wakahalalisha kupigana na khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Na lau kama wangelisimama sawasawa juu ya njia tungeliwanywesha maji kwa wingi.

Haya ni maneno mengine wakikusudiwa majini na watu. Makusudio ya njia hapa ni sharia ya haki na uadilifu. Maji mengi ni kinaya cha raha na ukunjufu wa riziki, kwa sababu maji ni asili ya uhai. Maana ni kuwa lau watu wangelimwamini Mwenyezi Mungu kwa ukweli, wakatumia sharia kwa uadilifu na wakajiepusha na dhulma na uadui, basi wangeliishi katika ukunjufu, raha na amani.

Ili tuwajaribu kwa hayo.

Yaani hayo ya raha. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawapa neema kisha aangalie, wakizidi imani na ikhlasi kwayo basi watakuwa wema duniani na Akhera na wakiibadilisha basi atakuwa anawangoja.

Na anayepuuza kumkumbuka Mola wake atamsukuma kwenye adhabu ngumu.

Kila anayekumbushwa haki akaidharau, Mwenyezi Mungu atamwadhibu adhabu chungu.


21

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا ﴿١٨﴾

18. Na hakika misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuombe yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.

وَأَنَّهُ لَمَّا قَامَ عَبْدُ اللَّـهِ يَدْعُوهُ كَادُوا يَكُونُونَ عَلَيْهِ لِبَدًا ﴿١٩﴾

19. Na hakika Mja wa Mwenyezi Mungu aliposimama kum­womba, wao walikuwa karibu kumzonga!

قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا ﴿٢٠﴾

20. Sema: Hakika mimi namwom­ba Mola wangu tu, wala simshirikishi na yeyote.

قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا ﴿٢١﴾

21. Sema: Mimi sina mamlaka ya kuwadhuru wala kuwaon­goza.

قُلْ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ اللَّـهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا ﴿٢٢﴾

22. Sema: Hakika hapana yeyote awezaye kunilinda na Mwenyezi Mungu, wala sitap­ata pa kukimbilia isipokuwa kwake Yeye tu.

إِلَّا بَلَاغًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِسَالَاتِهِ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ﴿٢٣﴾

23. Ila kwa kufikisha Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala zake. Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele.

حَتَّىٰ إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ أَضْعَفُ نَاصِرًا وَأَقَلُّ عَدَدًا ﴿٢٤﴾

24. Hata watakapoyaona wanayoahidiwa, ndipo watakapojua ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi.

قُلْ إِنْ أَدْرِي أَقَرِيبٌ مَّا تُوعَدُونَ أَمْ يَجْعَلُ لَهُ رَبِّي أَمَدًا ﴿٢٥﴾

25. Sema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayoahidiwa, au Mola wangu atayawekea muda mrefu.

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا ﴿٢٦﴾

26. Ni Mwenye kujua ghaibu, wala hamdhihirishii yeyote ghaibu yake.

إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُولٍ فَإِنَّهُ يَسْلُكُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ رَصَدًا ﴿٢٧﴾

27. Isipokuwa Mtume aliyemridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.

لِّيَعْلَمَ أَن قَدْ أَبْلَغُوا رِسَالَاتِ رَبِّهِمْ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيْهِمْ وَأَحْصَىٰ كُلَّ شَيْءٍ عَدَدًا ﴿٢٨﴾

28. Ili ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao, Na anajua vyema yote waliyo nayo na amedhibiti idadi ya kila kitu.

HAKIKA MISKITI NI YA MWENYEZI MUNGU

Aya 18 – 28

MAANA

Na hakika misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuombe yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.

Wametofautiana kuwa kauli hii ni ya Mwenyezi Mungu au ni ya majini? Vyovyote iwavyo maana ni moja, kwamba sehemu zote za kuabudu ni kwa ajili ya kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumtii Yeye tu; iwe zime­jengwa na kuimarishwa na waislamu au wengineo.

Na hakika Mja wa Mwenyezi Mungu aliposimama kumwomba, wao walikuwa karibu kumzonga!

Makusudio ya mja wa Mwenyezi Mungu hapa ni Muhammad(s.a.w.w) , aliyemuomba, ni Mwenyezi Mungu; na waliomzonga ni maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Maana ni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alipotoa mwito wa haki vilijitokeza vikundi vya upotevu na kumzonga kutokana na wingi wao; kama nywele au sufu zinapojizonga zonga. Katika hilo Imam Ali (a.s) anasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) aliingia kwenye kila majonzi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Ndugu zake wa karibu walimbadilikia na wa mbali wakaungana dhidi yake.

Waarabu walilegeza hatamu zao dhidi yake na wakamvalia njuga kumpiga vita, mpaka wakamjia maadui kutoka sehemu mbali mbali.

Linalofahamisha kuwa haya ndio makusudio yake ni kauli yake Mwenyezi Mungu moja kwa moja:

Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu tu, wala simshirikishi na yeyote.

Sema ewe Muhammad kuwaambia wale walioungana kukupiga vita: Je, nimewakosea nini? Je, nimewataka ujira au nimetaka cheo? Hapana isipokuwa ninamwabudu Mwenyezi Mungu na kumfanyia ikhlasi. Yeye ndiye aliyoyeumba ulimwengu wote pamoja na ardhi yake na mbingu yake, je hii ni dhambi isiyosameheka?

Sema: Mimi sina mamlaka ya kuwadhuru wala kuwaongoza ; yaani kuwanufaisha. Maana ni kuwa sema ewe Muhammad kuwaambia washirikina: Mimi ni mtu kama nyinyi tu sidai kuwa na uweza wa hatima yenu, wala madhara na manufaa yenu; amri yote ni ya Mwenyezi Mungu peke yake.

Sema: Hakika hapana yeyote awezaye kunilinda na Mwenyezi Mungu, wala sitapata pa kukimbilia isipokuwa kwake Yeye tu. Ila kwa kufikisha Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala zake.

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) akizembea kufikisha ujumbe alioaminiwa nao basi atakuwa hana pa kumkimbia Mwenyezi Mungu.

Aya hii ni miongoni mwa makumi ya Aya yanayofahamisha kwa uwazi kuwa Uislamu unakataa fkra ya kuweko wasta (wa katikati) baina ya Mwenyezi Mungu na mja wake, na inamweka mja mbele ya Mola wake moja kwa moja; azungumze naye, amnong’oneze vile atakavyo na ajikurubishe kwake kwa kufanya heri bila ya kuweko muombezi wala mgombezi.

Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele.

Hili ni onyo, hadhari na kiaga kwa waasi waliopituka mipaka, kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) anapasa kutiiwa, hata kama hakutoa tahadhari na onyo; sikwambii tena akitoa onyo na tahadhari kama hii.

Hata watakapoyaona wanayoahidiwa, ndipo watakapojua ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi.

Washirikina walikuwa wakiwaona dhaifu wasisidizi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na wakiwaona ni wachache, wakimwambia: sisi ni zaidi yako wewe kwa mali na watu. Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawaambia kesho mtajua ni nani aliye na nguvu na ninani aliye dhalili. Amesema kweli Mwenyezi Mungu mtukufu, hazikupita siku Uislamu ukawa na nguvu na akawainua waislamu kwa uweza wake na makafiri watakuwa na adhabu ya kuungua huko Akhera.

Sema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayoahidiwa, au Mola wangu atayawekea muda mrefu.

Washirikina waliposikia kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘ndipo watakapojua ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi,’ wal­imuuliza Mtume(s.a.w.w) : yatakuwa lini hayo; ndio Mwenyezi Mungu akamwamrisha Nabii wake awaambie ilimu yake iko kwa Mola wangu na wala sijui iko karibu au iko mbali.

Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Au atayawekea muda inafupishwa na neno mbali; kama ilivyo katika kauli yake:

وَإِنْ أَدْرِي أَقَرِيبٌ أَم بَعِيدٌ مَّا تُوعَدُونَ ﴿١٠٩﴾

“Wala sijui yako karibu au mbali hayo mliyoahidiwa. Juz. 17 (21:109).

Ni Mwenye kujua ghaibu, wala hamdhihirishii yeyote ghaibu yake, isipokuwa Mtume aliyoemridhia.

Ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu na yule aliyemwamini kwa wahyi wake na akamchagua kupeleka ujumbe wake kwa waja wake, huyo anaweza kujua ghaibu aliyojulishwa na Mwenyezi Mungu: “Utakatifu ni wako hatuna elimu isipokuwa ile uliyotufundisha.” Juz. 1 (2:32).

Kundi la wafasiri, akiwemo Ar-Razi na Al-Maraghi wamesema asiyekuwa Mtume anaweza kujua ghaibu na kuitolea habari, lakini kauli hii haifikia­ni na dhahiri ya kauli yake isipokuwa Mtume aliyemridhia.

Ndio, ni kweli kuwa kuna baadhi ya watu wanaweza kutabiri mambo yatakayotokea mbele na wakawa wakweli katika nyingi ya dhana zao, lakini hayo wanayatoa kutokana na vigezo na alama zinazowadhihirikia kwa ufahamu na ilimu. Sasa ni wapi na wapi haya na ilimu ya ghaibu ambayo haidhihirishi Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa mitume na manabii?

Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.

Yanayokuja haraka kwenye ufahamu wetu kutokana na Aya hii, ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawalinda manabii wakiwa wanatekeleza ujumbe wake na anawahifadhi na kila kikwazo cha kufikisha ujumbe kwa njia yake; ni sawa kizuizi hicho kiwe kinatoka ndani, kama vile kupuuza na kusahau, au kiwe kinatoka nje, kama vile ushawishi wa maadui nk. Kwa maneno mengine ni kuwa Aya hii inathibitisha umasumu wa manabii kati­ka utekelezaji wa wahyi.

Ili ajue yaani ifichuke ilimu ya Mwenyezi Mungu na uhakika wake,kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao, kwa uhalisia wakena Yeye anayajua vyema yote walio nayo . Yaani kila waliyosema manabii; haimpiti hata herufi moja. Fauka ya hayo ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amevizunguka kwa ujuzi viumbe vyake vyote vidogo na vikubwa.

Na amedhibiti idadi ya kila kitu. Atashindwaje kuwadhibiti wajumbe wake kwenye kauli zao na pumzi zao na hali wao wanafikisha risala yake kwa waja wake? Lengo la msisitizo huu ni kutanabahisha kwamba manabii wamelindwa; hawakosei katika kufikisha wahyi ‧ hawapunguzi herufi wala kugeuza herufi kwa herufi nyingine.

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

“Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni wahyi uliotolewa.” Juz. 27 (53: 3-4).

MWISHO WA SURA YA SABINI NA MBILI: SURAT AL-JINN


22

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sabini Na Tatu: Surat Al Muzzammil. Imeshuka Makka Ina Aya 20.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehmu.

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ ﴿١﴾

1. Ewe uliyejizongazonga nguo!

قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٢﴾

2. Simama usiku, ila kidogo tu!

نِّصْفَهُ أَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا ﴿٣﴾

3. Nusu yake, au ipunguze kidogo.

أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا ﴿٤﴾

4. Au izidishe, na soma Qur’an kwa utaratibu.

إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا ﴿٥﴾

5. Hakika tutakuteremshia kauli nzito.

إِنَّ نَاشِئَةَ اللَّيْلِ هِيَ أَشَدُّ وَطْئًا وَأَقْوَمُ قِيلًا ﴿٦﴾

6. Hakika kuamka usiku kunakanyaga zaidi, na ni vizuri zaidi kutamka.

إِنَّ لَكَ فِي النَّهَارِ سَبْحًا طَوِيلًا ﴿٧﴾

7. Kwani hakika mchana una shughuli nyingi.

وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلًا ﴿٨﴾

8. Na lidhukuru jina la Mola wako, na ujitupe kwake kujitu­pa kabisa.

رَّبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَاتَّخِذْهُ وَكِيلًا ﴿٩﴾

9. Mola wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipokuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa.

EWE MWENYE KUJIZONGAZONGA NGUO

Aya 1 – 9

MAANA

Ewe uliyejizongazonga nguo!

Aya hii na zinazofuatia ni miongoni mwa Aya za mwanzo mwanzo kumshukia Mtume(s.a.w.w) . Ama Aya ya mwanzo kabisa au Sura ya kwanza, yatakuja maelezo yake katika Juzuu inayofuatia sura 96.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) hapa amemwita Nabii wake mtukufu hivyo, kwa sababu alikuwa amejizongozonga nguo kutokana na sababu fulani. Ndio maana Mtukufu akamwita kwa sifa aliyokuwa nayo kwa kuzungumza naye kwa upole. Katika mfano kama huu ni kauli yake Mtume(s.a.w.w) kumwambia Ali: “Simama ewe Abu Turab (Baba wa mchanga),” kwa sababu alikuwa amelala mchangani. Pia kauli yake Nabii kumwambia Hudhayfa Al-Yamani: “Simama ewe mlalaji,” kwa vile alikuwa amelala.

Simama usiku, ila kidogo tu!

Wacha kujifunika nguo ewe Muhammad! Na ukeshe usiku kwa Swala na ibada nyingine, isipokuwa sehemu ndogo ya usiku utakayopumzika kwenye kitanda chako kwa usingizi. Kwa maneno mengine ni kuwa usiku wako ugawanye sehemu mbili; sehemu ya Mola wako na sehemu nyingine ya nafsi yako. Msemaji mmoja amesema kuwa kwa hili Mwenyezi Mungu alitaka kumwandaa Nabii mtukufu kwa jihadi ndefu, kuvumilia matatizo ya ufik­shaji na maudhi atakayopambana nayo kutoka kwa washirikina.

Hizi ni njozi tu, kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t) alikwishamwandaa Muhammad, kwa ajli ya amana kubwa atakayoichukua, kwa maumbile yake tangu siku aliyozaliwa.

Nusu yake, au ipunguze kidogo, au izidishe kidogo pia.

Huu ni ubainifu na tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘sima­ma usiku ila kidogo.’ Maana yake ni kuwa ewe Muhammad unaweza kusi­ma nusu yote ya usiku au chini yake kidogo au zaidi kidogo. Tafsiri hii, kikanuni ya nahw, inatubainishia kuwa nusu yake ni bada ya usiku na sio ya uchache. Pia inawezekana kuwa ni bada ya uchache na siyo ya usiku, na maana yawe unaweza kulala nusu yote ya usiku au upunguze au uzidishe kidogo. Hakuna tofauti ya maana baina ya irabu mbili hizi za kinahw.

Wafsiri wengi wameleta natija kutokana na neno kidogo katika Aya hii kuwa nusu inatakikana isizidi theluthi na ziada isizidi nusu mbili, kwa hiyo hiyari inakuwa baina ya nusu, theluthi au theluthi mbili na Aya ya 20 ya Sura hii imeeleza nyakati hizi tatu.

Na soma Qur’an kwa utaratibu.

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume(s.a.w.w) , lakini makusudio ni kwa wote. Maana ni kuwa usifanye haraka kusoma, kwani lengo la kusoma Qur’an ni kuzingatia msomaji maana yake na malengo yake, anufaike na hukumu zake, mawaidha yake na ahadi zake, aweze kuhisi hofu ya adhabu chungu kutokana na maasi na kutumaini thawabu nyingi kutokana na utiifu; vinginevyo kutingisha ulimi na kuzitoa herufi kwa matokeo yake tu, sio malengo.

HAIBA YA MTUME MTUKUFU

Hakika tutakuteremshia kauli nzito.

Qur’an kwa maana yote yaliyo katika maneno haya, ni nzito kwa vile imeshinda na imedumu. Pia ni nzito katika itikadi na sharia yake na kupigana vita kwake dhidi ya wafisadi wenye nguvu na mataghuti wapenda anasa.

Wafasiri wengi wamesema Qur’an ni nzito kwa sababu ya taklifa zake zenye mashaka; mfano kudumisha Swala tano, kuamka mwisho wa usiku kwa jli ya Swala ya alfajiri, kutawadha na kuoga kwa maji baridi mara nyingi, kufunga siku za joto, kuamka mwisho wa usiku, kuhiji na masha­ka yake ya ihramu kufanya sa’yi na tawafu.

Hakuna mwenye shaka kwamba haya ni mazito isipokuwa kwa wenye kunyenyekea, lakini kubwa na zito zaidi ya hayo yote ni taklifa ya jihadi ambayo iko namna nyingi, na iliyo nzito zaidi ni jihadi ya kubadilisha nyoyo na hisia, kubadilisha imani mbovu zilizorithiwa na kung’oa mizizi ya ufisadi.

Haya ndiyo aliyobebeshwa Abul-Qasim, Muhammad mwana wa Abdillah. Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimtuma kukamilisha maadili mema ya utu wote na awatoe watu kutoka gizani kuwapeleka kwenye nuru. Je, kuna mzigo mzito na wenye tabu kuliko huu?

Ni nani anayeweza kugeuza maadili ya mkewe na watoto wake, hasa kati­ka zama za ujahilia, zilizokuwa na ufisadi wa kupindukia na kupituka mipaka zaidi? Lakini Muhammad aliweza kuyakamilisha hayo. Siri ya hilo inakuwa katika haiba ya Muhammad(s.a.w. w ) , nguvu yake, ukuu wake na uvumilivu wake wa kushangaza katika maudhi kwenye njia ya mwito wake. alikuwa akizidi kuwa na subira na upole kila waasi walivyozidisha maudhi. Hakuwa akizidisha kauli yake: “Ewe Mwenyezi Mungu waseme­he watu wangu, hakika wao hawajui… ikiwa wewe hunikasirikii basi sijali.” Hapa ndio tunapata tafsiri sahihi zaidi ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

اللَّـهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ﴿١٢٤﴾

“Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi wa kujua mahali anapoweka ujum­be wake.” Juz. 8 (6:124).

Ndio! Mwenyezi Mungu anajua kuwa haiba ya Muhammad ina nguvu zaidi kuliko imani na itikadi na watu wote, ndio maana akamtuma kuka­milisha tabia njema: “Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya alivyoipa.” Juz. 28 (65:7). Hakika hii ameigundua mwanafasihi mashuhuri wa kimataifa, Bernard Show, pale aliposema; “Lau Muhammad bin Abdillah angelikuwa kwenye karne ya ishirini angemaliza ufisadi na upotevu.”

Hakika kuamka usiku kunakanyaga zaidi, na ni vizuri zaidi kutamka.

Katika Bahrf Al-muhit, imeelezwa kuwa maana ya kuamka usiku ni saa yake, kukanyaga zaidi, ni mashaka zaidi, na vizuri zaidi kutamka, ni kutamka kwa usawa na uthabiti.

Ni kama kwamba muulizaji ameuliza: Kwa nini Mwenyezi Mungu akamwamuru Nabii wake mtukufu kuabudu sehemu ya usiku? Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akajibu, kwa sababu mtu kuacha kitanda chake baada ya utulivu wa usiku kuna mashaka makubwa zaidi katika nafsi, na bora ya amali ni ile yenye mashaka zaidi. Na kwa kuwa moyo wa mtu usiku unakuwa safi na mtulivu zaidi, basi kisomo chake kinakuwa sahihi na uthabiti zaidi. Vile vile kinakuwa na mwitikio zaidi pamoja na Aya.

Imesemekana kuwa neno watw’a, tulilolifasiri kwa maana ya kukanyaga, hapa lina maana ya kuafikiana baina ya moyo na ulimi.

Kwani hakika mchana una shughuli nyingi.

Neno shughuli tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu sabhU lenye maana ya kuogelea; yaani mtu anajigeuzageuza kwenye shghuli za hapa na pale, kama anayeogelea.

Usiku ni wa ibada na tahajudi na mchana ni wa kufanya kazi na kuhangai­ka kutafuta maisha, nao ni mrefu unaotosheleza mahitaji ya mtu.

Sheikh Abdul-Qadir Al-Maghribi, katika kufasiri Aya hii, anasema: “Mpingaji anaweza kusema kuwa kuamka usiku kunadhoofisha. Hilo amelijibu Bwana wetu Ali (r.a) kwa kusema: ‘Kama mtu akisema: ikiwa hali ya mwana wa Abu Twalib ni hii basi hataweza kupamabana na mashujaa. Juweni kwamba mti wa msituni una mbao laini na matawi ya kijani yana magome laini, na mti wa mbugani una kuni ngumu na zinazochelewa kuzimika. Mimi na Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kama mwanga unao­tokana na mwanga, na kama pacha, na kama kigasha na sehemu ya juu ya mkono.’

Yaani yeye na Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ni asili moja katika utendaji na mfumo wa maisha; kwa hiyo hali ya ke ni kama hali ya Mtume, shujaa, mwenye azma ya nguvu, ingawaje maisha yake yalikuwa magumu.”

Na lidhukuru jina la Mola wako, na ujitupe kwake kujitupa kabisa.

Makusudio ya kumdhukuru Mwenyezi Mungu hapa ni kumlingania. Neno kujitupa tumelifasiri kutokana na neno abattul, linalotokana na batl. Neno hili hutumika katika kuachana na dunia; miongoni mwayo ni Batul, msimbo wa Bibi Maryam.

Maana ni kuwa baada ya kukesha sehemu ya usiku kwa ibada ewe Muhammad na kupumzika, basi lingania haki na kufanya juhudi katika njia ya Mwenyezi Mungu peke yake. Kama kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamfahamisha Mtume wake mtukufu kuugawanya usiku mafungu matatu: Fungu la ibada, la jihadi na la kupumzika ili aweze kuendelea na ibada yake na juhudi zake.

Mola wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipokuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa.

Ufalme katika mashariki na magharibi na mbinguni na ardhini ni wake peke yake, hana mshirika. Ikiwa viumbe wote ni wa Mwenyezi Mungu basi ni wajibu kwa mja kumtegema Yeye tu na wala asikimbilie kwa yey­ote asiyekuwa Yeye.

Hapa kuna ishara kwamba viumbe wanafahamisha kuweko muuumbaji na kwamba kunyenyekea viumbe kwenye siri ya maumbile yenye kuthibiti bila kugeuka ni dalili wazi kuwa muumba ni mmoja katika dhati yake na sifa zake.

وَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَاهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا ﴿١٠﴾

10. Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kujitenga vizuri.

وَذَرْنِي وَالْمُكَذِّبِينَ أُولِي النَّعْمَةِ وَمَهِّلْهُمْ قَلِيلًا ﴿١١﴾

11. Na niache Mimi na wanaokadhibisha, walioneemeka, na wape muda kidogo!

إِنَّ لَدَيْنَا أَنكَالًا وَجَحِيمًا ﴿١٢﴾

12. Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unaowaka kwa ukali!

وَطَعَامًا ذَا غُصَّةٍ وَعَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٣﴾

13. Na chakula kinachokwama kooni, na adhabu inayoumiza.

يَوْمَ تَرْجُفُ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ وَكَانَتِ الْجِبَالُ كَثِيبًا مَّهِيلًا ﴿١٤﴾

14. Siku ambayo ardhi itatikisika na milima, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga.

إِنَّا أَرْسَلْنَا إِلَيْكُمْ رَسُولًا شَاهِدًا عَلَيْكُمْ كَمَا أَرْسَلْنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ رَسُولًا ﴿١٥﴾

15. Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tulivyomtuma Mtume kwa Firauni.

فَعَصَىٰ فِرْعَوْنُ الرَّسُولَ فَأَخَذْنَاهُ أَخْذًا وَبِيلًا ﴿١٦﴾

16. Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamtesa mate-so mazito.

فَكَيْفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرْتُمْ يَوْمًا يَجْعَلُ الْوِلْدَانَ شِيبًا ﴿١٧﴾

17. Basi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wawe wazee?

السَّمَاءُ مُنفَطِرٌ بِهِ كَانَ وَعْدُهُ مَفْعُولًا ﴿١٨﴾

18. Mbingu zitapasuka! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa.

إِنَّ هَـٰذِهِ تَذْكِرَةٌ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا ﴿١٩﴾

19. Kwa hakika haya ni ukum­busho. Mwenye kutaka atashika njia ya kwendea kwa Mola wake.

JITENGE NAO KWA UZURI

Aya 10 -19

MAANA

Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kujitenga vizuri.

Maadui wa Mwenyezi Mungu walisema mengi juu ya Muhammad(s.a.w. w ) , ndio Mwenyezi Mungu akamwamuru avumilie na aachane nao bila ya kuwafanya lolote.

Hayo yalikuwa mwanzo mwanzo mwa utume ambapo waislamu walikuwa kidogo na makafiri ni wengi; mpaka ilipofikia Hijra na waislamu wakawa na nguvu ndipo Mwenyezi Mungu alipowaruhusu kuwahami wadhulumiwa kutokana na madhalimu.

Umetangulia mfano wake katika Aya kdhaa ikiwemo Juz. 9 (7:199).

Na niache Mimi na wanaokadhibisha, walioneemeka, na wape muda kidogo!

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kumwambia Nabii wake mtukufu kuwa aachane nao hao wanaomkadhibisha na kumpa sifa ya uchawi, mwendawazimu na mshairi, sasa anamwambia niachie nao mimi hawa waliolevyeshwa na mali na kuwapofua wasione kitu isipokuwa starehe na anasa zao. Waache wala wasikushughulishe, ni hivi karibuni tu itawapata adhabu na maangamizi.

Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unaowaka kwa ukali! Na chakula kinachokwama kooni, na adhabu inayoumiza.

Haya ndiyo aliowaahidi Mwenyezi Mungu: mbingu, moto ambao kuni zake ni watu na mawe, chakula cha miba kisichoshuka kooni wala kutoka na aina nyinginezo za adhabu, kama vile nguo za moto na makomeo ya chuma.

Siku ambayo ardhi itatikisika na milima, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga.

Huu ndio wasifu wa siku ya Kiyama na vituko vyake: ardhi itatetemeka na milima iwe kama rundo la mchanga unaotawanyika kwa sababu ndogo tu.

Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu.

Maneno yaneelekezwa kwa wakadhibishaji walioneemeka, makusudio ya mtume na shahidi ni Muhammad(s.a.w. w ) ; kama ilivyo katika Juz. 7 (4:41). Yaani Muhammad(s.a.w. w ) atatoa ushuhuda kuwa aliwafikishia ujumbe wa Mola wao, lakini wakaukadhibisha na kuupuza.

Kama tulivyomtuma Mtume kwa Firauni. Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamtesa mateso mazito.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anapiga mfano wa Firauni na wale walioneeme­ka waliomkadhibisha Muhammad(s.a.w. w ) , kuwa hali yao ni sawa na hali ya watu wa Firauni walivyokuwa na Musa. Mwenyezi Mungu anawahad­harisha, kama wataendelea na upotevu yatawapata yaliyompata Firauni na watu wake; maangamizi na adhabu chungu duniani na Akhera.

Basi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wawe wazee? Mbingu zitapasuka! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa.

Makusudio ya mkikufuru ni mkibakia kwenye ukafiri. Maana ni kuwa mta­jiokoa na nini nyinyi mnaopituka mipaka na adhabu kubwa siku itakapopa­suka mbingu na mtoto kuwa mzee kutokana na vituko vya siku hiyo. Siku hiyo itafika tu, hilo halina shaka, kwa sababu Mwenyezi Mungu hakhalifu kiaga. Ilivyo ni kuwa kuzeeka ni fumbo la yatakayowapata wakosefu, kwa sababu watoto hawatahisabiwa wala kuadhibiwa.

Kwa hakika haya ni ukumbusho. Mwenye kutaka atashika njia ya kwendea kwa Mola wake.

Haya ni hayo yaliyotangulia ya Aya za maonyo na kiaga. Ukumbusho ni mazingatio na mawaidha. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anabainisha njia mbili za heri na shari. Akaamrisha hili na kuliahidia thawabu na akakataza lile na kuliahidia adhabu; kila mtu atajichagulia neema au moto.

إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِن ثُلُثَيِ اللَّيْلِ وَنِصْفَهُ وَثُلُثَهُ وَطَائِفَةٌ مِّنَ الَّذِينَ مَعَكَ وَاللَّـهُ يُقَدِّرُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ عَلِمَ أَن لَّن تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرْضَىٰ وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِي الْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ وَآخَرُونَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٠﴾

20. Hakika Mola wako anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe. Na Mwenyezi Mungu anaukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuwe­ka hisabu, basi amewasamehe. Basi someni kilicho chepesi katika Qur’an. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo. Na simamisheni Swala, na toeni Zaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na kheri yoyote mnayoitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina ujira mkubwa sana. Na mtakeni maghufira Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kure­hemu.

SOMENI KILICHOCHEPESI KATIKA QUR’AN

Aya 20

MAANA

Hakika Mola wako anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe.

Mwanzoni mwa sura Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwamuru Nabii wake mtukufu na walio pamoja naye wafanye ibada theluthi mbili za usiku au nusu yake au hata theluthi, ni hiyari ya mtu.

Basi wakasikiliza na wakatii. Baadhi ya maswahaba wakawa wanaona uzito kuupanga wakati, kwa hiyo wakawa wanakesha usiku kucha, mpaka badhi yao wakavimba miguu kutokana na kusimama mda mrefu. Walifanya hivi kujitoa shaka kwenye dini yao na kumridhisha Mola wao.

Katika Aya hii tuliyo nayo Mwenyezi Mungu (s.w.t) anampa habari Mtume wake kwamba yeye na walio pamoja naye wamefikia ukomo wa kumwabudu na kumtii Mwenyezi Mungu na Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa malipo bora na ya ukamilifu.

Na Mwenyezi Mungu anaukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu, basi amewasamehe. Basi someni kilicho chepesi katika Qur’an.

Kuweka hisabau ni hiyo theluthi mbili na nusu yake na theluthi yake. makusudio ya kuwasamehe ni kuwaondolea taklifa.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewafanyia usiku na mchana kwa kiwango maalum, lakini mswahaba walikuwa hawajui nyakati kwa kiwango chake; isipokuwa walikuwa wakitegema dhana tu na ijtihadi; ambapo wakati huo hakukua na saa za kudhibiti dakika na sekunde.

Kwa hiyo akawaondolea kisimamo cha usiku cha theluthi mbili za usiku, nusu yake au theluthi moja; kwamba wasome Qur’an kiasi watakachoweza.

Mwenye ajamul-bayaa amewanukuu wafasiri wengi wakisema kuwa makusudio ya kitakachokuwa chepesi ni Swala ya usiku.

Ni sawa iwe makusudio ni kisomo au Swala, lakini ieleweke kuwa amri hapa ni ya Sunna sio wajibu.

Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu.

Hii ni hikima ya pili ya kuhafifishwa na kuondolewa taklifa ya kusimama kwenye theluthi mbili za usiku au nusu yake au theluthi yake; nayo ni kuwa miongoni mwa waja watakuweko wagonjwa watakaokuwa na uzito wa kumaliza masaa mengi usiku kwa kuswali, vile vile kutakuweko wasafiri wanaotafuta maisha na bila shaka safari inahitaji mapumziko na kulala usiku, vinginevyo itakuwa uzito kufanya kazi mchana kwa msafiri. Vile vile kutakuwa na wapiganaji wanaohitajia mapumziko usiku ili wawe na nguvu za mapambano mchana.

Basi Mwenyezi Mungu akawawahafifishia wote kwa sababu ya hawa watatu. Aya inaashiria mambo mawili muhimu: Kwanza, hikima ya kuon­doa taklifa kwa wote hailazimishi kushindwa wote, bali inatosha tu kushindwa baadhi na kuondolewa kwa wote. Pili, kazi ya kutafuta riziki ya halali ni jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu; sawa na jihadi ya kupigana na maadui wa Mungu na wa ubinadamu.

Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amelikariri jambo hili kwa kukaririka sababu zake; ya kwanza ilikuwa ni kutodhibiti wakati na ya pili ni ugonjwa, safari na vita.

Na simamisheni Swala ; yaani Swala tano. Hizi haziondoki kwa hali yoyote ile, si kwa safari, wala ugonjwa au jihadi. Kila mtu ataitekeleza kulin­gana na uwezo wake.Na toeni Zaka ya wajibu katika mali zenu.Na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema . Yaani vile vile toeni kwa kujitolea katika njia za heri na hisani; kwani kutoa huku kunawarud­ishia ziada juu ya ziada.

Amri hii ya kutoa imekaririka mara saba mpaka sasa; ya kwanza ni ile iliyo katika Juz. 2 (2:245).

Na kheri yoyote mnayoitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina ujira mkubwa sana.

Kheri haihusiki na kutoa mali tu; kila lililo na masilahi kwa watu basi ni heri; iwe ni kauli au kitendo. Mwenye kufanya wema anajifanyia mwenyewe na mwenye kufanya ubaya pia ni juu yake.

Na mtakeni maghufira Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

Mwenye kuzembea na akapituka mipaka basi anamfungulia mlango wa toba, na ni muhali kuufunga mlango wa maghufira.

MWISHO WA SURA YA SABINI NA TATU: SURAT AL MUZZAMMIL


23

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sabini Na Nne: Surat Al- Muddathir. Imeshuka Makka Ina Aya 56.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ ﴿١﴾

1. Ewe uliyejigubika!

قُمْ فَأَنذِرْ ﴿٢﴾

2. Simama uonye!

وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ ﴿٣﴾

3. Na Mola wako mfanyie takbira!

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ ﴿٤﴾

4. Na nguo zako zitwaharishe.

وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ ﴿٥﴾

5. Na mabaya yaambae!

وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ ﴿٦﴾

6. Wala usitoe kwa kutaka kingi.

وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ ﴿٧﴾

7. Na kwa ajili ya Mola wako, fanya subira!

فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ ﴿٨﴾

8. Basi litapopulizwa barugumu.

فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ ﴿٩﴾

9. Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu.

عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ ﴿١٠﴾

10. Kwa makafiri haitakuwa nyepesi.

EWE ULIYEJIGUBIKA

Aya 1 - 10

MAANA

Aya hizi zinaashiria wadhifa wa Muhammad(s.a.w.w) kama mjumbe wa haki kwa viumbe. Pia kuna ishara kuwa watu wote mbele ya Mwenyezi Mungu wako sawa; ufafanuzi ni kama ufufatavyo:­

Ewe uliyejigubika!

Huyo ni Mtume mtukufu(s.a.w.w) . Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemwita kwa sifa hii kwa sababu wakati huo alikuwa katika hali hiyo kutokana na sababu fulani; kama tulivyosema mwanzo wa Sura iliyopita.

Simama uonye!

Neno linaweza kuwa na maana moja ya kilugha, lakini maana hayo, mara nyingi, yanatofautiana kulingana na msemaji na anayeambiwa. Mfano neno ‘onya,’ maana yake katika kamusi za lugha lina maana ya kuhofisha na kuhadharisha.

Kwa mfano ukimuona mtu anachimba shimo njiani na kumwambia toa onyo, utakuwa unamaanisha atangaze na kuwaonya wapita njia wasiingie shimoni. Ukimwambia mwana fakihi katika kijiji: ‘onya.’ Utakuwa unamaanisha awafundishe watu wa hapo hukumu za dini na kuwahofisha kuzihalifu.

Ama kauli ya Mtukufu kwa Nabii wake; ‘simama uonye,’ Maana yake ni pambana na waasi wenye nguvu na kiburi kwa neno la haki na uwambie: nyinyi ni wapotevu wafisadi na mtajua kesho hizaya na udhalili utakaowapata, kama hamtarudi kuuacha upotevu wenu. Ukiwambia hivi uvumilie yatakayokupata kutoka kwao na umsabihi Mola wako na kumshukuru.

Tukiona jinsi Muhammad(s.a.w.w) alivyopambana na makuraishi wakiwa na nguvu na kauli na yeye hana chochote zaidi ya ikhlasi na imani, hapo ndio tunabainikiwa na yaliyomsibu kutoka kwao: walimpa sifa ya uchawi, uwongo, ushairi na hata wendawazimu. Walimshakizia watoto wamfanyie masikhara na kumtupia mawe; wakawaambia wanawake waweke miba kwenye njia atakayopita na wasafihi wamwekee uchafu na najisi njiani; hata kuna mmoja wao aliyewahi kumvua kilemba Mtume na kukifunga shingoni mwake. Fauka ya yote hayo makuraishi waliweka azimio la kumwekea vikwazo Mtume na watu wake na kumzuia asiwe na mahusiano na jamii.

Pamoja na yote hayo Nabii(s.a.w.w) alivumilia na kuendelea na mwito wake bila ya kujali hali ngumu waliyompa makuraishi, wakaunda vikosi na majeshi. Akavumilia, akawa imara na subira na kuitikia kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Ewe uliyejigubika! Simama uonye.”

Haya yanatuwekea wazi kuwa wadhifa wa Mtume ni kuonya pamoja na uvumilivu wa tabu na mashaka. Hili ndilo jambo la kwanza. Ama la pili, ni usawa baina ya watu, linalofa­hamika kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Na Mola wako mfanyie takbira!

Ukimwambia mtu wa kawaida: Mfanyie takbira Mwenyezi Mungu, tutafa­hamu kuwa unataka asema Allahf akbar; kama vile ukisema: mswalie Mtume.

Lakini kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kumwambia Nabii wake: ‘Na Mola wako mfanyie takbira, ina maana kubwa na nzito zaidi, ambayo ni: Ewe Muhammad(s.a.w.w) waambie usoni mwao wale wanoji­fanya majabari wenye kiburi kuwa enzi ni ya Mwenyezi Mungu na Yeye pekee ndiye mkubwa aliye juu, na kwamba nguvu, utukufu na utawala ni wa mmoja aliye pekee asiyekuwa na mshirika kutoka kwenye miungu wenu au nyinyi wenyewe au kutoka kwa wengine; na kwamba watu wote wako sawa katika kumwabudu Mwenyezi Mungu; hakuna tofauti baina ya mweusi na mweupe wala baina ya tajiri na fukara.

Muhammad aliitikia mwito wa Mola na kuwaambia mataghuti mengi tu; miongoni mwayo ni: “Hakika nyinyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannam, mtaifikia.” Juz. 17 (21:98).

Na nguo zako zitwaharishe.

Vile vile hii inafungamana na kulingania na kuonya. Hakuna anayetia shaka kuwa usafi wa mwili na nguo ni katika imani, lakini makusudio hapa ni zaidi ya hivyo; kwamba Mtume(s.a.w.w) atoe mwito wa usafi wa nje, kama vile uchafu, na usafi wa ndani, kama vile udanganyifu na hiyana, ria na unafiki, ujinga na kuhadaika na madhambi mengineyo.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) hayo ameyatolea ibara ya usafi wa nguo, kwa kutumia des­turi ya waarabu; wanaposema: Fulani ni msafi wa mapindo ya nguo yake, wakimaanisha kuwa ni msafi wa moyo na dhati.

Na mabaya yaambae!

Hii inakuwa ni tafsiri na ufafanuzi wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na nguo zako zitwaharishe,’ kama ilivyosemekana. Pia imese­mekana makusudio ni ushirikina na kuabudu masanamu.

Wala usitoe kwa kutaka kingi.

Makusudio ya kutaka kingi hapa ni kujiona umefanya mengi. Maana ni kuwa Ewe Muhammad! umewafanyia watu mema mengi na fadhila nyin­gi, lakini usimsimbulie yeyote kwa hilo ukajiona kuwa umefanya mengi, ukasema mimi nimefanya hili ni kawafadhili lile. Kwani kila ulilojitolea ni fadhila yako kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kuna fadhila gani na tukufu zaidi kuliko kuafikiwa kufanya kheri?

Mara nyingi huko nyuma tumeeleza kuwa makatazo yanafaa hata ikiwa anayeambiwa hana azma ya kufanya hilo linalokatazwa, mbali ya kuwa amri za Mwenyezi Mungu na makatazo yake yanawahusu waja wake wote, hata wale wenye takua.

Imesemwa katika Nahjul-balagha: “Kutekeleza haja hakuwezi kuendelea ila kwa mambo matatu: Kwa kuifanya ndogo itakuwa kubwa, kwa kuificha itajitokeza na kwa kuiharakisha itasifika.”

Na kwa ajili ya Mola wako, fanya subira!

Mwenyezi Mungu hakumwamrisha Nabii wake mtukufu jambo lolote la taklifa ya kufikisha na utume ila analikutanisha na subira, kama ilivyose­mekana, kwa sababu ya kujua kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu maudhi atakayopambana nayo kutoka kwa wenye inadi.

Basi litapopulizwa barugumu; siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu; kwa makafiri haitakuwa nyepesi.

Ni kama mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ ﴿١٠١﴾

“Basi itakapopuziwa parapanda, Juz. 18 (23:101).

Baada ya Mwenyezi Mungu kumwamuru Mtume wake kuwa na uvumilivu kutokana na adha ya wakadhibishaji, sasa anawahadharisha na Siku ya Kiyama ambayo itakuwa ngumu na kali sana kwao; itakuwa nzito isiyofu­atiwa na wepesi. Yametangulia makumi ya Aya kuhusiana na aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu kwa wakosefu; yakiwemo chakula, kinywaji na adhabu kali.

ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا ﴿١١﴾

11. Niache peke yangu na niliye­ muumba.

وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَّمْدُودًا ﴿١٢﴾

12. Na nikamjaalia kuwa na mali mengi.

وَبَنِينَ شُهُودًا ﴿١٣﴾

13. Na wana wanaoonekana.

وَمَهَّدتُّ لَهُ تَمْهِيدًا ﴿١٤﴾

14. Na nikamtengenezea mipan­go.

ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ ﴿١٥﴾

15. Kisha anatumai nimzidishie!

كَلَّا إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا ﴿١٦﴾

16. Sivyo! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!

سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا ﴿١٧﴾

17. Nitamtesa kwa mateso ya hali ya juu.

إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ ﴿١٨﴾

18. Hakika yeye alifikiri na akapima.

فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ ﴿١٩﴾

19. Basi amelaaniiwa! Vipi alivyopima!

ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ ﴿٢٠﴾

20. Tena amelaaniiwa! Vipi alivyo pima!

ثُمَّ نَظَرَ ﴿٢١﴾

21. Kisha akatazama.

ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ ﴿٢٢﴾

22. Kisha akakunja uso na aka­nuna.

ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ ﴿٢٣﴾

23. Kisha akageuka, na akatak­abari.

فَقَالَ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ ﴿٢٤﴾

24. Akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulionukuliwa.

إِنْ هَـٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ ﴿٢٥﴾

25. Haya si chochote ila ni kauli ya binadamu.

سَأُصْلِيهِ سَقَرَ ﴿٢٦﴾

26. Nitamtia kwenye Saqar.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ ﴿٢٧﴾

27. Na nini kitakujulisha ni nini Saqar?

لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ ﴿٢٨﴾

28. Haubakishi wala hauachi.

لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ ﴿٢٩﴾

29. Unababua ngozi.

عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ ﴿٣٠﴾

30. Juu yake wapo kumi na tisa.

وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ ﴿٣١﴾

31. Na hatukuwafanya walinzi wa Moto ila Malaika, Wala hatukufanya idadi yao ila kuwa jaribio kwa wale waliokufuru. Ili wawe na yakini waliopewa Kitabu na wazidi imani wale walioamini, wala wasiwe na shaka wale waliopewa Kitabu na waumi­ni, na wapate kusema walio na maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye na humwongoza amtakaye. Na hapana ajuae majeshi ya Mola wako ila Yeye. Na huo si chochote ila ni ukumbusho kwa watu.

NIACHE PEKE YANGU NA NILIYEMUUMBA

Aya 11 - 31

KISA KWA UFUPI

Walid bin Al-Mughira Al-Makhzumi, alikuwa ni miongoni mwa vigogo wa kikuraishi, akiwa na mali nyingi na watoto. Siku moja akamsikia Mtume akisoma Aya mojawapo ya Qur’an, akasema: “Hii sio maneno ya binadamu wala jinni. Wallah, hakika kauli yake ‧ yaani Qur’an ‧ ina utamu na ina mvuto na kwamba juu yake kuna matunda na chini yake kumejaa. Hakika iko juu na haishindwi.”

Basi makuraishi waliposikia hivi waka­hofia maneno ya Walid kama yakienea kwa watu, watamwamini Muhammad(s.a.w.w) . Wakamtaka Walid ampinge Mtume. Akasema nisemeje sasa? Niseme ni mwendawazimu, nani ataamini? Au niseme ni kuhani, naye hakuwahi kuwa kuhani kabisa.

Nikisema ni mshairi, yeye hajawahi kutamka shairi na nikisema ni mwongo, hakuna yeyote aliyewahi kusikia uwongo kwake. Kisha akafiria akaona ampe sifa ya uchawi na kwamba yeye ameichukua Qur’an kutoka kwa wachawi.

MAANA

Niache peke yangu na niliyemuumba.

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Makusudio yake ni kumkemea na kumhadharisha Walid bin Mughira kwa maafikiano ya wafasiri. Maana ni kuwa niachie mimi huyo ewe Muhammad, usijishughulishe naye, wala na yale anayokuzulia. Mimi peke yangu ndiye nitakayempiga vita na kumpa adhabu.

Mwenyezi Mungu alifikia ghadhabu hii kwa Walid, kwa sababu yeye alip­ituka mipaka na uovu; akakufuru neema ya Mwenyezi Mungu na akaipin­ga haki na kuifanyia kiburi haki na watu wake. Kila mwenye kuipinga haki basi ni mlengwa wa ghadhabu hii na makemeo haya; kama vile Walid Bin Mughira, kwa vile sababu ya kushuka Aya haihusiki na aliyeteremshiwa tu, bali inaenea, kama tulivyosema mara nyingi.

Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:Na nikamjaalia kuwa na mali mengi, inaashiria kuwa linasobabisha na kuleta msukumo wa kufanya uovu ni utajiri na wingi wa mali. Aya kadhaa zianaashria hakika hii, ikiwemo Aya 11 ya sura iliyopita na pia kauli yake Mwenyezi Mungu akimsimulia muasi aliyojifaharisha kwa mtu mwema:

أَنَا أَكْثَرُ مِنكَ مَالًا ﴿٣٤﴾

“Mimi nimekushinda kwa mali” Juz. 15 (18:34).

Inatosha kuwa ni ushahidi wa hayo kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾ أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾

“Hakika mtu hupituka mipaka, kwa kujiona amejitosheleza.” (96:6-7).

Kwa kutegemea Aya hizi na nyingine zilizo mfano wake, inawezekana kusema, ijapokuwa ni kwa kubuni, kwamba asili ni kuwa kila tajiri ni muasi, mpaka ithibitike kinyume. Imelezwa kwenye Nahjul-balagha: “Ni uzuri ulioje wa matajiri kuwanyenyekea mafukara kwa kutaka yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu! Na uzuri zaidi kuliko huo ni maringo ya mafukara kwa matajiri kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu.”

Kuna Hadith isemayo: “Heri zote ni za aliyesilimu na ikawa maisha yake ni kutosheka.. ewe Mwenyezi Mungu mruzuku Muhammad na kizazi cha Muhammad kujichunga na kutosheka.”

Na wana wanaoonekana , wakiwa pamoja naye wakishindana kumhudu­mia.Na nikamtengenezea mipango . Nimemsahilishia njia ya jaha na mali akiogelea kwenye neema atakavyo.

Kwa mnasaba huu tunaashiria kwamba neema za dunia hazifahamishi kuridhiwa na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Hakika maisha ya dunia ni mchezo na upuzi tu.” Juz. 26 (47:36). Kwenye Hadith amesema: “ Lau dunia mbele ya Mwenyezi Mungu italinganishwa na kheri kwa ubawa wa mbu, basi kafiri asingekunywa hata tama moja la maji.”

Ilijitokeza dunia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, mbora wa viumbe wa Mwenyezi Mungu, akaikataa, lakini Walid, muovu wa viumbe wa Mwenyezi Mungu, ilikithiri mali yake,kisha anatumai nimzidishie ! Yaani ana tamaa ya kuzidishiwa mali yake ili azidi uovu na uadui.

Haiwezekani kuchanganyika wema na tamaa katika moyo mmoja. Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) anasema: “Tamaa ni ufunguo wa kila maasi na ni msingi wa kila hatia na ni sababu ya kuanguka mambo mema.”

Sivyo! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!

Tokomea mbali ewe mpinzani mwenye hiyana! Hivi una tamaa kwa Mungu na wewe unaifanyia inadi haki na kuizuia kwa kutangaza vita kwa watu wa haki? Wapokezi wanasema kuwa iliposhuka tu Aya hii Walid alibadilika kutoka kwenye enzi na kuwa dhalili, utajiri kuwa fukara, na akafa na hali mbaya.

Amesema kweli aliyoesema: “Hawakusema watu kwa jambo lolote kuwa lina heri ila kuna shari iliyofichwa na nyakati.” Hii ni duniani, ama malipo yake huko Akhera yanaelezwa na Aya hii:

Nitamtesa kwa mateso ya hali ya juu.

Hali ya juu inaweza kuwa ni ukali na mashaka na inaweza kuwa ni zaidi. Mfumo wa maneno unajulisha maana zote mbili na kwamba adhabu siku hiyo itazidi kiwango na kiaina, muda baada ya muda.

Hakika yeye alifikiri na akapima.

alifikiria kuhusu Qur’an na akaandaa kauli ya uzushi kwamba Qur’an ni uchawi ulionukuliwa, kama itakavyokuja mbele.

Basi amelaaniwa! Vipi alivyopima! Tena amelaaniwa! Vipi alivyopima!

Amelaaaniwa kisha akalaaniwa katika kufikiria kwake na kupanga kwake kauli, vitendo na makusudio yake yote. Hakuna kitu kinachofahamisha ufasaha zaidi kuliko kukaririka laana kwa waovu.

Kisha akatazama . Baadaa ya kufikiria aliinua jicho lake kwa vigogo wa kikuraishi,kisha akakunja uso , kwa kukunja nyusi zakena akanuna ; uso ukamuiva.

Kisha akageuka, na akatakabari.

Alihakikisha alipofikiria kuwa Qur’an ni haki isiyokuwa na shaka, lakini pamoja na hayo aliipinga na akaitukukiaakasema: “Haya si chochote ila ni uchawi ulionukuliwa. Haya si chochote ila kauli ya binaadamu ,” aliyoichukua Muhammad kutoka kwa makuhani wa kichawi.

Picha hii ya Walid iliyopigwa na Qur’an, ya kufikiri, kupima, kukunja uso na kununa, inatujulisha kuwa yeye alikuwa hana la kufanya katika kupanga uwongo kwenye jambo analoliamini kuwa ni haki na kweli.

Nitamtia kwenye Moto waSaqar . Atakayetiwa ni huyo huyo Walid. Saqar ni miongoni mwa majina ya Jahannam.Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto waSaqar ? Kwani umefika kikomo cha kutisha; miongoni mwayo ni kwamba huohaubakishi yeyote katika wakosefuwala hauachi aina yoyote ya adhabu ila inawashushia naunababua ngozi .

Makusudio ya kubabua hapa ni kuiva, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا ﴿٥٦﴾

“Kila zitakapoiva ngozi zao, tutawabadilisha ngozi nyingine.” Juz. 5 (4:56).

Juu yake wapo kumi na tisa.

Yaani juu ya hiyo Saqar. Kumi na tisa ni walinzi wa Jahannam. Je, kumi na tisa ni idadi, au aina au ni viongozi? Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.

Kuna riwaya isemayo kuwa Abu Jahl, aliwaambia makuraishi: ‘’Hamna maana ninyi! Hivi watu kumi katika nyinyi wanashindwa kumshika mmoja katika hao 19?”

Mmoja alieyitwa Abul-Mushid alisema: “Mimi peke yangu nitawatoshea na 17, nyinyi shikeni wawili tu.” Huyu alisema kwa madharau kama alivyosema Abu Jahl.

Na hatukuwafanya walinzi wa Moto ila Malaika.

Walinzi wa moto si katika aina ya binadamu; bali ni malaika wakali wenye nguvu; hakuna anayewazidi nguvu isipokuwa aliye pekee, Mwenye nguvu ambaye ameumba kila kitu.

Kama kwamba muulizaji ameuliza: Nini makusudio ya kutajwa idadi, jambo ambalo linafungua mlango wa madharau kwa wapinzani? Ndio aka­jibu Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwamba kutaja kwake kuna faida tatu:

1.Wala hatukufanya idadi yao ila kuwa jaribio kwa wale waliokufuru.

Ndio! Mwenyezi Mungu anajua kwamba washirikina watakaposikia idadi watacheka na kufanya stihizai, lakini pamoja na hayo ametaja, kwa sababu haki inapaswa itangazwe, hata kama natija yake ni madharau ya wanaod­harau. Kwa maneno mengine ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawa­jaribu waja, naye ni mjuzi zaidi kuliko nafsi zao. Anawajaribu kwa raha na dhiki. Vile vile anasema haki ili vijitokeze vitendo vyao vinavyostahiki thawabu na adhabu.

Kutajwa idadi kumedhihirisha hakika ya washirikina ya kudharau ghaibu, hivyo wakastahiki ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu; kama kulivyodhihirisha hakika ya waumini wakastahiki radhi za Mwenyezi Mungu na thawabu zake, kama yatakavyokuja maelezo. Zaidi ya hayo ni kuwa kutangaza Mtume neno la haki bila ya kuangalia yatakayompata kwa ajili yake, ni dalili mkataa kwamba hana jingine analolitaka isipokuwa kui­hakikisha haki na kuibatilisha batili.

2.Ili wawe na yakini waliopewa Kitabu.

Ulama wa kiyahudi na wa kinaswara wakati huo walishuhudia kwa imani na yakini kwamba walinzi idadi yao ni 19, kwa sababu hilo linaafikiana na waliyoyasoma katika Tawrat na Injil.

3.Na wazidi imani wale walioamini.

Wahyi wa mambo ya ghaibu unawazidisha makafiri upinzani na jeuri na waumini wanazidi imani. Imesemekana kuwa waumini huzidi yakini waki­ambiwa na watu wa Kitabu kuwa idadi imo kwenye vitabu vyao. Usawa ni kuwa kila Aya katika Aya zake Mwenyezi Mungu Mtukufu inawazidisha waumini yakini kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake; ni sawa watu wa Kitabu wakubali au wapinge. Ni kweli kwamba kukubali kwao ni hoja kwa wapinzani.

Wala wasiwe na shaka wale waliopewa Kitabu na waumini.

Huu ni ufafanuzi na msisitizo wa yaliyokuwa kabla yake, kwa sababu kutokuweko shaka ni kuwa na yakini na kuzidi imani.

Na wapate kusema walio na maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu?

Vile vile huu ni ufafanuzi na msisitizo wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Wala hatukufanya idadi yao ila kuwa jaribio kwa wale walioku­furu,” pamoja na kufafanua aina ya makafiri ambao ni wanafiki walio na maradhi katika nyoyo zao. Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:26).

Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye na humwongoza amtakaye.

Mwenye kufuata njia ya upotevu Mwenyezi Mungu humpoteza:

فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ ﴿٥﴾

“Walipopotoka, Mwenyezi Mungu alizipotoa nyoyo zao.” Juz. 28 (61:5).

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ﴿١٠﴾

“Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi.” Juz. 1 (2:10).

Na mwenye kufuata njia ya uongofu Mwenyezi Mungu humuongoza: “Na ambao wameongoka anawazidishia uongofu.” Juz. 26: (47:17).

Umetangulia mfano wake katika Juz. 22 (35:8).

Na hapana ajuae majeshi ya Mola wako ila Yeye.

Askari wa Mwenyezi Mungu sio wale 19 tu, viumbe wote wanatii matak­wa hata wanyama, wadudu, ndege, upepo, matetemeko, matufani na men­gineyo ambayo hakuna anayejua isipokuwa mwanzishaji wa viumbe na mrudishaji.

Na huo si chochote ila ni ukumbusho kwa watu.

Huo ni huo moto wa Saqar. aliyoumba Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kuwa­hadharisha nao ili wayaogope maasi kwa ndani na nje.


24

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

كَلَّا وَالْقَمَرِ ﴿٣٢﴾

32. Sivyo! Naapa kwa mwezi!

وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ ﴿٣٣﴾

33. Na kwa usiku unapokucha!

وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ ﴿٣٤﴾

34. Na kwa asubuhi inapopam­bazuka!

إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ ﴿٣٥﴾

35. Hakika huo ni mojawapo ya mambo makubwa!

نَذِيرًا لِّلْبَشَرِ ﴿٣٦﴾

36. Ni onyo kwa watu.

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ ﴿٣٧﴾

37. Kwa anayetaka miongoni mwenu kwenda mbele au kurudi nyuma.

كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ ﴿٣٨﴾

38. Kila nafsi iko kwenye rahani kwa iliyoyachuma.

إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ ﴿٣٩﴾

39. Isipokuwa watu wa kuliani.

فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٤٠﴾

40. Watakua katika mabustani wakiulizana.

عَنِ الْمُجْرِمِينَ ﴿٤١﴾

41. Kuhusiana na wakosefu.

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ ﴿٤٢﴾

42. Ni kipi kilichowapeleka Motoni?

قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ ﴿٤٣﴾

43. Watasema: Hatukuwa mion­goni mwa waliokuwa wak­iswali.

وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ ﴿٤٤﴾

44. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini.

وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na tulikuwa tukijiingiza pamoja na wanaojiingiza.

وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿٤٦﴾

46. Na tulikuwa tukikadhibisha siku ya hukumu.

حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ ﴿٤٧﴾

47. Mpaka ikatujia yakini.

وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿٤٦﴾

46. Basi hautawafaa uombezi wa waombezi.

حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ ﴿٤٧﴾

47. Basi wana nini wanapuuza ukumbusho huu?

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ ﴿٤٨﴾

48. Kama kwamba wao ni punda waliotimuliwa.

فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ ﴿٤٩﴾

49. Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?

كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ ﴿٥٠﴾

50. Kama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa,

فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍ ﴿٥١﴾

51. Wanaomkimbia simba!

بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً ﴿٥٢﴾

52. Bali kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo­funuliwa.

كَلَّا بَل لَّا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ ﴿٥٣﴾

53. Sivyo! Bali hawaiogopi Akhera.

كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ ﴿٥٤﴾

54. Sivyo! Kwa hakika hiyo ni ukumbusho.

فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ ﴿٥٥﴾

55. Basi atakaye ataukumbuka.

وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ ﴿٥٦﴾

56. Na hawatakumbuka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu.

TUKIJIINGIZA PAMOJA NA WANAOJIINGIZA

Aya 32 – 56

MAANA

Na hawatakumbuka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu.

Sivyo! Komeni enyi washirikina kucheza na moto na kuwadharau walinzi wake.

Naapa kwa mwezi na kwa usiku unapokucha na kwa asubuhi inapopambazuka. Hakika huo ni mojawapo ya mambo makubwa.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwakemea wapinzani, sasa anaapa kwa mwezi, usiku na mchana kwamba Moto ni kweli isiyokuwa na shaka na ni adhabu ambayo haina mfano na hakuna adhabu nyingine inayoishinda hiyo. Kuapa kwa maumbile haya ni kuashiria kuwa wenye busara wanap­ata dalili ya mtengenezaji kutokana na ubunifu wa utengenezaji, na kwam­ba mwenye kufanya kitu bila ya chochote, anaweza kuipa uhai mifupa iliyochakaa.

Ni onyo kwa watu, kwa anayetaka miongoni mwenu kwenda mbele au kurudi nyuma.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewahadharisha waja na moto na akawafa­hamisha njia yake na kuwambia jichagulieni wenyewe kuundea au kuwa mbali nao. amejitoa lawamani Mwenye kuonya.

Kila nafsi iko kwenye rahani kwa iliyoyachuma.

Hii ni sababu ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa anayetaka kwenda mbele au kurudi nyuma. Maana ni kuwa jichagulieni wenyewe, nyinyi mmefungika kwenye rahani ya mliyoyafanya na mna deni la mliyoyatanguliza; ikiwa ni heri basi mtalipwa heri na ikiwa ni shari basi ni shari. Umetangulia mfano wake katika Juz. 21 (30:44).

Isipokuwa watu wa kuliani.

Qur’an inawaita watu wa upande wa kulia wale wanaomcha Mungu na wakosefu inawaita watu wa upande wa kushoto, Tazama Juz. 27 (56: 8-9, 38-41).

Maana ni kuwa hakuna mtu yeyote ila nafsi yake inakuwa ni mateka wa matendo yake; isipokuwa wenye takua, wao wamelipa madeni yao na wamezifungua nafasi zao kwa matendo yao mema, na malipo yao ni Bustani za milele zinazopitiwa na mito.

Watakua katika mabustani wakiulizana kuhusiana na wakosefu: Ni kipi kilichowapeleka Motoni.

Baada ya kutulia watu wa Peponi wataulizana wenyewe kwa wenyewe: Wako wapi wakosefu waliokuwa wakitupa tabu?

Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawaonyesha walipo katika Jahannam, ili wazi­di furaha, kama yalivyoeleza baadhi ya mapokezi.

Atawauliza kwa kuwatahayariza: ni jambo gani lililowapeleka kwenye makazi haya?Watasema kwa lugha ya hali au ya maneno:Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakiswali . Yaani hatukuacha machafu na maovu duniani. Tafsiri hii tumeichukua katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ﴿٤٥﴾

“Hakika Swala inakataza machafu na maovu.” Juz. 21 (29:45)

Wala hatukuwa tukiwalisha masikini, bali tulilimbikiza mali bila ya kuyatoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.Na tulikuwa tukijiingiza pamoja na wanaojiingiza.

Makusudio ya kujiingiza hapa ni kupiga porojo. Maana ni kuwa tukidha­rau kila jambo isipokuwa upuzi na mchezo na tukijiingiza kila mahali isipokuwa kwenye haki na kheri.

Na tulikuwa tukikadhibisha siku ya hukumu, mpaka ikatujia yakini, yaani mauti.

Neno hukumu tumelifasiri kutokana neno Din. Sheikh Abdul-Qadir Al-Maghribi anasema: “Siku ya Kiyama imeitwa hivyo kwa sababu ndani yake mna malipo, hisabu na hukumu. Yote haya ni katika maana ya neno din. Vile vile inaitwa siku ya ufufuo, kuhukumiwa watu, mlipaji na hakimu.

Wamesema Ali bin Abi Twalib ni hakimu wa umma huu baada ya Nabii; yaani baada ya Nabii(s.a.w.w) yeye alikuwa na aina ya pekee ya kuhukumu baina ya mahasimu. ( kwa kutumia neno din kwa maana ya hukumu)”

Basi hautawafaa uombezi wa waombezi

Hakuna muombezi atakayefaa wala udhuru utakaokubalika, isipokuwa toba na matendo mema.

Basi wana nini wanapuuza ukumbusho huu; kama kwamba wao ni punda waliotimuliwa, wanaomkimbia simba.

Wanaambiwa washirikina, makusudio ya ukumbusho ni Qur’an na punda ni wa mwituni. Maana ni kuwa wananini hawa wanakimbia uongofu na haki kama wanaokimbia mauti?

Bali kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizofunuliwa.

Kuna riwaya isemayo kuwa washirikina walimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu: “Hatutakuamini mpaka umteremshie kila mmoja wetu waraka usemao fulani bin fulani mfuate Muhammad(s.a.w.w) .”

Iwe sawa riwaya hii au la, lakini inafasiri dhahiri ya Aya. Hilo linatiliwa nguvu na Aya isemayo:

وَلَن نُّؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَابًا نَّقْرَؤُهُ ﴿٩٣﴾

“Na hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie Kitabu tukisome.” Juz. 15 (17:93).

Lakini wao hawawezi kuamini hata kama wangeliitikiwa matakwa yao, kama ilivyoliweka wazi hilo kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَابًا فِي قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ لَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٧﴾

“Na lau tungelikuteremshia maandishi katika karatasi na wakayagusa kwa mikono yao, bila shaka wale waliokufuru wangelisema: Haya si chochote ila ni uchawi dhahiri.” Juz. 7 (6:7).

Siri katika hilo ni kupupia kwao masilahi yao na mambo yao na wala sio hasadi, kama walivyosema baadhi ya wafasiri. Dalili ya hayo tuliyoyasema ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyokuja moja kwa moja:Sivyo! Bali hawaiogopi Akhera . kwa sababu wao hawajui isipokuwa maisha ya dunia wala hawategemei isipokuwa anasa zake na starehe. Ama ubinadamu, haki na heri kwao ni maneno yasiyokuwa na maana.

Sivyo! Kwa hakika hiyo ni ukumbusho.

Mara nyingine tena Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawakemea wakadhibisha­ji na kuwabainishia kuwa hii Qur’an ni mawaidha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa waja wake na wala sio kauli ya mchawi wala mshairi.

Basi atakaye ataukumbuka.

Yaani atanufaika na hukumu zake na mawaidha yake.

Na hawatakumbuka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu.

Unaweza kuuliza : Kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘atakaye ataukumbuka,’ inaonyesha kuwa mtu ana hiyari ya uhuru wake na utashi wake. Na kauli hii ‘Hawatakumbuka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu,’ inaonyesha kuwa mtu hana hiyari, anaendeshwa na hana uhuru wala utashi; sasa ni vipi mgongano huu?

Jibu : Makusudio ya matakwa ya kwanza, ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemwachia mtu hiyari ya kujichagulia imani au ukafiri. Na makusudio ya ya matakwa ya pili ni kuwa mpinzani anayekana hawezi kuamini mpaka Mwenyezi Mungu amlazimishe kwa nguvu. Kwa hiyo maana ya kauli mbili ni kuwa Mwenyezi Mungu amemwamchia mtu hiyari ya kuamini au kukufuru; kama isemwavyo kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ فَمَن شَاءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَاءَ فَلْيَكْفُرْ ﴿٢٩﴾

“Sema hii ni kweli itokayo kwa Mola wenu, basi atakaye aamini na atakaye akufuru.”

Juz. 15 (18:29).

Lakini mpinzani mwenye inadi hawezi, kwa hali yoyote ile, ila akifany­ishwa kwa nguvu na Mwenyezi Mungu; na hili haliwezi kuwa kabisa, kwa vile linapingana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu na hikima yake. Kwa sababu uadilifu wake Mwenyezi Mungu Mtukufu na desturi yake kwa waja wake, ni kuwabainishia njia ya heri na kuwahimiza na kuwabinishia njia ya shari na kuwahadharisha nayo.

Kwa hiyo kila mmoja anakuwa na hiyari yeye mwenyewe ya mwishilio wake; vinginevyo thawabu na adhabu zitakua hazina maana yoyote.

Hili linaungwa mkono na kauli yake Mwenyezi Mungu iliyokuja moja kwa moja:

Takua ni kwake na maghufira ni yake.

Yaani yeye Mwenyezi Mungu ambaye imetukuka hikima yake, ndiye anayestahiki kutiiwa katika maamrisho yake na makatazo yake, na kuogopewa kwa ghadhabu yake na adhabu yake. Vile vile yeye ndiye mwenye kuwahurumia waja na kuwasamehe wanao­tubia na kurejea.

Kwa mnaeno machache na ya uwazi zaidi ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemuumba mtu akiwa na hiyari, mwenye akili na utashi, akamto­fautisha na mnyama kwa hilo; kwa hiyo akamkalifisha utiifu na msimamo. Kama angelitaka Mwenyezi Mungu angelimuondolea utashi wa akili na kumfanya kama mnyama au chini yake zaidi.

MWISHO WA SURA YA SABINI NA NNE: SURAT AL- MUDDATHIR


25

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sabini Na Tano: Al-Qiyama. Imeshuka Makka. Ina aya 40.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ ﴿١﴾

1. Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!

وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ ﴿٢﴾

2. Na ninaapa kwa nafsi inayoji­laumu!

أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُ ﴿٣﴾

3. Hivi anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?

بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُ ﴿٤﴾

4. Kwanini! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!

بَلْ يُرِيدُ الْإِنسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ ﴿٥﴾

5. Lakini mtu anataka afanye maovu mbele yake.

يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ ﴿٦﴾

6. Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?

فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ ﴿٧﴾

7. Basi jicho litakapofanya kiwi.

وَخَسَفَ الْقَمَرُ ﴿٨﴾

8. Na mwezi utapopatwa.

وَجُمِعَ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ﴿٩﴾

9. Na likakusanywa jua na mwezi.

يَقُولُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ الْمَفَرُّ ﴿١٠﴾

10. Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?

كَلَّا لَا وَزَرَ ﴿١١﴾

11. Sivyo! Hapana pa kukimbilia!

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمُسْتَقَرُّ ﴿١٢﴾

12. Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako.

يُنَبَّأُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ ﴿١٣﴾

13. Siku hiyo ataambiwa mtu aliy­oyatanguliza na aliyoy­aakhirisha.

بَلِ الْإِنسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ ﴿١٤﴾

14. Bali mtu anajiona mwenyewe.

وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُ ﴿١٥﴾

15. Ingawa atatoa nyudhuru zake.

لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ ﴿١٦﴾

16. Usiitikisie ulimi wako kwa kuifanyia haraka.

إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ ﴿١٧﴾

17. Hakika ni juu yetu kuiku­sanya na kuisoma.

فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ ﴿١٨﴾

18. Hivyo tunapoisoma, basi fuatiliza kusoma kwake.

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ ﴿١٩﴾

19. Kisha ni juu yetu kuibainisha.

KIAPO KWA SIKU YA KIYAMA

Aya 1 - 19

MAANA

Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!

Yaani ninaapa kwa hiyo siku. Tafsiri hii ni ikiwa herufi la` ni ziada kiirabu ya nahw, kama walivyosema wafasiri wengi. Lakini ikiwa ni ya kukanusha kama walivyoona wengine, basi tafsiri yake itakuwa: Siapi kwa siku ya Kiyama; yaani hakuna haja kamwe ya kufanya hivyo, kwa sababu inaeleweka wazi. Kwa tafsiri zote mbili kuna maneno ya kukadiriwa ambayo ni hakika nyinyi mtafufuliwa kwa umbo jipya.

Na ninaapa kwa nafsi inayojilaumu!

Wafasiri wana kauli nyingi kuhusiana na maana ya nafsi inayojilaumu. Tuonavyo sisi ni kuwa mara nyingi sana mtu hujilaumu kutokana na matendo aliyoyafanya au kuyaacha yeye mwenyewe, baada ya kum­bainikia kuwa kufanya au kuacha kunamletea madhara ya kiafya, kama vile kula chakula alichokatazwa; au hasara aliyoipata kutokana na bei aliy­oifanya na mengineyo katika madhara ambayo hayana uhusiano na dini au muumba wake kwa namna yoyote ile. Haya sio maana yaliyokusudiwa hapa katika nafsi inayojilaumu.

Mara nyingine mtu anaweza kuhisi majuto na masikitiko kutokana na kuk­iuka miko ya haki na kupuuza kufanya heri; ni sawa awe amefanya hivyo kwa makusudi na kujua au amefanya bila ya kujua na kutokusudia; kisha ikambainikia hakika, kama itakavyokuwa hali ya kafiri Siku ya Kiyama. Maana haya ndiyo yaliyokusudiwa hapa kuhusu nafsi yenye kujilaumu.

Hivi anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? Kwanini! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!

Wanaokanusha ufufuo wanasema ni muhali kupata uhai mifupa iliyokuwa mchanga. Wameyasema hayo kwa mifumo mbali mbali, na Mwenyezi Mungu naye akawajibu kwa aina mbali mbali ya mifumo; miongoni mwayo ni Aya hii tunayoifasiri.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu ndiye atakayeikusanya na kuipa uhai, wala hakuna ajabu katika uweza wake Mtukufu asiyeshindwa na chochote. Fauka ya hayo Yeye atairudisha mifupa kwa ukamilifu, kama ilivyokuwa, hata ile midogo na myembamba; kama vile mifupa ya vidole vya mkono, itarudi kama ilivyokuwa, pamoja na ngozi yake, rangi yake na nywele; bali hata alama za vidole zilizokuwako.

Hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi. Kwa sababu yule aliyepangilia mwanzo na kuzifanya alama za vidole zitofautiane kutoka mtu mmoja hadi mwingine, kuanzia binadamu wa kwanza hadi wa mwisho, ni wepesi zaidi kwake kuzirudisha kama zilivyokuwa kwa sifa zake zote. Kwa sababu kutofautiana alama za vidole kwa mfano huu ni dalili ya nguvu zaidi juu ya uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko kuirudisha mifupa na wafu.

Lakini mtu anataka afanye maovu mbele yake.

Maovu ni madhambi, mbele yake ni kuendelea. Kwa hiyo basi makusudio ya mtu hapa yatakuwa ni muovu mwenye dhambi. Ujumla wa maana ni kuwa mwenye dhambi huyu anataka kuendelea na dhambi zake mpaka siku yake ya mwisho. Ndio maanaanauliza kwa madharau:Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama ni mbali au karibu?

Basi jicho litakapofanya kiwi, Na mwezi utapopatwa, na likakusany­wa jua na mwezi.

Mwenye inadi aliuliza ni lini Kiyama? Ndio Mwenyezi Mungu akazitaja sifa zake, jicho litaduwaa mwanga wa mwezi utaondoka na kugongana na mwezi kutokana na kuharibika nidhamu ya ulimwengu.

Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio kulikimbia janga hili? Sivyo! Hapana pa kukimbilia! Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako. Yeye peke yake ndiye marejeo ya waja siku hiyo na viumbe wote watanyenyekea kwenye hukumu yake.

Siku hiyo ataambiwa aliyoyatanguliza na aliyoyaakhirisha.

Makusudio ya aliyoyatanguliza ni aliyoyafanya katika heri na shari, na aliyoyaahirisha ni aliyoyaacha katika wajibu uliofaradhishwa kwake, maana ni kuwa mtu atakaposimama mbele ya Mola wake kesho kwa his­abu, yatamfunukia matendo yake yote ya heri na shari kuanzia mwanzo hadi mwisho wake. vile vile yata mfunukia majukumu aliyoyaacha.

Bali mtu anajiona mwenyewe, ingawa atatoa nyudhuru zake.

Kila mtu anajijua, anayajua aliyoyafanya na aliyoyaacha wala haihitajii kuambiwa. Yeye anajua tu hata kama atajaribu kutoa vijisababu.

Usiitikisie ulimi wako kwa kuifanyia haraka. Hakika ni juu yetu kuikusanya na kuisoma. Hivyo tunapoisoma, basi fuatiliza kusoma kwake. Kisha ni juu yetu kuibainisha.

Maneno yanaaza upya, kama ilivyo kawaida ya Qur’an kutoka kwenye maudhui moja hadi nyingine; iwe kuna jambo la kunasibiana au hakuna. Imam Ja’far As-Sadiq(a.s ) anasema: “Aya moja inaweza kuwa na jambo mwanzo wake na mwisho wake ni jambo jingine.”

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume(s.a.w.w) . Ni juu yetu kuikusanya yaani kuikusanya kwenye moyo wako. Tunapoisoma, yaani tunapoimaliza kuisoma.

Ujumla wa maana ni kuwa Jibril anapokusomea Qur’an, ewe Muhammad, usiwe na haraka ya kusoma kwa kuhofia kukupita kitu, sisi tutaifanya kamili katika moyo wako, mpaka akimaliza Jibril nawe anza kusoma. Ni juu yetu kukulinda usisahau wala kukosea kuisoma, au kubainisha hukumu yake na pia kuitumia.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:114).

كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ ﴿٢٠﴾

20. Sivyo! Bali nyinyi mnapenda ya sasa.

وَتَذَرُونَ الْآخِرَةَ ﴿٢١﴾

21. Na mnaacha Akhera.

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ ﴿٢٢﴾

22. Nyuso siku hiyo zitang’ara.

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ ﴿٢٣﴾

23. Zinamtazama Mola wake.

وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ بَاسِرَةٌ ﴿٢٤﴾

24. Na nyuso nyingine siku hiyo zitakunjamana.

تَظُنُّ أَن يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ ﴿٢٥﴾

25. Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.

كَلَّا إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِيَ ﴿٢٦﴾

26. Sivyo! Itakapofikia kwenye mitulinga.

وَقِيلَ مَنْ رَاقٍ ﴿٢٧﴾

27. Na pakasemwa: Nani wa kum­ganga?

وَظَنَّ أَنَّهُ الْفِرَاقُ ﴿٢٨﴾

28. Na akajua kuwa huko ndiko kufariki.

وَالْتَفَّتِ السَّاقُ بِالسَّاقِ ﴿٢٩﴾

29. Na utapoambatishwa muundi kwa muundi.

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمَسَاقُ ﴿٣٠﴾

30. Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako!

فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ ﴿٣١﴾

31. Basi hakusadiki, wala hakuswali.

وَلَـٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿٣٢﴾

32. Bali alikanusha, na akageuka.

ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰ أَهْلِهِ يَتَمَطَّىٰ ﴿٣٣﴾

33. Kisha akenda kwa watu wake kwa matao.

أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ ﴿٣٤﴾

34. Ole wako, tena ole wako!

ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ ﴿٣٥﴾

35. Kisha Ole wako, tena ole wako!

أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَن يُتْرَكَ سُدًى ﴿٣٦﴾

36. Hivi anadhani mtu kuwa ataachwa bure?

أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَىٰ ﴿٣٧﴾

Je, hakuwa ni tone la manii lililoshushwa?

ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٣٨﴾

38. Kisha akawa pande la damu, tena akamuumba na akam­linganisha sawa?

فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ ﴿٣٩﴾

39. Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke?

أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ ﴿٤٠﴾

40. Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?

MNAPENDA YA SASA

Aya 20 - 40

MAANA

Sivyo! Bali nyinyi mnapenda ya sasa, na mnaacha Akhera.

Ya sasa ni maisha ya dunia. Maneno yanaelekezwa kwa yule mwenye kuiuza dini yake kwa dunia yake na kuathirika na maisha yanayoisha badala ya yanayobakia, awe mwislamu au sio mwislamu. Aya iko wazi kwa hilo, haikubali taawili.

Nyuso siku hiyo zita ng’ara, zinamtazama Mola wake.

Shia Imamiya na Mu’tazila wamesema haiwezekeani Mungu kuonekana duniani wala Akhera, na wakasema vile vile kuwa kutazama hapa ni kwa akili sio kwa macho au ni kungoja, kwa maana ya kuwa zitangojea na kutazamia neema ya Mwenyezi Mungu na karama yake.

Ashaira wamejuzisha kumuona Mwenyezi Mungu kwa macho. Hayo tumeyazungumzia kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 1 (54-57) kifungu cha ‘Kumuona Mungu.’ Kwamba utafiti wa maudhui haya hauna faida, kiu­jumla wala kimahsusi na huenda ukaongeza mpasuko baina ya Waislam, na Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakumkalifisha nayo yeyote.

Vyovyote iwavyo ni kuwa wenye takua kesho watafufuliwa katika hali ya uso mwangavu wakiwa na furaha kwa fadhila aliyozowapa Mwenyezi Mungu.

Na nyuso nyingine siku hiyo zitakunjamana. Zitajua ya kuwa zitafiki­wa na livunjalo uti wa mgongo.

Wakosefu watakuwa kinyume kabisa na wenye takua; watafufuliwa waki­wa na nyuso zilizokunjana na kusinyaa na nyoyo zao zinazotetemeka kwa hofu ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (3:106).

Sivyo! Itakapofikia rohokwenye mitulinga, Na pakasemwa: Nani wa kumganga? Na mwenyeweakajua kuwa huko ndiko kufariki.

Aya hizi zinaelezea hali ya kukata roho na kufikiwa na mauti ambayo hataokoka nayo yeyote; awe Nabii, muovu, mdogo au mkubwa.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameanza na neno sivyo, baada ya kutangulia maneno bali nyinyi mnapenda dunia na kuiacha Akhera, kwa hiyo ikanasabiana kuyakemea hayo. Maana ni, ewe mkosefu acha kuathirika na ulimwengu unaoisha badala ya ule wa kubakia, na ukumbuke mauti yanay­ovunja dhati na kukata matamanio, kumbuka pumzi za mwisho wakati roho inapofika kooni, huku watu wako, baada ya kushindwa kukutibu wak­iuliza ni nani tabibu mzuri wa kukutibu, na wewe mwenyewe ukiwa na uhakika kuwa unayafikia mauti yasiyokuwa na tiba wala dawa

Na utapoambatishwa muundi kwa muundi.

Muundi mmoja wa anayekata roho utakuwa juu ya mwingine kutokana na shida ya kukata roho. Imesemekana kuwa ni kinaya cha kuelezea jambo gumu, kwa waarabu, wanasema kuhusina na jambo gumu: ‘limepandiwa na muundi.’

Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako.

Mwenye kufa hana kwengine kwa kwenda isipokuwa kwa Mungu tu. Miongoni mwa maneno ya Imam Ali(a.s ) , akisifia hali ya mwenye kuka­ta roho, anasema:

“Wakati yeye akiicheka dunia na dunia nayo inamcheka kutokana na kujisahau kwake. Mara wakati unamkanyaga kama mwiba, na siku zikaanza kudhoofisha nguvu zake na mauti yakianza kumkodolea macho kwa karibu, na huzuni ambayo hajawahi kuwa nayo ikaanza kumshika, na ugonjwa ukamshika… Muuguzaji akachoka na watu wake wakashindwa kuelezea ugonjwa wake…Hakika mauti yana uchungu usioweza kusifika au kuingia kwenye akili za watu wa dunia.”

Basi hakusadiki, wala hakuswali, bali alikanusha, na akageuka, kisha akenda kwa watu wake kwa matao.

Wafasiri wengi wamesema kuwa Aya hii ilishuka kwa Abu Jahl, nayo ni picha inayofuata asili ya sifa zake, kwa sababu hakumsadiki Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) wala hakuwahi kuswali hata kwa kupepesa jicho, bali alikadhibisha haki, akaivuruga, akaipinga na akaidharau. alikuwa akienda kwenye vikao vya Mtume(s.a.w.w) na kusikiliza Qur’an, kisha anarudi kwa watu wake kwa maringo.

Vyovyote itakavyokuwa sababu ya kushuka Aya ni kuwa dhahiri ya Aya inaenea kwa kila mwenye kuifanyia inadi haki na kuikalia juu, kwa sababu linalozingatiwa ni kuenea Aya, sio kuhusisha sababu.

Ole wako, tena ole wako! Kisha Ole wako, tena ole wako!

Lengo la kukaririka huku ni kuzidisha kuhadharisha na kiaga. Maana ni maangamizi na adhabu inakustahili wewe ewe mwenye dhambi.

Wafasiri wengi wamesema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alimshika mkono Abu Jahl na kumwambia:“Ole wako tena ole wako!” Mja wa laana huyu akasema: Unanitisha ewe Muhammad! Wallahi wewe huwezi kunifanya kitu wala Mola wako! Wallahi tena, hakuna anayenishinda katika bonde hili…”

Mtume alikuwa akasema: ‘Kila umma una Firauni wake na Firauni wa umma huu ni Abu Jahl.’ Naye aliuliwa kifo kibaya sana kwenye vita vya Badr.

Hivi anadhani mtu kuwa ataachwa bure?

Hatumjui yeyote anayefikiri na kudhania kuwa hana majukumu yoyote, kwa namna yoyote ile atakavyokuwa mjinga na mpotevu. Kama yuko mwenye kudhania hivi basi atakuwa amejishusha chini kufikia daraja ya wadudu na wanyama.

Lau Mwenyezi Mungu (s.w.t) angelimwacha bure bure angelikuwa Mwenyezi Mungu amefanya mchezo katika vitendo vyake. Ametakata Mwenyezi Mungu Mtukufu na hayo kabisa: “Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yao kwa mchezo.” Juz. 17 (21:16).

Je, hakuwa ni tone la manii lililoshushwa?

Huyu anayekanusha ufufuo, hakuwa ni maji tu yaliyomininwa kwenye mfuko wa uzazi,kisha akawa pande la damu, tena akamuumba na akamlinganisha sawa? Tone la manii lilikuwa umbo baada ya umbo ndani ya viza vitatu, kisha akatoka humo akiwa mtu kamili baada ya kuwa chini ya walio chini.

Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t) baada ya kulifanya tone la manii ni binadamu kamili, ametoa humo watoto wa kike na wa kiume.

Je! Huyo Mungu aliyyeyafanya maji hafifu kuwa ni mtu wa ajabu katika sura yake, akili yake na vipawa vyake na akatoa humo wanawake na watoto,hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?

Kwanini! Yeye ana uweza wa kila kitu na hakuna chochote kilichopo ila kinatamka uweza wake na kumsifu kwa sifa sifa zake. Wala kuumbwa mtu si kitu kulinganisha na kuumbwa ulimwengu:

لَخَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٧﴾

“Hakika umbo la mbingu na ardhi ni kubwa zaidi kuliko umbo la watu. Lakini watu wengi hawajui.” Juz. 24 (40:57).

Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 (22:5).

MWISHO WA SURA YA SABINI NA TANO: AL-QIYAMA


26

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sabini Na Sita: Al-Insan. Imeshuka Makka Ina 31. Imesemekana isiyokuwa hivyo.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

هَلْ أَتَىٰ عَلَى الْإِنسَانِ حِينٌ مِّنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْئًا مَّذْكُورًا ﴿١﴾

1. Je, kilimpitia binaadamu kipin­di katika zama ambacho hakuwa kitu kinachotajwa?

إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿٢﴾

2. Hakika tumemuumba mtu kutokana na tone la manii lililochanganyika, tumfanyie mtihani. Tukamfanya ni mwenye kusikia, mwenye kuona.

إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا ﴿٣﴾

3. Hakika tumemwongoza njia, ama awe ni mwenye kushuku­ru, au mwenye kukufuru.

إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَلَاسِلَ وَأَغْلَالًا وَسَعِيرًا ﴿٤﴾

4. Hakika tumewaandalia makafiri silsili na pingu na Moto mkali.

إِنَّ الْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا ﴿٥﴾

5. Hakika watu wema watakuny­wa katika glasi zilizochanganyi­ka na kafuri.

عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللَّـهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا ﴿٦﴾

6. Ni chemchem watakayoinywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiitiririsha mtiririko.

JE, KILIMPITIA BINADAMU KIPNDI

Aya 1 – 6

MAANA

Je, kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho hakuwa kitu kinacho tajwa?

Wamesema wafasiri kuwa herfi hal, tuliyoifasiri kwa maana ya je, ni ya uhakika, kwa maana ya hakika kilimpitia…

Aya hii iko katika picha ya swali na maana yake ni kusisitiza na kuhakik­isha. Lengo la Aya ni kuwa mtu anatakikana afikirie akilini mwake na kuji­uliza kuhusu uweza uliyomfanya yeye aweko baada ya kutokuweko. Ni kitu gani kimemfanya apatikane? Amepita vipi kutoka hali moja hadi nyingine? Je, anakwenda wapi?

Katika hili Imam Ali(a.s) anasema:“Amrehemu Mwenyezi Mungu mja aliyejua ametoka wapi, yuko wapi na anakwenda wapi.” Hili ndilo lengo la Aya hii. Ufuatao ni ufupi wa ufafanuzi wa yaliyoashiriwa na Aya hii na nyingine zinazofuatia katika hali ya kutoka mtu kwenye ngazi moja hadi nyingine mpaka kukamilika kwake. Ama kuhusu yuko wapi na anakwenda wapi tumekwisha fafanua huko nyuma katika kufasiri Aya za dunia na Akhera:­

1.Je, kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho hakuwa kitu kinachotajwa?

Ulipita muda mrefu sana ambao mtu hakuwa na atahari yoyote ya kuweko: “Je hakumbuki mtu ya kwamba tulimuumba kabla na hali hakuwa cho­chote?” Juz. 16 (19:67). Wataalamu wanasema kuwa mtu alipatikana hapa ardhini tangu miaka milioni 5: ” Na Mola wako anawajua vilivyo waliomo mbinguni na waliomo ardhini.” Juz. 15 (17:55).

2.Kisha Mwenyezi Mungu akamuumba Adam, baba wa watu, kutokana na udongo:

“Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kutokana na udongo.” Juz. 3 (3:59). Hapa aligura mtu kutoka hali ya kukosekana hadi kupatikana akiwa mchanga usiokuwa na uhai.

3.Hakika tumemuumba mtu kutokana na tone la manii lililochanganyika, tumfanyie mtihani.

Hii ni ishara ya kugura mtu kutoka udongo hadi kuwa majimaji, ambayo ni tone la manii lililokuwa kutokana na mfungamano wa aina mbali mbali ali­zoziashiria Imam Ali(a.s) kwa kauli yake:“Na jinsi yenye mchanganyiko wa udongo wa rangi tofauti, na vitu vyenye kufanana na kuafikiana, na vitu vilivyo kinyume visivyoafikiana, na viliyochanganyika vinavyobainika.”

Mingoni mwa atahari za udongo wa rangi tofauti ni tunavyomuona mtu akiwa na macho meusi na uso mweupe, katika vyenye kufanana na kuafikiana ni mifupa ya mikono na miundi na katika athari ya vilivyo kinyume visivyoafikiana ni mapenzi na chuki, tamaa na kukinai, kunyenyekea na kutakabari, mapambano ya akili na matamanio n.k. Hapa ndio tunapata tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Tumfanyie mtihani,’ pale anapopata mapambano makali mtu baina ya dhamiri yake na matamanio yake.

4.Tukamfanya ni mwenye kusikia, mwenye kuona.

Hii ni ishara ya kugura mtu kutoka tone la manii lililopata uhai ndani ya tumbo lake baada ya kupita siku kadhaa akiwa kwenye giza lisilokuwa na usikizi wala uoni hadi kwenye mng’ao pamoja na usikizi na uoni, lakini bila ya akili wala utambuzi, sawa na mnyama.

5.Hakika tumemwongoza njia, ama awe ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anaashiria kugura mtu kutoka kwenye maisha ya mnyama hadi kwenye maisha ya ubinadamu; yaani baada ya kutimia kwake kuwa mwili ulio na hisia, Mwenyezi Mungu akampa akili na utambuzi ili aweze kupambanua baina ya haki na batili na uongofu na upotevu. Vile vile amempa uhuru ili kwa akili yake na uhuru wake aweze kubeba majukumu na kustahiki thawabu na adhabu, baada ya kubainishiwa na kupewa hoja.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameuletea ibara ya shukrani, uongofu, kwa sababu ni kumtii Mwenyezi Mungu, na uovu akauita ukafiri kwa sababu ni kumuasi yeye.

Kwa ufafanuzi zaidi wa hayo tutaashiria hali ya uwiano baina ya mtu na viumbe vingine wa ardhini kwa ujumla: Viumbe hivi vinagawanyika kwenye viumbe vilivyotulia, vizisivyokuwa na uhai wala kukua; kama vile mchanga, miamba na madini, na viumbe vingine vyenye uhai. Vyenye uhai navyo vinagawanyika mafungu matatu:

1. Uhai wa mimea; hii ina harakati na kukua bila ya kuwa na hisia wala utambuzi. Kwa hiyo mimea haisikii wala haioni, pia haina akili.

2. Ni maisha ya wanyama; miongoni mwa sifa za wanyama ni kuwa na harakati, kukua, kuhisi, kusikia na kuona, lakini bila ya kuwa na akili wala utambuzi kwa aghlab, au utambuzi wa kimafungu sio wa kiujumla

3. Ni maisha ya kiutu; miongoni mwa sifa za mtu ni kuwa na harakati, kukua, kusikia kuona, fauka ya hayo anakuwa na utambuzi wa kimafungu na wa kiujumla; kwa hiyo anajua mengi yaliyokuwa na yatakayokuwa. Ni kwa utambuzi huu na maarifa haya ndio akawa tofauti na viumbe wengine wote wa ardhini.

Kwa hiyo basi mtu anakuwa na uwiano na vitu vilivyotulia, kwa vile yeye alikuwa mchanga, anaoana na mimea kwa vile alikuwa tumboni mwa mama yake akikua pole pole na kutaharaki bila ya kusikia wala kuona, na anawiana na wanyama kwa sababu alipokuwa mtoto alikuwa na hisia, kusikia na kuona, lakini bila ya utambuzi na akili. Kisha akatofautiana na vyote kwa akili na utambuzi. Kuanzia hapa ndio akawa anabeba majuku­mu na kustahiki thawabu na adhabu, kinyume na viumbe wengine.

Hapa inatakikana kujiuliza: Ni nani aliyemgurisha mtu kutoka kipindi cha kutokuwepo, hadi kwenye mchanga uliotulia, na kutoka hapo hadi mmea unaotaharaki, hadi kufikia mnyama mwenye usikizi na hatimae binadamu kamili mwenye akili inayompa habari ya yaliyopita na yatakayokuja, akaweza kutengeneza maendeleo, na kutawala viumbe vingi, hata mnyama mwenye usikizi na uoni? Je, hali hii na mengineyo yasiyokuwa na idadi yana tafsiri nyingine zaidi ya kuweko muumba mwenye uwezo ambaye akili zinashindwa kumuwazia na ndimi haziwezi kumsifia?

Baada ya Mwenyezi Mungu kuashiria majukumu ya mtu kwa kauli yake: “Hakika tumemwongoza njia, ama awe ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru,” amefuatilia kutaja aliyowaandalia makafiri kwa kusema:

Hakika tumewaandalia makafiri silsili na pingu na Moto mkali.

Silisili ni za miguu na pingu ni za mikono na moto ni wa mwili.

Hakika watu wema watakunywa katika glasi zilizochanganyika na kafuri.

Glasi ni chombo cha kioo cha kunywea. Pia neno hili hutumika kwa kiny­waji chenyewe, na haya ndiyo maana yaliyokusudiwa hapa. Wafsiri wengi wamesema kuwa kinywaji cha watu wa peponi kina harufu nzuri, kama harufu ya kafuri, na sisi tunasema kuwa mchanganyiko wa kafuri ni uhakika, kama inavyofahamisha dhahiri ya Aya. Ikiwa ladha ya kafuri duniani inachukiza, basi sio lazima ya Peponi nayo iwe hivyo hivyo. Pombe ya dunia inaleta uzito kichwani na maumivu, lakini kinywaji cha pombe ya Peponi:

لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ ﴿٤٧﴾

“Hakina madhara, wala hakiwamalizikii.” Juz. 23 (37:47).

Ibn Abbas anasema: “Kila lilichotajwa na Mwenyezi Mungu katika Qur’an kuhusu vilivyo Peponi, hakiko duniani isipokuwa jina tu.”

Ni chemchem watakayoinywa waja wa Mwenyezi Mungu, waki­itiririsha mtiririko.

Yaani itapita kadiri watakavyo, ni kiasi cha kutaka tu. Aya kadhaa zimekwishapita zinazosifia aliyowaandalia Mwenyezi Mungu waja wake wenye takua, na kwamba wao watastarehe humo starehe ambazo hakuna jicho lililowahi kuona wala siko lilowahi kusikia au kuwaziwa na moyo wa mtu. Na wakosefu nao wataadhibiwa kwa namna isiyosemeka wala kuwazika.

يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا ﴿٧﴾

7. Wanatimiza nadhiri, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea.

وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا ﴿٨﴾

8. Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na mateka.

إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّـهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا ﴿٩﴾

9. Hakika tunawalisha kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu tu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.

إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا ﴿١٠﴾

10. Hakika tunaogopa kutoka kwa Mola wetu siku ya kukunja uso yenye giza kali.

فَوَقَاهُمُ اللَّـهُ شَرَّ ذَٰلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا ﴿١١﴾

11. Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha.

وَجَزَاهُم بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا ﴿١٢﴾

12. Na atawalipa Bustani za hariri kwa vile walivyosubiri.

مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا زَمْهَرِيرًا وَلَا ﴿١٣﴾

13. Humo wataegemea juu makochi, hawataona humo jua kali wala baridi kali.

وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَالُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا ﴿١٤﴾

14. Na vivuli vyake vitanawiri juu yao, na mashada ya matunda yake yataning’inia chini chini.

وَيُطَافُ عَلَيْهِم بِآنِيَةٍ مِّن فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا ﴿١٥﴾

15. Na watapitishiwa vyombo vya fedha na bilauri za kioo.

قَوَارِيرَ مِن فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا ﴿١٦﴾

16. Kioo kinachotokana na fedha, wamezikadiria kwa vipimo.

وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا ﴿١٧﴾

17. Na humo watanyweshwa kikombe kilichochanganyika na tangawizi.

عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًا ﴿١٨﴾

18. Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil.

وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَّنثُورًا ﴿١٩﴾

19. Na watawazungukia wavulana wasiochakaa, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizotawanywa.

وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا ﴿٢٠﴾

20. Na utakapoyaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa.

عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا ﴿٢١﴾

21. Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao atawanywesha kinywaji safi.

إِنَّ هَـٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَاءً وَكَانَ سَعْيُكُم مَّشْكُورًا ﴿٢٢﴾

22. Hakika haya ni malipo yenu; na mahangaiko yenu yameshukuriwa.

HUWALISHA CHAKULA JUU YA KUKIPENDA KWAKE

Aya 7 – 22

MAANA

Baada ya kuashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t) baadhi ya yale aliyowaan­dalia watu wema kesho, hapa anasema wanastahiki hayo kutokana na sifa tatu:

1.Wanatimiza nadhiri.

Nadhiri kilugha ni ahadi, na kisharia ni kujilazimishaa mtu, aliyebaleghe na kuwa na akili timamu, kufanya jambo au kuliacha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; kutenda au kuacha kuwe kunamridhisha Mwenyezi Mungu; vinginevyo itakuwa sio nadhiri, kama wanavyosema wahakiki.

Tamko la nadhiri ni kusema mwenye kuweka nadhiri: Nimejilazimisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, au nimeweka nadhiri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Haiwezi kuwa nadhiri ikiwa hakuna mojawapo ya majina ya Mwenyezi Mungu; kama vile Mwingi wa rehema, Muumba, Muhuyishaji, Mfishaji n.k. Lau atasema: nimeweka nadhiri kuwa nitafanya jambo kadhaa, basi itakuwa ni mchezo.

Ahadi katika istilahi ya wanafiqh wengi, ni kusema yule mwenye kuweka ahadi: Ninamuahidi Mwenyezi Mungu, au nimejilazimisha kumwahidi Mwenyezi Mungu jambo fulani. Yamini ni kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu (kiapo). Yametangulia maelezo kuhusu Viapo katika Juz. 7 (5:59). Mwenyezi Mungu (s.w.t) anapenda na anamlipa thawabu kila mwenye kusadikisha na kufanya vizuri katika kitendo au kauli; ni sawa iwe ni kauli, ahadi, nad­hiri, kiapo, ushahidi au habari yoyote.

2.Na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea.

Wanamtii Mwenyezi Mungu katika kila kitu kuhofia siku ambayo shari yake inaenea kwa kila mwenye kumwasi Mwenyezi Mungu na akamhali­fu katika hukumu miongoni mwa hukumu zake.

3.Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yati­ma, na mateka.

Wanajitolea kila kizuri tena wakiwa wanakihitajia sana; mfano wake ni kauli ya Mwenyezi Mungu:

وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ﴿٩﴾

“Na wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.” Juz. 28 (59:9).

Mateka hapa, imesemekana ni mateka aliyetekwa na waislamu katika vita na maadui wa Mwenyezi Mungu na wa Uislamu. Imepokewa riwaya kuwa maswahaba walikuwa wakimpeleka mtu waliyemteka, basi mtume humk­abidhi kwa mmoja wa waislamu na kumwambia kaa naye vizuri. Akimchukua nyumbani kwake na kumtunza kuliko yeye mwenyewe na familia yake.

Hakika tunawalisha kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu tu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. Hakika tunaogopa kutoka kwa Mola wetu siku ya kukunja uso yenye giza kali.

Hatutaki malipo kutoka kwenu wala kwa mwingine; isipokuwa tunawal­isha na kujitolea kwa msukumo wa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kuhofia siku ya kuchunguzwa matendo na yenye vituko vingi. Waliyasema haya kwa lugha ya maneno na ya matendo au amewasemea Mwenyezi Mungu kwa kujua imani na ikhlasi iliyo nyoyoni mwao.

Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha.

Walihofia siku ya mkusanyiko wakapata kinga ya shari yake kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kumfanyia ikhlasi, wakabadilishiwa hofu yao kuwa amani, nyuso zao zikaangaza nuru ya furaha.

Na atawalipa Bustani za hariri kwa vile walivyosubiri.

Walivumilia njaa ili wamshibishe mwingine, malipo yao yamekuwa Bustani iliyo na kila kinachotamaniwa na nafsi na kuburudika na macho. Katika tafsiri nyingi imeelezwa kuwa Aya hizi zilimshukia Imam Ali bin Abi Twalib; miongoni mwazo ni ibara ya Ar -Razi, ninamnuku: “Ametaja Al-Wahidi, katika watu wetu ‧ yaani Sunni ‧ na mwenye Al­kashaf katika Mu’tazila, kwamba Hasan na Husein(a.s) walikuwa wagonjwa, Mtume(s.a.w.w) na watu wengine wakaenda kuwaamkia, wakasema: “Ewe Abul-Hasan, unaonaje lau utaweka nadhiri kwa ajili ya wanao. Basi akaweka nadhiri Ali, Fatima na Mtumishi wao Fidha, kufunga siku tatu ikiwa watapona.

Basi wakapona. Ali akakopa pishi tatu za shairi. Fatima akasaga pishi moja na kutengeneza mikate mitano kulingana na idadi yao. Wakaiweka ili wafuturu, akaja muombaji, akasema: As-salamu alaykum, enyi watu wa nyumba ya Muhammad! Maskini jamani, nilisheni atawalisha Mwenyezi Mungu Peponi. Basi wakampa bila ya kuonja kitu isipokuwa maji, wakaamkia saumu.

Ilipofika jioni na kuleta chakula aliwasimamia yatima wakampa. Akaja mateka usiku wa tatu, wakafanya hivyo hivyo. Ilipofika asubuhi Mtume wa Mwenyezi Mungu akawaona wanatetemeka kama vifaranga, akasema: “Ni huzuni kubwa iliyoje kuwaona katika hali hii! Jibril akashuka na kusema:“Chukua ewe Muhammad! Mwenyezi Mungu anakupongeza kwa watu wa nyumba yako, soma Sura hii.”

Humo wataegemea juu makochi, hawataona humo jua kali wala bari­di kali.

Humo ni humo Peponi. Jua kali ni kinaya cha joto. Maana yako wazi. Umetangulia mfano wake katika Juz. 15 (18:31).

Na vivuli vyake vitanawiri juu yao, na mashada ya matunda yake yataning’inia chini chini.

Neno kunawiri tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu daniU ambalo lina maana ya kuwa karibu, kama walivyofasiri hivyo wafasiri wengi. Lakini pia lina maana hiyo tuliyoitumia. Tumetumia maana hiyo kwa vile inaendana na kivuli, pia inaendana na herufi alayhim, (jua yao); kama inge­likuwa na maana ya karibu ingelitumika herufi ilayihim. Kuwa chini matunda maana yake ni kuweza kuchumwa bila ya kizuizi chochote. Umetangulia mfano wake katika Juzuu hii tuliyo nayo (69:23)

Na watapitishiwa vyombo vya fedha na bilauri za kioo; kioo kinachotokana na fedha, wamezikadiria kwa vipimo.

Ni watu wa Peponi hao, na ndio watakaokadiria. Maana ni kuwa rangi na ukubwa wa vikumbe utakua vile wanavyotaka watu wa Peponi, vile watakavyokadiria kwenye nafsi zao na kuleta picha kwenye akili zao. Wafasiri wameleta swali kuhusu Aya hii, kwamba chombo cha kioo kinawezaje kuwa cha fedha, je, ni sawa kusema kioo kinatokana na fedha na maji yanatokana na udongo? Wamejibu kuwa madini ya bilauri yametokana na fedha, lakini ni nyem­bamba zinaonesha kama kioo[10] .

Na humo watanyweshwa kikombe kilichochanganyika na tangawizi.

Wafasiri wanasema kuwa waarabu walikuwa wakipenda kuweka tangaw­izi kwenye vinywaji, ndio maana Mwenyezi Mungu (s.w.t) akakisifia kinywaji cha Peponi kwayo.

Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil ambayo ni tamu mno, kinywaji chake kinashuka vizuri,Na watawazungukia kuwatumikiawavulana wasiochakaa, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizotawanywa.

Wao ni kama lulu kwa uzuri wao na kunyinyirika kwao. Waliotawanywa ni ishara ya wingi wao na kuweko huku na huko.

Na utakapoyaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa.

Ukiingia Peponi utaona ambayo hayajaonekana wala kusikiwa na kuwaziwa.

Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao atawanywesha kinywaji safi kabisa.

Watavaa Hariri nyembamba na nzito, vile vile mikononi mwao mtakuwa na bangili na watakunywa kinywaji safi. Umetangulia mfano wake katika Juz. 15 (18:31). Hakika haya ni malipo yenu; na mahangaiko yenu yameshukuriwa. Baada ya takrima yote hiyo wataaambiwa huu ndio mshahara wenu wa matendo yenu mliyoyafanyia juhudi. Umetangulia mfano wake katika Juz. 15 (17:19).

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ تَنزِيلًا ﴿٢٣﴾

23. Hakika Sisi tumekuteremshia Qur’an kidogo kidogo.

فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ آثِمًا أَوْ كَفُورًا ﴿٢٤﴾

24. Basi subiri hukumu ya Mola wako wala usimtii miongoni mwao mwenye dhambi au

mwenye kufuru.

وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿٢٥﴾

25. Na lidhukuru jina la Mola wako asubuhi na jioni.

وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا ﴿٢٦﴾

26. Na usiku msujudie Yeye, na umsabihi usiku mrefu.

إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ يُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَاءَهُمْ يَوْمًا ثَقِيلًا ﴿٢٧﴾

27. Kwa hakika watu hawa wanapenda ya sasa, na wana­iacha nyuma yao siku nzito.

نَّحْنُ خَلَقْنَاهُمْ وَشَدَدْنَا أَسْرَهُمْ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَا أَمْثَالَهُمْ تَبْدِيلًا ﴿٢٨﴾

28. Sisi tumewaumba, na tukavi­imarisha viungo vyao. Na tuk­itaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao.

إِنَّ هَـٰذِهِ تَذْكِرَةٌ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا ﴿٢٩﴾

29. Hakika haya ni mawaidha; basi anayetaka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake.

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٣٠﴾

30. Wala hamuwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ilimu, Mwenye hiki­ma.

يُدْخِلُ مَن يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿٣١﴾

31. Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kud­hulumu amewawekea adhabu iliyo chungu.

WANAPENDA YA SASA

Aya 23 – 31

MAANA

Hakika Sisi tumekuteremshia - ewe Muhammad(s.a.w.w) -Qur’an kidogo kidogo.

Ni haki isiyokuwa na shaka na tumekuahidi kukunusuru, kwa sharti la kuvumila maudhi kutoka kwa wenye inadi na upinzani.

Basi subiri hukumu ya Mola wako.

Hukumu yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kupita mambo kwa desturi yake ya maumbile na kupatikana kwa wakati wake maalum. Njia ya uon­gofu kwa mwenye kuipendelea ni nasaha na uongofu, na njia ya nusra ni kuwa na subira katika jihadi.

Wala usimtii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru.

katika yale wanayokuzuwia nayo na wanayokuvutia nayo. Washirikina walimwekea mtume mali, wanawake na uongozi ili aache mwito wake wa kumlingania Mwenyezi Mungu, akawa anakataa. Hilo linaashiriwa na kukatazwa kumtii mwenye dhambi na mwenye kufuru. Makusudio ya mwenye kufuru ni kila mpinzani.

Kundi la wafasiri wamesema kuwa makusudio ya mwenye dhambi hapa ni Utba bin Rabia, kwa sababu alikuwa amezama kwenye starehe, mwenye kufuru ni Abu Jahl au Walid bin Mughira. Vyovyote iwavyo sababu ya kushuka, lakini haihusishi tamko.

Na lidhukuru jina la Mola wako asubuhi na jioni.

Yaani kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu katika mambo yako yote na wakati wako wote wala usiogope lawama. Umetangulia mfano wake katika Juz. 23 (33:42).

Na usiku msujudie Yeye, na umsabihi usiku mrefu.

Fanya tahajudi usiku muda kiasi. Amri hii ni ya Sunna sio ya wajib kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ ﴿٧٩﴾

“Na katika usiku amka kwayo, ni ziada kwa ajili yako.” Juz. 15 (17:79).

Kwa hakika watu hawa wanapenda ya sasa, na wanaiacha nyuma yao siku nzito.

Hawa ni ishara ya washirikina na kila mwenye kuipenda dunia, ikamtawala na kuichukia akhera na kuifanyia uadui. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameita siku nzito kwa vile itakuwa ngumu kwa makafiri.

Sisi tumewaumba, na tukaviimarisha viungo vyao.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye aliyewaleta kutoka kutokuwepo, akawatia sura na kuzifanya nzuri sura zao, vipi wanamkana na kuasi amri zake na makatazo yake?

Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao.

Huu ni ukemeo kwa wale wanokadhibisha kwamba Mwenyezi Mungu anaweza kuwangamiza na kuwaleta watu wengine bora kuliko wao. Umetangulia mfano wake katika Juz. 26 (47:38)

Hakika haya ni mawaidha.

Haya ni haya yaliyo katika Sura hii tuliyo nayo, ndani yake mkiwa na maonyo na mapendekezo, yakiwa ni mawaidha kwa mwenye moyo au akatega sikio naye ni shahidi.

Basi anayetaka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake; wala hamuwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amebainisha njia mbili ya kheri na shari. Akakataza hii na akaamrisha ile, akamwacha mtu ajichagulie mwenyewe, lakini mwenye inadi hawezi kufanya heri ila akifanyishwa kwa nguvu na Mwenyezi Mungu, na hili haliwezi kuwa kwa sababu litakwenda kinyume na uadilifu wake Mwenyezi Mungu Mtukufu, hikima yake na desturi yake kwa viumbe wake. Tazama Juzuu hii tuliyo nayo (74:56), tumefafanua zaidi huko.

Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ilimu, Mwenye hikima.

Mwenye kujua hali za waja wake, ana hikima kwa sababu hatoi amri ila kwa lenye heri na masilahi, wala hakatazi ila lenye shari na ufisadi.

Humuingiza amtakaye katika rehema yake.

Makusudio ya rehema hapa ni Pepo na matakwa yake ni kuwa hamwingizi Peponi yoyote yule ila kwa juhudi na kuifanyia kazi; hivyo ndivyo anavyotaka.

Aya zinazofahamisha hivyo ziko nyingi na wazi; miongoni mwazo ni: “Je, mwadhani mtaingia peponi na hali Mwenyezi Mungu hajawajua wale waliofanya jihadi miongoni mwenu na kuwajua wale waliofanya subira? Juz. 4 (3:142). Vipi atataka Mwenyezi Mungu (s.w.t) kumwingiza Peponi asiyestahiki na hali alimtoa humo Adam alipoasi.

Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu.

Wenye takua watapata rehema ya Mwenyezi Mungu na wakosefu watapa­ta ghadhabu na adhabu yake.

MWISHO WA SURA YA SABINI NA SITA: AL-INSAN


27

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sabini Na Saba: Al-Mursalat. Imeshuka Makka Ina Aya 50.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا ﴿١﴾

1. Naapa kwa wanaotumwa kwa wema!

فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفًا ﴿٢﴾

2. Na wanaokwenda kwa kasi!

وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرًا ﴿٣﴾

3. Na kwa wanotawanya mtawanyo kamili!

فَالْفَارِقَاتِ فَرْقًا ﴿٤﴾

4. Na wanaofarikisha mbali mbali!

فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرًا ﴿٥﴾

5. Na wanaopeleka ukumbusho!

عُذْرًا أَوْ نُذْرًا ﴿٦﴾

6. Kuondoa udhuru au kuonya!

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِعٌ ﴿٧﴾

7. Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka yatakuwa!

فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ ﴿٨﴾

8. Basi nyota zitakapofutwa.

وَإِذَا السَّمَاءُ فُرِجَتْ ﴿٩﴾

9. Na mbingu zitakapopasuliwa.

وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ ﴿١٠﴾

10. Na milima itakapopeperushwa­

وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ ﴿١١﴾

11. Na wajumbe watakapo­ wekewa wakati.

لِأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ ﴿١٢﴾

12. Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda?

لِيَوْمِ الْفَصْلِ ﴿١٣﴾

13. Kwa siku ya upambanuzi!

وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ ﴿١٤﴾

14. Na nini kitakachokujulisha ni nini siku ya upambanuzi?

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١٥﴾

15. Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha!

أَلَمْ نُهْلِكِ الْأَوَّلِينَ ﴿١٦﴾

16. Je, hatukuwaangamiza waliotangulia?

ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الْآخِرِينَ ﴿١٧﴾

17. Kisha tukawafuatilizia wengine?

كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ ﴿١٨﴾

18. Ndio kama hivyo tutawafanya wakosefu!

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١٩﴾

Ole wao, siku hiyo wanaokad­hibisha!

أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ ﴿٢٠﴾

20. Je, hatukuwaumba kwa maji ya kudharaulika?

فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ ﴿٢١﴾

21. Kisha tukayaweka mahali makini pa utulivu?

إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ ﴿٢٢﴾

22. Mpaka makadirio maalumu?

فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ ﴿٢٣﴾

23. Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٢٤﴾

24. Ole wao, siku hiyo wanaokad­hibisha!

أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا ﴿٢٥﴾

25. Je, hatukuifanya ardhi ni chombo?

أَحْيَاءً وَأَمْوَاتًا ﴿٢٦﴾

26. Kwa walio hai na wafu?

وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُم مَّاءً فُرَاتًا ﴿٢٧﴾

27. Na ndani yake tukaweka mil­ima mirefu na tukawanywe­sha maji matamu?

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٢٨﴾

28. Ole wao, siku hiyo wanaokad­hibisha!

NAAPA KWA WANOTUMWA KWA WEMA

Aya 1 – 28

MAANA

Sura hii imeelezea kuhusu Akhera na adhabu yake na vituko vyake. hayo yametangulia kwenye Aya kadhaa; ndio maana tutafupiliza kwa kufasiri kilugha, bila ya kuingia ndani, kama tulivyofanya katika sura yingine.

Naapa kwa wanaotumwa kwa wema.

Imesekana kuwa wanaotumwa hapa ni malaika, kwa maana ya kuwa Mwenyezi Mungu anawatuma malaika kwa ajili ya kufikisha wahyi kwa mitume na mengineyo ya kheri. Pia imesemekana makusudio ni upepo na tafsri iwe Naapa kwa zinazotumwa kwa kufuatana, yaani Mwenyezi Mungu anatuma Pepo kwa kufuatana.

Na wanaokwenda kwa kasi na kwa wanotawanya mtawanyo kamili!

Malaika wanaeneza rehema za Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake au kwamba Pepo zinatawanya mawingu angani.

Na wanaofarikisha mbali mbali!

Malaika wanashuka na Aya za Mwenyezi Mungu ambazo zinafarikisha baina ya haki na batili; au Pepo zinafarikisha mvua pembe za ulimwengu.

Na wanaopeleka ukumbusho! Kuondoa udhuru au kuonya.

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawatuma malaika na wahyi ili kuwaonya waja na wala wasiwe na udhuru. kwa tafsiri ya upepo ni kuwa makusudio ya ukumbusho ni mvua, kwa sababu inakumbusha kuhusu Mwenyezi Mungu na rehema yake; kwa hiyo mumin anamshukuru Mwenyezi Mungu inaposhuka mvua na kujiondolea udhuru wa uzembe alioufanya nyuma. Na kafiri anazidi uasi kwa kuwa mvua inazidisha utajiri wake, na hatimaye mvua au upepo humuonya na adhabu kali.

Huu ni muhtasari wa waliyoyasema wafasiri kuhusu Aya hizi saba. Tafsiri zote mbili (malaika na upepo), zinafaa, kwa sababu Mwenyezi Mungu anapeleka upepo; kama alivyosema:

وَهُوَ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ﴿٥٧﴾

“Na yeye ndiye azipelekaye pepo kuwa ni bishara kabla ya kufika rehema yake.” Juz. 8 (7:57).

Vile vile amewapeleka malaika; kama alivyosema:

اللَّـهُ يَصْطَفِي مِنَ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا ﴿٧٥﴾

“Mwenyezi Mungu huteua wajumbe miongoni mwa Malaika.” Juz. 17 (22:75).

Vyovyote iwavyo sisi hatutaulizwa kuhusu utafiti huu mbele ya Mwenyezi Mungu, wala kuujua hakuna mahusiano yoyote na maisha yetu, kwa sababu yoyote ile. Kwa hiyo bora hilo tuliachie ujuzi wake Mwenyezi Mungu Mtukufu, tukiamini kuwa yeye pekee ndiye msababishaji wa sababu.

Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka yatakuwa!

Mnayoahidiwa ni siku ya kiyama. Maana ni kuwa Kiyama kitafika tu, hilo halina shaka.

Basi nyota zitakapofutwa, yaani kuondoka mwanga wake.

Na mbingu zitakapopasuliwa, sayari zake zitapasuliwa.

Na milima itakapopeperushwa, kuwa vumbi na kwenda na upepo.

Na wajumbe watakapowekewa wakati.

Wajumbe hapa ni malaika. Mwenyezi Mungu amewawekea wakati maalum wa kuja kutoa ushahidi kwa waja, kisha wawapeleke wanaomcha Mungu Peponi na wakosefu kwenye Jahannam.

Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda hao mitume?

Kwa siku ya upambanuzi!

Swali limekuja kwa kuikuza siku yenyewe na vitu vyake. Imeitwa siku ya upambanuzi, kwa vile watu watapambanuliwa kwa haki, bila ya upendeleo.

Na nini kitakachokujulisha ni nini siku ya upambanuzi?

Yaani nini kitakachokufahamisha kuhusu siku hiyo ambayo vituko vyake havina mfano?Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha! Hili ni onyo kwa wenye kukadhibisha siku ya malipo. Vile vile kwa mwenye kuiamini lakini asiifanyie kazi.

Je, hatukuwaangamiza waliotangulia? Kama vile kaumu ya Nuh, kwa vile waliwakadhibisha mitume?

Kisha tukawafuatilizia wengine? Kama kaumu ya Lut.

Ndio kama hivyo tutawafanya wakosefu! Waliomkadhibisha Muhammad(s.a.w.w) . Kwa vile sababu ni moja -kuipinga haki.

Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha!

Aya hii imekarika mara kumi katika sura hii kufuatana na maana ya Aya iliyo kabla yake.

Je, hatukukuwaumba kwa maji ya kudharaulika? Kisha tukayaweka mahali makini pa utulivu? Mpaka makadirio maalumu? Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.

Je, mnakana ufufuo na mnasema: Ni nani atakayefufua mifupa iliy­ochakaa, na hali nyinyi mnajua kuwa Mwenyezi Mungu amewaumba kutokana na maji ya yaliyo duni, na mkawa kwenye viza vitatu kwa muda maalum, mkigura kutoka umbile moja hadi jingine, na muda huu akaupan­ga kwa umakini kabisa. Baada ya yote haya bado mnakufuru neema za Mwenyezi Mungu na mnakadhibisha uweza wa ufufuo, hisabu na malipo?

Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha! Je, hatukuifanya ardhi ni chombo? Kwa walio hai na wafu? Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameifananisha ardhi na chombo, kwa vile inakusanya na kuhifadhi. Maana ni kuwa ardhi inakusanya na kuhifadhi walio hai kwenye mgongo wake na wafu tumboni mwake.

Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, ili ardhi isiyumbe na tukawanywesha maji matamu? Ambayo ni uhai wenu na wa ardhi, inayowapatia heri na baraka. Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha!

انطَلِقُوا إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿٢٩﴾

29. Nendeni kwenye yale mliyokuwa mkiyakadhibisha!

انطَلِقُوا إِلَىٰ ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ ﴿٣٠﴾

30. Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!

لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّـهَبِ ﴿٣١﴾

31. Hayaleti kivuli, wala hayae­pushi mwako.

إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ ﴿٣٢﴾

32. Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!

كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ ﴿٣٣﴾

33. Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٣٤﴾

34. Ole wao, siku hiyo wanaokad­hibisha!

هَـٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ ﴿٣٥﴾

35. Hii ni siku ambayo hawatatamka.

وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ ﴿٣٦﴾

36. Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٣٧﴾

37. Ole wao, siku hiyo wanaokad­hibisha!

هَـٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ ﴿٣٨﴾

38. Hii ndiyo siku ya upambanuzi.Tumewakusanya nyinyi na waliotangulia.

فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ ﴿٣٩﴾

39. Ikiwa mnayo hila, nifanyieni!

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٤٠﴾

40. Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha!

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ ﴿٤١﴾

41. Hakika wenye takua watakuwa katika vivuli na chemchem.

وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na matunda wanayoyapenda

كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾

43. Kuleni na kunyweni kwa raha kwa sababu ya mliyokuwa mkiyatenda.

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٤٤﴾

44. Hakika ndio kama hivyo tunavyowalipa watendao mema.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٤٥﴾

45. Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha!

كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ ﴿٤٦﴾

47. Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٤٧﴾

47. Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha!

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ ﴿٤٨﴾

48. Na wakiambiwa: Rukuuni hawarukui.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٤٩﴾

49. Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha!

فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٠﴾

Basi ni mazungumzo gani baada yake watakayoyaamini?

KIVULI CHENYE MAPANDE MATATU

Aya 29 – 50

MAANA

Nendeni kwenye yale mliyokuwa mkiyakadhibisha.

Waliikadhibisha adhabu ya Mwenyezi Mungu, bali waliidharau pamoja na yule aliyewapa ahadi hiyo. Kesho mazabania wa Jahannam watawaambia kwa madharau; kama vile wao walivyodharau mitume: Haya nendeni, hivi sasa, kwenye lile mlilolifanyia mzaha.

Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu kinachotokana na moshi wa Jahannam: pande la kwanza litawafunika kichwani, pande la pili kuliani kwao na la tatu kushotoni.Hayaleti kivuli, wala hayaepushi na mwako . ni kivuli jina tu, lakini hakiwakingi wanaojifunika nacho na moto bali kinawazidishia adhabu juu ya adhabu. Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na kivuli cha moshi mweusi, si baridi wala starehe.” Juz. 27 (56:43-44).

Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!

Yaani moto wa Jahannam utaruka na kujaa hewani, kila cheche itakuwa kubwa kama jumba na rangi kama ya ngamia wa rangi ya manjano.

Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha! Hii ni siku ambayo hawatatamka, wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.

Siku ya Kiyama kuna sehemu baadhi ya watu watapewa idhini kusema, na wengine hawatapewa idhini. Tazama Juz. 23 (36:65). Imesemekana maana ni kuwa wakosefu hawatatamka yatakayowafaa wala hawatakuwa na udhuru kwa Mwenyezi Mungu.

Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha! Hii ndiyo siku ya upambanuzi.

Itapambanuliwa haki kwa viumbe.

Tumewakusanya nyinyi na waliotangulia, waliofanya makosa kama nyinyi na tumewakusanya nyote sehemu moja ili tuangalie hisabu, kisha mpelekwe kwenye makao mamoja ambayo ni Jahannam iliyo makao mabaya.

Ikiwa mnayo hila, nifanyieni!

Huu ndio mwisho wenu, ikiwa mna hila au nyenzo yoyote ya kuwazuia na adhabu basi ileteni. Hapa kuna kutahayariza kutokana na vitimbi vyao na hadaa yao katika maisha ya dunia.

Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha!

Hakika wenye takua watakuwa katika vivuli na chemchem na matun­da wanayoyapenda.

Hii ndio ada ya Qur’an Tukufu, inakutanisha adhabu ya wakosefu na thawabu kwa wanaomcha Mungu, kwa lengo la kupendekeza na kuhad­harisha. Wakosefu watakuwa na vivuli vya Jahannam na wenye takua watakua na vivuli vya Peponi, chemchem zinazopita na matunda aina kwa aina pamoja na takrima za hali ya juu; miongoni mwazo ni kauli ya malaika:

Kuleni na kunyweni kwa raha kwa sababu ya mliyokuwa mkiyatenda.

Umetangulia mfano wake kwa herufi zake katika Juz. 27 (52:19).

Hakika ndio kama hivyo tunavyowalipa watendao mema.

Hii ndio desturi yetu katika viumbe:

إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ مَنْ أَحْسَنَ عَمَلًا ﴿٣٠﴾

“Hakika sisi hatupotezi ujira wa anayefanya mazuri.” 15 (18:30).

Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha!

Kuleni na mjifurahishe kidogo tu.

Maneno yanaelekezwa kwa wakosefu. Makusudio yake ni kuhadharisha na kutoa ahadi. Maana yake ni stareheni kwenye dunia, vile mtakavyo, lakini hizo ni siku chache, kisha zitaondoka starehe kama mawingu yanay­opita,hakika nyinyi ni wakosefu! Desturi ya Mwenyezi Mungu kwa wakosefu ni kuwapa muda kidogo, kisha awaonjeshe adhabu ya moto.

Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha!

Na wakiambiwa: Rukuuni hawarukui.

Mtume akiwaamuru kumnynyenyekea Mwenyezi Mungu wanapandwa na kiburi.

Sheikh Abdul-Qadir Al-Maghribi, katika kufasiri Aya hii anasema: “Imepokewa kuwa Mtume(s.a.w.w) alimuuliza Hind, mke wa Abu Sufyan, bada ya kusilimu siku ya kuiteka Makka: Unauonaje Uisalmu? Akasema: “Ni mzuri isipokuwa mambo matatu: Kuinama ‧ yaani kurukui na kusuju­di katika Swala-ushungi, na huyu mtumwa mwesi kupanda Al-Kaa’ba ‧ akimkusudia Bilal na adhana yake kutoka juu ya Al-Kaa’ba.” Mtume(s.a.w.w) akamjibu: “Hakuna Swala bila ya kuinama, ushungi ni sitara nzuri kabisa, ama huyu mweusi basi ndio mja bora zaidi.”

Ole wao, siku hiyo wanaokadhibisha!

Basi ni mazungumzo gani baada yake watakayoyaamini?

Utukufu wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) umejitokeza kwenye Qur’an yote, kama ulivyojitokeza katika ulimwengu. Basi ambaye hatakinai wala kun­ufaika na Qur’an, huyo hawezi kukinaishwa na kitu chochote. Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 9 (7:185).

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

YALIYOMO

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 1

IMEANDIKWA NA: SHEIKH MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYA 1

IMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HASAN MWALUPA 1

IMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED 1

IMEPANGWA KATIKA KOMPYUTA NA: UKHT PILI RAJABU 1

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI 1

MAKOSA YA CHAPA 2

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 3

DHIHAR 3

LUGHA 3

KISA KWA UFUPI 4

MAANA 4

KUNONG’ONEZANA 6

MAANA 6

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 10

FANYENI NAFASI MWENYEZI MUNGU ATAWAFANYIA NAFASI 10

MAANA 10

KUKAA MBELE KWENYE KIKAO 11

WAMEFANYA VIAPO VYAO NI NGAO 13

MAANA 13

BILA SHAKA NITASHINDA MIMI NA MITUME WANGU 15

MAANA 15

MWISHO WA SURA YA HAMSINI NA NANE: AL–MUJADALA 16

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 17

VINAMSABIHI MWENEYEZI MUNGU 17

KISA CHA BANI NADHIR KWA UFUPI 17

MAANA 18

PROPAGANDA ZA UPOTOFU NA WAKATI MNASABA 19

MALI ISIZUNGUKE KWA MATAJIRI 21

MAANA 21

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 24

WANAWAPENDELEA KULIKO NAFSI ZAO 25

MAANA 25

AKIKUFURU HUMWAMBIA MIMI NIKO MBALI NAWE 27

MAANA 27

LAU TUNGELIITERMSHA HII QUR’ANI JUU MLIMA 29

MAANA 29

MWISHO WA SURA YA HAMSINI NA TISA: SURAT AL-HASHR 30

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 31

MSIMFANYE RAFIKI ADUI WANGU NA WENU 31

KISA KWA UFUPI 31

MAANA 32

KIGEZO CHEMA 33

MAANA 33

MUNGU HAWAKATAZI WASIOWAPIGA VITA 35

MAANA 35

Dola Rafiki Na Dola Adui 35

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 38

WAKIWAJIA WANAWAKE WAHAJIRI 38

MAANA 38

WANAWAKE WAUMINI WAKIKUBAI 40

MAANA 40

MWISHI WA SURA YA SITINI: SURAT AL – MUMTAHINA 41

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 42

KAMA KWAMBA WAO NI JENGO 42

MAANA 42

KUPOTOLEWA TAWRAT 44

MWENYEZI MUNGU ANAKAMILISHA NURU YAKE 47

MAANA 47

MWISHO WA SURA YA SITINI NA MOJA: SURAT AS – SAFF 49

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 50

NDIYE ALIEWAPELEKEA MTUME 50

MAANA 50

KAMA MFANO WA PUNDA WAALIOBEBA VITABU 52

MAANA 52

SWALA YA IJUMA 54

MAANA 54

MWISHO WA SURA YA SITINI NA MBILI: SURAT AL-JUM’A 55

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 56

HAO NI MAADUI JIHADHARI NAO 56

MAANA 56

MWENYE NGUVU ATAMFUKUZA MNYONGE 59

MAANA 59

MWISHO WA SURA YA SITINI NA TATU: SURAT AL- MUNAFIQUN 61

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 62

MIONGONI MWENU KUNA KAFIRI NA MUUMIN 62

MAANA 62

HII NI SIKU YA HASARA 65

MAANA 65

UADUI WA WAKE NA WATOTO 68

MAANA 68

MWISHO WA SURA YA SITINI NA NNE: SURAT AT – TAGHABUN 70

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 71

TALAKA KWA WAKATI WA EDA 72

MAANA 72

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 77

MWENYE WASAA AGHARIMIE 77

MAANA 77

MIJI MINGAPI 79

MAANA 79

MBINGU SABA NA ARDHI 80

MWISHO WA SURA YA SITINI NA TANO: SUARAT AT-TALAQ 81

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 82

KWA NINI UNAHARIMISHA ALICHOKUHALILISHIA MWENYEZI MUNGU? 82

KISA KWA UFUPI 82

MAANA 83

KUNI ZAKE NI WATU NA MAWE 86

MAANA 86

MKE WA NUH NA MKE WA LUT 88

MAANA 88

MWISHO WA SURA YA SITINI NA SITA: SURAT AT –TAHRIM 89

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 90

AMETUKUKA MWENYE UFALME WOTE 91

MAANA 91

TEMEBEENI KATIKA PANDE ZAKE 94

MAANA 94

ANAYEKWENDA AKISUNUKIA 96

MAANA 96

MWISHO WA SURA YA SITINI NA SABA: SURAT AL-MULK 99

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 100

WEWE SI MWENDAWAZIMU 101

MAANA 101

LIKAWA KAMA LIMEFYEKWA 104

MAANA 104

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 107

KWANI TUTAWAFANYA WAISLAMU KAMA WAKOSEFU? 107

MAANA 107

NIACHENI NA WANAOKADHIBISHA 110

MAANA 110

MWISHO WA SURA YA SITINI NA NANE: SURAT AL- QALAM 111

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 112

TUKIO LA HAKI 113

MAANA 113

WABEBAJI ARSHI 115

LAITI YANGELIKUWA NI YAKUMALIZA 117

MAANA 117

MNAVYOVIONA NA MSIVYOVIONA 119

MAANA 119

MWISHO WA SURA YA SITINI NA TISA: SURAT AL-HAQQA 120

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 121

KADIRI YAKE NI MIAKA HAMSINI ELFU 122

MAANA 122

SHETANI NA UTAFITI WA GHAIBU 122

NI NANI HAO WANAOSWALI? 125

MAANA 125

WAACHE WAPIGE POROJO 128

MAANA 128

MWISHO WA SURA YA SABINI: SURAT AL- MAA’RIJ 129

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 130

NILIWALINGANIA WATU WANGU 131

MAANA 131

IMANI NA RAHA 132

AMEWAUMBA KATIKA HALI MBALIMBALI 134

MAANA 134

WALA MSIMWACHE WADDA WALA SUWAA 135

MAANA 135

MWISHO WA SURA YA SABINI NA MMOJA: SURAT NUH 137

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 138

KUNDI MOJA LA MAJINI 138

MAANA 138

TULIZIGUSA MBINGU 141

MAANA 141

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 144

HAKIKA MISKITI NI YA MWENYEZI MUNGU 144

MAANA 145

MWISHO WA SURA YA SABINI NA MBILI: SURAT AL-JINN 147

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 148

EWE MWENYE KUJIZONGAZONGA NGUO 148

MAANA 148

HAIBA YA MTUME MTUKUFU 149

JITENGE NAO KWA UZURI 152

MAANA 152

SOMENI KILICHOCHEPESI KATIKA QUR’AN 153

MAANA 154

MWISHO WA SURA YA SABINI NA TATU: SURAT AL MUZZAMMIL 155

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 156

EWE ULIYEJIGUBIKA 156

MAANA 156

NIACHE PEKE YANGU NA NILIYEMUUMBA 160

KISA KWA UFUPI 160

MAANA 160

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 165

TUKIJIINGIZA PAMOJA NA WANAOJIINGIZA 166

MAANA 166

MWISHO WA SURA YA SABINI NA NNE: SURAT AL- MUDDATHIR 169

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 170

KIAPO KWA SIKU YA KIYAMA 171

MAANA 171

MNAPENDA YA SASA 174

MAANA 174

MWISHO WA SURA YA SABINI NA TANO: AL-QIYAMA 176

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 177

JE, KILIMPITIA BINADAMU KIPNDI 177

MAANA 177

HUWALISHA CHAKULA JUU YA KUKIPENDA KWAKE 181

MAANA 181

WANAPENDA YA SASA 184

MAANA 184

MWISHO WA SURA YA SABINI NA SITA: AL-INSAN 186

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 187

NAAPA KWA WANOTUMWA KWA WEMA 188

MAANA 188

KIVULI CHENYE MAPANDE MATATU 191

MAANA 191

SHARTI YA KUCHAPA 193

MWISHO WA JUZUU YA ISHIRINI NA NNE 193

YALIYOMO 194



[1] . Imesemekana kuwa makusudio ya Aya hii ni kama makusudio ya Aya iliyopita. Wengine wakasema makusudio ni jizia na kodi. Ikasemekana ni nyara iliy­opatikana kwa njia yoyote ile. Pia imesemekana kuwa Aya imeondolewa hukumu yake (mansukh) na Aya ya Juz. 10 (8:41). Na yamesemekana mengine zaidi ya hayo. Tuliyoyasema, kuwa Aya iliyotangulia hii inahusika na mali ya Bani nadhir na hii inahusika na mali nyinginezo, ndio tafsiri yenye nguvu zaidi kwa rai yetu. Mwenyezi Mungu ndiye ajuae zaidi aliyokusudia.

[2] . Talaka rejea ni ile ambayo mtaliki anaweza kumrudia mtalikiwa ndani ya eda bila ya ndoa. Na baini ni ile asiyoweza kumrudia mpaka ndoa mpya; kama talaka ya tatu na kuendelea, ya ambaye hajaingiliwa nk. Maelezo zaidi yako kwenye vitabu vya fiqh –Mtarjumu.

[3] . Utomvu mtamu wenye harufu mbaya. Na Mtume(s.a.w.w) alikuwa akichukia kuwa na harufu mbaya.

[4] . Juz. 8 (7:70).

[5] . Juz. 26 (51:14).

[6] . Juz. 17 (21:97).

[7] . Baadhi ya waswahili nao, wanaangalia kujikunguwaa (kujikwaa) mguu wa kulia au wa kushoto kwenye jambo wanaloliendea. Mtarjumu.

[8] . Haya ni mahisabu ya miaka ya 70 –Mtarjumu.

[9] . Inawezekana kuwa hiyo ni kwa wale majini wa mwanzo mwanzo mwa Uislamu, kwani hata waislamu wa mwanzo pia walikuwa wakiifanyia kazi Aya mara tu walipoisikia. ‧Mtarjumu.

[10] . Mimi ningeifasiri kwa namna ambayo haitaleta swali: “Na bilauri za kauri,” kwa kufasiri qawariru kwa maana ya madini ya kauri, ambayo ni udongo mweupe mwepesi unaong’aa na unaotengenezewa vyombo; kwa kudhani kuwa waswahili wamelichukua neno kauri kutoka neno hilo la kiarabu qarura. ‧Mtarjumi.