AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU
Kuweka vikundi Imam Ali bin Husein (A.S)
mwandishi Ali ibn al - Husayn Imam Zaynul al - Abidin (a.s.)
Lugha ya kitabu سواحیلی
mwaka wa kuchapisha 1404

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

KIMEANDIKWA NA: ALI IBN AL - HUSAYN IMAM ZAYNUL AL - ABIDIN (A.S)

KIMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HAROON PINGILI

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Tunamshukuru Allah (s.w.t) na baraka za Mtukufu Mtume(s.a.w.w) na Ahlul Bayt(a.s) kwa kutujaalia kuweza kufanikia juhudi zetu hizi katika kuchapisha kitabu hiki "Sahifatul Kamillah Al-Sajadia".

Kitabu kilochopo mikononi mwako ni tafsiri ya kitabu cha Kiarabu, kiitwacho "As-Sahifatul Kamillah Al-Sajadia" kilichoandikwa na Imamu wa Nne Al-Imam Zainul Abdeen(a.s) . Ndani ya Kitabu hiki Imam(a.s) ameelezea Du'a mbali mbali.

Sababu iliyoifanya Mission yetu isimamie kazi hii ni kama zile za mwanzo, ambayo zinatokana na maombi ya Maulamaa wengi katika Afrika Mashariki kututaka tukifanyie tarjuma kitabu hiki kiingie kwenye lugha ya Kiswahili.

Tunamshukuru Shaikh Harun Pingili kwa kutukubalia ombi letu na kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja, na vile vile Bilal Muslim Mission of Scandinavia kutukubalia kukichapisha kitabu hiki.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tena kwani vitabu vyetu vya mwanzo vimependwa mno na wasomaji na hivyo kutupa ari ya kuchapisha hiki ulichonacho mkononi na kitakachofuatia Insha-Allah.

Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa wale wote ambao kwa juhudi zao kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi na waliosaidia kwa njia moja au nyingine katika tarjuma na uchapishaji wa kitabu hiki. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) awalipe malipo mema hapo Duniani na baadaye huko, Akhera.

Wa Ma Tawfeeq Illa Billah

Bilal Muslim Mission of Tanzania


UTANGULIZI

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.

Utangulizi Na: Allamah Sayyid Muhammad Rizvi

Du'a, Sala, kwa maana ya mawasiliano na Allah (s.w.t), ni sehemu ya maumbile ya Mwanadamu. Mara nyingi, umuhimu wa Du'a upo dhahiri, na hata hivyo, katika nyakati zingine, dhiki na majanga humpelekea mwanadamu kujutia na kuomba msaada kutoka kwa Allah (s.w.t). Utafiti wa Kisayansi wa hivi karibuni uliofanyika mwaka 1999, katika Hospitali ya Maradhi ya Moyo Jijini Kansas U.S.A, umethibitisha kupona kwa njia ya Sala kwa Wagonjwa wenye kusali (bila ya wao wala daktari wao kufahamu) walionekana kupona maradhi yao kwa kupimwa na vyombo 35 vya vipimo vya afya ukilinganisha na Wagonjwa Wasiosali.. Allah (s.w.t) amesema wazi wazi kuwa wakati wote milango yake ipo wazi na kwamba (Allah) yupo karibu na (mja wake) mwanadamu wakati wote kuliko alivyo yeye Mwanadamu na mshipa wa shingo yake. Qur'an tukufu inasema: "Na Mwenyezi Mungu ana Majina mazuri mazuri, muombeni kwayo". (7:180) katika Aya nyingine Mwenyezi Mungu ansema: "Na Mola wenu anasema: "Niombeni nitakujibuni: Kwa hakika wale wajivunao kufanya ibada yangu, bila shaka wataingia Jahanamu, wadhalilike." (40:60) Ingawaje inaruhusiwa kuomba (du'a) kwa Allah (s.w.t) kwa njia yeyote tuipendayo, Mtume na Maimamu wa Ahlul Bayt(a.s) pia wametuongoza katika jambo hili. Miongoni mwa miongozo ya hekima ya Maimamu ni as-Sahifah as-Sajjadiyya ya Imamu 'Ali ibnul Husayn(a.s) . Imam 'Ali ibnul Husayn anafahamika na Waislamu wote kuwa ni Kiongozi Mkuu wa Imani ya Kiroho. Hii inaelezewa kwa majina yake maarufu: Zaynul 'Abidin kiongozi (mtukufu) wa Wachamungu na Sayyidus Sajidin, kiongozi wa wale wanaosujudu chini na kuabudu.

Kitabu chake cha as-Sahifah as-Sajjadiyya ni kitabu chenye mpangilio madhubuti wa Sala na Du'a. na kinajumuisha vipengele vyote anavyopambana navyo mwanadamu katika maisha yake, Matatizo ya Afya hadi Utajiri, furaha hadi upweke na unyonge; matukio ya mafanikio na mahitajio, siku za wiki hadi siku kuu maalum n.k. Mwanachuoni maarufu wa Ki-Sunni wa Misri (Egypt) Shaykh at-Tantawi al-Jawhari ameandika yafuatayo kuhusiana na Kitabu cha Sahifah. "Nimekisoma kitabu hiki kwa makini, NimezisomaDu'a zake na Munajjat kwa jicho la utafiti, nimeshangazwa na mantiki na falsafa lliyomo ndani yake. Nimevutiwa mno kwa ubora na mtiririko wa maandishi (tungo) haya. Ninashangaa ni vipi Waislamu kwa muda mrefu wamekuwa hawajui (jahili) kuhusu hazina hii tukufu. Wamekuwa katika usingizi mzito kwa karne nyingi. Hawakuweza hata kuzinduka na kutambua kuwa Allah (s.w.t) amewapatia Hazina hii kubwa ya Elimu. Tungo za Kitabu hiki zaweza kuwekwa katika mitazamo miwili mikubwa; kwanza ni kutafuta Elimu na mwongozo ili kujitenga mbali na madhambi na vitendo viovu wakati ambapo mtazamo mwingine ni kufuata na kuyatenda matendo mema ya kiroho ambayo tunaweza kusema matendo haya yaliyojaa maarifa na mwongozo mwema ni Hazina ya ajabu na ni siri iliyojaa Hekima. Mikakati yote hii inapatikana katika sehemu ya mwanzo ya Kitabu na sehemu ya pili imejaa sifa za Allah (s.w.t), Uumbaji wa viumbe na miujiza ya Allah (s.w.t). "Je hii haishangazi? Je hii sio siri ambayo hawa Watukufu wanaweka dhahiri siri nyingi kwa kusoma na kuiweka wazi Elimu ya Waislamu ambao wanaonekana hawajui kitu? Na huu ni ukweli kwamba mambo ya Wanadamu yamegawika katika sehemu mbili kubwa. Kwanza ni yale yanayohusiana na kujitenga (kuwa mbali) na vitendo viovu na pili ni yale matendo mema pamoja na kutambua kuwepo kwa Allah ambayo ni muhimu kwa utakaso binafsi na ukamilifu wa roho" (At-Tantawi Ad'iyyatu 'Ali Zayni 'l-'Abidin katika jarida la Huda 'l-Islam la Misri (Egypt)). Nina uhakika kwa kukisoma hiki kitabu kikubwa kutoka kwa Ahlul Bayt, sio tu utapata njia sahihi ya kuwasiliana na Allah, lakini pia kitakuweka karibu na Itikadi sahihi kuhusu uwezo na rehema ya Allah (s.w.t). Hatimaye utatambua kuwa maarifa (Elimu) sahihi ya Allah inapatikana tu kwa kupitia mafundisho sahihi ya Maimamu wa Ahlul Bayt wa Mtume. Allah, subhanah wa Taala, wakati wote yupo tayari kutusikiliza na Imam Zaynul Abidin(a.s) ametuwekea njia sahihi ya kuwasiliana na Allah. Hivyo huhitajii kwenda kwa mshauri yeyote au mganga wa kienyeji ambao kwao utatoa pesa ili kusikiliza matatizo yako; Allah (s.w.t) wakati wote yupo tayari kukusikiliza, bila muda maalum wala malipo yoyote!

Sayyid Muhammad Rizvi


NENO LA WACHAPAJI

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.

Allah (s.w.t) ameumba uhai na umauti kwa makusudio maalum Amelielezea hilo kwa njia ya vitabu vinavyobainisha wazi wazi kati ya matendo mema na maovu. Maelezo fasaha na yenye mtiririko mzuri yanatuthibitishia kuwa kila mmoja wetu na wa kila rika na jamii tofauti anaweza kukielewa kitabu hiki kwa urahisi. Imani ya Dini imemuweka mwanadamu katika upeo wa juu ambao haulinganishwi na zama za Kijahiliyya. Kwa kuujua uwezo wa Allah (s.w.t) huwapelekea watu kuwa na matumaini na furaha katika maisha ya hapa Ulimwenguni na Akhera. Katika mada hii Quran tukufu inasema: "Ambao ni wale walioamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Sikilizeni! Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia" Al-Raad:28. Hapana yeyote mwenye kuujua udhaifu wa mwanadamu na mapenzi ya Allah (s.w.t); atashindwa kubadilika kwa mafunzo yaliyomo katika Sahifa. Ndani yake tunapata mafunzo ya kiroho ya Kiislam au mafundisho ya kina na mapana ya Dini ya Kiislamu yanayohusu matendo na ukweli katika maisha na mahusiano kati ya mwanadamu na Allah (s.w.t) ambayo yameandikwa katika lugha za Kimataifa kwa kuweka misingi imara ya kiroho kwa ukamilifu. Kwa Niaba yetu sote tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Mtukufu Allah (s.w.t) na kwa mwandishi wa kitabu hiki kitukufu kilichotuwezesha kuandika tafsiri ya pili na tunaungana na kufurahia kazi ngumu ya tafsiri yake ya Kiswahili pamoja na Mzee wetu Ayatullah Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi wa Bilal Mission of Tanzania. Tunamuomba Allah (s.w.t) ambariki na amlipe kwa kazi yake kubwa aliyoifanya katika nyanja hii; pamoja na wale waliotoa mchango wao wa hali na mali Mission na Mwandishi pia wanatoa shukurani zao za dhati kwa wale wote waliotoa mchango wao katika kazi hii. Tunaweka kalamu yetu chini kwa kumalizia na methali ya Kiswahili isemayo, "Fuata nyuki ule asali."

DIBAJI KUHUSIANA NA USHUHUDA - THABITI WA SAHIFA

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema - Mwenye Kurehemu

Mtukufu Sayyed Najmu Deen Bahausharafu Abul-Hasan Muhammad bin Ahmad bin Ali bin Muhammad bin Umar bin Yahya Al-Alawi Al-Husayn - Mungu amrehemu - alituhadithia Alisema: Alitupa khabari Shaikh heri zimfikiye Abu Abdilahi Muhammad bin Ahmad bin Shahriyar muweka hazina wa hazina ya Amiyrul Muuminen Maulana Aliy bin Abiy Taalib alayhis-salaam katika mwezi wa Rabi-u-Awal (mwezi wa tatu A.H.) mwaka wa 516 mwezi May - June wakati Sahifa ilikuwa inasomwa mbele yake nami nasikia.

Alisema nimeisikia kutoka kwa Shaikh ikisomwa mbele yake Shaikh Swaduqu Abiy Mansoor Muhammad bin Muhammad ibun Ahmad bin Abdil-Aziz Al-Ukbari mwadilifu Mungu amreheu kutoka kwa Abil-Mufazzali Muhammad bin Abdilahi ibnil-Mutalib Ashaybaanee. Alisema: Sharifu Abu Abdilahi Jaafar bin Muhammad ibun Jaafar ibunil Hasani ibin Jaafar ibunil Hasan Ibunil Hasan ibun Ameril-muumineena Aliy ibn Abiy Taalib amani juu yake ametuhadithia. Amesema: Ametuhadithia Abdulahi ibin Umar ibin Khataab Azaya mwaka wa mia mbili sitini na tano 265 (878-9) Amesema: Ametuhadithia mjomba wangu Ali bin Anuumani Al-Aalamu. Amesema: Ametuhadithia Umairi bin Mutawakili Athaqafiyu Al-Balakhiyu naye... kutoka kwa baba yake Mutawakili bin Haroon. Alisema nimekutana na Yahya bin zaid bin Aliy Alayhi-salaam naye akiwa yu aelekea khurasani baada ya kuuliwa baba yake nilimsalimia. Aliniuliza umetoka wapi? Nikasema kutoka Hajji. Aliniuliza kuhusu Ahli wake na watoto wa ami yake huko Madina na alisisitiza swali kuhusu Jaafar bin Muhammad amani iwe juu yake.Nilimuelezea khabari zake na khabari zao na huzuni walionayo kuhusu baba yao Zaid bin Aliy amani iwe juu yake. Aliniambia: Ami yangu Muhammad bin Aliy amani iwe juu yake alimshauri baba yangu asitoke na alimjulisha kuwa endapo atatoka na kuiacha Madina mambo yatavyomuwia. Je ulipata kukutana na mtoto wa ami yangu Jaafar bin Muhammad amani iwe juu yake? Nikamwambia ndio. Akasema je ulipata kumsikia anasema chochote kunihusu? Nikasema ndio.

Akasema: Alisema nini kunihusu? Nikasema nimejitoa muhanga kwako sipendi nikukabili kwa yale niliyoyasikia kutoka kwake. Akasema wanitishia umauti? Lete ulichosikia. Nikasema nimemsikia akisema kwa hakika kabisa kuwa utauliwa na utasulubiwa kama alivyouliwa baba yako na alisulubiwa. Basi uso wake ulibadilika na akasema: (Mungu huyafuta apendayo na huyathibitisha na kwake ipo asli ya kitabu). Ewe! Mutawakilu hakika Mwenyezi Mungu mwenye enzi na ametukuka ameliunga mkono jambo hili kupitia kwetu na ametupa sisi elimu na upanga. Haya mawili yameunganishwa na sisi na wamepewa wana wa ami yetu khususan elimu tu peke yake. Nikasema nimejitoa kwako muhanga mimi naona watu wanaelemea sana kwa mwana wa ami yako Jaafar amani iwe juu yake kuliko kwako na kwa baba yake. Akasema: kwa hakika ami yangu Muhammad na mwanawe Jaafar amani iwe juu yao wamewaita watu kwenye uhai na sisi tumewaita kwenye umauti. Nikasema ewe mwana wa mjumbe wa Mungu je wao wanaelimu zaidi au ninyi? Aliinama punde kisha akainuwa kichwa chake na akasema: Sote tunaelimu isipokuwa wao wanayajua yoote tuyajuwayo nasi hatujuwi yote wayajuwayo. Kisha aliniambia: Je umeandika chochote kutoka kwa mwana wa ami yangu? Nikasema naam. Akasema nionyeshe, nikamtolea aina kadhaa za elimu na nikamtolea duwa nilizoandika kutoka kwake Abiy Abdilahi amani iwe juu yake. Na alinihadithia kuwa baba yake Muhammad bin Aliy amani iwafikie alimwandikia kwa imla na akampa khabari kuwa ni miongoni mwa DU'A za baba yake Aliy bin Husain amani ziwe juu yao ni miongoni mwa DU'A za Sahifa al-Kamila. Yahya aliiangalia mpaka mwisho wake na aliniambia: Je waniruhusu niinakili? Nikasema Ewe mwana wa mjumbe wa Mungu waomba ruhusa kile ambacho ni kutoka kwenu? Akasema hakika nitakutolea Sahifa ya DU'A kamili zile alizozihifadhi baba yangu kutoka kwa baba yake na kwa hakika baba yangu ameniusia kuilinda na kutompa asiyestahiki. Umairu alisema: Alisema baba yangu: Basi nilisimama na kumwendea nikabusu kichwa chake. Na nikamwambia naapa ewe mwana wa mjumbe wa Mungu hakika mimi nitafanya dini ya Mungu kupitia upendo wenu na kuwatii ninyi, nami nataraji anipe Mungu maisha ya faraja na umauti mwema kwa wilaya yenu (kuwa penda). Basi alitupa zile kurasa zangu nilizompa kwa mtoto alikuwa pamoja naye na akasema andika DU'A hii kwa hati bayana nzuri kisha nipe huenda nikaihifadhi kwani nilikuwa naiomba kutoka kwa Jafari Mungu amhifadhi naye alikuwa akiniziwiya nayo. Mutawakilu alisema: Nilijutia nililofanya sikujuwa la kufanya na Abu Abdilahi amani imfikiye hakuniambia kuwa nisimpe yeyote! Baadaye aliagiza kisanduku ambacho humo alitowa sahifa iliyofungwa na kupigwa muhuri akauangalia ule muhuri na akaubusu akalia akavunja na kufunguwa kufuli. Kisha aliikunjuwa ile sahifa na akaiweka kwenye macho yake na kuipitisha usoni kwake na akasema walahi ewe! Mutawakilu lau kama kwa ajili ya yale uliyoyasema miongoni mwa usemi wa mwana wa Amiy yangu yakuwa mimi nitauwawa na kusulubiwa nisingekupa hii sahifa ningeifanyia ubakhili. Lakini natambua kuwa usemi wake ni wa haki ameuchukua kutoka kwa baba zake na itatimia hivyo basi nimeogopa elimu kama hii iwafikie baniy Umayya wataificha katika kabati zao kwa ajili yao tu. Ichukue ihifadhi kwa niaba yangu na ungoje ukiwa nayo Mungu atapopitisha jambo langu na jambo la hawa watu na atapitisha.

Basi hiyo ni amana yangu kwako mpaka uifikishe kwa wana wawili wa Amiy yangu Muhammad na Ibrahim wana wawili wa Abdilahi bin Hassan bin Hassan amani iwafikie. Kwa sababu wao ndio watakaoshika jambo hili baada yangu.Mutawakilu akasema: Niliipokea sahifa. Na alipouliwa Yahya bin Zaid nilikwenda Madina nikakutana na Aba Abdilah, amani imfikie. Nilimsimulia zile khabari kumuhusu Yahya alilia sana na huzuni kumuhusu ilikithiri na akasema: Mungu mrehemu mwana wa Amiy yangu na amkutanishe na baba zake na babu zake. Wallahi ewe Mutawakilu halikunizuwia kumpa ile DU'A yeye isipokuwa lile alilolihofia kuhusu sahifa ya baba yake, basi iwapi sahifa? Nikasema: Ni hii.Aliifungua na akasema: Wallahi hizi ni hati za Amiy yangu Zaid na ni DU'A ya babu yangu Aliy bin Hussain amani iwafikie. Kisha alimwambia mwanawe: Simama ewe Ismael niletee ile DU'A ambayo nilikuamuru uihifadhi kwa moyo na kuilinda Ismael alisimama na aliitowa ile sahifa kama ile aliyo mkabidhi Yahya bin Zaid Abu Abdilahi aliibusu na aliiweka machoni kwake na akasema huu ni mwandiko wa baba yangu na aliiandika kwa imla aliyoifanya babu yangu amani iwe juu yao mimi nikiwa naona. Nikasema ewee mwana wa Mtume wa Mungu waonaje nikiilinganisha na sahifa ya Zaidi na Yahya? Aliniruhusu kufanya hivyo na alisema: Nakuona wafaa kwa hilo.Nikazichunguza naona kuwa zi kitu kimoja sikuipata hata herufi moja inatofautiana na zilizo kwenye sahifa nyingine. Kisha nilimwomba ruhusa Aba Abdilah amani iwe juu yake ili niwape sahifa watoto wawili wa Abdilahi bin Husain. Akasema (hakika Mungu anakuamrisheni kuzifikisha amana kwa wenyewe) ndio wape hao wawili.Nilipoinuka ili kukutana nao aliniambia: bakia mahali pako. Kisha alituma waitwe Mohammad na Ibraheem, na akasema huu ni urithi wa mwana wa Amiy yenu Yahya kutoka kwa baba yake amempeni ninyi khususan na kuwaacha ndugu zake. Nasi tunakuwekeeni sharti. Wakasema sema kwani kauli yako yakubalika. Akasema musitoke nayo sahifa hii nje ya Madina.Wakasema: Kwanini iwe hivyo? Akasema: Kwa hakika mwana wa Amiy yenu aliihofia jambo nami nalihofia kwenu. Wakasema kwa hakika aliihofia alipojua kuwa atauwawa. Akasema Abu Abdilah amani imwendee; na ninyi musijiaminishe, kwa kweli najua kuwa ninyi mutapinga kama alivyopinga na mutauwawa kama alivyouwawa. Walisimama huku wakisema hapana hila wala nguvu ila kwa kuwezeshwa na Mungu aliye na enzi ya juu mno mtukufu.Walipokwisha toka akaniambia Abuu Abdilahi amani imfikiye: Ewe Mutawilu: vipi Yahya alikwambia kuwa hakika Amiy yangu Mohammad bin Aliy na mwanawe Jaafar wanawaita watu kwenye uhai nasi tunawaita kwenye umauti? Nikasema ndio Mungu akuweke katika islahi aliniambia hivyo mwana wa ami yako Yahya. Akasema Mungu amrehemu Yahya, hakika baba yangu alinihadithia naye alihadithiwa na baba yake naye toka kwa babu yake toka kwa Aliy amani juu yake kuwa mjumbe wa Mungu(s.a.w.w) alisinzia kidogo akiwa juu ya membari yake akaona akiwa katika usingizi wake kuwa watu wanaruka ruka juu ya membari yake kama ngedere na kuwafanya watu warudi kinyume nyume.Mtume wa Mungu alikaa sawasawa(s.a.w.w) hali ikiwa huzuni imetanda usoni kwake. Jibrilu (a.s) alimjia na aya hii: (Hatukuifanya njozi tuliyokuonyesha isipokuwa ni mtihani kwa watu na mti ulio laaniwa katika Qur'an na tunawahofisha lakini haiwazidishii ila kuvuka mipaka kukubwa) Awakusudia Baniy Umayya kwa tamko la mti uliolaaniwa katika Qur'an.

Akasema ewe Jibril watakuwa katika muda wangu na katika wakati wangu? Akasema la hapana lakini kinu cha Uislamu kitazunguka toka kuhama kwako na kubaki miaka kumi baada ya hapo kinu cha Uislam kitazunguka mpaka miaka thelathini na tano toka kuhama kwako. Baada ya hapo kitabaki miaka mitano kisha hapana budi kutakuwa na maongozi potovu ya kuwa katika muhimili wake kisha kutakuwa na ufalme wa mafirauni. Akasema na Mungu mtukufu aliteresha aya ya Qur'an kuhusiana na hayo: (Kwa hakika tumeiteremsha usiku wa maazimio kitu gani kitakujulisha usiku wa maazimio nini usiku wa maazimio ni bora kuliko miezi elfu). Watamiliki Baniy Umayya wakati ambao hautakuwa na usiku wa maazimio. Akas.ema Mwenyezi Mungu mtukufu alimjulisha Nabiy wake(s.a.w.w) utawala wa umaa huu na mamlaka yao muda wote huu. Hata lau milima ingerefuka kupita kiasi wangejirefusha na wao hata kushinda mirima mpaka Mungu mtukufu aidhinishe kutoweka ufalme wao na wao katika wakati huo wote wamepandisha bendera ya chuki na bughudha dhidi yetu sisi Ahla Bayt. Mungu alimpasha khabari Nabiy wake yale watakayopambana nayo Ahli Bayt wa Muhammad na wapenzi wao na Shia wao toka kwao (Baniy Umayya) katika siku za ufalme wao. Akasema: Mungu ameteremsha kuhusu hawa watu: (huwaoni ambao wameibadilisha neema ya Mungu kwa kukufuru na kuwafanya watu wao kubaki katika maangamizi wataunguwa katika jahannam na ni makazi mabaya mno.) Na neema ya Mungu ni Muhammad na Ahli Bayt wake kuwapenda wao ni iymani yaingiza peponi na kuwachukia ni ukafiri na unafiki uingizao motoni.Mtume wa Mungu aliiweka siri hiyo kwa Aliy na kwa Ahli Bayt wake. Akasema: Kisha Abu Abdilahi amani iwe juu yake alisema: Hajatokea wala hatotokea kati yetu Ahli Bayt yeyote mpaka siku ya kusimama na kujitokeza kwa qaim wetu Imamu Mehdi ili aziwiye dhulma au kuifanya haki itekelezeke ila atagongana na balaa na itakuwa kujitokeza kwake ndio sababu ya kuzidisha uadui na msiba juu yetu na Shia wetu. Mutawakilu bin Haroon alisema: kisha Abu Abdilahi aliniandikia DU'A kwa njia ya imla nazo zikiwa katika milango 75 imenipotea kutokana nazo milango kumi na moja na nimehifadhi miongoni mwa DU'A hizo milango sitini na kitu. Ametuhadithia Abul-Fazzal amesema: Na amenihadithia Muhammad bin Al-Hassan Ibun Ruzbih Abu Bakr Al-madaini mwandishi ni mkazi wa Arrah'ba alitusimulia akiwa nyumbani mwake. Amesema: Amenihadithia Mohammad bin Ahmad bin Muslim Al-Mutaharyu, amesema: amenihadithia baba yangu kuutoka kwa Umairi bin Mutawakili Al-Balkhiyi toka kwa baba yake Al-Mutawakilu bin Haroon. Alisema: Nilikutana na Yahya bin Zain bin Aliy amani iwe juu yao na aliitaja hadithi kikamilifu mpaka ile njozi ya Nabiy(s.a.w.w) ambayo Jaafar bin Muhammad aliitaja toka kwa baba zake amani iwafikie. Na katika riwaya ya Almutahari imetajwa milango nayo ni:

1. Kumuhimidi Mungu mwenye enzi na ametukuka.

2. Sala kwa Muhammad na Ali wake.

3. Sala kwa wabeba arshi (kitanda.)

4. Sala kwa wanomsadiki Mtume.

5. DU'A kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wamuhusuo.

6. DU'A ya kila asubuhi na jioni.

7. DU'A yake kwa ajili ya mambo yanayotisha na muhimu.

8. DU'A yake kwa ajili ya kujikinga.

9. DU'A yake kwa ajili ya ayapendayo.

10. DU'A yake kwa kutaka Mungu awe ndio kimbilio lake.

11. DU'A yake kwa ajili ya mwisho mwema.

12. DU'A yake kwa ajili ya kukiri.

13. DU'A yake kwa ajili ya mahitaji.

14. DU'A yake kwa ajili ya matendo ya dhuluma.

15. DU'A yake wakati wa ugonjwa.

16. DU'A yake kutaka ufumbuzi.

17. DU'A yake dhidi ya shetani.

18. DU'A kwa kujihadhari na hatari.

19. DU'A yake kuomba maji.

20. DU'A yake kwa ajili ya kuwa na tabia njema.

21. DU'A yake akihuzunishwa na jambo.

22. DU'A yake wakati wa shida.

23. DU'A yake kwa ajili ya afya njema.

24. DU'A yake kwa ajili ya wazazi wake wawili.

25. DU'A zake kwa ajili ya watoto wake.

26. DU'A yake kwa ajili ya majirani zake na rafiki zake.

27. DU'A yake kwa ajili ya walinda mipaka.

28. DU'A yake katika mfadhaiko.

29. DU'A yake inapokuwa haba riziki.

30. DU'A zake ili kupata msaada wa kulipa deni.

31. DU'A yake kwa ajili ya toba.

32. DU'A yake katika sala za usiku.

33. DU'A yake katika kumwomba Mungu amchagulie lililobora (istikhara)

34. DU'A yake apatwapo na balaa au aona balaa ya nyemelea

kumfedhehesha kwa dhambi.

35. DU'A yake kuonyesha ridha kwenye maamuzi ya Mola.

36. DU'A yake asikiapo radu.

37. DU'A yake katika kuonyesha shukurani.

38. DU'A yake kuomba udhuru.

39. DU'A yake kuomba msamaha.

40. DU'A yake akumbukapo umauti.

41. DU'A yake kuomba kusitiriwa na hifadhi.

42. DU'A yake wakati wa kuhitimisha Qur'an.

43. DU'A yake anapouona mwezi mwandamo.

44. DU'A yake uingiapo mwezi wa Ramadhani.

45. DU'A yake kuuaga mwezi wa Ramadhani.

46. DU'A yake kwa ajili ya Iddi ya Fitri na Ijumaa.

47. DU'A yake siku ya Arafat.

48. DU'A yake siku ya uzhiya (kuchinja) na siku ya Ijumaa.

49. DU'A yake kujikinga na vitimbi vya maadui.

50. DU'A yake wakati wa hofu.

51. DU'A yake katika kumwomba Mungu sana na unyenyekevu.

52. DU'A yake katika kuomba kwa bidii.

53. DU'A yake katika kujidhalilisha (mbele ya Mungu).

54. DU'A yake ili kuondoa maudhi.

Ama milango iliobaki ni kwa matamko ya Abiy Abdilahi Al-Hasaniy rehma za Mungu zimfikie.

Ametuhadithia Abu Abdilah Jaafar bin Mohammad Al-Hasaniy, amesema: Ametuhadithia Abdulahi bin Umairi bin Khataab Azzayatu. Amesema: Amenihadithia mjomba wangu Aliy bin Annuumani Al-Halam.

Amesema: Amenihadithia umairu bin Mutawakilu Athaqafiyu Al-Balakhiyu kutoka kwa baba yake Mutawakilu bin Haroon. amesema amenifanyia imlaa bwana wangu Aswadiqu Abu Abdilahi Jaafar bin Muhammad.

Amesema: Babu yangu Aliy bin Husain alimfanyia imla mbele ya macho yangu baba yangu Muhammad bin Aliy, juu ya wote amani ya Mungu iwafikie.


1

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

DUA YA KWANZA

Na Alikuwa(a.s) Akianza Kuomba Du'a Huanza Kumhimidi Mungu Mtukufu Na Kumsifu Husema Hivi:

Sifa Njema Zote Ni Zake Mwenyezi Mungu. Ambaye ni wa mwanzo bila ya chanzo kilikuwa kabla yake, na wa mwisho bila ya cha mwisho kitakuwa baada yake: Ambaye yameshindwa kumwona macho ya watazamaji, yameshindwa kumuainisha mawazo ya wasifiaji. Kwa uwezo wake alianza kuumba viumbe. Aliwabuni (viumbe) kwa utashi wake wa kubuni, Kisha aliwapitisha njia ya utashi wake. Na aliwatuma katika njia ya upendo wake. Hawana uwezo wa kuchelewesha alichowatangulizia. Wala hawawezi kutanguliza alichowacheleweshea. Na ameifanyia kila roho miongoni mwao lishe ijulikanayo iliyogawanywa kutoka kwenye ruzuku yake. Mpunguzaji hawezi kumpunguzia aliye mzidishia. Wala mzidishaji hawezi kumzidishia aliempunguzia.

Kisha akaipigia kila nafsi muda wenye kikomo. Na akaisimamishia kila nafsi muda wenye mpaka. Yanatembea kuuelekea, kupitia siku za umri wake. Anaufikia kupitia miaka ya muda wake. Mpaka afikapo hatua ya mwisho, na kutimiliza hesabu za umri wake. Mungu humshika na kumpeleka kwenye thawabu zake nyingi au kwenye adhabu yake aliyo muhadharisha nayo. Ili awalipe ambao wamefanya vibaya waliyotenda, na awalipe wema ambao wamefanya mema. Ikiwa ni uadilifu kutokana naye. Yametakasika majina yake. Neema zake zimejitokeza!

"LA YUS'ALU AMMA YAF'ALLU' (Haulizwi atendayo) "WA HUM YUS' ALUNA" (Wao ndio wataulizwao). Sifa njema zote ni za Mungu ambaye lau angewaficha waja wake utambuzi wa Himidi yake, juu ya aliyowafanyia majaribu kwa neema zake zenye kufuatana, na amewakithirishia neema zake za wazi, wangezitumia neema zake, bila ya kumhimidi! Na wangejitanua katika riziki yake bila ya kumshukuru.

Na wangekuwa hivyo wangetoka nje ya mipaka ya ubinadamu na kuingia kwenye mipaka ya unyama na wangekuwa kama alivyo waelezea katika kitabu chake thabiti:

"IN HUM ILA KAL AN AAMI BAL HUM ADWAllU SABIILA" (Hakika wao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu mno wa njaa). Sifa njema ni za Mungu juu ya ujuzi aliotupa kumtambua yeye binafsi, na ametupa ilhamu ya kumshukuru. Ametufungulia milango ya elimu ya kutambua kuwa yeye ndiye Bwana. Na ametuelekeza tuwe wanyofu kwake katika kumpwekesha. Ametuepusha na upotovu na kuwa na mashaka katika amri yake. Sifa njema ambazo kwazo tutapata maisha marefu miongoni mwa viumbe wake walio muhimidi, na kwazo tumpite aliye tangulia kwenye ridhaa yake na msamaha' wake. Sifa njema ambazo zitatuangazia giza la BARZAKH na iturahisishie njia ya kufufuliwa. Ienzi mafikio yetu kwenye kisimamo cha mashahidi

'YAUMA TUJ'ZA KULU NAFSIN BIMA KASABAT WA HUM LAA YUDH'LAMUUN"

(Siku ambayo kila nafsi italipwa ilichotenda nao hawato dhulumiwa). "YAUMA LA YUGHNIIMAULA AN MAUL.4 SHA-I-AN WALA HUM YUN SWARUN"

(Siku ambayo Bwana hatomfaa chochote mtetezi wake nao hawatopata usaidizi) Sifa njema itatunyanyuwa juu mpaka juu zaidi ya walio juu) "FIKITABINMARQUMI. YASH'A HADU HUL-MUQARABUN"

(Katika kitabu kilicho andikwa. Wakishuhudia walio sogezwa karibu.) Sifa njema ambayo macho yetu yatapata utulivu pindi macho yatafanywa kiwi na kwayo sura zetu zitafanywa ziwe nyeupe pindi ngozi zitafanywa nyeusi. Sifa njema ambazo kwazo tutaachwa huru, kutoka moto mkali wa Mungu natuingiye kwenye karama ya ujirani wa Mungu. Sifa njema ambazo kwazo tutasongamana na Malaika wake walio kurubishwa, na tuungwe kwayo na Manabii wake waliotumwa.

Katika nyumba ya kudumu haitoweki, na mahali pa ukarimu wake ambao haubadiliki. Sifa njema ni za Mungu ambaye ametuchagulia maumbile mazuri.Na ametutunukia riziki muwafaka.Ametupa ubora kuvitawalia viumbe vyote. Viumbe wake wote wako chini ya utii wetu kwa Qudra yake waja kwenye kututii kwa enzi yake. Sifa njema ni zake Mungu ambaye amefunga kwa ajili yetu mlango wa mahitaji isipokuwa kwake. Kwa hiyo vipi tutaweza kumsifu? Au lini tutaweza kutekeleza shukrani zake Lahasha! Lini? Na sifa njema ni za Mungu ambaye ameunganisha katika sisi viungo vya mwili vyenye kupanuka, na ametujaalia viungo vya kushika. Ametustarehesha kwa roho ya maisha. Ametuunganishia kuwa imara viungo vya kazi. Na ametupa lishe maridhawa. Ametutosheleza kwa fadhila zake ili tusiwe na haja.

Ametumilikisha kwa wema wake. Kisha ametupa amri ili kututihani utiii wetu. Na ametukataza ili ajuwe shukrani zetu. Tumehalifu njia ya amri yake. Tumeparamia migongo ya makaripio yake! Hata hivyo hakutuharakishia adhabu yake, wala hakutuharakishia kisasi chake. Bali alikwenda nasi pole pole kwa huruma yake ikiwa ni takrima. Alitungoja turejee kwa huruma yake, ni upole (wake). Sifa njema ni za Mungu ambaye ametuonyesha jinsi ya kufana toba ambayo hatungefaulu isipokuwa kwa fadhila zake. Lau hatungeweza kuhesabu fadhila zake isipokuwa haya majaribu yake kwetu yamekuwa mema kwetu. Hisani zake kwetu ni kubwa mno. Fadhila zake kwetu ni za kutosha. Si kama hivi ulikuwa mwendo wake katika toba kwa waliokuwa kabla yetu. Ametuondolea lisilokuwa katika uwezo wetu. Hajatukalifisha isipokuwa lililo kwenye uwezo wetu hajatulazimisha jambo ila ni jepesi. Hajamwachia yeyote kati yetu udhuru wala hoja. Basi mwenye kuangamia kati yetu ni yule mwenye kuhiliki japo hataki.

Na mwenye heri kati yetu ni yule mwenye kumronga yeye. Na sifa njema ni za Mungu kwa kila aliye mhimidi malaika wake wa karibu naye. Na viumbe wake walio na heshima sana kwake, na wenye kumridhisha mno miongoni mwa wanao muhimidi. Sifa njema zilizo bora kuliko zote kama ubora wa Mola wetu juu ya viumbe wake wote. Kisha zake ni sifa njema mahali pa kila neema yake juu yetu na juu ya waja wake wote waliopita na waliobaki kwa idadi ya yaliyo zungukwa na elimu yake, toka vitu vyote. Na mahali pa kila moja miongoni mwazo idadi yake ni zaidi na zaidi milele mpaka siku ya Qiyama. Sifa njema isiokuwa na mwisho. Idadi yake haihesabiki. Mwisho wake haufikiwi. Muda wake hauna mwisho. Sifa njema itakuwa kiungo cha utii wake na msamaha wake, na ni sababu ya maridhawa yake. Na njia ya kwenye msamaha wake. Na njia ya kwenye pepo yake. Na mlinzi wa malipizi yake. Na ni usalama kwa ghadhabu yake. Usaidizi wa utii wake. Kizuizi cha maasi yake. Ni msaada wa kutekeleza haki yake na wajibu wake. Sifa njema ambazo zitatupa furaha miongoni mwa wenye furaha katika mawalii wake. Na kwayo tutakuwa katika daraja ya waliouliwa kwa upanga wa maadui wake. Hakika yeye ni mpendwa msifika.

DUA YA 2

NA ILIKUWA KATIKA DU'A YAKE(A.S) BAADA YA KUMUHIMIDI MUNGU KAMA HIVI: HUANZA KUMTAKIA REHMA MJUMBE WA MUNGU(S.A.W.W)

Sifa njema ni zake Mungu ambaye amekuwa na huruma kwetu kupitia Nabiy wake Muhammad(s.a.w.w) mbali na umma zilizopita na vizazi vilivyopita. Kwa uwezo wake ambao haushindwi kitu japo kiwe kikubwa mno. Wala haupitwi na kitu japo kiwe chepesi, au chenye hila nyingi, janja. Na alihitimisha kwetu kwa wote waumba na kutufanya tuwe mashahidi kwa wanaopinga. Kwa wema wake ametufanya tuwe wengi kwa walio wadogo. Ewe Mola mrehemu Muhammad mwaminifu wako juu ya wahyi wako (ufunuo) mteule wako kati ya viumbe wako mwenye kujitoa wakfu katika waja wako. Imamu wa rehema. Kiongozi wa mema. Funguo wa baraka. Aliye jitaabisha nafsi yake kwa ajili ya mambo yako. Amejitoa mwili wake kuyakabili yachukizayo kwa ajili yako. Alijionyesha kwenye uadui wa wazi toka kwa ndugu zake kwa kuwaita kwako. Amepigana na famili yake kwa ajili ya ridhaa yako. Amejikata na kujiweka mbali na watu wa ukoo wake ili kuihuisha dini yako. Aliwaweka mbali na ndugu wa karibu kwa upinzani wao. Aliwasogelea walio mbali kwa kuitikia kwao wito wako. Aliwafanya marafiki watu wa mbali kwa ajili yako. Na aliwafanya maadui kwa ajili yako watu wa karibu. Alijibidisha nafsi yake kuifikisha risala yako.

Aliichosha nafsi yake kuwalingania watu kwenye dini yako. Alijishughulisha kwa kutoa nasaha kwa watu waliostahiki wito wako. Alihamia ugenini mahali mbali na maeneo ya vipandwa vyake na maweko ya miguu yake mbali na alipozaliwa mbali na maeneo yafurahishayo nafsi yake. Akitaka kuienzi dini yako na kuomba msaada dhidi ya makafiri wasiokuamini wewe. Mpaka yalitimia aliyojaribu kuyafanya dhidi ya maadui wako. Na yalifanikiwa aliyoyapanga kwa ajili ya wapenzi wako. Aliibuka na ushindi kwa msaada wako akiwa na nguvu kwa nusura yako pamoja na udhaifu wake. Aliwapiga wakiwa ndani ya miji yao.

Aliwahujumu ndani ya makazi yao mpa amri yako ilishinda neno lako likawa juu kabisa ingawaje washirikiina walichukia. Ewe Mwenye enzi Mungu mwinuwe kwa kuwa ametaabika kwa ajili yako, afikie daraja la juu kabisa katika jannah zako ili asilingane kwa daraja. Ili asiwe rika katika daraja wala malaika waliokaribu wasimkurubie hata Nabiy mursalu. Umtambulishe katika Ali wake waliotakaswa na umma wake walio waumini kuwa watakuwa na uombezi mwema zaidi ya vile ulivyo muahidi. Ewee mtekelezaji wa ahadi mtimizaji wa qauli. Ewee! mwenye uwezo wa kubadilisha maovu kwa mema mengi hakika wewe ndio mwenye fadhila tukufu mno.

DUA YA 3

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE KWA MALAIKA WABEBAO ARSHI NA KWA KILA MALAIKA

Ewe Mola na kwa wabeba arshi yako ambao hawalegei kukusabihi wala hawachoki kukutakasa, wala hawafifii kukuabudu wewe hawazembei kufanya bidii katika amri yako. Na wala hawaghafiliki kuwa na nguvu ya mapenzi yako. Na Israafil malaika wa baragumu amesimama tayari angoja idhini yako tu na amri yako ili awazinduwe kwa pulizo waliotupwa chini makaburini. Na Mikail mwenye hadhi kwako na nafasi ya daraja la juu katika kukutii wewe. Na Jibril atambulikaye kwa uaminifu kufikisha wahyi (ufunuo) wako, mwenye kutiiwa na wakazi wa mbingu yako mwenye kuheshimiwa mbele yako na mwenye kusogezwa karibu na wewe. Na roho ambaye yuna ngazi ya juu miongoni mwa malaika wa hijabu, na roho ambaye ni amri yako, Ewe Mola warehemu na wale malaika walio chini yao miongoni mwa wakazi wa mbingu zako ambao ni miongoni mwa waamini wao kwa risala yako (jumbe) ambao hawachoshwi na hali ya kudumu wala hawaishiwi nguvu kwa kazi ngumu wala hawalegei. Wala hawasumbuliwi na matamanio ili waache kuku takasa wewe. Hawakatishwi na wakati wa usahaulifu katika kukutukuza. Wanyenyekevu wa macho hawathubutu kuinua macho yao kukuangalia videvu vyao viko chini ambao utashi wao umekuwa mrefu kwa yaliyo kwako. Wamerukwa na akili kwa upendo wa kuzitaja neema zako. Wanyenyekevu mbele ya utukufu wako na utukufu wa ukubwa wako. Wasemao waangaliapo jehanam ikiunguruma kwa ajili ya wanaokuasi, utakasifu ni wako hatujakuabudu ipasavyo kukuabudu wewe. Hivyo basi uwarehemu na rawhaniyyeena miongoni mwa malaika wako na wale wenye ukaribu kwako.Na wale wapelekao mambo yaliyo ghaibu kwa mitume wako na walioaminiwa kwa wahyi wako.Na kabila za malaika uliowafanya mahsusi kwa ajili yako na uliowaepusha na haja ya chakula na kinywaji kwa kukutakasa wewe uliowafanya waishi ndani ya tabaka za mbingu zako. Na ambao watasimama kwenye mipaka ya mbingu iteremkapo amri kwa kutimia ahadi yako.

Wahifadhi wa mvua na watawanyaji wa mawingu ambaye kwa sauti ya karipio lake husikika muungurumo wa radu. Na mrindimo wa mawingu unapoelea kuelekea kwenye umeme sauti ya muwako itajitokeza. Na mpelekaji wa theluji na baridi na wateremkao na matone ya mvua yateremkapo na walinzi wa hazina za upendo. Mawakala wa ulinzi wa mirima isije poromoka. Na wale uliowajulisha uzito wa maji na vipimo vilivyomo katika mvuwa kubwa na wingi wake. Na malaika ambao ni wajumbe wako kwa wana ardhi kwa mambo yachukizayo na yashukayo miongoni mwa balaa na raha ipendwayo. Na malaika watukufu waandishi na malaika wa mauti na wasaidizi wake. Na Munkari na Nakiiri. Na Ruman mtahini wa kaburini na wazunguka Baitul-maamur na Maliki malaika mlinzi wa moto na Rizwan malaika walinzi wa jannah. Na ambao (hawamuasi Mungu aliyowaamrisha na wafanya wanayo amriwa). Na ambao husema (salamu iwe juu yenu kwa vile mulivumilia neema ni nyumba ya mwisho). Na Mazabaniya ambao wakiambiwa: (Mchukuweni mtupeni kisha mchomeni katika jehannam) watamharakia upesi sana hawatompa muda.Na yule ambaye tumeshindwa kumtaja na hatukujua mahali pake kwako na kwa jambo gani umemuwakilisha.Na malaika wakazi wa hewani na ardhini na majini, na wale uliowawakilisha kwa viumbe.Warehemu siku ambayo kila nafsi itakuja ikiwa na msukumaji na shahid. Uwarehemu kwa rehema zitakazo wazidishia heshima juu ya heshima zako na kuwazidishia usafi juu ya usafi wao. O Mola ukiwarehemu malaika wako na wajumbe wako na kuwafikishia (maombi yetu ya) rehma kwao (twakuomba) uwarehemu kwa kauli njema uliotufungulia kwa ajili yao. Wewe ni mpaji mkarimu.

Dua ya 4

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE AMANI IMFIKIE KATIKA KUWA TAKIA REHMA WAFUWASI WA MITUME NA WALIO WASADIKI MITUME

Ewe Mola na kwa ajili ya wafuasi wa mitume na waliowasadiki bila kuonekana miongoni mwa wana wa ardhini wanapokabiliwa na upinzani wa wale wanaowapinga kwa kuwafanya waongo. Na kuwaonea shauku mitume kwa njia ya iymani ya hakika. Ulituma katika kila muda na zama uliwatuma mitume wakiwa na dalili kwa ajili ya watu. Tokea Nabiy Adam mpaka zama za Muhammad (s.a.w.) miongoni mwa maimamu waongofu na viongozi wa wachamungu wote amani iwafikie. wakumbuke kwa msamaha na ridhaa. Ewe Mola khususan kwa swahaba wake Muhammad waliokuwa wema katika usuhuba. Waliokuwa na majaribu mema katika kumsaidia na kumhami. Walimwitikia kwa haraka alipowasikilizishia hoja za ujumbe wake. Walitengana na wake, na watoto ili kulidhihirisha neno lake. Waliwapiga vita mababa na watoto ili kuuthibitisha unabiy wake kupitia kwake walishinda. Waliozingirwa na upendo wake watarajia biashara ambayo haitokuwa na hasara katika upendo wake. Na wale waliotengwa na jamaa zao pale tu waliposhikamana naye, na ukiraba kwao ulikwisha ili tu wakitulia chini ya kivuli cha ukaribu wake. Hivyo basi ewe Mola usiwasahau kwa yale waliyoyaacha kwa ajili yako na katika wewe waridhishe kwa ridhaa zako. Kwa ajili ya faida ya viumbe wamejitoa kwako. Walipokuwa na mjumbe wako walikuwa walinganiaji wako kwa ajili yako, waonyeshe ridhaa yako kwa kuhama nyumba za watu wao kwa ajili yake na kutoka kwao nje ya maisha ya wasaa na kwenda kwenye maisha ya dhiki. Wale ambao kwa kudhulumiwa kwao umewazidishia ili kuienzi dini yako. Ewe Mola wape taabeena waliotenda mema kwa kufuata nyayo za masahaba.Wanasema: (Ee! Mola wetu tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa iymani) malipo yako yaliyomema kwa waliokwenda njia yao waliochagua mwendo wao na walikwenda kwa utaratibu wao hawakugeuzwa upande na shaka katika utambuzi wao. Na wala hawakuingiwa na shaka katika kufuata nyayo zao na kuongoka na mwongozi wa nuru yao.Waendesha dini yao hali ya kuwahami na kuwasaidia.Wanaongoka kwa mwongozo wao, wanawafikiana nao. Wala hawawatuhumu kwa yale waliowapa. Ewe Mola wape rehma taabeena toka siku yetu hii mpaka siku ya malipo na rehma iwafikie wake zao na kizazi chao na wale waliokutii miongoni mwao. Rehma ambayo itawalinda wasikuasi na itawapatia nafasi katika maeneo ya janna yako.

Na itawakinga na makidi ya shetani. Na itawasaidia kwa yale waliokuomba msaada kwa ajili yake miongoni mwa wema. Na itawalinda na matukio ya ghafla ya usiku na mchana isipokuwa tukio lijalo kwa wema. Kwazo utawaimarisha kuwa na iymani ya matarajio mema kwako na kutumai yale uliyonayo. Na watokane na tuhuma kwa ajili ya yale yaliyomo mikononi mwa waja. Ili uwarejeshe kwenye upendo wako na kukuogopa wewe. Washawishhi waache kupigania wingi wa mapato ya haraka. Na uwapendezeshe kufanya mema kwa ajili ya baadaye na kujiandaa kwa yatakayojitokeza baada ya umauti. Na uwafanyie wepesi kila tatizo litakalo wafika siku nyoyo zitokapo nje ya viwili wili vyake. Na uwaepushe na yaletayo fitna miongoni mwa yaliyo hadharishwa, kutupwa motoni na kubaki milele humo.Uwafanye wawe katika amani miongoni mwa makazi ya wachamungu.


2

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

DUA YA 5

NA ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE KWA AJILI YAKE MWENYEWE (A.S) NA KWA WALIO CHINI YA WILAYA YAKE

Ewee! ambaye maajabu ya utukufu wake hayatokwisha. Mrehemu Muhamadi na Ali zake tuzuwiye kupotoka katika utukufu wako. O we ambaye muda wa ufalme wake hautakoma. Mrehemu Muhammad na Aali zake zikomboe shingo zetu na lipizi zako. Oh! wee ambaye hazishi hazina za rehma zake mrehemu Muhammad na Aali zake. Na utupe sehemu katika rehema zako, Oh wee ambaye macho yanashindwa kumwona. Mrehemu Muhammad na Aali zake, tusogeze karibu yako. Oh! wee ambaye unakuwa mdogo ukubwa wa kila kikubwa mbele yake. Mrehemu Muhammad na Aali zake utupe heshima. Oh, wee ambaye mbele yake hujitokeza kila kilichojificha. Mrehemu Muhammad na Aali zake. Usitufedheheshe mbele yako. Ewe Mola! tuonndolee haja ya hiba ya watowao hiba kupitia hiba zako. Tutosheleze tusisumbuliwe na kitwea cha wajitengao nasi kwa mawasiliano yako ili tusimsihi yeyote pamoja na kuwa wewe watupa bure. Wala tusione kitwe kutokana na yeyote ikiwa fadhila zako twazipata. Ewee Mola! Mrehemu Muhammad na Aali wake. Na utupangie wala usipanguwe dhidi yetu. Tupe ushauri kwa faida yetu wala si kinyume chake. Mzunguko wa neema udumishe kwetu wala usiuelekeze kwingine. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aali zake na utulinde sisi kuwa dhidi yako. Na utulinde kupitia wewe mwenyewe.

Utuongoze kuelekea kwako wala usituweke mbali na wewe. Kwa hakika umlindaye huwa salama. Na umwongozaye hujuwa. Umwekaye karibu nawe hupata ngawira. Ewee Mola mrehemu Muhammad na Aali zake. Na tukinge na makali ya mabadiliko ya wakati, na shari ya windo la shetani. Na ukali wa udhalimu wa kisultani Ewe Mola kwa hakika wajitoshao wajitosha kwa fadhila za uwezo wako. Msalie Muhammad na Aali zake kwa hakika hutowa watowao kupitia wingi wa utajiri wako. Mrehemu Muhammad na Aali zake na utupe, huongoka waongokao kwa nuru ya uso wako, msalie Muhammad na Aali wake na tuongoze. Ewe Mola hakika uliyemfanya rafiki hakumdhuru kutelekezwa na watelekezaji. Na uliyempa hapungukiwi kwa kunyimwa na wanyimaji. Na uliyemwongoza haumpotezi upotovu wa wapotovu. Mrehemu Muhammad na Aali zake. Na utuzuiye (tusidhuriwe na waja wako) kwa nguvu zako. Tutosheleze tusimhitaji mwingine mbali na wewe kwa kuungwa mkono na wewe. Tupitishe njia za haki kwa mwongozo wako. Ewe Mola msalie Muhammad na Aali zake. Na jaalia usalama wa nyoyo zetu kwa kukumbuka utukufu wako. Na nafasi ya wazi ya miili yetu iwe twakushukuru neema zako. Na ujaaliye mtiririko wa ndimi zetu uwe katika kusifu ihisani zako. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aali zake. Tujaalie tuwe miongoni mwa wahitaji wako wanaowaita watu kuja kwako na viongozi wako waongozao kuelekea kwako. Na tuwe miongoni mwa watu makhsusi uliowafanya wawe makhsusi kwako. Ewe mwenye kurehemu mno kuliko wenye kurehemu wote.

DUA YA 6

NA ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE A.S. NYAKATI ZA ASUBUHI NA JIONI

Sifa njema ni za Mungu ambaye ameumba usiku na mchana kwa nguvu zake. Na amezipambanuwa kwa uwezo wake. Na amekifanyia kila kimoja kati ya hivi viwili mpaka wenye kikomo na muda ulio na mwisho. Hukiingiza kila kimoja ndani ya mwenzake. Na humwingiza mwenzake ndani.yake. Kwa mpango kutokana na yeye, kwa ajili ya waja kwa vile awalishavyo na kwa hivyo ndivyo awakuzavyo. Amewaumbia usiku ili wapumzike humo kutokana na harakati za taabu na juhudi zenye kuchosha. Na ameufanya (usiku) kuwa vazi ili wajisitiri kwa mapumziko humo kwa kulala, iwe kwao kiburudisho na nguvu mpya na waifanyie kwa huo usiku furaha na matamanio. Na amewaumbia mchana uwezeshao kuona ili wazifikie fadhila zake. Na iwe sababu ya kuipata rizki yake. Na wazunguke kwa uhuru katika ardhi yake wakitafuta kipato cha mwenye haraka ya dunia yake na kufanikiwa ya baadaye katika maisha ya akhera. Kwa yote hayo awawekea sawa hali yao na kuuzifanyia mtihani khabari zao, ili awaangalie wakoje wakati wa utii wake na mahali mwa wajibu zake. Na sehemu za hukumu zake.(Ili awalipe waliotenda maovu kulingana na waliyotenda. Na awalipe waliotenda mema wema.) Ewe Mola! sifa zote njema ni zako. Kwa kutukunjulia asubuhi, na kutufanya tufurahie mwanga wa mchana. Na umetufanya tuone jinsi ya kuitafuta chakula na umetulinda na maafa. Tumekuwa asubuhi na vimekuwa vitu vyote pamoja ni vyako. Mbingu, ardhi na ulicho kitawanya kwa kila mmoja wao chenye kutulia na chenye kufanya harakati kikazi na chenye kusafiri na kirukacho juu kabisa angani na kijifichacho chini ya ardhi twapambazukiwa na asubuhi katika ushiko wako. Twazingirwa na ufalme wako na mamlaka yako. Tumo ndani ya utashi wako. Tunakwenda hapo na pale kwa amri yako. Tunageuka geuka ndani ya mpango wako.Hatumiliki letu jambo ila ulilolipitisha, wala hatulimiliki jambo la kheri isipokuwa ulilotoa. Na hii siku mpya imekuja, itakuwa shahidi madhubuti kwetu, tukifanya mema itatuaga iondokapo kwa sifa njema. Na tufanyapo maovu itatuacha kwa lawama. Ewe! Mola msalie Muhammad na Aali wake. Na utupe uzuri wa kusuhubiana naye na utulinde na kutengana naye vibaya, kwa kutenda yasiyofaa au kutenda dhambi yeyote ile ndogo au kubwa. Tufanye tuwe na matendo mema mengi humo na tuepushe na matendo maovu humo. Na jaza kwa ajili yetu kati ya ncha zake mbili sifa njema na shukrani, ujira na akiba, fadhila na ihsani. Ewe Mola wepesisha mizigo yetu kwa waandishi watukufu, na lijaze mema yetu katika sahifa zetu (karatasi za hesabu) usitudharaulishe kwako kwa matendo yetu maovu. Ewe Mola tujaaliye hadhi toka kwa waja wako katika kila sehemu ya shukurani zako. Na ushahidi wa kweli miongoni mwa malaika wako.

Ewe Mola msalie Muhammad na Aali zake. Utuhifadhi mbele yetu na nyuma yetu kuliani kwetu na kushotoni kwetu na pande zetu zoote, hifadhi inayotulinda na kukuasi wewe, yenye kutuongoza kwenye utii wako, yenye kutekeleza upendo wako. Ewe Mola! msalie Muhammad na Aali zake. Na utukubalie katika siku yetu hii na usiku wetu huu na katika siku zetu zoote kuitenda kheri na kuihama shari na kuishukuru neema na kuzifuata sunnah na kujiepusha na bidaa, na tuwe wenye kuamrisha mema na kukemea maovu. Kuulinda Uislamu na kuutweza ubatili na kuudhalilisha ili kuinusuru haki na kuipa nguvu kumwongoza aliyepotoka kumsaidia mnyonge kumkomboa aliyekatika taabu. Ewe Mola msalie Muhammad na Aali zake. Na ifanye (siku) kuwa ya baraka mno kuliko siku ya baraka tuijuayo na mwenzi bora kuliko mwenzi yeyote tumepata kuwa naye na wakati uwe ni wakati bora kuliko wakati wowote tumepata kuwa chini ya kivuli chake. Na utufanye tuwe wenye kuridhiwa mno miongoni mwa waliopitiwa na usiku na mchana katika jumla ya viumbe wako. Wenye kushukuru sana kati yao kwa mema uliowapa miongoni mwa neema zako. Watekelezaji kwa uthabiti mno wa sheria uliowawekea miongoni mwa sheria zako. Na wenye kujizuia sana na uliyo yahadharisha miongoni mwa makatazo yako. Ewe Mola mimi nakufanya shahidi nawe nishahidi tosha. Na ninazifanya mbingu zako na ardhi zako na uliowafanya kuwa wakazi wa mbingu na ardhi kuwa mashahidi miongoni mwa malaika wako na viumbe wako wengine. Katika siku yangu hii saa yangu hii usiku wangu huu na kikazi changu hiki. Hakika mimi nashuhudia kuwa hakika wewe ni Mungu ambaye hapana Mungu mwingine isipokuwa ni wewe! mwenye kuidhibiti adala uko mwadilifu katika hukumu mwenye huruma kwa waja-u-Mfalme wa Wafalme mwenye huruma kwa viumbe. Yakuwa Muhammad ni mja wako na ni mjumbe wako mteule wako miongoni mwa viumbe wako. Umembebesha risala yako na ameitekeleza. Ulimuamuru kuitowa nasaha kwa umma wake na aliunasihi. Ewe Mola msalie Muhammad na Aali zake. Zaidi ya vile ulivyomsalia yeyote katika viumbe wako. Umpe kwa niaba yetu kilicho bora ulichompa yeyote katika waja wako. Na umlipe kwa niaba yetu kilicho bora na hheshima zaidi kuliko ulichomlipa yeyote miongoni mwa Manabiy wako kwa niaba ya umma wake. Hakika wewe ndiye mtowaji kwa wingi na msamehevu wa makubwa nawe u mwenye huruma zaidi kuliko mwenye huruma yeyote. Msalie Muhammad na Aali zake wema waliotahirika wateule waheshimiwa.

DUA YA 7

NA ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE (A.S) ANAPOTOKEWA NA JAMBO SUMBUFU AU KUSHUKIWA NA TAABU NA WAKATI WA KUKERWA

Oh! we ambaye kwake hufunguka mafundo ya mambo yachukizayo. Ee! wee ambaye kwake makali ya shida huwa butu. Ee we! ambaye huombwa njia ya kutoka kuelekea kwenye burudisho la faraja. Magumu yamekuwa dhalili mbele ya nguvu zako. Kwa huruma zako sababu zimepatikana. Kwa nguvu zako hukumu zimepita. Kwa utashi wako vitu vimekwenda kama ilivyotakiwa. Kwa utashi wako bila ya kauli yako vimewajibika. Kwa utashi wako vimejiziwiya bila ya kutumia katazo lako, wewe ndiye wa kuombwa wakati wa jambo litishalo. Na ndio kimbilio la wakati wa shida haiondoki isipokuwa ile shida ulioiondowa. Haitoki isipokuwa uliyoitowa, yameniteremkia ewe Mola wangu ambayo uzito wake umenielemea.Juu yangu kumeshuka jambo ambalo uzito wake umenishinda. Kwa nguvu zako umeshusha juu yangu kwa mamlaka yako umeelekeza kwangu.

Hakuna wa kuondowa ulichokileta, wala kuziwiya ulichokielekeza, wala wakufunguwa ulicho funga, wala wakufunga ulichokifunguwa, wala wa kufanya kiwe chepesi ulichokifanya kigumu, wala wakumsaidia uliyemwacha. Msalie Muhammad na Aali zake, na nifungulie ewe Mola wangu mlango wa faraja kwa rehma zako, niondolee mamlaka yatishayo kwa nguvu zako. Unipe mtazamo mzuri kwa malalamiko yangu. Unionjeshe utamu wa matendo kwa niliyoomba. Na unipe kutoka kwako rehmah na faraja njema. Na nijaalie mwanya wa kupenya kutoka kwako. Usinifanye nijishughulishe na mengine na kuacha wajibu wako. Na kuifanya sunnah yako. Nimezikika na yaliyo nishukia Ee Mola wangu nimejawa na huzuni kwa kuyabeba yaliyo niteremkia.Wewe ndiye mwenye uwezo wa kuondoa yaliyo nifika na kuyaweka mbali niliyoangukia, nifanyie hivyo ingawaje sistahiki kwako hivyo Ewee! bwana wa arshi tukufu.

DUA YA 8

DU'A ZAKE KATIKA KUJILINDA NA MAMBO YACHUKIZAYO NA TABIA MBAYA NA MATENDO YALAUMIWAYO

Ewe Mola najilinda na wewe dhidi ya uchochezi wa pupa na ukali wa ghadhabu na kuhemewa na husda na kudhofika kwa subira na uchache wa kutosheka na ukali wa tabia.Na uchochezi wa harara. Na kumilikiwa na msukumo wa tabia au jadhba. Na mgeuzo wa nia na kwenda kinyume na uongofu na sinzio la kughafilisha na kujikalifisha (yaani kujitwisha mambo zaidi ya uwezo) kuchaguwa batili na kuiacha haki. Na kujibakisha na kuendelea na madhambi na kuyadogesha maasi na kuukuza utii. Na kujifaharisha kwa matajiri na kuwadharau masikini na uangalizi mbaya kwa walio chini yetu. Na kutokuwa na shukrani kwa waliotutendea mema au tumsaidiye dhwalimu au kumtelekeza mwenye taabu au kujitakia yasiyo haki. Kwetu au tuongee kuhusu elimu bila ya elimu au kujihusisha na kumghushi yeyote na kujionea fahari matendo yetu. Na kuwa na matumaini marefu. Na tunajilinda na wewe kuwa na undani na kukidharau kidogo. Na kudhibitiwa na shetani. Au kuhujumiwa na wakati, au kudhulumiwa na mtawala. Na tunajilinda na wewe kufanya israfu na kuwa na kisichotosha. Na tunajilinda na wewe na masimango ya maadui. Na kukosa wenzi, na kuishi katika shida na kufa bila ya maandalizi. Na twajilinda na hasara kubwa mno na msiba mkubwa na twajilinda na mwisho mbaya, na kunyimwa thawabu na kufikwa na adhabu. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aali zake na unilinde na yote hayo kwa huruma yako na waumini wote wanaume na wanawake. Ewe! mwingi wa rehma kuliko wenye kurehemu wote.

DUA YA9

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE AKIWA NA SHAUKU SANA YA KUOMBA MSAMAHA KWA MWENYE ENZI MUNGU MTUKUFU

Ewe Mola msalie Muhammad na Aali zake, tufanye tuelekee kwenye toba uipendayo. Na ututoe tusiendelee kutenda uchukialo. Oh! Mola tusimamapo kati ya hali mbili ya upungufu iwe siku ya dini au dunia uiondoe hali ile ya upungufu haraka iishe. Na ujaalie kwangu toba iwe ya kubaki sana miongoni mwa mawili hayo. Na tuyakusudiapo mambo mawili moja la kuridhisha kutoka kwetu na la pili lakuchukiza toka kwetu. Tufanye tuelemee kwenye lile likuridhishalo toka kwetu. Dhoofisha nguvu zetu kwenye linalokuudhi na kutuchukia kwa ajili yake. Usiziache nafsi zetu kuchaguwa kwa sababu zenyewe huchaguwa batili isipokuwa ulizozipa taufiki. Na zenye kuamrisha mabaya isipokuwa ukirehemu. Ewe Mola kutokana na unyonge umetuumba, na umetujenga juu ya hali duni umetuanza (kutuumba) kutokana na maji hafifu. Hatuna uwezo isipokuwa kwa nguvu zako, wala nguvu hatuna isipokuwa kwa msaada wako. Tuwezeshe kwa kutufanikisha. Tuongoze kwenye njia ya sawa kwa mwongozo wako.

Ipofushe nguvu ya kuona ya nyoyo zetu dhidi ya yaendayo kinyume na mahaba yako. Usikijaalie chochote katika viungo vyetu vya mwili upenyo wa kwenye maasi yako. Ewe Mola! mrehemu Muhammad na Aali zake. Na jaalia nong'ono za nyoyo zetu na harakati za viuongo vyetu na mitupo ya macho yetu na semi za ndimi zetu viwe kwa ajili ya mambo yawajibishayo thawabu zako. Ili tusije pitwa na jema twastahiki kwalo malipo yako. Na usitubakishie tendo baya ambalo tutastahiki kwa ajili yake adhabu yako.

DUA YA 10

MIONGONI MWA DU'A ZAKE AKIOMBA KIMBILIO KWA MUNGU

Ewe Mola! Ukipenda tusamehe kwa fadhila zako na ukipenda utatuadhibu na hiyo itakuwa kwa uadilifu wako. Hivyo basi tufanyie wepesi msamaha wako kwa huruma yako. Tuepushe na adhabu yako kwa subira zako. Kwa kuwa hatuna uwezo kuukabili uadilifu wako. Wala hakuna atayeokoka bila ya msamaha wako. Ewe mwenye kujitosheleza kuliko matajiri wote. Tu hapa waja wako mbele yako. Nami ni fakiri kuliko mafakiri wote kwako. Urekebishe ufakiri wetu kwa wasaa wako. Usikate matumaini yetu kwa zuio lako, utakuwa umemdhalilisha mwenye kukuomba heri. Na umemnyima aliyekuomba fadhila zako. Kwa hiyo tugeukie kwa nani mbali na wewe, twende! Wapi kama si mlangoni kwako! Utakatifu ni wako, sisi ni wenye kudhikika ambao umewajibisha kuwakubalia. Ni wenye uovu uliowaahidi kuwaondolea uovu wao. Ni kitu chafanana sana na utashi wako. Na ni bora kulingana na utukufu wako, kumuhurumia aliye kuomba umuhurumie. Kumsaidia aliekuomba msaada uhurumie ungamo letu kwako. Tutosheleze tujitupapo mbele yako. Oh! Mola wetu hakika shetani ametusimanga, kwa kuwa tumemfuata katika kukuasi wewe. Mrehemu Muhammad na Aali zake usimwache atusimange baada ya kuwa tumemwacha kwa ajili yako. Tumemtelekeza na kuelekea kwako.

3

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

DUA YA 11

DU'A ZAKE KWA AJILI YA MWISHO MWEMA

Ewe! mwenye utajo wake ni heshima kwa wamtajao. Ewe! mwenye shukrani yake ni ufanisi kwa wenye kumshukuru. Owe! Mwenye utii wake ni uokovu kwa wenye kumtii. Mswaliye Muhammad na Aali zake. Zihangaishe nyoyo zetu katika kukutaja wewe na kuziweka mbali na utajo mwingine wote. Na zihangaishe ndimi zetu katika kukushukuru na ziwe mbali na shukuru zingine zote. Na viungo vyetu vya miili vihangaike kukutii wewe na kuwa mbali na utii mwingine wowote. Ukitupangia wakati wa faragh (usio na kazi) basi jaalia faragha iliyo salama. Tusifuatwe na lipizi baya, wala usituambatanishie humo na kuchoshwa, ili watuondokee waandishi wa maovu na nyaraka tupu zisizotaja chochote katika maovu yetu. Na warudi waandishi wa mema kutoka kwetu wakiwa na furaha na waliyoyaandika miongoni mwa mema yetu. Na ziishapo siku za maisha yetu na kumalizika kwa muda wa umri wetu. Na kutufikia wito wako ambao hapana budi utufikie na pia hapana budi kuujibu. Msalie Muhammad na Aali zake. Na jaalia mwisho wa matokeo ya hesabu ya waandishi wa mabaya yetu kuwa toba yenye kukubaliwa. Usitusimamishe na dhambi tuliyotenda baada yake, wala maasi tuliyoyafanya, wala usifichue sitara uliyotusitiri mbele ya mashahidi siku zitakapojaribiwa khabari za waja wako. Hakika wewe ni mpole kwa akuombaye na u mwenye kuitika kwa akuitaye.

DUA YA 12

DU'A ZAKE KATIKA KUKIRI NA KUOMBA TOBA KWA MUNGU MTUKUFU

Ewe Mola! tabia tatu zaniziwiya kukuomba na moja yanihimiza nikuombe, iniziwiayo jambo umeamrisha na nikazembea kulifanya. Na katazo umenikataza nikaharakia kulitenda. Na neema ulinineemesha nayo nikashindwa kuishukuru. Na linihimizalo kukuomba ni fadhila zako kwa mwenye kuelekeza uso wake kwako. Na akaja kwa dhana nzuri kwako kwa kuwa ihsani zako zote ni fadhila. Na kwa sababu neema zako zote ni mwanzo mpya. Basi mimi huyu hapa Ewee! Mola wangu mwenye kusimama kwenye mlango wa enzi yako msimamo wa aliyesalim amri dhalili.Nikikuomba nikiwa na haya ombi la fakiri hohe hahe mnyonge. Mwenye kukiri kwako, sikusalimu amri wakati wa ihsani yako isipokuwa kwa kujiweka mbali na maasi yako. Sijapata kuwa katika hali zangu zote bila ya huruma zako. Je kutanifaa ewe Mola wangu kukiri kwangu kwako kwa maovu niliyotenda? Je kutaniokoa kutambua kwangu kwako kwa mabaya niliyotenda? Au utawajibisha makasiriko yako kwangu katika kikao changu hiki? Au chukio lako litaniambata wakati wa DU'A yangu? Utakatifu ni wako, sikati tamaa nawe hali umenifungulia mlango wa toba kwako. Bali nasema usemi wa mja mnyonge mwenyekujidhulumu nafsi yake, mwenye kuifanya haramu ya Mola wake kuwa kitu chepesi. Ambaye dhambi zake zimekuwa kubwa mno. Ambaye siku zake zimemtumbia mgongo na kutokomea. Mpaka aonapo muda wa kazi ya ibada umeisha. Na upeo wa umri umekwisha. Na akawa na yakini kuwa hana njia ya kujiepusha nawe, na hana kimbilio litalomweka mbali nawe.

Akugeukia kwa marejeo ya mara kwa mara, na kufanya toba kwako kwa ikhlaswi. Atasimama mbele yako kwa moyo safi kabisa. Na kukuomba kwa sauti dhalili ya chini, ameinama mbele yako na kujipinda hali ameinamisha kichwa chake chini, woga wake watetemesha miguu yake machozi yamtiririka mashavuni mwake. Akuomba akisema Ewe mwingi wa kurehemu kuliko wote! Ewe mwingi wa kurehemu wa wanaorejea kwake wakimwomba huruma. Ewee mwenye huruma mno kwa wenye kumzunguka waombao msamaha. Ewe ambaye msamaha wake ni mwingi kuliko malipizi yake. Ewe ambaye ridhaa yake ni nyingi sana kuliko makasiriko yake. Ewe yule ambaye amesifika kwa waja wake na njema saburi njema. Ewe ambaye amewazowesha waja wake kwa kukubali marejeo yao ya mara kwa mara. Oh! yule ambaye amewarekebisha waharibifu wao kwa njia ya tobah. Oh! yule ambaye ameridhika na madogo katika matendo yao. Oh! yule ambaye huwalipa mengi kwa machache yao. Oh! yule ambaye amechukuwa dhamana kwa ajili yao kuzikubali DU'A. Oh! yule ambaye amewaahidi mwenyewe binafsi kwa fadhila zake malipo mema. Mimi sio muasi zaidi kuliko waliokuasi na umewasamehe, wala mimi si mlaumiwa mno miongoni mwa walioomba udhuru kwako na umewakubalia, wala mimi si mdhalimu mno miongoni mwa waliotubu kwako na umepokea toba yao. Natubu kwako katika kikao changu hiki toba ya mwenye kujutia waliyompita. Mwenye kutambua yaliyomzunguka, mwenye haya sana kwa yaliyo mfika, ajua kuwa kuisamehe dhambi kubwa mno haliwi jambo kubwa kwako.

Na kuyafumbia macho madhambi makubwa kabbisa haiwi ngumu kwako. kuyavumilia makosa mabaya sana ya jinai hayakupi tabu. Na yakuwa mja wako mpendwa sana kwako ni mwenye kuacha kibri mbele yako. Na akajiepusha na kung'ang'ania, kashikamana na kuomba msamaha. Nami najitakasa kwako nisiwe na kibri na ninajilinda kwako nisiwe mwenye kung'ang'ania nakuomba msamaha kwa nililozembea. Naomba msaada kwa nililohemewa ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Nipe yaliyowajibu wangu kwako, niondolee ninayostahiki kwako. Nitakase na wayaogopayo waovu. Wewe ni mwingi wa msamaha, mwenye kutumainiwa msamaha, wajulikana kuwa umvumilivu. Haja yangu haina pakuitafutia isipokuwa kwako. Wala dhambi zangu hazina wakuzisamehe asiyekuwa wewe. Je! lawezekana hilo? Sijihofu binafsi ila kwako, hakika wewe ni mstahiki wa taqwa na mstahiki wa msamaha.Mrehemu Muhammad na Aliy zake nikidhie haja yangu. Fanikisha ombi langu. Nisamehe dhambi zangu. Nipe dhamana ya woga wa nafsi yangu hayo ni mepesi kwako, aameen ewe bwana wa maumbile yote.

DUA YA 13

DU'A ZAKE KUMWOMBA HAJA MUNGU MTUKUFU

Oh Allah. Ewe! mwisho wa maombi ya haja zote. Ewe! ambaye kupitia kwake mahitaji hupatikana. Ewe! ambaye hauzi neema zake kwa thamani. Oh! yule ambaye hakipaki tope akitowacho kwa masimbulizi. Ewe! yule ambaye hutosheka kwa kupitia kwake hatosheki mtoshekaji bila ya yeye. Ewe yule ambaye hutakiwa na hauwi utashi kando na yeye. Ewe yule ambaye hazina zake hazimalizwi na maombi. Ewe yule ambaye sababu hazibadilishi hikima yake. Oh! yule ambaye hazishi kwake haja za wahitaji. Oh! yule ambaye hayampi dhiki maombi ya waombao, umesifika kwake kutokuwa muhitaji toka kwa viumbe wako. Wewe wastahiki kuwa uwahitajii wao, umewahusisha na ufakiri wao ndio wahitaji kwako. Hivyo basi mwenye kujaribu kuziba pengo lake kupitia kwako. Na akusudia kujiondolea ufakiri kwa njia yako. Atakuwa ametafuta mahitaji yake mahali pafaapo. Na atakuwa ameyaleta mahitaji yake katika njia zake. Na mwenye kuelekeza mahitaji yake kwa yeyote miongoni mwa viumbe wako au kuifanya sababu ya kufanikiwa kwake kando na wewe atakuwa amejiweka kwenye hatari ya kunyimwa. Na atakuwa amestahiki kwako kukosa ihsani. Oh! Allah ninahaja kwako. Juhudi yangu imeshindwa, mbinu zangu zimeshindwa kuifikia nafsi yangu imenishawishi kuifikisha haja yangu kwa awezaye kuifikisha kwako. Wala hajitoshi katika mahitaji yako kando na wewe, na huku ni kuteleza miongoni mwa mtelezo wa watenda makosa na ni kujikwaa wanako jikwaa watenda madhambi. Kisha nilizinduka kwa kumbusho lako kwangu kutokana na mghafala wangu. Nimeinuka kwa taufiki yako kutoka kwenye mtelezo wangu.

Nimeimarika kwa imarisho lako na kujitoa kwenye telezo langu. Nasema subhana Rabiy (utakatifu ni wa Mola wangu), vipi muhitaji amwomba muhitaji mwingine? Ni vipi asiyekuwa na kitu amwomba asiyekuwa na kitu mwingine! Hivyo nimekuja kwako ewe Mola wangu kwa upendo, nimeyaelekeza matumaini yangu juu yako kwa kukuamini. Na nimejua kuwa mengi nikuombayo ni kitu kidogo mbele ya utajiri wako. Mazito nikuombayo ni kidogo kulinganisha na wasaa wako. Na ukarimu wako hautakuwa mdogo kwa sababu ya ombi la yeyote. Na kwa hakika mkono wako kwa utowaji uko juu kuliko kila mkono. Ewee Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake, nichukuwe kwa ukarimu wako kwa kunifadhili. Na usinichukuwe kulingana na uadilifu wako si kwa ninavyostahiki. Mimi si wa kwanza kukusihi miongoni mwa aliokusihi umempa hali ilikuwa astahiki kunyimwa. Na wala si kuwa mwombaji wa kwanza katika aliyekuomba na ukamfadhili hali ya kuwa alikuwa apaswa kunyimwa. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Na nikubalie ombi langu kwa wito wangu kuwa karibu. Uhurumie unyenyekevu wangu, isikilize sauti yangu, usiyakate matumaini yangu, usikate kiungo changu na wewe. Usinielekeze kwa haja yangu hii au nyingine kwa mtu mwingine. Nitilie manani ili kufanikisha ombi langu, na kidhi haja yangu ili kukipata nilichokiomba kabla sijatoka hapa niliposimama, kwa kunirahisishia kwako mimi magumu. Na uzuri wa kunikadiria kwako katika mambo yote. Mrehemu Muhammad na Jamiy yake, rehema ya kudumu na yenye kukuwa, kuendelea kusiko katika. Muda wake uwe hauna mwisho. Fanya hivyo iwe ni msaada kwangu, na iwe ndio sababu ya kufanikiwa ombi langu.Wewe ni mwenye wasaa mkarimu na miongoni mwa haja zangu ewe bwana wangu ni fulani na fulani (hapo utafanya sijda na kuisema haja yaneyewe badala fulani fulani). (Useme haya ukiwa ndani ya sijda):- Fadhila zake zimenipa raha. Ihsani yako imenionyesha njia. Nakuomba kwako na kwa Muhammad na Aliy wake ziwafikie rehma zako usinirudishe kinyume na matumaini yangu.

DUA YA 14

MIONGONI MWA DU'A ZAKE AKIFANYIWA UCHOKOZI NA AONAPO ASIYOYAPENDA TOKA KWA WADHALIMU

Ewe! ambaye hazifichiki kwake habari za waliolemewa. Oh! wee ambaye kuhusu visa vyao ahitajii ushahidi. Oh! wee ambaye msaada wake upo karibu na wadhulumiwa. Ewe! ambaye msaada wake uko mbali na wadhalimu. Unajua ewe Mola wangu alivyoniumbua (fulani bin fulani) uliyomhadharisha na amekiuka kwangu uliyomkataza. Akionyesha hali ya kutokuwa na shukrani kwa neema zako kwake. Akidanganyika na uliyomkataza. Ewe Mola! mrehemu Muhammad na Aliy zake. Mchukue aliyenidhulumu adui yangu kwa nguvu zako. Dugisha makali yake dhidi yangu kwa uwezo wako. Mshughulishe na aliyonayo, na ashindwe kumfikia amfanyiaye uadui ewe Mola! msalie Muhammad na Aliy zake, usimwachie anidhulumu. Nipe msaada mwema dhidi yake, nilinde na mfano wa vitendo vyake, usiniweke katika hali kama yake, ewe Mola! wangu mswalie Muhammad na Aliy zake. Na unisaidie dhidi yake msaada wa papo kwa papo, uwe kitulizo cha ghadhabu yangu kwake na kumaliza makasiriko yangu kumwelekea 'yeye. Ee Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake.Nifidie msamaha wako kwa dhulma yake kwangu. Nibadilishie uovu wa matendo yake kwangu iwe rehma zako kwangu. Kila chukizo kubwa liko chini kuliko ghadhabu zako. Na kila afa si sawa kulinganisha na ghadhabu zako. Ewe! Mola wangu kama ulivyonifanya nichukie kudhulumiwa, basi nilinde nisidhulumu. Ewe Mola sitolalamika kwa yeyote mbali na wewe. Na sitoomba msaada kwa hakimu ambaye si wewe. Vipi nithubutu hivyo! msalie Muhammad na Aliy zake. Iunganishe DU'A yangu na jibu, yakutanishe malalamiko yangu na mabadiliko. Ewe Mola wangu, usinifanyie majaribu ya kukata tamaa na insaafu yako. Wala usimfanyie yeye majaribu ya kujiona yuko salama na makatazo yako, asijeendelea kunidhulumu. Na kunizuia nisipate haki yangu. Mtambulishe haraka ulivyomuahidi mtenda dhulma. Na nijulishe mimi ahadi yako kuwajibu wenye kuzidiwa.

Ewe Mola msalie Muhammad na Aliy zake, unipe taufiki ya kukubali uliyoniamulia kwa faida yangu na kinyume chake, nifanye niridhie uliyochukua kwa ajili yangu na uliyoyacbukuwa kutoka kwangu.Niongoze kwenye lililo sawa, na nitumikishe kwa lililo salama. Ewe Mola ikiwa ni bora kwangu uonavyo ni kuahirisha kuchukua kwa ajili yangu na kuacha kulipiza kisasi kwa aliyenidhulumu mpaka siku ya maamuzi na mkusanyiko wa magonvi! basi msalie Muhammad na Aliy zake.Nipe nguvu kutoka kwako kwa nia ya kweli na subira ya kudumu, nilinde na utashi mbaya na pupa ya wachoyo. Nifanyie picha ya mfano moyoni mwangu wa ulicho nihifadhia miongoni mwa thawabu zako na ulilomwandalia mgomvi wangu miongoni mwa malipo yako na adhabu yako. Fanya hilo iwe ndiyo sababu ya kukinai kwangu uliyohukumu na ithbati kwangu kwa uliyoyachagua. Ameen Oh! bwana wa malimwengu hakika wewe u mwenye fadhila kubwa na wewe u muweza wa kila kitu.

DUA YA 15

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE (A.S.) AKIWA MGONJWA AU AKISUMBULIWA NA JAMBO AU KUPATWA NA BALAA

Oh! Mola wangu sifa njema ni zako kwa vile nipo katika hali ya salama ya kiwiliwili changu. Sifa njema ni zako kwa kuwa ndio sababu ya uele kiwili wili changu. Sijui ewe Mola wangu ni ipi katika hali mbili hizi unastahiki kushukuriwa zaidi? Na upi katika nyakati mbili hizi uliobora kukuhimidi? Je ni wakati wa siha njema ambao umenipendezesha humo riziki zako nzuri, na umenipa uzima humo nitake radhi zako na fadhila zako. Kwayo umenipa nguvu kwa yale uliyonipa taufiki katika utii wako? Au wakati wa uele ambao humo umenichuja. Na neema ambazo umenitunukia? Ili kufanya wepesi yaliyonitopea juu ya mgongo wangu miongoni mwa makosa na kunitakasa maovu niliyozama ndani yake. Na kuniongoza kwenye toba na ukumbusho wa kuondoa matendo yasiyofaa kwa njia ya neema za hapo nyuma. Na kwa yote hayo yale waliyoniandikia malaika wawili waandishi wa matendo yangu mema ambayo moyo haukuweza kuyafikiria wala ulimi haukuweza kutamka wala kiungo cha mwili hakijatenda bali ni ufadhili mtupu toka kwako kwa ajili yangu.

Na hisani miongoni mwa matendo yako ya hisani kwangu. Ewe Mola msalie Muhammad na Aliy zake. Nipendezeshe uliyoyaridhia kwangu. Nifanyie wepesi uliyoniteremshia, nitakase uchafu nilioutanguliza. Nifutie shari niliyoitanguliza. Nionyeshe utamu wa afya njema, nionjeshe hali poa ya usalama. Na jaalia kutoka kwangu kwenye uele iwe kuelekea kwangu kwenye msamaha wako. Na mgeuko wangu toka kwenye kulemewa kwangu uwe ndio mwelekeo wangu kwenye kufumbiwa macho kwako. Epuko langu toka kwenye dhiki yangu liwe kuelekea kwenye burudisho lako. Usalama wangu toka kwenye shida hii uwe kuelekea faraja yako. Hakika wewe ni msifika kwa ihsani mwingi wa ihsani na huruma. Mpaji mkarimu mwenye utukufu na wema.

DUA YA 16

DU'A ZAKE AOMBAPO KUJITOA KWENYE DHAMBI ZAKE AU AKINYENYEKEA KUOMBA MSAMAHA WA DOSARI ZAKE

Oh! wee ambaye kwa rehma zake wanaomba msaada watenda dhambi. Oh! wee ambaye kwa kukumbuka ihsani yake hukimbilia wenye dhiki. Oh! wee ambaye kwa kumwogopa hulia wakosaji. Oh! wee faraja ya kila mpweka mgeni, Oh! we mfariji wa kila mwenye huzuni. Oh! wee msaada wa kila aliyetelekezwa mpweka. Oh! we msaidizi wa kila muhitaji aliyefukuzwa. Wewe ndiye ambaye umeeneza kwa kila kitu rehma na elimu. Na wewe ndiye ambaye umemfanyia kila kiumbe awe na hisa katika neema zako. Nawe ndiye ambaye msamaha wake uko juu zaidi kuliko adhabu zake. Wewe ndiye ambaye zatiririka rehma zake mbele ya ghadhabu zake. Na wewe ndiye ambaye upaji wake zaidi kuliko nyimo lake. Na wewe ndiye ambaye viumbe wote wamefunikwa na rehema zake, wewe ndiye ambaye hapendi malipo toka kwa aliyempa. Wewe ndiye ambaye hazidishi adhabu ya aliyemuasi. Mimi ewe! Mola wangu ni mja wako ambaye uliyemuamuru kukuomba. Akasema: Labeika na niko chini ya utumishi wako. Ni hapa ewe! bwana wangu nimejitupa mbele yako. Mimi ndiye yule ambaye makosa yameuzidi uwezo wa mgongo wake. Mimi ni yule ambaye madhambi yamemaliza umri wake. Na mimi ni yule ambaye kwa ujinga wake amekuasi, hali ukiwa haukustahiki hivyo toka kwake. Je! ewe Mola wangu utamrehemu akuombaye ili nikithirishe DU'A? Au utamsamehe mwenye kukulilia ili nifanye haraka kulia. Au wewe ni mwenye kumfumbia macho mwenye kutia mchanga uso wake kwa ajili yako akijidhalilisha? Au wewe ni mwenye kumtosheleza mwenye kushitakia kwako ufakiri wake akiwa na matumaini! Ewe Mola wangu usimvunje moyo ambaye asiye mpata mpaji mwingine mbali nawewe.

Usimtelekeze asiyeweza kujitosheleza kando yako na mwingine yeyote. Ewe Mola wangu mrehemu Muhammad na Aliy zake. Usinitumpie hali nimekuelekea. Usininyime hali nimekuomba, usinipige kofi la uso kwa kunikatalia hali nimesimama mbele yako. Wewe ndiye uliyejisifu nafsi yako kwa rehema. Basi mswalie Muhammad na Aliy zake nirehemu. Wewe ndiye uliyejiita mwenyewe kuwa umsamehevu, basi nisamehe. Waona ewe Mola wangu mbubujiko wa machozi kwa kukuogopa, yote hayo ni haya nionayo kwa ubaya wa matendo yangu. Kwa ajili hiyo imezima sauti yangu kukulilia. Umebutuka ulimi wangu sinong'oni nisalipo. Ewe Mola wangu yako ni sifa njema aibu ngapi umenisitiri hukunifedhehi dhambi ngapi umezifunika kwa ajili yangu hukunifanya niwe mashuhuri kwazo. Makosa mangapi nimeyatenda wala hukunichania pazia la sitara, wala haukunibandika utepe wa chuki ya fedheha yake, wala haukudhihirisha aibu yake kwa atafutaye aibu zangu miongoni mwa majirani wangu na wenye husda ya neema zako kwangu. Hata hivyo hayakuniziwiya yote hayo nimepita kwenye maovu uliyoyajuwa kwangu. Hivyo basi ni nani mjinga zaidi wa mwongozo wake ewe Mola wangu kuliko mimi?

Nani mwenye kughafilika mno na hadhi yake kuliko mimi? Nani yu mbali sana na kuirekibisha nafsi yake kuliko mimi? Kwa kuwa naitumia riziki yako uliyoniruzuku katika mambo uliyonikataza miongoni mwa maasi yako. Nani aliyezama mbali sana katika mambo ya batili na mwenye kuyaendea maovu kuliko mimi? Nisimamapo kati ya wito wako na wito wa shetani huufuata wito wake bila kuwa niko kipofu katika kumjua wala sifanyi hivyo kwa kuwa kuna usahaulifu katika kumtambua. Hali yakuwa ninayakini kuwa mwisho wa wito wako ni peponi. Na mwisho wa wito wake ni motoni, utakatifu ni wako. Ajabu iliyoje juu ya ushahidi ni ubebao dhidi yangu mwenyewe. Na hesabu toka yaliyojificha katika mambo yangu? Ajabu kubwa kuliko hiyo ni ule upole wako kwangu na kwenda kwa utaratibu bila kuniharakishia. Hiyo si kwamba ninayo heshima kwako; bali ni uvumilivu wako kwangu, na ni fadhila zako juu yangu.Ili nijiepushe na maasi yako ya kukasirishayo, nipate mwanya wa kujing'oa toka maovu yangu yaniaibishayo. Kwa sababu kunisamehe wapendezwa sana kuliko kuniadhibu. Bali mimi ewe! Mola wangu ninadhambi nyingi sana na nyayo mbaya sana na matendo ya ovyo mno. Najitumbukiza vibaya sana katika batili. Niko dhaifu mno kuwa macho katika utii wako.

Ni mchache mno wakuzindukana na makamio yako na kuyachunga. Kwa kiasi cha kuweza kuzidhibiti aibu zangu. Au kuweza kuzikumbuka dhambi zangu kwa hayo nailaumu nafsi yangu tu nikiwa na tamaa ya huruma yako ambayo kwayo ndiyo kurekebika kwa mambo ya wenye dhambi. Na kutaraji rehma zako ambazo kwazo ndiyo ukombozi wa shingo za wakosaji. Oh! Mola hii ni shingo yangu imeshikwa utumwa na dhambi, msalie Muhammad na Aliy zake. Ikomboe kwa msamaha wako. Huu mgongo wangu umetopewa na makosa. Msalie Muhammad na Ali zake, uupunguzie uzito wake kwa huruma yako. Ewe Mola wangu lau ningekulilia mpaka zidondoke mbone za macho yangu na niliye mpaka ikatike sauti yangu. Na nisimame kwa ajili yako mpaka zifure nyayo zangu, na nirukuu kwa ajili yako mpaka ung'oke mgongo wangu, na nisujudu kwa ajili yako mpaka macho yangu yang'oke, na nile mchanga wa ardhini umri wangu wote, na ninywe maji yenye jivu mpaka mwisho wa umri wangu, na niwe na kutaja muda wote huo mpaka ulimi wangu uwe butu nisiinuwe uso wangu vyote hivyo nikikuonea haya isingewajibika kufutiwa ovu moja miongoni mwa maovu yangu. Ingawaje ulikuwa wanisamehe inapobidi nipate msamaha wako, na wanisamehe ninapostahiki msamaha wako. Kwani hilo haliwi wajibu kwa ajili yangu kwa kustahiqi wala silipati hilo kwa kuwa ni wajibu. Kwa kuwa malipo yangu toka kwako toka nilipokuasi kwa mara ya kwanza ilikuwa ni moto. Hivyo basi endapo utaniadhibu wewe sidhwalimu kwangu. Oh! Mola wangu kwa vile ulisitiri aibu yangu wala haukunifedhehi, ulinivumilia kwa ukarimu wako wala haukuniharakia. Ulinifanyia huruma kwa fadhila zako hukuibadilisha neema zako kwangu wala hukuyaboronga matendo yako mema kwangu. Hurumia unyenyekevu wangu wa muda mrefu. Na ukali wa umasikini wangu. Hali yangu mbaya. Ewe Mola msalie Muhammad na Aliy zake. Nilinde na maasi, nifanye niwe mtii, niruzuku kurejea kwako mara kwa mara, nisafishe kwa toba, nipe nguvu kwa kunilinda, nirekebishe kwa afya, nionjeshe utamu wa msamaha, nijaalie niwe niliye kombolewa kwa msamaha wako na niliyekombolewa utumwa kwa rehma zako, niandikie dhamana ya kutokasirikiwa nawe, nipe bishara ya haraka si ya baadaye bishara niitambuayo, itambulishe kwa alama nitaibainisha nayo. Hilo halikupi dhiki katika wasaa wako, wala halikusumbui katika nguvu zako, wala haliuzidi upole wako, wala haikuchokeshi katika hiba zako tukufu ambazo zimeonyeshwa na aya zako. Hakika wewe wafanya ulitakalo na wahukumu upendalo. Hakika wewe nimuweza wa kila kitu.

DUA YA 17

DU'A ZAKE(A.S) AMTAJAPO SHETANI HUJILINDA NAYE NA HUJILINDA NA UADUI WAKE NA VITIMBI VYAKE

Ewe Mola kwa hakika twajilinda kwako na mvuto wa shetani maluuni na vitimbi vyake na mitego yake. Na kuwa na matumaini ya ahadi zake.Udanganyifu wake na mawindo yake na asijipe tamaa nafsini mwake ya kutupoteza mbali na utii wako. Na kutotweza kwa sababu ya kukuasi tusije yaona kuwa ni mazuri aliyotufanya tuyaone mazuri. Na yasije onekana mazito kwetu aliyoyachukiza kwetu. Ewe Mola mtupe mbali nasi kwa njia ya ibada yako. Mtupe chini kwa upendo wetu wa kudumu kwako. Weka kati yetu na yeye kiziwizi asichoweza kukiondoa. Na kinga madhubuti hawezi ikiuka. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Mshughulishe awe mbali na sisi kwa baadhi ya maadui wako. Utulinde naye kwa uzuri wa uangalizi wako. Tufanye atusumbuliwi na khiyana yake, tugeuzie mgongo wake. Ukate kabisa ufuatilio wake kwetu. Ewe Mola msalie Muhammad na Ali zake. Tufurahishe kwa kutupa uongofu mfano wa upotovu wake. Tuzidishie uchamungu dhidi ya ushawishi wake. Tupitishe katika uchaji mungu kinyume na njia yake ya maangamio.

Ewe Mola usimjalie upenyo mioyoni mwetu. Usimfanyie makazi kwa yale tuliyonayo. Ewe Mola tutambulishe njia potovu atufanyiazo. Na tuitambuapo tulinde nayo tuonyeshe cha kumrubuni nacho. Tupe ilhamu ili kujiweka tayari naye tuamshe ili tutokane na sinzio la mghafala wa kumtegemea yeye. Ufanye uzuri msaada wako kwetu dhidi yake. Ewe Mola zinyweshe nyoyo zetu kuyakanusha matendo yake. Tufanyie upole kwa kutangua hila zake. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake.Yageuze mamlaka yake mbali nasi, kata matumaini yake kwetu, mziwie uchu wake kwetu, Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake.Wajaalie baba zetu, mama zetu, watoto wetu, ahli zetu, ndugu zetu wa karibu na majirani zetu miongoni mwa waumini wanaume na waumini wanawake katika ulinzi madhubuti dhidi yake. Na ngome yenye hifadhi na pango lenye kizuizi. Wavishe dhidi yake kinga iwalindayo, wape silaha dhidi yake silaha kali kali Ewe Mola waeneze hayo wenye kushuhudia kuwa wewe ndiyo Rabbu. Na akakutengea wewe umoja. Na amfanyiaye uadui (shetani) kwa ajili yako kwa hakika ya uja. Na akuomba msaada dhidi yake kwa maarifa ya elimu za kiungu.

Ewe Mola! fungua aliyoyafunga na rarua aliyoyashona. Haribu aliyoyapanga, mvunje moyo anapoazimia, yaharibu aliyoyafanya. Ewe Mola lishindishe jeshi lake, batilisha vitimbi vyake, bomoa pango lake, isuguwe pua yake chini ya ardhi. Ewe Mola! tuweke sisi katika ngazi ya maadui zake tutoe tusiwe katika idadi ya marafiki zake ili tusimtii anapotushawishi. Tusimwitikie atuitapo, tumpe amri mwenye kutii amri yetu amfanyie uadui, na tumuwaidhi ili asimfuate mwenye kufuata karipio letu. Ewe Mola! mrehemu Muhammad mwisho wa manabiy na bwana wa mitume na warehemu ahli bayt wake wema na wasafi. Na utulinde sisi na ahali zetu, ndugu zetu na jumla ya waumini wanaume na waumini wanawake, yale tuliyojilinda nayo. Na ututakase kwa yale tuliyokuomba ututakase nayo kwa hofu yake. Tusikilize tuliyokuomba na utupe tuliyoghafilika kuyaomba, ulinde na tuliyoyasahau. Kwa yote hayo tufanye tuwe katika daraja za watu wema na ngazi za waumini - Aameen ewe Mola wa ulimwengu wote.

DUA YA 18

LINDWA NA JAMBO ANALOLIHOFIA AU KUHARAKISHIWA AYATAKAYO

Oh! Mola sifa njema ni zako kwa uzuri wa utekelezaji wako. Kwa kuniondolea mitihani yako, usiijaalie hadhi yangu katika rehma zako ile ulioniharakishia katika afya yako nisije kuwa duni kwa niliyo nikiyapenda. Na mwingine awe na maisha mema kwa yale niliyoyachukia. Ikiwa hali njema niliyo nayo mchana wote au usiku wote kwa afya hii itafuatiwa na balaa isiyokoma na mzigo wa dhambi ambao usiotoweka.! Bora nitangulizie ambacho ungekichelewesha na nicheleweshee ambacho ungenitangulizia. Kwa kuwa ambacho mwisho wake ni kuteketea hakina wingi. Na ambacho matokeo yake ni kubakia hakina udogo. Msalie Muhammad na Aliy zake.

DUA YA 19

DU'A ZAKE(A.S) KUOMBA MAJI WAKATI WA UKAME

Oh! Mola tupe maji kwa kutuletea mvua. Tukunjulie rehma zako kwa mvua yako nyingi kutoka mawingu yasukumwayo kwenye mimea ya ardhi yako muwafaka kwa kuotesha katika zoni zote. Wahurumie waja wako kwa kuivisha matunda. Irudishie uhai nchi yako kwa kutungika maua. Wafanye malaika wako waheshimiwa waandishi kuwa mashahidi kwa mvua yenye manufaa toka kwako. Wingi wake uwe wa daima, mbubujiko wake uwe wa wasaa, mvua nyingi ya haraka, kwayo uirudishie uhai iliyonyauka, ukilete kwayo kinachokuja, kwayo ulete chakula nyingi, mawingu yenye kurundikana yenye kutosheleza, katika tabaka za mawingu yatoayo sauti mvua inyeshayo sio ile isiyo simama kuwe na umulikaji wenye matunda. Oh! Mola tupe mvua, yenye kusaidia, iletayo mazao yenye rutuba, yenye kuenea, nyingi, yakutosha inayotengeneza upya kilichovunjika. Oh! Mola tupe mvua, itakayofanya mawe ya mlimani yaporomoke itakayojaza visima, itakayoifanya mito itiririke, itakayootesha miti, itakayofanya bei za vitu irudi chini katika nchi zote, itakayo tia uzima wanyama na viumbe vingine, itakayotukamilishia chakula yakufaa, itakayotuoteshea mimea, itakayoongeza mtiririko wa maziwa katika chuchu za wanyama, itakayo tuongezea nguvu kwenye nguvu zetu. Ewe Mola usijaalie kivuli chake juu yetu kuwa upepo uunguzao, wala usiifanye baridi yake kwetu ya kukata, usiufanye mbubujiko wake kwetu kuwa ni pigo la mawe, wala usiyafanye maji yake kwetu kuwa ya chumvi. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Turuzuku miongoni mwa baraka za mbingu na ardhi. Hakika wewe u muweza wa kila kitu.


4

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

DUA YA 20

DU'A ZAKE KATIKA TABIA NJEMA NA VITENDO VYA KURIDHISHA

Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Ifanye iymani yangu ifikiye daraja kamilifu ya iymanni. Na ifanye yakini yangu iwe yakini bora. Na ifikishe nia yangu kwenye nia nzuri mno. Ewe Mola kwa huruma zako ikamilishe nia yangu. Ifanye yakini yangu iwe sahihi kwa yale uliyonayo. rekebisha kwa uwezo wako kilicho haribika kwangu. Ewe Mola msalie Muhammad na Aliy zake. Niepushe na hima inishughulishayo na kunirudisha nyuma. Nitumikishe katika ambayo utaniuliza kesho. Ziache siku zangu zitumike kwa yale tu ambayo kwa ajili yake uliniumba. Nitosheleze unipanulie riziki yako, usinipe mtihani wa kutokuwa na shukrani. Nipe enzi usinitihani kwa kunifanya niwe na kibri. Nifanye niwe nakuabudia wewe usiiharibu ibada yangu kwa kujisifu. Ipitishe mikononi mwangu kheri kwa watu usiifute kwa masimbulizi yangu kwao. Nipe tabia njema za hali ya juu kabisa. Nilinde na kujifaharisha. Ewe Mola wangu mrehemu Muhammad na Aliy zake. Wala usinipandishe daraja kwa watu ila uwe umeniteremshia nafsini mwangu mfano wake, usinifanyie utukufu wa wazi isipokuwa uwe umenifanyia udhalili wa ndani ya nafsi yangu kwa kadiri ile ile. Ewe Mola msalie Muhammad na Aliy zake. Na unistareheshe kwa mwongozo mwema ambao sitoubadilisha. Na njia ya haki ambayo sitopotoka na nia ongofu ambayo sitokuwa na mashaka nayo. Nipe maisha ikiwa maisha yangu yatakuwa zawadi ya bure kukutii wewe. Na endapo maisha yangu yatakuwa malisho mema ya shetani nichukuwa kwako kabla haijatangulia chuki yako kwangu au kabla haijachukuwa nafasi ghadhabu zako juu yangu. Ewe Mola usiiache sifa ambayo kwayo nitaaibishwa isipokuwa utakuwa umeirekebisha. Au aibu nalaumiwa kwayo ila itakuwa umeirekebisha. Wala daraja bora linakasoro uwe umelikamilisha.

Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Nibadilishie bughudha ya watu wenye chuki kwa upendo. Na nibadilishie husda ya mafedhuli iwe mapenzi, na dhana ya watu wema iwe uaminifu, na uadui wa makaraba uwe urafiki, na kutojaliwa na watu wa tumbo moja kuwe wema, na kutupiliwa mbali na ndugu wa karibu kuwa ni msaada, na upendo wa wabembe uwe upendo uliorekebika upendo sahihi, na kukataliwa na wenzi kuwe heshima na urafiki. Uchungu wa kuwaogopa wadhalimu uwe utamu wa uaminifu. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Unijaalie niwe na mkono wa juu dhidi ya wanaonidhulumu, na ulimi wa juu dhidi ya wanaonigomba, ushindi kwa anayemng'ang'ania kunikaidi. Nipe mbinu dhidi ya anayenifanyia vitimbi, na uwezo dhidi ya anayenikandamiza na kumkanusha anayenikebehhi, nipe usalama kwa anayenikamia, nipe taufiki ya kumtii anayeniweka sawa. Kumfuata anayeniongoza. Ewe Mola msalie Muhammad na Aliy zake. Niweke sawa ili nimpinge anayenighushi kwa nasaha, mlipe anayejitenga na mimi kwa wema umlipe mwenye kuninyima kwa kutoa bure, umlipe mwenye kujitenga na mimi kwa mawasiliano, nimpinge mwenye kunisengenya kwa kunitaja vyema, na niwezeshe kushukuru yaliyomema na kuyafumbia macho maovu, ewe Mola mrehemu Muhammad na Ali zake, nipambe kwa mapambo ya watu wema nivishe pambo la wachamungu kwa kueneza uadilifu. Kujizuiya na ghadhabu, kuuzima moto wa chuki, kuwaleta pamoja watu waliotawanyika, kusuluhisha mizozo ya wasiopatana, kueneza mema, kusitiri aibu, kuwa na tabia ya upole, kushusha bawa chini, mwendo mwema, uvumilivu, uzuri wa mwenendo, na kuharakia maadili, kuchagua fadhila, kuacha kuaibisha, kumfadhili asiyestahiki, kusema yaliyo haki japo ni machungu, kuudogesha wema japo uwe mwingi, kwa kauli yangu au kwa kitendo changu, nakuikithirisha shari japo iwe ndogo kwa kauli yangu au kitendo changu. Nikamilishie hayo mimi kwa kudumisha utii, na kujiambatanisha na jamaa na kuwakataa wazushi na watumiao rai zao za kubuni. Ewe Mola mrehemu Muhammad na aliy zake. Na jaalia riziki yangu iwe riziki ya wasaa mno kwangu endapo nitakuwa mtu mzima. Na mwenye nguvu sana katika nguvu zako nitakapoishiwa nguvu. Usinipe mtihani wakuwa mvivu katika ibada yako. Wala kuwa kipofu wakutoiona njia yako, wala kujihusisha na linalopingana na mapenzi yako, wala kujiunga na ambaye amejitenga na wewe, wala kujitenga na aliyejiambatanisha na wewe.

Ewe Mola nifanye niwe narukia kwako wakati wa dharura. Nakuomba wakati wa haja, nanyenyekea kwako wakati wa shida, usinipe mtihani wa kuomba msaada kwa mwingine mbali na wewe nikiwa nimedharurika wala kunyenyekea kwa ombi kwa mwingine mbali na wewe niwapo fakiri, wala kunyenyekea kwa ambaye ni chini yako nikiwa na woga. Kwa kufanya hivyo nitastahiki kutupiliwa mbali na wewe na kukabiliwa na zuio lako na kutumbiwa mgongo na wewe. Ewe mwingi mno wa kurehemu kuliko wanaorehemu wote. Ewe Mola fanya anachonitupia shetani moyoni miongoni mwa tamaa, dhana, na husda iwe ni kumbusho la utukufu wako kuitafakari nguvu yako, na iwe ni onyo dhidi ya adui wako. Nayafanye ayapitishayo ulimini mwangu miongoni mwa tamko baya au kebbehi au ushahidi batili, au kumsengenye muumini asiyekuwapo au kumtusi aliyopo na yaliyomfano wa hayo iwe ni tamko la kukuhimidi wewe. Na kuzama katika kukusifu wewe na juhudi katika kukuenzi wewe na shukrani kwa ajili ya neema zako. Nakutambua ihisani yako, na kuhesabu huruma yako. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Nisidhulumiwe hali wewe ni muweza wakunilinda, wala nisidhulumu nawe waweza kunizuia, usiache nipotee hali waweza kuniongoza, usinniache niwe masikini na hali kwako kuna yakunitosheleza. Nisivuke mipaka haki kwako ndio utajiri wangu. Ewe Mola, nimekuja kwenye msamaha wako, naelekea msamaha wako. Ninashauku na kufumbiwa macho kwako ninaithibati na fadhila zako, sina kinachoweza kuwajibisha msamaha wako kwangu, wala katika kazi yangu hakuna ninachoweza kustahiki msamaha wako, sina chochote baada ya kujihukumia mwenyewe dhidi ya nafsi yangu kinifaacho ila fadhila zako, mrehemu Muhammad na Ali zake, nipe fadhila zako. Ewe Mola, nitamkishe uongofu, nipe mwongozo wa uchamungu, niwafikishe fanaka katika ambacho ni safi mno, nitumikishe kwa ambalo lakuridhiwa ewe Mola nipitishe njia ya mfano bora. Yafanye maisha yangu katika mila yako kufa na kupona. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Nifanye wakufurahiya iktiswadi (yaani uwekevu), nifanye niwe miongonni mwa watu wa sawa miongoni mwa waongofu, miongoni mwa waja wema, niruzuku kuwa mwenye kufaulu marejeo na usalama wa mawindo.

Ewe Mola, chukuwa kwa ajili yako kutoka nafsini mwangu kitachoitakasa, nabakisha kwa ajili ya nafsi yangu kutoka nafsi yangu kitakachoifanya iwe njema kwa kuwa nafsi yangu ni yenye kuangamia isipokuwa ukiilinda. Ewe Mola, wewe ndio kifao changu ni huzunikapo wewe ndio kimbilio langu ninyimwapo kwako ndio mahali pa kuomba msaada nikiwa katika taabu. Na kwako kuna badali ya yaliyopotea na marekebisho kwa kilichoharibika. Na mabadiliko kwa ulichokikaa, nihurumie kwa kunipa afya kabla ya balaa. Na mali kabla ya kuomba, na kabla ya kupotea uongofu, nitosheleze nisipatwe na mzigo wa aibu kwa waja, unipe amani siku ya marejeo, nipe mwongozo mwema, ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Nilinde kwa rehma yako, nilishe kwa neema zako, nisawazishe kwa ukarimu wako, nitibu kwa wema wako, nifunike kwa kivuli chako, nienezee ridhaa zako.

Niwafikishe ili nifikie jambo lenye mwongozo mno endapo mambo yatachanganyika mbele yangu, nifikie kwenye kazi iliyo safi mno endapo kazi zitashabihiyana, nifikie kwenye itikadi iridhiwayo endapo itikadi zitapingana, ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake, nivishe taji la kuridhika. Nipe malezi mema, nipe mwongozo sahihi, usinipe mtihani kwa kuwa na nafasi, unipe maisha mema, usiyafanye maisha yangu kuwa ya taabu na shida, usiirudishe DU'A yangu kwangu kwa kuikataa. Kwa hakika mimi sikufanyii yeyote kuwa dhidi yako, wala simwombi yeyote pamoja na wewe nikimfanya kuwa yu sawa na wewe, ewe Mola msalie Muhammad na Aliy wake. Niziwie ili nisiwe mfujaji, ilinde riziki yangu na uharibifu, zidisha mali zangu kwa kuzibariki, niwafikishe njia ya mwongozo kwa wema wa niyatumiayo, ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Niepushe na mzigo wa kuchuma, na unipe bila ya hesabu, kutafuta kusiniziwie kufanya ibada yako, nisibebe mzigo wa matokeo mabaya ya uchumaji. Ewe Mola nipe niyatafutayo kwa uwezo wako, nipe kimbilio safi kwa nguvu zako kwa nihofiayo, ewe Mola msalie Muhammad na Aliy zake uhifadhi uso wangu kwa kuwa na nafasi bora ya maisha, usiidhalilishe heshima yangu kwa ufakiri ili nisije waomba riziki uliowaruzuku au niwaombe kipawa watu washari katika viumbe wako. Kwa hiyo nitakuwa katika fitna ya kumsifu atakaye nipa na kuingia katika balaa la kumlaumu atakaye nikatalia.

Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aliy zake. Na wewe siwawo ndio Bwana wa utoaji na uzuiaji. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Alali zake. Na unipe siha katika ibada, nijihusishe na zuhud, na elimu katika matendo, na kujiepusha katika kipimo. Ewe Mola hitimisha muda wangu kwa msamaha wako. Nayathibitishie matarajio ya Rehma zako matazamio yangu. Wepesisha njia zangu kufikia Ridhaa zako. Amali zifanye nzuri katika hali zote. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aali zake. Nizinduwe kukukumbuka nyakati za mghafala. Nitumikishe katika utii wako siku za Raha. Nifanyie njia nyeupe na rahisi kuelekea mapenzi yako. Nikamilishie kwayo kheri ya dunia na Akhera. E Mola mrehemu Muhammad na Aali zake. Kwa ubora ule uliomrehemu yeyote katika viumbe vyako kabla yake. Na ule ambao utamrehemu yeyote baada yake. Tupe mema hapa duniani na mema akhera. Na unilinde kwa rehema zako na adhabu za mto

DUA YA 21

NA ALIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) AKIHUZUNISHWA NA JAMBO NA YA MUOGOPESHAPO MAKOSA

Ewe Mola! Ewe mwenye kumtosheleza mpweka dhaifu. Mlinzi wa jambo lihofiwalo. Makosa yamenitenga wala sina mwenzi nimekuwa dhaifu kwa ghadhabu zako hakuna wakunipa nguvu. Nimeikaribia hofu ya kukutana na wewe hakuna wakuituliza hofu yangu nani anipe amani kwako na wewe ndiye umeniogopesha? Hatowi kimbilio Ewe! Mola wangu ila Bwana mlezi kwa awaleao hatowi amani ila mshindi kwa mshindwa. Hakuna asaidiaye juu ya chenye kuombwa ila ni mwombaji. Na mkononi mwako Ewe! Mola wangu kuna sababu zote hizo. Kwako ndio kwa kukimbilia na ndio kimbilio msaliye Muhammad na Aali zake. Na nipe kimbilio kwa ajili ya kimbilio langu fanikisha ombi langu. Ewe Mola hakika wewe ukinigeuzia uso wako mtukufu mbali nami au ukiniziwiya fadhila zako kubwa, au kunikataza riziki yako. Au ukikata mbali namimi sababu yako sitoipata njia kufikia chochote katika matumaini yangu bila ya wewe. Wala sitoweza kuyapata yaliyo kwako kwa msaada wa mwingine. Mimi ni mja wako niko mashikoni mwako. Nyele zangu za mbele zi mikononi mwako. Sina amri pamoja na amri yako hukumu yako yatekelezeka kwangu. Maamuzi yako kwangu ni ya kiadilifu. Sina uwezo wakutoka nje ya mamlaka yako. Wala siwezi kuzikurubia nguvu zako wala siwezi kuelemeza upendo wako. si ufikii upendo wako. wala sitoyapata yaliyokwako isipokuwa kwa utii wako nakwa fadhila za rehema zako Oh! Mungu wangu! muda wote niko mjawako wa ngazi ya chini kabisa. Si miliki manufaa kwa ajili ya nafsi yangu wala madhara isipokuwa kwa njia yako.

Nashuhudia hilo mwenyewe binafsi. Natambua udhaifu wa nguvu zangu na uhaba wa mbinu zangu: Hivyo basi nipe ulilo niahadi. Nitimizie ulilonipa Mimi ni mja wako Masikini, mnyonge Dhaifu mwenye dhiki Dhalili, mwenye kudharauliwa, mnyonge fakiri. Aliyeshikwa na woga aombaye hifadhi, Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aali zake. Ala mwenye kughafilika ihsani yako uliponipa mtihani. Wala kukata tamaa na jibu lako japo lije polepole sana kwangu. Sawa niwe katika neema au katika taabu. Shida au raha. Katika hali njema au katika balaa. Katika maafa au katika raha. Katika utajiri au hangaiko. Ufakiri au utajiri. Ewe Mola mrehemu Muhammadi na Aali zake. Na jaaliya kukusifu kwangu kwa sifa njema, kukuhimidi, na kukutukuza kuwe katika hali zangu zote. Ili niwe sifurahii ulionipa katika dunia. Wala nisihuzunikie ulionizuia humo. Upe moyo wangu kukuogopa wewe utumikishe mwili wangu kwa lile unalolikubali kutoka kwangu. Ishughulishe nafsi yangu katika utii wako kwa kila liingialo kwangu kiasi chakuwa nisikipende chochote kinachokukasirisha.

Wala nisichukie chochote kikufurahishacho. Ewe Mola msalie Muhammad na Aali zake. Ufanye moyo wangu uwe tupu ila kukupenda wewe. Na ushughulishe kukukumbuka wewe. Uhuishe kukuogopa na utishike na wewe upe nguvu kukusihi wewe. Uelemeze kwenye utii wako. Upitishe katika njia zipendwazo sana na wewe. Udhalilishe kupenda ulichonacho siku zote za uhai wangu. Kukuogopa wewe Duniani iwe ndio masurufu yangu. Safari yangu iwe kuielekea Rehma za kuingia kwangu kuwe katika maridhawa yako. Jaalia makazi yangu yawe katika jannah yako. Nipe nguvu za kubeba kila kitu ukipendacho. Jaalia kukimbia kwangu iwe kuja kwako na kupenda kwangu kile kilichokuwa kwako. Uvishe moyo wngu kuwaona watenda shari katika viumbe wako kuwa si wako kawaida. Nipe urafiki na wewe na marafiki zako na watu wako watii. Wala usimjaalie muwovu wala kafiri fadhila juu yangu, wala asiwe na mkono kwangu, wala ni siwee na haja kwake. Lakini jaalia utulivu wa moyo wangu, Raha ya nafsi yangu, kujitegemea, kwangu na kujitosheleza kwangu kwako. Na kwa viumbe wako wazuri mno. Ewe! Mola mrehemu Muhammad na Aali zake nifanye niwe rafiki kwao. Nifanye niwe msaidizi kwao. Nitunukie niwe na shauku ya upendo wako na kufanya mema kwa ajili yako yale uyapendayo na wayaridhiya. Hakika wewe ni muweza wa kila kitu. Na hayo kwako ni mepesi.

DUA YA 22

DU'A ZAKE(A.S) KATIKA SHIDANA JUHUDI NA MAMBO YANAPOKUWA MAGUMU

Oh! Allah Hakika umeniagiza jambo lihusulo nafsi yangu ambalo wewe wahusika nalo zaidi kuliko mimi. Uwezo wako juu yake na juu yangu ni mkubwa mno kuliko uwezo wangu. Hivyo basi nipe mimi ndani ya nafsi yangu linalokuridhisha kutoka kwangu na chukuwa kwa ajili ya nafsi yako ridhaa zake toka nafsini mwangu, katika hali ya afya njema. O Allah! Sina ustahimilivu katika juhudi wala sina subira katika balaa, sina nguvu za kuubeba mzigo wa ufakiri hivyo usikataze Riziki yangu, wala usiniwakilishe kwa viumbe wako ishughulikie haja yangu peke yako. Shikilia mwenyewe kunitosheleza. Niangalie nichunge, katika mambo yangu yote kwa kuwa wewe ukiwakilisha kwangu mwenyewe nitakuwa nimehemewa na sitofanya lenye maslahi. Kwa nafsi yangu. Endapo utaniwakilisha kwa viumbe wako watanikunjia uso, Ukinifanya nikimbilie kwa ndugu zangu wa karibu wataninyima. Na kama watanipa watanipa kidogo shingo pembeni. Na watanisimbulia saana mda mrefu na huku wakinilaumu sana. Hivyo basi kwa fadhila zako O Allah! Nitosheleze. Na utukufu wako ni nyanyuwe, kwa wasaa wako ikunjuwe mikono yangu. Nitosheleze kwa yaliyo kwako. O Allah! Msalie Muhammad na Aali Zake. Na uniweke mbali na husda nitenge mbali na dhambi nifanye niogope kutenda haram. Nisithubutu kutenda maasi. Fanya upendo wangu kwako na Ridhaa yangu iwe kwenye kinifikiacho kutoka kwako. Kibariki kwa ajili yangu, ulichoniruzuku. Na ulichonijaalia. Na ulichonineemesha.

Nijaaliye katika hali zangu zote mwenye kuhifadhiwa mwenye kulindwa. Mwenye kusitiriwa mwenye kuzuiliwa. Mwenye kukingwa kupewa kimbilio. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aali zake. Nifanye nitekeleze yote ulionilazimisha na uliyoyafaradhisha juu yangu kukuelekea wewe. Katika namna moja miongoni mwa aina zako za kukutii. Au kwa ajili ya kiumbe miongoni mwa viumbe wako. Japo mwili wangu uwe dhaifu kwa hilo na kudhoofu kwa hilo nguvu zangu. Uwezo wangu ukashindwa kulifikia hilo na mali yangu yakawa kidogo na hata kilichomkononi mwangu. Sawa niwe nakumbuka au nasahau. Mola wangu ni miongoni mwa uliyo yadhibiti hisabu yake dhidi yangu. Wakati mimi binafsi nimeghafilika. Ni jaaliye kutekeleza kwa wingi wa utoaji wako na kwa ukubwa wa ulichonacho. Kwa kuwa wewe unawasaa mno na ni mkarimu. Ili kwangu kisibakie kitu ambacho wataka kunifuatilia hesabu yake miongoni mwa maovu yangu siku nitakutana na wewe o Mola wangu! Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aali zake. Niruzuku upendo wa kutenda mema kwa ajili yako ili itengenee kheri yangu. Nijuwe ukweli wa hilo moyoni mwangu. Na kujinyima starehe ya dunia kuwe ndio mshindi. Nitende mazuri kwa shauku kabisa niwe katika usalama wakutotenda matendo maovu kwa kitisho na woga.

Nipe mwanga uniwezeshao kutembea kati ya watu. Utakao niwezesha kupata mwongozo gizani. Ning'arishe kwa mwanga huo shaka na mambo yanapokuwa si dhahiri. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Na uniruzuku kuogopa mayonzi ya kitisho. Na niruzuku kuwa na shauku ya thawabu iliyoahidiwa kiasi kwamba ni ipate ladha ya yale nikuombayo. Na niyapate majonzi ya kile nikiombeacho kimbilio kwako. Oh Allah! Wajua fika kitakachoweka sawa mambo ya dunia yangu na Akhera yangu. Hivyo basi kuwa na upendeleo kwenye mahitaji yangu. Oh Allah! mrehemu Muhammad na Aali Zake. Uniruzuku haki ninaposhindwa kukushukuru ipasavyo kwa ajili ya Neema zako ulizonineemesha. Nikiwa katika nafasi nzuri na katika matatizo. Katika siha njema na katika ugonjwa kiasi kwamba niwe natambua mwenyewe. Faraja ya maridhawa na utulivu wa nafsi kwa yaliyo wajibu kwako ambayo yazukayo katika hali ya hofu na amani. Hali ya ridhaa na ya makasiriko ya madhara na manufaa. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake.

Na uniruzuku usalama wa kifua kuepukana na husuda. Ili nisimhusudu yeyote katika ujumbe wako juu ya kitu chochote miongoni mwa fadhila zako. Kiasi kwamba nisione neema katika neema zako kwa yeyote miongoni mwa viumbe wako kwa yeyote miongoni mwa viumbe wako sawa iwe katika dini au dunia katika hali njema ya maisha au uchamungu. Sawa iwe wasaa au Raha. Isipokuwa niwe natarajia kwa ajili ya nafsi yangu yaliyo bora ya hayo kwako kutoka kwako peke yako huna mshirika. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Na uniruzuku kujilinda na makosa na niogope kuteleza hapa duniani na Akhera. Katika hali ya ridhaa na ghadhabu kwa kiasi isiwe sawa kwangu liingialo kati ya hayo mawili. Nitende utii wako nichaguwe ridhaa zako na kuacha yasiyokuwa hayo mawili. Kwa marafiki na maadui. Ili hata aduwi wangu awe katika amani mbali na dhulma yangu na maovu yangu. Na akate tamaa rafiki yangu na elemeo langu na kupinda kwenye matamanio yangu. Na ni jaalie niwe miongoni mwa wakuombao kwa unyofu katika raha ombi la wakuombao katika hali ya unyofu wamedharurika kukuomba. Hakika wewe wastahiki sifa njema u mtukufu.

DUA YA 23

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) AMWOMBAPO MUNGU HALI NJEMA NA ANAPOISHUKURU

Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Nivishe afya yako. Niviringishe afya yako. Niweke kwenye ngome ya afya yako. Nipe heshma kwa afya yako. Nitosheleze kwa afya yako.Nipe sadaka kwa afya yako. Nitunukiye afya yako Nitandikiye afya yako. Niwekee sawa afya yako. Usinitenge mbali na afya yako. Duniani na Akhera. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake nipe afya. Afya ya kutosha iponyeshayo, ya hali ya juu ikuayo. Afya izalishayo mwilini mwangu afya njema. Afya njema duniani na akhera. Nifanye niwajibike kwa siha na amani. Na usalama katika Dini yangu na Mungu wangu. Na ufahamu moyoni mwangu. Na uwezo wa kuyapitisha mambo yangu na kukuogopa wewe. Na kukuhofia wewe. Niwe na nguvu juu ya uliyoniamrisha katika kukutii. Na kujiepusha na uliyo nikataza miongoni mwa maasi yako. Oh Allah! Nifadhili kwa kufanya hija na umra na kuzuru kaburi la Mtume wako, Rehema zako na baraka zako zimfikie na ziwafikiye watu wa nyumba ya Mtume wako. Milele pindi unibakishapo katika mwaka wangu huu na katika kila mwaka. Naijaalie iwe yenye kukubaliwa yenye kushukuriwa. Yenye kutajwa mbele yako. Yenye kuhifadhiwa kwako. Utamkishe ulimi wangu shukrani yako, kukukumbuka wewe na kukusifu kwa sifa njema. Ukunjuwe moyo wangu kwa mwongozo wa dini yako. Na unipe mimi na kizazi changu ulinzi dhidi ya shetani aliyelaaniwa. Na shari ya chuki na uharibifu na jicho baya. Na shari ya kila shetani muasi. Na shari ya kila mtawala mkaidi Na shari ya kila mkwasi mtumikiwa. Na shari ya kila dhaifu na mwenye nguvu.

Na shari ya kila mdogo na mkubwa, na shari ya kila wakaribu na wa mbali na shari ya kila mwenye kufanya uaduwi kwa Mtume wako na watu wanyumbani mwake miongoni mwa jini au mtu. Na shari ya kila kiumbe kitambaacho ambacho wewe umezishika nyele zake mbele ya kichwa. Hakika wewe uko juu ya njia ilinyooka. Oh Allah! Mrehemu Muammad na Aali zake. Endapo yeyote atanitakia uovu niondolee naye mbali. Niondolee mbali vitimbi vitmbi vyake. Ikinge mbali na mimi shari na virudishe vitimbi vyake kooni kwake.

Na weka mbele yake boma ili ufanye macho yake yasinione na umfanye Asisikiye utajo wangu uufunge moyo wake usihihisi. Uzimishe ulimi wake dhidi yangu kiziwiye kichwa chake. Utweze utukufu wake. ivunje jeuri yake. Idhalilishe shingo yake. Haribu kibri chake, niweke katika amani na madhara yake yote na shari yake. Na masingizio yake, masengenyo yake na uchokozi wake. Husuda yake na uaduwi wake. Mtego wake na mawindo yake. Waenda kwa miguu wake na wapanda farasi wake. Hakika wewe muweza na mwenye nguvu.

DUA YA 24

DU'A ZAKE(A.S) KWA AJILI YA WAZEE WAKE(A.S)

Oh Allah! Mrehemu Muhammad mja wako na mjumbe wako na warehemu Ahlul-Bayt wake watakatifu. Na uwahusishe kwa ajili yao peke yao kwa fadhila zako na rehema zako na baraka zako na amani yako. Wahusishe Oh Allah! wazazi wangu wawili kwa heshima mbele yako na Rehema kutoka kwako. Oh! We mwenye kurehemu sana miongoni mwa wanaorehemu Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Na unifundishe kwa hamu elimu ya mambo ambayo ni wajibu wangu kwao. Na unikusanyie Elimu ya yote hayo kikamilifu. Kisha nitumikishe kwa yale unifundishayo kwa Il-ham. Niwafikishe kutekeleza elimu uliyonipa ili yasinipite matumizi ya kitu ulichonifundisha. Wala viungo vyangu visiwe vizito kutekeleza uliyonifundisha kwa njia ya Il-hamu. Oh Allah! Mrenemu Muhammad na Aali zake.

Kama ulivyotupa heshima kupitia kwake. Na mrehemu Muhammada na Aali zake kama ulivyowajibisha juu yetu haki juu ya viumbe kwa sababu yake. Oh Allah! Nifanye natishika nao (wazazi wawili) kitisho cha mtu mbele ya mtawala mshari nifanye niwe mwema kwao kama wema wa mama mwenye huruma. Na ufanye utii wangu na wema wangu kwao kuwa ni kitulizo cha macho yangu sana kuliko usingizi wa mwenye usingizi mzito. Na yawe baridi mno kwenye kifua changu kuliko kinywaji cha mwenye kiu kali. Ili niliweke walipendalo mbele kuliko nilipendelealo.Na niitangulize ridhaa yao mbele ya ridhaa yangu. Na niuone wema wao kwangu kuwa ni mkubwa japo uwe kidogo. Na niuone wema wangu kwao ni mdogo sana japo uwe mwingi. Oh Allah! Irudishe sauti yangu chini mbele yao. Yafanye maneno yangu kwao kuwa maneno yanayokubalika. Ifanye tabia yangu kuwa ya upole mbele yao. Ufanye moyo wangu laini kwao nifanye niwe mwenzi mwama, mwenye kuwahurumia.

Oh Allah! Washukuru kwa malezi yangu na walipe mema kwa kunipa mimi heshima. Na wahifadhi kama walivyokuwa wananihifadhi nilipokuwa mdogo. Oh Allah! Na kwa aina yoyote ya maudhi yaliwagusa kutoka kwangu na mambo yachukizayo yaliwafika kutoka kwangu. Au haki yao iliopuuzwa na mimi basi fanya iwe ni sababu ya kupunguza dhambi zao. Na kupanda kwao daraja yao. Na kuzidi kwa mema mengi sana. Oh Allah! Neno lolote liwalo walilonikosea au hawakuwa waadilifu kwangu katika tendo waliipoteza haki yangu. Au walizembea kutekeleza wajibu wao kwangu. Nawazawadia na kuwapa wao kama tulizo nakusihi kuwaondolea malipizi dhidi yao kwani mimi siwashitaki kwa ajili yangu. Wala siwaoni kuwa wamefanya goi goi katika kunitendea wema. Wala si chukii jinsi walivyo yapeleka mambo yangu. Ewe Mola wao wanahaki juu yangu zaidi hisani yao ndiyo ya kwanza zaidi kunifikia. Huruma yao ni kubwa mno kwangu kuliko niwezavyo kuwa fuaatilia kwa uadilifu. Au niwalipe kulingana nao. Uwapi basi Ewe Mola wangu urefu wa shughuli yao kunilea? Iwapi basi taabu kubwa ya kunilinda kwao mimi?

Kuwapi kujinyima kwao wenyewe ili wanipe mimi kwa wingi baada yao? Haiwezekani! Hawawezi kupata haki yao kamili kutoka kwangu. Wala siwezi kutekeleza yaliyowajibu juu yangu kwao. Wala siwezi kukamilisha wajibu wangu kwao kuwahudumiya. Hivyo basi mrehemu Muhammad na Aali zake. Na nisaidie Ewe mbora wa waombwa msaada. Na nifanikishe Ewe mbora wa waombwao mwongozo wake. Usinifanye niwe miongoni mwa wasio wathamini baba zao na mama zao (siku ambayo kila nafsi italipwa ilichochuma nao hawatodhulumiwa). Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake na dhuria zake. Uwatengee wazazi wangu wawili fadhila makhsusi uliyowatengea wazazi wa waja wako waumini na mama zao. Ewe Mwingi wa Kurehemu! Oh Allah! Usinisahaulishe kuwa kumbuka. Baada ya sala zangu. Nawakati wowote ule katika nyakati za usiku. Na katika kila saa miongoni mwa saa za mchana wangu. Oh Allah! Msaliye Muhammad na Aali zake. Ni ghofiriye kwa sababu ya DU'A yangu kwao. Na waghofiriye wao kwa wema wao kwangu ghofira ya sawa sana. Waridhiye kwa maombezi yangu kwa ajili yao ridhaa za yakini kabisa. Kwa ukarimu wako wafikishe makazi ya salama. Oh Allah! Na endapo ghofira zako zimetangulia kuwafika basi zifanye ziwe mwombezi wangu na ikiwa ghofira zako zimenifikia mwanzo. Nifanye niwe mwombezi wao. Ili tuweze kukutana pamoja kwa huruma zako. Katika nyumba ya heshima yako na mahali pa msamaha wako na rehema zako. Kwa hakika wewe ni mwenye fadhila nyingi na huruma ya kale. Na wewe ni mwenye Rehema sana kuliko wenye kurehemu wote


5

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

DUA YA 25

DU'A ZAKE(A.S) KWA AJILI YA WATOTO WAKE(A.S)

Oh Allah! Nihurumie kwa kubaki watoto wangu, na kuwa kwao wema kwangu, na kwa kufurahikiwa nao kwangu, Mola wangu. Refusha umri wako kwa ajili yangu wazidishie muda wao kwa ajili yangu mlee kwa ajili yangu mdogo miongoni mwako. Mpe nguvu aliyedhaifu miongoni mwao vipe siha kwa ajili yangu viwili wili vyao, miili yao na dini yao natabia zao. Wape afya nafsini mwao, viungo vya miili yao na kwa kila chenye umuhimu kwangu katika mambo yao. Nitiririshie juu ya mikono yangu riziki zao. Na wafanye wawe wema, wacha mungu watambuzi. Wasikivu watii kwao na kwa mawalii wako wana wapenda na kufuata ushauri wao. Na kwa maaduwi zako wote wana wapinga vikali ameen.

Oh Allah! Ipe nguvu mikono yangu kupitia wao kupitia wao unyoshe mgongo wangu uliotopewa. Iongeze Idadi yangu. Kupitia wao yapambe maudhurio yangu. Kupitia wao huisha utajo wangu. Kupitia wao nitosheleze nikiwa sipo. Kupitia wao nisaidiye Haja zangu. Wafanye wanipende wanielekee wanyofu watii kwangu. Wasiwe waasi wala watovu wa heshima wasiwe wafanyao kinyume wala wakosaji. Nisaidiye malezi yao kuwa adabisha na kuwafanya wawe wema. Unipe mimi pamoja na wao kutoka kwa watoto wa kiume. Hivyo ni kheri kwangu uwajaalie wawe msaada kwangu juu ya niliyokuomba. Nilinde mimi na kizazi changu na shetani mlaaniwa. Kwa kuwa wewe umetuumba, umetuamuru na umetukataza. Na umetupendezesha malipo kwa uliyotuamuru, na kutuogopesha adhabu yake. Umetufanyia aduwi anatushauri vibaya umemuwezesha kwetu juu ya ambayo hukutuwezesha sisi juu yake. Umemuwezesha kuketi vifuwani mwetu na kumpitisha ndani ya mishipa yetu ya damu. Haghafiliki tughafilikapo. Hasahau tunaposahau! Anatufanya tuone tuko salama na adhabu yako. Na yu atuogopesha na mwingine asiyekuwa wewe. Tukusudiapo kutenda yasiyofaa anatushajiisha. Na tukusudiapo kufanya tendo jema atuvunja moyo. Anatupinga kwa vishawishi. Hutuwekea mashaka. Akitupa ahadi hudanganya akitupa matumaini atatufanyia kinyume chake. Kama hautotuondolea vitimbi vyake atatupoteza. Kama hautotulinda na maovu yake atatutekelezesha.

Oh Allah! Ushinde uwezo wake kwetu kwa uwezo wako. Ili umzuiye mbali nasi kwa wingi wa DU'A zetu kwako. Mpaka tuwe miongoni mwa waliohifadhiwa na wewe mbali na vitimbi vyake. Oh Allah! Nipe mimi niliyoyaomba yote. Na kidhi haja zangu. Usiniziwiye itikio hali ulikwishachukuwa dhamana yake kwa ajili yangu usiizibe duwa yangu kwako hali uliniamuru nikuombe. Kuwa mwema kwangu kwa kila kitakachoniweka sawa katika dunia yangu na akhera yangu. Nikumbukacho na ni nachosahau. Ninachodhihirisha na ninachokificha. Nilichokitangaza au kukifanya siri nifanye kwa yote hayo kwa maombi yangu kwako kuwa miongoni mwa watu wema. Walio fanikiwa kwa kukuomba wewe wasio zuiliwa kwa kutegemea juu yako waliokingwa kwa kuomba kinga kwako waliopata faida kwa kufanya biashara na wewe. Waliopewa kimbilio kwa enzi yako. Waliopewa riziki nyingi ya halali kwa fadhila zako zenye wasaa na upaji, na ukarimu. Walioepushwa na dhulma kwa uadilifu wako. Waliowekwa mbali na balaa kwa rehma zako. Waliotajirishwa baada ya ufakiri kwa utajiri wako. Waliohifadhiwa mbali na dhambi kuteleza, na makosa kwa kukuogopa wewe. Waliofanikishwa kwa mema, mwongozo, na umakini kwa kukutii wewe. Waliokingwa kati yao na dhambi kwa uwezo wako. Walioacha maasi yako yote. Wakazi jirani na wewe. Oh Allah! Tupe yote hayo kwa kufanikishwa na wewe na kwa huruma yako. Tuepushe na adhabu ya moto. Uwape Waislamu wote wanaume na Waislamu wanawake wote.

Waumini wanaume na waumini wanawake. Kama yale niliyokuomba kwa ajili ya nafsi yangu na kwa watoto wangu. Kwa haraka ya hapa duniani na baadaye akhera. Hakika wewe ukaribu na mwenye uwezo wa kujibu. Msikilizaji mjuzi. Mwenye kughofiria mwenye kusamehe mpole mwenye huruma. Na tupe sisi mema duniani na mema akhera na tulinde na adhabu ya moto.

Dua ya 26

DU'A ZAKE(A.S) KWA AJILI YA MAJIRANI ZAKE NA MARAFIKI ZAKE AWATAJAPO

Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Nitumikishe kwa majirani zangu na marafiki zangu waitambuayo haki yetu na wapiganao na maaduwi zetu kwa utumishi ulio bora. Wafanikieshe. Kutekeleza sunnah 'yako. Nakuchukuwa adabu zako nzuri. Katika kuwatendea kwa upole wanyonge wao. Na kurekibisha dosari yao. Kuwatembelea wagonjwa wao. Kumwongoza atakayemwongozo. Kumpa nasaha mwenye kuwataka ushauri. kumpokea msafiri wao anaporudi. Kuwafichia siri zao. Kusitiri aibu yao. Kumsaidia mdhulumiwa wao. Kushirikiana nao vizuri katika matumizi ya vyombo. Nakuwapa yaliyo wajibu kwao kabla hawajaomba Nijaalie Oh Allah! Nimlipe mema muovu wao Nitupilie mbali kwa uvumilivu maovu ya dhalimu wao. Kuwadhania dhana njema wote. Niwatendee wema wote. Nirudishe macho yangu chini kujizuia na tamaa. Niteremshe upande wangu kwao kwa unyenyekevu. Niwe mpole kwa waliokumbwa na balaa miongoni mwao kuwa hurumia. Niwafurahishe wakiwa hawapo kwa upendo Nipende wabakiye na Neema kwa nia njema wape ambalo niwapalo jamaa zangu. Niwachungiye ambalo niwachungialo Marafiki zangu mahsusi. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Niruzuku kwa kadiri hiyo hiyo toka kwao. Nijaaliye hadhi ya kutosha katika waliyonayo wazidishiye utambuzi katika haki yangu, Na elimu ya ubora wangu. Ili wafanikiwe kupitia mimi na nifanikiwe kupitia wao. Ameen, E! Bwana wa Ulimwengu wote.

DUA YA 27

DU'A ZAKE(A.S) KWA WATU WA MPAKANI

Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Uimarishe mstari wa mbele wa Waislamu kwa uwezo wako. Wape nguvu walinzi wake kwa nguvu zako. Kithirisha wapewacho kwa utajiri wako Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Zidisha idadi yao. Nowa silaha zao. Ilinde nchi yao. Yalinde mapambano yao. Unganisha mkusanyiko wao. Pangilia mambo yao. Fululiza posho lao. Peke yako chukuwa jukumu la kuwatosheleza posho lao. Waunge mkono kwa ushindi wasaidie kuwa na subira. Wape werevu kwenye vitimbi. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Watambulishe wasio yajuwa Wafundishe wasiyoyajua Waoneshe wasiyoyaona

Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Wasahaulishe wakati wa kutanapo na aduwi. Kuikumbuka Dunia yao babaishi danganyifu. Futa toka mioyoni mwao fikra ya mali ipendezayo sana. Na ifanye Jannah iwe mbele ya macho yao. Waoneshe baadhi ya uliyowaandalia humo machoni mwao. Miongoni mwa makazi ya kudumu. Nyumba za heshima. Huri warembo. Mito ibubujikayo kwa aina aina za vinywaji. Miti iliyojiangika karibu ikiwa na sampuli tofauti za matunda. Ili yeyote miongoni mwao asiwe na wazo la kutumba mgongo, Wala asijishauri kumkimbia mpinzani wake. Oh Allah! Kwa hayo mshinde aduwi yao. Mkate makucha yake kutoka kwao, waweke mbali na silaha zao. Ondoa uthabiti wa mioyoyao. Waweke mbali na akiba yao. Watundu waze katika njia zao. Wapotoshe toka kwenye mwelekeo wao. Wakatie msaada. Wapunguze idadi. Wajaze woga mioyoni mwao. Igandishe mikono yao isiweze kukunjuka, zifunge ndimi zao zisiongee, watawanye walio nyuma yao. Wape funzo walio nyuma yao. Zikate tamaa za watakaokuja baada yao. Kwa kuwa dhalilisha. Oh Allah! Yafanye tasa matumbo ya wanawake wao. Vikaushe viuno vya wanaume wao Kikate kizazi cha wanyama wao Usiiruhusu mbigu yao kunyesha Wala mmea katika ardhi yao Kwa kufanya hayo uupe nguvu ujasiri wa Uislamu. Boresha kwa hayo ngome za nyumba zao. Kwa hayo wazidishiye mali zao. Waweke mbali na kupambana nao kwa ajili ya ibada yako na mbali na kulumbana nao ili wapate muda wa kujitenga wakiwa na wewe. Ili asiabudiwe ardhini asiyekuwa wewe wala paji lau uso la yeyote miongoni mwao lisisuguliwe kwenye mchanga kwa ajili ya yeyote mbali na wewe. Oh Allah! Wapeleke washambulizi kutoka kila upande wa Waislamu kwa washirikina waliomuka bala wao. Na uwaongezee msaada wa malaika kutoka kwako kwa daraja. 111 wawatimuwe mpaka mwisho wa nchi kwa kuwa uwa katika ardhi yako na kuwateka au wakubali kuwa wewe ndiye Allah ambaye hapana miungu isipokuwa wewe tu, peke yako huna mshirika. Oh Allah ! Waingize kwa hilo maadui zako katika maeneo ya nchi za India, Urumi, Uturuki, Khazars, Abyssinia, Uhabeshi, Noubah Zanji na Daylamite. Na umma zingine za washirikina ambao majina yao na sifa zao zafichika lakini ni ambao umejua hesabu yao kwa maarifa yako. Na umewaona kwa uwezo wako. Oh Allah ! Washughulishe washirikina wao kwa wao ili wasiifikie mipaka ya Waislamu wazuiye kwa kuwa punguza kutoka upungufu wao.

Wazuie kwa mgawanyiko utakaowafanya washindwe kujikusanya dhidi yao. Oh Allah ! Ondoa usalama mioyoni mwao na ondoa nguvu milini mwao, iziwie mioyo yao isiweze kuwa na mbinu, dhoofisha viungo vyao wasiweze kupambana na wanaume. Wafanye wawe waoga kiasi cha kuwa hawawezi kupambana na mashujaa, watumie askari kutoka miongoni mwa malaika wako kwa ukali kutoka ukali wako. Kama ulivyofanya siku ya badri uikate mizizi yao kwa hilo, kwa hilo uiondoe miba yao na uitawanye idadi yao. Oh Allah ! changanya maji yao maradhi yakuambukiza na vyakula vyao na maradhi, iangamize miji yao kwa kuifuta kabisa. Na wahangaishe kwa kutupiwa, wazuiye kwa ukame. Na ijaalie rizki yao kwenye ardhi yenye ukuba mno miongoni mwa ardhi zako, ardhi iliyo mbali sana nao, wazuie wao kwenye ngome zake (ardhi) wape njaa ya mara kwa mara na ugonjwa uumizao. Oh Allah! Na mshambuliaji yeyote akiwashambulia kutoka watu wa mila yako, au mpambanaji akipambana kutoka wafuasi wa sunnah yako, ili dini yako iwe juu. Na kundi lako liwe ndilo kundi lenye nguvu mno. Na hadhi yako iwe kamili. Mpe nafuu, mpangie mambo, mpe mafanikio, mchagulie wenzi, umpe nguvu mgongo wake, mzidishiye nafaka, umstareheshe kwa uzima na nguvu. Umzimishie joto la shauku, mpe kimbilio kutokana na huzuni ya upeka. Msahaulishe kuwakumbuka mke na watoto, mpitishie kuchagua nia njema mpe afya.

Mwambatanishie usalama mwepushe na woga, mpe ushujaa, mpe nguvu, msaidie kwa kumpa ushindi. Mfundishe sera njema na sunnah, mweke sawa katika kuhukumu. Mwondolee riyaa, mwepushe na kupenda kusifiwa, na ifanye fikra yake, kumbukumbu yake, safari yake, na kaa yake iwe katika wewe na kwa ajili yako. Asimamapo safu kwa adui yake na adui yako waonyeshe mbele ya macho yake kuwa ni wadogo. Udogeshe umuhimu wao moyoni mwake zamu ya ushindi dhidi yao iwe yake, wala usiifanye zamu ya ushindi kuwa yao, lakini endapo utamuhitimishia na heri na kumwamulia kupata shahadat. Acha iwe baada ya kumng'owa adui yako kwa kumuuwa na baada ya kutekwa kumewachujusha. Na baada ya kuwa mipaka ya Waislamu iko salama. Na baada ya kuwa adui yako amekwisha tumba mgongo akimbia.

Oh Allah! Muislamu yeyote akimwacha mpiganaji au askari mlinzi katika nyumba yake akatunza alivyoviacha nyuma yake. au akamsaidia kwa sehemu ya mali yake au kumsaidia kwa vyombo au kumnowa kwa ajili ya vita au kumwagizia mbele ya uso wake DU'A au kumhifadhia heshima nyuma yake. Mpe malipo mfano wa malipo yake uzito kwa uzito. Na mfano kwa mfano, mpe malipo ya kitendo chake malipo ya haraka ambayo ataharakia kunufaika na alichokitanguliza na kufurahia alichokileta mpaka wakati uishiye kwenye yale uliyompa miongoni mwa fadhila zako. Na uliyomwandalia kutokana na ukarimu wako. Oh Allah ! Muislamu yeyote atilia manani suala la Uislamu na kumuhuzunisha ushirikiano wa washirikina dhidi yao. Kwa hiyo akawa na nia ya kwenda vitani au akusudia jihadi. "Lakini udhaifu ukamzuia au umasikini umemchelewesha au tukio la bahati mbaya likamzuia au amezukiwa na jambo kinyume na utashi wake. Basi andika jina lake miongoni mwa wachamungu wajibisha kwake thawabu za wapiganaji jihadi. Na mweke katika daraja ya mashahidi na watu wema. Oh Allah ! Mrehemu Muhammad mja wako na Mjumbe wako na Ali wake Muhammad Rehma ya hali ya juu. Juu ya rehma na maamkizi Rehma haina mwisho wala idadi yake haikatiki kama Rehma zako zilizokamili mno miongoni mwa zilizopita kwa yeyote miongoni mwa mawalii wako. Hakika wewe mwema mwenye kuhimidiwa, mwanzilishi na mwenye kurudisha mtekelezaji wa utakalo.

DUA YA 28

DU'A ZAKE ANAPOKIMBILIA KWA ALLAH

Oh Allah! Nimekuwa mnyofu kwa kukata mawasiliano na kingine chochote isipokuwa kwako, mzima na kwa yote nimeelekea juu yako. Nimeugeuza uso wangu toka kwa ambaye yu ahitajia au ni yako. Nimeacha maombi kwa asiyejiweza bila ya fadhila zako. Nimeona kuwa muhitaji kumwomba muhitaji kama yeye ni upuuzi wa maoni yake. Na ni upotovu wa akili yake, ni wangapi nimewaona ewe Mola wangu miongoni mwa watu.! Wameomba utukufu kwa asiyekuwa wewe wakadhalilika, walitaka mali kwa mwingine ambaye si wewe wamekuwa masikini, walijaribu kupanda wakaanguka. Kwa kuona mifano yao humsahihisha mwerevu. Uangalifu wake umemfanikisha, uchaguzi wake umemwongoza kwenye njia ya sawa. Hivyo basi wewe ewe bwana wangu mbali na mwombaji yeyote ndio mahali pa maombi yangu. Ndio mfadhili wa haja yangu mbali na mwingine yeyote ambaye maombi hufanywa kwake. Wewe tu wahusika pekee kwa wito wangu kabla ya mwombaji mwingine yeyote.

Hakuna ashirikishwaye na wewe katika matumaini yangu. Wala yeyote hawafikiani na wewe katika DU'A zangu. Wala hapana yeyote ajiungaye na wewe katika hili. Kwako wewe tu ndiyo maombi yangu. Wako ewe Mola wangu, ni umoja wa idadi, na miliki ya uwezo wa milele, na ubora wa uwezo na nguvu, na daraja ya utukufu wa juu kabisa, na yeyote ambaye si wewe ni wakuhurumiwa maishani mwake, mwenye kuhemewa katika mambo yake. Mwenye kushindishwa na hali yake mambo yake tofauti, zabadilika sifa zake, hivyo basi uko juu mbali na kufanana na vitu au kitu kuwa dhidi yako. Umetukuka huwi mfano wa chochote na dhidi yeyote kwako. Utakatifu ni wako hapana miungu isipokuwa ni wewe.

DUA YA 30

DU'A ZAKE(A.S) KWA AJILI YA KUOMBA MSAADA WA KULIPA DENI

Oh Allah ! Mrehemu Muhammad na Aliy zake. Nikombowe kutokana na deni ambalo lachakaza uso wangu laichanganya akili yangu, latawanya fikra yangu ili kulipa shughuli yangu inakuwa ndefu, na ninajikinga kwako Ewe bwana wangu kutokana na woge wa deni na fikra zake. Mshughuliko wa deni na mkesho wake msalie Muhammad na Aliy zake, nilinde nayo. Naomba hifadhi kwako ewe, Mola wangu ili niepukane na dhila yake maishani na kufuatiliwa kwake baada ya kufa. Mrehemu Muhammad na Aliy zake. Na unipe hifadhi niepukane nalo kwa kunipanulia fadhila au kwa kufululiziwa utoshelezi wako.

Oh Allah ! Mrehemu Muhammad na Aliy zake, nizuwie kufanya israfu na kutumia zaidi ya haja. Niweke sawa katika kutoa kwa ukarimu na wastani. Nifundishe uzuri wa kukadiria, nikamate kwa upole wako nisifuje, ipitishe rizki yangu kwa njia ya halali, uelekeze utowaji wangu kwenye milango ya wema. Niepushe na mali itakayonisababishia majivuno au kunifanya niwe jeuri au itakayonifikisha kwenye kukiuka mipaka. Oh Allah ! nipendezeshe kusuhubiana na mafakiri nisaidie katika kusuhubiana nao kuwa na saburi njema. Uniondoleapo mafao ya dunia ya mpito nihifadhiye nayo katika hazina zako za kudumu.Jaalia uliyonitunukia miongoni mwa mabomoko yake na vifaa vyake ulivyo harakisha kunipa, viwe ni njia ya kuufikia ujirani wako na kiungo cha ukaribu wako' na ni sababu ya kuifikia janna yako kwa hakika wewe ni mwenye fadhila kubwa na wewe ni mpaji mkarimu.


6

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

DUA YA 31

DU'A ZAKE (A.S) KATIKA KUIELEZEA TOBA NA KUIOMBA

Oh Allah! Oh yule ambaye hazi sifa za wenye kumsifu kumsifia. Oh we ambaye hayamvuki matarajio ya watarajiao. Oh we ambaye kwake hayapotei malipo ya watenda mema. Oh we ambaye yeye ndiye mwisho wa hofu ya wachapa ibada. Oh we ambaye ni upeo wa woga wa wachamungu. Hiki ni kituo cha aliyepitiwa na madhambi mkono kwa mkono. Hatamu za makosa zimemwongoza na shetani amemtawala. Amezembea kutekeleza uliyomwamrisha kwa kupuuza. Na akajipa uliyomkataza ajiepushe nayo katika hali ya kudanganyika akiwa kama asiyejua uwezo wako juu yake, au akiwa kama mfano wa akanushaye ubora wa ihisani yako kwake! Mpaka jicho la uongofu litakapo mfungukia. Viwingu vya upofu vitakapomtanduka atahesabu vile ambavyo ameidhulumu nafsi yake. Na atatafakari katika yale amemkhalifu bwana wake. Hivyo ataona ukubwa wa maasi yake kuwa ni mkubwa na uzito wa kumkhalifu kwake kuwa ni mzito. Kwa hiyo ataelekea upande wako akikutumainia, akikuonea haya. ataelekeza maombi yake kwa kukuamini atakuwa amejitengeneza upya kwako kwa tamaa zake akiwa na yakini. Amekukusudia moja kwa moja kwa hofu na unyofu, tamaa zake zimeepukana na yote ya kufanyiwa tamaa bali ni wewe tu.

Kwa hiyo amesimama mbele yako akijitetea ameyaelekeza macho yake chini mnyenyekevu, ameinamisha kichwa chake kwa ajili ya utukufu wako mwenye kujidhalilisha. Akudhihirishia siri zake ambazo wewe wazijua vizuri mno kuliko yeye hali ya unyenyekevu. Atakuwa amezihesabu dhambi zake kwa unyenyekevu hali wewe wazijua vizuri mno idadi yake. Atakuomba sana msaada kwa lakutisha ambalo ameangukia humo katika elimu yako Na kwa ajili ya baya lililomfedhehesha katika hukumu yako miongoni mwa dhambi ambazo starehe zake zimetumba mgongo na kutokomea ambazo matokeo ya ubaya wake yamethibiti na kulazimu. Hato kanusha Oh! Mola wangu uadilifu wako endapo utamwadhibu wala hatouzingatia msamaha wako kuwa ni jambo kubwa endapo utamsamehe na kumuhurumia kwa sababu wewe ni bwana mkarimu ambaye hadogeshwi na msamaha wa dhambi kubwa. Oh Allah ! mimi ni huyoo! Nimekujia hali nikiwa mtii wa amri yako kwa kuwa umeamuru kuomba DU'A kwa hiyo nakuomba kutekeleza ahadi yako kwa uliyoahidi kujibu kwa vile wasema: (niombeni nitakujibuni). Oh Allah! mrehemu Muhammad na Aliy zake, kutana na mimi kwa msamaha wako kama nilivyokutana na wewe kwa kukiri kwangu. Niinuwe kutokana na mweleka wa dhambi kama nilivyojitupa chini kwako, nisitiri kwa sitara yako kama vile ulivyoacha kunifanyia haraka malipizi. Oh Allah! Iimarishe nia yangu katika utii wako upe nguvu ufahamu wangu katika ibada yako, nipe tawfiki katika matendo mema ambayo yataniosha uchafu wa makosa. Nifishe nikiwa katika mila yako na mila ya Nabiy wako Muhammad amani imfikie Oh Allah!, Hakika mimi natubu kwako katika kikao changu hiki kuwa nitaacha madhambi yangu makubwa na madogo.

Maovu yangu ya ndani na nje kupotoka kwangu kulikotangulia na kwa hivi sasa toba ya mtu asiyeweza fanya maasi wala hana dhamira ya kurejea kwenye makosa. Na kwa hakika umekwisha sema ewee Mola wangu katika kitabu chako thabiti kuwa hakika wewe waikubali toba ya waja wako na wasamehe maovu. Na unawapenda wanaotubu basi ikubali toba yangu kama ulivyoahidi na nisamehe maovu yangu kama ulivyochukua dhamana. Na niwajibishie mapenzi yako kama ulivyoweka sharti, sharti yangu kwako Oh bwana wangu sitorudi kwenye machukio yako na dhamana yangu nitoayo ni kuwa sitorudi kwenye yalaumiwayo na wewe. Na ahadi yangu ni kwamba nitayahama maasi yako yote. Oh Allah! hakika wewe wajua zaidi niliyoyatenda. Basi nighofirie uliyoyajua niepushe kwa uwezo wako na nielekeze kwenye ambayo wayapenda. Oh Allah ! na dhidi yangu kuna haki daiwa nimezihifadhi, na haki daiwa nimezisahau zote hizo zi jichoni mwako ambalo halilali. Na elimu yako ambayo haisahau wafidie wenye haki na nipunguzie mzigo wake, nifanyie wepesi uzito wake, nilinde nisiikurubie iliyo mfano wake. Oh Allah! kwa hakika sina uwezo wa kutekeleza toba yangu isipokuwa kwa kulindwa na wewe wala kujiziwiya na makosa isipokuwa kwa uwezo wako nipe uwezo wa kutosha. Nipe ulinzi wako wenye kuzuiya. Oh Allah! mja yeyote ametubu kwako naye katika elimu yako ya ghaibu ataitanguwa toba yake, na atarejea katika dhambi zake na makosa yake. Kwa hakika mimi najilinda kwako nisiwe kama vile, ifanye toba yangu hii toba sihitajii baada yake toba yeyote. Iwe toba iwajibishayo kufuta yaliyotangulia, na ya salama kwa yaliyobaki. Ewe Mola! Hakika mimi nakuomba msamaha kwa sababu ya ujinga wangu. Nakuomba usitilie manani vitendo vyangu viovu, niunganishe kwenye kivuli cha rehma yako kwa ihsani, nisitiri kwa sitara ya afya yako kwa fadhila zako. Oh Allahl kwa hakika mimi ninatubu kwako kutokana na kila kilichokwenda.

Kinyume na utashi wako au kimekuwa mbali na mapenzi yako kutoka mawazo ya moyoni mwangu, mtizamo wa macho yangu na hekaya za ulimi wangu.Toba ambayo kila kiungo cha mwili wangu kitabaki salama bila malipizi yako na kitakuwa na amani bila ya woga wa yale wayaogopayo wakiukaji miongoni mwa machungu ya adhabu zako. Oh Allah! Uhurumie upweke wangu mbele yako, na kupondekana kwa moyo wangu kutokana na kukuogopa wewe. Nakutetemea kwa viungo vya mwili wangu kwa ajili ya haiba yako. Ewe Bwana wangu! Dhambi zangu zimeniweka weko la kudharauliwa uwanjani pako. Nikinyamaza hakuna atakayenisemea na nikiomba Shafaa sikuwa miongoni mwa wenye haki ya kupata Shafaa. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali Zake Ufanye ukarimu wako kwa mwombezi wa makosa yangu. Yarejelee maouvu yangu kwa msamaha wako. Usinilipe malipo ninayostahiki katika adhabu zako. Ni kunjuliye juu yangu ihisani zako ni viringishe sitara yako. Nitendee kitendo cha mtu mwenye enzi wakati mtumwa dhalili amnyenyekeapo na akamuhurumia. Au tendo la mtu tajiri fakiri anapomnyenyekea naye akamtajirisha. Oh Allah! Sina wakunilinda dhidi yako hivyo basi naomba Enzi yako inilinde. Sina mwombezi kwako hivyo basi fadhila zako ziwe ndiyo mwombezi wangu. Makosa yangu yamenitia hofu wacha msamaha wako unipe amani. Siyo yote niliyotamka kwa ujinga wangu kwa sababu ya ufuatiliaji wangu mbaya wala sikusahau yaliyopita miongoni mwa matendo yangu yastahiliyo kulaumiwa.

Lakini ili mbingu zako zisikie na waliomo humo na ardhi yako na waliomo juu yake niliyokudhihirishia miongoni mwa majuto. Na nimekimbilia kwako kutubu. Huwenda baadhi yao kwa Rehema Zako watanirehemu kwa sababu ya ubaya wa kikao changu. Au mtu ashikwe na huruma juu yangu kwa sababu ya ubaya wa hali yangu. Huenda nikapata kutoka kwake DU'A ambayo sikilizwa mno kwako kuliko Duwa yangu. Au ombezi lenye nguvu mno kwako kuliko ombezi langu. Humo utakuwa uwokovu wangu epukana na ghadhabu zako. Na kufuzu kwangu kwa ridhaa zako

Oh Allah! Ikiwa kujuta ni toba ya kukubaliwa kwako, basi mimi ni mjutaji mno wa wajutaji wote. Na ikiwa kuacha kukuasi ndio kurejea kwako, basi mimi ni mrejea wa kwanza kwako kuliko warejeao wote. Na ikiwa kuomba ghofira ni sababu ya kupunguziwa dhambi, basi mimi ni miongoni mwa wakuombao ghofira. Oh Allah! Kama ulivyoamrisha toba na ukachukuwa dhamana msalie Muhammad na Aali zake ikubali toba yangu. Wala usinirudishe Rudisho la kutofanikiwa Rehma zako. Hakika wewe ni mwingi wa kupokea toba ya watenda dhambi. Na mwenye Rehma sana kwa wakosaji wanaorejea kwako. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali Zake. Na kama vile umetuongoza kwa sababu yake mrehemu Muhammad na Aali zake. Kama ulivyotuokowa kwa sababu yake mrehemu Muhammad na Aali Zake Rehema itakayotuombea siku ya Kiyama na siku ya kukuhitajia. Hakika wewe ni muweza wa kila kutu na ni rahisi kwako.

DUA YA 32

DU'A ZAKE BAADA YA KUMALIZA SALA ZA USIKU

Oh Allah! mmiliki wa ufalme wa kudumu wa melele. Utawala usioshindika bila ya askari wala wasaidizi. Na enzi ya kubaki miaka nenda miaka rudi zama nenda zama rudi siku nenda siku rudi. Yana Enzi mamlaka yako Enzi isiyo na mpaka wa mwanzo wala mwisho. Ufalme wako umekuwa wa juu zaidi vimeporomoka vitu bila ya kuufikia muhula wake. Sifa zenye uwezo wambali za wenye kusifu hazitoweza kukufikia kile kidogo mno ulichojitengea kwa ajili yako. Kwako sifa zimepotoka. Zimeshindwa kukufikia sifa. Mawazo yame DU'A mbele ya utukufu wako. Kwa ajili hiyo wewe ni wa Daima hutoweki. Nami ni Mja dhaifu wa matendo mwenye matumaini makubwa kabisa. Sababu za kuwasiliana zimeponyoka toka mikononi mwangu isipokuwa zilizo wasilishwa na Rehma zako. Hamana za matumaini zimenikatika isipokuwa ni ishikiliayo katika msamaha wako. Kimekuwa kidogo mno niwezacho kukihesabu katika utii wangu kwako. Yamekithiri dhidi yangu maasi yangu kwako haitokuwia dhiki kumsamehe mja wako japo afanye maovu basi nisamehe Oh Allah!

Elimu yako ya chunga kazi zilizojificha kila kilicho sitirika kimefichuka mbele ya utambuzi wako. Hayafichiki kwako mambo madogo sana na viroja vya siri kabisa havifichiki kwako. Adui yako amenishinda nguvu adui ambaye alikuomba umbakishe ili anipotoshe na ulimbakisha. Alikuomba umpe muhla wa kubakia mpaka siku ya hukumu ili anipoteze ulimpa muhula. Hivyo basi amenitupa chini ingawaje nimekimbilia kwako kutokana na madhambi madogo madogo angamizi na amali kubwa ziuwazo mpaka nilipotenda maasi yako na kwa ubaya wa juhudi yangu nimewajibika chuki yako. Amegeuza toka kwangu ugwe ya udanganyifu wake. Akakutana na mimi kwa neno lake la kufuru. Akajitenga na mimi. Akatumba mgongo anikimbia. Kwa hiyo akanitupa kwenye jangwa la ghadhabu zako peke yangu. Amenitoa nje na kuniweka kwenye uwanja wa malipizi ya kisasi chako nikiwa mwenye kufukuzwa. Hakuna mwombezi atakayeniombea kwako wala mlinzi atakayenifanya niwe na amani kwako. Wala hakuna ngome itakayonificha wewe usinione. Wala hapana kimbilio niwezalo kukimbilia kukukimbia wewe. Hivyo hiki ni kikao cha ajilindae na wewe nani mahali pa mtu akutambuaye. Basi fadhila zako zisinijie finyu, wala usikose kunifika msamaha wako wala nisiwe miongoni mwa waja wako wasio fanikiwa mno katika waja wako waliotubu. Wala nisiwe miongoni mwa wakata tamaa miongoni mwa wajao kwako wakiwa na matumaini. Nisamehe hakika wewe mghofiri bora miongoni mwa wenye kughofiri. Oh Allah! Hakika umeniamrisha nikaacha. Umenikataza nikafanya. Mawazo mabaya yamenifanyia majaribu kufanya mabaya nikazembea. Wala siwezi kutolea ushahidi funga yangu mchana. Wala siwezi kuomba kimbilio kwa ajili ya sala yangu ya Tahajudi usiku wala Sunnah hainipi sifa kwa kuihuisha.

Isipokuwa faradhi zako ambazo atakayezembea atahiliki siwezi kutaka wasila kwako kwa fadhila za sala za naafila hali yakuwa mengi nimeghafilika kuyatenda miongoni mwa nyadhifa za faradhi zako na nimevuka mipaka yako. Na kukiuka sehemu takatifu. Madhambi makubwa nimeyatenda ingawa afya yako ilikuwa kwangu ndio sitara kwa kuepukana na fedheha yake. Haya ni makazi ya mwenye kujionea haya binafsi mbele yako, na ameikasirikia nafsi yake, na ameridhika na wewe. Kwa hiyo akutana na wewe kwa moyo mnyenyekevu. Shingo iliyoinama chini. Mgongo mzito kwa makosa. Amesimama akibabaika kati ya kukupenda na kukuogopa. Na wewe ni bora wa aliowatumainia. Na umwenye haki mno kati ya alio waogopa na kuwa hofu. Basi nipe ewe Bwana wangu niliokutumainia. Nipe Nipe amani kwa niliyojihadhari nayo nihurumie kwa huruma za Rehema yako hakika wewe u mkarimu mno miongoni mwa wenye kuombwa. Oh Allah! kwa vile umenisitiri kwa afya yako. Na umenikinga kwa fadhila zako katika makazi yenye mwisho mbele ya marika nipe kimbilio la kujiepusha na fedheha za makazi ya kubaki milele waliko simama mashahidi. Miongoni mwa malaika walioletwa karibu na mitume waheshimiwa na watu waliokufa mashahidi na watu wema. Miongoni mwa jirani nilikuwa na mficha maovu yangu. Na ndugu watumbo moja nilikuwa namwonea haya siri zangu. Sikuwa na waamini kunisitiri Oh Rabi! Nimekuamini wewe Oh! Mola wangu, katika kunighofiria. Na wewe ni bora mno wa kuaminiwa. Na u mtowaji mno kuliko wote waombwao u mwema mno kuliko wote wanaoombwa Rehema, hivyo ni Rehemu. Ewe Mola wewe ndiwe uliye nifanya nitoke kwenye asili ya maji duni. Kutoka kiuno chenye mifupa miembamba na mapito ya shida.

Mpaka kwenye tumbo jembamba uliloli sitiri kwa mifuniko. Wani hamisha toka hali moja kwenda hali nyingine. Mpaka ulinimalizia kwenye umbo lililo kamilika. Ukaniweka viungo vya mwili, kama ulivyoaridhia katika kitabu chako (tone la Manii) kisha pande la Damu, kisha nyama, kisha mifupa, kisha uliivisha mifupa na nyama, kisha ulinifanya umbo jingine) kama ulivyopenda mpaka nilipohitaji riziki yako siku jitosha bila ya msaada wa fadhila zako. Ulinifanyia chakula chenye lishe kutoka fadhila ya chakula na kinywaji ulichomtunukia kijakazi wako ambaye tumbo lake ulifanya kuwa makazi yangu. Uliniweka chini ya tumbo lake la uzazi. Ewe Mola wangu! Lau ungeniwakilisha katika hali zile kwenye uwezo wangu au ungenifanya ni lazimike kutumia nguvu zangu. Uwezo ungekuwa haupo kwangu. Na nguvu zingekuwa mbali na mimi. Ulinipa lishe kwa fadhila zako lishe ya mtu mwema mwenye huruma. Wanitendea hayo kwa wema tu juu yangu mpaka kwenye mwisho wangu huu. Siyakosi mema yako. Mema yako haya niachi ningojee, pamoja na yote hayo 'ithibati' yangu haijaimarika. Kiasi cha kuwa niwe nina nafasi kwa ajili ya lile ambalo lina hadhi sana kwangu mbele yako.

Shetani ameshika barabara hatamu yangu kupitia dhana yangu mbaya. Na udhaifu wa yakini. Kwa hiyo mimi na nung'unika ubaya wa ujirani wake na mimi, na nafsi yangu kumtii yeye! Nakuomba hifadhi niepukane na utawala wake. Ninanyenyekea kwako ili niondolewe vitimbi vyake dhidi yangu. Sifa njema ni zako kwa sababu ya kuanza kwako Neema kubwa na kwa sababu ya Il-Hamu yako iwezeshayo kutambuwa ihsani na neema. Msaliye Muhammad na Aali Zake na unirahisishiye riziki yangu na unifanye niwe natosheka na makadirio yako kwangu. Unifanye ni ridhike na hisa yangu katika ulichonigawiya. Na ujaaliye kilicho toweka toka mwili wangu na umri wangu kiwe ni kwa ajili ya njia ya utii wako. Hakika wewe ni mbora wa watowao riziki.

Oh Allah! Hakika mimi najilinda nawe ili kuepukana na moto ulioutia makali dhidi ya watakaokuasi. Moto ambao umemuonya mwenye kugeuka mbali na ridhaa zako na moto ambao mwanga wake ni giza. Ambao nafuu yake ni machungu na umbali wake ni karibu. Kutokana na moto ambao baadhi yake yaila baadhi nyingine. Moto ambao waiacha mifupa imekwisha teketeza. Unawanywesha watu wake maji yachemkayo. Moto ambao haumwachii mwenye kukiri kwake. Hautomhurumia mwenye kuomba Rehema. Hauwezi kujipunguza makali kwa mwenye kuunyenyekea na kusalimu amri kwake. wapambana na wakazi wake kwa joto ililo nalo kwa mateso yaumizayo na ghadhabu kali mno. Najilinda kwako na nge wake walio midomo wazi. Na nyoka wake wenye meno yagege DU'A yo. Na kinywaji chake kinacho kata utumbo na nyoyo za wakazi wake na kuutowa ubongo wao. Nakuomba mwongozo kutoka kwako wa kile ambacho kitaweka mbali na huwo moto na kuufanya urudi nyuma. Oh Allah!

Mrehemu Muhammad na Aali Zake nipe kimbilio ili niepukane nao kwa fadhila za Rehema Zako. Nisamehe kujikwaa kwangu kwa uzuri wa msamaha wako. Wala usinitupe Ewe Mbora wa kutowa kimbilio. Oh Allah! Hakika wewe wahifadhi lichukizalo, Na watowa lililo zuri. Watenda upendalo, na U-muweza juu ya kila kitu. Oh Allah! mrehemu Muhammad na Aali Zake watajwapo watu wema. Na mrehemu Mhammad na Aali Zake kwa kadiri ya usiku na mchana unavyopishana kwa heri. Rehema ambazo ongezo lake halikatiki idadi yake haihesabiki. Rehema itakayojaza anga, na itajaaza ardhi na mbingu. O Allah! Mrehemu yeye mpaka aridhike O Allah! Mrehemu yeye na Aali Zake baada ya kuridhika. Rehema zisizo na mpaka wala mwisho OWEE Mwingi wa Kurehemu miongoni mwa wanaorehemu.

Dua ya 33

MIONGONI MWA DUWA ZAKE KATIKA ISTIKHARA

Oh Allah! Hakika mimi nakuomba ambalo ni zuri zaidi katika ujuzi wako. Msaliye Muhammad na Aali Zake na tuamuliye lililo zuri zaidi. Na tupe Il-Hamu ya maarifa ya kuchagua. Na ifanye iwe ni sababu ya kuridhiya uliyo yapitisha kwa ajili yetu na kusalimu amri kwa uliyotuhukumia tuondolee mashaka ya kusita sita tu imarishe kwa yakini ya watu wanyofu. Usitupatilize kwa kushindwa kutambua uliyo yachagua tusije tukadharau kadirio lako. Na tusije chukia mahali pa ridhaa zako na kuelemea kwenye ambalo li mbali na mwisho mwema na li karibu sana na kinyume cha afya njema.Tupendezeshe tukichukiacho katika Agizo lako. Na tusahilishiye tuonacho kuwa kigumu katika hukumu yako. Tufunulie kuwa wasikivu kwa uliletalo kwetu katika utashi wako mpaka iwe hatupendi kuchelewesha uliloliharakisha wala kuharakisha uliyolichelewesha. Wala tusichukie ulichopenda wala kuchaguwa ulichokichukia na tuhitimishiye kile chenye mwisho wenye sifa njema mno na matokeo yenye heshima zaidi hakika wewe unafisha chenye heshima na watowa kingi, watenda utakalo nawe u muweza wa kila kitu.

Dua ya 34

DU'A ZAKE AKIPATWA NA BALAA AU AMWONAPO MWENYE KUPATWA NA FEDHEHA, KWA AJILI YA DHAMBI

Oh Allah! Himidi ni yako kwa sababu ya kusitiri kwako baada ya kujuwa kwako. Na msamaha wako baada ya kuelewa kwako. Kila mmoja kati yetu amefanya aibu lakini hukumtangaza na amefanya tendo la utovu wa adabu na wala haukumfedhehesha. Na Alijisitiri kwa maovu wala haukumuonesha. Ni makatazo yako mangapi tumeyatenda! Amri yako umetuagiza na tumeikiuka; matendo maovu tumeyatenda. Makosa tumeyatenda. Ulikuwa ukiyaona na watazamaji wengine hawaoni.

Na muweza wa kuyatangaza kuliko wawezao wote. Uislama uliotupa ni pazia mbali na macho yao. Na kiziwizi dhidi ya masikio yao. Ifanye aibu uliyotufichiya na mambo ya ndani uliyoyaficha yawe onyo kwetu. Na kemeo dhidi ya matendo mabaya na kutenda makosa. Na viwe kichocheo cha juhudi ya kufanya toba ifuatayo na njia yenye kuhimidiwa na usogeze wakati wa toba. Usitupatilize kwa kukusahau kwa hakika sisi twakuomba. Na twatubu kwa kuacha dhambii. Oh Allah! Na mrehemu mteule wako katika viumbe wako Muhammad na kizazi chake, wateule miongoni mwa viumbe wako wa Taharifu. Na tujaaliye sisi kuwa wasikivu na watii kwao kama ulivyoamrisha.

DUA YA 35

MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA RIDHAA AWAANGALIAPO WANA WA DUNIA HII

Sifa njema ni za Allah kwa kuridhika na hukumu ya Allah Nimeshuhudia kuwa Mungu amegawa maisha ya waja wake kwa uadilifu. Amechukuwa jukumu la fadhili viumbe wake wote. Ewe Allah! Mrehem Muhammad na Aali zake. Usinifanyie kishawishi kwa uliyowapa viumbe wako. Wala usiwafanyiye kishawishi kwa uliyoninyima, ili nisije mwonea husuda kiumbe wako na kuyadharau maamuzi yako. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali Zake. Ipendezeshe nafsi yangu maamuzi yako. Kipanuwe kifuwa changu katika maeneo ya maamuzi yako. Nipe imani ili nikirikwa imani hiyo ya kuwa maamuzi yako hayafanyiki ila kwa kheri. Na ifanye shukurani yangu kwako juu ya ulichokiondoa kwangu iwe kubwa zaidi kuliko shukrani yangu kwako juu ya ulichonipa.

Unilinde nisije dhaniya kuwa kutokuwa na kitu kwa mtu ni kudunishwa au ni mdhaniye mwenye utajiri kuwa mwenye ubora (kwa Mungu). Kwa kuwa mbora ni yule aliye boreshwa na utii wako. Na mwenye enzi ni yule aliye enziwa na Ibada zako. Mswalie Muhammad na Aliy zake tupe starehe kwa mali isiyokwisha. Tupe nguvu kwa Enzi isiyotoweka. Tupe nafasi katika ufalme wa milele. Hakika wewe ni Mmoja peke yako kimbilio la milele. Haukuzaa wala haukuzaliwa, wala hakuna anayelingana na wewe.

DUA YA 36

DU'A ZAKE AANGALIAPO MAWINGU NA UMULIKAJI NA ASIKIAPO SAUTI YA RADI

Oh Allah! hakika hizi ni alama zako mbili na hawa ni wasaidizi wako wawili wa harakiao utii wako imma kwa Rehema yenye manufaa au kisasi kiumizacho. Usituteremshie kutoka kwa wawili hao mvua mbaya. Usituvishe toka kwa wawili hao vazi la balaa. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Na ututeremshie manufaa ya mawingu haya na baraka zake. Na utuondolee adha yake na madhara yake. Usitufikishie maafa kutokana nao usitutumie uharibifu wowote katika maisha yetu. Oh Allah! Ikiwa umewapeleka hao kwa kisasi na umewatuma kwa makasiriko basi twakuomba kimbilio ili kuepukana na ghadhabu zako.

Tunakusihi utupe msamaha wako elemea kwa washirikina kwa ghadhabu. Tupa jiwe la ghadhabu zako kwa makafiri. Oh Allah! Ondoa ukame wa nchi yetu kwa maji yako. Ondoa ukorofi wa vifua vyetu kwa riziki yako. Usituzuie kwako kwa kutushughulisha na kingine mbali na wewe. Usitukatie sote sisi vitu vya wema wako, kwa kuwa tajiri ni yule uliyemtajirisha aliyesalimika ni yule uliyemlinda. Hakuna yeyote mwenye ulinzi bila ya wewe. Hapana yeyote awezaye kuzuia adhabu yako. Waamua utakalo kwa umtakaye. Wapitisha utakalo kwa umtakaye. Sifa njema ni zako kutulinda na balaa. shukrani ni zako kwa kutupa neema. Sifa njema zitakazo ziwacha nyuma sifa njema za wenye kusifu kwa sifa njema. Sifa njema zitakazojaa ardhi yake na mbingu yake. Hakika wewe mwenye huruma nyingi mpaji wa neema nyingi. Mpokeaji wa sifa kidogo mwenye kushukuru ihisani ndogo matenda mema mtenda mzuri mfadhili. Hapana muabudiwa ila wewe. Na kwako ndio Marejeo.


7

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

DUA YA 37

DU'A ZAKE(A.S) ANAPOTAMBUWA KUSHINDWA KUTEKELEZA SHUKRANI IPASAVYO

Oh Allah! Hakika hakuna awezaye kufikia upeo wa kukushukuru isipokuwa atakuwa amepata hisani yako ambayo pia itamlazimu akushukuru. Wala hafikii kiwango cha kutosha katika kukutii japo afanye juhudi atakuwa chini ya haki yako kwa sababu ya uwingi wa fadhila zako. Kwa hiyo, mwenye shukrani zaidi miongoni mwa waja wako ashindwa kukushukuru ipasavyo. Na mcha mungu mno miongoni mwao yuko chini ya kiwango cha kukutii. Si wajibu kwa yeyote umsamehe kwa kuwa yu astahiki kusamehewa. Wala hana haki ya kuwa umridhiye kwa kustahiki umghofiriyae ni kwa sababu ya huruma zako. Na umridhiaye ni kwa sababu ya ukarimu wako. Waridhika na shukrani ndogo ulioshukuriwa. Walipa kiasi kikubwa kwa kadiri ndogo uliyotiiwa. Hata yaonekana kana kwamba. Shukurani ya waja wako ambayo umewajibisha malipo yao kwa ajili yake. Na umekithirisha malipo yao kwa sababu yake ni jambo wanamiliki uwezo wa kujizuia bila ya wewe na utawalipa na wala haikuwa sababu yake mkononi mwako ndio ukawalipa! Ukweli ni kuwa umemiliki Ewe Mola wangu! Mambo yao kabla ya waja wako hawajamiliki ibada yako. Uliandaa malipo mema kwa ajili yao kabla hawajaanza kukutii wewe. Hiyo ni kwa sababu sunnah yako ni kufadhili. Na tabia yako ni kufanya ihsani na njia yako ni kusamehe. Kwani kila kiumbe cha tambuwa kuwa wewe si dhalimu kwa uliyemwadhibu. Na chashuhudia kuwa unafanya ukarimu kwa uliyemsamehe, kila mmoja anakiri nafsini mwake kuwa hafanyi uliyowajibisha juu yake ipasavyo.

Lau si kama shetani kuwahadaa na kuwaweka mbali na utii wako asingekuasi mwenye kukuasi lau asingewaonesha batili katika mfano wa haki asingepotea njia yako mpoteaji. Hivyo basi utukufu ni wako ubainifu ulioje wa ukarimu wako katika kumtendea anayekutii au anayekuasi. Wamridhia mtii hali yakuwa wewe ndiye uliyesimama kwa ajili yake. Ulimpa muda mfanya maasi hali yakuwa ulikuwa na uwezo wa kumuharakishia adhabu yake. Kila mmoja wao umempa asilopaswa kupewa. Umempa fadhila kila mmoja wao isio lingana na kazi yake. Lau ungemlipa mtii kulingana na kiwango cha utii wake. Angekaribia kukosa malipo yao mema. Na imtoke neema yako. Lakini kwa ukarimu wako umemlipa muda mfupi uishao kwa muda mrefu wakudumu. Na badali ya upeo wa karibu wakutoweka. Kwa upeo mrefu wakubaki milele kisha hukumfanyia kisasi kwa ajili ya aliyokula miongoni mwa riziki yako inayompa nguvu ya kukutii. Wala haukumdadisi kuhusu viungo vya mwili ambavyo matumizi yake imekuwa ndio sababu ya kuufikia msamaha wako. Ungemfanyia hivyo yangekwenda yote aliyotaabikia na yote aliyoyafanyia juhuudi. Ikiwa ni malipo ya kidogo mno miongoni mwa nufaisho lako na huruma yako. Na angebakia rehani mkononi mwako kuhusiana na neema zako zingine. Basi vipi atakuwa anastahiki kupata chochote katika thawabu zako hakika ni vipi? Hii ewe Mola wangu ndio hali ya aliyekutii na aliyefanya ibada kwa ajili yako. Vipi hali ya mwenye kuasi amri yako na kutenda katazo lako!

Wala haukumuharakishia adhabu yako ili aibadilishe hali yake katika kukuasi wewe na hali ya kurejea kwenye utii wako. Alikuwa anastahiki O Mola wangu! Pale mwanzo alipokuasi kila ulilowaandalia viumbe wako wote miongoni mwa adhabu zako. Kwa hiyo yote uliyoyachelewesha miongoni mwa adhabu na umemcheleweshea kumtia adabu. Ni kuiacha haki yako na kuridhia bila ya wajibu wako. Basi E Mola wangu! Ni nani mkarimu zaidi kuliko wewe? Nani mwenye hali mbaya zaidi kuliko aliyeangamia kwa kutokukujali wewe! Hapana ni Nani? U mwenye baraka mno haiwezekani usifike isipokuwa kwa ihsani, umkarimu mno haiwezekani uogopwe isipokuwa uadilifu. Huogopwi kuwa utamdhulumu aliye kuasi. Wala haiogopwi kuwa utaghafilika kumpa malipo aliyekuridhisha msaliye Muhammad na Aali Zake na unipe matumaini yangu. Nizidishiye mwongozo wako utakaonifikisha kufanikisha amali yangu. Hakika wewe mwenye huruma mkarimu.

DUA YA 38

DUWA ZAKE(A.S) KATIKA KUOMBA RADHI KWA KUWATENDEA VIBAYA WAJA WA MWENYEZI MUNGU KWA KUTOWAJIBIKA IPASAVYO KUHUSU HAKI ZAO NA KUIKOMBOA SHINGO YAKE IEPUKANE NA MOTO

Oh Allah! Mimi nakuomba msamaha kutokana na mdhulumiwa alidhulumiwa mahali mimi nipo na sikumsaidia. Na kutokana na wema nimetendewa sikuwa mwenye shukurani. Na mtenda maovu aliniomba msamaha sikumsamehe. Mwenye shida aliniomba sikumpa kipaombele kuliko nafsi yangu. Na haki ya mwenye haki iliyo nilazimu ya muumini sikuitekeleza. Na aibu ya muumini ilinidhihirikia na sikumsitiri. Na kila aina ya dhambi ilijitokeza mbele yangusikuihama. Nakuomba msamaha Ewe Mola wangu kwa yote haya na kwa yafananayo na haya. Msamaha wa kujuta ambao utakuwa onyo kwa yaliyo mfano wake hapo baadaye. Msaliye Muhammad na Aali zake na jaaliya kujuta kwangu juu ya yale niliyojiingiza katika mitelezo iwe azma ya kujiepusha na yanayojitokeza mbele yangu miongoni mwa maovu. Iwe toba itakayo niwajibishia mapenzi yako. Ewe mpenzi wa wafanyao toba.

DUA YA 39

DUWA ZAKE(A.S) KATIKA KUOMBA MSAMAHA NA REHEMA

Oh Allah! msaliye Muhammad na Aali zake.Yavunje matamanio yangu ya kila haramu. Uondowe uchu wangu wa kila tendo la dhambi. Niziwiye kumuudhi muumini yeyote Muislamu mwanaume na mwanamke. Oh Allah! mja yeyote amenitendea baya ulilo hadharisha kwake na amekiuka kwa kunitendea ulilo mgombeza na amekufa na aliyo nidhulurnu au nimemlalamikia akiwa hai. Msamehe aliyonitendea na umuwiye radhi kwa yale aliyenitumbiya mgongo. Msimsimamishe kumtaka aliyonitendea. Usimuumbue kwa aliyoyachuma kwangu. Na jaaliya niliyosamehe kwa kuwawia radhi na niliyojitolea miongoni mwa sadaka kwao iwe sadaka safi mno miongoni mwa sadaka za watoao sadaka. Na zawadi ya hali ya juu mno miongoni mwa zawadi za watafutao ukaribu na wewe. Nifidiye msamaha wangu kwao kwa msamaha wako. Na DU'A yangu kwao nipate rehema zako ili kila mmoja wetu apate hali njema kwa fadhila zako. Na ili aokoke kila mmoja wetu kwa huruma zako. Oh Allah!

mja yeyote katika waja wako amepata kutoka kwangu ovu au aliguswa na madhara kutoka kwangu au lisilofaa limemfika kupitia kwangu au kwa sababu yangu amedhulumiwa. Nimeshindwa kuwa mwangalifu wa haki yake au nimekwenda (kufa) na haki yake iliyo dhulumiwa. Mswalie Muhammad na Aali zake mridhishe kwa ajili yangu kutaka utajiri wako. Mpe haki yake kamili kutoka kwako kisha nilinde na liwajibishalo hukumu yako kwa ajilii yake. Na niepushe na lihukumiwalo na uadilifu wako. Kwa sababu nguvu zangu haziwezi kuhimili adhabu yako. Na kwa sababu uwezo wangu hauwezi kusimama mbele ya makasiriko yako. Kwa hakika ikiwa utanilipa kulingana na haki utanihilikisha. Na kama hautonikinga na rehema zako utaniangamiza. Oh Allah ! hakika mimi nakuomba Ewe Mola wangu ambacho kukitowa kwake hakukupunguzii (chochote).

Nakuomba kubeba ambalo uzito wake haukutopei. Nakuomba uipe nafsi yangu Ewe Mola wangu! Ambayo haukuiumba ili ujikinge na uovu au iwe ndio njia ya manufaa, bali umeiumba ili kuthibitisha uwezo wako kwa nyingine iliyo mfano wake na kwa sababu iwe ni hoja dhidi ya iliyo mfano wake. Nakuomba ubebe mizigo yangu ya dhambi ambayo uzito wake umenishinda nguvu kubeba. Naomba msaada kwako kwa ajili ya ambalo uzito wake umenielemea. Msaliye Muhammad na Aali zake uipe nafsi yangu ingawa imetenda maovu. Iwakilishe Rehma yako kubeba mzigo wangu (dhambi). Wangapi miongoni mwa watenda mabaya imewafika Rehma zako! Wadhalimu wangapi msamaha wako umewajumuisha. Mswaliye Muhammad na Aali Zake. Na nifanye mimi mfano wa ulio wainuwa kwa kuwastahmilia kutoka kwenye mweleka wa wakosefu. Na umemwokowa kwa tawfeeki yako kutoka kwenye hali mbaya ya waovu. Na akawa aliyeachwa huru na msamaha wako kutoka pingu za makasiriko yako.

Na aliyeachwa huru na wema wako toka kamba za uadilifu wako. Hakika wewe ufanyapo hayo Ewe Mola wangu! wamfanyia ambaye hakanushi kustahiki kwake adhabu yako wala haji takasi nafsi yake kutoka wajibikiwa na malipizi yako. Wamfanyia hivyo Ewe Mola Wangu! Ambaye hofu yake kwako ni nyingi kuliko tamaa yake kwako. Na yule ambaye kukata tamaa kuwa hatofanikiwa ni saana kuliko matumaini yake ya kuokoka. Sio kutokuwa na matumaini kwake ni kukata tamaa au matumaini yake yawe ni kughurika (kudanganyika). Bali ni kwa sababu ya uchache wa mema yake kati ya maovu yake na udhaifu wa hoja zake katika matendo yake yote. Na wewe Ewe Mola wangu, ni mstahiki wa kuwa asi danganyike mbele yako mkweli. Wala asikatishwe tamaa na wewe muovu kwa sababu wewe ni bwana mtukufu ambaye fadhila zake hamziwii yeyote. Wala hamfuatilii yeyote haki yake. Jina lako litukuzwe zaidi ya watukuzwao, yametakasika majina yako zaidi kuliko wote watajwao. Neema zako kwa viumbe wote zimewaenea; zako ni sifa njema kwa yote hayo Ewe Bwana wa Ulimwengu wote.

DUA YA 40

MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) AKITANGAZIWA KIFO CHA MTU AU AKUMBUKAPO UMAUTI

Oh Allah! Msaliye Muhammad na Aali Zake. Tutosheleze na matumaini marefu tupunguzie nayo kwa kazi ya ukweli ili tusitumainiye kuikamilisha saa baada ya saa. Wala kuikamilisha siku baada ya siku wala kukutana pumzi na pumzi nyingine. Wala kukutana hatuwa na hatua nyingine, Tusalimishe na udanganyifu wake tupe amani na shari yake. Uweke umauti mbele yetu dhahiri usijaaliye kumbukumbu yake kwetu kuwa ni ya mara moja na kupotea utujaaliye kuwa miongoni mwa watenda mema. Ili tuone kwa ajili yake kuja kwako kuna chelewa mpaka ifikiye tuuone umauti ni jambo tunalopendezwa nalo. Na tuone umauti ni mahali tulipopazowea tuna shauku napo na mlinzi wetu tumpendaye kuwa karibu naye. Ukiuleta kwetu na kututeremshia tufanye tuwe na furaha nao kama mgeni aliyekuja kututembelea. Tuweke katika raha naye ajapo usitufanye tuwe katika mashaka ya kumpokea kwake. Usitudhalilishe katika kumpokea kwake. Wala usitutweze kwa ziara yake. Mfanye kuwa mlango miongoni mwa milango ya ghofirani zako awe ufunguo miongoni mwa funguo za Rehma zako. Tufishe katika hali ya uongofu si katika hali ya upotovu tuwe watii si wenye kukirihishwa. Wenye kutubu si katika hali ya uasi wala wenye kung'ang'ania maasi. Ewe mwenye kudhamini malipo ya watendao mema. Na mrekebishaji wa matendo ya waharibifu.

DUA YA 41

DU'A ZAKE(A.S) KATIKA KUOMBA SITARA NA ULINZI

Oh Allah! Msaliye Muhammad na Aali Zake. Nitandikiye kitanda cha heshima yako nipeleke kwenye manyweo ya maji ya rehema zako. Nikalishe kati kati ya bustani yako usinipe mtihani wa kukataliwa na wewe. Usininyime kwa kutokukutumainia. Usinifuatilie niliyoyatenda. Wala usinifuatilie nilioyafanya. Usiyadhihirishe yaliyofichika na kwangu wala usiyafichuwe yaliyositirika kwangu. Usiyaweke matendo yangu katika mizani ya uadilifu. Usizitangaze habari zangu mbele ya macho ya kundi la watu. Wafiche lile ambalo kulitangaza ni aibu kwangu. Likunje mbali nao litakaloniaibisha mbele yako. Ipe heshima daraja yangu kwa ridhaa zako. Nikamilishiye heshima yangu kwa ghofirani zako. Nipange katika watu wa mkono wa kulia, niongoze katika mapito ya walio katika amani. Nifanye niwe katika kundi la waliofaulu. Visitawishe vikao vya watu wema kwa kunitumikisha. Aameen. Ewe Bwana wa ulimwengu.

Dua ya 42

DU'A YAKE(A.S) WAKATI WA KUHITIMISHA QUR'AN

Oh Allah! Hakika wewe umenisaidia kuihitimisha Qur'ani kitabu chako ambacho umekiteremsha kikiwa nuru na umekifanya mlinzi wa kila kitabu ulichokiteremsha. Na umekiboresha juu ya kila hadithi uliyoisimulia. Na ni kitenganishi kwacho umetenganisha kati ya halali yako na haramu yako. Qur'an ambayo kwayo umeiweka wazi sheria ya hukumu yako. Kitabu umekipambanuwa kwa waja wako upambanuzi wa wazi. Ni Wahyi ulio uteremsha uteremsho kwa Nabii wako Muhammad Rehma Zako zimfikie na ziwafikiye Aali zake. Umeifanya kuwa nuru ituongoze katika giza ya upotevu na ujinga kwa kuifuata. Kiponyesho kwa mwenye kuisikiliza kwa kuifahamu na kuisadiki. Ni mizani ya kiadilifu isiyopotoka ulimi wake na kuwa mbali na haki. Nuru ya uongofu ambayo Burhani yake haiwazimikii watizamaji wake. Na alama ya uokovu ambayo hapotei mwenye kufuata mafunzo yake. Wala haitomfikia mikono ya maangamizi mwenye kujiambatanisha na kishiko chake cha ulinzi. Oh Allah! Kwa vile umetusaidia kuisoma. Na umeturahisishia ugumu wa ndimi zetu kwa uzuri wa ibara yake hivyo basi tufanye tuwe miongoni mwa wanaoichunga haki ya kuichunga na wakutumikia kwa itikadi ya kusalimu amri ya aya zake zilizothabiti waombao kimbilio kwa kuzikubali zile aya mutashabih na zile ufafanuzi wake uko bayana. Oh Allah! Hakika wewe umeiteremsha kwa Nabii wako Muhammad Rehema za mungu zimfikiye yeye na Aali zake kwa ujumla.

Na umeturithisha sisi Elimu yake tukiwa wafasiri. Na umetuboresha juu ya wasioijuwa elimu yake. Umetupa nguvu juu yake ili utunyanyuwe juu ya wasio weza Ibada. Oh Allah! kama vile umezifanya nyoyo zetu kuwa zenye kuibeba. Na kwa rehema zako umetutambulisha utukufu na ubora wake. Basi msaliye Muhammad, muhubiri wake na Aali zake wahifadhi wa Qur'ani. Utujaalie kuwa miongoni mwa wanaotambuwa kuwa yatoka kwako. Ili isituzukiye shaka katika kuisadiki. Wala upotovu usitutikise na kututowa nje ya njia yake nyofu. Ewe Allah, mswaliye Muhammad na Aali Zake. Na tujaaliye sisi kuwa miongoni mwa wanaoshikamana na kamba yako, na wakimbiliao kutoka kwenye aya mutashabihati kwenda kwenye ngome yake madhubuti na kuketi kwenye kivuli cha bawa lake, na aongokaye na mwanga wake wa asubuhi. Aongokaye na kuchomoza kwa mng'aro wake. Anamulika kwa taa yake. Wala hatafuti uongofu katika kitu kingine.

Ewe Mola! Kwa hiyo Qur'an umemweka Muhammad kuwa alama ya kukujuwa wewe. Na kupitia Ahlul-Bayt wake umeweka wazi njia za ridhaa zako. Msaliye Muhammad na Aali Zake na ifanye Qur'ani kwetu kuwa njia za kwenye daraja la utukufu. Na iwe ngazi tuipandayo kwenda mahali pa salama. Na iwe sababu tutakayolipwa uokovu kwenye uwanja wa kiyama. Na njia ambayo kwayo tutazifikia neema za nyumba ya kudumu. Ewe Allah! Msaliye Muhammad na Aali Zake. Kwa Qur'ani tupunguziye uzito wa dhana utupe sifa njema za watu wema na tufanye tufate athari za waliosimama kwa ajili yako nyakati za usiku na mwisho wa mchana. Ili ututakase na kila uchafu kwa utakaso wake. Utufanye tufate athari ya walioangaza kwa nuru yake. Wala matumaini hayakuwa zuiya kutenda kazi iliyowatenge mbali kwa vitimbi vya udanganyifu wake. Ewe Allah! Mrehemu Muhammad na Ali Zake. Rekebisha kwa Qur'an upungufu wetu tusiwe mafakiri. Kwa Qur'ani tusukumiye maisha ya raha na wasaa wa riziki. Tuepushe kwayo na tabia mbaya na mwenendo duni. Tuhifadhi kwa Qur'ani tusiingiye ndani ya shimo la maangamizi kufuru na mwendo wa kinafiki.

Ili iwe mwongozo uelekezao kwenye maridhawa yako na bustani zako siku ya kiyama. Na iwe kwetu mlinzi hapa duniani dhidi ya makasiriko yako na kukiuka mipaka yako. Na iwe kwa yale uliyonayo kwa kuhalalisha halali yake na kuharamisha haramu yake shahidi. Ewe Allah! Mrehemu Muhammad na Aali Zake na kwa Qur'ani urahisishe umauti nafsini mwetu wakati wa kufa. Na usumbufu wa kukokotwa (Roho) Uuguaji. Na taabu ya mauguzi, na mfuatano wa kutatarika. (Ifikapo roho kooni na itasemwa: Mganga ni nani?) Atajitokeza Malaika wa umauti ili aichukue toka nyuma ya pazia ya mambo yasiyojulikana. Na kuitupa toka upinde wa umauti kwa mshale wa kuachwa peka na kuwa changanyiya sumu iuwayo kwenye kikombe chenye mwonjo wa sumu wakati msafara wa kuelekea akhera ukitusogelea. Kazi zitakuwa ukosi wa shingo makaburi yatakuwa ndio kimbilio mpaka wakati wa siku ya kukutana. Ewe Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake. Na utubariki wakati wa kuingia nyumba ya kuoza na makazi ya muda mrefu kati ya tabaka za udongo. Yajaaliye makaburi baada ya kuiaga dunia yawe mafikio yetu mema tupanulie mbano wa mwana ndani zetu kwa rehema zako Usitufedheheshe mbele ya walio hudhudhiria siku ya Kiyama kwa sababu ya madhambi yetu ya angamizayo. Kwa Qur'ani irehemu hali yetu duni katika kikao cha kuletwa mbele yako Kwa Qur'ani zithibitishe nyayo zetu zisiteleze wakati daraja la Jehannam litakapoyumba yumba.

Kwayo ing'arishe giza ya makaburi yetu kabla ya kufufuka. Utuokowe kwa Qur'ani na kila taabu ya siku ya Kiyama na shida za kutisha siku ya maafa. Zing'arishe nyuso zetu siku ambayo nyuso za wadhalimu zitakuwa nyeusi siku ya kuhasirika na majuto. Utujaaliye upendo ndani ya nyoyo za waumini. Usiyafanye maisha kwetu kuwa ya shida. Ewe Allah! mrehemu Muhammad mja wako na mjumbe wako kwa vile ameifikisha risala yako na alitekeleza amri yako. Aliwanasihi waja wako Ewe Allah! Mjaaliye Nabii wetu Rehema Zako ziwe juu yake, na juu ya Aali zake - Awe karibu mno na wewe siku ya kiyama miongoni mwa Manabii watakaokuwa karibu ya kikao. Na mwenye uwezo mkubwa sana kwako wakuombea. Mwenye Enzi kubwa miongoni mwao kwako. Mwenye cheo kikubwa mno mbele yako. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali wa Muhammad. Itukuze nyumba yake, Bur'hani yake itukuze, Mizani yake ipe uzito, ya kubali maombezi yake usogeze karibu wasila wake, ufanye uwe mweupe uso wake, ikamilishe nuru yake iinue daraja yake. Tufanye sisi tuishi na sunna yake, tufishe tukiwa katika mila yake, tupeleke tufikishe kwenye njia yake. Tupitishe njia yake. Tujaaliye tuwe miongoni mwa watu watii wake.

Tufufuwe katika kikundi chake tuelekeze kwenye dimbwi lake, tunyweshe kwa bilauri yake. Rehemu Muhammad na Aali zake. Rehema ambayo utamfikisha nayo kwenye ubora asio uwazia miongoni mwa kheri na fadhila zako, na heshima zako. Hakika wewe ni mwenye Rehma kubwa na fadhila tukufu. Oh! Allah mlipe kwa aliyoyafikisha katika jumbe zako. Na amefikisha aya zako, amepigana jihadi katika njia yako malipo yaliyo bora umepata kumlipa yeyote miongoni mwa Malaika wako wa karibu na Manabii wako walio Mursali wateule. Amani imfikie yeye na iwafikiye watoto wake watakatifu wema, na rehema za Mungu na baraka zake.

DUA YA 43

MIONGONI MWA DU'A ZAKE AUONAPO MWEZI MWANDAMO

Ewe Kiumbe mtii. Mwenye mwendo wa haraka usiochoka. Wenye kurudia rudia katika mafikio yalio kadiriwa. Wenye kupita katika mviringo uliopangwa. Na mwamini ambaye kwa kukutumia wewe ameangaza nuru kwenye giza na ameangaza kupitia wewe weusi na amekufanya alama katika alama za ufalme wake. Na alama miongoni mwa alama za mamlaka yake. Na amekufanya mnyenyekevu kwa kuzidi na kupunguwa. Kuchomoza na kuzama, kung'ara na kupatwa uko mtii kwake kwa yote hayo. Na kwenye utashi wake uko haraka ajabu ilioje mpango wake katika mambo yako. Werevu ulioje aliofanya katika kazi yako. Amekufanya kuwa ndio mwanzo wa mwezi mpya na hali mpya. Na mwomba Mungu Bwana wangu na Bwana wako, Muumba wangu na Muumba wako. Muweka vikomo wangu na muweka vikomo wako. Mfanya taswira wangu na mfanya tasweira wako. Amrehemu Muhammad na watoto wake. Na akufanye wewe uwe mwezi mwandamo wenye baraka isiyo futwa na kupitiwa na usiku. Na usafi usiochafuliwa na dhambi. Mwandamo wenye amani bila ya maafa na salama bila maovu. Mwandamo wenye heri bila ya ndege mbaya na ufanisi bila ya shida. Mwandamo wenye urahisi usiochanganyika na ugumu.

Na wenye heri isio changanyika na shari. Mwanadamo wa amani na imani neema na hisani. Salama na Uislamu. Ewe Mola mrehemu Muhammad na Aali zake. Na tujaalie sisi kuwa wenye kuridhika mno miongoni mwa waliochomozea nao. Na wasafi mno miongoni mwa waliouangalia. Na waliobahatika mno katika wale waliokuabudu katika huwo. Utukubalie humo toba utulinde utulinde humo na matendo yasiyofaa utuhifadhi humo tuwe hatujihusishi na kukuasi wewe. Utugawiye humo kushukuru neema zako. Na utuvalishe humo kwa sitara ya afya njema. Tukamilishiye neema zako kwa ukamilifu wa utii wako. Kwa hakika wewe mwenye huruma msifika wa sifa njema. Na Rehema za Allah zimfikiye Muhammad na Aali zake wema waliotahirika.

DUA YA 44

MIONGONI MWA DU'A ZAKE UINGIAPO MWEZI WA RAMADHANI

Utukubalie humo toba utulinde litulinde humo na matendo yasiyofaa utuhifadhi humo tuwe hatujihusishi na kukuasi wewe. Utugawiye humo kushukuru Neema zako. Na utuvalishe humo kwa sitara ya afya njema. Tukamilishiye Neemza zako kwa ukamilifu wa utii wako. Kwa hakika wewe mwenye huruma msifika wa sifa njema. Na Rehema za Allah zimfikie Muhammad na Aali zake wema waliotahirika. Sifa njema ni za Allah ambaye ametuongoza kwenye sifa zake na kutujaalia sisi kuwa wastahiki wake. Ili tuwe wenye kushukuru ihsani zake. Ili atulipe kwa hilo malipo ya watu wema. Sifa njema ni za Allah ambaye ametupendelea kwa dini yake. Na ametuhusisha na mila yake na ametuelekeza katika njia za hissani zake. Ili tuzipate kwa upaji wake tuzifikie radhi zake. Himidi ambayo ataikubali kutoka kwetu, na ataridhika nayo. Sifa njema ni za Mungu ambaye amejaalia miongoni mwa njia hizo mwezi wake.

Mwezi wa Ramadhani mwezi waswiyam mwezi wa Uislamu. Mwezi wa usafi na ni mwezi wa mchekecho. Mwezi wa kusimama kwa ajili ya Sala. Mwezi ambao Qur'ani iliteremshwa humo ili iwe mwongozo kwa watu na ni ubainifu katika mwongozo na kitenganishi. Amebainisha ubora wake kwa kulinganisha na miezi mingine. Kwa kuwa ameujaalia matakatifu mengi na mengi yaliyo bora na mashuhuri. Hivyo basi ameharamisha humo ambayo aliyoyahalalisha katika miezi mingine ili kuuadhimisha. Ameziwia humo malaji na vinywaji ili kuupa heshima. Ameujaalia wakati bainifu, haruhusu Mtukufu Mwenye Enzi utangulizwe kabla ya wakati wake. Wala hakubali ucheleweshwe. Kisha ameuboresha usiku mmoja miongoni mwa usiku wake kwa daraja ya sawa na miezi elfu moja. Na ameuita Laylatul-qadri (Malaika na Arruhu huteremka usiku huo kwa idhini ya bwana wao na kila amri). Amani yenye baraka ya kudumu mpaka kuchomoza kwa alfajiri kwa amtakaye katika waja wake kwa aliyohukumu kulingana na maamuzi yake. Ewe Allah mrehemu Muhammad na Aali zake. Tupe Ilhamu ya kutambuwa ubora wao, na kutukuza heshima yake. Na kuchunga uliyoyazuiya. Tusaidie kutekeleza funga yake kwa kuvizuia viungo vya mwili visikuasi na kuvitumia humo (mwezini) kwa yakuridhishayo.

Kwa kiasi kwamba hatusikilizi kwa masikio yetu maongezi ya ovyo. Na tusiharakie kwa macho yetu kwenye upuuzi; na kwa kiasi kwamba hatunyoshi mikono yetu kwenye ambayo yamehadharishwa. Wala tusipige hatua kwa miguu yetu kuyaelekea yaliyokatazwa. Hata tusishibishe tumbo zetu isipokuwa iliyohalalishia, ndimi zetu zisitamke isipokuwa yale yaliyo mfano. Wala tusijibebeshe isipokuwa yanayosogeza karibu na thawabu zako wala tusijishughulishe isipokuwa na yale tu yanayozuia adhabu yako. Kisha yote hayo yaepushe na riya ya wapendao kusifiwa na yaepushe na kusikika kwa wapendao umashuhuri. Tusimshirikishe (kwenye matendo hayo yote) yeyote asiyekuwa wewe. Tusitaraji kwayo mradi usiokuwa wewe. Ewe Allah! mrehemu Muhammad na Aali zake na tujaalie humo kuhudhuria nyakati za Sala tano. Kwa mipaka yake uliyoiweka na wajibu uliowajibishia na nyadhifa zake ulizoziweka na nyakati zake ulizoweka. Na katika sala tuweke weko la waliofanya sawa mahali mwake, wenye kuhifadhi nguzo zake, watekelezao kwa wakati wake. Kama alivyofanya mja wako na mjumbe wako. Rehma zako zimfikie yeye na Aali zake.

Katika rukuu na katika Sijida na fadhaili zake zote kwa ukamilifu wa Twahara na wa sawa kabisa. Na unyenyekevu uliobayana na wa uhakika. Na tupe taufiki ndani yake ili tuunganishe udugu kwa mema na kujitolea. Na kuwa pamoja na majirani wetu kwa kuwafadhili. Tuziepushe mali zetu na madai na zitakase kwa kutoa zaka. Tumwendeee aliye tuwekea upasi na tumtendee uadilifu aliye tudhulumu. Tumsalimishe mwenye kutufanyia uadui isipokuwa yule afanyiwaye uadui kwa ajili yako kwa kuwa yeye ndiye adui ambaye hatutamfanya rafiki na ni kundi ambalo hatutalitakasa na tujikurubishe kwako humo kwa amali safi ambayo kwayo utatutakasa nayo na kutuweka mbali na dhambi. Utuhifadhi humo na kuzirudia aibu ili asikuletee malaika yeyote isipokuwa machache tuyaletayo katika milango ya utii wako na aina za ukaribu kwako. Ewe Allah hakika mimi nakuomba kwa haki ya mwezi huu. Na kwa haki ya walio abudu kwa ajili yako humo toka mwanzo wake mpaka wakati wa kwisha kwake, miongoni mwa Malaika uliyemsogeza karibu au Nabii uliyemtuma au mja mwema umemchagua makhsusi. Umrehemu Muhammad na Aali zake na utuandamishiye kwa yale uliyo waahidi wapenzi wako miongoni mwa karama zako. Twajibishiye humo uliowa wajibishia watu waliokwenda mbali sana katika kukutii.

Tuweke katika daraja la walio stahiki ngazi ya juu kwa rehema zako. Ewe Allah mrehemu Muhammad na Aali zake tuepushe na kupotoka katika kukupwekesha. Na kutofanya ipasavyo katika kukutukuza. Na kuwa na shaka katika Dini yako na kutoiona njia yako na mghafala wa heshima yako. Tuepushe na kudanganywa na adui yako shetani aliyewekwa kando na rehema zako.

Ewe Allah, mrehemu Muhammad na aali zake, tuelemeapo upande katika huu mwezi tuweke sawa. Tukienda kombo humo tuweke sawa. endapo adui wako shetani atatudhibiti tuokoe. Ewe Mola ujaze kwa Ibada zetu kwako zipambe nyakati zake kwa utii wetu kwako. Tusaidie katika nyakati zake za mchana kuufunga na usiku wake. Utusaidie kutekeleza sala na kukuomba wewe na kukunyenyekea kujidhalilisha mbele yako. Ili mchana wake usiwe shahidi dhidi yetu kwa mghafala wala usiku wake kwa kuzembea. Ewe Allah tujaaliye katika miezi mingine na mchana hivyo hivyo kwa kadiri utupavyo uzima. Tufanye tuwe miongoni mwa waja wako wema (ambao watarithi Janna ya Firdausi humo watabaki milele). ( Na wale ambao wanatoa wakitoacho hali ya kuwa nyoyo zao zaogopa kuwa watarejea kwa Mola wao) na miongoni mwa ambao (wanaharakia katika mambo ya kheri nao kwayo ni wenye kushinda). Ewe Allah! Mrehemu Muhammad na Aali Zake katika kila wakati na muda wote na hali zote kwa idadi uliomrehemu. Na zaidi ya yote hayo kwa ziyada ambayo hawezi kuihesabu asiyekuwa wewe! Hakika wawe ni mtendaji wa utakalo.


8

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

DUA YA 45

ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KUUAGA MWEZI WA RAMADHANI

Oh Allah! Ewe ambaye hapendi alipwe, Ewe ambaye hajutii kwa sababu ya kutoa. Ewe ambaye hamlipi mja wake sawa kwa sawa. Huruma zako ndio mwanzo, Msamaha wako ni ufadhili, Adhabu yako ni uadilifu, Hukumu yako ni uchaguzi mwema. Ukitoa huutii doa utowaji wako kwa masimbulizi. Ukiziwiya (kutoa) hauwi uziwiyaji wako uchokozi. Wamshukuru anayekushukuru na wewe ndiye uliyempa ilhamu ya kushukuru wamlipa mwenye kukuhimidi na wewe ndiye uliyemfundisha kukuhimidi wamsitiri ambaye lau ungependa ungemfedhehesha. Wamfanyia hisani ambae lau ungependa ungemnyima. Wote hao wawili wastahiki kutoka kwako fedheha na kunyimwa, isipokuwa wewe umefanya msingi wa matendo yako kufadhili. Umepitisha uwezo wako katika msamaha. Umemlaki aliye kuasi kwa huruma umempa muhula mwenye kukusudia kujidhulumu nafsi yake. Unawangoja kurejea kwa saburi yako. Unaacha kuwa harakia kwenye toba ili mwangamiaji asije angamia kwa sababu yako mwenye kuangamia miongoni mwao. Na asije kuwa na hali mbaya kwa neema zako mwenye hali mbaya wao isipokuwa kwa ajili ya udhuru wako mrefu kwake, na baada ya mfululizo wa hoja dhidi yake. Ikiwa ni ukarimu wa msamaha wako Ewe Mkarimu! Na ni tendo la huruma Ewe mpole. Wewe ndie uliyefungua mlango wa msamaha wako kwa waja wako, na umeuita "TOBA" na umeweka juu ya mlango huo dalili kwa ufunuo wako ili wasiupotee ndipo ulisema - jina lako limebarikiwa: (Tubuni kwa Mungu toba isiyo ya kurudi nyuma huwenda Mola wenu akakuondoleeni maovu yenu na akakuingizeni katika Jannah ambazo chini yake mito yatiririka. Siku ambayo Mungu hatomwaibisha huyu Nabii na walioamini pamoja naye nuru yao yakimbia (pita) mbele yao na kuliani kwao wakisema Mola wetu tutimiziye nuru yetu na tughofirie kwa hakika wewe umuweza juu ya kila kitu). Basi ni udhuru gani atakuwa nao mwenye kughafilika kuingia nyumba ile baada ya mlango kufunguliwa na kuwepo dalili?

Na wewe ndiye ambaye ulijizidishia bei dhidi yako mwenyewe kwa faida ya waja wako ukiwatakia faida yao kwa biashara yao na wewe. Na kufuzu kwao kwa kukufika wewe na ziada kutoka kwako. Ukasema jina lako limebarikiwa na uko ngazi ya juu (mwenye kuleta tendo jema atapata malipo yaliyo sawa na mema kumi, na mwenye kuleta tendo ovu moja hatolipwa ila sawa na malipo ya ovu hilo moja) na umesema: (mfano wa ambao watoao mali zao katika njia ya Mungu ni mfano wa punje moja imetoa masuke saba katika kila suke kuna punje mia moja Mungu humzidishia amtakaye). Na ulisema: (nani ambaye atamkopesha Mungu mkopo mzuri? Naye atamzidishia zidisho jingi. Na ulizoteremsha fano wao katika Qur'ani miongoni mwa aya zielezazo miongoni mwa ongezeko la malipo ya matendo mema. Na wewe ndiye uliyewajulisha kwa kauli yako toka ghaibu yako na himizo lako ambalo lina hadhi yao ndani yake, lau ungelificha kwao macho yao yasingelidiriki. Masikio yao yasingelisikia. Akili zao zisingelifikia. hivyo basi ulisema: (Nikumbukeni nitawakumbuka nishukuruni wala musinikufuru) na ulisema: (mukiwa wenye kushukuru nitawazidishieni lakini mkikufuru (kuacha shukrani) hakika adhabu yangu ni kali). Na ulisema: (Niombeni nitakujibuni hakika wanaofanya kibri kuniabudu mimi wataingia Jehannam wakiwa duni) umeiita DU'A yako Ibada, na kuacha kukuomba ni kibri, na umekamia mwenye kuacha kukuomba ataingia jehannam akiwa duni.

Hivyo basi wamekutaja kwa ukarimu wako. Na wamekushukuru kwa fadhila zako na wamekuomba kwa amri yako. Na wametoa sadaka wakitaka ziada yako. Na katika yote hayo umekuwa uokozi wao kwa kuepukana na ghadhabu zako na kufuzu kwao kupata ridhaa zako. Lau kiumbe mwenyewe angemwongoza kiumbe mwingine mfano wa yale uliyowaongoza waja wako angekuwa asifike kuwa ni muhisani na angesifika kuwa ni mwema na angehimidiwa na kila ulimi. Sifa njema ni zako. Kipatikanacho katika mwenendo wa sifa zako hapana tamko libakialo kwa sifa usifiwazo na maana ya sifa ya kuelekea wewe. Oh yule ambaye amesifika kwa waja wake kwa hisani na ufadhili. Na amewaeneza ukarim na umbuji wingi ulioje wa neema zako zilizotuenea? Ukarimu wako mwingi mno kwetu umetufanya makhsusi kwa wema wako. Umetuongoza kwenye dini yako ambayo umeichagua. Na mila yako uliyoiridhia, na njia yako uliyoirahisisha. Na umetuoneysha ukaribu kwako, nafika kwenye ukarimu wako. Oh Allah! Miongoni mwa teule mno katika nyadhifa hizo na zilizo makhsusi sana miongoni mwa faradhi hizo ni mwezi wa Ramadhani ambao umeufanya kuwa makhsusi kwa kuulinganisha na miezi mingine. Umeuchagua toka zama zote na nyakati zote. Umeupenda kuliko nyakati zote za mwaka kwa sababu umeteremsha humo Qur'an na nuru. Humo umezidisha imani na umewajibisha humo (mwezi wa Rama...) Funga, na umependezewa humo kisimamo cha sala Na umeutukuza kwa Laylatul-qadir ambayo ni bora kuliko usiku elfu moja. Kisha umetupendelea sisi kwayo kuliko umma zingine. Kwa ubora wake umetuchagua mbali na watu wa mila. Tumefunga kwa amri yako mchana wake tumesimama tukisal usiku wake tukijishughulisha kuufunga na kusali humo. Kwa vile umetuonesha kwa ajili yake rehema zako. Kwa ajili yake tumekuwa na sababu kuelekea thawabu zako. Na wewe uko daraja la juu zaidi kuliko kile kwa ajili yake watakiwa. Umkarimu uombwacho kwa fadhila zako.

Ukaribu kwa mwenye kujaribu kuupata ukaribu wako. Mwezi huu umetusimamishia msimamo wa sifa njema, umesuhubiana na sisi usuhuba wa mtu mwema. Umetufidisha faida bora ya viumbe wa ulimwengu. Kisha umetuacha ulipotimia wakati wake na kukatika kwa muda wake na kutimiza idadi yake. Nasi tu wenye kuuaga uwagaji wa ambaye kujitenga nae kwake kwa umiza juu yetu. Kumetusononesha na kutuacha peka, kutoweka kwake, mbali na sisi, kwa ajili yake umetulazimu ulinzi ulihifadhika. na heshima yenye kuangaliwa, na haki tekelezwa. Hivyo twasema: Assalaamu Alayka Ewe mwezi wa Mungu mkubwa kabisa Ewe Iddi ya wapenzi wake (Mungu). Assalaamu Alayka, Ewe wakati ulio bora kuwa nao miongoni mwa nyakati. Ewe mbora wa miezi katika siku na saa Assalaamu Alayka mwezi matumaini yamekurubia. Kazi njema humo zimetawanywa. Assalaamu Alayka Ewe rafiki ambaye thamani yake iliyopo imetukuka. Kutoweka kwake kwa tia simanzi. Machungu ya kutengana naye kwake yatazamiwa. Assalaamu Alayka msuhuba ambaye ujaji wake huleta raha hufurahisha ambaye aondokapo huleta kitwea. Assalaamu Alayka jirani ambaye nyoyo hulainika kwa ajili yake. Dhambi mwake zimepungua. Assalaamu Alayka msaidizi asaidiae dhidi ya shetani. Mwezi arahisishaye njia za ihsani. Assalaamu Alayka wengi walioje wakombolewa wa Mungu ndani yako.

Furaha iliyoje kwa wenye kuchunga heshima yako kwa msaada wako. Assalaamu Alayka umekuwa mfutaji mno wa dhambi. Umesitiri sana wa aina mbali mbali za aibu. Assalaamu Alayka umekuwa na uvumilivu kwa watenda dhambi wa tisha mno mioyoni mwa waumini. Assalaamu Alayka mwezi ambao siku hazishindani nao. Assalaamu Alayka mwezi ambao amani katika kila jambo. Assalaamu Alayka mwezi ambao kuwa pamoja nao kwake hakuchukizi, wala kuchanganyika pamoja nao kwake hakulaumiki. Assalaamu Alayka kama ulivyoingia kwetu kwa baraka nyingi na umetoa uchafu wa makosa. Assalaamu Alayka si muagwa achukizaye wala hakichoshi kilichoachwa na saumu yake. Assalaamu Alayka mtafutwa kabla ya wakati wake. Na muhuzunikiwa kabla ya kwisha kwake. Assalaamu Alayka maovu mangapi yamezuiliwa yasitufike kwa wewe. Mema mangapi tumebubujishiwa kwa sababu yako. Assalamu Alayka wa Alaa Laylatil Qadr ambayo ni bora kuliko miezi elfu moja. Assalamu Alayka tulipupia sana jana tutakuwa na shaka sana na wewe kesho. Assalaamu Alayka na juu ya fadhila zako zilizo haramishwa kwetu na juu ya baraka zako zilizopita ambazo hivi sasa tumepokonywa. Oh Allah! Sisi ni wana, mwezi huu ambao umetuboresha kwako (kwa huo mwezi). Na kwa huruma yako umetupa taufiki. walipokosa kuujua wakati wake. Na wamenyimwa fadhila zake kwa ajili ya uovu wao. Na wewe ndiye mfadhili wa elimu zake ambazo umetupendelea maarifa yake.

Umetuongoza kwenye utekelezaji wa sunna zake. Kwa tawfiki yako tumebeba jukumu la kuufunga na kusali kwa kiwango kidogo sana. Tumetekeleza humo kidogo sana miongoni mwa kingi. Oh Allah! sifa njema zote ni zako. Twakiri maovu. Twatambua kuzembea. Katika nyoyo zetu kuna fundo la majuto kwako. Ulimini mwetu kuna ukweli wa kukuomba udhuru. Tupe thawabu kwa yaliyotupata ingawaje tumezembea. Huenda tutaifikia kwayo fadhila itakiwayo na kwayo tufanikiwe aina mbali mbali za vifaa vilivyohifadhiwa. Wajibisha kwa ajili yetu udhuru wako kwa tuliyoshindwa kutekeleza ipasavyo miongoni mwa haki zako. Umri wetu tulio nao ufikishe mwezi wa Ramadhani ujao tukiufikia tusaidiye kufanya ibada unayostahiki. Tufanye tuwe twatekeleza yapasayo (ndani ya) mwezi huu yastahikiyo katika utii. Tutunukiye Amali njema itayotekeleza haki yako katika miezi miwili miongoni mwa miezi ya Dahar. Oh Allah! Tuliyoyatenda katika mwezi wetu huu miongoni mwa dhambi ndogo au kubwa. Au dhambi tumeangukia Emo na kosa tulilotenda makusudi au kwa kusahau. Tumejidhulumu nafsi zetu. Au tumemvunjia heshima mtu mwingine. Mswaliye Muhammad na Aali zake. Na utusitiri kwa sitira yako. Tusamehe kwa msamaha wako wala usituweke mbele ya macho ya wasimbuliaji. Wala usitukunjulie ndimi za wa umbuwaji. Tutumikishe kwa yatakayokuwa ndiyo punguzo na kafara ya usilolikubali kutoka kwetu. Kwa huruma yako isiyokwisha na fadhila yako isiyopanguliwa. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali Zake uuponye msiba wetu kwa mwezi wetu. Utubariki siku ya Iddi yetu na siku yetu ya kwanza kufunguliwa.

Ijaaliye kuwa miongoni mwa siku ya kheri mno imetupitia yenye kuleta msamaha sana na yenye kufuta mno dhambi. Tughofiriye zilizojificha katika dhambi zetu na zilizotangazika. Oh Allah! tutowe kwa kutoweka mwezi huu makosa yetu tuvuwe kwa kutoweka kwake maovu yetu. Tufanye miongoni mwa watu wenye heri mno kwa huwo (mwezi). Na wenye hisa kubwa mno humo na wenye hadhi mno humo. Oh Allah! mwenye kuchunga haki ya mwezi huu kwa haki, na kuhifadhi heshima yake kwa haki, na kutekeleza mipaka yake kwa haki. Na kuchelea dhambi zake kwa haki yake. Au akajikurubisha kwako kwa ujikurubishaji uwajibishao ridhaa yako kwake na huruma yako ikamwelekea juu yake. Tupe sisi mfano wake kutoka kwenye ukwasi wako. Tupe na sisi zaidi yake kwa fadhila zako. Hakika fadhila zako hazipunguwi kwa hakika hazina zako hazipunguwi bali huzidi. Ni kweli kabisa kuwa chimbuko la hisani zako hazishi. Upaji wako ni upaji wapendeza sana. Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali Zake, tuandikie ujira mfano wa ujira wa mwenye kuufunga au amekuabudu ndani yake mpaka siku ya Kiyama.

Oh Allah! Hakika twatubu kwako siku ya kwanza ya kufuturu kwetu ambayo umeifanya kwa waumini kuwa ni Idi na furaha. Na kwa watu wa mila yako wakati wa mkusanyiko na mjumuiko kutokana na kila dhambi tumeitenda au ovu tumelitanguliza, au fikra ya shari tumeificha iwe toba ya asiyeficha dhamira ya kurudi kwenye dhambi wala harejei baada yake kwenye makosa. Toba ya nasuha iliyeepukana na shaka na wasiwasi. Ikubali kutoka kwetu tu iridhiye tuimarishe juu yake. Oh Allah! Turuzuku kuogopa adhabu za kamio na shauku ya thawabu iliyo ahidiwa ili tuipate ladha ya kile tukuombacho kwa ajili yake na huzuni ya tukuombeacho kimbilio kwa ajili yake. Tujaaliye tuwe miongoni mwa walio tubu kwako. Ambao umewajibisha mapenzi yako. Oh! Umwadilifu mno wa waadilufu, Oh Allah! Wavumilie baba zetu na mama zetu na watu wote wa Dini yetu waliotangulia kati yao na watakaopita mpaka siku ya Kiyama. Oh Allah! Mrehemu Muhammad Nabii wetu na Aali Zake kama ulivyowarehemu malaika wako waliokurubishwa. Na umswali yeye na Aali zake. Kama ulivyowasalia Manabii wako wajumbe. Mswaliye yeye na Aali zake kama ulivyowasalia waja wako wema na bora zaidi kuliko hivyo Ewe Bwana wa Ulimwengu Swala Baraka zake zitufikie. Nafu yake ihifike, kwayo DU'A zetu zijibiwe. Hakika wewe u umkarimu mno wa waombwao. Na umtoshelezaji mno wa wanaotegemewa. Na umpaji mno wa waombwao fadhila yake. Na u muweza juu ya kila kitu.

DUA YA 46

DU'A ZAKE(A.S) KATIKA SIKU YA IYDI AL-FITRI

Akimaliza kusali husimama kuelekea Qibla na siku ya Ijumaa husema: Ewe! Unayemrehemu asiyerehemewa na waja. Ewe ambaye humkubali asiyekubaliwa na nchi. Ewe ambaye hawadharau wenye haja kwake. Ewe ambaye hamtowi matumaini mwenye kumsihi sana. Ewe ambaye hawakabili kwa kutowakubalia wenye msimamo mgumu kwake. Ewe ambaye akusanyae kidogo apewacho na ashukurue kidogo atendewacho. Ewe ashukuruye kidogo na hulipa kikubwa. Ewe ambaye humsogelea kwa amwendaye karibu yake. Ewe ambaye humwita kwake mwenye kumtumbia mgongo! Oh we! ambaye haibadilishi neema wala aharakii kulipizi. Oh We! ambaye huzalisha jema ili likuwe na hufumbia macho ovu ili asamehe hurudi tumaini kutoka kwake na haja yake bila kufikia uelewa na kiwango cha ukaribu wako. Vyombo vya haja vimejaa upaji wako sifa zimeshindwa kufikia sifa zako katika kukusifu. Ujuu wa juu kabisa ni wako uko juu kabisa kuliko kila aliyejuu. Utukufu mkubwa kabisa juu ya utukufu wote. Kila mtukufu kwako ni mdogo kila kitukufu kwenye utukufu wako ni kinyonge. Wameshindwa kupata waya tarajiayo wa mwenoeaye asiyekuwa wewe. Wamehasirika wajipelekao mbele isipokuwa kwako. Wamepotea wakaao ispokuwa na wewe wamekuwa wa kiwa wenye kukimbilia isipokuwa waliokimbilia fadhila zako. Mlango wako uko wazi kwa waronga - Rongao. Upaji wako kwa ajili ya waombao msaada wako ukaribu na waombao msaada. Wenye matumaini hawa katishwi tamaa wajiletao kwako hawatokwi na matumaini na upaji wako. Hawapatwi na hali mbaya kwa ajili ya lipizi lako wenye kuomba ghofirani.

Riziki yako imekunjuka mpaka kwa wanaokuasi. Huruma yako ya mwendea akupingaye, tabia yako ni kuwatendea hisani waovu desturi yako kuwabakisha wachokozi, mpaka kuwangojea kwako kumewadanganya wasirejee. Kuwapa kwako muhla kunawazuia kukoma. Hakika hukuwafanyia haraka ili warudi kwa amri yako. Mwenye kuwa miongoni mwa wema mulihitimishia. Na mwenye kuwa miongoni mwa anayestahiki hali mbaya wa mwacha bila msaada wako wote hao watakuwa kwenye hukumu yako, na mambo yao yazuilika na amri yako. Mamlaka yao hayadhoofiki kwa muda wao mrefu wote. Dalili yako haikuvunjwa kwa kuacha kuwaharakia! Hoja yako ipo haivunjwi, na ufalme wako uko thabiti haitoweki. Ole wake yule atakayeelemea mbali na wewe. Kuachwa kusiko kuwa na msaada ni kwa yule mwenye kuachwa na wewe shakawa iliyo mbaya sana ni ya aliye danganyika nawe. Atafanyaje ndani ya adhabu yako? Mahangaiko yake marefu yaliyoje ndani ya adhabu yako? Upeo wake wa faraja umbali ulioje? Kukatishwa tamaa kwake kulioje na urahisi wa kutoka? Ni uadilifu kutokana na uamuzi wako hudhulumu katika maamuzi.

Ni usawa wa hukumu yako huwezi muonea. Umesaidia hoja na kuzijaribu nyudhuru. Ulianza na tishio. Umekuwa mpole katika kuhimiza na umefanya mifano. Na umerefusha kutoa muhla. Umechelewesha ukiwa muweza wa kufanya haraka. Umefanya bila haraka hali ukiwa umejaa haraka. Kutoharakia kwako hakukuwa kwa sababu ya kushindwa, wala kutoa muhla kwako ni unyonge wala kujiziwia kwako si mghafala. Wala kungoja kwako si upendeleo, bali ili hoja yako iwe yenye nguvu zaidi na ukarimu wako uwe kamili na ihsani yako iwe ya kutosha. Neema zako ziwe timilifu. Yote hayo yamekuwa na yangali yataendelea kuwa haitokoma. Hoja yako ni kubwa mno kuliko vile vya weza kuelezwa yote. Utukufu wako uko juu zaidi hauwezi kufanyiwa mipaka kwa kiini chake. Neema zako nyingi haziwezi kuhesabiwa zote. Hisani zako nyingi kuliko vile zishukuruwe hata kwa kiasi chake kidogo. Ukimya umenifanya nishindwe kukuhimidi. Kujizuiya kumenifanya nishindwe kukutukuza. Niwezalo kulifanya ni kukiri kushindwa kwangu. Si kwa kupenda Ewe Mola wangu! Bali ni kutoweza, Mimi ni huyu hapa naja tena mbele yako. Nakuomba usaidizi mwema. Mrehemu Muhammad na Aali zake. sikiliza mnong'ono wangu. Kubali duwa yangu, wala usiihitimishe siku yangu kwa kukatishwa matumaini. Wala usinikabili kwa kurudisha ombi langu bila jibu. Uheshimu utokaji wangu kwako. Marejeo yangu ni kwako. Hakika wewe hudhikiki na ulipendalo. Na si mshindwi wa uombwalo We u muweza juu ya kila kitu. Hapana hila wala nguvu isipokuwa kuwezeshwa na Allah Mtukufu mkubwa.


9

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

DUA YA 47

DUWA ZAKE(A.S) SIKU YA ARAFA

Sifa Njema Ni Zake Allah Bwana Wa Ulimwengu. Oh Allah! Sifa Njema ni Zako. Mbuni wa mbingu na Ardhi. Mwenye Utukufu na ukarimu. U bwana wa Mabwana. Mwabudiwa wa kila mfanya ibada. Muumba wa kila kiumbe. Mrithi wa kila kitu (Hapana kitu mfano wake) wala kwake haifichiki elimu ya kitu. Na yeye akizunguka kila kitu. Yeye akichunga kila kitu. Wewe ndiye Allah..Hapana Miungu Ila ni wewe. Huna kifani peke yako. Mmoja mwenye kujitenga. Wewe u Allah! Hapana miungu isipokuwa wewe. U mkarimu mpaji! U Mtukufu mwenye kutukuka. U mkubwa mwenye kujitukuza. Wewe ndiye Allah hapana miungu isipokuwa ni wewe. Ungazi ya juu kabisa mwenye kujinyanyuwa. Mwenye Nguvu Stadi. Wewe ndiyo Allah. Hapana Miungu isipokuwa wewe. Mwingi wa Rehema mwenye huruma. Mjuzi wa kila kitu mwenye hekima. Wewe ndiye Allah. hapana Miungu isipokuwa wewe. Msikiaji Muonaji. Wa Tangu na Elewa. Wewe ndiye Allah. Hapana Mingu isipokuwa wewe. Mkarimu mkarimu mno.

Wa milele wamilele mno! Wewe ndiyo Allah. hapana Miungu isipokuwa wewe. Huna mwanzo upo kabala ya chochote. Utaendelea kuwa baada ya kila idadi. Wewe ndiye Allah. hapana Miungu isipokuwa Wewe. Aliye karibu katika kuwa kwake ngazi ya juu. Na u Daraja ya juu katika ukaribu wake. Na wewe ndiyo Allah. hapana miungu isipokuwa wewe. Mwenye uzuri na Utukufu. Mwenye Utukufu na sifa njema. Wewe ni Allah hapana miungu isipokuwa Wewe ambaye amevifanya vitu viwe bila ya asili. Umevianzisha ulivyo vianzisha bila kuiga. Wewe ndiye ambaye umekadiria kila kitu makadirio. Umekirahisisha kila kitu rahisisho. Umekipanga kilicho chini yako kwa mpango. Wewe ndiye ambaye hakukusaidia katika kuumba kwako mshirika. Wala hakukusaidia katika amri yako waziri. Wala hujawa na shahidi wala kifani. Wewe ndiye ambaye umetaka likawa ulilotaka bila muhali. Umehukumu ikawa hukumu yako adilifu. Wewe ndiye ambaye mahali hapawezi kukufanya uwe ndani yake. Haijapata kuwa mamlaka mbele ya mamlaka yako. Wewe ndiye ambaye umekihesabu kila kitu kwa idadi. Umekifanyia kila kitu muda, umekifanyia kila kitu makadirio. Wewe ndiye ambaye akili zimeshindwa kuitambuwa dhati yako. Zimehemewa fahamu kutambuwa namna yako. Macho yameshindwa kudiriki ulipo! Wewe ndiye ambaye huwekewi mipaka. usijezingirwa ndani ya mipaka Hujafanyiwa mfano usije kuwa upo ndani ya mifano. Hukuzaa usije kuwa mzaliwa. wewe ndiye ambaye huna aliye kinyume nawe asije kukupinga.

Hapana kilicho sawa na wewe kisije kukushinda. Wala huna mpinzani ili akupinge. Wewe ndiye ambaye aliyeanzisha na kubuni. Amezusha na kuanzisha. Amefanya vizuri kutengeneza aliyotengeneza. Utakatifu ni wako. utukufu ulioje washani yako. Miongoni mwa mahali. mahali pako ni pa juu sana. Imeipasua haki furkani yako, Utukufu ni wako umpole ulioje upole wako? Mwenye huruma ilioje huruma yako! Mwenye hekima ulioje ujuzi wako! Utakatifu ni wako Mfalme huonekani mpaji mwenye wasaa. Uko wa daraja ya juu, ilioje daraja yako ya juu! Mwenye Uzuri na utukufu, ukubwa na sifa njema. Utakatifu ni wako umekunjuwa mikono yako kwa mema. Mwongozo umejulikana kutoka kwako mwenye kukuomba. Dini au dunia atakukuta. Utakatifu ni wako. Atanyenyekea mwenye kukutambuwa. Walio chini ya arshi yako wamenyenyekea kwa ajili ya utukufu wako. Wamefuata ili kusalimu amri kwako viumbe wako wote. Utakatifu ni wako, uhisiwi wala huguswi. Huguswi wala hudanganywi. Hutolewi wala hupingwi, hukurubiwi wala hubishwi. Uhadaiwi wala hufanyiwi vitimbi Utakatifu ni wako. Njia yako ni ardhi laini amri yako ni ongofu nawe uko hai kimbilio la milele. Utakatifu ni wako. kauli yako ni maamuzi thabiti. Na hukumu yako hapana budi. Utashi wako thabiti. Utakatifu ni wako. hapana wakukataa utashi wako. Wala hapana mbadilishaji wa maneno yako. Utakatifu ni wako, mwenye alama zitiazo kiwi macho. Muumba wa mbingu. muumba wa Roho, Himidi ni yako, himidi ya kudumu kwa kudumu kwako. Sifa njema ni zako. sifa njema za kudumu kwa neema zako. Sifa njema ni zako sifa njema iendayo sambamba na fadhila zako. Sifa njema ni zako. sifa njema zazidisha radhi zako. Sifa njema ni zako. sifa njema zi pamoja na kila mwenye kukuhimidi. Shukrani huwa ndogo mbele yake shukrani ya kila mwenye kushukuru. Sifa njema haipaswi kwa yeyote isipokuwa wewe. Hautafutwi ukaribu kwa yoyote isipokuwa ukaribu kwako. Sifa njema ambayo kwayo huidumisha (Fadhila) ya kwanza. Na huwa ni sababu ya kudumu ya mwisho. Sifa njema huongezeka kila zinapokariri zama. Sifa njema wanashindwa wahifadhi kuihesabu, inazidi ile walioihesabu katika kitabu chako waandishi. Sifa njema itauzidi uzito wa arshi yako Tukufu, na kulingana na kiti chako kilichoinuka. Sifa njema ambazo malipo yake yatakamilishwa na wewe malipo yake yataenea juu ya malipo yote. Sifa njema ambazo sehemu yake ya nje ina uwiano na ya ndani. Na sehemu yake ya ndani yalingana na ukweli wa nia. Sifa njema hajakusifu hajapata kukusifu kiumbe mfano wake. Wala fadhila zake hazijui yeyote asiyekuwa wewe. Sifa njema ambazo mwenye kujitahidi kuzizidisha husaidiwa.

Haitokuwa Rehema ikiwa kuishinda. mrehemu Rehema yenye kuridhisha ambayo haitokuwa rehma juu yake. Mola wangu Mrehemu Muhammad na Aali zake. Rehema itakayomridhisha na itayozidisha juu ya ridhaa yake. Mrehemu Rehema itakayokuridhisha na itazidisha Radhi yako kwake. Mrehemu Rehema ambayo hutomridhia ila kwayo. Wala hautoiona nyingine kuwa na thamani. Mola wangu mrehemu Muhammad na aali zake. Rehema ambayo itakayoivuka ridhaa zako. Na itaungana na muungano wa kubaki kwako. Wala haitokwisha kama vile maneno yako hayatokwisha. Bwana wangu mrehemu Muhammad na Aali zake. Rehema zitakazo jinadhimu na Rehema za Malaika wako na Manabii wako na Mitume wako na watii wako na ndani yake mutakuwa na swala za waja wako miongoni mwa majini wako na wanaadamu wako na za wenye kukubaliwa nawe. Na zitaungana na sala za kila ulichokiumba miongoni mwa jinsi ya viumbe wako. Mola wangu Mrehemu yeye na Aali zake Rehema itayoizunguka kila Rehema iliyopita na itakayo kuja. Mrehemu yeye na watu wa nyumbani mwake. Rehema ikuridhishayo na kila aliye chini yako italeta pamoja na hiyo Rehema utaongezeka pamoja nayo Rehema hizo. Na kuzidi kwa kadiri siku zinavyorudia ziada yenye kuongezeka. Hatoweza kuihesabu asiyekuwa wewe. Mola wangu warehemu walio wema zaidi katika Aali zake. Ambao umewachagua kwa ajili ya amri yako. Uliowafanya kuwa hazina ya Elimu yako. Na walinzi wa Dini yako. Ni Makhalifa wako katika ardhi yako. Wao ndio hoja yako dhidi ya viumbe (waja) wako.

Umewatakasa kutokana na uchafu na ujusi na kuwafanya tohara kwa utashi wako. Na umewafanya njia ya kwenye Jannah yako. Mola wangu mrehemu Muhammad na Aali zake Rehema itayowakithirishia kitu katika kipaji chako na ufadhili wako. Itayowajazia hadhi ya huruma zako na manufaa yako kwao. Mola wangu Mrehemu Muhammad na Aali zake Rehema ambayo mwanzo wake kikomo wala muda wake hauna mwisho. Mwendeleo wake hauna mwisho. Mola wangu warehemu Rehema inayolingana na uzito wa arshi yako na walio chini yake. Rehema zijaazo mbingu zako na vilivyo juu yake, (zenye) kulingana na idadi ya ardhi zako na vilivyo chini yake na vilivyo kati yake Rehema itakayowasogeza karibu yako. Itakayokuridhisha na wao wataridhika. Na kuungana na walio mfano wako milele. Oh Allah! Hakika wewe umeiunga mkono dini yako nyakati zote kwa Imamu uliomweka akiwa mwongozo kwa waja wako na mnara katika nchi yako. Baada ya kuwa umeunga kamba yao na yako. Na umeifanya kuwa ni sababu ya kuifikia ridhaa zako. Na umewajibisha utii wake. Na umehadharisha kumuasi. Umeamrisha kutekeleza amri zake. Na kujiziwiya na katazo lako, na asimtanguliye mwenye kumtanguliya wala asibaki nyuma yake mwenye kubaki nyuma. Yeye ni kinga ya waombao hifadhi na ni kimbilio la waumini na kishiko cha wenye kushikamana. Ni mwanga wa ulimwengu. Oh Allah! mwongoze walii wako kushukuru juu ya uliyomneemesha nayo. Wasituongoze mfano wake kumuhusu yeye. Mjaalie kutoka kwako uwezo wa kumsaidia. Mfunguliye ufunguzi rahisi. Msaidie kwa nguzo yako yenye uwezo mkubwa. Uzidishe nguvu mgongo wake. Utie nguvu mkono wake. Msaidie kwa Malaika wako. Mwongozee Malaika Askari wako washindi, kupitia yeye kiimarishe kitabu chako na mipaka yako na sheria yako na Sunna za Mjumbe wako. Rehema zako.

Oh Allah! iwe juu yake na Aali zake. Kupitia yeye huisha walichokifisha wadhalimu miongoni mwa mwongozo wa dini yako. Kupitia yeye isuguwe kutu ya dhuluma itoweke mbali na njia yako Kupitia yeye iondowe shida iwe mbali na njia yako. Kupitia yeye waondolee mbali waliopotoka kombo na njia yako. Wafuate kupitia yeye waitakiao njia yako iliyonyooka kupinda pinda. Lainisha upande wake kwa ajili ya marafiki zake. Mkunjuliye mkono wake juu ya maadui zako. Tupe huruma yake, Rehema zake upendo wake. Tujaaliye kuwa wenye kumsikiliza watii kwake wenye bidii kwa limridhishalo, wenye kuungana katika kumsaidia na kumlinda. Tuwe karibu nawe na kwa Rasuli wako. Rehema zako Oh Allah! ziwe juu yake na Aali zake. Oh Allah! warehemu wapenzi wao watambuwao daraja yao. Wafuatao njia yao, wafuatiliao athari zao, wenye kushikamana na mashiko yao, wenye kushikamana na wilaya yao, wafuatao Uimamu wao, wenye kusalimu amri yao, wenye kujitahidi kuwatii, wenye kungoja siku zao, wenye kuelekeza macho yao kwao, Rehema na baraka zenye kuongezeka safi mpya mpya zenye kunukia, uwape wao usalama na wa roho zao, yaweke pamoja mambo yako katika Ta'kwaa, iweke sawa hali yao. Warejelee. Hakika wewe ni mwingi wa kurejea mwenye Rehema na mbora wa wenye kusamehe na tujaaliye tuwe pamoja nao katika nyumba ya salama. Kwa Rehema zako. Ewe Mrehemu zaidi kuliko warahimu wote. Oh Allah hii ni siku ya Arafa. siku ulioipa Utukufu, heshima, na ukubwa, umetawanya humo Rehema zako, umeonesha humo wema kwa msamaha wako. Umekithirisha humo upaji wako kwayo umewafadhili waja wako. Allah nami ni mja wako ambaye ulimneemesha kabla hujamuumba, na baada ya ulivyomuumba ukajaaliya kuwa miongoni mwa uliowaongoza kwa ajili ya Dini yako. Na ulimuwafikisha kwa ajili ya haki yako, ulimuhifadhi kwa kamaba yako, ulimwingiza katika kundi lako na umemwongoza kuwa rafiki wa rafiki zako. Na kuwa adui kwa maadui zako, kisha ulimwamuru hakufuata amri yako, ulimkemea hakukemeka, umemkataza asikuasi, amekhalifu katazo lako na kutenda katazo lako, si kwa kukupinga wala kuonesha kiburi dhidi yako, bali matamanio yake yamemtuma afanye ulichokitenga na kumuhadharisha akisaidiwa kwa hilo na adui yako na adui wake. Akajitosha kwenye hilo (katazo) hali yu atambua fika kamio lako akiwa na ithibati na uvumilivu wako ingawaje alilazimika mno katika waja wako kwa ajili ya uliyompa asingethubutu kufanya. Mimi ni huyo mbele yako! mwenye kudharaulika, dhalili mnyenyekevu, duni mwenye woga nakiri mzigo mkubwa wa dhambi nimeubeba na makosa makubwa nimeyatenda naomba hifadhi ya msamaha wako nakusihi sitara katika rehema zako nikiwa na yakini kuwa hakuna awezae kunilinda dhidi yako mlinzi. Wala hawezi kuniziwiya dhidi yako mziwiyaji, hivyo basi ni hurumiye kama umuhurumiavyo mwenye kutenda dhambi, nikirimu kama unavyomkirimu mwenye kujitupa mbele yako kwa msamaha wako. Ni hurumie kwa ambalo haliwi kubwa kwako kumhurumia mwenye kukutazamia kutokana na msamaha wako. Nijaaliye katika siku hii sehemu natapatapa kwa ajili yake, hadhi katika ridhaa zako wala usinirudishe mikono mitupu kama ambavyo warudivyo wafanya Ibada yako miongoni mwa waja wako. Ingawaje sijatanguliza mema kulinganisha na waliyotanguliza miongoni mwa mema. Hakika nimetanguliza Tawheed yako na kukanusha dhidi na kufanana na wewe na nimekuja kwako kupitia milango ambayo umeamrisha ujiwe. Na nimejikurubisha kwako kwa namna ambayo hajikurubishi yeyote kwako ila kwa kujikurubisha kwayo. Kisha nimefatilia hayo kwa kurejea kwako kwa kujidhalilisha na kujitweza kwako na kwa dhana njema kwako na kuwa na imani na ambayo uliyonayo, nimefanya jozi ya matumaini kwako ambayo mara chache hukosa mwenye kukutumainia. Nimekuomba ombi la mtu duni, dhalili, msikitikiwa, misikini, mwenye woga, mwomba hifadhi, yote hayo akiwa na woga akijitetea akiomba kinga na kusitiriwa. Si mwenye ufedhuli kwa kiburi cha wafanyao kibri. Si mwenye kujitukuza na utashi wa watii wala mwenye kutumainia uombezi wa waombezi ningali mnyonge wa wanyonge. Dhalili wa madhalili. Ni mfano wa chembe ndogo mno ya vumbi. Oh! We ambaye hawaharakii watenda maovu wala hawaziwii wenye maisha ya raha. Oh! yule ambaye atendea ihsani kwa kuwaokoa waliojikwaa. Na huwafadhili kwa kuwapa muda. Watenda makosa:

Mimi ni mtenda maovu, mwenye kukiri mkosefu. Mwenye kujikwaa. Mimi ndiye ambaye nimethubutu mbele yako. Mimi ndiye ambaye amekuasi makusudi. Mimi ndiye ambaye nimejificha nisikuabudu na kujitokeza mbele yako kwa majivuno. Mimi ndiye ambaye amewaogopa waja wako na kujiaminisha kwako. Mimi ndiye ambaye hakuogopa adhabu yako wala kuhofia ukali wako. Mimi ni mwenye kujikosea binafsi. Mimi niko rehani wa kujisibu kwangu. Mimi sina haya. Mwenye taabu sana, kwa haki ya uliyemuainisha katika viumbe wako. Na kwa uliyemchaguwa kwa ajili yako. Kwa haki ya uliye mteua kutoka viumbe wako. Na uliyempembuwa kwa kazi yako. Kwa haki uliye unganisha utii wake na utii wako. Na uliyemfanya kumuasi yeye ni kama kukuasi wewe. Kwa haki ya uliyeunganisha kumpenda kwake na kukupenda kwako. Na uliyeambatanisha kumfanyia uadui ni kukufanyia uadui. Nikinge katika siku yangu hii kwa kile ambacho wamkinga nacho mwenye kukuomba kwa shauku kubwa akijitakasa. Akiomba hifadhi kwa msamaha wako akitibu nichunge kwa ambacho unawachunga nacho watu wako watii na wakaribu kwako na wenye daraja kwako. Nipembuwe kwa unachowapembulia wenye kutekeleza ahadi yako. Na aliyejitaabisha nafsi yake kwa ajili yako ameishughulisha katika ridha zako. Usinichukuliye makosa kwa kuzembea kwangu kuhusu haki yako. Na kuvuka kadiri yangu kwenye mipaka yako. Na kukiuka hukumu zako. Usinivute kwa kunipa muda (huku ukijaza maovu yangu kwenye daftari ya maovu) mvuto wa aliyeniziwiya kheri zilizo kwake wala hakukushirikisha katika kuteremsha neema zake kwangu. Nizinduwe kutoka usingizi wa walio ghafilika na usingizi wa wafujaji na sinzio la waliotupiliwa mbali. Uchukuwe moyo wangu kwenye lile ulilo watumikisha wafanya ibada waliojitowa. Na ulikowatiisha wachamungu na kwayo umewaokoa wenye kuzembea. Nikinge mbali na kitacho niweka mbali na wewe. Na kitakachoziwiya kati yangu na hadhi yangu kwako. Na ziwiya juhudi yangu kwako Nirahisishiye njia ya kheri kuelekea kwako.

Na kupambana kuzielekea kama ulivyoamuru usinifute katika uwafutao miongoni mwa wanaopuuza uliyoahidi. Wala usiniangamize pamoja na uwaangamizao miongoni mwa wajitiao katika hatari ya chuki yako. Wala usinitanguwe katika uwatanguwao miongoni mwa waliopotoka toka kwenye njia zako. Niokoe kutoka kwenye funiko la fitina. Niepushe toka kwenye umio la balaa. Nikinge na kuchukuliwa na kuwepwa muda. Zuwia kati yangu na adui anipotezaye na upuuzi uniangamizao na dosari inipatayo. Usinigeuziye uso mgeuzo wa usiye mridhia baada ya ghadhabu yako. Usinikatishe tamaa kukutumainia ili nisije zidiwa na kutokwa na matumaini ya rehema zako. Wala usinipe mtihani ulio zaidi ya uwezo wangu ili usije ukanifanya nizidiwe na uzito wa unitwishacho kutokana na fadhila za mahaba yako. Usinitume kutoka mkononi mwako utumwaji wa asiyekuwa na kheri yeyote, wala umuhitajii wala harejei kwako. Usinitupe mtupo wa aliyetoka nje ya jicho la uangalizi wako. Aliyezingirwa na udhalilisho wako. Ni afadhali unishike mkono ili uniokowe kutokana na hamaniko la waliopotoka, na kuteleza kwa waliodanganyika, na hali mbaya ya walioangamia. Ni feleti kutokana na balaa ulio waonjesha tabaka za waja wako na vijakazi wako. Nifikishe ngazi za uliyemtilia manani uliyemneemesha, uliyemridhia, umemfanya aishi kwa sifa njema. Na ukamchukua kwako kwa heri, univike utepe wa kujitoa kwenye (mambo) yanayo haribu matendo mema, yaondoayo baraka. Ufunulie moyo wangu kujiziwiya na matendo mabaya, matendo yafedheha.

Usinishughulishe kufanya ambalo siwezi lifikia isipokuwa kupitia kwako, kwa kuwa mbali na ambalo huridhiki na mimi isipokuwa kwa hilo. Ondoa moyoni mwangu kupenda dunia nyonge iziwiayo kilicho kwako, inaziba kumpata mtetezi kwako, inaondoa jaribio la kupata ukaribu na wewe. Na pambambiye kubakia peka kwa ajili ya ibada yako usiku na mchana. Nipe hifadhi itakayo nikurubisha kukuogopa wewe. Itakayo niweka mbali na kutenda uliyo yaharamisha. Itakayonikomboa kutokana na utumwa wa dhambi kubwa itishayo. Nipe utakaso kutokana na uchafu wa maaswi. Niondolee uchafu wa makosa. Nivike na vazi la hali njema. Nivishe joho la msamaha wako. Niviringishe katika wingi wa neema zako. Nivishe na fadhila zako na ihsani yako. Nipe nguvu kwa tawfiki yako na mwongozo wako. Nisaidiye kuwa na nia njema na kauli ya kuridhisha, na kazi ikubaliwayo. Wala usiniwakilishe kwenye uwezo wangu na nguvu zangu, mbali na uwezo wako na nguvu zako. Usinidhili siku utakayonifufua kukutana na wewe. Usiniumbuwe mbele ya wapenzi wako, wala usinisahaulishe kukukumbuka. Usiniondolee shukrani yako, bali nilazimishe nayo katika hali ya kusahau wakati wa mghafala wa wasio zijua neema zako. Niongoze (moyoni) kusifu ulionitendea, na niyatambue uliyonitunukia nayo.

Jaalia londeo langu kwako zaidi kuliko londeo la wa londeawo. Na himidi yangu kwako iwe zaidi kuliko himidi ya wenye kukuhimidi. Usinitupe wakati wa haja yangu kwako. Usiniangamize kwa ajili ya niliyokutendea. Usinichape kofi kama ulivyowachapa kofi wakupingao. Kwani mimi nasalimu amri kwako. Najua kuwa hoja ni yako, na wewe ni mbora wa fadhila, mzoefu wa kufanya ihsani. Ni mwenye kustahiki kuogopwa, wastahiki kutoa msamaha, na kwamba kwako msamaha bora kuliko uadhibu. Na kwamba wewe kusitiri kwako ni karibu mno kuliko kufichuwa sitara. Nihuishe maisha mema yatakayo lingana na nitakayo, na yatayafikia niyapendayo kwa namna ambayo siyafanyi uyachukiayo, wala sitendi uliyoyakataza. Nifishe kifo cha ambaye nuru yake yapita mbele yake na kuliani kwake. Nidhalilishe mbele yako nitukuze mbele ya viumbe wako. Niteremshe nikiwa peke yangu kwako, ninyanyuwe kati yawaja wako. Nitosheleze kwa asiye na haja na mimi nizidishiye haja na ufakiri kwako. Nikinge na masimbulizi ya maadui na kushukiwa na balaa, udhalili na shida. Nikinge na lile ulionalo kwangu kwa ajikingacho nacho mwenye uwezo wa kupiga kwa nguvu lau si huruma yake. Nakushika kwa sababu ya dhambi lau kama si saburi yake. Uwafanyiapo gumu mtihani au uovu niokoe kwa kuwa naomba sitara yako. Kwa kuwa hujasimamisha kisimamo cha fedheha katika dunia yako, usinisimamishe kisimamo mfano wake katika akhera yako. Nifanyie ihsani mbili ya mwanzo kwa ya mwisho wake. Mafao yako yametangulia kwa matukio yake. Usinirefushie muda ambao moyo wangu utakuwa mgumu kwa ajili yake. Usinigonge na kigongo ambacho kunawiri kwangu kutatoweka. Usinitupe udhalili ambao utaidogesha hadhi yangu wala upungufu kwa ajili yake tamaa haitojulikana nafasi yangu. Usinihofishe hofu ambayo itanikatisha wala woga ambao kwa ajili yake nitabakia na woga. Jaalia woga wangu uwe katika tishio lako, na hadhari yangu iwe katika kutoacha kwako kwangu udhuru na onyo lako. Woga wangu uwe nisomapo aya zako usitawishe usiku wangu kwa kuamka humo kwa ibada yako. Nakubaki peke yangu nikikesha kwa ajili yako. Utulivu wangu ni kwako tu, na kuzileta haja zangu kwako. Na kukulalamikia wewe katika kuikomboa shingo yangu iepukane na moto wako. Na unipe kimbilio kutoka mahali ambapo watu wake ana adhambu. Usiniache kipofu nikitangatanga katika ujeuri wangu, wala katika mfadhaiko wangu mpaka muda.

Usinifanye niwe onyo kwa mwenye kuonyeka. Wala mfano wa adhabu kwa mwenye kuzingatia. Wala usiwe jaribio kwa mwenye kuangalia. Usinifanyie vitimbi pamoja na uwafanyiao vitimbi. Usinibadilishe na mwingine. Usinibadilishe jina, wala usinibadilishe mwili, usinifanye kichekesho kwa viumbe wako wala kuwa mfuasi wa chochote isipokuwa ridhaa zako. Wala kuwa mtumishi kwa yeyote isipokuwa kulipiza kisasi kwa ajili yako. Nionyeshe ubaridi wa msamaha wako, na utamu wa rehema zako, na raha zako, utulivu wako, na bostani ya kipeo cha raha yako. Nionjeshe utamu wa kuwa na faragha kwa uyapendayo, kwa wasaa katika wasaa wako. Na kufanya juhudi katika mambo ambayo yaletayo ukaribu na wewe na kwako. Nizawadie kwa zawadi miongoni mwa zawadi zako. Ifanikishe biashara yangu; rejeo langu lisiwe la hasara. Nihofishe mahali pako, nipe shauku ya kukutana na wewe. Ipokee toba yangu toba isio rejelewa dhambi usibakishe pamoja nayo dhambi ndogo wala kubwa. Usiache kosa pamoja na (Toba) lawazi wala la siri. Niondolee chuki kifuani mwangu kwa waumini lifanye moyo wangu uelemee kwa wanyenyekevu. Kuwa kwangu kama uwavyo kwa watu wema ni pambe na mapambo ya wachamungu nijaalie usemi mkweli kwa waliopita na utajo wenye kukuwa katika wakati ujao nichukuwe kwenye uwanda wa watu wa kwanza. Nikamilishiye neema yako, nidhihirishiye ukarimu wako. Ijaze mikono yangu faida zako. Nisongezee zawadi ya ukarimu wako. Nifanye jirani wa watu wema miongoni mwa mawalii wako, katika janna uliyoipamba kwa ajili ya wateule wako. Nizingirishe kwenye zawadi zako tukufu mahali palipo andaliwa kwa ajili ya wapenzi wako. Nijaalie kwako mahali nitakuwa nakimbilia nikiwa mtulivu. Na marejeo nitarejeako na macho yangu kupata utulivu. usinipime kwa ukubwa wa maovu yangu wala usinihilikishe siku siri zitakapo fichuliwa. Niondowe kila aina ya shaka na hali isiokuwa wazi. Nijaalie njia katika ukweli kutoka kila aina ya rehema. Nizidishie sehemu ya zawadi katika ukitowacho. Nipe hadhi kubwa ya ihsani katika utoaji wako wa ufadhili. Ujaalie moyo wangu kuwa na itibari na yaliyopo kwako. Hima yangu iwe kwa ajili ya ambalo ni lako. Nitumikishe kwa yale uwatumikishayo wenye ikhilaasi kwako. Unyweshe moyo wangu utii wako wakati nyoyo zitakapovutwa vingine.

NA ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) SIKU YA KUCHINJA, SIKU YA IJUMAA

O h Allah! Hii ni siku yenye baraka yenye heri. Waislamu katika siku hii wamejikusanya katika sehemu ya ardhi yako. Miongoni mwao akiwemo mwombaji, atafutaye alondeaye mwenye woga. Nawe ukiwa mwangaliaji wa haja zao kwa hiyo nakuomba kwa upaji wako na ukarimu wako na urahisi wa nilichokuomba. Mrehemu Muhammad na Aali zake. Na ninakuomba Oh Allah Mola wetu. Kwa sababu ufalme ni wako na zako ni sifa njema. Hapana Mungu isipokuwa ni wewe. Mwenye huruma mkarimu. Mpendwa wa wote mwema kwa wote. Mwenye Enzi na upaji. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Ugawanyapo kati ya waja wako waumini miongoni mwa heri au hali bora, au baraka au mwongozo au kazi ya utii wako au heri kwa tunukiayo unawaongoza kwayo kuja kwako. Au unawanyanyua kwako daraja au unawapa kwayo heri miongoni mwa heri ya dunia na akhera. Nizidishiye hisa yangu na sehemu yangu. Nakuomba Oh Allah Mola wetu kwa kuwa wako ni ufalme na zako ni sifa njema hapana muabudiwa ila ni wewe. Mrehemu Muhamrnad (Na Ali zake) mja wako na mjumbe wako mpenzi wako mteule wako mchaguliwa wako katika viumbe wako na ziwe juu ya Ali wa Muhammad watu wasafi wateuliwa. Rehema ambazo hana uwezo yeyote wa kuzihesabu isipokuwa wewe. Tushirikishe na wema waliokuomba katika siku hii miongoni mwa waja wako waumini.

Oh Bwana wa Walimwengu wote. Tusamehe sisi na wao. Hakika wewe ni Muweza juu ya kila kitu. Oh Allah! Kwako nimekusudia kwa haja zangu. Kwako nimekabidhi hii leo umaskini wangu haja zangu na taabu yangu. Kwani kwenye msamaha wako na rehema zako naani mno kuliko aamali yangu (Kazi). Msamaha wako na rehema zako zinawasaa zaidi kuliko dhambi zangu. Mrehemu Muhammad na Aali wa Muhammad shikilia kukidhi kila haja ambayo ni yangu. Kwa uwezo wako juu yake na urahisi wa hilo kwako. Na kwa sababu ya ufakiri wangu kwako, na kwa sababu ya kutonihitajia kwako. Sipati heri kabisa isipokuwa kutoka kwako. Haniondolei yeyote ovu kabisa isipokuwa wewe. Simtumainii kwa mambo ya akhera yangu na dunia yangu asiyekuwa wewe. Oh Allah! Mwenye kujiandaa na kujitayarisha kumwendea kiumbe akitarajia msaada wake na jaalio lake na kutaka kupata na tuzo lake. Basi kwako Ewe Mola wangu , ndio maandalizi yangu na utayarifu wangu hii leo. Maandalizi yangu na kuwa tayari kwangu kutaraji msamaha wako na msaada wako na kukupata wewe na kupata zawadi zako.

Oh Allah! Mrehemu Muhammad na Aali wa Muhammad usinitowe matumaini leo, hayo ndiyo matarajio yangu. Oh yule ambaye hasumbuliwi na mwombaji wala hapunguzwi na mpata (mahitaji). Hakika mimi sikukujia kwa kujiamini kuwa nina aamali njema nimeitanguliza au uombezi wa kiumbe niutarajiao. Isipokuwa uombezi wa Muhammad na Ahl-Bayt wake. Juu yake na juu yao amani iwafikie amani yako. Nimekujia nikiwa mwenye kutambua makosa na maovu kwa ajili ya nafsi yangu. Nimekujia nikitaraji kupata utukufu wa msamaha wako ambao kwa huwo umewasamehe wakosefu. Kisha muda mrefu wa kubaki kwao katika madhambi makubwa haukukuzuia kuwa rejelea na Rehema na msamaha. Oh yule ambaye rehema zake zinawasaa na msamaha wake mkubwa. Ewe Mtukufu Ewe Mtukufu. Ewe Mkarimu Ewe Mkarimu! Mrehemu Muhammad na Aali wa Muhammad. Nirudilie kwa Rehema zako kuwa mpole kwangu kwa fadhila zako nienezee msamaha wako. Oh Allah! Hakika nafasi hii ni ya makhalifa wako wateule kwako.

Na nafasi ya waaminifu kwako katika daraja ya juu ambayo umeifanya kuwa ni mahususi kwao wamenyang'anywa wewe ndio mpangaji wa hayo. Amri yako hailemewi. Wala hauvukwi mpango wako wa lazima. Upendavyo wakati upendao. Kwa ambalo wewe wajuwa zaidi, hutuhumiwi kwa kuumba kwako wala kwa utashi wako. Kitabu chako kimebeuliwa. Faradhi zako zimepotoshwa toka malengo ya sheria zako sunna za Nabii wako zimeachwa. Oh Allah! walaani maadui toka wa mwanzo mpaka wa mwisho pamoja na aridhikaye. Pamoja na mwenye kuridhika na vitendo vyao na wenye kuambatana nao na wafuasi wao. Oh Allah mrehemu Muhammad na Aali wa Muhammad. Hakika ewe ni mwenyestahiki ya kuhimidiwa na kutukuzwa. Mfano wa Rehema zako na baraka zako na maamkizi yako kwa wateule wako Ibrahimu na wana wa Ibrahim. Oh Allah! waharakishie faraja Raha, msaada, imarisho na kuungwa mkono. Oh Allah! nifanye mimi niwe miongoni mwa wenye kukupwekesha na kukuamini na kumsadiki mtumishi wako na maimamu ambao umeamuru utii wao miongoni mwa ambaye kwake wapitisha hayo na mkononi mwake. Ameen Rabbal-Alameen.

Oh Allah! Hapana kirudishacho ghadhabu zako isipokuwa huruma zako. Wala kiirudishacho kasiriko lako ispokuwa msamaha wako. Wala hakuna atowaye kimbilio la kuepuka adhabu ila ni Rehema zako. Hakuna kitakachoniokoa kutoka kwako isipokuwa kunyenyekea kwako mbele yako. Mrehemu Muhammad na Aali wa Muhammad na utupe kutoka kwako Ewe Mola wangu Faraja kwa nguvu ambazo kwayo wa Huisha wafu wa waja. Na kwayo unarudisha uhai wa wafu wa wala usinihilikishe Ewe Mola wangu katika majonzi kabla hujanijibu na kunijulisha jibu katika duwa yangu. Nionjeshe utamu wa kuwa na hali njema mpaka mwisho wa muda wangu. Usimpe fursa kunisimanga aduwi yangu, wala usiiweke shingo yangu chini ya uwezo wake usimpe mamlaka juu yangu. Oh Mungu! Wangu ukiniinuwa ni nani atanitweza? ukinitweza ni nani ataniinuwa? Ukinipa heshima ni nani atakayenidunisha ukinidunisha ni nani atakayenipa heshima? Ukiniadhibu ninani atakayenihurumia? Ukinihilikisha ni nani atakayekupinga katika mja wako au akuulize kuhusu mambo yalee? Nijuavyo ni kwamba hapana dhulma katika hukumu yako, wala haraka katika malipizi yako. Kwa kuwa hufanya haraka aogopaye kukosa na ni hakika kabisa kuwa aihitajie dhuluma ni yule ambaye ni dhaifu. Na hakika umetukuka Ewe Mola wangu! Umbali na hayo utukufu wa juu kabisa. Oh Allah mrehemu Muhammad na Aali wake. Usinifanye kuwa shabaha ya mabalaa wala nisiwe lengo la kisasi chako nipe muda nipe raha. Niondoshee kujikwaa kwangu Watambuwa udhaifu wangu na uhaba wa hila yangu na maombi yangu kwako. Na maombi yangu kwako najikinga kwako Oh Allah dhidi ya ghadhabu yako hii leo. Mrehemu Muhammad na Aali wake ni kinge na kuomba amani ili niwe mbali na adhabu yako.

Mrehemu Muhammad na Aali wake, na unipe amani. Nakuomba mwongozo basi mrehemu Muhammad na Aali wake na ni ongoze. Naomba kwako msaada basi mrehemu Muhammad na Aali wake na unisaidiye na kuomba rehema, basi mrehemu Muhammad na aali wake na unirehemu. Nakuomba kujitosheleza basi mrehemu Muhammad na Aali wake na unistosheleze. nakuomba riziki basi mrehemu Muhammad na Aali wake na uniruzuku. Nakuomba mssada basi mrehemu muhammad na Aali wake na unisaidie. Nakuomba msamaha kwa yaliyopita katika dhambi zangu mrehemu Muhammad na Aali wake na unisamehe. Nihifadhi basi mrehemu Muhammad Na Aali wake na unihifadhi. Kwa kuwa sitorudia kitu ulichokichukia kutoka kwangu ukipenda hivyo. Yaa Rabbi yaa Rabbi Oh Mola wangu! Oh Mola wangu! Yaa Hannaan yaa Hannan mpenda wote ya Dhal-Jalaal Wal-Ikram Oh Mwenye Ufalme na ukarimu.

Mrehemu Muhammad na Aali zake na nijibu kwa yote niliyokuomba na nimeyataka kutoka kwako na nilio kulondea agiza, gadiria, nihukumiye nipitishiye. Nipe kizuri katika ukipitishacho, nibariki nacho. Nifadhili nacho, Nifanye niwe na furaha na unipacho nizidishie fadhila zako na wasaa kwa uliyo nayo. Kwani wewe ni mwenye wasaa mpaji na unganisha hayo na heri ya Ahera na Neema Zake. Ewe Mwenye Rehema sana miongoni mwa wenye kurehemu (hapo omba upendayo na utamsalia Mtume Muhammad na Ahli wake mara 1000 elifu moja. Hivi ndivyo alivyokuwa akifanya amani iwe juu yake).


10

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE (A.S) KATIKA KUJIKINGA NA VITIMBI VYA MAADUI NA KUONDOWA MACHUNGU YAO

Mola wangu uliniongoza nikabeuwa. Uniwaidhi moyo wangu ukawa mgumuUlinitaribu kwa uzuri nimeasi. Baadaye nilitambuwa uliyo amrisha uliponitambulisha. Nikaomba ghofirani ukaondowa nikarudia ukasitiri. Zako Mola wangu ni sifa njema. Nimetosha katika bonde za kuangamiza nimejiweka kwenye hatari ya dhahbu zako na ni mashukio ya adhabu zako. Njia yangu kwako ni Tawheed. Nasababu zangu za kufika kwako ni kuwa sija kushirikisha na kitu chochote sijaambatanisha pamoja na wewe Mungu nimekimbilia kwako na nafsi yangu. Kwako ndio kimbilio la mtenda maovu aliyepoteza hadhi ya nafsi yake na kuomba kimbilio. Kiasi gani cha aduwi amechoomowa kwa ajili yangu upanga wa uaduwi wake! Na amechongowa makali ya ncha ya upanga wake kwa ajili yangu! Na kunowa kwa ajili yangu bapa la makali yake. Ameichanganya sumu yake iuwayo kwa ajili yangu. Na kuelekeza kwangu mishale yake iliyonyooka irukayo. Wala halikulala jicho lake linichungalo. Na kisiri siri akakusudia kunifanyia makuruuhi. Ana nitakia mimi uchungu wa chuki yake umeona O Mungu wangu udhaifu wangu kuibeba mizigo mizito na kushindwa kwangu kupata ushindi dhidi ya aliyenikusudia kwa kupigana naye. Na upeka wangu mbele ya idadi kubwa ya aliye na uaduwi na mimi. Anivizia kwa balaa ambalo sikuliwazia fikrani mwangu.

Ulianza kunisaidia kwa nusura yako uliimarisha mgongo wangu kwa nguvu zako. Uliyafanya butu makali yake. Baada ya mkusanyiko mwingi umemfanya abakiye peke. Umekiinua kisigino changu juu yake na kumfanya aliyonilenga yamrudie ulimrudisha nyuma. Hakuzituliza ghadhabu zake. Hakukoza kiu chake. Ameuma kidole chake. Aligeuza mgongo na kukimbia mpango wake haukutimia. Ni mara ngapi mdhalimu amenifanyia udhalimu kwa vitimbi vyake amenitegea mtego wake. Akaniwekea uangalizi wa walinzi wake akaniwinda uwindaji wa mnyama mkali awindapo windo lake.

Naye unidhihirishia tabasamu ya mwenye kujipendekeza. Huku akiniangalia kwa ghadhabu kali ulipoona Ewe Mungu wangu! Umebarikiwa na umetukuka ubaya wa fikra zake za siri na ubaya wa aliyo nayo. Ulimtupa kichwa chini ndani ya shimo lake mwenyewe. Na umemtumbukiza katika maporomoko aliyochimba. Alidogeshwa dhahili baada ya kujitukuza kwake ndani ya tanzi la mtego wake ambao alipanga anione nimenasa humo. Kama si Rehema zako yangenifika yaliyomfika. Wangapi miongoni mwa hasidi amenisonga koo kwa maumivu makubwa sana. Kwa ukali wake amenihuzunisha amenikata kwa ncha ulimi wake alinifanyia kijicho heshima yangu ilikuwa lengo lake ili kuiharibu. Amenivisha utepe wa aibu ambao ungalipo. Amenifanyia vitimbi ameniknga na hila zake. Hivyo basi nikakuita Oh Mungu wangu nikiomba msaada kwako. Nikiwa na uhakika wa haraka ya jibu lako. Nikijua kuwa hatendewi vibaya mwenye kukimbilia kwenye kivuli cha hifadhi yako. Hatofadhaika mwenye kukimbilia kwenye ngome ya ushindi wako. Ukanihifadhi na ukali wake kwa uwezo wako. Kiasi gani cha mawingu makuruhi umeniondolea mbali. Na mawingu ya neema umenyeshesha rehema zake juu yangu. Vijimto vya rehema umevitiririsha na halki njema umenivika nayo macho ya misiba umeyapofowa. Mfululizo wa mfuniko wa majonzi umeitanduwa. Dhana nzuri ngapi umeithibitisha na ukosefu umesawazisha ugonjwa umeuponya. Umasikini umeubadilisha. Yoote hayo ni neema na ufadhili kutoka kwako. Na katika hali yoote hiyo umeendelea ushupavu kutoka kwangu wa kukuasi. Matendo yangu maovu hayatakuzuiya kutimiza ihsani ufanyayo.

Hakika uliombwa ukatowa usipo ombwa ulianza (kutowa) uliombwa ufadhili wako haukutowa kwa unyimivu. Umekataa Oh Mungu wangu isipokuwa kufanya ihsani na ufadhili na kuneemesha. Nimekataa kila kitu isipokuwa kujitosa katika yaliyoharamisha. Na kuvuka mipaka yako. Na kutotiliya mananni makamio yako. Yako ni sifa njema Oh Mungu wangu! muweza asiye shindwa. Na saburi hafanyi haraka. Hiki ni kisimamo cha mwenye kutambuwa wingi wa neema na umeikabili kwa kiwango cha chini ya vile inavyobidi. Na amejishuhudiya binafsi kutowajibika. Oh Allah mimi najikurubisha kwako kupitia daraja ya juu ya Muhammad na kwa mwanga wa daraja ya juu ya Aali. Naelekea kwako kupitia wao wawili unilinde kutokana na shari fulani na fani. Hakika hayo hayakutii dhiki katika utajiri wako. Wala haikupi taabu katika nguvu zako na wewe ni muweza juu ya kila kitu. Basi nipe Oh Mungu wangu katika rehema zako na taufiki yako ya kudumu ambayo nitaifanya ngazi niipandayo ili kuifikia ridhaa yako. Ili niwe na amani mbali na adhabu yako. Oh Mwingi wa rehema kuliko wote wenye kurehemu.

NA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA HALI YA WOGA

Oh Allah hakika wewe umeniumba katika hali sawa bila dosari. Umenikuza nilipokuwa mdogo, uliniruzuku vya kutosha. Oh Allah hakika mimi nimekuta katika uliyoteremsha kitabuni mwako na umewabashiria hayo waja wako umesema: Oh! Waja wangu ambao wamezifuja nafsi zao, musikate tamaa na rehema za Allah. hakika Mungu hughofiria dhambi zote. Na yametangulia toka kwangu katika uliyoyajuwa na ambayo wewe ni mjuzi zaidi kuliko mimi. Aibu iliyoje kwa yale ambayo kitabu chako kimeyahifadhi dhidi yangu. Lau kama si sehemu ambazo nina matumaini ya msamaha wako ambao umeenea kila kitu ningejitupa chini (nikikata tamaa). Lau kama yeyote angeweza kumkimmbia Mola wake ningekuwa na haki zaidi ya kukukimbia. Na wewe hakifichiki kwako chenye kujificha kiwe ardhini au mbinguni ila utakileta. Wewe ni mwenye kujaza tosha na wewe ni mhasibu tosha. Oh Allah! hakika wewe utanitafuta endapo nitakimbi utanipata endapo nitapiga mbio hivyo basi mimi ni huyo ni mbele yako mnyenyekevu dhalili mwenye kujitweza. Ukiniadhibu ninastahiki, nayo Oh! Mola wangu ni uadilifu kutoka kwako. Na ukinisamehe toka zamani nimeingizwa katika msamaha wako. Na umenivika hali njema yako. Hivyo basi nakuomba Oh Allah! kwa majina yako yaliyo katika hazina na kwa utukufu wako uliyo nyuma ya pazia, ikiwa hautoihurumia nafsi hii yenye mashaka na hii mifupa iliyo sumbuka ambayo haiwezi joto la jua lako, itawezaje joto kali la moto wako ambayo haiwezi kuvumilia sauti ya radi yako. Vipi itaweza kuivumilia sauti ya ghadhabu yako. Hivyo basi nihurumie. Oh Allah! mimi ni mtu mnyonge, thamani yangu ndogo, kuniadhibu kwako hakuuzidishii ufalme wako uzito hata kama ule wa chembe ya vumbi.. Lau kama kuniadhibu kwako mimi kungezidisha chochote katika ufalme wako, ningekuomba niiivumiliye (adhabu), na ningependa iwe yako. Lakini mamlaka yako Allahumma ni Mtukufu mno, na ufalme wako ni wa kudumu mno kuliko ule wa kuongezwa na utii wa watii au upunguzwe na maasi ya watenda dhambi. Nihurumiye Ewe mwenye rehema zaidi ya woote wenye kurehemu. Nivumiliye Ewee mwenye enzi na ukarimu. Nirejelee, hakika wewe ni mwingi wa kukubali toba mwenye huruma kuliko wote.

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA KUSIHI NA KUNYENYEKEA

Oh Mungu wangu nakuhimidi na wewe ni mwenye kustahiki kuhimidiwa, kwa ihisani yako kwangu, na wingi wa neema zako kwangu, na kwa wingi wa utowaji wako kwangu, na kwa uliyonifadhili katika rehema zako. Umenikamilishia neema zako.Umenitendea mema kwa kiwango nashindwa kutekeleza shukurani yake. Lau kama si ihisani yako kwangu, na wingi wa neema zako kwangu, nisingeifikia hadhi yangu, wala nisingeiweka nafsi yangu sawa. Lakini wewe ulianza kunihisani na uliniruzuku vya kutosha katika mambo yangu yote. Uliniondolea taabu ya balaa. Uliziwiya kwa ajili yangu maamuzi yako yakuogofya.

Mungu wangu, balaa ngapi zitaabishazo umeniondolea. Neema ngapi za ukarimu umeniletea karibu. Matendo yako mangapi ya ukarimu kwangu! Wewe ndiye ambaye ulinijibu wakati wa dharura ombi langu. Na ulidogesha nilipojikwaa mtelezo wangu na ulinichukulia kutoka kwa maaduwi niliodhulumiwa. Oh! Mungu wangu sijakukuta bakhili nikuombapo. Wala mwenye kujikunja nilipo kutaka, bali nilikukuta mwenye kusikiliza DU'A yangu. Na mpaka wa matakwa yangu. Nimekuta neema zako kwangu nyingi. Katika kila jambo miongoni mwa mambo yangu. Na kila zama katika zama zangu wewe kwangu ni mwenye kuhimidiwa na matendo mema yako kwangu yenye kuheshimiwa. Nafsi yangu, ulimi wangu, akili yangu, vya kuhimidi himidi ifikiye tekelezo na hakika ya kushukuru. Himidi iwe kiwango cha ridhaa zako kwangu. Niokowe toka kwenye makasiriko yako. Oh! Mwokozi wangu nijikwaapo, lau si kama sitara yako aibu yangu, ningekuwa miongoni mwa wenye kufedheheka. Oh! Muungaji wangu mkono kwa msaada kama si msaada wako kwangu ningekuwa miongoni mwa wenye kushindwa. Oh! We ambaye wafalme wamemwekea kongwa ya udhalili shingoni mwao wakiogopa adhabu zake.

Oh! Mwenye stahiki ya kutukuzwa. Oh! Mwenye majina mema. Nakuomba unisamehe na unighofiriye siko mweupe bila dhambi, ili niweze kutowa udhuru. Wala sina nguvu, niwe na weza kupata ushindi wala sina kimbilio niweze kukimbilia. Ninakuomba uniokowe toka kwenye kujikwaa kwangu. Najitenga mbele yako na dhambi zangu ambazo zimeniweka pabaya na zimenizunguka na kunihilikisha. Kutokana nazo nimekimbilia kwako Mola wangu mwenye kutubu nikubaliye toba yangu. Najikinga kwako nipe kinga. Nikiomba hifadhi usiniache. Nikiomba usininyime. Nikishikilia usiniache. Nikiomba usinirudishe mikono mitupu. Nimekuomba Ewe Mola wangu niko hali mbaya mnyonge. Mwenye hofu mwoga. Mwenye kutapatapa fakiti. Nimedharurika kwako. Nakulalamikia Ewe Mola wangu, udhaifu wa nafsi yangu kutoharakia kwenye kile ulichowaahidi marafiki zako. Nakujiepusha na ulicho wahadharisha maadui zako. Na kukithiri mayonzi yangu na wasiwasi wa nafsi yangu. Mola wangu hujanifedhehesha kwa ajili ya fikra zangu za siri, wala hujanihilikisha kwa maovu yangu, nakuita wanijibu japo nipo goigoi unaponiita. Nakuomba nipendapo haja zangu. Popote niwapo naweka siri zangu kwako. Simwombi yeyote bali ni wewe tu. Simtumainii yeyote asiyekuwa wewe. Labeika Labeika. Wamsikia anayekunung'unikia, wampokea akutegemeaye. Wamwokoa mwenye kuomba hifadhi kwako. Wamfariji akimbiliyae kwako. Mola wangu usininyime mwisho mwema na mwanzo mwema kwa uchache wa shukrani wangu. Nighofirie ujuayo katika dhambi zangu. Ukiadhibu ni kwa kuwa mimi ni dhalimu, mzembe, mwenye kupuuza, mwenye dhambi, mwenye kuachwa mvivu. Mwenye kughafirika na hisa yake binafsi. Ukinisamehe ni kwa sababu wewe ni mwenye huruma mno kuliko wenye huruma wote.

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA KUMSIHI ALLAH (s.w.t)

Oh Allah! ambaye hakifichiki kitu chochote kwake katika ardhi au mbinguni. Vipi kifichike kwako Ewee Mola wangu ambacho wewe umekiumba? Vipi usijuwe idadi ya ambacho wewe umekiumba! Au vipi kisionekane kwako ambacho wewe wakimiliki. Oh Allah! Hapana kirudishacho ghadhabu zako isipokuwa huruma zako. Wala kiirudishacho kasiriko lako ispokuwa msamaha wako. Wala hakuna atowaye kimbilio la kuepuka adhabu ila ni Rehema zako. Hakuna kitakachoniokoa kutoka kwako isipokuwa kunyenyekea kwako mbele yako. Mrehemu Muhammad na Aali wa Muhammad na utupe kutoka kwako Ewe Mola wangu Faraja kwa nguvu ambazo kwayo wa Huisha wafu wa waja. Na kwayo unarudisha uhai wa wafu na wala usinihilikishe Ewe Mola wangu katika majonzi kabla hujanijibu na kunijulisha jibu katika duwa yangu. Nionjeshe utamu wa kuwa na hali njema mpaka mwisho wa muda wangu. Usimpe fursa kunisimanga aduwi yangu, wala usiiweke shingo yangu chini ya uwezo wake usimpe mamlaka juu yangu. Oh Mungu! Wangu ukiniinuwa ni nani atanitweza? ukinitweza ni nani ataniinuwa? Ukinipa heshima ni nani atakayenidunisha ukinidunisha ni nani atakayenipa heshima? Ukiniadhibu ninani atakayenihurumia? Ukinihilikisha ni nani atakayekupinga katika mja wako au akuulize kuhusu mambo yalee? Nijuavyo ni kwamba hapana dhulma katika hukumu yako, wala haraka katika malipizi yako. Kwa kuwa hufanya haraka aogopaye kukosa na ni hakika kabisa kuwa aihitajie dhuluma ni yule ambaye ni dhaifu. Na hakika umetukuka Ewe Mola wangu! Umbali na hayo utukufu wa juu kabisa. Oh Allah mrehemu Muhammad na Aali wake. Usinifanye kuwa shabaha ya mabalaa wala nisiwe lengo la kisasi chako nipe muda nipe raha. Niondoshee kujikwaa kwangu Watambuwa udhaifu wangu na uhaba wa hila yangu na maombi yangu kwako. Na maombi yangu kwako na jikinga kwako Oh Allah dhidi ya ghadhabu yako hii leo. Mrehemu Muhammad na Aali wake ni kinge na kuomba amani ili niwe mbali na adhabu yako. Mrehemu Muhammad na Aali wake, na unipe amani. Nakuomba mwongozo basi mrehemu Muhammad na Aali wake na ni ongoze. Naomba kwako msaada basi mrehemu Muhammad na Aali wake na unisaidiye na kuomba rehema, basi mrehemu Muhammad na aali wake na unirehemu. Nakuomba kujitosheleza basi mrehemu Muhammad na Aali wake na unitosheleze. nakuomba riziki basi mrehemu Muhammad na Aali wake na uniruzuku. Nakuomba mssada basi mrehemu muhammad na Aali wake na unisaidie. Nakuomba msamaha kwa yaliyopita katika dhambi zangu mrehemu Muhammad na Aali wake na unisamehe. Nihifadhi basi mrehemu Muhammad Na Aali wake na unihifadhi. Kwa kuwa sitorudia kitu ulichokichukia kutoka kwangu ukipenda hivyo. Yaa Rabbi yaa Rabbi Oh Mola wangu! Oh Mola wangu! Yaa Hannaan yaa Hannan mpenda wote ya Dhal-Jalaal Wal-Ikram Oh Mwenye Ufalme na ukarimu.Mrehemu Muhammad na Aali zake na nijibu kwa yote niliyokuomba na nimeyataka kutoka kwako na nilio kulondea agiza, gadiria, nihukumiye nipitishiye. Nipe kizuri katika ukipitishacho, nibariki nacho. Nifadhili nacho, Nifanye niwe na furaha na unipacho nizidishie fadhila zako na wasaa kwa uliyo nayo. Kwani wewe ni mwenye wasaa mpaji na unganisha hayo na heri ya Ahera na Neema Zake. Ewe Mwenye Rehema sana miongoni mwa wenye kurehemu (hapo omba upendayo na utamsalia Mtume Muhammad na Ahli wake mara 1000 elifu moja. Hivi ndivyo alivyokuwa afanya amani iwe juu yake).

NA ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA KUJIDHALILISHA KWA MUNGU MWENYE ENZI MTUKUFU

Oh Mola wangu zimeninyamazisha dhambi zangu maneno yangu yamekatika sina hoja nimekuwa mateka wa balaa yangu. Niko rehani kwa matendo yangu. Mwenye kutaradadi katika makosa yangu nimechanganyikiwa katika makusudio yangu. Nimezuilika. Nimejikwamisha binafsi mahali pa madhalili wenye dhambi. Mahali pa wenye hali mbaya wanaothubutu dhidi yako, ambao waifanyao ahadi yako nyepesi. Sub'haanaka-utakatifu ni wako. Ni ufedhuli ulioje nimekufanyia! Kudanganyika gani nimejidanganya nafsi yangu Mola wangu uhurumiye mtelezo wangu ulioniweka fudi fudi. Na kuteleza kwa nyayo yangu nitendee kwa upole wako kulingna na kutojuwa kwangu. Na kwa ih'sani yako juu ya uovu wangu. Mimi ni mwenye kukiri dhambi yangu.Mwenye kutambuwa makosa yangu. Huu mkono wangu na paji langu la uso. Najitoa kwa malipizi nafsi yangu, zihurumie mvi zangu na kwisha kwa siku zangu. Na kukurubia muda wangu, udhaifu wangu taabu yangu, na uchache wa hila yangu Mola wangu nihurumie pindi athari yangu ikatikapo duniani. Na kufutika kwa viumbe utajo wangu nikawa miongoni mwa waliosahaulika kama ambaye amekwisha sahauliwa. Mola wangu nihurumie libadilikapo umbo langu na hali yangu uozapo mwili wangu na kutawanyika viungo vyangu. Oh! mghafala ni wangu kwa yaliyotakiwa kwangu. Oh Mola wangu! nihurumie siku ya kukusanywa kwangu na kufufuka kwangu. Jaalia siku ile kisimamo changu niwe pamoja na mawalii wako. Matokeo yangu yawe pamoja na wapenzi wako. Makazi yangu yawe karibu yako. OhMola wa ulimwengu.


11

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

MIONGONI MWA DU'A ZAKE KUONDOWA MASHAKA

Oh mfariji wa mashaka, muondoa huzuni mwenye reh'ma ya dunia na akhera na mwenye huruma kwa zote mbili (dunia na akhera). Mrehemu Muhammad na Ali wa Muhammad. Nifariji mashaka yangu. Niondolee huzuni yangu. Oh we! mmoja Oh wee pekee! Oh we kimbilio la kudumu! Oh we ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa halingani na mmoja yeyote. Ni hifadhi, nifanye niwe safi niondolee balaa langu. Na hapa watakiwa isome;Ayatal-Kursiyi Na Qul Audhu Birabil-Falaq Na Qul-Audhu Bira Binnasi Na Qul-Huwallahu Ahadu.

Kisha soma DU'A hii: Oh Allah hakika mimi nakuomba ombi la ambaye hajja yake ni kubwa sana, nguvu zake zimedhoofu dhambi zake zimekithiri ombi la ambaye hampati wakumsaidia mahitaji yake, wala wakurudisha nguvu kwenye udhaifu wake wala wa kumghofiria dhambi zake asiyekuwa wewe, Oh mwenye utukufu na ukarimu. Nakuomba amali ambayo waipenda mwenye kuitenda na yakini itamfaa mwenye kuwa na yakini ya kweli katika kutekeleza amri yako. Oh Allah mrehemu Muhammad na Ali wa Muhammad ichukuwe nafsi yangu ikiwa katika hali ya kusadikisha, iondolee hajja yangu ya dunia na jaalia upendo wangu uwe katika yale yaliyo kwako nikiwa na shauku ya kukutana na wewe. Nipe ukweli wa kukutegemea na kuomba kheri iliyoachwa na kitabu kitakatifu na ninajikinga kwako na shari ya iliyoachwa na kitabu kitakatifu.

Nakuomba hofu ya wanao kuabudu na ibada ya wakunyenyekeao kukuogopa na yakini ya wanaokutegemea na kukutegemea kwa waumini. Oh Allah ufanye utashi wangu katika maombi yangu mfano wa utashi wa mawalii wako katika maombi yao. Na woga wangu mfano wa woga wa mawalii wako. Nitumikishe katika maridhawa yako aamali sitoacha pamoja nayo kitu chochote katika dini yako kwa kumwogopa yeyote katika viumbe wako. Oh Allah hii ni hajja yangu ukuze utashi wangu humo, dhihirisha humo udhuru wangu, nifundishe humo hoja yangu na humo kipe afya kiwili wili changu. Oh Allah mwenye kufikiwa na asubuhi akiwa na matumaini au tarajio kwa asiyekuwa wewe, nimefikiwa na asubuhi na wewe ni matumaini yangu na ndio tarajio langu katika mambo yote niamulie ambalo linamwisho mwema na uniepushe na fitna potovu, kwa huruma yako, ewe mwenye huruma zaidi ya wenye huruma wote. Mungu mbariki muheshimiwa wetu Muhammadi na mjumbe wa Mungu mteule na wabariki ali zake waliotahirika.

MIONGONI MWA TASBEEHI ZAKE NAMKUSUDIA ZAYNUL-AABIDEENA(A.S) ALAYHIS-SALAAM

Utakatifu ni wako Oh Allah na ninakuomba uangalizi wako wenye upendo. Utakatifu ni wako Oh Allah na umetukuka juu kabisa. Adhama ni yako Oh Allah na enzi ni shuka yako utakatifu ni wako Oh Allah na dhama ni joho lako utakatifu ni wako Oh Allah na ukubwa ni mamlaka yako. Utakatifu ni wako, ulioje utukufu wako! Utakatifu ni wako umetukuzwa juu, wasikia na waona kilicho chini ya udongo. Utakatifu ni wako washuhudia kila nong'ono, utakatifu ni wako mahali ambapo malalamiko yote huwekwa hapo. Utakatifu ni wako uko hadhiri katika kila mkusanyiko. Utakatifu ni wako ni lengo la kila matumaini. Utakatifu ni wako wakiona kilicho chini kabisa ya maji. Utakatifu ni wako wasikia pumzi za samaki waliochini kabisa ya bahari. Utakatifu ni wako wajuwa uzito wa mbingu. Utakatifu ni wako wajuwa uzito wa ardhi zote. Utakatifu ni wako wajuwa uzito wa jua na wa mwezi. Utakatifu ni wako wajuwa uzito wa giza na nuru. Utakatifu ni wako wajuwa uzito wa kivuli na wa hewa. Utakatifu ni wako wajuwa uzito wa upepo mara ngapi kubwa kuliko uzito wa chembe ya vumbi. Utakatifu ni wako Qudusu Qudusu utakatifu ni wako mwenye kukutambuwa vipi asikuogope. Utakatifu ni wako Oh Allah sifa njema ni zako. Utakatifu ni wa Mungu mtukufu mkubwa.

Zuh'riy alieleza habari kutoka kwa Saeedi bin Musayyib amesema: Qaumu ya watu walikuwa hawatoki nje ya mji wa Makka mpaka atoke Aliy bin Husayn bwana wa wafanya ibada amani iwe juu yake. Hivyo basi alitoka nikatoka pamoja naye alisimama katika moja ya vituo akasali rakaa mbili akawa yu afanya tasbihi hii: (hapo juu) haukubaki mti wala kidongo isipokuwa kilifanya tasbihi pamoja naye. Tukafazaika, akainuwa kichwa chake akasema: Ewe Saeed umefadhaika? Nikasema ndiyo ewe mwana wa Mjumbe wa Mungu! Akasema hii ni tasbihi tukufu amenihadithia baba yangu kutoka kwa babu yangu mjumbe wa Mungu(s.a.w.w) dhambi haitobaki pamoja na tasbihi hii, kwamba mungu umetukuka utukufu wake alipomuumba Jibrail alimfundisha tasbihi hii nayo ni jina kubwa la Mungu.

DU'A NA KUMADHIM KWAKE

Sifa njema ni za Allah ambaye amejitokeza nyoyoni kwa utukufu. Na amejificha kando na macho kwa nguvu akajiwezesha juu ya vitu kwa uwezo macho hayathubutu kumwona, wala mawazo hayafikii kiini cha utukufu wake. Ameonyesha nguvu zake na ukubwa amejizinga nguvu wema, na utukufu na amejitakasa kwa wema na uzuri. Ametukuka kwa fahari na uzuri. Amejitanda utukufu na neema. Amejichagulia nuru na mwanga. Muumbaji asiye na kifani pekee hana mpinzani, kimbilio la milele halingani mungu hana wa pili pamoja naye. Mwanzilishi hana mshirika, mtowa rizki hana msaidizi. Wa kwanza bila ya kutoweka wadaima bila kutoweka. Msimamizi bila taabu, mtowa amani bila mwisho, mwanzilishi bila muda, mtengenezaji bila ya kitu, bwana mwenye bila mshirika, muumbaji bila ya takalifu, mtekelezaji bila ya ajizi hana mpaka wa mahali, hana upeo katika zama, alikuwapo, yupo, ataendelea kuwa yupo kama alivyo, bila kikomo. Yeye ni Allah yu hai mwenye kujisimamia wa daima wa tangu, muweza mwenye busara, mungu wangu mbele yako watetemeka watetemekaji wa chaji. Na kwako wamekuwa na ikhlasi waliaji wakikuogopa na wakitarajia msamaha wako ewe Mungu wa haki. Ihurumiye DU'A ya waliowakiomba msaada, samehe dhambi za walioghafilika, zidisha ihisani za warejeao siku ya kuja kwako Oh mkarim.

DU'A ZAKE KATIKA KUWATAJA ALI WA MUHAMMAD(A.S)

Oh Allah ambaye umemteuwa Muhammad na Ali wake kwa heshima na kuwapendelea kwa risala na kuwachagua makhsusi kwa uombezi na kuwafanya kuwa ni mawarithi wa Manabiy na kwao ndio umehitimishwa uwasii na Maimamu na amewafundisha elimu ya mambo yaliyokuwa na yanayoendelea, na kuzifanya nyoyo za watu zielemee kwao mrehemu Muhammad na Ali zake waliotahirika tufanyiye yale ambayo wewe ni mwenye kustahiki katika dini na dunia na akhera, hakika wewe ni muweza wa kila kitu.

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE KATIKA KUMTAKIA REHMA ADAM(A.S)

Oh Allah Adamu ni shani ya maumbile yako, wa kwanza kuumbwa kutokana na udongo mwenye kutambua ubwana wako, mwanzo wa haja yako kwa waja wako na viumbe wako, na dalili ya kuomba hifadhi ya msamaha wa adhabu yako, na ni mfunguzi wa njia za toba yako, na ni wasila kati ya viumbe na kukujuwa wewe na ambaye umemfikishia uliyoyaridhia kwake kwa huruma yako kwake na rehema zako, ni mwenye kurejea kwako ambaye hakung'ng'ania kukuasi, mtangulizi wa wajidhalilishao kwa kunyoa kichwa chake katika haram yako, mwenye kutafuta wasila baada ya uasi kukutii ili aufikiye msamaha wako, baba wa Manabiy ambaye ambao wameudhiwa kwa ajili yako, ambaye amepambana sana kati ya wakazi wa ardhini katika kukutii. Hivyo mrehemu Oh we mwingi wa rehema na malaika wako na wakazi wa mbingu zako na ardhi yako, kama alivoadhimisha amri zako zisizoweza vurugwa, ametujulisha sisi njia za ridha zako Oh we mwingi wa rehema miongoni mwa wenye kurehemu.

MIONGONI MWA DU'A ZAKE KATIKA USUMBUFU NA KUOMBA FARAJA

Oh Mola wangu usimwache adui wangu anisimange, wala usimuumize mpenzi na rafiki yangu kupitia mimi. Mola wangu nipe mtazamo miongoni mwa mitazamo yako uniondolee humo uliyonisibu nayo. Ili unirudishe kwenye kawaida yako iliyo nzuri zaidi kwangu, nikubalie maombi yangu na maombi ya ambaye mwenye ikhilasi kwako ombi lake.Hakika nguvu zangu zimedhoofika werevu wangu ni mdogo, hali yangu imekuwa mbaya, nimekata tamaa na yaliyo kwa viumbe wako hakuna lililobaki kwangu isipokuwa kukutumainia wewe. Oh Mola wangu, hakika uwezo wako wa kuniondolea nilionayo ni kama uwezo wako juu ya yaliyonisibu, hakika kukumbuka mazuri yako kwangu kwanipa raha, na kutumainia fadhila zako na neema zako kwanipa nguvu, kwa sababu sijapata kuwa bila ya neema zako toka ulivoniumba, wewe ndio Mungu wangu ndio kimbilio langu ngome yangu, muhifadi wangu mlinzi wangu, mwenye upendo kwangu, mwenye rehema kwangu, mlinzi wa rizki yangu. Katika amri yako imekuwa yaliyo halali kwangu, kwa elimu yako ndiyo nilivyojaalia ee bwana wangu Sayyidi wangu ulichokikadiria na kuamuwa kwa ajili yangu, ulichokifanya hapana budi, kwa hali njema yangu ambacho ndani yake kuna manufaa yangu na kupata faraja kwa kuepukana na niliyo nayo. Mimi simtarajii yeyote kuzuwia hilo asiyekuwa wewe, simtegemei kwa hilo isipokuwa kwako basi ewe mwenye utukufu na heshima kuwa kwenye dhana yangu nzuri mno kwako.

Uhurumie udhaifu wangu na uchache wa werevu wangu, niondolee shida zangu, nikubaliye maombi yangu, niokowe toka kwenye kujikwaa kwangu, nionyeshe huruma kwa hilo na kila mwenye kukuomba, umeniamuru ewe bwana wangu kuomba na ulijipa jukumu la kuikubali ahadi yako ni thabiti haikhalifu wala kubadilika. Hivyo basi mrehemu Muhammad Nabiy wako na mja wako, na waliotahirika katika Ahli-Bayt wake. Nisaidie kwa kuwa wewe ni msaada kwa asiyekuwa na msaada na ngome kwa asiyekuwa na hifadhi. Nami ni mwenye dhiki ambaye umewajibisha kumjibu na kumwondolea aliyo nayo miongoni mwa maovu. Nijibu niondolee huzuni yangu irejeshe hali yangu kwenye ubora zaidi kuliko ilivyokuwa. Usinilipe kama ninavostahiki lakini nilipe kwa kulingana na rehema zako ambazo zimeenea juu ya kila kitu, ewe mwenye utukufu na heshima mrehemu Muhammad na Ali wa Muhammad sikiliza na ujibu owe mwenye enzi.

DU'A ZAKE A.S. KWA AYAHOFIAYO NA KUYAOGOPA

Oh Mola wangu hakuna liwezalo kuziwiya ghadhabu zako isipokuwa huruma zako, wala liokowalo toka kwenye adhabu yako isipokuwa msamaha wako. Hakuna liwezalo kuokowa kutoka kwako isipokuwa rehma zako na kunyenyekea kwako. Hivyo basi nipe ewe Mola wangu faraja kwa nguvu ambazo kwazo wahuisha mauti wa nchi na kwayo wazifufuwa roho za waja, wala usiniangamize na unipe maarifa ya jibu. Ewe Mola wangu niinuwe usinirudishe chini, nisaidie nipe rizki, ewe Mola wangu, ukiniinuwa nani atanirudisha chini, ukinirudisha chini nani ataniinuwa? Nimejuwa ewe Mola wangu katika hukumu yako hakuna dhuluma wala hapana haraka katika malipizi yako. Afanyaye haraka yule ahofiaye kukosa na aihitajiaye dhulma ambaye ni dhaifu, nawe uko juu kabisa mbali na hayo ewe bwana wangu. Mola wangu usinifanye kuwa lengo la shabaha ya balaa wala nisiwe ndio kiguzo cha malipizi yako, nipe muhula nipe raha, niokowe toka kwenye kujikwaa kwangu usinifuatilie kwa balaa baada ya balaa. Umeona udhaifu wangu na uchache wawerevu wangu, nipe uvumilivu kwa hakika mimi ni dhaifu nanyenyekea kwako ewe Mola wangu, ninajikinga kwako kutoka kwako basi nipe kinga. Naomba hifadhi kwako kutokana na kila balaa nipe kimbilio, najisitiri na wewe nipe sitara ewe bwana wangu na ambayo nayaogopa na kujihadhari nayo, wewe ni mtukufu mno u mtukufu kuliko kila kitukufu, bika bika bika nimejisitir ya Allah yaa Allah ya Allah (kariri hiyo mara kumi) Mrehemu Muhammad na Ali zake wataharifu.

MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA KUJIDHALILISHA

Mola wangu Mola wangu, wewe ni Mola na mimi ni mja yeyote amrehemu mja! Ni Mola tu Mola wangu Mola wangu, wewe u mtukufu namimi ni dhalili, yeyote amuhurumia dhalili ni mwenye utukufu tu. Mola wangu Mola wangu, wewe ni muumba na mimi ni kiumbe amuhurumia kiumbe ni muumba tu, Mola wangu Mola wangu, wewe ndio mpaji na mimi ni mwombaji, anayemuhurumia mwombaji ni mpaji tu. Mola wangu Mola wangu, wewe ni msaidiaji na mimi nimtaka msaada, anayemuhurumia mtaka msaada ni msaidiaji tu. Mola wangu Mola wangu, wewe ni mwenye kubakia na mimi ni mwenye kuhiliki, anayemrehemu mwenye kuhiliki ni mwenye kubaki tu. Mola wangu Mola wangu, wewe ni wa daima na mimi ni wakutoweka, anamrehemu mwenye kutoweka isipokuwa ni wa daima. Mola wangu Mola wangu, wewe u hai na mimi ni mayiti, anayemrehemu mayiti isipokuwa aliyehai. Mola wangu Mola wangu, wewe ni mwenye nguvu na mimi ni dhaifu amrehemu dhaifu isipokuwa mwenye nguvu, Mola wangu Mola wangu, wewe ni tajiri na mimi ni miskini anayemuhurumia miskini isipokuwa tajiri. Mola wangu Mola wangu, wewe ni mkubwa na mimi ni mdogo, anamrehemu mdogo isipokuwa mkubwa. Mola wangu Mola wangu, wewe ni mwenye kumiliki na mimi ni mwenye kumilikiwa, amuhurumiaye mmilikiwa ni mmiliki tu.

DU'A ZAKE SIKU YA JUMAPILI

Kwa Jina la Mwenjzi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenje Kurehemu. Kwa jina la Allah ambaye siitarajii isipokuwa fadhila zake. Wala siogopi isipokuwa uadilifu wake, sitegemei isipokuwa kauli yake sishikamani isipokuwa na kamba yake. Kwako naomba hifadhi , Oh mwenye msamaha na ridhaa kutokana na dhulma na uaduwi na kutokana na mabadiliko ya zama na kurudia rudia kwa huzuni na kutokana na pigo la matokeo mabaya nakwisha kwa muda kabla ya maandalizi na utayarifu. Kwako tunaomba mwongozo kwa ambayo ndani yake kuna wema na marekebisho, kwako naomba msaada wa ambalo lina mafungamano na mafanikio na jibu muwafaka, na kwako tunaloendea vazi la hali njema na ukamilifu wake na kuenea kwa amani na kudumu kwake. Ninajikinga kwako Oh Mola wangu na shinikizo la shetani, na ninaomba ulinzi kwa mamlaka yako na dhulma ya watawala, hivyo basi zikubali sala zangu zilizopita na swaumu yangu, na ijaaliye siku yangu ya kesho na ya baadaye iwe bora kuliko saa yangu hii na siku yangu, nienzi mimi katika ukoo wangu na kaumu yangu, ni hifadhi nikiwa macho na nikiwa nimelala. Wewe ni Allah muhifadhi bora na wewe ni mwingi mno wa rehma kuliko wote wenye kurehemu Oh Allah hakika mimi nina uhama ushirikina na kufuru, katika siku yangu hii na baada yake miongoni mwa siku za jumapili ninakuomba kwa unyofu kabisa ili nipate jibiwa, mrehemu Muhammad na Ali wa Muhammad, viumbe wako bora mwitaji wa kwenye ukweli wako, nitukuze kwa utukuzo wako ambao haudhuriwi, nihifadhi kwa jicho lako ambalo halilali, hitimisha mambo yangu kwa kujikata na mengine yoote isipokuwa kwako nahitimisha maisha yangu kwa ghofira hakika wewe ndio mghofiri mwingi wa huruma.

DU'A YAKE YA SIKU YA JUMATATU

Kwa Jina la Mwenjezi Mungu, Mwingi wa Kehema Mwenye Kurehemu. Hakumruhusu yeyote kushuhudia alipoziumba mbingu na ardhi, wala hakumchukuwa msaidizi alipoziumba nafsi, hakushirikisha katika uungu wala hakukusaidiwa katika umoja, ndimi ziko butu kufikia kikomo cha sifa yake. Akili zimeshindwa kumtambuwa yeye, wadhalimu wamenyenyekea kwa kumwogopa yeye, nyuso zimenyenyekea kwa kumwogopa kila mtukufu ametii utukufu wake (Mungu). Wako ni utukufu tena na tena wenye uwiano mfululizo kwa utaratibu ziwe baraka zake kwa mjumbe wake milele. Na amani yake ya daima bila mwisho Oh Allah jaalia mwanzo wa siku yangu hii iwe njema na kati yake iwe ya ufanisi. Mwisho wake uwe wa mafanikio na ninajikinga kwako na siku mwanzo wake ni hofu na katikati yake ni mashaka na mwisho wake maumivu Oh Allah kwa hakika mimi nakuomba msamaha kwa kila nadhiri nimeifanya na kila ahadi nimeiahidi kisha sikuitekeleza kwa ajili yako. Na ninakuomba kuhusu malalamiko ya waja wako kwangu hivyo basi mja yeyote katika watumwa wako au mjakazi miongoni mwa vijakazi wako alikuwa na malalmiko dhidi yangu nimemtendea vibaya yeye mwenyewe au katika heshima yake au katika mali yake, au katika ahli wake au mtoto wake au nimemsengenya au kumsingizia kwa kuelemea upande fulani dhidi yake au utashi wa moyo wivu, kujionyesha au upendeleo awe yupo hayo yakitendeka au hayupo, akiwa hai au amekufa. Kwa namna ambayo mkono wangu ulishindwa au sikuwa na wasaa wa kumrudishia na kujitowa kuwa dhidi yake. Nakuomba ewe mwenye kumiliki haja nazo hutolewa kwa utashi wake na ziko haraka kwenye irada yake, umrehemu Muhammad na Ali wa Muhammad, umridhishe kwa ajili yangu upendavyo nipe rehema kutoka kwako hakika yeye hapungukiwi kwa kughofiri kutoa hakumdhuru. Ewe mwingi wa rehema miongoni mwa wenye kurehemu. Oh Allah nipe mimi kila siku ya jumatatu neema mbili kutoka kwako, heri mwanzoni mwake kwa kukutii wewe na neema mwishoni mwake kwa msamaha wako, Oh ambaye ndiyo Allah. Haghofiri dhambi asiyekuwa yeye.


12

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

DU'A YAKE SIKU YA JUMANNE

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Sifa njema ni zake Allah na himidi ni haki yake kama anavyostahiki himidi nyingi, na ninajikinga na yeye na shari ya nafsi yangu (Innan-nafsa-la-ammaratun bis-suuin illaa ma rahima rabiy) (12:53)

Hakika nafsi ni yenye kuamrisha uovu isipokuwa Mungu wangu akiirehemu.

Na ninajikinga naye (Mungu) na shari ya shetani ambaye huniongezea dhambi kwenye dhambi zangu. Naomba ulinzi kwake dhidi ya kila fedhuli muovu, na mtawala dhalimu na aduwi mwenye mabavu. Oh Allah nifanye kuwa miongoni mwa askari wako kwa sababu askari wako ndio washindi, nifanye niwe kwenye kundi lako kwa sababu kundi lako ndilo lenye ufanisi, nifanye miongoni mwa Mawaliy wako kwa sababu Mawaliy wako hawatokuwa na hofu wala hawatohuzunika.

Oh Allah niwekee sawa dini yangu kwa sababu ndio hifadhi ya mambo yangu, niwekee sawa ahera yangu kwa kuwa ndio nyumba ya makazi yangu ya kudumu, na ndio kimbilio langu la kuwa jirani na waovu. Ujaaliye uhai uwe ndio zidisho langu la kila kheri, na kifo kiwe raha kwangu kwa kuepukana na kila shari. Oh Allah mrehemu Muhammad na khaataman Nabiyyin na ambaye timizo la idadi ya wajumbe. Na warehemu Aali wake wema walio tahirishwa. Na sahaba wake wateule. Nipe mimi siku ya jumanne mambo matatu: Usiniachie dhambi ila iwe umeisamehe, wala mayonzi ila uwe umeyaondowa, wala adui ila uwe umemsukuma nyuma. Kwa jina la Allah ni jina bora miongoni mwa majina Bismillahi bwana wa ardhi na mbingu najikinga na kila makuruhi mwanzo wake kasiriko lake, na ninaleta kila lipendwalo mwanzo wake ridhaa yake, ni hitimishiye kwa msamaha toka kwako ewe muhisani.

DU'A YAKE SIKU YA JUMATANO

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Kehema Mwenye Kurehemu. Sifa njema ni zake Allah ambaye ameujaalia usiku kuwa ni vazi, na usingizi kuwa ni pumziko. Na ameujaalia mchana kuwa wakati wa kuinuka. Sifa njema ni yako umeniinuwa toka usingizini mwangu. Lau ungependa ungejaalia wa milele. Sifa njema daima haikatiki, idadi yake viumbe hawaiwezi. Oh Allah! zako ni sifa njema kwa kuwa umeumba na ukakadiria. Ulikadiria na kuamuru, umeweka umauti na uhai, umeuguza na umeponya, umetowa afya na umeweka balaa, umetawalia kitanda cha enzi, ufalme ukauzingira, nakuomba ombi la ambaye uombezi wake umedhoofika, ujanja wake umekatika, muda wake umekurubia, matumaini yake duniani yamenywea, mahitaji yake ya rehma zako yameshika kasi, majuto yake kwa kupuuza kwake yamekuwa makubwa, kuteleza kwake na kujikwaa kumezidi, toba yake kwa ajili ya uso wako imekuwa nyofu, mrehemu Muhammad hitimisho la manabiy na warehemu watu wa nyumbani mwake wazuri waliotahirishwa, nitunukiye uombezi wa Muhammad. Oh Allah mbariki yeye na Ali zake, usininyime kuwa pamoja naye, kwa hakika wewe ni mwingi mno wa kurehemu katika wanao rahemu. Oh Allah niamuliye siku ya jumatano mambo manne: Ijaaliye nguvu yangu katika utii wako, na furaha yangu iwe katika ibada yako, upendo wangu uwe katika thawabu zako, kujiepusha kwangu kuwe katika ambalo linawajibisha kwa ajili yangu maumivu ya adhabu yako, kwa hakika umpole kwa umpendaye.

DU'A YAKE SIKU YA ALHAMISI

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Kehema Mwenye Kurehemu Sifa njema ni za Allah ambaye ameuondowa usiku wenye giza kwa uwezo wake, na ameleta mchana wenye mwanga kwa rehma yake, amenivisha mimi mwanga wake na amenipa neema za (mchana). Oh Allah kama ulivyonibakisha kwa huo mchana nibakishe kwa mfano wake. (mchana mwingine). Mrehemu Nabiy Mohammad na Ali zake usinipe mahangaiko humo na katika usiku mingine na mchana kwa kufanya yaliyoharamu na kutenda dhambi, niruzuku kheri zake na kheri zilizomo humo na kheri ya baadaye. Niondolee shari yake na shari iliyomo humo na shari ya baada yake. Oh Allah hakika mimi kwa hifadhi ya Uislam naomba wasila wa kuelekea kwako. Na kwa heshima ya Qur'an isiodhurika nakutegemea. Na kwa Muhammad mteule rehema za Allah zimfikie yeye na Ali zake naomba shafaa kwako. Tambuwa Oh Allah! dhimma yangu ambayo nimeitarajia kukidhi haja zangu. Ewe mwenye rehma nyingi kuliko wote wenye kurehemu. Oh Allah nikidhiye katika siku ya Al-hamisi matano hakuna wasaa kwayo isipokuwa ukarimu wako. Hakuna aya wezae isipokuwa neema zako; usalama unipe nguvu kwa ajili ya utii wako. Ibada ilinistahiki kwa ajili yake wingi wa thawabu zako. Hali ya wasaa kutokana na riziki ya halali. Uniweke katika amani mahali tuwa hofu kwa amani yako. Niweke katika ngome yako dhidi ya mahangaiko na mayonzi, mrehemu Muhammad na Ali wake jaalia wasila wangu kupitia yeye wenye mafanikio siku ya kiyama yenye manufaa kwa hakika wewe ni mwenye huruma zaidi miongoni mwa wenye huruma.

DU'A YAKE SIKU YA IJUMAA

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mnringi 'wa Kehema Mwenje Kurehemu. Sifa njema ni zake Allah wa kwanza kabla ya kuumba na kutoa uhai, wa mwisho baada ya kwisha vitu, mjuzi wa yote ambaye hamsahau mwenye kumkumbuka. Hampunguzi anayemshukuru haachi kumtekelezea amwombaye hakati matumaini ya mwenye kumtumainia. Oh Allah mimi nakuomba ushuhudiye nawe ni shahidi tosha na nawaomba washuhudie malaika wako wote na wakazi wa mbungu zako nawabeba arshi yako na uliowatuma miongoni mwa Manabiy wako na Mitume wako na uliowaumba miongoni mwa sampuli za viumbe wako. Kwamba mimi nashuhudia kuwa hakika wewe ni Allah hapana miungu isipokuwa wewe peke yako huna mshirika wa kulingana. Halishindwi neno lako wala kubadilika na hakika Muhammad ni rehema na amani zimfikie yeye na Ali zake ni mtumwa wako na mjumbe wako. Ametekeleza amefikisha ulilo mtuma kwa waja na amefanya juhudi kwa ajili ya Mungu aliye mtukufu juhudi ya haki na kwamba yeye alibashiri ambayo ni haki miongoni mwa thawabu na ameonnya ambayo ni kweli miongoni mwa adhabu. Oh Allah niimarishe katika dini yako pindi unibakishapo hai, usiupotoshe moyo wangu baada ya kuwa umeniongoza nipe rehema kutoka kwako hakika wewe ni mtowaji sana mrehemu Muhammad na Ali wa Muhammad nifanye mimi niwe miongoni mwa wafuasi wake na Shia wake, nikusanye mimi katika kundi lake ni wafikishe kutekeleza faridha ya Ijumaa zote, na uliyowajibisha humo kwangu miongoni mwa utii, na umegawa kwa watu wake chakutowa siku ya malipo, hakika wewe ni mwenye nguvu mwenye hekima.

DU'A YAKE SIKU YA JUMAMOSI

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Bismillaahi ni neno la wenye kushikamana kwake. Na niusemi wa watakao ulinzi kwake, najikinga kwa Mungu mtukufu na jeuri ya wajeuri na vitimbi vya mahasidi na uchokozi wa madhalimu na ninamuhimidi zaidi ya himidi ya wenye kumuhimidi. Oh Allah wewe ni mmoja bila mshirika na u mfalme bila kutawazwa. Hupingwi katika hukumu yako hushindwi katika ufalme wako nakuomba umrehemu Muhammadi na Ali zake mtumwa wako na mtume wako, niongoze kushukuru neema zako (shukrani) itakayo nifikisha upeo wa ridhaa zako, unisaidie kukutii wewe na kujilazimisha ibada yako ili nistahiki thawabu zako kwa huruma ya uangalizi wako. Nihurumiye na uniziwiye maasi yako kwa kadiri uniwekapo hai, uniwafikishe linaloninufaisha kadiri unibakishapo. Kipanuwe kifua changu kwa kitabu chako, punguza kwa kukisoma kwake mzigo wangu wa dhambi. Nitunukiye salama katika dini yangu na nafsi yangu usinifarakishe na wapenzi wangu timiliza ihisani yako katika umri wangu uliobaki. Kama ulivyofanya ihisani katika umri wangu uliyopita, Oh wee mwenye huruma nyingi kuliko wote wenye huruma.

MNONG'ONO WA IBADA YA WENYE KUJUTA

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Oh Mungu wangu makosa yamenivika nguo ya udhalili wangu, kuwa mbali na wewe kumenifunika vazi la huzuni yangu kuu. Dhambi yangu kubwa imefisha moyo wangu, hivyo basi uhuishe kwa kutubu kwako. Oh we tumaini langu na lengo langu. Oh we ndio utashi wangu na hitajio langu. Kwa uwezo wako, simpati wakusamehe dhambi zangu ambaye si wewe, simwoni yeyote wakuganga vunjiko langu ambaye si wewe. Nimenyenyekea kwa kurejea kwako, nimenyongeka kwa kujiweka chini kwako. Ikiwa utanifukuza toka mlangonni kwako ni kwa nani nitapata kimbilio! Ukinirudisha nyuma toka upande wako ni kwa nani nitajikinga. Huzuni iliyoje kwa kuaibika kwangu na kufedheheka. Oh wee huzuni ni yangu kutokana na matendo yangu maovu na yale niliyoyatenda. Nakuomba ewe mwenye kughofiria dhambi kubwa.

Oh wee mwenye kuganga mfupa uliovunjika, yafumbiye macho matendo yangu yaangamizayo. Na unisitiri siri zangu za kufedhehesha, usinitowe siku ya ushuhuda wa kiyama toka kwenye baridi ya msamaha wako na ghofira yako. Yapeleke mawingu ya msamaha wako juu ya aibu yangu. Mola wangu, harejei mtumwa aliyekimbia isipokuwa kwa bwana wake. Je yeyote aweza kumpa kimbilio toka makasiriko yake asiyekuwa yeye. Mola wangu! Ikiwa kujuta kwa ajili ya dhambi ni toba hakika mimi naapa kwa uwezo wako ni miongoni mwa wajutao. Ikiwa kuomba ghofira kutokana na makosa ni kupunguza, hakika mimi ni mwenye kuomba ghofira kwako, kwako narejea ili uridhike. Oh Mungu wangu kwa uwezo wako juu yangu nikubalie toba yangu. Kwa huruma yako kwangu nisamehe na kwa kunijuwa kwako mimi nifanyiye upole. Mola wangu wewe ndiye ambaye umefunguwa mlango wa msamaha wako kwa waja wako umeuita toba ukasema (tubuni kwa Allah toba ilioimara) ni udhuru gani atakuwa nao mwenye kughafilika kuingia mlango ule baada ya kufunguliwa kwake! Mola wangu! Ikiwa dhambi iko mbaya toka kwa mtumwa wako, msamaha uwe mwema kutoka kwako. Mola wangu mimi si wa kwanza kukuasi ulimkubalia toba yake au aliyejitahidi kutaka mema yako ulimfadhili. Oh we mwenye kumjibu aliye dharurika. Oh we mwenye kuondowa dhara. Oh we mkubwa wa mema. Oh we mjuzi wa yaliyo siri. Oh wee mzuri waa kusitiri! Ninaomba kwako shifaa kwa ukarimu wako na upaji wako. Naomba kwa upande wako na huruma yako nikubalie Du'a yangu kwako usininyime kufanikiwa kwako matumaini yangu. Nikubalie toba yangu. Nifichie makosa yangu kwa huruma yako. na rehema zako ewee mwingi wa kurehemu miongoni mwa wenye kurehemu.

NONG'ONO LA SALA YA MNUNG'UNIKAJI

Kwa Jina la Mwenyezi Mwingi wa Rehema Mwenje Kurehemu. Mola wangu nanung'unika kwako nafsi yenye kuamrisha maovu, yenye kuharakia kwenye makosa inabidii kwenye maasi yako, ikijiweka kwenye hatari ya kasiriko lako, yaipeleka mapito ya kuhilikisha yanifanya mimi mbele yako mwenye kuhiliki rahisi kabisa nyudhuru nyingi. Ikiwa na matumaini marefu, ikiguswa na shari yafadhaika na endapo itaguswa na kheri yazuiya yenye kuelemea sana kwenye mchezo na upuuzi. Imejawa na mghafala na kusahau yaniharakishia kwenye matendo yasiyotakiwa. Yanifanya nichelewe kutubu. Mola wangu nanung'unika kwako adui anipoteza na shetani anipotosha. Amekijaza wasi wasi kifuwa changu ushauri wake umejaa moyo wangu anaunga mkono upuuzi dhidi yangu. Yanipambia kuipenda dunia yazuia kati yangu na utii na ukaribu. Mola wangu kwako nanung'unika moyo mgumu wageuka pamoja na wasi wasi imejivisha kutu na kupigwa muhuri na jicho lisilo lia kwa hofu yako na kwa mambo yanayolifurahisha lina tamaa nayo. Mola wangu, hapana hila wala nguvu ila kwa nguvu zako, wala sina uwokozi kutokana na makuruhi ya dunia ila kwa hifadhi yako kwa hiyo nakuomba kwa umbali unaofikia hekima zako na upenyo wa utashi wako, usiniache nijitose kusiko kuwa na upaji wako, usinifanye nijiingize kwenye fitna kuwa mwenye kunisaidia dhidi ya maadui na mwenye kunisitiri kwenye fedhea na aibu. Na mlinzi kwenye balaa na mhifadhi kwenye maasi kwa huruma yako na rehema zako.

NONG'ONO LA SALA YA MWENYE HOFU

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Mola wangu, waona baada ya kuamini utaniadhibu! Au baada ya upendo wangu kwako utanifurusha. Au pamoja na matumaini yangu rehema zako na msamaha wako uninyime utanitupa pamoja na kukuomba kwangu saana hifadhi. Vipi uso wako mkarimu unifanyie kinyume na matumaini lau ningejua ni kwa ajili ya balaa na udhalili mama yangu amenizaa. Au ili nitaabike amenilea, ni afadhali basi asingenizaa wala asingenilea, afadhali ningejua umenijaalia kuwa miongoni mwa watu wa heri na umenichagua kuwa miongoni mwa wa karibu wako. Ili lifurahiwe kwa hilo jicho langu, na kwalo nafsi yangu iwe na utulivu Mungu wangu, hivi utaziweusisha nyuso ziliporomoka chini zikisujudu kwa utukufu wako, au utazifanya bubu ndimi zilitamka sifa za utukufu wako na enzi yako, au utazipiga muhuri nyoyo ndanimwe mulikuwa na upendo wako, au utayafanya kiziwi masikio yaliona ladha kusikia utajo wako kwa utashi wako, au utaifunga pingu mikono ambayo matumaini yameinyanyuwa kwako ikitazamia huruma yako au utaiadhibu miili imekonda katika juhudi kukutii wewe, au utaiadhibu miguu imefanya bidii katika ibada yako. Oh Mola wangu usimfungie mlango wa rehema zako akupwekeshaye. Usiwazuiye wenye shauku nawe kuangalia uzuri wa mtazamo wako. Mola wangu nafsi uliyoienzi kwa kunena tawhidi yako vipi utaidhalilisha kwa twezo kuiacha kwako. Dhamira imejifunga kwa mapenzi yako vipi utaiunguza kwa joto la moto wako. Mola wangu, nikinge na ukali wa ghadhabu zako na kasiriko lako kubwa, Oh mpendwa Oh mwenye huruma Oh mpole Oh mwenye huruma, Oh jabbar Oh mshindi, ewe msamehevu Oh msitiri, kwa rehema yako niokowe tokana na adhabu ya moto na fedheha ya aibu wajitengapo watu wema kando na washari. Na zibadilikapo sura hali ya kutisha itakapo chukuwa nafasi, wema watakapoletwa karibu waovu wawekwapo mbali (na kila nafsi zitapopewa yoote iliyo ikiyafanya wao hawato dhulumiwa).

NONG'ONO LA SALA YA WENYE MATUMAINI

Kwa Jina la Mwenyezi Mwingi wa Kehema Mwenye Kurehemu. Oh ambaye mja wake amwombapo humpa, akiyatumainia aliyo nayo humpa utashi wake. Akimsogelea humkurubisha na kumleta karibu, akimdhihirishia maasi humsitiri dhambi zake na huifunika, akimtegemea humtosheleza. Mola wangu nani afikaye kwako akiomba takrima yako na usimkarimu, nani ateremkiaye mlangoni kwako akitarajia wema wako na usimwonyeshe, je ni vizuri nirejee toka mlangoni kwako hali nimeondolewa bila ya matarajio yangu nami simjuwi bwana mfadhili mwenye kusifika kwa hisani asiyekuwa wewe. Vipi nimtarajiye asiyekuwa wewe hali yakuwa heri zote ziko mikononi mwako. Vipi nimtumainiye mwingine hali kuumba na amri ni vyako, vipi nitumai wengine.

Nikate matarajio yangu kwako hali ya kuwa umenionyesha ukarimu wako kwa ambalo sikuliomba katika fadhila zako je utanifanya niwe muhitaji kwa aliye mfano wangu, hali nikishikamana na kamba yako! Oh yule ambaye wamekuwa na maisha ya furaha kwa rehema zake wenye juhudi, wala hawakuwa duni kwa kisasi chake waomba ghofira, vipi nikusahau hali ungali wanikumbuka. Vipi nitageuzwa mtazamo mbali na wewe hali wewe wanichunga. Mola wangu kwenye pindo la ukarimu wako nimeangika mkono wangu ili kukifikia ukitowacho nimenyosha matumaini yangu, unipe safi Ikh'laasi kwa kunena tawheed yako, nijaaliye niwe miongoni mwa waja wako wateule. Oh ambaye kila akimbiaye kuelekea kwake hupata kimbilio, ni tumaini la kila mtafutaji, ewe mbora wa atarajiwaye, ewee mkarimu mno wa wenye kuombwa, ewe ambaye hamkatalii mwombaji wake wala hamsitukizi kwa kutomtekelezea amtumainiaye. Oh wee ambaye mlango wake uwazi kwa mwombaji wake, pazia yake imenyanyuliwa kwa mwenye matumaini kwake. Nakuomba kwa ukarimu wako unionyeshe huruma kwa bakshishi yako iwezayo kutuliza jicho langu. Na kwa kukutarajia wewe ambako kutaipa nafsi yangu utulivu, na kwa yakini ambayo itanifanyia wepesi misiba ya dunia, na kuniondolea kifuniko cha upofu toka kwenye ufahamu wangu. Kwa huruma yako ewe mwenye huruma zaidi ya wote wenye kuhurumia.

NONG'ONO LA WENYE KUSIHI SANA

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Mola wangu ikiwa masurufu yangu ni madogo katika msafara wangu kuelekea kwako, basi dhana yangu imekuwa nzuri kwa kutawakali kwako. Ingawaje dhambi zangu zimenihofisha adhabu yako matumaini yangu yamenitambulisha kuwa nitakuwa katika amani bila malipizi yako. Ingawa dhambi zangu zimenichongea kwenye adhabu yako uzuri wa imani yangu umenipasha khabari ya kupata thawabu yako. Ingawaje mghafala umenilaza nisiandae kukutana na wewe maarifa yamenizindu'a kwa ukarimu wako na neema zako japokuwa kutotii na maasi yaliyo kithiri kumefarikisha kati yangu na wewe, bishara ya msamaha na ridhaa zimenifurahisha na kunifanya nihisi ni karibu. Nakuomba kwa fahari ya uso wako na kwa nuru za utukufu wako, nakuomba sana kwa upole wa huruma yako na raufu ya wema wako nithibitishiye dhana yangu ninayoyatumainia, katika wingi wa takrima yako.

Na uzuri wa neema zako kwa ukaribu na wewe na ujirani kwako napendezwa na kukutazama wewe. Mimi ni hapa! Nimejiweka kwenye kibaridi cha upya wako na huruma yako. Nataka msaada wa mvuwa ya ukarimu wako na huruma yako, nikikimbia toka kwenye kasiriko lako kuelekea ridhaa zako. Nakimbia kutoka kwako nikielekea kwako nikitumai kizuri mno kilicho kwako nikitegemea matunzo yako, muhitaji wa uangalizi wako. Mola wangu, fadhila zako ulizozianza zitimize fadhila zako ulizo nitunukia, usiziondowe na ambalo umenisitiri usinifichuwe nalo, ambalo umelijuwa mionngoni mwa matendo yangu mabaya ni ghofiriye. Oh Mola wangu, naomba mwombezi kwako kwa ajili yako ninaomba hifadhi kuja kwako kutoka kwako nimekuja kwako, nikitumai hisani yako, nikitaka wema wako, nikiomba maji ya mvuwa ya fadhila zako, nikiomba mawingu ya mvuwa za fadhila zako, nikiomba ridhaa zako, nikija upande wako, nikija mahali patekwapo maji ya msaada wako, nikiomba mema ya hali ya juu kutoka kwako. Naja kwenye hadhara ya uzuri wako nikitaka uso wako, nikigonga mlango wako, nikijidhalilisha mbele ya utukufu wako na adhama yako. Nifanyie ghofira na huruma ambazo wastahiki, wala usinifanyie ambayo mimi nastahiki miongoni mwa adhabu na malipizi, kwa huruma yako ewe mwenye huruma mno kuliko woote wenye huruma.


13

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

MNONG'ONO WA SALA ZA WENYE KUSHUKURU

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Kehema Mwenye Kurehemu. Mola wangu umenisahaulisha kukushukuru mfululizo wa umbuji wako wingi wa fadhila zako umenifanya nishindwe kuhesabu sifa zako, mtiririko wa mema yako kwangu umenishughulisha nisitaje sifa njema zako. Mfululizo wa nufaisho lako kwangu kumenishindisha kutangaza fadhila zako, hiki ni kituo cha aliyetambua wingi wa neema na akazikabili kwa uzembe ameshuhudia dhidi yake mwenye kutojali na kuzembea, wewe ndio mwenye huruma na mpole, mwema mkarimu, ambaye amvunji moyo amwendeaye. Wala hamfukuzi toka ukumbi wake amtumainiaye, uwanjani kwako kwaishia misafara ya wenye matumaini katika kituo cha uwanjani mwako husimama matumaini ya waomba msaada, usiyakabili matumaini yetu kwa kutotekelezewa na kukatishwa tamaa.

Shukurani zangu zimekuwa ndogo mbele ya ukubwa wa ufadhili wako, himidi yangu na tangazo langu zimenywea mbele ya takrima yako kwangu, neema zako zimenifunika mavazi ya nuru ya iymani, umakii wa wema wako umenifunika pazia la kupendeza. Wema wako umenivika mkufu ambao hauto vulika na umenivika tepe ambazo hazito vunjika, fadhila zako chungu tele ulimi wangu umedhoofika kuzihesabu, neema zako nyingi fahamu zangu zimeshindwa kuzifahamu sembuse kuzitafiti. Hivyo basi vipi nitafanikiwa kushukuru hali yakuwa shukrani yangu kwako yahitaji ishukuriwe kila nikwambiapo Al-hamdulillahi itakuwa wajibu juu yangu nikwambie Al-hamdulillahi!

Mola wangu kama ulivyotulisha kwa upole wako na ukatulea kwa fadhila zako, tukamilishie fadhila nyingi, tukinge na makuruhi za malipizi. Utupe hisa za makazi mawili zilizo juu mno na bora mno zote mbili za papo kwa papo na za baadaye. Nawastahiki sifa njema kwa uzuri wa majaribu yako na wingi wa neema zako sifa njema ziwafikianazo na ridhaa yako na ivutayo wema wako mkubwa na utu wako, yaa adhiim yaa kareem, kwa rehema zako ewee mwingi wa huruma kuliko wote wenye huruma.

NONG'ONO LA WATU WA MUNGU

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Oh Allah tufundishe utii wako, tuepushe maasi yako, tufanyie wepesi kufikia tunayoyatamani miongoni mwa utashi wa ridhaa zako. Tuweke katikati ya janna yako, tanduwa toka kwenye ufahamu wetu mawingu ya shaka, fungua nyoyo zetu zingo na pazia la shaka. Ondoa ubatili toka dhamiri zetu, imarisha haki katika fikra zetu za siri, kwa sababu shaka shaka na dhana ni virutubisho vya fitna na vichafuzi vya usafi wa tuzo na wema. Oh Allah tujaalie tuwe katika safina za uokovu wako, tupe ladha ya sala ya kunong'ona na wewe, tunyweshe vidimbwi vya upendo wako, tuonjeshe utamu wa upendo wako na ukaribu wako, jaalia juhudi yetu kwa ajili yako na hima yetu iwe katika utii wako isafishe nia zetu kwa kazi yako tu. Kwa hakika sisi tupo kwa kuwapo kwako na tu wako, hatuna njia ya kufikia kwako isipokuwa ni wewe. Ewe Mungu wangu niweke mimi pamoja na wateule wema, niunge na wema watawa waliotangulia kuifikia zawadi ya ukarimu wenye haraka kwenye matendo mema watenda mema yenye kubaki wenye juhudi kuinuwa daraja, hakika wewe ni muweza juu ya kila kitu, kwa kujibu ndio wafaa, kwa rehema zako ewe mwingi mno wa wenye kurehemu.

NONG'ONO LA SALA YA WANA MUREEDI

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Kehema Mwenye Kurehemu. Utakatifu ni wako, njia nyembamba zilioje kwa usiyemwongoza! Haki yawazi iliyoje kwa uliye mwongoza njia yake! Mola wangu tupitishe njia za kufika kwako, tuendeshe katika njia ya karibu mno kufika kwako, tufanyie karibu mbali, na turahisishie gumu la taabu. Na utukutanishe na waja wako ambao kwa kuwahi kwako waharakia, daima wabisha hodi mlangoni kwako usiku na mchana wakuabudu wewe tu, nao waiogopa haiba yako, ambao umewasafishia manyweo. Na umewafikishia wayapendayo, umewapa wayatakayo, umewatekelezea kwa fadhila zako, utashi wao, umejaza upendo wako ndani ya dhamira zao, umetosheleza kiuzao kwa kinywaji chako safi, kupitia wewe wamewasili kwenye ladha ya kunong'ona na wewe, kutoka kwako wamefikia malengo yao ya mbali sana. Oh we ambaye kwa wale wamwendeaye huwaendea na huwapa zawadi na huwatunukia fadhila kwa upole, mwenye huruma na mwema kwa walioghafilika kumkumbuka, mpendwa mwenye huruma kwa kuwavuta kuelekea mlango wake.

Nakuomba unijaalie niwe miongoni mwa wenye hisa kubwa mno kubwa, na mwenye daraja ya juu zaidi kwako na miongoni mwa wenye hisa ya mapenzi kubwa kwako na mwenye hisa bora zaidi katika kukutambua, hima yangu imekatika isipokuwa kwako tu, utashi wangu umeelekea kwako tu, wewe tu ndio kusudio langu sio mwingine, kwa ajili yako tu kuamka kwangu na kukesha kwangu, wala si kwa ajili ya mwingine. Kukutana na wewe ndio tulizo la jicho langu. Kuungana na wewe ndio utashi wa nafsi yangu, shauku yangu ni kwako katika upendo wako ndio shauku yangu, kujiambatanisha na wewe ndio bidii yangu, ridhaa zako ni lengo niombalo.

Kukuona wewe ndio haja yangu, ujirani na wewe ndio ombi langu, ukaribu na wewe upeo wa ombi langu, sala ya kunong'ona na wewe ndio pumziko na raha yangu, kwako kuna dawa ya ugonjwa wangu na ponyo la moyo wangu unao unguwa, burudisho la shauku yangu, na kitu cha kuondoa taabu yangu. Kuwa mwenzi wangu katika upeka wangu, tulizo la kujigonga kwangu uwe mwenye kuni ghofiria kuteleza kwangu, mwenye kukubali toba yangu, mwenye kuitikia Du'a yangu, mfadhili wa kunihifadhi na dhambi, mwenye kunitoa toka ufakiri wangu, usikate mawasiliano yangu nawe. Oh we jaha yangu na bostani yangu, Oh we ambaye ndio dunia yangu na akhera yangu, Oh wee mwenye rehema nyingi kuliko wote wenye kurehemu.

NONG'ONO LA SALA YA WAPENZI

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Mola wangu ni nani ambaye ameonja utamu wa mapenzi yako kisha amkusudie mwingine badala yako! Ni nani ambaye umekuwa wa moyoni kwake kwa ukaribu wako naye kisha akamtaka mwingine na kujitoa mbali nawewe! Mola wangu tujaaliye tuwe miongoni mwa uliowachagua kuwa wakaribu na wewe na wapenzi wako, uliyemtakasa kwa upendo wako na mahaba yako, umempa shauku ya kukutana na wewe umemfanya apende maamuru yako, na umemtunuku kuangalia uso wako, na umempendelea ridhaa zako. Umempa kinga ya kutokukuhama na kukukirihi, umemfanyia makazi ya uhakika karibu na wewe, umemteuwa kwa ajili ya ukweli wa kukujua wewe, na kumfanya yu astahiki kukuabudu, umeutiisha moyo wake kwa utashi wako.

Umemchagua ili kukushuhudia, umeuweka tupu mtizamo wake kwa ajili yako, umeweka wazi moyo wake kwa upendo wako, umempendezesha yaliyo kwako umemwongoza utajo wako, umemgawiya shukrani yako umemshughulisha kwa utii wako. Umemfanya kuwa miongoni mwa viumbe wako wema, umemchagua kwa sala ya kunong'ona na wewe, umekata kutoka kwake vitu vyote vimkatavyo kutoka kwako. Oh Allah tujaalie tuwe miongoni mwa ambao mwendo wao ni kukufurahia wewe na upendo na nyakati zao ni kupiga kite na kulia, paji zao za uso zi katika hali ya sijda kwa taadhima yako.

Macho yao yakesha yakiwa chini ya huduma yako, machozi yao yatiririka kwa kukuogopa nyoyo zao zimejitundika kwa upendo wako, viini vyao vyatikisika kwa kukuogopa, Oh we ambaye nuru ya utukufu wake huvuta macho ya wapenzi wake, utukufu wa uso wake huamsha upendo wa nyoyo za wamjuao. Oh we utashi wa nyoyo za wenye shauku, Oh wee upeo wa matumaini ya wapenzi, naomba kwako upendo kwa ajili yako, na kuwapenda wanaokupenda, nakupenda kila tendo linifikishalo karibu yako.Na jaalia umpendwa mno kwangu kuliko mwingine yeyote, na jaalia upendo wangu kwako uwe mwongozo kwenye ridhaa zako, na shauku yangu kwako iwe kinga ya kutokukuasi, niangalie kwa jicho la upendo na huruma, usiugeuze uso wako mbali na mimi, nijalie niwe miongoni mwa watu wenye furaha na wewe na wenye hadhi kwako Oh mwenye kuitikia, Oh we mwenye huruma kuliko wote wenye huruma.

NONG'ONO LA SALA YA WAOMBAO WASILA

Kwa Jina la Mwenyez mwingi wa Rehema Mwenje Kurehemu. Mola wangu sina wasila kufikia kwako isipokuwa matendo ya upole wa huruma yako, wala njia yeyote ya kunifikisha kwako isipokuwa fadhila za upole wa rehema zako, na uombezi wa Nabiy wako Nabiy mwenye huruma, mwokozi wa umma toka kwenye bumbuwazo. Jaalia viwili hivyo kwangu ndio sababu ya kupata ghofira yako, vifanye viwili hivyo kwangu kiungo cha kufuzu ridhaa zako, matumaini yangu yamefika kwenye kitalu cha ukarimu wako, tamaa zangu zimetuwa kwenye ukumbi wa upaji wako. Matumaini yangu yameimarika kwako, hitimisha amali yangu kwa muhuri wa kheri nijaalie niwe miongoni mwa wateule wako ambao umewaweka katikati ya janna yako na umewaweka nyumba ya ukarimu wako uliofurahisha macho yao kwa kukuangalia wewe siku ya kukutana na wewe, uliowarithisha vituo vya ukweli karibu yako. Hawafiki wafikaji kwa mkarimu mno kuliko yeye, wakusudiaji hawampati mwenye rehema zaidi kuliko yeye, Oh mbora wa mwenye kuwa naye peke yake. Oh we mpole wa mwenye kukimbilia ya kwake hali amefukuzwa, nimenyosha mikono yangu kuelekea wasaa wa msamaha wako, kwenye ncha ya ukarimu wako nimetungika mkono wangu, usininyime, wala usinipe balaa la kutofanikiwa na kuhasirika. Oh we msikiaji Du'a, Oh we mwenye kurehemu mno kuliko wote wenye kurehemu.

NONG'ONO LA SALA YA MAFAKIRI

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Kehema Mwenye Kurehemu. Mola wangu mvunjiko wangu haugangwi ila na upole wako na upendo wako, ufakiri wangu hautoshelezi yeyote isipokuwa na upendo wako na hisani yako, woga wangu hautulizi yeyote isipokuw na amani yako. Udhalili wangu hawezi kuuenzi yeyote isipokuwa mamlaka yako, hatonifikisha kwenye matumaini yangu isipokuwa fadhila zako, hawezi kurekebisha ukosefu wangu isipokuwa umbaji wako. Hawezi kukidhi haja yangu asiyekuwa wewe, hawezi kunifariji dhiki yangu isipokuwa rehema yako. Madhara yangu hayaondowi yeyote ila huruma yako, kiu yangu iunguzayo hawezi kuiburudisha yeyote isipokuwa mawasiliano yako, shauku yangu hawezi kuizima yeyote isipokuwa kukutana na wewe. Shauku yangu kwako hakuna wa kuituliza isipokuwa kwa kuangalia uso wako.

Kuwa imara kwangu hakuwezi kufanyika isipokuwa kwa kusogea karibu yako, woga wangu hautulizi yeyote isipokuwa tulizo lako ugonjwa wangu hawezi kuutibu yeyote isipokuwa dawa yako, mayonzi yangu hayatowi yeyote isipokuwa kwa kuwa karibu yako, jeraha langu hawezi liponya yeyote isipokuwa msamaha wako, kutu ya moyo wangu haiondowi yeyote isipokuwa msamaha wako, wasi wasi wa moyo wangu hauondowi yeyote isipokuwa amri yako. Oh we upeo wa matumaini ya wenye kutumaini, Oh we upeo wa ombi la waombaji, Oh we umbali wa utashi wa watakaji, Oh we ambaye ndio juu kabisa wa takwa la watakaji, Oh we mfadhili wa watu wema, Oh we ambaye ni amani ya walio na woga, Oh we mwenye kujibu maombi ya wenye madhara, Oh we ambaye ni bohari ya wasiokuwa na kitu, Oh we ambaye ni hazina ya wanyonge, Oh we mwenye kukidhi haja za mafakiri na masikini, Oh we mkarimu mno wa wakarimu. Ewe mwenye rehema zaidi ya wenye kurehemu, Kunyenyekea kwangu na ombi langu ni kwako, utetezi wangu na ombi langu sana ni kwako nakuomba unipe tulizo la bidhaa yako, udumishe kwangu neema za huruma yako.

Mimi ni huyu! Mwenye kusimama kwenye mlango wa ukarimu wako, nimejiweka kwenye baridi ya wema wako, nimeshikilia kamba yako madhubuti, nimeshikamana na kishiko chako thabiti. Mola wangu muhurumie mja wako dhalili, mwenye ulimi butu na amali (kazi) ndogo, mpe kwa hisani zako nyingi mno, mhifadhi chini ya kivuli chako kikubwa, ewe mkarimu, ewee mzuri, ewee mwingi wa huruma kuliko wote wenye huruma.

NONG'ONO LA SALA YA WAJUZI

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Mola wangu, ndimi zimeshindwa kuifikia sifa yako njema, kwa kiwango kinacholingana na utukufu wako, akili zimeshindwa kuifikia hakika ya uzuri wako, macho yamehasirika bila ya uwezo wa kuangalia utukufu wa uso wako, wala haujamfanyia kiumbe njia ya kukujua wewe, isipokuwa kwa kutoweza kukujua. Mola wangu tujaalie sisi tuwe miongoni mwa ambao imeimarika miti ya shauku yako katika bostani za vifuwa vyao, nguvu ya shauku ya upendo wako imechukuwa mioyo yao yote, wao wakimbilia kwenye viota vya fikra wajilisha katika bostani ya ukaribu na ufunuo. Wanywa kwa glasi ya upendo pamoja na upole wa vikombe vya fadhila, waingia sehemu za maji yenye vuguvugu la upendo, vifuniko vimeondolewa toka macho yao giza la mashaka limewatoka kwenye akida zao na dhamira zao, zimetoweka ingio za shaka nyoyoni mwao na fikra zao za siri.

Vifua vyao vimekunjuka kwa kuthibitisha elimu ya kweli, hima zao zimepanda ili kuwahi maisha ya furaha katika zuhudi kinywaji chao kimekuwa kitamu katika chemchemu ya kazi njema, fikra zao za siri zimekuwa nzuri katika kikao cha moyoni.

Akili zao zimekuwa na amani sehemu za hofu, nyoyo zao zimetakata kwa kurejea kwa bwana wa mabwana, nyoyo zao zimeyakinisha kufaulu na ufanisi, macho yao yamefurahishwa na kumwangalia mpendwa wao, yameimarika makazi yao kwa kupata ombi na kuyafikia matumaini. Biashara yao imepata faida kwa kuiuza dunia kwa akhera, fikra za il-hamu zinaladha ilioje kwa kukukumbuka moyoni, unautamu ulioje msafara wa kifikra kuelekea kwako katika njia isioonekana, wapendeza mno utamu wa upendo wako. Kitamu kilioje kinywaji cha kuwa karibu nawewe, tukinge na fukuzo lako na kuwekwa mbali na wewe, tujaalie tuwe miongoni mwa mahsusi wakujuao, na waja wako wema mno, na wa kweli mno katika waja wako watii na wenye ikhlasi mno katika waja wako wachamungu. Oh we mwenye adhama mwenye ufalme, Ewe mkarimu ewe mtowaji, kwa rehema zako na huruma yako ewe mwngi wa rehema kuliko wenye kurehemu wote.

NONG'ONO LA SALA YA WENYE KUMBU KUMBU

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Kehema Mwenye Kurehemu. Mola wangu lau si wajibu kukubali amri yako ningekutakasa kuwa uko mbali sana na kukukumbuka kwangu wewe, kwa sababu kukukumbuka kwangu wewe ni kwa kadiri yangu si kwa kadiri yako, kadiri yangu haiwezi kufikia mahali pa kukutakasa wewe. Miongoni mwa neema kubwa sana juu yetu kuipitisha dhikri yako ndimini mwetu, na idhini yako kwetu kwa Du'a na kukutakasa na kukusabbihi mungu wangu tia moyoni mwetu utajo wako kando ya watu na katika mkusanyiko. Usiku na mchana, kwa kutangaza na kwa siri wakati wa mafanikio na wataabu, tuambatanishe na utajo wa siri tutumikishe na aamali iliyo safi, na juhudi yenye kuridhiwa na wewe tulipe kwa mizani iliyojaa. Mola wangu!

Nyoyo zenye upendo zafurahiwa na wewe kwa ajili ya kukutambua. Na kwa ajili ya upendo wako zimekusanywa nyoyo zilizotengana. Kutengana nyoyo hazitulii safi isipokuwa kwa kukukumbuka wewe, wala nafsi hazitulii isipokuwa zikuonapo. Wewe ni mwenye kutukuzwa kila mahali, mwabudiwa katika kila zana, upo kila wakati, muombwa kwa kila lugha mwenye kuadhimishwa katika kila moyo, nakuomba unisamehe katika kila ladha imepita bila ya kukukumbuka. Na katika kila raha bila ya kujiambatanisha na wewe, na katika kila furaha bila ya kujikurubisha kwako, na katika kila shughuli bila ya utii wako. Mola wangu! Wewe umesema na usemi wako ni wa haki (o ninyi mlioamini mkumbukeni Mungu sana na mumtukuze asubuhi na jioni) ulisema na usemi wako ni wa haki: (nikumbukeni nitakukumbukeni) ulituamrisha tukukumbuke na ulituahidi kuwa utatukumbuka ili kuinuwa heshima yetu na kututukuza sisi na hao twakukumbuka kama ulivyo tuamuru. Hivyo basi tutekelezee uliyotuahidi, Oh we mkumbukaji mno miongoni mwa wakumbukaji, Oh we mwenye huruma mno miongoni mwa wenye huruma.

NONG'ONO LA SALA YA WENYE KUSHIKAMANA

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Oh Allah Oh we kimbilio la wakimbiliao! Oh we kinga ya wenye kujikinga! Oh we mwokozi wa wahilikio! Oh we mhifadhi wa wanyonge! Oh we mwenye huruma kwa masikini! Oh we mwenye kuwajibu wenye shida! Ewe hazina ya wenye hajja! O we mwenye kuwaganga waliovunjika! Ewe kimbilio la waliokatikiwa! Oh msaidizi wa wanyonge! Oh we mtowa hifadhi kwa wenye hofu! Oh msaidia wenye taabu! Oh ngome ya wakimbizi! Ikiwa sikujikinga na uwezo wako ni kwa nani nitajikinga naye? Endapo sikuomba kimbilio kwa uwezo wako kwa nani nitakimbilia! Dhambi zimenifanya nishike upindo wa vazi la msamaha wako! Makosa yamenifanya niombe kubisha hodi kwenye mlango wa msamaha wako. Maovu yamenifanya niteremke kwenye ukumbi wa utukufu wako. Hofu ya adhabu yako imenichukuwa nishikamane na kishiko cha huruma yako.

Si haki kwa ambaye ameshikamana na kamba yako atupiliwe mbali. Wala haiwi sawa kwa ambaye ameomba hifadhi kwa enzi yako asalimishwe au atelekezwe! Oh Mola wangu usitutowe nje ya himaya yako. Usituvue uangalizi wako. Tulinde kwenye njia za kuangamiza. Hakika sisi tuko machoni mwako. Na tu katika bawa lako. Nakuomba kwa wateule wako miongoni mwa malaika wako na walio wema miongoni mwa viumbe wako. Utujaaliye juu yetu mlinzi atakaye tuokowa kutoka kwenye maangamizi, na utuepushe na maafa. Tufiche kutokana na misiba mibaya. Tuteremshie utulivu wako na funika nyuso zetu kwa nuru ya mahabba yako. Utupe hifadhi kwenye ngome yako. Tukusanye chini ya bawa la uhifadhi wako. Kwa huruma yako na rehema yako. Ewe mwenye huruma nyingi kuliko wote wenye huruma.

NONG'ONO LA SALA YA WATAWA

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Mola wangu umetuweka katika makazi yaliyotuchimbia shimo la vitimbi vyake. Umetuambatanisha kwenye mkono wa umauti katika kamba ya usaliti wake. Kwako twakimbilia toka kwenye vitimbi vya ujanja wake. Kwako twaomba hifadhi ili tusighurike na mng'aro wa mapambo yake. Kwa sababu yenyewe ni yenye kuwaangamiza wayatafutayo, yenye kuwaharibu wakazi wake, yamejaa maafa, misiba. Mungu wangu tushawishi kujiepusha nayo.

Tupe salama mbali nao kwa tawfiki yako na hifadhi yako. Tuvuwe majoho ya kukuhalifu wewe, yasimamie mambo yetu kwa uzuri wa utoshelezaji wako. Tuongezee ziada yetu kutoka wasaa wa rehema yako. Jaalia majazi yetu toka kwenye wingi wa ruzuku zako. Panda mioyoni mwetu miti ya upendo wako tutimiziye nuru ya maarifa yako, tuonjeshe utamu wa msamaha wako na ladha ya maarifa yako, yafurahishe macho yetu siku ya kukutana na wewe kwa kukuomba wewe. Toa kuipenda dunia ndani ya mioyo yetu kama ulivyo wafanyia watu wema miongoni mwa wateule wako, na watu wema miongoni mwa watu wako mahsusi. Ewe mwingi wa rehema kuliko wote wenye kurehemu. Oh wee mkarimu mno kuliko makarimu wote.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU


YALIYOMO

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 1

KIMEANDIKWA NA: ALI IBN AL - HUSAYN IMAM ZAYNUL AL - ABIDIN(A.S) 1

KIMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HAROON PINGILI 1

UTANGULIZI 2

NENO LA WACHAPAJI 4

DIBAJI KUHUSIANA NA USHUHUDA - THABITI WA SAHIFA 4

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 10

DUA YA KWANZA 10

DUA YA 2 12

NA ILIKUWA KATIKA DU'A YAKE(A.S) BAADA YA KUMUHIMIDI MUNGU KAMA HIVI: HUANZA KUMTAKIA REHMA MJUMBE WA MUNGU (S.A.W.W) 12

DUA YA 3 13

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE KWA MALAIKA WABEBAO ARSHI NA KWA KILA MALAIKA 13

Dua ya 4 14

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE AMANI IMFIKIE KATIKA KUWA TAKIA REHMA WAFUWASI WA MITUME NA WALIO WASADIKI MITUME 14

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 16

DUA YA 5 16

NA ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE KWA AJILI YAKE MWENYEWE (A.S) NA KWA WALIO CHINI YA WILAYA YAKE 16

DUA YA 6 17

NA ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE A.S. NYAKATI ZA ASUBUHI NA JIONI 17

DUA YA 7 18

NA ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE (A.S) ANAPOTOKEWA NA JAMBO SUMBUFU AU KUSHUKIWA NA TAABU NA WAKATI WA KUKERWA 18

DUA YA 8 19

DU'A ZAKE KATIKA KUJILINDA NA MAMBO YACHUKIZAYO NA TABIA MBAYA NA MATENDO YALAUMIWAYO 19

DUA YA9 19

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE AKIWA NA SHAUKU SANA YA KUOMBA MSAMAHA KWA MWENYE ENZI MUNGU MTUKUFU 19

DUA YA 10 20

MIONGONI MWA DU'A ZAKE AKIOMBA KIMBILIO KWA MUNGU 20

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 21

DUA YA 11 21

DU'A ZAKE KWA AJILI YA MWISHO MWEMA 21

DUA YA 12 21

DU'A ZAKE KATIKA KUKIRI NA KUOMBA TOBA KWA MUNGU MTUKUFU 21

DUA YA 13 23

DU'A ZAKE KUMWOMBA HAJA MUNGU MTUKUFU 23

DUA YA 14 24

MIONGONI MWA DU'A ZAKE AKIFANYIWA UCHOKOZI NA AONAPO ASIYOYAPENDA TOKA KWA WADHALIMU 24

DUA YA 15 25

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE (A.S.) AKIWA MGONJWA AU AKISUMBULIWA NA JAMBO AU KUPATWA NA BALAA 25

DUA YA 16 25

DU'A ZAKE AOMBAPO KUJITOA KWENYE DHAMBI ZAKE AU AKINYENYEKEA KUOMBA MSAMAHA WA DOSARI ZAKE 25

DUA YA 17 27

DU'A ZAKE(A.S) AMTAJAPO SHETANI HUJILINDA NAYE NA HUJILINDA NA UADUI WAKE NA VITIMBI VYAKE 27

DUA YA 18 28

LINDWA NA JAMBO ANALOLIHOFIA AU KUHARAKISHIWA AYATAKAYO 28

DUA YA 19 29

DU'A ZAKE(A.S) KUOMBA MAJI WAKATI WA UKAME 29

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 30

DUA YA 20 30

DU'A ZAKE KATIKA TABIA NJEMA NA VITENDO VYA KURIDHISHA 30

DUA YA 21 33

NA ALIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) AKIHUZUNISHWA NA JAMBO NA YA MUOGOPESHAPO MAKOSA 33

DUA YA 22 34

DU'A ZAKE(A.S) KATIKA SHIDANA JUHUDI NA MAMBO YANAPOKUWA MAGUMU 34

DUA YA 23 36

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) AMWOMBAPO MUNGU HALI NJEMA NA ANAPOISHUKURU 36

DUA YA 24 36

DU'A ZAKE(A.S) KWA AJILI YA WAZEE WAKE(A.S) 36

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 39

DUA YA 25 39

DU'A ZAKE(A.S) KWA AJILI YA WATOTO WAKE(A.S) 39

DUA YA 27 40

DU'A ZAKE(A.S) KWA WATU WA MPAKANI 40

DUA YA 28 43

DU'A ZAKE ANAPOKIMBILIA KWA ALLAH 43

DUA YA 30 43

DU'A ZAKE(A.S) KWA AJILI YA KUOMBA MSAADA WA KULIPA DENI 43

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 45

DUA YA 31 45

DU'A ZAKE (A.S) KATIKA KUIELEZEA TOBA NA KUIOMBA 45

DUA YA 32 47

DU'A ZAKE BAADA YA KUMALIZA SALA ZA USIKU 47

DUA YA 35 50

MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA RIDHAA AWAANGALIAPO WANA WA DUNIA HII 50

DUA YA 36 51

DU'A ZAKE AANGALIAPO MAWINGU NA UMULIKAJI NA ASIKIAPO SAUTI YA RADI 51

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 52

DUA YA 37 52

DU'A ZAKE(A.S) ANAPOTAMBUWA KUSHINDWA KUTEKELEZA SHUKRANI IPASAVYO 52

DUA YA 38 53

DUWA ZAKE(A.S) KATIKA KUOMBA RADHI KWA KUWATENDEA VIBAYA WAJA WA MWENYEZI MUNGU KWA KUTOWAJIBIKA IPASAVYO KUHUSU HAKI ZAO NA KUIKOMBOA SHINGO YAKE IEPUKANE NA MOTO 53

DUA YA 39 53

DUWA ZAKE(A.S) KATIKA KUOMBA MSAMAHA NA REHEMA 53

DUA YA 40 55

MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) AKITANGAZIWA KIFO CHA MTU AU AKUMBUKAPO UMAUTI 55

DUA YA 41 55

DU'A ZAKE(A.S) KATIKA KUOMBA SITARA NA ULINZI 55

Dua ya 42 55

DU'A YAKE(A.S) WAKATI WA KUHITIMISHA QUR'AN 55

DUA YA 43 58

MIONGONI MWA DU'A ZAKE AUONAPO MWEZI MWANDAMO 58

DUA YA 44 58

MIONGONI MWA DU'A ZAKE UINGIAPO MWEZI WA RAMADHANI 58

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 61

DUA YA 45 61

ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KUUAGA MWEZI WA RAMADHANI 61

DUA YA 46 64

DU'A ZAKE(A.S) KATIKA SIKU YA IYDI AL-FITRI 64

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 67

DUA YA 47 67

DUWA ZAKE(A.S) SIKU YA ARAFA 67

NA ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) SIKU YA KUCHINJA, SIKU YA IJUMAA 73

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 77

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE (A.S) KATIKA KUJIKINGA NA VITIMBI VYA MAADUI NA KUONDOWA MACHUNGU YAO 77

NA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA HALI YA WOGA 78

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA KUSIHI NA KUNYENYEKEA 79

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA KUMSIHI ALLAH (s.w.t) 80

NA ILIKUWA MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA KUJIDHALILISHA KWA MUNGU MWENYE ENZI MTUKUFU 81

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 82

MIONGONI MWA DU'A ZAKE KUONDOWA MASHAKA 82

MIONGONI MWA TASBEEHI ZAKE NAMKUSUDIA ZAYNUL-AABIDEENA(A.S) ALAYHIS-SALAAM 82

DU'A NA KUMADHIM KWAKE 83

DU'A ZAKE KATIKA KUWATAJA ALI WA MUHAMMAD(A.S) 83

NA MIONGONI MWA DU'A ZAKE KATIKA KUMTAKIA REHMA ADAM(A.S) 84

MIONGONI MWA DU'A ZAKE KATIKA USUMBUFU NA KUOMBA FARAJA 84

DU'A ZAKE A.S. KWA AYAHOFIAYO NA KUYAOGOPA 85

MIONGONI MWA DU'A ZAKE(A.S) KATIKA KUJIDHALILISHA 85

DU'A ZAKE SIKU YA JUMAPILI 86

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 88

DU'A YAKE SIKU YA JUMANNE 88

DU'A YAKE SIKU YA JUMATANO 88

DU'A YAKE SIKU YA ALHAMISI 89

DU'A YAKE SIKU YA IJUMAA 89

DU'A YAKE SIKU YA JUMAMOSI 90

MNONG'ONO WA IBADA YA WENYE KUJUTA 90

NONG'ONO LA SALA YA MNUNG'UNIKAJI 91

NONG'ONO LA SALA YA MWENYE HOFU 91

NONG'ONO LA SALA YA WENYE MATUMAINI 92

NONG'ONO LA WENYE KUSIHI SANA 93

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU 94

MNONG'ONO WA SALA ZA WENYE KUSHUKURU 94

NONG'ONO LA WATU WA MUNGU 94

NONG'ONO LA SALA YA WANA MUREEDI 95

NONG'ONO LA SALA YA WAPENZI 95

NONG'ONO LA SALA YA WAOMBAO WASILA 96

NONG'ONO LA SALA YA MAFAKIRI 97

NONG'ONO LA SALA YA WAJUZI 97

NONG'ONO LA SALA YA WENYE KUMBU KUMBU 98

NONG'ONO LA SALA YA WENYE KUSHIKAMANA 99

NONG'ONO LA SALA YA WATAWA 99

SHARTI YA KUCHAPA 100

MWISHO WA KITABU 100

YALIYOMO 101