MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
AYATULLAHIL- UDHMAA SAYYID SWAADIQ AL-HUSAINIY SHIRAZIY
HUKUMU ZA KIISLAAM PAMOJA NA USUULUD-DIN- FURUUD-DIN- UBORA WA QUR'ANI TUKUFU- MFUMO WA UTAWALA KATIKA UISLAAM- MAMBO YA WAJIBU- HARAAM- MAADILI NA MAS'ALA MAPYA
KWA MUJIBU WA FAT'WA ZA AYATULLAHIL- UDHMAA SAYYID SWAADIQ AL-HUSAINIY SHIRAZIY (Mungu amzidishie uhai)
Ni wajibu kwa mukallaf kujifunza mas'ala ambayo anayahitajia sana katika maisha yake ya kila siku. (Mas'ala 12)
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu. Sifa zote njema ni za Allah mola wa viumbe wote na sala na salam ziwe juu ya mbora wa viumbe wote, Mohammad Mustafa na kizazi chake kilicho twahara, na laana iwe juu ya maadui zao wote milele na milele. Amma baad: Inampasa kila muislaam asitosheke katika uislaam wake kwa kuwa na jina pekee la Uislaam (kwa kusema mimi ni Muislaam) na katika Qur'ani asitosheke kwa kusoma na kuwa na maandishi ya Qur'ani pekee, bali ni vema kwake kuufanyisha kazi Uislaam na kutekeleza hukumu za Qur'ani katika maisha yake yote na katika mambo yake yote, (yawe ni mambo yake binafsi, kimajii, kiuchumi, na kisiasa na mengineyo), ili awe Muislaam kwa maana halisi ya neno Uislaam, awe mtu mwema na mwenye kufaulu katika dunia na mwenye kufuzu na mwenye kuneemeka katika Akhera.
Na ni jambo lililo wazi kuwa saada ya Dunia na kufaulu katika Akhera, vitu hivi havipatikani kwa kushikamana na jina pekee na wala havipatikani kwa maombi pekee (Dua) bali jambo liyafanikishalo na kuyathibitisha kwa Muislaam ni kufanya matendo kwa mujibu wa mafunzo ya kiislaam na kutekeleza hukumu za Qur'ani za sawa na zenye kuleta maendeleo-baada ya kuwa na itikadi madhubuti ya Usulud-dini (misingi ya dini) ya kiislaam itikadi za kweli na za haki.
Kutokana na haya inamlazimu kila Muislaam anae taka kuishi maisha mema na yenye mafanikio katika Dunia na anataka mafanikio na awe ni mwenye kufaulu na mwenye neema katika Akhera- na sisi sote tunayataka ahayo-afanye juhudi za kujifunza itikadi zilizo sahihi na za haki za Uislazam na kuyatambua pia kuyaelewa mafunzo ya hali ya juu na mazuri ya Uislaam na kuzifahamu vema hukumu za Qur'ani zilizo madhubuti na za kiwango cha juu, kisha kuitakidi kimadhubuti kabisa itikadi ya kweli na kutekeleza matendo kwa wakati wote kwa mujibu wa mafunzo ya kiislaam na kutekeleza kiukamilifu hukumu za Qur'ani, hadi kufikia hatua ya kukusanya au kuoanisha kati ya jina na mwenye jina, na hivyo kuwa waislaam wenye kuridhiwa mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu na kwa Mtume wake(s.a.w.w) na tuwe ni wenye kuridhiwa kwa Ahlul bayti wake Mtume walio Maasuuminiin(a.s) na ili tuwe miongoni mwa watu wenye saada katika Dunia na wenye kufaulu katika Akhera.
Na ufuatao ni utangulizi ubainishao mambo ambayo ni wajibu kwa Muislaam kuyafahamu katika uwanja huu, na kwa muhtasari tunasema kama ifuatavyo: Hakika mafunzo matukufu na ya kiwango cha juu kabisa ya Uislaam na hukumu zenye kupea za Qur'ani yanagawanyika kwa muhtasari katika makundi matatu yafuatayo:
1. Usulud-din (Misingi ya dini)
2. Furuud-din (Matawi ya dini)
3. Maadili (Tabia Akhlaaq na adabu za kiislaam).
Kwa hivyo basi mwenye kuitakidi Usuulud-din na kufanya matendo yake kwa mujibu wa Furuud-din na kujipamba kwa maadili na adabu za kiislaam, atakuwa ni mtu mwenye saada katika nyumba mbili (Duniani na Akhera), na atapata faida katika sehemu mbili hizo na ataishi hali ya kuwa ni mwema na mwenye saada na kufa hali ya kuwa ni mwenye kusifiwa, na ufuatao hivi sasa ni ufafanuzi kwa ufupi wa kila moja kati ya makundi matatu haya tuliyo yataja.
1
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
AYATULLAHIL- UDHMAA SAYYID SWAADIQ AL-HUSAINIY SHIRAZIY
1. TAWHIID (Kumpwekesha Mwenyezi Mungu)
2. AL-ADLU (Uadilifu wa Mwenyezi Mungu)
3. AN-NUBUWWATU (Utume)
4. AL-IMAMATU (Uimamu)
5. AL-MA'AAD (Marejeo ya kiama)
Tawhiid: ni mwanadam kufahamu ya kuwa ulimwengu unae muumba alie uumba na kuufanya uwepo baada ya kuto kuwepo na ni mwenye kila kitu.. kama uumbaji, utoaji wa riziki na utoaji wa neema na mzuiaji mwenye kuhuisha na kufisha na mwenye kutoa swiha na ugonjwa , yote hayo yako chini ya utashi wake. Amesema mwenyezi Mungu mtukufu:
إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾
(Hakika si jambo jingine pindi atakapo jambo au kitu chochote huliambai kuwa na likawa).
Na dalili juu ya kuwepo kwa Mwenyezi mungu mtukufu: Ni vitu tuvionavyo mbingu na vilivyomo ndani ya mbingu hiyo, kama jua lenye kuangaza na mwezi wenye kutoa nuru na nyota zenye kumeremeta na mawingu, pepo na mvua. Pia Ardhi na vilivyomo ndani yake, kama Bahari, Mito, Matunda, Miti, madini ya aina tofauti na yenye thamani kama Dhahabu na fedha na Zamrad na mengineyo.
Na katika aina tofauti za wanyama wenye kupaa angani na wenye kuogelea majini na watembeao nchi kavu (yaani juu ya ardhi), wakiwa ni wa aina tofauti na wenye sauti zenye kutofautiana na ukubwa wenye kushabihiana (kufanana) na usio shabihiana. Na mwanadamu wa ajabu mwenye hisia tofauti au mwenye viungo tofauti vya kuhisia kama kusikia, kuona, kunusa, kuonja, na kugusa na kuwazia na mwenye viungo vingi vingine, kama macho, masiko,ulimi, moyo, mikono miguu, afya, ugonjwa, maridhio, ghadhabu, huzuni, furaha na mengi mengineyo. Yote hayo ni dalili juu ya kuwepo kwa mola mwenye hekima na mjuzi, tunamuitakidi na kumuabudu na kumtegemea kutupa usaidizi na kutawakali kwake.
MWENYEZI MUNGU MTUKUFU NA SIFA ZAKE NJEMA
Mwenyezi Mungu alie takasika anazo sifa nyingi kama:
ELIMU : Yeye ni mwenye kufahamu kila kitu, kikubwa na kidogo na anayafahamu yaliyomo ndani ya nyoyo.
UWEZO : Yeye ni mwenye uwezo juu ya kila kitu, ana uwezo wa kuumba, kutoa riziki, kufisha na kuhuisha na mengineyo.
UHAI : Yeye yu hai hafariki.
UTASHI : Yeye hukitaka kitu ambacho kina maslahi ndani yake na wala hakitaki kitu ambacho ndani yake kuna ufisadi au uharibifu.
KUDIRIKI : Yeye hukiona kila kitu na husikia kila sauti hata kama itakuwa ni kwa kunong'onezana masikioni au wahm (kufikiria).
UTANGU : Yeye Mwenyezi Mungu pekee ndie wa tangu na tangu na ndie wa milele, yaani yeye alie takasika alikuwepo kabla ya kila kitu kisha akaviumba vitu vyote na atabakia kuwepo baada ya vitu hivyo hadi milele na ulimwengu wote huu ni miongoni mwa uumbaji wake, au ni viumbe vyake, viumbe hivyo ni vyenye kumuhitajia si katika kupatikana kwake pekee bali katika kubakia kwake na kuendelea kuwepo kwa vitu hivyo pia, na kila kilicho umbwa basi kitu hicho ni chenye kuzuka, kwa hivyo basi hakuna wa tangu na tangu isipokuwa Mwenyezi Mungu mtukufu.
KUZUNGUMZA : Yeye Mwenyezi Mungu ni mwenye kuzungumza, humsemesha amtakae katika waja wake wema walio takasika na kutakaswa, mitume wake na malaika wake.
UKWELI : Yeye ni mkweli katika yale ayasemayo na hakhalifu ahadi zake (yaani haendi kinyume na ahadi zake), kama ambavyo yeye alie tukuka ni muumba, mtoaji wa riziki, muhuishaji, mtoaji, mzuiaji, mwenye huruma, msamehevu, mtukufu, mbora na mkarimu , n.k
Mwenyezi Mungu si mwenye kiwiliwili na wala si murakkab (yaani hakuunganika kwa sehemu tofauti) hana sehemu wala mahala maalum. Na haiwezekani kumuona Mwenyezi Mungu mtukufu, si katika Dunia wala Akhera, na wala hatokewi na mabadiliko, hapatwi na kiu, hashikwi na njaa, hazeeki hamaliziki, hashikwi na mghafala wala kulala. Na hana mshirika wala mwenza, bali yeye ni mmoja na wa pekee, mmoja mwenye kutegemewa, hana mke wala mtoto. Na sifa zake ndio dhati yake yenyewe, hakuna uwili kati yake na sifa zake, yeye ni muweza mjuzi hadi mwisho wa sifa zake njema kuanzia tangu na tangu, si kama sisi, kwani tulikuwa ni wajinga kisha tukajifunza na hatukuwa ni wenye uwezo kisha tukawa ni wenye uwezo. Na yeye ni ghanii (tajiri na mwenye kujitosheleza) na hakihitajii chochote na yeyote, hahitaji ushauri wa yeyote, au msaidizi au waziri, au askari na mfano wa hayo.
Maana yake ni kuwa: Mwenyezi mungu ni muadilifu hamdhulumu yeyote na hafanyi mambo yaliyo kinyume na hekima, kwa hivyo uumbaji wote, na utoaji wa riziki, utoaji na uzuiaji, vyote hivyo vimefanyika kutokana na maslahi au hufanyika kwa maslahi hata kama hatuyajui maslahi hayo, kama ambavyo Daktari anapo mtibu mtu fulani kwa kumpatia dawa fulani hufahamu ya kuwa dawa hiyo inamanufaa hata kama hatukufahamu maslahi yenyewe yaliyomo kwenye dawa hiyo. Kwa hivyo basi tutakapo ona ya kuwa Mwenyezi Mungu amemtajirisha mtu fulani au mtu fulani amemtia ufukara, au mtu fulani amemfanya kuwa mtukufu (sharifu) na mwingine hakumfanya hivyo, au amemtia ogonjwa mtu fulani na hakumfanya mtu mwingine kuwa mgonjwa, na mfano wa hayo, nilazima kuitakidi ya kuwa yote hayo yamefanyika kutokana na maslahi na hekima hata kama hatufahamu hekima yake na maslahi yake.[1]
Na imepokelewa katika hadithi kuwa: Mussa(a.s) alimuomba Mwenyezi Mungu mtukufu amfahamishe na kumtambulisha sehemu fulani ua uadilifu wake kati ya mambo ambayo dhahiri yake ni mushkeli (ni tatizo kuyaelewa), Mwenyezi Mungu akamuamrisha aende kwenye kisima chenye chemchem jangwan, ili akaangalie ni kitu gani kitafanyika huko, pindi Mussa(a.s) alipo toka alimuona mpanda farasi akija na kufika kwenye kisima hicho na kutelemka kutoka juu ya farasi wake na kukidhi mahitaji yake sehemu hiyo, na baada ya kumaliza alianza safari na kuondoka na kusahau mfuko wake wa pesa sehemu hiyo, kisha baada ya muda fulani akaja mtoto mdogo aliekuwa mumayyizi (yaani mwenye kutambua mambo) mtoto yule aliuona mfuko ule ukiwa umedondoka chini pembezoni mwa kisima kile, akauokota kwa furaha kubwa na kuondoka kwa haraka kurejea aliko toka, kisha baada ya muda akaja kipofu kwa ajili ya kutawadha kwenye kisima kile, ghafla yule mpanda farasi akarudi na kufika mahala pale huku akitafuta mfuko wake wa pesa, baada ya kuutafuta na kutouona akamtuhumu yule kipofu ya kuwa ndie alie chukua na kukapita mvutano kati yao, mvutano ulio pelekea yule bwana kumuua kipofu na yule mpanda farasi kujificha na hapo Mussa akastaajabu kutokana na yale aliyo yaona na kushangaa sana, Mwenyezi Mungu mtukufu akamtelemshia wahyi kwa mambo yaliyo ondoa mshangao wake, kwani alimwambia: Mpanda farasi alikuwa ameiba mali ya baba wa yule mtoto, kwa hiyo ile mali tukairudisha kwa mrithi ambae ni yule mtoto ambae umemuona, na yule kipofu alikuwa ni muuaji wa baba wa mpanda farasi, kwa hiyo mrithi akachukua haki yake na kulipiza kisasi kwa kipofu yule.[2]
Na hivyo ndivyo hukumu ya Mwenyezi Mungu inavyo kuwa na uadilifu wake japokuwa kwa mtazamo wa juu juu jambo hilo liko mbali na kanuni.
Mwenyezi Mungu alie takasika alipo muumba mwanadam, alimtakia mwanadam huyo saada na kheri katika Dunia na neema pia pepo katika Akhera na haya hayathibiti na kupatikana isipokuwa mwanadam huyu atakapo kuwa na mipango au program inayo kwenda sambamba na akili yake na maumbile yake na awe na mfumo unao wiana na roho yake na kiwiliwili chake, na program hiyo au mpango huo uziguse na kuyahusu mambo yote au mahitaji yote ya akili na maumbile, na uwe ni mfumo ulio kamili na wenye kukidhi matakwa yote ya kiroho na kimwili, haiwezekani kuwekwa kanuni hiyona mtu mwingine isipokuwa na muumba wa huyu mwanadam mwenye ujuzi wa matakwa na mahitaji yote ya mwanadam na vitu avipendavyo.
Na kutokana na ukweli kuwa ni Mwenyezi Mungu alie mtakia mwanadam saada wakati alipo muumba, basi ilikuwa ni juu yake kuipanga program na kuuweka mpango huo unao zihusu na kuzigusa sehemu zote za mwanadam (kiroho na kimwili) na kuweka mfumo ulio kamili uwezao kumfikisha mwanadam kwenye saada hiyo, kisha mfumo na program hiyo kuituma na kuifikisha kwa watu kupitia kwenye mikono ya watu waaminifu kati ya viumbe wake na waja wake walio hifadhiwa na utendaji wa makosa au kukosea na kusahau na walio twahirishwa kutokana na aibu mbalimbali na madhambi, nao si wengine bali ni manabii na mitume. Kwa msingi huo: Nabii ni mtu ambae Mwenyezi Mungu humtelemshia wahyi (humletea ufunuo kutoka kwake) kwa maana hiyo ni kuwa Nabii au Mtume hutoa habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu bila kuwepo kiunganishi cha kiumbe yeyote, na manabii wamegawanyika makundi mawili:
1. Nabiyyun mursal: (Nabii alie tumwa): Huyu ni yule Nabii alie tumwa kwa ajili ya kuwaokoa watu, kutoka kwenye kiza hadi kwenye nuru na kuwatoa kwenye batili hadi kwenye haki na kuwatoa kwenye mambo ya kupanga yasiyo na ukweli wala uhakika na kuwafikisha kwenye uhakika wa mambo, na kuwatoa kwenye ujinga na kuwafikisha kwenye elimu.
2. Nabiyyun ghayri mursali: (Nabii asie tumwa) Nae ni yule ambae hutelemshiwa wahyi kwa ajili yake mwenyewe na hakuamrishwa kufikisha hukumu kwa watu.
Na idadi ya mitume ni laki moja na ishirini na nne elfu (124000) na kati ya hao walio tumwa kufikisha hukumu kwa watu ni wachache. Na Mtume wa kwanza ni Aadam(a.s) na wa mwisho wao ni Mohammad(s.a.w.w) . Na manabii walio tumwa kufikisha ujumbe wamegawanyika makundi mawili:
1- Ulul-azmi
2- Wasio Ulul-azmi. Ulul-azmi: ni wale ambao walitumwa na Mwenyezi Mungu mtukufu katika ardhi hii kuanzia mashariki hadi magharibi na kwa watu wote, nao ni watano.
1. Ibrahiim(a.s) .
2. Nuhu(a.s) .
3. Mussa(a.s) .
4. Issa(a.s) .
5. Mohammad(s.a.w.w) .
Na Mayahudi ni miongoni mwa wafuasi wa Mussa(a.s) , Wakiristo ni miongoni mwa wafuasi wa Issa(a.s) na Waislaam ni wafuasi wa Mohammad(s.a.w.w) .
Lakini Uislaam ulifuta Dini zote zilizo tangulia, kwa hivyo basi haijuzu kuendelea kufuata Dini hizi bali ni lazima kwa watu wote kufuata mafunzo ya Uislaam kama Mwenyezi Mungu mtukufu alivyo sema:
وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾
Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri[3] .
Kwa hivyo basi Uyahudi na Ukiristo ni batili, na Uislaam unabakia kuwa ndio sheria ya Mwenyezi Mungu hadi siku ya kiama na haitafutwa kamwe milele na milele. Na Mitume wasio ulul-azmi: ni wale ambao walitumwa na Mwenyezi Mungu mtukufu kwenye sehemu maalum na nchi fulani au sehemu fulani tu na kwa watu maalum.
Hakika umekwisha fahamu ya kuwa Mohammad(s.a.w.w) ndie Mtume wa mwisho na kwamba dini yake- ambayo ni Uislaam- imefuta Dini zilizo tangulia na kwamba sheria yake itaendelea kuwepo na itabakia hadi siku ya kiama na kwamba ndio sheria pekee yenye uwezo wa kumfikisha mwanadamu kwenye saada na kuyathibitisha matarajio yake na matamanio yake katika maisha ya Dunia na Akhera kama ambavyo Mtume(s.a.w.w) ndie pekee ambae ni kigezo cha wanadamu na kigezo kilicho kamili katika upande wa kheri na mambo ya fadhili (ubora) kwa waislaam wote bali kwa ulimwengu wote ikiwa watajitakia kheri wao wenyewe, kwa kuifuata sera yake na kujipamba kwa tabia yake(s.a.w.w) na kuifahamu sehemu fulani ya historia yake(s.a.w.w) ni lazima kutaja baadhi ya sifa na mwenendo wake [4] . Yeye ni Mohammad bin Abdallah(s.a.w.w) na mama yake ni Aamina binti wahab. Alizaliwa katika mji wa Makkatul mukarramah, siku ya ijumaa tarehe kumi na saba (17) mwezi wa Rabiiul-awwal (mfungo sita) baada ya kuchomoza Al-fajiri mwaka wa tembo katika zama za mfalme muadilifu[5] (Kisraa)
Mtume(s.a.w.w) alipewa ujumbe wa kiislaam mnamo tarehe (27) mwezi wa Rajabul murajjab baada ya kutimiza miaka (40) katika umri wake mtukufu, kwani alishukiwa na jibrilu(a.s) ambae ni malaika mtukufu na alie karibu na Mwenyezi Mungu mtukufu na wakati huo Mtume(s.a.w.w) alikuwa katika pango la (Hiraa) nao ni mlima ulioko kwenye mji wa Makka na alitelemka kwake akiwa na aya tano za suratul Alaq kama zifuatazo:
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu[6] .
Baada ya tukio hilo Mtume(s.a.w.w) alisimama kwenye mlima wa Swafa na katika masjidul-haraam na katika makundi ya watu na katika sehemu za makutanio ya watu, kwa ajili kufikisha ujumbe wa mola wake na kuwaita watu na kuwaongoza kwa Mwenyezi Mungu mtukufu na kumuamini huku akisema:
أَیُّهَا النّاسُ قُولُوا لا اِلهَ الاّ اللّه تُفْلِحُوا
Enyi watu semeni hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mungu mmoja mtafaulu [7] .
Na kutokana na ukweli kuwa watu wa Makkah walikuwa ni washirikina na maraisi (viongozi) wao walikuwa wakiona maslahi yao binafsi yako kwenye shirki na kwa kuogopea maslahi yao wakawa wakimfanyia shere (wakimfanyia istihzaa na kumkebehi pia kumuudhi), na Mtume kila alivyo kuwa akiendelea na kazi yake ya wito wa kuwaongoza washirikina, pia wao waliendelea na kuzidisha maudhi yao kwa Mtume(s.a.w.w) mpaka akafikia hatua ya kusema:
ما أوذی نبي مثل ما أوذیت
Hakuudhiwa Mtume yeyote kama nilivyo udhiwa mimi (au hakuna Mtume yeyote aliepata maudhi mfano wa maudhi niliyo yapata mimi)[8] .
Na hawakumuamini isipokuwa watu wachache, wa kwanza wao akiwa Amirul muuminiin Ali bi Abi Twalib(a.s) na katika wanawake Khadijah binti Khuwailid(a.s) .
Na pindi mashinikizo ya washirikina kwake yalipo kithiri akaamua kuhamia kwenye mji wa Madinah, na kuhama huko au hijira hiyo ndio mwanzo wa tarehe ya Waislaam. Na huko ndiko Waislaam waliko ongezeka na kukithiri na nguvu yao kuongezeka, na kwa ubora wa wafunzo ya hali ya juu ya Mtume na kutokana na sheria ya Uislaam iliyo nyepesi na yenye hekima, wakawa ni mifano bora kabisa katika tabia, maadili na utu, na wakawa ni mifano bora katika utamaduni na wakawa wananchi bora, na kutokana na mafunzo hayo wakawapita na kuzivuka au kuzipituka tamaduni zote za ulimwengu na Dini zote za mbinguni na zisizo za mbinguni.
Na Mtume(s.a.w.w) wakati akiwa katika mji wa Madinatul Munawwarah alitokewa na vita pia mapigano mbalimbali, na vita vyote hivyo vilikuwa ni vita vya kujihami na kujibu uchokozi wa Washirikina, Mayahudi na Wakristo waliyo kuwa wakiyaelekeza kwa Waislaam, na Mtume(s.a.w.w) katika vita vyote akiangalia sana upande wa amani, huruma, usamehevu na ubora (fadhila), kwa hivyo ndio maana utakuta kwamba walio uwawa kati ya pande mbili hizo Waislaam na Washirikina katika vita vyake vya kujihami ambavyo vilifikia Thamanini na zaidi hawakuwa zaidi ya elfu moja na mia nne (1400), kama historia zilivyo nukuu na kusajili kwenye kumbukumbu zake.
2
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
KUFARIKI KWAKE KWENYE KUSIKITISHA NA KUHUZUNISHA
Tangu Mtume(s.a.w.w) alipopewa utume rasmi na kukabidhiwa ujumbe wa kiislaam mpaka kufariki kwake na kuiaga kwake Dunia hii alikuwa akiungwa mkono na wahyi (ufunuo), na Aminul-wahyi Jibraaillu(a.s) alikuwa akishuka kwake akiwa na Qur'ani tukufu au akimletea Qur'ani tukufu kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kidogo kidogo na katika matukio mbali mbali, hadi kitabu hiki adhiim kikakamilika katika muda wa miaka ishirini na tatu (23), na Mwenyezi Mungu akamuamuru kukikusanya na kukipanga kama kilivyo hivi sasa. Ndio, Mtume(s.a.w.w) alikuwa akipangilia na kuiwekea nidham Dini ya Waislaam na Dunia yao, na alikuwa akiwafundisha kitabu na hekima na akiwabainishia kanuni za ibada na twaa (utiifu) na maingiliano kati yao na uwiano wa kijamii na siasa, uchumi na mengine mengi.
Na baada ya Dini kukamilika- kwa kumtawalisha Ali bin Abi Twalib(a.s) Amirul muuminiin na Imam wa wachamungu na khalifa wa Mtume(s.a.w.w) baada yake na hili kufanyika katika siku ya Ghadiir tarehe kumi na nane (18) ya mwezi wa Dhil-hajjil haraam katika mwaka wa hijja ya kuaga na kumshukia kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ﴿٣﴾
Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini[9] .
Mtume(s.a.w.w) aliugua ogonjwa mdogo na wa kawaida tu, lakini maradhi au ugonjwa ule ukawa ukizidi na kuongezeka hadi kuaga Dunia na kurejea kwa mola wake tarehe ishirini na nane (28) ya mwezi wa Safar mwaka wa kumi na moja (11) hijiria, na wasii wake pia khalifa wake baada yake kusimamia jukumu la kuandaa mazishi yake nae ni Amirul muuminiin Ali(a.s) na kumzika katika chumba chake kwenye mji mtukufu wa Madina mahala ambapo ndipo lilipo kaburi lake tukufu kwa hivi sasa.
Hakika Mtume(s.a.w.w) katika hali zake zote na katika maisha yake yote alikuwa ni mfano wa hali ya juu katika uaminifu, utakasifu wa moyo (ikhlaas), ukweli, utekelezaji wa ahadi, uzuri wa tabia, ukarimu, elimu, upole, usamehevu, ulain, ukarimu, ushujaa, uchamungu, zuhudi (kujiepusha na ladha au anasa za kidunia), unyenyekevu, na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na alikuwa ni mwenye kusifika kwa uzuri wa maumbile ya kimwili na alikuwa ni mzuri: uzuri wenye kulingana na umbile lake na unao nasibiana na umbile hilo, uso wake ulikuwa ni wenye kumeremeta na wenye nuru sana kama mbalamwezi yenye kuangaza katika usiku wa ukamilifu wake, kama ambavyo moyo wake mtukufu na roho yake ya hali ya juu na kubwa vilikuwa vimefikia kileleni mwa ukamilifu wa kiroho, kama upatikanao kwenye tabia na maadili, na sira yake pia sunna au mienendo yake ni nyeupe yenye kutoa miali kama jua lenye kuangaza katika nusu ya mchana.
Kwa sura ya ujumla, hakika Mtume(s.a.w.w) alikuwa amekusanya ubora wote na fadhila zote na alikuwa ndio mahala pa utukufu na ukarimu na kitongoji cha elimu, uadilifu, uchamungu na ubora, na alikuwa ndio ofisi ya mambo ya Dini na Dunia na Dunia na Akhera, hakutokea kuwepo mfano wake kati ya walio tangulia na hata tokea mfano wake hadi milele. Huyu ndie Mtume wa Waislaam na hii ndio Dini ya kiislaam, hakika Dini yake ni Dini bora kuliko Dini zote, na kitabu chake ni bora kuliko vitabu vyote, kwani ni kama vile Mwenyezi Mungu alivyo sema:
لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ ﴿٤٢﴾
Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa[10] .
Na Uimam - kama walivyo uarifisha - ni uongozi wa jumla katika mambo ya Dini na Dunia, na uongozi huo (uraisi) unakuwa ni wa mtu mmojawapo kati ya watu akiwa ni naibu wa Mtume(s.a.w.w) na Uimam ni wajibu kuwepo kwa hukumu ya akili, kwa sababu Uimam ni (lutfu) huruma ya Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunafahamu kwa yakini ya kuwa watu wanapo kuwa na Raisi mwenye kuwaongoza na kuwaelekeza watu na mwenye kusikilizwa na kutiiwa na anae chukua haki ya mwenye kudhulumiwa kutoka kwa dhalimu na kumzuwia dhalimu kufanya dhulma yake watu hao watakuwa karibu zaidi na maisha mema na saada, na watakuwa mbali zaidi na ufisadi na uovu[11] .
Na bahthi ya Uimam ni miongoni mwa bahthi zinazo fuatia bahthi ya Utume na ni matawi yake, kwa sababu Uimam ni uendelezaji wa kazi ya Utume na kubakia kwake, na ni wajibu katika Uimam yote yaliyo wajibu kwenye Utume kama Ismah na utwaharifu, na kwamba ni lazima Imam ateuliwe na Mwenyezi Mungu mtukufu kwa Nasi (dalili ya wazi) na kumuainisha kwa jina, na kwa neno moja ni kuwa Imam anashirikiana pamoja na Mtume katika kila kitu isipokuwa wahyi (ufunuo), kwani Imam hatelemshiwi wahyi. Kwa hivyo basi: Kama ambavyo Mwenyezi Mungu mtukufu anavyo wateua na kuwachagua mitume na manabii vivyo hivyo maimam na mawasii wa Mtume na makhalifa wake.
Na kwa hakika alimuainisha na kumteulia Mtume wetu Mohammad(s.a.w.w) mawasii na makhalifa kumi na mbili (12) na hawa ndio maimam kumi na mbili walio mashuhuri kwa waislaam wote[12] nao ni hawa wafuatao kwa utaratibu wao.
1. Imam Amirul muuminiin Ali bi Abi Twalib(a.s) mtoto wa ami yake Mtume(s.a.w.w) na mume wa binti yake Fatuma(a.s) .
2. Imam Hassan bin Ali(a.s) na mama yake ni Fatuma binti Mohammad(s.a.w.w) .
3. Imam shahidi Hussen bin Ali(a.s) na mama yake ni Fatuma bint Mohammad(s.a.w.w) .
4. Imam Zainul aabidina: Ali bin Hussen(a.s) .
5. Imam Baaqir(a.s) : Mohammad bin Ali(a.s) .
6. Imam Swaadiq: Jaafar bin Mohammad(a.s) .
7. Imam Kaadhim: Mussa bin Jaafar(a.s) .
8. Imam Ridhaa: Ali bin Mussa(a.s) .
9. Imam Jawaad: Mohamma bin Ali (a.s).
10. Imam Al-hadiy: Ali bin Mohammad(a.s) .
11. Imam Askariy: Hassan bin Ali(a.s) .
12. Imam Mahdiy: Mohammad bin Hassan Al-qaaim (atakae simama) na mwenye kungojewa (Mwenyezi Mungu aharakishe faraji yake na kudhihiri kwake), na hawa maimam ndio hoja wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe wote na makhalifa wa Mtume wake(s.a.w.w) walio barikiwa, nao wote wanatokana na nuru ya Mtume(s.a.w.w) , na walikuwa kama Mtume(s.a.w.w) katika elimu, upole, na fadhila, zuhdi (kuitupamkono dunia), uadilifu, Ismah,tabia njema na tabia bora, na sifa zingine njema. Vipi wasiwe na sifa kama hizo? Ili hali wao ni makhalifa wake na mawasii wake na maimamu wake (viongozi) kwa viumbe wake na hoja za Mwenyezi Mungu juu ya viumbe (wanadamu) wote baada yake. Na ufuatao ni muhtasari wa historia ya kila mmoja kati yao (a.s) na historia ya binti wa Mtume(s.a.w.w) mke wa wasii wa Mutme(s.a.w.w) Fatuma Zahraa (a.s) .
Yeye ni Fatima Zahraa(a.s) baba yake ni Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) Mohammad bin Abdillah, na mama yake ni Sayyidah Mtukufu Khadijah(a.s) mama wa waumini, na mumewe ni bwana na wasii wa Mtume Ali Amirul muuminiin, na watoto wake pia wajukuu wake ni maimam watwaharifu(a.s) .
Alizaliwa(a.s) tarehe (20) ya mwezi wa Jamaddul-akhir mwaka wa (45) tangu kuzaliwa Mtume(s.a.w.w) na alikufa shahidi akiwa ni mwenye kudhulumiwa tarehe 3 Jamaadul Aakhir[13] siku ya juma nne mwaka wa kumi (11) hijiria akiwa na umri wa miaka (18) katika umri wa kuchanua maua waridi (yaani katika umri wa ujana wake). Na Amirul muuminiin ndie alie simamia suala la kuandaa mazishi yake na kumzika katika mji wa madina na kulificha kaburi lake kutokana na usia wake ikiwa ni hoja kutokana na dhuluma aliyo fanyiwa na haki yake iliyo porwa na kuchukuliwa kwa nguvu. Na Fatima alikuwa kama baba yake katika ibada na uchamungu na ubora na Zuhdi, na Mwenyezi Mungu aliteremsha aya kadhaa kuhusiana na hadhi yake (kuhusiana nae)[14] .
Na Mtume(s.a.w.w) ndie alie muita kwa laqabu (jina mashuhuri) ya (Sayyidatu nisaail aalamiin) Mbora wa wanawake wa ulimwenguni, na kumuita kwa kunia ya Ummu abiiha (Mama wa baba yake) na alikuwa akimpenda sana na kumtukuza sana na kwa kiwango kikubwa, hata ilifikia hatua kwamba anapo ingia kwa Mtume humkaribisha na kusimama kwa heshima yake na kumkalisha mahala pake na pengine alikuwa akiibusu mikono yake na Mtume(s.a.w.w) alikuwa akisema: Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwa maridhio ya Fatima na anachukia kwa kuchukia Fatima [15] . Alimzalia Amirul muuminiin(a.s) watoto wafuatao: Imam Hassan(a.s) na Imam Hussen(a.s) na Muhsin(a.s) lakini Muhsin mimba yake ilitoka kabla ya muda wake kutokana na maudhi na masaibu yaliyo mfika mama yake, na Sayyidatu Zainab(a.s) na Sayyidah Ummu kuluthuum(a.s) .
Yeye ni Ali bin Abi Twalib(a.s) , na mama yake ni Fatuma binti Asad(a.s) nae ni mtoto wa Ami yake Mtume wa Allah(s.a.w.w) na mume wa binti yake na wasii wake na khalifa wake kwa watu baada yake, Amirul muuminiin na baba wa maimam(a.s) . Alizaliwa ndani ya Kaaba tukufu katika mji wa Makkah, siku ya ijuma tarehe kumi na tatu (13) ya mwezi wa Rajab baada ya miaka thalathini (30) tangu kuzaliwa kwa Mtume(s.a.w.w) na alikufa shahidi usiku wa siku ya ijumaa katika msikiti wa Al-kufa katika mihrab, kwa upanga wa Ibnu Muljim Al-muradiy na bwana huyu alikuwa ni miongoni mwa Makhawariji- na ilikuwa ni tarehe kumi na tisa (19) ya mwezi mtukufu wa Ramadhan na kukutana au kurejea kwa mola wake baada ya siku tatu tangu apate dharuba lile na alikufa shahidi katika usiku wa tarehe (21) akiwa na umri wa miaka sitini na tatu (63), na maimam wawili Hassan na Hussen(a.s) ndio walio simamia suala la mazishi yake na kumzika katika mji wa Najaful-ashraf mahala ambapo ndipo lilipo kaburi lake hivi leo na kulificha kaburi lake kutokana na usia wake(a.s) , ili liwe katika amani kutokana na mashambulizi ya makhawariji na wenye kulitembelea kaburi lake wasiweze kulifikia na kunufaika kwa kufanya hivyo[16] kisha imam Swadiq(a.s) akalitambulisha kwa watu pia imam Kaadhim(a.s) .
Na anazo fadhila na sifa nyingi sana na zisizo hesabika, hakika yeye alikuwa ndie mtu wa kwanza kumuamini Mtume(s.a.w.w) na hakumshirikisha Mwenyezi Mungu hata chembe na wala hakusujudia sanamu kamwe na kutokana na hilo ndio maana ikasemwa kuwa linapo tajwa jina lake yasemwe maneno yafuatayo:Karrama llahu wajhahu (yaani Mwenyezi Mungu autukuze uso wake) na ushindi katika vita ulikuwa umefungamanishwa na bendera yake katika vita vyote, mwenye kusimama madhubuti na asie kimbia vitani, hakugeuka nyuma katika vita na wala hakukimbia kamwe na kutokana na hukumu zake nzuri (au uzuri wa utoaji wa hukumu wa Ali Mtume akasema kuhusia nae:
أقضاکم عليّ
Hakimu bora zaidi kati yenu ni Ali [17] .
Na kutokana na wingi wa elimu yake Mtume(s.a.w.w) akasema:
أنا مدینة العلم وعليّ بابها
Mimi ni jiji la elimu na Ali ni mlango wake [18] .
Na kutokana na kushikamana kwake na haki Mtume akasema:
عليّ مع الحق والحق مع عليّ
Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali [19] .
Na alikuwa ni muadilifu kwa watu wake, akitoa haki kwa sawa, mwenye kujiepusha na mali za kidunia, na alikuwa akija na kuingia kwenye hazina ya Waislaam (Baytul mali) na kuziangalia Dhahabu na Fedha na kusema:
یا صفراء ویا بیضاء غرّي غیري
Ewe mwenye rangi ya manjano (Dhahabu) na ewe mwenye rangi nyeupe (Fedha) mghuri (mdanganye) mwingine tofauti na mimi [20] .
Kisha kuzitawanya kwa watu na habakishi hata tembe moja, na alikuwa akiwahurumia masikini na akikaa pamoja na mafukara na kukidhi haja za watu na akizungumza maneno ya haki na kweli na kuhukumu kwa uadilifu na kuhukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu.
Na alikuwa akitekeleza hukumu za Mwenyuezi Mungu, na akifuata mwenendo wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) mpaka kheri ikaenea sehemu zote na baraka kutangaa na maisha bora na yenye neema (mazuri) kuwaenea waja wote na katika miji yote.
Kwa ufupi ni kuwa: Yeye(a.s) alikuwa kama Mtume(s.a.w.w) katika sifa zote na mambo yote, isipokuwa katika suala la Wahyi na Utume na kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu akamfanya katika aya ya maapizano (Mubahala) sawa na nafsi ya Mtume(s.a.w.w) [21] .
Yeye ni Haassan bin Ali(a.s) bin Abi Twalib, na mama yake ni Fatima Zahraa(a.s) binti Mohammad(s.a.w.w) nae ni mjukuu mkubwa wa Mtume(s.a.w.w) na ni khalifa wake wa pili na Imam wa watu baada ya baba yake Amirul muuminiin (a.s) .
Amezaliwa katika mji wa Madinatul munawwarah siku ya juma nne katikati ya mwezi wa Ramadhan mwaka wa tatu wa hijiria, na alikufa shahidi kwa sumu ambayo alitegeshewa na Muawia bin Abi Sufyaan kupitia mkewe Imam Hassan ambae ni Juudah binti Ash'ath na hilo lilifanyika siku ya Al-khamisi tarehe saba (7) ya mwezi wa Safar[22] mwaka wa (50) hijiria, na alisimamia mazishi yake ndugu yake Imam Hussen(a.s) na kumsitiri katika makaburi ya Bakii'i katika mji wa Madinatul munawwarah, mahala ambapo ndipo kilipo kiwiliwili chake kwa hivi sasa (ndipo mahala lilipo kaburi lake) na-kwa masikitiko makubwa - kaburi lake lilivunjwa na Mawahabi pia walivunja kuba la kaburi lake hilo.
Na Imam Hassan(a.s) alikuwa ni mfanya ibada kwa wingi kati ya watu wa zama zake na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na mbora na alikuwa ni mwenye kumfanana sana Mtume(s.a.w.w) , na alikuwa ni mkarimu zaidi kati ya Ahlul bayti wake katika zama zake na alikuwa ni mwenye huruma zaidi.
Na miongoni mwa ukarimu wake(a.s) ni kuwa alipewa mafuta uzuri na mjakazi mmoja wapo kati ya vijakazi wake, akasema kumwambia mjakazi yule: Wewe uko huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha akasema: Hivi ndivyo alivyo tuadabisha Mwenyezi Mungu pale alipo sema:
وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ﴿٨٦﴾
Mnapo amkiwa kwa maamkizi basi itikieni kwa maamkizi mazuri zaidi kuliko mliyo amkiwa au rudisheni kwa yale maamkizi mliyo amkuliwa[23] .
Na miongoni mwa upole wake(a.s) ni kuwa mtu mmoja wa Sham alimuona akiwa amepanda mnyama, yule bwana akawa akimlaani Imam na Imam hakumjibu kwa chochote, yule bwana alipo maliza kutoa laana zake na matusi yake Imam Hassan akamwendea na kusema:
Ewe shekh nadhani ni mgeni na huenda umenifananisha, lau unge omba tukuridhishe basi tunge kuridhisha, na lau kama unge tuomba kitu fulani tunge kupatia na lau kama unge taka tukuongoze tunge kuongoza na lau unge tutaka tukubebee mzigo wako tunge kubebea na ikiwa unanjaa tunge kushibisha na kama unge kuwa uchi tunge kuvisha na kama ni muhitaji tutakutajirisha na ikiwa umefukuzwa tutakuhifadhi na kukusitiri na ikiwa unahaja tutaitatua haja yako[24] .
Yule bwana alipo sikia maneno yale alilia na kusema: Nina shuhudia ya kuwa wewe ni Khalifa wa Mwenyezi Mungu katika Ardhi yake, hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kufahamu vema mahala pa kuuweka ujumbe wake.
Yeye ni Hussen bin Ali bin Abi Twalib(a.s) na mama yake ni Fatima binti Mohammad(s.a.w.w) nae ni mjukuu wa Mtume(s.a.w.w) na Khalifa wake wa tatu na baba wa maimam tisa walio kuja baada yake na ni Imam wa watu baada ya nduguye au kaka yake Hassan (a.s) .
Alizaliwa katika mji wa Madinatul-munawwarah tarehe tatu (3) ya mwezi wa Shaaban mwaka wa nne hijiria na kuuwawa kwa dhulma kwa upanga hali ya kuwa ni mwenye kiu, mauaji yaliyo fanya na bani Umayyah kwa amri ya Yazid bin Muawia katika tukio mashuhuri la Ashura, siku ya juma mosi tarehe kumi (10) ya mwezi wa Muharram mwaka (61) hijiria, na jeneza lake pia kiwiliwili chake kitwaharifu na kilicho katwa katwa kwa mapanga pamoja na viwiliwili vingine vya mashahidi walio kufa mashahid pamoja nae vilizikwa baada ya siku tatu tangu kuuwawa kwao wakiwa mashahidi na alaie mzika ni mwanae Imam Zainul aabidiin(a.s) na kumzika mahala ambapo ndipo kaburi lake lilipo hivi sasa katika mji mtukufu wa Karbalaa, mji ambao uliangukia mikononi mwa Saddam na kundi lake na Mwenyezi Mungu kuukomboa kutoka mikononi mwao-pamoja na sehemu zingine tukufu zilizoko Iraq.
Na fadhila zake ni nyingi sana kiasi kwamba ni vigumu kuweza kuzitaja zote, kwani yeye ni ua zuri la Mtume(s.a.w.w) ambae Mtume alisema kuhusiana na yeye:
حسین مني وأنا من حسین
Hussein anatokana na mimi na mimi natokana na Hussen [25] .
Na pia amesema kuhusiana nae na kuhusu nduguye Hassan(a.s) :
هما ریحانتاي من الدنیا
Wao wawili ni maua yangu mazuri duniani [26] .
Pia amesema(s.a.w.w) :
الحسن والحسین سیدا شباب أهل الجنّه
Hassan na Hussedin ni mabwana wa vijana wa peponi [27] .
Pia amesema(s.a.w.w) :
الحسن والحسین إمامان إن قاما وإن قعدا
Hassan na Hussein ni maimam sawa wakiwa wamesimam au wamekaa [28] .
Na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na mfanya ibada sana kati ya watu, hakika alikuwa akisali kila usiku rakaa elfu moja kama baba yake Amirul muuminiin(a.s) na mara nyingi alikuwa akibeba mfuko wa ngozi wenye vyakula usiku na kuwapelekea mafakiri hadi ilionekana alama na athari yake mgongoni mwake baada ya kuuliwa na alikuwa ni mkarimu, mtukufu, mpole, na alikuwa mkali sana pindi anapo asiwa Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwa ukarimu wake ni pale alipojiwa na bedui mmoja akimuomba na kumuimbia shairi lisemalo: Hakwenda kombo kwa hivi sasa mwenye kukuelekea kwa matarajio na alie bisha mlangoni kwa mara kadhaa, wewe ni mkarimu na wewe ni mwenye kutegemewa, baba yako alikuwa ni muuaji wa mafasiki, lau kama si yule ambae alikuwa mwanzoni mwenu, basi sisi sote tunge enewa na kuzungukwa na moto wa jahannama.
Imam Hussen akampatia dinari elfu nne na akmuomba msamaha kwa kusema: Zichukue hakika mimi nakuomba samahani na fahamu ya kuwa mimi ni mwenye huruma sana kwako, lau kama mwendo wetu kesho ungekuwa ni mwema, na anga letu lingekumiminia kheri nyingi, lakini matatizo ya zama ni ya aina tofauti na yenye kubadilika kwa hivyo na mkono wangu ni wenye kutoa kidogo. Na kwa hakika Imam(a.s) kwa kisimamo chake cha kishujaa-na ambacho hakina mfano katika ulimwengu-aliweza kuihuisha sheria ya kiislaam na dini ya babu yake Mtume(s.a.w.w) bali aliuhuisha ulimwengu wote hadi siku ya kiama, kwa hivyo yeye ni bwana wa mashahidi na ni mtu bora baada ya kaka yake na nduguye Hassan(a.s) .
3
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
Yeye ni Imam Ali bin Hussen(a.s) na mama yake ni Shahri banuu binti wa mfalme Yazdjard na Imam huyu(a.s) alikuwa akiitwa Mtoto wa wateule wawili, kutokana na kauli ya Mtume(s.a.w.w) :
Hakika mwenyezi Mungu ana wateule wawili katika waja wake, mteule wake katika waarabu ni Quraishi na katika waajemi (wasio waarabu) ni Mfursi. Na kwa kuyazingatia maana ya maneno haya Abul Aswad akaimba shairi lifuatalo:
Hakika mtoto alie zaliwa kati ya Kisraa na Haashim ni mkarimu zaidi ya watoto wote walio vishwa hirizi shingoni mwao.
Amezaliwa(a.s) katika mji wa Madinanatul-munawwarah siku ya Alikhamisi mwezi mtukufu wa Shaaban[29] mwaka (38) hijiria na kufa shahidi kwa sumu siku ya juma mosi tarehe (25) mwezi wa Muharram[30] mwaka (95) akiwa na umri wa miaka (57), na mwanae Imam Baaqir(a.s) ndie alie simamia suala la mazishi yake na kumzika karibu na kaburi la Ami yake Imam Mujtaba(a.s) katika mji wa madinatul-munawwarah.
Na alikuwa ni wa aina yake (kwa maana ya kuwa hakuwa na mfano) katika zama zake katika suala la elimu, ibada, fadhila, uchamungu, kuwasaidia watu wenye kuomba misaada na wenye kutaka usaidizi na mengineyo, na maulamaa wengi pia mafaqihi wamepokea riwaya nyingi sana na zisizo hesabika kutoka kwake na kuhifadhi kutoka kwake dua na mawaidha mengi na karama mbalimbali na mengine mengi yasiyo hesabika. Na alikuwa akitoka usiku wa kiza na kubeba mfuko mabegani mwake ukiwa na Dinari na Dirham napengine alikuwa akibeba mgongoni mwake mfuko wa vyakula, au kuni na kupita mlango mmoja mmoja akibisha hodi na kumpatia kila atokae kwenye nyumba hizo pesa hizo, na alikuwa akifunika kichwa chake ili mafakiri wasimfahamu, na pindi alipo fariki watu wa madina wakafahamu na kuelewa ya kuwa yeye(a.s) ndie ambae alikuwa akibeba mfuko na kuwapatia vyakula.
Pamoja na hayo akipendezewa sana kula pamoja na mafukara au kuhudhuria kwenye chaku chake mayatima na mafakiri na kula pamoja nae. Na miongoni mwa tabia zake njema(a.s) ni kuwa katika kila mwezi alikuwa akiwaita wahudumu wake na kusema: Mwenye kutaka kuolewa kati yanu nitamuoza, au akitaka kuuzwa nitamuuza, au akitaka kuachiwa huru nitamuachia huru. Na pindi alipokuwa akijiwa na muombaji husema: Karibu wewe ambae huibeba akiba yangu ya akhera.
Na kutokana na uchaji mwingi wa mola ni kuwa alikuwa akisali kwa usiku na mcana wake rakaa elfu mmoja na anapo kuwa kwenye sala ngozi yake husinyaa na kukunjamana na rangi yake kubadilika na kuwa ya njano na kutetemeka kama kuti la mtende, na miongoni mwa laqabu zake ni Dhuthafanaati (mwenye sugu au magamba), kutokana na athari za sajda katika paji lake la uso na vitanga vyake pia magotini mwake. Mtu mmoja alimtusi na kumtolea maneno machafu na mabaya na yeye(a.s) akiwa kimia hazungumzi wala kasema chochote na baada ya muda Imam(a.s) akamwendea, waliokuwa wamehudhuria wakadhania ya kuwa anataka kumfanya kama alivyo fanya yeye, mara akasoma aya ifuatayo:
وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾
Na wenye kuvunja ghadhabu na kuwasamehe watu na Mwenyezi Mungu anawapenda watu wema[31] .
Kisha akamsimamia bwana yule na kusema: Ewe ndugu yangu hakika wewe ulisimama kwangu (ulinisimamia) muda ulio pita na kusema uliyo yasema, ikiwa umeyasema kwangu hayo uliyo yasema, basi mimi nina muomba Mwenyezi Mungu msamaha na ikiwa umesema mambo ambayo siko nayo, Mwenyezi Mungu akusamehe[32] .
Yeye ni Imam Mohammad bin Ali Al-baaqir(a.s) na mama yake ni Fatuma binti Hassan(a.s) alizaliwa katika mji wa madina siku ya Ijumaa mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Rajab[33] mwaka (57) hijiria.
Na yeye ndie mtu wa kwanza katika kizazi cha Ali alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi hicho cha Ali, na ni mtu wa kwanza wa kizazi cha Haashim alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi cha Haashim, na ni mtu wa kwanza alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi cha Fatuma, kwani yeye ndie wa mwanzo alie kusanya kati ya kizazi cha maimamu wawili Hassana na Hussen(a.s) na alikufa shahidi kwa sumu siku ya juma tatu tarehe (7) Dhul hajjil haraam mwaka (114) hijiria akiwa na umri wa miaka (57) na mwanae Imam Swaadiq(a.s) ndie alie simamia suala la maandalizi ya mazishi yake na kumzika pembezoni mwa kaburi la baba yake Imam Sajjad(a.s) na Ami wa baba yake na babu yake Imam Mujtaba(a.s) katika makaburi ya Baqii'i kwenye mji wa Madinatuil munawwarah. Na alikuwa ni mwenye fadhila kubwa mkarimu na mwenye kushikamana na dini na alikuwa ni mwenye elimu nyingi na kubwa na mpole sana, pia mwenye tabia njema na mwenye kufanya ibada sana, mwenye unyenyekevu, ukarimu, ukunjufu na alifikia kwenye kilele katika tabia zake njema, mkiristo mmoja alimwambia: Wewe ni mfunguzi na mpasuaji! Imam akasema: Mimi ni Mfuinguzi.
Akasema wewe ni mtoto wa mpishi. Imam akasema:Hiyo ni kazi yake . Akasema: Wewe ni mtoto wa mtu mweusi na mbaya. Imam(a.s) akasema:
Ikiwa umesema kweli Mwenyezi Mungu amsamehe na ikiwa umesema uongo Mwenyezi Mungu akusamehe . Yule Mkiristo akasilimu.
Na katika elimu alikuwa kama Bahari yenye mawimbi mengi, akijibu kila mas'ala na swali lolote analo ulizwa bila kusita.
Na Ibnu Atwaa Al-makiy amesema: Sija wahi kuona kamwe wanazuoni na maulamaa kwa mtu yeyote alie kuwa mdogo zaidi kuliko nilivyo waona kwa Baaqir(a.s) hakika nilimuona Al-hakam bin Utaybah-pamoja na utukufu wake na heshima yake kati ya watu-akiwa mbele yake kama mtoto akiwa mbele ya mwalimu wake, na Mohammad bin Muslim amesema: Sikujiwa na fikra yoyote isipokuwa nilimuuliza Mohammad bin Ali(a.s) mpaka nilimuuliza hadithi elifu thalathini (30).
Na Imam(a.s) alikuwa ni mwenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wakati wote, mpaka Imam Swaadiq(a.s) akasema: Baba yangu alikuwa ni mwenye kumtaja sana Mwenyezi Mungu, nilikuwa nikitembea pamoja nae hali ya kuwa akimtaja Mwenyezi Mungu na alikuwa akizungumza na watu na lisimshughulishe hilo kunako kumtaja Mwenyezi Mungu[34] .
Na Imam alikuwa ni mwingi wa tahajjud (sala za usiku) na ibada, mwenye kulia sana na mwenye mazingatio.
Yeye ni Jaafar bin Mohammad As-swaadiq(a.s) na mama yake ni Fatuma alie kuwa akiitwa kwa kunia ya (Ummu farwah) alizaliwa(a.s) katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarehe (17) mwezi wa Rabiiul Aawwal (mfungo sita) siku ya kuzaliwa Mtume(s.a.w.w) mwaka (83) hijiria na kufa shahidi kwa sumu siku ya juma nne tarehe (25) mwezi wa Shawwal (mfungo mosi) mwaka (148) hijiria akiwa na umri wa miaka (65), na mwanae Imam Kaadhim kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika katika makaburi ya Baqii'i pembezoni mwa kaburi la baba yake Imam Baaqir(a.s) na babu zake wawili: Imam Sajjad na Imam Mujtaba(a.s) .
Na alikuwa na Fadhila nyingi zisizo hesabika kama elimu, fadhila, hekima, fiqhi, zuhdi, uchamungu, ukweli, uadilifu, ubora, furaha na utoaji, ukarimu, ushujaa na fadhila zinginezo.
Na kwa hakika Mufiid alisema (Mwenyezi mungu autukuze utajo wake): Na maulamaa hawakunukuu kwa yeyote kati ya Ahlul bayti wake kama walivyo nukuu kutoka kwake na hakuna yeyote kati ya watu wakusanyao hadithi na wakusanyaji wa habari, mfano wa Jaafar bin Mohammad As-swaadiq(a.s) hakika walikusanya majina ya wapokezi kutoka kwake kati ya watu waaminifu pamoja na kutofautiana kwao kirai na itikadi, na walikuwa ni watu elfu nne (4000)[35] . Hadi mwisho wa maneno yake.
Na Abu hanifa Imamu wa madhehebu ya hanafi alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wake moja kwa moja, kama ambavyo maimam wengine wa madhehebu za Ahli sunna walikuwa ni wa wanafunzi wake pia(a.s) lakini si moja kwa moja bali kwa kupitia wanafunzi wake na kwamba elimu nyingi na mpya kama vile Kemia, Fizikia na elimu ya maumbo na nyota na elimu ya ugunduzi wa madini na kuchimbuaji wa hazina zilizoko ardhini na zinginezo nyingi ambazo Imam ndie alie weka misingi yake na kuwaongoza watu kwenye elimu hizo.
Hakika Imam(a.s) alitumia fursa iliyopatikana ya ugomvi kati ya bani Abbas walio fanya mapinduzi dhidi ya bani Umayyah na kati ya bani umayya walio kuwa mbioni kuanguka na kutoweka dola lao, alitumia fursa hiyo kuanzisha Madrasa kubwa ya kielimu na kujishughulisha na kazi ya ulezi wa wanafunzi na watafutaji wa elimu na kuwabainishia mafunzo ya kiislaam na uzuri wa sheria zake na kuwafafanulia fikra za batili na mbaya zilizo ingia kwenye Uislaam na kubatilisha shubha zitolewazo, mpaka misingi ya sheria ikaimarika na ubainifu wa Uislaam kudhihiri na kubainika wazi na akafahamika(a.s) kama Raisi na kiongozi wa Madhehebu ya Jaafaria, kama ambavyo wafuasi wake(a.s) walifahamika pia kwa jina la Shiatu Jaafar (wafuasi wa Jaafar au mashia wa Jaafar).
Na miongoni mwa uongofu wake(a.s) ni kuwa yeye alikuwa akila siki na mafuta na kuvaa kanzu ngumu na nzito napengine alikuwa akivaa nguo yenye viraka na alikuwa akifanya kazi zake mwenyewe kwenmye mabustani na mashamba yake.
Na miongoni mwa Ibada zake ni kuwa alikuwa akisali sana na pengine alikuwa akizimia katika sala na kuitwa watu wa kumsaidia usiku, Mtumishi wake anasema: Nilikwenda mlangoni kwake na nikamkuta katika chumba chake cha faragha akiwa ameweka shavu lake juu ya udongo hali akiomba kwa kuinua vitanga vyake na huku kukiwa na athari ya mchanga usoni mwake na kwenye shavu lake.
Na Imam(a.s) alikuwa ni mwingi wa kutoa, mwenye tabia njema, mwenye maneno laini, mwenye vikao vizuri na mwenye bashasha kwa kila mwenye kukutana nae na alikuwa na muashara mzuri kwa kila anae kutana nae.
Yeye ni Imam Mussa bin Jaafar Al-kaadhim(a.s) na mama yake ni Hamidah Al-muswaffah, alizaliwa(a.s) katika sehemu iitwayo (Ab'waa) nayo ni sehemu iliyoko kati ya Makka na Madina siku ya juma pili tarehe (7) mwezi wa Safar mwaka (128) hijiria na aliiaga Dunia akiwa na umri wa miaka (55) kwa kulishwa Sumu na kufa shahidi katika jela ya Haroun baada ya kumfunga kwa muda mrefu kwa muda wa miaka (14) kwa dhuluma na uadui, na alifariki siku ya Ijumaa tarehe (25) ya mwezi wa Rajab mwaka (183) na mwanae Imam Ridhaa(a.s) kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika mahala lilipo kaburi lake tukufu kwa hivi sasa katika mji wa Kaadhimiyyah huko Iraq.
Na Imam alikuwa ndie mwenye elumu zaidi kati ya watu wa zama zake na mbora wao na mkarimu zaidi kati yao na shujaa zaidi na amwenye tabia njema, mwenye umbile bora na mororo, mwenye kudhihiri juu yake fadhila, elimu na mwenye hadhi tukufu, mwenye kufanya sana ibada na mwenye kurefusha sijda zake, na kutokana na kuvunja kwake ghadhabu na kuto kasirika akaitwa Al-kaadhim, na kutokana na wema wake na utukufu wake alikuwa akiitwa Al-abdus swalih (mja mwema). Na kutokana na elimu yake nyingi aliweza kudhihirisha elimu za aina tofauti, elimu ambazo ziliwashangaza watu, na kati ya elimu hizo ni hadithi ya (Burayha)[36] mkuu wa Wakiristo alie mashuhuri alie shindwa na Imam na kukosa la kusema mwishowe kusilimu na kuwa muislaam safi.
Na miongoni mwa ukarimu wake(a.s) ni kuwa: fakiri mmoja alimuomba Dinari mia moja na Imam kwa kutaka kumjaribu akamuuliza mas'ala au swali moja ili kujua kiwango cha maarifa yake, yule fakiri alipo jibu mas'ala yale Imam akampatia Dinari elfu moja. Na Imam(a.s) alikuwa ni mwenye sauti nzuri sana pindi anapo soma Qur'ani na alikuwa ni mfanya ibada sana kati ya watu na kusoma sana Qur'ani, na alikuwa ni mwenye kurefusha sana sijda na rukuu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na mwenye kulia sana na mwenye mazingatio, na alifikiwa na shahada hali ya kuwa yuko kwenye hali ya kusujudu (yaani akiwa ni mmwenye kusujudu).
Yeye ni Imam Ali bin Mussa Ridhaa(a.s) na mama yake ni Sayyidah Najmah, alizaliwa(a.s) siku ya Al-khamisi tarehe (11) mwezi wa Dhulqaadatul-haraam, mwaka (148) hijiria katika mji wa Madina na kufa shahidi kwa sumu siku ya Ijumaa mwishoni mwa mwezi wa Safar, mwaka (203) na mwanae Imam Jawaad(a.s) kusimamia suala la maandalizi ya mazishi yake na kumzika katika sehemu ya khorasani sehemu ambayo ndiko liliko kaburi lake tukufu. Na Imam(a.s) alikuwa mashuhuri sana kwa elimu nyingi, fadhila, ukarimu, mwingi wa kutoa, mwenye tabia njema, mnyenyekevu, na mwenye kufanya ibada sana.
Maamun-kutokana na vitimbi na hadaa-alimuita Imam Ridhaa(a.s) kutoka Madinah hadi Khorasani (Iran) na kumtaka achukue ukhalifa wa kiislaam-badala yake-lakini Imam alikuwa amejiweka kando na kuyapa mgongo mambo ya kidunia (yaani alikuwa ni mwenye zuhdi) na hakukubali, kwani alifahamu matokeo ya maombi hayo, kuwa ni vitimbi na hadaa, kama ambavyo babu yake Amirul muuminiin(a.s) alivyo kataa Ukhalifa-katika shura-wakati Ibnu Auf alipo mpatia Ukhalifa huo kwa sharti kwamba afuate sera ya mashekhe wawili walio mtangulia, (Abubakar na Omar), kwani Imam aliona ya kuwa Ukhalifa wakati huo ulikuwa umesimama juu ya jambo moja wapo kati ya mambo mawili, na mambo yote mawili hayo ni ya uongo na si yenye kukubaliwa na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu mtukufu: Ama jambo la kwanza ni kuwa Imam(a.s) akubali sharti kisha asilitekeleze -kama alivyo fanya Othumani - na huo ni uongo wa kikauli na wenye kuchukiwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Ama jambo la pili ni kuwa: Imam akubali sharti na atekeleze, maana yake ni kuwa aridhie sera ya mashekhe wawili pamoja na kuwa hakuwa na ridhaa na hakuridhishwa na matendo yao na huo ni uongo wa kimatendo na ni wenye kukemewa mbele ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo basi Imam hakuona njia yenye kuridhiwa na Mwenyezi Mungu tofauti na kukataa na kupinga na kuto kubali[37] .
Na baada ya Imam Ridhaa(a.s) kuukataa Ukhalifa, Maamun alishikwa na butwaa na kunyongea sana kwani aliona ya kuwa mpango wake ambao kwa ajili yake alimuita Imam umeshindwa na kufeli, hapo alimtaka achukue wilayatul ahad - cheo cha waziri mkuu- na kumlazimisha kukubali(a.s) lakini Imam(a.s) alimuwekea sharti ya kuwa hato ingilia katika jambo lolote kati ya mambo ya dola na kukubali cheo hicho kwa sharti hilo. Imam(a.s) alikuwa ni mrithi wa baba zake watukufu(a.s) katika elimu na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na elimu yake ilionekana na kudhihiri kiasi kidogo kuhusiana na mambo ya dini na Madhehebu fikra na Itikadi-katika kikao cha majadiliano ambacho kiliandaliwa na Maamuun-na yaliyo jitokeza kwenye hadithi ya Rukbaan.
Vile vile katika ibada alikuwa(a.s) akikesha katika masiku mengi kwa ibada na kuhitimisha Qur'ani kwa muda wa siku tatu na mara nyingi alikuwa akisali usiku na mchana rakaa elfu moja, na mara nyingi alikuwa akisujudu kwa muda mrefu, pengine alichukua masaa kadhaa kwenye sijda na alikuwa ni mwengi wa kufunga. Na Imam(a.s) alikuwa ni mwingi wa kutenda mema, na akitoa sana sadaka na sadaka nyingi alikuwa kizitoa kwa siri na hasa kwenye usiku wa kiza.
Na miongoni mwa tabia zake na adabu zake(a.s) ni kuwa hakumuudhi mtu yeyote kwa maneno kamwe na wala hakumfanyia ukali mtu yeyote katika kauli, na hakuwa akiegemea kukiwa kuna watu wamekaa mbele yake na hakuwahi kucheka kwa sauti kubwa na ya juu kamwe, na hakuwahi kutema mate mbele ya yeyote kamwe, na chakula kilipo kuwa tayari mezani huwaita ahli zake wote na wahudumu wake na kula pamoja nao.
4
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
Yeye ni Imam Mohammad bin Ali Al-jawaad(a.s) na mama yake ni Sayyidah Sabiika, alizaliwa(a.s) siku ya Ijumaa tarehe (10) katika mwezi mtukufu wa Rajab, mwaka (195) hijiria, katika mji wa Madinatul munawwarah na kufa shahidi kwa sumu katika mji wa Baghdaad, mwishoni mwa mwezi wa Dhul-qaadah (mfungo pili) mwaka (220) hijiria, na mwanae Imam Al-hadiy(a.s) kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika kwenye maburi ya Makuraishi pembezoni mwa kaburi la babu yake Muusa bin Jaafar(a.s) katika mji wa Kaadhimiyyah mahala lilipo kaburi lake kwa hivi sasa.
Na Imam(a.s) alikuwa ni mjuzi zaidi kati ya watu wa zama zake na mbora zaidi kuliko watu wote, mkarimu, pia mwingi wa kutoa na mwenye vikao vizuri, na alikuwa ni mwenye tabia njema, mfasaha na kila alipo kuwa akipanda mnyama wake hubeba Dhahabu na Fedha na hakuna aliekuwa akimuomba isipokuwa humpatia, na alie kuwa akimuomba pamoja na wingi wao alikuwa hampatiii chini ya Dinari Khamsini (50) na alie kuwa akimuomba kati ya shangazi zake alikuwa hampi chini ya Dinari ishirini na tano (25).
Na miongoni mwa elimu yake kubwa ambayo ilidhihiri kwa watu: Ni kuwa wanazuoni thamanini kati ya wanazuoni wa miji mbalimbali walikusanyika kwake baada ya kurudi kwao kutoka kwenye ibada ya hijja na kumuuliza kuhusiana na mas'ala mbali mbali na yeye(a.s) kuwajibu, namiongoni mwa mambo ya ajabu yaliyo simuliwa kutoka kwake(a.s) ni kuwa watu wengi walikusanyika kwake na kumuuliza mas'ala thelethini elfu-katika kikao kimoja nacho ni kikao kiitwacho kwa siku hizi kwa jina la kongamamno, kongamano ambalo hufanyika na kuendelea kwa muda wa siku kadhaa na Imam kuwajibu mas'ala hayo bila kusita kufanya hivyo wala kukosea na wakati huo akiwa na umri wa miaka tisa (9), lakini jambo kama hili si jambo la ajabu na la kushangaza kutokea kwa Ahlul bayti-watu wa nyumba ya Wahyi na mahala alipokuwa Jibril(a.s) akitelemka akiwa na Qur'ani na hasa baada ya Qur'ani kuzungumzia kuhusiana na kupewa kwa Issa bin Maryam kitabu na Utume hali ya kuwa bado yuko kwenye kitanda chake akiwa mtoto mchanga. Kisha ni kuwa khalifa Alimuoza binti yake na hilo lilifanyika baada ya kumtahini kwa maswali (mas'ala) muhimu na kuyajibu yote-katika kisa mashuhuri.
Yeye ni Imam Ali bin Mohammad Al-hadiy(a.s) mama yake ni Sayyidah Samanah. Alizaliwa(a.s) katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarehe (2) mwezi mtukufu wa Rajab, mwaka (212) hijiria na kufa shahidi kwa sumu kwenye mji wa Samarraa siku ya juma tatu tarehe (3) mwezi wa Rajab, mwaka (254) hijiria, na mwanae Imam Askariy(a.s) kusimamia maandalizi ya mazishi yake, na kumzika ndani ya nyumba yake kwenye mji wa Samarraa mahala lilipo kaburi lake kwa hivi sasa na mahala kilipo lazwa kiwili wili chake kitukufu. Na Imam(a.s) alikuwa ni mtu bora kati ya watu wa zama zake na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na alie kusanya fadhila zote na mkarimu sana na mwingi wa kutoa na alikuwa ni mwenye maneno laini na aliekuwa akimuabudu sana Mwenyezi Mungu na mwenye sera nzuri nasafi na mwenye tabia njema.
Na miongoni mwa ukarimu wake ni kisa kilicho pokelewa na (Ardabiliy) katika kisa chake ya kuwa: Khalifa alimtumia Dirham elfu thalathini, Imam akampatia bedui mmoja wa Al-kufa kama zawadi na akamwambia: Toa kiasi ulipe madeni yako na kiasi kitakacho bakia kitumie kwa ajili ya matumizi na mahitaji ya familia yako na ahali zako na utusamehe. Yule bedui akamwambia Imam: Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika deni nililo kuwa nalo halifikii theluthi ya pesa hii. (Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kufahamu vema mahala pakuuweka ujumbe wake), na akachukua pesa zile na kwenda zake[38] .
Yeye ni Imam Hassan bin Ali Al-askariy(a.s) na mama yake ni Sayyidah Hadiitha. Alizaliwa katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarhe nane (8) mwezi wa Rabiul-aakhir, na inasemekana kuwa amezaliwa tarehe kumi na mbili (12) Rabiul-aakhir[39] mwaka (232) hijiria na kufa shahidi kwa Sumu siku ya Ijumaa tarehe nane (8) mwezi wa Rabiul-awwal mwaka (206) hijiria, na mwanae Imam Hujjatul-muntadhar (mwenye kungojewa) ndie alie simamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika karibu na kaburi la baba yake Imam Al-hadiy(a.s) katika mji wa Samarra, mahala ambapo ndipo lilipo kaburi lake kwa hivi sasa.
Na Imam(a.s) alikuwa ni mfano wa juu kabisa katika ubora, elimu, utoaji, sharafu, furaha na ukarimu, ibada, unyenyekevu na tabia zingine nyingi njema, na alikuwa ni mfano wa kuigwa na kigezo chema kwa wengine, na alikuwa ni mwenye urefu wa wastani na mzuri wa umbile, mwenye uso mzuri na kiwiliwili cha wastani, mwenye heshima na hadhi kubwa kwenye nyoyo na mwenye nafasi ya juu na tukufu katika nafsi za watu, na Imam(a.s) alikuwa akimfanana sana babu yake Mtume(s.a.w.w) katika tabia zake na mwendo wake mwema na uzuri wa kuishi vema na watu.
Na miongoni mwa visa vya ukarimu wake ni kisa kilicho pokelewa na Ismail kisemacho: Nilimkalia na kumsubiri Imam(a.s) katikati ya njia, alipo fika na kupita mahala nilipo kuwa nikamueleza ufukara wangu. Imam akasema(a.s) : Unaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo kwani umefukia Dinari miambili chini ya Ardhi na kusema kwangu maneno haya si kwa sababu ya kuto taka kukupa, ewe ghulam (Mhudumu) mpatie ulicho nacho, akasema: Yule mhudumu akanipatia Dinari mia moja[40] . Na kuna mtu mwingine alimwendea Imam-alipo sikia ukunjufu wake na ukarimu wake-na alikuwa akihitaji Dirhamu mia tano, Imam(a.s) akampatia Dirham mia tano na kumuongezea Dirhamu zingine mia tatu[41] .
Na kwa hakika watu wote walitoa ushahidi na kuthibitisha ubora wake na ukarimu wake, hata wakiristo walimshuhudia(a.s) ya kuwa yeye anafanana na masihi (Yesu) katika ubora, elimu, ukarimu na miujiza yake, na Imam(a.s) alikuwa ni mwenye kufanya sana ibada, akisali sala za usiku (tahajjud) daiama na alikuwa ni mwenye mandhari ya wema, na mwenye heba kubwa.
IMAM WA KUMI NA MBILI: IMAM AL-MUNTADHAR(a.s) (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake)
Yeye ndie Imam na Al-hujjatul-mahdiy(a.s) , Mohammad bin Hassan(a.s) na mama yake ni Sayyidah Narjis. Alizaliwa(a.s) katika mji wa Samarraa usiku wa nusu ya mwezi wa Shaaban, mwaka (255) hijiria. Na yeye(a.s) ndio hoja wa mwisho wa Mwenyezi Mungu juu ya ardhi na Khalifa wa mwisho wa Mtume(s.a.w.w) na Imam wa mwisho wa Waislaam, maimam ambao ni kumi na mbili na Mwenyezi Mungu-kwa utashi wake - ameurefusha umri wake mtukufu katika Dunia hii ili ardhi isibakie bila hujja wa Mwenyezi Mungu, kwani kama kusinge kuwa na hujja basi ardhi inge didimia pamoja na watu wake na yeye Imam haonekani kwa watu na Mwenyezi Mungu atamdhihirisha katika Aakhiriz-zamani (Zama za mwisho) baada ya Dunia kujawa na dhuluma na ujeuri (uovu), ili aijaze dunia hiyo kwa uadilifu na usawa.
Hakika Mtume(s.a.w.w) na maimam watwaharifu walitoa habari ya kuwa yeye atakuwa na ghaibah (Atatoweka na kuto onekana) kwa muda mrefu, na hatakuwa thabiti kwenye juu ya Uimam na wilaya yake na kumuamini isipokuwa yule ambae Mwenyezi Mungu ameujaribu moyo wake kwa Imani, na katika siku za ghaiba yake atakuwa katika hali ya kuwafikishia manufaa watu wa Ardhini kama jua lifikishavyo manufaa na faida zake kwa watu hao hata kama litakuwa limefunikwa na mawingu, na Mwenyezi Mungu atambakiza hai mpaka utakapo fika wakati wa kudhihiri kwake, na hapo kudhihiri kwa idhini yake Mwenyezi Mungu mtukufu na kuimiliki (kuitawala) Dunia yote na kueneza uadilifu na usawa Duniani na kueneza Uislaam na misingi yake yote na kuitekeleza Qur'ani na amri zake kwa watu wote na katika nyanja zake zote za maisha, na hapo Kheri kuenea na saada kutangaa kwenye miji yote na kuwaenea waja wote na kuthibitika kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo:
لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ ﴿٣٣﴾
Ili auidhihirishe Uislaam juu ya dini zote hata kuma washirikina watachukia [42] .
Ewe Mwenyezi Mungu harakisha faraja yake na kufanye kwepesi kudhihiri kwake na utujaalie tuwe miongoni mwa wasaidizi na answari wake. Baada ya hayo ni jambo lililo wazi ya kuwa Imam Al-mahdiy(a.s) alipokuja kuandaa mazishi ya baba yake Imam As-kariy(a.s) na kumsalia watawala waovu walifahamu kuwepo kwa mrithi na mshika nafasi baada ya Imam Askariy(a.s) na hili lili waogopesha sana juu ya utawala wao na wakafikiria njia ya kumkamata na kumuua kama walivyo waua baba zake(a.s) ili kwa kufanya hivyo waokoke na kujinusuru na habari zilizo wafikia kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kuhusiana na habari za Imam wa kumi na mbili na kwamba yeye ndie ambae atakae maliza na kuangamiza utawala wa waovu na kuchukua utawala huo, na Imam Mahdiy(a.s) alikuwa ameamuriwa na Mwenyezi Mungu mtukufu kuwa kwenye ghaiba na kuto onekana kwa watu.
Na pindi majasusi wa Khalifa walipo muona na kuivamia nyumba yake akaghibu na kutoweka na kuto onekana kwa watu na kufichika kunako macho yao, na hilo lilifanyika kwa Imam kutokea kwenye mlango mwingine ulio kuwa wazi wenye kutokea kwenye Sirdab (nyumba ya chini) iliyo kuwa na mlango wa kutokea nje bila yeyote kati yao kumuona, na kutokana na ukweli kwamba sehemu ambayo ilikuwa ndio mahala pa kughibu kwake ni nyumba yake(a.s) Waislaam wakaifanya ile sehemu inasibishwayo kwake-katika mji wa Samarra-iliyo mashuhuri kuwa ni sirdab ya kughibu kwake, wakaifanya kuwa msikiti na mahala pa kufanyia ziara (kutembelea).
5
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
Maana yake ni kuwa: Mwenyezi Mungu mtukufu anamuhuisha na kumfanya mwanadamu awe hai katika Akhera baada ya kumfisha duniani, ili amlipe thawabu mtu mwema juu ya wema wake na kumlipa muovu kwa uovu alio ufanya. Kwa hivyo basi mwenye kuamini na kutenda matendo mema na kusali, kufunga, katoa sadaka (zaka) na kumtakasia nia Mwenyezi Mungu (kuwa na ikhals) na kuwahifadhi Mayatima na kuwalisha Masikini na mengineyo mengi, hakika yeye Mwenyezi Mungu humpa thawabu mtu huyo kwa kumuingiza kwenye pepo yenye neema ambayo hutiririka chinio yake mito, na yenye vivuli vyenye kumfunika na yenye rehma nyingi sana na majumba ya kifalme na kifakhari na mahurulaini walio fungiwa kwenye majumba yao na kupata maridhio ya Mwenyezi Mungu ni kukubwa zaidi.
Na mwenye kukufuru na kufanya matendo mabaya na kusema uongo, kufanya khiyana, kuua, kuiba, kuzini, kunywa pombe, na mfano wa hayo, hakika Mwenyezi Mungu humlipa kwa kumuingiza katika jahannama iliyo jawa na moto na adhabu, na chakula chake ni cha miti ya miba na kinywaji chake ni maji ya moto na wakati yuko kwenye matatizo na adhabu yenye kudhalilisha na ya milele isio katika wala kukoma.
Na kuna visimamo vingine viwili kabla ya moto na pepo:
1. Kaburi: Nayo ni sehemu au hatua ya kwanza kati ya hatua za ulimwengu wa barzakh baada ya kuwa mauti ni mlango wa kuingia kwenye ulimwengu huo, kwa hivyo kila mmoja huulizwa aliyo yafanya akiwa kaburini mwake, na kupewa thawabu kwa matendo mema aliyo yatenda na kuadhibiwa juu ya matendo mabaya na kutokana na hayo Mtume(s.a.w.w) akasema:Kaburi ima ni shimo kati ya mashimo ya moto, au ni bustani kati ya mabustani ya peponi [43] na hali ya mwanadamu akiwa kaburini kwa mfano na kwa kutaka kukuletea karibu maana na hali yake ni kuwa: ni kama hali ya mtu alie lala ambae anaota ndoto nzuri na kufurahi kwa ndoto hiyo, au kuota ndoto mbaya na kuteseka na kuadhibika kwa ndoto hiyo, wakati ambapo yule ambae humkaribia yule mtu alie lala na kumuona, hafahamu ya kuwa yuko kwenye raha au kwenye adhabu, vilevile walio hai huwaoni watu walio kufa katika hali ya kuwa ni vilivyo haribika, ama kujua ya kuwa wana adhibiwa au wako kwenye neema, hawalihisi hilo na hilo linatokana na ukweli kuwa vipimo katika ulimwengu wa barzakh ni vipimo vipya tofauti na vipimo vya duniani, na havifanani na vipimo vya maisha ya kidunia ambavyo tunavifahamu na tumevizowea.
2. Kiama: Nayo ni kuwa baada ya kuvifufua viwiwili hivi na kuvitoa kwenye makaburi, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu atavifufua katika siku hiyo vyote katika jangwa kubwa na pana kwa ajili ya hesabu na malipo na huko kuwekwa mahakama kubwa na kuwekwa vipimo na mahakimu kuhudhuria-nao ni mitume wa Mwenyezi Mungu na mawasii wao-na kugawiwa madaftari ya matendo: Nyaraka za matendo ya waja na mashahidi kwa ajili ya kutoa ushahidi, na viungo vya mwanadamu kukiri juu ya matendo yaliyo tendwa na mwanadamu na kuyafanya, na waumini wale ambao walifanya matendo mema duniani kuneemeka kwa kuingia peponi na waovu wale ambao walikuwa wakitenda maovu duniani kuwa katika hali mbaya ya uovu na kuingia motoni. Kwa hivyo ni juu ya mwanadamu kujitahidi kwa kadri ya uwezo wake katika kutekeleza matendo mema na kujiepusha na matendo maovu, ili asije kuwa muovu huko katika Akhera uovu wa milele na milele, uovu usio kuwa na makimbilio wala muokozi, kiasi kwamba waovu watabakia jela wakati wote na wakiwa kwenye adhabu ya milelel.
Mwenyeziu Mungu anasema:
فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾ وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾
Mwenye kufanya matendo ya kheri hata kama ni kiasi cha tembe moja atayaona. Na mwenye kufanmya matendo ya shari kiasi cha tembe moja atayaona[44] .
Kabla ya kuanza kubainisha na kufafanua sehemu ya pili katika mafunzo ya juu ya Uislaam, hapana budi kuashiria hapa ya kuwa sehemu ya kwanza ya mafunzo ya kiislaam ya hali ya juu na yaliyo matukufu yaani: Usulud-dini ambazo tumezi zungumzia, ni lazima mwanadamu aziitakidi au awe na itikadi nazo-kwani misingi hiyo ndio inayo husiana na ukafiri na itikadi- kutokana na ijtihadi na kwa kutegemea dalili na wala haitoshi kwenye misingi hiyo kujitegemeza sehemu fulani au kwa mtu fulani na kumfuata mtu huyo.
Wakati ambapo Furuud-dini (matawi ya dini), ambayo hivi sasa tuko mbioni kuyafafanua na kuyazungumzia, hakika matawi hayo yameenea na kuzihusu sehemu na nyanja zote za maisha na yanazihusu harakati zote za mwanadamu na matendo yake yote kabla ya kuzaliwa kwake mpaka baada ya kufariki kwake na maranyingi mwanadam-kwa sababu ni mambo yanayo husiana na matendo kama harakati za mwanadamu na kutulia kwake na utendaji au utekelezaji wa mambo ya aina tofauti na mabadiliko-hawezi kufanya ijtihadi (kujitahihi) katika mambo yote hayo na kufahamu hukumu zake kutokana na dalili zake kwa uchambuzi wake ulio tajwa katika vyanzo vine vya sheria: Qur'ani tukufu, Sunna sharifu- Yaani hadithi za Mtume(s.a.w.w) na riwaya za Ahlul bayti(a.s) - na Ijmaa (Makubaliano ya wanazuoni) na Akili, kwa hivyo Uislaam ukajuzisha (ukamruhusu) kwa mwanadamu kumfuata mujtahidi alie kusanya masharti ya kufuatwa (kufanyiwa taqliid) kwenye mas'ala hayo na kurejea kwake katika mas'ala hayo kwa ajili ya kumfanyia wepesi na kumrahisishia mambo.
Ndio, hakika matawi ya dini ni mengi sana na sisi tuta ashiria yale yaliyo muhimu sana nayo ni kumu yaliyo maarufu, kisha tutabainisha na kufafanua yale ambayo yanahitaji kufafanuliwa kati ya hayo inshaa allah taala ama matawi hayo kumi yaliyo maarufu ni kama yafuatayo:
1. Sala
2. Saumu (Funga)
3. Khumsi
4. Zaka
5. Hajji
6. Jihadi
7. Kuamrisha mema
8. Kukataza maovu
9. Kuwatawalisha mawalii wa Mwenyezi Mungu
10. kujitenga na kujiepusha na maadui wa Mwenyezi Mungu.
Kwa kuyafahamu hayo ni jambo lililo wazi kuwa matawi haya pamoja na kuongezea matawi mengine kama uuzaji (bayii) na ununuzi na Nikah (Ndoa) na Talaka, Kisasi na Diyaa (fidia), hayo yamefafanuliwa na kufanyiwa bahthi kwa upana zaidi katika kitabu hiki-katika kifungu cha masaail-lakini baadhi yaliyo muhimu kati ya hayo yamebakia na ambayo ni katika mambo yaliyo sambamba na yenye kuwiana na zama hizi tunazo ishi, kama jamii ya wanadamu na nidhamu ya kijamii na kisiasa, Uchumi, Jeshi na nguvu zadola, kama Jeshi la ulinzi na polisi, Mahakama na utoaji hukumu, Utamaduni na Vyombo vya habari, Afya na nyenzo za tiba, Uhuru wa kila mtu mmoja mmoja na uhuru wa jamii na mengineyo, haya ndio ambayo tutayazungumzia katika sehemu hii kwa utashi wake Allah.
Hakuna shaka ya kuwa Uislaam unayo nidhamu maalum ya utawala na uendeshaji wa mambo ya kijamii, kama ambavyo hakuna shaka ya kuwa nidhamu hii maalum ya kiislaam imekuwa ikitekelezwa katika nchi za kiislaam kwa muda wote wa karne kumi na tatu (13) mpaka lilipo anguka dola la kiislaam kabla ya zaidi ya nusu karne - sawa utekelezaji huo ulikuwa ni utekelezaji kamili wa kanuni zote au ulikuwa ni utekelezaji pungufu- Kisha mtu ana weza kusikia ya kuwa utamaduni wa kiislaam (Al-hadharatul- islaamiyyah) ulikuwa ni utamaduni wa aina yake na bora kwa kiwango kikubwa na ulio pituka tamaduni zingine zote, na anaweza kusikia ya kuwa Uislaam - kutokana na hekima za kanuni zake zitokazo mbinguni na zilizo na uadilifu-umebeba jukumu la kutatua matatizo yote ya ulimwengu na kwamba kanuni hizo lau kama zitatumika na kurudishwa kwenye utawala, dunia itabadilika na kuwa pepo yenye neema na watu kuishi kwenye kivuli na neema zake raha mustarehe, na wangeishi maisha mema na yenye raha tele.
Kwa msingi huo: Basi nidhamu hiyo ni ipi? Na je kuna uwezekano wa Nidhamu na Utawala wa kiisalam kurudi tena kwenye uhai katika zama hizi za upanukaji wa dunia na maendeleo ya kianga na maendelo ya atomi na katika zama za maendeleo ya Internet na kupanuka kwa habari na vyanzo vyake? Na ikiwa Uislaam utachukua Utawala vipi utaweza kutatua matatizo yaliyopo ya kiulimwengu? Hakika haya ni maswali yanayo paswa kupatiwa majibu
Na Pengine - majibu ya maswali tutakayo yataja hapa - yakaamsha hali ya mshangao na kustaajabu na msomaji kupigwa na butwaa na kudhania ya kuwa sisi tunazungumzia kuhusu mji ulio bora kabisa, pamoja na kuwa sisi tuna maandalizi kamili na tuko tayari kuondoa mshangao huo na kustaajabu huko kwa kutoa dalili na ushahidi wa kiisalaam juu ya majibu hayo[45] , na kutoa mifano hai na ya wazi kabisa kutoka kwenye historia ya utawala wa kiislaam ulio safi na halisi, jambo linalo thibitisha uwezo wa Utawala na Nidhamu ya kiislaam kurudi tena na kwa mara nyingine kwenye uhai na kushika hatamu ya uongozi na kuendesha mambo kwa ujasiri kamili na kwa umadhubuti bila kuteteleka, kwani Nidhamu ya kiisallam ndio Nidhamu pekee kati ya Nidhamu zote za ulimwengu- kuanzia hizo za zamani na za hivi sasa na zitakazo jitokeza kwa siku za baadae-kutokana na hekima za kanuni na sheria zake zitokazo mbinguni- yenye uwezo wa kuuendesha ulimwengu wenye maendeleo na ulio funguka au ulio wazi, uendeshaji uwezao kuufikisha kwenye matarajio yake na kuyathibitisha matumaini yake na kuutatulia matatizo yake na kuuondolea matatizo unayo kabiliana nayo na kuuondolea mambo yanayo usibu kama Uovu Madhara Ujinga Maradhi na kuufikisha ulimwengu huo kwenye ukingo wa Amani na Matumaini na kuufikisha kwenye ufukwe wa sa'aada na Amani, na Nidham hii imekusanya sababu na nyenzo zote za kuuletea maendeleo na kuufisha kileleni na kuyathibitisha yote ayatakayo mwanadamu katika nyanja hizi: kama Siasa Uchumi Uhuru na mengineyo ambayo tutayaelezea kwa muhtasari:[46]
Swali : Je katika Dini ya kiislaam kuna siasa?
Jawabu : Ndio, ndani ya Uislaam kuna sehemu au fungu bora kabisa kati ya mafungu ya siasa na kuna aina nzuri kabisa kati ya aina za idara na uendeshaji wa nchi na wananchi (waja wa Mwenyezi Mungu).
Swali : Je utawala katika Uislaam ni utawala wa kijamhuri au ni utawala wa kifalme?
Jawabu : Utawala katika Uislaam si utawala wa kijamhuri wala wa kifalme-kwa maana ya kiistilahi ya maneno hayo yalivyo elezwa kwenye kamusi za ulimwengu wa kimagharibi (yaani kama yanavyo elezwa kwenye makamusi ya nchi za magharibi katika zama hizi-bali ni utawala wa mashauriano ya watu na inasihi kuuita kuwa ni utawala wa kijamhuri, kutokana na kuwa ni utawala unao tegemea mashauriano ya wananchi, kwani katika Uislaam hakuna utawala wa kifalme wa kurithishana.
Swali : Ni zipi sifa za mtawala (kiongozi) wa kiislaam?
Jawabu : Kiongozi wa kiislaam ni mtu muumini, mwenye elimu ya sheria ya dini ya kiislaam kikamilifu na mwenye kufahamu mambo ya kidunia na mwenye kusifika na sifa ya uadilifu kikamilifu, kwa hivyo basi mtu yeyote atakae kamilisha masharti haya na watu wengi kumridhia, basi anakuwa mtawala na akipungukiwa na moja wapo kati ya masharti haya atauzuliwa na kutolewa kwenye cheo chake kwa haraka sana, lakini ikiwa umma (watu) hawakuridhia abakie kwenye cheo chake hicho na kuwa raisi, na wanayo haki ya kumbadilisha na kumuweka mwingine alie kusanya masharti hayo.
Swali : Ni nani anae mteua mtawala wa kiislaam?
Jawabu : Sehemu kubwa ya umma (watu walio wengi) na hii inahusika tu ikiwa mtawala huyo au kiongozi huyo si maasuum alie teuliwa na Mwenyezi Mungu alie takasika na mtukufu kama Mtume(s.a.w.w) na maimamu watwaharifu(a.s) .
6
Swali : Je katika utawala wa kiisalam kuna suala la uchaguzi na utoaji wa maoni na upigaji wa kura na je kuna bunge la wawakilishi wa watu na vikao vya manispaa na mikoa na mfano wa hayo?
Jawabu : Ndio yote hayo yamo ndani ya Uislaam- hasa katika zama zetu hizi ambazo Imam Mahdiy(a.s) yuko mafichoni (katika Ghaiba) - lakini kwa mfumo wa kiisalaam, kwa mfano: Bunge jukumu lake ni kutekeleza na kufuatisha au kutekeleza kanuni za ujumla kwenye sehemu zake na maswaadiki zake, na jukumu lake si kuweka sheria mpya na kutunga sheria mpya, kwa sababu utungaji wa sheria na kanuni kwanza kabisa hiyo ni haki ya Mwenyezi Mungu mtukufu na pili ni kuwa hakuna upungufu katika hukumu za kiislaam na wala hakuna kasoro wala upungufu, mpaka tuhitaji kutunga sheria mpya na kutunga kanuni zingine, kwa mfano imepokelewa katika hadithi kwamba:Hakika Uislaam umetubainishia hukumu za kila kitu hata hukumu ya dia (fidia) ya mkwaruzo) (yaani mtu akimkwaruza mwenziwe kuna hukumu yake) na imepokelewa katika hadithi nyingine ya kuwa: (Halali ya Mohammad(s.a.w.w) ni halali hadi siku ya kiama na haramu yake ni haramu hadi siku ya kiama) [47] .
Kwa hivyo basi: Mtu yeyote hana haki ya kuharamisha jambo fulani na kuhalalisha jambo lingine bali haki yake ni katika kutekeleza na kutenda, kwa mfano: Uislaam umehukumu ya kuwa biashara katika nchi ni haki ya watu na wafanya biashara, kwa hivyo bunge halina haki ya kubadilisha sheria hii au kuibadilisha kwa kuifungamanisha au kuihusisha na watu fulani tu au kuihusisha tu na serikali, wakati ambapo Uislaam haukuhukumu ya kuwa utembeaji bara barani na majiani uwe kwa upande wa kulia au upande wa kushoto, kwa hiyo katika sehemu kama hizi ni haki ya bunge kuainisha kuwa iwe ni upande wa kulia au kushoto, na imekuwa hivyo kwa sababu Uislaam umeamrisha kuwepo nidhamu na kuto kuwa na fujo na kila mtu kufanya atakavyo, na suala la kuainisha upitaji wa mabarabarani au njiani iwe ni upande wa kulia kwa mfano ni kutekeleza nidhamu ambayo imehukumiwa na Uislaam na kuweka sheria yake na hali ni hiyo hiyo katika mambo mengine mfano wa hilo.
Swali : Sasa kwa nini hivi leo tunaona katika nchi za kiisalam upungufu na matatizo na utungaji wa sheria na kanuni?
Jawabu : Hakika nchi hizo ni nchi za kiisalaam kwa jina tu na kwa alama na si zaidi ya hivyo na Mwenyezi Mungu mtukufu amekwisha sema:
وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ ﴿١٢٤﴾
Na mwenye kujiepusha na utajo wangu (Qur'ani) hakika mtu huyo ana maisha ya taabu na siku ya kiama tutamfufua akiwa kipofu.[48]
Kwa hivyo yule ambae anachukua jukumu la kutunga sheria na kuacha au kujiepusha na hukumu za Mwenyezi Mungu anayafanya maisha yake kuwa finyu na ya dhiki - kama maisha ya nchi za kiislaam yalivyo kuwa finyu-na mtu huyo katika Akhera ana aibu na moto.
Swali : Ni lipi jukumu la utawala wa kiisalaam kuuelekea Umma?
Jawabu : Jukumu lake ni kuhifadhi na kulinda uadilifu kati ya watu- ndani ya nchi na nje ya nchi-na kuyafanya maisha yaendelee na kuondoa mahitaji kwa kukithirisha mahitaji ya watu: kuwapatia riziki, mali, kuwapatia elimu na kuwapatia elimu za juu na kuhifadhi Amani na usalama wao na utulivu wao.
Swali : Ni kanuni ipi ambayo hutekelezwa na dola la kiislaam?
Jawabu : Ni kanuni itokanayo na kitabu na Sunna za Mtume(s.a.w.w) na Ijamaa na Akili.
Swali : Ni nani mwenye kuweka kanuni ili ziweze kutekelezeka?
Jawabu : Huwekwa na mafaqihi (maulamaa wa fiqhihi) walio waadilifu ambao ndio marejeo ya Umma yaani wanazuoni wa mambo ya dini na Dunia, ambao watu hurejea kwao katika taqliid.
Swali : Je katika Uislaam kuna makundi mbali mbali ya kisiasa?
Jawabu : Hakuna shaka kuwepo kikundi ambacho kiko chini ya uangalizi wa maulamaa ambao ndio marejeo ya watu, ikiwa kikundi au chama hicho ni utangulizi wa kuunda bunge la wananchi amabalo ndio linalo takiwa kutekeleza na kufuatilia utekelezaji wa sheria, ama kikundi ambacho kitakuwa ni utangulizi wa kusimamia utungaji wa sheria hakifai kuwepo na hilo linatokana na ukweli kuwa utungaji na uwekaji wa sheria hilo ni jukumu maalu tu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu alie takasika.[49]
Swali : Je katika Uislam kuna mfumo maalum wa kiuchumi?
Jawabu : Ndio na ulio bora zaidi kuliko mifumo iliyo wahi kujulikana katika ulimwengu huu.
Swali : Je mfumo wa kiuchumi wa kiislaam ni wa kibepari (Capitalism), au kijamaa? au ni wa Makomonisti au ugawaji kwa sawa?
Jawabu : Hakuna Ubepari wala ujamaa katika Uislaam,- kwa maana ifahamikayo hivi leo - na wala si wa kikomonisti wala ugawaji.
Swali : Basi mfumo wa kiislaam uko je?
Jawabu : Uchumi wa kiislaam unaheshimu umiliki wa mtu mmoja mmoja na unaukiri kwa sharti kwamba umiliki huo usitokane na mali ya haramu, na nisharti kutekeleza na kutoa haki zake za kisheria[50] .
Swali : Basio dola (serikali) linapata vipi mapato yake?
Jawabu : Dola linapata mapato yake kwa kukusanya haki za kisheria zilizo thibitishwa ndani ya Uislaam.
Swali : Ni zipi hizo haki za kisheria zilizo wajibu?
Jawabu : Haki hizo ni nne: Khumsi, Zaka, Kodi za Ardhi, na Jizya (mali ichukuliwayo kutoka kwa Mayahudi na Wakiristo walio wekaeana mikataba na dola la kiisalaam kwa ajili ya kuwalinda).
Swali : Tufafanulieni haki hizi ambazo ndio vyanzo vya mapato katika Uislaam kama mlivyo taja hapo kabla?
Jawabu : "Khumsi" ni mali au pesa ichukuliwayo na mtawala wa kiislaam (Haakim) nayo ni asilimia (20%) katika faida zote za kisheria na katika Madini, Mali iliyo fichwa chini ya ardhi, na Mali itolewayo baharini kwa kuzamia, na Mali ya halali iliyo changanyika na haramu na Mali iliyo patikana kwenye vita kati ya Waislaam na Makafiri na sehemu fulani ya Ardhi. Na "Zaka" ni mali ichukuliwayo na mtawala wa kiisalaam moja ya (40) na moja ya (100), na Zaka huchukuliwa katika Mbuzi, Ng'ombe, Ngamia, Dhahabu, Fedha, Tende, Zabibu, Shairi na Ngano. Na "Kharaaj" Ni kodi zichukuliwazo na mtawala wa kiislaam kutoka kwa wakulima, katika ardhi zilizo kombolewa bila mapigano au bila kutumia nguvu. Na "Jizya" ni mali ichukuliwayo na mtawala wa kiisalaam kutoka kwa Mayahudi, Wakiristo na Majusi walio wekeana mikataba, na makafiri wengine kwa ajili ya kuwahami na kuwalinda au kwa ajili ya dhimma fulani.
Swali : Je katika Uislaam kuna Mabenki?
Jawabu : Ndio lakini mabenki ya kiislaam hayana riba wala nyongeza, kwani riba katika Uislaam ni sawa na kumtangazia vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake, pamoja na kutekeleza sheria zake zote za kiislaam za mali na mambo ya wafanyakazi huendeshwa na mapato mengine na ikiwa hayakutosheleza, basi hukamilishwa kutoka katika hazina (baytul mali) ya dola la kiislaam:
Swali : Je dola au serikali huchukua mali zingine kutoka kwa watu tofauti na hizo zilizo tajwa, kati ya mafungu yaliyopo hivi sasa?
Jawabu : Hapana, kwani dola la kiislaam halina haki ya kuchukua zaidi ya mafungu manne yaliyo tajwa - kamwe-na imepokewa katika hadithi kama ifuatavyo: (Mwenye kuchukua mali kwa yeyote bila ya ridhaa yake, Mwenyezi Mungu ataichukua mali hiyo siku ya kiama kutoka kwake, badala ya kila Dirham atachukua sala mia saba kati ya sala zake zilizo kubaliwa na kumpatia mwenye mali).
Swali : Dola la kiislaam, huzifanyia nini pesa au mali lizichukuazo na kuzikusanya kutoka kwa watu?
Jawabu : Kwa hakika katika dola la kiislaam kuna idara au Wizara kwa istilaha ya kisasa ijulikanyo kwa jina la (Baytul mali) katika wizara hii hukusanya mali yote ikusanywayo kutoka kwa watu na mali hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kutatua mahitaji yote ya Waislaam, pamoja na kuwa dola husimamia mipango yote ya kimaendeleo ujenzi na maendeleo mengine ya nchi, pia hutenga fungu fulani la mali na kumpatia kila fakiri kiasi cha pesa kimtoshelezacho kuendesha mambo yake ya kimaisha, ili asibakie fakiri katika nchi (kwa maana kuwa huweka mpango wa kupiga vita ufukara nchini) na hukidhi haja ya kila muhitaji, kwa mfano mwenye kutaka kuoa, au mtaji wa kuanzisha biashara, au kujenga nyumba na kuanzisha duka, au kwa ajili ya matibabu, au kwa mwenye safari ya lazima kutokana ya haja au tatizo, au humpatia mtu alie katikiwa na matumizi akiwa safarini na hakuwa na pesa ya kumrudisha nyumbani kwake, au kuwasaidia wanafunzi wanao hitajia pesa katika masomo yao kama kulipia karo, na mfano wa hayo kwa kurejea kwenye baytul mali- na kuithibitishia-kwa njia za kawaida, kama kuleta mashahidi, au kuapa- ya kuwa anahaja ya kitu fulani na hana pesa, wakati huo baytul mali humpatia kiwango kinacho tosheleza kukidhi haja yake kulingana na hadhi yake na chenye kumtosheleza, na kwa msingi huu hakutabakia katika dola la kiislaam fakiri au muhitaji-kamwe-.
Swali : Je haki na pesa hizo za aina nne zilizo tajwa zinatosheleza mahitaji yote hayo?
Jawabu : Ndio, inatosha ukiongezea mapato liyapatayo dola la kiisalaam kutokana na ghanima (Ngawira) na imepokelewa katika hadithi ya kuwa: (Lau kama pesa hiyo haikutosheleza basi Mwenyezi Mungu angeongezea katika kiwango chake) (yaani angeongeza katika kiwango kinacho takiwa kutolewa)[51] .
Swali : Vyanzo vya mapato vilivyo tajwa na ambavyo ni vichache, vinatosheleza vipi wakati tunaona ya kuwa hivi leo kuna vyanzo vikubwa na vingi vya mapato na bado havitoshelezi mahitaji ya serikali na watu?
Jawabu : Vinatosheleza kutokana na uchache wa muundo wa dola na uchache idara (Wizara) na wafanya kazi wake kuwa waaminifu na mambo kuwaachia watu wenyewe, kwa mfano: Wafanya kazi katika dola la kiislaam ni wachache sana, kwa sababu idara au wizara nyingi dola la kiislaam halina haja nazo, kisha ni kuwa kazi nyingi ambazo husimamiwa na dola na serikali-kwa hivi sasa-husimamiwa na watu binafsi katika dola la kiisalaam na hakubakii katika majukumu ya dola na serikali ya kiislaam isipokuwa kazi chache kiasi kwamba dola linakuwa na uwezo wa kuzitekeleza kwa haraka sana na kwa urahisi zaidi kadri iwezekanavyo na ni jambo lililo wazi kuwa: pindi idadi ya wafanya kazi inapokuwa chake na mishahara kupanda na mambo ya watu kuwaachia watu wenyewe na wasimamizi kuwa waaminifu hapo mali hukithiri na kuwa nyingi[52] .
Swali : Je walio staafu kazi hupewa pensheni?
Jawabu : Ikiwa ni fakiri asie jiweza hupewa kulingana na mahitaji yake, si kwa kiwango maalum-kama ijulikanayo katika serikali na madola mbali mbli ya siku hizi[53] .
7
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
Swali : Je katika Uislaam kuna dhamana ya kijamii?
Jawabu : Ndio na ni bora kabisa kati ya aina ya dhamana za kijamii na za kiwango cha juu kabisa.
Swali : Je mnaweza kutubainishia na kutufafanulia sehemu fulani ya dhamana hiyo ya kijamii katika Uislaam?
Jawabu : Dhamana ya kijamii katika Uislaam inatokana na shauku na mapenzi ya kibinadamu na kiutu tena ya kiwango cha juu kabisa kwa maana hiyo hakika Uislaam una anzia kwenye nukta ya utu au ubinadamu, na huitoa dhamana hii ikiafikiana na hali ya kibinadamu na kiutu na ikilenga kwenye upeo wake na katika nyanja zake za ubora na kwa kusisitiza hilo historia haikuwahi kushuhudia kabla ya Uislaam na historia haikunukuu utamaduni wa aina yoyote baada ya Uislaam hadi hivi leo dhamana ya kijamii yenye kina kilicho sawa na kina cha dhamana ya kijamii katika Uislaam.
Hakika dhamana ya kijamii katika Uislaam inasema yafuatayo:
1. Hakika kila mtu anae kufa hali ya kuwa na madeni, au ameacha familia bila msimamizi na mtu wa kuitunza familia yake, ni juu ya Imam wa Waislaam kulipa madeni yake, kama ambavyo ni juu yake kuitunza na kuilea familia yake.
2. Kila anae fariki hali ya kuwa ana mali, mali yote ni ya warithi wake.
3. Pamoja na hayo, huduma za kimali ambazo hutolewa na Baitul mali ya Waislaam kwa kila mtu katika umma wa kiislaam, ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya mwanzo na kwa ajili ya kujipatia maisha mema.
Je unadhani-pamoja na yote hayo- unadhani kunadhamana kama hii ambayo imo ndani ya Uislaam, hata kama ni katika utamaduni ulio endelea na wenye kina kikubwa zaidi? Kwa hakika na bila shaka yoyote hakuna kitu kama hicho, bali ukweli ni kuwa mifumo mingine ya utawala ya kiulimwengu na ya kijahili iliyo kuwepo kabala ya Uislaam vilevile mifumo ya ulimwengu inayo dai kuwa imeendelea na iliyo kuwa na maendeleo ya kielimu na iliyo staarabika katika zama zetu hizi huwajibisha kutoa mapato makubwa kwenye urithi, kama ambavyo wao hawalipi deni la yeyote na wala hawabebi jukumu la kuitunza familia ya marehemu na hakuna shaka hapa kutaja baadhi ya mifano ya kiislaam juu ya jambo hili.
Katika Nusuus (dalili) za kisheria za kiislaam, kuna dalili nyingi zinazo tilia mkazo juu ya haya tuliyo yataja ya dhamana ya kijamii ya kiislaam na dalili hizo bila shaka zinatujulisha juu ya namna Uislaam unavyotilia mkazo na hima juu ya jamabo hili na katika upande huu wa kibinadamu na kijamii ulio mkubwa, kiasi kwamba imekaririwa kwa mara kadha zikinukuliwa dalili juu ya suala hilo kutoka kwa Mtume wa Uislaam(s.a.w.w) na maimam wa kizazi kitwaharifu cha Mtume(s.a.w.w) . Kwa mfano imepokelewa kutoka kwa Abi Abdillah Jaafar bin Mohammad As-swaadiq (a.s) Imam wa sita wa Ahlul bayti(a.s) , ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema:
أنا أولی بکل مؤمن من نفسه وعلي أولی به من بعدي
Mimi ni bora kabisa au mwenye haki zaidi kwa kila muumini kuliko nafsi yake na Ali (a.s) ni bora zidi na mwenye haki zaidi kwa kila muumini kuliko nafsi yake baada yangu .
Akaulizwa: Nini maana ya maneno hayo? Akasema: Kauli ya Mtume(s.a.w.w) :Mwenye kuacha deni, au familia basi ni juu yangu mambo hayo na mwenye kuacha mali basi ni ya warithi wake [55] .
Ali bin Ibrahiim katika tafsiri yake ametoa hadithi, kwa sanadi yake iliyo tajwa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ya kuwa yeye alikuwa akisema:
Hakuna mdai yeyote alie kwenda na mdaiwa wake kwa mtawala kati ya watawala wa kiislaam na ikabainika kwa yule walii ya kuwa ni tajiri na mwenye uwezo, isipokuwa humuokoa yule fakiri kutokana na deni lake, na deni hilo kuhamia kwenye dhima ya mtawala yule wa Waislaam kutokana na mali iliyoko mikononi mwake kati ya mali za Waislaam [56] .
Amesema Imam Swadiq(a.s) baada ya kunukuu hadithi hii kutoka kwa Mutme(s.a.w.w) : Na hakukuwa na sababu ya kusilimu Mayahudi wote isipokuwa baada ya kusikia kauli hii kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) na kwamba wao walipata tumaini juu ya nafsi zao na juu ya familia zao [57] .
Shekh Mufiid (Quddisa sirruhu) ametoa hadithi katika kitabu chake Al-majaalis, kwa sanadi yake kutoka kwa Imam Abi Abdillah As-swadiq(a.s) ya kuwa alikuwa akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alipanda kwenye Mimbari, vitukuta vyake vikabadilika na rangi yake kumeremeta, kisha akageuza uso wake na kusema:Enyi waislaam! Hakika si jambo jingine mimi nimetumwa na kiama, kama vitu viwili hivi- hadi akasema- enyi watu! Mwenye kufariki na kuacha mali basi mali hiyo ni ya warithi wake na mwenye kuacha deni au familia bila muangalizi, ni juu yangu na hurejeshwa kwangu [58] .
Pia ametoa hadithi kutoka kwa Abi Abdillah As-swadiq(a.s) ya kuwa amesema: Yeyote atakae kuwa na mali (yaani atakae chukua deni) kwa mtu fulani na hakuitumia mali hiyo vibaya (kwa israfu), au katika maasi, na ikamuwia vigumu kulipa deni hilo, ni juu ya mwenye mali kumpa muhula (muda) mpaka Mwenyezi Mungu amruzuku na aweze kulipa deni hilo na ikiwa Imam muadilifu yupo, ni juu yake kumlipia deni hilo, kutokana na kauli ya Mtume(s.a.w.w) :Yeyote atakae acha mali basi mali hiyo ni ya warithi wake na mwenye kuacha deni au familia, ni langu na ni juu yangu na ni juu ya Imam kuchukua dhamana aliyo ichukua Mtume (s.a.w.w) [59] .
Hakika Uislaam - kwa ubora wa mfumo na nidhamu yake uliyo nayo ya Baytil mali ya Waislaam na dhamana ya kijamii ya kiislaam- imeufanya umma wa kiislaam kuwa tajiri na ufakiri katika dola hilo umekaribia kuwa sawa na khabari ya kana (khabari iliyo kuwa) kutokana na dola la kiislaam, ambalo lemeenea kila mahala, na lenye ardhi kubwa na pana na zilizo mbali, ardhi ambayo takariban zaidi ya tatu ya nne ya ardhi hiyo ni yenye kukaliwa na watu, na yenye wakazi wengi. Ndio, hakika Shekh Hurrul Amiliy ametaja katika kitabu chake maarufu: (Wasaailu-shia) kisa kifuatacho akisema: Hakika Imam Amirul muuminiin Ali bin Abi Twalib(a.s) alikuwa akitembea katika mitaa na vichochoro vya mji wa Al-kufa, ghafla akamuona mtu mmoja akiomba watu misaada: akastaajabu sana kutokana na mtu huyo na akawageukia walio kuwa pembezoni mwake akijiuliza: Ni kitu gani hiki?
Akajibiwa: kuwa ni Mkiristo amezeeka na kuwa na umri mkubwa na hana tena uwezo wa kufanya kazi na hana mali ya kumuwezesha kuishi, kwa hivyo ndio maana anawanyooshea watu mkono kwa kuomba. Imam(a.s) akasema hali ya kuwa ni mwenye ghadhabu: Mmemfanyisha kazi wakati akiwa kijana mpaka alipo fikia utu uzima na uzee mkamtelekeza na kumuacha? Kisha Imam(a.s) akaamuru atengewe fungu yule Mkiristo katika baytul mali ya Waislaam litakalo mfanya aishi maadamu bado yuko hai[60] .
Hakika kisa hiki kinatufahamisha ya kuwa ufukara ulikaribia kutokuwa na nafasi katika dola la kiislaam, hadi ilifikia Imam Amirul muuminiin(a.s) akimuona fakiri mmoja hushangaa na kustaajabu na kuliona tukio hilo kuwa ni tukio lisilo la kawaida na hali isiyo ya kawaida na halinasibiani na jamii ya kiislaam na dola au nidhamu ya kiislaam, kisha wakati huo akamuwekea fungu litakalo mfanya aishi maisha mazuri na yenye furaha pamoja na kuwa ni Mkiristo na hafuati dini ya kiislaam, na alifanya hivyo ili kusiwe katika nchi ya kiisalaam mfano au tukio moja linalo onyesha hali ya ufukara na kutokuwa na kitu na ili ulimwengu ufahamu hali waliyo nayo Waislaam: Ya kuwa serikali ya kiislaam inampango wa kuangamiza janga la ufukara na kuinua hali ya maisha ya mafakiri na masikini na si kwa mustawa wa Waislaam pekee yao, bali inaupiga vita ufukara hata kwa Makafiri maadamu wako chini ya uangalizi wa dola la kiislaam.
Shekh Kulayni ametoa hadithi kwa sanadi yake iliyo tajwa kutoka kwa Hassan amesema: (Hakika Ali alipo washinda Twalha na Zubayri) katika vita vya Jamal na katika vita vyake alivyo pigana pamoja na wapingaji (Naakithiin) watu walirejea wakiwa wameshindwa, na wakampitia mwanamke mmoja alie kuwa mja mzito njiani, na alipo waona akashikwa na fazaa na mshutuko mkubwa na ikawa ni sababu ya kutoka kwa kilicho kuwa tumboni mwake kikiwa hai na kutatizika hadi akafariki, kisha mama wa mtoto huyo nae kafariki baadae, Imam Ali(a.s) akampitia mama huyo yeye na maswahaba zake hali ya kuwa mama yule akiwa amelala chini na mwanae akiwa njiani, akawauliza kuhusiana na kilicho msibu mama huyo? Wakasema: Hakika alikuwa ni mja mzito na akashikwa na fazaa na mshutuko wakati alipo ona mapigano na namna walivyo shindwa.
Akasema: Akawauliza: Ni yupi alifariki kabla ya mwengine? Akajibiwa: Hakika mwanae ndie alie fariki kabla ya mama.
Akasema: Imam(a.s) akamuita mumewe baba wa mtoto alie fariki akampa theluthi ya fidia kama urithi wa mwane, kisha akamrithisha mama yake theluthi nyingine ya fidia, kisha akamrithisha mume vilevile kutoka kwa mkewe nusu ya fidia ambayo aliirithi kutoka kwa mwanae na kuwarithisha jamaa au ndugu wa mke alie fariki fidia iliyo bakia, kisha akamrithisha mume pia katika fidia ya mkewe alie fariki nusu ya fidia nayo ni: Dirhamu elfu mbili na miatano na jamaa za mwanamke alie fariki akawarithisha nusu ya fidia nayo ni:Dirhamu elfu mbili na mia tano na alimpa kiasi hicho kutokana na kutokuwa na motto mwingine tofauti na yule alie toka kutokana na fazaa iliyo mshika.
Akasema: Na Imam(a.s) alitoa mali yote hiyo kwenye Baytul mali ya Basrah[61] .
Ndio, hivi ndivyo Uislaam ulivyo weka Baytul mali ya Waislaam kwa ajili ya manufaa ya Umma na kutatua matatizo yao na kuwapa haki zao, kwani - kama ilivyo pokelewa katika hadithi tukufu -(Haki ya muislaam haipotei) na katika hadithi nyingine imepokewa ikisema:Damu ya Muislaam haimwagiki bure [62] na kwa dalili hizo Uislaam ukauwekea Umma wa kiisalaam mahitaji yenye kumtosheleza kupitia mpango wake wa dhamana yake ya kijamii yenye uadilifu.
8
Swali : Je katika Uislaam kuna jeshi maalum lililo pangwa na lenye nidham maalum?
Jawabu : Ndio na lenye nidhamu iliyo bora kabisa na lililo pangwa katika sura iliyo bora kabisa.
Swali : Je katika Uislaam kuna sheria ya kujiunga na jeshi kwa lazima bila ya hiari?
Jawabu : Hapana, kujiunga na jeshi katika Uislaam ni suala la hiari[63] .
Swali : Basi inakuwa vipi kujiunga kwake na uandaaji wa jeshi?
Jawabu : Hakika dola au serikali ya kiislaam huandaa sehemu kubwa na mahala maalum nje ya miji, iliyo andaliwa kwa aina tofauti za silaha na kuwahiarisha watu kwenda kushiriki katika mazoezi ya kijeshi katika sehemu hizo katika nyakati zao za faragha kama siku ya Ijumaa na ziku zinginezo ambazo hawako kazini, bila ya kutofautisha kati ya yeyote atakae kushiriki, wakubwa kwa wadogo[64] .
Na kwa njia hii takriban watu wote hushiriki katika hufanya mazoezi na kuiondolea serikali matumizi ambayo inge yatoa kwa ajili ya jeshi, kama ambavyo wafanya kazi hubakia makazini na kwenye familia zao, kwa hivyo kila mtu hufanya mazoezi kila siku-kwa muda wa saa moja au masaa mawili, kwa mfano-kisha kurudi kwenye kazi yake na kubakia na familia yake. Na pindi adui anapo ivamia nchi au dola inakuwa ni wajibu kwa wote kupigana kwa kuutetea Uislaam na mwenye kupendezewa kulitumikia dola na serikali kwa hiari yake, hupangiwa mshahara maalum, ili abakie wakati wote na bila kusimama akiwa ni mhudumu wa dola la kiislaam.
Swali : Ni upi mtizamo wa kiislaam kuhusiana na vifaa vya kisasa vya kivita?
Jawabu : Mtazamo wa kiislaam ni kuwa niwajibu kutengeneza na kuwa na vifaa vitakavyo liwezesha dola au serikali ya kiislaam kujibu mashambulizi na kujilinda na kulinda heshima ya Uislaam na amani ya waislaam[65] na hilo linatokana na kauli yake Mwenyezi Mungu:
وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ ﴿٦٠﴾
Na waandalieni nguvu kwa kadri ya uwezo wenu[66]
Swali : Dola au serikali huwa na mipango gani kuhusiana na familia za wanajeshi wanao kufa vitani?
Jawabu : Ikiwa familia hiyo ni mafukara na wasio jiweza, hupewa kiwango cha kutosheleza mahitaji yao kulingana na hadhi yake na kama familia hiyo haikuwa hivyo, haipewi kitu isipokuwa ikiwa katika kuwapa chochote kuna maslaha na mfano wa hayo.
Swali : Ni upi msimamo wa Uislaam kuhusiana na amani na vita?
Jawabu : Uislaam ni dini ya amani na utulivu kama alivyo sema Mwenyezi Mungu alie tukaka:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً ﴿٢٠٨﴾
Enyi mlio amini ingieni kwenye Uislaam wote[67] .
Na Uislaam hufanya kazi ya kueneza amani na usalama uli mwenguni na huenda mbio kuzima chochoko ya vita na kuzima moto wake wenye kulindima na kung'oa mizizi ya chanzo chake kati ya watu, kwa kung'oa vyanzo na sababu zipelekeazo kutokea kwa vita na badala yake kuweka vyanzo vinavyo chochea mapenzi na kuelewana na vinavyo chochea kuwepo sulhu na utulivu na kuacha kabisa suala la vita na kuwa na utulivu hata kama adui atakuwa anafanya hadaa na kutoa wito wa kutaka kuwepo amani, amesema Mwenyezi Mungu alie takasika:
وَإِن جَنَحُوا لِلسَّلْمِ فَاجْنَحْ لَهَا ﴿٦١﴾
Na ikiwa wataelek ea na kumili kwenye amani basi nanyi elekeeni kwenye amani[68] .
Na wakati huo huo Uislaam unaharamisha mambo ya kutumia nguvu na vitisho na mauaji ya kuvizia au mauji ya kawaida na inapiga vita kila jambo lipelekealo kuwa na khofu na kuogopa na wasiwasi na kutokuwa na utulivu kati ya watu.
Swali : Je kuna uhuru katika Uislaam?
Jawabu : Ndio, tena uhuru ulio bora kabisa kati ya migawanyo ya uhuru, na ambao ulimwengu hauja wahi kuufikiria wala kuuotea katika utamaduni wa juu kabisa kati ya tamaduni za hapa ardhini.
Swali : Ni upi uhuru wa kiislaam?
Jawabu : Uhuru wa kiislaam ni wa aina nyingi, na hapa tutataja baadhi tu kati ya aina hizo za uhuru huo kama ifuatavyo:
1. Uhuru wa kufanya kazi na kufanya Biashara, kila mtu kati ya watu wa Umma wa kiislaam anayo haki ya kujichagulia kazi au shughuli aitakayo kuifanya kwa ajili ya uchuuzi au kuwa ndio chanzo cha mapato yake, kwa hivyo akichagua uwindaji ni juu yake, au kuchimba madini na ngawira zilizoko ardhini, au kukusanya mambo ya mubaha na kuyamiliki na mengineyo kati ya vyanzo halali vya uchuuzi, kama ambavyo ni ni haki ya mfanya biashara kuingiza nchini bidhaa azitakazo au kusafirisha nje ya nchi bidhaa azitakazo, au kununua na kuuza bidhaa azitakazo, katika upande huo kahakuna kizuizi kamwe, katika Uislaam hakuna ushuru (Tax) wala hakuna Leseni ya biashara wala sharti, ndio hushurutishwa bidhaa zisiwe za haramu-kama mvinyo - (vileo) na kusiwe na riba katika biashara hiyo au isiwe ni biashara ya haramu na mfanya biasha asifiche bidhaa wakati wa mahitaji kwa ajili ya kusubiri msimu ambao kutakuwa na uhaba wa bidhaa hizo na katika biasha hiyo kusiwe na madhara kwa watu na katika uchumi wao.
2. Uhuru katika kilimo na viwanda, kwa maana mwenye kutaka kujishughulisha na kilimo kiasi chochote cha ardhi akitakacho na kwa aina yoyote ile aitakayo, anayo haki ya kufanya hivyo na wala hakuna katika Uislaam kitu kiitwacho ( kilimo cha kisasa) mpango ulio ingizwa kutoka katika nchi zisizo za kiislaam, ndio ardhi hiyo ikiwa ni ardhi iliyo (kombolewa kwa nguvu) ni wajibu kwa mkulima kutoa malipo ya ukodishaji wa ardhi hiyo-kwa kiasi kidogo sana-na kuilipa serikali au dola na hiyo ndio iitwayo kwajina la (kodi) ya ardhi, na mkulima ikiwa ni fakiri ni wajibu kwa serikali kumkidhia haja yake kulingana na hadhi au hali yake na hakuna kizuizi cha mtu kulima kiasi chochote cha ardhi akitakacho kwa sharti kwamba asiwanyime wengine nafasi na fursa ya kulima na alime mazao yoyote ayatakayo isipokuwa yatakayo kuwa na madhara kama na serikali haina haki kuchukua mapato isipokuwa (Khumsi) na (Zaka) pamoja na kuchunga masharti yake kama tulivyo eleza hapo kabla, na vilevile viwanda vyote, viko huru- kwa maana kamili ya uhuru-isipokuwa katika vitu vilivyo haramu katika Uislaam kama viwanda vya pombe (Vileo) na madawa ya kulevya.
3. Uhuru wa ujenzi na uendelezaji wa ujenzi wa nchi na miji, mwenye kutaka kuiendeleza ardhi kwa namna yoyote ile iwayo, anayo haki ya kufanya hivyo, kwa hivyo basi mtu yeyote chini ya kivuli cha serikali ya kiislaam anayo haki ya kujitengea ardhi ya halali na kujenga akitakacho kwenye ardhi hiyo kama nyumba au sehemu ya kibiashara, au kiwanda, msikiti, Husainiyya, Madrasa, Dispensari, Hospitali, au mfano wa havyo kwa uhuru kamili na katika ujenzi na uendelezaji hakuna kabisa kitu kiitwacho Leseni na serikali au dola halina haki kuchukua chochote kwa mtu huyo walau senti moja kwa ajili ya ardhi au kinginecho, hakika Uislaam umeweka kanuni isemayo kuwa (Mwenye kuhuisha ardhi zilizo kufa yaani zilizo telekezwa basi ardhi hiyo ni milki yake)[25] isipokuwa ardhi hiyo ikiwa (imekombolewa kwa nguvu) wakati huo ni juu ya mwenye kuiendeleze ardhi hiyo kutoa malipo ya ukodishaji kwa serikali. Na ikiwa hukumu hii itatekelezwa katika ardhi na uendelezaji wa ardhi basi itakuwa inatosheleza kukidhi haja za watu katika suala la makazi, na kutoweka tatizo la makazi lililo enea katika nchi zote za kiislaam.
UHURU WA MTU KUISHI NA KUSAFIRI MAHALA APATAKAPO
4. Uhuru wa kusafiri na kuishi, yaani mwenye kutaka kuishi mahala fulani, au kusafiri mahali fulani anahiari ya kufanya hivyo bila sharti wala kikwazo, katika Uislaam hakuna mipaka ya mahala, wala vikwazo vya kijinsia wala ubaguzi wa kirangi, lugha na kwa uhuru huu suala la uraia na jinsia na suala la pasport za kusafiria huporomoka na mengine yote yanayo ambatana na hayo, kama ambavyo nchi nyingi za ulaya zilivyo andoa vitu hivyo na kupinga bidaa hii yenye kuwaudhi na kuwakera wananchi wake na nchi zao.
5. Uhuru wa kutoa huduma za kijamii au kuihudumia jamii na harakati za kisiasa bila kuwa na vikwazo,-isipokuwa harakati zilizo haramishwa na Uislaam nazo ni chache sana, kwa maana hiyo hakuna idara ya upelelezi kamwe, kwani haijuzu kumfanyia yeyote upelelezi au tajassusi, kwa hivyo katika Uislaam hakuna wizara ibebayo jina la Wizara ya upelelezi na mfano wa hayo, isipokuwa wizara ya kukusanya habari (Wizara ya habari) kwa ajili ya maslahi ya Umma na kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi na usalama wake, kwa hivyo katika dola la kiisalaam[26] kila mtu yuko huru kuandika na kubainisha ayatakayo na katika maneno yake na auandishi wake wa vitabu na yuko huru kuunda vikundi mbali mbali vya kijamii na jumuia na vikundi vya ushirika na vikundi vya kheri na kukusanya misaada mbali mbali na vitu vya kujitolea na kutoa au kuchapisha majarida mbali mabli na magazeti na kuanzisha redio na televisheni na visivyo kuwa hivyo.
6. Uhuru wa nashati zingine za mtu mmoja mmoja au za kijamii, kwa mfano: kila mtu mwenye kufahamu udreva, yuko huru kuendesha bila ya haja ya kumpatia leseni au mfano wake, kama ambavyo maiti hahitajii ruhusa ili aandaliwe na kuzikwa, bali ni juu ya jamaa zake kusimamia suala la kumuandaa na kumzika sehemu yoyote waitakayo au sehemu aliyo iusia yeye mwenyewe marehemu, bila ya haja ya kutoa kodi au Risiti au mfano wa hayo na hukumu ni hiyo hiyo katika mambo mengine.
Swali : Kutokana na mliyo yataja itapelekea kufungwa kwa ofisi na idara nyingi?
Jawabu : Ndio na hivyo ndivyo dola la kiislaam lilivyo kuwa, halikuwa na idara isipokuwa chache sana na kwa maana hiyo ndio maana tukasema-hapo kabla-ya kuwa wafanya kazi katika dol a au serikali ya kiislaam ni wachache sana, na ni wachache kupita kiasi na kwa sababu ya uchache wa wafanya kazi majukumu ya serikali na mzigo wa serikali na dola la kiislaam utapungua na wala muundo wa serikali au dola hauta beba mzigo wa matumizi mengi ya pesa (yaani dola halita tumia pesa nyingi katika bajeti yake).
Swali : Je katika Uislaam kuna hakimu na utoaji wa hukumu?
Jawabu : Ndio, katika Uislaam kuna aina nzuri sana ya utoaji hukumu na kuna mahakimu walio waadilifu zaidi.
Swali : Hakimu na utoaji wa hukumu huwa vipi katika Uislaam?
Jawabu : Katika Uislaam Hakim ni wajibu au ni lazima awe ni muumini na muadilifu, mwenye elimu ya utoaji hukumu na awe ni Mujtahidi katika mas'ala ya utoaji hukumu na katika hukumu zake na utoaji hukumu ni wajibu uwe kwa kutegemea dalili na viapo, bila kuwa na vikwazo katika mahakama wala kusiwe na mizunguko na bila ya kuwepo ufunguzi wa mafaili wala stakabadhi wala ulipaji wa malipo kamwe na hakuna haja ya kutanguliza ufunguaji wa faili la mashtaka na mfano wa hayo kama mafaili ya mashtaka yatumikayo katika zama hizi kwenye mahakama mbalimbali na katika utoaji wa hukumu. Na kwa ajili ya urahisishaji, uadilifu huu uliopo kwenye mahakama za kiislaam na kutoa egemea au kumili sehemu fulani kuliko shurutishwa kwa Hakimu katika Uislaam, Hakimu au Kaadhi mmoja anaweza kusikiliza madai ya pande zote mbili mshitaki na mshitakiwa na kutoa hukumu kwa haraka sana iwezekanavyo na hilo hufanyika juu ya vipimo na misingi ya Uislaam na ushahidi wa mashahidi walio waadilifu na kutokana na hali hiyo ndio maana Kaadhi mmoja alikuwa akihukumu mji mmoja wenye (Mamilioni) ya watu kiasi kwamba hakuna tatizo lolote libakialo linalo husiana na mambo ya mahakama au utoaji hukumu kamwe.
Swali : Hakimu hupata wapi riziki yake kwa kazi aifanyayo?
Jawbu : Hupata riziki yake kutoka kwenye Baytul mali.
Swali : Ni ipi kazi ya Kaadhi (Hakimu)?
Jawabu : Kadhi kwa kusaidiwa na wasaidizi wake hufanya kazi zifanywazo na ofisi au idara nyingi katika serikali tawala, katika zama hizi, hakika yeye husimamia mambo ya waqfu na kuwasimamia watumishi wa waqfu hizo na hukusanya mali ya watoto wadogo na kuiihifadhi ili baadae awape wenyewe pindi masharti yanapo kamilika na huizuia mali ya punguwani na kufungisha ndoa na kutoa au kusimamia suala la talaka na huuza na kununua na kuwekesha reheni na kukodisha na kutatua mizozo kati ya watu na kutekeleza hududi za kisheria kati yao na mengineyo[69] .
Swali : Je katika Uislaam kuna mfumo wa mawakili, kwa namna hii ijulikanayo katika mahakama za kisasa?
Jawabu : Katika Uislaam hakuna mfumo wa uwakili kwa namna hii iliyopo hivi sasa na wala Uislaam hauhitaji idadi hii kubwa ya mawakili, kwani mambo yote na hasa mambo ya mahakama na utoaji hukumu katika dola la kiislaam huendeshwa kwa njia nyepesi na kwa urahisi sana tena kwa amani na uaminifu.
Swali : Uislaam huwafanyisha nini au huwatumikisha vipi mawakili na wafanyakazi ambao dola la kiislaam haliwatambui kutokana na kazi zao, ikiwa utashika hatamu ya uongozi na kuendesha serikali?
Jawabu : Hakika Uislaam hauushutukizi umma au watu kwa mabadiliko au marekebisho ya ghafla bali katika kufanya mabadiliko na marekebisho huwa nao sambamba na kwa njia ya taratibu, kwanza kabisa wale ambao haizitambui kazi zao huwaandalia kazi zinazo wiana na hadhi au utaalamu wao au zinazo nasibiana nao, kisha kuwalipa kutoka kwenye hazina ya dola au serikali kiwango kitakacho weza kuwasaidia katika mambo yao ya kimaisha, mpaka ifikie kupata kazi ambazo wao wenyewe wanataka kuzifanya, je baada ya hatua hizi kuna yeyote kati ya wale ambao serikali haizitambui na kuzikiri kazi zao atakae chukua hatua yeye mwenyewe na kuitilia mgomo serikali ya kiislaam baada ya kuwa serikali ya kiislaa imemuandalia kazi inayo nasibiana na utaalamu wake au nafasi yake kati ya kazi zilizo huru na zenye manufaa na kumsaidia mpaka akawa na uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa fakhari na kwa raha mustarehe bila ya kukereka? Na vilevile Uislaam hufunga kabisa sehemu ziuzazo pombe kama Mabaa na majumba ya ufuska na mfano wa hayo pamoja na kutilia mkazo kwa kiwango kikubwa mambo ya maisha yao na kuanzisha vituo au kazi zinazo wiana na sehemu na hadhi zao kama kazi ambazo zitawafanya wapate riziki zao za halali na kuwazuwia kazi hizo kufanya matendo ya haramu.
SWALI : Je katika Uislaam kuna nidham na mfumo wa mambo ya kiafya?
Jawabu : Ndio na mfumo ulio bora kabisa kuliko mifumo na nidhamu iliyopo ya kinga na utibabu, na inamifumo iliyo makini zaidi na mipana na yenye kuhusika na nyanja zote, kwa mfano inayo mifumo inayo husu afya ya mwili, roho na afya ya mtu mmoja mmoja na jamii na mifumo ya usalama wa hali ya hewa anga na mazingira.
Swali : Mfumo wa kiislaa wa kiafya uko vipi?
Jawabu : Uislaam huweka jedwari kwa sura ya ujumla linalo husiana na afya ya ujumla kwa kuweka kanuni ya mambo matatu:
1. Kanuni ya kinga: Hakika kanuni hii hulinda na kumhifadhi mtu mmoja mmoja, Jamii na Mazingira ili yasienewe na maradhi ya kuambukiza au kuhamia kwa watu wengine na kinga hiyo hutimia kwa mambo yafuatayo:
A. Kuharamisha vitu ambavyo ni sababu ya kuzuka kwa maradhi na uambukizaji., kwa mfano: Pombe, madawa ya kulevya, uzinifu, kulawitiana, kusagana kati ya wanawake, mambo yenye madhara, miziki na mambo yasababishayo kero na Mabaa (sehemu za kuuza vileo) na madanguro (majumba ya ufuska) na vikao ambavyo watu hukaa uchi (yaani sehemu za shoo ambapo wanawake hukaa uchi) na mfano wa hayo.
B. Kwa kuweka kanuni ya mambo na adabu kumi za sunna zenye kumuelekea mtu mmoja mmoja na jamii, kama kanuni ya Usafi, Kuoga, Kutoa damu kwa ajili ya kusafisha mwili (Hijaama) na kutoa damu katika baadhi ya mishipa kwa kuchanja (Al-fasdi), kufunga, Kujipaka mafuta, Kuoa, kutumia tiba ya kunusa dawa, kutumia wanja, na kutumia (Nura) dawa ya asili kwa kujisafishia, namna ya kula na kunywa na namna ya kuvaa, sehemu ya kuishi, kulala, kuamka, na mengiyo.
2. Tiba: Na hutimu hilo kwa kuelekeza baadhi ya madawa ya miti shamba na vyakula vyenye manufaa na vinavyo saidia katika kutibu magonjwa na yote hayo hufanyika kwa njia ya kawaida na nyepesi na njia hii japokuwa haienei na kuyahusu magonjwa yote, isipokuwa ukweli ni kuwa hufukuza marahi na hasa yanapo kuwa yana anza, kama ilivyo elezwa katika kitabu (Twibbun-nabiiy)(s.a.w.w) na katika kitabu (Twibbul-aimmah)(a.s) na mfano wa hayo.
3. Kuchukua tahadhari: Hakika Uislaam huchukua tahadhari na kulinda suala la usafi wa mazingira na hufuatilia suala la usafi wa mazingira kutokana na kuchafuliwa na hufuatilia kwa makini afya ya kila mtu na kumlinda asipatwe na magonjwa ya kuambukiza, kama ambavyo huwachunga matabibu na madaktari kwa makini kabisa na kuwajaza ndani ya nyoyo zao hali ya kiutu na dhamira safi na khofu ya Mwenyezi Mungu na kuwaadhibu pindi wanapo kiuka maadili, kwani utakuwa imefikia kuweka kanuni isemayo (Tabibu au Daktari ni mwenye dhamana hata kama ni hodari na mwenye uhakika na kazi yake) kitu ambacho humfunga na kumtia dhamana Daktari asiweze kupuuzia katika kumuangalia mgonjwa au kupuuzia katika kutoa matibabu, au kuto sema ukweli, bali kanuni hiyo inamfanya awe na hali ya umakini na umadhubuti wa hali ya juu kabisa na tahadhari kubwa na mwenye kujichunga sana katika kumuandikia mgonjwa dawa na katika kuyafanyia uchunguzi maradhi na kuyatibu kwake maradhi hayo.
Swali : Je si kweli kwamba tiba ya kisasa imepata maendeleo makubwa na yenye kushuhudiwa ulimwenguni?
Jawabu : Hakuna shaka yoyote juu ya maendeleo yaliyo patikana katika tiba ya kisasa lakini ile misingi ambayo tumeitaja na ambayo ndio nguzo na vizingiti vya msingi na sababu za kiafya na swiha, misingi hiyo imevunjwa na kubomolewa, kwa maana hiyo ndio maana tunakuta kwamba maradhi yamekuwa yakiwashambulia wanadamu kwa njia za ajabu sana na kwa sura ya kushangaza, hata imefikia wingi wote huu wa madaktari na maduka ya madawa na mahospitali na mfano wa hivyo, havitoshelezi kurejesha hali nzuri ya kiafya duniani kwa sura ya ujumla. Na kwa msingi huo bado tuna wakumbuka mababu zetu na mababa zetu ambao-kwa kuchunga na kulinda kwao nidhamu ya kiislaam katika mambo ya kiafya-wakiishi raha mustarehe na wakiwa na afya kamili na swiha nzuri na wakiwa na nguvu zao timamu mpaka wanapo fikia hatua ya kufariki, wakati ambapo tunaona katika zama zetu hizi ya kuwa kila nyumba haikosi kuwa na mgonjwa au maradhi na watu wengi utakuta kuwa wamekumbwa na ugonjwa au magonjwa ya aina tofauti.
Swali : Sasa ni ipi njia ya kurekebisha na kutibu hali hii?
Jawabu : Njia ya kurekebisha na kutibu hali hii ni kufanya kila njia na kwenda mbio kurudisha ile mipango na ratiba na kanuni za ujumla za kiafya zilizomo katika Uislaam na kuzifanyisha kazi au kuzitekeleza katika jamii zetu na kuchukua tiba ya kisasa yenye manufaa na mambo mapya yaliyo gunduliwa katika tiba ya kisasa na kutoa mambo ya haramu na mambo yenye madhara katika tiba hiyo na kufungua njia na milango ya kufaidika na tiba ya miti shamba au tiba ya kizamani (kama waiitavyo wataalamu wa kisasa) na ambayo ni mujarrabu, ili zichanganyike tiba hizo mbili tiba ya zamani (yaani ya miti shamba) na tiba ya kisasa na kwa kufanya hivyo wanadamu na viumbe waweze kuokoka na kuepukana na maraadhi au magonjwa pia mabalaa na majanga ya kibina damu chini ya kigezo cha maradhi ya kushutukiza na kuua kwa ghafla.
9
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
Swali : Je katika Uislaam kuna mifumo ya tamaduni za aina mbamlimbli?
Jawabu : Ndio, katika Uislaam kuna mifumo iliyo bora kabisa ya kitamaduni.
SWALI: Ni ipi mifumo hiyo?
JAWABU: Hakika Uislaam umefaradhisha na kuwajibisha suala la kutafuta elimu kwa mwanamke na mwanamume na ukaitambulisha elimu ambayo ni wajibu kwa watu kuitafuta katika makundi matatu:
1. Elimu ya Usulud-dini (Misingi ya dini) na elimu ya Furuud-dini na elimu ya Akhkaq (maadili) na adabu za kiisalaam na ikahimizwa kutafuta elimu zingine, na ikakuhesabu kufanya hivyo kuwa ni fadhila kwa mwanadamu na sharafu kubwa kwake, na ukahimiza na kusisitiza kuitekeleza elimu hiyo kwa matendo na kuandaa nyenzo na ukailazimisha serikali kutoa usaidizi katika utekelezaji wa yoye hayo.
Swali : Hakika yote mliyo yataja yanawalazimisha wawe na maendeleo na wawe wamefikia hatua ya juu kabisa katika maendeleo, sasa kwa nini wamekuwa nyuma kimaendeleo?
Jawabu : Hakika Waislam wamechelewa na kuto endelea tangu wakati ambapo Uislaam ulipo achwa kutekelezwa ulimwenguni na tangu walipo acha na kuuweka kando mfumo wa kiisalaam katika mambo ya kiutamaduni, ama wakati walipo kuwa wameshika hatamu ya utamaduni wa kiislam na wenye kuutekeleza Uislaam, hakika wakati huo utamaduni wao uliupituka utamaduni wa kimagharibi wa hivi leo na hakuna dalili bora kabisa ya hilo kuliko wamagharibi kukiri wao wenyewe juu ya suala hilo, kwa mfano ukiangalia kiwango cha vitabu vyao maktaba zao shule zao na wataalamu wao, pamoja na ukiangali nyenzo walizo kuwa wakizitumia katika zama hizo, ni vingi sana ukilinganisha na vitabu, maktaba, shule, na wataalamu katika zama hizi pamoja na kuwa kuna maendelea katika nyenzo na sababu za kuyatekeleza hayo.
Swali : Ni upi msimamo wa kiisalaam kuhusiana na vyombo vya kisasa vya kuwaelimisha watu na kwa ibara nyingine: je Uislaam unaharamisha mashule, vyuo, Magazeti, majarida, televitioni, Redio, Sinema, na Satalaiti, Internet na mfano wa hayo?
Jawabu : Hakika Uislaam husisitiza na kuhimiza kila kinacho saidia au kuchangia kwa njia moja au nyingine kuwaelimisha watu na kueneza tamaduni za kibinadamu katika Umma, ndio, hakika Uislaam unaharamisha ufisadi na vyombo vyenye kusababisha uharibifu kati ya nyenzo hizi za kisasa, kwa hivyo ikiwa vitasafishwa na kuepukana na ufisadi basi Uislaam uko msitari wa mbele kabisa katika kuvikubali na kuzipokea nyenzo hizo.
Swali : Ni ipi tofauti ya ujulma kati ya mfumo wa kiisalam wa kitamaduni na kati ya mfumo wa kitamaduni wa kimagharibi katika siku hizi?
Jawabu : Tofauti ya msingi ni kuwa: Uislaam umechanganya kati ya elimu na imani na utamaduni na Maadili na fadhila (ubora), wakati ambapo utamaduni wa kimagharibi kwa hivi leo hauna kitu kiitwacho imani, maadili na fadhila, na kwa kufuatia suala hilo elimu mbayo ndio wasila na nyenzo bora kabisa ya kukuza utamaduni na kuleta maendeleo vitu ambavyo ndio nyenzo yenye nguvu zaidi ya kuleta maelewano na kufahamiana na amani na usalama katika umma, bali katika ulimwengu wote imekuwa ndio nyenzo ya kuwafanya watu wamomonyoke kimaadili na kutengana na kimekuwa chombo cha kusabibisha khofu, fazaa, fujo na kutokuwa na utulivu na vita na uharibifu katika umma, bali katika ulimwengu wote.
Swali : Je Uislaam ni dini ya vita, au ni dini ya amani?
Jawabu : Uislaam ni dini ya amani, Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً... ﴿٢٠٨﴾
Enyi mlio amini ingieni katika Uislaam wote[70] .
Ama ikiwa mtu mmoja atamshambulia mtu fulani, au akaanzisha vita na kuwapiga vita Waislaam, wakati huo Uisla am haukai kimia na kusimama ukiwa una agaalia tu bila kufanya chochote, bali unajibu mashambulizi na kujitetea kwa ajili ya kuhakikisha uadilifu unapatikana na ukweli unakuwepo na kuzuwia uadui na kuondoa dhuluma itakayo kuwa ikifanywa.
Swali : Uislaam unaihami vipi amani?
Jawabu : Uislaam unaona ya kuwa kuna wajibu wa kuenea na kutawala Amani ndani ya nchi na nje ya nchi, ama kuhusiana na ndani ya nchi huzuia kufanyika kwa maovu na nje ya nchi haifanyi uchokozi kwa nchi yeyote au mtu yeyote na hutoa kipigo kwa wale wachokozi na wenye kuvuka mipaka ya nchi.
Swali : Uislaam unapinga vipi maovu?
Jawabu : Uislaam unapinga maovu na maasi kuanzia kwenye mizizi yake na kutibu sababu zake, kwani sababu za maovu ni kama zifuatazo: Ufukura, Mambo yasabaishayo ufisadi, Ujinga, Uadui, Matatizo, na mfano wa hayo na Uislaam unayapiga vita mpaka uhakikishe umeyaondoa kabisa, na mambo hayo yanapo toweka, maovu yatapungua yenyewe. Kwa hivyo basi kutokana na ubora wa mifumo ya Uiislaam iliyo madhubuti na mipango yake iliyo salama, inauwezo wa kutokomeza ufukara na kuwatajirisha mafukara au kuwafanya wasiwe wahitaji na kuwajulisha watu madhara ya ufisadi wa kijinsia na ufisadi wa kunywa pombe, kwa kupambika na tabia ya kanaa'a (kutosheka na unacho kipata) hujizuia na mambo ya kifahari na kunywa pombe na kueneza elimu na utamaduni na kuteketeza kabisa sababu za uadui na chuki na kutatua matatizo kwa njia nyepesi na utoaji hukumu wa haraka, kwa kufanya hivyo unaweza kung'oa mizizi ya maovu na kupandikiza mbegu za mapenzi na maelewano na umoja na amani kati ya umma na katika ulimwengu wote.
Swali : Anae fanya uhalifu katika Uislaam huadhibiwa vipi?
Jawabu : Hakika Uislaam - baada ya kuandaa mazingira mazuri na kuteketeza sababu za uhalifu katika jamii - wakati huo inaweka adhabu kwa mhalifu na mwenye kufanya maovu, kwa sababu atakuwa amefanya maovu na uhalifu huo kutokana na uchafu wake mwenyewe wa kimaadili na kupotoka kwake kimaadili na kutokana na upotovu wake na uadui wake kwa jamii yake na wananchi wenzake ambao ni waaminifu, hakika muhalifu wakati huo atakuwa ameitia doa na kuharibu sifa ya jamii yake na kuvunja Usalama na Amani ya jamii na anakuwa amewapora utulivu wao kwa hiyo huadhibiwa kwa adhabu kali, na adhabu hiyo hutekelezwa kwa haraka sana, na Uislaam wakati huo hulisafisha anga ili matendo maovu kama hayo yasiweze kukaririka katika jamii.
Kutokana na haya inabainika wazi kabisa kuwa Uislaam hauruhusu kutekeleza kanuni za kuwajazi wahalifu peke yake na kuzitekeleza bila ya hukumu zingine, kama ilivyo zoeleka katika zama hizi katika baadhi ya nchi za kiisalaam, na Uislaam huliona kuwa tendo kama hilo lenyewe ni uhalifu dhidi ya Uislaam, kwa sababu ndani yake kuna udhalilishaji wa Uislaam wenyewe na heshima yake na heba yake na kushikamana na tuhuma na sababu za kuwa Uislaam ni dini ya nguvu na ugumu kwa wananchi si dini yenye huruma na iliyo laini katika hukumu zake.
Swali : Uislaam huzifanyia nini jela?
Jawabu : Hakika Uislaam unaona ya kuwa kanuni zilizo wekwa na wanadamu na zitumikazo kwenye nchi mbali mbali hazina maana na kima chochote kamwe bali kanuni iliyo bora na yenye maana ni kanuni iliyo telemka kutoka mbinguni au kanuni ya Mwenyezi Mungu tu na kwa msingi huu makosa mengi na uhalifu mwingi wa kikanuni katika zama hizi si makosa wala uhalifu katika mtizamo wa kiisalaam, mpaka ifikie hatua ya kumtia jela mwenye kukiuka kanuni hizo, ama uhalifu na makosa yanayo zingatiwa na Uislaam kuwa ni makosa na ni uhalifu, kama Wizi, Uzinifu, Uislaam umekwisha ainisha na kubainisha adhabu kali na ya haraka dhidi ya makosa hayo na si kufungwa jela, ndio kuna makosa na uhalifu mdogo ambao Uislaam umeyawekea adhabu ya kukaa jela-kama mtu mwenye uweze (tajili) anae zembea na hataki kulipa deni lake-na Jela katika Uislaam ni ibara ya kuwa Kaadhi wa kiislaam humkabidhi muovu na mhalifu anae stahili kukaa jela kwa mtu fulani ili amzuwie na kumfungia katika chumba cha nyumba yake-kwa mfano-na kwa maana hiyo katika Uislaam hakuna jela kwa maana na mafhumu yajulikanayo katika zama hizi na yaliyo enea katika nchi za kiislaam kamwe na unapo lazimika kujenga jela, ujenzi huo unakuwa ni ujenzi wa jela ya kawaida, (si kama jela tuzionazo katika nchi za kimagharibi), kwa hakika jela hizo zina kuwa ni shule za malezi kwa wahalifu na sehemu ya kuwaelimisha kwa kuwafundisha tamaduni na elimu za kibinadamu zilizo sahihi.
Swali : Uislaam unaweza vipi kuhifadhi na kulinda amani nje ya dola la kiisilaam na kwa watu wote?
Jawabu : Hakika Uislaam haufanyi uchokozi kwa yeyote kamwe na wala hauvuki mipaka na kufanya uadui na uchokozi kwa dola au nchi yoyote, na dola lolote au nchi yoyote inapo taka Amani kati yake na dola la kiislaam, Uislaam nao humili kwenye amani hiyo, Mwenyezi Mungu alie takasika amesema:
وَإِن جَنَحُوا لِلسَّلْمِ فَاجْنَحْ لَهَا ﴿٦١﴾
Na ikiwa watamili kwenye Amani basi nayi elekeni kwanye amani hoyo[71] .
Na dola la kiislaam linapo fanyiwa uchokozi na kushambuliwa, Uislaam unasimama na kujitetea na kuutetea umma kwa sura iliyo bora kabisa ambayo historia haija wahi kuona mfano wake, na dola lolote linapo fanya uchokozi juu ya dola la kiislaam au nchi ya kiisalaam, Uislaam hutoa majibu ya uadui huo kwa kiwango kidogo iwezekanavyo na kukomea kwenye mipaka yake (na si kuvuka mipaka katika kujibu mashambulizi).
Swali : Uislaam unahifadhi vipi Amani na Usalama serikalini na kati ya watu?
Jawabu : Hakika utawala au serikali ya-kiisalaam-ni serikali ya wananchi kwa maana sahihi ya neno hilo, watu au wananchi wanataka nini tofauti na kushiriki katika kuchangia rai serikalini, na utajiri, Elimu, Uhuru, Amani, Afya, na fadhila za kimaadili, vitu ambavyo Uislaam unafanya kila mbinu kuhakikisha vitu hivyo vinawafikia wananchi na vinakuwepo tena kwa njia iliyo bora? Na kutokana na sababu hiyo ndio maana tunaona ya kuwa serikali sahihi na utawala safi katika Uislaam ulikuwa ukidumu kwa muda mrefu sana na hilo lilitokana na mapenzi yaliyo kuwepo kati ya wanacnhi na serikali au utawala wao na Raisi (kiongozi wa juu serikalini) hakuna siku yoyote ambayo alikuwa akihitajia (Amani) (Ulinzi) (upelelezi) na mfano wa hayo, mpaka ahitaji watu wa kumlinda na kumuwekea watu wa kumuhami kutokana na watu.
Swali : Ni upi mtazamo wa kiisalaam kuhusiana na Familia?
Jawabu : Mtazamo wa Uislaam kuhusiana na familia-baada ya kumuangalia mtu mmoja mmoja-ni kuwa familia ndio msingi wa kwanza au tofali la kwanza la msingi katika kujenga jemii njema kwa hivyo Uislaam unakwenda mbio kuhakikisha familia zina kuwa ni familia njema ili jamii iwe njema na nzuri (kwani usafi wa familia ndio sababu ya usafi wa jamii) na kutokana na manti hii tunaona kuwa Uislaam unafaradhisha (kuvaa hijab) kwa mwanamke, Mwenyezi Mungu amesema:
وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ﴿٥٣﴾
Na mnapo wauliza au mnapo waomba mahitaji basi waombeni kwa nyuma ya pazia[72] .
Na kwa kufanya hivyo mat atizo na mabalaa yanapungua na mahusiano ya mume na mkewe na mke na mumewe yanashika kasi na kuimarika, na hapo familia inakuwa na utulivu na kuishi kwenye anga tulivu na safi, familia yenye kugubikwa na mapenzi na maelewano na utulivu, ikijua ya kuwa Hijab ni: Mwanamke kuto dhihirisha nywele na viungo vyenye kusababisha fitina.
Swali : Je Uislaam unaharamisha kwa mwanamke kujielimisha na kufanya kazi?
Jawabu : Hapana, hakika Uislaam haukuharamisha kamwe kwa mwanamke kujielimsha na kufanya kazi, bali Uislaam wakati mwingine umefaradhisha kwa mwanamke kujielimisha na kufanya kazi na kuvifanya kuwa suna au kuvihimiza kwake wakati mwingine, isipokuwa ilicho kiharamisha Uislaam ni utokaji usio wa kisheria katika nyumba kutojipamba na kujifukizia manukato na na kuonyesha au kudhihirisha mapambo kwa watu wa nje na kuto jisitiri (yaani kutembea bila sitara ya kisheria) kama ambavyo umeharamisha kwa mwanamke kufanya matendo yanayo pingana na sitara yake (iffa) na heba yake.
Swali : Ni ipi rai au mtazamo wa Uislaam kuhusiana na mwanamke?Jawabu : Uislaam ni Dini yenye huruma sana na hii ni itikadi ambayo imefahamika kwayo Uislaam katika historian na kuitekeleza katika sehemu mbali mbali, ama kuhusiana na mwanamke Uislaam unaona kuwa maisha ya familia hayatimii na kukamilika isipokuwa kwa kuhangaika na kutaabika nje ya nyumba na kuhangaika kwa ajili ya makazi na kufanya kazi ndani ya nyumba, na hapo Uislaam ukagawanya majukumu ya maisha kati ya wawili wenye kuoana kutokana na misingi ya mapenzi na kusaidizana kati yao, mwanamume: ikampatia majukumu ya nje ya nyumba na mwanamke: ukampatia majukumu ya ndani ya nyumba.
Bali kazi za ndani ya nyumba na utulivu wa ndani ya nyumba majukumu hayo iliyafanya kuwa ni ya mwanamke, kwani mwanamke ndie bora zaidi kuliko mwanamume katika kuendesha mambo ya ndani ya nyumba na hasa katika masuala ya malezi ya watoto kuwalea malezi yaliyo mema na yenye manufaa, mwanamke ni mahala bora kabisa pa malezi na uangalizi na ukuzaji wa kimwili na kiakili na mwenye upole kwa watoto, na Uislaam wenye kusifika kwa sifa ya hekima, umeona ya kuwa lau kama mwanamke ange chukua jukumu la kufanya kazi za mwanamume nje ya nyumba, wakati huo hapana budi azitelekeze kazi zake za nyumbani kwa wanaume na katika kufanya hivyo kuna upoteaji wa nguvu mbili, nguvu ya mwanamke ya huruma na nguvu ya mwanamume ya kufanya kazi, kazi ni ile ile, isipokuwa ni kuwa imegeuzwa na kupinduliwa na hali ikiwa hivyo, katika hali kama hii kwa hakika kutajitokeza au kutatokea natija isiyo ridhiwa wala kuridhisha, kwa hivyo ikapendekeza kuwa mwanamke afanye kazi za ndani ya nyumba na mwanamume ikampatia jukumu la kazi za nje ya nyumba na ambazo ni ngumu[73] .
Swali : Ni ipi rai au mtazamo wa kiisalaam kuhusiana na ndoa?
Jawabu : Uislaam unaona kwamba inajuzu na inafaa kuoa na inatilia mkazo na kusisitiza kufanya hivyo na ina amrisha kuoa na inahimiza kupendekeza jambo la kuoa mapema na uoaji huo ufanyike wakati kila mmoja kati ya mwanamke na mwanamume wamekamilisha miaka ifuatayo, Mwanamke kutimiza miaka tisa (9) pamoja na kufikia ukubwa (kiasi kwamba anakuwa na uwezo wa kuendesha mambo yake) na mwanamume kukamilisha miaka kumi na tano (15), pamoja na kuwa na uwezo wa kuendesha mambo yake pia, na unapo fika wakati huo Uislaam unatilia mkazo kuoa, ili maovu na ufisadi usiweze kutokea.
Swali : Ni upi mtazamo wa kiisalaam kuhusiana na mchanganyiko wa mabinti na wavulana (yaani watoto wa kike na kiume), katika tabaka tofauti za uhai wao?
Jawabu : Mchanganyiko wa mabinti na wavulana kwa mtazamo wa kiisalaam - Uislaam ambao unatilia hima kubwa juu ya usalawa wa jamii na saada ya jamii-mchanganyiko huo haufai kamwe, sawa iwe sehemu za kuogelea, mashuleni, au kwenye sinema, au sehemu za kazi, au kwenye mikusanyiko mbalimbali, au kwenye makongamano, au kwenye sehemu zingine, na Uislaam unaona kuwa mchanganyiko huo unasabaisha ufisadi, wakati ambapo ni wajibu kuilinda jamii na ufisadi huo, isipokuwa utakapokuwa mchanganyiko huo una usalama kamili na ulinzi makini na huku kukiwa na hijabu, itara na kutokuwepo uwezekano wa kutokea maovu kwa kuchanganyika kwao kama kuchanganyika katika hijja na sehemu takatifu na mfano wa hizo.
Swali : Kwa mtazamo wa kiislaam ni yapi majukumu ya mke na mume katika maisha ya kifamilia?
Jawabu : Kwa mtazamo wa kiislaam ni juu ya mume suala la matumizi yote ya mwanamke na kumtosheleza mwanamke matakwa yake ya kimwili-kama ilivyo pangwa katika sheria-na ni juu ya mke kumtii mumewe katika suala la kutoka nyumbani na katika kustarehe, ama mambo ya ndani ya nyumba si wajibu juu ya mke bali Uislaam unapendekeza kwa mwanamke kufanya hivyo, kwa ajili ya kulinda hali ya kusaidiana na mapenzi kati yao wawili, kisha ni kwamba Uislaam umeifanya nikah (Ndoa) kuwa haifungiki isipokuwa kwa maridhio ya wote wawili na-Umeiweka talaka-kwa ajili ya maslaha ya kijamii-kuwa ni haki ya mume pekee, isipokuwa ikiwa katika kufunga ndoa watawekeana sharti kuwa talaka iwe ni haki ya mwanamke pia.
Swali : Ni ipi rai ya Uislaam kuhusiana na kuoa wanawake zaidi ya mmoja?
Jawabu : Uislaam unaona kuwa inajuzu na inafaa kuoa wanawake zaidi ya mmoja hadi kufikia wanawake wane kwa ndoa ya daima lakini kwa sharti kuwa kuwe na ufanyike uadilifu kati yao na kwa hukumu hii Uislaam ukawa umetatua tatizo la wanawake wasio olewa na wajane, kwa sababu imekuwa maarufu katika jamii mbali mabli na ni jambo lenye kufanyika pia na limethibiti kwa kufanya sensa kuwa wanawake ni wengi zaidi kuliko wanaume, kwa hivyo basi ikiwa hakukuwekwa ufumbuzi wa kiwango kilicho zidi itakuwa maana yake ni kwamba wanawake wengi watabakia bila kuolewa na bila ya waume.
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
YALIYOMO
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO 1
AYATULLAHIL- UDHMAA SAYYID SWAADIQ AL-HUSAINIY SHIRAZIY 1
HUKUMU ZA KIISLAAM PAMOJA NA USUULUD-DIN- FURUUD-DIN- UBORA WA QUR'ANI TUKUFU- MFUMO WA UTAWALA KATIKA UISLAAM- MAMBO YA WAJIBU- HARAAM- MAADILI NA MAS'ALA MAPYA 1
KWA MUJIBU WA FAT'WA ZA AYATULLAHIL- UDHMAA SAYYID SWAADIQ AL-HUSAINIY SHIRAZIY (Mungu amzidishie uhai) 1
UTANGULIZI 1
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO 3
AYATULLAHIL- UDHMAA SAYYID SWAADIQ AL-HUSAINIY SHIRAZIY 3
KIFUNGU CHA KWANZA 3
USULUD-DIN (MISINGI YA DINI) 3
1. TAWHIID (Kumpwekesha Mwenyezi Mungu) 3
MWENYEZI MUNGU MTUKUFU NA SIFA ZAKE NJEMA 3
MWENYEZI MUNGU AMETAKASIKA NA SIFA MBAYA 4
MWENYEZI MUNGU ALIE TAKASIKA NA KUTUKUKA AMEEPUKIKA NA SIFA ZA UPUNGUFU 4
2. UADILIFU WA ALLAH 4
3. UTUME 5
MTUME WA MWISHO (s.a.w.w) 7
KUPEWA UTUME KWA MTUKUFU MTUME (s.a.w.w) 7
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO 9
KUFARIKI KWAKE KWENYE KUSIKITISHA NA KUHUZUNISHA 9
UIMAM 10
BINTI WA MTUME FATIMA ZAHRAA(a.s) 11
IMAMA WA KWANZA IMAM AMIRUL MUUMINIIN (a.s) 12
IMAM WA PILI: IMAM MUJTABA (a.s) 14
IMAM WA TATU: IMAM SHAHIID (a.s) 15
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO 17
IMAM WA NNE: IMAMA SAJJAD (a.s) 17
IMAM WA TANO: IMAM BAAQIR (a.s) 18
IMAM WA SITA: IMAM SWAADIQ (a.s) 19
IMAM WA SABA: IMAM KAADHIM (a.s) 20
IMAM WA NANE: IMAM RIDHAA(a.s) 21
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO 23
IMAM WA TISA: IMAM JAWAAD(a.s) 23
IMAMA WA KUMI: IMAM AL-HADIY(a.s) 23
IMAM WA KUMI NA MOJA: IMAM ASKARIY(a.s) 24
IMAM WA KUMI NA MBILI: IMAM AL-MUNTADHAR(a.s) (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake) 25
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO 27
MAREJEO YA KIAMA 27
SEHEMU YA PILI MATAWI YA DINI 28
JAMII NA DOLA (NIDHAM) LA KIISLAAM 29
UISLAAM NA SIASA 30
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO 32
AINA YA UTAWALA NA NAMNA YA KUTAWALA 32
MAJUKUMU YA UTAWALA WA KIISALAAM 33
UCHUMI WA KIISLAAM 33
VYANZO VYA MAPATO KATIKA UISLAAM 34
BAYTUL- MAALI YA WAISLAAM (HAZINA YA WAISLAM) 34
UCHACHE WA WIZARA NA WAFANYA KAZI 35
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO 36
DHAMANA YA KIJAMII KATIKA UISLAAM 36
MIFANO YA DHAMANA YA KIJAMII YA KIISLAAM 36
MFANO WA KWANZA 37
MFANO WA PILI 37
MFANO WA TATU 37
MFANO WA NNE 38
MFANO WA TANO 39
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO 40
UISLAAM NA JESHI 40
VIFAA VYA KIVITA 40
UHURU KATIKA UISLAAM 41
UHURU WA BIASHARA NA UCHUUZI 41
UHURU WA VIWANDA NA UKULIMA 42
UHURU WA UJENZI NA UENDELEZAJI WA MIJI 42
UHURU WA MTU KUISHI NA KUSAFIRI MAHALA APATAKAPO 42
UHURU WA NASHATI ZA KIJAMII NA KISIASA 43
UHURU WA HARAKATI NA NASHATI ZINGINEZO 43
UTOAJI WA HUKUMU NDANI YA UISLAAM 43
UWAKILI KATIKA UISLAAM 44
SWIHHA NA AFYA KATIKA UISLAAM 45
UISLAAM NA TIBA YA KISASA 46
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO 47
UTAMADUNI WA KIISLAAM 47
NYENZO ZA KISASA ZA KUELIMISHA WATU 47
AMANI KATIKA UISLAAM 48
UFUATILIAJI WA WAHALIFU NA KUWAADHIBU 48
ADHABU YA KIFUNGO JELA 49
AMANI KWA WOTE 49
UISLAAM NA FAMILIA 50
RAI YA UISLAAM KUHUSIANA NA MWANAMKE 51
NDOA KATIKA MTAZAMO WA KIISALAAM 51
SHARTI YA KUCHAPA 52
MWISHO WA KITABU 53
YALIYOMO 54
[1] . Pamoja na haya ukiongezea mambo mengine mengi yaliyo tajwa kama ufukara Magonjwa na mfano wa hayo yanatokana na matumizi mabaya ya mwanadamu mwenyewe na kuto pangilia vema au kuto weka mipango mizuri. Zingatia katika hilo.
[2] . Buharul-anwaar: juzu ya 61/ 117 malango wa 2/ chapa ya Bairut.
[3] . Suratu Aalimraan aya 85.
[4] . Kwa ajili ya ufafanuzi zaidi rejea kitabu (Waliawwali marrat fii tariikhil- Adam, juzu ya 1-2 na kitabu (Baaqatun Atwiratun fii Ahwalil khatamin-nabiyyiin) na (Swiraatul fawaha) pia (Mohammad (s.a.w.w) wal-qur'an) kilicho andikwa na ayatullahil- udhmaa Sayyid Mohammad Al-husseiny shiraziy (mwenyezi Mungu amtakase).
[5] . Yaani alie muadilifu kwa asilimia Fulani ukimlimganisha na mwingine.
[6] . Suratul-alaq aya 1-2.
[7] . Al- manaaqib juzu ya 1/ 56, sehemu isemayo Katika mahali alipo kutana na makafiri katika kitabu chake.
[8] . Kashful-ghumma: juzu ya 2/ 537, sehemu ya 4/ mlango wa 5.
[9] . Suratul maidah aya ya 3.
[10] . Suratu fuswilat aya 42/.
[11] . Na inawezekana kuifafanua kwa kutoa mfano ufuatao: nao ni kwamba nchi ya Iraq na Japan baada ya vita vya pili vya dunia, nchi hizi mbili zilikuwa katika msitari mmoja wa uharibifu na ubomozi na kurudi nyuma kimaendeleo, na kuto songa mbele kimaendeleo, lakini Japan baada ya muda kadhaa iliweza kuwa sawa bali kuzipita kwa kiwango kikubwa nchi na madola makubwa ya magharibi katika fani mbali mbali na katika viwanda, maendeleo na kushamiri kwake, wakati ambapo Iraq ilibakia ikiwa ni yenye kuharibika na kurudi nyuma kimaendeleo ikiwa masikini mwenye kuhitaji, ikiingiza kila kitu kutoka nje ya nchi hata ngano na nyama na hata nyuzi za kushonea na sindano, na wataalam pia wachambuzi wa mambo walio toa sababu na illa ya tofauti kati ya nchi mbili hizo ya kuwa viongozi wan chi ya Japan walikuwa ni wenye uwezo wa kuongoza na viongozi walio iongoza Iraq hawakuwa na uwezo wa kustahili kuongoza, haya ni katika upande wa kimadda, ama kwa upande wa kimaanawia pia ni jambo lililo wazi, kwa hivyo katika hadithi tukufu isemayo: (asie kuwa na maisha hana marejeo) inamaanisha kuwa: Ufukara wa duniani ni hasara katika Akhera, ukionhezea na mengine yaliyo pokelewa kutoka kwa Fatuma Zahraa (a.s) ya kuwa amesema: Lau kama wasinge upora ukhalifa, dunia wa watu ing kuwa njema na yenye neema na Akhera yao pia na kusinge kuwa na tofauti tofauti kati ya watu wawili.
[12] . Kwa ajili ya ufafanuzi zaidi rejea kitabu: Min mawsuuatul- fiqhil-kitab (Assiyaasah) siasa na (Al-iqtiswaad) uchumi (Al-ijtimaau) jamii na (Al-idaratu) idara (uendeshaji wa mambo) (Al-hukumu) utawala katika uislaam, na (Al-hurriyatu) uhuru, na kitabu (Idha qaamal islaam fil-iraq) na (Sabilun ilaa inhaadhil muslimiin) na ( As-swiyaaghatul jadiidah) na (Mumaarasatu-taghyiir) na cha marehemu Ayatullahil udhmaa Sayyid Mohammad Shiraziy (Mwenyezi Mungu autakase utajo wake).
[13] . Inasemekana ya kuwa kufariki kwake ilikuwa ni baada ya siku 75 tanfu kufariki kwa Mtume (s.a.w.w) na inasemekana ilikuwa ni baada ya siku 95 tangu kufariki kwa Mtume (s.a.w.w).
[14] . Rejea kwenye kitabu: ( Fatwimatuz-zahraa fil qur'ani) cha Ayatullahil udhmaa Sayyid Swaadiq Shiraziy (Mwnyezi Mungu amhifadhi).
[15] . Rejea kitabu Ihtijaaj ukurasa 354, mahojiano ya Abi Abdillahi (a.s) na katika majadiliano hayo kuna maneno yafuatayo: ya kuwa Mtume (s.a.w.w) alimwambia Fatuma: (Ewe Fatuma hakika mwenyezi Mungu anachukia kwa kuchukia kwako na anaridhia kwa kuridhia kwako).
[16] . Kwa sababu Hajjaj- kama ilivyo nukuliwa kwenye historia ua kuwa alifukua makaburi laki moja akitafuta kaburi lake (a.s).
[17] . Kasful ghumma: Mujaalad wa 1/ 263, na Al-ihtijaaj: Ukurasa 391.
[18] . Al-aamaaly cha Shekh Swaadiq: Ukurasa 345, majlis ya Khamsini na tano (55).
[19] . Al-jamal: ukurasa 81 na Al-fusuulul mukhtaar: Ukurasa 97.
[20] . Al-manaaqib: Mujallad wa 3/ 257 katika sehemu izungumziayo: Fii musawaatihi ma'a Daud wa Twaluut wa Sulaiman (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).
[21] . Suratu Al-imaraan aya 61.
[22] . Na inasemekana kuwa ni Safar 28.
[23] . Suratun-nisaa aya 86.
[24] . Al-manaaqib: Mujallad wa 4/ 19 sehemu ya Makaarimul-Akhlaaq.
[25] . Al-irshaad: Mujallad wa 2/ 127, mlango wa Twarafun min fadhaailil-hussein (a.s).
[26] . Al-manaaqib: Mujallad wa 4/ 76, sehemu ya Fii ma'aali Umurihi.
[27] . Al-aamaliy cha Shekh Swaduuq: Ukurasa 57, hadithi ya 10.
[28] . Ilalush-sharaai'I: Ukurasa 211, hadithi ya 2, mlango wa Al-illatullatiy min ajliha swaalahal hassan bin Ali (a.s).
[29] . Na inasemekana ya kuwa: Mwaka w tano mwezi wa Shaaban.
[30] . Na inasemekana ya kuwa ni tarehe 12 au 18 ya mwezi wa Muharram.
[31] . Suratu Al- Imraan aya 134.
[32] . Aalamul-waraa: Ukurasa 216, sehemu ya nne: Fii dhikri baadhi mu'ujizaatihi wa manaaqibihi wa Fadhaailihi.
[33] . Na inasemekana kuwa ni: Tarehe mosi Mwezi wa Rajab.
[34] . Uddatud-daiy: Ukurasa 248, mlango wa tano: Fiima Ulhiqa bidduaa wahuwa Adhikri.
[35] . Na inasemekana ni Elfu ishirini.
[36] . Attawhiid: Ukurasa 27, mlango wa Arrad alaa lladhiina qaalu Inna llah thaalithu.
[37] . Rejea Nahjul balagha: Sharhu ya Ibnu Abil hadiid: Mujallad wa 1/ 188 kisa cha shuraa.
[38] . Kashful- ghumma: Mujallad wa 2/374, Dhikru Imamul Aashir Abil Hassan Ali (a.s).
[39] . Na inasemekana ni wa: nane.
[40] . Al-irshaad: Mujallad wa 2/332, mlango wa Dhikru Twarafun min Akhbaar Abi Mohammad.
[41] . Al-irshaad: Mujallad wa 2/326, mlango wa Dhikru Twarafun min Akhbaar Abi Mohammad.
[42] . Suratu-tawbah aya 33.
[43] . Rejea kwenye kitabu Al-aamaaly cha Shekh Mufiid, ukurasa 265, majlis ya thalathini na moja (31).
[44] . Suratuz-zilzaalah aya 7-8.
[45] . Kwa ajili ya ufafanuzi zaidi rejea kitabu: Min mawsuuatul- fiqhil-kitab (Assiyaasah) siasa na (Al-iqtiswaad) uchumi (Al-ijtimaau) jamii na (Al-idaratu) idara (uendeshaji wa mambo) (Al-hukumu) utawala katika uislaam, na (Al-hurriyatu) uhuru, na kitabu (Idha qaamal islaam fil-iraq) na (Sabilun ilaa inhaadhil muslimiin) na ( As-swiyaaghatul jadiidah) na (Mumaarasatu-taghyiir) na.. cha marehemu Ayatullahil udhmaa Sayyid Mohammad Shiraziy (Mwenyezi Mungu autakase utajo wake).
[46] . Al-kafiy: Mujallad wa 2/17.
[47] . Bali matokeo ya maneno hayo ni kuwa: Nidhamu ya utawala wa kiislaam ni bora zaidi kuliko utawala wowote ulio wahi kutokea na kujulikana katika historia.
[48] . Suratu twaha aya 125.
[49] . Kama ambavyo hakuna shaka juu ya kuwepo kwa vyama au vikundi ambavyo vinafana kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo ya ujenzi wa nchi ikiwa havipingi kuwepo kwa sheria.
[50] . Yaani haki za kisheria, kama Khumsi na Zaka.
[51] . Hili kwa sharti kwamba zisivunjwe wala kupuuzwa haki za watu wengine na miongoni mwao ni vizazi vijavyo.
[52] . Hakika magazeti na mawakala wa habari wametaja ya kuwa nchi moja wapo kati ya nchi za magharibi yenye nafasi na nguvu katika nchimza magharibi kabla ya miaka kadhaa iliyo pita ilikuwa na tatizo kubwa na uhaba mkubwa wa pesa ya bajeti ya serikali kiasi kwamba inakadiriwa ya kuwa ilikuwa na upungufu wa maelfu kadhaa ya mamilioni ya dola, lakini nchi hiyo iliweza kuziba pengo hilo la bajeti kwa kutumia njia ya kupunguza watumishi wa serikali kwa muda mchache ikaweza kutatua tatizo hilo kubwa na kujilimbikizia hazina kubwa ya ziada inayo kadiriwa kiasi cha mamilioni elfu kadhaa ya dola na kuziweka akiba kwa ajili ya kuinua uchumi wake na hali maisha ya wananchi wake na ni jambo la lisilo fichika ya kuwa, kuwa na watumishi wachache ni jambo lililo amrishwa na uislaam na ni jambo lililo faradhishwa kwa dola la kiislaam, na ni jambo la kusikitisha sana kuona kwamba waislaam wana acha mafunzo ya uislaam wao na wasio waislam kuyatumia mafunzo hayo na wao kupata maendeleo na kutawala na sisi kudhalilika na kubakia nyuma kimaendeleo.
[53] . Kama makubaliano ya kisheria au sharti lililo ndani ya makubaliano au mfano wa hayo.
[54] . Kipande hiki ambacho kina anwani ya: (Dhamana ya kijamii) kimechukuliwa pamoja na kufanya marekebisho kadhaa kutoka kwenye kitabu: Assiyaasatu min waaqiul- islaam. Cha Mheshimiwa Ayatullahil-udhmaa Al-haji Sayyid Swaadiq Shiraziy (Mwenyezi Mungu amhifadhi) na kitabu hicho kimechapishwa Iraq mwaka 1381 hijiria, na msambazaji.
[55] . Tafsiru Nuuru thaqalayni: Mujallad wa 4/ 240 na Adhiyaau na Al-aailatu.
[56] . Wasailush-shia: Mujallad wa 13/ 151, akinukuu kutoka kwenye kitabu Al-khilaaf.
[57] . Mustadrakul-wasaail: Mujallad wa 2/ 490.
[58] . Mustadrakul-wasaail: Mujallad wa 4/ 490.
[59] . Mustadrakul-wasaail: Mujallad wa 4/ 492.
[60] . Wasailush-shia: kukiwa na marekebisho kadhaa.
[61] . Buharul-anwaar: Mujallad wa 32/ 214, kutoka kwa katika kitabu Al-kafiy: Mujallad wa 7/ 354, Mustadrakul- wasaail: Mujallad wa 17/ 446.
[62] . Manlaa yahdhuruhul faqiih: Mujallad wa 4/100.
[63] . Na uchambuzi wa hayo linabakia ni jukumu la bunge la wanazuoni au jopo na shura ya maulamaa na mafaqihi na maraajiu.
[64] . Na hili halipingani na kuyapanga hayo, bali makusudio ni kuwa inapsa kuwafundisha wote wakubwa kwa wadogo.
[65] . Kama ambavyo inalazimika kuwazuia watu kutengeneza na kupanua uwezo wa makombora au mabomu ya nyukilia ambayo yanamadhara kwa wanadamu na watu wote, kwani (Hakuna madhara wala kudhuriana katika uislaam) Wasailush-shia: Mujallad wa 17/ 376, mlango wa 1-h 11.
[66] . Suratul-anfaal aya 60.
[67] . Suratul baqarah aya 208.
[68] . Suratul anfaal aya 61.
[69] . Tahdhiibul-ahkaam: Mujallad wa 7/52, hadithi ya 22. Na rejea Wasailush-shia: Mujallad wa 17/ 328, hadithi ya 32228.
[70] . Suratul baqarah aya 208.
[71] . Suratul Anfaal aya 61.
[72] . Suratul Ahzaab aya 53.
[73] . Hata kama haikuharamishwa kwake kazi za nje ya nyumba kwa kuzingatia masharti yake.