USUULID DIIN
UIMAMU
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote, na rehma na amani ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad na Kizazi chake Kitukufu.
"Uimamu" kwa waislamu ni miongoni mwa maudhui ambayo yamezungumzwa sana na kufanyiwa utafiti sana, hadi vitabu vilivyo tungwa kuhusu maudhui haya kufikia maelfu kwa maelfu.
Kisha yakaendelea mazungumzo kuyahusu maudhui hayo, na watafiti kugundua wingi wa kuchipuka kwa matawi yake na upana wa maudhui haya katika utungaji wa vitabu, na kwa hivyo kila kundi kati ya watunzi hao likachukuwa tawi moja wapo kati ya matawi yale au upande mmoja wapo wa maudhui hayo, na matokeo ya kufanya hivyo ukatokea upande ufanyao utafiti na kujihusisha na suala la uimamu ndani ya Qur'ani.
Na upande mwengine ukajihusisha na suala hilo kwa upande wa hadithi za Mtume, na kuna upande uliojihusisha na uimamu kwa mtizamo wa elimu ya akida, au kwa upande wa historia, au kuuangalia uimamu kwa kuzingatia mipaka ya yale yaliyo tokea kwenye Saqifa bani Saida pindi alipo fariki Mtume(s.a.w.w) , kisha yaliyo husiana na maisha ya Maimamu na historia zao, na kue-ndelea.
Pamoja na vitabu vilivyo tungwa kuwa vingi na idadi kuwa kubwa, hakika vitabu vingi kati ya hivyo, havikuandikwa kwa roho ya kuyatazama maudhui yenyewe tu yakiwa yameepukana na matamanio na ghera (taasubi) juu ya madhehebu fulani, matokeo yake ni kudhihiri utafiti na vitabu vilivyo jawa na taasubi (ghera) iliyo kemewa, na hisia zikaenda kinyume cha ukweli, na kutolewa hukumu zenye kufuata matakwa na mata-manio, na kubeba mambo ambayo akili na mantiki haiyakubali wala kuyaridhia.
Na hapa ikaonekana kuwa maudhui ya uimamu yamezungu-kwa na sura tofauti za kiakili ambazo hazilisogezi karibu lililo mbali na wala haziondoi tofauti iliyopo na hazisaidii kuleta uelewano wala muungano.
Na sura hizi zilizoko akilini hazikuwa na chimbuko lingine tofauti na vitabu hivyo vilivyo tungwa na vilivyo toka kwenye maadili ya utunzi wa vitabu na uandishi wa kimaudhui, na wala si chimbukizi tofauti na picha mbaya iliyotolewa yenye kuchukiza ya mwendo (historia) wa kiislamu kwa karne zote hizo.
Na kwa uwazi kabisa:
Tunapo taka kufanya utafiti wa maudhui ya uimamu hivi leo na baada ya kupita karne kumi na nne tangu lifanyike tukio la "Saqifa" na matukio yake mengine, kwa nini tujaalie kuwa tutatofautiana. Na ikiwa tutatofautiana (na kwa wafanyao utafiti suala la kutofautiana ni la kawaida kwao) kwa nini tunapatwa na ghera (asabiya) ya kupenda kutetea kitu hata kama si cha sawa na kuwa wakali na wenye ghadhabu, wakati ambapo kutofautiana kwa rai hakuharibu mapenzi ya kitu?.
Na je katika utafiti huu kuna jambo limletealo mwanadamu wa leo faida ya mali au kumfikisha kwenye msimamo fulani ambao anaweza kuutumia kwa maslahi yake? Au je kwenye utafiti huu kuna kitu kitakachomtia mtu wa zama hizi gharama au kuleta maudhi yawezayo kumpata huyu au yule katika wana-damu?
Hakika waislamu wa leo, wote kwa ujumla wanakubaliana kutokuwepo kwake kunaweza kupelekea watu kutofautiana katika kumpa baia (kiapo cha utiifu) au kutompa baia, kwa hivyo basi hakuna ugomvi uogopewao au mapigano yenye kuogopewa lau kama mtu fulani atasema maneno yake katika maudhui haya.
Na huenda muulizaji akauliza:
"Ikiwa hali ni hivyo, kwanini -basi- kufanyike utafiti kama huu na juhudi kama hizi"?
Jawabu:
Hakika sisi tunataka kufanya utafiti wa mas'ala haya ili kutoa msimamo wa uislamu (kwa kuzingatia kuwa uislamu ni dini na sheria na ni nidham ya maisha) kwenye maudhui haya hatari, na tunataka kutoa majibu yenye maswali yatatanishayo yenye kiu cha kupata majibu sahihi:
Nini maana ya "Uimamu" katika uislamu?Je "Uimamu" ni lazima kuwepo? Na vipi? Je Uislamu ulifaradhisha kuwepo uimamu, na je ulimteua Imamu au mtu anae faa kuwa Imamu kwa dalili au liliachwa suala hilo kwa ajili ya kufanywa uchaguzi?
Je uimamu kwa kuteuliwa ni fikra ya "kitheokrafia" (theocracy- utawala wa dini) au ya kidikteta au fikra ya kidemo-krasia?
Na pande zingine ambazo ni lazima kuzifanyia utafiti kwa undani na kwa uhuru, huenda kufanya hivyo kukawa na faida au kutuletea ukweli na kutupa msingi na msimamo wa kiislamu kuhusu mas'ala haya yenye msisimko mkubwa.
Na mfumo wa kitabu hiki utawatolea wasomaji natija iliyo salama na utakuwa na muelekeo usio gusa au kuyapa umashuhuri madhehebu haya au yale kati ya fikra na mielekeo ya vikundi mbalimbali vya kiislamu au fikra ya mtu huyu au yule kati ya wanazuwoni wa kiislamu, na nimeuepusha na kuto zungumzia au kutoifanyia utafiti historia ya mambo yaliyo tokea siku aliyo fariki Mtume(s.a.w.w) kutokana na mgawanyiko na tofauti zilio tokea, ili kuepukana na mambo kadhaa ambayo yaweza yakasa-babishwa na bahthi hiyo, kama vile kuziamsha hisia na mapenzi au kulitonesha jeraha wakati ambapo tunataraji kwa nia safi jambo hili (jeraha hili) litulie na lipone kutokana na usaha wake wenye kuumiza na kusikitisha.
Na matarajio yangu yote ni kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, anisaidie katika njia yangu hii na anisaidie kupita kwenye njia na mipaka niliyo jiwekea na kujifunga nayo na kujilazimisha kuifuata kwenye utafiti nilio tangulia kuufanya, na aiepushe kalamu yangu kutokana na usahaulivu na ukosevu, na auelekeze mkono wangu kwenye kauli aziridhiazo na kwenye matendo ayaridhiayo, hakika yeye ni msaidizi bora na muwafikishaji.
Na maombi ya mwisho, tunasema sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote.
Kaadhimiyya - Iraq
MUHAMMAD HASSAN AALI YAASIN
Imam (kama lugha ya kiarabu ilivyo muarifisha), ni mtu mwenye kuwatangulia kaumu yake au watu wake, pia mwenye kufuatwa na mwenye kufanywa kuwa kiongozi na msimamizi wa mambo.[1]
Na uimamu (kwa maana hii) unakuwa na maana ya uongozi na uraisi na kufuatwa na kuwatangulia watu, na kwa hivyo mtu mwenye kuwatangulia watu kwa ajili ya sala atastahiki kuitwa "Imamu" kwa sababu anawatangulia na kuwaongoza wote kwa pamoja.
Na kwa maana hii ya kilugha Qur'ani imekuwa ikilitumia neno "Imam" kama alivyo litumia kwenye kauli yake tukufu:
"Hakika mimi nimekufanya wewe uwe imamu (kiongozi) kwa watu.
"Na kabla yake kulikuwa na kitabu cha Mussa, imamu (kiongozi) na rehma".
"Na utufanye tuwe maimamu )viongozi( wa wachamungu".
"Siku ambayo tutawaita watu wote na imamu wao (kiongozi wao).
Na aya zingine zilizo kuja kwenye Qur'ani tukufu katika matumizi ya neno "Imamu".
Na neno Khalifa (kama ambavyo lugha ilivyo liarifisha vilevile), ni kiongozi na mtawala mkubwa na mwenye kuchukua nafasi ya mtu aliekuwa kabla yake au alie mtangulia.[2]
"Ewe Daudi hakika sisi tumeku-fanya uwe khalifa (mtawala) katika ardhi".
"Yeye ndie aliekufanyeni kuwa watawala kwenye ardhi".
"Na kumbukeni pale alipo kufanyeni kuwa makhalifa (watawala) baada ya watu wa Nuhu"
Na aya zinginezo ambazo ziliyatumia maneno hayo.
Na ikiwa wanazuwoni wa lugha wamekubaliana katika maana hii ambayo ina ashiriwa na neno "imamu" na "khalifa" na wafuasi wao wametofautiana kuhusu maneno hayo mawili ya kwamba je! Yana maana moja au maana mbili tofauti?. Kwa mfano Al-mawridy anatoa taarifa ya uimamu kuwa ni "Umewekwa kwa maana ya khilafa ya kushika nafasi ya mtume (kuchukuwa nafasi baada ya mtume) katika kuilinda dini na kuingoza dunia".[3]
Na Ibnu Khaldun anatoa taarifa ya neno khilafah kuwa "ni kuwaongoza (kuwaelekeza) watu wote kufatana na mtazamo wa kisheria kwenye maslahi yao ya kiakhera na kidunia maslahi ambayo hurejea kwa utawala huo".[4]
Na anatilia mkazo na kusema "Hakika mikakati ya kidini na kisheria huingia chini ya uimamu mkuu ambao ndio ukhalifa.[5]
Na mtu wa tatu kaunganisha "kati ya ukhalifa kwa kuuzinga-tia kuwa ndio uimamu (uongozi) mkuu na swala kwa kuuzingatia kuwa ni uimamu (uongozi) mdogo.[6]
Na maana ya yote hayo ni kuwa maneno haya mawili yanamuelekeo mmoja au makusudio mamoja.
Na huenda "uraisi" au "uongozi" ndio maana zenye kuku-sanya na kutosheleza ambazo zinawezekana kutumiwa kuyatafsiri maneno mawili hayo na kukubaliana juu ya maana hiyo.
Lakini tunapo fuatilia nyanja ambazo uongozi huu au uraisi huu huingia hasa kwenye viwanja vya kazi au sehemu za kazi hakika tunahisi kuwepo tofauti inayo tenganisha kati ya maneno mawili haya au itenganishayo kati ya neno moja na lingine na kuyapambanua kati yake na kuonyesha kutofautiana, tofauti ambayo hulipa kila tamko kati ya matamko mawili hayo ukubwa wake na upana wake.
Basi uimamu (kama ambavyo dalili za dini zinavyo tuonyesha) ni uongozi wa juu wa kidini. Na Khilafa (kama zijulishavyo dalili vilevile) ina maana kuwa ni uongozi wa juu wa dola.
Na,"Imamu kwa wanafikra wa kiislamu, wawe masuni au mashia, amekuwa na maana ya kuwa ni mwenye haki ya kisheria, wakati ambapo tamko khalifa linamuashiria mwenye utawala au nguvu za kiutawala kwa wakati ule"[7] , na kutokana na haya "Ukhalifa wa Abubakar baada ya Mtume, katika serikali yake au utawala wake ulikuwa ni utawala wa zama hizo na si utawala wa kidini".[8]
Na kwa kuyazingatia hayo kila tamko linakuwa na sehemu zake na nyanja zake maalum na mipaka yake maalum ambapo hufanya kazi ndani ya mipaka hiyo. Na pamoja na tofauti hii iliyopo kwenye nyanja za utekelezaji wa maneno hayo nje, hakika sisi tunaamini (kwa kuzirejelea dalili za kidini) kuwa anwani hizi mbili ni lazima ziungane na zikusanyike kwa mtu mmoja, kwa sababu hatukubali, katika uislamu fikra ya kutenganishwa dini na serikali au dola.
Na ikiwa jamii ya watu wa ulaya ambayo ndio iliyotuletea fikra hii ya kutenganisha dini na serikali wananyudhuru na sababu za kujenga fikra hiyo na waliyoyafanya katika kufanya mapinduzi dhidi ya utawala wa kanisa na kuingilia kwake mambo yote, kwa kuzingatia kuwa ukristo haukuwa na nidhamu ya dola au utawala na mifumo ya kutawala, basi sisi waislamu hatuna udhuru wowote au sababu yoyote iwezayo kutufanya kubeba wito huo au fikra hiyo, maadamu dini yetu kiukweli na uhakika wake ni ujumbe wa dini na ni nidhamu ya dola na utawala.[9]
Kwa hivyo basi, ni lazima kukusanyika uongozi wa dini na wa dola kwa mtu mmoja ili tusije kutumbukia kwenye fikra ya "uwili" ambao athari yake ya mwanzo huwa ni ugonjwa wa kutokuwa na msimamo wa rai moja katika nafsi ya muislamu.
Na ikiwa kati ya wislamu kuna watu wasemao kuwa uimamu ni kitu na ukhalifa ni kitu kingine, hakika waliyapata haya kutokana na historia ya waislamu na matukio yaliyo tokea, wakati ambapo ulitengana ukhalifa na uimamu, na kiongozi wa dini akawa sie raisi wa serikali au dola, na lilikuwa si jambo lenye kuingia akilini, khalifa kama Yazidi bin Muawiya kwa mfano awe ni "Imamu" wa waislamu wakimtegemea na kumkimbilia katika utatuzi wa mas'ala ya dini na mambo ya itikadi.
Hakika Uimamu, kama Shia Imamiyah walivyo ufahamu, ni sehemu ikamilishayo ujumbe wa Mtume na iufanyayo ujumbe huo uendelee kuwepo. Na akili inahukumu ulazima wa kuwepo kwake kwa sababu Uimamu ni huruma ya Mwenyezi Mungu na kila huruma (Lutfu) ni wajibu kwa Mwenyezi Mungu kufatana na hukumu ya akili yenye misingi ya mfumo wa akili katika elimu ya akida.
Ama uimamu kuwa ni Lutfu (Upole au huruma ya Mwenyezi Mungu), ni kwa sababu huruma au lutfu ni kitu kimkaribishacho mja kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu na kumweka mbali na maasi na kumpeleka na kumpitisha kwenye njia ya haki na maana hii huthibitishwa na uimamu kwa uwazi kabisa.
Na kila mmoja anafahamu kuwa kuwepo kiongozi mwenye kusikilizwa na mwenye utawala wenye nguvu, huzuwia dhuluma, na kumpa kila mwenye kudhulumiwa haki yake, na mambo yote ya watu huyawekea nidhamu kwa moyo safi na imani na kuepu-kana na matamanio na ubinafsi na kupenda kujitolea, mambo ambayo humkaribisha mwanadamu kwenye utiifu na kumtenga na maovu na humtia hamasa ya kufuata mfumo ambao Mwenyezi Mungu Ameuchagua.
Na hii ndio maana ya "Lutfu" (upole au huruma ya Mwenyezi Mungu) tuukusudiao kwenye sehemu kama hii.
Na jambo ambalo halihitaji maneno mengi ni kuwa hakika kila jamii ya watu, iwe ya zamani au ya hivi sasa, ni lazima iwe na raisi (kiongozi) mwenye kuyapangilia mambo yake, na nilazima kuwe na katiba na kanuni yenye kuweka nidhamu katika mambo ya jamii hiiyo. Na ikiwa jamii ya leo hii ina hisi kuwepo haja kubwa na umuhimu wa kuwepo raisi na serikali, yaani kuwepo utawala unao simamia mambo ya maisha kwa ajili ya jamii ile kama vile mambo ya kisiasa, ya kijeshi, kiuchumi, ya mahkama na ya malezi na vinginevyo, basi uislamu unamuangalio raisi wa dola kwa mtizamo mpana zaidi na wenye kukusanya vitu vyote, kwa kuwa yeye ni mwenye majukumu na ni mtekelezaji wa mambo yote ya dini na dunia, mambo yale ambayo yamebebwa na sheria au yamo ndani ya sheria kama mifumo ya tabia na mwendo wa mwananchi muislamu, sawa uwe ni mwenendo wa kumuelekea mola wake na mtu yeyote kati ya wanadamu.
Na kwa kuzingatia kuwa katiba nyingi na kanuni nyingi zitumikazo katika jamii za watu zimetungwa na kuwekwa na wanaadamu na zenye uwezekano wa kubadilika na kugeuka kufatana na mahitaji ya wakati na sehemu, na uislamu ukiwa umetoka na uko nje ya kanuni hizo na katiba hizo kwa kuzingatia kuwa ni sheria ya mbinguni ambayo haifai kuguswa au kufanyiwa mabadiliko yoyote, lakini uislamu huo pamoja na kukamilika kwake na kutimia kwake na kuto juzu kuchezewa bado umefungi-ka katika baadhi ya dalili zake na ina kanuni za ujumla na nguzo za msingi katika dalili zake zingine. Na ilikuwa ni lazima, ulazima ambao hauna shaka yoyote, kusema kuwa ni lazima awepo mwenye kutekeleza hukumu na kufafanua na kubainisha na kutoa ufumbuzi na kuelekeza sehemu ya utekelezaji wa kila hukumu. Na hivyo hivyo kila dalili ijulishayo ulazima wa kuwepo utume na wajibu wake itakuwa inafaa kuitumia kama dalili vilevile juu ya ulazima na uwajibu wa kuwepo uimamu, kwa sababu kuwepo utume bila ya uimamu ni sawa na kukatika na kutoendelea kuwepo jambo hilo, na jambo hilo linapingana na uislamu ulio simama kwenye msingi wa kuendelea kuwepo kwa ujumbe wake hadi siku ya kiama.
Kwa hivyo basi utume ni mwanzo wa maisha na uimamu ni kundelea kwa maisha hayo. Na lau kama ingefaa kwetu kukubali utume bila uimamu, ingefaa pia kusema kuwa ujumbe wa Mtume unamtizamo finyu na wenye mipaka maalumu ambao haukuweza kujikadiria umri mrefu hata baada ya kumalizika maisha ya Mtume wake, na haukuweza kuyawekea malengo yake mrithi (au muusiwa) atakae endeleza na kuendelea na kazi yake.
Na kutokana na kuwa uislamu unalenga kwenye dola kubwa ambalo litawajumuisha watu wote pamoja na kuwa wako kwenye nchi tofauti na wenye rangi tofauti, hakuna budi uislamu kuya-andalia malengo hayo uongozi wa kuyatekeleza na kuyafanya hayo, uongozi huo ukionekana wazi kwa mtume katika maisha yake na kwa khalifa wake ambae atakae shika nafasi yake baada ya kufariki kwake.
Na muhtasari wa hayo tuliyoyasema ni kuwa Uimamu kwa hakika ni ukamilisho wa maana ya utume, na kuwepo kwa Mtume na ufanyakazi wake hautasimama madhubuti bila kuwepo Imamu. Na kwa sababu hii Shia Imamiya wanaamini kuwa Uimamu ni wajibu kuwepo au ni lazima kuwepo kama ambavyo ni lazima kuwepo kwa utume, na dharura ya kuwepo uimamu ni sawa na dharura ya kuwepo utume au Mtume. Na haya yana dalili bora ambayo ni hadithi ya mtume iliyo mashuhuri:
"Mwenye kufa hali ya kuwa hamjui Imamu wa zama zake (basi) amekufa kifo cha kijahili". Na ikiwa uimamu ni jambo la lazima ambalo ni lazima kuwepo kwake, kama tulivyo eleza hivi punde, je uislamu uliwaachia watu jukumu la kumchagua Imamu ambae atasimamia kazi za cheo hiki muhimu na cha hatari au suala la Imamu linahusika na dalili (kauli) za Mwenyezi Mungu na Mtume katika kumteuwa na kumthibitisha?.
Shia na Muutazila walio wengi wao wamesema kuwa Imamu ni lazima awe ameelezwa (ametajwa) kwa dalili kutoka kwa mtume na awe amemuainisha yeye mwenyewe.Wamesema haya wakijitegemeza kwenye dalili kuwa, kwa kuzingatia kuwa uima-mu ni kuendelea kwa cheo cha utume, ni lazima kwenye uimamu huo kama ulivyo utume, kuwe na uteuzi na uainishaji maalumu uonyeshao uteuzi wa Mwenyezi Mungu kwa Imamu huyo na kumridhia kwake.
Kama ambavyo hakuna utume au mtume achaguliwae na kuteuliwa kwa kufanya mashauriano, hivyo hivyo, hakuna uima-mu au imamu ateuliwae kwa kufanya shura (kushauriana) na kwa uchaguzi. Na mfumo huu ndio mfumo thabiti ufuatwao na madhehebu hayo mawili katika mas'ala ya uimamu na imamu.
Ama makundi mengine ya kiislamu hayakuchagua mfumo maalum wa utawala katika uislam.[10] Bali walisema kuwa kila mwenye kushika utawala na kudai kuwa yeye ni imamu basi huyo ndie imamu. Sawa awe amefika kwenye utawala huo kwa njia ya uchaguzi kama ilivyo fanyika kwa Abubakar na Uthumani na Ali na Hassan, na haukufanyika kwa mwingine yeyote kwenye historia ya kiislamu, au amefika kwenye utawala kwa kuwekwa na yule alie mtangulia kama ilivyo tokea kwa Omar Binil-Khattab na makhalifa wengine wa bani umayya na bani Abbasi na Uthmaniyyah, au afike hapo kwa nguvu na kwa kutumia silaha kama ilivyo tokea kwa Muawia bin abi Sufiyani na Abul Abbas Assafah.
Na miongoni mwa dalili walizo zitolea ushahidi mashia juu ya ulazima wa kuwepo dalili inayo onyesha kuteuliwa kwa Imamu ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
"Na Mola wako Ana-umba Akitakacho na Anamchagua Amtakae , hawana hiyari katika hayo ".
Kwani aya hii imetujulisha kwa matamshi yake yaliyo wazi kuwa suala la kuwachagua mitume ambao ni waaminifu juu ya sheria na walinzi wa dini sio katika haki ambazo Mwenyezi Mungu aliwaachia watu wafanye watakavyo, bali suala la kuwachagua watu hao wa nafasi ya utume hufanyika kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na linahusika na Mola pekee.
Ama jibu la mwenye kupinga haya na kusema ya kuwa uteuzi huo unahusiana na suala la Utume tu na aya imeliangalia tu jambo hilo wala haikuligusia jambo lingine, ni maneno yasiyo kubalika, kwani mwanzoni mwa aya au mwishoni mwake hakuna kitu kitujulishacho -hata kama kwa njia ya siri- kuwa aya hii inahusika tu na mitume bali kutofungika kwake na jambo fulani (ujumla wake), na kutokana na uwazi wa matamshi yake, (ujumla huu) una kataa na haukubali kuyafunga maneno yake kwenye utume tu wala kuyafanyia taawili yoyote, na vipi yasikatae taawili wakati ambapo uimamu huzingatiwa kuwa ni kuendelea kwa cheo cha Utume, na kuutimiza ujumbe kunahitajia masharti hayo hayo yaliyo wekwa na kuzingatiwa kwa mtume katika upande huu.
Na ukweli kuwa, lau kama usia usingethibiti kutoka kwa mtume(s.a.w.w) kwa njia ya riwaya na habari zilizo nukuliwa, hakika akili pekee ni yenye kuhukumu ulazima wa kuwepo usia na kuwa suala la usia lilifanyika. Na kwamba yeyote katika sisi haridhii katika nafsi yake kusafiri na kuziacha mali zake zenye kumalizika au zenye uwezekano wa kutoweka au utawala wake wenye kutoweka na kuviacha vitu vyake kama mali yake chache aliyo nayo bila kuiweka mali hiyo chini ya ulinzi wa mtu aliemuusia na alie muaminifu, atakae iangalia na kuilinda pia kuiangalia isiweze kupotea. Je, inafaa kwa Mtume wa Uislam kuuacha urithi wake ulio mkubwa na urithi huo ukiwa ni kwa ajili ya wanadamu kwa zama zake zote bila kumuacha mtu alie usiwa atakae uchunga urithi huo na kuulinda kama itakiwavyo?
Hakika mazingira na matukio yote yaliyo uzunguka Uislamu wakati wa kifo cha Mtune(s.a.w.w) yanatufanya tuamini kuwa ni lazima atakuwa alitoa usia, na kwamba mmea wake wenye baraka hakuuacha jangwani hivihivi ukipigwa na upepo mkali au kwenye joto kali liumizalo au jambo lolote lingine liwezalo kujitokeza na kuufanya mmea huo utoweke na usiwepo tena.
Na hakika dini ambayo imefaradhisha kanuni na hukumu na sheria mbali mbali katika kila jambo kati ya mambo ya kidunia na kila upande kati ya pande za maisha na kila kitendo kati ya vitendo vya mwanadamu kama kuuza, kununua, kuhamishwa deni kutoka kwa mdaiwa na kuhamia kwa mdhamini (hawala), na kuchukua dhamana, kukodisha na kuweka wakala, kulima na kumwagilia, kukopa na kuweka rehani, kuoa na kutaliki, kuwi-nda na kuchinja, na kuhusu vyakula na vinywaji, hukumu na kulipa fidia. Hakika dini kama hii haiwezekani kwake kuliacha na kutolitilia umuhimu suala la uimamu, nalo kama lilivyo katika umuhimu wake na nafsi yake katika uwekaji wa sheria na kuongoza dola na majukumu yake ya kuwaelekeza watu kwenye mwendo wa kiislamu, kuelekea kwenye kukamilisha aliyo yaanzisha Mtume(s.a.w.w) katika ujenzi wa jengo jipya.
Na kuwa uislamu ambao ulilenga katika sheria zake zote kuweka uadilifu na usawa na utulivu kwa ajili ya waislamu na kumpatia amani kutokana na mambo yake yenye kuogopesha, na kumlinda na maovu yote, chini ya itikadi tukufu yenye kumu-unganisha na Mwenyezi Mungu Mtukufu na viungo vyake kutawaliwa na tabia zilizomo ndani ya nafsi yake zimzuwiazo kufanya khiyana na uovu na uharibifu na kutenda mambo mabaya.
Hakika uislamu hauwezi kulithibitisha na kulifikia lengo hilo kubwa -kwa mtazamo wetu mdogo- bila kuwepo Imamu alie teuliwa kwa dalili, na Imamu huyo awe mbali na mambo wayafa-nyayo watu wengine kama kukosea au kutetereka na kuyafata matamanio na kufanya uharibifu, yaani mambo maovu au kusema kauli mbaya na kuathirika na matendo yasiyo ya uadilifu matendo ambayo humfanya hakimu kuwa muovu, na kwa kuhari-bika kwa hakimu na kuwa muovu hupelekea maisha ya watu kuharibika na pia dini yao na nidhamu yao kwa ujumla.
Ni lazima kwa ajili ya kuepukana na maovu yote hayo awepo Imamu alie chaguliwa na Mwenyezi Mungu alie kusanya sifa zote za ukamilifu, alietakasika na sifa yoyote ichukizayo, na kuepuka-na na aina zote za uovu katika matendo na kukosea kwenye makadirio na kwenda kinyume na mafundisho ya sheria na haya ndio tuyaitayo kwa jina la "Ismah". Ni jambo lililo wazi kuwa kumteua mtu aliekusanya sifa zote hizi ni jambo gumu kwa raia wenye kutawaliwa na wenye kuchagua. Kwa hivyo basi ni lazima kuwepo dalili ya Mtume na zikiainishi kuhusu suala hili na kitu cha kuuongoza umma na kuuelekeza katika suala hili.
Na Ismah (yaani kuhifadhika huku kutokana na kutotenda madhambi) kuliko ashiriwa si jambo la kushangaza au kustaaja-bisha kama ionekanavyo kwenye maneno ya baadhi ya watafiti kwenye madhehebu za kiislamu, na hasa kwa mustashrikina, bali si miongoni mwa vitu vya lazima kwa mtawala au hakimu ambae miongoni mwa majukumu yake ni kuitafsiri na kuifafanua Qur'ani tukufu na kutekeleza hukumu zake na kuyatolea ufafanuzi na ufumbuzi mambo yake yaliyo fungika na yasiyo eleweka.
Hakika, Ismah katika maneno ya waarabu ina maana ya kuzuwia[11] na maana hii ndio tuikusidiayo kwenye istilahi zetu, na Ismah katika istilahi hii ina maana ya uzoefu wa kinafsi kumtawala au kummiliki mwanadamu na kumzuwia kufanya maasi na kuuacha utiifu na kuitawala akili yake na hisia zake na viungo vyake na kumfanya awe ni mwenye kuamka na kuelewa kwa kiasi kikubwa (kwa wakati wote) na kumfanya asiwe ni mwenye kusahau wala kughafilika wala kufanya matendo yasiyo ridhiwa na Mwenyezi Mungu.
Hakika mwenye kufanya maasi ni dhalimu katika istilahi ya Qur'ani.
"Na mwenye kuvuka mipaka ya mwenyezi Mungu hakika hao ndio madhalimu "
"Na mwenye kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu hakika amesha idhulumu nafsi yake ".
"Hawa ndio ambao walimsingizia uwongo Mola wao, hakika laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya madhalimu ".
"Kisha tutawaokoa wale ambao walimcha Mwenyezi Mungu na tutawaacha madhalimu humo wakiwa wamepiga magoti ".
Na mfano wa aya hizo ambazo ni nyingi ndani ya Qur'an tukufu.
Na mfanya maasi huyo ambae Qur'ani imemuita "dhalimu" hawezi kuvumilia kubeba majukumu ya sheria yenye kuhusiana na Mwenyezi Mungu Mtukufu na dini yake na sheria yake. Hayo ndio yaliyo tajwa waziwazi na Qur'ani tukufu kwa kusema:
"Na pindi Mola wako alipomfanyia majaribio Ibrahim kwa maneno akayatimiza (Mwenyezi Mungu) Akasema:"Hakika mimi nimekufanya uwe Imamu kwa watu. (Ibrahim) akasema na katika kizazi changu je! (Mwenyezi Mungu) Akasema: Ahadi yangu haiwapati madhalimu ".
Na bwana Fakhru Razi amesema katika kuitafsiri aya hii:"Imethibiti kwamba makusudio ya ahadi kwenye aya hii ni uimamu Na ikiwa aya inajulisha kuwa Imamu hawi muovu, basi aya hii kutujulisha kuwa Mtume haifai kuwa muovu na mwenye kufany a madhambi na maasi ni kwa njia bora zaidi[12] .
Kwa hivyo inaonekana kuwa maana ya "Ismah" na kuijalia kuwa ni sharti la uimamu na imamu sio fikra ngeni au itikadi ya ajabu, bali hiyo ndio maana inayo wiana na dalili za kisheria zilizo sahihi na ni fikra ya asili ya dini.
Dr Ahmad Mahmoud Subhi katika maelezo yake juu ya mas'ala ya "Ismah" kwa mashia amesema:
"Hakika wanafalsafa wote wa siasa walipo yazungumzia na kuyafanyia utafiti maudhui ya uongozi au utawala wa juu katika dola na serikali au kiongozi wa juu kabisa katika serikali, waliiweka na kuipa nafasi ya juu ya kiwango cha Shubha (kisichokubali kuingiwa na shaka) na wanafalsafa pia wanasiasa wenye kuamini siasa ya kidikteta na wale waliothibitisha kuwa kiongozi wa juu kabisa serikalini ni hakimu (mtawala) walithibiti-sha sharti la ismah hata ingawa walichagua sifa zingine anazota-kiwa kuwa nazo.
Na vilevile wanafalsafa wa mfumo wa demokrasia waliwasifia wananchi au wawakilishi wao au katiba kuwa ni vyenye ismah (yaani wasio fanya makosa). Na inadhihirika kuwa kuhifadhika na kutotenda makosa (Isma) ni lazima kuwe ni sifa ambayo anasifika nayo mwenye jukumu la uongozi wa juu katika dola kama dhamana pekee ya kubakia kwa nidhamu ya utawala na sababu ya kuungwa mkono na wananchi.
Hakika nidhamu zote au mifumo yote ya kisiasa pamoja na tofauti zake, zinakubaliana juu ya ulazima na wajibu wa kuwepo serikali ya juu kabisa ambayo ndio inayo kuwa marejeo ya hukumu zote, na yeyote hawezi kuwa ni mwenye cheo au madara-ka kwenye serikali hiyo vyovyote atakavyo kuwa amemtawala yeyote au utashi wa watu wote au katiba isipokuwa tu atakapo kuwa amepambika na aina fulani ya utakasifu na kusifiwa na sifa ya Ismah (yaani asiwe ni mwenye kufanya makosa).
Kwa hivyo basi, ismah ya Imamu wa kishia si jambo lenye kushangaza, vyovyote neno hili litakavyo onekana kuwa na habari za ghaibu (za mbinguni). Na ikiwa mashia ndio wa mwanzo walianzisha utafiti kuhusu uhakika na undani wa Ismah na mipaka yake lakini si wao peke yao ambao wameshikamana na kauli hiyo.[13]
Na vyovyote mambo yatakavyo kuwa, imekwisha dhihiri kutokana na yaliyotangulia kuwa mashia katika upingaji wao wa kuchaguliwa imamu na watu, hawakutoa upingaji huo kutokana na mwelekeo fulani wenye kutawaliwa na hisia kwa mtu fulani au kutokana na rai fulani ya kisiasa kwa maana inayo eleweka ya kisiasa, bali waliona kutoka kwenye uteuzi kupitia dalili (Qur'ani na Sunna ya mtume) dhamana ya maisha mema na nyenzo salama ya ujenzi,[14] wao hupata msukumo wa kuiunga mkono rai hii kutokana na roho ya imani ya uislamu na kuwa na ikhlasi ya kufikia lengo (walilo umbwa kwa ajili yake) na kwa kuhisi maslahi yaliyopo. Na hivyo inatuwia wazi kuwa kauli isemayo kuwa ni lazima kuwepo uteuzi:
1- Inaungana moja kwa moja pamoja na hisia za kimaumbile ndani ya mwanadamu, kitu kinacho zaa hisia ya kuwepo mahita-jio ya nguvu ya ghaibu na kuitii kwa mambo yote.
Na uimamu -kama tunavyo fahamu- ndio kichwa cha mambo hayo ambayo humfungamanisha mwanadamu na nguvu hiyo ya ghaibu kwa kupewa hali ya kuhisi utulivu na raha na kusalimu amri kiukamilifu kwenye njia ya salama na mwendo wake kuwa thabiti kwenye njia hiyo.
2- Kauli hiyo inaungana vilevile pamoja na elimu ya nafsi isemayo kuwa ni lazima kung'oa mizizi ya vitu vimpelekeavyo mtu kuwa na hali ya kuchukia na kuwa na wasiwasi na ni lazima kumkataza au kumzuwia asiwe na roho ya kutoitii kanuni.
Na pindi Imamu anapo kuwa ameteuliwa na yule Mwenye wahyi (au Mtume) moja kwa moja, kila mtu atakuwa na matu-maini ya mia kwa mia ya kuenea na kutawala uadilifu na utakasifu na usawa wa kweli na ikhlasi iliyo ya kweli. Na kwa kufanya hivyo mambo yote yasababishayo wasi wasi au kero au uchovu na kutozitii amri yatatoweka.
3:Na pia inaungana na rai waliyo shikamana nayo wanazuwoni wote wa mambo ya jamii kuwa dini ni mfumo wa juu zaidi wa kuunganisha na kuleta mshikamano kwenye maisha ya jamii, na yale yahisiwayo na watu wa dini hizo kama udugu na umoja na kuridhiana kiukamilifu.
Na Imamu alieteuliwa kwa dalili ndie mtu wa juu kabisa na hakuna shaka yeyote katika kazi ya kuunganisha na kuleta mshikamano ulio ungana na chanzo cha juu kabisa (Mwenyezi Mungu) na katika kuhifadhi imani kuwa uchaguzi wake ulikuwa mzuri na uteuzi wake ulikuwa salama.
Na fikra hii haitoweza kudhurika baada ya kuthibiti asili yake kuwa ni ya kiislamu, iliyo chukuliwa kutokana na dalili za Qur'ani na hadithi za Mtume, na baada ya kuthibitika uwiano na muungano wake pamoja na hisia za kimaumbile na misingi ya kielimu ya elimu ya nafsi na elimu ya jamii, hata kama mtu yeyote atajitokeza na kuipinga au kuibeza au kuipa majina tofauti atakayo.
Naam, uimamu hautodhurika baada ya kuthibitika yote hayo yaliyo tangulia kwa kuitwa na baadhi ya waandishi kwa jina la "Theocracy"[15] (yaani utawala wa kidini). Hakika jina hili likikusu-diwa "Hukumu ya dini" halina matatizo, bali hali ndivyo ilivyo kiukweli wake. Na ikikusudiwa kwa jina hilo kuwatawala "kimabavu" watu kwa jina la dini kwa kulinganisha na utawala mbaya wa kanisa siku za kale, kufanya hivyo ni kinyume na uhakika wa uimamu katika nadharia na katika utekelezaji.
Na kwa kuyazingatia hayo Dr.Majiid khaduri alilipinga jina hilo kwa kutowiana kwake na ukweli ulivyo, na akachagua jina lingine alilo litoa kwenye mifumo madhubuti ya uislamu nalo ni "Nemocracy"[16] yaani utawala ambao uongozi wake ni wa kanuni.
Na huu ndio ukweli ambao mwenye shaka na mpingaji hawezi kuupinga vyovyote watakavyo zama kwenye shaka na upingaji. Na uimamu vile vile hautadhurika ikiwa baadhi ya waandishi watauita kwa jina la "udikteta". Kwani utawala wa kidikteta ni utawala ambao nafasi ya uongozi wa juu ni ya mtu mmoja au watu kadhaa maalumu, kwa hivyo dola linakuwa ni milki au mali ya watu wale na huzichezea kanuni na sheria kama watakavyo, na haya yana pingana -kiukamilifu- na mfumo wa utawala wa kiislamu ambao unauzingatia uongozi wa juu kuwa ni uongozi wa kanuni pekee, na sio wa kitu kingine. Na nijambo lililo wazi kuwa uongozi wa kanuni kama alivyo utekeleza Mtume na kuonekana kwenye zama zake au utawala wa Imamu wa kwanza Ali bin Abi Twaalib(a.s) katika hali ya kawaida na wakati wa vita, uongozi huo na udikteta ni vitu viwili vinavyo pingana.
Kisha uimamu hautodhurika kuitwa kwa jina la "Utawala wa kitabaka" au utawala wa tabaka fulani, kama ulivyo itwa na baadhi ya waandishi. Na ni jambo lenye kueleweka kuwa utawala wa "tabaka fulani" maana yake ni kuidhoofisha sheria yote kwa ajili ya maslahi ya tabaka lile na kuvielekeza vyombo vyote vyenye nguvu kuyaendeleza maslahi makhsusi na ya kibinafsi ya tabaka hilo. Na hayo ni mambo ambayo hayana ukaribu na uhusiano wowote na Uislamu kwa aina yoyote ile na kwa mahusiano ya aina yoyote.
Hakika uongozi wa kanuni ya kuvitawalisha vyanzo vya sheria na kutomruhusu yeyote hata Imamu mwenyewe kubadili-sha dalili (Qur'an na suna) na kuzigeuza hukumu kunakata mahusiano kati ya Uimamu na kila fikra ya utabaka ambayo huenda baadhi wakajaribu kuilinganisha na kuihusisha na nidhamu hii (ya uimamu).
Na mwisho - na sio mwishoni- uimamu hauto dhurika kuitwa kuwa ni mfumo "usio wa kidemokrasia". Kwa hakika thamani ya kimsingi ya demokrasia -ikiwa kama nadharia- hudhihiri katika msemo wake usemao "Utawala wa wananchi"(au utawala wa watu) nayo thamani ya kimsingi ya watu na utawala wao inatokana na kuamini kuwa "watu ndio chanzo cha tawala zote" (au serikali zote).
Na kutokana na ukweli kuwa Mwenyezi Mungu -kwa nadharia ya kiislam- ndie afanyae alitakalo, ilikuwa ni lazima kukiri na kukubali kuwa yeye ndie kauli ya mwisho katika kila jambo kati ya mambo ya utawala na nidhamu.
Na ukizingatia kuwa Mtume ndie mtamkaji pekee kwa jina la chanzo cha tawala na muwakilishi muaminifu wa huyo mwenye kauli ya mwisho (Mwenyezi Mungu) hakika kumteuwa kwake Imamu unakuwa ni uteuzi wenye kuridhiwa utokeao kwenye chanzo hicho cha sheria, na kwa kufanya hivyo atakuwa ameungana na mantiki (fikra) ya kisiasa isemayo kuwa ni lazima kukitaka ushauri chanzo cha tawala zote katika uchaguzi na uteuzi.
Muhtasari wa sehemu iliyo tangulia ni kama ifuatavyo:
Hakika uimamu ni lazima kuwepo ili kuendesha na kundeleza mwendo wa kiislam. Na uimamu haupatikani isipo-kuwa kwa kutumia dalili na uteuzi kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) mwenyewe kwa kuzingatia kuwa ni mtu ambae hatamki kwa matamanio au matakwa yake.
Na kwa kumaliza sehemu hiyo ya utafiti kwa muhtasari huo ulio wazi tuna hamia kwenye hatua mpya inayo kusudia kumtafuta imamu alie teuliwa kwa dalili na kuzitafuta dalili tukufu ambazo zimemtaja imamu mwenyewe.
Na kutokana na kuwa dalili za uimamu riwaya zake ni nyingi sana pamoja na wapokezi wake na ni zenye mifumo tofauti ya kutoa ushahidi na ambazo hazihesabiki kwenye sehemu finyu kama hii, sisi tutakomea katika kuzitaja tatu kwa haraka, tukiyaacha mazungumzo marefu na mapana yenye kuelezea pande zake zote kwenye vitabu vikubwa vilivyo jihusisha na maudhui haya.
Hadithi ya nyumba (Hadithu ddarr)
Ameitoa Ibnu jariir At-twabari kwa upokezi wake kwamba Mtume(s.a.w.w) pindi ilipo telemka kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:
"Na waonye jamaa zako wa karibu"ali-waita wana wa Abdul-Muttwalib kwake, wakiwemo ami zake (baba zake wadogo ), kama vile Abu-Twalib, Hamza, Abbas na Abu Lahab.
Na walipo maliza kula Mtume wa Mwenyezi Mungu akasimama kati yao kwa ajili ya mazungumzo na akasema:"Enyi wana wa Abdul-Muttwalib, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi simjui kijana yeyote katika waarabu alie waletea kaumu yake (watu wake) kitu bora zaidi ya kile nilicho kuleteeni. Hakika mimi nimekuleteeni kheri ya dunia na akhera. Na Mwenyezi Mungu ameniamuru nikuiteni kwenye kitu hicho, sasa ni yupi miongoni mwenu atanisaidia juu ya jambo hili ili awe ndugu yangu na wasii wangu na khalifa wangu kati yenu? Watu wote wakanyamaza. Ghafla Ali(a.s) akasimama na kusema:"Mimi, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nitakuwa waziri wako (msaidizi) juu ya jambo hilo". Mtume(s.a.w.w) akasema: "Hakika huyu ni ndugu yangu na wasii wangu na khalifa wangu kwenu msikilizeni na mumtii". Watu wale wakasimama huku wakicheka na wakimwambia Abu Twalib:"Hakika amekuamuru umsikilize mwanao na umtii".[17] Hakika dalili hii ya kihistoria imekusanya sifa tatu za Ali:
1- Waziri (Msaidizi)
2- Wasii (Muusiwa)
3- Khalifa (Mshika makamu)
Na ni haki yetu kujiuliza na kusema:
Kwa nini Mtume alimpa Ali sifa hizo tatu na asiwape wengine? Na ni kwanini alichagua mjumuiko wa kwanza kufanyi-ka baada ya kupewa utume kwa ajili ya kufanya jambo hilo?
Na ikwa usaidizi ni lazima kwake kwa kuzingatia kuwa yeye alihitajia -kwa wakati huo- kuwa na msaidizi na waziri kwa nini basi, aliongeza cheo cha wasii na khalifa kwa matamshi haya mawili? Na kuna uhusiano upi kati ya usia au muusiwa na khalifa katika kuwaonya jamaa zake na kuwaita watu wa familia yake kwenye uislamu?
Na kwa ajili ya kuweka wazi jawabu la maswali haya, ni lazima tusisahau na kughafilika kuwa Mtume(s.a.w.w) katika mazungumzo haya anatangaza kwa mara ya kwanza mwanzo wa dola jipya na zama mpya na jamii mpya.
Na anatangaza kuwa utawala wowote au jambo lolote ili libakie hai na liwe ni lenye kuendelea ni lazima liwe na raisi au kiongozi wa juu kabisa mwenye kuongoza jambo hilo na kuuelekeza usukani wake na nilazima kuwepo naibu wake ambae watu watamrejelea ikiwa raisi atapatwa na jambo fulani la kumfanya asifanye kazi yake.
Na Mtune(s.a.w.w) katika mazungumzo na msimamo ule alikuwa akilenga kuwafahamisha watu wale walio hudhuria kwamba mas'ala haya ya kidunia na kidini sio mas'ala ya kutawala tu na kuyatumia kujikingia kwa kivuli chake au ni uraisi anao utumia na kufaidika nao maadamu yuko hai, bali ni ujumbe kutoka mbinguni na ni ujumbe wa milele hautokufa kwa kufariki kwake na hautakwisha kwa kumalizika kwa umri wake bali utabakia kwa muda wote wa kubakia kwa mbingu na ardhi, na baada yake kutakuwa na mtu atakae beba majukumu hayo na kutekeleza mambo yake yote, nae ni kijana huyu ambae anatangaza uwezo wake na maandalizi yake ya kujitolea muhanga na kujitoa fidia na kuwa msaidizi, na si mwingine tumkusudiae, bali ni Ali bin Abi Twalib(a.s) .
Na haya yote tunayapata pindi tunapofanya utafiti na kudadisi kwa uwazi kwenye hadithi tukufu ya Mtume tuliyo itaja hapo punde.
Na Imamu Raazi kutokana na kutopata kigezo cha kuto ikubali na kukiri usahihi wa hadithi hii na sanadi (upokezi wake) na kuwa ni dalili iliyo wazi, akafanya haraka kutia shaka kwenye maana ya ukhalifa ulio tajwa kwenye hadithi, akidai kuwa Mtume(s.a.w.w) angekuwa amekusudia pindi alipo fanya hivyo kumteuwa khalifa baada ya kufariki kwake asinge ishia kusema "na khalifa wangu kwenu", bali ange ongezea kwenye ibara hiyo neno "bada yangu" ili iwe ni dalili iliyo wazi.
Na ukweli ni kuwa sisi hatuoni tofauti kati ya ibara hizi mbili. Na ikiwa "Khalifa wangu kwenu baada yangu" iko wazi katika ushahidi wake, vile vile "Khalifa wangu kwenu" ni hivyo hivyo, kwa sababu maana yake ni kuwa Ali ndie ambae atakaekuwa khalifa wangu na atakae chukua nafasi yangu kwenu ikiwa nitapatwa na jambo lichukizalo (yaani kifo), na hii ni dalili juu ya ukhalifa baada ya kufariki, na maana hii inatiliwa mkazo na neno "wasii" alilo taja Mtume.
Usia katika Uislam unakusudiwa baada ya kifo, kiasi kwa-mba muusiwa (wasii) hufanya aliyotakiwa ayafanye yule alietoa usia. Na jambo hilo kama lingekuwa linahusu mambo yaliyo kabla ya kifo angesema "Wakili wangu" na asinge sema "Wasii wangu", kwa sababu uwakili ndio ibara itumikayo kwenye uislamu kwa anaetakiwa kutekeleza baadhi ya mambo ya mtu aliepo na alie hai.
Kwa hivyo basi, dalili iko wazi kuwa Mtume(s.a.w.w) tangu siku ya kwanza alichagua mtu atakae kuwa baada ya kufariki kwake kwa ajili ya kuendeleza kazi ya wito na atakuwa ni wasii wake katika kuyalinda mambo ya waislamu, ili jahazi lisiende mrama na kuwa chini ya huruma ya mawimbi na pepo kali baada ya kufariki nahodha wake. Na huu ni mwanzo uliodhihiri na kuchomoza pamoja na sauti ya kwanza iliyo sikika ya wito wa kiislamu, wito ambao nafasi yake ilikuwa ni finyu na katika siku zake za mwanzo, na akaendelea kusisitiza na kutilia mkazo kwenye mwanzo huo hadi siku ya mwisho ya umri wake Mtume wa uislamu.
Hadithi ya cheo (Hadithul-manzilah)
Ameitoa Muslim kwa upokezi wake kwamba Mtume(s.a.w.w) alimwambia Ali:
"Wewe kwangu ni sawa na cheo cha Haruna kwa Mussa, isipokuwa hakuna Mtume baada yangu ".[18]
Hadithi hii tukufu, pamoja na ufupi wa matamshi yake inaashiria kwenye maana nyin gi ambazo huenda zisionekane wazi kwa mtizamo wa haraka haraka, lakini maana hizo zina onekana wazi bila kizuizi pale msomaji atakapo fanya udadisi kidogo kwenye upana wa maneno na maana zake na makusudio yake.
Hakika hadithi ina ashiria kuwa Ali:
A: Ni waziri wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwani Haruna alikuwa ni waziri wa Mussa, kama aya isemavyo:
"Na uniwekee waziri (msaidizi) kutokana na jamaa zangu ".
B: Ni ndugu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Kwani Haruna alikuwa ni nduguye Mussa kama aya isemavyo: "Haruna ndugu yangu ".
C: Ni mshirika wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwani Haruna alikuwa ni mshirika wa Mussa kama aya isemavyo:
"Na mshirikishe kwenye jambo langu".
D: Ni khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwani Haruna alikuwa ni khalifa wa Mussa kama aya ilivyo sema:
"Na akasema Mussa ku-mwambia nduguye Haruna:"Kuwa Khalifa wangu kwenye jambo langu hili".
E: Ni uimamu chimbuko lake kuwa ni utume, kwani dhamiri " anta" iliyo tumika kwenye hadithi inauelezea uimamu na dhamiri ya (yee) kwenye tamko (minniy) ina uelezea utume, na herufi ya jari hapo ina maana ya kuanza na kuwepo, na ili isitumike katika uanzaji huu na chimbuko hili kuwa kuna ulingano kati ya maana zake au vitu hivyo kuwa sawa Mtume akafafanua kuwa kuna tofauti ya msingi ambayo ni utume akasema:"Isipokuwa ni kwamba baada yangu hakuna utume"
Na kutokana na kuwa Mussa alikuwa ame-muo mba Mola wake amuwekee waziri (msaidizi) kutokana na jamaa zake, kama aya ilivyo tujulisha, hakika hilo linatujulisha kuwa ukhalifa na uwaziri kwa ajili ya Mtume unawekwa na kujaaliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na sio uchaguzi wa watu au kwa uteuzi wao.
Na hivi ndivyo mtazamo wa udadisi unavyo tuwekea wazi zile maana pana za mbali ambazo hadithi hupanuka na kuzifikia, nazo ni maana zenye kina, ambazo haifai kuzitafsiri kwa msingi tu wa kumtukuza na kumfurahisha Ali(a.s) , bali nyuma yake kulikuwa na lengo kubwa, nalo ni kuutanabahisha umma na kuu-fahamisha atakae shika nafasi ya Mtume baada ya kufariki kwake katika suala la kuliongoza dola na kuliongoza jahazi na kuuelekeza usukani wake.
Na ushirika ulio elezwa na hadithi hii, ushirika wa Ali kwa Mtume -Sio ushirikiano wa kibiashara kwenye bidhaa au uundaji au kilimo- unakusudiwa ni ushirika katika kubeba majukumu ya uislamu na kutekeleza mambo muhimu yanayo husiana na dini hii. Na kutokana na kuwa ushirika huenda mipaka yake ikafi-chika na isieleweke kwa msikilizaji wa kawaida (na hasa baada ya kufahamu utume wa Haruna). Mtume akaielezea hadithi ya cheo kwa kueleza mambo yanayo ondoa dhana na kuelezea makusudio ya ushirika huo akapinga kuwepo kwa Utume kwenye ushirika huo moja kwa moja na kuuweka utume nje ya ushirika huo kama tulivyo tangulia kusema.
Na huenda mambo yadhihirishayo wazi umuhimu wa hadithi hii na ushahidi wake na dalili yake na upana wake ni kufahamu kuwa: Sababu iliyo mpelekea Mtume kutangaza cheo hiki ilikuwa ni wakati alipo muacha Ali akiwa naibu wake na mshika nafasi yake kwenye mji wa madina pindi alipo toka kwenda kwenye vita vya Tabuk.
Na Sheikh Ibnu Taimiyya alipinga na kusema kuwa katika mnasaba wa tukio hili hakuna kitu kithibitishacho fadhila yoyote kwa Ali kamwe kwenye hadithi hii kwa sababu Mtume alifuatana na maswahaba wengi na muuminina, na Ali hakumuacha isipo-kuwa na wanawake na watoto, seuze wale ambao hawakwenda vitani na wanafiki na kumuacha mtu kwenye uangalizi wa watu kama hawa hakuna maana yoyote kati ya maana za utukufu na kukirimiwa.[19]
Lakini mwenye kufanya mazingatio na kuelewa mambo atatoka na natija nyingine, tofauti na natija aliyo iona Ibnu Taimiyya anapo soma mazingira ya hadithi hii:
Mji wa madina, ulikuwa ni mji mkuu wa dola na makao makuu ya Utume na Mtume. Na pindi raisi anapo safiri na kuacha mji mkuu na kwenda sehemu ya mbali, kama Tabuuku, na kwa kutumia nyenzo za kizamani na za mwanzo katika mawasiliano na zenye kutumia muda mrefu, na vita havieleweki ni lini vitamalizika, na ni wakati gani watarudi kutoka vitani, bila shaka kuchagua kwa raisi huyu naibu atakae shika nafasi yake kwenye mji mkuu, na hasa mji mkuu ambao ulikuwa umezingi-rwa na hatari mbali mbali na wanafiki na maadui wenye kusubiri fursa yoyote na wakati wowote ili wauchukue mji huo au cheo hicho, mazingira hayo yana tufafanulia kwa uwazi maana kubwa na ya hatari katika uchaguzi huo na uteuzi huo.
Hadithi ya bonde la ghadiir. (Hadithul Ghadiir).
Wameipokea hadithi hii maswahaba wengi sana na taabiina, na maulama na mahufadhi wameipokea pia.[20]
Na kwa ajili ya kufupisha tutachukua kwenye hadithi sehemu ya ushahidi, sehemu ambayo imeungana na hadithi moja kwa moja juu ya uimamu na uteuzi wa imamu. Msimuliaji wa hadithi hii amesema:
Mtume alipokuwa njiani akitokea kwenye hija ya kuaga (ya mwisho) na alipo kuwa amefika sehemu iitwayo Ghadir-Khum, alisimama baada ya sala ya adhuhuri ili kuhutubia kati ya waislamu na miongoni mwa mambo aliyo wambia ni kama ifutavyo:
"Enyi watu! Huenda nikaitwa na kuitika, na mimi nitauli-zwa, nanyi mtaulizwa ni kitu gani mtakacho sema? Wakasema: "Tunashuhudia ya kuwa wewe umefikisha ujumbe na umepigana jihadi na umetoa nasaha. Mwenyezi Mungu akulipe kheri. Mtume akaendelea kuzungumza hadi akasema:"Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtawala (Bwana) wangu, na mimi ni mtawala (Bwana) wa waislamu, na mimi ni bora zaidi kwao kuliko nafsi zao. Kwa hivyo basi yeyote ambae mimi nilikuwa mtawala (Bwana) wake huyu Ali ni mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu mpende mwenye kumpenda Ali na mfanyie uadui mwenye kumfanyia uadui Ali, na mnusuru mwenye kumnusuru Ali, na ifanye haki, iwe pamoja na Ali popote atakapo kuwa.
Na mtume akamalizia maneno yake nao watu wakamki-mbilia Ali na kumpongeza na kusema: "Hongera! Hongera! Ewe Ali! Umekuwa mtawala wetu na mtawala wa kila muumini wa kiume na wa kike". Kisha akateremka Jibrilu na wahyi wa Mwenyezi Mungu na kusema:
"Hivi leo nimekukamilishieni dini yenu, na nimezitimiza kwenu neema zangu, na nimeridhia kwenu uislamu kuwa ndio dini". Huu ndio ufupi au muhtasari wa hadithi ya Ghadiri Khum na mazingira yake, na haya ndio matamko yaliyotumika kama yalivyo simuliwa na wathibitishaji. Na imekuja ikiwa wazi kabisa katika kuthibitisha fikra ya "Uimamu" yenye utawala wote na majukumu yaliyo mapana na katika kumteua "Imamu" mwenye majukumu baada ya kufariki Mtume(s.a.w.w) . Na inatutosha dalili moja juu ya uwazi huo nayo ni waislamu kufahamu hivyo na kuharakia kutoa baia, kitendo ambacho kilikuwa ni natija ya kufahamu kwao jambo hilo, na kwenda kumpongeza na kuonye-sha furaha yao kwa mnasaba huu au tukio hili tukufu na zuri.
Na wakajitokeza kwetu baada ya muda fulani, watu wenye kudai kimakosa kuwa ni wenye falsafa, na kusema baada ya kufahamu usahihi wa hadithi hii na kutokuwepo uwezekano wa kuipinga, kuwa haikuwa ni dalili juu ya suala hilo, kwa sababu tamko "maula" katika lugha ya kiarabu linatafsiriwa kwa maana nyingi, kama mfuasi, mwana wa baba mdogo, rafiki, mrithi, na mfano wa hizi, na hatufahamu Mtume alikusudia nini kwa kutumia tamko hilo, na ni maana ipi kati ya maana hizo aliikusudia.
Na huku kujifanya wanafilosofia (wachambuzi) kulitokana na matamanio na malengo fulani, na yaliyo mbali na utafiti wa kina na kimaudhui. Na inatosha katika kubatilisha madai haya kufanya mazingatio ya kina kwenye mambo yafuatayo:
1- Kuteremka kwa aya ya tablighi kabla ya Mtume(s.a.w.w) kusimama na kutangaza utawala (wilaya). Wanahistoria wamesimulia na mufassirina kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimle-tea wahyi Mtume wake akiwa ametokea Makka baada ya hija ya kuaga na kusema:
"Ewe Mtume fikisha ulicho teremshiwa kutoka kwa Mola wako, na kama hukufanya utakuwa hukufikisha ujumbe wake na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu ".[21]
2- Mtume(s.a.w.w) kusimama katikati ya jangwa na kwenye jua kali la adhuhuri kwa ajili ya kutangaza utawala huo.
3- Kuelezwa tawala za aina tatu kwenye maneno ya Mtume(s.a.w.w) :
A: Mwenyezi Mungu ni Mtawala wangu.
B: Mimi ni mtawala wa waumini.
C: Yeyote ambae nilikuwa ni mtawala wake huyu Ali ni Mtawala wake[22] .
4: Kumalizia khutuba au mazungumzo yake kwa kumuombea:
"Ewe Mwenyezi Mungu mpende ampendaye na mfanyie uadui mwenye kumfanyia uadui na umnusuru mwenye kumnusuru na muache mwenye kumuacha na ifanye haki iwe pamoja naye popote atakapo kuwa".[23]
Na kwamba dua haiwiani kamwe na jambo au maana nyingine tofauti na utawala wote (mpana) na uongozi juu ya waumini.
5- Kuteremka kwa aya ya kukamilisha dini tuliyo itaja hapo kabla:
Ijulishayo kutokea kwa jambo la hatari na muhimu ambalo Mwenyezi Mungu aliikamilisha dini na kuitimiza neema ya jambo hilo.[24]
6- Na waislam walio kuwepo kwenye tukio hilo kumponge- za Ali kwa mfumo tulio utaja.[25]
Hakika kwa kufanya udadisi kwenye pande zote hizi sita kunatufanya tuamini kwa imani kamili na yakini kamili kuwa makusudio haikuwa kuwazindua waislam kwamba Ali ni mrithi au mfuasi wa Muhammad au ni rafiki yake au kuwa ni mwana wa ami yake.
Na mas'ala ya urithi au kunusuru, lau kama Mtume angetaka kuyazungumzia hayo yalikuwa hayahitajii kuyaelezea kwenye hali na mazingira kama yaliyo kuwepo siku ya tukio la Ghadir Khum, kama vile mazingira yenyewe na kwenye mnasaba ule, pia kuteremshwa kwa aya na Mwenyezi Mungu kati ya aya zilizo wazi, na kutumika mifumo maalumu ya kumpongeza Ali na kumbariki bali yote hayo hayatakuwa na maana yenye kukuba-lika kama usingekusudiwa uimamu na kumteua khalifa na kutoa kiapo cha utiifu (bai'a).
Na huenda Dr Ahmad Muhammad Subhi akawa ameuleta karibu ukweli au ameufikiria, kwa yale aliyo yatolea ushahidi katika kutoa sababu ya kukataa kwa walio kataa hadithi hii pale alipo sema:
"Kwa kuwa Ahlu dhaahiri na Salafiya walikuwa wakimfuata Muawiya kama mtawala hakika hawakuwa na kimbilio tofauti na kuchagua ima kuuacha utawala huo au kuipinga hadithi hii kwa kutumia nyenzo mbali mbali. Na pamoja na kuwa ni wajibu itikadi zetu zifuate dalili, isipokuwa ukweli ni kuwa watu wengi wenye madhehebu, walizifanya hadithi ziwe ni zenye kuyanye-nyekea matakwa yao na madhehebu yao.[26]
Kwa hivyo imethibiti kutokana na yote yaliyo tangulia kwamba Mtume(s.a.w.w) alitoa dalili juu ya Imamu ambae atachu-kua nafasi yake katika kuuongoza umma huu. Na dalili iliyo ashiriwa, hata kama matamshi yake yatatofautiana na minasaba yake, ilikuwa iko wazi na mafhumu yake yalikuwa bayana.
Lakini: Je kuthibitika dalili juu ya Imamu wa kwanza Ali inatosha kuitumia na kuwateuwa maimamu wengine au ni lazima kuwepo na dalili inayo wahusu wao vilevile?
Kwa hivyo basi vipi umeweza kuthibiti uimamu wa maimamu wengine? Na iliwezekana vipi idadi yao kuifunga kwenye kumi na mbili haizidi wala kupungua?
Hakika ulithibiti uimamu wa maimamu wengine kwa njia mbili:
Njia ya kwanza:
Hadithi nyingi za Mtume(s.a.w.w) ambazo wingi wake umefikia kiwango cha kuwa mashuhuri sana, kama kauli yake(s.a.w.w) akimuelezea Hassan na Hussen:
"Nyinyi wawili ni maimamu na mama yenu ana uombezi ".[27]
Na kauli yake(s.a.w.w) akimuashiria Hussen:
Huyu ni imamu, mwana wa imamu, ndugu wa imamu, baba wa maimamu ".[28]
Na hadithi zenye mfumo kama huu ni nyingi, na ambazo riwaya zake zimo kwenye vitabu vya hadithi na historia na masomo ya juu yaliyo husika na maudhui au bahthi ya uimamu.
Njia ya pili:
Ni dalili ya alietangulia kumthibitisha atakae fuatia. Na dalili au hadithi inayotoka kwa aliyemtangulia mwenzake kumthibi-tisha wa baada yake ni hoja na ni lazima kuifuata na kuifanyisha kazi na kuitii maadamu tuna itakidi uimamu wake uliosimama juu ya msingi wa kuwa yeye ni mkweli na muaminifu juu ya wadhifu wa kuihifadhi dini (uimamu)[29] .
Ama uthibitisho wa kuwa maimamu ni kumi na mbili hawazidi wala kupungua ni nyingi vile vile.[30]
Na inatutosheleza kwa yote hayo hadithi ya Mtume iliyo mashuhuri ambayo wanazuoni wamekubaliana juu ya upokezi wake, pia mashekhe wa hadithi na mahufadhi wa sunna ya Mtume walio maarufu nayo ni kauli yake isemayo:
"Dini itaendelea kusimama hadi kiama kisamame, na kuwe juu yenu makhalifa kumi na wawili wote watokanao na (kabila la) Makuraishi ".[31]
Na katika hadithi nyingine imekuja kwa matamshi mengine:
"Hakika jambo hili halitamalizika mpaka wapite maimamu kumi na mbili ".[32]
Na pindi tunapofanya udadisi kwenye hadithi hii, ambayo waislamu wote wamekubaliana juu ya usahihi wake, tunaikuta kuwa inaweka wazi mambo mawili:
1: Kuendelea kuwepo dini hadi siku ya kiama.
2: Kuwepo makhalifa kumi na mawili tu, kwa muda wote ambao dini ita kuwepo na ikisimamia na kuyachunga mambo ya waislamu na uislamu.
Na jambo lililo wazi ni kuwa Mtume(s.a.w.w) aliposema kuwepo kwa makhalifa kumi na mbili hakuwakusudia makhalifa wale ambao waliwatawala waislamu kwa muda wa karne kumi na nne zilizo pita, kwani wao ni zaidi ya "kumi na mbili" kwa mara kadhaa, na kwamba wengi wao walikuwa hawafuati kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume, kwa hivyo haiwezekani kuwahesabu kuwa ni makhalifa wa kweli kwa ajili ya ujumbe wa Mwenyezi Mungu na Mtume(s.a.w.w) , kwa hivyo basi, ni lazima makusudio ya hadithi yawe watu wengine wasiokuwa hawa.
Na hakuna wengine wasio kuwa hawa isipokuwa Ali na wanae kumi na moja ambao waislamu wote wamekubaliana juu ya suala la wajibu wa kuwapenda na kuwatukuza, na kuchukuwa kwao hukumu za dini, na kurejea kwao katika matatizo yatupa-tayo kifikra na kisheria, na kukimbilia au kujitegemeza kwao kila linapo jitokeza tatizo au kila upepo mkali wa zama uvumapo au matukio ya zama yajitokezapo.
Na mwenye kutaka kuelewa zaidi dalili au hadithi za Mtume kuhusu suala la kuteuliwa imamu na kuelezwa idadi yao anaweza kurejea kwenye vitabu vikubwa vilivyo elezea kwa upana zaidi suala hili na masomo yaliyo panuliwa yaliyo jihusisha na maudhui haya.
Ni lazima kwangu, Ili kuukamilisha mtiririko wa hadithi hii na kukamilisha mfumo wake, kueleza kwa muhtasari, majina ya maimamu watwahirifu na mazingira ya kisiasa yaliyo mzunguka kila mmoja wao, na nina ashiria kwa muhtasari vile vile urithi mtukufu walio tuachia na historia ya maisha yao mema kwa sura ya ujumla, pamoja na kujilazimisha kiukamilifu kufupisha maelezo hayo, ili ukubwa wa kitabu usivuke kiwango kilicho kubaliwa kwenye maudhui yetu na mtiririko wetu huu.
Na yote ninayo yatarajia ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, nae ndie msaidizi na atoae tawfiiq, ni kwamba awe ndie mwenye kunisaidia kuiandika historia ya maimamu hawa watukufu, kwenye vitabu maalumu vyenye kumkusudia kila mmoja wapo kati ya maimamu kumi na wawili, ili vijana wetu wa zama hizi wawe na maarifa kamili ya mwendo na sira za viongozi wa dini yake na urithi wa kielimu walio uacha kwa ajili ya watu wa zama zote zitakazo pita, urithi ambao ni chimbuko la utajiri na nguvu, na ni sababu ya utukufu na kupata daraja za juu, na ndio mwanzo wa utamaduni na maendeleo. Hakika yeye, alie tukuka, ndie Bwana wa usaidizi na tawfiiq.
Ajulikanae kwa lakabu (sifa) yake maarufu aliyo pewa na Mtume(s.a.w.w) "Amirul-muumini " [33] .
Alizaliwa kwenye mji mtuku-fu wa Makka ndani ya nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu (kaaba) tarehe kumi na tatu (13) mwezi wa Rajab mwaka 30 tokea mwaka wa tembo.[34]
Mtume alimchagua kukaa nae akiwa bado mtoto mdogo, ili kumpunguzia kazi ya malezi Amu yake Abu Twalib, na Mwenyezi Mungu akataka Ali apate hadhi ya kulelewa na Mtume(s.a.w.w) na kumuelekeza mwenendo mwema tangu utotoni mwake.
Wakati mtume alipo tumwa na kupewa uislamu, Ali alikuwa ndie wa mwanzo kuamini na kusilimu.[35]
Na alipo waita watu wake kwenye uislamu mwanzoni mwa utume, alimteuwa Ali kuwa waziri (msaidizi) na wasii na khalifa, kama tulivyo elezea. Na Mtume alipo kusudia kuhama kutoka Makka kwenda Madina, Ali alijitolea fidia nafsi yake kwa ajili ya Muhammad(s.a.w.w) akalala kitandani kwa Muhammad ili kuwaonyesha makuraishi kuwa bado yupo kwenye sehemu yake.
Na baada ya kuhamia Madinatul-Munawwara, Ali alishiriki vita vyote vya kiislamu na kubeba bendera ya Mtume kwenye nyanja zote, na hakubakia nyuma kwenye vita vyote vya Mtume isipokuwa vita vya Tabuuk, kwani Mtume alimuacha Madina auhami na kuulinda mji mkuu wa uislamu kutokana na hatari, kama tulivyo eleza.
Mwenyezi Mungu na Mtume walimkirimu kwa kumchagua kwake awe mume wa binti pekee wa Mtume Muhammad ambae ni Fatuma Zahraa.
Na Mtume hakuyamaliza maisha yake isipokuwa tu baada ya kumteuwa Ali kuwa Imamu wa watu kwenye hadithi ya Ghadiri kama tulivyo elezea.
Hata pamoja na matukio yote aliyo yaona na kuishi nayo baada ya kufariki Mtume(s.a.w.w) hakika hakubakisha nafasi katika kutoa juhudi na nasiha na kutoa nasaha za kuutumikia uislamu na kwa ajili ya kuyatumikia maslahi ya uislamu na kuendeleza mwendo mtukufu ambao ulikuwa ni lazima uendelee na kuuhami usitetereke na kugeuka kutokana na mazingira na hali yoyote itakayo jitokeza.
Waislamu walimkimbilia baada ya kuuliwa Uthumani waki-mtaka akubali ukhalifa akaukubali hali ya kuwa ni mwenye kulazimishwa na akilazimika kuuchukua na kuukubali. Lau kama si kuhudhuria kwa watu wale walio hudhuria na kusimama kwa hoja ya kuwepo kwa wasaidizi, na kuwepo kwa ahadi aliyo-ichukua Mwenyezi Mungu juu ya maulamaa ya kuwa wasikubali shibe ya dhalimu wala njaa ya mwenye kudhulumiwa, angeitupia kamba ya uongozi huo juu ya yule wa mbali na angemnywesha wa mwisho wao kwa glasi ya yule wa mwanzo wao, na watu wangeikuta dunia yao hii kwa Ali kuwa ni kitu duni sana kuliko tembe ya maji ya puwani, kulingana na maneno yake(a.s) .
Imam alipata mitihani katika kipindi cha utawala wake kwa kupigana na Naakithiina (waliovunja bai'ah) wafuasi wa ngamia
(As-habu), na Qaasitwini (wenye nyoyo ngumu) wafuasi wa Muawiya, na Maariqina (walio toka kwenye utifu wake) nao ni makhawariji (walio toka kwenye dini).
Alifariki kwenye mji wa Al-kufa kutokana na njama chafu zilizopangwa, katika usiku wa ishirini na moja, katika mwezi wa Ramadhani, mwaka wa 40 Hijiria, na akazikwa sehemu ya juu pembozoni mwa mji wa Al-kuufa sehemu iitwayo "An-najaful Ashraf".
1
USUULID DIIN
UIMAMU
IMAMU WA PILI
HASSAN BIN ALI(a.s)
Alie maarufu kwa lakabu (jina na umashuhuri) ya "Azzakiyu"na "Al-mujtaba". Alizaliwa Madina katikati ya mwezi wa Ramadhani mwaka wa 3 H.
Amekulia kwenye malezi ya Utume na uwanda wa Qur'ani na kwenye nyumba iliyo kuwa ukishuka wahyi ndani yake. Alikuwa ni mmoja wa "Maimamu wawili wa uongofu"[36] na mmoja kati ya "mabwana wawili wa vijana wa peponi"[37] , na mmoja wapo kati ya watu wawili ambao kizazi chote cha mtume kimetokana nao, nae ni mmoja wapo kati ya watu wanne ambao Mtume aliwachukua kwa ajili ya maapizano na manasara (wakristo) wa Najran, na ni mmoja wapo kati ya watu watano ambao Mwenyezi Mungu aliwatakasa na kuwaondolea uchafu kiukamilifu.
Aliishi miaka saba pamoja na babu yake Mtume(s.a.w.w) kisha alikuwepo kwenye matukio yote ambayo baba yake alikumbana nayo na kutaabika kwa machungu yake na kuyavumilia maumivu na machungu yake, ukhalifa ulimfikia kutokana na kufariki kwa baba yake(a.s) na ulimwengu wote wa kiislamu ukampa baia (kiapo cha utii) isipokuwa Mu'awiya na watu wa miji ya Sham na akalazimika, ili kutekeleza wajibu wa kuihifadhi hii amana ya dini, kulipeleka jeshi lake ili kupambana na Muawiya na jeshi lake. Kisha utokaji ule ulimalizika kwa kufanya suluhu ambayo ni maarufu. Imamu huyu alikuwa kama babu yake alivyo sema kumuhusu: "Hakika mwanangu huyu ni Sayyid, Mwenyezi Mungu atafanya suluhu kupitia kwake kati ya makundi mawili makubwa.[38]
Utafiti kuhusu suluhu yake pamoja na Muawiya kwa kuangalia utangulizi na mazingira yake, na sababu zilizo mfanya Imamu kufanya suluhu hiyo na siri ya msimamo alio uchukua kwenye suluhu hiyo na vifungu vya mkataba wake, na masharti yake, pia ahadi zake. Kisha kuangalia ni kwa kiasi gani Muawiya alitekeleza masharti yale, ni bah'thi ambayo nafasi haituruhusu kuweza kuyaelezea, na ni juu ya mwenye kutaka ufafanuzi zaidi asome kitabu "Sulhul-Hassan". Muandishi amekusanya na kuhifadhi na akafanya utafiti mzuri, na kitabu hicho kimechapi-shwa zaidi ya mara moja.
Hakika wapigaji kelele walipandikiza na kumzulia mambo Imamu(a.s) na kudai kuwa alikuwa ni mwingi wa kuoa na kuacha, hadi mmoja wapo kati yao alidai kuwa idadi ya wakeze ilikuwa kati ya miatatu na mia tisa,[39] Lakini uchunguzi wa kihistoria haukuthibitisha kuwa na wake walio maarufu zaidi ya saba au wanane.[40] Kama ambavyo utafiti wa kihistoria haukuthi-bitisha matukio ya talaka kwa imamu zaidi ya tatu.[41]
Na Dr.Ahmad Mahmood Sub'hi amesema akifafanua suala la Imamu kuwa na wake wengi: "Huenda kuwa na wake wengi alikuwa akikusudia kuwa na wake wengi kwenye makabila ya waarabu, kwa sababu mtawala, kama maelezo ya Ibnu Khaldun yasemavyo, hutegemea katika utawala wake ukabila. Na kutoka-na na kuwa bani Umaya hawakushinda na kujimakinisha kwenye ardhi isipokuwa kutokana na asabiya (hisia ya ukabila) waliyo kuwa nayo. Hassan alielewa mambo yatakayo kuja kuwatokea watu wake wa karibu na kizazi chake kama vile kubanwa na kuuliwa ambako hakutakifanya kizazi cha Mtume kibakie na kiwe ni chenye kuhifadhiwa isipokuwa kwa kuoa kwake wake wengi na kuwa na kizazi kingi.[42]
Alifariki kwa sumu ya Muawia, kwenye mji wa Madina kwenye mwezi wa Safar, mwaka wa (50) Hijiria.[43] Na akazikwa kwenye ardhi ya Baqii' iliyotwahara.
Alie maarufu kwa lakabu ya "Seyyidu shuhadaa" (bwana wa mashahidi).
Amezaliwa katika mji wa Madina, tarehe tano mwezi wa shaaban mwaka 4.H.Alikuwa kwenye kivuli cha utume na sehemu iliyo shushwa ujumbe wa Mwenyezi Mungu, na sehemu ambayo Malaika walikuwa wakipishana, na kwenye chimbuko la elimu.
Alishirikiana pamoja na kaka yake Hassan katika sifa zote za msingi:Yeye kama nduguye, ni mmoja kati ya "maimamu wawili wa uongofu", na mmoja wapo kati ya mabwana wawili wa vijana wa peponi" na ni mmoja kati ya watu wawili ambao kizazi chote cha mtume kinatokana nao, na ni mmoja kati ya wanne ambao Mtume aliwachukua kwa ajili ya maapizano na wakiristo na ni mmoja kati ya watu watano walio takaswa kutokana na uchafu na walio twahirishwa kiukamilifu.
Aliishi miaka sita kwenye malezi ya babu yake(s.a.w.w) na akawepo kwenye matukio yote yaliyo wasibu watu wa nyumba ya Mtume tangu alipofariki babu yake hadi kuuliwa kwa kaka yake kwa sumu, na kupitiwa na mambo yaliyo msibu mama yake na yaliyo mtaabisha baba yake, na yaliyomkumba kaka yake.
Na wakati alipokufa Muawiya na yazidi kurithi ukhalifa, waumini walimtaka akubali suala la uongozi na kufanya mapinduzi dhidi ya khalifa mpya, akaitika wito au maombi yao na akatangaza kupinga kwake kutoa baia (kiapo cha utii) kwa kijana huyo mwenye pupa. Na tunaweza kuzieleza kwa ufupi sababu zilizo mfanya afanye mapinduzi katika sababu tatu za msingi:
1- Yazidi kuto stahiki na kutofaa kuwa khalifa.
2- Kumalizika kazi ya mkataba uliofungwa kati ya kaka yake Hassan na Muawiya, nao ni mkataba ambao ulielezea kwenye madda au kifungu chake cha pili kwamba "Utawala uwe kwa Hassan baada ya Muawiya na ikiwa Hassan atapatwa na tukio lolote (kifo) utawala utakuwa kwa nduguye Hussen, na haimpasi Muawiya kumpa ukhalifa huo mtu yeyote"[44] . Na maana ya mane-no haya ni kuwa Hussen baada ya Muawiya kufariki, amekuwa mwenye haki rasmi ya kuwa khalifa kwa kukubali kwa Muawiya (kukiri), pale alipo tia sahihi yake kwenye mkataba huo.
3- Mazingira yote kwa ujumla ambayo yalikuwa yakimla-zimisha kutekeleza wajibu huo. Hussen alikuwa ameshaelezea hali na mazingira pindi alipo taja sababu zilizo msukuma kufanya mapinduzi kwenye hadithi yake alipo sema: "Hakika mimi sikutoka kwa ujeuri na kiburi wala kwa kutaka shari wala nikiwa mharibifu wala sikutoka nikiwa dhalimu. Hakika nimetoka kutafuta suluhu kwenye umma wa babu yangu Muhammad(s.a.w.w) ninataka kuamrisha mema na kukataza maovu".[45]
Na amesema akiashiria kwenye mazingira hayo katika barua alizo zituma kwa baadhi ya mashia wake (wafuasi wake): "Ninaapa kwa umri wangu, si imamu isipokuwa mwenye kuhukumu kwa Kitabu, mwenye kusimamia uadilifu, mwenye kufuata dini ya kweli, mwenye kuifunga nafsi yake juu ya dhati ya Mwenyezi Mungu".[46]
Na sababu hizi zinapokuwa wazi na bayana na kudhihiri sababu za kiislamu zitiazo msukumo mkubwa wa mapinduzi hayo hapo huonekana ukubwa wa makosa aliyo fanya Abubakari Bin Araby na mfano wake pale walipo sema kuwa Hussen alifanya makosa kwenye mapinduzi yake, na wakaona kuwa ilikuwa ni bora kwake kutoa baia (kiapo cha utii) na kunyamaza.[47] Na vipi itakuwa bora kwake kunyamaza wakati ambapo wajibu wake wa dini unamlazimisha afanye mapinduzi, na yaliyoandikwa kwenye mkataba ambao Muawiya alitia sahihi yake yanampa haki ya kutotoa baia na kutonyamaza.
Na hivi ndivyo Hussen alivyo kuwa mshindi na mwana mapinduzi mkubwa katika historia, hata kama alipata hasara kwenye mapigano ya kijeshi yaliyo fanyika kwa wakati maalumu katika uwanja wa karbalaa, nao walio muuwa wakawa ni wenye kulaaniwa na vizazi vyote kwa muda wa historia ya wanadamu, hata kama walipata ushindi kwenye mapigano yao, huo ni ushindi wa wakati mfupi tu, bali "historia haijaweza kuwajua watu fulani walio fanya harakati fulani na kupata ushindi, kisha wakawa wakijiuma vidole kwa kujuta (alama za majuto) kama wale ambao walishinda kwenye uwanja wa Karbalaa".[48]
Alikufa shahidi tarehe kumi ya mwezi wa Muharram baada ya adhuhuri, mwaka 61H,[49] na kuzikwa pale pale alipo fia akiwa shahidi kwenye ardhi ya Karbalaa.
Ajulikanae kwa lakabu mbili maarufu "Assajjad" na "Zainul-Abidiina" (yaani mwingi wa kusujudu) na (pambo la wafanya ibada).
Alizaliwa kwenye mji wa Madina mwaka 37 H. Na alikuwepo kwenye zama za tukio la kuuliwa Amirul Muuminiin, akiwa ni mdogo na pia alikuwepo kwenye zama za baba yake mkubwa au ami yake Hassan alipo patwa na mitihani iliyo mpata na ambayo ilimfanya afanye suluhu pamoja na Muawiya (na tumeelezea kuhusiana na mtihani huo).
Kisha akaishi, akiwa kijana kwenye matukio ya huzunishayo na ya kikatili ya Karbalaa na kuyaona machungu yake na jinsi yanavyo sikitisha na kuhuzunisha. Na akachukuliwa hadi Sham akiwa miongoni mwa mateka.Yeye pamoja na Shangazi yake walikuwa na dauru kubwa katika kuifanya mikakati ya bani umayya ishindwe.
Mikakati yenye kutisha iliyo kusudiwa kufuta uovu wa kuuliwa kwa Hussen(a.s) na kuyafanya yaliyo tokea kuwa ni tukio la kijeshi la kuwaadabisha watu walio asi na kutoka kinyume cha dini na serikali (utawala).
Kisha akaendelea kuishi hadi mwaka wa pili, tangu kuuliwa baba yake, na kushuhudia tukio la "Harra" na maovu yake yote, na fedheha waliyo ifanya. Na pale wana mapinduzi walipo amua kuwafukuza bani Umayya wengine kutoka kwenye mji wa Madina, Mar'wan binilhakam hakupata makimbilio ya kumuha-kikishia usalama wake na familia yake isipokuwa nyumba ya Imamu Assajad na kuiacha familia yake kwa Imamu.[50] Na Imamu kuwakubali na kuwapokea wakimbizi hao lilikuwa ni somo kubwa lililo dhihirisha mbele ya watu na historia maana ya uimamu kwa mafhumu yake ya mbinguni yaliyo takasika na matukufu.
Imamu alichukua msimamo wa upinzani dhidi ya serikali ile, na msimamo huu wa upinzani ulionekana na kudhihiri kwenye mfumo au umbile la dua na nyuradi walizo kuwa watu wakijifunza kutoka kwake na kuzitawanya kati yao. Hakika Imamu aliweza kueleza kwenye dua na nyuradi hizo mambo yenye kuhitaji kufanyiwa mazingatio na kuangaliwa kwa makini kabisa, Kwani yalikuwa yakielezea uhakika wa serikali ilivyo dhalimu na ukubwa wa dhuluma yake na jeuri kubwa waifa-nyayo, na pia alikuwa akiziamsha akili na mabongo ya watu juu ya mambo yaliyo fanywa na watawala wale ya kuyafisha mafundisho ya dini na kuitumia nafasi ya wateule na waaminifu wa Mwenyezi Mungu kuyapotosha mambo ya faradhi ya dini na kukiacha kitabu na kuziacha sunna.[51]
Na wakati huo huo akijaribu kulitibu lile tatizo la kitabia ambalo lilikuwa ni kali na ambalo lilikuwa likiitaabisha jamii kutokana na athari zake mbaya kwa wakati huo.
Na dua hizo zilikusanywa kwenye kitabu kiitwaho "Swahifatu-Sajjadiya". Dua hizo zimekuwa ni mfano kwetu sisi na vizazi vyetu vyote vijavyo na sehemu muhimu ya urithi wa Imamu, na kitabu hiki kimechapishwa mara nyingi sana.
Kama ambavyo miongoni mwa urithi wenye kubakia milele wa Imamu, ni ujumbe wake au kijitabu chake kihusianacho na "Haki" na alikusudia kwenye kijitabu hicho kuweka wazi au kubainisha haki makhsusi kwa watu makhsusi na haki za watu wote kwa jumla ambazo ndizo ziwekazo nidhamu ya mahusiano na mwenendo kati ya mtu na Mola wake, au mtu na viungo vyake, au mtu na watu wengine katika jamii yake, na kijitabu hiki kimechapishwa zaidi ya mara moja.
Alifariki (Rehma na Amani ziwe juu yake) kwenye mji wa Madina, mwaka 95H,[52] na kuzikwa kwenye makaburi ya Baqi'i tukufu.
Alie maarufu kwa lakabu ya "Al-baaqir"aliyopewa na babu yake Mtume(s.a.w.w) . Alizaliwa Madina, mwaka 57.H.
Aliyashuhudia, akiwa bado ni mtoto, matukio ya kuhuzuni-sha ya Karbalaa na akaishi kwenye ujana wake, katika matatizo hayo na mitihani hiyo na machungu yake, matukio ambayo baba yake Sajjad aliyo yapata na watu wengine wa familiya yake. Ali pindi uimamu ulipomfikia, baada ya kufariki baba yake, aliamua kuwa na msimamo wa upinzani dhidi ya serikali iliyo kuwa ikiwatawala kwa Uhuru wote na kutoshiriki kwa aina yoyote ile kwenye matukio ya zama zake, bali aliamua kuutumia wakati wake wote kwenye juhudi za kufundisha dini na kuufafanua Uislamu Sahihi na wa kweli na kuondoa athari za kutu na mawingu yaliyo tanda juu ya sheria, fiqhi na hadithi katika zama za bani umaya wa mwanzo.
Pamoja na kukatika mawasiliano kati yake na watawala wa zama zake, wao walikuwa wakimkimbilia kwenye baadhi ya matatizo yote ya ujumla wakimtaka ushauri na nasaha, na Imam alikuwa hafanyi ubakhili wa kuwapa nasaha na kuwaelekeza ili kulinda na kuhifadhi jengo la Uislamu yaani mujtamaa na maslahi yake ya juu.
Kama mfano juu ya ushauri alio kuwa akiutoa ni kuwa baadhi ya wanahistoria wamesimulia kwamba Khalifa Abdul Maliki bin Mar'waan alizuwia kuenea kwa aina fulani ya vyombo na nguo zilizo kuwa zikitengenezwa na baadhi ya wakristo kwenye nchi ya misri na juu yake wakivipamba na kuweka juu yake nembo au alama ya baba, mwana, na roho mtakatifu kwa Lugha ya kisiriyaniya na kukafanyika mazungumzo kati ya khalifa na mfalme wa Roma kuhusu suala hilo, na Khalifa alikuwa akikataa na kupinga na kutokubali maombi au matakwa ya mfalme huyo wa Roma ya kuendelea kuuza bidhaa zile, na mwishowe mfalme akatishia, ikiwa Khalifa hata kubali maombi yake, kuwa ataweka sentensi za kumtusi Mtume wa Uislamu juu ya dirhamu na dinari (aina za pesa za wakati huo) zitumikazo kati ya waislamu na hadi wakati huo pesa zilikuwa zikitengenezwa kwenye nchi ya Roma.
Na pindi Abdul-Malik alipo tatizika kuhusu suala hilo, hapakuwa na budi isipokuwa ni kumtaka Imam Baaqir, ushauri kuhusiana na suala hilo, na akamuita hadi Sham kwa lengo hilo. Imamu akaitika wito wake na kwenda Sham, na baada ya kufika tu akakutana na Abdul-Malik. Khalifa yule akamueleza tatizo lenyewe. Alicho kifanya Imamu ni kumuamuru kuwaleta wahunzi. Khalifa akawaleta, Imam akawafahamisha jinsi na namna ya kutengeneza dirham na dinar na kuunda umbo au muundo wake na kupima kiwango chake.
Na kwa ushauri huu akaweza kulishinda tatizo lile na kuvunja mbinu na mikakati iliyo kuwa imewekwa na kupangwa na mfalme wa Roma, ya kuwafanya waislamu wafuate na kuvinyenyekea vitisho vyake visivyo na haya.[53]
Wanafunzi wa Imamu ni wengi sana na hatuna nafasi ya kuwaorodhesha. Na urithi wake uliohifadhiwa ni wenye thamani na mzuri, na riwaya zake zimo kwenye vitabu vya tafsiri na fiqhi na hadithi, pia kwenye vitabu vya akida na historia. Alifariki kwenye mji wa Madina mwezi wa dhul hijja, mwaka 114H na kuzikwa kwenye makaburi ya "Baqi'i"tukufu.
Alie maarufu kwa lakabu ya "Aswaadiq". Amezaliwa kwenye mji wa Madina mwaka 83 H. Alikuwepo kwenye zama ambazo dola la bani umaya lilidhoofu na kuanguka, na mwanzoni mwa dola la bani Abbas, na jinsi walivyo kuwa wakijishughulisha na uwekaji wa nguzo za utawala mpya. Mazingira haya yalimsaidia sana kuwafaidisha watu na kuwafundisha, pia kuwapatia elimu na malezi wanafunzi wengi na wanazuwoni ambao walikuwa na athari kubwa katika kuzipa msukumo harakati za kielimu na kuzifanya zisonge mbele na kupanuka (kwa kuzama kwenye elimu kadha) kwenye ulimwengu wa kiislamu.
Na kutokana na wingi wa wanafunzi wake na riwaya zake kuwa nyingi, ushia katika matumizi ya watu uliitwa kwa jina la "Madhehebu ya Jaafariya" kwa kuyanasibisha na Imam Jaafar Aswadiq(a.s) wakati ambapo ushia ni mfumo wa Ahlul baiti wote bila kuhusika na Imamu fulani au kuyafungamanisha nae pekee.
Na inatosha kufahamu nafasi ya Imamu huyu katika kazi na ujuzi aliokuwa nao kwa kuyasoma yaliyo andikwa na mmoja wapo kati ya wanahistoria kwa kuorodhesha idadi ya wapokezi wa hadithi kutoka kwa Imamu waliofikia watu elfu nne.[54] Na pia kwa kusoma maneno yaliyo wazi ya Abul-Hassan Al-washau, pale alipo sema kwenye moja wapo kati ya mazungumzo yake kuhusu hadithi zake:
"Niliwaona kwenye msikiti huu (akikusudia msikiti wa kufa) mashekhe mia tisa na wote wakisema: Amenieleza Jaafar bin Muhammad".[55] Kisha inatutosha kuelewa urithi wa Imamu wa kielimu aliotuachia tangu siku hizo kwa kuelewa kiasi tu, ili tuone ukubwa na utukufu wenye kudhihiri kwa Imamu huyu mtukufu.
Hakika zimepokelewa kutoka kwa Imamu hadithi nyingi katika kuitafsiri Qur'ani na katika elimu ya fiq'hi na sheria, pia katika falsafa na akida, na mambo mengine mengi, lau kama yangekusanywa yange weza kuunda au kufikia kitabu kikubwa sana na kisicho na mfano.
Kisha miongoni mwa urithi ulio patikana kwake ni zile kanuni za tiba na vyanzo vya msingi katika masuala ya afya kwa ujumla, urithi ulio kusanywa kwenye vitabu viwili kama vifuatavyo[56] "Tawhidul-mufadhal" na "Al-ihliilijah".Vitabu hivi vimekusanya maudhui mbali mbali, kati ya maudhui zilizomo kwenye vitabu hivyo ni kuelezea wazi kwa ufafanuzi wenye kutosheleza kuhusu mas'ala ya "ugonjwa wa kuambukiza" ambao hupelekea kuvifahamu "vijidudu vya magonjwa" (mikrobu) ambavyo nafasi yake kwenye elimu ya magonjwa inafahamika. Kama ambavyo vimeelezea pia jinsi Imamu(s.a) alivyo tangulia kugundua siri ya mzunguko wa damu kabla hajaweza kuugunduwa na kuuelewa Dr.Harfi kwa karne nyingi.
Na mwisho, ikiwa si mwishoni, kuna mambo katika urithi wa Imamu ambayo alimueleza mwanafunzi wake ayaandike ambae ni Jaabir bin Hayani, zikiwemo kanuni za kikemia na misingi yuke, na kwa kufanya hivyo alikuwa ametoa elimu ya kemia kidhati kama Dr Muhammad Yahya Al-hashimy alivyo muita[57] .
Naye mwalimu Donald Son anazungumzia njia ya Imamu katika ufundishaji na anasema: "Hakika njia yake ilikuwa kama Sokrati, yeye alikuwa akiwaanzia wanafunzi wake kwa mazungu-mzo na majibizano na akienda hatua kwa hatua kwenye maudhui madogo na mepesi hadi kufikia kwenye maudhui magumu na yaliyo fungika na siri zisizo fahamika"[58] .
Amefariki Imamu (Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kwenye mji wa Madina katika mwezi wa mfungo mosi (Shawwal) mwaka 148.H[59] na kuzikwa kwenye uwanja wa "Baqi'i"ulio mtukufu.
Alie mashuhuri kwa lakabu mbili za "Al-kaadhim" na "babul-hawaaij".
Alizaliwa kwenye sehemu iitwayo Ab'waa, karibu na mji wa Madina, mwaka 128.H. Aliyamaliza masiku ya maisha yake akiwa ni mwenye kuadhibiwa na kufukuzwa na watoto wa ami yake Banu Abbas. Akapambana na vikwazo vyao, nae akiwa huru, pia kupambana na maudhi yao, akiwa jela mambo ambayo hayawezi kuelezeka. Siku za mtawala Rashiid zilikuwa ni zama mbaya sana kwa Imamu.
Na baadhi ya wanahistoria wanasimulia sababu ya kuwepo hali hiyo ni kuwa: Rashiid wakati alipo kwenda Madina na kuingia kwenye msikiti wa Mtume, akizungukwa na viongozi mbali mbali na maraisi alilielekea kaburi tukufu la Mtume, akamsemesha mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kwa kusema:
"Amani iwe juu yako ewe Mwana wa ami yangu". Alijaribu kwa kusema vile kuwahadaa watu kuwa anahaki ya ukhalifa kwa sababu ya ukaribu uliopo kati yake na Mtume. Imamu hakuna alilo lifanya isipokuwa ni kuweka wazi udhaifu wa hadaa hiyo, pale nae alipo msemesha Mtume(s.a.w.w) kwa kusema:"Amani iwe juu yako ewe baba". Uso wa Rashiidi ukageuka na kudhihiri alama za hikidi (chuki) na uovu (shari).
Na kulifanyika mazungumzo mengi kati ya Imamu na Rashiid kuhusiana na maudhui haya, na mazungumzo yalihu-siana na kumbainisha na kumfahamu alie karibu zaidi na Mtume kati yao na mambo muhimu aliyokuwa akiyasema Rashiid katika mazungumzo hayo ni kukataa kwake na kupinga watoto watoka-nao na binti kuhesabiwa kuwa ni katika "kizazi" (dhuria) na kuhesabika kuwa ni "watoto" wa babu yao kwa sababu maneno haya mawili "dhuria" na "abnaau" (watoto) yanakusudia kizazi au watoto watokanao na waendelezao kizazi kwa upande wa baba na si upande wa mama.
Na muhtasari wa majibu ya Imamu yalikuwa kama ifuatavyo:
1- Lau kama Mtume(s.a.w.w) angekuwa hai au angefufuka, anaweza kumchumbia binti yake Rashiid na kumuoa. Lakini asingeweza kumchumbia na kumuoa binti wa Imamu.
2- Kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo "Yeyote mwenye kukutolea hoja kuhusiana nao (Uislamu) baada ya kukujia elimu sema"Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu ". Na waislamu wote wali fahamu kuwa watoto waliotoka na Mtume kwa ajili ya maap izano walikuwa ni Hassan na Hussen watoto wa Fatuma(a.s) na Qur'an imewaita watoto "abnaau"
3- Kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo kutoka kwa Ibrahim Alkhalil (Rafiki wa Mwenyezi Mungu) "Na katika kizazi chake ni Daudi na Sulaiman na Ayyub na Yusufu na Mussa na Harun na hivyo ndivyo tuwalipavyo watu wema. Na zakaria na Yahya na Issa..". Issa nae hana baba, na Qur'ani imemuhesabu kwenye kizazi cha Ibrahim kwa sababu ya mama yake. Na yote hayo yana maana kuwa mwenye ukaribu kupitia kwa mama ni katika "Ukoo au kizazi" (dhuria) vile vile kama Qur'ani ilivyo elezea wazi.
Pamoja na matatizo aliyo kumbana nayo Imamu na jela mbali mbali alizo kuwa akihamishiwa, hakika alikuwa haiachi nafasi yoyote ipite bila kuwafundisha watu na kuwafaidisha, na kutokana na baraka za muda mchache alio kuwa huru aliweza kutuachia urithi mkubwa ambao umo kwenye vitabu vikubwa vya kiislamu.
Alifariki (Rehema na amani ziwe juu yake) tarehe sita mwezi wa Rajabu mwaka 183 h,[60] na kuzikwa kwenye makaburi ya makuraishi yafahamikayo hivi leo kwa jina la "Kaadhimiya" ikinasibishwa sehemu hiyo na Imamu mwenyewe.
Ni maarufu kwa lakabu ya "Ar-ridhwa". Alizaliwa Madina mwaka 148.H. Alikulia kwenye zama za mtawala wa kwanza wa bani Abbas. Na akaishi kwenye machungu na maumivu yote yaliyo msibu baba yake kwenye jela na kuwekwa mahabusu. Na ukhalifa ulipo mfikia Maamun nchi zote za kiislamu kwa ujumla zilikuwa na matatizo mengi ya kimsingi yaliyo kuwa ni muhimu zaidi, kati ya hayo ni: Kudhoofu heshima ya dola baada ya mapigano ya Amini na Maamun, (Wana wa Harun Rashid) na bani Abbas pamoja na wafuasi wao kuchukizwa sana na kitendo cha Maamun kuhamishiwa mji mkuu wa ukhalifa au utawala na kupelekwa Iran na kujikurubisha kwake (Maamun) sana kwa wafursi. Kisha harakati za mapinduzi zilizo kuwa zikiongozwa na Alawiyyiin (kizazi cha Imam Ali) katika mji mtukufu wa Makka Yemen, Al-kufa, Basra na Khurasaan.
Maamun alifikiria sana jinsi ya kutatua tatizo hilo, na hakuwa na budi isipokuwa ni kumwita Imam Ridhwa kwenda sehemu iitwayo Mar'wo, na akamfikishia fikra ya kujitoa na kujiweka kando na ukhalifa kwa ajili yake pindi tu alipo kutana nae, kisha akakazania na kumsisitiza Imam kwa usisitizaji ambao hauna jinsi ya kulikimbia au kulihepa jambo hilo kuwa akubali cheo cha wilayatul ahdi (Mrithi wa ukhalifa) baada ya kukikataa cheo cha ukhalifa Lau kama Maamun angelegeza msimamo wake.
Na sababu zilizo mfanya khalifa kufanya vile ni kujiokoa kutokana na hali ya hatari iliyokuwa imefikia kwa wakati huo, na hasa mapinduzi yaliyokuwa yakifanywa au kufanyika pande zote za ulimwengu wa kiislamu, kiasi kwamba aliona kuwa kushiriki kwa Imamu Ridhwa kwenye utawala wake itakuwa ni Sababu ya mapinduzi yale kupoteza moto na kasi yake na kupunguza utetezi wa watu walio wengi kuendelea, ambao ni kuwapenda kizazi cha Ali na kuwaita watu kumuelekea Imamu Ridhwa ambae ni katika kizazi cha Muhammad.
Na sababu iliyo mfanya Imamu kukataa ni kufahamu kwake kuwa Maamun ameamua kusisitiza suala hilo kutokana na maslahi ya kisiasa yaliyokuwepo kwa wakati huo, na huenda siku za mbele akawa ni kiongozi wa harakati za kisiasa zilizo dhidi yake, au atawaweka baadhi ya Alawiyyin (watu wa kizazi cha Ali) wafanye maelewano nae na kuwasukuma kuuza dhamiri pamoja nae, na kuwa kiongozi wa mbele wa harakati zile zilizo dhidi yake.
Lakini Imamu, pamoja na kuyajua yote hayo, alikuwa akihisi taabu kuhusiana na suala hilo alilo ambiwa, kwa sababu kukataa moja kwa moja itamaanisha kuwa anakubali na kukiri kuwa hana haki ya suala lile, na kuwa hana uwezo wa kustahmili mikiki yake, kwa maana hiyo akakubaliana na fikra ya wilayatul ahdi (mrithi wa ukhalifa) ili kiwe ni kipimo cha majaribio na mtihani kwa Maamun. Basi Imamu akawa mrithi wa ukhalifa rasmi wa serikali.
Na mambo ya fitina na kuzuwa mambo ya kuwachanganya watu yakaanza kusukwa na kutengenezwa hapa na pale, kisha Imamu akafariki kwenye mazingira yenye kutatanisha yasiyo epukana na shaka na tuhuma, mambo ambayo nafasi yetu haitu-ruhusu kuyaelezea.
Ama urithi wa kielimu wa Imamu ni riwaya nyingi zinazo-patikana kwa mwenye kufanya utafiti kwenye vyanzo (vitabu) vikubwa vya kiislamu. Na kati ya urithi huo ni kitabu chake cha tiba kiitwacho "Adhahabiya" alicho kiandika kwa jina lake "Twibu Arridhwa", na Dr Swahib Zayni alikifafanua na kukishe-rehesha kwa kulinganisha kati ya madhumuni yake na mambo mengine yaliyo gunduliwa na kufahamika kwenye tiba ya kisasa na asili ya kitabu hicho ilichapishwa pamoja na sherehe yake huko Baghadad kabla ya miaka kadhaa iliyo pita.
Alifariki (rehema na amani ziwe juu yake) sehemu iitwayo Tuusi katika mwezi wa Safar mwaka 303 H[61] , na kuzikwa huko na hivi sasa sehemu aliyozikwa huitwa "Mash'had" kwenye mkoa wa Khorasani, huko Iran.
2
USUULID DIIN
UIMAMU
Ni maarufu kwa lakabu ya "Al-jawad" na "Attaqii". Alizali-wa kwenye mji wa Madina katika mwezi wa Ramadhan mwaka 195 H.
Aliishi mwanzoni mwa utoto wake katika zama za utawala wa khalifa Maamun, ambae pamoja na mambo yote yaliyo uzunguka utawala wake, alikuwa akionyesha kuwa na mapenzi na kuwatawalisha Ahlul Bayti(a.s) . Naye Imamu Ridhwa(a.s) alipo fariki na watu kuzielekeza tuhuma za kifo cha Imam kwa Maamun, na mazungumzo hayo kuenea kwenye vinywa vya watu kuwa yeye ndie aliemuua Imam, Khalifa alijaribu kukanusha suala hilo na kutoa dalili ya kivitendo ili kuyabatilisha hayo, na hima zake zote kuzielekeza kwa mwana wa Imamu Ridhwa, kwa kumpenda na kujikaribisha kwake, hadi kufikia kuchukua uamuzi wa kumuoza Imamu binti yake na kuimarisha mahusiano kati ya familia mbili hizo.
Nao bani Abbasi wakamchukia Maamun kwa kufanya hivyo na wakamwambia wazi kutoridhishwa kwao, na kumsisitizia kua-chana na jambo hilo analo taka kulifanya, huku wakimtaka awatendee wana wa Ali na kuwa pamoja nao kama walivyo kuwa wakiwatendea na kuwa nao makhalifa walio tangulia, waki-kusudia kuwafanyia chuki na kukata mawasiliano na kuwafanyia uadui.
Maamun akalikataa hilo na kuwaeleza wazi ulazima wa kuondoa hali yiho ya dhuluma na uadui iliyo rithiwa, kwa sababu kufanya hivyo ni kukata udugu na kuwafanyia uadui wana wa Ali bila sababu na bila ya dalili, na akawawekea wazi na kuwabaini-shia kuwa kumchagua Imam ili amuozeshe binti yake hakikuwa ni kitendo cha kuathirika kwa hisia au kitendo kisicho na faida, bali alifanya hivyo kutokana na kuona sifa au hali tofauti ambayo inamtofautisha na kumpambanua na watu wote wenye elimu na wenye sifa bora akiwa bado ni mdogo.
Walipo muona Maamun harudi nyuma na kuacha msimamo wake ule wakamtaka ampe muda Imamu hadi akasome elimu ya fiqhi vizuri na aweze kujifunza. Maamun akawaambia "Hakika huyu ni katika watu wa nyumba ya Mtume, elimu yao hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mkitaka mfanyieni majaribio ili muweze kufahamu jambo hili. Watu wale wakakubali kufanya hivyo, na wakafanya maandalizi yenye kufaa, na wakamuomba Qadhil-Qudhati (hakimu wa mahakimu) alie kuwa akiitwa Yahya bin Aktham amuandalie Imam maswali ambayo yatadhihirisha kuto-kuwa na uwezo na kushindwa kwake kuyajibu.
Na mtihani ule ukafanyika kwenye siku yake iliyo pangwa, na matokeo yake ilikuwa ni kadhi yule kushindwa kwenye majaribio yake na Imamu kudhihirisha kiwango cha juu zaidi na kikubwa kwenye fiqhi ya kiislamu jambo ambalo hatuna nafasi ya kulie-lezea kwa upana. Kisha ndoa ikafanyika na kukawa na mahu-siano ya kina kati ya Imam na Maamun.
Ukhalifa ulipomfikia Muutaswim alimuita Imamu kwenda Baghdaad na kumuweka kwenye nyumba maalum, kisha Imam hakubakia kwa muda mrefu, kwani alifariki haraka sana baada ya kufika huko na alikufa kwenye mazingira yasiyo eleweka ambayo yalielekewa na vidole vya tuhuma, vikimtuhumu Muuta-swim kuwa yeye ndie alie muwekea sumu Imamu kupitia mkewe Umulfadhli.
Hata ingawa utawala ulikuwa umembana Imam na hasa kipindi alicho kaa Baghdad, zimebaki kutoka kwake athari za kielimu zenye thamani zilizomo kwenye vyanzo vikubwa (vitabu) na mashuhuri vya kiislamu.
Alifariki (rehema na amani ziwe juu yake) katika mwezi wa dhulqaada mwaka 220H, na kuzikwa pembezoni mwa babu yake Imam Kadhim Kwenye makaburi ya makuraishi "Al-kadhimiyya".
Alie maarufu kwa lakabu zake "Al-haad"na "Annaqi".
Alizaliwa Madina katikati ya mwezi wa dhul-hijja, mwaka wa 212 H Aliishi miaka kadhaa kwenye zama za utawala wa Muutaswim, nazo ni zama za kuanzishwa mji wa Surra man ra'a (Samarra) na Khalifa kushughulikia matatizo ya waturuki waliokuwa watumwa na walio kuwa wakilitawala jeshi na dola. Kisha zikaja zama za utawala wa Waathiq, na ni zama ambazo hapakuwa na tukio lolote isipokuwa hali ya kupendana kati ya Khalifa na Imam. Kisha zikafuatia zama za Mutawakil, nazo ni zama za utawala ulio kuwa ukienda kinyume na Ahlulbait(a.s) na kutangaza wazi uadui wao na kuwapiga vita kwao.
Mtumishi wa Mutawakil aliekuwa Madina alipofahamu malengo ya Khalifa, akawa akituma ripoti kwenda mji mkuu wa utawala, na ripoti zote zikimtuhumu Imamu kwa kuandaa mapinduzi na kusisitiza juu ya hatari ya Imamu huyu kwa dola.
Na ripoti hizo zilipo kithiri Mutawakil akamuandikia Imamu barua akimpa pendekezo ndani ya barua hiyo kuwa aende Samarra pamoja na yeyote atakae taka kufuatana nae katika familia yake na watu wa nyumbani kwake, ili kujadidisha uhusiano wao (kuufanya upya) na ili kuzima joto ya hamu na shauku ya kukutana naye kama ambavyo Mutawakili alivyo muandikia pia mtumishi wake wa Madina na kumueleza, ikiwa Imamu ataazimia kusafiri awatume walinzi na watu watakao fuatana nae ili kuonyesha zaidi umuhimu na heshima nyingi aliyokuwa nayo Khalifa kwa Imam.
Kutokana na yote hayo Imamu akaona kuwa yeye ni lazima asafiri, na baada ya kutulia kwa muda kiasi kwenye nyumba ya pekee aliyo tayarishiwa na Mutawakil, akahamia kwenye nyumba aliyo inunua yeye mwenyewe kwa mali yake ili kuepuka kuwa mgeni wa Khalifa, nayo ni nyumba ambayo baada ya kufariki kwake ilikuwa ni sehemu yake ya kuzikwa na ni sehemu ambayo watu huifanyia ziara.
Na Imamu akabakia Samarra akiwa mateka na kukaa pale kwa lazima (kifungo cha nyumbani) hadi alipo fariki. Na pamoja na yote hayo uchunguzi ulikuwa ukiendelea wa kumchunguza Imamu, na wachochezi wakiendelea na kazi yao kwa bidii zote, na nyenzo zote za kumfanyia maudhi Imamu zikifanya kazi, ikiwemo kuvamiwa nyumba ya Imamu usiku kwa madai ya kutafuta mali na silaha anazo ziandaa kwa ajili ya mapinduzi dhidi ya utawala wa Mutawakili.
Pamoja na uchokozi wote huo na usumbuaji, khalifa wakati mwingine alikuwa akilazimika kumkimbilia Imamu anapo patwa na masuala magumu na mazito ya sheria ambayo kwenye serikali au watu wa karibu wa khalifa, hakuna alie kuwa akiyafahamu vizuri na mwenye uwezo mzuri wa kuyajibu.
Na katika urithi wa Imamu wa kielimu kilibakia kwetu kitu cha thamani sana, na miongoni mwa urithi huo ni kitabu madhu-buti kilicho tilia mkazo maudhui ya "Al-jabri wa Tafwidh", kwani alielezea kwenye kitabu hicho mas'ala haya pande zake zote, na kubainisha mielekeo yake, na kuyabainisha mambo yake yaliyo fichika na matatizo yake, na kutoa ufafanuzi kamili wa yale aliyo yakusudia babu yake Jaafar bin Muhammad(a.s) alipo sema "Hakuna kutenzwa nguvu wala kuachiliwa huru, bali jambo hilo ni kati kwa kati.[62]
Alifariki kwenye mji wa Samarra katika mwezi wa Rajab mwaka 254 H.[63] na kuzikwa kwenye nyumba yake huko, sehemu ambayo ndiyo ifanyiwapo ziara yake kwa hivi sasa.
Ajulikanae kwa lakabu maarufu ya "Askari" na hilo ni jina moja wapo kati ya majina ya mji wa Samarra.
Alizaliwa kwenye mji wa Madina katika mwezi wa Rabiiul-akhir, mwaka wa 232 H, aliishi katika siku za uhai wake, kwenye zama za watawala na zama hizo kuanzia kwa Khalifa Al-muutazzu, na hapakumtokea Imamu kwenye zama hizo pamoja na Muutazzu suala lolote kama kuwa na msimamo wa aina yoyote wenye sura ya kumfanyia uchunguzi wa karibu Imamu.
Na hilo lilitokana na Khalifa kujishughulisha na matatizo ya askari jeshi wa kituruki walio kuwa wakilidhibiti dola na serikali na kueneza fujo na uharibifu kwenye sehemu za dola hilo, hadi kufikia hatua ya kumshika mateka, kumtia kizuwizini khalifa na kumvua madaraka.
Khalifa Al-Muhtadi, mahusiano yake na Imamu yalikuwa mazuri, kutokana na kufahamika kwake khalifa huyu kuwa ni mwenye kujiepusha na unywaji pombe na vikao vya taarabu na ngoma, na kujiweka kando, na kujidhihirisha kwenye madh'hari ya wema na upole.
Khalifa Al-Muutamad alikuwa ni mkali na mwenye kutumia nguvu kwa Ahlulbaiti, na Imamu aliwekwa jela kwenye utawala wa khalifa huyu Muutamad kwa muda kadhaa, kisha khalifa akalazimika kumuachia huru Imamu pale walipo mtatiza viongozi wa kikristo katika tukio lililo tokea baina yao nayeye, na kisa chake kime simuliwa na baadhi ya wanahistoria. Khalifa akakimbilia kwa Imamu ili awape majibu ya kuwaziba midomo na kudhihirisha uongo na udhaifu wao mbele ya halaiki ya waislamu.
Na Muutamad alikuwa na dauru isiyo njema na isiyotukufu pale alipo fikiwa na habari za kufariki kwa Imamu, kwani aliwaamuru askari wake kumtafuta "Muhammad Almahdi", mtoto wa Imamu Askari, huku akimtumia katika tukio hilo Jaafar bin Ali, ami yake Almahdi, kwa kumlimbikizia mali na kumpatia cheo, ili amsaidie kumtafuta mtoto wa nduguye.
Lakini pande hizo mbili hazikufaulu katika matakwa yao. Imamu Al-mahdi akatoweka kwenye macho ya maadui zake na Mwenyezi Mungu akamuokoa kutokana na vitimbi vya watu hao wafanyao vitimbi.
Pamoja na kuwa mazingira ya Imamu yalikuwa ni magumu na yenye matatizo, wapokezi wa riwaya wamesimulia na kupokea kutoka kwake mambo mengi ya kielimu na yenye manufaa na muelekeo wa uongofu na ujuzi wenye kueleweka na wa kweli.
Alifariki (rehema na amani ziwe juu yake) katika mji wa Samarra tarehe 8 mwezi wa Rabiul awwal mwaka 260 H.[64] na kuzikwa kwenye mji huo karibu na baba yake, kwenye nyumba yao makhsusi.
Alie maarufu kwa lakabu ya "Al-mahdi" na "Al-qaa'im-Al-Muntadhwar".
Alizaliwa kwenye mji wa Samarra wakati wa Alfajiri, tarehe 15 ya mwezi wa Sha'aban mwaka 255 H. Alitoweka kwenye macho ya Serikali ya wakati huo pale walipo taka na kufanya juhudi kubwa za kumtafuta, kufuatia kufariki kwa baba yake.
Kipindi cha mwanzo cha kughibu kwake aliteuwa wawaki-lishi maalumu watakao kuwa wakiwasiliana nae na kumpelekea barua za mashia na masuali yao, na pia kupokea majibu ya maswali yao, na kuyafikisha kwa wenyewe. Na mawasiliano haya yalipo onekana kuwa ni hatari vilevile, pamoja na kuwa yalikuwa yakifanywa kwa tahadhari na siri, Imamu akayamaliza mawasi-liano yale na uwakilishi ule, na mawasiliano ya moja kwa moja yakakatika, kwa pande zote, kati yake na wafuasi wake.
Na Mwenyezi Mungu atamdhihirisha baada ya kutoonekana (kughibu) kwa muda mrefu. Na atakapo dhihiri ataijaza ardhi kwa uadilifu na usawa kama ulivyo jazwa dhuluma na ujeuri. Kufuatana na bishara aliyo itowa babu yake Mtume(s.a.w.w) kwenye hadithi nyingi kama kauli yake isemayo:
"Hakika Ali ni wasii wangu na katika kizazi chake atatoka Al-qaa'im Almuntadhwar Mahdi " (Mwenye kufanya mapinduzi mwenye kusubiriwa kuja kwake alieongozwa), ambae ataijaza ardhi uadilifu na usawa kama ilivyo jazwa ujeuri na dhulma".
Pia kauli yake Mtume(s.a.w.w) :
"Mfurahieni Mahdi, (au pokeeni bishara ya mahdi) ni mtu atokanae na kabila la kikuraishi, ni mtu atokanae na kizazi changu. Atatoka wakati watu watakapo tofautiana na kuwepo mtetemeko, na ataujaza ulimwengu na ardhi kwa uadilifu na usawa kama ulivyo jazwa dhuluma na ujeuri ".[65]
Na kutokana na umuhimu wa maudhui ya Mahdi tumeyawekea kitabu makhsusi na tumegawanya mazungumzo yake katika sehemu tatu:
Sehemu ya kwanza ina husu kuitoa na kuiweka wazi fikra ya "Al-mahdi" na kiwango cha mahusiano na maungano yake na uislamu.
Na sehemu ya pili, inaelekea kwenye suala la kumbainisha na kumu ainisha "Mahdi" kutokana na dalili za hadithi za Mtume zilizokubaliwa kati ya waislamu wote.
Na sehemu ya tatu, inazungumzia uwezekano wa kughibu kwa Imamu na dalili zake. Na mwenye kutaka ufafanuzi zaidi arejee kwenye vitabu tulivyo viashiria hapo kabla.
Na baada ya hayo: Huu ndio "uimamu" kama ambavyo akili ilivyo tuongoza na kama dalili zilizo nukuliwa zilivyo eleza wazi. Na hizi ndio "dalili" zikiwa wazi na zikiainisha na kupambanua. Na hawa ndio "maimamu" na urithi wao ulio mkubwa, na historia yao yenye kutoa marashi (yaani nzuri) na mienendo yao yenye kupendeza na kuvutia. Je msomaji anaona ya kuwa kuwa-fuata na kupitia kwenye miongozo yao na kufuata nyayo zao ni kutoka kwenye uislamu na kuwafuata mayahudi?
Na je inafaa kusemwa, kutokana na yote yaliyo tangulia, ya kuwa ushia umedhihiri kwenye zama za khalifa Othumani binil Afan na kufuatia mapinduzi dhidi yake yaliyo fanywa na waislamu kupitia kwa yahudi alie ingia kwenye Uislamu kwa ajili ya kuubomoa uislamu aitwae Abdallah bin Sabai?!
Je Abdallah bin Sabai, ana uhakika wowote wa kuwepo kwenye historia ili awe atanasibishiwa kuanzisha Ushia na kuweka misingi yake?! Hakika Dr.Barnado Luise alilizingatia Suala la kuwepo Abdallah bin Sabai kuwa ni suala au picha iliyo simama kwenye msingi wa khayali na dhana, na akasisitiza kuwa mambo aliyo husishwa nayo ni mambo yaliyo undwa na watu walio kuja mwishoni.[66]
Naye Dr Twaha Hussen ameyatilia shaka mambo yote yaliyo nasibishwa kwa Ibnu Sabai miongoni mwa matukio mbali mbali na akaweka maelezo yake juu ya riwaya za wanahistoria kwa kusema:"Ni uovu ulioje wa masingizio waliyoyasingizia maadui wa mashia kwa mashia!.[67]
Naye Dr. Jawad Ali amezitilia shaka habari zinazo husiana na Ibnu Sabai kwa sababu riwaya zote zimetoka kwa Saifu bin Omar, na hazitoki kwa mwenginewe.Na Saifu huyu ametuhumiwa kuhusu ukweli wake na riwaya zake.[68]
Naye Dr. Ali Al-ward, ameonelea kuwa Ibnu Sabai ni jina la umashuhuri walilo litoa bani umayya na kulitumia kwa sahaba mtukufu Ammar bin Yaasir, na akatoa dalili kadhaa zinazo unga mkono maneno yake juu ya rai yake hiyo.[69]
Kisha akaja Ustadh Ahmad Abbas Swaleh mwishoni na kutilia mkazo kuwa "Ni ukosefu wa akili kufikiria kuwa huenda yupo kweli mtu kama huyu". Na akasema katika mazungumzo yake kuhusiana na Ibnu Sabai yafuatayo:
"Na Abdallah bin Sabai ni mtu wa kupandikizwa bila shaka yoyote..na fikra yenye kuelekea kuunda mtu kama huyu wa kupandikizwa asie na ukweli wowote ni fikra finyu na potovu bila shaka yoyote, ili aipe athari katika matukio yaliyo tokea" na "visa vyote vilivyo undwa kuhusiana na Abdallah bin Sabai ni mambo yaliyo wekwa (kutungwa) na watu walio kuja nyuma wala hakuna dalili juu ya kuwepo kwake kwenye vitabu mama vya zamani ukiachilia mbali ubovu wa fikra hiyo ya kutarajia kuwa na asili ya kuwepo kwake".[70]
Na ikiwa Ibnu Sabai, kama tulivyo tangulia kusema, ni mtu wa kupandikizwa, na historia haikupata habari zake wala kumjua, basi ni nani alianzisha Ushia? Na ni nani alikuwa wa mwanzo kulitumia neno hilo?
Jawabu :
Hakika ni Muhammad bin Abdillah(s.a.w.w) mwenyewe. Twabari na Al-haafidh bin Hajari wametoa kwa mashekhe wao ambao ni mahufadhi walio mashuhuri, kwamba Mtume(s.a.w.w) siku moja alisoma kauli ya Mwenyezi Mungu:"Hakika wale ambao wameamini, na wakafanya matendo mema, hao ndio viumbe bora zaidi". Kisha akamgeukia Ali bin Abi Twalib (a.s) na kusema: "Watu hao ni wewe na mashia wako (wafuasi wako).[71]
Na ikiwa Muhammad bin Abdillah(s.a.w.w) ndie wa mwanzo kutumia neno hili na akawakusudia kwa kutumia wafuasi wa Ali kwa dhati, basi Ushia hautadhurika na maneno au uzushi wa wazushao maneno ya uongo, na shaka za wenye kuutilia shaka na kauli za wasemao.
Na sifa zote ni za Mwenyezi Mungu ambae ametuongoza kwa hili na hatukuwa ni wenye kuongoka kama si Mwenyezi Mungu kutuongoza, na amani ziwe juu ya mitume wote na himidi zote ni za Mola wa viumbe wote.
Na huwenda mwenye kufanya utafiti na mdadisi wa hali iliyokuwa wakati wa kufariki Mtume(s.a.w.w) atafahamu kiukamilifu hali hiyo na mambo mengine yaliyo kuwa yakitarajiwa kutokea. Na alifahamu hivyo kwa hukumu ya ufahamu wake wa ukweli wa mambo, na kwa hukumu ya kupewa habari na Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya hayo yatakayo tokea kama Mwenyezi Mungu alivyo sema: "Je ikiwa atafariki au kuuwawa mtageuka na kurudi kwenye visigino vyenu ".
Sasa kwa nini Mtume hakumteua na mtu mwengine akateua? Je Muhammad alikuwa ana ufahamu mdogo zaidi wa kuijua hatari na kuhis i majukumu juu ya umma huu kuliko walioteua?
Ili kujua kuwa Fatima ndie binti pekee wa Mtume rejea kwenye bahthi yetu kuhusu "Utume"katika ukurasa wa 45-55-chapa ya Baghdad 1392 H.
Mtume alimpa habari kwamba yeye atapigana vita na watu hawa, rejea Taarikhu Baghdaad Juzuu 8/340 na 13/187 na Al-istiaab 3/53.Ili kujua usiku alio kufa rejea Muruju Adhahabi:2/291,na al-kaafi 1/452, na pia Irshaad-6 na Twabari, kwenye historia yake amesema katika juzuu 5/143 kuwa pigo la Abdurrahman bin Muljim alilo mpiga Ali lilikuwa usiku wa 17 au 19 na kutokana na kuwa alibakia hai kwa muda wa siku mbili baada ya pigo hilo kifo chake kinakuwa usiku wa 21 kulingana na mojawapo kati ya riwaya mbili za Twabari.
MAHDI MTARAJIWA KATI YA TASWAWWUR NA TASDIQ
"Na hakika yeye ni alama ya Kiama ". Suratu-Zukhruf:61
Muqaatil bin Sulaiman amesema na mufasirina wengine walio mfuata: "Hakika aya hii imeteremka kumhusu Almahdi".
Ibn Hajar Al-haitami As-shaafii: Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Ili aidhihirishe juu ya dini zote, hata kama washirikina watachukia". Surat Aswaf:9.
Said bin Jubair amesema: "Ni Mahdi atokanae na kizazi cha Fatima(a.s) ".
Al-haafidh Al-Kanjiy As-shaafii.
Kwa jinala Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema
Mwenye kurehemu.
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu kwa neema alizotoa na kutupa ilhaam. Na rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad na Ali zake wema.
Zilitolewa na kuzalishwa shub'ha na shaka kuhusu maudhui ya Mahdi mtarajiwa na kutawaliwa na majibizano, kati ya viku-ndi vya waislamu, hata baadhi ya waandishi na watunzi wa vitabu kufikia hatua ya kusema na kuona kuwa kumuamini Mahdi au fikra ya Mahdi ni sawa na kuamini mambo yaliyo pandikizwa yasiyo na ukweli au kuamini visa vya watu wa kale.
Kwa hivyo ilikuwa ni lazima kwa watafiti walio jihusisha na masomo ya kiislam, kutokana na hali hii, kuyaelekea na kuyafanyia utafiti maudhui haya, kwa kiwango kikubwa na kuyapa umuhimu mkubwa, na kuziandaa kalamu zao kwa ajili ya utafiti kuhusu masuala haya kwa uhuru kamili na uwazi, ili waweze kuondoa shub'ha zenye kutokea, na kuzibatilisha shaka zitokanazo na dhana, na kuyabatilisha madai yaliyo zuiliwa, na kuondoa pazia kwenye ukweli ulio wazi ili uweze kuonekana mbele ya watu wote kwa uhakika wake wa Uislamu au kama yalivyo kiuhakika wake ndani ya Uislamu wenye kumeremeta na kutoa mwanga.
Na huenda kati ya watu kuna wanao dhania kwamba kuyazungumziya maudhui haya na mengine mfano wake ni miongoni mwa mas'ala ambayo yanaweka kizuwizi cha kuleta ukaribu na kuelewana kati ya waislamu na kuchochea moto wa tofauti kati yao uzidi kuwaka na kulindima, na kwamba kuweka na kubakiza sitara au pazia kwenye mambo haya ni vizuri na ni jambo lenye manufaa zaidi, lakini kufikiria hivyo, kama ninavyo amini, ni dhana zisizo kuwa na ukweli na zisizo ufikia ukweli kwa aina yoyote, kwa sababu kuficha jambo haijawahi kuwa ni utatuzi wa matatizo kama haya, bali kufanya hivyo hakutatoa athari yoyote isipokuwa ni kuandaa mazingira mapana ya kupatikana dhana mbaya na kubobea hali ya kutofautiana na kuyachanganya mambo tofauti, kwa sababu hii kufanya utafiti wa makusudi kabisa kwa uwazi na ukweli ni jambo lenye athari ya upeo wa juu na lenye faida nyingi, kwani ukweli utadhihiri (uliokua haufaha-miki) na uongo wa kuunda na ulio zuliwa utakuwa wazi, na madirisha au nafasi za kutia shaka na kutoamini zitajifunga.
Na kutokana na haya, matarajio yangu kwenye kurasa hizi yalikuwa ni kwamba hizi kurasa ziwe hatua tuzifanyazo kwenye njia hii kuelekea kwenye lengo kubwa na ziweze kuwa juhudi zenye nia safi katika kujaribu kuleta mtazamo ulio salama na mafundisho yaliyo wazi na kuziba nyufa.
Na katika kijitabu hiki sintakuwa na nafasi kubwa -kwani kinaandikwa kwa msukumo huu mtukufu na kutaka kulithibi-tisha lengo hilo la juu kabisa- isipokuwa ni kuyadhihirisha kwa ukweli na kutoa hukumu iliyo salama, na kufanya utafiti ulio epukana na matamanio na mapenzi ya upande fulani.
Na matarajio yangu yote ni kuwa msomaji mtukufu apate ndani yake dalili zitakazo ondoa wingu jeusi ambalo limetanda juu ya maudhui haya kwa karne zote zilizo pita na apate dalili zinazo weka wazi msimamo wa Shia Imamiyya kuhusu mas'ala ya Mahdi na (kuhusu) fikira ya Mahdi.
Na himidi zote ni za Mwenyezi Mungu ambae alituongoza kwa hili, na hatukuwa ni wenye kuongoka lau kama si Mwenyezi Mungu kutuongoza.
Muhtasari wa maudhui tuliyo yamaliza kwenye utafiti wa "Uimamu"[72] ni kuwa Uimamu kwa hukumu ya Hadithi, Qur'an na Akili ni sehemu ikamilishayo ujumbe, na ni sehemu iufanyayo ujumbe wa kiislamu uendelee kuwepo, na kwamba dalili zote zilizo julisha ulazima wa kuwepo utume na uwajibu wake zinafaa kuzinukulu na kuzitumia kutolea dalili juu ya ulazima wa kuwepo uimamu, kwa sababu kuwepo kwa utume bila ya uimamu ni kuwepo kuliko katika kusiko endelea, na hali hiyo inapingana na jengo la Uislamu lililo simama juu ya msingi wa kuendelea ujumbe hadi siku ya mwisho.
Kwa hivyo basi utume ni mwanzo wa uhai, na uimamu ni kuendelea kwa uhai ule na lau kama ingefaa kwetu kusema na kukubali utume bila uimamu, ingefaa kusema kuwa ujumbe wa Mtume una mtazamo finyu na wenye mipaka maalumu, hauku-weza wenyewe kujikadiria umri wa kuendelea kuwepo baada ya uhai wa Mtume wake, na haukuweka akiba kwa ajili ya kuyathi-bitisha malengo yake kwa kumteua Wasii ili aendeleze kazi na kuwepo kwa ujumbe wake.
Na ukweli ni kwamba, lau kama usia usingethibiti kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kwa njia ya riwaya na habari zilizo nukuliwa, hakika akili pekee ni yenye kuhukumu ulazima wa kuwepo usia na kuwa ulifanyika, na kwamba mtu yeyote miongoni mwetu haridhii kughibu na kuacha mali zake ziwezazo kutoweka au kufa na kuacha vitu mbali mbali hata kama ni vichache, bila kuzikabidhi mali hizi au zile kwa mtu alie muusia na muaminifu aziendeshe na kuzipangilia na kuzilinda.
Basi je ina juzu kwa Mtume wa Uislamu kuuacha urithi wake mkubwa, urithi ambao ni wa watu au wanadamu kwa zama zote, bila kumuweka wasii atakae uchunga na kuulinda urithi huu na kuuangalia kama inavyo stahili?!
Hakika mazingira yote yaliyo uzunguka Uislamu siku au wakati alipo fariki Mtume(s.a.w.w) yanatuita na kutulingania kuamini kuwa Mtume aliusia, na kwamba hakuliacha pandikizo lake lenye baraka jangwani, lipigwe na upepo mkali au joto kali lenye kuunguza au tukio lenye kulitokea, na kulifanya litoweke. Na hivyohivyo ina dhihiri wazi kuwa Shia Imamiyya hawakutoa maneno yahusianayo na kupinga kwao uchaguzi kutokana na hisia ya chuki kwa mtu fulani, au kutokana na rai yao ya kisiasa kwa maana ifahamikayo na yenye kuenea ya siasa, bali waliona kwenye Qur'an na Hadith dhamana sahihi ya maisha na nyenzo ya ujenzi iliyo salama, na basi wakawa wamevutiwa katika kuunga mkono rai hii kwa roho ya imani juu ya Uislamu na ikhlasi kwa ajili ya malengo na kuhisi maslahi ya Uislamu.
Ali bin Abi Twalib(a.s) alikuwa ni Imamu wa kwanza alie thibitishwa kwa dalili kwani riwaya za Mtume(s.a.w.w) ni nyingi sana nani "mutawaatiri" kumhusu yeye, baadhi zikimuelezea wazi na zingine zikimuashiria. Na riwaya zote hizo pamoja na kutofautiana matukio yake na minasaba yake na mifumo yake zinalenga, kama tulivyo tangulia kusema, kwenye kitu kimoja nacho ni kumteua mwenye cheo cha uimamu na ukhalifa baada ya kufa kwake Mtume(s.a.w.w) .
Na imamu wa pili alikuwa ni Hassan bin Ali Na watatu ni Hussen bin Ali. Na wa nne ni Ali bin Hussen Assajad. Na wa tano Muhammad bin Ali Albaaqir. Na wa sita ni Jaafar bin Muhammad Asswadiq. Na wa saba Mussa bin Jaafar Al-kaadhim. Na wa nane Ali bin Mussa Al-ridhaa. Na wa tisa Muhammad bin Ali Al-jawaad. Na wa kumi ni Ali bin Muhammad Alhaadi. Na wa kumi na moja ni Al-Hassani bin Ali Al-askari. Kisha alikuwa Muhammad binil-Hassan al mahdi ndie Imamu wa kumi na mbili[73] , na alighibu kwenye macho ya watu hadi Mwenyezi Mungu atakapo toa idhini ya kudhihiri kwake na "kuujaza ulimwengu kutokana na yeye, uadilifu na usawa kama ulivyo jawa na dhuluma na ujeuri"[74] .
Na mishale ya kutuhumu na kupinga ikamuelekea Almahdy kwa nguvu zote na kwa kutia mkazo na kusisitiza, na maneno yakawa mengi kwenye maudhui haya ya ghaiba (kufichika na kutoonekana) hadi kufunikwa na mawingu mazito ambayo hayakuwezeshi kuona na kufahamu na kukupa uwezo wa kudadisi na kupambanua lililo sahihi, na watafiti wengi ambao ni wenye ikhlasi wakajiweka kando na maudhui haya kwa kuyakimbia matatizo yake na ugunu wake, na sauti za wapingaji zikaja juu na kusikika kwa kudhalilisha na kufanya istihizaa nazo zikidhania kuwa silaha yake iliyo simama kwenye msingi wa kufanya maskhara na kutoa hila kuwa ni silaha kali yenye kukata isiyo katwa na wala haishindwi.
Na hivyo ndivyo utafiti wa "Almahdi na fikra ya kuwepo Almahdi" ulivyo jitenga na kuwa mbali na mfumo wa kielimu ulio salama. Na ukawa si utafiti wa kimaudhui wenye amani na ikhlasi, na ukawa chini ya msukumo wa mapenzi ya nafsi yaliyo mbali na akili na mantiki.
Na kutokana na hayo ilikuwa mfumo wetu kwenye kijitabu hiki ni lazima ufuate upande na mfumo usiofuata mapenzi na uwe ni mfumo wa kimaudhui, ili tujiepushe na tofauti ambazo wengi walizitumbukia. Na mfumo huu utasimama juu ya msingi wa kuyagawa mazungumzo hayo sehemu tatu
Sehemu ya kwanza inakusudia kuitoa fikra yenyewe ya (Mahdi) na jinsi mahusiano yake na Uislamu yalivyo, na sehemu ya pili inaelekea kumuonyesha na kumuainisha (Mahdi) kwenye dalili zilizo pokelewa za Mtume, na sehemu ya tatu inazungumzia maudhui ya uwezekano wa kughibu na kutoonekana, na dalili zake.
Na mwendo huu ulioandaliwa na ufanyao uchunguzi, kama ninavyo itakidi, utachukuwa dhamana ya kutoa ufafanuzi na kuweka wazi kiukamilifu mambo yatakavyo gundulika na kupatikana kwenye mwendo huu na matokeo yake, na kutoa ufahamu makini wa matatizo yake kwa uhakika wake na ukweli wake wa asili ulio mbali na mapenzi na matamanio na malengo mengine.
3
USUULID DIIN
UIMAMU
SEHEMU YA KWANZA
FIKRA YA KUWEPO KWA MAHDI
Lau kama tutavitupia jicho la haraka vyanzo vya historia, na hasa historia ya dini mbali mbali, tungeweza kuelewa na kuona kwa uwazi kuwa kumuamini au Imani ya "Mahdi" sio jambo lihusikanalo na shia Imamiyya tu na sio katika mambo ambayo haya kuwepo kwenye dini na wao wakalizuwa, kama wasemavyo baadhi ya waandishi, bali jambo hilo sijambo lihusikanalo na waislamu peke yao na kutowahusu watu wengine wafuatao dini mbalimbali za mbinguni. Bali ukweli ni kuwa mayahudi na wakristo wana itakidi kuwepo kwa msuluhishi mwenye kutara-jiwa kuja katika zama za mwisho nae ni Eliya kwa mayahudi na Issa (Yesu) mwana wa Maryam kwa wa Kristo.
Kama ambavyo waislamu kwa ujumla, pamoja na madhehe-bu yao na vikundi vyao tofauti tofauti wanaamini hivyo kwani Shia Imamiyya (Ithina asharia) na kiisaniyya na Ismailiyya, wao wana amini kuwepo kwa "Mahdi" na wanasema wazi kuwa hilo ni katika mambo ya lazima ya madhehebu yao. Nao masunni wameamini vivyo hivyo (kuwepo kwa Mahdi) kwa kushikamana na rai hiyo kupitia maimamu wa madhehebu zao na wapokezi wao wa hadithi na baadhi yao wakadai kuwa wao ni akina Mahdi kama ilivyotokea Morocco, Libya na Sudan.
Na hivi ndivyo dini tatu za mbinguni (Uislamu,Ukristu na uyahudi) zinavyo kutana katika kuamini fikra hii ya Mahdi.
Na hivyohivyo mashia wanakutana na ndugu zao waislamu kwenye suala hili. Na wanaitakidi kuhusu Mahdi, mambo aliyo yasimulia Dr. Ahmad Amiin katika rai za masuni kuhusu huyo Mahdi kuwa" Yeye ni katika alama za kiama, na kwamba ni lazima adhihiri kwenye zama za mwisho mtu atokanae na kizazi cha Mtume, atakae iendeleza dini na kudhihirisha uadilifu na waislamu watamfuata na atayatawala madola ya kiislamu, na anaitwa Al-mahdi".[75]
Na kwamba rai yao kuhusu suala hilo ni kama rai ya Sheikh Abdul-Azizi bin Baaz, raisi wa chuo kikuu cha Kiislamu cha Madina pindi alipo sema:"Hakika suala la Mahdi ni suala lenye kueleweka na hadithi kuhusu suala hilo ni mustafiidha (zimepo-kewa na wapokezi watatu kwenye kila tabaka) bali ni mutawaatir (wapokezi wake ni wengi sana) na zenye kuungana , na zo kwa ukweli kabisa zina thibitisha kuwa kuja kwa mtu huyu alie ahidiwa, ni jambo lililo thibiti na kutokea kwake ni jambo la Haki".[76]
Na kutokana na haya hakika fikra hii (fikra ya kuja kwa Mahdi) yenyewe ni sahihi kama asemavyo muandishi wa Misri wa zama hizi aitwae Abdul-Hasiib Twaha Hamud.[77]
Lakini la kustajabisha na kuchekesha kuhusu suala hili, ni kuwa Abdul-Hasiib huyu hakugundua pale alipo isahihisha fikra hii kama ilivyo tangulia, ya kwamba alijipinga yeye mwenyewe, na alisahau kuwa alishawahi kutoa kauli ya kuwa:"Fikra ya Mahdi ni mojawapo kati ya matunda ya itikadi za (dini ya) Sabaiyyah"[78] , nae kwa kusema hivyo anakusudia kuwa fikra hii imechukuliwa kutoka kwenye itikadi za mayahudi na haina mahusiano yoyote na Uislamu, hata ingawa hakusudii kwenye ibara yake hii isipokuwa kuwatuhumu Mashia ya kuwa wamechu-kua itikadi zao kutoka kwa mayahudi na kuwa hazina mahusiano yoyote na dini ya Kiislamu lakini kwa hakika amewatuhumu waislamu wote bila ya kutambua, kwa tuhuma mfano huo, na akazizingatia na kuzihesabu fikra alizoziita kuwa ni fikra sahihi hapo mwanzo kuwa ni moja wapo kati ya matunda ya itikadi za sabaiyyah, na huku ni kupingana kimaneno na kutetereka. Na ikiwa yatatujulisha juu ya jambo lolote maneno hayo, hapana shaka yanatujulisha nia mbaya na maradhi ya nafsi aliyo nayo, na hasa ukizingatia kuwa utafiti wa kihistoria wa zama zetu hizi umethibitisha kuwa hakuna mtu alieitwa Abdullah bin Sabai na kwamba huyu ni mtu alietengenezwa katika akili na kuundwa na akapambwa na kupewa sifa za kuwa ni mtu muhimu, na ana fikra fulani na ndie muwekaji wa itikadi na rai kadha, na huenda wale watu ambao walikuwa wakilirudia mara kwa mara jina la Abdullah bin Sabai mwanzoni mwa Uislamu walikuwa wakiku-sudia swahaba mtukufu Ammar bin Yaasir, kama wasemavyo baadhi ya watafiti.[79]
Na vyovyote iwavyo hakika natija ipatikanayo kutokana na utafiti wa kina na ulio safi usio na uchafu ni kuwa, Shia hawaku-zua fikra ya Mahdi, na wala hawakufuata itikadi ya dini ya Sabaiyyah au dini nyingine isiyo kuwa ya Sabaiyya, bali ni kwamba fikra ya kuwepo Mahdi ni fikra iliyo bashiriwa na dini tatu za mbinguni (Uyahudi, Ukristo na Uislamu), na kwamba Uislamu ulipotilia mkazo juu ya ukweli wa kielimu wa fikra ya Mahdy waislamu walifanya haraka kuikubali na kuinukulu na kusalim amri mbele ya fikra hiyo kwa kukubali kikamilifu.
Na haiwezekani yote haya yawe ni kunyenyekea kwa kitu kiitwacho kwa jina la "upotovu wa Shia na bidaa zao", bali ni kukubali na kunyenyekea kuliko sahihi kwenye ukweli utokanao na itikadi za Kiislamu na hadithi za Mtume(s.a.w.w) .
Na mwanazuoni mtukufu wa kisuni wa Iraq, alitoa muhtasari wa ukweli huu aitwae Sheikh Swafau ddin Aalu-Shaykh Al-halkah na akasema: "Ama Mahdi mtarajiwa, hadithi zilizopoke-lewa kumhusu zimefikia kiwango kikubwa na ni zenye kutuachia matumaini kwamba huyu atakuwapo zama za mwisho, na ataurudishia Uislamu usalama wake na imani, atairudishia nguvu yake, na dini atairudishia uzuri wake , nazo ni hadithi muta-waatir bila shaka yoyote wala shub'ha, bali inasihi kutumia sifa ya mutawaa tir kwa zinginezo zilizoduni yake, kufuatana na istilahi zote zilizo andikwa kwenye elimu ya Usuul".
Ama athari tuzipatazo kutoka kwa maswahaba, zisemazo wazi kuwepo kwa Mahdi, ni nyingi sana zina hukumu ya Raf'u (kuinuliwa hadithi bila kutaja baadhi ya wapokezi).
Hakika hadithi alizo zitaja Al-barzanji kwenye kitabu cha Al-isha'ah Liasharaatisaa'a, na Aalusi kwenye Tafsiri yake, na Tirmidhy na Abu Dawud na Ibnu maaja na Alhakim na Abu ya'ali na Tabaraan na Abdur-rrazaaq na Ibn Hanbali, na Muslim, Abu Naiim, na Ibn Asakir, na Bayhaqiy, na Al-khatiib kwenye historia yake na Daruqutniy na Rady aany, na Naiim bin Hamad katika kitabu Alfitan na Ibnu Abu Sh'eiba na Abu Naiim Al-kuufiy, na Al-bazzaz, na Dailamiy na Abdul-Jabbar Al-khul'aniy kwenye Kitabu chake cha historia, na Aljuwainiy na Ibnu Habban na Abu Amru Addamiy kwenye sunani zake, katika yote hayo kuna dalili za kutosha.
Kwa hivyo kuamini kutokea kwa Mahdi ni waajibu, na kuitakidi kudhihiri kwake ni kuzikubali na kuziswadikisha hadithi za Mtume(s.a.w.w) .[80] Na wanazuoni wengi wa kiislamu walifanya haraka kukubali na kukiri fikra ya Mahdi na kuzisahihisha habari zake kwa kutunga vitabu na vijitabu vya kutoa fat'wa na kufutu mas'ala katika maudhui hayo ili vizazi vijavyo viweze kufahamu suala hili na ukweli wake kama ilivyo pokelewa kwenye sheria kupitia kwa Mtume Mtukufu(s.a.w.w) na miongoni mwa waandishi hao wa maudhui haya, tukitaja baadhi kwa mfano, walikuwa ni:
1- Ubad bin Yaaqub al-rawajiniy alie kufa mwaka 250 H. Ana kitabu kiitwacho "Akh'baarul-Mahdi".
2- Abu naiim Al-Isbihaaniy alie fariki mwaka 430h. Ana kitabu kiitwacho "Ar-baina hadithan fi amril-Mahdi"[81] na kitabu "Manaaqibul Mahdi"[82] na kitabu "Na'atul Mahdi".
3- Mohammad bin Yuusuf Al-Kanjy Ashaafiiy aliefariki mwaka 658 H, ana kitabu kiitwacho "al-bayaan fi akh'bari Swahib zzamaan", kimechapishwa.
4- Yuusuf bin yahya Assalmy Ashaafiiy alie fariki mwaka 685 H. Ana kitabu kiitwacho "Uqad-Addurar fi Akh-baaril Mahdiyil Muntadhar".[83]
5- Ibnu Qayyim Al-jauziya aliefariki mwaka 751 H, ana kitabu kiitwacho "Al-Mahdiy".
6- Ibnu hajar Al-haitamy Ashaafii alie fariki mwaka 852 H, ana kitabu kiitwacho "Al-qaulul-mukhtasar fi alaamatil Mahdiy-Almuntadhar".[84]
7-Jalaalu ddin Asuyutwiy alie fariki mwaka 911 H, ana kitabu
"Al-urful-wirdiy fi akhabaril-Mahdy" kimechapishwa na kitabu "Alamaatul-Mahdi"
8- Ibnu Kamaal basha Al-hanafi aliefariki mwaka 940 H, ana kitabu "Tal-khisul bayan fi alaamat Mahdiyyi Aakhiriz -zamaan".[85]
9- Mohammad bin tuuluun Ad-damash-qi alie fariki mwaka 952 H, ana Kitabu "Al-muhdi ila ma-warada fil Mahdi".[86]
10- Aly bin Hussaamud-din Al-mutaqiy Al-hindiy alie fariki mwaka 975H, ana kitabu "al-burhaan fi alaamati mahdiy Aakhiriz-zaman" na kitabu "Talkhiisul-Bayaan fi akhbari Mahdiy Aakhiriz-zaman".[87]
11- Ali Al-qaariy Al-hanafiy aliefariki mwaka 1014 H, ana kitabu "Arrad alaa man hakama wa qadha annal Mahdy jaa'a wa madhwa".
Na kitabu "Al-mashrabul-wirdiy fi akh-baril Mahdy".[88]
12- Mar-ii bin Yusuf Al-Karamiy Al-hanbaliy alie fariki mwaka 1031 H, ana kitabu "Faraidu-fawaidul-fikri fil Imamil-Mahdiyil-Muntadhwar".[89]
13- Al-Qaadhi Muhammad bin Ali Ash-shaukani alie fariki mwaka 1250 H, ana kitabu "Ataudhihu fi tawaturi majaa'a fil Mahdiy Almuntadhar wad-dajaali wal-masiih.[90]
14- Rashid Arrashid Atadhafiy Al-halabiy wa zama hizi ana kitabu "Tanwiir Ar-rijaal fi dhuhuril-Mahdy wa dajjal" kime chapishwa.
Hivyo hivyo washairi walikuwa pamoja na "fikra ya mahdi" na "Mahdi mwenyewe", kwani kaswida zao zilikuwa na madhumuni na maana yaelezayo fikra hiyo na ambao ni wengi, na kaswida zao ni zenye kuelezea kutarajiwa kutokea siku yake, na kukiri kuja kwake kusiko na shaka na miongoni mwa washairi hao kwa mfano na kama ushahidi na sio kuwataja wote ni:
1- Al-Kumeit bin Zaid Al-asadi, aliefariki mwaka 126 H, na kuhusu suala hilo anasema:"Ni wakati gani itasimama haki kwenu na wakati gani atasimama Mahdy wenu wa pili.[91]
2- Ismaa'il bin Muhammad Al-himyari alie fariki mwaka 173H, nae anasema kuhusu hilo"Ni kwamba Bwana wa utawala na mwenye kusimama (na kuleta mabadiliko) ambae nafsi yangu inamuelekea kwa kuimba, anayo ghaiba, ni lazima aghibu. Basi Mwenyezi Mungu amrehemu mwenye kughibu, atakaa kipindi fulani kisha atadhihiri kipindi kingine, na kuujaza uadilifu mashariki yote na magharibi".[92]
3- Da'abal a-Khuza'iy aliefariki mwaka 246 H, anasema kuhusu hilo:"Kutoka kwa Imamu hakuna shaka atatoka. Atasi-mama juu ya jina la Mwenyezi Mungu na baraka zake, na atatu-pambanulia haki na batili na atatoa malipo kwa neema na adhabu.[93]
4- Mihyaar-Ad-daylamy aliefariki mwaka 428 H, anasema kuhusu hilo:"Huenda zama za kesho zikaiponya mioyo ya wenye ghadhabu kutokana na wenye kukufanyia uadui.
Huenda ushindi wa haki ukawa juu ya jambo lisilo wezekana, huenda upungufu ukashindwa na utukufu na ubora kwa kusikia kwangu wito wa huyo mtu wenu atakae simama akiitikiwa na kila mwenye kuomba msaada.
5- Ibnu Muniir Attaraabilsiy aliefariki mwaka 548 H, amese-ma kuhusu hilo kwa njia ya mzaha na utani "Nimewatawalisha watu wa kizazi cha umayya walio safi watukufu na walio barikiwa na ninamkadhibisha mpokezi na ninatia ila kwenye kudhihiri kwa Mahadi".[94]
6- Muhammad bin Twalha Ashaafiy aliefariki mwaka 652 H, anasema: "Na alisema Mtume(s.a.w.w) kauli tuliyo ipokea". Akaendelea hadi kusema "Na hakika alimdhihirisha kwa kueleza nasaba yake na sifa zake na kumuita jina lake, na inatosha kauli yake kuwa "anatokana na mimi" kudhihiri uhai na maisha yake na katika pande la nyama yake ni Zahra ndio mahala pake na sharafu yake watakao sema ni Mahdi hawa kukosea kwa hilo walilo litamka".[95]
7- Ibnu Abil-hadiid Al-Mu'utazilii alie fariki mwaka 656 H, amesema kuhusu hilo: "Hakika nimefahamu ya kuwa ni lazima aje Mahdi wenu, na siku ya kuja kwake ninaitarajia. Atahudu-miwa na vikosi vya jeshi la Mwenyezi Mungu, kama mtu mwenye maumivu amekuja akiwa ni mwenye ushindi na kikisonga mbele kizazi cha Abil-hadidi wa kiwa mashujaa na walio mashuhuri na mikuki iliyo inuliwa juu.[96]
8- Shamsud-din Muhammad bin Tuulun Al-Hanafy Ad-damsh-qiy aliefariki mwaka 953H, anasema kwenye kasida yake akiyataja majina ya Maimamu kumi na wawili:"Na Askari Hassan alietwahirika Muhammadul-Mahdi atadhihiri".[97]
9- Abdullah bin Alawi Al-hadaad Attarimy Ashaafi'i, alie fariki mwaka 1132 H, na kuhusiana na hayo amesema: "Muhammad Al-mahdi ni khalifa wa Mola wetu, Imam wa uongofu na dola lake linasimama kwa uadilifu kana kwamba namuona (siku hizo) akiwa baina ya maqaam na nguzo yake (yaani kati ya nguzo ya kaaba na maqam ya Ibrahim) wakimpa baiya kila upande wenye kumpongeza". Na anasema katika sehemu nyingine: "Na kwetu kuna Imam umefika wakati wa kutoka kwake, atasimama kwa amri ya Mwenyezi Mungu kama ipasavyo, na kuujaza ulimwengu kwa haki na uadilifu na uongofu, kama ulivyo jazwa jeuri kwa dhulma ya watu waovu.[98]
Hakika Uislamu uliipinga rai ya mayahudi ya kuwa "Elia" ndie msuluhishaji mwenye kusubiriwa na pia rai ya wakristo isemayo kuwa yeye ni "Issa mwana wa Maryam".Vilevile hali ya wazi ya matokeo ya nje imeipinga rai ya madhehebu ya kiisaaniya ya kuwa huyo mwenye kusubiriwa ni "Muhammadi bin Alhanafiya" na madhehebu ya "Ismaailiyya, ya kuwa huyo ni "Ismaail bin Jaafar" kwani imethibiti kufariki kwa Muhammad na Ismaili na kubatilika fikra ya kubakia kwao. Basi imebaki tofauti na hitilafu kati ya Ahli sunna na Shia Imamiya katika kumuainisha Mahdi ni nani.
Na muhtasari wa itikadi za Ahli sunna ni kuwa Mahdi atadhihiri zama za mwisho na atasimama kwa upanga na kwamba "Habari zake zimekuwa mutawaatiri (nyingi sana na zingine mustafidhi, kwenye kila tabaka kuna wapokezi wawili au watatu" kwa wingi wa wapokezi wake kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kuhusu kutokea kwake na kwamba yeye anatokana na kizazi chake Mtume, na kwamba atamiliki au kutawala kwa muda wa miaka saba.
Na kwamba ataijaza ardhi na ulimwengu kwa uadilifu, na kwamba atatoka pamoja na Issa(a.s) na kuwa yeye atawaongoza kwenye sala umma huu na Issa atasali nyuma yake.[99]
Na muhtasari wa itikadi ya Shia Imamiyya ni kuwa atadhi-hiri katika zama za mwisho Mahdi atokanae na nasaba ya Ali na atasimama kwa upanga, na kwamba ataujaza ulimwengu uadilifu na usawa na atatengeneza mazingira yawezeshayo kuutekeleza Uislamu kiukamilifu katika ardhi yote.
Kwa hivyo ni sehemu ipi yenye tofauti kati ya kauli mbili hizi?
Hakika kati yao imefungika kwa upande wa masunni kwenye kauli au kwenye itikadi yao ya kuwa, Mahdi huyu atazaliwa katika zama za mwisho, na hivi sasa hayupo, na haijulikani ni wakati gani atakao zaliwa na baba yake ni nani? Kwa msingi huu aliweza Sunuusiy huko Libia na Abdul-Rahmaan wa huko Sudan na wengineo kudai kuwa wao ni akina Mahdi na kusimama kwa upanga (Silaha).
Ama Shia Imamiyya, wao rai yao ni kuwa Mahdi ni Muhammad bin Hassan bin Ali bin Muhammad bin Ali bin Mussa bin Jaafar bin Muhammad bin Ali bin Hussen bin Ali bin Abi twaalib(a.s) na kwamba yupo kwenye dunia hii lakini watu hawamtambui. Na hii ndio nukta yenye tofauti kati ya pande hizi mbili.
Kutokana na ukweli kuwa mwenye kutoa madai ndio huiti-shwa dalili ya madai yake, kama ilivyo katika fiqhi (sharia) ya kiislamu, basi sisi tutatoa ushahidi ambao wana utegemea Mashia kwenye kuthibitisha yale wanayo yaitakidi, na tutaonyesha usha-hidi mwingine walio utumia kuzibatilisha rai za wapingao fikra hii, ili jambo hili liweze kuonekana na kujulikana wazi kwa kila mwenye macho mawili. Na kutokana na ukweli kuwa mashia kama tulivyo eleza mwanzoni mwa maudhui haya kuwa wana amini kuwa uimamu ni cheo cha kupewa na Mwenyezi Mungu na kina hitajia dalili na uteuzi, wame amini kuwa uimamu wa Mahdi, Muhammad bin Hassan kufuatana na dalili zilizopo na kwa kuzitii dalili hizo, na kufuatana na matamshi yake yaliyo wazi kabisa.
Huenda kukawa na mwenye kuuliza, dalili hizo ni zipi na lafdhi zake ni zipi na ni nani alie zisimulia na kuzipokea?
Ili kulifafanua jawabu la swali hilo ni lazima kuashiria kuwa dalili hizo zimhusuzo Mahdi haikuwa ni habari ( hadithi) moja au mbili, bali ni habari nyingi zilizotoka kwa Mtume(s.a.w.w) na zilizo mutawaatir zilizovuka mamia, na zilipokewa na idadi kubwa ya maswahaba, na zikatolewa na idadi kubwa nyingine ya mahuffa-dhi na wapokezi, na kwa wingi wa istifadha (wapokezi watatu kwenye kila tabaka) tawaatur (wapokezi wengi sana) haikuwa tena ni sahihi kufanya mjadala kuhusu usahihi wa hadithi hizi na kuhusu yakini zinazo tuletea katika kuthibitisha swala hilo. Na kwa ajili ya udadisi zaidi na utafiti wa kimaudhui tunasema:
Hakika hadithi hizi kwa sanadi yake na dalili yake zimegawa-nyika kwenye makundi matatu:
Kundi la kwanza:
Zenye sanadi sahihi na dalili yake ni ya dhahiri zisizo na shaka yoyote, na maimamu wa hadithi na mahufadhi wakubwa walithibitisha juu ya usahihi wake au kuwa ni hassan[100] (nzuri) na kuwa baadhi yake ni sahihi kufuatana na masharti ya mashekh wawili, Bukhari na Muslim.
Na hakuna shaka katika uwajibu wa kuzichukuwa hadithi za kundi hili na kuzifanyia kazi na kuyaamini mambo yanayo zungumziwa na kujulishwa na hadithi hizo.
Kundi la pili:
Ni hadithi zisizo sahihi katika sanadi yake hata kama dalili yake (yaani maneno yake) iko dhahiri. Kanuni zilizo kubaliwa kwenye elimu ya hadithi zinatulazimisha kuzichukua hadithi hizo vilevile, kwa kuungana kwake na kusahihishwa kwake na kundi la kwanza na kwa kuwa mashuhuri ya kuwa wanazuoni wame-zikubali, bali wanazuoni wote wamefanya ijmai kuafikiana juu ya madhumuni yake.
Na kundi la tatu:
Limekusanya sahihi na dhaifu, lakini hadithi hizo zinapi-ngana na hadithi zingine zote ambazo ni mustafidhi na zilizo mutawaatir. Basi kitu cha lazima ni kuziacha, na kujiepusha nazo, ikiwa haikuwezekana kuzifanyia ta'awili, kwa mfano zilizosema kuwa jina la Mahdi ni Ahmad au zilizo sema kuwa jina la baba yake linafanana na jina la baba yake mtume(s.a.w.w) au zisemazo kuwa yeye anatokana na watoto wa Abi Muhammad Hassan Az-Zakiy, kwani habari hizi ni habari chache na nadra ambazo wanazuoni mashuhuri wamejiepusha nazo.[101]
Hadithi za makundi mawili la kwanza na la pili hizo ndizo ambazo tumebainisha kuwa ni wajibu kuzichukuwa zilikuwa zikielekeza kwenye lengo kwa ibara tofauti tofauti na zikikusudia kumtambulisha na kumuainisha kwa matamshi tofauti tofauti na tunaweza kuufupisha muhtasari wake kama ifuatavyo:
Baadhi ya hadithi hizo zimethibitisha kuwa Mahdi anatokana na kabila la kikuraishi. Ametoa Ahmad na Al-manwardi ya kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:
"Pateni bishara ya Mahdi, ni mtu atokae kwenye kabila la kuraishi, atokae kwenye kizazi changu. Atatoka watu watakapo hitilafiana na kuwepo mtetemeko, na kuijaza ardhi kwa uadilifu na usawa kama ilivyo jazwa dhuluma na ujeuri".[102]
Na zingine zimethibitisha, kuwa Mahdi ni katika watoto wa Abdul-Mutwalib.
Ametoa Ibn Maaja kwa sanadi yake kutoka kwa Anas bin Maalik, amesema: Nilimsikia Mtume(s.a.w.w) akisema:
"Sisi watoto wa Abdul-Mutwalib ni mabwana wa watu wa peponi, Mimi na Hamza na Ali na Ja'afar na Hassan na Hussen na Mahdi".[103]
Na zingine zimethibitisha kuwa yeye ni katika Aalu Muhammad (Kizazi cha Mtume,(s.a.w.w) . Amesema Mtume(s.a.w.w) :
"Atatoka katika Zama za mwisho mtu atokanae na kizazi changu, jina lake ni kama jina langu, na kuniya yake ni kama yangu (jina la ubaba kwa mfano baba ya fulani) ataijaza ardhi kwa uadilifu kama ilivyo jazwa ujeuri, na huyo ndie M ahdi". Na hii ni hadithi mashuhuri.[104]
Na zingine zimethibitisha kuwa ni katika kizazi chake. Ametoa Abu Daud kwa Sanadi yake kutoka kwa Ummu Salama (Mungu amuwie radhi) amesema:"Nilimsikia Mtume(s.a.w.w) akisema:
"Madhi anatoka katika kizazi changu ".[105]
Na zingine zimethibitisha kuwa yeye ni katika Ahlul bayti. Amesema Mtume(s.a.w.w) :
"Lau kama isingebakia isipokuwa siku moja Mwenyezi Mungu angetuma mtu atokanae na Ahlul-bayti wangu aujaze ulimwengu uadilifu kama ulivyo jazwa ujeuri .[106]
Na zingine zimethibitisha kuwa, anatokana na watoto wa Ali(a.s) , kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibnu Abbas (Mungu awawie radhi) amesema: "Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu:
"Hakika Ali (a.s) ni wasii wangu na katika kizazi chake atatoka huyo mwenye kusimama (dhidi ya dhulma) na mwenye kusubiriwa (almuntadhar), ambae ni Mahdi atakae ijaza ardhi usawa na uadilifu kama ulvyo jazwa ujeuri na dhulma ".[107]
Na zingine zimethibitisha kuwa ni katika watoto wa Fatima.
Ametoa Muslim na Abu daud na Nasai na Ibnu Maaja na Bayhaqiy na wengine:
"Mahdi ni katika kizazi changu ni katika watoto wa Fatuma ".[108]
Na wengine wamethibitisha kuwa ni katika watoto wa Hussen, Amesema Mtume(s.a.w.w) :
"Haitaondoka dunia mpaka ausimamie umma wangu mtu atokanae na kizazi cha Hussen, aijaze ardhi kwa uadilifu kama ilivyo jazwa dhulma ".[109]
Na zingine zimethibitisha kuwa ni wa tisa katika kizazi cha Hussen. Kutoka kwa Salmani Al-faarisi (Mungu amuwie radhi) amesema:"Niliingia nyumbani kwa Mtume(s.a.w.w) mara nika-muona Hussen akiwa mapajani mwake akilibusu shavu lake na kuulamba mdomo wake na akisema:
"Wewe ni Sayyid mtoto wa Sayyid, nduguye Sayyid, na wewe ni Imam Mtoto wa Imam na ndugu wa Imamu, na wewe ni Hujja mtoto wa Hujja ndugu wa Hujja baba wa Mahujja tisa, wa tisa wao ni yule atakae simama (dhidi ya dhulma) ambae ni Mahdi.[110]
Na zingine zilithibitisha kuwa yeye ni wasii wa kumi na mbili. Na Imamu wa kumi na mbili na khalifa wa kumi na mbili.
"Hakika wasii wangu ni Ali bin Abi twalib na baada yake ni wajukuu wangu wawili Hassan na Hussen watafuatiwa na maimamu tisa watokao kwenye uti wa mgongo wa Hussen(a.s) , akasema:"Ewe Muhammad nitajie majina yao". Akasema: "Aki-ondoka Hussen ni mwanae Ali akiondoka Ali ni mwanae Muhammad, akiondoka Muhammad ni mwanae Jaafar, akiondo-ka Jaafar ni mwanae Mussa, akiondoka Mussa ni mwanae Ali, akiondoka Ali ni mwanae Muhammad, akiondoka Muhammad ni mwanae Ali akiondoka Ali ni mwanae Hassan, akiondoka Hassan ni mwanae Alhujja Muhammad Al-mahdi hawa ndio maimamu kumi na mbili".
Yahya binil Hassan ametaja kwenye kitabu Al-umda kupitia njia ishirini za upokezi ya kwamba makhalifa baada ya Mtume(s.a.w.w) ni kumi na mbili na wote wanatokana na kabila la kikuraishi, katika Bukhari kupitia njia tatu za wapokezi, na katika Muslim kupitia njia tisa na kwa Abi Daud kupitia njia tatu, na katika Tirmidhi kupitia njia moja na katika Al-hamiidi kupitia njia tatu".[111]
Na zingine zimethibitisha kuwa ni mtoto wa Hassan Al-askari.
Katika manaaqib kutoka kwa Jaabir bin Abdillahi al-answary kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) :
"Basi baada yake ni mwanae Hassan aitwae Al-askari, na baada yake ni mwanae Muhammad aitwae Mahdi na mwenye kusimama kwa haki (Al-Qaaim) na Al-hujja, atatoweka na kutoonekana kisha atatokea, na atakapotokea ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama ulivyo jazwa ujeuri na dhuluma .[112]
Na hivyo hivyo tunakuta kuwa hadithi hizi kwa wingi huu na tofauti zake zimemuelezea Mahdi wa umma huu, na kusema kuwa ni mtoto wa Hassan Al-askari, nayo ni matokeo au natija thabiti ambayo haina kasoro ndani yake.
Na msomaji ili awe na ujuzi zaidi wa jambo hili tunatoa katika sehemu ifuatayo majina ya wapokezi wa hadithi za Mahdi zilizotajwa hapo kabla na hasa majina ya maswahaba, kwani utafiti wetu huu wa haraka hauna nafasi kubwa ya kuweza kuandika majina ya wapokezi wote kutoka kwenye matabaka mengine:
01- Abu Amama al-baahily
02- Abu Ayyub
03- Abu Said Al khudri.
04- Abu Sulaiman-mchungaji mifugo wa Mtume(s.a.w.w)
05- Abu tufail.
06- Abu Huraira.
07- Ummu Habiba mama wa waumini.
08- Ummu Salama mama wa waumini
09- Anas bin Maaliki.
10- Thubaan-mtumwa wa Mtume (s.a.w.w).
11- Jaabir bin Samrah.
12- Jaabir bin Abdillahi al-Answari.
13- Hudhaifa binil Yamaan.
14- Salman Al-faarisi.
15- Shahr bin Hawhab.
16- Twalha bin Ubaidullah.
17- Aisha mama wa waumini.
18- Abdur-rahmaan bin Auf
19- Abdallah bin Haarith bin Hamzah.
20- Abdallah bin Abbas.
21- Abdallah bin Omar.
22- Abdallah bin Amrubinil Asi.
23- Abdallah bin Masoud.
24- Othmani bin Affan.
25- Ali bin Abitwalib.
26- Ali Alhilaali.
27- Ammar bin Yaasir.
28- Umraan bin Haswiin.
29- Auf bin Maalik.
30- Qurrat bin Iyaas.
31- Mujmau bin Jariyah Al-answari.[113]
Ama ambao walitoa hadithi kuhusu Mahdi kati ya mahufadhi wa hadithi na wenye vitabu vya sahihi na sunanu, ni shekh Abdul-Muhsin Alubad aliwahesabu na kufikia "38" ambao ni mashuhuri na walio wema[114] , na miongoni mwao ni:
01- Abu Daud katika Sunani yake.
02- At-tirmidhi kwenye kitabu chake kiitwacho "Jami'u".
03- Ibnu Maaja kwenye Sunani yake.
04- An-nasai kwenye kitabu chake Alkubra.
05- Ahmad kwenye Musnadi wake.
06- Ibnu Habban kwenye Swahihi yake.
07- Al-haakim kwenye Mustadrak.
08- Abubakar bin Abi Shaiba kwenye "Al-munswif".
09- Naim bin Hamad kwenye Kitabu Al-fitani.
10- Abu Naiim kwenye kitabu "Al-Mahdi wal-hilyah".
11- At-twabaraniy kwenye kitabu "Al-kabiir wal-awsat wa As-swaghiir.
12- Ad-daru-qutni kwenye kitabu "Al-ifrad".
13- Al-baarudy kwenye kitabu "Ma'arifat As-swahaba".
14-Abu Ya'ala al-muuswiliy kwenye Musnad yake.
15- Al-bazzar kwenye Musnad yake.
16- Al-haarith bin Abi Usamah kwenye Musnad yake.
17- Al-khatib kwenye kitabu chake"At-talkhisul-mutashabih" na katika "Almut- tafaq wal-muftaraq".
18- Ibnu Asakir kwenye kitabu cha historia.
19- Ibnu Mundih kwenye kitabu chake cha historia "Taarikh Isbahan".
20- Abul-hassan Al-harbiy kwenye kitabu chake "Al-awwal minal-harbiyaati".
21- Tamam Ar-raziy kwenye "Fawaid".
22- Ibnu Jariri kwenye "Tahdhibul-Athar".
23- Abubakari bin Al-muqri kwenye "Mu'ujam" wake.
24- Abu Amru Addani kwenye Sunani yake.
25- Abu Gharam Al-kuufiy kwenye kitabu chake "Al-fitani".
26- Ad-daylamiy kwenye kitabu chake "Musnadul-fir dausi".
27- Abu Bakar Al-Iskaf kwenye "Fawaidul Akhbaar".
28- Abul-Hussen binil Munawiy kwenye kitabu chake "Al- malaahim".
29- Albaihaqi kwenye "Dalailu An-nubuwah".
30- Abu-Amru Al-muqri, kwenye Sunani yake.
31- Ibnul Jawzi kwenye kitabu chake cha Historia.
32-Yahya Al-hamaniy kwenye Musnad wake.
33- Ar-ruyaaniy kwenye musnad wake.
34- Ibnu Sa'ad kwenye "Twabaqaat".
Imam (Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alizaliwa kwenye mji wa Samarra wakati wa Al-fajiri tarehe kumi na tano ya mwezi wa Sha'aban mwaka 255H.[115] na baba yake akamuita Muhammad, na huo ulikuwa ni uthibitisho wa hadithi ya Mtume(s.a.w.w) iliyo maarufu isemayo "Jina lake ni sawa na jina langu"[116] na Kuniyah yake (Jina lake la ubaba) akumuita Abul-Qaasim.[117]
Na wapokezi wa riwaya wa Shia Imamiyya walisalim amri juu ya ukweli huu na wengine wengi wa makundi mengine ya kiislamu. Lakini baadhi ya waislamu pamoja na kuikubali kwao fikra ya kuja mahdi walimkataa Mahdi kwa hoja ya kuwa hakuna mtoto wa Askari, na wakatoa dalili nne kuthibitisha hoja hiyo, na tutazielezea kwa ufupi, kama ifuatavyo:
1- Walisema kuwa Askari alipo karibia kufa alimuweka mama yake (Umul-Hassan) kuwa ndie muusiwa wake wa kuya-angalia yote aliyo kuwa akiyasimamia kama vitu vya wakfu na sadaka na mambo mbali mbali mengine, kama angekuwa na mtoto asingemuacha kumuusia na kumuusia mtu mwingine.
2- Ni kuwa Jaafar bin Ali ami yake Mahdi alipinga kuwepo mtoto wa kaka yake, na ushahidi wa baba mdogo kwenye jambo kama hili ni wenye umuhimu mkubwa.
3- Hakika mashia wanadai kuwa Askari alificha suala la mwanae kwa watu wasio maalumu na wasio wa karibu, kwa nini alifanya hivyo pamoja na kuwa maswahaba wake walikuwa ni wengi katika siku hizo huku wakiwa na nguvu, mali na uwezo wakati ambapo maimamu walio tangulia kwenye zama za utawala wa bani umaya na bani Abbas walikuwa kwenye hali ngumu zaidi na wali banwa zaidi, pamoja na hayo hawakuficha suala la watoto wao kama ufichaji huu.
4- Hakika vitabu vya historia havikumfahamu na kumuelezea mtoto wa Hassan Al-Askari wala havikusimulia habari yake yoyote. Na kwa dalili hizi nne wakapinga wapingaji kuzaliwa kwa Imam Muhammad binil-Hassan.
Tutatowa sehemu ifuatayo kwa ufupi jawabu la dalili hizi ili jambo hili liweze kuwa wazi na iweze haki kudhihiri, na kwa hivyo tunasema:
Ama jawabu la dalili ya kwanza ni kuwa:
Hakika kumuusia mama haifai kuwa ni dalili ya kupinga kuwepo kwa mtoto, na lengo la Imam kutoa usia huo ni kuwafa-nya watu wasimuelekee na kutaka kujua habari za mwanawe na watu kutojishughulisha nae na mazingira kugubikwa na suala lake na kuwajulisha maadui zake kutokuwepo mwanae, bali aliwazidishia dhana hiyo kwa kuwafanya kuwa mashahidi wa Usia huo watu wengi katika wakubwa wa serikali ya wakati huo juu ya usia huu.[118]
Na Imam alikuwa kwenye matendo yake hayo akifuata mfumo wa babu yake Jaafar bin Muhammad As-swadiq(a.s) pale alipojiwekea wausiwa watano baada ya kufariki kwake nao ni Al-mansuril Abbasi na Arrabi'u na Kadhi wa madina ukiongezea mkewe Hamidah, na mwanae Mussa bin Jaafar(a.s) na lengo lake kwa kufanya hivyo ni kuyaweka mbali macho ya watawala na maadui yasimuelekee mwanae Mussa[119] , kwa sababu lau kama angemuusia yeye peke yake, bani Abbasi wangeweza kufanya jambo lolote lingine tangu siku ya kufariki baba yake, na Mansur alipofikiwa na habari za kufariki Imamu Swadiq(a.s) alimuandi-kia gavana wake wa Madina, akimuamuru azidi kumbana wasii wa Jaafar bin Muhammad, yule gavana akamuandikia Mansuur, baada ya kufanya uchunguzi, akimfahamisha kuwa walio usiwa ni watu watano na kuwa wa mwanzo wao na ambae ni muhimu ni khalifa mwenyewe. Na kwa kufanya hivyo ilikuwa ni kumuepu-shia Imamu Mussa bina Jaafar(a.s) maudhi.
Ama jawabu la dalili ya pili ni kuwa:
Hakika Jaafar ni katika watu wa kawaida, na inawezekana kwake kufanya mambo kama wafanyavyo watu wengine wa kawaida kama kukosea na kuasi na kutoa madai ya batili, na inatosha akawa kama mfano wa Kaabiil, pindi alipomuua ndugu-ye au mfano wa watoto wa Yaakub walipomtumbukiza ndugu yao kwenye kisima na wakamuudhi baba yao na kuapa viapo vya uongo ya kuwa ndugu yao ameliwa na mbwa mwitu.
Na Jaafar alidhania, nae akifahamu kufichwa suala la mtoto wa kaka yake kwa watu wasio maalumu kati ya maswahaba wa baba yake, ya kuwa atakuwa Imamu kwa kupinga kule, na kwa-mba mali za kisheria zitakusanywa kwake kutoka kila pembe na kila upande, lakini Irada ya Mwenyezi Mungu ndio yenye kushi-nda, kwani ni haraka sana ulidhihiri uongo na ubaya wa suala lake, kisha akajuta kwa yale aliyoyafanya na akatubia kutokana na uovu alio ufanya hadi kuwa mashuhuri kwa jina la " Ja'afar Attawaab". (Mwenye kutubia)
Na si jambo la ajabu baba mdogo kusimama kidete dhidi ya mtoto wa nduguye. Hapo zamani Abu Lahab na Abbas walikuwa ni viongozi wa kikundi cha maadui dhidi ya mtoto wa ndugu yao, Muhammad(s.a.w.w) kwani walipinga utume wake na kumuhusisha na uchawi na wendawazimu na kuyaongoza majeshi kumpiga vita na wakaweka mipango na mikakati ya kumua.
Ama jawabu la dalili ya tatu ni kuwa:
Hakika jambo lililo mfanya Imamu Askari kuficha suala la mwanae ni kutokana na kufahamika na kuwa mashuhuri ya kuwa Imam atasimama kwa upanga ili kuondoa dola la batili na kusi-mamisha dola la haki, kwa hivyo watawala walikuwa wakimu-ogopa mwana mapinduzi huyo na wakijiandaa na kuandaa mipango ya kumuua kwa aina yoyote ile, lau wangefahamu suala lake na kujua habari zake. Kutokana na hali hii akalazimika Imam Askari kuficha na kutozisema habari za mwanae na kuzihi-fadhi habari zake kwa siri kwa maswahaba wake maalumu. Na jambo linaloweka wazi na kuyaunga mkono maneno haya ni kuwa serikali tawala za wakati huo waliharakisha kuwatuma wapelelezi wao wakati wa kufariki Imam Askari kwenye nyumba yake ili wamkamate mtoto yoyote atakae kuwa ndani ya nyumba hiyo.[120] Lau kama si utashi wa Mwenyezi Mungu ambao ulimfanyia wepesi Muhammad bin Hassan kukimbia na kujificha, wange-muua.
Na Imamu Askari katika ufichaji huu alikuwa na kigezo cha mama yake Mussa bin Imran alipo shushiwa wahyi kuwa ni lazima kumficha na kufanya siri kuhusu suala la Nabii Mussa kwa kumkhofia Fir'auni wa zama zake kama Qur'an tukufu ilivyoelezea kuhusu swala hilo.
Ama maimamu walio tangulia ilikuwa si lazima kwao kusimama kwa upanga, bali suala hilo liliachiwa kulingana na mazingira na mambo ya zama hizo na kufanya kulingana na mahitajio ya kila zama na mazingira yake kwa kujua ni hukumu gani au taklifu ipi inatakiwa, kwa hivyo walikuwa na amani kiasi na uhuru kwa kiwango fulani, hata kama haikuwa ni amani na uhuru kwa maana yake sahihi.
Ama jawabu la dalili ya nne ni kuwa:
Hakika kujulikana utoto au mtoto huyu kuwa ni wa huyu huthibitika katika sheria, kwa kauli ya mkunga au wanawake ambao huwepo kwenye uzazi ule (yaani mama yule anapo jifungua) na kwa kukubali mwenye kitanda (baba mzazi) na kushuhudia wanaume wawili walio waislam juu ya kukiri na kumkubali baba mtoto wake. Na pande hizi tatu zilithibitika na kupatikana kwenye uzazi ule.
Kwa mfano, Sayyida Hakimah binti wa Imam Jawaad(a.s) ndie ambae alisimamia jambo hilo la uzazi na akashuhudia uzazi huo. Na Imam Askari ndie baba na alikubali kuzaliwa kwa mtoto huyo mbele ya maswahaba wake maalumu.[121]
Na waislamu wa zama hadi zama zinginezo zilizo fuatia, wanasimulia habari hizo na wanashuhudia juu ya usahihi wake. Na miongoni mwa waliopokea na kusimulia uzazi huu, ukiongezea juu ya kukubaliana mashia Imamiyya wote juu ya suala hili kati ya wanazuoni wa kiislamu, kuna idadi isiyo chache ya wana historia na waandishi, kwa mfano kuna hawa wafuatao:
01-Muhammad bin Twalha Ashaafii,aliefariki mwaka 652 H.[122]
02- Sibti ibn Jawziy, aliefariki mwaka 554 H.[123]
03- Al-kanji Ashaafi'i , aliefariki mwaka 658 H.[124]
04- Ibnu Khalakaan Ashafi'i, aliefariki mwaka 681 H.[125]
05- Swalahud-dini As-swafadi aliefariki mwaka 764 H.[126]
06- Ibnu Hajar Al-haytami Ashaafi'i aliefariki mwaka 852 H.[127]
07- Ibnu Swabbagh Al-maaliki, aliefariki mwaka 855 H.[128]
08- Ibnu Tuuluum Ad-damashqi, aliefariki mwaka 953[129]
09- Al-Hussen bin Abdallah Assamar qandi, aliefariki mwaka 1043.[130]
10-Mohammad As-swaban Ashaafi'i, aliefariki mwaka 1206.[131]
11- Sulaimani Al-kanduzi'ii, Al-hanafiy aliefariki mwaka 129 H.[132]
12- Mohammad Amin As-suwaydi aliefariki mwaka 1246 H.[133]
13- Mu'umin Ashablanji Ashaafi'i, aliefariki katika karne ya 14 H.[134]
4
USUULID DIIN
UIMAMU
SEHEMU YA TATU
UWEZEKANO WA KUGHIBU NA DALILI ZAKE
Imetuthibitikia kutokana na yote yaliyo tangulia kuwa fikra ya (kuja kwa) Mahdi, ni fikra iliyochimbuka kwenye sheria halisi ya kiislamu, na Mtume(s.a.w.w) alitoa bishara ya fikra hiyo katika hadithi zilizo kuja kutoka kwake, na wanazuoni wa hadithi tabaka kwa tabaka wakarithishana na kupeana riwaya hizo kama ilivyo thibiti vilevile ya kuwa Mahdi aliezungumziwa kwenye hadithi ni Muhammad bin Hassan Al-askari, na kwamba alizali-wa kwenye mji wa Sammarraa na habari za kuzaliwa kwake kujulikana kwa siku ile aliyo zaliwa kwa watu maalumu katika maswahaba wa baba yake, kisha akawa mashuhuri baada ya kuzaliwa kwake kwenye vitabu vya historia.
Na ni lazima kwetu baada ya kuthibitika sehemu mbili za mwanzo tuhamie kwenye maudhui ya sehemu ya tatu na ya mwisho inayo husiana na hatua ifuatiayo baada ya kuzaliwa Muhammad bin Hassan na kuthibiti kuwa yeye ndie Mahdi.
Na huenda ikawa bora zaidi ili kufuata mfumo maalumu na ili kuweka wazi jambo hilo, twende hatua kwa hatua kwenye mazungumzo yetu kufuatia mtiririko ufuatao:
01: Je Mahdi alighibu (alifichika na kutoonekana)?
02: Tukijaalia kuwa kuna uwezekano wa kughibu, je mtu anaweza kubakia akiwa hai kwa muda wa karne zote hizo?
Na ni vizuri kwetu, na huku tukiwa tumefikia sehemu nyeti na ya muhimu zaidi katika utafiti huu, tutangulize utangulizi ufuatao kabla ya kuingia kwenye kina cha maudhui yenyewe, ili utusaidie kufikia natija zilizo safi na malengo kuwa wazi.
Hakika Uislamu uliifanya akili kuwa ndio chimbuko la itikadi na msingi wa Imani, na ukakataa kufanya taklidi (kuwa-fuata watu ufuataji usio na dalili) na ufuataji wa kiupofu, na lengo la kufanya hivyo ni kuwa misingi ya itikadi na mizizi yake ijitege-meze kwenye akili na kuitegemea akili, na misingi hiyo ipate nguvu yake na kujizatiti kutokana na akili pekee, bila kushiriki kitu kingine chochote kwenye suala hilo kama matamanio ya nafsi na kutawaliwa na hisia za ndani na kufuata watu wengine.
Na hivyo ndivyo akili ilivyo kuwa ni dalili ya kumtambulisha Mwenyezi Mungu, nayo ndiyo iongozayo kwenye Imani. Katika kuwepo Mwenyezi Mungu na Umoja wake na katika ulazima wa kuwepo kwake, kisha akili vilevile ili kuwa ni dalili ya kuthibiti-sha ulazima wa kuwepo utume na uimamu na kuwepo marejeo ya kiama yakiwa ni matawi ya Imani ya Mwenyezi Mungu alie tukuka.
Ama maneno mengine ya hukumu za sheria na dalili za kidini hazihitajii dalili ya kiakili, na si lazima kwa mambo yao kusima-misha dalili kama hii, bali inatosha kulazimika kuyakubali kwa kutolewa tu dalili yenyewe ya aya au riwaya, juu ya suala hilo kwa njia za kisheria zilizo thibitisha ulazima wa kuzitii na kuzi-fuata dalili za kidini (aya na riwaya).
Kutokana na haya waislamu wakaamini kwa ukweli na kwa yakini, mas'ala ya kuwepo malaika kwa mfano, au kuamini kuwa Issa alizungumza akiwa mtoto mchanga au habari za mawe kumsabihi Mwenyezi Mungu yakiwa mikononi mwa Mtume(s.a.w.w) , kwa ajili ya kuzungumziwa mambo haya kwenye Qur'an tukufu na sunna sahihi.
Na sisi tunapofanya utafiti kuhusu maudhui ya Mahdi na kughibu kwake tunayafanyia utafiti pamoja na waislamu wenye kukubali misingi ya uislamu na misingi ya sheria, bila ya kuwahusisha wengine wapingao kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu au ambao bado hawajawa waislamu, na kufanya hivyo ni kwa sababu mas'ala yenyewe yalivyo, yanategemea kutolewa dalili na ushahidi wa Qur'an tukufu na Sunna tukufu, kwa hivyo haifai kuyazungumzia mas'ala haya pamoja na mtu asie kiamini kitabu na sunna.
Kwa ibara nyingine, hakika sisi tunayafanyia utafiti maudhui haya juu ya msingi wa itikadi ya dini yenye kujitegemeza kwenye dalili za kisheria ambazo waislamu wote wamekubaliana na kuafikiana ya kuwa ni wajibu kuvifuata na kuvifanyisha kazi na si kwa kufuata msingi mwingine wala mas'ala haya kwa hali yoyote hayajawahi kuwa kama kazi ya kimahesabu ya kawaida kama jibu la 2 2 au kama kanuni ya kifalsafa ambayo haiwe-zekani kuzungumziwa na kujadiliwa kama kubatilika kwa dauru (mzunguko usio na mwisho) au tasalsulu (silsila ya vitu vyenye uhusiano isiyo kuwa na kikomo).
Kwa hivyo basi, na awe msomaji mtukufu ni mwenye kufahamu ya kuwa sisi tutayazungumzia na kuyafanyia utafiti mas'ala haya au tatizo hili kwa pande zake zote kwa kufuata msingi wa kitabu na sunna kwa sababu vitu hivi viwili ndio chimbuko la sheria na mlango wa maarifa na elimu kwa waislamu, na kwamba kuvipinga na kutoka kwenye msingi wa kuvifuata ni sawa na kuupinga Uislamu na kutoka dhidi ya hukumu zake na amri zake.[135]
Ukiwa wazi utangulizi huu, tunasema:
Hakika hadithi tukufu za Mtume ambazo zimepokelewa na mahufadh wa hadithi, na wakiwemo kati yao wale ambao waislamu wamekubaliana juu ya usahihi wa hadithi zao, zimekariri mara kadha neno la "kughibu".[136]
Na kati ya hadithi zingine zinasema "Ataghibu", kutakuwa na hali ya watu kutapatapa na kutahayari, na kaumu zitapotea kwenye hali hiyo ".[137]
Na katika riwaya nyingine:
Na katika riwaya nyingine "Ataghibu na kuto onekana kwa wapenzi wake, kuto onekana ambako hatabakia kwenye Imani na kauli ya Uimamu wake isipokuwa yule ambae Mwenyezi Mungu amempa mtihani moyo wake kwa Imani .[138]
Na katika hadithi ya Ibnu Abbas:
"Atatumwa Mahdi baada ya kukata tamaa, na mpaka watu waseme:Hakuna Mahdi ".[139]
Neno "ghaib" kama hadithi tulizo zitaja zilivyo,haina maana ya kumuhuisha Mahdi baada ya kufa kwake, na kumrejesha duniani baada ya kufa kwake bali hadithi hizo zina angalia kwenye ile hali ya kuto onekana kwake na kufichika kwake na watu kutomuona na kumshuhudia, na haya ndio yafahamikayo kwa haraka kwa kila msomaji pindi anapo soma hadithi hii na kulipima neno (ghaiba) lililo kaririwa kwenye hadithi hizo.
Na hadithi tukufu ambazo waislamu wamekubaliana juu ya riwaya yake.
"Mwenye kufa na hakumjua Imamu wa zama zake amekufa kifo cha kijahili ".
Hadithi hii iko wazi katika kuonyesha ulazima wa kuwepo Imamu katika kila zama na kila wakati.
Na baada ya kuthibiti kuzaliwa kwa Muhammad bin Hassan kwa dalili zisizo na shaka, neno "ghaiba" na ulazima wa kuwepo Imamu katika kila zama na kuwa ni dalili mbili za wazi zithibitishazo kuendelea kuwa hai kwa Mahdi kwa muda wa karne zote hizi na zinakuwa dalili za kupinga maneno mengine yasemayo kuhusu maudhui haya, maneno yenye kutilia shaka na kutowezekana kufanyika kitu kama hicho.
Na kauli ya kuwa Mahdi amekufa, pamoja na kuwa inapi-ngana na hadithi za ghaiba na hadithi za kuendelea kuwa hai kwa uimamu, hakuna mwana historia yeyote alieitolea ushahidi, na haikutajwa kwenye kitabu chochote ikiwa miongoni mwake vitabu vya wapingao suala hili Amekufa lini? Na katika siku ipi na mwezi gani na mwaka gani na wakati gani, alipelekwa kuzikwa na ni akina nani walio hudhuria mazishi yake na amezikwa w api na katika nchi gani?
Hakika yote haya yanatilia mkazo kuwa Mahdi, yuhai hakufa na kwamba yeye alighibu na kufichika mbali ya macho ya maadui zake, ili kuyahifadhi maisha yake na kuiokoa nafsi yake na kufichika kwake kulikuwa ni kwa aina mbili.
Aina ya kwanza:
Kutoonekana kwa watu pale jeshi la khalifa walipo ivamia nyumba ya Imamu Askari baada ya kufariki kwake. Na katika kipindi hiki alikuwa akiwasiliana na mawakili wake na kuwapatia majibu juu ya maswali na matatizo ambayo mashia wakiyaele-keza kwake.
Aina ya pili:
Ni kutoonekana kwake kiukamilifu kwenye macho ya watu kiasi kwamba alikuwa hawasiliani na yeyote.[140]
Hakika suali la muhimu linalojitokeza kwenye akili, baada ya kuthibitika kuwepo kwa Mahdi na kufichika kwake na maisha yake kuendelea hadi leo, ni hili: Je anaweza kubakia hai kwa muda wa miaka yote hiyo? Na je, akili ina kubaliana na hilo?
Kabla ya kujibu swali hilo tunapenda kumkumbusha mso-maji yaliyo tangulia kusemwa kuwa, mambo ya kweli ya kisheria yakithibitika kwa habari za kunukuliwa zilizo sahihi, basi sisi kwa kuzingatia kuwa ni Waislam, ni lazima kwetu kufuata na kutii habari hizo na kuikubali hata kama akili zetu hazikupata njia na muongozo wa kufahamu falsafa yake na kujua siri zake.
Kwa hakika kutofahamu hekima ya hukumu hii au sababu yake, haiwi ni dalili ya kuipinga na kuikataa, bali ni lazima kusalimu amri na kutekeleza kwa hali yoyote, na haifai katika Uislamu, Muislamu kupinga hukumu moja wapo kati ya hukumu zake au kuitoa na kutolikubali suala lolote lililo elezewa kwa hoja ya kutofahamu siri au kutokinaika na sababu iliyotolewa.
Ama umri kuwa mrefu na maisha kuendelea kuwepo kwa muda wote huo kwa mamia ya miaka sio katika mambo yaliyo muhali, na kutowezekana kama wanavyo dhania baadhi ya watu bali imepokelewa riwaya na wana historia na kusimulia juu ya kutokea hilo kwa wingi, kwenye historia ya wanadamu ambayo ni ndefu. Kwa mfano Adam(a.s) alipewa umri na kuishi kwa muda wa miaka elfu moja. Na Lukman mwenyewe alipewa umri wa miaka elfu tatu na miatano (3500). Na Salman Al-faarsi (Mungu amuwie radhi) aliishi muda mrefu hapa aridhini, na baadhi ya wana historia wanadai kuwa aliishi zama za Masihi Issa(a.s) na kuudiriki Uislamu na akafariki kwenye zama za Khalifu Omar binil Khattab.
Na wengine wengi waliopewa umri wa mamia ya miaka na habari zao kusimuliwa na wanahistoria na hasa Assajastani alie kusanya habari zao kwenye kitabu alicho kiita "Al-muammarun" (waliopewa umri mrefu) kilicho chapishwa kwa mara ya kwanza Misri mwaka 1323 H, 1905 AD. Huu ni uthibitisho kwa upande wa kihistoria.
Ama Qur'ani tukufu ndio kauli iliyo ya kweli zaidi na hoja yenye nguvu zaidi kuliko mwana historia yeyote na riwaya yeyote.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu na kauli yake ni ya kweli: Hakika Nabii Nuhu(a.s) alikaa katika kaumu yake akiwalingania kwenye Imani ya Mwenyezi Mungu kwa muda wa miaka "950" na Mwenyezi Mungu ndie ajuae ni muda gani alio ishi kabla ya kuanza wito na baada ya tuufani.
Na kwamba Mtume Yunusu(a.s) alibakia kwenye tumbo la nyangumi kwa muda mrefu na lau kama si fadhila za Mwenyezi Mungu wake angebaki kwenye tumbo lake hadi siku ya kiama.
"Basi iseng elikuwa ya kwamba yeye alikuwa ni miongoni mwa wenye kumsabihi Mwenyezi Mungu bila shaka angekaa kwenye tumbo lake hadi siku ya kufufuliwa".
Na maana ya kukaa huku ni kubakia kwake akiwa hai hadi siku ya kiama na nyangumi nae kubakia hai pamoja nae kwa muda wote huo ulio mrefu. Na kwamba watu wa pango (kahfu):
"Walikaa kwenye pango lao miaka mia tatu na wakazidisha tisa" wala hatufahamu ni kwa muda gani waliishi kabla ya kuingia pangoni na baada ya kutoka kwao
Na kwamba:
"Au kama yule ambae alipita kwenye kijiji (akakikuta) kikiwa kimeharibika na majumba yake kubomoka akasema:Vipi Mwenyezi Mungu anaweza kuvihuisha vitu hivi baada ya kufa kwake? Mwenyezi Mungu akamfisha kwa muda wa miaka mia moja, kisha akamfufua akasema, umekaa hapa kwa muda gani? Akasema: Nimekaa kwa muda wa siku moja au nusu siku. Akasema: Bali umekaa kwa muda wa miaka mia moja, basi kiangalie chakula chako na kinywaji chako hakikugeuka wala kuharibika, na muangalie punda wako".
Huwenda kubakia chakula na kinywaji (maziwa) kwa muda wa miaka mia moja bila kuharibika au kugeuka, ni jambo la ajabu zaidi kuliko umri mrefu wa mwanadamu na lengo lenye kustaajabisha zaidi.[141]
Yote haya kwa kuongezea na mambo mengine waliyo yaandika waandishi wa historia na wana hadithi na wakayapokea kwa kuyakubali na kuhusu uhai wa Khidhiri ambae alikuwepo kabla ya zama za Mussa(a.s) na ataendelea kuwepo hadi zama za mwisho.
Je tuyaamini na kuyakubali yote hayo yaliyo zungumzwa na Qur'an na kupokelewa kwa wingi kwenye suna au la? Na je ina swihi kwetu kuyapinga na kuyakataa ilimradi tu akili ya mwanadamu kwa kiwango chake ilicho nacho haijaweza kufaha-mu siri ya mambo haya na bado haijaweza kufichua na kugundua mambo mengine yaliyo fichika na yasiyo julikana?
Maudhui ya kughibu kwa Mahdi mfano wake ni kama haya kiukamilifu, na ni lazima kwetu kukiri kuwa maisha na uhai wake ni wenye kuendelea kufuatia ushahidi na dalili hizo na kumswadikisha mtume(s.a.w.w) ambae "hatamki kwa matamanio yake bali ayasemayo ni wahyi ulio teremshwa" na kutekeleza amri yake Mwenyezi Mungu.
"Aliyo waleteeni Mtume yachukueni", na imani yetu kwa vitu hivyo haitakuwa ni ajabu au jambo geni, au kuliamini jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye Uislamu, bali kufanya hivyo ni sawa na kuamini umri mrefu wa Nabii Nu hu na kukaa kwa Yunusu kwenye tumbo la nyangumi, na kubakia kwa chakula na kinywaji (maziwa) kwa muda wa miaka mia moja bila kuharibika na bila kugeuka au kupatwa na uharibifu.
Na ikiwa dalili ya Qur'an na hadithi tukufu zimejulisha uwezekano wa mwanadamu kubakia hai zaidi ya miaka elfu moja na kutufahamisha kutokea hilo kwenye kaumu zilizo tangulia, basi hiyo haimaanishi kuwa jambo hilo liko juu ya uwezo wa kielimu na juu ya uwezo wa kiakili, na hii ni elimu ya kisasa inatueleza wazi ya kuwa mwanadamu anauwezo wa kubakia kwa maelfu ya miaka ikiwa ataweza kutayarishiwa nyenzo za kuzihifa-dhi nguvu za kimwili ambazo ndizo zimsaidiazo kubakia hai.
"Hakika maulamaa wenye kutegemewa kwa elimu zao wanasema: "Hakika chembe chembe za msingi kwenye kiwiliwili cha wanyama, zinakubali kubakia kwa muda mrefu usio na mwisho, na kuwa kuna uwezekano wa mwanadamu kubakia hai kwa maelfu kadha ya miaka ikiwa hakutokewa na vitu au vikwazo viwezavyo kukata kamba ya uhai wake, na kauli yao hii si dhana tu bali ni natija na matokeo ya majaribio (au kazi iliyo fanyiwa majaribio".
"hakika mwanadamu hafi kwa sababu kuwa ameishi kwa muda wa miaka kadhaa, sabini au thamanini au mia moja au zaidi, bali kuna vitu vinavyo ingia kwenye baadhi ya viungo vyake na kuviharibu na kuto kuwepo mawasiliano kati ya viungu vyake vyenyewe na vyote vinakufa, na elimu ikiwa itaweza kuondoa vipingamizi vitokeavyo kwenye mwili au kuzuwia ufanyaji kazi wake au kuathirika kwake, hakutabakia kizuwizi kizuwiacho kuendelea kuishi mamia ya miaka".[142]
Naye John Roston anaitakidi kutokana na ugunduzi na majaribio ya kielimu kuwa kufuata njia ya kumhifadhi mwana-damu, halijabakia kuonekana kuwa ni jambo muhali lisilo wezekana[143] , kwani ugunduzi ulio thibitishwa na kuandikwa na wana-zuoni na wataalamu mashuhuri tangu karne moja takriban unatupa na kutuachia matumaini ya uwezekano wa kufikia kufahamu na kugundua chembe zenye uwiano na chembe za mwilini zitakazo saidiana kuongeza kuishi kwa miaka mingi, kwa kutegemea majaribio ya kielimu aliyo yaandika Brown Sickward, Alexy Carl, Voronor, na Minsha bonkov na Bogau Molites,Vilator na wengineo".
"Ama Robert Itinger, ambae aliweka mwishoni kitabu kizuri na makini kwa anwani "Je mwanadamu anaweza kubakia milele akiwa hai", hakika alileta matarajio mapya pale alipo sema: "Hakika mwanadamu ambae anaishi na kupumua kwa hivi sasa anamiliki uwezo wa kubakia kwa upande wa kifizikia".[144]
Haya yote ukiongezea na maneno mengine mengi yaliyo semwa wazi yaelezeayo uwezekano wa kuyahifadhi maisha ya mwanadamu kwa maelfu ya miaka ikiwa mwanadamu atagandi-shwa kwa kipindi hiki, kwa kuzingatia kuwa kugandishwa kunazihifadhi seli (chembe) zote za uhai, na wakati wowote inapotakiwa kumrudishia mwanadamu aliegandishwa ufanyaji kazi wa mwili wake hupewa au huwekewa kiwango fulani cha joto kilicho lazima kwenye mwili na kumfanya kurudi kwenye hali yake, kama alivyo kuwa mwenye nishati kwa harakati na mwenye uhai mwingi ndani yake.
Na vyovyote iwavyo, hakika maneno ya wazi ya wataalamu wa zama hizo yanasisitiza uwezekano wa umri wa mwanadamu kuwa mrefu, na kwamba uwezekano huo ndio kitu kikubwa kiwapacho msukumo juu ya kuendelea na kufanya juhudi za kutaka kuelewa nyenzo za vitu vinavyo weza kulifanya jambo hilo lifanikiwe.
Na ikiwa inafaa mwanadamu kuweza kurefuka umri wake kutokana na maandalizi na maumbile aliyo nayo, itakuwa ni jambo linalo wezekana umri wa Mahdi(a.s) kuwa mrefu kwa karne zote hizi kutokana na hali ya kimaumbile na utashi wa Mwenyezi Mungu.
Na baada ya hayo:
Hakika wanadamu ambao wanaishi kwenye zama hizi ni wenye mazingira magumu sana ya kifikra na ambao ni wakati hatari sana wa utamaduni na wenye kuhitajia sana msuluhishaji huyu mwenye kutarajiwa na kusubiriwa, ambae ni lazima atoke siku fulani ili aweze kurudisha mwendo wa wanadamu kwenye njia au mfumo wake sahihi, na kumpitisha kwenye njia iliyo nyooka.
Bila shaka akili ya wanadamu, muislamu na asie muislamu, ikipata habari za mtu au msuluhishaji mfano wa huyo mwenye kungojewa, inakubali na kukiri kuwa ni lazima aje na ni lazima awepo, hata kama kusinge kuwa na dalili ya Qur'ani au hadithi juu ya mtu huyo au ishara juu ya mtu huyo. Bali hata mwana-falsafa wa Uingereza alie mashuhuri Bernard Show, alitoa bishara ya msuluhishaji huyo kwa msukumo wa fikra zake halisi na akaandika kitabu kuhusiana na hilo alicho kiita kwa jina la "Al-Insaan wa superman" na amesema kuwa msuluhishaji huyu mwenye kungojewa "ni mwanadamu alie hai mwenye ujenzi wa kiwiliwili ulio sahihi na uwezo wa kiakili wa kiwango cha juu sana kisicho cha kawaida, ni mtu wa kiwango cha juu sana na mtu huyu wa chini (yaani wa hali ya kawaida) atamfikia baada ya juhudi za muda mrefu" na kwamba yeye "umri wake utakuwa mrefu hata kuzidi miaka mia tatu, na anaweza kunufaika na vitu alivyo vikusanya kwenye zama zote hizo na alivyo vikusanya kwenye muda wote wa uhai wake ulio mrefu".[145]
Na Abbas Mahmud al-a'qqad amesema akiongezea maelezo yake juu ya hilo: "Inatudhihirikia kuwa Superman show si jambo la muhali kuwepo na kwamba wito wake kwake haukosi ukweli ulio thabiti.[146]
Na hatuwezi kupata kheri mwishoni mwa mazungumzo hayo zaidi ya kumuelekea Mwenyezi Mungu na kumuomba kwa kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunashitakia kwako kumkosa nabii wetu, na kughibu kwa mtawala wetu, na kuzidi kwa maadui wetu, na idadi yetu kuwa chache, na fitina (mitihani) kwetu kuwa mikali na zama kutugeuka na kushinda. Basi mrehemu Muhammad na (Aali) jamaa zake, na utusaidie juu ya hayo kwa ushindi wa haraka utokao kwako, na kwa kuondoa taabu na madhara na kwa ushindi uutukuzao, na utawala wa haki uudhihirishao"
"Ewe Mwenyezi Mungu mnusuru kwa nusra iliyotukufu, na umpe ushindi ulio mwepesi na utujalie tuwe ni katika wafuasi wake na wasaidizi wake, hakika wewe ni msikivu na mwenye kujibu maombi".
"Na mwisho wa maombi yetu ni kuwa tunamshukuru Mwenyezi Mungu mola wa viumbe wote".
Baada ya kutoka chapa ya kwanza ya kitabu hiki nilipokea barua kutoka kwa mheshimiwa Ustadh Muhammad Ridh'waan Al-Kasam kutoka Damaskas akipinga baadhi ya mambo yaliyo kuwemo kwenye bahthi yetu (utafiti).
Na ninafurahi sana kuelezea au kutoa shukurani zangu za dhati kwa Sheikh Al-kasam, kwa kutoa mwishoni mwa chapa hii baruwa yenyewe na jibu langu juu ya barua hiyo, huenda mso-maji mtukufu akapata ndani yake manufaa na faida fulani.
Na Mwenyezi Mungu ndie atoae tawfiqi.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu.
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe na rehma na amani ziwe juu ya Mtume wa mwisho.
Mheshimiwa Sayyid Muhammad Hassan Aalu Yaasin, Assalam alaykum wa rahmatullahi wa barakatuhu. Ama baada ya hayo.
Hakika nimesoma kitabu chako kiitwacho "Al-Mahdil-Muntadhar baina At-taswawuri wa At-tasdiiq" na uliyo yataja ndani ya kitabu hicho na kutokana na kauli yako kwamba ni utoaji wa habari ulio wa kweli na ni utoaji hukumu wenye amana na ni utafiti ulio safi ulio epukana na matamanio na mapenzi. Hakika jambo zuri lililo nistaajabisha kwenye kitabu hicho ni kauli yako kwenye ukurasa wa 50:
"Hakika Uislamu umeifanya akili kuwa ni chanzo cha itikadi na msingi wa Imani na ukakataza kufanya taklidi (kuwafuata watu fulani) ufuataji wa kiupofu "usio na ushahidi wala dalili".
Nina sema ewe Sayyid mtukufu hakika kutokana na haya, ilikuwa haiwezekani kwangu isipokuwa kukutolea mambo ambayo ni lazima kuelezwa kati ya mambo niliyo yafahamu kutokana na masomo yangu, kwa kuzingatia kuwa ni mmoja wapo wa wafanyao kazi kwenye uwanja huo wa kiislamu ili kubainisha ninayo yaona ni sawa, na maelezo yangu ndio haya:
Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ametukataza moja kwa moja katika aya nyingi kuitakidi itikadi yoyote isiyo na yakini ndani yake na akasema "Sema je mna ujuzi wowote kuhusu hili mkatutolea", na akasema tena "Kwa nini hawawaletei ushahidi ulio wazi, basi ni nani dhalimu zaidi kuliko aliemzulia Mwenyezi Mungu uongo", na akasema tena "Hawana ujuzi wowote kuhusu suala hilo isipokuwa ni kufata dhana".
Kwa hivyo yeye Mwenyezi Mungu anatutaka tuwe na ujuzi na maarifa na ushahidi na anatukataza kuwa na dhana na makatazo yake hayo anayaunganisha na ahadi na vitisho. Kutoka-na na hayo tunaweza kusema kuwa itikadi hazichukuliwi isipo-kuwa kutokana na yakini.
Na baada ya kukisoma kwa uchambuzi Kitabu chako na kuandika maoni yangu kukihusu, nimeona kuwa wewe umetaja kuwa fikra ya "Mahdi" imesimama juu ya msingi wa yakini na elimu au ujuzi ulio mutawatir na ukasema kwenye ukurasa wa "14": "Kutokana na dalili za Mtume kuwa mutawatir katika haki ya Mahdi, mara kwa kueleza wazi na mara nyingine kwa kuashiria" na ukamalizia pembezoni mwa kitabu kuwa mtu anaweza kurejea kwenye kitabu muraja'ati cha Sheikh Sayyid Abdul-Hussen Sharafud dini na kitabu Al-ghadiir juzuu ya kwanza cha Al-Amiini.
Na kwa kurejea kwenye vitabu viwili hivyo hapakuwa ndani ya vitabu hivyo chochote kinacho faa kuwa ni dalili na ushahidi wa fikra hii, isipokuwa hadithi ambazo sanadi yake ni Auhaad (zisizofikia kiwango cha mutawatir) na si hadithi zilizo mutawa-tiri. Je hadithi sahihi zina kupatieni yakini katika nadharia yenu?
Hakika suala hili ni la kushangaza.
Kisha kuna jambo lingine ni vizuri kulitilia umuhimu nalo ni pale ulipo taja kwenye ukurasa "14" kama ifuatavyo: "Na ni-lazima ili kujiepusha na maovu haya awepo Imamu alie chaguliwa na mwenye sifa zote za ukamilifu, alie epukana na kutakasika na mambo yote yachukizayo, na alie mbali na kila aina ya uovu katika matendo na kutoka kwenye kanuni za sheria na hali hiyo ndiyo tuiitayo kwa jina la Isma" na kuendelea.
Ndugu yangu mpenzi, hiyo ni Ismah gani?
Je kuna mwanadamu yeyote mwenye Ismah basi utasemaje kuhusu kauli ya Mtume(s.a.w.w) isemayo "Kila mwanadamu ni mwenye kufanya makosa na watu bora (kati ya wafanyao makosa) ni wale wafanyao tauba (yaani waombao msamaha) ".
Je Mtume aliposema kila mwanadamu ni mwenye kukosea alimtoa kwenye hukumu hiyo mtu yeyote? Basi hoja na dalili ya Ismah iko wapi? Ukiongozea pamoja na haya kuwa wewe umetoa ushahidi wa hadithi sahihi ukurasa "53" "Mwenye kufa hali ya kuwa hakumfahamu Imamu wa zama zake amekufa kifo cha kijahili", na ukafahamu kutokana na hadithi hiyo kuendelea kwa Uimamu wa Muhammad bin Hassan.
Ni mtu gani anae kubali kauli hii. Hakika sisi tunasema ya kuwa, hakika hadithi kwa matamshi yake na mafuhumu yake inasema kuwa ni juu ya kila muislamu kumfahamu Imamu wa zama zake, na ampe baia juu ya kukitekeleza au kukifuata kitabu na suna na haijulishi juu ya Imamu fulani maalumu.
Sasa kumuaminisha na kuufunga uimamu kwa maimamu kumi na mbili kumetoka wapi? Je si umeyasema hayo bila dalili?
Ikiwa tunamtaka Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, ni juu yetu kufuata dalili ya kidini, itakayo kuwa ni madhubuti tunachu-kua itikadi kutoka humo na hukumu, na itakayo kuwa ni yenye kutoa dhana tutachukua humo hukumu pekee, na haifai kwa muisilamu alie na ufahamu kamili abakie akiitakidi mambo yenye kudhaniwa na kuyaweka kwenye kiwango cha mambo ya itikadi bila kuwa na dalili na kusema kuwa Mahdi atakuja, na akaamini hivyo wakati ambapo hana dalili yoyote kati ya dalili za wahyi atakazo zitolea ushahidi juu ya kauli yake.
Na mimi ninatarajia kwa ndugu Ustadh na wafuasi wake watukufu kuwa maneno hayo niliyosema, yatulie na kukaa kwenye nafsi zao zilizo tulia ili kupata thawabu za Mwenyezi Mungu na radhi zake.
Wassalamu alykum warahmatullahi wabarakatuhu.
Damaskas, 15/Rabiiul-thani/89. (29/07/69).
MUHAMMAD RIDHWANI Al-KASAM.
Assalamu alaykum warahmatullahi wa barakatuhu.
Ama baada ya salamu,
01: Bado nina sisitiza kauli yangu ya kuwa "Uislamu umeifa-nya akili kuwa ni chimbuko la itikadi na msingi wa Imani", na mimi niko pamoja nanyi katika kusema kuwa "Itikadi hazichuku-liwi isipokuwa ni kutokana na yakini", na sitorudi nyuma kuhu-siana na haya hata kidogo, sawa natija au matokeo ya hadithi hii yawe ni yangu au yawe juu yangu.
02: Hakika hadithi za Mtume kuwa mutawatiri kwa kuelezea wazi na kuashiria (tuliko kuashiria kwenye ukurasa wa 14 kwenye chapa ya kwanza) zina mhusu Ali(a.s) na kuwa yeye ndio Imamu wa kisheria baada ya kufariki Mtume(s.a.w.w) . Na tumekusudia kwa neno mutawatiri, tawaturi ya kimaana na sio ya kimatamshi, na tunasema hivyo kwa sababu hadithi zote zilizo zungumzia suala hilo pamoja na kusisitiza kwake, zinaelekea kwenye suala la uimamu wa mtu huyu kidhati na kumuainisha, na lau kama hadithi ambazo sanadi yake inakuwa ni ya Aahaad [147] [76], (kufuatana na ibara uliyotumia) zingeelekea kulielezea jambo moja pekee hakika bila shaka yoyote, jambo hilo litakuwa mutawaatir.
03: Tulifanya bahthi ya "Ismah" kwa upana kwenye kitabu chetu "Al-Imamah" na ninatarajia utakisoma na kunipa rai yako kwenye maudhui hayo.
04: Ama kauli yako isemayo "uteuzi na uainishaji na kulifu-nga jambo hilo kwenye idadi ya kumi na mbili, umetokea wapi? Na umekuja kutoka wapi? Je haya si umeyatowa bila dalili"? Utapata jibu lako kwenye kitabu "Al-Imamah" kilicho ashiriwa vile vile.
05: Ama uliyo yataja mwishoni mwa barua yako kuwa Mahdi ni miongoni mwa masuala yanayo dhaniwa ambayo haifai kuyapa daraja ya kuwa ni jambo la kiitikadi, hakika maneno haya ni dalili ya kuwa hukukisoma kitabu hicho kwa mazingatio, na lau kama ungerudia kukisoma ungeona majina ya maswahaba ambao wamepokea na kusimulia hadithi za Mahdi kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) na majina ya wanazuoni ambao wametunga vitabu kuhusu Mahdi, na majina ya mahufadhi walio mashuhuri ambao wamezi-thibitisha hadithi hizi kwenye vitabu vyao, na ushahidi wa wahe-shimiwa wengi juu ya kuwa hadithi za Mahdi ni mutawaatir na kukata shauri juu ya usahihi wake.
Basi ni vipi yakini isithibiti na kukata shauri kwa yakini juu ya suala hili na kuwa na yakini kwa kuyashuhudia yote haya?
Na amani iwe juu ya mwenye kufuata uongofu na mwisho wa maombi yetu ni kuwa tuna mshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu.
5
USUULID DIIN
MAREJEO YA KIAMA
MAREJEO YA KIAMA
"Suratu At-taghaabun". "Wale ambao wamekufuru walidai kuwa hawatafufuliwa, sema ndio, ninaapa kwa (haki ya) Mola wangu, bila shaka mtafufuliwa kisha mtapewa habari za yale mliyo yafanya, na jambo hilo ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu".
"Suratul- Jaathiya"
"Mwenyezi Mungu anakuhuisheni kisha atakufisheni kisha atakukusanyeni siku ya kiama, hakuna shaka kuhusu (suala) hilo".
"Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu.
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe, na rehma na amani ziwe juu ya mbora wa viumbe vyake Muhammad na jamaa zake walio wema na walio twahirika.
Uislamu huu mtukufu na yote uliyo kuja nayo kwa viumbe mingoni mwa hukumu na amri, na kwa yote uliyo yakusanya kwenye pande zake kama kuwataka kutekeleza vitendo fulani au kuviacha vingine, na kwa yote uliyo yakusudia na kuyalenga kama kuyajenga maisha juu ya misingi madhubuti kati ya mahu-siano yote kwa ujumla, mahusiano ya mtu na jamii yake, na mahusiano ya jamii na watu wake na mahusiano ya wote hao na serikali au dola, na mahusiano ya dola na watu wake, kisha juu ya mahusiano hayo, akaweka uhusiano wa mtu na Mola wake,na mfumo au mwenendo wake kwenye ibada na kwenye kujikari-bisha kwa Mwenyezi Mungu.
Uislamu huu wenye kubakia milele na yote uliyo nayo kati ya hukumu hizo na mambo yaliyo amrishwa kufanywa, na nidhamu au mpangilio wa mambo, na mafunzo mbalimbali, je umemuachia muislamu nafasi ya kufanya matendo na kufanya amali zake juu ya msingi wa uhuru na uteuzi, na kutekeleza amri hizo akitaka mwenyewe na kutofanya akitaka vilevile?
Au umemuwekea hali ya lazima ambayo haifai kujighafilisha nayo na kuzembea kwenye hali hiyo, na ili kudhamini kuwa ataji-lazimisha na kutekeleza, ukamuekea mwenye kukhalifu amri zile au mambo yale ya lazima adhabu na athari zingine zimfanyazo muislamu awe ni mwenye kutii moja kwa moja na kuyatekeleza yote kiukamilifu bila kughafilika?
Na ikiwa hukumu hizo amelazimishwa Muislamu kuzite-keleza bila kukhalifu hata kidogo, je adhabu ina husika tu na kule kwenda kinyume ambako habari zake huifikia serikali na serikali kumpitishia aliefanya matendo haya au alie khalifu amri hizo hukumu iliyo wekwa na kanuni ya maovu kwenye hali kama hii, kisha suala hilo linaishia au kukomea kwenye mipaka hiyo tu?
Na upi msimamo kuhusu maovu na ukiukaji au kukhalifu ambako hufanywa siri na habari zake kutojulikana na kupotea njia zake na asitokee yeyote kuyafahamu wala kanuni kutekelezwa?
Na ni upi msimamo wa ukiukaji ule ambao haumhusu yeyote kati ya watu ili aweze kusimama dhidi ya ukiukaji huo mwenye kutoa habari za kufanyika kwake na kutoa dalili juu ya kuonyesha kuwa amefanya makosa alie kiuka na kufanya mambo yake, bali kila kilichopo katika ukiukaji huo ni kuwa ni uasi wa amri moja wapo kati ya amri za Mwenyezi Mungu katika kitendo kimojawapo kati ya vitendo vya sala au hukumu moja wapo kati ya hukumu za funga kwa mfano?
Na hata ukiukaji ule ambao hutekelezwa hukumu yake (kuadhibiwa kama kupigwa viboko au mawe) kwa Mwenye kutenda au kuchukuliwa fidia kutoka kwa mtendaji. Je ukiukaji huo hufuatia juu yake haki ya Mwenyezi Mungu (nayo ni ile iitwayo kuwa ni haki ya jumla kwenye istilahi ya kanuni zilizo wekwa) au ni kwamba kutekelezwa hukumu au kutoa fidia kunatosha kumtoa mfanyaji wa ukiukaji ule kwenye dhima ya haki nyingine yeyote?
Na muislamu huyu ambae anaitakasa nia yake kwenye utiifu na kuizuia nafsi yake na vitu vingi vyenye ladha na kujiziwia na matamanio yake na matakwa yake na vitu mbalimbali vipendwa-vyo na nafsi, kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujikaribisha kwake, kama vile mwenye kufunga ambae kiu na njaa humtaabisha na akaendelea kubakia kwenye hali hiyo na kutovijali vitu hivyo, au kama muuzaji ambaye anaweza kupu-nguza kipimo au kughushi (kudanganya) kwenye bei ya bidhaa lakini asifanye hivyo, na mfano wa hao watu ambao wanauwezo wa kufanya matendo ya haramu lakini wakajizuwia nayo na kujiepusha nayo.
Muislamu huyu ambae anajiwekea kwenye nafsi yake vitu kama hivi na kujinyima huku kuliko kukubwa, je matokeo ya kujinyima kule yanakuwa ni kuonyesha kuwa amemtii mola wake jinsi inavyo takiwa na hakuna kitu kingine nyuma ya utiifu huu, au kuna maana kuwa kuna malipo badala ya kujinyima kule anayo yahisi mwanadamu atakayo pewa badala ya kuwa amejinyima na kwamba matamanio ya kimaisha ya dunia yaliyo mpita haikuwa na hasara kwa maana ya kawaida ya hasara, bali ilikuwa ni aina fulani ya kujiwekea akiba na hazina, kiasi kwa-mba atayapata siku fulani yale malimbikizo yake ambayo ni mengi na matokeo yake ya manufaa na faida, na akahisi wakati huo raha na utulivu na kupata msukumo zaidi wa kuweka hazina na kujilimbikizia kwa hamasa kubwa na ikhlasi?
Na mbadala huu tulio uashiria ikiwa utasihi basi ni lini utafanyika? Na itakuwa vipi, yaani utatekelezwa vipi?
Ni lazima ufanyike mbadala huo baada ya kuwa mwanadamu ameukamilisha umri wake wote na siku zingine za uhai wake ili ionekane wazi ni kwa kiasi gani anastahili malipo haya katika hali ya kumrudia Mola wake na kufanya utiifu, au kustahili kupata mateso na adhabu, katika hali ya kuvuka mipaka na kufanya maasi.
Kwa hivyo ni lazima kuwe na hali ya kurejea baada ya kifo kwenye hesabu na kuhukumiwa ili kumpa kila mtu anayo stahili kupewa kati ya wema au ubaya yakiwa ni malipo ya matendo aliyo yatanguliza na kazi alizozifanya. Lakini je linawezekana hilo? Na dalili yake ni ipi? Na je mwanadamu mwenye akili na busara anaweza kuamini kuwa kuna uwezekano wa kurejea baada ya kufa, kwa ajili ya kufanywa hesabu na kumuangalia au kumuainisha anaestahili kupata thawabu au adhabu.
Hayo ndio yatakayo elezewa kwenye kijitabu hiki kwa kuya-bainisha na kuyafafanua, na kukiwa na matarajio ya kuyaweka wazi mas'ala hayo na kuyadhihirisha kwa msomaji mwenye kutaka kuelewa, tukilazimika katika kufanya hivyo kutumia ibara zilizo salama, na fikra zilizo wazi, na kurahisisha kwa haya tuyazungumziayo, na kujiepusha na istilahi za kifalsafa na mambo mengine yaliyomo kwenye falsafa hizo kama kutumia maneno magumu na yasiyo eleweka.
Na matarajio yangu yote ni kuwa kurasa hizi zimekusanya mambo na malengo yaliyo kusudiwa, na zenye kufikia na kuyathi-bitisha makusudio, na kuyaelezea kama inavyo stahili kwenye ufafanuzi wa mas'ala haya, na kuyabainisha kiukweli wake wa asili ulio safi.
Na jambo linalopaswa kusemwa ni kuwa:
Huenda msomaji akawa na matarajio kutoka kwangu, nami nikizungumzia msingi huu muhimu kati ya misingi ya uislaam kuwa bahthi yangu ni bahthi ya kiakili tu iliyo wazi kwa kuzichukua rai na kuzijibu, kama vile ambavyo hufanya bahthi kwenye mas'ala ya kifalsafa na kutoa msimamo kutoka kwenye bahthi hiyo kwa uhuru kamili wa kupinga na kukubali.
Lakini, uhakika wa mambo hapo unatulazimu kufuata mfumo mwingine unaotofautiana na huo unaotarajiwa kwa tofauti kidogo.
Tunafanya hivyo kwa sababu sisi tunaishi katika hali ya kuamini marejeo kwa ujumla wake na tukiwa ndani ya uzio wa itikadi na hukumu za sheria, na ni lazima kwetu, kutokana na hali hii, tuzitegemee dalili na ushahidi wa Mwenyezi Mungu (ushahidi wa Qur'an) kifikra, kimfumo na kidalili na kurudi kwenye Qur'an kila tunapo taka kuchagua kilicho bora au kinacho faa kati ya vitu vinavyo dhaniwa kuwa vinafaa, vitolewavyo kwa ajili ya kufanyiwa utafiti na kujadiliwa, na kwamba tusivuke na kutoka kwenye mambo hayo kwa ujumla, kwenye duara hilo lililothabiti na lenye mipaka maalumu ambayo haifai kuivuka kwa hali yoyote ile.
Na kulazimika kufanya hivyo hakuna aibu yoyote au jambo la kushangaza au upingaji wa hukumu ya kiakili, bali huenda ikawa ndio natija ya kimantiki pekee ambayo haina shaka yoyote kuisema na kuifuata miongozo yake, maadamu inawekwa na hali ya kwenda hatua kwa hatua kwenye Imani ya misingi ya itikadi, na kuifanya kuwa ni "mfumo" kwa maana kamili ya neno hilo, na wenye kuwiana wenyewe kwa kiwango cha juu kabisa.
Hakika tumemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Muumba na Muwekaji wa vitu vyote, na hatukuwa na dalili juu ya Imani hiyo isipokuwa akili pekee.[148]
Na tukaamini, kutokana na hayo na kwa kukubali na kuwa chini ya hukumu ya dalili, uadilifu wake ulio takaswa na matama-nio na uongo na dhulma na makusudio mabaya.[149]
Kisha tukaamini, kutokana na hayo vilevile, na kwa kukubali kuwa chini ya hukumu ya dalili, utume na ujumla wa mitume wote, na utume wa mwisho ( wa Mtume Muhammad)(s.a.w.w) pamoja na yote yaliyomo ndani yake kama vile wahyi na kuwe-kwa kwa sheria.[150]
Na kwa kuamini kwetu sehemu hizi tatu zenye kufuatana moja baada ya nyingine, bahthi ya kiitikadi kuhusu "ma'aadi" ina kuwa ni sehemu ifuatayo sehemu zilizo tangulia, kwa sababu sehemu hii inategemea kwanza msingi wa Imani juu ya Mwenyezi Mungu Muumba, Muadilifu, na pili Imani ya Mtume aliye Mkweli na mwenye kuswadikishwa, na tatu kukiamini kitabu cha Mwenyezi Mungu kilicho teremshwa.
Baada ya hayo hakutabakia jambo la kushangaza ikiwa tutafanya kuwa ni lazima mazungumzo yahusianayo na itikadi yasitoke, kufuatana na hali inavyo lazimu kwenye mipaka ya Kitabu hiki (Qur'an) na sheria zake maalumu, kwa kuzingatia kuwa kitabu hiki ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake(s.a.w.w) .
Pamoja na yote hayo hakika sisi kwenye mwendo wetu ndani ya maudhui haya hatuta jiepusha na akili na dalili au ushahidi wake, bali tutaielekea kwa heshima ya kiwango cha juu, ili tuiulize ni kiwango gani imekinaika na mas'ala ya marejeo (kiama) na kwamba ni jambo ambalo ni muhali kuwa au linawezekana? Na kwamba je ni katika vitu ambavyo akili ina uwezo wa kuwaza kutokea kwake au haiwezi kuliwaza na kulifikiria? Na je jambo hili linawiana na akida au haliwiani?
Na kwa kufanya hivyo, yote hayo kwa muhtasari wake yanakuwa ni mchanganyiko mzuri wa kufuata dalili (Qur'an) na kutokiuka kamwe, na kufuata muongozo wa akili, bila kupunguza haki au kupitukia kwenye haki ya upande wowote kati ya pande mbili (Qur'ani na akili).
Na Mwenyezi Mungu amesema kweli pale aliposema:
"Mwenyezi Mungu hakuna Mungu isipokuwa yeye, atakukusa-nyeni katika siku ya kiama hakuna shaka kwa hilo, na ni nani mkweli zaidi kwenye mazungumzo kuliko Mwenyezi Mungu"?
"Na wanasema:Ahadi hiyo ni lini (itakuwa), ikiwa nyinyi ni wakweli? Sema:"Mnayo miadi (marejeo) siku ambayo hamtache-leweshwa hata saa moja wala kutanguliziwa".
"Siku ambayo kila nafsi itayakuta mambo yote ya kheri iliyo yatenda yakiwa yameletwa mbele yake na maovu aliyoyatenda".
"Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye na mama yake na baba yake, na mkewe na watoto wake. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na jambo lenye kumshughulisha. Nyuso siku hiyo zitakuwa ni zenye kumeremeta zikicheka na zenye bishara na furaha, na nyuso zingine siku hiyo zitakuwa na mavumbi juu yake zikiwa zimefunikwa na giza na weusi".
Na mwisho wa maombi yetu ni kuwa tunamhimidi Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe.
Hakuna budi kwa mwenye kufanya utafiti wa kimaudhui, kwenye mas'ala ya "Al-ma'aad" (marejeo) kwanza kabisa asimame katika mwendo wa utafiti wake kwenye fikra ya "Al-ma'aad" akiwa hana rai yoyote ihusianayo na maudhui haya kama maelezo na ufafanuzi juu ya masuala haya, ili uweze kuthibiti ukubwa na ulazima wa kuwepo marejeo na kuwa ni lazima yatokee kwenye ulimwengu wa itikadi na aweze kufahamu sababu zifanyazo kuwa ni lazima marejeo yatokee na ulazima wake na dalili zake za kidini.
Na mwenye kufanya utafiti akiweza kusimamisha dalili juu ya jambo hili la lazima, hapo atakuwa na uwezekano wa kuhamia kwenye hatua ya utafiti mwingine na kutoa au kuendelea kutoa maelezo kuhusu maudhui hayo, na kufanya hivyo ni kwa sababu ya kuwa, kuikubali hatuwa hii inakuwekea msingi mzuri na madhubuti au ina kuandalia njia ya kuyakubali mambo yanayo-tokana na kukiri huku ambayo ni kama matawi ya jambo hili la asili.
Na hatutoweza kufikia kwenye natija itakiwayo isipokuwa kwa kwenda taratibu hatua kwa hatua kuelekea kwenye natija hiyo kwa kupitia hatua ambazo zote zina ungana na kila ifuatayo ikiwa imeungana na iliyotangulia kwa kiunganishi madhubuti ambacho kitatuondolea pazia na ukweli kuonekana:
01: Je mwenyezi mungu aliamuru na kukataza?
Sidhani ya kuwa kuna watu wenye kuelewa na wenye akili timamu wasio elewa -kwa maana halisi ya kuelewa- ya kwamba Mwenyezi Mungu ameamrisha na kukataza na kwamba sheria ya kiislamu ni mkusanyiko mkubwa wa amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu.
Na usomaji wa haraka kwenye Qur'ani tukufu unatupa dalili isiyo na shaka juu ya hilo, amesema Mwenezi Mungu Mtukufu:
"Simamisheni Swala na mtoe zaka"
"Imefaradhishwa juu yenu funga kama ilivyo faradhishwa juu ya wale ambao walikuwa kabla yenu".
"Na amefaradhisha Mwenyezi Mungu juu ya watu kuhiji kwenye nyumba (Tukufu)".
"Na fahamu ni ya kwamba kitu chochote mtakacho kipata kama ghanima (faida) hakika khumsi yake ni ya Mwenyezi Mungu".
"Piganeni kwenye njia ya Mwenyezi Mungu ki kweli kweli".
"Mwenyezi Mungu amehalalisha biasha- ra na ameharamisha riba".
"Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na ihsani (wema) na kuwapa haki watu wa karibu, na anakataza machafu na maovu na uzinifu".
"Na baadhi yenu wasiwasengenye baadhi (wengine)"
"Msichunguzane".
"Hakika huzua uongo wale ambao hawaziamini aya za Mwenyezi Mungu".
"Jiepusheni sana na dhana".
"Ole wao wenye kupunguza vipimo".
Na aya tukufu nyingine zilizo mfano wa hizi zilizo jaa amri na makatazo mbali mbali ya Mwenyezi Mungu.
Kwa hivyo basi, hakuna shaka hata kidogo kuwa Mwenyezi Mungu ame amuru na kukataza.
02: Je amri hizi na makatazo hayo yalikuwa ni mambo ya lazima au ni muongozo?
Hakika elimu ya Usulul-fiqhi imemaliza kuyafanyia utafiti mas'ala haya kwa upana zaidi, na muhtasari wa utafiti huo kuhusu maana ya amri ulikuwa ni kwamba: "Amri ni dalili ya uwajibu (wa jambo) na iko dhahiri katika uwajibu pale ambapo amri hiyo itakuwa haina alama ijulishayo kuwa ni jambo la mustahabu (lisilo lazima bali linapendeza)". Na kwamba "Uwajibu unatokana na hukumu ya akili kwamba ni lazima kutii amri ya mola (bwana) na kwamba ni wajibu kutekeleza amri yake kwa ajili ya kutekeleza haki ya utawaliwa na kuwa mja". Kama ambavyo muhtasari wa Nahyi (Katazo) ni kuwa neno la kukataza ni "Kama neno la amri katika kujulisha kwake (ni dalili) juu ya ulazima (wa kuacha kitendo) kiakili na katazo liko dhahiri katika kujulisha kuwa jambo lililo katazwa ni haramu". Na kwamba swigha ya kukataza ikitoka kwa mtu ambae anawajibika kutiiwa, itakuwa natija na matokeo ya ulazima wa kumtii mtawala huyo n a uharamu wa kumuasi, kwa hukumu ya akili, kwa kutekeleza haki ya utumwa na utawaliwa, ni kutofaa kuacha kitendo ambacho amekikataza.[151]
Na vipi amri isiwe hivyo wakati Mwenyezi Mungu amesema:
"Alicho kupeni Mtume kichukueni na alicho kukatazeni kiacheni".
Na anasema Mwenyezi Mungu:
"Na wajihadhari wale ambao huenda kinyume na amri zake kupatwa na mitihani au kupatwa na adhabu iumizayo".
Kwa hivyo basi, hapana budi kusema kuwa amri na maka-tazo ya Mwenyezi Mungu ni mambo ya lazima kwa maana kamili ya neno hilo, na hakuna nafasi ya kuchagua (khiyari) na kutoa ruhusa.
03: Ni nini matokeo ya kukhalifu amri na makatazo?
Na ikiwa Mwenyezi Mungu ameamuru na kukataza, na amri zake na makatazo yake yakawa ni mambo ya lazima, haifai kuyakiuka na kwenda kinyume nayo, basi je matokeo ya ukiukaji huu ni mateso na adhabu, kwa maana ya kimadi, au masuala haya hayavuki athari za kiadabu na kimaanawiya ya ukiukaji tu.
Na inatosha kujibu swali hili kuonyesha aya za Qur'ani zifuatazo ili tuweze kuelewa matokeo ya ukiukaji wa amri za Mwenyezi Mungu na matokeo yake.
Anasema:
"Na mwenye kwenda ki-nyume miongoni mwao na amri zetu tutamuonjesha adhabu ya moto".
"Hakika mimi nina ogopa, ikiwa nitamuasi Mwenyezi Mungu, adhabu ya siku kubwa".
"Na ni kijiji gani kilicho kwenda kinyume na amri za mola wake na Mtume wake tukakipa hesabu iliyo kali na tukakiadhibu kwa adhabu iumizayo".
"Ni kitu gani kilicho kuingi-zeni motoni? Wakasema hatu kuwa ni miongoni mwa wenye kusali".
"Ole wao wale ambao walidhu-lumu kutokana na adhabu ya siku iumizayo (kali)". Kwa hivyo basi, hapana budi kusema kuwa kutakuwa na adhabu za kimwili juu ya kila mwenye kukiuka amri na m akatazo ya Mwenyezi Mungu ambazo kwa ujumla wake huunda kitu tukiitacho kwa jina la "Sheria za kiislamu".
04: Je Ahadi Za Thawabu Na Adhabu Za Mwenyezi Mungu Ni Vitu Vya Kweli Au Zina Malengo Ya Kuwahimiza Watu Kufanya Twaa'a??
Zimenifikia habari ya kuwa kuna watu wasemao kwamba: "Hakika Qur'an kurudia mara kwa mara kutaja marejeo baada ya kufa, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu aliwaahidi malipo mema watiifu na akaahidi kuwaadhibu waasi, hakika kufanya hivyo ni katika njia ya kuhimiza na kuwatisha tu ili watu waweze kuwa na msukumo wa kufanya utiifu na kujitenga na maasi, bila kuwepo lengo la kweli la maana ya kimaddi la kufikia kwenye neema au adhabu, kana kwamba msemaji huyu katika maneno yake haya ameyasema kutokana na itikadi yake isemayo kuwa kiwiliwili hupotea na kupukutika, na kwa kufa haiwezekani kukirudisha baada ya kupukutika kutokana na kuwa ni muhali kukirudisha kwenye hali yake ya mwanzo kitu ambacho kimetoweka, na wakati huo hakubakii nafasi ya kuwepo neema na adhabu kwa maana yake ya kimaddi, kwa Hivyo waadi (kuahidi) na waidi (kutishiwa) vina kuwa ni vitisho tu visivyo na maana yoyote kati ya maana za kutekeleza.
Na ukweli ni kuwa sisi tunapo soma Qur'an tukufu, na Mwenyezi Mungu aliiteremsha kwa lugha ya kiarabu iliyo wazi, na sisi ni wana lugha yake na wenye kufahamu zaidi sehemu za kutumia maneno yake na maana yake na matamshi yake, hatuoni sababu yoyote itupayo ruhusa ya kulitafsiri tamko tofauti na dhahiri yake na maana yake kwa sababu limekuja tamko hilo likiwa halina alama ijulishayo kukusudiwa maana iliyo tofauti na dhaahiri ya maneno yake.
Na ikiwa matamshi yatumikayo kwenye sehemu ambazo Qur'ani inawahutubia watu yametumika bila kuwa na alama inayo ruhusu kufanya taawili, ina lazimika basi kuyachukulia matamshi hayo kwenye maana yake halisi na ya asili, na haifai kwetu kwa hali yoyote kuyachukulia kwenye maana ya majazi (yasiyo ya hakika) au mubalagha (kusisitiza) au vitisho au ahadi za uongo ziwatiazo watu hamasa ya kufanya kitu fulani.
Na tutatoa, katika sehemu ifuatayo, baadhi ya aya tukufu ambazo zinakusudia kutaja ufufuo na marejeo na zikisisitiza kutokea kwa mambo haya kwa masisitizo kamili, ili tuweze kufahamu kwa uwazi wake usio na kipingamizi na usio na taawili, na ubainifu wake ulio safi ambao haukubali maana yoyote kati ya maana za kufunga na za mzunguko.
"Kama tulivyo anza kumuumba kiumbe wa mwanzo tutamrudisha, ni ahadi iliyo juu yetu hakika sisi ni wenye kufanya hivyo".
"Amewawekea muda maalumu usio na shaka kutokea kwake".
"Na tumewafufua hatukumuacha yeyote miongoni mwao".
"Na kitawekwa kitabu, na utawaona watu waovu wakiyaogopa yaliyomo ndani ya kitabu hicho na wakisema, ole wetu kina nini kitabu hiki hakiliachi jambo dogo wala kubwa isipokuwa tu kimetoa hesa bu yake na watakuta waliyo yafanya yamewahu-dhuria (mbele yao) na Mola wako hatamdhulumu yeyote.
"Kisha nyinyi baada yake mtakufa kisha hakika nyinyi siku ya kiama mtafufuliwa".
"Je mnadhania ya kuwa tumekuumbeni kwa mchezo na kwamba nyinyi hamtarejea kwetu"?
"Ewe Mola wetu hakika wewe ni mwenye kuwakusanya watu siku ambayo haina shaka ndan i yake (juu ya kuwepo kwake). Hakika Mwenyezi Mungu haendi kinyume na ahadi zake".
"Enyi majini na watu je hawakukujieni M itume watokanao nanyi, wakikusomeeni na kukusimulieni aya (dalili) zangu na wa-kikuonyeni kuhusu kukutana na siku yenu hii? Wakasema: Tunashuhudia juu ya nafsi zetu, na maisha yao ya dunia yakawa-hadaa".
"Hakika siku ya kutolewa hukumu ni yenye kupangwa na kuahidiwa kwa wakati maalumu".
"Hiyo ni siku ya haki basi mwenye kutaka ashike njia na aende kwa Mola wake".
"Na kila nafsi ikapewa malipo ya matendo iliyo yafanya, na yeye Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi wa mambo wayafanyayo".
"Na wakasema wale ambao walikufuru, hakitatujia kiama. Sema ndio na ninaapa kwa haki ya Mola wangu hakika kitakujieni hicho kiama, (Mwenyezi Mungu ni) Mjuzi wa mambo ya ghaibu, hakuna kijifichacho kwake hata kama ni kiasi cha tembe ndogo iliyoko mbinguni na wala ardhini, na hata kilicho kidogo zaidi ya hicho wala kikubwa isipo kuwa kimo kwenye kitabu kilicho wazi, ili awalipe wale ambao walio amini na wakafanya matendo mema. Hao wana msamaha na riziki iliyo bora.
"Na wakaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa viapo vyao vya nguvu kwamba Mwenyezi Mungu h atowafufua walio kufa. Kwa nini (asiwafufue)? Ni ahadi iliyo lazimika kwake (kuwafufua na kuwalipa) lakini watu wengi hawajui. Ili awabainishie yale ambayo walikuwa wakitofautia ndani yake na ili wale walio kufuru waelewe ya kuwa wao walikuwa ni waongo".
"Na ni kipi kikujulishacho ni ipi siku hiyo ya mwisho? Kisha ni kipi kikujulishacho ni ipi hiyo siku ya mwisho? Siku ambayo nafsi haitamiliki kwa ajili ya nafsi nyingine kitu chochote na amri siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu". Kwa hivo natija ni ipi?
Ikiwa Mwenyezi Mungu ameamrisha na kukataza, na amri zake na makatazo yake yakawa ni ya lazima kutekelezwa.
Na ikiwa kukiuka amri hizi na makatazo haya humlazimu mtu kupata adhabu.
Na adhabu hiyo ikawa ni adhabu ya kimada kwa maana yake maalumu na sio kwa ajili ya kuogopesha watu na ya uongo.
Basi kwa hivyo ni lazima tuseme ya kwamba: Marejeo ni jambo la lazima na hakuna makimbilio kwa muislamu, ila kusema hivyo na kuamini ulazima wake na kwamba bila shaka yatatokea.
Na haya ndio ambayo tumefahamishwa na aya tukufu tulizo zitaja, kwa kusema wazi kuwa marejeo ni jambo "lisilo na shaka kutokea kwake" nayo "ni siku ya haki" ambayo haitacheleweshwa kwa muda wa saa moja wala kutangulizwa saa moja, na kwamba lengo la kuwekwa siku hiyo ni kuwahesabia watu na kuwahu-kumu, ambapo hupewa "kila nafsi malipo yake iliyo yatenda", kufuatia kitabu kisicho acha jambo dogo wala kubwa isipokuwa hutoa hesabu yake, kwani ndani ya kitabu hicho "kila nafsi itakuta mambo ya kheri iliyo yatenda yakiwa yamehudhuria mbele yake, na mambo mabaya iliyo yatenda, na wakati huo waovu watakuwa "wakiogopa yaliyomo ndani yake.
Na kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kurejea ni ahadi "iliyo ya haki juu yake" na ni nani mkweli zaidi kuliko Mwenyezi Mungu katika uzungumzaji, na kwamba wale ambao walidai ya kuwa hawatofufuliwa na kwamba hakitawajia kiama ni makafiri na waongo, na "adhabu kali siku hiyo itakuwa kwa wakadhibi-shaji, wale ambao wanaikadhibisha siku ya mwisho, na haika-dhibishi siku hiyo isipokuwa kila mwenye kukiuka na mwenye dhambi". Amesema kweli Mwenyezi Mungu mtukufu.
Na tunapofikia kwenye natija hii kutokana na mtiririko wa mazungumzo, inakuwa ni lazima, ili bahthi hii ienee pande zake zote, tusimame sehemu hii kwa muda ili tuchunguze kwa yakini ni "kitu" gani hasa kitakacho rejea?
Je "roho" pekee kama walivyo dai wasemao kuwa ni muhali kurejea kiwiliwili? Au "mwili" pekee, kama Jubai alivyosema na wafuasi wake kuwa "roho na mwili vile vile"? Au ni "roho na mwili" kama waaminivyo wana fikra wengi wa kiislamu?!
Hakika lifahamikalo haraka akilini, na kwenye ufahamu kutokana na mfumo wa aya za Qur'an zinazo husu maudhui haya, ni kuwa marejeo yatakuwa ni ya mwili ulio hai wenye kuhisi na kufahamu ladha ya neema na machungu ya adhabu, yaani "mwili wenye roho" ukiwa una sehemu zake zote uzitumiazo na kufaidika nazo na sifa zake na tofauti zake.
Na kwamba aya hizo kutokana na maana yake kuwa wazi na makusudio na maana kuwa bayana na lafdhi, zinakataa aina yoyote ya kutafutwa maana kwa ujanja au kufanyiwa taawili ambayo pengine wanaweza kuitegemea watafutao maana kwa ujanja na wafanyao taawili. Basi huenda ikawa ina uwazi wa hali ya juu katika maana na madhumuni, uwazi ambao unazuwia kusiwezekane kuificha na kuifunika funika na kuzungusha huku na kule kwa aina yoyote ile.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Na (wakumbushe) siku maadui wa Mwenyezi Mungu watakapo kusanywa katika moto wakawa manatengwa makundi makundi, hata watakapo ujia (moto huo), macho yao na masikio yao na ngozi zao vitatoa ushahidi juu ya yale waliyokuwa wakiyatenda. Na wataziambia ngozi zao: "Kwa-nini mnatushuhudilia"? Zitasema: "Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambae alie kitamkisha kila kitu na ndie alie kuumbeni kwa mara ya mwanzo, na kwake mnarudishwa". Na hamkuwa ni wenye kujifichia yasiweze kutoa ushahidi juu yenu macho yenu wala masikio yenu wala ngozi zenu, lakini mlidhani kuwa Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika yale yote mnayo yafanya ". Suratu-fuswilat:18-22
"Hivi leo tunaweka vizibo juu ya midomo yao, na mikono yao itazungumza nasi, na miguu yao itashuhudia waliyo kuwa wakiya-chuma ". Surat-Yassin:56
"Suratu Annisaa:56"."Hakika wale ambao walikufuru aya zetu tutawaingiza motoni, kila zitakapo iva ngozi zao tunawabadili-shia ngozi zingine, ili waonje adhabu ". Suratul-Kiyama 3-4.
"Je mwanadamu anadhani ya kuwa hatutaikusanya mifupa yake? Kwa nini! Sisi ni wenye uwezo wa kukusanya misitari ya ncha za vidole vyake".
Hakika usomaji wa uchunguzi makini wa aya hizi, unatuju-lisha kwa dalili iliyo wazi na kwa ubainifu ulio mkubwa juu ya kuwa, marejeo yatakuwa ni "mwili na roho" kwa hali yake ya kawaida, ukiwa na masikio, macho, ngozi, midomo, mikono, miguu na mifupa, kuhisi maumivu na adhabu. Na maneno haya hayawezi kudhaniwa kwa aina yoyote ya dhana na shaka na taawili
Na hapa ni lazima tusiache na kusimama angalau kidogo kwenye aya mbili za mwisho ili tusimame kwenye nukta zile za kielimu ambazo zimeashiriwa na kuelezwa na aya mbili zilizo-tajwa, na kwenye uhakika ule ambao aya hizo mbili zimetunaba-hisha juu yake kabla hazijagunduliwa na elimu ya kisasa kwa muda wa karne na karne, mambo ambayo tunaweza kuyachu-kulia kuwa ni miongoni mwa dalili kubwa kabisa zilizo wazi za kuonjesha umuujiza wa kitabu hiki cha muujiza na cha milele.
Hakika sababu ya kufanya hivyo ni mambo yaelezwayo na tiba ya kisasa kwamba "mishipa ya maumivu iko kwenye tabaka la ngozi, ama viungo vya ndani na mishipa yenye nyama na viungo vilivyomo ndani hisia zake ni dhaifu, kutokana na hali hiyo daktari huelewa kwamba kuungua kidogo ambako hakuvuki kwenye ngozi huwa na maumivu makali sana tofauti na kuungua sana ambako huvuka kwenye ngozi hadi kufika kwenye viungo vya ndani, kwa sababu pamoja na kuungua sana nakuwepo kwa hatari, hakutoi maumivu makali, na Mwenyezi Mungu ana-tuambia: "Hakika moto kila unapo ila ngozi ile yenye mishipa ya maumivu tunaibadilisha na kuweka ngozi mpya ili maumivu yaendelee bila kukatika, na ili waonje adhabu iumizayo".
Na hapa inadhihiri na kuonekana hekima ya Mwenyezi Mungu kabla mwanadamu hajafahamu, na Mwenyezi Mungu ni Mtukufu na mwenye hekima.[152]
Ama aya ya pili ndio aya ambayo inawapinga wasio amini marejeo kwa kutoamini kwao marejeo, kisha inasisitiza juu ya marejeo: Kwa nini! tunaweza kuiweka sawasawa mistari ya ncha za vidole vyake (au viganja vyake). Basi ni zipi sifa hizi za mistari hii?
Elimu ya kisasa inasema:
Hakika "Banaan" ni mpangilio wa kitaalamu ulio mzuri na wa ajabu uliopo kwenye mistari ya ncha za vidole Michoro ya misitari ya vidole vya mwanadam, na kwamba kila mwanadamu ana michoro na miundo ya kitaalamu yenye kutofautiana kiuka-milifu na miundo ya mtu wa pili vyovyote watakavyo kuwa karibu kwenye damu au kizazi au nasabu (ukoo), na hakuna kwenye jamii ya wanadamu wa ulimwengu huu watu wawili wenye kufanana misitari ya vidole vyao.
Na katika uchunguzi wa ncha za vidole vya mwanadamu uliofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1884 A.D, uchunguzi ulio kuwa makini baada ya kugunduliwa vyombo vya kukuza vitu, elimu iliweza kuthibitisha kuwa kila mwanadamu ana ramani yenye umbo maalumu na yenye sehemu madhubuti na makini za mistari iliyo pangika ambayo zimechukua umbo maalumu zuri na lenye kupendeza kwenye ngozi ya vidole vyake, vikionyesha hali yake ya siri ambayo imewekwa na uwezo wa Mwenyezi Mungu wa hali ya juu kwenye vidole vyake.
Hakika mistari hii huwa ni yenye kuonekana wazi na yenye ncha iliyo pinda na iliyo chimbika na yenye umbile jembamba sana, kiasi kwamba huonekana sehemu zake zote zilizo nyembamba na michoro yake na miundo yake juu ya karatasi pindi unapo pakazwa juu ya karatasi wino na kukandamiza juu ya karatasi.
Vilevile huonekana na kubakia mistari hii ikiwa thabiti juu ya madini yaliyo mororo na kioo na ubao ulio safi kutokana na ngozi ya ncha za vidole kuwa na tezi zitoazo jasho na mafuta.
Na sensa ya ulimwengu wa leo iliyofanywa kwa ajili ya kufanya utafiti wa elimu ya mistari ya vidole imeeleza kwamba katika kila watu milioni mianne, hupatikana alama moja inayo ashiria kufanana kiukamilifu kwa mistari yote kati ya watu wawili, isipokuwa ni kwamba kufanana huko hakuwi na kufikia kiwango cha kuwa sawa na kufanana kiukamilifu.
Na hivi leo vimefunguliwa vituo maalum vya kielimu pembe zote za dunia ya leo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa elimu ya mistari ya vidole, ili kuwajua na kuwatambua watu kwenye miamala na matendo yao na kwenye matukio ya uovu na wizi, kiasi kwamba hugundua kuwa kwa kugusa tu kioo au kuishika silaha au chombo chochote huacha juu yake alama na athari zikiwa zimethibiti, na kisha alama na athari hizi huchapishwa kwenye karatasi kwa njia maalumu ili kuzihifadhi na kuzifanyia uchunguzi na kuzifanya kubwa kwa ajili ya kuzilinganisha na mistari ya vidole vya watuhumiwa na washukiwa.
Na miongoni mwa mambo ya ajabu sana ni kuwa maumbo haya ya kitaalamu yaliyo jipanga vizuri kwenye ramani ya ncha za vidole vya mwanadamu, yanabaki yakiwa thabiti tangu saa ya mwanzo ya kuzaliwa na muda wote wa uhai, kiasi kwamba misingi yake haiathiriki kwa kukua kwa mwili bali huwa vikubwa na kupanuka pembe zake bila mabadiliko yoyote, kana kwamba yamewekwa chini ya chombo cha kuzikuza wakati wa kuzili-nganisha kati ya ramani mbili katika siku za utotoni na wakati anapo kuwa mkubwa na utaziona kuwa ni nuskha (kopi) iliyo sawasawa na asili yake kabisa bila kubadilika.
Na miongoni mwa mambo yashangazayo kweli kweli ni kuwa ramani ya mistari ya vidole inapopatwa na uharibifu au kasoro kutokana na kusagana au kusagika wakati wa kazi au pindi inapo jeruhiwa na kuungua kwa kiasi kikubwa, na kuungua juu juu, viungo vya mwanadamu hukua ili kuirudisha ramani ile ile ya asili na sehemu zake zote zikiwa zimepangika kwa umakini wake wa kiwango cha juu sana na sifa zake za hali ya juu za kitaalamu na muungano wake wenye kupendeza kama kwamba kuna mkono uliojificha unaoziamrisha chembe zake zikue kwa muelekeo maalumu na kuweka picha iliyo sawa na ile ya asili ya msitari iliyo haribika bila kukosea au kutofautiana.
Na hakika elimu na utafiti wa mistari ya vidole zimethibitisha kuwa umbo na ramanai zake za kitaalamu na mistari yake yenye kupambwa hurejea kwenye maungio manne ya msingi:
01- Kiungio cha mistari iliyo pinda kama upinde.
02- Kiungio cha mistari iliyo nyooka.
03- Kiungio cha mistari ya kudumu au kuendelea, yenye mzunguko ulio unganika kwenye sehemu kuu au kituo kikuu na iliyo ingiliana na mingine na ambayo hukua umbo lake taratibu ikianzia ndani hadi kutokezea nje, nayo hushirikiana kwenye kituo kimoja kikuu katikati ya kiganja.
04- Kiungio cha mistari iliyo pandana, nayo ni mchanganyiko wa mistari ya viungio vitatu. Kiungio cha mistari iliyo pinda kama upinde, na ilio nyooka, na ya kudumu au ya kuendelea, kiasi kwamba vinakuwa vimeungana na vingine kwenye umbo gumu na la kustaajabisha.
Hakika michoro ya vidole hivi leo inacheza dauru kubwa na la hatari, kwenye ulimwengu wa maovu na wizi na kuwatambua watu pande zote za ulimwengu.
Fadhila yote ya kuyatambua maelfu ya matukio na wasababi-shi wake inarudia siri hii ya Mwenyezi Mungu ambayo ni ya ajabu ambayo aliiumba na kuiweka kwenye ngozi ya vidole katika mwili wa mwanadam.
Uislamu wetu mtukufu hufahamika kuwa ndie mgunduzi wa mwanzo wa siri hii ya ajabu na ngeni katika miili ya wanadamu na ambayo ni ngumu, pale Qur'an ilipo ashiria kuhusu suala hilo ikizitanabahisha akili kuhusu umuhimu wa maumbile haya yaliyo pangiliwa kwa makini kwenye ncha za vidole vya mwanadamu, na kuhusu kila mwanadamu kuwa na ramani yake maalumu ya utaalamu maalumu.[153]
6
USUULID DIIN
MAREJEO YA KIAMA
UWEZEKANO WA KUWEPO MAREJEO NA DALILI ZAKE
Tumetaja kwenye utangulizi wa kijitabu hiki ya kuwa sisi tunaishi na suala la marejeo kwa ukamilifu wake ndani ya jengo la itikadi na ndani ya maeneo yake maalumu.
Na tumeashiria sehemu hiyo ya kuwa Imani ya marejeo ni hatua itokanayo na Imani ya ule msingi mkubwa, na tunakusudia Imani ya Mwenyezi Mungu mtukufu muumba wa ulimwengu na muanzilishi wa kuwepo kwa ulimwengu na walimwengu na ni sababu ya juu kabisa ambayo sababu zote hurejea kwake, pasina kuwepo sababu ya kuwepo kwake au sababu ya kusaidizana nae katika kuanzisha kuwepo kwa ulimwngu.
Na inapothibiti Imani kama hii iliyo thabiti na madhubuti ya kumuamini Mwenyezi Mungu na kwamba yeye ndiye chanzo cha viumbe na chanzo cha ulimwengu na kwamba madda ni moja kati ya viumbe vyake hata kama watadhania na kuamini kuwa ni ya tangu na tangu kama wasemavyo baadhi ya wanafikra wa kimadda (materialists)[154] , hakutakuwa na kizuwizi mbele ya mwanadamu kitakacho mzuwia kuamini kuwepo kwa marejeo na ufufuo na kukubali uwezekano wa kutokea na kuwa si muhali kutokea kwake.
Hakika akili kumuamini mfanyaji wa kwanza inajifungulia njia ya kuamini uwezo wa mfanyaji huyo wa kuweza kufanya kitendo chake kwa mara ya pili na kwa mara elfu kadha, na kwamba jambo hilo ni miongoni mwa mambo ya badaha , yaani ya wazi kwenye akili yasiyo hitaji ufafanuzi wala dalili na ushahidi zaidi, na inatosha kutoa mfano juu ya jambo hilo kwa kumuangalia mtu alie weza kuunda kitu fulani, kwa mfano mashine itumiayo nguvu za umeme yenye uwezo mkubwa, hakika uwezo wa mtu huyo wa kuweza kutengenza tena kitu kile halitakuwa ni jambo la kusitasita au kulitilia shaka, madamu tumekinaika kuwa yeye ndie muundaji wa kitu kile kwa mara ya kwanza.
Hakika muundaji wa gari lau kama atasambaratisha gari lile na kuliweka kwenye vipande tofauti vidogo vidogo maelfu kwa maelfu, kisha akasema kuwa anaweza kuliunda na kulirudisha gari lile ikiwa limeungwa kama ilivyo kuwa, hakuna mtu yeyote ulimwenguni atakae jitokeza na kumtaka atoe dalili juu ya uwezo huo, na haitafanyika hivyo isipokuwa ni kwa sababu mfanyaji wa kitu kwa mara ya mwanzo ana uwezo wa kukifanya kwa mara ya pili na ya tatu na kwa mara mia kadha na kwa mara milioni na kwa njia hii ya utoaji ushahidi juu ya uwezekano wa kurejea na kwa mujibu wa utaratibu huu wa kupanda kwenye ngazi ya akida, Qur'ani tukufu imetoa dalili juu ya ubadaha (uwazi wa akilini) wa marejeo baada ya kifo (yaani ni suala lisilo hitaji dalili).
Na hebu tutoe baadhi ya aya hizo tukufu ambazo zilihusika na kuweka wazi ukweli huu na kufafanua uwezekano wake kwa kila mwenye akili na ufahamu na uelevu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Na wakasema, tutakapo kuwa mifupa na mapande yaliyo sagikasagika, je sisi tutafufuliwa kwa maumbile mapya? Sema kuweni mawe au chuma au kiumbe kingine ambacho kinaone-kana kikubwa au kigumu kwenye nyoyo (fikra) zenu. Hapo watasema, ni nani atakae turudisha (kwenye hali yetu ya mwzanzo)? Sema ambae alikuumbeni kwa mara ya mwanzo . "Suratu-Israai:49-51".
"Na mwanadamu anasema:"Ikiwa nitakufa je nitatolewa tena nikiwa hai"? Je mwanadamu hakumbuki ya kuwa sisi tumemu-umba hapo kabla na hakuwa ni chochote ".Suratu Maryam:66.
"Siku ambayo tutaikunja mbingu kama ukunjaji wa kurasa (karatasi) zilizo andikwa, kama tulivyo kianzisha kiumbe cha kwanza tutakirudisha (hivyo). Ni ahadi juu yetu hakika sisi ni wenye kufanya hivyo ". Suratul-ambiyaa: 104.
"Mwenyezi Mungu huwaanzi-sha viumbe kisha atawarudisha kisha mtarudishwa kwake ". "Suratu-Al-ruum:11".
"Na watasema:Tutakapo kuwa mifupa na mapande yaliyo sagika sagika je sisi tutafufuliwa kwa maumbile mapya? Je hawa-kuona ya kuwa Mwenyezi Mungu alieumba mbingu na ardhi ni Mwenye uwezo wa kuumba mfano wao "."Suratul-Israai: 49-51.
"Hakika tulimuumba mwanadamu kutokana na chembe chembe za udongo, kisha tukamfanya kuwa ni mbengu za uzazi kwenye mahali madhubuti, kisha tukaumba kutokana na mbengu za uzazi pande la damu, na tukalifanya pande la damu kuwa pande la nyama, na pande la nyama tukaliumbia mifupa, na mifupa tukaivisha nyama kisha tukakiumba kiumbe kingine, ametakasika (Mwenyezi Mungu) mbora wa uumbaji, baadae hakika nyinyi mtafishwa, kisha nyinyi siku ya kiama mtafufuli-wa". "Suratul-muuminuuna :12-16.
"Sisi tumekuumbeni, basi kwa nini hamsadiki? Je mmeyaona maji ya uzazi myatoayo? Je nyinyi ndio myaumbayo au sisi ndio wenye kuyaumba? Sisi tumekikadiria kifo kati yenu, nasi si wenye kushindwa kuleta viumbe mfano wenu na kukuumbeni kwenye umbo msilolijua, na hakika mnajua umbo la kwanza (kuumbwa kwenu) kwanini hamkumbuki"? "Suratul-Waaqia:57-62.
"Je anadhani mwanadamu ya kuwa ataachwa hivi hivi? Je hakuwa ni mbegu ya uzazi ya manii yatokayo kwa kuchupa, kisha akawa pande la damu na (Mwenyezi Mungu) akamuumba na kumuweka kwenye umbo la sawa, na akamfanya namna mbili mwanamume na mwanamke. Je (alie kufanya hivyo) hakuwa ni muweza wa kuwahuisha na kuwarudisha kwenye uhai walio kufa? "Suratul-qiyama:36-40".
"Je hawakuona ya kuwa Mwenyezi Mungu ambae ameumba mbingu na ardhi na hakuchoshwa na kuwaumba kwao ni Mwenye uwezo wa kuwahuisha walio kufa ? Naam hakika yeye ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu" "Suratu-Ahqaafi:33".
"Je hatukukuumbeni kutokana na maji yaliyo dhalili na tukayaweka mahali pa utulivu hadi muda maalumu na tukakadi-riya (wakati wa kutoka mtoto). Na si ni wazuri kabisa wa kukadiria. Ole wao siku hiyo wanaokadhibisha"! "Suratul-mursalat:20 -24".
"Je mwanadamu hakuona ya kuwa sisi tumemuumba kutokana na maji ya uzazi, na ghafla ana kuwa ni adui wa wazi, na akatupigia mfano na kasahau kuumbwa kwake akasema: "Nani ataihuisha mifupa ikiwa imeharibika na kusambaa"? Sema ataihuisha yule amabae aliiumba kwa mara ya mwanzo, nae ni mjuzi wa kila kitu."Suratul Yaasin 77-79".
"Je alie umba mbingu na ardhi si mwenye uwezo wa kuumba viumbe mfano wao? Naam, na yeye ndie Mwingi wa kuumba na Mjuzi"."Suratu-Yaasin 81".
Je tulichoka kwa kuumba kwa mara ya kwanza? (Hata tushindwe kuumba umbo la pili). Basi wao wako kwenye shaka juu ya umbo jipya". "Suratu-Qaf:15".
"Hakika kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi (na kugumu) kuliko kuwaumba watu, lakini watu wengi hawajui".
"Enyi watu ikiwa mko kwenye shaka kuhusu ufufuo, hakika sisi tumekuumbeni kutokana na udongo kisha mbegu za uzazi kisha pande la damu kisha pande la nyama lenye umbile (kamili), na lisilo na umbile (kamili), ili tukubainishieni. Nasi tunavithibi-tisha kwenye mifuko ya uzazi tuvitakavyo hadi muda uliowekwa kisha tunakutoweni mkiwa watoto, kisha tunakuleeni ilimfikie kuwa wakubwa, na kuna wanao kufa na kuna warudishwao kwenye umri dhalili, ili asijue chochote baada yu kuwa alikuwa akijua mambo".
Na unaiona ardhi ikiwa imetulia kimya na tunaposhusha juu yake maji inataharuki na kukuwa na kuotesha kila aina ya mimea iliyo mizuri. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ndie haki na kwamba yeye anawahuisha wafu na kwamba yeye ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu, na kwamba kiama kitakuja hapana shaka ndani yake, na hakika Mwenyezi Mungu atawafufua waliomo makaburini. "Suratul-Hajji:5-7.
"Hakika mmetujia kama tulivyo waumba kwa mara ya mwanzo bali mlidhani ya kuwa hatukukuwekeeni miadi hii". "Suratul-kahfu:48".
Kwa hivyo inatudhihirikia wazi kuwa "hakika Mwenyezi Mungu ambae ameumba mbingu na ardhi ni mwenye uwezo wa kuumba viumbe mfano wa hivyo" kama alivyo kiumba kiumbe cha mwanzo atakirudisha hivyo hivyo. Na kwamba uumbaji wa pili hautatofautiana na uumbaji wa mwanzo tunao ufahamu kwa kuushuhudia kwa macho yetu. Na kuwa alieipa mbegu ya uzazi uwezekano na nguvu ya kukua hadi kufikia kuwa pande la damu kisha kuwa pande la nyama kisha kuwa mtoto na kuwa kijana hadi kuwa mzee, ni Mwenye uwezo wa kuifanya tena kazi ya uu mbaji na kuvifufua na kuvihuisha na kuvirudisha kama vilivyo kuwa.
Kwa hivyo ataihuisha mifupa nayo ikiwa imebadilika na kuwa mchanga kama alivyo iumba hapo kabla na haikuwa ni chochote. Na hilo si la ajabu maadamu yeye Mwenyezi Mungu "ndiye ambae aliviumba vitu kwa mara ya mwanzo", nae ndie ambae ameiumba mbingu na ardhi na hakuchoshwa na kuviu-mba na ni mwingi wa kuumba na mjuzi".
Ametakasika yule ambae ufalme wa kila kitu umo kwenye miliki yake" "Ametakasika mola wa walimwengu". Na hii ndio mantiki ya akili na maumbile na dhamiri, vikiwa vime epukana na aina yoyote ya shaka na dhana.
Ama mwenye shaka na kujitatiza kwenye ukweli huu ulio wazi hatumzingatii kuwa ni mwenye shaka kuhusu marejeo ili tuweze kuingia kwenye mazungumzo yenye kumuhusu, bali shaka yake hii inajulisha kutokuwa mkweli kwenye madai yake ya kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ndie Muumbaji wa mwanzo, na wakati huo hatastahili kutaka zitolewe dalili kuhusu suala la marejeo au kudai kulipinga suala hilo au kutokinaika na suala hilo, bali inampasa atafute dalili za kuamini kwa uumbaji wa mwanzo, na muumbaji wa mwanzo, kwa kuzingatia kuwa marejeo -kama tulivyo tangulia kusema- ni kurudia kufanya kitu ambacho hapo kabla kilikwisha tengenezwa na kutokea, na Imani ya hayo yaliyo tangulia inapothibiti kwa kukinai na kwa yakini kutakuwa hakuna shaka kamwe katika kuthibiti marejeo.
Huenda kukawa na mwenye kutoa pingamizi kuhusiana na haya yaliyo tangulia na akasema: "Hakika kupinga kwetu suala la marejeo sio kupinga kuumba kwa Mwenyezi Mungu na kuviweka kwake viumbe, bali ni kusalimu amri juu ya hukumu ya akili katika hukumu yake kuwa ni muhali kurejea, baada ya mwanadamu kutokana na kifo chake kuwa ni kitu kilicho potea na kutoweka, na nijambo lililo wazi kuwa kilicho kwisha potea na kutoweka ni muhali kukirudisha, na sijambo la kiakili mtu mwenye akili kuamrishwa kuamini mambo yasiyo wezekana (yaliyo muhali).!
Huu ndio muhtasari na ufupi wa shub'ha ambayo wenye kuikubali ni wengi na waisemayo ni wenye kuhesabika, baada ya jambo hilo kuwatatiza na kuchanganya kati ya hili na lile au wakaghafilika kunako maana ya kweli ya kifo na marejeo.
Lau kama wenye shub'ha (shaka inayofanana na haki) hiyo wangetaka kuzama na kuliangalia kwa ndani, kidogo wangeweza kuelewa uwazi wa jambo hilo, kwani ingemuwia wazi ya kuwa kifo kilivyo, si kutoweka viungo vya mwanadamu, bali ni kuvitenganisha na kuvisambaza viungo vile, na baadhi ya watu walidhani ya kuwa mwili baada ya kuachana na kusambaa vinapotea na kutoweka haviwi tena, lakini ukweli ni kuwa viungo hivyo vipo vikiwa vimetawanyika na chembe zake kusambaa, na Mwenyezi Mungu anapotaka kuvirudisha atavikusanya kwa uwezo wake viungo hivi vilivyo sambaa na kuviunganisha na kuviweka kwenye hali yake ya mwanzo ukiwa ni mwili na roho na sifa zake, na hayo ndio marejeo (kiama).
Na tunaelekezwa na kuongozwa mwongozo bora kwenye maana hii na maneno yaliyo zungumzwa kwenye Qur'an tukufu kutokana na suali la Ibrahimul-Khalil(a.s) alipo muuliza Mola wake kwa kusema: "Nionyeshe vipi unawahuisha wafu"?
Na jawabu la Mwenyezi Mungu aliyetakasika kwa Ibrahim lilikuwa ni kauli yake "Chukua ndege wanne wakatekate" yaani Ibrahim awakatekate vipande vidogo vidogo na avichanganye vyote uchanganyaji ambao hauwezi kutofautisha wala kutengani-sha kati ya ndege wale,"Kisha weka juu ya kila mlima kati ya vipande hivyo kipande kimoja" yaani kipande kimoja kati ya vile alivyo vichanganya, kisha waite, watakujia wakitembea kwani Mwenyezi Mungu atapambanua viungo vya kila ndege kuvito-fautisha na ndege mwingine, na kukusanya kila kipande kuki-weka na chenzake vikijitenga na vinginevyo, na kuviwekea uhai wakati ndege anapo kamilika kwenye umbo lake maalumu.
Na mfano huu wa Qur'ani ulio makini na ulio wazi ya kuwa kifo ni sawa na kuvitenganisha viungo na sio kutoweka kama wadhaniavyo baadhi ya wapingaji.
Kwa hivyo basi, kwenye jambo hili hakuna maana yoyote kati ya maana za kutowezekana na kuwa muhali wala shub'ha yoyote kati ya shub'ha zipingazo kwa kusema ni jambo lisilowezekana kiakili kama wanavyodai baadhi ya watu hao.
Kutokana na kuwa marejeo, kama tulivyo tangulia kusema, yana maana ya kurudi kwa watu wote, baada ya kufa kwa malengo ya kufanyiwa hesabu na kuhukumiwa, kisha kupewa thawabu (yaani malipo mema) na kuadhibiwa kutokana na matokeo ya hukumu ile "Na tutawafufua na hatutamuacha miongoni mwao yeyote" "Siku ambayo kila nafsi itayakuta iliyo yatenda kati ya mazuri yakiwa yameletwa mbele yake, na maovu aliyo yatenda".
Hakika marejeo haya ni lazima yatanguliwe na kumalizika kwa ulimwengu na vyote vilivyomo, vitu na wanadamu kiasi kwamba uhai utasimama kufanya kazi na vyote vilivyo hai kufariki "siku ambayo tutaikunja ardhi kama ukunjaji wa kurasa zenye maandishi" "siku ambayo ardhi itabadilishwa tofauti na ardhi hii, na mbingu (vile-vile)".
Je hilo linawezekana kiakili? Na je elimu ya kisasa inaweza kutuongezea na kutuelekeza kwenye uwezekano huu kutokana na kufungukiwa na nyanja mbali mbali na sehemu nyingi za ugunduzi wa vitu au habari zisizo julikana na kutoa habari za mambo yatakayo tokea siku za usoni?
Profesa Frank Allen anasema:
"Hakika kanuni za mwendo wa joto (dynamic law), zinajuli-sha kwamba vitu vitoavyo nguvu kwenye ulimwengu huu vinapotelewa na kuondokewa na joto lake taratibu, na kwamba vitu hivyo vinaelekea kwenye siku ambayo vitakuwa vyote kwenye siku hiyo, chini ya kiwango cha joto cha chini kabisa ambacho ni sifuri, na siku hiyo nguvu yote itakosekana na itakuwa ni muhali kuwepo uhai. Hakuna budi kutokea kwa hali hii ya kutoweka kwa nishati zote (energy) wakati kiwango cha joto cha vitu kitakapo-fikia chini ya sifuri kwa kupita kwa muda".
Naye Profesa Edward Luther Keel anasema:
"Kuna uhamaji wa joto wenye kuendelea kutoka kwenye vitu vya joto na kuhamia kwenye vitu vya baridi, na haiwezekani kutokea kinyume kwa nguvu za kidhati (ya kibinafsi) kiasi kwamba joto likarudi (lenyewe binafsi) na kuhama kutoka kwenye vitu baridi kwenda kwenye vitu vyenye joto. Na maana ya hayo ni kwamba ulimwengu unaelekea kwenye kiwango cha joto ambacho vitu vyote vitakuwa na kiwango cha joto kilicho sawa na ndani yake nguvu ya usaidizi. Na siku hiyo hakutakuwa na kazi ya kemia au maumbile, na hakutakuwa na athari ya uhai wenyewe kwenye ulimwengu huu".
Naye Profesa Claud M.Nathaway anasema:
"Sir (bwana) Isack Newton alikuja kufahamu ya kuwa nidhamu ya ulimwengu huu inaelekea kwenye kusimama (kuisha) na kuwa inakaribia kwenye hatua ya kiwango cha joto cha vitu vingine (vitoavyo nguvu) kuwa sawa na utafit i wa joto umeunga mkono rai hizi na umetusaidia kupambanua kati ya nishatiweza (energy potential) na isiyoweza, na imegundulika kwamba kunapo tokea mabadiliko yoyote ya joto hakika sehemu fulani ya nishatiweza, na kwamba hakuna uwezekano mwingine ila kuwa na mabadiliko haya kwenye maumbile kwa njia ya kinyume".
Naye Boltsman alitilia umuhimu uchunguzi wa kutaka kufahamu hali hii, na katika uchunguzi wake akatumia uwezo wake wote wa kugundua na vipimo vyake vya mahesabu, hadi akathibitisha kuwa kukosekana kwa nishati weza (energy potential) ambayo ina ashiriwa na kanuni ya pili ya mwendo joto ya joto (dynamic law of heat), si jambo lingine isipokuwa ni hali mahsusi katika matukio mengi ya jumla inayo ashiria kuwa mabadiliko yoyote au mgeuko wa kimaumbile hufuatiwa na hali ya kuzorota au kuwepo upungufu kwenye nidhamu ya ulimwe-ngu. Na katika hali ya joto kubadilika kwa nishati kutoka kwenye nishati weza na kuwa nishati isiyo weza, huchukuliwa kuwa ni ukosefu au upungufu wa nidhamu katika kiungo fulani au kwa ibara nyingine, ni kuzorota na kuharibika kwa jengo".
Naye Dr Muhammad Jamalud- din Afandi:
"Wataalamu wa sayari wote wanasisitiza ya kuwa jua, kama sayari nyingine yoyote ni lazima ipatwe na hali ya kuzidi kwa ghafla kwenye joto lake na ukubwa wake na miaka yake kwa kiwango ambacho akili haiwezi kukikubali, na wakati huo anga lake la nje litapanuka pamoja na vilivyomo ndani ya anga lake, navyo ni moto na moshi hadi kuufikia mwezi na kusababisha kasoro kwenye uwiano (nidhamu) wa jamii ya sayari zote. Na kila jua kwenye anga (mbinguni) ni lazima lipitie kwenye hali kama hizi kabla halijafikia kwenye uwiano wake wa daima, na jua letu kwa dhati yake halijapitia mzunguko huu bado.[155]
Amesema mwenyezi Mungu mtukufu:
"Basi ingoje siku ambapo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri " "Suratud- dukhan:10"
"(Itakuwa siku hiyo) wakati litakapo parama jicho, na mwezi utakapo patwa, na jua na mwezi kukusanywa, siku hiyo mtu atasema makimbilio yako wapi "? "Suratul-Qiyamah:7-10".
"Na ardhi na majabali yatabebwa na kupigwa pigo moja" "Suratul-Haaqqah:14". Kwa hivyo basi, siku ya marejeo na dalili zake na kila litufahamishalo kuhusu siku hiyo, kama vile kumali-zika kwa ulimwengu na kutoweka kwa uhai, ni siku ambayo inawezekana kutokea kwa hali yoyote, bali ni jambo la lazima na lisilo na shaka kwenye ufahamu wa kielimu ya kisasa.
Na elimu ya kisasa ikiwa imezidi kutupa matumaini ya ukweli huu basi hakika baadhi ya wanafalsafa wa zamani ambao elimu haikuwasaidia kwenye zama zao kuweza kufahamu ukweli, walishikilia na kuchukua kauli zisemazo kuwa ulimwengu utabakia kwenye hali yake ya hivi sasa bila kumalizika wala kuondoka, kwa kutoa ushahidi wa jua juu ya hayo, ambalo pamoja na kuwa lina umri mrefu sana, halijatokewa na mabadi-liko yoyote yanayoashiria kupungua au kuyayuka kwake na haya yana maana kwamba litabakia milele na milele, kwani lau kama lingekuwa limepangiwa kumalizika kungedhihiri kwenye jua hilo vitu vijulishavyo kumalizika huko kama upungufu au kubadilika au kuyayuka.
Ubatilifu wa madai haya unakuwa wazi kutokana na kufaha-mu uhakika ufuatao:
01- Hakika kanuni ya diynamic ya joto imetufahamisha ya kuwa joto halitadumu milele, na kwamba siku ya kumalizika kwake ambako kutapelekea kumalizika kwa ulimwengu bila shaka yoyote itakuja na kutokea kama tulivyo elezea kwa upana.
02- Hakika wachunguzi wametoa habari za kutokea kwa milipuko mingi juu ya anga la jua kwa kiwango cha masafa makubwa sana na mapengo yamedhihiri katika sehemu zilizoto-kea milipuko hiyo ambayo haiwezi kufasiri isipokuwa kwa kusema kuwa ni kulika (kuisha) kwa sayari ya jua
03- Wataalamu wa sayari kusisitiza kwa hali ya kupanuka anga la nje la jua hadi kufikia kwenye mwezi, kiasi kwamba uwiano wa sayari zote unaingiwa na kasoro, kama tulivyo tangu-lia kusema.
Na maana ya yote hayo ni kuwa kumalizika kwa ulimwengu ni jambo la lazima, hakuna makimbilio, na kwamba kauli ya kubakia milele kwa jua ni kauli isiyo kuwa na dalili yoyote.
Ama dalili ya wale wasemao ya kuwa hakuna marejeo kwa kutumia kanuni ya kuwa "Madda haimaliziki" ili kuyafanya sahihi madai yao, ni dalili yenye kupingwa kwa hali yoyote ile kwa sababu kauli isemayo kutomalizika kwa madda, imekuwa ni miongoni mwa kauli za zamani, ambazo elimu imezivuka na kusema kuwa itamalizika. Na sawa mada imemalizika au haikumalizika, kwani mas'ala haya hayana mahusiano yoyote na maudhui ya bahthi yetu, kwa sababu marejeo ni mabadiliko kwenye sura ya madda na sio kumalizika kwake.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu "Siku itakayo badili-shwa ardhi isiwe ardhi hii na mbingu hii" na ni tofauti kubwa iliyopo kati ya kubadilika na kumalizika.
Na muhtasari wa kauli ni kuwa:
"Hakika kiama kitakuja, hakuna shaka ndanyi yake, na Mwenyezi Mungu atawafufua waliomo makaburini".
"Na hakika wale ambao hutia shaka kuhusu kiama wako kwenye upotevu wa mbali na siku kitakapo simama kiama siku hiyo watapata hasara wenye kubatilisha ( kuwepo kwa kiyama)".
Na kiyama hicho kitakuja "pindi ardhi itakapofikia kileleni mwa utamaduni wake na mwanadamu kufikia mwisho wa maendeleo yake, na ardhi kuchukua mapambo yake, na mwana-damu kudhania ya kuwa anakihukumu kila kitu na akawa ni mwenye uwezo wa kufanya kila kitu, basi yeye akawa ana hukumu na kutawala suala la mvua, na kupandikiza au kulima kwenye ardhi yenye changalawe, na kwenye jangwa na kuhami-sha nyoyo na macho kutoka kwa wafu na kuwawekea watu walio hai, na akawa anasafiri kwenye sayari na anapasua chembe chembe za atom, na anahamisha majabali. Hakika Mwenyezi Mungu anatuahidi kwa kutuonya.
Hadi ardhi itakapo pambwa na kuwa vitu vya kuvutia na watu wake kudhania kuwa ni wenye uwezo juu yake, itawajia amri yetu usiku na mchana na tutawafanya kuwa kama mavuno kana kwamba hayakuwa ni mimea siku ya jana.
Na katika aya hii kuna uzuri (jamala) na siri (fumbo). Mwenyezi Mungu anasema, hakika kiama kitakuja usiku au mchana, na hakuna tafsiri ya maneno hayo isipokuwa ardhi iwe kama tufe la duara, nusu yake ni usiku na nusu nyingine ni mchana, basi kitakapo kuja kiama, nacho kitakuja ghafla,"na hakikuwa kiyama isipokuwa ni kama kupepesua jicho au karibu zaidi ya hivyo", nusu ya wakazi wake watakuwa kwenye usiku na nusu ya pili watakuwa kwenye mchana.
Kisha Qur'ani inatufikisha kwenye alama ya mwisho kati ya alama za kiama nayo ni kupulizwa kwa balagumu na kusimama kwa kiama.
Na matukio ya kiama yanayo simuliwa na Qur'an ni ya kutisha, kwa kuyasikia damu huganda kwenye mishipa kwamba jua litapatwa na mwezi kushikwa na majabali yatang'oka na nyota zitatawanyika, na mabahari yatapasuka, na ardhi itat ete-meka na viumbe hai vyote ardhini na mbinguni vitapiga kelele.
Yatatokea haya wakati wa kupulizwa parapanda la mwanzo. Na likipulizwa kwa mara ya pili watafufuka wote na kuanza hesabu.[156]
"Na kitabu kitawekwa, na utawaona waovu wakiyaogopa yaliyomo ndani yake, na wakisema:"Ole wetu kina nini kitabu hiki hakiachi jambo dogo wala kubwa isipokuwa hulihesabu". Na watayakuta mambo waliyo yatenda yakiwemo, na Mola wako hamdhulumu yeyote ". (Suratul-kahfu :49).
"Na kitabu kitawekwa na wataletwa manabii na mashahidi na itatolewa hukumu kati yao kwa haki, na wao hawatadhulumi-wa. Na itapewa kila nafsi malipo ya matendo iliyo yatenda, na yeye ni Mjuzi zaidi wa mambo wayafanyayo ". "Surat-uz-zumar: 69-70".
AMESEMA KWELI MWENYEZI MUNGU ALIE TUKUKA NA ALIE ADHIM
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
YALIYOMO
USUULID DIIN 1
UIMAMU 1
UTANGULIZI 1
UIMAMU KWA MAANA YAKE YA UJUMLA 3
DALILI YA KUTEULIWA KWA IMAMU 12
DALILI YA KWANZA: 12
DALILI YA PILI: 14
HADITHI YA TATU: 16
MAIMAMU (REHMA NA AMANI ZIWE JUU YAO) 20
IMAMU WA KWANZA 21
ALI BIN ABI TWALIB(a.s) 21
USUULID DIIN 23
UIMAMU 23
IMAMU WA PILI 23
HASSAN BIN ALI(a.s) 23
IMAMU WA TATU 24
HUSSEN BIN ALY(a.s) 24
IMAMU WA NNE 26
ALI BIN HUSSEN(a.s) 26
IMAMU WA TANO 27
MUHAMMAD BIN ALI(a.s) 27
IMAM WA SITA 28
JAAFAR BIN MUHAMMAD(a.s) 28
IMAM WA SABA 30
MUSSA BIN JAAFAR(a.s) 30
IMAMU WA NANE 31
ALI BIN MUSSA(a.s) 31
USUULID DIIN 33
UIMAMU 33
IMAM WA TISA 33
MUHAMMAD BIN ALI(a.s) 33
IMAMU WA KUMI 34
ALI BIN MUHAMMAD(a.s) 34
IMAMU WA KUMI NA MOJA 35
ASSAN BIN ALI(a.s) 35
IMAMU WA KUMI NA MBILI 36
MUHAMMAD BIN HASSAN(a.s) 36
MAHDI MTARAJIWA KATI YA TASWAWWUR NA TASDIQ 39
KUMFAHAMU NA KUMSADIKI 39
UTANGULIZI 39
MUHAMMAD HASSAN AALU-YAASIN 40
USUULID DIIN 43
UIMAMU 43
SEHEMU YA KWANZA 43
SEHEMU YA PILI 48
MAHDI NI NANI? 48
USUULID DIIN 58
UIMAMU 58
SEHEMU YA TATU 58
NYONGEZA 65
BARUA YA SHEKH AL-KASAM 65
JAWABU LA BARUA 67
USUULID DIIN 69
MAREJEO YA KIAMA 69
MAREJEO YA KIAMA 69
UTANGULIZI 69
MAREJEO NI LAZIMA 72
USUULID DIIN 81
MAREJEO YA KIAMA 81
UWEZEKANO WA KUWEPO MAREJEO NA DALILI ZAKE 81
SHARTI YA KUCHAPA 88
MWISHO WA KITABU 88
YALIYOMO 89
[1] . Lisanul-arab juzuu 12/25-madda (Ama).
[2] . Lisanul-arab juzuu 9/83-84-89 madda "khalafa".
[3] . Al-ahkaam as-sultwaniya-3.
[4] . Muqaddimat Ibnu Khaladun-159.
[5] . Muqaddimat Ibnu Khaladun-183.
[6] . Nadhariyatul-Imamiya-22.
[7] . Nadhariyyatul-imamiyyah 24.
[8] . Nadhariyyatul-imamiyyah 20.
[9] . Rejea kwenye utafiti wa "Al-Islamu dinun wa daula" katika kitabu chetu "Mafahiimul Islam".
[10] . Dr.Ahmad Mahmood Swabahy anasema:Hakika utatuzi wa Abubakar na Omar ulikuwa ni utatuzi wa muda tu ili kuondoa fitina iliyotarajiwa kutokea, bila kuweka msingi kamili wa nidhamu ya utawala. Rejea Nadhariyatul Imamiya-26.
[11] . Tafsiri-Razy juzuu 4/43.
[12] . Tafsiru-razy juzu 4/43.
[13] . Nadhariyatul-Imamiya-135-139.
[14] . Na miongoni mwa mambo yanayo takiwa kuangaliwa kwa makini ni kuwa wale wasemao suala la uchaguzi siku aliyofariki Mtume(s.a.w.w) , walilazimika kukubali kuwepo uteuzi na kuutetea pale khalifa wa kwanza wa Uislamu alipo mteua atakae shika nafasi yake baada yake, na wakatoa sababu kwa kitendo hicho kuwa hali iliyokuwepo kwa ujumla ilimfanya atoe usia na kuteuliwa khalifa, kwa kuzingatia kuwa na vita vya ukombozi vilivyo kuwa vikifanyika, na kwamba ilikuwa inaogopewa kuwepo kwa wapinzani au waasi na mashambulizi yao.
[15] . Theokrasia kwa kiswahili.
[16] . Nadhariyatul-Imamiyah-62.
[17] . Tumeinukuu kwa ufupi kutoka kwenye taarikhu Atwabari, juzuu 2/319-321 iliyo chapwa na darul maarif ya Misri, chapa ya mwaka 1961 AD.Na miongoni mwa yasemwayo ni kuwa Dr Muhammad Hussen Haykal ameithibitisha hadithi hii kwenye kitabu chake kiitwacho "Hayatu Muhammad" chapa ya mwaka 1970 ukurasa 104. Kisha katika chapa ya pili akaifuta hadithi hiyo.
Pia rejea ili kujua vitabu vilivyo taja hadithi hii na silsila ya wapokezi wake kwenye kitabu Al-ghadiir juzuu 2/252-260.
[18] . Sahihi Muslim juzuu 7/120.Pia rejea kuhusu vitabu vilivyo taja hadithi hii na wapokezi wake kwenye kitabu Al-ghadir Juzuu 1/48-49 na 3/173.
[19] . Nadhariyatul-imamiya-229.
[20] . Ili kuyajua majina ya hao maswahaba na maulama na ma hufadhi na wana mashairi na wapokezi na vitabu vilivyo wataja na riwaya zao angalia kwenye kitabu ghadiri Juzuu ya kwanza yote.
[21] . Suratul-maaidah-67, pia rejea katika kitabu cha Addurul-manthuur juzu ya 2/298 na Fathul-Qadiir juzuu 2/60 na vitavu vingine vilivyo tajwa kwa mapana zaidi kwenye kitabu Al-ghadiir Juzuu ya 1/196-209 ili kujua sababu ya kuteremka aya hii.
[22] . Usudul-Ghaba Juzuu 4/28 na Albidaya wannihaya Juzuu 5/209-213 na vyanzo vingine vilivyo tajwa katika kitabu Al-ghadiri juzuu 1.
[23] . Sunanu Ibnu Maja juzuu 1/43 na Al-bidaya wannihaya 5/210 na Wafiyatul-A'ayaan 4/318 na vyanzo vingine vilivyo tajwa kwenye kitabu Al-ghadiir.
[24] . Suratu-maidah-3 na ukitaka kuelewa uteremkaji wa aya hii na kwa mnasaba huu rejea Taarikh Baghdaad Juzuu 8/290 na Durrul-manthuru 2/259 na vitabu vingine vilivyo tajwa kwa upana kwenye kitabu Al-ghadiir juzuu 1/120-217.
[25] . Taarikh Baghdaad Juzuu 8/190 na albidayaa wanihaya 5/210 na vyanzo vingine vilivyo elezwa kwenye al-ghadiir Juzuu ya 1.
[26] . Nadhariyatul Imama Uk:221/222.
[27] . Nuzhatul-majaalis 2/476.
[28] . Minhaaju ssunna 4/210.
[29] . Rejea kwenye dalili za Mtume katika kuwateuwa Maimamu na pia ushaidi wa kila imamu,alie tangulia kumtolea dalili ajae, vitabu Al-irshaad cha Mufid, Al-manaqib cha Ibnu Shahri ashuub asarawi, na Al-fusulul-muhimma cha Ibnu-Swabagh Almaliki, na Matwalibu ssaul cha Ibnu Twalha Ashafii, pia Yanabiul-mawaddah cha Al-Qanduzi Al-hanafi na vinginevyo.
[30] . Sheikh Alqanduzi, na wengineo wametoa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kauli yake isemayo: "Mimi ni Bwana wa Manabii wote, na Ali ni Bwana wa Mawasii wote, na hakika Mawasii wangu baada yangu ni kumi na wawili". Rejea kweye kitabu yanabiul-mawadda ili uione hadithi hii na hadithi zingine zinazo elezea idadi ya kumi na mbili, ukurasa 441-486-487-488-492-493.
[31] . Sahihi Bukhari 9/101 na Sahihi Muslim 6/3, na Sunanu Tirmidhi 4/50 na Sunanu Abi Dawud 2/42, na Jamiul-Usul 4/440-442. Na Kadhi al-Qanduzi amesema kuhusiana na njia ya hadithi hii, katika Bukhari imepokelewa kwa njia tatu, na katika Muslim kwa njia tisa, na katika Abu Daud kwa njia tatu, na katika Tirmidhi kwa njia moja, na Hamiidi kwa njia tatu, Rejea yanabiul-Mawadda:444.
[32] . Sahihi Muslim Juzuu 6/4.
[33] . Hil-yatul-awliya juzuu 1/63.
[34] . Al-irshaad cha Mufiid:3.
[35] . Ili kujua ni nani wa mwanzo kusilimu rejea Al-ghadiir Juzuu 3/192-209 kwani ametoa maswahaba na taabiin 66 walio sisitiza kuwa Ali ndie muislamu wa kwanza.
[36] . Nuzhatul-majlisi Juzuu 2/476.
[37] . Sunanu Attirmidhi 5/656.
[38] . Sunanu Attirmidhi 5/658.
[39] . Akiidatu Ashia:90.
[40] . Ahlul-bayti 280/282.
[41] . Ahlul-bayti 282.
[42] . Nadhariyatul-Imama :328-329.
[43] . Al-wiladah wal-wafat minal-ishad:191-197.
[44] . Sulhul-Hassan:259-260.
[45] . Almanaaqib Juzuu 2/208.
[46] . Al-irshaad:210.
[47] . Al-awasim minal-qawasim:231.
[48] . Nadhariyatul-imama:336.
[49] . Taarikhul-wilada wal-wafat kwenye kitabu cha Al-irshaad:203.
[50] . Al-kaamil 3/311.
[51] . Ukitaka kuyaelewa hayo rejea kwenye kitabu Swahifatu-Assajadiya ukurasa 25-38-56-82-107-167-196-236-261-262-304-308.
[52] . Tarehe ya kuzaliwa kwake na kufariki kwake rejea Al-irshaad:270.
[53] . Ili kukielewa zaidi kisa hiki rejea kwenye kitabu Al-mahaasin wal-masawii cha bayhaqi.Juzuu 2/232-236.
[54] . Al-manaqib Juzuu 2/324.
[55] . Ashi'atu min hayati Asswadiq 1/85.
[56] . Vimechapishwa kwa mara kadha huku Najaf na Qairo,Iran na Bairut.
[57] . Rejea kwenye kitabu chake kiitwacho "Imamu Aswadiq mul-himul-kimyaa"chapa ya pili-Syria 1958 A.D.
[58] . Majallatul balaagh-mwaka wa pili-toleo la pili ,ukurasa:83.
[59] . Al-irshaad:289.
[60] . Al-irshaad: 307.
[61] . Al-irshaad: 325.
[62] . Barua hiyo iko kwenye kitabu Tuhafil uquul:341-356.
[63] . Al-irshaad:352.
[64] . Al-irshaad:360.
[65] . Hadithi ya kwanza inapatikana kwenye kitabu yanabiul-mawada ukurasa 448. Na yapili kwenye kitabu:Swawaiqul-muhrika 99, na kwa madhumuni hayo, hadithi zingine utazipata kwenye sunanu Abi daud Juzuu ya 2/422 na Al-haawi 2/124-125.
[66] . Usulul-Ismailiya:86-87.
[67] . Al-fitnatul-Kubra juzuu 1/131-134.
[68] . Jarida la majmaul-Ilmiy la Iraq kitabu cha tatu, Juzuu ya kwanza ukurasa 53.
[69] . Wu'aadhu ssalatwin.
[70] . Al-yamiin wal-yasaar fil-Islam :96.
[71] . Tafsirut -twabari 30/265 na Swawaiqul-muhriqa:96. Na rejea kwenye Nihaya cha Ibnul-Athir 3/276 na Tafsir Addurr-Almanthur cha suyuti:6/379.
[72] . Rejea kwenye kitabu chetu "Al-Imama"chapa ya Beirut mwaka 1392 H (1972 AD).
[73] . Rejea sehemu yetu ya uimamu.
[74] . Hii ni hadithi yenyewe ya mtume, ameitoa Ibnu Hajar Al-haitamiy katika Swawaiqul-Muhriqa ukurasa 99.
[75] . Almahdi wal-mahdawiya cha Dr Ahmad Amin Ukurasa 110.
[76] . Jarida la chuo kikuu cha kiislam Toleo la 3 ukurasa 161-162.
[77] . Adabu Shiia ukurasa 101 na anayaunga mkono Dr Abdul-haliim Annajaar kwenye utangulizi wake wa kitabu Al Mahdiyyi fil-Islam. Hakika maulamaa wa hadithi wanasimulia kuwa fikra ya mahdy imefikia daraja ya kuwa mutawaatir kwa maana (yaani hadithi nyingi zimekuja kwa maana hii hata ingawa matamshi yametofautiana).
[78] . Adaabu Shia:16.
[79] . Wu'aadhu ssalaatwiin cha Dr Ali Al-wardu.
[80] . Jarida la Atarbiyatul-Islamiyah/mwaka 14 toleo la 7/ukurasa:30.
[81] . Alisimulia na kupokea kutoka kwake Ibnu Swabbagh Al Maaliky katika Alfusulul-Muhimma:275.
[82] . Amepokea kutoka kwake Al-haafidh Al-kanjii Asshaafii kwenye kitabu chake (Al-bayaan).
[83] . Na kuna Nus'kha (kopi) iliyo chapwa na taasisi ya Ma'ahadul makhtutwatil- arabiya ya Kairo.
[84] . Zimepokewa hadithi kutoka kwenye kitabu hicho katika As-afu-rraghiin:139, na kuna kopi zake zillizo andikwa kwa mkono katika mji wa Halab na Istambuli. Na ninayo kopi iliyo tolewa na kusomwa kwa mtunzi na iliyo hifadhiwa huko halab.
[85] . Kuna kopi iliyo andikwa kwa mkono huko Istambuli.
[86] . Mtunzi amekitaja kwenye kitabu chake "Al-aimatul-Itha ahar ",Uk:118.
[87] . Kati ya vitabu hivyo viwili kopi iliandikwa kwa mkono iko Istambuli na ninayo kopi iliyochukuliwa kutoka kwenye asili ya kitabu cha.
[88] . "Alburhani" kilichoandikwa kwa mkono na kilicho hifadhiwa huko Makka Mukarramah kwenye maktaba ya Haramul Makki. 5.Kitabu cha kwanza kopi ilio andikwa kwa mkono iko India na kopi ya Kitabu cha pili kiko Istambul.
[89] . Kuna kopi yake iliyo andikwa kwa mkono Istambuli.
[90] . Majalatul-jaamia Al-Islamiyah: Toleo 3/ukurasa 131.
[91] . Al-ghadir 2/184 chapa ya najaf 1365 H.
[92] . Al-ghadiir 2/223.
[93] . Diiwaanu, Da'abul:42.
[94] . Al-ghadiir 4/279.
[95] . Matwaalibu ssaul 2/79.
[96] . Sharhul-qawaid Assab'ul Alawiyat, Uk:70.
[97] . Al-aimatul Ithna-ashar :118.
[98] . Diiwan Abdallah bin alawiy iitwayo "Ad-duruhl-mandhum" Uk:18 na 146.
[99] . Swawaiqul-muhriq:99. Na irejee "Al-Mahdi wal-mahdawiya".
[100] . Hassan ni sifa ya hadithi kutokana na wapokezi wake.
[101] . Rejea kitabu Al-mahdi:9.
[102] . Aswawaiqul-muhriqa:99 na Is-aafu-raaghibiin:243 na Al-hawiy 2/124.
[103] . Sunanu Ibnu maja:2/1368 rejea Al-fusulul-Muhimma:276 na Yanabiul-mawaddah:435 na Al-hawiy:2/124.
[104] . Tadhkiratul-khawaas: 377. Na rejea Sunani Abi Daud: 2/422 na Swawaiqul muhriqa:98 na Nurul-Abswar: 156-157 na Al-hawiy :2/129-137.
[105] . Sunanu Abi Daud:2/422, na Aswawaaiqul-muhriqa:97 na Is-aafur-raghi-biin:131 na Al-hawiy:2/124.
[106] . Sunanu Abi Daud:2/422 na Aswawaiqul-muhariqa:97,na Nurul-abswar:157 na Al-hawiy:2/124-126 na katika Musnad Ahmad bin Hanbali 1/376 na 377-430-448 "Haitaondoka dunia au haitamalizika dunia mpaka awatawale waarabu mtu kutoka kwenye Ahlul-bait wangu,jina lake linafanana na jina langu". Na mfano wa hadithi hii iko kwenye Sunan At-tirmidhi:4/505 na Tadh-kiratul-hufadh:2/488 na rejea Sunanu Ibnu Maaja:2/1366.
[107] . Yanabiul-mawaddah:448 na Al-hawiy:2/190.
[108] . Sunanu Abi-daud:2/422na Al-bayaan:64 na Swawaiqul-Muhriqa:97 na Is-aafur-raaghibiin:131, na Sunanu Ibnu Maaja:2/1368 na Al-hawiy:2/124 na 137.
[109] . Yanabiul-Mawadda:455, na katika Al-bayaan:82 na miongoni mwa hadithi ya Mtume ambayo ni ndefu, Kisha akapiga kwenye bega la Hussen na kusema "Atatokana na huyu mahdi wa umma huu".
[110] . Yanabiiul-mawaddat:445.
[111] . Yanabiul mawadda:441/445.
[112] . Yanabiul mawadda:443 na Is-aaf Ar-raaghibiin:139-140.
[113] . Kuhusu orodha hii rejea, kwa kuongezea vyanzo tulivyo vitaja hapo nyuma-bahthi ya Shekh Abdul Muhsin Al-abal kwenye majallatul-jaamiatul Islamyiyya toleo:3/128, nayo ina anuwani ya "Aqidatu ahlisunna wal-athar fil-mahdiy Al-muntadhar".
[114] . Majallatul jaamiatil-Islamiyyah Toleo:3/129.
[115] . Al-Irhaad: 372 na Yanabiul-mawadda 451-452.
[116] . Swahihu al-tirmidh :2/270 na Aswawaiqul-Muhriqa:97.
[117] . Tadhkiratul-khawas:377 na matwalibus-saul:2/79 na Swawaiqul- Muhriqa :124 na Nurul Abswar:154.
[118] . Alfusuulul-Ashara cha Shekhe Mufiid :13-14.
[119] . Alfusuulul-Ashara cha Shekhe Mufiid: 14.
[120] . Al-Irshaad:372.
[121] . Al-Irshaad:372.
[122] . Matwaalib As-sauli:2/79.
[123] . Tadhkiratu-Khawaasi:377.
[124] . Al-bayaan:102-112.
[125] . Wafiyatul-A'ayan:3/316.
[126] . Al-wafiy bil-wafiyaat:2/336.
[127] . Aswawaiqul-muhriqa:124.
[128] . Al-fusulul muhimmah:274.
[129] . Al-aimatul-Ithna ashar:117.
[130] . Tuhfat Al-twalib :17/A (imeandikwa kwa mkono na iko kwenye maktaba ya Haram ya Makka katika namba 33/historia/Dahlawi).
[131] . Is-aafur-Raghibiin:140.
[132] . Yanabiul-mawaddah:450-451.
[133] . Sabaik Adhahab: 78.s
[134] . Nurul-Abswar: 154.
[135] . Na mambo ya ajabu sana aliyo yasimulia Dr Ahmad Amini kwenye kitabu chake "Al-Mahdi wal-mahdawiyat, Uk:108 kuhusu mas'ala haya alipo sema ya kuwa Madhehebu ya Ibnu khaladuni ni kukubali (Alkhabarul Wahid) habari moja (hadithi) ikiungwa mkono na hukumu ya akili, na kuzikataa hadithi nyingi ikiwa akili haikuziunga mkono na kwamba yeye alipinga kuwepo kwa Mahdi na fikra ya Mahdi kwa sababu fikra hiyo inapingana na hukumu ya akili yake!.
[136] . Rejea Kitabu Al-bayan cha Al-haafidh Al-kanji Ashaafii:102-113.Na sheikh Kanduzi Al-hanafii kwenye yanabiul-Mawadda ametoa hadithi ukurasa:448 kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibnu Abbas (radhi za Allah ziwe juu yao) wamesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w):" Hakika Ali ni wasii wangu na katika kizazi chake atatoka mwenye kusimama (juu ya haki) na mwenye kungojewa ambae ni Mahdi, ambae ataijaza ardhi kwa usawa na uadilifu kama ilivyo jazwa dhuluma na ujeuri. Nina apa kwa yule ambae amenituma kwa haki nikiwa mtoabishara na muonyaji, hakika wenye kusimama madhubuti juu ya kauli ya uimamu wake zama za kughibu kwake ni wachache zaidi kuliko baruti. Akasimama Jaabir bin Abdullah akasema:" Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je huyo mwenye kusimama kutoka kwenye kizazi chako atakuwa na ghaiba (atatoweka na kuto onekana)"?? Akasema Mtume: "Ndio, ninaapa kwa jina la Mola wangu, Mwenyezi Mungu atawachekecha wale ambao wameamini na atawaangamiza makafiri. Kisha akasema: Ewe Jaabir hakika hili ni jambo kati ya mambo ya Mwenyezi Mungu na siri kati ya siri zake Mwenyezi Mungu, jiepushe kuwa na shaka kwani kutia shaka kwenye jambo la Mwenyezi Mungu ni kufuru".
[137] . Yanaabiul-mawadda:488.
[138] . Yanaabiul- mawadda:495.
[139] . Al-hawiy :2/152.
[140] . Dr Ahmad Amin anawanasibishia mashia kuwa wao wana itakidi kuhusu Mahdi "ya kuwa pamoja na kuwa yuko mafichoni huwatia hamasa wafuasi wake ili waondoe dhuluma" na kwamba yeye anaishi mafichoni na huwaelekeza akiwa nyuma ya pazia kwa kuamuru na kukataza. Kitabu "Al-mahdy wal-mahdawiya" Uk:109na119 na vitabu vyote vya Shia vinasema wazi kuwa ameghibu na hawasiliani na yeyote, sasa ziko wapi kauli za kweli na iko wapi amana katika kunukuu habari?.
[141] . Pamoja na dalili zote hizi za Qur'ani zilizo wazi,hakika Dr Ahmad Amiin anaonelea kuwa mwanadamu "hawezi kufichika na akabaki mafichoni kwa mamia ya miaka bila Mwenyezi Mungu kumpitishia hukumu ya kifo".Na akasema kuwa hilo haliwezekani" isipokuwa kwa wajinga ambao wameondo-kewa na akili zao". Al-mahdy wal-mahdawiya:96.
Je Dr Ahmad anaonelea kuwa kusadikisha suala la kutohukumiwa kwa kifo kwa Nuhu na Yunusu na Nyangumi na watu wa Kahfu (pango) ni dalili ya ukosefu wa akili?.
[142] . Majallatul-Muqtatwaf,mwaka wa 59/juzuu ya tatu.
[143] . Kutumia neno muhali si sawa, na sawa ni kuwa haionekani kuwa ni jambo lililo mbali kufanyika.
[144] . Jaridatul-ambaa Aljarida Albaghdaadiya, toleo namba:40/mwaka wa kwanza/27 march/mwaka:-1965 A.D. 1.Bernardshow, cha Abbas Mahmud Al-aqqad/Silsila ya Iq'rau/Tolea.
[145] . 89/Ukurasa 124-125.
[146] . Kwenye kitabu hicho "Berardshow".
[147] . Aahaad ni hadithi ambayo sio mutawatir iwe imepokewa na mpokezi mmoja au zaidi.
[148] . Rejea Kitabu "Allah-bainal-fitrat wad-dalil" chapa ya Bagh'daad 1389 H=1967 A.D, na Bairut 1392 H=1972 A.D.
[149] . Rejea Kitabu chetu "Al-adlul-ilahi bainal jabri wal-ikhtiyaar", Baghdaad 1389 H=1970 A.D, Bairut 1392=1972 A.D.
[150] . Rejea Kitabu chetu "An-nubuwat"Baghdaad 1392 H=1972A.D, Bairut 1392=1972 A.D.
[151] . Usulul-fiq'hi cha mudhwaffar, 1/55-59-89-90.
[152] . Al-Islam wat-Twibul-hadith:66.
[153] . Dr Ibrahim Ar-rawiy-Majallatu Al-adlu Annajafiya toleo la 1 ukurasa 1/6-2-6.
[154] . Rejea kwenye bahthi ya kuwa madda si ya tangu na tangu na majadiliano na wasemao ya kua ni ya tangu na tangu kwenye kitabu (Hawaamishu ala kitabi. Naqdi fikrid-dini) Chapa ya Bairut/1391h-1971 A.D.
[155] . Rejea kwenye kitabu "Allah yatajalla fi-asril ilm" Ukurasa:8-29-92-167.
[156] . Al-Qur'ani, cha Mustafa Mahmud:207-209.