MEZA YA UCHUNGUZI
KIMEANDIKWA NA: OMAR JUMAA MAYUNGA
KIMETOLEWA WAVUNI NA: TIMU YA AHLUL BAYT DIGITAL ISLAMIC LIBRARY PROJECT
"Enyi waumini, mkimcha Mwenyezi Mungu atakuongozeni njia ya haki na atawafutieni makosa yenu na atakusameheni ". 8:29.
Uchamungu ni moja ya pambo Ienye thamani kwa binadamu na nikipimo cha haki na batili na kila ambacho kinamfanya mwanadamu kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, kwani uchamungu ni vazi zuri Ienye thamani kila ataelivaa, hupata ukunjufu wa moyo na hima ya kutafuta haki hadi kufikia kikomo na kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, kando ya neema zake, zikitiririka bila ya hesabu. Katika ulimwengu huo ambao umejaa ibilisi wenye rangi tofauti, wakiwa na mitego tofauti ili kuwanasa wanadamu kwa vishawishi vipotovu na kuwatowa katika misingi ya haki na ya ukweli na yenye mwelekeo wa tawhid. Wale ambao waliofahamu hila za ibilisi na wakakana kudhalilishwa kwa kufuata vishawishi vyake, kwa hakika hawa ni katika waongofu.
Jambo lakusikitisha, kwamba kwa upande mwingine makafiri wanahila zao, nara zao zaweza kuwa ni uchamungu na wakafanya vitendo viovu wakiona ni vyakumridhisha Mwenyezi Mungu, hali ya kughafilika kwamba huo ni upotovu na ni chanzo cha kuangamia, lakini Mwenyezi Mungu amewaahidi wale wamchae kuwaonyesha njia ya haki. Kitengo cha Utamaduni Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, unayo furaha ya kuchapisha kitabu, kwa jina: (MEZA YA UCHUNGUZI) kimeandikwa na mtafiti wa haki, si mwingine nae ni Sheikh Omar Juma Mayunga, mwandishi wa kitabu hiki amepata misuko suko mingi mpaka kufikia upeo wa haki, yeye ni mfano wa kuigwa kwani wengi bado wanayumba yumba katika kutafuta ukweli. Kwani haki ni lulu yenye thamani hupatikana kwa juhudi, ongeza uchamungu. Kwani uchamungu ni taa yenye kung'arisha njia ya haki, na wale ambao si wachamungu wakiitafuta haki hawaiyoni.
Sheikh Omar Jumaa Mayunga katika kitabu chake ametowa dalili za Qur'an na Sunna za Mtume(s.a.w.w) , ongeza tajruba zake katika kuitafuta haki na Uislam wa kweli ulioletwa na Mtume Muhammad(s . a . w .w ) akisaidiwa na nuru ya uchamungu ameweza kufikia chemchem ya chimbuko la haki. Tukiacha kupendelea katika itikadi na matamanio ya nafsi na wasi wasi wa ibilisi, tukiangalia kwa jicho la haki kitabu hiki kinaweza kuwa muamuzi na sababu ya kupata kheri za dunia na akhera. Kitengo cha Utamaduni kinasisitiza kuwa yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki ni yake Muandishi, Kitengo cha Utamaduni kimesaidia kuchapa copy 10,000 tunawaombea Mungu wote wanaotafuta haki na Uislamu wa kweli. Mustaffa Najarian Zadeh Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Dar es Salaam – Tanzania.
Sheikh Umar Juma Mayunga alikwenda Kenya ambako baada ya mazungumzo ya kidini, alishauriwa na Sheikh Abdallah Nasser (wa Nairobi) na Haji Ali Muhammad Jaffer (wa Mombasa) kuwa atakaporudi Dar es Salaam aonane nami kwa maelezo zaidi. Alikuja kuonana nami, na swali lake la kwanza lilikuwa juu ya Taqiyah. Nilimpa jibu lililomtosheleza kutoka kwenye Qur'ani Tukufu na Ahadithi. Baada ya hapo alikuwa akinitembelea mara kwa mara na mambo yote aliyokuwa akiyaelewa vibaya (kutokana na propaganda za kiovu za Wahabiyyah) aliyaelewa vipasikavyo. Baada ya hapo aliyachambua matukio ya mwenye wakati wa mwisho wa maisha ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w) na mara tu baada vitabu muhimu vya historia ya Kiislam kama vile Taarikh at-Tabari, Taarikh al-Kamil na Sirah Ibn Hisham; Sura zihusikanazo na historia za vitabu vya Ahadith kama vile Sahih Bukhari, Sahih Muslim, Kanzul Ummal, n.k. Baada ya kujifunza matukio hayo, alijifunza vitabu vya Kishia; na akavutiwa na ukweli wauzungumzao Shia.
Tangu hapo, amekuwa akizitembelea sehemu nyingi za Tanzania na Kenya. Huko Mombasa alitoa hotuba juu ya Ndoa ya Mut'a na baada ya hapo aliandika juu ya mada hiyo na kikachapishwa. Hivi hapa, ili kuusherekea mwaka wa 1400 wa Tukio la GhadiirKhum, amekiandika kitabu ulichokishika. Nimekicheki kitabu hiki na ninathibitisha kwamba rejea zilizotajwa kitabuni humu na tafsiri zao ni sahihi. Ninamwomba Allah Subhanahu wa Taala Akijaalie kitabu hiki kuwa njia ya hidaya kwa ajili ya watu na Amjaalie mwandishi wake Tawfiiq zaidi kuihudumia dini ya Mwenyezi Mungu kama inavyofundishwa mwenye Qur'an na Ahlul Bayt(a.s) .
Iwapo msomaji ye yote yule atataka kujua zaidi juu ya jambo lo lote lile lililotajwa kitabuni humu, anakaribishwa kumwandikia mwandishi huyu ambaye anwani yake imo kitabuni humu. Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Mhubiri Mkuu Dar es Salaam Bilal Muslim Mission of Tanzania.
Jina langu ni OMAR JUMAA MAYUNGA. Nimezaliwa mwaka 1947 Mkoa wa Tabora katika Wilaya ya Igunga Tarafa ya Simbo. Mwaka 1957 baba yangu alianza kunisomesha Quran Tukufu, ilipofika mwaka 1959 nilianza masomo ya Kizungu katika Shule ya Msingi ya Simbo hadi mwaka 1962 nilipokaa nyumbani kuendelea na masomo ya Qur'an. Mwaka 1968 baba yangu alinipeleka mjini Tabora kusoma kwa Sheikh Mzee Fereji Farahani (Mwenyezi Mungu amrehemu) mpaka mwaka 1972 nilipokwenda Mombasa kujiunga na Madrasa ya Tahdhib Muslim School ambayo iliongozwa na Almarhum Al'ustadh Alwy Qasim. Kwa kipindi nilichosoma katika Madrasa hii, siwezi kusahau ukarimu niliopata nikiwa ugenini.
Kwanza kabisa Sheikh Muhamad Amran Bushir, ambaye yeye ndiye aliyenipokea kwa mara ya kwanza nyumbani kwake. Akanikirimu kwa ukarimu mkubwa, akanifanyia mambo yote na watoto wake.
Pili; Ustadh AIwy Qasimu aliyenipenda sana, akanisomesha kwa juhudi kubwa. Ustadh Alwy alinipatia vitabu vingi mbali mbali na akanisomesha kwa undani zaidi vitabu vya ibn Taymiyya, Ibn Qayyim Aljawziyya, na vya Muhammad Abdulwahabi.
Tatu; Maulamaa Sheikh Abdallah Saleh Alfarsy na Sheikh Muhammad Kasim Mazrui, ambao walikuwa machifu Kadhi wa Kenya. Kila mmoja alinisaidia sana kunipa maarifa na mwongozo mwema. Nilibaki katika Madrasa hii mpaka alipofariki Ustadh kwa ajali ya gari. Mwaka 1975 nilikwenda kusoma Ujiji - Kigoma, kwa Sheikh Khalfani Muhammad Kiumbe hadi 1976. Nikiwa Ujiji, Almarhum Mzee Husein Taufik Msanga alinihudumia kwakunipa kila masaada kwa muda wote nilioutumia katika masomo.
Mwaka 1976 nilikwenda kusoma Iringa kwa Sheikh Harith Khelef Khamis. Sheikh Harith kwa mapenzi yake makubwa juu yangu alinisomesha masomo mengi yenye maana sana. Nikiwa Iringa. Al'marhum Mzee Hasan Souf Imam wa Msikiti Mkuu wa Iringa, alinipokea akanipa chumba. Nilipata miada mingi mbalimbali kwa; Mzee Ali Fundi, Mzee Muhammad Bunnu, Mzee Muhammad Mbarak. Mpenzi wa roho yangu niliyeshikamana naye wakati mwingi, Al-haji Saburi Goha Momba ambave hatimaye alinioza binti yake.
Mwaka 1978 niliajiriwa katika Chuo cha Kiislamu- Chang'ombe, Dar es Salaam.
Mwaka 1980 Sheikh Abdallah Idd Chaurembo (Mwenyezi Mungu amrehemu) alinitaka niasisi "Madrasatu Ahli Sunnatu Waljamah" katika Msikiti wa Mtoro. Nilisomesha miezi mitatu nikaandika barua ya kujiuzulu ya tarehe 2J.5.1980 kwa nia ya kuasisi Madrasa yangu binafsi. Mwaka 1982 niliandika kitabu: "Jawabu la wazi kwa wateteao bid'a" kilichochapishwa Dar es Salaam tarehe 27.1J.1982.
Kitabu hiki kilitetea msimamo wa Kiwahabi, na kabla ya hapo niliandika Makala mbali mbali kwa mujibu wa matukio yaliyotokea kati yangu na baadhi ya Masheikh. Aidha mwaka 1982 nilikwenda mara nyingi Bujumbura, huko nilitoa mihadhara mingi mikubwa katika Msikiti wa Bwiza. Mihadhara hiyo niliielekeza Bujumbura tokea mwaka 1982 hadi 1985. Kisha nilielekeza mihadhara hiyo mjini Lusaka - Zambia. Mwaka 1985 vile vile nilikwenda Saudi Arabia katika Ofisi ya Muslim World League mara tatu, kwa lengo la kupanua mawasiliano baina ya Madrasa yangu na taasisi mbali mbali za Kimataifa.
Mwaka 1986 nilikwenda Mombasa - Kenya huko nilikutana na Sheikh Abdillah Nasir: Nilipata nafasi ya kuzungumza naye mambo mengi kuhusu msimamo wa dini. Jambo lililojitokeza zaidi katika mazungumzo yetu ni Usunni na Ushia, na ilipohitajika kupata vitabu vya Kishia ndipo aliponikutanisha na Sheikh Ali Muhammad Jaafar, Kiongozi wa Bilal Muslim Mission ya Kenya. Naye alinipatia vitabu "Aslus Shia wausuluha, Al-murajaatu, Fadhailu Lkhamsa." Niliporudi Dar es Salaam nilivisoma kwa makini na kufuatilia vitabu vya Kisunni vilivyoonyeshwa humo. Na nilikuwa karibu sana na Mwanachuo wa Kishia hapa Dar es Salaam Maulana Sayyid Saeed Akthar Rizvi. Nilikuwa na nukta kadhaa zilizonikera dhidi ya Shia, kwa hivyo nilimuomba Maulana Rizvi anipatie wakati wa kutosha ili tuzijadili hizo nukta. Mbali na shughuli zake nyingi alizokuwa nazo, Maulana alinipatia siku mbili kwa wiki. Baadhi ya nukta tulizozichambua ni:- Tahriful Qur'an, Imamah, Taqiyya, na Mut'a. Sayyid Saeed Akthar Rizvi mbali na kunijibu nukta hizi, lakini pia amenifundisha na kunionyesha mengi sana yaliyomo katika vitabu vya Kisunni. Kisha alinipa kitabu "AIghadir" akaninyesha yaliyomo humo, na Kisha tulifuatilia baadhi ya nukta zilizotajwa katika "Alghadir" kwa vitabu vya Kisunni. Kwa utafiti huu wa pamoja katika vitabu vya kutegemeka vya Kisunni, ambavyo ndivyo vimenifanya kuwa Shia lthnaasheri. Baadhi ya vitabu hivyo ni:- Sahihi Bukhari, Sahihi Muslim, Tarikhut Tabari, Tarikh Ibn Athir, Mizanul Itidal na Tafsir nyingi za Quran, nimeamua kuwa: "Mimi ni Shia Ithna-asheria, nitafuata sheria na kanuni zake katika uhai wangu na baadaye Insha-Allah". Tarehe J.9.1986 nilialikwa na Bilal Muslim Mission ya Kenya, katika Majlis ya kukumbuka mauaji ya Imam Husein(a.s.) .
Tarehe 8.9.1986 mimi nilisoma Majlis katika ukumbi wa Huseiniyya Mombasa. Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kupanda katika Mimbari na kusoma habari za watukufu wa nyumba ya Mtume(s.a.w.w) . Tarehe 20.1J.1987 nilialikwa kuhudhuria Mkutano mjini Tehran-Iran, mkutano ambao ulizungumzia mauaji ya kinyama walio fanyiwa ndugu zetu Mahujaji na askari wa Kisaudia katika Haram ya Makka. Katika Mkutano huo mimi nilipata nafasi ya kuhutubia kwa kulaani kitendo cha kinyama cha mauaji ambayo askari wa Kisaudi waliwauwa Mahujaji wasio na hatia. Mwaka 1987 nilifasiri Dua Kumayl kilichochapishwa Mombasa - Kenya Mwaka 1989, Tarehe 24.10.1989 niliandika kitabu:- "Mut'a ndoa sahihi" kilichochapishwa Dar es Salaam tarehe 8.3.1990. Tarehe 8.7.1990 nilialikwa kuhudhuria sherehe ya Imam Ali(a.s) mjini London. Sherehe ambayo mwaka 1410 Hijiria ilikuwa inatimia karne kumi na nne tokea Imam Ali(a.s) atangazwe na mtume(s.a.w.w) hadharani katika bonde la Khum. Nilibahatika kuchaguliwa na kamati ya maandalizi ya Mkutano huu kuwa mmoja wa watakaohutubia katika hafla hii. Tarehe 13.7.1990 katika majira ya jioni, nilihutubia katika ukumbi wa Hotel ya Ramada mjini London. Katika hafla hii kuna zawadi maalum ilitengwa kwa ajili ya wale watakaofanya vizuri. Mimi nilibahatika kutunikiwa saa yaa mkono yenye nembo ya ujumbe maalum wa lile agizo la Mtume(s.a.w.w) juu ya Imam Ali (a.s) siku ya Ghadir Khum, kuwa yeye Imam Ali(a.s) ni Kiongozi wa Waumini baada yake aliposema: "Ambaye mimi ni kiongozi wake, basi huyu Ali ni kiongozi wake".
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwafikisha mara nyingine kukamilisha kuandika kitabu hiki, baada ya kitabu chetu:- "Mut'a ndoa sahihi." Mambo yanayoweza kuamsha misimamo ya watu na kuleta msukumo mpya katika kumwandaa binadamu ili apige hatua mbele, ni kujua habari za watukufu wao waliotangulia. Kwa sababu kujua habari za watangulizi wetu ni mizani ya kutupimia sisi tunaokuja baada yao. Katika kitabu hiki, nimetaja mambo ambayo ingawa yanajulikna na wengi, lakini ni mageni katika kusema. Wanaoyajua kuwa ni kweli si kidogo, lakini wengi wanaogopa kuyasema au wametiliwa itikadi potovu kuwa hayafai kusema. Bila shaka yakionekana katika kitabu hiki itakuwa dhambi kubwa kwao. Sisi nasi tunaamini kuwa Haki ni lazima isemwe, sawa sawa itawaridhi watu au haitawaridhi.
"Na lau haki ingefuata mapenzi yao basi mbingu na nchi zingeharibika ." 23:71.
Ninawashukuru wote waliokipitia Kitabu hiki kukisahihisha, na wakanipa maoni yao yenye thamani kubwa. Mwenyezi Mungu awalipe malipo mema duniani na akhera.
Msimamo wa Aya zilizokuja juu ya uongozi
ukisoma yalioandikwa katika vitabu mbali mbali na Hadithi zilizothibiti, na tarikh inayoonyesha katika jambo hili, utapata mambo makuu matatu ambayo yanaonyesha kuwa: Uimam (Ukhalifa) lazima uteuliwe na Mwenyezi Mungu. Na kwa upande wa pili utaona kuwa Nyimati zilizopita zilifuata uongozi uliochaguliwa na Mwenyezi Mungu, wala jambo hilo halikuachiwa watu wenyewe kwa njia ya kuchaguwana. Jambo la kwanza lililoongoza baina ya Mtume waliopita ilikuwa ni kusalimu amri na kufuata uongozi wa Mwenyezi Mungu, na kila alipoondoka Mtume aliweka atakaeshika nafasi yake. Wengi wao waliorithi kazi zoa walikuwa Manabii, hata hivyo baadhi yao hawakuwa Manabii bali walikuwa Mawasii tu. Jambo la pili: Uongozi katika nyimati zilizopita ulipatikana kwa njia ya kurithi baina ya vizazi katika koo za Mitume kama tunavyosoma katika Aya zifuatazo:
A. "Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na Kizazi cha Ibrahim na Kizazi cha Imrani juu ya walimwengu wote. Ni kizazi cha wao kwa wao, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua " (Qur’an: 3:33-34)
B. "Na tulimpa Isihaqa na Yaaquubu na tukaweka katika Kizazi chake Unabii na Kitabu , na tukampa ujira wake katika dunia. Nae katika akhera kwa hakika atakuwa miongoni mwa watu wema ." 29:27
C. "Na hakika tulimpeleka Nuhu na Ibrahim na tukauweka katika kizazi chao Unabii na kitabu ." 57:26
D.Mwenyezi Mungu alimweka Ibrahim kuwa Imam (Kiongozi wa watu). Ibrahim alimuomba Mola wake awape nafasi hiyo vile vile katika kizazi chake. Mwenyezi Mungu hakumkemea wala kumgombeza, ila alimwambia ya kuwa: "Haiwafakii ahadi yangu (Unabii and Uimam) watu madhalimu ." 2:124.
Nabii Musa(a.s) alipoomba kwa Mwenyezi Mungu ndugu yake Haruna awe msaidizi wake katika uongozi, Mwenyezi Mungu hakumkasirikia wala kumkatalia ombi hilo.
وَاجْعَل لِّي وَزِيرًا مِّنْ أَهْلِي ﴿٢٩﴾ هَارُونَ أَخِي ﴿٣٠﴾ اشْدُدْ بِهِ أَزْرِي ﴿٣١﴾ وَأَشْرِكْهُ فِي أَمْرِي ﴿٣٢﴾ كَيْ نُسَبِّحَكَ كَثِيرًا ﴿٣٣﴾ وَنَذْكُرَكَ كَثِيرًا ﴿٣٤﴾ إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرًا ﴿٣٥﴾ قَالَ قَدْ أُوتِيتَ سُؤْلَكَ يَا مُوسَىٰ ﴿٣٦
"Na unijaalie waziri katika jamaa zangu, Haruna ndugu yangu. Uniimarishe kwake nguvu zangu, na umshirikishe katika kazi yangu. Ili tukutukuze sana, na tukutaje kwa wingi. Hakika wewe unatuona, akasema hakika umepewa maombi yako ewe Musa" 20:29-36.
Musa alimweka Haruna kuwa Khalifa wake alipoondoka, kama Quran inavyosema:
وَوَاعَدْنَا مُوسَىٰ ثَلَاثِينَ لَيْلَةً وَأَتْمَمْنَاهَا بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِيقَاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٤٢﴾
"Na tulimwahidi Musa siku thelathini na tukatimiza kwa kumi ikatimia miadi ya Mola wake siku arobaini. Na Musa akamwambia ndugu yake Haruna: Shika mahala pangu katika watu wangu na usuluhishe wala usifuate njia ya waharibifu." 7:142.
Katika Aya hizi tumeona nafasi ya Uongozi unavyoendelea kati ya Kizazi na Kizazi baina ya koo za Manabii.
Mtiririko huu ikiwa umejengeka kwa Wahyi katika nyimati zilizopita katika suala la Khilafa, basi kubadili utaratibu huo katika Islam lazima ipatikane dalili na ufafanuzi. Jambo la tatu: Kumbukumbu za tarikh ya Mitume inaonyesha waziwazi kuwa: Kila alipoondoka Mtume aliweka mtu wa kushika mahala pake, na hapa tutaonyesha kwa ufupi: Wakati iliposhuka Aya 214 katika Sura ya Ash'Shuaraa, Mtukufu Mtume(s.a.w.w) alisema:
"Enyi Bani Abdil Muttalib! Hakika mimi wallahi simjui kijana yeyote katika Waarabu, aliyewaletea watu jambo bora kabisa kuliko nililokuleteeni mimi. Hakika mimi nimekuleteeni kheri ya dunia na ya akhera, Mwenyezi Mungu ameniamrisha nikuiteni kwake, basi nani kati yenu atakaenisaidia jambo hili ili awe ndugu yangu na wasii wangu na Khalifa wangu kwenu? Watu wote wakanyamaza, nikasema (Ali) na mimi ni mdogo wao kwa umri mng'avu wao wa macho, mkubwa wao wa tumbo, mnene wa miundi, mimi ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu nitakuwa waziri wako. Pale pale akanishika shingo yangu, kisha akasema: Hakika huyu ni ndugu yangu, na wasii wangu, na Khalifa wangu kwenu, basi msikilizeni na mtiini ".
Akili, na maandiko, pamoja na matukio ya tarikh, vyote vinaonyesha kwa pamoja kuwa: Msingi wa asili katika hukumu ni maamuzi ya Mwenyezi Mungu tu peke yake, na yeye ndiye anayemtawalisha amtakae katika waja wake. Tukio la Ghadir Khum ni tangazo muhimu Ia uongozi mkuu, lililokamilisha dini na neema na radhi ya Mola. Tarehe kumi na nane mfungo tatu Mtukufu Mtume(s.a.w.w) alipokuwa akirejea Madina kutoka Makka katika mwaka wa kumi baada ya kumaliza ibada ya Hija alifika mahali katika bonde la Khum akiwa na Waislam zaidi ya laki moja. Mwenyezi Mungu akateremsha Aya: "Ewe Mjumbe fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako, na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu, hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu wanaokufuru " 5:67.
Baada ya kushuka Aya hii, Mtume(s.a.w.w) alimshika mkono Imam Ali(a.s) akasema: "Ambaye mimi natawalia mambo yake, basi huyu Ali ni mtawala wake. Ee Mola! Muunge atakae muunga, na mfanyie uadui atakae mfanyia uadui ". Ilipokamilika hutuba ya Mtume(s.a.w.w) Masahaba walianza kutoa kiapo cha utiifu kwa Imam Ali (a.s) kama tunavyomnukuu hapa Umar bin Khattab:
"Hongera ewe mwana wa Abu Twalib sasa umekuwa kiongozi wangu na kiongozi wa Waislamu wote ".
Taz; Tarikhu Dhahbi J.2 Uk. 197 Tariku Baghdad J.8 Uk. 290 Tarikhu Ibn Asakir J.2 Uk. 45 Al Isaba J.1 Uk. 305 Tafsirul Kabir J.12 Uk. 49 Addurrul Manthur J.5 Uk. 182 Ansabul Ashraf J.2 Uk. 315 Albidayatu Wannihaya J.7 Uk. 359.
Hata hivyo, wako baadhi ya Masahaba waliopinga kitendo hiki cha kutoa kiapo cha utiifu kwa Imam Ali(a.s) Baada ya Masahaba kutoa kiapo cha utiifu kwa Imam Ali(a.s) Harithi bin Nuuman Al'fahri, alimkabili Mtume(s.a.w.w) akamwambia: Ewe Muhammad! umetuamrisha kushuhudia kuwa hapana apasae kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu na wewe ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekubali. Umetuamrisha kusali mara tano kila siku, tumekubali. Umetuamrisha kutoazaka katika mali yetu, tumekubali. Umetuamrisha kufunga mwezi wa Ramadhani kila mwaka, tumekubali. Umetuamrisha Kuhiji AI'kaaba, tumekubali. Kisha hukutosheka yote haya mpaka umempandisha mtoto wa ammi yako juu ya shingo zetu! Hili ni wazo lako au ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu?" Mtume(s.a.w.w) akajibu: "Wallahi, hapana apasae kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu, hili si langu isipokuwa ni Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ". Harithi akaondoka zake na huku akisema: "Ee Mola! ikiwa haya anayosema Muhammad ni kweli, basi tuteremshie mvua ya mawe au tuletee adhabu nyingine kali". Naam, pale pale alipokuwa, Mwenyezi Mungu akamdondoshea kijiwe kikagonga utosini kikatokezea kwenye tundu ya nyuma akafa papo hapo. Mwenyezi Mungu akateremsha Aya ya kwanza na ya pili katika Suratul Ma'ariji: "Muombaji aliomba juu ya adhabu itakayotokea, kwa makafiri hapana awezae kuzuia"
Taz: Tafsirul Qurtubi J.18 Uk. 278.
Tukio la Ghadir Khum ni ujumbe muhimu sana kwa Waislamu, na kila anayeshuhudia: "LAA ILAHA ILLA LLAHU MUHAMMADUN RASULULLAH" Lazima vile vile atoe kiapo cha utiifu kwa uongozi wa Ahlul Bait(a.s) . Kwa sababu tarikh inaonyesha kuwa Masahaba waliokataa kutoa kiapo chao kwa Imam Ali, Mwenyezi Mungu aliwaadhibu. Katika hao walioadhibiwa ni huyu Harithi bin Nuumani Al'fahri, kama ulivyoona kisa chake hapo juu. Pia tarikh inaonyesha kuwa Sahaba Zaid bin Ar'qam alipotengua kiapo chake cha utiifu kwa Ahlul Bait, alipofuka macho yake mara moja. Taz: Manaqibul Imam Ali Uk. 23.
Kabla hatujaingia ndani kuzungumzia suala la Mubahala, kwanza ni vizuri tufahamishe maana ya Mubahala. Muhabala ni: Kuapizana. Ujumbe wa Kikristo kutoka Najran ulifika kwa Mtume kujadili suala la Nabii Isa(a.s) . Mtume aliwajulisha kuwa:
إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّـهِ كَمَثَلِ آدَمَ خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٥٩﴾
Hakika mfano wa Isa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, aliumbwa kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa naye akawa. (Qur’an 3:59).
Kwakuwa Nabii Isa alizaliwa bila baba, Wakristo wamedhani kuwa baba yake ni Mwenyezi Mungu. Aya hii inaondoa dhana hiyo ambayo inapingana na utukufu wa Mwenyezi Mungu, na inawapigia mfano wa ajabu zaidi katika kuumbwa Adam bila ya baba wala mama. Aliumbwa kwa udongo kisha akaambiwa: kuwa naye akawa, na kwa neno hilo hilo Nabii Isa(a.s) ndivyo alivyoumbwa. Ujumbe huo ulipokuwa haukukubaliana na hoja hii, Mwenyezi Mungu akateremsha Aya:
فَمَنْ حَاجَّكَ فِيهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ فَقُلْ تَعَالَوْا نَدْعُ أَبْنَاءَنَا وَأَبْنَاءَكُمْ وَنِسَاءَنَا وَنِسَاءَكُمْ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَتَ اللَّـهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ ﴿٦١﴾
"Na atakayehojiana nawe (Muhammad) katika hili baada ya ujuzi uliokufikia, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafis zenu, kisha tuombe kwa kunyenyekea tuijaalie laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo." (Qur’an 3:61).
Hili ilikuwa tarehe ishirini na nne mfungo tatu mwaka wa kumi, Mtume akawaita ili waanze kuapizana. Wakajibu: "Ngojea tujadiliane". Walipokwenda faragha, wakamuuliza Askofu Abdul Masih; ana Maoni gani katika suala hili? Akajibu: Enyi Wakristo: Wallahi nyinyi mnajua kuwa Muhammad ni Nabii aliyeletwa na amekuja na ushahidi ulio wazi juu ya jambo la huyu (isaa.s. ). Wallahi hakuna watu walioapizana na Nabii wakasalimika, ikiwa mtaapizana naye mtaangamia". Usqufu yeye aliwaambia: "Enyi Wakristo: Mimi naziona nyuso hizi (kundi la Mtume) kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, Wallahi atauondoa. Msiapizane naye mtaangamia, na hatabaki Mkristo ye yote hapa duniani mpaka siku ya Kiama ".
Alipoulizwa Ahtam, akawaambia: Niacheni nikamuulize Muhammad, alipomkabili Mtume akamuuliza, "Ewe Abulqasim'! Unatoka na kina nani kwa ajili ya maapizano haya?" Mtume(s.a.w.w) akamjibu: "Ninaapizana nanyi nikiwa na watu bora hapa duniani na watukufu mno mbele ya Mwenyezi Mungu, nao ni hawa (akawaonyesha) Ali, Fatima, Hasan na Husein." Wakaogopa kuapizana na Mtume, na badala yake wakaomba sulhu kwa Mtume(s.a.w.w) kwa kutoa dirham arobaini elfu.
Taz: Tarikh Ibn Athir J.2 Uk. 200. Tafsirul Qurtubi J.4 Uk. 104. Tafsirul Ibn Kathir J.1 Uk. 376-379. Tafsirul Khazin J.1 Uk. 359-360. Tafsirul Maragh J.3 Uk. 175. Tafsirul Kabir J.8 Uk. 81. Zadul Masir J.1 UK. 399.
Katika Ayatul Mubahala, iliposema: "Tuwaite watoto wetu " Mtume(s.a.w.w) alimwita:Hasan na Husein . Iliposema: " Na wanawake wetu " Mtume(s.a.w.w) alimwita: "Fatima bint Muhammad ". Iliposema: " Na nafsi zetu " mtume akamwita: "Ali ". Kwa hivyo Ali bin Abi Talib ni nafsi ya Mtume Muhamad(s.a.w.w) . Tukio hili Ia Mubahala tukilitazama kwa upande wa pili, linatukumbusha lile tukio la "Kisaa " Iliposhuka Ayatut Tat'hir:
إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴿٣٣﴾
Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni sana sana" (Qur’an 33:33).
Iliposhuka Aya hii Mtume alimchukua Ali na Fatima na Hasan na Husein, akawafunika nguo kisha akasema: "Ee Mola! Hawa ni watu wa nyumba yangu, basi waondolee uchafu na uwatakase sana sana ". Mama Ummu Salma (mke wa Mtume) alipotaka kuingia humo, Mtume(s.a.w.w) akamzuia: Kama ambavyo kwenye tukio la Mubahala ulipofika wakati wa kuomba maombi maalum kwa ajili ya maapizano kati yake na Wakristo wa Najrani, Mtume alimchukua Ali na Fatima na Hasan na Husein tu. Ingawa wakati huo Mtume(s.a.w.w) alikuwa nao wakeze, na Masahaba ambao ni marafiki zake pia, lakini hapa hawakuingia. Wake za Mtume na Masahaba hawakuingia katika "KISAA" na hawakusimama katika uwanja wa Mubahala, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwahusisha darja hii Ahlul Bait tu peke yao. Taz: Tafsirul Khazin J.3 Uk. 259 Tafsirul Ibn Kathir J.3 Uk. 494 Tafsirul Qurtubi J.14 Uk. 183 Zadul Masir J.6 Uk. 381.
1
MEZA YA UCHUNGUZI
QURAN NA AHLUL BAIT
Imepokewa kutoka kwa Sahaba Zaid bin Arqam: Amesema Mtume(s.a.w.w) : "Mimi ninakuachieni vizito viwili ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu, Quran na AhIul Bait wangu, viwili hivi havitaachana mpaka vitakaponifikia katika Haudh. "
Taz: Tafsir Ibn Kathir J.4 Uk. 122 Tafsirul Khazin J.1 Uk. 4 Tarikh Bughdad J.8 Uk. 442 Sahihi Muslim J.4 Uk. 1873 Sahihi Tirmidh J.2 Uk. 308 Jamiul Usul J.1 Uk. 187 AIbidayatu Wannihaya J.7 Uk. 362 Majmauz Zawaid J.9 Uk. 163.
Hadithi hii inathibitisha kuwa baada ya kuondoka Mtume watakaoshika mahala pake ni Ahlul Bait(a.s) ambao tumekwisha waona katika tukio Ia "KISAA" na katika tukio la "Mubahala" Mwenyezi Mungu ameamrisha kufuata uongozi wao aliposema: "Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msitengane".(Qur’an 3:103).
Tamko la kamba hapa ni Ahlul Bait" na hapa tutaonyesha maneno ya Imam Shaafy "Na nilipowaona watu Madhehebu yao yamewapeleka katika bahari yao ya upotovu na ujinga, nikapanda kwa jina Ia Mwenyezi Mungu katika meli yenye kuokoa, nao ni watu wa nyumba ya Mtume mwisho wa Mitume. Na nikaishika kamba ya Mwenyezi Mungu nayo ni kuwatawalisha (Ahlul Bait) kama tulivyoamuriwa kushikamana na kamba, watakapo farakana katika dini makundi sabini na kidogo kama ilivyokuja katika Hadithi. Na asipatikane wa kuokoka miongoni mwao isipokuwa kundi moja, niambieni ni kundi gani hilo enyi wenye akili na maarifa je! Katika makundi yatakayoangamia mojawaponi ni lile kundi la watu wa Muhammad? Au wao ni katika kundi litakalo salimika, niambieni. Ikiwa utasema kundi la Muhammad ni katika kundi litakalookoka, basi huo ni msimamo wa kweli, na ukisema kundi hilo ni katika makundi yatayoangamia bila shaka umepotosha uadilifu, basi niachie Ali awe kiongozi wangu na kizazi chake, na wewe bakia katika mapambo ya ulimwengu." Imam Shaafy hapa anatukumbusha tamko muhimu Ia Mtukufu Mtume(s.a.w.w) aliposema: "Mfano wa Ahlul Bait wangu ni kama mfano wa Meli ya Nuhu, atakaepanda humo ataokoka, na atakaebaki nje atazama ".
Taz: Manaqib Ali Uk. 132 Mustadrakus Sahihain J.2 Uk. 343 Majmauz Zawaid J.9 Uk. 168 Kanzul Ummal J.6 Uk. 216 Hilyatul Awliyaa J.4 Uk. 306.
Mwenyezi Mungu anasema: "Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na Ulul'amri katika nyinyi ." 4:59.
Katika Aya hii kuna mambo matatu muhimu:
(a) Kumtii Mwenyezi Mungu
(b) Kumtii Mtume
(c) Kuwatii Ulul'amri.
Kumtii Mwenyezi Mungu, maana yake ni kushika amri zake na kuacha makatazo yake. Kama ambavyo; kumtii Mtume(s.a.w.w) maana yake ni kufuata uongozi wake. Katika Aya hii mwenyezi Mungu anaamrisha wa atiiwe Ulul'amri na yeyote ambaye Mwenyezi Mungu anaamrisha atiiwe lazima awe maasum (Mwenye kuhifadhiwa na makosa). Basi, lazima Ulul'amri waliotajwa katika Aya hii wawe Maasum. Naam; kidogo tujikumbushe lile tukio Ia "KISAA" Mwenyezi Mungu aliposema:
"Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni sana sana." (Qur’an 33:33).
Hapa tutaangalia Nukta mbili katika Aya hii:
(a) Ar'rijsu = Uchafu, matendo mabaya, Haramu Laana, Kufru, Adhabu. Taz: Al-Muujamal wasit (kamusi) Kwa mantik hii utaona kuwa: Ahlul Bait, Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na matendo mabaya. Amewaepusha haramu, hawana Iaana, wanarehema, amewaondolea kufru na adhabu.
(b) At'tuhru: Kutokuwa na uchafu wa aina yoyote.
Taz: Al-muujamal wasit (Kamusi) Kwa hiyo; Ahlul Bait(a.s) hawana uchafu wa aina yo yote. Natija inaonyesha kuwa: Ahlul Bait ni Watakatifu na ni Maasum.
Katika mwaka wa kumi Hijjra, Mtukufu Mtume(s.a.w.w) alipeleka jeshi kwenda kupigana Roma. Katika jeshi hilo Mtume aliamuru liongozwe na Usama bin Zaid akasema: "Nenda ukapigane alikouliwa baba yako".
Uteuzi huu Masahaba haukuwapendeza, kwa hiyo walisikika wakipinga amri hiyo wakisema: "Itakuwaje mtoto mdogo huyu apewe madaraka makubwa juu yetu? Ilipomfikia habari hii Mtume(s.a.w.w) aliwaambia: "Nimesikia lawama zenu nilivyomtawalisha Usama katika jeshi hili, sioni ajabu, maana mlikwisha nilaumu zamani nilipomtawalisha baba yake kabla yake. Wallahi baba yake alikuwa ni mtu aliyefaa kushika uongozi wa jeshi hilo, kama ambavyo mtoto huyu anastahiki kabisa uongozi wa jeshi hili". Mtume(s.a.w.w) akasisitiza watu wote isipokuwa Ali, waende na jeshi Ia Usama akisema: "Andaeni jeshi la Usama, Mwenyezi Mungu amlaani atakaebaki asiende na jeshi hilo ".
Taz: AI-miIalu Wannihal J.1 Uk. 20.
Alipofika nje kidogo ya mji, Usama aliweka kambi ili watu wakusanyike pamoja tayari kwa msafara. Hapo Abubakar akaanza kumahawishi Usama kwamba asipeleke hilo jeshi kwa sababu haiwezekani kutoka na kumwacha Mtume(s.a.w.w) akiwa hali hii ya maradhi. Abubakar alikuwa ni mtu mzima kwa umri kuliko Usama, takriban umri wa Abubakar wakati huo si chini ya miaka hamsini, na umri wa Usama si zaidi ya miaka Kumi na Tisa.
Abubakar alitumia hila mbali mbali kwa kuendesha majadiliano kati yake na kijana mdogo Usama, baina ya jeshi liende kupigana Roma kama alivyoamuru Mtume, au lisiende kama anavyotaka Abubakar. Hali hii ilichelewesha na kuchukua muda mrefu bila ya kwenda alikoamrisha Mtume, mpaka mauti yakamfikia akafa Mtume(s.a.w.w) .
Mwenyezi Mungu anasema:
وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦﴾
"Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapohukumu jambo lo lote wawe na khiari katika hukumu hiyo. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotevu ulio wazi". (Qur’an 33:36).
Amri aliyohukumu Mtume hapa ni Usama kuwa Mkuu wa jeshi litakalokwenda kupigana Roma, matoke ni kwamba; baadhi ya Waislamu hawakutii amri hiyo. Katika Aya, iliposema: "Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotevu ulio wazi." Hapa Abubakr na Umar wanapatikana na hatia ya kumuasi Mtume(s.a.w.w) , na mwenye kumuasi Mtume amemuasi Mwenyezi Mungu.
Waandishi wa tarikh na Hadithi wamelieleza tukio la Karatasi kama hivi: "Mtume(s.a.w.w) alipokuwa mgonjwa mahtuti, watu wengi walikusanyika ndani ya nyumba ya Mtume akiwamo Umar Ibn Khattab. Mtume(s.a.w.w) aliwaambia kuwa: "Nileteeni Karatasi niwaandikieni maandiko hamtapotea baada yake." Umar akasema: Mtume anaweweseka! Mtume akawaambia: "Niondokeeni" wakaondoka. Katika kauli nyingine inasema: Umar alimwambia Mtume baada ya kuagiza karatasi: "Mtume yamemzidi maradhi inakutosheni Quran mliyo nayo". Kauli ya kwanza na ya pili utazipata katika: Sahih Bukhar Kitabul Ilmi Sahih Bukhar Kitabul Tibb Sahih Bukhar Kitabun Nabi ila Kisra Sahih Bukhar Babu Karahiyatul Khilaf Sahih Bukhar Babu Jawaizil wafdi Sahih Muslim Babu Tarikil Wasia Tarikhut Tabari J.2 Uk. 436 Sharhush Shifaa J.2 Uk. 353.
Mwenyezi Mungu anasema:
وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾
"Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake) hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa." (Qur’an 53:3-4).
Amesema Abdallah bin Amri: "Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) ili nikihifadhi, Makuraishi wakanikataza wakanambia: Wewe unaandika kila kitu unachokisikia kwa Mtume!? Na Mtume ni binadamu, anazungumza (wakati mwingine) katika hali ya ghadhabu. Basi nikajizuia kuandika, nikamjulisha hayo Mtume(s.a.w.w) . Akasema Mtume, "Andika, na muape ambae nafsi yangu imo katika milki yake, mimi sisemi isipokuwa haki tupu".
Taz: Tafsir Ibni Kathir J.4 Uk. 264 Tafsir Maraghi J.27 Uk. 45.
Somo hili linatufundisha kuwa: Wakati wote Mtume(s.a.w.w) anaposema, huwa ni Wahyi. Sawa sawa awe katika furaha kubwa au katika ghadhabu, na awe katika maradhi au afya. Sasa: kwa nini Umar kuzuia usiandikwe Wahyi na nini hukumu ya mtu kama huyu? Sikiliza, Mwenyezi Mungu anasema:
وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿١١٥﴾
"Atakaempinga Mtume baada ya kudhihirikiwa muongozo, na kufuata njia isiyokuwa ya waumini, tutamgeuza alikogeukia mwenyewe, na tutamwingiza katika moto wa Jahannamu." (Qur’an 4:115).
Imepokewa kwa Mwana Aisha kuwa, Mtume(s.a.w.w) alipougua maradhi aliyofia, aliamrisha kuwa: Abubakr aslishe watu, mimi (Aisha) nikasema, Abubakr ni mtu mpole sana, atakaposimama mahala pako atashindwa (kusalisha) Mtume akaamuru: Abubakr asalishe. Nikasema kama nilivyosema kwanza, Mtume akakasirika akasema: Nyinyi ni watu wa Yusuf. Mara Mtume akahisi woga moyoni mwake, akatoka akichechemea kwa kushikiliwa na watu wawili (Ali na Abbas) alipofika Msikitini, Abubakr akarudi nyuma ya safu ya kwanza. Mtume akakaa kuongoza swala, Abubakr akawa anafuata sala ya Mtume(s.a.w.w) na Waislamu wakawa wanapokea kwa Abubakr."
Taz: Tarikhut Tabari J.2 Uk. 439.
Afatu As'habil Hadithi Uk. 13-30 Hapa pana mambo matano yanahitaji kuangaliwa:
(a) Abubakr ni katika watu walioamriwa na Mtume kutoka pamoja na jeshi Ia Usama bin Zaid. Kwa hiyo basi, amma Abubakr aliwenda pamoja na jeshi hilo, na kwa hivyo hakusalisha maana hakuwepo. Amma alikuwapo mjini, kwa hivyo alipinga amri ya Mtume(s.a.w.w) na kwa hivyo Abubakr amelaaniwa.
(b) Mtume(s.a.w.w) alipougua maradhi aliyofia, alikuwa ndani ya nyumba ya Mwana Aisha, Mtume alisema: "Niitieni Ali" Aisha akajibu: "Laiti ungemwitisha Abubakr" Hafsa (mtoto wa Umar) akasema: "Laiti ungemwitisha Umar" (kila mmoja akamwita baba yake) wakakusanyika mbele ya Mtume. Alipowaona Mtume akawaambia "Ondokeni nikikuhitajini nitakuiteni". Taz: Tarikhut Tabari J.3 Uk. 439.
(c) Mtume(s.a.w.w) alipowaambia Aisha na Hafsa, "Nyinyi ni watu wa Yusufu" hapa inaonyesha kuwa amri ya kusalisha Abubakr si ya Mtume(s.a.w.w) , hali ya kisa cha wanawake waliomtaka Nabii Yusufu (a.s) na yeye akajizia, na kisa cha Aisha na Hafsa kuwatanguliza mbele baba zao ni jambo lililofanana.
(d) Mtume(s.a.w.w) alitoka akichechemea taabani na watu wawili wamemshikilia, Abubakr akapisha mahala hapo, na Mtume(s.a.w.w) akashika mwenyewe kusalisha. Ni jambo gani lililomlazimisha kutoka akiwa hali hii, ikiwa yeye ndiye aliye amuru Abubakr asalishe? Jambo gani lililomsonga asalishe watu hali amekea chini kwa taabu na dhiki kubwa?
(e) Kuonyesha dalili zote hizi, haina maana kuwa: kama itasihi kuwa Abubakr amesalisha, basi itapasisha Abubakr kushika uongozi baada ya kuondoka (kufa) Mtume(s.a.w.w) . Hii haina maana, kwa sababu nafsi ya kusimama mbele na kusalisha watu si jambo lenye kima na thamani tukufu ambalo litampasisha kupata kila apitae mbele na kusalisha watu!! Kwa mujibu wa Hadithi za ndugu zetu Masunni, inasema kuwa: Mtume(s.a.w.w) amesema, "Salini nyuma ya kila mwema na muovu ". Na kwa msingi huu Madhihabi ya Imam Shaafy na Imam Ahmad na wengine wamepasisha Mwislamu asali nyuma ya ye yote japokuwa Fasiq.
Taz: Assunanu Walmubtadiatu Uk. 182.
Lakini pia tukiliangalia kwa wema suala hili tunaona kuwa: Mtume(s.a.w.w) alipokuwa akitoka kwenda vitani, nyuma alikuwa akiweka mtu wakushika mahala pake katika masuala mbalimbali, ikiwa ni pamojana kusalisha.
Kwanza; ni vizuri kujua maana ya neno: Saqifa: Ni Klabu au ukumbi. Amesema Mwana Aisha kuwa: "Zilipotangazwa habari za kifo cha Mtume(s.a.w.w) Umar bin Khattab na Mughira bin Shuubam waliingia ndani alikolazwa Mtume(s.a.w.w) . Umar akasema: Oh msiba mzito kwa kuondokewa na Mtume, kisha walitoka nje, walipokuwa mlangoni Mughira akasema: Ewe Umar! Kwa kweli Mtume amekufa, Umar akajibu: Wewe muongo, Mtume hajafa isipokuwa wewe ni mtu unayesumbuliwa na fitina. Mtume hatakufa mpaka wanafiki wamalizike wote.
Taz: Albidayatu Wannihaya J.5 Uk. 212.
Hatimae Umar alikamata upanga akaonya kuwa: Ye yote atakaesema kuwa Mtume amekufa atakata kichwa chake. Alipofika Abubakr, Umar akanyamaza na akaweka upanga wake chini. Kisha Abubakr akatangaza kuwa Mtume amekufa, na hapo ndipo alipoondoka yeye na Umar kwenda mwenye ukumbi wa Bani Saida. Huko walijumuika na Masahaba kutoka Ansar wa Madina tayari kwa uchaguzi. Abubakr alitoa hutuba ndefu katika mkutano huo akiwakumbusha kuwa wao (Muhajir) ndio wenye haki ya kushika uongozi mahala pa Mtume(s.a.w.w) . Hutuba ambayo ilijibiwa baadae na Hubab bin Mundhir katika Ansar, naye akionyesha kuwa ma-Ansar wanayo haki zaidi yao, kwa sababu kwao (Madina) ndiko kuliko shamiri na kukomaa nguvu za Uislam, na Waislamu kupata Uhuru wa kuabudu. na ikiwa hapana budi basi kwa Muhajir atoke mmoja na kwa Ansar atoke mmoja. Hapo ndipo Umar aliposimama akasema: "Hilo haliwezekani, panga mbili hazikai katika ala moja, Wallahi Waarabu hawakubali kuwatawalisheni na hali Mtume wao hatokani na nyinyi".
Baada ya mabishano makali na kushutumiana, karibu wauwane, hatimae Abubakr akachaguliwa. Kama asemavyo Umar: "Kuchaguliwa kwa Abubakr kulitokea ghafla, Mwenyezi Mungu alizuia shari zake, na atakaerejesha kitendo kama hiki auliwe".
Taz. Tarikhul Tabari J.2 Uk. 446/457 Tarikh Ibn Athir J.2 Uk. 223 Sahih Bukhar J.8 Uk. 210 Albidayatu Wannihaya J.5 Uk. 215.
Abubakr na Umar hawakuwahi kumzika Mtume(s.a.w.w) .
Taz: Kanzul Ummal J.5 Uk. 652.
Wakati wote huo Imam Ali yuko nyumbani kwa Mtume(s.a.w.w) akishughulikia maandalizi ya kumzika Mtume. Kisha baada ya kumzika Mtume(s.a.w.w) Imam Ali alibaki nyumbani kwake yeye na mkewe Mwana Fatima (a.s) wakawa wanakusanyika hapo Bani Hashim. Abubakr baada ya kutawalishwa alimpeleka Umar bnil Khattab nyumbani kwa Mwana Fatima(a.s) ili akawatoe wote waje kumbai Abubakr akamwagiza kuwa: Endapo watakataa kutoka kuja kumbai, awauwe. Umar akaenda na kijinga cha moto, Mwana Fatima alipomuona mlangoni na kijinga hicho akamuuliza: Ewe Umar! Umekuja iwasha nyumba yetu? Umar akajibu Ndiyo Wallahi nitakuunguzeni au mtoke kwenda kumbai Abubakr". Inasemekana kuwa: Umar alipoingia nyumbani kwa Mwana Fatima, alimpiga ngumi ya tumboni, ngumi ambayo iliumiza ujauzito na kuzaliwa mtoto aliyekufa! Na kwa sababu ya kipigo hicho, afya ya Mwana Fatima ilidhoofu sana na baadae kufariki. Umar alikuwa akiyakumbuka haya, mwenyewe husema "Laiti ningelikuwa kondoo niliyefugwa, nikanenepeshwa kiasi cha kupendeza. Akija mgeni nikatwekatwe sehemu nyama yangu ikaangwe na sehemu ibanikwe, kisha wanile na wanitoe nikiwa mavi nisiwe binadamu".
Taz: Kanzul Ummal J.12 Uk. 619.
Mwana Aisha amesema kuwa:- "Ali (a.s) hakumbai Abubakr ila bada ya miezi sita kupita ". Abubakr alikwenda nyumbani kwa Imam Ali(a.s) akawakuta Bani Hashimu wamekusanyika, Imam Ali akamwambia "Sisi haikutuzuilia kukubali ewe Abubakr, kwa kupinga heshima yako wala ubora aliokupa Mwenyezi Mungu, lakini sisi tunaamini kuwa jambo hili (la uongozi) ni letu na nyinyi mmelipokonya kwetu ". Kisha akawa anamtajia nafasi aliyonayo kwa Mtume(s.a.w.w) na haki zake mpaka Abubakr akaangua kilio.
Taz: Tarikhut Tabari J. 2 Uk. 448
Abu Bakr Aliposhika utawala, alitoa hotuba kwa mara ya kwanza, na hii ni sehemu ya hotuba hiyo "Hakika mimi ninae shetani hunifikia mara kwa mara basi wakati wo wote atakaponifikia muniepuke ".
Taz: Tarikhut Tabari J.2 Uk. 460.
Mwenyezi Mungu anasema "Hakika sisi tumewajaalia mashetani kuwa marafiki wa wale wasioamini " 7:27.
Abubakr anae shetani, na kila mwenye kuambatana na shetani si muumin, Abubakr ni nani? Mwenyezi Mungu anasema: "Na yule ambaye amekuwa shetani ndiye rafiki yake, basi ana rafiki mbaya sana " 4:38
Mwenyezi Mungu anasema:
إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّـهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا فَأَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَيْهِ وَأَيَّدَهُ بِجُنُودٍ لَّمْ تَرَوْهَا ﴿٤٠﴾
"Kama hamtamsaidia basi Mwenyezi Mungu amekwisha msaidia walipomfukuza wale waliokufuru, alipokuwa wa pili katika wawili walipokuwa wote, wawili katika pango. Alipomwambia swahibu yake; usihuzunike hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Ndipo Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake na akamsaidia kwa majeshi msiyoyaona" 9:40.
Uchunguzi wetu katika Aya hii utahusu silabi zilizotumika katika mfumo wa Aya hii, kwa hiyo tutajadili hapa nukta saba:
(a) Amekwisha msaidia
(b) Walipomfukuza
(c) Alipokuwa wapili katika wawili
(d) Alipomwambia swahibu yake
(e) Usihuzunike
(f ) Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi
(g) Akamteremshia utulivu wake.
(a) Amekwisha msaidia lliposemwa "Mwenyezi Mungu amekwishamsaidia". Hapa pana dhamiri ya mmoja aliyesaidiwa, naye ni Mtume Muhammad(s.a.w.w)
(b) Walipomfukuza lliposemwa:- "Walipomfukuza" ni mtu mmoja aliyefukuzwa, Mtume Mohammad(s.a.w.w) .
(c) Alipokuwa wa pili katika wawili lliposemwa "Alipokuwa wa pili katika wawili". Hii ni jumlatul haliyya, swahibul hali ni dhamiri katika: "Akhrajahu" inayomrejea Mtume Mohammad(s.a.w.w) . Natija inasema "Walimfukuza peke yake".
(d) Alipomwambia Swahibu yake lliposemwa "Alipomwambia Swahibu yake" watu wengi wanafikiri kuwa Mwenyezi Mungu kulitumia tamko la "Swahibu" katika Aya hii ni ibara inayompa sharaf kubwa Abubakr. Ni vizuri kuliangalia tamko Ia "Swahibu" linavyotumiwa katika Quran: "Akamwambia Swahibu yake hali akibishana naye, mimi nina mali nyingi kuliko wewe na nguvu zaidi kwa wafuasi. Na akaingia bustani yake hali ya kujidhulumu nafsi yake, Swahibu yake akamwambia hali ya kubishana naye. Je! Umemkufuru yule aliyekuumba kwa udongo tena kwa tone Ia manii kisha akakufanya mtu kamili? 18:34-37 Mazungumzo haya yalikuwa kati ya muumini na kafiri, wakiambizana "Swahibu yangu".
(e) Usihuzunike Iliposemwa "Usihuzunike", hapa pana Suratun Nahyi, ambayo Huzuni imepatikana kwa Abubakr ama kwa Sura ya Twaatullah au kwa Sura ya Maaswiyatullah!! Ikiwa ni twa'atullah, basi Mtukufu Mtume(s.a.w.w) hakatazi twa'a bali anaiamrisha na kuwataka Waislamu wawe watiifu. Na ikiwa ni maasi, basi Mtume(s.a.w.w) ameyakataza, Abubakr alihuzunika na Mtume(s.a.w.w) akamkataza.
(f) Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi Iliposemwa "Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi" Naam: "Hawashauriani kwa siri watatu ila Mwenyezi Mungu ni wa nne wao. Wala watano ila Mwenyezi Mungu ni wa sita wao, wala wachche kuliko hao wala zaidi ila Mwenyezi Mungu huwa pamoja nao popote walipo " 58:7.
(g) Akamteremshia utulivu wake Iliposemwa: "Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake " Assakiina (utulivu) ni jambo wanalolipata watu wema tu. Hapa tutataja taratibu za matumizi ya tamko hili lilivyokuja katika Quran:
a. Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha Utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya waumini" 9:26.
b. "Yeye ndiye aliyeteremsha Utulivu katika nyoyo za waumini ili waongezeke imani juu ya imani yao" 48:4.
c. Basi akateremsha Utulivu juu yao (waumini) na akawapa ushindi wa karibu" 48:18.
d. Mwenyezi Mungu akateremsha Utulivu wake juu ya Mtume na juu ya waumini" 48:26
Lakini katika pango tunasoma hivi "Mwenyezi Mungu akamteremshia Utulivu wake na akamsaidia kwa majeshi msiyoyaona". Aliyeteremshiwa hapa ni Mtume Muhammad tu peke yake.
Abubakr alipokuwa mgonjwa taabani alimwitisha Uthmani bin Affan ili aandike wasia juu ya Umar binil Khattab, akamwambia: "Andika Bismillahir Rahmanir Rahimi, hili ni agizo la Abubakr bin abi Quhafa kwa Waislamu wote" mara Abubakr akazimia Uthman akaendelea kuandika: "Amma baada ya haya, nimekutawalisheni Umar bnil Khattab na sikuacha kukupendeleeni kheri". Kisha Abubakr akazimuka, akauliza: Umeandika nini? Uthmani akassomea yale aliyoyaandika, Abubakr akashangilia sana kisha akasema Uliogopa kuwa khitilafu ingetokea kama ningezimia moja kwa moja? Uthmani akajibu: "Ndiyo Abubakr akasema Mwenyezi Mungu akulipe wema". Umar akashika mahala pa Abubakr.
Taz: Tarikhut Tabari J.2 Uk. 618 Tarikh Ibn Athir J.2 Uk. 292.
Katika tukio la Ghadir Khum, vitabu vya tarikh vimeonyesha kuwa Umar alitoa Baia kwa Imam Ali bin Abi Talib(a.s) . Na katika kumbukumbu ya tarikh vile vile vitabu kama vile: Assunanu Walmubtadia'tu ukurasa wa pili, inasimuliwa kuwa: Katika zama za Mtume(s.a.w.w) Waislamu wawili waligombana wakaenda kwa Mtume kuamuliwa. Mtume(s.a.w.w) baada ya kusikiliza ugomvi baina yao, mmoja akamtia makosa na wa pili akampa haki. Yule aliyeonekana na makosa mbele ya Mtume (s.a.w.w) akakafaa kukubali makosa yake, kwa hiyo akashauri kesi yao ipelekwe kwa Abubakr. Wakaenda kwa Abubakr, wakamhadithia namna kesi yao ilivyosikilizwa na kuhukumiwa na Mtume(s.a.w.w) , Abubakr akasema: Sina zaidi ya alivyohukumu Mtume(s.a.w.w) . Hapo vile vile ikashindikana, wakaamua kwenda kwa Umar binil Khattab, wakamhadithia walivyoanzia kwa Mtume kisha kwa Abubakr. Umar akachomoa upanga akakata kichwa cha aliyekataa kutii hukumu ya Mtume(s.a.w.w) . Pale pale Mwenyezi Mungu akateremsha Aya ya 65 ya Sura ya 4 kuwa:
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾
"Naapa kwa Mola wako, hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye hakimu wao katika yale waliyohitilafiana kati yao, kisha wasione dhiki katika nyoyo zao kwa hukumu uliyotoa na wanyenyekee sana sana".
Ikiwa Umar amekata kichwa cha mtu aliyekataa kutti hukumu ya Mtume, kisha Mwenyezi Mungu akambariki kwa kitendo hicho.
(a) Kwa nini Umar hakukata kichwa cha Abubakr aliyekwenda kinyume na Aya ya 67 ya Sura ya 5 ambayo imeshuka kwa ajili ya kumtawalisha Imam Ali bin Abi Talib(a.s) . Kitendo ambacho kilihudhuriwa na zaidi ya Waislamu laki moja, akiwamo Abubakr na yeye mwenyewe Umar?
(b) Na; kwa nini Umar hakukatwa kichwa kwa kuipinga Aya 67 ya Sura ya 5 ambaye alionekana hadharani akitoa BAIA kwa Imam Ali(a.s) kuwa ndiye Imam wake baada ya kuondoka Mtume?
Umar binil Khattab ameondoa: "Ndoa ya Mut'a na Tamattuu ya hija." Taz: Tafsirut Tabari J.5 Uk. 9 Tafsirul Qurtubi J. 5 Uk. 130 Tafsirul Razi J. 3 Uk. 200 Umar ameondoa: "Hayya a'la khairil-amal" (katika adhana na Iqama). Taz: Lisanul Mizani J.1 Uk. 268 Mizanul Itidal J.1 Uk. 139 Sunanul Bayhaq J.1 Uk. 524 Da'aimul Islami J.1 Uk. 45.
Umar binil Khattab aliweka: "Talaka tatu kuwa tatu" (zinazotolewa kwa mara moja)
Taz: Tafsirul Qurtubi J.3 Uk. 130 Sahihi Muslim J.4 Babut Talaka Fiq'hus Sunna J.2 Uk. 231 Musnadu Ahmad J.1 Uk. 314.
Umar ameweka: "Assalatu khairun minan-nawm" (katika adhana ya asubuhi). Taz: Al-Muwattau J.1 Uk. 25.
Umar aliweka: "Swala ya Tarawih" (kwa jamaa).
Taz: Tarikhu Ibn Athir J. 3 Uk. 31 Tabaqatul Kubra J. 3 Uk 281 Tarikhul Khulafai Uk. 136.
Imepokewa kwa Qatada kuwa: Umar alipozidiwa karibu atakufa, aliwaita Waislamu mbele yake akasema: "Laiti Abu Ubaida bin Jarrahi angelikuwa hai ningelimchagua kuwa khalifa wenu, na laiti Salim mtumwa wa Hudhaifa angekuwa hai ningemchagua kuwa Khalifa wenu". Siku ya pili Umar akamwita Ali bin Abi Talib, Uthman bin Affan, Saad bin Abi Waqas, Zuberi bin Awwam, Abdur Rahman bin Awf, akawaambia: "Nimefanya uchunguzi kutafuta atakaeshika mahala pangu, sikuona mwingine isipokuwa nyinyi. Shaurianeni kwa muda wa siku tatu mchague mmoja atakaekuwa Khalifa wenu, Katika siku tatu hizo za mashauriano atakusalisheni Suhaibu, na Talha bin Ubeidillahi. Mchague mmoja atakaekuwa Khalifa wenu. Katika siku tatu ni mwenzenu katika mashauri haya, akirudi katika siku tatu hizi mtieni katika wagombea. Na asipowahi basi chagueni na yeye yuko pamoja nanyi, mwanangu Abdillahi atahudhuria kikao chenu kama mashauri tu. Watano kati yenu wakimchagua mmoja, na mmoja akipinga, basi kateni kichwa chake. Wanne wakichagua mmoja, na wawili wakikataa, basi wauweni. Ikiwa watatu wakikubaliana mmoja wao, na watatu wakikataa, elekezeni shauri hili kwa mwanangu Abdillahi. Kama atakataa, basi angalieni upande aliosimama Abdur Rahmani bin Awf, ndio ulio na haki na watatu waliobaki wauliwe".
Waislamu wakamuomba ajaribu kumpendekeza anayemuona anafaa kushika mahala pake. Umar akawaambia: "Wallahi hainizi wilii kukupa Ukhalifa ewe Saadi isipokuwa ukatili ulio nao na kwamba ni mpiganaji.
Na haikuniziwia kukupa wewe Abdur Rahmani ila ni kwa sababu wewe ni firauni wa umma huu. Na haikuniziwia kukupa wewe Zuberi isipokuwa tabia uliyonayo, unapofurahi huwa muumini kweli kweli na uanapoghadhibika huwa kafiri hasa. Siku moja unakuwa shetani, siku nyingine unakuwa binadamu. Unaonaje siku unayokuwa shetani nani atashika Ukhalifa siku hiyo? Na sitaki kumpa Talha kwa sababu ya majivuno yake, na kama atashika Ukhalifa akili yake yote itafikiria wanawake. Na sitaki kumpa Uthmani kwa sababu uongozi atawaachia Bani Umayya. Na haikuniziwilia kukupa wewe Ali isipokuwa pupa uliyo nayo, na wewe ndiye bora ya watu wote, ikiwa utashika Ukhalifa bila shaka utasimamia sheria za Mwenyezi Mungu". Baada ya kufa Umar, ile kamati ikakutana, Talha akajitoa katika wagombea, na haki yake akamwachia Uthman bin Affan. Zubeir naye akajitoa na haki yake akaiacha kwa Ali.
Saad yeye naye akaacha haki yake kwa Abdur Rahman. Kwa hiyo wagombea wakabaki watatu: Ali, Uthman, na Abdur Rahman. Walipokaa kikao, Abdur Rahman aliuliza: "Nani kati yenu atajitoa katika kugombea ili awe na haki ya kuchagua mwingine"? Jamaa wakakaa kimya. Abdur Rahman akawaambia Nimefanya utafiti kujua nani mnampendelea kuwa Khalifa wenu, nimegundua ama Ali au Uthman. Kisha baada ya majadiliano marefu siku ya tatu, Abdur Rahman akamwita Ali akamshika mkono na kumwambia: "Toa ahadi kuwa utaongoza kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume wake na utafuata mwenendo wa Abubakr na Umar". Ali akajibu: "Hapana, isipokuwa nitafuata Quran na Sunna za Mtume"(s.a.w.w) Abdur Rahman akamwachia mkono kisha akamwita Uthman naye akamshika mkono na kumwambia: "Toa ahadi kuwa utaongoza kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake na utafuata mwenendo wa Abubakr na wa Umar?" Uthman akakubali; "Ndio" Abdur Rahman akasema, "Ee Mola! Sikia na ushuhudie, mimi nampa dhamana hii Uthman". Ali bin Abi Talib akatoka nje huku akisema: "Ipo siku itafikia".
Taz: Tarikhut Tabari J.3 Uk. 301 Tarikh Ibn Athir J.3 Uk. 34 Kanzul Ummal J.5 Uk. 741.
2
Mara alipochaguliwa Uthman, Abu Sufiyan alikwenda kumpongeza Uthman. Katika baadhi ya risala yake alisema hivi "Sasa (utawala) umekufikia baada ya kushikiliwa na Bani Taymi, basi zungusha kama mpira (wanavyopasiana) na weka viongozi wake wakuu Bani Umayya. Kwa sababu huu sasa ni ufalme, wala sina habari kama kuna pepo wala moto". Taz: Al-Istiia'b J.2 Uk. 690.
Abdullahi bin Saad bin Abi Sarhi, huyu ni ndugu ya Uthman wa kunyonya. Alisilimu kabla ya Fat'hu Makka, akawa pamoja na Mtume katika vikao mbalimbali, kisha baadae Alirtaddi (alitoka katika Uislamu) akawa pamoja na Makuraishi akiwaambia: "Nilikuwa nikimkejeli Muhammad namna nipendavyo".
Ilipokuwa siku ya Fat'hu Makka Mtukufu Mtume alitoa agizo ya kwamba:- Abdullah bin Saad bin Abi Sarhi auliwe po pote atakapokuwa japokuwa awe katika pazia la Kaaba". Wanafiki wakamjulisha habari hii Abdullah bin Saad bin Abi Sarhi, naye akakimbilia kwa Uthman bin Affan. Uthman akamficha, mpaka bali ilipotulia, Uthman akaenda naye kwa Mtume kumuombea msamaha. Mtume akakaa kimya kwa muda mrefu kisha akajibu, "Ndiyo" Alipoondoka Uthman na mtu wake, Mtume(s.a.w.w) akawauliza waliokuwapo hapo: "Sikunyamaza kitambo chote kile ila nilingoja miongoni mwenu asimame amkate kichwa chake" Mtu mmoja katika Ansar akamwambia Mtume: Mbona hukunikonyeza ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtume(s.a.w.w) ? Akajibu, "Kukonyeza si tabia ya Mtume ".
Taz: Usudul Ghaba J.3 Uk. 173.
Mali yote iliyopatikana baada ya kufutuhiwa Afrika mpaka Tanjat, Uthman akampa Abdullah bin Saad bin Abi Sarhi. Baadae Uthman katika mwaka wa ishirini na tano alimtawalisha Abdullah kuwa Gavana wake katika nchi ya Misri baada ya kumuuzulu A'mri. Abdullah bin Abi Sarhi akakaa miaka mingi akiwa mtawala wa Misri, watu wa Misri wakapeleka malalamiko yao kwa Uthman dhidi ya utawala wa Ibni Abi Sarhi. Uthman akaandika barua ya kumkanya Ibnu Abi Sarhi lakini hakusikia. Hapo Waislamu hawakuvumilia tena vitendo viovu aliivyokuwa akiwafanyia na kuamua kwenda kuonana na Uthman. Walipofika kwake na kumueleza yote, Uthman akawaambia: "Chagueni mtu mmoja atakaekuongozeni mahala pa Ibni Abi Sarhi. Watu wote wakamchagua Muhammad bin Abi Bakr. Uthman akampa Muhammad makaratasi ya kumtambulisha kuwa yeye ni gavana wake katika nchi ya Misri. Watu wote katika Muhajir na Ansar wakatoka kushuhudia tukio hilo, na Muhammad bin Abi Bakr gavana mteule akiwa na ujumbe wake wakaondoka kwenda Misri. Walipokuwa njiani mara aliwatokea kijana mmoja aliyekuwa na ngamia wake mwenye mbio za ajabu. Walipomuuliza anakwenda wapi na kuna nini alisema, yeye ametumwa na Uthman kwenda kwa kiongozi wa Misri. Jamaa wakamwambia Kiongozi wa Misri ni huyu (Muhammad bin Abi Bakr) kijana akajibu: "Huyu siye niliyetumwa kwake." Alipoulizwa kuwa anayo barua? Akajibu, "Sina". Wakampekuwa wakamkuta nayo barua aliyoificha, walipoifungua kuisoma ilikuwa hivi: Atakapokufikia Muhammad bin Abi Bakr na wenziwe, fanya kila njia uwauwe na upuuze barua yao, na wewe uendelee kukalia kiti chako". Walipoisoma barua hiyo, Muhammad na ujumbe wake, walifadhaika sana na wakaamua kurudi Madina. Walipofika huko wakakusanyika: Talha, Zubeir, Ali, Saad, na Masahaba wengine wengi, ikasomwa barua hiyo mbele yao na wote wakahuzunika mno. Kisha wakaafikiana kwenda kumuona na kumuuliza Uthman juu ya barua hiyo. Walipofika kwake, wakiwa pamoja na barua hiyo na kijana aliyepewa barua, Imam Ali akamuuliza: "Huyu ni kijana wako? Uthman akajibu: "Ndiyo" Ali akasema: "Ngamia huyu ni wako?" Uthman akajibu "Ni wangu" Ali akauliza: "Wewe ndiye uliyeandika barua hii? (akaonyeshwa) Uthman akajibu: "Hapana" Akaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa yeye hakuandika barua hiyo wala hakuagiza iandikwe. Ali akamuuliza: "Huu muhuri ni wako?" Uthman akajibu: "Ni wangu" Imam Ali akamuuliza: "Itawezekanaje kijana wako amchukue ngamia wako na barua iliyo na muhuri wako na wewe usiwe na habari yo yote?"
Taz: Tarikhul Khulafai Uk. 156-160.
Uthman alimuuzulu Saad bin Abi Waqqas katika mkoa wa Kuufa na mahala pake akamtawalisha Al'Walid bin Uqba ndugu yake kwa upande wa mama. Saad alipoona hivyo alishangaa na kuuliza: "Hivi wewe umekuwa mwema baada ya kuondoka mimi huko Madina, au mimi nimekuwa mjinga sikujui?" Al'walid akajibu: "Yote hayo hayakutokea (mimi si mwema na wewe si mjinga) huu ni ufalme asubuhi huliwa na hawa na jioni ukaliwa na wengine".
Taz: Tarikh Ibn Athir J.3 Uk. 42.
Waislamu yalipowachosha matendo ya Uthman ya kuwatawalisha Bani Ummayya na kuwauzulu Masahaba wakubwa, walimfuata Abdur Rahmani bin Awf wakamwambia: "Hii ndiyo kazi yako na uchaguzi wako kwa Umat Muhammad." Uthman akaanza kusambaza misaada kwa Bani Umayya akichota katika Baitilmal. Akampa Marwan bin Al'hakam aliyompa, akampa Harith bin Al'hakam bin Abil'As dirham laki tatu, akampa Zaid bin Thabit Al'ansary dirham laki moja. Hapo Abudharril Ghifar akawa anawakumbusha Waislamu Maneno ya Mwenyezi Mungu.
وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٣٤﴾ يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ ﴿٣٥﴾
"Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu basi wape habari za adhabu iumizayo. Siku itakapotiwa joto (mali yao) katika moto wa Jahanamu na kwa moto huo vitachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao. Haya ndiyo mliyoyakusanyia nafsi. zenu, basi onjeni (adhabu) ya yale milyokuwa mkikusanya" 9:34-35.
Uthman akamfukuza Abudharri akaamuru apelekwe Rabadha (mji mdogo ulio karibu na Makka) akaagiza Mar'wan bin Al'hakam ndiye atakaempeleka huko. Na hakuna ruhusa kwa mtu ye yote kutoka kumuaga wala kumsalimia Abudharri, na watu wote wakajifungia majumbani isipokuwa Imam Ali na nduguye Aqil na Hassan na Husein na Ammar, wao walitoka kumsindikiza.
Taz: AI'Ansab J.5 Uk. 52 - 54 Tabaqatul Kubra J.4 Uk. 168.
Uthman alimrejesha Madina ammi yake Al'hakam bin Abil'As ambaye Mtume(s.a.w.w) alimfukuza Madina akampeleka Taif.
Taz: Usudul Ghaba J.2 Uk. 34. Al'bidayatu Wannihaya J.8 Uk. 262.
Uthman alimpa Abu Sufiyan dirham laki mbili katika Baitulmal, akampa Abdullah Ibn Abi Sarhi dirham laki moja. Uthman alimgawia dirhamu milioni mbili na laki mbili Talha bin Ubeidillah, na Zubeir akampa dirhamu hamsini na tisa milioni na laki nane. Alhakamu bin Abil'As ammi yake Uthman ambaye alifukuzwa na Mtume yeye alipomrudisha Madina akampa dirhamu laki tatu. Na familia ya Alhakamu akaipa dirhamu milioni mbili na ishirini elfu, na wengine wengi katika Bani Umayya.
Imam Ali(a.s) ni; "Ndugu ya Mtume na Wasii wake na Khalifa wake kwa Waislamu wote".
Taz: Tarikhut Tabari J.2 Uk. 63 Tarikh Ibn Athir J.2 Uk. 62 Tarikh lbn Asakir J.1 Uk. 85 Assiratul Halabiyya J.1 Uk. 311 Musnad Ahmad J.5 Uk. 41 Kanzul Ummal J.15 Uk. 115 Kifayatut Talibi Uk. 620 Mizanul Itidal J.2 Uk. 273 Majmauz Zawaid J.9 Uk. 113 Manaqib Ali Uk. 200.
Maana ya "WASII" ni mtu anayesimamia kuendesha mambo ya mtu. Kwa kuwa Ali ni Wasii wa Mtume(s.a.w.w) maana yake Ali atasimamia na kuendesha mambo ya Waislamu baada ya Mtume(s.a.w.w) . Maana ya 'KHALIFA" ni mtu anayekuja kukaa mahala pa mtu baada yake. Kwa kuwa Ali ni Khalifa wa Mtume(s.a.w.w) manna yake Ali atashika mahala pa Mtume(s.a.w.w) baada yake. Mtume(s.a.w.w) amesema: "Wewe (Ali) nafasi yako uliyonayo kwangu mimi, ni (kama) Haruna (nafasi aliyonayo) kwa Musa, isipokuwa hakuna Utume baada yangu".
Taz: Sahih Bukhari Kitabu Maghazy Sahih Bukhari Kitabu Badi Ilkhalq Sahih Muslim Kitbul Fadhail Sahih Tirmidh J.5 Uk. 301 Musnad Ahmad J.3 Uk. 50 Mustadrakul Hakim J.3 Uk. 109 Ansabul Ashraf J.2 Uk. 106 Al-Isaba J.2 Uk. 507 Kifayatut Talib Uk. 281 Usudul Ghaba J.4 Uk. 26.
Ujumbe uliomo katika Hadithi hii ni kwamba "Ali ni Haruna wa Muhammad isipokuwa hakuna Utume baada yake. Haruna mbali ya kuwa ni Khalifa wa Musa, lakini pia ni Nabji, hii ndiyo manna ya Hadithi kusema kwamba: "Ali na Haruna ni kwa kila kitu isipokuwa Unabii". Mtume(s.a.w.w) amesema, "Mimi ninakuachieni vizito viwili ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu, Quran na Ahlul Bait, viwili hivi havitaachana mpaka vitakaponifikia katika Haudh" Taz: Tafsir Ibn Kathir J.4 Uk. 122 Tafsir Khazin J.1 Uk. 4 Tarikh Bughdad J.8 Uk. 442 Sahih Muslim J.2 Uk. 1873 Sahihut Tirmidh J.2 Uk. 308 Jamuil Usul J.1 Uk. 187 Albidayatu Wannihaya J.7 Uk. 362 Majmauz Zawaid J.9 Uk. 163 Usudul Ghaba J.2 Uk. 12 Addurrul Manthur J.2 Uk. 60.
Ahlul Bait ni cha pili katika vitu viwili ambavyo Mtume(s.a.w.w) ameacha katika umma huu. lliposemwa: "Viwili hivi havitaachana mpaka vitakaponifikia katika Haudh" Maana yake, Quran na Ahlul Bait viko pamoja na vitakuwa pamoja mpaka siku ya mwisho. Kwa maneno mengine, uongozi wa Ahlul Bait uko sambamba na uongozi wa Quran. Kwa kuwa Ali ni Imam wa kwanza katika AhIul Bait, basi Waislamu kama watashikamana naye (kwa kufuata uongozi wake) hawatapotea baada ya Mtume.
Jamal: Ni ngamia. Inaposemwa: Tukio la Ngamia, maana yake; yule ngamia aliyempanda Mwana Aisha akaenda nae katika uwanja wa Basra. Katika mwaka wa thelathini na sita Hijria, Talha na Zubeir walimuomba ruhusa Imam Ali kwenda Makka kwa ajili ya Umra. Walipokuwa njiani wakakutana na Mwana Aisha akawauliza habari za Uthman, wakamwambia kuwa Uthman ameuliwa. Mwana Aisha akasema "Muuweni na'athala hakika amekufuru".
Taz: Tarikh Ibn Athir J.3 Uk. 206 Lisanul Arab J.14 Uk. 193 Assiratul Halabiyya J.2 Uk. 286.
Na'athala: Maana yake; Myahudi mmoja aliyekuwa akiishi Madina, ambaye alikuwa na manywele mwili mzima. Mwana Aisha anamfananisha Uthman na myahudi yule. Imam Ali(a.s) aliposhika uongozi, Mwana Aisha alitoka akilia na huku akisema: "Uthman ameuliwa kwa dhulma " Ammar bin Yasir akamuuliza: "Ni vipi wewe jana ulikuwa ukimlaani na leo hii unamlilia".
Taz: Ansabul Ashraf J.5 Uk 75 Tarikh Ibn Asakir J.7 Uk. 319.
Mwana Aisha alipokuwa njiani kuelekea Basra alifika mahala akabwekewa na mbwa wengi. Mwana Aisha alishtuka akauliza hapo ni mahala gani? Akaambiwa: "Ni Hauab" Mwana Aisha akalalamika sana akataka arudishwe nyumbani, jamaa wakamgomea. Alipoulizwa kwa nini kulalamika hivyo akajibu: "Nimemsikia Mtume(s.a.w.w) akituambia: Nani katika nyinyi atabwekewa mbwa wa Hauab"? Imam Ali(a.s) alipigana na majeshi yakiongozwa na Mwana Aisha, Talha, na Zubeir watu kiasi elfu kumi walikufa katika vita hivyo.
Taz. Tarikhut Tabari J.3 Uk. 543.
Baada ya kumalizika vita, Imam Ali(a.s) alimpeleka Abdullah lbn Abbas kwa Mwana Aisha kumuamuru amrudishe Madina. Akapanga kikosi cha wapiganaji thelathini akiwamo ndugu yake Abdur Rahman bin Abi Bakr. Na mabibi watukufu wa Basra ishirini, waliovalia sare za jeshi la Ali pamoja na silaha. Akawausia kuwa; "Wasimuonyeshe Mwana Aisha kuwa wao ni wanawake". Imam Ali akaamuru mara moja jeshi hilo kumrudisha Mwana Aisha Madina.
Tukio Ia Jamal, Mwana Aisha hakulisahau maishani mwake, na kila alipolikumbuka alikuwa akijuta akisema: "Laiti ningelikuwa uchafu uliotupwa ".
Taz: Tadhkiratul Khawas Uk. 81.
Amesema Ibn Hajar katika utangulizi kwa Kitabu chake: "Al'isaba" kuwa: "Sahaba ni mtu aliyekutana na Mtume(s.a.w.w) akamwamini na akafa katika imani hiyo. Hapa anaingia aliyeishi naye kwa muda mfupi aliyepokea kwake au hakupokea, vile vile anaingia aliyepigana pamoja naye au hakupigana, aliyemuona japo mara moja au hakumuona, kwa sababu ya matatizo fulani kama upofu". Hata hivyo suala Ia Sahaba linagawanyika makundi mawili:
(a) Kwamba; Masahaba wote ni waadilifu, hawana makosa, huu ni msimamo wa Masunni
(b) Kwamba; Masahaba kama watu wengine kuna walio waadilifu, na kuna wanafiki na mafasiq. Hupimwa kwa mujibu wa matendo yao, mwema atalipwa kwa wema wake na muovu ataadhibiwa kwa mabaya yake. Huu ni msimamo wa Mashia Ithnaa'shar.
Mwenyezi Mungu anasema:
لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا ﴿١٨﴾
"Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewawia radhi waumini walipofu ngamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo mioyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao na akawalipa ushindi wa karibu" 48:18.
وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٠٠﴾
"Na waIiotangulia wa kwanza katika wahajiri na Ansar na wale waliofuata kwa ihsani. Mwenyezi Mungu amewaridhia nao pia wameridhia na amewaandalia bustani zipitazo mito chini yao, kukaa humo milele huku ndiko kufaulu kukubwa" 9:100.
لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ ﴿٨﴾ وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٩﴾
"Ni kwa mafukara waliohama, ambao walifukuzwa katika nyumba zao na mali zao wakitafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio wa kweli. Na wale waliofanya maskani na kushika imani kabla ya hao, wanawapenda waliohamia kwao wala hawapati dhiki mioyoni mwao kwa hayo waliopewa. Na wanawapendelea kuliko nafsi zao ingawa wenyewe wana hali duni, na aepushwae na ubahili wa nafsi yake basi hao ndio wenye kufaulu". 59:8-9.
"Bora ya umati wangu ni karne yangu kisha wanaofuatia, kisha watakaofuata, kisha watakuja watu viapo vyao vitakuwa mbelembele kuliko kuonyehsa ushahidi wao. Na watatoa ushahidi kabla ya kuombwa hilo."[1] "Msiwatukane Masahaba wangu, Wallahi laiti atatoa dhahabu mmoja wenu iliyo kubwa kama mlima wa Uhud, hawezi kufikia ubora wao"[2] "Nilimuuliza Mola wangu kuhusu Masahaba wangu watakao khitilafiana baada yangu Mwenyezi Mungu akaniambia: Ewe Muhammad, Sahaba wako kwangu mimi ni kama nyota zilizoko juu, baadhi yake zinang'aa sana kuliko zingine. Basi atakafuata lolote walilonalo katika khitilafu zao, huyo kwangu mimi yuko katika uongofu"[3] "Mwenyezi Mungu amenichagulia mimi na akachagua Masahaba wangu, akawafanya (baadhi yao) wakwe zangu (baadhi yao) Ansar wangu, na katika Zama za mwisho watatokea watu watawadharau. Sikilizeni msiwaoze wala msioe kwao, sikilizeni msisali nao wala msiwasalie (wakifa) imewashukia laana"[4] _
Taz: Tarikhut Tabari J.3 U.K 411.
Katika mwaka wa arobaini Imam Ali(a.s) akauliwa. Kisha Muawia katika mwaka wa arobaini na moja aliamrisha watu wote wamlaani Imam Ali.
Taz: Tarikhut Tabari J.4 Uk. 188
Taz: Sahih Bukhari Kitabul Jihad Sahihut Tirimidhi J.5 Uk. 333 Mustadrakul Hakim J. 2 Uk. 148 Tarikh Ibn Athir J. 3 Uk. 310.
Ammar ameuliwa katika vita vya Siffin akiwa upande wa Imam Ali. Kwa hiyo basi, inaonyesha kuwa watu waliosimama dhidi ya Imam Ali walikuwa watu wa motoni, ambao walikuwa: Muawia na Masahaba wengine. Lakini hapa tunaambiwa kuwa wote hawa ni wema, waliokuwa upande wa Imam Ali(a.s) na pia waliokuwa dhidi yake wote wema!!.
Mwenyezi Mungu anasema:
وَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنَّهُمْ لَمِنكُمْ وَمَا هُم مِّنكُمْ وَلَـٰكِنَّهُمْ قَوْمٌ يَفْرَقُونَ ﴿٥٦﴾ لَوْ يَجِدُونَ مَلْجَأً أَوْ مَغَارَاتٍ أَوْ مُدَّخَلًا لَّوَلَّوْا إِلَيْهِ وَهُمْ يَجْمَحُونَ ﴿٥٧﴾
"Na wanamuapa Mwenyezi Mungu kuwa wao ni pamoja nanyi hali wao si pamoja nanyi bali wao watu wanaogopa. Kama wangelipata pa kukimbilia mapangoni au mahala pengine pa kuingia, bila shaka wangeligeukia huko hali ya kukimbia". 9:56-57.
وَيَقُولُونَ طَاعَةٌ فَإِذَا بَرَزُوا مِنْ عِندِكَ بَيَّتَ طَائِفَةٌ مِّنْهُمْ غَيْرَ الَّذِي تَقُولُ وَاللَّـهُ يَكْتُبُ مَا يُبَيِّتُونَ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٨١﴾
"Na wanasema: Tunatii, lakini wanapotoka mbele yako, kundi moja miongoni mwao (Masahaba) linashauriana usiku kinyume cha yale uliyoyasema. Na Mwenyezi Mungu huyaandika wanayoshauriana usiku, basi waachilie mbali na umtegemee Mwenyezi Mungu na atosha Mwenyezi Mungu kuwa mlinzi." 4:81.
وَمِمَّنْ حَوْلَكُم مِّنَ الْأَعْرَابِ مُنَافِقُونَ وَمِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ مَرَدُوا عَلَى النِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ ﴿١٠١﴾
"Na katika mabedui wanaokaa pembezoni mwenu kuna wanafiki, na katika wenyeji wa Madina pia (wako wanafiki) wamebobea katika unafiki. (Wewe Muhammad) huwajui, sisi tunawajua, hivi karibuni tutawaadhibu mara mbili kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa". 9:101.
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا قُلْ مَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ مِّنَ اللَّـهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ وَاللَّـهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١﴾
"(Masahaba) wanapoiona biashara au mchezo wanavikimbilia, na wanakuacha umesimama (peke yako unakhutubu ukiwa na Masahaba wachache)" 62:11.
Siku ya Kiama Mtume(s.a.w.w) atawaona baadhi ya Masahaba waki pelekwa motoni aseme: "Sahaba wangu ataambiwa: Wewe hujui waliyoyazua baada yako, wao walirudi nyuma (ukafirini) tokea ulivyowaacha. Nitasema kama alivyosema Mja mwema, nilikuwa nikiyaona nilipokuwa nao, uliponifisha, wewe umekuwa ndiye mwangalizi wao na wewe ni shahidi juu ya kila kitu. Ikiwa utawaadhibu hao ni waja wako, na kama utawasamehe bila shaka wewe tu Mwenye ushindi Mwenye hekima". Taz: Tafsirul Qurtubi J.6 Uk. 377 Mukhtasar Tafsir lbn Kathir J.1 Uk. 565 Zadul Masir J. 2 Uk. 465 Tafsirul Maragh J. 7 Uk. 65.
Wakati wa Mtume(s.a.w.w) Masahaba walikuwa wakigombana na kutukanana, na hilo halikuathir chochote heshima yao. Bali la muhimu ilikuwa kusuluhisha kati yao, na mara moja walitukanana na kupigana mbeleya Mtume(s.a.w.w) .
Taz: Tafsirul Qurtubi J. 16 Uk. 315 Sahihi Muslim J. 3 Uk. 1424.
Mtu mmoja alimtukana Abubakr na Mtume(s.a.w.w) yupo kakaa, akawa anatabasam.
Taz: Hayatus Sahaba J. 2 Uk. 414.
Umar Ibn Khattab alimpiga bakora Abu Huraira mpaka akamtoa damu, kwa sababu ya ubadhirifu aliofanya Bahrain.
Taz: Tarikh Ibn Kathir J.8 Uk.113 Shaikhul Mudhira Uk. 80 Quddama bin Madh'un, ni katika Waislamu wa kwanza kwanza, amewahi kuhamia Habash na amepigana vita vya Badr na vya Uhud pamoja na Mtume(s.a.w.w) . Pia ni shemeji ya Umar ibn Khattab, bwana huyu alikuwa mlevi na Umar alimpiga hadd. Taz: Al'Isaba J. 3 Uk. 228 Usudul Ghaba J.4 Uk. 198.
Abdur Rahman bin Udais Al'balawiyyu, huyu alikuwapo katika Baia'tur ridhwan na alishiriki pamoja na wenziwe. Lakini, yeye ndiye aliyeuongoza msafara uliokwenda kuzingira nyumba ya Uthman bin Affan wakamuua.
Taz: Tarikhut Tabari J.3 Uk. 411 Usudul Ghaba J. 3 Uk.309.
Tha'alaba bin Hatib bin Umar bin Umayya alipigana vita vya Badr na vya Uhud. Lakini alizuia zaka ya mali yake, na Mwenyezi Mungu akateremsha Aya ya kumlaumu sana.
Taz: Tafsir Ibn Kathir J.2 Uk. 388 Fat'hul Qadir J.2 Uk. 367 Al-walid bin Uqba, Mwenyezi Mungu amemwita Fasiq, soma Aya 6 ya Sura 49.
Tena Sahaba huyu alikuwa mlevi, aliwekwa na Uthman bin Affan kuwa gavana wake katika Mkoa wa Kuufa. Siku moja alilewa alfajiri na mapema akasalisha sala ya asubuhi, akapiga rakaa nne, akageuka kuwauliza: Nikuongezeni?
Taz: Tarikh Ibn Athir J.3 Uk. 53 Usudul Ghaba J.5 Uk.91 AI'bidayatu Wannihaya J.8 Uk. 216 Mwana Aisha, alisujudu sijda ya kumshukuru Mwenyezi Mungu mara alipopata habari kuwa: Imam Ali(a.s) ameuliwa. Taz: Maqatilut Talibina Uk. 27.
Jina lake ni: Muawia bin Abi Sufiani bin Harb bin Umayya. Muawia baada ya kuandikiana mkataba wa amani kati yake na Imam Hasan(a.s) alikwenda Madina. Alipofika nyumbani kwa Uthman bin Affan akamkuta Aisha bint Uthman, alipomuona tu, Aisha akaangua kilio kumkumbuka baba yake. Muawia akamtuliza akamwambia: "Ewe mtoto wa ndugu yangu! Watu wametutii nasi tumewapa amani, tumeonyesha upole ndani yake kuna chuki na wao wametuonyesha udhalili ndani mna fundo, basi kila mtu ameshika silaha yake na anamwangalia adui yake alipo, tukianza mashambulizi na wao watajibu. Na hatujui tutapigwa au tutawapiga, wewe kuendelea kuwa mtoto wa Amirul Muuminina ni bora kuliko kuwa mateka wa watu." Taz: Shaikhul Mudhira Uk. 181 Muawia alipompeleka Mughira bin Shuuba kuwa gavana wake katika Mkoa wa Kuufa, mwaka arobaini na moja, alimwita akamwambia: "Nilitaka kukuusia mambo mengi sana, lakini ninakuachia wewe na akili yako katika yale yatakayo niridhisha na kuinua utawala wangu, na kupatanisha raia. Na sitaacha kukuusia jambo moja, usiache kumtukana Ali na kumkashifu, na kumhurumia Uthman na kumuombea msamaha. Na kuwatia aibu watu wa Ali na kuwatenga mbali, na kuacha kuwasikiliza mahitaji yao".
Taz: Tarikhut Tabari J.4 Uk. 188 Tarikh Ibn Athir J.3 Uk. 234.
Muawia aliwaandikia magavana wake katika miji yote kuwa: "Ye yote mtakaemgundua anawaheshimu watu wa nyumba ya Mtume, basi aadhibiwe mara moja". Muawia aliamuru akamatwe Abdur Rahman bin Hasan Al'a'nz apelekwe kwa Ziyad, kwa sababu Abdur Rahman alikuwa akiwataja kwa wema watu wa nyumba ya Mtume akakamatwa mara moja akapelekwa kwa ziyad naye akamzika akiwa hai!! Kama ambavyo jeshi la Muawia lilimkamata Muhammad bin Abi Bakr, likamfunga katika kiriba, kisha akawashwa moto mpaka akafa.
Taz: Tarikhut Tabari J.4 Uk. 79 Tarikh Athir J.7 Uk. 313 Annujumuz Zahira J.1 Uk. 110.
Muawia alipokuwa karibu atakufa, alimuusia mwanawe Yazid kuwa: "Tahadhari sana na watu wa Madina hasa Husein. Ukiona mambo yanabadilika haraka mpeleke Muslim bin Uqba." Jeshi la Muslim liliingia Madina likabaki hapo kwa muda wa siku tatu, binadamu wengi sana waliuliwa, na wasichana bikira elfu moja walinajisiwa na jeshi hilo.
Taz: Al'bidayatu Wannihaya J.6 Uk. 239 Tarikhut Tabari J.4 Uk. 374.
Jina lake ni: Abu Abdur Rahman Ahmad bin Shua'ib Annasai. Alikuwa Imam wa Hadith katika zama zake, na kitabu chake ni mojawapo ya Sihahi sita zinazotegemeka sana kwa ndugu zetu Masunni. Alipoandika Kitabu: "Alkhasais" kilichotaja ubora wa Imam Ali(a.s) , Annasai anasema: "Nilipofika Damashq (Syria) na nikawaona wapinzani wengi wa Ali, nikaandika Kitabu nikitaraji kuwa watakapokisoma Mwenyezi Mungu atawaongoa" Akaulizwa: "Kwa nini hakuandika fadhaili za Muawia"? Annasai akawajibu: "Niandike fadhla gani!! Sina ninayoijuwa isipokuwa moja tu, Mtume(s.a.w.w) aliyomwambia: "Ee! Mola, usilishibishe tumbo lake". Hapo akashambuliwa na kupigwa ndani ya Msikiti, kisha akatolewa akatupwa katika kijiji cha Ramala. Imam Annasai amekufa kwa kipigo hicho!!
Taz: Al'bidayatu Wannihaya J.11 Uk. 132.
Lile agizo la Muawia kupitia kwa magavana wake ya kuwa: "Wasiache kumtukana Ali na kumkashifu, na kumhurumia Uthman na kumuombea msamaha, na kuwatia aibu watu wa Ali na kuwatenga mbali......." Agizo hilo limefika mbali sana na sumu yake inaendelea mpaka leo hii. Hapa tutataja baadhi ya Makada wa Muawia ambao wako katika mstari wa mbele wa usimamiaji wa siasa hiyo.
Haijapata kutokea katika zama za Ujahili, au hata katika zama za Uislam, kuwa mtu ye yote ametiliwa shaka kujua jina lake na jima la baba yake isipokuwa Abu Huraira. Wamekhitilafiana jina la baba yake na jina lake kwa kauli thelathini.
Taz: Al'Isaba J. 7 Uk. 199 Usudul Ghaba J.5 Uk. 315
Abu Huraira anasema: "Hatukuweza kusema chochote juu ya Hadithi za Mtume mpaka alipokufa Umar lbn Khattab, tukiogopa bakora".
Taz: Al'bidayatu Wannihaya J.8 Uk. 210.
Sayyid Muhammad Rashid Ridha amesema: "Laiti Umar angebakia mpaka kufa Abu Huraira, zisingetufikia Hadithi nyingi namna hii". Abu Huraira anasema: "Laiti nitakusimulieni Hadithi za Mtume nilizonazo Wallah mtanipiga mawe" "Laiti nitakuelezeni ninayoyajua, Wallahi watu watanitukana waseme Abu Huraira mwenda wazimu". "Hakika Mwenyezi Mungu ameamini katika Wahyi wake watatu: Jibril, Mtume Muhammad na Muawiya".
Taz: Mustadrakul Hakim J.3 Uk 509 Tabaqatul Kubra J.4 Uk. 7 Shaikhul Mudhira Uk. 230.
Abu Huraira ameifanyia marekebisho Aya ya 214 katika Sura ya 26. Iliposhuka Aya hii kama inavyoonyesha Tarikh Mtume(s.a.w.w) alitoa tamko: Hakika huyu (Ali) ni ndugu yangu na wasii wangu na Khalifa wangu kwenu, basi msikilizeni na mumtii". Tazama vitabu vya Tarikh na vitabu vya Tafsiri utayaona. Lakini kwa bahati mbaya sana, Abu Huraira ameikata Hadithi hii akaondoa na kupachika maneno yake, kama hivi: Enyi Makuraishi! Mimi sitakufaeni chochote kwa Mwenyezi Mungu, enyi kizazi cha Abdul Manaf mimi sitakufaeni cho chote kwa Mwenyezi Munge, ewe mwanangu Fatima, niombe unachotaka katika mali yangu, mimi sitakufaa cho chote kwa Mwenyezi Mungu".
Taz: Sahih Bukhari J. 4 Uk. 7.
La ajabu zaidi mbali ya kuzua uongo huu, Aya hii imeshuka katika mwaka wa tatu wa Utume, wakati huo Abu Huraira ni kafiri yuko Yemeni hana habari na Uislamu. Vile vile Tarikh inaonyesha kuwa: Wakati ikishuka Aya hii, ilikuwa ni mwaka wa tatu wa kupewa Utume Mtume Muhammad(s.a.w.w) , wakati ambao Mwana Fatima bint Muhammad hajazaliwa bado!! Kwa sababu Tarikh inaonyesha kuwa: Mwana Fatima(a.s) amezaliwa mwaka wa tano baada ya kupewa Utume Mtume Muhammad(s.a.w.w) . Kwa hiyo Abu Huraira siyo mwongo tu, bali ni mwendawazimu kama asemavyo mwenyewe. Ndiyo maana unaweza kuona baadhi ya vitabu vya Tafsir au vya Tarikh ikifikia kutajwa madhumuni ya tukio hili huandikwa: "Hakika huyu ni ndugu yangu na kadha wa kadha, basi msikilizeni na mumtii".
Jina lake ni: Ismail bin Umar bin Kathir Addamashqi. Amesema: "Ama yale wanayohadaika nayo wajinga wengi wa Kishia na watoa visa wapumbavu, yakuwa Ali ameusiwa Ukhalifa, ni uongo.........." Taz: Al'bidayatu Wannihaya J.7 Uk. 226 Wajinga na wapumbavu, watoa visa vya uongo, kuwa Ali ni wasii na khalifa wa Mtume(s.a.w.w) ni hawa:
(a) Imam Ali bin Abii Talib(a.s)
b) Abu Ayyub Al'Ansar(a.s)
(c) Abu Said Al'khudury(a.s)
(d) Abu Dharri Al'ghifari(a.s) Na wengine wengi katika Masahaba wakubwa wa Mtume(s.a.w.w) . Je! Masahaba hawa tuliowataja hapa ni wapumbavu, wajinga wenye kutoa visa vya uongo.
Jina lake ni: Abu Muhammad Ali bin Ahmad bin Said bin Hazmi. Amesema: "Hakuna hitilafu kwa ye yote katika umma kuwa, Abdur Rahman bin Muljam hakumuua Ali ila alifanya jitihada akidhani anafanya sawa, na ndiyo maana Imran bin Hattan amesema: Ewe dharba ya mcha Mungu, hakuikusudia ila apate radhi ya Mwenyezi Mungu. Mimi naikumbuka siku hiyo, basi najua atapata malipo makubwa kwa Mwenyezi Mungu"
Taz: Al'MuhalIa J. 10 Uk. 484.
Ibn Hazmi anasema: Abul'A'dia Yasir bin Sab'i Assalmi (aliyemuua Ammar bin Yasir) ni mtu aliyejitahidi akakosea, atapata malipo ya kujitahidi. Lakini huyu si sawa na waliomuua Uthman, kwa sababu watu hao hawana nafasi ya kujitahidi kumuua".
Taz: Al'Fisal J. 4 Uk. 161.
Jina lake ni: Abul Abbas Ahmad bin Abdul Halim bin Abdus Salami bin Abdullah Muhammad bin Alkhudhar bin Muhammad bin Alkhudhar bin Ali bin Abdullah bin Taymiyya. Amesema: "Mambo mengi yaliyofanywa na Masahaba wakubwa yanasamehewa, na mahala pake huwekwa katika nafasi ya "Jitihada" ambayo mwenye kupata hulipwa thawabu mbili na mwenye kukosa hulipwa thawabu moja. Taz: Minhaj Sunna J. 3 Uk. 19/261.
Jina lake ni: AInnad ibn Muhammad bin Muhammad bin Ali bin Mahmuud bin Ahmad bin Ahmad bin Al'Asqalan. Amesema: "Wamekhitilafiana kusema: Alayhis salamu kumwambia mtu mwingine asiyekuwa Mtume(s.a.w.w) . Ingawa wamekubaliana kuwa ni sharia kwa Mwislamu kumsalimu; Assalamu Alaykum. Kwa kuwa jambo hili linatumiwa sana na Mashia, vyema sasa kuliacha, bali kuacha ni sunna na kulitumia ni bid'a.
Taz: Fat'hul Bari J. 11 Uk. 142.
Jina lake ni: Abu Hamid Muhammad bin Muhammad bin Muhammad Al'ghazaly. Amesema "Inakatazwa kwa kiongozi wa dini na mwingine yeyote kusoma matukio ya mauwaji ya Husein na kuyasimulia. (Haifai kutajwa) yaliyopita kati ya Masahaba, na kuwakosoa makosa yao kwa sababu wao ni viongozi wa dini na yaliyotokea kati yao huchukuliwa kwa nia nzuri, na pengine hayo yametendeka kwa makosa katika kujitahidi na wala si kwa kutaka ukubwa.
Taz: Ruhul Bayan J. 4 Uk. 142.
Hawa ni baadhi ya Makada wachache wa Muawia, ambao wake katika mstari wa kwanza kufuta - ikiwezekana - athari za Ahlul Bait(a.s) .
Kipimo cha kumpima mtu kuwa anafaa kupokea kwake mafundisho ya dini kwa salama na sahihi ni kutirnia sharti tano hizi:
(a) Uwepo uadilifu wa mapokezi, maana yake kila mpokezi katika wapokezi wake awe Mwislamu, aliye balighi, asiwe fasiq na asiwe muongo.
(b) Yakamilike mafungamano ya Sanad, maana yake kila mpokezi katika wapokezi wake awe amepokea moja kwa moja mpaka kufikilia kwa Mtume(s.a.w.w) .
(c) Kuwepo udhibiti wa mapokezi, yaani kila mpokezi katika wapokezi wake awe mwenye kudhibiti vyema, sawasawa iwe kwa kuhifadhi moyoni au kuhifadhi kwa maandiko.
(d) Kukosekane Shadh, yaani hadithi isiwe Shadh. Na maana ya Shadh ni: Kupinga hoja au msimamo wa walio wengi wenye kutegemeka zaidi.
(e) Kukosekana aibu, maana yake hadithi isiwe na aibu. Yaani mmoja wa wapokezi wa hadithi hiyo asijulikane na aibu yo yote. Sharti tano hizi zinapokamilika katika hadithi, huwa hadithi hiyo ni sahihi. Na hadithi kama hizi zikikusanywa katika kitabu, hujulikana kitabu hicho kuwa ni sahihi. Ndiyo maana kwa ndugu zetu Masunni kuna vitabu viwili vilivyokusanya hadithi zilizotimiza sharti hizo. Kwa pamoja Masunni wamekubaliana kuwa: Baada ya Quran Tukufu, kitabu kilicho sahihi mno ni Bukhari na Muslim".
Taz: Sharhus Sahih Muslim J. 1 Uk. 14 Mustalahul Hadithi Uk. 36.
Sasa; nitataja majina ya watu waliomo katika Sanad za hadithi zilizomo ndani ya vitabu viwili hivi (Bukhari na Muslim). Kisha msomaji atazame sharti tano tulizokwishazitaja, na watu hawa kuwamo katika Sanad za hadithi hizi sahihi.
(1) Aban bin Taghlib Alkufy. Huyu ni Shia. Imam Ahmad bin Hanbal, Yahya bin Muin, Abu Hatim na Ibn A'diyy. Hawa wamemthibitisha kuwa: "Ni mkweli anategemeka katika hadithi" Walipoulizwa: Kwa nini kumkubalisha Shia? Na hali mtu anapimwa kwa sharti tano ndipo akubalike na Shia hapati sharti hizo! Pakajibiwa: "Kama zitakataliwa hadithi za hawa (Mashia) basi zitapotea hadithi zote za Mtume"
Taz: Mizanul Itidal J. 1 Uk. 5 Imam Muslim ametegemea hadithi zake nyingi.
(2) Ismail bin Aban Al'azdy Alkufy. Huyu ni Shia. Imam Bukhari amesoma kwake, na akamtaja kuwa: Ismail ni mkweli sana anategemeka katika hadithi.
(3) Ismail bin Abdir Rahman bin Abi Karimah Alkufy. Huyu ni Shia. Huyu ni Mfassir wa Quran, na anayejulikana sana kwa jina la Assudy katika tafsir mbali mbali za Kisunni. Yeye alikuwa akimtukana Abubakr na Umar, hata hivyo amesema Imam Ahmad bin Hanbal, Ibn Addiyy, Yahya Alqattan, na Yahya bin Said kuwa: "Ismail bin Abdir Rahman ni mkweli anategemeka katika hadithi".
(4) Khalid bin Mukhlad Alkufy. Huyu ni Shia. Imam Bukhari amesoma kwake. Alikuwa akiwaalani (baadhi ya Masahaba) Imam Bukhari na Imam Muslim wametegemea hadithi nyingi kutoka kwake.
(5) Ali bin AI'juud. Huyu ni Shia. Imam Bukhari amesoma kwake, hadithi nyingi ametegemea kutoka kwa Ali bin Al'juud.
(6) Hisham bin A'mmar. Huyu ni Shia. Imam Bukhari amesoma kwake, na hadithi nyingi zilizomo katika kitabu chake amepokea kwa Hisham bin A'mmar.
(7) U'beidullah bin Musa Alkufy. Huyu ni Shia. Imam Bukhari amesoma kwake na kupokea hadithi nyingi.
(8) Said bin Ash'wa'a. Huyu ni Shia. Imam Muslim na Imam Bukhari wametegemea hadithi zake.
(9) Alhakam bin U'taiba Alkufy. Huyu ni Shia. Imam Bukhari na Imam Muslim wametegemea hadithi zake nyingi. Hapa nimeshughulikia tu kuonyesha baadhi ya watu ambao majina yao katika Sanad za Hadithi zilizomo katika Sahihi mbili, Bukhari na Muslim. Nikizingatia lile kongamano la Masunni kuwa: "Baada ya Quran Tukufu, kitabu kilicho sahihi mno ni Bukhari na Muslim". Ni vizuri nitaje hapa tamko la Maimam wa Kisunni walioshughulika kwa undani kuchambua fani ya Hadithi kuwa: Ikiwa zitakatiliwa hadithi za Mashia, basi hadithi zote za Mtume zitapotea". Kwa maneno mengine: "Kumtenga Shia katika Uislamu ni kufuta hadithi za Mtume, ukifuta hadithi za Mtume katika Uislamu ni kufuta Uislamu".
"Ni Nini Basi Baada Ya Haki Isipokuwa Upotovu ?!" Quran 10:32.
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
YALIYOMO
MEZA YA UCHUNGUZI 1
KIMEANDIKWA NA: OMAR JUMAA MAYUNGA 1
KIMETOLEWA WAVUNI NA: TIMU YA AHLUL BAYT DIGITAL ISLAMIC LIBRARY PROJECT 1
PONGEZI 1
UTANGULIZI 2
MWANDISHI WA KITABU HIKI 2
UTANGULIZI 4
OMARI JUMAA MAYUNGA UIMAM 5
MUBAHALA 7
MEZA YA UCHUNGUZI 10
QURAN NA AHLUL BAIT 10
JESHI LA USAMA 11
TUKIO LA KARATASI 12
RIWAYA KUHUSU SWALA 12
SAQIFA 14
ALI HAKUMBAI ABUBAKR 15
TUKIO LA HIJRA 15
ABUBAKR AMTEUA UMAR 16
MAMBO ALIYOYAONDOA KATIKA DINI 17
MAMBO ALIYOYAWEKA KATIKA DINI 17
TUKIO LA SHURA 18
MEZA YA UCHUNGUZI 20
UTHMAN BIN AFFAN 20
IMAM ALl 22
TUKIO LA JAMAL 23
SAHABA 23
MASAHABA WEMA 24
UBORA WA SAHABA KWA ITIKADI ZA SUNNI 24
MASAHABA WAOVU 25
HABARI ZA MUAWIA 27
TUKIO LA HARRA 27
ANNASAI 28
VIBARAKA WA BANI UMAYYA 28
(1) ABU HURAIRA 28
(2) IBN KATHIR 29
(3) IBNI HAZMI 29
(4) IBN TAYMIYYA 29
(5) IBN HAJAR 30
(6) AL'GHAZALY 30
SHIA WALIMU WA SUNNI 30
SHARTI YA KUCHAPA 31
MWISHO WA KITABU 31
YALIYOMO 32
[1] . Mara baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w) Masahaba wengi walikimbilia kwenye ukumbi wa Bani Saida. Baada ya mabishano makali na kushutumiana, hatimae Abubakr akachaguliwa kwa taabu. Kwa kitendo hiki Abubakr na Umar hawakumzika Mtume (s.a.w.w). Ilipokuwa tarehe kumi na nane mfungo tatu mwaka thalathini na tano Hijria Uthman bin Affan aliuliwa na Masahaba.
[2] . Kwa sababu hii Muawia akaanza kumlaani Imam Ali(a.s) mpaka alipokuja Umar Abdul Azizi.
[3] . Mtume (s.a.w.w) alisema kumwambia Ammar bin Yasir: "Utauliwa na kundi potovu".
[4] . Inajulikana kuwa: Kuwaua Masahaba kama Ammar bin Yasir, au kuwapiga, kama Abdullah bin Masuud (ambaye Uthman bin Affan aliamuru Abdullah bin Zam'a ampige Abdullah bin Masuud; Abdullah bin Zam'a alimpigiza chini Abdullah bin Masuud mpaka ukavunjika ubavu mmoja). Au kuwafukuza Madina kama Abudharri yote hayo si kitu, lakini kuwadharau ni dhambi.