ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
Kuweka vikundi Imam mahdi (a.s)
mwandishi Marehemu Mulla Muhammad Jaafar Sherif Dewj
Lugha ya kitabu سواحیلی
mwaka wa kuchapisha 1404

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

MUANDISHI: MAREHEMU MULLA MUHAMMAD JAAFAR SHERIF DEWJI

DIBAJI

kitabu hiki kinatoa ufafanuzi wa hadithi maarufu ya mtume muhammad(s.a.w.w) ambaye amesema:

"Yeyote atakayekufa pasina kumtambua imamu wake atakufa mauti ya mpagani." kila mwislamu mwenye kuamini kauli ya bwana mtume(s.a.w.w) hana budi kufanya kila juhudi ya kumtambua imamu wake wa wakati huu maana dunia hii haiwezi kubaki hata sekunde moja bila ya hujjah ya mwenyezi mungu (s.w.t) kuwapo. ama kwa hakika, kuwa na imani katika imami ni mzizi mmoja wapo wa dini, maana kazi ya kuiongoza na kuihifadhi dini ni wajibu wa imamu baada ya kuondoka duniani bwana mtume(s.a.w.w) .

Ndipo kitabu hiki kinafaa kisomwe na kila mwislamu! na kutafakari aya za kurani, hadithi za bwana mtume(s.a.w.w) za maimamu waliotajwa na mtume(s.a.w.w) na maelezo ya kihistoria yaliyomo ndani yake. kila neno lina maana na maarifa yake.

Mwalifu wa kitabu hiki, marehemu mulla muhammad jaafar sherif dewji, amefanikiwa kueleza kwa uwazi dhana ya uimamu ambaye ni usuli unaofafanuliwa kwa masimulizi kuhusu kuzaliwa, na kughibu na maisha yake marefu, ungojaji wa waumini kutokeza kwake, mahala aishipo, na ishara na dalili za kujitokeza kwa imam mehdi. vilevile ameeleza faradhi za waumin miongoni mwa mambo mengine mengi ya msingi na muhimu. mtarjumi wa kitabu hiki kwa lugha ya kiingereza kutoka lugha ya kigujarati ni alhajj murtaza a. lakha na alhaj z; m. s. lakha amekitarjumi kwa kiswahili chepesi na chenye ufasaha.

Maulana seyyid sabir husein musawi, qibla, ametilia shime kitabu hiki kichapishwe kwa kiswahili na mkarimu mmoja amejitolea kugharimia uchapishaji wa hiki kitabu.

Alla subhanahu wa taala kwa wasita wa mtume muhammad(s.a.w.w) na mwanae imam mehdi(a.s) atawajazi kila lililo jema mchapishaji huyo na wengine waliosaidia kwa dhati dhamira , hali na mali kueneza habari hizi muhimu zinazohusu imani na amali za waumini wa dini ua uislaam. miye, al-hakiri, ninashukuru kupewa fursa hii ya kuandika dibaji na ninaamini kuwa nami pia nitakubaliwa na imamu wangu kuwa mmojawapo wa mfuasi wake na kupata shifaa yake siku ya kiyama na pia hadhi ya kukutana naye hapa duniani.

alhaji muhsin m.r.alidina

Dare -es-Salaam

25 shawwal, 1409.


SHUKRANI

kitabu hiki kimetarjumiwa kutoka lugha ya kiingereza. kama ilivyoelezwa katika dibaji, sina budi kumshukuru alhaj muhsin m. ali dna ambaye alinihamasisha kuendelea kukitarajumi baada ya kukatishwa tamaa ya kumpata mtu wa kusahihisha na kunyoosha lugha. ijapokuwa alhaj muhsin m.r. alidina alipitia muswaada kikamilifu na kutoa mapendekezo muafaka au naksi yoyote iliyobaki ni 'dhima yangu. ninatumai wasomaji watazisamehe kasoro za lugha na kujali zaidi ujumbe uliomo katika kitabu hiki. alhaj zakirihusein m.s lakha mtarjumi. imam al zaman (imam wa wakati huu) hadhrat mehdi(a.s) kwa jina la mwenyezi mungu mwenye rehema na huruma


1

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE SURA 1

UTANGULIZI

Kitabu hiki hakikuandikwa kwa ajili ya kuleta majadiliano au mabishano na waumini wa dini zingine au madhehebu mengine ya kiislamu, bali kimeandikwa kwa ajili ya waumini wa jamii yangu, hasa kwa ajili ya vijana wanaokua ili waweze kufahamu na kutambua vema manufaa na ukweli wa imam wa wakati, hadhrat mehdi(a.s) , uongozi wake wa kiimamu, kughibu na hatimaye kuonekana kwake tena mara ya pili. ni katika kuthibitisha ukweli na uhakika wa imam huyo na maimamu kumi na wawili ndipo kitabu hiki kimenukulu-kauli kutoka vitabu vya madhehebu mbalimbali ya kiislamu na dini zingine.

Kwa vile uimamu ni mojawapo wa maadili matano ya dini yetu (shia ithnaashery) mwumini wa madhehebu shurti awe na yakini na imani juu ya itikadi hii kama vile shurti afahamu na kuamini kwa makini upweke wa mungu,uadilifu wa mungu, manabii walioletwa na mungu na siku ya kiyarna. kwa hivyo ni lazima mtu awe na yakini juu ya uimamu. hivyo hamna budi mtu kufahamu, kukubali na kuamini kwamba maimamu hao ni warithi na makaimu wa mtume wa mwisho. katika hao maimamu kumi na wawili ni imam wa kumi na mbili, imam wa wakati huu, hadhrat mehdi(a.s) ambaye yungali hai, bali kwa sababu mbalimbali ameghibu. wakati mungu atakapo mwamrisha, imam mehdi(a.s) atajitokeza na atatawala ardhi (dunia) hii kwa kueneza usalama na uadilifu kadri ile hivi inavyotawaliwa na dhuluma na maonevu, na ataeneza dini ya uislam.

Kiini cha hitilafu kati ya madhehebu 73 katika dini ya uisla ni suala la uimamu. Juu ya suala la upweke wa mungu, manabii, korani takatifu, na siku ya kiyama madhehebu yote yanaafikiana katika imani zao (isipokuwa makadiani, mabahai na madhehebu machache yaliyojitokeza katika karne mbili zilizopita). Lakini suala la uimamu ni jambo muhimu mno.

Waislamu wote wanaamini kwa kauli moja hadithi ya mtume mtukufu(s.a.w.w) kwamba "yeyote anayefariki bila kumtambua imamu wa wakati hufa kifo cha upagani (kutokuwa na imani ya dini), yaani, kifo cha kutokuwa mwislamu." vile vile hadithi ya mtume(s.a.w.w) inayokubalika kwa waislamu kwamba "wafuasi wangu watagawanyika katika makundi 73, na watapotoka kwenda motoni ila kundi moja tu ambalo iitakuwa katika njia ya haki." Haiyumkiniki kwamba firka zote 73 ziwe kwenye sirat-al-mus takim. kadhalika kila firka inamwona mwingine kapotoka. Hivyo kila mwislamu anawajibika kutafuta na kukubali madhehebu ya kweli na ya haki. kwani kwa mujibu wa hadithi ya mtume(s.a.w.w) "Mtu anayekufa bila kumtambua imam wake wa wakati hufa kifo cha kutokuwa na dini na vitendo vyake vyote, swala saumu zake zote huwa hazina thamani yoyote ." Kwa vile imani katika uimamu hufarakanisha madhehebu mbalimbali, basi hilo ni suala muhimu na zito sana.

Uislam umeweka maadili matano ya kuthibitisha ukweli wa mahehebu. kwa hivyo kila mwislamu anayejibidiisha kwa dhati kujipatia ridhaa ya mwenyezi mungu na uokovu wake na aliye jiandaa na yuko tayari kuacha ukaidi wake na dhana alizofuga bila shaka ataweza kutambua dini iliyokuwa ya haki na yenye ukweli. mwenyezi mungu amesema katika kitabu chake:

وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا وَإِنَّ اللَّـهَ لَمَعَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٦٩﴾

"Wale ambao wanajitahidi kwa ajili yetu kwa hakika wataongozwa kwenye njia yetu ya haki na iliyonyooka." (29:69).

maadili matano hayo ni:

1) Qur'ani takatifu.

2) Hadithi sahihi za mtume ambazo hazipingani na au kuwa kinyume cha Qur'ani takatifu

3) Tawarikh (historia).

4) Uhakikawatukio.

5) Utumiaji wa akili (urazini)

Katika kufahamu na kuelewa maana halisi ya qur ani takatifu, ujuzi wa hadithi sahihi, historia, uhakika wa matukio na utumiaji wa akili ni muhimu sana. udogo wa kitabu hiki hauruhusu majadiliano bayana juu ya mambo hayo. tangu kughibu kwa imam mehdi(a.s) , zaidi ya miaka elfu moja iliyopita, mamia ya waislamu wamedai utume, uimamu na hata kuwa mehdi(a.s) . wadanganyifu wengi walidai kuwa mehdi wametoka bara arabu, iran, bara hindi na afrika. lakini kwa hakika hata mmoja wao hakuwa mehdi wa kweli kama ilivyoelezwa katika kitabu kitakatifu. hadithi na historia huthibitisha kwamba atakuwa mehdi mmoja tu. kwa hivyo wenye. kudai kuwa mehdi ni wazushi, waongo na kwa udanganyifu wao wamemkebehi mungu na mtume wake. Aidha dalili moja muhimu katika kutafuta madhehebu ya haki ambayo itamletea uokovu mwanadamu ni kwamba kila firka ya uislarnu hukubali atukufu wa aila ya mtume(s.a.w.w) .

Yeye mwenyewe, Ali, Fatima, Hassan na Hussein (rehma ya mungu iwe juu yao), ni watu waliotakasika kikamiliru na walio juu ya siratul-mus-taqim (njia ya haki) na ambao wanastahiki utukufu na taadhima ya haki. Kwa hivyo, bila pingamizi lolote, amri zao, hadithi zao na mafunzo yao yanapatia watu uokovu. Hakuna mwislamu yeyote ambaye anaweza kuyapinga mafunzo ya hao watano. Kila mwislamu anawajibika kutafiti maisha waliyo ishi hao watano, maagizo na mafundisho yao ili kuweza kufuata madhehebu ya haki.

Inawezekana kujua namna ya maisha yao, vitendo vyao maagizo ya hao "watano" sio tu kutoka katika vitabu vya madhehebu ya shia ithnaashery, bali pia katika vitabu vilivyoandikwa na waandishi maarufu wa madhehebu ya sunni. Wafuasi wa kila madhehebu ya kiislam huwakubali hao watano ambao walikuwa juu ya haki na mfuasi wa madhehebu hudai kwamba ni mfuasi wa hao watano. Aidha madai hayo ya firka mbali mbali kuhusu maagizo yanayohitilafiana, ni kinyume cha busara na hayawezi kukubaliwa. Kitabu hiki kitajaribu kubainisha maelezo ya watano hao pamoja na maelezo kuhusu madhehebu ya kweli na ya kumtambua imamu mehdi(a.s) , imam wa wakati huu.

Zaidi ya hayo kuhusu hao watukufu watano kuna hadithi mashuhuri ya mtume(s.a.w.w) ambayo inakubaliwa na wote; nayo ni:"Mimi ninawaachieni vitu viwili muhimu (vizito) mno: kitabu cha mungu na dhuriya yangu (Ahlul-bait). kama mtashikamana na vyote viwili hamtapotea kamwe."

Familia tukufu ya mtume mtukufu(s.a.w.w) imetajwa katika kitabu kitukufu na mwenyezi mungu kuwa ni yenye watu watakatifu na waliotakasika kutokana na kila uovu. bila shaka, licha ya kuwa katika njia ya haki, watu hao pia ni viongozi wa umma kwenye njia ya uokovu. kwa hivyo wafuasi wanaowapenda watano, huzingatia na kufuata mafunzo pia maagizo yao na kuwa maadui wa wauaji wa Ahlul Bayt, kwa hakika ni wafuasi wa dini ya haki na wanastahili uokovu.

Madhehebu yote ya kiislam hukubali kwamba qur'ani ni neno la mwisho la allah lililoteremshwa juu ya mtume(s.a.w.w) kuwa yanawajibika kufuata maagizo yake (ila makadiani ambao wanashaka na qur'ani kwa sababu imo katika lugha ya kiarabu kwa hivyo ni kwa ajili ya waarabu tu). Iwayo yote itakavyokuwa mgeni anapozuru jiji, ikiwa mchana jua linapowaka, au usiki taa zinapomeremeta kama haujui huo mji hataweza kufika kokote bila mwongozi. Vivyo hivyo, qur'ani ni mfano wa mwanga wa jua; kwa hivyo, tunahitaji mwongozi kutuongoza kwenye siratul mustakiim (ajia ya haki). kama vile mwongozi anahitajika kuwa mwenyeji na kufahamu mambo yote katika jiji hulo,vivyo hivyo, hainabudi kwa maimamu kuwa na ujuzi kamili na wa kweli wa qur'ani iliyoteremshwa kwao na mwenyezi mungu mwenyewe. Kwa hiyo Mtume(s.a.w.w) katika hadithi yake madhukura amesema kwamba ameachia vitu viwili vizito: kitabu cha mungu na dhuriya wake, na yeyote atakayeshikamana na hivyo viwili hatapotoka kabisa.

Hoja inayotolewa na wapinzani wa imamu wetu ni kwamba imam lazima awe anaonekana siku zote na kuwa awe hadharani mwa watu na kwamba imam aliyejificha hawezi kuwa imam au hawezi kutoa mwongozo mwema au kusaidia si hoja thabiti. Iwapo hatuwezi kumkubali imam tusiyemwona, basi kuwepo kwa mungu mwenyewe ambaye hatumwoni bapa duniani na hata baadaye (siku ya akhera) vile vile, naudhubillah, hubatilisha kuwepo kwake. hata hivyo, kukubali kuwepo kwa mungu ni imani muhimu katika dini zote. licha ya hayo viumbe wengi wa mungu ambao hawaonekani, lakini kuwepo kwao hakupingwi. Mathalan roho ya binadamu inayoingia katika kijusi kilichopo tumboni mwa mama na roho inapotoka mwilini mwa binadamu vile vile haionekani. kuongezea hayo, hewa na malaika hawaonekani, lakini hatuvikanushi.

Mtume adhimu wa uislamu alilazimika kujificha na kuishi katika pango kwa muda wa miaka mitatu. Vile vile manabii mussa, suleiman, ibrahim na issa kwa baadhi za nyakati waliona dharura ya kujificha. Kadhalika manabii khidhri na elias wapo hapa duniani kwa muda wa maelfu ya miaka na huo ni ukweli unaokubaliwa na waislamu wote.

licha ya hayo, shetani "iblis"na wafuasi wake na majini wapo hai duniani na hawaonekani. Dajjal na yajuj majuj (agog na magog) na mataifa yao yanakubaliwa kuwa wapo hai lakini hawaonekani. Qur'an takatifu yenyewe imeeleza juu ya imani ya ughaibu na tutaeleza aya hizo za qur'an pahala pengi katika kitabu hiki. Hali itakayokabiliwa katika kaburi, siku ya hukumu (kiyama) pepo, moto, mizani, sirat (njia nyembamba siku ya kiyama) arsh na kiti cha enzi (kursy) na kadhalika havionekani. Licha ya waislam kuwa na itikadi juu ya hayo yote, hata wakristo, mayahudi na mabaniani pia huyaamini. kwa hivyo hakuna sababu ya kusaili kutoonekana kwa imam.

Jamii ya kibohora huamini kwamba imam wao tayyab ametoweka tangu 524 a.h. na kwa muda wa miaka 876 haonekani. Kwa hivyo wao hawawezi kusema kwamba kutoonekana kwa imam wetu wa kumi na mbili haimkiniki. Vile vile ismailia, wafuasi wa agakban, "wamesimulia katika vitabu vyao kuwa baadhi ya maimam wao walikuwa hawaonekani. Hivyo kuzaliwa kwa imam wa wakati, imam Mahdi(a.s) , na kuwa hai na kughibu kunathibitika na aya za qur'an, hadithi za mtume mtukufu, historia na akili na hakuwezi kubatilishwa kwa kisingizio hicha kutoonekana kwake. Kwa hiyo suala muhimu linalojitokeza si kwamba, je, iwapo imamu haonekani au kufikiwa anawezaje kuutumikia uislam na waislamu na kwa nini asijitokeze kuondoa ukafiri? hayo ni masuala ambayo yatajadiliwa kwa makini katika kitabu hiki katika sura zinazofuata ili idhihirike kwamba ijapokuwa imam haonekani lakini uislam na waislamu hupata manufaa na fadhila nyingi kutoka kwake imam(a.s) .

Maismailia wanaomfuata agakhan pamoja na viongozi wa dini hiyo wanasema kuwa maneno ya qur'ani "imaulmubin" yanamaanisha imam aliyekuwa mbele ya macho yetu, na siyo imam aliyejificha. walakini neno "mubin" halimaanishi tu "kitu kinachoonekana bayana". neno hilo limetumiwa pahala pengi katika qur'an takatifu kwa maana anuwai k.m.

1) Kifungu "imamul mubin" kimetumiwa katika sura ya 36 (surat-yasin) aya 12 "na sisi tumehifadhi kila kitu katika imamu aliyebainika". Katika kamusi za kiarabu kiingereza neno "mubin" humaanisha, "bayana", "dhahiri" na "wazi wazi".

2) Katika sura hiyo hiyo ya yasin, neno la "mubin" limetumiliwa katika muktadha wa "yeye ni adui dhahiri" (36:60). Aya hiyo bila shaka inamzungumzia shetani kuwa ni adui anayejulikana waziwazi na hakuna ushahidi wa aina yoyote wa kusema shetani anaonekana. kwa hiyo imedhihirika kwamba neno "mubin" halimaanishi "dhahiri" kwa macho tu. katika sura hiyo hiyo, aya 24 inasema, "nikifanya hivyo nitakuwamo katika upotofu bayana". Katika aya hii upotofu unasibishwa na sifa "mubin" (bayana). Hapo tena inakubalika kwamba kosa sio kitu kinachoonekana.

3) Katika sura ya "nyuki", sura ya 16, mwisho wa aya 35, kuna maneno yafuatayo: "basi kunawajibu'. Mwingine wa mitume pia kufikisha ujumbe waziwazi?" neno "mubin" hapa limenasibi- shwa na ufikishaji ambao ni kitu kisichoweza kuonekana.

4) Neno hili pia limetumika katika sura 26 kuhusu washairi ambamo katika aya 195 inasomeka: "katika lugha ya kiarabu dhahiri", lugha siyo kitu kinachoweza kuonekana kwa macho.

5) Katika sura ya yasin, aya ya 17: "na hakuna kitu kinachowapasa ila ufikishaji wa ujumbe bayana". ujumbe sio kitu kinachoweza kuonekana kwa macho. 7) tena katika sura ya "nyuki" aya ya 4:" amemuumba binadamu kutokana na chembe ya uhai bali anakuwa mpinzani bayana." kwa hivyo, ni dhahiri kwamba kukubali kwamba neno la "mubin" linamaanisha tu kuweza kuonekana kwa macho ni uwongo na udanganyifu. Wakati huo huo imethibitika kwamba hata mitume waliishi maisha ya kutoonekana bayana. mabohora na waismailia pia huamini kama baadhi ya maimam wao walijificha. katika mpangilio wa kurithiana, maimamu watatu wa kiaghakhan, wafi ahmed, taki mohamed na raza abdullah waliishi maisha ya mafichoni. licha ya hayo hakuna habari yoyote juu ya maisha na wasifu wa wengi wa maimamu wao 48.

Mwisho :

Sifa za imam zimeelezwa bayana katika qur'an na katika hadithi za mtume(s.a.w.w) . sifa hizo zitajadiliwa katika kitabu hiki katika sura zijazo. kitu muhimu cha kuzungumzia hapa ni mazingira au hali inayohitajika kufanya imam mehdi(a.s) kujitokeza. iwapo hali zilivyoelezwa katika qur'an tukufu na hadithi za mtume(s.a.w.w) hazikutimia, basi mdai veyote hatakubaliwa na mwislamu kuwa yeye ndiye mehdi. sifa zinazohusu ni zifuatazo:

1. Jina tukufu la mehdi ni hadhrat muhammad(a.s) . ukweli wa maneno hayo umethibitishwa kutokana na hadithi na historia ya uislam. kwa hivyo, wenye majina ya gulam ahmed, mohamedali bab, bahauddin au mwenye jina lolote lingine hawezi kukubalika kuwa mehdi.

2. Hadhrat mehdi'(a.s) yungali hai hadi hii leo na hakujitokeza kwa sababu ishara zinazohusika na wakati wa kujitokeza kwake kama zilivyo elezwa katika qur'an na hadithi hazikudhihirika.

3. Ishara moja muhimu kabla ya kujitokeza kwake ni kuonekana kwa dajjal ambaye atauliwa na imam(a.s) . japokuwa baadhi ya watu waliodai kuwa mehdi wameshajitokeza na kupotea, lakini mpaka leo dajjal hajaonekana. (mirza wa kadiani alieleza kuwa kampuni ya gari la moshi ya uingereza (british railways) ni punda wa dajjal asiyekuwa na mkia, lakini baadaye yeye mwenyewe na wafuasi wake walimpanda huyo punda (gari moshi).

4. Kitambo tu baada ya kujitokeza kwa mehdi duniani kutakuwa na uadilifu na amani. hali kama hiyo bado haijapatikana hadi leo ingawa wadanganyifu wengi waliodai umahdi wamejitokeza. kinyume cha hayo uonevu, uovu na dhuluma umezagaa. nabii issa atateremka kutoka mbinguni na atafika kwa hadhrat mehdi(a.s) . jambo hilo bado halijatokea. mirza kadiani na mithili yake wengine vile vile walidai kuwa wao ndio nabii issa.

Kufuatana na kauli ya wanahistoria na wanahadithi wa kiislamu, hadhrat mehdi(a.s) atajitokeza wakati uliopangwa na mungu, na ni mwana wa imam wa kumi na moja, imam hassan askari(a.s) na anatokana na dhuria (kizazi) ya imam hussein(a.s) mwana wa mwana-fatima(a.s) , binti wa mtume mtukufu(s.a.w.a) . yeye atakuwa kwenye kizazi cha tisa cha imam hussein(a.s) na imam wa kumi na mbili katika urithi huo.

5. Pia hadhrat mehdi(a.s) atakuwa ni mwana wa wazazi walio wacha mungu wa hali ya juu na watakatifu na atakubaliwa na waislamu wote. kwa hivyo, kwa vile wadanganyifu wote kutoka bara arabu, pakistan, iran na punjab waliodai kuwa mehdi hawakutokana na kizazi hicho kamwe. kwa hiyo hawakubaliki.

6. hadhrat mehdi(a.s) atakuwa na vitu maalum vya wadhifa wake kama mitume walio pita k.m. pete ya nabii suleiman, fimbo ya nabii mussa, jiwe la nabii mussa ambalo alipolipiga fimbo yake liliibua chemchem kumi na mbili na bendera ya mtume(s.a.w.w) . wadanganyifu waliodai kuwa wao ni hadhrat mehdi(a.s) hawakuwa na hata kitu kimoja kati ya vile vilivyo tajwa hapo. Vile vile maayari hao wataweza kuwa na daawa hiyo?


2

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 2

AYA ZA QUR'ANI KUHUSU UIMAMU, KUGHIBU NA KUONEKANA TENA KWA IMAM WA WAKATI WETU HADHRAT MEHDI(A.S)

"Alif laam mim. kitabu hiki, bila shaka ni mwongozo kwa wale wanaoepukana na maovu. wale ambao wanaamini visivyoonekana".

kuna aya nyingi katika qur'an tukufu kuhusu kuwa na imani ya mambo yasiyoonekana. "mwenyezi mungu ameahidi baina yenu kwa wale ambao hutenda vitendo vyema kwamba bilashaka atawateua wraithi juu ya ardhi (duniani) kama alivyo teua warithi, kabla ya hao na bilashaka atastawisha dini wanayo fuata (uislam) aliyoichagua yeye (mungu) na kwa hakika baada ya hali ya hofu kubadilika kuwa pa imani ili wanaomwabudu mungu na kutomshirikisha yeyote nayeye (mungu) na yeyote ambeye hataleta imani baada ya hayo,hao ndio ambao ni waovu." (55).

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ ﴿٩﴾

"Ni yeye (mungu) ndiye alie mtuma mtume wake pamoja na mwongozo na dini ya haki ili ishinde dini zote japokuwa washirikina watakasirihishwa na hilo. " (61:9).

Mtume mtukufu(s.a.w.w) katika uhai wake hakuweza kushinda dini zote wala kuwashinda washirikina. Kwa hivyo ahadi hiyo itatimizwa na kukamilishwa katika kipindi cha utawala wa hadhrat mehdi(a.s) .

Katika ufafanuzi wa aya hiyo mwanazuoni mashuhuri sana wa kisunni, imam fakhruddin razi, anasimulia kutoka kwa Abu hureira kwamba mtume(s.a.w.w) amesema kwamba: Ahadi hiyo iliyotolewa na Allah kuupa uislam ushindi juu ya dini zote itatekelezwa na hadhrat mehdi(a.s) atakapojitokeza na watu wote kukubali dini ya uislam.

Hadithi nyingi kuhusu hadhrat mehdi(a.s) zimo katika vitabu vya kisunni.

وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِي الزَّبُورِ مِن بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الْأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ ﴿١٠٥﴾

"Na kwa hakika tuliandika katika zaburi baada ya ukumbusho ya kwamba waja wangu watakatifu watarithi (watatawala) ardhihii".(21:105).

وَلَقَدْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَبَعَثْنَا مِنْهُمُ اثْنَيْ عَشَرَ نَقِيبًا ﴿١٢﴾

"Na bilashaka allah amewaahidi wana wa israil kwamba amewateua viongozi kumi na wawili" (5:12).

Sahih Bukhari na Sahih Muslim ambavyo ni vitabu vinavyo aminiwa sana na masunni, vinasimulia hadithi ya mtume(s.a.w.w) kuwa:

"Hadi hapo itakapo kamilika silsila ya warithi wangu kumi na wawili dunia hii itaendelea, nao watakuwa maimam kumi na wawili."

"(Kumbukeni) siku ambayo kila watu wataitwa pamoja na imam wao." (17:71).

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِمْ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَإِقَامَ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءَ الزَّكَاةِ وَكَانُوا لَنَا عَابِدِينَ ﴿٧٣﴾

"Na sisi tumewateua maimam miongoni mwao watakao ongoza binadamu kwa amri yetu (amri ya mungu) ya kutenda mema, kuendeleza swala na kutoa sadaka na walitutumikia sisi peke yetu" (21:73).

Maimamu wameagizwa kutenda vitendo vyema, kuendeleza swala, kulipa zaka, kumwabudu mungu na kuwaongoza watu kufuatana na maagizo ya mungu. Kwa hiyo, ni watu hao tu ambao waliojiwajibisha - kutenda hivyo na kuwaongoza wengine kufuatana na maagizo ndiyo wanaoweza kuwa maimam; na sio wale ambao hutenda kinyume (kuasi amri ya mungu). 8)

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ ﴿٤١﴾ وَأَتْبَعْنَاهُمْ فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ هُم مِّنَ الْمَقْبُوحِينَ ﴿٤٢﴾

"Na sisi tumewafanya maimam ambao huwavuta watu motoni; na siku ya kiyama hao hawatasaidiwa. na sisi tumesababisha maafa kuwazingira duniani na siku ya kiyama hao watakuwa katika kikundi cha watu wataotisha." (28:41-42)

لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ ﴿٣﴾ تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ ﴿٤﴾ سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ ﴿٥﴾

Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri!" (97:3-5).

Malaika huteremka kwa idhini ya mola kwa ajili ya kila amri. lakini malaika hao huenda wapi na hayo mambo huelekezwa wapi na je, hao wanaoteremka hawakamilishi ujumbe? hivyo inathibitika kwamba duniani kuna mwakilishi wa mungu na ni mrithi wa mtume(s.a.w.w) anayetimiza wajibu wa imam. kila mwaka katika usiku huo mtukufa malaika huteremka na kumkabidhi ujumbe wa mungu. Kutokana na hoja za aya za qur'an, hadithi za mtume(s.a.w.w) na akili, mtu aliyekamilika na anayestahili heshima hiyo na kutembelewa na malaika hawezi kuwa yeyote mwingine ila hadhrat mehdi (a.s) katika kitabu hiki kwingineko tutaelezea kwamba hawezi mtu mwingine kudai hadhi hiyo ila hadhrat mehdi(a.s) .


3

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 3

UTEUZI WA MAIMAMU, SIFA ZAO NA WAAJIBU WA VEEO VYAO

Imam ni neno la kiarabu linalomaanisha, "mkuu", "kiongozi", na "mwongozi."

Uteuzi wa imam hufanywa na mungu na kumjulisha mtume wake, ambaye hutangaza uteuzi wa imam huyo kwa wafuasi wake. mwenyezi mungu amesema katika qur'an "na bwana wenu anayeumba na kumchagua anayempenda, na siyo hiari yao, na kutukuzwa ni yeye ambaye ni juu ya vyote anavyo shirikishwa nae" kuna aya nyingi katika qur'an zinazoeleza kwamba uteuzi wa imam ni wa mungu na hufanywa na mungu mwenyewe. kwa mfano kuhusu nabii adam:

وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ﴿٣٠﴾

Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa ...(2:30).

Kuhusu Nabii Daudi, Mungu amesema katika Qur'an:

يَا دَاوُودُ إِنَّا جَعَلْنَاكَ خَلِيفَةً فِي الْأَرْضِ فَاحْكُم بَيْنَ النَّاسِ بِالْحَقِّ ﴿٢٦﴾

Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki... (38:26).

Kuhusu Nabii Ibrahim, Qur'an imeleza:

وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾

Na Mola wake Mlezi alipo mjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza, akamwambia: Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu. Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu." (2:124).

Kutokana na aya hizo imedhihirika kwamba mtume(s.a.w.w) humteua (tangaza) imam kutokana na amri ya mungu tu. La sivyo, yeye hana uwezo wa kumteua imam kwa sababu imam lazima awe mwenye hekima yote na. awe maasum (asiyekosa, asiye na dhambi na kuwa taahir).

Qur'an inazungumzia maimam aina nyingi, k.m.

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِمْ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَإِقَامَ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءَ الزَّكَاةِ وَكَانُوا لَنَا عَابِدِينَ ﴿٧٣﴾

"Na sisi tumewafanya kuwa maimam wanao ongoza watu kwa amri yetu na tumewaamrisha kutenda wema, kuimarisha swala na kutoa zaka na sisi peke yetu tu wao hututumikia." (21:73).

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ ﴿٤١﴾

"Na sisi tumewafanya maimam ambao huwaongoza watu kwenda motoni, na siku ya hukumu hao hawatasaidiwa." (28:41).

Yafuatayo ni madondoo machache ya wanazuoni mashuhuri wa kisunni kuhusu imam na sifa zake. aalim mashuhuri wa kihindi katika kitabu chake madhahibul islam katika ukurasa 106 aandika:

Imam ni mwakilishi wa mtume(s.a.nv.w) na kwa niaba yake ni mtawala na mhifadhi wa mambo yao duniani na mtoaji mwongozo kuhusu mambo ya kidini, kudumisha elimu ya dini, kutekeleza maagizo ya kiislam, kuamrisha watu kutenda mema, na kuwakataza watu waache maasi, kupingana na makafiri na kuwapa adhabu wahalifu kufuatana na mwongozo wa dini."

licha ya hayo, katika madhehebu ya sunni neno la "imam" hutumika katika maana ya kawaida tu. Mtu yeyote ambaye ni mtaalamu katika hadithi na sheria ya kiislam vile vile huweza kuitwa imam. k.m.

Imam ghazali, imam shafi, imam abu hanifa. lakini hata hivyo wanaamini kwamba kuwa mrithi (mwakilishi) wa mtume(s.a.w.w) na faradhi za mtume(s.a.w.w) imam lazima awe na masharti yafuatayo.

Imam lazima awe:

1) Mwislam.

2) Mwanamume.

3) Mtu huru (asiwe mtumwa)

4) Awe na akili timamu.

5) Awe amebaleheghe (siyo mtoto mdogo)

6) Awe mcha mungu (asiwe mtenda maasi)

7) Awe anatokana na kabila la quraishi.

8) Asiwe na kilema cha aina yoyote; kiziwi, bubu au kipofu.

9) Awe mtaalam katika sheria ya kiislam.

Imam wa 32 wa ismaili (wafuasi wa aga khan) shah mustansir billah, ameandika sifa za watakatifu katika kitabu chake kiitwacho "fidi aad jawan mardi".

Kitabu hiki kinahesabika kuwa ni cha uhakika wa hali ya juu kwa waismailia na vile vile kuna makala ya watakatifu. toleo moja la kitabu hiki kilichapishwa katika mwaka wa hindoo 1961 na laljibhai devraj katika lugha ya kiajemi (persian) lakini katika hija ya kihindi. katika ukurasa wa 94 sifa za watakatifu zimeelezwa "eh waumini, jueni kwamba "peer" (mtakatifu) huwa mtu thabiti, pili humkumbuka na kuamini mungu, na wajibu wake ni kutafakari, kuhubiri na kuhutubia juu ya ukweli.

Yeye lazima kwanza hujitaradhia nafsi yake kabla ya kuwasihi wengine." "tena katika kurasa 94-96 anaendelea: "mtakatifu wa haki ni yule ambaye ni mwenye matamanio katika makuu ya dunia, huepuka kwenda pahala pasipo pazuri na vitendo vya fuska, mwenye subira, makini, mkweli na mcha mungu". mwishowe tunasimulia hadithi moja kuhusu sifa za imam, kutoka kitabu cha shia ithnaasheri. hassan bin fadhal asimulia kutoka kwa baba yake kwamba Imam Ali-ridha(a.s) , imam wa nane, ameeleza sifa 30 zinazo mhusu imam, nazo ni:

1. Imam lazima awe na elimu zaidi kuliko watu wote wa wakati huo.

2. Awe kiongozi na mwamuzi wa watu wote.

3. Awe ni mtu mwenye subira zaidi kuliko wote katika karne

anayoishi.

4. Awe mcha mungu zaidi kuliko watu wote wa wakati wake.

5. Awe shujaa kuliko wote.

6. Awe mtu mwenye dini na mwabudu mungu zaidi kuliko wote.

7. Awe mkarimu kuliko wote.

8. Awe amezaliwa akiwa ametahiriwa.

9. Huzaliwa msafi na huwa mcha mungu.

10. Huweza kuona nyuma yake kama anavyoona mbele bila kugeuka nyuma.

11. Hawi na kivuli cha mwili wake.

12. Anapozaliwa papo hapo huweka viganja vyake juu ya ardhi

(Sakafu).

13. Hutoa shahada juu ya upekee wa mungu na utume (unabii) wa

Mtume muhammad(s.a.w.w)

14. Hapati ndoto za unyevunyevu.

15. Hata akiwa amelala huwa macho kifahamu.

16. Malaika huja kumwamkia na kuzungumza naye.

17. Deraya ya mtume(s.a.w.w) humtosha barabara.

18. mkojo au kinyesi chake hakionekani na mtu yeyote. hunyonywa

(mezwa) na ardhi, haiwi na harufu mbaya lakini hutoa harufu ya

ambari na miski."

19. Hudhibiti maisha ya watu.

20. Huwa na huruma zaidi juu ya watu kuliko wazazi wao.

21. Huwa mnyenyekevu mno katika swala zake na ibada ya mungu.

22. huwa wa kwanza katika kutekeleza amri za mungu.

23. Hujizui kwa dhati na juhudi kuepuka na maasi.

24. Dua zake zote hutakabaliwa na allah na hakuna kitu anachomwomba mola hukataliwa na mungu, akimwomba mungu jiwe gumu lipasuke hupasuka.

25. Huwa anamiliki deraya ya mtume(s.a.w.w) pamoja na upanga wake dhulfikar.

26. Huwa na daftari lenye orodha ya wafuasi wake wote pamoja na

wale ambao watakao zaliwa mpaka siku ya hukumu.

27. Huwa na kitabu chenye orodha ya maadui wake wote.

28. Huwa na jaamiah yenye urefu wa yadi 70 ambamo kuna maelezo kamilifu kuhusu mambo ya dunia.

29. Huwa na nyaraka kubwa iliyo tengenezwa kwa ngozi ya mbuzi na nyingine ndogo iliyotengenezwa kwa ngozi ya kondoo ambazo huitwa jafar kuu na jafar ndogo ambazo zinaeleza kanuni zote za kidini hata kuhusu mambo madogo kama vile sheria inayomhusu mtu akimcho mamwezie kwa ukucha.

30. Huwa na kitabu alicho rithishwa kutoka mwana fatima(a.s) binti muhammad(s.a.w.w) .

Ikiwa mtu hana hizo sifa 30, basi kwa mujibu wa itikadi ya shia ithnaashery hawezi kamwe kukubaliwa kuwa imam.

Kwa hakika ni wajibu wa mtume(s.a.w.w) na warithi wake kumi na wawili kuishi maisha kwa mujibu wa amri za mola na kanuni zilizoandikwa katika qur'an tukufu na kuongoza waislamu ili kuishi maisha ya kidini bila kuleta mabadiliko ya aina yoyote katika amri takatifu. kuhusu jambo hilo tunakumbusha aya chache zinazohusika za qur'an:

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa (53:3- 4).

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٤٤﴾

"Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri." (5:44).

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٥﴾

"Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu." (5:45).

ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٨﴾

"Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu". (45: 18)

وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ ﴿٤٤﴾ لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ ﴿٤٥﴾ ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ ﴿٤٦﴾ فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ ﴿٤٧﴾

Na angalikuwa amezua chochote kinyume cha amri zetu, kwa hakika tungelimtwaa upande mkono wa kuume na baadaye tungelikata mishipa yake ya damu upande wa kushoto wa moyo. Na hakuna hata mmoja katika nyinyi angeweza kumkinga." (69:44-47).

Wakati hata mtume mtukufu(s.a.w.w) hana madaraka ya kuongeza au kupungu za, kubadilisha au kugeuza yaliyoteremshwa (wahyi) na allah kama ilivyoelezwa katika qur'an tukufu. Basi kwa hakika imam(a.s) pia hana uwezo wa namna hiyo. Maimam wote(a.s) ni viongozi wa wafuasi, huwafunza amri za mungu kama alivyofunza mtume(s.a.w.w) .

Kwa hiyo ni jambo la lazima kuwa elimu ya maimam(a.s) kuhusu qur'an tukufu na hadithi iwe bora kuliko ya waislam wote.


4

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 4

UIMAMU NA UKHALIFA

Uteuzi wa imam na khalifa ulifanywa na mtume mtukufu(s.a.w.w) kutokana na agizo la mungu peke yake. Kwa hiyo hakuna imkani yoyote ya kuwahusisha watu katika uteuzi huo. mwenyezi mungu amesema katika qur'an:

وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ سُبْحَانَ اللَّـهِ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٨﴾

Na Mola wako Mlezi huumba na huteuwa atakavyo. Viumbe hawana khiari. Mwenyezi Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanao washirikisha naye (28:68).

Katika qur'an tukufu allah amewateua manabii Adam na Daudi kuwa makhalifa tu; wawakilishi wake duniani

يَا دَاوُودُ إِنَّا جَعَلْنَاكَ خَلِيفَةً فِي الْأَرْضِ ﴿٢٦﴾

Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. (38:26).

Hata hivyo licha ya kumteua awe nabii na khalifa vile vile alimpa hadhi ya kuwa imam". kwa hakika mimi nitakufanya wewe imam". (2:124).

Kutokana na hadithi mashuhuri ya mtume(s.a.w.w) , watakuwa warithi kumi na wawili baada yake. Wanazuoni mashuhuri wa madhehebu ya kisunni wameukubali ukweli wa hadithi hiyo na kunakili katika vitabu vyao. vile vile katika historia ya kiislam, banu ummaya, na banu abbasi walikuwa watawala wa kidunia tu, wao kamwe hawakuteuliwa na mtume mtukufu(s.a.w.w) . kwa hakika kufuatana na hadithi zingine, mtume(s.a.w.w) mewaatangaza hao kuwa ni waghasibu wa ufalme.

Kwa hakika warithi na makhalifa wa mtume(s.a.w.w) ni maimam kumi na wawili ambao kama mtume(s.a.w.w) mwenyewe, ni katika kizazi bora cha hashim wa kabila la quraishi na kupewa madaraka juu ya viumbe vyote. walikuwa na elimu na uwezo wa kufanya (kuleta) miujiza na sifa zote alikuwa nazo mtume(s.a.w.w) . kama alivyo yeye (mtume) walikuwa wametakasika kwa kila uovu na dhambi. Hawa ni maimamu waliotajwa na allah katika qur'an tukufu kuwa ni "watu wa kweli wenye madaraka na walio takasika". mwanazuoni wa kisunni fak-ruddin Razi, katika kitabu cha Tafsir Al-kabir, juzuu ya 3, ukurasa 357, kilichochapishwa misri, ameeleza kwamba amri ya "kumtii mungu, mtume wake na wale wenye madaraka" (4:54). Inamaanisha kwamba: wale wenye madaraka ambao utii wao uliamrishwa katika qur'ani ni wale tu wasio kuwa na dhambi na wasioweza kukosa; la sivyo, inamaanisha kwamba mungu ametuam risha kuwafuata wale wanaoweza kukosa kueleza amri za mungu.

Utambulisho wa hao maimam kumi na wawili warithi wa mtume(s.a.w.w) , umethibitishwa na hadithi chache ambazo zimenakiliwa katika vitabu vya kisunni. Shaikhul islam, sheikh suleiman hanafi nehshabandi kanduzi balkhi aliyefariki 1294 (a.h.) na aliyekuwa mtakatifu mkuu wa sultani wa istanbul (uturuki) abdul aziz khan, ameandika katika kitabu cha: Yanabiu Al-mawaddah kurasa 369-71 (kama ilivyotafsiriwa katika kiingereza) "yahudi mmoja mwenye jina la naathal alikuja kuonana na mtume(s.a.w.w) na kutaka maelezo kuo.ndosha shaka alizokuwa nazo na kuahidi kwamba akipata maelezo ya kumtosheleza kutoka kwa mtume(s.a.w.w) atakubali dini ya uislam.

Mtume(s.a.w.w) alimruhusu kuuliza maswali yake. kwanza yeye (naathal) aliuliza juu ya upwekee wa allah na sifa zake, na kupata majibu ya kumtosheleza. baadaye akauliza maswali, juu ya urithi wa mtume(s.avw.w) na wa kila mtume na utangazaji wa warithi wao (warithi wa mitume kabla ya muhammad(s.a.w.w) , kabla kufariki dunia k.m. nabii moosa alimteua yushae bin noon, mtume(s.a.w.w) akajibu "mrithi wangu mimi ni ali ibn abi talib, baada yake watakuwa wajukuu wangu wawili hassan na hussein na baada ya hao watakuwa maimam tisa ambao watatokana na kizazi cha hussein (a.s) ; nao ni warithi wangu". hapa huyo yahudi aliuliza majina ya hao maimam tisa na mtukufu mtume alisema "baada ya hussein atakuwa mwanawe ali ibni hussein, na baada yake atakuwa mwanawe muhamedl bin ali (baqir)na baada yake jaffer sadiq na baada yake mussa kadhim na baada yake ali ridha na baada yake muhamad taki na baada yake ali naqi na baada yake hassan na baada yake mwanawe muhammad mehdi.

Hayo ndiyo majina ya warithi wangu kwa mpangilio huo". Myahudi yule tena alimwomba mtume(s.a.w.w) amweleze hao warithi wake watatu yaani ali, hassan na husein watafariki dunia namna gani. Mtume(s.a.w.w) akamjibu "hadhrat ali (a.s) atauawa na upanga, hassan atapewa sumu na hussein atauawa kwa (kuchinjwa) huku ana njaa na kiu ya siku tatu". myahudi tena akamwuliza mtume(s.a.w.w) kama hao mashahidi watakuwa na mtume(s.a.w.w) huko peponi. Na hapo mtume(s.a.w.w) akajibu "hao watakuwa na mimi peponi". Hapo myahudi akakiri shahada takatifu, na akawa mwislamu, na akasema "eh mtume wa mungu bila shaka hao uliowataja ni warithi wako. Hao wametajwa kwa kirefu katika vitabu vya manabii waliopita na vilevile katika maagano ya nabii mussa. Imeelezwa wazi humo kwamba atakuwa nabii katika kipindi cha mwisho akijulikana kwa majina ya ahmad na muhammad na ndiye wa mwisho wa manabii na baada yake hatakuwa nabii yeyote.

Yeye (nabii) atakuwa na warithi kumi na wawili; wa kwanza ni binamu yake na mkwewe; wa pili na watatu watakuwa ndugu. Mrithi wa kwanza atauawa kwa upanga, wa pili kwa sumu na watatu atauawa jangwani pamoja na wanawe na masahaba wake wakiwa na njaa na kiu ya siku tatu. watakabili misiba yote kwa subira na watapewa jazaa na mungu na kutukuzwa na uwezo wa kuokoa marafiki na wafuasi wake kutoka kwenda motoni. walio biki lisa watatokana na kizazi chake (hussein) na kwa ujumla watakuwa kumi na wawili kama idadi ya "asbat". Mtume mtukufu(s.a.w.w) baadaye akamwuliza kama anajua habari za asbat. Yeye akajibu "ndiyo walikuwa kumi na wawili na katika hao lawa bin barkhya alighibu na kujitokeza tena na kupigana na mfalme wa karastya na kumwua". Mtume mtukufu(s.a.w.w) akaendelea kusema: "kwa hakika yale yaliyo wakabili mayahudi yatajiri kwa wafuasi wangu. Mrithi wangu wa kumi na mbili ataghibu. katika siku hizo uislam utabakia kwa jina tu . Qur'an itasomwa kama kawaida ya dini lakini bila kufuatwa kwa vitendo.

Wakati dhulma (kufuru) itakapokuwa imetawala mrithi wangu wa kumi na mbili atajitokeza na kuufufua tena uislam, haki na insafu. watao bahatika ni wafuasi wale ambao wataomtii yeye (mehdi) na ghadhabu ya mungu itawasubiri wale ambao watamhalifu yeye (mehdi)." tena katika kitabu hicho, ukurasa 371, sura ya 77, kuhusu hadithi ya mrithi wa kumi na mbili ameeleza chini ya kichwa cha 'tahkik' (uthibitisho) kuwa: "imesimuliwa kwamba jabir bin saamra, mmojawapo wa masahaba wa mtume(s.a.w.w) , amesema kwamba uislam utadumu kwa sababu mrithi wangu wa kumi na mbili atakuwepo na warithi wangu wote watatokana na nambari ya qureish." vitabu vilivyo andikwa na bukhari, muslim na tirmidhi vinaeleza hadithi hiyo ilivyo. Zaidi ya hayo yahya bin hassan katika kitabu chake umdah ameelezea kwamba kuna hadithi 20 za mtume mtukufu(s.a.w.w) za kusimulia kwamba warithi wake kumi na wawili wote watatokana na mbari ya quraish.

Vitabu mashuhuri vya sunni kama vile vya bukhari na hamid vimesimulia hadithi tatu na. Tirmidhi vile vile kaandika hadithi moja juu ya jambo hilo. Muslim aandika kwamba abdi saad, sahaba wa mtume(s.a.w.w) alimwandikia samra kumwuliza kwamba alisikia hadithi yoyote kutoka kwa mtume(s.a.w.w) . samra katika jibu akaeleza kwamba siku ya ijumaa ambayo aslami alipigwa mawe mpaka akafariki, mtume(s.a.w.w) alisema uislam utaendelea mpaka siku ya kiyama na watakuwa warithi wake kumi na wawili baada yake na wote watatokana na ukoo wa quraishi. Hadithi nyingi zilizoandikwa katika vitabu vya sunni zathibitisha kuwapo kwa warithi kumi na wawili waliotajwa na mtume(s.a.w.w) wanatokana na ukoo wa quraishi. Kwa hakika warithi kumi na wawili waliotajwa hawawezi kuwa wengine ila wale tu wanaokubaliwa na mashia ithnaasheri. hawawezi kuwa na uhusiano wowote na makhalifa wa bani umayya kwa sababu hawakuwa kumi na wawili na ambao walikuwa wadhalimu ila mmoja omar bin abdulaziz ambaye alikuwa mwema. Vile vile hao bani umayya hawakuwa katika kizazi cha hashim kama ilivyoelezwa katika hadithi nyingi za mtume(s.a.w.w) . vile vile hawawezi kuwa makhalifa wa bani abbas kwa sababu hawakuwa kumi na wawili na walikuwa madhalimu na maadui wa ahlul-bait wa mtume(s.a.w.w) .

Hivyo, uhakika ni kuwa warithi kumi na wawili waliotangazwa (tajwa) na mtume(s.a.w.w) ni maimam kumi na wawili kutokana na dhuria ya mtume(s.a.w.w) na katika uhai wao hawakuwa na mtu yeyote aliyelingana nao katika elimu, ibada, atakuwa na ushujaa. hakuna wengine wanaostahili sifa zilizoelezwa kutokana na hadithi za mtume(s.a.w.w) isipokuwa hao maimam kumi na wawili. tena katika kitabu hicho hicho sura ya 78, ukurasa 374, mwandishi amenakili: "katika kitabu faraedussimtayn imeelezwa kwamba mtume mtukufu(s.a.w.w) ameeleza bayana kwamba yeyote asiye amini katika kujitokeza kwa mehdi ni kafiri na yeyote asiye amini kuja kwa nabii issa kutoka mbinguni vile vile ni kafiri na yeyote asiye amini kujitokeza kwa dajjal mwenye jicho moja tu vile vile ni kafiri."

zaidi ya hayo, katika kitabu hicho hicho imesimuliwa hadithi kutoka kwa mtume mtukufu(s.a.w.w) iliyo andikwa na ibnu abbas kwamba yeye (mtume) amesema "watakuwa warithi kumi na wawili baada yangu ambao watakuwa hujjah (dalili) ya mungu juu ya viumbe wake. Wa kwanza atakuwa hadhrat ali(a.s) na wa mwisho hadhrat mehdi(a.s) . wakati huo wa mehdi(a.s) ardhi itang'aa na utawala wake utaenea kote kote duniani".

Waislamu wote, mashia na masunni, huamini kwamba watakuwa warithi kumi na wawili wa mtume(s.a.w.w) . hivyo imebainika kutokana na hadithi mashuhuri kwamba warithi wa kweli kumi na wawili kufuatana na hadithi za mtume(s.a.w.w) ni wale kumi na wawili wanao kubaliwa na shia ithnaasheri; wa kwanza ni ali ibn abi talib (a.s) na wa mwisho wao ni imam wa kumi na mbili imam hadhrat muhammad mehdi(a.s) . hata hivyo, kuna hadithi mbili katika vitabu vya sunni zinazonakili majina ya maimam kumi na wawili. Itabainika kuwa kukamilisha idadi hiyo ya kumi na wawili, hadithi hizo zinamtaja muawiyya pamoja na mwanawe yazid n.k. ambao hawastahili kuitwa warithi wa mtume(s.a.w.w) . mulla alikari katika kitabu cha 'sharhe mishkat' na tena katika kitabu 'sharhe akber' amenakili majina kumi na mbili y amakhalifa wanao aminiwa na masunni.

1) Abu Bakar

2) Omar

3) Othman

4) Ali bin Abi Twalib(a.s)

5) Muawiyya

6) Mwana wa muawiya Yazid

7) Abdul Malik bin Marwan na wanawe wane

8) Walid

9) Suleiman

10) Hisham

11) Yazid

12) Omar bin Abdulaziz.

Suyut katika kitabu 'tarikhul khulafaa' (historia ya makhalifa) amenakili kutoka sahihi bukhari na sheikhul islam ibnu hajar kuwa: "kutokana na hadithi zinazo kubalika, waislamu wanakubaliana kuwepo makhalifa wafuatao:

1. Abubakar

2. Omar

3. Othman

4. Ali bin Abi Twalib(a.s) na baadaye hapakuwa na makubaliano juu ya urithi wa imam hassan(a.s) kulikuwa na mapatano ya kumkubali

5. Muawiya na baadaye imam hussein(a.s) ambaye hakurithi kwa sababu aliuawa "shaheed", kwa hivyo

6. Yazid alikubaliwa na watu wakala kiapo cha utii kumkubali yeye yazid. baada ya kifo cha yazid kulikuwa na mafarakano juu ya urithi lakini wengi wakamkubali abdul malik baada ya kuuawa ibnu zubeir. (baada ya yazir marwan alitawala kwa muda ya miezi sita tu na mwanawe abdul malik aliendelea kwa miaka 21 lakini wote wawili hao hawakuorodheshwa).

katika orodha ya makhalifa kutoka taarifa tuliyotaja kwanza abdul malik ametajwa ni khalifa wa saba lakini katika orodha ya pili ya makhalifa hakutajwa kabisa.

7. Baada ya yazid wana wanne wa abdul malik wanakubaliwa kuwa warithi, nao ni walid

8. Suleiman

9. Yazid

10. Hashim na baada ya hao

11. omar bin abdulaziz (kama alivyoorodheshwa wa kumi na mbili katika orodha ya kwanza kutokana na hadithi)

12. walid ibnu yazid ibnu abdul malik bin marwan (ambaye kutokana na hadithi iliyotajwa atakuwa khalifa wa kumi na tatu).

kwavyo, huthibitika kutokana na maandishi ya waislamumashuhuri na hadithi za kuaminika kwamba maimam kumi na wawili wanaofuatwa na shia ithnaasheri ni warithi wa kweli. katika hao wa kwanza ni hadhrat aii ibn abi talib(a.s) na wa mwisho ni hadhrat mehdi(a.s) ..


5

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 5

HADITHL KUHUSU KUWEPO KWA IMAM WA ZAMA HIZI

Hadhrat Mahdi(a.s) wanazuoni wengi mashuhuri wa madhehebu ya kisunni wameandika kuhusu kuwapo kwa hadhrat mehdi(a.s) katika vitabu vyao. kati ya hao tunaorodhesha majina ya wanazuoni 14:

1) Shaikh Kamil Abdul Wahab Sharam.

2) Mulla Ali Asadullah Akbar bin Mawdudi.

3) Mulla Nurdin bin Abdulrahman bin Ahmad jamii.

4) Khaja muhammad parsa, Ahmad bin Mahmoud Al hafizi.

5) Sheikh Abdul Haqi Muhadith Dehlawi,

6) Allama Sheikh Nuruddin bin Sabag Maliki.

7) Shah Waliyullah Muhaddis Dehlawi.

8) Allam Hamwayn Shafi'i mwandishi wa Faraidu Simtayn.

9) Sheikh ata Naishapuri.

10) Sheikh Kabir Shamshudin Tabrizi.

11) Sheikh Neimkillah Al Walli.

12) Sheikh Kamil Arif Matuk Misri.

13) Sheikh Saad bin Hamawi.

14) Shaik Suleiman bin Ibrahim Balkhi Kunduzi sheikhul islam wa Istambul (uturuki) na mwandishi wa wa kitabu kinacho julikana sana katika madhehebu ya sunni Yanabiu Al-Mawaddah.

Waandishi hao wote wameandika katika vitabu vyao kuwa mwana wa hadhrat Imam hassan askari(a.s) , hadhrat Mahdi(a.s) yu hai na ameghibu.

Licha ya hayo wanazuoni wengi wengine wamenakili taarifa kama hizo katika vitabu vifutavyo:

1. Kitabu cha Jaamiul- Usul, kikitumia ushuhuda uliopo katika Bukhari, Muslim. Abu Dawood na Tirmidhi wamenakili matamshi ya Abu Hureira kwamba: Mtume(s.a.w.w) alisema:"Miongoni mwa wafuasi wangu kikundi kimoja kitatangaza jihadi ya kushinda vita vyote. hapo nabii Issa atateremka kutoka mbin guni na kiongozi wa hicho kikundi hadhrat mehdi (a.s) atamkaribisha nabii Issa kuongoza swala ya jamaa lakini nabii Issa atajibu "wewe ndiye mwenye mamlaka (madaraka) juu ya viumbe wa Mungu na kutokana na dhuria ya mtume Muhammad (s.a.w.w) Mwenyezi Mungu amekutunukia heshima na ubora kuliko waumini wote wa wakati huu". kanji, mfuasi wa ushafi'i, vile vile amenakili hadithi hii na ametilia mkazo kwamba hadithi hiyo ni sahihi.

2. Hafidh Abu Nairn na Tabarani katika kitabu chao Muazamu -akber wamenakili kwamba mtume muhammad(s.a.w.w) amesema: "Baada yangu watakuja makhalifa ambao baadhi yao watakuwa watawala na baadhi yao watakuwa wafalme dhalimu.

Baada ya hapo atakuja mehdi kutokana na kizazi changu kama mungu alivyoahidi na atatokeza na kueneza unyoofu na uadilifu katika dunia hii.

3. mwanazuoni anaye aminiwa sana katika madhehebu ya sunni huko india obeidullah amratsari, amenakili katika kitabu chake arjahul ma talib, ukurasa 472, kwamba sheikh abu abdullah na muhammad bin yusufu kanji shafi katika kitabu chao al bayan fi akhbare-sahibuz-zaman ameandika kwamba hadhrat mehdi(a.s) yu hai na ameghibu na kuna sababu nyingi za kuthibitisha hayo. Kwa mfano nabii issa, nabii idris na nabii ilyas ni mitume ambao wamekuwa hai kwa miaka maelfu na vile vile katika maadui wa mungu, dajjal na iblis watakuwa hai mpaka muda maalum; kwa hivyo hakuna cha kustaajabisha kwamba hadhrat mehdi(a.s) yuna umri wa miaka 1100.

4. Ibnu hajar hanafi makki katika kitabu chake sawaikul muhrika, ukurasa 481, ameandika kwamba jina la hadhrat mehdi(a.s) ni muhammad na majina mengine yake maarufu yanayo julikana ni: abul qasim na lakabu ni mehdi, saleh, qaaim, muntadhar, na sahibuz-zaman. wakati alipofariki baba yake hadhrat imam hassan askari(a.s) , imam mehdi(a.s) alikuwa na umri wa miaka mitano tu. mwenyezi mungu alimjaalia elimu hekima katika utoto wake. sababu ya kupatiwa lakabu ya qaaim ni kuwa yupo hai lakini ameghibu na maskani yake hayajulikani.

5. Katika kitabu hicho hicho, ukurasa 102, imeandikwa kwamba hadhrat mehdi(a.s) atajitokeza kabla kurudi (kuteremka kutoka mbinguni) nabii issa. katika hadithi nyingi mtume mtukufu(s.a.w.w) amesisitiza kwamba hadhrat Mahdi(a.s) atatokana na kizazi chake na baada ya kujitokeza atatawala kwa muda wa miaka saba na kustawisha insafu duniani na baada ya muda mfupi tu nabii issa atateremka kutoka mbinguni na hadhrat mehdi(a.s) atamwua dajjal.

Kuna hadithi nyingi kuhusu hadhrat mehdi katika vitabu vinavyojulikana sana katika madhehebu ya sunni lakini bado baadhi ya wanavyuo wa kisunni wanaamini kwamba hadhrat medhi hajazaliwa bado na baadaye ndiyo ataeneza insafu duniani. ijapokuwa hiyo ni baadhi ya imani ya maulamaa wa kisunni, lakini kutokana na wingi wa hadithi na ushahidi wa kihistoria ni dhahiri kwamba hadhrat mehdi(a.s) alikwisha zaliwa tarehe 15 shaban 255 a.h. kwa hiyo, si jambo la kubishana tena juu ya kuzaliwa kwake. mwanazuoni wa kuaminika mno wa kisunni, muhammad yazeed hafiz bin maajah (aliyefariki dunia 273 a.h.) katika kitabu chake sunan ibni maajah ameandika (kurasa 518/519) kwamba zipo hadithi nyingi za mtume muhammad(s.a.w.w) kuhusu hadhrat mehdi(a.s) kuwa atatokana na dhuria yake na kizazi cha binti wake fatima(a.s) . atakuwa ameteuliwa kwa amri ya allah na atakuwa mrithi wake. Mtume mtukufu(s.a.w.w) tena amewataradhia waislamu wote kwamba wakipata bahati ya kuonana naye (kuwa hai katika karne ya hadhrat mehdi(a.s) basi wamtii yeye. vile vile ameeleza kwamba hamza, jaffar, ali, hassan, hussein na mehdi watakuwa viongozi huko peponi.

Imam Ahmad bin Hambal (aliyefariki 240 a.h.) mwandishi maarufu wa vitabu vya kisunni amearidhia katika sehemu ya kwanza ya kitabu chake musnad, ukurasa 99, kwamba imesimuliwa kuwa "mwenyezi mungu atamleta mehdi(a.s) aliyetokana na dhuria yangu kutoka mafichoni kabla ya siku ya kiyama, japokuwa ikibakia hata siku moja kabla mwisho wa dunia, naye ataeneza haki, usawa na usalama duniani na kutokomeza dhuluma na ukandamizaji." sheikh-ul-islam wa istanbul, sheikh suleiman nakshbandi hanafi, katika kitabu cha yanabeeul-mawaddah, katika ukurasa wa 494, amenakili masimulizi kutoka kwa jabir bin abdullah ansari kuwa Mtume(s. a.w.w) amesema: "Baada yangu watakuwa maimam 12; wa kwanza ni Ali, na watakaofuata baada ya Ali ni Hassan, Hussein, Ali bin Hussein, Muhammad bin Ali(a.s) (Baqir). Eh! Jabir wewe utabahatika kuonana na huyo Baqir(a.s) , tafadhali mpe salam zangu. Na baada yake, Jaffar bin Muhammad. Mussa bin Ali bin Muhammad, Hassan bin Ali na Baada yao atakuja msubiriwa Mahdi(a.s) . Mahdi atakuwa mrithi wa kumi na mbili na wa mwisho. yeye atakuwa na jina langu na lakabu ya kassim. atakuwa mwana wa Hassan bin Ali, Al-Askari.

ahmad bin hajar makki katika kitabu chake sawaikulmuh-rika, ukurasa wa 116, na vile vile tirmidhi katika kitabu chake jame-a, ukurasa wa 33, wamenakili kwamba mtumemtukufu(s.a.w.w) amesema, "baada yangu watakuwa warithi wangu kumi na wawili ambao watakuwa makhalifa wangu na hao wote watatokana na mbari ya quraishi".

Sheikhul-kamil, Abdul Wahab, amearidhia katika kitabu chake yawakit wa jawahir kuwa, "wakati dunia itapojaa ukandamizaji na ukafiri ndipo hadhrat mehdi(a.s) atatokeza. yeye (hadhrat mehdi(a.s) ni mwana wa hadhrat hassan al- askari(a.s) , alizaliwa tarehe 15 shaaban 255 a,h. na yupo hai duniani. wakati nabii issa atapoteremka kutoka mbinguni yeye (mehdi a.s.) atatokeza na kuishi naye; wakati wa kuandika kitabu hiki umri wake (hadhrat mehdi a.s.) ulikuwa umekwisha timia miaka 1146."

Abu Abdullah muhammad bin muhammad bin yusuf muhammad bin kanji shafii amenakili katika kitabu chake "kifayya tut-talib" kuwa: "haiwezi kupingwa kwamba hadhrat mehdi(a.s) yu hai hadi leo. Dalili kwamba yeye anaweza kuwa hai kwa muda mrefu inatokana na uhakika kwamba manabii issa, khidhr na elias wapo hai duniani kwa miaka elfu kwa maelfu. Hao ni manabii wa mungu, lakini maadui wake (mungu) pia kama dajjal mwenye jicho moja na lblis aliye laaniwa wapo hai hadi leo kama ilivyo thibitishwa katika qur'an.


6

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 6

HADHRAT MAHDI (A.S.) NI IMAM WA KUMI NA MBILI

Kuna hadithi nyingi mno katika madhehebu ya shia ithnaasheri kuthibitisha kwamba hadhrat mehdi(a.s) ni imam wa kumi na mbili. katika sura hii tutanakili mateuzi machache kutoka vitabu vya kisunni na vya ismaili, wafuasi wa agakhan, kuthibitisha ukweli huo. Waislamu wote wanakubaliana kwa kauli moja ukweli wa hadithi ya mtume mtukufu(s.a.w.w) kwamba baada yake idadi ya warithi wake itakuwa kumi na wawili. mwandishi wa kisunni abdul wahab katika kitabu chake "Al- yawaqit wal Jawahir" amenakili kuwa "wakati dhuluma na kufuru itapozagaa duniani hadhrat mehdi(a.s) atatokeza, yeye ni mwanae imam hassan askari(a.s) alizaliwa tarehe 15 shaaban mwaka 255 (a.h) na ataishi mpaka atapokutana na nabii issa."

Shaikhul islam, mwanazuoni wa kisunni Ahmed Jami, katika kitabu chake 'nafsatulanas' katika lugha ya kiajemi amesimulia kishairi, kwa mapana na marefu majina ya maimam kumi na wawili na ameeleza kwamba: "hadhrat imam Hassan askari(a.s) ni mwanga unaoongoza dunia na mwanae hadhrat mahdi(a.s) hana kifani duniani. molvi jallaludin rumi katika tenzi zake za "divan" ametaja majina ya maimam kumi na wawili na kuthibitisha kwamba hadhrat mehdi(a.s) ni imam wa kumi na mbili.

Katika 'Tadhkiratul Kiram' ya Molavi shah mohamed kabir, ukurasa 270, imearidhiwa kutoka masimulizi sahihi kwamba kutakuwa na urithi wa namna mbili: moja bayana na moja ya kisiri (kufichika), urithi wa namna moja tu utaendelea mpaka

Imam Hassan Al-askari(a.s) , lakini baada yake namna zote mbili zitatokeza na hapo baadaye imam wa kumi na mbili atafuata.

Shah Abdul Aziz na imam ghazali katika' Ihyaul-uloomm. mulla moin katika 'dirasatul labib na ibne Hajar As-kalani katika 'FAthul Bari wote ambao wanazuoni mashuhuri wa kisunni wanakubaliana kwa pamoja kwamba elimu ya maimam kumi na wawili hutoka kwa allah moja kwa moja. maimam kumi na wawili pamoja na mtume mtukufu(s.a.w.w) na binti yake fatima(a.s) ni watakatifu kikamilifu (masumin) na kuhusu hao kumi na wanne kuna makubaliano ya kauli moja baina ya waislam kwamba tokea kuzaliwa mpaka kufa kwao hawakutenda dhambi ya aina yoyote wala kukosea. (tarikhul islam, .juzu 1, ukurasa 29).

Katika kitabu chake kiitwacho 'Kanzul Masaib" kurasa 9-10 na 22 na 23, aga khan, his highness hassanali shah saheb amearidhia juu ya imani ya maimam kumi na wawili. uthibitisho wa ziada umeelezwa katika hukumu iliyotolewa na jaji maarufu wa kiparisi katika daawa ya "mahuwa commission" ambayo imenakiliwa kwenye ukurasa wa 56 kuwa: "kanzul Masaib" ni kitabu cha lugha ya kiajemi (irani) na imeandikwa kwa amri na msaada wa muadham muhammad hassan el husseini. Mualifu wa kitabu hicho ni Ibrahim Isfahani na kitabu hicho kilichapishwa mwaka 274 a.h. katika kurasa 22 na 23 za. kitabu hiki majina ya maimam kumi na wawili yametajwa bayana".

Ibratulafza' ni kitabu katika lugha ya farsi kilicho andikwa na agakhan i kuhusu maisha yake mwenyewe. mateuzi hayo yalitafsiriwa katika lugha ya gujarati mwaka 1865 b.k. na bawana karim dadaji na kuchapishwa na oriental press bombay. Katika ukurasa 19, ameandika, "kwa karne nyingi baba zangu walikuwa na vyeo vya uwaziri katika serikali ya misri. wao walikuwa wanafuata kanuni za imani ya jaafery na sheria zilizowekwa na maimam kumi ria wawili."

Aga Jahangir shah mwana wa aga khan i, amechapisha risala yake kuhusu ibada katika farsi. Hiyo ilichapishwa na datprasad printers bombay mwaka 1313 a.h. humo yeye ameandika kwamba: mimi natoa ushahidi kwamba hadhrat ali murtadha(a.s) na wanawe (watoto wake kutokana na kizazi chake) kumi na moja ni warithi wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) na kila mmoja ni imam wa kweli (haki). kutokana na mateuzi hayo matokeo ya 'mahuwa commission ukurasa 57 imearidhia kuwa: "aga khan wa karne hii amekubali mahakamani ukweli wa mateuzi hayo. zaidi ya hayo kulikuwa na ushahidi kwamba mama yake aga khan bibi alishah na mkewe vile vile wakiamini maimam kumi na wawili.

Aga Khan wa pili, his highness aga ali shah, alitoa mateuzi yake kuhusu kanuni za swala na mfungo wa ramadhani katika lugha ya kisindhi. kwenye ukurasa wa 15, mstari wa 17 katika "mahuwa commission report," kumeelezwa kuhusu maamkizi kwa imam wa kumi m mbili(a.s) . vile vile mstari wa 17 ukurasa 34 kuna maagizo kuhusu maamkizi kwa imam hussein(a.s) .kadhalika, katika mstari wa 6 ukurasa 35 kumeelezwa juu ya maamkizi kwa imam wa kumi na mbili. kwenye ukurasa huohuo, mstari wa kumi, unatoa amri ya kum womba mungu kwa kutaja majina ya "Muhammad, Ali, Fatima, Hassan, Hussein watakatifu mahsusi na pamoja na maimam tisa walio tokana na dhuria ya imam hussein. zaidi ya hayo mtu ataka dalili (uthibitisho) gani?

Varas wa Junaghat (india) kassambhai ismail alimwandikia barua mfawidhi wa jamnagar (india) kassambhai devji kuthibitisha kwamba siku hizo makhoja ismaili wafuasi wa aga khan wakiamini maimam kumi na wawili na watakatifu kumi na nne na vile vile wakitoa maamkizi kwa imam wa nane. mateuzi halisi katika barua hiyo ni yafuatayo "jamnagar 927-55 shah peer amjalie mfawidhi kassam devji raha milele. kutoka varas kassam vares ismail wa jamnagar na tafadhali kubali salaam zake. pili, khudavand, maadham, his highness, ameandika barua kutoka zanzibar tarehe 19 shravan kwamba khudavand ataondoka zanzibar kwenda mombasa tarehe 20 septemba na baadaye atawasili india na ameamrisha jumuia zote na kamadia wote wajulishwe kwamba:

a) Maelezo kuhusu tukio la karbala yasisomwe kila mara, lakini yasomwe katika siku za muharram tu, na maamkizi kwa imam hussein baada ya hotuba yaendelee, lakini maamkizi mawili kwa imam ar-ridha(a.s) na muhammad mehdi(a.s) yasiendelee.

b) Baada ya majlis maamkizi moja tu yaendelee kuelekea magharibi.

c) katika kumbukumbu na vitabu vinavyowekwa na jamati (jumuiya) au kumbukumbu za hesabu zinazo hifadhiwa na mfawidhi au katika kumbukumbu za ndoa, majina ya maimam kumi na wawili pamoja na watakatifu kumi na wanne yasitumike tena. Juma mosi tarehe 17 bhardva 1956 kassam ismail.

katika mwaka 1941 wa hindoo; aladin gulamhusein, mfuasi madhubuti wa aga khan, alichapisha kitabu chake kisindhi, katika gulamhussein press ambacho sasa hakipatikani (kimezuiliwa). imeandikwa: "huko mtume, amirul mumiiin mola murtadha Ali na maimam kumi na wawili pamoja na malaika jibraeel na israel watahudhuria." (kurasa 18-19). Katika kitabu hicho ukurasa 43 imearidhiwa "nuru ya pepo itamfikia yule ambaye atakuwa na imani juu ya upekee wa mungu na unabii wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) na atayefuata Ahlul-Bait na kutambua maimam kumi na wawili na hadhi ya waumini hao itakuwa ya juu.' (kimenakiliwa kutoka Risala ya Imam Ja’afer Sadiq. uk. 43).

Kwa kweli ijapokuwa sifa nyingi mno ziliturnika kwa ajili ya his highness, yeye hakukubaliwa kama ni imam wa wakati huu katika barua iliyoandikwa na varas kassam ismail. hii inathibitisha pasi shaka kwamba mpaka wakati huo aga khan hakuhesabiwa kuwa ni imam, bali ni peer tu (kiongozi). varas: ni cheo katika jumuia ya makhoja wafuasi wa aghakhan. majlisi: mkutano maalum panapodhikiriwa kisa cha karbalaa.


7

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 7

KUTAJWA KWA HADHRAT MAHDI (AS.) KATIKA GINAN ZA PEER (VIONGOZI) (NYIMBO ZA DINI ZA WATAKATIFU WA KIISMAILI)

Katika kitabu cha Sala ya waismailia, wafuasi wa Aga Khan, kiitwacho so ginan, sehemu ya kwanza ukurasa 70, katika sala ya nne ya peer shams imeandikwa kwamba huyo mehdi aliyetakasika atakuja amepanda farasi duldul.

Katika kitabu hicho hicho, sehemu 2, ukurasa wa 3, katika sala ya peer ismaili shah yafuatayo yameandikwa: "yeyote asiyemtambua mehdi shah atahesabika hakuelimika (mjinga) na atakabiliwa na hasara duniani na akhera na hataokoka. mehdi ataua makafiri wote na atafundisha qur'an na kufuta ujinga."

Katika kitabu hicho hicho sehemu ya 6, kuna sala za peer hassan kabirdin ambaye amearidhia "imam wa mwisho imam Mahdi(a.s) atakuja. Yeye (Mahdi) ni mtakatifu mno na watakaomfuata watakuwa wamebahatika. Wa kwanza ni ali(a.s) , mwisho ni mehdi(a.s) ambaye ni imam mtukufu. Yeyote atayemkataa na kutomfuata yeye (Mahdi) aamali (sala zake) hazitakubaliwa."

Sala nyingine ya peer Hassan Kairdin, katika kitabu hicho hicho inasema: "Mahdi aliye shujaa atafundisha kiarabu na jina lake litakuwa Mahdi Shaah. yeye atawaua iblis na Dajjal na kutawala bara zote duniani."

Tanbihi: wadanganyifu wote waliodai kuwa wao ni mehdi hawakuweza kutawala hata kijiji kidogo licha bara zote duniani. Kutokana na hizo sala zote nne zilizotajwa uhai wa hadhrat mehdi(a.s) umethibitika na kuja kwake kutawala ulimwengu na kuleta usawa na amani vile vile kumebitika.

SURA 8

KUZALIWA KWA HADHRAT MEHDI (A.S)

Mwenyezi Mungu amesema katika qur'an:

يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّـهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ ﴿٣٢﴾

" Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia."(9:32).

Maadui wa allah hawakuacha jambo lolote katika jitihada zao za kumwumbua mtume mtukufu(s.a.w.w) na ahlul-bait wake(a.s) . wamewaua kwa kuwachinja au kwa kuwapa sumu dhuria ya mtume(s.a.w.w) moja baada ya mmoja, iakini "nuru" imeendelea kuangaza na itaangaza hadi siku ya kiyama. khalifa mo'tamid aliyekuwa katika makhalifa wa bani abbas alimweka kizuizini imam wa kumi na moja, hadhrat imam hassan askari(a.s) , miaka mingi gerezani. alikuwa ana habari kamili juu ya hadithi ya mtume muhammad(s.a.w.w) kwamba imam hassan .askari atapata mwana hadhrat mehdi(a.s) na huyo ataanzisha na kustawisha utawala wa dhuria ya mtume(s.a.w.w) ulimwenguni na kuangamiza maadui wa Ahlul-Bait na wa mtume(s.a.w.w) . kwa hivyo alimweka imam hassan askari (a.s) gerezani kwa muda mrefu sana ili kuzuia bishara ya mtume(s.a.w.w) .

Firaun alidai kwamba yeye mungu. wanajumi walimshauri kwamba kutokana na kizazi cha bani israel atazaliwa mtoto ataye angamiza ufalme wake, kumwua yeye (firaun), wafuasi na masahaba wake. kwa hiyo firaun aliweka ulinzi mkali juu ya wanawake wa bani israel. kila mtoto akizaliwa akiuliwa ili kuzuia kuzaiiwa kwa nabii musa. Hata hivyo, alivyotaka mungu ikawa. nabii musa alizaliwa katika nyumba hiyo hiyo ya firaun. Licha ya kuzaliwa tu, hata kalelewa nyumbani mwa firaun. kama vile alivyo firaun, mo'tamad alitaka hadhrat mehdi(a.s) asizaliwe. Lakini hakuna mtu anayeweza kufaulu kuzuia amri ya mungu.

Katika kipindi imam hassan askari(a.s) alipokuwa kizuizini kulitokea ukame mkali sana samarra. kwa muda mrefu hapakunyesha hata tone moja la mvua. waislamu waliswali swala maalum ya kuomba mvua inyeshe lakini hawakufanikiwa.

Wakati waislamu wote walipokusanyika nje ya jiji la samarra, padri mmoja wa kikristo akanyanyua mikono yake kuomba mungu na papo hapo mawingu yakakusanyika na myua ikanyesha kidogo. Kuona hivyo waislamu wote walibabaika. Wakaanza kupatwa na wasiwasi kwamba labda ukristo ni dini ya kweli. Khalifa papo hapo akaitisha baraza lake na kuchukua ushauri wa wanavyuo, mawaziri na maofisa wake. Wote walipigwa butaa. Mmoja wa washauri wake akatoa wazo kwamba yuko mwokozi mmoja tu ambaye anaweza kuwaokoa, naye ni imam hassan askari(a.s) ambaye alifungwa gerezani. khalifa alikuwa na hakika (yakini) juu ya elimu, ukweli na uimam wa imam hassan askari(a.s) na haki yake ya utawala (ukhalifa). akamwita imam hassan askari katika baraza la kifalme.

Hadhrat imam hassan askari(a.s) alipofika kasri, khalifa akasimama kwa taadhima, akamkaribisha, na akamkalisha karibu na kiti cha kifalme na kumweleza mambo yote. Imam akasema "usiwe na wasiwasi. Hilo si jambo kubwa. Waamrishe waislamu wote wakusanyike nje ya jiji kesno ili waswali na kuomba mvua inyeshe. Na wakati huo huo mwamrishe huyo padri wa kikristo alike". Kesho yake waislamu wote pamoja na yule mkristo walikusanyika huko. Imam akamwambia huyo padri aombe mungu na papo hapo mawingu yakakusanyika. Irnam akamwomba khalifa kumtuma mtu akalete kile kitu padri huyo alichoficha katikati ya vidole vyake. Khalifa aliamrisha afisa wake akamnyang'anye mfupa uliofichwa katikati ya vidole vya padri, na akamkabidhi imam hassan askari(a.s) . imam Hassan Askari(a.s) akaufunika huo mfupa katika leso na kuiweka hiyo leso mfukoni mwake. papo hapo mawingu yaliyokusanyika yakatawanyika. Hapo hadhrat akamwambia huyo padri amwombe mungu ili inyeshe mvua. Padri huyo alijitahidi sana kumwomba mungu lakini hakufanikiwa hapo imam akamjulisha khalifa kwamba ule mfupa ulikuwa wa nabii mmojawapo na wakati wowote unapowekwa chini ya mbingu basi mawingu hukusanyika imam akiwaongoza waislamu katika swala akanyanyua mikono yake mitakatifu. Papo hapo mawingu yakakusanyika pande zote. Imam akawaamuru watu waende makwao na baadaye mvua kubwa ikanyesha. imam na khalifa walirudi kitaluni na hilo lilikuwa jambo pekee likizungumzwa na kila mtu. Khalifa alifurahi mno kwa sababu uislam ulinusurika.

Khalifa na watu wote waliamini mafaa ya swala, ukweli na utawala wa imam. Baada ya muda imam(a.s) akaondoka. Khalifa alipomwuliza alikokuwa anaelekea imam akamjibu kuwa alikuwa anarudi kifungoni alimo wekwa na khalifa. Kusikia hayo, khalifa aliona haya sana na akasema, "eh mjukuu wa mtume, tafadhali rudi nyumbani kwako". Hapo imam alirudi nyumbani kwake. Katika muda huo narjis-khatun (mama yake imam wa kumi na mbili akawa mja mzito).

يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّـهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ ﴿٨﴾

"Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia." (61:8).

Jina la mama yake hadhrat mehdi(a.s) hasa lilikuwa narjis khatun. majina yake mengine yalikuwa malika, sausan na 'rayhana. Yeye ni mjukuu wa mfalme wa utawala wa uturuki. Historia ya kuvutia ya narjis khatun kufika samarra ni kama ifuatavyo: imesimuliwa na bashir bin suleiman kuwa: "niliitwa na imam ali naqi (baba yake imam hassan askari(a.s) , imam wa kumi na kuambiwa: 'wewe ni katika kizazi cha wasaidizi wetu na marafiki zetu. Nitakupa shughuli muhimu kwa sababu mimi nina imani na wewe: mimi nilimwomba aniamrishe tu kwa sababu nilijiandaa kutimiza anachotaka. ameniambia kwamba anahitaji kumnunua kijakazi.

Akaniamrisha niende baghdad kwa ajili ya shughuli hiyo, na nitapofika huko niende kwenye ukingo wa mto. Huko mimi nitaona majahazi mengi na mateka wa kike wakiuzwa. Mimi niende kwa mtu mmoja aitwaye omar bin yazid ambaye atakuwa na mtekwa wa kike aliyevaa nguo mbili za hariri. yeye (huyo mtekwa wa kike) atakataa kuuzwa kwa mnunuzi yeyote na atakuwa anazungumza lugha ya kituruki. Imam ali naqi akanipa dinar 120 akaniambia kwamba mwuzaji atakubali kumwuza huyo mtekwa kwa hiyo bei. Vile vile alinipa barua ya kumpa huyo mtekwa wa kike.

Mimi nilikwenda baghdad kama nilivyoagizwa na kwa alama nilizo elezwa na imam ali naqi, nilimtambua huyo mtekwa na nikampa barua. kusoma barua hiyo tu huyo bibi machozi yalimjaa machoni mwake na akamwambia maliki wake kwamba hatakubali kununuliwa na mtu yeyote ila miye (bashir bin suleiman). Kwa hivyo nilirudi nyumbani (huko baghdad) na huyo mtekwa ambaye aliweka barua hiyo juu ya macho yake na kulia sana. Nilimwuliza kwa nini anabusu hiyo barua na kulia wakati yeye ni mgeni kutoka uturuki na hamjui mwandishi wa barua hiyo. Yeye akasema: "Sikiliza, mimi ni mjukuu wa kaisar, mfalme wa uturuki na jina langu ni malika.

Jina la baba yangu ni yashua na jina la mama yangu ni shamunusafaa. baba yangu aliandaa mipango niolewe na mpwa wake. Siku moja aliwaita mapadri wote, mawaziri, viongozi na wafuasi wake, na kumkalisha mpwa wake juu ya kiti cha enzi ambacho kilipambwa na almasi na kumwomba padri afunge ndoa yetu. Padri alipoanza kufungua kitabu kutaka kufunga ndoa masanamu waliotundikwa ukutani waliporomoka na mwana mfalme (mpwa wa babu yangu) akazirai na kuanguka na kiti cha enzi kilivunjika vipande vipande. mapadri walitetemeka na kumwomba msamaha baba yangu mfalme, kwa sababu hawakutarajia kutatokea balaa hiyo.

Mfalme alihuzunika sana. Akaona ndoa hiyo ilikuwa na nuksi na kwa hivyo aliagiza kiti kingine cha enzi na kutundika masanamu tena ukutani. padri tena akaanza kufunga ndoa na tukio hilo hilo likatokea tena. waliohudhuria wote walishtuka sana na wakaondoka papo hapo. baba yangu alifedheheshwa sana na siku nyingi alikuwa hakutoka nje ya kasri.

Usiku huo huo nilimwona nabii issa katika ndoto. Yeye alikuwa pamoja na masahaba wake waliokuwa wamehudhuria sherehe ya ndoa yangu. kiti kirefu cha enzi kiliwekwa pahali palipo wekwa kiti cha mwana wa mfalme (aliyetaka kunioa) na kilikaliwa na mtu mkubwa mwenye uso uliojaa nuru. Baada ya muda mfupi tu niliwaona watu wenye nyuso za nuru na hapo nabii issa alisimama kuwakaribisha na kuwapa nafasi karibu yake. Nilimwuliza mtu mmoja anijulishe hao waliokuja walikuwa nani? nikaarifiwa kwamba hao ni mtume wa uislam pamoja na mrithi wake na maimam kumi na moja wanaotokana na dhuria yake.

Mtume mtukufu hapo akamwomba nabii issa kumcchumbia malika binti wa shamunusaafa mjukuu wake imam H assan askari ambaye uso wake uking'aa kwa nuru (ombi hilo lilifanywa kwa nabii issa kwa sababu malika alitokana na kizazi cha hadhrat shamoon mrithi wa nabii issa). Nabii issa akamwomba hadhrat shamoon atoe kibali chake na papo hapo hadhrat shamoon akakubali kwa kuona hiyo ni heshima kuu. Kwa hiyo ndoa yangu ikafungwa na imam hassan askari(a.s) . macho yangu yakafunguka ghafla na mimi nilijawa na furaha. Nilikumbuka hiyo ndoto. Hata hivyo niliogopa sana na sikumhadithia ndoto hiyo mtu yeyote. Hapo baadaye mimi nikaanza kuwa mgonjwa ona kumkumbuka imam hassan askari na hali yangu ikaanza kudhoofu. Safari moja nilimwona binti wa Mtume(s.a.w.w) mwana Fatima(a.s) na katika ndoto mimi nilisimama kwa taadhima na nikamweleza hali yangu na kutomwona imam hassan askari(a.s) . aliniamrisha nisome "shahada", nikawa mwislamu na baadaye kila usiku nilimwona imam hassan askari katika ndoto akinituliza. Mara moja imam hassan askari aliniambia kwamba babu yangu atatuma jeshi kuivamia nchi ya waislamu na mimi nibadilishe mavazi yangu niungane na jeshi kama mtumishi mmojawapo. Waislamu watashinda vita hivyo, na mimi nitatekwa na kwa hivyo niungane na mateka wengine, mpaka baghdad."

Mimi (bashir bin suleiman) niliposikia hayo nilijawa na furaha na nilimleta bibi narjis khatun samarra kwa imam ali naqi(a.s) . imam Ali naqi(a.s) alimkaribisha pia akamkabidhi kwa dada yake Halima Khatun. Baadaye imam ali naqi(a.s) alimwozesha bibi narjis khatun na mwanawe imam Hassan Askari(a.s) akawabashiria kwamba watampata mwana ambaye atakuwa hujjat (dalili) duniani wa kuthibitisha kuwepo kwa mungu. Wakati dunia itapokuwa imeghariki katika ukandamizi, uovu na ulaghai yeye atakuja kutawala na kuleta insafu na usawa. Imam Mahdi(a.s) alizaliwa samarra iraq alfajiri siku ya ljumaa tarehe 15 shaaban 255 a.h. nyumbani kwa baba yake mtukufu. Alizaliwa tohara na amekwishatahiriwa na uso wake ulivyojaa na nuru ambayo ilipenya paa na kuelekea mbinguni. Alipozaliwa tu, kwanza alisujudu na huku akiwa amenyosha kidole chake cha shahada kuelekea samawati na kuthibitisha upweke wa mungu na unabii wa mtume muhammad(s.a.w.w) na uimamu wa Ali(a.s) pamoja na warithi wake kumi kuwa ni maimam wa kweli. Hapo baadaye akamwomba mungu atimize ahadi yake.

Halima khatun, binti wa imam wa tisa, hadhrat imam mohammed taqi(a.s) , shangazi yake imam hassan askari(a.s) , akamnyanyua mtoto aliyezaliwa na kumpa baba yake ambaye alimpakata. Imam Mahdi(a.s) papo hapo akamwamkia baba yake ambaye alimjibu na akamwambia aendelee kusema kwa amri ya mungu. hapo tena hadhrat mehdi(a.s) akarudia kuthibitisha upweke wa mungu, utume wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) urithi wa maimam kumi na moja na kusoma aya ya qur'ani "tumekusudia kuwajalia jamala yetu wale ambao waliofikiriwa ni wanyonge duniani na kuwateua maimam na kuwafanya warithi duniani" (28:5). Hapo baadaye imam Hassan askari(a.s) akamrudisha huyo mwana kwa bibi Halima Khatun na Halima Khatun akamrudisha mtoto kwa mama yake. Mwana huyo alimwamkia mama yake vile vile. Katika Sherehe ya akika imam Hassan Askari(a.s) alimwamrisha wakili wake Othman Saidi Omari kuwagawia maskini nyama ya mbuzi 10,000 na mikate 10,000.

Kuna marejeieo mengi katika vitabu vya kisunni kuhusu kuzaliwa kwa hadhrat mehdi(a.s) . tuna nakili madondoo machache pamoja na ushahidi. mwanazuoni wa kisunni, ubeidullah amrat-sari katika kitabu chake sawanahe umry hadhrat Ali(a.s) ukurasa 433, kuhusu imam hassan askari(a.s) . ameandika, "hakuna mwana yeyote aliyeishi baada yake ila mwanawe aabdal qassim mohammad al-hujjat tu" zanabl katika kitabu chake tarikhul islam ameandika kwamba imam wa kumi na mbili amezaliwa katika mwaka 256 a.h.

Sheikhul Sislam wa istanbul, sheikh suleiman balkhi kanduzi, katika kitabu chake yanabiul mawaddah ameeleza bayana kuhusu kuzaliwa kwa hadhrat mehdi(a.s) kama vile maelezo yaliyomo katika vitabu vya ithnaasheri. Yeye ameandika kuwa hadhrat mehdi(a.s) alizaliwa mwaka 250 a.h. ambayo nitofauti kidogo na hiyo ilisababishwa na kosa la uchapishaji. katika kitabu maarufu sana cha kisunni tarikh ibnul khaladun juzuu la pili, ukurasa 24, mwandishi anaeleza "Mahdi(a.s) anaye subiriwa alizaliwa siku ya ijumaa tarehe 15 shaaban 255 a.h. na baba yake ni imam hassan askari (a.s.). 5) mulla abdur-rahman jami katika shawahidu Nubakhat, ukurasa 247, ameandika kuwa "mwana wa imam ridha ni muhammad, na mwanawe ni ali na mwanawe hassan na mwanawe ni muhammad mehdi(a.s) , huyu wa mwisho alizaliwa samarra 255 a.h.


8

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 9

IDDUL-BARAAH (KISMATU RIZKI)

Iddul-Baraah ambayo ni tarehe 15 shaaban ni usiku wa baraka na furaha kwa waislamu wote. usiku huo umependekezwa sana kwa ajili ya ibada na hasa Duau Kumail (dua ambayo imam Ali(a.s) alimfunza sahaba wake qumail ibne ziyad) na ziara (mamkizi) ya imam hussein(a.s) . mamilioni ya wanazuoni hukusanyika huko karbala katika usiku huo. waislamu duniani kote husherehekea usiku huo kwa kuwasha taa kwa wingi majumbani mwao ili kuzidisha utukufu katika kukumbuka na kusherehekea kuzaliwa kwa imam wa kumi na mbili. kuna hadithi nyingi katika vitabu vya sunni na shia kuhusu iddul-baraah na hapa tunanakili chache zinazohusika: kwanza, neno "baraat" katika lugha ya kiarabu lina maana ya "kumwachia huru," "kufungua," "kuruhusu" au "msamaha". kufanya ibada usiku huo humpatia mja rehema na msamaha wa mwenyezi mungu. mtume mtukufu(s.a.w.w) amesema kwamba:Usiku huo Mwenyezi Mungu hupanga riziki, umri wa kila mtu na orodha ya watu watao kwenda kuhiji mwaka huo.

Mtume(s.a.w.w) vile vile amesema kwamba:katika usiku huo Mwenyezi Mungu anawasamehe waumini wengi mno kuzidi hata manyoya ya kondoo wa kabila la kalb. akaongezea kunena kuwa:"Mwenyezi mungu hukubali ibada zote usiku huo, na kuwasamehe waumini wote ila tu wale wanao abudu miungu, wale ambao huanzisha mambo mapya"

Katika dini kinyume cha amri ya mwenyezi mungu, wale wanaodharau ndugu na jamaa zao, na waasi wanaoendelea kutenda maasi bila ya kutubia. Mtume(s.a.w.w) amewasihi wanafunzi wake kukesha usiku wa l5 Shaaban katika ibada na kumwomba mwenyezi mungu na kufunga siku ya pili kwa sababu mungu anawasubiri sana usiku huo kuwasamehe viumbe wake wanao kumbuka madhambi yao na kuomba toba na huwazidishia riziki yao wale wanao omba hivyo.

Imam Jaffar Sadiq(a.s) amependekeza kwamba mtu awe tohara kwa kukoga usiku huo ili uzito wa dhambi upunguzwe na vile vile kusoma ziara (maamkizi) ya imam hussein(a.s) ili asamehewe madhambi yake.

Imam Zainul Abidin(a.s) amesema: ikiwa mtu anatamani kuwaamkia manabii 124,000 basi siku hiyo azuru kaburi la imam hussein(a.s) na kusoma ziara yake (imam hussein) usiku wa 15 shaaban kwa sababu mitume wote pamoja na malaika wote wanazuru kaburi la imam hussein(a.s) . kwa hakika waliobahatika ni wale wanaokuwa karbala usiku huo na kuweza kusoma ziara ya imam hussein(a.s) .

Imam Muhammad Baqir(a.s) amesema kwamba: Baada ya 'lailatul Qadri' katika mwezi wa ramadhani, usiku wa 15 shaaban umebarikiwa zaidi kuliko nyusiku zote. Mwenyezi mungu ameahidi kukubali dua ya waumini na hatakataa ombi lolote ila tu ombi hilo likiwa kinyume cha amri zake. kwa kweli usiku huo mtu asomaye subhanallah, alhamdu lillah lailaha illallah, allahu akbar, madhambi yake yatafutwa na ibada yake kukubaliwa.

SWALA NA DUA ZILIZO PENDEKEZWA SANA

A. DUA-UL-KUMAIL.

B. SWALA YA RAKAA NNE (Kila baada ya rakaa mbili unatoa Salam)

katika kila rakaa baada ya suratul-Faatiha Utasoma Suratul-Ikhlas mara 100.

kuna swala na ibada nyingi zingine ambazo zimeelezwa katika vitabu vya ibada.

Kama ulivyo usiku huo, siku ya 15 shaaban vile vile imebarikiwa namo imependekezwa ibada na dua pamoja na kusoma ziara ya imam hussein(a.s) . sura 10.

Utoto (ujana) wa hadhrat Mahdi(a.s) mwenyezi mungu alimjalia hadhrat mehdi(a.s) hekima na ubora tangu kuzaliwa kwake. kama vile mitume issa na yahya walivyokuwa na maarifa na hekima, imam mehdi(a.s) pia alijaaliwa na uwezo wa kuonyesha miujiza, uwezo wa kusema na kusoma qur'an akiwa susuni bado. siku ya pili baada ya kuzaliwa hadhrat mehdi(a.s) , mhudumu mmojawapo, nasseem khatoon, alipokaribia susu yake alienda chafya. imam(a.s) kama vile ilivyo mila ya kiarabu akamwambia "mungu akuteremshie rehma" na akamweleza "mtu yeyote anaye enda chafya anahakikishiwa kwamba hatafariki kabla ya siku tatu kupita". mhudumu mwingine masr alipokaribia susu, hadhrat mehdi(a.s) alimwomba amletee sandali nyekundu. alipoleta sandali imam(a.s) akamwuliza "unanijua mimi?" mhudumu akajibu, "wewe sayyid yangu na mwana wa tajiri yangu." Imam akasema: "Mimi sikuuliza hayo. mimi ni imam wa kurni na mbili, imam wa mwisho. mwenyezi mungu atajaalia ushindi dhuria ya mtume mtukufu(s.a.w.w) kwa mkono wangu namimi nawafuasi wangu tutakomesha dhuluma na maafa duniani".

Siku arobaini baada ya kuzaliwa imam(a.s) , bibi halima khatoon alipokwenda kwa imam hassan askari(a.s) alishangazwa kumwona hadhrat mehdi(a.s) amekua kama mwana wa miaka miwili. imam hassan askari(a.s) akamweleza kwamba wana wa imam hukua kwa haraka kuliko watoto wengine. miujiza mingi ilionyeshwa na hadhrat mehdi(a.s) wakati yungali mtoto bado. mmojawapo ni kamaufuatao: ahmed bin ishak bin sadulashary anahadithia kwamba safari moja alikwenda kwa imam hassan askari(a.s) kutaka kumwuliza nani atakuwa imam baada yake. kabla hajamaliza kuuliza suala hilo, imam Askari(a.s) akasema "Eh Ahmad, Mungu haachi pengo la hujjah wake duniani na hujja wake atakuwepo mpaka siku ya hukumu na kwa sababu ya kuwepo kwake ndiyo Mwenyezi Mungu huteremsha rehema na kuepusha maafa ." baada ya hapo akauliza swali. hapo imam Hassan Askari(a.s) akamleta mtoto mmoja wa miaka mitatu mwenye uso uliojaa nuru na akamwambia Ahmad, "Eh Ahmad, wewe ni katika masahaba waaminifu na kwa hivyo ninakuonyesha mwana wangu; yeye ni hujjat wa mungu, imam baada yangu na mrithi wangu. Yeye ataeneza insafu na usawa duniani. " Ahmad aliposhangazwa na hayo akamsikia huyo mtoto akisema: "Eh Ahmad, mimi ni mrithi wa mwisho na maimam wa haki. dunia itaendelea kwa sababu yangu. mimi nitachukua kisasi na kuwaadhibu maadui wa dini. wakati dunia itapoghilibiwa na ulaghai, dhuluma, ukandamizaji na uovu, mimi nitajitokeza kwa amri ya mungu na nitatawala kwa insafu na usawa ."

Siku ya Shahada ya imam Hassan Askari(a.s) jiji zima la Samarra liligubikwa na huzuni. Hata mayahudi na wakristo walihuzunika. maduka yote yalifungwa. Imam Hassan Askari(a.s) alifariki dunia tarehe 8 rabiul awwal (mfungo sita) .mwaka 260 a.h. umri wake ulikuwa miaka 28-29. wakili wake, othman bin said, aliandaa mazishi ya imam hassan askari(a.s) . jeneza lilipokwisha kuwa tayari mashia (wafuasi wa maimam kumi na wawili) na waislamu wote, pamoja na wakuu wa jeshi walikutanika nyumbani mwa imam hassan askari(a.s) kuomboleza msiba huo. ndugu yake imam hassan askari(a.s) , baba mdogo wa imam mehdi(a.s) jaffar tawwab akajitokeza na kutaka kuongoza swala ya maiti.

Alisimama karibu na jeneza na watu wote walikwisha jipanga katika safu ili waswali. jaffer alipotaka kuanza swala, mtoto mdogo mmoja, uso wake uking'ara kama mbalamwezi akaja na kumwambia Jaafar "Eh baba mdogo, jongea mbali, mimi ninastahili zaidi kuliko wewe kuongoza swala ya maiti ya baba yangu mzazi". jaffar alikuwa hajawahi kumwona hadhrat mehdi(a.s) kabla ya hapo na kwa hivyo alibabaika na kurudi nyuma. hadhrat mehdi(a.s) akaongoza swala na kuondoka. hakuna mtu aliyeweza kujusuru kumwuliza chochote hadhrat mehdi(a.s) wala kuweza kuzungumza naye.

Baada ya kuongoza swala, hadhrat mehdi(a.s) alikwenda kuonana na mtumishi wa baba yake kwa jina la adyan na kumwuliza juu ya barua aliyopewa. adyan alimkabidhi barua hiyo imam mehdi(a.s) . kabla ya kufariki imam hassan askari(a.s) alimtuma adyan kwenda baghdad kupeleka barua na alimweleza kuwa atakaporudi na jibu yeye (imam hassan askari(a.s) atakuwa amekwishafariki dunia na kwa hiyo amkabidhi jibu mtu atakaye ongoza swala ya maiti na atakayedai barua hiyo kutoka kwake (adyan). alimwambia kuwa mtu huyo ndiye atakuwa mrithi wake na imam wa wakati huo.

Jaafar tawwab alijitahidi sana ili apate mali ya kaka yake pamoja na uimam. alikwenda mpaka kwa khalifa wa wakati huo kutaka msaada wake. lakini khalifa alimjibu kwamba kumpatia uimam haikuwa kazi yake ila shia wa nduguze wakimkubali na kumtambua ndipo jaffar ataupata uimamu. matukio mengi yalitokea katika utoto wa imam(a.s) , lakini hatusimulii katika kitabu hiki. imam zaman(a.s) katika kasri ya khalifa mu'tamid abbasi.

Mmoja wa wahudumu wa imam hassan askari(a.s) . ali bin zamahyar anasimulia kwamba kazi yake moja wapo ilikuwa kumleta imam mehdi(a.s) kwa imam hassan askari(a.s) kutoka ghorofa ya chini (sardab) ambako imam mehdi(a.s) akiishi na mama yake narjis khatun na baada yake kumrudisha tena huko chini (Sirdab). wakati baba (imam hassan askari(a.s) alipokuwa na mwanaye (imam mehdi a.s) na kuzungumza naye ali zamahyar alikuwa hawezi kufahamu mazungumzo hayo. siku moja tarishi kutoka kwa khalifa mu'tamid abbas alitumwa kwenda kwa imam hassan askari(a.s) kuleta salamu ya khalifa kwamba amepata habari kwamba imam hassan askari(a.s) amebarikiwa na mwana lakini hakumjulisha khalifa ili yeye (khalifa) aweze kushirikiana na imam kufurahia kwa kuzaliwa huyo mwana. kwa hiyo khalifa alikuwa anasubiri kwa hamu sana kumwona huyo mtoto. hapo imam hassan askari(a.s) akamwamrisha ali bin zamahyar kumleta huyo mtoto (imam mehdi(a.s) na kumchukua kwa khalifa. kusikia hayo ali zamahyar alijawa na hofu kwa sababu alikuwa na uhakika khalifa atamwua huyo mwana (imam mehdi a.s.). imam hassan askari(a.s) alipomwona ali zamhayar amehofishwa sana akamwambia asiogope kumpeleka huyo mtoto kwa khalifa kwa sababu allah mwenyewe atamhifadhi hujjat (dalili ya kuwepo kwa mungu.

ali Zamhayar anasema: "Mimi nilikwenda ghorofa ya chini na nikaona nuru iliyoje iking'aa usoni mwa imam mehdi(a.s) , nuru ambayo sikuwahi kuiona maishani mwangu. kiwaa kwenye shavu la kulia kiking'ara kama nyota. nilimbeba mabegani na nilipotoka nje ya nyumba niliona uso wake umetoa nuru ambayo ilimulika jiji la samarra mpaka mbinguni. wakazi wa mjini waliacha shughuli zao na kumwaangalia macho huyo mtoto (imam mehdi a.s.). wanawake na watoto walikuwa wakimchungulia huyo mtoto mwenye nuru, kutoka madirishani na ghorofani. punde si punde barabara zilijazana kwa watu na ilikuwa shida kwangu kupita nifike kwa mfalme. tarishi wa mfalme ilimbidi aniongoze njia nzima.

Nilipofika kitaluni niliona khalifa na washauri wake na walinzi waliaibika na ung'avu wa uso wa lmam mehdi(a.s) . mimi nikaenda moja kwa moja mpaka kwa mfalme na nikasimama upande wa kulia nikimbeba imam mehdi mabegani na kumkabili khalifa. baada ya muda mrefu waziri aliyesimama karibu na khalifa akamnong'oneza khalifa. mimi nilikuwa na hakika kwamba walizungumza juu ya kumwua imam mehdi(a.s) na hapo mwili wangu mzima ukatetemeka. khalifa papo hapo aliamrisha walinzi wake wamwue mtoto (imam mehdi a.s.). walijaribu kuvuta panga zao kutoka kwenye ala zao lakini panga hazikutoka.

Khalifa akasema hizo panga zimekwama kwa mazingaombwe ya mwana wa hashim (maimam wote wanatokana na ukoo wa bani hashim). kwa hivyo aliamrisha uletwe upanga kutoka beit al mal (hazina ya serikali) ambao hautaathirika na uchawi. upanga uliletwa kutoka beit-al-mal lakini huko pia ulikwama katika ala. khalifa pamoja na washauri wake walipigwa na butaa. hapo tena khalifa aliamrisha waletwe simba watatu wakali kutoka matundu yao. papo hapo wakaletwa hao simba.

"Mimi (Ali zamahyar) niliamrishwa nimweke mtoto (imam Mahdi a.s.) mbele ya simba hao. nilitetemeka nilipopewa amri hiyo katili. ghafla mtoto (imam mehdi(a.s) akaninong'oneza na kusema: "usiogope, niweke mbele ya simba hao." nikatimiza amri yake. nilishangazwa sana kuona kwamba hao simba watatu walinyanyua mikono yao na kunisaidia kumweka mtoto juu ya sakafu. baadaye wakasimama kwa taadhima mbele ya imam(a.s) huku wameinamisha vichwa vyao. simba mkongwe ghafla akaanza kusema katika kiarabu fasihi kuthibitisha upekee wa mungu, unabii wa mtume muhammad(s.a.w.w) na kutaja majina ya maimam kumi na moja na kumwamkia huyo mtoto (imam mehdi a.s.) na kuendelea, "wewe ni hujjat wa mungu duniani. mimi ninataka kushtaki kwako. hawa simba wawili vijana wanavamia chakula chote tunacholetewa na kuninyima hata hisa yangu, na ninaendelea kubaki na njaa."

mtoto (imam a.s.) akatamka adhabu ya dhuluma (kosa) hiyo na kusema kuwa hao simba vijana wageuke wakongwe na huyo mkongwe arudishiwe ujana wake na afya yake. Kabla imam(a.s) hajamaliza hayo matamshi simba wawili vijana wakazeeka na kudhoofu na yule mkongwe akageuka kijana na mwenye nguvu. kuishuhudia miujiza hiyo khalifa na washauri wake wote wakanadi allahu akbar kwa mshangao na msisimko. hapo khalifa akaamrisha kwamba huyo mtoto (imam a.s.) arudishwe kwa wazazi wake. mimi (ali zamhayar) nilimshukuru mola na nikambeba imam a.s. kurudi naye nyumbani. njiani barabara zote zilijaa watu na kila mtu alishangazwa na nuru ya imam(a.s) . nilipofika nyumbani nikamhadithia yote imam hassan askari(a.s) ambaye alifurahi na kumshukuru mungu."


9

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 11

KUGHIBU KWA MUDA MFUPI (GHAIBATU-S-SUGHRA) NA MAWAKILI WA IMAM

Baada ya kifo cha baba yake na kufuatana na maagizo yake imam hassan askari(a.s) , imam wetu wa wakati, hadhrat mehdi(a.s) amejificha kutoka macho ya watu, tarehe 10 shawwal 260 a.h. umri wake ulikuwa miaka mitano. kujificha kwake kwa kipindi hicho huitwa kughibu kwa muda mfupi (ghaibatu-Sughra). hata hivyo aliteua baadhi ya masahaba wake kuwa mawakili ambao wakiandikiana na wafuasi wake na kujibu maswali kwa maandishi. kipindi hicho kiliendelea kwa muda wa miaka sabini na baada ya hapo kukatokea kughibu kwake kwa muda mrefu ambao unaendelea hadi leo. katika kipindi hicho cha kughibu kwa muda mrefu hakuteuliwa mwakilishi yeyote na mawasiliano kwa maandishi yamesimama. kwa hiyo, imam(a.s) sasa anasubiri amri ya mungu ili ajitokeze. mada hii tutaizungumza kwa marefu na mapana katika sura ifuatayo. Mawakili katika muda wa kughibu kwa (imam mehdi a.s.) muda mfupi

Wakili wa kwanza alikuwa Othman bin Said ambaye alikuwa wakili wa Imam wa kumi pia na imam wa kumi na moja. Yeye alikuwa mwenye umri mkubwa na mwanazuoni mwenye hekima kubwa. Akawa wakili wa imam mehdi(a.s) kwa muda mfupi tu wa kipindi cha mwaka mmoja na nusu. imam mehdi(a.s) alimwarifu kwamba atafariki dunia baada ya muda mfupi na amteue mwanae muhammad kuwa wakili na kuwa uteuzi huo utangazwe hadharani.othman bin saidi alifariki baghdad na kuzikwa huko, waumini wengi mara kwa mara huzuru kaburi lake.

Wakili wa pili alikuwa muhammad bin othman imam(a.s) alimwandikia "Eh Muhammad bin Othman, baba yako alibahatika sana kupata mwana mwema kama wewe mwenye sifa nyingi njema. kila siku mwombe mungu akujalie rehema yake. mwenyezi mungu akusaidie." muhammad bin othman alikuwa mwanazuoni mcha mungu. alikuwa mtu mwenye msaada mkubwa kwa mashia na akiendesha uwakala wa imam(a.s) kufuatana na maagizo ya imam(a.s) . alipokaribia kufariki dunia imam(a.s) alimtumia ujumbe wa kumteua hussein bin rauh kuwa wakili kumrithi yeye (Muhammad bin Othman). muhammad bin othman akafariki dunia 305 a.h. baada ya kuwa wakili wa imam(a.s) kwa muda wa miaka hamsini. amezikwa baghdad na waumini wengi huzuru kaburi lake. wakili wa tatu alikuwa sheikh abui kassim hussein bin rauh. alikuwa mwanazuoni mashuhuri, mcha mungu, mwenye tabia nzuri na akiheshimiwa na kupendwa na masunni wengi. alimtumikia imam(a.s) na mashia wake kwa dhati na kwa bidii. mengi aliyokamilisha yameelezwa katika vitabu vingine. Abul kassim hussein bin rauh alifariki dunia 326 a.h.

Wakili wa nne alikuwa aly bin muhammad samary. Yeye alikuwa wakili wa mwisho. Na uwakala wake ulidumu kwa muda wa miaka mitatu. Muda mfupi kabla ya kufariki dunia alipata ujumbe ufuatao kutoka kwa imam(a.s) "kwa jina la mungu: ali samary, mungu awajaalie subira na jazaa waumini wenzake kutokana na kifo chake. Baada ya siku sita wewe utafariki dunia hii. Kwa hivyo, kamilisha mambo yako yote, kwa sababu baada yako hatateuliwa mrithi wako kuwa wakili wangu kwa sababu nimeamrishwa na mungu nighibu kwa muda mrefu. katika muda wa kughibu kwangu watu watakuwa na roho ngumu, maafa na dhuluma zitaenea na wazandiki wengi watajitokeza. Kutakuwa na alama mbili za kuashiria kujitokeza kwangu. sufiani (ukoo moja na jeshi lake) atatokea kutoka syria na sauti kubwa mno itasikika kutoka mbinguni ambayo mataifa yote yatasikia na watu wote bila kujali lugha wanayotumia watasikia na kufahamu. Kama alivyosema imam(a.s) ali samary alifariki baghdad tarehe 15 shaaban na kuzikwa huko huko. Watu huenda kuzuru kaburi lake kama wanavyokwenda kwenye makaburi ya mawakili wenzake waliotangulia.

SURA 12

KUGHIBU KWA MUDA MREFU (GHAIBAT-AL-KUBRA) SIRI YAKE NA MAJIBU YA UWAMBI DHIDI YAKE

Katika kipindi cha kughibu kwa muda mfupi imam(a.s) akijibu maswali ya mawakili na wafuasi wake moja kwa moja. baadaye mungu alimwamrisha aghibu kwa muda mrefu na tokea siku hiyo imam(a.s) haonekani. katika kipindi hicho imam(a.s) hataonekana dhahiri, na hakuna mtu yeyote atakayeweza kudai kuwa ni wakili aliyeteuliwa na imam(a.s) wala kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na imam. Kwa hivyo badala ya mtu maalum kuteuliwa naibu wake, wanazuoni wacha mungu huhesabiwa ni kama mawakili wa imam(a.s) . ili kuwatambulisha wale wanaostahili kukubaliwa kama manaibu wake, imam(a.s) ametangazakuwa:"wale wanazuoni wa kidini ni watetezi wa dini, wanaojizuia nafsi zao dhidi ya maasi na kumfuata imam (a.s). kila muumini anawajibika kuwafuata wanazuoni hao. wanazuoni hao ni manaibu wetu kama vile sisi tulivyoteuliwa na mungu. wataowapinga hao watakuwa wapinzani wetu na hao watakaotupinga sisi ni wahalifu wa mungu."

Uwambi mwingi umeelekezwa dhidi ya kughibu kwa imam(a.s) kwa muda mfupi na muda mrefu. inasemekana kwamba imam(a.s) amejificha kwenye ghorofa ya chini kwa kuogopa na kwa hivyo hatupati faida yoyote ilihali yule imam wa wawambi anaonekana dhahiri. kwanza ni lazima kuthibitisha ukweli wa daawa hilo la uimam; la sivyo, kuonekana kwa imam haina faida yoyote. Katika sura mojawapo iliyotangulia katika kitabu hiki imekwisha thibitika kwa aya za qur'an na hadithi kwamba imam mendi(a.s) ni imam wa kweli wa wakati huu na imam wa kumi na mbili. sura hii itazungumzia kuwa kughibu kwake hakukufanyika kwa woga au kitisho ila iliamuliwa na mungu kuwa hivyo. Kama vile dunia inanufaika wakati jua linapojificha nyuma ya mawingu, vivyo hivyo viumbe wa mungu wanafaidika ijapokuwa imam haonekani.

Nabii Musa alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu mwenye kila uwezo wa kumhifadhi. Lakini nabii Musa alikimbia na kwenda kujificha kutokana na dhuluma za firaun. Kama ilivyoelezwa katika qur'an (28:21): "kwa hivyo yeye ameondoka akiwa na hofu, na kusubiri".

Wakati huo allah angeliweza kumjalia nabii Musa muujiza wa "fimbo" na kumwamrisha amkabili firaun. Lakini Mungu hakufanya hivyo ila kumwamrisha Musa akimbie kutoka Misri na kujificha kutoka kwa Mayahudi kwa muda wa miaka kumi au kumi na tano. Katika kipindi hicho Waisraeli (Mayahudi) waliteseka chini ya utawala wa firaun. je, kwa muda huo wote Mungu hakuwa na uwezo? hiyo ilikuwa kwa ridhaa na uamuzi wake mungu kuwatahini firaun na wafuasi wake waasi na washirikina na kutahini subira na imani ya wafuasi wa musa. mwenyezi mungu hafanyi haraka kumwadhibu mtu. Kutokana na hayo imedhihirika kwamba kujificha kwa nabii musa kulikuwa ni jaribio kwa binadamu duniani. Kwa hivyo alijificha kwa amri ya mungu kwa muda maalum uliowekwa na mungu.

Baada tu ya kifo cha hadhrat Imam Hassan Askari(a.s) imam wa kumi na moja, papo hapo imam mehdi(a.s) angeweza kuanza kuwaadhibu wadhalimu makafiri na waovu kwa uwezo wanaopewa maimam na uwezo aliojaliwa na mungu kudhibiti viumbe wake. Kwa hivyo, imam angelazimika kuwaua waislamu wengi sana wakati ambapo waumini walikuwa wachache tu. wengi wa hao waislamu (wafuasi wa banu umayya na bani abbasi wenye tamaa na vile vile washirikina na makafiri) wangepaswa wauliwe na katika muda mfupi tu umati mkubwa wa watu duniani ungemalizika. kwa hivyo, kusingetokea fursa ya watu kuzaliwa kwa wingi na kusubiri mpakaimammehdi(a.s) kujitokezailiwaweze kujaribiwa subira na imani zao juu ya mungu. watu wote hao waliozaliwa na kuishi kwa imani juu ya mungu wamejipatia pepo, kadhalika na wale watakao zaliwa kabla kujitokeza kwa Imam(a.s) . kwa hivyo, kughibu na kujitokeza kwake (imam a.s.) ni hiari ya mwenyezi mungu ambaye hana mshiriki, mshauri au msaidizi. mwenyezi mungu ameiumba dunia hii kutokana na mapenzi yake na kuwajaribu binadamu. katika sura 29 ya qur'an, Al-anakabut (buibui), aya 2, Mwenyezi Mungu anasema:"je watu wataachiwa tu kwa kusema tu sisi tunaamini bila kujaribiwa?"

Wafuasi wa Nabii Nuh walijaribiwa vikali kama inavyoelezwa bayana katika qur'an, hadithi na historia. vivyo hivyo na wafuasi wa kila nabii. kwa muda wa miaka mitatu mtume muhammad(s.a.w.w) ilimbidi akabili njaa na dhiki katika pango kutokana na vitisho vya makuraishi wa makkah. baada ya washirikina kuzingira nyumba yake kutaka kumwua ilimbidi aondoke nyumbani mwake peke yake katika usiku wa manane na kuihama makkah. kwa amri ya mwenyezi mungu alimteua hadhrat ali(a.s) alale kitandani mwake. je, mungu hakumjalia huyo nabii nguvu za kutosha kuwaangamiza maadui wa mungu na kueneza dini ya mungu? ahadi ya mungu ilikuwa bado kufika ili amri yake ipate ushindi dhahiri. kwa hivyo, kufuata amri ya mungu, mtume(s.a.w.w) ilimbidi ahame kutoka makkah. Yeye (Mtume) alikuwa bado hajaamrishwa kuchukua silaha kwa msaada wa pekee wa mtoto wa ami yake ali(a.s) na masahaba wake wachache.

Juu ya hayo, kufuatana na hali ilivyo katika nyakati mbali mbali manabii ibrahim na suleiman na manabii wengine waliamrishwa na mungu kujificha. mambo hayo yameelezwa katika qur'an na vile vile katika historia, ila hatuyaelezi hapa kwa sababu kitabu hiki kitakuwa kirefu. Ingawa imam(a.s) wa wakati huu ameghibu, lakini kuwepo kwake ni fadhila na huruma ya Mwenyezi Mungu. Kwa hakika, asaa hiyo nuru ya Mungu yaani walii wake na mrithi wa mtume(s.a.w.w) asingekuweko duniani, dhambi na dhuluma zingeghariki dunia kiasi ambacho dunia isingenusurika hata kwa muda mfupi kutokana na ghadhabu ya mungu. kutokana na qur'an na hadithi ardhi ingelinyimwa mvua na hakuna tunda iolote lingeliota kuwapatia viumbe chakula. hao ambao hawamwamini mungu, mtume wake(s.aw.w) na qur'an wasingekubaliana na maadili hayo. hivyo, kutoamini na kuwa na msimamo wa kiburi haiwahusu waumini.

Zaidi ya hayo, imani na waumini hupata mwongozo na msaada kutoka kwa imam wa wakati huu. tunaeleza mifano michache hapa ili kufariji imani za waumini. kiasi cha maili mia moja kutoka najaf (alipozikwa imam ali(a.s) ambayo ni kituo maarufu cha taalimu cha mashia, akiishi mwanazuoni mashuhuri sana. (mujtahid sheikh allam hilli). Siku moja watu wengi walimwuliza juu ya amrisho kuhusu mazishi ya mwanamke mjamzito aliyefariki dunia, lakini mwenye mtoto hai tumboni mwake. walimwuliza kwamba huyo mama azikwe hivyo hivyo au kwanza wamtoe mtoto tumboni mwake? aliwashauri kwamba huyo mama azikwe kama alivyo. baada ya watu kumaliza ada zote kuhusu maiti, walibeba jeneza na kuelekea makaburini. hapo wakamkuta mtu mmoja aliyepanda farasi anawazuia njiani, na kuwaambia kwamba huyo allama amebadilisha uamuzi wake wa kwanza na kuagiza kwamba huyo mama asizikwe kama alivyo, bali atolewe mtoto kwanza kabla ya kuzikwa. Mtoto alitolewa kwa usalama na mama kuzikwa.

Baada ya muda wa miaka miwili au mitatu huyo allama alitembelewa na mtu mmoja akifuatana na mtoto mdogo (aliyetolewa kutoka tumboni mwa mama aliyefariki). Huyo mtu alimwuliza allama: "je, unamjua huyu mtoto? huyu ni yule ambaye kufuatana na amri yako alitolewa tumboni mwa mama yake aliyefariki. Wewe kwanza ulishauri kwamba mama yake azikwe pamoja na mtoto aliyekuwa tumboni mwake, lakini baadaye ulimtuma mtu aliyepanda farasi kuja na amri kwamba mtoto atolewe tumboni mwa mama yake". Allama alishangazwa sana kusikia hayo na uso wake uligeuka rangi kwa sababu alivyokumbuka yeye hakumtuma yeyote kubadilisha uamuzi wake. Alingamua kuwa iwapo imam mehdi(a.s) asingekwenda kumsaidia, angekabiliwa na dhambi ya kusababisha kumzika mtu aliye hai. tokea siku hiyo akajifungia mlango na akaamua kutotoa uamuzi wowote juu ya mambo yanayohusu dini ili asijerudia kosa lile tena. baada ya muda mfupi alipokea barua kutoka kwa imam(a.s) ikimwambia kwamba asijali mambo hayo yaliyopita na aendelee kutoa fatuwa. Ikiwa kwa bahati mbaya atakosea basi imam(a.s) anaelewa mambo yote na anafika kuwasaidia mashia - wafuasi wake. licha ya wafuasi kunufaika kwa uongozi wa imam(a.s) ijapokuwa angali ameghibu, iakini msaada wake pia unafika wakati unapohitajika.

Imenakiliwa katika biharul anwar kwamba katika enzi za utawala wa kiingereza watu wote wa bahrain walikuwa waisiam na mfuasi wa madhehebu ya kisunni aliteuliwa gavana wa nchi hiyo. Nchini humo walikuwa mashia wengi iakini gavana huyo na waziri wake walikuwa na uadui na mashia. Siku moja waziri alimzawadia gavana makudhumani ambao juu yake alidai kwamba majina ya makhalifa wanne wa kiislamu yalijitokeza kwa kudra ili kuhakikisha ukweli wa madhehebu ya sunni na makhalifa wanao aminiwa. Hapo akamshawishi gavana kuwaita wanazuoni wa kishia awaonyeshe hilo tunda ili waache madhehebu na itikadi ya kishia na kukubali ukweli wa itikadi ya kisunni. Akasisitiza kwamba wakikataa kukubali ukweli wa itikadi ya kisunni basi wasihesabiwe tena kama waislamu na wauawe au walazimishwe kulipa kodi (jiziya) maalum ambayo hulipwa na wakazi wasio waislamu.

Gavana alipoangalia hilo tunda na kuona mwandiko "lailaha illa allah, muhammadun rasulullah - Abu Bakar, Omar, Othman Ali khulafau Rasulullah" aliathirika sana na kutokana na ushauri wa waziri akawaita wanazuoni wa kishia, akawaonyesha tunda hilo na kuwapa hiari tatu kama alivyoshauriwa na waziri wake. Wanazuoni wa kishia walistaajabishwa. wakaomba muda wa siku tatu kutoka kwa gavana, ambaye aliwapa huo muda kwa ridha yake, ili wampatie jibu. waligharikika na mshangao na hatimaye wakaamua kuomba msaada kutoka kwa imam wao hadhrat mehdi(a.s) . wanazuoni wacha mungu watatu wakateuliwa na ikaamuliwa kwamba kila mmoja wao kila usiku atoke nje ya jiji na kwenda kumwomba auni Imam(a.s) . siku mbili za kwanza wanazuoni wawili wakakesha kuswali na kumwomba mungu awapatie msaada wa imam(a.s) lakini bila mafanikio. usiku wa tatu mwanazuoni' wa tatu akaenda nje ya jiji kuomba kwa bidii mno ili apate msaada kutoka kwa imam(a.s) . alfajiri alimwona mtu mwenye haiba ambaye alijitambulisha kwamba ni imam wake. huyu mtu akamwuliza mwanazuoni shida yake. mwanazuoni akamjibu kwamba kama kweli yeye ni imam(a.s) basi anaelewa tatizo linalomkabili. imam(a.s) akamjibu kwamba yeye ana habari kamili ya balaa iliyowapata lakini wasikate tamaa ila wafuate maagizo yake. kisha imam akasema, "kesho asubuhi wewe na wenzako mwende kwenye kasri ya gavana na kumwambia kuwa mtampatia jibu nyumbani kwa waziri.

Waziri atakataa jibu hilo lakini lazima msisitizie hilo na mhakikishe kwamba waziri hafiki nyumbani kabla nyinyi kufika. mwende nyumbani kwa waziri mkifuatana pamoja naye hadi paani. waziri atababaika sana na atajitahidi kutangulia lakini nyinyi mumziwie kutangulia na kufika kabla nyinyi hamkufika. huko ghorofani mtaona mfuko katika kishubaka ukutani. mfungue huo mfuko na mumwonyeshe gavana vitu vilivyomo mle. humo ndani kutakuwemo kalibu ambayo juu yake mtaona maandishi yaliyotokeza juu ya komamanga. hizo ni kalibu zilizovishwa na waziri juu ya makomamanga yalipoanza kuota na zilipoanza kukomaa maandishi hayo yalizidi kuimarika. gavana ataathirika na hayo na atakubali kwamba jambo hilo lilikuwa ulaghai wa waziri. 58

Baadaye mwambieni gavana kwamba kuna ushahidi mwingine kuhusu ulaghai huo. mumwombe gavana amwamrishe huyo waziri avunje hilo tunda mbele yenu na gavana ataathirika na uwezo wa mungu na ulaghai uliofanywa. asubuhi ifuatayo huyo mwanazuoni (muhamad bin ali) akaenda nyumbani kwa gavana pamoja na wenzake. walimwomba gavana wafuatane nyumbani kwa waziri pamoja naye (waziri) kama alivyoagizwa na imam(a.s) . mwishowe gavana akamwamrisha waziri avunje hilo tunda. alipolivunja tunda hilo vumbi nyeusi likatoka na kumwingia machoni na kwenye ndevu huyo waziri. hapo kila mtu akacheka. gavana ilimbidi kusadiki ulaghai uliotendwa na waziri na kuamuru waziri huyo kuuliwa. wanazuoni wa kishia waliondoka hapo kwa heshima. tukio hilo linajulikana sana. kaburi la huyo mwanazuoni aliyeonana na imam(a.s) limehifadhiwa na waislamu wengi huzuru kaburi hilo. hakika hizo huthibitisha kwamba imam(a.s) yu hai, yupo na sisi na inapolazimika huja kuwasaidia mashia wanapokabiliwa na msiba. matukio mengi kama hayo yameorodheshwa katika kitabu hiki kwingineko. imam hadhrat mehdi(a.s) alizaliwa samarra na alighibu kupitia ghorofa ya chini iliyoungana na jengo la maziara ya maimam wa kumi na wa kumi na moja. uwingi wa umati wa samarra ni masunni (90-95%) ambao wanaamini juu ya uhai wa hadhrat mehdi(a.s) kwa sababu miujiza mingi hutokea huko. zaidi ya hayo, imam(a.s) anapokuja kuzuru makaburi ya baba na babu yake (maimam wa kumi na kumi na moja) jiji zima hujaa nuru. waarabu wa huko hufurahia kwa msisimko na wanawake hupanda juu maghorofani kufurahia kuja kwa imam(a.s) .

Hata katika usiku wa giza, Imam(a.s) anapozuru, hilo jiji hung'aa kwa nuru. ikiwa mtu yeyote akinyosha kidole au akitoa ufunguo na kuuning'iniza basi hutoa mwanga kama mshumaa. hata baada ya miujiza mingi kutokea samarra, hao waarabu hawaachi kuwasumbua mashia wanao kuja kwa ajili ya ziara. allah maisha hukamilisha mathibitisho yake. miujiza mingi na dalili nyingi hutokeza kuthibitistia ukweli wa imam(a.s) na uhai wa hadhrat mehdi.(a.s) ili imani ya waumini iimarike na uwe uthibitisho kwa wabishi. hata hivyo, bado kuna maswali machache yanayoulizwa na majibu yake ni kama yafuatayo: suali: ikiwa imam mehdi(a.s) atajitokeza sasa, bila shaka uovu na ukandamizi na kufuru vitakoma duniani, amani, usalama na utii kwa mungu utadhihirika, na waumini hawatakua na shaka yoyote.

Jibu: dunia hii ni pahala pa majaribio kwa binadamu. mwenyezi mungu amekamilisha mathibitisho yake juu ya kila mtu. kujitokeza kwa imam(a.s) hutegemea amri ya mungu. mtu yeyote hana haki ya kuharakisha au kudadisi dadisi. iicha ya hayo, hata baada ya kuja kwa imam(a.s) waliopotoshwa watapotoka. wengi waliomwona mtume(s.a.w.w) na maimam wetu, kushuhudia miujiza na kusikia maagizo yao, lakini walipotoshwa kwa tamaa ya dunia na wakabakia bila imani hata kuwasaidia wadhalimu (bani umayya na bani abbas) na kusahabisha upinzani na uadui dhidi ya maimam wetu na hatimaye kuwaua. kwa hivyo, ni jambo dhahiri kwamba mwenyezi mungu hutenda kila jambo kwa kupenda yeye mwenyewe.

Swali : waislamu wengi huishi katika hali ya vitisho kutoka maadui wao, hudharauliwa na kuteswa. huomba msaada kutoka kwa imam(a.s) lakini matatizo yao hubakia pale pale. kwa hivyo shaka nawasiwasi huingia moyoni mwao ambalo siyo jambo jerna.

jibu : siku moja mwana mmoja wa mama mmoja akawa mgonjwa mahututi sana na hapakuwa na tamaa yoyote ya huyo mwana kupona, huyo mama alisema kwamba ikiwa mungu yupo naye ndiye mwenye kila uwezo na mwenye rehema bila shaka huyu mwana atapona tu, au la sivyo imani yake juu ya mungu haina maana. huyu mtoto akafariki. je, uwezo wa mungu na rehema ya mungu hubatilika kwa hayo?

Ikiwa huyo mtu anayeomba msaada kutoka kwa imam(a.s) ni mkandamizi na asiye na imani na haswali basi hastahili msaada wowote. kwa hivyo, huyo mtu akipata au asipate msaada haitaathiri ukweli wa imam(a.s) . haina umuhimu wowote kwa imam(a.s) ikiwa mtu anaamini uimam au dalili, alama, aya za qur'an na hadithi za kuthibitisha uimam wa hadhrat mahdi(a.s) kuukubali uimam wake humletea manufaa mwumini mwenyewe na kwa ajili ya wokovu wake binafsi. katika jambo la dini hakuna mtu anaye lazimishwa. baada ya mtume(s.a.w.w) , mwenyezi mungu ameteua warithi kumi na moja, mmoja baada ya mmoja, huku duniani kwa ajili ya mwongozo wa binadamu na wote wameuliwa kwa upanga au sumu na wadhalimu kama yazid, bani umayyah au bani abbas.

Zaidi ya hayo, hao maimam wlikuwa wanaonekana na kuishi pamoja na watu na vilevile kuonyesha miujiza mingi. wao (maimam) wameongoza waislaam, wachache tu waliwaamini na wengi wao (waislaamu) wakawaacha hao maimam(a.s) . hata kama huyo imam wa kumi na mbili (hadhrat mahdi a.s) angekuwa anaonekana angalikabiliwa na mambo hayo hayo. kwa hivyo mwenyezi mungu amemhifadhi kwa muda maalum.


10

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 13

MAISHA MAREFU YA HADHRAT MAHDI IMAM WETU WA ZAMA HIZI

Hadhrat Mahdi(a.s) alizaliwa mwaka 255(a.s) na yu hai hadi leo. watu hutilia shaka juu ya maisha yake marefu ya zaidi ya miaka elfu moja. ubishi upo kwamba mtu akitimiza miaka mia huwa mdhoofu, hajiwezi na pungwani, kwa hivyo vipi mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 1100 huweza kuwa na afya nzuri? suala hili hujibiwa kwa aya nyingi za qur'an, hadithi na kwa dalili za kiakili. kwanza, ni jambo dhahiri lililothibitishwa kihistoria kwamba watu wengi wakiwemo waumini na makafiri miongoni mwao, wanajulikana kuwa wameishi zaidi ya miaka elfu moja, kwa hakika tutathibitisha katika sura hii kwamba baadhi ya hao wapo hai hadi leo.

Qur'an tukufu inapozungumzia juu ya nabii yunus imeeleza:

فَلَوْلَا أَنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُسَبِّحِينَ ﴿١٤٣﴾ لَلَبِثَ فِي بَطْنِهِ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤٤﴾

Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa." (37:143 - 144).

Nabii Yunus alikuwa binadamu. Ikiwa allah kwa uwezo wake anaweza kumweka hai binadamu tumboni mwa samaki bila huyo binadamu kupata mwangaza, upepo, chakula hata maji mpaka siku ya kiyama, kwa nini haiwezekani kwake kumweka mtume wake (au mrithi wa mtume wake) hai kwa muda wa miaka 1,000 au 2,000? hakuna mtu anayeweza kutia shaka juu ya uwezo wa mungu. kwa hivyo, swali linaloweza kuulizwa ni je, ni kweli hadhrat mehdi(a.s) yu hai, na kama yupo hai kwa nini haonekani? masuala hayo yamezungumziwa katika sura nyingine ya kitabu biki. hata masunni wamekubali na kuandika juu ya maisha marefu ya hadhrat mehdi(a.s) hayo pia katika sura nyingine katika kitabu hiki. wafuatao ni binadamu, mitume watukufu na vile vile washirikina na makafiri ambao walijaliwa maisha marefu mno: mitume na waumini:

Nabii Nuh miaka 2,000 hadhrat lukman miaka 3,800 nabii suleiman miaka 700 miaka nabii hood miaka 464 nabii adam ambaye aliishi miaka 930 na kuacha ayali ya watu .40,000 nabii shish miaka 900 bibi hawa (mke wa nabii adam) miaka 930 manabii wanne ambao wangali hai hadi leo mbinguni kwa maelfu ya miaka: nabii idris alichukuliwa mbinguni wakati umri wake ulikuwa umekwishatimia miaka 890 na yupo huko kwa miaka elfu kwa maelfu. nabii issa yupo mbinguni kiasi cha miaka 2,000. makafiri na washirikina: iblis tangu milele, anak binti wa nabii adam, miaka 3,000. ouj bin anak, miaka 3,600 mfalme jamshed miaka 1,000 zahaq tazi (mpwa wa jamshed) miaka 1,000 aaad bin our bin irem saam bin nooh miaka 1,200 shaddaad, miaka 900. cyrus, mfalme wa iran miaka 1,000 dajjal, miaka 1,375 na yu hai hadi leo.

Duniani nabii khidhr yu hai leo miaka 4,000 na hutembea dunia nzima. nabii elias yu hai kiasi cha miaka 4,000-5,000 na hutembea dunia nzima. hatimaye, hoja moja ya kirazini. ikiwa atatokea mtu mmoja akada kwamba anaweza kutembea juu ya maji, bila shaka watu wote watamzunguka na kuona kwamba kweli huyo anatembea juu ya maji na kushangazwa na kumwamini yeye kama mtu mtakatifu. lakini ikiwa baada ya rnuda mfupi atatokea mtu mwingine na kudai hilo, mshangao wa watu utapungua na hawatakuwa wengi kumwangalia mdai wa pili kama walivyomwangalia wa kwanza. dai kama hilo halitakuwa tena jambo la kushangaza. kama akitokea mdai wa tatu watu hawatashangazwa hata kidogo na hakitakuwa kitu kipya tena.

Vile vile, ikiwa watu wengi wamekwishaishi maisha ya maelfu ya miaka ya maelfu na kwa hakika manabii khidhr na elias wamekwishaishi maisha zaidi ya miaka 4,000-5,000, na wakiwa na afya nzuri huku wakitembea dunia nzima, basi haliwezi kuwa jarnbo la kustaajabisha kuwepo hai na mwenye afya nzuri kwa imam wetu wa kumi na mbili(a.s) kwa miaka 1,110-1,200. si ajabu wala kustaajabisha tena wakati wakristo na waislamu hukubali iblis na dajjal wapo hai hadi leo na agog magog wapo hai kwa tangu maelfu ya miaka ya zama ya alexander mkuu.

Kwa hakika manabii khidhr na elias wapo hai ijapokuwa kipindi chao cha unabii na uongozi umemalizika. hiki ni kipindi cha unabii wa mtume muhammad(s.a.w.w) na kanuni za kiislamu zilizopangwa kutokana na aya za qur'an zitadumu hadi siku ya kiyama. kwa hivyo, muda mrefu wa uhai wa manabii na mfano bora sana kuhusu maisha marefu ya imam wa zama hizi, hadhrat mehdi(a.s) aliyejaliwa na mungu.

Idadi kubwa ya wanazuoni wa kisunni wamenakili katika vitabu vyao habari juu ya kuzaliwa kwa hadhrat mehdi(a.s) katika mwaka 255 a.h. na kuwepo hai kwake hadi leo na vile vile kunakili habari za watu walionana naye. hata hivyo, wengi wao huamini kwamba hadhrat mehdi(a.s) hajazaliwa bado na atazaliwa katika siku za mwisho na yeye ndiye atatawala kwa insafu na usawa. sababu kuu kuhusu itikadi hii ni kwamba wakimkubali kuwa hadhrat mehdi(a.s) amekwishazaliwa watalazimika kumkubali kama yu hai na ameghibu na bidhaa yake itakuwa kuacha imani juu ya makhalifa kumi na wawili wanaowakubali, na kufuata itikadi ya ithnaasheri ambayo inaamini kwamba ukhalifa unakomea kwa hadhrat mehdi(a.s) , imam wa kumi na mbili.

Kwa wanaomkataa hadhrat mehdi(a.s) amekwishazaliwa na yungali hai, kuwa ana pahala pake anapoishi, watoto na wahudumu wake na kukutana na watu kwa sababu tu kwamba pahala anapoishi hapakuonyeshwa katika ramani na si rahisi kufika ni kujidanganya nafsi zao. papo hapo, hao wanaomkataa imam mehdi(a.s) wenyewe wanawaamini wale waliojificha na hawaonekani na kwamba maskani yao hayajaweza kutambulika. kwa mfano, katika kitabu cha "rehla eibne battuta" (ibne battutta aliyefariki 779 a.h.), ambacho kinaeleza juu ya safari yake ndefu kwenda arabuni, iraq, asia na china, katika juzuu la pili ukurasa 64 imenakiliwa kuwa: "katika safari yangu nilifika had! china ambako nilisimuliwa juu ya sheikh wa ajabu mwenye umri wa miaka 200, lakini hakuna mtu yeyote aliyemwona akila, kunywa wala kuzungumza na mtu mwingine. alikuwa na afya nzuri lakini hakufunga ndoa, akiishi ndani ya pango lakini akitoka nje wakati akitaka kufanya ibada. hivyo niliamua kwenda pamoja na sahibu zangu kumwona huyo sheikh pangoni mwake.tuiipofika tulimwona amesimama nje ya pango lake. Nilimsalimu na akanijibu. Baadaye akaushika mkono wangu na maneno yake yalifasiriwa kwangu na mkalimani kwamba mimi ninaishi upande wa magharibi wa dunia na yeye anaishi upande wa mashariki wa dunia.

Tena akaniambia kwamba katika safari yangu nimeona vitu vya kumstaajabisha na ninakumbuka kuzuru kisiwa ambamo kulikuwa hekalu moja na humo ndani nilimwona mtu ambaye alinipa sarafu kumi za dhahabu. nikamjibu kwamba tukio hilo nakumbuka vizuri sana. akanijibu kwamba mtu yule alikuwa yeye mwenyewe (sheikh). papo hapo nilimbusu mkono wake, naye akanyamaza kimya kwa muda mrefu. ghafla yeye akaingia ndani ya pango. tulimsubin nje kwa muda mrefu sana lakini hakutokea, kwa hivyo tuliamua kumfuata ndani lakini tuliambiwa kwamba hatutaweza kumwona tena. mtumishi wake alikuwa na vipande vya karatasi ambavyo alinikabidhi na humo ndani kuliandikwa kwamba sheikh amemkabidhi zawadi kwa ajili ya wageni na kwa hivyo mimi niondoke. niliposisitiza kutaka kumwona huyo sheikh mhudumu akaniambia kwamba hata nikisubiri miaka kumi sitaweza kumwona tena kwa sababu yeye haonani na mtu yeyote mara ya pili.

Mimi nilihisi kuwa huyo mtu alikuwa pale pale na mimi, ila alikuwa haonekani tu. sisi tuliduwazwa na tukatoka kwenye hilo pango. mwandishi aliendelea kusema "mimi niliwasimulia tukio hakimu shaikhul islam na awahududin bukhari nao walithibitisha kwamba mtu yeyote aliyemwona huyo sheikh (huko china) mara ya kwanza hawezi kumwona tena na yule mhudumu aliyewakabidhi hiyo bahasha ni huyo mtu mwenyewe lakini alibadilisha sura yake. sahaba wake mmojawapo alithibitisha kwamba aliwahi kujificha kwa miaka 50 na kujitokeza ghafla. hakuna cho chote katika pango hilo lakini mhitaji yeyote aombapo msaada hupatiwa pesa. huyo sheikh (wa china) alisimulia hadithi ya mtume(s.a.w.w) na kuzungumza mambo yaliyopita. yeye hudai kwamba angalikuwa wakati wa mtume mtukufu(s.a.w.w) angalimsaidia bila wasiwasi wowote. naye huwalaani vikali mno muawiya na yazid.

Zaidi ya hayo katika kitabu hicho hicho juu ya safari zake mwandishi aandika kwamba awahuddin bukhari alimwambia kwamba yeye (bukhari) aliwahi kuingia ndani ya hilo pango na huyo sheik alipeana naye mkono. anakumbuka kwamba alikuwa katika kasri kubwa iliyopambwa sana na sheikh huyo alikaa juu ya kiti cha enzi na kuvaa taji kichwani mwake huku akizungukwa na magashi. aliona mito hupita na vile vile miti yenye matunda matamu. aliokota tunda moja ili ale lakini ghafla alijikuta yuko peke yake nje ya hilo pango. mandhari yale yalipotea na akajikuta peke yake. papo hapo akaondoka. mambo ya kustaajabisha kama hayo yanayomhusu sheikh yamenakiliwa katika vitabu vya sunni na huonekana kwamba waislamu wapo tayari kumwamini huyo sheikh, kuhusu kujificha kwake na miujiza ya kustaajabisha wakati hata jina lake halifahamiki. lakini, bado wanatia shaka juu ya hadhrat mehdi(a.s) , wakati qur'ani tukufu, hadithi na historia na vitabu vilivyoandikwa na waandishi wa kiislamu hutoa maelezo ya kutosheleza juu yake, kughibu kwake na miujiza yake.

SURA 14

KUGHIBU KWA MITUME

Sheikh Abu Jaafer Muhammad bin Babawayhi anayejulikana kwa jina la S heikh Saduq amenakili kwamba: aliambiwa na sheikh Najmuddin Abu Said Muhammad bin Hassan kuandika kitabu juu ya hadhrat Mahdi(a.s) na aliahidi kuandika atakapo rudi nyumbani tehran. aliporudi tehran hakuweza kuitimiza ahadi hiyo kwa sababu alishughulikia familia yake na matatizo mengine. siku moja aliota ndoto kwamba yuko makkah anatufu kaaba. 'alipomaliza kutufu mara yasaba na kubusu hajaril aswad (jiwe jeusi) alimwona mtu mtukufu mwenye uso uliokuwa unatoa nuru karibu na mlango wa kaaba. yeye alitia shaka kwamba huyo ni imam wake na akamwamkia ipasavyo. huyo mtu akamjibu na kumwuliza kwa sababu gani hakuandika kitabu juu ya kughibu (ghaibat). Sheikh akajibu kwamba amekwishaandika mengi kuhusu ghaibat lakini huyo mtu akasema: "la, sasa katika kitabu hicho eleza ghaiba ya manabii waliotangulia". huyo sheikh akaamka usingizini mwake na akalia. usiku kucha akakesha katika ibada na siku ya pili akaanza kuandika kitabu kuhusu [kughibu kwa imam(a.s) .

Katika sura hii, tutaelezea kwa ufupi kuhusu kujificha kwa manabii wawili. kujificha kwa Nabii Musa(a.s) sheikh sadooq ananakili kutoka kwa imam wa nne(a.s) kuwa kabla ya kufariki dunia nabii yusuf aliwakusanya ayali wake na wafuasi wake na kubashiri yatakayo tokea. akawaambia kwamba watapata rnateso makubwa katika utawala wa firaun. firaun atawafanya wanaume wao watumwa na kuwachinja na ataamrisha matunbo ya wake zao yakatwe ili watoto wauawe kabla ya kuzaliwa. allah atamwamrisha hadhrat mussa mwana wa lavi bin yakub kutokeza. atakuwa rnrefu wa kimo na mwenye uso wa rangi ya hudhurungi.

kwa muda wa miaka 400 chini ya utawala dhalimu wa firaun, waisraeli waliteseka. mtume alikaa mafichoni. Waisraeli waliomba mungu kwa bidii sana kuja kwa nabii mussa. baada ya muda mrefu walipata ishara ya kuz.aliwa kwa nabii mussa ambayo iliwapatia matumaini makuu. miongoni mwa hao waisraeli alikuwa mwanazuoni mcha mingu ambaye akiwatuliza hao waisraeli kuwabashiria juu ya kuzaliwa kwa nabii musa na ushindi wake juu ya firaun. Mateso ya firaun yaliendelea na ilimlazimu huyo mwanazuoni kujificha pangoni mwituni. Baada ya waisraeli kuchoka kuendelea kuvumilia mateso ya kubebeshwa magogo na mapande mazito mazito ya mawe walituma ujumbe kwa huyo mwanazuoni kuhusu mateso waliyopata. Wakamweleza kwamba maneno yake kuhusu ushindi ulikuwa 'faraja kwao na wakamwomba arudi kuishi nao na kuwafariji tena katika mateso.

Mwanazuoni huyo akawaalika Waisraeli hao kwake msituni. Wachache wakaenda kumtembelea. Usiku mmoja wenye mwangaza akatabiri kwamba wakati wa kuja. kwa mkombozi ulikaribia. walipokuwa wame.shughulika katika mazungumzo yao. wakamwona kijana mmoja mrefumwenye uso mwangavu mbele yao. Huyo mwanazuoni ambaye akizijua sifa za nabii musa papo hapo akasujudu kumshukuru mungu na waisraeli wote walienda sijda kumshukuru mola. walibusu miguu ya nabii musa na kueleza mateso waliyopata kutoka kwa firaun. Nabii Musa akawatuliza na kuwahakikishia kwamba ushindi umekaribia na akapoteamachoni mwao. Nabii Musa akaelekea madyan nyumbani kwa nabii shuaib na akafunga ndoa na binti wa nabii shuaib kwa sharti ya kumtumikia nabii shuaib kwa muda wa miaka kumi.

Kipindi cha kwanza cha kujificha kwa nabii musa ni sawa na kughibu kwa hadhrat mehdi(a.s) kwa muda mfupi. usumbufu kwa waisraeli ulizidi kuongezeka na subira ilikuwa inapungua. kwa hivyo, baada ya miaka kumi walienda kamwona huyo mwanazuoni ambaye aliwaarifu kuwa alikuwa amepata ilhamu kutoka kwa mwenyezi mungu ya kuwa ushindi wao ungepatikana katika miaka arobaini. kusikia hivyo, wao wakatamka "alhamdulillah" (sifa zote ziwe kwa mungu). Kushukuru huku kulimfurahisha mungu. naye akawapunguzia muda wa kuteseka uwe wa miaka ishirini. habari hii njema alipashwa mwanazuoni huyo na mungu. mwanazuoni akawaeleza waisraeli kuwa shukraini zao zimeleta faida hiyo. kusikia tu hivyo, waisraeli wakasema "rehema na huruma zote hutoka kwa mwenyezi mungu peke yake". Hapo tena mwanazuoni huyo akapata ilhamu ya kuwa mwenyezi mungu amewapunguzia huo muda uwe wa miaka kumi. waliposikia hayo wakasema kuwa hapakuwa na mwingine ila mwenyezi mungu mwenye uwezo wa kuwakomboa.

Punde si punde, wakamwona nabii musa ametokeza. wakasujudu kwa mwenyezi mungu na kumbusu miguu nabii musa ambaye aliwafikishia habari njema ya kuwa aliamrishwa na allah kujitokeza ra kumkabili firaun na akawaamrisha waondoke. baada ya hapo nabii mussa akaelekea kwenye kasri ya firaun ambaye akaamrisha wachawi wake wahudhurie. nabii musa akatoka misri na waisraeli 600,000, wake kwa waume, wazee na vijana, na akavuka mto. lakini firaun na wafuasi wake wengi walipojaribu kuuvuka mto wakazama. Hivyo inathibitika kujificha kwa hadhrat musa na majaribio na mitihani kwa wafuasi wake. vivyo hivyo wafuasi wa mtume muhammad(s.a.w.w) hujaribiwa na kutahiniwa. kujificha kwa nabii suleiman nabii dawood alirithiwa ufalme na nabii suleiman. baadaye nabii suleiman kwa amri ya mungu akajificha kutoka wafuasi wake na tatika kipindi hicho akapata taji ya ufalme. hadithi yake ni kama ifuatayo: nabii dawood aliimarishwa na mungu kumteua mwanawe wa mwisho suleiman kuwa mrithi wake. nabii dawood aliwajulisha wanawe na wafuasi wote juu ya uamuzi huo. waisraeli hawakupendezwa na uamuzi huo eti ulikuwa sio wa insafu kwa sababu nabii suleiman alikuwa mdogo kuliko wote na kaka zake walikuwa wenye uwezo na ujuzi.

Nabii Daudi akawaambia kwamba: hakuna yeyote anayeweza kutengua amri ya Mungu. Lakini kuwatosheleza akawaomba wanawe kuweka vitawi vilivyoandikwa majina yao katika chumba maalum, na vile vile akamwomba nabii suleiman kuweka vitawi vilivyo andikwa jina lake katika chumba hicho maalum. Siku ya pili wote walitakiwa wafike kuangalia kwamba vitawi gani vime mea na kuota majani na matunda. mwenye vitawi vilivyo mea na kuota majani na matunda ndiye atakuwa mrithi wake. wote waliridhika na wazo hilo na wakaleta vitawi. Siku ya pili walipofungua hicho chumba ilionekana kuwa vitawi vya nabii suleiman tu vilikuwa vimeota majani na kuzaa matunda. kwa hivyo wote walikubali uteuzi wa nabii suleiman.

Kuthibitisha zaidi ustahilifu wa Nabii Suleiman, nabii Daudi akamtahini elimu yake na uwezo wake kadamnasi ya waisraeli. akamwuliza "kitu gani humpa mtu furaha na utulivu wa moyo?" nabii suleiman akajibu "kusamehewa na mungu na kusameheana watu wenyewe". nabii dawood tena akamwuliza: "kitu gani chenye ladha mno?" "huba na urafiki wa ukweli kwani upendo na urafiki wa ukweli ni zawadi na rehema kutoka kwa mungu juu ya viumbe wake." (katika zamana hii zawadi ya mungu ya mapendano na urafiki imepotea na badala yake uadui, husuda na dhuluma imezagaa ambayo ni adhabu kutoka kwa mwenyezi mungu). nabii dawood alifurahishwa sana na ubora na usahihi wa jibu kutoka kwa mwanae. akawauliza waisraeli kama wameridhika kwamba nabii suleiman alistahili urithi kwa kila njia.

Baada ya kifo cha nabii dawood, nabii suleiman kutokana na amri ya mungu alienda kujificha. Katika kipindi hicho wafuasi wake waliteseka na kupata shida. nabii suleiman alikwenda kujificha katika nchi ya jirani ambako aliolea na kuishi na wakwe zake. Siku moja mkewe akamwambia kwamba anampenda sana kwa tabia zake, sifa na ukarimu wake. lakini huona dhila kutegemea wazazi wake na alimpa wazo la kujitafutia maisha yake na kujitetegemea kimapato. Nabii Suleiman akajibu kwamba: hakuwa na ujuzi wa kazi yoyote ya kujikimu kistahiki kwa sababu hakuhitajika kufanya kazi (kwa muda alikuwa mwana wa mfalme). Hata hivyo, aliahidi kwamba siku ifuatayo atakwenda sokoni kujitafutia mapato. alijiandaa kwenda kufanya kazi, lakini hakufanikiwa chochote. mkewe mwema akamtuliza moyo na akampa hima kwamba ajaribu sikuya pili.

Siku ya apili vile vile nabii suleiman akarudi mikono mitupu. tena mkewe akamsihi asivunjike moyo na kumhakikishia kwamba kutokana na rehema ya mungu atafanikiwa. siku ya tatu nabii suleiman akenda pwani na kumwomba amtumikie mvuvi kwa ujira wowote, mvuvi akakubali ombi na jioni yake akampa nabii suleiman samaki wawili kama ujira wake. nabii suleiman alifurahi na akamshukuru mungu nabii suleiman akamkata samaki huyo vipande na kumsafisha. tumboni mwa samaki mmoja nabii suleiman akapata pete moja. kwa vile alikuwa nabii, akatambua kuwa hiyo pete ni dalili yq ufalme. akasafisha hiyo pete akaiweka kwenye leso na kuweka mfukoni mwake. baadaye, akawachukua hao samaki wawili na kwenda nyumbani, ambako akamwona mkewe amefurahi sana.

Huyo mkewe akamwita baba yake akamwonyesha samaki wawili, nabii suleiman hapo akamwuliza baba mkwe " unajua mimi nani" huyo baba mkwe akajibu kwamba nabii suleiman alikuwa mtu mwema na yeye (bab mkwe) akimhesabu kama mwanawe lakini alikuwa hamjui kama yeye ni nani. Hapo nabii Suleiman akamsimulia kwamba yeye ni mwana wa Nabii dawood, mwana wa mfalme na mriuthi wa kiti cha ufalme. akatoa hiyo pete kutoka mfukoni mwake na kuivaa. papo hapo, majini na ndege kutoka pande zote walikusanyika bele yake. Nabii Suleiman akaelekea kwenda mji mkuu pamoja na mkewe na wakwe zake. Wafuasi wake walifurahi sana kumwona nabii Suleiman na wakamshukuru Mungu. Hii ni mifano miwili kuhusu kujificha kwa mitume. Wafuasi wa kila mtume walijaribiwa. kujificha kwa manabii Yusuf Ibrahim na Idris kumeelezwa katika vitabu vingine. Kwa kufupisha kitabu hiki hatuandiki habari hiyo humu.

11

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 15

HADHARAT MAHDI (A.S) NA WSIO WAISLAM

Allamah Gulam Husein Kanturi ameandika katika kitabu chake Intisarul islam (1917) kwamba: jamaa yake wa karibu Hakim Seyyid Zafer Mahdi alirudi lahore baada ya kwenda kuhiji pamoja naye. Mnajimu mmoja wa kihindi alimjia na akamwomba Seyyid amwulize swali. Seyyid alimwomba apokee zawadi bila ya kumuuliza swali, lakini huyo mnajimu alikataa kupokea zawadi bila kuulizwa swali. Huyo Seyyid alikerwa sana kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa mnajimu. lakini, hata hivyo, alimwuliza ili aweze kujua kwamba huyo mnajimu alikuwa anaweza kubashiri juu ya mambo yajayo, mambo ya kale na kumweleza nini alikuwa anafikiria.

Huyo mnajimu aliendelea kueleza juu ya jambo gumu; Seyyid huyo akamwomba amweleze juu ya mtu anayemfikiria kwa wakati huo. huyo mnajimu akafikiria na kufanya hesabu kwa uwezo wake wote lakini bila mafanikio. mwishowe akaweza kupata undani wa habari ya huyo anayefikiriwa; sura yake na sifa zake ambazo zilimshangaza yeye mwenyewe. huyo mnajimu akamwambia seyyid kwamba huyo mtu anayefikiriwa ni mfalrne wa dunia na akhera. ameng'amua kwamba hata akijitahidi maisha yake yote hataweza kujua habari kamili ya buyo mtu. akaeleza kwamba huyo ni mfalme wa duniani na akhera, na vile vile mfalme wa wafalme duniani.

Kusikia hivyo, huyo seyyid alifurahishwa sna na akasema kwakmba kwa wakati huo alikuwa akimfikiria imam mahdi(a.s) ambaye mnajimu aliweza kumtambua. hapo sayyid akamwamrisha mhudumu wake kuleta kashida nzuri sana na kumvika begani. mnajimu huyo alikataa kupokea zawadi yoyote na machozi yalimlenga lenga. "sitaki ,sitaki, sihitaji zawadi ya kashida. leo kutokana na suala lako nimepata ufumbuzi mkubwa na wenye thamani kuliko ufalme wowote duniani. Nimeongozwa kwenye njia ya ukweli na nimemfahamu bwana wangu wa kweli. Sina tama ya kitu chochote duniani" hapo mnajimu akalia sana na seyyid na wenzake wote pia wakalia.

Mwandishi (hayati) wa kitabu hiki alitembelewa katika mwaka 1930 a.d. na mnajimu mmoja kutoka bombay ambaye alikuwa na umri mkubwa, ndevu nyeupe na akijitambulisha kuwa ni husein brahmin. baniani wa aina ya brahmin alietokana na kizazi cha wafuasi wa iamam husein (a.s) alimwomba mwandishi amwulize suali lakini kwa vile hayati alikuwa na shughuli nyingi hakumjali. hata hivyo, mnajimu huyo aliendelea kukaa hapo na baada ya muda mfupi akaanza kumweleza habari ya maisha yake yaliyopita nay a baadaye, biashara yake, burudani, tabia zake njema na mbaya na vilevile afya yake, mwandishi alishangazwa; kwa hiyo, alianza kumsikiliza kwa makini. asilimia tisini na tisa ya aliyoeleza yalikuwa ya kweli. kwa hivyo, mwandishi akasema: "nimejishughulisha kwa muda mrefu sasa kujua habari za rafiki yangu. Nataka kujua yuko wapi, ana hali gani, yu hai au amefariki dunia, ana raha au ana shida na kama kuna uwezekano wowote wa kuonana naye. ukinipa jibu la kunitosheleza nitakupa rupia 25 za kihindi."

Kusikia hayo, mnajimu huyo akaanza kupiga mahesabu yake juu ya karatasi. kabla ya hayo alimsimulia mwandishi mambo mengi bila ya kufanya mahesabu yoyote. Mwandishi alipomwuliza kwa nini anafanya hivyo, mnajimu akamjibu kwamba aliweza kutoa habari zote kwa kutazama paji la uso wake, lakini sasa anahitaji msaada wa kalamu ili aweze kutafuta habari za rafiki yake. baada ya michoro mingi juu ya karatasi na mahesabu ya vidole na kuinamisha kichwa mara kwa mara kwa muda wa robo saa akasema: "Bila shaka rafiki yako unayemfikiria ni mtu mkubwa sana. yeye hutawala juu ya ulimwengu na mbinguni, hana wasiwasi wala shida yoyote ila fikra juu ya dini ya jadi yake. bila shaka yu hai na ana raha ya kila aina. karibu atajitokeza kutawala india, asia na dunianzima, na akaendelea kueleza sifa nyingi njema ya huyo rafiki (imam Mahdi a.s) ambazo zilimfurahisha mwandishi kiasi cha kumpa mnajimu rupia 25. mwandishi tena akamwuliza siku gani huyo mfalme atajitokeza ? akafanya mahesabu na akasema karibu sana katika muda wa miaka 25 au 30 atajitokeza na kushinda dunia nzima. (tanbihi: hakuna mtu yeyote anayeweza kutoa taarifa kwa uhakika siku gani mungu ataamua kumwamrisha imam mehdi(a.s) kujitokeza.

Hata hivyo mahesabu ya wanajimu yamethibitisha kuweko na kughibu kwa hadhrat mehdi(a.s) . muhaki-el-tusi, mwanazuoni maarufu wa shia ithnaasheria, alisumbuliwa sana na suala la "upekee wa mungu", ambalo aliulizwa na mlahidi (asiye amini mungu). alifanya mahesabu ya kinajimu kutafuta wapi hadhrat mehdi(a.s) atakuwa kwa wakati huo na akaona kwamba atakuwepo masjid-ul-kufa. kwa hivyo papo hapo aliondoka najaf, akakutana na imam(a.s) na akapata jibu la kumtosheleza na kutatua tatizo lake.

Imam(a.s) akamwuliza vipi alijua kwamba yeye yupo pale (masjid-ul-kufa). akamjibu kuwa kutokana na mahesabu yake, imam(a.s) akamsihi kwamba asirudie tena jambo hilo na muhakiki Attusi aliomba msamaha na kueleza kwamba alifanya hivyo kwa sababu ya tatizo alilo nalo na kuahidi kuwa asingerudia padri mmoja wa kiingereza alichapisha kitabu kiitwacho "maajabu arubaini ya siku zijazo" kutokana na kitabu cha nabii. daniel, kubusu vita, njaa na alama zingine zitakazo jitokeza katika siku za mwisho wa dunia. Kitabu hicho kilipendwa sana na kilichapishwa 1925 a.d., ambacho "hayati mwandishi alikisoma mwenyewe. padri huyo kaandika kuwa kutakuwa vita kuu katika siku zijazo na nchi tisa tu za ulaya zitasalimika.

Nchi ya kumi itakuwa syria ambayo mfalme wake yumkini atakuwa muhammad mehdi. huyo mehdi atakuwa mpinzani mkali wa ukristo. atavamia ulaya, atashinda na hatimaye kushinda dunia nzima. lakini atatawala kwa miaka saba tu na baadaye nabii issa atatokeza na ukristo utaenea duniani kote. hapo nabii issa atatawala miaka elfu moja. mwandishi (hayati) mwenyewe binafsi amekiona kitabu hicho toleo la l6 na kusoma yaliyomo, lakini katika matoleo yaliyo fuata jina la. mehdi limefutwa. padri huyo labda alitanabahi kwamba jina hilo huthibitisha ukweli wa uislam na wa imam mehdi(a.s) . Hata hivyo, ufutaji wa jina la Mahdi(a.s) hauwezi kukanusha ukweli. yeyote ambaye anaweza kupata nakala ya toeo la 16 la kitabu hicho ataweza kuhakikisha kwa dhati jina la imam mehdi(a.s) lilivyotajwa bayana.

Kwamba hadhrat mehdi(a.s) atatawala dunia nzima ni ushahidi madhubuti kuhusu kujitokeza kwake. kwamba baada ya utawala wake wa miaka saba utafuata uenezi wa ukristo duniani na nabii issa atatawala kwa miaka elfu moja si jambo la kuwababaisha wafuasi wa hadhrat mehdi(a.s) . ni imani yetu kwamba nabii issa atakuja baada ya muda mfupi wa kujitokeza kwa hadhrat mehdi(a.s) na dini pekee ya ukweli, uislam, itaenea dunia nzima. nabii isa kamwe hakudai kuwa mwana wa mungu na hakufundisha kwamba kuna mungu zaidi ya mmoja na huyu mungu ana mshirika yeyote. yeyote anaye amini katika upekee wa mungu, mtume muhammad(s.a.w.w) pamoja na manabii wote ni mwislamu. waumini wa nabii adam na manabii waliofuata ambao wamezingatia mafundisho yao, na kujizuia na maasi wote ni waislamu. katika qur'an tukufu kuhusu nabii Ibrahim Mungu anasema: "Amewaiteni jina la waislam ." (22:78).

Katika zaburi aliyoteremshiwa nabii dawood, aya ya nne, sura 19, murmuz, imeandikwa kwamba katika siku za rnwisho za dunia atakuja mtu mmoja ambaye atakuwa na kivuli cha wingu juu yake na ambaye ataeneza usawa na insafu.

katika kitabu cha mtume safyay, aya ya 3, imeandikwa: "Tahadharini kwamba katika siku za mwisho duniani atatokeza mtu mmoja ambaye atasababisha watu wote kumwabudu mungu mtindo mmoja (wote wataamini katika upekee wa mungu). Katika kitabu cha mabaniani (hindoo) fat ankal imeandikwa kuwa, "maisha duniani yatagawanyika katika vipande vinne, na kila kipindi kitagawanyika katika mida maalum na kila muda utakuwa wa kipindi cha miaka elfu nne. dunia itaendelea kwa muda wa miaka 256,000 na mwisho atatokeza mtu rnmoja muadham. huyo atatokana na kizazi cha viongozi wakuu wawili, mtume wa mwisho(s.a.w.w) na mrithi wake ajulikanaye kwa jina la bishan. Jina la huyo mtu atakaye tokeza itakuwa mwongozi (Mahdi) na atakuwa walii wa ram (Mungu).yeye atatawala dunia kama walivyotawala mitume walio pita na ataonyesha miujiza mingi; yeyote atakayemkubali huyo (Mahdi) ataokoka. Atakuwa na maisha marefa na ataishinda dunia nzima, atabomoa jumba la masanamu somnath na kutokana na amri yake sanamu kuu jaganath litapata uwezo wa kusema na baadaye litaporomoka. mwishowe kwa agizo lake masanamu yote yatavunjwa duniani kote.

Katika kitabu cha dini ya hindoo kiitwacho nasak, imeandikwa kuwa: "wakati dunia itakapo karibia kwisha kutakuwa ufalme ambamo ukweli na insafu itatawala. hazina zilizojificha chini ya bahari kuu, majabali au ardhi zitajitokeza na kuanza kuelezea siri zitajitokeza na kuanza kuelezea siri zote za duniani na mbinguni. katika kitabu cha dini ya waabudu moto "zand vapa zand" ambacho huaminiwa kama kataremshiwa nabii zardosh, kuhusu hadhrat mehdi(a.s) . vile vile katika vitabu vingine "kosab na azwasan' imeandikwa juu ya habari za imam mehdi(a.s) . Hakim jamasap katika kitabu kuhusu Mtume(s.a.w.w) na warithi wake amearidhia: "mtume mmoja atazaliwa katika milima ya uarabuni, atapanda ngamia na atakaa na kula na watumwa (hatakuwa mtu mwenye kiburi).

Yeye atafuta dini zingine zote, atashinda iran na kubatilisha dini ya waabudu moto. mrithi wa mwisho wa huyo mtume(s.a.w.w) atakayetokana na kizazi cha binti wa mtume(s.a.w.w) atatawala dunia nzima kwa uwezo aliopewa na mungu. utawala wake utaanzia makkah na utaendelea mpaka siku ya kiama. Atamkamata na kumfunga adui wa mungu, aharman (iblisi) na malaika kutoka mbinguni watafika kwake. atawafufua (waliokufa na kupata uhai kwa amri ya mungu) wema na waovu. atawapa jazaa wema na kuwaadhibu waovu. atamfufua baba yake nabii khidhr, nabii elias, mahras, lafvas baba wa ahasata lalis, nuh, shamasun na solan shamueel. Vile vile atawafufua namrood, firaun, hamman na kuwachoma moto."

Mengi yameandikwa kuhusu huyo mfalme (hadhrat Mahdi a.s.) wa siku za mwisho za dunia. katika vitabu vingi vya manabii wa zamani na vile vile katika vitabu vitukufu: torat, injiil na zabur na vile vile katika vitabu vingine vya dini zingine (zisizokuwa za kiislamu). zaidi ya hayo, wakristo, mayahudi, waabudu moto na mabaniani wanamsubiri mwongozi. wakristo humsubiri nabii issa na mayahudi nabii mussa. kwa hivyo, dunia nzima humsubiri huyo 'hadi' ambaye atasafisha dunia hii kutokana na maovu, fitina, ugomvi, vita, maafa, mateso au ulahidi na kueneza usawa wa uadilifu. kwa jumla, imani ya watu wote duniani huthibitisha imani yao juu ya "anayesubiriwa" na huimarisha hoja ya kwamba hao wote waliodai kuwa mehdi ni wadanganyifu tu. hawakuweza kutimiza chochote kama anavyotarajiwa kutimiza mehdi wa kweli.

Bayasajee aliandika kitabu 'bothiran sandhram' na gosai tulsidasji alitafsiri hicho kitabu katika lugha ya kihindi. Katika sura ya 12; ya tafsiri hiyo, ukurasa 212, ameandika: "Mimi sitaandika chochote kutokana na maoni yangu lakini ukweli mtupu ulioandikwa katika ved na purana. Katika muda wa miaka kumi nguvu zote zitamalizika na hakuna yeyote atakuwa na nguvu kama hiyo tena. badala ya hayo nyota itang'aa pahala patakatifu duniani. Miujiza yasiyoaminika yatafanyika na walii aliyekamilika atateuliwa duniani. yeyote atakayetamani kupata ridhaa ya mungu atawajibika kumtii muhammad. baadaye atatoka mtu atayejulikana kwa jina la mehdi. uwezo wote utakuwa wake (imenakiliwa kutoka gazeti la kisunni molvi-delhi- rasool, safar/rabiul awwal. 135z ah).


12

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 16

HADITHI KUHUSU MUDA WA KUSUBIRI (INTIDHAR) NA MAJARIBIO YA MUDA HUO

1. Hadhrat imam Ali Ridhaa(a.s) amessema kwamba: katika qur'ani Mwenyezi Mungu amezungumzia juu ya kugojea:

"Basi ngojeni; ngojea hapo. mimi vilevile nitakuwemo katika wale wanaongojea" (7:71).

2. Hadhrat Ali(a.s) amesema:"ngojea (msubiri) kutokeza imam mehdi; hivyo, yeyote atakayesubiri amri zetu atazawadiwa cheo cha shahidi anayegalagala katika damu yake" .

3. Hadhrat imam Jaafar Sadiq(a.s) ameeleza: "kutakuwa kipindi ambamo imam(a.s) atakuwa haonekani kwa wafuasi wake ambao itawabidi wavumilie mateso kutoka maadui wao kwa muda mrefa mmo siku ya kiyama watapewa habari njema kutokana na imani yao juu ya imam aliyeghibu, madhambi yao yatasamehewa na mema yao yatazawadiwa, na kwa sababu ya hao waumini duniani kutanyesha mvua na kuota vyakula. wasingekuwepo allah aangeliwateremshia adhabu hao wahalifu.

4. Imam Jaafar Sadiq(a.s) amesema kwamba:"Mwumini yeyote atakaye msubiri imam wake aliyeghibu kwa makini akifariki dunia atapewa jazaa ya kuishi na imam mehdi (a.s)." .

5. Imenakiliwa kutoka abdulhamid wasti kwamba yeye alilalamika kwa imam hadhrat muhammad baqir(a.s) kwamba kusubiri daima usiku na mchana kwa ajili ya mwokozi wa mwisho huathiri shughuli za kila siku maishani. imam akajibu "yeyote mwenye imani kuwa mungu atamwokoa kwa mkono wa wokovu, mungu mwenyewe humtimizia mambo yake. mwenyezi mungu amteremshie rehema huyo mwumini ambaye huvumilia shida kwa ajili yetu na hueneza hdithi zetu (mambo ya dini) kwa waumini wengine." adbulhamid akauliza tena, kama huyo mtu akifariki dunia kabla kujitokeza imans(a.s) je? imam akamjibu kwamba yeyote anaetamani kwamba atakapojitokeza hadhrat mehed(a.s) yeye awe mmoja wa wasaidizi wake kwenda vitani naye, atapata daraja kama ya mtu yule ambaye aliyeishi pamoja na hadhrat mehdi(a.s) na kupigana vita vya dini kutokana na amri yake (imam mehdi).

6. Mtume mtukufu(s.a.w.w) aliwaambia masahaba wake: " katika siku za mwisho za dunia wema wa mwumini mmoja utazidi wema wa watu 25 wenu". Masahaba wakalalamika kwamba wao walikuwa pamoja na mtume(s.a.w.w) na wamekwenda vitani naye. lakini mtume(s.a.w.w) akajibu, "siku za mwisho duniani waumini watakuwa wamezingirwa na maadui, kuzungukwa na maafa yaliyo sababishwa na maadui wao, lakini hata hivyo watakuwa imara katika imani yao kiasi hata nyinyi hamtaweza kulingana nao.

7. Imam wa tano, hadhrat muhammad baqir(a.s) . akiwahutubia marafiki na mashia juu ya dhuria ya mtume(s.a.w.w) akasema:"kumbukeni kwamba bila shaka rntatahiniwa katika uthabiti wa imani yenu na hiyo imani itatoweka bila nyinyi kufahamu. hilo jambo litakuwa kama mfano wa wanja, unapokuwa machoni hudhihirisha athari yake lakini hutoweka (yeyuka) bila mtu mwenyewe kufahamu. vilevile kati yenu watakuwa watu ambao asubuhi wataamka waumini lakini magharibi watakuwa wamepotelewa na imani yao bila wao wenyewe kufahamu" .

8. Hadhrat imam Jaafar Sadiq(a.s) amesema:"Wakati waovu namakafiri watakapoeleza (julikana) imani yao kadamnasi na waumini kudhihirisha imaniyao na tofauti baina ya waumini na makafiri kudhihirika, na watu kukata tamaa na kufa moyo ndipo imam (a.s) atajitokeza." maana ya hadithi hii ni kuwa yatakuwa majaribio magumu mno. wale watu ambao hawajali dini yao na kwa hivyo ni wazembe wa kuswali, au kufunga na kutekeleza maagizo mengine ya kidini, waliojishughulisha katika mambo ya dunia, na ni wadhalimu watafedheheka, na kwa upande mwingine wale wacha mungu waswalihina, wanaofunga mwezi wa ramadhani na kutekeleza maagizo mengine, wema, waoambao toba, wenye huruma na wathabiti katika imani yao watafaulu majaribio hayo.

9. Zaidi ya hayo imam Jaafar Sadiq(a.s) alimwambia Abu Basir kwamba: theluthi mbili ya wafuasi wa hadhrat hujjat(a.s) wataacha dini (kwa sababu ya dhambi zao na uzembe wao watakata tamaa na kwanza kuuliza ikiwa imam(a.s) yupo ughaibuni kwanini hajitokezi? Kwa hivyo, watapoteza imani yao juu ya imam(a.s) .

10. hadhrat imam muhammad baqir(a.s) amesisitiza kwamba bidii ifanywe ya kuwasimulia waumini hadithi ya kughibu na kuonekana tena kwa hadhrat imam mehdi(a.s) na wale wasioamini waache walivyo.

11. Hadhrat Ali(a.s) ameserna: "Nyinyi waumini ni kama nyuki. Watu duniani watafikiri nyinyi wanyonge, wanyenyekevu, na msiothaminika. hawatatambua sifa zenu. kumbukeni kwamba imam wenu hatatokeza mpaka nyinyi mtapo gombana na kila mtu kumwita mwenzie mwongo kutokana na mafarakano baina yenu. katika siku hizo za majaribio na mitihani wachache mno watabakia juu ya imani yao kwa uthabiti".

SURA 17

ALAMA ZITAKAZO DHIHIRIKA KATIKA SIKU ZA MWISHO ZA DUNIA

Wakati huu, yaani siku za mwisho (Akhiru Zamani) dunia imezingirwa na ulahidi, ukafiri, udhalimu, uovu na ukandamizi. binadamu amezongwa na ugomvi, vita, jefule na amepoteza imani juu ya mungu. Hata hivyo, kipindi hiki kinajulikana kama ni kipindi cha ustaarabu, elimu, utafiti, ufumbuzi na hekima. jumuia zingine zimefuata nyayo ya maendeleo ya kipindi hiki nasi twashawishika tufuate mtindo huo. Hata hiyyo, maendeleo yote ya zamana hii humezwa na ugomvi, vita na dhuluma.

Hadhrat Ali(a.s) amesema kwamba:katika siku za mwisho za dunia binadamu atapoteza busara yake na kupotoshwa katika mawazo yake, kila kilichokuwa chema atakiona kibaya na kiovu, lakini uzushi (bidaat) katika mambo ya dini, uasherati, uhayawani utatukuzwa . kuna hadithi nyingi zinazoeleza alama za siku za mwisho za dunia. nyingi zimekwisha dhihirika na zingine zinadhihirika. alama muhimu zitadhibirika katika muda mfupi kabla ya kujitokeza kwa imam(a.s) .

Hadithi chache kuhusu alama hizo ni kama zifuatazo:

1. Mtume mtukufu(s.a.w.w) ameridhia kuwa utafika wakati:

a) Mtu atamthamini mwanazuo (Aalim) kufuatana na mavazi mazuri yake.. (wataangalia mapambo ya mwanazuoni, mwanazuoni wa kweli atadharauliwa na atabaki fukara).

b) watu watatamani kusikia qur'ani kutokana na uzuri wa sauti ya wasomaji (qur'ani husikilizwa katika redio, na kaseti kutokana na uzuri wa sauti ya wasomaji).

c) watu watamwabudu mungu katika mwezi wa ramadhani tu. (katika miezi mingine usomaji wa qur'ani, ibada na saumu vitasahaulika). ukija wakati kama huo watu watateseka kutokana na watawala dhalimu.

2. hadhrat ali (a.s) amesema kwamba: "katika siku za mwisho za dunia mfalme wa iran atapinduliwa. ataomba msaada kutoka wasio waislamu. mashavu ya miguu yake yatakuwa membamba (yeye kwa maumbile atakuwa mnene mno). jina la mfalme huyo litakuwa ahmed (huyo alikuwa mfalme wa mwisho katika ukoo wa kajar). alipopinduliwa alikimbilia paris (ufaransa) na kufia huko huko. hata jina lake lilibashiriwa miaka 1300 kabla ya hadhrat ali(a.s) .

3. Hadhrat ali(a.s) vile vile alisema katika siku hizo waislamu watavaa vitambaa vya rangi shingoni mwao.

4. Vilevile amesema: "tehran itakuwa kama gereza na jahannam kwa waumini, lakini pepo kwa wale wasio na imani. hapatakuwa kitu chochote cha dini (uislam), wanaume watakuwa na tabia za kike na wanawake watadharau buibui, watatembea uso wazi masokoni na kujazana barabarani.

5. katika vyuo watakuwa wanafunzi wa aina mbili:

a) Wale ambao wanajifunza falsafia.

b) Wale ambao wanajifunza mambo yasiyo husiana na uislamu.

6. Hadhrat imam Jaafar Sadiq(a.s) amesisitiza kuwa: "Wakati nchi zinazingirwa na balaa, fitina na uovu inafaa mtu ahame kwenda kuishi katika jiji la qum, iran, ambalo litakuwa pahala pa amani na kuepukana na maafa, vyuo vya elimu vitahamia qum kutoka najaf, karibu na wakati wa kujitokeza kwa imam mehdi(a.s) . qum kutakuwa makao makuu ya kujipatia masomo ya dini ya kiislam.

7. Namna wanawake wanaotembea bila haya na kutojifunika huku kujipamba ni mojawapo ya alama za mwisho wa dunia. kuna hadithi nyingi kuhusu alama kama hii na tunazinakili chache tu.

a) Hadhrat Ali(a.s) amesema"Wanawake watakuwa hawana haya. watajihusisha na wanaume wasiokuwa waume zao. mitindo ya usukaji wa nywelie utafanana na nundu iliyojitokeza ya ngamia. wanawake hao katu hawataingia peponi" (kitu kilichobashiriwa na mtume(s.a.w.w) na maimamu kabla ya miaka 1300 kinaonekana dhahiri kabisa na kuthibitisha ukweli wa hadithi hizo, na wa uislaam).

Mwanazuoni huyo akawaalika waisraeli hao kwake msituni. wachache wakaenda kumtembelea. usiku mmoja wenye mwangaza akatabiri kwamba wakati wa kuja. kwa mkombozi ulikaribia. walipokuwa wame.shughulika katika mazungumzo yao. wakamwona kijana mmoja mrefumwenye uso mwangavu mbele yao. huyo mwanazuoni ambaye akizijua sifa za nabii musa papo hapo akasujudu kumshukuru mungu na waisraeli wote walienda sijda kumshukuru mola. walibusu miguu ya nabii musa na kueleza mateso waliyopata kutoka kwa firaun. nabii musa akawatuliza na kuwahakikishia kwamba ushindi umekaribia na akapoteamachoni mwao. nabii musa akaelekea madyan nyumbani kwa nabii shuaib na akafunga ndoa na binti wa nabii shuaib kwa sharti ya kumtumikia nabii shuaib kwa muda wa miaka kumi.

Kipindi cha kwanza cha kujificha kwa nabii musa ni sawa na kughibu kwa hadhrat mehdi(a.s) kwa muda mfupi. usumbufu kwa waisraeli ulizidi kuongezeka na subira ilikuwa inapungua. kwa hivyo, baada ya miaka kumi walienda kamwona huyo mwanazuoni ambaye aliwaarifu kuwa alikuwa amepata ilhamu kutoka kwa mwenyezi mungu ya kuwa ushindi wao ungepatikana katika miaka arobaini. kusikia hivyo, wao wakatamka "alhamdulillah" (sifa zote ziwe kwa mungu). kushukuru huku kulimfurahisha mungu. naye akawapunguzia muda wa kuteseka uwe wa miaka ishirini. habari hii njema alipashwa mwanazuoni huyo na mungu. mwanazuoni akawaeleza waisraeli kuwa shukraini zao zimeleta faida hiyo. kusikia tu hivyo, waisraeli wakasema "rehema na huruma zote hutoka kwa mwenyezi mungu peke yake". hapo tena mwanazuoni huyo akapata ilhamu ya kuwa mwenyezi mungu amewapunguzia huo muda uwe wa miaka kumi. waliposikia hayo wakasema kuwa hapakuwa na mwingine ila mwenyezi mungu mwenye uwezo wa kuwakomboa.

Punde si punde, wakamwona nabii musa ametokeza. wakasujudu kwa mwenyezi mungu na kumbusu miguu nabii musa ambaye aliwafikishia habari njema ya kuwa aliamrishwa na allah kujitokeza ra kumkabili firaun na akawaamrisha waondoke. baada ya hapo nabii mussa akaelekea kwenye kasri ya firaun ambaye akaamrisha wachawi wake wahudhurie. nabii musa akatoka misri na waisraeli 600,000, wake kwa waume, wazee na vijana, na akavuka mto. lakini firaun na wafuasi wake wengi walipojaribu kuuvuka mto wakazama. hivyo inathibitika kujificha kwa hadhrat musa na majaribio na mitihani kwa wafuasi wake. vivyo hivyo wafuasi wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) hujaribiwa na kutahiniwa.

Kujificha kwa nabii suleiman nabii dawood alirithiwa ufalme na nabii suleiman. baadaye nabii suleiman kwa amri ya mungu akajificha kutoka wafuasi wake na tatika kipindi hicho akapata taji ya ufalme. hadithi yake ni kama ifuatayo: nabii dawood aliimarishwa na mungu kumteua mwanawe wa mwisho suleiman kuwa mrithi wake. nabii dawood aliwajulisha wanawe na wafuasi wote juu ya uamuzi huo. waisraeli hawakupendezwa na uamuzi huo eti ulikuwa sio wa insafu kwa sababu nabii suleiman alikuwa mdogo kuliko wote na kaka zake walikuwa wenye uwezo na ujuzi.

Nabii dawood akawaambia kwamba hakuna yeyote anayeweza kutengua amri ya mungu. Lakini kuwatosheleza akawaomba wanawe kuweka vitawi vilivyoandikwa majina yao katika chumba maalum, na vile vile akamwomba nabii suleiman kuweka vitawi vilivyo andikwa jina lake katika chumba hicho maalum. siku ya pili wote walitakiwa wafike kuangalia kwamba vitawi gani vime mea na kuota majani na matunda.

Mwenye vitawi vilivyo mea na kuota majani na matunda ndiye atakuwa mrithi wake. wote waliridhika na wazo hilo na wakaleta vitawi. siku ya pili walipofungua hicho chumba ilionekana kuwa vitawi vya nabii suleiman tu vilikuwa vimeota majani na kuzaa matunda. kwa hivyo wote walikubali uteuzi wa nabii suleiman.

Kuthibitisha zaidi ustahilifu wa nabii suleiman, nabii dawood akamtahini elimu yake na uwezo wake kadamnasi ya waisraeli. akamwuliza "kitu gani humpa mtu furaha na utulivu wa moyo?" nabii suleiman akajibu "kusamehewa na mungu na kusameheana watu wenyewe". nabii dawood tena akamwuliza: "kitu gani chenye ladha mno?" "huba na urafiki wa ukweli kwani upendo na urafiki wa ukweli ni zawadi na rehema kutoka kwa mungu juu ya viumbe wake." (katika zamana hii zawadi ya mungu ya mapendano na urafiki imepotea na badala yake uadui, husuda na dhuluma imezagaa ambayo ni adhabu kutoka kwa mwenyezi mungu).

Nabii daudi alifurahishwa sana na ubora na usahihi wa jibu kutoka kwa mwanae. akawauliza waisraeli kama wameridhika kwamba nabii suleiman alistahili urithi kwa kila njia. baada ya kifo cha nabii dawood, nabii suleiman kutokana na amri ya mungu alienda kujificha. katika kipindi hicho wafuasi wake waliteseka na kupata shida. nabii suleiman alikwenda kujificha katika nchi ya jirani ambako aliolea na kuishi na wakwe zake. siku moja mkewe akamwambia kwamba anampenda sana kwa tabia zake, sifa na ukarimu wake. lakini huona dhila kutegemea wazazi wake na alimpa wazo la kujitafutia maisha yake na kujitetegemea kimapato. nabii suleiman akajibu kwamba hakuwa na ujuzi wa kazi yoyote ya kujikimu kistahiki kwa sababu hakuhitajika kufanya kazi (kwa muda alikuwa mwana wa mfalme).

Hata hivyo, aliahidi kwamba siku ifuatayo atakwenda sokoni kujitafutia mapato. alijiandaa kwenda kufanya kazi, lakini hakufanikiwa chochote. mkewe mwema akamtuliza moyo na akampa hima kwamba ajaribu sikuya pili. siku ya apili vile vile nabii suleiman akarudi mikono mitupu. tena mkewe akamsihi asivunjike moyo na kumhakikishia kwamba kutokana na rehema ya mungu atafanikiwa. siku ya tatu nabii suleiman akenda pwani na kumwomba amtumikie mvuvi kwa ujira wowote, mvuvi akakubali ombi na jioni yake akampa nabii suleiman samaki wawili kama ujira wake. nabii suleiman alifurahi na akamshukuru mungu nabii suleiman akamkata samaki huyo vipande na kumsafisha. tumboni mwa samaki mmoja nabii suleiman akapata pete moja.

Kwa vile alikuwa nabii, akatambua kuwa hiyo pete ni dalili yq ufalme. akasafisha hiyo pete akaiweka kwenye leso na kuweka mfukoni mwake. baadaye, akawachukua hao samaki wawili na kwenda nyumbani, ambako akamwona mkewe amefurahi sana. huyo mkewe akamwita baba yake akamwonyesha samaki wawili, nabii suleiman hapo akamwuliza baba mkwe " unajua mimi nani" huyo baba mkwe akajibu kwamba nabii suleiman alikuwa mtu mwema na yeye (bab mkwe) akimhesabu kama mwanawe lakini alikuwa hamjui kama yeye ni nani. hapo nabii suleiman akamsimulia kwamba yeye ni mwana wa nabii daudi, mwana wa mfalme na mriuthi wa kiti cha ufalme. akatoa hiyo pete kutoka mfukoni mwake na kuivaa. papo hapo, majini na ndege kutoka pande zote walikusanyika bele yake.

Nabii Suleiman akaelekea kwenda mji mkuu pamoja na mkewe na wakwe zake. wafuasi wake walifurahi sana kumwona nabii suleiman na walimshukuru mungu. hii ni mifano miwili kuhusu kujificha kwa mitume. wafuasi wa kila mtume walijaribiwa. kujificha kwa manabii yusuf ibrahim na idris kumeelezwa katika vitabu vingine. kwa kufupisha kitabu hiki hatuandiki habari hiyo humu.


13

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 18

BIBI, AZALI, BAHI KAMA VILE HUKO PUNJAB

Mirza alifanya daawa ya utume na umehdi, huko iran, kabla ya miaka 100, yalizuka madhehebu mapya ya babi, azali na bahai. wafuasi wa madhehebu hayo hadi leo wako iran na india. katika kitabu kidogo kama hiki haiyumkiniki kueleza maisha ya babi azali na bahai na ubatilisho wa madai yao. hata hivyo, tutaeleza kwa muhtasari historia ya madhehebu haya.

Mwanzilishi wa ubabi alikuwa mirza ali mohammad mirza raza shirazi. vichepuko vya madhehebu ya babi vikawa madhehebu ya azali na bahai yakimhesabu baab kuwa mtume na ishara ya habari njema kwa sababu alibashiria juu ya ndugu hao wawili. katika mabahai, baab hujulikana kuwa ni mtu mmoja tu aliyebaki hai kutokana na dhuria ya mtume(s.a.w.w) na mirza husseinali ni nabii issa wa pili anaye subiriwa. baada ya kifo cha mirza muhammad baab, wafuasi wake hawakumtambua au kumkubali mirza yahya subhe azal au mirza husseinali kama walivyomkubali baah. mirza alidai kwamba baab alitangaza kuja kwake (mirza yahya). Mirza husseinali baha mwanzoni alimkubali ndugu yake na kueneza madhehebu yake kwa niaba ya nduguye lakini baadaye akageuka na kutangaza kuwa madhehebu ya nduguye ni udanganyifu na kubatilisha madai yake kuwa ni ya uongo kuanza kueneza madhehebu yake mwenyewe ya ubahai.

Kutokana na mafarakano baina ya ndugu wawili hao, damu nyingi ilimwagika. Wafuasi wa mirza yahya wakajitambulisha kuwa maazali na wa mirza husseinali kuwa mabahai siku hizi wamisionari wa kibahai wameenea kote katika mabara ya asia, ulaya na afrika. Vipi mtu anaweza kuwa na daawa ya kuteremshiwa wahyi wakati yeye mwenyewe amebadilisha dini yake mara tatu! Kwanza alikuwa shia ithnaasheri, baadaye akaungana na madhehebu ya ubabi na baadaye kuwa misionari wa madhehebu ya nduguye mirza yahya azali. Hatimaye akawa mwanzilishi wa madhehebu yake na kujitangazia kuwa yeye ni mehdi anayesubiriwa. Madhehebu yake ni mchapuo wa madhehebu ya ubabi.

Albayan husemekana ni kitabu alichoteremshiwa mwanzilishi wa madhehebu ya baab. maadili kadhaa kutoka kitabu hicho yanaorodheshwa hapa. Itadhihiri kwamba maadili yote ni kinyume cha maagizo ya qur'an na hadithi.

1. Swala ya jamaa hukatazwa.

2. Badala ya raka 17 za kila siku mtu aswali rakaa tisa tu na kuna mabadiliko mengi katika hizo swala.

3. Kufunga katika mwezi wa ramadhan kumekatazwa na badala yake mtu afunge siku 19 tu kuanzia tarehe 1 machi (asrarul akaeed, uk. 830.

4. Kuoga tohara baada ya mtu kujamiiana na mwanamke au kutoka manii usingizini sio lazima.

5. Mwanamke yeyote, ila mama mzazi, huweza kufungwa naye ndoa.

mwanzoni, mwanzilishi wa madhehebu ya babi mirza muhammadali baab alikuwa shia ithnaasheri. alikuwa mwanazuoni wa kidini huko najaf-iraq. Baadaye alikwenda iran na akaanza uombezi. alikuwa akisimama kichwa wazi juani kwa muda mrefu. mwishowe, akapotelewa na akili na kujitangazia kila daawa. Katika 1844 a.d., mirza ali muhammad akaanza kutangaza dini yake. Akatangaza yeye ni mlango wa mungu (huwezi kumfikia mungu bila kupita kwake), mti wa toor, mehdi anayesubiriwa na mwishowe nabii.

Katika majadiliano bayana na mwanazuoni wa shia itbnaasheri akatangasza "kauli zangu ni bora na zenye ufasaha zaidi kuliko qur'ani. Madhehebu yangu hubatilisha uislaam. Tahadharini mimi nitawaua wapinzani wangu wote". Aliwaamuru wafuasi wake kuongeza katika adhana kauli ya ushahidi kwamba ali muhammad ni dalili ya mungu na vile vile natoa shahada kwamba ali muhammad ni mlango wa mungu".

Katika washabiki wakuu wa kueneza na kukubali madhehebu ya babi alikuwa mwanamke mmoja, kurratui ayn, ambaye alikuwa binti wa mwanazuoni naye aliolewa na mwanazuoni. Alikuwa mwanamke mjanja, aliyeelimika na msemaji hodari. Jina lake la mwanzo lilikuwa zarrin taj na alikuwa mwanamke mwenye sura nzuri sana. Kutokana na mafarakano na mumewe akaungana na madhehebu ya babi ili alipize kisasi dhidi ya mumewe. Kila alipopata fursa alionyesha umbo na uzuri wake kwa kuvua buibui lake hadharani. Siku moja alipanda juu ya mimbari mbele ya watu wengi, akavua buibui na kutangaza: "marafiki na maadui! Kutokeza kwa madhehebu ya babi kumebatilisha uislam.

Amri zote kuhusu swala, saumu, kutoa sadaka na kadhalika zimetanguliwa. Tahadharini hadhrat baab ataiteka dunia nzima na karibuni hakutakuwa na dini yoyote duniani ila ubabi na kwa hivyo kila mtu anawajibika kuungana nasi kwa wingi kadri iwezekanavyo." achilieni mbali buibui ambalo lawatenganisheni na wanawake. Mkumbuke kuwa mwanamke ni ua linalonukia la bustani la dunia hii. hivyo, lichume na kulistaladhi. ua huzawadiwa kwa marafiki. tamaa mbele giza. msikose kuwapa marafiki zenu, wake zenu na maana vikwazo kama hivyo vimekwisha ondolewa katika madhehebu ya ubabi. Staladhi raha zote za dunia maana hakuna lolote baada ya kifo." mwenye akili hahitaji maelezo zaidi kuhusu imani ya madhehebu hayo.

Ubahai ubahai ulianzishwa 1853 b.k. na mwanzilishi wake ni hussein ali ambaye hujulikana kama bahaullah, huko mazinderan iran baada ya kuacha madhehebu ya ubabi. Watu wengi waliuawa. Mwishowe kwa amri ya shah wa iran, nasiruddin, bahaullah akafungwa jela na kufia huko gerezani 1886. Alirithiwa na mwanawe abbas effendi ambaye alistakimu katika jiji la akka huko falestina.

Profesa browne aandika kwamba ubahai ni muundo mpya wa ubabi. kama vile mababi humtukuza ali mubammad (baab) kuwa mtukufu mno vivyo hiyyo mabahai vile vile humfikiria mirza husseinali bahauddin kuwa mtu mtukufu mno. mabahai huamini kwamba ali muhammad baab alibashiri tu juu ya kutokeza kikamilifu kwa amri ya mungu na hilo likafuatwa na kuzaliwa kwa bahauddin kwa sababu mirza hussein ali alikuwa kiwiliwili cha mungu. Hata bahaullah mwenyewe alipokuwa gerezani alitangaza kwamba "hakuna mungu ila mimi mwenyewe aliyefungwa na kukandamizwa." Mtu atamfikiria nini huyo mungu anayefungwa gerezani na anayekandamizwa? madhehebu hayo vipi huweza kuhesabiwa kuwa na uhusiano wowote na uislam?

Kitabu cha kwanza cha mabahai kilikuwa aykaan. baada ya kujitangazia kama yeye mwenyewe ndiye mungu akachapisha kitabu cha pili kiitwacho aqdas ambacho kinadaiwa kuwa ni bora kuliko vitabu vyote vya dini. Katika humo imearidhiwa: "mama zenu tu hamwezi kulala nao na ustaarabu tu unakataza kutoa kanuni kuhusu kumfeli mtoto mwanamume mwenye sura ya kupendeza". hivyo, inamaanisha kwamba mtu anaruhusiwa kuingiliana na kila mwanamke ila mama yake mzazi na vile vile kufeliana na mwanaume mwenzie. Uchochezi wa babi-bahai ulisababisha umwagaji mkubwa wa damu huko iran. wanazuoni, mawaziri na mwishowe shah wa iran nasirrudin shah waliuawa. Idadi kubwa ya mababi na mabahai waliokuwa iran ni mayahudi wa hamadan kashan na yazd waliokubali madhehebu hayo, na vile vile maparisi wa iran na india. waislamu wachache mno walikubali madhehebu hayo.

Mmisionari mkuu wa madhehebu ya bahai, mirza hassan niku, alikuwa mwakilishi wa abbas effendi, mwana wa bahaullah. Abbas ambaye alitunukiwa jina kuu la "jibrael" na mabahai. Jina lake la kiislaam lilikuwa abdulhussein ayni naye alikuwa mfuasi mkuu wa madhehebu hayo. Hao wote pamoja na wamisionari wakuu wa madhehbu hayo wakatubu na kuandika vitabu dhidi ya ubahai na kufichua mabaya ya madhehebu hayo. Avarah katika kitabu cha kashful hiyal amechapish kibayana picha zinazofichua siri za madhehebu hayo. Kwa sababu tu kuimarisha upinzani dhidi ya uislaam huko iran ndiyo mayahudi na maparisi walijiunga na madhehehbu hayo.

Mdai umehdi katika karne ya 13 na 14, mirza kadiani mwanzoni mwanazuoni mubalighi wa kisunni. pole pole, akaanza kudai umehdi, unabii na mwishowe uungu. Vile vile, mirza mohammad ali baab wa ubaabi na husseinali bahaullah wa ubahai mwanzoni walikuwa mashia kila mmoja akaanzisha madhehebu mapya na wakadai kuwa ni wawakilishi wa baab, mehdi, nabii na mwishowe mungu.

Babu zake his highness agakhan walikuja india kutoka iran wakiwa shia ithnaasheri na kuamini maimam kumi na wawili, watukufu kumi na wanne na wakifuata sheria za kuswali, kufunga ramadhaai na kanuni zote za madhehebu ya shia. Siku za mwanzoni, viongozi wa dini ya agakhan walijulikana kwa jina la 'peer' jamatini watu wa kiswali na kufunga ramadhani. Qur'an ikisomwa na watu wakiamini maimam kumi na wawili. Pole pole katika karne hii maaghakani ikaanza daawa ya umehdi, unabii na hatimaye kiwiliwili cha mungu.

Mwanzoni wafuasi wa agakhan wakijulikana kwa jina la bhagat na mashia ithnaasheri subhanya. baadaye waaghakani wakajigeuza kuwa maismaili na kitambo kidogo wamekuwa wakijitambulisha kama shia imami ismailia. kwa upande mwingine, kwa mujibu wa itikadi ya shia ithnaasheri, tangu kuja kwa uislam, imani katika qur'an, maimam kumi na wawili, kuzaliwa kwa hadhrat mehdi(a.s) , kughibu kwake na kutokeza mara ya pili kumethibitishwa kutokana na qur'an, hadithi na historia. Dalili madhubuti za uhakika huo na ufanunuzi wake umeelezwa kikamilifu katika kitabu hiki.

Waliodai umehdi walijitokeza mmoja baada ya mwingine, na kueleza nadharia zilizokuwa kinyume na tofauti na maadili ya kiislam kama ilivyoelezwa katika qur'an na hadithi. Hapana shaka wadai wote hao hawawezi kuwa wakweli kwa sababu ubashiri uliopo ni wa mehdi mmoja tu. Hadithi maarufu ya mtume mtukufu(s.a.w.w) kwamba watakuwa maimam kumi na wawili baada yake na wa mwisho ni hadhrat mehdi(a.s) imenakiliwa na wanazuoni maarufu wa kisunni katika vitabu vifuatavyo:

1. Kanzul umal, juzuu la 6, uk. 198

2. Sunan Abi Daud uk. 588

3. Jaamiu Tirmidhi uk. 269

4. Sahih Muslim, juzuu la pili, uk. 119

5. Sahih Bukhari, kitabul fitan, babul istikhlaf, juzuu la 29, uk.629

bila shaka mtume mtukufu(s.a.w.w) alitangaza hadithi hiyo kuhusu maimam kumi na wawili kutokana na amri ya mwenyezi mungu mwenyewe. Kwa hivyo, lazima wawe warithi 12 wa mtume(s.a.w.w) . Basi imani yoyote kuamini warithi zaidi ya kumi na wawili wa mtume(s.a.w.w) haiwezi kuwa na ridhaa ya mungu na mtume(s.a.w.w) .

Ifuatayo ni orodha ya madai ya warithi wa mtume(s.a.w.w) :

1. Msururu wa kwanza ni wa khulafaul rashidin ambao walikuwa wanne tu na sio kumi na wawili.

2. Msururu wa pili wa daawa ya urithi ni kutoka nasaba ya bani umayya ambao walikuwa kumi na wanne.

3. Msururu wa tatu ulikuwa wa bani abbasi ambao walikuwa 37 (thelalhini na saba).

4. Msururu wa nne ulikuwa mchanganyiko wa watu wa misri na bani abbas ambao walikuwa kumi na wanane. halaku khan alikomesha ukhalifa wa bani abbas huko baghdad, na mfalme wa misri alimtawaza mwana wa mfalme wa bani abbas kuwa khalifa na kufanya idadi yao iwe kumi na wanane.

5. Msururu wa tano unatokana na makhalifa wa kituruki. khalifa wa kwanza wa kituruki salim sultan aliiteka misri na kuanzisha ukhalifa wa kituruki. idadi ya makhalifa hao ilikuwa thelathini, lakini alipokuja mustafa kamal pasha akakomesha ukhalifa huo; kwa hivyo, duniani sasa hayupo khalifa wa kisunni.

Madai ya madhehebu mengine:

1. Madhehebu ya babi azali na bahai, ambayo yamejitenga mbali na itikadi ya uislam, hayawezi kufikiriwa kwamba ni madhehbu ya kiislaam.

2. Vile vile ukadiani hupinga moja kwa moja imani ya uislam na kwa hivyo madhehebu hayo pia siyo ya kiislaam.

3. Hata hivyo waumini wa madhehebu ya dawoodi bohora ni waislamu lakini huamini maimamu ishirini na mmoja na vile vile huamini hadi leo kuwa imam wao wa mwisho, imam tayab, amejificha, hivyo daawa yao huzidi idadi ya imam kumi na wawili.

4. Waismailia wafuasi wa agakhan, huamini imam wao wa kipindi hiki ni wa 49; kwa hiyyo, idadi yao buzidi idadi iliyotajwa na mtume(s.a.w.w) zaidi ya mara nne.

5. Ni shia ithnasharia peke yao tu ndio wanawaamini maimam kumi na wawili, kama ilivyosimuliwa na hadithi ya mtume(s.a.w.w) . imam wa kwanza ni hadhrat ali(a.s) na wa kumi na mbili ni hadhrat mehdi(a.s) kama ilivyoridhiwa katika vitabu vitano mashuhuri vya madhehebu ya kisunni na kutajwa katika vitabu vingi vingine. jina maalum la kila imam(a.s) lilitajwa na mwenyewe mtume(s.a.w.w) . ukweli huu vile vile umethibitishwa katika vitabu maarufu vya kisunni, k.m.

1. "Mawaddatul Qurba" uk. 34, kilicho andikwa na allama seyyid alihamdani, kilichochapishwa bombay press.

2. "Arjahul Matalib", uk. 402, lahore press.

3. Yanabiul Mawaddah", uk. 445, kilichoandikwa na allama

sheikh Suleiman Kanduzi, sheikh wa istanbul. istanbul turkish press.

4. Tarikhul Rawzatul Ahbab", Yanabiuel Mawadda juzuu 3, uk. 27. licha ya hivyo, kuna vitabu vingi vimetaja majina halisi ya imam mehdi(a.s) .

5. Babu zake agakhan wa siku hizo wakiamini maimam kumi na wawili kama ilivyoelezwa katika vitabu vyao ambavyo tumekwishavitaja.


14

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA19

MAKAZI YA HADHRAT MEHDI (A.S) JAZIRATUL KHADHRAA NA MENGINEYO

Hadhrat Mahdi(a.s) yupo hai duniani na huwaokoa wafuasi wake wanapohitaji msaada wake. Mahala pengi pameainishwa kuwa ni makazi yake. Miongoni mwao ni rabwa huko yemen, zituwa n.k. kama ilivyoelezwa katika dua mbalimbali. Zaidi ya hayo, jaziratul khadhraa (kisiwa kijani) ni nchi kubwa mno katika ufalme wa imam(a.s) na kuna majiji mengi makubwa yenye umati mkubwa wa kishia. Hayo hutawaliwa na wana wa imam(a.s) kundi la visiwa linalojulikana kwa jina hilo lipo katikati ya bahari nyeupe (white sea) magharibi ya uingereza. Kwa amri ya mwenyezi mungu wengi wamekwishawahi kuzuru visiwa hivyo. Hata hivyo, kutokana na vitabu vya historia mizunguko mikali ya maji huzingira visiwa hivyo na huwa ngumu na hatari kwa vyombo kufika huko.

Kuna hoja inayotolewa kwamba ikiwa visiwa hivyo ni vikubwa kiasi hicho basi kutokana na maendeleo ya vyombo vya angani na vyombo vya kupigia picha vya ramani, kutoonekana kwa kisiwa hicho katika ramani ya dunia humfanya mtu asiamini kuwa kipo. kwa hivyo, kabla ya kueleza mahali penyewe, tunajibu hoja hiyo.

1. Amerika ambayo ni bara kubwa mno lililotanda karibu nusu ya dunia lilivumbuliwa katika karne ya 18. Je tunaweza kujenga hoja ya kusema kuwa bara hili halikuwapo kabla ya karne ya 18?

2. Ugunduzi wa nchi zilizofunikwa na barafu kwenye kizio cha kaskazini (north pole) bado unaendelea hadi leo.

3. kuna visiwa vingi katika bahari kuu na vichache tu vinajulikana.

4. kuna nchi nyingi ambazo kuwapo kwazo zimethibitika kihistoria, lakini mahala penyewe hapajulikani na hata ramani hazijachorwa; mathalan, kaskazini mwa afrika kuna eneo linalokaliwa na umati wa agog-magog nalo hujulikana kama saadal sikandari. nabii suleiman alijenga ngome kubwa huko kaskazini mwa afrika na kuficha hazina nyingi mno. tena kuna makazi ya masahaba wa gofu (as'habul kahf), bustani ya aden na janna ya shaddad. kuwepo pahala hapo pote pamethibitika kihistoria lakini hapawezi kufikiwa (ila tu watu wachache walioweza kufika huko); hata ndege za nchi zilizoendelea hazikufika huko.

5. Miaka michache iliyopita wakati vita vya korea vikiendelea habari zifuatazo ziliwasilishwa na shirika la habari la reuter. tadriki ya kusini kwenye kizio cha kusini cha dunia (south pole) baada ya vita vya korea. rear admiral byrd (mkuu wa jeshi la majini) mwenye umri wa miaka 64 ametangaza kwamba ataongoza tadriki nyingine kusini kwenye kizio cha kusini (south pole) mara tu baada ya vita vya korea kumalizika.

Yeye amesema: "kuna ardhi huko antarctic, yenye eneo kubwa kama amerika, ambayo mpaka leo halijafikiwa na mtu yeyote". "hivyo chemchem hiyo yenye mali asili isitekwe na adui yeyote." alizungumzia uwezekano wa kutumia bomu la haidrojeni au silaha nyingine ya nuklia kuyeyusha maeneo makubwa ya barafu ili aweze kupata mali iliyo chini ya ardhi. (reuter). kwa hivyo ni dhahiri kuwa kuna mahala pengi ambapo bado hapajagunduliwa. kadhalika, jaziratul khadhraa, ambayo habari zake kihistoria zimezungumzwa karne nyingi zilizopita na kuna ushahidi wa watu waliofika huko pamoja na majina na tarehe ya kufika.

Haramu za misri mwanazuoni mkuu wa kishia, allama majlis(a.s) na wanazuoni wengi wengine wameandika kwamba abdulhasan hammad bin ahmad aliwahi kuona hazina kubwa mno ambayo mtu yeyote hakuwahi kupata mali hapo kabla. kwa hivyo tama yake ilizidi na aliamrisha haramu za misri zibomolewe na mali yote iliyofukiwa chini yake ichukuliwe. washauri wake walijaribu kumsihi asibomoe haramu, kwa sababu maisha yake yatafupika. hata hivyo hakukubaliana nao na akawatuma watu elfu moja wafanye kazi hiyo.

Waliendelea kuchimba kwa muda wa mwaka mzima lakini hawakupata chochote. basi aliamua wasiendelee na uchimbaji. Siku ya mwisho wachimbaji waliona shimo refu na waliamua kuingia humo. kabla hawajafika mwisho wa hilo shimo wakaona bamba kubwa mno. Wakaling'oa hilo bamba. Ndani ya bamba hilo kulikuwa na michoro ambayo hakuwa hata mtu mmoja huko misri hakuweza kuifahamu.

hatimaye abi abdulla madini akasema kwamba anamjua mzee mmoja huko uhabeshi (ethiopia) mwenye umri wa miaka 360 ambaye angeweza kufafanua maana ya michoro hiyo. basi salaam zilitumwa kwa mfalme wa uhabeshi kumwomba ampeleke huyo mzee misri, lakini mfalme wa uhabeshi alisema hataweza kumwomba mtu mwenye umri kama huo asafiri maana safari hiyo ingeweza kusababisha kifo chake.

Mfalme alipendekeza kwamba masuala yote yanayotakiwa kumwuliza huyo mzee yatumwe kwa maandishi. kwa hivyo, hilo bamba likapelekwa uhabeshi. huyo mzee akatafsiri michoro hiyo katika lugha ya uahabeshi na tafsuru yake ikafanywa katika lugha ya kiarabu. bamba hilo lilisema kuwa limetoka kwa: rayan bin doneta mfalme wa misri, ambaye katika kipindi cha utawala wake nabii yusuf alikuwa nabii huko misri. azizi (mtawala wa misri) aliishi miaka 700 na baba yake rayyan 1700 na babu yake domag 3000. iliendelea "niliamua kuona chanzo cha mto wa nile. nilisafiri na masahibu wangu kw muda wa miaka minane. mwishonikafika pahala penye giza totoro. katika msafara huo masahibu wangu wote, ila 400, walikufa na kwa hivyo niliamua kurudi misri na kujenga haramu mbili. ndani humo nilificha mali yangu, vito vyenye thamani n.k mali hiyo wala vitabu vya elimu havitaharibika. baadaye ilifuata tafsiri ya maandiko yaliyoandikwa juu ya bamba: "elimu yangu imenipa mwanga juu ya undani wa maajabu machache.

Hata hivyo, mungu anajua kikamilifu habari za vitu vilivyojificha. mimi nilisafiri kwa muda wa miaka thamanini hata nikafika kwenye giza totoro. hatimaye nikafahamu kwamba sitaweza kwenda mbele na mtu yeyote mwingine hataweza kufika huko nilikofika. kwa hivyo, nilirudi nyumbani misri na nikajenga haramu mbili kama mfano wa nguvu na ujasiri wangu. hazitachakaa wala kuharibika. hakuna yeyote atakayeweza kufikia mali nyingi mno wala kufungua hilo shimo niliyofukia mali na niliyoimarisha, ila katikas siku za mwisho za dunia walii mmoja wa mungu atafichua hazina hii yangu ya ajabu.

Walii huyo ataonyesha hiyo mali katika kaaba. bila shaka, kila kitendo chake kitakuwa kikamilifu na atakuwa na uwezo wa kumdhibiti kila mtu. jina ka allah litaenea duniani kutokana na juhudi zake. huyo atapokuja watu 313 wataleta imani juu yake na yeyote atakayepinga atauwawa.baada ya hapo watu 99 walio kufa wa taif watafufuka na kuchimbua hiyo hazina niliyofukia ambayo itatumika katika vita vya dini. Hapa nimedokeza kuhusu mabao yatakayo tokea. kwa hakika wote tutakufa, hata mimi mwenyewe".

Baada ya kusoma hayo mfalme abdul hassan hammad aliyakinika kwamba hakuna mtu yeyote atakayeweza kufukua hiyo hazina ila hadhrat mahdi(a.s) . kwa hivyo, alirudisha hilo bamba pahala pake pa asili. katika muda mfupi wa miezi kumi na mbili hammad alipokuwa katika usingizi wa sakarani aliuliwa na mmoja wa watumwa wake, taher. hazina iliyofichwa na nabii suleiman katika ngome za shaba (madina-tunnahas) jiji la shaba.

Madinatunnahas ni mojawapo ya maajabu makuu ulimwenguni. ngome hiyo ilijengwa na nabii suleiman huko andolusia, afrika mashariki kwa msaada wa majini kwa kuyeyusha risasi. eneo lake ni maili kumi na mbili za mraba na kuta zake ni futi 75 kwa urefu. na ameficha mali ya ajabu yenye thamani kuu. ipo dokezo kuhusu hiyo katika qur'ani tukufu: "na kamyeyushia chemchem ya shaba. na kati ya majini walikuwepo wale waliofanya kazi chini ya uongozi wake kwa amri ya mola wake". (34:12).

Kwa amri ya allah kulitokeza chemchem ya shaba kujengea ngome. katika utawala wa khalifa bdul malik bin marwa wa bani umayya, mtu mmoja aliwahi kufika kwenye ngome hiyo. (ilikuwa niamri ya allah huyo mtu afike huko ili aje kuwasimulia watu wa bani umayya na waislaam wa wakati huo na watakaozaliwa baadaye alama zake (mungu) na hadhi ya hadhrat mehdi(a.s) . huyo mtu alimhadithia khalifa mambo yote ya ngome hiyo na khalifa papo hapo akamwamrisha gavana wa andolusia kuanza msafara wa kutafuta ngome hiyo na kupatiwa taarifa.

Gavana huyo alifunga hiyo safari. Alifika kwenye ngome lakini alishindwa kuingia ndani yake. Sauti za ajabu zilisikika kutoka ngomeni. karibu na ngome hiyo kulikuwa na ziwa moja ambamo maji yalikuwa yanajaa kila saa na maji hayo yalikuwa yakitoa povu kama vile maji ya moto yanapochemka. gavana akawaamrisha wapigambizi wazame ziwani, nao walileta vyombo duara vya mabati na risasi. juu ya hivyo vyombo vilikuwa mihuri. gavana akaamrisha vyombo hivyo vivunjwe. humo ndani ya vyombo vikatokeza masanamu yaliyopanda farasi yakipiga kelele." eh mtume wa mungu tunaomba amani kwako". Gavana alisadiki kwamba hao walikuwa majini wahalifu ambao walifungwa na nabii suleiman.

Gavana alimpatia khalifa taarifa kamili. vile vile aliongeza kwmba alitekeleza agizo lake la kwenda kwenye ngome dhidi ya ushauri wa wahenga ambao walimwonya kuwa kabla ya hapo hakuna mtu yeyote aliyefanikiwa kuingia ndani ya hiyo ngome., sikander mkuu (alexander the great) alijitahidi kufikia hiyo ngome na kutuma watu wake waingie humo lakini baada ya muda mrefu walirudi bila mafanikio. Kwa hiyo, sikander alikata tamaa na kuacha jambo hilo; hata hivyo, gavaha alipeleka watu waliojiandaa kikamilifu. Alikabili matatizo mengi na katika safari hiyo aliishiwa hata chakula. ijapokuwa aliifikia ngome hiyo lakini alishindwa kuingia ndani. Kuta za ngome zilikuwa na urefu wa futi sabini na tano ambazo zilizojengwa kwa shaba na juu ya hizo kuta kulikuwa maandishi maalum katika lugha ya kiarabu. Gavana aliagiza maandishi hayo yanakiliwe na kupelekwa kwa khalifa.

Hayo maandishi yalikuwa katika lugha ya kiarabu fasaha na kiini na muhtasari wake ulikuwa hivi: "hakuna kiumbe atakayeishi milele. iwapo kungekuwapo mtu mwenye nguvu na heshima ambaye angeweza kuishi milele basi pasina shaka kuwa nabii suleiman angeishi maisha marefu mno. mwenyenzi mungu alinitayarishia chemchem ya shaba na kukiamrisha kikundi cha majini kunijengea ngome kutokana na hiyo shaba iliyo yayuka na ambayo itadumu hadi siku ya hukumu (kiyama). Na haitachakazwa kwa urefu wa muda au umri. Mimi niliamrisha zijengwe kuta ndefu sana, ziimarishwe na shaba iliyoyayuka na kuhifadhi humo hazina yangu kubwa mno, ili muda wowote ukipita hata chembe moja ya hiyo hazina isiharibike. kwa hakika fahari (makuu) ya mfalme yeyote haiwezi kudumu daima.

Mwisho wa kila mfalme ni kulala peke yake kaburini. Na hivyo divyo itakuwa hali yangu. kwa hivyo, watu wajue kwamba ufalme wa milele ni wa mungu peke yake. Baada ya kufa kwangu kutakuja kipindi ambacho mtu aliye bora kuliko wote kutoka katika sulbi ya adrian na hashim atazaliwa. Mungu atamjalia miujiza, kudra yake na utume. Atakuwa mwongozi wa viumbe wote duniani. atakuwa na funguo zote za hazina za dunia nzima na warithi wake vile vile watakuwa na sifa hizo. Warithi hao watakuwa kumi na wawili-na wote watakuwa makhalifa wa mungu duniani. Mrithi wa mwisho atatokeza (baada ya kughibu kwa kipindi maalum) kwa amri ya mola. Jina lake litatangazwa kwa sauti kubwa huko mbinguni na huyo mtukufu atafungua hiyo ngome yangu na kudhihirisha hazina hii."

Alipomaliza kusoma hiyo taarifa, mjumbe aliyeleta barua, talib (bin mudrik, akaongezea na kusema kwamba yeye binafsi pamoja na gavana walifika kwenye hiyo ngome ya kusoma maandishi hayo juu ya kuta zake. kusikia hayo khalifa akamwuliza muhammmad bin shahad zohri aliyekuwa pale, na ambaye alikuwa mmojawapo wa masahaba wa imam wa nne (zainul abidiin a.s.) na mwenye kupenda familia ya mtume atoe maoni yake. Yeye (zohri) akasema kwamba hiyo ngome iko chini ya utawala wa majini ambao huzuia watu kuingia humo. hapo khalifa alisisitiza sana apatiwe jibu kwa sababu jambo hilo lilikuwa la muhimu mno na alimtaka zohri aelezee kinaga ubaga habari hizo bila kuchelea kuwa maelezo yatamuudhi khalifa kwa sababu mfalme alikuwa na hamu ya kujua jawabu.

Baadaye zohri akahadithia kwamba hadhrat ali bin hussein (imam wa nne a.s.) alimjulisha yeye kuwa huyo mehdi(a.s) atatokana na dhuria ya fatima(a.s) binti wa mtume mtukufu(s.a.w.w) , khalifa abdulmalik akamkata kauli na kwa hali ya kugugumia akasema: "nyinyi wote wawili waongo. mehdi atatokana na ukoo wa umayya". Zohri akamwambia kwamba anaweza kuthibitisha kutoka imam ali bin hussein(a.s) yote aliyosema lakini khalifa akajibu kuwa hapakuwa na dharura ya uthibitisho huo. Baadaye akamnong'oneza zohri, "tahadhari, mtu yeyote asipate kujua ukweli kuhusu hiyo ngome na maandishi yaliyokuwa ukutani". Zohri aliahidi kama hatamhadithia mtu yeyote maneno hayo.

Andolusia imeonyeshwa katika ramani ya afrika. waingereza walifika nchi hiyo lakini hawakufanikiwa kufikia hiyo ngome. Wangalifanikiwa kufikia hiyo ngome wangejitahidi kadri ya uwezo wao kupata hiyo hazina iliyohifadhiwa. kwa hivyo, si jambo la kuajabia kwamba jazeeratul khadhraa na nafasi nyingi zingine hazikugunduliwa na binadamu. Hadhrat Mahdi(a.s) ana makazi mengi lakini makazi hayo hayafikiwi na watu wa kawaida ila ayali yake na wahudumu wake wa karibu mno. Hata yeye (hadhrat mehdi(a.s) anapokuja kumwokoa mtu yeyote hatambuliki. baada ya kumuawini mtu na kutoweka, baada ya kutoa msaada kimuujiza huthibitika kwamba huo umetoka kwake hadhrat mahdi(a.s) na humfnya mtu awe na majonzi ya kukosa kumtambua imam wake.

katika mwezi mtukufu wa ramadhani imam pengine huhudhuria msikiti wa kufa, au wa najaf na vile vile kerbala. Katika kila msimu wa hija yeye huenda kuhiji. Baadhi ya makazi yake yametajwa katika vitabu vingi, k.m. majiji makubwa chini ya utawala wake ktika makundi ya visiwa vinavyojulikana kama jazeeratul khadhraa huko bahari nyeupe ambako huweza kufika baada ya safari ya siku kumi na tano hadi ishirini kwa meli kutoka mwambao wa kaskazini magharibi (northwest) ya afrika. majina ya majiji hayo ni haya yafuatayo:

1. Mubaraka: gavana wa kisiwa hicho ni hadharat tahir, mwana wa imam(a.s) na makao makuu ya kisiwa hiki ni jiji linaloitwa zahera.

2. Raequa: gavana wa huko ni mwana wa pili wa imam(a.s) , aitwaye hadhrat qassim.

3. Sfiya: lililo chini ya utawala wa hadhrat ibrahim ambaye vile vile ni mwana wa imam(a.s) .

4. Zaloom: hiko gavana ni hadhrat abdulraman ambaye pia ni mwana wa imam(a.s) .

5. Panatis: mtawala wa huko ni mwana wa imam.

mbali na visiwa hivi vitano, imamu anayo maskani mengine ya upekee huko yemen na iraq ambapo waumini wachache wameweza kuzuru na maelezo yake yametolewa kwingine katika kitabu hiki.

Masimulizi kuhusu visiwa hivyo

1. seyyid muhammad sharif rishtia ametuuusia kwamba katika kipindi cha ughaibu wa imam(a.s) waumini wajaribu kumkumbuka imam(a.s) mara kwa mara kwa sababu yeye hutupenda sisi na yu muhibu wetu kuliko wazazi wetu. tujitahidi mno kutenda mambo ya kumfurahisha yeye (imam a.s.). ameandika kwamba kila mara akimwomba imam(a.s) amwonyeshe jaziratul khadhraa, bahari nyeupe na nchi za ufalme wake ambazo yeye na wanawe wanatawala. anaendelea kusimulia kuwa: "safari moja usiku wa ghadir (siku ya kutangazwa kwa imam Ali(a.s) kuwa khalifa baada ya mtume(s.a.w.w) uliangukia usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa. nilikuwa natembea bustanini mwangu baada ya ibada za usiku wa manane huko beedabad bazar katika mji wa isfahan (iran). ghafla nikakutana na seyyid mwenye haiba aliyevaa mavazi ya wanazuoni wa kiislamu. baada ya kunisalimu akaniuliza: "wewe una hamu ya kuona jaziratul khadraa kuongeza yakini yako na imani za wengine?" kwa unyenyekevu nikajibu, "bwana wangu, nina hamu sana ya kuiona."

Akaniambia nikamate mkono wake, kufumba macho yangu na kumswalia mtume(s.a.w.w) pamoja na dhuria yake mara 7. Mimi nilifanya hivyo. nilihisi mvumo mkali wa upepo huku nikipaa angani. Punde si punde, akaniambia nifungue macho yangu na kusifu uwezo wa kuumba wa mwenyezi mungu. Nilipofumbua macho yangu nilijikuta niko kwenye jiji zuri lenye barabara pana na majumba yaliyo karibu karibu. Chemchem za maji zilikuwa kote kote na mabustani ya kupendeza yaliyojaa aina nyingi ya miti iliyozagaa kwa matunda. Nilihisi nipo peponi.

Seyyid huyo alinionyesha msikiti uliotazamana na bustani na kunijulisha kwamba watu walikwisha kusanyika kwa ajili ya swala ya asubuhi ambayo itaongozwa na abdulrahman, mjukuu wa kizazi cha saba cha imam mehdi(a.s) . akanielekeza niswali nyuma ya huyo kiongozi wa swala na kuwa ataonana na mimi baada ya swala. mimi nilikwenda msikitini. Mashaallah! ulikuwa msikiti wa ajabu.

Nilipoingia tu niliona watu wamekwisha jiandaa kwa ajili ya swala itakayoongozwa na mcha mungu mwenye uso uliojaa nuru na ambaye alikuwa amekwishafika katika mihrab. Baada ya kujidukiza katika umati wa watu nikafika kwa kiongozi huyo na nikamsalimia na kumbusu mikono yake. Alinikaribisha kwa taadhima na kuniambia kwamba nilibarikiwa na allah kufika msikitini huko. Nilimwuliza maswali machache ambayo yalikuwa yakinitatanisha kwa muda mrefu na papo hapo nikapata majibu ya kunitosheleza. Punde ukafika wakati wa swala.

Baada ya swala nikakumbuka kwamba mimi huongoza swala katika msikiti wa isfahan na watu watakuwa wananisubiri na pengine kukata tamaa. Nilipotamka maneno hayo nikamkuta yule bwana aliyenileta kutoka isfahan amesimama karibu yangu na kunipa mkono wake na kuniambia nifumbe macho. Katika muda mfupi mno nilijikuta kwenye msikiti wa isfahan ambapo watu walikuwa wamekwishajiandaa na kunisubiri mimi. niliongoza swala na baada ya hapo sikumwona seyyid yule tena".


15

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 20

HADITHI KUHUSU KUJITOKEZA KWA IMAM MAHDI(A.S) NA ALAMA MAALUM ZITAKAZO TANGULIA

Vitabu vyote vya sunni vimehadithia hadithi juu ya kujitokeza kwa imam(a.s) . hii ni dalili kwamba imam(a.s) wa wakati huu yu hai, kwa sababu mtu atakayeweza kujitokeza lazima awe hai na aliyeghibu na si yule ambaye bado hajazaliwa.

1) Imenakiliwa katika juzuu la pili la tarikhe khamis kuwa: "wakati atakapojitokeza mehdi, muhammad bin hassan askari(a.s) malaika watatangaza kujitokeza kwake. Yeye ni khalifa aliyeteuliwa na mungu na katika kipindi cha utawala wake mbuzi watakuwa malishoni pamoja na mbwa mwitu na watoto wa binadamu watakamata nyoka na visusuli na kucheza nao."

2) Katika kitabu cha asafurraghbin, ukurasa 140, sheikh muhyiddin amenakili kutoka kitabu cha kiarabu futuhat kuwa: "hakuna shaka yoyote kwamba hadhrat imam mehdi(a.s) atatokeza, lakini wakati ule dunia nzima itakuwa imejaa udhalimu, ukandamizi, na dhambi na huyo imam as. atasafisha hayo yote na ataijaza dunia kwa insafu na usawa. "yeye atatokana na dhuria ya mtume mtukufu(s.a.w.w) kutokana na binti yake fatima(a.s) kwa utaratibu ufuatao: mwana wa fatima atakuwa imam hussein(a.s) atakayemzaa alia zainul abedin(a.s) ambaye atamzaa muhammad ai-baqhir(a.s) atakayemzaa jaffar sadiq(a.s) atakayemzaa musa(a.s) atakaye mzaa ali ridha(a.s) ambaye atamzaa hassn askari(a.s) ambaye mwanaye atakuwa muhammad mehdi(a.s) atakaye pokea kiapo cha utii katika kaaba takatifu".

3) Ibne abbas amearidhi katika faraidussimtayn kutoka mtume mtukufu(s.aw.w) kuwa: "watakuwa makhalifa 12 walioteuliwa na mungu, wa kwanza wao ni hadhrat ali(a.s) na mwisho atakuwa mwanangu mehdi(a.s) . nabii issa atakapoteremka kutoka mbinguni ataswali nyuma ya mehdi(a.s) . dunia nzima itang'aa kwa nuru ya mungu. utawala wa hadhrat mehdi(a.s) utaenea kutoka mashariki mpaka magharibi duniani kote (hadithi tatu hizi zote zilizotajwa zimehifadhiwa katika vitabu vya sunni).

vitabu hivyo vya kisunni vile vile vimethibitisha kwamba hadhrat mehdi(a.s) atakapojitokeza atastawisha uislam kuwa ni dini ya pekee duniani kote na kueneza insafu na huyo atakuwa mwana wa imam hassan askari(a.s). hao wote waliodai kuwa mehdi (kadiani mirza na wengineo) na wale ambao hudai kuwa imam wa wakati huu na mehdi hawakuweza kushinda dhuluma na ukandamizi kwa namna yoyote. alama zitakazoashiria kujitokeza kwa imam mehdi(a.s) alama zitakazotangulia kabla ya kujitokeza kwa imam hadhrat mehdi(a.s) na hali ya dunia itakavyokuwa imekwisha elezwa. Sasa tutazingatia alama maalum ambazo zitatangulia kabla imam hajajitokeza:

i) Dajjal atatokeza.

ii) Sauti kubwa itasikika kutoka mbinguni.

iii) Sufiani atatokea na ataanzisha vita vikali.

iv) Jeshi la sufiani ghafla litamezwa na mpasuko wa ardhi baina ya makkah na madina.

v) Seyyid mahshumu na mcha mungu atauawa makkah.

vi) Seyyid anayetokana na dhuria ya imam hassan(a.s) atatokeza na jeshi lake.

vii) Sura ya binadamu itaonekana mbinguni kabili ya juwa.

viii) Kutatokea kupatwa mwezi na juwa mara mbili katika mwezi mtukufu wa ramadhan kinyume cha hali ya kawaida na hesabu: kutakuwa kupatwa juwa

tarehe 15 na tarehe ya mwisho wa mwezi.

ix) Nyakati tatu itasikilizana sauti kubwa kutoka mbinguni katika mwezi mtukufu wa ramadhan. alama hizi zimekwishaelezwa bayana kwingineko.

Imam Jaafar Sadiq(a.s) amesema kwamba: kutakuwa kupatwa kwa jua na mwezi kinyume cha hali ya kawaida na kabla ya tukio hilo thuluthi mbili ya waislamu watakuwa wamegeuka makafiri.

Hadhrat Ali(a.s) amesema kwamba kabla ya kujitokeza kwa hadhrat mehdi(a.s) kutamwagika damu kwa uwingi, vifo kwa tauni vitakithiri na mchwa watatokeza kwa wingi mara mbili.

SURA 21

KAFIRI DAJJAL CHONGO

siku moja hadhrat Ali(a.s) mwishoni mwa hotuba yake katika msikiti wa kufa aliwaomba watu wamwulize maswali wanayotaka kabla yeye kufariki dunia. Sasa bin sawhan akasimama na kuuliza: "eh kiongozi wa waumini! Wakati gani hadhrat hujjat atatokeza"? Imam Ali(a.s) akajibu: "kwanza zitatokeza alama nyingi moja baada ya moja. Sikiliza kwa makini kuhusu hizi alama na uzikumbuke. Watu watapotosha dhana ya ibada, watakhini amana, watahalalisha uongo, watakula riba, watakuwa waovu, na waasharati na hawatawapenda jamaa zao, wataona fahari kufanya dhuluma, watapamba Qur'an tukufa, misikiti yenye minara mirefu itajengwa, wataheshimiwa waovu na wadhalimu, misikiti itajaa watu wa kuswali lakini watu hao hawatakuwa na umoja, watawashirikisha wake zao katika biashara ili kupata utajiri, wataamini maneno ya waasi na kuwatii, waovu na wapotovu watakuwa viongozi wa majamii, wataweka vifaa vya ghina (muziki) (gita na piano), wanawake watapanda farasi (baiskeli) na kuwaiga wanaume (kwa mavazi ya kiume), watu watajishughulisha na kutekeleza mambo ya dunia kabla ya kuswali faradhi na kuonekana waungwana lakini mioyo yao itakuwa imejaa ufasiki".

Alipofika hapo asbag bin nabata akauliza, dajjal ni nani? imam ali(a.s) akajibu: "jina la Dajjal ni sayad bin sed. Waovu tu ndio watamfuata na waungwana watamkimbia. Dajjal atatokea yahudiyya mjini isfahan Iran. atakuwa na jicho moja na hilo jicho litakuwa kwenye paji la uso na litang'aa sana. Mboni ya jicho lake litakuwa wekundu na karibu na jicho lake litakuwa limechorwa neno kafiri ili lisomeke na wote. Mbele yake kutaonekana mlima wa moshi na kisogoni kwake kutaonekana kilima cheupe. Yeye atatokeza wakati wa njaa kali, watu watababaika na vilima hivyo kufikiria hiyyo ni vyakula na kumkimbilia huyo dajjal. Atapanda punda rangi ya majivu ambaye hatua yake moja itakuwa sawa na masafa ya maili moja.

Akipita karibu na mto wowote maji yake yatakauka. kwa sauti kubwa itayosikika na watu na majini wote yeye atanadi, "eh nyinyi rafiki zangu, njooni kwangu mbio. Mimi ni muumba wa vyote ulimwenguni. Nimeumba vitu katika maumbile mbalimbali na mimi ndiye mtoa riziki mimi ninawaita kwenye maongozi yangu kwa sababu mimi ni mungu na nina uwezo juu ya vitu vyote."

Imam Ali(a.s) tena aliendelea kuwatahadharisha watu kwamba yule adui wa mungu ni mdanganyifu wa nafsi yake kwa sababu yeye anakula na kunywa. zaidi ya hayo mungu wenu siye chongo, wala hali wala kunywa, hana mwili na haondoki kutoka pahala pamoja na kwenda pengine. mjitahadhari! wafuasi wa huyo mwovu watakuwa watoto wa haramu na mayahudi. hadhrat mehdi(a.s) atamwua dajjal huko sham kwenye mlima mkubwa unaoitwa tallu affik siku ya ijumaa saa tatu baada ya jua kuchwa. baadaye kutatokeza tukio kuu. akasoma aya kutoka qur'an tukufu isemayo:

"Na sisi tuliwasimulia kwamba kuna mtu hutembea kwa wepesi na kuzungumza nao ". (27.28).

Mtu huyo (Imam a.s) atatokeza kutoka mlima wa saffa uliopo makkah. atakuwa amevaa pete ya nabii suleiman na kushika asa ya nabii mussa.

Atagusa paji la uso la waumini kwa pete hiyo na papo hapo kutachoreka maneno "hadha mu'min" (huyu ni mtu aliyeamini). Atagusa paji la uso la makafiri na papo hapo patachoreka maneno "hadha kafir (huyu kafiri). Juwa litachomoza kutoka magharibi na yeye atanyanyua kichwa mbele ya juwa na watu wote duniani wataweza kumwona. wakati huo mlango wa toba utafungwa na vitendo havipatiwi jazaa ila vya wale walio amini kabla ya tukio hilo kwa sababu imani bila amali haikamiliki."

Katika kitabu kimoja cha kisunni, kamaluddin, abdulla bin umar amesimulia kwamba siku moja baada ya swala ya asubuhi mtume mtukufu(s.a.w.w) pamoja na masahaba zake walikwenda kutembea mjini. mtume(s.a.w.w) akasimama karibu na nyumba moja na kugonga mlango wa nyumba hiyo. alitoka mwanamke mmoja aliyemtambua mtume(s.a.w.w) na kumwuliza kwamba angeweza vipi kumsaidia mtume(s.a.w.w) . mtume akamjibu kwamba alitaka kuonana na mwanae, abdulla. mama huyo alijibu kwamba mwanae alikuwa mgonjwa wa akili na kwa hivyo huchafua nguo zake na kuzungumza maneno ya kiburi mara kwa mara. mtume(s.a.w.w) akaomba ruhusa ya kuingia ndani kumwona huyo mgonjwa. mama huyo akamruhusu mtume(s.a.w.w) lakini aliomba asamehewe ikiwa mwanawe huyo atazungumza vibaya na mtume.(s.a.w.w) .

Mtume(s.a.w.w) akaingia ndani pamoja na masahaba. yule maluuni alikuwa amevaa nguo nene na kuzungumza peke yake. mama yake akamwambia anyamaze kwa sababu mtume mtukufu(s.a.w.w) alikuja kuonana naye. kusikia hivyo akanyamaza. mtukufu mtume(s.a.w.w) akasema: "ingelikuwa huyo mama asingemwambia kunyamaza, mngelisikia anayosema na mngeelewa hali nilivyoeleza". tena mtume(s.aw.w) akamwuliza kwamba anaona nini. alijibu, "mimi ninashuhudia haki na ubatili na nina ona arsh ya mungu inaelea juu ya maji". bwana mtume(s.a.w.w) akamsihi atoe shahada juu ya upweke wa mungu na unabii wake. naye akajibu, "ninatoa shahada juu ya upekee wa allah na mimi mwenyewe ni mtume wa mungu kwa sababu wewe hustahili utume zaidi yangu." mtume(s.a.w.w) akaondoka.

Siku ya pili mtume mtukufu(s.a.w.w) , pamoja na masahaba wake walikwenda kumwona tena nyumbani kwake. kwa idhini ya mama akaingia ndani na wakamwona amekaa juu ya mtende anapayukapayuka tena mama yake akamgombeza na kumwambia akae kimya na kuteremka chini. siku hiyo tena mtume akachukiwa na akasema "ingekuwa mama yake asingemwambia kunyamaza, nyinyi mngeamini kwamba huyo ni dajjal mfasiki, ambaye nimekwisha watahadharisheni naye" mtume(s.a.w.w) akaondoka. mtume(s.a.w.w) tena pamoja na masahaba wake akaenda kumwona siku ya tatu na alipoingia ndani akamwona huyo abdulla akicheza na mbuzi waliokuwa karibu naye.

Mtume(s.a.w.w) akamsihi akubali upekee wa mungu na unabii wake na akamwambia aseme mtume(s.a.w.w) alikuwa na wazo gani. huyo akasema "addhukh adhukh" (dukh maana yake mvuke na siku hiyo hiyo suratul dukhan iliteremshwa na mtume(s.a.w.w) alisoma sura hiyo aliposwalisha swala ya alfajiri. mtume(s.a.w.w) akamjulisha 'atakayo mungu ' ndivyo huwa na wewe hutafikia mradi wako." mtume mtukufu(s.a.w.w) baadaye akawaeleza masahaba "wake kwamba huyo abdulla ndiye dajjal mfasiki ambaye habari zake alikwishawaeleza. atatokeza duniani siku za mwisho na kabla ya hapo mungu atakuwa amemweka mahabusu katika kisiwa kimoja. atawaletea watu utatanishi mkubwa siku za mwishoni. manabii wote kabla ya mtume mtukufu(s.a.w.w) waliwatahadharisha wafuasi wao kuhusu dajjal. kadhalika, mtume wetu(s.a.w.w) ametutanabahisha sisi kuhusu huyo dajjal na akaongeza "msidanganyike na huyo: mungu wetu siyo chongo, wala hana mwili na huyo mwovu (dajjal) atajitokeza siku za mwisho amepanda punda".

Dajjal atajitokeza siku za mwisho na ataishi kwa muda wa siku arubaini na atatembelea kila sehemu ya dunia juu ya punda wake. mwisho atauliwa huko syria kwa mikono ya imam mehdi(a.s) .

SURA 22

HAKIKA KUHUSU KUJITOKEZA KWA IMAM WA KIPINDI HIKI

Imam Mahdi(a.s) wakati uliopangwa wa kujitokeza kwa hadhrat mehdi(a.s) utapowadia upanga wake "dhulfiqar" utajitokeza nje ya ala yake na kwa kudra ya mungu utapata kauli na kusema: "Eh hujjat wa Mungu, wakati wa kujitokeza kwako umewadia. tafadhali jidhihirishe mbele ya watu duniani" Imam jaafar Sadiq(a.s) amesema: "Atakapojitokeza imam mehdi (a.s) ataingia katika jiji la makkah. atakuwa amevaa mavazi ya mtume (s.a.w.w). kilemba cha njano, na atashika fimbo na kuvaa viatu vya mtume (s.a.w.w). mbele yake watakuwa mbuzi wachache waliodhoofika ".

Hakuna mtu katika makkah atakayeweza kumtambua imam mehdi(a.s) . ataingia kaaba akionekana kijana kabisa. ataignia katika kaabah tukufu usiku wa manane. Jibriil, Mikaiil na malaika wengine katika vikundi vikubwa watateremka kutoka mbinguni kuja ka’aba na kumwamkia imam Mahdi(a.s) . Jibril atampasha imam habari kuhusu maagizo ya Mungu Subhana wa taala kwamba chochote atakachopenda na kuamrisha kitakuwa. Imam(a.s) hapo atachukua mkono wake wa kulia na kuweka juu ya uso wake na kusema:

وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي صَدَقَنَا وَعْدَهُ وَأَوْرَثَنَا الْأَرْضَ نَتَبَوَّأُ مِنَ الْجَنَّةِ حَيْثُ نَشَاءُ فَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿٧٤﴾

"Nao watasema: Alhamdulillah, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye tutimizia ahadi yake, na akaturithisha ardhi, tunakaa katika Bustani popote tupendapo. Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao!." (39: 74).

Baadaye hadhrat hujjat(a.s) atasimama kwenye pembe moja ya kaaba tukufu na kutangaza "Eh nyinyi mlioteuliwa mahsusi na allah kunisaidia mimi tafadhali mje kwangu" sauti hiyo itasikika katika kila nchi lakini khassa na waumini 313 katika asia, afrika na china. baadhi ya hao waumini watakuwa juu ya miswala, wengine watakuwa wamelala, lakini wote watafunga safari kwenda makkah na katika muda mfupi mno watajikuta wamekwisha fika kwa imam(a.s) .

Wakati huo Jibreel atabusu mkono wa Imam(a.s) na kula kiapo cha utii kwa imam(a.s) . na kufuatwa na malaika wengine. baadaye viongozi wa majini na hao waumini 313 watakula kiapo cha utii. watu wa makkah kutahamaki hayo watashangazwa na watauliza hao watu ni nani na wanatokea wapi? vile vile watajiuliza kwa sababu gani usiku huu umekuwa marini na kwa miujiza mingi inaonekana. wengi wao watajibu kwamba hawajui; ila watu wanne kutoka madina ambao watawajulisha kwamba kiongozi wao mwenye uso marini ni imam(a.s) .

Baada ya kupambazuka kutasikika sauti (mwito) katika lugha ya kiarabu duniani kote ikitangaza: "eh nyinyi viumbe mliokuwa mbinguni na ardhini, shaksi aliyejitokeza ni mehdi anayetokana na dhuria ya mtume(s.a.w.w) . baadaye hiyo sauti (tangazo) itaeleza majina kamili ya hadhrat mehdi na nasaba yake mpaka imam hussein(a.s) na itawataka watu kula kiapo cha utii kwa imam(a.s) na kuwaonya kwamba kuhalifu ni kugeuka kafiri. malaika, majini na wale 313 pamoja na waumini wengine watadhihirisha imani yao na utii kwa imam(a.s) .

Huo mwito utasikika vizuri mno katika nchi zote, misitu na milima yote na wanaume kwa wake na watoto wote watashangazwa nao. Wakati wa machweo kutasikika mwito mwingine ukitangaza: "Eh watu, sikilizeni. mungu wenu amejitokeza kutoka misitu ya yabis (palestine) na jina lake ni othman bin amsasah anayetokana na ukoo wa umayyah na dhuria ya yazidi bin muawiyah. Mwelekee kwake na kula kiapo cha utii mwongozwe njia ya haki". Malaika majini na waumini halisi watabatilisha tangazo hilo kuwa ni uzushi na uwongo mtupu. Makafiri wanafiki na wasioamini dini watababaishwa na tangazo hilo na kupotoshwa.

Baadaye imam Mahdi(a.s) akishikilia kaaba tukufu atanadi "Eh viumbe vyote wa mungu nisikilizeni! mimi nimejaliwa na wema, uwezo na miujiza yote ya mitume wote, pamoja na sifa zote za mtume mtukufu (s.a.w.w) na maimam na elimu ya vitabu vitakatifu vyote. " waumini wote watakubali tamko hilo. hapo tena mtu mmoja ajulikanaye kama dabbatul ardh atatokeza baina ya rukn na maqam akishika fimbo na pete mkononi. huyo. (dabbatui ardh) atapoiweka pete hiyo kwenye paji la uso wa waumini papo hapo maneno "huyu mwumini" yatajitokeza na atapoiweka hiyo pete juu ya paji la uso wa makafiri maneno "huyu kafiri" yatajitokeza.

Baada ya hapo mtu mwenye uso wake uliogeuka nyuma atafika kwa imam(a.s) na kusema, "eh bwana wangu! Mimi na ndugu yangu tulikuwa katika jeshi la sudani na tulivamia ardhi yote baina ya damascus na baghdad kusababisha hasara na maangamizi. Baadaye tulielekea madina na makkah na jeshi la watu 300,000 tukikusudia kuingia makkah kubomoa kaaba tukufu na kuua umati mzima wa jiji.

Tulifika usiku jangwa la bayadana lililopo baina ya madina na makkah. Baada ya usiku wa manane tulisikia sauti: "Eh bayadana, waangamize makafiri wadhalimu. Papo hapo kwa amri ya allah ardhi ikapasuka na maaskari wetu 300,000, mali zetu pamoja na wanyama wetu wakamezwa na ardhi, haikubakia alama yoyote. Mimi na ndugu yangu tu tulisalimika. akatokea malaika mmoja na kutupiga makofi kwa nguvu mno na kusababisha nyuso zetu kuelekea nyuma (migongoni). Hapo huyo malaika akinielekea mimi akaniambia, "eh bashir elekea makkah na mpe imam(a.s) taarifa njema kuhusu maangamizi ya jeshi la sufiani. Tena baadaye alimwelekea ndugu yangu na kusema: "eh nazir elekea damascus na mwarifu sufiani kuhusu kuangamia jeshi lake na vilevile mpe taarifa ya kujitokeza kwa hadhrat mehdi(a.s) huko makkah. Msihi aje ajisalimishe kwa imam(a.s) na kuomba msamaha kwa maovu yake na akifanya hivyo toba yake itakubaliwa. (lakini hata hivyo huyo mtu mwovu hataomba msamaha na atajitumbukiza jahanam). Baada ya kusikia hayo yote imam(a.s) kwa mikono yake iliyo barikiwa ataurudisha uso wake uwe sawa. hadhrat mehdi(a.s) ataelekea kufa kutoka makkah na jeshi kubwa la malaika na majini. msikiti wa kufa utakuwa mahakama na msikiti wa sahlah makazi yake.

Mtume mtukufu(s.a.w.w) amebashiri kwamba imam Mahdi(a.s) . atapata ushindi katika usiku mmoja na kukamilisha malengo yake. Hadithi hii ya mtume mtukufu(s.a.w.w) ni ushahidi kamili wa kubatilisha daawa ya wale wote waliojidai kuwa wao ni mehdi(a.s) na vilevile ya wale ambao watafanya daawa ya kuwa mehdi(a.s) . Mji mkuu wa utawala wa imam(a.s) utakuwa kufa ambao utakuwa umepanuka hata kumeza jiji la najaf. kila inchi ya ardhi hiyo itathaminika sana na waumini kutoka kote kote dumanai watakutana huko (kufa). Jiji la kufa litakuwa na urefu wa maili 54 na kuungana na mji wa kerbala, katika zamana hiyo mwenyezi mungu subhana wa taala atatimiza kila matilaba ya waumini.

Imam(a.s) hapo atatuma jeshi kubwa kwenda damascus ambalo litashinda jeshi la sufiani na kumwua sufiani. Sawia ya hapo imam husein(a.s) pamoja na masahaba wake 72 ambao waliuawa karbalaa pamoja na waumini halisi watarudi duniani kwa amri ya mola. Hao watu watafika mbele ya imam mehdi hadhrat ali(a.s) na maimam wengine watarudi duniani. Mtume mtukufu(s.a.w.w) pamoja na masahaba wake waliouawa vitani (jihadi) vilevile watarudi duniani. wale ambao hawakumwamini mtume(s.a.w.w) , kumsumbua, kumzulia kuwa ni mchawi na kumtuhumu maovu mengine watarudishwa duniani na kuadhibiwa kwa dhuluma na uonevu waliotenda. vilevile atarudi nabii issa na mitume wengine pamoja na waumini. Hakutakuwa dini ila moja tu, uislaam, ulimwenguni kote. Dunia hii itajaa baraka za mungu. hali itakayokuwa wakati huo imekwisha elezwa katika vitabu vingine.


16

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 23

MAREJEO (RAJ'AAT)

raj'aat maana yake ni kurudi duniani (kupata maisha mapya) kwa wale waliokufa. Ni lazima kuamini kuwa baada ya kujitokeza kwa hadhrat mehdi(a.s) wenye sifa nzuri na hata wadhalimu, maadui wa aila ya mtume mtukufu(s.a.w.w) watapatiwa uhai mara ya pili. Kuna aya nyingi za qur'an kuhusu raj'aat na vilevile hadithi nyingi za mtume mtukufu(s.a.w.w) zimenakiliwa katika vitabu vya kisunni kuthibitisha ukweli wa raj'aat. Sio hivyo tu, bali hata vitabu vya wakristo, mayahudi, waabudu moto na mahindoo vimetaja dhana hiyo. Katika sura hii tunaeleza kwa ufupi itikadi hiyo kutokana na aya za Qur'an tukufu na hadithi.

وَيَوْمَ نَحْشُرُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ فَوْجًا مِّمَّن يُكَذِّبُ بِآيَاتِنَا فَهُمْ يُوزَعُونَ ﴿٨٣﴾

1. "Na Siku tutapo kusanya kutoka kila umma kundi katika wanao kadhibisha Ishara zetu, nao watagawanywa mafungu mafungu. " (27.83).

kwa upande wa pili kuhusu siku ya kiyama qur'an tukufu imearidhi.

وَحَشَرْنَاهُمْ فَلَمْ نُغَادِرْ مِنْهُمْ أَحَدًا ﴿٤٧﴾

"Na tukawafufua - wala hatutamwacha hata mmoja kati yao ." (18:47).

Aya hii inatuthibitisha kwamba siku ya kiyama viumbe wote watahuishwa bali katika aya iliyotangulia baadhi ya wafuasi wa kila mtume watapatiwa uhai. kwa hiyo, hii ishara ya dhahiri kuwa wachache watarudi duniani baada ya kufa.

وَحَرَامٌ عَلَىٰ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا أَنَّهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿٩٥﴾

2. "Na haiwi kwa wana-mji tulio uangamiza, ya kwamba hawatarejea".(21:95).

Aya hii inathibitisha bayana kurudi tena duniani kwa sababu siku ya kiama, mwenyezi mungu atawapa uhai viumbe wote.

قَالُوا رَبَّنَا أَمَتَّنَا اثْنَتَيْنِ وَأَحْيَيْتَنَا اثْنَتَيْنِ فَاعْتَرَفْنَا بِذُنُوبِنَا فَهَلْ إِلَىٰ خُرُوجٍ مِّن سَبِيلٍ ﴿١١﴾

3. "Wao watasema: "bwana wetu ametufisha mara mbili na umetuhuisha mara mbili". (40:11)

aya hii inazungumzia kufa na kupatiwa uhai mara mbili, kwa hivyo humaanisha kurudi duniani baada ya kufa.

فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ أُولَاهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَّنَا أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا خِلَالَ الدِّيَارِ وَكَانَ وَعْدًا مَّفْعُولًا ﴿٥﴾

4. Basi itapo fika ahadi ya kwanza yake tutakupelekeeni waja wetu wa kali kwa vita. Watakuingilieni ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyo timizwa.." (17:5).

إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ ﴿٥١﴾

5. "Kwa hakika sisi tunawaauni mitume wetu, na wale walioamini katika maisha ya dunia hii." (40:51).

6. Kuna aya nyingi katika qur'an tukufu kuhusu kuwapa uhai (kuwarudisha duniani) waliofariki. zaidi ya hayo, "kurudishwa" (kupatiwa uhai mara ya pili) kulitokea katika baadhi ya wafuasi wa mitume waliopita na katika wale waliokufa walipatiwa uhai mara ya pili, kwa hivyo kuamini kwamba waliofariki duniani hawatapatiwa uhai mpaka siku ya kiyama ni hoja isiyo na uzito.

1. Nabii musa aliwachukua masahaba 70 wateule kumwomba mungu na kusikia maagizo ya mungu. walidai kutaka kumwona mungu kwa macho yao. Kwa hivyo wote walikumbwa na kifo. Kwa dua ya nabii musa, mungu aliwarudisha duniani hao wote waliokufa. Hiyo imeelezwa katika qur'an tukufu.

2. Katika qur'an tukufu sura ya pili ya Al-baqarah (Ng'ombe) aya 243 huaridhi.

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ الْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ اللَّـهُ مُوتُوا ثُمَّ أَحْيَاهُمْ﴿٢٤٣﴾

"Hukuwaona wale walio toka majumbani kwao kwa maelfu kwa kuogopa mauti? Mwenyezi Mungu akawaambia: Kufeni! Kisha akwahauisha.".

Aya hii inasimulia kisa cha nabii hizkil na wafuasi wake wenye familia 70,000. wakati ugonjwa wa tauni ulipoenea jijini kwao wote waliacha jiji. kabla kupata makazi mengine kulitokea amri ya mungu, wote wafe na papa hapo wakafa na miili yao ikaanza kuozeana na kubaki mifupa tu. siku moja nabii mmojawapo wa bani israil akapita hapo (mtume armiya au hizkil) na kumwomba mungu awapatie uhai hao kutokana na uwezo wake ili jiji hilo lipate watu wa kumwabudu yeye (Mungu). Mwenyezi Mungu akamwamrisha huyo nabii anyunyizie maji juu ya hiyo mifupa. siku hiyo ilikuwa ya nairuzi. mtume akatekeleza hivyo na hao wote wakawa hai na kuingia jijini kwa mara ya pili. wakawa wafuasi wa mtume na wakafanya ibada na kuwa watiifu wa allah.

Katika kipindi cha raj'aat ("kurudi") waumini thabiti na makafiri waovu watahuishwa. vile vile baadhi ya manabii, mtume wetu mtukufu, maimam kumi na mmoja na baadhi ya masahaba wake na mashahidi wa karbala vile vile watarudi. kuna hadithi nyingi kuhusu jambo hili lakini tunaeleza machache tu.

1. Imam Jaafar Sadiq(a.s) amearidhia kwamba: katika kipindi cha raj'aat baada ya kujitokeza kwa Imam Mahdi(a.s) , kwanza imam Hussein(a.s) pamoja na masahaba wake waliouawa karbala watarudi tena duniani. pamoja na imam hussein(a.s) watakuwa manabii 70. Wakati umri wa hadhrat mahdi(a.s) utakapomalizika atamkabidhi pete yake imam hussein(a.s) ambaye atashungulikia mazishi ya hadhrat mehdi(a.s) baada ya kufa kwake.

2. zaidi ya hayo imam jaffar sadiq(a.s) amesema "baada ya raj'aat, imam mahdi(a.s) ataingia kufa na kutokea makaburini ya najaf panapoitwa waadis-ssalam allah atawapa uhai waumini thabiti 70,000 ambao watamsaidia hadhrat mahdi(a.s) .

3. vile vile imam(a.s) amesema kwamba wakati atakapojitokeza hadhrat mahdi(a.s) malaika mmoja atakwenda kwenye kaburi la kila mwumini na kumjulisha kujitokeza kwa hadhrat mahdi(a.s) na kumwambia asimame ikiwa anataka kufika kwa imam(a.s) wakati huo kila mwumini apendaye kwenda kwa imam(a.s) atatoka nje ya kaburi lake.

4. imam jaffar sadiq(a.s) vile vile amesema kwamba mwumini yeyote ambaye husoma Duaul-Ahad (dua inayohusu maamkizi kwa imam mahdi(a.s) atakuwepo miongoni mwa masahaba wa hadhrat mahdi(a.s) na akiwa amefariki Imam Mahdi(a.s) kudhihiri atapewa uhai na kuamshwa kutoka kaburini mwake.

5. Baada ya masimulizi hayo, imam(a.s) amesema kwamba kabla ya dhuhur (kujitokeza kwa mara ya pili) ya imam mabdi(a.s) kwa muda wa siku arubaini kuanzia mwezi mzima wa jamadiul akhir (mfungo tisa) hadi siku kumi za mwanzo wa mwezi wa rajab mvua zitanyesha kwa wingi mno kiasi ambacho hazikunyesha kamwe kabla ya hapo, napo ndipo mwenyezi mungu ataunganisha mifupa na nyama za wafu. waumini watajitokeza makaburini mwao huko wakijipangusa mchanga kichwani. kuna hadithi nyingi kuelezea hali hiyo lakini hatutaeleza hapa.

6. Haras bin Abdallah Rabai anahadithia kwamba: safari moja alikaa pamoja na khalifa mansur kwenye daraja la baghdad. ubavuni mwa khalifa alikuwa waziri mkuu wake sawaar. pamoja nao alikuwa mshairi seyyid hamyari ambaye alikuwa anasoma shairi alilotunga kumsifu huyo khalifa ambaye alifurahishwa sana na hilo shairi. waziri mkuu alipogundua kwamba khalifa alinogewa sana aliingiwa na husda na kusema, "eh kiongozi wa waumini, huyu seyyid kwa hakika hakupendi, bali anawapenda na kuwaheshimu viongozi wake: familia ya mtume(s.a.w.w) . licha ya hayo yeye hawakubali makhalifa na masahaba wa mtume(s.a.w.w) na ni adui yako."

Huyo Seyyid akajitetea: "huyu waziri wako hulalamika dhidi yangu kwa sababu ya husda. jamii yake nzima kabla ya kusilimu na kukubali dini ya uislam walikuwa na uadui dhidi ya nasaba yako. hata Mungu alimjulisha hivyo mtume(s.a.w.w) katika qur'an.

إِنَّ الَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَاءِ الْحُجُرَاتِ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿٤﴾

"Hakika hao wanao kuita nawe uko nyuma ya vyumba, wengi wao hawana akili." (49:4)

katika hao mmojawapo ni huyu waziri wako. khalifa akatabasamu na kusema: "hayo ni kweli". waziri mkuu hapo akapandwa na ghadhabu zaidi na kusema "huyu seyyid huamini katika raj'aat". seyyid akajibu "kwa hakika mimi ninaamini raj'aat kwa sababu allah amezungumzia juu ya raj'aat katika qur'an tukufu (na huyo seyyid akasoma aya tulizotaja za qur'an na vile vile hadithi nyingi za mtume mtukufu(s.a.w.w) kuhusu jambo hili.

Hapana shaka kuwa hadithi nyingi za mtume mtukufu(s.a.w.w) kwamba siku ya kiyama wenye kiburi watakuwa na sura ya chungu. aliendelea kusema kuwa katika siku za mwisho duniani wafuasi wake wengi watamezwa na ardhi na wengine watageuka kuwa na sura ya kima na nguruwe na kadhalika, itikadi yangu kuhusu raj'aat ni ya hakika na hutokana na agizo la qur'an tukufu na hadithi nyingi na kunithibitishia kwamba katika raj'aat huyu waziri atapatiwa uhai mara ya pili lakini atageuka sura ya mbwa, nguruwe au kima. kwa jina la allah, huyu waziri ni mdhalimu, mstakadhari na kafiri. kusikia maneno hayo machungu khalifa akatabasamu na kusema : "unayosema wewe ni kweli."

Katika kipindi cha raj'aat hadhrat mahdi(a.s) atalipiza kisasi kikamilifu dhidi ya wakatili wa imam hussein(a.s) na maimam wengine na waumini. wale waliouliwa bila kosa watarudishwa duniani ili waweze kumaliza umri waliojaaliwa na watapatiwa haki zao kutoka wakatili wao na hao wakatili vile vile watauliwa. Katika siku hizo hadhrat mahdi(a.s) atatawala kwa uadilifu kutokana na uwezo aliojaliwa na allah, hatahitaji mashuhuda. kipindi hicho kitajulikana kama kiyamat-al-sughra (kiyama-ndogo).

7. Imam Muhamad Baqir(a.s) amesema kwamba: siku ya ashura (siku ambayo imam Hussein(a.s) pamoja na aila masahaba zake waliuawa huko karbala) imam hussein(a.s) aliwaarifu masahaba wake kabla ya kuanza vita kwamba mtume mtukufu(s.a.w.w) alimjulisha kwamba baada ya kufariki kwake (mtumes.a.w.w ) maadui wake watamwalika imam Hussein (a.s) kwenda iraq na kumwua pamoja na masahaba wake. Imam Hussein(a.s) akaendelea: "mimi ninaona kuwa hawa makafiri watatuua sisi sote. kwa hakika baada ya kifo chetu sisi tutaonana na mtume mtukufu(s.a.w.w) na tutakaa naye kwa muda mfupi. tena katika kipindi cha raj'aat mimi (imam) nitakuwa wa kwanza kutoka kaburini mwangu. sisi tutapigana na hao maadui wa allah tukisaidiana na malaika ambao hawajawahi kuteremka ardhini nao watateremka pamoja na jibraeel, mikaeel na israfeel kuungana nasi. wakati huo mtume mtukufu(s.a.w.w) , Imam Ali (a.s) , ndugu yangu imam hassan(a.s) pamoja na maimam wote wanaotokana na dhuria yangu watakuwa nasi mtume mtukufu(s.a.w.w) atatweka bendera yake pamoja na upanga wake na kumkabidhi Imam Mahdi(a.s) . Masahaba wangu wote watakuwa na mimi na wataishi duniani kwa muda aliopanga allah.

Baadaye hadhrat ali(a.s) atanikabidhi mimi upanga wa mtume mtukufu(s.a.w.w) na atanituma pamoja na jeshi kwenda mashariki ya dunia (bara la asia). Huko nitapigana na maadui wa dini na kuwaua wote, nitafika barahindi na kuiteka na kuisafisha na kuondoa makafiri na washirikina. Nitawaua wanyama wote ambao nyama zao ziliharamishwa. nitawasihi wakristo, wayahudi na washirikina waje kwenye njia ya haki. Wale watakaobakia bila dini nitawaua. Katika kipindi hicho mwenyezi mungu atawahifadhi waumini kutoka kila balaa na ugonjwa na kuwajalia baraka na rehema. Matawi ya miti yatakuwa yamejaa matunda. Yale matunda yanayopatikana katika msimu wa joto yatapatikana katika kipupwe na yale ya kipupwe vile vile atapatikana katika msimu wa joto".

Baadaye imam Hussein(a.s) akawaambia masahaba wake kwamba allah amesema katika qur'antukufu kwamba

وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِن كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٩٦﴾

"Na lau kama watu wa mji wangeliamini na kuepukana na maovu, sisi tungewapatia baraka kutoka mbinguni na aridhi, lakini walikadhibisha; kwa hivyo sisi tumewahukumu kufuatana na vitendo vyao." (7:96).

8. Nabii Idris alighibu kwa muda wa miaka ishirini. Alipojitokeza akaonyesha miujiza kwa kumrudisha duniani mtu aliyefariki. Mama wa huyo mtu aliyepatiwa uhai mpya akawajulisha jamii yake na wote wakaja kwa nabii kuomba msamaha na kumlalamikia awaondoshee hiyo gumba iliyowakabili kama bidhaa ya uhalifu wao. Nabii akawaombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu na wote wakaokoka. Kwa hiyo, kuna mifano mingi ya watu waliokufa na kuhuishwa mara ya pili na ambao waliishi muda mrefu, kufunga ndoa na kuzaa watoto, udogo wa kitabu hiki haurulmsu kueleza kwa urefu mifano hlyo. Lakini lazima ieleweke bayana kwamba idadi maalum ya watu waliopatiwa uhai (kurudi duniani) baada ya kufariki kwa amri ya allah hujulikana kama raj'aat. kwa hivyo hakuna chochote cha kustaajabisha kwamba wakati wa zuhuru (kujitokeza baada ya kughibu) ya imam mahdi(a.s) kutakuwa raj'aat ya manabii, maimam(a.s) waumini thabiti na wadhalimu wakatili.


16

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 24

WAJIBU WA WAUMINI NA DUA YA WAUMINI KATIKA KIPINDI CHA GHAIBA (KUGHIBU) KWA IMAM (A.S)

Ijapokuwa imam wetu(a.s) ameghibu machoni mwetu, lakini yeye ana habari zote kuhusu ibada zetu, vitendo, mashughuli yetu, matatizo na maafa tunayoyakabili. Mwumini yeyote wakati wa shida akiomba msaada kwa dhati hakosi kupata kutoka kwa imam(a.s) . Kuna masharti fulani ambayo waumini wanawajibika kutimiza ili kuthibisha ukweli wa itikadi yao:-

1. ni wajibu wa kila mwumini kwa dhati na kwa mapenzi kumkumbuka imam wake ambaye ni kiongozi wake wa kweli duniani na kesho akhera na kusoma dua mbali mbali katika kipindi hicho k.m. dua-ul-ahad kila siku baada ya swala ya asubuhi, dua-ul-nudba kila ijumaa na ziyarah (maamkizi).

2. ni wajiba wa kila mwumini kujikumbusha kwamba madhalimu wameghasibu haki ya imam(a.s) na kuwa yamefanyiwa mabadiliko na mageuzi katika kanuni za dini na kuwa wapenzi na wafuasi wa dhuria ya mtume mtukufu(s.a.w.w) ni wachache na wanadharauliwa, lazima huyo mwumini aombe mungu aondoshe hiyo balaa na aharakishe ukombozi wa mwisho.

3. Ni wajibu wa kila mwumini kuhakikisha kwamba dini inabaki,waumini wanaendelea kuimarisha imani yao na kujitahidi kadri ya uwezo wao kueneza dini pamoja na kuanzisha madarasa ya dini na kuchapisha vitabu vya dini.

4. Kama vile mtu hutoa sadaka kukinga balaa juu ya wazazi wake na familia yake, vivyo hivyo lazima atoe sadaka kwa ajili ya imam(a.s) kwa sababu yeye ni mtakatifu, hii ni alama ya mapenzi yakweli. kama ilivyoamrishwa kumswalia (salawat) mtume mtukufu(s.a.w.w) na aila yake ijapokuwa hawahitaji, lakini hiyo ni alama ya upendo na njia ya kujipatia jazaa kubwa, na vilevile utoaji wa sadaka kwa ajili ya imam(a.s) ni kuamini utukufu wake.

5. Ni lazima kila mwumini amfurahishe imam(a.s) kwa kusoma qur'an kila wikati, kuzuru pahala ptakatifu pa karbalaa na kwenda hajj kwa niaba yake na kadhalika. Imam(a.s) humwomba mungu awahifadhi na kuwasamehe waumini wake kwa sababu imam(a.s) huwa na taarifa kuhusu vitendo vyetu. mara moja abu muhammad adaji alimtuma mwumini mmoja kwenda kuhiji kwa niaba imam Mahdi(a.s) .

Huyo mtu alikuwa na wana wawili, mmoja wao mwumini na wa pili mpotovu. kutokana na pesa aliyopata kwenda kuhiji akampa fedha kidigo mwanawe mpotovu. alipofika arafah akakutana na mtu mwenye uso unaong'aa ambaye alimwambia, " Eh shekh, huni hata aibu? " huyo shekh akauliza, ' kwa sababu gani ?' huyo mtu akamjibu: 'Unajua kwamba huyo mtu uliokuja kuhiji kwa niaba yake ni imam wako na kwa hivyo anaelewa habari yote. Hata hivyo, katika pesa ulizopewa kufanyia hija ulimpa mwanao mpotovu. Utakuwa kipofu haraka sana' baada ya kusema hayo huyo mtu akaondoka. Siku chache baada ya kurudi nyumbani kwake akaumwa macho na kuyapoteza.

6. Katika kipindi cha shida na matatizo imam(a.s) huja kutoa msaada. lakini, shuruti yule mtu anaeomba msaada kwa imam(a.s) awe anaswali kila siku, kufunga kama ilivyoamrishwa, lifanya kila bidii kuepukene na maasi, kuomba toba kwa maasi aliyotenda, kuwa na mapenzi kwa ajili ya imam(a.s) , kumkumbuka imam katika maombi, dhikiri na maamkizi. Mtume mtukufu amesema:

'Hata unapokuwa umewekewa kisu shingoni ukimkumbuka imam wako wa wakati (imam al-zaman) bila shaka imam (a.s) atakuja kukusaidia' . Kuna nyakati imam(a.s) alitoa misaada na hilo litazungumzwa katika sura zinazo husika.

7. Ni faradhi ya kila mwumini wakati anapotaja jina la imam(a.s) katika maombi, maamkizi au mazungumzo kusimama na kuweka mkono wake wa kiume juu ya kichwa chake. hii ni alama ya mapenzi, heshima na taadhima kwa imam(a.s) .

8. Kuna hadithi nyingi zinazoeleza namna mbali mbali ya kuomba msaada wakata wa dhiki na shida. hadithi moja ni hii ifuatayo:- kataka kipindi cha utawala wa shah fatehali huko iran kulitokea mafarakano baina ya wanazuoni mashuhuri kuhusu suala la waqfu. Wanazuoni walio husika walikuwa agha haji muhammad ebrahim na agha mirza muhammad mabdi. kwa hiryo, shah wa iran alimtuma mwanazuoni wake mashuhuri sana mulla kassam isafahani kwenda kusuluhisha mafarakano hayo. alifanya hivyo na kuwapatanisha wanazuoni hao. Katika safari yake siku moja alikwenda makaburini huko isfahan akifuatana na msaidizi wake. Siku hiyo madhali haikuwa "alhamisi hawakuwa watu wengi huko makaburini na mikahawa ilifungwa. Baada ya kusoma suratul fatiha huko makaburini akamwambia msaidizi wake, "hapa hakuna mkahawa. mimi ninatamani kuvuta rushba".

Msaidizi wake akamjibu, "ungeniambia hayo tulipokuwa mjini ningeleta huka." basi, mulla kassam akaenda kwenye kaburi la mwanazuoni mashuhuri hayati mirza muhammad baqir damad. kaburi hilo lilijengwa vizuri na alipoingia humo alimwona sheikh kaketi juu ya mswala. mulla kassim alisogelea hilo kaburi na kuanza kusoma fatiha. kuyo mtu akamwambia: "mulla kasam, nyinyi mulla inaonyesha hamna tabia nzuri. kwa nini hukunisalimu wakati ulipo ingia?" mulla kassim alishangazwa na haiba ya huyo mtu na akainamisha shingo yake na kusema kwa unyenyekevu: baada ya kumaliza kusoma fatiha ningefika kwako na kukusalimia". baada ya kusema hayo akamsalimia huyo mtu ambaye alijibu na kusema, "tafadhali kaa, baba yako alikuwa mwana mwadilifu. Alimwomba mungu amjaalie mwana mwadifu ambaye atakuwa mwanazuini. Dua yake mungu ameikubali na amejaaliwa mwana mwadilifu na mwenye elimu kama wewe."

Baadaye huyo mtu akamwuliza mulla kassim kama angependa kuvuta huka. mulla kassam akajibu kwamba alidhani kwamba huko makaburini kutakuwa maduka na hivyo hakuleta huka yake. Mtu huyo akasema: 'tafadhali nenda ukalete huka katika kikapu changu." mulla kassam akaangalia ndani ya mkoba akaona huka, tumbaku na makaa ya kutosheleza pamoja na kibiriti. Mulla kassam aliamua kumwita msaidizi wake amtayarishie huka. Huyo mtu alimkataza asimwite mhudumu wake bali atayarishe huka yeye mwenyewe. Basi mulla kassam akatoka nje kutayarisha huka na kuvuta huko huko. Baada ya kuvuta huka. Mulla kassam akasafisha na kuirudisha kwenye mkoba. huyo mtu tena akamwuliza kwamba alikuwa na haja yoyote". Mulla kassam akamwomba chakula kidogo lakini mtu huyo akamwambia, "usiombe kitu cha dunia". mulla kassam akasema kwamba alikuwa tayari kupokea kitu chochote atakachopewa. kwa hiyo, akasema: "mimi ninakufundisha dua mbili na usome hizo wakati wote unapohitaji chochote au unapohitaji msaada wangu katika dhiki na papo hapo mimi nitakuja kukusaidia. hata hivyo, dua mojawapo ni kwa ajili yako tu, na ya pili kwa ajili ya kila mwumini".

Mulla kassam akaomba msamaha kwa sababu ya kutokuwa na karatasi au kalamu. Mtu huyo akamwelekeza akachukue kutoka mkobani. Mulla kassam alipoangalia mkobani aliona hakuna huka aliouweka humo yeye mwenyewe. aliona dawati, kalamu na karatasi tu. Akachukua hizo na kuanza kuandika. Kwanza huyo mtu akamwandikisha dua iliyokuwa kwa ajili yake tu. baadaye akamwandikisha dua nyingine ya kusoma mara sabini ambayo inamhusu kila mwumini akiwa na haja au anakabiliwa na dhiki "ya allah, ya muhammad, ya ali, ya fat1ma, ya sahibuzzaman adrikny wala tuhlikny". mulla kassam alipofikia neno la mwisho alisita maana katika vitabu vingine vimeandikwa adrikuuny 'katika uwingi' (nyinyi wote njooni kwa kunisa1dia). Huyo mtu akasema: "kwa nini huandiki. adrikny katika umoja ni sahihi kwa sababu mimi peke yangu naja kusaidia na mimi ni hujjat (khalifa) wa mungu katika muda huu na nina uwezo wote. kwa hivyo msaada wangu tu unaombwa. majina ya mungu, mtume mtukufu 'hadhrat ali(a.s) na fatima(a.s) yanatajwa kwa pamoja, kwa sababu wao ni wasila.

Mwombaji msaada ameomba msaada wangu kwa kutumia majina yao". kwa hivyo mulla kassam aliandika hivyo na kurudisha wino na kalamu mkobani. Akainua kichwa chake kutaka kusoma hizo dua il kuangalia kama kuna kosa. aliponyanyua kichwa chake hakumwona mtu yeyote, mswala wala mkoba. Papo hapo akaelekea mlangoni na kuangalia kote lakini hakumwona mtu yeyote. akamwuliza msaidizi wake, naye akajibu hakumwona mtu yeyote. mulla kassam hapo akaamini kwamba huyo mtu alikuwa imam wake(a.s) naye alionyeshwa miujiza na imam wake. kwanza imam(a.s) alijua alichotamani mulla kassam, katika mkoba wake hakikuwemo kitu chochote, tena kuona vifaa vya kuandika na hiyo huka kutoweka. akamshukuru mungu kwa nafasi hiyo aliyopatiwa lakini alisikitika kukosa fursa ya kumwuliza imam(a.s) masuala mengine.

9. Mwanazuoni mtakatifu seyyid ibne tawoos alimwusia mwanawe wa kwanza yafuatayo:- "mimi nakujulisha wewe, ndugu zako na yeyote atakayefahamu yaliyomo katika wasia huu kwamba mwenyezi mungu na mtume wake mtukufu(s.a.w.w) ametujulisha kuhusu bwana wetu imam wa wakati huu hadhrat imam mehdi(a.s) na vilevile kuhusu heshima, taadhima, misaada na manufaa wanayopata wafuasi wake kutoka kwake. sisi tusiwe tunamsahau na kutokumbuka kwa mapenzi hata kwa muda mfupi. ikiwa mtu atajishughulisha katika mambo ya dunia tu, utajiri, watoto, majumba na biashara basi atapendelea vitu duni vya dunia badala ya kumpenda imam wake."

Zaidi ya hayo, ikiwa mtu anajishughulisha nafsi yake na wafalme, wakuu duniani na viongozi, na kila saa anajibidiisha kuwafurahisha hao, kwa matumaini ya kunufaika kutoka kwao, basi naye daima atapenda uongozi na utawala wa wakuu hao uendelee. kwa hivyo, hatapata kujitokeza kwa imam(a.s) na utawala wake uanze kwa sababu utawala huo hautompendeza. kiini cha itikadi yetu ni kuwa imam wa wakati huu ni mtawala mstahilifu wa falme zote, na mali yote ni yake. Utawala na madamaa yote ni yake aliyopewa na mwenyezi mungu. Hata baada ya kuwa na itikadi kama hiyo ikiwa mwumini hachukizwi na hali ilivyo duniani na haombi mungu kuwa udhalimu wa haki za imam ukome basi huyo si mwumini mwenye imani halisi juu ya imam".

Dondoo hilo limechukuliwa kutoka wasia hiyo. kwa hakika, ikiwa mtu ana imani juu ya imam(a.s) basi lazima atamkumbuka imam wake. wakati wowote waumini wanapokutana jambo la kwanza la kuzungumzia liwe ughaibu wa imam(a.s) , upinzani dhidi ya uislam na masikitiko ya waumini. hivyo ndivyo inatakiwa iwe hali halisi. kwa hali ilivyo kwa wakati huu, ijapokuwa waumini wanamwamini humkumbuka imam(a.s) lakini mwaka mara moja tu, tarehe 15 shaaban au wanaposoma dua-ul-iftitah (dua inayosomwa usiku wa ramadhani) lailatulqadr, au katika maamkizi baada ya swala za kila siku. ni jambo la kuhuzunisha kwamba baada ya nyakati hizo hatuzungumzii chochote juu ya imam(a.s) wala hatumkumbuki. katika mikutano yetu hupitisha maazimio kuwatakia kheri watawala wa dunia, lakini hatufanyi hivyo kwa ajili ya mfalme wa dunia na akhera, baba yetu wa kiroho, na wala hatuombi msaada kutoka kwake kufanikisha mikutano yetu au kupatiwa faraja kutoka kwake (imam a.s.).

Kwa hiyo, ni wajibu wa viongozi wetu wa jamii, masheikh, wahubiri, pamoja na ulama kuendelea kueleza na kuhubiri habari za imam(a.s) , kughibu kwake na alama zitazotokeza siku za mwisho za dunia. Kwa kufanya hivyo, watachomeza hisia na kuzidisha matumaini ya waumini na kuepusha jamii kutokana na maasi, faraja na burudani, eti ndiyo maendeleo hayo! Lazima tutambue kuwa kughibu kwa imam(a.s) ni jaribio gumu kwa waumini. Mwenyezi Mungu aliwajaribu wafuasi wa mitume waliopita kama ilivyoelezwa bayana katika kitabu kitukufu na hadithi tulizonakili.

Ni ole wetu kuwa hata katika nyakati za taklifu na dhiki hatumkumbuki mhifadhi na imam(a.s) wetu na kuomba msaada wake. tunaamini kwamba mwenyezi mungu hakubali ibada zetu bila wasila ya imam(a.s) lakini bado tunaghafilika na imam wetu.

10. Katika zama za imam Ali(a.s) Sahaba wake mmoja ramila alisimulia: "safari moja nilipata homa kali. baada ya siku chache nikapata ahueni. ilikuwa siku ya ijumaa. kwa hivyo, niliamua kuoga tohara na kwenda msikitini ili niswali nyuma ya imam wangu na kufanya ziara yake. nikaoga na kubadilisha nguo zangu na kwenda msikitim. katikati ya hotuba nilikuwa ninahisi baridi na mwili wangu ukitetemeka lakini nikasubiri. Baada ya swala imam ali(a.s) alikwenda nyumbani na mimi nilimfuata nyumbani kwake.

Alinikaribisha na kuniambia kwamba nilikuwa natetemeka wakati hotuba ilipokuwa inatolewa. mimi nikamweleza hali yangu na imam(a.s) akssema: "oh Ramila, wakati wowote dhiki inapowakabili wapenzi wetu au wanapokuwa wagonjwa sisi vile viie huathirika kwa yale yanayowakabili wapenzi wetu". Mimi nikamwuliza: "Eh bwana wangu, hii athari hutokea kwa wakazi wa kufa tu wanapokabiliwa na dhiki?" imam(a.s) akajibu, "mfuasi wetu anapokabiliwa na tatizo au kuwa mgonjwa popote duniani sisi hupata taarifa papo hapo na kuathirika".

11. ikiwa kuna madhara au hofu kutokana na adui lazima tuombe msaada kutoka imam wa wakati huu kwa kuswali rakaateeni, kusoma ziara (maamkizi) kwa imam(a.s) na kusoma dua ifuatayo mara 70. ya mawlay, ya sahibazzamani; ana mustageethum bika, ya mawlay ikfini sharra many;udhini.

12. Namna nyingine ya kumkaribia na kuomba msaada kutoka kwa imam(a.s) ilivyonakiliwa katika vitabu vingi ni kumtumia aridhah na hayo hutupwa baharini, mtoni au ziwani. jambo hilo sana hufanywa siku ya 15 shaaban baada ya swala ya alfajiri kabla ya jua kuchomoza. aridhi hiyo huandikwa juu ya karatasi nadhifu na tohara na hufukizwa kwa udi na uturi na kufungwa katika udongo tohara na kutupwa majini kwa taadhima.

ili kufupisha maelezo hatuelezi kwa urefu dua inayosomwa wakati wa kutupa aridha hiyo majini, lakini mwumini yeyote anayetaka kupata msaada kwa kutumia njia hii anaweza kupatiwa aridha na dua inayohusika. bila shaka malalamiko haya humfikia imam(a.s) . mwumini yeyote mwenye imani madhubuti juu ya imam(a.s) na kuishi maisha ya kidini kwa kuswali, kufunga mwezi wa ramadhani na kujiepusha na maasi, anaweza kuomba msaada kutumia njia hii siku yoyote (siyo lazima iwe 15 shaaban). utaratibu huu humpa mtu nafasi kueleza bayana mapenzi na imani yake juu ya imam(a.s) na heshima ya kumtumia salaam kwa njia ya maandishi. hapa tunaeleza visa viwili kuhusu namna aridhi zilivyomfikia imam(a.s) na wahusika walivyo saidiwa.

1. Agha Mirza ibrahim shirazi anasimulia: "nilipokuwa shirazi nilikuwa na haja zangu chache ambazo zilikuwa zikinisumbua sana. kuiiko zote shauku ya kwenda karbala kuzuru kaburi la imam hussein(a.s) ilikuwa kubwa mno. ili kupata msaada wa imam-al-zaman(a.s) nilituma aridha kwa imam(a.s) . siku moja saa za jioni bila mtu yqyote kuniona nikatupa aridha yangu katika ziwa lililojaa maji. bila mwenyezi mungu hakuna aliyeshuhudia kitendo hicho.

Siku ya pili kama desturi nilikwenda darasani. walikuwa wanafunzi wengi huko darasani. mwalimu wangu kwa kunitaja jina alinijulisha kwamba ardhilihali yangu ilikwishamfikia imam(a.s) . Nilifurahi mno. Hata hivyo, nilimwuliza mwalimu wangu alipata vipi habari hiyo na akanijulisha: "jana usiku nilimwona hadhrat salman farsi katika ndoto. alikuwa na watu wengi pamoja na rundo kubwa la barua iliyokuwa mbele yake na ambazo akizikagua. aligeuka upande wangu na kunitajia jina lako pamoja na wachache wengine ili niwajulishe kwamba aridhi zenu zimekwishamfika imam(a.s) . baadaye niliona kwamba karatasi zilizokuwa mikononi nwa hadhrat salman zilikuwa na mhuri wa imam(a.s) .

Kwa hivyo, mimi nilielezwa kwamba aridha zote zilizoshughuiikiwa zilipatiwa muhuri wa imam(a.s) na zile zisizofanikiwa zilikosa muhuri. wanafunzi waliobaki waliniuliza kuhusu aridha hiyo na ndoto ya mwalimu wetu. niliwasimulia kuhusu aridha yangu ambayo iliwayakinisha kuhusu ndoto ya mwalimu wetu. kwa ufupi, nilipatiwa mahitaji yangu yote na vilevile nilifanikiwa kwenda karbalaa." Seyyid Muhammad Seyyid Abbas mkaazi wa Jabalul Amil, anahadithia: "mimi nilikuwa ninaishi najaf katika nyumba mojawapo iliyojengwa katika eneo la kaburi la hadhrat Ali(a.s) . nilikabiliwa na ufukara sana. mara nyingi ilibidi nipitishe siku zangu kwa kula tende kidogo na kunywa maji tu. Nilimwomba Mwenyezi Mungu kila siku nifarijike lakini sikumweleza mtu dhiki iliyonikabili. mwishowe nikaamua kutuma aridha kwa imam(a.s) .

Kila asubuhi wakati mlango wa najaf (mji mmoja huko iraq na pahala alipozikwa Imam Ali(a.s) ulipokuwa unafunguliwa nikienda kutupa aridhia yangu mtoni, siku 39 zilipita. Siku hiyo nilipokuwa ninarudi baada ya kutupa hiyo aridha nilihisi kama kuna mtu ananifuata. Nilipogeuka kuangalia nyuma nilimwona mwarabu kama mkaazi wa jabalu amil, akanisalimu na akaanza kufuatana nami. mimi nilijibu hiyo salam. yeye aliniuliza: "Sayyid Muhammad kwa muda wa siku 39 zilizopita kila asubuhi unapofunguliwa mlango wewe unatoka nje na kutupa aridha yako mtoni. una haja gani? unafikiri kama imam wako haelewi mahitaji yako?" mimi nilishangazwa vipi huyu mtu amejua shughuli zangu za kila siku maana sikumweleza mtu yeyote."

Papo hapo nikafahamu kwamba huyu anaweza kuwa imam(a.s) . nilisoma katika vitabu kwamba kitanga cha mkono uliobarikiwa wa imam(a.s) huwa chororo mno, hivyo kujitopsheleza nikakunjua mkono ili tupeane mikono. huyo imam(a.s) akanipa mkono wake na kitanga kilikuwa chororo mno. nilithibitisha kwamba huyo mtu alikuwa imam(a.s) na papo hapo niliinama ili nimbusu mikono lakini ghafla nikajikuta niko peke yangu. lakini nilifarijika kujua kwamba aridha yangu ilimfikia imam(a.s) na nilikuwa na bahati nzuri ya kuonana naye. Baada ya muda mfupi tu hali yangu ikatengemaa.


17

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 25

JE INAWEZEKANA KUONANA NA IMAM MAHDI(A.S) KATIKA KIPINDI CHA KUGHIBU KWAKE KWA MUDA MREFU (GHAIBATULKUBRA)?

Wapinzani wetu wanatucheka itikadi yetu kwamba hadhrat mahdi(a.s) ameishi maisha ya kutoonekana kwa muda wa miaka elfu na mia moja. kwa mfano, munshi khadim hussein anaandika katika gazeti la kikadiyani la lugha ya urdu na ambalo hutolewa kila mwezi kwa jina la tahshizulazham katika sura iitwayo tahkike akheruzzaman kwamba huona ajabu kabisa kwamba ijapokuwa hadhrat mahdi(a.s) yu hai kwa miaka 1100 hakuna mtu anadai kwamba kaonana naye (hadhrat mahdi a.s.). hoja hii ya gazeti hilo haina msingi wala itibari maana watu wengi wanaonana na hadhrat mahdi(a.s) na taarife kamili imeelezwa katika vitabu vya shia ithnaasheri. katika sura ya mwisho ya kitabu hiki tumesimulia habari za watu wachache waliokwisha bahatika kukutana naye. hata hivyo vitabu vikuu vingi vya kisunni vimeeleza habari za waislamu walio onana na hadhrat mahdi(a.s) .

Mwanazuoni mashuhuri wa kisunni, allama sha'arani, amenakili katika kitabu chake lawakihul .anwar kwamba sheikh hassan iraqi amesimulia kuwa: "siku moja nilipoingia ndani ya msikiti wa ijumaa wa ummayad niliwaona watu wengi wameketi kumzungukia mtu mmoja aliyekuwa akihutubia juu ya hadhrat mahdi(a.s) . mimi niliathirika sana na hiyo hutuba na nikaanza kupata shauku ya kutaka kuonana na hadhrat mahdi(a.s) na tokea siku hiyo nilikuwa namwomba mungu anijalie bahati hiyo. muda wa mwaka mmoja ulipita. siku moja nilikwenda katika msikiti huo kwa ajili ya swala ya magharibi na baada ya swala hiyo nilimkuta mtu aliyevaa kilemba cha kiirani akinijongelea. akanigusa begani na kuniuliza sababu gani nilikuwa nikimwomba mungu kwa bidii kuonana naye. mimi nikamwuliza yeye nani na akanijibu kwamba ni hadhrat mahdi(a.s) . papo hapo nikambusu mkono wake na nikamkaribisha nyumbani kwangu akakubali mwaliko wangu na kuwa mgeni wangu kwa muda wa siku saba. katika muda huo alinielimisha juu ya mambo ya dini na kunishauri nifunge kila siku moja na kuacha rnoja na koswali rakaa mia tano kila siku. siku ya saba wakati wa kuniaga akanishauri kutoonana na mtu yeyote, bali kujishughulisha katika ibada ya mungu na nisisumbuke kuhusu riziki yangu kwa sababu hiyo nitapatiwa.

Nilimsindikiza hadi mlangoni na akaniambia nirudi nyumbani mwangu. tokea siku hiyo nilikaa nyumbani kwangu kwa usalama. mwandishi anasema kwamba alipomwuliza umri wake wakati huo imam(a.s) akajibu kwamba umri wake ulikuwa miaka 620. mwandishi huyo huyo amenakili tukio hilo katika kitabu chake kingine yawakit wal jawahir ukurasa 288 kilichochapishwa misri.

Isitoshe visa hivyo vya watu kuonana na hadhrat mahdi(a.s) na majina yao yamehifadhiwa katika vitabu vya kisunni k.m. kifayatuttalib, matalibul usul na yanabiul mawadah na kadhalika. katika kitabu cha mwisho kilichoandikwa na sheikhul islam wa istanbul, sheikh Suleiman Kanduzi, sura ya 83 imetengwa kwa ajili ya maelezo ya watu walio onana na Imam Mahdi(a.s) .

1. Maelezo hayo yanatolewa kwa muhtasari tu hapa Ali abdulla bin saleh anaeleza kuwa: "Nilipomwona Imam Mahdi(a.s) huko makkah karibu na hajarul as-wad (jiwe jeusi) watu walikuwa wakisukumana ili wapate kusonga mbele. HapoImam Mahdi(a.s) akawaambia kwamba kitendo hicho ni kinyume cha amri ya Mungu.

2. Muhammad bin Shazan Kabuli anasimulia kwamba: alipoonana na Imam Mahdi(a.s) imam huyo alimwita kwa jina lake maalum linalojulikana na watu wa nyumbani mwake tu na kupatiwa majibu ya kutosheleza maswali aliyomwuliza ima(a.s)

3. Muhammad bin Othman alimwona Imam Mahdi(a.s) huko kaaba amenyanyua mikono yake kuomba dua na kusema "eh mungu timiza ahadi ulionipa mimi".

4. Zarif Abunasr anahadithia kwamba: alipobahatika kuonana na Imam Mahdi(a.s) yeye (imam as.) alisema: "mimi ni mrithi wa mwisho wa mtume mtukufu(s.a.w.w) na kwa ajili yangu watu wataepuka na maafa duniani."

5. Muhammad bin Abdulla Kufi ametoa taarifa ya majina ya watu kumi na wawili ambao walikuwa watumishi wa serikali na wengine 53 ambao wote walionana na hadhrat mehdi(a.s)

6. Hassan ibne wajna nasibi ameeleza kuwa: "mimi nilihiji mara 53 na kila mara huko kaaba nilikuwa nikimwomba mungu amjalie kuonana na imam(a.s) . mara moja katika safari ya 54 nilipokaa huko makkah alitokea mwanamke mmoja ambaye akahiita kwa jina langu hassan na kuniomba nifuatane naye. tulipofika kwenye nyumba ya bibi khadija (mke wa kwanza wa mtume(s.a.w.w) tukasimama. imam mahdi(a.s) mwenyewe akaja mlangoni. mimi nikamwamkia na akaniambia "hassan, mimi niko na wewe kila mwaka unapokwenda kuhiji. sasa wewe acha nyumba yako na uende kuishi katika nyumba ya imam jaffar sadiq(a.s) na usisumbuke kuhusu maisha yako. utapatiwa chakula na mavazi unayohitaji." vile vile akanifundisha dua moja.

Niliishi katika hiyo nyumba kwa muda mrefu na nilipatiwa mahitaji yangu juu ya wakati.

7. Ali bin Ahmed Kufi anasimulia kwamba: mara moja alipokuwa akitufu kaaba akashituka ghafla kumwona kijana mwenye uso unaong'aa. katika msituko huo akamwuliza huyo kijana yeye nani, na akajibiwa: "Mimi ni imam na wakati huu na ni mahdi ambaye atajaza dunia kwa uadilifu na usawa. Kwa hakika hujja (khalifa wa mungu) daima huwapo duniani." baadaye akatupa fimbo aliyoshika mkononi mwake. Mimi nikanyanyua hiyo fimbo na nilipoiangalia nimeona imegeuka ya dhahabu, nikamrudishia hiyo fimbo.

Rashid hamdani anasimulia: "mara moja nilipokuwa narudi kutoka hijja nilipotea njia. nilijikuta peke yangu msituni. nilikwenda hatua chache tu nikaona bustani ambayo ikinukia viziiri. ghafla nikaona hema moja zuri na nje yake walikuwa wahudumu wawili. waliponiona mimi mmojawapo akaingia ndani na baada ya muda mfupi akarudi na kunikaribisha ndani ya hema. Ndani humo alikuwa ameketi mtu mwenye haiba na uso unaong'aa. Juu ya kichwa chake kulikuwa upanga mrefu ulioning'inia hewani. nikamsalimia, naye akanijibu na kusema: "mimi ni qaim (aliyesimama) ambaye nitajitokeza siku za mwisho wa dunia na kwa upanga huu nitatawala dunia kwa insafu na usawa." mimi nikapiga magoti na yeye akasema:

Hakuna wa kumsujudia yeyote ila mungu; nyanyua kichwa chako jina lako ni rashidna wewe ni mkazi wa hamdan. Unahitaji nini? je, unahitaji kufika nyumbani kwako? mimi nikajibu, "ndio seyyid yangu, mimi nina hamu sana kufika nyumbani kwangu" akanizawadia mkoba mmoja na kumwagiza mhudumu mmoja anifikishe nyumbani kwangu. tukaondoka pale na baada ya hatua chache tu mhudumu akaniambia: "angalia, hapa ni makazi yako; endelea. Nilipogeuka na kumwangalia huyo mhudumu sikumwona. nilipofika nyumbani niliona kuwa katika mkoba huo hadrat mahdi alinizawadia sarafu hamsini za dhahabu. sarafu hizo zilitufanya tuishi kwa raha sana."

Hayo yote yameandikwa katika kitabu kimoja kiitwacho yanabiul-mawaddah. Licha ya hayo, kuna visa vingi vilivyonakiliwa katika vitabu vingi vya kisunni na hata kutaja majina ya watu walio onana na imam(a.s) na sababu za kuonana naye. bila shaka katika vitabu vya shia kuna visa vingi vilivyohadithiwa. udogo wa kitabu hiki hauruhusu kuingiza maelezo marefu.

SURA 26

VISA SITA VYA WATU KUKUTANA NA IMAM MAHDI(A.S)

Kisa cha kwanza: uwekaji wa jiwe jeusi (hajar-ul-aswad) pahal a pake na imam wetu wa wakati huu hadhrat mahd(a.s) . mwanazuoni wa kishia, abil kassim jaffar ibne muhammad kavliyah, amenakili katika kitabu chake kuwa: "katika 307 a.h. jeshi la karamala lilivamia kaaba. tukufu na kuondosha jiwe jeusi (Hajarul Aswad). Baadaye waliamua kurudisha hilo jiwe wakati ambapo mimi nilikuwa nikijiandaa kwenda kuhiji na nilifika baghdad. mimi nilijua kwamba atakayeweza tu kuweka hilo jiwe jeusi (Hajarul Aswad) ni imam wa wakati huu na ilikuwa kwa nia hiyo ya kuonana na imam(a.s) ndiyo niliamua kwenda kuhiji mwaka huo. kwa bahati mbaya huko baghdad nikawa mgonjwa sana. Kwa hiyo nikamwomba ibne hashim aende kuhiji kwa niaba yangu na nikampa fedha za kugharimia safari hiyo pamoja na barua. nikamsisitizia kwamba kwa hali yoyote lazima aonane na mtu yule atakayeweka hilo jiwe jeusi (Hajarul Aswad) na kumkabidhi barua hiyo".

Ibn Hashim anahadithia: "Mimi nilikwenda makkah na nikawalipa fedha nyingi wahudumu huko kaaba ili wanipatie nafasi karibu na Hajarul Aswad. umati rnkubwa wa watu ulikusanyika huko msikitini. nilishuhudia kwamba watu wakuu na wanazuoni walijaribu kulirudisha hiio jiwe jeusi (Hajarul Aswad) pahala pake lakini bila mafanikio; jiwe hilo liliendelea kucheza. ghafla kijana mmoja mwenye haiba na uso wa kung'aa akajitokeza na kwa mikono yake iliyobarikiwa akaliweka jiwe hilo nafasi yake. hilo jiwe likaganda barabara.

Umati walipata msisimko na kwa furaha wakasema kwa sautikubwa "allahu akbar". Baada ya kuweka hilo jiwe kijana huyo akaondoka. Mimi nilimfuata nikiwasukuma watu kama kichaa. Huyo kijana alikuwa anakwenda polepole lakini sikuweza kumfikia ijapokuwa mimi nilikuwa nakwenda mbio mno. mwisho tukafika msituni nje ya jiji. huyo kijana akasimama, akageuka na kuniomba hiyo barua. bila kusoma hiyo barua akaniambia "mwarifu mwandishi wa barua hii kwamba, atapona ugonjwa wake na ataishi muda wa miaka 30 mingine".

Kusikia hayo mimi nililia kwa kuhemkwa. katika kipindi hicho huyo mtukufu alitoweka machoni mwangu." Ibn Hashim alirudi kwa ibne kavliyah na kumsimulia maneno aliyoyasema imam(a.s) na kama alivyobashiri imam mwanazuoni huyo aliishi miaka 30 zaidi. kisa cha pili kuonekana kwa hadhrat mehdi(a.s) huko" kandhar afghanistan katika jawabu lake kwa mwanazuoni mwingine, mulla abul kassim kandhaar amesimulia kuwa: katika mwaka 1266 a.h, mimi nilikuwa kandahaar, huko afghanistan nikihudhuria darasa la unajimu na falsafa kutoka kwa mwana wa mulla abdulrahim mulla habibullah. siku moja ya ijumaa nilimtembelea nyumbani kwake.

Alikuwa amekaa sebuleni akiwa pamoja na wanazuoni wengi, mahakimu na viongozi wa jiji walioegemea kuta. Kati yao alikuwa mulla gulam muhammad, kadhim mkuu, sadra muhammad ali khan na mwanazuoni kutoka misri ambao wote hao walikuwa masunni. mfanyabiashara mmoja wa kishia, wana wa mwenyeji, mwana wa kadhi na mimi tulikuwa tumekaa kuelekea qibla. majadiliano ya mantiki na ya kidini yakaanza. kadhi mkuu alizungumzia kwa kirefu dhidi ya shia, kuwakashifu mashia na kudai namna shia walivyokuwa wajinga na wapuuzi kwa kuamini kwamba hadhrat mahdi(a.s) amekwisha zaliwa kutokana na hadhrat imam hassan askari(a.s) mwaka 255 a.h. na kughibu katika mwaka 260 a.h. na kuwa yungali hai hadi leo. Wote waliafikiana naye, ila mtu mmoja tu: mwanazuoni aliyetoka misri ambaye alikuwa sunni na alishiriki katika majadiliano ya awali ya kukashifu mashia.

Lakini katika suala hilo yeye hakuwaunga mkono masunni wenzake. alipomaliza mazungumzo yake kadhi mkuu, mwanazuoni kutoka misri akasema: " sasa nisikilizeni mimi kwa makini. "Mimi nilikuwa ninapata mafunzo ya hadithi kutoka kwa mufti katika shule moja huko tawleen. Mufti alizingumzia sura, urefu na jamali ya hadhrat mahdi(a.s) . kulikuwa mazungumzo marefu juu ya somo hilo. Ghafla wote tukakaa kimya kwa sababu kijana mmoja mwenye sifa hizo na urefu huo alionekana amekaa na sisi. kila mtu akainama na kunyamaza. hakuna mtu aliyethubutu kunyanyua jicho lake au kunene neno".

Mwanazuoni wa kimisri alipomaliza kusema hayo waliohudhuria wote wakainamisha vichwa vyao na wakakaa kimya. Baada ya muda mfupi tu wote waliloana kwa jasho. mimi mara moja tu nilinyanyua macho yangu ili nimwone imam(a.s) . alikuwa amekaa katikati yetu na kila mtu alikuwa kimya akimwangalia mwenzake. kwa hakika mimi nilishtuka. hata hivyo, sikuthubutu kusema neno. mmoja baada ya mmoja wakaanza kuondoka bila kuagana. usiku huo mzima mimi sikupata usingizi na nilikuwa katika hali ya furaha mno kwa kupata fursa ya kuweza kuonana na imam(a.s) . zaidi ya hayo, wapinzani walipata jibu muafaka la hoja yao juu ya wakati, yaani kuwepo kwa imam(a.s) , kughibu na uwezo wake juu ya dunia nzima kulithibitika bayana'. Hata hivyo, mimi nilihuzunika sana kwa sababu niliweza kumwona imam wangu mara moja tu, lakini ukweli ni kwamba sikuthubutu kunyanyua kichwa changu mara ya pili."

Mulla abdul kassim anaendelea kusema: "siku ya pili nilihudhuria darasa la mulla abdulrahim ambako imam(a.s) alitutembelea. mwalimu wangu akaniita faraghani katika maktaba na kuniuliza", je uliona kulitokea nini jana? hadhrat mahdi(a.s) mwenyewe alitutembelea na sisi sote tuliloana kwa jasho, tulipigwa na butaa na hivyo tuliondoka bila hata kuagana. Kwa hofu nikasema kuwa sijaona kitu chochote. yeye (mwalimu) akasema: "hilo ni jambo dhahiri, kwa nini unakanusha? wengi waliohudhuria jana wameniandikia kuhusu waliyoyaona jana na kushangazwa na kisa kilichotokea jana." Siku ya pili mtaani nikaonana na huyo mfanyabiashara. Yeye akasema "Mwenyezi Mungu ametusaidia kwa kutupatia nafasi ya kuonana na hujjat (khalifa) wake duniani. zaidi ya hayo sardar alikhan akasadiki ukweli kuhusu imam mahdi(a.s) na kugeuka shia".

Baada ya siku chache nilionana na mwana wa pili wa kadhi mkuu ambaye aliniambia kwamba baba yake angependa nimtembelee. mimi nilikataa moja kwa moja lakini alishikilia nimtembelee baba yake na mwishowe nililazimika kwenda kuonana na kadhi mkuu. nilikwenda kuonana na huyo kadhi mkuu na nikamwamkia. akanijibu na kunikaribisha kuketi karibu naye. wakati huo mwanazuoni wa kimisri na watu wengi walikuwa wamekaa hapo. huyo kadhi mkuu akaniuliza juu ya tukio la usiku huo. mimi nikajibu kwamba nilichoona tu ni watu kuondoka (kutawanyika) bila kuagana. wote waliohudhuria wakaniita 'mwongo'. wakasema kwamba walimwona mtu mwenye haiba alikuwa amekaa nao amepinda magoti yake. kadhi alisema kuwa mimi ni mwanafunzi wa fiqhi (elimu kuhusu maamrisho ya kidini). "hawezi kusema uwongo. huwezekana kwamba wale watu waliokuwa na shaka kuhusu imam mahdi(s.a) wamemshuhudia. lakini huyu akiwa shia mwenye itikadi thabiti. Juu ya imam(a.s) hakushuhudia hayo."

Waliohudhuria wote walitoshelezwa na maelezo ya kadhi. kisa cha tatu ziara ya hadhrat mahdi(a.s) nyumbani kwa mwanazuoni maarufu -agha seyyid mahdi - huko hilla iraq huko hilla kulikuwa na mfanyabiashara mmoja kwa jina la shekh ali ambaye alikuwa mmojawapo wa waumini. anaeleza kuwa "siku moja asubuhi niliamua kwenda nyumbani kwa agha seyyid mahdi bahrul-uluum kumsalimia. njiani nikapita karibu na kaburi la seyyid muhammad zidmeah. nikamwona mtu mwenye haiba kuu amesimama karibu na hilo kaburi akisoma suratul fatiha. huyo alikuwa mwarabu mwenye uso unaong'aa. nilipomwona mtu huyo na mimi nikasimama kusoma fatiha. baadaye nikamsalimu. akanijibu na kuniambia "o Ali, unakwenda kumwona seyyid muhammad ?" mimi nikajibu "ndiyo". njiani akaniambai, "o Ali usikate tamaa. Umepata hasara kubwa katika biashara. Hiyo ndiyo hali ya utajiri kwa sababu fedha haikai daima kwa mtu mmoja. mungu atakusaidia wewe ijapokuwa ulikuwa umewajibika kwenda kuhiji lakini hukutekeleza. hata hivyo, usijali, utakuwa tajiri tena. Mimi nilishangazwa sana vipi mtu nisiyefahamiana naye alipata habari kuhusu hasara niliyoipata? hata hivyo, nikajibu kuwa mungu ndiye anayestahili sifa zote na apendaye yeye ndio huwa. Hapo tulikuwa tumekwishafika nyumbani kwa mujtahidi (mwanazuoni). Mimi nikangoja na nikamwomba atangulie. yeye akajibu 'ana sahibuddar' kumaanisha: "mimi ndiye mwenye nyumba" (moja wapo ya sifa na majina ya heshima ya imam mahdi(a.s) ni sahibuddar".

Hapo akanikamata mkono na kunitanguliza na akanifuata. katika nyumba hiyo kulikuwa chumba kikubwa ambamo huyo mujtahid akiendesha darasa. Wanafunzi wake walikuwa wanamsubiri. nafasi hiyo ya mujtahidi ilikaliwa na huyo mtu (imam mahdi(a.s) na mimi nikakaa kando karibu na nafasi ya mujtahidi. Huyo mtu akanyanyua kitabu kimoja kilichoandikwa na mujtahidi mwenyewe na akaanza kusoma na kuwaelekeza wanafunzi kuwa: "kitabu hiki ni cha maana sana. Kuna dalili thabiti kuhusu kanuni za dini". katika muda huo mujtahid alitoka chumbani mwake na kumwona huyo mtu mwenye haiba amekaa juu ya nafasi yake. Kumwona mujtahid, huyo mtu akasimama na kumpisha nafasi yake, lakini huyo mujtahid akasisitiza akae hapo hapo na mujtahid akakaa kwa heshima mbele yake. Mujtahid huyo alishawishika sana kumwuliza jina lake huyo mtu na anatokea wapi lakini alishindwa. Mujtahid akaanzisha mafunzo kama kawaida na mtu huyo akatoa maoni yake. Kabla ya hapo sijapata kusikia dalili na maelezo kamilifu kwa ufasaha na uwazi kama alivyoeleza mtu huyo. Mwanafunzi mmoja mjinga na mjeuri akamkatiza kauli na kumwuliza kwamba yeye anafahamu nini juu ya swala hilo, lakini huyo mtu alitabasamu na kukaa kimya.

Baadaye huyo mtu akaomba maji na msaidizi akaanza kujaza maji katika bilauri kutoka kwenye mtungi mkubwa. Huyo mtu akasema 'hayo maji katika mtungi huu siyo safi kwa sababu kuna mjusi amefia humo" na akaomba maji kutoka mtungi mwingine. Maji yaliletwa na huyo mtu akayanywa. Mujtahid hapo akamwuliza anatokea wapi, akajibu kuwa ametoka mji wa suleimanlyya. Mujtahidi akamwuliza alianzalini safari yake kutoka suleimaniyya, naye akajibu "niliondoka jana. Najibpasha amekwishaingia mjini na jeshi la serikali na kuliteka. amemweka kizimbani gavana mwasi ahmed na badala yake amemteua abdulla pasha kuwa gavana" umbali kutoka suleimaniyya hadi hilla ulikuwa safari ya siku kumi na mimi nilishangazwa huyo mtu amefika hapa namna gani katika muda mfupi ilihali gavana wa hilla au mtu yeyote mwingine hana taarifa juu ya ziara yake. Hata hivyo, nikanyamaza kimya!

Hapo teaa huyo muadham akasimama ili aondoke. Mujtahid akamsindikiza mpaka mlangoni. Kurudi tu mujtahid akawauliza wanafunzi kwa sababu gani hawakumwuliza huyo muadham ameweza vipi kusafiri umbali kutoka suleimaniyya mpaka hilla katika usiku mmoja wakati safari kutoka suleimaniyya mpaka hilla huchukua siku kumi? Wanafunzi wakamwuliza mujtahid sababu gani yeye mwenyewe hakumwuuliza muadham swali hilo.

Mujtahid akajibu kuwa wakati huo alipotelewa na fahamu. Yeye (mujtahid) akatuomba sisi sote tutoke nje kumtafuta huyo muadham ijapokuwa yeye alikuwa na uhakika kwamba hatutamwona kwa sababu aliamini kwamba huyo muadham alikuwa imam mahdi(a.s) mwenyewe. chombo kilichokuwa na maji hakikuwepo usoni lakini alijua kwamba mjusi alifia ndani humo. Ili kuhakikisha ukweli ukweli huo, hicho chombo kililetwa na kweli alionekana mjusi mmoja mrefu humo. tena katika maswali ya dini alikuwa anaelewa mambo yote na kueleza kikamilifu.

Hapo tena mimi nikaeleza vipi nilikutana naye njiani na alinizungumzia juu ya biashara yangu na hasara niliyoipata, na mimi kutokwenda kuhiji. wote waliamini kwamba huyo muadham hakuwa mtu yeyote mwingine ila hadhrat hujjat(a.s) mwenyewe. Baada ya siku kumi gavana wa hilla akapata taarifa ya kutekwa kwa suleimanniyya ambayo iliimarisha zaidi imani ya wote kwamba walibahatika kuonana na hadhrat mahdi(a.s) na wakamshukuru mungu kisa cha nne mwanafunzi wa najaf aonana na hadhrat mehdi(a.s) katika msikiti wa kufa mwanazuoni wa najaf, sheikh abdul hadi anahadithia kuwa: "Muumini mmoja katika mji wa Najaf, haji ali, akienda msikiti wa sahlah kila usiku wa kuamkia jumatano. siku moja nilimwuliza kama aliwahi kubahatika kuonana na imam mahdi(a.s) .

Akanijibu kwamba miaka mingi kabla yeye pamoja na wanafunzi wenzake na waumini(wengine walikuwa wakienda kukesha huko msikitini kufa kila usiku wa jumatano. (msikiti wa sahlah uko kufa, iraq). Walikuwa kumi na mmoja na kila wiki mmojawao huleta chakula, chai na tumbaku, siku moja ilikuwa zamu ya mwenye duka, yeye aliandaa kila kitu lakini alisahau kuvichukua alipokwenda msikitini. Tulikwenda msikiti wa sahlah na baada ya kuswali swala ya isha tukaenda msikiti wa kufa na baadaye tukakusanyika katika chumba kimoja kula chakula. Wote walikaa kimya. hata huyo mwenye duka aliyewajibika kuleta chakula vilevile alikaa kimya na kuinamisha kichwa chake kwa fedheha. Alikiri kwamba ijapokuwa aliandaa vifaa vyote lakini alisahau kuleta pamoja naye. Aliahidi kwamba atakapofungua duka siku ya pili atatuonyesha alivyokiandaa. Kwa hivyo, sisi tulijiandaa kupitisha usiku huo wa baridi kwa njaa. Ghafla tukasikia mlango ukibishwa na mmoja wetu ambaye alishikwa njaa sna usiku huo wa baridi alikwenda kufungua mlango na kuuliza nani alikuwa anagonga mlango usiku wote huo.

Huko mlangoni akakutana na mtu mwenye uso wa kung'aa na wenye haiba na akasalimiana naye pale pale. alijibiwa kwa sauti ya kufurahisha. rafiki yetu akamwuliza huyo (mgeni) akauliza: 'mtapendelea kupata mgeni usiku huu? rafiki yetu akamkaribisha kwa dhati. huyo mgeni akaingia ndani na kukaa pamoja na sisi. Tulihisi furaha na faraja mioyoni mwetu kwa sababu ya huyo mgeni kuwa nasi. Alianza kuzungumza taratibu na kwa sauti ya kupendeza. Alitusimulia hadithi za mtume mtukufu(s.a.w.w) na kumtaja mtume(s.a.w.w) kuwa ni babu yetu'.

Baada ya muda mfupi, akatuambia kuwa hatukuwa tumekunywa chai na kuwa yeye alileta viungo vyote vya chai katika mfuko wake. sisi sote tulifurahika mno kwa sababu usiku huo wa baridi kama tusingeweza kupata chakula basi hata chai ingetutosheleza. mmoja wetu akatoa viamkajengo vyote pamoja na sufuria na makaa. mwenzetu alipokuwa anapika chai mgeni alikuwa akitufarajisha na hadithi muhimu sana. baada ya kunywa chai tukarudisha vyombo vyote na akanendelea kuzungumza na sisi. baada ya muda mfupi tu akatamka: "nyinyi nyote mna njaa kwa sababu hamkuwa na chakula chochote. toeni chakula mfukoni mwangu mle. sisi tulifurahi sana na ukarimu huo na tukamshukuru mungu. mmoja wetu akatoa chombo kilichojaa chakula kutoka katika mkoba huo.

Tulipofunua hicho chombo tuliona wali uliopikwa vizuri pamoja na nyama. chakula kilikuwa moto nacho kilipikwa muda mfupi tu uliopita. tukala mpaka kushiba. alipoona chakula kimebaki akatuambia tumpelekee mhudumu wa msikiti.

Usiku wa manane mgeni huyo akatushauri tulale. hivyo sote tukapata usingizi na kulala. Tulipoamka asubuhi tukaswali swala ya asubuhi na baadaye tulipokuwa tunajiandaa kurudi najaf tukamkumbuka mgeni wetu. Tukaanza kumtafuta kila mahali msikitini lakini hatukumwona. tulimwuliza mhudumu wa msikiti kama alimwona mtu yeyote lakini alijibu hakumwona mtu yeyote kuingia msikitini usiku maana milango ya msikiti ilifungwa. kwa hivyo, hakuna aliyeweza kuingia au kutoka.

kwa hivyo, sisi sote tulistaajabishwa. Baadaye tukang'amua kwamba vipi katika ule mkoba mdogo tuliweza kuona vyombo vya kupikia chai bila kuwemo vyakula humo ndani na baada ya muda mfupi tuliweza kupata vyombo vilivyojaa vyakula bila kuona alama yoyote ya vyombo vya kupikia chai. Zaidi ya hayo saa nyingi zilipita tangu huyo mgeni (imam Mahdi a.s.) alipofika na wakati chakula kilipoanza kugawanywa kilikuwa kimoto na chenye ladha na kututosheleza sote kumi na mmoja mpaka tushibe. hivyo, tukaamini kwamba hayo yote yaliyotokea yalikuwa miujiza. tena tukakumbuka kwamba huyo muadham (imam mahdi a.s.) alipokuwa akisimuli hadithi za mtume(s.a.w.w) akimtaja mtume(s.a.w.w) kuwa ni babu yake na mwishowe kutoweka machoni mwetu. Sote tulikuwa na hakika kwamba mgeni wetu aliyetufikia usiku uliopita hakuwa mtu yeyote mwingme ila imam wetu hadhrat hujjat (a.s) . tulisikitishwa sana kwamba hatukuweza kumtambua imam wetu usiku huo.

Kisachatano maskani ya imam wetu (imam mahdi a.s) katika hilla (iraq) agha hujjatul islam seyyid ali akbar khui mwanazuoni maarufu huko mashhad (iran) amesimulia: "nilipokwenda iraq kuzuru makaburi ya maimam wetu(a.s) nilikwenda hilla ambako niliona jengo lenye kuba. kwenye mlango mkuu niliona maandishi yakisema: "makamu sahebuzzaman" na watu wengi huzuru mahala hapo. Niliuliza watu kuhusu jengo hilo na nikaambiwa kwamba hilo jengo lilikuwa mali ya mwanazuoni agha sheikh ali hallawi ambaye alikuwa mcha mungu na kila saa akimkumbuka imam wetu(a.s) .

Yeye alikuwa akiuliza sababu gani imam(a.s) ilikuwa hajitokezi wakati hadithi husema kwamba masahaba 313 wa imam wanahitajika na wakati huu kuna waumini wengi duniani na hilla peke yake ina wanazuoni wacha mungu zaidi ya elfu moja. Hilo lilikuwa hoja kuhusu kujitokeza kwa imam(a.s) lililosumbua mara kwa mara alipokuwa anatembelea bustani nje ya mji. alikuwa amepotea katika mawazo hayo. Ghafla akamwona mwarabu mmoja anamkaribia na baada ya kusalimiana naye mwarabu huyo akamwuliza sababu iliyofanya azungumze peke yake kwa hasira. Akajibu kwamba dhuluma na dhambi zimetawala duniani kote lakini imam(a.s) hajitokezi.

Yeye (imam a.s.) anahitaji masahaba waaminifu 313 tu, ilihali katika hilla peke yake kuna wanazuoni wacha mungu zaidi ya elfu moja. Huyo sheikh akajibiwa: "eh sheikh, mimi ni imam wako na sivyo kama wewe unavyofikiri. katika hilla nzima wewe na yule mchinja nyama tu mnastahili kuwa masahaba wangu halisi. Nitakuthibitishia hayo. Nenda ukachague wanazuoni 40 wacha mungu katika hilla na uwaambie kwamba usiku wa alhamisi imam(a.s) atafika nyumbani kwako (kwa aga sheikh ali hallawi). Waalike kuja nyumbani kwako baada ya swala ya isha. wewe uwalete mbuzi wawili na uwafunge nyumbani kwako ghorofani na umwambie huyo mchinja nyama alete buchari yake.

Waweke hao wageni wakae sebuleni na mimi mwenyewe nitafika huko. sheikh alifurahi mno kusikia hayo lakini mara alijikuta yuko peke yake papo hapo, akaenda kuonana na mchinja nyama na kumhadithia mambo yote. baadaye kama alivyoagizwa akawaalika wanazuoni wacha mungu arubaini. ambao walifurahi sana kujua kuwa watamwona imam(a.s) kama ilivyoahidiwa. 'sheikh ali akanunua mbuzi wawili. usiku wa alhamisi watu walioalikwa walikusanyika nyumbani kwa sheikh ali na kujishughulisha katika dhikri ya mungu na kumswalia mtume(s.a.w.w) pamoja na dhuria yake. katika muda mfupi harufu nzuri ikatapakaa kote na mwanga wenye nguvu ukamulika nyumba. Mwanga huo pole pole ukawapitia wote waliohudhuria sebuleni na ukaendelea huko juu ghorofani. Wote walishangaa na mshangao kusema kuwa imam(a.s) amefika na wakasoma takbir na salawat (takbir ni allahu akbar salawat ni kumswalia mtume(s.a.w.w) pamoja na dhuria yake). Waliuona mwanga tu. hawakuona umbile la mtu yeyote.

Baada ya muda mfupi wakasikia sauti kutoka juu ikimtaka sheikh ali kumpeleka huyo mchinja nyama. Mchinja nyama huyo alipanda juu. Imam(a.s) akamwamrisha amchinje mbuzi mmoja. Kwa miujiza ya imam(a.s) huyo mbuzi hakupiga kelele hata kidogo. Damu ya huyo mbuzi aliyochinjwa ikatiririka kutoka darini mpaka chini uani. wageni walipoona hiyo damu wakaingiwa na hofu. wote hao wakaamini kwamba imam(a.s) amemchinja mwuza nyama. hapo tena wakasikia sauti nyingine kumtaka sheikh ali aende juu. sheikh ali alipoflka juu imam(a.s) akaamrisha huyo mbuzi wa pili achinjwe. Damu ya huyo mbuzi wa pili ilitiririka mpaka waliko wageni. Wageni hao wakatetemeka na kuamini kwamba hata sheikh ali amechinjwa. waliogopa na kufikiria kwamba sasa itakuwa zamu yao ya kuchinjwa. Basi wote wakakimbia na hata mmoja hakubakia.

Hapo tena imam(a.s) akamwambia sheikh ali aende huko chini na kuwaleta hao wageni, lakini alimwarifu kwamba hatamkuta hata mtu mmoja. sheikh ali alipofika sebuleni akaona watu wote wameondoka. kurudi juu kwa imam(a.s) alipigwa na butwa. Imam(a.s) hapo akamwuliza: "je, umesadiki hao watu wana imani namna gani juu ya imam wao?" kuokoa maisha yao wote wamekimbia, hawakuwa na subira hata ya kuonana na mimi. Kwa hivyo sasa wacha kukereka rohoni mwako kuhusu kujitokeza kwangu. katika wale watu arubaini uliowateua katika hilla, bila nyinyi wawili wote wamekimbia. Hali hiyo iko katika nchi". Baada ya kusema hayo imam(a.s) akatoweka. "kutukuza ziara ya imam(a.s) nyumbani kwa shekh ali, yeye (shekh ali) akatengeneza nyumba hiyo kwa upya na akatoa wakf na kuipa jina la "makamu sahiuz-zaman" hadi leo nyumba hiyo ipo hilla na watu wengi huizuru. Wengi wameomba haja zao na wamefanikiwa. Licha ya hilla tu kuna pahala pengine panapohusika na kufika kwa imam mahdi(a.s) .

1. Katika maziara ya wadisusalaam huko najaf kuna pahala panapojulikana kama makamu Sahibu zaman ambapo watu hufika kwa ajili ya ziara na hufanikiwa wanachoomba.

2. Baina ya kufa na najaf kuna msikiti unaojulikana kama sahla ba humo kuna nafasi inayonasibishwa na imam(a.s) .

3. Katika mji wa naa'maaniyyah, ulioko kati ya baghdaad na wasta kuna nafasi iliyopatiwa jina la imam(a.s) na watu wengi huenda huko kwa ajili ya ziara.

Kuna pahala pengine ambapo imam(a.s) hutembelea. nafasi hizo zilizotembelewa na imam(a.s) watu huenda kuzuru na kuomba dua zao. kama tulivyoeleza juu, katika pahala paitwapo na'maniyyah mwanazuoni mmoja sheikh ibne abil jawad alibahatika kuonana na imam(a.s) . Yeye anahadithia: "mimi nilibahatika kuonana na imam(a.s) na nikamwambia kuna pahala pawili patakatifu pamepatiwa jina lake, moja huko na'maniyyah na kwingine huko hilla. yeye (imam a.s.) akajibu" usiku kuamkia jumanne na siku ya jumanne mimi huja na'maniyyah. usiku wa kuamkia ijumaa na siku ya ijumaa mimi huenda hilla. Lakini wakazi wa hilla hawana tabia nzuri. hawaniheshimu mimi wala hawapaheshimu pahala pangu. Wanapoingia hawanisalimii na wala hawawaswalii babu zangu kumi na wawili. Mwumini yeyote akizuru pahala pangu hilla, akiniamkia asome salawat mara kumi na mbili, aswali rakaa mbili asikitike kwa mungu kumwomba mungu haja zake zisikilizwe.

Mimi (abiljawad) nikamwomba: "Eh bwana wangu, nifundishe hiyo dua inayotakiwa kusomwa hilla". Imam(a.s) akanisomea hiyo dua mara tatu ili niweze kuihifadhi kwa moyo. Dua biyo ni kama ifuatayo: "Allahumma kad akhzattaadibu minnl hatta massanniyadhur waanta arhamur raahimiiin, wain kana maktarafu minaaddhunub astahikku bihi azaf azaf ma addabtani bihi anta halimunzu antin ta'fuan kasir hatta yasbiku afwaka adhabak". Dua hiyo isomwe mara tatu na baada yake isomwe salawat.

Kisa cha sita mwujizawa kuponyesha jeraha pajani mwa ismail harkali mwanazuoni wa kishia ali ibne issa arbali amesimulia katika kitabu chake kashful ghumma tukio la ismail bin hassan harkali lililotokea katika kipindi cha utawala wa khalifa mustansir ukoo wa bani abbas. Yeye anahadithia kwamba ismail bin hassan harkali alifariki dunia akiwa rika yake lakini hakuwahi kuonana naye. Hata hivyo, alisimuliwa na mwanae harkali, shamsudin, hadithi alivyopokea kutoka baba yake. (ismail bin hassan harkali). Wakati nilipokuwa kijana nilipata jeraha kwenye paja la mguu wa kulia. Hilo jeraha lilizidi kachimba ndani kwa ndani na wakati wa kipupwe jeraha hutumbuka na kutoa damu na usaha kwa nguvu. Mimi nilisafiri kutoka mji wangu harkal kwenda hilla kupata ushauri wa mwanazuoni maarufu wa kishia mujtahid agha raziyyudin ali ibni tawiis.

Akanichukua kwa waganga wa hilla na kuwaonyesha jeraha lakini wote wakatoa ushauri mmoja kwamba hilo jeraha limechimba mpaka mishipa ya damu na kwa hivyo upasuaji wa jeraha hilo huweza kuhatarisha ukataji mishipa na kusababisha kifo popo hapo. kwa hivyo amenishauri nifuatane naye baghdad ambako tutaweza kuonana na waganga wa kikristo. Waganga wa kikristo baada ya kuangalia jeraha waliniambaia kwamba hakuna matibabu yake. Katika hali hiyo nikawaza kwamba huko kabla ya kurudi nyumbani nitazuru makaburi ya maimarn huko samarra. Mujtahid aliafikiana na wazo hilo na hata kunifanyia mpango wa fedha na mambo rnengine kuhusu safari hiyo. Nilipofika huko samarra (pahala walipozikwa maimam wawili):

1. Imam wa kumi, muhammad taqi aqs.

2. Imam wa kumi na moja, hassan askari(a.s) nikazuru makaburi mawili hayo na nikenda huko sardab sehemu iliyo chini ya ardhi. Huko nikasoma ziara, nikaomba mungu nikalia na kuomba msaada wa imam mahdi(a.s) .

Alhamisi asubuhi nikaenda nje ya jiji nikaoga mtoni, nikafua nguo zangu na nikarudi mjini. Nilipokaribia kuta za jiji nikawaona watu wanne juu ya farasi; wawili wao walikuwa vijana, na mmoja wa makamu na katika hao alikuwa mmoja mwenye haiba na uso mwangavu na upanga kiunoni. Mimi nilidhani hao ni wachungaji. Waliponiona wakasimama na kunisalimu na mimi nikajibu. Yule mtu mwenye haiba aliyekuwa katikati akasema: 'Ismail unataka kurudi nyumbani kwako kesho? Mimi nikajibu "ndio, ninahamu sana ya kurudi nyumbani." Mtu huyo akaniambia nimkaribie nami nikamkaribia na kufika karibu na farasi wake. Akauweka mkono wake mmoja begani kwangu na kuinama chini akalibinya jeraha langu kwa nguvu sana kwa mkono wa pili. Iliniletea maumivu mno. Baadaye akarudi kwenye farasi wake. mtu wa makamu aliyekuwa upande wa kulia akaniambia, "eh ismail umeponyeshwa" mimi nikajibu, "kwa rehema ya mungu sote tutapata uokovu. mimi nilishangazwa kuona kwamba ingawa jina langu lilikuwa likitajwa kila mara, lakini mimi nilikuwa simjui hata mmojawapo na nilikuwa mgeni kabisa katika hilo jiji. Baadaye huyo mtu wa makamu akanisimulia kwamba yule mtu aliye katikati ni mwenyewe imam Mahdi(a.s) .

Papo hapo nikamwangukia na kumbusu mguu wake. yeye akatangulia na mimi nikamfuata nyuma. Hapo hadhrat imam mahdi(a.s) akaniambia nirudi mjini lakini nikasema baada ya kuonana na imam(a.s) kamwe sitaachana naye. Hata hivyo, imam(a.s) akaniamrisha nirudi na kuongezea kwamba jambo hilo (la kurudi jijini) lilikuwa bora kwangu. Lakini mimi niliendelea kumfuata nyuma. mtu wa makamu akasema: "eh ismail huoni hata haya wakati imam anakwambia mara mbili mbili uende zako na wewe unaendelea kutotii amri yake?" mimi nikahuzunika sana na nikapigwa na bumbuwazi. Imam(a.s) akageuka na kuniambia: "utakapofika baghdad, khalifa abu jaffar mansur atakutumia mtu na atakapojua kuwa wewe umepona atakuzawadia dinari elfu moja. Usikubali zawadi hiyo, mwombe mwanangu seyyid ibni tawoos kwa kunitaja mimi amwandikie barua mfanyabiashara ali ibni awz akupe pesa kadri unavyohitaji na mimi vilevile nitamshauri huyo mfanyabiashara akupe pesa wewe."

Na hapo hao wapanda farasi wanne wakatoweka mimi nikabakia katika huzuni kuu na nikalia kwa nguvu sana. mwisho nikarudi samarra hali yangu ghairi na masikitiko. wahudumu wa makaburi ya maimam(a.s) waliponiona hali yangu walistaajabika na wakaniuliza kuhusu afya yangu. mimi nikawauliza hao wapand farasi wanne waliotoka nje ya jiji walikuwa nani? wao wakafikiri walikuwa wachunga wanaoishi karibu na jiji. nikawaeleza kwamba mmojawapo katika wale alikuwa hadhrat mahdi(a.s) . wao wakapigwa na butaa na wakasema wanashangazwa kwa nini mimi sikumwomba (imam mahdi a.s) aniponyeshe ugonjwa wangu. Hapo nikawaeleza tukio zima na nikaondoa nguo iliyofunika jeraha. (kabla ya hapo kwa majonzi ya kuachana na imam(a.s) mimi hata sikufikiria kuangalia jeraha). Wao wakasema kwa msisimko vilevile kwamba hakuna alama ya aina yoyote kuonyesha kulikuwa jeraha kwenye mapaja yote mawili. Papo hapo mimi nikazingirwa na watu wote ambao wakaanza kusoma salawat kwa ajili ya mtume mtukufu(s.a.w.w) . kwa furaha kuu wakaanza kuchana nguo yangu ili kila mtu atabaruku na kipande cha hicho kitambaa.

Niliogopa kwamba watanikanyaga na nitakufa. wahudumu wakaingiwa na hofu na wakanibeba na kunitoa katika kikundi cha watu na kuniweka mahala pa usalama. Baada ya muda mfupi hakimu kutoka jiji akaja kwangu na kuniuliza siku gani niliondoka baghdad na mimi nikamjibu niliondoka wiki moja iliyopita. Siku ya pili saa nane nikaondoka kuelekea baghdad. nikapitisha usiku huo kwenye makazi nje ya baghdad na asubuhi yake nikaingia mjini. Habari kuhusu tukio langu zilikwishafika baghdad na umati mkubwa wa watu ulikuwa baghdad ukinisubiri kunikaribisha. Nilipofika darajani watu hao wakaniuliza jina langu. Waliposikia jina langu wakanizingira. wakaanza kuchana chana vipande vipande nguo zangu. polisi wakaingilia kati na kuniokoa. Wakanichukua mjini nako vilevile nikazungukwa na watu. Mujtahidi Seyyid Ali ibni Tawoos alikuja kuniona na mimi nikamhadithia tukio zima.

Huyo mujtahid aliwahi kuona jeraha hiyo na akainua nguo yangu kuangalia jeraha mwenyewe. Alipoona kuwa jeraha limepona kikamilifu na hakuna alama yoyote kuonyesha kidonda alizimia hapo hapo. alipopata fahamu akalia kwa nguvu sana na akanichukua kwa waziri wa khalifa mustansir. Waziri huyo alikuwa mkaazi wa qum na shia. Akaangalia mapaja yangu yote mawili na alipothibitisha kwamba hakuna alama yoyote us jeraha akawaita waganga wale bingwa wa kikristo nilioonana nao ili wajitosheleze nafsi zao. Hao waganga walithibitisha kwamba waliokwisha ona jeraha hilo na kwamba tiba ya pekee ilikuwa kupasua jeraha hilo ambalo lingeweza kuhatarisha maisha yangu. Waziri tena akawauliza hao waganga ingelichukua siku ngapi hilo jeraha kukauka limngekuwa limepasuliw? wakajibu muda usioweza kupungua miezi miwili, lakini kovu na hilo shimo lingebakia pale pale.

Waziri tena akawauliza kwamba muda gani umepita tokea wao kuona jeraha hilo na wakajibu ni siku kumi tu. Hapo waziri akanyanyua nguo yangu kwenmye paja na waganga wakashangazwa kuwa hapakuwa hata alama au kovu pahala pa jeraha, ila ngozi nyororo. Mganga mmoja wa kikristo akasema kwamba hiyo ni kazi ya bwana yesu. Waziri akajibu kwamba wao walishindwa kutibu hilo jeraha ambalo limetibiwa bila kuacha kovu au alama na waziri alielewa vizuri huo mwujiza ulikuwa wa nani.

Waziri akamjulisha khalifa mustansir ambaye akaniitisha kwake na kuangalia paja langu ili kujitosheleza nafsi yake kwamba huo mwujiza ulikuwa wa hadhrat mahdi(a.s) . Akanipa sarafu elfu moja za dhahabu lakini nilikataa kuzipokea. akaniuliza sababu gani nimekataa kuzipokea. nikamjibu kwamba imam(a.s) aliyeniponyesha ugonjwa wangu alinikataza kupokea hizo sarafu. Kusikia hayo khalifa alihuzunika na kulia. Mimi nikaondoka sebuleni kwake. kufuatana na maagizo ya imam(a.s) mujtahid seyyid ali ibni tawoos akaniandikia barua kwa ali ibni awz ambaye akanipa fedha nilizohitaji.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU


YALIYOMO

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 1

MUANDISHI: MAREHEMU MULLA MUHAMMAD JAAFAR SHERIF DEWJI 1

DIBAJI 1

SHUKRANI 2

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE SURA 1 3

UTANGULIZI 3

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 9

SURA 2 9

AYA ZA QUR'ANI KUHUSU UIMAMU, KUGHIBU NA KUONEKANA TENA KWA IMAM WA WAKATI WETU HADHRAT MEHDI(A.S) 9

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 11

SURA 3 11

UTEUZI WA MAIMAMU, SIFA ZAO NA WAAJIBU WA VEEO VYAO 11

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 15

SURA 4 15

UIMAMU NA UKHALIFA 15

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 20

SURA 5 20

HADITHL KUHUSU KUWEPO KWA IMAM WA ZAMA HIZI 20

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 23

SURA 6 23

HADHRAT MAHDI (A.S.) NI IMAM WA KUMI NA MBILI 23

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 26

SURA 7 26

KUTAJWA KWA HADHRAT MAHDI (AS.) KATIKA GINAN ZA PEER (VIONGOZI) (NYIMBO ZA DINI ZA WATAKATIFU WA KIISMAILI) 26

SURA 8 26

KUZALIWA KWA HADHRAT MEHDI (A.S) 26

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 31

SURA 9 31

IDDUL-BARAAH (KISMATU RIZKI) 31

SWALA NA DUA ZILIZO PENDEKEZWA SANA 32

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 36

SURA 11 36

KUGHIBU KWA MUDA MFUPI (GHAIBATU-S-SUGHRA) NA MAWAKILI WA IMAM 36

SURA 12 37

KUGHIBU KWA MUDA MREFU (GHAIBAT-AL-KUBRA) SIRI YAKE NA MAJIBU YA UWAMBI DHIDI YAKE 37

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 43

SURA 13 43

MAISHA MAREFU YA HADHRAT MAHDI IMAM WETU WA ZAMA HIZI 43

SURA 14 46

KUGHIBU KWA MITUME 46

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 49

SURA 15 49

HADHARAT MAHDI (A.S) NA WSIO WAISLAM 49

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 53

SURA 16 53

HADITHI KUHUSU MUDA WA KUSUBIRI (INTIDHAR) NA MAJARIBIO YA MUDA HUO 53

SURA 17 54

ALAMA ZITAKAZO DHIHIRIKA KATIKA SIKU ZA MWISHO ZA DUNIA 54

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 59

SURA 18 59

BIBI, AZALI, BAHI KAMA VILE HUKO PUNJAB 59

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 64

SURA19 64

MAKAZI YA HADHRAT MEHDI (A.S) JAZIRATUL KHADHRAA NA MENGINEYO 64

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 70

SURA 20 70

HADITHI KUHUSU KUJITOKEZA KWA IMAM MAHDI(A.S) NA ALAMA MAALUM ZITAKAZO TANGULIA 70

SURA 21 71

KAFIRI DAJJAL CHONGO 71

SURA 22 73

HAKIKA KUHUSU KUJITOKEZA KWA IMAM WA KIPINDI HIKI 73

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 77

SURA 23 77

MAREJEO (RAJ'AAT) 77

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 82

SURA 24 82

WAJIBU WA WAUMINI NA DUA YA WAUMINI KATIKA KIPINDI CHA GHAIBA (KUGHIBU) KWA IMAM (A.S) 82

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE 88

SURA 25 88

JE INAWEZEKANA KUONANA NA IMAM MAHDI(A.S) KATIKA KIPINDI CHA KUGHIBU KWAKE KWA MUDA MREFU (GHAIBATULKUBRA)? 88

SURA 26 90

VISA SITA VYA WATU KUKUTANA NA IMAM MAHDI(A.S) 90

SHARTI YA KUCHAPA 100

MWISHO WA KITABU 100

YALIYOMO 101