TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN
Kuweka vikundi tafsiri ya Qurani
mwandishi Muhammad Hussein Tabaatabaai
Lugha ya kitabu سواحیلی
mwaka wa kuchapisha 1404

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

DIBAJI YA AL-MIZAN

Katika kazi nyingine alizozifanya mfasiri mkubwa allama tabatabai Al-Mizan inachukuwa nafasi ya kwanza katika kutambuliwa, kwa sababu ya sifa zake zisizokuwa na kifani. Jambo hili si katika vitabu vyake tu bali ni katika vitabu vyote vya Kiislamu vilivyo andikwa kuhusu Dini, Sayansi, Falsafa, na hasa kuhusu aina zote za tafsiri ya Qur'an mpya ama zamani zilizoandikwa na Sunni ama Shia. Maelezo haya hayawezi kueleza kwa urefu mambo yaliyomo lakini yanaweza kuwasaidia wasomaji kwa kuwapa fununu juu ya umaridadi wa Al Mizan. Ninaona kwamba sistahili kuifanya kazi kubwa kama hii kama watu wakubwa mfano Ayatullah Mutahhari ambaye yeye mwenyewe ni mtu mwenye fikra mpya, mjuzi wa Qur'an na mfasiri vile vile, aliposema: "Al- Mizan ni tafsiri kubwa zaidi ya Qur'an iliyowahi kuandikwa tangu kuanza Uislamu; na itachukua miaka sitini ama mia moja mpaka watu wetu kuutambua umuhimu wa Al-Mizan ya Allama Tabatabai. "Wanachuoni wengine, wajuzi na watu walio na busara walitoa maoni kama haya kuhusu kitabu hiki. Majaribio yoyote ya kuonyesha maana ndani ya Al- Mizan hata kama ni kwa njia ya juujuu, katika maelezo mafupi kama haya, ni kama kujaribu kuitia bahari ya Atlantiki katika chungu kidogo.

Hata hivyo ninatarajia kukusanya matone machache katika bahari hii ya elimu ya Kiislamu kulingana na uwezo wangu ili nitosheleze kiu yangu. Nataraji roho njema ya mwandishi mcha Mungu wa kitabu hiki cha milele, itaniwia radhi kwa kazi hii ndogo nitakayoitanguliza.

Historia Ya Al-Mizan Kabla ya kugusia zile alama zinazoipambanua tafsiri hii na nyinginezo, tutaandika historia fupi ya Al- Mizan. Allama Tabatabai, aliyekuja katika hawzah ya Qum mwaka wa 1325 A.H aliandika na akatoa hotuba kuhusu matawi mbali mbali ya elimu za Kiislamu. Tafsiri na maelezo ya Qur'an lilikuwa ni somo moja katika mazungumzo yake, aliyoyafanya na wanachuoni na wanafunzi na "Hawzeh Ilmiyyah" ya Qum. Kuhusu azimio lake la kuandika Al- Mizan, Allama Tabatabai alisema kwamba, alipokuja Qum kutoka Tabriz alijaribu sana kutathmini mahitaji ya jamii ya Kiislamu, na vile vile alzingatia hali iliyokuwapo katika Hawzah Ilmiyyah ya Qum. Baada ya kulizingatia jambo hili, suluhisho lilikuwa, shule ile ilihitaji maelezo ya Qur'an ili waweze kuielewa vyema na kuzifahamu sharia zake na vilevile kuyaelewa maana halisi ya vitabu vyote vya Kiislamu na maandishi yote yaliyo na vipaji vikubwa.

Kwa upande mwingine kwa vile nadharia za mada zilikuwa zikipata nguvu siku hadi siku, palikuwa na haja kubwa ya kupata hoja za kiakili na kifalsafa ili kuiwezesha Hawza kukabiliana na hali mpya na kuchambua misingi ya kifikra na imani ya Uislamu, pamoja na msaada wa hoja za kiakili ili kutetea maoni ya Uislamu. Basi aliona ni jukumu lake kufanya juhudi ili ayatimize mambo haya mawili muhimu kwa msaada wa Mwenyezi Mungu aliye Mtukufu zaidi. Alipanga masomo ya tafsiri ya Qur'an kwa mpango huu. Pengine Alama Tabatabai alitoa masomo ya Qu'ran nzima kwa wanafunzi kwa mara nyingi na huku akiandika yale aliyofundisha. Wakati wa darasa hizi zilizoandaliwa vizuri kwa undani wa fikra, pengine, alitoa vikao hivi vya masomo kwa ufasaha , na baadae yalichapishwa katika mijalada ya vitabu.

Uchapishaji wa kwanza wa Al - Mizan ambao ulikuwa katika lugha ya Kiarabu ulifanyika Iran na ilirudiwa kuchapishwa huko Beirut. Mpaka wakati huu, zaidi ya chapa tatu zimechapishwa huko Iran na Beirut kwa idadi nyingi zaidi. Ni Maktaba chache za watu binafsi na za serkali ambazo hazina seti kamili ya Al Mizan. Vile vile maktaba zote zinayo baadhi ya majalada ya tafsiri hii juu ya rafu zao. Kitabu cha asili cha Al Mizan ambacho kinakusanya majalada ishirini kiliandikwa katika lugha la Kiarabu. Kila mjalada una kurasa mia nne. Ilikusudiwa kwamba watu wote waliyopenda kusoma tafsiri ya Qur'an, wawe watapata faida ya kutosha kutokana na mafundisho ya Quran. Baadhi wa wanafunzi wa Allama Tabatabai walikifasiri kitabu hiki katika lugha ya Kifursi chini ya uongozi na usimamizi wake. Kila mjalada mmoja wa lugha ya Kiarabu ulifasiriwa katika mijalada miwili ya lugha ya Kifursi na idadi ya mijalada hii ikawa arobaini. Jukumu hili lilichukuliwa na Syed Muhamad Baqir Musawi Hamadani. Ili tafsiri ya Al Mizan iliyokuwa katika lugha ya kifursi isionekane tofauti, jambo ambalo lingeharibu usomaji wa kitabu hicho, Allama Tabatabai alimpa mijalada ya mwanzo ya Al Mizan kuifasiri tena.

Ni lengo letu kwamba tafsiri hii ya maneno matukufu ya Qur'an itafasiriwa katika lugha nyengine pia, ili iwe rahisi kwa wale wanaotaka kuondoa kiu ya elimu tukufu na kwa wale wanaotaka kuzijua sheria za Kiislamu zenye kuokoa maisha. Ingekuwa bora tafsiri hii kufanywa na watu na wanachuoni ambao wanaijua vyema lugha ya Qur'an. Ingekuwa ni kazi nzuri kama ujumbe wa Qur'an Tukufu ungetolewa katika njia hii ili uwafikie binadamu na kuwaokoa na mila za makafiri. Elimu ya kumwabudu Mwenyezi Mungu katika Qur'an humwepusha binadamu na aina zote za aibu na utumwa.

Alama Zinazoipambanua Tafsiri Ya Al Mizan: Al Mizan inakusanya aina mbali mbali za elimu: kama vile ya Sayansi, Ufundi, Usanifu na Uzuri. Vile vile Falsafa, Elimu ya Adabu (literature), Historia, Elimu ya Jamii na Elimu ya Hadithi (za Mtume(s.a.w.w) Mambo matatu kati ya haya hayako wazi wakati mengine yanahusiana nayo.

1. Tafsiri Ya Qur'an Kwa Qur'an: Allama Tabatabai katika maelezo yake juu ya Qur'an kwanza anonyesha asili ya kuingiliana kwa aya mbalimbali, na vile vile kusibitisha kwamba, kwa sababu hii ya kuingiliana kwa aya, aya hizi hufasiriana na kujieleza zenyewe. Kwa maneno mengine Allama Tabatabai anaonyesha kwamba baadhi ya sehemu ya Qur'an hufasiri sehemu nyingine.

Ili kuzielewa aya tukufu za Qur'an na Tafsiri zake ni lazima tutafute msaada kutoka katika Qur'an yenyewe. Alizungumzia tatizo la tafsiri ya Qur'an katika kitabu chake " Qur'an dar Islam" (Mahali pa Qur'an katika Uislamu). Baada ya kufafanua jambo hili; Allama Tabatabai alisema ' kwamba tafsiri sawa ya Qur'an inawezekana kupitia kufikiria kwa makini na kushauri aya nyingine kuutazama mwongozo wa aya za Qur'an. Kwa maneno mengine, zipo njia tatu ambapo njia yoyote kati yake iko wazi kwetu kuitumia katika tafsiri ya sawa ya aya.

1.Tafsiri ya aya zozote bila ya kuhusisha maana ya aya nyinginezo; na kwa msaada wa maelezo ya elimu maelezo za Sayanzi tuliyo nayo; au pasi na elimu hizo.

2. Tafsiri ya aya ikiwa na mwongozo na Hadith, ikichukuliwa kutoka kwa mmoja wa Ma'sumin(a.s) , inayofuatia aya.

2. Tafsiri ya aya kwa kufukiria kwa makini maneno na maana ya aya kwa kutumia msaada wa aya zinazohusika. Vile vile kutafuta ushauri katika Hadith mahali inapopasa. Njia ya tatu ndiyo iliyoelezewa katika sura iliyopita (nayo ni mahali pa Qur'an katika Uislamu). Hii ndiyo njia aliyoitumia Mtume(s.a.w.w) na Maimami(a.s) , kama tunavyosoma katika mafundisho yao. Mtume(s.a.w.w) alisema: "Aya nyengine huzungumzia baadhi ya aya nyengine na baadhi yake huzithibitisha nyengine."

Allama huyu mwisho anatukumbusha jambo muhimu; nalo ni kwamba, Qur'an hutafasiriwa kwa Qur'an. Siyo kwa maoni ya mfasiri - njia ambayo imekataliwa na Hadith mushuhuri ya Mtume(s.a.w.w) . Mwisho Allama Tabatabai anazifananisha na kuzieleza njia hizi tatu za tafsiri, kwa urefu. Kisha anasema, njia ya tatu ndiyo njia bora ya kuifahamu Qur'an kulingana na majadilano ya Qur'an na uthibitisho wa hadith. Mwisho wa sehemu hii ya mazungumzo anatuonyesha mfano na tafsiri ya Qur'an kwa Qur'an ambao hatuwezi kuonyesha hapa kwa ajili ya kufupisha. Al-Mizan inaonyesha jambo muhimu la kuzielewa sifa za miujiza ya Qur'an tukufu kufanana na kuingiliana kwa ya zake.

2. Upande Wa Kijamii:

Tafsiri zote za Qur'an kwa uchache ama kwa wingi zimejadili mambo muhimu kuhusu mazingira ya jamii, lakini Al-Mizan haina mfano ikifafanishwa na tafsiri myengine. Mijadala ya kuhusu jamii iliyomo katika Al-Mizan ina kina kikubwa sana cha thamani kwa wingi. Kwa namna alivyoitazama migawanyiko mingi na matatizo ya kijamii, Allama Tabatabai alifaulu kuyatatua kwa kutumia aya za Qur'an. Ametoa mwangaza mpya kuhusu baadhi ya matatizo hAya Na kijamii kwa maoni ya Qur'an, matatizo ambayo mpaka kufikia wakati huu yalikuwa yamepuuzwa. Allama Tabatabai amefungua ukumbi mpya kwa wasomaji walio na ari ya kuvumbua sehemu mpya katika maana ya Qur'an tukufu.

3. Upande Wa Falsafa:

Allama Tabatabai ambaye ni mwanafalsafa mwenye mwelekeo wa mustakbali na usanii nadra na wa asili, alifanya kazi kubwa katika elimu ya tafsiri, kufafanua ughaibu wa Qura'n, jambo ambalo linatupa uoni mkunjufu na wenye faida katika kufahamu bara bara maisha ya ughaibu Aliyakanusha makosa yote yasiyo na msingi yaliyotolewa katika Qur'an. Kwa maoni yake, ughaibu wa Uislamu una mizizi yake katika Qur'an, nayo ni ufafanuzi wa Qur'an kuhusu Mwenyezi Mungu, binadamu na ulimwengu. Allama Tabatabai vile vile anaonyesha kwamba ada ya kuogopa kuzungumzia mambo ya ughaibu (yasiyoonekana), inatokana na ukosefu wa kufahamu mambo hayo na kutokuwa na habari sahihi kuhusu mambo hayo.

Katika vitabu vyake kama vile Usul-e-Falsafa wa Rawish-e-Riyalism (Misingi ya falsafa na utaratibu wa madhehebu ya ukweli), maelezo juu ya kitabu kiitwacho Al-Asfar cha Mulla Sadra, katika makala mbili za (Bidayat, Al-Himah, na Nihayat, al-Hikmah), alieleza na kuyasawazisha makosa yote juu ya asili ya ughaibu. Katik Al-Mizan amezungumza masuala hAya Na a falsafa kadhaa za kifalsafa kutokana na aya hizo. Hili ni jambo ambalo halina mfano katika historia ya tafsiri ya Qur'an. Katika kutafsiri kwake aya za Qur'an na kuelezea uhusiano wake na fikra za ughaibu, alionyesha uthabiti wa Qur'an na vile vile kuonyesha upuuzi na ukosefu wa msingi wa falsafa ya mada. Sehemu hii ya tafsiri yake ni ya asili na vile vile ni mpya katika uwanja wa masomo ya falsafa. Mijadala yake hii ina undani wa maana ulio nadra, usahihi na ustadi ambao utaendelea kuwavutia wasomi katika siku za usoni.

Katika Juzuu Ama masomo mabili mbali ambayo yanazungumzwa kulingana na Sura ni

1. Mazungumzo kuhusu maumbile ya binadamu kutoka katika Qur'an.

2. Mazungumzo kuhusu viapo katika Qur'an orodha ya vitu ambavyo Mwenyezi Mungu anaapia katika kitabu kitukufu.

3. Mazungumzo kuhusu maana ya Roho (Ruh) katika Qur'an.

4. Mazungumzo kuhusu vipi malaika wanafanya kazi kama mawakili katika hali ya maisha.

Mwisho ni lazima nikiri kwamba maarifa yangu machache ambayo huenda yameathiri katika kufahamu undani wa na upana wa fikra za historia zilizomo katika Al-Mizan, yametia kasoro na dosari kubwa. Allah aiweke pema roho ya Allama Tabatabai kwa kazi yake kubwa aliyoifanya.

Abu-Al-Qasim Razzaqi

Kwa Wasomaji Sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyenipa uwezo wa kutafsiri tafsiri hii ya Qur'an iliyoandikwa na mwanachuoni mkubwa Bwana Muhammad Hussein Tabatabai. Ni lazima ieleweke kwamba haikuniwiya rahisi kazi hiyo hasa kwa kuzingatia undani na upana wa fikra za mwanachuoni huyo. Ugumu zaidi ulikuwa pale niliposhindwa kupata maneno ya Kiswahili yatakayotoa maana halisi yaliyokusudiwa jambo ambalo limenilazimisha kuacha baadhi ya ibara hasa zile za kanuni za lugha ya Kiarabu (Nahwu). Hata hivyo nimejitahidi kugusia kila ambacho ni muhimu katika tafsiri hiyo. Kwa vile tafsiri hii imeelezewa kwa undani sana na kwa njia ya kifalsafa, jambo ambalo pengine halikuzoeleka kwa vitabu vya dini vilivyoandikwa kwa Kiswahili, basi ndugu msomaji nawe itakubidi uisome kwa undani na wala sio kuipitia juu juu. Pengine itakubidi urudierudie baadhi ya ibara.

Ndugu msomaji ikiwa macho yako utayafungua kwenye makosa tu, na kuyafumba kwenye usawa na faida, basi ninakwambia Mungu akusamehe na aniongoze mimi na wewe. Hata hivyo sina maana ya kukukataza kunikosoa, bali ninakuomba hasa ufanye hivyo na Inshallah Mwenyezi Mungu atakulipa kwa nia yako. Kwani walikwishasema wahenga : "Binadamu si kamili". Shukrani: Shukrani zangu za dhati ziwaendedd London Islamic Foundation kwa kujitolea kuisimamia na kuigharimia kazi ya kukichapisha kitabu hiki. Pia shukrani nyingi zimwendee Sheikh Islam Khiyar Islam kwa taabu kubwa aliyoichukuwa ya kusahihisha kitabu hiki. Na wengineo ambao kwa namna moja au nyingine wamechangia kukitayarisha kitabu hiki; Mungu awajaze heri ya dunia na akhera (Amin).

Desemba 1988 Hassan Ali Mwalupa


1

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURAT NABA (HABARI)

SURAT NABA (HABARI) (NA. 78) INA AYA 40

Aya ya 1 -16

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ ﴿١﴾

1. Ni lipi wanaloulizana?

عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ ﴿٢﴾

2. Ni habari kubwa.

الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ ﴿٣﴾

3. Ambayo wao wanahitalifiana.

كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٤﴾

4. Si hivyo! Karibu watajua.

ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٥﴾

5. Tena si hivo! Karibu watajua.

أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا ﴿٦﴾

6. Jee, Hatukuifanya ardhi kuwa ni tandiko?

وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا ﴿٧﴾

7. Na majabali kuwa ni vigingi?

وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا ﴿٨﴾

8. Tukawaumba nyinyi wanawake na wanaume?

وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا ﴿٩﴾

9. Tukaufanya usingizi wenu ni raha?

وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا ﴿١٠﴾

10. Tukaufanya usiku ni sitara?

وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا ﴿١١﴾

11. Tukaufanya mchana ni (wa kutafutia maisha)?

وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا ﴿١٢﴾

12. Tukajenga juu yenu mbingu saba madhubuti?

وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا ﴿١٣﴾

13. Tukaufanya na taa yenye kung'aa?

وَأَنزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا ﴿١٤﴾

14. Tukateremsha kutoka mawinguni maji yenye kububujika?

لِّنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا ﴿١٥﴾

15. Ili kwayo, tutoe nafaka na mimea.

وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا ﴿١٦﴾

16. Na mabustani yenye kushindamana.

UBAINIFU

Sura inakusanya habari za kuja siku ya kupambanuliwa hukumu, na kuitolea hoja kwamba ni kweli, haina shaka. Imeanzia na kuuliza kwao habari yake; kisha ikataja katika mpangilio wa jawabu na kuogopesha kwamba wao watajua. Kisha imetoa hoja ya kuthibiti kwake, kwa kuonyesha nidhamu inayoonekana katika ulimwengu, kutokana na yaliyomo ndani yake, katika mipangilio ya kihekima, yenye dalili waziwazi, kwamba baada ya umbile hii lenye kubadilika na kuzunguuka, kuna umbile lenye kuthibiti na kubakia, na kwamba baada ya nyumba hii yenye kazi bila malipo, iko nyumba yenye malipo bila kazi basi iko siku itakayobainishwa nidhamu hii.

Kisha inasifu siku watakapo hudhirishwa watu, na kugeuka wale wanaopetuka mipaka kwenye adhabu chungu na wenye kumcha Mwenyezi Mungu kwenye neema za kudumu, na yanaishia maneno kwa kuonya. Sura imeshuka Makka kwa ushaidi wa mpangilio wa aya zake.

Aya Ya 1

Kuulizana hapa, ni kwa maana ya kuulizana baadhi yao kwa baadhi nyengine, au ni kuuliza baadhi yao baada ya wengine ijapokuwa mwenye kuulizwa ni mwengine, kwa hiyo ama walikuwa wakiulizana baadhi yao baada ya baadhi nyengine walikuwa wakimuuliza Mtume(s.a.w.w) kuhusu jambo. Ilivyokuwa mpangilio wa jawabu una maonyo zaidi na makamio, inatilia nguvu kuwa wenye kuulizana ni makafiri wa Makka katika wanaomshirikisha Mungu waliokanusha Utume na Marejeo. Kuulizana kwa wanaomshirikisha Mungu, na kukuelezea huko kuulizana kwao, kwa njia ya swali ni kufahamisha udhaifu wake, kwa kuwa jawabu la swali liko wazi.

Aya Ya 2-3

Makusudio ya habari kubwa ni habari ya ufufuo na Kiyama ambayo Qur'an imetilia umuhimu katika Sura zilizoshuka Makka, hasa zile sura zilizoshuka mwanzo mwanzo. Mpangilio huo unatilia nguvu kutokana na maelezo yake ya sifa za siku ya upambanuzi na hoja zilizotangulia kuwa siku hiyo ni kweli kutukia kwake. Imesemwa kuwa habari kubwa ni Qur'an tukufu.

Pia imsemwa habari kubwa ni vile walivyokuwa wakihitalifiana katika kuthibitisha mtengenezaji na sifa Zake, Malaika, Mitume, Ufufuo, Pepo na Moto n.k.

Anayesema haya amezingatia yaliyo katika Sura kuonyesha uhaki wa yote yaliyo katika mlingano wa Kiislamu. Yote hayo yanapingwa kutokana na kuwa ishara ya yote hato ni katika sharti za sifa ya siku ya ufufuo yenye kukusanya mafungu ya itikadi ya haki na amali njema, ukafiri na makosa. Zaidi ya hayo ni kuwa hawa wenye kuulizana ambao ni washirikina wanathibitisha mtengenezaji na Malaika na wanakanusha yaliyotajwa.

Kusema kwake "ambayo wanahitalifiana" Ni kwamba walihitalifiana katika upande wa kukataa, na wanaafikiana kuikanusha. Baadhi yao walikuwa wakiona kuwa ni muhali kama anayosema Mwenyezi Mungu: "Na walisema wale ambao wamekufuru (kuambiana wenyewe kwa wenyewe): "Je, tuwajulishe mtu anayewaambia ya kwamba mtakapochambuliwa vipande vipande (makaburini) kuwa atakuwa katika umbo jipya?! " (34:7)

Wengine walikuwa wakiiweka mbali na kuikanusha. Kama walivyosema: "Je, anawaahidi ya kwamba mtakapokufa na mkawa udongo na mifupa kuwa mtatolewa. Hayawi! Hayawi! Hayo mnayoahidiwa ." (23:35-36). Wengine walikuwa wakiitia shaka na kukanusha: anasema Mwenyezi Mungu: "Kwani imefikia wapi elimu yao (kujua) akhera (hata wanauliza Kiyama?) Bali wao wamo katika shaka nayo, bali wao ni vipofu nayo." (27:66) Na wengine walikuwa na yakini lakini hawaamini kwa inadi tu. Kwa hiyo wanakanusha, kama vile ambavyo hawaamini Tawhid, na Utume, baada ya kutimia hoja; Mwenyezi Mungu anasema: "Bali wao wanaendelea tu katika uasi na chuki ." (67:21)

Maana inayopatikana katika mpangilio wa aya tatu na zinazofuatia, ni kwamba wao waliposikia vile Qur'an inavyowaonya kuhusu jambo la ufufuo na malipo siku ya upambanuzi, waliliona zito hilo, ndipo wakawa wanaulizana kuhusu habari hii ya ajabu ambayo inagonga masikio yao mpaka leo. Walikuwa wakimrudia Mtume(s.a.w.w) na waumini, kuwauliza sifa ya hiyo siku, kwamba kitakuwa lini hicho kiaga mkiwa mnasema kweli? Na huenda walikuwa wakirudiana wao wenyewe katika baadhi ya waliyogonga masikio yao katika hakika za Qur'an. Ameishiria Mwenyezi Mungu katika Sura hii kisa cha kuulizana kwao kwa njia ya swali na jawabu, akasema: "Ni lipi wanaloulizana?" Kisha akasema: "Ni habari kubwa ambayo wao wanahitalifiana." Hilo ni jawabu na maelezo ya kile wanachoulizana. Kisha akasema: "so hivyo! Karibu watajua" na ni hilo ni jawabu la kuulizana kwao.

Wafasiri wana njia nyingi kuhusu tafsiri ya matamko ya aya hizo tatu; tumeziacha kwa kutoafikiana kwake na mpangilio. Yale tuliyoyaleta ndiyo yanayoafikiana na mpangilio wa maneno.

Aya Ya 4-5

Ni kupinga kuulizana kwao; yaani na wakome kuulizana, kwa sababu watafunukiwa kwa kutokea habari hii na wataijua. Katika ibara hii kuna utisho, kama ilivyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu: "Watajua wafanyao dhuluma ni mgeuko gani watakaogeuka " (26:227).

Kurudia tena maneno hayo katika aya ya (5) ni kutilia mkazo kukataza na utisho. Ufahamisho wa utisho ni kuonyesha kuwa wenye kuulizana ni washirikishaji wanaokanusha ufufuo na malipo, kinyume cha waumini na washirikishaji wengine.

Aya Ya 6

Kuanzia aya hii mpaka aya ya 11 ni mfumo wa kutoa hoja juu ya kuthibiti ufufuo na malipo na kuhakikika habari hii kubwa. Kuthibiti kwa habari hiyo kubwa kunalazimisha usahihi wa neno la Mwenyezi Mungu "Watajua" linaloelezea kwamba wao watashuhudia siku hiyo, hivyo watajua. Uthibitisho wa hoja ni kuwa ulimwengu huu tunaouona, pamoja na ardhi yake na mbingu yake, pia usiku wake na mchana wake, pamoja na watu wanaozaana, nidhamu yenye kupita katika hayo, mipangilio iliyotengenezwa kwa ustadi kabisa, ni muhali kuwa yote hayo ni mchezo usiokuwa na lengo lenye kuthibiti na kubakia. Kwa hiyo ni lazima kwa nidhamu hii yenye kugeuka geuka ifuatiwe na ulimwengu wenye nidhamu yenye kuthibiti na kubakia, ije na kubakia, ije idhihiri athari ya kutengemaa kunakopendelewa na maumbile ya mtu, na vile vile uje udhihiri ufisadi unao katazwa. Kwani katika ulimwengu wetu huu tunaouona, hakudhihiri wema wa wamchao Mwenyezi Mungu uovu wa mafisadi.

Ni uhali kwa Mwenyezi Mungu kutoa umbile linalolingania kufuata silika au kukataza kwenye jambo ambalo haliathari na wala lisitokee. Basi iko siku itakayomfikia mtu na kulipwa katika siku hiyo amali yake, ikiwa ni kheri na ikiwa shari ni shari. Aya hizi ziko katika maana ya aya zinazosema:

"Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake bure. Hiyo ni dhana ya wale waliokufuru. Basi adhabu kali ya moto itawathubutikia wale waliokufuru. Je tuwajaalie wale walioamini na kutenda mema kuwa sawa na wafanyao ufisadi katika ardhi? Au tuwajalie wacha Mungu kuwa sawa na waovu? " (38:27-28).

Kwa ubainifu huu inathibiti kwamba iko siku ya malipo. Kwa hiyo hakuna haja kwa wanaomshirikisha Mungu kuhitalifiana na kutiliana shaka, ikiwa kundi jengine linaona ni muhali, jengine haliamini kwa inadi. Basi siku hiyo ni lazima kutokea na malipo, hakuna shaka. Baadhi wamesema kuwa aya hizi ziko katika mfumo wa kuthibitisha uwezo na kwamba marejeo yanaanzia mwanzo; Mwenye kuweza kuanzisha pia anaweza kurejesha. Hoja hiyo ingawaje ni kamilifu na imetokea katika maneno yake Mwenyezi Mungu, lakini ni hoja ya kueleza uwezekano na sio kutukia. Na mfumo tulionao sisi ni mfumo wa kutokea hasa na wala sio kuwezekana. Hivyo yenye kunasibiana zaidi ni yale tuliyoyatanguliza kuyafafanua.

Vyovyote iwavyo maana ya aya ya (6) ni kuwa: tumefanya ardhi ni kituo chenu cha kutulia na kuitumia.

Aya Ya 7

Huenda yamehisabiwa majabali kuwa ni vigingi kutokana na kuwa majabali yanatokana na kazi ya volcano. Kwa kupasuka ardhi, na kutoka vitu katika ardhi vilivyoyeyuka vinasimama kwa kulundikana kwenye mdomo wa shimo lililopasuka kama kigingi kilichosimamishwa. Chini yake kunakuwa na mchemko wa volcano ambao unanyanyua sehemu ya ardhi kutokana na kutetemeka. Baahi wamesema kwamba makusudio ni kujaalia vigingi ni nidhamu ya masiha ya watu duniani kutokana na manufaa yake na lau si hayo majabali, basi ardhi ingeliwayumbisha yumbisha yaani wasingeliweza kunufaika. Laikini kuiacha dhahiri ya tamko bila dharura hakufai.

Aya Ya 8

Yaani tumewaumba mume na mke ili kizazi kiendelee mpaka atakapotaka Mwenyezi Mungu.

Imesemwa kuwa makusudio yake ni maumbile yaani kila mtu ana umbile la mwenzake.

Pia imsemwa ni aina tofauti, kama weupe, weusi, wekundu, njano n.k. Vile vile imesemwa kuwa ni kuumbwa kwa manii ya aina mbili (ya mume na mke). Hizi ni njia dhaifu.

Aya Ya 9

Kuwa usingizi ni raha ni kwa kuwa unatuliza kiwiwili baada ya kuwa macho katika kutaabika kupitia matumizi ya nafsi. Imsemwa kuwa maana ya "Subata" ni kukata, kwamba usingizi unakata matumizi ya nafsi katika mwili. Maana hiyo iko karibu kuliko iliyotangulia. Imesemwa ni mauti na Mwenyezi Mungu amehisabu usingizi kuwa ni mauti aliposema: "Naye ndiye anayewafisha wakati wa usiku ." (6:60).

Lakini kauli hii iko mbali na maana ya aya hii, imehisabu usingizi kwa kuchukua roho lakini haikuuhisabu usingizi ni mauti kama inavyofafanua Qur'an sehemu nyengine: "Allah huchukua roho wakati wa mauti yake na zile ambazo hazijakufa (pia anazichukua) katika usingizi wake ." (39:42).

Aya Ya 10

Yaani unasitiri. Kutokana na giza lake, na hii ni sababu ya Mungu ya kuwataka watu wa ache harakati zao usiku na kuelekea nyumbani kwa watu wao. Baadhi wamesema makusudio ya kuwa usiku ni sitara nikuwa unasitiri mchana. Na kauli hayo ni kama unavyoina.

Aya Ya 11

Neno maisha linahusika na maisha ya wanyama; haiwezekani kusema maisha ya Mungu au ya Malaika. Maana ya aya nikuwa tumeufanya mchana ni wakati wa kutafuta maisha, kutafuta fadhila kutoka mola wenu.

Aya Ya 12:

Yaani mbingu saba zilizo madhubuti katika mjengo wake.

Aya Ya 13:

Makusudio ya taa yenye kuang'aa ni jua.

Aya Ya 14

Maana ya neno Mu'usirat ni mawingu ya mvua. Imesemwa ni pepo ambazo zinakamua mawingu ili inyeshe mvua.

Aya Ya 15

Nafaka hizo na mimea ni kwa ajili ya chakula cha binadamu na wanyama wengine.

Aya Ya 16

Inaungana na aya iliyotangulia. Kushindana ni kushindana kwa miti.

Utafiti Wa Hadith Katika baadhi ya habari zilizokuja ni kwamba habari kubwa ni Ali(a.s) . Katika Nahjul-Balagha, amesema Ali(a.s) : "Na ameuzuia mtingishiko wa ardhi yake kwa kupiga vigingi kwa majabali ."

Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu aya ya (10) amsema: Usiku unausitiri mcha. Huenda makusudio ya hadithi hiyo ni kuficha yanayodhihiri mchana.


2

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURAT NABA' (HABARI)

SURAT NABA' (HABARI)(NA. 78)

Aya 17 - 40

17. Hakika siku ya upambanuzi imewekewa wakati maalum.

إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا ﴿١٧﴾

18. Siku itakayopulizwa parapanda, mje makundi makundi.

يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا ﴿١٨﴾

19. Na mbingu zifunguliwe, ziwe milango.

وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا ﴿١٩﴾

20. Yaondolewe majabali yawe mlenge.

وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا ﴿٢٠﴾

21. Hakika Jahannam ni malindilizo.

إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا ﴿٢١﴾

22. Ni marejeo kwa wenye kupetuka mipaka.

لِّلطَّاغِينَ مَآبًا ﴿٢٢﴾

23. Watakaa humo karne nyingi.

لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا ﴿٢٣﴾

24. Hawataonja humo raha wala kinywaji.

لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا ﴿٢٤﴾

25. Isipokuwa maji ya moto na usaha.

إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا ﴿٢٥﴾

26. Malipo yalitosawa (na makosa yao).

جَزَاءً وِفَاقًا ﴿٢٦﴾

27. Kwa sababu wao walikuwa hawaogopi kuhesabiwa.

إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا ﴿٢٧﴾

28. Wakazikadhibisha sana aya zetu.

وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا ﴿٢٨﴾

29. Na kila kitu tumekidhibiti kwa kukiandika.

وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا ﴿٢٩﴾

30. Basi onjeni, hatutawazidishia ila adhabu.

فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا ﴿٣٠﴾

31. Hakika wanaomcha Allah wana mahali pa kufuzu.

إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا ﴿٣١﴾

32. (Wana) mabustani na mizabibu.

حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا ﴿٣٢﴾

33. Na wasichana walio marika.

وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا ﴿٣٣﴾ وَكَأْسًا دِهَاقًا ﴿٣٤﴾

34. Na vikombe vilivyojaa.

لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا ﴿٣٥﴾

35. Hawatasikia humo upuuzi wala kukadhibishana.

جَزَاءً مِّن رَّبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا ﴿٣٦﴾

36. Wamelipwa na Mola wako kipawa chenye kutosha.

رَّبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرَّحْمَـٰنِ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا ﴿٣٧﴾

37. Bwana wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake, Mwingi wa Rehema Ambaye hawataweza (siku hiyo) kusema naye.

يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّا لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا ﴿٣٨﴾

38. Siku ambayo atasimama roho na Malaika, wamepiga safu hawatazungumza ila aliyepewa ruhusa na (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa Rehema na akasema yaliyosawa.

ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ مَآبًا ﴿٣٩ ﴾

39. Hiyo ndiyo siku ya haki. Basi anayetaka naashike njia ya kurejelea kwa Mola wake.

إِنَّا أَنذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَا لَيْتَنِي كُنتُ تُرَابًا ﴿٤٠﴾

40. Hakika sisi tunawaonya nyinyi adhabu iliyo karibu. Siku ambayo mtu ataona kilichotangulizwa na mikono yake, na kafiri atasema: laiti ningelikuwa mchanga.

UBAINIFU

Aya zinasifu siku ya upambanuzi ambayo imetolewa habari kwa ujumla na aya ya 4. Kisha inasifu yale yatakayowapitia wanaopetuka mipaka na wanaomcha Mwenyezi Mungu. Mwisho Sura inamalizia kwa tamko la kuonya, na hilo ndilo kama natija.

Aya Ya 17

Ni kuingilia kusifu yale yanayokusanywa na habari kubwa ambayo imetolewa utisho katika aya ya 4; Kisha Mwenyezi Mungu akasimamisha hoja juu ya hayo kuanzia aya ya 6 na kuendelea. Mwenyezi Mungu ameiita siku hiyo siku ya upambanuzi na akaielezea kuwa ni siku ya kupambanuliwa hukumu. Kuleta ibara ya tamko "kanat" ni dalili ya kuthibiti kwake na kubainishwa kwake katika ujuzi wa Mungu kutokana na hoja iliyotangulia kutajwa. Maana yake hakika siku ya upambanuzi wa hukumu ambayo habari yake ni kubwa, imekua katika ujuzi wa Mwenyezi Mungu tangu siku aliyoumba mbingu na ardhi na akapitisha katika siku hiyo nidhamu. Yeye Mwenyezi Mungu alikuwa anajua kwamba umbile hili aliloliumba haliwezi kutimia bila ya kukomea kwenye siku ya kupambanuliwa hukumu.

Aya Ya 18

Yamekwisha tangulia maelezo kuhusu maana ya kupuziwa parapanda. Maneno yamekuja kwa njia ya kuambiwa watu kwa kuelezea haki ya kiaga. Kama kwamba aya iko katika mwelekeo wa aya inayosema: "Siku tutakapowaita kila watu pamoja na kiongozi wao ." (17:71)

Aya Ya 19

Utaungana ulimwengu wa watu na ulimwengu wa Malaika. Imesemwa kuwa kukadiria kwake ni: 'zikawa zenye milango.' Na imesemwa ni njia katika hizo mbingu. Lakini njia zote hizo mbili haziepukani na kuangaliwa vizuri.

Aya Ya 20

Kuondolewa majabali na kugongwa kunaishia kwenye kutawanyika vipande na kuondoka umbo lake kama ilivyotokea katika maneno yake Mwenyezi Mungu wakati wa kusifu tetemeko la Kiyama na athari yale alopisema: "Na majabali (yang'oke) yawe yanakwenda mwendo (mkubwa) " (52:10).

Na amesema: "Na ikaondolewa ardhi na majabali ikavunjwa mvunjo mmoja ." (69:14).

Amesema tena "Na majabali ya kawa kama sufi iliyopurwa ." (101:5).

Na amesema: "Na majabali yakasagwasagwa " (56:5).

Amesema: "Na pindi majabali yatakaposagwasagwa ." (77:10).

Ndio kunaishilia kusagwasagwa kwake kwenye kukosekana na kupotea kabisa umbo lake. Majabali yaliyokuwa yamekita kabisa yaliyokuwa yakionekana na nguvu yasiyoweza kutingishwa na kimbunga, leo yana pondwapondwa na kupotea. Aya hii iko katika mwelekeo wa aya inayosema: "Na unayaona majabali unayadhania yametulia, nayo yanakwenda kama mawingu ." (27:88). Yaani hiyo siku ya mtetemeko wa Kiyama.

Aya Ya 21

Mwenyezi Mungu ameita Jahannam ni malindilizo kwa kuwa watu wataipitia. Mwenyezi Mungu anasema: "Wala hakuna yoyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia (hiyo Jahannam) " (19:71).

Aya Ya 22

Kuihisabu Jahannam ni marejeo, ni kwamba wao walijiandalia wenyewe marejeo walipokuwa duniani. Kisha waliachana na dunia na kurejea.

Aya Ya 23

Maana ya neno Ahqab ni muda mrefu usio na kikomo. Wamehitalifiana kuhusu neno hilo. Baadhi yao wamesema ni miaka 80 au miaka 80 na kitu. Wengine wakaongezea kusema kwamba mwaka katika hiyo Ahqab una siku 360 na kila siku inalingana na miaka elfu. Wengine wamesema ni miaka 40 na wengine wamesema ni miaka 70,000. Wala hakuna dalili yoyote kutoka katika Qur'an inayofahamisha juu ya viwango hivi, wala haikuthibiti katika lugha. Ukweliulivyo ni kuwa neno "Ahqab" ni muda wa wakati usiojulikana.

Kwa dhahiri ni kwamba makusudio ya waliopetuka mipaka ni wale waliofanya inadi katika makafiri.

Hayo yanatiliwa nguvu na aya ya (27) ya Sura hii inayosema; "Kwa sababu wao walikuwa hawachi kuhesabiwa ."

Imesemwa kuwa aya zinazofuatia ni sifa ya hilo neno (Ahqab) maana yake ni kuwa watakaa humo karne nyingi katika sifa hizi nazo nikuwa wao hawataonja raha wala kinywaji isipokuwa maji ya moto na usaha, kisha watakuwa kwenye sifa nyengine kwa muda usiokuwa na kikomo. Kauli hii ni nzuri kama ingelisaidiwa na mpangilio wa maneno.

Aya Ya 24-25

Zinaelezea hali watakayokuwa nayo ndani ya Jahannam.

Aya Ya 26

Ni dalili ya kuwafikiana kwenye kutimia kati ya malipo na amali. Mtu kwa amali yake anataka malipo yaliyo sawa na kazi yake. Mwenyezi Mungu amesema: "Enyi mliokufuru msitowe udhuru leo; Hakika mnapewa malipo ya yale mliyokuwa mkiyatenda ." (66:7).

Aya Ya 27 – 28

Ni sababu ya kufafanua muwafaka wa malipo yao kwa amali yao. Kwamba wao hawakutarajia kuhisabu siku ya upambanuzi wakaona kuwa hakuna maisha ya akhera, wakazikadhibisha aya zinazofahamisha hayo wakakanusha Tawhid na Utume na wakaakiuka kuwa wenyewenyekevu katika amali zao, hivyo wakamsahau Mwenyezi Mungu naye amewasahau na kuwanyima wema wa nyumba ya akhera. Kwa hiyo hawakubakiwa na chochote isipokuwa machukivu na ndio kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Basi onjeni! Hatutawazidishia ila adhabu ".

Aya hii ya (27) ni dalili ya kuafikiana kwenye kutimia kati ya malipo na amali. Mtu hutaka malipo kwa amali yake aliyoifanya. Anasema Mwenyezi Mungu katika aya ya 30 ya Sura hii: "Enyi mliokufuru! Msilete udhuru leo; Hakika mnapewa malipo ya yale mliyokuwa mkiyatenda ." (66:7).

Aya Ya 29

Yaani kila kitu tumekidhibiti na tukakibainisha katika kitabu. Aya hii iko katika mwelekeko wa aya inayosema: "Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari linalobainisha ." (36:12)

Au makusudio yake ni kuwa na kila kitu tumekihifadhi hali ya kuwa ni chenye kuandikwa katika "Lawh Mahfudh" (ubao wenye kuhifadhiwa) au katika karatasi za amali. Na wamejuzisha kuwa maana ya neno "Ihsau" ni kuandika, maana yake itakuwa na kila kitu tumekiandika kitabuni. Kwa vyovyote vile makusudio ya aya ni kutoa sababu ya yaliyotangulia; maana yake; malipo ni yenye kuwafikiana na amali zao, kwa sababu wao walikuwa kwenye hali kadha wa kadha na tumezihifadhi, kwa hiyo tumewalipa malipo yenye kiafiki.

Aya Ya 30

Ni mtiririko wa yaliyotangulia unaoelezea kuwakatisha tamaa ya kutarajia kuokoka. Kuwasemesha kwa kutumia neno "Basi onjeni" ni kwa kutahayariza; Makusudio ya kuwaambia "Basi onjeni hatutawazidishia ila adhabu" ni kuwa mnayoyaonja baada ya adhabu ni adhabu nyengine, hiyo ni adhabu baada ya adhabu na adhabu juu ya adhabu, hamtaepukana na kuongozewa adhabu mpya kwenye ile adhabu ya zamani, basi kateni tamaa katika mnayoyataka na mnayoyapenda. Aya hii haiepukani na kudhihiri kuwa makusudio ya aya 30 ni kukaa milele bila kikomo.

Aya Ya 31-35

Zinaelezea kufuzu kwa wale wamchao Mwenyezi Mungu kwa kupata heri na salama.

Aya Ya 36

Yaani wamefanyiwa wale wanaomcha Mwenyezi Mungu yake waliyofanyiwa hali ya kuwa ni malipo kutoka kwa Mola wako na kipawa chenye kuhisabiwa. Imesemwa kuwa kutegemezwa neno malipo kwa Mola kisha kwa Mtume ni kwa ajili ya kuyatukuza na halikutegemezwa kwa Mwenyezi Mungu neno malipo ya wenye kupetuka mipaka, kwa ajili ya kumtakaza nayo Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani shari yao iliyowapata imetokana na wao wenyewe. Mwenyezi Mungu anasema: "Hayo ni kwa sababu ya yale yaliyofanywa na mikono yenu. Na hakika Allah si mwenye kuwadhulumu waja ". (8:51)

Kutokea tamko la hisabu katika mwisho wa malipo ya wenye kupetuka mipaka na wenye kumcha pamoja ni kuthibitisha yale yanayoishiriwa na siku ya upambanuzi yaliyotokea mwanzo wa maneno.

Aya Ya 37

Ni ubainifu wa neno "Mola wako" inakusudiwa kuwa ubwana wake Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni wenye kuenea kwa kila kitu na kwamba Mola ambaye Mtume anamfanya kuwa Bwana na kulingania watu kwake, ni Mola wa kila kitu sio kama walivyokuwa wakisema washirikina kwamba kila taifa lina Mola na Mwenyezi Mungu ndiye Bwana wa mabwana, au kama walivyokuwa wakisema wengine kwamba Yeye ni Mola wa mbingu. Kumsifu Mola kwa kuwa "Mwingi wa Rehema" ni kuonyesha kuenea rehema yake na kwamba hiyo ni alama ya uungu wake hakizuilii chochote na kupata rehema hiyo isipokuwa mtu kujizuilia mwenyewe kwa kuzembea kwake na ubaya wa uchaguzi wake. Na katika uovu wa hao waliopetuka mipaka ni kwamba wao wamejinyima hiyo rehema kwa kutoka katika hali ya unyenyekevu.

Kuhusu "ambaye hawataweza (siku hiyo) kusema naye" kutokana na kuanza aya na "Bwana wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake Mwingi wa Rehema" ni dalili kwamba makusudio ya hawataweza kusema naye ni kumsemesha katika baadhi ya aliyo yafanya kwa njia ya swali kama kusema: kwa nini umefanya hayo? Na kwa nini hukufanya. Kwa hiyo jumla "hawataweza kusema naye" inakuwa katika maana ya neno lake Mwenyezi Mungu: "Haulizwi (Mwenyezi Mungu) anayoyafanya, lakini wao (viumbe) wataulizwa .." (21:23)

Lakini aya inayofuatia baada ya jumla hii inaonyesha kuhusika na Malaika yaani hao Malaika hawatasema na Mwenyezi Mungu katika atakavyopitisha kwa kumwingilia au kuwaombea kama alvyosema Mwenyezi Mungu: "kabla ya haijafika siku ambayo hapatakuwa kujikomboa wala urafiki (wa kusaidiana) wala uombezi ." (2:254)

Aya Ya 38

Makusudio ya roho ni kiumbe kinachohusikana na Mwenyezi Mungu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "sema roho ni jambo linalohusika na Mola wangu ". (17:85)

Imesemwa kuwa ni mtukufu wa Malaika. Imesemwa ni Malaika mwenye kuchukua roho, lakini hakuna dalili juu ya kauli hizi. Imesemwa makusudio ni Jibril, imesemwa ni roho za wanaadamu na kusimama kwao pamoja na Malaika. Katika wakati ulio kati ya mipuzio miwili ya parapanda kabla ya kuingia roho katika viwiliwili hali ya kupiga safu. Na imesemwa ni Qur'an na makusudio ya kusimama kwake ni kudhihiri athari yake siku hiyo katika wema wa waumini na uovu wa makafiri.

Lakini hizi kauli tatu zinapingwa, kwamba ingawaje ametumia Mwenyezi Mungu neno roho katika kila moja yao lakini ni pamoja na kuifunga (kuihusisha) na kitu chengine. Kama katika kauli yake: "Na kumpulizia roho inayotokana na mimi ." (15:29).

Na kauli yake: "Ameyateremsha hayo roho (Jibril) mwaminifu"

(26:193). Na kusema kwake: "....Na tukampelekea roho wetu ." (19:17).

Na kauli yake: "Sema ameiteremsha roho mtakatifu ." (Jibril) (16:102).

Na kauli yake:

"Namna hivi tumekufunulia (Qur'an) kwa roho atokaye kwetu ". (42:52) Kusema kwake "Hawatasema" ni ubainifu wa neno "ambaye hawataweza kusema haya". Dhamiri ni ya kundi lote la roho, Malaika, Watu na Majini kutokana na unavyofahamisha mpangilio wa maneno. Imesemwa dhamiri ni ya roho na Malaika. Na imesemwa ni ya watu lakini kutokea neno hawataweza na hawatasema katika muundo mmoja hakuafikiani na kauli hizo mbili.

Kusema kwake "Ila aliyepewa ruhusa na Allah, Mwingi wa Rehema" ni yule atakayeweza kusema. Jumla hiyo iko katika maana ya kauli yake: "wakati itakapokuja (siku hiyo) kiumbe chochote hakitasema ila kwa ruhusa yake (Mwenyezi Mungu)". (11:105).

Kusema kwake "Na akasema yaliyo sawa " yaani ni neno lililosawa lisiloingiliwa na kosa, ni haki isiyoingiliwa na batili. Kwa hakika jumla ni kuifunga idhini na haki, ni kama vile imesemwa 'wala hatapewa idhini isipokuwa yule atakayesema yaliyosawa." Kwa hiyo aya iko katika maana ya aya inayosema: "Wala hawana uwezo wa uombezi wale wanaowaomba badala yake ila wale wanaokiri (hii) haki, wakaijuwa ." (43:86).

Kuhusu Roho Katika Qur'an Limekaririka tamko la roho katika maneno ya Mwenyezi Mungu, na maana inayofahamika haraka ni kitu ambacho no msingi wa uhai. Na Mwenyezi Mungu hakulitumia neno hili kwa mtu au kwa mtu na mnyama pekee, bali amelithibitisha sehemu nyengine; kama katika kauli yake "na tukampelekea Mariam roho wetu.. " (19:17).

Na kusema kwake: Namna hivi tumekufunulia (Qur'an) kwa roho atokaye kwetu." (42:52) Kwa hiyo roho ina uthibitisho kwa mtu na penginepo, kauli inayoweza kuielezea roho zaidi ni ile ya Mwenyezi Mungu isemayo "Na wanakuuliza habari ya roho. Sema roho ni amri ya Mola wangu". Na ameielezea amri kwa kusema kwake: "Hakika amri yake anapotaka chochote ni kukiambia kuwa kikawa. Ametutuka yule ambaye mkononi mwake umo ufalme wa kila kitu, na kwake mtarejezwa nyote ." (36:82-83)

Kwa hiyo amebainisha kwamba hiyo roho ni tamko linalofanya kitu kipatikane; hii ikimaanisha kwamba hilo tamko ndiyo kupatikana (kwa kitu) kwa vile kunavyonasibiana na Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anavyosifika na kupatikana huko, na siyo huko kupatikana kunavyonasibiana na ila au sababu za nje. Kwa makusudio haya amemuhisabu Masihi (AS) kuwa ni tamko na roho kutoka kwake aliposema: "Na tamko lake alilompelekea Mariam. Na ni roho iliyotoka kwake ." (4:171).

Hapo ni wakati alipompa Mariam, Isa (AS) kwa njia isiyokuwa ya kawaida. Inakurubia katika makusudio hayo kauli yake Mwenyezi Mungu: "Hakika mfano wa Isa kwa Allah ni kama mfano wa Adam alimuumba kwa udongo, kisha akamwambia kuwa, basi akawa ". (3:59).

Na Yeye Mwenyezi Mungu ingawaje aghlabu ameitaja hiyo roho kwa kutegemeza au kwa kuifunga na kitu; kama kauli yake "na kumpulizia roho inayotoka na mimi " (15:29).

Na kauli yake: "na akampulizia roho yake " ( 32:9). Na kauli yake:

"na tukamplelekea roho wetu ." (19:17).

"Na ni roho kutoka kwake.. " (4:17)

"Na tukamtia nguvu kwa roho mtakatifu . " (2:87).

Na mengineyo, lakini pia yamekuja baadhi ya maneno yake kwa kutaja roho bila ya kuitegemeza au kuifunga na chochote. Kama kauli yake; "Hushuka Malaika na roho katika Lailatul-Qadri kwa amri ya Mola wao kwa ajili ya kila jambo ". (97:4).

Dhahiri ya aya hiyo ni kwamba roho hapo ni kiumbe kingine cha mbinguni ambacho ni Malaika. Aya hiyo iko katika mwelekeo wa kauli yake: "Malaika na roho hupanda kwake katika siku ambayo muda wake ni miaka elfu hamsini " (70:4). Ama roho yenye kufungamana na binadamu ameitolea taabiri Mwenyezi Mungu kwa mfano wa kauli yake: "Na kumpulizia roho inayotokana na mimi ." (15:29).

Na "na akampulizia roho inayotoka kwake ." (32:9) Na ameleta neno "Min" lenye kufahamisha umwanzo. Na kitendo cha kuleta "umwanzo" akakiita kuwa ni "kupulizia'. Ametaja roho aliyowahusisha waumini kwa mfano wa kauli yake " na akawatia nguvu kwa roho itokayo kwake." (58:22).

Ameleta herufi "Ba" katika aya hiyo yenye kufahamisha sababu na akakiita kitendo hicho 'kutia nguvu'. Ametaja roho aliyowahusisha mitume katika mfano wa kauli yake "na tukamtia nguvu kwa roho mtakatifu" (2:87).

Kwa hiyo akaongezea utakatifu, pia ametaja kuwa ni kutia nguvu.

Kwa kuzikusanya aya hizi pamoja na mfano wa aya, iliyoko katika Sura ya Qadr inadhihiri kwamba mnasaba kati ya roho yenye kutegemezwa kitu ambayo iko katika aya hizi, na roho ambayo haikusasibishiwa chochote ni kama kunavyonasibishwa kumimina na mmiminaji au kivuli na chenye kuleta kivuli. Vinaponasibishiwa na idhini ya Mwenyezi Mungu.

Vile vile roho yenye kufungamana na Malaika, isipokuwa ni kwamba hakusema katika roho ya Malaika kwa kupuzia na kutia nguvu, kama alivyosema kwa binadamu bali ameita roho tu kama katika kauli yake: "Na tukampelekea roho wetu." (19:17). Na kusema kwake: "Sema ameiteremsha roho mtakatifu " (16:102). Kwa sababu Malaika ni roho pekee, kulingana na kuhitalifiana daraja zao katika ukaribu na umbali na Mola wao. Wanavyoonekana na viwiliwili ni kwa kujifananisha tu; kama linavyoonyesha neno lake: "Na tukampelekea roho wetu akajifananisha kwake na (sura ya) binadamu aliye kamili ". (19:17). Kwa sababu hiyo hawakuambiwa roho zao 'zimepuliziwa' tofauti na binadamu ambaye ana sehemu ya kiwiliwili ambacho ni maiti na roho ambayo iko hai, huyu inanasibu kusema amepuliziwa; kama anavyosema Mwenyezi Mungu: "Nikishamkamilisha na kumpulizia roho yangu, angukeni mumsujudie." (15:29).

Kama ambavyo umbile la roho ya mwanadamu ni tofauti na ile ya Malaika, kwa vile katika mwanadamu kuna'kupulizia' na katika Malaika hakuna, hivyo ndivyo tofauti kati ya roho inavyopatikana. Tofauti ya maisha ya roho kuwa mazuri au mabaya, imeleta tofauti katika kuielezea roho inayohusika. Hivyo ndivyo 'kutiwa nguvu' kwa Malaika, na waumini. Miongoni mwa roho, ni roho zenye kupuliziwa kwa mtu anasema "nikapuzia roho itokayo kwangu ". (15:29).

Na roho zenye 'kutiliwa nguvu' ni roho za waumin. Mwenyezi Mungu anasema: "Hao ndio ambao (Mwenyezi Mungu) ameandika nyoyoni mwao imani na akawatia nguvu kwa roho itokayo kwake " (58:22).

Hiyo ni daraja ya juu zaidi katika roho za kibinadamu kama inavyoelezea kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) ambayo iko katika maana ya aya hii tuliyoitaja sasa hivi: "Je aliyekuwa maiti kisha tukamfufua na tukamjaalia nuru, kwa nuru hiyo hutembea mbele za watu, atakuwa sawa na yule ambaye hali yake yuko gizani asiweze kutoka humo ". (6:122).

Kwa hiyo amemuhisabu muumin ni hai mwenye nuru anayotembea kwa nuru hiyo, ni athari ya roho. Na kafiri amemuhisabu kuwa maiti naye ni mwenye roho ya kupuliziwa.

Kwa hiyo inadhihiri kwamba daraja za roho kuna zile zilizo katika mimea kutokana na athari ya uhai. Zinazofahamisha hilo ni aya zenye madhumuni ya kuihuyisha ardhi baada ya kufa. Miongoni mwa aina za roho ni zile wanazotiliwa nguvu mitume nazo. Ama kauli yake: "Hupeleka roho kwa amri yake kwa amtakaye miongoni mwa waja wake, ili kuwaonya siku ya kukutana (naye)" (40:15) Na kauli yake: "Namna hii tumekufunulia roho kwa amri yetu ". (42:52).

Inawezekana kuwa roho zinazozungumziwa katika aya mbili hizo, ni roho ya Imani au roho mtakatifu (Jibril).

Aya Ya 39

Ni ishara ya hiyo siku ya upambanuzi. Kuishiria kwa ishara ya mbali ni kuonyesha uzito wake. Kauli yake "Basi anayetaka naashike njia ya kurejelea kwa Mola wake." ni mtiririko wa habari za siku ya upambanuzi maana yake mwenye kutaka kurudi kwa Mola wake na arudi.

Aya Ya 40

Makusudio ya adhabu hapa ni adhabu ya akhera na kusema iliyokaribu ni kwa kuwa ni kweli hapana shaka kuileta, na kila linalokuja liko karibu. Kuhusu ambacho kimetangulizwa na mikono yake ni amali yake aliyoifanya mwenyewe. Mwenyezi Mungu anasema: "Siku ambayo itakuta kila nafsi mema iliyoyafanya yamehudhurishwa na pia ubaya ulioufanya ". (3:30). Kusema kafiri laiti ningelikuwa mchanga yaani atatamani hivyo kutokana na shida ya siku hiyo kwamba yeye lau angelikuwa kitu kisichokuwa na hisiya yoyote.

Utafiti Wa Hadith Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu aya ya (19) amesema: "Itafunguliwa milango ya peponi " na kuhusu aya ya (20) anasema: yatakwenda majabali mfano wa mlenge ambao unametameta katika jangwa. Katika hiyo hiyo Tafsiri ya Qummi kuhusu aya ya (23) amesema neno "Ahqab" ni miaka na mwaka una siku 360 na siku moja huko ni kama miaka elfu mnayoihisabu. Katika Majmau amepokea Nafi'i kutoka kwa Ibn Umar amesema: amesema Mtume(s.a.w.w) 'Hatatoka motoni mpaka akae humo kitambo cha Huqb nyingi na Huqb moja ni miaka 60 na kitu na mwaka mmoja ni siku 360, kila siku ni kama miaka elfu mnavyohisabu kwa hiyo asitegemee yoyote kutoka katika moto. Riwaya kama hiyo imekuja katika Durril Manthur na imepokewa vile vile riwaya nyengine kutoka kwake(s.a.w.w) kwamba "Huqb" ni miaka 40. Katika hiyo hiyo amepokea Iyashi kwa isnadi yake kutoka kwa Hamran amesema: 'Nilimwuliza Abu Jaffar(a.s) kuhusu aya hii akasema: "Aya hii inawahusu ambao watatoka motoni ."

Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu aya (31) amesema: "Watafuzu ". Na aya (33) ni wake wa watu wa peponi. Katika riwaya ya Abul Jarud kutoka kwa Abu Jaffar(a.s) kuhusu aya (31) amesema ni utukufu. Na aya (33) amesema ni wasichana wenye matiti yaliyosimama. Katika Durril Manthur ametoa Ibn Abu Hatim, Abush Shaykh katika Adhama na Ibn Murdawayh kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtume(s.a.w.w) amesema: "Roho ni askari katika askari wa Mungu sio Malaika wana vichwa, mikono na miguu, kisha akasema "Siku atakayosimama Roho na Malaika wamepiga safu akasema: Hao ni askari na hao ni askari ." Imekwisha tangulia riwaya katika aya zinazoelezea roho kutoka kwa Maimamu(a.s) .

Ndio katika riwaya ya Qummi aliyoipokea kutoka kwa Himran ni kwamba Roho ni malaika mkubwa kuliko Jibril na Mikail na alikuwa pamoja na Mtume(s.a.w.w) na yuko pamoja na Maimamu(a.s) . Huenda makusudio ya Malaika ni kwa vile yuko mbinguni au hizo ni dhawa za wapokezi wa hadith katika kunakili maana wala hakuna hali ya kufahamisha kuwa kila kinachopatikana mbinguni ni malaika bali iko dalili ya kinyume cha hilo kama inavyofahamisha kauli yale Mwenyezi Mungu: "Ewe Ibilisi! Kipi kilichokuzuia kumsujudia yule niliyemuumba kwa mikono yangu? Je, umetakabari au umo miongoni mwa wakubwa ". (38:75).

Katika Usul-Kafi kwa isnadi yake kutoka kwa Muhammad bin Al-Fadhil naye kutoka kwa Abul Hassan(a.s) amesema: Nilisoma aya; "Siku ambayo atasimama Roho na Malaika, wamepiga safuu hawatazungumza ila aliyepewa ruhusa na (Allah) Mwingi wa Rehema na akasema yaliyosawa ." Niliposoma aya hiyo akasema: "Wallah sisi ndio tutakaopewa idhini siku ya Kiyama na ndio wenye kusema yaliyosawa ." Nikasema : "Mtasema nini? " Akasema: "Tutamsifu Mwenyezi Mungu na kumswalia Mtume wetu na kuwaombea wafuasi wetu wala hataturudisha Mola wetu ".

Katika Majmau imepokewa hadith hiyo Iyash ikiwa Marfua kutoka kwa Muawiya bin Ammar naye kutoka kwa Abu Abdillah(a.s) . Riwaya hii ni kwa upande wa kuelezea baadhi ya mambo yanayosadikiwa, kwani wako waombezi wengine, katika malaika, mitume na waumini watapewa idhini katika kuzungumza. Na wako mashaidi wa uma watakaopewa idhini ya kuzungumza; kama inavyoeleza Qur'an na hadith.


3

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURAT NAAZIA'AT (KUTOA KWA NGUVU)

SURA NAAZIA'AT (KUTOA KWA NGUVU) (NA. 79 )

INA AYA 46

Aya 1 - 41

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا ﴿١﴾

1. Naapa kwa (Malaika) wanaotoa roho (Kwa nguvu).

وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا ﴿٢﴾

2. Na wanaotoa roho (kwa upole).

وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا ﴿٣﴾

3. Na wanokwenda (nazo hizo roho) kwa haraka.

فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا ﴿٤﴾

4. Na wenye kutangulia mbio mbio.

فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا ﴿٥﴾

5. Na wenye kupanga mambo.

يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ ﴿٦﴾

6. Siku itapolia parapanda (ya kwanza)

تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ ﴿٧﴾

7. Ifuatiwe na yenye kufuatia (ya pili).

قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ ﴿٨﴾

8. Nyoyo siku hiyo zitatemeka.

أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ ﴿٩﴾

9. Macho yake yatatazama chini.

يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ ﴿١٠﴾

10. Wanasema: Je, ni kweli sisi tutarejezwa katika hali ya kwanza?

أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَّخِرَةً ﴿١١﴾

11. Pindi tutakapokuwa mifupa iliyooza?

قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ ﴿١٢﴾

12.Watasema: Hayo, hapo, yatakuwa marejeo ya hasara.

فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ ﴿١٣﴾

13. Hakika hayo yatakuwa ni ukelele mmoja tu.

فَإِذَا هُم بِالسَّاهِرَةِ ﴿١٤﴾

14. Mara wao watakuwa juu ya Ardhi.

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ ﴿١٥﴾

15. Je, imekujia habari ya Musa?

إِذْ نَادَاهُ رَبُّهُ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى ﴿١٦﴾

16.Wakati Mola wake alipomlingania katika wangwa mtakatifu wa Tuwa.

اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ ﴿١٧﴾

17. (Akamwambia) nenda kwa Firaun, hakika yeye amepetuka mipaka.

فَقُلْ هَل لَّكَ إِلَىٰ أَن تَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾

18. Umwambie: Je, unataka kujitakasa?

وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ ﴿١٩﴾

19. Ni kuongoze kwa Mola wako ili umche?

فَأَرَاهُ الْآيَةَ الْكُبْرَىٰ ﴿٢٠﴾

20. Akamwonyesha miujiza mikubwa.

فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ ﴿٢١﴾

21. Akakadhibisha na akaasi.

ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ ﴿٢٢﴾

22. Kisha akapa mgongo akaanza kufanya jitihadi.

فَحَشَرَ فَنَادَىٰ ﴿٢٣﴾

23. Akakusanya (watu) akatangaza.

فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٤﴾

24. Akasema: Mimi ndiye Mola wenu mkubwa.

فَأَخَذَهُ اللَّـهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَىٰ ﴿٢٥﴾

25. Allah akampatiliza kwa adhabu ya Akhera na ya ulimwengu.

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ ﴿٢٦﴾

26. Hakika katika hayo mna mazingatio kwa anayemcha (Mwenyezi Mungu).

أَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُ بَنَاهَا ﴿٢٧ ﴾

27. Je, nyinyi ni wenye umbo gumu zaidi, au mbingu alizozijenga?

رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا ﴿٢٨﴾

28. Akainua kimo chake akazipanga vizuri.

وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا ﴿٢٩﴾

29. Akautia giza usiku wake, akaudhihirisha mchana wake.

وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا ﴿٣٠﴾

30. Na ardhi baada ya hapo, akaitandika.

أَخْرَجَ مِنْهَا مَاءَهَا وَمَرْعَاهَا ﴿٣١﴾

31. Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake.

وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا ﴿٣٢﴾

32. Na majabali akayathibitisha.

مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ﴿٣٣﴾

33. Kwa manufaa yenu na wanyama wenu.

فَإِذَا جَاءَتِ الطَّامَّةُ الْكُبْرَىٰ ﴿٣٤﴾

34. Basi pindi itakapokuja balaa kubwa.

يَوْمَ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ مَا سَعَىٰ ﴿٣٥﴾

35. Siku ambayo mtu atakumbuka alichokitenda kwa bidii.

وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ ﴿٣٦﴾

36. Na moto udhihirishiwe wenye kuona.

فَأَمَّا مَن طَغَىٰ ﴿٣٧﴾

37. Ama aliyepetuka mipaka.

وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿٣٨﴾

38. Akapendelea zaidi maisha ya dunia.

فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَىٰ ﴿٣٩﴾

39. BAsi moto ndio makazi yake.

وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٤٠﴾

40. Na ama yule aliyegopa cheo cha Mola wake, akaizuilia nafsi (yake) na matamanio.

فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ ﴿٤١﴾

41. Basi pepo ndiyo mashukio yake.

UBAINIFU

Katika Sura hii kuna habari za kutilia mkazo tukio la ufufuo na Kiyama. Na kutoa hoja kutokana na njia ya mpangilio wa Mwenyezi Mungu yenye kutoa natija kuwa watu siko hiyo watagawanyika makundi mawili, watu wa peponi na watu wa motoni. Inamalizia Sura kuonyesha kumwuliza kwao Mtumwe(s.a.w.w) kuhusu wakati wa Kiyama pamoja na jawabu lake. Sura hii imeshuka Makka kwa ushahidi wa mpangilio wa aya zake.

Aya Ya 1-5

Wafasiri wamehitalifiana kiajabu tafsiri ya aya hizi, ingawaje wameafikiana kuwa ni kiapo. Kauli ya wengi wao nikuwa jawabu la kiapo limeondolewa, kukadiria kwake ni Ninaapa kwa. mtafufuliwa.

Aya ya 1

Imesemwa makusudio yake ni Malaika wanaotoa roho kutoka katika viwiliwili neno "Gharqa" nikutilia nguvu kutoa. Imesemekana kuwa makusudio yake ni Malaika wanaotoa roho za makafiri kutoka katika viwiliwili vyao kwa nguvu. Pia imesemwa ni mauti yanatoa roho kutoka katika viwiliwili kwa nguvu sana. Imesemwa ni nyota zinatoka na kutua. Imesemwa ni upinde unatoa mshale yaani kuvutwa kwa nguvu. Kwa hiyo kuapa kwa upinde ni wale wanaopigana Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Vile vile imesemwa makusudio ni mnyama mwitu anayeendea malisho.

Aya ya 2

Makusudio yake ni kutoa kwa upole yaani Malaika ambao wanatoa roho katika viwiliwili. Imesemekana kuwa makusudio yake ni Malaika ambao anatoa roho za waumini kwa upole, kama vilke ambavyo makusudio ya aya 1:ni Malaika waotoa roho za makafiri .

Imesemwa ni Malaika wanaotoa roho za makafiri kutoka katila viwiliwili vyao. Imesemwa ni roho za waumini. Imesemwa ni nyota zinatoka katika pembe moja mpaka nuengine. Imesemwa ni mshali unaotoka katika upinde siku ya vita. Imsesemwa ni mauti yanayotoa roho kutoka katika viwiliwili. Na imesemwa ni mnyama mwitu anayetoka upande mmoja kwenda upande mwengine.

Aya ya 3

Imesemwa kuwa makusudio yake ni kwenda haraka na roho za waumini peponi na roha za makafiri motoni. Imesemwa na Malaika wanazichukua roho za waumini. Imesemwa ni Malaika wanaozitoa kwa upole roho za waumini, kisha wanaziacha zistarehe kama anavyoogelea mtu na kitu katika maji na kukiacha.

Imesemwa ni Malaika wanaoshuka kwa haraka kutoka mbinguni. Na imesemwa ni nyoota zinazoogelea; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na vyote vinaogelea katika njia zao ."(36:40).

Vile vile imesemwa ni farasi wa vita wanaokimbia kwa kasi. Imesemwa ni mauti yanaogelea katika nafsi za wanyama. Imesemwa ni majahazi yanayoelea majini. Imesemwa ni mawingu: Na imesemwa ni wanyama wa baharini.

Aya ya 4

Imesemwa kuwa ni Malaika, kwani wao wametangulia binadamu kwa heri, imani na amali njema. Imesemwa ni Malaika wa mauti wanatangulia kuipeleka roho ya muumini peponi na ya kafiri motoni. Imesemwa ni Malaika wa wahyi (ufunuo) wanawatangulia mashetani kwa Mitume kwa kuwapa wahyi. Imesemwa ni roho za wauminii zinawatangulia Malaika wazozichukua, kwa shauku ya kuonana na Mola wao. Imesemwa ni nyota zinazotanguliana katika kwenda. Imesemwa ni farasi wa vita wanatanguliana katika vita. Na imesemwa ni mauti yanatangulia tamaa.

Aya ya 5

Imesemwa ni Malaika woote wanaopanga mambo. Wafasiri wengi wamesema hivyo mpaka ikadaiwa kuwa wameafikiana wafasiri. Hata hivyo pia imesemekana kuwa makusudio ni Malaika wanne wenye kupanga mambo ya Dunia:

1. Jibril: anayepanga mambo ya upepo, askari na wahyi.

2. Mikail: anayepanga mambo ya mvua na mimea.

3. Izrail: Mwenye kuwakilishwa kuchukua roho.

4. Israfil: Mwenye suri (parapanda).

Imesemekana kuwa ni falaki zinatokewa na jambo la Mwenyezi Mungu, halafu (athari) ya hukumu ya Mwenyezi ikaonekana duniani. Kuna kauli kwamba kiapo katika aya zote tano kiko katika tamko lililoondolewa, kukadiria kwake ni "naapa kwa Mola wa Malaika wanaotowa roho." Kwa kuangalia kwako mwenyewe utaona kwamba mpangilio wa aya tano ni mpangilio mmoja wenye kuambatana na kufanana mafungu yake, hauafikiani na nyingi ya kauli hizi kwa kuhitalifiana maana ya chenye kuapiwa; kama vile kuwa makusudio ya aya ya kwanza yawe Malaika wenye kuchukua roho za makafiri na aya ya pili iwe ni wanyama mwitu, ya tatu majahazi ya nne mauti kutangulia tamaa na ya tano iwe ni falaki. Zaidi ya hayo nyingi katika kauli hizo hazina dalili kwa upande wa mpangilio isipokuwa kuangalia kilugha tu. Tena nyingi katika kauli hizo hazinasibiana na mpangilio wa aya za Sura ambayo inataja ufufuo na kutoa hoja juu ya kutukia kwake, kama ilivyo katika Sura ya Al-Mursalaat (77) ambayo ina mazungumzo yenye kunasibiana katika kiapo na jawabu yake.

Tunayoweza kusema:

Na Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi - ni kwamba yale yaliyomo katika aya hizi katika sifa za chenye kuapiwa yanakubali kufungamana na sifa za Malaika katika kufuata amri wanazopewa kutoka katika upande wenye nguvu amri zinazofungamana na kupanga mambo ya ulimwengu huu wenye kushuhudiwa; kisha wasimamie (malaika) mipango yenyewe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Aya hizo zinafanana na aya za mwanzo wa Sura ya Assaffat zinazosema:

"Naapa kwa Malaika wajipangao safu tena kwa wale wanaokataza mabaya. Kisha kwa wale wasomao mawaidha (ya Mwenyezi Mungu)." (37: 1-3).

Pia zinafanana na aya za mwanzo za Sura Wal-Mursalaat. "Naapa kwa (kundi la Malaika) linalopelekwa kwa kufuatana. Wakafuatana kama pepo zinazovuma kwa kasi. Na kwa (Malaika) wanaotawanya (kurasa zenye kuandikwa wahyi). Wakapambanua (haki na batili na halali na haramu). Wakapeleka wahyi (kwa Mitume). Kwa ajili ya kuondosha udhuru au kuhadharisha". (77:1 - 6).

Zote hizo zinasifu Malaika kufuata kwao amri ya Mwenyezi Mungu, hizo zinasifu Malaika wa wahyi, lakini Sura hii inasifu Malaika wote katika kupanga mambo ya ulimwengu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kisha linalodhihirisha zaidi sifa zilizotajwa katika aya hizi tano katika kufungamana na Malaika, ni neno lake "na wenye kupanga mambo". Ikiwa aya ya 3, imeanza na herufi "Fa" inayofahamisha kuwa sifa ya kupanga imetokana na sifa ya kutangulia. Vile vile aya ya 4 imekutanishwa na herufi "Fa" kufahamisha kuwa sifa ya kutangulia imetokana na kufanya haraka, hayo yanafahamisha kuwa maana ya aya tatu (3, 4 na 5) ni ya jinsi moja. Ufahamisho wake ni kuwa wao wanapanga mambo baada ya kutanguliana na kwenda haraka. Kwa hiyo makusudio ya wenye kwenda haraka na wenye kutangulia, ndio wale wenye kupanga mambo. Kwa kuzingatia kushuka kwao kwenye lile waliloamrishwa kulipanga. Aya hizo tatu ziko katika maana ya aya hii: "Ana (kila mtu) kundi (la Malaika) mbele yake, nyuma yake wanamuhifadhi (na kuyadhibiti anayoyafanya) kwa amri ya Allah." (13:11)

Ikiwa makusudio ya aya tatu ni kuonyesha kuharakisha Malaika kushuka kwenye lile waliloamrishwa na kutangulia na kulipanga, inaonyesha aya ya (1-2) ni kutoka kwao pale wanapoambiwa kuliendea lile waliloamrishwa na kutoka kwao sehemu zao. Kama vile, ambavyo aya ya (3) ni kuharakisha kwao baada ya kutoka. Na hilo linafuatiwa na kutangulia kwao na kupanga mambo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo aya tano ni kiapo kwa sifa wanazokuwa nazo wakati wanapoamrishwa kupanga mambo ya ulimwengu, kuanzia wanapoanza kushuka mpaka kutimia kupanga.

Pia zinaonyesha nidhamu ya mpangilio wa Mwenyezi Mungu, wakati wa kuzuka tukio; kama vile ambavyo aya zinazofuatia (yaani aya ya 15..) zinaonyesha mipango ya Mungu iliyowazi katika ulimwengu huu. Katika mipangilio ya Malaika ni hoja juu ya ufufuo na malipo; kama vile ambavyo mipangilio ya kidunia yenye kushuhudiwa ni hoja juu ufufuo; kama yatakavyokuja maelezo (Inshallah) katika utafiti wa hadith.

Malaika Ni Mawakala Katika Kupanga Mambo Malaika ni mawakala kati yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) na vitu, tangu mwanzo hadi marejeo, kutokana na maana yanayotolewa na Qur'an, kwamba wao ni sababu ya matukio zaidi ya sababu zinazoonekana katika ulimwengu huu tunaouona, kabla ya kufa watu na kugura kwenye ufufuo wa akhera na baada yake. Uwakala wa Malaika uko wazi katika marejeo ambayo ni hali ya kudhihiri mauti, kuchukuliwa roho, kuulizwa kaburini ikiwa ni pamoja na thawabu zake na adhabu yake na kuuliwa wote kwa mpuzio wa suri.

Vile vile kufufuliwa, kupewa kitabu, kuwekwa mizani (hisabu) na kupelekwa peponi au motoni, katika yote hayo uwakala wa Malaika uko wazi. Na aya zinazofahamisha hilo ni nyingi hazina haja ya kuzirudia. Vile vile hadith za Mtume(s.a.w.w) na Maimamu hazina hesabu. Ama uwakala wao katika kupanga mambo unafahamishwa na yaliyoko mwanzo wa Sura hii. Aya ya (1-5) kama yalivyotangulia maelezo. Vile vile kauli yake Mwenyezi Mungu: "Aliyewafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa, mbili mbili, tatu tatu na nne nne.. " (35:1).

Yaani Malaika wote wameumbwa kuwa mawakala kati yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) na viumbe vyake. Wanapelekwa kutekeleza amri yake, kama linavyofahamisha neno lake Mwenyezi Mungu: "..bali hao (Malaika) ni waja waliotukuzwa. Hawamtangulii (Mwenyezi Mungu) kwa neno na wao wanafanya kwa amri yake ." (21:25-26).

Na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Wanamwogopa Allah aliye juu yao na wanatenda wanayoamrishwa ." (16:50) Kwa hiyo Malaika hawana shughuli yoyote isipokuwa uwakala kati ya kiumbe na Mwenyezi Mungu S.W.T kwa kutekeleza amri yake, bila ya tofauti yoyote. Mwenyezi Mungu anasema : "Hakika Mola wangu yuko juu ya njia ilinyooka ." (11:56) Anasema tena: "Wala hutapata mabadiliko katika kawaida (desturi) ya Allah wala hutakuta mageuzo katika kawaida (desturi) ya Allah ." (35:43)

Katika uwakala baadhi yao wana vyeo vya juu kuliko wengine na mwenye cheo cha juu humwamrisha wa chini katika kupanga mambo. Kwa mfano Malaika wa mauti anamwakilisha Mwenyezi Mungu kwa kutoa amri kwa wasaidizi wake wachukue roho. Mwenyezi Mungu anasema kuzungumzia Malaika: "Na hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake maalum ." (37:164) Na anasema tena: "Mwenye kutiiwa huko mwaminifu ." (81:21)

Aya Ya 6-7

Imefasiriwa ya kwanza kwa maana ya ukelele mkubwa wa kwanza ambao una migongano. Na ya pili imefasiri kuwa ni ukelele wa pili. Kwa hiyo zinafungamana aya mbili na kelele mbili za parapanda ambayo inafahamishwa na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na itapigwa parapanda watoke roho, watu waliomo mbinguni na waliomo ardhini ila yule amtakaye Mwenyezi Mungu. Tena itapigwa mara nyengine hapa watafufuka wawe wanatazama (nini kitatokea) ." (39:67)

Imesemekana kuwa maana yake ni mtetemeko na makusudio yake vile vile ni mpuzio wa kwanza utakaotetemesha ardhi na majabali. Imesemwa makusudio yake ni mbingu na nyota ambazo zitatetemeka na kugongana na kupasuka. Njia zote hizo mbili haziepuki kuwa mbali na maana hasa ya mwisho. Kwa hali yoyote lenye kunasibiana zaidi ni kuwa aya hizo ni jawabu la kiapo kilichoondolewa kwa kufahamisha juu ya uzito wake nacho ni: naapa mtafufuliwa.

Aya Ya 8-9

Kunasibisha macho na nyoyo mahali pamoja ni kwamba makusudio ya nyoyo katika mfano wa sehemu hizo ambazo zinaegemezwa sifa za utambuzi kama elimu, hofu, matarajio na n.k., ni nafsi. Na kunasibisha kunyenyekea kwa macho ambako ni katika hali za moyo, ni kwa kudhihiri athari ya moyo yenye kufahamika katika macho yenye nguvu zaidi kuliko viungo vyengine.

Aya Ya 10

Ni kueleza kusema kwao kuwa ufufuo uko mbali; na kuonyesha kuwa hawa ambao nyoyo zao zitatetemeka na macho yao kuinama chini siku ya Kiyama ni wale wanaokanusha ufufuo katika dunia. Neno Hafira - kama ilivyosemwa- lina maana ya mwanzo wa kitu, Na swali limekuja kwa maana ya kukanusha maana yake ni: Je, hivi sisi tutarudisha hali yetu ya mwanzo baada ya kufa?

Imesemekana kuwa maana ya neno "Hafira" ni ardhi ya kaburi, maana yake ni: Je, tutarudi kuwa hai na kutoka katika makaburi yetu baada ya kufa? Pia imesemwa aya inatolea habari kukiri kwao ufufuo siku ya Kiyama. Na maneno hayo watayasema baada ya kufufuliwa. Swali ni la kushangaa; kana kwamba wao watapofufuliwa wakashuhudia waliyoyashuhudia watashangaa, na watataka kujua walivyorudi hai baada ya mauti. Haya ni maana mazuri, kama sikuhitalifiana na mpangilio wa maneno.

Aya Ya 11

Kukaririka kuuliza ni kwa ajili ya kukokoteza kuliweka mbali suala la ufufuo.

Aya Ya 12

Ishara ya kusema "hayo" ni hayo ya kurudi kunakofahamishwa na aya ya 10. Kauli yao hiyo ni kwa njia ya kucheza shere. Au ni kwa kukadiria kuwa watasema hivyo wakati wa kufufuliwa kwa njia ya kuona wameharibikiwa.

Aya Ya 13-14

Dhamiri ni ya marejeo. Imesemwa kuwa ni ua ukelele wa pili. Aya hizi mbili ziko katika mahali pa jawabu la swali lililoulizwa katika aya ya 10-11.

Maana yake: Sio uzito kwetu kuwafufua baada ya kuwafisha. Kwani huko kuwarudisha au huo ukelele wa pili utakuwa ni ukelele mmoja tu! Mara wao watakuwa juu ya ardhi baada ya kuwa ni wafu ndani yake.

Aya hizo ziko katika maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: "Wala halikuwa hilo jambo la Kiyama ila ni kama kupepesa jicho au ni karibu zaidi.. " (16:77)

Aya Ya 15

Kuanzia aya hii mpaka ya 26 ni kuonyesha kwa ujumla kisa cha Nabii Musa na ujumbe wake kwa Firaun aliyepinga mlingano wake na kupatwa na adhabu ya akhera na ulimwengu. Katika kisa hicho mawaidha na maonyo kwa wanaomshirikisha Mungu, wenye kukanusha ufufuo. Hawa wamefanya kukanusha kufufuliwa kuwa ni kisingizio cha kukanusha mlingano wa kidini kwa sababu hakuna maana ya sheria ya dini la hakuna krejeshwa tena kuwa hai. Na katika kisa hicho pamoja na hayo ni kutuza moyo wa Mtume(s.a.w.w) kutokana na kukadhibishwa na watu wake.

Pamoja na yote hayo kisa kizima ni hoja ya kutokea ufufuo na malipo. Kwani kuangamia kwa Firaun na jeshi lake- kisa ambacho ni cha kufazaisha ni dalili juu ya ukweli wa Mtume Musa kutoka upande wa Mwenyezi Mungu kwenda kwa watu. Wala hautimii ujumbe wake kutoka upande wake Mwenyezi Mungu Mtukufu isipokuwa kwa uungu wake kwa watu, kinyume na wanavyodai wanashirikisha Mungu kwamba hakuna uungu kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t), kwa watu na kwamba kuna waungu wengine, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkuu wa miungu hiyo tu. Kwa hiyo aya hii ya (15) ni swali la kumkaribisha msikilizaji katika kusikia mazungumzo ili atuze moyo wake na iwe ni onyo na kutimiza hoja kwa wale wanaokanusha.

Aina hii ya swali haikanushi kwa msikilizaji anayajua hayo yenye kuzungumza, kwa sababu makusudio ni kuuelekeza mtazamo wa msikilizaji kwenye mazungumzo na wala sio swali la kihakika au kutaka kufahamisha. Kwa hiyo inawezekana kuwa aya hizi ndiyo mwanzo wa Mwenyezi Mungu kusimulia kisha cha Musa au kuwa zilikwishatanguliwa na masimulizi mengine ya Musa. Kama katika Sura ya Al-Muzzammil (73) kilivyosimuliwa kisa kwa ujumla. Sura hiyo imetangulia sura hii An-Nazia'at kwa kuteremshwa. Vile vile katika Sura ya A'araf (7), Twaha (20) n.k.

Aya Ya 16

Hapo ilikuwa ndiyo mwanzo wa kupewa wahyi Mtume Musa(a.s) .

Aya Ya 17

Ni tafsiri ya mlingano.

Aya Ya 18

Makusudio ya kujitakasa hapa, ni kujitakasa na uchafu wa kupetuka mipaka.

Aya Ya 19

Inaungana na aya iliyotangulia. Makusudio ya kumca Mwenyezi Mungu ni kumcha kwenye kulazimiana na imani inayompelekea kufanya twaa, kujikinga na maasia baada ya kujitakasa kwa toba.

Aya Ya 20

Makusudio ya muujiza mkubwa ni muujiza wa fimbo. Imesemwa makusudio yake ni mkusanyiko wa miujiza ya Nabii Musa aliyomwonyesha Firaun.

Aya Ya 21

Yaani alimkadhibisha Musa na akamwita mchawi. Na akamwasi kwa aliyomwamrisha au alimwasi Mungu.

Aya Ya 22

Yaani alifanya jitihadi kubatilisha jambo la Musa na kumpinga.

Aya Ya 23

Maskusudio ya watu aliowakusanya ni watu wa mamlaka yake. Imesemwa kwa makusudio yake ni kuwakusanya wachawi kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Basi Firaun akawatumwa wakusanyo watu katika miji ." (26:53)

"Basi Firaun akapa mgongo na akatengeneza hila yake kisha akaja. " (20:60) Lakini hakuna dalili ya kuwa makusudio ya kukusanya katika aya hii ndiyo hayo hayo yaliyoko katika aya mbili hizo.

Aya Ya 24

Kwa dhahiri ni kuwa yeye alidai kuwa juu zaidi ya waungu wengine waliokuwa wakiabudiwa na watu wake wanaoabudu masanamu. Huenda makusudio ya kujifanya Mungu bora, pamoja na kuwa Yeye naye anaabudu miungu, ni kwa kujiona kwamba yeye ni Mungu aliyekaribu, riziki zao zinapitia mikononi mwake na yeye ndiye anayewatengenezea maisha yao na ndiye anayechunga utukufu wao; na miungu wengine hawana sifa hizi. Imesemwa makusudio ya aliyoyasema, ni kujifanya bora kwa kila kiongozi wa mamlaka yake; yaani kujifanya mfalme na kwamba yeye ndiye aliye juu ya wanaoshikilia mamlaka mbali mbali kama vile mahakimu n.k. Kwa hiyo aya inakuwa katika maana ya aya inayosema: "Na Firaun alitangaza kwa watu wake, akanena: Enyi watu wangu! Utawala wa Misri si wangu, na pia mito hii ipitayo mbele yangu? Je, hamuoni? " (43:51).

Lakini hayo ni kinyume na dhahiri ya maneno yaliyo katika aya hii: "Enyi watu wakuu simjui kwa ajili yenu Mungu asiyekuwa mimi ." (28:37)

Aya Ya 25

Maana yake Mwenyezi Mungu akamwadhibu Firaun adhabu ya dunia na akhera; ama adhabu ya dunia ni kumgharikisha yeye na jeshi lake, na adhabu ya akhera nu kumwadhibu baada ya mauti. Kwa hivyo makusudio ya "Akhirata wal-ula"ni akhera na ulimwengu.

Imesemwa makusudio yake ni tamko lake (Firaun) la kwanza alilosema kabla hii ambalo ni "Simjui kwa ajili yenu Mungu asiyekuwa mimi ." (28:38).

Na la pili ni pale aliposema "Mimi ndiye Mola wenu mkubwa." Lakini maana haya yamejificha sana, Imesemwa kuwa "ula" ni kukadhibisha kwake na kuasi kwake kulikotajwa katika mwanzo wa kisa na "Akhirata" ni kusema kwake "Mimi ni Mola wenu mkubwa." Lakini maana haya pia yamejificha sana." Pia imesemwa "ula" ni mwanzo wa maasi yake na "Akhirata" ni mwisho wake. Lakini kauli zote hizo haziko wazi.

Ay Ya 26

Inaishiria kwenye mazungumzo ya Musa. Maana yake mazungumzo haya ya Musa mna mazingatio kwa mwenye kucha na akawa na maumbile ya kuucha uovu na adhabu, ambayo ni ya mtu mwenye umbile la sawasawa. Imesemekana kuwa kuna maneno yalioondolewa; kukadiria kwake ni 'kwa anayemcha Mwenyezi Mungu.' Lakini njia tuliyoelezea kwanza ndiyo inayowakilisha maana zaidi.

Aya Ya 27

Ni matahayarizo kwa njia ya lawama kwa wanaomshirikisha, wenye kukanusha ufufuo na wenye kucheza shere. Pia inakusanya jawabu la kuweka mbali kwao ufufuo, kwa neno lao lililo katika aya ya (10-11) katika Sura hii. Kwamba Mwenyezi Mungu ameweza kuumba vitu vilivyo na umbo gumu zaidi yenu basi kuwaumba na kuwafufua tena anaweza tu. Pia inakusanya hoja ya kutokea ufufuo kutokana na kutaja mpangilio wa kijumla wa kilimwengu, kufungamana kwake na ulimwengu wa kibinadama ambako kumelazimisha kuweko Mwenyezi Mungu na kuweko Utume na sharia na hayo yamelazimu na malipo ambayo sehemu yake ni ufufuo. Ndio maana Mwenyezi Mungu akafuatisha aya hizi na aya inaoelezea Kiyama (aya ya 34). Kwa hiyo aya ya 27 ni swali la kutahayariza kwa kuondoa madai yao ya kuuweka mbali ufufuo baada ya kufa. Kufafanua mbingu kwa ksemwa "alizozijenga" ni dalili ya kuthibitisha kuwa mbingu ina umbo gumu zaidi.

Aya Ya 28

Yaani kuinua sakafu yake na kuifanya sawa kulingana na mafungu yake kwa kuliweka kila moja mahali pake panapopitishwa na hekima.

Aya Ya 29

Mchana na usiku umenasibishwa na mbingu kwa sababu ya asili ya vitu hivyo ni ya mbiguni, nayo ni kwamba maumbo ya vitu vyenye giza yanasababishwa kwa kujificha nuru hasa ya jua na inapodhihiri ndipo maumbo ya vitu hivyo pia yanang'aa. Wala hauhusiki usiku na mchana na ardhi tunayoishi tu, bali na maumbile ya vitu vingine kadhaa.

Aya Ya 30

Yaani akaitandika ardhi baada ya kuijenga mbingu. Imesemwa kuwa maana ya neno "Baada" ni pamoja na wala sio baada. Kama ilivyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu aliyotumia tamko "Baada" kwa maana ya pamoja. "Mwovu sana pamoja na hayo ni mtu asiyekuwa na asili ." (69:13).

Aya Ya 31

Makusudio ya kutoa maji ni kufungua chemchemi na kupitisha mito juu ya ardhi inayootesha mimea ambayo ni chakula cha binadamu na wanyama. Kwa hiyo makusudio ya neno "Mar-a" ni mmea wote wa chakula cha watu na wanyama kama inavyo tambulisha aya inayofuatia. Wala sio malisho ya wanyama tu; Kama ilivyozoeleka kutumika tamko hilo.

Aya Ya 32

Yaani ameyathibitisha katika ardhi ili zisiwayumbishe. Na akaweka hazina ya maji na madini kama zinavyofahamisha aya nyengine.

Aya Ya 33

Yaani yote yaliyoumbwa yaliyotajwa mbingu, ardhi n.k. ni kwa ajili ya manufaa yenu na ya wanyama wenu ambao amewalishieni ili mustarehe nao katika maisha yenu. Kwa hiyo maumbile haya na mipangilio hii ni migumu kimaumbile kuliko kuumbwa kwenu; basi si sawa kuona ajabu kuumbwa kwenu mara ya pili.

Aya Ya 34

Makusudio ya balaa kubwa ni Kiyama kwani ni balaa ya mabalaa. Kuanza aya hii kwa herufi "Fa" ya kuunganisha na kuonyesha kuwa Kiyama ni katika mambo yanayolazimiana na kuumbwa mbingu na ardhi na mipangilio yake.

Aya Ya 35

Ni siku hiyo ya balaa kubwa.

Aya Ya 36

Yaani utadhihirishwa moto kwa kuondolewa pazia, aushuhudie kila mwenye kuona kwa macho yake. Aya iko katika maana ya aya inayosema: "Kwa hakika ulikuwa umo katika kughafilika na jambo hili; basi tumekuondolea pazia yako; kuona kwako leo kumekuwa kukali ." (50:22).

Isipokuwa ay hii ina upana zaidi wa maana. Vile vile ayah ii ya 36 inadhihirisha kuwa moto ni wenye kuumbwa kabla ya siku ya Kiyama, na kwamba utadhihiri siku hiyo kwa kuondolewa pazia.

Aya Ya 37 - 41

Ni ufafanuzi wa hali za watu siku hiyo katika kugawanyika kwao. Mwenyezi Mungu S.W.T. amewagawanya watu wa motoni na wa peponi. Ametanguliza sifa za watu wa motoni kwa sababu maneno zaidi yameelekezwa kwa wanaomshirikisha Mungu. Amewasifu watu wa motoni kwa kupituka mipaka na kupendelea maisha ya dunia. Kinyume chake ni vile alivyowasifu watu wa peponi kwa kuogopa kusimama mbele za Mola na kuizuilia nafsi na matamanio. Ikiwa makundi mawili yanakabiliana hali zao, itakuwa kila sifa ya kundi moja ni mkabala wa sifa ya kundi jengine. Kwa hiyo hofu ya kumwogopa Mwenyezi Mungu na kuizuilia nafsi na matamanio mkabala wake ni kupetuka mipaka ambako ni kukosa kuathirika kwao na kusimama mbele ya Mola wao kwa kiburi na kutoka kwao na kipambo cha utumwa hawanyenyekei, hawapiti katika sehemu wanazotakiwa kupita wala hawachagui waliyochaguliwa miongoni mwa wema wa milele, bali wanafuata mapenzi ya nafsi zao katika anasa za maisha ya ulimwengu.

Kwa hiyo kupetuka kwao mipaka ni kuchagua kwao maisha ya dunia kama alivyowasifia Mwenyezi Mungu kwa kusema "Akapendelea zaidi maisha ya dunia". Ikiwa kupetuka mipaka ni kuikataa akhera na kuathirika na maisha ya dunia ambako ni kufuata nafsi vile inavyotaka na kuitii na kumkhalifu Mwenyezi Mungu Mtukufu itakuwa mkabala wake ni kuogopa kufuata matamanio ya nafsi, ambako ni chimbuko la kujizuilia na kushikamana na maisha ya dunia. Ndivyo alivyowasifu Mwenyezi Mungu watu wa peponi kwa kusema:"Akaizuilia nafsi na matamanio" baada ya kuwasifu kuwa wanaogopa.

Hakjika Mwenyezi Mungu amesifu "kuzuilia nafsi na matamanio" bila ya kusema kuacha kuifuata kimatendo. Kwa sababu binadamu ni mdhaifu, huenda akasukumwa na ujinga kwenye maasia bila ya kiburi. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe kama alivyosema: "Ni vya Allah vilivyomo mbinguni na ardhini ili awalipe wabaya kwa hayo wanayoyatenda, na kuwalipa mema wale wanaofanya mema. Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu isipokuwa makosa hafifu, hakika Mola wako ndiye mwenye maghufira mengi ." (53:31-32).

Amesema tena:

"Kama mkijiepusha na maovu makubwa mnayokatazwa, tutawafutia makosa yenu madogo na tutawaingiza mahali patukufu ." (4:31)

Maana inayopatikana katika aya tatu ni kuwa watu wa motoni ni watu wa kufuru na ufasiki na watu wa peponi ni watu wa imani na takuwa. Kuna makundi mengine katika wanyonge na ambao wamekiri dhambi zao wamechanganya amali njema na mbovu na wengineo jambo lao liko kwa Mwenyezi Mungu, huenda Mwenyezi Mungu atawakusanya kwenye maghufira kwa kuombewa n.k.

Neno "Maqam" kwa asili ni mahali kinaposimama kitu au kusimama, lakini mara nyengine huja kwa ibara ya sifa na hali kwa mahali kama Cheo; Mwenyezi Mungu amelitumia neno hilo kwa maana hayo aliposema: ",,,,Basi wawili wengine watasimama mahali pao ." (5:107).

Kwa hiyo cheo chake Mwenyezi Mungu penye kunasibishiwa naye, ni sifa ya Ubwana wake inayolazimiana na sifa zake tukufu; kama ujuzi, uwezo, nguvu, ushindi, rehema na ghadhabu na yanayonasibiana na sifa hizo. Mwenyezi Mungu anasema: "Wala msipetuke mipaka katika hayo, isije ikawashukia ghadhabu yangu. Na ambaye imemshukia ghadhabu yangu, huyo ameangamia " (20:81 - 82).

Amesema tena: "Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ni Mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Kurehemu. Na hakika adhabu yangu ni adhabu inayoumiza kweli kweli ." (15:49-50).

Basi daraja ya Ungu wake ndiyo inayoogopesha waja wake, nayo ni msingi wa Rehema Yake, na msamaha wake kwa mwenye kuamini na Kumcha Mwenyezi Mungu na ni uchungu wa adhabu yake kwa mwenye kukadhibisha na kuasi. Imesemwa kuwa makusudio ni kusimama mbele ya Mola wake siku ya Kiyama wakati atakapoulizwa amali zake. Pia imesemwa maana yake ni kumwogopa Mola wake.

Utafiti Wa Hadith Katika Faqih amepokea Ali bin Mahziyar amesema: Nilimuuliza Abu Jaffar(a.s) kuhusu viapo anavyoapia Mwenyezi Mungu kama kuapia kwa usiku wa manane n.k. Akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu anaweza kuapa kwa viumbe vyake vile anavyotaka lakini viumbe hawawezi kuapia kitu chengine isipokuwa Yeye Mwenyezi Mungu." Katika Durril Manthur ametoa Said bin Al-Mansur Ibn Al-Mundhir kutoka kwa Ali kuhusu aya ya 1 akasema: "Ni Malaika wanaotoa roho za makafiri na aya ya (2) ni Malaika wanaing'oa roho kati ya kucha na ngozi mpaka waitoe. Aya ya (3) ni wanaogelea na roho za waumini kati ya mbingu na ardhi. Aya ya (4) ni Malaika wanaotanguliwa na roho za waumini kwa Mwenyezi Mungu. Aya ya (5) ni Malaika wanaopanga mambo ya waja."

Katika hiyo Durril Manthur, ametoa Ibn Abu Hatim kutoka kwa Ali bin Abu Twalib, kwamba Ibnul Kawwa alimuuliza kuhusu aya ya (5) akasema ni Malaika wanaozingatia utajo wa Mwenyezi Mungu na amri yake. Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu aya ya (6) amesema itapasuka ardhi na neno "Radifa" ni ukelele. Katika hiyo tafsiri kuhusu aya ya (10) amesema: Walisema Maquraish hivi tutarudi baada ya kufa?

Tena katika hiyo hiyo Tafsiri ya Qummi kuhusu aya ya (12) anasema walisema hivi kwa njia ya kucheza shere. Katika hiyo hiyo tafsiri katika riwaya ya Abul Jarud kutoka kwa Abu Jaffar(a.s) amesema kuhusu aya ya (10) wanasema kuhusu umbo jipya ama aya ya (14) walikuwa katika makaburi waliposikia ukelele walitoka katika makaburi yao wakawa juu ya ardhi.

Katika Usulul-Kafi kwa kutegemezwa kwake kwa Daud Arraqi kutoka kwa Abu Abdillahi kuhusu kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na mwenye kuogopa cheo cha Mola wake atapewa mabustani (pepo) mawili ." (55:46). Amesema: Mwenye kujuwa kwamba Mwenyezi Mungu anamuona, na kusikia anayoyasema na kujuwa anayoyajua katika heri au shari hilo litamzuwiya na kufanya matendo mabaya huyo ndiye yule anayeogopa cheo cha Mola na akaizuilia nafsi na matamanio.

Hadith hiyo inatilia nguvu maana yaliyotangulia kuelezwa kuhusu kuogopa cheo chake Mwenyezi Mungu (s.w.t) Katika hiyo Usulil-Kafi kwa kutegemezewa Yahya bin Akil amesema: Amesema Amirul Mominin(a.s) : Hakika mimi ninaogopa kwenu mambo mawili; kufuata matamanio na tamaa ndefu. Ama kufuata matamanio hakika kunazuia haki. Ama tamaa ndefu inasahauliza akhera.

Aya Ya 42 - 46 42.

يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ﴿٤٢﴾

42. Wanakuuliza habari ya Kiyama kutokea kwake kutakuwa lini?

فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾

43. Ujo wapi wewe na kuwatajia (habari ya Kiyama).

إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَاهَا ﴿٤٤﴾

44. Ukomo (wa ujuzi) wake ni kwa Mola wako peke yake.

إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَاهَا ﴿٤٥﴾

45. Wewe ni mwonyaji tu. Kwa anayekiogopa.

كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا ﴿٤٦﴾

46. Siku watakayoiona, watakuwa kana kwamba hawakukaa ila kitambo cha jioni moja na asubuhi yake.

UBAINIFU

Ni kuonyesha kuuliza kwao Kiyama na majibu yake, kwamba ujuzi wa Kiyama uko kwa Mwenyezi Mungu tu.

Aya Ya 42

Kwa dhahiri ibara ya wanakuuliza inafahamisha kuendelea; walikuwa wanaomshirikisha Mungu baada ya kusikia mazungumzo ya Kiyama wakimrudia Mtume(s.a.w.w) na kumtaka awaelezee hasa wakati wa Kiyama. Walikuwa wakiendela hivyo. Qur'an imelikariri hilo mara nyingi. Kusema: Kutokea kwake kutakuwa lini na kubainisha swali na maana yake: wanakuuliza hawa wanakanushaji kuhusu Kiyama kwa kucheza shere.

Aya Ya 43

Ni swali la kukanusha; yaani hataweza kukijua kwa kukitaja sana. Au ikiwa "Dhikra" ni kwa maana ya kuhudhuria hakika ya kitu katika moyo wa mtu, maana yake ni: huna ujuzi nacho hata uweze kujua hakika yake. Maana haya ndiyo yanayosibiana zaidi kuliko yaliyotangulia. Imesemwa maana yake ni: kukitaja hicho Kiyama sio mambo yanayofungamana na ujumbe wako, wewe umepelekwa kumwonya anayekiogopa. Imesemwa maana yake ni kukanusha kuuliza kwao, kwa maana ya kuwa; swali hili ni lanini, na hali wewe utakitaja tu, kwa sababu hilo linafungamana na utume wako kwa kuwa wewe ni Mtume wa mwisho. Imesemwa aya ni swali kamili walilouliza wanaomshirikisha Mungu kwa Mtume(s.a.w.w) . Maana yake: Unajua nini kuhusu Kiyama na wakati wake? Au umepata kujua nini na kukitaja kwako sana? Wewe mwenyewe msomaji unajua zaidi kwamba mpangilio wa aya hauoani kabisa na chochote katika maana haya.

Aya Ya 44

Ni sababu ya maneno yaliyotangulia maana yake: wewe hujui wakati wake kwa sababu ukomo (wa ujuzi wake) ni kwa Mola wako. Haijulikani hakika yake na sifa zake. Sio mbali - Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi - kuwa aya iko mahali pa sababu ya maana nyengine nayo ni kuwa Kiyama kitasimama kwa kuishi vitu na kuondoka sababu zote, na kudhihiri kuwa hakuna ufalme isipokuwa wa Mwenyezi Mungu pekee mwenye kushinda, hainasibishwi siku isipokuwa kwake Yeye Mwenyezi Mungu bila ya kuingiliwa kati na sababu yoyote. Kwa hivyo siku hiyo haikubali kuwekewa wakati kwa hakika.

Kwa hiyo ndio maana hayakuja katika maneno ya Mwenyezi Mungu maelezo ya kuelezea siku halisi isipokuwa tu, kuelezea siku kwa kwisha dunia, kama vile kusema kwake:

"Na itapigwa parapanda watoke roho watu waliomo mbinguni na waliomo ardhini (39:68). Miongoni mwa maana ya aya hiyo ni kufahamisha juu ya kuharibika dunia kwa kubadilika ardhi, mbingu na kupukutika nyota n.k. Sehemu nyengine ameielezea siku kwa kufananisha tu, kama vile aya ya mwisho wa Sura hii, na pia kauli yake Mwenyezi Mungu: "Siku watakayoyaona waliyoahidiwa itakuwa kama kwamba hawakukaa ulimwenguni ila saa mmoja ya mchana " (46:35).

Kisha anataja uhakika wa kauli katika hilo kwa kusema: "Na waliopewa ilimu na imani watasema: Hakika nyinyi mmekaa kwa hukumu ya Allah mpaka siku ya kufufuliwa, basi hii ni siku ya kufufuliwa ." (30:56) Yanafahamisha maneno ya Mwenyezi Mungu kwamba Kiyama kitafika kwa ghafla tu. Mwenyezi Mungu anasema: "Hakitawafikia ila kwa ghafla (tu!) ." (7:187).

Hii ni njia iliyondani sana inayohitaji ukamilifu wa kufikiria vizuri, ili kuondoa shaka ya yanayodhihiri katika aya nyingi za kiyama. Hebu angalia vizuri aya hii: "Kwa hakika ulikuwa umo katika kughafilika na jambo hili, basi tumekuondolea pazia yako; kuona kwako leo kumekuwa kukali ." (50:22).

Pamoja na aya nyengine zenye maana haya. Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kutakwa msaada.

Aya Ya 45

Yaani tumekukalifisha kumwonya anayekiogopa Kiyama, sio kutolea habari wakati wake. Kwa hiyo hakuna haja ya kuwajibu kuhusu wakati wake. Makusudio ya kuogopa kutokana na kunavyonasibiana na mahali hapa, ni kuogopa kinapotajwa.

Aya Ya 46

Ni ubainifu wa kukaribia Kiyama kwa njia ya kufananisha. Imedhihiri kwamba makusudio ya kukaa ni kukaa kati ya uhai wa dunia na kufufuliwa yaani kukaa makaburini. Imesemwa kuwa makusudio ya kukaa ni baina ya wakati wa hayo hayaafikiani na dhahiri ya aya nyengine zinazoonyesha kukaa kwao dhahiri ya aya nyengine hayo hayaafikiani na dhahiri ya aya nyengine zinazoonyesha kukaa kwao kabla ya kufufuliwa; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Atasema: Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya miaka? Watasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku ." (23: 112-113)

Utafiti Wa Hadith Katika Tafsiri Al-Qummi kuhusu aya ya (40-41) amesema ni mja akiwa kwenye maasi na akawa anaweza kuyafanya; kisha akayawacha kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu na makatazo yake, akaizuilia nafsi, basi malipo yake ni pepo. Katika Durril Manthur ametoa Ibn Hatim na Ibn Murdawayh kwa Isnad dhaifu kutoka kwa Ibn Abbas amesema: Hakika washirikishaji Mwenyezi Mungu wa Makka walimuuliza Mtume(s.a.w.w) kwa kumchezashere: Ni lini kitakuwa Kiyama? Ndio ikashuka aya hiyo ya (42).

Katika hiyo hiyo Durril Manthur ametoa Al-Bazzar, Ibn Jariyr, Ibn Al-Mundhir na Ibn Murdawayh kutoka kwa Aisha amesema: "Hakuwacha kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu anauliza kuhusu Kiyama mpaka ziliposhuka aya hizo (44-45) ndipo hakuuliza tena. Amepokea vile Urwa kutoka kwa masahabu wengi, vile Shihab bin Twariq kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) lakini mpangilio hauafikiani kuwa ni jawabu la swali la Mtume(s.a.w.w) na hali Mtume alikwisha pewa wahyi katika Sura nyingi za Qur'an hasa zile zilizoshuka Makka kwamba ujuzi wa Kiyama unahusika na Mwenyezi Mungu (s.w.t) haijuwi isipokuwa yeye tu, na akaamrishwa kumjibu anayemuliza wakati wake, kuwa hajuwi.


4

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA ABASA (ALIFINYA USO (NA. 80)

INA AYA 42)

AYA 1-16

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١﴾

1. Alikunja uso akapa mgongo.

أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ ﴿٢﴾

2. Kwa sababu alijiwa na kipofu.

وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ ﴿٣﴾

3. Ni lipi la kukujulisha huenda akajitakasa.

أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٤﴾

4. Au akawaidhika ukamfaa waadhi?

أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ ﴿٥﴾

5. Ama ajionaye amejitosha.

فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ ﴿٦﴾

6. Wewe ndiye unayemshughulikia.

وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ﴿٧﴾

7. Wala si juu yako asipojitakasa.

وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ ﴿٨﴾

8. Ama yule anayekujia mbio mbio.

وَهُوَ يَخْشَىٰ ﴿٩﴾

9. Na hali yeye anamcha (Mungu)

فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ ﴿١٠﴾

10. Wewe unajipurukusha naye!

كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ ﴿١١﴾

11. La usifanye! Hakika hizo (aya za Qur'an) ni waadhi.

فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ ﴿١٢﴾

12. Anayependa ataukumbuka.

فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ ﴿١٣﴾

13. Umo katika vitabu vitakatifu.

مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ ﴿١٤﴾

14. Vyenye kutukuzwa, vyenye kutwahirishwa.

بِأَيْدِي سَفَرَةٍ ﴿١٥﴾

15. Vimo katika mikono ya wajumbe.

كِرَامٍ بَرَرَةٍ ﴿١٦﴾

16. Watukufu watenda njema.

UBAINIFU

Zimekuja riwaya katika njia ya Ahli Sunnah kuwa aya ziliteremshwa katika kisa cha Ibn Umma Maktuum kipofu aliyeingia kwa Mtume akamkuta yuko na mabwana wa Kiquraysh anawaelezea jambo la Uislamu, Mtume akafinya uso wake. Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamlaumu kwa aya hizi. Ziko baadhi ya riwaya za Shia zinazosema hivyo. Baadhi ya riwaya za Shia zinasema kuwa mwenye kukunja uso ni mtu moja katika Bani Umayya, alikuwa kwa Mtume akaingia Ibn Ummi Maktuum, akafinya uso yule mtu ndio zikashuka hizo aya, Utakujia ufafanuzi wa utafiti wa hilo katika utafiti wa hadithi (Inshallah). Vyovyote iwavyo kusudio la aya ni lawama kwa yule anayewatanguliza matajiri kuliko wanyonge na maskini walio waumini. Anawatukuza watu wa dunia na kuwaangusha watu wa akhera. Kisha zinakusudia kuonyesha vile anavyopuuza mtu kuumbwa kwake na kujizulia kwake kuzingatia vizuri jambo lake. Pia Sura inataja kwa Muhtasari kufufuliwa kwa mtu na kulipwa kwake, kama onyo. Sura hii imeshuka Makka bila ya ubishi.

Aya Ya 1-2

Ni maelezo ya kukunja uso na sababu yake.

Aya Ya 3-4

Makusudio ya kujitakasa hapa ni kujitakasa kwa amali njema baada ya kuwaidhika na kuzinduka kuitakidi haki. Kufaa waadhi ni kule kulingana kwake kujitakasa na imani na amali njema. Katika aya hizo nne mna lawama kubwa. Kunazidisha lawama kuzileta aya mbili za mwanzo kwa mfumo wa kumweleza mtu asiyekuwepo, kisha kuzileta aya mbili nyengine kwa mfumo wa kumwelekeza mtu kwa kutahayarisha na kuzidisha lawama.

Ibara ya kuja kipofo nayo inazidisha lawama, kwa vile haja ya kumshughulikia kipofu ambaye haja ya dini yake imemwacha ahangaike kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu, ilikuwa ni zaidi kumhurumia na kumpokea wala sio kumkunjia uso. Imesemwa kwamba ikiwa aya zinamhusu Mtume, kuleta ibara ya dhamiri ya mbali kwa aya mbili za mwanzo ni kumtukuza Mtume kwa kuchukulia, kuwa aliyefinya uso ni mtu mwengine sio Mtume(s.a.w.w) . Na kuleta aya mbili nyengine kwa dhamiri ya kumsemesha ni utukuzo pia kwa kuwa inaonyesha kumliwaza (Mtume) baada ya kumkaripia.

Lakini hayo hayaafikiani na dhamiri ya kusemesha iliyo katika aya zinazofuatia. (Ama ajionaye amejitosha. Wewe diye unayemshughulikia) ambazo zinalawama zaidi ya zilizo tangulia.

Aya Ya 5 -7

Makusudio ya kujitosha ni kujitosha na kuonekana mkubwa katika macho ya watu na kutakabali katika kuifuata haki. Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika mwanadamu hupetuka mpaka kwa kujiona amejitosha " (96:67).

Kwa hivyo sio juu yako kumshughulikia huyo na kumwacha anayetaka kujitakasa na huku anamwogopa Mwenyezi Mungu. Ni kitu gani kinachokulazimu, ikiwa hakujitakasa na kufuru na uovu? Kwani hakika wewe ni mjumbe, ni juu yako kufikisha tu! Imesemwa kuwa maana ya aya "7" ni usijali kwa kukosa kujitakasa kwake na uchafu wa kufuru na uovu. Maana haya yanasibiana zaidi na mpangilio wa lawama.

Aya Ya 8-9

Kumcha Mwenyezi Mungu ni alama ya kuwaidhika. Mwenyezi Mungu anasema: "Hatukukuteremshia Qur'an ili upate mashaka. Bali ni mawaidha kwa wanaomcha (Mwenyezi Mungu) ." (20:2-3).

Amesema tena: "Atawaidhika nao mcha (Mungu) ". (19:10). Kutanguliza dhamiri "wewe" ni kuthibitisha lawama.

Aya Ya 11 - 12

Ni makatizo ya yale aliyolaumiwa kwayo ambayo ni kufinya uso kupa mgongo, kumshughulikia anayejiona amaejitosha na kujipurukusha na anayemcha Mwenyezi Mungu. Kusema kwake "Mwenye kutaka ataukumbuka" ni jumla yenye kuingia kati. Dhamiri ni ya Qur'an au yanayowaidhiwa na Qur'an. Ibara hii inaonyesha kuwa hakuna kulazimisha kuwaidhika, kwani hakuna manufaa yanayomrudia mwenye kutoa mawaidha isipokuwa anayenufaika ni yule mwenye kuwaidhiwa, kwa hiyo na chague anayoyachagua.

Aya Ya 13-14

Neno Suhuf lina maana ya chenye kuandikiwa; ni habari ya aya ya 11. Hiyo inadhoofisha kauli inayosema kuwa makusudio ya "Suhuf" ni ubao wenye kuhifadhiwa Lawhin Mahfuudh. Wala hakuna katika maneno ya Mwenyezi Mungu kukusudia ubao wenye kuhifadhiwa kwa tamko la wingi. Pia kuna udhaifu wa kauli ya kuwa makusudio ya Suhuf ni vitabu vya Mitume kwa sababu ya kutoafikiana na aya ya 15. Kusema kwake kutakaswa, ni kutakaswa na uchafu wa batili, maneno ya upuuzi, shaka na kupingana. Mwenyezi Mungu anasema: "Haiifikii batili mbele yake wala nyuma yake ." (41:42). Na amesema tena: "Hakika (hii Qur'an) ni kauli ya haki wala si upuuzi " (86:14).

Amesema tena:

"Hiki ni kitabu kisicho na shaka ndani yake ." (2:3).

Amesema: "Na kama ingelitoka kwa asiyekuwa Allah bila shaka wanagalikuta ndani hitilafu nyingi ". (4:82).

Aya Ya 15

Neno Safarah ni wingi wa Safiyr kwa maana ya mjumbe. Ni sifa baada ya sifa. Watukufu ni sifa ya hao wajumbe kwa kuzingatia dhati zao na watenda njema ni sifa kwa kuzingatia kazi yao. Maana ya aya hizi ni kwamba Qur'an ni waadhi uliyoandikwa katika vitabu vitukufu vilivyo toharishwa na kila aina ya uchafu, vilivyomo mikononi mwa Malaika, Watumishi ambao ni watukufu mbele za Mwenyezi Mungu kwa vile wao wenyewe ni tohara, na ni wema mbele ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya matendo yao yaliyo mema matupu.

Inadhihiri katika aya kwamba wahyi unashughulikiwa na Malaika kwa kuchukua vitabu na kutoa wahyi. Wao ni wasaidizi wa Jibril wako chini ya amri yake. Kunasibisha wahyi kwa Malaika wengine, hakukanushi kunasibika nao Jibril katika mfano wa kauli yake. "Ameyateremsha Ruuh mwaminifu juu ya moyo wako " (26:193-194).

Na amemsifu Mwenyezi Mungu katika kauli yake: "Hakika hii (Qur'an) ni kauli ya mjumbe mtukufu mwenye nguvu, mwenye daraja mbele za mwenye ufalme. Mwenye kutiiwa huko mwaminifu "; (81:19-21).

Kwa hiyo yeye ni mwenye kutiiwa na Malaika, mwenye kutoa amri yake. Na kitendo chake na chao, vyote ni vya Malaika. Inasemekana kuwa makusudi ya "Safarah" ni waandishi katika Malaika lakini maana iliyotangulia ndiyo iliyowazi zaidi. Pia inasemekana kuwa makusudio ni wasomaji, wanayaandika kisha wanayasoma.

Utafiti Wa Hadithi Katika Majmau imesemwa aya ziliteremshwa kwa sababu ya Abdallah bin Ummi Maktuum, naye ni Abdallah bin Sharih bin Malik bin rabia Al-Fahri katika ukoo wa Amir bin Luayyi. Ni kwamba yeye alimjia Mtume(s.a.w.w) akiwa anawasemesha Utba bin Rabia, Abu Jahl bin Hisham, Abbas bin Abdul-Muttwalib, Ubayya na Ummayya Khalaf akiwalingania kwa Mwenyezi Mungu na hali anawatarajia wasilimu. Akasema Ibn Ummi Maktuum: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nifundishe aliyokufundisha Mwenyezi Mungu." Akawa anasema kwa nguvu na kulikariri hilo wala hajui kwamba yeye ni mwenye kushughulika na wengine. Mpaka kukadhihiri kuchukia katika uso wa Mtume(s.a.w.w) kwa kukatishwa maneno yake akawa Mtume anasema kimoyo: 'hawa wakuu watasema wafuasi wake ni vipofu na watumwa'. Kwa hivyo akampa mgongo na akawaelekea watu aliokuwa akiwazungumza nao; ndio zikashuka aya hizo.

Baada ya hapo Mtume akawa anamtukuza. Kila amwonapo husema: "Karibu ewe ambaye amenilaumu Mola wangu kwaye". Kisha humwambia, Je, unayo haja. Aliwahi kumfanya kaimu wake Madina mara mbili katika vita. Amepokea Suyut katika Durril Manthur kisa hicho kutoka kwa Aisha, Anas na Ibn Abbas kwa hitilafu ndogo.

Lakini aya haziko dhahiri kufahamisha kuwa makusudio ni Mtume(s.a.w.w) bali katika hadithi; hakufafanuliwa aliyehusika. Na tukichunguza vizuri katika aya hiyo tutafahamu anayekusudiwa si yeye; kwani kukunja uso si katika sifa ya Mtume(s.a.w.w) hata kwa adui aliyewaziwazi, sembuse kwa waumini wenye kutaka uongofu. Kisha kumsifu kwamba yeye anawashughulikia matajiri na kujipurukusha na makafiri hakufanani kabisa na tabia zake. Mwenyezi Mungu amezitukuza tabia zake aliposema katika Sura ya Al-Qalam (68) iliyoshuka kabla ya hii ambayo wapokezi wenye kubainisha utaratibu wa kushuka Sura wameafikiana kuwa imeshuka baada ya Sura ya Iqraa' (96). (Sura ya kwanza kushuka).

Aya inasema: "Hakika wewe unatabia njema " (68:4).

Itaingiaje akilini kuwa Mwenyezi Mungu amtukuze mwanzo wa Biitha yake kisha arudie kumlaumu juu ya tabia yake na amshutumu kwa mifano hiyo ya kuwashughulikia matajiri hata wakikufuru na kujipurukusha na makafiri hata wakiamini na kutaka kuongoka. Vile vile Mwenyezi Mungu amesema: "Na uwaonye jamaa zako waliokaribu. Na uinamishe bawa lako kwa yule anayekufuata katika wale waliomini ." (26:214-219).

Hapo ameamrishwa kuwachukulia upole waumini. Surah hiyo imeshuka Makka. Na mpangilio wa kusema kwake "Waonye jamaa zako walio karibu", ni wa kushuka mwanzo mwanzo wa mlinganio. Pia kauli yake Mwenyezi Mungu: "Usinyooshe (usidokowe) macho yako (kutazama) yale tuliyowastareheshea makundi mbali mbali ya hao (wabaya) wala usiwahuzunikie (huzuni kubwa ya kujiumiza nafsi yako) na inamisha bawa lako kwa waumini " (15:88).

Na katika kauli yake: "Basi yatangaze uliyoamrishwa na ujitenge mbali na hao washirikina " (15:94).

Sasa vipi itawezekana kwa Mtume kukunja uso na kuwapa mgongo waumini huku akiwa ameamrishwa kuheshimu imani zao na kuwainamishia bawa na kutoikodolea macho dunia. Hayo tuliyoyaelezea, pia ni jibu la yale yaliyosemwa kuwa Mwenyezi Mungu hakumkataza kitendo hicho ila wakati huo tu!, kwa hivyo hakikuwa haramu kwake kabla ya kukatazwa, bali ni haramu baada ya kukatazwa.

Katika Majmau imepokewa hadith kutoka kwa As Sadiq(a.s) kuwa aya hizo zilishuka kwa mtu mmoja katika Bani Umayya, alikuwa mbele za Mtume(s.a.w.w) akaja Ibn Ummi Maktuum, alipomwona akamkunjia pua kwa kumwona mchafu na akamkunjia uso na kumpa mgongo, ndio akalielezea Mwenyezi Mungu hilo. Katika hiyo hiyo Majmau imepokewa kutoka kwa Asswadiq(a.s) kwamba yeye amesema: Alikuwa Mtume(s.a.w.w) anapomwona Abdallah Ibn Ummi Maktuum husema. Marhaba! Marhaba! Waallahi hatanilaumu Mwenyezi Mungu kwa sababu yako milele. Na alikuwa akimfanyia upole mpaka akawa anajizuia na Mtume, yaani alikuwa anajizuia kuwa na Mtume kwa jinsi anavyomshughulikia sana.


5

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA ABASA (ALIFINYA USO)

Aya Ya 17-42

قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ ﴿١٧﴾

17. Amelaniwa mwanadamu si ukafiri wake huo!

مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ﴿١٨﴾

18. ( Jee anajua) kwa kitu gani amemuumba ?

مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ ﴿١٩﴾

19. Kwa tone la manii amemuumba akamwezesha.

ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ ﴿٢٠﴾

20. Kisha akamfanyia nyepesi njia.

ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ ﴿٢١﴾

21. Kisha akamuua, akamfanyia kaburi.

ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ ﴿٢٢﴾

22. Kisha anapotaka atamfufua.

كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ ﴿٢٣﴾

23. Hakika hajatekeleza aliloamrishwa

فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ ﴿٢٤﴾

24. Basi mtu naatazame chakula chake.

أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا ﴿٢٥﴾

25. Sisi tumemebubujiza maji.

ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا ﴿٢٦﴾

26. Kisha tukaipasua Ardhi.

فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا ﴿٢٧﴾

27. Tukaotesha humo nafaka.

وَعِنَبًا وَقَضْبًا ﴿٢٨﴾

28. Na zabibu na mboga.

وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا ﴿٢٩﴾

29. Na zaituni na mitende.

وَحَدَائِقَ غُلْبًا ﴿٣٠﴾

30. Na mabustani yenye miti mingi.

وَفَاكِهَةً وَأَبًّا ﴿٣١﴾

31. Na matunda na malisho.

مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ﴿٣٢﴾

32. Kwa manufaa yenu na wanyama wenu.

فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ ﴿٣٣﴾

33. Basi itakapokuja sauti ya nguvu.

يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴿٣٤﴾

34. Siku ambayo mtu atamkimbia ndugu yake.

وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ ﴿٣٥﴾

35. Na mama yake na baba yake.

وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ ﴿٣٦﴾

36. Na mke wake na watoto wake

لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ ﴿٣٧﴾

37. Kila mtu katika wao siku hiyo atakuwa na jambo limshughulishalo.

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ ﴿٣٨﴾

38. Nyuso siku hiyo zitanawiri.

ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ ﴿٣٩﴾

39. Zitacheka na kufurahika.

وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ ﴿٤٠﴾

40. Na nyuso nyingine siku hiyo zitakuwa na mavumbi.

تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ ﴿٤١﴾

41. ( Zitakuwa) zimefunikwa na weusi weusi.

أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ ﴿٤٢﴾

42. Hao ndio makafiri, watendao maovu.

UBAINIFU

Aya Ya 17- 42

Ni kumwombea laana mtu na kumstaajabia kwa kuendelea kwake kuukanusha ubwana wa Mola wake. Kwani yeye mtu hawezi hata chembe kujiumba na kujiangalia. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyeuumba katika tone la manii lililo duni. Akamkadiria akamzua kisha akamfanyia nyepesi njia kisha akamuua. Akamfanyia kaburi kisha atakapotaka atamtafufua. Basi yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye Mola wake aliyemuumba, mwenye kuangalia vizuri mambo yake katika hali zote. Na yeye mtu hatekelezi aliyoamrishwa na Mola wake, wala haongoki kwa ungozi wake. Lau angelitazama mtu chakula chake tu! ambacho ni onyesho moja katika maonyesho ya mazingatio yake na ukufi mmoja tu! Katika bahari ya rehema yake, angeliona wasaa wa mapitilizo na upole wa utengenezaji ambao utaishangaza akili yake. Ni neema zisizohisabika. "Kama mkitaka kuzihesabu neema zote za Mwenyezi Mungu hatamweza ." (14:34). Kwa hiyo kuficha mtu kumzingatia Mola wake na kuacha kushukuru neema zake ni jambo la ajabu. Hakika mwanadamu ni dhalimu mkubwa nwa mwenye kukufuru sana.

Aya hizi kama unavyoona hazikatai kuambatana na aya zilizotangulia katika mfumo mmoja ingawaje baadhi wanasema zimeshuka kwa sababu nyengine kama ukavyoona. (Inshallah).

Aya Ya 17

Ni kumwombea laana mtu kutokana na tabia yake ya kujiingiza kufuata matamanio na kuusahau ubwana wa Mola wake, na kuwa na kiburi katika kufuata amri zake. Makusudio ya ukafiri ni hali yoyote ya kuficha haki iliyowazi na unafungamana na kukanusha uungu na kuacha ibada. Yanatilia nguvu hayo yale yanayoonyesha mazingatio ya Mungu. Baadhi yao wamefasiri ukafiri kwa kuacha kushukuru na kuzikanusha neema. Ingawa hivyo ni sawa, lakini yanayonasibiana zaidi kwa kuangalia mpangilio, ni yale yaliyotangulia. Amesema katika Kash-shaf: "Amelaaniwa mtu" ni dua ya kumwombea laana na kauli na "namna gani alivyoendelea na ukafiri wake" ni kustajaabu kutokana na kupetuka mpaka katika kuzikufuru neema za Mwenyezi Mungu. Huwezi kuona mfumo mkali wa kulaani zaidi ya huo. Imesemekana kuwa jumla na "Namna gani alivyoendelea na ukafiri" ni swali na maana yake ni jambo gani lilimfanya kuwa kafiri? Lakini maana yaliyotangulia ndiyo yaliyokaribu zaidi.

Aya Ya 18

Maana yake ni kuwa ni kitu gani alichoumbiwa mtu hata ikawa anapetuka mpaka na kiburi katika imani na twaa? Swali hili ni la mkazo yale yaliyotangulia (ya kustaajabu). Mastaajabu yanakuwa katika matukio yasiyokuwa na sababu kwa hivyo. Kwanza: Inafahamisha kuwa ni katika maajabu kwa mtu kupetuka mpaka katika kufuru. Pili: Panaulizwa je, katika umbile lake aliloumbwa na Mwenyezi Mungu kuna linalowajibisha kukufuru? Jibu ni hakuna? Wala hapana hoja atakayoitoa wala udhuru kwani yeye ni kiumbe aliyeumbwa na maji duni. Hamiliki chochote katika umbile lake wala katika kuangalia mambo ya uhai wake, kifo chake na kufufuliwa kwake. Jibu la swali hili liko katika aya zinazofuatia.

Aya Ya 19

Kuleta neno Nutfa (tone la manii) kwa njia ya (Nakra) kutojulikana kwa kudharau yaani ametokana na tone la manii lililoduni, dhalili katika umbile lake, kwa hivyo hana haki ikiwa asili yake ni hii, kupetuka mpaka kwa kufuru yake na kuwa na kiburi na twaa. Kusema kwake Akamwezesha yaani akampa uwezo katika dhati yake, na sifa zake na vitendo vyake; kwa hivyo hafai kupetuka kiasi alichowezeshwa na kupetuka mipaka aliyowekewa. Yamemzunguka yeye maangalizi ya Mungu katika kila upande. Haifai kwake kujihukumia kupata yale asiyowezeshwa.

Aya Ya 20

Kwa dhihiri ya mpangilio ulivyo, makusudio yake ni kukanusha udhuru wa mtu wa kufuru yake na kiburi chake, kwamba makusudio ya njia ni njia ya twaa ya Mwenyezi Mungu na kufuata amri, ukipenda unaweza kusema njia ya kheri kwa hivyo aya itakuwa inaondoa mushkili, kwa sababu ikisemwa "kwa tone la manii alimuumba kisha akamuwezesha" inawezekana kumfahamikia msikilizaji kwamba ikiwa kuumba na kuwezesha kumemzunguka mtu kwa kila upande, itakuwa vitendo vya mtu kwa dhati yake na sifa zake ni vyenye kuwezeshwa na kufungamana na matakwa ya Mungu ambayo hayahalifu. Kwa hivyo mtu atakuwa ni mwenye kutenzwa nguvu, asiyekuwa na hiyari. Hivyo ukafiri siyo matakwa ya mtu wala ufasiki. Kwa sababu hayo yanakuwa kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu (s.w.t) Kwa hiyo hakuna shutuma wala lawama kwa mtu.

Kwa sababu hiyo, Mwenyezi Mungu ameondoa mushkeli huo kwa kusema "Kisha akamfanyia nyepesi njia" inafahamisha kuwa kuumba na kukadiria hakukanushi hiyari ya mtu katika lile aliloamrishwa miongoni mwa imani na twaa. Anayo njia ya kuendea wema alioumbiwa. Hivyo ni kwamba kuwezesha ni kwenye kuwa juu ya vitendo vya mtu kwa njia ya hiyari yake na matakwa ya Mungu ni yenye kufungamana na vitendo vya mtu kwa matakwa yake na hiyari yake. Kitendo ni chenye kutokana na mtu kwa hiyari yake ambayo kwa kuwa ni hiyari basi ni yenye kufungamana na uweza. Kwa hivyo mtu ana hiyari katika kitendo chake lakini ni mwenye kuulizwa juu ya hivyo vitendo. Utafiti juu ya suala hili utaelezewa mara nyingi katika aya zinazofanana na hii.

Imesemekana makusudio ya kufanya nyepesi njia ni kutoka katika tumbo la mama yake kwa maana ya: Kisha akafanyiwa nyepesi mtu njia ya kutoka hali yakuwa ni mtoto mchanga aliyeumbwa kutokana na tone la manii. Imesemekana kuwa makusudio yake ni kuongoza kwenye dini na kubainisha njia ya heri na shari kama alivyosema: "Na tukambainishia njia mbili" (90:10) lakini yaliyotangulia ni bora.

Aya Ya 21

Makusudio ya "Akamfanyia kaburi" ni kumzika na kumficha ndani ya ardhi. Hii ni kuchukulia vile walivyozowea watu. Kwa mnasaba huo ndio akaunasibisha kwake Mwenyezi Mungu; kwa sababu Yeye ndiye aliyewaongoza kwenye hilo la kufanya kaburi na akawafahamisha. Imesemekana kuwa makusudio ya kumfanyia kaburi, ni amri yake Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kumtukuza ili kuuficha mzoga usiwaudhi watu. Nja iliyoelezwa kwanza ndiyo yenye kunasibu zaidi.

Aya Ya 22

Mpangilio ni kumfufua anapotaka yaani kuwa huo ufufuo utakuwa ni wa ghafla hajui isipokuwa yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Aya Ya 23

Kutokana na mpangilio wa manno ulivyo neni " Kalla" ni la kukataa. Ni kama kuna swali; yaani baada ya kuonyeshwa kuwa binadamu ni kiumbe mwenye kuangaliwa vizuri na Mwenyezi Mungu, tangu kupatikana kwake mpaka mwisho wake; kuumbwa, kukadiriwa, kufanyiwa nyepesi njia, kuuliwa, kutiwa kaburini na kufufuliwa. Yote hayo ni neema kutoka kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa hivyo likaja swali amefanya nini mtu? Je, amemnyenyekea Mola wake? Au je, ameshukuru neema? Pakajibiwa" hapana sivyo hivyo; kisha pakafafanuliwa zaidi kwa kusemwa: "hajatekeleza alioamrishwa." Kwa hiyo imedhihiri kuwa dhamiri ya neno hajatekeleza inamrudia mtu. Vile vile imedhiri kuwa shutuma na lawama zilizomo katika aya hiyo ni za mtu kutokana na tabia yake na kupetuka mipaka katika kufuru na inadi. Imedhihiri kutokuwa sawa yale waliyoyasema baaadhi, kuwa aya inaenea kwa kafiri na muislam. Kwa sababu dhamiri ya mtu aliyetajwa ni kwa kutokana na tabia yake inayompelekea kukufuru basi inafungamana na mwenye vitendo hivyo.

Aya Ya 24

Ni mtiririko wa yaliyotangulia kwa ajili ya kufafanua. Ndani yake mna maelekezo ya kuangalia mtu chakula chake tu, ambacho anakila na kukitegemea ili aishi. Hilo ni jambo moja tu, kati ya yasiyohisabika liloandaliwa na maangalizi mazuri ya Mungu, ili aweze mtu kuchunguza na kushudia upana wa maangalizi mazuri ya Mungu ambayo yataweza kuishangaza akili yake. Makusudio ya mtu kama ilivyosemwa sio yule mtu aliyetajwa katika aya ya 17. Kwani makusudio ni kumhusu mtu mwenye kukufuru sana, kinyume cha mtu yule aliyetajwa katika aya ile aliyeamrishwa kuangalia vizuri, hii ni yenye kuenea kwa kila mtu. Ndio maana ikaletwa kwa dhahiri bila ya dhamira.

Aya Ya 25-32

Ni ubainifu wa ufafanuzi wa maangalizi mazuri ya Mwenyezi Mungu. Makusudio ya kububujiza maji nikuteremsha mvua ya Ardhi, wala sio mbali kuwa ni pamoja na mito na chemchemi kwa sababu hazina ya maji iliyo ndani ya ardhi inatokana na mvua. Kuipasua ardhi ni kwa mmea unaotoka. Neno Qadhba lina maana ya kukatakata; yaani mboga anyoikatakata mtu na kuila. Imesemekana kuwa makusudio ni chakula cha wanyama. Imesemekana kuwa yametajwa yale matunda mengine kwanza kwa majina yao kwa ajili ya kuyapa kipaumbele (umuhimu). Kuacha dhamiri ya asiyekuwepo na kuleta dhamira ya wenye kusemeshwa na kwa ajili ya kutilia mkazo neema alizowaneemesha.

Aya Ya 33

Makusudio ya sauti ya nguvu ni kupuziwa Suur. Yaani siku ya Kiyama. Hiyo ni kuishiria ule mwishilio wa yaliyotajwa katika mipangilio ya Mungu kwa ajili ya mtu, kwamba kuna jambo la Mungu kwa mja nalo ni siku ya Kiyama ambayo atalipwa mtu malipo ya matendo yake.

Aya Ya 34-37

Ni kuonyesha ugumu wa siku hiyo ya Kiyama. Wale ambao mtu aliwahesabu kuwa ni jamaa zake wa karibu na wanaomuhusu ambao alikuwa nao na kuwafanya ni nguzo na wasaidizi wa kuwategemea katika dunia, lakini leo anawakimbia kutokana na matatizo yaliyomzunguuka, kiasi ambacho hayamruhusu kumshughulikia mwengine vyovyoye atakavyokuwa. Balaa likiwa kubwa na likizidi, mtu kujivutia mwenyewe na kuwaacha wengine. Dalili ya maana hii ni aya inayosema: "Kila mmoja katika wao siku hiyo atakuwa na jambo la kumshughulisha". Zimesemwa sababu nyengine za mtu kuwakimbia jamaa zake wanaomuhusu, ambazo hazina dalili yoyote kwa hivyo tumezifumbia macho.

Aya Ya 38-39

Ni ubainifu wa kugawanyika watu siku hiyo mafungu mawili; watu wema na waovu, na kuonyesha kuwa watajulikana kwa alama zao za nyusoni mwao. Kunawirika uso ni kuangaza kunawirika uso kwa furaha na kushangilia kwake kushuhudia yale yenye kufurahisha.

Aya Ya 40

Vumbi ni alama ya hamu na ghamu.

Aya Ya 41

Yaani zitakuwa na giza na weusi. Imebainishwa hali ya makundi mawili katika aya nne kwa ubainifu wa nyuso, kwa vile uso ndio kioo cha moyo katika furaha yake na kuchukiwa kwake.

Aya Ya 42

Yaani wenye kukusanya ukafiri kiitikadi na kiuovu. Hayo ni maasi mabaya sana.

Utafiti Wa Hadith Katika Durril Manthur ametoa Ibn Al-Munathir kutoka kwa Akram kuhusu aya ya 17: amesema. "Imeshuka kwa Utbah bin Abilahab wakati aliposema: "Nimemkufuru Mola wa nyota zinapoanguka". Mtume akamwapiza, akauawa na simba katika njia ya Sham. Katika Ihtijaj imepokewa kutoka kwa Amirul Muminin(a.s) hadith ndefu kuhusu aya hiyo yaani amelaaniwa mtu. Katika Tafsiri al Qummi kuhusu aya ya 20 amesema amemfanyia nyepesi njia ya heri. Makusudio yake ni kumfanya ni mwenye kuchagua katika kitendo chake kinachomsahilishia kufuata kwake njia ya wema na kufika kwenye ukamilifu ambao amemuumbia. Haya yanafungamana na yale tuliyotangulia kuyaeleza katika tafsiri ya aya.

Katika Durril Manthur ametoa Abu Ubayd katika Fadhail kutoka kwa Ibrahim Attaymi amesema: aliulizwa Abu Bakr As-Swiddiq kuhusu neno "Abba" akasema: "Ni mbingu gani itakayonifunika na ni ardhi gani itakayoniua kama nikisema katika kitabu cha Mwenyezi Mungu jambo nisilolijua". Katika hiyohiyo Durril Manthur ametoa, Sadi Bin Mansuur, Ibn Jariyr, Ibn Saas, Abd bin Hamid, Ibn Al-Mundir, Ibn Murdawayh na Bayhaqi katika Shiilbul-Iman, na Khatib, na Al-Hakim. Ikasahihishwa kutoka kwa Anas kwamba Umar alisoma juu ya mimbar aya ya 28 - 31 akasema 'yote haya tumeyajua' basi ni nini "Abba"?' Kisha akainyanyua fimbo yake iliyokuwa mkononi mwake akasema; "Hii naapa kwa umri wa Mwenyezi Mungu ndio taklifa, lakini si lawama kwako kutojua nini "Abba" fuateni yale aliyowabainishia uongozi wake katika kitabu muyafanye na msiyoyajua yategemezeni kwa Mungu."

Katika Irshadul-Mufid imepokewa kwamba Abu Bakr aliulizwa kuhusu neno lake Mwenyezi Mungu (s.w.t) Abba hakujua maana yake akasema; Ni mbingu gani itakayonifunika au ni ardhi gani itakayoniua au nitafanya nini nikisema katika kitabu cha Mwenyezi Mungu sijui? Ama Fakiha tunajua, lakini Abba Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi."

Yakamfikia hayo Amirul Muuminin Ali(a.s) akasema: Subhannallah hajui kuwa "Abba" ni malisho na kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu "Na matunda na malisho" ni kuhesabu Mwenyezi Mungu neema zake juu ya viumbe vyake katika alivyowalisha na kuwaumbia kwa ajili yao na kwa ajili ya wanyama wao ambavyo vinawapa uzima na kuimarisha miili yao. Katika Majmau imepokewa kutoka kwa Ataa' bin Yasar naye kutoka kwa Sawdah mke wa Mtume(s.a.w.w) amesema: Amesema Mtume: "Watafufuliwa watu uchi, bila viatu, wenye mizunga, wakitokwa na majasho yanayofikia ndewe za masikio ". Anasema Sawdah, nikamuuliza: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tutaangaliana uchi". Akasema: "Watu hawatakuwa na habari na hilo". Akasoma Mtume wa Mwenyezi Mungu: "Kila mtu katika wao siku hiyo atakuwa na jambo limshughulishalo".


6

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA TAKWIR (KUKUNJA) (NA. 81)

INA AYA 29.

Aya 1 - 14

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ﴿١﴾

1. Jua litakapokunjwakunjwa.

وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ ﴿٢﴾

2. Na nyota zitakapoanguka.

وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ ﴿٣﴾

3. Na majabali yatakapoendeshwa.

وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ ﴿٤﴾

4. Na ngamia wenye mimba watakapotupiliwa mbali.

وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ ﴿٥﴾

5. Na wanyama wa mwitu watakapokusanywa.

وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ ﴿٦﴾

6. Na bahari zitapowashwa moto.

وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ ﴿٧﴾

7. Na nafsi zitakapokutanishwa.

وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ ﴿٨﴾

8. Na kijana mwanamke aliyezikwa angali hai atakapoulizwa.

بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ ﴿٩﴾

9. Kwa makosa gani aliuawa?

وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ ﴿١٠﴾

10. Na madaftari yatakapofuniliwa.

وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ ﴿١١﴾

11. Na mbingu zitakapoondolewa mahali pake.

وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ ﴿١٢﴾

12. Na moto utapokokwa.

وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ ﴿١٣﴾

13. Na pepo itakaposogezwa.

عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ ﴿١٤﴾

14. Itajua nafsi ilichokihudhurisha.

UBAINIFU

Sura inataja siku ya Kiyama, kwa kutaja baadhi alama zake na matukio yake. Inaisifu siku hiyo kwamba yatafunuka ndani ya siku hiyo yale aliyoyafanya mwanadamu. Kisha inaisifu Qur'an kwamba aliyeileta kwa Mtume ni mjumbe wa mbingu ambaye ni Malaika wa wahyi na sio shetani, wala Mtume sio mwenda wazimu aliyepagawa na mashetani. Sura hii inakubaliana kwa mpangilio wake kuwa ni katika Sura za mwanzo. Hili linaungwa mkono na maelezo yaliyomo ndani yake yanayohusu kumtakasa Mtume(s.a.w.w) na visingizio vya kuwa ni mkichaa; ambavyo makafiri walimsingizia mwanzo wa utume wake. Vile vile Sura Al Qalam ambayo ni katika Sura za mwanzo nayo ina maelezo ya kumtakasa Mtume(s.a.w.w) . Sura imeshuka Makka bila ya ubishi.

Aya Ya 1

Maana ya neno Takwir ni kukunja kwa kuzungusha; kama kukunja kilemba juu ya kichwa. Huenda makusudio ya kukunjwa jua ni kuwa giza umbo lake kwa mzunguko.

Aya Ya 2

Neno Inkadarat lina maana ya kuanguka kutoka hewani mpaka kwenye ardhi. Huenda ikawa ni kwa maana ya kugeuka, ikawa makusudio ni kuondoka mwanga wake.

Aya Ya 3

Yaani yataendeshwa kutokana na mtingishiko wa Kiyama yawe kama vumbi lenye kupeperushwa.

Aya Ya 4

Imesemwa kuwa neno Ishar wingi wake ni ushara naye ni ngamia mwenye mimba ya miezi kumi, huitwa hivyo mpaka azae, huenda akaitwa hivyo hata baada ya kuzaa. Na ngamia ndiyo mali yenye thamani zaidi kwa waarabu. Kana kwamba ni ishara ya fumbo kwamba mali yenye thamani ambayo wanaishindania watu itabakia bila ya mtu wa kuimiliki na kuitumia, kwa sababu watu watakuwa wanajishughulisha na kuokoa nafsi zao tu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Kila mtu katika wao siku hiyo atakuwa na jambo la kumshughulisha ". (8:37).

Aya Ya 5

Dhahir ya aya kulingana na mpangilio wa aya za kukisifu Kiyama ni kwamba hata wanyama mwitu pia watakusanywa kama watu. Hayo yanatiliwa nguvu na kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Na hakuna mnyama katika ardhi wala ndege arukaye kwa mbawa zake mbili ila ni umati kama nyinyi. Hatukupuuza kitabuni (mwetu) kitu chochote kisha watakusanywa kwa Mola wao ". (6:38).

Ama hali yao baada ya kukusanywa haikuelezwa katika maneno yake Mwenyezi Mungu wala yale yanayotegemewa katika hadith. Ndiyo kusema kwake Mwenyezi Mungu katika Sura (6:38). ni umati kama nyinyi na kusema kwake "Hatukupuuza kitabuni kitu chochote" huenda hayo yakafafanua hali yao kwa mwenye huzingatia na kuangalia kwa makini. Pengine husemwa, kukusanywa wanyama ni katika alama za Kiyama na si katika matukio ya Kiyama. Hivyo itakuwa maana ya kukusanywa wanyama; ni kule kutolewa kutoka mwituni na mapangoni mwao.

Aya Ya 6

Imefasiriwa Sujjirat kwa kuwako moto na imefasiriwa kwa kujaa.

Aya Ya 7

Nafsi njema zitakutanishwa na wanawake wa peponi Mwenyezi Mungu anasema: "Humo watakuwa na wake waliotakaswa ". (4:57).

Amesema tena: "Na tutawaoza Mahurilaini " (44:54).

Ama nafsi za waovu zitakutanishwa na mashetani, Mwenyezi Mungu anasema: "Wakusanyeni wale waliodhulumu (nafsi zao) pamoja na wenziwao na wale waliokuwa wakiwaabudu ." (37:22).

Na amesema: "Na mwenye kuyafanyia upofu maneno ya mwingi wa rehema tunamwekea shetani kuwa rafiki yake " (43:36).

Aya Ya 8

Waarabu walikuwa wakiwazika wazima watoto wa kike kwa kuogopa aibu; kama kunavyoonyesha kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Anapopewa habari mmoja wao ya (kuzaliwa) mtoto wa kike husawijika uso wake akajaa sikitiko". Anajificha na watu kwa sababu ya habari mbaya ile aliyoambiwa! (Anafanya shauri) Je, akae naye juu ya fedheha hiyo au amfukie udongoni? " (16:58 - 59).

Mwenye kuulizwa kwa hakika ni baba yake aliyemzika nzima ili asiaibishwe, lakini amehisabiwa kuwa mwenye kuulizwa ni kijana mwanamke kwa namna ya kuaibishwa na kufedheheshwa huyo muuaji na kumsahilishia huyo kijana wa kike kumuomba Mwenyezi Mungu amwadhibu muuaji wake. Maneno yako katika mfano wa kusema kwake Mwenyezi Mungu kuhusu Isa(a.s) :

"Na (kumbuka) Allah atakapo sema: "Ewe Isa bin Maryam! Je, wewe uliwaambia watu 'Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Allah ? " (4:116).

Imesemwa kuwa kutegemeza kuuliza kwa kijana wa kike ni kwa njia ya fumbo. Makusudio yake ni kuuliziwa, mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu: "Kwa hakika ahadi itaulizwa ". (17:34)

Aya Ya 10

Yaani yatafunuliwa kwa ajili ya hisabu. Ama watu wa peponi watakutanishwa na wanawake wema. Ama watu wa motoni kila mtu atakuwa na shetani; yaani nafsi za makafiri na wanafiki zitakutanishwa na mashetani ndio marafiki zao". Katika Durril Manthur ametoa Ibn Abu Maryam, Addiylamiy kutoka kwa Abu Maryam kwamba Mtume(s.a.w.w) amesema kuhusu kauli yake "Jua litakapokunjwa kunjwa ", amesema: "Litakunjwa katika Jahanam ".

Aya Ya 11

Maana ya neno Kushitwat ni kubanduliwa. Kisha Mwenyezi Mungu ataikunja; kama ilivyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na mbingu zitakunjwa kwa uweza wake" (39:67) Na siku itakapopasuka mbingu zilete chungu ya mawingu " (25:25).

Aya Ya 12

Yaani utakokwa mpaka uzidi kuwa mkali.

Aya Ya 13

Makusudio ya kusogezwa ni kwa ajili ya kuingia watu wake.

Aya Ya 14

Makusudio ya nafsi ni jinsi ya nafsi yoyote. Na makusudio ya ilichokihudhirisha ni amali yake iliyoifanya. Aya iko katika maana ya aya inayosema: "Siku ambayo kila nafsi itakuta mema iliyoyafanya yamehudhurishwa na pia ubaya ilioufanya ." (3:30).

Aya Ya 15-29

فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ ﴿١٥﴾

15. Naapa kwa nyota zirudizo nyuma.

الْجَوَارِ الْكُنَّسِ ﴿١٦﴾

16. Ziendazo na kujificha.

وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ ﴿١٧﴾

17. Na kwa usiku unapotoka.

وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ ﴿١٨﴾

18. Na asubuhi inapotoa mwanga.

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿١٩﴾

19. Hakika hiyo (Qur'an) ni kauli ya Mjumbe Mtukufu.

ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ ﴿٢٠﴾

20.Mwenye nguvu, Mwenye daraja mbele za Mwenye ufalme.

مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ ﴿٢١﴾

21 Mwenye kutiiwa huko, Mwaminifu.

وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ ﴿٢٢﴾

22. Wala mwenzenu si mwendawazimu.

وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ ﴿٢٣﴾

23. Na hakika alimwona pambizoni mwa mbingu mlimo wazi.

وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ ﴿٢٤﴾

24. Wala yeye kwa jambo la ghaibu si mwenye kutuhumiwa,

وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ ﴿٢٥﴾

25. Wala (Qur'an) si kauli ya shetani aliyefukuzwa.

فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ ﴿٢٦﴾

26. Basi mnakwenda wapi?

إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿٢٧﴾

27. Hi (Qur'an) siyo ila ni waadhi kwa walimwengu.

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ ﴿٢٨﴾

28. Kwa anayetaka kunyooka katika nyingi.

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٩﴾

29. Wala hamtataka ila kwa matakwa ya Allah Mola wa viumbe.

UBAINIFU

Niutakaso kwa Mtume(s.a.w.w) kwa wazimu na kwamba Qur'an inayomjia Mtume haina mwingiliano wowote na shetani. Na hiyo Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) tu anayoletewa Mtume na Malaika wa wahyi ambaye hafanyi hiyana katika ujumbe wake. Na kwamba hiyo Qur'an ni waadhi kwa walimwengu, yenye kuongoza kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kwa anayetaka kuongoka katika nyinyi.

Maana yake ninaapa hakika Mtume alimwona Jibril akiwa pambizoni mlimo wazi, ambayo ni sehemu ya juu kabisa kuliko sehemu zote zinazonasibiana na ulimwengu wa Malaika. Imesemwa kuwa maana yake ni hakika Mtume alimwona Jibril na sura yake ya asili wakati wa kuchimbuka jua akiwa yuko sehemu ya juu kabisa upande wa Mashariki. Hakuna dalili inayofahamisha hayo hasa kufungamana kuona kwa sura yake ya asili au kumwona kwa mfano wowote. Ni kama vile zimechukuliwa baadhi ya riwaya kwamba alimuona mwanzo wa Biitha na yeye yuko kati ya mbingu na ardhi amekaa juu ya kiti. Hayo yamechukuliwa kwa kufananisha.

Aya Ya 15 - 16

Aya mbili zinazofuatia hizi zinatilia nguvu kuwa makusudio ya nyota zirudizo nyuma, ziendazo na kujificha, ni nyota zote au baadhi yake. Lakini sifa za baadhi ya nyota zinanasibiana zaidi na sifa zilizoapiwa ambazo ni kurudi nyuma na kwenda kwa kujificha. Nazo ni sayari tano Zohal (Saturn), Mushtara (Jupitar), Mirikh (Mars), Zuhura (Venus) na Zebaki (Mercury). Kwani hizo zina sifa ya kwenda na kurudi na kujificha katika maficho yake kama wanyama wa porini. Imesemwa kuwa makusudio yake ni nyota yoyote. Ama kurudi nyuma ni kule kujificha mchana chini ya mwanga wa jua. Kwenda kwake ni kwenda kunakoonekana usiku na kujificha kwake ni kutua upande wa magharibi yake. Imesemwa kuwa makusudio yake ni Nyati na Paa. Sio mbali kuwa kutaja nyati au paa ni kwa upande wa mithali tu. Na kwamba makusudio ni mnyama wowote wa mwituni. Kwa vyovyote ilivyo, kauli ya kwanza iko karibu zaidi, ya pili iko mbali na ya tatu iko mbali zaidi.

Aya Ya 17

Inaungana na aya mbili zilizotangulia. Neno As'as huja kwa maana ya kuingia usiku na kutoka usiku. Raghib anasema; Ni mwanzo wa usiku na mwisho. Kwa hiyo As'as ni giza jembamba. Yanayosibiana zaidi na jumla na aya inayofuatia ni kuwa makusudio yake ni kutoka kwa usiku. Imesemwa makusudio yake ni kuingia, lalini kauli hii iko mbali.

Aya Ya 18

Inaungana na aya iliyotangulia limetumiwa neno kupumua kwa maana ya kutoa mwanga, kwa sababu asubuhi unakunjuka mwanga wake kwenye anga na giza lililoufunukia linaondoka. Ametaja Zamakhshari njia nyengine katika Kash-Shaf: ukisema nini maana ya kupumua asubuhi? Nitasema: "Ikija asubuhi huja upepo wa asubuhi kwa hiyo umejaaliwa juo upepo ndio pumzi zake". Kauli ya kwanza ndiyo iliyokaribu zaidi.

Aya Ya 19 -21

Ni jawabu la kiapo dhamiri ni ya Qur'an au ni ya yaliyotangulia katika Sura hii kwa maana ya kuwa ni Qur'an. Makusudio ya mjumbe hapa ni Jibril, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Sema: Anayemfanyia ushinde Jibril hakika yeye ameiteremsha Qur'an moyoni mwako kwa idhini ya Allah (2:97). Kulitegemeza neno kwake kama mjumbe ni dalili kwamba neno ni la Mwenyezi Mungu. Amemsifu Mwenyezi Mungu Jibril kwa sifa sita: Mjumbe: Inafahamisha ujumbe wake na kuleta kwake wahyi wa Qur'an kwa Mtume(s.a.w.w) . Mtukufu: Yaani mwenye utukufu na cheo. Mwenye Nguvu: Yaani mwenye uwezo wa kutekeleza.

Mwenye Daraja mbele ya Mwenyezi Mungu : Yaani mwenye nafasi ya ukaribu mbele za Mwenyezi Mungu. Mwenye kutiiwa huko: Yaani mbele ya

Aya Ya 22

Inaungana na aya ya 19, kupinga kumsingizia kwao wazimu. Kuleta ibara ya "mwenzenu" ni kukadhibisha masingizio yao. Kwa kuonyesha kuwa huyo ni mwenzenu amekaa nanyi akatangamana nanyi kwa muda mrefu, nanyi mnajua zaidi mlivyomkuta na ukamilifu wa akili, rai ya sawa na ukweli wa maneno. Mwenye sifa hizi haambiwi kuwa ni mwenda wazimu. Kumsifu Jibril kwa sifa zilizopita bila ya kumsifu Mtume(s.a.w.w) sio dalili ya ubora wa Jibril kuliko Mtume. Kwa sababu maneno yanakusudia kubainisha kuwa Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyoteremshwa kwa Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya wahyi sio kwa njia ya fikra za kiwenda wazimu kutoka kwa shetani. Yaani makusudio yake ni kubainisha kusalimika njia ya kushuka na kumtukuza yule anayeiteremsha kwa kutaja sifa zake tukufu na kuzidi kumtakasa na makosa na hiyana. Ama yule mwenye kuteremshiwa hakuna haja ya kutaja sifa nyingi zaidi ya zile wanazomtilia shaka.

Ni miongoni mwa maneno yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) kumsifu Mtume(s.a.w.w) hata kwa yale asiyotiliwa shaka katika ubora wake kuliko Malaika wote. Na Mwenyezi Mungu aliwafanya Malaika wote wamsujudie Mtume ambaye ndile Khalifa wake katika ardhi.

Mwenyezi Mungu kuna Malaika anawaamrisha na wanamtii, hapa inaonyesha kuwa ana msaada wa Malaika anaowaamrisha. Muaminifu: Yaani hafanyi hiyana kwa yale anayoamrishwa. Imesemwa Rasul ni kwa maana ya Mtume(s.a.w.w) , lakini kama unavyoona hayo hayaafikiani na aya inayofuatia.

Aya Ya 23

Dhamira ya mwenye kuona inamrudia "mwenzenu" yaani Mtume na mwenye kuonwa ni Jibril. Kwa dhahir pambizoni mlimo wazi ni kama vile ilivyoonyesha aya inayosema: "Na yeye yuko pambizoni juu kabisa " (53:7).

Aya Ya 24

Dhamiri inamrudia Mtume. Jambo la ghaibu ni Wahyi kutofanya ubakhili yaani haufichi huo wahyi wala haubadilishi baadhi yake au wote. Anawafundisha watu kama alivyofundishwa na Mwenyezi Mungu na anawafikishia yale aliyoamrishwa kuyafikisha.

Aya Ya 25

Ni kanusha la kuitegemeza Qur'an na shetani. Shetani ni kwa maana ya yule aliye mwovu aliyefukuzwa, kama vile anavyoitwa na Mwenyezi Mungu Iblis na kizazi chake. Vile vile anaitwa hivyo majini wengine waovu. Mwenyezi Mungu anasema: "Allah akasema: "Basi toka humo kwani umebaidishwa na rehema ." (38:77).

Anasema tena: "Na tumezilinda na kila shetani aliyefukuzwa ." (15:17). Maana yake nikuwa Qur'an siyo ushawishi wa shetani na askari wake wala sio kupagawa na majini waovu kama wanavyopagawa wenda wazimu.

Aya Ya 26

Ameweka wazi Mwenyezi Mungu katika aya ya saba zilizotangulia uhaki wa Qur'an hali ya kuikinga na mashaka wanavyomsingizia aliyekuja nayo kuwa ni mwenda wazimu.

Pili : Kwamba imeteremshwa na malaika wa mbinguni, mwenye cheo kikubwa ambaye ni mwaminifu wa wahyi naye ni Jibril asiyekuwa na kizuwizi chochote kati yake na Mwenyezi Mungu wala kati yake na Mtume.Tatu : kwamba aliyeteremshiwa ni mwenzenu ambaye hali yake haikujificha kwenu, sio mwenda wazimu kama wanavyomzulia. Hakika alimwona malaika mwenye kuchukua huyo wahyi na akauchukua kwake wala si mwenye kuficha aliyopewa wahyi wala kugeuza.

Nne : Kwamba sio ushawishi na kiibilisi na askari zake wala sio kupatwa na shari za majini. Natija ya ubainifu huu ni kwamba Qur'an ni kitabu cha uongofu, anaweza kuongoka nacho mwenye kutaka kwa kuongoka kwenye haki. Ndio kusema kwake Mwenyezi Mungu "Hii (Qur'an) siyo ila waadhi kwa walimwengu." Kusema kwake "Basi mnakwenda wapi?" ni kianzio cha kutaja natija ya ubainifu huo, swali katika aya hii ni la kutahayariza; maana yake ikiwa ni hivi basi mnakwenda wapi, mnaiacha haki yenu nyuma yenu?

Aya Ya 27

Yaani ni waadhi kwa watu, katika wale wanaoweza kuiona haki.

Aya Ya 28

Ni ubainifu kuwa sharti ya kunufaika na waadhi huo ni kutaka kunyooka juu ya haki nako ni kuwa na uthabiti wa utii.

Aya Ya 29

Yameelezwa zaidi maana yake katika aya zilizotangulia zenye kufanana na hii. Aya hii kwa unavyofahamisha mpangilio wa Sura hii ni kuwa iko katika maana ya kukinga uwezekano wa tuhuma kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu "kwa anayetaka katika nyingi kunyooka" kwamba wana uhuru wa kutaka kunyooka. Wakitaka watanyooka, wasipotaka hawatanyooka; kwa hiyo Mwenyezi Mungu, kwa kutaka hao wanyooke, ana haja fulani kwao. Ndipo fikira hiyo ikaondolewa na aya hii, kwamba huko kutaka kwao kunyooka hakuwezekani ila tu anapopitisha Mwenyezi Mungu hilo. Hivyo ni kusema vitendo vya mwanadamu vile anavyoitaka, Mwenyezi Mungu pia amevitaka (vitokeo) kupitia kwa matakwa ya binadamu. Yaani ni Mwenyezi Mungu kumtakia mwanadamu afanye kadha wa kadha kwa mapenzi yake (mwanadamu) mwenyewe.

Utafiti Wa Hadith Katika Durril Manthur ametoa Said bin Mansur, Al-Fariyabi, Abdu bin Hamid, Ibn Jariyr, Ibn Hatim na Hakim na amesahihisha kutoka katika njia ya Ali, kuhusu kauli yake "Naapa kwa nyota zirudizo nyuma" amesema ni nyota zinazorudi usiku na kujificha mchana zikiwa hazionekani. Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu aya hiyo hiyo anasema: maana yake ni: Ni naapa kwa Al-Khunnas (jina la nyota) ziendazo kwa kujificha amesema: zinajificha mchana hazibainiki. Katika Majmau kuhusu "zirudizo nyuma"-amesema zinarudi nyuma mchana na zinadhihiri usiku. "Ziendazo" ni sifa yake kwa sababu zinatembea katika Falaki (njia yake). "Ziendazo kwa kujificha" ni katika sifa yake vile vile kwa sababu zinajificha katika ngome zake kama anavyojificha paa kwenye nyumba yake; nazo ni nyota tano Zohal, Mushtara, Mirikh, Zuhura na Zebaki. Hadith hiyo imepokewa kutoka kwa Ali. Kuhusu aya ya 17 inapoingia yaani linapoondoka giza lake. Kutoka kwa Ali.

Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu aya ya 17 amesema ni kuingia giza na kuhusu aya ya 18 ni kuondoka giza. Katika Durril Manthur ametoa Ibn Asakir ktuoka kwa Muawiya bin Qurrat amesema: Anasema Mtume(s.a.w.w) kumwambia Jibril ni uzuri ulioje wa alivyokusifu Mola wako. Mwenye nguvu, mwenye daraja, mbele za mwenye ufalme. Mwenye kutiiwa huko, na muaminifu. Ni zipi hizo nguvu zako? Na ni upi huo uaminifu wako? Akasema Jibril: "Ama nguvu zangu ni wakati nilipopelekwa katika miji ya lut nayo ni minne. Katika kila mji kuna wapiganaji laki nne nikawanyanyua kutoka katika ardhi ya chini mpaka wakasikia watu wa mbingu sauti za kuku na kelele za mbwa, kisha nikawaporomosha, wakafa. Ama umanifu wangu sikuamrisha kitu chochote nikakipeleka kwa mwengine.

Riwaya hii haiwezi kupita hivihivi. Ameidhoofisha Ibn Askari. Katika Khiswal kutoka kwa Abu Abdillahi amesema: mwenye kusema katika kila siku ya Shabaan " Astaghfirullaha lladhiy laa ilaha huwa rrahmanurrahim. Al-hayyul qayyuum wa atubu ilayh" mara sabaini huandikwa katika pambizoni mwa mbingu mlimwowazi. Akasema nikauliza nini pambizoni mwa mbingu? Akasema ni sehemu katika Arsh yenye mito yenye kupita. Katika Tafsiri ya Qummi katika hadith aliyoitegemeza kwa Abu Abdillah kuhusu aya ya 25 amesema shetani mwenye kufukuzwa ni makuhani wa Maquraish yananasibishwa maneno yao na maneno ya mashetani.


7

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA INFITAR (KUPASUKA) (NA. 82)

INA AYA 19

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾

1. Mbingu zitakapopasuka.

وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ ﴿٢﴾

2. Na nyota zitakapoputika.

وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ ﴿٣﴾

3. Na bahari zitakapofunguliwa na kuchanganyika.

وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ﴿٤﴾

4. Na makaburi yatakapopinduliwa.

عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ ﴿٥﴾

5. Nafsi wakati huo itajua ilichokitanguliza na ilichobakisha nyumba.

يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ ﴿٦﴾

6. Ewe mwanadamu! Ni nini kinachokughuri kwa Mola wako Mtukufu.

الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ ﴿٧﴾

7. Ambaye amekuumba, akakukamilisha, akakulinganisha?

فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاءَ رَكَّبَكَ ﴿٨﴾

8. Akakufanya kwa Sura aliyoipenda.

كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ ﴿٩﴾

9. Hapana sio hivyo! Bali mnayakadhibisha malipo.

وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ ﴿١٠﴾

10. Na hakika mna wenye kuwatunza.

كِرَامًا كَاتِبِينَ ﴿١١﴾

11. Watukufu wenye kuandika.

يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ ﴿١٢﴾

12. Wanajua mnayoyatenda.

يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ ﴿١٢﴾

13. Hakika watu wema watakuwa katika neema.

وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ ﴿١٤﴾

14. Na hakika watu waovu watakuwa katika moto.

يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ ﴿١٥﴾

15. Watauingia siku ya malipo.

وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ ﴿١٦﴾

16. Wala hawatakuwa mbali nao.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٧﴾

17. Ni lipi la kukujulisha ni ipi siku ya malipo.

ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٨﴾

18. Kisha ni lipi la kukujulisha ni ipi siku ya malipo?

يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْئًا وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّـهِ ﴿١٩﴾

19. Ni siku ambayo nafsi haitamilikia chochote nafsi nyengine , na amri siku hiyo ni ya Allah (peke yake).

UBAINIFU

Sura inajulisha siku ya Kiyama kwa kutaja baadhi ya alama zake zenye kulazimiana nayo na zenye kuambatana nayo. Inakisifu hicho Kiyama kwa yale yatakayotukia ndani ya siku hiyo; ambayo ni kukumbuka mtu alilolitanguliza na aliloliacha nyuma katika amali zake njema na mbaya - ambayo yamehifadhiwa na malaika wanaohusika nayo - na kulipwa amali yake. Akiwa ni mwema, basi atalipwa wema na akiwa ni mwovu mwenye kukadhibisha siku ya malipo, basi atalipwa moto atakaouingia hali ya kudumu humo. Kisha inaanzia tena kusifu hiyo siku; kwamba ni siku ambayo nafsi haitamilikia nafsi nyengine kwa chochote na amri siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu. Sura hii imeshuka Makka bila ya ubishi wowote.

Aya Ya 1

Aya hii iko kama aya inayosema: "na mbingu zitapasuka, basi siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa ." (69:16).

Aya Ya 2

Kupukutika nyota yaani kutawanyika kwa kuondoka sehemu zake zilipowekwa. Zimefananishwa nyota na lulu zilizotungwa ushanga, kisha ukakatika uzi wake, zikapukutika na kutawanyika.

Aya Ya 3

Yaani nahari zitafunguliwa kwa kuondoka kizuizi na yachanganyike maji ya tamu na ya chumvi na kuwa bahari moja. Haya ndiyo maana yanayosabiana na tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu. "Na bahari zitakapofurika " (82:6).

Aya Ya 4

Katika Majmau amesema neno Buuthirat lina maana ya kupindua chini juu. Kwa hivyo maana yake ni utakapogeuzwa mchanga wa makaburi na kugeuzwa ndani nje ili kuwatoa wafu na kufufuliwa kwa ajili ya malipo.

Aya Ya 5

Makusudio ya kujua hapa ni kujua kwa upambunuzi matendo yake aliyoyatenda duniani. Na haya sio kuwa yanapatikana kwa kupewa kitabu la! Mwenyezi Mungu anasema: "Bali mtu ni shahidi juu ya nafsi yake ingawa anatoa nyudhuru zake " (78:15).

"Siku atakayokumbuka mtu alichokitenda ". (79:35).

"Siku ambayo kila nafsi itakuta mema iiyoyafanya yamedhuhurishwa na pia ubaya ilioufanya ". (3:30).

Makusudio ya nafsi ni jinsi ya nafsi yoyote, na makusudio ya ilichokitanguliza, ni kile ilichokifanya katika uhai wake. Na kile ilichokibakisha nyuma ni kile ilichokianzia ikiwa kheri au shari na kikafanywa baada ya kufa kwake huandikwa katika karatasi ya amali yake. Mwenyezi Mungu anasema: "..na tunaliandikia kile walichokitanguliza (bila ya kuacha athari) na (kile walichokifnya kikaacha) athari zao ". (36:12) Inasemekana kuwa makusudio ya aya ni kile ilicho kifanya mwanzo wa umri wake na kile ilichokifanya mwisho wa umri wake. Kwa hiyo inakuwa ni fumbo la uchunguzi zimesemwa maana nyengine ambazo hazihitaji kutajwa hapa. Mwenye kuzitaka na ajipatie vitabu vilivyorefushwa tafsiri.

Aya Ya 6-8

Ni lawama na kumkemea mtu. Makusudio ya mtu hapa ni yule mwenye kukadhibisha siku ya malipo kama unavyofahamisha mzunguuko mzima wa maneno unaokusanya "Bali nyinyi mnakadhibisha malipo". Na kuikadhibisha siku ya malipo ni kufuru na kukanusha sheria ya malipo, na kuikanusha kwake ndio kukanusha ubwana wa Mwenyezi Mungu S.W.T. Msemo umeelekezwa kwa mtu kwa kuwa yeye ni mtu ili iwe ni hoja kwa kuthibiti mambo yaliyotajwa ya neema zinazohusikana naye kama mtu. Amefungamanisha kuhadaika na sifa mbili za ulezi wake na ukarimu wake Mwenyezi Mungu (s.w.t), ili iwe ni hoja katika kuelekeza lawama. Kwani hakika mwenye kulewa, akimwasi mlezi wake ambaye anaangalia mambo yake na kumfunika na neema zake ndani na nje, ni ukafiri usiokuwa na shaka katika ubaya wake na katika kustahiki kwake adhabu, hasa akiwa mlezi ni karimu asiyetaka kulipwa chochote katika neema yake na anachokitoa, anayesamehe makosa yanayotukia kwa kutojua. Basi ikiwa hivyo ukafiri wakati huo utakuwa mbaya zaidi, na shutuma na lawama zitakuwa kali zaidi. Kwa hivyo aya ya (6) ni swali la kukemea analokemewa mtu kwa sababu ya ukafiri, hasa usiokuwa na udhuru, nao ni ukafiri wa kukufuru neema ya Mola wake aliyekarimu.

Hawezi mtu kujibu kwa kusoma "Ewe Mola wangu umenihadaa ukarimu wako" kwani Mwenyezi Mungu amekwishayapitisha aliyoyahukumulia na kumfikishia mtu kupitia kwa ulimi wa Mitume yake; kama alivyosema; "Kama mkishukuru nitawazidishieni, na kama mkikufuru, (jueni) kuwa adhabu yangu ni kali sana." (14:7).

"Ama aliyepetuka mipaka. Akapendelea zaidi maisha ya dunia. Basi moto ndio makazi yake ." (79:39).

Zaidi ya hizo kuna aya nyenginezo zinazoelezea kwamba hakuna kuokoka kwa wale wenye kufanya inadi na adhabu; na ukarimu hautawafikia siku ya Kiyama. "Na rehema yangu inaenea kila kitu, lakini nitawaandikia wale wanaojikinga na yale niliyoyakataza ". (7:156) Lau kungemtosheleza mtu mwenye kuasi kusema "umenihadaa ukarimu wako" basi angeliepuka na adhabu kafiri mwenye kufanya inadi, kama itakavyoondolewa kwa muumini aliyeasi. Wala hapana udhuru baada ya ubainifu.

Aya Ya 7

Ni ubainifu wa ulezi wake wenye kuwa pamoja na ukarimu, kwani ni katika kuangalia kwake vizuri kumuumba mtu kwa mafungu yake yote na kumfanya sawa kwa kuweka kila kiungo mahali pake panaponasibiana nacho; kisha akalinganisha baadhi ya viungo vyake na akavitia nguvu kwa baadhi ya viungo vyengine kwa kufanya wizani na ulinganifu kati yao. Kwa hivyo kiungo hakiwezi kukidhoofisha kuingo chengine; kama vile kula kwa kumega tonge ambako ni kwa ajili ya mdomo na mdomo nao unalikata tonge na kulitafuna, hilo linatimia kwa meno tofauti, halafu inahitajika kulipeleka tonge katika pembe za mdomo na kuligeuza, na kazi hiyo inafanywa na ulimi. Na mdomo katika kula unahitaji kuwekewa chakula, hilo linafanywa na mkono na kazi hiyo inatimizwa na kiganja na kufanya kazi kwake ni kwa vidole vyenye manufaa tofauti. Mkono nao unahitaji kuchukua na kuweka mahali na hilo linafanywa na mguu. Ni kama hivyo kazi za viungo vyengine. Ni maelfu kwa maelfu yasiyohisabika katika mipango yake Mwenyezi Mungu, ambaye anayafanya yote hayo bila ya kutaka kujinufaisha au kumzuia yeye mambo ya mtu ya kusahau shukrani na kuikufuru neema. Yeye Mwenyezi Mungu ni Mola Mkarimu.

Aya Ya 8

Ni ubainifu wa kauli yake "Akakulinganisha sawa" yaani katika Surah yoyote aliyopenda akakufanya - wala hataki ila lile lenye hekima - akakufanya mke na mume, mweupe na mweusi, mrefu na mfupi, mzuri na mbaya na mwenye nguvu na mnyonge na mengineo. Vile vile viungo vyenye kushurikiana kati ya watu kwa namna tofauti mfano mikono miwili , miguu miwili na macho mawili. Pia kichwa na kiwiliwili na kulingana sawa kimo nk. Yote hayo ni katika kulinganisha baadhi ya viungo na vyengine. Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika tumemuumba mwanadamu katika hali nzuri mno ." (95:4). Yote hayo yanaishilia kwenye mazingatio mazuri yake Mola hakuna utengenezaji wa mtu katika hilo.

Aya Ya 9

Ni kuzuia kughurika mtu na ukarimu wa Mwenyezi Mungu na kulijaalia hilo ni wasila wa kufuru na uasi, yaani msighurike hakutawafaa kughurika.

Aya Ya 10 - 12: Ni ishara ya kwamba amali za mtu zitahudhurishwa na ni zenye kuhifadhiwa siku ya Kiyama kwa njia nyengine isiyokuwa kukumbuka kwake mtu. Njia ambayo ni kwa kuandika waandishi wa amali katika malaika wenye kuwakilishwa kwa mtu kwa kumchukulia hisabu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na tutamtolea siku ya Kiyama daftari (iliyoandikwa amali yake) atakayoikuta imekunjuliwa (aambiwe) soma daftari yako, nafsi yako leo inakutosha kukuhisabu ". (17:13-14).

Kwa hivyo kusema kwake Mwenyezi Mungu : "Na hakika wenye kuwatunza" Yaani hakika mna wenye kuwatunza kutoka kwetu wanaohifadhi amali kwa kuziandika. Kusema kwake "watukufu wenye kuandika" yaani wenye utukufu na enzi mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Imekaririka katika Qur'an tukufu kuwasifu Malaika kwa utukufu, na hilo sio mbali kuwa makusudio yake kwa kusaidiwa na mpangilio wa maneno, ni kuwa wao kimaumbile ni wenye kuhifadhiwa na madhambi na maasi.

Hilo linatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Bali (hao Malaika) ni waja waliotukuzwa. Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake ". (21:26-27).

Hilo linafahamisha kuwa wao hawataki isipokuwa analolitaka Mwenyezi Mungu, wala hawafanyi ila waliloamrishwa na Mwenyezi Mungu. Vile vile kauli yake: "Watukufu watenda njema ". (80:16).

Makusudio ya kuandika ni kuandika amali kwa kukutanisha na kauli yake wanajua mnayoyafanya. Kauli yake Mwenyezi Mungu: wanajua mnayoyafanya ni kukanusha makosa yao katika kuihusisha heri na shari kama ilivyotangulia aya ya kuwaepusha na madhambi na maasia, wao ni wenye kuzunguukwa na matendo kama yalivyo na sifa zake, lakini ni wenye kuhifadhiwa nayo. Imekuja katika tafsiri ya aya: "Hakika Qur'an ya Al-Fajiri inashuhudiwa (na Malaika) ". (17:78).

Kwamba waandishi wa amali wa mchana wanapanda nayo, baada ya kutua jua na wanashuka wengine wanaadhika amali ya usiku mpaka Al-Fajiri wanapande na wanashuka Malaika wa mchana na kadhalika.

Aya Ya 13 -14

Ni maelezo yanayobainisha natija ya kuhifadhi amali kwa kuandikwa na waandishi nayo ni kudhihiri siku ya Kiyama. Wema ni wale wenye amali njema na waovu ni wale wenye dhambi.

Aya Ya 15

Dhamiri ni ya moto; yaani waovu watalazimiana nao siku ya malipo.

Aya Ya 16

Inaungana na aya iliyotangulia, inatilia nguvu maana ya kulazimiana nao na moto na kukaa kwao milele. Makusudio ya kutokuwa mbali nao ni kutotoka humo. Aya hii iko katika maana ya aya inayosema: "wala hawatakuwa wenye kutoka motoni ". (2:167).

Aya Ya 17

Ni utisho na kulikuza jambo la siku ya malipo; yaani haiwezi kujulikana nini hakika ya siku ya malipo. Hii ni ibara ya fumbo la kulikuza jambo.

Aya Ya 18

Ni kutilia mkazo ukubwa wake.

Aya Ya 19

Ni ubainifu wa kijumla wa hakika ya siku ya malipo. Hilo ni kwamba athari zote zenye kufungana na sababu za dhahiri ni zenye kukatika, kama kunavyofahamisha kusema kwake Mwenyezi Mungu: "na yatakatika mafungamano yao ". (2:166).

Kuhusu kusema kwake "na amru siku hiyo ni ya Allah" yaani yeye ni mwenye kumiliki amri si mwengine; kama alivyosema: "Leo ufalme ni wa nani" Ni wa Allah mmoja mwenye kushinda " (40:16).

Kusema kuwa neno Amr lina maana ya jambo hakuafikiani. Na mahali hapa.

Utafiti Wa Hadith Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu kusema kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t) "Na makaburi yatakapopinduliwa" amesema yatapasuka na watatoka watu. Katika Durril Manthur ametoa Hakim na akaisahihisha kutoka kwa Hudhayfa amesema: "Amesema Mtume(s.a.w.w) : Mwenye kuanzisha heri ikafuatwa atakuwa na malipo mfano wa malipo ya wanaomfuata bila ya wao kupungukiwa. Na mwenye kuanzisha shari ikafuatwa basi atapata dhambi zake na dhambi za mfano wa wanaomfuata bila ya wao kupungukiwa. Akasoma Hudhayfa "Itajua nafsi na ilichokitanguliza na ilichokibakisha nyuma". Katika hiyo hiyo Durril Manthur ametoa Abd bin Hamid kutoka kwa Saleh bin Miswar amesema: "Imenifikilia mimi habari kwamba Mtume(s.a.w.w) amesoma aya hii: "Ewe mwanadamu! Ni nini kinachokughuri kwa Mola wako Mtukufu; kisha akasema ni ujinga wake ".

Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu "Akakufanya kwa sura yoyote aliyopenda" anasema: Lau angetaka angekufanya sura isiyokuwa hii. Katika hiyo hiyo Tafsiri kuhusu "na hakika mna wenye kuwatunza" amesema: "Ni Malaika wawili wawakilishi kwa mtu." Kutoka kwa Saad Assu'ud ni kwamba hao Malaika wawili wanamjia Muumin wakati wa swala ya Al-Fajiri wakishuka wale wengine wa usiku huondoka, linapotua jua hushuka wale wa usiku na kuondoka wa mchana. Hiyo inakuwa ni ada yao mpaka anapofikiwa na mauti yake wakati yakifikia mauti yake husema hao Malaika wawili kumwambia mtu mwema: "Allah akulipe uliyosuhubiana nasi kwa kheri, amali ngapi njema umetuonyesha! Kauli ngapi nzuri umetusikilizisha! Na ni vikao vingapi vya kheri umetupeleka! Basi leo sisi tuko juu ya lile unalolipenda na waombezi kwa Mola wako."

Akiwa ni asi (muovu) humwambia: "Mungu akulipe uliyesuhubiana nasi kwa shari, ulikuwa ukituudhi, ni amali ngapi mbaya ulizotuonyesha! Ni kauli ngapi mbovu ulizotusikilizisha! Na ni vikao vingapi viovu ulivyotupeleka! Basi sisi leo tuko juu ya lile unalolichukia na mashahidi mbele za Mola wako." Katika Majmau kuhusu "Na amri siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu" amepokea Amr bin Shamr kutoka kwa Jabir naye kutoka kwa Abu Jaffar(a.s) amesema: "Amri siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu na siku yote ni ya Mwenyezi Mungu. Ewe Jabir siku ya Kiyama mahakimu wote watakomea, hatabakia hakimu isipokuwa Mwenyezi Mungu."

Makusudio yake Imam ni kwamba, kuwa amri ni ya Mwenyezi Mungu, hakuhusika na siku ya Kiyama tu, bali amri ni ya Mwenyezi Mungu milele, na kuihusisha na siku ya Kiyama, ni kwa kuzingatia kudhihiri hiyo amri na wala sio asili yake yaani kudhihiri kwa kuonekana; siku hiyo hakutakuwa na amri ya mwengine yoyote isipokuwa Yake Yeye Mtukufu.

8

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA MUTAFFIFIN (WAPUNGUZAJI VIPIMO) (NA. 83)

Aya ya 1-21

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ ﴿١﴾

1. Ole wao wenye kupunguza (vipimo).

الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ ﴿٢﴾

2. Ambao wakijipimia kwa watu kwa pishi hujikamilishia.

وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ ﴿٣﴾

3. Na wanapowapimia wao kwa pishi au kwa mizani, hupunguza.

أَلَا يَظُنُّ أُولَـٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ ﴿٤﴾

4. Jee, hawadhani hao kuwa watafufuliwa?

لِيَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥﴾

5. Katika siku kubwa.

يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦﴾

6. Siku ambayo watu watasimama mbele ya Mola wa viumbe.

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ ﴿٧﴾

7. Si hivyo! Hakika maandishi ya watu waovu yamo katika Sijjin.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ ﴿٨﴾

8. Ni lipo la kukujulisha nini hiyo Sijjin.

كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٩﴾

9. Ni daftari iliyoandikwa (amali za watu waovu).

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١٠﴾

10. Ole wao siku hiyo wenye kukadhibisha.

الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿١١﴾

11. Ambao hukadhibisha siku ya malipo.

وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ ﴿١٢﴾

12. Wala haikadhibisha ila kila mpetuka mipaka mwingi wa madhambi.

إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣﴾

13. Ambaye anaposomewa aya zetu husema: ni ngano za watu wa kale.

كَلَّا بَلْ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٤﴾

14. Si hivyo! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao waliyokuwa wakiyachuma.

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ ﴿١٥﴾

15. Si hivyo! Hakika wao siku hiyo watazuiliwa kupata rehema ya Mola wao.

ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ ﴿١٦﴾

16. Kisha wao wataingia motoni.

ثُمَّ يُقَالُ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿١٧﴾

17. Kisha wataambiwa: Hili ndilo ambalo mlikuwa mkilikadhibisha.

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ ﴿١٨﴾

18. Si hivyo! Hakika maandishi ya watu wema yamo katika Illiyyin?

وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ ﴿١٩﴾

19. Ni lipi la kukujulisha ni nini Illiyyin?

كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٢٠﴾

20. Ni daftari iliyoandikwa (amali za watu wema).

يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ ﴿٢١﴾

21. Ambayo hushuhudiwa na wenye kukurubishwa.

UBAINIFU

Sura inaanzia kwa kutoa makamio kwa wale wenye kupunguza vipimo katika pishi au mizani na kuwaonya kwamba wao watafufuliwa kwa ajili ya malipo katika siku iliyokuwa kubwa, nayo ni siku ya Kiyama. Kisha inafafanua yale yatakayowapitia siku hiyo waovu na wema. Inavyonasibu zaidi kwa kuangalia mpangilio ni kuwa mwanzo wa Sura unaoelezea makamio kwa wenye kupunguza kipimo, umeshuka Madina. Ama aya zinazofuatia mpaka mwisho wa Sura zinakubali kufungamana na mpangilio wa Makka na Madina.

Aya Ya 1

Ni makamio juu ya wanaopunguza vipimo. Mwenyezi Mungu amelikataza hilo, na ameliita ufisadi katika nchi, kama alivyolielezea katika kauli ya Mtume Shuayb. "Na enyi watu wangu! Timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu wala msiwapunguzie watu vitu vyao, wala msieneze uovu katika nchi mkafanya ufisadi ." (11:85).

Aya Ya 2-3

Madhumuni ya aya zote mbili ni shutumu ya aina moja; hayo ni kwamba wao wanachunga haki yao tu! Na wala hawachungi haki ya wengine. Kwa maneno mengine, hawachungi haki za wengine, kama vile wanavyochunga haki zao. Jambo hilo linaleta ufisadi katika jamii ya watu iliyojengwa juu ya uadilifu na haki. Haikutajwa mizani katika aya ya 2 kama ilivyotajwa katika aya ya 3 kwa sababu imesemwa kuwa wapunguzaji vipimo aghlabu walikuwa wakinunua nafaka na mazao, kisha wanachuma, kwa kuyauza kidigo kidogo. Desturi yao ilikuwa zaidi ni kunuliwa kwa pishi, sio kwa mizani ndio ikatajwa pishi peke yake katika aya ya pili. Imesemwa kuwa haikutajwa mizani kwa sababu mizani na pishi ni za kununua na kuuza, ikitajwa moja yao, inatosha kufahamisha juu ya nyengine na yale yaliyotajwa katika pishi yanapita pia katika mizani. Njia hiyo haiwezi kuepuka kuangaliwa vizuri. Imesemwa kuwa aya mbili zinaelezea mazoea waliyokuwa nayo wale ambao Sura imetereshwa kwa sababu yao. Walikuwa wakinunua kwa pishi tu! Na wakiuza kwa mizani na pishi. Njia hii ni madai yasiyokuwa na dalili. Mengi yametajwa kwa njia ya kufupisha juu ya pishi ambayo hayaepukani na udhaifu.

Aya Ya 4-5

Ni swali la kukanusha na kustaajabu. Kuishiria wenye kupunguza vipimo kwa neno "hao" nikuishiria kwa umbali, kwa maana ya kuwa kwao mbali na Rehema ya Mwenyezi Mungu. 'Siku kubwa' ni siku ya Kiyama. Kutosheka kutaja ufufuo kwa kudhani tu, pamoja na kuwa ni wajibu kuitakidi kwa kujua na sio kwa kudhani, ni kwamba, kudhania hatari katika amali yoyote kunawajibisha kuepuka kuifanya amali hiyo hata kama haikujulikana. Kwa hiyo kudhania ufufuo katika siku kubwa ambayo atawaadhibu Mwenyezi Mungu watu kwa yale waliyoyachuma kunakataza kufanya dhambi kubwa ambayo itawajibisha adhabu yenye machungu. Imesemekana kuwa dhana hapa ni kwa maana ya kujua. Aya Ya 6: Makusudio ya kusimama ni fumbo la kuwa kwao hai baada ya kufa, ili waende kwenye hukumu yake Mwenyezi Mungu.

Aya Ya 7 -10

Ni kupinga yale waliyokuwa nayo katika kupunguza vipimo na kughafilika na ufufuo na hisabu. Kuhusu maana ya Sijjin mwenye kuangalia vizuri na kufikiri katika mpangilio wa aya nne, kwa kupima baadhi yake na nyengine na kupima mkusanyiko wake na mkusanyiko wa Illiyyin mpaka kutimia aya nne, ni kwamba makusudio ya Sijjin ni mkabala wa makusudio ya Illiyyin na neon Illiyin linatokana na neno Alaa yaani "juu" kwa hiyo Sijjin ina maana ya chini na kufungika; kama inavyoonyesha kauli yake Mwenyezi Mungu: "Kisha tukamrejeza chini ya waliochini (95:5).

Karibu zaidi ni kuwa maana yake ni jela kwa maana ya kufunga. Makusudio ya maandishi ya watu waovu ni yale aliyowakadiria Mwenyezi Mungu katika malipo na kuyathibitisha kwa hukumu yake. Tunayoyapata katika aya, ni kwamba yule ambayo ameyathibitisha Mwenyezi Mungu katika malipo yao au aliyowaandalia yako katika jela ambayo atafungwa mwenye kuiingia kifungo kirefu au milele.

Maana ya neno Marquum kama alivyosema Raghib ni hati nene. Na imesemwa ni kupanga kitabu. Na neno lake Mwenyezi Mungu ni lenye kuchukua njia zote mbili. Maana ya pili ndiyo yenye kunasibiana zaidi. Kwa hivyo inaishia kwamba maana yake ni kuwa, yale waliyoandikiwa ni yenye kubainishwa; yasiyokuwa na utatanishi wowote. Yaani hukumu ni lazima haibadiliki. Na imefahamika kuwa ni yenye kuhukumiwa wao, yenye kuthibitishwa na yenye kufafanuliwa bila utatanishi wowote. Kauli yake Mwenyezi Mungu: "Ole wao siku hiyo wenye kukadhibisha", ni kuwatakia shari waovu. Yaani na waanagamie waovu,- ambao ni wale wenye kukadhibisha siku hiyo yatahakikika yale aliyowaandikia Mwenyezi Mungu na kuwahukumia malipo. Haya ndiyo yanayofahamika kutokana na kuangalia vizuri (Tadabbur) aya hizi nne, nazo zina mpangilio mmoja wenye kuafikiana.

Watu wana kauli mbalimbali katika tafsiri ya matamko na jumla za aya hizi nne kama vile kuwa maana ya neno kitab ni maandishi ya matendo yao. Na imesemwa ni kuandika na kwamba kuna neno lilioondolewa kukadiria kwake ni: 'hakika kuandika amali ya watu waovu ni katika Sijjin. Imesemwa neno " hakika waovu" ni lenye kuenea zaidi kuliko wenye kukadhibisha kwa sababu linakusanya ukafiri na ufasiki. Na wamesema: " makusudio ya Sijjin ni ardhi ya saba chini, huweka maandishi ya watu waovu." Na imesemwa ni bonde katika Jahannam. Pia imesemwa ni shimo katika Jahannam na imesemwa ni jina la kitabu chao. Imsemwa Sijjin ya kwanza ni mbali ambapo panawekwa kitabu chao na Sijjin ya pili ni jina la kitabu chao. Imesemwa ni kitabu chenye mkusanyiko wa amali mbovu za majini na watu. Imesemwa ni hasara na utwezo. Wamesema kuwa aya ya (9) sio tafsiri ya Sijjin bali ni tafsiri ya kitabu kilichotajwa katika aya ya (7). Lakini ukiangalia vizuri utakuta nyingi za kauli hizi ni kujiamulia tu bila ya dalili yoyote.

Aya Ya 11

Ni tafsiri ya aya iliyotangulia. Kwa dhahiri makusudio ya kukadhibisha ni kukadhibisha kwa kauli iliyowazi, kwa hivyo inahusika na kuwatusi makafiri, wala haiwachanganyi mafasiki katika watu wa imani pia haihusiki na yeyote mwenye kupunguza kipimo bali ni makafiri katika wao. Hayo yanatiliwa nguvu na aya inayofuatia. Lakini kama ikikusudiwa kukabidhisha kimatendo, itakuwa inakusanya waovu katika wenye imani, kama vile ambavyo huenda hayo yanatiliwa nguvu na aya ya (4) "Je, hawadhani hao kuwa watafufuliwa?"

Aya Ya 12

Inajulikana kuwa kizuizi pekee cha maasi si kuamini ufufuo na malipo. Na mwenye kung'ang'ania kwenye matamanio, na kuufungamanisha moyo wake kwa kupetuka mipaka katika dhambi, inakataa nafsi yake kusalimika na kujizuia na yanayokatazwa na kuishia kukadhibisha ufufuo na malipo. Mwenyezi Mungu anasema: "Kisha ulikuwa mwisho wa wale waliofanya ubaya ni kuzikadhibisha aya za Allah na walikuwa wakizicheza shere " (30:10).

Aya Ya 13

Makusudio ya aya za Qur'an, kwa kuunganisha na neno "wakisomewa". Maana yake ni wakisomewa aya za Qur'an ambazo zinawahadharisha na maasi na kuwaonya kwa ufufuo na malipo, husema ni ngano za watu wa kale.

Aya Ya 14

Ni kupinga yale waliyoyasema wenye kukadhibisha kuwa ni ngano za watu wa kale. Anasema Raghib: Rana ni kitu inayokuwa juu ya kitu safi. Mwenyezi Mungu anasema: "Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao" yaani hilo limekuwa kama kutu juu ya usafi wa moyo, wakapofuka kujua kheri na shari. Kuwa waliyokuwa wakiyachuma ni kutu juu ya nyoyo zao nikuwa dhambi ni kizuwizi cha kuipata haki kama ilivyo. Katika aya yanadhiri mambo yafuatayo:

Kwanza : Kwamba amali mbaya zina nakshi na picha.

Pili : Kwamba nakshi hizo na picha hizo zinazuiya nafsi kuipata haki kama ilivyo na kuiwekea kizuwizi. Tatu: Kwamba tabia ya mwanzo ya nafsi ni usafi unaotambua haki kama ilivyo na kuipambanua na batili na kupambanua kati ya twaa na maasia Mwenyezi Muungu amesema: "Na (kwa) nafsi na aliyelingamanisha akaifahamisha maasia yake na twaa yake ".(91:7-8).

Aya Ya 15

Ni kukataza kuchuma madhambi yenye kuweka kizuwizi kati ya moyo na kuipata haki. Makusudio ya kuwa wao ni wenye kuzuiliwa na Mola wao siku ya Kiyama, ni kizuiliwa na utukufu wa ukaribu na cheo. Huenda makusudio ni yale aliyoyasema msemaji: "hakika makusudio, ni kuwa wao ni wenye kuzuiliwa na Rehema ya Mola wao". Ama kuondoka kizuizi kwa maana ya kuondoka sababu zenye kuwa kati yake Mwenyezi Mungu na viumbe vyake na maarifa yenye kutimia ya kumjua Mwenyezi Mungu, hilo linapatikana kwa kila mtu. Mwenyezi Mungu amesema: "..na watajua kwamba Allah ni haki iliyodhahiri ."(24:25).

Aya Ya 16

Yaani wataingia na kubaki ndani yake au watafukizwa joto lake kama walivyofasiri wengineo.

Aya Ya 17

Ni kuaibisha. Na mwenye kuyasema hayo ni mtunzaji wa moto au watu wa peponi.

Aya Ya 18-20

Illiyyin ni juu na inafungamana na daraja za juu na vyeo kama vile ambavyo kinyume chake ni Sijjin. Maana ya aya tatu hizi ni mfano wa maana ya aya tatu zilizotangulia ambazo zinakabiliana nazo (aya ya 7, 8 na 9).

Kwa hivyo maana ni kwamba yale ambayo yameandikwa kwa ajili ya watu wema na kuhukumuliwa kuwa ni malipo ya wema wao, yako katika Illiyyin. Ni lipi la kukujulisha nini Illiyyin? Ni jambo lenye kuandikwa na lenye kuandikwa na lenye kupitishwa kwa hukumu ya mkato iliyowazi bila ya uficho. Watu wana kauli nyingi kuhusu aya hizi kama ilivyo katika zile zilizotangulia, isipokuwa miongoni mwa kauli kususu Illiyyin ni kwamba hiyo ni mbingu ya saba chini ya arshi ambako kuna roho za waumini. Na imesemwa ni Sidratul-Muntaha ambako kunaishia amali. Imesemwa ni ubao wa zabarjadi ulioko chini ya arsh, wenye kutungikwa na wenye kuandikwa amali.

Aya Ya 21

Yenye kunasibu zaidi kutokana na maana ya aya zilizotangulia ni kuwa maana ya kushuhudia ni kuona na wenye kukurubishwa ni watu wa peponi, walio na daraja ya juu zaidi kuliko watu wema wote, kama yatakavyokuja maana ya aya ya 28.

Makusudio ya kuona ni kuoneshwa na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu amesema mfano wa hayo kuhusu moto. "Si hivyo! Lau mngejua ujuzi wa yakini. (Msingejishughulisha na hayo). Hakika mtauona moto ". (102:56). Katika hilo inadhihiri kuwa wenye kukurubishwa ni watu ya yakini. Imesemwa kuwa kushuhudia ni kuhudhuria na wenye kukurubishwa ni Malaika. Makusudio yake ni kuhudhuria Malaika kwenye maandishi ya amali zao wanapoyapeleka kwa Mwenyezi Mungu. Imesemwa wenye kukurubishwa ni watu wema na Malaika wote. Kauli hizo mbili zina muweko wa kuwa makusudio ya kitabu ni maandishi ya amali. Lakini umekwisha elezwa udhaifu wake.

Utafiti Wa Hadith Katika Tafsiri ya Qummi katika Riwaya ya Abul-Jarud kutoka kwa Abu Jaffar(a.s) amesema: Iliteremshwa Sura ya Al-Mutwaffifin kwa Mtume(s.a.w.w) wakati alipofika Madina, wakati huo wakazi wa hapo walikuwa ni waovu zaidi ya watu wote kwa kipimo na wakawa wazuri. Katika Kafi kwa isnadi yake kutoka kwa Abu Hamza Ath-Thimali amesema: "Nimemsikia Abu Jaffar(a.s) , akisema: "Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametuumba katika watu walio juu zaidi wa Illiyyin. Akaumba nyoyo za wafuasi wetu katika lile tuliloumbiwa sisi isipokuwa viwiliwili vyao. Kwa hivyo nyoyo zao zinapondokea kwetu, kwa sababu zimeumbwa kutokana na lile tuliloumbiwa sisi, kisha akasoma aya hizi (18, 19, 20 na 21). Na ameumba nyoyo za maadui zetu kutoka katika Sijjin na akaziumba nyoyo za wafuasi wao kutokana na lile waliloumbiwa wao isipokuwa viwiliwili vyao, kwa hiyo nyoyo zao zinapondekea kwao kwa sababu zimeumbiwa lile waliloumbiwa wao;" kisha akasoma aya hizi (7, 8, 9, na 10).

Imepokewa hadith mfano wa hiyo katika Kafi kwa njia nyengine kutoka kwa Athimali naye kutoka kwa Abu Jaffar(a.s) .

Na amepokea mfano wake katika Ilalish-Sharaii kutoka kwa Zaid Ash-Shahham kutoka kwa Abu Abdillahi. Na Hadith - kama unavyoona - inatilia nguvu yale tuliyoyatanguliza kuyaeleza katika maana ya aya. Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Hakika maandishi ya watu waovu yamo katika Sijjin", anasema : yale aliyowaandikia Mwenyezi Mungu katika adhabu yamo katika Sijjin. Katika hiyohiyo Tafsiri ya Qummi katika riwaya ya Abul-Jarud kutoka kwa Abu Jaffar(a.s) amesema: "Sijjin ni ardhi ya saba na Illiyyin ni mbingu ya saba ".

Lau riwaya hiyo ni sahihi basi itakuwa pepo na moto ziko pande mbili ya juu na ya chini. Kwa hiyo iko haja ya kuangalia vizuri riwaya hiyo; kama vile kuhisabu kaburi kuwa ni bustani ya peponi au ni shimo la Jahannam, na kuhisabu jangwa la Barhut kuwa ni mahali pa Jahannam. Katika Durril Manthur ametoa Ibn Al-Mubarak kutoka kwa Said bin Al-Musayyib amesema: "Salman alikutana na Abdallah bin Salaam, akasema mmoja wao kumwambia mwenzake ukifa kabla yangu njoo uniambie aliyokufanyia Mola wako nami nikifa kabla yako nitakuja kukupa habari. Akasema Abdalla vipi itakuwa? Akasema ndio hakika roho za waumini zinakuwa katika Barzakh katika ardhi zinakwenda popote zinapotaka na za makafiri zitakuwa katika Sijjin, na Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi."

Katika Usulul-Kafi kwa isnadi yake kutoka kwa Zurara naye kutoka kwa Abu Jaffar(a.s) amesema: "Hakuna mja yoyote ila katika moyo wake kuna doa jeupe, akifanya dhambi kutokea doa jeusi, akitubia huondoka huo weusi, akiendelea na dhambi, huzidi weusi mpaka unafunika weupe. Ukifunikwa weupe, mwenye moyo huo hawezi kurudi kwenye heri milele. Na hiyo ndiyo kauli yake Mwenyezi Mungu: "Si hivyo! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao waliyokuwa wakiyachuma".

Imepokewa hadith kwa maana haya katika Durril Manthur kutoka kwa maswahaba kadhaa, kutoka kwa Abu Huraira naye kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) . Katika hiyo hiyo Durril Manthur kwa isnadi yake kutoka kwa Abdalla bin Muhammad Al-Hajjal kutoka kwa baadhi ya maswahaba zetu amesema: "Amesema Mtume(s.a.w.w) kumbushaneni, kutaneni na zungumzeni, kwani mazungumzo ni usafi wa moyo. Hakika nyoyo zinashika kutu kama unavyoshika kutu upanga na usafi wake ni mazungumzo.

Kutoka kwa Rawdhatul-Waidhiya amesema: "amesema Al-Baqir(a.s) : "Hakika kitu kinachoharibu moyo kama makosa. Hakika moyo unapofanya makosa basi huendelea kuwa nayo mpaka uyashinde." Amesema Mtume(s.a.w.w) : Hakika muumin akifanya dhambi kunakuwa na doa jeusi katika moyo wake akitubia na kutka msamaha hukwatuka, akizidi na dhambi nalo huzidi. Hiyo ndiyo kutu aliyoitaja Mwenyezi Mungu aliposema: "Si hivyo! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao waliyokuwa wakiyachuma ".

Aya 22-36

إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿٢٢﴾

22. Hakika watu wema watakuwa katika neema.

عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ ﴿٢٣﴾

23. Wakiwa juu ya malili wanatazama.

تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ ﴿٢٤﴾

24. Utaona katika nyuso zao kunyinyirika kwa neema.

يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ ﴿٢٥﴾

25. Watanyweshwa mvinyo wenye kufunikwa.

خِتَامُهُ مِسْكٌ وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ ﴿٢٦﴾

26. Mwisho wake (ni) miski na katika hayo nawashindane wenye kushindana.

وَمِزَاجُهُ مِن تَسْنِيمٍ ﴿٢٧﴾

27. Na cha kuchanganyia ni Tasnim.

عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ ﴿٢٨﴾

28. Chemchemi ambayo hunywewa na wenye kukurubishwa.

إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ ﴿٢٩﴾

29. Hakika wale ambao wamefanya makosa walikuwa wakiwacheka wale walioamini.

وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ ﴿٣٠﴾

30. Na walipokuwa wakiwapitia wakikonyezana.

وَإِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمُ انقَلَبُوا فَكِهِينَ ﴿٣١﴾

31. Na walipokuwa wakirudi kwa watu wao wakirudi huku wakiona raha.

وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَضَالُّونَ ﴿٣٢﴾

32. Na walipokuwa wakiwaona wakisema: "Hakika hawa wamepotea!"

وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ ﴿٣٣﴾

33. Wala hawakupelekwa wao kuwatunza.

فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ ﴿٣٤﴾

34. Basi leo wale ambao wameamini wanawacheka makafiri.

عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ ﴿٣٥﴾

35. Wakiwa juu ya malili wanatazama.

هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٣٦﴾

36. Ja, makafiri wamelipwa kwa waliyokuwa wakiyafanya.

UBAINIFU

Ni ubainifu ulio na baadhi ya ufafanuzi wa utukufu wa cheo cha watu wema na ukubwa wa daraja yao mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kwamba wao kwa kuwa walikuwa wakidharauliwa na makafiri na kuchekwa na wao watawacheka na kuangalia adhabu wayoipata.

Aya Ya 22

Neno Naim lina maana nyingi. Yaani hakika watu wema watakuwa katika neema nyingi zisizoweza kusifiwa.

Aya Ya 23

Malili ni viti vya enzi vya kifahari vyenye kupambwa. Kutaja kutazama tu; Bila ya kusema ni kutazama kitu gani, kunatilia nguvu kuwa ni kutazama mandari ya pepo yenye kufurahisha na neema zilizomo. Imesemwa kuwa makusudio ya kutazama hapa ni kutazama yale wanayolipwa makafiri.

Aya Ya 24

Hayo anaambiwa Mtume(s.a.w.w) . Na hukumu ni yenye kuenea kwa wote; kwa maana kila mwenye kuangalia kwenye nyuso zao ataona kwenye nyuso zao kupendeza, kwa neema waliyonayo.

Aya Ya 25

Ni mahali pake kusifiwa kwa sifa ya kufungwa kwa vizibo, kwa sababu huzibwa kitu kisafi ili kisalimike na hadaa yoyote na kuchanganyika na kitu kitakachokiharibu.

Aya Ya 26

Imesemwa maana yake ni kufungwa kwake miski badala ya udongo. Na imesemwa maana yake ni kuwa mwisho wa ladha anayoipata mnywaji ni harufu ya miski. Kuhusu kauli yake "nawashindane wenye kushindana" ni kuvutiwa kuyapata yale yaliyosifiwa katika mvinyo wenye kufungwa. Neno "Na katika hayo" ni kusisitiza kuvutia kwa kuihusisha hukumu baada ya kuieneza. Maana yake: Nawashindane wenye kushindana katika neema ya pepo na katika mvinyo wenye kufunikwa ni watu mahsusi ambao watakunywa.

Aya Ya 27

Tasnim kutokana na inavyofasiriwa na aya inayofuatia ni mto katika pepo ambao Mwenyezi Mungu ameuita Tasnim. Temko Tasnim lina maana ya kunyanyua na kujaza.

Aya Ya 28

Aya hii inafahamisha kuwa wenye kukurubishwa watakunywa Tasnim bila ya kuchanganywa. Hayo yanafahamisha haya yafuatayo:

Kwanza : Kwamba Tasnim ni bora kuliko mvinyo wenye kufungwa ambao unazidi tamu kwa kuchanganywa na Tasnim.

Pili : Kwamba wenye kukurubishwa wana daraja ya juu zaidi kuliko wema waliotajwa katika aya (mbali mbali).

Aya Ya 29

Mpangilio unaeleza kuwa makusudio ya wale ambao wameamini ni wale watu wema wenye kusifiwa katika aya, wametajwa wale ambao wameamini kwa sababu imani yao ndiyo sababu ya kuchekwa na kudharauliwa na makafiri na wametajwa makafiri kwa sifa ya wale ambao wamefanya makosa, kwa kuwa huko kuwacheka wale walioamini ni katika makosa.

Aya Ya 30

Yaani wanakonyeza kwa kuonyesha dharau.

Aya Ya 31

Neno Fakihu lina maana ya furaha iliyozidi kiasi yaani baada ya kuwacheka wenye kuamini wanarudi hali ya kuona raha na kufurahi kwa waliyoyafanya. Au linatokana na Fakaha lenye maana ya mazungumzo ya kupumbaza, kwa maana ya kuwa wakirudi kwa jamaa zao wanazungumzia waliyoyafanya hali ya kupumbazika.

Aya Ya 32

Wanawaona wamepotea kwa njia ya kuona au kuwahukumia tu! Kuwa wamepotea.

Aya Ya 33

Yaani hawakupeleka hao makafiri kuwa wawachunge waumini, na kuwahukumia katika haki yao kwa wanavyotaka wao. Aya hii ni kuwaumbua wenye kuwafedhehesha waumini.

Aya Ya 34

Makusudio ya keo, ni siku ya malipo. Na wale ambao wamefanya makosa kuwaita makafiri ni kurudia hakika ya sifa yao.

Aya Ya 35-36

Neno thawabu kwa asili lina maana ya malipo ijapokuwa linatumiwa zaidi katika kheri. Kwa ujumla maana ya aya ni wake ambao wameamini watakuwa katika vyandarua wakiangalia malipo ya makafiri malipo ya matendo yao waliyokuwa wakiwafanyia katika dunia kama kuwacheka kukonyezana wanapowapitia na kurudi kwa jamaa zao hali yakufurahi baada ya kuyafanya hayo na kusema kwao "Hakika hawa ni wenye kupotea".

Utafiti Wa Hadith Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu kusema kwake Mwenyezi Mungu "Na katika hayo na washindane wenye kushindana" amesema: Ni katika tuliyoyataja miongoni mwa thawabu anazozitafuta Muumin. Katika Majmau kuhusu kusema kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t) "Na walipokuwa wakiwapitia wakikonyezana." Imesemwa imeshuka kwa Ali bin Abutwalib(a.s) na kundi la waislamu waliokuwa wakielekea kwa Mtume(s.a.w.w) wakadharauliwa na wanafiki, wakawacheka, na wakakonyezana; kisha wakarudi kwa watu wao wakaambia tumemwona kipara tukamcheka; Ndio ikashuka aya hiyo kabla ya kufika Ali(a.s) na wenzake kwa Mtume(s.a.w.w) . Hadithi hiyo imepokewa kutoka kwa Muqatil na Kalbi.

Imepokewa hadithi hiyo katika Kash shaf. Katika hiyo hiyo Kash shaf ametaja Al-Hakim Abul-Qassim Al-Hasakani katika kitabu Shawahidu tanzil kutoka kwa Abu Swaleh naye kutoka kwa Ibn Abbas amesema: "Hakika wale ambao wamefanya makosa ni wanafiki wa Kiquraish na wale 'ambao wameamini' ni Ali bin Abu-Twalib na wenzake."


9

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA INSHIQAAQ (KUPASUKA)( NA: 84)

INA AYA 24

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾

1. Mbingu zitakapopasuka.

وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٢﴾

2. Zikamtii Mola wake na zikafanya ndivyo.

وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ ﴿٣﴾

3. Na ardhi itakaponyooshwa.

وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ ﴿٤﴾

4. Ikatupa vilivyomo na ikawa tupu;

وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٥﴾

5. Ikamtwii Mola wake na ikafanya ndivyo.

يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ ﴿٦﴾

6. Ewe mwanadamu: Hakika wewe ni mwenye kufanya juhudi mpaka (kufikilia) kwa Mola wako; basi ni mwenye kukutana naye.

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ ﴿٧﴾

7. Ama atakayepewa kitabu chake kwa kuumeni kwake.

فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ﴿٨﴾

8. Atahisabiwa hisabu nyepesi.

وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا ﴿٩﴾

9. Awarejee (atarudi kwa) watu wake huku akiwa na furaha.

وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ ﴿١٠﴾

10. Ama atakayepewa kitabu chake nyuma ya mgongo wake.

فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا ﴿١١﴾

11. Yeye atauita ole wake.

وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا ﴿١٢﴾

12. Aingie na motoni.

إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا ﴿١٣﴾

13. Maana yeye alikuwa kati ya watu wake (ulimwenguni) ni mwenye furaha.

إِنَّهُ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ ﴿١٤﴾

14. Kwa kudhaani kwamba hatarejea (kwa Mola wake).

بَلَىٰ إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا ﴿١٥﴾

15. Kwani? Hakika Mola wake alikuwa akimjua.

فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ ﴿١٦﴾

16. Naapa kwa mawingu mekundu.

وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ ﴿١٧﴾

17. Na usiku na ulichokikusanya.

وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ ﴿١٨﴾

18. Na mwezi unapotimia.

لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ ﴿١٩﴾

19. Mtakutana na hali baada ya hali.

فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠﴾

20. Basi wananini hao hawaamini.

وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ ﴿٢١﴾

21. Na wanaposomewa Qur'an hawanyenyekei.

بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ ﴿٢٢﴾

22. Bali wale ambao wamekufuru hukadhibishwa.

وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ ﴿٢٣﴾

23. Na Allah ni mjuzi wa waliyoyakusanya.

فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢٤﴾

24. Basi wape habari ya adhabu yenye uchungu.

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٢٥﴾

25. Ila wale ambao wameamini wakatenda amali njema (wao) watapata malipo mema yasiyokoma.

UBAINIFU

Sura inaishiria kusimama Kiyama na inakumbusha kwamba mtu ni mwenye kwenda kwa Mola wake mpaka akutane naye atamuhisabu kwa mujibu wa kitabu chake. Sura hii inatilia mkazo jambo hilo na pia imesisitiza zaidi upande wa maonyo kuliko ule na biashara. Mpangilio wa aya ni wa Makka.

Aya Ya 1

Ni sharti ambalo jawabu lake limeondolewa kukadiria kwake ni: Mbingu zitakapopasuka, mtu atakutana na Mola wake atahisabiwa na kulipwa yale aliyoyatenda. Kupasuka kwa mbingu ni katika alama za Kiyama kama kukunjwa jua, kukutana jua na mwezi, kupuputika nyota, n.k.

Aya Ya 2

Kusikiliza ni fumbo, maana yake ni kutii na kufuata. Kufanya ndivyo: ni kufanya ndivyo huko kumtii na kufuata; yaani zikamtii Mola wake na zikafanya ndivyo kumtii na kumfuata.

Aya Ya 3

Kwa dhahiri makusudio ni kufanywa pana ardhi; Mwenyezi Mungu anasema: "Siku ambayo ardhi hii itabadililishwa kuwa ardhi nyengine ." (14:48).

Aya Ya 4

Yaani itatupa vilivyomo ndani yake katika wafu na kuwa tupu. Imesemwa kuwa makusudio ni kutupa wafu na hazina; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na ikatoa ardhi mizigo yake " (99:2) Imesemwa maana ni kutupa vilivyo ndani yake nakuwa tupu na vitu vilivyo juu yake miongoni mwa majabali na bahari. Huenda maelezo ya kwanza ndiyo yaliyo karibu zaidi na maana.

Aya Ya 5

Dhamiri hapa ni ya ardhi na maana ni kama yaliyotangulia katika mbingu.

Aya Ya 6

Anasema Raghib maana ya neno Kad-h ni kwenda na kufanya juhudi. Na imesemwa maana yake ni juhudi ya nafsi katika amali. Kwa hivyo maana itakuwa ni kwenda, kwa dalili ya herufi ila yenye maana ya mpaka. Kauli ya: "basi ni mwenye kukutana naye" (kuwa katika hukumu yake) inaungana na neno kad-h. Mwenyezi Mungu amebainisha kwa neno hii (Kad-h) kwamba ukomo na mwenendo huu na mahangaiko haya ni kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), kwa kuwa yeye ndiye Mola Mlezi. Yaani, kwa kuwa mtu ni kiumbe mwenye kulelewa, kumiliki na mwenye akili, daima ni mwenye kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kawa sababu yeye ndiye Mola wake mwenye kupanga mambo yake. Mja hajiamulii mwenyewe alitakalo au alifanyalo. Yeye anao uwezo wa kutaka, lakini anafanya tu lile alilolitaka Mwenyezi Mungu na kumwamuru alifanye, sababu yeye ndiye bwana wake. Hivyo mja anachukua jukumu la aliyoyapenda na kuyatenda.

Kwa hivyo hapa yanadhihiri mambo haya:

Kwanza : "Hakika wewe ni mwenye kufanya juhudi mpaka (kufikilia) kwa Mola wako" ni hoja huu ya marejeo ya Kiyama kwa vile ulivyo kuwa ubwana hautimii ila pamoja na jukumu na utumwa, wala hautimii utumwa ila pamoja na jukumu na halimtii jukumu ila kwa kurejea na kuhisabiwa na hakutimu kuhisabiwa ila kwa malipo.

Pili : Kwamba makusudio ya kukutana naye ni kuishia kwake, ambako hakuna hukumu isipokuwa hukumu yake bila ya kuweko kuziwizi chochote.

Tatu : Mwenye kuambiwa ni jinsi ya mtu yeyote, hivyo ulezi wa Mungu ni wenye kuenea kwa kila mtu.

Aya Ya 7

Ni ufafanuzi wa mpangilio juu ya yale yalioelezewa na aya iliyotangulia, kwamba kuna marejeo na maswali juu ya amali na hesabu, na makusudio ya kitabu ni karatasi ya matendo (amali).

Aya Ya 8

Hisabu nyepesi ni ile iliyosahilishwa na ikawa haina malumbano yoyote.

Aya Ya 9

Makusudio ya watu wake hapa ni wale aliomwanadalia Mwenyezi Mungu katika pepo miongoni mwa Hurulaini, watumishi, n.k. Haya ndiyo yanayofahamika kutokana na mpangilio wa aya. Imesemwa kuwa makusudio ni jamaa zake waumini atakaoingia nao peponi, Imesemwa kuwa waumini hata kama sio jamaa zake; kwa sababu waumini wote ni ndugu. Njia zote mbili haziepukani kuwa ziko mbali zaidi na maana.

Aya Ya 10

Huenda ikawa kupewa vitabu vyao nyuma ya migongo yao ni kwa sababu ya kugeuzwa nyuso zao visogoni mwao kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "..kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni. ." (4:47).

Hapana mgongano kati ya kupewa vitabu vyao nyuma ya migongo yao na kupewa kushotoni mwao; kama ilivyo katika kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Ama atakayepewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto. Basi atasema Oo! Laiti nisingelipewa daftari langu ."(69:25).

Yatakuja maelezo zaidi kuhusu maana ya kupewa kitabu nyuma ya migongo katika utafiti wa hadith (Inshallah).

Aya Ya 11

Yaani atakaposema kitabu chake ataita "Oo kuangamia.

Aya Ya 12

Yaani moto wenye joto kali ambao hauna mfano kwa adhabu yake wala hauna kiasi kwa joto lake.

Aya Ya 13

Yalimfurahisha yale aliyokuwa akiyapata katika starehe za dunia na kuvutika na anasa za dunia. Hilo lilimsahaulisha mambo ya akhera. Mwenyezi Mungu anaishutumu furaha ya mtu kutokana na kheri za dunia anazozipata na ameiita furaha pasi na haki. Anasema Mwenyezi Mungu baada ya kuutaja moto na adhabu yake: "Haya (yaliyowapata) ni kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafurahia duniani pasi na haki na yale mliyokuwa mkijivunia ." (40:75)

Aya Ya 14

Makusudio ni kurejea kwa ajili ya hisabu na malipo. Hakuna kinachomsababisha kudhania hivyo isipokuwa kujiingiza katika dhambi kunakopelekea kuona kufufuliwa ni jambo lisilo wezekana.

Aya Ya 15

Ni jibu la dhana yake; kwamba sio hivyo anavyodhania, kwani hakika Mwenyezi Mungu(s.w.t) ndiye Mola wake na mfalme wake mwenye kuzingatia jambo lake. Anamjua na kuona yote aliyokuwa akiyafanya katika matendo yake. Na matendo yake yana malipo mema au mabaya. Kwa hiyo hapana budi kurudi kwake na amlipe yale yanayostahiki matendo yake. Kwa hali hiyo inadhihiri kuwa kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Hakika mola wake alikuwa akimwona" ni katika kutoa hoja juu ya kupasa marejeo; aya hii ni kama ile iliyotangulia katika kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Hakika wewe ni mwenye kufanya juhudi mpaka (kufikilia) kwa Mola wako."

Vile vile inadhihiri kutokana na mkusanyiko wa aya hizi tisa, kwamba utoaji wa vitabu ni kabla ya hisabu kama kunavyofahamisha kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Na kila mtu tumemfungia vitendo vyake shingoni mwake; na tutamtolea siku ya Kiyama daftari atakayoikuta imekunjuliwa. (Ataambiwa), Soma daftari yako, hii leo nafsi yako inatosha kukuhisabu ." (17;13).

Aya Ya 16

Ni wekundu unaofuatiwa na manjano kisha weupe ambao unatokea magharibi mwanzo wa usiku

Aya Ya 17

Yaani kukusanya vile vilivyotawanyika wakati wa mchana miongoni wa watu na wanyama kwani wao hytawanyika mchana na kurudi katika makazi yao usiku na kutulia. Baadhi wamefasiri neno Wasaq kwa maana ya kufukuza yaani usiku unazifukuza nyota kutoka katika kujificha kwenda kwenye kudhihiri.

Aya Ya 18

Yaani kukusanyika nuru yake na kuwa mwezi mtimilifu.

Aya Ya 19

Ni jawabu la kiapo. Makusudio yake ni mtakutana na hali baada ya hali kwa namna yoyote yatakavyokuwa masafa anayoyakata mtu katika kufikia kwa Mola wake, kutoka katika maisha ya dunia, kisha mauti kisha maisha ya Barzakh, kisha kwenda akhera kisha maisha ya akhera kisha hesabu na malipo. Kiapo - kama unavyoona - ni kutilia mkazo yale yalio katika aya ya 6 na yaliyo baada yake katika hanari za ufufuo Aya hii pia inaonyesha kuwa vipindi anavyopitia mtu ni vyenye kupangwa katika kumfikia Mola wake.

Aya Ya 20 -21

Ni swali la kustaajabu na kutayarisha, kwa hiyo limeoana na mgeuko huu wa ghafla kutoka kwenye mazungumzo ya ana kwa ana na kuwa anamzungumzia mtu mwingine asiyekuwepo; kana kwamba yeye alipowaona kuwa hawaidhiki kwa waadhi wake, aliachana nao na kumwelekea Mtume kwa kumwambia: "wana nini hao hawaamini"

Aya Ya 22-24

Yaani hawakuacha imani kwa sababu ya upungufu wa ubainifu, au kwisha dalili, bali wao wamefuata majadi wao na viongozi wao, wakazama katika kufuru na wakaendelea na kukadhibisha. Mwenyezi Mungu anayajua waliyoyakusanya katika nyoyo na waliyoyaficha katika nyoyo zao, miongoni mwa ukafiri na ushirikina. Imesemwa kuwa makusudio yake ni kuwa wana kitu walichoficha katika nyoyo zao ambacho hakiwezi kuelezwa kwa ibara yoyote: Hakijui isipokuwa Mwenyezi Mungu tu! Lakini maelezo hayo yako mbali na mpangilio wa aya. Kuita maonyo ya adhabu kuwa ni biashara hii ni namna Fulani ya mabezo. Jumla hii ni fungu la (malipo ya) kukadhibisa.

Aya Ya 25

Hapo wanavuliwa na hayo walio amini.

Utafiti Wa Hadithi Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu "mbingu zitakapopasuka" amesema ni siku ya Kiyama. Katika Durril-Manthur ametoa Ibn Abu Hatim kutoka kwa Ali amesema : Itapasuka mbingu hii yenye nyota. Katika Tafsiri ya Qummi: Na ardhi itakaponyooshwa, ikatupa vilivyomo, na ikawa tupu, amesema itanyooshwa ardhi itapasuka wa watatoka watu. Katika Durril Manthur ametoa Hakim kwa isnadi nzuri kutoka kwa Jabir naye kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) amesema: itanyooshwa ardhi siku ya Kiyama kama inavyonyooshwa ngozi kisha mwanadamu hatakuwa na mahali isipokuwa mahali pa nyayo zake.

Katika Ihtijaj kutoka kwa Ali(a.s) katika hadith amesema: watu siku hiyo watakuwa na sifa na daraja mbali mbali. Kuna katika wao atakayehisabiwa hisabu nyepesi na kurudi kwa watu wake huku akiwa na furaha, na katika wao kuna ambao wataingia peponi bila ya hisabu kwa sababu hawakuvaana na jambo lolote la dunia. Hii ni kwa sababu kisabu huko ni kwa wale waliovaana na dunia. Na muka katika wao watakaohisabiwa hisabu isiyopungua hata chembe na kuwa katika adhabu ya moto mkali.

Katika Maani kwa isnadi yake kutoka kwa Ibn Abu Jaffar(a.s) amesema: Amesema Mtume(s.a.w.w) kila mwenye kuhisabiwa ni mwenye kuadhibiwa akaambiwa: "Basi nini maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) "Atahisabiwa hisabu nyepesi?" Akasema: Hilo ni kwa kusamehe. Imepokewa hadith mfano wa hiyo katika Durril Manthur kutoka kwa Bukhari, Muslim, Tirmidhi na wengineo kutoka kwa Aisha.

Katika Tafsir ya Qummi katika riwaya ya Abul-Jarud kutoka kwa Abu Jaffar(a.s) kuhusu kauli yake Mwenyezi Mungu: "Ama atakayepewa kitabu chake kwa kuumeni kwake" yeye ni Abu Salama Abdulla bin Abdul-Aswad bin Hilal Al-Makhzumi. "Ama mwenye kupewa kitabu chake nyuma ya mgongo wake" ni ndugu yake ambaye ni Al-Aswad bin Abdul-Aswad Al-Makhzumiy aliyeuliwa na Hamza bin Abdul-Muttalib siku ya vita vya BAdr.

Katika Majmau kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mtakutana na hali baada ya hali". Amesema: Maana yake ni shida baada ya shida ya uhai kisha mauti, kisha kufufuliwa, kisha malipo. Hadithi hiyo imepokewa marfui. Katika Jawaamiul-Jami kuhusu aya hiyo hiyo, kutoka kwa Abu Abayadah: Mtakutana na desturi ya waliokuwa kabla yenu na hali zao. Na yamepokewa hayo kutoka kwa Imam Sadiq(a.s) .


10

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA BURUJ (BURUJI) (NA. 85)

INA AYA 22

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa mbingu zenye buruji.

وَالْيَوْمِ الْمَوْعُودِ ﴿٢﴾

2. Na siku iliyotolewa kiaga.

وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ ﴿٣﴾

3. Na shahidi na chenye kushuhudiwa.

قُتِلَ أَصْحَابُ الْأُخْدُودِ ﴿٤﴾

4. Wamelaaniwa wenye handaki.

النَّارِ ذَاتِ الْوَقُودِ ﴿٥﴾

5. (Lenye) moto wenye kuni.

إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌ ﴿٦﴾

6. Walipokuwa pambizoni mwake wamekaa.

وَهُمْ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ بِالْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌ ﴿٧﴾

7. Na wao, kwa yale wanayowatendea wenye kuamini washuhudia.

وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَن يُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿٨﴾

8. Wala hapana lililowachukiza kwao ila kwamba walimwamini Allah. Mwenye kushinda Mwenye kusifiwa.

الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٩﴾

9. Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi. Na Allah ni mwenye kushuhudia kila kitu.

إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ ﴿١٠﴾

10. Hakika wale ambao wanawaudhi waumini wanaume na wanaumini wanawake, kisha wasitubie watapata adhabu ya kuungua.

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْكَبِيرُ ﴿١١﴾

11. Hakika wale ambao wameamini wakatenda amali njema, watapata mabustani yanayopita mito chini yake; huko ndiko kufaulu kukubwa.

إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ ﴿١٢﴾

12. Hakika mashiko ya Mola wako ni makubwa.

إِنَّهُ هُوَ يُبْدِئُ وَيُعِيدُ ﴿١٣﴾

13. Hakika Yeye ndiye anayeanza na kurejeza

وَهُوَ الْغَفُورُ الْوَدُودُ ﴿١٤﴾

14. Naye ndiye Mwingi wa kusamehe, Mwenye mapenzi.

ذُو الْعَرْشِ الْمَجِيدُ ﴿١٥﴾

15. Mwenye ufalme mkubwa.

فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ ﴿١٦﴾

16. Mwingi wa kutenda alipendalo.

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْجُنُودِ ﴿١٧﴾

17. Jee, imekujia habari ya majeshi.

فِرْعَوْنَ وَثَمُودَ ﴿١٨﴾

18. (Ya) Firaun na Thamud.

بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي تَكْذِيبٍ ﴿١٩﴾

19. Lakini ambao wamekufuru wamo katika kukadhibisha.

وَاللَّـهُ مِن وَرَائِهِم مُّحِيطٌ ﴿٢٠﴾

20. Na Allah kwa nyuma yao amewazunguka.

بَلْ هُوَ قُرْآنٌ مَّجِيدٌ ﴿٢١﴾

21. Bali hii ni Qur'an tukufu.

فِي لَوْحٍ مَّحْفُوظٍ ﴿٢٢﴾

22. Katika ubao uliohifadhiwa.

UBAINIFU

Sura ya maonyo na biashara, ndani yake mna makamio kikali kwa wale wanaowaadhibu waumini wanaume na waumini wanawake kwa sababu ya kumwamini kwao Mwenyezi Mungu; kama walivyokuwa washirikina wa Makka wakiwafanyia hivyo wale waliomwamini Mtume(s.a.w.w) . Wanawaadhibu ili warudie shirki yao ya kwanza. Wakawa katika wao kuna ambao walikuwa wakisubiri wala hawarudi kwa hali yoyote ile na kuna katika wao walikuwa wakirudi na kurtadi nao ni wale wadhaifu wa imani, kama kunavyoonyesha kusema kwake Mwenyezi Mungu:

"Na katika watu kuna wanaosema: tumemwamini Allah lakini wanapoudhiwa katika (njia ya) Allah hufanya vile vituko vinavyowakuta kwa watu kama ni adhabu ya Allah " (29:10).

Na kusema kwake: "Na katika watu wako wanaomwabudu Allah ukingoni. Ikiwafikia heri hutulia kwayo na ikiwafikia fitina (misukosuko) hubwatika juu ya uso wake (akasunukia, hataki kuuna tena uislamu) ." (22:11). Ametanguliza Mwenyezi Mungu S.W.T. ishara hiyo katika kisa cha wenye handaki, kuwahimiza waumini kuwa na subira katika upande wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) Na akafuatisha kuishiria habari ya askari wa Firaun na Thamud na hilo ni kuituliza nafsi ya Mtume kwa kiaga cha ushindi na kuwatisha wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu.

Sura hii imeshuka Makka kwa ushahidi wa mpangilio wa aya zake.

Aya Ya 1

Neno Buruj lina maana ya kudhihiri, aghlabu kutumiwa kwa jumba kubwa kwa vile linawadhirikia watazamaji. Na jengo lenye kujengwa juu ya ukuta wa mji kwa ajili ya kujikinga huitwa Buruji. Hayo ndiyo makusudio katika aya hii, kutokana na kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Na hakika tumeweka katika mbingu, buruj (vituo vya nyota) na tumezipamba kwa ajili ya wale wanaozitazama ". (15:16).

Basi makusudio ya Buruj ni mahali pa nyota katika mbingu. Kwa hivyo inadhihiri kwamba kutafsiri Buruj kuwa ni nyota 12 zilizokubaliwa katika elimu ya nyota sio sawa. Katika aya kuna kiapo kwa mbingu yenye kuhifadhiwa na buruji na kiapo hicho kinanasibiana sana na kisa kitakachoelezewa. Pia kunafuatia kiapo cha makamio na kiaga.

Aya Na 2

Inaungana na Aya Na kwanza. Siku iliyoagwa ni siku ya Kiyama ambayo Mwenyezi Mungu ametoa kiaga kwa kuhukumu baina ya waja wake.

Aya Na 3

Pia inaungana na aya mbili zilizotangulia. Viapo vyote hivyo viko juu ya yale yaliyokusudiwa kubainishwa katika Sura, nayo-kama ilivyotangulia kuelezwa - ni makamio kikali kwa mwenye kuwaudhi waumini wanaume na waumini wanawake kwa sababu ya imani yao. Na kiaga kizuri kwa wale waliomini na wakatenda amali njema. Ni kama vile kusema: "Ninaapa kwa mbingu zenye buruji" ambazo kwa buruj hizo Mwenyezi Mungu anazikinga mbingu hizo na mashetani, hakika Mwenyezi Mungu anaikinga imani ya waumini ni vitimbi vya mashetani na marafiki zao katika makafiri. "Na ninaapa kwa siku iliyotolewa kiaga ambayo watalipwa watu matendo yao. Na ninaapa kwa shahidi anayeshuhudia matendo ya hao makafiri na vile wanavyowafanyia waumini kwa sababu ya imani yao kwa Mwenyezi Mungu. Na ninaapa kwa kile chenye kushuhudiwa atakachokishuhudia kila mmoja".

Juu ya hivyo basi inakubalika kuwa "Shahid" ni Mtume kwa kushuhudia kwake vitendo vya umma wake, kisha atavitolea ushahidi siku ya Kiyama. Na inakubalika kuwa chenye kushuhudiwa ni adhabu ya makafiri kwa sababu ya hawa waumini na yale waliyofanyiwa katika maudhi. Ukipenda unaweza kusema ni malipo yake au unaweza kusema juu ya yale yatakayotukia siku wa Kiyama katika mateso na thawabu kwa hao madhalimu na wadhulimiwa. Kuna kauli nyingi juu ya tafsiri ya shahidi na chenye kushuhudiwa; baadhi yao wamefikisha kauli thelathini (30). Kama vile kuwa shahidi ni siku ya Ijumaa na chenye kushuhudiwa ni siku ya Arafa, Siku ya Idd na siku ya Arafa, siku ya Arafa na siku ya Kiyama, kuwa shahidi ni Malaika wanaowashuhudia wanaadamu na chenye kushuhudiwa ni siku ya Kiyama, kuwa shahidi ni ni siku ya Kiyama. Na kuwa shahidi ni wale wanaowashuhudia watu na chenye kushudiwa ni wale wanaoshuhudiwa.

Vile vile kuwa shahidi ni umma huu na chenye kushuhudiwa ni umma wengineo. Shahidi ni viungo vya binadamu na chenye kushuhudiwa ni nafsi zao. Shahidi ni jiwe jeusi (Hajarul-Aswad) na chenye kushuhudiwa ni mwenye kuhiji. Shahid ni Mitume na chenye kushuhudiwa ni Mtume Muhammad(s.a.w.w) ni kwamba shahidi ni Mwenyezi Mungu na chenye kushudiwa ni tamko la Lailah illa llah. Pia iko kauli kuwa shahidi ni Mwenyezi Mungu na chenye kushuhudiwa ni siku ya Kiyama. Shahidi ni Adam na kizazi chake na chenye kushuhudiwa ni siku ya Kiyama. Shahidi ni siku ya Tarwiya na chenye kushudiwa ni siku ya Arafa, siku ya Jumatatu na Ijumaa. Shahidi ni wenye kukurubisha na chenye kushuhudiwa ni illiyuuna. Shahidi ni mtoto ambaye alimwambia mama yake. "Subiri hakika wewe uko kwenye haki" katika kisa cha wenye handaki na chenye kushuhudiwa ni tukio lenyewe na kauli kuwa shahid ni Malaika wanaofuatilia kuandika vitendo, na chenye kushudiwa ni Qur'an ya Al-fajr na kauli nyengine nyingi.

Nyingi katika kauli hizi zinachukulia ushahidi kwa maana ya kutekeleza yale yaliyochukuliwa katika ushahidi na baadhi yake zinatofautisha kati ya shahidi na chenye kushuhudiwa katika maana ya ushahidi na umekwishajua udhaifu wake. Linalonasibu zaidi ni kuchukua ushahidi kwa maana ya kuona ijapokuwa unalazimisha maana ya kutekeleza siku ya Kiyama na kwamba ushahidi unakubaliana kufungamana na Mtume(s.a.w.w) . Vipi isiwe hivyo na hali Mwenyezi Mungu amemwita shaahid aliposema: "Ewe Mtume hakika sisi tumekutuma (uwe) shahidi na mtoaji habari nzuri na mwonyaji ". (33:45).

Na amemwita shaahid aliposema: "ili awe Mtume shahidi juu yenu ." (22:78). Kisha jawabu la kiapo limeondolewa linajulishwa na kusema kwake: "Hakika wale ambao wamewaudhi waumini wanaume na waumini wanawake" mpaka mwisho wa aya mbili. Vile vile hilo jawabu la kiapo linafahamishwa na kusema kwake: "Wamelaaniwa wenye handaki ." na hicho ni makamio cha wale wanaoudhi na ni ahadi kwa waumini wema kwamba Mwenyezi Mungu atawawafikisha kwa subira na atawapa nguvu juu ya kuhifadhi imani yao kutokana na vitimbi vya wachimba vitimbi, ikiwa watafanya Ikhlas (kumtakashia Mwenyezi Mungu amali) kama walivyofanya waumini katika kisa cha handaki.

Aya Na 4

Ni ishara ya kisa cha handaki ili iwe ni mwanzo wa yatayokuja katika kauli yake "Hakika wale ambao wamewaudhi " na sio jawabu la kiapo kabisa. Watu wa handaki ni wale waliochimba handaki na kuwasha moto ndani yake, kisha wakawaumuru waumini waingie ndani yake wakawachoma kwa kuwatesa kwa ajili ya imani yao. Na neno Wamelaaniwa ni dua ua kuwaombea laana. Imesemwa kwa makusudio ya watu wa handaki ni waumini wanaume na waumini wanawake waliochomwa ndani ya handaki na kwamba neno Qutila ni kwa maana ya kuuliwa yaani kuuliwa hao waumini kwa kuchomwa, na wala sio dua ya laana. Lakini hayo yanadhoofishwa na kudhihiri dhamiri katika jumla ya walipokuwa pambizoni mwake, wao kwa yale wayatendayo na hapana lililowachukiza kwao. Dhamiri zote hizo haziwezi kuwarudia waumini.

Aya Na 5

Kuusifu moto wenye kuni ni ishara ya kuonyesha ukali wa moto na mwako wake.

Aya Na 6

Pambizoni mwake ni huo moto yaani hao watu makatili wenye kiburi walikuwa wamekaa pambizoni mwa huo moto.

Aya Na 7

Yaani waumini wanaona na kushuhudia kuunguzwa kwao.

Aya Na 8-9

Yaani walichukizwa na imani yao. Kuanzia mwenye kushinda mpaka mwisho wa Aya Na 9 ni sifa zenye kupita katika jina la Mwenyezi Mungu zinazoonesha kuwa hao waumini. Walikuwa juu ya haki katika imani, wenye kudhulumiwa katika waliyofanyiwa, haijifichi hali yao kwa Mwenyezi Mungu na atawalipa malipo mema na kwamba hao makatili walikuwa kwenye batili wenye kumkosea Mwenyezi Mungu, madhalimu kwa waliyoyafanya na wataonja ubaya wa mambo yao. Hilo ni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kushinda, mwenye kusifiwa, yaani yeye ni mshindi asiyeshindika kwa hali yoyote, ni mzuri katika vitendo vyake, ni wake peke yake kila utukufuru na uzuri. Kwa hivyo ni wajibu kumnyenyekea na kutompinga. Ikiwa ni wake ufalme wa mbingu na ardhi basi yeye ni mwenye kumiliki hali zote, amri ni yake na hukumu ni yake, Yeye ni bwana wa viumbe vyote. Hivyo ni wajibu kumfanya ni Mola wa kuabudiwa na kutomshirikisha na yoyote. Basi waumini wako kwenye haki na makafiri wako katika upotevu.

Kisha hakika Mwenyezi Mungu- ambaye ndiye aliyepatisha kila kitu- juu ya kila kitu ni mwenye kushuhudia, hakifichiki kwake kitu chochote katika viumbe vyake wala vitendo vyovyote katika vitendo vya viumbe vyake wala haifichiki hisani na mwenye kufanya hisani au uovu wa mwenye kufanya uovu, atamlipa kila mmoja kwa aliyoyafanya. Kwa ujumla, ikiwa Mwenyezi Mungu mwenye kutukuka ndiye mwenye kusifika na sifa hizi tukufu itakuwa ni juu ya hao waumini kumwamini, na ni jambo lisilotakikana kwa hao maharamia kuwaingilia waumini wala kuwafanyia uovu wowte.

Baadhi ya wafasiri wamesema kuhusu makusudio ya kuleta sifa katika aya: Hao watu ikiwa walikuwa ni washirikina, basi jambo liliokuwa likiwaudhi kutokana na waumini halikuwa ni kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali lilikuwa ni kukanusha yale yasiyokwuwemo katika ibada zao batilifu. Na kama walikuwa ni wakanushaji wa sifa za Mwenyezi Mungu, basilinalowaudhi ni kuthibitisha Mwenye kuabudia wasiyemzoea. Lakini ilivyokuwa makusudio ya mambo yote hayo mawili (kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kukanusha sifa), ni kumkanusha mwenye kuabudiwa kwa haki mwenye kusifika na sifa za uungu na utukufu, basi ndipo zikaletwa ibara za sifa za Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Katika mghafala waliokuwa nao makafiri ambao ni waabudu masanamu, hawakuwa wakinasibisha kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kutengeneza na kupatisha tu! Ama uungu ambao unawajibisha ibala walikuwa wakitosheka na waungu wao tu! Mwenyezi Mungu kwao alikuwa ni Mungu wa waungu tu! Na sio zaidi ya hapo.

Aya Na 10

Neno Fitna hapa ni kwa maana ya misukosuko na adhabu, na hilo linaenea kwa watu wa handaki na makafiri wa kiquraysh waliokuwa wakiwaadhibu wenye kumwamini Mtume(s.a.w.w) katika waumini wanaume na waumini wanawake kwa aina za adhabu ili warudi katika dini yao. Amesema katika Majmau "pameulizwa vipi kutofautisha kati ya adhabu ya Jahannam na adhabu ya kuungua? Pakajibiwa kwamba makusudio yake ni kwamba wao wana aina za adhabu katika Jahannam ambazo sio kuungua mfano Zakkum(mti wa uchungu), maji ya ushaha na marungu, pamoja na hayo watachomwa kwa moto.

Aya Na 11

Kiaga kizuri kwa waumini cha kuzituliza nafsi zao.

Aya Na 12

Aya hiyo na zinazofuatia mpaka kutimia Aya Na saba ni kuhakikisha na kutilia mkazo yaliyotangulia katika makamio na kiaga kwa makafiri na ahadi ya waumini. Kutegemeza neno "Mashiko" Kwa Mola na kutegemeza neno mola kwa dhamiri ya mwenye kuambiwa ni kuituliza nafsi ya Mtume(s.a.w.w) kwa kumpa nguvu na ushindi na kuonyesha kuwa watu wenye kiburi katika umati wake, vile vile wana fungu katika makamio yaliyotangulia kuelezwa.

Aya Na 13

Neno Yubdiu kwa kulilinganisha na Yuid lenye maana ya kurejeza, lina maana ya kuanza. Wamesema halikusikika neno hilo kwa waarabu, lakini kisomo kiko hivyo. Katika baadhi ya visomo vyengine visivyokuwemo katika istihali husomwa kwa fatha ya yei na dali Yabdau. Kwa vyovyote iwavyo aya iko mahali pa ila (sababu) ya ukali wa mashiko yake Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Hilo ni kwamba yeye Mwenyezi Mungu mwenye kutukuka ni mwenye kuanza. Hupatisha kila anachokikusudia kupatisha kwa kuanza bila ya kumtegemea mwengine. Yeye Mwenyezi Mungu atarudisha kila kilichokuwa vile kilivyokuwa. Yeye Mwenyezi Mungu S.W.T hazuiliki na alilokusudia wala halimpiti. Ikiwa ni hivyo, basi yeye ni muweza wa kumchukulia hatua ya adhabu ya zaidi ya uwezo wake yule mwenye kupetuka mpaka wake, na kumhifadhi juu ya yale aliyo nayo, ili aonje adhabu, Mwenyezi Mungu anasema: "Na wale ambao wamekufuru wana wao moto wa Jahannam, hawatahukumiwa kufa, wala kawatapunguziwa adhabu yake " (35:36).

Yeye nu muweza juu ya kurudisha vile vilivyoharibiwa na adhabu katika hali yake ya kwanza, ili aonje mkosaji adhabu bila ya kwisha; Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika wale ambao wamezikanusha aya zetu, tutawaingiza katika moto. Kila ngozi zao zitakapoiva, tutawabadilisha ngozi nyingine ili wawe wanaonja (uchungu wa) adhabu ." (4:56).

Kwa ubainifu huu yanafunuka mamba hAya Na fuatayo:

kwanza : Mpangilio wa kauli yake "Hakika yeye" mpaka mwisho unafahamisha kuwa kuanzisha kupatisha na kurudisha ni kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), kwa sababu matengenezo na kupatisha kunakomea kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) peke yake.

Pili : Mipaka ya vitu vyote iko kwake Mwenyezi Mungu akitaka kitu kisiwe na mpaka, huwa; au kubadilisha mpaka mwengine. Yeye ndiye ambaye ameweka mpaka (ukomo) wa adhabu ya dunia kuwa ni mauti, na lau asingelitaka kuiweka ukomo angefanya kama ilivyo katika ahabu ya akhera. Tatu: Kwamba makusudio ya mashiko makubwa ni kwamba hakuna wa kumzuia Mwenyezi Mungu na adhabu yake wala haukna wa kuipinga hukumu yake vyovyote vile anavyohukumu.

Aya Na 14

Yaani ni mwingi wa maghufira na mapenzi kwa kuangalia ahadi ya waumini; kama ilivyo katika aya iliyotangulia kwa kuangalia kiaga cha makafiri.

Aya Na 15-16

Arshi ni arshi ya ufalme. Kusema: Mwenye arshi ni fumbo la ufalme yaani Yeye ni mfalme anaweza kufanya vile atakavyo katika mamlaka yake. Mwenye kutenda alipendalo yaani haligeuki analolitaka, si kwa sababu ya ndani kama vile uvivu au kuchoka, wala kwa sababu za nje kwa kizuizi kitakachoingia kati yake na kati ya analolitaka. Kwa hivyo anaweza kuwapa kiaga wale waliowaadhibu waumini wanaume na waumini wanawake kwa moto na kuwaahidi wale walioamini na wakatenda amali njema kwa pepo kwa sababu Yeye ndiye mwenye arshi tukufu, wala hawezi kuvunja ahadi yake, kwa sababu Yeye ni mwingi wa kutenda alipendalo.

Aya Na 17-18

Ni tikrari ya yaliyotangulia katika mashiko yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuwa Yeye ni mfalme mkubwa mwenye kutenda alitakalo. Na hilo nikuituliza nafsi ya Mtume(s.a.w.w)

Aya Na 19

Sio mbali kutokana na mpangilio wa aya kuwa makusudio ya wale ambao wamekufuru ni katika kaumu ya mtume Muhammad(s.a.w.w) . Aya inaonyesha kususiwa mauidha yaliyotangulia, yaani haitakikani kutarajia kwao kuamini aya hizi zilizowazi, kwani wale ambai wamekufuru ni wenye kuendelea na kukabidhisha kwao, hawatanufaika na mawaidha au joha.

Aya Na 20

Nyuma ya kitu ni pambizoni mwake mnamokizunguuka. Inaonyesha kawaba wao hawawezi kumshinda Mwenyezi Mungu Yeye ni Mwenye kuwazuguuka ni muweza juu yao kwa kila upande. Na hilo pia ni katika kuituliza nafsi ya Mtume(s.a.w.w) .

Aya Na 21-22

Ni kupinga kuendelea kwao Kuikadhibisha Qur'an. Maana yake nikuwa sio kama wanavyodai, bali Qur'an ni kitabu kikubwa katika maana yake chenye kushinda katika maarifa yake kiko katika ubao wenye kuhifadhiwa na uongo na batili, na yeye ni yenye kuhifadhiwa kuguswa na shetani.

Utafiti Wa Hadith Katika Durril Manthur ametoa Ibnu Murdawayh kutoka kwa Jabir bin Abdillah kwamba Mtume(s.a.w.w) aliulizwa kuhusu mbingu yenye buruji akasema ni nyota. Akaulizwa kuhusu "ambaye amejaaliwa katika mbingu buruji" akasema ni nyota. Akaulizwa kuhusu Buruujum mushayyadah akasema ni majumba makubwa. Katika hiyo hiyo Durril Manthur ametoa Abdu bin Hamid Attrimidhiy na Ibn Abidduniya katika Usuul; Ibn Jariyr, Ibn Al-Mundhir, Ibn Hatim, Ibn Murdawayh na Bayhaqi katika Sunan yake kutoka kwa Abu Huraira amesema: Amesema Mtume(s.a.w.w) : siku iliyoagwa ni siku ya Kiyama na siku yenye kushuhudiwa ni siku ya Arafa na shahidi ni siku ya Ijumaa.

Imepokea hadith mfano wa hiyo kwa njia nyengine kutoka Abu Malik Said Bin Al-Musabbib na Jubayr bin Mut'imu kutoka kwake Mtume(s.a.w.w) ; Shahid ni siku ya Ijumaa na chenye kumshuhudiwa ni siku ya Arafa. Imepokewa kwa tamko hili kutoka kwa Abdurrazzaq, Fariyabiyy, Abdu bin Hamid, Ibn Jariyr na Ibn Mundhir kutoka kwa Ali bin Abu Twalib. Katika hiyo hiyo Durril Manthur ametoa Ahmad bin Hamid, Ibn Al-Mundhir kutoka kwa Ali amesema: siku iliyoagwa ni siku ya kiyama, shahidi ni siku ya ijumaa na chenye kushuhudiwa ni siku ya Idd ((Idd-el-Hajj)

Katika Majmau imepokewa kwamba mtu mmoja alingia katika msikiti wa Mtume(s.a.w.w) mara ikawa mtu mmoja anazungumzia Mtume(s.a.w.w) . Amesema: "nikaamuliza kuhusu Shahid na mwenya "kushuhudiwa", akasema: Ndio shahidi ni siku ya Ijumaa na chenye kushuhudiwa ni siku ya Arafa, nikampita na kumfuata mwengine naye pia anamzungumzia Mtume(s.a.w.w) nikamuuliza hilo, akasema: "ama shahid ni siku ya Arafa na chenye kushuhudiwa ni siku ya Idd." Nikawapita wote hao wawili nikaenda kwa kijana uso wake kama Dinar naye anamzungumzia Mtume(s.a.w.w) , nikamwambia: "nifahamishe kuhusu shahidi na chenye kushuhudiwa", akasema: ndio ama shahidi ni Muhammad na chenye kushuhudiwa ni siku ya Kiyama kwani hukusikia kauli yake Mwenyezi Mungu?: "Ewe Mtume hakika sisi tume kutuma (uwe) shahidi na mtoaji habari nzuri na mwonyaji ?" (33:45)

Akaendelea kusema: hiyo siku ya kukusanya watu, ndiyo siky yenye kushuhudiwa. Nikauliza ni nani yule wa kwanza? Wakasema: ni Ibn Abbas, wapili ni Ibn Amr na watu wakasema ni Hasan bin Ali." Hadith hiyo ni yenye kupokewa kwa njia tofauti na matamko yenye kukurubiana. Imetangulia katika tafsir ya aya kwamba aliyoyasema Hasan(a.s) ndiyo yaliyo wazi zaidi kwa kuangalia mpangilio wa aya, ingawaje tamko la shahidi na chenye kushuhudiwa halikatai kufungamana na jambo jengine vile vile.

Katika Tafsir ya Qummi kuhusu "wamelaaniwa wenye handaki" anasema: sababu yake ni kwamba yule ambaye aliitingisha Uhabeshi kwenye vita vya Yaman ni Dhu Nawas naye ndiye mfalme wa mwisho katika ukoo wa Himyar, aliingia katika dini ya Uyahudi na akawakusanya watu wa kabila ya Himyar na kuwafanya kuufuata Uyahudi. Yeye akajiita Yusuf na alidumu hivyo kwa muda mrefu. Akapata habari kwamba huko Najran kuna watu wamebaki kwenye dini ya Unasara (Ukristo) na wanahukumu kwa Injili na kiongozi wa dini hiyo ni Abdallah bin Baryam. Kwa hiyo akachukuwa watu wa dini yake kuwaendea hao Manasara ili wawaingize katika dini ya Kiyahudi. Alipofika Najran akawakusanya wale waliokuwa katika dini ya Kinasara kisha akawelezea dini ya Kiyahudi na kuwahimiza waingie. Akajadiliana nao na akatoa jitahad zake zote lakini walikataa na wakajizulia kuingia dini ya Kiyahudi.

Basi akafanya handaki, akakusanya kuni na akawasha moto. Kuna katika wao waliounguzwa wengine waliouliwa kwa upanga na akawafanyia vya kufanya, ikafikia iadadi ya waliouawa 20,000 (ishirin elfu). Akawaponyoka mtu mmoja anyeitwa Dawshi Dhu Thaalaban na farasi wake, wakamfuata mpaka akawashinda kwa mbio, akarudi Dhu nuwasi kwa askari wake. Ndio Mwenyezi Mungu akasema "wamelaaniwa wenye handaki mpaka mwisho wa Aya Na 8."Katika Majmau amepokea Said bin Jubayr amesema: waliposhindwa watu wa Isfand-han alisema Umar bin Al-Khattab: wao sio wayahudi wala wanasara wala hawana kitabu chochote na walikuwa ni Majusiy, akasema Ali bin Abi Twalib: Hapana wao walikuwa nacho kitabu, lakini kikaondolewa. Sababu ya kuondokwa kitabu nikwamba mfalme wao siku moja alilewa akamwingilia binti yake au dada yake, ulevi ulipomtoka akamwambia: "Itakuwaje kwa nililyoyanfanya? Akamjibu: "Wakusanye watu na mamlaka yako na uwaambie kwamba wewe unapendekeza watu kuonana na mabinti zao na kwamba wewe unawaamrisha walihalilishe hilo."

Kwa hivyo akawakusanya na akawapa habari ya hilo. Wakakataa kumfuata. Akawachimbia handaki katika ardhi na akawasha moto. Ikawa mwenye kukataa humtupa katika moto na mwenye kukubali humwacha. Imepokewa hadith kwa maana haya katika Durril Manthur kutoka kwa Abd bin Hamid kutokana naye Ali(a.s) . Katika Tafsir ya Iyashi, imepokewa kutoka kwa Jabir(a.s) amesema: Alitumwa Ali(a.s) kwa askofu wa kinajrani kumuuliza kuhusu wnye handaki, akamuelezea, kisha Ali(a.s) akamwambia sio kama ulivyosema, lakini nitakueleza: "Hakika Mwenyezi Mungu alimpa utume mtu mmoja wa Kihabeshi, wakamkadhibisha na kupingana naye. Wakawaua wafuasi wake, wakateka nyara na wafuasi wake. Kisha wakamjengea boma wakalijaza moto.

Wakawakusanya watu wakawaambia: "Ambaye yuko kwenye dini yetu na mambo yetu na ajitenge na ambaye tuko kwenye dini ya hawa na ajitupe mwenyewe moto. Wakawa wafuasi wake wanashindana kujitupa katika moto. Akaja mwanamke na mtoto mdogo wa mwezi mmoja. Alipotaka kujitupa aliogopa na akamuhurumia mtoto wake. Mtoto akanadi: 'usiogope nitupe mimi wa wewe katika moto kwani hakika Wallahi adhabu hii kwa Mwenyezi Mungu ni chache'. Akajitupa katika moto pamoja na mwanawe. Na huyo mtoto akawa miongoni mwa waliozungumza uchangani." Imepokewa hadith kwa maana haya katika Durril Manthur kutoka kwa Ibn Murdawayh, naye kutoka kwa Abdillahi bin Naja naye kutokana na Ali(a.s) . Vile vile imepokewa kutoka kwa Ibn Hatim, Ibn Al-Mundhir katika njia ya Hasan kutokana na Ali(a.s) kuhusu "wenye handaki" amesema hao ni wahabeshi.

Sio mbali kufahamika kwamba hadith ya wenye handaki ni matukio mbali mbali yaliyotukia uhabeshi, Yemen na Uajemi. Ziko hadith zinazozungumzia kisa chake bila ya kutaja mahali maalum pa tukio lenyewe. Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu aya "bali hii ni Qur'an tukufu katika ubao uliohifadhiwa" una ncha mbili kuumeni mwa Arshi kwenye paji la Israfil, anaposema Mwenyezi Mungu ambaye umetukuka utajo wake - wahyi, ubao hupiga paji la Israfil naye huangalia kwenye ubao na kuupeleka wahyi kwa Jibril".

Katika Durril Manthur ametoa Abu Shaykh, na Ibn Murdawayh kutoka kwa Ibn Abbas amesema: 'amesema Mtume(s.a.w.w) : ameumba Mwenyezi Mungu ubao kutokana na lulu nyeupe. Umezungushiwa Zabrajad ya kijani, maandishi yake ni ya nuru, huchunguzwa mara mia tatu na sitini (360) kila siku. Anahuisha na kufisha. Anaumba na kuruzuku. Anatukuza na kudhalilisha na anafanya analotaka.' Riwaya kuhusu Lawh ni nyingi zenye kuhitalifiana, nazo ziko juu ya namna ya kufananisha tu!.


11

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA TARIQ (CHENYE KUJA USIKU) (NA. 86)

INA AYA 17

Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa mbingu na chenye kuja usiku.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الطَّارِقُ ﴿٢﴾

2. Na lipi la kukujulisha ni nini chenye kuja siku.

النَّجْمُ الثَّاقِبُ ﴿٣﴾

3. Ni nyota inayong'ara usiku.

إِن كُلُّ نَفْسٍ لَّمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ ﴿٤﴾

4. Hakuna nafsi isipokuwa kuna mwenye kuitunza.

فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ مِمَّ خُلِقَ ﴿٥﴾

5. Basi mtu na ajitazame ameumbwa kwa kitu gani..

خُلِقَ مِن مَّاءٍ دَافِقٍ ﴿٦﴾

6. Ameumbwa kwa maji yanayotoka kwa nguvu.

يَخْرُجُ مِن بَيْنِ الصُّلْبِ وَالتَّرَائِبِ ﴿٧﴾

7. Yanayotoka baina ya uti wa mgongo na mifupa ya kifua.

إِنَّهُ عَلَىٰ رَجْعِهِ لَقَادِرٌ ﴿٨﴾

8. Hakika yeye ni mweza wa kumrejeza.

يَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ ﴿٩﴾

9. Siku zaitakapofunuliwa siri.

فَمَا لَهُ مِن قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ ﴿١٠﴾

10. Basi hatakuwa na nguvu wala wa kumnusuru.

وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الرَّجْعِ ﴿١١﴾

11. Naapa kwa mbingu yenye kurudi.

وَالْأَرْضِ ذَاتِ الصَّدْعِ ﴿١٢﴾

12. Na ardhi yenye mipasuko.

إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ ﴿١٣﴾

13. Hakika hii (Qur'an) ni kauli yenye kupambanua.

وَمَا هُوَ بِالْهَزْلِ ﴿١٤﴾

14. Wala si upuuzi.

إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا ﴿١٥﴾

15. Hakika wao wanakuchimbia vitimbi.

وَأَكِيدُ كَيْدًا ﴿١٦﴾

16. Nami (pia) ninawachimbia vitimbi.

فَمَهِّلِ الْكَافِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًا ﴿١٧﴾

17. Basi wape muhula makafiri wape muhula kidogo.

UBAINIFU

Katika Sura hii kuna maonyo kwa marejeo ya akhera na kufufuliwa. Na hayo yanafamisha uwezo wake Mwenyezi Mungu. Na inamalizia Sura kwa kueleza kiaga cha makafiri. Sura hii imeshuka Makka bila ya ubishi.

Aya 1-3

Neno Twariq asili yake- kama ilivyosemwa- ni kugonga kiasi cha kutoa sauti, miongoni mwao, ni nyundo na lina maana njia. Njia imeitwa hivyo kwa vile mpita njia anaigonga kwa nyayo zake. Kywa hivyo likaenea neno hilo kutumiwa kwa njia, kisha likahusishwa na kuja usiku, kwa sababu mwenye kuja usiku aghlabu hukuta milango imefungwa, kwa hiyo hugonga, kisha likaenea hilo neno kwa kila chenye kuhidhiri usiku. Makusudio ya neno hilo katika aya ni nyota yenye kutokeza usiku. Neno Thaqb asili yake ni kupasua; kisha likawa ni nuru yenye kuangaza, kwa sababu inapasua giza, na linakuja kwa maana ya kuwa juu kama kusema: imepaa juu ndege, nikama vile inapasua anga kwa kuruka kwake. Kwa hivyo makusudio ya Aya Na kwanza ni kuapa kwa mbingu na nyota inayotokeza usiku. Na Aya Na pili ni kwa ajili ya kulikuza jambo la chenye kuapiwa ambacho ni hicho chenye kutokeza usiku. Aya Na tatu ni ubainifu wa hicho chenye kutokeza usiku. Jumla hiyo ni jawabu ya swali.

Aya Na 4

Ni jawabu la kiapo. Herufi Lamma ni kwa maana ya illa (isipokuwa). Makusidio ya kutunza hapa ni kuandika matendo yake mema na maovu, ili yaweze kuhisabiwa siku ya Kiyama na kulipwa. Kwa hivyo mtunzaji ni malaika na chenye kutunzwa ni matendo, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na hakika mna wenye kuwatunza watukufu wenye kuandika ." (82:10-11).

Sio mbali kuwa makusudio ni kutunza nafsi dhati yake na vitendo vyake, kwa hiyo inafahamisha kuwa nafsi ni zenye kutunzwa hazimaliziki kwa mauti wala haziharibiki mpaka Mwenyezi Mungu atakapovifufua viwiliviwili, atavirudisha nafsi na atakuwa mtu kama alivyokuwa mtu wa duniani kwa dhati yake; kisha alipwe kwa mujibu wa vitendo vyake vyenye kuchungwa, vikiwa ni kheri au shari. Hilo linatiliwa nguvu na aya nyingi zinazofahamisha juu ya kutunzwa vitu, kama vile kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Sema atawaua Malaika wa mauti aliye wakilishwa kwenu kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu. " (32:11).

"Allah huzichukua roha wakati wa mauti yake na zile zisizokufa katika usingizi wao. Basi huzizuwiya zile alizozihukumia mauti. ." (39:42).

Hayo hayakanushi dhahiri ya Aya Na Sura ya (82:10).

kuwa kutunza kwa Malaika ni kuandika, kwa sababu kuitunza nafsi pia kutokana na kuandika kama anavyofahamisha Mwenyezi Mungu kwa kusema: "Hakika sisi tulikuwa tukiandika yale aliyokuwa mkiyatenda ." (45:29).

Kwa njia hii kunabatilika kutia makosa juu ya yale yanayofahamisha juu ya marejeo ya Kiyama katika kuenea Kudura, kwamba kumrusisha mtu kwa dhati yake ni muhali kwa sababu mtu ataumbwa tena mara ya pili mfano wa yule mtu wa duniani aliyeumbwa kwanza, lakini si yule yule na mfano wa kitu sio kitu chenyewe. Njia ya kubatilisha hoja hiyo ni kwamba: utu wa mtu unatokana na mtu kwa nafsi yake sio kwa kiwilikiwili chake na nafsi ni yenye kihifadhiwa kwa hivyo akiumba kiwilikiwili na kukifungamanisha na nafsi atakuwa ndiya yule yule mtu wa duniani kwa utu wake, ijapokuwa sio dhati yake.

Aya Na 5

Yaani aangalie nini mwanzo wa umbile lake? Na ni kitu gani ambacho Mwenyezi Mungu amekifanya kuwa mtu? Jumla hii ni mtiririko wa aya iliyotangulia. Maana yanavyofahamisha kutokana na mpangilio wake, ni kwamba, ikiwa kila nafsi ni yenye kuhifadhiwa kwa dhati yake na vitendo vyake, bila ya kwisha hiyo nafsi na kusahauliwa vitendo vyake basi akubali mtu ukweli kwamba yeye atarudi kwa Mola wake na kulipwa aliyoyatenda, wala hilo asilihisabu kuwa ni mbali. Naangalie ukweli huu kwenye asili ya umbile lake na akumbuke kwamba yeye ameumbwa kwa maji yanayoka kwa nguvu yanayotoka baina ya uti wa mgongo na mifupa ya kifua. Basi yule aliyeanza kumuumba kutokana na maji haya anaweza kumrudisha na kumuhuisha baada ya mauti.

Aya Na 6

Maji yenye kutoka kwa kuruka ni manii. Jumla hiyo iko katika jawabu la swali.

Aya Na 7

Neno Sulb lina maana ya mgongo na Taraib ni mifupa wa kifua. Wamehitalifiana kiajabu kwenye matamko yao katika aya hii na iliyo kabla yake. Kwa dhahiri makusudio yake ni sehemu iliyokatikati ya uti wa mgongo na mifupa ya kifua.

Aya Na 8

Yaani ambaye amemuumba mtu kutokana na maji, sifa yake ni hiyo hiyo, ni mwenye kuweza kumrudisha na kumuhuisha baada ya mauti.

Aya Na 9: Ni siku yatakayofichuka yale alioyoyaficha mtu na kuyafanya siri katika itikadi na matendo ya kheri au ya shari. Aya hii iko katika maana ya aya inayosema "Na mkidhihirisha yaliyomo katika nyoyo zenu au mkiyafichua, Allah atawataka hisabu ya (yote) hayo ." (2:284)

Aya Na 10

Hana uwezo katika nafsi yake utakaomzuia na adhabu ya Mwenyezi Mungu wala hana wa kumnusuru atakayemkinga na adhabu yaani hakutakuwa na uwezo wowote utakaomkinga na shari kutoka kwake au kwa mtu mwengine.

Aya Na 11

Kiapo baadha ya kiapo, ni kwa ajili ya kutilia mkazo jambo la Kiyama na kurejea kwa Mungu. Makusudio ya kurudi ni kuhisi kwenda kwake kwa kuchimbuka nyota na kutua. Imesemwa kuwa makusudio yake ni mvua. Makusudio ya kupasuka ni kupasuka kwa ajili ya mimea.

Aya Na 12-13

Maana ya neno Fasl ni kupambanua kati ya vitu viwili. Aya hizi mbili ni jawabu la kiapo kwa maana; ninaapa kwa hivyo nilivyoviapia hakika Qur'an ni neno lenye kupambanua kati ya haki na batili na sio maneno yasiyokuwa na maana. Yale inayoyahakikisha ni haki isiyokuwa na shaka na yale inayoya batilisha ni batili isiyokuwa na shaka. Kwa hiyo yale iliyoyatolea habari katika ufufuo na marejeo ni haki isiyokuwa na shaka ndani yake. Imesemekana kuwa dhamiri katika neno Innahu ni ya hayo yaliyotangulia kuelezwa katika habari ya marejeo lakini tuliyoyaeleza mwanzo ndiyo yanayoelekea zaidi.

Aya Na 15

Yaani makafiri wanaichimba vitimbi wakikusudia kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu na kubatilisha mlingano wako.

Aya Na 16

Ikiwa wao wanavyo vitimbi na mimi ninavyo vitimbi. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kushinda juu ya jambo lake, kwa hivyo wangojee tu; wala usifanye haraka, ngoja kidogo tu! Yatawajia yale waliyoahidiwa, na kila linalokuja liko karibu.

Utafiti Wa Hadithi Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu kusema kwake Mwenyezi Mungu "Hakika kila nafsi ina mwenye kuichunga" amesema ni Malaika. Na kuhusu "Ameumbwa kwa maji yanayotoka kwa nguvu" amesema ni manii ambayo hutoka kwa nguvu". Kuhusu "yanayotoka kati ya uti wa mgongo na mifupa ya kifua" amesema uti wa mgongo ni mwanaume na mifupa ya kifua ni mwanamke. Katika Majmau imepokewa hadith marfuu kutoka kwa Abu Dardai amesema: "Amesema Mtume(s.a.w.w) :Amedhamini Mwenyezi Mungu kuumba kwake vitu vine: Swala, Zaka, Kufunga Ramdhan na kuoga janaba na hizo ndizo siri alizozisema Mwenyezi Mungu "Siku itakayofunuliwa siri ."

Huenda ikawa maana ya hadithi hiyo ni kutaja baadhi ya mambo ya ukweli, kama inavyotilia nguvu hilo hadithi inayofuata. Katika hiyo hiyo Majmau kutoka kwa Muadh bin Jabal amesema: "Nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu: ni siri zipi ambazo Mwenyezi Mungu atawafunuliwa waja katika akhera? Akasema siri zenu ni matendo yeno ya swala, kufunga, zaka, udhu, kuoga janaba na kila lenye kufaradhiwa, kwa sababu matendo yote ni siri yenye kufichamana, mtu akitaka anaweza kusema ameswali na asiwe ameswali au aseme ametawadha kumbe hakutawadha. Basi ndiyo kusema kwake Mwenyezi Mungu "siku itakayofunuliwa siri."

Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu kauli yake Mwenyezi Mungu: "Basi hatakuwa na nguvu wala wa kumnusuru." Amesema: hatakuwa na nguvu yoyote kwa muumba wake wala wa kumnusuru kama Mwenyezi Mungu akimtakia uovu. Katika hiyo Tafsiri ya Qummi amesema kuhusu neno Raj'n amesema ni mvua na ardhi yenye mipasuko ni ardhi yenye mimea. Katika Majmau kuhusu : "hakika hii Qur'an ni kauli ya haki" amesema "Hakika Qur'an inapambanua kati ya haki na batili kwa kuibainisha kila moja. Hayo yamepokewa kutoka kwa Imam Assadiq(a.s) .

Katika Durril Manthur ametoa Ibn Abi Shayba, Addarami, Tirmdhi, Muhammad bin nasr na Ibn el- Ambari katika Masahif kutoka kwa Harith el-Aa'war amesema: Niliingia msikitini mara watu wakaingia katika mazungumzo. Nikamwendea Ali nikampa habari; akasema: "Je wamekwishafanya? Mimemsikia Mtume(s.a.w.w) akisema: "Kutatokea fitna. Nikasema: Ni kitu gani cha kutokea katika fitna hiyo Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Je ni sawa hapa? Akasema:kitabu cha Mwenyezi Mungu kina habari za kabla yenu baada yenu na kimekwisha wahukumia, ni upambanuzi na sio upuuzi, mwenye kukiacha Mwenyezi Mungu kumuangamiza, mwenye kukusudia pengine Mwenyezi Mungu humpoteza .

Ni kamba madhubuti, mauidha yenye hekima na njia yenye kunyooka. Ni ambachi hakipotezi wala hawashibi nacho wanavyuoni, hazitatiziki nacho ndimi wala haiishi ajabu yake. Ndicha ambacho majini waliposikia walisema: " Hakika tumesikia Qur'an ya ajabu inaongoza kwenye uongofu." Mwenye kusema kwacho huwa mkweli, mwenye kuhukumu kwacho amefanya uadilifu na mwenye kuganya amali kwacho amepata thawabu, na mwenye kulingania kwenye kitabu hicho ameongoka katika njia iliyonyooka. Amepokea karibu na maana hayo Muadh bin Jabal kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) .


12

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA A'ALAA (MTUKUFU) (NA. 87)

INA AYA 19

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى ﴿١﴾

1. Litakase jina la Mola wako aliye Mtukufu.

الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٢﴾

2. Ambaye ameumba (kila kitu) akakiweka sawa.

وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ ﴿٣﴾

3. Na ambaye amekadiria (kila kitu) na akakiongoza.

وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَىٰ ﴿٤﴾

4. Na ambaye ameotesha malisho.

فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَىٰ ﴿٥﴾

5. Kisha akayafanya makavu yenye kupiga weusi.

سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰ ﴿٦﴾

6. Tutakusomesha wala hutasahau.

إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ ﴿٧﴾

7. Ila anachopenda Allah. Hakika yeye anayajua yaliyowazi na yaliyofichika.

وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٨﴾

8. Tutakusahilishia njia nyepesi.

فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ ﴿٩﴾

9. Basi waidhisha ikiwa utafaa waadhi.

سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ ﴿١٠﴾

10. Atawaidhika nao mcha (Mungu).

وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى ﴿١١﴾

11. Na atajiepusha nao asiyemcha.

الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَىٰ ﴿١٢﴾

12. Ambaye atauingia moto mkubwa..

ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ ﴿١٣﴾

13. Kisha humo hatakufa wala hatokuwa hai.

قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ ﴿١٤﴾

14. Hakika amekwishafaulu mwenye kujitakasa.

وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ ﴿١٥﴾

15. Akakumbuka jina la Mola wake na akaswali.

بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿١٦﴾

16. Lakini nyinyi mnapenda zaidi maisha ya ulimwengu.

وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿١٧﴾

17. Hali akhera ni bora na yenye kubaki.

إِنَّ هَـٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ ﴿١٨﴾

18. Hakika hAya Na mo katika vitabu vya kwanza.

صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ ﴿١٩﴾

19. Vitabu vya Ibrahim na Musa.

UBAINIFU

Ni amri ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu juu ya yale yanayoelekeana na upande wake Mtukufu na kuitakasa dhati yake tukufu na kutaja pamoja na jina lake Mtu mwengine au kutegemeza kwa mwengine yale yanayopasa kutegemezwa kwake, kama kuumba kuangalia vizuri mambo na kuruzuku. Na nikiaga chake kwa Mtume kwa kumpa nguvu kwa elmu, hifadhi na kummakinisha katika njia ambayo ni nyepesi kwa tabligh na inayonasibiana zaidi na mlingano. Mpangilio wa aya katika mwanzo wa Sura ni mpangilio wa ki Makka. Ama mwisho wake yaani kuanzia Aya Na 14 mpaka mwisho wa Sura, imepokewa katika njia ya Maimamu wa Ahlul Bait vile vile katika njia ya Ahli Sunnah kwamba, makusudio yake ni zaka ya fitr, na swala ya Idd, na ni maalum kuwa saumu na yanayofuatia saumu miongoni mwa zaka ya fitr na swala ya Idd ilianzishwa Madina baada ya Hijra. Hivyo zitakuwa aya za mwisho zimeshuka Madina. Katika hiyo Sura mwanzo wake ni Makka na mwisho wake ni Madina, wala hayo hayakanushi yale yaliyokuja kuwa Sura imeshuka Makka, kwani ilivyo nikuwa haikataliki kuchukulia hivyo mwanzo wa Sura.

Aya Na 1

Ni amri ya kulitakasa jina lake Mwenyezi Mungu S.W.T. na kulitukuza. Na kwa vile hapa kutakaswa Mwenyezi Mungu kumefungamanishwa na jina yake, basi huko kumtakasha kunamaanisha asitajwe yeyote ambaye yeye Mwenyezi Mungu ametakata naye. Kwa sababu jina linatokea katika kusema. Hivyo isitajwe pamoja na jina lake miungu wengine washirikina, waombozi na kuwanasibishia uungu. Na vile vile kama kutaja baadhi ya yanayohusika naye Mwenyezi Mungu (s.w.t) kama kuumba kupatisha, kuruzuku, kuhuisha na kufisha na mfano wake kwa kuyanasibisha kwa asiyekuwa yeye Mwenyezi Mungu Au kama kutaja baadhi ya yasiyofanana na upande wa utakatifu wake, katika vitendo kama kushindwa, ujinga, dhuluma, mghafala na mfano wake katika sifa za upungufu na aibu kwa kuyanasibisha kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Kwa ujumla kulitakasa jina lake ni kuepuka kauli na kutaja yasiyonasibiana kuyataja kwake na jina lake Mwenyezi Mungu (s.w.t), na huko ni kumtakasa katika kiwango cha kauli kwenye kuafikiana na kumtakasa kwake katika kiwango cha kitendo. Hiyo inalazimisha Tawhid (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) iliyo kamili kwa kukanusha kumshirikisha Mwenyezi Mungu kuliko waziwazi; kama ilivyo katika kusema kwake Mwenyezi Mungu:

"Na anapotajwa Allah peke yake nyoyo za wale wasioamini akhera, huchukiwa na wanapotajwa wale walio kinyume naye, mara wanafurahi ". (39:45).

Na pia kusema kwake: "Na unapomtaja Mola wako katika Qu'ran peke yake, basi wao hugeuza migongo yao kwa kuchukia ." (17:46).

Kutegemeza jina Mola kwa dhamiri ya mwenye kusemeshwa (jina la Mola wako) ni kutilia nguvu yale tuliyotangulia kuyataja, kwani maana ni litakase jina la Mola wako ambaye umemfanya ni Mola na wewe unalingania kuwa yeye ni Mola wa waungu, basi isitokee katika maneno yako pamoja na kutaja jina lake kwa uungu wake na kutaja mwengine, kwa kiasi ambacho kitakanusha kumwita Mungu kama alivyojijulisha kwako.

Kusemwa kwake: Mtukufu ni ambaye yuko juu ya aliye juu na kushinda kila kitu, hiyo ni sifa ya Mola wako yaani litakase jina lake kwa sababu yeye ni Mtukufu zaidi. Imesemwa kuwa maana ya aya hii ni kusema "Subhana rabial aala" hayo ni kutoka kwa Ibn Abbas, pia amesema, ni kuswali. Imesemwa makusudio ni jina vile, anavyoitwa yaani mtakase Mwenyezi Mungu S.W.T. na kila sifa na vitendo visivyofanana naye. Imesemwa kuwa makusudio ni kuyatakasa majina yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) na yale yasiyofanana naye wala haitwi asiyekuwa yeye na jina linalomhusu yeye Mwenyezi Mungu, wala halitamkwi katika mahali pasipo nasibiana naye kama chooni n.k. Yale tuliyotanguliza kuyataja katika maana ndiyo mapana zaidi na yenye kukusanya zaidi maana na ndiyo yanayonasibiana zaidi na aya inayosema "tutakusomesha wala hutasahau" na "tutakusahilishia njia nyepesi". Kwa sababu mpangilio ni wa kupewa utume mpaka kwenye ukumbusho na tabligh. Hivyo ikaanzwa kwa maneno yake Mtume(s.a.w.w) ya kumtakasa na kila linalo tambulisha shirika kwa uwazi au kwa undani. Akamwahidi mara ya pili kumsomesha kiasi ambacho hataweza kusahau chochote katika yale aliyopewa Wahyi na kusahilishiwa njia ya Tabligh.

Aya Na 2

Kuumba kitu ni kukusanya mafungu yake na kuyapanga sawasawa kiasi ambacho huwekwa kila kitu mahali pake panapo nasibiana napo na kukipa haki yake, kama kuweka kila kiungo katika viungo vya binadamu mahali panapo nasibu. Ayah ii mpaka mwisho wa Aya Na nne zinasifu mipangilio mizuri, ya Mungu na hayo ni dalili ya uungu wake Mwenyezi Mungu (s.w.t)

Aya Na 3

Yaani ni kuvifanya vitu alivyoviuumba juu ya kiasi mahususi na mipaka yenye kuonyesha dhati zake na sifa zake na vitendo vyake visivyozidi kipimo chake na akaviandaa na yale yanayonasibiana na yaliyokadiriwa. Kwa hiyo kila mmoja anafuata upande wa yale yaliyokadiriwa kwake, kwa uongozi wa Mungu, kama mtoto kuendea titi la mama yake, kifaranga kutegemea riziki ya mama yake, mwanamume kwa mwanamke na mifano ya hayo. Mwenyezi Mungu anasema:"Na hakuna kitu chcochote ila hazina yake iko kwetu wala hatukukiteremsha ila kwa kipimo maalum ." (15:21).

Amesema tena: "Kisha akamfanyis nyepesi njia " (80:20). Amesema tena: "Kila mmoja ana mwelekeo wake wa kuelekea ." (2:148).

Aya Na 4 -5

Kutoa malisho kwa ajili ya chakula kisha kuyafanya makavu meusi ni katika usadikisho wa mipangilio ya Mungu na dalili zake; kama ilivyo katika kuumba, kulinganisha sawa, kukadiri na uongozi.

Aya Na 6-7

Amesema katika Mufradati: "Kusoma ni kukusanya herufi na matamko pamoja katika kusoma, lakini sio mkusanyiko wowote ni kusoma, huwezi kusema umewasoma watu, kama ukiwakusanya." Hiyo inafahamisha kuwa hakuwezi kuitwa kusoma kwa herufi moja. Katika Majmau anasema kusomesha ni kuchukua kisomo kwa msomaji kwa kumsikiliza ili usahihishe makosa.

Kumsomesha kwake Mtume, sio kama vile tunavyosemeshana sisi kwa kumsikiliza msomaji kisha kumsahihisha anayoyakosa. Haikuwa kwa Mtume kusoma chochote katika Qur'an akakikosea au asahau wahyi kisha asome ndipo arekebishwe la, bali makusudio yake ni kumwezesha Mtume (SAWW) kuisoma Qur'an kama ilivyoteremsha bila ya kuibadilisha, kwa kuzidisha kitu au kupunguza au kuifanya kombo kwa sababu ya kusahau. Kwa hivyo kauli yake Mwenyezi Mungu tutakusomesha hutasahau ni kiaga kitokacho kwake Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kumuwezesha kuijua Qur'an na kuifikisha kama ilivyoteremshwa, kiasi ambacho hataisahau. Huo ni msingi wa kufikisha wahyi (ufunuo) kama iluvyofunuliwa. Kusema kwake "Ila anachopenda Allah, ni kuvua kunakofahamisha uwezo wa Mungu ulio huru na kwamba kipawa hiki cha kutosahau sio kuwa Mungu amelazimika macho. Yeye anao uwezo wa kukusahaulisha kama akitaka.

Ayah ii kwa mpangilio wake, haiepukani kuwa inatilia nguvu yale yaliosemwa kwamba Mitume(s.a.w.w) alipokuwa akiletewa wahyi (ufunuo) na Jibril humsomea kwa kuogopa kusahau, ikawa Jibril akimaliza tu naye huanza. Basi iliposhuka ayah ii hakusahau kitu baadaye. Inakurubia kuzingatia kuwa ayah ii tutakusomesha hutosahau ilishuka kwanza ndipo ikashuka aya inayosema: "Usiutikise ulimi wako kwa (kuufanyia haraka) wahyi kwa hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. Wakati tunapokusomea, basi fuata kusomwa kwake, kisha ni juu yetu kuubainisha ". (75:17-19).

Kisha aya inayosema: Usiifanyie haraka (hii) Qur'an kabla haujamalizika wahyi (ufunuo) wake, Na (uombe) useme. Mola wangu nizidishie elimu" (20:114).

Kusema kwake "Hakika anajua yaliyowazi na yaliofichika" kuwa wazi ni kwa kuona au kusikia kama Qur'an inavyosema: "Wakasema tuonyeshe Mungu waziwazi ". (4:153).

"Hakika yeye anajua kauli iliyo dhahiri ". (21:110) Jumla ya aya iko katika mahali pa sababu kwa maana tutakufanyia uzuri katika kupokea wahyi (ufunuo) na kuuhifadhi kwa sababu sisi tunajua dhahiri na ndani ya hali yako na vile unavyojihimu katika jambo la wahyi na unavyopupia twaa katika yale uliyoamrishwa.

Aya Na 8

Wepesi ni sifa yenye kusimama mahali pa msifiwa yaani njia nyepesi, kwa maana ya kuwa daima tutakufanyia njia ya tabligh ni nyepesi kwa maneno na vitendo utaongoza watu na itatimia hoja kwa wengine na utafanya subira juu ya maudhi yao.

Aya Na 9

Ni mtiririko wa amri iliyotangulia ya kulitakasa jina la Mola wake kuahidiwa kwake kusomeshwa wahyi kiasi ambacho hatasahau, na kusahilishiwa njia nyepesi, hizo ni sharti za kidharura ambazo zinaweza kuzuwia kufaulu mlinganio wa kidini. Maana ni kuwa ukitimiza amri ya kufuata yale tuliyokuamrisha, kukusomesha hutosahau na kukusahilishia njia ya wepesi, basi waidhisha ikiwa utafaa (huo) waadhi.

Imeshartiwa kuwa waadhi uwe wenye kunufaisha. Na hilo ni sharti juu ya uhakika wake. Kwani ikiwa waadhi hautanufaisha basi itakuwa ni upuuzi, naye Mwenyezi Mungu ametakata na kuamrisha upuuzi. Kwa hiyo kumwadhia mwenye kumcha Mwenyezi Mungu kwanza kunafahamisha kupondokea haki na hayo ndio manufaa yake (huo waadhi), vile vile kuwaidhika kama alivyosema: "Atawaidhika anayemcha (Mungu). Na kumwaidhia muovu ambaye haogopi katika moyo wake, kwanza kunafahamisha kutimia hoja juu yake na ndio manufaa yake (huo waadhi) na kunalazimisha kuejiepusha kwake, na kuikataa kwake haki kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na atajiepusha nayo muovu". Waadhi baada wa waadhi haunufaishi na chochote kwa hiyo kukaamriwa kuachana naye. Mwenyezi Mungu amesema: "Basi jiepushe na wale wanaoupa mgongo ukumbusho wetu huu na wala hawataki ila maisha ya dunia ." (53:29)

Imesemekana kuwa sharti ni sharti la kisura tu! Sio la kihakika, kwamba ni kutolea habari kuwa waadhi ni wenye kunufaisha katika kuzidisha twaa na kukoma na maasi, kama inavyosemwa: Muulize inafaa kumuuliza, kwa hiyo ndio baadhi yao wakasema: "Herufi In katika aya ni kwa maana ya (Qad) hakika". Na imesemwa kuwa maneno ni ya mkato kwa kuondoa maneno mengine, kukadiria kwake ni "Basi waidhisha ikiwa utafaa waadhi na hata ukitofaa". Hilo ni kwamba yeye Mtume(s.a.w.w) amepelekwa kwa waadhi na kuonya. Kwa hiyo ni juu yake kuonya na kutoa waadhi uwe una manufaa au usiwe na manufaa; Kwa hiyo aya inaelekeana na aya inayosema: "Na amewafanyia kanzu zinazowakinga na joto (na baridi) ". (16:81).

Imesemwa kuna ishara ya kuweka mbali manufaa ya hawa wenye kutajwa; Ni kama vile imesemwa: Fanya unayoamrishwa hata kama hayatanufaisha.

Aya Na 10

Yaani atawaidhika na Qur'an yule ambaye moyoni mwake mna kitu cha kumwogopa Mwenyezi Mungu na kuogopa mateso yake.

Aya Na 11

Dhamiri ni ya mawaidha. Makusudio ya neno Ashqa kwa kulinganisha na aya iliyotangulia, ni yule asiyemwogopa Mwenyezi Mungu.

Aya Na 12

Mto mkubwa ni moto wa Jahanam, ni mkubwa kulinganisha na wa dunia. Imesemwa makusudio yake ni daraja ya chini ya Jahanam ambayo ina adhabu kali zaidi.

Aya Na 13

Makusudio ya kutokufa wala kuwa hai, ni kutookoka kabisa kwa maana ya kuwa adhabu haitakwisha wala maisha hayatabadilika kuwa mazuri. Kwa hiyo makusudio ya uhai ni maisha mema; kama alivyosema katika Ardhi; "Si hai wakutarajiwa wala si maiti wakusahauliwa".

Aya Na 14 -15

Makusudio ya kujitakasa hapa, ni kujitakasa na uchafu wenye kufungamana na dunia kwa dalili ya kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Lakini nyinyi mnapendelea zaidi uhai wa kilimwengu." Kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa kumuelekea yeye Mwenyezi Mungu ni kujitakasa. Kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kujitakasa na uchafu unaofungamna na mali. Hata udhu wa swala ni mfano wa kujitakasa na yale yaliyochumwa na nyuso, mikono na miguu. Kusema kwake: Akalikumbuka jina la Mola wake akaswali, makusudio yake kwa dhahiri ni kumtaja Mwenyezi Mungu kwa kutamka, na kuswali ni swala ya kawaida ya Kiislamu. Aya mbili hizi kwa dhahiri ufahamisho wake ni kuenea a kila kitu, lakini imepokewa kutoka kwa Maimamu wa Ahlul Bait(a.s) kuwa aya hizo zinahusu zaka ya fitri na swala ya Idd. Vile vile hayo yamepokewa katika Ahli Sunnah.

Aya Na 16

Msemo huo unaelekezwa kwa watu juu ya tabia yao ya kiutu inayopelekea kufungamana kabisa na dunia na kujishughulisha na kuiamirisha. Imesemwa kuwa msemo unawaelekea makafiri tu. Kwa hali yoyote maneno ni yenye kuelekezwa kwenye lawama.

Aya Na 17

Imehisabiwa akhera ni yenye kubakia kulinganisha na dunia, pamoja na kuwa yenyewe akhera ni yenye kubaki milele, kwa sababu ya kupima kati ya dunia na akhera.

Aya Na 18-19

Neno haya "Linaonyesha yale yaliyobainishwa kuanzia aya 14 mpaka 17. Imesemwa kuwa ni hAya Na kuwa akhera ni bora na ni yenye kubaki. Imesemwa kuwa kusema vitabu vya kwanza tu. Kisha kuvibainisha kuwa ni vitabu vya Ibrahim na Musa ni kwa ajili ya kutukuza na kukuza jambo.

Utafiti Wa Hadith Katika Tafsiri ya Iyashi kutoka kwa Uqba bin Amir El-Jahaniy amesema iliposhuka aya inayosema: "Litakase jina la Mola wako aliye mkuu" Mtume(s.a.w.w) alisema ifanyeni katika kurukui kwenu. Na iliposhuka "Litakase jina la Mola wako aliye Mtukufu akasema": Ifanyeni katika kusujudi kwenu. Hadith hiyo pia imepokewa katika Durril Manthur kutoka kwa Ahmad, Abu Dawud, Ibn Maja Ibn El-Mundhir na Ibn Murdawayh nao wamepokea kutoka ka Uqba naye kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) .

Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu Aya Na kwanza amesema: "utakata ni kwa Mola wangu aliye Mtukufu". Kuhusu na ambaye ameumba akakamilisha na ambaye makadirio ya mwanzo kisha akaviongoza.

Katika Durril Manthur ametoa Ibn Murdawayh kutoka kwa Ibn Abbas amesema: "Mtume(s.a.w.w) alikuwa anajikumbusha Qur'an kwa kuhofia kusahau akaambiwa tumekutoshea na hilo", na ikashuka aya Tutakusomesha wala hutasahau. Katika Faqih aliulizwa Imam As Sadiq(a.s) kuhusu kusema kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t) "Hakika amefaulu mwenye kuitakasa " Akasema: "Ni mwenye kutoa zaka ya fitr". Akaulizwa: na akamkumbuka Mola wake, akaswali? Akasema ni aliyetoa uwanjani akaswali. Amepokea hadith kwa maana hii Hammad, naye kutoka kwa Jarir naye kutoka kwa Abu Baswir na Zurarah kutoka kwake Imam Jaffar As Sadiq(a.s) . Katika Durril Manthur ametoa Ibn Murdawayh kutoka kwa Abu Said Al-Khudri amesema: Mtume(s.a.w.w) alikuwa akisema: "Hakika amefaulu mwenye kujitakasa na akamkumbuka Mola wake akaswali " Kisha hugawanya zaka ya fitr kabla ya kwenda kwenye mswala siku ya Idd-ul-fitr.

Vile vile kumepokewa kushuka aya mbili hizo katika zaka ya fitri na swala ya Idd kwa njia mbili kutoka kwa Abu Said, vile vile kwa njia mbili kutoka kwa Ibn Umar kwa njia moja kutoka kwa Naila bin Al-Asqa, kwa njia mbili kutoka kwa Abu Aliya na kwa njia moja kutoka kwa Atau. Vile vile kwa njia moja kutoka kwa Muhammad bin Sirin, kwa njia moja kutoka kwa Ibrahim Annakhyi na kutoka kwa Amru bin Awf naye kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) .

Katika Khiswali imepokewa kutoka kwa Utbah bin Amru Allaythi naye kutoka kwa Abu Dharr katika hadith inayosema: "Nilimuuliza Mtume(s.a.w.w) ni kitu gani katika dunia alichokuteremshia Mwenyezi Mungu kilichokuwa katika vitabu vya Ibrahim na Musa? Akasema, Ewe Abu Dharr, soma: hakika amefaulu mwenye kujitakasa akalikumbuka jina la Mola wake akaswali. Lakini nyinyi mnapendelea zaidi uhai wa kilimwengu. Hali akhera ni bora na yenye kubaki. Hakika hayo yamo katika vitabu vya kwanza vitabu vya Ibrahim na Musa. Hadithi inatilia nguvu kuwa ishara na neno "haya" ni mkusanyiko wa aya nne kama ilivyotangulia. Katika Baswir kwa isnadi yake kutoka kwa Abu Baswir amesema Abu Abdillah: Tunazo suhuf alizozitaja Mwenyezi Mungu katika Aya Na 19: Nikamwambia ni mbao? Akasema ndio. Amepokea vile vile kwa njia nyengine Abu Baswir kutoka kwake Abu Abdillah(a.s) . Kwa dhahiri ni kwamba makusudio ya kuwa Suhuf ni mbao nikuwa ni Taurat yenye kuelezewa katika Qur'an kama mbao; kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t): "Na ukamwandikia katika mbao kila kitu ." (7:145).

Na pia kusema kwake Mwenyezi Mungu:'na akazitupa mbao .." (7:150). Na kusema kwake "aliziokota zile mbao " (7:154).

Katika Majmau imepokewa kwa Abu Dharr, yeye amesema: "Nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu ni Mitume wangapi? Akasema: Ni laki moja na ishirini na nne elfu (124,000) nikamuuliza ni wangapi walio Mursaal katika wao? Akasema mia tatu na kumi na tatu (313). Nikasema Adam alikuwa Mtume. Akasema ndio Mwenyezi Mungu alimsemesha na amemuumba kwa mkono wake. Ewe Abu Dharr, Mitume waarabu ni Hud, Saleh, Shuayb na Mtume wako.

Nikasema tena: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ameteremsha vitabu vingapi? Akasema mia moja na nne (104). Kwa Adam mbao kumi, kwa Shiyth hamsini kwa Ukhnun ambaye ni Idris thelathini naye ndiye wa kwanza kuandika kwa kalamu, Ibrahim kumi na Taurat, Injil, Zabur na Qur'an. Yamepokewa hayo katika Durril Manthur kutoka kwa Abd bin Hamid, Ibn Murdawayh na Ibn Asakir nao kutoka kwa Abu Dharr isipokuwa hazikutajwa mbao za Adam na zimetajwa mbao kumi za Musa kabla ya Taurat.


13

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA GHASHIYA (KIYAMA) (NA. 88)

INA AYA 26

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwnye kurehemu

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ ﴿١﴾

1. Je, imekujia habari ya Kiyama?

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ ﴿٢﴾

2. Nyuso siku hiyo zitadhalilika.

عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ ﴿٣﴾

3. Zitatumika na kutaabika.

تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً ﴿٤﴾

4. Zitaingia katika moto mkali.

تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ ﴿٥﴾

5. Zitanyweshwa maji ya chemshemi ichemkayo.

لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ ﴿٦﴾

6. Hawatakuwa na chakula isipokuwa cha miba.

لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِن جُوعٍ ﴿٧﴾

7. Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ ﴿٨﴾

8. Nyuso siku hiyo zitanawiri.

لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ ﴿٩﴾

9. Zitakuwa radhi kwa amali yake.

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ ﴿١٠﴾

10. (Zitakuwa) katika pepo iliyo tukufu.

لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً ﴿١١﴾

11. Hazitasikia humo upuuzi.

فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ ﴿١٢﴾

12. Humo mna chemichemi inayotiririka.

فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ ﴿١٣﴾

13. Mna malili yaliyotukuzwa.

وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ ﴿١٤﴾

14. Na vikombe vilivyowekwa.

وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ ﴿١٥﴾

15. Na mito iliyopangwa.

وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ ﴿١٦﴾

16. Na mazulia yaliyotandikwa.

أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ ﴿١٧﴾

17. Je, hawamtazami ngamia namna gani alivyoumbwa.

وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ ﴿١٨﴾

18. Na mbingu namna gani zilivyoinuliwa?

وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ ﴿١٩﴾

19. Na majabali namna gani yalivyo simamishwa.

وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ ﴿٢٠﴾

20. Na ardhi namna gani ilivyotandikwa.

فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ ﴿٢١﴾

21. Basi kumbusha, hakika wewe ni mkubushaji tu!

لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ ﴿٢٢﴾

22. Wewe si mtenza nguvu.

إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ ﴿٢٣﴾

23. Lakini mwenye kupa mgongo akakufuru.

فَيُعَذِّبُهُ اللَّـهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ ﴿٢٤﴾

24. Allah atamwadhibu adhabu kubwa mno!

إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ ﴿٢٥﴾

25. Hakika ni kwetu sisi marejeo yao.

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم ﴿٢٦﴾

26. Kisha ni juu yetu sisi hesabu yao.

UBAINIFU

Ni Sura ya maonyo na biashara. Inasifu Kiyama kwa hali ambayo watu watakuwa nayo ya kugawanyika makundi mawili: Wema na waovu, na kutua kwao katika sehemu walizoandaliwa miongoni mwa pepo na moto. Inamalizia kwa kumwamrisha Mtume(s.a.w.w) kuwakumbusha watu fani za mazingatio ya Mungu katika ulimwengu zenye kufahamisha juu ya uungu wake, na kurudi kwao kwake kwa ajili ya kuhisabiwa. Sura imeshuka Makka kwa ushahidi wa mpangilio wa aya zake.

Aya Na 1

Ni swali linalopelekea kukuza mambo. Limetumiwa neno kufudikiza (Ghashiya) kwa maana ya Kiyama, kwa sababu kitawafudikiza watu na kitawazingira kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na tutawafufua wala hatutamwacha hata mmoja katika wao ." (18:47). Au kimeitwa hivyo kwa kuwa kitafudikiza nyuso za makafiri kwa adhabu.

Aya Na 2

Yaani nyuso ni zenye kudhalilika kwa ghamu na adhabu itayozifunika. Kudhalilika kutawapata wenye nyuso, lakini hapa kumenasabishwa kwenye nyuso, kwa sababu kunadhihiri katika uso.

Aya Na 3

Makusudio yake kwa kulinganisha na aya inayokabiliana nayo katika sifa ya watu wa peponi inayosema "Zitakuwa radhi kwa mali yake" ni kuwa kutumika kwake ni katika dunia na kutaabika kwake ni katika akhera. Hakika mtu anafanya anayoyafanya katika dunia ili atengenekewe, na apate matakwa, lakini amali zao ni bure tu; Hazitawafaa na chochote, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na tutayaendea yale waliyoyatenda katika amali tuyafanye kama mavumbi yaliyitawanywa ". (25:23).

Kwa hiyo hakirudi chochote katika waliyoyafanya isipokuwa taabu, kinyume cha watu wa peponi, kwani hakika wao mahangaiko yao waliyohangaika katika dunia ni kibali kitakachowapeleka katika pepo siku ya Kiyama. Imesemwa makusudio yake ni kutumika katika dunia kwa maasi na kutaabika katika moto siku ya Kiyama.

Aya Na 4

Yaani ni moto katika ukomo ya joto.

Aya Na 5

Yaani ni yenye joto kali.

Aya Na 6

Dhwarii ni aina ya miba ambayo watu wa Hijazi wanaita hivyo inapokauka. Na chakula kibaya sana, hawawalishi hata wanyama wao. Huenda hiyo ya motoni imeitwa hivyo, kwa kufanana.

Aya Na 7

Kunawiri ni fumbo la furaha inayodhihiri usoni kama ilivyosemwa: "utaona katika nyuso zao mng'ao wa kunawiri ." (83:24). Au itakuwa kwa maana ya kuneemeka. Imesemwa haikuwekwa herufi za kuunganisha kwa kuonyesha ubainifu kamili kati ya hali za makundi mawili.

Aya Na 8

Makusudio ya amali njema yaani imeridhia amali yake njema kwa kulipwa malipo mema.

Aya Na 9-16

Ni utukufu wa daraja yake, kwani katika hiyo pepo kuna maisha yasiyokuwa na kifo, ladha isiyokuwa na machungu yoyote, na furaha isiyokuwa na huzuni. Kusema kwake "Hazitasikia humo upuuzi" yaani hizo nyuso hazitasikia tamko lolote lisilokuwa na faida. Kuhusu chemchemi makusudio yake ni jinsi yake, na amezihesabu Mwenyezi Mungu chemchemi katika hiyo pepo katika maneno kama Salsabil Kinywaji kitakatifu nk.

Aya Na 17

Baada ya kumaliza kukisifu Kiyama na kubainisha hali za makundi mawili wa waumini na makafiri, amefuatishia kuishiria kijumla mipangilio mizuri ya Mungu ambayo inabainisha uungu wake, inayohukumilia kumwabudu kwake, na hilo likafuatiwa na hisabu ya matendo na malipo ya muumin kwa imani yake na kafiri kwa kufuru yake. Wakati wake hayo ni siku ya Kiyama. Kwanza amewaambia kuangalia ngamia vile alivyoumbwa. Vipi alivyoitia sura Mwenyezi Mungu ardhi isiyokuwa na uhai wala hisia, kwa Sura hii ya ajabu katika viungo vyake, nguvu zake na vitendo vyake. Akaitiisha kwao ili wanufaike nayo kwa kuipanda, uchukuzi, nyama yake, maziwa yake, ngozi yake na sufu yake. Na hata mkojo wake na kinyesi chake. Je, yote hAya Na mezuka tu kwa bahati bila ya kupangwa? Kuhusisha kutaja ngamia ni kwa njia kuwa Sura imeshuka Makka na ngamia alikuwa ndio nguzo ya maisha ya waarabu.

Aya Na 18

Imepambwa hiyo mbingu kwa jua, mwezi na sayari nyenginezo kwa manufaa ya watu wa dunia; na amejaalia hewa ambayo wanalazimika wanyama kuivuta.

Aya Na 19

Majabali ndio vigingi vya ardhi vinavyoizuia ardhi isitetemeke na hazina ya maji ambapo mito na chemchem hububujika kutoka huko na ni hifadhi za madini.

Aya Na 20

Yaani imatendikwa ili mwanadamu aweze kukaa na kumsahilikia kuguru hapa na pale na matumizi mengine ya kiufundi. Basi mipangilio yote hii imetegemezwa kwa Mwenyezi Mungu bila ya wasiwasi wowote. Yeye ni Mola wa mbingu ardhi na vilivyo ndani yake. Yeye ni Bwana wa ulimwengu wa kibinadamu, niwajibu kwao kumfanya ndiye Mola, kumpwekesha na kumwabudu na mbele yao kuna Kiyama ndiyo siku ya hesabu ya malipo.

Aya Na 21

Ni sehemu ya yaliotangulia maana yake ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola na hakuna Mola asiyekuwa yeye na mbele yao kuna siku ya hesabu na malipo kwa aliyeamini katika wao au aliyekufuru, basi wakumbushe hilo. Kusema kwake "Hakika wewe ni mkumbushaji tu " ni ubainifu wa kuwa kazi ya Mtume ni kukumbusha tu kwa kutarajia kuitikiwa na kuaminiwa bila ya kulazimisha.

Aya Na 22

Ni ubainifu na tafsiri ya aya iliyotangulia.

Aya Na 23

Hapo anavuliwa na ukumbusho yule mwenye kupa mgongo na kukufuru. Ilivyo ni kuwa kukanusha kumekuja baada ya ukumbusho; kukanusha kwa kuvua, ni ukumbusho baada ya ukumbusho. Ni kama vile imesemwa wakumbushe na udumishe ukumbusho isipokuwa yule ambaye umemkumbusha akapa mgongo na kukufuru. Kwa hiyo huna haja ya kudumisha kumkumbusha bali achana naye. Mwenyezi Mungu atamwadhibu adhabu kubwa. Aya Na 21 - 24 katika Sura hii zinalingana na Aya Na 9 -12 ya Sura ya Al-A'laa (87). Imesemekana kuwa sio kuvuliwa na ukumbusho bali nikuvuliwa kutenza nguvu, na maana ni wewe simtenza nguvu isipokuwa juu ya yule mwenye kupa mgongo akakufuru ndio Mwenyezi Mungu anakusaliti naye na kukuamrisha kufanya jihadi; utapigana naye na kumuua. Na imesemwa kuvua hapa ni kwa kukataa tu, Kwa maana; wewe si mtenza nguvu, lakini mwenye kupa mgongo akakufuru katika wao hataachwa bure. Atamwadhibu Mwenyezi Mungu adhabu kubwa. Tuliyoyatanguliza kuyataja yako karibu na yenye nguvu zaidi.

Aya Na 24-25

Imetangulizwa "ni kwetu sisi" kwa sababu ya kutilia mkazo. Na aya hiyo iko katika mahali pa illa (sababu) ya kuadhibu kulikotajwa katika aya iliyotangulia.

Utafiti Wa Hadith Katika Majmau imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas amesema: "Amesema Mtume(s.a.w.w) Dhwarii ni kitu katika moto kinafanana na mwiba kichungu kuliko shubiri. Kinanuka uvundo kuliko mzoga na ni kikali kuliko moto. Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu kwake Mwenyezi Mungu "Hawatasikia humo upuzi" ni upuuzi na uwongo." Kuhusu Aya Na 22 amesema yaani sio mwenye kuwachunga. Katika Durril Manthur ametoa Ibn Jariyr, Hakim, Ibn Murdawayh na Bayhaqi kutoka kwa Jabir amesema: 'Amesema Mtume(s.a.w.w) : "Nimeamrishwa kupigana na watu mpaka waseme: "La ilaha illa llahu" wakisema, damu yao na mali zao zitakuwa zimesalimika isipokuwa kwa haki yake, na hisabu yao iko juu ya Mwenyezi Mungu, kisha akasoma aya "Basi kumbusha hakika wewe ni mkumbushaji wewe si mtenza nguvu ". Hakuna dalili yoyote kwamba kuvua kunatokana na dhamiri ya wao na hilo ni dhahiri.

Katika hiyo Durril Manthur katika hadith iliyopokewa kutoka kwa Abu Jaffar(a.s) kuhusu kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Lakini mwenye kupa mgongo na akakufuru" anakusudia yule asiyewaidhika, na asiyesadiki akakanusha uungu na akakufuru neema. "Atamwadhibu Allah adhabu kubwa mno!" anakusudia adhabu nzito ya milele. "Hakika ni kwetu sisi marejeo yao" anakusudia mwisho wao "kisha hakika ni juu yetu sisi hesabu yao" anakusudia malipo yao. Katika Nahj aliulizwa Ali(a.s) vipi atawahisabu Mwenyezi Mungu watu na wingi wao huo? Akasema: Kama vile anvyowaruzuku na wingi wao. Kukaulizwa vipi atawahisabu na hawamuoni? Akasema kama anavyowaruzuku na hawamwoni.

Katika hiyo hiyo Nahj amesema As Sadiq, kila Umma utahisabiwa na Imam wa zama zake. Na wanawajua maimam marafiki zao na maadui zao kwa alama zao na ndio maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na juu ya mahali hapo palipoinuka watakuaweko watu hao watakaowafahamu wote kwa alama zao ". (7:46). Imepokewa hadith kwa maana haya katika Baswir kutoka kwa Sadiq, katika Kafi kutoka kwa Baqir na Kadhim(a.s) na katika Faqih kutoka kwa Hadi(a.s) .


14

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA AL-FAJR (ALFAJIRI) (NA. 89)

INA AYA 30

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

وَالْفَجْرِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa Alfajiri.

وَلَيَالٍ عَشْرٍ ﴿٢﴾

2. Na (kwa) masiku kumi.

وَالشَّفْعِ وَالْوَتْرِ ﴿٣﴾

3. Na (kwa) shufwa na witiri.

وَاللَّيْلِ إِذَا يَسْرِ ﴿٤﴾

4. Na (kwa) usiku unapopita.

هَلْ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجْرٍ ﴿٥﴾

5. Katika hayo mna kiapo kwa mwenye akili.

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ ﴿٦﴾

6. Je, hujui jinsi Mola alivyoifanya (kabila) ya Aad.

إِرَمَ ذَاتِ الْعِمَادِ ﴿٧﴾

7. Iram wenye nguzo ndefu?

الَّتِي لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِي الْبِلَادِ ﴿٨﴾

8. Ambayo haikuumbwa mfano wake katika miji.

وَثَمُودَ الَّذِينَ جَابُوا الصَّخْرَ بِالْوَادِ ﴿٩﴾

9. Na (kabila) ya Thamud ambao walikua wakipasua majabali katika (mji wa) waad.

وَفِرْعَوْنَ ذِي الْأَوْتَادِ ﴿١٠﴾

10. Na Firaun mwenye vigingi.

الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ ﴿١١﴾

11. Ambao walipetuka mipaka katika miji.

فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ ﴿١٢﴾

12. Wakazidisha humo mambo maovu.

فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ ﴿١٣﴾

13. Akawateremshia Mola wako namna za adhabu.

إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ ﴿١٤﴾

14. Hakika Mola wako ni Mwenye kuotea.

فَأَمَّا الْإِنسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ ﴿١٥﴾

15. Ama mwanadamu - Mola wake anapomjaribu, akamtukuza, akamneemesha, husema: Mola wangu amenitukuza.

وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ ﴿١٦﴾

16. Ama anapomjaribu akampunguzia riziki yake husema Mola wangu amenitweza.

كَلَّا بَل لَّا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ ﴿١٧﴾

17. La, si hayo tu! Bali nyinyi humumtukuzi yatima.

وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿١٨﴾

18. Wala hamhimizani katika kumlisha maskini.

وَتَأْكُلُونَ التُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا ﴿١٩﴾

19.Na mnakula mirathi kula kwa pupa.

وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا ﴿٢٠﴾

20. Na mnapenda mali mapenzi makubwa.

كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا ﴿٢١﴾

21. Si hivyo! Ardhi itakapo pondwa pondwa!

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا ﴿٢٢﴾

22. Akaja Mola wako na Malaika (wamejipanga) safu kwa safu.

وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَ ۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٢٣﴾

23. Ikaletwa siku hiyo Jahannam! Siku hiyo ndipo mwanadamu atakapokumbuka, lakini kutamfaa nini kukumbuka (kwake)?!

يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي ﴿٢٤﴾

24. Atasema laiti niliyatangulizia (wema) maisha yangu.

فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ ﴿٢٥﴾

25. Basi siku hiyo hapana yoyote atakayeadhibu kama adhabu yake (Mwenyezi Mungu).

وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ ﴿٢٦﴾

26. Wala hapana yoyote atakayefunga kama kufunga kwake.

يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ ﴿٢٧﴾

27. Ewe nafsi iliyotua!

ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً ﴿٢٨﴾

28. Rejea kwa Mola wako hali yakuwa uradhi (na) mwenye kuridhiwa.

فَادْخُلِي فِي عِبَادِي ﴿٢٩﴾

29. Kisha ingia katika waja wangu (wema).

وَادْخُلِي جَنَّتِي ﴿٣٠﴾

30. Na uingie katika pepo yangu.

UBAINIFU

Katika Sura hii kuna makemeo juu ya kufungamana na dunia kwenye kufuatiwa na kupetuka mpaka na ukafiri, na kuwaogopesha watu wenye mambo hayo na ukali wa adhabu ya Mwenyezi Mungu katika dunia na akhera. Kwa hiyo Sura inabainisha kuwa mtu kwa ufupi wa mtazamo wake na ubaya wa fikra yake anaona kuwa anayoletewa na Mwenyezi Mungu miongoni mwa neema yake ni katika ukarimu wake Mwenyezi Mungu, na yale anayovaana nayo miongoni mwa ufakiri ni utwezo. Kwa hiyo anapetuka mpaka na kuwa mfisadi katika ardhi anapopata na anakufuru anapokosa. Basi yanayompata katika cheo na utajiri na katika ufakiri na dhiki ya maisha, ni mitihani na balaa za Mungu ili adhihirishe kwayo yale atakayoyatanguliza akhera yake kutoka katika dunia yake.

Basi mambo hayako kama vile anavyofikiri mtu na anavyosema, bali mambo yalivyo kama atakavyoyakumbuka itakapotuka hisabu na kuletwa adhabu, kwamba yaliyompata miongoni mwa ufakiri au utajiri na nguvu au unyonge yalikuwa ni mitihani ya Mungu. Ilikuwa inamuwezekania yeye kutangulizia kesho yake kutokana na leo yake, lakini hakufanya na akaathirika na mateso kuliko thawabu. Basi haitapata maisha mema katika akhera isipokuwa nafsi iliyotua kwa Mola wke, isiyoyumba kwa vimbunga vya balaa wala kupetuka mpaka kwa kipato au kukufuru kwa kukosa. Sura hii imeshuka Makka kwa ushahidi wa mpangilio wa aya zake.

Aya Na 1-4

Aya hizo zote ni kiapo. Huenda dhahiri ya neno Alfajiri, Alfajiri yoyote, lakini sio mbali kuwa makusudio yake ni Alfajiri ya usiku wa Ijumaa. Imesemwa ni swala ya Alfajiri na imesemwa ni mchana wote na imesemwa ni kupasuka chemchem katika miamba na mengineyo. Njia zote hizi ziko mbali. Kuhusu masiku kumi huenda makusudio ni masiku kumi ya mwanzo katika mwezi wa Dhulhijja. Imesemwa makusudio ni siku za mwisho za mwezi wa Ramadhan, na ikasemwa ni za mwanzo wake. Pia imesemwa ni siku kumi za mwanzo za mwezi wa Muharram na ikasemwa kuwa ni ibada ya masiku kumi kuchukulia kuwa makusudio ya Alfajiri ni swala ya Alfajiri. Kuhusu Shufwa wa Witiri maana yanakubali kufungamana na kuwa ni siku wa Tarwiya (tarehe 8 Dhul-hijja) na siku ya Arafa (tarehe 9 Dhul-hijja). Imesemwa kuwa makusudio yake ni swala mbili ( rakaa mbilimbili na rakaa moja) katika mwisho wa usiku. Na imesemwa ni swala yoyote, ziko mbili mbili na moja.

Pia imesemwa kuwa Shufwa ni siku ya Idd ya Dhul-hijja wa Witiri ni siku ya Arafa, na imesemwa Shufwa ni viumbe vyote, kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema: "Na tukawaumba wanawake na wanaume " (78:8).

Na Witiri ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) Kuna riwaya nyingi zitakazokuja juu ya kauli hizi katika utafiti wa hadith 8 Vile Vile imesemwa makusudio yake ni hisabu ya viwiliviwili na kimojakimoja na kwamba kuapa kwa hisabu, ni kuwa kudhibiti idadi katika kiasi ni katika nema kubwa itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Imesemwa kuwa ni viumbe vyote, kwa sababu vitu vyote ama vitakuwa ni jozi au kimoja. Imesemwa kuwa makusudio ya Witiri ni Adam na Shufwa ni kuwa pamoja na mkewe Hawa.

Na imesemwa Shufwa ni mchana, na usiku, na Witiri ni mchana ambao, hauna usiku nao ni siku ya Kiyama. Imesemwa Shufwa ni Safa na Marwa na Witiri ni Al-Ka'aba, na imesemwa ni siku za kabila la Ad na Witiri ni nyusiku zake. Na imesemwa Shufwa ni milango ya motoni saba. Na zaidi ya hayo mengi yaliyosemwa zaidi ya kauli thelethini na sita (36). Kuhusu kauli yake; Na (kwa) usiku unapopita ni kama Aya Na 33, Sura ya 74 inayosoma: "Na (kwa) usiku unapokucha".

Kwa dhahiri herufi Lam ni ya jinsi yaani usiku wowote, lakini wengine wamesema ni usiku wa Muzdalifa (usiku wa kuamkia Idd) ambao mahujaji wanapita kutoka Arafa mpaka Muzdalifa wanakusanyika Mahujaji kwa kumtii Mwenyezi Mungu kisha wanaamkia kwenda Mina kwa hiyo kama unavyoona itakuwa makusudio ya usiku kumi ni usiku kumi za mwanzo katika mwezi wa Hijja (Dhul-Hijja).

Aya Na 5

Ni ishara ya yaliyotangulia katika kiapo na ni swali la kuthibitisha, maana yake kwa ujumla, ni kwamba, katika hayo tuliyoyatanguliza kuyaapia yanatosha kwa mwenye akili ya utambuzi wa maneno inayopambanua haki na batili. Na Mwenyezi Mungu akiapa naye haapi isipokuwa lile lenye utukufu na daraja linakuwa ni neno la haki lenye kutiliwa mkazo ambalo halina shaka katika ukweli wake. Jawabu la kiapo limeondolewa linafahamika kutokana na yatakayotajwa katika adhabu ya watu waliopetuka mipaka na ukafiri katika dunia na akhera na thawabu ya nafsi yenye kutulia na kwamba kuneemesha kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t) juu ya aliyomneemesha na kumzuilia, hakika hayo ni majaribio na mitihani. Kuondoa jawabu la kiapo na kulileta kwa njia ya fumbo, ni kutilia mkazo zaidi katika hali ya kuonya na kutoa biashara.

Aya Na 6

Ni kabila la Aad wa kwanza nao ni kaumu ya Mtume Hud(a.s) . Vimekaririka visa vyao katika Qur'an tukufu na imeonyesha kwa wao walikuwa watu wa nchi yenye machunguu ya michanga. Yameelezwa yale yanayopatikana katika visa vyao katika Sur ya Hud (11).

Aya Na 7-8

Neno Imad ni nguzo za nyumba. Kwa dhahiri ya aya mbili hizi, ni kuwa Iram ulikua ni mji uliokuwa wa aina yake wenye majumba marefu na maguzo marefu. Hakika habari zao zimekatika na athari zao zimefutika, kwa hiyo hakuna njia ya ufafanuzi itakayoeleza hali zao kiasi cha kuituliza nafsi isipokuwa yale tu, yaliyohadithiwa na Qur'an tukufu kwa ujumla juu ya kisa chao; kwamba wao walikuwa baada ya kaumu ya Nuh, wakazi wa nchi yenye machuguu ya mchanga, na walikuwa ni wenye umbo kubwa na nguvu kubwa zaidi na walikuwa na maendeleo, miji yenye majengo mengi ardhi za rutuba zenye mabustani ya mitende na mimea na mahali pazuri. Kimeelezewa zaidi kisa chao katika Sura ya Nuh.

Imesemwa kuwa makusudi ya neno Iram ni hao kaumu ya Aad - na sili na neno hilo ni jina la baba yao kwa hiyo wakaitwa kwa jina la baba yao, kama inavyosemwa Quraish kwa kukusudia wanawe au Israil kwa kukusudia wana Israil. Makusudio ya kusema wenye maguzo marefu ni kuwa wao ni watu wenye nguvu, na maana yake ni Je, hujui jinsi Mola wako alivyoifanya (kabila) ya Aad Iram wenye nguvu ambao haukumbwa mfano wao katika miji, au katika dunia nzima, lakini hayo hayaepukani na kuwa mbali na dhahiri ya tamko. Ya umbali zaidi ya yaliyosemwa kwamba makusudio ya kuwa wao ni wenye maguzo marefu, ni vile kuwa wao walikuwa ni watu wa kuazimia kusafiri katika wakati wa maleleji na mimea inaponyauka basi hurudi majumbani mwao. Kisa cha bustani ya Iram kilichopokewa kutoka kwa Wahb bin Manbih na Kaabulahbar, ni katika ngano za watu wakale tu!

Aya Na 9

Yaani walipasua miamba ya milima kwa kuichonga kuwa nyumba. Aya hii iko katika maana ya aya inayosema: "Na mnachonga milimani majumba mkastarehe tu! " (26:149)

Aya Na 11

Huyo ni Firaun wa Musa, ameitwa mwenye vigingi- kutokana na yaliyo katika baadhi ya riwaya - kwamba yeye alikuwa akitaka kumuadhibu mtu humnyoosha juu ya ardhi na kuipingilia mikono yake na miguu yake kwa vigingi vine katika ardhi, au humnyoosha juu ya ubao na kumfanyia hivyo. Hayo yanatiliwa nguvu na yale aliyoyasimulia Mwenyezi Mungu kuhusu kauli yake Firaun akiwatisha wachawi walipomwamini Musa kwa kusema: "Nitawasulubu katika mashina ya mitende ." (20:71).

Hakika wao walikuwa wakiwamba mikono ya msulubiwa na miguu yake juu ya ubao wa kusulubu.

Aya Na 12

Ni sifa wa waliotajwa, Ad, Thamud na Firaun, maana yako wazi.

Aya Na 13

Ametaja kumimina kwa njia ya fumbo kwa maana ya kufuatana, maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu aliteremsha kwa mataghut wote hawa wenye kukithirisha uharibifu mara tu, baada ya kupetuka kwao mipaka na ufisadi wao, adhabu kali ya aina yake yenye kufuatana mfululizo.

Aya Na 14

Kuwa Mwenyezi Mungu yuko katika kuotea, ni istiara ya kufananisha Mwenyezi Mungu anavyochunga matendo ya waja wake na mtu anayeotea mtu apite amchukue, bila ya kutambua. Basi Mwenyezi Mungu anachunga matendo ya waja wake, wakipetuka mipaka na kukithirisha ufisadi tu, huwaadhibu kwa adhabu kali. Aya hiyo ni sababu ya yaliyotangulia katika mazungumzo ya kuadhibu wanaopetuka mipaka wenye kukithirisha ufisadi. Kuongeza dhamira katika neno Mola na kuwa "mola wako", ni kuonyesha kuwa desturi hiyo ya adhabu ilikuwa ni yenye kupita katika umma wake Mtume(s.a.w.w) kama ilivyopita katika umati zilizotangulia.

Aya Na 15

Ni mtiririko wa yaliyotangulia, ndani yake mna ufafanuzi kuhusu hali ya mtu anapopewa neema ya dunia au anapozuiliwa, ni kama vile imesemwa: Hakika mtu yuko chini ya ulinzi wa Mungu, anaotewa na Mola wake kuwa je, atatengenea au ataharibika?. Kwa hiyo anamjaribu na kumtahini katika yale atakayompa katika neema yake au kunyima kwake. Ama mtu yeye akineemeshwa huhisabu kwamba huo ni utukuzo wa Mungu kwa hiyo anaweza kufanya vile anavyotaka. Hivyo anapetuka mipaka na kukithirisha ufisadi. Na akimzuilia na kuifanya chache riziki yake, huhisabu kuwa ametwezwa na Mungu, basi hukufuru na kulalamika Makusudio ya mtu ni jinsi ya mtu. Kusema kwake: akamtukuza akamneemesha ni tafsiri ya majarabio yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemtukuza na akampa nema iliamshukuru na amuabudu, lakini yeye mtu mwenyewe anajaalia ni mateso juu ya nafsi yake yanayofuatiwa na adhabu. Kuhusu neno "husema Mola wangu amenitukuza" yaani amenijaalia juu ya ukarimu unaotokana naye kwa neema ambazo amenipa, kwa hiyo ninaweza kufanya lile ninalo taka.

Kusema "Mola wangu amenitukuza" kuko katika mnasaba wa kumzingatia Mungu - hayo hayasemwi na waabudu masanamu na wanaomkanusha Mungu - na ni kwenye kujengwa juu ya kumkubali Mungu kwa kiasi cha maumbile yalivyo ijapokuwa ulimi unajizuia na hilo, vile vile aya inayofuatia.

Aya Na 16

Yaani akifanya mtihani ikawa dhiki riziki yake, basi husema Mola wangu amenidhalilisha. Kutokana na aya hizi (15 na 16) yanadhihirika mambo yafuatayo:

Kwanza : Kukaririka majaribio na kuthibitika katika sura mbili za neema na kuzuiliwa, ni kwamba kupewa neema na kuzuiliwa vyote ni katika majaribio na mitihani ya Mungu kama alivyosema: "Tutawajaribu kwa (mambo) ya shari na heri " (21:35).

Pili : Kupewa neema kwa kuwa ni fadhila na rehema, ni utukufu iwapo wanadamu hawakukubadilisha kuwa adhabu. Tatu: Mtu anaona wema wake katika maisha ya dunia ni kuneemeshwa katika dunia ka neema za Mwenyezi Mungu, hivyo anaona ndio utukufu na kunyima kunakotokana na Mwenyezi Mungu anakuona kuwa ni uovu. Ilivyo nikuwa, utukufu uko katika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa imani na amali njema, ni mamoja iwe ni utajiri au ufakiri, kupata au kukosa, yote hayo ni mitihani. Wanayo maana nyengine kuhusu aya hizi mbili lakini tumeacha kuyaonyesha kwa kutokuwa na umuhimu wowote.

Aya Na 17

Na makemeo kwa yale wanayoyasema kwamba utukufu uko katika utajiri na kwamba ufakiri na kukosa ni madhila. Basi si hivyo isipokuwa kutoa kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t) neema, na kuizuia yote hayo ni mitihani anayojaribiwa mtu. Kusema kwake Mwenyezi Mungu: Bali nyinyi hamumtukuzi yatima, ni kutilia mkazo makemeo kwa kutaja baadhi ya neema ambayo haikusanyi utukufu kabisa, kama kukosa kumtukuza yatima kwa kula urathi wake na kumzuilia nao na kukosa kuhimizana juu ya kumlisha maskini kwa ajili ya kupenda mali. Kuacha kumtukuza yatima ni kumzuilia na urathi wa mzazi wake kama walivyokuwa wakiwazuilia watoto wadogo na kurithi, kama inavyotia nguvu aya inayofuatia.

Aya Na 18

Yaani hamuhimizani kutoa sadaka. Hayo yanatokana na kupenda mali sana kama ilivyo katika aya inayofuatia.

Aya Na 19

Maana ya neno Lamma ni mtu kula fungu lake na la mwengine, na kula chochote anachokipata kiwe kibaya au kizuri. Aya hii ni tafsiri ya kukosa kumtukuza yatima kama iliyotangulia.

Aya Na 20

Aya hiyo nayo inafasiri kukosa kuhimizana katika kumlisha maskini kama ilivyotangulia.

Aya Na 21

Makusudio yake ni kufika siku ya Kiyama. Hilo ni kemeo la pili kutokana na yale anayoyasema mtu katika hali mbili za utajiri na ufakiri. Aya hii inasimamia sababu za makemeo kwa maana ya kuwa, sio kama anavyosema mtu, kwani yeye atakumbuka kitakaposimama Kiyama kwamba maisha ya dunia na vilivyomo ndani yake miongoni mwa utajiri na ufakiri sio makusudio kwa dhati, bali yamekuwa ni majaribio na mitihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) Anapambanua kutokana na mitihani hiyo mwema na mwovu na inamuandalia mtu yale atakayoishi kwayo katika akhera. Hakika mtu ametatizika akadhania kuwa utukufu ndio makusudio kwa dhati akajishughulisha nao na wala asitangulize chochote kwa maisha yake ya Akhera. Kwa hiyo wakati huo atatamani huku akisema: Laiti mimi niliyatanguliza (wema) maisha yangu, lakini matamani hayatatoshelezea lolote na adhabu.

Aya Na 22

Kunasibisha kuja Mungu ni katika mikanganyo ambayo inahukumuliwa na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) "Hakuna chochote mfano wake " (42:11). Na yaliyokuja katika alama za Kiyama, ni katika upambanuzi wa kuondoa sababu na mapazia yaliyowaziba na kushihiri kwamba Mwenyezi Mungu ni haki iliyo wazi. Kwa hiyo yale yaliyopokewa katika hadith yanalirudia hilo kwamba makusudio ya kuja kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni kuja amri yake kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na amri siku hiyo ni ya Allah " (82:19).

Kunatilia nguvu njia hii kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Je, kuna jengine wanalongojea ila kuwafikia Allah katika vivuli vya mawingu na kuwafikia malaika na imekwishapitishwa amri ". (2:210).

Kama tukikikutanisha na kusema kwake. "Je, wanangoja jengine (hawa makafiri) ila wawafikie Malaika? Au iwafikie amri ya Mola wako? " (16:33). Kwa hiyo basi kuna neno lililondolewa, kukadiria kwake ni: ikaja amri ya Mola wako. Au kunasibisha kuja Mungu ni kwa majazi (fumbo) ya kiakili.

Aya Na 23

Sio mbali kuwa makusudio ya kuletwa Jahannam ni kudhihirishwa, kama ilivyo katika kauli yake. "Basi tumekuondolea pazia yako kuona kwako leo kumekuwa kukali " (50:22).

Kusema kwake "Siku hiyo atakumbuka mtu" yaani atakumbuka kwa uwazi zaidi kwamba yale yaliyokuwa yakimjia katika maisha ya dunia miongoni mwa heri au shari yalikuwa ni majaribio ya Mwenyezi Mungu na mitihani yake na yeye akapuuza. Hivyo ndivyo unavyofahamisha mpangilio wa maneno. Kusema kwake "wapi kutamfaa kukumbuka" ni fumbo la kukosa kunufaika na kukumbuka isipokuwa kukumbuka kungefaa kama angekuunganisha na kutubia na kutenda amali njema kwa yale aliyoyapuuza, na leo ni siku ya malipo sio siku ya kutubia na kufanya amali.

Aya Na 24

Maisha hapa ni ya akhera au ni maisha ya kihakika ambayo ndiyo hayo maisha ya akhera, kama kulivyozindua kusema kwake: "Na hayakuwa haya maisha ya dunia ila ni upuzi na mchezo; na nyumba ya akhera ndio maisha hasa: Laiti wangalijua ". (29:64) Makusudio ya kuyatanguliza maisha ni kuyatangulizia amali njema.

Aya Na 25-26

Dhamir katika neno adhabu na kufunga inamrudia Mwenyezi Mungu. Yaani siku hiyo hakika adhabu yake na kufunga kwake kutakuwa zaidi ya adhabu ya kiumbe chochote. Wengine wamesoma kwa Fat'ha ya Dhali na Thau. Dhamir kwa kisomo hiki itakuwa inamrudia mtu, yaani hataadhibishwa yoyote siku hiyo mfano wa adhabu ya mtu wala hatafungwa yoyote siku hiyo mfano wa kufunga kwa mtu.

Aya Na 27

Mpangilio wa maneno uonaokubaliana na 'nafsi' hii kutokana na yale yaliyotajwa kabla yake katika sifa zinazofungamana na dunia, upitukaji mipaka, ufisadi na ukafiri na yale yaliyoahidiwa katika mwisho mbaya, unaonyesha kuwa nafsi yenye kutulia ni ile inayotulizana kwa Mola wake na kurudhia kile kinachoridhiwa na Mola wake, inajiona kuwa ni mtumwa asiyejimiliki na chochote katika kheri na inaiona dunia ni nyumba ya kupita, na inayoyakabili katika hiyo dunia miongoni mwa utajiri au ufakiri, manufaa au madhara, ni majaribio na mitihani ya Mungu. Kwa hiyo mtiririko wa neema haumpelekei kupetuka mipaka, kufanya ufisadi mwingi au kujifanya mkubwa wala ufakiri na kukosa kitu hakumuingizi katika ukafiri na kuwacha kushukuru, bali yeye ni mwenye kutulizana, hakosei njia yake yenye kunyooka kwa kupetuka mipaka au kuwapitusha mipaka wengine.

Aya Na 28

Kuisifu nafsi kwa hali yakuwa radhi ni kwamba kutulizana kwale kwa Mola wake kunalazimisha kuridhia kwake yale yaliyokadiriwa na kuhukumiliwa na wala hayamchukizi. Mtu akimridhia Mola wake naye humridhia, kwani Mwenyezi Mungu S.W.T. huchukia sana kutoka mja katika kipambo chake. Basi akilazimiana na njia ya kuwa mja wa Mwenyezi Mungu, litawajibisha hilo radhi ya Mola wake, kwa hiyo ndio maana hali ya kuridhia imefuatishwa na kuridhiwa.

Aya Na 29

Inaungana na aua iliyotangulia inafahamisha kuwa mwenye nafsi yenye kutulia yuko katika kundi la waja wa Mwenyezi Mungu. Hilo ni kwamba alipotulia kwa Mola wake alijiondoa kujiona huru, na akaridhia ile iliyohaki kwa Mola wake, akaona dhati yake, sifa zake na vitendo vyake ni miliki ya Mola wake. Hakupita katika yaliyokadiriwa kuhukumiliwa wala katika yaliyo amrishwa na kukatazwa isipokuwa yale anayoyataka Mola wake. Huko ndiko kudhihiri uja wenye kutimia. Kwa hiyo kusema kwake "ingia katika waja wangu" ni ikrari ya mahali pa uja wake hiyo nafsi. Neno lake "na ingia katika pepo yangu" ni kubainisha kituo chake. Kuitegemeza pepo kwa dhamiri ya mwenye kusema (pepo yangu) ni utukuzo mahsusi wala halipatikani hilo katika maneno yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) isipokuwa katika aya hii tu!.

Utafiti Wa Hadithi Katika Majmau kuhusu kusema kwake "na (kwa) Shufwa na Witiri, imesemwa kuwa Shufwa ni kuumba kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema: "Na tukawaumba nyinyi wanaume na wanawake (jozi) " (78:8). na Witiri ni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hadithi hiyo imeyoka kwa Atiyal-Aufiy, Abu Saleh, Ibn Abbs na Mujahid, hiyo ni riwAya Na Abu Saad El-Khudriy naye amepokea kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) .

Imesemekana kuwa Shufwa na Witiri ni swala: kuna katika hiyo swala ya Shufwa na ya Witiri. Hiyo ni riwAya Na Ibn Haswin naye amepokea kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) .

Imesemwa kuwa Shufwa ni siku ya kuchinja na Witiri ni siku ya Arafa, kutoka kwa Ibn Abbas Akrama na Adh-Dhah-hak nayo ni riwAya Na Jabir kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) .

Imesemwa kuwa Shufwa ni siku ya Tarwiya (siku ya nane ya mwezi Dhul-Hijja) na Witiri ni siku ya Arafa (siku ya tisa ya Dhul-Hijja), hayo yamepokewa kutoka kwa Abu Jaffar na Abu Abdillah.

Riwaya hizo tatu zimepokewa kwa njia ya Ahli Sunnah. Inawezekana kukusanya kati ya hizo riwaya kwamba makusudio ni Shufwa na Witiri yoyote. Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu "Masiku kumi" amesema ni ya mwezi wa Dhul-Hijja na "Shufwa na Witiri" amesema ni rakaa mbili na moja. Katika hadith Shufwa ni Hassan na Hussein na Witiri ni Amiirul Muuminiin(a.s) . Katika riwAya Na Abu Jarud, kutoka kwa Abu Jaffar kuhusu Aya Na tano anasema ni "Mwenye akili". Katika ulal kwa isnadi yake kwa Abana Al-Ahmar amesema: "Nilimuuliza Abu Abdillahi kuhusu kusema kwake Mwenyezi Mungu. Na Firaun mwenye vigingi, kwanini ameitwa hivyo?" Akasema : "Kwa sababu alikuwa anapomwadhibu mtu humtandaza juu ya ardhi na kumnyoosha mikono yake na miguu yake kisha humwamba kwa vigingi vinne. Mara nyengine humtandaza juu ya ubao na kumwamba miguu yake na mikono yake kwa vigingi vine, kisha humwacha mpaka afe, ndio Mwenyezi Mungu akamwita mwenye vigingi."

Katika Majmau kuhusu "Hakika Mola wako ni mwenye kuotea" imepokewa kutoka kwa Ali(a.s) kwamba yeye amesema: Hakika maana yake ni kwamba Mola wako ni muweza wa kuwalipa waasi malipo yao. Katika hiyo hiyo Majmau imepokewa kwa Swadiq amesema maana ya neno Mirswad ni korongo kwenye Swirat halipiti korongo hilo mja ambaye hakujiweka kimja. Kutoka kwa Ghawali naye kutoka kwa Aswadiq(a.s) katika hadithi ya kutafsiri kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t): "Na dhun-nun (Yunusi) alipoondoka hali amechukiwa na akadhani ya kwamba hatutamdhikisha." (21:87) Amesema: Husikii kauli yake Mwenyezi Mungu. "Ama amjaribupo, akamdhikisha riziki yake, husema: Mola wangu amenitweza"? Katika Tafsiri ya Qummi katika riwAya Na Abu Jarud, kutoka kwa Abu Jaffar(a.s) kuhusu kauli yake "si hivyo ardhi itakapopondwa pondwa' Amesema hilo ni tetemeko.

Katika Durril-Manthur ametoa Ibn Murduwayh kutoka kwa Ali bin Abu Twalib amesema: "Amesema Mtume(s.a.w.w) he, mnajua nini tafsiri ya aya hii! "Si hivyo ardhi Takapondwa pondwa ikaleta siku hiyo Jahannam" akasema: Kitakapokuwa Kiyama Jahannam itaongozwa kwa hatamu elfu sabini kwa mikono ya Malaika elfu sabini itachomoza mchomozo mmoja, lau Mwenyezi Mungu sikuifunga ingeliunguza mbingu na ardhi. Hadith hii pia ni yenye kupokewa kutoka cha Amali Sheikh kwa isnadi yake kutoka kwa Arridha naye kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa Ali(a.s) naye kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) .

Katika Uyun katika mlango wa yaliyokuja kutoka kwa Arridha katika Akhbaru Tawhid kwa isnadi yake kutoka kwa Ali bin Fadh-dhal naye kutoka kwa baba yake amesema: Nilimuuliza Arridha(a.s) kuhusu kusema kwake Mwenyezi Mungu "Na akaja Mola wako na Malaika (wamejipanga) safu kwa safu" Akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hasifiwi na kuja na kwenda isipokuwa maana ni, na ikaja amri ya Mola wako."

Katika Kafi kwa isnadi yake kutoka kwa Sadiyr Asswayrafiy amesema: "Nilimwambia Abu Abdillah(a.s) niwe mkombozi wako ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, Je, muumin anachukia anapotolewa roho yake akasema: Hapana, hakika yeye anapojiwa na Malaika wa Mauti kuchukua roho yake hufadhaika, Malaika wa Mauti huwambia: Ewe walii wa Mwenyezi Mungu usifadhaike, ninaapa kwa ambaye amempa utume Muhammad, hakika mimi nitakufanyia wema na upole kuliko mzazi, fungua macho uone.

Hapo atafanishiwa Mtume(s.a.w.w) , Amirul Muminiin, Fatima, Hassan and Hussein na Maimamu katika kizazi chao(a.s) ataambiwa hawa ni marafiki zako. Atafungua macho yake na atanadi mnadi kutoka mbele ya Mwenyezi Mungu atasema; Ewe nafsi iliyotua! Kwa Muhammad na Ahlul Bait wake rudi kwa Mola wako hali ya kuridhia wilaya na hali ya kuridhiwa thawabu, ingia katika waja wangu yaani Muhammad na Ahlul Bait wake na ingia katika pepo yangu. Litakua ni jambo la kupendeza kwake kutolewa roho yake na kumsikia mnadi. Amepokea Qummi riwaya kwa maana haya katika Tafsiri yake na Al-Barqi katika Mahasin.


15

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA BALAD (MJI) (NA. 90)

INA AYA 20

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

لَا أُقْسِمُ بِهَـٰذَا الْبَلَدِ ﴿١﴾

1. Naapa ka mji huu.

وَأَنتَ حِلٌّ بِهَـٰذَا الْبَلَدِ ﴿٢﴾

2. Na hali yakuwa wewe ni mkazi wa mji huu.

وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ ﴿٣﴾

3. Na (kwa) mzazi na alichokizaa.

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي كَبَدٍ ﴿٤﴾

4. Hakika tumemuumba mwanadamu, katika mateso.

أَيَحْسَبُ أَن لَّن يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ ﴿٥﴾

5.Je anadhani kwamba hatawezekana na yeyote?

يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُّبَدًا ﴿٦﴾

6. Anasema: Nimepoteza mali mengi!

أَيَحْسَبُ أَن لَّمْ يَرَهُ أَحَدٌ ﴿٧﴾

7. Anadhani kwamba hakuonekana na yeyote?

أَلَمْ نَجْعَل لَّهُ عَيْنَيْنِ ﴿٨﴾

8. Ja hatukumpa macho mawili?

وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ ﴿٩﴾

9. Na ulimi na midomo miwili?

وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ ﴿١٠﴾

10. Tukamuonyesha njia mbili?

فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ ﴿١١﴾

11. Basi mbona hakupita njia nzito?

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ ﴿١٢﴾

12. Na umejuaje, ni ipi njia nzito?

فَكُّ رَقَبَةٍ ﴿١٣﴾

13. Ni kumwacha huru mtumwa.

أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ ﴿١٤﴾

14. Au kumlisha siku ya njaa.

يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ ﴿١٥﴾

15. Yatima aliye jamaa.

أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ ﴿١٦﴾

16. Au maskini mwenye haja.

ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ ﴿١٧﴾

17. Kisha akawa ni katika ambao wameamini, wakausiana kusubiri na wakausiana kuoneana huruma.

أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ ﴿١٨﴾

18. Hao ndio watu wa heri.

وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ ﴿١٩﴾

19. Na ambao wamezikanusha alama zetu, hao ndio wa shari.

عَلَيْهِمْ نَارٌ مُّؤْصَدَةٌ ﴿٢٠﴾

20. Juu yao ni moto uliokomewa.

UBAINIFU

Sura inataja kwamba umbo la mtu ni lenye kujengwa juu ya tabu na mashaka. Huwezi kukuta jambo lolote katika mambo ya maisha isipokuwa litakuwa limekutanishwa na matatizo na tabu, tangu roho inapoingia katika kiwiliwili chake mpaka anapokufa. Hana raha inayoepukana na tabu na mashaka, wala furaha isiyoandamana na misukusuko au huzuni isipokuwa katika nyumba ya akhera tu, mbele ya Mwenyezi Mungu. Basi mtu na avumulie uzito wa taklifa za Mwenyezi Mungu kwa kusubiri juu ya kufanya twaa na kuepukana na maasia. Na ajitahidi kueneza huruma juu ya wale waliopatwa na majaribio na balaa za dunia kama uyatima, ufakiri na maradhi ili awe ni katika watu wa heri. Kama si hivyo, basi akhera yake itakuwa kama dunia yake na atakuwa katika watu waovu juu yao ni moto uliofungiwa.

Mpangilio wa Aya Na Sura nii unafanana na wa Makka, kwa hiyo unatilia nguvu kuwa Sura imeshuka Makka. Baadhi wamedai kuwa hilo (la kushuka Makka) ni kwa Ijmai (mkusanyiko wa makubaliano ya wanazuoni). Imesemekana kwamba Sura hii imeshuka Madina na kwamba mpangilio wa aya za mwanzo hausaidii kusema kuwa imeshula Makka. Na pia imesemwa imeshuka Madina isipokuwa aya nne za mwanzo. Utakuja ufafanuzi katika utafiti wa hadith (Inshallah).

Aya Na 1

Wametaja kuwa makusudio ya mji huu ni Makka na hilo linatilia nguvu kuwa Sura imeshuka Makka.

Aya Na 2

Kuliweka jina dhahiri mahali pa dhamir ni kwa ajili ya kuadhimisha (mji huo) na kushughulika nao ambao ni mji mtukufu. Neno Hillun ni masdar kiarifa chenye kutumika kama jina kwa maana ya kukaa na kuthibiti mahali. Masdar hapa imekuja kwa maana ya (fail) Mtendaji maana yake kwa ujumal: ninaapa kwa mji huu na hali ya kuwa wewe ni mkazi wake. Na hilo uzindushi juu ya utukufu wa Makka kwa sababu ya kukaa kwake Mtume(s.a.w.w) na kuwa ni mahali pake pa kuzaliwa.

Inasemekana jumla hiyo imeingia kati tu; kati ya kiapo na chenye kuapiwa na makusudio yake ni kuhalalishwa. Anasema katika Kash-shaf "Na ameingilia kati ya kiapo na chenye kuapiwa kwa Kusema: "Na hali yakuwa wewe ni mwenye kuhalalishwa katika mji huu" yaani ni katika mateso kwamba mfano wako wewe juu ya ukubwa na utukufu wako unahalalishwa katika mji huu mtukufu, kama linavyohalalishwa windo nje ya haram. Wanaharamishwa kuua windo na kupukusa majani, lakini wanahalalisha kukutoa wewe na kukuua. Hadith hiyo imepokewa katuka kwa Sharhabil. Katika hilo ni uthabiti kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na uwezekano na mateso aliyokuwa akiyapata kutoka kwa watu kustajaabu kutokana na hali yao ya uadui. Kisha akasema: "au alimfariji Mtume kwa kuapa kwa mji wake kwamba mtu haepukani na shida kisha akaingilia kati kwa kusema kuwa kiaga chake cha ushindi wa Makka kitatimu ili kumpa faraja, kwa hiyo akasema: na hali ya kuwa wewe ni mwenye kuhalalishiwa (yaliyoharamu) katika mji huu yaani na hali wewe utahalilishiwa hapo mbeleni utafanya ndani ya mji huu yale utakayoyataka maka kuua na kuteka".

Kwa hiyo inakuwa tafsiri ya neno Hillum ni kwa maana ya mwenye kuhalilishiwa kinyume chake ni mwenye kuharamishiwa; yaani tutakuhalalishia siku ya ushindi wa kuichukua Makka kwa muda utapigana na utamuua unayemtaka.

Aya Na 3

Ni kulazimisha namna ya kunasibika na kufungamana kati ya kiapo na chenye kuapiwa, kunapelekea kuwa makusudio ya mzazi na alichokizaa, kwamba kuna mnasaba iliowazi kati yake na mji wenye kuapiwa. Hilo linakubaliana na Ibrahim na mtoto wake Ismail(a.s) . Wao ndio chanzo cha kujengwa mji wa Makka na ndio wajenzi wa Al-Ka'aba tukufu: Mwenyezi Mungu anasema; "Na (kumbukeni) alipoinua Ibrahim kuta za nyumba (Al-Ka'aba) na Ismail (pia); (wakaomba wakasema) Ewe Mola wetu tutakabalie (amali yetu). Hakika wewe ndio mwenye kusikia, na mwenye kujua ." (2:127).

Kuleta herufi "Maa" yenye maana ya ambacho badala ya kuleta Man yenye maana ya ambaye, ni kwa ajili ya kulikuza jambo na kulistaajabia jambo lenyewe; kama alivyosema; "na Allah anajua zaidi alichokizaa ." (3:36).

Maana kwa ujumla ni naapa kwa mzazi mwenye jambo kubwa ambaye ni Ibrahim na alichokizaa ambacho ni mtoto wa ajabu wa jambo lake mwenye kubarikiwa; naye ni Ismail. Na wao wawili ndio waliojenga Al-Ka'aba. Ufahamisho wa aya tatu ni kuapa kwa mji mtukufu Makka kwa Mtume ambae amekaa katika mji huo na kwa Ibrahim na Ismail ambao wameujenga. Inasemekana kuwa makusudio ya mzazi ni Ibrahim na alichokizaa ni watoto wake wote Waarabu. Lakini ni umbali kwa Mwenyezi Mungu kuwa Mtume (SAWW) na Nabii Ibrahim(a.s) awakutanishe na watu kama akina Abu Lahab, Abu Jahal na wengineo katika viongozi wa ukafiri na awaapie wote. Na Ibrahim(a.s) alijiepusha na kila asiyemfuata katika watoto wake juu ya Tawhid wakati aliposema: "Na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu. Mola wangu! Hakika (masanamu) hawa wamepoteza watu wengi. Basi aliyenifuata ni wangu mimi na aliyeniasi (unaweza kumsamehe) kwani wewe ni mwingi wa msamaha na Mwingi wa rehema ". (14:35-36).

Basi mwenye kufasiri alichokizaa kuwa ni watoto wa Ibrahim, ni juu yake kuwahusisha waislamu tu, katika kizazi chake, kama ilivyo katika dua ya Ibrahim. "Ewe Mola wetu! Utufanye tuwe wenyenyekevu kwako. Na miongoni mwa kizazi chetu (pia ufanye) umma mnyenyekevu kwako na utuonyeshe njia ya ibada yetu na utusameha ." (2:128).

Inasemekana kuwa makusudio ya mzazi na alichokizaa na Adma(a.s) na kizazi chake chote kwa kuzingatia kuwa kilichoapiwa viapo hivi ni kule kuumbwa mwanadamu katika mateso. Na Mwenyezi Mungu ameweka utaratibu wa kuzaliana ili kuhifadhi jinsi hii. Kwa hiyo ameapia katika aya hizi kwa kupitia utaratibu huu na matokeo yake - nayo ni mzazi na alichokizaa - kuwa mtu yuko katika tabu na mateso kulingana na namna ya kuumbwa kwake kuanzia anapopata uhai mpaka kufa.

Maelezo haya hayana ubaya, lakini kunabakia kubainisha mnasaba uliopo kati ya mji wa Makka na mzazi na kila mwenye kuzaliwa katika kuwakusanya kwenye viapo. Pia imesemwa kuwa makusudio ni Adam na watu wema katika kizazi chake. Maelezo haya ni kama yanamtakasa Mwenyezi Mungu kuapia kwa maadui wake wenye kupetuka mipaka na wafisadi katika makafiri.

Imesemwa kuwa makusudio ni kila mzazi na kila mwenye kuzaliwa na pia imesemwa kuwa ni mwenye kuzaa na asiyezaa kwa kuchukulia herufi Maa kuwa ni ya kukanusha. Vile vile imesemwa makusudio ya mzazi ni Mtume na alichokizaa ni umati wake kwa sababu yeye yuko katika daraja ya baba kwa umati wake; lakini hayo yote ni maelezo yaliyo mbali.

Aya Na 4

Jumla hiyo ni jawabu ya kiapo. Mateso katika umbile la binadamu na tabu katika mambo yake yote ya uhai ni jambo lisilofichika kwa kila mwenye roho. Mwanadamu hakusudii neema yoyote katika neema ya dunia ila huwa na matatizo katika dunia uzuri wako. Wala hawezi kupata kitu chochote katika dunia ila kitakuwa kimechanganyika na usumbufu pamoja na matatizo na mateso kuongozea misiba ya balaa za dunia na matukio ya ghafla.

Aya Na 5

Katika natija ya hoja iliyotangulia, uthibitisho wake ni kuwa; kwa kuwa mtu umbile lake limejengewa tabu, hapati kitu chochote katika anavyovitaka ila hupata asivyotaka, basi yeye ni mwenye kuzungukwa katika umbile lake, mwenye kushindwa katika matakwa yake na ni mwenye kushindwa nguvu katika analoliweza. Anayemshinda katika matakwa yake na kumshinda nguvu kufanya mambo anayoyaweza ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) naye ni muweza katika kila upande, yeye anaweza kumfanyia mtu lolote analolitaka na kumchukua wakati anapomtaka.

Kwa hiyo mtu asifikirie kuwa hawezwi na yeyote, kwani fikra hiyo itampelekea kujifanya mkubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na kutakabari katika kumwabudu. Au akitoa katika baadhi ya aliyoamrishwa, na kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi anajiona ni mwingi wa mali, na husimbulia baada ya kufanya ria, kwa kusema: "Nimepoteza mali mengi!'.

Aya Na 6

Mpangilio wa aya na nyengine zinazofuatia mpaka mwisho wa Sura unaonyesha kuwa kulikuwa na baadhi ya wenye kudhihirisha Uislamu; akitoa baadhi ya mali yake anajifaharisha kuwa ametoa sana kwa kusema: nimepoteza mali mengi! Ndio ikashuka aya kumjibu, kwamba kufuzu kwa kheri za uhai hakutimu ila kwa kupita njia nzito ya kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuingia katika kundi la wale ambao wameamini wakausiana kusubiri na kuoneana huruma. Yatatilia nguvu hilo yale yatakayokuja katika utafiti wa hadith (Inshallah).

Aya Na 7

Ni kukanusha hilo neno la mtu kwa njia ya fumbo. Maana yanayopatikana ni kwamba vile mtu anavyolazimika kusema kuwa amepoteza mali mengi, akafikiria kuwa mimi nimeghafilika na sijui, yale aliyotoa? Basi amekosea katika hilo na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuona aliyoyatoa, lakini kiasi hicho hakitoshi kumfanya awe ni mwenye kufuzu kwa maisha ya kheri bali hana budi kuvumilia zaidi ya hayo katika mashaka ya kimja, apite njia nzito na awe pamoja na waumini katika yote waliyonayo.

Aya Na 8-10

Yaani tumemtayarisha katika mwili wake kwa yale anayoonea ili apate elimu ya vinavyoonwa kwa kadri ya upana wa elimu hiyo Na je, hatukumpa ulimi na midomo miwili vitakavyomsaidia kutamka yaliyo katika dhamir yake miongoni mwa elimu na aongoke kwa hilo mwenzake kwa kujua mambo yaliyofichika na macho? Na tumemfahamisha njia ya heri na ya shari kwa ilhamu itokayo kwetu, hivyo yeye anujua heri na anapambanua shari. Na aya hii ya tisa iko katika maana ya Aya Na nane ya Sura Shams Na. (91).

Aya hizo tatu ni hoja juu ya kauli yake Mwenyezi Mungu "Anadhani kwamba hakuonekana na yeyote" Yaani Yeye Mwenyezi Mungu anaona matendo ya waja wake na anajua yaliyo katika dhamiri yao kwa njia ya matendo na anapambanua kheri na shari na mema na mabaya. Kwa ujumla ni kuwa hakika Mwenyezi Mungu S.W.T. ndiye ambaye anamfahamisha yenye kuonekana kupitia macho yake mawili na namna anavyoweza kupiga picha kumfahamisha jambo asilolijua, na ni Yeye ambaye anamfahamisha yaliyo katika dhamiri kupitia kusema Je, inaingilika akilini kuwa Mwenyezi Mungu amfunulie mtu mambo ambayo Yeye mwenyewe hayajui?

Na yeye ndiye ambaye anampambanulia mtu heri na shari kwa ilhamu, Je, inawezekana kuwa Yeye hawezi kujua wala kupambanua? Yeye Mwenyezi Mungu anaona aliyoyafanya mtu na najua anayonuia kuyafanya na kuyapambanua kuwa ni kheri au shari.

Aya Na 11

Maana ya neno Iqtahama ni kuingia kwa haraka na kwa shida kujigagamiza na neno Aqaba ni njia nzito yenye vikwazo vya kupanda majabali. Kujigagamiza kuparamia njia nzito ni ishara ya kutoa (mali) ambako kunakuwa vigumu kwa mtoaji, kama itakavyoelezwa. Inasemekana kuwa jumla yote ni dua dhidi ya mtu anayesema nimepoteza mali mengi lakini si hivyo.

Aya Na 12

Ni kulikuza jambo lenyewe, kama ilivyopita katika mtazamo wake.

Aya Na 13

Yaani njia nzito ni kumwachia hutu mtumwa. Makusudio ya njia nzito ndiyo huko kuacha huru ambako ni kitendo chenyewe, na kujigagamiza kunaamanisha kukitenda. Kwa hiyo basi inaharabika kauli ya baadhi ya wanaosema kwa kumwachia huru mtumwa ndiko kupita njia nzito lakini sio njia nzito yenyewe, kwamba kuna mudhafu (neno lenye kutegemezwa) uliondolewa kukisia kwake ni: Na umejuaje ni nini kupita njia nzito, kupita njia nzito ni kumwacha huru mtumwa. Hayo yaliyotajwa katika kubainisha njia nzito ambayo ni kumwacha huru mtumwa au kulisha siku ya njaa, katika kueneza huruma yamehusishwa kutajwa kutokana na umuhimu wake. Na kumetangulizwa kuacha huru mtumwa kwa sababu dini imeshughulikia sana suala hilo.

Aya Na 14-16

Neno Matraba linatoka katika neno Turab (mchanga) na maana yake ni kushikwa na mchanga (vumbi) kutokana na shida ya ufakiri. Maana yake kwa ujumla ni, au kumlisha siku ya njaa. Yatima mwenye udugu au maskini mwenye ufakiri sana.

Aya Na 17

Kuusiana kusubiri ni kuusiana kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu na kuusiana kuoneana huruma ni kuusiana kuwaonea huruma wenye ufakiri na umaskini. Jumla nzima inaungana na jumla ya kupita njia nzito.

Aya Na 18

Neno Maymana limekuja kwa maana ya heri kinyume chake na Mash'ama uovu. Kuleta ishara ya neno (hao) kwa unavyofahamisha mpangilio wa maneno uliotangulia, ni kuwa: Wale ambao wamepita njia nzito na wakawa katika wale ambao wameamini, na wakausiana kusubiri na wakausiana kuoneana huruma ni watu wa heri. Walilolifanya katika imani na amali yao ni njema wataliona ni jambo lenye kubarikiwa, zuri na lenye kurudhiwa. Imesemekana kuwa makusudio ya Maymana ni Yamin upande wa kuume na watu wa upande ya kuume ndio ambao watapewa vitabu vyao kwa upande wao wa kuume, lakini hilo halifuatani na neno Mash'ama (uovu).

Aya Na 19

Alama zetu ni alama za mbinguni na za kinafsi nazo zinafahamisha juu ya umoja katika uungu na kuzikanusha ndio kumkanusha Mwenyezi Mungu, vile vile ni kukanusha Qur'an tukufu na aya zake na yote yaliyoshuka na kufikishwa kwa njia ya ujumbe.

Utafiti Wa Hadith Katika Majmau Aya Na 2 imesemwa kuwa maana yake ni na hali ya kuwa ni halali kwako kumuua unayemwona anastahiki kuuliwa katika makafiri. Hilo ni wakati alipoamrishwa kupigana siku wa kuichukua Makka; Mwenyezi Mungu akamhalalishia hata akaweza kupigana na kuua. AmesemaMtume(s.a.w.w) haikuhalalishiwa kwa yoyote kabla yangu wala haitakuwa halali baada yangu kwa yoyote, na mimi sikuhalalishiwa isipokuwa saa moja katika mchana. Hadith hiyo imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas, Mujahid na Ata.

Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah amesema: "Maquraish walikuwa wakiuadhimisha mji na kumuhalalisha Muhammad(s.a.w.w) katika mji huo, akasema: Naapa kwa mji na halo ya kuwa wewe ni mwenye kuhalalishwa katika mji huu anakusudia kusema kuwa wao wamehalalisha kukuudhi kukuadhibisha na kukutukana. Na wao walikuwa hawamwadhibu hata mtu aliyeua baba wa mmoja wao. Na walikuwa wakivaa majani wa mti kumpa amani, lakini wakahalalisha kwa Mtume(s.a.w.w) yale ambayo hawakumuhalalishia mwengine. Katika hiyo Majmau kuhusu Aya Na tatu imesemwa kuwa ni Adam an alichokizaa katika Mitume, mawalii na wafuasi wao. Hadith hiyo imepokewa kutoka kwa Abu Abdillahi.

Maana yaliyotangulia pia yamepokewa katika njia ya Ahli Sunna. Pia amepokea Qummi katika Tafsiri yake. Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu Aya Na sita amesema maana ya neno Lubada ni mkusanyiko. Na katika Majmau kuhusu aya hiyo hiyo imesemwa huyo aliyesema hivyo ni Harith bin Naufal bin Abdul Manaf, wakati alipofanya dhambi fulani, akataka fatuwa kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) akamwamrisha kutoa kafara, akasema: Tangu nilipoingia dini ya Muhammad mali yangu imeisha katika makafara na kulisha. Hadith hiyo imepokewa na Muqatil. Katika hiyo hiyo Majmau, imesemwa kuwa, aliulizwa Amirul-Miminin Ali(a.s) kwamba watu wanasema kuhusu neno ya Mwenyezi Mungu "Na tukamuongoza njia mbili" kwamba hizo njia mbili ni matiti? Akasema hapana njia mbili hizo ni heri na shari.

Katika Kafi kwa isnadi yake kutoka kwa Hamza bin Muhammad naye kutoka kwa Abu Abdillahi(a.s) amesema nilimuuliza kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu tukamwongoza njia mbili akasema ni njia ya heri na shari. Imepokewa riwaya hii katika Durril Manthur kwa njia ya Ali(a.s) Anas, Abu Amama na wengineo kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) .

Katika Kafi kutoka kwa Jaffar bin Khilad amesema: Alikuwa Abul-Hassan Ridha(a.s) anapokula, huletewa chano karibu na chakula chake, anaangalia chakula kizuri katika vyakula alivyoletewa na kukiweka katika chano, kisha anaamrisha kipewe masikini kisha anasoma ayah ii: 'Haya naapite hiyo njia nzito 'kisha anasema: "Mungu anajua kuwa sio kila mtu anaweza kuacha huru mtumwa kwa hiyo amewafanyia njia nyengine ya kwenda peponi".

Katika Majmau imepokewa hadith Marfuu kutoka kwa Baraa bin Azib amesema: "Alikuja bedui kwa Mtume(s.a.w.w) akasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nijulishe amali itakayonitia peponi" Mtume akasema: "Ukiwa umefupisha hotuba basi umerefusha masuala; muache huru mtu, na uifungulie shingo." Akasema yule bedui "kwani yote hayo sio kitu kimoja?" Akasema Mtume: La! Kuacha huruni kumuacha aende zake na kuifungulia shingo ni kumsaidia katika thamani yake. Kama si hivyo, basi mlishe mwenye njaa, na mnyweshe mwenye kiu na uamrishe mema na ukataze maovu na uzuiye ulimi isipokuwa katika jambo la kheri tu. Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu kauli yale Mwenyezi Mungu : "Au maskini mwenye shida" ni yule asiyeweza kujikinga na mchanga (vumbi).


16

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA SHAMS (JUA) (NA. 91)

INA AYA 15

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا ﴿١﴾

1. Naapa kwa jua na mwanga wake.

وَالْقَمَرِ إِذَا تَلَاهَا ﴿٢﴾

2. Na (kwa) mwezi unapoliandamana.

وَالنَّهَارِ إِذَا جَلَّاهَا ﴿٣﴾

3. Na (kwa) mchana unapoifunia.

وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَاهَا ﴿٤﴾

4. Na (kwa) usiku unapoifunika.

وَالسَّمَاءِ وَمَا بَنَاهَا ﴿٥﴾

5. Na (kwa) mbingu na aliyeziweka.

وَالْأَرْضِ وَمَا طَحَاهَا ﴿٦﴾

6. Na (kwa) ardhi na aliyeitandika.

وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا ﴿٧﴾

7. Na (kwa) nafsi na aliyelingamanisha.

فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا ﴿٨﴾

8. Akaifahamisha maasia yake na twaa yake.

قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا ﴿٩﴾

9. Hakika amefaulu mwenye kuitakasa.

وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا ﴿١٠﴾

10. Na hakika amepata hasara mwenye kuitweza.

كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا ﴿١١﴾

11. Ilikadhibisha (kabila ya) thamud kwa kupetuka mipaka.

إِذِ انبَعَثَ أَشْقَاهَا ﴿١٢﴾

12. Wakati walipomshakiza mwovu wao (kumuua ngamia).

فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّـهِ نَاقَةَ اللَّـهِ وَسُقْيَاهَا ﴿١٣﴾

13. Akawaambia Mtume wa Allah, (tahadharini na) ngamia wa Allah na maji yake.

فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنبِهِمْ فَسَوَّاهَا ﴿١٤﴾

14. Wakamkadhibisha (na) wakamchinja. Mola wao akaeneza (adhabu) kwa sababu ya madhambi yao, na akaifanya sawa.

وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا ﴿١٥﴾

15. Wala haogopi matokeo yake.

UBAINIFU

Sura inataja kwamba kufaulu kwa mtu ni kuitakasa nafsi yake na kuikuza makuzi mema kwa kuipamba na takua na kuitakasa na uovu. Na kupata hasara na kuzuiliwa wema ni kwa mwenye kuitweza. Yanatolea ushahidi hilo yale yaliyowapitia kabila la Thamud walipong'olewa na adhabu pale walipomkadhibisha Mtume was Saleh na kumchinja ngamia. Hilo ni kuwaonyesha watu wa Makka. Sura imeshuka Makka kwa ushahidi wa mpangilio wake wa maneno.

Aya Na 1

Maana ya neno Dhuhaa ni kukunjuka jua na kuenea mchana na neno hilo limetumiwa kwa wakati. Katika aya hii kuna kiapo kwa jua na kuangaza kwake juu ya Ardhi.

Aya Na 2

Inaungana na Aya Na kwanza na nikuapa kwa mwezi hali yakuwa unaandamia jua. Makusudio ya kuandamia ikiwa inamaanisha kule kupata mwezi nuru yake kutoka kwa jua, basi itakuwa ni kuapa kwa wakati wote wa mwezi. Na ikiwa ni kuchimbuka kwa mwezi baada ya kutua jua, basi itakuwa kuapa ni tangu kuwa mwezi mchanga mpaka kuwa mpevu.

Aya Na 3

Maana ya neno Jallaha ni kudhihirisha na dhamir ni ya Ardhi kwa maana ya kuwa: ninaapa kwa mchana unapoidhirisha ardhi kwa macho. Inasemekana kuwa dhamir ya (mtendaji) ni ya mchana na dhamir ya (mtendwa) ni ya jua, kwa maana ya kuwa, ninaapa kwa mchana wakati Mwenyezi Mungu anapolidhihirisha jua, na hiyo ni njia iliyo mbali.

Aya Na 4: Yaani unapoifunika ardhi, dhamir ni ya ardhi kama katika aya iliyotangulia. Na inasemekana kuwa ni ya jua na hiyo pia ni njia iliyo mbali, kwa sababu usiku haufuniki jua isipokuwa unafunika ardhi na vilivyo juu yake. Ibara ya kufunika ardhi imekuja kwa (kitendo cha sasa) kinyume cha aya zilizotangulia ambapo ibara zake zimekuja kwa kitendo cha muda uliopita. Hiyo ni kufahamisha kufunika uovu wa ardhi kwa wakati uliopo ambao ndio mwanzo wa kudhihiri mlingano (mwito) wa Kiislamu, kutokana na yaliyotangulia kuwa kuna muungano kati ya kuapa na mwenye kuapiwa.

Aya Na 5-6

Herufi Maa katika neno Maabanaaha na Maatwahaaha ni kiwakilishi yaani na ambaye ameziweka na kuitandika ni Mwenyezi Mungu. Kuleta ibara bila ya kumtaja Mwenyezi Mungu ni athari ya kuficha kunakofahamisha ukubwa na ajabu, kwa maana ya kuwa; Ninaapa kwa mbingu na kitu chenye nguvu cha ajabu kilichoziweka. Na ninaapa kwa ardhi na kitu chenye nguvu cha ajabu kilichoitandika. Imesemwa kuwa Maa ni kiarifa chenye kutumika kama jina kwa maana ninaapa kwa mbingu na kuziweka kwake. Na ardhi na kuitandika kwake, lakini mpangilio wa maneno katika Sura kama vile aya inayofuatia haulisaidii hilo.

Aya Na 7

Yaani ninaapa kwa nafsi na kitu chenye uwezo, ujuzi na hekima ambacho kimeilingamanisha, kuipanga umbo lake na viungo vyake na kuilingamanisha sawa nguvu yake. Makusudio na nafsi ni nafsi ya mtu yoyote. Imesemwa kuwa makusudio ni nafsi na Nabii Adam(a.s) , lakini mpangilio wa maneno hauafikiani na hilo hasa Aya Na tisa na kumi.

Aya Na 8

Neno Fujuur kama alivyotaja Raghib ni kupasua sitara ya dini. Makatazo ya Mungu ya kufanya au kuacha, ni sitara iliyowekwa kati ya binadamu na Mwenyezi Mungu na kufanya yaliyokatazwa ni kupasua sitara hiyo. Neno Taqwa kama alivyotaja Raghib ni kuifanya nafsi katika kinga ya yanayohifiwa. Makusudio ya Taqwa kwa kuilinganisha na aya inayofuatia ni kujiepusha na maovu na kujilinda na yaliyo katazwa. Imefasiriwa katika hadith kwamba ni kujichunga ya yaliyoharamishwa.

Kuifunga silika (Ilham) juu ya anuani mbili za uovu wa nafsi na takua yake, ni kwa ajili ya kufahamisha kwamba makusudio ni kwamba Mwenyezi Mungu anamfahamisha mtu sifa ya kitendo chake kuwa ni kizuri au kibaya, baada ya kumfahamisha kitendo chenyewe hasa, kwa kuangalia asili yake ya mwenzo, ambapo kitendo kinaweza kuwa ni kizuri na kibaya wakati mmoja. Kwa mfano kula mali ya yatima ambako ni kuovu na kula mali yake mwenyewe ambako ni kitendo kizuri au kuvaana na mwanamke ambako kunashirikiana kati ya zina ambayo ni uovu na ndoa ambayo ni takua. Kwa ujumla makusudio na kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemfahamisha mtu kuwa kitendo anachokifanya ama kitakuwa cha uovu au cha takua na akampambanulia takua na uovu.

Kuifuatisha silika juu ya usawa katika kauli yake: "na mwenye kuilingamanisha. Akaifahamisha." ni kuashiria kuwa (mtu) kufahamu uovu na heri - ambapo ndiyo akili ya kimatendo - ndiyo kusawazisha nafsi. Na hiyo ni miongoni mwa sifa za umbile la hiyo nafsi; kama alvyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t): "Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawasawa ndiyo umbile Allah alilowaumbia watu; hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Allah. Hiyo ndiyo dini iliyo haki " (30:30).

Kutegemeza uovu na takua kwenye dhamir na nafsi ni kuonyesha kwamba makusudio ya uovu na takua zinafahamishwa hapa ni uovu na wema kuhusika na hii nafsi iliyoelezewa ya mtu na zile za majini kama ilivyodhihiri katika Qur'an tukufu kuwa wao ni wenye kukalifiwa na imani na kutenda amali njema.

Aya Na 9 -10

Kufaulu ni kushinda matakwa na kupata matakwa, kinyume chake ni kupata hasara. Kutakata ni kukua kwa makuzi mema yenye baraka. Na kutweza ni kuingiza kitu katika kitu chengine, makusudio yake kwa kukutanisha na aya, inayokabiliana na kutakasa, ni kuikuza nafsi katika misingi inayohitalifiana na tabia yake na kuipandanisha nayo. Aya hizo mbili ni jawabu la kiapo na Aya Na pili inaungana na ya kwanza. Kuleta ibara ya kutengenea nafsi na kuharibika kwake kwa neno kutakasa na kutweza ni udhihirisho wa inavyofahamisha kauli yake Mwenyezi Mungu. Akaifahamisha maasi yake na twaa yake, kwamba ni katika ukamilifu wa nafsi ya kiutu kwamba hiyo nafsi kimaumbile inapambanua uovu kutokana na twaa, yaani dini ya Kiislamu ni dini ambayo Mwenyezi Mungu anaikusudia kwa maumbile ya mtu, kwa hiyo kuipamba nafsi kwa twaa ni kuitakasa.

Aya Na 11

Aya hii na zinazofuatia mpaka mwisho wa Sura ni ushuhuda na uthibitisho wa yaliyotangulia katika kauli yake Mwenyezi Mungu: "Hakika amefaulu mwenye kuitakasa ".

Aya Na 12

Makusudio ya mwovu wa Thamud ni yule aliyemchinja ngamia. Jina lake kutokana na yaliyo katika riwaya ni Qidar bin Salif. Na kushakiza kulikuwa na kushakiza kwa watu kama zinavyofahamisha aya zinazofuatia kutokana na dhamir zake za wingi.

Aya Na 13

Makusudio ya Mtume wa Mwenyezi Mungu hapa ni Saleh(a.s) Mtume wa Thamud. Maana yake: akawaambia Mtume Saleh kwa ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu: "Tahadharini na ngamia wa Allah na maji yake wala msimtaaradhi kuwa kutaka kumuua au kumzuwia na zamu yake ya kunywa maji ." Mwenyezi Mungu amekifafanua kisa hiki katika Sura ya II (Hud) na nyenginezo.

Aya Na 14

Kusema kwake akaifanya sawa, kwa dhahiri dhamir ni ya Thamud kwa kuzingatia kuwa ni kabila yaani akalifanya sawa na ardhi hilo kabila au ni kufanya sawa kwa maana ya kuitandaza hiyo ardhi. Inasemekana kuwa dhamir ni ya neno kueneza kwa maana ya kuwa akawaeneza adhabu na akaifanya sawa kwa wote hila ya kuangalia mwenye nguvu, wala myonge au mkubwa wala mdogo.

Aya Na 15

Dhamir ni ya kueneza au kufanya sawa yaani Mola wao haogopi mwisho wa kueneza adhabu na kuifanya sawa, kama wanavyoogopa wafalme na wenye nguvu mwisho wa mateso kwa maadui zao; kwa sababu mwisho wa mambo ni vile anavyotaka yeye Mwenyezi Mungu na kuafikiana na anavyoidhinisha. Aya hii iko karibu katika maana na aya inayosema: "Haulizwi anayoyafanya, lakini wao wataulizwa " (21:23).

Inasemekana kuwa dhamir ya neno haogopi ni ya mwovu kwa maana ya kuwa haogopi mchinjaji ngamia mwisho wa aliofanya. Na pia imesemekana kuwa dhamir ya haogopi ni ya Saleh na dhamir ya mwisho wake ni ya kueneza adhabu kwa kutegemea kuokoka. Udhaifu wa njia zote hizo mbili uko wazi.

Utafiti Wa Hadith Katka Tafsiri ya Qummi kuhusu Aya Na saba amesema: Akaiumba na kuitia Sura. Katika Majmau amepokea Zurarah na Hamran, na Muhammad bin Muslim kutoka kwa Abu Jaffar na Abu Abdillah(a.s) katika kauli yake Mwenyezi Mungu: Akaifahamisha maasis yake na twaa yake, ni kuwa ameibanisha yale ya kufanya na ya kuwacha. Na katika kauli yake Mwenyezi Mungu: "Hakika amefaulu mwenye kuitakasa". Amesema: "Hakika amefaulu mwenye kutwii" Na kuhusu na hakika amepata hasara mwenye kuitweza. Amesema: "Hakika amepata hasara mwenye kuasi".

Katika Durril Manthur ametoa Ahmad, Muslim, Ibn Jariyr, Ibn Mundhir, Ibn Murdawayh kutoka kwa Amran bin Haswiyn kwamba mtu mmoja alisema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu unaona wanayoyafanya watu leo wanajitahidi katika jambo ambalo limekwisha hukumuliwa na kupitishwa katika kadar iliyotangulia? Au katika ambayo wanamkubalia Mtume wao"? Akasema: "Bali ni jambo lililokwisha pitishwa.' Akasema huyo mtu kwa nini wanafanya basi? Akasema Mtume: "Ambaye Mwenyezi Mungu amemuumbia kwa moja ya daraja mbili humuandalia kuifanya. Na ukweli wa hayo ni katika kitabu cha Mwenyezi Mungu: "Na (kwa) nafsi na aliyelingamanisha akaifahamisha maasia yake na twaa yake ."

Ufafanuzi Wa Hadith Hiyo Aliposema au katika wanayomkubalia Mtume wao, inaungana na sehemu ya kwanza kama swali yaani, Je, katika kumtii Mtume wao kumepitishwa na kukadiriwa tayari? Aliposema: "Kwa nini wanafanya basi, yaani nini maana ya amali yao na kutugemezwa kitendo kwao"? Na aliposema; "Ambaye Mwenyezi Mungu amemuandalia " Maana yake ni kuwa: Matokeo ya kutenda wema au uovu yanatokana na wao pamoja na kuangalia kuwa yamekwishapitishwa na kukadiriwa; huko hakukanushi kutokea kwake kwa kumwangalia mtu na hiyari yake. Na hayo yamefafanuliwa mara nyingi. Katika utafiti uliotangulia katika kitabu hiki.

Katika hiyo Durril Manthur, ametoa Ibn Abu Hatim,Abu Shakh, Ibn Murdawayah na Addilami kutoka kwa Juwaybir naye kutoka Adh-dhahak naye kutoka kwa Ibn Abbas amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) akisema: "Hakika amefaulu mwenye kuitakasa". Imefaulu nafsi aliyoitakasa Mwenyezi Mungu na imepata hasara nafsi aliyoihasirisha Mwenyezi Mungu na kila heri".

Kunasibisha utakaso na hasara kwa Mwenyezi Mungu S.W.T. ni kwa njia ambayo haikanushi kunasababishwa twaa na maasi kwa mtu. Na hakika hunasababishwa upotevu kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa njia ya fumbo; kaa S.W.T. kwa njia ya fumbo; kama alivyosema Mwenyezi Mungu "Na hamwachii yoyote kupotea kwa mfano huo isipokuwa wale wavunjao amri zake (mafasiki) " (2:26).

Katika Majmau anasema: " Imesihi riwaya kwa kutegemeza Uthman bin Suhaib naye kutoka kwa baba yake amesema" "Mtume(s.a.w.w) alisema kuumuliza Ali bin Abu Twalib: ni nani mwovu zaidi wa watu wa mwanzo?" Akasema: " aliyemchinja ngamia". Mtume akasema, "umepata". "Na nani mwovu wa watu wa mwisho?" Akasema "sijuwi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu." Akasema Mtume: "Ambaye atakupiga kwenye huu (akaonyesha utosi wake)". Na imepokewa hadith nyengine kwa maana haya haya kutoka kwa Ammar bin Yassir. Katika Tafsiri ya Burhan amepokea Thalaabi ne Wahidi kwa kutegemezwa kwao, kutoka kwa Ammar na kutoka kwa Athman Bin Suhaib na kutoka kwa Adh-dhahhak.

Na amepokea Ibn Murdawayh kutoka kwa Jabir bin Samra; na kutoka kwa Ammar kutoka kwa Ibn Adi na amepokea Attabari na Muswili. Amepokea Ahmad kutoka kwa Adh- dhahhak naye kutoka kwa Ammar kwamba yeye amesema: Amesema Mtume(s.a.w.w) : "Ewe Ali mwovu zaidi wa kwanza ni mchinja ngamia na mwovu zaidi wa mwisho ni muuaji wako ".


17

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA LAYL (USIKU) (NA. 92)

INA AYA 21

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa usiku unapofunika

وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ ﴿٢﴾

2. Na (kwa) mchana unapofunuka.

وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ ﴿٣﴾

3. Na (kwa) mwenye kuumba kiume na kike.

إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ ﴿٤﴾

4. Hakika matendo yenu ni mbali mbali.

فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ ﴿٥﴾

5. Ama mwenye kutoa akamcha (Mwenyezi Mungu).

وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٦﴾

6. Akalisadiki jambo jema.

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٧﴾

7. Tutamsahilishia njia ya wepesi.

وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ ﴿٨﴾

8. Ama mwenye kufanya ubakhili akajiona hana haja.

وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٩﴾

9. Akalikadhibisha jambo jema.

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ ﴿١٠﴾

10. Tutamfanyia nyepesi njia ya uzito.

وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ ﴿١١﴾

11. Hayatamfaa mali yake atakapopomoka.

إِنَّ عَلَيْنَا لَلْـهُدَىٰ ﴿١٢﴾

12. Hakika na juu yetu kuongoza.

وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَىٰ ﴿١٣﴾

13. Na hakika ni yetu sisi akhera na ulimwengu.

فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ ﴿١٤﴾

14. Basi ninawahadharisha na moto unaowaka kwa nguvu.

لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى ﴿١٥﴾

15. Hatauingia ila mwovu mno!

الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٦﴾

16. Ambaye amekadhibisha akapa mgongo.

وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى ﴿١٧﴾

17. Na ataepushwa nao mwenye kucha (Mungu).

الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾

18. Ambaye hutoa mali yake kwa (kutaka) kujitakasa.

وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ ﴿١٩﴾

19. Na hali ya kuwa hakuna yoyote aliyemfanyia hisani ili awe anamlipa.

إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٠﴾

20. Isipokuwa ni kwa kutaka radhi ya Mola wake aliye Mtukufu mno.

وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ ﴿٢١﴾

21. Basi hapo ataridhia.

UBAINIFU

Lengo la Sura hii ni kuonya. Inaelezea huko kuonya kwa kufuata njia ya kuonyesha tofauti ya matendo ya watu: Kwamba katika wao, mwenye kutoa, akamcha Mwenyezi Mungu na akalisadiki jambo jema, basi Mwenyezi Mungu atammanikisha katika maisha mema ya milele. Na katika wao mwenye kufanya ubakhili, akajiona hana haja na akalikadhibisha jambo jema, basi Mwenyezi Mungu atamwelekeza kwenye uovu. Sura hii inatilia umuhimu zaidi jambo la kutoa mali. Kulingana na mpangilio wake inawezekana kuwa imeshuka Makka au Madina.

Aya Na 1

Mwenyezi Mungu anaapa kwa usiku unapofunika mchana; kama alivyosema: "Huufunika usiku kwa mchana " (7:54). Inawezekana kuwa makusudio yake ni kufunika ardhi au jua.

Aya Na 2

Inaungana na Aya Na (1). Maana ya neno Tajallaa ni kudhihiri kitu baada ya kujificha. Amesema katika Majmau ni kudhihiri huo mchana kutoka katika giza. Hili ni neema kubwa, kwani lau wakati wote ungekuwa ni giza, basi watu wasingeweza kutafuta maisha.

Aya Na 3

Pia inaungana na aya iliyotangulia herufi Maa ni kiwakilishi na makusudio yake ni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Imekuja ibara hiyo bila ya kumtaja Mwenyezi Mungu kwa kutambulisha utukufu wake; Maana yake; ninaapa kwa kitu cha ajabu ambacho kimeleta kiume na kike ambavyo ni namna moja, lakini vimetofautina. Imesemwa kuwa herufi Maa ni kiarifa chenye kutumika kama jina; Maana yake ni ninaapa kwa kuumba kiume na kike lakini njia hii ni dhaifu. Mukusudio ya kiume na kike hapa ni aina yoyote ya kiume na kike. Imesemwa kuwa ni mtu mume na mke na pia imesemwa kuwa ni Adam na mkewe Hawa, lakini njia iliyo na nguvu zaidi, ni hiyo ya kwanza.

Aya Na 4

Neno Saa'ya lina maana ya kwenda haraka, na makusudio yake hapa ni ketendo kwa vile mtu anajihimu nacho, nalo liko katika maana ya wingi. Jumla hiyo ni jawabu la kiapo na maana yake; Ninaapa kwa vitu hivi vyenye kutofautiana kwa umbo na athari, hakika matendo yenu ni yenye kutofautiana hayo yenyewe na athari zake. Kuna katika hayo ni ya kutoa, kumcha Mwenyezi Mungu na kusadikisha, yana athari inayohusika nayo. Na kuna katika hayo ni ya ubakhili, kujitosheleza na kukadhibisha nayo yana athari inayohusika nayo.

Aya Na 5-6

Ni ufafanuzi wa kutofautiana matendo yao na kutofautiana athari yake. Makusudio ya kutoa ni kutoa mali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kinyume chake ni ubakhili wa kujizuia kutoa mali. Na kusema kwake: "Hayatamfaa mali yake atakapopomoka." Na kusema kwake : "Na akamcha Allah" ni kama anafasiri kutoa, makusudio yake ni kutoa kwa njia ya (taqwa) uchaji Mungu. "Jambo jema" ni sifa yenye kusimama mahali pa chenye kusufiwa, kwa dhahiri kukadiriya kwake ni maandalizi mema ambayo ameyatolea ahadi Mwenyezi Mungu Katika thawabu ya kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) Na huko kutoa ni kusadikisha ufufuo na kuamini Mwenyezi Mungu na kulazimisha imani kwa umoja wake Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika ubwana na kuuamini utume. Hiyo ndiyo njia ya kufikia yale aliyoyatolea ahadi Mwenyezi Mungu kupitia kwenye ulimi wa Mtume wake.

Aya Na 7

Makusudio ya kumsahilishia njia ya wepesi ni kumwafikisha kwa mali njema kwa kuzifanya nyepesi bila ya uzito wowote. Au kumfanya ni mwenye kujiandaa kwa maisha mema mbele ya Mola wake na kuingia peponi kwa sababu ya amali njema anazozifanya. Hii njia ya pili ni karibu na iko wazi zaidi kutokana na yale yaliyotolewa ahadi katika viaga vya Qur'an.

Aya Na 8 -10

Ubakhili ni kunyume cha kutoa. Makusudio ya kukadhibisha jambo jema ni kukanusha mambo mema na thawabu za Mwenyezi Mungu ambazo wamezielezea Mitume. Na hayo yanarudia kukanusha ufufuo. Makusudio ya 'kusahilishiwa uzito' ni kutofanikiwa kwake kwa kukosa kuwafikishwa kwenye amali njema, kwa kuwa nzito na kukosa kukunjuliwa moyo wake na imani au ni kuandaliwa adhabu.

Aya Na 11

Herufi Maa ni swali yaani mali yake itamfaa namna gani atakapokufa na kuangamia. Au ni ya kukanusha, yaani haitamfaa mali yake atakapoangamia.

Aya Na 12-13

Ni sababu ya yaliyotangulia katika kuzungumzia wepesi na uzito Au nikuelezea kwa ufafanuzi zaidi kwamba hakika sisi tunafanya huu wepesi au tunaubainisha ubainifu huu, kwa sababu unatokana na uongofu na ni juu yetu kuongoza na wala hakituzuii kitu chochote. Kwa hivyo kusema kwake "Hakika ni juu yetu kuongoza", kunamaanisha kwamba kuongoza watu alikokupitisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) amejiwabisha mwenyewe kwa mujibu wa hekima, na hilo ni kwamba yeye amewaumba ili wamwabudu; kama alivyosema: "Sikuumba majini na watu ila waniabudu ". (51:56).

Kwa hiyo amefanya kumwabudu ndiyo lengo la kuumbwa kwao na akaifanya hiyo ibada ni njia yenye kunyooka ya kumwendea yeye; kama alivyosema: "Hakika Allah ni Mola wangu na ni Mola wenu, basi mwabuduni hii ndiyo njio iliyonyooka " (3:51) "Hakika wewe unaongoza njia iliyonyooka " (42:52).

Mwenyezi Mungu amejihukumilia kuwabainishia watu njia yake na kuwaongoza kwake, kwa maana ya kuwaonyeshea njia, ikiwa wataifuata au wataiwacha, kama alivyosema: "Na Allah ndiye anayesema kweli, naye kuongoa njia (ya uongofu) (33:4). Amesema tena: "Hakika sisi tumemuongoa njia, basi ama atakuwa mwenye kushukuru au kukufuru ". (76:3).

Hayo yote hayapingi kuwa mtu mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu kuweza kusimamia jambo hili kwa idhini yake Mwenyezi Mungu, kama vile mitume; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Hakika wewe (Muhammad) unaongoza njia iliyonyooka " (42:52). Amesema tena: "Sema, hii ndiyo njia yangu ninailingania kwa Allah kwa ujuzi wa kweli, mimi (ninafanya hivi) na wanaonifuata " (12:108)

Hayo ni ikiwa uongozi ni kwa maana ya kuonyesha njia. Ama ikiwa uongozi ni kwa maana ya kufikisha kwenye matakwa - na matakwa ni athari nzuri ambazo zinafuatana na kuongoka kwa uongofu wa Mwenyezi Mungu kama maisha mema ya dunia na ya akhera ya milele - basi kwa ubainifu zaidi itakuwa ni kwa upande wa kutengeneza na kupatisha ambako anahusika nako Mwenyezi Mungu (s.w.t) Hayo ni katika yale aliyoyahukumilia Mwenyezi Mungu na kujiwajibishia na kuyasajili kwa kiaga chake cha haki; Mwenyezi Mungu anasema: "Basi atakayeufuata uongofu wangu hatapotea wala hatataabika ." (20:123).

"Mwenye kufanya mema miongoni mwa wanaume au wanawake na hali ya kuwa yeye ni muu'min tutamuhuyisha maisha mema na tutawapa ujira wao mkubwa kwa sababu ya yale mema waliyokuwa wakiyatenda ." (16:97).

Amesema tena: "Na wale waliomaini na wakatenda njema tutawaingiza katika mabustani yapitayo mito chini yake watakaa humo milele. Ndiyo ahadi ya Allah iliyokweli. Na ninani mkweli zaidi kwa usemi kuliko Allah ? (4:122). Kunasibishiwa uongozi mtu mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kwa kuingia kati huyo mtu na hayo yanayonasibishwa kwa Mwenyezi Mungu. Hii ikiwa ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hivyo Mwenyezi Mungu atakuwa ndiyo asili ya uongozi, na mtu huyo ni mfuasi. Maana ya aya, ikiwa makusudio ya uongofu ni kuonyesha njia, ni: hakika sisi tunawabainisha yale tunayoyabainisha, kwa sababu ni juu yetu kuonyesha njia ya kuabudu. Ikiwa ni kwa makusudio ya kufikisha kwenye matakwa, ni: hakika tunawasahilishia hawa wepesi wa amali njema, au na maisha mepesi ya milele na kuingia peponi; kwa sababu hilo ni katika kuvifikisha vitu kwenye lengo lake, na hilo ni juu yetu. Ama kusahilishia njia ya uzito ni kuzuilika na kupata wepesi, "Ili Allah apate kuwapambanua walio wabaya na walio wazuri na kuwaweka wabaya juu ya wabaya wengine na kuwarundika wote pamoja na kuwatupa katika Jahanam ". (8:37).

Mwenyezi Mungu amekwishasema: "Na tunateremsha katika Qur'an (Hayo mafundisho yake) ambayo ni ponyo na rehema kwa wanaoamini wala hayawazidishi (mafundisho hayo) madhalimu ila hasara tu! (kwani hawakubali kufuata) ." (17:82).

Inawezekana kuwa maana ya ungozi hapa - kwa vile tamko 'uongozi' halikutegemezewa sharti yeyote - ni kwamba huu uongozi, pasi na kutajwa katika jambo gani, una maana mapana zaidi kuliko uongozi uliotajwa kama katika mazingatio ya sheria n.k. - kwa hiyo Mwenyezi Mungu ni wake uongozi wa kiuhakika kama alivyosema: "ambaye amekipa kila kitu umbo lake kisha akakiongoza ." (20:50).

Na ni wake uongofu wa kimazingatio, kama alivyosema: "Hakika sisi tumemuongoa (tumembainishia) njia (ya kheri nay a shari) , basi (mwenyewe tena) atakuwa mwenye kushukuru au kukufuru .(76:3).

Kuhusu Aya Na (13) ni ulimwengu wa mwanzo na ulimwengu wa kurudi; kila kinachohisabika ni kitu basi ni milki yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa milki ya uhakika ambayo inasimamia kupatikana kwa kiti hicho, kisha ndipo inakuja milki wa kimazingatio ambayo katika athari zake ni kujuzu kukifanya lolote.

Kwa hiyo yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamiliki kila kitu kwa kila upande hakuna mpinzani anayempinga wala mzuwiyaji atakayemzuwiya, wala hakuna kitu kinachomshinda, kama alivyosema: "Na Allah huhukumu hakuna wa kupinga hukumu yake "(13:41).

Na amesema tena: "Na Allah hufanya apendavyo." (14:27).

Na amesema tena: "Na Allah ndiye mwenye kushinda juu ya jambo lake (alitakalo lazima liwe) ." (12:21).

Aya Na 14-16

Ni mtiririko wa yaliyotangulia; yaani ikiwa uongofu ni juu yetu, basi ninawatahadharisha na moto wa Jahannam. Na kwa hilo anauelekeza msemo katika kauli yake (ninawatahadharisha) kutoka katika wenye kusema wengi kwenda kwa mwenye kusema mmoja pekee, yaani ikiwa uongofu ni wenye kupitishwa, basi muhadharishaji wa asili ni Mwenyezi Mungu ijapokuwa ni kupitia kwa ulimi wa Mtume wake. Makusudio ya moto uwakao ni Jahannam kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Lakini wapi! Kwa hakika huo ni moto uwakao ". (70:15).

Makusudio ya mwovu mno ni kafiri yeyote ambaye anakufuru kwa kukadhibisha na kupa mgongo. Kwani yeye ni mwovu zaidi ya waovu wengine. Mwenye kuwa na balaa katika mwili wake amepata uovu, mwenye kupatwa na balaa katika mali yake au mtoto wake pia amepata uovu na mwenye kupata hasara katika mambo yake ya akhera amekuwa mwovu, lakini huyu ni mwovu zaidi ya wengine kwa vile uovu wake ni wa milele hakuna tamaa ya kuepukana nao. Kinyume cha uovu wa mambo ya kidunia, kwa sababu uovu unakatika na ni wenye kutarajiwa kuondoka haraka.

Kwa hiyo makusudio ya mwovu mno hapa ni kafiri mwenye kukadhibisha mlingano wa haki, kama alivyomwelezea Mwenyezi Mungu kwa kusema: "Ambaye amekadhibisha na akapa mgongo." Ama kusema muovu zaidi ni kwa maana ya muovu wa watu wote ni jambo ambalo halisaidiwi kabia na mpangilio wa maneno. Makusudio ya neno Yaswlaaha ni kuufuata huo moto na kulazimiana nao (kuwa nao) kwa hiyo inafahamisha kudumu kwenye huo moto. Hayo ni katika aliyoyahukumilia Mwenyezi Mungu katika haki ya kafiri, kama alivyosema: "Na wale ambao wamekufuru na wakayakadhibisha maneno yetu hao ni watu wa motoni, watakaa milele humo ." (2:39).

Hilo basi linapinga yale yaliyosemwa kwamba maana ya neno: "Hatauingia ila mwovu mno" kwamba mafasiki katika waislamu hawataingia motoni, isipokuwa inaonyesha kuwa asiyekuwa kafiri hatadumu , lakini atauingia.

Aya Na 17-19

Makusudio ya neno Atqaa ni yule mwenye kumcha Mungu zaidi: Wako watu hucha kupotea nafsi kama kwa kifo au kuuawa, na wengine hucha kuharibika mali na wengine hucha ufakiri, kwa hiyo wanajizuia kutoa mali. Na wengine humcha Mwenyezi Mungu tu; kwa hiyo wanatoa mali. Basi huyu ndiye mwenye kucha zaidi ya wote, anatoa mali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Ukipenda unaweza kusema: hucha hasara ya akhera , kwa hiyo anajitakasa kwa kutoa. Yule ambaye hachi kwa kutoa mali anashindwa na huyo anayetoa mali, ijapokuwa hucha mambo ya kidunia au humcha Mungu kwa baadhi ya matendo mema.

Ayah ii inaenea kwa wote na sio mahsusi kwa mtu, kulingana na inavyofahamisha, na kunafahamisha hilo, kumsifu mwenye kucha zaidi kwa aya inayofuatia. "Ambayo hutoa mali yake" hiyo ni sifa ya yeyote yule amayetoa, lakini hili halikanushi kuwa aya au Sura yote imeshuka kwa sababu mahsusi kama ilivyopokewa katika sababu za kushuka. Ama kumuhusisha mbora zaidi mmoja tu! Juu ya watu wote, wabaya au wema katika wote au katika kila zama na iwe maana ni "ataepushwa nao mwenye kucha zaidi ya watu wote, na hatauingia ila mwovu zaidi ya watu wote", ni jambo ambalo halisaidiwi na mpangilio wa aya za mwanzo wa Sura vile vile hakuna maana ya kusema "Ninawahadharisha nyote na moto ambao hatadumu ndani yake ila mmoja katika nyinyi na hataokoka ila mmoja katika nyinyi".

Aya Na (18) ni sifa ya yule mwenye kumcha zaidi yaani ambaye anatoa mali yake hali ya kutaka kwa hilo ziada njema.

Aya Na (19) ni ya kuthibitisha madhumuni ya aya iliyotangulia yaani hana yoyote mbele zake ihsani itakayolipa hiyo ihsani yake isipokuwa anatoa kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu. HAya Na natiliwa nguvu na aya inayofuatia.

Aya Na 20

Maana yake ni lakini yeye anatoa mali yake hali ya kutaka radhi ya Mola wake Mtukufu. Maelezo zaidi ya Mola Mtukufu yako katika Sura ya 87.

Aya Na 21

Yaani huyu mchaji zaidi ataridhia yale anayopewa na Mola wake Mtukufu kutokana na malipo mema yaliyo mazuri. Kutaja sifa mbili za Mola na Utukufu, ni kufahamisha kwamba yale malipo anayopewa ni malipo ya neema zaidi na ya utukufu zaidi (juu zaidi) nayo ni yenye kunasibiana na Uungu na Utukufu.

Utafiti Wa Hadith Katika Kafi kutoka kwa Muhammad bin Muslim amesema: "Nilimuuliza Abu jaffar(a.s) kuhusu maneno ya Mwenyezi Mungu: "Naapa kwa usiku unapofunika, na naapa kwa nyota zinapoanguka (zinapokuchwa) " na mifano ya hayo. Akaniambia: "Hakika Mwenyezi Mungu anaweza kuapia chochote anachotaka katika viumbe vyake, lakini viumbe haviwezi kumwapia asiyekuwa Yeye (Mwenyezi Mungu). Imepokewa katika Faqih kutoka kwa Ali bin Mahziyar kutoka kwa Abu Jaffar wa pili(a.s) na katika Tafsiri ya Qummi kuhusu Aya Na kwanza anasema: Ni wakati unapofunikwa mchana, na hicho ni kiapo. Kutoka kwa Humayri naye kutoka kwa Ahmad bin Muhammad naye kutoka kwa Ahmad bin Muhammad bin Abu nasr naye kutoka kwa Abul-Hassan Arridhaa(a.s) kuhusu tafsiri ya Sura ya Al-layl anasema:

"Hakika mtu mmoja alikuwa na mtende katika ukuta wa Mtu mwengine na huyo mwenye mtende alikuwa akimdhuru huyo mwengine; akamshtakia Mtume akaitwa yule mwenye na Mtume akamwambia nipe mtende wako kwa mtende wa peponi, akakataa. Na kulikuwepo mtu mwengine anayeitwa Abu Dahdaah aliyesikia hayo akamwendea mwenye mtende akamwambia niuzie mtende wako kwa ukuta wangu akamuuzia. Abu Dahdaah akwamwendea Mtume akamwambia nimeununua mtende fulani: kwa ukuta wangu. Mtume akamwambia "utapata badala yake mtende katika peponi ndipo akateremsha Mwenyezi Mungu: "Na mwenye kuumba kike na kiume. Hakika matendo yenu ni mbalimbali. Ama mwenye kutoa (yaani mtende) na akamcha Allah na akalisadiki jambo jema (yaani lililo mbele ya Mtume(s.a.w.w) mpaka Aya Na 11.

Katika Tafsiri ya Qummi mwenye kucha Mwenyezi Mungu zaidi ni Abu Dahdaah. Hayo ni kwa upande wa Shia kutokana na Maimamu wa Ahlul Bait. Kwa upande wa Ahli Sunna amepokea Tabrasi katika Majmau kwamba kisa hicho kimepokewa kwa Wahidi naye kutoka kwa Akrama naye kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Ansari mmoja alipiga bei na mwenye mtende akaununua kwa mitende arubaini, kisha akampa Mtume naye Mtume akampa mwenye nyumba. Amepokea Tabrasi kutoka kwa Ata kwamba jina la huyo mtu ni Abu Dahdaah. Na amepokea Assuyuti katika Durril Manthur kisa hicho kutoka kwa Ibn Abu Hatim naye kutoka kwa Ibn Abbas, lakini ameifanya dhaifu riwaya hiyo.

Imepokewa tena, katika njia ya Ahli Sunna kwamba Sura hii ilishuka kwa Abu Bakr. Amesema Arrazi katika Tafsiri Kabir: "Wamekongamana wafasiri katika sisi kwamba makusudio katika aya ni Abu Bakr. Anaendelea kusema Arrazi: "Jua kwamba Mashia wote wanakanusha riwaya hii, wanasema imeshuka katika haki ya Ali bin Abu Twalib na dalili juu ya hilo ni juu ya aya inayosema: "Na hutoa zaka na hali yakua wao wanaswali " (5:55).

Kwa hiyo neno lake Mwenyezi Mungu: "Mwenye kumcha (Mungu) zaidi ambaye hutoa mali yake kwa kujitakasa " linaishiria kwenye aya hiyo (5:55).

Ama yale yaliyonasibishwa kwa Mashia wote, yenye kutegemewa katika njia zao ni Sahihi ya Al-Himyariyy iliyotangulia kueleza yaliyo katika riwAya Na nayofahamisha kushuka aya kwa Abu-Dahdaah El- Ansari.

Ndio, imekuja riwaya dhaifu kutoka kwa Barqi naye kutoka kwa Ismail bin Mahraan naye kutoka kwa Ayman bin Muhriz naye kutoka kwa Abu Basiyr naye kutoka kwa Abu Abdillah amesema: Ama kauli yake: Na ataepushwa nao mwenye kumcha (Mungu) zaidi, mwenye kumcha (Mungu) zaidi ni Mtume(s.a.w.w) na wafuasi wake na Ambaye hutoa mali yake kwa (kutaka) kujitakasa, huyo ni Amiirul-Mui'miniin Ali(a.s) na ndiyo kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na wanatoa zaka na hali wao ni wenye kuswali ." (5:55).

Na kuhusu aya "Na hali ya kuwa hakuna yoyote aliyemfanyia hisani ili awe anamlipa " huyo ni Mtume(s.a.w.w) ambaye hana yoyote wa kumlipa hisani na hali hisani zake ni zenye kuenea kwa watu wote.

Riwaya hiyo ni dhaifu kwa upande wa mapitio yake na kufuatilia kwake bila ya kuangalia tafsir. Dalili iliyowazi ya udhaifu wake ni vile kufuatilia kwake kuwa mwenye kusifiwa ni Mtume na sifa iwe juu ya Ali(a.s) kisha aya inayofuatia tena juu ya Mtume. Na kama hilo lingekuwa katika tafsiri ingeliharibika nidhamu yake kabisa. Na huyo Ayman bin Muhriz hajulikani.

Imepokjewa kutoka kwa Al Himyariyy kutoka kwa Ahmad bin Muhammad bin Abu Nasr naye kutoka kwa Abul hassan Arridha(a.s) amesema: Niliulizwa kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: "Hakika Allah humwongoza anayemtaka na kumpoteza anayetaka. Nikamwambia: Mwenyezi Mungu akufanye uwe mwema "Hakika watu katika watu wetu wanadai mwamba maarifa ni yenye kuchumwa na kwamba wao wakiangalia vizuri wanapata heri". Akakanusha hilo na akasema: "Hawa watu hawachumi heri wao wenyewe, hakuna yeyote katika watu isipokuwa ni wajibu kuwa heri inatokana na yule ambaye heri inatoka kwake.

Ama uongofu ambao makusudio yake ni kufikisha kwenye matakwa, huo ni wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ni katika mambo ya Mungu. Ama upotevu ambao makusudio yake ni kupoteza kwa upande wa njia na wala sio kupoteza kwa kuanzia ambako hakuegemezwi kwa Mwenyezi Mungu, ni kwa Mwenyezi Mungu pia, kwa kuwa yeye ni mwenye kuzuwiya kushusha rehema na kukosekana uongofu. Ikiwa uongofu unatokana naye basi kuzuilika nako pia kunatokana naye.


18

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA ADHUHAA (DHUHA)(NA. 93)

INA AYA 11

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa mwanzo wa mchana.

وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾

2. Na kwa usiku unapotuwa.

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾

3. Hakukuacha Mola wako wala hakukukasirikia.

وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ الْأُولَىٰ ﴿٤﴾

4. Hakika akhera ni bora kwako kuliko ulimwengu.

وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰ ﴿٥﴾

5. Na atakupa Mola wako utaridhia.

أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ ﴿٦﴾

6. Je, hakukuta ni yatima akakuhifadhi?

وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ ﴿٧﴾

7. Akakukuta umedangana akakuongoza?

وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ ﴿٨﴾

8. Akakukuta ufakiri akakutajirisha.

فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾

9. Basi yatima usimdhalilishe.

وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾

10. Na mwenye kuoma usimkaripie.

وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ ﴿١١﴾

11. Na neema ya Mola wako, izungumze.

UBAINIFU

Inasemekana kuwa Mtume(s.a.w.w) alikatikiwa na wahyi kwa siku kadhaa mpaka watu wakawa wanasema: "Hakika Mola wake amemwachilia mbali". Basi ndio akateremsha Mwenyezi Mungu Sura hii kuituliza nafsi yake. Sura hii inawezekana kuwa imeshuka Makka au Madina.

Aya Na 1-2

Maana ya neno Dhuhaa ni kuangaza jua na kuenea mchana na neno Sajaa nikutulia yaani kuingia giza.

Aya Na 3

Ni jawabu la kiapo. Mnasaba wa nuru ya mchana na giza la usiku kwa kushuka wahyi na kukatika kwake uko dhahiri.

Aya Na 4

Maana yake kutokana na inavyofahamisha aya iliyotangulia ni kama vile anaambiwa Mtume: Yale uliyonayo miongoni mwa fadhila na rehema ni muda wa kuwa uko hai katika dunia na uhai wako wa akhera ni bora kwako kuliko maisha yako ya dunia.

Aya Na 5

Ni uthibitisho wa aya iliyotangulia na imekusanya kiaga cha kutoa kutakakofuatiwa na kuridhia. Imesemwa aya hii inaangalia pande zote mbili (maisha ya dunia na akhera) na wala sio akhera tu!

Aya Na 6

Inaishiria baadhi ya neema zake Mwenyezi Mungu kwa Mtume; alifiwa na baba yake akiwa tumboni mwa mama yake, kisha akafa mama yake akiwa na miaka miwili, tena akafa (mlezi wake) babu yake naye akiwa na miaka minane, basi ndio akachukuliwa na ami yake kumlea. Inasemekana makusudio ya yatima hapa ni yule mtu aliye peke yake. Kwa hiyo maana inakuwa; Je hakukuta peke yako kati ya watu, akawakusanya watu kwako?

Aya Na 7

Makusudio ya neno Dhwallan ni kudangana kukosa ungofu na makusudio ya kudangana kwake Mtume(s.a.w.w) ni ila hali ya kukatikiwa na ungofu wake Mwenyezi Mungu Mtukufu na hapana uongofu kwa Mtume(s.a.w.w) wala kwa yoyote katika viumbe ila kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo nafsi yake ilikuwa imedangana, ijapokuwa uongofu wa Mwenyezi Mungu ni wenye kulazimiana naye. Aya hii iko katika maana na aya inayosema: "Ulikuwa hujui kitabu nini wala imani " (42:52).

Vile vile iko katika maana ya neno la Musa, kama anavyosimulia Mwenyezi Mungu katika Qur'an. "nimeyafanya hayo nilipokuwa miongoni mwa waliodangana ." (26:20) yaani wakati bado sijapata uongofu wa utume.

Yanakurubia maana hayo na yale yaliyosemwa kuwa makusudio ya Dhwallan ni kuondokewa na elimu (kutokujua) kama ilivyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu."..ili kama mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine " (2:282).

Hayo yanatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu: "na hakika ulikuwa kabla ya haya ni miongoni mwa wasio na habari hizi ." (12:3).

Imesemwa maana yake ni akakukuta umepotea kati ya watu hawajui haki yako akawaongoza kwako na akawajulisha kuhusu wewe.

Imesemwa ni ishira ya kupotea njia ya Makka alipokuwa mdogo. Pia imesemwa ni ishara ya kupotea kwake ndani ya msafara wa Maysara mtumishi wa Khadija, wakati alipokwenda Sham pamoja na ami yake, Abu Twalib. Na yamesemwa zaidi ya hayo ni hizo zote ni njia dhaifu.

Aya Na 8

Fukara ni yule ambaye hana mali. Alikuwa Mtume(s.a.w.w) ni fukara akatajirishwa na Mwenyezi Mungu baada ya kumuoa Bibi Khadija ambaye alikuwa na mali nyingi akampa Mtume.

Aya Na 9-11

Aya zote hizi tatu zinatokana na aya zilizotangulia na zinataja wema wake Mwenyezi Mungu (s.w.t), ni kama anasema: "Umeyapata yale yanayompata yatima katika udhalili na upweke kwa hiyo basi usimdhalilishe yatima kwa kuidhalilisha nafsi yake au mali yake." Na mara nyingi umeipata haja ya mwenye kupotea vile anavyohitajia uongofu na fakiri anavyohitajia utajiri, basi usimkaripie mwenye kuomba kuondolewa haja yake ya uongofu au maisha. Vile vile umeona kuwa neema ulizonazo amekuneemesha Mola wako kwa ukarimu wake, basi ishukuru neema yake kwa kuizungumza wala usiifiche. Maamrisho yote haya ni kwa watu wote ingawaje yanaelekezwa kwa Mtume.

Utafiti Wa Hadith Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu neno la Mwenyezi Mungu Dhuhaa anasema ni wakati wa kupanda jua na Sajaa anasema ni wakati wa giza. Na kuhusu neno la Mwenyezi Mungu Maqalaa anasema ni "hakukukasirikia". Katika Durril Manthur kuhusu Aya Na tano, ametoa Ibn Abu Shayba kutoka kwa Ibn Masud amesema: "Amesema Mtume(s.a.w.w) "Sisi Ahlul Bait Mwenyezi Mungu ametuchagulia akhera kuliko dunia ."

Katika hiyo hiyo Durril Manthur ametoa Askary katika Mawaidh, Ibn Laali na Ibn Najjar kutoka kwa Jabir bin Abdillahi amesema; "Mtume(s.a.w.w) aliingia kwa Fatima akiwa anatwanga kwa jiwe huku amevaa nguo za sufu za ngamia". Alipomwangalia akasema: "Ewe Fatima fanya haraka umeze uchungu wa dunia kwa neema na akhera kesho." Akateremsha Mwenyezi Mungu aya hiyo ya tano. Riwaya hii inachukulia kuwa aya hiyo ilishuka peke yake baada ya kushuka aya zilizo kabla yake katika Sura hii kisha kuunganishwa. Kuna uwezekano wa Aya hiyo kushuka peke yake kwa mara nyingi.

Katika hiyo hiyo Durril Manthur ametoa Ibn El Mundhir,Ibn Murdawayh na Abu naim katika Hilyat kutoka katika njia ya Harb bin Sharih amesema:"Nilimwambia Abu jaffar Muhammad bin Ali bin Hussein(a.s) unaonaje hii Shafaa (uombezi) wanayoizungumzia watu wa Iraq ni kweli? Akasema: "Kabisa Wallah". Alinizungumzia Ami yangu Muhammad bin El-Hanafiya kutoka kwa Ali kwamba Mtume(s.a.w.w) alisema: "nitauombea shafaa umati wangu mpaka Mola wangu anisemeshe: Umeridhika ewe Muhammad? Na nisema: Ndio ewe Mola wangu nimeridhika." Kisha akanikabili na kuniambia: "Hakika nyinyi watu wa Iraq mnasema: Hakika aya yenye kutarajiwa zaidi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ni ile inayosema: "Sema, enyi waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu! Msikate tamaa na Rehema ya Allah; Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote " (39:53). Nikasema ndio sisi tunasema hivyo. Akasema: Basi sote sisi Ahlul Bait tunasema: "Hakika aya inayotarajiwa zaidi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ni ile inayosema: "Na atakupa Mola wako nawe utaridhia". Yaani uombezi. (Aya Na tano katika Sura hii).

Katika Tafsiri ya Burhan kutoka kwa Baabwayh kwa isnadi ya Ibn Jaham kutoka kwa Ridhaa(a.s) katika kikao pamoja ya Maamun alisema huyo Ridhaa; "Anasema Mwenyezi Mungu (s.w.t) kumwambia Mtume wake Muhammad(s.a.w.w) . "Je hakukuta ni yatima akakuhifadhi?" Anasema: "Je hakukuta peke yako akakusanyia watu? Na akakukuta umedangana yaani mbele ya watu wako "akakuongoa" yaani akawongoa watu wakakufahamu. Na akakukuta ufakiri akakutajirisha". Anasema "akakutajirisha kwa kujaalia dua yako ni yenye kutakabaliwa?" Akasema Maamun: "Mwenyezi Mungu akubarikie ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu".

Katika hiyo hiyo Tafsiri ya Burhan kutoka kwa Barqi kwa isnadi yake kutoka kwa Amru bin Abu Nasr amesema: Alinizungumzia mtu mmoja katika watu wa Basra akasema: "Nilimuona Hussein bin Ali(a.s) na Abdallah bin Umar wanatufu Al-Kaaba. Nikamuuliza Ibn Umar: Kuhusu neno lake Mwenyezi Mungu "Na neema ya Mola wako izungumze", Akasema : "Ni kuzungumza aliyoneemesha Mwenyezi Mungu." Kisha nikamuuliza Hussein bin Ali(a.s) akasema: "Nikuzungumza aliyoneemesha Mwenyezi Mungu katika dini yake." Katika Durril Manthur kutoka kwa Bayhaqi naye kutoka kwa Hassan bin Ali kuhusu ayay hiyo ya 11 akasema: "Ukipata heri wazungumzie ndugu zako".

Katika hiyo Durril Manthur ametoa Abu Dawud kutoka kwa Jabir bin Abdillahi kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) amesema: "Mwenye kujaribiwa kwa kupewa misukosuko akaizungumza, hakika huyo amemshukuru Mwenyezi Mungu, na mwenye kuficha atakuwa amemkanusha (uweza) wa Mwenyezi Mungu. Na mwenye kujinasibishia asilokuwa nalo, hakika yeye ni kama amevaa nguo za uzushi.


19

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA INSHIRAAH (UKUNJUFU) (NA. 94)

INA AYA 8

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenya kurehemu

أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ ﴿١﴾

1. Je, hatukukunjulia moyo wako?

وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ ﴿٢﴾

2. Tukakuondolea uzito wako.

الَّذِي أَنقَضَ ظَهْرَكَ ﴿٣﴾

3. Ambao uliuelemea mgongo wako?

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾

4. Tukakutukuzia utajo wako?

فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٥﴾

5. Hakika pamoja na uzito kuna wepesi.

إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٦﴾

6. Hakika pamoja na uzito kuna wepesi.

فَإِذَا فَرَغْتَ فَانصَبْ ﴿٧﴾

7. Basi ukishamaliza (amali yako) jitaabishe kwa ibada.

وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَارْغَب ﴿٨﴾

8. Na Mola wako (peke yake) mtake haja.

UBAINIFU

Ni amri ya kujitaabisha kwa ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kujipendekeza kwa kumtaka haja. Sura hii inawezekana kuwa imeshuka Makka au Madina, na mpangilio wa aya zake unawafikiana zaidi na Madina. Katika baadhi ya riwaya za Maimamu wa Ahlul Bait(a.s) zinasema kuwa Sura ya Adh-dhuha na Al-Inshiraah ni Sura moja. Na yamepokewa hayo vile vile kutoka kwa Twaaus na Umar bin Abdul-Aziz.

Amesema Arrazi katika Tafsiri Kabir baada ya kuwanakili hao wawili: Jambo lililofanya Twaaus na Umar kusema kuwa hizo ni Sura moja ni kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t): "Je hatukukukunjulia moyo wako ?" Nikama linaungana na neno; "Je hakukukuta ni yatima akakuhifadhi?" Lakini sababu hiyo siyo, kwani neno la kwanza kushuka kwake, lilikuwa ni katika hali ya kuwa Mtume(s.a.w.w) yuko kwenye ghamu kutokana na maudhi ya makafiri, akawa katika hali ya misukosuko na dhiki ya moyo. Na neno la pili linahukumilia kuwa liliposhuka, Mtume alikuwa katika hali ya kukunjuka na kutulia moyo, basi yataungana vipi haya?

Katika hiyo hiyo Tafsiri Kabir imesemwa makusudio ya kuukunjua moyo wake Mtume(s.a.w.w) ni kufanywa Mtume anakunjukiwa na hakika zote anazopewa wala hapati dhiki yoyote kutokana na maarifa yanayomshukia na wala hapati dhiki kutokana na adha ya watu katika kuyafikisha hAya Na nayomshukia. Na wala sio kutulia moyo na furaha, kama yatakavyokuja maelezo zaidi (Inshallah). Yanafahamisha hayo yale yaliyopokewa na Ibn Abu Hatim kutoka kwa Said bin Jubayr naye kutoka kwa Ibn Abbas amesema: Amesema Mtume(s.a.w.w) : "Nilimuuliza Mola wangu masuala ambayo nilitamani nisingemuuliza. Nilimwambia "Ewe Mola wangu Mitume waliokuwa kabla yangu kuna katika wao waliofanyiwa upepo uwatii na waliokuwa wakiwafufua wafu. Ndio akasema Mwenyezi Mungu: "Je sikukuta ni yatima nikakuhifadhi?" Nikasema: "Kwa nini?" Akasema: "Je sikukuta umedangana nikakuongoza?" Nikasema: "Bila shaka ewe Mola wangu." Akasema: "Je sikukukunjulia Moyo wako na nikakuondolea uzito wako?" Nikasema "Bila shaka ewe Mola wangu." Maelezo zaidi yako katika Tafsiri ya Sura Quraish (Liiylafi Quraish).

Aya Na 1

Asili ya neno Nashrah ni kuichangua nyama na mfano wake, na miongoni mwa maana yake ni kukunjua moyo yaani kuukunjua kwa nuru ya Mungu na utuvu unaotokana upande wa Mwenyezi Mungu na Roho inayotoka kwake. Qur'an inasema: "Ewe Allah nikunjulie moyo wangu ." (20:25).

"Je hatukukunjulia moyo wako?" "Je ambaye amekunjuliwa moyo wake na Allah " (39:22).

Kuzifuatisha aya tatu za mwanzo katika madhumuni yake kisha kuzibainisha kwa kauli "Hakika pamoja na uzito kuna wepesi", kwa dhahiri inaonyesha kufungika hali yake Mtume katika mwanzo wa mlingano wake, katikati yake na mwisho wake. Kisha kukaririka kuthibitisha ila na kuzifanya aya mbili za mwisho kuwa ni sehemu yake. Yote hayo yanashuhudia kuwa makusudio ya kukunjua moyo wake Mtume(s.a.w.w) ni kuukunjua kiasi ambacho yatakunjuka yale yanayomfikia miongoni mwa wahyi, yale anayoamrishwa kuyafikisha na yale yanayompata katika maudhi na adha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kwa maneno mengine tunaweza kusema ni kuifanya nafsi yake tukufu ni yenye kujiandaa kwa ukamilifu kwa kukubali yale yanayoifikia hiyo nafsi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Aya Na 2-3

Makusudio ya kuondoa uzito wake kutokana na unavyofahamisha mpangilio wa maneno ni kutekeleza mlingano wake na kupitisha juhudi zake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa kuwafiki sababu. Kwani hakika ujumbe (Utume), na mlingano ndio uzito aliochukua mara tu! Baada ya kukunjuliwa moyo wake. Inasemekana kuwa kuondoa uzito kunaonyesha kunaelekeana na yale yaliyopokewa kwamba Malaika wawili walimshukia Mtume wakakipasua kifua chake na wakautoa moyo wake wakautoharisha, kisha wakaurudisha mahali pake. Maelezo zaidi yatakuja baadae.

Inasemekana makusudio ya uzito ni yale yaliyomtokea kabla ya kupewa utume, pia imesemwa ni kupatwa kwake na mshangao katika baadhi ya mambo kama kutekeleza haki ya ujumbe na imesemwa kuwa ni uadui wa watu wake na maudhi yao mengi. Pia imesemwa ni huzuni yake kwa kufiwa na ami yake Abu Twalib na mkewe Khadija. Na ikasemwa uzito ni maasi na kuondolewa uzito ni isma (kuhifadhiwa na dhambi) yake na imesemwa kuwa uzito ni dhambi za uma wake na kuondolewa uzito huo ni kusamehewa. Njia hizi baadhi yake ni za kipuuzi na baadhi yake ni dhaifu zisizoafikiana na mpangilio wa maneno. Nazo ziko kati ya imesemekana na inawezekana tu! Hazina uhakika wowote.

Aya Na 4

Kuutukuza utajo maana yake ni kutajwa sana jina lake kuliko mtu mwengine. Miongoni mwa kuutukuza utajo wake ni kukutanisha Mwenyezi Mungu jina lake pamoja na jina la Mtume. Kwani jina la Mtume liko pamoja na la Mola wake katika shahada mbili ambazo ndizo msingi wa dini na ni wajibu kwa kila muislamu kumtaja Mtume pamoja na Mola wake katika swala tano za wajibu kila siku. Ni katika wema kutokea kutukuzwa utajo baada ya kuondolewa uzito.

Aya Na 5

Siyo mbali kuwa ni sababu ya yale yaliyotangulia (kuondoa uzito na kulitukuza jina). Yale aliyobebeshwa na Mwenyezi Mungu na akaamrishwa kuyalingania - ambayo ni mazito kwa mtu kuyachukua - yalikuwa yamezidi. Vile vile watu wake walizidi kumfanya mwongo kwa mwito wake, kumdharau na kujitahidi kuuzima utajo wake (jina lake). Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamwondolea uzito wake ambao ameuchukua kwa kuwafanya watu kumwitikia mwito wake na akautukuza utajo wake ambao walikuwa wanataka kuuzima.

Hayo yanayotokana na desturi yake Mwenyezi Mungu katika ulimwengu kuleta wepesi baada ya uzito, kwa hiyo huenda kumwondolea shida kulikotajwa ni katika desturi yake. Basi kwa hali hii herufi lam katika neno Usri ni ya Jinsiya yaani jinsi ya uzito baadhi yake na wala sio kila uzito. Na huenda desturi na desturi ya kubadilisha matukio na hali isibakie milele.

Amesema Zamakh-Shari katika Kash-Shaff: Washirikishaji Mwenyezi Mungu walikuwa wakimkashifu Mtume(s.a.w.w) kwa ufukara na dhiki mpaka akatambua Mtume kuwa wao wanajiepusha na uislamu kwa sababu ya ufakiri wa watu wake. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu anamkumbusha yale aliyomneemesha miongoni mwa neema nyingi kisha akasema: "Hakika pamoja na uzito kuna wepesi". Kana kwamba amesema: "Tumekufadhili yale tuliyokufadhili basi usikate tamaa na fadhila za Mwenyezi Mungu, kwani uzito ulio nao uko pamoja na wepesi." Kwa dhahiri herufi lam ni ya Ahdiyya na wala sio Jinsiyya yaani uzito maalum uliokusudiwa na kwamba makusudio ya wepesi ni ghanima nyingi walizoruzukiwa waumini na Mwenyezi Mungu.

Lakini hayo ni yenye kupingika kwani utambuzi wake Mtume (SAWW) ni mkubwa zaidi kuliko kuogopea hali zao. Kuwa wanajiepusha na usilamu kwa sababu ya ufakiri wa watu wake. Isipokuwa wao walikuwa wakiukataa mwito wake kwa kiburi tu! Na Mwenyezi Mungu alikwishamkatisha tamaa Mtume wake kuwa wengi wao hawataamini aliposema: "Hakika imehakikika kauli juu ya wengi katika wao; kwa hivyo hawaatamini " (36: 7-10).

Na aya hizo zilishuka Makka. Na aya nyengine iliyoshuka Madina inayosema: "Hakika wale ambao wamekufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye hawataamini ". (1:6).

Lau inachukuliwa kuwa wepesi baada ya uzito ni nguvu ya kiislamu na kuinuka kwake baada ya kuwa chini pamoja na kuchukulia kuwa Sura imeshuka Makka, basi kusingekuwa na ubaya sana.

Aya Na 6

Ni kutilia mkazo na kusisitiza. Imesemekana kuwa ni kuanza upya na wametaja kwamba katika aya mbili hizo (5 na 6) kuna ufahamisho kuwa pamoja na hali nzito moja pana nyepesi mbili. Kwa kawaida jina lenye herufi lam likirudishwa mara ya pili katika maneno, linakuwa kama lile la kwanza kinyume cha jina lisilokuwa na lam. Lakini kawaida hii sio ya lazima, huwa ikabadilika.

Aya Na 7-8

Inatokana na yote yaliyobainishwa mwanzo, miongoni mwa kuchukua ujumbe na kumneemesha kwake Mwenyezi Mungu kwa kuukunjuwa moyo na kuondoa uzito na kuunyanyua utajo na yote hayo ni wepesi baada ya uzito. Kwa hiyo maana inakuwa, ikiwa uzito unafuatiwa na wepesi na mambo yote yanatokana na Mwenyezi Mungu tu! Basi ukimaliza yale uliyofaradhiwa, itaabishe nafsi yako kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa ibada zake na dua zake na umtake kukuneemesha raha baada ya taabu hii na wepese baada ya uzito huu.

Imesemwa makusudio yake ni ukiishamaliza faradhi, jitaabishe katika suna na pia imesemwa ukishaswali jitaabishe na dua. Na madhumuni ya kauli mbili hizi ni baadhi ya yanayokubalika. Imesemwa maana yake ni ukishamaliza vita, jitahidi katika ibada. Na pia imesemwa makusudio yake, ukisha maliza yale ya duniani jitaabishe katika akhera yako. Na yemesemwa zaidi na hayo, lakini zote hizo ni njia dhaifu.

Utafiti Wa Hadith Katika Durril Manthur ametoa Abdalla bin Ahmad katika Rawaid ez-zuhd kutoka kwa Ubayya bin Kaab kuwa Abu Hurayra alisema kumuuliza Mtume(s.a.w.w) : "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni jambo gani uliloona kwanza kuhusu utume?" Mtume(s.a.w.w) akakaa vizuri akasema: "Umeuliza swali ewe Abu Huraira. Mimi nilipokuwa na umri wa miaka ishirini na miezi kadhaa siku moja nilisikia maneno juu ya kichwa changu mara tu mmoja akawa anamwambia mwenzake ndiye huyu? Wakanikabili na sura ambazo sijaziona kwa kiumbe yoyote na roho ambao sijazipata kwa mtu yoyote na nguo sijaziona kwa mtu yoyote kabisa. Wakaja kila mmoja akanishika mkono.

Mmoja wao akamwambia mwenzake mlaze, akanilaza bila kuchelewa, mmoja akasema mpasue kifua chake, akashika kifua changu na kukipasua katika hali ambayo sikuona damu wala maumivu. Akamwambia mwenzake na mfundo wa hasadi, akatoa kitu mfano wa pande la damu kisha akikitupilia mbali akamwambia tia upole na huruma. Mara akatia kitu mfano wa kile kilichotolewa, lakini kikiwa mfano wa fedha, kisha akatingisha kidole gumba cha mguu wangu wa kulia na akasema: "Ondoka uko salama". Basi nikarudi nikawa nina mfanyia upole mdogo na kumuhurumia mkubwa."

Baadhi yao kama katika Rauhilmaani wamesema kwamba alikuwa na umri wa miaka kumi. Na katika baadhi ya riwaya kimenukuliwa kisa wakati wa kushuka Sura ya Alaq (96).

Na wengine kama katika Sahih ya Bukhari, Muslim, Tirmidhi na Nasai, kimenukuliwa kisa wakati wa Israi wa Mtume. Kisa hiki kwa hali yoyote ni cha kufananisha tu! Sio tukio la kweli na wamefanya upekuzi mrefu kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa tukio la kweli wakautia nguvu hup upekuzi wao kwa njia ambazo hazina faida kujishughulisha nazo.

Katika hiyo Durril Manthur ametoa Abu Yaala, Jariyr, Ibn Mundhir, Ibn Hatim, Ibn Habban, Ibn Murdawayh na Abu Naim katika Dalail wamepokea kutoka kwa Abu Said El-Khudri naye kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) amesema: "Alinijia Jibril akasema: Hakika Mola wako akasema: "Je, unajua vipi alivyotukuza utajo wako?" Nikasema, "Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi ". Akasema: "Nikitajwa, unatajwa pamoja nami." Katika hiyo hiyo Durril Manthur ametoa Abdurrazzaq, Ibn Jariyr, Hakim na Bayhaqi, kutoka kwa Hassan amesema: Siku moja alitoka Mtume(s.a.w.w) akiwa na furaha na kucheka huku akisema: "Nzito moja haiwezi kushinda nyepesi mbili".

"Hakika pamoja na uzito kuna wepesi, hakika pamoja na uzito kuna wepesi." Katika Majmau kuhusu Aya Na 7 na 8 maana yake ukimaliza kuswali swala ya faradhi jitaabishe kwa Mola wako kwa dua na umtake haja. Na hayo pia yamepokewa kutoka kwa Abu Jaffar na Abu Abdiallah(a.s) .


20

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA TIN (TIN) (NA. 95)

INA AYA 8

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa tini na zaituni.

وَطُورِ سِينِينَ ﴿٢﴾

2. Na kwa Mlima Sinai.

وَهَـٰذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ ﴿٣﴾

3. Na kwa mji huu wenye amani.

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ﴿٤﴾

4. Hakika tumemuumba mwanadamu katika hali nzuri mno.

ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ ﴿٥﴾

5. Kisha tukamrudisha chini ya walio chini.

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٦﴾

6. Ila wale walioamini wakatenda mema; wao wana malipo mema yasiyokoma.

فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِالدِّينِ ﴿٧﴾

7. Basi ni lipi baada ya hayo, linalokufanya ukadhibishe malipo?

أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ ﴿٨﴾

2. Je, Allah si bora ya mahakimu?

UBAINIFU

Sura hii inataja kufufuliwa na malipo, na inaeleza hayo kwa kufuata njia ya kueleza kuumbwa mtu katika hali nzuri, kisha kukhitalifiana watu; Wengine wakatoka na kuanguka chini ya waliochini. Pia inaeleza wajibu wa kihekima wa kupambanua kati ya hayo makundi mawili katika malipo. Sura hii imeshuka Makka, lakini inawezekana kuwa imeshuka Madina. Hata hivyo aya inayosema: "Na kwa mji huu wenye kuaminika," inatilia nguvu kuwa Sura hii imeshuka Makka.

Aya Na 1-3

Inasemekana makusudio ya Tini na Zaituni ni matunda maarufu na Mwenyezi Mungu ameapa kwa matunda hayo kwa sababu ya faida zake nyingi na majani yake yenye manufaa. Pia imesemwa makusudio yake ni mti wa Tini na wa Zaituni. Imesemwa makusudio ya Tini ni jabali iliyoko Damascus na Zaituni ni jabali liliyoko Al-Baytul Muqaddas (Palestina), na kwamba huenda makusudio ya hayo matunda mawili yaliyopo juu ya hayo majabali ni kwa vile hayo matunda yanaota katika majabali hayo na kwamba Mwenyezi Mungu ameapa kwa sehemu hizo kwa vile Mitume wengu wamepewa utume sehemu hizo. Na yamesemwa zaidi ya yaho.

Makusudio ya Turisinin ni jabali ambalo Mwenyezi Mungu Mtukufu alizungumza na Musa bin Imran(a.s) . Vile vile linaitwa Mlima Sinai. Makusudio ya mji huu wenye kuaminika, ni Makka kwa sababu Haram imepewa amani mahsus, ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t): "Je, hawaoni ya kwamba tumeifanya ni nchi takatifu (Haram) na ya amani ." (29:67).

Na katika dua ya Ibrahim(a.s) , aliyoizungumzia Mwenyezi Mungu katika Qur'an tukufu: "Ewe Mola wangu, ufanye mji huu wa Makka uwe wa salama ". (2:126).

Kutumia tamko 'mji huu' ni kuthibitisha utukufu wake kwa kuuhusisha huo mji tu. Na kuusifu kwa neno amani inaweza kuwa ni kwa maana ya mji wenye amani au ni kwa maana ya mji wenye kuaminiwa, haohofiwi na shari.

Aya Na 4

Ni jawabu la kiapo. Makusudio ya kuwa mwanadamu ameumbwa katika hali nzuri, ni kuwa hali nzuri na bora katika mambo yake yote. Maana kwa ujumla ni kuwa mtu ameumbwa katika hali nzuri ya maumbile. Maana ya hali nzuri ya kimaumbile kutokana na ufahamisho wa aya inayofuatia (kisha tukamrudisha chini ya waliochini) ni kutengemaa kimaumbile kwa kupanda daraja ya juu na kufuzu kwa maisha ya milele mbele ya Mola wake, yaliyo mema na yasiyokuwa na uovu wowote. Hayo yametokana na vile alivyoandaliwa na Mwenyezi Mungu, pamoja na elimu yenye manufaa na kummakinisha kutokana na elimu hiyo katika amali njema; Mwenyezi Mungu anasema: "Na kwa nafsi na aliyeilingamanisha, akaifahamisha maasia yake na twaa yake ." (92:7-8).

Kwa hiyo akiamini lile alilolijua akaingilia kufanya amali njema Mwenyezi Mungu humnyanyua, kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

"Kwake hupanda maneno mazuri na amali njema huyapandisha (hayo maneno mazuri) " (35:10). "na lakini inamfikia twaa yenu " (22:37).

"Allah atawainua wale walioamini miongoni mwenu; na waliopewa elimu katika daraja ." (58:11).

Kuna aya nyengine zisizokuwa hizo zinazofahamisha kuwa kuinuka kwa mtu kufikia daraja ya juu ya kufikilia kwake imani na matendo mema ni zawadi isiyokatika. Na Mwenyezi Mungu ameiita 'malipo' kama alivyosema katika Sura hii. "Wana malipo mema yasiyokatika."

Aya Na 5

Makusudio ya chini ya waliochini ni mahali palipo chini kabisa pa watu waovu na wa hasara; yaani "kisha tukamrudisha chini ya walio chini" katika watu wa adhabu. Inawezekana kuwa maana ya kurudisha ni kufanya yaani kisha tukamfanya chini ya waliochini, au inaweza kuwa kwa maana ya kubadilisha yaani kisha tukambadilisha. Makusudio ya chini kwa hali yote ni ouvu na adhabu.

Imesemwa makusudio ya hali nzuri ni ujana, nguvu ukamilifu wa Sura na uzuri wa umbo. Na kwamba kurudishwa chini wa waliochini ni kurudishwa kwenye uzee kwa kudhoofika nguvu za binadamu za dhahiri za batini na kurudishwa nyuma umbo lake; kwa hiyo aya inakuwa sawa katika maana na aya inayosema: "Na tunaempa umri tunamrejeza nyuma katika umbo ". (36:68).

Lakini hayo hayakubaliani na aya inayofuatia "Ila wale waliomaini na wakatenda amali njema." Kwa sababu kusema kuwa waumini hawawi wazee ni upuuzi tu. Vile vile kusema kuwa makusudio ya mtu ni kafiri na kwamba kurudishwa ni kwa maana ya kurudishwa katika Jahannam au kubadilishwa umbo hakukubaliana na aya inayofuatia.

Aya Na 6

Hapo inavuliwa jinsi ya mtu. Neno "malipo yasiyokatika" linatilia nguvu kuwa makusudio ya chini ya waliochini ni kumrudisha kwenye uovu na adhabu.

Aya Na 7

Hapa anaulizwa mtu kwa kuzingatia jinsi ya mtu yeyote. Imesemwa ni Mtume(s.a.w.w) . Neno dini hapa limekuja kwa maana ya malipo. Na maana yake - kutokana na yale yaliyosemwa - ni, nilipi lilokufanya ukadhibishe malipo ya siku ya Kiyama baada ya kuwa tumewafanya watu makundi mawili: kundi lenya kurudishwa chini yawaliochini na kundi lenye kulipwa malipo yasiyokatika?

Aya Na 8

Kuhusu "Je Allah si hakimu bora wa mahakimu (wote)?" ni swali la kutaka kuthibitisha. Kuwa Mwenyezi Mungu ni hakimu bora na kwamba Yeye yuko juu ya mahakimu wote katika kuzingatia hukumu na haki yake na kuipitisha bila kutokea mgongano wowote au makosa yoyote. Kwa hiyo Yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t) anahukumu katika viumbe vyake kwani hekima inawajibisha kuhukumu kwa uzuri na kutekeleza hiyo hukumu. Ikiwa Mwenyezi Mungu ni hakimu bora wa mahakimu wote na watu wakiwa ni makundi mawili tofauti kwa kiitikadi na kimatendo, basi ni katika wajibu kihekima kupambanua kati ya hayo makundi mawili kwa malipo katika maisha yao yatakayobakia, ambayo ni ufufuo.

Kwa hivyo ikiwa watu wote wameumbwa katika hali nzuri (iliyo sawasawa); halafu wakatofautina, likapatikana kundi lililojitoa katika hali yake ya usawa ya umbile lake la kwanza, na kama Mwenyezi Mungu mwenye kuzingatia mambo yao ni hakimu bora wa mahakimu wote, na vile vile ikiwa ni lazima makundi hayo yatofautiane kimalipo, basi iko siku ambayo litalipwa kila kundi kutokana na yale liliyoyafanya, na hili ni jambo lisilokatalika. Aya hizi - kama unavyoziona - ziko katika maana ya aya zinazosema: "Je tuwajaalie wale walioamini na kutenda mema kuwa sawa na wale wafanyao uharibifu katika ardhi? Au tuwajaalie kuwa sawa na waovu? " (38:28).

"Je, wanafikiri wale ambao wamefanya maovu kuwa tutawafanya kama wale walioamini ." (45:21).

Baadhi ya wale wanaosema kuwa Mtume ndiye anaembiwa katika Aya Na "7" wameifanya Maa kuwa na maana na Man (nani), na neno Ahkam kwa maana ya kadhi (mwamuzi). Kwa hiyo maana kwa ujumla itakuwa: Ikiwa watu wanatofautiana, na hilo likalazimisha kutofautiana malipo yao katika siku ya malipo, basi ni nani anayekunasibishia uongo kwa malipo? Je, hakuwa Mwenyezi Mungu ni kadhi bora wa makadhi wote. Basi Yeye ataamua kati yako na ya wale wanaokadhibishia malipo." Lakini kama unavyoona, tafsiri hii ina taklifa isiyokuwa na lazima yeyote.

Utafiti Wa Hadith Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu Aya Na 1-3: Tini ni Madina, Zaituni ni Baytul Muqadas, Turisinin ni Kuffa na mji wenye kuaminika ni Makka. Imepokewa hadith katika maana hayo hayo katika baadhi ya riwaya za Musa bin Jaffar kutokana na mababu zake(a.s) nao kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) . Na katika baadhi ya riwaya nyengine ni kwamba Tini na Zaituni ni Hassan na Hussein Tur ni Ali na mji wenye kuaminika ni Mtume(s.a.w.w) , lakini hayo hayamo katika tafsiri. Katika Durril-Manthur ametoa Ibn Murdawayh kutoka kwa Khuzayma bin Thabit (siye Ansari) alimuuliza Mtume(s.a.w.w) kuhusu mji wenye kuaminika akasema ni Makka.


21

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA ALAQ (PANDE LA DAMU) (NA. 96)

INA AYA 19

Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾

1. Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba

خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾

2. Ameuumba mwanadamu katika pande la damu!

قْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾

3. Soma na Mola wako ni Mkarimu mno.

الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾

4. Ambaye amefunza (kuandika) kwa kalamu.

عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾

5. Amefunza mwanadamu asilolijua.

كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾

6. Si hivyo! Hakika mwanadamu hupetuka mipaka.

أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾

7. Kwa kujiona amejitosha

إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ﴿٨﴾

8. Hakika marejeo ni kwa Mola wako.

أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾

9. Je, umemwona ambaye humkataza.

عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾

10. Mmja, ( wa Mungu) anaposwali?

أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ﴿١١﴾

11. Je, inaonaje! Ikiwa yuko katika uongofu.

أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ﴿١٢﴾

12. Au akawa anaamrisha wema?

أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٣﴾

13. Je, unaonaje! Akikadhi bisha na akaipa mgongo.

أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ ﴿١٤﴾

14. Je, hajui kwamba Allah anaona?

كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ ﴿١٥﴾

15. Naakome! Naapa asipokoma, tutamkokota kwa nywele za utosi.

نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ﴿١٦﴾

16. Utosi wenye kusema uongo, wenye kufanya makosa.

فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾

17. Haya na awaite wanachama wenzake.

سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾

18. Na sisi tutawaita Malaika wa adhabu.

كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ﴿١٩﴾

19. Naakome! Usimtii (bali) sujudu (swali) na ujikurubishe ( kwa Mola wako).

UBAINIFU

Amri kwa Mtume kupokea Qur'an kwa Wahyi utokao kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t) Hii ni ndio Sura ya kwanza kushuka katika Qur'an na mpangilio wake wa maneno haukatai kwa imeshuka kwa mpigo (mkupuo mmoja) kama tutakavyoeleza - Nayo imeshuka Makka , bila ya shaka yoyote.

Aya Na 1

Amesema Raghib kusoma ni kukusanya herufi na matamko, lakini sio mkusanyiko wowote ni kusoma. Haiwezekani kusema umewasomesha watu kwa kuwa umewakusanya. Kwa vyovyote iwavyo husemwa umesoma kitabu kama ukizikusanya herufi na matamko na kuyachunguza katika bongo hata kama hukuyatamka. Na husemwa umesomea mtu kama ukimkusanyia herufi na matamko katika usikizi wake; vile vile hutumiwa neno Tilawa kwa maana ya kisomo kama alivyolitumia Mwenyezi Mungu neno hilo katika Sura ya (98:2): Naye (ni) Mtume aliyetoka kwa Allah anayewasomea madaftari yenye kutakasika.

Kwa dhahiri maana ya neno Soma ni amri ya kupokea yale anayopewa wahyi na Malaika. Kwa ujuma ni amri ya kusoma kitabu ambayo inatokana na kitabu hichi hicho; kama alivyosema msemaji mmoja katika mwanzo wa kitabu chake kwa yule aliyempeleka "Soma kitabu changu hiki na ukifanyie kazi" kwa hivyo hiyo amri ya kusoma kitabu, imetokana na kitabu chenyewe. Mpangilio huu wa maneno:

Kwanza : unatilia nguvu yale yaliyopokewa kwamba Sura hii ni ya kwanza kayika Qur'an kwa Mtume(s.a.w.w) .

Pili : Kwamba makusudio yake ni kusoma Qur'an au yaliyo katika maana yake, na sio makusudio ya kusoma chochote au kuwasomea watu ijapokuwa hilo ni miongoni mwa lengo la kushuka kwake, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na Quran tumeigawanya sehemu mbali mbali. Ili uwasomee watu kwa kituo ".(17:106)

Na pia sio makusudio yakuwa lisome jina la Mola wako. Makusudio hasa ni kwamba jumla ya "kwa jina la Moa wako" inafungamana na kitu kilichoondolewa; kukadiriwa kwake ni hali ya kuanza na hali ya kufungua. Hilo halipingi Bismillahi inayoanza katika Sura hiyo, kuwa ni fungu katika Sura, kwani hayo ni katika maneno ya Mwenyezi Mungu aliyoanzia na kuamrisha kuanzia nayo. Kuhusu "Mola wako ambaye ameumba; inaonyesha milki ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyote, kwani wanaoamshirikisha Mungu walikuwa wakisema Mwenyezi Mungu kazi yake ni kuumba na kupatisha vitu tu! Lakini hana ufalme wowote juu yake. Mwenyezi Mungu analipinga hilo kwa kusema 'Mola wako ambaye ameumba' kwa kutumia neno Rabb ambalo limaana ya kumiliki na kukiangalia vizuri kile kinachimilikiwa kwa hiyo kuumba na kumiliki ni kwake Yeye peke yake.

Aya Na 2

Neno Alaq lina maana ya damu iliyoganda na makusudio yake ni ile inayogeuka kutoka tone la manii katika mfuko wa uzazi. Hiyo inaonyesha vile Mwenyezi Mungu anavyoangalia vizuri na kupanga mambo ya mtu, tangu anapokuwa pande la damu mpaka anapokuwa mtu kamili kwa namna ya kiajabuajabu kiasi ambacho akili zinakwama kujua hilo. Hivyo mtu hatimii wala hakamiliki ila kwa mipangilio inayotokana na Mungu ambayo ni kutoka umbo moja baada ya jingine. Kwa hiyo mtu hana budi kumfanya Mungu pekee ndiye mlezi. Na maneno haya ni hoja ya kuwa Mmoja Mlezi (Mungu).

Aya Na 3

Amri ya kusoma hapa ni ya kusisitiza ile amri ya kwanza. Imesemwa makusudio yake hapo ni kuamrisha kisomo kwa watu yaani kuwafikishia (Tabligh) kama ilivyosemwa kwamba amri ya kwanza ya kusoma na hii ya pili zote ni kwa ajili ya kuwasomea watu. Lakini njia zote mbili hizi haziko wazi

Aya Na 4-5

Herufi Ba ni yakusababisha, kwa maana ya amemfundisha mtu kusoma au kuandika kupitia kalamu. Maneno haya ni kwa ajili ya kuitia nguvu nafsi ya Mtume(s.a.w.w) na kumwondoa kiherehere; kwa kuamrisha kusoma na hali ya kuwa yeye ni ummiy haandiki wala hasomi. Kama vile ameambiwa; soma kitabu cha Mola wako anachokufunulia wala usipogope na hali ya kuwa Mola wako ni Mtukufu ambaye amefundisha mtu kusoma kupitia kalamu, kwa hiyo yeye anaweza kukufundisha kusoma maandishi yake na hali ya kuwa wewe ni ummiy (usiyejua kusoma wala kuandika).

Kisha akaeneza Mwenyezi Mungu (s.w.t) neema, akataja kumfundisha kwke mtu asilolijua akasema: Amemefundisha mtu asilolijua. Hilo ni kuzidisha kuutia nguvu moyo wa Mtume(s.a.w.w) .

Makusudio ya mtu kwa dhahiri ni jinsi ya mtu yoyote. Imesemwa makusudio yake ni Mtume(s.a.w.w) . Na imesemwa ni Mtume Idris(a.s) kwa sababu yeye ndiye mtu wa kwanza kuandika kwa kalamu; Pia imesemwa ni kila Mtume aliyekuwa akiandika. Lakini njia zote ni dhaifu zilizo mbali na ufahamu.

Aya Na 6-7

Makatazo ya kukufuru neema, baada ya Mwenyezi Mungu kumneemesha mtu kwa neema kubwakubwa; mfano kumfundisha kwa kalamu na mengineyo. Ni juu ya mtu kumshukuru juu ya hilo, lakini mtu hukufuru neema zake Mwenyezi Mungu Mtukufu na kupetuka mpaka. Na hiyo ni kutokana na kwamba yeye anajishughulisha na sababu za kidhahir ambazo zinamfikisha kwenye makusudio yake. Kwa hiyo anaghafilika na Mola wake na kuona kuwa hana haja na kumkumbuka na kumshukuru juu ya neema yake, ndipo anamsahau na kupetuka mpaka.

Aya Na 8

Kwa dhahiri maana ya neno marejeo hapa ni kiaga cha mauti na kufufuliwa. Hapa anaambiwa Mtume(s.a.w.w) na imesemwa anaambiwa mtu. Kauli ya kwanza ndiyo iliyodhahiri zaidi.

Aya Na 9-13

Yanatajwa baadhi ya mambo ya mtu mwenye kupetuka mpaka. Makusudio ya mja anayeswali hapa ni Mtume(s.a.w.w) kutokana na unavyofahamisha mwisho wa aya za mwisho wakati Mwenyezi Mungu anapomwamrisha Mtume(s.a.w.w) kusujudu na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kumkataza kumtii huyo anayekataza. Mpangilio wa aya hizi kwa kukadiri kuwa Sura ni ya kwanza kushuka na kushuka kwake mara moja, basi unafahamisha kuwa Mtume alikuwa akiswali kabla ya kushuka Qur'an na pia unafahamisha utume wake kabla ya risala yake ya Qu'an. Ama yale waliyoyataja baadhi yao kwamba swala haikufaradhiwa mwanzo wa utume isipokuwa ilifaradhiwa usiku wa Miraj kwa kusema kwake Mwenyezi Mungu: "Simamisha swala jua linapopinduka mpaka giza la usiku na Qur'an ya Alfajiri "(17:78).

Hiyo inafahamisha kuwa swala tano za kila siku zilifaradhiwa kwa namna yake hasa rakaa mbili mbili, katika usiku wa Miraji, lakini hakuna linalofahamisha kuwa haikuweko kabla yake. Na zimeshuka Sura nyingi kuwa haikuweko kabla yake. Na zimeshuka Sura nyingi kabla ya sura ya 17 (Israi) zinazotaja swala kama Al- Muddathtir, Al-Muzammil nk. kwa ibara tofauti ijapokuwa namna ya swala yenyewe haikudhihirishwa, isipokua ilikuwa ni namna ya kusoma Qur'an na kusujudu, vile vile zimepokewa baadhi ya riwaya za swala ya Mtume(s.a.w.w) pamoja na Khadija bin Ali katika mwanzo wa utume, ingawaje haikutajwa namna ya swala yenyewe. Kwa ujumla maana ya aya ni kumfahamisha yule ambaye anamkataza mja anaposwali na huyo anayekataza anajua kuwa Mwenyezi Mungu anamwona yale anayoyafanya. Nifahamishe huyo anaemkataza mja anayeswali aliye juu ya uongofu au anayeamrisha kumcha Mwenyezi Mungu anamwona?, Je, hastahiki adhabu?

Aya Na 14

Kuhusu "Hivi hajui kuwa Mwenyezi Mungu anamwona ". Makusudio ya kujua hapa yamekuja kwa njia ya kulazimsha kujua. Kwa sababu kuitakidi kuwa Mwenyezi Mungu ni Muumba wa kila kitu kunalizimisha kuitakidi kuwa Yeye (Mwenyezi Mungu) ana ujuzi wa kila kitu. Na huyo mkatazaji alikuwa ni mshirikishaji Mungu anayeabudu masananmu, na wanaobudu masanamu wanakubali kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu na wanamtakasa na sifa za upuungufu, kwa hiyo wanaona kuwa Mwenyezi Mungu hapitwi na kitu wala kushindwa na kitu chochote.

Aya Na 15 - 16

Kuusifu utosi wenye kusema uongo ni kwa njia ya fumbo kwa maana ya uongo wa mwenye utosi huo. Maana ya aya kwa jumla ni makemeo na utisho; nikuwa mambo hayako kama anavyotaka yeye. Ninaapa kama hatajizuia na makatazo yake, tutamchukua kidhalili na kumkokota mwenye adhabu ya utosi ambao mwenye utosi huo ni mwongo kwa anayosema na mkosaji kwa anayofanya. Imesemwa maana yake ni tutautia kovu utosi wake kwa moto na kuufanya mweusi.

Aya Na 17-18

Anaeleza Mwenyezi Mungu udhaifu ya huyo mwenye kukataza mja kuswali, kwa kusema: Haya na awaite hao watu wa baraza lake (wanachama wenzake) na sisi tutawaita Malaika wa motoni, wakali wenye nguvu, ambao hawana wa kuwazuyiwa.

Aya Na 19

Ni kusisitiza makemeo. Makusudio ya "Usimtii " ni usimtii anayekukataza swala. Hii inafahamisha kuwa makusudio ya kusujudu ni swala. Huenda swala aliyokuwa akiiswali Mtume(s.a.w.w) wakati huo ni tasbih na kumsujudia Mwenyezi Mungu. Imesemwa makusudio yake ni kusujudu kwa ajili ya kisomo cha Sura hi ambayo ni moja ya Sura nne za Azaim ( zenye sijda za wajib). Na kujikurubisha ni kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Imesemwa ni kujikurubisha kutokana na thawabu za Mwenyezi Mungu.

Utafiti Wa Hadithi Katika Durril-Manthur ametoa Abdurrazzaq, Ahmad, Abdu bin Hamid, Bukhari, Muslim, Ibn Jariyr na Ibn Ambari katika Masahif. Vile vile Ibn Murdawayh na Bayhaqi katika njia ya Ibn Shihab kutoka kwa Urwa bin Zubeir naye kutoka kwa Aisha mama wa waumin amesema "mwanzo wa kudhihirikiwa Mtume(s.a.w.w) na wahyi ni ndoto njema katika usingizi. Na alikuwa haoti ndoto ila itadhihiri mfano wa Falaq (nyota ya asubuhi).

Kisha akawa anapendelea kukaa mbali na alikuwa akipendelea kwenda Jabal Hiraa na kuabudu huko kwa idadi ya nyusiku kadhaa akiwa amechukua chakula, kisha hurudi kwa Bibi Khadija kuchukua chakula. Alikuwa akifanya hivyo mpaka ilipomjia haki naye akiwa huko Jabal Hiraa. Akamjia Malaika akasema: "Soma" akamwambia "Mimi si msomaji". Mtume anasema: Akanishika na kunikamua mpaka nikafikiwa na kughumiwa, kisha akaniacha, akasema "Soma" nikasema "mimi si msomaji" akanishika tena na kunikamua kama kwanza kisha akaniacha akaniambia "Soma" nikamwambia "mimi si msomaji". Akanishika tena mara ya tatu kisha akaniwacha akaniambia: "Soma kwa jina la Mola wako ambaye ameumba (kila kitu). Amemuumba Mtu kutokana na pande la damu. Soma na hali yakuwa Mola wako ni Mkarimu. Ambaye amemfundisha (mtu) kuandika kwa kalamu".

Akarudi Mtume(s.a.w.w) kwa Bibi Khadija akiwa anatetemeka moyo wake, akasema: "Nifunikeni, nifunikeni" wakamfunika mpaka ilipomwondokea fazaa, akamuhadithia Khadija habari hiyo na akamwambia 'ninaogopa juu ya nafsi yangu' Khadija akamwambia 'Hapana Mwenyezi Mungu hakukufedhehesha kabisa. Hakika wewe utaunga udugu, utachukua taabu, utawakaribisha wageni na utasaidia upande wa haki'.

Akaondoka Khadija mpaka kwa binamu yake anayeitwa Waraqah bin Naufal bin Asad bin Abdulaziz naye alikuwa ni mkristo katika zama za ujahili na alikuwa akiandika Kiibrania, akawa anaandika Injili kwa Kiibrania; wakati huo alikuwa mzee sana na kipofu. Khadija akamwambia "Ewe binamu nisikilize". Akamwambia "umeona nini?". Akamfahamisha yale aliyoyaona Mtume(s.a.w.w) . Akamwambia "huyo ni msiri ambaye alimshukia Musa! Natamani ningelikuwa kijana, natamani niwe hai wakati watakapokutoa watu wako!" Akasema Mtume(s.a.w.w) "hivi watanitoa?" Akasema, "ndio hakuna mtu yeyote aliyekuja na mfano wa uliyokuja nayo wewe ila hupingwa na nikiwahi siku yako hiyo nitakusaidia." Lakini hakuendelea kuishi Waraqah na akafa katika kipindi cha wahyi.

Amesema Ibn Shihab: "Amenifahamisha Abu Salama bin Abdurrahman kwamba Jabir bin Abdillahi El-Ansari amesema: "Amesema Mtume(s.a.w.w) - akiwa anazungumzia kipindi cha wahyi akasema katika mazungumzo yake mbiguni, nikanyanyua macho yangu, nikamwoma Malaika yule aliyenijia katika Jabal Hiraa kwenye kiti kati ya mbingu na ardhi, nikamwogopa na kurudi nyumbani, nikasema nifunikeni nguo! Nifunikeni! Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha aya: "Ewe mwenye kujifunika maguo, simama uonye (watu) na Mola wako umtukuze. Na nguo zako uzisafishe na mabAya Na puuze ." (74:1-5).

Katika hiyo hiyo Durril-Manthur ametoa Ibn Abu Shaybah, Ibn Jariyr nna Abu Naim kutoka kwa Abdalla bin Shaddad amesema: "Jibril alimjia Muhammad(s.a.w.w) akasema: "Ewe Muhammad "Soma". Akasema "Nisome nini?" Akamshika kisha akasema ewe Muhammad "Soma". Akasema "nisome nini?" Akasema : "Soma kwa jina la Mola wako ambaye ameumba (kila kitu) mpaka akafikia amemfunza mwanadamu asilolijuwa."

Mtume akaja kwa Khadija akamwambia, "Ewe Khadija naona amenidhuru." Akasema Khadija: "Hapana Mola wako hawezi kukufanya hivyo na wala kukufanyia ubaya wowote". Basi Khadija akamwendea Waraqh bin Naufal, akampa habari hiyo akasema. "Ukiwa unasema kweli, basi mumeo ni Mtume na atapata tabu kutokana na umati wake nakama nikimuwahi nitamwamini."

Kisha akachelewa Jibril kumjia, akasema Khadija naona Mola wako amechukia ndio Mwenyezi Mungu akateremsha: "Naapa kwa mwanzo wa mchana. Na kwa usiku unapotulia hakukuacha Mola wako wala hakukukasirikia ". (93:1-3).

Lakini kisa chote hiki hakiwezi kuepukana na shaka. Miongoni mwa shaka yake ni vile kutia shaka Mtume(s.a.w.w) kuwa yule aliyoyaona ni wahyi wa Mwenyezi Mungu kutoka kwa Malaika wa Mbinguni, bali hata kudhani kuwa ameshikwa na shetani aliyemtia wazimu. Na shaka zaidi ni vile kumtegemea Mkristo Mtawa kuwa ndiye atakayemtuliza nafsi yake kwa kumfahamisha kuwa yeye ni Mtume, na hali Mwenyezi Mungu amesema: "Sema hii ni njia yangu ninailingania kwa Allah kwa ujuzi wa kweli, mimi na wanaonifuata. (12:108). "Sasa je, ujuzi wa kweli ndio huko kutulizwa moyo na neno la Waraqah? Na amesema Mwenyezi Mungu:

"Sema mimi ninayodalili wazi itokayo kwa Mola wangu ". (6:57)

Sasa dalili gani iliyo wazi katika neno la Waraqah? Na amesema tena Mwenyezi Mungu: "Hakika sisi tumekuletea wahyi kama tulivyowapelekea Nuh na Manabii (wengine) baada yake ." (4:163). Je hao Mitume wengine walikuwa wakitegemea kupata utume wao mfano wa kisa hiki?

Ilivyo ni kwamba wahyi wa utume unalazimisha kuwepo yakini kutoka kwa Mtume mwenyewe kuwa umetokana na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hayo ndio yaliyopokewa kutokana na Maimamu wa Ahlul Bait. Katika Majmau kuhusu Aya Na tisa; ni kuwa Abu Jahl alisema; "Je Muhammad anaweka uso wake mchangani (anaswali) mbele yenu?" Wakasema "ndio". Akasema "Ninaapa kwa yule anayeapiwa, nikimwona nitaikanyaga shingo yake". Akaambiwa "huyo anaswali". Akawa anakwenda kumkanyaga mara akawa anarudi nyuma huku akijikinga kwa mikono yake wakasema: "Unanini ewe Abul Hakam?" Akasema: "Hakika kati yangu na yake kuna handaki la moto na hawa wenye mbawa". Akasema Mtume: "Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko katika uweza wake, lau angelinikurubia tu! Wangelimchanachana Malaika. Ndipo akateremsha Mwenyezi Mungu Aya Na tisa mpaka mwisho wa Sura. Hayo ameyapokea Muslim katika Sahih.

Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu aya hiyo hiyo nikuwa ilishuka juu ya Walid bin El-Mughira aliyekuwa akiwakataza watu kuswali na kutiiwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ufahamisho wa hayo haupingi kuwa mwenye kuswali ni Mtume(s.a.w.w) .

Katika Majmau kwenye hadith ya Abdallah bin Masud kwamba Mtume(s.a.w.w) amesema: "Mja anakuwa karibu zaidi na Mwenyezi Mungu anapokuwa amesujudu". Katika Kafi kwa isnadi wa Wash-shai amesema: "Nimemsikia Arridhaa(a.s) akisema: "Karibu zaidi anapokuwa mja na Mwenyezi Mungu ni anaposujudu, ndio maana akasema Mwenyezi Mungu "Sujudu na ujikurubishe (kwa Mola wako)".

Katika Majmau amepokea Abdulla bin Sinan kutoka kwa Abu Abdillahi amesema: Al - Azaim (Sura Sajda za wajibu) ni nne (Sura ya 32, 41, 52 na 96), zisizokua hizo katika Qur'an ni sunna tu, kusujudu!.


22

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA QADR (QADR) (NA. 97)

INA AYA 5

Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾

1. Hakika sisi tumeiteremsha Qur'an katika Laylatul Qadri.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ ﴿٢﴾

2. Na ni lipi la kukujulisha wewe ni nini Laylatul Qadri?

لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ ﴿٣﴾

3. Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.

تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ ﴿٤﴾

4. HushukaMalaika na Roho katika (usiku) huo kwa amri ya Mola wao kwa ajili ya kila jambo.

سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ ﴿٥﴾

5. (Ni) amani mpaka alfajiri.

Ubainifu Sura hii inaelezea kushuka Qur'an katika usiku wa "Laylatul -qadr" na kuutukuza usiku huo kwa kuufanya bora kuliko miezi elfu. Sura hii inawezekana kuwa imeshuka Makka au Madina, lakini yale yaliyopokewa kwa Maimamu katika Ahlul Bait wa Mtume(s.a.w.w) kuhusu sababu za kushuka kwake, yanatilia nguvu kuwa Sura hii imeshuka Madina.

Aya Na 1

Dhamira katika neno "tumeiteremsha" ni ya Qur'an. Kwa dhahiri inaonyesha kushuka Qur'an yote na wala sio baadhi ya aya zake. Hilo linatiliwa nguvu na ibara ya neno "Anzalnahu" ambalo kwa dhahir lina maana ya kushuka kwa mkupuo mmoja; kinyume cha neno "Tanziyl" ambalo kwa dhahiri lina maana ya kushuku kwa awamu nyingi. Katika maana ya aya hiyo Mwenyezi Mungu anasema: "Naapa kwa kitabu kinachobainisha. Hakika sisi tumeiteremsha (Qur'an) katika usiku uliobarikiwa ". (44:2-3).

Kwa dhahiri hapo Mwenyezi Mungu anaapa kwa jumla ya kitabu chote kisha anatolea habari ya kila kilichoapiwa. Kwa hiyo ufahamisho wa aya ni kuwa Qur'an imeshuka jumla kwa Mtume.

Hakuna katika manen ya Mwenyezi Mungu yanayobainisha kuwa usiku huo ni usiku wowote na kwamba sio usiku ulio katika neno lake Mwenyezi Mungu: "Ni Mwezi wa Ramadhan ambao imeteremshwa ndani yake Qur'an " (2:185) kwa sababu aya hii ikichanganywa na Aya Na Sura ya Al-Qadr (tunayoizungumza) inafahamisha kuwa usiku huo ni katika nyusiku za Ramadhan. Mwenyezi Mungu ameuita usiku huo Laylatul Qadri. Kwa dhahiri inaonyesha kwamba makusudio ya neno Qadri ni kukadiria. Kwa hiyo ni usiku wa kukadiria ambao anakadiria Mwenyezi Mungu matukio ya mwaka mzima kama vile uhai, mauti na riziki. Vile vile wema, uovu nk, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Katika usiku huo hubainishwa kila jambo la hekima. Ndio hukumu inayotoka kwetu; kwa hakika sisi ni waletao mitume. Ni rehema itokayo kwa Mola wako " (44:4-6).

Kwa hivyo hakukuwa kubainisha jambo la hekima ila ni hekima za matukio yenye kutuka katika sehemu zake zinazohusika kwa kukadiria. Hilo linafahamisha kwamba usiku huo unakaririka kwa kukaririka miaka. Kwa hiyo katika mwezi wa Ramadhan wa kila mwaka kuna usiku unaokadiriwa mambo ya mwaka. Kwa sababu hakuna maana ya kuukadiria usiku mmoja (ulioshuka Qur'an) kwamba umekadiriwa ndani yake matukio ya kabla yake na baada yake. Na neno 'hubainisha' ambalo kwa dhahiri linaonyesha kuendelea vile vile neno 'hushuka' Malaika yanatilia nguvu hilo.

Basi hakuna njia inayoonyesha yale yaliyosemwa kuwa usiku huo ni ule usiku mmoja tu ulioteremshwa Qur'an. Au kwamba ulikuwa ukikaririka katika miaka ya zama za Mtume(s.a.w.w) kisha Mwenyezi Mungu akauondoa. Vile vile hakuna njia inayoonyesha kuwa usiku huo upo katika miaka yote, lakini unabadilika kwa kukaririrka miaka; kwamba mwaka mwengine uwe katika mwezi wa Ramadhan, mwengine uwe katika mwezi wa Shaaban, nk. Imesemwa neno Qadr limekuja kwa maana ya hadhi na heshima na kwamba umeitwa usiku wa hadhi kutokana na umuhimu wa hadhi yake, au kwa hadhi ya wale wenye kuabudu katika usiku huo. Imesemwa tena Qadr ni kwa maana ya ufinyu, na kwamba umeitwa usiku finyu kwa sababu ardhi inakuwa finyu kutkana na kushuka Malaika.

Maana ya aya ni kwamba huo ni usiku ulio katika mwezi wa Ramadhan katika kila mwaka ambao ndani yake mnahukumiwa mambo kwa kiasi cha makadiro. Hilo halikanushi kutokea mabadiliko katika muda wa mwaka kwa sababu kuhakikika kile chenye kukadiriwa ni jambo jengine na mbadiliko katika kukadiria ni jambo jengine; kama vile kutokea mabadiliko ya matukio ya kilimwengu kwa kiasi cha matakwa ya Mungu, hakukanushi kuainiwa kwake katika "Lauhil Mahfudh"! Amesema Mwenyezi Mungu: "Na asili ya hukumu zote iko kwake " (13:39).

Uwezekano wa kutokea mambo kwa kuhakikika kwake kuna mipangilio kwa kutimia na kupungua. Inawezekana kutokea baadhi ya mipangilio katika Laylatul-Qadr na kuchelewa kutimia kupitishwa mpaka wakati mwengine, lakini hadithi zitakazokuja haziwafiki hilo.

Aya Na 2

Ni fumbo la utukufu wa cheo cha usiku na daraja yake kubwa. Hilo linatiliwa nguvu na kudhihiri kwa jina la huo usiku mara kwa mara, pale iliposemwa: "Nini Laylatul-Qadr, Laylatul-Qadr ni bora ". Na wala isisemwe nini huo, huo ni bora.

Aya Na 3

Ni ubainifu wa kijumla kwa lile limaloishiriwa na aya tatu katika ukubwa wa jambo la huo usiku. Makusudio ya kuwa ni bora kuliko miezi elfu ni ubora wa ibada kama walivyofasiri wafasiri. Hilo ni lenye kunasibiana na makusudio ya Qur'an na kuwatia hima watu kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo kuufanyia ibada ni bora kuliko ibada ya miezi elfu na baraka iliyotajwa katika Sura ya (44:3) inafahamisha hilo. Na kuna maana mengine yatakayokuja katika utafiti wa hadith (Inshallah).

Aya Na 4

Kwa dhahiri roho hapa ni roho iliyotajwa katika Aya Na (85:17) "Sema roho ni jambo linalohusika na Mola wangu ". Herufi Min katika neno Min Kulli imesemwa kuwa imekuja kwa maana ya herufi Ba yaani kwa kila jambo. Na imsemwa ni ya kuanzia makusudio na kufahamisha sababu yaani kwa sababu ya kila jambo la Mungu. Pia imesemwa ina maana ya sababu ya lengo, yaani kwa ajili ya kuzingatia kila jambo katika mambo. Kwa kweli hasa ikiwa makusudio ya neno Amr ikiwa ni amri ya Mungu inayofasiriwa na neno lake Mwenyezi Mungu katika Sura (36:82): "Hakika amri yake anapotaka chochote ni kukiambia kuwa kikawa". Basi Min ni ya kuanza na kufahamisha sababu kwa maana ya "Hushuka Malaika na Roho katika Laylatul-Qadr kwa idhini ya Mola wao hali ya kuanza kushuka kwao kutokana na kila amri ya Mungu ".

Ikiwa Amr ina maana ya kilimwengu, basi itakuwa kwa maana ya Lam ya kwa ajili, yaani kwa idhini ya Mola wao kwa ajili ya kuzingatia kila jambo katika mambo ya kilimwengu.

Aya Na 5

Amesema katika Mufradat neno Salaam lina maana ya kuepukana na maafa ya nje na ndani. Kwa hivyo neno hilo katika aya linaonyesha hifadhi ya Mungu kwa kueneza rehema kwa waja wake wenye kuelekea kwake na kuziba mlango wa mateso. Aya mbili hizi za mwisho ni tafsiri ya Aya Na tatu.

Utafiti Wa Hadith Katika Tafsiri ya Bur'han kutoka kwa Sheikh Tusi naye kutoka kwa Abu Dharri amesema: Nilimuuliza Mtume(s.a.w.w) : "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Laylatul-Qadr ni jambo linalokuwa katika zama za Mitume, wakiondoka nalo linaondoka?" Akasema "La! bali Laylatul-Qadr inaendelea mpaka siku ya Kiyama". Na imekuja hadithi hiyo katika maana mbali mbali katika njia ya Ahli Sunnah. Katika Majmau kutoka kwa Hammad bin Uthman, naye kutoka kwa Hassan bin Abu Ali amesema, "nilimuuliza Abu Abdillahi(a.s) kuhusu Laylatul-Qadr akasema: 'Utafute katika usiku wa 19, 21 na 23". Katika baadhi ya habari zilizopokewa ni kuwa kati ya usiku wa 21 na 23 kama inavyoeleza riwAya Na Iyashi kutoka kwa Abdul-Wahid naye kutoka kwa Baqir(a.s) .

Imefahamika kutoka katika riwaya kwamba haukuainiwa (haukutajwa) kwa ajili ya kuutukuza ili usidharauliwe kwa kufanyiwa maasi. Katika hiyo hiyo Majmau katika riwAya Na Abdillahi bin Bakir kutoka kwa Zurara kutokana na mmoja wa Maimamu wawili (Abu Abdillahi na Baqir) amesema: "Hakika usiku wa Laylatul-Qadr ni usiku wa "Jahaniy". Hadith ya Jahaniy ni kwamba yeye alisema kumwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Hakika nyumba yangu nimeijenga nje ya mji niamrishe usiku wa kuingia kwenye nyumba hiyo, akamwamrisha usiku wa 23. Hadith ya Jahaniy imepokewa kwa njia ya Ahli Sunnah vile vile katika Durril Manthur kutoka kwa Malik na Bayhaqi. Katika Kafi kwa isnadi ya Zurarah amesema; "Amesema Abu Abdillahi(a.s) kukadiria ni mwezi 19, kukata hukumu ni mwezi 21, na kutia saini ni mwezi 23." Na kuna riwaya nyengine zenye maana hiyo.

Zimeafikiana habari za Ahlul Bait kwamba usiku huo ni wenye kubakia ukikaririka kila mwaka na kwamba huo ni usiku katika usiku wa mwezi wa Ramadhan na kwamba uko katika moja ya nyusiku tatu. Ama kwa upande wa Ahli sunnah riwaya zimehitalifiana kiajabu kiasi kisicho dhibitika na lililo maarufu ni kwamba huo ni usku wa mwezi 27 ambao imeshuka Qur'an. Katika Durril Manthur ametoa Hatib kutoka kwa Ibn El-Musabbib amesema: "Amesema Mtume(s.a.w.w) niliona katika ndoto Bani Umayya wakipanda mimbari yangu likanitia dhiki hilo, ndio akateremsha Mwenyezi Mungu Sura ya Qadr.

Imepokewa mfano wa hadith hiyo kutoka kwa Hatib katika Tarekh yake naye kutoka kwa Ibn Abbas, vile vile imepokewa katika maana hayo kutoka kwa Tirmidhi, ibn Jariyr, Tabrani Ibn Murdawahyh na Bayhaqi katoka kwa Hassan bin Ali. Na ziko riwaya nyingi katika maana haya kwa upande wa Shia kutoka kwa Maimam wa Ahlul Bait(a.s) . Katika riwaya hizo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfariji Mtume wake(s.a.w.w) kwa kumpa Laylatul Qadr na kuifanya bora kuliko miezi elfu ambao ni muda wa ufalme wa Bani Umayya. Katika Kafi kwa isnadi yake kutoka kwa Ibn Abu Umayya naye kutoka kwa watu zaidi ya mmoja nao kutoka kwa Abu Abdillah(a.s) kwamba walimuuliza baadhi ya sahaba zetu wala simjuwi ila Said Assiman: "Vipi itakua Laylatul Qadr ni bora kuliko miezi elfu?' "Akasema amali katika usiku huo ni bora kuliko amali ya miezi elfu bila Laylatul Qadr".

Katika hiyo hiyo Kafi kwa isnadi yake kutoka kwa Fadhili, Zurara na Muhammad bin Muslim, kutoka kwa Humran kwamba yeye alimuuliza Abu Jaffar(a.s) kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: "Hakika sisi tumeiteremsha (Qur'an) katika usiku uliobarikiwa". Akasema: "Ndio Laylatul Qadr nao uko katika kila mwaka katika mwezi wa Ramadhan katika kumi la mwisho, haikushuka Qur'an illa katika Laylatul Qadr, amesema Mwenyezi Mungu: "Katika (usiku) huo hubainishwa kila jambo la hekima ." (44:4).

Akaendelea kusema: "Hukadiriwa katika Laylatul Qadr kila kitu kinachokuwa mwaka huo kwa mkabala wake; heri na shari, utii na uasi na kuzaliwa na ajali au riziki. Kinachokadiriwa katika usiku huo na kupitishwa basi kimekwishapitishwa. Na Mwenyezi Mungu ana matakwa yake katika hilo. Akasema tena: "Na amali njema katika usiku huo kama vile swala, zaka na namna ya mambo ya heri, ni bora kuliko amali katika miezi elfu isiyokuwa na Laylatul Qadr."

Kuhusu jumla ya "Mwenyezi Mungu ana matakwa yake katika hilo" anakusudia uhuru wa kudura yake. Anaweza kufanya analotaka hata kama amelipitisha. Kwani kuwajibisha jambo hakuwezi kuufunga uweza, kwa hiyo anaweza kuichangua hukumu aliyoipitisha. Katika Majmau amepokea Ibn Abbas kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kwamba yeye Mtume amesema: "Unapokuwa Laylatul Qadr hushuka Malaika ambao ni wakazi wa Sidratul Muntaha miongoni mwao akiwa ni Jibril. Anashuka pamoja na bendera, bendera moja anaisimamisha kwenye kaburi yangu, nyengine kwnye Baytul-Muqadas, nyengine Masjidul-Haram, na nyengine anaisimamisha Mlima Sinai. Wala hamwachi yeyote mwanamume au mwanamke ila humpa salam isipokuwa, mnywaji tembo, mwenye kula nyama ya nguruwe na mwenye kujipaka zafarani".

Katika Tafsiri ya Bur'han kutoka kwa Said bin Abdillahi naye kutoka kwa Abu Baswiyr amesema. "Nilikuwa pamoja na Abu Abdillahi(a.s) akataja kitu kuhusu kuzaliwa Imam, akasema inawajibisha kuzidi Roho katika Laylatul Qadr , nikamwambia: niwe mkombozi wako kwani Roho si Jibril? Akasema Jibril ni katika Malaika na Roho ni mkubwa kuliko Jibril huoni Mwenyezi Mungu anasema: "Hushuka Malaika na Roho". Riwaya ni nyingi sana zinazoeleza ubora wa Laylatul Qadr na baadhi yake zimetaja alama ambazo tumezifungia jicho; kama kutokeza mwanga wa jua na kulingana sana hewa, nk.

SURA BAYYINA ( HOJA) (NA. 98)

INA AYA 8

Kwa jina la Allah. Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿١﴾

1. Hawakuwa wale ambao wamekufuru katika watu wa kitabu na washirikina, ni wenye kuachana na waliyonayo mpaka iwajie hoja.

رَسُولٌ مِّنَ اللَّـهِ يَتْلُو صُحُفًا مُّطَهَّرَةً ﴿٢﴾

2. (Nayo) ni Mtume atokaye kwa Allah awasomee kurasa zilizotakaswa.

فِيهَا كُتُبٌ قَيِّمَةٌ ﴿٣﴾

3. (Ambazo) ndani yake mna maandishi yaliyosawasawa

وَمَا تَفَرَّقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿٤﴾

4. Wala hawakutengana wale waliopewa kitabu ila baada ya kuwajia hiyo hoja.

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾

5. Na hawakuamrishwa ila wamuabudu Allah kwa kumtakasia yeye dini, hali wameshikamana na haki na wasimamishe swala na watoe zaka na hiyo ndiyo dini iliyo sawasawa

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ ﴿٦﴾

6. Hakika wale ambao wamekufuru katika watu wa kitabu na wenye kushirikisha (wataingia) katika moto wa Jahannam watakaa humo milele na hao ndio waovu wa viumbe.

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ هُمْ خَيْرُ الْبَرِيَّةِ ﴿٧﴾

7. Hakika wale amabo wameamini wakatenda (amali) njema hao ndio bora wa viumbe.

جَزَاؤُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ رَبَّهُ ﴿٨﴾

8. Malipo yao kwa Mola wao ni mabustani ya milele yanayopita mito chini yake watakaa humu milele. Allah yuradhi nao na wao waradhi naye. Na hayo ni kwa mwenye kumcha Mola wake.

UBAINIFU

Sura hii inasajili ujumbe wa Muhammad kwa wote wale waliopewa kitabu na washirikina. Kwa maneno mengine, kwa wote wale wenye mila na wasiokuwa na mila. Ujumbe huo ni katika utaratibu wa Mwenyezi Mungu - desturi za uongofu - ambazo zimeelezwa katika Qur'an; kwa mfano kamanalivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t): "Hakika sisi tumemuongoa (tumembainishia) njia, basi ama atakua mwenye kushukuru au mwenye kukufuru ." (76:3).

Na amesema tena Mwenyezi Mungu : "Na hakuna umma wowote ila alipitia humo muonyaji ." (35:24).

Ujumbe wa Muhammad(s.a.w.w) unatoa hoja kuwa ni kwa ajili ya watu wote, kwa vile unakusanya maslahi ya jamii ya binadamu ikiwa ni pamoja na itikadi na matendo; kama utakavyokuja ufafanizi (Inshallah). Sura hii inauwezekano wa kuwa imeshuka Makka au Madina, ingawaje mpangilio wake unaonyesha kuwa imeshuka Madina.

Aya Na 1

Ayah hii ambayo ndiyo kichwa cha maneno ya Sura, inaonyesha kusimama hoja juu ya wale ambao wamekufuru na wale waliopewa kitabu wakati walipoanza kuhitalifiana. Makusudio hasa ni kuwa Mtume(s.a.w.w) ni mmojawapo wa waliyothibitisha hoja ya Mwenyezi Mungu ana wajibu wa kuleta mwokozi kwa watu. Hii ni kutokana na (uadilifu) wa mwenendo wake. Makusudio ya 'waliokufuru' hapa ni waliokanusha mwito wa utume wa kiislamu. Herufi: min ni ya kuelezea baadhi, yaani baadhi ya waliopewa kitabu. Washirikina ni wale wanaoabudu masanamu na wengineo.

Kwa ujumla ni kuwa; wale walioukanusha ujumbe wa Mtume(s.a.w.w) walikuwa ni wenye kuhitajia kusimamishiwa hoja wakati wote, mpaka alipokuja Mtume(s.a.w.w) wajibu huo wa kupatiwa hoja ulikwisha. Wamehitalifiana kiajabu katika tafsiri ya ayah ii na maana yake, mpaka baadhi yao wakasema kwamba aya hiyo ndiyo ngumu zaidi katika Qur'an kimpangilio na kitafsiri. Maana haya tuliyoyaleta ndiyo yanayolingana sawa na mpangilio wote wa Sura bila ya kupingana na aya. Mwenye kutaka maelezo zaidi na ayatafute haya katika vitabu vilivyorefushwa maelezo.

Aya Na 2

Neno Suhuf lina maana ya kitu kinacho andikiwa juu yake. Makusudio yake hasa ni mafungu ya Qur'an yanayoshuka kwa ujumla. Neno hili limekaririka katika maneno yake Mwenyezi Mungu kwa maana ya mafungu ya vitabu vya mbinguni; kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t): "Huo waadhi umo katika kurasa tukufu. Zenye kutukuzwa (na) zenye kutakaswa. Zimo katika mikono ya waandishi. Watukufu watenda mema ." (8:13-16).

Makusudio ya kuwa kurasa. Zimetakaswa, ni kuwa imetakaswa na uchafu wa ubatilishi kwa kuguswa na shetani. Na imekaririwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwamba hayo ni maandishi ya haki yenye kuhifadhiwa na muingilio wa kishetani. Mwenyezi Mungu kasema: "Hapana aigusaye ila waliotakaswa na mabaya" (56:79).

Aya Na 3

Neno kutubu lina maana ya kila chenye kuandikwa, iwe ni ubao au karatasi nk. Vile vile lina maana ya hukumu: Kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t); "Mmehukumiwa (mmelazimishwa) kufunga ".(2:183).

"Na mmehukumiwa (mmelazimishwa) kupigana vita " (2:216).

Kwa dhahiri ni kuwa makusudio yake ni maandishi yaliyomo katika kurasa zenye hukumu za Mungu zenye kufungamana na itikadi na matendo. Dalili yake ni kuyasifu kwa neno Qayyima linalotokana kusimamia kitu kwa maana ya kukihifadhi, kuchunga maslahi yake na kudhamini wema wake. Inajulikana kuwa vitabu vya mbinguni vinasimamia mambo ya jamii ya watu, na kuchunga maslahi yake kutokana na hukumu zake zenye kufungamana na itikadi na amali. Kwa hiyo maana ya aya hizi mbili ni kuwa: hoja iliyowazi ambayo amewaletea Mtume(s.a.w.w) kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwasomea vitabu vya mbiguni vyenye kutakaswa na batili, ni hukumu zenye kusimamia mambo ya jamii ya watu, zenye kuchunga maslahi yake.

Aya Na 4

Aya Na kwanza ilikuwa inaonyesha kumkanusha kwao Mtume na kitabu chake chenye kudhamini mlingano (mwito) wa haki. Aya hii inaonyesha kukhitalifiana kwao juu ya mlingano wa Kiislamu. Hayo yameonyweshwa kwenye sehemu nyengine katika Qur'an kama: "Na hawakukhitalifiana waliopewa kitabu ila baada kuwajia elimu ". (3:19).

Kuwajia hoja ni ubainifu wa utume ambao umewabainikia katika vitabu vyao au ule waliofafanuliwa na mitume yao, kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t): "Na alipofika Isa kwa dalili zilizo wazi, alisema "Nimekujieni na elimu (yenye nafuu na nyie), na ili nikuelezeni baadhi ya yule mliyohitalifiana; basi mcheni Allah na nittini. Kwa hakika Allah ndiye Mola wenu; basi muabuduni, hii ndiyo njia iliyonyooka, lakini yalihitalifiana makundi wao kwa wao ". (43:63-65).

Kama ukiuliza, kwa nini imeelezwa kutengana kwa watu wa kitabu na haikuelezewa kutengana kwa washirikina.

Jibu ni kuwa, sio mbali kuwa neno: wale ambao wamepewa kitabu, lililoko katika ayah ii linawachanganya watu wa kitabu na washirikina. Limebadilishwa neno 'watu wa kitabu' ambao katika Qur'an wanajulikana kuwa ni Mayahudi, Wakristo na Majusi, kuwa wale ambao 'wamepewa kitabu'. Bila shaka ibara hizi mbili zinatofautiana. Mwenyezi Mungu amefafanua kuwa Yeye ameteremsha kitabu ambacho ni sharia iliyofaradhaiwa juu yao yenye kuhukumu katika hitilafu za mambo yao ya kimaisha - tangu mwanzo zilipodhihiri hitilafu zao za kimaisha wao wakahitalifiana katika dini baada ya kuwabainikia wao haki na kuwasimamia wao hoja. Kwa hiyo watu wote wameletewa kitabu; kisha wakahitalifiana, kuna katika wao waliosahau kile walichopewa, kuna waliochukulia kimakosa na kuna wale waliohifadhi kile walichopewa wakakiamini. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: "Watu wote walikuwa wa dini moja (kisha wakahitalifiana). Basi Allah akawaleta manabii watoao habari njema na waonyao na pamoja nao akawateremshia vitabu vilivyoshikamana na haki ili vihukumu baina ya watu katika yale waliyokhitalifiana na hawakuhitalifiana katika hayo ila wale waliopewa vitabu hivyo; baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi kwa sababu ya uhasidi (uliokuwa) baina yao ." (2:213).

Katika maana hayo Mwenyezi Mungu anasema: - mpaka aliposema- Na kama Mwenyezi Mungu angelitaka wasingelipigana wale waliokuwa baada yao (baada ya mitume) baada ya kuwafikia hoja zilizowazi. Lakini walihitalifiana, kwa hiyo wako katika wao walioamini na wako katika wao waliokufuru.. (2:253).

Kwa ujumla neno wale ambao wamepewa vitabu linaenea kwa wote, watu wa kitabu na washirikina.

Aya Na 5

Dhamira katika neno hawakuamrishwa inawarudia wale waliokanusha katika waliopewa kitabu na washirikina. Makusudio yake ni kuwa, ujumbe wa Mtume(s.a.w.w) na maandishi yaliyomo katika kurasa na wahyi, hayakudhamini kitu isipokuwa ibada ya Mwenyezi Mungu kwa kuifunga pamoja na Ikhlas katika dini na kutomshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote. Neno Hunafaa lina maana ya kuondoka kwenye upande wa kupetuka mipaka na kuelekea kwenye kulingana sawa (kuwa ndani ya mipaka ya Mwenyezi Mungu). Na Mwenyezi Mungu ameiita Dini ya Kiislamu Hanifa kwa vile Uislamu unaamrisha 'uwastani' katika mambo yote na kujiepusha na kukiuka vipimo. "Kisha wasimamshe swala na watoe zaka". Baada ya kuelezea dini kwa ujumla anaelezea mafungu ya dini yenye kuhusikana. Swala na kutoa zaka ni miongoni mwa nguzo za Uislamu ambazo ni mwelekeo wa kiibada unaomhusu Mwenyezi Mungu na kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Makusudio ya dini iliyo sawasawa ni dini ya maandishi yenye msimamo ulio sawasawa kama walivyofasiri. Ikiwa makusudio ya maandishi ni maandishi yote ya mbiguni kama maandishi ya Nuh na wengineo katika mitume, maana yake yatakuwa hAya Na liyoamriwa na kulinganiwa katika mlingano (mwito) wa Muhammad, ndio yale yale waliyoamriwa katika vitabu vyao vyenye msimamo na wala sio jambo la kuzusha, kwani dini ya Mwenyezi Mungu ni moja na ni juu yao kuifuata dini hiyo, kwa sababu ndiyo yenye msimamo. Na ikiwa makusudio ya maandishi yenye msimamo ni yale wanayosemewa na Mtume(s.a.w.w) kutoka katika maandishi yaliyomo katika kurasa zenya kutoharishwa, basi itakuwa maana yake ni kuwa wao hawakuamrishwa ila kufuata hukumu zenye msimamo na zenye maslah ya jamii ya kiutu.

Kwa vyovyote iwavyo aya inaishiria dini ya Tawhid (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ambayo inadhaminiwa na Qur'an inayosadikisha vitabu vilivyo kabla yake na kuhukumia yale yanayoamrisha jamii ya watu, hali ya kusimamia mambo yao na kuchunga maslahi ya maisha yao; kama alivyo lifafanua hilo Mwenyezi Mungu kwa uwazi katika neno lake: "Basi uelekeze uso wako katika dini iliyosawasawa, ndilo umbile ambalo Allah amewaumbia watu (dini iliyosawa). Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Allah. Hiyo ndiyo dini ya sawa (30:30).

Kwa aya hii basi, yanakamilika ubainifu wa kuenea ujumbe wa Mtume(s.a.w.w) na kuenea mwito wa Kiislamu kwa watu wote. Kwa hiyo neno lake Mwenyezi Mungu: "Hawakuwa wale ambao wamekufuru katika watu wa kitabu" mpaka mwisho, linaonyesha kuwa kuna ulazimu kutokana na desturi ya uongozi wa Mungu, kutimiza hoja kwa yule mwenye kuukanusha mwito miongoni mwa watu wa kitabu na washirikina. Kuhusu neno lake Mwenyezi Mungu "Mtume atokae kwa Allah" inaonyesha kuwa hiyo hoja ni Mtume Muhammad(s.a.w.w) . Kufarikiana kwao na kukanusha kwao haki kwa zamani, pia kuliendelea baada ya kuja Mtume Mhuhammad(s.a.w.w) kama anavyosema Mwenyezi Mungu katika Sura hii: "Wala hawakutengana".

Aya Na 6-7

Baada ya kuelezea ukanushaji wao wa hoja na mambo wanayolinganiwa, sasa anaingilia kutoa onyo kwa wale wakanushaji na kuwapa biashara waumini. Maana ya Aya Na ko wazi hakuna haja ya ufafanuzi.

Aya Na 8

Maana halisi ya neno Adn ni kutulia na kuthibiti, kwa hiyo makusudio yake ni pepo ya kudumu. Mwenyezi Mungu analisisitiza hilo kwa kusema: "Watakaa humo milele".

Mwenyezi Mungu kuwa radhi nao ni uhakika wa thawabu alizowapa, ikiwa ni malipo ya imani zao na matendo yao. "Hayo ni ya mwenye kumuogopa Mola wake" hiyo ndio chapa ya wema wa akhera na Mwenyezi Mungu amesema: "Kwa hakika wale wanaomuogopa Allah miongoni mwa waja wake ni wale wataalamu (wanavyuoni) ". (35:28).

Kwa hiyo kumjua Mwenyezi Mungu kunafuatia kumuogopa na kumuogopa kunafuatia kumuamini kwa maana ya kuamini kimoyo uungu wake kisha kutenda amali njema. Kuna hitilafu kubwa sana katika kufasiri aya hizi. Hitilafu hizi hazina umuhimu wa kuzielezea. Mwenye kutaka kuzijua na aangalie vitabu vyenye maelezo marefu.

Utafiti Wa Hadith Katika Tafsiri ya Qumii katika riwAya Na Abu-Jarud kutoka kwa Abu Jaffar(a.s) anasema: Hoja ni Muhammad(s.a.w.w) . Katika Durril Manthur ametoa Ibn Murdawy kutoka kwa Aisha amesema: "Nilimuuliza ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu" Ni nani Mtukufu zaidi wa viumbe kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ewe Aisha kwani hukusoma aya inayosema: Hakika wale ambao wameamini na wakatenda matendo mema hao ndio bora wa watu?" Katika hiyo hiyo Durril-Manthur ametoa Ibn Asaki, kutoka kwa Jabir bin Abdillahi amesema: "Tulikuwa mbele ya Mtume akaja Ali akasema Mtume(s.a.w.w) . "Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake hakika huyu na wafuasi wake ndio wenye kufuzu siku ya Kiyama." Kisha ikashuka aya hiyo, ikiwa masahaba wa Mtume(s.a.w.w) wakijiwa na Ali husema: "Amekuja bora wa watu."

Imepokewa hadith kwa maana hiyo kutoka kwa Addi kutoka kwa Ibn Abbas, vile vile kutoka kwa Ibn Murdawayh, naye kutoka kwa Ali(a.s) . Na imepokewa vile vile katika Bur'han kutoka kwa Muwaffaq bin Ahmad katika kitabu Manaqib kutoka kwa Yazid bin Sharahiyl El-Ansari, vile vile katika Majmau kutoka katika kitabu cha Shawahiduttanzil cha Hakim naye kutoka kwa Yazid bin Sharahiyl kutoka kwa Ali amesema: Wakati Mtume(s.a.w.w) akikaribia kufa, na mimi nimemwigamiza katika kifua changu, aliniambia: "Ewe Ali hivi hukusikia neno la Mwenyezi Mungu. "Hakika wale ambao wameamini na wakatenda (amali) njema hao ndio bora wa viumbe". Wao ni wafuasi wako na kukutana kwangu na nyinyi ni kwenye birika wakati utakapokusanyika umati kwa ajili ya hisabu. Wafuasi wako watakuwa wana mapako yenye kung'aa (katika viungo vya udhu).

Katika Majmau kutoka kwa Muqatil bin Salman, naye kutoka kwa Adh-dhah-hak naye kutoka kwa Ibn Abbas kuhusu neno lake Mwenyezi Mungu: "Hao ndio bora wa viumbe" amesema ilishuka kwa Ali na Ahlul Bait wake.


23

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA SILZAAL ( TETEMEKO)(NA. 99)

INA AYA 8

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema , Mwenye kurehemu

إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا ﴿١﴾

1. Itakapotetemeshwa ardhi huo mtetemeko wake.

وَأَخْرَجَتِ الْأَرْضُ أَثْقَالَهَا ﴿٢﴾

2. Na ikatoa ardhi mizigo yake.

وَقَالَ الْإِنسَانُ مَا لَهَا ﴿٣﴾

3. Na akasema mwanadamu ina nini?

يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا ﴿٤﴾

4. Siku hiyo itatoa habari zake.

بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَىٰ لَهَا ﴿٥﴾

5. Kwa kuwa Mola wako ameiamrisha.

يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ ﴿٦﴾

6. Siku hiyo wataondoka watu wametawanyika tawanyika ili kuonyeshwa amali zao.

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾

7. Basi atakayefanya wema (hata) uzani wa sisimizi atauona.

وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾

8. Na atakayefanya uovu (hata) uzani wa sisimizi atauona.

UBAINIFU

Sura hii inaelezea Kiyama, kutolewa watu kwa ajili ya malipo ya sharti za kiyama ambazo ni tetemeko la ardhi na kuzungumza habari zake. Sura hii inawezekana kuwa imeshuka Makka au Madina.

Aya Na 1

Mwenyezi Mungu anasema "Itakapotetemeshwa ardhi huo mtetemeko wake" kwa maana ya kuwa tetemeko hilo ni la aina yake, kutokana na ukubwa wake.

Aya Na 2

Neno athqal lina manna ya mizigo. Kwa vyovyote vile iwavyo makusudio ya aya ni kuwa ardhi itatoa mizigo yake iliyoichukua ambayo ni wafu kama ilivyosemwa au hazina za madini au vyote hivyo. Kauli ya kwanza (wafu) ndyo iliyokaribu zaidi na maana.

Aya Na 3

Yaani mtu atapigwa na mshangao wa ajabu kutokana na tetememko hilo kiasi cha kujiuliza: Ina nini ardhi? Mbona inatetemeka hivi? Imesemwa kuwa makusudio ya mtu hapa ni kafiri asiyeamini ufufuo, na yamesemwa zaidi ya hayo kama yatakavyokuja maelezo (Inshallah).

Aya Na 4 -5

Ardhi itakuwa shahidi wa vitendo vya mwanadamu, kama vile vitavyokuwa shahidi viungo vya binadamu na maandishi ya Malaika. Hiyo ni kutokana na amri ya Mwenyezi Mungu. Na hii inafahamisha kuwa vitu vina uhsai na hisia, ijapokuwa sisi hatujui hilo, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na hakuna chochote ila kinamsabihi (Mwenyezi Mungu) kwa sifa zake njema lakini nyinyi hamfahamu kusabihi (kutukuza) kwake.." (17:44).

Akasema tena: "Hata watakapoujia (huo moto), hapo ndipo masikio yao, na macho yao na ngozi zao zitakapotoa ushahidi juu yao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.. Na wao waziambie ngozi zao; "Mbona mnatushuhudilia? "Nazo ziwaambie: "Allah aliyekitamkisha kila kitu ndiye aliyetutamkisha, naye ndiye aliyekuumbeni mara ya kwanza. Na kwake hivi sasa) mnarudishwa (41:20-21).

Kumekuwa na hiitilafu kubwa juu ya maana ya kuzungumza ardhi; kuwa itapewa uhai na hisia au itaumbwa sauti tu! Lakini hatuna haja na hitilafu hizo, kwa sababu vyovyote iwavyo ni kwamba ardhi itatoa ushahidi.

Aya Na 6

Makusudio ya kuondoka kutawanyika tawanyika, ni kuenda zao kwenye makazi yao katika pepo na katika moto. Na kuona matendo yao ni kuona malipo ya matendo ya au kuona umbo halisi la hayo matendo. Imesemwa kuwa makusudio yake ni kutoka makaburini mwao kuelekea kwenye mkusanyiko wakitofautina kwa nyuso nyeusi na nyeupe,na kwa fazaa na amani, ili yafahamike malipo yao kwa kuangalia tu!, kama alivyosema Mwenyezi Mungu; "Siku ambayo kila nafsi itakuta mema iliyoyafanya yamehudhurishwa, na pia ubaya iliofanya .(3:30).

Kauli ya kwanza ndiyo iliyo karibu zaidi na maana.

Aya Na 7-8

Dharra ni chembe ndogo za vumbi zinaonekana katika mwanga wa jua au sisimizi wadogo. Aya hiyo inatilia mkazo yaliyotangulia kuwa amali yoyote hata iwe ndogo kiasi gani, itaonekana. Lakini aya hizo hazikanushi kuharibika kwa amali, au kugura amali kwenda kwenye nafsi nyingine; kama kugura mema ya mwuuaji kwenda kwa mwenye kuuwa, au kubadilika maovu kuwa mema kwa baadhi ya wenye kutubia, nk; kama ilivyoelezwa katika Sura zilizotangulia kama aya inayosema: "Ili Allah apate kuwapambanua walio wabaya na walio wazuri ." (8:37).

Kwa hiyo aya hizo zinahukumia aya hizi mbili, kwani mwenye kuharibikiwa na amali yake ya heri, ni kuwa hana amali ya heri atakayoiona. Na juu ya mfano huu unaweza kukisia na kufahamu..

Utafiti Wa Hadith Katika Durril Manthur, ametoa Ibn Murdawayh na Bayhaqi kutoka jwa Anas bin Malik, kwamba Mtume(s.a.w.w) amesema: "Hakika Ardhi itatoa habari siku ya Kiyama kila lililofanywa juu ya mgongo wake, na akasoma Mtume(s.a.w.w) : "Itakapotetemeshwa ardhi huo mtetemeko wake" mapaka alipofikia: "Siku hiyo itatoa habari zake" akasema " Je, mnajua habari yake? Jibril amenijia akaniambia kuwa; kitakapokuwa Kiyama ardhi itatoa habari ya kila yaliyofanywa juu ya mgongo wake". Na imepokewa hadith ya mfano huo kwa Abu Huraira.

Ametoa Hussein bin Sufiani na Abu Naim kutoka kwa Shaddad bin Aus; amesema: Nimemsikia Mtume(s.a.w.w) akisema: "Enyi watu, hakika dunia ni maonyesho ya sasa hivi anakula mwema na muovo. Na hakika Akhera ni kiaga cha kweli, atahukumu huko Mfalme muweza, itathibiti haki na itabatilika batili, Enyi watu kuweni watoto wa akhera wala msiwe watoto wa dunia, kwani kila mtoto humfuata mama yake. Fanyeni amali kwa tahadhari. Jueni kwamba mtaonyeshwa amali zenu na mtakutana na Mwenyezi Mungu. Basi mwenye kufanya wema (hata) uzani wa sisimizi atauona na mwenye kufanya uovu (hata) uzani wa sisimizi atauona! Katika Tafsiri ya Qummi, kuhusu Aya Na 2, amesema: Mizigo ni watu. Na kuhusu aya 4-6 amesema: Yatakuja makundi ya waumin, makafiri na ya wanafiki ili waone matendo yao. Katika riwAya Na Abu Jarudi kutoka kwa Ab Jaffar(a.s) kuhusu Aya Na 7-8 anasema: Ikiwa mtu ni katika watu wa motoni na amefanya amali ya heri ya uzani wa sisimizi itakuwa ni majuto ikiwa ameifanya siyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na akiwa ni mtu wa peponi na amefanya amali ya shari ya uzani wa sisimizi, ataonyeshwa shari hiyo, kisha atasamehewa.

SURA ADIYAAT (FARASI) (NA. 100)

INA AYA 11

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema , Mwenye kurehemu.

وَالْعَادِيَاتِ ضَبْحًا ﴿١﴾

1. Naapa kwa farasi wanaokwenda mbio wakihema.

فَالْمُورِيَاتِ قَدْحًا ﴿٢﴾

2. Wanaotoa moto, kwa kupiga kwata.

فَالْمُغِيرَاتِ صُبْحًا ﴿٣﴾

3. Wanaowashambulia maadui ghafla wakati wa asubuhi.

فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا ﴿٤﴾

4. Wakatifua vumbi wakati huo.

فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا ﴿٥﴾

5. Wakaliingilia kati wakati huo kundi (la maadui).

إِنَّ الْإِنسَانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ ﴿٦﴾

6. Hakika mwanadamu ni mwenye utovu wa shukrani sana kwa Mola wake.

وَإِنَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ ﴿٧﴾

7. Na yeye ni shahidi wa hilo.

وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيدٌ ﴿٨﴾

8. Na hakika yeye kwa sababu ya kupenda mali ni bakhili.

أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِي الْقُبُورِ ﴿٩﴾

9. Je, hajuwi watakapofufuliwa waliomo makaburini.

وَحُصِّلَ مَا فِي الصُّدُورِ ﴿١٠﴾

10. Yakadhihirishwa yalipo nyoyoni.

إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّخَبِيرٌ ﴿١١﴾

11.Hakika Mola wao siku hiyo ni mjuzi mno wa hali zao.

UBAINIFU

Sura inataja ukanushaji wa mtu kwa neema ya Mola wake na kupenda kwake sana heri. Na yeye atahisabiwa juu ya hayo. Sura hii imeshuka Madina kwa ushahidi wa habari ya vita inayoelezwa katika Sura hiyo kwa mfano: "Naapa kwa farasi wa wapigania Jihadi"; kama yatakavyokuja maelezo yake. Na vita vya jihadi vilianza baada ya Hijra. (kuhama wa Mtume(s.a.w.w) . Hayo yanatiliwa nguvu na hadith zilizopokewa na Shia kutoka Maimamu wa Ahlul Bait kuwa, Sura hiyo ilishuka kwa ajili ya Ali(a.s) katika vita vya Salasil (Minyororo). Yatakuja maelezo yake katika utafiti wa hadith (Inshallah) kwa kufuatana na mapokezi ya Ahli Sunnah.

Aya Na 1

Mwenyezi Mungu anaapa kwa farasi wanaokwenda mbio wakihema; yaani wakitoa sauti ya pumzi mbele ya maadui na hali hiyo ni maarufu kwa farasi, ingawaje inadaiwa kuwa wanyama wengine wanayo. Maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu anaapa kwa jeshi lililo na farasi wa namna hiyo. Imesemwa kuwa makusudio yake ni ngamia wa mahujaji wanapokuwa Mina siku wa Nahr (ya kuchinja). Na pia imesemwa kuwa ni ngamia wa vita. Lakini aya zinazofuata hazionyeshi kuwa makusudio yake ni ngamia !

Aya Na 2

Yaani farasi wanaotoa moto kwa kupiga kwato katika mawe au ardhi ngumu. Imesemwa kuwa makusudio ya kuwasha moto hapa ni hila za wanaume katika vita. Na imesemwa kuwa ni kuwasha moto tu! Na pia imesemwa kuwa makusudio ni ndimi za wanaume zinazowasha moto kutokana na uzito wa yale wanayoyasema. Lakini njia zote hizo ni dhaifu kwa dhahiri kabisa.

Aya Na 3

Wanatajwa farasi kuwa ndiyo wenye kushambulia maadui kwa njia ya fumbo kwa maana ya wenye farasi hao.

Aya Na 4

Watawatimulia vumbi maadui kutokana na mashambulizi.

Aya Na 5

Yaani kuliingilia kati kundi la maadui. Imesemwa kuwa maana yake ni kuingia kati ngamia katika Mina siku ya Hijja. Lakini kuzifikiria aya zote tano kuwa na maana ya ngamia wa mahujaji wanaomiminika kwenda Mina, ni kinyume kabisa. Ilivyo hasa makusudio yake ni farasi wa vitani. Na mpangilio wa aya inayosema: (Wanaoshambulia maadui ghafla wakati wa asubuhi:) na (wakaingia katikati ya kundi), unafahamishwa kuwa Mwenyezi Mungu anaapa kwa farasi wa vita. Ne herufi fa katika aya nne, inafahamisha mpangilio wa kufuatana kila moja baada ya nyingine.

Aya Na 6

Ni jawabu ya Qasam (kiapo) inayotolea habari yale yaliyo katika tabia ya mtu, kama kufuata matamanio, kuyavamia na mambo ya dunia yanayokwisha na kuacha kumshukuru Mola wake juu ya alivyomneemesha. Inaonyesha aina ya watu wanaoshambuliwa. Inaonyesha kuwa makusudio ya kukanusha kwao, ni kukanusha neema ya uislamu aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu juu yao. Nayo ni neema kubwa waliyopewa na kutengeneza vizuri maisha yao ya dunia na wema wa maisha yao mengine ya milele.

Aya Na 7

Dhamira katika neno "na yeye" inamrudia mtu, kwa hiyo makusudio yanakuwa: mtu yeye mwenyewe anashuhudia juu ya kukanusha na kukufuru kwake. Kwa hiyo aya iko katika maana ya aya nyengine inayosema: "Bali mtu juu ya nafsi yake ni mwenye kushuhudia ". (75:14).

Na imesemwa kuwa dhamira inamrudia Mwenyezi Mungu, kwa maana kuwa yeye Mwenyezi Mungu ni shahidi. Lakini mpangilio wa dhamira hauliwafiki hilo.

Aya Na 8

Neno Khayr hapa limekuja kwa maana ya mali, yaani mtu kwa ajili ya kupenda sana mali anakuwa bakhili. Imesemwa kuwa makusudio yake ni hakika mtu ni mwingi wa kupenda mali na hilo linampelekea kujuzuwiya na kutoa haki ya Mwenyezi Mungu na kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Namna hii wamefasiri. Lakini hayo hayaweki mbali kuwa makusudio ya Khayr ni kheri ya aina yoyote. Na kwamba kupenda kheri ni maumbile ya kiutu, ndipo mtu anaona anasa za dunia ndio kheri, kwa hiyo zinamuingia na zinamsahauliza kumshukuru Mola wake.

Aya Na 9 – 10

Yaliyo katika nyoyo ni sifa ya imani au ukafiri, kama alivyosema Mwenyezi Mungu "Siku itakayofuniliwa siri ". (87:9).

Na maana kwa ujumla - na Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi - ni kuwa; hivi hajui mtu kuwa kwa sababu ya kukanusha kwake na kumkufuru kwake Mola wake atalipwa? Wakati watakapotolewa waliomo makaburini na kudhihirishwa siri za nafsi, miongoni mwa imani na kufuru na utii na uasi. Hakika Mola wao, siku hiyo ni mjuzi mno wa hali zao, kwa hiyo atawalipa.

Utafiti Wa Hadith Katika Majmau imesemwa kuwa; Mtume(s.a.w.w) alipeleka kikosi katika makao ya ukoo wa Kinana kikiongozwa na El-Mundir bin Amri El-Ansari mmoja wa Makamanda. Walipochelewa kurudi, Mwenyezi Mungu akampa khabari Mtume(s.a.w.w) kwa kusema: "Naapa kwa farasi wenye kwenda mbio wenye kuhema." Imesemwa kuwa Sura hii ilishuka wakati Mtume(s.a.w.w) alipompeleka Ali(a.s) kwa Dhatus-Salasil (Wenye Minyororo) na akawashinda. Na hilo ni baada ya kuwapeleka masahaba wengine mara nyingi. Wote wakarudi kwa Mtume bila ya kufaulu. Hadith hii imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah(a.s) katika hadith ndefu. Na vita hivyo viliitwa vya minyororo kwa sababu baadhi yao walitekwa, wakauawa na wakafungwa mateka kwa kamba za mikoni kama vile wamefungwa na nyororo.

Utafiti Wa Hadith Iliposhuka Sura hii Mtume(s.a.w.w) alitoka akawaswalisha watu swala ya asubuhi na akasoma katika swala Sura hiyo. Alipomaliza kuswali masahaba zake wakasema: "Sura hii haituijui", Mtume(s.a.w.w) akasema: "Ndio hakika Ali amewashinda maadui wa Mwenyezi Mungu na Jibrail amenifahamisha hilo usiku huu. Baada ya siku kidogo Ali akafika pamoja na ngawira na mateka kadhaa ."


24

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA QAARIA ( KIYAMA) (NA. 101)

INA AYA 11

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehemai, Mwenye kurehemu

الْقَارِعَةُ ﴿١﴾

1. Kiyama!

مَا الْقَارِعَةُ ﴿٢﴾

2. Ni nini Kiyama?

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْقَارِعَةُ ﴿٣﴾

3. Na nini lipi lakukujulisha ni nini Kiyama?

يَوْمَ يَكُونُ النَّاسُ كَالْفَرَاشِ الْمَبْثُوثِ ﴿٤﴾

4. Ni siku ambayo watu watakuwa kama panzi waliotawanywa.

وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ الْمَنفُوشِ ﴿٥﴾

5. Na yakawa majabali kama sufi iliyopurwa.

فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ ﴿٦﴾

6. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito.

فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٧﴾

7. Yeye atakuwa katika maisha yenye kuridhiwa.

وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ ﴿٨﴾

8. Na yule ambaye mizani yake itakuwa nyepesi.

فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ ﴿٩﴾

9. Basi makaza yake yatakuwa ni Hawiya.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا هِيَهْ ﴿١٠﴾

10. Na ni lipi la kujulisha wewe nini hiyo ( Hawiya).

نَارٌ حَامِيَةٌ ﴿١١﴾

11. (Hawiya) ni moto uliomkali mno.

UBAINIFU

Sura hii inatoa onyo juu ya Kiyama.Imeshuka Makka.

Aya Ya 1-3

Neno Qari'ah linatokana na Qur'u lenye maana ya kugonga sana, nalo ni mojawapo katika majina ya Kiyama. Imesemwa kuwa Kiyama kimeitwa hivyo, kwa sababu kinagonga nyoyo fazaa na kinawagonga maadui wa Mwenyezi Mungu kwa adhabu.

Aya Ya 4

Yaani siku hiyo ya Kiyama watu watakuwa kama panzi waliotapanyika, kutokana na mfazaiko. Imesemwa kuwa watu siku ya kufufuliwa wamefananishwa na panzi, kwa vile panzi wanaporuka hawaeleki upande mmoja kama desturi ya ndege wengine. Bsi vile vile watu watakapotoka makaburini mwao watakuwa wameshikwa na fazaa; wataelekea pande mbali mbali; au wataelekea sehemu zao mbalimbali za uovu au wema.

Aya Ya 5-7

Inaashiria juu ya uzani wa amal ( Matendo); kwamba kuna matendo mazito ambayo yana daraja mbele ya Mwenyezi Mungu nayo ni iman na twaa (Utii) na kuna yale ambayo hayana uzani wowote nayo ni kufuru na uasi. Kwa hiyo mwenye kuwa na amali zenye uzani uzito atakuwa katika maisha atakayoyaridhia.

Aya Ya 8

Neno Hawiya lenye maana ya kuporomoka ni mojawapo ya majina ya Jahannam; imeitwa hivyo kwa vile mtu atakayeingizwa humo ataporomoka hadi chini ya waliochini; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Kisha tukamrudisha chini ya waliochini, ila wale walioamini "(95:5-6)".

Kuusifu moto kwa neno Hawiya ni fumbo kama fumbo la kuyasifu maisha ya kuridhiwa kuileta ibara ya makazi kwa neno Ummu lenye maana ya mama, ni kwa sababu ndiyo marejeo ya huyo mwenye uzani mwepesi, kama anavyorejea mtoto kwa mama yake. Imesemwa kuwa makusudio ya Ummu ni Ummur- ra'as yaani fuvu la kichwa chake, kwa maana yakuwa ataangukia kichwa chake katika Jahannam, lakini kauli inawekwa mbali na kubakia dhamiri bila ya mahali inapoashiria katika neno Maahiya inayofasiriwa na aya 11.

Aya Ya 10

Jumla hiyo ni kulifanya kubwa jambo la huo moto.

Aya Ya 11

Moto mkali, yaani wenye kuchomwa sana. Na hilo ni jawabu na tafsiri ya aya 1.

Utafiti Wa Hadith Katika Tafsri ya Qummi katika neno lake Mwenyezi Mungu " Na yule ambaye mizani yake itakuwa nyepesi". Yaani wepesi katika mambo mema. Na kuhusu Ummu amesema ni fuvu la kichwa chake yaani atatupwa katika Jahannam kichwa- kichwa.

Katika Durril Manthur ametoa Ibn Murdawayah kutoka kwa Abu Ayyub El- Ansari, kwamaba Mtume(s.a.w.w) amesema: " Hakika nafsi ya muumin inapochukuliwa hukutana na watu wa rehema katika waja wa Mwenyezi Mungu na watu wema kutoka duniani; watasema: Mwaangalieni mwenzenu anastarehe kwani yeye alikuwa katika mashaka makubwa; kisha watamuuliza: fulani na fulani wamefanya nini? Je Fulani ameolewa? Na watakapomuulizia mtu aliyekufa kabla yake, atasema: huyo amekufa kabla yangu. Halafu watasema: " Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea. Amekwishapelekwa kwenye makazi yake ya Hawiya, ni makazi mabaya na malezi mabaya." Na imepokewa hadith kwa maana haya kutoka kwa Anas bin Malik, na kutoka kwa Hassan na Ash'ath bin Abdalla Ama.

SURA TAKATHUR ( KUTAKA WINGI WA MALI) (NA. 102)

INA AYA 8

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ ﴿١﴾

1. Kumewashughulisha mno kutaka wingi wa mali.

حَتَّىٰ زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ ﴿٢﴾

2. Mpaka mzuru makaburi.

كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣﴾

3. Komeni! Hapo mtajua.

ثُمَّ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٤﴾

4. Kisha komeni! Hapo mtajua.

كَلَّا لَوْ تَعْلَمُونَ عِلْمَ الْيَقِينِ ﴿٥﴾

5. Si hivyo! lau mngejua ujuzi wa yakini (msinge jishughulisha na hayo).

لَتَرَوُنَّ الْجَحِيمَ ﴿٦﴾

6. Hakika mtauona moto.

ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيْنَ الْيَقِينِ ﴿٧﴾

7. Kisha mtauona kwa jicho la yakini.

ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ ﴿٨﴾

8. Lisha mtaulizwa siku hiyo matumizi ya neema mlizopewa.

UBAINIFU

Makaripio makubwa kwa watu kutokana na kujishughulisha kwao kwa wingi wa mali na watoto na kusahau mambo yanayofuatia miongoni mwa hasara na adhabu. Vile vile ni utisho kwamba wao watajua, wataona adhabu na kuulizwa neema waliyopewa ili washukuru, lakini wakabadilisha neema hiyo kuwa kufuru. Sura hii uinaweza kuwa imeshuka Makka au Madina Maelezo zaidi yatakuja katika utafiti wa hadithi kuhusu sababu za kushuka kwake, (Inshallah).

Aya Ya 1-2

Maana ya aya hizi mzunguko ni kuwa: mmeshughulika sana na kuzama katika starehe za dunia na vipambo vyake na kushindana katika wingi wa vitu, jambo ambalo limewafanya muache jambo muhimu la kumtaja Mwenyezi Mungu, mpaka mkafikiwa na kifo. Kughafilika kwenu kumewatia upofu katika maisha yenu yote. Imesemwa kuwa maana yake ni kuwa kumewashughulisha nyinyi kujifaharisha kwa wingi wa watu. Hawa wanasema "Sisi tuna watu wengi zaidi". Na wengine wanasema "Sisi tuna watu wengi hata mlipomaliza kuhisabu waliohai mkaenda makaburini kuwahesabu waliokufa katika watu wenu. Hivyo basi mkashindana pia kuwahisabu wafu wenu".

Maana haya ndiyo yaliyoko katika mpangilio wa yale yaliyopokewa kuhusu sababu za kushuka Sura hii, kwamba makabila mawili katika Ansar yalijifakharisha waliohai na waliokufa. Katika baadhi ya yaliyopokewa ni kwamba hayo yalikuwa Makka kati ya Abdu Manaaf na Bani Sahm. Kitakuja kisa chake katika utafiti wa hadithi (Inshallah).

Aya Ya 3

Makemeo na vitisho kutokana na kujishughulisha na mambo yasiyokuwa na umuhimu wowote.

Aya Ya 4

Kusisitiza yale yaliyotangulia katika aya ya 3. Imesemwa kuwa makusudio ya aya ya 3 ni kwamba watayojua hayo wakati wa kufa, na aya ya 4 kuwa watayajua wakati wa kufufuliwa.

Aya Ya 5

Makemeo baada ya makemeo, kwa kusisitiza. Na 'yakini' ni elimu ambayo haina shaka yoyote. Jawabu la 'Lau' limeondolewa, ambalo makadirio yake ni "Lau mngejua ujuzi wa yakini msingejishughulisha na hayo".

Aya Ya 6

Ni jumla nyengine inayoanza, na wala siyo jawabu la lau ya aya ya 5. Makusudio yake ni kuuona moto kwa moyo kabla ya kuuona kwa macho siku ya Kiyama, kutokana na inavyoonyesha katika neno lake Mwenyezi Mungu: "Na utadhihirishwa moto kwa mwenye kuona ". (79:36).

Aya Ya 7

Makusudio yake ni kuona kabisa kwa macho siku ya Kiyama, kutokana na dalili ya aya ya mbele (Kisha ataulizwa siku hiyo neema zote). Kuna kauli zinazosema: Kuuona kwa kwanza ni kabla ya kuuingia moto na kuuona kwa pili ni baada ya kuuingia. Kauli nyengine inasema, kwanza ni kuujua huo moto na pili ni kuuona. Na imesemwa makusudio yake ni kuuona baada ya kuuona, kwa kuonyesha kuendelea na kudumu. Na mengine zaidi ya hayo yamesemwa.

Aya Ya 8

Mzunguko wote wa maneno, unaonyesha kuwa maneno haya yanaelekezwa kwa watu wote wale ambao neema za Mwenyezi Mungu zimewafanya wamsahau Mwenyezi Mungu. Na binadamu ni mwenye kuulizwa juu ya neema zote alizopewa na Mwenyezi Mungu. Neema-Jambo ambalo linamuafiki yule mwenye kuneemeshwa na kumpa heri na manufaa-inakuwa neema kulingana na yule mwenye kuneemeshwa anavyoitumia. Kinyume cha hivyo, basi itakua ni balaa, ijapokuwa yenyewe nineema. Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemuumba mtu na akajaalia makusudio ya kumuumba kwake, ni kumuabudu. Kama alivyosema: "Sikuumba majini na watu ila waniabudu " (51:56).

Huo ndio utawala wa Mungu kwa mja wake, na Mwenyezi Mungu amemuandalia huyo mja wake, kila linalomnufaisha katika kulifikia lengo ambalo amemuumbia kwalo.

Kwa hivyo kuitumia neema hii katika njia anayoiridhia Mwenyezi Mungu na itakayomfikisha mtu kwenye lengo lake analolitaka, ndiyo njia ya kufikia lengo muhimu ambalo ni twaa (Utii). Kuitumia neema kinyume cha anavyoridhia Mwenyezi Mungu na kusahau lengo lake, ni upotevu na kukosa kulifikia lengo. Mwenyezi Mungu amekwishatoa hukumu ambayo haibadilishwi, kuwa mtu atarudi kwake na kumuuliza juu ya amali (matendo) yake, kisha amuhisabie na kumlipa. Matendo (amali) yake ni matumizi ya neema ya Mwenyezi Mungu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na kwamba mtu hatapata isipokuwa yale aliyoyatenda. Na kwamba matendo yake yataonekana. Kisha atalipwa malipo yaliyo kamili. Na kwamba mwisho (wa kila jambo) unarejea kwa Mola wako ." (53:39-42).

Utafiti Wa Hadithi Katika Majmau imesemwa kuwa Sura hii ilishuka kwa Mayahudi waliosema: "Sisi ni wengi zaidi kuliko ukoo fulani". Na ukoo fulani ni zaidi ya ukoo fulani". Wengine wamesema kuwa ilishuka kwa makabila mawili katika Ansar walipojifaharisha, na imesemwa kuwa imeshuka kwa Maquraish ukoo wa Abdu Manaaf bin Quswai na wa Sahm bin Amr wakajifaharisha na wakahesabu watukufu wao, Abdu Manaaf wakawa wengi. Kisha wakasema twendeni makaburini, tuwahisabu wafu wetu. Wakawa wengi ukoo wa Sahm, kwa sababu wao walikuwa wengi wakati wa ujahili. Katika Tafsiri ya Bur'han kutoka kwa Barqi kutoka kwa baba yake kutoka kwa Ibn Abu Umayr, kutoka kwa Hisham bin Salim naye kutoka kwa Abu Abdillahi, kuhusu neno la Mwenyezi Mungu "Lau mngelijua kujua kwa yakini". Amesema: Nikuona kwa macho. Na riwaya hii inatilia nguvu yale tuliyotangulia kuyaeleza katika maana ya aya". Katika Tafsiri ya Qummi kwa isnadi yake kutoka kwa Jamil naye kutoka kwa Abu Abdillahi(a.s) amesema: "Nilimwambia kuhusu mtaulizwa siku hiyo neema zote" akasema: "Utaulizwa uma huu juu ya neema aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kisha kwa Ahlul Bayt wa Mtume(s.a.w.w) .

Katika Kafi kwa isnadi yake kutoka kwa Abu Khalid El-Kabili amesema: "Nilliingia kwa Abu Jafar(a.s) akaniita chakula cha mchana nikala pamoja naye chakula ambacho sijapata kukila kwa uzuri wake. Tulipomaliza kula akasema: "Ewe Abu Khalid umekionaje chakula chetu?" Nikasema, "Sijakula chakula kizuri na kisafi kama hicho, lakini nimekumbuka aya ambayo iko katika kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t) inayosema: "Kisha mtaulizwa siku hiyo neema zote". Abu Jaffar akasema: "Hakika mtaulizwa yale mliyo na haki nayo ".

Katika hiyo hiyo Kafi kutoka kwa Abu Hamza amesema: "Tulikuwa kundi kwa Abu Abdillahi(a.s) akatuita chakula ambacho hatujapata kuona mfano wake, kutokana na ladha yake na kupendeza kwake, na akatuletea tende zilizo nzuri na safi, mtu mmoja akasema: "Mtaulizwa neema hii mliyoneemeshwa nyumbani kwa mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema Abu Abdillahi(a.s) : Hakika Mwenyezi Mungu ni mkarimu sana, hawezi kuwalisha chakula kisha awaulize, isipokua atawauliza neema aliyowaneemesha kwa Muhammad na kizazi cha Muhammad(s.a.w.w) ." Zimepokewa riwaya zenye maana haya kwa njia nyengine na ibara zenya kukhitalifiana. Baadhi ya riwaya zinasema kwamba neema ni wilaya (Utawala) wa Ahlul Bait wa Mtume na imetafsiriwa, kuwa ni neema zote alizozineemesha Mwenyezi Mungu.

Ubainifu wa hayo, ni kwamba neema hiyo sio kuwa itaulizwa kama kitu kwa mfano nyama, mkate, tende au maji baridi. Au kwamba neema hiyo ni usikizi, uoni, mkono au mguu. Hapana sio hivyo; isipokuwa itaulizwa neema ambayo Mwenyezi Mungu amemuumbia mtu, kama ameitumia katika njia ya ukamilifu wake na kupata ukaribisho na ibada, na akahimiza kuitumia kwa kushukuru, sio kuikufuru. Neema itaulizwa vipi ilivyotumiwa? Inayoelezea jinsi ya kutumia neema, ni dini aliyokuja nayo Mtume(s.a.w.w) na kuusimamisha ubainifu wake, na maimamu kutoka katika Ahlul Bayt wake Mtume.

Kwa hiyo kuulizwa neema, maana yake ni kuulizwa amali ya dini katika harakati zote. Na kuulizwa juu ya Mtume(s.a.w.w) na Maimamu walio baada yake ambao amewajibisha Mwenyezi Mungu kuwatii na akawajibisha kuwafuata katika njia ya kumuendea yeye Mwenyezi Mungu, ambayo njia yenyewe nu kuitumia neema kama ilivyobainishwa na Maimamu. Kuulizwa neema maana yake ni kuulizwa dini, kunaonyeshwa na riwaya ya Abu Khalid inayosema: "Hakika mtaulizwa yale mliyo na haki nayo". Kuulizwa dini maana yake ni kuulizwa juu ya Mtume na Ahlul Bayt wake, hili linaonyeshwa na riwaya mbili za Jamil na Abu Hamza zinazosema. "Atauliza Mwenyezi Mungu umma huu juu ya alivyowaneemesha kwa Mtume wake na Ahlul Bait wake".

Kuna baadhi ya riwaya zinazosema neema ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa watu wa ulimwengu kuwaokoa na upotevu. Na neema ni utawala wa Ahlul Bait, na utawala wa Ahlul Bait, unawajibisha kuwatii na kuwafuata katika ibada. Katika Majmau, imesemwa kuwa neema ni uzima na wasaa juu ya marifa. Riwaya hii inasaidiwa na riwaya iliyopokewa na Ibn Abbas kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) amesema: "Watu wengi wamehadaiwa na neema mbili, uzima na wasaa".

Katika hiyo hiyo Majmau imesemwa kuwa neema ni amani na uzima. Riwaya hii imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Masud na Mujahid. Katika riwaya nyingine kutoka katika njia ya Ahli Sunnah zinasema: "Neema ni tende, maji baridi, nk. Na katika hadithi nyingine kutoka katika njia hiyo hiyo ya Sunni inasema: "Mambo matatu hataulizwa mtu; kitambaa kinachousitiri uchi wake, kipande cha tonge kinachozuiya njaa yake au nyumba inayomsitiri joto na baridi". Na Mwenyezi Mungu ndie mjuzi zaidi.

SURA ASR (ZAMA) (NA. 103)

INA AYA 3

Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

وَالْعَصْرِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa zama.

إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ ﴿٢﴾

2. Hakika mwanadamu yumo katika hasara.

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ ﴿٣﴾

3. Ila wale ambao wameamini wakatenda amali (matendo) njema, wakausiana (kushikamana na) haki, wakausiaana kusubiri.

UBAINIFU

Sura hii Muhtasari wa maarifa yote ya Kiqur'an na imekusanya makusudio ya Qur'an kwa maelezo mafupi (Muhtasar). Sura hii inawezekana kwa imeshuka Makka na Madina, lakini inavyoelekea imeshuka Makka.

Aya Ya 1

Ni kuapa kwa majira maalum. Na hii ndiyo tafsiri nzuri, kwa vile aya mbili zinazofuatia, zimejumlisha watu wote wa ulimwengu katika kupata hasara, isipokuwa wale waliofuata ukweli na wakasubiri. Sifa hizo ni za waumini wanaofanya mema. Hivyo makusudio ya majira (asr) yanakuwa ni zama za Mtume(s.a.w.w) ambazo ni zama za kutokeza Uislamu kwa jamii ya watu na kudhihiri haki juu ya batili. Inasemekana pia kuwa makusudio ya Asr hapa ni wakati wa Alasiri ambao ni sehemu ya mwisho katika mchana, kwa kufahamisha mipangilio ya Mungu kwa kuchwa jua na kuja usiku pamoja na kuondoka ufalme wa jua. Na imesemwa kuwa makusudio ya Asr hapa ni swala ya Alasiri ambayo ni swala katikakati na ni bora katika swala za faradhi za kila siku.

Pia inasemeka makusido ya Asr ni usiku na mchana, na imesemwa kuwa makusudio ni zama ndefu za maisha kutokana na matukio ya kiajabu yanayofahamisha uwezo wa Mungu nk Imepokewa kutoka katika baadhi ya riwaya kwamba makusudio yake ni zama za kudhiri Mahdi(a.s) kwa kutumia kudhihiri haki juu ya batili.

Aya Ya 2

Yaani hasara ya kupungua raslimali ya mtu.

Aya Ya 3

Mwenyezi Mungu anawatoa katika hasara wale wenye kuvaana na imani na matendo mema, hao ni wenye kusalimika na hasara. Hapa kitabu cha Mwenyezi Mungu kinabainisha kuwa mtu anayo maisha ya milele ambayo hayakatiki kwa kifo, bali kifo ni kugura kutoka ulimwengu mmoja mpaka ulimwengu mwengine, kama alivyosema Mwenyezi Mungu "(Hatutashindwa) kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyingi katika umbo (jengine) msilolijua ".(56:61).

Qur'an inabainisha kwamba sehemu ya maisha hayo ambayo ni maisha ya dunia ni mtihani wa sehemu ya mwisho ya maisha ambayo ni akhera ya milele; kuwa yatakuwa mazuri au mabaya anasema Mwenyezi Mungu: "Na uhai wa dunia kwa mkabala wa akhera si kitu isipokuwa ni starehe ndogo tu ".(13:26).

Na amesema tena: "Kila nafsi itaonja mauti, na tuna kufanyieni mitihani kwa (mambo ya) shari na ya kheri, na kwetu (nyote) mtarejea " (21:35).

Vile vile inabainisha kwamba kitu cha kukitanguliza katika maisha haya ya dunia kwa ajli ya maisha ya akhera ni itikadi na vitendo. Kwa hiyo itikadi ya kweli na amali njema ndivyo vyenye kumiliki wema wa akhera, na ukafiri na ufasiki utasababisha uovu akhera. Mwenyezi Mungu amesema: "Na kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyatenda. Na kwamba matendo yake yataonekana. Kisha atalipwa malipo yaliyo kamili ." (41:39-41)

Amesema tena: "Anayekufuru, (madhara) ya kufuru yake ni juu yake (mwenyewe); na wafanyao mema (hao) wanazitengeza nafsi zao ".(44:46). Kwa hali hiyo basi, imebainika kwamba uhai wa dunia ni rasilimali ya mtu, anachuma yale atakayoishi nayo katika maisha ya akhera. Kama akifuata haki katika itikadi na amal (vitendo) basi amepata faida katika biashara yake, amebarikiwa katika chumo lake na amesalimika na shari katika mustakabali wake. Kama akiifuata batili na akaacha imani na matendo mema, basi biashara yake itakuwa na hasara na atazuiliwa heri katika mwisho wake. Hilo ndilo neno lake Mwenyezi Mungu. " Hakika wanadamu wote wako katika hasara, isipokuwa wale ambao wameamini na wakatenda amali njema". Makusudio ya imani, ni kuamini Mwenyezi Mungu na miongoni mwa mambo ya kumuamini Mwenyezi Mungu ni kuamini Mitume yako yote na kuamini siku ya mwisho.

Mwenyezi Mungu ameeleza katika Sura ya (4:150-151), kuwa yule asiyeamini baadhi ya Mitume yake au siku ya mwisho, basi sio muumin. Kukusiana (kushikamana na) haki na kuusiana kusubiri, ni kuusiana watu kushika hiyo haki, kuifuata na kudumu nayo. Dini ya kweli haiwi isipokuwa kwa kuifuata haki kwa itikadi na vitendo. Na kuusiana kushikamana na haki ni kukubwa zaidi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya, kwa sababu kunakusanya itikadi na kuhimiza amali njema.

Kisha kuusiana haki na katika amali njema, na kumetajwa baada ya amali njema kutokana na umuhimu wake. Na kuusiana kusubiri ni katika kuusiana haki, limetajwa neno kuusiana mara mbili kwa ajili ya kusisitiza. Kumetajwa kuusiana baada ya kutajwa iman na amali njema, kwa kuashiria kwanza kwenye uhai wa nyoyo zao na kukunjuka nyoyo zao kwa Uislamu, kisha kuieneza haki hiyo kwa watu wote. Subira imeelezwa kwa ujumla, kama kusubiri juu ya kumtii Mungu, kusubiri juu ya kuacha maasai na kusubiri juu ya misiba inayompata kwa kadari ya Mungu.

Utafiti Wa Hadithi Katka Tafsri ya Qummi kwa isnadu yake kutoka kwa Abdurrahman bin Kathiyr naye amepokea kutoka kwa Abu Abdillahi(a.s) katika neno lake Mwenyezi Mungu "Ila wale ambao wameamini" amewavua Mwenyezi Mungu watu wa ikhlas katika viumbe vyake. Katika Durril Manthur, ametoa Ibn Murdawayh, kutoka kwa Ibn Abbas kuhusu neno lake Mwenyezi Mungu: "Hakika wanadamu wote wako katika hasara" anakusudia Abu Jahl bin Hisham. Na kuhusu "Ila wale ambao wameamini na wakatenda mambo mema" ametajwa Ali na Salman.


25

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA HUMAZA (MRAMBA KISOGO) (NA. 104)

INA AYA 9

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ﴿١﴾

1. Ole wake kila anyeramba kisogo, anayesengenya.

الَّذِي جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُ ﴿٢﴾

2. Ambaye amekusanya mali na kuyahesabu.

يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُ أَخْلَدَهُ ﴿٣﴾

3. Anadhani kwamba mali yake itambakisha milele.

كَلَّا لَيُنبَذَنَّ فِي الْحُطَمَةِ ﴿٤﴾

4. Na akome! Atatupwa katika Hutama!

مَا أَدْرَاكَ مَا الْحُطَمَةُ ﴿٥﴾

5. Na ni lipi la kukujulisha nini hiyo Hutama?

نَارُ اللَّـهِ الْمُوقَدَةُ ﴿٦﴾

6. Ni moto wa Allah uliowashwa.

الَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى الْأَفْئِدَةِ ﴿٧﴾

7. Ambao hupanda mpaka nyoyoni.

إِنَّهَا عَلَيْهِم مُّؤْصَدَةٌ ﴿٨﴾

8. Hakika (Moto) huo utafungiwa juu yao.

فِي عَمَدٍ مُّمَدَّدَةٍ ﴿٩﴾

9. Kwa magogo marefu marefu.

UBAINIFU

Sura hii inatoa makamio makali ya Mwenyezi Mungu kwa wale wenye kuzama katika kukusanya mali, wakajifanya juu kuliko watu wengine, wakatakabari na kuwaaibisha wenzao. Sura hii imeshuka Makka.

Aya Ya 1

Amesema katika Majmau: "Neno Humaza lina maana ya mwingi wa kuwaaibisha na kuwashutumu wengine kwa mambo wasiyokuwa nayo. Asili ya neno hilo ni kuvunja na humaza ni aibu. Vile vile amesema kwamba humaza na lumaza ni kwa maana moja. Lakini imesemwa kuwa kuna tofauti kati ya maneno hayo mawili, humaza ni yule anayeaibisha mtu akiwa hayupo na lumaza ni yule anayeaibisha mtu mbele yake. Pia imesemwa kuwa humaza ni yule anayemuudhi mtu aliekaa naye kwa maneno mabaya na lumaza ni yule anaye mvunjia macho mtu aliyekaa naye huku akiashiria kwa macho yake na kichwa chake. Kwa hiyo maana kamili ya aya ni: "Ole wake kila anaewatia aibu watu sana, mwenye kusengenya sana." Wengine wamefasiri kwa maana nyengine kulingana na tafsiri zao.

Aya Ya 2

Ni ubainifu wa yule mwenye kuramba kisogo mwenye kusengenya. Pia ni ubainifu wakuidunisha mali. Kwani mali ijapokuwa nyingi kiasi gani, haiwezi kumfaa mwenye kuwa nayo na kitu chochote zaidi ya matumizi ya nafsi ya kitabia, kama vile kula, kunywa, nk. Neno Addadah lina maana ya hesabu yaani kwa sababu ya kuipenda mali sana, basi anaikusanya na kuihesabu mara kwa mara huku akifurahiwa wa wingi wake. Na imesemwa kuwa maana yake ni kuirundika mali, kwa kutaraji itamfaa wakati wa shida (akiba).

Aya Ya 3

Yaani anafikiria kuwa mali yake hiyo itamzuia kufa? Mtu huyu kwa sababu ya kutaka kuishi kwake katika ardhi, na kuzama kwake katika tama ndefu, hakinai na mali ambayo inamuondoshea haja za maisha yake mafupi na siku zake zenye kuhesabiwa, bali kadiri mali inavyozidi ndivyo anavyozidi kuwa na tamaa isiyokua na mwisho. Hivyo hali yake inaonyesha kwamba yeye anaona kua hiyo mali itambakisha ulimwenguni. Na kwa sababu ya mapenzi yake ya kitabia ya kutaka kubaki, basi anajishughulisha na kuikusanya mali na kuihesabu. Baada ya kuipata hiyo mali na kujiona tajiri, anajifanya mkubwa mbele za watu kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Hakika mwanadamu hupetuka mpaka, kwa vile kujiona ametajirika." Na kiburi hicho ndicho kinachomfanya arambe visogo vya watu.

Neno akhladah limekuja kwa njia ya muda uliopita lakini hapa lina maana ya muda ujao kutokana na kukutana na neno yahsabu ambalo ni la muda ujao.

Aya Ya 4

Inapinga fikra za kudhania kudumu milele kwa mali. Neno hutama hapa limekuja kwa maana ya kula. Na hiyo hutama ni moja kati ya majina ya moto kama inavyo fasiriwa na aya ya 6. Yaani ayah hii inakusudia kusema kwa: Mtu huyo hataweza kubakishwa milele na mali, bali atakufa kisha atupwe katika Hutama.

Aya Ya 5

Ni utisho na kulifanya kubwa jambo.

Aya Ya 6

Ni kwa ajili ya kulifanya kubwa jambo na kuogopesha.

Aya Ya 7

Moto huo utatokeza kwenye nyoyo, kwa vile moyo ndiyo msingi wa utambuzi wa mtu na fikra yake nao ndiyo nafsi ya kiutu. Inaelekea kuwa makusudio ya kutokeza juu ya nyoyo, ni kwamba unamchoma banadamu ndani na nje alvyosema Mwenyezi Mungu: "Kuni zake ni watu na mawe ." (2:24).

Aya Ya 8

Yaani moto huo utatiwa komeo amabyo hawataweza kutoka wala kuokoka.

Aya Ya 9

Maguzo marefu; Imesemwa kuwa ni maguzo ambayo yatakua ni komeo ya moto. Pia imesemwa kuwa ni miti ambayo watafungiwa watu wa motoni kama ile miti inayofungiwa wezi. Na yamesemwa zaidi ya hayo.

Utafiti Wa Hadithi Katika Ruwhel Maani kuhusu aya ya 1 kutokana na alivyotoa Ibn Hatim kutoka katika njia ya Ibn Ishaq kutoka kwa Athman bin Umar, kwamba imeshuka juu ya Ubayya bin Khalaf. Na kutokana na aliyo yatoa Sudiyy, kuwa imeshuka juu ya Ubayya bin Amru El-Thaqafi, mashuhuri kwa jina la Akhnas bin Shariq, kwani yeye alikuwa akimsengenya Mtume katika matukio mengi. Na kutokana na yale aliyoyasema Ibn Ishaq kuwa imeshuka kwa Umayya bin Khalaf El-Jamhi ambaye alikuwa akimramba kisogo Mtume(s.a.w.w) .

Kutokana na aliyotoa Ibn Jariyr na wengineo kutoka kwa Mujahid, ni kwamba ayah ii imeshuka juu ya Jamil bin Amir, na imesemwa pengine, kwamba imeshuka juu ya Walid bin Mughirah kwa kumsengenya kwame Mtume(s.a.w.w) na pia imesemwa kuwa imeshuka kwa Asi bin Wail. Kisha amesema katika hiyo Ruwhel Maani kuwa inawezekana kuwa imeshuka kwa wote hao waliotajwa. Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu aya ya 1 amesema ni yule ambaye anawakonyeza watu na kuwadharau mafakiri. Kuhusu neno humaza ni yule ambaye anageuza shingo yake na kichwa chake (anabeza) na anachukia anapomuona fukara au muombaji.

Kuhusu aya ya 2 ni yule aliyeiandaa mali na kuiweka. Katika Majmau amepokea Iyashi kwa isnadi yake kutoka kwa Muhammad bin Annu'man El-Ahwal, naye kutoka kwa Hamran bin aa'yan naye kutoka kwa Abu Jaffar (AS) amesema: "Hakika makafiri na washirikina watawaaibisha watu wa Tawhid katika moto huku wakisema: "Tunaona Tawhid yenu haiwafai chochote, nyinyi na sisi tuko sawa tu!" Basi hapo Mwenyezi Mungu atawatoa aibu kwa kuwaambia Malaika: "Waombeeni". Nao watawaombea. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawambia Mitume: "Waombeeni" Mitume nao watawaombea. Tena Mwenyezi Mungu atawaambia waumini, "Waombeeni" basi waumini watawaombea Mwenyezi Mungu atasema: "mimi ni Mwingi wa rehema wenye kurehemu, tokeni kwa Rehema Yangu." Ndiyo watatoka kama wanavyotoka panzi; kasha itavutwa nguzo na wale watu wa motoni watatiliwa komeo kama walivyokuwa".

SURA FIL (NDOVU) (NA.105)

INA AYA 5

Kwa jina ya Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَابِ الْفِيلِ ﴿١﴾

1. Je, hukujua jinsi Mola wako alivyowafanya wenye ndovu?

أَلَمْ يَجْعَلْ كَيْدَهُمْ فِي تَضْلِيلٍ ﴿٢﴾

2. Je, hakukifanya kitimbi chao nichenye kupotea bure?

وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ ﴿٣﴾

3. Akawepelekea ndege makundi makundi.

تَرْمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ ﴿٤﴾

4. Wakiwatupia kwa mawe ya udongo mkavu.

فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍ مَّأْكُولٍ ﴿٥﴾

5. Akawafanya kama ganda tupu lililoliwa ( kokwa yake)

UBAINIFU

Sura hii inaeleza kisa cha watu wenye ndovu, walipokwenda Makka, ili kuharibu Al-Ka'aba tukufu, lakini Mwenyezi Mungu akawaangamiza kwa kuwapelekea makundi ya ndege. Kisa hicho kilichowazi ni katika alama ya Mwenyezi Mungu. Na Majahili walikitaja katika Sura hii imeshuka Makka.

Aya Na 1

Neno Alamtara hapa lina maana ya kujua kuliko dhahir, kwa maana ya kuwa, je hukujua namna gani alivyowafanya Mola wako watu wenye ndovu? Tukio hili lilikuwa mwaka aliozaliwa Mtume(s.a.w.w) .

Aya Na 2

Makusudio ya vitimbi vyao ni makusudio yao mabAya Na kwenda Makka kutaka kuivunja nyumba tukufu (Al-Ka'aba), lakini vitimbi vyao vilipotea bure. Walikwenda kwa ajili ya kuivunja Al-Ka'aba, wakaishilia kuangamia wao wenywe.

Aya Na 3 -4

Neno Ababil lina maana ya makundi makundi, yaani Mwenyezi Mungu aliwapeleka hao waliotaka kuivunja Al-Ka'aba makundi ya ndege, waliowatupia mawe.

Aya Na 5

Asf ni jani la mmea ambao mbegu yake imeliwa, au ganda tupu la tembe ambayo imeliwa kokwa yake. Yaani wao walirudi kuwa viwiliwili bila ya roho, au kwamba vile vijiwe kutokana na joto lake, viliunguza miili yao kwa ndani. Imesemwa kuwa makusudio yake ni majani yaliyoliwa na wadudu. Na imefasiriwa aya hii baadhi ya njia ambazo hazilingani na fasihi ya Qur'an.

Utafiti Wa Hadithi Katika Majmau wapokezi wamesema mfalme wa Yemen ambaye alikusudua kuivunja Al-Ka'aba ni Abraha bin Assabahi El-Ashram, na inasemekana alikuwa akijulikana zaidi kwa jina la "Abu Yaksum". Imenukuliwa kutoka kwa Waqidi kuwa yeye ni babu wa Mfalme Najashi aliyekuwa katika zama za Mtume(s.a.w.w) . Kisa kinaendelea kueleza kuwa huyo mfalme alijenga Ka'aba huko Yemen akaweka makuba ya dhahabu, na akaamrisha watu wa mamlaka yake kuhiji hapo, kwa kuifananisha na ile ya Makka.

Mtu mmoja katika Bani Kinana, alikwenda Yemen akaangalia jingo hilo, kisha akaenda kunya humo ndani. Abraha alipoingia na kukuta uchafu huo , alisema: Ni nani aliyenionyesha jeuri hii? Ninaapa kwa Ukristo wangu nitaivunja ile Al-Ka'aba yao ili wasiende tena watu kuhiji milele". Basi akaitisha ndovu na akatoka pamoja wa wafuasi wake katika watu wa Yemen. Wafuasi wake zaidi walikuwa ni makabila ya Akka, Ash-Aruun na Khath'am. Alipokuwa njiani, akamtuma mtu mmoja katika Bani Salim, ili awalinganie watu kwenda kuhiji nyumba yake aliyoijenga. Basi huyo mjumbe akakutana na mtu mwengine kutoka katika Bani Kinana akauliwa. Hilo likamzidisha mori zaidi wa kwenda.

Alipofika Taif, akawaomba wampatie muonyeshaji njia, wakampatia mtu mmoja katika ukoo wa Hudhayl anayeitwa Nufayl. Akawa anawaongoza mpaka walipofika Maghmas maili 6 kutoka Makka, wakatua, kisha wakapeleka watangulizi. Maquraish wakatoka makundi wakasema : Hatuna nguvu za kukabiliana na watu hawa, " hakubaki hapo Makka isipokuwa Abdul Mutwalib bin Hashim akiwa mahali pake pa kunywesha maji na Shaybah bin Uthman bin Abdiddar akiwa kwenye kizuizi cha Al-Ka'aba. Akawa Abdul Mutwalib anashika mihimili ya mlango huku akisema: 'Ewe Mwenyezi Mungu hakika mtu anataka kuzuwiya utukufu wako basi uzuwiye msafara wake, ili usiweze kushinda msalaba wao na uadui wao. Wasiweze kuingia mji huu mtukufu basi jambo limekudhihirikia."

Wale watangulizi wakapora ngamia wa Maquraish na wakapora ngamia mia mbili wa Abdul Mutwalib. Abdul Mutwalib alipopata habari hizo, akawaendea. Mlinzi wa Abraha alikuwa ni mtu mmoja katika Ash'an ambaye alikuwa akimjua Abdul Mutwalib. Basi yule mlinzi akamtaka idhini mfalme, akimwaambia: "Ewe Mfalme amekujia Bwana wa Maquraish, ambaye huwalisha binadamu mjini na wanyama majabalini. Akamwambia mwache aingie.

Abdul Mutwalib alikuwa ni mtu mwenye umbo kubwa, mzuri. Basi Abu Yaksum (Abraha) alipomwona hakuona vyema kumkalisha chini yake wala hakupendelea kumkalisha juu ya kitanda chake. Kwa hivyo akashuka chini akakaa pamoja na Abdul Mutwalib, kisha akamuuliza: "Nini haja yako?" akajibu: " Haja yangu ni ngamia mia mbili walioporwa na watu wako". Akasema Abu Yaksum: " Hakika umenishangaza sana". Akasema: " kwa nini ewe Mfalme". Akasem:" " Mimi nimekuja kwenye nyumba ya utukufu wenu, ya ubora wenu kwa watu na ya dini yenu ambayo mnaabudia. Nimekuja niivunje na ni nikapora ngamia wako mia mbili, sasa ninakuuliza nini haja yako, unaniambia ni ngamia tu! Wala huukulizia habari ya nyumba yenu (Al-Ka'aba)."

Abdul Mutwalib akamwambia: "Ewe mfalme mimi ninakusemesha katika mali yangu na hii nyumba ina mwenyewe ( Mungu) mwenye kuilinda. Mimi si lolote si chochote. HAya Na limshtusha Abu Yaksum. Basi Abu Yaksum akaamrisha kurudishwa ngamia wa Abdul Mutwalib, kisha akarudi na wale wakakesha katika usiku ambao anga yake ilichafuka, wakawa wanahisi adhabu.

Jua lilipochomoza, wakatokewa na ndege wakiwa wamechukua mawe, wakawa wanawatupia, kila ndege katika mdomo wake kuna jiwe moja na kwenye miguu kuna mawe mawili. Ndege akitupa jiwe likimpata mtu kwenye tumbo linampasua na linatoboa mifupa. Abu Yaksum akaamua kurudi, huku akiwa amepatwa na baadhi ya mawe akawa kila anapopiga hatua hukatika kiungo mpaka alipofika Yemen hakubakiwa na kiungo chochote. Alipofika, kikachanika kifua chake na likapasuka timbo lake akaangamia. Kunahitilafu kubwa katika kisa hiki, mwenye kutaka zaidi na asome vitabu vya sera na historia vyenye kueleza kwa urefu.

SURA QURAISH (QURAISH)(NA. 106)

INA AYA 4

Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

لِإِيلَافِ قُرَيْشٍ ﴿١﴾

1. Kwa ajili ya kuzowea Maquraish.

إِيلَافِهِمْ رِحْلَةَ الشِّتَاءِ وَالصَّيْفِ ﴿٢﴾

2. Kuzowea kwao safari ya kusi na kaskazi.

فَلْيَعْبُدُوا رَبَّ هَـٰذَا الْبَيْتِ ﴿٣﴾

3. Na wamwabudu Mola wa nyumba hii.

الَّذِي أَطْعَمَهُم مِّن جُوعٍ وَآمَنَهُم مِّنْ خَوْفٍ ﴿٤﴾

4. Ambaye amewalisha wakati wa njaa, na akawasalimisha na khofu.

UBAINIFU

Sura hii inaeleza neema ya Mwenyezi Mungu juu ya Maquraish kwa kuweza kusafiri katika wakati wa kusi na kaskazi na kufanya biashara kwa usalama, kwa hivyo wambudu Mola wa nyumba tukufu (Al-Ka'aba). Sura hii imeshuka Makka. Kwa kuwa madhumuni ya Sura hii yanafungamana na madhumuni ya Sura ya Fil, basi wamesema jamaa katika Shia na Ahli Sunnah kuwa Fil na Quraish ni Sura moja; kama ilivyosemwa katika Sura Adhuha na Alamnashrah (Al Inshirahi).

Kwa upande wa Ahli Sunnah waemetegemea mapokezi yao kuwa Ubayya bin Kaab, hakuweka Bismillah kati ya Sura ya Fil na Quraish katika msahafu wake. Na pia mapokezi yaliyotokana na Maymun El-Azadi amesema: "Niliswali maghrib nyuma ya Umar bin El-Khattab akasoma katika rakaa ya kwanza Sura ya Wattin na katika rakaa ya pili akasoma Alamtara na Liilafi bila ya kusoma Bismillahi kati yake. Lakini riwAya Na kwanza imejibiwa kuwa riwaya hiyo inapingana na riwaya nyingine inayosema kuwa Bismillah ipo katika huo msahafu wa El-Azadi. Na riwAya Na pili imejibiwa kuwa inawezekana huyo mpokeaji wa riwaya hiyo hakusikia tu! Au pengine hiyo Bismillah ilisomwa bila sauti.

Ama kwa upande wa Shia wametegemea yale yaliyo katika Majmau: Kutoka kwa Abul Abbas, naye kutoka kwa mmoja wa Maimamu(a.s) amesema: "Alamtara na Lillafi ni Sura moja". Na wametegema yale yaliyo katika Tahdhib kwa isnadi ya Alaa, kutoka kwa Zaid Shaham amesema: "Abu Abdillahi(a.s) alituswalisha Alfajiri, akasoma Alamnashrah na Adhuha katika rakaa moja. Na yaliyo katika Majmau, kutoka kwa Iyash naye kutoka kwa Mufadhil bin Saleh kutoka kwa Abu Abdillahi(a.s) amesema: "Nimemsikia akisema huyo Abu Abdillahi(a.s) : Hazichanganywi Sura mbili katika rakaa moja illa Alamtara na Ilafi na Alamnashra na Adhuha. Na amepokea Muhakkik kwa kunakili kutoka katika kitabu Jamiu cha Ahmad Muhammad bin Abu Nasr. Lakini riwAya Na Abul Abbas ni dhaifu. Ama riwAya Na Shahham, imepokewa kutoka kwake kwa njia mbili nyengine Ya kwanza ni ile iliyo katika Tahdhib kutoka kwa Ibn Miskan, naye kutoka kwa Zaid Shahham amesema: "Abu Abdillahi alituswalisha, akasoma Sura ya Wadhuha na Alamnashra.

Na riwAya Na pili imepokewa kutoka kwa Ibn Abdi Umar naye kutoka kwa baadhi ya masahaba zetu, kutoka kwa Zaid Shham amesema: " Abu Abdillah(a.s) alituswalisha akasoma katika rakaa ya pili Sura ya Wadhuha na katika rakaa ya pili Sura ya Alamnashrah." Kwa hali yeyote itakayokuwa ni kwamba riwaya hizo, zinafahamisha kujuzu kusoma Sura mbili Alamnashrah na Adhuha katika rakaa moja au Alamtara na Liilafi katika rakaa moja, jambo ambalo halijuzu katika Sura nyengine.

Aya Na 1-2

Maquraish ni ukoo wa Mtume(s.a.w.w) , wao ni kizazi cha Nadhr bin Kinanah aliyekuwa akijulikana kwa jina la Quraish, "Msafara wa kusi na kaskazi" ni msafara wa Maquraish wakawa wanaishi kwa biashara tu! Walikuwa wana misafara miwili kwa kila mwaka, msafara wakusi ulikuwa wa Yemen na msafara wa kaskazi ulikuwa wa Sham (Syria). Na walikuwa wakiishi kwa hilo na watu wakiwaheshimu, hawaulizwi njiani, wala mji hauvamiwi, kwa sababu ya nyumba tukufu (Al-Ka'aba). Herufi Fa katika neno Fal-ya'abudu ni ya kueleza maana ya sharti yaani: kwa vyovyote iwavyo, basi wamwabudu Mola wa nyumba hii kwa ajili ya kuwazowesha kwake misafara miwili. Kwa ujumla maana ya aya hizi tatu ni kuwa; Maquraish wamwabudu Mola wa nyuba hii(Al-Ka'aba) kwa ajili ya kuwazowesha msafara wa kusi na kaskazi huku wakiwa katika amani.

Hii ni kwa kuangalia kuwa Sura hii imeepukana na Sura ya Alamtara. Ama kwa kukadiri kua Sura hii ni sehemu ya Sura ya Alamtara, basi herufi Lam katika Liilafi, itakuwa ni Ya taalil yenye kufungamana na yale yaliyo katika Sura ya Alamtara, kwa maana ya kuwa tumefanya hayo tuliyowafanyia watu wenye ndovu, hali yakuwa ni neema itokayo kwetu juu ya Maquraish kuongezea neema ya misafara yao ya kusi na kaskazi. Yaani kama vile amesema kutoka neema moja mpaka neema nengine kwa hivyo ndio maana kasema kuwa herufi lam inatekeleza maana ya Ilaa (mpaka). Na hilo ni neno lake Farra (Mwanachuoni wa kinahaw) Pia imesemwa kuwa: tumewafanyia hilo watu wenye ndovu ili wazoee Maquraish Makka na waweza kukaa hapo. Au ili wazowee Maquraish hapo kwa vile walimkimbia Abraha alipoikusudia Al-Ka'aba, hivyo tukawangamiza Abraha na watu wake, ili warudi Maquraish Makka, wazowee hapo na azaliwe Muhammad(s.a.w.w) awe muonyaji kwa watu.

Aya Na 4

Inaishiria yale yaliyomo katika neema zilizo wazi, amabazo ni kupata chakula katika ardhi iliyo kame na kuwa katika amani, jambo ambalo halikuweko kwa watu wengine, kwa hiyo basi na wamwabudu Mola anayezingatia vizuri mambo yao ambaye ndiye huyo Mola wa hiyo nyumba (Al-Ka'aba)

Utafiti Wa Hadithi Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu Sura hii anasema " Imeshuka kwa ajili ya Maquraish, kwa sababu maisha yao yalikuwa yakitokana na misafara miwili msafara katika kusi kuelekea Yemen na msafara katika kaskazi kuelekea Sham (Syria) na walikuwa wakichukua kutoka Makka siagi, lozi na vitu vinavyoota pembeni mwa bahari, kama pilipili na vyenginevyo, na walikuwa wakinunua nguo, unga mweupe na nafaka huko Sham, na walikuwa wakitembea vikundi, kila kikundi kina kiongozi katika viongozi wa Kiquraish.

Basi Mwenyezi Mungu alipompeleka Mtume wake wakawa hawana haja na hayo tena, kwani walikuwa watu wakija kwa Mtume(s.a.w.w) na kuhiji Al-Ka'aba, kwa hivyo ndio Mwenyezi Mungu akasema: " Na wamwabudu mola wa nyumba hii, ambaye amewalisha kwa ajili ya njaa na akawasilimisha na khofu" (yaani hofu ya njiani)". Lakini maneno haya (kuanzia Mwenyezi Mungu alipompeleka Mtume?.) yamefichika katika anuani ya aya za Sura hii, au huenda huyo Qummi ameyachukua kutokana na baadhi ya yaliyopokewa kutoka kwa Ibn Abbas.


26

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA MAUN ( MANUFAA) (NA. 107)

INA AYA 7

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

أَرَأَيْتَ الَّذِي يُكَذِّبُ بِالدِّينِ ﴿١﴾

1. Je, umemwona (unamjua) yule ambaye anakadhibisha dini.

فَذَٰلِكَ الَّذِي يَدُعُّ الْيَتِيمَ ﴿٢﴾

2. Huyo ni ambaye humsukuma yatima.

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿٣﴾

3. Wala hahimizi kulisha maskini.

فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ ﴿٤﴾

4. Basi ole wao wenye kuswali.

الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ ﴿٥﴾

5. Ambao wanapuuza swala zao.

الَّذِينَ هُمْ يُرَاءُونَ ﴿٦﴾

6. Ambao wao hujionyesha.

وَيَمْنَعُونَ الْمَاعُونَ ﴿٧﴾

7. Na wakazuilia (watu) manufaa.

UBAINIFU

Sura hii inaelezea kiaga anachopewa yule mwenye kusifika na sifa za kiunafiki kama vile kuipuuza swala kufanya ria na kuzuwiya misaada. Sura hii inawezekana kuwa imeshuka Makka au Madina. Na inasemekana nusu yake imeshuka Makka na nusu yake imeshuka Madina.

Aya Na 1

Neno Araayta lina maana ya kuona kwa macho au kwa kiakili. Makusudio ya dini hapa ni malipo siku ya malipo na kukadhibisha malipo maana yake ni kukadhibisha kufufuliwa. Imesemwa kuwa makusudio ya dini ni kwa maana ya mila.

Aya Na 2

Neno yaduu lina maana ya kusukuma na kufukuza kwa nguvu na jeuri. Hapa ina maana ya yule anayemsukuma na kumfukuza yatima kwa nguvu na jeuri bila ya kujali matokeo ya mabaya hayo ayafanyao. Lau hakukataa siku ya malipo angeliogopa siku hiyo. Na lau aliigopa siku hiyo angelimhurumia yatima.

Aya Na 3

Yaani ni yule ambaye hapendelei watu wawalishe maskini. Imekuja ibara ya kuhimiza, kwa vile kuhimiza kunaenea zaidi kuliko kufanya tu! Inasemekana kuna neno Twaam lina maana ya chakula kama lilivyo, kwa kufahamisha kwamba yule mwenye kupewa ni kama vile anamiliki kile anachopewa, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na katika mali zao ilikuwako haki ya kupewa maskini aombae na ajizuiae kuomba ." (51:19).

Na inasemwa Twaam katika aya ina maana ya kulisha.

Aya Na 4-5

Wanaopuuza swala ni wale wasiopatiliza swala wala hawajali kukosa swala zote au baadhi, au kuchelewa na wakati wake bora (wa mwanzo). Aya hii inawaunganisha wale wanaopuuza swala na wale wanaokadhibisha malipo, kufahamisha kuwa wao hawaachani na unafiki wao kwa vitendo huku wakijidhihirisha kwa imani.

Aya Na 6

Wanaojionyesha ni wale wanaofanya ibada kwa kujionyesha kwa watu, kwa hiyo wanafanya ibada kwa ajili ya watu na sio kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Aya Na 7

Neno Maun lina maana ya msaada wa aina yoyote inayoondoa dhiki au tatizo la aina yoyote kama vile kumkopesha mtu pesa, au kumfanyis wema au kumuazima chombo cha nyumbani.

Utafiti Wa Hadithi. Katika Tafsiri ya Qummi kuhusu Aya Na 1 anasema ilishuka kwa Abu Jahl na makafiri wa Kiquraish, na kuhusu Aya Na 5 wanakusudiwa wale wanaocha swala na wala sio kusahau, kwa sababu kila mtu anaweza kusahau katika swala. Amesema Abu Abdiallah(a.s) : "Ni kuichelewesha swala na wakati wake bila ya udhuru ". Katika Khiswal katika hadith ya mia nne imepokewa kutoka kwa Ali(a.s) amesema: "Hakuna amali inayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuliko swala, kwa hivyo kisiwashughulishe chochote na swala kwani Mwenyezi Mungu amewashutumu watu kwa kusema: "Wale ambao swala zao wanazipuuza" yaani wanaopuuza wakati wake.

Katika Kafi kwa isnadi ya Muhammad bin Alfadhil, anasema: "Nilimuuliza mja mwema(a.s) kuhusu Aya Na 5 akasema ni kupuuza, na ziko riwaya nyingi katika madhumuni haya haya. Katika Durril Manthur ametoa Ibn Jariyr, Ibn Hatim na Bayhaqai kutoka ka Ali bin Abu Twalib kuhusu neno, wale amabo wanafanya ria ni kufanya ria katika swala. Katika hiyo hiyo Durril Manthur ametoa Abu Naim, Dilami na Ibn Asakir kutoka kwa Abu Hurayra naye kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kuhusu Aya Na 7 ni vitu wanavyosaidiana watu kama shoka, ndoo, sufuria nk.

Katika Kafi kwa Abu Baswir naye kutoka kwa Abu Abdiallah(a.s) amesema: "Na neno lake Mwenyezi Mungu (s.w.t): Na wakazuilia (watu) na manufaa" ni kuzuilia kukopeshana na kufanyiana mema na kuazimana vyombo vya nyumbani na pia kuzuilia zaka. Kilifasiri neno Maun kwa maana ya zaka pia imepokewa kwa njia ya Ahli Sunnah, kutoka kwa Ali(a.s) kama ilivyo katika Durril Manthur kuwa tamko Maun ni zaka ya wajibu. Yaani wanajionyesha katika swala zao na huku wanazuia zaka zao.

Katika hiyo Durril Manthur ametoa Ibn Qani kutoka kwa Ali Ibn Abu Twalib(a.s) amesema: "Nimemsikia Mtume(s.a.w.w) akisema: "Muislamu ni ndugu ya muislamu mwengine anapokutana naye humuamkia kwa salam na humpatia kila chenye heri na hamzuilii Maun nikasema, "Ewe Mtume wa Mungu nini maun" akasema Mtume "ni jiwe, chuma, maji nk." Amefafanua Mtume(s.a.w.w) katika hadith nyengine kuwa chuma ni sufuria za shaba na shoka ya chuma. Na mawe ni nyungu za mawe.

SURA KAWTHAR (HERI NYINGI) (NA. 108)

INA AYA 3

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ ﴿١﴾

1. Hakika sisi tumekupa kheri nyingi.

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

2. Basi mswalie Mola wako na uchinje mnyama.

إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الْأَبْتَرُ ﴿٣﴾

3. Hakika mwenye kukubughudhi wewe yeye ndiye mwenye kuishiwa.

UBAINIFU

Sura hii inaeleza kuneemeshwa kwa Mtume kwa kupewa neema nyingi. Na Sura hii ndiyo Sura fupi katika Qur'an. Mapokezi yamekithalifiana kuwa Sura imeshuka Makka au Madina, lakini inaonyesha kwamba imeshuka Makka. Wengine wamesema imeshuka mara mbili.

Aya Na 1

Imesemwa katika Majmau kwamba neno Kawthar liko katika kipimo cha Faw-al yenye maana ya wingi, kwa hiyo Kawthar ni heri nyingi. Wamehitilafiana kiajabu sana katika tafsiri ya neno Kawthar. Imesemwa kuwa ni heri nyingi, wengine wamesema ni mto peponi, wengine wamesema ni birika ya Mtume katika pepo au katika siku ya kukusanywa watu. Pia imesemwa ni watoto wake, masahaba wake, wafuasi wake mpaka siku ya Kiyama, au wanavyuoni wa umma wake.

Na imesemwa ni Uislamu, Tawhid, elimu na hekima, ubora wake, maqamu yenye kusifiwa, nuru ya moyo wake na zaidi ya hayo yamesemwa mpaka kufikia kauli ishirini na saita (26). Baadhi ya riwaya zimetegemea kwenye kauli mbili za mwanzo (heri nyingi na to katika pepo). Lakini kauli nyingine pia haziwezi kuachwa. Kwa hali yoyote iwayo. Neno abtar kwa dhahiri lina maana ya mwenye kukatikiwa na kizazi. Kwa hiyo makusudio hapa ya kawthar ni kizazi kingi, au heri nyingi kwa maana ya kuwa hicho kizazi ni heri nyingi lau kama si hivyo, basi ingelikuwa jumla ya aya ya haina faida yoyote.

Hadith zimeeleza kwamba Sura hii ilishuka, kutokana na mtu mmoja aliyemtusi Mtume(s.a.w.w) , kwa kuwa eti amekatikiwa na kizazi chake kutokana na kufa kwa watoto wake wa kiume (Kassim na Abdulla). Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamrudishia majibu kwa kusema huyo mwenye kukubughudhi wewe ndiye abtar aliyekatikiwa na heri zote: Neno "hakika sisi tumekupa wewe", limekuja kwa wingi kwa kuadhimisha tu. Jumla yote hiyo ya maneno inafahamisha kuwa kizazi cha Fatima(a.s) ni kizazi cha Mtume(s.a.w.w) . Mwenyezi Mungu amekifanya kingi sana kizazi hicho kuliko kizazi kingine chochote pamoja na misiba iliyowashukia na kuuliwa kwa makundi katika mauaji ya kuchukiza na ya kinyama.

Aya Na 2

Kushukuru neema ni jambo linalotakikana. Hapa Mwenyezi Mungu anamwamrisha Mtume wake kuwa tumekupa heri nyingi, basi wewe shukuru neema hiyo kwa kusali na kuchinja mnyama. Imesemekana maana ya ayah ii ni kuswali swala ya Idd na kuchinja mnyama. Pia imesemwa maana ya neno wanhar ni kunyanyua mikono miwili katika swala wakati wa kusoma takbira.

Aya Na 3

Imesemwa maana ya neno abtar hapo ni kuepukana na heri au kuepukana na watu wake. Yatakuja maelezo katika utafiti wa hadith. Neon shani ni yule mwenye kubughudhi naye ni Asi bin Wail.

Utafiti Wa Hadith Katika Durril Manthur ametoa Bukhari, Ibn Jariyr na Hakim kwa njia ya Abu Bashar kutoka kwa Said bin Jubayr naye amepokea kutoka kwa Ibn Abbas kwamba yeye amesema: "Kawthar ni heri alizopewa Mtume". Abu Bashar akasema kumwambia Said bin Jubayr: "Hakika watu wanadai kuwa kawthar ni mto katika pepo". Akajibu "mto katika pepo ni katika heri ya Mwenyezi Mungu aliyompa Mtume wake." Katika hiyo hiyo Durril Manthur ametoa Ibn Abu Hatim, Hakim, Ibn Murdawayh na Bayhaqi katika hadith zake kutoka kwa Ali bin Abu Twalib(a.s) amesema:

"Iliposhuka Sura ya Kawthar, Mtume(s.a.w.w) alisema kumwambia Jibril: Ni uchinjo gani huu alioniamrisha Mungu? Jibril akasema: "Sio uchinjo isipokuwa anakuamrisha kunyanyua mikono yako katika swala wakati wa kuhirimia, kurukui na wakati wa kunyanyua kichwa baada ya rukui, kwani hiyo ndiyo swala yetu na swala ya Malaika walioko katika mbigu saba, na kwamba kila kitu kina kipambo chake na kipambo cha swala ni kunyanyua mikono miwili kila unaposoma takbira. Katika Majmau imepokewa kutoka kwa Muqatil naye kutoka kwa Asbagh bin Nabata, kisha akasema wamepokea Thaalabi na Wahidi katika tafsiri zao, kwamba imepokewa kutoka kwa kizazi chote kitakatifu cha Mtume kitabu hicho hicho ametoa Ibn Jariyr kutoka kwa Abu Jaffar kwamba maana ya msalie Mola wako, ni swala na maana ya wanhar ni unyanyue mikono miwili unapotoa takbira mwanzo wa swala.

Tena katika hiyo hiyo Majmau ametoa Ibn Murdawayh kutoka kwa Ibn Abbas kuhusu Aya Na 2 amesema: Hakika Mwenyezi Mungu alimpelekea Wahyi Mtume wake kwa kusema : "Nyanyua mikono yako muelekeo wa sehemu ya juu ya kifua hiyo ndiyo nahr". Katika hiyo hiyo Majmau imepokewa kutoka kwa Umar bin Yazid amesema: "Nimesikia Abu Abdillahi akisema? Maana ya wanhar ni kunyanyua mikono yako pambizoni mwa uso wako. Na pia imepokewa kutoka kwa Abdulla bin Sinan mfano wa hadith iliyo karibu na maana hayo kutoka kwa Jamil. Katika Durril Manthur ametoa Ibn Saad na Ibn Asakir katika njia ya Kalabi kutoka kwa Abu Saleh naye kutoka kwa Ibn Abbas amesema: "Alikuwa mtoto mkubwa wa Mtume(s.a.w.w) ni Kassim kisha Zaynab, Abdulla, Ummu Kulthum, Fatima na Ruqayya. Akafa Kassim, naye ndiye maiti wa kwanza katika kizazi chake, kisha akafa Abdullah. Ndipo akasema Asi bin Wail Assahmi :"Kizazi chake kimekwisha katika, kwa hiyo yeye ni abtar. Basi akateremsha Mwenyezi Mungu; Hakika mwenye kukubughudhi wewe yeye ndiye abtar (mwenye kuepukana na heri zote)".

Katika hiyo hiyo Durril Manthur ametoa Ibn Abu Hatim kutoka kwa Assadi amesema. "Walikuwa Maquraish wakisema: mtu anapofiwa na mtoto wa kiume, ni abtar basi alipokufa mtoto wa Mtume(s.a.w.w) , Asi bin Wail akasema Mtume ni abtar. Tena katika hiyo hiyo Durril Manthur ametoa Zubeir bin Bakar na Ibn Muhhamd kutoka kwa baba yake amesema: "Alikufa Kassim mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu huko Makka, Mtume alipokuwa akitoka kuzika akapita kwa Asi Bin Wail akiwa na mtoto wake Amru, akasema alipomwona Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . "Mimi ninamchukia sana." Akasema Asi: "Achana naye kwani yeye ameshakua Abtar". Mwenyezi Mungu ndio akateremsha Sura hiyo.

Ibn Abi Hatim amepokea kutoka kwa Assadi amesema: "Mtu anapofiliwa na mtoto wa kiume, Quraish walikuwa wakisema: "Fulani ameshakuwa abtar." Basi alipokufa mtoto wa Mtume(s.a.w.w) Asi bin Wail alisema : "Amekuwa abtar". Wamehitalifiana juu ya aliyembughudhi Mtume(s.a.w.w) ; wengine wanasema ni Walid bin Al-Mughira, wengine wanasema ni Abu Jahl, wengine ni Uqbah bin Abu Muiit na wengine wanasema ni Ka'ab bin Ahsraf. Lakini kauli yenye tutegemewa ni ile inayomtaja Asi nin Wail.

Hayo yanatiliwa nguvu na yale yaliyo katika Ihtijaj ya Tabrasiy kutoka kwa Hasan bin ali(a.s) katika hadith anayomwambia Amru bin Al-Asi: "Hakika wewe umezaliwa kutokana na kitanda kilichoshirikianwa, wakabishana juu yako wanaume wa Kiquraish ambao ni Abu Sufyan bin Harb, Walid bin Al-Mughira, Uthman bin Al-Harith, Annadhri bin Al-Harith bin Kaldah na Asi bin Wail. Kila mmoja anadai kuwa wewe ni mtoto wake, ndipo akashinda yule mchafu wao zaidi.

Katik Tafsiri ya Qummi amesema Kawthar ni mto katika pepo aliopewa Mtume badala ya mtoto wake Ibrahim (aliyekufa). Kwa vyovyote iwavyo kutafsiri Kawthar kuwa ni mto katika pepo hakupingani na tafsiri ya heri nyingi, kama yalivyokwisha tangulia maelezo ya Ibnu Jubeir.

SURA KAFIRUN (MAKAFIRI)(NA. 109)

INA AYA 6

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ ﴿١﴾

1. Sema: Enyi makafiri

لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ ﴿٢﴾

2. Mimi siabudu mnachokiabudu.

وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ ﴿٣﴾

3. Wala nyinyi hamkiabudu ninachokiabudu mimi.

وَلَا أَنَا عَابِدٌ مَّا عَبَدتُّمْ ﴿٤﴾

4. Wala mimi sitaabudu mnachokiabudu nyinyi.

وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ ﴿٥﴾

5. Wala nyinyi hamtakiabudu ninachokiabudu mimi.

لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ ﴿٦﴾

6. Nyinyi mna dini yenu, na mimi nina dini yangu.

UBAINIFU

Katika Sura hii Mwenyezi Mungu anamwamrisha Mtume kudhihirisha kujitenga kwake na dini yao. Dini yake haingilii dini yao wala dini yao haingilii dini yake. Yeye katu haabudu lile wanaloliabudu wala wao katu hawaabudu anachokiabudu. Kwa hivyo wakate tamaa na namna yoyote ile ya kudanganya. Wamekhitalifiana wafasiri kuwa Sura imeshuka Makka au Madina, lakini mpangilio wa maneno unaonyesha kuwa imeshuka Makka.

Aya Na 1

Kwa dhahiri ni watu maalum sio makafiri wote. Hilo linafahamisha kuamrishwa kwake Mtume(s.a.w.w) kuwambia makafiri kutakasika kwake na dini yao na kujizuilia kwao na dini yake.

Aya Na 2

Makusudio ya kile mnachokiabudu, ni masanamu waliyokuwa wakiyaabudu. Herufi laa hapa ni ya kukanusha kwa muda ujao (mustaqbal) na herufi maa ni ya muda wa sasa hivi. Yaani siabudu milele kile mnacho kiabudu hivi sasa katika msanamu.

Aya Na 3

Pia ni ya kukanusha kwa muda ujao yaani kumpa habari Mtume(s.a.w.w) kwamba makafiri hawataabudu kile anachokiabudu Mtume(s.a.w.w) kama walivyokuwa wakidai. Kwa kuunganisha amri iliyo katika mwanzo wa maneno, aya hizi mbili zinaonyesha ya kwamba Mwenyezi Mungu ameniamrisha kudumu kumuabudu Yeye. Halikadhalika ameniamrisha kuwaeleza kama nyingi hamtamuabudu katu. Kwa hivyo hapana ushirikiano wa dini kati yangu na nyinyi. Ayah ii ina maana sawa na ile aya isemayo: "Bila shaka kauli (ya adhabu) imehakikika juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini ." 36:7.

Halikadhalika inakubaliana na aya isemayo: "Hakika wale waliokufuru (Kwa ukaidi na inadi) ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini ". (2:6). Ilikuwa sawa ni kusema: "Wala nyinyi siwenye kuabudu ninayemuabudu". Lakini imesemwa "Ninachokiabudu". Kwa jili ya kufuata mpangilio ulioanzia: "Siabudu mnachokiabudu".

Aya Na 4-5

Ni kutilia mkazo yale yaliyotangulia, kama ilivyo katika Sura ya (102: 3-4); aliposema: "Komeni punde kidogo tu! Mtajua kisha komeni punde kidogo tu! Mtajua ". Na katika Sura (74: 19-29):

"Amelaaniwa, namna gani alivyokadiria (kutia ila Qur'an) kasha amelaaniwa, namna gani aliyokadiria (kutia ila Qur'an) ."

Imesemekana kuwa ma katika neno Abadtum sio mausul yenye maana kurejea kwenye jina, bali ni ya masdariya ya kufanya jina la kitendo yenye maana wa Wala mimi siabudu ibada yenu wala nyinyi siwenye kuabudu ibada yangu. Kwa maana kuwa siwashirikishi wala hamnishirikishi si katika mwenye kuabudiwa wala ibada. Ninayemuabudu mimi ni Mungu na mnayeabudu nyinyi ni sanamu. Na ibada yangu ni ile aliyoiweka Mwenyezi Mungu, lakini ibada yenu ni ile mliyoizusha wenyewe kwa ujinga na uzushi. Yatakuja maelezo katika utafiti wa hadith (Inshallah).

Aya Na 6

Nikuzidi kutilia mkazo kukanusha kushirikiana. Na herufi lam ni ya kuhusisha, yaani dini yenu ya kuabudu masanamu inahusika na nyinyi na hii dini yangu inahusikana na mimi tu! Inasemekana kwamba dini hapa ina maana ya malipo yaani; Mna malipo yenu na nina malipo yangu. Na inasemekana pia kuna kitu kilichoondoshwa yaani, mna malipo ya dini yenu nami nina malipo ya dini yangu. Lakini njia mbili zote hizo, ziko mbali na ufahamu.

Utafiti Wa Hadithi Katika Durril Manthur ametoa Ibn Jariyr, na Ibn Abu Hatim na Ibn Anbari, kutoka kwa Said Ibn maynai Huru (aliyekuwa mtumwa) wa Abul Bakhtari amesema: "Walid bin El-Mughira, Asi bin Wail, sa-wad bin El-Mutwalib na Umayya bin Khalaf, walikutana na Mtume wakamwambia "Ewe Muhammad ! njoo tuabudu kile unachokiabudu na wewe uabudu kile tunachokiabudu na tushirikiane sisi na wewe katika mambo yetu yote, ikiwa haya yetu ni sahihi zaidi kuliko yako, basi utakuwa umepata cha kupata, na kama ikiwa yale unayoyaabudu wewe ni sahihi zaidi kuliko yetu, basi tutakuwa tumechukua la kuchukua". Mwenyezi Mungu ndio akateremsha Sura hiyo yote.

Katika Tafsiri ya Qummi amepokea kutoka kwa baba yake naye amepokea kutoka kwa Ibn Abu Umeir amesema: "Abu Shakir alimuuliza Abu Jaffar El-Ahwal kuhusu Sura ya Kafirun "Jee Mwenye hekima anasema maneno kama haya na kuyarudia mumo kwa mumo? "Abu Jaffar El-Ahwal hakuwa na jibu. Basi akaenda Madina kumuuliza Abu Abdillahi(a.s) akasema: :Sababu ya kushuka Sura hiyo na kukariri maneno hayo, ni kwamba Maquraish walimwambia Mtume(s.a.w.w) : 'abudu miungu wetu mwaka mmoja na tuabudu Mungu wako mwaka mmoja na tena abudu miungu wetu mwaka moja na tuabudu Mungu wako mwaka mmoja".

Mwenyezi Mungu akawajibu kama vile walivyo sema. Akasema juu ya yale waliyoyasema kuwa aabudu miungu yao mwaka alisema: Sema enyi makafiri. Mimi siabudu mwachokiabudu. Na katika yale waliyoyasema kuwa watamwabudu Mungu wake mwaka alisema: Wala nyinyi hamkiabudu ninachokiabudu mimi. Na juu ya yale waliyosema aabudu miungu yao mwaka mmoja alisema: Wala mimi siabudu mnachokiabudu nyinyi.

Na katika yale waliyoyasema wataabudu Mungu wake mwaka mmoja alisema: Wala nyinyi hamtakiabudu ninachokiabudu mimi. Nyinyi mna dini yenu na mimi nina dini yangu. Akarudi Abu Jaffar El-Ahwal kwa Abu Shakir akampa habari juu ya hayo!


27

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA NASR (MSAADA)NA 110

INA AYA 3

Kwa jina la allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّـهِ وَالْفَتْحُ ﴿١﴾

1. Utakapokuja msaada wa Allah na ushindi.

وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّـهِ أَفْوَاجًا ﴿٢﴾

2. Ukawaona watu wanaingia katika dini ya Allah makundi makundi.

فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا ﴿٣﴾

3. Basi hapo mtakase Mola wako pamoja na kumsifu na umwombe maghufira. Hakika yeye ni mwingi kukubali toba.

UBAINIFU

Mwenyezi Mungu alimwahidi Mtume(s.a.w.w) ushindi na kwamba yeye atawaona watu wakiinga katika Uislamu makundi kwa makundi, akamwamrisha kufanya tasbih, tahlil na istighfar. Sura hii imeshuka Madina baada ya Sul-hul Hudaibiya (mapatano ya Hudaibiya) na kabla ya ushindi wa Makka, kama vile itakavyobainika.

Aya Na 1

Idha ni neno linaloonyesha muda ujao, kwa hiyo madhumuni ya aya hii ni kulitolea habari jambo litakalo hakikika baadaye. Ikiwa jambo linalotolewa habari ni msaada na ushindi na hilo ni katika mambo yanayomtuliza moyo Mtume, basi ni ahadi nzuri na biashara kwake. Msaada na ushindi uliokusudiwa hapa sio ule ambao amempatia Mwenyezi Mungu katika msimamo wake wote kama vile ushindi juu ya maadui zake katika vita na iman ya Ansar na watu wa Yemen, wala pia sio makusudio ya Sulhul Hudaibiya (mapatano ya amani ya Hudaibiya) ambayo Mwenyezi Mungu ameyaita ushindi wakati aliposema: "Hakika sisi tumekupa ushindi ulio wazi ". (48: 1).

Kwa vile Aya Na pili haioani na madhumuni yake. Kwa hiyo makusudio hapa ni ushindi wa kuiteka Makka ushindi ambao ulikuwa ndio mama wa ushindi wake Mtume(s.a.w.w) katika zama za ushindi wake na ulikuwa msaada wa ushindi ambao ulivunja vizingiti vya ushirikina katika Bara-arabu.

Hayo yanatiliwa nguvu na kiaga cha msaada uliotajwa katika aya zilizoshuka katika Sul-hul Hudaybiya: "Hakika sisi tumekupa ushindi ulio wazi, ili Allah akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yanayokuja, na kukutimizia neema zake na kukuongoa katika njia iliyonyooka. Na akunusuru Allah nusura (msaada) yenye nguvu habisa " (48:1-3).

Lililo karibu zaidi kufahamika kutokana na yaliyomo katika aya hizo ni msaada wa Mwenyezi Mungu kwa Mtume(s.a.w.w) wake juu ya Maquraish kwa kuichukua Makka ijapokuwa ni baada ya kupita miaka miwili baada ya ushindi wa Alhudaibiya. Pia hayo ni jawabu la madai kuwa ni kuitikia watu wa Yemen kuiingia kwao katika Usilamu, bila ya vita. Yenye kukubalika ni kuwa kusudio la ushindi hapa ni ushindi wa Mtume(s.a.w.w) juu ya Maquraish na kuiteka Makka. HAya Na nadhihirisha kuwa Sura hii iliteremka baada ya Sulhul Hudaibiya kuteremka Suratul Fath (ushindi) na kabla ya kutekwa Makka.

Aya Na 2

Raghib amesema: Fawj ina maana ya makundi yanayopita kwa haraka. Wingi wa Fawj ni Afwaja. Maana ya kuingia watu makundi ni kuingia kundi baada ya kundi jengine. Makusudio ya dini, ni dini ya Kiislamu, kama alivtyosema Mwenyezi Mungu: "Hakika dini mbele ya Allah ni Uislamu ." (3:19)

Aya Na 3

Msaada huu na ushindi huu, ni namna mojawapo ya kuidhalilisha shirki na kuipa nguvu Tawhid. Au kwa maneno mengine, kuibatilisha batili na kuihakikisha haki. Basi hayo yananasabiana na kumtakasa Mwenyezi Mungu, na kumsabihi kwa upande wa kwanza na kumsifu (Sifa) Menyezi Mungu na kumshukuru kwa upande wa pili. Ndio akaamrishwa Mtume(s.a.w.w) ikasemwa (Mtakase mola wako pamoja na kumsifu na umtake msamaha.) Mwelekeo mwengine wa amri ya kumtakasa Mungu, kumsifu na kumtaka msamaha, ni kwamba ni juu ya mja kumkumbuka mola wake kwa sifa za ukamilifu wake, na kujikumbusha (mja) upungufu wake na haja yake. Ilivyokuwa kwamba ushindi huu umemaliza lile alilokuwa akilihangaikia Mtume(s.a.w.w) katika kuondoa batili na kukata shina la ufisadi, basi ameamrishwa Mtume(s.a.w.w) kumkumbuka Mola wake kwa utukufu na mwisho kujikumbusha upungufu wake wa kumhitajia kwake Mwenyezi Mungu ambako nikutaka maghufira. Maana ya kutaka maghufira, (msamaha) hapa ni kudumu hayo maghufira, kwani Mtume(s.a.w.w) amekwisha ghufiriwa.

Utafiti Wa Hadithi Katika Majmau imepokewa kutoka kwa Muqatil. Iliposhuka Sura hii, Mtume(s.a.w.w) aliwasomea Masahaba zake, wakafurahi. Alipoisikia Abbas alilia. Mtume(s.a.w.w) akamwambia: "Ni lipi linalokuliza ewe ami?" Akasema Abbas: "Ninadhani umejitolea habari za kifo chako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu." Akasema Mtume(s.a.w.w) : "Ndio kama unvyosema". Basi akaishi baadae miaka miwili, hakuonekana akicheka kwa furaha. Simepokewa hadith nyingi kwa maana haya. Katika hiyo Majmau, imepokewa kutoka kwa Ummu Salama, amesema: "Alikuwa Mtume(s.a.w.w) siku za mwisho hasimami wala hakai, wala hendi au kuja mahali illa husema: "Subhanallahi wabihamdihi, astaghfirullah waatubu ilaihi." Kutakakata na maovu ni kwa Mwenyezi Mungu na pamoja na kumsifu. Namtaka maghufira Mwenyezi Mungu na ninarejea (tubia) kwake." Tukamuuliza juu ya hilo, akasema: "Hakika mimi nimeamrishwa hilo" kisha akasoma "Sura ya Idhaa- jaa (Nasr).

Pia ziko hadith zaidi zilizokuja kwa maana haya, lakini kwa kuhitalifiana yale aliyoyasema Mtume(s.a.w.w) . Katika kitabu cha Uyun kwa isnadi yake kwa Hussein bin Khalid, amesema: "Amesema Ridha(a.s) : "Nimemsikia baba yangu anazungumza kutokana na baba yake(a.s) kwamba Sura ya kwanza ni Iqraa (Alaq) na Sura ya mwisho kushuka ni Idha-jaa (Nasr)". Huenda ikawa makusudio ni Sura ya mwisho kushuka ikiwa kamilifu.

Katika Majmau, katika kisa cha ushindi wa Makka imesemwa: Alipotiliana mkataba wa amani Mtume(s.a.w.w) pamoja na Maquraish, katika mapatano ya Hudaibiya (Sulhul-Hudaibiya), ilikuwa moja ya masharti ni kwamba atakayetaka kujiunga na Mtume(s.a.w.w) aruhusiwe. Basi kabila la Khuzaa likajiunga na Mtume(s.a.w.w) , na Bani Bakr wakajiunga na Maquraish, makabila haya mawili yalikuwa na ugomvi mkubwa sana tangu zamani. Baadaye vikazuka vita kati ya Bani Bakr na Khuzaa. Maquraish wakawa wanawapa silaha Bani Bakr, na pia wakawa wanawasidia kupigana wakati wa usiku hali ya kujificha. Miongoni mwa waliokuwa wakiwasaidia ni Akrama bin Abu Jahal na Suhail bin Amru.

Mtu mmoja katika Khuzaa anayeitwa Amru bin Salim, akasafiri hadi Madina kwa Mtume(s.a.w.w) . Na hilo lilikuwa ni miongoni mwa mambo yaliyoleta harakati za ushindi wa kuiteka Makka. Basi Salim akasimama mbele ya Mtume alipokuwa msikitini katikati ya watu na akasema: "Leo mimi meazimu mumwona Muhammadi Rafiki mwema rahimu Ja mzaziwe wa jadi Quraishi madhalimu wamepangua ahadi Miadi yako muhimu wameivunja kusudi wakatuua kaumu Rukuuni na Sujudi". Mtume akasema kumwambia Amru: :Inatosha ewe Amr". Kisha akasimama akaingia nyumba ya mkewe Maymuna Akamwambia: "Nimiminie maji" Akawa anajiosha huku akisema "Kama sikulisaidia kundi la Amr basi itakuwa sikusaidia kitu." Baadaye akaja tena kwa Mtume(s.a.w.w) Badil bin War'qai na kikundi cha Bani Khuzaa wakampasha habari Mtume(s.a.w.w) yale wanayofanyiwa na Maquraish na jinsi walivyojitokeza kuwasaidia bani Bakr.

Kisha wakaenda zao kurejea Makka. Mtume(s.a.w.w) alikuwa ameshawaambia watu: Naona kana kwamba Abu Sufiani atakuja kuitilia nguvu mkataba na kuongeza muda wake. Walipofika sehemu inayoitwa Asfa na wakakutana na Abu Sufiani akiwa ametumwa na Maquraish ili aongeze muda wa Mkataba. Basi Abu Sufiani alipokutana na hao jamaa alimuuliza Badil, "umetoka wapi?" Badil akamwambia "nimekwenda katika mwambao huu ndani ya wangwa huu". Akauliza tena Abu Sufiani, "hukumwendea Muhammad ?" Akajibu, "La!" Basi alipoondoka Badil kuelekea Makka Abu Sufiani akajisemea, "Ikiwa ametoka Madina atakuwa amemlisha ngamia wake kokwa za tende," kwa hivyo akaenda pale alipokuwa ametulia ngamia wa Badil akachukua kinyesi chake na kukichangua, akaona kokwa za tende, akasema,: "Ninaapa kuwa Badil ametoka Madina kwa Muhammad".

Kisha katoka Abu Sufiani mpaka kwa Mtume(s.a.w.w) akamwambia "Ewe Muhammad ilinde damu ya watu, upatane na Maquraish na uongeze muda wa Mkataba wetu." Mtume(s.a.w.w) akasema: "Ewe Abu Sufiani mnajifanya wajanja !" Akasema "La! Sisi bado tunashikilia mkataba wetu na amani" Akatoka Abu Sufiani akakutana na Abu Bakr akasema "Fanya mapatano na Maquraish." Aby Bakr akajibu "Ole wako! Kuna mtu anayeweza kufanya mapatano zaidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ". Kisha akakutana na Umar akamwambia hivyo hivyo. Kisha akatoka akaingia nyumbani kwa Ummu Habiba, (mke wa Mtume) akawa anataka kukaa kwenye tandiko. Ummu Habiba akanyanyua tandiko na kulikunja, akasema: "Ewe binti yangu kwa nini unanikataza kukalia hili tandiko?" Akasema: "Ndio hili ni tandiko la Mtume wa Mwenyezi Mungu haiwezekani ulikalie wewe najisi unayemshirikisha Mwenyezi Mungu."

Basi akatoka akaingia nyumba ya Fatima(a.s) akamwambia: "Ewe binti wa bwana wa waarabu, hufanyi mapatano na Maquraishi na kuongeza muda wa mkataba ili uwe bibi mkarimu zaidi katika watu?" Akasema" "Mapatano yangu ni mapatano ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Kisha akasema: "Basi waamrishe watoto wako (Hassan na Hussein) wafanye mapatano" Akasema: "Hawajafikia watoto wangu kufanya mapatano, na hakuna yeyote anayeweza kufanya mapatano zaidi ya Mtume(s.a.w.w) .

Akasema: Abu Sufiani "Ewe Abul-Hassan(a.s) naona mambo yamekuwa magumu, nishauri". Akasema Ali(a.s) "Wewe ndiwe mzee wa Maquraish, basi simama msikitini uwapatanishe Maquraish. Halafu wende zako kwenu". Abu Sufiani akasema: "Unaona kua hilo litatosha?" Akasema: "Hapana wallah sioni hivyo, lakini sina jengine zaidi ya hilo". Basi akasimamam Abu Sufiani msikitini akasema: "Enyi watu! Hakika mimi ninataka mapatano kati ya Maquraish". Akapanda ngamia wake akaenda zake, alipofika kwa Maquraish akaulizwa, akawapa kisa, wakasema: "Wallah Ali Bin Abu Twalib hakukufanyia lolote ila kukuchezea tu". Tumefaidika nini kwa hayo uliyasema? Akasema : "Lakini sikupata jengine zaidi ya hilo.

Mtume(s.a.w.w) akaamrisha maandalizi ya vita vya kuipiga Makka. Akawaamrisha watu wajitayarishe. Akaomba dua kwa kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu yapoteze macho na ziepushe habari zetu hizi na Maquraish mpaka tuwaiingilie mjini mwao ghafla". Hatib bin Abu Bal-Taah akawaandikia Maquraish kuwafahamisha habari hizi za vita, lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu akapata habari kutoka mbinguni, akamtuma Ali(a.s) na Zubeir kuchukua barua ka mwanamke aliyetumwa na Hatib. Kisa cha barua hii kimeelezwa zaidi katika Sura ya 60.

Kisha mtume(s.a.w.w) akatoka na jeshi la Waislamu elfu kumi wakiwemo wapanda farasi mia nne. Hakubakia yeyote katika Muhajirina na Ansar. Akamwacha Abudharr El- Ghifari kuwa khalifa wake hapo Madina. Ikatokea Abu Sufiani bin Harith bin Abdul Muttwalib na Abdalla bin Ummay kukutana na Mtume(s.a.w.w) kati ya Makka na Madina wakaomba kukutana na Mtume lakini hakuwapa idhini. Ummu Salama akamwambia Mtume: "Ewe Mtume na Mwenyezi Mungu binamu yako ni mkoi wako aliye mkweo (hao hapo)." Mtume akasema: "Sina haja nao; huyo binamu yangu ndiye aliyevunja heshima yangu na huyo mkoi aliye mkwe wangu ndie aliyesema aliyoyasema juu yangu huko Makka." Basi walipopopata habari hiyo, Abu Sufiani ambaye alikua pamoja na mtoto wake akasema: "Wallah! kama hataniruhusu kusema naye nitakwenda mbali pamoja na mtoto wangu huyu mpaka tufe kwa kiu na njaa." Mtume alipopata habari hiyo akawaonea huruma, hivi akawaruhusu kuzungumza naye na wakasilimu."

Mtume(s.a.w.w) alipopita Dhahran, huku Maquraish wakiwa hawana habari yoyote, alitoka usiku huo Abu Sufiani bin Harb, Hakim bin Huzam na Badil bin Warqai wakipeleleza Abbas alikuwa amekwishasema usiku huo: "Ee kupambaukiwa kubaya kwa Maquraish; kama Mtume akifanikiwa kuwavamia kuingia Makka, basi ndio itakuwa kuangamia kwa Maquraish milele." Akaendelea kusema: " Wacha nitoke huenda nitakamwona, kidomo domo au muuza maziwa au yeyote yule anayeingia Makka ambaye anaweza kwenda kuwapa habari Maquraish wakaweza kumjia Mtume(s.a.w.w) .

Abbas anaendelea kusema: "Wallah nilipokua nazunguuka kwenye miti ya miswaki, mara nikasikia sauti ya Abu Sufiani, Hakim bin Hizam na Badil bin Warqai, nikamsikia Abu Sufiani akisema: "Wallahi sijaona moto kama huu wa leo", akasema Badil: "hii ni mioto ya Bani Khuzaa." Akasema Abu Sufiani "Khuzaa niwachache kuliko hao". Basi nikajua sauti yake nikamwambia: "Ewe Abu Handalah (Abu Sufiani)!" Akasema "Ewe Abul Fadhli" nikasema "Naam!" Akasema" "Labeka! Baba yangu na mama yangu wawe wakombozi wako! Niambie kuna nini nyuma yako? Nikamwambia " Huyo hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu amekuja na kundi la Waislamu wasiopungua Elfu Kumi (10,000).

Akasema : "Sasa unasemaje?" Nikamwambia "Panda juu ya mgongo wa ngamia huyu na nitakutakie amani kwa Mtume: "Kwani naapa kwa Mwenyezi Mungu wakikupata wataikatilia mbali shingo yako." Basi nitatoka naye, kila nilipokuwa nikipita kwenye kikundi fulani walikuwa wakisema huyo ni Ami wa Mtume na yuko juu ya ngamia wa Mtume mpaka tulipofika katika kundi la Umar bin Al-Khattab akasema Umar: "Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ametuwezesha kukupata wewe bila ya taabu wala mapatano yoyote."

Kisha tukafanya haraka tukaelekea kwa Mtume(s.a.w.w) , akatangulia Umar kwa Mtume, akasema : "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu huyu Abu Sufiani adui wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amekuletea bila matatizo yoyote, kwa hiyo wacha nimkate shingo yake!" Nikasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mwacheni kwanza." Lakini Umar alikuwa bado anashikilia tu! Basi nikwambia" "Ngoja ewe Umar". Huyu mtu ni katika watu wa Bani Abdu Manaf, lau angelikuwa ni katika Bani Adi nisingesema, hivyo Akasema Mtume(s.a.w.w) : "Nenda naye mpaka kesho."

Basi kulipopambazuka, nikaenda naye kwa Mtume(s.a.w.w) , alipomwona akasema: "Ole wako ewe Abu Sufiani! Bado hujafikiwa kujua kuwa hapana Mola illa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mkombozi wako ni baba yangu na mama yangu ni huruma zako zilioje na upole wako!, Wallah nimedhani kwamba, lau angelikuwako Mungu mwingine, basi angelitosheleza siku ya vita vya Badr na Uhud". Akasema tena Mtume(s.a.w.w) : "Je, bado hujafikiwa kujua kwamba mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ama hili moyoni mwangu mna kitu". Basi nikamwambia: "Ole wako! Toa shahada ya kweli kabla hawajakiondoa kichwa chako", basi akashahadia."

Mtume(s.a.w.w) akamwambia Abbas: "Nenda naye na umfunge kwenye njia ya jangwani mpaka jeshi la Mwenyezi Mungu lipite." Anaendelea kusema Abbas: "Nikamfunga kwenye jabali, yakawa yanapita makabila mbali mbali na yeye anasema : "Ni nani hawa" nikamjibu: "Aslam, Juhayna na Fulani na ?.." mpaka akapita Mtume(s.a.w.w) katika kikosi cha kijani wakiwemo Muhajirina na Ansar akiwa amezungukwa huko na huko. Akasema Abu Suffiani "Ni kina nani hawa? Nikamwambia: "Huyu ni Mtume, wa Mwenyezi Mungu akiwa pamoja na ndugu yako amekuwa mfalme mkubwa" Nikamwambia: "Ole wako! Huo si ufalme, bali ni utume" akasema "Ndio hivyo, sasa!"

Akaja Hakim bin Hizam na Badil bin Warqai kwa Mtume(s.a.w.w) , wakasilimu na wakambai. Basi Mtume(s.a.w.w) akawatuma kwa Maquraish kuwalingania katika uislamu. Akasema Mtume(s.a.w.w) "Mwenye kuiingia nyumba ya Abu Sufiani iliyoko sehemu ya juu ya Makka, amesalimika na mwenye kuinigia nyumba ya Hakim iliyoko chini ya Makka, amesalimika, na mwenye kufunga mikono yake amesalimika. Alipotoka Abu Sufiani na Hakim kuelekea Makka, Mtume alimpeleka Zubeir bin Awam, akamwamrisha kukita bendera yake sehemu ya juu ya Makka na akamwambia " Usiondoke mpaka nije huko." Kisha Mtume(s.a.w.w) akaingia Makka na akapiga kambi. Akaanza kumpeleka Saad bin Ubadah na kikosi cha Ansar na akampeleka Khalid bin El-Walid pamoja na wale waliosilimu katika Kudhaa na Bani Salim, akamwamrisha kuingia sehemu ya chini ya Makka na kukita bendera yake kando ya majumba.

Mtume(s.a.w.w) akaamrisha wote kuizuwiya mikono yao, wasipigane na mtu yoyote isipokuwa yule anayetaka kupigana nao Na akamrisha kuuliwa watu wane, (1) Abdalla bin Saad bin Abu Sarh (2) Huwayrith bin Nufayl (3) Ibn Khatal (4) Muqbis bin Dhubaba. Pia akamrisha kuuwawa wajakaza wawili waliokuwa wakiimba nyimbo za kumkebehi Mtume. Akasema Mtume(s.a.w.w) : "Wauweni hao hata kama mkiwakuta wamejifunika pazia ya Al-Kaaba." Ali(a.s) akamuuwa Huwayrith bin Nufayl, na mmoja wa wajakazi wawili na mjakazi mwingine akatoroka, akamuuwa Muqbis katika soko na akamkuta Ibn Khatwal amejifunika na pazia ya Al-kaaba, wakatangulia Said bin Hureith na Ammar bin Yassir , Said akatangulia yeye akamuuwa. Abu Sufiani akamuendea Mtume akachukua kikuku chake cha kupandia farasi akakibusu, kisha akasema: "Makombozi wako ni baba yangu na mama yangu hivi hukusikia yale anayosema Saad: "Leo ni siku ya vitakuu, leo wanawake watatekwa."

Mtume(s.a.w.w) akamwambia Ali mfuate, uchukue bendera kwake, na uwe wewe ndiye utakayeingia nayo na uingie nayo kwa upole. Basi ali akaichukua akaingia nayo kama alivyoamrishwa. Mtume(s.a.w.w) alipoingia Makka, alikwenda kusimama kwenye mlango wa Al-Kaaba akasema: "Hapana Mola isipokua Allah hali ya kuwa yupekee yake, ametekeleza ahadi yake. Na amemnusuru mja wake, amevishinda vikundi vya madui hali yakuwa yupeke yake. Jueni kwamba mambo yote na damu inayodaiwa, vyote hivo viko chini ya miguu yangu hii, isipokuwa utumishi wa Al-Kaaba na kunywesha mahujaji. Hivyo viwili vitarudishiwa wenyewe. Jueni kwamba Makka ni yenye kuharamishwa kwa uharamisho wa Mwenyezi Mungu, haikua halali kwa yeyote aliyekuwa kabla yangu na haikua halali kwangu isipokuwa saa moja katika mchana, nayo ni yenye kuharimishwa mpaka Kiyama; Haukatwi mti wake wala hawindwi mnyama wake, wala sihalali kuokota kitu ila kwa atakayekitangaza kisha akasema: "Eee! Majirani wabaya wa Mtume(s.a.w.w) mlikuwa mkifanya mrongo, mkamfukuza na mkamuudhi; kisha hamkutosheka na hayo mpaka mkanifuata katika mji wangu kunipiga vita, basi nendeni nimewasamehe. Wakatoka watu kama walifufuliwa kutoka makaburini na wakaingia katika Uislamu. Mwenyezi Mungu alikuwa amemwezesha Mtume kuwachukua mateka, lakini akaacha, kwa hiyo wakaitwa watu wa Makka 'walioachiwa'. Kisha akaja Ibn Zabary akasilimu.

Imepokewa kutoka kwa Ibn Masud amesema: aliingia Mtume(s.a.w.w) siku ya kuichukua Makaa akakuta katika Al-Kaaba sanamu mia tatu na sitini, akawa anazichoma kwa mti aliokuwa mkononi mwake huku akisema: "Imekuja haki na batil haina msingi wala haitarudi tena, imekuja haki na imeondoka batil, hakika batil ni yenye kuondoka."

Imepokewa kwa Ibn Abbas, amesema: "alipofika Mtume Makka alikataa kuingia Al- Kaaba ikiwa na masanamu akamrisha yatolewe miongoni mwayo yalikuwepo masanamu ya Ibrahim na Ismail(a.s) yakiwa na miti ya kupigia mburuga mikononi mwake. Mtume(s.a.w.w) akasema: " Mungu awatokemeze. Kwa hakika walijua kuwa hawakuwa wakipiga mburuga kabisa." Hadith katika kisa hiki cha ushindi wa Makka ni nyingi na yaliyotangulia ni kama muhtasar tu!


28

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN

SURA LAHAB (MIALI) (NA. 111)

INA AYA 5

Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ ﴿١﴾

1. Imehasirika mikono miwili ya Abu Lahab, naye amekwisha hasirika.

مَا أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُ وَمَا كَسَبَ ﴿٢﴾

2. Haitamfaa mali yake wala alichokichuma.

سَيَصْلَىٰ نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ ﴿٣﴾

3. Atauingia moto wenye miali.

وَامْرَأَتُهُ حَمَّالَةَ الْحَطَبِ ﴿٤﴾

4. Yeye na mkewe hali ya kuchua kuni.

فِي جِيدِهَا حَبْلٌ مِّن مَّسَدٍ ﴿٥﴾

5. Ambaye ana katika shingo yake kamba ya ndifu.

Ubainifu Kiaga kikali kwa Abu Lahab, kwa kuangamia nafsi yake na matendo yake katika moto wa Jahannam, na mkewe hali kadhalika. Sura hii imeshuka Makka.

Aya Na 1

Neno Tab lina maana ya kuhasirika na kuangamia kama alivyosema Jawhari. Na kudumu kuhasirika kama alivyosema Raghib. Imesemwa kuwa maana yake ni kutokuwa na lolote, pia imesemwa kuwa maana yake ni kuepukana na kila la heri. Maana yote hayo yanakurubiana. Mkono wa mtu ndio kiungo ambacho anakitumia kupata makusudio yake, na kazi nyingi za mtu zinanasibishwa kwenye mikono yake. Kwa hivyo kuhasirika mikono yake ni kupata hasara katika chumo lake. Ukitaka unaweza kusema kubatilika kwa amali yake anayoifanya kwa mikono yake miwili, bila ya kufikilia kwenye lengo analolitaka na kukosa kunufaika na kitu chochote katika hiyo amali yake, na kuhasirika nafsi yake kwa kuzuiliwa na wema wa milele.

Kwa hivyo kusema kwake Mwenyezi Mungu : "Imehasirika mikono miwili ya Abu Lahab ni dua ya kumtakia kuangamia na kubatilika ile kazi aliyokuwa akiifanya kwa kujaribu kuizima nuru ya Utume au lile alilokuwa akilipitisha Mwenyezi Mungu. Abu Lahab huyu, ni Abu lahab ami yake Mtume (Abu Lahab bin Abdul Muttwalib). Alikuwa ni adui mkubwa ma Mtume, akimpinga na kumuudhi sana Mtume kwa kiasi anachoweza kwa maneno na vitendo. Ndiye ambaye alimwambia Mtume "Umehasirika wewe!" Aliyasema haya wakati Mtume alipowalingania kwenye Uislamu kwa mara ya kwanza. Ndipo ikashuka Sura na akamrudishia Mwenyezi Mungu maangamizi juu yake. Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa Abu Lahab ni jina lake halisi ijapokuwa hapa limekuja kama kinaya. Inasemekana kama jina lake halisi ni Abdul Uzza, wengine wengine wamesema jina lake halisi ni Abdu Manaf. Sawa zaidi ni yale yaliyosemwa kwamba hiyo ni Kun-ya yake, kwani hilo ni kwa istihzai (kudharau) kwa sababu Abu Lahab inamaanisha kunasibika na miali ya moto, kama vile inavyosemwa, Abul Khayri, Abul Fadhli au Abu Shari, kwa kunasibishwa kwenye Heri, Fadhli na Shari Mwenyezi Mungu aliposema: "Atauingia moto wenye miali" imefahamisha kuwa kuitwa kwake Abu Lahab kumenasibishwa kwenye miali ya moto.

Imesemwa kuwa hakutajwa kwa jina lake ( Abdul-Uzza) kwenye aya, kwa sababu linamaanisha mtumwa wa Uzza, Uzza ni jina la sanamu mojawapo kati ya miungu ya Maquraish. Kwa hiyo ikawa makruh kutaja neno la asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kiasi cha kumnasibisha mtu na asiyekuwa Mungu na hali ya kuwa kila mtu ni 'Abdullah' mtumwa au mja wa Mungu.

Aya Na 2

Mali yake ambayo ameichuma kwa mikono yake miwili ni amali yake.

Aya Na 3

Moto yenye miali ni moto wa Jahannam.

Aya Na 4-5

Inaonekana kuwa makusudio ya aya mbili hizi, ni kwamba huyo mkewe Abu Lahab atauingia moto siku ya Kiyama katika kipambo alichokua akijipamba nacho duniani, nacho kuwa ni yeye alikuwa akichukua matawi ya miba na mengineyo akitupa usiku katika njia ya Mtume kwa ajili ya kumuudhi. Kwa hiyo naye ataadhibiwa kwa moto hali ya kuchukua kuni na katika shingo yake kuna kamba ya ndifu. Katika Majmau amesema: "Kama ikisemwa kwamba je, Abu Lahab alikuwa akilazimiwa kuamini baada ya Sura hii? Na kama angeamini, basi habari za Mwenyezi Mungu kuwa Abu Lahab atauingia moto wenye miali, zingekua za uwongo?"

Jibu: Imani inamlazimu yeye, kwa sababu takilifu ya imani ni yenye kuthibiti juu yake, na kwamba kiaga cha Mwenyezi Mungu ni kwa sharti ya kutoamini. Mushkili huu unatokana na kughafilika kuwa hukumu inayotokana na Mwenyezi Mungu haiwajibishi kutokuwepo kwa hiari ya mtu, wala haiwajibishi kulazimika mtu na kitendo, kwani matakwa ya Mwenyezi Mungu, hayafungamani na hiyari ya mtu, yaani afanya vile anavyotaka. Kwa hiyo ikiwa jambo lenye kufungamana na hukumu ya Mungu, linawajibisha hiyari, basi kuliwacha pia ni hiyari, hata kama halitokei. Imebainika kwamba Abu Lahab alikuwa katika hiyari ya kuamini na kuiokoa nafsi yake na moto ambao alikuwa amehukumiwa kuuingia kutokana na kufuru yake."

Katika Majmau kuhusu aya inayosema: "Na waonye jamaa zako walio karibu" (26:214), Ibn Abbas amesema: "Iliposhuka aya hii Mtume alipanda Jabal Safa akasema: "Enyi wenzangu!" wakasema Maquraish: 'una nini?' Akasema Mtume: "Je, mtaniamini kama nikiwaambia kuwa adui atawavamia asubuhi au jioni?" wakasema Maquraish: "Kwa nini tusikuamini", akasema: "basi mimi ni muonyaji wenu kabla ya kufika adhabu kali." Akasema Abu Lahab: "Kuhasirika kwako ewe Muhammad, hivi umetuitia jambo hili!". Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Sura ya Tabbat.

Katika hiyo Majmau, kutoka kwa Tariq El Muharibi amesema: "Wakati mmoja nilipokuwa katika soko linaloitwa Dhul Mezaj mara nikamwona kijana mmoja akisema: 'enyi watu semeni hapana apasaye kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu' mtafaulu. Huko nyuma kuna mwanaume mmoja akimtupia mawe mpaka miundi yake ikaiva damu na huku anasema: "enyi watu huyo ni muongo msimuamini." Nikauliza, ninani huyu? Nikaambiwa "Huyo ni Muhammad anadai kuwa yeye ni Mtume na huyu ni ami yake Abu Lahab anadai kuwa ni mwongo."

Katika isnadi ya Musa bin Jaffar(a.s) katika hadith ndefu anayotaja alama za Mtume(s.a.w.w) , amesema: "katika alama hizi ni kwamba, wakati iliposhuka Sura ya Tabbat Yada, Ummu Jamil, mke wa Abu Lahab, alimjia Mtume akiwa pamoja na Abu bakr bin Abu Quhafa, Abu Bakr akamwambia Mtume: huyu hapa Ummu Jamil amekasirika anataka kukupiga mawe. Mtume akamwambia Abu Bakr: 'hataniona'.

Yule mwanamke akamwambia Abu Bakr: "yuko wapi sahibu yako?" Abu bakr akamjibu: "yuko pale anapotaka Mwenyezi Mungu"; kisha akasema: "Nimemfuata yeye na lau ningemwona ningempiga mawe, kwani yeye amenitukana. Naapa kwa Lata na Uzza kuwa mimi ni malenga." Kisha Abu Bakr akamuuliza Mtume, kwa nini hakukuona? Akajibu Mtume(s.a.w.w) : "Mwenyezi Mungu ameweka pazia kati yangu na yeye." Imepokuwa hadith iliyokaribu na maana haya katika upande wa Ahli Sunnah.

Katika Tafsiri ya Qummi katika neno lake Mwenyezi Mungu: "Yeye na mkewe hali ya kuchukua kuni.", mke mwenyewe ni Ummu Jamil bint Sakhar, na alikua akimkejeli Mtume kisha ananakili habari kuwapelekea makafiri.

SURA IKHLAS (IKHLASI) (NA. 112)

INA AYA 4

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾

1. Sema huyo Allah ni mmoja tu!

اللَّـهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾

2. Allah ndiye Mwenye kukusudiwa kwa haja zote.

لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾

3. Hakuzaa wala hakuzaliwa.

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾

4. Wala hakuwa yeyote mfano wake.

UBAINIFU

Sura hii inamsifu Mwenyezi Mungu kwa umoja wa dhati, na kumrejea Yeye Mwenyezi Mungu katika haja zote, bila ya kumshirikisha Yeye Mwenyezi Mungu na kitu chochote, si katika dhati yake wala katika sifa zake na wala katika vitendo vyake. Hiyo ndiyo Tawhid ya Kiqur'an ambayo inahusika na Qur'an tukufu ambayo maarifa yote ya Kiislamu yanatokana nayo. Zimukuja hadith nyingi sana juu ya ubora wa Sura hii, kiasi ambacho imepokewa kutoka kwa Shia na Sunni, kwamba Sura hiyo inalingana sawa na theluthi ya Qur'an, kama yatakavyokuja maelezo yake (Inshallah). Sura hii inawezekana kuwa imeshuka Makka au Madina lakini kutokana na baadhi ya yaliyopokewa katika sababu za kushuka kwake, ni kwamba imeshuka Makka.

Aya Na 1

Neno Ahad lenye maana ya mmoja tu; ni sifa yenye kuchukuliwa katika neno Wahid lenye maana ya moja lakini neno Ahad linatumiwa juu ya kitu ambacho hakihisabiki yaani hakikubali wingi si kwa dhahiri wala kwa kiakili. Kwa hiyo neno Ahad haliingii katika idadi kinyume cha neno Wahid, kwani kila moja ina ya pili na ya tatu na kadhalika. Ama katika neno Ahad kila unapokadiria kitu cha pili, kinakuwa ni hicho hicho hakizidi kitu. Kwa mfano mtu akisema: "Ma Jaani Minal Qaumi Ahad" yenye maana hakunijia mimi yeyote katika watu, atakuwa anakanusha kuja kwa yeyote katika wao; wawili, watatu, au zaidi, lakini kama akisema :Ma Jaani Wahidu Minhum," yenye maana hakunijia mmoja wao, hapo atakuwa anakanusha kuja kwa yeyote mmoja tu!, lakini si wawili au zaidi. Kwa maana hayo neno hili ni lazima litumike pamoja na kutegemezwa kwenye kitu kingine isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu linatumika bila ya kutegemezwa kwenye kitu kingine chochote.

Aya Na 2

Asili ya neno Swamad, ni kukusudia pamoja na kutegemea. Wameifasiri Swamad ambao ni sifa kwa maana nyingi. Zaidi wameeleza kuwa ni Bwana mwenye kukusudiwa kwa haja zote. Kwa kuwa katika aya hili neno hili limetajwa bila ya kutegemezwa katika neno jengine, basi moja kwa moja maana yake ni mwenye kukusudiwa kwa haja zote. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyepatisha kila chenye kupatikana (kisichokuwa Yeye), basi kila kisichokuwa Yeye kitakua kinakusudia kwake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Fahamuni kuwa kuumba (ni kwake tu!) na amri zote ni zake ."(7:54).

Na amesema tena "Na kwamba mwisho (wa kila jambo) unarejea kwa Mola wako. "(53:42).

Ama kulileta tena neno Allah katika aya hii kwa kusema: "Allah ndiye Mwenye kukusudiwa katika haja zote." Na wala asiseme ' Yeye ndiye Mwenye kukusudiwa kwa haja zote', hiyo ni kuonyesha kwa kila moja kati ya jumla hizi mbili inaweza kutosheleza katika kumweleza Mwenyezi Mungu. Aya hizi mbili zinamsifu Mwenyezi Mungu kwa sifa ya dhati ya kitendo. Kwa hiyo neno Allahu Ahad lenye maana ya Mwenyezi Mungu ni mmoja, ni sifa ya dhati yake na Mwenyezi Mungu na Allahu Swamad lenye maana ya Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kukusudiwa kwa haja zote, ni sifa ya kitendo ambayo inamsifu Mwenyezi Mungu kwa kuishia kwake kila kitu. Pia imesemwa kuwa maana ya neno Swamad ni ambaye hali, wala hanywi, halali, hazai wala hazaliwi. Kwa hiyo aya inayofuata (hakuzaa wala hakuzaliwa), ni tafsiri ya Swamad.

Aya Na 3-4

Aya hizi mbili zinakanusha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amezaa kitu kwa kugawa kitu au kutoa kitu kutokana na Yeye, kama wanavyodai wakristo kuhusu Masih(a.s) kuwa eti yeye ni mtoto wa Mungu au kama wanavyodai waabudu masanamu kuhusu baadhi ya waungu wao kuwa ni watoto wa Mungu. Vile vile aya hizi mbile zinakanusha kuwa Yeye amezaliwa au ametokana na kitu kingine, kama wanavyodai waabudu masanamu. Katika miungu yao, kuna Mungu baba, Mungu mama na Mungu mwana. Pia aya hizi zinakanusha kuwa kuna anayefanana na Mungu katika vitendo vyake, kama walivyodai akina Firaun na Namrud kuwa eti ni miungu. Kuzaa ni namna moja ya kugawanyika kwa maana yoyote ile utakavyofasiri, itakuwa yule mwenye kuzaliwa ni lazima aambatane na yule aliyemzaa, kwani itakuwa yule mwenye kuzaliwa ni fungu la yule mwenye kuzaa na bila shaka itakuwepo haja ya kuhitajiana kati yo mafungu hayo, na Mwenyezi Mungu (s.w.t) hahitaji chochote isipokuwa vitu vyote vinamhitajia. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu hakuzaa.

Ama kuwa hakuzaliwa, ni kwamba kinachozaliwa, ni lazima kitakuwa kinamuhitajia yule aliyekizaa, na Mwenyezi Mungu siyo muhitaji, hivyo hakuzaliwa. Ama kuwa hana kifano, ni kwamba hakuwezi kuhakikika kupwekeka kwake ni kujitosheleza kwake ikiwa yuko mwenye kufanana na Yeye. Mwenyezi Mungu pekee ndiye Mwenye kukusudiwa kwa haja zote, hivyo hana kifano. Kwa hiyo imebainika kuwa aya hizi mbili zinaeleza maana ya Swamad na kuthibitisha umoja wake Mwenyezi Mungu katika dhati Yake na sifa zake na vitendo vyake na kuongeza yale yanayoambatana na ukubwa wake na utukufu wake. Kwa hiyo Sura nzima hii, inaeleza sifa yake Mwenyezi Mungu kwamba Yeye ni mmoja tu. Pia imesemekana kwamba maana ya neno Kuf-wan ni mke, kwa sababu mke ni kifano cha mume, kwa hiyo aya inakuwa katika maana ya aya inayosema: "Utukufu wa Mola wetu umetukuka kabisa, hakujifanyia mke wala mtoto ."(72:3).

Utafiti Wa Hadithi Katika Kafi kutoka kwa Muhammad bin Muslim kutoka kwa Abu Abdillah(a.s) amesema: "Hakika Mayahudi walimuuliza Mtume wakasema. 'Tusifie Mola wako! Akaongojea M tume(s.a.w.w) siku tatu bila kuwajibu, kisha ikashuka ' Qulhuwallah' mpaka mwisho." Katika Ihtiyaj imepokewa kutoka kwa Askary(a.s) , kwamba aliyemuuliza Mtume ni Abdallah bin Suriyyah (Myahudi). Katika baadhi ya riwaya za ahli Sunnah ni kuwa muulizaji alikuwa Abdallah bin Salam, alimuuliza Mtume alipokuwa Makka kisha akasilimu, lakini akaficha imani yake. Riwaya nyingine katika Sunni zinasema kuwa ni watu katika Mayahudi na nyengine zinasema waabudu masanamu waliouliza ni watu wa Makka wanaowamshirikisha Mungu.

Katika Ma'an kwa isnadi kutoka kwa Asbagh bin Nabata kutoka kwa Imam Ali(a.s) amesema: " Sifa za Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni Qulhuwallah". Na katika Ilal kwa isnadi kutoka kwa Imam Sadiq(a.s) katika hadithi; kwamba Mwenyezi Mungu alimwambia Mtume soma Qulhuwallah kwani hiyo Qulhuwallah ni sifa yangu. Imepokewa kutoka kwa Musa bin Jaffer(a.s) kwa maana hayohayo, na zimepokewa riwaya nyingi sana kwa maana hayo katika njia za Ahli Sunnah kutoka kwa Masahaba wengi, kama vile Ibn Abbas, Abu Dardai, Jabir bin Masud, Abu Sais El- Khudr, Muadh bin Anas, Abu Ayyub, Abu Amama na wengineo. Vile vile zimepokewa hadithi nyingi kwa upande wa Shia. Wameieleza Sura hii kuwa inakuwa sana na theluthi ya Qur'an kwa njia tofauti, moja wapo ni kwamba, maelezo yaliyomo katika Qur'an yanaeleza misingi mitatu: Tawhid, Utume na Marejeo ya Akhera, na Sura hii (Ikhlas) inaeleza moja ya msingi hiyo, Tawhid.

Katika Tawhid imepokewa kutoka Amirul Muminin Ali(a.s) amesema: "Nilimwona Khidhr(a.s) katika usingizi siku moja kabla ya vita vya Badri, nikamwambia: Nifundishe kitu kitakachonilinda na maadui, akasema: " Sema; Yaa huwa man la huwa illa huu ewe ambaye hapana mwengine ila Yeye." Basi nilipoamka nikamuhadithia Mtume(s.a.w.w) , akaniambia ewe Ali umefundishwa jina tukufu. Kwa hiyo likawa katika ulimi wangu siku ya vita vya Badri. Hakika Amirul Muminin alisoma Qulhuwallah, alipomaliza akasoma "(Ya! Huwa man la huwa illa huu! Ighfirliy wansurni alal qawmil kafirin)." Ewe ambaye hapana mwengine ila yeye nisamehe na uninusuru na makafiri. Katika Usulul Kafi kwa isnadi yake kutoka kwa Daud bin El-Qassim Jaffari, amesema: "Nilimuuliza Abu Jaffar(a.s) : nini maana ya Swamad, akasema: "ni Bwana Mwenye kukusudiwa kwa kichache na kingi ."

Katika tafsiri ya Swamad maana nyengine zilizopokewa kutoka kwa Maimamu(a.s) . Kutoka kwa Baqir(a.s) : amesema Swamad ni Bwana Mwenye kutiiwa ambaye hakuna zaidi yake. Na kutoka kwa Husayn(a.s) Swamad ni ambaye hana mfano, ambaye halali na ambaye hakuwacha kuwa ni Mwenye kupatikana na wala hatawacha kuwa ni Mwenye kupatikana. Kutoka kwa Assajjad(a.s) : Swamad ni yule ambae kitu hukiambia kuwa kikawa na Swamad ni yule ambaye amezusha vitu na akaviumba namna moja na vinahitalifiana kwa namna mbali mbali na kwa kiume na kike. Asili ya maana ya neno Swamad ni ile tuliyoipokea kutoka kwa Abu Jaffer wa pili, kutokana na maana hasa yaliyomo katika mada yake nayo ni kukusudiwa. Kwa hivyo maana mbalimbali yaliyopokewa na kunakiliwa kutoka kwa Maimamu(a.s) katika tafsiri ya Maimamu(a.s) yanalazimisha kuwa maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusudiwa katika kila haja. Kwa hiyo vitu vyote vinakomea kwake, bila ya yeye kuhitaji chochote.

Katika Tawhid imepokewa kutoka kwa Wahab bin Wahab El- Qurashi naye amepokea kutoka kwa Assadiq(a.s) naye kutoka kwa wazazi wake(a.s) kwamba watu wa Kuffa walimwandikia Husayn(a.s) wakimuuliza maana ya Swamad, kisha akawarudishia majibu hivi: "Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, amma baadu; msingilie Qur'an wala msiifanyie mjadala bila ya kuwa na elimu yoyote, kwani nimemsikia babu yangu (Mtume) akisema: Mwenye kusema juu ya Qur'an bila ya elimu yoyote, basi na ajichagulie mahali pake katika moto. Na Mwenyezi Mungu ametafsiri Swamad aliposema: "Allah ni mmoja tu! Allah ndiye Mwenye kukusudiwa kwa haja zote, kisha akaifasiri kwa kusema: Hakuzaa wala hakuzaliwa wala hakuwa kifano cha mtu yoyote". Katika hiyo Tawhid kwa isnadi yake kwa Ibn Abu Umair kutoka kwa Musa bin Jaffar(a.s) kwamba yeye amesema "Jua kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni mmoja tu! Mwenye kukusudiwa haja zote, hakuzaa akarithiwa wala hakuzaliwa akashirikishwa."

Katika hotuba nyingine ya Ali(a.s) anasema: "Hakuzaliwa asijekuwa na mshirika katika utukufu wake, wala hakuzaa ili asiwe mwenye kurithiwa .." katika maana hayo yaliyotangulia kuna riwaya nyingi.

SURA FALAQ (ASUBUHI) (NA. 113)

INA AYA 5

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾

1. Sema ninajilinda kwa Mola wa asubuhi.

مِن شَرِّ مَا خَلَقَ ﴿٢﴾

2. Na shari ya alichokiumba.

وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ ﴿٣﴾

3. Na shari ya usiku wa giza unapoingia.

وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ ﴿٤﴾

4. Na shari ya wenye kupuliza katika mafundo.

وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ ﴿٥﴾

5. Na shari ya hasidi anapohusudu.

UBAINIFU

Aliamrishwa Mtume kujikinga na shari zote na baadhi ya shari nyengine maalum. Sura hii imehuka Madina, kutokana na ilivyopokewa katika sababu za kushuka kwake.

Aya Na 1

Mwenyezi Mungu ametumia neno Falaq lenye maana ya kupasua kwa maana ya asubuhi, kwa sababu asubuhi inapasuliwa kutoka katika giza. Kwa hivyo maana yake ninajilinda kwa bwana wa asubuhi ambaye anaipasua. Na ibara hii inaamanisha kutaka hifadhi na shari ambayo inafunika heri. Imesemwa kuwa maana ya Falaq ni kila kinachoumbwa na kupatikana. Kupatikana kitu kunakuwa baada ya kukosekana, yaani kupatikana kumepasua kukosekana, na kutoa kile kinachopatikana. Pia imesemwa kuwa maana ya Falaq ni shimo katika Jahannam na baadhi ya riwaya zimetilia nguvu hilo.

Aya Na 2

Maana ya shari ya alichokiumba, anakusudia yoyote mwenye kuchukua shari katika watu, majini, wanyama na viumbe vinginevyo vyenye shari.

Aya Na 3

Shari imenasibishwa na usiku kwa sababu giza linmsaidia mshari katika shari yake, kwa vile linamsitiri, kwa hiyo usiku unakuwa na shari zaidi kuliko mchana, na mtu anakuwa mnyonge kuweza kuikabili shari wakati wa usiku kuliko mchana. Mwenyezi Mungu ametanguliza kutaja shari ya usiku baada ya kutaja shari ya kiumbe kwa kuzidisha uzito wa shari ya usiku. Mwenyezi Mungu ametilia umuhimu katika Sura hii namna tatu za shari (shari ya usiku, shari ya wachawi na shari ya hasidi), kwa vile watu wanaghafilika sana katika vitu hivi.

Aya Na 4

Yaani wanawake wachawi ambao wanafanya uchawi wao kwa namna hiyo ya kupuliza katika mafundo. Wamehusishwa wanawake na uchawi kwa sababu wanawake walikuwa wanapendelea uchawi zaidi kuliko wanaume. Hii inathibitisha kuweko athari za uchawi, kwa jumla; kama vile alivyosema Mwenyezi Mungu katika kisa cha Haruta na Maruta: "Na wakajifunza kwao mambo ambayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawakua ni wenye kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Allah ". (2 : 102).

Na vile vile athari hii inadhihirika katika kisa cha uchawi wa Fir'aun. Pia imesemwa kuwa maana ya wanawake wenye kupuzia katika mafundo ni wanawake ambao wanabadilisha maoni ya waume zao katika yale wanayoyataka wao tu! Kwa hiyo maoni ni mafundo na kupuzia katika mafundo ni kuyatatua maoni hayo. Lakini kauli hii iko mbali na maana.

Aya Na 5

Inasemekana kuwa aya hii inakusanya msaidizi wa hasidi na husuda, kwa hiyo msaada wa hasidi ni namna mojawapo ya husuda.

Utafiti Wa Hadithi Katika Durril Manthur, ametoa Abdi bin Hamid kutoka kwa Zaid bin Aslam, Amesema: "Mtu mmoja katika Mayahudi alimroga Mtume(s.a.w.w) akawa hajisikii vizuri, akajiwa na Jibril, akamteremshia Sura mbili (Nas na Falaq), akasema Jibril, hakika mtu katika Mayahudi amekufanyia uchawi na uko katika kisima Fulani." Basi Mtume akamtuma Ali akaulete ule uchawi. Jibril akamuamrisha Mtume kuufungua huku akisoma aya mpaka Mtume akasimama akiwa amechangamka. Mfano wa hadith hii unapatikana katika Twibbul Aimma kwa isnadi hya Muhammad bin Sinan kutoka kwa Mufadhal naye amepokea kutoka kwa Imam Sadiq(a.s) , na riwaya nyingi kutoka katika njia za Ahli Sunnah kwa tofauti ndogo tu! Baadhi ya riwaya za pande zote mbili zinasema kuwa Mtume alimpeleka pamoja na Ali, Ammar bin Yaasir na Zubeir.

Watu wengine wameiitilia mashaka hadith hii, wakisema kwamba Mtume ni mwenye kuhifadhiwa na kuathiriwa na uchawi. Lakini vipi wanatia mashaka na hali Mungu aliposema: "Na madhalimu wakasema nyinyi hamumfuati ila mtu aliyerogwa. Tazama jinsi wanavyokupigia mifano (isiyoelekea), basi wamepotea wala hawataweza (kushika) njia iliyonyooka : (25:8-9).

Hapa Mungu anamkinga Mtume kwamba makusudio kwa aliyerogwa ni kuharibikiwa na akili kwa uchawi. Ama kuathirika na uchawi kwa maradhi yanayompata katika mwili wake, na mfano wa hayo, hakuna dalili ya kuhifadhiwa kwake.

Katika Majmau imepokewa kwamba Mtume mara nyingi akiwatakia hifadha Hassan na Hussein kwa kuwasomea Sura mbili hizi. Na katika hiyo Majmau kutoka kwa Uqba bin Amir amesema; 'Amesema Mtume(s.a.w.w) ': "Nimeteremshiwa aya ambazo hazijatereremshwa mifano yake, nazo ni Almuawwidhatyn (Qul audhu bi Rabbi nnasi na Qul audhu bi Rabbil Falaq)."

Hadith hii inapatikana katika Sahih na imetegemezwa kwa Tirmidhi, Nasai na wengineo katika Durril Manthur. Na vile vile imepokewa hadith kwa maana haya kutoka kwa Tabrani kwa wasta wa Ibn Masud. Na huenda maana ya kuwa hazijateremshwa mifano yake, ni katika aya za hifadhi tu; lakini si katika Qur'an yote.

Katika Durril Manthur ametoa Ahmad, Bazzar, Tabrani na Ibn Murdawayh katika njia sahih imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas na Ibn Masud, kwamba huyo Ibn Masud alikuwa akizifuta Muawwidhatayn (Nas and Falaq) katika msahafu na alikuwa hazisomi; kisha akasema Suyuti amesema Bazzar; "Hakuna sahaba yeyote aliyemfuata Ibn Masud. Na imethibitishwa kutoka kwa Mtume, kwamba yeye alikuwa akizisoma Sura hizo mbili katika swala na zimethibiti katika msahafu. Katika Tafsiri ya Qummi kwa isnadi yake kutoka kwa Abu Bakr El-Hadhrami amesema: "Nilimwambia Abu Jaffar(a.s) ; Hakika Ibn Masud alikuwa akifuta Muawwidhatayn katika msahafu. Akasema hakika baba yangu alikuwa akisema; "Hakika Ibn Masud ameyafanya hayo kwa maoni yake tu!"

Ziko riwaya nyingi katika njia ya Kisunni na Kishia zilizopokewa na vikundi vyote vya Kiislamu Mutawatir Qat'iyy kwamba Muawwidhatayn ni katika Qur'an. Wametia mashaka baadhi ya wakanushaji juu ya muujiza wa Qur'an kwamba, kama Qur'an ingekuwa ni muujiza kwa ufasaha wake, basi kusingekuweko na hitilafu kuwa Sura mbili hizi ni katika Qur'an. Wamejibiwa kwamba kukubaliana watu wengi kuwa ni katika Qur'an (Tawatur Qat'iyy) imetosha katika hilo na kwamba haikunukuliwa kutoka kwa yeyote kuwa Sura hizo hazikumshukia Mtume au kwamba Sura hizo si muujiza kutokana na ufasaha wake, bali wmaesema tu; kuwa ni fungu katika Qur'an na hilo limeshindwa nguvu na hadith Mutawatir.

Katika Durril Manthur ametoa Ibn Jaffar kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kwamba yeye amesema Falaq ni kisima katika Jahannam kilichofunikwa. Na maana yake siyo moja katika hadith; kuna riwaya nyenginezo zinasema kuwa Mtume amesema: Falaq ni mlamgo katika moto, unapofunguliwa huwaka na hadith nyengine inasema kuwa ni kisima katika Jahannam, inapowaka Jahannam nacho huwa na moto. Katika Majmau imesema kuwa Falaq ni kisima katika Jahannam watataka hifadhi watu wa Jahannam kutokana na joto lake kali. Imepokewa kutoka kwa Abu Hamza na Ali bin Ibrahim katika Tafsiri zao na katika Tafsiri ya Qummi kutokana na baba yake kutoka kwa Naufal naye kutoka kwa Sukuni naye kutoka kwa Abu Abdillahi(a.s) amesema: "Amesema Mtume(s.a.w.w) :'Unakurubia ufakiri kuwa ni ukafiri na husuda inakurubia kushinda Qadar ."

Hadith hii pia imepokewa kutoka kwa Anas kwa lafdh hiyo na katika Uyun kwa isnadi yake kutoka kwa Sultiy kutoka kwa Ridha(a.s) kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) Amesema: "Hasadi inakurubia kushinda Qadar". Na katika Durril Manthur ametoa Ibn Shayba kutoka kwa Anas, amesema: 'Amesema Mtume(s.a.w.w) ': "Hakika Husuda Inakula Mambo Mema Kama Vile Moto Unavyokula Kuni ."

SURA NAS ( WATU) (NA: 114)

INA AYA 6

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾

1. Sema ninajilinda kwa Bwana, Mlezi wa watu.

مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢﴾

2. Mfalme wa watu.

إِلَـٰهِ النَّاسِ ﴿٣﴾

3. Mungu wa watu.

مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ ﴿٤﴾

4. Na shari ya mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma.

الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ ﴿٥﴾

5. Ambaye hutia wasiwasi katika nyoyo za watu.

مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ ﴿٦﴾

6. (Ambaye ni) katika majini na watu.

UBAINIFU

Ni amri kwa Mtume(s.a.w.w) ya kujilinda na hari ya mwenye kutia wasiwasi. Sura hii imeshuka Madina kama Sura iliyotangulia. Haya ni kwa mujibu wa ufahamisho wa sababu za kuteremshwa kwa Sura hii. Bali pia imefahamika kutokana na riwaya kwamba Sura hii na Falaq zimeshuka pamoja.

Aya Na 1 – 3

Ni tabia ya mwanadamu, anapokabiliwa na shari ( hatari) anayoiogopea nafsi yake, na anapojiona kuwa yeye ni mnyonge, huwa anataka msaada kwa yule ambaye anamwona kuwa ana nguvu zaidi za kuweza kumlinda na kumkinga na shari hiyo isimfike. Kwa hiyo anaeyefaa kumtegemea na kumshikilia katika jambo hilo ni mmoja kati ya watatu. Ama mlezi ambaye anamlea na kumtekelezea haja zake zote; na miongoni mwa yale anayohitajia katika maisha yake ni kumkinga na mambo yanayomwogopesha; na hii ni sababu inayobaki milele katika nafsi yake ( kutaka awe na mwenye kumtegemea). Au mwenye nguvu ya utawala - nguvu za kupinduukia na utawala unaokubalika - amkinge anapotaka kinga, na amwepushie shari kwa kufuatana na uwezo wake, kama mfalme yeyote anavyofanya. Na hii vile vile ni sababu inayobaki milele katika nafsi yake (kutaka awe na mwenye kumtegemea). Ama, wa tatu, ni Mungu mwenye kuabudiwa, kwani lazima ya kuabudiwa Mungu hasa akiwa ni mmoja asiyekuwa na mshirika, ni kumpwekesha, kutomwomba asiyekuwa Yeye, asitake isipokuwa alitakalo Yeye, wala asifanye isipokuwa alipendalo Yeye.

Na mwenyezi Mungu (s.w.t) ni Mlezi wa watu, Mfalme wa watu na Mungu wa watu, kama alivyoikusanya sifa tatu katka neno lake; "Huyu ndiye Allah, Mlezi wenu. Uflame ni wake, hakuna Allah ila Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi? " (39:6).

Halikadhalika ameishiria sababu za ulezi wake na uungu wake kwa kusema:"(Yeye ndiye) mola wa Mashariki na Magharibi hakuna Allah ila Yeye, basi mfanye kuwa mlinzi(wako) " (73:9).

Na ameishiria sababu ya Ufalme wake kwa kusema: "Ni wake Ufalme wa mbingu na ardhi, na mambo yote yanarudishwa kwa Allah " (57:5).

Kwa mwanadamu akitaka kujilinda kwa mlezi na shari inayomwogopesha, basi mwenyezi Mungu (s.w.t), ndiye Mlezi. Hakuna Mlezi isipokuwa Yeye. Na akitake kujilinda kwa mfalme, basi Mwenyezi Mungu ndiye Mfalme wa haki. Ufalme ni wake na Utawala ni wake. Na pindi mwanadamu atakapotaka Mungu amlinde, basi yeye ndiye Mungu; hapana mwengine. Kyw hiyo kusema kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t): "Sema ninajilinda kwa Bwana Mwenye kuwalea watu?" mpaka mwisho. Ni amri kwa Mtume(s.a.w.w) kutake hifadhi Kwake, kwani huyo Mtume ni katika watu na Yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mlezi wa watu, Mfalme wa watu na Mola wa watu. Na kutokana na hayo yaliyotangulia, imetudhhirikia sifa zote tatu za Mwenyezi Mungu; na zimetajwa sifa hizo tatu kwa mpangilio:

Kwanza : Mlezi - kwa vile mtu anakuwa karibu na mlezi na anakuwa ndiye anayemuhusu zaidi kwa utawala.

Pili : Mfalme- kwa vile ingawaje hayuko karibu zaidi na mtu, lakini anakuwa ni mtawala, hivyo anakuwa ni mtawala wa kila mtu ambaye hana mtu wa karibu wa kumkinga. Na mwisho, ni Mungu- kwa vile Yeye ni walii anayekusudiwa na watu kwa amali bila ya kuwa na mshirika katika ibada.

Kutokana na kutajwa sifa zote moja kwa moja bila ya kuweka kiunganishi atfu inaonyesha kuwa sifa zote hizo tatu pamoja na ni sababu ya kujikinga na shari. Yaani ulinzi na hifadhi unatokana na sifa hizo tatu, na Mwenyezi Mungu pekee ndiye mwenye kuzikusanya: ni Mlezi, ni Mfalme , na ni Mungu, kama ilivyoelezwa katika Sura ya (112:2): "Allah ndiye Mwenye kukusudiwa kwa haja zote"

Aya Na 4

Imesemwa katika Majmau kuwa wasiwasi ni mazungumzo ya nafsi kama sauti yenye kujificha. Mwenye kurejea nyuma (shetani), ni yule mwenye kujificha baada ya kudhihiri. Imesemwa kuwa shetani ameitwa "mwenye kurejea nyuma" kwa sababu anapomtia mtu wasiwasi, mtu yule akimtaja Mwenyezi Mungu, basi hurudi nyuma; na kama akighafilika, basi shetani hurudi tena kumtia wasiwasi.

Aya Na 5

Wasiwasi unafungamana na msingi wa utambuzi wa mtu, na in nasi yake (moyo). Mwenyezi Mungu ametumia neno Suddor yaani vifua, kama alivyosema katika Sura ya (22:46): "lakini zimepofuka nyoyo zao ambazo zimo vifuani ??"

Aya Na 6

Kila mwovu anafaa kuitwa shetani hata kama ni binadamu , kama alivyosema Mwenyezi Mungu katika Sura ya (112:6) "Mashetani katika watu na katika majini"

Utafiti Wa Hadithi Katika Majmau Abu Khadija amepokea kutoka kwa Abu Abdillah(a.s) kwamba amesema: "Alikuja Jibril kwa Mtume na hali ya kuwa Mtume hajisikii vizuri; akamwagua kwa Almuawwidhatayn (Sura Nas (114) na Falaq (113) na Qul huwa Allah (112) Akasema Jibril: "kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Mwenyezi Mungu akupoze kila ugonjwa unaokuudhi. Akasoma Qul audhubi Rabbi n-nasi mpaka mwisho."

Na imepokuwa kutoka kwa Anas bin Malik, amesema: "Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: "Hakika shetani hukweka pua yake juu ya moyo wa binadamu. Kama binadamu akimtaja Mwenyezi Mungu, shetani hurudi nyuma; na kama akimsahau, basi hummeza. Basi huyo ndiye mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma." Na katika hiyo Majmau, imepokewa kya Iyash, kwa isnadi yake kutoka kwa Aban bin Taghlab kutoka kwa Jaffar bin Muhammad(a.s) amesema: "Amesema Mtume(s.a.w.w) : "Hapana Mumin yeyote ila pana katika moyo wake, ulioka kifuani mwake, tundu mbili: tundu moja inapulizwa na Malaika na tundu nyingine unapulizwa na mwenye kutia wasiwasi, mwenye kurejea nyuma." Mwenyezi Mungu (s.w.t) humpa nguvu Mumin kwa Malaika kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t): "Na akawatia nguvu kwa roho atokaye kwake " (58:22).

Katika Amali ya Saduq kwa isnadi yake kwa Imam Sadiq(a.s) , amesema: "Iliposhuka aya hii: "Na ambao wanapofanya uchafu au kudhulumu nafsi zao humkumbuka Allah " (3:135), Iblis alipanda jabali linaloitwa Thuwayr lililoko Makka, akapiga kelele kuwaita maafriti wake, wakakusanyika na kumuuliza: "Umetuitia nini ewe bwana wetu?"

Akasema: "Imsehuka aya hii, basi nani awezaye kupambana nayo?" Akasimama Afriti akasema: "Mimi naiweza. Nitapambana nayo kwa namna kadhaa." Akasema Iblis: "Sio yako" Akasimama mwengine akasema hivyo hivyo, Iblis akamwambia: "Hapana! hutoiweza." Akasimama Wasiwasil Khannas (mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma) akasema:

"Mimi naiweza." Akaulizwa: "Vipi utaiweza?" Akasema: "Nitawapa ahadi na kuwatamanisha kufanya hayo madhambi mpaka wafanye. Pindi watakapofanya madhambi hayo, nitawasahaulisha kuomba msamaha." Hapo basi Iblis akamwambia: "Wewe kweli utaiweza Aya hiyo." Akamstakabadisha mpaka siku ya Kiyama.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU


YALIYOMO

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 1

DIBAJI YA AL-MIZAN 1

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 5

SURAT NABA (HABARI) 5

SURAT NABA (HABARI) (NA. 78) INA AYA 40 5

Aya ya 1 -16 5

UBAINIFU 5

Aya Ya 1 6

Aya Ya 2-3 6

Aya Ya 4-5 7

Aya Ya 6 7

Aya Ya 7 8

Aya Ya 8 8

Aya Ya 9 8

Aya Ya 10 9

Aya Ya 11 9

Aya Ya 12: 9

Aya Ya 13: 9

Aya Ya 14 9

Aya Ya 15 9

Aya Ya 16 9

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 10

SURAT NABA' (HABARI) 10

SURAT NABA' (HABARI)(NA. 78) 10

Aya 17 - 40 10

UBAINIFU 11

Aya Ya 17 11

Aya Ya 18 11

Aya Ya 19 11

Aya Ya 20 12

Aya Ya 21 12

Aya Ya 22 12

Aya Ya 23 12

Aya Ya 24-25 12

Aya Ya 26 12

Aya Ya 27 – 28 13

Aya Ya 30 13

Aya Ya 31-35 13

Aya Ya 36 13

Aya Ya 37 14

Aya Ya 38 14

Aya Ya 39 17

Aya Ya 40 17

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 19

SURAT NAAZIA'AT (KUTOA KWA NGUVU) 19

SURA NAAZIA'AT (KUTOA KWA NGUVU) (NA. 79 ) 19

INA AYA 46 19

Aya 1 - 41 19

UBAINIFU 21

Aya Ya 1-5 21

Aya ya 1 21

Aya ya 2 21

Aya ya 3 21

Aya ya 4 22

Aya ya 5 22

Aya Ya 6-7 24

Aya Ya 8-9 24

Aya Ya 10 25

Aya Ya 11 25

Aya Ya 12 25

Aya Ya 13-14 25

Aya Ya 15 25

Aya Ya 16 26

Aya Ya 17 26

Aya Ya 18 26

Aya Ya 19 26

Aya Ya 20 26

Aya Ya 21 26

Aya Ya 22 26

Aya Ya 23 26

Aya Ya 24 26

Aya Ya 25 27

Ay Ya 26 27

Aya Ya 27 27

Aya Ya 28 27

Aya Ya 29 27

Aya Ya 30 28

Aya Ya 31 28

Aya Ya 32 28

Aya Ya 33 28

Aya Ya 34 28

Aya Ya 35 28

Aya Ya 36 28

Aya Ya 37 - 41 28

Aya Ya 42 - 46 42 30

UBAINIFU 31

Aya Ya 42 31

Aya Ya 43 31

Aya Ya 44 31

Aya Ya 45 32

Aya Ya 46 32

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 33

SURA ABASA (ALIFINYA USO (NA. 80) 33

INA AYA 42) 33

AYA 1-16 33

UBAINIFU 33

Aya Ya 1-2 34

Aya Ya 3-4 34

Aya Ya 5 -7 34

Aya Ya 8-9 35

Aya Ya 11 - 12 35

Aya Ya 13-14 35

Aya Ya 15 35

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 38

SURA ABASA (ALIFINYA USO) 38

Aya Ya 17-42 38

UBAINIFU 39

Aya Ya 17- 42 39

Aya Ya 17 39

Aya Ya 18 40

Aya Ya 19 40

Aya Ya 20 40

Aya Ya 21 41

Aya Ya 22 41

Aya Ya 23 41

Aya Ya 24 41

Aya Ya 25-32 42

Aya Ya 33 42

Aya Ya 34-37 42

Aya Ya 38-39 42

Aya Ya 40 42

Aya Ya 41 42

Aya Ya 42 42

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 44

SURA TAKWIR (KUKUNJA) (NA. 81) 44

INA AYA 29 44

Aya 1 - 14 44

UBAINIFU 44

Aya Ya 1 45

Aya Ya 2 45

Aya Ya 3 45

Aya Ya 4 45

Aya Ya 5 45

Aya Ya 6 45

Aya Ya 7 45

Aya Ya 8 46

Aya Ya 10 46

Aya Ya 11 46

Aya Ya 12 46

Aya Ya 13 46

Aya Ya 14 46

Aya Ya 15-29 47

UBAINIFU 47

Aya Ya 15 - 16 48

Aya Ya 17 48

Aya Ya 18 48

Aya Ya 19 -21 48

Aya Ya 22 48

Aya Ya 23 49

Aya Ya 24 49

Aya Ya 25 49

Aya Ya 26 49

Aya Ya 27 50

Aya Ya 28 50

Aya Ya 29 50

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 52

SURA INFITAR (KUPASUKA) (NA. 82) 52

INA AYA 19 52

UBAINIFU 53

Aya Ya 1 53

Aya Ya 2 53

Aya Ya 3 53

Aya Ya 4 53

Aya Ya 5 53

Aya Ya 6-8 54

Aya Ya 7 54

Aya Ya 8 55

Aya Ya 9 55

Aya Ya 13 -14 56

Aya Ya 15 56

Aya Ya 16 56

Aya Ya 17 56

Aya Ya 18 56

Aya Ya 19 56

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 58

SURA MUTAFFIFIN (WAPUNGUZAJI VIPIMO) (NA. 83) 58

Aya ya 1-21 58

UBAINIFU 59

Aya Ya 1 59

Aya Ya 2-3 59

Aya Ya 4-5 59

Aya Ya 7 -10 60

Aya Ya 11 61

Aya Ya 12 61

Aya Ya 13 61

Aya Ya 14 61

Aya Ya 15 61

Aya Ya 16 62

Aya Ya 17 62

Aya Ya 18-20 62

Aya Ya 21 62

Aya 22-36 63

UBAINIFU 64

Aya Ya 22 64

Aya Ya 23 64

Aya Ya 24 65

Aya Ya 25 65

Aya Ya 26 65

Aya Ya 27 65

Aya Ya 28 65

Aya Ya 29 65

Aya Ya 30 65

Aya Ya 31 65

Aya Ya 32 65

Aya Ya 33 66

Aya Ya 34 66

Aya Ya 35-36 66

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 67

SURA INSHIQAAQ (KUPASUKA)( NA: 84) 67

INA AYA 24 67

UBAINIFU 68

Aya Ya 1 68

Aya Ya 2 68

Aya Ya 3 68

Aya Ya 4 68

Aya Ya 5 68

Aya Ya 6 69

Aya Ya 7 69

Aya Ya 8 69

Aya Ya 9 69

Aya Ya 10 69

Aya Ya 11 70

Aya Ya 12 70

Aya Ya 13 70

Aya Ya 14 70

Aya Ya 15 70

Aya Ya 16 70

Aya Ya 17 70

Aya Ya 18 70

Aya Ya 19 71

Aya Ya 20 -21 71

Aya Ya 22-24 71

Aya Ya 25 71

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 73

SURA BURUJ (BURUJI) (NA. 85) 73

INA AYA 22 73

UBAINIFU 74

Aya Ya 1 74

Aya Na 2 75

Aya Na 3 75

Aya Na 4 76

Aya Na 5 76

Aya Na 6 76

Aya Na 7 76

Aya Na 8-9 76

Aya Na 10 77

Aya Na 11 77

Aya Na 12 77

Aya Na 13 78

Aya Na 14 78

Aya Na 15-16 78

Aya Na 17-18 79

Aya Na 19 79

Aya Na 20 79

Aya Na 21-22 79

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 82

SURA TARIQ (CHENYE KUJA USIKU) (NA. 86) 82

INA AYA 17 82

UBAINIFU 83

Aya 1-3 83

Aya Na 4 83

Aya Na 5 84

Aya Na 6 84

Aya Na 7 84

Aya Na 8 84

Aya Na 10 84

Aya Na 11 84

Aya Na 12-13 84

Aya Na 15 85

Aya Na 16 85

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 87

SURA A'ALAA (MTUKUFU) (NA. 87) 87

INA AYA 19 87

UBAINIFU 88

Aya Na 1 88

Aya Na 2 89

Aya Na 3 89

Aya Na 4 -5 89

Aya Na 6-7 89

Aya Na 8 90

Aya Na 9 90

Aya Na 10 91

Aya Na 11 91

Aya Na 12 91

Aya Na 13 91

Aya Na 14 -15 91

Aya Na 16 92

Aya Na 17 92

Aya Na 18-19 92

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 94

SURA GHASHIYA (KIYAMA) (NA. 88) 94

INA AYA 26 94

UBAINIFU 95

Aya Na 1 95

Aya Na 2 95

Aya Na 3 95

Aya Na 4 96

Aya Na 5 96

Aya Na 6 96

Aya Na 7 96

Aya Na 8 96

Aya Na 9-16 96

Aya Na 17 96

Aya Na 18 96

Aya Na 19 97

Aya Na 20 97

Aya Na 21 97

Aya Na 22 97

Aya Na 23 97

Aya Na 24-25 97

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 99

SURA AL-FAJR (ALFAJIRI) (NA. 89) 99

INA AYA 30 99

UBAINIFU 100

Aya Na 1-4 101

Aya Na 5 101

Aya Na 6 102

Aya Na 7-8 102

Aya Na 9 102

Aya Na 11 102

Aya Na 12 103

Aya Na 13 103

Aya Na 14 103

Aya Na 15 103

Aya Na 16 104

Aya Na 17 104

Aya Na 18 104

Aya Na 19 104

Aya Na 20 104

Aya Na 21 104

Aya Na 22 105

Aya Na 23 105

Aya Na 24 105

Aya Na 25-26 105

Aya Na 27 106

Aya Na 28 106

Aya Na 29 106

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 109

SURA BALAD (MJI) (NA. 90) 109

INA AYA 20 109

UBAINIFU 110

Aya Na 1 110

Aya Na 2 110

Aya Na 3 111

Aya Na 4 112

Aya Na 5 112

Aya Na 6 112

Aya Na 7 112

Aya Na 8-10 113

Aya Na 11 113

Aya Na 12 113

Aya Na 13 113

Aya Na 14-16 114

Aya Na 17 114

Aya Na 18 114

Aya Na 19 114

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 116

SURA SHAMS (JUA) (NA. 91) 116

INA AYA 15 116

UBAINIFU 116

Aya Na 1 117

Aya Na 2 117

Aya Na 3 117

Aya Na 5-6 117

Aya Na 7 117

Aya Na 8 118

Aya Na 9 -10 118

Aya Na 11 119

Aya Na 12 119

Aya Na 13 119

Aya Na 14 119

Aya Na 15 119

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 121

SURA LAYL (USIKU) (NA. 92) 121

INA AYA 21 121

UBAINIFU 122

Aya Na 1 122

Aya Na 2 122

Aya Na 3 122

Aya Na 4 122

Aya Na 5-6 123

Aya Na 7 123

Aya Na 8 -10 123

Aya Na 11 123

Aya Na 12-13 123

Aya Na 14-16 125

Aya Na 17-19 125

Aya Na 20 126

Aya Na 21 126

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 129

SURA ADHUHAA (DHUHA)(NA. 93) 129

INA AYA 11 129

UBAINIFU 129

Aya Na 1-2 129

Aya Na 3 129

Aya Na 4 129

Aya Na 5 130

Aya Na 6 130

Aya Na 7 130

Aya Na 8 130

Aya Na 9-11 130

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 133

SURA INSHIRAAH (UKUNJUFU) (NA. 94) 133

INA AYA 8 133

UBAINIFU 133

Aya Na 1 134

Aya Na 2-3 134

Aya Na 4 135

Aya Na 5 135

Aya Na 6 135

Aya Na 7-8 136

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 138

SURA TIN (TIN) (NA. 95) 138

INA AYA 8 138

UBAINIFU 138

Aya Na 1-3 138

Aya Na 4 139

Aya Na 5 139

Aya Na 6 140

Aya Na 7 140

Aya Na 8 140

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 142

SURA ALAQ (PANDE LA DAMU) (NA. 96) 142

INA AYA 19 142

UBAINIFU 143

Aya Na 1 143

Aya Na 2 143

Aya Na 3 144

Aya Na 4-5 144

Aya Na 6-7 144

Aya Na 8 144

Aya Na 9-13 144

Aya Na 14 145

Aya Na 15 - 16 145

Aya Na 17-18 145

Aya Na 19 145

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 149

SURA QADR (QADR) (NA. 97) 149

INA AYA 5 149

Aya Na 1 149

Aya Na 2 150

Aya Na 3 150

Aya Na 4 150

Aya Na 5 151

SURA BAYYINA ( HOJA) (NA. 98) 153

INA AYA 8 153

UBAINIFU 153

Aya Na 1 154

Aya Na 2 154

Aya Na 3 154

Aya Na 4 155

Aya Na 5 155

Aya Na 6-7 156

Aya Na 8 156

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 158

SURA SILZAAL ( TETEMEKO)(NA. 99) 158

INA AYA 8 158

UBAINIFU 158

Aya Na 1 158

Aya Na 2 158

Aya Na 3 158

Aya Na 4 -5 158

Aya Na 6 159

Aya Na 7-8 159

SURA ADIYAAT (FARASI) (NA. 100) 160

INA AYA 11 160

UBAINIFU 160

Aya Na 1 161

Aya Na 2 161

Aya Na 3 161

Aya Na 4 161

Aya Na 5 161

Aya Na 6 161

Aya Na 7 161

Aya Na 8 162

Aya Na 9 – 10 162

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 163

SURA QAARIA ( KIYAMA) (NA. 101) 163

INA AYA 11 163

UBAINIFU 163

Aya Ya 1-3 163

Aya Ya 4 163

Aya Ya 5-7 164

Aya Ya 8 164

Aya Ya 10 164

Aya Ya 11 164

SURA TAKATHUR ( KUTAKA WINGI WA MALI) (NA. 102) 164

INA AYA 8 164

UBAINIFU 165

Aya Ya 1-2 165

Aya Ya 3 165

Aya Ya 4 166

Aya Ya 5 166

Aya Ya 6 166

Aya Ya 7 166

Aya Ya 8 166

SURA ASR (ZAMA) (NA. 103) 168

INA AYA 3 168

UBAINIFU 168

Aya Ya 1 168

Aya Ya 2 169

Aya Ya 3 169

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 171

SURA HUMAZA (MRAMBA KISOGO) (NA. 104) 171

INA AYA 9 171

UBAINIFU 171

Aya Ya 1 171

Aya Ya 2 171

Aya Ya 3 172

Aya Ya 4 172

Aya Ya 5 172

Aya Ya 6 172

Aya Ya 7 172

Aya Ya 8 172

Aya Ya 9 172

SURA FIL (NDOVU) (NA.105) 173

INA AYA 5 173

UBAINIFU 173

Aya Na 1 174

Aya Na 2 174

Aya Na 3 -4 174

Aya Na 5 174

SURA QURAISH (QURAISH)(NA. 106) 175

INA AYA 4 175

UBAINIFU 176

Aya Na 1-2 176

Aya Na 4 177

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 178

SURA MAUN ( MANUFAA) (NA. 107) 178

INA AYA 7 178

UBAINIFU 178

Aya Na 1 178

Aya Na 2 178

Aya Na 3 178

Aya Na 4-5 179

Aya Na 6 179

Aya Na 7 179

SURA KAWTHAR (HERI NYINGI) (NA. 108) 180

INA AYA 3 180

UBAINIFU 180

Aya Na 1 180

Aya Na 2 180

Aya Na 3 181

SURA KAFIRUN (MAKAFIRI)(NA. 109) 182

INA AYA 6 182

UBAINIFU 182

Aya Na 1 183

Aya Na 2 183

Aya Na 3 183

Aya Na 4-5 183

Aya Na 6 183

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 185

SURA NASR (MSAADA)NA 110 185

INA AYA 3 185

UBAINIFU 185

Aya Na 1 185

Aya Na 2 186

Aya Na 3 186

TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN 192

SURA LAHAB (MIALI) (NA. 111) 192

INA AYA 5 192

Aya Na 1 192

Aya Na 2 193

Aya Na 3 193

Aya Na 4-5 193

SURA IKHLAS (IKHLASI) (NA. 112) 194

INA AYA 4 194

UBAINIFU 194

Aya Na 1 194

Aya Na 2 195

Aya Na 3-4 195

SURA FALAQ (ASUBUHI) (NA. 113) 197

INA AYA 5 197

UBAINIFU 198

Aya Na 1 198

Aya Na 2 198

Aya Na 3 198

Aya Na 4 198

Aya Na 5 198

SURA NAS ( WATU) (NA: 114) 200

INA AYA 6 200

UBAINIFU 200

Aya Na 1 – 3 201

Aya Na 4 202

Aya Na 5 202

Aya Na 6 202

SHARTI YA KUCHAPA 203

MWISHO WA KITABU 203

YALIYOMO 204