TADWIN AL HADITH

UANDISHI WA HADITH

UCHUNGUZI WA KIHISTORIA JUU YA UKUSANYAJI NA UANDISHI WA HADITH

Kimeandikwa na:

RASUL JA'AFARIYAN

Kimetarjumiwa na

AMIRALY M. H. DATOO

(BUKOBA - TANZANIA)

UTANGULIZI

Umuhimu wa Hadith katika maadili ya mafunzo ya Kiislamu - ikiwemo Tafsir, Fiqh (Sharia), na maadili, n.k.- unakubalika katika madhehebu yote ya Kiislamu. Leo itakuwa ni vigumu kumpata mtu yeyote yule aatakayekuwa akidai kuwa Qur'an Tukufu inajitosheleza kwa Shariah ya mafunzo ya Kiislamu pamoja na maelezo bila ya msaada wa Sunnah na Hadith. Zaidi ya hayo, yapo matamko mengi ya Mtumes . a.w.w , na baadhi ya taarifa katika Qur'an yenyewe, ambazo zinaelekeza katika umuhimu wa amri na matendo ya Mtumes.a.w.w , Kwa hivyo ni dhahiri umuhimu uliopo juu ya Hadith na Sunnah za Mtumes.a.w.w , hivyo hapana shaka wala haja ya ushahidi kwa swala hili.

Madhumuni ya kitabu hiki ni kuchambua na kutazama vile mfumo wa Hadith ulivyokuja kuandikwa na kutazama muda uliotumika kukusanya matamko (kauli), matendo (fi'l) na kukubaliwa kwa ukimya (taqrir) wa Mtumes.a.w.w hadi kufikia katika sura ya ukusanyaji na uandishi. Ni dhahiri, swala hili linaweza kuwa na umuhimu wa kuchambua ushahidi wa mfumo wa Hadith.

Ama kuhusu swala la Qur'an, sisi twajua kuwa hapakuwapo na pengo la muda baina ya kufunuliwa Ayah za Qur'an na kuandikwa kwao. Vivyo hivyo, hapana shaka juu ya usahihi wa Qur'an, kwani Mtumes.a.w.w alikwishawachagua waandishi kuanzia mwanzoni mwa ufunuo na hapo walipatiwa kazi za kuzikusanya na kuzindika. Hata hivyo, utaratibu huu haukutumika katika swala la Hadith, ambavyo imekuja kupokelewa vinginevyo. Umuhimu wa hadith na daraka lake katika maswala ya kijamii na kisiasa vimesababisha baadhi ya makundi kuonyesha hali ya kiasi fulani cha kutovumilia kelekea hayo. Kutovumilia huku ndiko kuliko sababisha Hadith kucheleweshwa kusimuliwa na kuandikwa na kuenezwa. Na kwa masikitiko makubwa, kucheleweshwa huku kumeleta hali ya mtatanisho kwa ajili ya uthamini wake kwa vizazi vya baadaye.

Hata hivyo, ni lazima kutambulisha kuwa hali ya Hadith katika Shiah ilikuwa ni tosauti na ile hali ya Hadith za Ahl al-Sunnah Tofauti hii inatokana na imani ya Mashiah kuhusu Uimamu wa Shia wa Ahl al-Bayt a.s. ambapo kuwapo kwao ulikuwa ukiendelea hadi katikati ya karne ya 3 A.H. / 9 A.D. Kwa hivyo, Hadith zilizonakiliwa na Mashiah hazikukumbwa na matatizo ya kucheleweshwa kwa kuandikwa. Hapa sisi tutatazama kwa kimukhtasari sana uthibitishaji kuhusu swala hili, lakini sehemu kubwa ya uchambuzi huu utakuwa ukihusiana na historia ya uandikaji wa Hadith miongoni mwa zile za Ahl as-Sunna. Historia hii inaonyesha kuwa Hadith zilikuwa hazikuandikwa kwa kioindi fulani. Siyo hayo tu, hata kuzieneza kwao pia kulipigiwa marufuku kwa muda fulani, kwa kipindi cha miaka mia moja. Ahadith (wingi wa Hadith) zilienezwa kwa desturi ya matamshi tu. Ingawaje sehemu ya Hadith ilianza kuandikwa katika karne ya 2 A.H. / 9 A.D., sehemu yake kubwa iliandikwa tu baada ya muda wa kutosha kupita.

Hapa sisi tutatazama kwanza Maimamu( a.s ) wa Kishia wakisisitiza uandikaji wa Hadith. Na baadaye tutachukua historia ya uandikaji wa Hadith miongoni mwa Ahlal-Sunnah. Uchunguzi wa aina hii utatusaidia kama mwongozo kwa ajili ya kuthamini misingi halali ya Hadith ya Madhehebu zote za Islam na kutudhihirishia ipi iliyo na ufululizo wa uandikaji wa Hadith (bila ya kuvunjika kwa mfululizo huo) Umuhimu mkubwa wa uchunguzi huu ni utamini kwa undani wa sanad na mutun (kiini) cha Hadith, jambo ambalo linalohitaji utafiti maalum ingawaje baadhi ya kazi kama hizi zimeshaandikwa juu ya somo hili, lakini bado kunahitajika juhudi zaidi katika uchunguzi kama huu.

Kwa kifupi, kitabu hiki ni mkusanyiko wa makala yaliyokuwa yakichapishwa katika jarida la Al-Tawhid J. V, II uk. 39-55; j. V, III & IV uk. 71-84 na VI, I uk. 19-35 - Sazmaan Tablighaat Teheran Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Niliona kuwa itakuwa ni kazi yenye manufaa iwapo nitayakusanya hayo na kuyatarjumu katika lugha ya Kswahili katika sura ya kitabu.

Amiraly M.H.Datoo

P.O.Box 838

BUKOBA - TANZANIA


UANDISHI WA HADITH

1. MAIMAMU WA SHIA KATIKA UANDIKAJI NA UENEZAJI WA HADITH

Katika sehemu hii, twategemea kuzungumzia kwa mukhtasari msimamo wa Shia kuhusu uandikaji wa Hadith kutokea mwanzoni. Itaonekana kuwa ni kinyume na msimamo wa wengine kuhusu swala hili. Msimamo wa Kishia ulisisitiza mno juu ya uandikaji wa Hadith zikisaidia uhifadhi wake wakati ambapo Maulamaa mashuhuri wa Kisunni, hata kufikia mwanzoni mwa karne ya 3A.H./9 A.D. walikuwa wakipinga uandikaji wa Hadith. Ni baada ya uandikaji wa Hadith ulipokuwa dhahiri hao wanaopinga walipoanza kwenda kinyume na Hadith walizokuwa wamezitoa wakipinga uandishi na uenezaji wake na hapo wakaanza kuziandika. Alba ibn al-Ahmad ananakili kuwa mara moja Ali ibn Abi Talib a.s. wakati akitoa Hotuba juu ya mimbar, alibainisha: "Je, ni nani atakayeinunua elimu kwa Dirhamu moja?" Al-Harith ibn al-A' war alinunua karatasi yenye thamani ya Dirhamu moja na kumwijia Imam Ali ibn Abi Talib a.s. na kuandika kiasi cha kutosha cha elimu juu yake. Riwaya hii inatuonyesha vile Imam a.s. alivyokuwa akisisitiza juu ya uandikaji.

Imam Hassan ibn Ali ibn Abi Talib( a.s ) ameripotiwa akiwashauri watoto wake kama ifuatavyo:-

"Nyinyi sasa ni watoto wa Ummah ambao katika maisha ya mbeleni mtakuwa wakubwa wao. Jielimisheni Elimu; na yeyote yule miongoni mwenu atakayeweza kuhifadhi (kukariri) elimu (yaani Hadith), basi aiandike na kuiweka nyumbani mwake."

Imeripotiwa kuwa Hijr ibn Adi, mmoja wa Sahaba wa Mtumes.a.w.w na Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) , aliziandika Hadith za Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) katika kitabu na kuzirejea pale alipohitaji msaada wa mwongozo katika masuala mbalimbali Mifano hii inadhihirisha umuhimu aliokuwa ameuambatanisha Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) , watoto wake na Sahaba wake katika uandikaji wa Hadith. Mifano miwili ifuatayo itaonyesha dhahiri vile Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) alivyokuwa akisisitiza umuhimu wa Hadith na kuzihifadhi.

Umar ibn Ali anaripoti kuwa mtu mmoja alimwuliza Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) ni vipi kuwa yeye (Ali) aliweza kunakili na kusimulia Hadith nyingi za Mtumes.a.w.w kuliko Sahaba wengineo. Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) alijibu:"Hii ni kwa sababu daima nilipokuwa nikimwuliza swali Mtume s.a.w.w, alikuwa akinijibu maswali yangu. Na pale nilipokuwa nikiwa kimya, basi Mtume s.a.w.w alianzisha mazungumzo mwenyewe."

Ali ibn Hawshab anaripoti kutoka Makhul, mwanachuo kutokea Syria, kuwa Mtumes.a.w.w. aliisoma Ayah (69:12) Na hapo alimwambia Imam Ali ibn Abi Taliba.s "Mimi nimemwomba Allah swt kuwa masikio hayo yawe ni yako." Baadaye Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alisema: "Mimi kamwe sikusahau Hadith yoyote au chochote kile kilichosikilizwa na sikio langu kikisemwa na Mtumes.a.w.w .

Umar ibn al-Harith anasema: "Wakati mmoja Alia.s aliuelekeza uso wake kuelekea mbinguni na kuurudisha chini akisema: "Mwenyezi Mungu na Mtume wakes.a.w.w. wamesema kweli." "Je, kilikuwa nini? "Kikundi cha watu kiliuliza. Imam Imam Ali ibn Abi Taliba.s alisema:"Mimi ni mpiganaji wa vita na vita vinarithishia mtu ulaghai. Vivyo hivyo, ninaweza kukubali iwapo nitaporomoka kutokea mbinguni kwa ajili ya kunaswa na ndege kuliko kumsingizia uwongo Mtume wa Allah swt. Kwa hivyo fuateni chochote kile mukisikiacho kikitoka kwangu........" Kauli juu ya uandishi wa Hadith pia zimenakiliwa kutoka Maimamu wengine.

Al-Imam al-Sadiqa.s alisema:"Andikeni na kuieneza elimu yenu miongoni mwa ndugu zenu, na iwapo mtafariki basi watoto wenu watarithi vitabu vyenu. Itafika siku ambapo patatokea machafuko na hapatakuwapo na mtu wa kumfanya rafiki na wala hapatakuwa na chochote cha kuweza kutegemewa isipokuwa ni vitabu tu.... "

Al-Imam al-Sadiqa.s pia amenakiliwa kwa kusema:"Hifadheni vitabu vyenu kwani mutakuja kuvihitaji hivyo siku moja." Vile vile ameripotiwa akisema kuwa: nguvu za moyo na kuhifadhi akilini inategemea mno juu ya maandishi.

Abu Basir anaripoti kuwa aliambiwa na Imam al-Sadiqa.s : "Baadhi ya watu waliotoka Basrah walikuwa wakija na kuniuliza kuhusu Hadith na waliziandika. Je, kwa nini nawe hauziandiki?" Na aliongezea kusema,"Elewa wazi wazi kuwa wewe kamwe hautaweza kuhifadhi Hadith bila ya kuiandika."

Idadi kubwa ya mapokezi yanaonyesha kuwa Maimamua.s walikuwa navyo vitabu na maandishi ambavyo walirithi kutoka vizazi vilivyowatangulia. Katika riwaya nyingine Imam Ali ibn Abi Taliba.s ameripotiwa akiwa amesema:"Ikamateni elimu (kwa kuiandika)," ambavyo aliirejea mara mbili.

Imeripotiwa kutoka kwa Ja'bir kuwa Abu Hanifa alikuwa akimwita al-Imam al-Sadiqa.s "Kutubi" (yaani mwenye vitabu) kwa sababu ya kutumia mno vitabu, na Imama.s alifurahishwa kwa jina kama hilo. Vile vile imeripotiwa kuwa al-Imam Muhammad ibn Ali al-Baqira.s ameziandika Hadith za Mtumes.a.w.w. ambazo zilikuwa zikinakiliwa na Jaabir ibn Abdullah Ansaari. (Ingawaje taarifa hii inaonyesha kuwa siyo ya ukweli kwani Jaabir alikuwa ameshakwisha kufariki wakati Imama.s alikuwa na umri wa miaka mitano tu, labda inawezekana kuwa Hadith ziliandikwa na mjumbe).


UANDISHI WA HADITH

2. MASHIA NA UANDISHI WA HADITH

Kwa kuwa riwaya (desturi) ya uandishi wa Hadith ilikuwapo miongoni mwa Shia tangia mwanzoni, wao walikuwa wanaongoza katika uandishi wa Hadith na Fiqh. Dr. Shawqi Dayf anaandika: "Mwelekeo na umuhimu wa Mashia katika uandishi wa Fiqh umekuja daima ni madhubuti mno. Sababu nyuma yake ilikuwa ni imani yao katika Maimamu wao ambao walikuwa ni kiongozi wao (haad) na wakiwa wameo ngozwa na Allah swt (mahdi) na fatawa zao zimekuwa zimeshikamana. Kwa hivyo, wao walipatiwa uzito na umuhimu katika misemo ya Imam Ali ibn Abi Taliba.s Na kwa sababu hiyo, mkusanyiko wa kwanza ulifanywa na Mashia, ulifanywa na Sulaym ibn Qays al-Hilali, katika zama za al-Hajjaj." Al-Allamah al-Sayyid Sharaf al-Din anaandika: "Imam Imam Ali ibn Abi Taliba.s na wafuasi wake walitilia mkazo na kufuatilia swala la uandishi kuanzia mwanzo kabisa. Jambo la kwanza kabisa lililotiliwa mkazo na kufuatiwa na Imam Ali ibn Abi Taliba.s ilikuwa ni kuiandika Quran nzima, ambayo aliifanya baada ya kifo cha Mtumes.a.w.w. kwa kuiandika kimpangilio wa ufunulio wa Aya za Qurani.Katika Qurani hiyo pia alikuwa ameonyesha ni aya zipi zilizokuwa 'amm au khass, mutlaq au muqayyad, muhkam au mutashabih. Baada ya kukamilisha hayo, aliendelea na kazi ya ukusanyaji wa kitabu kwa ajili ya Fatimah, ambacho kilikuwa kikijulikana kwa vizazi vyao kama Sahifat Fatimah. Baada ya hayo, aliandika kitabu juu ya diyat (fidia) ambacho kilijulikana kama Sahifah. Ibn Sa'id amenakili hivyo katika musnad kutoka kwa Imam Ali ibn Abi Taliba.s mwishoni mwa kazi yake mashuhuri al-Jami.' Mtunzi mwingine wa Kishia ni Abu Rafi, ambaye alikusanya maandiko yakiitwa kitab al-Sunan wa al-ahkam wa al-qadhaya. "

Marehemu Sayyid Hassan al-Sadr anaandika kuwa Abu Rafi, aliyekuwa mawla wa Mtumes.a.w.w. ndiye aliyekuwa wa kwanza miongoni mwa Mashia kwa kukikusanya kitabu. al-Najashi katika Fihrist ameelezea kuwa Abu Rafi alikuwa ni mtunzi katika kizazi cha kwanza cha Mashia. Mfuasi wa Imam Ali ibn Abi Taliba.s Abu Rafi alishiriki katika vita vya Imam Ali ibn Abi Taliba.s na alikuwa ni mwangalizi wa hazina ya Serikali huko Kufah. Kitabu chake kilichokuwa kikiitwa Kitab al-Sunan wa al-ahkam wa al-qadhaya, ambacho kilikuwa kimeanza kwa sura izungumziayo Salat, kufuatiwa na sura juu ya Saumu, Hajj, Zakat, kutolewa kutoka kwa Imam Ali ibn Abi Taliba.s katika Kufah, Kitabu hiki kilinakiliwa na Zayb ibn Muhammad ibn Ja'afer ibn al-Mubarak katika nyakati za al-Najashi. Ali ibn Abi Rafi, mwana wa Abu Rafi, aliye tabi't na Mshia khalisi ameweza vile vile kukusanya kitabu kilichokuwa na sura mbali mbali juu ya mambo ya Sheria kama vile wudhuu, Salaat, n.k.

Kama ilivyoelezwa hapo awali, abu Hanifa alimwita al-Imam al-Sadiqa.s kutubi (akisema 'innahu kutubi') sifa ambayo ilimtambulisha na wengineo. Wakati Imama.s aliposikia kuhusu hayo, alicheka na kusema, "...... lakini kila alichokisema kuwa kwangu suhufi ni kweli; mimi nimesoma suhuf (vitabu) vya mababu zangu." Riwaya hii inaonyesha kwa wazi wazi kuwa Imam a.s. alikuwanavyo vitabu fulani ambavyo alipewa na mababu zake, na hiki kilikuwa ni kipindi ambacho Ahl al-Sunnah walikuwa hawakutilia mkazo katika uandishi wa Hadith. Miongoni mwa mapokezi ambayo inatuonyesha kuwa ma-Imam a.s. walikuwa navyo vitabu kama hivyo, ni mojawapo iliyoripotiwa na Muhammad ibn 'Udhafir al-Sayrafi anasema: "Mimi nilikuwa pamoja na al-Hakam ibn Utaybah na tulimtembelea al-Imam al-Baquira.s Al-Hakam alimwuliza swali Imama.s Abu Ja'afera.s alikuwa akimstahi sana. Wao walitofautiana juu ya swala fulani na hapo Abu Ja'afer alisema: "Mwanangu (mtoto wake), inuka na ukilete kitabu cha Imam Ali ibn Abi Taliba.s Huyo mtoto alimletea kitabu kikubwa, ambacho Imama.s alikifungua, na kulipitishia macho hadi kulipata swala walilokuwa wakilizungumzia. Na hapo Abu Ja'afera.s alisema:"Haya ni maandish i ya Imam Ali ibn Abi Talib a.s na yaliyosemwa na Mtume s.a.w.w..........."

Katika riwaya nyingineyo ameripotiwa Imam al-Baquira.s akisema: "Katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Taliba.s nimepaona ambapo Mtumes.a.w.w . akisema:'Wakati zakat itakapokuwa hailipwi, basi baraka itapotea kutoka ardhi." Vile vile ipo imeripotiwa kuwa Imam al-Sadiq a.s amesema: Baba yangu alisema: "Mimi nimesoma katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Taliba.s kuwa Mtumes.a.w.w . ameandika mkataba baina ya Muhajirun na Ansar na watu wengineo wa Yathrib ambao waliungana naye, ikisemwa humo hivi:"Jirani ni sawa na mtu mwenyewe; asitendewe visivyo haki au kutendewa madhambi. Utukufu wa jirani wa mtu ni sawa na ule utukufu wa mama yake." Katika riwaya nyingine al-Imam al-Sadiq a.s amesema: Imeelezwa katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Taliba.s "Mfano wa dunia ni sawa na mfano wa nyoka: ngozi yake nyororo mno, lakini ndani yake ni sumu kali mno. Mtu aliye mwenye busara hujiweka naye mbali, lakini jahili anafanya kila aina ya jitihada ya kutaka kuikaribia."

Kwa mujibu wa riwaya nyingineyo, habari ifuatayo imetoka katika kitab adab Amir al-Muminiin: Mtu yeyote asijaribu kurejea katika mithali katika masuala ya Din, kwani amri ya Allah swt haiwezi kutambuliwa kwa mithali. Watatokezea watu ambao watakuwa wakirejea katika mithali, na hao watakuwa na uadui pamoja na Din. Zurarah anaripoti: Nilimwuliza al-Imam al-Baquir a.s. kuhusu hisa ya babu katika urithi. Imama.s. alijibu:"Sijawahi kumwona mtu yeyote yule akilisemea swali hili bila ya kuongezea mawazo yake ya kibinafsi, isipokuwa Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Talib a.s.." Mimi nilimwuliza: "Na jee alisema nini?" Imama.s alinijibu:"Njoo kesho, mimi nitakusomea kutoka kitabuni." Mimi nilisema, "Mimi niwe fidia juu yako, naomba uiseme katika mtungo wa Hadith kwani Hadith zako ni afadhali kwangu kuliko kukisoma kitabu." Imama.s alisema:"Tafadhali usikilize kile nilichokuambia. Njoo kesho na mimi nitakusomea kutoka kitabu hicho." Siku ya pili mimi nilimwendea Imama.s wakati wa adhuhuri. Jaafer ibn Muhammad mwanae Imama.s alinikaribia na Imama.s alimwambia kunisomea kitabu hicho........

Katika riwaya nyingine, Imam al-Sadiqa.s anasema: "Ipo imeelezwa katika Kitabu cha Imam Ali ibn Abi Taliba.s kuwa mtu anywaye pombe na mwenye kumsaidia aliyelewa (muskir) basi wote wanastahili kuadhibiwa, ambavyo ni sawa katika sura zote mbili." Muhammad ibn Muslim, Sahaba wa Imam al-Baquira.s asema: "Abu Jaafer alinisomea kitabu kitab al-faraidh, ambacho yalikuwemo yaliyosemwa na mtumes.a.w.w. na kuandikwa na Imam Ali ibn Abi Taliba.s : "Habari zote zilizotajwa hapo juu, ambazo ni chache sana kutokea riwaya nyingi mno kama hizo, zinatudalilisha kuwa desturi ya Mashia ya kuandika Hadith imetangulia mawaidha ya ma-Imama.s kwa sahaba wao kuhusu uandishi wa Hadith. Ilikuwa ni desturi ambayo ilianzia katika zama za Mtume Mtukufus.a.w.w . na ilikuwa imeanzishwa na Imam Ali ibn Abi Taliba.s . Zipo Hadith, nyingi katika desturi ya Mashia ambazo zimetimiza kanuni za tawatur, na vile vile yapo marejeo katika Sunni ambazo zinathibitisha na kushuhudia Hadith kama hizo.

Mambo yote hayo yanakuelekeza katika uimara na uhakikisho wa usahihi wa Hadith zilizonakiliwa na Mashia. Hii ni kwa sababu pamoja na kuendelea na maongozo ya Maimamua.s hadi kufikia katikati ya karne 3 A.H./9 A.D., Hadith za Mashia zilitoa watunzi wengi mno na ambao maandishi yao kuanzia kipindi cha al-Imam al-Sadiqa.s yamekuwa kwa hakika ni katika idadi kubwa sana. Iwapo mtu ataweza kutupia macho Rijal al-Najashi, basi huyo ataweza kuona kuwa wafuasi wa Imam a.s. wametupatia kazi kubwa ambazo zimetumika kama misingi ya Fiqh katika Ushia.

Ukweli ni kwamba, Mashia idadi yao ndogo kwa upande mmoja na maisha ya hatari waliyokuwa wakiishi kwa upande wa pili ambayo iliwazuia watu waovu na wenye kuvizia majukumu kuingia katika Ushia pamoja na umuhimu uliosisitizwa na Maimamua.s na wafuasi wao katika uandishi, ndivyo vilivyoleta matokeo ya utajiri na usahihi wa Fiqh ya Kishia. Haya ndiyo faida ambazo hazikupatikana kwa Ahl al-Sunnah kwani, kwanza, wingi wa idadi yao, pili, kwa kuwa madhehebu ya Sunni ndiyo iliyokuwa Dini ya utawala wa Dola, na tatu, kwa sababu ya ukosefu wa Hadith zilizoandikwa kwa Waislam kwa ujumla kuyafuatilia yale yanayotokana na ukweli wa misingi ya kihistoria.


UANDISHI WA HADITH

3. HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KATIKA SUNNI

Kazi zote zilizopo hadi leo zinazohusu Hadith zilikuwa zimekusanywa katika kipindi cha karne 2 A.H./8 A.D. au katika karne ya 3 A.H./9 A.D. Historia inatuonyesha kuwa katika kukaribia karne ya 2 A.H. kulitokezea idadi ndogo ya Muhaddithun ambao walianza kuziandika Hadith, ingawaje hazikuwa na mpangilio. Baadaye mkusanyiko huu mdogo ulikuwa kiini cha kazi zote kubwa. Hata hivyo wingi wa Hadith zilizopo sasa kwa kukusanywa, zilienezwa kwa desturi ya kutamkwa (kusemwa), na wakati zilipokuja kuandikwa vitabuni, zilikuwa hazikuwahi kuandikwa popote kabla yake. Ucheleweshwaji katika kuandikwa kwa Hadith ni swala mojawapo muhimu katika historia ya Hadith. Umuhimu wake ni wa ukweli kwamba kucheleweshwa huu kuliathiri hasa kuhusu utunzi na idadi ya Hadith pamoja na uwepesi wao wa kuzushwa (zikaongezwa na kupunguzwa na hatimaye zikawa ni zile zilizo na uongo) na matatizo mengi mengineyo yanayohusiana.

Jambo la umuhimu huu katika swala hili linawahusu wale ambao ndio waliokuwa wamesababisha ucheleweshwaji huo wa kuandikwa kwa Hadith. Mwelekeo wao ulikuja kama ni mfano kwa ajili ya wengine katika kutoziandika Hadith. Katika sehemu yetu hii, tutaweza kuchambua makusudio yao na athari za mwenendo wao wa aina hiyo juu ya Hadith. Kila kinachoweza kukusanywa kwa shida katika Historia ni kwamba baadhi ya Makhalifa walizuia uandikaji wa Hadith kwa sababu fulani fulani. Baada yao kikundi cha Sahaba na Tabiun waliwafuata katika swala hili. Kwa mujibu wa msemo "Watu hufuata dini ya wafalme wao," wao walijiepusha na uandikaji wa Hadith kwa kukubali na kuridhia kwa kuharamishwa hivyo.

Wao walizihifadhi Hadith za Mtumes.a.w.w . kwa kuzikariri tu (kwa kuzihifadhi akilini mwao tu). Kama vile tutakavyoona hapo mbeleni, wao nyakati zinginezo walijaribu kurejea katika kuziandika, ili kuyateketeza maandishi yao katika kipindi cha mwisho wa maisha yao, kama kwamba maandishi hayo yaliwasaidia wao tu katika kuhifadhi kwao. Kumbukumbu hizo za Hadith zilizokuwa zimeandikwa hazikutumiwa kwa kutaka kuzihifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo. Ni jambo la kuvutia sana kuona kuwa kupigwa marufuku wa uandikaji wa Hadith katika Sunni ulitolewa na watawala wao; na vile vile ile amri ya kuziandika Hadith pia zilitolewa na watawala wao.

Al-Zuhri anasema: "Sisi tulikuwa tukichukia mno uandishi wa elimu, hadi hapo wakuu wetu walipotulazimisha kuyaandika hayo. Hapo baadaye tulikuja kugundua kuwa hapakuwapo na yeyote miongoni mwa Waislam waliopinga. "Al-Zuhri anaendelea kusema: "Wafalme waliniambia kuandika elimu ('ilm, i.e. Hadith) kwa ajili yao. Baada ya kuwaandikia kwa muda fulani, mimi nilishikwa na aibu mbele ya Allah swt; (mimi nilijiuliza): Je, kwa nini nimejitayarisha kwa ajili ya kuwaandikia wafalme na wala si kwa ajili ya watu wengineo!?" Ni dhahiri, kama vile itakavyokuja kuonekana kwamba Hadith hazikuwa ni kweli kwa ajili ya Sahaba na Tabiun wote. Wengi wao na akiwemo Ali ibn Abi Taliba.s waliziandika Hadith na vile vile waliwaambia wengine kufanya hivyo. Wengine walianza kuziandika Hadith wakati sheria zilizowekwa na Makhalifa juu ya kutoziandika Hadith zilipobadilishwa na amri ya Kikhalifa kutoka kuziandika Hadith.

'Umar ibn Abd al-Aziz (101 A.H./719 A.D.) ndiye aliyekuwa Khalifa wa kwanza kuamrisha wanazuoni wa miji mbalimbali kuziandika Hadith na kumpelekea huyo Khalifa maandishi yote. Imeripotiwa kuwa Khalifa alimwandikia Muraah ibn Kathir akimwomba amwandikie Hadith za Mtumes.a.w.w Vile vile yeye alimwandikia Abu Bakr ibn Muhammad Hazm:"Andika Hadith yoyote ile ya mtume s.a.w.w uliyonayo na kunitumia na chochote kile kilichonakiliwa kutoka kwa Umar, kwa sababu ninayo hofu kuwa utafika wakati ambapo Hadith zitakuwa zimetoweka." Yeye pia aliwaandikia watu wa Madinah akiwataka wamwandikie chochote kile kilichobakia cha Hadith za Mtumes.a.w.w .

Ripoti hizi zinaonyesha wazi wazi kuwa uandikaji wa Hadith haukuwa jambo lenye umuhimu hadi wakati huo, hata hivyo, haimaanishi kuwa hapakuwepo na Hadith zilizokuwa zimeandikwa hadi wakati huo. Pamoja na kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz kazi hii haikufuatiliwa na Makhalifa waliofuata, na kwa mara nyingine tena uandikaji wa Hadith uliangukia katika kusahauliwa. Kukariri (kuhifadhi katika akili) ndiyo iliyokuwa njia iliyobakia. Hadith za kusemwa mdomoni tu (bila ya maandiko) ndiyo iliyokuwa njia ya uenezaji wakati ambao Sunni walirithi kutoka vizazi vyao vilivyowatangulia, ilisababisha upinzani mkubwa mno katika kuziandika Hadith. Sisi twaweza kuelewa vyema hali hii wakati tutakapokuja kujua kuwa baadhi ya Muhaddithun walichukizwa mno na uandishi wa Hadith hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. Kauli za wanahistoria kuhusiana na ukusanyaji wa Hadith hapo mwanzoni zinaelezea hayo hayo.

Abd al- Razzaq anaelezea kuwa mtu wa kwanza kuzikusanya Hadith alikuwa Abd al-Malik ibn Jurayj, aliyejulikana kama Ibn Jurayj (150 A.H./767 A.D.) Vile vile Abd al-Rahman Al-Awzai (88-157 A.H./707-773 A.D.) alikuwa ni miongoni mwa wale walioanza kuzikusanya Hadith. Al-Dhahabi anaandika kuwa, katika kipindi hiki ndipo Wanazuoni wa Kiislamu walianza kuandika Hadith, Fiqh na tafsiri katika mwaka 143 A.H./760 A.D. Wafuatao ndio waliokuwa wakiongoza katika kazi hizo nao ni Ibn Jurayj katika mji wa Makkah, Malik (179 A.H./795 A.D.) huko Madinah, al-Anzai katika Syria, Said ibn Abi Urwah (156 A.H./783 A.D.) huko Basrah, Muammar huko Yemen, Sufyan al-Thawri (156 A.H./783 A.D.) huko Kufah. Kabla ya kipindi hicho, hata hivyo, Muhaddithun waliongoza wakiripoti Hadith kutokea kukariri au kutokea kwa waliotegemewa lakini zilikuwa ni mikusanyo isiyokuwa na mipangilio.

Mahali pengine yeye ni mbainifu zaidi wakati asemapo: "Ibn Jurayj na Ibn Abi Urwah walikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith na Muammar ibn Rashid alikuwa ni wa kwanza miongoni mwao huko Yemen." Ipo habari iliyoripotiwa na Abd al-Aziz ibn Muhammad al-Darwardi kuwa mtu wa kwanza kukusanya elimu alikuwa Ibn Shihab al-Zuhri. Ibn Shihab al-Zuhr (124 A.H./742 A.D.) mwenyewe anaripotiwa akiwa amesema: "Umar ibn Abd al-Aziz alituamrisha kuzikusanya Hadith za Mtumes.a.w.w Kufuatiwa hayo sisi tuliandika katika sura ya kitabu, na kupeleka nakala ya kitabu hicho katika sehemu zote za utawala wake." Ni dhahiri, ingawaje Hadith zilikuwa zikikusanywa kwa kiasi fulani katika siku hizo, kazi ya ukusanyaji ilianza kuzorota kwa sababu ya upingamizi uliofuatia kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz, na vile anavyosema al-Dhahabi, kazi hiyo ya ukusanyaji wa Hadith uliahirishwa au kuachwa kwa kipindi cha nusu karne.

Ibn Hajar anasema: "Kazi ya ukusanyaji na upangaji (tabwib) wa Hadith ulianza katika miaka ya mwishoni mwa kipindi cha tabi'un, yaani ni kwamba; wakati ambapo Wanazuoni wa Kiislam walipokuwa wameenea katika miji. Wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith walikuwa ni Rabi ibn Subayh na Sa'id ibn Abi Urwah......hadi wakuu miongoni mwa Wanazuoni wa tabaka la tatu walipokusanya ahkam.

Al-Dhahabi pia anaelezea kitu kama hicho. Kutokana na taarifa hizo inaweza kudadisiwa kuwa ukusanyaji wa Hadith uliotokezea katika sehemu mbili: Sehemu ya kwanza ni mkusanyiko usio kamilifu mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. na sehemu ya pili ni ukusanyaji uangalifu katika sehemu yake ya pili. Hajji Khalifah anakubaliana na haya pale asemapo: "Wakati Islam ilipoenea katika sehemu mbalimbali, na miji ya Islam ilipopanuka, tabi'un walisambaa mote humo. Baada ya muda, mkuu wao alipofariki dunia na hivyo ndivyo ilivyokuwa imekuja kuathiri ukusanyaji wa Hadith.

Wanazuoni walianza kuhisi haja ya kuziandika Hadith na kuzihifadhi kwa njia ya kuziandika. Katika maisha yangu, lilikuwa ni jambo la maana la kuziandika Hadith, kwa sababu kukariri tu kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kuja kupoteza fahamu au kuzipotoa. Baada yao, kulitokezea kipindi cha wataalamu wa Hadith kama Ibn Jurayj na Malik ibn Anas. Inasemekana kuwa mtu wa kwanza katika kukusanya Hadith alikuwa Rabi ibn Subay wa Basrah. Baada yahuyo, zoezi kama hili lilikuwa ni la kawaida.

Kutokana na taarifa hizo, tunaweza kumalizia kuwa, kotekote, kulikuwapo na vipindi vitatu katika mpitilio wa Hadith za kutamkwa. Kipindi cha kwanza kilichukua/kilidumu mwanzoni hadi mwishoni mwa karne ya 1 A.H. /7 A.D. katika kipindi hiki uandishi wa Hadith haukuwapo wala haukujaribiwa isipokuwa tu katika hali chache ambapo Sahaba walijaribu kuziandika kwa kwenda kinyume na amri ya Makhalifa. Katika kipindi cha pili, kuanzia mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. hadi kwa kufikia katikati, kulitokezea uandishi na ukusanyaji wa Hadith katika hali isiyokuwa kamilifu na pia mambo yaliyoandikwa yaliweza kukusanywa. Katika kipindi cha tatu, kilichoanzia katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., uangalifu mkubwa ulielekezwa katika ukusanyaji na uandikaji wa Hadith ikiwa ni shughuli muhimu kimsingi. Vitabu vichache mno vilivyoandikwa katika kipindi hiki vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana- kama vile musannaf Ibn Abi Shaybah, musannaf ya Abd al-Razzaq na Muwatta ya Malik ibn Anas yalikuwa yameanzishwa katika sehemu ya pili ya karne ya 2 A.H./8 A.D. Kwa mujibu wa ripoti ya al-Dhahab, musnad ya kwanza ilikusanywa na Nu'aym ibn Hammad. Yahya al-Hamani huko Kufah na al-Musd huko Basrah nao ndio waliokuwa wa kwanza miongoni mwa Wanazuoni wa miji hii katika kukusanya musnad.

1

TADWIN AL HADITH

UANDISHI WA HADITH

4. SABABU ZA KUCHELEWA KUANDIKA HADITH

Inafahamika vyema kabisa kuwa Mtumes.a.w.w , kuanzia mwanzoni kabisa mwa Utume wake, aliupatia umuhimu zaidi kuhusu uandishi wa Qurani. Kimatokeo Qurani ikawa ipo mbali na makosa au mabadiliko (tahrif). Hata hivyo, katika hali ya Hadith kwa mujibu wa imani yetu mbali na ruhusa au amri ya Mtumes.a.w.w kwa kuhusiana na uandishi wa Hadith na mbali na ukweli kwamba Hadith zilikuwa zimeandikwa katika zama za uhai wa Mtumes.a.w.w , sio kwamba tu kuwa haukupewa umuhimu kwa kazi, pia iliweza hata kupingwa. Upingamizi huo ulisababisha matatizo mengi kuhusiana na Hadith, ambayo tutayaona hapo mbeleni.

Uchelewesho huo wa kuziandika Hadith na matokeo yenye hatari yalifanya kikundi kimoja kumtupia lawama na 'udhubillah' Mtumes.a.w.w.

Wao walitambua wazi kuwa upingamizi wa uandishi wa Hadith iwapo itatokea kwa Mtumes.a.w.w , basi haitaweza kulaumiwa, kwani Mtumes.a.w.w hawezi kulaumiwa; hata hivyo, iwapo wataielezea kwa wengine basi itatoboa udhaifu wao. Kwa hivyo, walimwelekezea Mtumes.a.w.w kuwa ndiye aliyekataza kuandikwa kwa Hadith.

5. RIWAYA YA ABU SA'ID

Riwaya ifuatayo imenakiliwa kwa mamlaka ya Abu Sa'id al-Khudhri: "Musiandike chochote kile kutoka kwangu isipokuwa Qurani tu, na yeyote yule aliyekwisha andika chochote kile basi ni lazima ayateketeze yote." Taarifa hiyo ni wazi na yenye maana isiyofahamika. Maana inayotakiwa kuelezwa ni kwamba hakuruhusiwi kuandikwa kwa Hadith. Kwa mujibu wake, mtu yeyote aliyekuwa ameandika chochote kile basi lazima akiteketeze. Ni sawa kabisa kwa sababu ya uwazi wa ubainishi wake, vile vile pamoja na sababu zinginezo, ndiyo maana sisi hatuwezi kuikubali uhakiki wa taarifa hiyo au nyinginezo kama hizo. Sababu zetu za kutokubaliana na Hadith hiyo ya juu ni kama zifuatazo:

1.Kwanza : iwapo sisi tutaikubalia Hadith hii basi hatuwezi kuifungia kipindi cha muda. Iwapo uandishi wa Hadith ulikatazwa na haram, basi ni haram katika kila zama. Hata hivyo, sisi twaona wanaoinakili Hadith hii, wao wenyewe hawakuifuatilia na wao hatimaye waliziandika na kuzikusanya Ahadith. Uandishi huu, kama ilivyoonekana hapo juu, ulianza katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., na kukosekana kwa utiifu wa Hadith inatuonyesha kuwa hao wanainakili Hadith walikuwa hawakuichukulia kama sahihi na kweli; kwani hao walijua kuwa chochote kile kilichoharamishwa na Shariah haiwezi kubadilishwa kikawa halali. Jambo la kuvutia humu ni kwamba wao wameirekodi hata Hadith hii, ambavyo wao hawakuifuatilia, kwa kalamu zao zilizobarikiwa! Je, itawezekanaje sisi kuiamini kuwa ni sahihi na kweli?

2.Pili : waandishi hawa hawa pia wamezinakili Hadith zinginezo zinazozungumzia kuruhusiwa kuandikwa kwa Hadith, na iwapo sisi tutazichukulia Hadith zote mbili kuwa ni sawa katika maelezo na maelekezo, basi itatulazimu kuziachia mbali Hadith zote mbili hizo kwa sababu ya kupingana kwao kwenyewe. Kwa hivyo, katika hali kama hii Hadith hizi zote mbili zinapoteza ustahi wa kuaminika; navyo hata sisi, kwa kudhania tu, hatuwezi kamwe hata kutumia njia zinginezo kusadikisha Hadith ambayo ipo inakataza uandishi wa Hadith za Mtumes.a.w.w .

3.Tatu : Abu sa'id al-Khudhri, ambaye anatajwa hapo juu kwa wingi katika kuinakili taarifa hiyo, pia anatoa taarifa nyingine inayopingana na ile ya kwanza, yeye anasema:

"Katika siku hizo, sisi tulikuwa hatuandiki chochote kile isipokuwa Qurani na tashahud."

Nukta mbili zinaweza kufahamika kwa kujua sababu zake kutokana na taarifa za Abu Sa'id.

Kwanza : Abu Sa'id haelezi kuwa kutoandika kwao Hadith kulitokana na amri ya Mtumes.a.w.w kwani kama ingalikuwapo, basi angalionyesha hayo, hadi hapo isemwe kuwa maelezo kama hayo hayakuazimiwa hapa. Uwezekano huu wa pili uliotolewa, ingawaje unaweza kuchukuliwa kwetu sisi, inaonekana ya mbali mno. Na nukta ya pili ni kuongezwa kwa neno tashahhud katika taarifa hii, kitu ambacho hakipatanishi pamoja na kusudi la uharamisho wa kuandika isipokuwa Quran tu. Ni jambo la kutilia maanani kwamba Hadith nyingine kutoka kwa Ibn Mas'ud, neno istikharah limeongezwa pamoja na tashahhud.

Kwa kuhusiana na Hadith hii, inawezekana kukaulizwa, je, ni kwa nini Mtumes.a.w.w aruhusu uandishi wa tashahhud pekee yake, ambapo inatambuliwa kuwa kutapotea vile wakati uendeleavyo, hayo pia yaliweza kutokea pamoja na Hadith zinginezo, baadhi yao ambazo zilikuwa na maongozo muhimu kabisa ya Shariah za Dini. Na katika upande wa pili, iwapo kulikuwapo na madhara yoyote katika kuziandika Hadith, basi madhara hayo pia yaliweza kutokezea katika kuandika tashahhud au chochote kile. Kwa hivyo, haikubaliki kimantiki kudai kuwa Mtumes.a.w.w ndiye aliyeharamisha kuandikwa kwa Hadith.

4.Nne : kile kinachoweza kukusanywa kutokana na historia- ambacho sisi tutalisemea kwa zaidi hapo mbeleni - Abu Bakr, na hata Khalifa wa pili, walipendekeza kuandikwa kwa Hadith mwanzoni mwa Ukhalifa wao. Hata hivyo, hapo baadaye wao waliharamisha kwa kutolewa kwa sababu zao. Hao Makhalifa kamwe hawakusema kuwa kazi kama hiyo ilikuwa imeharamishwa na Mtumes.a.w.w . Zaidi ya hayo wao waliposhauriana na Sahaba wengineo kuhusu kuandika Hadith, nao pia walipendezewa na shauri hilo. Hii pia linatuthibitishia kuwa hapa kutolewa amri na Mtumes.a.w.w . ya kuharamisha kuandika kwa Hadith.

5. Katika mojawapo ya Hadith Abu Basir anaripotiwa akiwa amemwambia Abu Sa'id al-Khudhri: "Sisi twaandika chochote kile tukisomacho." Abu Sa'id alimwambia: "Je, wataka kuyakusanya ili ukitengeneze Kitabu? Mtumes.a.w.w . ametuelezea Hadith nasi pia twakuambia wewe, nawe pia kama sisi ni lazima uzikariri tu kwa mdomo bila ya kuandika." Nukta mbili hapa zinastahili kuchunguzwa.

Kwanza, Abu Sa'id hasemi kuwa Mtumes.a.w.w . ndiye aliyeharamisha uandikwaji wa Hadith. Pili, sababu aitoayo kwa kutoziandika Hadith ni sawa na zile zilizoripotiwa kutokea kwa Khalifa wa pili, ambaye naye pia hamsemi Mtumes.a.w.w . kuwa ndiye aliyeharamisha uandishi wa Hadith. Katika hali yoyote ile, ni jambo la kuyakinisha kuwa Mtumes.a.w.w . kamwe hakuharamisha uandishi wa Hadith.

6.Sita , kuna taarifa katika Hadith, moja kwa moja baada ya kutajwa hiyo ya juu, na kuwapo kwake pia kunatudalilishia kule kutothaminiwa kwake: "Simulieni (chochote kile utakacho) kutokea Waisraili. Hakuna madhara ndani yake." Kuanzia mwanzoni kabisa, kwa upande mmoja Mtumes.a.w.w anafahamika kwa kuchukizwa mno katika kusikia hadithi za Mayahudi (hujulikana kama Israiliyyat) -na kwa upande wa pili, Wanazuoni wa Kiislam wamekwisha zitambua madhara ya mawazo yanayoenezwa nayo, inaweza kusemwa kuwa Hadith hiyo nzima ni kazi ya uzushi mtupu. Hadith hii inawataka Waislam kwa upande mmoja, waziandike Hadith za Mtumes.a.w.w, na hatimaye kwamba zitaweza kusahauliwa pole pole; na upande wa pili, inawapatia leseni ya bure ya kuunganisha chochote kile wakitakacho kutoka kwa Mayahudi, Haya ndiyo maazimio maovu kabisa za Hadith kama hizi za kuzuliwa. Je, kunaweza mtu yeyote mwenye akili timamu akasema kuwa Mtume s.a.w.w. ndiye aliyetoa amri kama hiyo?

Ipo Hadith nyingineyo kutokea Abu Sa'id al-Khudhri ambayo inatuletea uwezekano wa Mtume s.a.w.w. kutomruhusu Abu Sa'id kuandika Hadith kutokana na sababu maalum, ingawaje, katika mtazamo wetu, uwezekano wa kuruhusiwa katika swala hili pia ni kwamba Hadith hii vile vile ni uzushi. Abu Sa'id asema:"Mimi nilimwomba Mtume s.a.w.w. ruhusa ya kuandika Hadith, lakini yeye alikataa kunipa idhini." Je kwa sababu zipi ? Hadith hii inatuunga mkono katika uwezekano wa Mtume s.a.w.w. kwa kumkatalia ruhusa ya kuandika Hadith katika swala la Abu Sa'id. Wakati inapozingatiwa katika nuru ya Hadith, ambazo sisi tutazinakili hapo mbeleni, ambapo Mtume s.a.w.w. yupo anaripotiwa kwa kutoa idhini kwa watu wengineo basi uwezekano huu utajipatia nguvu zaidi.

7. KUTOKUBALIKA KWA HADITH ZA ABU HURAYRAH

Kuhusiana na hayo, kuna Hadith kutoka kwa Abu Hurayrah ambayo pia imehusika. Abu Hurayrah asema: "Mtumes.a.w.w . alitufikia wakati tulipokuwa tunaziandika Hadith. "Je, mwaandika nini?" Aliuliza Mtumes.a.w.w mimi nilijibu: "Haya ni mambo ambayo sisi tumeyasikia kutoka kwako." Mtumes.a.w.w . alisema: "Je, munataka kuandika kitabu mbali na Kitabu cha Allah swt? Hakuna kilichopotosha mataifa isipokuwa tu pale wameandika kitabu mbali na Kitabu cha Allah (Quran)" Hadith hii pia haikubaliki kwa sababu zifuatazo:

1. Kwa sababu ya wengi waliokwisha kutoa sababu zao katika masomo yao na ambazo sisi pia tumeziona kuwa zinaweza kukubalika baada ya kuchunguzwa, hivyo usadikifu ('adalah) wa Abu Hurayrah hauwezi kukubaliwa. Vile vile inawezekana kuwa Hadith hii imezuliwa na wengine halafu wakaja kumtaja Abu Hurayrah kuwa ndiye aliyeiripoti.

2. Pili, mazungumzo yaliyomo ni sawa kabisa, kama vile yalivyokuwa yametolewa na Khalifa Umar wakati alipokuwa ameamua kuziandika Hadith na baadaye kughairi. Lakini Khalifa mwenyewe kamwe hakumsingizia Mtumes.a.w.w . Wakati ambapo Abu Hurayrah, au wale wote wengineo wakimsingizia Mtumes.a.w.w ., hawakutupatia mwanya wa kubishana nao kwa madai yao (kwani madai yao ni kuwa Mtumes.a.w.w . tu ndiye aliyeyasema, hivyo hakuna ubishi juu yakauli ya Mtume): Khalifa Umar kama vile tutakavyoona hapo mbeleni, alifikia maamuzi hayo baada ya kuzingatia mambo fulani fulani.

3. Tatu, mazungumzo yaliyomo na yanayonekana katika Hadith hii ingawaje inaonekana kuwa inayo mizizi katika kauli ya Mtumes.a.w.w . ambayo itazungumzwa hapo mbeleni, inazungumzia juu ya Mtumes.a.w.w . kuharamisha vitabu vya Mayahudi na Wakristo, na wala si kuharamishwa Hadith za Mtumes.a.w.w. ambazo ni kitu kilicho kamili baada ya Quran.

4. Nne, je inawezekana kwa Mtumes.a.w.w. kuharamisha kuandikwa kwa Sunnah, ambayo ndiyo inayofuatia baada ya Quran? Au aliharamisha kuwa hivyo isibakie sambamba na Quran? Je, ni nafasi ipi iliyo ya Sunnah ya Mtumes.a.w.w. isiokuwa ubavuni mwa Quran? Je, ni ukweli unaoweza kupingwa kuwa Quran na Sunnah ndivyo kwa pamoja vinafanya Shariah za Kiislam? Ipo Hadith nyingine ivutiayo, ambayo inadhihirisha tabia ya udanganyifu wa Hadith kama hizo, nayo ni ile iliyonakiliwa na Abu Hurayrah. Baada ya kuelekezea kama taarifa tuliyonayo ipo, inaendelea kuongezea mambo mengi ambayo yanatudhihirishia upotofu katika upande wa Abu Hurayrah, au mzushi aliyezusha juu yake. Kwa mujibu wa Hadith hii, Mtumes.a.w.w. aliwasikia watu wameziandika Hadith zake. Papo hapo, alikwenda juu ya Mimbar na baada ya kumsifu Allah swt alisema: "Ni aina gani ya vitabu hivi ambavyo nimesikia mmeviandika? Kwa hakika mimi ni mwanadamu tu. Yeyote aliyeandika chochote kile, basi ni lazima aniletee mimi." Hadith hiyo kwa wazi wazi inakanusha Sunnah ya Mtumes.a.w.w. kwani Mtumes.a.w.w. yupo anakana uwezekano na uhalali wake wa utume kwa kusema kuwa yeye alikuwa ni mtu kama watu wengine wa kawaida. Hili ni jambo ambalo mtu yeyote hawezi kulikubali kwani ni uzushi mtupu. Jambo la kuvutia zaidi ni kuhusu kusema kwa Mtumes.a.w.w. hapa ('mimi ni mwanadamu') ipo imeelezwa katika Hadith nyingine kuwa hayo yalisemwa na kikundi cha watu wa Quraysh kuhusu Abd Allah ibn Amir ibn al-As, ambaye alikuwa ameandika Hadith za Mtumes.a.w.w. Hapo Mtumes.a.w.w. hatilii maanani maoni yao kwa hakika yupo anayakanusha. Anasema:"Mimi hakuna nilisemalo isipokuwa ni haki tupu."

5. Tano, ipo imeripotiwa kutoka Abu Hurayrah mwenyewe kuwa hakuna mtu yoyote yule anayemzidi katika kunakili Hadith, isipokuwa Abdallah ibn Amribn al-As, kwa sababu huyu alikuwa akiziandika wakati ambapo Abu Hurayrah hakuwa akifanya hivyo. Taarifa hii inaonyesha kutokuwapo kwa uharamisho Abdallah aliziandika Hadith zote, ambapo zipo sababu za kibinafsi zilizomfanya Abu Hurayrah asiziandike. Hivyo, inatuonyesha wazi wazi kuwa hapakuwepo na amri yoyote yenye kuharamisha kuandikwa kwa Hadith za Mtume s.a.w.w.; wote waliotaka kuziandika waliziandika, na yeyote asiyetaka kuziandika hakuziandika lakini kwa sababu zao binafsi bila ya kuzuiwa.

6. Sita, katika ripoti nyingineyo Abu Nuhayk, mwanafunzi wa Abu Hurayrah, asema: "Mimi nilikuwa nikiviazima vitabu kutoka kwa Abu Hurayrah, nilinakili, na kumchukulia (makala zangu) Abu Hurayrah na kumsomea. Kwa kila Hadith nilikuwa nikimwuliza iwapo amewahi kumsikia Mtume Mtukufus.a.w.w. akiisema, naye alikuwa akiitikia." Hadith hii pia inaonyesha uongo wa Hadith isemayo kuharamishwa uandishi wa Hadith, ambayo amesingiziwa Abu Hurayrah.

7. Imeripotiwa na Hamman ibn Munabbih, mwanafunzi wa Abu Hurayrah kuwa alikusanya mus-haf iliyokuwa na Hadith zote zilizokuwa zimenakiliwa na mwalimu wao katika uhai wake. Hayo pia yanatuonyesha kupingana na Hadith hiyo, kwani isingewezekana kwa Abu Hurayrah kunakili Hadith inayoharamisha uandishi wa Hadith wakati ambapo wanafunzi wake wameziandika Hadith mbele yake na katika uhai wake, au tuseme labda kuwa Abu Hurayrah hakutekeleza Hadith ipigayo marufuku uandishi wa Hadith kwa kunakili Hadith na kuzifundisha.

Vile vile ipo Hadith nyingineyo iliyoripotiwa na Zayd ibn Thabit kwamba siku moja alimwendea Muawiya, ambaye alimwuliza kuhusu Hadith fulani. Hapo Muawiya alimwambia mtu fulani kuiandika. Hapo Zayd alisema: "Mtume Mtukufus.a.w.w. ametuambia tusiandike Hadith ya aina yoyote ile." Sisi twaamini kwa uhakika uliowazi kuwa Hadith zilikuwa zimeandikwa na Tab'un na Tabi'in na baadhi ya wanazuoni wa Sunni, wanathibitisha kutotegemewa kwa Hadith kama hizo. Hapo mbeleni katika kulichambua swala hili, sisi tutaona uthibitisho utakaoonyesha sababu za kweli katika kuharamisha uandishi wa Hadith za Mtume Mtukufus.a.w.w. Uhakika na uthibitisho huu unaonyesha kuwa sahihi kwa kumsingizia Mtumes.a.w.w. kwa taarifa kama hizo. Pia imeripotiwa kuwa Ibn Mas'ud alielezea katika usia wake kuwa mkusanyo (sahifa) wa Hadith zilizofanywa naye, ziteketezwe. Katika sura hii, haionyeshi wazi iwapo tendo hili lilikuwa limejibu amri ya Mtume Mtukufus.a.w.w. Labda inawezekana, alikuwa akifuata amri ya Makhalifa. Pili, kama vile tutakavyozungumza hapo mbeleni, tendo hilo linaelezea kuhusu kuteketeza riwaya na mapokezi ya Mayahudi (Israilliyyat) na wala si Hadith za Mtumes.a.w.w. Vile vile imeripotiwa kuwa Abu Musa al-Ash'ari aliziteketeza Hadith zilizokuwa zimeandikwa na mtoto wake. Tukichukulia utiifu wa Abu Musa kwa Khalifa wa Pili, labda inaweza kusemwa kuwa tendo lake hili lilikuwa bila shaka chini ya ushahidi kuonyesha kuwa Abu Musa alitenda kwa kuvutiwa na uharamisho huo wa Mtumes.a.w.w. kuhusu Hadith.

Moja ya kitu kinachoonyesha kutokuwa halisi kwa mapokezi hayo yaliyozuliwa juu ya Mtumes.a.w.w. kuharamisha uandishi wa Hadith, ni kauli aliyoitoa Umar kuhusiana nalo kwa nia yake ya kutaka kukusanywa kwa Hadith za Mtumes.a.w.w. Umar anaripotiwa akiwa amesema: "Mimi nilinuia kuziandika Sunnah za Mtumes.a.w.w. Lakini lilikuja wazo akilini mwangu kuwa watu waliopita walikuwa wameandika baadhi ya vitabu na walikuwa wakivitegemea mno, hatimaye wao waliacha kukitegemea Kitabu cha Allah swt. Kwa kiapo cha Mungu, mimi sitakubaliana na chochote kile kitakachoweza kukifunika (kuachwa) Kitabu cha Allah (Quran)."

Katika riwaya ya hapo juu, inaonyesha kuwa Khalifa wa Pili alinuia kuandika Hadith hapo awali. Katika baadhi ya tafsiri ya riwaya hii inaelezea kuwa aliwashauri Sahaba wengine kuhusu swala hili nao pia walilikubalia (kuandika Sunnah za Mtumes.a.w.w; lakini hapo baadaye yeye alilibadilisha shauri lake hilo kwa sababu zake alizozitaja, na wala si kwamba Mtumes.a.w.w. ndiye anayehusika katika kuharamisha.

Jambo lingine ambalo linaloweza kuonekana kama uthibitisho wa kukanusha uhalisi wa Hadith isemayo juu ya uharamisho wa kuandika Hadith, ni maneno aliyoyasema Mtumes.a.w.w. siku ya Alhamisi ya mwisho katika maisha yake (yaani kabla ya kufariki). Siku hiyo, walikusanyika Sahaba wote katika kitanda chake Mtumes.a.w.w. na hapo Mtumes.a.w.w. aliwaambia: "Nileteeni wino na karatasi ili niweze kuwaandikieni mambo fulani fulani ambayo hapo baadaye nyie mnapashwa kujitahadharisha msitumbukie katika makosa." Hapo baadhi ya watu wakiongozwa na Umar walipinga hayo wakisema "Kitabu cha Allah kinatosheleza kwetu sisi." Riwaya hii inatuonyesha kuwa uandishi wowote mbali na Quran haukupigwa marufuku tu, bali hata ulichukuliwa na Mtumes.a.w.w. kuwa ni lazima ili kuokoa Ummah kuangukia makosa na upotofu. Wakati Mtumes.a.w.w.

alipokuwa akiulizia vifaa vya kuandikia na kikundi cha Sahaba- kikiongozwa na Khalifa wa Pili kwa mujibu wa al-Shahristani katika al-milal wa al-nihal- walimpinga Mtumes.a.w.w ., kwani Mtumes.a.w.w. alikuwa akielewa wazi maafa yatakayotokea hapo baadaye kutokea tukio au kisa hiki. Hapo mbeleni sisi tutachambua kwa undani zaidi yaliyokusanywa na kusemwa na wanazuoni wa Sunni kuhusu athari mbaya zilizotokana na kutoandikwa kwa Hadith lakini ni lazima tujiulize "Je, ni sahihi kwa kumdhania Mtumes.a.w.w. katika kuharamisha kuziandika Hadith zake, jambo ambalo limeleta maovu makubwa katika utamaduni wa Kiislamu na kusababisha Sunnah za Mtumes.a.w.w. kuchezewa na Hadith hizo za kuzuliwa? Je, ni kweli kuwa Mtumes.a.w.w. ndiye anayehusika moja kwa moja katika upotofu huu na madhara yote yaliyotokea?"

8. HADITH ZA MTUME S.A.W.W. KATIKA KURUHUSU UANDISHI WA HADITH

Hadith zimepokelewa kutoka Mtumes.a.w.w. ambamo yeye ameruhusu uandishi wa Hadith kijumla au kuruhusu kikundi fulani. Hadith hizi, zenyewe, zinatosheleza kukanusha Hadith zilizotangulia zinazozungumzia kuhusu kuharamishwa kwa uandishi wa Hadith, au tuseme haikosi, kuleta vurugu la riwayaat (wingi wa riwaya) katika hali yoyote, zinashindwa kubakia na uhai wao (hujjiyyah);kwani idadi ya Hadith hizi ni kubwa mno, na kwa kutilia maanani ya makanusho yaliyonayo dhidi ya Hadith zinazozua juu ya kutoandika Hadith, basi uhalisi wa Hadith kama hizi ni zenye kusadikiwa kabisa. Hadith hizi si kwamba zinazoruhusu kuandika Hadith bali pia zinatuamrisha kuziandika Hadith za Mtumes.a.w.w.

Hadith ifuatayo imenakiliwa kupitia mfululizo wa upokezi kuwa kulikuwapo na mtu aliyemlalamikia Mtumes.a.w.w. juu ya udhaifu wake wa kuhifadhi mambo katika akili yake. Mtumes.a.w.w. alimwambia: "Chukua msaada wa mkono wa kulia (i.e. kuandika) dhidi ya udhaifu wa hifadhi ya akili yako." Mtumes.a.w.w. yupo anaripotiwa akisema: "Ikamateni (hifadheni, iandikeni) elimu kwa njia ya kuandika."

Imeripotiwa kutoka Rafi' ibn Khadij kuwa yeye alisema: "Sisi tulimwuliza Mtumes.a.w.w. ,'Je tunaweza kuandika baadhi ya mambo ambayo twayasikia kwako?' Mtumes.a.w.w. alijibu, 'Andika hayo na wala hakuna madhara ndani yake.' Imeripotiwa kwa mamlaka ya Amr ibn Shu'ayb kuwa baba yake alimwuliza Mtumes.a.w.w : "Sisi tukisikia mambo kutoka kwako ambayo hatuwezi kuhifadhi akilini mwetu kwa kipindi kirefu, je, tunaruhusiwa kuyaandika?" Hapa Mtumes.a.w.w . alijibu:Naam, muyaandike"

Imeripotiwa kupitia mifululizo ya wanaonakili, kutoka Abdallah ibn Al-As kwa kusema: "Mimi nilimwuliza Mtumes.a.w.w .: 'Je, tunaweza kuandika kile tukisikiacho kutoka kwako? Mtumes.a.w.w. alijibu, 'Naam.' Mimi niliulizia. 'Bila ya kujali wewe ukiwa umeghadhabika au mpole? Mtumes.a.w.w. alijibu,"Naam mimi sizungumzi chochote kile isipokuwa haki tupu, hata kama nikiwa nimeghadhabika au nikiwa nimefurahishwa." Katika Hadith nyingine, msimulizi anaripotiwa kwa kumwuliza Mtumes.a.w.w. "Je, twaweza 'kuikamata' elimu?" Mtumes.a.w.w. alijibu:"Naam." Huyo huyo Abd Allah ibn Amr anaripotiwa kuwa,"Nilikuwa nimezoea kuandika chochote kile nilichokisikia kutoka kwa Mtumes.a.w.w . kwa ajili ya kurekodi. Baadaye Maqureyshi walinizuia kufanya hivyo, na mimi pia niliachilia kuandika. Baadaye, mimi nilimwelezea Mtumes.a.w.w. swala hilo. Naye alisema:"kwa kiapo cha Mungu ambaye anayamiliki maisha yangu, mimi kamwe sitamki chochote kile isipokuwa haki tupu."

Imeripotiwa na Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Taliba.s kuwa Mtumes.a.w.w alisema:"Andikeni elimu (ilim) kwani mutafaidi nacho humu duniani na akhera vile vile. Eleweni kuwa elimu haikubali mmiliki wake ateketee."

Hadith nyingine mashuhuri ya Ma-Imam wa Ahl al-Bayta.s ambayo imesimuliwa na chanzo cha Sunni na Shia, inaelezea maandiko (sahifah) juu ya upanga wa Mtumes.a.w.w. Al-Imam al-Sadiqa.s anaripotiwa akiwa amesema: "Kulikuwapo na Sahifah katika mpini wa upanga wa Mtumes.a.w.w. yakisomwa:"Amelaaniwa yule anayeiba mipaka ya ardhi. Amelaaniwa yule ajifanyiaye marafiki mbali na mawali wake." Au alisema:"amelaaniwa yule ambaye anakana neema za Mola wake aliyempatia."

Abu Hurayrah anaripotiwa akisema: "Hakuna yoyote yule anayeweza kuelewa zaidi yangu kuhusu Hadith za Mtumes.a.w.w. isipokuwa Abd Allah ibn Amr, kwa sababu yeye alikuwa akiyaandika kwa mkono wake, na kuhifadhi akilini mwake, ambapo mimi nilikuwa nikiyahifadhi tu bila ya kuyaandika. Naye huyo alikuwa amepatiwa idhini na Mtumes.a.w.w. kwa ajili ya kuziandika Hadith zake." Abd Allah ibn amr anaripotiwa kwa kusema: "Mimi nataka kusimulia Hadith zako na iwapo wewe utaniruhusu mimi nitaweza kuutumikisha mkono wangu (i.e. katika kuandika) ili kuusaidia moyo wangu (i.e. kuhifadhi). Na Mtumes.a.w.w. alisema, 'iwapo ni Hadith zangu, basi lazima uchukue msaada wa mkono wako.''' Yeye pia anaripotiwa kuwa na sahifah ambayo ilijulikana vyema kama al- Sahifat al-Sadiqah, ingawaje wengine wanakana kama ilikuwa na Hadith za Mtumes.a.w.w. Al-Mughirah ibn Shu'bah anaripotiwa kwa kuthibitisha kuwa Abd Allah ibn Amr alikuwa na Sahifah iliyoitwa al-Sahifah al-Sadiqaah.

Katika Hadith nyingine, Mtumes.a.w.w. anaripotiwa akisema:"Wakati mumin anapokufa, karatasi alimoandika elimu (ilim) itabakia daima na itakuwa ni pazia baina yake na moto wa Jahannam Siku ya Qiyama."

Al-Tirmidhi ameripoti kuwa Sa'id ibn Ubadah alikuwa na sahifah ambamo alikusanya idadi kubwa ya Hadith za Mtumes.a.w.w. Mtoto wake pia alikuwa anayo mazoea ya kunukuu Hadith kutoka sahifah hiyo. Kwa mujibu wa riwayah za al-Bukhari, ilikuwa ni nakili ya sahifah ya Abdallah ibn Awfi ambaye alizoea kuandika Hadith ndani mwake kwa mikono yake mwenyewe. Samurah ibn Jundab pia alikusanya Hadith nyingi katika kitabu chake kikubwa na mtoto wake, Sulayman, aliyerithi, alizoea kunakili Hadith kutokea humo. Bila shaka yalikuwa ni maandiko haya ambayo Ibn Sirin anayasemea: "Katika risalah aliyoiacha Samurah kwa mtoto wake, humo kuna kiwango kikubwa mno cha ilimu.

Imeripotiwa na Anas akisema huku amenyooshea mkono kwa mus-haf: "Hizi ni Hadith ambazo mimi nimezisikia kutoka kwa Mtume Mtukufus.a.w.w. Mimi niliziandika na nilimpatia Mtumes.a.w.w. (kwa ajili ya uthibitisho wake)." Al-Imam Jaafer al-Sadiq a.s . anasimulia kutokea Mababu zakea.s . kwamba Mtumes.a.w.w. alisema:"Wakati unapoandika Hadith, andika pamoja na sanad yake (ufululizo wa upokezi wake). Iwapo itakuwa ni kweli, basi utagawana thawabu zake; na iwapo zitatokezea kuwa ni za uongo, basi madhambi yake yatamwia aliyesema."

Mtumes.a.w.w. pia anaripotiwa kwa kusema:"Ikamateni elimu." Na alipoulizwa ni nini alichokuwa akimaanisha, alielezea kuwa yeye alikuwa akimaanisha uandishi. Umma Salma R.A. ameripotiwa akiwa amesema: "Mtumes.a.w.w. aliulizia adim ya kondoo iliyotiwa dawa ili isioze iletwe mbele yake. Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa pamoja naye. Baadaye aliyazungumza mambo mengi mno kwa Imam Ali ibn Abi Taliba.s. hadi kukaandikwa sehemu zote mbili za ngozi hiyo na vile vile kingo zake pia zilijaa maandishi."

Hadith zote hizi zinathibitisha wazi kuwa Mtumes.a.w.w. aliruhusu uandishi wa Hadith. Wapo Wanzuonini wengi ambao wanashikilia kwamba Mtumes.a.w.w. alikuwa ameharamisha hapo mwanzoni na kuruhusu hapo baadaye. Iwapo ndiyo hali ilivyo, je, ilikuwa ni kwa misingi gani ambapo baadhi ya Makhalifa waliharamisha uandishi wake na baada ya Hadith nyingi mno kuandikwa, tukamsingizia ati kuwa ni Mtumes.a.w.w. ndiye aliyeharamisha uandishi wa Hadith? Rashid Ridha amezichambua Hadith zinazoharamisha na zenye kuruhusu kuandika Hadith.Yeye anajaribu kuthibitisha kuwa Hadith zinazopiga marufuku zinashinda zile zenye kuruhusu, hivyo Hadith zinazoelezea kuharamishwa kwa kuandika Hadith ni lazima zichukuliwe kuwa ni halisi na kweli. Yeye anaandika:

"Iwapo tutachukulia kuwapo kwa mgogoro baina ya Hadith zenye kupiga marufuku na zile zenye kuruhusu, basi mtu anaweza kusema kuwa mojawapo baina yao imetengua (batilisha) nyenzio kwa kuthibitisha kuwa Hadith zinazoharamisha zinashinda zile zenye kuruhusu, kwa sababu mbili: Kwanza, Sahaba walisimulia Hadith zinazoharamisha hata baada ya Mtume s.a.w.w. Pili, Sahaba hawa kuziandika Hadith; kwani iwapo wao wangalikuwa wameziandika, basi zingalikuwa zimetufikia sisi." Sisi hatuwezi kukubaliana na maelezo hayo kwa sababu zifuatazo: Kwanza, Sahaba ndio waliosimulia Hadith zenye kuruhusu uandikaji wa Hadith pamoja na zile zinazoharamisha, na kama vile tulivyokwisha ona hapo juu, baadhi ya Sahaba waliendelea na kuziandika hizo Hadith.

Pili, sababu ya Sahaba kutojishughulisha na ukusanyaji wa Hadith kulitokana na kutolewa kwa amri ya kuharamishwa na Makhalifa wa kwanza na pili, na wala si kuwa ni Mtumes.a.w.w. aliyeharamisha. Tatu, kwa kuwa haiwezekani sisi tukadai kuwa aina moja ya Hadith hizi zinashinda aina ya pili yake, sisi twaweza kusema kuwa ugomvi wao unazifanya zote ziwe zimebatilika na wala si kwamba mojawapo inaishinda ya pili yake. Kuhusiana na kukubali kwa Abu Hurayrah kuwa Abd Allah ibn Amr alizoea kuandika Hadith, Rashid Ridha anasema: "Hakuna sababu ya kwamba sisi tuchukulie hivyo kama uthibitisho wa ruhusa ya kuandika Hadith, kwa sababu haijaelezwa katika Hadith kuwa Abdallah aliandika Hadith kwa kuruhusiwa na Mtumes.a.w.w.

Sisi tulikwishawaonyesha hapo juu riwaya zinazoonyesha kuwa Abd Allah ibn Amr kwa hakika alikuwa amepatiwa ruhusa kama hiyo. Zipo riwayat nyingi ambazo zimeshuhudia hayo, na mojawapo hapo juu Abu Hurayrah kwa kusisitiza anasema kuwa Abd Allah ibn Amr alikuwa amepatiwa ruhusa na Mtumes.a.w.w. kama hiyo. Ama kwa upande wa upinzani, wengineo, kama Abu Zuhra, wenye mawazo ya kusema kuwa Mtumes.a.w.w. aliruhusu uandishi wa Hadith kufikia mwishoni mwa Utume wake ambapo hapakuwapo na hatari ya kuzichanganya Hadith pamoja na Aya za Quran. Iwapo sisi tutachukulia kusema kuwa matendo ya baadhi ya Sahaba, hasa yale ya Makhalifa, sisi hatuwezi kuikubalia hivyo, ama kwa upande wa pili, iwapo tutakubalia, basi itatubidi kuwalaumu baadhi ya Makhalifa kwa mienendo yao. Sisi hatujui iwapo Bwana Abu Zuhrah ataupendelea uelekeo upi.


2

TADWIN AL HADITH

UANDISHI WA HADITH

9. MAONI YA BAADHI YA SAHABA KUHUSIANA NA UANDIKAJI WA HADITH

Mbali na imani ya baadhi ya Sahaba kuwa Hadith zisiandikwe, kikundi miongoni mwao kiliendelea kufanya hivyo. Ukweli huu ni dalili yenyewe inayoelezea kuwa kuharamishwa kwa uandishi wa Hadith ulitokana na Makhalifa na wala si Mtumes.a.w.w. kama inavyodaiwa. Miongoni mwa Sahaba waliokuwa wakiamini ruhusa ya uandishi wa Hadith walikuwa Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Taliba.s. na mwana wake al-Hasana.s. ambao si tu kwamba waliziandika Hadith, bali walitilia mkazo juu ya uandikaji wake pia.

Abdallah ibn al-Abbass, imeripotiwa kuwa alizoea kusema, "Ikamateni (kuitia mahabusi) 'ilim kwa njia ya kuiandika." Harun ibn Antarah anaripoti kutokea baba yake kuwa abd Allah ibn al-Abbass baada ya kuitamka hiyo Hadith aliyomwomba aiandike. Salami anaripoti kuwa yeye aliona vipande vya maandishi kwa Ibn abbass ambamo alikuwa ameandika matendo ya Mtumes.a.w.w. kama vile ilivyokuwa imesimuliwa na Abu Rafi. Imeripoti kuwa Anas ibn Malik alizoea kumwambia mwanae:"Ikamateni ilim kwa kuiandika." Al-Kattani anaripoti kuwa Ayadh alizoea kusimulia ruhusa ya kuziandika Hadith kutokea Sahaba na Tabi'un. Hata hivyo, wengi wa Sahaba, inavyoonekana, ama walikuwa hawana uhakika katika yale waliyoyaandika kuhusu kuruhusiwa kwa kuziandika Hadith au hawakuwa na ari ya kuyazingatia na kuyasisitiza hayo kimatendo; uthibitisho huo ni kule kujiepusha kwao katika ukusanyaji wa Hadith.

Zaazan anaripoti: "Mimi nilichukua baadhi ya maandishi (tasabih) kutoka Umm Ya'fur na kumwendea Imam Ali ibn Abi Taliba.s. Naye alinifundisha hayo na baadaye aliniambia nikayarudishe kwa Umm Ya'fur."

Imenakiliwa pia kwamba Ibn Abbass alizoea kuziandika Sunan za Mtumes.a.w.w. juu ya vibao vya kuandikia, ambazo alizichukua mwenyewe hadi pale palipokuwapo na mkusanyiko wa Wanazuoni. Pia imeanakiliwa kwa wingi (mutawatir) kuwa alipofariki aliacha vitabu vingi mno vinavyoweza kupakiwa juu ya ngamia mmoja. Kwa mujibu wa ripoti kuwa Abu Bakr aliandika baadhi ya Hadith baada ya Mtumes.a.w.w. na baadaye alizichoma moto, nayo pia inadalilisha kuwa uandishi wa Hadith ulikuwa ni desturi iliyokuwa inakubaliwa miongoni mwa Sahaba.

Riwaya iliyonakiliwa kutoka Imam Ali ibn Abi Taliba.s ambamo alisema kuwa yeyote aandikaye Hadith basi aandike pamoja na sanad yake navyo pia inaungana na mawazo hayo. Vianzio vyote vyote ni dhahiri kuwa idadi ya Sahaba walikubaliana kuwa uandishi wa Hadith ulikuwa umeruhusiwa. Ripoti kuhusu Sahifah ya Ja'abir ibn Abd Allah ambayo ilikuwanayo Hadith za Mtumes.a.w.w. pia inaunga mkono juu ya tabia na mazoea ya Sahaba katika uandishi wa Hadith zilikuwapo miongoni mwa Sahaba. Katika misingi hiyo, tunaweza kumalizia kuwa uandishi wa Hadith ulikuwa umekubaliwa na vikundi vya Sahaba na upinzani wa Mahalifa juu ya uandishi wa Hadith haukutokana na kukatazwa na Mtumes.a.w.w. kama inavyodaiwa, bali ulitokana na uamuzi wao wenyewe.

9. AL-QURAN NA UANDISHI

Al-Khatib al-Baghdadi, ili kuunga mkono maelezo yake juu ya ruhusa ya uandikaji wa Hadith, anaelezea uthibitisho kutokea aya za Qurani.Katika misingi ya Quran inayotuamrisha kuandika vyote vile ambavyo vina hatari ya kuweza kusahaulika, yeye anaelezea kuwa Hadith, ambayo pia ipo hatarini kupotea, basi ni lazima ziandikwe. Katika uhusiano huu yeye anaelezea aya zifuatazo za Quran 2:282, 6:91 na 31:157 Al-Tahawi, pia anaelezea akitoa Aya: "Wala msipuuze kuandika, mapatano yawe ni madogo au makubwa mpaka muda wake" (2:282) kuhusu uandishi wa madeni, anasema kuwa pale Mwenyezi Mungu anapotuamrisha kuandika madeni ili kuepukana na kutokezea mashaka na mizogo, na uhakika wa elimu ambavyo pia kuuchunga kwake ni vigumu kabisa na muhimu mno kuliko kurikodi madeni basi inasimama pamoja na umuhimu mno katika kuandikwa ili kuepukana na mashaka yaliyoelezwa hapo juu. Abu Hanifa, Abu Yusuf na Muhammad ibn al-Hassan al-Shaybani pia ni watu waliokuwa na msimamo kama huo.

10. MTUME S.A.W.W. KUHARAMISHA UANDISHI WA HADITH NA SABABU ZA KWELI

Uchambuzi wetu wa hapo mwanzoni unatuonyesha kuwa lawama zozote katika ucheleweshwaji wa uandishi wa Hadith hauwezi kamwe kutupiwa Mtumes.a.w.w. kwani riwaya zote zilizozuliwa juu yake haziwezi kamwe kukubaliwa kwa sababu mbali mbali. Katika jaribio hili, sisi tutakuwa tukitegemea mno juu ya riwaya zitegemewazo na Ahl al-Sunnah na penginepo tutatumia riwaya za Mashia. Ni mategemeo yetu kuwa msomaji ataweza kukadiria usahihi na ukweli wa uchambuzi huu kwa makini.

Aisha anaripotiwa kusema: "Baba yangu alikuwa amezikusanya Hadith mia tano za Mtumes.a.w.w. Asubuhi moja, alinijia na kusema,''Lete Hadith zote zilizopo kwako.' Nami nilizileta mbele yake. Yeye aliziunguza zote kwa moto na kusema: 'Nisije mimi nikafa huku nimekuachia vyote hivi.''

Imeripotiwa kwa mamlaka ya al-Zuhri kuwa: Umar alikuwa akitaka kuandika Sunan ya Mtumes.a.w.w. Yeye alikuwa akilifikiria kwa muda wa mwezi mmoja, alitarajia mwongozo kutokea kwa Allah swt katika swala hili. Siku moja asubuhi, alichukua uamuzi na kubainisha: "Mimi niliwakumbuka watu wote wale waliokwisha nitangulia, ambao waliandika na wakawa wamevutiwa mno katika yale waliyokuwa wameyaandika na ambao hatimaye walikiacha kitabu cha allah (yaani Quran)."

Abd al-'Ala ansema: "Qasim ibn Muhammad ibn Bakr alizoea kutamka Hadith mbele yangu. alisema kuwa kulikuwapo na ongezeko katika Hadith katika zama za Umar. Naye Umar aliamrisha Ahadith zote zikusanywe, na zilipokusanywa, alizichoma moto zote kwa pamoja, akibainisha: Kama muthnat ya Ahl al-Kitab 'Mathnat' kama inavyoonekana kilikuwa ni kitabu ambacho Mayahudi walikiandika wao wenyewe na ambacho kilikuwa ni tofauti na Taurati. Hapa Umar alikilinganisha kitabu hicho pamoja na Hadith za Mtumes.a.w.w. , ambavyo alikuwa hataki ziwepo pamoja na Kitabu cha Allah (yaani Quran). Yahya ibn Ju'dah naye pia ameripoti kuwa 'Umar alidhamiriwa kuandika hadith na Sunan. Lakini alibadilisha dhamira yake na kutuma ujumbe wake katika miji yote, ikibainisha:"Yeyote yule aliyenacho chochote kutokana na hayo, ayateketeze yote."

Imeripotiwa kutoka 'Urwah ibn al-Zubayr kuwa, "Umar ibn al-Khattaab alikuwa akitaka kuandika Sunan ya Mtumes.a.w.w. Kuhusiana na swala hili, alishauriana na Sahaba wengineo. Sahaba wote waliafikiana kuwa Hadith zote ziandikwe.Lakini Umar alikuwa akizingatia swala hilo hadi ikafika asubuhi moja alipochukua uamuzi wake wa kughairi hivyo, na akasema, 'mimi nilitaka kuandika sunan. Lakini baadaye nilijikumbusha watu walionitangulia ambao waliandika vitabu na kukiacha kitabu cha Allah (yaani Quran). Kwa kiapo cha Allah swt mimi sitakifunika Kitabu cha Allah kwa kitu chochote kile." Riwaya hii inatuonyesha kuwa Sahaba wote au angalau wale waliokuwa wameshauriwa walikubali juu ya uandishi wa Hadith. Lakini Khalifa, baada ya kufikiri kwa muda wa mwezi mmoja hivi, aliharamisha uandikaji wa Hadith katika misingi aliyoelezea yeye mwenyewe, jambo ambalo, bila shaka, halikuwepo pamoja na Sunnah za Mtumes.a.w.w. .

10. UPINZANI WA BAADHI YA SAHABA NA TABIUN KATIKA UANDISHI WAHADITH

Baada ya Khalifa kukataza uandishi wa Hadith, kwani mienendo yao ilichukuliwa na watu kama ni Sunnah, basi kikundi cha Sahaba na Tabiun pia walijiepusha na uandishi wa Hadith na walikuwa wakitegemea mno juu ya kile kimehifadhiwa akilini mwao.Wao walieneza Hadith kwa midomo tu na walichukia wazo la kuziandika. Kwao ilikuwa sivyo sahihi katika kuziandika Hadith za Mtumes.a.w.w . ambapo Quran na Mtumes.a.w.w . vyote vimeweka msisitizo mkubwa juu ya uandishi kwa ujumla. Abu Burdah anaripotiwa akisema kuwa baba yake alimwambia Abu Musa al-Ash'ari amletee chochote kile alichokuwa amekiandika kutokana na riwaya za baba yake.Na yote yalipoletwa, aliyaangamiza yote na alisema, "Wewe nae pia, kama sisi, lazima ukariri tu bila ya kuandika chochote." Abd al-Rahman ibn Salamah al-Jamhi anaripoti: "Mimi nilisikia Hadith ya Mtumes.a.w.w. kutoka kwa Abd Allah ibn Amr na niliiandika. Na baada ya kuhifadhi (kuikariri) akilini mwangu, nilikiteketeza kile nilichokiandika."

Asim alisema: "Mimi nilitaka kumwachia Ibn Sirin kitabu, lakini yeye alikataa kukiweka, akisema kuwa yeye hakutaka kuwa na kitabu chochote karibu yake." Abu Nadhrah asema: "Mimi nilimwambia Abu Sa'id awe akituandikia sisi, yeye alijibu, 'mimi sitawaandikieni na mimi siwezi kuwafanyieni chochote kama Quran kwa ajili yenu. Wewe uichukue (Hadith) kutoka sisi vile tulivyopokea kutoka Mtumes.a.w.w. ' Abu Sa'id alizoea kusema, Simulieni Hadith miongoni mwenu, kwani mmoja wenu anamkumbusha mwingine vile kujali." Imeripotiwa kuwa mamlaka ya Ibn Abi Tamin kuwa Ibn Sirin na wenzake wasingeliziandika Hadith.

Al-Harawi anaandika kuwa Sahaba na Tabiun walikuwa hawaziandiki Hadith na walikuwa wakizihifadhi akilini mwao, isipokuwa kitabu cha Sadaqa. Al-Nuwawi anaandika: "Mwelekeo wote wa Sahabah ulikuwa juu ya jihad, harakati dhidi ya matamanio ya mwili, na vile vile juu ya ibadah. Kwa hivyo wao hawakuwa na muda wa kunakili na kuandika (!).

Kwa sababu kama hizo, Tabiun pia hawakuweza kuleta chochote kile kilichoandikwa (tasnif)." Abu Kathir al-Ghubri anamnakili Abu Hurayrah akiwa amesema:"Ahadith zisifichwe wala zisiandikwe." Abd Allah ibn Muslim anaripoti kuwa Sa'id ibn Jubayr alikuwa anachukizwa na uandishi. Vivyo hivyo, Ibrahim al-Nakhai alibainisha kuwa yeye kamwe alikuwa hajawahi kuandika chochote. Wakati alipoulizwa sababu ya kutoandika, yeye alijibu, "Wakati mtu anapoandika kitu chochote, basi huja kutegemea juu ya yale aliyoyaandika."

Habib ibn Abi Thabit anaripotiwa kusema: "Mimi sina kitabu chochote ulimwenguni kote, isipokuwa kwa ajili ya Hadith ambayo ni kwa ajili ya sanda yangu."

Al-Hassan ibn Abi al-Hassan wakati wa kifo chake alimwamrisha mfanyakazi wake aliwashe tanuru na kuvitupa vitabu vyote alivyokuwa navyo isipokuwa kimoja tu. Ibn Sirin alikuwa akisema: "Iwapo mimi nitahitaji kuandika kitabu basi nitaandika kitabu juu ya barua za Mtumes.a.w.w. "

Yahya ibn Sa'id anasema: "Mimi niliwaona Wanzuonini katika hali ambayo wanapingana juu ya kunakili na kuandika." Suleyman ibn Harb anaripoti: "Yahya ibn Sa'id alitujia na alikuwa akisema Hadith. Mwanzoni mwenzi wetu walikuwa hawaziandiki Hadith alizokuwa akizisimulia, lakini baada ya muda kupita, wao walianza kuziandika."

Qasim ibn Muhammad ibn Abi Bakr alikuwa akimwambia Abd Allah ibn 'Ala asiwe akiandika Hadith. Sufyan ameripoti kuwa, pale alipoambiwa Amr ibn Dinar kuwa yeye alikuwa akiziandika Hadith za Amr, 'Amr alisimama na kusema, "Yeyote yule anayeziandika Hadith basi atoke hapa kwangu." Sufyan anasema kuwa kuanzia hapo hakuandika chochote kile alichokisikia kutoka Amr isipokuwa alikuwa akihifadhi tu.

Imeripotiwa kutoka Ibn Tawus kuwa baba yake alisema: "mtu mmoja alimwuliza Abd Allah ibn Abbass, swali ambalo lilimfurahisha mno. Huyo mtu alimwomba Ibn Abbass amwandikie jibu lake.Lakini Ibn Abbass alisema kuwa wao kamwe hawaandiki chochote kile kilicho cha 'ilim' Riwaya hii ipo katika mzozano pamoja na riwaya zinginezo zilizotangulia za Ibn Abbass.

Malik ibn Anas anaripoti kuwa Ibn Musayyab alipofariki, hakuacha hata kitabu kimoja. Vivyo hivyo ndivyo ulivyokuwa ukweli wa Qasim ibn Muhammad, Urwah ibn al-Zubayr na Ibn Shihab al-Zuhri. Mansur ibn Mu'tamir ameripotiwa akiwa amesema: "Mimi sijaandika chochote hadi leo." Na taarifa kama hiyo hiyo ipo imeripotiwa kutokaYunus ibn Ubayd. Imeripotiwa kuhusu Ibn Abi Dhu'ayb kuwa yeye alikuwa akikariri tu Hadith. Yeye alitokana na tabaka la tano na aliishi katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D. Imesemwa kuhusu Sa'id ibn Abd al-Aziz alikuwa haandiki chochote. Ismail ibn Ayyash, aliyetokana na tabaka la sita alikuwa amehifadhi akilini mwake kiasi cha Hadith elfu kumi lakini hakuandika hata moja. Abu Hatim anaripoti kuwa yeye kamwe hakuona chochote kilichoandikwa mikononi mwa Abd al-Walid al-Tayalisi. Wote hao walikuwamo katika tabaka la saba na walichukia mno uandishi wa Hadith. Pia imesemwa kuwa al-Nufayli kamwe hakuonekana pamoja na kitabu chochote. Vile vile Sahib al-Basri inasemekana alichukia mno uandikaji.

12. KITABU KINGINECHO MBALI NA QURAN

Kama itakavyoonekana kutokana na riwayah zinazotokana na wale wote waliokuwa wakizingatia kuharamishwa kwa Hadith kuandikwa, kwamba madai yao yote ya hasa kuficha ukweli yalikuwa ni khofu ya kutokezea kwa 'kitabu kinginecho mbali na Quran', na kwamba matokeo yake yatakuwa ni kutumika vitabu vingine na kuachwa kwa Quran. Hapa sisi tutajaribu kuchambua uhakika wa khofu kama hiyo na itaonekana wazi kuwa hayo yalikuwa ni hoja za kutaka kuuficha ukweli na wala hapakuwapo na makusudio mengineyo. Al-Quran na Sunnah vinakamilishana, na kama vile Waislamu wote wanavyoelewa kuwa kimoja hakikamiliki bila ya kingine - isipokuwa tu labda wale wenye kusema kuwa:"Kitabu cha Allah kinatutosha."

Jambo ambalo linahitaji kuzingatiwa hapa ni kuwa wale mabingwa wote wa kuharamisha uandishi wa Hadith iwapo wao walikuwa ni Makhalifa au wale waliofuata katika swala hili na waliweza kutumia hivyo kwa kuhalalisha tendo lao- walikuwa wakijua kauli ya Mtumes.a.w.w . kuhusu "Kitabu ubavuni mwa Kitabu cha Allah swt." Hata hivyo kimakosa au kimakusudi wao waliitumia visivyo hivyo kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ni kweli kuwa katika zama za uhai wa Mtumes.a.w.w. baadhi ya Sahaba waliweza kujipatia vitabu vya Taurati na vitabu vinginevyo vya Mayahudi. Na Mtumes.a.w.w. alipokuja kupata habari kuhusu hayo, aliwaambia wasivilinganishe sambamba na Kitabu cha Al-lah, al-Quran. Katika uhusiano huu itatubidi kuzingatia riwaya ifuatayo iliyonakiliwa na Jaabir. Jaabir anaripoti kuwa Umar al-Khattab alileta nakala moja ya Tawrati mbele ya Mtumes.a.w.w. na kusema: "Hii ni nakala ya Tawrati ambayo mimi huwa ninaisoma." Mtumes.a.w.w.

alikaa kimya lakini rangi ya uso wake ulibadilika. Abu Bakr aliiona hali hiyo, na alimwambia Umar, "Mama yako alie katika kilio chako, je, hauoni uso wa Mtumes.a.w.w .! Umar alipouona uso wa Mtumes.a.w.w. akasema, "Mimi najikinga na Mungu kwa ghadhabu za Mtumes.a.w.w. Mimi namkubalia Allah kama mmiliki wa vyote, Islam kama Dini na Muhammad kama Mtume." Juu ya hayo Mtumes.a.w.w. alisema:"Kwa kiapo cha Mungu, iwapo Musa angalitokea hapa na wewe umfuate yeye kwa kuniacha mimi, basi ungalikuwa umepotoka njia ya haki. Iwapo Musa angalikuwa hai na kuniona mimi, angalikuwa akinifuata mimi."

Mapokezi haya yanatuonyesha Mtumes.a.w.w. alivyokuwa amekasirishwa kwa sababu Umar alikuwa amekichukulia kitabu kingine sambamba na Quran. Katika mapokezi mengine kama haya, mtu kutoka Ansaar anachukua nafasi ya Abu Bakr. Inawezekana kuwa mapokezi hayo mawili yanatuelezea matukio mawili tofauti na kwamba tunaweza kuelewa kuwa matukio hayo mawili yametokea katika nyakati mbalimbali. Imepokelewa kutoka Abu Qalabah kuwa mara moja Umar ibn al-Khattab alipita karibu na mtu aliyekuwa akisoma kitabu. Baada ya kumsikiliza kwa muda mfupi, Umar alipendezewa na kile alichokisikia. Basi alimwomba mtu yule amwandikie kutoka kitabu hicho. Mtu huyo alikubali kumwandikia hivyo. Hapo Umar alilinunua jani na kumletea huyo mtu, ambamo mtu yule aliandika kwa kujaza sehemu zote mbili.

Baadaye Umar alifika mbele ya Mtumes.a.w.w. na kumsomea yaliyokuwa yameandikwa. Papo hapo rangi ya Mtumes.a.w.w. ilibadilika kwa ghadhabu. Basi hapo mtu aliyetokana na Ansaar alimwambia Umar: "Mama yako alilie kilio chako! Je, hauoni uso wa Mtumes.a.w.w. ? "Kwa hayo Mtumes.a.w.w. alisema: "Mimi nimetokezea kama Mtume, kama mfunguzi (fatih) na kama mfungaji (khatim), na mimi nimeleta kila kitu ambacho ilinibidi kujanacho (hivyo hakuna kilichobakia hadi nyinyi) kwenda kuvitafuta kutoka kwa watu wengineo."

Imeripotiwa kwa mamlaka ya al-Zuhri kuwa Hafsah binti yake Umar, alikileta kitabu chenye Hadith (masimulizi za Mtume Yusufa.s mbele ya Mtumes.a.w.w . Yeye alianza kukisoma huku Mtumes.a.w.w . akiwa akisikiliza na uso wake kubadilika rangi kuwa mwekundu. Hapo ndipo Mtumes.a.w.w . aliposema, "kwa haki ya Mungu, iwapo Yusuf mwenyewe angalikuja hapa na iwapo wewe ungalimfuata yeye na kuniacha mimi basi wewe ungalikuwa umepotoka." Riwaya hizi zote zinatuonyesha kile alichokuwa akikichukia Mtumes.a.w.w. kilikuwa ni maandishi mapotofu ambayo athari zake zilikuwa ni kueneza imani potofu za Mayahudi ambazo zilikuwa zikiitwa Israilayyat - miongoni mwa Waislamu. Mtumes.a.w.w. alikuwa hataki vile vitabu vya Mayahudi viwe sambamba na Quran Tukufu, maneno yote ambayo yalikuwa ni maneno ya Allah swt; katika vitabu vya Mayahudi kulikuwamo na visa na Hadithi za uwongo na zenye imani za ushirikina na kuamini uchawi, vinaweza kumfanya mtu apotoke na njia iliyo na mafundisho halisi ya Quran ambayo yameelezwa mbele yao.

Riwaya zilizoelezwa hapo juu pia zinaonyesha kuwa Khalifa na binti yake walikuwa wakipendezewa mno na usomaji wa vitabu kama hivyo na mara nyingine ilitokea kuchunguzwa na Mtumes.a.w.w. Hata hivyo, kwa bahati mbaya, tunaona kuwa baadaye ambapo Ka'aba al-Ahbar, Myahudi aliyesilimu kidhahiri tu, alipomwijia Umar na kumwomba ruhusa ya kuisoma Tawrati, Umar alimwambia: "Iwapo wewe unajua kuwa hiyo ndiyo Tawrati aliyokuwa ameteremshiwa Musaa.s . huko katika Milima ya Sinai, basi uisome usiku na mchana." Na haya ndiyo yaliyokuwa majibu ya Umar baada ya Mtumes.a.w.w. kumkataza yeye mwenyewe kutoisoma Tawrati wala mambo yoyote kama hayo.

Zipo riwaya zingine ambazo zinathibitisha fikara zetu kuwa Mtumes.a.w.w . alichokuwa akiharamisha kuwapo kwa kitabu sambamba na Quran yalikuwa ni maandiko ya Mayahudi yaliyokuwa yakitumiwa na Waislamu. Ipo imeripotiwa kuwa Abdallah ibn Mas'ud aliposikia kuwa watu walikuwanacho kitabu ambacho walistaajabishwa na yale yaliyokuwemo,basi alikichukua na kuki teketeza, akisema:"Watu wa vitabu (Ahl al-Kitaab) waliangamia kwa sababu wao walikuwa wakitegemea mno maandiko ya Wanazuoni wao (ulamaa) na walikuwa wamepuuzia Kitabu cha Allah (yaani Tawrati)" Neno ulamaa katika Waarabu wa zama hizo ilikuwa ikimaanisha Wanazuoni wa Kiyahudi na Kikiristo na vitabu vinavyozungumzwa katika riwaya hizi ni maandishi ya Kiyahudi.

Riwaya ifuatayo inaelezea vizuri zaidi swala hili. Murrah al-Hamdani anasema: Abu Murrah al-Kindi alikileta kitabu kutoka Syria (al-Shaam) na alimpatia Ibn Mas'ud alikipitia kitabu hicho, akaleta maji na kuyaosha yale maandishi yaliyokuwa yameandikwa katika kitabu hicho. Na hapo alisema, 'Watu walioishi kabla yenu waliangamia kwa sababu ya kuvifuata vitabu kama hivi na kukiacha cha Allah (yaani Quran)" Al-Husayn anasema, "Kwa hakika asingeteketeza maandishi hayo kama yangalikuwa ni Quran na Sunnah (yaani Hadith za Mtumes.a.w.w. Bali kilikuwa ni kitabu cha Ahl al-Kitaab."

Imam Ali ibn Abi Taliba.s . ameripotiwa akisema:"Yeyote yule miongoni mwenu aliyenacho kitabu (mbali na Quran na Sunnah) akiteketeze.Watu waliowatangulia nyinyi waliangamizwa kwa sababu ya kufuata masimulizi ya Wanazuoni wao huku wakikiacha Kitabu cha Allah (yaani Quran)."

Al-Imam al-Sadiqa.s . ameripotiwa akisema: "Baadhi ya Wanazuoni wapo wanafuatilia riwaya za Mayahudi na Wakristo, huku wakitegemea kuongeza elimu yao. Watu kama hao, nafasi yao ipo chini mno ndani mwa Jahannam. Imeripotiwa kwa mamlaka ya amr ibn Yahya ibn Ju'dah kuwa kilipokuwa kimeletwa kitabu mbele ya Mtumes.a.w.w. alisema: "Inatosheleza kwa upumbavu na upotofu wa Ummah kwa kuyaacha yale yaliyokuwa yameletwa na Mtume wake na kuanza kuangalia yaliyokuwa yameletwa na Mitume mingine." Riwaya hii pia inatuonyesha aina ya kila kitabu kilichokuwa kimeletwa mbele ya Mtumes.a.w.w. na pia kutupia nuru juu ya maana ya: 'Kitabu sambamba na Kitabu cha Allah (yaani Quran).'

Vile vile Ibn Abbass anasema: "Je utawaulizaje swali Ahl al-Kitaab kuhusu matatizo wakati ambapo Al-Qur'an ipo miongoni mwetu ?" Riwaya na masimulizi na mapokezi yote haya yanaonyesha kuwa Mtumes.a.w.w. aliharamisha kutayarishwa kwa kitabu sambamba na Quran huku akitahadharisha hatari ya uingiliaji wa Israiliyyat na kamwe, vyovyote vile, hakumaanisha Sunnah yake, ambayo ipo imeshikamana (wajib al-'ita'ah), kama vile wanavyokubalia Waislamu wote. Mabishano yetu yanazidi kupata nguvu kwa uhakika kuwa Wanazuoni wa Hadith wa Islam walikuja baadaye wakaziandika na kuzikusanya Hadith. Ama kwa mfano wa wale kama 'Urwah walichoma moto Hadith walizokuwa wameziandika kwa kudai kuwa "sisi hatutaki kuwanacho kitabu sambamba na Kitabu cha allah (al-Quran),' basi ni lazima tuseme kuwa wao walitenda kwa sababu ya kutoelewa vyema mafhumu ya kauli ya Mtumes.a.w.w.

Kama itakavyokuwa imeonekana hapo awali kuwa sisi hatuwezi kusema kuwa Mtumes.a.w.w. ndiye aliyehusika na uharamishwaji huo wa kuziandika Hadith; na msimamo kama huo unaweza kuchomoza maswali ambayo hayana majibu. Ilieleweka hapo awali kuwa baadhi ya Makhalifa walihusika moja kwa moja katika swala hili la kutoziandika Hadith na wao ndio walioharamisha uandishi wa Hadith. Hapa, baada ya kutaja sababu zilizotolewa nao kwa kuchukuwa hatua kama hiyo, sisi tutajaribu kutafuta maelezo yake. Baada ya kuthamini sababu chache zilizotolewa nao katika swala hili, sisi tutajaribu kuelezea kile tunachokiona kuwa ndiyo sababu maalum kuhusiana na uharamishwaji huo, pamoja na uthibitisho wa kutosheleza katika kuugana na maelezo yetu.

13. SABABU ZILIZOTOLEWA KWA KUHARAMISHA UANDISHI WA HADITH ZA MTUME S.A.W.W.

1. Sababu ya kwanza iliyotolewa ni khofu ya watu kushindwa kutofautisha baina ya Quran na Hadith za Mtumes.a.w.w. ambazo zingalisababisha uharibifu (tahrif) wa maandiko ya Quran, madhambi yasiyo samehewa. Mazungumzo haya, ambayo hayawezi kukubalika, yamekanushwa na Ustadh Abu Riyyah katika maneno yafuatayo: "Mtu kama huyo anaweza kuwashawishi watu wa kawaida, lakini haiwezi kukubalika kiutafiti. Kwa sababu itakuwa ikimaanisha kuwa ufasaha wa Quran unasimama sawasawa na ufasaha wa Hadith za Mtumes.a.w.w. Kile anachokimaanisha hapa ni muujiza wa ufasaha wa Quran unavyo tambulikana miongoni mwa watu, hatuwezi kudai kuwa wao wangalikuwa chini ya upotofu kwa kuzichanganya aya za Quran kwa Hadith za Mtumes.a.w.w, ambazo zipo chini kwa kulinganishwa na ufasaha wa Quran. Msimamo kama huu, kwa hakika unamfanya mtu akipingana na muujiza wa Quran.

Zaidi ya hayo, kuamini katika uwezekano wa kuchanganyika kwa Aya za Quran na Hadith ni sawa na kuamini katika uwezekano wa kuja kupotea kwa maandiko ya Quran. Imani kama hiyo inakanushwa kwa sababu uhalisi wa Quran upo unathibitishwa na Allah swt katika Quran: Sura Hijr, 15:9. Tunaweza kusema zaidi ya hayo kuwa kikundi cha Sahaba walikuwa wamehifadhi moyoni mwao Quran nzima, na kwa uangalifu mkubwa na upendo wao mkubwa juu ya Quran. Hatuwezi kamwe kuwafikiria kuwa wao walikuwa na hatari ya kuchanganyikiwa baina ya Quran na Hadith. Sisi twaweza kusema kuwa labda kulikuwapo na hatari ya uwezekano tu, na uwezekano huo hauwezi kupewa uzito sawa na madhara na hatari za kutoziandika Hadith. Madhara yaliyokuwa yameshajulikana kuanzia awali kabisa Shabaha hawakukubaliana miongoni mwao katika siku za awali kuhusu baadhi ya Shariah za Kiislamu na ilikuwa ni dhahiri kuwa athari za ufarakano huo ungelikuwa na hatari kubwa iwapo Hadith za Mtumes.a.w.w. zingalikuwa hazikuandikwa. Lakini hatari hiyo ilitokea tu. Baina ya tishio la zamani na hatari fulani, iliwabidi wao walitilie mkazo swala la uandishi wa Hadith, ingawaje, kimsingi swala la kutoruhusu uandishi wa Hadith halikuwa na uzito wowote.

2. Maelezo ya pili yatolewayo na Abu Riyyah yanasema baada ya kukubalia uharamisho wa kuandika Hadith ulitokana na Mtumes.a.w.w. kwamba Mtumes.a.w.w. alitaka maamrisho ya Shariah yawe katika mipaka iliyodhibitiwa na alipinga kueneza zaidi kwa maamrisho ya Shariah (adillah). Haya, kwa mujibu wake, ni sababu ambayo pia inatokana na nyakati zinginezo ambapo Mtumes.a.w.w. alichukia kuulizwa maswali. Sababu hiyo hiyo ipo inatumika katika hali ambapo Hadith ambazo zilikuwa sahihi katika kipindi fulani na ambapo haikuruhusiwa kufuata hapo baadaye.

Sisi tunachukulia maelezo hayo kuwa ni dhaifu mno, kwani haiwezekani kamwe kudai kuwa Mtumes.a.w.w. alipinga kwa kuenea Hadith halali kisheria zikitumika kama misingi ya kanuni halali za shariah. Je, itawezekanaje kwetu sisi kukubaliana nayo wakati Quran na Hadith kwa pamoja zinawajibika kujibu mahitaji katika sura mbalimbali ya Shariah kwa ajili ya siku ya Kiyama na siku zote kutoa maongozi kwa mwanadamu? Pamoja na hayo, sisi tutaelezea tena kwa mara ya pili kuwa sisi hatuamini ya kwamba Mtumes.a.w.w. alitoa amri ya kuharamisha uandishi wa Hadith.

3. Al-Awzai anatoa maelezo mengineyo, anaandika: "Sayansi ya Hadith ni tukufu pale inapoenezwa kwa mdomo tu, inawafanya watu wakumbushana daima Hadith. Lakini, pale inapoandikwa, nuru yake inafifia na pia huweza kufikia mikono ya watu wasiostahili kupatiwa." Sisi tunaweza kuonyesha kuwa ingawaje kuenezwa kwa Hadith kwa mdomo kuna faida ya kukumbusha watu yaliyomo ndani mwa Hadith, utumiaji wake kama halisi, na pekee, njia za kuzirekodi hizo zipo mashakani. Kwa hakika, faida kama hizo ziliambatana na madhara makubwa mno. Hata hivyo, hii ndiyo sababu mojawapo ambayo al-Awzai ameibuni, na ipo inashukiwa iwapo ikizingatiwa na wale waliokuwa wameharamisha uandishi wa Hadith.

4. Ibn Abd al-Birr, anaandika wakati wa kutoa maelezo kama hayo: Uandishi wa Hadith uliharamishwa ili watu wasitegemee mno yale yaliyoandikwa na wao, wakiepukana na huzihifadhi. Katika hali kama hiyo, desturi ya kuhifadhi moyoni Hadith ingalikuwa imepotea. Wazo kama hilo pia haliwezi kukubalika, kwa sababu madhara yaliyotokana na kushindwa kuziandika Hadith yalikuwa ni makubwa mno kwa kulinganishwa na faida iliyotokana na kupigwa marufuku kwa uandishi wa Hadith. Ustaarabu na utamaduni wa mwanadamu umekuwa ukilindwa kwa kupitia maandishi na wala si kwa kusema tu, ingawaje kuhifadhi Hadith kwenyewe ni tabia nzuri na yenye maana.

5. Sababu nyingine imetolewa pamoja na haya ni kwamba iwapo Hadith zingalikuwa zimeandikwa basi watu wangalikuwa wameiacha Quran huku wakizipatia Hadith umuhimu wote. Mazungumzo hayo pia hayawezi kuchukuliwa kuwa ni kinga, kwani jambo kama hilo linaweza kusemwa iwapo Hadith itakayomaanishwa itakuwa ni zile zisemwazo kwa mdomo tu, na Quran kwa upande wa pili. Ni kweli kabisa kuwa kupitia umuhimu wote Hadith ni upotofu ambao wale wafanyao hivyo waonywe na wachukue umuhimu kama huo katika Quran. Lakini uharamisho wa uandishi wa Hadith, umeleta uharibifu usioweza kutegemewa katika utamaduni wa Islam, kwa njia hiyo si ya kupatikana kwa matokeo sahihi.

6. Abjad al-'ulum anaandika: "Sahaba na Tabi'un, kwa sababu ya uhalisi wa imani yao na kuwapo kwao karibu na kipindi cha Mtumes.a.w.w ., na kutokuwapo kwa mabishano na uwezekano wa kuwaelekea watu waliotegemewa, hawakuwa na hitajio la kuziandika Hadith na shariah.Lakini vile Islam ilipoanza kuenea penginepo, wao walianza kuzikusanya na kuziandika Hadith, Fiqh na tafsiri ya Quran.' Kile anachokitaka kukisema huyu mwandishi siyo sababu ya kupinga kwa baadhi ya Sahaba kwa ajili ya uandishi wa Hadith, bali ni maelezo tu- nayo pia siyo sahihi- ni kwa nini Hadith hazikuandikwa; sababu yake halisi ilikuwa ni kupingwa kwa uandishi wa Hadith, na wala si kutohitajika kama vile anavyodai mwandishi huyo. Zaidi ya hayo, ueneaji wa Islam ulitokea katika miaka ya ishirini au zaidi ya miaka hamsini baada ya kifo cha Mtumes.a.w.w. Uandishi na ukusanyaji wa Hadith ulicheleweshwa hadi kufikia nusu ya karne ya 2 A.H./8 A.D. mbali na nukta hizo mbili inaeleweka kuwa sifa hii ya kumzulia Mtumes.a.w.w. ilianza katika maisha yake, na hatimaye iliweza kuongezeka kwa sababu ya kutokuwepo kwa Hadith zilizoandikwa. Pia ilikuwa ni wajibu wa Sahaba, ambao walitofautiana miongoni mwao katika mambo ya Shariah, kuzuia kukua kwa upotoshi na tofauti kwa kuanza kuziandika Hadith.

8. Sababu hasa ambayo ipo nyuma ya kuharamishwa kwa uandishi wa Hadith, ambayo mimi ninaamini, imeelezwa na mwanachuo mashuhuri aitwaye Sayyid Jaafar Murtadha na imethibitishwa kwa ushahidi uliopo:- Kulikuwapo na madhehebu mawili miongoni mwa Mayahudi. Dhehebu moja waliamini katika uandishi wa Hadith, ambapo dhehebu la pili halikuafiki hivyo, waliamini katika kutoandika chochote kile isipokuwa Taurati peke yake. Kundi hili la pili liliitwa Qurra (wasomaji). Haya yapo yamedokezwa na Dhadha katika kitabu chake cha fikara za Dini ya Kiyahudi. Ka'aba al-Ahbar Myahudi aliyesilimu (katika zama za Umar) alitokana na kundi hilo la pili. Mara moja Umar alimwuliza swali kuhusu mashairi ya vitu avisemavyo kuhusu Waarabu, kuwa kikundi cha kizazi cha Ismail, walikuwa wamehimili Biblia katika nyoyo zao na walizungumza kwa busara.....Labda inawezekana kuwa Khalifa alilichukua wazo hilo (la kutoandika chochote kile isipokuwa Quran tu) kutoka kwa Ka'b al-Khalifa na vile vile alikuwa akiheshimiwa kwa ushauri wake.

Zaidi ya hayo, uharamisho juu ya uandishi wa Hadith ulikuwa ukienda vyema pamoja na Siasa za tawala, kwani waliweza kuyazima malalamiko dhidi yao na kuendelea kuimarisha utawala wao. Kwa hakika hatua kama hiyo inawezekana kuwa na matokeo ya upotezi wa sehemu ya Hadith izungumziayo juu ya haki za wapinzani na ustahiki na ambayo ilifaa kuletea nguvu sehemu walizokuwa wamezidhibiti. Mtunzi huyo, kama vile taarifa yake ionyeshavyo, anadhani zipo sababu mbalimbali zilizosababisha kuharamishwa kwa Hadith, moja na muhimu kabisa ni kushawishiwa kwa mawazo ya Ahl al-Kitab juu ya Khalifa wa pili, ambaye, inavyoonekana, alipenda kusoma vitabu vyao kuanzia wakati aliposilimu. Uthibisho unaothibitisha ushawishi huu ni riwaya ya Urwah ibn al-Zubayr, isemayo kuwa Khalifa alikuwa amenuia kukusanya 'sunan' na hata pia aliwasiliana na Sahaba wengineo juu ya mpango wake huo. Wao walikubaliana nalo, lakini alibadilisha mpango wake huo kwa kusema kuwa watu wa Ahl al- Kitaab waliviacha vitabu vitukufu na kuanza kuvifuata vile walivyokuwa wameviandika na hivyo yeye hakutaka kufuata kitakachotokea juu ya Quran kama hivyo ilivyokuwa imetokea.

Ni jambo la kuweza kutokea kuwa maelezo hayo ya Khalifa yaliletwa na Ka'b al-ahbar, aliyetokana na kikundi cha Qurra, ambaye alijiepusha na kuandika chochote kile mbali na Tawrati. Ka'b alikuwa na njama mbaya dhidi ya Islam; ingawaje Khalifa alikuwa hana nia kama hizo, naye, kwa bahati mbaya, alishindwa kuona kwa kupitia ulaghai wa Ka'b. Mabishano ya Umar dhidi ya uandishi wa Hadith yalirudiwa na wengineo. Abu Burdah anaripoti kutokea baba yake aliyesema: "Banu Israil waliandika vitabu na kukiacha Kitabu cha Allah." Hakam ibn Atiyyah anaripoti kutokea Muhammad (bila shaka, Muhammad ibn Sirin) kuwa alizoea kusema: "Imenukuliwa kuwa Banu Israil walipotoshwa kwa sababu ya vitabu walivyovirithi kutokea mababu zao."

Mwanachuoni mwingine anaandika: "Moja ya ushawishi mkubwa wa Mayahudi juu ya Waislamu ulikuwa ni kuepukana na desturi ya kuandika Hadith. Imeandikwa katika Talmud, "Nyinyi hamna haki ya kuandika mambo ambayo munayazungumzia tu. "Huwezi kupinga kuwa Waislamu hawaku shawishiwa na Ka'b al-ahbar katika swala hili, ingawaje wao waliileta mbele katika sura ya Hadith ya Mtumes.a.w.w. Ushahid wake ni amri iliyotolewa na Khalifa baada ya kuzichoma Hadith alizokuwa amezikusanya: "Mathnat (au Mishnah) kama Mathnat ya Ahl al-Kitab." Maneno haya pia yanatuonyesha vile alivyokuwa ameshikamana pamoja na desturi za Mayahudi. Abu Ubayd katika Gharib al-Hadith, anaandika: "Mimi nilimwuliza mwanachuo wa Taurati na Injili kuhusu neno 'Mathnat.' Yeye alinijibu: "Mapadre wa Kiyahudi na waalimu wa Kiyahudi waliviandika baadhi ya vitabu baada ya Musa, mbali na vitabu vitukufu, na ambavyo wao waliviita kwa jina la 'Mathnat.'

Ni dhahiri kuwa Khalifa alikuwa akiufuata mfano wa Mayahudi ambao wao walikuwa katika kambi mbali na iliyoelezwa hapa. Abu Ubayd anaendelea kusema: Baada ya kupata maelezo hayo, mimi nimeelewa maana ya riwaya hii. Na hii ndiyo iliyokuwa sababu Abd Allah ibn Amr ibn al-As alikuwa akichukia kukichukua chochote kile kutokea kwa Ahl al-Kitaab, ingawaje yeye alikuwa na baadhi ya vitabu alivyovipata wakati wa kampeni ya Yarmuk (kutokea Makanisa ya Kiyahudi).

Abu 'Ubayd anaongezea: "Ni lazima, uharamisho (wa uandishi na usambazaji) haukuhusiana na Hadith na Sunnah za Mtumes.a.w.w. , kwa sababu itawezekanaje kuharamisha uandishi wa Hadith wakati ambapo wengi wa Sahaba wenyewe walikuwa wakinakili Ahadith. Hii inatuonyesha waziwazi kuwa Umar aliharamisha uandishi wa Hadith za Mtumes.a.w.w. na Sunnah zake kwa sababu yeye alichukulia msimamo kama ule wa maandishi yaliyokuwa yametolewa na waalimu wa Kiyahudi. Kwa hivyo, badala ya kuangalia na kuchunga kuenea kwa imani za Isra'iliyyat, yeye alikuwa ameshawishiwa nayo, ushawishi ambao ulisababisha katika kuangamizwa kwa Sunnah za Mtumes.a.w.w. Vile vile ni lazima iongezwe kuwa Abd Allah ibn Amr mwenyewe alikuwa mmoja wa waenezaji wa 'Isra'iliyyatambaye kamwe alikuwa si mtu aliyechukiwa mbele yao. Ilikuwa ni kwa sababu ya elimu yake ya Tawrati kwamba watu walimwambia awaeleze tabia ya Mtume mmoja.

Kile kilichotokea, katika mtizamo wetu, ni hivi: "Hadith za Mtume s.a.w.w. kwa ujumla hazikuandikwa hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 1 A.H./7 A.D., ingawaje baadhi ya Sahaba walipendelea uandikaji wake na vile vile wengineo walikuwa na vibao vilivyokuwa vimeandikwa Hadith. Uandikaji wa hapa na pale ulianza kutokea katika karne ya 2 A.H. /8. A.D. , lakini ukusanyaji na uandikaji wa Hadith ulianza kwa nguvu mwishoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D., na hasa katika karne ya 3A.H./8 9 A.D. Ingawaje inawezekana kuwa wakusanyaji walikuwa na mkusanyiko usio na utaratibu (kwani walikuwa wakikusanya chochote kile walichokipata bila ya kufanyia utafiti juu ya usahihi wake au ni nani aliyeileza), ni dhahiri kuwa wingi wa Hadith walizozikusanya zilikuwa zimetokana na kutamkwa tu. Ushahidi uliopo ni kwamba uandishi mdogo kabisa-ambao hauwezi kulinganishwa na kazi kubwa ya ukusanyaji wa Hadith-zipo dalili kidogo kabisa zenye kuonyesha kuwa kulikuwepo na uandishi wa Hadith katika karne ya 2 A.H./88 A.D. Hivyo inaweza kusemwa kuwa Hadith hazikuwa zikiandikwa kwa kipindi kirefu na zilikuwa zikisemwa kwa midomo tu bila ya kuandikwa katika kipindi hicho.


3

TADWIN AL HADITH

UANDISHI WA HADITH

14. MATOKEO YA KUTOZIANDIKA HADITH

Kulitokea matokeo mabaya kwa sababu ya kutokuwa na Hadith zilizoandikwa wakati wa kuzieneza. Hapa sisi tutajaribu kuzizungumzia baadhi yao.

1. Upoteaji mkubwa mno wa Hadith: Haya yalikuwa ni matokeo ya kutoandikwa kwa Hadith. Kwa Sahaba, uhifadhi moyoni ulileta matokeo ya kuhifadhika kwa idadi kubwa ya Hadith, na pia tukubali kuwa kulisababisha katika kupotea Hadith chungu nzima kwani kuhifadhi moyoni ni njia isiyoaminika katika kuhifadhi. Kukiri na kukubali kwa Muhaddithun (waliohadithia) katika jambo hili ni ushahidi ulio bora kabisa kwa ajili ya hayo. Ibn Qulabah anasema, "vitabu na maandiko ni bora kabisa kuliko kupotea kwa fahamu na hatimaye kusahau." Yahya ibn Sa'id anaandika, "mimi niliwaona Wanazuoni katika hali ya kuchukia uandishi wa Hadith. Laiti tungalikuwa tukiziandika, basi sisi tungalikuwa tunayo elimu kubwa mno ya Sa'id ibn Musayyab na vile vile mashauri yake." Yahya hapa anasikitikia upoteaji wa idadi kubwa ya Hadith zilizosimuliwa na Sa'id na vile vile mashauri yake yote kwa sababu ya kutoziandika.

Urwah ibn al-Zubayr anaandika, "mimi niliandika idadi kubwa ya Hadith na hapo baadaye niliziteketeza. Sasa ninaona kuwa laiti nisingeziteketeza badala yake ningelikuwa nimetoa mali na fidia ya watoto wangu kwa kuzibakiza. Hisham bin Urwah anaelezea "Baba yangu alivichoma vitabu vyake vyote alivyokuwanavyo katika tukio la Harrah (mnamo mwaka 63 A.H./ 283 A.D. ambapo jeshi la Syria liliposhambulia mji wa Madinah na kuuteketeza mji huo); baadaye aliniambia, 'Laiti ningalikuwa nimeviweka, kwa hakika ingalikuwa bora kabisa kwangu kubakia na Hadith kuliko mali na watoto nilionao kwa hivi sasa." Pia Yahya ibn Sa'id alikuwa akisema kama hayo. Taarifa hizo zinatuonyesha vile baadhi ya watu walivyokuwa wakisikitika kwa kuteketeza vitabu vyao kutokana na sababu moja au nyingine.

Mu'ammar asema, "mimi nilimsimulia baadhi ya Hadith Yahya ibn Kathir. Yeye aliniambia kumwandikia Hadith fulani fulani. Lakini mimi nilimwambia kuwa sisi tulichukia maandishi ya Ilm. Yeye aliniambia, "Andika, kwani usipoandika, utapoteza yote." Al-Mansurr asema, Laiti ningalikuwa nimeziandika Ahadith..........Kwani nimekwisha zisahau kwa idadi sawa na zile nizikumbukazo. Laiti ningalikuwa nimeziandika! Sasa nipo ninazikumbuka nusu tu ya Hadith ya zile nilizokuwa nimezisikia." Ibn Rushd anaandika, "iwapo Wanzuonini wasingalikuwa wamehifadhi elimu kwa kuandika na iwapo wasingalikuwa wameweza kutofautisha katika uhalisi na uzushi, basi elimu yote ingalikuwa imeshapotea na kusingalikuwapo na mwelekeo wowote ule wa Din. Mungu awajaze jazaa iliyo bora kabisa. Mwanzo wa kuandikwa kwa Hadith, mbali na kucheleweshwa kwake, yalikuwa ni maendeleo yaliyokuwa yamekaribishwa, khususan ilifuatia baada ya kuhifadhi Hadith moyoni zikiwemo halisi na zile zilizozuliwa.

Rashid Ridha anaandika, "sisi tuna uhakika kuwa sisi tumeshasahau na kupoteza idadi kubwa ya Hadith za Mtumes.a.w.w. kwa sababu Wanazuoni hawakuziandika Hadith walizokuwa wakizisikia. Lakini kile kilichopotea hakikuhusiana na Quran wala hakikuhusiana na maswala ya dini." Baada ya kuukubali ukweli wa kupotea kwa Hadith, yeye anajaribu kutuonyesha kutokuwapo kwa umuhimu wake kwa kusema kuwa kila kilichopotea hakikuwa juu ya Quran wala hakikuhusiana na maswala ya Dini. Mawazo kama hayo hayawezi kukubaliwa: Je, inawezekanaje kwa kitu kiwe ni Hadith ya Mtumes.a.w.w. na papo hapo kisiwe na uhusiano na maswala ya Dini? Vyovyote vile, yeye anatuthibitishia kuwa baadhi ya Madhehebu ya Kiislamu hawana mafunzo yote ya Mtumes.a.w.w. ambayo yalihifadhiwa na Ahl al-Bayt a.s yake.

Ibn Abd al-Birr aandika, "leo hakuna yeyote achukiae kuandika Hadith. Iwapo Hadith hazitaandikwa basi idadi kubwa ya elimu itaweza kupotea bure." Umar ibn Abd al-Aziz asema, "Wakati nilipotoka Madinah mimi ndiye niliye kuwa mwenye elimu zaidi kuliko wote, lakini kufikia Syria mimi nilikwisha sahau nilichokijua." Yazid ibn Harun alisema, "Mimi nilihifadhi Hadith elfu sabini kutoka Yahya ibn Sa'id. Lakini nilisahau nusu ya Hadith hizo pale nilipougua ugonjwa." Ibn Rahewayh anaandika:"Mimi nilikuwa nimehifadhi moyoni mwangu Hadith elfu sabini na niliweza kujikumbusha zaidi ya Hadith laki moja. Mimi nilikuwa sikisikii chochote kile isipokuwa nilikiweka katika hifadhi yangu moyoni. Lakini baada ya muda mimi nilisahau yote."

Al-Sha'bi anasema, "Hadi sasa mimi sijaandika hata ukurasa mmoja, na hadi leo hakuna yeyote aliyenielezea Hadith hata moja ambayo ilikuwa imeandikwa bali aliisimulia kwa mdomo tu, na wala sikupenda kusimuliwa kwa mara ya pili. Pamoja na hayo nimekuja kusahau mimi kiasi kikubwa cha elimu (ilm), kiasi kwamba iwapo mtu yeyote atakuwa na elimu hiyo basi atakuwa mwanachuo mkubwa katika zama zake." Ishaq ibn Mansur anaandika,"Mimi nilimwuliza Ahmad ibn Hanbal kuhusu wale waliochukia kuandika 'ilm. Yeye alisema kuwa baadhi walichukia na baadhi waliipendelea. Mimi nilidokeza iwapo 'ilm isingaliandikwa basi ingalipotea kabisa. Yeye alikubaliana akisema, 'iwapo kusingaliandikwa kwa 'ilm,' je tungalikuwa na nini hivi leo."

Ahmad ibn Hanbal anasema, "Baadhi walitusimulia kutoka fahamu zao na wengineo kutokea vitabuni. Hadith zilizotakana na vitabu zilithaminiwa zaidi." Ahmad mwenyewe kamwe hakusimulia Hadith ila kutokea vitabuni tu. Ibn Salah anaandika, "Iwapo Hadith isingalikuja kuandikwa, basi 'ilm yote ingalikuja kupotea katika zama zilizoifuatia." Taarifa hizo zinatosheleza kuelezea maelezo yetu.

2. Uenezaji wa uongo na masingizio: Uovu mwingine wa matokeo ya kutoandika Hadith ni kukua kwa Hadith zilizozuliwa na za uongo. Haikuwezekana kudhibiti hali halisi ya Hadith na muundo wake halisi. Hapo mwanzoni, kama inavyoeleweka, watu hawakuupa umuhimu wa sanad (mfululizo wa watu waliosimulia Hadith) kwani hali ya kuaminiana ilikuwapo zamani na ilikuwa imeenea kote. Siku hizi, Wanazuoni wa Hadith, ili kukwepa kukiri kuwa kulikuwapo jambo kama hili la ukweli wa kihistoria, wanasema kuwa hapakuwapo na Hadith zozote zilizozuliwa katika zama za Sahaba. Lakini katika uchunguzi na utafiti uliofanywa siku hizi, imethibitishwa kuwa baadhi ya watu kama Abu Hurayrah, walizua Hadith nyingi mno. Ni kweli kuwa zilifanywa jitihada nyingi katika kuzitofautisha Hadith zilizo halisi na zile zilizo za uongo, lakini haya yalikuwa yametokea katika kipindi ambapo idadi kubwa ya makundi yalijitokeza katika jamii pamoja na mambo ya Imani na Siasa hadi kwamba utofautisho wa halisi (thiqah) pia ulikuwa ukitofautiana na watu walivyokuwa wakielewa. Ni dhahiri kuwa jitihada kama hizi zinaweza kuleta matokeo ya uthamini sahihi wa Hadith na mapotoshi ya aina gani yaliyokuwapo.

Juu ya kuandika somo hili, abu Riyyah anasema, "Wakati Ahadith za Mtumes.a.w.w. zilipoachwa kuandikwa na Sahaba hawakuchukua hatua kuzikusanya, milango ya masimulizi ya Hadith kwa midomo ilifunguliwa kwa ajili ya wacha Mungu na vile vile hali hiyo kwa ajili ya waongo, wapotofu na wazushi, ambao walisimulia chochote kile walichokitaka bila ya kuwa na woga wa yeyote." Mwandishi mwingine anaandika, "Moja ya sababu ya kuchomoza kwa waliokuwa wakibuni Hadith ni kwa sababu ya kutoziandika Hadith na Sahaba waliridhika kwa kusimuliwa kimdomo tu bila ya maandiko yoyote."

Abu al-Abbas al-Hanbali (716 A.H./1316 A.D.) anaandika: Moja ya sababu ya kutofautiana kimashauri miongoni mwa maulamaa ni Hadith na maelezo yanayotofautiana. Baadhi yao wanafikiria kuwa Khalifa Umar ibn Khattab ndiye aliyehusika, kwa sababu Sahaba walimwomba ruhusa ya kuandika Hadith, lakini, yeye aliwazuia, mbali na kutambua ukweli wa amri ya Mtumes.a.w.w. ya kuandika hotuba yake ya Hijja ya mwisho kwa ajili ya Abu Shat na vile vile Mtume s.a.w.w.alikuwa amesema: "Ikamateni elimu yenu kwa kuiandika.'Iwapo kila Sahaba angaliandika alichokisikia kutoka kwa Mtumes.a.w.w. , basi Sunnah zingalinakiliwa bila ya kuwapo na msimulizi zaidi ya mmoja (mfululizo wa wanaosimulia) baina ya Mtumes.a.w.w. na (kizazi kilichofuatia) Ummah."

Ni jambo la kuvutia sana kwa kuangalia kuwa Abu al-Abbass alishutumiwa kuwa ni rafidh (aliyeasi) na tashayyu (kuwa Shiah) kwa sababu ya maelezo yake hayo! Abu Riyyah katika maelezo yake mengineyo, yeye anajitokeza katika kukana imani kuwa Mtumes.a.w.w. ndiye alitoa amri ya kutoandikwa kwa Hadith, anasema: "Je ni sahihi kuwa Mtumes.a.w.w. atakuwa amepuuzia nusu ya kila alichofunuliwa, akiicha bila kuhifadhiwa katika mioyo ya watu, ambamo mmoja wao anakumbuka, na mwingine, anasahau wakati huo huo na mwingine anaongezea atakacho kwa yale yasiyoandikwa......? Je uangalifu wa Sahaba upo wapi vile walivyoijali Quran? Hakuna kingine chochote kile kwa sababu ya dharau isipokuwa ni matokeo ya kutoandikwa huku kwa nusu ya ufunuo na wao wote ni wenye madhambi katika swala hili."

Ibrahim ibn Sa'id ameelezea zaidi kuwa uandishi wa Hadith ulianza pale ambapo palipogunduliwa kuandikwa kwa Hadith za uongo na uzushi. Yeye anasema, "Kama isingalikuwa kutokezea kwa Hadith kutokea Mashariki, sisi tusingalikuwa tumeandika Hadith hata moja, wala kusingaliruhusiwa kuandikwa kwake." Habari kama hiyo pia imeelezwa na Ibn Shihab al-Zuhri. Hata hivyo, Hadith ziliandikwa kwa kuchelewa mno. Uchelewesho huo unaweza kuonekana kutokana na ukweli kuwa sahih ya al-Bukhari alichaguliwa miongoni mwa Hadith laki saba na Abu Hanifa alizikubali Hadith 150 tu kati ya Hadith milioni moja!

5. Kusimulia Hadith kwa kutoa maana tu na wala si kwa maneno yake Mojawapo ya athari za kutoandika kwa Hadith ni kule kusahauliwa kwa maneno halisi ya Hadith na lilikuwa ni jambo la kawaida kutokea masimulizi yaliyokuwa juu ya maana tu. Ni jambo la kawaida pia kwa mtu aliyesikia Hadith miaka ishirini iliyopita kuielezea kwa maana yake tu wakati aisimuliapo. Kuongezwa na kupunguzwa ni mambo ya kawaida katika hali kama hizo. Hata hivyo, iwapo Hadith zingalikuwa zimeanza kuandikwa kuanzia hapo mwanzoni, uwezekano wa janga kama hilo lingalikuwa dogo.

Imran ibn al-Husayn anasema: "Kwa kiapo cha Mungu, nilitaka kusimulia Hadith za Mtumes.a.w.w. kwa mfululizo wa siku mbili, lakini kile kilichonizuia kilikuwa ni kuwaona kwangu wale waliosikia Hadith kama mimi, lakini wao walisimulia Hadith katika sura isiyokuwa ya halisi.(Kusimulia kwa kuelezea maana tu).Nami nilikuwa nikiogopa nisije nikasimulia Hadith kama wao. Lakini nakuambia, wao wanafanya makosa mengi katika kusimulia Hadith, ingawaje ni bila ya kunuia."

Sufyan anasema: "Mimi nilisikia kupitia wasimulizi wa Hadith kutokea Bara' ibn Azib kutokea Mtumes.a.w.w. kuwa: "Nilimwona Mtumes.a.w.w. akiinua mikono yake alipokuwa akiianza sala." Na pale nilipokwenda Kufah, nilimwona msimulizi Ibn Abi Layla, akiongezea maneno "Hapo baadaye hakurudia hivyo' katika hayo. Inaonekana kuwa fahamu zake zilikuwa nzuri pale alipokuwa Makkah. Mimi niliambiwa kuwa fahamu zake zimepata mabadiliko kidogo." Ibn al-Jawzi, katika kuelezea habari za wasimulizi wa Ahdith zenye uzushi, anaandika: Aina ya kwanza ni wale, ambao chini ya ushawishi wa utawa, polepole walipuuzia kuhifadhi Hadith pia kuzitambulisha Hadith na wale, katika hali ya makosa walisimulia Hadith kutokana na hifadhi zao baada ya vitabu vyao kupotea au kuungua au kuzikwa. Aina hii ya watu mara nyingi walisimulia Hadith mursal kama marfu', mawqul kama musnad na mara nyingi waliziingiza Hadith za hapa kuingia pale na za pale kuingizwa hapa.

4. Ufarakano miongoni mwa Waislamu: Matokeo mengineyo ya kutoandika Hadith ni kugawanyika na kufarakana kwa mashauri ya Waislamu katika mambo ya halali (Shariah), hadi kufikia ufarakano wao katika fatawa na imani. Na haya yalitokana na Hadith zilizotofautianan, ndivyo ilivyokuwa hali ya Waislamu katika nyakati hizo. Kufuatia ushindi wa awali, Islam ilienea katika maeneo mapya. Sahaba na Tabiun ambao walielekea sehemu mbali mbali zilizokuwa mpya, kila mmoja wao alichukua sehemu ile tu ya Hadith ambayo alisikia kutokea kwa Mtumes.a.w.w. au Sahaba. Kutoka Madinah, baadhi yao walikwenda Makkah na Yemen, baadhi yao walikwenda Syria na Palestina, na baadhi yao waliishi katika miji ya Iraq kama vile Kufah na Basrah. Matokeo ya hayo, ni kwamba kila mmoja wao alichukuliwa msimamo wake kwa mujibu wa Ahdith alizokuwanazo. Bila ya kujua Ahdith walizonazo wengineo, kila mmoja wao alifuata fatawa tofauti. Ufarakano huu ulipotambuliwa katika kipindi cha Tabiun, wao walianza kusafiri ili kuzuru miji tofauti, na hivyo ndivyo 'Safari ya kutafuta Hadith' (al-rihlah talab al-Hadith) ilivyokuja kubuniwa.

Wingi wa safari hizi zilitokea katika karne ya 2 A.H./8 A.D. na 3 A.H./9 A.D. , na hata baada ya hapo sababu ya uhakika nyuma yao ilikuwa kutawanyika kwa Hadith kwa kupitia miji tofauti na Wanazuoni waliotembea huko na huko katika kutafuta na kuleta namna moja ya Hadith baina ya Hadith za sehemu moja na nyingine; lakini wakati mwingine ilitokea kwamba Hadith moja iliweza kusimuliwa tofauti katika sehemu zinginezo - jambo ambalo mfano wake tumeulezea hapo awali. Sisi twaambiwa kuwa Abd Allah ibn Mubarak alisafiri hadi Yemen, Misri, Syria na Kufah kwa madhumuni ya kukusanya Hadith.

Abu Hatim al-Razi anaandika: "Safari zangu za awali zilinipeleka katika kutafuta Hadith, zilinichukua miaka saba. Mimi nilipiga hisabu ya umbali niliosafiri kwa miguu nikapata jumla ya 'Parasang' (parasang moja ni sawa na takriban maili nne hivi) elfu moja. Basi mimi nilikuwa nikiendelea kuongezea hivyo hivyo hadi zilipokuwa zikifikia parasang elfu moja......Mara nyingi nilisafiri kutoka Makkah kwenda Madinah na kutoka Misri hadi Ramlah, kutoka hapo hadi Asqalan, Tabariyyah, Demascus, Homs...... Ibn Musayyat anasema: "Mimi nilikuwa nikisafiri usiku na mchana katika kutafuta Hadith moja." Safari hizi zilikuwa zimeenea sana hadi al-Khatib alikusanya maandiko juu ya somo hilo kwa kukipatia jina la al-rihlafi talab al - Hadith na vile vile al-Ramhurmuzi aliandika sura juu ya somo hilo katika kitabu chake al-Muhaddith al-fadhil.

Safari hizi za kutafuta Hadith zilikuwa muhimu mno hadi Yahya ibn Muin ilimbidi aseme: "Kuna aina nne ya watu ambao hawawezi kutegemea kukomaa kwao....mmoja wao ni yule ambaye atabakia mjini mwaka akiandika Hadith hapo, na hakusafiri hadi miji mingine katika kutafuta Hadith." Matatizo kama hayo, ambayo ni matokeo yenyewe ya kutoandika Hadith, hayakutokea katika swala la Quran.Iwapo Hadith za Mtume s.a.w.w. zingalikuwa zimeshaanza kuandikwa kutokea miongoni, kwa ushirikiano wa Sahaba wote kwa pamoja, Vyuo vyote vya Kisheriah - na hata kiitikadi na kisiasa - zilizotokezea hapo baadaye basi zisingaliweza kuwapo. Vyuo vyote hivi vinategemea imani zao juu ya Ahdith. Je kwa kiasi gani Hadith hizo zilikuwa Sahihi? Je kwa kiasi gani zilikubaliwa na wengine? Kwa kiasi gani wengineo walikubalia maagizo yake iwapo masimulizi yalitegemea maana tu? Haya ni maswali ambayo hayakupatiwa majibu.

Abu Suhrah anaandika: Wakati Umar alipofariki na Sahaba walipoondoka kwenda miji tofauti, kila mmoja wao alianzisha Chuo cha Sharia kwa ajili yake na hivyo kila mmoja wao aliifuata njia yake. Ulipofika wakati wa Tabiun, kila mji ulikuwa na Chuo chake cha Sharia na mitazamo yao ilikuwa tofauti na mbali na zingine kama vile miji yenyewe ilivyokuwa mbali na nyingine. Siku moja, al-Mansur alimwambia Malik ibn Anas, juu ya nia yake ya kutumia muwatta Malik kama ndiyo Shariah ya Dini, kwa kutegewa na Waislamu wote wa miji hiyo na kufundisha na kufuata yaliyokuwamo na kujiepusha na chochote kile (kama ndiyo mamlaka ya Shariah), na hivyo ingalifanyika kwa kutengeneza nakala zaidi ya hivyo kwa ajili ya miji yote. Malik alimwambia, "Ewe Amir al-Muminiin, usithubutu kufanya hivyo. Watu hawa wanazo itikadi zao, wakiwa wamesikia kila Ahadith na kuzisimulia, na kila mmoja wao anaamini katika kile alichokuwanacho. Waache peke yao watu wa kila mji pamoja na kila walichojichagulia wao wenyewe."

5. Kuenea kwa Ra'y: Athari nyingine ya kushindwa kwa uandikaji wa Hadith ilikuwa ni kutokezea na kutumika zaidi mno kwa ra'y (hukumu zisizo halisi au hukumu za kibinafsi) miongoni mwa Mahakimu wa Kiislamu, kwa sababu kila mmoja wao alikuwa na kiasi kidogo tu cha Hadith alizokuwa akiweza kuzifikia, kwani mno ama zilipotea au hazikuweza kufikiwa. Watu walishindilia kutoa fatawa wakati ambapo wao walikuwa hawana kiasi cha kutosheleza cha Hadith kuwasaidia katika hatua hiyo. Kwa hivyo wao iliwabidi kuchagua njia ya ra'y ili kuweza kuwajibu watu. Zaid ya hayo, wengineo walikuwa ni mabingwa katika ra'y kwa sababu ya kutokuwa na imani katika Hadith, na hii ni wazi kwa kutokezea kwa sababu ya ukosefu wa Hadith zilizoandikwa.

Wakati fulani, katika mji mmoja hukumu ilitegemea Hadith iliyokuwapo, ambapo pengine hukumu ilikuwa inategemea uamuzi wa kibinafsi. Kwa bahati mbaya, baada ya muda fulani, zile hukumu za ra'y zilijipatia nafasi za mamlaka halisi ya hukumu kwa ajili ya wengine ambao wao pia hawakuwa na ufikio wa kutosheleza katika Hadith, wao walipendelea kufuatilia ra'y za mababu zao badala ya wao kubuni maamuzi yao ya kibinafsi (vile walivyokuwa .wakipendelea wao wenyewe). Kutanda huku kwa tabia ya ra'y kwa kufikia kiasi hiki miongoni mwa Ahl al-Sunna kulitokana na kutokuwapo na kutosheleza kwa Hadith, ambavyo kwa upande wa pili ulitokana na kupotea kwa idadi kubwa mno ya Hadith za Mtumes.a.w.w. na Sunnah zake.

15. UHARAMISHO WA KUSIMULIA HADITH

Sisi tumezungumzia hapo awali vile uandihi wa Hadith ulivyoharamishwa na kile kilichotokea athari yake. Mazungumzo yetu hapa yanaelezea ukweli kuwa kama vile historia inavyoelezea, baadhi ya Sahaba walijaribu hata kuzuia kusimulia Hadith kwa mdomo pia.Wao walizuia uandishi wa Hadith kwa kisingizio cha Quran kulindwa, na wao waliharamisha kusimulia kwa mdomo pia kwa kisingizio cha kuwazuia watu wasitilie mkazo mambo mengine isipokuwa Quran tu, kama kwamba azma yao ilikuwa kuifanya Hadith ionekane kuwa ni kitu kisicho na maana wala kisipewe umuhimu wowote na vyovyote vile, kuna uwezekano wa kuwapo kwa sababu za kisiasa katika hatua hizo.

Qurzah ibn Ka'b anasema: Sisi tuliondoka Madinah kwenda Iraq.Umar alitusindikiza hadi kufikia nje ya Mji. Yeye alituambia, "Je mnajua kwa nini mimi nimekuja nanyi hadi hapa?" Sisi tulijibu, "Labda` umekuja kutuaga, kwani sisi ni Sahaba wa Mtumes.a.w.w. " Umar alisema, "Mimi nimekuja kuwaambieni kuwa nyie muuweke mkazo wenu zaidi juu ya Quran na kwamba musizisimulie Hadith za Mtumes.a.w.w. kwa zaidi, ila kidogo tu. Sasa endeleeni kwani mimi ni mshiriki wenu katika swala hili."

Qurzah anaongezea katika riwaya nyingine: Pale mimi nilikuwa nimeketi miongoni mwa watu waliokuwa wakisimuliana Hadith. Ilionekana kuwa mimi ndiye niliyekuwa nikizijua Hadith nyingi kuliko wao. Lakini nilijikalisha kimya pale nilipokumbuka ushauri wa 'Umar.' Katika mapokezi ya al-Dhahabi, yeye anaripotiwa akiwa amesema, wakati wao waliponiomba kusimulia Hadith za Mtumes.a.w.w ., mimi niliwaambia kuwa Umar ameniharamishia kufanya hivyo. Vile vile imeripotiwa kuwa wakati Khalifa alipomtuma Abu Musa al-Ashari kwenda Iraq, alimwambia, "Usiwashughulishe watu katika Hadith. Mimi ni mshiriki wako katika swala hili."

Riwaya hizi zinatuonyesha majaribio yaliyofanywa katika kuzuia kuenezwa kwa Hadith Mtumes.a.w.w ., si pekee kwa maandishi tu. Ibn Asakir anaripoti haya yaliyosemwa na Ibrahim ibn Abd Rahmaan: Haki ya Mungu, Umar hakufariki kabla ya kuwaita Sahaba wa Mtumes.a.w.w. kama vile Hudhayfah ibn al-Yamani, Abu al-Darda, Abu Dhar, Aqabah ibn Amir na ......Yeye aliwaambia: "Je ni Hadith zipi hizi ambazo nyinyi mnazieneza pembe zote?" Wao walimjibu, "Je, wewe unatuzuia kusimulia Hadith?"

Kwa mujibu wa riwaya iliyorikodiwa na al-Tabarani, Ibrahim ibn Abd Rahman alikuwa na uzoefu wa kusema: "Umar alimwita Abd Allah ibn Mas'ud, Mas'ud al-ansari na Abu Darda. Yeye aliwaambia, "Je, ni Hadith zipi hizo za Mtumes.a.w.w. ambazo mnazisimulia kwa kupita kiasi?" Na kuanzia hapo aliwazuia Madinah tu hadi kufariki kwake (waliwekwa chini ya kifungo)." Ni dhahiri kuwa watu hawa walikuwa ni miongoni mwa watu maarufu kabisa katika Sahaba wa Mtumes.a.w.w. , Ahl al-Sunnah hawana shaka juu ya watu kama hawa juu ya usadikifu wa watu kama Hudhayfah, Abu Darda na Ibn Mas'ud hadi kuwa alipomtuma Iraq, aliwaandikia, "Mimi nimependelea faida yenu kuliko hasara yangu kwa kuwatumieni Ibn Mas'ud kwenu nyinyi."

Ibn Sazm amechukizwa mno na shutuma hiyo dhidi ya Khalifa, lakini, hakuthubutu kushutumu tendo la Khalifa, yeye anazusha mashaka kuhusu ukweli wa riwaya. Yeye anasema: "Hadith hii ni mursal, na yenye mashaka kwa sababu ya mmoja wa watu katika mfululizo wa wasimulizi ni Shu'bah. Hivyo haiwezi kuchukuliwa kuwa ni uthibitisho." Lakini sisi twaelewa kuwa Hadith hiyo ipo imepokelewa kwa kupitia mifululizo ya wasimulizi. Zaidi ya hayo, Ibn Haytham, katika Majma al-Zawaid (Vol. 1 uk. 147), baada ya kuitenga Hadith hii ni sahihi, ameandika: "Msemo huo wa Umar ni sahihi (inayosadikiwa) na ipo imesimuliwa kwa kupitia mifululizo ya masimulizi mengi."

Hata hivyo, Ibn Hazm, wakati akiichambua Hadith, anasema: Riwayah hii kwa uthibitisho ni uongo; kwani aliyesema itatubidi tuseme kuwa amejitoa katika mipaka ya Islam, kwa sababu jitihada zake zililenga katika kufunika na kupuuzia Hadith za Mtume wa Allah swt. Mwandishi wa al-Sunnah qabl al-tadhwin anaandika: Ukweli kuwa kuwekwa mahabusu (habs) kwa Sahaba (katika Madinah) kulitokana na wao kusimulia Hadith za Mtumes.a.w.w. , sivyo sahihi. Kwa sababu Abu Hurayrah alikuwa mmoja wa watu wa aina hiyo, na ambapo yeye hakuwekwa mahabusi (na Umar). Habari ya hapo juu si ya kweli, kwa sababu Abu Hurayrah mwenyewe alikuwa ni mmoja wa wale waliopigiwa marufuku na Umar katika kusimulia Hadith za Mtumes.a.w.w. Abu Hurayrah alitekeleza maamrisho ya Umar na hivyo aliweza kusimulia Hadith kidogo mno katika uhai wa Umar. Imekamilika, wal hamdu lillah.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s) Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA WA KITABU


YALIYOMO

TADWIN AL HADITH 1

UANDISHI WA HADITH 1

UCHUNGUZI WA KIHISTORIA JUU YA UKUSANYAJI NA UANDISHI WA HADITH 1

RASUL JA'AFARIYAN 1

AMIRALY M. H. DATOO 1

UTANGULIZI 1

UANDISHI WA HADITH 3

1. MAIMAMU WA SHIA KATIKA UANDIKAJI NA UENEZAJI WA HADITH 3

UANDISHI WA HADITH 5

2. MASHIA NA UANDISHI WA HADITH 5

UANDISHI WA HADITH 8

3. HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KATIKA SUNNI 8

TADWIN AL HADITH 11

UANDISHI WA HADITH 11

4. SABABU ZA KUCHELEWA KUANDIKA HADITH 11

5. RIWAYA YA ABU SA'ID 11

7. KUTOKUBALIKA KWA HADITH ZA ABU HURAYRAH 13

8. HADITH ZA MTUME S.A.W.W. KATIKA KURUHUSU UANDISHI WA HADITH 16

TADWIN AL HADITH 20

UANDISHI WA HADITH 20

9. MAONI YA BAADHI YA SAHABA KUHUSIANA NA UANDIKAJI WA HADITH 20

9. AL-QURAN NA UANDISHI 21

10. MTUME S.A.W.W. KUHARAMISHA UANDISHI WA HADITH NA SABABU ZA KWELI 21

10. UPINZANI WA BAADHI YA SAHABA NA TABIUN KATIKA UANDISHI WAHADITH 22

12. KITABU KINGINECHO MBALI NA QURAN 24

13. SABABU ZILIZOTOLEWA KWA KUHARAMISHA UANDISHI WA HADITH ZA MTUME S.A.W.W 26

TADWIN AL HADITH 32

UANDISHI WA HADITH 32

14. MATOKEO YA KUTOZIANDIKA HADITH 32

15. UHARAMISHO WA KUSIMULIA HADITH 37

SHARTI YA KUCHAPA 39

MWISHO WA WA KITABU 39

YALIYOMO 40